Simulizi : Wauaji Walitumia, Chai, Miavuli Na Hata Sumu Kuwaangamiza Wapinzani
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Mwanasiasa huyo aliuawa na mtu aliyekuwa amevalia kama dubu mwaka 1639.
Bwana Jenatsch, ambaye alikuwa amesifika kwa huduma yake alikuwa katika sherehe wakati kundi moja la watu lilipowasili na kutaka kujiunga nao.
Kiongozi wa kundi hilo alikuwa amevaa kama dubu.
Kundi hilo liliruhusiwa kuingia na dubu huyo ambaye utambulisho wake haukujulikana kabla ya kumkata bwana Jenatsch hadi kufa kwa kutumia shoka.
Inadaiwa kuwa shoka lililotumiwa ndio hilo hilo alilotumia kumuua mpinzani wake.
Chuma cha moto
Zaidi ya miaka 700 huenda imepita tangu mfalme Edward wa pili alipouawa kati mji wa Gloucestershire, lakini bado tunaweza kukumbuka.
Tunachojua ni kwamba mfalme Edward wa pili alikamatwa na kulazimishwa kuwachia ufalme kwa niaba ya mwanawe ambaye alikuwa Edward wa tatu baada ya mkewe Isabella na mpenziwe Roger Mortimer kuvamia Uingereza mwaka 1326.
Edward wa pili baadaye alifungiwa huko Berkeley ambapo alifariki mwaka uliofuatia.
Wana historia wamehoji ni vipi Edward wa pili alifariki.
CHANZO CHA PICHA,HULTON ARCHIVE/GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Wana historia wamehoji ni vipi Edward wa pili alifariki.
Lakini kulingana na habari zilizopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine hakufariki usingizini kama ilivyodaiwa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment