Search This Blog

Saturday, 24 December 2022

WAUAJI WALITUMIA, CHAI, MIAVULI NA HATA SUMU KUWAANGAMIZA WAPINZANI - 3

   http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/wauaji-walitumia-chai-miavuli-na-hata_10.html

Simulizi :  Wauaji Walitumia, Chai, Miavuli Na  Hata Sumu Kuwaangamiza Wapinzani 

Sehemu Ya Tatu (3)


Mwavuli uliowekwa sumu.

Raia wa Bulgaria Georgi Markov alikuwa akisubiri kupanda basi mnamo tarehe 7 mwezi Septemba wakati alipohisi amedungwa kisu katika paja lake.


Bwana Markov mwenye umri wa miaka 49 aliangalia nyuma na kumuona mtu ambaye alikuwa amebeba mwavuli akikimbia na kupanda teksi.


Ni baadaye alipokamilisha kazi yake ya huduma ya BBC nchini Bulgaria aliporudi nyumbani na kuanza kuugua.


Bwana Markov ambaye alikuwa mpinzani wa serikali ya kikomyunisti ya Bulgaria alifariki miaka minne baadaye.


Maafisa baadaye waligundua kwamba aliwekewa sumu ya ricin ambayo ilidaiwa kutiwa katika mwavuli huo.


Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji yake ikiwa ni mabaya zaidi katika vita baridi, lakini Bwana Markov alisema kuwa anaamini kwamba majasusi wa Urusi KGB walihusika katika shambulio lake.


Dubu aliyebeba shoka.

Jörg Jenatsch alikuwa muhubiri ambaye alibadilika na kuwa mwanasiasa maarufu katika vita vya miaka 30 nchini Switzerland.


Lakini licha ya mafanikio yake yote ni kifo chake mwaka 1639 katika nyumba moja ya kulala huko Chur ambacho kitakumbukwa sana.


Mwanasiasa huyo aliuawa na mtu aliyekuwa amevalia kama dubu mwaka 1639.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog