IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
*********************************************************************************
Simulizi : Kiapo Cha Jasusi
Sehemu Ya Kwanza (1)
DAR ES SALAAM 20/04/2032..
Saa kumi alasiri muda ambao jiji la Dar es salaam limezoeleka kuwa na pilika pilika nyingi za wakaazi lakini kwa siku hii ya leo hali ilikuwa tofauti sana na siku nyingine.Jiji lilikuwa kimya.Ni watu wachache tu walioonekana mabarabarani mida hii.Mitaa mingi na barabara zilikuwa tupu.Sehemu za starehe hazikuwa na watu na nyingi zilifungwa.Licha ya shughuli nyingi kusimama lakini Katika baadhi ya nyumba za ibada milango ilikuwa wazi na watu walionekana ndani wakifanya maombi.Juu angani kulitanda mawingu mazito meusi na mvua nyepesi iliyoambatana na upepo mkali ilikuwa inanyesha.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Hali hii iliyolikumba jiji hili kuu la kibiashara Tanzania ilitokana na onyo lililotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ikitahadharisha wakaazi wote wa jiji la Dar es salaam kubaki katika nyumba zao kufuatia kimbunga Oba chenye kasi na nguvu kubwa kuikaribia pwani ya Dar es salaam.Kabla ya kufika pwani ya Dar es salaam kimbunga Oba kilipiga pwani ya Madagascar na kuleta maafa makubwa sana kikiwaacha maelfu ya watu wakikosa makazi na mamia kufariki.Kwa vipimo vya wataalamu kimbunga hiki kiliendelea kuongezeka ukubwa na kasi kila knavyozidi kuikaribia pwani ya Dar es salaam na litabiriwa kwamba kitapiga pwani ya jiji la Dar es salaam kuanzia saa kumi na mbili za jioni.
Mamlaka zinazohusika na majanga tayari zilikwisha jiandaa kukabiliana na athari zitakazotokana na kimbunga Oba.Jeshi la wananchi wa Tanzania nao walikwisha jiandaa kwa ajili ya kutoa msaada wa haraka pindi utakapohitajika.Wote wanaoishi sehemu za mabondeni walihamishwa na kutafutiwa makazi ya muda ili kuepuka mvua kubwa zitakazoambatana na kimbunga hicho zinazoweza kusababisha mafuriko makubwa.Kwa ujumla serikali na vyombo vyake vya majanga na uokozi walikwisha jiandaa vya kutosha kuweza kukabiliana na athari za tufani hii kubwa kuwahi kulikumba jiji la Dar es salaam.
Katika ikulu ya Dar es salaam,Dr Enock Mwaibule rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alihamishiwa katika makazi salama ya rais yaliyopo chini ya jengo la ikulu ambako hutumika kumuhifadhi rais ,familia yake na viongozi wote wa juu wa serikali nyakati zile za hatari.Akiwa huku chini rais huendelea kufanya kazi zake zote kwani ni sehemu iliyo na kila kitu anachohitaji kumuwezesha kufanya kazi zake.
Katika chumba cha mikutano rais,makamu wa ras,waziri mkuu na baadhi ya mawaziri wa wizara kadhaa walikuwa wanafuatilia mwenendo wa kimbunga Oba kupitia runinga kubwa iliyokuwa ukutani vile vile walikuwa wakipokea taarifa za hatua mbali mbali zinazoendelea kuchukuliwa na vikosi mbali mbali vya uokozi vilivyosambaa kila kona ya jiji la Dar .
Saa kumi na mbili na dakika ishirini na tisa mvua kubwa ikaanguka katika jiji la Dar es salaam ikiambatana na upepo mkali .Tayari kimbunga Oba kilikwisha wasili katika pwani ya Dar es salaam kikiwa na nguvu kubwa sana.
Wakati rais Enock na wasaidizi wake wakiendelea kufuatilia hali ya mambo simu ya Dr Enock ikaita akatazama mpigaji halafu akawaomba radhi viongozi wale aliokuwa nao akatoka nje ya chumba kile kwa ajili ya kuipokea.Alikwenda hadi katika chumba cha mazungumzo ya faragha akajifungia humo halafu akampigia yule mtu aliyempigia
"Mheshimiwa rais habari za muda huu? ikasema sauti nzito upande wa pili
"Mheshimiwa jaji mkuu,habari yangu ni nzuri ninafuatilia hali ya kimbunga inavyoendelea.Wewe uko sehemu salama?
"Mimi niko salama kabisa mheshimiwa rais"
"Nafurahi kusikia hivyo"
"Mheshimiwa rais nimekupigia ili tuzungumze kidogo.Nilipenda sana kama ningezungumza nawe ana kwa ana kwani sipendi sana kutumia njia ya simu kwa maongezi nyeti lakini kwa hali ilivyochafuka leo sintaweza kufika huko kuonana nawe"
"Usijali mheshimiwa jaji mkuu simu yangu hii ni salama kabisa na usiogope kunieleza kitu chochote.Hii ni simu ya rais na haiwezi kudukuliwa" akasema Dr Enock
"Ahsante sana mheshimiwa rais.Nilitaka tuzungumze kuhusu suala la rais mstaafu Dr Alfredo kitwe"
"Ndiyo nakusikiliza mheshimiwa" akasema rais
"Kesho kama tukijaaliwa uzima ndiyo siku ya hukumu yake"
"Oh kumbe ni kesho.Nimesahau kabisa.Nimejielekeza sana katika suala la hiki kimbunga nikasahau kuhusu Dr Alfredo "akasema Dr Enock
"Mheshimiwa rais,kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka,mahakama imejiridhisha kwamba mheshimiwa rais mstaafu Dr Alfredo ana hatia na anastahili adhabu kwa kosa alilolitenda wakati akiwa madarakani.Kesho hukumu hiyo itasomwa na mimi mwenyewe ambaye ndiye niliyekuwa kiongozi wa jopo la majaji waliosikiliza kesi hiyo.Ninataka kusikia maoni yako kabla ya hukumu haijasomwa hapo kesho.Una mawazo yoyote kuhusiana na mheshimiwa Dr Alfredo kitwe?akauliza mheshimiwa jaji mkuu wa Tanzania profesa Sixmund Mlekwi.Dr Enock akakaa kimya akavuta punzi ndefu halafu akasema
"Adhabu gani atakayoipata Dr Alfredo kitwe?
"Ni adhabu ya juu kabisa kwa kosa la mauaji ambayo ni kifungo cha maisha gerezani"
Akavuta pumzi ndefu tena akatafakari na kusema
"Natamani adhabu ya kifo isingeondolewa kwani ndiyo anayostahili mtu kama yule.Lakini hata hiyo ya kifungo cha maisha gerezani inamfaa pia ila ongeza na kazi ngumu.Anapaswa apate mateso makali"
"Mheshimiwa rais hiyo ni adhabu ya juu kabisa tuliyonayo kwa kosa la mauaji.Hata hivyo huyu jamaa tayari anakaribia miaka sitini na nane ni mzee tayari na hata afya yake hairidhishi.Unaonaje mheshimiwa rais endapo tukimpunguzia adhabu na kumpa kifungo cha miaka kadhaa gerezani kuliko adhabu ya kifungo cha maisha?
"No ! akasema Dr Enock
"Dr Alfredo hapaswi kuonewa huruma hata kidogo.Alistahili adhabu ya kifo lakini kwa vile hatuna adhabu hiyo kwa sasa basi afungwe maisha gerezani ili afie huko huko" akasema Dr Enock
"Nimekuelewa mheshimiwa rais.Ahsante sana kwa maoni yako"
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"Ahsante sana mheshimiwa jaji mkuu na hongera sana kwa kuifanikisha kesi hii.Nakutakia kila la heri katika kuisoma hukumu hiyo hapo kesho" akasema Dr Enock na kukata simu
"Bazazi yule anastahili adhabu kali sana.Anatakiwa apate mateso makali ili ajutie unyama alioufanya.Atateseka mno na ataomba Mungu amchukue lakini hatakufa.!! akawaza Dr Enock halafu akarejea tena katika chumba kile maalum wakiendelea kufuatilia hali ilivyokuwa inaendelea jijini Dar es salaam kufuatia kimbunga Oba
21/04/2032
Habari kuu iliyotawala vyombo vingi vya habari vya ndani na nje ya nchi ni kuhusiana na kimbunga Oba kilichopiga jiji la Dar es salaam na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu ikiwemo na vifo kadhaa huku idadi kubwa ya wananchi wakiachwa bila makazi.Barabara nyingi hazikuwa zikipitika kutokana na kujaa maji na nyingine kufunikwa na miti iliyoangushwa kufuatia mvua kubwa iliyoonyesha takribani usiku kucha ikiambatana na upepo mkali sana.Nyumba nyingi zilizojengwa sehemu za mabondeni zilifunikwa na maji na nyingine kusombwa.Huduma ya umeme ilikatika karibu sehemu kubwa ya jiji kutokana na nguzo nyingi kuanguka.Kwa ujumla hali ya jiji la Dar es salaam ilikuwa mbaya na vikosi vya uokozi vikisaidiana na vile vya jeshi la wananchi na polisi pamoja na watu waliojitolea vilikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha huduma za muhimu kama vile maji safi na umeme vinarejea kwa muda mfupi.Waathirika wa kimbunga Oba walikusanywa katika kambi maalum na kupatiwa mahitaji ya muhimu.
Wakati watu wakiendelea na jitihada za kukabiliana na athari za kimbunga Oba kuna tukio kubwa lilitokea nchini Tanzania ambalo wengi hawakulisikia au kulitilia maanani kutokana na wengi kujielekeza katika athari za kimbunga.Mahakama kuu ya Tanzania iliwakuta rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr Alfredo kitwe na wenzake kumi na sita na hatia kwa kosa la mauaji ya kukusudia wakati wa utawala wa rais huyo hivyo kuwahukumu kifungo cha maisha gerezani.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,rais kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya wakati akiwa madarakani.Hii iliwezekana baada ya kifungu cha katiba kinachozuia rais kutokushtakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa madarakani kurekebishwa na kuruhusu rais kuweza kushtakiwa kwa makosa aliyoyatenda wakati akiwa madarakani .
Mara tu baada ya adhabu ile kutolewa,rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyepo madarakani Dr Enock Mwaibule akampigia simu kamishna mkuu wa magereza Tanzania na kumuelekeza kwamba Dr Alfredo akafungwe katika gereza la Markubelo lililopo katika kisiwa cha Markubelo lenye ulinzi mkali mno.Alisisitiza pia kwamba Dr Alfredo asiruhusiwe kuonana na mtu yeyote hata familia yake.
"Hatimaye yametimia na moyo wangu una amani kubwa.Naamini hata wale ambao wapendwa wao waliuawa wakati ule watakuwa na furaha iliyopitiliza. Dr Alfredo hatasamehemwa kamwe ni kama vile ambavyo Mungu hawezi kumsamehe shetani.Ataozea gerezani.Atapata mateso makali na atakufa taratibu" akawaza Dr Enock huku uso wake ukiwa na tabasamu akampigia simu mke wake na kumpa habari ile ambao kwao ilikuwa ni habari njema sana.
MIAKA KUMI BAADAE - 2044
Tayari imetimia miaka kumi toka Dr Alfredo alipoanza kutumikia adhabu yake ya kifungo cha maisha gerezani.Kiumri ametimiza miaka sabini na nane.Kwa kipindi chote ambacho amekuwa gerezani hali yake ya kiafya imekuwa si nzuri na kwa muda wa mwaka mmoja sasa amekuwa kitandani akisumbuliwa na maradhi ya mgongo.Amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya gereza lakini baada ya madaktari kutokuona mafanikio, walipendekeza ahamishiwe katika hospitali kubwa ili aweze kufanyiwa upasuaji wa mgongo.Ilimlazimu mkuu wa gereza kutuma maombi maalum wizara ya mambo ya ndani ili apewe ruhusa ya kumuhamishia Dr Alfredo katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi kwani hali yake ilizidi kuwa mbaya siku hadi siku.Jitihada alizozifanya mkuu wa gereza hazikuweza kuzaa matunda kwani jibu alilopewa ni kwamba Dr Alfredo anatakiwa kutibiwa katika hospitali ile ya gereza na haruhusiwi kutoka nje ya gereza.
Akiwa ofisini kwake,kamishna msaidizi Dastan Mwaikambe mkuu wa gereza la Markubelo alikuwa amejiegemeza kitini akionekana kuzama katika mawazo
"Ni kawaida pale mfungwa anapohitaji matibabu makubwa zaidi ambayo hapa katika hospitali yetu ya gereza hatuwezi kuyatoa tunaomba kibali cha kumpeleka katika hospitali kubwa kutibiwa na huwa hakuna tatizo lolote.Kwa nini mzee huyu anafanyiwa hivi?Kwa nini imekuwa vigumu kutoa ruhusa akapatiwe matibabu nje ya gereza? Dastan akatolewa mawazoni baada ya mlango wake kugongwa akaingia Dr Williamn Mnonge daktari mkuu wa gereza.
"Karibu sana Dr William.Imekuwa vyema umekuja kwani nilikuwa najiandaa kuja ofisini kwako" akasema Dastan.
"Ahsante Mr Dastan" akasema Dr William na kuketi kitini
"Nimetoka kumtazama mzee Dr Alfredo kitwe,hali yake inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.Kuna taarifa yoyote kutoka wizarani?Wametoa kibali cha kwenda kumtibu Dr Alfredo nje ya gereza?akauliza Dr William
"Hilo ndilo lililotaka kunileta kwako ili tujadili.Nimepokea majibu leo hii kutoka makao makuu na wamekataa kutoa kibali cha Dr Alfredo kwenda kutibiwa nje ya gereza badala yake wamesema watawatuma madaktari bingwa kuja kumtibu hapa hapa gerezani" akasema Dastan na Dr William akainamisha kichwa
"Poor Dr Alfredo kitwe.Kwa nini wanamfanyia hivi? akauliza
"Dr Wiliam hilo ni suala ambalo liko nje ya uwezo wetu.Hatuwezi kupingana na maamuzi ya wakubwa zetu" akasema kamishna Dastan
"Hata wakiwatuma hao madaktari bingwa hawataweza kumtibu Dr Alfredo kitwe"akasema Dr William
"Kwa nini unasem hivyo Dr William? akauliza Dastan
"Nilikueleza kwamba nimetuma sampuli kwa siri katika maabara moja kubwa ili kujua nini hasa kinachomsumbua huyu mzee na leo nimepewa majibu.Kinachomsumbua huyu mzee ni saratani ya uti wa mgongo"
"oh my God ! Dastan akastuka
"Kuna namna yoyote ya kuweza kuitibu saratani hiyo?
"Kwa hatua ilipofikia haitawezekana kutibiwa tena."
"Thats means Dr Alfredomust die? Akauliza Dastan
"Yes .Matibabu anayoweza kupatiwa ni kwa ajili ya kuongeza siku zake za kuishi lakini hataweza kupona.Saratani imefikia katika hatua mbaya.Inasikitisha sana namna huyu mzee alivyotengwa kama vile hakuwahi kuwa mtu mkubwa hapa nchini.Wakati wa utawala wake aliwahi kufanya mambo mengi mazuri lakini yote hayo yamesahaulika na leo hii hakuna anayetaka hata kusikia habari zake.Tutamsaidiaje? akauliza Dr William
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"We have to tell him the truth.Anatakiwa afahamu kuwa hataweza kupona ili aanze kujiandaa" akasema Dastan
"Hilo litakuwa ni jambo jema.Twende wote tukaonane naye na tumueleze kuhusu suala hili"akasema Dr William wakaongozana hadi katika chumba alimolazwa Dr Alfredo kitwe
"Mzee Dr Alfredo shikamoo" Dastan akamsalimu Dr Alfredo ambaye alifumbua macho akamtazama
"Marahaba kijana wangu" akajibu mzee Dr Alfredo akionekana kuwa katika maumivu makali sana
"Vipi unaendeleaje?akauliza Dastan na kuvuta kiti akaketi.
"Hali yangu ni kama unavyoiona hakuna afadhali yoyote ninamuomba Mungu anichukue tu nikapumzike kwani mateso haya ninayoyapata ni makali sana"akasema Dr Alfredo kitwe
"Pole sana mzee wangu.Nilituma maombi makao makuu kuomba kibali kwa ajili ya kukutoa hapa nikupeleke katika hospitali kubwa nje ya gereza ukafanyiwe upasuaji lakini majibu niliyopewa si mazuri" akanyamaza na kumtazama mzee yule pale kitandani halafu akaendelea
"Wamekataa ombi langu na wanataka utibiwe hapa hapa ndani ya gereza.Wamesema watatuma madaktari bingwa kuja kukufanyia upasuaji hapa hapa"akasema Dastan halafu chumba kikawa kimya kwa muda.
"Mzee Dr Alfredo kuna jambo lingine pia ambalo Dr William anataka kukueleza" akasema Dastan na Dr William akamsogelea Dr Alfredo kitwe
"Mzee nilituma sampuli katika maabara ili kujua nini hasa kinachokusumbua na majibu yamerudi kwamba unasumbuliwa na saratani ya uti wa mgongo."
"Oh my God ! akasema Dr Alfredo na kuwatazama Dastan na Dr Wiliam halafu akasema
"You are scared to say, but I can read your faces.I'm going to die soon ,right? akauliza mzee Dr Alfredo kitwe.Dastan na Dr William wakatazamana kisha Dr William akasema
"Mzee lazima tuwe wakweli kwamba kwa mahala ilipofikia kansa hii haitaweza kutibika hivyo lazima utakufa" akasema Dr William na licha ya kuwa katika maumivu sura ya mzee Dr Alfredo ikaonyesha tabasamu kwa mbali
"Thats what I want.To die ! akasema Dr Alfredo na kuwatazama akina Dastan
"How many days do I have? akauliza
"I'm not sure but you dont have much time" akasema Dr William na kuitoa simu yake mfukoni iliyokuwa ikiita akazungumza na mpigaji halafu akamgeukia Dastan
"Mr Dastan nimeitwa kuna mgonjwa anahitaji huduma ya haraka.Tutaonana baadae" akasema Dr william na kutoka
"Dastan ahsante sana kwa kujaribu kunisaidia kijana wangu lakini nakuomba usisumbuke tena kwani kama alivyosema mwenzako sina maisha marefu.Ninashukuru umekuwa msaada mkubwa kwangu.Toka ulipofika hapa maisha yangu yamekuwa na ahueni kubwa.Umenisaidia sana katika mambo mengi.Walionileta hapa walikuwa na lengo nipate mateso makali hadi kufa lakini imekuwa tofauti.Nimeishi maisha mazuri mno japokuwa ni ya upweke mkubwa" akasema Dr Alfredo kitwe
"Mzee usikate tamaa.Nitafuatilia ili madaktari hao bingwa waweze kufika hapa kwa wakati na kukuhudumia ili uweze kuwa na siku nyingi zaidi.Mungu pekee ndiye muweza wa yote na ukimtegemea yeye hatakuacha kamwe na kwa sasa ni muhimu mno kujiweka karibu naye"
"Sitaki nipone kijana wangu.Nina miaka sabini na nane sasa na nimekwisha ishi vya kutosha ni wakati sasa wa kwenda kupumzika" akanyamaza na kufumba macho akijaribu kugeuka upande wa pili,Dastan akainuka na kumsaidia kugeuka
"Ahsante kijana" akasema mzee Alfredo
"Mungu atakusaidia mzee utapona" akasema Dastan
"Nimesema sitaki kupona.Nataka nife japo nataka nife kwa amri ya Mungu,sitaki kujiua.Nitavumilia mateso haya hadi pale Mungu atakaponiita" akasema Dr Alfredo halafu akamtazama kamishna Dastan kwa makini
"I can feel death" akasema kwa sauti ya chini
"I can feel it and I'm scared" akanyamaza tena akatazama juu kwa muda
"Hakuna mwanadamu anayetamani kufa.Kifo hakizoeleki na ndiyo maana tunapambana kwa kila hali kujitahidi kupata matibabu ya kina ili tusife lakini siku ikifika hakuna wa kuweza kuizuia zaidi ya Mungu mwenyewe" akasema Dastan
"Una roho nzuri sana kijana lakini ninasikitika kwamba hakuna kitakachofanyika ili kunipa mimi uhai mrefu zaidi.Siku zangu zimemalizika kabisa.It's over.Lakini....." akasema Dr Alfredo na kunyamaza akafumba macho kwa muda halafu akamtazama Dastan na kumfanyia ishara asogee karibu.
"Kuna kitu kimoja ambacho nataka unisaidie"akasema Dr Alfredo
"Sema mzee nikusaidie nini?
"Kwa miaka kumi sasa sijawahi kuonana na familia yangu na ninaamni hawajui nimefungwa gereza gani na hata kama wangefahamu wasingeruhusiwa kuja kuniona.Hii ni adhabu nyingine kubwa niliyopewa.Sitaki kufa bila kuonana na familia yangu hata kama ni kwa siri.Ninakuomba japo kwa siku moja tu unisaidie niweze kuonana na familia yangu.Ni muhimu sana" akasema Dr Alfredo
"Mzee ninatamani sana kukusaidia kuitafuta na kuileta familia yako hapa gerezani lakini tumepewa maelekezo na wakubwa kwamba asiruhusiwe mtu yeyote kuja kukuona na hapa gerezani kuna watu maalum wamewekwa kwa siri kukufuatilia na kuchunguza namna unavyoishi na kama kuna mtu yeyote anakuja kukuona na endapo nikithubutu kuitafuta familia yako na kuwaleta hapa habari zitafika huko kwa wakubwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yangu"akasema Dastan
"Nimekuelewa kijana wangu na sitaki kukuingiza katika matatizo kwani umekuwa msaada mkubwa kwangu lakini kuna kitu nataka unisaidie kukifanya.Naomba kalamu na karatasi" akasema Dr Alfredo na Dastan akampatia kalamu na karatasi kisha akaandika maneno machache katika karatasi ile na kumpatia.
"Karatasi hii naomba uipeleke Parokia ya Mt Elizabeth iliyoko Peninsula na umuulizie padre mmoja anaitwa Thadei Ambrosi.Ukimpata mwambie karatasi hii imetoka kwangu na ahakikishe inamfikia Mariana"
"Sawa nitafanya hivyo.Ni vipi endapo nitamkosa? Kuna mtu mwingine ninaweza kumpatia?
"Hakikisha unampata huyo huyo Padre yeye anajua ni wapi pa kumpata Mariana.Jitahidi sana ni muhimu mno kwangu.Huu ni msaada mkubwa ambao unaweza kunisaidia katika siku hizi chache zilizobaki.Nataka kuonana na Mariana" akasema Dr Alfredo kitwe
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"Huyu Mariana ni nani? Endapo nitamkosa huyu Padre Thadei kwa nini nisimtafute huyo Mariana na kumpa huu ujumbe?akauliza Dastan
"Nimekutuma kwa padre Thadei kwa ajili ya usalama wako.Mariana huwezi kumuona hivi hivi ni hatari sana kumfikia.Endapo utamkosa padre Thadei nitakuelekeza sehemu nyingine"
"Sawa mzee nitafanya hivyo.Nitahakikisha leo hii hii ujumbe huu unamfikia muhusika"akasema Dastan
"Nashukuru sana kijana wangu kwa msaada huu mkubwa ila ninakuonya uwe makini sana wakati ukipeleka ujumbe huu.Hakikisha hakuna yeyote anayefahamu kama nimekutuma zaidi ya padre Thadei" akaonya Dr Alfredo kitwe
"Nitajitahidi mzee usihofu" akasema Dastan na kutoka ndani ya kile chumba na moja kwa moja akaelekea ofisini kwake akajiegemeza kitini.Akatafakari yale yote aliyoyazungumza na Dr Alfredo halafu akakikunjua kile kijikaratasi akakisoma
"Im dying.I have few days left.meet me before I die"
Huu ndio ujumbe aliouandika Dr Alfredo kitwe
"Mariana ni nani?Kwa nini Dr Alfredo hakutaka kunielekeza nikamuone? Kwa nini ni hatari kumfikia?akawaza Dastan
"Dr Alfredo amefungwa kwa miaka yapata kumi sasa na kwa muda huu wote hajawahi kutembelewa na mtu yeyote na hana taarifa zozote za kinachoendelea huko nje na kuna uwezekano mkubwa hata huyo padre Thadei ambaye anataka nimpe ujumbe huu yawezekana amekwisha fariki au amehamishwa kwani kwa ninavyofahamu hawa watumishi huwa hawakai sehemu moja kwa muda mrefu.Nadhani litakuwa ni jambo zuri kama nikimtafuta kwa simu na kuwa na uhakika kama kweli yupo katika parokia hiyo aliyonielekeza Dr Alfredo " akawaza Dastan na kumuomba katibu wake muhtasi amletee kitabu chenye orodha ya namba za simu za taasisi mbali mbali akaitafuta namba ya simu ya jimbo kuu la Dar es salaam na kupiga akaomba apatiwe namba za simu za parokia ya Mt Elizabeth.Akaombwa apige baada ya dakika tano akakata simu na kupiga tena baada ya dakika tano akapewa namba za parokia ya Mt Elizabeth kisha akapiga na kumuulizia padre Thadei.
"Kwa sasa Padre Thadei amekwenda katika huduma labda upige tena baadae" akasema mwanadada aliyepokea simu
"Niko mbali kidogo na Dar es salaam na ninao ujumbe wake muhimu je unaweza kunipatia namba zake za simu ya mkononi niwasiliane naye?akaomba Dastan na ikamlazimu yule mama amueleze padre Dastan kwamba kuna mtu anataka kuzungumza naye kupitia simu yake ya mkononi na akaruhusiwa kumpa namba na bila kupoteza muda Dastan akapiga
"Hallo Padre Thadei"
"Hallo.Habari yako ndugu"
"Nzuri kabisa.Natumai hunifahamu.Ninaitwa Dastan Mwaikambile mkuu wa gereza la Markubelo"
"Nafurahi kukufahamu ndugu Dastan.Mimi naitwa Father Thadei Ambrose niko parokia ya Mt Elizabeth.Nikusaidie nini Dastan?akauliza padre Thadei
"Father Thadei nina ujumbe wako nimepewa nikupe umpatie Mariana"
Padre Thadei akasikika akivuta pumzi ndefu
"Padre Thadei" akaita Dastan
"Ujumbe huo umepewa na nani?
"Nimepewa na rais mstaafu Dr Alfredo Kitwe ambaye amefungwa hapa gerezani"
“oh Mungu wangu ! akasema Padre Thadei
"Dr Alfredo amefungwa katika gereza hilo?akauliza
"Ndiyo amefungwa hapa"
"Ujumbe huo unasemaje?
"Nitaupiga picha na kukutumia ujumbe huu katika simu yako ili uufikishe mahala husika"
"Vipi kuhusu hali ya Dr Alfredo kitwe?Anaendeleaje?akauliza padre Thadei
"Dr Alfredokwa sasa anaumwa sana na hali yake si nzuri hata kidogo"
"Nashukuru sana kwa taarifa hii.Tumekuwa tukihangaika kwa muda mrefu kujua mahala alikofungwa bila mafanikio.Nini hasa kinachomsumbua?
"Anasumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo na kwa mujibu wa madaktari hana muda mrefu wa kuishi" akasema Dastan
"Ahsante Dastan kwa taarifa hizi njema.Tafadhali naomba asifahamu mtu yeyote kama umepewa maagizo na Dr Alfredo unipatie mimi" akasema padre Thadei na kukata simu
"Padre Thadeo anadai wamekuwa wakitafuta gereza alikofungwa Dr Alfredo kwa muda mrefu bila mafanikio je naye ni mmoja wa wanafamilia? Huyu Mariana ni nani? akawaza Dastan na kuuchukua ujumbe ule wa Dr Alfredo akaukunja na kuutupa katika chombo cha takataka akatoka na kwenda kuendelea na shughuli zake.
IKULU DAR ES SALAAM 2044
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Enock Mwaibule alimaliza vipindi viwili vya utawala wake wa miaka mitano mitano kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Akiwa katika kipindi chake cha mwisho Dr Enock ambaye ni rais aliyetokea kupendwa sana na wananchi kwa mambo makubwa aliyoyafanya katika uongozi wake,alibadili vifungu kadhaa vya katiba na kuondoa kifungu cha katiba kinachoweka ukomo wa uongozi wa rais kuwa wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano na kuweka kifungu kingine ambacho kiliongeza muda wa rais na kuwa wa vipindi vitatu vya miaka nane.Mabadiliko hayo yalipelekwa kwa wananchi na kutokana na ushawishi mkubwa uliofanywa na kwa maendeleo aliyoyafanya wananchi wakayapitisha kwa kura ya maoni na hivyo kumuwezesha Dr Enock kuwa rais wa kwanza kuanza kutumikia kipindi cha miaka nane baada ya kumaliza miaka kumi katika uongozi.Suala hili la kuongeza muda wa rais lilipigiwa kelele mno na jumuiya ya kimataifa lakini kwa vile wananchi waliamua kuyapitisha mabadiliko yale kelele za jumuiya ya kimataifa hazikusaidia kitu.
Katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake Dr Enock alifanya mambo mengi makubwa kiasi cha kuipaisha Tanzania kiuchumi na kuwa rais aliyeingia katika historia baada ya kufanikiwa kuiiingiza Tanzania katka nchi ya kipato cha kati.Uchumi wa Tanzania uliimarika na kuwa ni taifa kubwa la pili kwa kuwa na uchumi mkubwa barani Afrika likitanguliwa na Afrika kusini.Viwanda vingi vilijengwa na kuleta ajira kwa watu wengi,miundo mbinu ya barabara na reli ilijengwa hadi vijijini na hivyo kurahisisha usafiri kwa mazao ya wakulima vijijini kufika sokoni kiurahisi.Serikali ilivuna pesa nyingi sana kutokana na rasilimali zake kama madini,mafuta na gesi na hivyo kufanya elimu ya kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita kuwa bure,huduma za afya pia ziliboreshwa na gharama zake kuwa ndogo sana kiasi cha kumuwezesha kila mwananchi kumudu.Kwa ujumla mambo mengi yalifanyika katika kipindi hiki cha miaka kumi na hii ndiyo sababu wananchi waliyapokea na kuyapitisha mapendekezo ya kubadili ukomo wa uongozi na rais Dr Enock akaendelea kutawala wakiamini endapo atakaa kwa muda mrefu zaidi nchi itapiga hatua kubwa kimaendeleo.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Alipoanza kutumikia kipindi chake kingine cha miaka nane Dr Enock alihamisha makazi ya rais kutoka Dodoma yaliko makao makuu ya nchi na kurejea Dar es salaam huku akianza mchakato wa kubadili makao makuu ya nchi kuwa Dar es salaam badala ya Dodoma.Alikuwa ni rais aliyejilimbikiza utajiri mkubwa sana nje ya nchi na alifanya mambo yake kwa siri.Hakutaka kupingwa na mtu yeyote na kila aliyeonekana kwenda kinyume naye alizimishwa kimya kimya.Wengi hususan viongozi waliopo serikalini na hata wale wa vyama pinzani walikuwa wanamuogopa sana kwani neno lake moja tu lilikuwa na uwezo wa kuondoa uhai wa mtu.Alikuwa ni rais asiyekaukiwa tabasamu usoni lakini kwa walio karibu yake wanalifahamu tabasamu hilo ni la kinafiki kwani hulitumia kuwahadaa wananchi huku roho yake ikiwa na ukatili usiopimika.
Dr Enock alikuwa na kikundi chake maalum cha siri ambacho hukitumia katika kufanikisha mambo yake mbali mbali ya siri kilichopewa jina la 100CHITAS.Hiki ni kikundi hatari sana kilichosheheni watu wenye ujuzi wa hali ya juu sana katika ujasusi.Ni kikundi kilichopenyeza mtandao wake sehemu mbali mbali hivyo kuweza kupata taarifa kirahisi za kila kinachoendelea nchini.Wanatumia teknolojia ya hali ya juu sana katika kuhakikisha wanapata taarifa nyeti wanazozihitaji.Lengo lao kuu la kuhakikisha rais anakuwa salama na nchi inakuwa salama kwa kupata taarifa ambazo vyombo vingine vya ulinzi na usalama haviwezi kuzipata kirahisi na kwa haraka.Kikundi hiki hakikujulikana serikalini na hakikuwa na bajeti ya kukiendesha ni Dr Enock pekee aliyefahamu zilikotoka fedha za kuendesha kikundi hiki ambacho kilitumia gharama kubwa mno kujiendesha.Kupitia kikundi hiki Dr Enock hakuwa na wasi wasi na maisha yake na aliamini kuwa anayeweza kuchukua uhai wake ni Mungu pekee.
Akiwa ofisini kwake simu yake ikaita na mpigaji alikuwa ni CT 01 Noah.Akainuka na kusogea pembeni kisha akaipokea ile simu
"Hallo Noah" akasema Dr Enock
"Mzee nimepokea taarifa kutoka gereza la Markubelo kwamba mkuu wa gereza hilo kamishna msaidizi Dastan amepewa ujumbe na Dr Alfredo aupeleke mahala fulani na mara tu baada ya kupewa ujumbe huo alisikika akiwasiliana na mtu fulani katika simu.Kwa mujbu wa mtu tuliyemuweka pale gerezani kwa ajili ya kutupa taarifa anadai kwamba aliingia ofisini kwa Dastan na kuchambua katika chombo cha takataka akafanikiwa kuvipata vipande vya karatasi ile ambayo Dr Alfredoalimpatia Dastan na baada ya kuiunganisha ilisomeka hivi "I'm dying.I have few days left.Meet me before I die"
Dr Enock akavuta pumzi ndefu na kusema
"Inaonyesha kuna mahala Dastan ametumwa aupeleke ujumbe huu.Lakini kwa nini autupe badala ya kuupeleka sehemu husika?
"Mara tu alipotoka kuonana na Dr Alfredo aliomba apatiwe kitabu cha simu chenye namba za taasisi mbali mbali na akasikika akipiga simu.Hakutumia simu ya ofisi bali alitumia simu yake ya mkononi"
"Mnaweza kufuatilia na kujua alimpigia nani na walizungumza nini?
"kwa bahati mbaya hatuna namba ya simu aliyoitumia kupiga.Amekuwa akiificha mno namba yake binafsi ya simu ya mkononi na huwa anaitumia mara chache sana.Mara nyingi hutumia simu ya ofisi au simu ya mkononi yenye laini inayotambuliwa na ofisi"
"Hiyo si kauli ya kuzungumza mtu kama wewe Noah.Go get that phone.Fuatilia ujue alikuwa anazungumza na nani na walizungumza nini.Nataka hadi saa mbili usiku wa leo niwe tayari nimepata majibu.Umenielewa?
"Ndiyo mzee nimekuelewa" akasema Noah
"Dr Alfredo anajua kwamba hawezi kupona na sasa anataka kuonana na watu wake wa karibu,kuna mambo naamini anataka kumueleza mtu huyo anayetaka kuonana naye.Siwezi kumpa hiyo nafasi ya kuonana na mtu yeyote.Familia yake wataiona maiti yake ndani ya jeneza na hawatamuona akiwa hai!! akawaza Dr Enock huku akiuma meno kwa hasira.
****************
Ni saa kumi na moja za jioni katika kisiwa cha Markubelo,kilichopo katika bahari ya Hindi ambacho kwa mujibu wa wataalamu kipo kati kati ya Dar es salaam na Pemba,Kamishna msaidizi Dastan Mwaikambile mkuu wa gereza la Markubelo baada ya kumaliza kazi zake za siku alikuwa amevalia mavazi yake ya kuogelea akapakia vifaa vyake katika boti yake ndogo tayari kuingia baharini kuvua samaki na kuogelea.Kila siku akitoka kazini huenda baharini kuvua samaki na kuogelea.Alihakikisha vifaa vyake vyote anavyovihitaji vipo halafu akawasha boti yake na kuelekea baharini kuvua samaki.Alifika mahala ambako aliona panafaa akazima boti na kabla hajaanza kuvua akasikia muungurumo wa boti kwa mbali,akatoa kiona mbali na kuangaza pande zote akafanikiwa kuiona boti moja ndogo ikija kwa kasi ikimfuata.Akaivuta karibu zaidi na kuona ndani yake kulikuwa na watu wanne lakini kilichomstua zaidi ni baada ya kumuona mmoja wa watu wale akiwa na bunduki kubwa yenye uwezo wa kulenga masafa marefu.
"Ni akina nani hawa watu?Ni majambazi?akajiuliza na kwa haraka akavaa mtungi wake wa gesi ,akachukua begi lake dogo lisilopenya maji lililokuwa na vitu vyake muhimu akalifunga kiuoni halafu akajirusha majini.Ile boti iliyokuwa inakwenda kwa kasi kubwa ikafika katika boti ya Dastan iliyokuwa tupu.
"Amekwenda wapi?akauliza mmoja wao
"Huyu yawezekana akawa ni shetani.Mbona amepotea ghafla?akauliza mwingine
"Fred ingia katika boti yake chunguza kama simu yake anayo" akasema mmoja aliyeonekana kama kiongozi wao na yule jamaa aliyepewa maelekezo akatoka katika boti yao akarukia katika boti ya Dastan akapekua kila mahali na wakati akiendelea na zoezi la kupekua ghafla Dastan akaibuka kwa kasi na kuachia risasi mfululizo kutoka katika bastora yake na kuwalenga wale jamaa waliokuwa wamebaki katika boti yao.Yule aliyekuwa ameingia katika boti yake akiipekua alipoona wenzake wameanguka kwa kupigwa risasi akachupa majini.Kilikuwa ni kitendo kilichotokea kwa haraka sana kiasi kwamba wale jamaa hawakuwa wamekitarajia.Yule jamaa alipochupa majini Dastan naye akazama majini na kuanza kuogelea akimfuata.Hakutaka kumuua alitaka kumpata akiwa mzima ili awafahamu ni akina nani.Kasi ya Dastan ilikuwa kubwa na akajikuta akimkaribia yule jamaa ambaye aligeuka ghafla na kumtandika Dastan teke zito na kuivunja miwani aliyovaa iliyokuwa inamsaidia kuogelea halafu akazama chini zaidi.Dastan akamfuata na alipomkaribia akavua mtungi wake wa gesi na kumpiga nao yule jamaa kichwani akaweweseka na kuanza kunywa maji.Aliishiwa nguvu.Haraka haraka akamshika mkono na kuanza kupanda naye juu.Hakuwa na fahamu.Akamtoa majini na kumpandsha katika boti yake akamfunga miguu na mikono kisha akaanza kumsachi akamkuta na shilingi laki nne na simu.
"who are these people?! akauliza Dastan na kurukia katika boti ya wale jamaa ambayo ilikuwa imetapakaa damu kila mahali akaanza kuwasachi na kuwakuta na bastora mbili na bunduki moja kubwa.
"Ni akina nani hawa?Wametokea wapi na kwa nini wananifuata?Ni majambazi?akajiuliza
"Walikuwa wamejiandaa vilivyo na kama nisingekuwa najiweza wangeniua.Lakini nini hasa lengo lao kwangu? akaendelea kujiuliza maswali halafu akaingia katika boti yake akaiwasha na kurejea gerezani.Alipomgusa yule jamaa aliyempiga na mtungi wa gesi akagundua kwamba hakuwa na uhai alikwisha fariki.Akawaelekeza askari wa gereza wende baharini na watakuta boti ikiwa na wale jamaa aliowaua ambao aliamini ni majambazi.Alipotoa maelekezo hayo akatembea taratibu kuelekea nyumbani kwake uku akitafakari.Tayari kiza kilikwisha anza kuingia.
"Watu wale kwa nini walikuwa wananifuata?Walifahamuje kama nimekwenda baharini kuvua samaki?Nini hasa walikihitaji kutoka kwangu? akajiuliza wakati akielekea nyumbani kwake.Mara tu alipofika katika mlango wa kuingilia ndani mwake akastuka.
"Some one was here" akawaza na kisha akachukua kile kibegi kidogo cha vitu vyake alichokuwa amekifunga kiuononi akatoa bastora yake na kukirusha kibegi kile katika maua taratibu akakiminya kitasa cha mlango akaingia ndani.Hakukuwa na mtu yeyote na taa ilikuwa imezimwa.Akawasha taa na kustuka baada ya kukuta sebule ikiwa imevurugwa hovyo.Kila mahala kulikuwa kumepekuliwa
"Watu wale naamini walikuwa hapa.wanatafuta nini kwangu? akajiuliza kisha akapiga magoti na kuanza kukusanya karatasi zilizotupwa chini.Mara ghafla akahisi kama kuna mtu ananyata nyuma yake akanyoosha mkono ili kuichukua bastora yake aliyokuwa ameiweka chini lakini akasikia sauti nyuma yake ikisema kwa ukali
"Hivyo hivyo ulivyo inua mikono yako juu halafu simama taratibu!!
Dastan bila ubishi akainua mikono juu na kisha taratibu akasimama
"Ipige teke bastora hiyo ije kwangu !! akaamuru tena yule jamaa na Dastan akafanya kama alivyoamriwa kisha yule jamaa akamuamuru jamaa mwingine akamfunge pingu mikononi
"Geuka unitazame!! ikasema sauti ile na Dastan akageuka taratibu akawakuta watu watatu wakiwa wamefunika nyuso zao.
"Ninyi ni akina nani?akauliza
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"Tunahitaji kitu kimoja tu kutoka kwako."akasema yule jamaa hukua kiwa amemuelekezea Dastan bastora
"Mnahitaji nini ?akauliza Dastan
"Simu yako iko wapi?
"simu yangu?
"Ndiyo iko wapi?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment