Simulizi : Njia Nyembamba
Sehemu Ya Pili (2)
“Yani Amadu, ulipewa barua na wewe ukaileta bila kusoma?” Farah aliuliza. Amadu akatikisa kichwa.
“Sasa nifungue ya nini na hainuhusu?”
“Haa! Kama ni ujumbe wa kukuua? … We unaleta tu.”
“Sidhani. Kama ingekuwa ni ujumbe mbaya kunihusu, wasingenituma. Ila tu nashangaa ujumbe huo ulivyokuwa wa siri mno kiasi cha kuulizwa ulizwa hivyo.”
“Kuna jambo.” Ussein alitia neno. “Unadhani, Amadu? Kutakuwa kuna kitu.”
Amadu alitabasamu akaendelea kunena na shoka lake aukate mti. Baada ya muda wa robo saa shughuli ikiwa inaendelea, Mou aliacha kukata mti akashika kiunoche.
“Yani mi nakata tu hapa basi, nimekasirika vibaya mno. Siamini kama kweli nafanya hii kazi kwa ajili ya Talib. Shenzi kweli!”
“Utafanyaje sasa na yamekwisha tokea, kaka?” Farah aliuliza huku akichakarika kukata mti.
“Ndio, yametokea lakini huku ni kuonewa sasa. Sijui Talib kamlisha nini General Kessy, hataki hata kutusikiliza.”
“Jamani tuendelee kupiga kazi. Tusije tukakawia tena yakawa matatizo mengine.” Amadu alishauri. Wanaume wakaendelea kupiga kazi. Yakiwa tayari magogo kumi na tano yamekatwa, wakina Amadu walirudi kambini kunywa maji. Hapo wakakutana na Talib ambaye mkononi alikuwa kabebelea chupa ya kilevi.
“We mbwa wewe! … Unajikuta mjanja, sio?” Mou aliwaka. Talib alikunywa fundo moja akatabasamu. “Hamuoni aibu mtu mmoja kuwazidi watano?”
Mou alitaka kumvamia Talib lakini wenzake walimtuliza wakimtaka aachane naye, walienda kunywa maji wakarudi kazini, ndani ya saa kumi ya jioni magogo yakawa tayari, yalibebwa na kuletwa mbele ya makao makuu kuonyeshwa. General aliyahakiki kwa idadi kisha akawaruhusu wakina Amadu waendelee na shughuli zao. Amadu alikwenda mtoni kuoga, aliporejea alienda chimbo mule walipo mke wa waziri na mtoto wake kuwajulia hali. Aliwakuta wapo hoi wamelala hawajiwezi. Alifungua mlango akainga ndani.
“Vipi, nini shida?”
“Njaa.” Alijibu binti kwa sauti kavu inayoyoma. Haraka Amadu akatoka chimbo na kuelekea hemani mwake kutafuta chakula. Alitafuta sahanini lakini hakupata. Alikwenda kwenye basi walilokuja nalo, humo akakuta mabaki ya chakula aliyoyachukua na kupeleka chimbo.
“Kuleni!”
Amadu alisema huku akitua masufuria mawili ya chakula. Mwana waziri aliwahi sufuria akapeleka matonge mawili mdomoni. Alimuamsha na mamaye akamlisha. Amadu aliwatizama na macho ya huruma wakiwa wanakata matonge kama watu ambao wamehaidiwa kutokula tena baada ya hapo.
“Hamkula tangu muda gani?”
“Tokea jana asubuhi.”
“Mmmh … Poleni.”
Mwana waziri hakujibu, aliendelea tu kula yeye na mamaye. Amadu hawakuongelesha tena. Alibakia wakiwatizama mpaka walipomaliza.
“Ahsante.”
Alisema mwana waziri. Mke waziri hakusema jambo, alijiegemeza ukutani na uso wa huzuni uliofanana na mwanae ambaye aliamua kulaza kichwa kwenye miguu ya mamaye.
“Kwanini mnatutesa hivi lakini? … Kama mnatuua tuueni tujue moja.” Alilalamika mwana waziri. Amadu alimtizama binti kwa muda kidogo kabla hajafungua mdomo wake.
“Nawaonea huruma sana kwa kuwa waathirika wa harakati za mapinduzi. Lengo letu sisi si kuwaumiza wana Sierra wenzetu, ila tunajua kwamba katika mapambano yetu hatuwezi kukwepa wachache kuumia kwa ajili ya wengi. Tusamehe sana.”
Mwana waziri alinyanyua sufuria akambamiza nayo Amadu.
“Toka! … Sitaki hata kukuona. Nenda … usiniletee unafiki wako hapa. Sitakusahau maisha yangu yote kwa kubadili maisha yetu juu chini. Sitokusahau kamwe!” Mwana waziri aling’aka. Amadu alimtizama akatikisa kichwa chake;
“Najua huwezi ukanielewa. Ila tambua kwamba, baba yako ni mojawapo wa watu waliofanya mamia na maelfu ya wa Sierra Leone kupata hida mno. Baba yako akiwa Mkuu wa jeshi la ulinzi aliungana mkono na waziri wake wa ulinzi, Louis Diarra, kuleta machafuko kwa kumtoa kimabavu raisi Assessoko. Watu wengi wakauwawa, ikiwemo wazazi na dada yangu. Watu wakawa vilema, ikiwemo ndugu, jamaa na rafiki zangu. Siwezi nikakaa tuli wakati damu zao zanidai. Siwezi nikatulia tuli kwa kuwa nimepata angalau nafasi ya kulilia damu za wapendwa niliowapoteza. Najua kwako si kitu, kwasababu wakati mimi na wana Sierra Leone wengine tukiwa tunakikimbia kifo mitaani dhidi ya wanajeshi wa pande mbili waliokuwa wanararuana, wewe na familia yako mlikuwa nje, ufaransa, mkiishi kwa amani, mkinywa juice huku mkitutizama runingani.”
Amadu alieleza ya moyoni. Mwana waziri alimtizama akabinua mdomo wake.
“Unajificha kwenye uvungu wa mapinduzi lakini wewe ni mlipiza kisasi tu. Upo tayari kwenda kuua tena wa Sierra Leone wenzako na kutengeneza watu wengine kama wewe, unadhani huo mduara utkwisha? Mtakapokuwa madarakani nao watataka kufanya kisasi kwa kuua familia zao, huoni kama unarudia kosa walilofanya wenzako?”
“Vyovyote vile!” Amadu alijibu kimapuuzi. Alinyanyuka akaondoka zake kurudi hemani. Alijilaza kwenye godoro lake akavuta begi lake lililokuwa kando akatoa picha ya baba, mama na dada yake akawa anazitizama kama mtu anayekumbuka jambo. Alifanya zoezi hilo mpaka pale kengele ya kwenda kula ilipogonga, akanyanyuka kuelekea kupata chakula. Alipanga mstari akawekewa chakula, alikula akakimaliza. Akaenda kuongeza tena. Mpakuaji alimtizama kwa macho ya jazba akamuuliza;
“Si umeshakula?”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Weka chakula kwani kimewekwa kwa ajili gani!” Amadu alifoka kwa ukali. Mpakuaji hakuuliza tena, aliweka chakula pomoni kwenye sahani. Amadu akatafuta sahani nyingine na kuleta iwekwe chakula, ikafanywa hivyo. Akiwa amebeba sahani zake mbili, Amadu alielekea chimbo sahani moja akamkabidhi Chui na nyingine akamkabidhi mwana waziri, ila hakujua, nyuma yake Talib alikuwa anamfuatilia akitizama kila kitu alichokuwa anakifanya.
Kesho asubuhi, baada ya kengele ya kifungua kinywa kugongwa, kengele ya mkutano iligongwa wapambanaji wote wa MDR wakakutana eneo lao moja. Hawakuwa katika idadi ile ya mwanzoni, 800, ni kama watu mia tatu hawakuwepo. General Kessy, akiwa mbele ya hadhira alianza kueleza nia ya makutano;
“Leo, kama ilivyo jana na juzi, vitaongezeka vikosi vingine viwili kwenda Kabala, ambavyo ni kikosi Simba na kikosi Tembo. Mbali na hayo, nadhani wote mnajua leo ni mwisho wa wiki na huwa kuna nini, bahati mbaya mkuu leo hatutokuwa naye kutokana na majukumu ya hapa na pale, ila mambo ni yale yale.”
Wafuasi walishangilia baada ya hiyo kauli.
“Na kwa wale wanaoenda Kabala, msihofu. Mtindo ni ule ule. Vinywaji na vyakula vyenu vitakuja huko huko. Sahauni matatizo yenu, leo ni siku ya kufurahi. Tunywe na kunywa! … Ila mchunge hizo mashine zenu huko mnakoenda kutafuta vipashio.”
General alimaliza kwa hayo maneno, wafuasi wakacheka. Haikupita muda mrefu, magari yaliyobebelea pombe yakaanza kumiminika, Vyakula navyo vikaanza kupikwa tofauti na siku za wiki. Jua lilipozama, sherehe ikachomoza. Wafuasi wa MDR wakanywa na kula. Wengine wakaenda kutafuta wanawake. Amadu alichukua chakula cha kutosha akapeleka chimbo kwa mateka. Wakati anafanya hivyo, Talib alikuwa anamtazama tena kila alichokuwa anakifanya.
Baada ya muda kidogo, Amadu akanyanyuka na kwenda hemani kwake. Talib alijificha asionekane. Amadu alivyopotelea, Talib akatoka alipokuwa amejificha na kuelekea chimbo. Mwendo wake ulikuwa wa kilevi akipepesuka. Macho yake yalikuwa legevu kama vile aangukia mbele. Alijishikizia kwenye kuta ya chimbo akarusha macho yake ndani kumtizama mke wa waziri pamoja na mwanae waliokuwa wamejilaza. Akatabasamu.
“Nyie mbwaa! Mmekula sasa mmelala eenh?” Alihororoja kwa kebehi. Mke wa waziri pamoja na mwana wakashtuka na kutizama kule sauti itokako.
“Si nawauliza nyie hamnisikii!”
Talib alifoka kisha akanyoosha mkono wake juu ya jengo akatoa ufunguo allioupenyeza kwenye kitasa kisha akaingia ndani.
“Mmmmh … mtu na mama yake, sio?” Talib aliongea kisha akajichekesha. Alimnyanyua mke wa waziri akampiga na kiwiko kichwani, mama akapoteza fahamu. Akamnyooshea bunduki binti waziri akimtaka anyamaze kimya na aongoze kwenda nje, binti akatii, huku mikono yake ikielekea juu alitoka nje ya chimbo na kwenda misituni.
“Kata kulia! … Tembea kabla sijakufumua ubongo! … Tembea haraka, si umetoka kula wewe!”
Talib aliropoka huku akimsukumiza binti waziri. Walipotembea baada ya dakika kumi na nane, Talib akamuamuru binti waziri asimame avue nguo zake. Binti aliposita alipigwa makofi kama si ngumi. Huku akibubujisha machozi akavua nguoze na kumgeukia Talib kama aelekezwavyo.
“Lala chini tanua miguu malaya wewe!”
Binti akajilaza chini na kutanua miguu yake. Talib akafungua zipu na kushusha suruali. Alipiga magoti akapeleka mkono wake sehemu za siri za binti waziri akaanza kuzichezea. Ingawa mtendwaji alikuwa amekunja sura kwa hasira, mtenda alikuwa anatabasamu, mkono wake wa kulia ulimnyooshea bunduki mtendwa asipate kujaribu fanya lolote.
Baada ya kuchezea sehemu za siri za binti waziri, Talib akatoa uume wake toka kwenye nguo ya ndani, akaupakaa mate uke wa binti waziri tayari kwa kufanya tendo la uingiliaji. Kabla hajafanikiwa kuingiza uume wake, binti waziri alikusanya fundo la udongo na mkono wake wa kuume akaurushia usoni mwa Talib. Talib akaweweseka, kabla hajatumia silaha yake, binti waziri alitumia mguu wake kuupiga teke mkono wenye bunduki kisha akavuta mti uliokuwepo kando na kumbamiza nao Talib kichwani kwanguvu, Talib akadondoka na kuzirai. Binti waziri alivaa nguoze akachukua silaha na kuanza safari ya kurudi kambini kwa machale. Kila aliposikia sauti ama kishindo, alijificha akiweka silaha yake tayari. Alipofika, kwa uangalifu mkubwa akafungua mlango wa chimbo akamfuata mamaye.
“Mama … Mama!”
Aliita lakini mamaye hakuamka. Baada ya kumtikisa tikisa, mama aliamka akavuta pumzi kwanguvu.
“Amka mama twende, amka!” Binti waziri alisihi kwa kunong’oneza. Mama akaamka na safari ya kuacha kambi ikaanza.
“Tunaelekea wapi sasa, mwanangu?”
“We twende tu mama. Tutajua huko huko!”
Wakapita miti mirefu na mifupi pamoja na vichaka vyake. Baada ya dakika ishirini walifika kwenye mto mkubwa, wakasimama.
“Huu mto unatokea Sierra, tuambae nao.” Binti waziri alisema.
“Una uhakika?”
“Sio sana. Ila ufahamu wangu wa jografia kidogo wanieleza hivyo. Lakini hata kama hatutotokea Sierra, basi tutatokea sehemu nyingine mbali na hii. Heri nusu shari kuliko shari kamili.”
Hao wakaanza kuufuata mto kwa pembezoni wakielekea kaskazini. Walipambana na matope pamoja na mawe ya mto wakiyaruka na muda mwingine wakijikwaa kutokana na uwepo wa mwanga hafifu lakini hawakukoma, waliendelea na safari. Ila si muda wote walifanikiwa, mke wa waziri alijikwaa akadondoka chini kichwa chake kikagonga juu ya jiwe. Damu zikamwagika. Hakupata hata mwanya wa kusema kitu, akawa amefariki.
Binti akaita na kumtikisa mamaye pasiwepo na matokeo. Wakati yu hapo analia, alisikia mlio wa mngurumo wa mnyama mithili ya mbwa ama simba. Akashtuka. Akatizama huku na huko na ghafla akaona kitu kama mnyama mkubwa kikimsogelea. Alinyoosha mkono wake wenye bunduki kuelekea huko huku akitizama kwa umakini. Loh! Akamuona simba tena simba dume akiwa anachechemea kumfuata.
Simba alinguruma kuonyesha mabavu. Macho yake yalikuwa yanang’azwa na mwanga wa mwezi na kumfanya atishe zaidi. Binti waziri alivuta pumzi ndefu akafyatua risasi. Simba akalalamika kwa maumivu. Kwa hasira sasa, akaongeza mwendo wake kumfuata binti waziri. Pasipo kufanya ajizi, binti akalenga tena risasi mara mbili, simba akadondoka. Alimnyanyua mama yake akamuweka mgongoni na safari ikaendelea ila sasa ikiwa na mwendo wa pole pole.
Baada ya dakika moja, binti akachoka. Alitua mwili wa mama yake chini avute pumzi. Alipopata tena nguvu akajitwika mwili wa mama yake na kuendelea safari. Alifanya hivyo kwa mara nne kabla hajapoteza nguvu kabisa na kulala chini akiwa analia. Alimuita tena mama yake lakini hakupata majibu, ni kama vile hakuwa anaamini kama mama yake kafariki. Aliweka sikio kifuani asisikie kitu. Aliweka vidole vyake pembezoni mwa pua asihisi kitu. Alishika tama machozi yakimtiririka, baada ya muda akasema;
“Nisamehe mama. Sina budi kutenda hili.” Akanyanyuka akakata matawi mengi ya mti, akamfunikia mamaye na kusali kisha akaendelea na safari.
Wakati anatembea, kwa mbali akaona mwanga wa taa. Akausogelea taratibu na kwa tahadhari, akaona kajumba kamoja kadogo. Alikasogelea akachungulia ndani, akamuona mwanaume mmoja mzee akiwa amevalia kofia chakavu amejilaza kwenye kiti. Kwa muda kidogo akawaza, mwishowe akaweka bunduki yake kwenye nguo ya ndani akaugonga mlango. Mzee aliyekuwepo ndani akashtuka. Alitizama kwa hofu. Alifuata dirisha lake na tochi akachungulia nje akiuliza;
“Nani?”
Binti waziri hakujibu kitu. Mwanga wa tochi uliommulika ulimpa Imani mwenyeji akafungua mlango.
“Karibu!”
“Ahsante.”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Binti aliingia ndani, na hapo ndipo akajiona aligeuza nguo zake.
“Vipi? Naweza nikakusaidia?”
“Samahani baba. Naitwa Ulsher; mtoto wa waziri wa ulinzi na usalama Sierra Leone. Naomba msaada wako.”
“Mtoto wa waziri wa ulinzi?”
“Ndio!”
“Bwana Mamadou Toure?”
“Ndio. Ni baba yangu!”
Mzee yule akamtizama Ulsher kama vile anamkagua. Alipomaliza akatabasamu.
“Baba yako huwa namsikia redioni!” Akaonyeshea redio yake ndogo aliyoitoa pembezoni mwa kiti.
“Karibu sana. Keti hapo kitini.”
Kwa furaha, mzee yule akamkaribisha Ulsher kwenye kiti chake yeye akasimama.
“Umetokea wapi? … Baba yako anakutafuta sana! Ametangaza donge nono la pesa kwa yeyote atakayetoa taarifa ya kupatikana kwako. Hatimaye nakuwa tajiri. Mama yako yupo wapi? enh?”
“Nimetokea huko kusini. Tulikuwa tumetekwa na waasi. Mama yangu amefia njiani tukija huku.”
“Eish! Pole sana. Hao waasi ni wa MDR?”
“Umejuaje?”
“Si nimekuambia huwa namsikia baba yako akiongea redioni. Unataka kuniambia ni kweli hao waasi wa MDR wapo Guinea?”
“Ndio!”
“Mbona raisi wetu wa Guinea huwa anakana!”
“Sijui. Ila inaonekana anajua kuhusu hawa waasi na kwa njia moja ama nyingine wanahusiana.”
Mzee yule akaonyesha kufikiri kisha akauliza;
“Kwanini sasa wafanye hivyo?”
“Sijui!” Ulsher akajibu kwa mkatisho na kuuliza; “Una simu?”
“Hapana!”
“Una kitu gani sasa cha mawasiliano?”
Mzee yule akaonyeshea redio. Ulsher akatikisa kichwa kusikitika.
“Kutembea hapa mpaka Sierra ni muda gani?”
“Mmmh kwa miguu kama siku mbili kwako wewe.”
“Kuna njia yoyore ile naweza nikaitumia?”
“Hapana! Njia ni hii hii ya msituni. Ila una bahati sana kufika hapa salama. Huko msituni si salama kabisa, kuna wanyama wa kila aina; nyoka wakali, simba, chui na kadhalika. Ni hatari kutembea usiku.”
“Sina namna. Unaweza ukanisaidia kunipelekea Sierra?”
“Ndio. Ila si saa hii.”
“Saa ngapi?”
“Jua likiamka. Muda huu ni hatari tunaweza tukamezwa hata na chatu!”
Ulsher akakubali japokuwa kishingo upande.
Keng! Keng! Keng! Keng! Keng! Keng! Keng! Kengele iliita kwanguvu wafuasi wakakusanyika kwa pamoja eneo lao. Wengine walikuwa wanayumba yumba kutokana na kunywa. Wengine walikuwa wamelala hata kujielewa hawakuwa wanajielewa, hivyo hawakufika makutanoni. Wengine hawakuwepo hata eneo la kambini, walikuwa masafa ya mbali kujivinjari.
General Kessy alisimama mbele ya umati. Macho yake yalikuwa mekundu yakiandamwa na ndita za hasira. Baada ya kwenda mbele hatua kadhaa na kuzirudia, alipaza sauti yake kali;
“Ni nani amefungulia mateka kule chimbo!”
Mizozo ikavuma miongoni mwa wafuasi. Amadu alitoa macho ya mshangao, wakati huo Talib akitizama tizama kiwizi wizi.
“Mateka wawili hawaonekani; mke wa waziri pamoja na mwanae. Mlango umekutwa wazi … Wazi kabisa! … Nauliza nani kafungulia mateka?!” General alitema moto. Minong’ono ikaendelea kuvuvuma bila ya kuwapo kwa majibu yoyote.
“Sasa basi. Kwanza, kuanzia leo hakutakuwa na sherehe tena! Naona hiyo ndiyo inawapa uzembe. Pili, adhabu kali itatolewa kwenu wote, hamtopokea pesa yoyote ya kujikimu kwa miezi mitatu na mtakula mara mbili tu kwa siku. Yote hayo yataanza kutekelezeka kuanzia leo endapo tu kama anayehusika na tendo hilo la kidhalimu hatowekwa wazi!”
Minong’ono ikaendelea kuita kwa wafuasi. Juuze sauti ya Talib ikapaza;
“Mkuu, mimi sifahamu haswa nani aliyefanya hilo tukio. Ila nataka tu nikutaarifu kwamba kuna mtu huwa anachukua chakula na kuwapelekea mateka mara kwa mara badala ya mara moja kwa siku. Lakini pia hukaa na kuongea nao kwa muda. Nadhani yeye atakuwa ana ufahamu kuhusu tukio hilo.”
“Ni nani huyo?” General akauliza.
“Ni Amadu!” Talib akajibu. Watu wote wakamtizama Amadu.
“Amadu ni kweli?”
Amadu alinyoosha shingo yake akajibu;
“Ndio, ni mimi.” Alisema kwa kujiamini.
“Amadu, haujui utaratibu? Au?”
“Najua, mkuu. Mke wa waziri hali yake …”
“Nyamaza!” General alifoka. “Nyamza mpumbavu wewe! … Umekuwaje siku hizi?”
“Ila mkuu, sijafunguli …”
“Nimesema nyamaza! … Hey! Kamateni huyo mumpeleke chimbo mkamfungie huko. Na asipewe chakula kwa siku tatu!”
Haraka wanaume watatu wakamkamata Amadu na kumpeleka chimbo. General akaendelea kuhutubia;
“Rosem, Sakho na Mohamed!” General aliita. Walengwa wakaitika.
“Nataka mateka hao warudi hapa kabla ya kesho jioni. Mnaujua msitu wote huu. Nendeni kfanyae kazi!”
Rosem Sakho na Mohamed wakaondoka kwenda kuchukua silaha na vifaa vingine kama darubini, kurunzi na miwani moja ya kuonea gizani. Safari ya kuwatafuta mateka ikaanza. Rosem akiwa kavalia miwani, Mohamed akiwa kashikilia kurunzi na wote wakiwa na bunduki, walitembea kwa kasi wakitizama alama za mtawanyiko na mpondeko wa nyasi wakajua Ulsher alipokatiza yeye na mamaye. Baada ya muda wakafika mtoni, hapo wakaanza kufuatilia nyayo za miguu zilizojichora kwenye tope mpaka wakafikia kwenye jiwe lililotapakaa damu pembeni yyake kukiwa na mzoga wa simba. Wakasimama hapo,
“Hii ina maanisha nini?” Rosem aliuliza.
“Kuna mtu aliteleza hapa, unaona huu mguu ulifyatuka. Na huyu simba alikuja baada ya wao kuwa hapa chini, kama isingekuwa hivyo, tungeona nyayo zote hizi zikiwa katika harakati ya kujikomboa.” Mohamed alielezea huku akinyooshea alama za miguu.
“Inaelekea huyu mtu kajeruhiwa vibaya sana, damu ni nyingi!” Sakho naye alichangia. Wakaendelea kidogo kutembea.
“Umeona hapa!” Rosem alionyeshea nyayo. “Mtu wa pili hayupo, sasa kuna nyayo ya mtu mmoja tu. Atakuwa kaenda wapi?”
Mohamed alichuchumaa akatizama zile nyayo akajibu, “Wapo pamoja!” Alinyanyuka akamtizama Rosem.”Nyayo iliyobakia yenyewe inaonekana imedidimia chini zaidi kuliko za mwanzo, atakuwa amebeba mzigo, atakuwa amembea mwenye jeraha.”
Wakaendelea kusonga mbele. Baada ya dakika kama tatu, wakaona majani mengi yametapakaa. Walipotizama tizama vizuri waliona alama za kuburuzwa zikiwa zimetapakaa damu. Wakaanza kufuatilia alama zile kwa tahadhari. Walipofika mbele zaidi wakakuta kipande cha mkono wa binadamu. Rosem akaubeba na kuutizama.
“Huu mkono ni wa kizee. Utakuwa wa yule mama.”
Waliporusha macho yao mbele wakaona vipande vipande vya nyama, mbavu pamoja na mifupa mingine.
“Keshaliwa!” Sakho alisema huku akibinua mdomo wake.
“Inaelekea alikufa baada ya kujigonga kwenye jiwe akazikwa kwa kufunikwa na majani!” Mohamed alibashiri. Waliachana na mabaki hayo ya mwili wakaendelea na safari yao kumtafuta Ulsher wakifuatisha vilivyo alama za nyayo zilizoachwa juu ya uso wa dunia.
Baada ya mwendo wa dakika tatu, sauti ya mngurumo ilisikika, wapambanaji wa MDR wakashtuka. Walisogeleana karibu wakiwa wameshikilia bunduki zao tayari kwa ajili ya kushambulia. Rosem alipepesa macho yake kushoto na kulia asione kitu. Mohamed naye alipeleka kurunzi yake kushoto na kulia pasipo kuona jambo. Walipogeuza macho yao nyuma, Loh! Wakaona simba akiwa hewani, mikono yake yenye kucha ndefu pamoja na mdomo vikiwa vimeachama. Ni kufumba na kufumbua, simba akawa amemdondokea Rosem na kumpeleka chini. Alinyanyua mkono wake wa kuume na kurarua uso wa Rosem. Mohamed pamoja na Sakho wakashambulia kwa kufyatua risasi. Kama vile simba hakusikia risasi, alimnyofofa nyofoa Rosem aliyekuwa anapiga kelele za maumivu. Pale Mohamed alipopiga kichwa cha simba mara mbili, ndipo simba akadondoka na kufa. Mohamed na Sakho wakamsogelea na kumtazama mwenzao. Alikuwa hatamaniki hata kidogo. Uso wote ulikuwa mwekundu uchuruzao damu nyingi toka kwenye makovu ya kina ya kucha za simba. Shingo yake ilikuwa imenyofolewa na kuachwa shimo kubwa hali kadhalika kifuache. Miwani yake ilikuwa imekatika katika ikiwa pembeni. Sakho na Mohamed wakaachama kwa bumbuwazi lililobeba taharuki ndani yake. Rosem alikuwa akipapatika papatika na baada ya muda, akakata roho.
“Eish! Sasa tunafanyaje?” Sakho aliuliza. Uso wake ulionyesha u njia panda pamoja na uoga vile vile.
“Hatuwezi tukambeba. Hatujui huko tuendako. Hatuwezi pia kumuacha hapa” Mohamed alifunguka.
“Na hatuwezi kurudi kambini pia!” Sakho naye akaongezea.
“Sasa tufanye hivi. Tumzike na tuache alama. Tutakuja kumfukua na kumrejesha kambini.” Mohamed alishauri.
“Sasa tunamzika na nini?”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Tuchukue miti tuchimbie.”
Walikata matawi manene ya mti wakaanza kufukua. Shukrani kwa ardhi pembezoni ya mto ilikuwa laini. Walifukua na kusogeza udongo kwa mikono yao mpaka shimo likapatikana japo halikuwa na urefu mkubwa. Waliingiza mwili wa Rosem humo wakafukia, juu yake wakachomeka mti.
“Pumzika kwa amani, mpambanaji.” Wote wakasema. Walipoteza masaa mawili, zaidi walimpoteza mwenzao. Mohamed alimulika mbele na kurunzi yake safari ikaendelea. Bahati kombo baada ya dakika kumi na tano za utembezi wao, nyayo walizokuwa wanazifuatilia zikapotea. Zilimezwa na maji ya mto baada ya kujaa. Sasa hapo Sakho na Mohamed wakabaki njia panda.
“Tunaenda wapi sasa?” Sakho aliuliza.
“Sijui hata!”
“Bora ingekuwa kwenye majani tungejua. Sasa hapa sijui atakuwa kaelekea wapi. Sijui alipanda juu ya mawe akaenda hukoo au hukuuu?!”
Hawakupata jibu. Mwishowe Sakho akatoa ushauri,
“Mohamed, tupumzike. Asubuhi tutaendelea!”
“Tupumzike?”
“Ndio! … Sasa hapa tutafanya nini? Usihofu huyo mateka hatokuwa amekwenda mbali. Kufika Sierra ni siku mbili, tena bila kusimama. Unadhani ataweza? Msichana? Asubuhi maji yatakuwa yamepungua, tutapata kuona hizo nyayo.”
“Lakini tukimkosa je? General atatuua nakuambia.”
“Hatuwezi tukamkosa bwana. Tutampata tu. Alafu unavyoniona hapa nimechoka kweli, si unajua tena tumekunywa sana ndugu yangu, au hukuniona ninavyopepesuka muda mwingine?”
“Na vipi kuhusu wanyama wakali humu?”
“Aaah Mudi! … Ni mara yetu ya kwanza hii kulala msituni? Si tunawasha moto tu.”
Mohamed akaridhia. Wakawasha moto na kujilaza kando kando yake. Hakuchukua muda mrefu, Sakho akapitiwa na usingizi tena mzito. Aliachama mdomo wake na kuchuruza mate lakini Mohamed alikuwa amelala mguu mmoja ndani mwingine nje. Kila aliposikia tu kamlio alifungua jicho kutizama. Ila naye baada ya muda, usingizi ukambeba. Labda pombe walizokunywa zilianza kufanya kazi. Hakufungua tena jicho.
****
Wakati Chui anageuka usingizini alimgonga Amadu na mguu wake, akashtuka. Amadu alikuwa ameketi kitako akiegemea ukuta, bado alikuwa macho. Chui alijikusanya akaketi na kumtizama Amadu kwa mshangao.
“Vipi, umekuja saa ngapi?” Akapangusa uso wake afute usingizi. “Umekuja muda mrefu? Mbona hujanishtua?”
“Wamenifunga.” Amadu alisema na kuongezea, “Wamenishtumu nimewafungulia mateka wakatoroka.”
Chui akaguna na kukunja sura.
“Wamekufunga?”
“Ndio!”
“Ila mbona aliyewafungulia mateka ni Talib?”
“Talib?”
“Ndio, Talib. Nimemsikia kwa masikio yangu akiwaongelesha mateka. Alimuamuru mmoja atoke na yeye na ajabu baadae nikasikia sauti ya yule aliyetoka naye akimuamsha mama yake. Nao wakatoka! Ila sikusikia tena sauti ya Talib!”
“Talib.” Amadu alisema huku akitikisa kichwa chake kwa masikitiko. “Nimekufanya nini unifanye hivi?” Alijiuliza. Macho yake yakawa mekundu. Akalaza kichwa chake ukutani akatizama juu.
“Usihofu, Amadu. Yatakwisha.” Chui alimpa moyo Amadu.
“Samahani sana, Chui. Hakika nimekuleta kwenye matatizo.” Amadu alisema kwa upole.
“Hapana, Amadu. Yote yana mwisho. Bado naamini kwako, kumbuka na wewe ndiye uliyenipa tumaini la kupigania haki.”
“Nashukuru sana kwa kuniamini, Chui. Ila naumia sana kuona nazidi kupoteza Imani yangu kwa mkuu wangu.”
“Usiogope. Maovu yote yana mwisho wake. Siku moja mkuu ataelewa kweli nawe utakuwa huru.”
Amadu akamtizama Chui na kumshika mkono wake wa kuume.
“Nashukuru sana kwa kunipa nguvu. Siku moja yote haya yatakuwa historia. Na tutakuwa washindi.”
“Amina.” Chui akasema kwa tabasamu.
“Ila … Huyo binti atakuwa kaenda wapi na mama yake?” Amadu aliuliza lakini akionekana hategemei kupata jibu.
“Sijui. Si ndo’ familia ya waziri?”
“Ndio.”
“Endapo wakifika Sierra Leone mtakuwa hatarini. Watatoa maelezo ya mpatikanapo na kutakuwa na mgogoro mkubwa kati ya Guinea na Sierra, hata vita pia.”
“Unachokiongea ni kweli lakini wataweza kweli kufika ama watakuwa kitoweo cha wanyama huko porini? …. Kuna wanyama wakali huko wa kila aina, ni hatari. Tena ni hatari zaidi kwao kama wanawake. Isitoshe yule mmama, mke wa waziri, anaumwa.”
“Unaonekana kujali sana, Amadu. Kwanini? Hiyo si sifa ya waasi.”
“Ndio mana nilikuambia sisi si kundi la wa …”
“Hapana! Wewe si muasi, ni mwanamapinduzi. Ila si wengine mithili ya Talib.”
“Nashukuru. Nyie wote ni wana Sierra Leone kama mimi, kuwatesa nyie ni kuuendeleza unyama ule ule uliotufanya tukaunda hili kundi. Wanaostahili mateso ni wale waliotuingiza hapa, si vinginevyo.”
“Hakika. Uongeacho ni sahihi ila sidhani kama ndilo hilo walifuatacho wenzako.”
“Ndicho hiko, sema tu kama unavyojua penye wengi pana mushkeli. Wote lengo letu ni hilo. Wote dhamira yetu ni kuikomboa Sierra Leone na si kuiangamiza.”
Amadu akatizama ukutani kama mtu anayewaza.
“Kuna kitu kimoja aliniambia yule binti waziri kila nikiketi kinanirudia. Endapo kama sisi tutatumia mabavu kuuondoa utawala kwa kuua na kutesa watu, hata tutakapo kaa madarakani yataibuka tena makundi mengine wakitaka kulipiza kisasi. Hivyo tutakuwa tumetengeneza mduara wa visasi na visasi.”
“Ni kweli. Sasa wewe una mawazo gani?”
“Kwanza, nataka nijitofautishe na mlipiza kisasi. Nataka niwe zaidi ya hapo, sitaki kuruhusu kisasi kiniendeshe bali dhamira yangu. Zaidi ya kupigania damu ya wazazi wangu, jamaa na marafiki, nataka niwapiganie wananchi wangu, wapate maji, wapate umeme, wapate huduma za afya, wapate barabara, wapate mlo wa kila siku, wajikomboe na maisha yao magumu.”
“Kweli, nakuunga mkono kwa asilimia zote. Inabidi tuwe kitovu cha mbadiliko wanayohitaji wananchi wetu. Ila unadhani tutaweza?”
Amadu akakunja ngumi yake kwanguvu akibinua mdomo wake.
“Tutaweza. Na hii sehemu tunayoyaongea haya itakuwa ya kihistoria.”
Chui akatabasamu.
“Roho yangu ilikuamini toka kitambo. Sitojutia huo uamuzi.”
Wakakumbatiana kwa furaha.
***
Jua taratibu lilianza kuchomoza. Uso wa dunia ukapokea mwanga wa jua kwa shangwe za ndege waliotapakaa kila kona ya msitu. Mohamed akaamka na kuangaza pembeni yake, hakumuona mwenzake kulikuwa tu na darubini. Akanyanyuka na kuangaza huku na kule bila kumuona Sakho. Akapata shaka. Aliweka darubini shingoni akaita;
“Sakhoo!”
Lakini hakukuwa na majibu. Alitizama moto uliokuwa unafifia akausogelea. Kwa kando kidoogo akaona bunduki ya Sakho. Akainyanyua na kuitizama.
“Sakho!”
Alizunguka zunguka maeneo yote ya karibu lakini hakumuona Sakho. Ila kuna kitu aligundua katika msako wake huo. Aliona alama. Alama za nyoka mkubwa akiwa ametambalia juu ya ardhi. Akaamua kuzifuatilia. Hatua kadhaa kwa umbali akamkuta nyoka mkubwa aina ya chatu akiwa kajipumzisha. Tumbo lake lilikuwa pana lisilojificha kwamba amemeza kitu, tena kikubwa. Mohamed akatumbua macho kwa taharuki.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Sakhoo!”
Kwa uchungu akanyanyua silaha yake na kumfyatua nyoka kichwani. Nyoka akafa papo hapo. Mohamed akakata tawi la mti saizi ya kati, akatoboa tumbo la nyoka na kumtoa Sakho humo akiwa hatamaniki; amejawa na ma ute ute mwili ukiwa umebabuka babuka; mbavu zikiwa zimevunjwa vunjwa pia na mifupa mingine ya mwili hali iliyofanya awe nyang’a nyang’a.
Mohamed akambeba Sakho na kumpeleka pembezoni mwa mto, kazi ya kuchimba shimo ikaanza. Akapoteza masaa mawili tangu alipoamka. Alipomaliza, akabeba bunduki yake na kusonga na safari ya kumtafuta mateka akifuatisha alama hafifu za miguu zilizoacha na maji ya mto. Lakini sasa uso wake ukiwa na jeraha la huzuni. Alikuwa yu peke yake wenzake wote akiwa kawazika. Na labda pia kazi iliyo mbele yake ilikuwa inamtafuna akili.
Baada ya muda wa dakika ishirini, Mohamed akaona kijumba juu ya mlima. Alivuka mto akafuata kijumba hiko akakuta mlango upo wazi. Akaingia ndani kwa tahadhari mkononi akiwa na bunduki. Akatafuta tafuta lakini hakuona kitu. Aliona sahani ya chakula mezani na si kingine. Akatoka nje na kuangaza macho ndio akaona alama ya buti kwenye udongo. Akafuatilia zaidi, akaona nyayo za kiatu cha binti. Akiwa huko kilimani, akapeleka darubini yake machoni na kuzungusha shingo yake huku na kule. Kwa mbaaali akamuona mateka akiwa pamoja na mwanaume. Tabasamu likajaza uso wa Mohamed. Alianza kukimbia haraka kuelekea kule aliposhuhudia jambo.
Baada ya dakika nane za kukimbia, akawa tayari ameshawafikia walengwa wake kasoro hatua kumi na tano. Akashikilia bunduki yake vyema kuiweka sawia na pambano baada ya kuona Ulsher ana bunduki ndogo mkononi. Sasa akiwa ananyata asizalishe kelele, alisogea kwa haraka. Punde tu, akasema kwa ukali;
“Hapo hapo mlipo, mikono juu!”
Ulsher na mzee aliyekuwa naye wakagutuka kwa hofu, mikono yao yote ikapanda juu.
“Tupia silaha chini, upesi!”
Amri Ilitolewa na Mohamed, Ulsher akatimiza.
“Geuka na mje kinyume nyume!”
Amri nyingine ikatolewa. Ulsher na mzee wake wakasonga kinyume nyume, Mohamed akawafunga mikono na mkanda wake kisha safari ya kurudi kambini ikaanza, Mohamed akisimamia zoezi kwa kuwashikia mateka bunduki nyuma ya migongo yao.
Walitembea kwa takribani lisaa bila ya kuweka kituo. Ulsher akachoka. Alisimama akamtazama Mohamed kwa sura yenye hasira na mchoko ndani yake, akasema kwa kiburi;
“Nimechoka, naomba nipumzike.”
“Hakuna!” Mohamed alifoka, “muda umeshaenda mno, unatakiwa ufike kambini kabla ya leo jioni.”
“Kuwa na huruma mwanangu.” Mzee naye alichangia. “Huyu ni binti si kama sisi, alafu si tayari umeshamkamata? Hofu yako ya nini?”
“Nimesema hakuna! Na wewe mzee unyamaze hivyo hivyo kabla sijakupasua ubongo wako. Wewe si ndo’ ulikuwa unamtorosha, twende ukapate chai yako huko!”
Hakukuwa tena na neno lingine zaidi ya mwendo kuendelea. Ila baada ya dakika tano, Ulsher akadondoka chini, na kwakuwa alifungwa pamoja na mzee, mzee naye akadondoka chini.
“Nyanyukaa!” Mohamed aliwaka.
“Nimechoka mno. Naomba nipumzike japo kidogo!” Ulsher alisema kwa sura ya huruma, kinyume kabisa na mwanzoni.
“Nimesema hakuna kupumzika, husikii? Ulizoea maisha mazuri enh? Hapa si kwenu. Nyanyuka kabla sijakumiminia risasi sasa hivi!” Mohamed alipaza sauti kali huku akiwa ametoa macho yake kama magololi. Mzee akamtizama Ulsher.
“Jitahidi mwanangu. Utauwawa!”
Ulsher akamtizama mzee na kumnong’oneza;
“Hawezi akaniua. Wananihitaji.” Kisha akaendelea kulala kama vile hakusikia alichoamriwa. Mohamed akapiga kelele na kutoa vitisho vya kuua lakini Ulsher hakuamka. Zaidi alimtaka Mohamed amuue maana hawezi akaendelea kwa kuwa amechoka.
Mwishowe, Mohamed akasalimu amri. Aliwapa dakika kumi na tano tu za kupumzika safari iendele. Ulsher pamoja na mzee wakaketi kitako kuvuta pumzi ya pumziko kwa muda. Mohamed naye akaketi ila macho yote yakawa yanawatizama mateka kwa uangalifu mkubwa.
Milio ya ndege, nyani na mangedere ilikuwa inasikika huku na huko. Lakini zaidi sauti ya maji ya mto ndio ilikuwa inapasua anga kwa wingi wake. Watu hawakuwa wanaongea, kila mtu alinyamaza. Ila juu ya uso wa mzee, machozi yalikuwa yanabubujika. Mohamed aligundua hilo, akauliza;
“Unalia nini wewe mzee?”
Mzee hakujibu. Alifumba macho yake kwanguvu kama mtu anayejitahidi kukausha machozi kisha akaendelea zake kutizama chini.
“Nini kinakuliza wewe mzee? Unaogopa kufa na umri wako umeshakaribia?” Mohamed alisema kwa dhihaka. Mzee akamtizama na kumwambia;
“Naomba uniachie mwanangu. Nisamehe. Hakika sikujua najiingiza kwenye matatizo gani. Umasikini wangu ndo umeniponza.”
Mohamed akatabasamu.
“Pole sana, mzee. Bahati mbaya siwezi nikakuacha uende.”
“Nakuomba, tafadhali. Nina familia inanitegemea.”
“Hapana. Kukuachia huru ni kuweka jumuiya yangu rehani.”
“Hamna, sitosema lolote. Nitanyamaza kimya niendelee na maisha yangu kama awali.”
“Hapana.”
“Nakuomba … Nakuomba.”
“Nimesema hapana, na sitaki kusikia kelele zako tena!” Mohamed alisema kwa ukali. Ila mzee hakukoma, alifungua mdomo kuomba tena aachiwe, Mohamed akamfyatulia bunduki kwenye mguu wake wa kulia. Mzee akapiga yowe kali la maumivu huku akitamani ashike mguu wake uvujao damu. Baada ya Mohamed kutishia kuujeruhi mguu mwingine kwa kutotaka kelele, mzee akajitahidi kunyamza. Alifunga mdomo wake kwanguvu, macho yake mekundu yakimtoka na jasho pia.
“Nyanyukeni tuondoke!” Mohamed aliamuru. Ulsher akanyanyuka na kumsaidia mzee kwa kumvuta, safari ikaendelea ila kwa mwendo pole, mzee alikuwa anachechemea huku akijisindikiza na mafua ya kilio, akivuta makamasi na kuyaachia. Dakika chache baada ya jua kuzama, wakawa wamewasili kambini. Moja kwa moja, Mohamed akawapeleka mateka wake mbele ya makao makuu. General Kessy akatoka nje kuwaona.
“Wapo wapi wenzako?”
“Wamekufa. Rosem alishambuliwa na simba na Sakho akamezwa na chatu. Miili yao nimeizika huko msituni. Ila nimewekea alama kwahiyo twaweza kuipata na kuileta kambini.”
“Yuko wapi mke wa waziri?”
“Ameliwa na wanyama. Tulikuta tu vipande vyake vya mwili!”
General alitikisa kichwa kwa manung’uniko. Alishusha pumzi ndefu akashika kiuno.
“Na huyu mzee ni nani?”
“Huyu mzee nimemkuta akijaribu kumtorosha binti waziri. Alikuwa anamepeleka Sierra Leone!”
General Kessy akamsogelea mzee na kumtazama usoni.
“Wewe ni nani?”
“Naitwa Buruwani.”
“Wewe ndio mtoroshaji, sio?”
“Hapana. Ni bahati mbaya tu, sikujua.” Mzee alijitetea.
Kessy alimtizama Mohamed akampa ishara ya kupandisha kichwa, Mohamed akawachukua mateka na kuwapeleka chimbo, Ulsher akaweka kwenye chumba chake binafsi, mzee akawekwa kwenye chumba cha Amadu na Chui, ila kabla Mohamed hajatoka, Amadu akataka kuongea naye kidogo;
“Samahani Moudy. Mmewapata wale watu?”
“Ndio, ila mmoja tu. Mke wa waziri ameuwawa na wanyama.”
“Pole sana kwa kazi. Vipi, wako wapi Rosem na Sakho?”
“Nao pia wamekufa msituni. Sababu ikiwa hiyo hiyo.”
“Pole sana.”
“Ahsante.”
“Samahani, naomba uwe unatuletea chakula ndugu yangu, si unajua huwa wanasahau sana huku.”
“Siwezi. Nitaingia matatizoni.”
“Hapana, Moudy. Tutakufa njaa.”
“Samahani sana. Lipo nje ya uwezo wangu.”
Mohamed alisema kisha akatoka ndani ya chumba na kufunga nje kwa ufunguo. Bila kugeuka nyuma Mohamed akapotea lile eneo. Amadu alitikisa kichwa chake akamtizama mzee mpya aliyeingizwa mule chumbani akaanza kumhoji, mzee akaeleza yote mpaka kufikishwa pale.
Yakapita masaa kadhaa giza likaivaa uso wa dunia, Farah akiwa anatembea kwa siri, alikuja chimbo akiwa amebebelea sufuria. Alipofika kwenye kuta, akaita kwa sauti ya chini;
“Amaduu …”
Amadu akaitika. Farah akafungua mlango na kumkabidhi Amadu sufuria.
“Nimekuletea chakula.”
“Ahsante sana.” Amadu akapokea sufuria na kuuliza, “Vipi huko, nini kinaendelea?”
“Vikosi vingine viwili vimekwenda Sierra akiwemo Mou na Ussein, na miili ya Sakho na Rosem imezikwa. Ila kuna taarifa mbaya huko Sierra, hali si nzuri. Kuna mapambano makali na watu wetu wengi wameuwawa, inasemekana serikali ya Liberia inamsaidia Diarra.”
“Sasa mkuu amechukua hatua gani?”
“Hatujajua bado ila hali si nzuri.” Farah alijibu kisha akanyanyuka, “Amadu, naomba niende nisije nikajipalia matatizo.”
“Ngoja kwanza!”
Amadu akavuta jani la mgomba pembeni yake akalikung’uta na kupakulia hapo nusu chakula kisha akampa Farah hilo jani.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Naomba umpatie huyo mwanamke aliyekuwepo chumba cha pili. Tafadhali.”
Farah akakubali, akaaga na kutimiza kile alichoambiwa. Amadu akaweka sufuria kati na kukaribisha watu wapate kula. Wakiwa wanafanya hilo zoezi la kupeleka chakula kinywani, Chui na Amadu wakaanza kuteta;
“Serikali ya Sierra Leone ina ushirikiano na Liberia, si tu kibiashara na kiuchumi, hata kijeshi. Si kitu cha kushangaza kusikia Liberia wakisaidia jeshi la Sierra. Hata kama wasingeisaidia kwa sasa, wangefanya hilo baadae.” Chui alifunguka akiwa anakata tonge.
“Sasa hapo tatizo linakuwa kubwa.” Amadu alisema huku akitafuna, “serikali ya Liberia itaisaidia Sierra Leone kwa uwazi kwa madai ya kupinga uasi, hata Afrika nzima itawaunga mkono kwa hilo. Ila kwetu, Guinea inatuunga mkono kwa siri kwa kuhofia wakigundulikana watapigwa vita hata kuwekewa vikwazo kwenye baadhi ya nchi.”
“Ni kweli usemacho, Amadu. Cha kufanya kwa sasa ni kuhakiksha mnazuia msaada toka Liberia kwa njia yoyote ile. Bila hivyo kuuondoa utawala wa Louis Diarra, itakuwa ni ndoto.”
“Kweli, ukizingatia tunapungua idadi. Inabidi hatua zichukuliwe.”
“Hakika. Ila muda nao hausubiri, hatua hizo inabidi ziwe za haraka na zenye nguvu.”
“Sijui kama mkuu atakuwa analifikiria hilo. Natamani nionane naye ila sidhani kama itawezekana.”
“Hakikisha kwanza kabla ya kutaka kuonana naye una cha kumuambia. Inabidi uwe na mipango yakinifu na yenye kuleta tija.”
Amadu akatikisa kichwa kukubaliana na alichokisikia. Alikula tonge moja akasimama kufuata kuta ya mitimiti ya chimbo akaishika na kurusha macho yake angani kutizama mwezi. Alitizama mwezi kwa muda kidogo kama vile kuna kitu anafikiri. Baadae Chui aliungana naye wakawa wanatazama wote mwezi. Kwa dakika kama ishirini walifanya hilo zoezi kwa pamoja kabla ya Amadu kufungua mdomo wake na kuvunja ukimya;
“Kila ninapotizama mwezi kwa muda, naona uso wa mama yangu. Namuona baba yangu na dada yangu. Ila baada ya muda, naona mwezi unabadilika rangi na kuwa mwekundu. Nikifikicha macho na kuutizama tena, naona umerudi katika hali yake ya kawaida.”
Chui akaguna. Akautizama mwezi kwa sekunde kama tatu kisha akasema;
“Mama yangu anaamini ukiutizama mwezi kwa muda, mwezi unaanza kuonyesha kilichopo kichwani mwako. Na sasa naanza kuamini. Inaelekea familia yako imetawala kichwani mwako.”
“Ni kweli. Miongoni mwa vitu nilivyofeli kuvitoa kichwani ni hiko.”
Baada ya hapo kimya kikapita kati yao.
Baada ya muda kidogo, kuna sauti ya gari ikasikika nje ya makao makuu. Lilikuwa ni gari aina ya Toyota Land Cruiser J200. Mlango wa gari ulifunguliwa, akatoka Assessoko akiwa ameongozana na wanaume watatu ambao walisimama nje wakati Assessoko akiingia ndani kukutana na Kessy.
Kessy alinyanyuka akampokea mkuu wake kwa salamu, ila Assessoko hakuonekana kuijali salamu hiyo, alikaa kitako kwenye kiti akiwa amekunja sura. Akabamiza meza kwa nguvu na ngumi yake.
“Unafanya nini sasa, Kessy? Mbona unaniangusha kiasi hiki? Watu wanateketea huko! Na mpaka leo jeshi halijakwenda lote huko, nini shida?” Assessoko alifoka.
“Mkuu kama unavyojua, tunaelemewa kwa kiasi kikubwa kwasababu ya muunganiko wa nguvu kati ya Sierra na Liberia. Wanajeshi wa Liberia wamekwenda huko na hata vifaa vile vile kwahiyo kidogo inakuwa tabu.”
“Inakuwa tabu! … Inakuwa tabu! … Inakuwa tabu! Sitaki kusikia hilo neno! Sasa kazi yako ni nini kama huwezi kupambanua akili yako kwa mujibu wa muktadha? Nataka kusikia toka kwako kwamba tunafanya hivi na hivi. Kumbuka hatuna milele hapa!”
“Najua mkuu. Nakuhakikishia kila kitu kitakwenda sawa. Kupeleka vikosi huko vyote kwa wakati mmoja si kitu kizuri kiusalama kwani inafanya nafasi ya kupata taarifa na kujipanga kuwa finyu. Ila bado mpaka sasa Kabala ipo chini yetu, na kwa vifaa na vikosi tulivyopeleka leo, bado inatuhakikishia hiyo nafasi. Lakini kuna haja kubwa ya kuongeza wafuasi, si tu kwa matumizi ya sasa, hata baadae.”
“Hilo la wafuasi, Kessy, lahitaji pesa zaidi. Inabidi kwa sasa tuje na njia mbadala ya haraka ya kutuweka vyema, la sivyo vyote tulivyokuwa tunafanya miaka yote hiyo itakuwa bure! Hatuwezi tukaruhusu kupungukiwa na wapambanaji zaidi. Kesho nataka kusikia toka kwako.”
Assessoko alihitimisha kisha akanyanyuka na kuondoka zake. Akamuacha Kessy akiwa na mawazo, amekaa akiwa kashika tama macho yake yakitizama chini. Kessy alikaa hapo mpaka akaanza kusinzia. Mwishowe alilaza kichwa chake juu ya meza usingizi ukampitia mpaka asubuhi.
*******
*******
Baada ya mlango wa chimbo kufunguliwa, sauti ilisikika;
“Amadu, toka nje!”
Alikuwa ni General Kessy mlangoni akiwa ameshikilia mlango. Amadu akainua uso wake na kutizama kisha akaurudisha uso chini na kuuliza;
“Unahitaji nini, mkuu?”
“Toka nje!”
“Siwezi nikatoka humu ndani kama sitatoka na mwenzangu.”
“Amadu, unanibishia, ama?”
“Tangu lini nikakubishia, mkuu? Sijakataa kutoka ila tu kama nitatoka na mwenzangu.”
“Amadu, nenda tu.” Chui alishauri.
“Hapana. Sitoenda popote bila yako. Ni bora tukaendelea tu kukaa humu.” Amadu alitia msimamo. General akamtizama kwa dakika kama mbili kisha akasema;
“Tokeni nje.”
Amadu pamoja na Chui wakatoka wakaongozana na general kuelekea makao makuu. Wakaketi, General Kessy akaweka chupa ya kilevi na ramani juu ya meza kisha akaanza kuongea;
“Amadu, kwa sasa hali yetu si nzuri huko Sierra. Silaha na majeshi toka Liberia yanatudhoofisa zaidi. Una shauri nini kifanyike?”
“Mkuu, hapo hakuna cha kufanya isipokuwa haya yafuatayo; Mosi, lazima tujue na tuzibe njia zitumikazo kupitishia silaha hizi. Pili, lazima Liberia awe distracted, kwa vyovyote vile inabidi tuhamishe focus yake ya majeshi toka kwetu kwenda sehemu nyingine, na njia rahisi ya kufanya hivyo ni kwa kutumia kundi la Le tueurs.” Amadu akafafanua kwa kujiamini.
“Kuhusu hilo kundi hamna shida naweza nikawapa order wakatii. Ila sasa hizo njia tutazitambuaje?” General aliuliza. Chui akachukua nafasi kutoa maelezo;
“Eneo la Monrovia, Liberia, ndipo penye kambi ya kijeshi iliyokaribu na Sierra Leone. Kwa namna yoyote ndipo patakuwa panasambaza silaha hizi za kijeshi kuja Sierra. Kwahiyo, moja, tunaweza tukaharibu daraja lile la mpakani mwa Sierra na Liberia linalopokea barabara tokea Monrovia ili kukata mawasiliano. Kisha pili, kambi ile ya Monrovia ingeshambuliwa kwa kushtukiza. Na tatu, jeshi la Liberia lingepewa kazi kubwa ya kutetea nchi yake na kuachana kabisa na Sierra.”
“Sasa, hiyo kazi ya kwenda kufumua daraja na kushambulia hiyo kambi, inaweza ikachukua muda gani?” General aliuliza.
“Ndani ya juma moja tu endapo utanipa watu ninaowataka kufanya nao kazi.” Amadu akajibu.
“Unawataka wakina nani?”
“Wale nilioenda nao kuchukua silaha Sulima kasoro Talib.”
“Kingine?”
“Uwe kwenye mawasiliano mazuri na kundi la Le tueurs katika muda huu kwani tutawahitaji kumalizia kazi tutakayoianza huko. Zaidi ya hapo, ni kikosi changu tu.”
“Sawa. Niachie hiyo kazi, jioni wenzako watakuwepo hapa!”
Kweli wakati jua lazama, Mou, Ussein na Farah wakawa tayari wapo makao makuu kukutana na Amadu na Chui. Mipango ikaanza kupangwa juu ya kile cha kufanya, Chui na Amadu wakiwa waelekezaji.
Jua lilipopotea, wanaume wakajiweka kwenye gari na safari ya kuelekea mpakani mwa Sierra na Liberia ikaanza. Ndani ya gari zilipakiwa kreti za bia nne na bunduki za kila mmoja pamoja na maguruneti. Safari hii hawakutumia tena njia ya Sierra Leone, walishika njia ya Guinea wakilenga kuingia Sierra Leone baadae kwa kupitia mji wa Kangama.
Ndani ya lisaa bila ya kupumzika wakawa tayari wamefika mji wa Banian. Baada ya masaa mawili wakafika mji wa Kissidougou, hapo wakaweka kituo wapate kula na kuvuta pumzi. Walipaki gari lao wakaingia mtaani kunyoosha nyoosha miguu huku wakipiga simulizi za hapa na pale. Cheko na tabasamu vikitawala nyuso zao. Walitumia lisaa tu katika huo mji wakarudi kwenye gari na kuendelea na safari. Ilipofika saa sita ya usiku wakawa ndio wanaingia ndani ya nchi ya Sierra Leone ili sasa waambae kutafuta mji wa Sulima wakapate kuharibu daraja. Mita chache wakiwa wameacha mpaka wakakutana na wanaume watano wa uhamiaji, gari likasimamishwa.
“Naombeni pasipoti zenu.” Mwanaume mmoja alisema huku akiwa amekinga mkono wake. Chui akasonya.
“Hivi nyie hamjui hata wenzenu?”
“Wewe ni nani?”
“Mimi ni huyu!” Chui akasema huku akionyeshea kitambulisho chake cha jeshi.
“Mnaelekea wapi usiku huu?”
“Aaah ndugu yangu, kwani hujui kinachoendelea? Tunaelekea Liberia kubeba silaha. Huku Guinea tumetoka kwa shemeji zenu!” Chui alisema kwa sauti yenye utani, wenzake wakaangua kicheko. Wakaruhusiwa kuondoka wakaendelea na safari yao, ndani ya asubuhi ya saa kumi na mbili wakawa tayari wameshafika mji wa Sulima. Waliweka pozi hapo wasome mazingira kwanza. Waliacha gari lao kando sehemu ya kificho kisha wakaanza kutembea tembea maeneo ya Sulima, baadae wakazamia kuingia nchini Liberia kwa kupitia mto wa Mane, wakaenda mpaka Monrovia huko nako wakijifanya wazururaji tu lakini waliokuwa na macho makali kutizama na kukariri mazingira.
Walipotimiza haja zao za moyo, wakarudi nchini Sierra Leone. Walitafuta sehemu ya kupumzikia wakapata nyumba moja ya wageni ya hadhi ya chini, hapo wakakodi vyumba vitatu lakini wakakutania sehemu moja na kuanza kuteta;
“Inabidi tuyarejee hayo mazingira na usiku pia tupate kuona ulinzi wake unakuaje.” Amadu alinena.
“Ni kweli hiko unachokiongea. Sehemu ninazoziona zina shida ni pale kambini kidogo, na hata pale darajani.” Mou alitema neno.
“Ila mimi nina wazo kidogo.” Chui aligusia, wenzake wote wakamuazima macho na masikio.
“Itabidi tujigawanye na kupeana majukumu, sidhani kama itakuwa busara tukaenda wote hasa kipindi hiko cha usiku. Lakini cha muhimu ni kuwa na mawasiliano kati yetu.”
“Wazo zuri!” Amadu akadakia huku akitikisa kichwa. “Au mnaonaje?”
“Kweli, wazo jema.” Wengine wakaliunga mkono.
“Sasa basi tutakachokifanya ni hivi, mimi na Mou tutakwenda mpaka kule kambini, Farah na Chui mtazunguka maeneo ya mtoni na darajani, Ussein utatembelea zile njia za panya tulizozipitia na kuzitizama kwa muda ule. Alafu tutakutana hapa saa nne ya usiku.” Amadu alifafanua mgawanyo. Wenzake wakakubali.
Baadae giza lilipotanda, wanaume wakajigawa na kwenda kutimiza majukumu yao kama vile walivyopeana. Mida ya saa nne ya usiku wakakutana pale pale walipopeana maelekezo kuleta mrejesho.
“Kwangu safi, hakuna shida. Njia zipo vyema hakuna cha kutisha zaidi tu ya walevi walevi kukatiza.” Ussein alielezea eneo lake.
“Kwetu maeneo ya darajani kuna shida kidogo, magari ya jeshi yanapita pita yakielekea na hata kurudi toka Sierra Leone kila baada ya dakika kama kumi na tano.” Chui alitia neno, Amadu naye akatoa majibu ya eneo lao.
“Kwa eneo letu kuna doria ila si ya kutisha. Wanajeshi wanapita wawili wawili, wawili upande wa magharibi na wawili upande wa mashariki. Nadhani doria yao ni hafifu kutokana na kutokuwa na sababu ya kuhofia na eidha kwasababu wapo ndani ya uzio.”
Baada ya hayo maelezo, wakaulizana;
“Muda gani mnaona ni sahihi kufanya tukio?”
“Usiku!” Wote wakajibu. Mipango ikaelezwa na Amadu;
“Kama tulivyojigawa leo, na kesho vile vile. La muhimu sana ni mawasiliano si kingine. Mtabandika mabomu pale madarajani na sisi tutayabandika mule kambini. Tukikutana hapa ndipo tutakapoyafumua. Sawa?”
“Sawa!”
Ngoma inogile kesho yake usiku ilipowasili. Wanaume wakagawana majukumu, Chui na Farah wakawa wa kwanza kutekeleza kazi yao kwa kubandika mabomu chini ya daraja huku Ussein akiwa anang’aza macho yake kwenye vinjia vyake endapo kama kuna lolote litatokea.
Amadu na Mou wakaongozana kwenda kambini. Waliruka ukuta wakaingia ndani kwa tahadhari kubwa. Wakiwa wananyata wakaanza kusogelea maeneo kadha wa kadha na kubandika mabomu toka kwenye mabegi yao waliyoyabebelea mgongoni. Baada ya kubandika maeneo manne, wakakutana na wanajeshi wawili walio doria. Bila ya kutengeneza sauti waliwakaba wanajeshi wale wa doria na kuwaburuzia gizani kisha wakaendelea na kazi yao ya ubandikaji wa mabomu. Walipomaliza waliruka ukuta, walipotua tu wakakutana na wanajeshi wengine wawili, hapo kukawa hamna jinsi. Amadu na Mou wakaachia bunduki zao ziseme na maadui na kufanya sauti za risasi kuvuma! Kisha mbio zikaanza.
“Tunakuja haraka! Kila kitu kipo sawa … Over?” Amadu aliongea na radio call huku wakiwa mbioni na mwenzake.
“Kila kitu kipo sawa … Over!” Sauti ya Chui ikajibu.
“Tunakimbizwa. Nitakapokushtua tu hakikisha unalipua daraja, sawa?”
“Sawa!”
Baada ya lisaa wakiwa wanakimbia Amadu na Mou wakafika darajani na kutoa taarifa kwa Chui, daraja likalipuliwa. Hao wakashika njia ya panya na kutokea eneo lao la mapumziko, wakiwa hapo wakafyatua na mabomu waliyoyapachika kambini mwa jeshi la Liberia kisha wakapanda gari lao na kuanza safari ya kurudi kambini kwao, Guinea.
Njiani Amadu akatoa radio call yake na kumtafuta General akampasha habari kisha akamtaka afanye jambo;
“Mkuu huu ndio wasaa wa Le tueurs kushambulia. Waambie wavamie Monrovia sasa hivi na waiweke kwenye himaya yao. Kama sio sasa, si milele tena.”
Ni ndani ya dakika kadhaa tu, waasi wa kundi la Le tueurs wakajitokeza na kushambulia kambi ya Monrovia wakaiweka himayani. General Kessy akawatafuta wafuasi wake na kuwapasha habari ya mafanikio hayo. Furaha ikatanda miongoni mwao. Walipeana mikono ya kheri ikisindikizwa na macheko na matabasamu. Walifungua vinywaji wakanywa mpaka basi. Baada ya kuzidiwa na kilevi, Amadu ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari aliamua apaki kando wapate kupumzika. Wakalala fofofo.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Jua lilipokucha safari ikaendelea na wakati jioni yawasili wakawa tayari wamefika kambini kwao. General akawapokea kwa uso wenye furaha na makumbato makubwa.
“Mmefanya kazi nzuri sana. Mkuu amenipigia simu ameona taarifa ya habari! Raisi wa Liberia amechanganyikiwa, sasa atatulia na yake!”
General alisema kwa bashasha ya furaha. Alileta chupa ya kileo akampa kila mmoja.
“Sasa huu ndio wakati wa kuongeza mashambulizi Sierra Leone, amekuwa yatima sasa.” General aliendelea kumumuya kifuraha. “Shambulizi letu limekuwa msaada mkubwa sana kwa Le tueurs, wamepata pa kuanzia. Hakika watatusaidia sana huko mbeleni tukiwa tupo ndani ya Sierra!”
Baada ya hayo maongezi na vinywaji kumalizika, wakina Amadu waliaga. Ila kabla hawajatoka, General akawapatia bahasha ya kaki. Walipotoka nje wakaifungua na kukuta pesa, wakagawana sawa kwa sawa kisha kila mtu akaelekea upande wake, Amadu pamoja na Chui wakaelekea hemani. Walihifadhi pesa zao na kujilaza kitandani wakawa wanateta;
“Nataka niwatumie wazazi wangu hizo pesa.” Chui alisema huku akimtizama Amadu.
“Usihofu. Kesho mida ya mchana nitakupeleka kwa wakala utume.”
“Nitafurahi sana.”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment