Search This Blog

Thursday, 29 December 2022

KUFA TU HAKUNA NAMNA - 2

   

Simulizi : Kufa Tu Hakuna Namna 

Sehemu Ya Pili (2)





"madam kasema hili tumwache hai yapaswa atupe hizo picha alompiga muheshimiwa"




Veko akadanganya kusudi wapate hizo picha kwani alijua akisema madam 's' katoa amri auawe basi asingetoa picha




Sudi pasina kujua akawa ambia picha na video ipo katika memori ya simu yake wakamnyang'anya simu na kuikagua ambapo kwanza walizikuta sms zake na za namba ambazo ziliseviwa 'my love' ambaye alionekana akichat naye kila hatua ambayo alikuwa akipitia...




Wakachukua namba za huyo binti ambaye awakumjua kama ni Sara mwandishi mkubwa tu wa habari,walijua naye lazima atakuwa na izo picha,wakaitoa memorycard,wakamuua Sudi na kumtupia kulekule kwenye pagara,wakatoweka nguvu zao wakiziamishia kumsaka Sara!




*** ** ***




Kwa Upande Wa Sara kazini alikaa avikukalika kila muda macho yake yalikuwa kwenye simu yake,toka asubuh alipomtumia mpz wake namba walikuwa wakichati na Sudi alikuwa akimwambia kila alipofikia




'dah mpz nimempigia kashtuka sana kakubali kutoa ela ndo naelekea kuonana naye'




'mpz,nipo hapa ndo namsubiri yule nimemuona kwel ana bruefcase mbili namuona anaziingiza ndani'




'katoka mpz'




'yah,kashapotea kwenye huu mtaa wacha nikazichukue tumetajirika mpz'




Sara anakumbuka ile ndo msg ya mwisho hata alipo mtext azikupokelewa na alipo mpigia aliambiwa simu aipatikani,




je ni iliisha chaji,au Sudi kakamatwa au kaingiwa na tamaa na kuamua kumtoroka?!




Maswali mengi yakatiririka katika kichwa chake yalokosa majibu na kumkosesha uvumilivu na kubaki akiangaika ofisini kwake...




mpaka baadaye katika habari zilizotufikia hivi punde aliposhughudia habar ya kifo tena cha kikatili cha mpz wake kukatwa katwa mapanga na watu wasojulikana,nguvu zilimwisha Sara,na ghafla akaenda chini...




DAH SARA NAYE ANAWINDWA NA USALAMA WA TAIFA,MPZ WAKE SUDI AUAWA KIFO CHA KIKATILI JE NIN KITAENDELEA?




UPANDE MWINGINE RAIS ANAPATA MAWAZO KWA MTOTO WAKE KUMTUMIA ZENA KATIKA MAMBO YAKE JE ATAFANIKIWA?










Msanii wa bongo Movie Mwenye umbo na mvuto wa kipekee Magreth au Miss g anaamua kumtafuta mwandish wa habar Sara na kumpa dili kuwa anatoka na kigogo wa serikalin




Anamwelekeza na hotel alofikia,Sara anafanikiwa kuwachukua video na kwenda kumuonesha mpz wake Sudi




Tamaa inamwingia Sudi,anamwambia asitangaze ile habari na badala yake wamuuzie mwenyewe mheshimiwa,




Kwa Uoga muheshimiwa anakubali kuinunua pasina kujua USALAMA WA TAIFA wanashtukia mchezo ule nao kuingilia kati,




Wakati Sudi kaenda kuchukua hizo hela usalama wa taifa wanamdhibiti na mwisho kumuua kama maagizo ya mkuu wao madam 's' yalivyosema




Sara akiwa kazini anapata habari ya kuuwawa kwa mpz wake nguvu zinamwisha hatimaye anapoteza fahamu




je nin kiliendelea?!




Wafanyakazi haraka haraka walimzunguka tayari kumpa huduma ya kwanza,wengi walimjua Sudi kuwa mpenzi wake ni Sara,




Sara baadaye alipopata fahamu alipewa pole nyingi alilia ikabidi apewe ruksa akaelekea hosptalin ulipoifadhiwa mwili wa mpenzi wake!




*** ** ***




Kitara cha polisi kilitia timu eneo la tukio,ni kutoka makao makuu ni baada ya kupigiwa simu na mtu alojiita mwananchi mwema na kutoa taharifa kukuta mwili ndani ya pagara




Alishuka Kijana nadhifu akiwa ndani ya sare za jeshi la polisi zilizo mkaa vyema nyota kadhaa mabegani huyu alitambuka kama inspekta Nurdin,




Wengi Wa Wapenz Na Wasomaji Wangu Watakuwa Wanamjua,inspekta Machachari muadilifu na makin katika kila kazi afanyazo,




Inspekta Nurdin akuwa peke yake aliongozana na mwanadada mrembo alotambulika kwa jina la Koplo Zena,huyu alikuwa ni mgeni katika idara ya jeshi la polisi,




Kutokana na makosa aloyafanya na kufukuzwa jeshini baada ya kuua alipata msamaha wa Raisi na kutokana na juhudi zake jeshine Raisi akapendekeza wamweke idara ya polisi kukabiliana na uhalifu uendelehao jijini,kuwa polisi badala ya mwanajeshi Ilikuwa ni kama kumshusha cheo kwa kosa lake la mauaji,




Lakin Rais alikuwa na siri yake moyoni!,baada ya kupata taharifa kwamba yupo anakumbuka siku hiyo Sara alikuwa na furaha sana kuwa huru akiwa nje ya geti la gereza lile ghafla gari jeusi likapiga breki pembeni yake vioo vikafunguliwa na kijana Dani akachungulia,




Walijuana,basi Dani akamvuta garini,Sara akuwa mbishi kitengo tu cha kuingia ndan ya gari alishtuka kumkuta muheshimiwa raisi haraka sana akamsalimia...




Rais akaitika akiwa na tabasamu kubwa sana usoni mwake,




"binti yangu unajua kwa nin nimekutoa gerezani?"




Zena akatingisha kichwa kutokujua




Raisi Asamoye akaendelea...




"kijana wangu naamin ufanyaji kazi wako,nimekutoa na kukusaidia hili nawe mwanangu uweze kunsaidia utafanya kazi chini yangu ila ripoti utonipa mimi,hapana...




Naitaji Uwe mwandishi wa habari ila ficha sura yako isitambulike ovu lolote utakalo liona katika serikali yangu nilione katika televisheni!..




...na maana yangu na najua ipo siku utajua nini na maanisha..




...najua ni kazi ngumu ninayokupa ila fanya kwa weledi utafanikiwa"




Baada ya maelekezo yale sara alishusha pumzi Rais akaendelea




...Hii kazi utakuwa ukiifanya kwa siri pasina kutambulika sura yako kama afanyavyo Sudi Brown,ila kazi ambayo utajulikana ni upolisi ili uishi uraiani huru na utaanza kama koplo,utaitwa Koplo Zena,ila Katika Uandishi utaligeuza jina lako KOPLO ZENA utaitwa 'ZK'




'Z' ikisimama kama Zena 'K' ikisimama kama KOPLO,baada ya raisi kumpa maelekezo yale akawasiliana na watu wake Zena akaingia idara ya polisi tena makao makuu,na leo ndo alikuwa na kijana Nurdin,wakashuka kwenye gari kuingia ndani ya pagara lile...




Kulikuwa na watu wengi wameuzunguka ule mwili,haraka Koplo Zena akautandika ule mwili picha kadhaa wakati inspekta akiendelea na uchunguzi haraka yeye akachoropoka na kutoa taharifa 'ukwel tv' televishen alokuwa akiifanyia kazi kwa muda huo akatuma na zile picha alizozipiga, akijitambulisha kwa jina la 'ZK' kisha akarudi zake ndani,




Habari ile ndiyo iliyo onwa na mwanadada Sara,akapoteza Fahamu,na Pia Waziri Mkuu...




"ni Nani alotupigia simu polisi au wakwanza kuona tukio hili?"




Inspekta Nurdin alihoji ila hakuna alojitokeza,akujua ni uoga au ni nini,mpaka mwili ule ukiingizwa ndani ya gari jingine la polisi hawakuwa wamepata alama yoyote ya ushahidi wakaelekea hosptalin na mwili ule...




*** ** ***




Salome akiwa sebuleni kwake anafatilia mchezo katika runinga yake ghafla simu yake ikaita ilikuwa ni namba geni akapokea...




"Nani mwenzangu?!"




"Naitwa Katarina ni mke wake bosi wako Zidu nakuomba achana na mume wangu kama unapenda kuendelea kuishi ni onyo tu nakupa ila ukiendelea kujifanya mjuaji mamy utakuwa ukijitafutia tiketi wewe mwenyewe ya kuelekea ahera Kama ni msikivu nadhani utakuwa umenielewa ila kama ni mbishi we endelea ila tusije laumiana tuka onana wabaya hapo baadaye ok!"




Salome akujibu kitu Katarina akata simu!




Mwili wote ulimloa jasho Salome alikuwa akitetemeka,








Katarina anampigia simu Salome na kumuonya kuendelea na mahusiano na mume wake Zidu,




Salome anaingiwa na uwoga mwili wote unamloa jasho hofu inamtanda,




Anamjua vizuri Katarina ila je ni kweli ataweza kukatisha penzi la Zidu na Salome lililomea kwa kasi?!....




Tusonge kuburudika zaidi.....




Hata hamu ya kuangalia tv ilimyeyuka akajinyanyua na kuelekea zake chumbani kwake kulala,




Akiwa kitandani ghafla simu yake ilianza kuita alipoangalia mpigaji 'bosi' ndilo jina lililoseviwa katika screen ya kioo cha simu yake,




Kwa dakika kadhaa akaacha ikaita mpaka ikakata,




Alikuwa akijishahuri apokee au lah ghafla ikaita tena akaona bora apokee amwambie ukweli tu Zidu kwamba wayavunje mahusiano yao wabaki tu kama mtu na mfanyakazi wake




Akapokea




"Beby mbona nakupigia, utaki kupokea,


Nini nimekukosea,


Wangu my dea,




Nambie usisite,


Nini wataka upate,


Au nikufate?!,


Ntakupa chochote,




Utakacho my dia,


Pls acha kulia,


Chochote ntakusaidia,


Wangu malkia,




Zidu ghafla akaacha kuimba baada ya kusikia mpz wake Kama analia




" unalia nini love?!...."




Akauliza kwa mshangao uloambatana na wasiwasi




"Naomba tuachane mpz!"




"Kwanini tena Salome aaaah ok kwa sababu tulipoachana hotelini sijakupigia nilipofika nyumbani mke Wangu alinletea shida tukazipiga ila pia nilipokea simu rafiki yangu Isack kashambuliwa na risasi na watu wasojulikana ikanibidi usiku ule twende hospitali mpaka saa tano ndo tulitoka na kwa Leo sijaja ofisini kwa kuwa bado nipo hospitalini kupeleleza alompiga Isack risasi tafadhali mpz wangu usichukie wala usijihisi vibaya kutokuja kazini na kutokukupigia simu"




"Izo ni shida zako mimi azinihusu ila nakuomba usahau kama mimi ni mpz wako kwaheri"




Salome akakata Simu,Zidu alichanganyikiwa akajaribu kupiga mara kadhaa ila akupata mrejesho wowote wakupokelewa simu mwisho alipopiga ilizimwa kabisa




Akaamua kwenda nyumbani kwa Salome usiku ule ule wa ile siku ya pili akajue kulikoni.....




***** ** *****




Katarina kila muda macho yake yaliangalia saa ya ukutani tayari ilishafika saa sita ila mumewe akurejea....




Alipo mpigia Mary hospitalin Mery akumficha alimwambia Zidu alitoka toka saa tatu pale hospitalin wakat mwanzo alisema angelala na mgonjwa na matokeo yake aliondoka tena bila hata kuaga




Katarina mara kadhaa alipiga simu ya mumewe ila aikupokelewa zaidi ya kukatwa,




Mapenzi yanauma,ndoa ni kasumba,ndoa ni mateso hata kama mtu alikupenda kitu kidogo tu kinaweza mbadilisha




Zidu alibadilika,




Katarina alikonda alikuwa mtu wa mawazo,mtu wa mahasira,alilala palepale sebuleni mezani akimsubiria mumewe aje wale wote kama yalivyo mazoea yao




Mfanyakazi wake Suzan mapema tu alishalala,




Saa tisa za usiku Suzy aliamka baada ya kiu kumkamata akashuka kitandani na kuelekea sebuleni ilipo friji akanywe maji




Alishtuka kukuta taa zinawaka si ndo akapiga hatua ndefu kuwah sebuleni,




Alishtuka baada ya kumkuta bosi wake Katarina akiwa kalaza kichwa chake mezani ambapo pia kulikuwa na vyakula ambavyo avikuliwa




Suzan akamsogelea katarina na kuanza kumuamsha




"Mamaa!,mama!,mama...."




Katarina aka amka alipiga miayo akajinyoosha macho yake yakadondokea ukutani!




"Baba yako amekuja?!"




"hapana mama sijui chumbani mbona ujala sasa mama"




Katarina akujibu kitu akaamka,na kuelekea chumbani akiwa na matumaini labda pengine angemkuta mumewe




Ola!....




Katarina alishindwa vumilia kulia,Dada Wa kazi akawa akim'bembeleza




"Kalale tu mdogo wangu..."




Suzan akatoka huku akimsikitikia bosi wake yule alompenda na kumlea kama binti yake,kazi alikuwa akimsaidia mshahara akimlipa mkubwa tena katika wakati muafaka




Suzan alimpenda sana Katarina ivyo kata alipokuwa akiumia naye alipata maumivu vile vile




Usiku ule katarina akulala




**** ** ****




Zidu baada ya kutoka hospitalini saa tatu ile alienda moja kwa moja mpaka alipokuwa akiishi mpz wake Salome,




Alikuwa kampangia nyumba kubwa akiishi yeye na mdogo wake wa kiume alokuwa akimsomesha




Akabonyeza kengele Sam mdogo wake na Salome akaenda kufungua,




Zidu akaingia,Sam akaingia zake chumbani Zidu naye akaelekea chumbani ambapo alimkuta Salome kajilalia




"Salome mpz wangu kitu gani nilichokukosea kwanini wataka kunipa adhabu kubwa kiasi icho umenionjesha asali kwa Nini wataka kunipa na shubiri nambie mpz....




Zidu aliongea kwa unyonge kwa hisia huku machozi yakimtiririka




Maneno yale yakamchoma Salome




" si Mimi mpz ni mkeo kanipigia simu kunionya niachane na wewe nakupenda sana Zidu ila sina budi bora tuachane tu ataniua eti yule mwanamke"




"Hapana Salome usiseme ivyo cheki nnavyokuthamini....




Zidu akaingiza mkono mfukoni akautoa ulikuwa Na kikopo kidogo vile viekeavyo pete akafungua kikopo kile na kutoa pete ya dhahabu




Salome akuamini akayatoa macho yake pima akifunua mdomo akauwekea mkono




Akajikuta akitoka kitandani na kwenda kumkumbatia Zidu,




Zidu akamvisha ile pete, Salome akasahau yote




" mpz na njaa ujapika"




Zidu akadeka




Salome chap akaingia jikon Zidu akuwa nyuma kumfata wakakarangiza mayai wakakaa mezani wakala....




Katu Zidu akujua mkewe alikuwa akimsubiria mezani wapate chakula,




Yeye na Salome wakala wakashiba wakaingia kitandani




Wakaendeleza penzi lao kila mmoja akionesha ufundi wake!




Hakika Salome alikuwa ni mtundu kitandani alimpagawisha kijana wa watu na kuzidi kuziteka hisia zake




Walilala kihasara hasara!




Kesho yake walioga pamoja wakaenda kazini Pamoja,




Zidu akumtafuta Katarina Na wala simu yake akupokea ndo kwanza baada ya kuona anasumbua sana akamweka black list.....




Alijua kufanya vile anamkomoa na katu akujua kwa kufanya vile aliyaweka maisha ya Salome hatarini




Salome naye akajisahau kama alishaonywa...




Na Katarina huwa aonyaji Mara mbili








Katarina anaingia kuionja chungu ya ndoa,


Ni baada ya kushindwa kupata mtoto kidume kinabadilika na kutoka na mfanyakazi wake hata baada ya Katarina kumuonya Salome ndo kwanza penzi linapea na kumzalishia maumivu makali Katarina




Je nini kitaendelea?!....




Twende pamoja kuburudika zaidi....




Upande wa pili Baada ya insp Nurdin akiambatana na Koplo Zena kuwasili hosptalin na kuukabidhisha mwili ule kwa madaktari kwa uchunguzi aukupita muda mrefu sana watu walojitambulisha kama wazazi wa Sudi wakawasili,




Walishindwa kustahimili kuutazama mwili wa mwanao pasina kuacha kuangua kilio...




Insp Nurdin na Koplo Zena ikabidi wabebe dhima ya kuwabembeleza




"je kuna mtu yeyote aliyewatilia mashaka ambao mnahis anaweza kuwa anausika kwa namna moja ama nyingine kwa tukio hili?"




Inspekta Nurdin akahoji wakati huo koplo Zena akiwatwanga picha wazazi wa Sudi,insp Nurdin alishangazwa kwa jambo lile ila akalipotezea,kabla wazaz wale awajajibu kitu ghafla mlango ukafunguliwa na binti mrembo akaingia akiangua kilio,wazazi wakampokea maeneo yale yakageuka kuwa msibani...




Nurdin na hata Zena Walimtambua yule mwanadada aliyeingia kama mwandishi wa habari atokaye tumain tv,




Basi baada ya kunyamazishana safari hii Zena akarudia lile swali ambalo awali kabla Sara ajawasili Nurdin alishaliuliza,




"je mnamtambua au hata kumuhisi mtu ambaye anaweza kuwa kwa namna moja au nyingine anahusika kwa mauaji haya?"




Zena alihoji akiwatazama mmoja baada ya mwingine,




"ndiyo,mimi namjua muuaji!"




Pasina Kupepesa macho Sara aliongea kwa uchungu huku machozi yakimchurika wote walipigwa na butwaa,




"basi sawa tutaondoka na wewe mpaka kituoni ukaandikishe maelezo ok?"




"amna shaka afande!"




Sara akajibu,baadaye kidogo wakaondoka mpaka kituoni ambapo Sara alitoa maelezo yake,kwanzia alipompiga picha mh waziri, akamshirikisha mpz wake tamaa ikamwingia Sudi,akaitaji Kumuuzia Wazir Picha zile wakaelewana wakutane mikoroshini


Sara alieleza kila kitu mpaka walipochati na Sms hata video pia walizionesha ambapo Zena alizichukua katika simu yake,ulikuwa ni ushahidi tosha wa kumfunga waziri,basi walimtoa shaka Zena na kumruhusu,




Kwa kuwa lilikuwa ni jambo nyeti ilipaswa Insp Nurdin akaliwasilishe swala lile kwa mkuu wake




"dah kaz kweli kwali lazima waziri mkuu atakuwa anahusika kabla atujafanya chochote wacha niwasiliane na usalama wa taifa kujua tutafanyaje"




Palepale Kamishna alokuwa ndo mkuu pale makao makuu baada ya kamishna Alex,akashika mkonga wa simu yake akaiweka masikioni akabonyeza tarakimu kadhaa,


simu ikaita!




"madam 's' hapa nambie kamishna"




"umeskia habari ya yule mtu alokutwa amekufa kwa kucharangwacharangwa na mapanga huko tmk"




"yah ndio kamishna..."




"waziri mkuu anahusika, ushahidi upo je kutakuwa na hali ya usalama ndan ya taifa ikiwa tutamkamata na kumuhoji"




"hapana kamishna,wazir ndo kiongoz wa serikali kwa usalama wa taifa achaneni na habari hii ishie tu juu juu waambie vijana wako waachane nayo,na pia huo ushahidi uteketezeni sawa?"




"sawa madam"




Kamishna akakata simu,akawageukia Ins Nurdin Na Koplo Zena Walokuwa Wakisubiri Mrejesho...




"habari ilotoka ngazi za juu ni kwamba yapaswa mfunge hilo faili achanen na hiyo kesi"




"kwa nin tena mkuu?"




Nurdin akahoji moyo wake ukiwa katika maumivu tele




"upaswi kujua kwa nin amri imetoka ngaz za juu kwa usalama wa taifa"




Insp Nurdin na mwenzake Koplo Zena wakainuka na kupiga saluti,wakatoka zao...




Tukio lile lilimkumbusha Insp Nurdin Mbali,ulimkumbusha kisanga cha riwaya ya 'mzimu ulorejea' tukio kama hili hili lilitokea,




Ni baada ya tajiri mkubwa kuuwawa kikatili na mwili wake kutupwa kandokando ya bahari,baada ya upelelezi sana mwisho Nurdin alikuja kumgundua muuaji ni tajiri mkubwa jijin Dar,alipofikisha habar ile kwa mkuu wake Kamishna,akaambiwa Wazi aachane na kesi ile,ikiwa ndo taharifa kutoka ngazi za juu kama leo hii anaambiwa vilevile,




je ni ipi haki ya maiti,au hana haki kwa kuwa hana uhai,ila akuwa na budi kuachana na habari hiyo kama alivyoamriwa,




Kwa upande wa koplo Zena ndo kwanza alikuwa kaingia idara ya jeshi la polisi,ila japo


alishangazwa na jambo lile,kumbe waziri anaweza fanya kosa asishtakiwe?!,




Akajikuta akitabasamu,kwa mara nyingine ndipo alipoelewa maana ya raisi Asamoye Kumtoa gerezani,serikalini kulioza...


akakumbuka tena kauli ya mh Rais siku ile wakiwa ndani ya gari nje ya gereza lile baada ya yeye tu kutoka...




"nakutoa kwa lengo moja tu,nakusaidia hili nami unsaidie,ntakuingiza ndani ya idara ya polisi na pia huku ukiwa mwandishi kificho,ovu lolote utakalogundua katika serikali yangu usiniripotie nahitaji nilione katika vyombo vya habari,utafanya kazi pale ukwel tv,ni televishen yangu ile japo watu awajui ila sura isionekane vaa mask,na pia kama habar ni mbaya sana pengine chafu,fungua ma akaunti yutube,instagram huko makundi ya whatsupp ukitumia jina la 'zk' sambaza huko...




Zena Kukumbuka Ivyo akacheka,Zena alibahatika kuwa na kipaji cha sauti toka mara ya kwanza anaingia 'ukwel tv' wengi walijua ni mwanaume kutokana na sauti yake nzito ya kiume alokuwa akiongea pindi akiripoti habari mkurugenzi wa televishen ile alitambua mtu yule wa mask aliwekwa na bosi wake ivyo alikuwa ni tofaut na wafanyakaz wengine




'ZK' akukaa ofisin wala akupangiwa eneo la kwenda kusaka habari...




Yeye alipopata habari alimpigia simu mkuu wake na kuipandisha moja kwa moja hewani...




Siku hiyo baada ya kutoka kituoni alipania kuvujisha siri ile usalama wa taifa waloamua kuificha,akatuma maelezo ikiwa kama 'breaking news'




"habari Ilotufikia hivi punde ni kwamba siri ya mauaji ya mtu alokatwa katwa mapanga na mwili wake kutupwa wilaya ya tmk maeneo ya mikoroshin ndani ya pagara bovu yafichuka...




Mwili huo inasadikika aliyenyuma ya tukio ni wazir mkuu mh John


Chanzo chetu kinaripoti...




Zena akapokea akiongea kwa sauti ya kiume,wengi wakimtambua kama mwanaume...




Zena alieleza kila kitu alichoelezwa na sara mpaka meseji walizotumiana na ushahidi wa video hiyo alieleza waz kuwa unapatikana ndani ya akaunti yake youtube 'ZK'




Kwa kashfa ile taifa likazizima,presha ikampanda muheshimiwa waziri mkuu akaenda nje kutibiwa...




"huyu ZK asakwe naye auwawe hiki kituo cha televisheni nacho kifungiwe"




Madam 'S' akiwa kapandwa na jazba akatoa amri...




Ukwel Tv,kikafungwa Kwa Mwezi Mmoja bila kutoa habari 'Zk' akaingia mitini...




Usalama wa taifa wakawa wakijiuliza kama Sara Wanaye Je hizi habar 'zk' hatakuwa kazipata wapi?!...




kwanza 'zk' ni nani!...




Siku hiyo kituo cha televishen ukwel tv kikavamiwa na vijana wa usalama wa taifa wakawapiga waandishi wakiwalazimisha waseme u kweli "ZK' ni nani na yupo wapi,




Waandishi wote walikana kuitambua sura yake,




Mwisho vijana wale wa usalama wa taifa wakaonelea waondoke na mkurugenzi wa chombo kile cha habari huyu wangembana vizuri bila shaka angesema








Mwanadada Katarina bado yupo katika maumivu makali ya mapenzi,kipigo ndo kimekuwa chakula chake kutoka kwa mume wake Zidu alompenda na kufikia hata kuisaliti nchi yake ya Ganyama Kipindi Iko,yote magumu waloyapitia Zidu anayasahau kisa tu kuchelewa kupata mtoto,


Zidu ana amua kutoka na mfanyakazi wake na kufikia hata kumvisha pete ya uchumba




Pia upande mwingine upelelezi wa mauaji dhidi ya Sudi unafanikiwa baada ya Sara Kueleza Kila Kitu Ila Maaskar Walokuwa Wakifatilia Kesi hiyo wanazuiwa kwa ajili ya usalama wa taifa,ila koplo Zena ana amua kuvujisha siri akitumia jina la "ZK" pia tulipata taharifa kuwa Sara alikamatwa kabla hata habari zile kuvuja madam 's' mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa anatoa amri huyo anayejiita "ZK" asakwe na kuuwawa mara moja,




Kituo Cha 'Ukwel Tv' ambacho anafanyia kazi kinavamiwa waandishi wanapigwa wakilazimishwa waeleze mahali alipo huyo 'zk' au watoe picha yake halisi,baada ya kutofanikiwa kwa jambo hilo mwisho wanaondoka na mkurugenzi wa kituo kile kwenda kusiko julikana...




Minong'ono uraiani inatawala...




twendelee...




Chombo kinachotetea vyombo vya habari kikapaza sauti,kulaani kitendo 'ukwel tv' walichofanyiwa,




Magazeti yakapambwa na vichwa vya habari vya kuilaani serikali,waziri wa habari yeye alikana serikali siyo walotuma watu kituoni pale,hata kamanda wa polis naye pia alikana akisema ni watu wasojulikana na jeshi lake wanafanya uchunguzi juu ya tukio ilo...




Siku hiyo hiyo katika akaunti ya utube 'ZK' akiwa katika mavazi yake meusi koti kubwa,na maski usoni akaripoti pia kupotea kwa mwandishi wa habari Sara,pamoja na mkurugenzi wao,chanzo akaweka wazi ni serikali wakimlinda waziri...




'ZK' akazidi kuwa maharufu mara dufu...




Rais alfrah, akaitisha kikao na madam 's' pamoja na baadhi ya washauri wake,na viongoz wa chama ofisini kwake...




"hili jambo sasa limechafua serikali yangu,John ananchafulia cv ya uongoz wangu wananchi wanatuelewaje sisi,hapo awali silaha zilikamatwa bandarini,serikal yangu ikachafuka wananchi wakajua angejiuzulu au mimi ningemuuzulu ila nlpo mtaka ajiuzulu akaja juu kwa kuwa yeye ndo ana nguvu kifedha na pia chama chake kinanguvu pia ilajua ananipa mimi wakati mgumu katika uongozi wangu...




na uchaguz ujao ikiwa tutamweka agombee wallah ikulu tutawaachia wenyewe wana mapinduzi...




nimeshangaa sana kwa usalama wa taifa kumlinda muhalifu tena kwa kuua mama kwa nin mnafanya ivyo?!..




sasa natoa amri mkurugenzi wa 'ukwel tv' mumuachie na si yeye tu pia huyo mwandishi alokuwa mpz wake marehemu pia aachiwe,




kingine vyombo vya habari viachiwe uhuru wao maswala sijui huyu kaficha sura asakwe huyu kafanya vile hii ni nchi ya amani na toka mwalimu Nyerere katupatia uhuru chama cha mapinduz kimetawala miaka yote mpaka wametuachia,




Wametuachia katika hali ya amani kila mwananchi akiwa na amani miaka miwili tu naanza kuona dalili za kupotea kwa amani,mimi ndo naumia,Wazir mkuu akitoka india kwa kashfa hii atake atajiuzulu asitake pia atajiuzulu kwa manufaa ya uongozi wangu"




Wajumbe Wote Waliyekuwa Kwenye Kile Kikao Wakapiga Makofi Kumuunga Mkono muheshiwa raisi..




Madam 's' naye akaongea..




"heshima kwako muheshiwa Raisi,heshima Kwa Wajumbe Wote Wa Kamati Kuu Uloyaongea yana tija tena kubwa mh Raisi,ila tambua mimi kama mimi najua nifanyacho ndo maana nikawekwa kwenye kitengo kama hiki kuhakikisha taifa linakuwa salama




Muheshimiwa Rais Kwanza nikutake radhi kwa nitakayokwambia na waheshimiwa wajumbe wote...




Aliyemuua Sudi si waziri mkuu lahasha ila ni vijana wangu,kwanin sasa nilifanya ivyo wengi najua mnataman kujua...




Baada ya Sudi kunasa picha za mh waziri alimpigia na kumtishia kuzisambaza mtandaoni ikiwa tu atompa kiasi cha ela,waziri alikubali kutoa icho kiasi cha ela ili kuficha siri yake ndipo Sudi alipo mtaka waonane mikoroshin na akimwambia asimwambie mtu yoyote,waziri akafanya ivyo,ila mimi baada ya kunasa maongez yao nikatuma vijana wangu kwa siri wamfatilie wazir na ndivyo walivyofanya,waziri akujua kama anafatiliwa akalipa hizo ela katika pagara lile akatoka zake huku nyuma Sudi alipoingia vijana wangu wakamtia nguvuni, wakamnyang'anya simu ilokuwa na hizo picha na kumuua




Walimuua ili kuua kabisa soo,kwa kuwa angeweza kurudi kumbughudhi tena muheshimiwa...




Kitu ambacho atukukijua ni kuwa mpz wake kumbe ni yule Sara Mwandishi wa tumaini tv,ivyo yeye Sara aliripoti polisi mkuu alipo nambia nilimwambia afute hiyo kesi na kuwa ambia vijana wangu wamkamate huyo Sara,naye yapaswa auawe!"




"kwa hiyo Sara naye kafa?"




"hapana,kagoma Mpaka Sasa Kusema mahali ilipo memorikad bado vijana wangu wanamshikilia,ila kinacho niumiza kichwa ni huyu 'ZK' mwandishi wa 'ukwel tv' ni nani hasa na habar zetu anazipata wapi?!...




'ZK' ndo aloharibu hali ya hewa mh hana shida,ila ripoti anazotangaza 'zk' ndo zinazo mchafua muheshimiwa na sisi kama usalama wa taifa lazima tu dili naye...




Wajumbe Wote Wakapiga makofi,mapigo ya moyo ya Rais yakaanza kwenda mbio,alishindwa cha kuongea...




angeongea nin sasa...




Na yule alomponda hapo awali kashasafishwa,mpaka kikao kinaisha Sara na 'zk' ndo walo onekana wanaotishia usalama wa taifa...




Rais akajua hapa kamweka mtoto wa watu matatizoni, aliujua ukatili wa kitengo kile cha kijeshi ambao waliyoko ndani yake wao walifunzwa kuua...




*** *** ***




Macho yalikuwa mazito kufunguka ila akajitahidi ivyo ivyo akayafungua ila akapokelewa na giza tororo akataman kupeleka mkono machoni ila akakutana na ukinzani akang'amua kwamba mikono ilifungwa katika kitanda alicholalia na sio mikono tu la hasha mpaka na miguu,mguu mmoja ulifungwa huku mwingine ukafungwa kule mikono hivyo hivyo akiwa kalazwa kimgongo mgongo mwili wote alihisi maumivu mpaka sehemu zake za siri,akajaribu kuvuta kumbukumbu zake,mwisho akakumbuka...




Ni wakati akitoka kituo kile cha polisi alipotoka kuripoti wakati akiwa hapo nje akisubiria daladala,kituo kile kilikuwa kandokando tu ya barabara,ghafla gari moja ikasimama pembeni yake mlango ukafunguka akashuka mtu,




Akijua yule mtu pengine labda angeenda na shughuli zake alimkwapua mpaka kwenye gari na gari ikatoka kwa kasi watu wachache waliyeona tukio lile awakulifatilia zaidi ya kuwaacha katika mshangao!....




Mpaka gari ile ikawapotea, kule ndani kulikuwa na vijana wa tatu dereva yule alomkwapua na alompokea ambao wao walikaa siti ya nyuma...




"kwa Nini Unapenda Kufatilia Watu Wakubwa?"




Watu wale walokaa nyuma walimuoji kabla ajajibu akapokea ngumi ya uso,ajakaa vizur wa pembeni akamla kibao




"tunahitaji ushahidi wote wa muheshimiwa waziri"




Yule alompiga awali aliongea ila Sara akuweza kujibu kitu zaidi ya kulia...




Watu Wale Waliendelea Kumpiga na kumtesa mpaka akapoteza fahamu wakimlazimisha aseme ilipo memori kadi kwani kwenye simu memori ilitolewa...




Baada ya kupoteza fahamu sasa ndo anazinduka mwili wote ukimuuma,alipo mkumbuka mpz wake akajikuta akianza kulia tena!...




ghafla mlango ukafunguliwa na taa ikawashwa,




Sara akatambua kumbe ilikuwa ni usiku hapo pia alijigundua kumbe yupo uchi kama alivyozaliwa




Akaingia mtu ambaye ndo mara ya kwanza alimuona si miyongon wa wale walo mteka,huyu alivaa singland ya kijesh na surual na buti za kijeshi,mkononi alishika mkanda wa jeshi,kwa hatua fupi fupi akamsogelea huku akiuzungusha ule mkanda tabasamu likipendezesha uso wake...




"ndo kwanza nimetoka kogoe katika kambi mpya ya jeshi miaka sita sijui ladha ya mapenz na nilivyokukuta,dah hiyo moja pili kamanda wangu alikuwa mwanamke kantesa sana mafunzoni kanifanya niwachukie wanawake ntakuonesha...




Akamtandika na ule mkanda wa tumbo,tena bila huruma,alimchapa mara tano tena eneo lile lile,Sara alilia akujali kilio chake...




"iko wapi hiyo memory ya waziri"




Akauliza huku akiendelea kutingisha mkanda wake uloloa damu...








Mapenzi Zidu anayoyapata kutoka kwa mfanyakazi wake Salome yanampagawisha na kumfanya asahau nyumbani siyo ivyo tu,hata hosptalin alipolazwa rafiki yake aliyepigwa risasi na watu wasojulikana anakata mguu wa kwenda




Mke wake Katarina asubuh asubuh ana amua kumfatilia huko anapewa taharifa zinazo mshtua zaidi,




Kwamba Zidu mida anayoingia kazin ni saa nne akija pamoja na katibu muhtasi wake na saa saba wakienda 'lunch' huwa awarejei mpaka kesho yake,Katarina anaaga ila anatulia nje punde Zidu na Salome wanawasili wanaingia ofisin huku wakiwa wameshikana mikono kama wapenzi,songa kujua kilichoendelea...




Moyo ulizidi kumwenda mbio,kizunguzungu kikali kikamjia sambamba na giza haraka sana Katarina akachuchumaa kwani alijua laiti kama angeendelea kusimama uwezekano wa kudondoka ulikuwa mkubwa,




Alichuchumaa pale chini kwa dakika kadhaa,mpaka kizunguzungu kile kilipotoweka akajinyanyua akiwa kashapata wazo jipya,




Akaondoka eneo lile mpaka maduka ya nguo akanunua hijabu na nikabu akavivaa palepale dukani,akachukua na gloves pia akazivaa mkononi akachukua boda boda mpaka nyumbani kwake ambapo alimwambia bodaboda amsubiri, akabonyeza kengele, msichana wa kazi akaja 'speed' kumfungulia...




"nikusaidie nin dada?!"




"ni mimi embu nipishe nipite"




Baada ya mfanyakazi yule kusikia ni sauti ya bosi wake akampisha njia huku kichwani kwake akiwa na rundo la maswali,




Alijua lazima bosi wake atakuwa kaamua kumsaliti mumewe,kwa nin avae vile kuficha sura yake hakuwa na shaka ni ili pindi atakapoingia gesti asigundulike,




Moyoni mwake mwanadada yule akazidi isikitikia familia ile...




Katarina aliingia chumbani kwake akafungua kabati lake la nguo akatoa ka begi chake kadogo cha kwapani ndani akatia kisu,na kitambaa akatoka...




Akaenda mpaka ilipo bodaboda ile na kupanda akamuelekeza eneo alilotaka ampeleke dereva bodaboda akaiwasha pikipiki hao mpaka kazini kwa bahati nzuri gari ya Zidu bado ilikwepo,Katarina akashuka akamlipa mida ya saa saba kasoro unifate hapa...




"sawa ma mdogo amna shida"




Bodaboda yule akaondoka,Katarina akaenda kuketi ndani ya kamgahawa kamoja akaagiza chai akawa akinywa huku macho yake yakiwa dirishani...




Muda ukasonga, dakika zikazidi kukimbia,masaa yakakatika hatimaye boda boda yule akawasili na kama tu Mungu alikuwa upande wake baada ya bodaboda yule kuwasili muda huo huo Zidu na Salome Ndo Walikuwa wanatoka ofisin wakaingia ndani ya gari yao!,




Katarina akachepuka kuifata ile pikipiki akaipakia,




"yapaswa kwa siri sana uifatilie hii gari mpaka mwisho wa safari yake hakikisha awagundui juu ya kufatiliwa kwao,barabara kuu acha hata gari mbili ziwe mbele...




"sawa ma mdogo"




Dereva bodabada yule akatia pikipiki yake mafuta akaanza kuifatilia ile gari akiiachia umbali kidogo...




Nyumba aliyokuwa akiishi Salome aikuwa mbali na pale kazini walipofika wakasimamisha gari wakipiga honi!




Katarina palepale akatoa hela na kumlipa yule boda boda akimwomba amuache palepale,akashuka akawa sasa akiifata ile nyumba ya Zidu ila kabla ajafika akakumbuka kitu,




Umakin kwake ulipotea,lengo lilikuwa amuue Salome,ila Je angemuuuaje na Zidu yupo ndani?,pili kama angemuulia pale ndani ingekuwa na uwezekano mkubwa wa yeye kugundulika na kukamatwa kirahisi hasa kwa ushahidi wa dereva bodaboda,kwani alipajua alipoishi na yeye mwenyewe ndo kampeleka!




Ikabidi asitishe swala la kuua adili kwanza na dereva bodaboda kumpoteza ili akija kuua kusiwe na ushahidi wowote palepale akatoa simu yake ndani ya begi lake na kumpigia ndan ya dakika tano aliwasili akapakia,safari hii Katarina alikuwa akimkumbatia dereva akazidisha madoido safari yao ikaishia katika gesti za uswahilini,




Baada ya masaa kadhaa habari zikasikika kukutwa kwa mwili wa mtu katika chumba cha gesti akiwa kachomwa kisu na kutobolewa macho,


huyu hakuwa mwingine zaidi ya yule dereva bodaboda!...




huku muuaji akutambulika...




Katarina alirejea nyumbani akaendelea na maisha yake,kila siku alikuwa akiwafatilia akitafuta njia ya kumwondosha Salome pasina kuipata nafasi hiyo kwani kika mahali walikuwa pamoja nyumban wakitoka pamoja wakirejea pamoja!,Zidu akumuachia nafas Salome ya kuwa peke yake na Salome vile vile akuamuachia nafasi Zidu ya kuwa pekee waligandana kama kumbikumbi...




'nitamuua hata wakiwa pamoja'




Katarina aliwaza saa tatu hiyo wakati akiwa ndani ya gari lake nje ya nyumba aloishi Salome Leo aliamua itakavyokuwa na iwe,mkononi mwake alikuwa na silaha akiwasubiria kwa hamu watoke...




Kweli geti likafunguliwa,na gari ya Zidu ikatoka Katarina alikuwa upande wa kushoto ivyo aliweza kumuona Vizuri Salome akaunyoosha mkono wake wenye silaha muda ule ule milio ya risasi ikasikika kutoka katika bastola aloishika Katarina...




*** ** ***




Viongozi Mbalimbali wa vyama pamoja na watu mbalimbali walifurika uwanjani kumpokea muheshiwa waziri mkuu,pia kwa upande wa waandishi wa habari walikuwa wengi tena wote wakiwa na mask usoni kama afanyavyo 'ZK' siku hiyo ilikuwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani,


'ZK' katika makundi mbalimbali ya whatsupp alipeleka ombi lake kama ku i sapraiz serikal wavae kama yeye,waandishi wakamuunga mkono na ndivyo ilivyokuwa...




Kitendo kile kikazidi kumchanganya muheshimiwa waziri mkuu,ulinzi ulikuwa wakutosha,maaskari wakawa wakiwazuia waandishi kwa kutaka kuwapiga na kuwakamata ila JJ akawazuhia kwani alijua angeruhusu hali ile ni kutafuta choko choko na waandishi na kitendo hiko kingemshusha yeye na chama chake kisiasa


"waacheni wanihoji maswali nitajibu ya wachache yanayojibika,hii ni nchi ya amani polisi waachieni hao"




Waandishi walokamatwa wakaachiwa...




Wakamsogelea Muheshimiwa Waziri na kuanza kumuhoji...




"muheshimiwa waziri unasemaje kuhusu tukio la kufa kwa kijana...na wewe kuhisiwa ndiye msababishaji unaongeleaje kuhusu swala hili?"




"ZM" akapata bahati ya kuwa muulizaji wa kwanza,hili astiliwe shaka alitumia sauti yake ya kike,watu walikuwa wakijua ZM niwakiume hata waandishi wenzake,swali lile lilikuwa ni gumu kwa muheshimiwa waziri,likaanza kumtoa jasho,akapatwa na kigugumizi cha ghafla




"ni..ni..ni..swala hili sitoliongelea kwa leo wacha nikapumzike hali yangu bado ijawa vizuri ntatafuta siku ntaitisha kikao cha waandishi ntaongelea kila kitu!"




"mh wazir na vipi kuhusu zile picha ukiwa na miss mage unaongeleaje swala hilo?"


"ZK" akampachika swali jingine mh Waziri akujibu kitu akaelekea mahali ulipo msafara wake walinzi wakimweka kati akaingia ndani ya gari msafara ukaondoka kutoka maeneo ya uwanja ule...




'ooh 'ZK' shit! sikutegemea kama ulohaidi lingetimia ni zaidi ya nilivyokuwa nikikufikiria hakika una iq kubwa'




Mh Rais aliwaza akiwa ikulu wakati akitazama kwenye runinga 'ZK' alipokuwa akimchapa maswali waziri,akujua binti yule alitumia njia gani kuwashawishi waandishi wote wale kuvaa kama yeye,akujua juu ya umoja wao huko whatsupp...








Wahenga waliponena mapenz yanaua, wala hawakukosea hasa ukitawaliwa na uwivu,jambo hili linajidhihirisha kwa Katarina baada ya kumpa onyo Salome mwanamke anayetembea na mume wake ahachane na mume wake ndo kama alimwambia hazidi kumteka pasina kujua Kwamba mwenye mume anaendelea kumchunguza na leo anamtandika risasi ndani ya gari je unahis nin kiliendelea tusonge...




Wakati Zidu alipokuwa akilitoa gari lake nje alishtuka kuikuta gari ya Katarina Kwa nje ikiwa inawasubiri wakati akiwa katika mshangao ule akashughudia Katarina akiunyoosha mkono wenye silaha haraka sana akapiga breki sambamba na kuinama akimwinamisha kichwa Salome,milio Kadhaa ya risasi ikasikika Salome akaachia yowe baada ya risasi moja kumtwanga maeneo ya begani,Katarina akarudisha gari nyuma akaligeuza na kutoweka maeneo yale...




Zidu wala akuangaika kumfatilia ndo kwanza akalitia gari mafuta kuelekea kituo cha polisi akaenda kutoa maelezo kuwa walivamiwa na mtu ambaye aliwashambulia kwa risasi,kituoni pale alimkuta Afande Nurdin,




"hey Koplo chukua maelezo ya huyo Zidu umkatie pf3 mpz wake akatibiwe,"




Koplo Zena, askari alokuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Inspekta Nurdin akachukua maelezo kwa Zidu Kama alivyohitajika ,




Zidu akuthubutu kumtaja mke wake kwamba ndiye aliye fanya tukio lile,wakaelekea hospitalin ambapo zoezi la kutolewa risasi liliendelea...




Wakati Salome akiendelea kutibiwa muda wa kuwaona wagonjwa ulipopita Zidu akatakiwa kutoka,akaingia ndani ya gari lake lililoharibiwa vibaya kioo cha upande wa siti ya pembeni ya dereva




Safari hii Zidu akaelekea moja kwa moja nyumbani kwake usoni akiwa kavimba kwa hasira...








Katarina hata hakuwa na wasiwasi ndo kwanza moyo wake ulijaa furaha,ni baada ya kumshambulia mwanamke alomkosesha amani,hakiwa jikoni anaosha vyombo wakati huo msichana wao wa kazi Suzan hakiwa anapika ghafla mlio wa honi nje ukasikika,wote wawili wakainuka kitendo kile kikawafanya wacheke




"haya nenda wewe kamfungulie baba yako mi niendelee kusonga huu ugali na kukarangiza, Suzani akacheka na kutoka kwenda kufungua,katarina akanawa mikono yake vizuri akaipangusa kisha akayasogelea majiko akaonja chumvi kwenye mboga mchuz wa nyama,akatabasamu akawa akiukoroga uji wa ugali ulikuwa tayari umechemka akachepuka kuelekea kabatin akatoa unga tayari kwa kuusonga...




Huku nyuma Suzan alifungua geti Zidu akaingiza gari alikuwa kanuna hata salamu yake akuitikia




"mama yako yupo wapi?"




"yupo jikoni"




Suzan akajibu huku akitetemeka miaka mitatu sasa alikuwa akifanya kazi pale toka kina Zidu wajitegeme kutoka katika familia ya Isack lakin hakuwai kumuona Zidu akiwa katika hali ile




Zidu akaelekea mpaka jikoni jazba zikiwa zimempanda kwa jinsi alivyokuwa akipiga hatua Katarina kule jikoni machale yakamcheza akajua Zidu yu aja kishari akafunika ule uji na kusitisha kusonga ugali ili ajipange,alikuwa ni mwanamke jasiri asiyependa kuonewa,asiyependa kupigwa,kupigwa labda aotewe katika kupigana muda mwingi alipenda kuvaa suruali,vikaptura au nguo yoyote inayoweza kumpa uhuru wa kurusha mguu wake teke...




Zidu akaingia...




"wewe mwanamke wantafuta nini hasa sasa leo utantambua!"




Zidu aliongea akimsogelea huku kapanua mkono wake amchape kibao ila Katarina akaudaka na kuushusha chini kwa nguvu,




"hayo ni malipo ya usaliti,nilimkanya akutaka kunisikia na huo ndo mshahara wake anaostahili akaadithie kuzimu,na nikwambie tu kila mwanamke utakayeamua kuwa naye kimapenz sitomuacha hai ntamuua kwa mkono wangu nadhan umensahau Zidu kutokuwa jeshini kwa muda mrefu hii aina maana sipo fiti,silaha nnayo uwezo wa kupata risas pia nnao,mbinu za mapigano pia nnazo ivyo wewe ndo utakayesababisha niue nitaua kwa ajili yako"




Katarina aliongea kwa hisia,Zidu akukubali naye akamjibu...




"lakin kabla ujaua mimi ntakutanguliza ili ukawatengenezee njia hili ukiwaua uwe tayari unajua wanaelekea wapi"




Ghafla Zidu akapeleka mkono wake mfukoni ile anauchomoa na kuunyoosha tayar Katarina alisha upiga teke risasi ikapaa ikatua pembeni kidogo ya Suzan




"mwanaume Kamili tena komandoo yakupasa upambane kwa kutumia mikono na miguu si bastola Suu okota hiyo bastola..




Kabla bado ajamalizia kutoa maelezo Zidu akamrukia teke lililo mfanya akapepesuka na kwenda kudondokea uji ulokuwa ukitokota ukamuunguza vibaya sana...




"mamaaaa!"




Suzan akaita kwa mshangao ulochanganyikana na woga,tena mbaya zaidi ulimuunguza maeneo ya mgongoni,



ITAENDELEA


imulizi : Kufa Tu  Hakuna Namna 


Sehemu Ya Tatu (3)




Zidu akabaki kaganda pasina kuamini kile kilichotokea,unajua shetan ni kiumbe mbaya sana ukushawishi kufanya kitu na kwa kukujaza hasira,chuki au tamaa ya hicho kitu ukishakitenda uondoka na kukaa pemben akikucheka huku akikwachia majuto na huzuni...




Ndicho kilichomkuta Zidu Katili pamoja na ukatili wake roho mbaya alokuwa nayo ilo mpelekea hata kumchukia mkewe akajikuta sasa akijilaumu akamkimbilia mpz wake




"nisamehe katarina..."




Katarina aliumuka vibaya sana mgongoni malenge lenge dah akawa akilia kwa uchungu ndipo akili zilipo mrudia Zidu,akamnyanyua mke wake




"fungua mlango"




Akamfokea Suzan alofungua mlango wa mule jikoni Zidu akatoka Suzy akafungua mlango wa koridoni zidu akapita akawah kufungua na mlango wa gari




"Ingia"




Suzan akaingia kiti cha nyuma akakaa na Katarina,Zidu akaingia Kiti cha mbele cha dereva gari ikawashwa alipofika getin akashuka akafungua geti na kulifunga kwa nje kwa namba zake maalumu wakaelekea hosptalin,hali ya Katarina ilikuwa ni mbaya sana...




Alifikishwa hosptalin madaktari wakamchukua haraka haraka tayar kwa kumuudumia wakimpaka dawa mgongoni...




Zidu akaambiwa tu ye aende arejee kesho akalipia kila kitu yeye na Suzan Wakaondoka,lau Kama angejua ni bora angemweka mmoja "vip" kutokana na kuchanganyikiwa akukumbuka ilo...




Katarina alipopakwa tu ile dawa kidogo ikampunguzia maumivu,Salome naye baada ya kutolewa risasi na kupigwa bandegi akaambiwa akapumzike wodini akipewa kitanda namba nne,wakati Katarina anaingizwa akaingizwa wodi ile ile mbaya zaidi akapewa kitanda namba tano ila muda huo Salome alikuwa kalala kageukia upande wa pili,




ivyo akumuona Katarina na kwa kuwa Salome aligeukia upande wa pili Katarina akumjua...




wodi ile ilikuwa na vitanda ishirini pande nne,kila pande ikibeba vitanda vitano ivyo katarina alipat kitanda cha kwanza mgonjwa alotoka Salome kitanda cha sita upande wa pili akiwa jiran na Kata










Jaribio la shambulio la kumtwanga risasi Salome linalofanywa na Katarina linashindwa




Zidu baada ya kumuwaisha hospitalini anarejea nyumbani,ugomvi mkali unazuka ugomvi unaopelekea Zidu kumuunguza mkewe na uji ulokuwa ukichemka,Zidu anamuwaisha hosptalini na kwa bahati mbaya zaidi Katarina anapewa wodi alolazwa Salome Je nin kitaendelea?




Siku ilofatia asubuh ndipo Katarina na Salome walipotambuana,Salome alishtuka kumuona Katarina,naye Katarina alishtuka kugundua kuwa Salome kuwa bado yu hai,akawa akimwangalia kwa macho makali yaliyozidi kumwogopesha binti yule,




Katarina akuweza kufanya chochote kwa kuwa wodi ile ilikuwa na wagonjwa wengi ila swala la kumwangamiza Salome lilikuwa palepale




'kama bado nataman kuendelea kuishi sina budi kutoroka hapa hospitalini'




Salome aliwaza kwani kwa sasa aliendelea vizuri,




Akakusanya vyombo vyake na nguo zake zote katika mfuko,akusubiri kuruhusiwa akajinyanyua kitandani ile anataka kuondoka akashtushwa na sauti nyuma yake...




"mke mwenzangu unaelekea wapi asbuh asbuh hii hata umeruhusiwa kweli?"




Baadhi ya wagonjwa wakainua vichwa vyao kumtazama Salome,binti kwa aibu akarejea kitandani kwake...




"mbona kama umeingiwa na uwoga,nilikukanya lakini,ole wako sasa uwaambie polisi kwamba unani hisi mimi utajirahisishia zaidi kifo chako,"




Katarina aliongea kwa sauti ya upole ilo mfikia Salome Pekee,ghafla Mlango ukafunguliwa na maskari wawili wakaingia,




Alikuwa Ni Koplo Zena akiambatana na Insp Nurdin wakiwa katika sare zao za jeshi la polisi wakaelekea mpaka mahala alipo Salome tayari kuanza kumuhoji,




"je unamuhisi nani alousika katika kukushambulia wewe risasi?"




Insp Nurdin baada ya kumpa pole akamtwanga na swali,Salome alipomtupia jicho Katarina alikutana na jicho kali akanywea




"ha..ha...hapana simuhisi mtu kwa kweli"




Jibu lile na hata kigugumizi cha ghafla alichokipata Salome kikawatia shaka wanausalama wale kabla awajauliza swali jingine ghafla mlango ukafunguliwa na Zidu akazama wodini, alishtuka kumuona Katarina kajilaza pembeni ya kilipo kitanda cha Salome,




Akapiga hatua mpaka kilipo kitanda cha Salome akawasalimia maaskari wale,




"unaendeleaje mgonjwa?"




"naendelea vizuri tu,"




"ok,n..nimekuletea chai"




Zidu aliongea akitoa chupa kwenye mfuko na kuiweka juu ya kakabati kadogo kalichokwepo pale,




Akatoa na nusu mkate akauweka pale,vilivyobakia akasogea navyo kitanda cha pembeni,




"unaendeleaje Katarina?"




Zidu akauliza uso ukiwa umemtawala haya,Katarina akujibu kitu Zidu akaendelea...




"amka basi unywe chai"




"tafadhali naomba niache"




Katarina aliongea usoni akionekana kuchukia




Kila Kitu maaskari wale walikishughudia sasa mashaka yakatawala katika nyuso zao,




Zena akajinyanyua na kusogelea kitanda cha pili akimwacha Nurdin Pale alipo Salome




"samahani Kaka huyu ni mke wako eeh?"




"yah ni mke wangu kwani vipi?"




Zidu akaitikia kwa hasira kama vile akupendezwa au tuseme akutaka kuendelea kuulizwa maswali yale,ila tofauti na mategemeo yake Koplo Zena akashusha tabasamu pana akamtwanga swali lingine...




"naona kabla ujaja hapa ulianza kwa yule pale naye ni nani wako?!"




Zidu akazidi kukunja sura kutopendezwa na maswali yale..




"secretary wang"




Akajibu kimkato,




"ahaaa turudi kwa mke wako ni kipi hasa kilichomkuta"




"kamwagikiwa na uji wakati anapika kwa bahati mbaya ndio ukamuunguza,




"ok,tukitoka itabidi tutoke wote kwa mahojiano zaidi..."




Palepale akamgeukia katarina alokuwa akiwasikiliza muda mrefu




"pole sana dada,unaendeleaje sasa?"




"kama unavyo niona!" Katarina akajibu...




"yule pale unamfahamu?!,"




"ndio ni mfanyakazi wa mume wangu"




"umemfahamu toka lini?!"




"zaidi ya miaka miwili toka alipoajiriwa?"




"unafanya kazi katika kampuni ya mume wako?"




"hapana mi sifanyi kazi"




"kama ufanyi kazi umemjuaje au mume wako kakuonesha picha za wafanyakaz wako wote na kukutambulisha majina yao?"




"hapana hapo mwanzo nilikuwa nikifanya kazi ila nikaacha"




"kwa nin uliacha kazi?"




"mume wangu aliniachisha"




"kwa nini akuachishe?"




"ilo swali labda umuulize yeye mwenyewe ndo anayeweza kukujibu"




"ok kaka kwa nini ulimuachisha mkeo kazi"




"niswala la kifamilia"




Zena akageukia upande wa katarina,yani alikuwa akiuliza swali pasina kufikiria tena akiwa chap...




"una ugomvi wowote na huyu mfanyakazi wa mume wako?"




"Hapana"




"ok,asante"




Zena alimaliza,wakijua kaishia pale akarukia kitanda kingine akajitambulisha




"kwa jina naitwa Koplo Zena kutoka makao makuu ya jeshi la polisi huyo binti hapo unayemuona kashambuliwa na risasi na watu wasojulikana na sisi tupo katika upelelez wa kumtambua mshambuliaji na maswali machache ya kukuuliza bibi




"s.sawa mwanangu"




"jina lako unaitwa nani?"




"bi z..zena!"




"haaa wajina..."


Wote wawili wakatabasamu...




"sema sasa mjukuu wangu"




"huko apa hosptalin toka lini bibi"




"nna..na..wiki sasa"




"yule mgonjwa pale kaletwa lini?"




Akamnyooshea kidole Salome




"Juzi mjukuu wangu tena akiwa katika hali mbaya"




"na huyu mwingine"




Akamnyooshea Kidole Katarina,




"jana usiku, huyu kaka ana mtihani wake zake wawili wote wagonjwa"




Zidu,Katarina Salome na hata insp Nurdin wote walishtushwa kwa kauli ya bibi yule




Zena akatabasamu!




"bibi kwani umejuaje kama hawa wote ni wake zake"




"haaa si huyo hapo mwenyewe kasema asbuh huyu alitaka kuondoka huyu mke mwenzake akamwambia mke mwenzangu unaenda wapi na ujaruhusiwa basi akarudi"




Katarina alikumbuka kwel aliongea maneno yale na hata Salome Kwel alisikia akiambiwa vile!




Zena akanyanyuka na kumsogelea Katarina,"je nikweli uliongea maneno hayo?"




"ndiyo"




Katarina akuona haja ya kubisha...




"ni kweli Salome alitaka kutoroka?"




"sina uhakika ungemuuliza yeye maana mi nilimwona kabeba mfuko wenye vitu vyake"




"je ana mahusiano yoyote tofaut na kaz na mumeo?"




"kwa ilo kwa kwel sijui mi najua hana na namwamin sana mume wangu"




"kwa nin sasa umwite mke mwenzako"




Katarina akatabasamu




"ndo tulivyokuwa tukiitana ivyo hata kazini"




Zena akasogea kitanda cha mgonjwa mwingine huyu alikuwa ni mtoto mdogo,




"ujambo mtoto mzuri?"




"sijambo shikamoo dada"

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog