Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (5)
Sehemu Ya Nne (4)
Hakukuwa na mtu aliyeshuhudia kitendo kile akiwa kama wanajeshi wa kambi ile akaanza kuondoka kuelekea getini hakuna aliye mtilia shaka kwa bahati nzuri pale getini alikuta kuna wanajeshi wawili tu waliolinda hiyo haikumpa tabu kutoka
Kwani kwa vyovyote vile Gambi ilikuwa ni lazima atoke kijeshi au hata kikomandoo ndani ya kambi ile
§§§
Nchi ya Kinte ilizizima kwa taarifa ya kutoroka kwa Gambi, jambo hilo liliwashangaza wananchi wa Kinte
Taifa lililojaliwa maliasili za kuvutia kitita kama zawadi kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake kilihamasisha msako kwa vijana msako wa chini kwa chini nako bado uliendelea bila mafanikio.
Gambi hakuonekana, inspekta Nurdin alizidi kuchanganyikiwa, vikao vya mara kwa mara havikuisha Ikulu, akiitwa mara kwa mara naye hakuwa na jibu stahiki la mahali alipo huyo kijana hatarishi kwa viongozi wa serikali ya Kinte,
mwisho serikali ikaongeza mainspekta wawili Kulwa Manyanga na Said Chezo wasaidiane kumtia Gambi nguvuni.
Walikuwa ni mainspecta wenye uelewa mkubwa na kazi yao;
Baada ya ujio wa ma inspecta hawa wawili mori ya kufanya kazi ikaongezeka wakipewa wiki mbili za awali.
Je wangefanikiwa?!
§§§§§
Giza lilitawala eneo lile ni wakati huo ndipo Gambi alipozidi kulisogelea geti kwa umakini wa hali ya juu kwa kawaida wanajeshi hawakuruhusiwa kutoka usiku bila ruhusa maalumu
Walinzi wale wawili walokuwa ndani ya kiofisi kidogo wakipiga story huku macho yao yakiwa yametumbuliwa wakimtazama Gambi alivyokuwa akiwasogelea
ni wazi kuwa hawakumtambua hivyo hakuwa na shaka na hilo!
Aliwafata mpaka ndani ya kile kibanda kidogo na kuingia ghafla alichomoa bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti na kufetua risasi kadhaa katika miili ya wanajeshi wale wakadondoka kama makuti bila hata kutoa sauti gambi akautumia mwanya uwo uwo kutoka nje bila kugundulika maafa aloyafanya.
Habari ya kuuwawa kwa walinzi wanajeshi wawili wa kambi ya kijeshi Isonga zilimfikia afisa Brown Stanpey ambaye akiongozana na jopo la wapelelezi Jonathan,
Kulwa na Said walifika kambini na kuchukua alama za vidole katika kijumba kile kwa kupitia ukutani na milangoni marehemu wakachukuliwa na kuwaishwa hospitali ya jeshi kwa uchunguzi na aina ya risasi zilizotumika zikitolewa.
Hakika lilikuwa ni jambo lililomshangaza Nurdin
Hakuelewa Gambi alihusika vipi na mauaji yale bado hakuwa na jibu ya kilichokuwa kikiendelea alikuwa kwenye giza ila alikuwa na uhakika ni gambi kutokana na alama za vidole alizoziacha ukutani,
Ina maana huyu mwana haramu alikuwa anaishi huko kambini?! au ilikuwaje?! Mbona kizaazaa?! Au ina maana aliingiaje mule?!'
Mawazo yakazidi kukisakama kichwa chake pasina majibu stahiki,hali ya mkanganyiko wa jinsi kesi hiyo ilivyokuwa ikimchanganya ikazidi kumchanganya Mara dufu!
Ila akupaswa kukata tamaa zaidi ya kujifariji kusudi hazidi kujitia nguvu
'Tutamtia nguvuni tu'
§§§§§
Mwanajeshi yeyote ni mtu anayethamin sana muda,
Hata kwa Gambi, nafasi ilipojitokeza hakudiriki kupoteza hata sekunde yake!,
ivyo aliendelea kutembea mpaka Stendi kuu alijiapiza kwa usiku huo kwa muda huo ilikuwa lazima afike mjini kabla "akijabambaruka" juu ya mauaji ya kule kambini,
Ilikuwa pia ni lazima afike mjini kusudi ajue ni jinsi gan atawamaliza wabaya wake.
Walousika na mauaji ya wazazi wake na kumtia kifungoni!
Na Kumpa jina la mfungwa!
Hapana
"Nisipowauwa, wenyewe wataniangamiza washe-nzi hawa",
Gambi aliendelea kuwaza hasira, ghadhabu ilojaa moyon mwake haikuwa na mfano roho yake ya upole ilibadilika roho ya unyama iliongezeka kila dakika iliposogea.
Alifika stendi na kupakia coster kwa kuwa alikuwa kavaa magwanda ya kijeshi na kofia kaishusha kuziba uso wake kidogo hakuna mtu alokuwa na habari na yeye mfukoni hakuwa ata na senti ilo alikumpa tabu kwani wana usalama wa Kinte walipakia magar bure
Safari katika hali ya utulivu na amani iliendelea mpaka mjini alimshukuru Mola wake ukaguzi haukumgundua kila kwenye vizuizi alionekana kama mwanajeshi na waliiruhusu gari iendelee maaskari, matrafki walishika picha yake wakikagua kila gari hakika msako ulikuwa ni mkali baada ya kufika stendi alishuka na kuingia katika mgahawa ulokuwa eneo lile kwani alihisi njaa ikimtafuna akaagiza chakula japo hakuwa na hela ilo akulijali macho yake yakatua kwenye runinga ilokuwa ikirusha taarifa ya habari,....
*MUUAJI ANAYESAKWA AENDELEZA MAUAJI KATIKA KAMBI YA JESHI ISONGA KAUA WANAJESHI WAWILI NA KUMVUA MMOJA NGUO NA KUTOKOMEA NAZO KWA YEYOTE ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWAKE ATAPATA ZAWADI NONO.....*
Gambi hakusubiri habar ile iishe alinyanyuka na kuelekea chooni akili yake ilifanya kazi zaidi ya kompyuta alihitajika kufanya kitu.
Eneo lile la chooni lilikuwa kimya ila kuna mlango ulifungwa kwa ndani kumaanisha kwamba kuna mtu ndani,
“haya mavazi si salama tena lazima nipate mengine mda huu na anza na huyuhuyu”
Gambi aliwaza na punde yule mtu alitoka chooni Gambi alimpokea kwa teke na kukikunja kichwa chake yule mtu akatulia tuli Gambi akamvua nguo zake na kuzivaa!
“Haya mavazi si salama tena lazima nipate mengine muda huu na anza na huyuhuyu”
Gambi aliwaza na punde yule mtu alitoka chooni Gambi alimpokea kwa teke na kukikunja kichwa chake yule mtu akatulia tuli
Gambi akamvua nguo zake za kisharobaro na kuzivaa naye akamvalisha gwanda zake huyoo mwanaume akasepa"
***
MERY muhudumu wa mgahawa mkubwa wa GARDEN INN macho yake yalikuwa kwenye televisheni,
Sura ile ya GAMBI haikuwa ngeni machoni pake alijua ni yule yule aliyemuhudumia alipoangalia sehemu yule mwanajeshi alipokaa alimshughudia akinyanyuka na kuelekea toilet naye akutaka kusubiri uchu wa mamilion kwa yeyote atakayewezesha kukamatwa kwa gambi ulimuingia akapiga simu polisi....
"una uhakika dada?..."
Jonathan alipopokea simu akahoji pasina kuamini kile akisikiacho..
"Ndiyo yeye kaelekea toilet"
muhudumu Yule kwa uhakika akajibu....
"Ok twaja saivi"
Jonathan alijibu na bila kupoteza muda aliwashtua wenzake Kurwa na Saidi safari ya matumaini ya kumtia nguvuni GAMBI ikaanza
Dakika tano baadaye waliwasili mgahawani pale kwa haraka wakaelekea chooni
Walipofika mlangoni wakapishana na kijana sharobaro alovaa 't shart' yake Kali na 'jeans' ya special chini alikuwa na raba Kali kichwani alikuwa na kofia aina ya kapelo!
Kwa kuwa maelezo yao ni kuwa Gambi alikuwa na sare za kijeshi na haraka walokuwa nayo pasina kumtilia Shaka mtu yule wakampita na kuelekea ndani ya vyoo vile.
Ahmadi! Wote walipigwa na butwaa baada ya kupokelewa na maiti ilovalishwa gwanda zile za kijeshi!
"Atakuwa si ndo huyo tulopishana naye?!"
Kurwa akauliza akiwatazama wenzake!
Kwa haraka wakageuka kurudi nje ya vyoo vile!
Patupu!!!
Walipofika kwa muhudumu yule kumuuliza kama kapita pale jibu ni hapana GAMBI toka aingie chooni akutoka,ikabidi warudi tu kwa yule maiti huku wakionekana wazi kuchangulia
kama kawaida vinasaba vikachukuliwa shingoni mwa marehemu tayari gambi alishaondoka Jona alizidi changanyikiwa akujua atampatia wapi...
***
LAURENT MERNEL GAMBI akiwa ndani ya t shart na jeans chini katupia raba na kofia aina ya kapelo kichwani mkononi alikuwa na saa na usoni alivaa mawani,
Kapelo ile aliigeuza nyuma baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya bar ile akaelekea saluni japo alikuwa na khofu ya kukamatwa ila alijihamini akupaswa kuwa muoga
Kwa bahati nzuri akukuta mtu ndani ya saluni ile akaketi katika kiti na kujifunika shuka jeupe kumsubiri kinyozi baada ya dakika chache jamaa huyo akaja!
"Sory bro kwa kukuchelewesha nilikuwa hapo jirani si yule muuaji anayesakwa gambi kafanya tukio na kusepa jamaa ni noma aisee"
Kinyozi yule pasina shaka akisafisha mashine yake akaanzisha stori moyo wa Gambi ulipasuka paaaaa kwa mshtuko
Lakini kwa kuwa alitambua ajagundulika akajitoa hofu! Na kujichekesha
"Daaah kashafika mtaa huu?!"
Gambi akaoji akijifanya kushtuka
"Stayle gani broo nkunyoe" jamaa kabla ajajibu akauliza!
"Zipunguze kiasi ndevu nyoa o! Kwa hiyo usiniambie jamaa bado analitia joto jeshi'
" si ndo hapo! nipo hapa mkuu si ndo ni kaona kipira cha polisi kikipita kwa spidi na makelele kutoka kumbe ni hapo Garden inn jamaa alikwepo nasikia chooni maaskari kuingia mtu kashafanya yake na kusepa"
Kinyozi yule akazidi kutoa ushuhuda huku akiendelea kumnyoa ndevu zake alizinyoa o ilomwongezea umaridadi,
Baada ya kumalizwa akaingiza mkono mfukoni na kutoa waleti akaifungua na kutoa 2000 akampa jamaa yule na kutoka zake!
Jamaa alionekana kabisa kuto kumtambua!
Kisura Gambi alikuwa kakomaa na mwili ulojengeka kimazoezi hivyo ile tshart aloivaa ilimbana vizur na kukionesha kifua chake kipana
Alikuwa ni bonge la sharobaro Handsomeboy mwenye mvuto kwa kila mwanamke amtazamaye
Ilikuwa ni kazi ngumu kumtambua kwa jinsi alivyokua mfukoni alikuwa na laki moja na nusu katika waleti ya yule sharo
Baada ya kutoka saluni akaelekea mtaa wa lowasa rod
Aliachana na barabara hyo ilowai kuzinduliwa na waziri mkuu mstahaf wa nch jiran ya Tanzania,
Nchi ilosifika kwa kuwa na amani ulimwenguni
Akaingia katika barabara ya kwakwen ilokuwa na vumbi ambapo alipanda bodaboda ilomfikisha katika kijiji kimoja kilichoitwa MZUVA LAND,
Kijiji hiki kilikuwa mpakani mwa ganyama na kinte,ni kijiji cha watu masikini ni kijiji ambacho hata komando chaka aliwai kujificha wakati alipotumwa kumuua rais wa ganyama Silvestar
Alijua kitendo chake cha kukaa huko kingemuwia vigumu kugundulika akujua kama anajidanganya na laiti kama angejua asingeish humo.
Alipata chumba cha bei poa elf tano kwa mwez akaya anza maisha akilala chini,huku akifikiria jins atakavyoanza kulipiza kisasi
Uclolijua ni sawa na usiku wa kiza!!!!
Daaaah nini kilichoendelea?!
Gambi atakamatwa?!,vipi maendeleo ya Katarina Zidu icu nchini Tanzania?!,na Kiapo cha Isack dhidi ya Zidu!..
Alijua kitendo chake cha kukaa huko kingemuwia vigumu kugundulika akujua kama anajidanganya na laiti kama angejua asingeish humo
Alipata chumba cha bei poa elf tano kwa mwez akaya anza maisha akilala chini,huku akifikiria jins atakavyoanza kulipiza kisasi
uclolijua?...
Ni sawa na usiku wa kiza!!!
***
Mainspekta hawa watatu walijigawa kila mmoja kwenda katika kasino lake kujaribu kama wangeweza kumbahatisha KURWA MANYANGA
Siku hiyo akil yake aikuwa sawa akiwa katika kasino lake la tripo h akiangalia walimbwende mawazo yakampeleka kwa mpenz wake SHANIA mtoto mrembo alojaliwa uzur wa haja,
japo alikuwa ni masikini na aliish kwa shida lakin uzur wake aukujificha kila siku ulizidi kuchomoza kama jua lichomozapo asbuh
Alimpigia simu dereva wake bwana Olomy Wakaelekea Mzuva Land katu hakujua na kama angelijua timbwil timbwil la huko ni bora asingeenda
Ni dakika kadhaa zilishapita,na alihisi hitaji la sigara akajinyanyua pale katika kona ya chumba alichoketi na kutoka nje akaelekea katika duka lililopo mtaa ule ule
Macho yake yalitua kifuani mwa dada yule mrembo, kwa sekunde chache alishindwa kutamka kitu na kubaki akimkodolea macho dada yule alokuwa akiuza duka kwa mara ya kwanza toka ajiunge na jeshi alihisi kumpenda tamaa ya ngono ikamvaa...
"Nilikuwa naitaji cocacola ya barid.,"
GAMBI aliagiza huku macho yake yakiendelea kumchombeza dada yule wazo la sigara liliyeyuka bado aliitaji kuwepo eneo lile...
"shadaash! bin moyo wang kama si hawa nyang'au angefaa kuwa mke cheki macho yake chek matiti yake dah! kuna vitu vilivyoshushwa hiki akikuzaliwa hiki..."
aliwaza huku akiendelea kumtazama kwa tabasamu mrembo yule
GAMBI aliendelea kuwaza huku hisia zikimpanda kwa kasi alihitaji awe naye hata mara moja tu akaona uwo ndo muda wake
"mimi naitwa Zuberi Maruma mwenzangu sijui unaitwa nani?"
Gambi alidanganya jina akitumia jina la mwandishi mmoja ambaye alikuwa akisoma stori zake fb na whatsupp
Mapigo ya moyo yaliongezeka kasi kila alipomwangalia dada yule.
Dada yule akacheka
"Heee wewe ndo yule mtunzi wa riwaya fb na Whatsupp unaye andikaga pia visa na mikasa ya watu
Mdada akahoji kumbe naye alikuwa ni mpenzi wa riwaya za kijana yule akatabasamu, tabasamu lililozidi kumchanganya gambi wakati gambi akisubiri jibu gari ilifika na INS KURWA MANYANGA na OLOMY wakashuka kurwa akamtumbulia macho
Macho ya wivu, Gambi naya akanyanyua kichwa kumwangalia kurwa ni kosa kubwa sana alilofanya
Macho yao yakagongana! Kurwa akamtambua gambi na bila kupoteza sekunde alichomoa bastola kibindoni
"upo chini ya ulinz nyoosha mikono yako ju..."
Kabla ajamalizia sentensi yake teke kali lilitua katika mikono yake na kuirusha bastola ile juu
Akajigeuza na teke lingne mpaka katika maeneo ya kifuani teke hilo lilionwa vizur na kurwa alorudi nyuma hatua tatu ndefu teke lile lika ambaa hewani na kumfanya gambi hakosi mhimili na kupepesuka.
kitendo kile kilimfanya kurwa aruke teke la jonchu la maeneo ya maungoni na kuziathiri korodani za komandoo yule.
Gambi akajipinda kuzishika kosa kubwa sana alifanya kwani kwa kasi ya ajabu kurwa alimjia kwa teke lililompeleka chini dakika hiyo hiyo akamfunga na pingu
Watu walishajaa eneo lile,
Kurwa akachukua simu yake na kuwajulisha wenzake!
Ila tamaa ya kuonekana shujaa na tamaa ya kupata "kibunda" ikamponza akusubiri wenzake waje! pengine mbali na tamaha yake pia alihofia kumpoteza gambi kwani eneo lile hakuliamin sana akafanya kosa.
kosa lililomgharimu tayar taarifa ilishazagaa katika idara ya polisi na wakuu mbalimbali walikubaliana kuonana makao makuu ya jeshi la polisi yaliyopo wami mjii mkuu wa kinte
Kurwa pamoja na dereva wake olomy wakiwa katika mwendo mkali wa kuelekea makao makuu ya jeshi la polisi ambacho hakujua kurwa ni kwamba OLOMY alishawasiliana na wenzake ODOVY KYELA na FATMA ambao mda huo huo walitoka kwenye nafasi zao za kazi na wote kuelekea uelekeo ambao olomy aliwaelekeza wakiita "safari ya matumaini"
Wakati gari ikiwa kwenye mwendo mkali ghafla OLOMY alipiga break ya ghafla kitendo kilichosababisha wote wagongane kwa kasi ya ajabu OLOMY alimtandika ngumi nzito KURWA kabla ajafanya kitu tayari alishamchoma kisu cha mbavu hakutaka kupoteza muda aliwasha gari na kuliondoa kwa kasi hakiwa kasha uondoa uwai wa mpelelez alo ongezwa KURWA muda wote gambi alikuwa akishangaa hakuweza kufanya kitu kwani pingu alizofungwa miguuni na mkononi zilimkaza madhubuti
***
Wakwanza kupata habar ya kifo cha mpelelezi KURWA alikuwa ni mpelelezi inspekta Jonathan
hakika ulikuwa ni utata mkubwa makao makuu ya jeshi la polisi maafisa wote walikuwa kimya wakimsikiliza rais.
"ni kazi gani mnayofanya ninyi? sasa natoa siku tatu laurent MERNELI GAMBI awe amepatikana lasi ivyo afisa upelelezi,jemedar mkuu,na viongozi wote wa jeshi mjiuzulu siwezi kufanya kazi na watu wasoweza kazi"
Rais alitoa tamko! viti vya maafisa wakubwa wa jeshi viliwaka moto
Rais laizer nyoshi alinyanyuka na kuondoka kwa hasira
maafisa wote walimwangalia afisa ALEKS kwa hasira kwa sababu kesi ilikuwa mikonon mwake naye alimwangalia insp Jonathan kwa hasira ambaye naye hakuwa na chakujieleza.
***
Inspekta Jona aliwasili eneo la tukio triple h kwa sababu mara ya mwisho KURWA alisema anaenda huko na kwenda moja kwa moja counter ambapo alimfata SHANIA alokuwa bado na majonzi
"za saivi shemeji...."
alisalimia
"nzur tu shemu"
"shemu unaweza kunambia siku ya tukio ilikuwaje?"
"mh! yani siamin shemeji alikuja kijana mmoja kimuonekano ni mzuri kisura kiumbo katupia pamba hakasimama hapa uliposimama akaagiza soda akaanza kunywa
wakati anakunywa si ndiyo kurwa akaja na aliposhuka tu alipomuona akamchomolea bastola wakaanza kupigana lakini KURWA alishinda na kumfunga pingu miguuni na mikononi...."
Jonathan aliendelea kuandika lakini ghafla akasita akashtuka na kunyanyua kichwa chake! akaoji peni yake ikiwa mdomoni kwa tafakari zito,..
"unasema alimfunga pingu miguuni na mikononi?"
"ndiyo shemu"
"Mh sasa itakuwa ajilifunguaje au huyu jamaa ana mtandao?"
Jonathan aliuliza taratibu kama vile anaongea mwenyewe umakini ukiongezeka katika ncha za akili yake akaendelea kumsikiliza dada yule mrembo....
"baada ya hapo wakambeba wawili wakampakia kwenye gari"
Jonathan akashtuka akaoji kwa shauku....
"unasema walimbeba wawili?"
"ndiyo shemu!,"
"huyo mwingine unamfahamu?!"
"ndiyo ni dereva wake"
"axante sana shemu nitarudi nikikuitaji"
Jonathan akutaka kupoteza muda alishajua pa kuanzia!
Kuna kitu alichohisi ni lazima ampate dereva yule!...
Jonathan akashtuka akaoji kwa shahuku....
"unasema walimbeba wawili?"
"ndiyo shemu!,"
"huyo mwingine unamfahamu?!"
"ndiyo ni dereva wake"
"axante sana shemu nitarudi nikikuitaji"
Jona akutaka kupoteza muda alishajua pa kuanzia!
Ilikuwa ni lazima dereva OLOMY apatikane kwa gharama yoyote aliondok hapo akiwa na tumaini jipya
***
Baada ya OLOMY kufanikiwa kumuua KURWA na kumtupa alirudi na kumfunga Gambi kitambaa cheusi usoni na kuliondoa gari kwa kasi
dakika chache baadaye gari nyingine iliwasili katika mtaa usokuwa na watu wengi
Wakashuka vijana wawili ambao walionekana kujuana na Olomy
OLOMY akafungua mlango akisaidiana na wale vijana wakambeba gambi na kumuingiza ndani ya gari walokuja nayo na ile ya KURWA wakaiacha hapo hapo
"kazi nzur sana " kijana mmoja hapo akampongeza Olomy
"DAH kwenye mapigano jamaa yuko fiti alishamdhibiti jamaa nikaona nimuondoshe tu duniani"
ITAENDELEA
imulizi : Kiapo Cha Mfungwa (5)
Sehemu Ya Tano (5)
Olomy aliwa ambia wenzake
"ok fatma yupo wapi?" Olomy akaoji
"yupo hotelini anatusubiri"
"poa mi kazi nshaharibu"
"kilichotuleta si tumefanikiwa?"
"ila saivi ujue wazee nami ntasakwa."
Olomy akasema
"kwani wana picha yako?"
"ndiyo"..Olomy akatamka kwa wasiwasi
" ooooh shit but siyo ishu twende hotelini tukayapange!"...
Muda wote ule bado LAURENT GAMBI hakujua hao walikuwa ni wakina nani na walimuokoa kwa sababu gani na wala hakuwa na haraka ya kujua...
"kama vipi si tumfungue kabisa hizo pingu awe huru"
Olomy akatoa wazo
" ok mfungue ila kitambaa muacheni nacho..."
Mmoja wapo wa vijana wale wawili akajibu
Gambi akafungunguliwa pingu zote mbili bado hakuongea kitu chochote
***
Inspekta Jonathan Alikaa ofisini kwake mawazo yakimsumbua hakujua dereva wake KURWA olomy alikuwa wapi!?
' au naye atakuwa kauwawa?!'...
alijiwazia...
'Lakini! kama kauwawa yeye atakuwa katupwa wapi!? na nani anayefanya mchezo huu!'
Bado maswali yalizidi kutiririka kichwani mwake pasina majibu kwa kuwa mainspekta wote walikuwa na madereva wao alishika simu yake na kupiga namba ya OLOMY iliita mara moja kabla aijakatwa na kuzimwa kabisa.
Akili ya Jona ikazidi kuchanganyikiwa hakuwa na budi kuamisha msako kusaka watu wawili kazi ikazidi kuwa ngumu
***
Kilikuwa ni kikao cha watu wa nne ambao ni Odovy Kyela, Olomy Msofe, binti Fatma na Laurent Gambi
ambaye macho yake yalikuwa mekundu ishara ya hasira dhahiri mbele ya watu kadhaa ambao ni wazi kuwa halikuwa na kisasi nao
Macho yake yaliyotisha yaliangaza kuwatazama watu wale watatu ambawo ndiye wakombozi wake
Akakohoa kidogo kusafisha koo lake lililokabwa na "kisasi" cha wazazi wake dhidi ya wabaya wake akatoa msokoto wa bangi akavuta na kuachia pafu moja
Fatma akupendezeshwa na jambo lile ila gambi akujali matokeo yake ndo akatoa tabasamu lisilopendeza kwa kiumbe chochote kimwangaliaye
likachanua katika kingo za papi za midomo yake
akatasua mdomo na kuongea kwa sauti kavu na ya jeuri
"nashkuru mapapaa kwa kuokoa life langu ila! ila! ila! siwezi kuondoka kinte mpaka niwa adibishe hawa wasen...ge waloniulia wazazi wangu....ndiyo! naweza kuja kulinda amani kongo lakin mpaka hawa mafedhuli niwaondoe...."
ghafla akakatishwa na Fatma
"lakini...."
Gambi akaikatisha kauli hyo kwa ukali
"lakini nini Fatma?!! Mabedui wawauwe wazazi wangu mimi niwa ache waendelee kutesa katika ardhi hii?? ,
No angekuwa Zidu ndo kawauwa nisingelipiza kwa kuwa dady ndo alikuwa na nia mbaya na yule sokwe, lakin alimsamehe iweje watu watoke from no where wampindue dady wanihukumu kifo!? siwezi kuwaacha wazima wale,siwezi nasema siwezi abadani!!!."
Aliendelea kujibu gambi akanyanyuka na kuidondosha bangi ile ilobakia kidogo akaikanyaga kwa soli ya kiatu chake ikazima akapiga hatua kutaka kuondoka lakini ODOVY akapiga hatua ndefu na kumshika begani
"unaenda wapi gambi?"
Odovy alioji kwa wepesi wa ajabu gambi aligeuka kwa ngumi nzito ilompata sawia odovy pembeni ya jicho na kumsababishia maumivu makali
"Upaswi kuniuliza wala kujua ninapoelekea!,nishasema siwezi kurudi kulinda amani kongo mpaka nikamilishe kazi nilonayo nadhani nshaeleweka sasa mwanaume aniguse"
Gambi akaongea kwa dharau na kupiga hatua ingine kuelekea ulipo mlango wa kutokea
Odovy akukubali akajirusha kumkabili Gambi kama umeme gambi akamkwepa na wakati huo huo akiachia pigo sehemu nyeti katika mwili wa kijana yule wa kikongo!
Olomy kuona hivyo akaupeleka mkono mfukoni lengo achomoe silaha!
Ila Gambi akajirusha kumvaa Olomy wote wakaenda chini!
Mwanaume akawah kusimama sasa macho yake yalikuwa kwa Odovy na Fatma ,
Olomy alikuwa akigugumia chini kwa maumivu
Fatma alikuwa amebaki ametahayari,Odovy akajirusha na teke ambalo Gambi alilipangua sambamba na kuachia pigo jingine juu kidogo ya kiuno yani maeneo ya kitovuni
Odovy akaenda chini,akajinyanyua tena,sasa macho yake yalikuwa kwa Fatma akimwangalia kumpa taharifa kama naye anajiweza aende!
Daaah nini kitaendelea?!,Gambi kaokolewa ila kawasaliti waokozi wake!? Mpaka alipe kisasi atafanikiwa?!
Fatma alikuwa amebaki ametahayari, Odovy akajirusha na teke ambalo Gambi alilipangua sambamba na kuachia pigo jingine juu kidogo ya kiuno yani maeneo ya kitovuni
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment