Simulizi : Mwanamke Mwenye Juba Jeusi
Sehemu Ya Tatu (3)
Punde Kishime, aliinua kichwa kutoka pale mezani alipojilaza baada ya kwisha kikao kile, mawazo yalimchukua nyuma kabisa ya ujana wake na kumrudisha Makutopola. Nafsi yake bado iliendelea kupigana na maamuzi yake lakini hakujua ni nini afanye, uzalendo ulimsuta, tamaa ilimtawala. Alinyanyuka kutoka pale alipo na kuuendea mlango wa kutokea.
Siku hiyo kwake ilikuwa ni ndefu mno ‘siku ndefu mno’, alicheka kidogo alipoikumbuka simulizi hii aliyowahi kuisoma huko Tanzania miaka ya nyuma. ‘nikubali, nisikubali?’ alijiuliza na kukosa majibu yeye mwenyewe...
‘Tutakaa masikini mpaka lini, wakati wenyewe wananenepesha matumbo yao sisi kazi kuwawekea saini tu wavute mahela’ bado Mh Punde Kishime alijiuliza maswali mengi sana lakini majibu yalikuwa machache, mara alikunja sura na mara alicheka yote yalijichanganya ndani ya sura moja ya mzee huyu wa makamo ambaye Taifa linamtegemea hasa katika kupambana na wala rushwa. Kazi kubwa iliyomkabili ni kumshawishi Mh Chakwima, kila alipolikumbuka hilo alijikuta anakuwa mzito mwili na roho kwa kuwa alimjuwa wazi Chakwima jinsi alivyo muaminifu katika kazi yake, mtiifu kwa serekali yake na mstari wambele katika chama chake ‘nitaanzia wapi?’ au ‘nitamshawishi nini’.
Punde Kishime alijinyanyua kutoka katika kiti kile na kuelekea katika chumba alichooneshwa, aliingia na kuketi, mezani kulikuwa na vinywaji aina aina, yeye aliviangalia vyote lakini hakuvutiwa na hata kimojawapo kwani mawazo yako yalishachanganywa na mambo mengi sana. Msichana mrembo aliyekuwa jirani naye alizunguka nyuma ya kiti alichokaa Mh Kishime na kuanza kumminyaminya mabegani, Mh Punde Kishime alihisi mwili wake kufa ganzi mara kwa mara alishusha pumzi ndefu, ni wawili hao tu waliokuwa ndani ya chumba hiko, Kishime alimshika mikono msichana yule na kumvutia mbele yake, bila ubishi msichana alikuja mbele yake na kujikaliza juu ya miguu ya Mheshimiwa, Kishime alipata shida kidogo katika maeneo yake, akajikohoza na kumuweka vizuri msichana yule kifuani pake
“Beibi” alijikuta akitamka maneno hayo ambayo daima aliyatumia kumwita mkewe Bi Sheiza tu wawapo falagha.
“Mmm darling” yule binti alijibu huku akijibinuabinua mgongo wake akiwa pale miguuni kwa Mh Kishime. Uvumilivu ulianza kumshinda Mh Kishime na kuanza kupeleka mikono yake kifuani kwa binti yule.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmmm darling,…” yule binti alilalama kidogo baada ya mikono ya Kishime kusika na kuminyaminya chuchu zake. Mzuka ulimpanda Mheshimiwa Kishime hata akasahau kila kitu isipokuwa mrembo yule aliyekuwa naye mahali pale.
“Just wait darling, please” msichana yule alilalama na kumueleza maneno yale mh Kishime huku akimtoa mikono yake kifuani pake, akanyanyuka na kuelekea mezani, alisimama kidogo na kugeuka kumwangalia Mh Kishime ambaye wakati huo alikuwa akitweta kama mbwa aliyekuwa akikimbiza digidigi na kumkosa, macho yake yalitua kwa msichana yule wa kiarabu mwenye nywele mpaka kiunoni. Akiwa bado kasimama alilishika vazi lake refu na kulitoa kuanzia mabegani na kulidondosha chini akabaki na bikini tu, akageuza macho kumwangalia Mh pale kitini na kumuona jinsi alivyozidiwa na aliyoyaona.
Mh Kishime alimeza funda kubwa la mate kwa jinsi alivyoona unono wa mrembo huyo,
“Karibu kinywaji” sauti nyororo ya msichana yule ilimkaribisha Mh Kishime kupata kinywaji. Bila kusita alikipokea na walipokwisha kugonga chiaz kila mmoja akamnywesha mwenzie kimahaba. Grass ziliwekwa chini na msichana yule akaendelea na vimbwanga vyake akiwa juu ya mapaja ya Kishime alimnyonya ndimi na kumbsu hapa na pale. Mh kishime alihisi mwili wake unachoka na mara kwa mara macho yake yalipambana na usingizi uliokuwa ukija kwa fujo muda si muda alikosa ujasiri na kujikuta hana uwezo tena wa mapambano hayo. Kiza kinene kilimfunika macho na fahamu zote zikalala.
ÑÐ
“Lete mkoba!” sauti yenye mkoromo ililifikia sikio la Mama Chakwima, alipogeuka alikutana uso kwa so na mtu asiyemjua kwa kuwa alimuona macho tu kwingine kote kulifunikwa na vazi kubwa jeusi. Mama Chakwima alisita, aliona labda kasikia vibaya
“Unasemaje?” alimuuliza mtu yule
“Lete hand bag haraka” yule mtu alimueleza Mama Chakwima. Mama Chakwima alijikuta akitazamana na domo la bastola, bila kubisha alitoa mkoba na kumpa yule mtu, yule mtu alitokomea nao kwenye foleni ya magari. Mama Chakwima alibaki akilia na kupigapiga usukani wa gari yake kwa hasira
“Nitamueleza nini Chakwima mume wangu!” alilia kwa uchungu akimuwaza mumewe ambaye alimtuma cd ile aliyopewa kwenye ndege, ambayo sasa Mheshimiwa Chakwima alihitaji ili aiwasilishe panapohusika. Mama Chakwima hakujua afanye nini mpaka aliposikia honi za magari ya nyuma na kelele za madereva wakimtaka kuondoa gari lake alipoinua macho alikuta taa ya kijani ikimuashiria kuondoka, aliondoa gari yake na kuipaki pembeni akanyanyua simu yake lakini hakujua amwambie nini mumewe, akaona busara ni kwenda kumueleza ukohuko hospitalini, aliwasha indiketa na kuingia tena barabarani na kuendelea na safari.
6
Amata Ga Imba aligonga kengele ya mlangoni na kufunguliwa na kijana mmoja mtanashati mwenye suti nyeusi, akakaribishwa ndani, kwa hatua za taratibu alifika katika sebule kubwa ambayo alikuwa ameshawahi kufika siku za nyuma, wasichana wengi walio katika shamrashamra hii na ile walipitapita
“Kadi yako tafadhali” mmoja wa wasichana wale alimuomba Amata, kadi ya mualiko ilikabidhiwa mkononi mwa dada yule, aliitazama na kumwangali Amata juu mpaka chini kasha akampa ishara ya kumfuata.
Burudani ya ngoma za kiarabu ilikuwa ikipigwa katika ukumbi huo vijana walikuwa wakicheza sana kwa ustadi wa hali ya juu, wageni mbalimbali walikuwa wameujaza kumbi ule wakinywa vinywaji vya aina tofati kila mtu na anachokipenda, Amata aliangalia kwa chati na miwani yake nyeusi aliyoivaa, kwa hatua za hesabu aliendelea kumfuata binti yule
“Ghorofa ya kwanza juu” yule msichana alimueleza Amata. Kwa mwendo wa kukimbia kidogo Amata alipanda ngazi zile na kufika eneo husika, watu wachache wasiozidi watano walikuwa mahali pale na kiti kimoja kilibaki wazi. Amata aliketi katika kiti hicho na kujichukulia kinywaji.
“Naitwa Amata, Amata ga Imba” alijitambulisha kwa mtu mmoja aliyeketi jirani naye, huku wakitazamana macho lakini Amata aliyaficha kwa miwani yake iliyomkaa sawasawa
“Niite Max Petito” yule mtu wa makamo naye alijitambulisha kisha wakapeana mikono. Max Petito alimuangalia Amata kwa makini sana kana kwamba alishawahi kumuona sehemu Fulani, akatoa ishara ya wale wengine kuondoka, wakatii, akabaki yeye na Amata
“Umekufa Rodolph!” Max Petito alimueleza Amata baada ya kumkumbuka kuwa ni yule Rodolph aliyekuja kwake na kupewa kazi.
“Nani aliniua?” Amata aliliza
“Sharifa ‘the killer’ alikuua” Max aliongeza
“Mimi si Rodolph, naitwa Amata ga Imba, Tanzania Secret Agency namba moja” Alijitambulisha tena mpaka kazi yake. Max Petito alipigwa na bumbuwazi, alibaki mdomo wazi kijasho cha kwapa kilianza kumtiririka, hakutegemea hata siku moja kukutana na mtu huyu ambaye mara nyingi alisikia watu wakimzungumzia kuwa ni hatari sana hata wengine kumfananisha na James Bond wa kwenye filam. Max Petito alikosa la kuzungmza alibaki akimtazama Amata na kushindwa kummaliza
“Nikusaidie nini?” Max alimuuliza Amata
“Unamjua BIG?” Amata aliuliza, Max alishtuka kidogo na kumuangalia vizuri Amata.
“Yeah! Ninamjua. Alikuwa mtu wangu wa karibu sana miaka ya nyuma katika kazi zetu za biashara” Max alijibu kwa kirefu.
“Biashara gani mlikuwa mkifanya? Na wapi?” Amata alisaili tena. Lakini kabla hawajaendelea binti mmoja aliingia mle ndani
“Samahani, Mzee kuna simu yako” yule binti alimuekeza Max Petito
“Dakika 5 tafadhali” Max alimueleza Amata, na Amata alijibu kwa kutikisa kichwa kushiria amekubaliana nae.
Amata ga Imba alitulia juu ya sofa lile akiendelea kuangalia ile ngoma ya kiarabu iliyopigwa kwa mtindo wa dufu, vijana waliovalia kisultani walikuwa wanacheza ngoma ile kwa madaha kabisa. Dakika saba zilikatika Max Petiti hajarejea mahali pake, kengele za hatari zililia kichwa ni mwa Amata akatua glass yak echini na kuelekea kule alikoelekea Max bastola mkononi, alitokea kwenye ukumbi mkubwa usio na kitu zaidi ya viti vichache na kijimeza, karibu na dirisha aliona kameza kadogo kenye simu, mkono wa simu hiyo ulikuwa pembeni mwa kitako chake, dirisha lilikuwa wazi, Amata hakumuona Max eneo lile, kwa hadhari kubwa alitembea bastola mkononi alipokaribia eneo lile alikuta mwili wa Max Petito melala chali sakafuni shingoni akiwa kazungushiwa waya wa simu, amenyongwa! Amata bila kuchelewa alirudisha bastola mahali pake na kuwahi pale dirishani na alipoangali chini aliona gari moja aina ya BMW nyeusi ikiwa imesimama, dirisha lile lilikuwa la alumminium alipita haraka na kushuka kwenye kiukuta kidogo kuliwahi gari lile, kabla hajafika mahali pa kushuka chini kabisa alihisi kama mtu anamshika mguu akageuka mara moja na kukutana uso kwa uso na jamaa mmoja ambaye mkononi mwake alishika kisu, Amata akiwa pale juu ya ukuta aliepa pigo la kisu lililolengwa tumboni mwake kwa kurudi nyuma kidogo, pigo la pili lilichana mkono wa koti alilovaa, yule jamaa akpiga tena kisu sasa kuelekea shingoni kwa Amata, kosa! Amata aliepa upande na mono wenye kisu kile ukapita pembeni kidogo mwa bega lake akaudaka na kujigeuza kasha akamnyanyua yule mtu na kumtupa kwa mbele, mguno wa maumivu ulisikika, Amata alimminya kifuani kwa goti lake la kulia
“Kwa nini umemuua Max?” Amata aliuliza lakini hajajibiwa aligundua jamaa yule alikuwa akitazama sana upande mmoja, Amata alipogeuka alikutana na domo la bastola kwa haraka akajiviringa na risasi ile ilipoachiwa Amata alikuwa tayari kajindondosha chini, yowe la kifo lilisikika yule jamaa alifumuliwa vibaya na risasi ile. Amata akanyanyuka na kutoa bastola yake, risasi ya kwanza ikapasua kioo cha nyuma cha gari ile, wakati huo gari ile iliingia barabarani kwa norinda, Amata akasimama katikati ya barabara akiiangalia gari ile inavyoondoka aliinua bastola yake na kulenga shabaha safi iliyofumua kisogo cha dereva, gari ile iliyumba na kuacha njia na kugonga nguzo ya umeme iliyobeba transfoma juu yake, mlipuko mkubwa ukatokea watu wakatawanyika uku na huko kelele na vilio vikasikika. Amata akakimbia na kuchukua gari yake kasha akafika eneo la tukio kwa haraka, akachungulia ndani ya gari ile na kuona yule abiri bado alikuwa anahangaika jinsi ya kutoka akamsaidi kumtoa na moja kwa moja akamtia kwenye buti ya gari yake na kuondoka upesi kabla watu hawajawa wengi maana kwa muda huo ni walevi tu waliotawanyika na kuacha vinywaji vyao.
ÑÐ
Mama Chakwima aliingia wodini akitweta, moja kwa moja alienda kitandani kwa mumewe na kupiga magoti
“Uniwie radhi mume wangu” aliomba radhi huku akifuta machozi, maana alimjua mumewe jinsi asivyopenda uzembe hata siku moja. Lakini alishangaa mumewe huyo hakuwa na hasira zake za kawaida kama siku zote.
“Usijali mpenzi nililitegemea hilo, hawajakudhuru?”alimuuliza mkewe
“Wameninyang’anya mkoba tu mume wangi na ile cd uliyoitaka ipo mle” mama Chakwima aliendelea kulia zaidi.
“Basi mpenzi nyamaza! Maada ma hawakukudhuru, hiyo cd si shida, waache wachukue ni ya kwao wametoka mbali sana kuifuata” Mh Chakwima alimueleza mkewe huku akikaa na kufunga kitabu chake cha kumbukumbu na kukiweka pembeni.
“Ilikuwaje mpaka wakachukua mkoba?” Chakwima alimuuliza mkewe
“Nilipofika nyumbani nilikuta kuna gari aina ya Noah nyeusi imesimama pale nje, nilipowauliza watoto wakanambia wao hata hawajaiona. Basi nikachukua ulivyoniagiza nikaondoka, nimekwenda vizuri tu mpaka nilipofika katika njia panda ya Mwenge, nikiwa nimesimama nasubiri taa ziniruhusu kupita ndipo niliposikia kioo changu kinagongwa niliposhusha nikakutana na mwanamke aliyevaa guo jeusi akionekana macho tu, nikamshangaa, akanambia nimpe mkoba nilipomuuliza wa nini akanitolea bastola sikuwa na jinsi nikampa akaondoka nao” Mama Chakwima akaanza kulia tena huku kajifunika mtandio wake.
“Sikiliza Mke wangu” Chakwima alitulia kidogo
“Tupo kwenye hatari kubwa sana hivi leo nimeshafanya booking ya ndege wewe, watoto na wafanyakazi wa nhyumbani wote muondoke muende Kigoma nyumbani kwa muda ili nilimalize ili swala” Chakwima alimueleza mkewe
“Kwani kuna nini mume wangu?”
“Ni stori ndefu mke wangu, kwa kifupi kuna watu wanataka kuniua ndiyo maana wamenifanyia ile ajali, wanataka hiyo cd waliyoichukuwa, tangu nipo Saudi Arabia walikuwa wananiandama sana, ah! Mke wangu. Naomba uende uwanja wa ndege moja kwa moja ukitoka hapa hao wafanyakazi watachukuliwa na gari ingine. Mi nitakuja weekend” Akamaliza na kumkumbatia mkewe na kumbusu.
“Nenda mke wangu usichukue chochote wewe nenda kama ulivyo, ukifika uwanja wa ndege piga simu namba hii, huyu dada atakusaidia kila kitu” Chakwima akamaliza kumueleza mkewe na kumpatia business card yenye namba aliyomueleza.
Saa tisa alasiri familia ya Chakwima iliondoka na ndege ya shirika la ndege la Tanzania kuelekea Kigoma kama ilivyoamriwa.
Mheshimiwa Punde Kishime alihisi kama yupo kwenye Chopa maana alihisi pangaboi kubwa likizunguka juu ya uso wake na vivuli vikipitapita huku sauti ya mvumo wake ikiyasumbua masikio. Alifumbua macho taratibu ndipo alipogundua kuwa kazungukwa na watu kama wanne hivi waliovalia kidaktari, alijiangalia na kujikuta yupo katika kitanda kidogo kizuri vitu kama kamba ndogo ndogo zilipachikwa kifuani pake alipoziangalia kwa makini aligunduwa kuwa ni electro cadiogram ili kufuatilia muenendo wa moyo wake.
“Mi siyo mgonjwa nyie vipi?” aling’aka lakini haikumsaidia kitu kwani aligundua hata mwili wake haukuwa na nguvu za kufanya lolote, alitulia palepale na kila alipojaribu kujitikisa haikuwa rahisi.
Baada ya muda mfupi walikuja watu aliowatambua kwa sura na majina, Inspekta Simbeye aliketi jirani kabisa na kitanda cha Mh Punde Kishime, walitazamana macho na wakajikuta kila mmoja ana la kumwuliza mwenziwe.
“Inspekta, nafurahi kukuona!” Kishime alimwambia Inspekta Simbeye
“Nami pia nafurahi kukuona maana ni muda mrefu hatujaonana karibu wiki sasa au siyo?” Inspekta alijibu huku akitoa tabasamu pana kwa Mheshimiwa Kishime.
“Tumekutafuta sana Mheshimiwa, siku nne hizi hatukulala, hebu tueleze kisa na mkasa” Inspekta Simbeye alieleza kwa mtindo wa kuuliza
“Inspekta, kwanza nawashukuru, lakini ningependa mnieleze mmeniokota wapi?” Mheshimiwa Kishime aliuliza
“Jana alfajiri majira ya saa kumi…http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TUKIO HALISI
…Askari wa doria walikuwa wakirudi toka katika maizunguko yao, katikati ya barabara ya Namanga dreva wa defender ya polisi aliona kwa mbali kitu kimelala mfano wa gogo, kwa spidi aliyokuwa nayo alifanikiwa kukikwepa na kusimama kwa mbele, wakashuka na kurudi kuangalia ndipo walipokuta ni binadamu. Walimtazama wakijua ni mlevi kama walevi wengine, baada ya kumpekua mifukoni ndipo wakakutana na kitambulisho chake cha kazi, walitazamana na kumbeba kumuweka ndani ya gari, walipiga redio kituo cha polisi cha Oysterbay na kupewa maelekezo kuwa wampeleke hospitali ya Jeshi ya Lugalo nao wakafanya hivyo. Walipohakikisha anepokelewa walirudi kituoni.
Habari za kupatikana Mh Punde Kishime ziliushtua moyo wa Inspekta Simbeye, alikurupuka na kukiacha kitanda
“Mume wangu mbona hivyo!!” Mkewe alishangaa alipomuona mumewe kawa kama mwehu. Alijiandaa harakaharaka na kupiga redio kituoni, dakika chache golf ya polisi ilikuwa mlangoni na moja kwa moja walielekea Lugalo. Inspekta Simbeye alitamani kumuona Mheshimiwa Punde Kishime yu hali gani maana taarifa ya kupotea kwake ilikuwa na utata mkubwa, alipofika pale alimkuta Mheshimiwa amelala usingizi
“Kwa sasa hamuwezi kuongea naye kwani tangu amefikishwa hapa hajaamka bado” Mganga wa zamu Luteni Kanali Kasiga alimueleza Inspekta Simbeye.
Majira ya saa nne Inspekta Simbeye alikuwa katika hospitali Ile akiwa na hamu ya kujua nini kilichojiri juu ya Mheshimiwa Kishime na kupotea kwake, aliamini majibu ya Kishime yangempa mwanga yeye kujua kama matukio yote yaliyoungana yana uhusiano au la…
… hivyo ndivyo ilivyokuwa Mheshimiwa” Inspekta Simbeye alimueleza kwa upole Mheshimiwa Kishime. Kishime aliketi kitandani, mwili wake haukuonekana kuteseka wala kupata shida Fulani mbaya kadiri ya kutoweka kwake. Inspekta Simbeye kwa kuona hilo alijua wazi kuwa huo haukuwa muda muafaka wa kuhojiana naye, aliongea na mganga wa zamu na kumwambia pindi tu atakapomruhusu atoe taarifa ili mahojiano yote yafanyike katika chumba maalumu huko makao ya polisi.
ÑÐ
Kasi iliyokuwa kwa gari ya Amata haikuwa ya kawaida, hasa alipogundua kuwa nyuma yake kuna gari mbili zinazomfuata. Aliongeza kasi na kuiacha barabara ya Jomo Kenyatta na kuingia Ali Hassan Mwinyi kuelekea daraja la Surrender, Mercedes Benz nyeusi ilikuwa tayari ubavuni mwake, mtu mmoja alitoa bastola kumlenga Amata. Amata hakutetereka aliiyumbisha gari yake na kuwagonga ubavuni kitendo kilichofanya mtu yule apoteze lengo na kukosa shabaha yake, Amata alifanya vile kwa mara ya pili na kuisukuma gari ile upande ikaenda na kugonga mwamba wa daraja, ikayumba na kunyanyuka kabla haijadondoka Amata alikuwa tayari ameshaitoa bastola yake na kupiga shabaha maridadi katika tenki la mafuta, mlipuko mkubwa ulitoke na gari ile ailitupwa chini ya daraja. Amata aliacha barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kukunja kushoto kuelekea Ocean Road, gari moja bado ilikuwa ikimfuata kwa kasi, Amata aliiona vizuri kupitia kioo cha kuendeshea, aliyakwepa magari ya mbele yake na kuichanganya ile gari isijue ameelekea wapi lakini bado baadae aliiona ikija kwa kasi aliongeza kasi na kufunga breki za ghafla ile gari ikagonga nyuma ya gari ya Amata na kuharibika vibaya, Amata alishuka bastola mkononi, aliinua mkono na bastola yake ikakohoa na kuondoa roho ya dereva, Amata aliona akilengwa akajitupachini na kujiviringa kupita uvunguni mwa gari yake na kutokea upande wa pili alijinyanyua na kupiga goti moja kabla hajakaa sawa alihisi kitu cha moto kimepita karibu kabisa ya mkono wake alisukumwa na kuanguka chini, akiwa hapo chini aliitumia bastola yake avizu na kumpiga jambazi aliyebaki ambaye alikuwa na shortgun mkononi, jambazi yule alitua barabarani akiwa hana uhai. Ving’ora vya polisi vilisikika kutoka Oyserbay, Amata bila kuchelewa huku damu zikimtoka aliingia garini na kutokomea.
Amata aliegesha gari katika chumba cha chini cha jengo la PPF Tower akazunguka na kufungua buti akawasha tochi na kumuona mateka wake akitweta akamtoa na kumtia kwenye buti ya gari ingine na kuondoka nae mpaka mpaka Kivukoni, akaegesha gari karibu kabisa na kituo cha polisi cha wanamaji, akasaidiwa kumtoa mateka yule na kumtia kwenye boti na kuondoka naye mpaka upande wa pili wa bahari ambako alimkuta Madam S akiwa na watu wengine watatu walimpokea Amata.
“Pole Kamanda” Madam S alimsabahi
“Asante, mzigo huo!” Amata alimjibu madam S huku akielekea kwenye gari iliyokuwa hapo. Walipompakia mateka wao wakaondoka na gari ile kuelekea mafichoni kwao, jumba lilelile aliloingia Amata na Gina ndiyo lilikuwa ofisi yao ya maficho, wakaingia namoja kwa moja kuelekea chumba cha chini kabisa katika jengo hilo ambalo kwa nje lilikuwa ni gofu tu.
ÑÐ
Mheshimiwa Punde Kishime alifikishwa katika chumba maalum na kuhifadhiwa akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
“Utakaa hapa, upumzike kwa ajili ya usalama wako na baadae tutakuwa na kikao kidogo” Inspekta Simbeye alimueleza Mheshimiwa Punde Kishime.
Mheshimiwa Punde Kishime alitulia ndani ya chumba hicho kipana kikiwa na kitanda na kiti kimoja, pembeni palikuwa na kijimeza kidogo ambacho juu yake kulikuwa na chumba ya maji na glass moja. Mheshimiwa Punde Kishime aliketi juu ya kitanda, sasa alijikuta kama yupo gerezani, hakuwa na njia yoyote ya mawasiliano na ulimwengu wa nje. Pembeni ya chupa ile ya maji kulikuwa na gazeti la nyuma kidogo, alilichukua na kujilaza kitandani na kuanza kusoma habari zilizomo ndipo alipokutana na habari ya ajali ya kutatanisha ya Mheshimiwa Chakwima, mshtuko mkubwa ulimfika moyoni, jinamizi la uchungu lilimtawala akaketi tena kitandani na kuliweka gazeti lile chini akabaki kajiinamia hajui nini cha kufanya, kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi sana, aliwaza na kuwazua akajikuta akitoa machozi kwa habari hiyo aliyoipata. ‘Sasa itakuwaje!’ alijikuta akitamka maneneo hayo bila kujua. Hakufahamu kabisa kama chumba hicho kimefungwa mitambo maalumu ya kunasa sauti, pembeni ya chumba hicho kulikuwa na dirisha pana lakini halikuweza kufunguka hata siku moja. Upande wa pili Inspekta Simbeye aliweza kumuona vizuri sana Mheshimiwa Punde Kishime akiwa katika mahangaiko yale. Kila alichonong’ona kilisikika kwa uzuri sana upande wa pili ambapo kulikuwa na mtambo unaorekodi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Simbeye hakuona kama kutoweka kwa Mheshimiwa Punde Kishime ni tatizo kubwa kama wengine walivyochukulia, yeye aliona wazi kuwa hapo kunamchezo uliofanyika, mara nyingi alifikiria juu ya barua aliyoambiwa na katibu wa Mheshimiwa Kishime kuwa aliipokea toka kwa mwananke yule aliyevalia vazi jeusi, alijaribu kuoanisha na yule aliyemuona pale kituo cha polisi kati ambaye alileta barua ofisini kwake, alijawa na hamu kujua nini kinajiri katika hili lakini kila alipofikiria aliona giza nene hakuona pa kukamata, kupatikana kwa Mheshimiwa Kishime kwake ilikuwa furaha kubwa, kwa wakati huo alimsahau Mh Chakwima kule hospitali, alimsahau mtuhumiwa wa ajali ya Chakwima aliyeuawa na jambazi mwanamke kule hospitali, zaidi ya hapo hakujua dunia ya pili inashughulika na nini katika hili, fikra zake nyingi zilimsababishia kupata kipara kwa kushika kichwa chake mara kwa mara apambanapo na jambo.
Punde Kishime alionekana kama kukumbuka jambo Fulani, alikurupuka kutoka kitandani, akaweka mikono yake kichwani huku akitikisa kichwa, akaishusha na kushika kiuno, alionekana ni mtu asiyejua la kufanya ‘barua’ alinong’ona, kisha akatulia tena kitandani.
“Kwa nini umemuua?” madam S alimuuliza Amata
“Sijamuua, huyu ndiye alemuua” Amata alimjibu Madam S huku akiinua bilauri iliyojawa na kinywaji kikali chenye barafu ndani yake na kujimiminia kinywani kisha akalegeza tai yake ili apate hewa ya kutosha.
“Kwa nini amemuua?” Madam S aliuliza tena
“Ndio maana nimemleta mumuulize nyie, mi kazi yangu imekwisha” Amata alijibu na kumpa ishara kijana mmoja aliyekuwa jirani hapo asogeze kiti cha chuma.
Jeraha llilikuwa mguuni mwa jambazi yule lilivuja damu nyingi, Masunga, kijana mcheshi anayefanya kazi katika kitengo maalum ndani ya jumba hilo alimtazama yule jambazi kwa makini na kumtupia swali
“Kwa nini umemuua Max Petito?”
Lile jambazi likaanza kucheka kwa nguvu kitendo kilichomkera Amata, alipandwa na gadhabu na kumsogelea akitaka kumchapa makonde
“Subiri Kamanda” Masunga alimuomba Amata.
“Niambie, kwa nini umemuua Max, na nani aliyekutuma?” Masunga alimsaili tena jambazi yule ambaye sasa alikuwa akimtazama Masunga kwa jicho la dharau. Masunga aligundua kuwa hapa wanapoteza muda, alivuta droo ya meza ndogo na kutoa kifaa cha kuchomea sakiti za redio ‘soldering iron’ akakiunganisha katika umeme, sekunde chache kikawa chamoto na kubadilika rangi kuwa chekundu, Masunga alikishika vizuri na kukichomeka katika jeraha lile la mguu, jamabazi yule alipiga yowe la maumivu
“Nasema nasema jamani niacheni nasema nasema nasema!!!”
“Sema sasa, kabla sijachoma tena!” aling’aka Masunga huku akimtolea macho jambazi yule
“Nilitumwa” alitoa jibu fupi
“Ulitumwa na nani?” Masunga aliuliza
“Mi simjui, mi nilitumwa tu” aliendelea kulia kwa uchungu, Masunga akaweka tena kile chuma jerahani sasa kwa nguvu zaidi huku akimhoji maswali
“Nani unayemfanyia kazi?” Masunga aliuliza kwa ukali huku akiendelea kuchoma jeraha lile
“Mi simjui jamani mnanionea, mi natumwa tu, nalipwa baada ya kazi” Jambazi lile lilitoa machozi.
“Kwa nini ulimuua Max?” Masunga aliuliza huku akiwa ameshika kile chuma sasa alikwishakitoa katika jeraha lile
“Ntasema jamani, ntasema kabisa, msiniunguze” jambazi lile lilia kwa uchungu. Madam S alishindwa kuvumilia na akataka kuondoka lakini Amata alimshika mkono na kumrudisha pale
“Usiondoke, simama hapa ili ujue kazi zetu zinavyokuwa ngumu, na sisi tukikamatwa tunafanywa vivi hivi” Amata alimueleza Madam S.
“Mimi huwa nakodiwa tu kuua, mteja wangu hunielekeza tu mtu wa kumuua basi, hakuna zaidi” yule jambazi aliendelea kusema
“Ok! Vizuri sasa nani ndiyo mteja wako aliyekutuma kazi hii?” Masunga aliendelea kumhoji.
“Kiundani simjui, ila tupo wengi sipo peke yangu jamani, tumepewa kazi yenye hela nyingi sana” yule jambazi aliendelea kusema huku akimumunya mdomo wake, Kamanda Amata aliijua janja hiyo aliruka kutoka aliposimama na kumbana koo jambazi yule
“Tema!” alimpigia kelele na jambazi yule alitema kitu kama pipi ambacho hutumia pindi wanapoona wamezidiwa na hawatakiwi kutoa siri. Kwa kumuachia Amata alimsukuma jambazi yule na kumdondosha pamoja na kiti chake mpaka chini, kisha wakamuinua tena.
“Sasa useme kwa ufasaha, ukileta jeuri tunapasua korodani” Masunga alimkemea jambazi
“Nitasema jamani, lakini msiniue mimi nina familia” jambazi lilizidi kulalama huku likikohoa baada ya koo lake kubanwa na mkono wa wenye nguvu wa Kamanda Amata.
“Haya sema haraka!” Masunga alisisitiza kwa sauti kali
“Mkitaka kujua habari yote mtafuteni BIG, yeye ndio mpango mzima” lile jambazi lilijibu huku likilia kama toto. Likiwa pale kitini likajiinamia na kutulia kimya, Amata alipata wasiwasi akamsogelea alipomuinua kichwa akakuta tayari ameshakufa.
“Shenzy taip limejiua…” Masunga aling’aka kwa hasira. Madam S alishusha pumzi ndefu na kuondoka mahali pale, Amata alimuachia yule jambazi kisha nay eye akaondoka huku akisikitika kwa mbinu chafu aliyotumia jambazi huyo kujiua ‘BIG’ alijiwazia huku akipanda ngazi kuelekea ghorofa ya juu.
Amata Ga Imba alikuwa mesimama mbeley kitanda cha Mheshimiwa Chiwawa Chakwima, alitabasamu kwa kumuona akaiandikaandika katika kitabu chake cha kumbukumbu. Mzee huyu aliyepata sifa kubwa katika mioyo ya Watanzania hasa kwa kufichua siri za mabilioni ya viongozi wa serekali yaliyowekezwa katika mabenki ya Ulaya na madhambi mengi ya ubadhilifu mkubwa wa fedha na mali za uma alikuwa ni mtu wa kawaida sana, katibu wa wizara ya fedha, lakini kwa sasa alikuwa akiangaliwa kwa jicho la husuda na kila aliyetajwa katika sakata hilo, kesi zilikuwa zikinguruma huku na huko, vigogo waliopo madarakani walisalimika kwa kinga walizowekewa kwa mujibu wa katiba lakini wale waliokwishastahafu walikuwa wakisota rumande kila kukicha.
Chakwima alimtazama kijana huyu aliyesimama mbele yake akiwa ndani ya suti maridadi ya mikono mifupi iliyomkaa sawia, mawani yake myeusi iliyomfanya aonekane ni kijana mtanashati asiye na mawaa yoyote. Amata alitoa miwani yake usoni na kuikunja kabla ya kuiweka mfukoni, macho yake yaliyojaa kila chembe ya huruma yalimtazama Mheshimiwa alivyokaa pale kitandani huku mguu wake mmoja ukiwa na POP.
“Shikamoo Mzee!” salamu hiyo kutoka kwa Amata ilimshtua Mheshimiwa, akayainua macho yake na kukutana na uso angavu wa kijana huyu jasiri.
“Marhaba kijana, karibu sana, kama nakukumbuka vile tulionana wapi?” Mheshimiwa Chakwima aliuliza
“Geneva, Uswiss” Amata alijibu huku akitabasamu
“Aaaaaa nimekumbuka sana, ndiyo ndiyo” Mheshimiwa alijibu kwa furaha sana huku akimpa mkono Amata kwa bashasha kisha akaendelea
“Nashukuru, sasa mkombozi wangu umefika” alimwambia maneno hayo huku akimkabidhi Amata kitabu kile cha kumbukumbu, Amata hakuelewa kwa nini, akakipokea na kukishika vizuri. Amata alipotaka kumuuliza swali Mheshimiwa alijikuta akishikwa bega
“Samahani kaka, bado hatujatoa kibali cha kuongea na mgonjwa mpaka madaktari wake kutoka Amerika wataporuhusu” yule muuguzi alimueleza Amata huku akimsukuma atoke nje. Mheshimiwa Chakwima alimwangalia Amata na walipogongana macho alimpa ishara ya kutoka nje. Amata alitii na moja kwa moja aliiendea gari yake aina ya Freelander, aliketi ndani na kujifungia mlango, kisha akachukua kile kitabu cha kumbukumbu alichokipata kwa Chakwima na kukifungua ndani kusoma…
Ilikuwa ni kumbukumbu ya muhimu sana kw aMheshimiwa Chakwima labda kama angekufa basi kitabu hicho kingesaidia kujua kila kitu, ndani ya kitabu hicho kulikuwa na kumbukumbu ya safari yote ya Chakwima ya kwenda Abu Dhabi na kila kilichojiri huko
…nilifika uwanja wa ndege wa kimataifa Riyadh saa kumi na moja jioni, nikapokelewa na wenyeji wangu, waarabu wawili ambao mikononi mwao walikuwa na kibao chenye jina langu, moja kwa moja nikapelekwa hotel ya Hilton yenye hadhi ya nyota tano kutokana na wadhifa wangu, pale nilikutana na wajumbe kutoka nchi mabalimbali hasa za Afrika ya kaskazini na Uarabuni kwenyewe. Tukiwa chakulani, mtu mmoja alikuja kuketi karibu yangu alivaa vazi la kiarabu haswa, hakuwa anajua kiingereza vizuri ila alikuwa anajua pia baadhi ya maneno ya Kiswahili, alinisabahi na kuniuliza mambo mengi sana juu ya Tanzania hasa mambo ya rasilimali (kwa kuwa sgenda kuu ya mkutano ule ilikuwa ni uwekezaji katika sekta ya mafuta ghafi). Maswali yake yalinifanya niogope kidogo hasa jinsi alivyouliza kwa ufundi mkubwa, alikuwa ni tajiri sana japo husingeweza kumjua kiurahisi nanma hii…
Amata alishusha pumzi ya kutosha, alijiona kama anasoma kitabu kilichotungwa na Hussen Tuwa, alifyatua na kulaza kiti ili ajue nini kiliendelea katika safari hiyo.
…Siku ilofuata tukiwa mkutanoni, kila mjumbe kadiri ya nchi watokazo walikuwa wakielezea rasilimali ile ya mafuta jinsi wanavyotumia na kunufaika nayo, kwa akili yangu niligundua kuwa kiwango kikubwa cha rasilimali hiyo kinapelekwa katika nchi hizo. Wakati wa mapumziko niliongea na bwana mmoja kutoka Nigeria, yeye alithibitisha kwamba mafuta mengi yanakwenda ughaibuni na wanachi wanabaki masikini ndiyo maana mapigano ya wenyewe kwa wenyewe hayamaliziki kwani serikali inauza ,mafuta na kupewa silaha za maangamizi.
Jioni ya siku hiyo tulipomaliza kikaonilitembelewa na wageni watatukwa haraka haraka walionekana ni matajiri wakubwakadiri ya utambulisho wao walikuwa wakitoka nch itofaut, walisema wanapenda sana kuja kuwekeza Tanzania hasa sekta ya Mafuta, Ges, Urenium, Dhahabu na Almasi. Jamaa hawa walikuwa na ramani ambayo ilikwisha ainisha maeneo yote yanayopatikana vitu hivi, kwa kweli jasho lilinitoka hasa waliponidokezea kile wanachokitaka kwa undani
“Tungependa kuwe na mtu atakayeendana na matakwa yetu, sio kuvuruga nchi bali kuwekeza kwa asilimia 99, wewe na viongozi wako mtapata tuzo mnazostahili…”
Ilikuwa ngumu kuelewa, nikagundua kumbe hawa jamaa kwa njama hii wamenunua serekali nyingi sana katika nchi zetu za dunia ya tatu…
Amata alihisi kama damu inataka kusimama akajinyoosha kidogo na kujiweka sawa, kisha alikodoa macho tena kusoma kitabu kile
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
(…) Tusipoangalia Taifa letu lililojawa na kila tunu ya utajiri, utulivu na amani litapotea katika umasikini, vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuna mbinu chafu inayofanyika sasa hasa katika nchi hizi masikini kuwahadaa viopngozi wenye majina. Kuna mpango wa kuvihadaa vyama vya siasa vyenye nguvu na kudhaminiwa mapesa ya kutosha ili viweze kupenyeza siasa chafu ambazo zitwafanya wananchi wagombane na serikali yao na kuuvunjwa utaifa.
Hili litiliwe mkazo
Tayari vibaraka wa mabwana hawa wamepandikizwa kila mahali katika sekta binafsi na serekalini wengine ni wafanya biashara wakubwa na majina yao yanalindwa na serikali iliyopo madarakani.
Baada ya maelezo marefu sana aliyoyaandika kwa mkono wake mwenyewe Mheshimiwa Chakwima alimalizia kwa ujumbe mzito.
Ninawindwa kila kona kutokana na msimamo mkali niliouonesha mbele yao huko Abu Dhabi, nimezungukwa na watu wanaoitaka roho yangu kwa hali na mali, taarifa hii iwe kama funguo katika utatuzi wa utata huu. Ni mtu mwenye akili tu anayeweza kuuelewa muandiko huu. Ushahidi upo wa yote na mpango mzima wa kufanikisha hili upo.
Naipenda Tanzani…
Amata alitulia kwa muda huku mikono yake ikitetemeka ilhali yeye mwenyewe hakulijua hilo, aliona kazi ngumu iliyo mbele yake akajaribu kuunganisha matukio hili na lile lakini hakupata muungano huo kwa usahihi, angalau sasa aliweza kupata picha kuwa ajali ya Chakwima ilidhamiriwa kumuua ili siri hii isitoke kirahisi namna hii lakini la, Mungu analipenda taifa lake, Chakwima aliumia sana lakini hakufa, kumbe hili halikuwa jaribio la kwanza la kumuua hata huko Abu Dhabi aliponea chupuchupu, kama hangekuwa kapitia japo jeshi kidogo tayari angeshakufa kiulaini.
SIKU CHACHE NYUMA
Abu bhabi
“Kama hutaki kukubaliana na sisi hutorudi kwenu…” sauti hii ilimsumbua sana Chakwima kila alipokaa maneno haya aliambiwa na mmoja wa wale wageni wake baada ya kumtaka kukubali mpango huo lakini Chakwima alipowasikiliza sera zao tayari alikuwa ameshaelewa mchezo huo ‘siwezi kusaliti taifa langu’, roho ya uzalendo ilimji mara kwa mara na alipokataa kwa sauti moja ndipo walipoadhimia kumpoteza ili asije kutoa siri ile kwa wengine.
Chakwima aliingia chumbani kwake ili kuweka vizuri begi lake tayarai kwa safari jioni ile, alichukua makabrasha yake yote ambayo ndiyo yalikuwa mali za serikali akatia katika briefcase yake na kuitupia kitandani. Akajiangalia kwenye kioo kama yuko sawa na nguo imemkaa vyema, aliporidhika mbele ya madini hayo ya ulanga akaiendea jokofu ndogo iliyopo chumbani hapo akafungua na kutaka kutoka kinywaji akasita kidogo, mpangilio wa chupa aliouacha haukua sahihi alitazama mara mbili tatu kengele za hatari zikagonga, lakini akajua labda ni wahudumu wamezigeuza akachukua moja na kuifungua kisha akajimiminia katika bilauri kinywaji hiko kitamu akakisogeza kinywani na kupiga funda moja ambalo lilipofika kati koromeo alihisi likishindwa kupita akafanikiwa kulirudisha kinywani lakini kiasi Fulani kilienda tumboni, akatulia kwa muda na kuanza kujishika tumbo, kizunguzungu kwa mbali kikaanza kuja, Chiwawa Chakwima alivuta chupa ya maji kutoka katika jokofu hilo akaidondosha chini, chupa ya pombe nayo ikavunjika chini, hali ikawa mbaya sana hana nguvu za kujongea hata mita tano alijivuta kwa kusota nyuma yake alihisi kama kuna mtu kamsimami akajua kwa vyovyote huyo ni Israel mtoa roho alipogeuka macho yake hayakumdanganya mtu mmoja alisimama akimwangalia na kupiga hatua moja kumfuata kila alipojongea. Mtu aliyevaa guo jeusi mwili mzima na alionekana macho tu mkononi alishika jisu refu, akamkanyaga Chakwima pale sakafuni na kumgusa koromeo kwa lile jisu lake, Chakwima alitulia kama maji mtungini akijua sasa kifo chake kimefika alitupa jicho kwa makini kuangalia kitufe cha dharula akgundua hakiko mbali, akamwanga lia yule jamaa alivyosimama kwa utulivu na kwa kumshtukiza aliuvuta mguu wake kitendo kilichomfanya yule bwana kupoteza muelekeo Chakwima akajiinua na milimita chache nyuma yake lile jisu lilipita karibu na kisogo na kuondoa nywele kidogo, kwa jinsi alivyonyanyuka Chakwima kichwa chake kilitua tumboni kwa jamaa yule na kumsukuma mpaka ukutani kitedo kilichofanya wote wawili kuanguka na hapo ndipo Chakwima Lipopata nafasi ya kubofya kile kitufe, yule jamaa alipoona hivo akajua mambo yameharibika aliingia mlango wa chooni na kupanda juu ya sinki la choo n akupita dirishani na kutokome. Mlango ukafunguliwa, Chakwima hoi sakafuni povu linamtoka mdomoni. Haraka haraka walimbeba na kuteremka nay echini kwa lifti kisha huduma ya kwanza ya kumpatia maziwa ikafanyika wakiwa ndani ya gari ya wagonjwa.
Alipojisikia nafuu hakupenda tena kubaki katika nchi hiyo aliamua kuondoka na ndege nyingine. Akiwa airport sehemu ya kusubiria waondokaji alimuona mtu mmoja mfupi aliyeshupaa mwili akimwangalia sana kila jambo anlofanya, Chakwima akajua kuwa kazi bado ni pevu. Aliona usalama wake ni yeye kuwa wa kwanza kuingia ndani ya ndege na akafanya hivyo na kutulia kitini akitafakari yote yaliyojiri katika safari yake.
(...)tunajua kuwa dhamana ya usalama wa jiji la Dar es salaam ipo mikononi mwako, tupe nafasi tufanye kazi yetu ambayo iko mbioni kuanza, mwisho wa siku utafurahi maana mtenda kazi anastahili ujira wake.
Wasalaam,
Ni sisi wapenda amani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Simbeye aliikunja barua ile na kuirudisha ndani ya bahasha yake, bahasha ndogo ya khaki iliyozungukwa kwa utepe wa dhahabu, haraka haraka unaweza ukasema ni kadi ya harusi. Aliivuta mtoto wa meza na kuitumbukiza ndani yake kisha kuyaelekeza macho yake kwenye luninga ndogo iliyopo ofisini kwake, hakuna cha maana alichokiona zaidi ya habari zilezile tu za mauaji ya Syria.
Alivuta faili moja lililokuwa mezani kwake ambalo lililetwa na mmoja wa askari upelelezi lililokuwa likihitimisha mswala ya kupotea kwa Mheshimiwa Kishime, aliliangalia harakaharaka maana aliona kuwa halina kazi tena na kisha akalitia kwenye shelf. Japokuwa kichwani mwake bado aliamini kesi hii lazima iendelee kuchunguzwa ili kubaini ukweli, haiwezi kwisha kirahisi namna hii, alitikisa kichwa kuonesha kuwa amekubaliana na mawazo yake mwenyewe. Sasa alivuta faili lingine na kuliweka mezani, akagundua kuwa alikuwa amelisahau kwa muda maana lilikuwa na vumbi na mikojo ya mende ‘uzembe’ alijiwazia, akiangalia huku na huku alikuta mafaili mengi yamemzunguka huku nahuko hakujua lipi aanze nalo na lipi amalizie, lile la kuokotwa kwa maiti ya mwanamke bwawani liko pembeni, lile la mauaji kanisani uchunguzi unaendelea, lile la kukamatwa kigogo wa serikali na madawa ya kulevya linapigwa danadana akajikuta mkononi mwake amelishika lile la Mheshimiwa Chakwima, aliligeuza geuza na kusoma kidogo lakini akaona haelewi kitu akaliweka mezani ‘traffic case’ akasema kimoyomoyo, ile shauku ya kutaka kujua muungano wa matukio haya ikawa inayeyuka taratibu, akaona wazi hakuna muungano wowote katika hilo, akashusha pumzi na kujinyoosha macho yake yakagongana na yale ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa pichani pale ukutani, na yeye akatabasamu. ‘Sasa naweza kwenda likizo, nikalime kidogo’ alijisemea moyoni na hapo ndipo alishutushwa na hodi kisha mlango ukasukumwa ndani, kijana ambaye hakumfikiria kwa muda huo aliingia akiwa kavalia nadhifu kama kawaida yake, Kamanda Amata alivuta kiti na kuketi kisha akatoa mawani yake na kuitia mfukoni.
“Karibu! Mbona leo bila taarifa?” Simbeye alimuuliza Amata
“Wakati mwingine ni bora kufanya hivi” Amata alijibu
“Karibu kijana! Umeniwahi kweli nilikuwa nataka kutoka nikapate japo kahawa” Inspekta Simbeye alimueleza Amata. Amata alifungua kijitabu chake kidogo na kusoma vitu fulanifulani.
“Mzee, ujio wangu hapa ni kutaka kujua mmefikia wapi juu ya kesi ya Mheshimiwa Punde Kishime, ningependa kusikia machache” Amata alimuuliza Inspekta ambaye wakati huo alikuwa akijitikisa pale lkatika kiti chake.
“Mi nafikiri Kamanda hilo lomeisha, mlengwa si amepatikana? Nini kitaendelea?” Simbeye alimjibu Amata huku sasa mikono yake ikiwa juu ya meza.
“Inspekta, hii kesi haiwezi kuisha hivi unavyoona wewe, lazima uchunguzi a kina ufanyike, mbona mnafanya kazi kienyeji hivi, ninyi ni polisi jamani. Tumieni akili” Amata aliongea kwa jazba akionesha wazi kutoridhika na jibu alilopewa na Inspekta. Inspekta Simbeye hakupenda hata kidogo kufundishwa kazi na mtu, daima aliona yeye yuko sawa, dharau ilikuwa ni jambo la kawaida sana kwake. Alimwangalia Amata kwa jicho la dharau
“Kijana ulipokuwa CCP pale Moshi mi nilikuwa nakufundisha, sasa leo we unataka kuwa mwalimu?” Simbeye alimuuliza Amata huku akisimama na kuvaa kofia yake, Amata naye akasimama
“Samahani Inspekta, mi nafikiri hiyo kazi haijaisha, haya matukio inawezekana yana uhusiano mkubwa kwa upande mmoja au mwingine.” Amata akashusha pumzi na kukatishwa na Inspekta
“Uhusiano unatoka wapt? Sisi tumefanya uchunguzi tumeona hilo, hamna uhusiano. Sasa tujadiliane tunafanya nini labda mwenzangu una wazo” Inspekta Simbeye alimtazama Amata huku akijishikashika tumbo lake kubwa lililojaa vizuri katika sare hiyo ya khaki.
“Hakuna uhusiano!? Kama simu zilizopigwa kwa Mheshimiwa Punde Kishime kabla hajatoweka location yake ni Keko, kwa nini ukufikiri kwamba na gari lililosababisha ajali lilitokea Keko hapo hakuna uhusiano?” Amata alimuuliza Inspekta. Inspekta Simbeye alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akarudi kitini na kutafakari mawili matatu.
“Karibu kiti kijana” alimkaribisha kiti Amata kana kwamba ndiyo kwanza wanakutana.
Baada ya kuwekana sawa mambo yao ya kiofisi kila kitu kilikuwa sawa. Mara fax ya ofisini kwa Simbeye iliita naye akairuhusu fax ile iendelee kuingia, ilipomaliza akaikata ile karatsi na kuisoma kisha akaikunja na kuiweka kwenye moja ya mafaili yaliyopo hapo mezani.
“Kuanzi sasa hili swala tunawaachi ninyi muendelee nalo ila kama mtahitaji msaada basi tuwasiliane kijana.”Inspekta Simbeye aliagana na Amata na kumkabidhi kopi za faili lililohusiana na Mheshimiwa Punde Kishime kisha kila mtu kuchukua njia yake.
7
Watu wengi walijaa katika viwanja vya jangwani wakisikiliza mkutano wa hadhara juu ya mustakabali wa siasa ya nchi yao, kelele za kushangilia zilizizima mitaa yote ya Jangwani, wingi wa watu uliokuwa pale haukuwahi kuonekana katika siku za karibuni.
Katika jukwaa kubwa la mbao mtu mmoja mnene mweusi aliyevaa suti ya kijivu alikuwa akifuta jasho lililomtiririka kwa wingi kana kwamba ana bomba la mvua mwilini, lakini haishangazi kwa kuwa joto la Dar es salaam hakuna hasiyelijua. Watu waliendelea kushangilia kwa nguvu, akina mama wakiwandani ya sare za rangi ya kijivu na bluu bahari wlipiga vigeregere visivyo na mwisho, vijana kwa maelfu walikuwa wakiimba nyimbo za kumpongeza msemaji wa chama hicho aliyekuwa akinguruma juu ya jukwaa hilo, akiwapa njia Watanzania hawa masikini kujua hali halisi na mustakabali wa siasa ya nchi yao
“Wameuza nchi kwa mataifa makubwa” alipiga kelele
“Wanatufanya sisi wajinga, hatuna akili, msiwachague”
“Msipoteze kura yenu, tumieni akili Watanzania” kelele za mashangilio zilisindikiza hotuba ile iliyokuna mioyo ya watu wengi kuanzia waliokuwa pale kiwanjani mpaka wale waliokuwa mbele ya luninga zao majumbani wakikodolea macho na kutega masikio kumsikia mwanasiasa huyu aliyeibuka ghafa katika uwanja wa siasa na kuanza kuunguruma majukwaani kama Simba mwenye njaa.
Punde Kishime sasa alikuwa rasmi katika orodha ya wanasiasa wa Tanzania, akiwa ndiyo muongeaji mkuu katika chama chao cha PDP (People’s Development Party), mzee huyu mwenye jazba na akili ya hali ya juu aliweza kuziteka nyoyo za Watanzania kwa muda mchache sana ukizingatia alishakuwa maarufu hasa pale alipowaumbua vigogo wa serikali wanaohujumu uchumi wa nchi, watu wa kila rika akina mama, wazee, vijana na hata watoto walipenda kumuita ‘Kishime Mkombozi’. Sasa alibaki kuwa mwanasiasa hakuwa na muda tena kwa kazi ya ofisi yake kama katibu mkuu wa wizara nyeti ya Nishati na Madini, alipewa barua ya kuachishwa kazi kutokana na kukiuka kanuni za Ilani ya chama tawala.
Alipigania kwa kipaza sauti haki za wanyonge zilizopotea lakini nyuma yake kulikuwa na mengi yanayosubiri kazi hiyo itimie.
‘Hata huyu?’ Chakwima alijiuliza pale alipokuwa akiangalia televisheni ya hospitalini, akiwa bado anuguza mguu wake, ‘Kweli siasa haina mwenyewe!’
“Hili ndilo nililokuwa nalisubiri sana, ila sikujua ni katika mtindo gani litakuja” Kamanda Amata alimueleza Madam S. Madam S alitulia juu ya kochi kubwa lililo sebuleni kwake akitazama televisheni yake kubwa sana iliyoweza kumletea ulimwengu waote sebuleni kwa muda mfupi.
“Sio bure, kila mtu serikalini ameshangaa na hatua aliyochukua Mheshimiwa” Madam S alimueleza Amata
(...) Mheshimiwa hongera kwa kazi yako nzuri, kila mtu hachoki kulitamka jina lako, na mi pia nafanya vivyo hivyo. Kwa kazi yako nzuri leo hautaliona jua la kesho lakini uhai wako hautapotea bure endapo ukikubali kuja nilipo na kuzungumza, ukichelewa vijana watakuja kuchukua mzigo (...).
Kamanda Amata alikumbuka maneno ya barua aliyoichukua ofisini kwa Punde Kishime usiku ule lakini kila alipojaribu lupiga simu kwa namba ambayo ilikuwa mle simu haikupatikana kabisa.
Sasa jambo jipya lilikuwa limeanza, kazi mpya ilikuwa inajitokeza, uanasiasa wa Punde Kishime, Tanzania Secret Agency namba 1, Kamanda Amata alianza kuuwekea uanasiasa huo alama za kujiuliza....
“Mamluki!” Madam S alisema neno hilo huku akiinuka na kuliendea fridge kubwa lililo katika kiujia cha kuendea jikoni, akalifungua na kutoa chupa moja kubwa ya grants kisha kwenye kabati la jirani akatoa sprite moja moto na kuelekea sebuleni akaketi tena mbele ya TV ile na kummiminia kinywaji Amata kisha wakaendelea kutazama matangazo yale ya moja kwa moja.
Kamanda Amata alitoa bahasha ndogo na kumtupia Madam S
“Weka muvi hii tuangalie” Amata alimwambia Madam S
“Hivi we una akili, huna?” Madam S alishusha bilauri yake kutoka kinywani na kumtupia swali hilo Amata ambaye alikuwa bize kucheza game za simu.
“We weka, si nimekwambia weka au?” Amata alimueleza madam S kiutani kama kawaida yake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Madam S, mwanamama jasiri na mtata, anayeishi peke yake maisha yake yote, mkuu wa kitengo maalum cha usalama wa taifa, alimzoea Amata na kumfanya kama mtoto wake. Tangu walipokutana na Amata kumuokoa kutoka katika mikono ya genge la waharifu huko Columbia alipokuwa akifanya upelelezi juu wapi dawa za kulevya zinazoua nguvu kazi ya taifa zinatokea na kujikuta mikononi mwa genge hilo hatari, akiwa amekwishakata tamaa ya kuuona uhai tena, asubuhi moja alimuona kijana huyu kama Malaika mlinzi, na jinsi alivyomuokoa ndicho kilichomfurahisa zaidi, wepesi wake wa kupigana na watu zaidi ya mmoja na ujuzi wa kutumia kila aina ya silaha iliyo karibu naye. Waliporudi nchini ndipo alipoomba rasmi kijana huyu machachari aingie katika kazi maalum ya utatuzi wa mambo mazito. Baada ya miaka kadhaa Mheshimiwa Rais alimteuwa Madam S kuwa incharge wa kitengo hicho akitokea idara ya usalama wa taifa.
Amata alijisikia faraja sana kufanya kazi na mwanamama huyu mtu mzima, aliyepita katika misukosuko mingi sana na asiyekubali kushindwa mwenye mbinu nyingi za kupambanua matatizo magumu kitaifa na kimataifa, aliyekomaa na mwenye mafunzo ya hali ya juu ya kijasusi aliyochukua huko katika shirika la kijasusi la Mossad.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment