Simulizi : Bomu
Sehemu Ya Tano (5)
Hannan aliingiza ile namba katika 'program' anayoijua yeye, tena kwa namna anayoijua yeye.
Akasema.
"Hii namba haipatikani kwa sasa, hivyo itakuwa ngumu kidogo kujua mahali alipo mmiliki wa namba hii.."
David alipiga kite cha ghadhabu.
Tumaini lililofufuka kwa kasi la kuipata familia yake lilipotea tena.
"Usihofu David, tutaiokoa tu familia yako. Hatujawahi kushindwa, siku zote sisi ni washindi" Daniel alisema kwa kujiamini.
"Hannan inamaana hakuna namna nyingine yoyote ya kuweza kupajua mahali alipo huyo Elia Kilasi?" Adrian aliuliza.
"Hivi kwanini tusiangalie uelekeo mwengine. Tumchunguze Mzee Msangi. Maana ni miongoni mwa watu waliowasiliana na Elia Kilasi? Tukimtia mikononi mwetu mzee Msangi atatuambia tu ana uhusiano gani na Elia Kilasi" Daniel alisema.
"Wazo zuri san Daniel, ila sasa changamoto nyingine ni, namba ya mzee Msangi tutaipata wapi?" Adrian aliuliza.
"Hii hapa nimeipata" Hannan alisema. Wote macho yao yakageuka kwa Hannan.
"Ni kweli Elia alikuwa anawasiliana na Mohammed Msangi mara kadhaa. Na hapa ndipo nilipoipata namba yake" Hannan alisema.
"Kazi nzuri sana Hannan, hebu i'track hiyo namba ya mzee Msangi. Tukamsangue" Daniel alisema.
Ukumbi mzima ulikaa kimya. Wote wakimsubiri Hannan afanye mambo yake. Ilikuwa inasikika sauti ya 'laptop' tu wakati ikibonyazwa na Hannan.
Ukumbi mzima ulikaa kimya. Wote wakimsubiri Hannan afanye mambo yake. Ilikuwa inasikika sauti ya 'laptop' tu wakati ikibonyazwa na Hannan.
Tusome ya leo..
Ilichukua kama dakika tano ya ukimya. David roho ikimdunda, alikuwa anaitegemea kitu kimoja tu, sauti ya matumaini kutoka kwa Hannan.
"Nimempata, nimempata Mzee Msangi" Hannan alisema kwa furaha, huku akirusha ngumi yake ya kulia hewani.
"Umempata mzee Msangi? Yupo sehemu gani?" David aliuliza kwa furaha. Tumaini likafufuka tena.
"Mzee Msangi sasahivi yupo katika nyumba moja huko Oyesterbay" Hannan alisema huku akiwa bado ameiinamia ile tarakilishi yake.
"Kazi imekwisha! Adrian utafuatana na David kwenda huko Oysterbay. Tunataka mtuletee mzee Msangi hapa bila kumuuliza chochote. Majibu yote ya maswali yetu atajibia akiwa hapa. Maelekezo yote sehemu alipo mtakuwa mnawasiliana na Hannan. Hakikisheni mnamleta hapa akiwa anapumua.." Daniel alisema.
"Sawa Daniel, tumekuelewa. Tutafanya kama ulivyosema" David alitikia.
Dakika hiyohiyo Adrian Kaanan na David Ngocho waliingia kazini. Huku wakiwa wamebebelea silaha zao. Wamejiandaa kikazi, na wakiwa tayari kwa kazi.
Waliondoka kamili gado, huku wakijua kuwa pamoja kuwa mzee Msangi kwasasa alikuwa ni mstahafu katika idara ya usalama wa taifa, lakini haitakuwa kazi ndogo hata kidogo kumkamata.
Walienda zao.
Walipotoka tu wakina David, Daniel Mwaseba alimpigia simu Chifu kwa kutumia simu nyingine aliyoichukua chumbani kwake. Alikuwa anataka kumpa taarifa juu ya misheni yao ilipofikia.
Simu ya Daniel ikapokelewa.
"Habari yako Daniel" Sauti kwenye simu iliongea.
Mstuko dhahiri ulionekana katika sura ya Daniel Mwaseba. Uso wake ulisawajika ghafla. Furaha yake ilipotea.
Kwani aligundua kwamba ile akiyoisikia haikuwa sauti ya Chifu.
"We ni nani uliyopokea simu ya Chifu?"Daniel aliuliza huku akiwa makini kuisikiliza ile sauti.
"Wananiita Imma Ogbo. Bila shaka haiwezi kuwa mara yako ya kwanza kulisikia jina hili..Immanuel Ogbo!" Sauti ya kwenye simu ilisema kwa majigambo.
"We mshenzi usinambie kuwa umemteka na Chifu? Omba isiwe hivyo, maana nitakachokufanya kitaandikwa katika vitabu vya kumbukumbu hapa duniani." Daniel alisema kwa hasira.
"Sijamteka Chifu wenu tu. Nipo poa na waziri wenu wa fedha mikononi mwangu. Na punde tu nitafanya tukio ambalo nina uhakika litaishangaza dunia." Imma Ogbo alisema bila ya hofu.
"Imma Igbo. Unajua madhara ya hiko kitu mnachokifanya?" Daniel aliongea baada ya Hannan kumwambia kwa ishara aendelee kuongea.
Huku yeye akibofya kwa kasi ile tarakilishi yake.
Alikuwa anajaribu kum'trace Imma Ogbo.
"Daniel, usibuy time kwa kudhani mtajua mahali nilipo. Mnajidanganya sana. Nimewazidi akili parefu sana. Mimi na nyinyi ni tofauti ya mbingu na ardhi" Imma Ogbo alitamba.
"Imma.." Daniel hakumalizia. Imma Ogbo alidakia.
"Sikiliza Daniel Mwaseba. Eti mpelelezi namba moja nchini Tanzania, hahaha. Ni hivi, huna haja ya kunitisha mimi. Sina msamiati wa hofu moyoni mwangu."
"Kwani mnataka nini nyinyi?"
"Ni hivi, kama mnawataka Chifu na waziri wenu wa fedha watoke salama hapa walipo, tunaweza kuongea. Lakini kama utaendelea kujifanya kiburi endeleza hiko kiburi chako. Nakuapia mtakosa yote..." Imma Ogbo alisema bila mas'hara.
"Kwani mnataka nini ili muwaachie salama?" Daniel aliuliza akiwa amekata tamaa.
"Tunataka kitu kidogo kutoka katika serikali yenu. Tunajua wewe una ushawishi mkubwa sana hapa nchini. Tumia ushawishi wako kumwambia rais wenu jambo hili. Afungue mipaka ya nchi, au mtutafutie njia ya kutoka hapa Tanzania. Tukitoka salama basi mjue na hawa watu wenu tutawaacha salama. Mkifanya kinyume na matakwa yetu, basi amini mtaokota maiti kila siku. Tutauuwa tupendavyo. Tutawatesa tujisikiavyo" Imma Ogbo alisema.
"Hatuna mpango wa kuwaacha mtoke salama ndani ya nchi hii. Mbinu zenu zimefika ukingoni. Tutawakamata hivi karibuni.." Daniel alisema.
"Hahaha unacheza wewe Daniel, naitwa Imma Ogbo, anaitwa Mark the sniper. Ninakuapia mtavikuta vichwa vya hawa watu wawili katikati ya uwanja wa taifa saa mbili asubuhi. Na hiyo inatokana na kiburi chako Daniel!!" Imma Ogbo alisema kwa hasira.
Daniel aliwaza kidogo. Na hakumpa muda wa kuwaza zaidi simuni.
Imma Ogbo akakata simu.
Baada ya simu kukatwa, Daniel alimgeukia Hannan, na kumuuliza.
"Vipi Hannan umefanikiwa kugundua simu imepigwa kutokea wapi?"
"Hapana Daniel. Kuna kitu cha kiteknolojia wamefanya. Na kitu hiko si cha kawaida. Simu hii haioneshi hapa jamaa alikuwa anaongea kutokea wapi?" Hannan alisema akiwa amechoka.
"Tunafanyaje sasa? Chifu na Waziri wa fedha wametekwa, na lengo lao ni kushinikiza wanapewa nafasi watoke hapa nchini. Yaani serikali iruhusu wahalifu waondoke hapa nchini?" Daniel aliuliza.
Ukumbi wote ulikuwa kimya. Hakukuwa na mtu mwenye njia mbadala.
Daniel hakujua kwamba hakupaswa kuuliza. Yeye ndio alipaswa kutoa majibu. Watu wote pale sebuleni walikuwa wanamtegemea yeye.
Walikuwa wanamsubiri awape mbinu mbadala.
Imma Ogbo alikuwa amewashika hapa!!!!
Ukumbi wote ulikuwa kimya. Hakukuwa na mtu mwenye njia mbadala.
Daniel hakujua kwamba hakupaswa kuuliza. Yeye ndio alipaswa kutoa majibu. Watu wote pale sebuleni walikuwa wanamtegemea yeye.
Walikuwa wanamsubiri awape mbinu mbadala.
Na hii ni sehemu ya thelathini na mbili..
Ilikuwa kweli, kama Imma Ogbo alivyosema wakati anaongea kwa simu na Daniel Mwaseba.
Walikuwa na Chifu. Mkuu wa Idara ya Usalama Taifa wa nchi. Walikuwa pia na Waziri wa mipango na fedha, mheshimiwa Elisha Salu.
Imma Ogbo alikuwa hadanganyi..
Kuwatia mikononi mwao watu hao wawili muhimu kwa nchi, ilikuwa ni kazi makini ya mwanaume, Imma Ogbo.
Haya yalikuwa ni matokeo ya kikao cha watu watatu. Imma Ogbo, balozi Agdir na Dr Luis. Waliamua hivyo baada ya mpango wao wa kuulipua ubalozi wa Uganda kushindwa kufanyika.
Katika kikao chao, walipanga mambo mawili, ambapo moja lilikuwa limekamilika. Jambo hilo likikuwa ni kumteka waziri wa fedha wa nchi. Na walifanikisha vizuri sana, na kwa bahati nzuri waziri Elisha alikuwa na kikao na Chifu. Na hivyo bastola ya Imma Ogbo kuweza kuwateka wote kwa wakati mmoja.
Sasa ilibaki kazi ya pili. Kazi ngumu zaidi ya hii ya awali. Kuteka watoto wa shule ya msingi ya St Joseph.
Na imma Ogbo alienda kuifanya kazi hiyo baada ya tu kuongea na Daniel Mwaseba. Yote hiyo ilikuwa kuilazimisha serikali iwape mpenyo wa kuondoka nchini Tanzania.
Saa kumi na mbili jioni, Imma Ogbo alifanikiwa kuliteka basi dogo la wanafunzi wa St Joseph waliokuwa wanatoka 'Beach' wakirejea shuleni kwao. Wanafunzi sitini na mbili na walimu wao watatu wakike pamoja na dereva walikuwa mikononi mwake.
Ilipotimu saa mbili usiku ndipo habari hii ikatangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali nchini. Ikiambatanishwa na ile ya kutekwa kwa Chifu Salimu Gulenga na Waziri wa mipango na fedha, Elisha Salu.
Habari hizi zikazua kizaazaa kipya nchini Tanzania!
Taifa likaingia katika taharuki kubwa. Iliyoambatana na kizaazaa haswa!
Kutoweka kwa wanafunzi sitini na mbili wa shule ya msingi St Joseph pamoja na walimu wao watatu ilikuwa habari kubwa sana katika taifa lisilozoea mshikemshike kama hiyo.
Askari polisi walihaha kuwasaka wanafunzi na walimu wao, bila kumsahau dereva. Wakati wazazi na ndugu wa watoto hao wakilia na kusaga meno ndani ya shule ya St Joseph. Waliapa hawatatoa miguu yao ndani ya shule hiyo mpaka watoto wao watakapopatikana.
Ilikuwa tafrani!!
***
Saa tatu zilizopita kabla ya taarifa ya kutekwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi St Joseph, Adrian Kaanan na David Ngocho walifika katika nyumba ambayo simu ya mzee Msangi ilionekana kwa mara ya mwisho. Ilikuwa maeneo ya Oysterbay. Wakifika kwa kutumia maelekezo wakiyopewa kwenye simu na Hannan.
Nyumba yenyewe, ilikuwa nyumba kubwa ya kisasa, yenye geti kubwa likilolindwa na walinzi wanne wenye silaha za moto pamoja na Mbwa!.
Kwa kutumia mbinu zao walifanikiwa kuwalaza walinzi wanne na mbwa wawili.
Lakini ndani ya nyumba hiyo hawakukuta kitu kingine chochote kile.
Mzee Msangi hakuwepo ndani ya nyumba hiyo, na hii ilizidisha hofu kuu katika moyo wa David.
Baadae wakaja kugundua kwamba mzee Msangi alikuwa anawasiliana na Elia Kilasi kwa kutumia simu ya mezani.
Walirudi nyumbani kwa Daniel Mwaseba na kuwaeleza wenzao yote yaliyotokea huko Oysterbay.
Na ndipo ilipotimu saa mbili usiku walishuhudia taarifa ya habari ya upotevu wa watoto sitini na mbili wa shule ya msingi St Joseph, pamoja na walimu wao.
"Jamani, hapa sasa hakuna siri tena. Watu wote wanajua nini kinaendelea hapa nchini. Na kam taifa limetupa sisi dhamana ya kuwaokoa watu hao wote waliotekwa. Adrian, kwanini usiwasiliane na IGP John Rondo na kumweleza shida yetu ya kuonana na rais?" Daniel aliuliza.
Adrian hakuuliza kitu. Alifanya kitu. Alichukua simu yake na kumpigia IGP John Rondo.
"Mambo gani haya mnafanya Adrian?. Kila siku mambo yanakuwa magumu kwa kushindwa kutekeleza kazi yenu. Ona sasa, Waziri wa fedha ametekwa, Chifu Salim ametekwa. Nani atakuwa salama sasa kama viongozi hao wakubwa wa nchi wanatekwa kiholela? Nani atashangaa kusikia watoto sitini na mbili wa St Joseph wametekwa ikiwa viongozi wao pia wametekwa?" IGP John Rondo alisema pindi tu alipopokea simu ya Adrian.
"Samahani sana mkuu. Na hiyo ndio sababu ya kukupigia simu usiku huu. Kwasasa tushawajua maadui tayari. Lakini kabla hatujawakamata tulikuwa tunaomba ruhusa ya kuonana na rais, kuna mambo tunataka kumueleza" Adrian alisema.
"Mambo gani hayo mnayotaka kumweleza rais? Niambieni mimi na nitalifikisha. Rais kwa sasa sidhani kama atakuwa tayari kuongea na nyinyi. Amechanganyikiwa sana na haya mambo yanayotokea hapa nchini" IGP John Rondo alisema.
"Naomba tutafutie nafasi kuonana na mheshimiwa rais, mkuu. Nakuhakikishia hili jambo linaenda kufika mwisho. Tutafutie nafasi ndogo tu ya kuongea na mheshimiwa rais" Adrian aliomba.
"OK ngoja niongee nae rais. Nitakujulisha kama atakubali kuonana na ninyi.." IGP John Rondo alisema.
Simu ikakatwa.
"Naomba tutafutie nafasi kuonana na mheshimiwa rais, mkuu. Nakuhakikishia hili jambo linaenda kufika mwisho. Tutafutie nafasi ndogo tu ya kuongea na mheshimiwa rais" Adrian aliomba.
"OK ngoja niongee nae rais. Nitakujulisha kama atakubali kuonana na ninyi.." IGP John Rondo alisema.
Simu ikakatwa.
Tusome ya Leo...
Sehemu ya Thelathini na Tatu
Dakika kumi baadae simu ya Adrian Kaanan iliita.
Alikuwa ni IGP John Rondo.
Adrian aliipokea simu.
"Adrian, rais amekubali muende kuonana naye. Amesema muende watu wawili tu" IGP John Rondo alisema.
"Amesema twende tukamuone muda gani?" Adrian aliuliza.
"Sasahivi. Hivi huko Mheshimiwa rais Mgaya anawasubiri ninyi. Mtapitia hapa makao makuu, maana ametaka twende wote" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu, tutakuwa hapo sio muda mrefu kuanzia sasa" Adrian alisema kwa furaha.
Simu ikakatwa.
Adrian akawaeleza wenzake kila kitu alichoongea na IGP John Rondo.
Ikaamuliwa, Adrian Kaanan na Daniel Mwaseba wajiandae kwa safari ya ikulu kuonana na mheshimiwa rais.
***
Wakati huo, mzee Msangi alikuwa kitalu C. Mahali ambapo walikuwepo pia wakina Elia Kilasi, Mark the sniper, Lameck na Luca.
Muda mfupi uliopita mzee Msangi alikuwa ametoka Tegeta Nyuki, ambapo kwa macho yake alishuhudia uharibu uliofanywa na kina Daniel Mwaseba.
Hakuamini kabisa kwa jinsi watu hao walivyofanikiwa kumuokoa Hannan.
Mzee Msangi alikasirika sana! Akampa likizo Anna arejee kwao. Na moja kwa moja ndio akaja kitaku C.
Nayeye pia, akiwa na wenzake waliipokea taarifa ya kupotea Chifu, waziri wa fedha na wanafunzi wa St Joseph wakiwa hapo.
Mzee Msangi moja kwa moja aliamini hiyo ni kazi ya Imma Ogbo. Huku akiwa haamini hatua aliyoichukua Imma Ogbo.
Hii ilitia uzito katika harakati zake za kumkamata Dr Luis.
Lakini kitu ambacho Mheshimiwa rais alikuwa hakijui, pamoja na kumpa kazi ya kumsaka Dr Luis mzee Msangi, lakini mzee Msangi naye alikuwa na mpango binafsi wa kumpata Dr Luis. Katika mpango huo alikuwa akishirikiana na Mwenyekiti, Antony Kyando.
Mpango wao ulikuwa ni kutengenezewa kirusi cha ajabu cha DH+.
Kirusi cha DH+ kilikuwa ni kirusi kipya katika dunia ya sayansi. Kirusi hiko kilikuwa kirusi hatari. Na aliyekiumba alikuwa ni Dr Luis.
Antony Kyando alikuwa anakihitaji kwa nguvu zote kukipata kirusi hiko kwa ajili ya kukitumia kwa wapinzani wake. Na mtu pekee aliyekuwa anaweza kukitengeneza kirusi hiko cha ajabu hapa duniani, alikuwa ni mwanzilishi wake..Dr Luis.
***
Saa tatu na dakika tano usiku, Daniel Mwaseba, Adrian Kaanan wakiongozana na IGP John Rondo waliwasili ikulu huko Magogoni.
Kwakuwa kulikuwa na taarifa wa ujio wao hapakuwa na shida yoyote ile. Baada ya kukaguliwa na kuambiwa waache vitu vyao vyote zikiwemo silaha zao katika cumba cha ukaguzi, moja kwa moja wakapelekwa katika chumba cha mikutano.
Ndani ya chumba cha mahojiano, walisubiri kama dakika tano hivi, ndipo Mheshimiwa rais Mgaya akaingia katika chumba cha mikutano.
Rais Mgaya alikuwa amevaa suti nzuri ya rangi nyeusi na tai nyeupe, chini alivaa viatu vya rangi ya kahawia. Ukiacha uchovu katika sura yake, lakini alikuwa amependeza sana.
"Poleni sana kwa kuwaweka hapa. Nilikuwa namaliza kikao na kamati ya ulinzi na usalama.." Rais alisema huku akilazimisha kutabasamu.
"Haina shida Mheshimiwa rais. Hata hivyo hatujakaa muda mrefu sana" IGP John Rondo alijibu.
"Nashukuru sana IGP John. Nimeitika wito wenu. Nawasikiliza ninyi IGP John kitu gani mlichoniitia hapa. Leo ratiba ilikuwa ngumu sana. Nilikuwa sina nafasi kabisa. Tangu asubuhi imekuwa ni siku ya vikao tu, lakini ulivyonambia kuna watu wana majibu juu ya kutekwa kwa Chifu, Waziri Elisha Salu na wale watoto wadogo wa St Joseph, nikaona nitenge angalau muda huu mdogo kuja kuwasikiliza" Rais Mgaya alisema.
"Ni kweli mheshimiwa rais. Najua ulikuwa hujapata bahati ya kukutana na watu hawa. Huyu hapa ni Daniel Mwaseba. Ni mpelelezi katika idara ya usalama wa taifa. Huyu hapa anaitwa Adrian Kaanan. Ni afisa wangu ninayemuamini sana. Hawa kwa pamoja na wengine ambao hawajapata nafasi ya kuja hapa leo ndio vijana wetu wanaounda kikosi cha B1. Kikosi kilichopewa kazi ya kumsaka rafiki yako Dr Luis.."
Msako dhahri ulionekana katika sura ya rais Mgaya baada IGP John Rondo kusema hivyo. Ni Daniel Mwaseba pekee ndio aliouona mstuko huo.
"... Aaah kumbe ndo kikosi cha B1 hiki. Daniel nimesikia sifa zako mara kadhaa, nafurahi leo kuonana nae kwa uso na macho" Rais Mgaya alisema akijibaraguza.
"Nami nashukuru sana mheshimiwa rais kuonana na wewe. Ni nafasi ya kipekee sana hii. Tulikuwa hatujaonana tangu umeingia madarakani. Nakupongeza sana kwa uongozi wako uliotukuka" Daniel alisema.
"Nashukuru sana Daniel, na huyu umesema anaitwa Adrian?" Rais Mgaya aliuliza akimwangalia IGP John Rondo.
"Ndio. Adrian Kaanan. Kwasasa Adrian ni kiongozi wa askari wetu wa misheni za siri na muhimu kwa nchi" IGP John Rondo alisema.
Rais Mgaya na Adrian Kaanan wakapeana mikono nao.
"Sasa mimi sitokuwa muongeaji mkuu. Kazi yangu ilikuwa ni kuwatambulisha tu. Hawa wenyewe ndio watakwambia lengo la ombi hili la kukutana na wewe" IGP John Rondo alisema.
"Karibuni sana" Mheshimiwa rais Mgaya aliwakaribisha.
"Kama tulivyotambulishwa na na IGP John Rondo. Mimi na Adrian tunaunda kikosi cha B1. Tukiwa pamoja na wenzetu, David Ngocho, Hannan Halfan na Martin Hisia.
Mheshimiwa rais, sisi kama kikosi cha B1 tulipewa kazi ya kumtafuta Dr Luis aliyetekwa katika kikosi cha B1, na mimi nikiwa kiongozi wake.
Kwanza niseme tu ni mimi ndiye niliyepewa na Chifu kazi ya kwenda kumpokea Dr Luis siku ile pale airport. Kwa maana hiyo nasikitika kusema Dr Luis alipotea katika mikono yangu katika hoteli ya Dos Santos.
Dr Luis hakupotea tu, na mimi niliishia kutekwa katika harakati za kumwokoa. Watekaji walinipeleka huko Mkuranga bila kujua kwamba nilitoa taarifa kwa mwenzangu ambaye alifatilia nyendo za watekaji.
Walinifikisha Mkuranga na kunifungia katika chumba kimoja kidogo. Nilijitahidi kujiokoa katika kile chumba. Nilivyotoka nje nilimkuta mwenzangu akiwa kapigwa risasi. Katika harakati za kumwokoa ndipo nilishuhudia nyumba ile ikilipuliwa kwa Bomu na helkopta ya jeshi.
Na hiyo ikawa sababu ya kuundwa kwa kikosi hiki.
Kikosi cha B1 kilifanya kazi yake kwa umakini mkubwa sana. Kabla ya kugundua kwamba kuna mwenzetu anatusaliti. Tulijaribu kumchunguza mwenzetu, tukagundua kwamba alikuwa anapewa maagizo na mtu anayeitwa Elia Kilasi, kwa shinikizo, kwakuwa familia yake ilikuwa imetekwa.
Tuliichunguza namba ya Elia Kilasi. Tukagundua ana mawasiliano na mzee Msangi!"
"Unasemaje wewe! IGP huu ndio upuuzi ulioniitia hapa!" Rais Mgaya alifoka. Ilikuwa kama anasubiri sehemu atakayotajwa mzee Msangi.
"Mheshimiwa rais huu sio upumbavu. Ni kitu cha ukweli na tuna ushahidi nacho!" Daniel alisema kwa hasira.
"IGP John Rondo ondoa hawa vikaragosi hapa. Hawa ni wanafiki, wanataka kuizika kazi aliyoifanya mzee Msangi kwa skendo za kutengeneza!" Rais Mgaya alifoka.
"Mhesh..." Daniel hakumalizia kuita.
"Na kuwnzia sasa kikosi cha B1 kivunjwe. Watafutwe watu wengine wa kuifatilia kesi hii!"
"Mhesh.." Daniel Mwaseba hakumaliza alichotaka kuongea.
"Naomba uwasikilize mheshimiwa rais" IGP John Rondo aliingilia.
Rais Mgaya alikaa kimya.
"Tunaomba umuite mzee Msangi hapa kama hautuamini! Asimame hapa mbele yetu kama atabisha.." Daniel alisema.
Rais Mgaya alikubali kwa kichwa.
"Ndio hiko tu ndicho kilichowaleta hapa?" Rais Mgaya aliuliza.
Daniel alianza kuelezea juu ya uhusika wa Imma Ogbo na rais Abayo katika sakata hili.
Hapo rais Mgaya ndo hakukubali kabisa.
"Kuhusu mzee Msangi mmesema nimpigie simu aje hapa. Je kuhusu Rais Abayo mna ombi gani?" Rais Mgaya aliuliza.
"Tupe kibali cha kuingia ubalozi wa Nigeria hapa nchini. Tuna uhakika tutapata kitu juu alipo Dr Luis" Daniel aliomba.
Rais Mgaya ameonesha kutoyakubali maelezo ya kina Daniek Mwaseba..
Je sasa atayakubali maombi yao?
ITAENDELEA
"Kuhusu mzee Msangi mmesema nimpigie simu aje hapa. Je kuhusu Rais Abayo mna ombi gani?" Rais Mgaya aliuliza.
"Tupe kibali cha kuingia ubalozi wa Nigeria hapa nchini. Tuna uhakika tutapata kitu juu alipo Dr Luis" Daniel aliomba.
Na hii ni Sehemu ya Thelathini na nne
Baada ya Daniel kusema hivyo. Rais Mgaya alichukua simu yake na kumpigia mzee Msangi.
"Hallo mzee Msangi" Rais Mgaya aliita simuni.
"Mheshimiwa rais, habari za sahivi"
"Nzuri mzee Msangi. Samahani nilikuwa nakuhitaji hapa Ikulu sasahivi. Nataka tuje kuongea kuhusu yale masuala yetu, maana siku ya kesho itakuwa ndefu sana kwangu" Rais Mgaya alidanganya.
"Sawa mheshimiwa rais. Nitakuwa hapo ndani ya nusu saa" Mzee Msangi alisema na simu ikakatwa.
"Kuhusu suala la kwenda kuuchunguza ubalozi wa Nigeria nimewakubalia. Nitaongea na balozi wao usiku huu. Kesho asubuhi mtaenda pale na watakuwa na taarifa zenu" Rais Mgaya alisema. Pamoja na yote yeye mwenyewe alikuwa anamuhitaji sana Dr Luis. Ili siri yake iendelee kuwa siri.
"Sawa, tunashukuru sana kwa ushirikiano wako" Daniel aliitikia kivivu.
"Lakini mnaamini hiyo inaweza kusaidia kuwapata wanafunzi waliopotea na viongozi wetu?" IGP John Rondo aliuliza.
"Hii ndio njia sahihi mkuu. Imma Ogbo mtu ambaye amewateka hao watu anapewa nguvu na rais wao. Ingawa mheshimiwa rais hapa hataki kukubali. Bila shaka rais Abayo anamtumis balozi wao. Nina imani tukienda pale ubalozi wao tutagundua kitu tu." Adrian alisema.
Rais Mgaya alikaa kimya. Hasira dhahiri ziliomekana usoni mwake.
Baada ya dakika thelathini na mbili aliingia mhudumu wa Ikulu. Na kumtaarifu rais Mgaya kwamba mzee Msangi amefika.
Moja kwa moja akaambiwa aingie ndani ya ukumbi wa mikutano.
Mzee Msangi, hakuamini macho yake alichokiona baada ya kuingia mle ndani.
"Mambo yameharibika" mzee Msangi alisema kifuani.
Mbele yake alikuwa anatazamana na watu ambao hakutaka kuwa nao meza moja hata siku moja.
"Mbona umestuka sana mzee Msangi?" IGP John Rondo aliuliza.
Mzee Msangi alikaa kimya.
"Karibu kitini mzee wangu" Daniel alisema. Aliiona ile ni nafasi pekee kumuonesha rais juu ya uhusika wa mzee Msangi.
Mzee Msangi alienda kukaa kwenye kiti huku uwoga dhahiri ukionekana katika macho yake na tembea yake pia ilijaa kitetemeshi.
"Mzee Msangi nimekuita hapa. Kuna vitu hawa vijana wanataka kukuuliza" Rais Mgaya alisema kwa upole.
"Mimi ninaitwa Daniel Mwaseba, na mwenzangu huyu anaitwa Adrian Kaanan. Tuna maswali machache ambayo tunaomba utujibu mbele ya mheshimiwa rais" Daniel alisema.
Mzee Msangi bado alikaa kimya.
"Kimya chako hakitakusaidia mzee, nakushauri ni bora ukaongea tu" Daniel alisema.
"Mnataka kujua nini kutoka kwangu" Mzee Msangi alisema kwa sauti ya kukwaruza.
"Naomba unisikilize. Nadhani bila shaka unafahamu upotevu wa Dr Luis. Sisi ndio tuliopewa jukumu la kuchunguza juu ya utekaji nyara huo. Lakini wakati tupo katika kazi yetu kuna mwenzetu familia yake ilitekwa, na hilo lilifanywa ili atusaliti sisi. Tulizitambua mapema hila hizo. Tukaichukua namba ya huyo mtu aliyekuwa anamtumia meseji mwenzetu na kuichunguza. Tukagundua kwamba huyo mtu anaitwa Elia Kilasi. Na tulivyoendelea kuichunguza namba hiyo tukagundua kwamba ana mawasiliano na wewe.
Swali ni, je unamjua mtu anayeitwa Elia Kilasi?" Daniel aliuliza.
Usoni mwa Mzee Msangi uwoga ulimshamiri. Alijua Daniel alikuwa anaelekea wapi pindi tu alipoanza habari yake. Mzee Msangi alimwangalia rais Mgaya, rais Mgaya akamfanyia jicho kwa chini.
Walijidanganya sana, jicho makini la Daniel Mwaseba liliona yote hayo.
"Mimi sielewi hizo hekaya za Abunuwas mnazonisimulia. Na wala simtambui huyo mtu anayeitwa Elia Kilasi" Mzee Msangi alisema. Mfinyo wa jicho wa rais Mgaya ulimpa nguvu. Aliona kuwa mheshimiwa rais yupo nyuma yake.
"Mheshimiwa rais, huyu mzee anajua kila kitu. Tunaomba utuachie tuondoke naye. Nakuhakikishia atafunguka kila kitu anachokijuw akiwa mikononi mwetu!" Adrian alisema kwa jazba.
Ukimya ukapita wakati rais Mgaya akiwaza lipi ni jibu sahihi. Alijua kuwaachia mzee Msangi ni kuanika uhusika wake wa kutekwa kwa Dr Luis mbele ya kina Daniel Mwaseba.
"Mimi ninaomba mkalishughulikie kwanza hilo suala la ubalozini. Mtakuja kumalizana na Mzee Msangi baada ya kufanikisha kumpata Dr Luis" Rais Mgaya alisema.
"Hilo haliwezekani Mheshimiwa rais. Familia ya mwenzetu imetekwa. Na mhusika yupo hapa. Hatuwezi kusubiri, lazima atupe majibu leo!" Daniel akasema kwa hasira.
IGP John Rondo alistushwa na kauli ya Daniel, alijua ni nini kinafuata.
"Kauli ya rais ni ya mwisho!" Rais Mgaya alisema taratibu.
"Sasa kwanini umemwita huyu mzee hapa kama ulikuwa unajua kauli ya yako ni ya mwisho?" Daniel aliuliza kwa hasira.
"Daniel! Kumbuka unaongea na rais!" IGP John Rondo aliiingilia kati. Aliona mambo yanatibuka.
"Hii haikubaliki mkuu. Hili jambo lazima lifike mwisho. Lazima tuhakikishe tunampata Dr Luis, lazima tuhakikishe familia ya David inapatikana, na mwisho kabisa kuwafikisha katika vyombo husika waharifu wote wa suala hili!" Daniel alisema.
"IGP John Rondo, naomba watoe hawa watu wako nje!" Rais Mgaya alisema kwa hasira.
"Unafanya kosa rais. Kosa ambalo utakuja kulijutia hapo baadaye!" Adrian alisema.
"Na sitaki mjihusishe kwa lolote kuhusu kupotea kwa Dr Luis, wala kwenda ubalozini, nitaongea na Rais Abayo na mambo haya yataisha" Rais Mgaya alisema.
Wote walibaki mdomo wazi.
"Kuna siri rais Mgaya anaficha" Daniel alisemea kifuani. "Ni siri gani hiyo?" Kabla Daniel hajapata jibu, alisikia sauti ya rais ikiita.
"Walinziii"
katika milango miwili wakatokea walinzi. Idadi yao ilikuwa yapata kumi.
Watano kutoka katika kila mlango. Walibeba wakina Daniel mkuumkuu, na kwenda kuwatupia nje ya geti la ikulu.
Hiyo ni baada ya kauli moja tu ya rais Mgaya.
Wakina Daniel wanafukuzwa ikulu na kuitwa wahuni!!
Katika milango miwili wakatokea walinzi. Idadi yao ilikuwa yapata kumi.
Watano kutoka katika kila mlango. Walibeba wakina Daniel mkuumkuu, na kwenda kuwatupia nje ya geti la ikulu.
Hiyo ni baada ya kauli moja tu ya rais Mgaya.
Wakina Daniel wanafukuzwa ikulu na kuitwa wahuni!!
Hii ni sehemu ya Thelathini na Tano
Daniel na Adrian walirejea maskani kwao. Njiani walikuwa kimya. Kila mmoja akitafakati kilichotokea ikulu.
"Kuna siri nzito rais anayo" Daniel aliwaza.
Walifika maskani kwao baada ya dakika hamsini na tano. Waliwakuta watu wote sebuleni wakiwasubiri wao.
Adrian alichukua usukani wa kuwaekeza wenzao kila kitu kilichotokea huko Ikulu. Daniel hakuweza hata kuzungumza, alikuwa amekabwa na donge la hasira.
Hii haikuwa habari njema hata kidogo kwa wote mle ndani.
Rais Mgaya alikuwa amewasaliti..
"Poleni sana ndugu zetu. Kwa mujibu wa maelezo yenu inaonesha kuwq rais Mgaya kuna kitu anaficha. Ingawa tumetolewa kufatilia kesi hii lakini hatupaswi kuacha hadi tujue ni kitu gani mheshimiwa rais anaficha?" Hannan alisema.
"Hannan, tunaweza kuendelea na kesi hii wenyewe. lakini itakuwa ngumu sana kwetu. Hatuna wa kushirikiana naye, kwa ujumla serikali imetutenga na suala hili. Kama tunaendelea na uchunguzi wetu basi kumbukeni tuna kazi kubwa sana ya kufanya. Je mko tayari tupambane wenyewe?" Daniel aliongea kwa mara ya kwanza tangu aingie mle ndani.
"Mimi nipo ndani. Liwe jua iwe mvua. Nitakuwa pamoja na wewe Daniel.." Martin aliwashangaza mle ndani. Alikuwa wa kwanza kukubali kuungana na Daniel Mwaseba.
"Nami nipo ndani ya misheni hii. Nitakuwa nawe bega kwa bega Daniel" Hannan akadakia.
"Nami pia nipo ndani! Nina uchungu na familia yangu. Nitakuunga mkono siku zote Daniel" David aliitikia.
"Sina haja ya kuongea sana. Sisi ni B1 na B1 haiwezi kufa kamwe. Wametuunganisha lakini hawawezi kututenganisha" Adrian naye alisema.
"Safi sana jamaa zangu. Mmenipa nguvu sana. Nimefuraahi sana kuona mnakuwa upande wangu. Taifa linatuhitaji sana, hatuwezi kukatishwa tamaa kwa maneno ya rais Mgaya. Maneno yake yatupe hali ya kupambana zaidi na zaidi!" Daniel alisema.
Daniel akaweka mkono, Hannan akaupandisha juu yake, akafuatia David, Adrian akafatia, kisha juu akamalizia Martin Hisia.
"Kazi nd'o inaanza!" Wakasema kwa pamoja.
Hiyo ilikuwa saa sita usiku.
***
Kulikucha. Siku nyingine tena ikachomoza jijini Dar es salaam.
Siku hii mpya ilikuja na habari iliyowastua sana watanzania. Ikikuwa kama alivyoahidi Imma Ogbo kwa Daniel Mwaseba jana yake.
Mwili wa waziri wa mipango na fedha, Elisha Salu, uliokotwa katikati ya uwanja wa Taifa kule Chang'ombe.
Kilichostua zaidi ni ujumbe uliokutwa pembeni ya maiti hiyo.
"Mtaokota maiti nyingine baada ya nusu saa!!"
Taarifa ya kifo cha waziri wa mipango na fedha ilimkuta rais Mgaya akiwa anasoma magazeti asubuhi.
Ilikuwa ni ada yake kusoma magazeti yote ya siku kila siku asubuhi.
Rais Mgaya aliipokea taarifa hiyo kwa mstuko mkubwa sana!!.
Moja kwa moja akampigia simu kamanda wa polisi wa mkoa wa Dar es salaam, kamanda Karim Gogo, akimtaka yeye na askari wake waashughulikie suala hilo kwa uwezo wao wote. Huku akimsisitiza pia juu ya kuwasaka na kuwaokoa watoto wengine sitini na mbili wa shule ya msingi St Joseph. Kamanda wa Polisi wa mkoa alikubali kwa utii agizo hilo. Bila kujua undani wa tukio hilo. Naye akaagiza askari wake waingie kazini, kuwasaka wahalifu hao.
Taarifa hiyo ya kifo cha waziri wa mipango na fedha iliwakuta wakina Daniel Mwaseba sebuleni, maskani kwao. Walikuwa wametulia wakipanga makakati yao. Taarifa hiyo iliongeza hofu juu ya usalama wa familia ya David, maana wao waliamini familia ya David ipo mikononi mwa watu hao. Mikononi mwa Imma Ogbo!
"Hawa jamaa sasa wameanza kuua watu. Hatujui ni nani atafuata baada ya mheshimiwa Elisha, pengine akawa Chifu au wale watoto wadogo wasio na hatia" Daniel aliwaambia wenzake.
"Mwanzoni hisia zetu wote zilituambia hawa watu wapo katika ubalozi wa Nigeria hapa nchini, lakini tatizo tumeshindwa kuthibitisha hisia zetu kwakuwa tumekosa kibali cha kuingia ubalozini kutoka kwa mheshimiwa rais Mgaya. Rais Mgaya amegoma kabisa sisi kuuchunguza ubalozi huo. Na ni ngumu sana kuvamia pale, maana hivi sasa balozi zote zina ulinzi mkali sana kutokana na lile tishio la kulipuliwa kwa ubalozi wa Uganda.
Lakini mimi nilikuwa nina wazo moja.." Adrian alisema.
"Una wazo gani Adrian?" Hannan aliuliza.
"Mnaonaje tukamteka balozi wa Nigeria!" Adrian alisema.
Ukumbi mzima ulikaa kimya.
Baada ya kama sekunde ishirini Hannan aliipata sauti yake.
"Hatuwezi kuzusha mgogoro wa kidiplomasia kweli?"
"Hapana Hannan, hatuwezi kuzusha mgogoro wa kidiplomasia, bali tutakuwa tunaelekea kuufikisha mwisho mgogoro huu.
Sisi sote hapa tunakubali kwamba serikali ya Nigeria inahusika kwa asilimia zote kwa haya mambo yanayotokea hapa nchini. Sasa kuna namna nyingine zaidi ya kumteka mwakilishi wa serikali hiyo? Aje hapa ili tumfungue, aseme kila kitu anachokijua kuhusu sakata hili. Na kama tukiona hahusiki kwa lolote, basi tunamwachia" Adrian alisema kwa kirefu.
"Umeongea vizuri sana Adrian. Mimi naunga mkono kila neno lako. Lakini tatizo lipo ni kwa jinsi gani tunampata huyo balozi. Kwasasa bila shaka si balozi tu zinazolindwa, hata mabalozi wenyewe wanalindwa pia. Watakuwa wapuuzi kiasi gani eti walinde jengo na kumuacha mtu?" David alisema.
"Sikia niwaambie. Sisi hapa, tukiamua inawezekana kumteka Balozi wa Nigeria. Sisi hapa, tukiamua pia tunaweza kuingia hata katika ubalozi wa Nigeria tena saa saba mchana, hata kama kuna ulinzi kiasi gani" Daniel alisema kwa uhakika.
Watu wote walimwangalia Daniel Mwaseba pale sebuleni.
Je nini kitatokea? Daniel Mwaseba kachanganyikiwa ama?
"Sikia niwaambie. Sisi hapa, tukiamua inawezekana kumteka Balozi wa Nigeria. Sisi hapa, tukiamua pia tunaweza kuingia hata katika ubalozi wa Nigeria tena saa saba mchana, hata kama kuna ulinzi kiasi gani" Daniel alisema kwa uhakika.
Watu wote walimwangalia Daniel Mwaseba pale sebuleni.
ENDELEA..
"Sio rahisi kihivyo Daniel" Martin alisema.
"Nakwambia hivi Martin, inawezekana.
Nyinyi hamjui tu nguvu yetu watu tuliokaa humu ndani. Mimi ninawaambia tunaweza kufanya chochote kile tutakacho. Muda wowote na kwa namna yoyote ile.
Mimi, Adrian, Martin, Hannan, nyuma yetu kuna Mwanasheria mlevi. Mimi ninawaambia hata tukitaka kuipindua dunia tunaweza!" Daniel alisema. Watu wote mle ndani walikuwa wanamwangalia yeye.
"Sasa ninasema hivi, tunaenda kumchukua balozi wa Nigeria sasahivi. Awe nyumbani kwake, awe ofisini kwake. Tunaenda kumchukua balozi wa Nigeria na kumleta hapa. Hannan utabaki hapa kutupa back up pale tutakapohitaji. Mimi, David, Adrian na Martin Hisia tunaingia kazini asubuhi hii. Na haturudi hapa mpaka tuwe na balozi wa Nigeria mkononi.
Tumeelewana?"
Daniel alisema na mwisho kuuliza.
"Tumeelewana Daniel.." Wote waliitikia kasoro Hannan.
Daniel alimwangalia Hannan, akamwita.
"Hannan!!"
Hannan akanyanyua sura yake iliyokuwa inatazama 'laptop'. Aliacha kubofya 'laptop' yake na kumwangalia Daniel Mwaseba huku akiongea..
"Agdir Okema. Ni raia wa nchi ya Nigeria kwa kuzaliwa. Agdir amezaliwa katika mji wa Abuja. Elimu yake alisomea hapohapo Abuja kabla ya kwenda Marekani kusomea shahada yake ya rasilimli watu, ambapo baba yake pia alihamia huko kikazi.
Agdir ana watoto wa kike wawili, mmoja akiwa na miaka mitano na mwengine akiwa na miaka Tisa. Catherine na Eva.
Agdir alimuoa mwanamke mwenye asili ya Ghana, kwa jina anaitwa Sophia.
Agdir alichaguliwa kuwa balozi wa Congo, ambapo alihudumu kwa miaka miwili tu. Kabla ya kuhamishiwa Tanzania." Hannan alisema bila kuangalia kwenye laptop yake.
"Umefanya kazi nzuri sana Hannan, tena kwa muda mfupi" David alisema kwa furaha.
"This girl is amazing!" Martin alisema kifuani "Ndani ya sekunde chache ameyapata yote hayo tena ameyahifadhi kichwani!"
"Safi sana Hannan. Umefanya kitu muhimu sana. Hayo maelekezo yako mazuri yamenipa kitu kingine cha kufanya.." Daniel alisema.
"Kitu gani hiko umepata Daniel?" Martin aliuliza.
"Kwasasa ninaona tuiteke familia ya Balozi Agdir na kuileta hapa. Tutaitumia familia hiyo kumfanya balozi Agdir afate matakwa yetu. Hii itakuwa ni njia nyepesi zaidi kwetu." Daniel alisema.
"Upo sahihi Daniel. Hiyo ni njia rahisi zaidi, na hatutatumia nguvu nyingi kama tukitaka kumteka balozi mwenyewe" Martin alikubali.
"Watoto wa balozi Agdir wanasoma katika shule ya St Anna iliyopo Upanga. Kwa majina ni Catherine na Eva. wanaingia shuleni saa mbili asubuhi, na kutoka saa nane mchana" Hannan alisema huku akiingalia 'laptop' yake safari hii.
"Safi sana Hannan. Tunaenda kuwachukua hao watoto shuleni kwao sasahivi.
Hiyo saa nane atakayeenda kuwachukua akute patupu" Daniel alisema.
Wote walikubaliana.
Je wafanikiwa mpango wao?
Naaaaam, Huu ni mwisho wa Season one, tukijiandaa kuisubiri Bomu Season Two (Sehemu ya Pili) basi leo jioni tutamsoma Daniel Mwaseba katika Riwaya nyingine. Cha kufanya mi wewe kuwaalika marafiki wapende ukurasa huu na kushare uwafikie wengi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment