Search This Blog

Friday 30 December 2022

KIAPO CHA MFUNGWA (5) - 5

    

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (5) 


Sehemu Ya Tano (5)

  



Odovy akaenda chini,



Akajinyanyua tena,sasa macho yake yalikuwa kwa Fatma akimwangalia kumpa taharifa kama naye anajiweza aende!



Ila tofauti na matarajio yake,Fatma akaufunua mdomo wake



"Tunajua una hasira na machungu kwa wabaya walousika kwa kifo cha wazazi wako ila kumbuka hasira aisaidii plz tukae chini tuyapange tupo kwa ajili ya msaada kwako Gambi"



Fatma aliongea kwa sauti ya upole! Ilojaa utii na maombi,Gambi akamwangalia kwa dakika kadhaa na kurudi kwenye kiti chake!...



***



Iliikuwa ni nyumba kubwa iliyozungushiwa mitambo maalumu ya ulinzi,



Mbali na mitambo hiyo kamera za DSTV zilikwepo pembezoni mwa geti kubwa katika taa mbili kubwa getini pale moja ilimulika nje na ya pili ilimulika ndani,



Ukuta ulizungushiwa nyaya maalumu zenye short na alamu pale mtu apandapo juu ya kuta hizo



Mbali na ulinzi huo kulikuwa na walinzi maalumu wa vikosi vya jeshi la jkt wakilinda kwa shifti katika hekalu hilo



Ndani ya nyumba hiyo aliishi mzee wa makamo mwenye kipara katikati ya kichwa chake,



hakiwa kavaa bukta pana na singland taulo fupi kalitupia shingoni hakiwa kakaa kwenye kochi



Hakukaa peke yake pembeni yake alikuwa binti mdogo yamkini ni kama binti yake akiwa kavaa upande laini wa khanga kamlalia mzee huyo mapajani akimchezea ndevu zake taratibu mzee huyo alijulikana kwa jina la JAMES JOHN JJ



Ndiye aliyekuwa waziri mkuu wa KINTE JJ alikuwa ni waziri ambaye hakuwa ameoa wala hakuwa na mtoto hilo lilimfanya abadilishe wanawake kama anavyotaka



Akimtumia dereva wake LAMBART kumpata mwanamke yeyote amtakaye kwa gharama yeyote ile



Alitembea na masta na warembo wa kila aina moyo wake ulimwendea mbio kila binti yule alipomchezea ndevu zake aliitaji kitu kingine ndiyo hakuona haja ya kwenda chumbani



Walimalizana palepale bila kujali kuwa vijana wa chumba cha dst Walishughudia na alijua fika sebuleni pale kuna camera ila angeogopa nini wakati alikuwa na uhuru na mali zake?....



Hayo ndo yalikuwa maisha ya JJ waziri mkuu wa KINTE



***



Kikao kile kiliendelea kati ya vijana wa KIKONGO na LAURENT GAMBI safari hii walifanikiwa kumshawishi waungane kwa minajili ya kumsaidia gambi baada ya mabishano ya kioja hatimaye gambi akakubali akaanza kuwatajia orodha ya watu aloitaji kuwa angamiza ilikuwa ni orodha ya watu wa 4 tu wakwanza akiwa rais LAIZER NYOSHI,



Kamishna Brown Stanley, waziri mkuu JJ,na LUTENI KANALI JONSON MWAKATABE.



Jambo lile lilikuwa zito kwa vijana wale watu aloitaji gambi kuwauwa walikuwa ndo serikali kamili ya kinte wote walikuwa wamepitia jeshi hakika waliyaona maisha yao hatarini



Naam hawakuwa na budi! kuwa na gambi bega kwa bega kwa kutoa msaada pale gambi alipoitaji tayari odovy na gambi walishabadilish

a sura za bandia ikawa vigumu kugundulika ila kwa upande wa FATMA na odovy walibakia hivyo hivyo kwa kuwa wao hawakuwa wakisakwa.



Ivyo wote walirudi kazini kwao kama kawaida FATMA akarudi ikulu na ODOVY akarudi jeshini.



***



Alamu ya saa yake ndiyo iliyomshtua,



alipitisha dakika kadhaa hapo kitandani akiyapembua mawazo yake yaliyomuumiza.



katika kazi zote alizowai kufanya Ins Jonathan alikiri hii ni ngumu hasa alikosa amani pale alipoitajika na mkubwa wake wa kazi kamishna Brown apeleke ripoti dhidi ya LAURENT GAMBI au dereva ake na KURWA ilo lilimchanganya



Alijiinua taratibu kitandani na kwenda kukoga alipomaliza alikunywa chai tayari saa moja na nusu alikuwa barabarani akielelea ofisini makao makuu ya jeshi la polisi alipiga miayo ya uchovu usiku hakulala kutokana na mawazo aliapa kumtesa vibaya sana Gambi siku akiingia mikononi mwake kama mshahara wa mateso ampayo.



Akasonya akishuka garini bado hakuwa na habar mpya katu hakujua ambacho kingetokea na hakujua kuwa Gambi yupo katika sura mpya



****



Mabadiliko haya hutokea mara kwa mara katika utumishi wa UMA bila viongozi wa utumishi wa uma kujua hasa hasa kwa wafanyakazi individual wadogo wadogo na masecretary ili kuepusha mianya ya rushwa.



mabadiliko haya yalimkumba FATMA aliyeamishwa IKULU na kupelekwa ofisi ya waziri mkuu kama secretari wa JJ ambaye ni hasimu mkubwa wa gambi.



Jj hakujua juu ya mabadiliko hayo wala hakutaarifiwa alimzoea MERY! Alishangaa kukuta mfanya kazi mpya FATMA alijistiri vizur macho tu ndo yaloonekana huo ulikuwa ni mtego wake kwa jj na kama alivyotarajia ukanasa jj alikuwa na hamu ya kumjua binti yule mpya aloletewa.



Sauti yake nyororo ilimvutia katika masikio yake kila alipojaribu kuzizuia hisia zake alishindwa na hatimaye aka amua kumwita binti yule hofisini FATMA aliingia....



Ndipo JJ alipomwomba aione sura yake FATMA kwa kuwa yule ni kiongozi wake tena bosi wake hakubisha akavua juba lake sura yake ya urembo ikaonekana



JJ akashindwa kuzizuia HISIA zake kigugumizi kikamtawala



ALISHAMPENDA!



Na alimuitaji bila kujielewa mikono yake akaipeleka usoni mwa FATMA binti yule akarudi nyuma kwa woga wa bandia waziri mkuu JJ akatahamaki na kuomba radhi,



Binti hakakubali waziri akaomba amtoe lanchi FATMA hakuwa na kizuizi kwa mh JJ ikawa tabia yake kumletea zawadi,kumtoa lanch kumpa hata fedha kwa minajili ya kumuweka karibu ilo alifanikiwa na hata alipompasulia FATMA ya kuwa ANAMPENDA binti hakuweka pingamizi



Japo hakuacha kuvaa JUBA akakataa kupelekwa katika ma hoteli makubwa ndipo JJ aka afiki kumpeleka nyumbani....



Hicho ndo kitu ambacho binti yule alikisubiri kwa hamu hakamuwaidi kesho yake ambaye ilikuwa week and juma mosi kumtembelea...



JJ hakujua kilichokuwa nyuma ya mawazo ya binti FATMA na laiti angejua?!!!......







Hakika moyo wa GAMBI kwa mara ya kwanza ulitabasamu,



Alimwangalia Fatma kwa macho ya kutoamini ayasikihayo Fatma alimweleza mpango wa kumnasa JJ ulivyo.



Na GAMBI kwa moyo mweupe aka afikiana naye kwa pongezi,yah!



Hakujua ni sangapi alimkaribia binti yule na kumkumbatia joto laini baina yao lika ambaa katika miili yao,



Mioyo yao ikasemezana waka angaliana kwa macho ya kimahaba kila mmoja akimtaman mwenzake



Lakini waliweza!



Waliweza kuzizuhia hisia za mioyo yao wakaachiana gambi aliufurahia msaada huo baada ya kupewa mawasiliano hakijifanya FATMA alivaa juba lile na kuingia ndani ya gari aina ya Ferrari la serikali safari ya kuelekea nyumbani kwa JJ ikaanza



Jj alishatoa taharifa getini mwanamke mwenye juba jeusi akija asikaguliwe aingie na ndivyo ilivyokuwa gambi aliingia mpaka ndani parking na kupaki gari lake na kushuka akifata maelekezo ya meseji alizotumiwa mpaka katika mlango wa chumbani akabisha hodi taratiiibu



Jj akafungua mlango uso wake ukipambwa na tabasamu alikuwa na bukta tu alimkumbatia Gambi bila kujua anamkumbatia nani!



Muemko wa mapenzi ukiwa umempanda akaanza kumvua juba lile.



Mwanaume alitulia hakivuliwa hasira za kuuwa zikiwa zimempanda maradufu



"jj" alishtuka baada ya kuiona sura hasiyoitarajia lakini alishachelewa mkono wenye nguvu ukiwa umekunja ngumi ulishushwa katika taya na kujigeuza kwa teke kali lililotua katikati ya kifua



Jj hakaenda kudondokea katika kitanda chake hakiona nyota nyota zinaelea hewani



"uliusika na mauaji ya wazazi wangu! nami lazima niusike na mauaji yako mwanahayuni weee!!!"



Gambi alifoka kwa hasira wakati huo huo akimwendea kwa kasi mwanajeshi huyo wa zamani katika utawala wa baba yake laurent gambi bwana MERNELI WA 11.



bila kuchelewa alimrushia ngumi mbili za haraka haraka moja akiipiga maeneo nyeti shingoni na nyingine tumboni



Jj hakuwa na shaka kuwa ngumi hizo zilivunja koromeo na kuchana utumbo na kupasua mishipa yote ya damu



Jj hakutaka kufa kikondoo alibeba kiti kilichokuwa karibu yake na kukirusha gambi alikikwepa na kwa hatua mbili ndefu na viatu vyake vya kike alirusha teke aina ya TANGKYU lipigwalo kwa kutumia kisigino maeneo ya kitovuni na kuvunja vipingili vya kiunoni



jj aligugumia kwa maumivu na hata pale wazo la kupiga kelele lilipopita katika kichwa chake na kutaka kulifanyia kazi mdomo ulikuwa mzito na aliisi ubaridi na maji ya unyevu nyevu yakitiririka kutoka kifuani macho yake yalipotua maeneo hayo



Alikishughudia kisu kikubwa kikiwa kimezama kabisa katika tumbo lake na kuacha mpini ghafla macho yakaanza kupoteza nuru yake ya asili giza likauvaa uso...



Sasa ndo nakufa mie jaman...



Jj aliserereka chini huwai ukauacha mwili



Gambi akatoa tabasamu lake lile baya na kuchovya kiasi cha damu na kuandika katika mpini wa kisu kile neno MFUNGWA.



Alipomaliza akaelekea bafuni akanawa vizuri akavaa juba lake akatoka akiurudishia mlango vizuri



Akaingia garini akuna alojua kitu getini aliwaaga walinzi kwa kuwapungia mkono mwanaume akaondoka mpaka ofisi za waziri mkuu akaliacha pale lile ferari akachukua tax mpaka hotelini anapoishi kule kusikokuwa na serikali



Akafungua dranka lake akatoa karatasi lenye majina ya alopaswa kuwa angamiza kunako jina la JJ akaweka tiki kumaanisha tayari







Ikulu hali aikukalika raisi alichukia sana



Sasa aliiona hatari mbele ya macho yake!,



"Lazima nifanye maamuzi sahii tofauti na ivyo tutateketea!..."



Akaongea kwa sauti kubwa viongozi wa juu wa taifa lile wakimsikiliza kwa makini



Kitendo cha kuuwawa kwa waziri mkuu wake aliona ni cha kizembe ,



Hasira,ghadhabu kwa Gambi ziliongezeka Mara dufu



Alitoa siku tatu za awali Gambi awe ametiwa nguvuni akiwa mzima au maiti imeshindikana na sasa kusababisha mauaji ya mmoja wa watu wakubwa katika taifa lake mwanamapinduzi mwenzake kilimuuma sana

Akafumbua mdomo wake



"Je kati yetu ni nani anayefatia upelelezi unaendelea bila mafanikio naomba maafisa wa ngazi ya juu kama mmeshindwa kazi mjiuzulu kamishna Brown mnafanya nini?! Au mpaka Gambi akufikie ndo utajua huyu jamaa ni hatari narudia tena naitaji Gambi atiwe nguvuni mapema sana ikishindikana Zidu aletwe!"



"Hapana mh raisi bado kijana wangu ajashindwa Gambi ni mwanajeshi Zidu komandoo tutakuwa tunamdhalilisha!...."



"Haaaaa kwa hiyo saizi yake ni polisi mbona mnafanya utani na huyu mtu nyie!"



"Hapana mkuu Jonathan si polisi kama unavyodhani naye ni mwanajeshi pia mpelelezi alojificha katika mwamvuli wa uinspekta bado ajakiri kushindwa tumpe muda!"



Kikao kiliendelea na hatimaye kikaisha chachu ya kumtia Gambi mkononi ikiwa imeongezeka Mara dufu



***



Insp Jonathan akiwa anaendelea na upelelezi wake aliingia ofisi ya waziri mkuu alishtuka baada ya kumkuta mwanamke alivaa juba!



Machale yakamcheza nywele zikamsisimka!



"Mheshimiwa Mara ya mwisho aliingia na mwanamke alovaa juba ambapo baadaye huyo mwanamke alitoka na gari ya ofisini na kuondoka asbuh ndipo tulipogundua muheshimiwa ametutoka"



Jona akakumbuka maojiano Yale aliyo ojiana na mlinzi wa getini nyumbani kwa marehemu,akabaki ameganda akimwangalia Dada yule!



"Samahani ni kusaidie nini kaka?!"



Fatma akamshtua na kumtoa katika Lindi la mawazo lililochanganyikana na butwaa



"Sory kwa jina naitwa inspekta Jonathan natoka makao makuu ya usalama wa taifa kitambulisho changu hiki hapa ni mfatiliaji wa kifo cha mh waziri"



"Ok nashkur kutambua hilo"



"Ok naitaji sapoti yako ningependa kujua mahala kamera za dstv za siri na za dhahiri zilipotegeshwa"



"Nadhani ofisi ya waziri mkuu aina camera za siri zaidi ya hizo unazoziona juu twende....



Wakaingia mpaka ofisi ya waziri mkuu!



"Pamoja na hizi"



Jonathan akapeleka mkono kukagua camera zile zilizopo ukutani zote ziliharibiwa!



Jona akashtuka!



"Unaweza kunionesha chumba cha mawasiliano"



Fatma akamuonesha Jona akaingia katika chumba kile ambacho vijana walikuwa wakiendelea na kazi



Jona akajitambulisha kama kawaida na kuwauliza juu ya kuaribika kwa camera zile ndani ya ofisi ya waziri mkuu



Makarani wale wakamjibu kuwa mheshimiwa mwenyewe ndo ameziharibu kutokana na kutotaka siri zake za umalaya zisionekane lakini hata ivyo wakamtoa khofu kwa kumwambia zipo za siri!



Hili hata Fatma akulijua

Wakasogeza compyuta zao vizuri na kuanza kuangalia picha zilizotoka katika camera ilotegeshwa kwa siri Sana ofisini kule kwa waziri mkuu



Picha zikaanza kufunguka

Akionekana mwanamke mwenye juba akiwasili katika ofisi zile Mara ya kwanza akapendwa na Jb na kumuomba ajifunue naye bila iyana akajifungua



Jona akapigwa na butwaa baada ya kumtambua ni Fatma

Kumbukumbu zikarudi nyuma alipo onana na Fatma ofisini kwa bosi wake Kamishna Brown Stanley kama sekretari



Alimjua vizuri Fatma kama mpelelezi na mwanajeshi kutoka Kongo,walishakutana kwenye mafunzo Cuba



Pia alikuwa ni jasusi mwenzake wa kimataifa( jwk)



Wakati akiendelea kusta ajabu picha za wawili wale wakiwa wamekumbatiana Jj akihema ghafla Fatma akamsukuma na kumuitaji wakafanyie nyumbani



Mpaka hapo akuwa na shaka Fatma akuwa na nia nzuri na taifa lile!,akamkumbuka na dereva Olomy ilikuwa lazima awafatilie!



Ni wazi sasa alijua fika Gambi hakuwa peke yake!



Ghafla akajitoa pale kwa spidi kwa lengo la kwenda kumkamata binti yule ambaye angemwezesha kukamatwa kwa Gambi!



Fatma akwepo!



Jona akazidi kuchanganyikiwa

Akajitoa katika ofisi ile kuelekea ofisini kwa bosi wake!



****



UWANJA WA NDEGE KIA



Ndege aina ya Boeing Mali ya Kinte ifanyayo safari kati ya marekani na Kinte ilitua chini taratibu

Mlango ukafunguka na watu wakaanza kushuka!



Kijana mrefu maji ya kunde alovaa suti ilomkaa vyema mkononi akiwa na brufcase yake taratibu naye akashuka!



Usoni alivaa miwani sijui ni yajua!

Akaangalia eneo lote lile la uwanja! Macho yakatua katika saa yake!



Akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa simu akafungua mfuniko wake na kutoa line akapachika line nyingine.



Akapiga na kusikiliza upande wa pili



"Nimefika salama ntakujulisha kila kitu mkuu"



Akakata na kuchepuka kutoka nje ya uwanja ule!



Daaah ni nani huyo tena na alikuwa anawasiliana na nani?!

Vipi Zidu,Katarina na Isack Tanzania wanaendeleaje,bado tuna safari ndefu.









Mtu yule alipofika nje ya uwanja akakuta kuna gari inamsubiri akaingia ndani ya gari na gari ikaondolew akiwa ndan ya gar kuna meseji ikaingia katika simu yake!,akaisoma



"tuelekee ikulu,"



Akamwambia dereva wake,ambaye alielekea uelekeo wa ikulu,alipofika alikuwa akipigiwa saluti na kila askari alompita akaingia ndani ya ikulu!,mtu yule alikuwa na mazungumzo nyeti sana na mh rais,



"karibu mh!" Mh Rais Akamsalimia Kwa Furaha Swaiba Wake Yule Waloshirikiana Katika Mapinduzi Ya Kumng'oa Mernel ii,tena huyu hasa ndo alo mtandika risasi,



"hali ni mbaya Gambi Katoroka Na Kashamuua Wazir Mkuu Jj Mpaka Sasa ajapatikana"



Rais Laizar Nyoshi aliongea kwa huruma



Mtu Yule akatabasamu,



Alionekana kujiamin kupita maelezo



"usijal mh rais kila kitu niachie mimi wacha nielekee kambin nkawapange vijana,ili mradi nimerudi hakuna kitakachoharibika,



Wakaagana Pale Mtu Yule Akatoka na kuelekea kambini



BAADA YA SIKU KADHAA



KAMBINI



"Wewe ni nani?!"



Mtu yule alioji!



",naitwa Gambi! , Laurent Mernel Gambi"



Mtu aloulizwa akajitambulisha,



Mtu yule akashtuka baada ya kuskia jina lile,



japo sura aikuwa ya Gambi ila sauti ilikuwa yake!..



'Bila Shaka kavaa ngozi bandia'



Akawaza mtu yule huku akipanga mapigo atakayo yatumia kummaliza kiumbe alokuwa mbele yake



'Sijatoka marekani bure'



Akamalizia kwa wazo hilo mtu yule...



Na hapo hapo akamfata speed Gambi,naye kijana yule akakaa stendy bay kumngojea kyare alipomfikia akarusha teke zake ambazo hata ivyo mtaalamu Gambi alizipangua sambamba na kurusha mateke yake mawili ya haraka haraka aina ya taekwando yalofanikiwa kuvunja miguu ya kanali yule!



Gambi alijua ni wapi apige!



Wakati kyare akiugulia maumivu Gambi akaingiza mkono mfukoni alipotoka ulikuwa na bastola akamuoneshea kamanda yule alochafuka 'v' mabegani



"Wewe ndiyo uliyowamiminia risasi wazazi wangu bila huruma mbele ya macho yangu baba na mama sitoweza kukuacha hai mwana haramu wewe ulolaaniwa wasalimie kuzimu"



Gambi hakuwa na mzaa akaachia risasi zikachimbua kifua cha mtu Yule kanali kyare na kuuondoa uhai wake,



Kijana yule bila kupoteza muda akachukua kiasi cha damu na kuandika katika nailoni la hema lile mfungwa no 02



Akimaanisha huyo ndo wapili kumuua,katika orodha yake alibakiwa na watu wawili tu



Kamishna Brown Stanley aliyewaig kumkamataga kipindi icho akiwa mwanajeshi Wa kawaida tu pamoja na mh Rais



Kwa kupitia njia za panya alizoelekezwa na Odovy Gambi akapotea eneo lile.



ILIVYOKUWA



Ni wakati kina Odovy wakiendelea na mazoezi kambini pale gari ile ilompakia luteni Johnson kyare iliwasili!...



Odovy hakupata tabu kumtambua Luteni yule kwamba ndo anayesakwa na gambi!,sasa ilikuwa ni jinsi ya kuufikisha ujumbe!



Wanajeshi wa kambi ile usiku kwa kutumia njia za panya baadhi walikuwa wakitoroka mpaka kijijini katika sherehe mbalimbali zikiwemo harusi na hata disko,uongozi wa kambi ile awakugundua hilo



Nafasi hiyo adimu ndiyo odovy aloitumia kufika katika kijiji kile wenzake walipojifichia na kumpa habari Gambi juu ya kuwasili kwa Kyare!



Gambi akaanza kujiandaa,akafika katika kijiji kilichokuwepo mpakani mwa kambi ile akajifanya yupo mafunzoni kwa miezi kadhaa ilo alifanikiwa kuwa hadaa wana kijiji wale pasina kujua mawazo ya kijana yule ambaye kwa siri sana usiku aliingia msituni na kutembelea kambi ile ya jeshi kwa uchunguzi



Taratibu akaanza kuwafatilia wanajeshi wale walokuwa wakitoroka usiku,siku hiyo wanajeshi wale walitembelea kilabu na kunywa pombe zile za asili



Wakati wanaondoka Gambi akiwa tayari ndani ya uniform alizopewa na Odovy aliwafata nyuma nyuma wanajeshi wale ambao awakugundua ufatiliwaji wao



Kwa kupitia njia za panya mpaka ndani kabisa ya kambi ile kwa kuwa ilikuwa ni usiku alijificha chini ya magari na kupitiwa na usingizi!



Alikuja kushtuka saa kumi usiku ni wakati wanajeshi wale wakitoka katika mapema yao,na kuanza mazoezi yeye ndo akapata upenyo wa kuingia katika moja ya hema lile ambalo alikagua silaha yake na kuipachika kiunoni wakati akiwa anawaza cha kufanya ghafla katika pembe ya jicho lake akamuona mbaya wake akija uelekeo wa hema lile!



Mwili wa Gambi ukamsisimka!



Hasira chuki zikamtawala, akakumbuka wakati mtu yule alipowamiminia risasi wazazi wake



Luteni Johnson kyare akijua pengine ni mwanajeshi anayetegea mazoezi akajipeleka kabla ajapokonywa roho yake na kiumbe kile hatari



Kisha Gambi akatoweka kwa kupitia njia zile zile za panya walomuonesha wenyewe



****



Baada ya kwisha kwa gwaride wanajeshi wale walirudi katika mahema yao kwa minajili ya kubadilisha uniform za mazoezi na kuvaa za gwaride



Kila siku asubuhi ilikuwa lazima wakimbie mchaka mchaka km kadhaa , wajipange mstari,wahesaba namba wa gwaride ,ndo waanze mazoezi ya ardhini,mapigano na baadhi ya mazoezi magumu



Baada ya hapo waende kuoga wapate kifungua kinywa ndo waanze mazoezi maalumu ya gwaride



Ni wakati wanajeshi wale wakiingia katika hema ghafla nje ya hema lile wakakutana na damu iloganda kwa haraka wakazama ndani walipoukuta mwili wa kiongozi wao auna uhai



Mauaji kambini hasa kwa kiongozi ilikuwa ni jambo la kawaida ila neno mfungwa no 2 ndilo lililoleta udadisi na kutambua kuwa muuaji akutoka ndani ya kambi ile!



Akuna ambaye alikuwa amtambui Gambi mfungwa alotoroka miezi kadhaa nyuma awakuwa na shaka ndo muhusika kutokana na neno mfungwa no 2



Wanajeshi wale wakaingia rasmi uraiani wakishirikiana na serikali kumsaka Gambi , Olomy na Fatma ndo walokuwa na picha zao!



Katu hawakujua kuwa wale walikuwa ndani ya sura mpya ,



Magari yalikagullwa usiku na mchana , picha zikisambazwa nchi nzima, vizuizi viliongezeka nyumba kwa nyumba zikikaguliwa na wanajeshi wale walotapakaa mtahani bila mafanikio



Na Hatimaye baada ya kupita katika nchi nzima bila mafanikio na sasa wakakivamia kijiji cha Mzuva land!



Kijiji kilichosaulika!....



Wenyewe wausika wakiwa katika moja wapo ya kilabu bila kujua juu ya kuvamia kwa kijiji kile w akaendelea kuleweka!



Walikuwa wako full



"Mimi ndo Gambi lazima niwamalize mafala hao!"



Gambi akaropoka pasina kujua wanajeshi walikuwa ndo wanaingia eneo lile!



"Baba yangu aliwa kosea nini mafala nyinyi mpaka mumuue mtanikoma mamae....."



Akaendelea kuropoka!



Ghafla akayatoa macho baada ya kuona mitutu ya bastola!....



Mkojo ukagonga chupi



"Tumekwisha!"



Fatma akanong'ona



"Wote mikono juuu"



Daaaaah embu niishie hapa!

Usikose mwendelezo hapa bado vipande viwili tuitimishe season 5 mkasa unakataa kuisha tuonane katika season 6 Kiapo ( Hitimisho) kuitimisha riwaya hii







"Mimi ndo Gambi lazima niwamalize mafala hao!"



Gambi akaropoka pasina kujua wanajeshi walikuwa ndo wanaingia eneo lile!



"Baba yangu aliwa kosea nini mafala nyinyi mpaka mumuue mtanikoma mamae....."



Akaendelea kuropoka!

Ghafla akayatoa macho baada ya kuona mitutu ya bastola!....



Mkojo ukagonga chupi



"Tumekwisha!"



Fatma akanong'ona



"Wote mikono juuu!"



Amri ikatoka walevi wote waliekwepo pale wakanyoosha mikono yao juu!



Wanajeshi wale wakakagua eneo lile!,



"Wakati taifa likiwa kwenye janga la uzuni nyinyi mnalewa tu!"



Aliye onekana kuwa kiongozi wao akafyoka akimwangalia mama muuzaji



Katu awakuwatilia shaka walevi wale dakika chache walokuwa wakiongea mahoka katika kilabu kile na wala hawakusikia kile Gambi alicho ongea kutokana na kelele nyingi



Watatu wale walikuwa na ngozi bandia usoni mwao Fatma alikuwa kamkalia Gambi kimahaba kanga imechanika hawakuwa tofauti na wakazi wa kule



Olomy naye aliketi pembeni yao!,wakakonyezana kupeana ishara ya kutoana khofu kwamba awaja julikana!



Wanajeshi wale walipita kwa mmoja mmoja wakionesha picha ya Gambi na Fatma na Olomy wakiuliza hakuna alowatambua

Mwisho wakatoka zao!



Nyuma walevi wale kila mtu akisema lake kulaani kitendo kile cha kunyooshewa silaha!



"Mama clareee chochea moto ulete ya moto moto hawatupati ng'ooooo"



Gambi akaanza tena kujigamba,hakuna alomfatilia!...



***



Gambi akiwa katika chumba chake alishika kile kikaratasi chake chenye orodha ya majina na pale katika jina la Luteni Kanali Johnson kyare akaweka tiki



Sasa alibaki akiya angalia majina mawili!...



"Kamishna Brown Stanley ndo anayefatia na wa mwisho ndo kiongozi wao rais Laizar nyoshi baada ya hapo ntakuwa tayari kuelekea na nyinyi Kongo"



Akaongea kwa sauti ya utulivu Fatma na Olomy wakimsikiliza kwa makini!



Akaendelea



"Kesho nitaenda jijini wami kuanza kuchunguza nyendo za huyo Brown baada ya hapo ntamzawadia kifo sina shaka na hili!"



Wakati Gambi akiwa katika mikakati ile upande wa kamishna walikuwa katika kikao kingine!



Kikao hiki walikuwa watatu tu!....



Insp Jonathan,Rais Laizar Nyoshi na Kamishna Brown Stanley



"Kazi imekuwa ngumu!,kwako na tukikuachia mwenyewe utoiweza tumeona tumlete Komandoo Gambi ujumuike naye kumsaka huyo mwana haramu!"



Jona akatabasamu aliujua uwezo wa Gambi



Rais akashika simu yake na kumpigia Gambi simu iliita bila kupokelewa!



Akajaribu tena



Jibu lilikuwa lile lile,wasiwasi ukaanza kumshika!



Ghafla ikakatwa na kuzimwa kabisa!



"Mbona apokei na kaizima?!"



Rais akaoji kwa wahka! Mpigie na mke wake Katarina!



Alipopiga simu ya Katarina nayo aikupatikana kabisa!



Kuna nini?!



Wote kwa pamoja wakawaza!



Ni wakati wakiwa katika mawazo Yale wakakumbuka kumpigia mwenyeji alopaswa kumpokea Zidu na mkewe nchini Tanzania



Simu ikaita na baada ya dakika kadhaa ikapokelewa....



"Rais Laizar Nyoshi hapa,rais wa Kinte naongea na Isack nataka kujua vipi Zidu alifika Tanzania salama?!"



"Ndi...ndo...ila yupo katika hali mbaya icu"



Isack akajibu



"Eti nini?!"



"Ndio muheshimiwa! Yeye pamoja na mkewe Katarina"



Isack akazidi kuabarisha



"Mbona amkunijulisha?!"



Isack kimya



"Oooh shit tumekwisha!"



Laizar akaongea kwa kukata tamaa



Ni wazi alichanganyikiwa ,Inspekta Jona na Kamishna walimwangalia raisi wao kwa wasiwasi!



"Zidu yu mahututi nani atatusaidia?!"



Kila mmoja kwa upande wake alichoka!



Wakati wale wakiwa katika mawazo yale ,wakifikiria kipi cha kufanya mwanaume Gambi akiwa katika kijiji kile akapakia pikipiki!



"Wapi mkuu?!"



"Uko full tank!"



"Kama kawaida man"



"Ganyama unaweza kufika?!"



Boda boda yule akakunja uso



"Poa nipeleke Kisangire"



Akaagiza boda boda yule akatia mafuta pikipiki na kuiondoa kwa mwendo wa taratibu!



Toka katika kijiji kile kuelekea Kisangire walipita katika pori

Huko ndipo ambalo mtaalamu Gambi alipanga kumnyang'anya jamaa yule pikipiki ile!



"Brooh embu simama nikojoe hapo kwanza"



Akamwambia yule jamaa ambaye bila shaka alisimama naye akashuka



"Daaaah nami pia nilibanwa kinoma nilijikaza tu"



Jamaa naye akaelekea pembeni ya alipo Gambi na kufungua zipu!



Ghafla alipokea bonge la Kofi nyota nyota zikasambaa katika uso wake kizungu zungu kikamtawala!



Gambi akakamata koo lake na kumkaba kwa mkono mmoja akamvutia mbele yake na kumzawadia ngumi yenye ujazo ilompeleka jamaa chini!



Gambi akamfata na kumshushia mguu wake ulovalishwa kiatu imara katika uso wake! Na kuondoka na uhai wa kiumbe Yule



"Ukuwa katika orodha yangu ila utansamehe"



Akamwambia akimvua koti lake akalivaa yeye!, akamvua gloves zake na kuzivaa yeye akaivaa na element akamsukumia katika vichaka



Mwanaume akapanda pikipiki! Akavuta mafuta na kuiondoa kwa speed



'Moja kwa moja mpaka jijini wami nakuja kamishna!'



Akajisemesha akizidi kuvuta mafuta!...



Sijui nini kiliendelea?!



Gambi atafanikiwa kuwamaliza wabaya wake?!



Tuonane katika sehemu ya mwisho ya season hii anza sasa kulipia agano ( hitimisho) seasom 6 kujua hatma ya yote haya







Gambi akamfata na kumshushia mguu wake ulovalishwa kiatu imara katika uso wake! Na kuondoka na uhai wa kiumbe Yule



"Ukuwa katika orodha yangu ila utansamehe"



Akamwambia akimvua koti lake akalivaa yeye!, akamvua gloves zake na kuzivaa yeye akaivaa na element akamsukumia katika vichaka



Mwanaume akapanda pikipiki!



Akavuta mafuta na kuiondoa kwa speed



'Moja kwa moja mpaka jijini wami nakuja kamishna!'



Akajisemesha akizidi kuvuta mafuta!...



***



Gambi akiwa juu ya pikipiki yake alifika mpaka katika jumba lile,



Ilikuwa ni jumba lenye ulinzi wa kampuni flani za ulinzi



Walinzi wale walikaa ndani ya geti mmoja akiwa pembeni ya geti na mwingine katika kijumba chake!



Gambi alifika na pikipiki yake akashuka na bila uwoga akalisogelea Geti na kuligonga



Mlinzi Yule alokuwa pale getini akafungua na kupokewa na tabasamu jepesi la kijana yule katili



"Nimemkuta mheshimiwa!"



Kwa sauti ya taratibu Gambi aliuliza!



"Yah yupo karibu ndani"



Jamaa yule akaongea akimfungulia mlango mdogo Gambi naye akazama ndani!



Akaelekea upande wa kile kijumba ambacho yule askari mmoja alikwepo ,lakini ghafla aliingiza mkono mfukoni na kuutoa ukiwa umeshika pistol yenye kiwambo cha kuzuia sauti



Na kwa wepesi wa ajabu akafyetua risasi zilizo kichimba kifua cha mlinzi yule alokuwa akielekea katika kiti chake kwa lengo la kukaa



Muda ule ule akadondokea chini uwahi ukiuacha mwili,



Yule mlinzi wa ndani alibaki na bumbuwazi mkono umeshika mkonga wa simu lengo ni kupiga ndani aeleze kuna mgeni kusudi apewe ruksa ya kumpeleka

Akabaki amenata vile vile

Naye tayari alishamfata mwenzake!,



Mwanaume akazidi kusonga kuelekea ndani ya nyumba ile!



Mahala alipo Kamishna Brown na familia yake!



****



Brown akiwa katika sebule yake macho yake yakiwa katika tv ghafla akaskia yowe la mke wake!



Kwa wepesi akajinyanyua kuelekea ilipotoka sauti ile,



Ghafla akapiga breki mbele yake alitazamana na bastola!



"Niliapa kuwaua wote mlioiangamiza familia yangu na na mshkuru Mungu nimefanikiwa juu ya ilo na baada ya wewe atabaki huyo kiongozi wenu rais Laizar Nyoshi"



"Gambi ni wewe?!"



Brown aliongea kwa mashaka!



"Ulijua sitofanikiwa kukuua,japo mara ya kwanza ulinizidi nguvu ila nimetoroka tena nikiwa na Kiapo cha kuwamaliza nyinyi nyote sina cha zaidi wasalimie kuzimu"



Bila huruma Gambi aka achia risasi ,wala Brown akufanya jitihada zozote za kujinasua akaporomoka chini macho akiyageuza ni kwamba alikufa akiwa katika butwaa



Gambi aka achia kicheko na kuchovya kiasi cha damu aka andika jina mfungwa 03 ukutani!



Baada ya tukio lile akageuka kurudi alipotoka akiiruka miili ile ukiwemo wa mke wa Brown watoto mpaka nje ya geti akajipakia katika pikipiki yake na kuondoka kwa kasi!....



"Mr Nyoshi salamu zikufikie joh nathani ndo kazi ngumu ilobakia moyo wangu uwe na amani nadhani hata wazazi wangu huko waliko wanafurahia kwa nnachokifanya nakuja kwa ajili yako my president"



Gambi akaongea mwenyewe akizidi kukata mitaa ile kuelekea eneo lake la maficho!



****



Ni wakati akiwa ndani ya ofisi yake katika ikulu yake yenye ulinzi mkali ghafla mlango wa ofisi ile ukafunguliwa na bastola ika anza kutangulia....



Rais Laizar Nyoshi akabaki katika butwaa pasina kujua ni nani anayeingia,ghafla kiatu kikatangulia ni kiatu cha kijeshi na mtu wa miraba minne akaingia akiwa ndani ya nguo za kijeshi!



Bastola akiwa ameielekezea usawa wake!,mapigo ya moyo wake yakaongeza kasi ya upigaji!



Kivipi kijana yule aweze ingia mahali pale penye ulinzi mkali



Hamu ya kutaka kujua walinzi wake wapo katika hali gani ikamkamata na kwa haraka macho yake akayaelekezea dirishani



Walinzi wakaonekana wakicheka bila khofu yoyote kama vile hakuna kilichotokea!



Kivipi sasa?!



Hapati jibu akayarudisha macho yake kwa mvamizi yule na kuendelea kulishughudia tabasamu lake baya



"Hakuna marefu yasiyo na ncha muheshimiwa president"



Mtu yule akamwambia kwa sauti kavu isiyo hata na chembe ya huruma ndani yake!,bado bastola akiwa kaishika vizuri katika mkono wake kumuelekezea yeye



"Nilihaidi kuwaua na sasa nimefanikiwa"



Mtu yule aliendelea kuongea huku akimsogelea na bastola yake mpaka akawa karibu yake umbali kati yao ukiwa ni kama hatua tano tu



"Gambi?!"



Laizar akaoji akiwa kama katega kitu



"Yah Mimi ni mtoto wa rais Mernal ulotoa idhini auwawe kikatili tena mbele ya macho...



Kabla ajamalizia Nyoshi akaruka na kuutandika mkono uloshika ile bastola teke bastola ikaruka na ilipotua ilikuwa katika mkono wake bila kupoteza muda ikacheua katika kifua cha Gambi na kumporomosha chini!



Gambi hakuwa na uhai tena!



Laizar Nyoshi akaangua kicheko akiusogelea mwili ule na kuukanyagia kanyagia chini kwa dharau....



Dah nini kiliendelea?! Gambi ndo kafa kizembe ivyo?!



Vipi Zidu na Katarina na Isack Tanzania!...



MWISHO WA SEASON 5, TWENDE TUMALIZE NA SEASON 6

0 comments:

Post a Comment

Blog