Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4)
Sehemu Ya Kwanza (1)
IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
********************************************************************************
Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Baada ya kukumbatiana, wakaachiana,wote watatu wakaingia ndani ya gari moja mali ya Richard Mombi au Isack kwa asilia ya jina lake,wakaelekea katika jumba lile la mfanya biashara yule Isack!...
Isack Alitafuta Mwanasheria Wa Kimataifa,kumsimamia,akatafuta Waandishi Wakajibandua Sura Zao Zile Za Bandia Na Kuelezea Taifa Historia Nzima Ya Maisha Yao!,
Zidu Alijieleza Jinsi Alivyo Kuwa Akitumiwa Kiuhalifu Na Mheshimiwa Alex,jinsi Alivyoingia Katika Zambi Ya Kumtesa Mtoto Isack Na Mara Zote Alimkosa!,mwisho Akatupwa Rumande!
Ni Mkasa Uliowasisimua Watanzania Wengi!,akiwemo Mtunzi Mahiri Zuberi Maruma Aloamua kuuandikia kitabu,ambacho hata ivyo kilinunuliwa na wengi!
Siku chache baadaye Isack na Mery Mtoto Wa Mh Alex Wakafungwa Ndoa Kubwa Iloudhuriwa Na Maelfu Ya Watu Akiwemo Rais Wa Marekani Na Waziri Wake Macdonald!
Mac Donald Akamuita Zidu Pembeni,"tunashukuru Umekamilisha Kazi Yetu,niwajibu Wako Kwenda Kulikomboa Taifa Lako,wewe Ni Komandoo Zidu,mi Nikutakie Kila La Kheri,maelezo Yote Anayo Mh Silvestar,daktari Alokubadilisha Ngozi!
Wakapeana Mikono,msafara Wa Rais Wa Marekani Hatimaye Ukaondoka!
Siku Chache Badaye Uchaguzi Ukafanyika Nchini Tanzania,akapatikana Rais Mwingine,uongozi Nao Ukabadilika!
KITABU CHA PILI
MTETEZI WA KINTE!
SURA YA KUMI NA SITA
NDANI YA NCHI YA KINTE
Mwaka 1964
MVUA KUBWA ilikuwa ikinyesha, radi likipiga na upepo mkali ukiezua baadhi ya mapaa dhaifu yaliyoshindwa kustahimili makeke hayo ya hali ya hewa.
Miti midogo iling’olewa na hata mikubwa ilijikuta katika wakati mgumu kupambana na hali ile ya hali ya hewa
Watu, wanyama walisombwa na mafuriko ambayo yaliacha maafa katika nchi hii ndogo ya Kinte,
Nchi iliyojiengua kutoka katika taifa la Ganyama na kujipatia uhuru wake na kujiongoza yenyewe kama Taifa huru.
Swala hilo nchi ya Ganyama hawakuafikiana nalo. Ilikuwa lazima wairudishe Kinte mikononi mwao.
Wakati hali ya hewa ikiendelea kuhatarisha maisha ya watu wa Kinte;
Katika msitu mmoja Mkubwa, msitu wenye wanyama wakali ulofungamana miti mikubwa iloleta giza lililoleta hali flani ya kutisha
Msitu huo ulijulikana kana msitu wa Lwana,au nyumba ya maiti
Katika usiku ule ulokuwa na dhoruba, ndege ndogo ya kijeshi ilitua katikati ya msitu huo ,
Wanajeshi watatu wakateremka!
Wawili walikuwa na asili ya kiafrika, mmoja alikuwa Chongo na wa pili kwa jinsi tu alivyoonekana kwa umbo, alikuwa Nunda;
kichwa chake kilichongoka, chale zilizagaa katika uso wake na wa tatu ambaye alionekana kama kiongozi wao kwa jinsi nyota zilizvyomchafua mabega yake; yeye alikuwa Mzungu.
Kwa ujumla wote hawakuonekana wema; sura zao zilijaa shari!
Wakaiacha ndege yao iliyochorwa bendera ya nchi ya Ganyama katika ubavu wake,
wao wakasonga mbele ndani ya msitu huku silaha zao zikiwa tayari kwa kazi, mabegi mgongoni
Kutoka mbali wakaiona ndege yao ikiondoka.
Wakaachana nayo,
Yule mzungu alokuwa Kama kiongozi wao akatoa jikaratasi flani kwenye mfuko wa kombati ya gwanda lake
Pasina kujali italoana akaikunjua na kuanza kuisoma,ilikuwa ni ramani ya walipokuwa wakielekea
Baada ya kupata muktadha akampa ishara mwenzake akatoa kitu mfano wa dira akasoma uelekeo,kisha kwa kujiamini akaongoza mbele silaha kailekezea mbele
Bila kujali mvua inyeshayo, radi lipigalo, wenzake nao silaha zikiwa tayari kwa shambulio lolote wakafata nyuma
walizidi kusonga mbele wakifuata ramani walokuwa nayo, ilivyowaelekeza.
Wakati wakiendelea kusonga mbele mzungu akiongoza nao wakifata nyuma ghafla mzungu akapiga breki akiachia yowe sambamba na silaha kumponyoka
Wale wa nyuma hawakuamini wanachokiona mapema namna hiyo,
mmoja wao yule Mzungu kashambuliwa?!....
Kwa haraka wakalala chini kwa sekunde kadhaa ili kukabili hatari yoyote itakayotokea.
Kwa pembe za macho yao, walimshuhudia mwenzao akitapatapa kwa nukta kadhaa kisha akatulia tuli.
Damu yake ikachanganyika na maji ya eneo lile, hakukuwa na milio ya bunduki wala mabomu
Walibaki wakijiuliza nini kilichotokea bila majibu
Ni wazi ndani ya msitu ule kulikuwa na mdunduaji ambaye aliifanya kazi yake sawiya
Ni nani huyo?!...
Hakuna alotambua hilo
"Kuna mdunguaji hapa!"
Walinong’onezana Wanajeshi wale ilhali bado wamelala chini, kwa umakini mkubwa walisikiliza, hawakusikia mtingisho wala mpapaso.
Ni wazi mdunguaji alikuwa akivizia wakatambaa hivyo hivyo wakiwa wameshika silaha zao tayari kwa lolote.
GANYAMA siku huyo hiyo
SIYO KINTE pekee, hali ya hewa ilikuwa mbaya hata katika nchi ya jirani yake Ganyama, nayo hali aikuwa shwari, mafuriko, miti kuangushwa vilishamiri
Ni nyumba moja ya kisasa ilokuwa na ulinzi imara haikutikisiswa na hali hiyo tete, wote waliokuwa ndani ya nyumba hiyo hawakuisikia mvua iliyokuwa ikinyesha. Mazungumzo yao, yaliendelea bila athari zozote.
“Kama nilivyokwisha kusema, inaonesha Makomandoo tuliowatuma Kinte,wameshindwa kufanikisha kazi tuliyowapa, na tumepoteza mawasiliano nao; kwa vyovyote wametekwa au wamekufa,”
aliongea aliyeonekana kuwa kiogozi wao.
“Ndiyo, yote yawezekana, sasa tutafanyeje? Tusikilize, kama wapo hai, tutajua, na kama wametekwa, pia tutajua, ila lazima Kinte irudi kwenye mikono yetu,”
aliongea Rais Goodluck Sylvester, Rais wa nchi ya Ganyama.
§§§§§
ZIDU KATILI ATUA KINTE
Zidu k' baada ya kumaliza matatizo yote nchini Tanzania alienda kuonana na dk Silvestar aliyempa maelekezo aliyopaswa kuyafahamu!
"Na kwanzia sasa utakuwa ukitumia jina la John Chaka,Zidu yapaswa ulisahau sasa"
Shushushu Yule Mwenye cheo kikubwa jeshini akazidi kumjuza,akampa viza ya kusafiria
Isack,Mery wakamsindikiza Zidu mpaka Ear port akaingia kwenye ndege badae dege likapaa na kuiacha ardhi ya Tanzania
Ndani ya ndege Zidu alikuwa na mawazo tele,akujua kazi atakayoenda kuifanya ni kazi ngumu ambayo ingeweza kuondoka na maisha yake
Japo akujua ni kazi gani angeipewa kulidhibiti taifa la Ganyama
Nusu saa baadae John Chaka aliwasili Kinte na kupokelewa na Maafisa mbalimbali wa Jeshi, aliingizwa kwenye gari jeusi na safari ya kuelekea Ikulu ikaanza
Alishangaa kuiona Kinte ilivyobadilika, haikuwa ile aliyoijua yeye
Ile aloikimbia miaka tele nyuma baada ya kuaribu jeshini na hatimaye yeye na kijo kufukuzwa,
nyumba zilibomoka, miti ilianguka, kiujumla hali ilitisha.
Baada ya mwendo mdogo waliwasili Ikulu kulipokuwa na tafrija ya kumpokea
Baada ya tafrija aliitajika na Rais kwa mazungumzo, moyo ukaanza kumwenda mbio akijua sasa ndo anaenda kukabidhiwa kazi ngumu ambayo mpaka wakati ule akuijua ni kazi gani
Na wala akujua ni kwa nini moyo ulimuuma vile,na nywele kumsisimuka
Ile ilikuwa ni ishara mbaya sana kwake!
Ishara ya hatari!!!!
Baada ya tafrija aliitajika na Rais kwa mazungumzo, moyo ukaanza kumwenda mbio akijua sasa ndo anaenda kukabidhiwa kazi ngumu ambayo mpaka wakati ule akuijua ni kazi gani
Na wala akujua ni kwa nini moyo ulimuuma vile,na nywele kumsisimuka
Ile ilikuwa ni ishara mbaya sana kwake!
Ishara ya hatari!!!!
Ila kwa komandoo kama Yule alijua alipaswa aiondoshe woga,na wasiwasi ulokuwa ukimjia kwa kasi,
Akakumbuka kazi za hatari alizokwisha kumbana nazo,akakumbuka mazoezi alokuwa akiyapata kambini!
Akajikuta tabasamu likimponyoka
Tabasamu lililolendana na fikra ya kinifu akuamini kama ipo siku moja angetembea katika taifa lake la Kinte kwa Uhuru namna ile,pindi aliporejea angepokewa kwa tafrija kama ile
Na leo anaenda kuonana na Rais wake, Zidu akajikuta akiongeza mwendo sambamba na kuongeza ukubwa wa hatua zake mpaka ilipo ofisi ya rais ikuluni pale
Nje palikuwa na mlinzi aloshusha saluti sambamba na kugonga mlango,alokuwa ndani akaufungua mwanaume akazama
Kalikuwa ni kaofisi kadogo tu palikuwa na mwanajeshi mmoja mlangoni huyu ndo alofungua mlango baada ya kuoneshewa ishara na raisi wake afanye ivyo
Pia nyuma ya raisi palikuwa na mlinzi mwingine ambaye tabasamu lilikuwa hadui yake
Rais akampa ishara aketi katika kiti kilichokuwa ofisini mule!
"Nashkuru kwa kuitika wito wangu Zidu,jina lako la kazi ni Chaka eeh?!"
"Yaaaah komandoo John Chaka"
Zidu akaongea akitabasamu,rais naye akaachia tabasamu lake!
"Lengo la kukuita ni kuitaji msaada kutoka kwako,kwa sifa zako tulizozipata ukiwa kambini na kwa kazi nzur uloifanya nchini Tanzania naomba basi uifanye na hapa!
Wewe ni Mwana Kinte hili ndo taifa lako,vipi ukubali kuona taifa lako likiteketea ni kipi *KIAPO* cha damu ulichokula wakati waingia jeshini?!
Raisi Kuongea Maneno Yale Yakampeleka Zidu Mbali Kimawazo Akikumbuka Kwa Mara Ya Kwanza,wakati Alipopelekwa Jeshini Na Baba Yake,
Alikuwa Ndo Kwanza Ana Miaka 18 Baada Ya Kuhitimu Masomo Yake Ya O Leval,akakumbuka Kiapo Alichoapishwa Kuwa Muwadilifu,kulilinda taifa,dhidi ya hatari yoyote!...
akakumbuka pia walipopewa visu wakaambiwa wajikate mkono kidogo damu yao ndo kiwe kiapo chao,ikiwa ndo wanakaribishwa katika mafunzo!
ghafla machozi yakaanza kumtoka,rais alimkumbusha mbali,sia ya kulilinda taifa lake likamvaa!
Alikumbuka Ubaya Alolifanyia Taifa Lake Kwa Kitendo Chake Yeye Na Mwenzake Kijo Kumbak
mkuu wao wa mafunzo brigedia lucy,kisa tu alikuwa akiwatesa!
Kazi ile ilipaswa ifute kosa lile,
"nipo tayari kufanya kitu chochote utakacho niagiza kulilinda taifa langu mkuu"
"vizuri!,miaka kadhaa nyuma tulijiengua katika taifa la ganyama baada ya kutoona faida ya muungano kwa muda mrefu,hiyo imeleta chokochoko,Rais wa nchi ya Ganyama Kila Mara Analeta Wanajeshi Wake Huku Wanaua Raia Waso Na Hatia,wanapora Tumechoka!
Kazi Iliyoko Mbele Yako Yapaswa Uende Ganyama,kwambinu Yako Yoyote Ile Uakikishe Unamuua Rais Wao,
Zidu Akashtuka!,kumuua Rais?,Rais Wa Ganyama Silvestar Nyoshi Alimtambua Fika,ukatili,roho mbaya yake,jeshi lake pia alilijua!
Ni Kama Wewe Hapo Leo Ukaambiwa Ukamuue Rais Wa Marekani,au Rais Wa Korea!,nchi Zilizojizatiti Kwa Ulinzi Ikiwemo Ardhini,majini Na Angani!
Zidu Alibaki Kaganda Akimtumbulia Macho Rais Wake Yule!,ghafla tu Mwili Wake Wote Ulimloa Jasho!
Kwenda Kule Ni Kukifata Kifo Chake!
"uwezo najua unao,kufa kwake kutaleta hali ya amani katika nchi zetu!"
"lakini muheshimiwa kwanini msitumie nguvu ya kijeshi 'vita' katika kumng'oa huyu mtu,kama jeshi unalo,zana za kivita unazo,kusanya jeshi vamia!"
"sawa tunaweza fanya ivyo,ila wale ki zana wapo vizur zaid yetu watatushinda tu,wale wana mpaka mabomu ya asidi,achana na hayo wana makombora ya masafa marefu,hiyo siyo ishu wana mpaka nyuklia kupambana nao ni kutaka kinte ibaki jangwa ndo maana nikaamua kutumia njia hii nenda kwa siri Ganyama Kaue Kwa Siri Kwetu Hii Ndo Njia rahisi Na Kwa Uwezo Wako"
"yote hayo Sijakataa Mkuu Ila Nadhani Pia Umesahau Juu Ya Rada Wanazomiliki Watu Wale,pia Umesahau Print Finga Na Vitu Vingine Kama Ivyo Maisha Yangu Yatakuwa Hatarini Mkuu!"
"ulikula *kiapo* Cha Damu Kulilinda taifa Lako Kivipi Saivi Usite,wewe Ni Hodari Ni Muda Wa Kuonesha Uhodari Wako,wewe Ni Shujaa Chaka Onesha Ushujaa Wak pambana kwa ajili ya nchi yako na ukifa kufa kwa ajili ya nchi yako,ni amri nenda Ganyama Akikisha Unamwangamiza Rais Wao,usirudi Hapa Bila Ushindi Labda Urudi Ukiwa Maiti Utazikwa Kishujaa Pia,utakuwa Umekufa Kwa Ajili Ya Nchi Yako,kuwa Mzalendo!...
Rais Mernel ii Ilibidi Sasa Aongee Kwa Ukali,ukali Ukiambatana Na Amri Za Kijeshi!
Zidu Hakuwa Na Budi Kuzifuata Akasimama Na Kusaluti,kukubali Amri Ile!
"andika Unavyoviitaji Utapatiwa Kajiandae Na Safari"
"sawa Mkuu!"
Zidu Akaelekea Chumbani Kwake Kule Ikulu,ni Chumba Alichoweka Mizigo Yake Akafungua Friji Akatoa Kilevi Akakigubia,kupunguza mawazo!
kazi ile aikuwa nyepesi hata chembe!!...
****
Katika Nchi Zote Ulimwenguni Huwa Mashushushu hawakosekani,ukaa katika sehemu nyeti wakipeleleza kitu na kuifikishia nchi yake,hawa walilipwa fedha nyingi sana,kwa kuwa uwezekano wa kuuwawa pindi wakigundulika ulikuwa ni mkubwa sana!,
Katika taifa dogo la kinte mashushushu wa Ganyama walikwepo,na katika taifa la Ganyama pia Mashushushu Wa kinte walikwepo,sia na nia nikuhakikisha habari na siri zote mipango nyeti wanazifujisha katika nchi zao!
Mfano wa shushushu mmoja hapo ni Antonio Reyland body gardy mkuu wa rais laizar ii wa nchini Kinte,huyu Alikuwa Ni Komandoo aliyeaminiwa na rais Laizar Ila Kumbe alikuwa ni mnafki,kivipi sasa?!
Tupate historia yake kwa ufupi kumjua mtu huyu,alitokea katika familia ya kijeshi,baba yake na mama yake walikutana jeshini wakapendana,ivyo walipokuja kupata mtoto wakamwingiza jeshini,kwa bahati mbaya au nzur mtoto walobahatika kumpata ni huyo mmoja tu!,wao walikuwa wakiishi upande wa kinte japo chimbuko la mama yake ni ganyama,badae nchi zilipokuja tengana,wazaz wake pia wakatengana mama akarudi ganyama baba akabaki kinte,naye akijifanya na mapenz mazito na nchi ya kinte akabaki,baba yake Reyland Akajitahid Kumuweka Karibu Na Rais,laizar Akamwamin Na Kumfanya Mlinzi Wake
pasina kujua habari zao nyeti yeye ndio aliyezivujisha Ganyama!
Hata habar ile ya kuwasili kwa Jitu Zidu katili nchini kinte na kwenda kuakikisha anamwangamiza Rais Silvestar Kama amri aliivujisha nchini ganyama!
Habari hiyo kuwa rais Laizar Moreti ii anamtuma mtu aje kumuua kilimuumiza sana rais wa Ganyama Silvestar,
Hasira Zake Zikaongezeka Mara Dufu,mwili Wake Ukamchemka,mbaya Zaidi Alitumiwa hadi picha ya Zidu, P.a.k komandoo Chaka!
"HUYU MWENDAWAZIMU AKITUA TU AKAMATWE ULINZI UIMARISHWE KATIKA VIWANJA VYOTE VYA NDEGE PICHA YAKE AGAWIWE KILA MWANAUSALAMA KWANZIA MGAMBO MPAKA MAKOMANDOO WETU"
Amri Ikatolewa Kwenye Viwanja Vyote Vya Ndege Ulinzi Imara Ukawekwa Kusudi Tu Zidu akitua akamatwe,mabasi ya mipakani yalikaguliwa picha ya Zidu 'wanted' ilisambazwa kila kona chini pakiwa na dau kubwa kwa atakayemuona na kupelekea kukamatwa kwake!
Ilikuwa mshikemshike mtahani watu wakitazamana,hakika palikuwa na msako mkali,rada ziliongezwa,askar maalumu wakitengo cha camera wakikagua kila mtaa kwa kutumia mitandao maalum!
hali ilikuwa niyakutisha.
***
Wakati hayo yakiendelea Zidu Mwenyewe Akutaka Kutumia Usafiri Wa Ndege,alijua Ilo Litatokea,
Alipewa Maelekezo Ya Njia Ambayo Alipaswa aitumie "njia za
Panya,ambapo kuna mtu maalumu ambaye angefikia kwake akuambiwa hata jina la mtu yule!,toka Sofya Mji Mkuu Wa Kinte Mpaka Ganyama Palikuwa Na Umbali Mrefu,kikiwa Kimebakia Kijiji Kimoja Ndipo Aingia Ganyama Mjini Akaweka tuo,kuna mahali ilipaswa apumzike kungoja usiku ndipo aingie sasa Ganyama,taifa lililokuwa likimsaka kwa udi na uvumbi
Mtu Yule Alompakia Katika Gari Yake Akamuonesha Kajumba Cha Makuti Ambacho Ndicho Kilipaswa Akae Mpaka Usiku Ndipo Aingie Ganyama!,wakaachana,Zidu akaelekea katika kajumba kale,
ile kuingia,akamkuta mtu kalala katika kakitanda cha kamba akinesanesa huku akiwa kajifunika kwa ngozi ya mnyama!
ile zidu anaenda kumfunua mtu yule akaruka na kutua nyuma yake!
Zidu Akapigwa Na Butwaa Na Kugeuka,akuamini Macho Yake!,
"haaa,ni Wewe?!" Aliuliza Pasina Kuamin Macho Yake!
"ni Mimi!"
Wakakumbatiana,ni Isack Yule Yule Alomwacha Nchini Tanzania!,
"dah Wewe Mery Na Eggy Awajambo? Imekuwaje Huko Hapa?"
"ha ha ha wapo tz,wanaendelea salama,ntakuachaje kaka kama tulivyopambana Tanzania Tutapambana Pia Ganyama Sipo Tayari Upambane Mwenyewe Kama Kufa tutakufa wote hiki ni kiapo nala mbele yako"
"aaah camon isack wataka kufanya nini?,umechanganyikiwa wewe?"
"sijachanganyikiwa hili naongea kutoka ndani ya moyo wangu,nimekuja kukusaidia hii opereshen,utoiweza peke yako!"
Jitu Zidu Likatingisha Kichwa Kusikitika!,kisha Likatabasamu!
"sitopenda Umuache Mery Mjane,bado Anakupenda,unategemewa Ila Mimi Mery Wangu Mwanangu Walishakufa Hakuna Anayenitegemea Sipendi Nawe Upotee Kwanza Wewe Ni Mtanzania Kaipambanie Nchi Yako Nami Ni Mkinte Nipo Kwa Ajili Ya Nchi Yangu Nakuomba Sana Usiingilie Hii Ishu Wewe Aikuhusu! Yangu Na Yako Tulishayamaliza Tanzania!"
Zidu Aliongea Kwa Hisia,badala Yake Isack Akaanza Kumcheka,
"mbona Wajidanganya Ivyo Zidu Eti Yangu Na Yako Yalishamalizika Tanzania Sawa Yale Yalipita hii opereshen mpya tunaianza pamoja na tutaimaliza pamoja utake usitake"
"mzee,mbona wataka kulazimisha mambo?,mimi kwenda katika hiyo opereshen nalipwa matrilion ya mabilion ya mafwedha,wewe je?!
Isack Akacheka Sana,akampa Barua Ambayo Ilitoka Katika Idara Ya Jeshi La Polis Nchini Tanzania Kumruhusu Kuisaidia Kinte,ikiwa Ni Kukubaliwa Kwa Ombi La Kinte Kumuitaji!
Zidu Akabaki Kaganda,pasina Kuamini Kile Alichokisoma,
"ongea Jingine Sasa Je Ningewakatalia!?"
Zidu Alibaki Kimya Pasina Kujibu Angejibu Nini Sasa? Machozi Yenyewe Yakaanza Kumchuruzika,ni Mara Ya Pili Hii Isack Kuyaona Machozi Ya Zidu,kitu kile kikamshangaza hiyo inamaana yale ni machoz ya furaha au?!
dah mambo yameanza je nin kitaendelea?
Baada Ya Kumkosa Kosa Mara Kibao Kumuua Ndani Ya Season One Na Two,three Mwishon Kwa Pamoja Wanaungana Kushirikiana Kuwaangamiza Wale Walokuwa Wabaya Wao!,
Kwa Ndinde Sana Wanafanikiwa,
Ila Zidu Linaitajika Nchini Kwake Kwenda Kulikomboa taifa lake,kashkash inatokea hapo anapewa kaz ya hatari kwenda kumuua rais wa ganyama mh Silvester mh katil tena mwenye roho mbaya!
Wakati Akiwa Amebakisha Vijiji Viwili Kuwasili Ganyama Anakutana Na Isack,kaja Wakashirikiane Naye,Zidu anapinga vikali,je nin kitaendelea songa nayo tuburudike!
SEHEMU YA TISINI NA TANO!
Isack alibaki kaganda akalishangaa chozi la mtu yule,ni ajabu kwake,komandoo kutoa chozi,kwake ni wazi moyo wake ulikuwa katika maumivu ya kiwango cha juu sana,kwa sauti ya taratibu, yakubembeleza na ya kusihi ikasikika kutoka katika domo la jamaa yule!...
"ni afadhal ya chozi langu limwagike mara moja kuliko lije limwagike tena,likiambatana na chozi la mkeo Mery,tena Mjamzito,tukiwa Wote Sitokuwa Na Furaha Kama Nikiwa Mwenyewe,nikiwa Mwenyewe Ntakuwa huru ntafanya kazi kwa ufanisi,tukiwa wawili ntakuwa na khofu ya kukupoteza,nakuomba nipo chini ya miguu yako rudi tz nakuhaidi nala *kiapo* kwako NITASHINDA
Hakika Yale yalikuwa ni maneno makali yaloenda yakakita katikati ya muyo wa Isack naye machozi yakaanza mtiririka!
"u.n..ani..a.pia..kamanda.uta.shinda?"
"nakuapia nitashinda we acha niende!"
Isack Akamfata Akakumbatia Kwa Nguvu!,wote Sasa Machoz Yakawa Yakiwatiririka,wakabaki Wamekumbatiana Vile Kama Dakika Tano Nzima!
Ghafla Zidu Akazinduka, akamuachia Isack!,
"dogo Jioni Hii Muda Umeenda wacha nikajiandae!"
Zidu Akalifata begi lake akalifungua akatoa ndevu za bandia akazivaa nywele zake akapaka rangi flani kama mvi kwa mbaali,akachukua rangi na kukolezea nyuzi zak weusi kidogo,yani kimuonekano alibadilika,akachukua koti lake kubwa akalivaa,mifuko ya ndani ya koti akazamisha visu kadhaa,bastola akaisweka kibindoni,kisha akamgeukia Isack,
Isack Alishtuka,kwani Muda Wote Alikuwa Amemwekea Mgongo,
"wallah Umebadilika Kaka, atakayekujua uyo mchawi kumbe si lazima tumtumie dokta kutubandika mingozi juu ya ngozi zetu umetisha mkuu!"
Zidu likaachia jicheko la kinafki,kisha akamaliza kwa kusema "upo right huu mwanzo sidhani kama yupo atayenijua!"
"ok twende nifate" Isack Akamwambia Zidu Naye Zidu akamfata,wakazunguka nyuma ya nyumba! katika kichaka flani!
Isack Akavuta Kwa Nguvu Yale Majani Pakafunguka,kumbe Kile Kichaka Bandia,si Cha asili,Zidu akabaki kushangaa,chini pakawa na shimo,Isack akampa ishara Zidu Aingie,
"kuna Nini humo?!"
"VVS.."
Isack akaongea kwa mkato,tayari Zidu Alishamwelewa Pale Alimaanisha Vitu Vya Siri,akuliza Swali Lingine taratibu akalisogelea shimo kuchungulia ndani kuna mwanga akashuka kupitia ngazi zilizoanzia pale pale juu,kushuka tu Isack akarudishia ule mfuniko wa ardhi juu yenye nyasinyas ngumu zilizolandana na nyasi za eneo lile,akasimama juu yake!,macho yake yakiwa katika simu ni baada ya dakika kumi ndo ilipaswa afungue ule mfuniko Zidu Atoke!
Kimbembe!
Zidu Sasa Kule Chini,aliposhuka Chini Kabisa Kwa Kutumia Zile Ngazi,mbele yake akapokelewa na nyumba nzuri,usingeweza kudhani wala hata kuhisi kule ni chini ya ardhi!,
Akapiga hatua kuifata ile nyumba, akagonga mlango, ghafla mlango ukafunguka wenyewe kufunguka tu kuna gari ni kama ilikuwa ikimsubiri dereva mwenye asili ya kizungu akampa ishara aingie naye akaingia,
Dereva akaiondoa ile gari,kutoka ndani ya nyumba ile,jamaa yule alikimbiza gari kama dakika tano wakawasili katika jumba jingine la kifahari,akampa ishara ashuke awakuongea kitu,nje Ya Jumba Lile Palikuwa Na Ulinzi Kama Wa Huku Juu Ya Ardhi,mlinzi Yule Akafungua Geti Wakaingia Ndani Wakaikwea Lift Mpaka Juu Katika chumba kimoja akampa ishara,agonge mlinzi yule akarudi zake Zidu kugonga mlinz mwingine akamfungulia na kumpeleka mpaka palipokwepo na mtu ambaye akumtegemea kabisa kama ipo siku angekutana naye katika maisha yake!
Ni mkuu wa majeshi katika taifa la kinte!...
akampa maelekezo yake,ikiwemo kula kiapo kingine mbele ya mawakili wa jeshi kutosaliti taifa lake!,akapewa jacket proof,akatoa lile alovaa akavaa ilo alopewa,wanajeshi kadhaa wakapanda na pikipiki juu ambayo angeitumia kama usafiri,alipewa pia na saa yenye mawasiliano na kule!
"ukiitaji msaada tumeweka kambi karibu kusudi tukusaidie kazi njema!"
Kila kitu Zidu Aliona yu ndotoni,yani juu palitengenezwa kinyumba cha makuti na alijua Isack pekee ndo anaish pale kwa kaz maalumu,kumbe chini kuna mambo,kuna watu zaidi ya mia tena wanausalama,ishi uone mengi,nje ya ile nyumba akakutana na yule mzungu alompakia tena katika gari lake mpaka pemben ya zile ngazi,ambapo pemben palikuwa na ile nyumba aloenda gonga,yeye akapanda ngazi kupanda juu,mzungu akarudisha gari ndani!...
nje alikuta pikipiki yake ishafikishwa mwanaume akaipakia!
"kesho ntarudi tz,kila la kheri kaka uje na ushindi!"
Zidu akamuonesha dole gumba,huyo akawasha pikipiki tayari kuondoka eneo lile!...
***
ZIDU ATUA GANYAMA!
ASHTUKIWA...
Zidu k kwa jina lingine John Chaka, usiku Ule Mida Ya Saa Mbili Alianza kuingia katika mji wa Bamala,mji Mkuu Wa Ganyama na palipo makao makuu ya taifa lile,akushangazwa sana na vizuizi alivyokumbana navyo na msako juu yake!,
Kimuonekano akushtukiwa mapema alifanikiwa kufika Bamala Salama, mji Ulikuwa umechangamka Kwa Muda huo alitafuta club moja na kukaa
Akaagiza bia yake moja kushtua ubongo akiburudishwa na wimbo wa alomide mamaa aloimbwa na mwanamziki wa kikongo kofii olomide,tayari wanawake wachache walishaanza kujipitisha kwake!,akuitaji kuisumbua sana akili yake kung'amua kwamba wale ni machangudog waloitumia miili yao kujipatia kipato!,
kwa kuuza penzi kwa thaman ndogo tu ya ela,kukumbuka vile kukamfanya amkumbuke mke wake Mery,mwanamke Alomsaliti Na Kutoka Na Kibopa Wa Serikali,wakati Akiwaza Vile Ghafla Macho Yake Yakatua Katika Meza Moja Aloketi Dada Mmoja Na Jamaa Ake,ni Kama Wapenzi,ila Walikuwa Wakimtazama Sana,Zidu Alipowatazama Kwa Ghafla Wakaamisha Macho Yao Kwa haraka na kuwa kama wanajadili yao!
Jitu Zidu alikuwa Jitu Jinga eti eeh!,kengele ya hatari ikagonga katika bichwa lake!,akajinong'oneza 'watakuwa wamenigundua nin?!,mbona mapema hivi,sindo nafika?..hapana,embu ngoja!'
Akajiwazia,muda huo huo akijinyanyua na kuelekea toilet akitafuta njia ya kuchoropoka pale,alihisi hali ya hewa kuaribika!
"kamanda,nahisi anataka asepe ndo yeye kabisa kama vipi wakati mimi nawashtua kikosi 'a' cha makomando wewe kamtange asisepe kama vipi hata funga mlango kwa nje asitoke"
mwanamke yule ambaye Zidu alimuhisi alimnong'oneza mwenzake alokuwa naye,bila kujibu kitu jamaa akajinyanyua silaha yake ndogo ikiwa mkononi akaelekea kule alipo elekea Zidu,kufika Zidu Ndo Alikuwa Akiingia Ndani Ya Chumba Cha Choo,akaenda Kusimama Pale Nje,kwa bahati mlango ukuwa na komeo la nje,ivyo silaha aliweka tayar,mwanaume akitoka tu anamtandika ya bichwa na kuutawanja ubongo,kama si ya tumbo na kutawanya mautumbo!...
ITAENDELEA
Simulizi : Kiapo (Mtetezi Wa Kinte) (4)
Sehemu Ya Pili (2)
Afisa Polisi Yoyote uongozwa na hisia (machale) na ni kosa kwa afisa polis yoyote kudharau hisia zake,hapo awali Chaka alihis watu wale wawili si wazuri kwake,na kuamua kujifanya kwenda toilet akiwa ndani ya choo kile hisia zake bado zilimtuma kuhisi kuna mtu ndani ya choo kile,tena kashika silaha,japo akuwa na mkojo ila alikojoa!,
Baada Ya Kumaliza Kukojoa Akaugeukia Mlango!,ramani Ikajichora Katika Kichwa Chake,nyuma Ya huu mlango kuna kiumbe kimesimama,kama si kale ka binti atakuwa ni yule jamaa,kashika pisto,na nikitoka ni kunisambaratisha ubongo,vile alivyohis ndivyo ilivyokuwa!
sasa afanyaje,mlango ule ulifunguka kwa nje nikiwa na maana ukiwa ndani utausukumia nje ndo utoke na ukiwa nje utauvuta kwa nyuma!,ivyo kwa kubahatisha tu aliushika kwa kutumia nguvu zake nyingi akausukuma kama vile uligoma kufunguka!
Mtu yule alosimama nyuma na silaha yake,pigo lile lilikuwa la ghafla,mlango ule ulimpiga,akaachia yowe silaha ikamponyoka akaserereka chini,ila kwa wepesi akanyanyuka akuangaika kuiokota silaha yake kama umeme akamjia Chaka Na Kumtandika Ngumi Ilompata Sawia Komandoo Chaka 'ck' mdomoni ikabadilisha ladha ya mate,ikawa na uchumvi chumvi,wakati Chaka Akista ajabu uhodari wa yule mtu,mtu yule alijirusha na kuachia mguu kwa mbele lililoenda kukita kifuani mwa Chaka,teke Lile Likampeleka Chaka Chini,yule Kijana alikuwa Ni Mwepesi,kc Kutokana Na Mafunzo Alopitia aligundua mtu yule hakuwa mtu wa kawaida!
alikuwa ni mwanajeshi,tena mwenye mafunzo maalumu ya kijeshi kama yake,si mwanajeshi wa kawaida yule!,ni komandoo kama yeye,mwenye mafunzo kama yake,au pengine ni zaidi yake,jitu likajitahadharisha
Likajua tayari lipo hatarini,nywele zilimsimama,mwili ulimsisimuka,ilipaswa akili yake aifanyishe kazi ya kufikiri zaidi,
Wakati huo yule mtu akamjia 'kc' kwa spidi,akiwa na lengo la kumpiga pigo moja takatifu,lakin Zidu Alilisoma akajipinda kidogo,jamaa akapita,'kc' akamuwah kwa kum'bandika teke moja zito la kiunoni,ambalo mtu yule akujua ujio wake,akaenda chini,yowe likimtoka!,kc,sasa akamsogelea,mtu yule alikuwa kama akijitahidi kuamka ila akuweza,kc akatabasamu kwa dharau
"hata ukipona utoamka tena,nishavunja mifupa ya kiuno haya ndo malipo ya kunifatilia!"
Mtu yule akaachia tabasamu la kujilazimisha,kwani bado uso ulijikunja kwa maumivu,kwa ghafla mtu yule akamtemea mate yenye mchanganyiko wa damu 'kc' usoni,lengo kumkasirisha azidi kumpiga na hatimaye akutwe,kwani uwezi wa kumzuhia pale akuwa nao tena!
Kwa Mbinu Ile Alikosea Sana,kutemewa mate usoni,Zidu alichukulia kama dharau,akaona ndo kajikatia tiketi ya akhera,kwani alipanga amuache hai ila kwa kitendo kile alimfata akakishika kichwa chake akamnong'oneza
"shadaaash bwege wewe wasalimie kuzimu" palepale akakikunja,akauondosha uhai wake!,akamsachi akakuta kitambulisho cha jeshi,kitengo maalumu,ndo icho cha ukomando,akakirudisha mfukoni,katika mfuko mwingine akakuta pesa,pesa mwanaharamu,hizo akuzirudisha akazisweka mfukoni mwake,akauruka ule mwili akaenda kuiokota ile pistol ilodondokea pembeni akaisweka kibindoni,sasa angetokaje,alihisi akipita mlango wa kawaida angekumbana na yule mwanamke pengine hata na jeshi zima,ghafla macho yake yakadondokea katika bomba kubwa lililopitisha maji taka,akajaribu kufungua mfuniko akafanikiwa,akajitumbukiza akaanza kutambaa mpaka nyuma ya klabu kulipokuwa na shimo refu kulipopokea maji yale,
Baada ya kutoka ndani ya bomba lile aliitazama fensi ndefu ya kutokea nje,katikati ya fensi ile kulikuwa na nguzo ambayo Zidu aliitumia kutokea nje na kupotea eneo lile!...
***
ILIVYOKUWA
Wakati Zidu akipita na pikipiki yake katika kizuizi kimoja wapo bila kugundulika na mtu yeyote,hali ilikuwa tofauti kwa mwanadada Katarina na mwenzake Lameck,bila kupoteza muda wakapanda katika pikipiki na kuanza kumfata kwa nyuma Zidu kwa lengo la kumchunguza kwanza
HILI NDO KOSA KUBWA WALILOLIFANYA
Zidu hakuwa mtu wa kuchunguzwa,safari zao ziliishia mpaka club ambapo baada ya Zidu kuhisi anaangaliwa sana na kuelekea chooni,
Katarina Akamwambia Lameck akamweke chini ya ulinzi naye akapiga simu makao makuu,kuitaji nguvu kazi,Lameck akamfata chooni na kuambulia kifo 'kc' akatoweka
Dakika tano badae gari ilojaza wanajeshi ilitia timu kwa mbwembwe hata kabla aijasimama makomandoo waliruka tayar walishajipanga wengine wakazunguka club ile huku wengine wakiingia ndani,kila mtu silaa ikiwa mkononi,kufika chooni wakakumbana na mwili wa Lameck Usio na uhai!,macho yao yakatua katika mfuniko ule ulokuwa wazi haraka sana wachache wakazama na kutokea upande wa pili!,
patupu!!
Mwanaume saa nyingi sana alishasepa,huzuni ikatawala ganyama,hakika jeshi la polisi lilikumbwa na huzuni kumpoteza Lameck,kijana alokuwa amefuzu katika kombi ya mapigano!
Jibu likapatikana kuwa
ZIDU K' A.K.A CHAKA YUPO GANYAMA KWA MUONEKANO MPYA
Katarina akaeleza jinsi 'kc' alivyo,picha ikachorwa na kusambazwa huku dau lake kwa atakayefanikisha kukamatwa hata kueleza tu mahali alipo likiongezwa,ikulu ulinzi ukiimarishwa maradufu!...
Wananchi wakazidisha kasi ya usakaji!,
kitimtim Ganyama!...
Baada ya nchi ya Kinte kujitenga,na kujipatia uhuru wake toka katika taifa la Ganyama,Rais Wa Nchi Ya Ganyama akubaliani na jambo hilo!,vita vya chini kwa chini vinazuka...
Wakati Machafuko Yakiendelea Kwa Siri sana Rais wa kinte Mernel ii anamtuma komandoo Zidu Ganyama akahakikishe anamwangamiza rais wa Ganyama,akiamini kufa kwake ungekuwa ndo mwisho wa machafuko yale!,Zidu akitumia jina la Komandoo Chaka 'kc' anatua Ganyama,kwa bahati mbaya katika kizuizi kimoja anashtukiwa anafatiliwa ila anafanikiwa kuwatoroka,baada ya kumuua kijana Lameck Aloenda Kumdhibiti
NA HII NI SEHEMU YA TISINI NA SITA
moyo wa Komandoo Chaka haukuwa na amani,kitendo cha kushtukiwa mapema kiasi kile kilimwogopesha,hakuwa tayari kuingia mikononi mwa Serikali ya Ganyama bila kurudi nyumbani na ushindi akiwa ndani ya chumba chake cha hoteli alofikia,baada ya kutoka pale club alijilaza kitandani,akarudisha kumbukumbu zake nyuma!...
Wakati Akiwa Mbele Ya Mh Rais akikabidhiwa kazi ile
"ulikula *kiapo* cha damu kulilinda taifa lako kivipi sasa usite?,wewe ni hodari ni muda wa kuonesha uhodari wako,wewe ni shujaa Chaka onesha ushujaa wako pambana kwa ajili ya nchi yako na ukifa kufa kwa ajili ya nchi yako,ni amri nenda Ganyama akikisha unamwangamiza raisi wao ukiwa kama mtetez wa Kinte usirudi hapa bila ushindi labda urudi ukiwa maiti utazikwa kishujaa pia,utakuwa umekufa kwa ajili ya nchi yako...
Kuyakumbuka Maneno yale kukampa ujasiri,akajinyanyua mpaka katika soketi akaiwasha tv ikawaka,alishtuka kuona picha yake katika runinga ikitangazwa na dau kubwa,sura yake ile ya sasa,mwili ukamsisimuka,ni kwa haraka eti,mambo yalikuwa yakimuendea kombo,hakuwa tayari kuendelea kubaki hapo kwani alikuwa na kumbukumbu jins dada wa mapokez alivyokuwa akimwangalia kimatamanio wakati akichukua chumba pale
angetokaje sasa pale na ilikuwa
lazima apitie mapokezi ndo atoke nje!,liwalo na liwe ile anatoka tu akashughudia chumba kinachofatia mdada alojifunga nikabu akiangaika kufungua mlango akazama ndani,palepale pasina kupoteza muda,Zidu likapiga hatua zake ndefu kukifata chumba kile akagonga mara moja tu,
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment