Search This Blog

Friday, 30 December 2022

KIAPO CHA MFUNGWA (6) - 3

    

Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (6) 


Sehemu Ya Tatu (3)


Kule katika chumba cha mikutano ,Isack akashika ile rimonti na kuelekeza kilipo chumba kile



Chumba no 5



Macho ya watu wote yakanata katika runinga wakitegemea kushughudia moto



Bomu lilikuwa eneo la kificho ambapo kati yao ( Katarina na Zidu) hakuna ambaye angeweza kuliona!.....



Isack akaanza kuhesabu tano....nne.....tatu...mbili.....moj



komandoo Zidu (kz) na Katarina hatarini tena



Nini kitawakomboa katika mikono ya Isack kijana hatari na kiongozi wa makomandoo wa mafia (MWM)



Katarina akamkimbilia mumewe na kuanza kumfungua katika kitanda kile



*******************



Rais Wa mapinduki Kinte mh Laizer Nyoshi akiwa mafichoni bado moyo wake ulienda mbio alijua kabakia yeye tu na kwa kipindi iko alijua mwanaume Wa Kazi Gambi ndo yupo katika harakat za kumsaka



Bado msako mkali uliendelea pasina kuzaa matunda,akashika simu yake kumpigia Zidu kujua kafika wapi kwani mara ya mwisho kuongea naye alimwambia yupo ndani ya ndege na masaa kadhaa ndege ingepaa kwa muda ule alitakiwa awe ameshafika Tanzania



Ila alishangaa akimpigia apatikani akaona isiwe tabu ampigie mwenyeji wake pale pale akatafuta namba ya Isack na kumpigia ikaita na kupolelewa



"Unasema?!....."



Akauliza kwa ukali pasina kuamin



"Katekwa?!....my God,sawa embu ntumie hizo namba walizokupigia nazo"



Rais aliongea akionekana wazi kuchanganyikiwa baada ya dakika chache mlio Wa msg ukaingia haraka sana akapiga zile namba huku mdomo akitetemeka kwa hasira ilochanganyikana na woga simu ikaita ghafla ikapokelewa kwa sauti nene nzito alijua huyo ndo Mr x mmiliki Wa kundi la Mafia na aliyekuwa akisakwa pasina kutambulika sura yake halisi



********************



Kule katika chumba cha mikutano ,Isack akashika ile rimonti na kuelekeza kilipo chumba kile



Macho ya watu wote yakanata katika runinga wakitegemea kushughudia moto...



Ila kabla Zidu ajabonyeza rimonti simu yake ikaita kuangalia ni mh rais wa Kinte akatabasamu na kupokea akiongea kwa majonzi



"Mh Rais Zidu ajafika Tanzania nimeenda uwanja wa ndege ila akwepo nimesikia kashukia njiani ila mkuu kingine nimepigiwa simu na watu nisiyo wafahamu wamesema wamemteka Zidu na mkewe kajitambulisha kama mr x I think ni mmiliki Wa kundi la mafia...."



"Unasema?!"



Upande Wa pili ukauliza kwa ukali



"Ndo ivyo mh Zidu katekwa na kundi la mafia"



"Katekwa?!,sawa embu nitumie hizo namba walizo kupigia nazo"



Palepale Isack akakata simu ile aliachia cheko Kali kama aloyafanya ni mazuri



Kisha akamtumia namba nyingine kwa laini yake ile ilotambulika kama ndo ya Isack aikupita hata dakika moja simu ilokuwa na iyo laini alomtumia mh Rais ikaita



Akaachia tabasamu jingine hafifu , akanyoosha mkono wake kuipokea kutoka kwa mmoja Wa vijana wake akisitisha zoezi lile la kulipua kwa muda akaangalia mpigaji akaachia tabasamu



"Niambie mh rais"



Akasema Isack kwa sauti nzito tofauti na ile alo ongelea awali watu wote walikuwa makini kumsikiliza.....



"Afadhali nimekupata hewani mkuu kwa habari niliyoipata kutoka kwa Isack Zidu ilikuwa aingie Tanzania Leo ila mmemteka yeye na mkewe Katarina,ila chonde chonde naomba msimwangamize,kuna kazi naitaji aje anisaidie na baada ya hapo ruksa kumfanya mtakavyo"



Rais Laizar aliongea kwa unyonge kwani akujua huyo alokuwa akiongea naye ndiyo Isack aliyeongea naye dakika chache kumuulizia kama Zidu amefika



Isack kwa masikitiko alimwambia ajafika ila amepokea simu kutoka kwa kiongoz Wa mafia Mr x akimwambia Zidu yupo mikononi mwake ivyo tusiangaike kumtafuta,na hapo alijua ndo anaongea na huyo Mr x kumbe ni mtu yuleyule



"Hiyo kazi uwezi kutupa sisi mpaka mumpe yeye?!...



Isack au Mr x kama Rais alivyomjua akauliza kwa sauti yake ile ile nzito



" hapana muheshimiwa ila niwahidi tu malipo yake ya kazi hiyo nitawapa nyinyi na baada ya kuifanya kazi hiyo ndiyo mumuue..."



"Sawa bwana Laizar kwa kuwa wewe ndiyo uliye waacha vijana wangu huru pindi huyo Zidu alipowaweka ndani nami ni muda wangu wa kukusaidia kwa hili tutamuachia ila naitaji akaunti yetu kwa sasa isome biliini 5 .5 "



"Sawa sawa mkuu hakuna shaka juu ya hilo jua maisha yangu yapo hatarini"



"Sawa usijali!,ilikuwa ni mmalize sasa nimeairisha ila NAAPA NITAMUUA KWA MKONO WANGU ZIDU kanitenda vibaya sana huyu mtu na nshaweka *agano la kiapo cha damu* kumwangamiza kwa alivyontesa kwanza amewaua vijana wangu wengi sana sitomwacha hai abadani"



"Sawa muheshimiwa"



Simu ikakatwa



"Hakuna haja tena ya kumuua kuna kazi wanaitajika wakafanye nchini kwao ila akiimaliza bado hatakuwa katika mkono wangu,black sqopion nifate"



Akamalizia Isack mkuu wa mafia akinyanyuka mchana kijana mmoja akimfata kwa nyuma



*********************



Katarina alimaliza kumfungua Zidu kamba



"Tumefikaje humu mpz wangu?!"



Zidu aliuliza kiboya,Katarina akamwangalia kwa sek kadhaa na kulishusha tabasamu



"Tutoke kwanza huku tutajua kila kitu!"



Katarina akaongea wakafungua mlango na kutoka nje



"Ina maana ndo wapo wa nne tu?!"



Katarina alijiuliza



"Kina nani hao?!"



Zidu akamjibu kwa kuuliza



"Tupo zaidi ya wa nne"



Ghafla wakasikia sauti nyuma yao kugeuka macho kwa macho na Black sqopion

Gaidi hatari, komandoo lililotafutwa na dunia kwa muda mrefu



Bila kusemezana Zidu na mkewe walikaa kimapigano,waka angaliana kwa ishara na wote wawili wakajirusha kumvaa black sqopion yule



Ni wazi awakumtambua vizuri jamaa Yule



Kwani ghafla black s aliinama Katarina na mwenzake wakapita na kutua chini!,wakaachia mayowe



"Sipo kama mfikiriavyo"



Black aliongea kwa kujiamini



"Lazima tukuue wewe"



Zidu akajibu akijinyanyua na kujipanga upya



"Ziduuuuuuuuuuuu"



Katarina akaita kwa uoga akifumba macho yake kutotazama kile kinachoenda kumtokea mume wake yule



Hatari sana!!!!!!!.....



Sipo kama mfikiriavyo"



Black aliongea kwa kujiamini



"Lazima tukuue wewe"



Zidu akajibu akijinyanyua na kujipanga upya



"Ziduuuuuuuuuuuu"



Katarina akaita kwa uoga akifumba macho yake kutotazama kile kinachoenda kumtokea mume wake yule



Zidu kugeuka nyuma akakumbana na mkono mzito ulokikamata kichwa chake ukakikunja

Zidu alipo achiwa akaporomoka chini!...



Katarina alichanganyikiwa,aliujua mkunjo ule wa kuvunja mfupa wa shingo ndiyo makomandoo wengi waliyo utumia kuua.



Akiwa na uchungu mkubwa akamkimbilia mumewe na kuanza kumwita kwa nguvu huku akimtingisha!



"Zidu!,Zidu! Mume wangu Zidu..."



Akamwangalia yule aliyesababisha lile kwa hasira!,



Akamnyanyukia ila kabla ajamvaa kitu kizito kikatua kichwani mwake!,



Nguvu zika anza kumwisha,aka anza kuona maruwe ruwe watu wawili wawili!



Ghafla nuru ikatoweka na kuanza kumuona mtu kavaa nguo nyeupe akimwita kwa tabasamu ni kama alikuwa akimkaribisha katika ulimwengu ule mpya!



Alipo mkazia macho kumwangalia zaidi alikuwa ni Zidu

Katarina akatabasamu!



Hakuwa na shaka kuwa wameshakufa!...



*



Baada ya Isack kumpiga na chuma cha kichwa Katarina aliye kuwa na malengo ya kumvamia Black sqopion aliye fanikiwa kumdhibiti Zidu,



Wakati wote Black sqopion alipokuwa akipambana na Zidu Isack alikuwa kajificha kwa pembeni,akichungulia,



Alishughudia mpaka kuzimishwa kwa Zidu wakati Katarina akimfata Black naye akajitoa akiwa kashika chuma alichomtandika nacho Karatina kichwani kwa malengo flani



Si ya kumuua hapana ni kumzimisha tu,



Isack akawaita vijana wake kadhaa na kuwapa ishara wakaitupe ile miili!



Zoezi hilo likafanyika Mara moja!



Ilikuwa lazima wafanye ivyo kuwaondoa eneo lile kwa mantiki kwamba wale wasingeondoka wangetaka kuchunguza zaidi....



***



Kilikuwa ni kikao kingine tena kilichojumuisha wana usalama wa taifa la Kinte wakiwemo polisi na wanajeshi!



Msemaji mkuu wa mkutano ule alikuwa ni rais wa mapinduzi GANYAKITE muheshimiwa Laizar Nyoshi



"Kazi hii kwa muda mrefu sasa si chini ya miezi miwili sasa toka mfungwa Gambi hatoroke gerezani na kusababisha mauaji ya viongozi mbalimbali wa taifa hili!



Tumemtafuta kila namna bila mafanikio na sasa nimeiona niongeze nguvu komandoo wa taifa letu Zidu na mkewe KATARINA walosafiri siku chache nyuma walipata matatizo kidogo ila kwa sasa siku yoyote anaweza kuingia nchini mtajulishwa wao ndio watakayemtia mkononi huyu mfungwa...



Makofi yakatanda kila mtu alionesha kufurahia kwa jambo lile!,wengi waliukubali uwezo wake!,rais akaendelea



"kwa sasa kazi bado ipo kwa insp Jonathan mpaka pale Zidu ntakapomkabidhi rasmi kazi hii"



Ghafla simu yake ikaita alipoangalia ni simu kutoka kwa Mr x kama alivyomjua yeye akaomba samahani na kunyanyuka kwenda "private" kuongea na simu ile!



"Aloooh Nyoshi!,njoo uchukue mizoga ya watu wako tumewatupa katika kisiwa cha Belgium"



Simu ile ikakata!,mwili wa rais Laizar ukaloa jasho!...



***



Miongoni mwa wanajeshi waliyokuwepo katika mkutano ule wa rais ni Odovy



Ujio ule wa Zidu kwake aukumfuraisha,aliujua moto wa jamaa yule na kwa vyovyote ilikuwa lazima aonane na wenzake Fatma,Olomy na Gambi kusudi wajue watafanyaje!



Alijua muda wowote Zidu angeingia na katu hakujua kuwa kuna habari nyingine za komandoo yule na mke wake! Juu ya khali zao



****



Walikuwa ni jumla ya watu wa nne (4)



Wote walikuwa kimya wakiwa katika tafakari kuu!,



Walihisi mambo yao sasa yanaenda kuwa magumu!



"Sasa tufanyeje?!"



Mmoja wapo kati ya wale watu akaoji!



Hakuna aliyefumbua mdomo wake kati ya wale watu kujibu!



"Tusipo angalia tutakwisha!"



Mtu yule aliye uliza awali hatimaye akamalizia!



"Kwa nini tusiachane na kazi hii Gambi?!"



Mwingine alidakia baada ya kimya cha muda mrefu huyu alikuwa ni Olomy aliye wahi kuwa dereva wa insp Kurwa



"Tumeianza kazi lazima tuimalize kazi kwani Zidu ndo nani?!"



Gambi alijibu kwa hasira muda wote alikuwa kimya akifikiria mbinu za kumvaa rais, habari za kwamba Zidu anakuja sijui azikumtisha kabisa!



"Siyo ivyo Gambi kumbuka yule ni komandoo na si mwanajeshi wa kawaida kama sisi..."



"Oterval! Ila lazima nimuue Nyoshi kwa njia yoyote ile kama nyinyi mmeingia upepo ni juu yenu ila Mimi sitorudi nyuma aletwe sijui Gambi hata ezrael bado sitorudi nyuma afe yeye nife Mimi!"



Gambi alizidi kuongea kwa kujiamini akaendelea...



"Sitokuwa na furaha pasina kumuua huyo mtu Laizar, kazi yote tuloifanya itakuwa kazi bure sitorudi nyuma nasema,labda aniue Mimi kama alivyowaua wazazi wangu ila tofauti na ivyo mapapaa amjanishauri kitu!"



Ghafla machozi yakaanza kumtiririka,mchomo mkali wa maumivu ukiuchoma moyo wake

Mwanajeshi alilia!!!...



Mbona hatari!



"Wewe ni mwanajeshi Gambi,na kwa kazi uloifanya nimekuvusha daraja u komandoo gambi,ila komandoo alihii wewe ni mtoto wa kiume jikaze tufikirie kipi cha kufanya ila Mimi Nina wazo!"



Muda wote alikuwa kimya binti yule sasa alivunja ukimya na wote wakamtazama kusikia wazo lake,ni binti mwenye akili sana kufikiria kipi afanye



Je Fatma anawazo gani na litasaidia ilo wazo lake?!







Muda wote alikuwa kimya binti yule sasa alivunja ukimya na wote wakamtazama kusikia wazo lake,ni binti mwenye akili sana kufikiria kipi afanye

Fatma akaendelea....



"Nishasoma stori nyingi sana za mtunzi ZUBERI MARUMA"



"Haaaaa zile za kufikirika?!"



Odovy akaongea kwa kejeli na kupelekea wote kucheka,



Fatma akakunja sura kutopendezwa na dharau zile!



"Odovy usikilize ni nini naongea si unaropoka"



Fatma akaja juu Odovy akawa kimya!



"Ok! Endelea mamaa!"



Gambi akampooza na hatimaye Fatma akaendelea...



"Huwa anamzungumzia sana katika kila Hadithi yake mganga mmoja nani vile?!"



"Ndumbwendumbwele"



Wote wakaitika kuonesha kwamba ni wapenzi wa kijana huyo!

aliyejipatia umaharufu kwa riwaya zake zile ,Fatma akaendelea...



"Wazo langu tukamuone mganga yule ndumbwendumbwele atupe dawa tusionekane au tukipigwa bastola idunde hiyo itaraisisha kazi kuwa raisi!"



Wote wa nne wakatazamana!



Mshangao ukiwavaa waziwazi



"Naona sasa Fatma unaleta utani!,habari za riwaya tena riwaya zenyewe za kufikirika kuziingiza katika uhalisia wapi na wapi?!"



Gambi akaongea kwa hasira,huku Odovy na Olomy wakatingisha kichwa kuafiki!



"Kivipi mpz!?" Kwa unyonge Fatma akahoji Gambi akajibu



"Unavyosema tukamuone ndumbwendumbwele yule si yupo tu katika riwaya kwani yupo katika ulimwengu huu?!"


ITAENDELEA

    

Simulizi : Kiapo Cha Mfungwa (6) 

Sehemu Ya Nne (4)



Fatma akayatoa macho ya mshangao,kisha kwa kujiamini akajibu...



"Ndumbwendumbwele yupo jamani katika ulimwengu huu na yupo Kinte hii hii ndani ndani ya kijiji cha Binyalia sijui katikati ya msitu gani uko!"



Wote wakayatoa macho kwa mshangao pasina kuamini kile wakisikiacho,



"Una uhakika?!"


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog