Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO (MTETEZI WA KINTE) (4) - 4

   


Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4) 


Sehemu Ya Nne (4)



Ghafla Monica akasikia sauti nyuma yake,ile kugeuka akuyaamini macho yake alipo onana uso kwa uso na mdomo wa bastola



"Hii bastola nimeivalisha kiwambo cha kuzuia sauti na kwa uzuri zaidi eneo hili amna watu zaidi yangu Mimi na wewe sasa usitake nikayakatisha maisha yako haraka sana geuka unipeleke hiko chumba"



Ilikuwa ndo Mara ya kwanza kunyooshewa bastola ile,mkojo wenyewe ukaanza kumchuruzika,akaanza kutetemeka



"Pita mbele uniongoze haraka!"



Monica ubishi ulimyeyuka,akapita mbele Zidu akamfata nyuma mpaka katika jengo moja akamuoneshea chumba kimoja kilichokuwa na maandishi 'chumba cha siri' juu kabisa ya mlango



Alafu pia kulikuwa na maandishi mengine kwenye mlango ule wa kuingilia ' Usiingie' *HATARI*



"Una uhakika na usemacho?!"



Monica akatingisha kichwa kuafiki kile asemacho,"ok,unaweza kwenda" Zidu akamnong'oneza ile kageuka kutaka kuondoka zake ghafla kitu kizito kikatua kichwani,akasimama akauweka mkono kichwani akaserereka kabla ajafika chini Zidu akamdaka kukwepa kutoa kishindo akampeleka chini kidogo kidogo



'Kumwacha hapa hatari sasa ntamweka wapi!'



Akawaza macho yake yakiangaza huku na kule kutafuta eneo zuri la maficho la kumuifadhi, akuona,sasa akapata wazo lingine la tofaut kabisa,



Ndio aliona hilo ndiyo sahihi haraka sana akamnyanyua Yule dada juu akampachika mabegani



SECRET ROOM



MEN



SIRUHUSA MTU YOYOTE KUINGIA NDANI



Chini ya ardhi kule upande wa kiume nje ya mlango kulikuwa na tangazo ilo,na ndani ya chumba iko kulikuwa na kitanda kimoja vikabati vile vya hospitali na kameza cha kimtindo, kilikuwa ni chumba cha 'privet',juu ya kitanda kile alilala mtu alokosa fahamu huyu alitambulika kwa jina la Isack

Pembeni yake alikaa mwanaume wa kazi 'Sai' akimwangalia Kwa tabasamu jepesi huku vingi tu kichwani kwake akijiwazia



'Baada ya wewe kutoka hapa ndani ya masaa 24 na uhakika tutakuwa tushamtia Zidu nguvuni Kwa kuwa kila utakachofanya sisi tutakiona kila utakapoenda utafatiliwa pasina mwenyewe kujua'



Kwa wazo lile akajikuta akiishia kutabasamu akimwangalia Isack usoni kwa furaha,aliyelala pasina ufahamu wowote



Ghafla simu yake ikaita,simu ya kazi 'kuna nini' akajiwazia akibonyeza batani ya kupokelea



"Kokwa maliasili kuna mauaji yametokea mauaji tata inasemekana Zidu ndo msababishi wahi haraka"



Haraka sana 'Sai' akanyanyuka pale akaufata mlango na kuufungua akatoka nje lengo aelekee wodi zile za kike akajue mpenzi wake anaendeleaje

Je kashatolewa mimba apate kuwaaga akiwa ambia amepata dharura



Akafika mpaka katika kile chumba ambacho Monica Nusu saa ilopita alimuonesha Zidu kwamba ndani yupo Dk Dani pamoja na Kk,akauendea mlango akashika kitasa akafungua akaingia



Alichokutana nacho akuamini macho yake,dk alilala chini katika dimbwi la damu ni wazi akuwa na uhai tena kucheki kitandani Kk akwepo nini kilichoendelea?!, akajikuta akifikiria pasina kupata jibu



Ghafla macho yake yakatua dirishani kioo kilivunjwa akavutika kwenda kuchungulia nje Shabaaaaash akuamini alipomuona Katarina akiwa kalala chini akiugulia maumivu



'Ni nini lakini kilichoendelea hapa'



Akawaza akiruka lile dirisha kumfata mpz wake



"Ninini kilichotokea?!"



Akaniuliza mkono wake akiuingiza kwenye shingo kumwinua kidogo!



"Z...z...zidu"



Kk aliongea kwa shida,



"Zidu?!,kaja huku"



Sai'; alihoji kwa mshangao Katarina ndo akaanza kumsimulia ilivyokuwa



"Baada ya daktari kuja wakati akiwa ndo anajiandaa kunipiga Nusu kaputi ghafla mlango ukafunguliwa sambamba na kushughudia daktari akienda chini mbele yangu alikwepo Zidu mkononi akiwa kashika bastola ndogo yenye kiwambo cha kuzuia risasi ikifoka Moshi kutoka katika bomba lake



" najua una mimba yangu na upo hapa kwa ajili ya kuitoa naomba usiitoe huyo mtoto hana hatia kumbuka tulifanya kwa makubaliano na sikukubaka ivyo kama ni uhadui ubaki wangu na wako ila usiwe na uhadui na mwanangu huyo ndo kakufanya nikuache hai ningeshakuua hata kama utomlea nizalie nitakuja kumchukua hospital mwanangu hiyo siku utakayo jifungua kwa shida nitamlea nwenyewe"



Zidu aliongea maneno Yale kwa hisia,nilibaki kuganda nikistaajabu,mambo mawili yalinishangaza sana moja maneno ya Zidu yaliniumiza na kuniuzunisha pili Zidu alijuaje kama mimi yu mjamzito palepale nikakumbuka kuwa mtu yule ndiyo nilokuwa nikimsaka Kwa muda mrefu kafanya nimetukanwa na raisi,nikamjibu kwa jeuri kuwa



"Mimba nitaitoa siwezi kuwa na mtoto wa shetani eti nisu biri nijifungue uje kumchukua miez nane na wiki moja unadhani bado utakuwa hai ni kwambie tu muda huu ungeutumia kufanya ibada"



Basi pale kwa ghafla niliinuka sekunde hiyo hiyo nikibinjua mto nikakwapua bastola yangu kumnyooshea Jamaa si akarukia dirishani kapasua vioo aka rukia nje nami sikutaka kupoteza muda nikamfata ile nami natua nje akanipokea na teke la mkonono risasi ikaniponyoka ndipo tukaanza kuzipiga kavukavu mwisho alinishinda akakimbia.....



"aaaah shit blood fackin"



Sai akajikuta akitukana baada ya kuadithiwa kilichotokea,pale pale kama kakumbuka kitu akasimama akakimbia 'kk' akimfata nyumanyuma huku akichechemea huku akimuuliza anakimbilia wapi ' Sai' akujibu yeye akazidi kukimbia kuelekea wodi za kiume



Mpaka katika chumba kile alicholazwa Isack,kwanza alishtuka kukuta mlango wazi na anakumbuka aliufunga kwa nje na funguo ni yeye pekee alikuwa nazo



Kuingia ndani olaaaaaaaaaaa



KITANDA AKIKUWA NA MTU



Sai akatoa macho yake kwa mshangao....



Na Katarina naye ndo alikuwa akifika naye kuona vile alishajua kilichotokea akupaswa kufaamishwa kwamba Mwana ume Wa kazi Zidu k alishafanya yake....



Wakabaki wameganda,wakitegeana nani aanze kuzungumza,macho yao kitandani....



UKUMBUKE NI CHINI YA ARDHI NDANI YA HOSPITAL YA 'SHERATON HOSPITAL'





         Wote Walibaki Wameganda Pasina Kuamin Kile Wakionacho,mapigo Ya Moyo Ya Mwanaume 'Sai' yaliongeza  upigaji khof ilitanda moyoni mwake!,

Ni vipi angemweleza mkubwa wake mh Rais aliyemwamin na kumpa kazi ile akakumbuka hoja ya muheshimiwa rais na jins alivyoipinga

"na kitu kingine unapaswa uelekee Masanja road taharifa tuloipata ni kwamba nchi ya Kinte Imepoteza Mawasiliano Na Zidu,na kwa fikra zao uhisi labda Zidu tumemwangamiza kimyakimya, hivyo wamemtuma mtu kwa siri kuja kuchunguza kama Zidu yupo hai au alishakufa?,kilichopo kawekeni kizuizi katika njia ya masanja road huyo chalii akipita mkamateni mumuue kikatili,mumchukue na kamera vyote vitumwe kinte"

Alikumbuka agizo la mh rais,akakumbuka alilipinga na kutoa rai yake,rai ambayo kwa saivi inaenda kumtokea puani,akajihisi yupo mbele ya jopo la viongozi wa nchi akisemwa vibaya!

Kwa Mara Ya Kwanza 'Sai' toka ameingia jeshini ajajikuta moyo wake ukiumia,kk' pekee akashika dhima ya kumbembeleza na kumtoa wasiwasi!,

"mpenz 'kc' namtambua fika ni kijana mjanja sana kukuponyoka usivunjike moyo bali tuongeze juhudi ya kumsaka mwisho tutamtia nguvuni"

'Kk' akajaribu kumpa moyo na huku akiwaza 'uliona ufahari mimi kunyang'anywa hii nafasi ukapewa wewe ukiona ni nafasi nyepesi,rahisi eeh,ngoja sasa yakukute mwanaume wewe!' usoni alionekana mwingi wa huzuni ila moyoni alifurahi,alitaman siku moja yeye ndo amkamate Zidu Katili Kwa Mikono yake amuwasilishe kwa raisi kurudisha heshima yake,

"ok! beby,nimekuelewa kwa sasa acha nikaonane kwanza na muheshimiwa raisi nimpe taharifa hii ya kutoweka kwa Isack,sijui ntamwambia nini anielewe mimi sindo atantukana mpaka basi na mzee yule ajuavyo kugomba!...

'ndo hapo sasa utakapo isoma no'

Kk akajiwazia huku akiendelea kumsikiliza 'Sai' akampa maagizo "wewe nenda kokwa maliasili kuna mtu nasikia amekutwa amekufa,upelelezi wa awali inasemekana Zidu Ndo Muhusika!...

"Zidu ndo muhusika?!,kivipi sasa yani!"

"sina muda wa kulijibu swali ilo  wewe ndo unapaswa uje unijibu swali ilo katika uchunguzi wako!,"

Sai' akamalizia kibabe na kutoka,kk' akatabasamu tena!

'na bado ujauona moto'

akawaza naye akitoka ndani ya wodi ile,naye akaelekea katika ngazi,zilizo mpandisha juu ya hospital ile,kwa kuwa gari alokuja nayo 'sai' alishaondoka nayo,alipofika barabarani akapanda bodaboda!

"kokwa maliasili" akamwambia dereva bodaboda yule,safar ikaanza!...

KOKWA MALIASILI

Kwanza alipatwa na mshangao kumwona kijana yule ndo aliyeuwawa,alimtambua,ni mmoja wapo wa kijana alokuwa akitumia kituo kile cha pale getini kwake!...

Pili alijua pengine,atakuta watu,lakini alishangazwa na kujikuta yeye ndo akiwa wa kwanza kufika eneo lile,hii ikiwa na maana mtu alompigia simu  'Sai' Kumtaharifu Juu Ya Kifo Kile Kwa Vyovyote Vile huyo ndo muuaji!,wakati akizidi kutafakari ghafla simu yake ikaita kuangalia no,ni geni haraka akapokea

"alooh mpenz!" 

Nisauti nzito ya mahaba,ilojaa hisia si kwamba iliishia tu katika masikio yake lahasha,bali ilifika mpaka moyoni mwake,na matokeo yake mapigo ya moyo yakaanza dunda kwa kasi sana!

"n.n.na...ni!"

"najua ushanijua la unataka tu kuhakikisha ujakosea mimi ni mpz wako mwenye mapenzi ya dhati kwako Zidu!,najua now upo mbele ya mwili wa huyo bodaboda na nadhani utajiuliza kwa nini nimemuua usipate shida wacha nikujibu swali ilo,sababu kubwa ilonifanya nikamuua huyo ni kimbelembele chake, alinigundua!,nikajua kumuacha hai ingenletea shida,tuachane na ilo pia nashkur nimemuokoa Isack Wangu,nasasa Najiandaa Kumpandisha Ndegeni akatibiwe nyumbani,nadhani wajiuliza sana nimejuaje mpo pale pia nimejuaje kwamba wewe unamimba yangu na unataka kuitoa,ntakujibu ila siyo sasa,nkutakie kazi njema,nyongeza pumzika mama achana na maswala ya kunifatilia,mtunze mwanangu!,usiwaze kumtoa!"

Akakata Simu,kk,akabaki kazubaa bado alijihisi yupo ndotoni haraka sana akapiga tena ile namba,ikawa aipatikani!,akapiga kitengo cha mawasiliano,

"naomba mnambie usajili wa hii line pili imepigwa kutoka eneo gani!"

"Subiri kidogo madamu...

usajili ni Zidu  Gaspar Kite,imepigwa Kutokea Maeneo Ya Town Senta Ghorofa Ya Sita"

"ok! asante" Katarina akazidi kushangaa,

Town Senta ilikuwa ni katikati ya mji,katika ghorofa moja refu kubwa la biashara,akapotezea!

Muda ule ule akapiga simu,madaktari Wa Jeshi,wakawasili Wakaanza Kuuchunguza Ule Mwili,

"inaonekana huyu kauwawa kwa kukanyagwa shingoni na mtu alovaa  kiatu aina ya raba yenye nembo ya c4 kwa chini!...

Daktar mmoja akamwambia, baadaye wakamchukua kumpeleka hosptal kwa uchunguzi zaidi!,'kk' aliandika baadhi ya vitu kwenye kakitabu chake,kama kumbukumbu,sasa aliitaji kuelekea nyumbani pale kituon kuuliza masa alimpakia mteja wa namna gani mteja wake wa mwisho,ila je kama Zidu akumpakia pale kituoni na alikutana naye njiani akataka kupuuza,kwa kujua Zidu asingeweza kutoka uko mafichoni kwake akaja pakia pikipiki pale!...

ila kitu kingine kikamwambia aulize tu kwani akiiuliza hata akiambiwa ni mtu wa kawaida angepungukiwa na nin,mwanausalama akutakiwa kudharau hisia zake!

Akafika Mpaka Nyumbani,kabla Ajalifata geti lake akawafata boda boda  walokwepo pale,ambao maskin awakujua kama mwenzao ameshakufa,

"hoy wana masa yupo wapi?!" akawahoji kihuni

"dah sistar toka ametoka asb ajarejea!"

"ah,alimpeleka abiria wa aina gani?"

"si babu?!"

kk' akashtuka,ila akuonesha mshtuko wake wa nje!

"poa wanangu! wacha nizame ndani!"

akaingia zake ndani ya geti ile anatupa macho mlangoni kuingia katika nyumba ya ndani,akakuta raba mpya zenye  alama ya c4 ubavuni mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio akaongeza mwendo akaenda kunyanyua kiatu kimoja akakinyanyua kukiangalia chini ile c4 ilikwepo!

'i..i..i..namaana babu ndo Zidu?'

Akawaza,palepale Akakumbuka hata ile siku alipompa taharifa juu ya kufa kwa familia yake akapoteza fahamu alihisi zile sharubu ni bandia alipotaka kuzing'oa kichefu chefu kikamkamata akaenda tapika,akatapika,alitapika alipomaliza akajisahau kumchunguza!...

'shetani mkubwa huyu kumbe siku zote tunamsaka mtu kumbe lipo ndani kwangu nalilisha wallah nikilikuta ni kulimiminia tu risasi amna mazungumzo wala maulizo'

akawaza,maskin muda huo Zidu alikuwa sebulen akicheki tv akujua ana sekunde kadhaa tu za kuishi,katarina akatoa silaha,sasa akawa akiingia silaha kainyoosha mbele!...





IKULU



Gari alopanda Sai Iliwasili Ikulu,'sai' akashuka,mwili wote ulikuwa ukimtetemeka na alijua siku hiyo nilazima angenyang'anywa ile tenda,kwake aliiona ile ni tenda ambayo kama angefanikiwa ni wazi angepandishwa cheo zaidi,akaenda mpaka kwa secretary wa rais ambaye alimruhusu aingie akaonane na mheshimiwa,baada ya raisi kumruhusu!,akafungua mlango na kuingia katika chumba kile ambacho mheshimiwa rais alikifanya cha mapumzko,rais akamkaribisha akaketi,



"nikijana mara nyingi ninayekuamini na bila shaka umekuja na habari njema"



Maneno Yale Yakazidi Kumuumiza 'sai' Akajikaza Kisabuni



"Isack katoroshwa mkuu!"



Rais alishtuka akatoa macho,ni kama alipokea habari ya msiba 'sai' alilitegemea lile,



"katoroshwaje na ilikuwaje?!"



Ikabidi Sasa 'sai' aanze kumsimulia ilivyokuwa toka alivyomteka akampeleka sheraton hosptal,alipopigiwa simu aliporejea chumba cha katarina na kumkuta katarina ayupo daktari kalala chini ameuwawa!,akampa na maelezo ya katarina,

"alijuaje kwamba Isack Yupo Pale?,pia amejuaje kwamba katarina anamimba yake na lengo la kwenda pale ni kuitoa"



"ndo hapo hata mimi nashindwa kuiewa mh rais"



"unamwamini sana katarina?"

tofauti na mategemeo yake alijua labda raisi angemkoromea ila ali ongea naye kirafiki zaidi!,'sai' alifarijika kwa ilo!



"ndiyo namuamin mheshimiwa rais"



"ndo kosa ulilofanya,hii kazi kwa sasa fanya wewe kama wewe usimwamini kiumbe chochote,na hisia kwamba katarina ayupo upande wetu,kumbuka yule tayar ana mimba ya adui lazima awe upande wake,yapaswa naye umchunguze kila hatua aipigayo hisia zangu zinanituma kuamini kuwa upo katika hatua za mwisho za kumkamatata huyo mwanaharamu zidu,nakuamin kijana wangu uhai wangu upo chini yako usikate tamaa"



Rais akazidi kumwelewesha kijana yule,ambaye alizidi farijika,mpaka anatoka katika chumba kile alikuwa katika hari nyingine



alitaka awamu nyingine akirejea pale aje na habari nzuri,kwani alitambua kuwa anayekupa moyo ukupaswa kumvunja moyo,



Akaingia Ndani Ya Gari Yake Tayari Kwa Kuelekea Nyumbani,dakika Tatu tu alikuwa nje ya jumba lake akapiga honi!



Wakati huo ndo ule wakati ambao 'kk' alikuwa kashika bastola akielekea sebuleni akiwa na nia za kummaliza Zidu,ghafla akasikia honi nje ya nyumba yake,palepale akasimama na kurudisha bastola mahali pake,alijua huyo ni mpenzi wake 'Sai' Na Kama Nilivyosema awali akutaka 'Sai' ajuwe chochote alichogundua yeye,aliamin Sai Ndo aliyefanya yeye akanyang'anywa kesi ile,alimchongea kwamba amefanya ngono zembe na mwalifu,hiyo ikafanya adhalilishwe mbele ya viongozi wakubwa wa serikali!,



'nitamchunguza mwenyewe na kama ni yeye nitamkamatisha polisi mwenyewe kurudisha heshima yangu kwa rais'



Akawaza huku akirejea nje kufungua geti,'sai' akaingiza gari lake ile kushuka tu 'kk' akamfata na kumkumbatia,akalaza kichwa chake katika kifua cha mwanaume wake yule!



"rais kakwambiaje mume wangu,kakutukana eeh!"



'Kk' akaanza kwa kuoji ile 'Sai' anajiandaa kumjibu akakumbuka kuwa rais alimwambia awe makini na mwanamke yule,



"Raisi kantukana sana,tena sana...



'na ukome' kk akawaza kimoyoni aki mcheka!,



"nimefika nimemweleza kila kitu kilivyotokea,kanipa barua yako kwanzia sasa wewe aupo tena katika msako huu,chukua..."



"what? kwa nin tena,nimekosa nini mim"



'Kk' aliongea huku akilia,unajua kuwa katika ile tenda ilikuwa ni bahati,kwani kila siku akaunti yako ujazwa ela, na ina marupurupu mengi,katarina Kuondolewa Kabisa Kwake Ilikuwa Ni Uchungu eti kisa kupigwa na adui



'dah najua ipo siku muheshimiwa ataniomba radhi kwa haya yote anayonifanyia kipindi ambacho ntamfikisha huyu punguani Zidu Katika Mikono Yake Pasina Msaada Wowote Wa Polisi,na Kama bado ningekuwa katika nafasi yangu mapema sana ungekuta tushamaliza huu mchezo'



'Kk' aliwaza,wakaingia sebuleni,kwanza kk' alishindwa kujizuia akajikuta kamkata jicho kali mzee lyatuu aloketi pale sebulen kuangalia tv

jicho lile lilimshtua hata Zidu Mwenyewe



Alikuwa Jicho La Wema Lile,



"usiwaze Sana Mke Wangu,ipo Siku Moja tutafanikiwa tu na huyu mwendawazimu nitamtia mkononi kwanza honey uko kokwa maliasili umegundua nini"



Swali Lile Lilikuwa Nila ghafla ambalo akulitegemea ilipaswa alijibu kiuangalifu,kwani ili pekee lingeweza kumkamatisha mzee yule na lengo lake 'sai' achunguze mwenyewe ajue kusiwepo na msaada wake!



'yeye si kaonekan hawezi'



"mpz zile namba ulizopigiwa na mtu alokwambia juu ya mauaji yale unazo?!"



'Sai' akujibu kitu akapekenyua simu yake akamtajia ndo zilezile za Zidu alizompigia



"Izo namba ni za Zidu!"



Mzee Pale Alipoketi Mwenyewe Alishtuka,mshtuko Ule Kk aliuona akazidi kujidhibitishia kile akiwazacho,tena alikuwa akiongea huku akimwangalia mzee lyatuu ilikuwa ni kama kumuabarisha kuwa nimeshakugundua



"unasema?!,kivipi?"



"yah,kufika eneo la tukio hapakuwa na mtu yeyote ikiwa na maana mimi ndo wa kwanza kufika pale,muda ule ule nikapigiwa simu kupokea mpigaji akajitambulisha kwa jina la Zidu akanambia boda boda huyo ni mmoja wa wapelelez wa fbi alokuja nchini kwa nia ya kumwangamiza,yeye kwake alikuwa ni hatari hata zaidi yetu kamuua,kwa usalama wetu tuache kumfatilia huyo mtu kwani nasi atatua hivyo hivyo!...



Zidu Pale Kwenye Kochi Alishangaa Mwanamke Yule Aliyatolea Wapi Maneno Kama Yale Mbona Siyo Aliyoyaongea?...



Katu Akujua Kuwa Ule Ni Mtego,kk Alomtega?,je Angeweza Kuuruka?!





TUSONGE......



Hakika astajabuye ya Musa ni wazi ajaona ya firauni na siku akija kuyaona ni wazi asingestahimili kuendelea kuyaona

Zidu maswali mengi sana yalijizalisha katika kichwa chake,



Kwanza jicho la 'kk' wakati anaingia pale sebuleni halikuwa jema kabisa kwa yeye kama mpelelezi aliliona hilo,kitu kingine uangaliaji wa 'kk' wakati anaongea na mpz wake alikuwa akimtazama yeye ishara kwamba amemtambua



Ila kama amemtambua hatakuwa kamtambuaje?!,na kama ni kweli kamtambua kwa nini akumkamata,au ni kwa sababu ana mimba yangu au hataki mwenzake ajue kwamba ndo yeye na kama ndo ivyo lipi lengo lake sasa?!



kuwa upande wake au!?



Hapana!,Akakataa baada ya kukumbuka mafunzo alopewa ya awali wakati akianza jeshi,katika nguzo au sheria kuu za jeshi,ipo I losema 'katu usimwamini aduh yako hata kama akikuonesha dalili za kuhitaji kukusaidia hiyo inaweza ikawa nyenzo ya kukumaliza'



Pale pale akafuta wazo lile,haraka sana akatengeneza lingine kusahihisha alipokosea kusudi akae huru hata kama alikuwa akitiliwa shaka aifute Shaka ile kama ni kwel kagundulika au vipi!,na kama kagundulika aweze kujinasua,atupe jiwe moja liue ndege wawili,yani afanye kitu ambacho kitamuwezesha agundue kwamba Katarina Ni Kweli Kamtambua?,na Ndani Ya Kile Kile Kitu Kama Kweli Katambulika,basi Kifute Mtambuliko Ule Apate Kuwa Huru na kuendelea na harakati zake!,



Ni Kitu Gani sasa angefanya,akalala akiwaza,mwanajeshi alitakiwa aumize ubungo,achanganye akili,mpaka anapata usingizi akujua ni kitu gani afanye...



Kwa Upande Wa 'Kk' Chumbani Kwake,naye aliwaza yake,japo alimuhisi yule mzee ni Zidu Kesho Yake alipanga kumaliza kazi wakati mwenzake akiwa kazini basi amwekee kinywaji mzee madawa kisha ampe mzee akinywa na kulala ajaribu kumnyofoa zile Sharubu,ikiwa Zitatoka,pale Pale akiwa kalala atamfunga pingu amuwasilishe moja kwa moja ikulu kwa raisi!...



Akatabasamu,akimwangalia 'sai' Alolala Pembeni Yake akikoroma kwa dharau



'mwanaume boya sana wewe unalala,kipindi changu mi nilikuwa silali,we unalala na unapata usingizi mpaka unakoroma teh teh teh'



Akamcheka Mawazoni huku akimgusa,kuikatisha ile koroma yake kwani ilikuwa inamboa!



pakapambuzuka!



Wakapata Chai,na baada ya kupata chai,'Sai' akaondoka na kuwaacha wawili,kwa Zidu Ilikuwa Sasa Ni Ule Muda Wa Kujisafisha,



Na Kwa 'kk' Ulikuwa Ni Ule muda wa kumaliza kazi,ilikuwa ni mida ya saa nne mzee akiwa chumbani kwake,pasina kujua hili wala lile,

kk' Sebuleni alichukua juisi akaiwekea dawa ya usingizi,akaelekea chumbani kwa mzee lyayatuu



akaingia pasina hata kugonga hodi!



kuingia kwake kwanza kulimshtua Zidu akajikausha



"mh mjukuu wangu unaingia tu bila hodi sijui ungekuta babu yako navaa ungefanyaje?"



"ah babu wala hata nisingejali,we ushazeeka hata nguvu sasa una ningeshangaa kwa kipi sasa!"



"wacha bwana,ng'ombe azeeki maini ati,"



Zidu alijibu akitabasamu,akafanya meno yake ya njano yakaonekana,ila meno yake halisi ayakuwa vile yale aliyapaka rangi kuleta uhalisia,mapigo yake ya moyo yalienda mbio akijiuliza binti yule kafata nin ndani,na ile juisi,bila shaka kaitia kitu ndani,



Akapata Wazo,pengine bado mwanamke yule anamtilia shaka ndo kamletea kile kinywaji ikiwa angekataa basi angemdhibitishia ndo yeye,na pengine labda akina kitu,ila je kama kina kitu na lengo lake ni jingine!



vyovyote,lazima mtego ule auruke...



"mh Babu Ina Maana Ujazeeka Maini,una Nguvu Zako Leo Nahtaji Nizione Kunywa Kwanza Hii Juisi Unishughulikie"



'kk' Akaongea Kimzaha Kwani Alijua mzee yule akinywa ile juisi angelala hapo angemkagua na kumfikisha kwa rais akiwa ana ufahamu ila



je angekataa kukinywa,



Basi hilo lingemdhibitishia kuwa yule ndo Zidu Ivyo ambacho kingefuata ni kujifanya kama anarudi akiwa mbal naye kidogo achomoe bastola ammalize palepale amtoe zile sharubu apeleke maiti ikulu...



ila mzee akiwa na furaha akakipokea na kukibugia,



akionekana kumtamani sana 'kata' ile kumaliza macho yakawa mazito...



Akadondokea Kitandani Usingizi Mzito Ukamvaa...



Kata' Akiwa katabasamu akamsogelea akapeleka mkono tayari kuzivuta sharubu kuzitoa,pamoja na ndevu



maskini Zidu!!!



****



UPANDE MWINGINE WA STORI



Si Kwamba Palikuwa Na Giza sana,wala siwezi kusema kulikuwa na mwanga,mandhari yake ilikuwa nitofauti na ya duniani,



Mchana palikuwa na mwanga wa mbalii,usiku palitawala giza,ni katika shimo moja refu,ninaposema refu ni refu ki kweli kweli!,ukiwa kwa juu usingeweza kuona mwisho wa shimo lile wala kilichopo chini yake,



Kwa Muda Wa Siku Nyingi Sana Mtu Yule alikuwa amefumba macho pasina ufahamu,usiku wa manane kuna mtu alikuwa akishuka kitaalamu kwa kamba aloifunga juu ya mti katika tawi kisha umlisha yule mtu na kupanda zake juu kisha kuondoka!



Leo hii mida ya usiku mtu yule alifumbua macho,mwili ulimlegea akajihisi uchovu,akajaribu kuamka ila akashindwa akajaribu kupapasa pale alipolala akajigundua kalala chini,akapekecha macho yake ili hata aone kiza kilitawala



'Nimekuwa kipofu au?'



Mtu yule akawaza mwaswali mengi yakamiminika kichwani kwake



'ni wapi nipo?!' akajaribu kuwaza ila akupata jibu akajaribu kuvuta kumbukumbu zake!,kwanza yeye ni nani!...



Kwa Mpelelezi Yoyote alishajengwa kisaikolojia kujiuliza swali ilo pindi apatapo fahamu ili kama atakuwa eneo la hatari ajue jinsi ya kurudisha kumbukumbu zake haraka haraka,kutotoa siri!...



'isack!,ndiyo Mimi Ni Isack John'



Hapo Sasa akawa kafanikiwa kurudisha kumbukumbu zake vizuri tu!,mara ya mwisho alikuwa mikononi mwa adui alomkamata masanja road,na mwisho anakumbuka alikuwa kalazwa hosptal akiwa chini ya mtu yule,sasa pale ni wapi!,akajaribu kupapasa tena,akajitahidi akaamka,bado palikuwa ni giza,akatembea akufika mbali akagonga mwisho,



Kwenda mbele napo akakuta mwisho kulia mwisho,kushoto akupiga hatua nyingi sana mwisho,



Sasa akapata picha,lile ni duara,kwa maana hiyo yupo shimoni!



Nani Kamuweka Huko Sasa?,bado ubongo wake aukumpa jibu la uhakika!...



ghafla akahisi mlio wa vuuuuu,kama mtu alikuwa akishuka,akakaa 'standbay' ile katua



"wewe nani?!"



akampiga swali,mtu yule kimya



"nakuuliza hivi wewe nani na huku ni wapi uliko nleta!"

ITAENDELEA

    

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4) 

Sehemu Ya Tano (5)





"uuu,uuuu"



'kumbe bubu' Isack Akawaza Akielekea Kukata tamaa lakini sasa akuelewa kama yule mtu ni mzuri au mbaya



"upaswi kunijua mimi ni nani!,ila tambua mimi ni msaada wako,chakula hiki kula! nimekuletea"



Ghafla akasikia sauti ambayo akuitambua ya nani akawa akipapasa,na ghafla akamgusa mtu yule,akamkabidhi vyakula kisha baada ya kukipokea



"naenda ntarejea kesho ugua pole"



Mtu Yule akaongea na muda ule ule akahisi kama mtu yule akipanda juu!,Isack akapapasa ile hotpot akafunua mfuniko akaanza kula,kwa giza lililokwepo,ilikuwa ni kama anaishi ndani ya ukipofu!



'lakini yule mtu ni nani?,huku ni wapi na kwa nin mwanzo aniongeleshee ukibubu na badae aje aongee je halikuwa na maana gani?!....



DAH ISACK YUPO CHINI YA SHIMO REFU NI WAPI HUKO?!,PILI MTU YULE ALOMSHUKIA NI NANI







Komandoo Katarina 'kk' anamtilia shaka mzee lyayatuu pengine ndo Zidu,kutokana Na Ushahidi Mbalimbali anayoikusanya ikiwemo alama ya kiatu,na ushahidi mwingine kuwa yeye ndo alopakiwa na marehemu mara ya mwisho,anamwekea dawa ya usingizi kwenye juice Lengo amtoe sharubu na ndevu,je nin kiliendelea?!



TUSONGE...



Mkono wake ukashika zile ndevu ukajaribu kuzivuta,wapi!,zilikuwa ngumu,ina maana kama zilikuwa ndevu za bandia zisingeng'ang'ania,ina maana zile ni ndevu zake,alipojaribu hata kwa sharubu hali ikawa ile ile,wazo kwamba yule ni Zidu taratibu zikaanza kuyeyuka,Zidu ndevu zake azikukaa vile zenyewe



Zilijichonga o,'pengine huyu mpuuzi anamtumia huyu kiumbe kusudi kuchanganya upelelezi,lazima nichunguze juu ya hili!'



Kk Akawaza huku akimwangalia mzee yule usoni,alikuwa na uhakika mzee yule alikuwa akitumika na Zidu Na aliapa kumtumia kumpata Zidu,embu Ngoja Lazima Nimzindue Nimtese Mpaka anieleze kila kitu!,kwanza ngoja nisachi humu ndani...



'kk' akafungua kabati akatoa nguo zote za zidu,zilikuwa ni nguo kuu kuu zilizochakaa mpya zilikuwa chache tena zile alizonunua hiyo juzi siku ya tukio!,kk akazidi changanyikiwa ni wazi akuielewa hali ile,mwisho aliona anapoteza muda wake kuumiza ubongo wake kufikiria kitu ambacho majibu yake alikuwa na uwezo wa kuyapata kwa kupitia kwa mzee alokwepo mbele yake,



Mzee ambaye aliamin angemtesa kidogo basi angemweleza siri zote azijuazo,palepale kata akatabasamu haraka sana akanyanyuka pale na kuelekea chumbani kwake,akafungua kabati na kutoka na bobo fulani aliloifadhia dawa,akachukua kidonge kimoja akakiponda ponda akakiweka kwenye maziwa akaenda kumnywesha mzee,kile kiliua nguvu zote za yale madawa ya usingizi kilichangamsha mwili...



Baada Ya Kumnywesha Ghafla Mzee alianza kukohoa,palepale Mwanamke Yule akapata wazo lingine akamwachia yule mzee na kutoka zake,akuona haja tena ya kumtesa pengine kwa kufanya vile angeweza kumshtua,Zidu na kuaribu mipango yake yote!....



Ivyo alipanga aendelee kumchunguza, mwisho angegundua kitu!,kama ni Zidu angejua na kama kibaraka wake pia angejua,haraka sana akarejea chumbani kwa Zidu kupiga chabo mlangoni kumwangalia mzee yule baada ya kuamka kipi angefanya au angewasiliana na nani!



Kwa upande wa Zidu baada ya kushtuka aliangaza macho akajaribu kukumbuka,haraka sana akapata jibu lazima yule mwanamke alimfanya kitu,alimwekea kitu katika juisi ile alokunywa,akapiga mwayo,alijua lazima kwa muda ule jicho la yule mwanamke litakuwa likimtazama ninin angefanya,'kama ni mchezo nami naweza ucheza ngoja nikuoneshe'



akawaza sambamba na kujiamsha pale kitandani akajifanya kujinyoosha nyoosha akipikicha macho yake,eti kazee kale kakaenda shika simu yake,kata pale anapomchungulia akajua sasa mambo yameiva cha ajabu kakaangalia muda na kuirudisha kitandani!,akaelekea bafuni...



kule bafuni akafungulia maji na kuanza kuoga,katarina Akaona ah arejee zake sebuleni ghafla simu yake ikaita kucheki namba ni zile zile za Zidu,jitu Linalo Mtesa,linalo Mnyima Raha,kabla ajapokea akapiga hatua haraka haraka mpaka chumbani kwa Zidu,akatupia Macho kitandani simu ya kale kazee ilikwepo,akaguna!,wazo kwamba yule mzee anaweza kuwa Zidu Likazidi Yeyuka,au ana Simu Mbili?!



Akakataa kwan asingeweza kupigia bafuni haraka sana akarejea sebuleni,na kuipokea simu ile!...



Kule Bafuni Zidu Alifunga Bomba La Maji,mkono Wake Ulovalishwa Saa Ulikuwa Maskioni



Akabonyeza taratimu kadhaa katika saa yake ile ya mkononi,akaipachika masikion,ndo simu ya kata ikaita!

'naona umefutwa kufatilia kesi hii lakin umekuwa mbishi nimeona nijaribu kumtumia huyo mzee kuchunguza kama unanifatilia au vipi,japo yeye ajui kama namtumia,nimegundua pamoja ya kusimamishwa kufatilia kesi yangu lakin bado ujakoma,waendelea kunifatilia,sasa nakupa onyo la mwisho acha kunifatilia ok!..."



Simu Ile Ikakatwa,haraka Sana 'kk' akapiga simu idara ya mawasiliano,embu tazama hii namba imepigwa wapi?!...

akauliza kwa amri!



"sheraton hotel"



Akajibiwa!,'bila Shaka Kiumbe Kile Kitakuwa Kimejificha Katika hotel hiyo ni lazima niende nikafanye uchunguzi,' akawaza,muda ule ule,akavaa,akamuaga mzee lyatuu akaingia ndani ya gari lake na kuondoka kuelekea katika hoteli ile,



Katu akujua mbaya wake kamuacha mulemule ndani,alichofanya Zidu alitegesha simu Sheraton Hotel chooni juu kabisa mahali ambapo ilikuwa ni vigumu kugundulika,ile simu aliiseti na saa yake ya mkononi,saa za kipelelezi,ivyo alivyobonyeza pale kwenye saa ilifika katika simu ile ivyo walipocheki kitengo cha mawasiliano walinasa eneo simu ilipo basi!...



Jambo Lile Likawa Ni Alama Nyingine Ya Ushindi Kwa Zidu!,katarina Alifika Sheraton Hotel akakagua kila eneo pasina mafanikio,kichwa kikazidi kumuuma,mpaka jion anarudi nyumbani alikuwa kachoka,kichwa kikimuuma zaidi,hakika Zidu Aliamua Kumchanganya...



Ilikuwa Mwendo Wa Saa Mbili na dakika kumi na tatu wakati ambao wawili wale walikuwa wameketi sebuleni wakipata chakula cha usiku,kila mtu alikuwa na mawazo yake kichwani,wakwanza ni Katarina Yeye Mawazo Yake Ni Jinsi Ya Kumtia Mkononi Zidu alomuumiza kichwa,alocheza na akili zake,pembeni yake alikuwa mpz wake naye kiu yake aikutofautiana na ya kwake,ili kujenga heshima yake kwa raisi Sai aliwaza ni njia ipi aifanye kusudi amnase Zidu,



"mzee Lyatuu Yuko Wapi Mbona ajumuiki kula na sisi?"

Sai akahoji baada ya kutomuona Mzee Pale Mezani



"leo ayupo sawa,anajisikia kuumwa kajilalia humo ndani" Kk akajibu akijua madawa yale ndo yalokuwa yamemlegeza mzee yule,ila ukwel ukuwa huo muda huo Zidu alikuwa chooni akiongea na raisi wake mh Moreti Wa Pili,alimpa maagizo usiku huo ndio angempeleka Isack Mpakani Kwa Sababu hali yake ni mbaya shimoni kule angekufa ivyo kuwepo na ndege ya kumpokea na wanajeshi kadhaa,



Rais Pasina Kujua Nyuma Yake Mlinzi Wake (body Gard) Ni adui afichuaye siri zao,akamwamini,mlinzi yule akaomba kwenda toilet chooni kule muda ule ule akampigia Sai,Sai Akiwa Sebulen Na Mke Wak Kk Wakila Ghafla Simu Yake Ikaita Kuangalia Ni

'Mr X' Ndivyo alivyoinakili namba ya mtu yule katika simu yake!,akanyanyuka na kwenda pembeni kuongea kusudi hata mke wake asisikie...

"Zidu usiku huu anategemewa kumtorosha Isack Masanja Road,kutakuwa Na Ndege Yenye Makomandoo Kadhaa Ni Muda Wako Sasa Wa Kumkamata Zidu,"



Baada Ya Maelezo yale simu ile ikakatwa,Sai akurudi tena kula,akamuaga mkewe...



"natoka nimepata dharura"



Kk Akupinga,mwanaume akatoka,kk baada ya kumaliza kula akaelekea zake kulala,



Usiku Mida Ya Saa Saba,kama Kawaida Yake Mzee Lyayatuu aliamka,usiku huu ndo alipanga kumtorosha Isack Masikin akujua mpango wake ulishashtukiwa na wanajeshi wa kutosha walitegeshwa mafichon 'masanja road' na hata ndege ile kotoka kinte ilipowasili,ikawekwa chini ya ulinzi kwani wanajeshi wa ganyama walikuwa wengi!



Mzee Akawasha taa akajiandaa,akatoka,siku ya kufa nyani miti yote uteleza,wakati anauparamia ukuta kumbe kk alimuona alipotoa naye kk akistaajabu akaupamia ukuta akatua upande wa pili kimyakimya,sasa akaanza kumfatilia kwa nyuma,ZIDU akujua kama anafatilia hata lile shimo kumbe alikuwa mbali sana akashika kamba akatua chini!,akaenda akamfunga ISack Mikono Sasa Akaanza Kumvuta Kwa Juu,akambeba Mabegani Ile anageuka machokwa macho na kk,Zidu alishtuka akajikuta anamuachia Isack!



Dah!,nin Kitaendelea?!,kk Macho Kwa Macho Na Zidu amjuaye kama Mzee Lyayatuu nin kitaendelea ukumbuke Kk anamjua Isack Na Isack Yupo Katika Sura Yake halisi

mbona kitimtim





Kutokana na hali ya Isack Kuwa mbaya Zidu anapanga kumtorosha usiku wa manane,



Pasina Kujua habari zile zinavuja,na kumfikia moja kwa moja kijana Sai naye anakusanya jeshi usiku ule ule na kuweka mtego 'masanja road' eneo analotegemea kulitumia Zidu,wanafanikiwa Kuiweka Chini Ya Ulinz Wao ndege ambayo ingetumika kumbebea Isack Na Sasa Wanamsubiria Zidu awasili 'sai' akamilishe kazi!...



Upande Mwingine Pia tulimwona Mzee Lyayatuu 'Zidu' akiamka usiku wa manane lengo lake akamtoroshe Isack,anauparamia Ukuta Pasina Kujua Mwanadada Machachari Katarina alikuwa akimfatilia safar yake ikaishia katika shimo lile akashuka,akamfunga Isack Kamba akapanda juu akawa sasa akimvuta!



Akambeba begani ile anageuka macho kwa macho na mtoto wa kike,Katarina,mwili wote ukamlegea,vinyweleo vikamsisimuka,akajikuta akimuachia Isack! Je Unahisi Nin Kiliendelea?!...



TUSONGE....



Komandoo Katarina 'Kk' alimwangalia kwa tabasamu baya,tabasamu la kumkejeli!



"mara nyingi nilikutilia mashaka sana we mzee,na leo afadhal nimekufuma na ushahidi huu, Zidu Yupo Wapi?"



Akili za Zidu muda ule zilifanya kazi kwa kasi,mara mbili ya zinavyofanyaga kazi,



alijua!...



Ilipaswa ajifanye mjinga,ilipaswa asijidhihirishe pale,kwani hakuwa akijua yule dada nyuma yake kwa siri sana kaongozana na wana usalama wangapi!,



"tafadhali usiniue,mi sijui yuko wapi ua anantuma t..!"



Paaaaaa!



Kibao Kikali Kikatua Shavuni Mwake,alihisi Kiling'oa Meno,akaanza Kutema damu



"nakuuliza Kwa Mara Nyingine tena Zidu Yupo Wapi Au Upo tayari kunipeleka alipo?"



"sijui kitu mjukuu wangu!" Zidu akazidi sisitiza,



"unaonekana wewe ni sugu ila nikwambie ukweli utanieleza ukwel wote,utake usitake!"



'Kk' aliongea huku akimfata kaugeuza mkono wake ukawa ukimjia kwa kasi Zidu,naye Mwanaume akawa akiuona ukija alitaman aukwepe ila alijua angeshtukiwa akawa akiusubiria ni Pigo Lijulikanalo Kama 'kelbu' Lipigwalo Kwa Kutumia Upande Wa Nyuma Wa Mkono...



Wakati 'Kk' akiutoa mkono wake,Zidu alihisi muwasho eneo la paja,kiza kikaanza kumtawala,uchovu,kizunguzungu kikali na ghafla akaenda chini!



'kk' akacheka ni baada ya kufanikisha kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi,akawavuta mpaka kwenye manyasi akawaifadhi,akarejea nyumbani akaruka ukuta,akaingia chumbani,akachukua funguo,kwa kuwa 'Sai' akwepo alikuwa na uhuru wa kutosha,akatoka mpaka 'parking' akaingia ndani ya gari akawasha akarudi nyuma akakata kona uelekeo wa lilipo geti,kufika getini akashuka akafungua geti,akatoka,kufika nje akasimama akarudi kufunga geti kwa ndani akauparamia ukuta,akapanchu kwa juu akatua nje upande wa pili akaelekea lilipo gari akaingia na kuondoka,



Mpaka eneo alipowaifadhi mzee lyayatuu na mwenzake,akawapakia katika gari,akaliondoa kwa kasi!...



Masame



Lilikuwa Ni eneo waliloishi matajiri geti tu ndizo zilizo onekana,hapa masame na kule ambapo Kk alikuwa akiishi na 'sai' Katika Jumba lile walilokabidhiwa na serikali palikuwa na umbali mkubwa tu!,Katarina binafsi alikuwa kashajijenga kabla hata ajaenda cuba tayari alikuwa na nyumba kadhaa mjini pale,katika nyumba zake za siri hii ilikuwa moja wapo,nyumba hii aikutambulika na mtu yeyote akashika rimont yake alokuwa nayo akaelekezea geti,lenyewe likafunguka akaingiza gari geti lenyewe likajifunga!


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog