Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (AGANO LA DAMU) (3) - 3

  


Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (3) 

Sehemu Ya Tatu (3)

'tutawanyikeni Kuwachanganya Kila Mmoja Apite Njia Yake'



Kila Mmoja Akapita Njia Yake,kule Nyuma Watu Tatu Walijua Ndo Walikuwa Wakiwakaribia Kutokana Na Mbwa Wao Kuzidi Kubweka,ubwekaji Ule Ukawapa Hari Nguvu Ya Kuzidi Kukimbia!



Mbio, Mbio, Mbio,



ghafla katika njia panda moja mbwa wale wakasimama!



ni pale walipogawanyika kila mmoja akapita njia yake Wale Nao Wakagawanyika Sambamba Na Wanajesh Wale Kila Mmoja Kwenda Upande Wake!



Hali ya mtafutano hali ya kivita ikatawala baina yao wazo lililokuwa kwa wanajeshi Wa mwaka Wa Tatu ni kuua tu

Kwani wanafunzi walosemekana kutaka kutoroka ndani ya kambi ile tena wakiwa na silaha walipofika uraiani walikuwa ni majambazi ivyo ikishtukiwa kuna watu wanatoroka adhabu yao ni kifo!!!



Yule aloelekea upande Wa kushoto alizidi kukimbia sasa pumzi zilimuishia,akawa akihema ghafla akaanza kuona kizungu zungu chini!



Habari Yake ikawa imeishia hapo!



Mbwa alipomfikia akammalizia



Upande Wa kulia mwanajeshi alokuwa nyuma Yake alipomuona tu akanyoosha silaha risasi zikatuagongoni mwake

Akaporomoka chini,huu nao ukawa mwisho wake



Wakawasiliana na kupeana taharifa wanajeshi wale ila tatizo redio call ya yule alonyoosha njia iliita tu bila kupokelewa

Hii ikawa ni kama alama ya hatari vichwani mwao

Kushoto akambeba mtu wake,kulia napo akambeba mtu wake wakakutana njia panda pale walipogawanyika



"Sasa tufanyaje?! Morn apatikan kapatwa na tatizo nini

mi naona tujulishe kambini mwaka wa pili wote wakaguliwe ikiwezekana tutumiwe rct tukague msitu wote huu kabla ajatoka nje ya mji



tukisema tuwafate kwa njia hii saiv watakuwa washafika mbal nakama Morn Kauwawa Huyu Mtu Atakuwa Hatar adhibitiwe Haraka sana!



Muda Ule Ule Wakawajulisha Kambini,kengele Ikagongwa Ukaguz Ukaanza Mara Moja Ni Mwanafunz Gan Ambaye Ayupo!



Wakat Ukaguz Ukiendelea Roketi Yenye Satelite Ikiwa Na Wanajesh Watat Ikatumwa Katika Msitu Ule Kukagua Mwanafunz Mmoja Yupo Wap?



Huku Chuoni Isack Akatambulika Ndiyo Mwanafunz Ambaye Ayupo!...



Kizaazaa...







ISACK anaingia katika hatari ingine ni baada ya kutoroka kambini kwa nia ya kutembelea mahafali katika chuo cha st lucy lengo ni kwenda kuonana na Mery!



Je Ninin Kilichoendelea?! Twende Pamoja Kujua Mwendelez Wa Riwaya Hii



NA HII NI SEHEMU YA SITINI NA SABA



Isack Alizidi Kukimbia,ila Mwisho Aligundua Anaishiwa Pumzi,pia Kwa Sasa Alisikia Sauti Ya Mbwa Mmoja Akupata Tabu Kugundua Kuwa Lazima Walokuwa Wakiwakimbiza Walipofika Njia Panda Walijigawanya akuona sababu ya kuendelea kukimbia akakikabili kichaka kilichokuwa karibu yake,macho yake yakatazama ule upande alotokea!



Ni Kama Dakika Moja Tu Alionekana mbwa akija kwa kasi nyuma yake akifatiwa na mwanajeshi



akashika bastola yake vizur na kumlenga yule mwanajeshi palepale akaachia risasi zilizompata vyema mtu yule kifuani! akaenda chini,



bastola akaielekezea kwa yule mbwa risasi kadhaa zikachomoka na kumwendea mbwa yule,naye akadondoka na kufia pale pale!...



sasa Isack Akatoka Katika Kichaka Kile Na Kuanza Kukimbia,ile Ilikuwa Ni Hatari,naye Kwa Muda Ule Alikuwa Ni Hatari,wakati Akiendelea Kukimbia Ghafla Akasikia Mlio Juu Akainua Shingo Yake Juu Kuangalia Ilibakia Kidogo Angezirai Kwa Kile Alichokiona!



kwa haraka sana akaenda chini na kuanza kutambaa kama nyoka,



kule ndani ya roketi walizidi kusachi kupitia satelite mazingira ya chini,ghafla satelite yao ikamnasa Isack Taratibu Ikaanza Kushuka



Isack Alizidi Kutambaa Lakin Ghafla Alishughudia Ile Sateline Ikishuka Wakati Akiendelea Kushangaa Aliona Maaskari Tena Walovaa Jacket Proof Wakishuka!



'huu Sasa Ni Mwisho Wangu'

Akajiwazia Akijaribu Kuendelea Kutambaa Kabla Ajashtushwa Na Sauti Kali

"isack Tunakuomba Usamli Amri Hapo Hapo Ulipo Simama Tupa Silaha Mbele Na Upge Magoti Unyooshe Mikono Mbele!'

Tayari Alishazingirwa Na Alipaswa Kujiokoa Afanye Kile Alichoambiwa!...



Akasimama Na Kutupa Silaha,kama alivyoagizwa!

japo alikuwa jasiri,ila hiyo aikuzuia machozi kumchuruzika!



alijua sasa mwisho wake umefika,akajuta kwa kutoroka kambini,ila alikiri ni kwel alimmis Mery Na Lengo Lake La Kutoroka Ni Kwenda Katika Mahafal Akamchukue Mery Na Hata Ikiwezekana Siku Hiyo Ndo Aiyanze Kwa Kumuua Bray Kwa Kosa La Kumuulia Mpz Wake Alice!



Matokeo Yake Visas Vyake Asingetekeleza,Mery wake asingemuona tena!

Machozi Ya Majuto Yakazidi Kumchuruzika!...



ST LUCY COLLAGE



Ni wakati mahafali yale yakiendelea,ndani ya chuo cha St Lucy Collage!



Ulinz Uliimarishwa Nje Na Hata Ndani Ya Chuo Kile Hii Ni Kutokana Na kuwepo kwa viongoz wa ngazi za juu wa serikal wa nchi mbalimbal wakiwemo , marais,mawazir,wabunge mabalozi!



ugawaji wa vyeti sambamba na zawadi ukamalizika salama!



wanachuo wakawa wakirudi kwenye mabweni yao huku wakiwa wameshika mazawadi walozawadiwa na ndugu jamaa na marafiki!



Mery Akiwa Chumban Kwake Aliendelea Kukagua Zawadi Zake Na Ghafla Alifungua Bahasha Moja Akatoa Macho Ya Mshangao Kwa Kile Alichokiona!



Kile Kilichokuwepo Ndani Ya Bahasha Ile!



Zilikuwa Ni Picha Kadhaa,ambazo Ziliambatanishwa Na Barua!



Picha Zile Zilikuwa Tatu,moja Ilimuonesha Isack Akiwa Hosptalin Kipind Iko Wakiwa Wadogo Naye



Mery Akiwa Pembeni,picha Ya Pili Ilimuonesha Isack Akiwa Katikat Ya Pori Wakiwa Wamefungwa Kamba Mtini! Mery Akimwangalia Isack Kwa Macho Ya Huruma,na Picha Ya Tatu Ilimuonesha Mpz Wake Bray Akimshindilia Kisu Alice



Mery Alichoka Akajaribu Kuvuta Kumbukumbu Alompa Bahasha Ile Ila Walotoa Zawadi Walikuwa Ni Wengi Hivyo Akuweza Kukumbuka!

Haraka Sana Akazirudisha Zile Picha Kwenye Bahasha Yake!

Akatoa Na Ile Barua Iliandikwa Maneno Machache Tu

'najua Unajua Nimekufa Ila Nipo Hai,nakupenda Mery' Chini Ikaandikwa Jina La Isack!



'isack?!' No! Akukumbuka Kama Aliiona Sura Ya Isack,isack Yupo Hai,ina Maana Bray ndo aliyemuua alice ili isack afungwe?!



hapana ilikuwa ni lazima achunguze ikiwezekana asirudi Tanzania Mpaka Ampate Isack!

Lazima Achunguze Jambo Lile Wakumwambia Ukweli Ni Nani Mdogo Wake!...



Ndiyo Yeye Pekee Ndo Wakumfungua Katika Fumbo Lile Lililomtatiza!



Ushahid Wa Picha Alikuwa Nao



Bas Taratibu Alimfata Mdogo Wake Na Kumuita Pembeni,wakateta Kidogo Wakatoka Nje Ya Bwen Lile Ilikuwa Ni Mida Ya Jioni Jion

Wakaelekea Uwanjani Baada Ya Mery Kuitaj Kwenda Kuongea Na Mdogo Wake Eneo Lenye Utulivu!



Muda Ule Spack Alikuwa Akitokea Toilet Kwa Mbali Alimuona Mery Na Mdogo Wake Wakiongozana Kuelekea uwanjani kwa tahadhar sana akaanza kuwafata kwa nyuma!



"Agnes naomba nieleze ukwel! kuhusu maisha yangu vip nilishapotezaga fahamu na isack tunamahusiano gani naye?"



"isack?,isack yupi yule mwanachuo aliyemuua alice"



"isack akumuua alice!"



Muda Huo Spack Alikuwa Kajibanza Akiwasikiliza!



"unasema? Kama Si Isack Ni Nani Sasa?"



Mery Akamkabidhi Zile Picha Kwenye Ile Bahasha!

Agnes Akazitoa!



Macho Ya Mshangao Yalimtoka!,



"hizi Picha Si Za Kwel Dada!...



Palepale Akataka Kuzichana Ila Mery Akawah Kumponyoka,muda Ule Ule Spack Akajitokeza,Mery akanyamaza kimwa mkono uloshika picha akauweka nyuma kusudi sparc asione!



"aina aja ya kumficha dada yako mueleze ukweli,kama uliyenieleza mimi!"



"ukwel gani spack?! naomba ukae mbal na maisha yetu!"



"mueleze ukwel wa maisha yake ayatambue kwa nin umfiche?!"



"naomba uondoke Spack Haya Ayakuhusu!"



"naomba Nieleze Shem Ukwel Gan Unaoujua Kuhusu Maisha Yangu?"



"siwez Kukuelezea Kitu Shem Muombe Huyo Huyo Mdogo Wako Akueleze!...



Wakat Wakiendelea Kubishana Pale Ghafla Bray Kwa Mbal Alionekana Akija Ikawalazimu Wabadilishe Mada!



Ila Mery Alikuwa Kapania Kuujua Ukwel Hata Kwa Kutumia Nguvu!



Je Ni Nan Aloleta Zile Picha?,Mery ataujua ukwel? na atachukua maamuz gani







Isack Anafanikiwa Kuwashawish Wenzake Watatu Kuelekea Katika Chuo Cha St Lucy Katika Mahafali!...



Inawalazimu Kupita Katikati Ya Pori Kabla Ya Kufika Mjin Mahal Kilipo Chuo Hiko



Kwa Bahati Mbaya Wanagunduliwa Na Wanajeshi Kadhaa Kutumwa Wenzake Wanauwawa,isack Anatiwa Nguvuni Je Nin Kiliendelea?



Songa Nayo!...



SEHEMU YA SITINI NA NANE



OFISINI kwa mkuu wa kambi ile alikwepo mh waziri wa ulinz mh alfonsor usoni akionekana kuwa na hasira,



mbele yake kwenye kiti alikaa Isack Akiwa Kifua Waz Mwili Wote Ulichanwachanwa Kwa Kipigo,suruali Ya Kijesh Aloivaa Ilitapakaa Damu!



"unafanya Nin Isack,kwa Nin Unakuwa na akili mbovu kiasi iko kwa nin usivumilie huo mwaka mmoja ulobakia ndo ukaenda lipiza kisasi unaona sasa umesababisha vifo vya wenzako wanne kwa nin unakuwa ivyo?!...



mh Alfonsor Aliongea Kwa Uchungu Ni Baada Ya Isack Kumuelezea Kuwa Lengo La Kutoroka Alikuwa Anataka Kwenda Kuianza Kazi Yakumuua Bray,



"usiwe Na Haraka Isack Kaz Utafanya We Vumilia Tu Sawa"



"sawa Mkuu!"



Mh Wazir Akaongea Na Jemedar Mkuu Wa Pale Wakayamaliza!

Isack Akasamehewa Akaendelea Na Masomo Kama Kawaida!



Usiku Disco Lilianza Wanafunzi Walicheza Kwa Furaha,ila Moyon Kwa Mery Akukuwa Na Furaha Kabisa!



"mpenz Twende Basi Tukacheze?



Bray Alimbembeleza Mery Wakacheze Ila Mery Akuwa Tayari,alijikuta Akimchukia Bray Kupitiliza



"najiskia Vibaya Bray Wacha Nikapumzike Ndani!"



Taratibu Akatoka Ndani Ya Ukumbi Ule Na Kuelekea Upande Wa Yalipo Mabweni Yao,



Akalngia Na Kujitupa Kitandani Akaanza Kuzitazama Zile Picha!

ITAENDELEA

Simulizi : Kiapo (Agano La Damu) (3) 

Sehemu Ya Nne (4)



Ghafla Mlango Ukafunguliwa Aliyeingia Alikuwa Ni Mdogo Wake Agnes!



"dada Unatatizo Gani Mbona Una Raha?"



"naomba Nieleze Ukwel Kuhusu Maisha Yangu Na Isack"



"ukweli Gan Lakini Dada!"



Ghafla Mery Akachukua Begi Lake Akatoa Vidonge...



"nipo Tayari Kufa,ila Kama Unanithamini Mimi Dada Yangu Naomba Nieleze Ukweli Lasivyo Navimez...



"dada unataka kujiua kwa sababu gani lakini,kipi ninachokuficha mimi?!...



Muda Ule Ule Mery Akawa Sasa Akivitupia Vidonge Vile Mdomoni Ila Egnes Akawai Kumzuia!



"acha Ntakwambia Ukweli Dada,nikweli Ulipoteza Fahamu!"



"nlipoteza Fahamu?,kitu Gani Kilichopelekea Nipoteze Fahamu Na Kwa Nini Ulikuwa Utaki Kunambia?!"



"ulipoteza Kumbukumbu kwa Sababu Ya Isack Na Baba Alintishia Kuficha Siri Hii Na Ikiwa Ntakueleza Basi Atatuuwa Sote Wawili"



Ikabidi Sasa Janeth Aanze Msimulia Mery Kila Kitu Kwanzia Mwanzo Mpaka Mwisho!



Mery Akuamin,moyo Wake Ulimuuma Kwa Yale Alomtendea Isack,kumbe Baba Yake Ni Mbaya Kiasi Kile,ila sasa je alomtumia zile picha ni nani!,na kwa nin alimtumia!,



au Isack Yupo Hai,akuwa Na Uhakika Wa Jambo Hilo Akamtoa Khof Mdogo Wake,kwamba Atofanya Mabadiliko Yoyote Kugundulika Kwamba Amejigundua Kama Alipoteza kumbukumbu!



Lakini Moyoni Mwake kulijenga chuki kali dhidi ya baba yake na ya yule alomwona mpz wake Bray Mwanaume Alompa Upendo Wake,kumbe Alimnyang'anya Rafki Yake Kipenz Isack Na Kumtengenezea Kesi Mwenzake Akafungwa Na Kunyongwa Ila Alipanga Kuchunguza Juu Ya Isack!...



Akaziifadh Zile Picha

Akutaka Kumuonesha Chuki Yoyote Bray!



Kesho Yake Wakafungasha Vitu Tayari Kurudi Tanzania!...



TANZANIA



Uwanja wa ndege wa kimataifa ulikuwa na ulinz wa kutosha ni kama kiongoz mkubwa alikuwa akija nchini!

viongoz mbalimbal wa nchi walikwepo uwanjani pale!



Ndege Ilokuwa Ikisubiriwa Hatimaye Iliwasili Ndani Ilibeba Watoto Wa Viongoz Wa Kubwa Wakubwa,akiwemo Kina Mery Na Bray



Mh Max Malwal Rais Wa Jamhur Ya Muungano Wa Tanzania Na Mwenzake Mh Alex Walikuwa Pamoja Kuwasubiria Watoto Wao!



Walikuwa Wakijua Juu Ya Mahusiano Yao Japo Wenyewe Waliyafanya Kwa Siri,na Leo Hii Walitaka Wawasapraiz!



Yalikuwa Nimapokez Ya Pekee Kwao,baada Ya Watoto Wale Kushuka,kila Mmoja Akaenda Kwa Mwenyej Wake,mzee Alex , mr max wakapeana ishara kila mmoja akampokea mtoto wake,wakaingia kwenye magari safar ya kutoka uwanjani ikafatia!



"baba tunaelekea wapi?"



Mery Alimuuliza Baba Yake



"hotelin Kuna Sapraiz Yako!"

Ndivyo Alivyojibiwa,hata Kwa Upande Wa Bray Naye Alimuuliza Baba Yake Naye Alijibiwa Ivyoivyo!



SEVEN EAR HOTEL



Wakwanza kuwasili katika hotel ile ni mh alex na wanawe...



wakashuka na kuingia ndani ya hoteli!



Si Mery Pekee Alopigwa Na Butwaa Kwa Kile Alicho Ona Hata Kwa Mdogo Wake Egy,

Ukumbi Ulipambwa ukapambika



Welcome Bray & Mery



Ilikuwa Ni Sapraiz Ambao Aikutegemewa,msafara Wa Rais Ukawasili,



Kama Ilivyokuwa Kwa Mery hata Bray Pia Alishtuka!,alishindwa Hizuia Furaha Yake Kwenda Kumkumbatia Mery!

Hapo Ndipo Bendi Maalumu Ilipotokea Na Kuanza Kuburudisha!



Waandishi Mbalimbali Walikwepo Kuripoti Tukio Lile Ilikuwa Ni Kama Siku Ya Harusi!

Waalikwaji Mbalimbali Walikwepo...



Pasina Kutegemea Siku Hiyo Ilipaswa Wavalishane Pete!



Ratiba Ikaanza!,Isack na Mery Wakaitwa Mbele

Katika Meza Kulikuwa Na Sahani Moja Ya Dhahabu Ilofunikwa Bray Akapewa Idhin Aifunue

Naye Akafunua Alitoa Macho Akaweka Mkono Mdomon Kwa Mshangao!



Uzuri Wa Pete Aloiona Hata Yeye Binafsi Katika Tembea Yake Akuwai Kuiona,taratibu Akapeleka Mkono Wake Kuichukua Pete Ile!



"prince Wetu Utamvisha Pete Hiyo Malkia Wako!"



Watu Wakashangilia,Mery kitendo kile akikumfuraisha,yule alikuwa ni adui yake aliyemuulia mpz wake,yeye kukubali kuvishwa pete ile ule ni usaliti,akajikuta machozi ya hasira yakimchuruzika,akaweka mkono wake nyuma! ishara ya kukataa bado machoz yaliendelea kutiririka kama bomba la maji!



Bray Akabaki Kaishika Pete Yake,huku Akishndwa Kulizuhia Butwaa Lake Kum'butwikia



Wakati Hayo Yote Yakiendelea Maeneo Ya Parking Katika Gari Moja Jeusi alionekana mtu mmoja alokuwa kavaa kepu kuficha sura yake akiikazia macho ile gari ya mh rais alokuja nayo!



Ghafla mlango wa gari ya mh rais ukafunguliwa akashuka dereva na kuelekea maeneo ya vilipo vyoo...



mtu yule naye akashuka



akistaajabu ulinzi ulokwepo pale akaelekea upande ule ule alipoenda dereva!



akasimama nje ya choo kimoja kilichokuwa kimefungwa,hakuwa na shaka dereva yule atakuwa ameingia mule!



kama dakika moja na nusu mlango ukafunguliwa ila kabla mtu wa ndani (dereva) ajatokeza nje jamaa aliusukuma kwa ndani mlango ule,naye akazama...



alipotoka alikuwa kavaa nguo za yule dereva suti uson alipiga miwani...



akaufunga ule mlango kwa nje,yeye akatoka akaelekea mpaka lilipo gari la muheshimiwa rais akaingia ndani



alitumia kama dakika nyingine tatu akatoka ndani ya gari lile akarudi zake kule chooni



akaingia kwenye choo kile kile alipotoka,alikuwa kavaa nguo zake zile za awali!



akarejea kwenye gari yake na kujiingiza ndani!



"taratibu fata maelekezo yangu usilete ubishi sitosita kukwangamiza aya we ni nan na umeweka nin kwenye ile gari!



alishtushwa na sauti kavu,macho yake akayaelekeza katika saidmirror aliyemuona ilibaki robo azirai!

alijiingiza matatani!

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog