Simulizi : Cosa Nostra
Sehemu Ya Pili (2)
Wakaanza shughuli za utekaji na kudai kulipwa ili kumuachia mateka (kidnapping for ransom), wakaanza na shighuli za usafirishaji wa binadamu na madawa ya kulevya. Lakini pia hawakuitelekeza shughuli yao ya miaka yote. Kuwalinda vidosi (protection), tofauti tu ni kwamba sasa walikuwa wanawalinda watu wenye utajiri mkubwa mkubwa sio vijisenti.
Hadi kufikia katikati ya miaka ya 1910 ushawishi wa Mtandao wa Mafia katika mji wa Socily ulikuwa ni mkubwa kupindukia.
Ndipo hapa ambapo wakachukua hatua nyingine ya ziada kuhakikisha wanakuwa imara zaidi.
Wakahakikisha kwamba Gavana wa mji huo wa Sicily anatoka katika mtandao wao katika kila uchaguzi uliokuwa unaitishwa.
Hili walifanikisha kwa kutisha wapiga kura na kuwalazimisha kuchagua mtu wao. Lakini pia waliwatishia maisha wagombea wengine na kuwalazimisha kujitoa kwenye kinyang'anyiro hivyo wagombea wao walipita bila kupingwa kwenye chaguzi nyingi.
Ushawishi wa Mafia katika mji wa Sicily ukaongezeka na kufikia kilele cha juu kabisa na ikawa kana kwamba wanaumiliki mji wa Sicily.
Mafia vs Benito Mussolini.
Mwanzoni mwa miaka ya 1920 Jimbo la Sicily lilirudishwa katika utawala wa nchi ya Italia. Katika kipindi hiki kiongozi mkuu wa nchi alikuwa ni Waziri Mkuu Benito Mussolini, kiongozi katili, na dikteta aliyeogopwa kila kona.
Mwaka 1924 Mussolini alifanya ziara ya kiserikali katika jimbo la Sicily.
Katika ziara yake alikaribishwa na Gavana wa mji wa Sicily aliyeitwa Fransesco Cuccia. Huyu licha ya kuwa Gavana wa jimbo la Sicily pia alikuwa ni moja ya mabosi wa ngazi za juu wa Mafia.
Katika mapokezi yake inasemekana alishangaa kuona Mussolini ameongozana na maafisa wengi wa Ulinzi kutoka Roma.
Ndipo hapa inaelezwa akamnongoneza Mussolini na kumwambia "Mtukufu Waziri Mkuu huitaji ulinzi wote huu ukiwa na mimi". Akimaanisha kuwa kwa kuwa yeye (wao mafia) wanaumiliki mji wa Sicily hivyo hakuna mtu yeyote anayeweza kuthubutu kumdhuru mgeni wa ngazi za juu aliyekuja kuonana na Gavana (Bosi wa Mafia).
Inasemekana Mussolini alikasirishwa vikali na kauli hii na akamkemea vikali Gavana Fransesco Cuccia na kumueleza kuwa haitaji Ulinzi wake.
Kitendo hiki cha kukemewa kilimuudhi sana Gavana, na akawaeleza vijana wake watoe maagizo kwa wananchi kuwa wasihudhurie mkutano wa Mussolini uliopangwa kufanyika kesho yake.
Ni kweli kesho yake Mussolini alipokwenda katika mkutano wa kuhutubia wananchi wa Sicily akajikuta yuko peke yake na walinzi wake. Hata Gavana hakuwepo.
Mussolini akauliza ni nini kimetokea? Ndipo akaambiwa kuwa Gavana huyo ni moja ya mabosi wa Mafia na alichukizwa na jinsi alivyo mkemea jana hivyo aliamuru wananchi wasijitokeze kwenye mkutano wa Mussolini.
Mussolini akachukia kweli kweli, hii ilikuwa ni dharau kubwa kwa mtu wa aina yake. Akarejea Roma na kuahidi kumfundisha somo Gavana Francesco Cuccia na watu wa dizaini yake.
Aliporejea Roma akateua kikosi maalumu cha kijeshi kilichoitwa Carabineti na kukiagiza kwenda jimbo la Sicily kuwakamata na kuwafunga wanachama wote wa Mafia na wanaowashabikia.
Kikosi hiki cha kijeshi kilikuwa ni moja wapo ya vikosi vya weledi (special forces) vya jeshi la Italia na kijulikana kwa ukatili wake na ufanisi.
Kikosi kikaingia ndani ya Italia na kuanza msako wa wanachama wa Mafia Jimbo zima, kitongoji kwa kitongoji, mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.
Oparesheni yao ilikuwa na mafanikio makubwa kwani walifanikiwa kuwatia gerezani zaidi ya wanachama 11,000 wa Mafia na kuwaua wengine.
Kwa miaka kadhaa Mafia ikafutika kabisa kwenye jimbo la Sicily na nchi ya Italia kwa ujumla.
Lakini mabosi wa juu wa Mafia (Dons) wengi wao walifanikiwa kutoroka na kukimbia nchi kwenda kuishi uhamishoni. Hii ndio ilikuwa mojawapo ya sababu kuu ya Mafia kuenea nje ya nchi ya Italia.
Mfano Don Carlo Gambino na Joseph Bonanno walikimbilia nchini marekani mji wa New York na kwenda kuanzisha upya shughuli za mafia huko na kuwa moja ya Mafia waliofanikiwa zaidi katika historia ya mtandao huu wa kihalifu.
MAFIA WANAANZA KUJIJENGA TENA UPYA.
'Habari njema' kwa mafia ilikuwa ni pale ilivyoanza vita kuu ya pili ya dunia.
Baada ya vita kukolea, majeshi ya umoja wa magharibi yakiongozwa na marekani (Allied Forces) mwaka 1943 yakavamia Italia na zaidi ya wanajeshi nusu milioni.
Mojawapo ya miji ya kwanza kabisa kuvamiwa na Majeshi ya Marekani na washirika wake ilikuwa ni jimbo la Sicily.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment