Simulizi : Ulimwengu Mzima Kiganjani Mwa CIA
Sehemu Ya Tano (5)
Allen Dulles ni kaka wa John Dulles, waziri wa mambo ya nje wa Marekani (Secretary of State) wakati wa utawala wa Rais Dwight Eisenhower ambaye ndiye amerithiwa na Kennedy miezi mitatu iliyopita, kwa hiyo inahitaji kujitoa ufahamu kumgusa mtu kama Allen Dulles. Na Kennedy alijitoa ufahamu na kumfuta kazi Allen Dulles mtu ambaye anapendwa na kuhusudiwa na majasusi wa CIA pengine kushinda hata Kennedy mwenyewe, Karatasi ya juu ya ripoti rasmi ya CIA ambayo ndani yake kuna baadhi ya paragraph zikionyesha kuwa CIA hawakuridhishwa na namna ambavyo Kennedy alifanya maamuzi juu ya kukataa mashambulio ya anga.
Wengine huenda mbali zaidi na kusema kwamba uvamizi wa Bay of Pigs ndivyo iliyochangia kifo cha Kennedy, kutokana na madhira ya vita vyenyewe na athari ya vita kwa CIA kuipoke kwa mtazamo kuwa John F. Kennedy kama chanzo ya Marekani kushindwa vita hiyo, japo hakuna ushahidi ulio wekwa wazi kuhusu hili.
Sababu ya Cuba kushinda na Marekani kushindwa uvamizi wa Bay of Pigs...
Kuna sababu nyingi zinazotolewa juu ya ushindi huo kwa Cuba. Mosi, ni taarifa za kiintelijensia kuwafikia mapema kupitia vyanzo vyao vya ndani ya Marekani, Baadhi ya duru hubainisha kuwa vyombo vya habari nchini Marekani hasa magazeti vilikuwa vikiripoti juu ya operesheni hiyo ya mafunzo ya siri, jambo lililosababisha Havana kupata taarifa mapema na kujiandaa vilivyo, sambamba na kupenyeza mashushu watiifu wa Castro ambao walijifanya waasi wakati upande wa pili walitii serikali ya Havana na kupeleka taarifa zote kwa Castro kupitia mashushushu wa mtaani, hii ni kwamba askali hao watiifu walipokuwa kambini walitoa taarifa zote zinazoendelea kwa raia wa Cuba ambao walilikuwa wafanya biashara ambako askali hao walikuwa wakienda kupumzika baada ya mafunzo.
Pili, inadaiwa kuwa kikosi hicho kujikanganya kwenye eneo mahsusi la kuingilia kisiwani, na kujikuta wakitia nanga Playa Giron au Bay of Pigs kimakosa, mkakati wa awali ulikuwa ni kuwa ni kikosi hicho kutia Nanga eneo la Bay of Pigs upande kusini mashariki, yani kilomita 1.7 upande wa chini ambao gridi reference yake ni 27ES na 57NE, eneo ambalo kulikuwa na miinuko ya miamba ambayo ingewapa urahisi wa kutoonekana kwa urahisi kwa askali wa Cuba, kinyume chake walijikanganya na kutia nanga eneo la kusini ambalo lipo wazi hivyo ilikuwa rahisi kushambuliwa kwa uwepesi.
Tatu, na mwisho, ni kwamba hali mbaya ya hewa na uwazi kimwonekano wa eneo la Bay Of Pigs walilotia nanga, Inadaiwa kwamba ilikuwa rahisi kwa makamanda wa Cuba kuwamaliza wavamizi sababu ya eneo hilo kuwa wazi na rahisi zaidi kwenye shabaha kutokea mafichoni.
Serikali ya Marekani haikukubaliana na matokeo ya kushimdwa vita ile hivyo Raisi Kennedy akataka uchunguzi ufanyike ili kubaini sababu za Marekani kushindwa vita ile, hivyo akaitaka ofisi wa utafiti chini ya Maxwell kuendesha uchunguzi ili kubaini hasa kwanini Marekani imeshindwa vita hiyo ya uvamizi wa Bay of Pigs.
Tume ya Maxwell Taylor Commission...
Mnamo tarehe 22 Aprili mwaka 1961, Rais Jonh F. Kennedy aliunda tume na kumteua Jenerali Maxwell D. Taylor, pamoja na Mwanasheria Mkuu Robert F. Kennedy, Admiral Arleigh Burke na Mkurugenzi wa CIA Allen Dulles, tume hii ilijulikana kama Maxwell Taylor commission, tume hii iliundwa ili kutafiti sababu za Marekani kushindwa vita ile ya Cuba, baada ya tume hiyo kufanya shuguri zote za kiuchunguzi, Jenerali Taylor aliwasilisha ripoti ya tume yake ya Uchunguzi kwa Rais Kennedy mnamo tarehe 13 Juni mwaka 1961, tume hiyo ilielezea sababu za Marekani kushindwa vita ile ni kwa ukosefu wa taarifa za uhakika na za mapema kwa raisi, pia tume ilielez kuwa sababu nyingine ni operation hiyo kuendeshwa kwa njia za siri, kitu ambacho vyombo vingine vilishindwa kushirikishwa ili kutoa ushauri wa kitaalam, tume hiyo pia iliiulaumu utawala wa Kennedy kwa kushindwa kuidhinisha mashambulizi ya ndege kwa wakati, pia tume iliuulaumu uongozi wa CIA kwa kutumia ndege zisizofaa, mambo mengine ambayo tume ilieleza ni pamoja na mapungufu ya silaha, marubani ambao awakuwa na uzoefu wa kutosha na eneo la Bay of Pigs na Cuba kwa ujumla.
Pia tume ilieleza suala la mashambulizi ya angani kutokutekelezwa ipasavyo, utawala wa Kennedy kitofuata mkakati uliowekwa na mtangulizi wake.
Ripoti ya tume hiyo ilikuwa na kurasa 201, hata hivyo baada ya ripoti hiyo kutolewa na kuwekwa hadharani ilikutana na ukosolewaji mkubwa, tume hiyo ilionekana kuwa na upendeleo ulioegemea kumshambulia raisi Kennedy pamoja na Mwanasheria Mkuu Robert F. Kennedy ndugu yake Rais Kennedy.
Mika 20 baada ya riporti hiyo ya Maxwell Taylor commission, Jack Pfeiffer, ambaye alifanya kazi kama mwanahistoria wa CIA hadi katikati ya miaka ya 1980, alitoa taarifa juu ya Marekani kushindwa mapigano ya Bay of Pigs kwa kunukuu taarifa ambayo Raúl Castro, kaka wa Fidel, alikuwa ametoa kwa mwandishi wa habari wa Mexico mnamo 1975, ambayo inasema kuwa ushindi wa vita ile kwa Cuba ulitokana na hofu ya Raisi Kennedy Juu ya Urusi na uchanga wake Juu ya maswala nyeti ya nchi, Raul Castro alikili wazi kuwa kama vita ile ingefanywa na mtangulizi wa Kennedy Raisi Dwight Eisenhower ingeifanya vita ile kuwa ngumu.
Ripoti ya Siri ya CIA...
Mnamo Novemba 1961, Mkaguzi Mkuu wa CIA Lyman B Kirkpatrick aliandika ripoti juu ya Utafiti wa Operesheni ya Cuba ripoti ambayo ilibaki kuwa siri (classified) hadi mwaka 1998, miaka 37 baadae ndipo ilipo wekwa hadharani kwa umma yani disclassified, ripoti hiyo ya CIA ilionesha mambo kadhaa yaliyopelekea Marekani kushindwa vita ile ambayo ni pamoja na;
Mosi, Marekani Kushindwa kutathmini kiuhalisia hatari na kuwasiliana vya kutosha na viongozi pamoja kukosekana kwa habari sahihi juu ya operation hiyo mezani kwa Raisi Kennedy na pia upatikanaji hafifu wa maamuzi ya ndani ya CIA na wakuu wengine wa serikali.
Pili, kukosekana kwa ushiriki wa kutosha wa viongozi wa serikali ya Kennedy na askali wa brigade 2506 katika uhamishwaji.
Tatu, CIA kushindwa kuandaa mpango huu vizuri ili kuwahusisha pia upinzani wa ndani ya Cuba, ambao wangesaidia sana kuhujumu serikali ya Castro kipindi ambacho vile ikiendelea.
Nne, CIA kushindwa kukusanya taarifa kwa ufanisi na kuzichambua taarifa hizo za kijasusi kuhusu vikosi vya jeshi la Cuba.
Tano, Ukosefu wa sera thabiti au mipango ya dharura kutoka ndani ya serikali juu ya operation hiyo.
Matokeo ya Marekani kushindwa vita ile ilipelekea mgogoro mkubwa kwa viongozi wa Juu wa CIA na serikali kuu hasa kuanzia Mkurugenzi wa CIA Allen Dulles, Naibu Mkurugenzi wa CIA Charles Cabell, na Naibu Mkurugenzi wa Mipango Richard Bissell wote walilazimishwa kujiuzulu mapema mwaka wa 1962.
Baada ya vita ile uhasama baina ya Cuba na Marekani uliongezeke na Marekani ilihaidi kulipiza kisasi kufatia aibu iliyopata mwaka 1961 katika vita ile ya Bay of Pigs, kufatia hatua hiyo ya kuzorota kwa diplomasia ya mataifa hayo ilipelekea kuongezeka kwa msuguano wa vita baridi, hasa mvutano baina ya Urusi na Marekani, mivutano hii ilipelekea viongozi wa Juu wa nchi hizo kuwekeana vitisho na Urusi kuionya Marekani kuacha kuthubutu kuivamia Cuba.
Jambo hili nimelielezea huko nyuma, nilisema mara zote Marekani ilihofu kuchochea mgogoro wowote na Cuba kwa kuhofia kuibuka kwa vita baina ya Marekani na Urusi, lakini baada ya Marekani kushindwa vita ile ya Bay of Pigs ilipelekea Marekani kujitafakari upya dhidi ya usalama wake dhidi ya Cuba na hasa hasa Urusi yenyewe ambayo ndio ilikuwa kiranja mkuu wa ujamaa duniani.
Basi bwana...
Marekani ikaanza kujiimarisha na kujiimarisha katika muungano wao wa NATO, hii NATO ni muungano wa mataifa ya kibepari kujihami dhidi ya mataifa ya kijamaa, hivyo Marekani na NATO wakaanza kujiandaa ili kuidhibiti Urusi, maana walijua wakidhibiti Urusi watakuwa wameidhibiti Cuba, baada ya Urusi nao kujua hilo nao wakanza kujizatiti ili kuidhibiti Marekani, ndio Urusi wakaunda umoja wao wa Warsaw Pact.
Kufatia hilo muungano huo wa mashariki kwa kipindi hicho ulioitwa Warsaw Pact ulianza kikao chake cha dharula mwezi February mwaka 1962 na ilipofika mwezi April mwaka 1962 walifikia uamuzi wa kuingia katika vita kamili ya kujihami dhidi ya umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO
Jumla ya askari 400,000 kutoka nchi mbali mbali za umoja wa kujihami wa nchi za mashariki walianza kusogea mipakani mwa nchi zao kujiandaa na vita dhidi ya umoja wa kujihami wa nchi za magharibi NATO
Ilipofika August mwaka 1962 meli za kivita za Urusi zikiwa zimebeba askari zaidi ya 100,000 pamoja nyambizi zilizobeba silaha kali za nyuklia zilitia nanga kisiwani Cuba
Dunia yataharuki...
Mwezi September mwaka huo wa 1962 Rais wa Urusi wa wakati huo Nikita Khruschev aliwahakikishia nchi washirika wake wa mashariki kuwa endapo askari hata mmoja wa NATO angevuka mpaka na kuingia katika nchi zao basi nae angejibu mapigo kwa kuangamiza sehemu kubwa ya nchi ya Marekani hususani majiji ya New York na Miami, Kwani tayari nae alikuwa ameshaweka silaha kali za nyuklia mkabala na nchi ya Marekani, Inaonekana kabisa kuwa silaha hizo zilipelekwa kwa siri katika nchi ya Cuba.
Tamko hilo la Rais Nikita Khruschev lilizua hali ya taharuki ndani ya nchi ya Marekani, Haraka sana idara ya ujasusi ya nchi hiyo CIA ilifanya upelelezi wa haraka na kugundua kuwa ni kweli kabisa silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuangamiza taifa la Marekani zilikuwepo katika kisiwa cha Cuba mkabala na nchi ya Marekani
Vita kamili...
Tarehe 12 October 1962 bunge la Marekani lilikutana na kwa pamoja lilipitisha azimio la kuivamia nchi ya Cuba kwa haraka sana, Rais John F Kennedy Sasa alikuwa kwenye shinikizo kubwa sana la kutangaza vita ambayo kwa hakika ingekuwa ndio vita kuu ya Tatu ya Dunia, Akilihutubia taifa la Marekani usiku wa tarehe 16 October Rais Kennedy alisema kuwa kamwe taifa la Marekani halitoweza kuvumilia kitendo hicho cha kutishiwa usalama wake na akasema kuwa jeshi la Marekani litakwenda nchini Cuba kuziondoa silaha hizo kwa nguvu kwa sababu njia zote za amani zilikuwa zimeshindikana
Tayari jumla ya askari wapatao 300,000 pamoja na meli za kivita pamoja na ndege za kivita ziliwasili katika jiji la Miami kujiandaa kuivamia nchi ya Cuba, Meli kubwa kabisa za kivita za Marekani zilisogea karibu kabisa na kisiwa cha Cuba tayari kuanza mashambulizi ya kukiteka kisiwa hicho, Majeshi ya Cuba na Urusi nayo yalijibu mapigo kwa kusogeza vikosi vyake katika fukwe za kisiwa hicho mkabala na Majeshi ya Marekani
Uwanja wa mapambano...
Meli za kivita za Urusi zikiwa zimebeba silaha kali kabisa za nyuklia zikiwa Sasa zinakabiliana ana kwa ana na meli za kivita za Marekani, Tarehe 27 October 1962 ni siku ya kukumbukwa sana Duniani, Siku hiyo wizara ya ulinzi ya Marekani ilitoa amri kwa ndege zake za upelelezi za kivita kuingia katika anga ya Cuba, ndege hizo zilikuwa na kazi ya kuangalia Majeshi ya adui yamejipanga vip ili kuweza kukabiliana nayo, Ndege hizo ziliweza kuonekana na rada za Majeshi ya Urusi na mara moja walianza kuzishambulia.
Majeshi hayo ya Urusi yalifanikiwa kuangusha ndege moja ya upelelezi ya jeshi la Marekani jioni ya siku hiyo ya tarehe 27 October 1962 na kusababisha kifo cha askari wa jeshi la anga la Marekani luteni Rudolph Anderson, Kifo cha rubani mdogo mwenye umri wa miaka 34 Luteni Rudolph Anderson kilimsikitisha sana Rais John F Kennedy, Asubuhi ya tarehe 28 October 1962 Rais Kennedy alikwenda hadi nyumbani kwa familia ya marehemu kutoa salamu za rambi rambi.
Katika Hali ya kuhuzunisha sana Rais John F Kennedy alianza kulia baada ya kumuona mke wa marehemu akiwa mjamzito na pia aliwaona watoto wadogo wa marehemu mmoja akiwa na miaka 5 na mwingine akiwa na miaka 3, taarifa za kuangushwa kwa ndege ya kivita ya Marekani zilienea kwa kasi sana Duniani na Kila mtu alijua tayari Sasa Vita imeanza, Jeshi la Uingereza usiku wa siku hiyo lilituma kikosi maalum cha makomandoo kwenye mstari wa mbele wa kivita huko mashariki ya ulaya
Vasil Arkshipov aiokoa dunia...
Usiku wa siku iyo ya tarehe 27 October 1962 nyambizi ya kivita ya Urusi B-59 ikiwa imebeba silaha kali za nyuklia ikiwa chini kabisa ya bahari pasipo kuonekana na rada za Majeshi ya Marekani ilisogea karibu kabisa na pwani ya Florida ili kuanza mashambulizi endapo jeshi la Marekani lingeanzisha vita.
Nyambizi hiyo iliongozwa na Captain Savitsky pamoja na Admiral Vassil Arkhipov iliingia usiku huo karibu na Florida, Ikiwa chini kabisa ya bahari walianza kuhisi kufuatiliwa na nyambizi za jeshi la Marekani.
Wasilokuwa wakilijua askari Hawa wa Urusi ni Kwamba nyambizi hizi za jeshi la Marekani zilikuwa katika doria yake ya kawaida na wala haikuwa ikiifuatilia nyambizi hiyo ya Urusi, Kwa kuwa walikuwa chini kabisa ya bahari hawakuwa na mawasiliano yoyote na wenzao, Kulinganisha na hali waliyokuwa wameiacha Cuba Nahodha wa nyambizi hiyo Captain Savitsky alijua kabisa kuwa Sasa Vita imeshaanza na kwa maagizo waliokuwa wamepewa ni kusubiria vita ianze na kushambulia pwani za Florida kwa makombora ya nyuklia.
Haraka sana Captain Savitsky alitoa amri ya kufyatua makombora ya nyuklia kwa nyambizi za Marekani na pia kwenye fukwe za Florida zilipokuwa kambi za kijeshi na kituo cha kijeshi cha Marekani kwa wakati huo, Ili kutekeleza amri hiyo ilihitajika idhini ya Admiral Vassil Arkhipov.
Vassil alikataa kata kata kuachia makombora ya nyuklia kwa nyambizi za Marekani akisema kuwa swala zito kama hilo linahitaji amri na idhini kutoka Moscow na sio kwa yoyote yule, Askari wote wa kwenye nyambizi hiyo walikuwa wakipingana na Vassil mabishano ndani ya nyambizi hiyo yaliwachukua saa nzima na hatimaye wote wakakubali amri ya Admiral Vassil Arkhipov ya kutokupiga makombora ya nyuklia na haswa baada ya kuona nyambizi za Marekani zikiondoka bila ya kufanya shambulizi lolote kwao.
Hakika kilikuwa kitendo cha ujasiri sana kwa Vassil kuwashawishi wenzake wasishambulie nyambizi za Marekani maana endapo nyambizi zile za Marekani zingewaona na kuanza kuwashambulia wao basi ni dhahiri kuwa nyambizi hiyo ya B-59 ya Urusi ingeteketea na wote waliokuwamo ndani yake wangeuawa
Nyambizi hiyo ya B-59 iliondoka haraka sana eneo hilo na kurudi ilipokuwa ngome yao katika pwani za kisiwa cha Cuba usiku huo huo wa tarehe 27 October 1962 na vita ikawa imesimama, toka hapo Urusi na Marekani wakaanza mazungumzo ya Amani ya kuiepusha dunia kuingia kwenye uwezekano wa kutoka vita.
Copyright 2021, All Rights Reserved.
Maktaba Kuu.
0 comments:
Post a Comment