Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

TAI KWENYE MZOGA - 5

  





    Simulizi : Tai Kwenye Mzoga

    Sehemu Ya Tano (5)





    “ Patrick...” Drel Fille aliniita wakati nikiendelea kupata kifungua kinywa.

    “ Naam!”

    “Mimi siyo Rosine wala...”

    “Nafahamu” nilimkatisha “Wewe ni Drel Fille mpelelezi kutoka D.R Congo

    sivyo? Drel hakunijibu mapema badala yake aliinua macho yake kunitazama

    huku akitabasamu.

    “Hilo ndilo jina langu mpenzi umelijuaje?

    Bila ya kuzungumza neno nililichukua lile gazeti nililolinunua njiani waka-

    ti nilipokuwa nikienda kule hospitali ya Kigali ambalo wakati huu nilikuwa

    nimekuja nalo pale mezani na hapo nikamtupia. Drel Fille alilichukua lile

    gazeti na kulifungua akipitia vichwa vya habari halafu baada ya muda nilim

    uona akiinua macho yake kunitazama lakini wakati huu uso wake ukiwa na

    taharuki.

    “Kwa hiyo wanatufahamu? hatimaye alizungumza kwa utulivu

    “Yoyote anaweza kusema hivyo na hapo ndipo majina ya Rosine na Patrick

    yalipofutika na majina ya Drel Fille na Luten Venus Jaka kuchukua nafasi

    yake” nilimwambia Drel Fille huku nikiumba tabasamu hafifu.

    “Mh! kwa hiyo wewe si Patrick tena na jina lako ni Venus Jaka?

    Sikumjibu neno na badala yake nilimtazama huku nikitabasamu na nilipov-

    uta funda moja la kahawa nikamtupia swali.

    “Hebu niambie yaliyokusibu kule msituni hadi tukapoteana”

    Bila kupoteza muda Drel Fille alianza kunisimulia mkasa wote tangu kule

    msituni akieleza namna alivyofanikiwa kutoroka kwenye ile nyumba baada

    ya kushtuka toka usingizini na kutoniona hadi namna alivyoweza kuutoroka

    msitu ule na kupata lifti kwenye gari ya Ghaspard Gahizi iliyomfikisha jijini

    Kigali.

    Kisha alinisimulia yote yaliyotokea katika nyumba ya Ghaspard Gahizi hadi

    aliponikiwa kumuua Ghaspard Gahizi na kutoroka kwenye ile nyumba nji-

    ani akipishana na gari la wanajeshi. Drel Fille aliendelea kunielezea namna

    alivyokuja kunitafuta kule hospitali ya Kigali na kunikuta nikiwa katikati ya

    mapambano makali na wale watu hatari. Kisha akanielezea namna alivyokuwa

    akinifuatilia kwa nyuma baadaya kutoka pale hospitali na namna nilivyokuwa

    nikimkimbia bika kujua.

    Kufikia hapo maelezo yake yakanifanya nikumbuke namna mtu fulani

    alivyokuwa akinifuatilia kwa nyuma mara baada ya kutoroka kule hospitali

    nilipofanikiwa kuwazidi ujanja wale watu hatari. Kumbukumbu hiyo ndiyo

    ikanifanya nifahamu kuwa yule mtu aliyekuwa akinifuatilia kwa nyuma mara

    baada ya kutoroka kule hospitali siku ya jana ambaye muda mfupi baadaye

    alinipotea katika mazingira yasiyoeleweka kumbe ndiye alikuwa Drel Fille.

    “Oh! sasa kweli nakumbuka kuwa kulikuwa na mtu fulani aliyekuwa aki-

    nifuatilia kwa nyuma mara baada ya kutoka kwenye ile hospitali siku ya jana

    lakini sikuweza haraka kumtambua mtu yule kuwa ulikuwa wewe. Hata hivyo

    nilikuwa najua kuwa wewe ulikuwa miongoni mwa wale watu hatari ndiyo

    maana nilikuwa nikiongeza jitihada za kukutoroka japokuwa nilishangaa sana

    wakati nilipogeuka nyuma na kutokukuona”

    “Ilinibidi niache kukufuatilia mara baada ya kuwaona wale watu walioku-

    wa wakikufukuza kule hospitali wakiwa hatua chache nyuma yangu. Hivyo

    niliamua kuwachenga na kutoweka mbele yao ingawaje roho iliniuma sana

    kwani sikujua kama tungeonana tena mpenzi”

    “Bila ya shaka kuonana kwetu huenda kukawa ni mpango wa Mungu”

    nilimwambia Drel Fille huku nikiumba tabasamu usoni baada ya kuvuta funda

    moja la kahawa na hapo nikaliona tabasamu lake hafifu likichanua usoni kisha

    akavishika vidole vyangu mkononi na hali hiyo ikanifanya nijisikie faraja.

    “Ulijuaje kama nilikuwa kule hospitali hadi ukaja kunifuatilia ile jana?

    “Nilimsikia Dr. François Tresor kule mapangoni wakati alipokuwa aki-

    kueleza kuwa endapo ungefanikiwa kutoroka ulipaswa kumtafuta Dr. Lisa

    katika hospitali ile hivyo sikuona sehemu nyingine ya kukutafuta zaidi ya kule

    hospitali ndiyo maana nilikuja kule hospitali kukutafuta na kama ningekukosa

    ningemtafuta huyo Dr. Lisa ambaye niliamini kuwa angenielekeza mahali

    ulipo”

    Nilimtazama Drel Fille na kumuona kuwa alikuwa msichana mwerevu,

    mjanja na mpelelezi aliyekomaa vizuri. Nikavuta funda moja la kahawa na

    nilipokiweka kikombe mezani nilimuuliza

    “Unafanya nini hapa Rwanda?

    “Kazi kama yako”

    “Kwani kazi yangu ni kazi gani?

    “Mpelelezi na upo hapa nchini Rwanda kupeleleza juu ya kifo cha mtanza-

    nia Tobias Moyo”

    “Umejuaje? nilimuuliza kwa mshangao.

    “Nilizipata taarifa zako kupitia Kanali Bosco Rutaganda wakati nilipotekwa

    na kupelekwa kule mapangoni”

    “Kanali Bosco Rutaganda alikwambiaje?

    “Mh! naona unanipeleleza sana” Drel Fille aliongea huku akiumba ta-

    basamu.

    “Hapana mpenzi napenda tu kufahamu”

    “Okay!... mara tu nilipokamatwa na kufikishwa kwa Kanali Bosco Rutagan-

    da alinieleza kuwa baada ya mimi kukamatwa mtu mwingine ambaye ange-

    fuatia ulikuwa ni wewe mpelelezi kutoka nchini Tanzania ambaye taarifa zako

    tayari yeye alikuwanazo. Hivyo ulikuwa ukisubiriwa ufike tu hapa Rwanda

    ili wakukamate. Vilevile aliniambia kuwa mimi na wewe ndiyo tuliyokuwa

    watu wa kuhofiwa katika kuitibua mipango yao na ndiyo hapo nilipozinasa

    tetesi zako”

    Nilitulia kidogo nikimtazama Drel Fille huku nikiyatafakari maneno yake

    kisha nikavunja tena ukimya nikimuuliza

    “Alikueleza kuwa nilikuwa nimetumwa kupeleleza juu ya kifo cha Tobias

    Moyo?

    “Ndiyo na inavyoelekea ni kuwa huyo Tobias moyo ni yeye aliyehusika

    katika kumuua kwani aliniambia kuwa wewe usingefanikiwa chochote kwani

    huyo Tobias Moyo alistahili kifo tu kama ambavyo na sisi tungestahili”

    Nilimtazama Drel Fille huku mawazo yangu yakiwa kwenye tafakari nzi-

    to ya kujaribu kufikiria ni wapi ambapo Kanali Bosco Rutaganda angekuwa

    amezipata taarifa zangu hata hivyo sikupata jibu japokuwa fikra zangu bado

    zilikuwa kwa mkuu wa kuratibu safari zangu za kijasusi Brigedia Masaki

    Kambona kwani yeye ndiye mtu pekee ambaye angeweza kuvujisha siri zangu

    kwa urahisi japokuwa sikutaka kukubaliana na hilo mapema kwa vile sikuo-

    na sababu ambayo ingempelekea kufanya hivyo. “Mbona hakuweza kufanya

    hivyo katika zile safari zangu nyingine za kijasusi zilizotangulia? nilijiuliza

    bila kupata majibu na mawazo yangu yakawa kama yanayocheza ulingo.

    Nilirudia tena kumtazama Drel Fille kwa udadisi huku nikivuta funda

    jingine la kahawa baada ya kutanguliza kitafunwa kinywani.

    “Na wewe je? nilimuuliza baada ya kuweka kikombe juu ya meza na hapo

    Drel Fille akanitazama kisha akatoa mkono wake uliokuwa umesalia juu ya

    kiganja changu na kuegemea meza.

    “Kabla ya mimi kutumwa hapa Rwanda mbele yangu alikuwa ametumwa

    mpelelezi mwingine kutoka nchini Kongo na jina lake aliitwa Kanza Dyan-

    sangu. Kanza Dyansangu alitumwa hapa Rwanda kuchunguza kama kulikuwa

    na ukweli wowote kuwa serikali ya Rwanda na baadhi ya maafisa wake wa

    kijeshi wasio waaminifu walikuwa wakihusika katika kuvisaidia silaha na fed-

    ha vikundi vya kijeshi vya waasi vinavyopigana na majeshi ya serikali katika

    eneo la mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika maeneo ya

    Boma, Bukavu, Kisangani na Kivu ya kaskazini.

    Kanza Dyansangu hakupata mafanikio sana katika kazi yake kwani miezi

    mitatu tu baada ya kuanza harakati zake hapa Kigali jioni moja mwili wake

    uligundulika ndani ya gari alilokuwa akilitumia ukiwa na matundu sita ya ri-

    sasi, manne kifuani kwenye moyo na mawili tumboni. Gari lake lilikuwa lime-

    telekezwa kando ya daraja la mto mmoja unaokatisha kando ya jiji la Kigali.

    Nashukuru Mungu nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuuona mwili

    wa Kanza Dyansangu katika gari hilo. Ilinibidi nifike hapa Kigali mapema

    sana baada ya kutumwa na idara ya ujasusi ya nchini kwangu mara baada ya

    taarifa za kifo cha Kanza Dyansangu kutufikia.

    Nilifika hapa Kigali usiku wa manane baada ya kuvuka mpaka wa Kongo na

    Rwanda katika njia zisizo rasmi na nilikuwa na bahati sana ya kuukuta mwili

    wa Kanza Dyansangu ukiwa bado haujaondolewa eneo la tukio na kwa yale

    mazingira niliyoyaona hadi sasa naamini kuwa Kanza Dyansangu aliuwawa

    kwanza sehemu fulani na baadaye mwili wake uliwekwa kwenye gari lake na

    kuendeshwa hadi kando ya daraja lile kabla ya kutelekezwa.

    Tangu hapo sikurudi tena nchini kwangu kwani nilihitajika na idara yangu

    ya kijasusi kuendelea na upelelezi wa kumtafuta aliyehusika na kifo cha Kanza

    Dyansangu lakini vilevile kuendelea na kazi ya Kanza Dyansangu pale ali-

    poishia. Katika harakati hizo ndiyo nikajikuta nikitumbukia kwenye mikono

    ya mtu hatari Kanali Bosco Rutaganda”

    “Kuna mafanikio yoyote katika kazi yako? nilimuuliza Drel Fille kwa utu-

    livu.

    “Mafanikio yaliyofikiwa ni makubwa mno na najivunia kwa hilo. Kwanza

    nimeweza kumtia mkononi mtu aliyehusika na kifo cha Kanza Dyansangu

    na hivi tunavyozungumza maafisa wa idara yangu ya ujasusi nchini Kongo

    wapo na mtu huyo kwa mahojiano zaidi lakini bila serikali ya hapa Rwanda

    kufahamu.

    Nimeweza pia kuithibitishia idara ya ujasusi ya nchini kwangu kuwa baadhi

    ya viongozi wasio waaminifu wa serikali ya nchi hii na wanajeshi wenye vyeo

    vya juu wanavisaidia vikundi hivyo vya kijeshi vya waasi wanaopigana dhidi

    ya majeshi ya serikali ya Kongo na sababu zinazowapelekea kufanya hivyo

    ni pamoja na sababu za unasaba wa kikabila na zile za kutaka kufaidika na

    madini mengi yanayopatikana nchini Kongo ambayo vikundi hivi vimekuwa

    vikiyatolea macho ya uroho” Drel Fille aliweka kituo akivuta funda la kahawa

    nami nikabaki nikimtazama huku nikiyatafakari maelezo yake na kwa kweli

    nilimuona Drel Fille kuwa ni msichana jasiri sana aliyehitimu vizuri katika

    harakati za kijasusi.

    “Hongera sana umefanya kazi nzuri ya kizalendo kwa nchi yako. Nadhani

    sasa upo tayari kunieleza ukweli wote kuhusu hii nyumba na mengineyo kwani

    mimi na wewe ni wapenzi sasa” nilimwambia Drel Fille huku nikimtazama

    kwa utulivu na hapo nikamuona akiumba tena tabasamu hafifu usoni mwake.

    “Mh! nilikudanganya Luteni hata hivyo uongo wangu ulikuwa na manu-

    faa na kwa kusema ukweli nyumba hii si yangu, si ya dada yangu wala si ya

    mumewe. Mimi ni mgeni katika nchi hii kama ulivyo wewe na istoshe kwa

    uhalisia tu mimi ni yatima nisiye na baba wala mama kwani mara baada ya

    kuzaliwa nilitupwa kwenye dampo moja maarufu lililopo eneo fulani katika

    jiji la Kinshasa. Niliokotwa na msamaria mwema mmoja na kulelewa kwenye

    kituo kimoja cha kulelea watoto yatima kinachomilikiwa na kanisa katoliki

    ambapo baadaye nilisomeshwa na kituo hicho na nilipohitimu nikajiunga na

    jeshi la nchi yangu nikichaguliwa katika idara ya ujasusi kwa hiyo mimi sina

    ndugu” Drel Fille aliweka kituo akinitazama kama anayewaza jambo kisha

    aliendelea

    “Nilipofika hapa Rwanda kupeleleza kifo cha Kanza Dyansangu na kuende-

    leza pale alipoishia nilianza upelelezi wangu kwa kufuatilia mahali alipokuwa

    akiishi Kanza na mahali hapo ni ndani ya nyumba hii. Sikuweza kupata cho-

    chote cha maana kwani niliikuta nyumba hii ikiwa imeshafanyiwa upekuzi wa

    kina huenda na hao watu waliomuua Kanza Dyansangu.

    Kitu pekee nilichokipata humu ndani ilikuwa ni picha ya Kanza Dyansangu

    akiwa na msichana fulani aliyekuwa na mahusiano naye na ilinichukua muda

    mfupi tu kugundua kuwa picha ya msichana yule ilielekea kufanana sana na

    mimi”

    Nikiwa nimeanza kuyashtukia maelezo ya Drel Fille mahali yalipokuwa

    yakielekea nilijikuta nikizidi kuhamasika kumsikiliza lakini badala ya Drel

    Fille kuendelea kunisimulia nilimuona akigeuka na kuitazama picha moja ili-

    yokuwa imetundikwa pale ukutani sebuleni ikimuonesha mwanaume na mwa-

    namke.

    “Yule ndiye Kanza Dyansangu na pembeni yake ndiye huyo msichana ali-

    yekuwa na mahusiano naye” Drel Fille aliniambia nami nikageuka kuitazama

    ile picha kwa makini ingawaje ile haikuwa mara yangu ya kwanza kuitazama

    ile picha hata hivyo mara hii nilishangaa kushikwa na taharuki pale nilipoita-

    zama picha ile na hapo nikagundua kuwa ni kweli yule msichana kwenye pi-

    cha aliyekuwa pembeni ya Kanza Dyansangu alikuwa akifanana sana na Drel

    Fille lakini sura yake pia haikuwa ngeni sana machoni mwangu.

    Akili yangu ikaanza kusumbuka nikifikiria ni wapi niliwahi kumuona msi-

    chana yule hata hivyo sikusumbuka sana jibu nikalipata. Msichana yule ali-

    kuwa akifanana sana na yule niliyeonana naye kwa mara ya kwanza wakati

    nilipokuwa nikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali ambaye pia

    nilimuona kule A half moon Bar na hapo nikataharuki. Drel Fille akashangaz-

    wa na taharaku niliyokuwa nayo.

    “Vipi kuna nini? Drel aliniuliza kwa mashaka

    “Namfahamu yule msichana ingawa sikuwa nimepata nafasi ya kuichungu-

    za vizuri ile picha lakini sasa nimemkumbuka vizuri” nilimwambia Drel Fille

    na hapo nikamuona akiachama mdomo kwa mshangao.

    Nikaanza kumhadithia Drel Fille mkasa wote tangu nilipofika jijini Kigali

    siku ya kwanza, jinsi nilivyoonana na msichana yule aliyejitia mkaguzi wa

    pasi za kusafiria wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali. Niliendelea ku-

    mueleza namna nilivyomfuatilia msichana yule kule A half moon Bar namkasa

    ulionikuta hadi kufanikiwa kuwatoroka wale askari wa Kanali Bosco Rutagan-

    da kule hospitali. Nilipomaliza kusimulia nilimuona Drel Fille akinikodolea

    macho kama ambaye haamini.

    “Sasa inavyoonekana ni kuwa msichana huyu alipandikizwa pale kwenye

    uwanja wa ndege wa Kigali na Kanali Bosco Rutaganda ili kuweza kuwa-

    fuatilia kwa urahisi watu wote wageni wanaoingia hapa Kigali”

    “Sina shaka na hilo na ndiyo maana siku ile ya kwanza nilipoingia hapa

    jijini Kigali nilifuatiliwa”

    “Lazima kuna mahusiano kati ya msichana huyu na Kanali Bosco Rutagan-

    da na bila ya shaka Kanza Dyansangu alikosea sana wakati alipojitumbukiza

    kwenye mahusiano ya kimapenzi na msichana huyu bila kujua kuwa alikuwa

    anaiuza roho yake”

    “Hiyo inaweza kuwa sababu ya chanzo cha kifo chake” nilimwambia Drel

    Fille huku nikimtazama na wakati huo mawazo yangu yalikuwa yamehamia

    kwa Niyonkuru huku nikijaribu kumuhusisha na kifo cha Tobias moyo. Wakati

    nikiwa katikati ya mawazo hayo nikakumbuka kuendelea na maongezi yetu.

    “Bado hujamaliza kunisimulia kuhusu hii nyumba mpenzi”

    “Oh! maongezi yamekuwa mengi hadi nimesahau. Mara baada ya kugundua

    kuwa huyu msichana aliyekuwa na mahusiano na Kanza Dyansangu alikuwa

    akifanana na mimi nilipata wazo la kuiweka picha yangu humu ndani nikiwa

    na hakika kuwa yoyote angeweza kuamini kuwa mimi na yeye ni mtu na dada

    yake”

    “Bado sijakuelewa”

    “Usijali muda mfupi utanielewa kwanini nililazimika kukudanganya kule

    mapangoni na kusudi langu lilikuwa hivi, sikujua nguvu ya adui ilikuwa kub-

    wa kiasi gani na kutokana na kifo cha Kanza Dyansangu ambaye nilimfaha-

    mu kama mpelelezi hodari mimi sikuwa zaidi yake hivyo nilijua isingekuwa

    kazi kubwa kwa adui kunifikia. Hivyo kwa kuiweka picha yangu humu ndani

    niliamini kuwa ingekuwa msaada mkubwa kwa mpelelezi ambaye angekuja

    nyuma yangu endapo ingetokea mimi nimeuwawa”

    “Una maana gani?

    “Sikumfahamu huyu msichana ni nani na kama si maelezo yako nisingemjua

    kabisa hivyo dhamira yangu ilikuwa kwamba endapo ningeuwawa mpelelezi

    mwingine ambaye angetumwa nyuma yangu asingesumbuka kumtafuta Kanza

    Dyansangu kwani taarifa zake kwenye idara yetu ya ujasusi ni kuwa ame-

    shakufa hivyo kwa vyovyote mpelelezi huyo angeweka jitihada zake katika

    kumtafuta huyu msichana aliyekuwa na mahusiano na Kanza Dyansangu

    kwani wakati huo mimi ningekuwa marehemu na kwa yeye kumtafuta msi

    chana huyu majibu yote yangepatikana” Drel Fille alimaliza kunielezea huku

    akimalizia funda la mwisho la kahawa kwenye kikombe chake, mimi nikabaki

    nikimtazama kwa udadisi huku nikipima ushawishi wa maelezo yake. Nikavu-

    ta funda moja la kahawa kusukuma kitafunwa kilichosalia mdomoni mwangu

    huku nikimtazama Drel Fille.

    “Una uwezo mkubwa wa kushawishi mpenzi” nilimwambia huku nikiumba

    tabasamu.

    “Inaonekana kama hivyo lakini hayo ndiyo yaliyokuwa mawazo yangu, sasa

    nilipokuona kule pangoni haraka nilikutambua kuwa ulikuwa na mipango ya

    kutoroka ndiyo maana nikajiweka karibu yako huku nikitunga uongo mzu-

    ri ambao nilijua kuwa kwa vyovyote ungekuwa na manufaa. Kwanza katika

    kukushawishi utoroke na mimi na kama hiyo ingeshindikana na wewe un-

    gefanikiwa kutoroka peke yako kwa vyovyote nilijua kuwa ungefika katika

    nyumba hii na wakati huo ukiwa na picha kamili ya kile nilichokueleza. Sasa

    hapo najua ungeanza kumtafuta Sam, yule mwanaume niliyekuambia kuwa

    amehusika na kifo cha dada yangu Diane ambaye ndiye huyo msichana hapo

    pichani na mumewe ndiye huyo Kanza Dynasangu. Hivyo ni huyo Sam am-

    baye angekueleza habari zote za hawa wapenzi wawili na hapo ungeweza

    kumnasa huyu msichana”

    “Lakini umesahau kuwa uliniambia kuwa huyu msichana naye pia alikufa”

    “Ndiyo nakumbuka kitu kama hicho anyway... labda sikuweza kukaa chini

    na kuutunga vizuri uongo wangu lakini nilipenda ionekane hivyo”

    “Mh! hongera umejitahidi kunidanganya”

    “Lakini vyovyote ilivyokuwa mimi kwa sasa nimefurahi kwa sababu nime-

    onana tena na wewe mpenzi wangu”

    “Hata mimi nimefurahi Drel lakini bado nina swali”

    “Swali gani mpenzi?

    “kuhusu huyu sam uliyenidanganya kuwa alikuwa rafiki wa mume wa dada

    yako yaani Jean Felix Akaga, hebu niweke wazi”

    “Oh! mpenzi bado unaendelea na mada hiyo anyway... ni hivi, huyo Jean

    Felix Akaga na huyo Diane ni majina ya kubuni tu na kwa maana nyingine

    huyo Jean felix Akaga ndiye huyo Kanza Dyansangu na huyo msichana ndiye

    huyo aliyekuwa mpenzi wake.

    Sasa ipo hivi huyu Sam ndiye mtu aliyeniteka mimi na wakati nikitekwa ka-

    tikati ya jiji na kuingizwa kwenye gari humo ndani nilimkuta huyu msichana

    ambaye ndiye alikuwa mpenzi wa Kanza Dyansangu. Nilimkumbuka haraka

    msichana huyo wakati nilipomtazama kwani picha yake nilikuwa tayari nime-

    kwishaiona”

    “Huyo Sam kwa sasa hayupo tena” nilimkatisha Drel Fille

    “Una maana gani?

    “Nimemuua kule hospitali”

    “Umefanya kazi nzuri kwani yeye ni miongoni mwao”

    Maongezi yaliendelea baina yetu tukizungumza hili na lile katika namna

    ya kuzidi kufahamiana zaidi na wakati huo huo nilipata nafasi ya kuweza kuz-

    ichunguza zile bahasha mbili nilizozichukua kwenye ile ofisi ya Dr.François

    Tresor kule hospitali.

    Nilitoa ile picha iliyomuonesha Dr.François Tresor na marafiki zake wa-

    najeshi wakistarehe mahali fulani kisha nikampa Drel Fille ili na yeye aita-

    zame kama ataweza kuwatambua wale watu wengine. Drel Fille aliipokea ile

    picha na kuitazama kidogo na hapo akamtambua mmoja miongoni mwa wale

    wanajeshi.

    “Huyu ndiye aliyemuua Kanza Dyansangu na nilishamtia mikononi na sasa

    hivi yupo D.R Congo akitakiwa kujibu tuhuma za mauaji ya Kanza Dyansan-

    gu. Huyu mwingine simfahamu lakini huyu mzungu si ni yule aliyeuwawa

    kule pangoni?

    Nilikubaliana na Drel Fille kwa kutikisa kichwa.

    “Huna idea yoyote kuwa urafiki wao ulitokana na nini, mwanajeshi wa cheo

    cha juu wa jeshi la wananchi wa Rwanda na daktari wa kujitolea na mwana-

    harakati wa haki za binadamu?

    “Siwezi kukuhakikishia moja kwa moja ila ninachoweza kusema ni kuwa

    huyu mwanajeshi aliyemuua Kanza Dyansangu alikuwa ni miongoni mwa

    washirika wa karibu wa Kanali Bosco Rutaganda na alikuwa akifanya biasha-

    ra ya madini kwa njia ya magendo akiwauzia wazungu kwa bei poa na madi-

    ni hayo yamekuwa yakiporwa migodini na vikundi vya waasi vinavyopigana

    dhidi ya majeshi ya serikali ya D.R Congo.

    Nilichoweza kufahamu ni kuwa Kanali Bosco Rutaganda na baadhi ya

    maafisa wa jeshi la Rwanda wasio waaminifu wamekuwa wakivisaidia silaha

    kwa siri vikundi hivi vya waasi huku serikali yao ikiwa haifahamu hilo na kwa

    kufanya hivyo wao wamekuwa wakipewa madini yanayoporwa na waasi hao

    kutoka katika hiyo migodi wanayoishikilia msituni huko D.R Congo. Wana-

    popewa madini hayo huyauza hapa Rwanda kwa baadhi ya wafanyabiashara

    wageni wanaoingia kwa siri hivyo huenda huyu mzee wa kizungu ni miongoni

    mwao hao wanunuzi wa hayo madini”

    Maelezo ya Drel Fille yalikuwa mazuri na yaliendana na kile nilichokuwa

    nikikiwaza kichwani hivyo nikabaki nikitabasamu kwa kuanza kupata mwan-

    ga katika suala hili na wakati huohuo nikijaribu kuyalinganisha maelezo yake

    na yale ya Dr. Amanda Albro juu ya tamaa ya utajiri wa madini aliyokuwa

    nayo Dr.François Tresor enzi za uhai wake.

    Nilimueleza Drel Fille juu ya mkasa wote hadi kilichonipelekea kudadisi

    juu ya Dr. François Tresor na nilipomaliza Drel Fille alihitimisha kuwa hata

    yeye aliona kuwa kulikuwa mahusiano makubwa kati ya Dr.François Tresor

    na wale wanajeshi katika ile picha na pengine hiyo biashara ya madini ndiyo

    iliyowakutanisha.

    Nilipoifungua ile bahasha ya pili niliuchukua ule ufunguo uliyokuwa ndani

    yake na kuanza kuuchunguza chunguza. Sikuwa na uelewa sana na masuala

    ya posta hivyo nilimuuliza Drel Fille kama angekuwa na ufahamu wowote

    kuhusiana na funguo ya namna ile kwani ilikuwa ni funguo tofauti kabisa na

    zile funguo nyingine nilizowahi kuziona.

    “Hiyo ni funguo ya posta mpenzi” Drel Fille aliniambia baada ya kuitazama

    ile funguo

    “Una hakika?

    “Nina uzoefu na funguo za namna hiyo kwani wakati fulani nilipokuwa

    kwenye kile kituo cha kulelea watoto yatima cha kanisa Katoliki jijini Kinsha-

    sa nilikuwa nikiongozana na Sister Hellen kila siku ya Ijumaa kwenda posta

    kuchukua barua za kanisa na ni wakati huo ndiyo nilipopata uzoefu na funguo

    za namna hiyo”

    Nilimtazama Drel Fille na kumuona kuwa alikuwa akimaanisha alichoku-

    wa akikisema na hapo swali libaki kuwa nitawezaje kujua namba ya sanduku

    la posta la funguo ile. Baada ya kufikiri hapa na pale nikapata jibu la swali

    langu hivyo nikaurudisha ule ufunguo mfukoni na ile picha kwenye bahasha

    nikaihifadhi.

    “Nitakwenda posta pengine nitapata chochote cha kunisaidia” nilimwambia

    Drel Fille

    “Utajuaje sanduku la posta la huo ufunguo?, istoshe kuna ofisi za posta

    nyingi hapa jijini Kigali hivyo naona kuwa ni vigumu kufahamu sanduku la

    posta la funguo hiyo lipo kwenye ofisi ipi miongoni mwa hizo”

    “Nitakachokifanya kwanza ni kufanya utafiti wa ofisi zote za posta zilizopo

    karibu na hospitali ile ambayo Dr.François Tresor alikuwa akifanya kazi na

    bila ya shaka nitafanikiwa,”

    “Mh! anyway... labda ujaribu pengine ukafanikiwa” Drel Fille aliniambia

    huku akijiegemeza vizuri kwenye kiti na nilipomtazama nikamuona ni kama

    aliyekuwa akifikiria jambo fulani.

    “Kanali Bosco Rutaganda na washirika wake wanapanga kufanya mapin-

    duzi hapa nchini” hatimaye aliongea kwa sauti tulivu.

    “Kwanini unasema hivyo?

    “Nilipata nyaraka kwenye nyumba ya Ghaspard Gahizi” akaniambia huku

    akitoa bahasha ndogo ndani ya blauzi yake na alipoifungua akatoa karatasi

    fulani na kunipa. Nikaipokea ile karatasi na kuanza kuisoma na maelezo yake

    yalikuwa kwa lugha ya kifaransa hivyo kwa kuwa sikuwa mzuri sana kwenye

    lugha hiyo kuna baadhi ya vipengele nilihitaji ufafanuzi toka kwa Drel Fille.

    Nilipomaliza kuisoma ile karatasi nikawa na picha kamili ya mambo yalivyo

    ingawaje bado sikuweza kuyajibu maswali yangu yote. Mwisho wa karatasi ile

    niliyaona majina matatu na sahihi zao na miongoni mwa majina hayo lilikuwe-

    po jina la Kanali Bosco Rutaganda kama katibu wa harakati.

    Nilimaliza kusoma nyaraka ile nikiwa katika tafakari nzito huku nikiwa

    nimeanza kuyakumbuka tena yale maneno ya Kanali Bosco Rutaganda wakati

    nilipokuwa kule kwenye mapango ya Musanze juu ya tukio walilopanga ku-

    lifanya katika hii nchi. Nilibaki nikimtazama Drel Fille huku mawazo yangu

    yakiwa mbali na mimi.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Kwa hiyo hivyo ndivyo mambo yalivyo Luteni!” Drel Fille alinikatisha.

    “Hawa watu ni hatari sana Drel tunahitajika kufanya kitu fulani ili kuzuia

    hili tukio. Vipi tukienda kuonana na ofisi ya rais au kiongozi yoyote wa seri-

    kali mwenye dhamana ya nchi hii kabla mambo hayajaharibika? na lini wame-

    panga kufanya hayo mapinduzi?

    “Sina majibu sahihi juu ya tukio hilo lakini muda tunao na tunaweza kufan

    ya uchunguzi wa kujiridhisha kabla ya kutoa taarifa kwa wahusika”

    “Ni lazima tufanye hivyo Drel kwani viongozi wa nchi hii ni lazima wafa-

    hamishwe mapema juu ya njama za hawa wahuni wachache na kwa kufanya

    hivyo serikali itakuwa na nafasi nzuri ya kuzima tukio hili la mapinduzi na

    ikiwezekana kuwatia mbaroni wahusika wote”

    “Ni wazo zuri Luteni lakini ni lazima tuwe waangalifu katika kufanya

    hivyo”

    “Ni kweli kuwa mafanikio ya mkakati wowote yanahitaji uangalifu lakini

    unadhani kuna tatizo lolote katika kufanya hivyo? nilimuuliza Drel Fille huku

    nikimtazama.

    “Tatizo linaweza kuwepo endepo tusipolifanya hili suala kwa umakini”

    “Kwa vipi? nilimuuliza Drel Fille huku nikijiegemeza vizuri kwenye meza.

    “Tatizo nchi hii imesongwa na suala la itikadi za kikabila kwa kiasi kikub-

    wa sana na hata viongozi waliopo madarakani au kwenye vyombo vya ulinzi

    kama polisi na jeshi nao pia wamegawanyika kwa kufuata maslahi ya makabi-

    la yao na si maslahi ya taifa. Hali hii ndiyo inayonifanya nianze kuhisi kuwa

    hata haya mapinduzi yanayopangwa kufanyika pengine yakawa yameegemea

    kwenye ukabila na upo uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya viongozi wa ser-

    ikali wa nchi hii wanafahamu mkakati wa mapinduzi haya.

    Hivyo ni muhimu kwanza kuchunguza na kufahamu ni akina nani hasa

    waliopo nyuma ya mpango huu na tutakapofahamu itatusaidia kujua ni nani

    anayepaswa kupelekewa hizo taarifa za tahadhari vinginevyo tunaweza kujik-

    uta tunawapelekea taarifa wahusika wa mapinduzi hayo”

    Niliyapima maelezo ya Drel Fille na kuyaona kuwa yalikuwa na mantiki.

    Uwezo wake wa kufikiri na kuunda hoja kichwani ulinishangaza sana na hapo

    nikajikuta nikianza tena kujivunia kwa kuwa na mpenzi wa namna hii. Nil-

    igeuka kuitazama saa iliyokuwa ukutani pale sebuleni na hapo nikagundua

    kuwa tayari ilikwishatimia saa tano na nusu asubuhi hivyo sikuona sababu ya

    kuendelea kukaa pale mezani.

    Nilimtazama Drel Fille na kumuona kuwa ni kama aliyekuwa akihitaji tuen-

    delee kukaa katika hali ile lakini kwa upande wa pili hisia zangu ziliniambia

    kuwa nilikuwa nikipishana na matukio mengi muhimu huko mitaani ambayo

    yangeweza kujibu maswali yangu.

    “Jiandae tunaondoka” hatimaye nilimwambia Drel Fille.

    “Tunaenda wapi tena?

    “Katikati ya jiji”

    “Kufanya nini?



    #186

    TEKSI TULIYOIKODI ILISIMAMA kiasi cha umbali wa mita ishirini kabla

    ya lilipo jengo la ofisi ya posta ya katikati ya jiji la Kigali, nikampa dereva

    pesa yake kisha tukashuka. Hali ya hewa ilikwishaanza kubadilika na dalili

    za kunyesha kwa mvua kama wingu zito angani na hali ya fukuto ilikuwa

    ikiongezeka.

    Watu wachache waliokuwa eneo lile waligeuka kututazama kwa wivu kama

    wapenzi tulioendana vizuri wakati tulipokuwa tukiharakisha kuufikia mlango

    mkubwa wa kuingilia ndani ya zile ofisi za posta. Hatukupenda kuvuta macho

    ya watu hivyo mara baada ya kuingia ndani ya ofisi zile kila mmoja alishi-

    ka uelekeo wake huku tukiwa makini kuzichunguza nyuso za watu wachache

    waliokuwa mle ndani wakihudumiwa.

    Drel Fille alikuwa amepata wazo la kupata huduma ya simu ili awasiliane na

    idara ya ujasusi ya nchi yake kuwaeleza hatua aliyofikia katika upelelezi wake

    na vilevile kupata taarifa kutoka kwao. Hivyo wakati mimi nikielekea kwenye

    idara ya mawasiliano ya posta kwa njia ya barua yeye alishika uelekeo wa ilipo

    idara ya mawasilino ya posta kwa njia ya simu lakini tukiwa tumekubaliana

    kuwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.

    Niliwakuta watu wachache wakingoja huduma kwenye kaunta ya idara

    ya mawasiliano ya barua kwa njia ya posta. Baadhi ya watu hao walikuwa

    wameegemea kwenye kaunta ile wakiandika barua na wengine wakibandika

    stempu. Hakuna aliyesumbuka kugeuka na kunitazama kwani kila mtu aliku-

    wa amezama kwenye shughuli yake.

    Mfanyakazi wa posta dada mrembo wa kinyarwanda mhudumu wa idara ile

    aliinua macho kunitazama huku akinionesha tabasamu la ukaribisho wa kipe-

    kee wakati nilipokuwa nikiikaribia kaunta ile nami nikamroga wa tabasamu

    langu lenye ulimbo mkali aghalabu nikilitumia kuwanasa wasichana warembo

    wa sampuli yake.

    “Karibu kaka tafadhali naomba nikusaidie? yule msichana akaniuliza kwa

    lugha ya kifaransa.

    “Nimepoteza funguo ya sanduku la posta tafadhali naomba unisaidie”

    “Nitajie namba ya sanduku lako na baada ya wiki moja funguo yako itakuwa

    tayari lakini utalipia gharama kidogo” yule dada aliniambia huku akiwa ame-

    pumbazika na uzuri wangu.

    “Wiki moja ni mbali sana dada yangu tafadhali naomba unisaidie niipate

    mapema zaidi. Ninaweza kulipa hizo gharama zote leo hii ili hiyo funguo iten-

    genezwe kwa huo muda wa wiki moja lakini kwa leo nina shida sana na barua

    zilizopo ndani ya hilo sanduku langu. Nitashukuru sana kama utanisaidia kuz-

    ipata hizo barua” nilimdanganya.

    “Hatuna utaratibu huo kaka”

    “Najua huo siyo utaratibu wenu lakini tafadhali nina shida sana na hizo

    barua kwa leo hii” niliendelea kumshawishi yule dada huku nikianza kuhisi

    kukata tamaa na hapo nikamuona akianza kulainika. Yule dada akanitazama

    kidogo kama anayefikiri jambo kisha akaongea kwa unyonge.

    “Ngoja niangalie kama ninaweza kukusaidia ila ni vizuri ukaelewa kuwa

    taratibu za kazi haziruhusu kufanya hivi” yule dada akaongea huku akichukua

    karatasi na kalamu toka kwenye droo ya kaunta na kisha kuviweka mezani.

    “Andika majina yako kamili na namba ya sanduku lako la posta”

    Nikaichukua ile kalamu na karatasi na kuanza kuandika jina la Dr. François

    Tresor lakini nikakwama kwenye namba ya sanduku la posta kwani nilikuwa

    siifahamu. Yule msichana aliponiona nasita kuandika akalihisi tatizo langu.

    “Umesahau namba ya sanduku lako? akaniuliza kama aliyeanza kuchoshwa

    na mambo yangu.

    “Loh! Nimesahau kwani ni muda mrefu sijafika kuchukua barua hapa” nili-

    jitetea.

    “Mh! huo ni usahaulifu wa kupita kiasi sasa nitakusaidiaje kaka? akaniuliza

    huku akiichukua ile karatasi”

    “Haya ndiyo majina yako kamili? akaniuliza.

    “Ndiyo dada tafadhali naomba unisaidie”

    “Kama hujakosea majina naweza kuzipata namba za sanduku lako kwa

    kuangalia kwenye kitabu cha orodha ya majina ya wateja wetu kinachoonesha

    majina na namba za masanduku ya posta ya wateja wetu”

    “Nitashukuru” nilimwambia yule dada na muda uleule nikamuona yule

    dada akielekea kwenye meza nyingine iliyokuwa jirani na eneo lile ambapo

    juu yake kulikuwa na kitabu cha rangi ya samawati.

    Yule dada alipokifikia kile kitabu akaanza kufunua kurasa moja baada ya

    nyingine hadi pale alipoifikia kurasa aliyokuwa akiihitaji na hapo akaweka

    kituo na kuanza kulinganisha taarifa zangu na zile zilizokuwa kwenye kile

    kitabu cha mezani.

    Haukupita muda mrefu nikamuona yule dada akigeuka kunitazama huku uso

    wake ukiwa umeumba tabasamu na hapo nikaingiwa na faraja. Muda mfupi

    uliyofuata nilimuona akiiacha ile meza na kushika uelekeo wa nyuma ya eneo

    lile la ofisi na sekunde chache zilizofuata yule dada akawa ametoweka kwenye

    usawa wa macho yangu. Nikashusha pumzi na kutabasamu kimoyomoyo huku

    nikiwa naomba nifanikiwe ingawaje sikuwa na hakika kama sanduku la posta

    la Dr. François Tresor lilikuwa katika ofisi zile za posta.

    Nilikuwa nimeyaweka mawazo yangu mbali kidogo na Drel Fille hivyo

    wakati nikimsubiri yule dada nikatumia muda huo kugeuka kule alipo Drel

    Fille na hapo nikamuona akiwa anazungumza na simu ndani ya kibanda kido-

    go chenye kuta za vioo kilichokuwa pembeni ya mlango wa kutokea nje, nika-

    jua kuwa tayari amekwisha unganishwa na opereta.

    Nikamfanyia ishara kuwa mambo yalikuwa yakielekea kuwa mazuri na

    yeye akanifanyia ishara kuwa alikuwa amampata mtu aliyekuwa akimhitaji

    kuongea naye. Kwa ujumla nikafurahishwa na namna mambo yalivyokuwa

    yakienda.

    Nikiwa nimesimama pale kaunta ya mapokezi niliendelea kusubiri huku

    nikizichunguza nyendo na nyuso za watu waliokuwa wakiingia na kutoka

    mle ndani na wakati huo huo mawazo yangu yakihama na kumkumbuka Dr.

    Amanda Albro huku nikijiuliza nini kilichokuwa kimemsibu kule nyumbani

    kwake na wakati huu alikuwa wapi.

    Kwa kweli sikuweza kufahamu ni masaibu gani yaliyomtokea na moyo

    wangu ulikuwa umeshawishika kwa kiasi kikubwa kumfuatilia na ikiweze-

    kana kumuokoa endapo angekuwa hayupo kwenye mikono salama lakini nil-

    ishindwa kabisa kufanya hivyo kwa kukosa sehemu ya kuanzia.

    Wasiwasi ulianza kuniingia baada ya kuanza kuhisi kuwa muda mrefu uli-

    kuwa umepita bila ya yule dada mfanyakazi wa posta aliyeenda kunitazamia

    barua kwenye sanduku la posta la Dr. François Tresor kurudi. Nikaitazama saa

    yangu ya mkononi na kutazama tena kwenye ule uelekeo alikopotelea yule

    dada bila kuona dalili zozote za uwepo wake na hapo hofu juu ya jambo fu-

    lani lisilo la kawaida ikazidi kuniingia sambamba na mapigo ya moyo wangu

    kuanza kupoteza utulivu.

    Niligeuka tena kumtazama Drel Fille nikamuona kuwa bado alikuwa

    kwenye maongezi ya simu na hakuwa na habari na mimi. Wasiwasi ukiwa

    tayari umeiteka nafsi yangu nikaanza kufikiria nini cha kufanya endapo yule

    msichana aliyeenda kunitazamia barua angeendelea kukawia. Lakini kabla

    sijaamua chochote mara nikamuona mwanaume mfupi na mnene kiasi ali-

    yevaa suti nadhifu nyeusi na viatu vya ngozi akitokea upande ule yule msicha-

    na alikopotelea muda mfupi uliyopita.

    Nilipomtazama yule mwanaume uso wake haukuonesha tashwishwi yoyote

    zaidi ya ule utulivu wa kawaida huku akizitupa hatua zake haraka na alipofika

    kwenye lile eneo la meza ya kaunta akatutazama kwa haraka watu wote tuli-

    yokuwa eneo lile na wakati akifanya hivyo nilipata nafasi ya kumchunguza

    vizuri. Wajihi wake ulieleza haraka kuwa yule mtu alikuwa ni miongoni mwa

    viongozi wakubwa wa ofisi ile ya posta kama siyo meneja.

    “Namhitaji Dr. François Tresor” hatimaye yule mtu aliongea baada ya kum-

    aliza kuwatazama watu wote eneo lile. Moyo wangu ukashtuka na kusita huku

    nikijishauri kuwa nijitokeze au niendelee kujifanya sio mimi lakini baadaye

    niliamua kujitokeza baada ya kuhisi kuwa sikuwa na namna nyingine ya ku-

    fanikisha nilichokua nikihitaji.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “François Tresor!...” yule mtu akaita tena kwa sauti kubwa zaidi.

    “Mimi hapa” nikaitikia huku nikijidai nilikuwa sijasikia na hapo yule mwa-

    naume mfupi akageuka kunitazama kama ambaye ameshikwa na mshangao

    halafu bila ya kupoteza muda akaniambia

    “Nifuate”

    Nikiwa nimejianda kwa tukio hilo nikapenya katikati ya uchochoro wa watu

    waliokuwa wamesimama eneo lile na kuanza kumfuata yule mtu lakini kabla

    sijafanya hivyo niligeuka kutazama ule upande aliokuwa Drel Fille nikiwa na

    dhumuni la kumpa ishara kuwa aendelee kunisubiri hata hivyo sikufanikiwa

    baada ya kumuona Drel Fille kuwa bado alikuwa amezama kwenye maongezi

    ya simu. Hivyo nilimuacha na kuanza kumfuata yule mtu mfupi kwa nyuma

    tukieleke kule ndani.

    Tulipofika ndani ya lile jengo upande ule yule dada alikopotelea tukawa

    tumetokezea kwenye korido pana yenye vyumba upande huu na ule. Niligun-

    dua kuwa vyumba vile vilikuwa ni vya ofisi za idara tofauti kwani ndani yake

    niliwaona wafanyakazi wengine wakiwa wanaendelea na shughuli mbalimbali

    za kiofisi kupitia kuta safi za vioo.

    Tulifika mwisho wa korido ile na hapo kulikuwa na mlango na juu ya mlan-

    go ule kulikuwa na kibao kidogo cheusi chenye maandishi meupe kilichoeleza

    kuwa ile ilikuwa ni ofisi ya meneja mkuu wa ofisi zile za posta na hapo nikajua

    kuwa kwa vyovyote mtu yule niliyeongozana naye ndiye aliyekuwa na cheo

    kile.

    Yule mtu akausukuma ule mlango na hapo tukaingia ndani lakini wakati

    tukiingia tulipishana na yule dada ambaye ndiye yule niliyekuwa nikimsubiri

    kule mapokezi. Hakunisalimia wala kuonesha tashwishwi yoyote usoni waka-

    ti nilipomtazama na badala yake aligeuka na kunitazama hadi pale nilipoufun-

    ga ule mlango nyuma yangu na tukio lile likanishangaza sana.

    “Karibu uketi ndugu” yule mtu niliyeongozana naye alinikaribisha mara

    baada ya kuingia ndani ya ofisi ile huku yeye akielekea kwenda kuketi kwenye

    kiti kipana kilichokuwa nyuma ya meza kubwa ya ofisi yenye vitabu na ma-

    faili chungu mzima.

    Nilitazama juu ya meza ile nikaona kibao kidogo chenye utambulisho wa

    jina la Betrand Masambu kama Meneja wa posta ile. Nilipotazama pembe-

    ni ya kibao kile nikaona bahasha moja kubwa iliyofungwa vizuri kwa gundi

    na juu ya bahasha ile kuliandikwa jina la Dr. François Tresor kwa maandishi

    makubwa na meusi.

    Niliitazama hati ile juu ya ile bahasha na hapo nikagundua kuwa ilikuwa

    inafanana na zile hati nilizoziona kule ofisini kwa Dr. François Tresor kule

    hospitali hivyo nikajua kuwa kwa vyovyote ile ilikuwa ni bahasha iliyotolewa

    katika sanduku la posta la Dr. François Tresor.

    “Jina langu ni Betrand Masambu, meneja wa posta hii. Nimepokea maombi

    yako toka kwa mfanyakazi wangu lakini nasikitika kukuambia kuwa tumesh-

    indwa kukubaliana na maombi yako” yule mtu mfupi aliongea kwa utulivu na

    hapo nikamtazama meneja yule huku nikijiuliza kuwa ile isingekuwa sababu

    iliyomfanya aniite mle ofisini kwake. Machale yakaanza kunicheza na hapo

    nikayazungusha macho yangu kuipeleleza ofisi ile kwa siri na sikuona cho-

    chote cha kukitilia mashaka hivyo niliyarudisha macho yangu tena kwake.

    “Ni utaratibu gani mnaoutumia kwa mtu mwenye tatizo kama langu? nilim-

    uuliza meneja yule wa posta huku nikimtazama kwa makini na hapo nikamu-

    ona akiangua kicheko hafifu. Kilikuwa kicheko cha dharau na kilinipandisha

    hisia mbaya moyoni mwangu hata hivyo nilivumilia kumtazama.

    “Wewe si Dr. François Tresor mmiliki halali wa sanduku hili la posta labda

    angekuwa ni yeye mwenyewe ningeweza kumjibu vizuri swali hilo” yule me-

    neja wa posta alinijibu huku akinitazama kwa udadisi na hapo nikajua kuwa

    uongo wangu ulikwisha fichuliwa.

    “Mbona sikuelewi?

    “Unanielewa vizuri Luteni sema tu unataka kurefusha huu mjadala”

    “Kama umeshindwa kunisaidia wacha niende zangu pengine nitapata mtu

    mwingine wa kunisaidia” nilimwambia huku nikisogeza kiti changu nyuma na

    kusimama lakini wakati huo macho yangu yakiwa makini kuitazama ile baha-

    sha iliyokuwa juu ya ile meza yenye jina la Dr. François Tresor juu yake. Hata

    hivyo sikufanikiwa katika hila yangu kwani nilijikuta nikirudishwa kitini kwa

    nguvu isiyo ya kawaida na mtu fulani aliyekuwa nyuma yangu. Nilipogeuka

    nikarudishwa kwa pigo kavu la ngumi nzito shingoni.

    “Tulia wewe mbona unaharakisha kuondoka wakati maongezi bado hay-

    ajaisha? ile sauti ya mtu aliyesimama nyuma yangu ilinionya huku nikihisi

    mdomo wa chuma baridi cha bastola ukikikuna kuna kisogo changu. Nikarudi

    kitini na kuketi huku nikijihisi kuchanganyikiwa kwa kuingia tena mtegoni.

    Nilijaribu kufikiria kuwa mtu yule angekuwa ametokea wapi na hapo

    nikayazungusha macho yangu kukipeleleza tena kile chumba cha ofisi na hapo

    nikayaona makabati mawili makubwa yaliyokuwa upande wa kushoto wa ofisi

    ile na kabati moja lilikuwa wazi na hapo nikajua kuwa ule ulikuwa ni mtego

    ulioandaliwa na kupangwa vizuri kuninasa na yule mtu nyuma yangu bila sha-

    ka alikuwa amejificha ndani ya lile kabati ambalo sasa lilikuwa wazi. Lakini

    pia nilishtushwa na ile sauti ya mtu aliyekuwa nyuma yangu kwani haikuwa

    ngeni sana masikioni mwangu.

    “Hivi ndivyo mnavyowafanyia wateja wenu? nilimuuliza yule meneja wa

    posta huku nikiwa nimeshikwa na hasira isiyoelezeka.

    “Mwenzako yuko wapi? yule mtu nyuma yangu aliniuliza

    “Mwenzangu nani mbona mnaongea kama walevi?

    “Nani mlevi, hebu wacha kutuchanganyia habari, tunamuulizia mwezako

    Drel Fille yuko wapi? yule mtu aliniuliza na kabla sijamjibu nilichapwa ma-

    kofi mawili yaliyonifanya nione nyota.

    “Mbona mnanipiga tena?

    “Tueleze mwenzako yuko wapi? yule meneja wa posta aliniuliza huku uso

    wake ukiumba tabasamu.

    “Mwenzangu nani mbona mimi nimezaliwa pake yangu?

    “Anatupotezea muda wetu huyu” yule mtu nyuma yangu alifoka

    “Kwani mnataka kuelekea wapi? niliwauliza wale watu huku nikiununua

    muda na muda uleule nikaanza kupewa mkong’oto na yule mtu nyuma yangu.



    #213

    Ulikuwa mkong’oto wa nguvu na usiokuwa na utaratibu maalum na wenye

    maumivu makali. Nikapiga mayowe na kumsihi yule mtu aniache na hatimaye

    akaniacha.

    “Tuambie mwenzako yuko wapi?

    “Oh! nimekumbuka, mwenzangu nimemwacha nyumbani” nikaamua ku-

    wadanganya wale watu baada ya kuhisi kuwa endapo ningeendelea na msima-

    mo wangu pengine hali ingezidi kuwa mbaya zaidi.

    “Nyumbani ni wapi? yule meneja wa posta akaniuliza

    “Hamuwezi kupafahamu mpaka niwapeleke” niliwaambia na hapo ukimya

    ukafuatia huku wale watu wakitazamana na wakati wakifanya hivyo akili yan-

    gu ilikuwa ikifanya kazi haraka nikifikiria namna ya kujinasua. Hata hivyo

    nilifarijika sana kuwa wale watu walikuwa hawajamuona Drel Fille.

    Niliitazama saa yangu ya mkononi na hapo nikagundua kuwa muda wa robo

    saa tayari ulikuwa umepita tangu nilipoingia ndani ya ofisi ile. Nikajikuta niki-

    waza namna ambayo Drel Fille angehangaika baada ya kutoniona mara baada

    ya kumaliza kuongea na simu.

    Nikiwa na hakika kuwa ombi langu sasa lilikuwa likifanyiwa kazi kwenye

    vichwa vyao niliamua tena kuununua muda wa ziada.

    “Lakini bado hamjaniambia kwa nini mnamuhitaji Drel Fille? niliwauliza

    wale watu na badala ya kunijibu walianza kuangua kicheko cha dhararu. Siku-

    taka kuendelea kupoteza muda kwani nilifahamu ni nini ambacho kingefuatia

    endapo ningeendelea kuzubaa pale.

    Hivyo toka pale kwenye kiti nilipoketi nilikusanya nguvu na kumtandika

    kichwa cha nguvu yule mtu aliyekuwa nyuma yangu na hapo akapiga yowe

    kali la maumivu huku akiiachia bastola yake mkononi wakati huo na mimi

    nikaanguka sakafuni kizembezembe. Yule meneja wa posta kuona vile akavuta

    droo ya meza yake na kuchukua bastola hata hivyo hakufanikiwa kuitumia

    kwani niliwahi kuisukuma ile meza kwa miguu yangu yote miwili na hapo

    nikamuona yule meneja wa posta akirushwa nyuma ya ile meza na kuangukia

    kwenye mafaili yaliyokuwa nyuma yake juu ya meza ndogo na ile meza ika-

    vunjika huku yale mafaili yakitawanyika kila mahali sakafuni.

    Nilitaka kunyanyuka lakini yule mtu nyuma yangu aliniwahi kunishika mi-

    guu na kunivuta na hapo nikaanguka chini kama gunia huku nikisikia maumi-

    vu makali ya mbavu. Akiwa bado ameishika miguu yangu sikutaka kumpa

    nafasi hivyo nikajizungusha na kumtandika teke la usoni yule mtu hali iliyom-

    pelekea aniachie mwenyewe bila kupenda lakini nilipokuwa nikisimama yule

    meneja wa posta aliiwahi bastola yake na kunilenga na hapo nikawahi kujitu-

    pa nyuma ya kabati kumpotezea shabaha hivyo risasi aliyoifyatua ikapekenya

    mbao za kabati lile na kuzivunja vipandevipande huku mshindo mkubwa wa

    risasi ukisikika mle ndani.

    Nikiwa naona hatari inazidi kunikaribia nikaupeleka mkono wangu mafi-

    choni na nilipoutoa nilikuwa nimeikamata vyema bastola yangu lakini wakati

    huo zile risasi zilikuwa zikiendelea kurindima ovyo pale nyuma ya kabati nili-

    pojificha hvyo ikanibidi niendelee kulala pale nyuma ya lile kabati.

    Nilipoona lile kabati linazidi kuchakazwa na risasi nikaamua kuhamisha

    maficho yangu lakini wakati huo pia nikifikiria namna ya kupunguza masham-

    bulizi. Lile kabati jingine lilikuwa kiasi cha urefu wa hatua mbili tu pembeni

    yangu hivyo nikaamua kujirusha nyuma ya kabati lile lakini wakati huo huo

    macho yangu yakitazama upande ule zile risasi zilipokuwa zikitokea. Nikamu-

    ona yule meneja wa posta akiwa kwenye uwazi mzuri hivyo nikavuta kilimi

    cha bastola yangu na kuziruhusu risasi mbili kufanya mjongeo na hapo hapo

    nikamuona yule meneja wa posta akirushwa hewani huku kichwa chake kiki-

    fumuliwa vibaya kwa risasi. Ubongo wake ukaruka na kutawanyika hewani

    huku mimi nikitua nyuma ya lile kabati na kujibanza chini na hapo mrindimo

    wa zile risasi ukawa umepungua na hatimaye kukoma kabisa.

    Nilitambaa sakafuni na kujibanza huku nikimchungulia yule jamaa mtata

    aliyesalia hata hivyo nilishangaa kutomuona lakini wakati nikiwa katika hali

    hiyo gafla nililiona lile kabati nililojibanza nyuma likiniangukia. Nikataka

    kulizuia lakini uzito wa kabati lile ulinionya kuwa nisingefanikiwa hivyo nili-

    wahi kujitupa pembeni na lile kabati likaanguka huku droo zake zikifunguka

    na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake vikatawanyika sakafuni na hapo vumbi

    likisambaa mle ndani.

    Kabla sijasimama ghafla nilishtukia nikitandikwa teke la tumbo na kurush-

    wa ukutani na ile bastola niliyoishika ikaniponyoka huku nikijisikia kutaka

    kutapika na kizunguzungu kikinikabili. Nilipotaka kunyanyuka yule mtu mta-

    ta alinitandika tena teke la tumbo na hali yangu ikazidi kuwa mbaya zaidi huku

    damu ikianza kunitoka puani. Kwa kweli nilijihisi kuchanganyikiwa na pigo

    jingine la teke kifuani likanirusha hadi pembeni ya ile maiti ya yule meneja

    wa posta. Nilipoyatupa macho yangu pembeni nikaiona ile bastola ya yule

    meneja wa posta ikielea kwenye dimbwi la damu yake na hapo tumaini jipya

    likachipua moyoni mwangu. Nikakusanya nguvu na kuirukia ile bastola lakini

    yule mtu mtata alikuwa tayari ameishtukia hila yangu hivyo akawahi kuipiga

    teke ile bastola mbele yangu na ile bastola ikateleza sakafuni na kupotelea

    chini ya kabati, na hapo tumaini langu likatoweka kabisa.

    Halafu muda uleule nilipigwa teke la kichwa na pigo hilo likanipelekea

    nisiweze kuona vizuri mbele yangu. Hofu ikaniingia juu ya hali yangu kuzidi

    kuwa mbaya huku nikianza kuhisi kuwa dakika zangu za kubaki duniani zili-

    kuwa zikihesabika.

    Sikuwahi kuogopa kifo hata siku moja katika maisha yangu kwani kama ni

    vifo nilishawahi kuviona vingi vya ajabu ajabu tena vingine vikipitia mikononi

    mwangu. Hivyo kifo hakikuniogopesha hata kidogo kwani hata mimi nilijua

    kuwa ipo siku moja ningekufa tu lakini kifo cha kizembe nilipingana nacho

    siku zote katika uhai wangu hivyo kuona kipigo kile kikinizidia nilianza ku-

    fikiria njia mbadala ya kujiokoa.

    Nikiwa bado najihisi kuchanganyikiwa nilikusanya nguvu na pigo jingine

    la teke lilipokuja niliwahi kulidaka kabla halijanifikia tumboni kisha nikauzu-

    ngusha mguu wa mtu yule kwa nguvu na kwa kasi ya ajabu na bila upinzani

    nikafanikiwa kuutengua mfupa wake wa goti lake na hapo yule mtu akapiga

    yowe kali la maumivu. Alipoanguka chini mfupa wa goti lake ulikuwa tayari

    umevunjika, nikawahi kunyanyuka na kumfuata lakini wakati nikifanya hivyo

    nilisita pale nilipojikuta nikitazamana na mtutu wa bastola yake mkononi.

    “Ulidhani utaondoka ukiwa hai humu ndani, unajidanganya bure Luteni

    kwani huendi kokote” yule mtu mtata alizungumza huku akicheka na safari

    hii sauti yake ilinikumbusha kitu fulani na nilipomtazama vizuri nikagundua

    kuwa alikuwa ni yule mtu aliyetupa hifadhi mimi na Drel Fille kule kwenye

    ile nyumba katikati ya msitu mara baada ya kuyatoroka mapango ya Musanze.

    “Umenikumbuka eh!, bila ya shaka umenikumbuka mimi ndiye Honey

    Burger king’ang’anizi hakuna aliyewahi kunipiga mgongo akafanikiwa kuon-

    doka”

    “Mbona unaongea kama mwanamke mwoga aliyefumaniwa na mumewe?

    nilimwambia kwa hasira.

    “Unajifariji bure Luteni kwani maneno yako hayatakusaidia kitu. Nita-

    kuchapa risasi za kutosha na kwa mpangilio maalumu mpaka utakapoaga dun-

    ia huku mdomo wako mchafu ukiwa wazi. Najua una matumaini makubwa

    kuwa utaondoka na ile bahasha ya Dr. François Tresor lakini hilo unapaswa

    kulisahau kabisa na badala yake ungemuomba Mungu aipokee roho yako huko

    iendako muda mfupi kuanzia sasa”

    Niliyasikiliza maneno ya yule mtu aliyejiita Honey burger mtata jina lake

    likiwa na maana ya Nyegere, mnyama mwenye tabia ya kung’ang’ania kitu

    bila kuchoka. Kwa kweli nilimuona akiendana kabisa na tabia hizo maana ali-

    kuwa ameanza kunifuatilia tangu nilipomtoroka kule msitunihadi huku mjini

    tena bila ya kukata tamaa akiwa na nia moja tu ya kunitia mikononi mwake

    kama si kuichomoa roho yangu kabisa.

    Bastola yake ikiwa imenionya kuwa nisipige hatua yoyote kumkabili, nili-

    simamahuku nikifikiria namna ya kufanya katika kujinasua katika kizingiti

    kile kilichoonekana kikubwa zaidi mbele yangu huku nikijua kuwa endapo

    nisipokuwa makini risasi zote zilizokuwa ndani ya ile bastola yake zinge-

    potelea mwilini mwangu. Niliendelea kumtazama yule mtu huku akili yangu

    ikiwa imefika kikomo cha ufikirivu bila kupata majibu na kwa kweli nilikata

    tamaa sana.

    “Unadhani utapata tena nafasi ya kuonesha umahiri wako?, usijidanganye

    Luteni kwani leo mwisho wako umefika. Mapinduzi yaliyopangwa katika nchi

    hii yatafanyika kama yalivyopangwa lakini wewe ukiwa hayati mbwa kacho-

    ka. Hili taifa ni mali yetu na hakuna mende yeyote wa kutuzuia na dunia laz-

    imailifahamu hilo”

    “Acheni ubinafsi wenu mapinduzi ya nini wakati hii ni nchi huru? nilimuuli-

    za huku nikiununua muda ingawaje mpaka wakati huu niliona kweli sikuwa na

    ujanja wa kujinasua katika kizingiti hiki cha kifo mbele yangu.

    “Usitake kujua kwani hiyo haitokusaidia kitu chochote. Nakuona nikama

    unayetafuta faraja ya kifo chako wakati kifo hakina faraja. Baada ya kukucha-

    pa risasi za kutosha Kanali Theoneste Bagasora atafika hapa kunichukua na

    harakati zetu zitaendelea kama kawaida wakati wewe ukiwa mfu” Honey

    Burger aliongea na niliweza kuipima sauti yake kuwa ilikuwa mbali na mza-

    hahali iliyonipelekea nitokwe na jasho jepesi kwa hofu. Kwa kweli nilikuwa

    kwenye mtego ambao kwa akili za kibinadamu nisingeweza kujinasua kirahisi

    hivyo nikabaki nikimwomba Mungu huku nikifikiria namna ya kuununua

    muda zaidi nikisubiri muujiza.

    “Huyo Kanali Theoneste Bagasora ni nani? nilimuuliza yule mtu na hapo

    nikamuona akianza kuangua kicheko huku akinitazama kwa mshangao.

    “Kweli sasa umechanganyikiwa Luteni, nimeshakuambia kuwa anaitwa

    Kanali Theoneste Bagasora halafu tena unaniuliza huyo ni nani. Kama huko si

    kuchanganyikiwa ni nini sasa?yule mtu aliendelea kuongea na kabla hajamal-

    iza nilishtuka kuuona ule mlango wa ile ofisi ukifunguliwa kwa kasi ya ajabu

    na sote tukashtushwa na tukio lile.

    Alikuwa Drel Fille, kufumba na kufumbua akafyatua risasi toka katika

    bastola yake mkononi kumlenga yule mtu na hapo ghafla nikamuona Hon-

    ey burger akirushwa hewani kwa nguvu yarisasi nne zilizouchakaza vibaya

    mgongo wake. Akapigizwa ukutani na alipotua chini alikuwa tayari amekata

    roho. Nikabaki nimesimama huku nikiwa siamini kilichotokea mbele yangu.

    “Drel...!” nikamuita.

    “Twende zetu mpenzi hatuna muda wa kupoteza wanajeshi wapo nje”

    Nilimtazama Drel Fille na kumuelewa kuwa alikuwa akimaanisha alichoku-

    wa akikisema na hapokwa haraka nikaenda kuichukua ile bahasha ya Dr.

    François Tresor iliyokuwa juu ya ile meza ya meneja wa posta marehemu Be-

    trand Masambu kisha nikazichukua zile bastola zote tatu yaani yangu na zile

    mbili, yaani ya Honey burger na ya Betrand Masambu. Wakati nikifanya hivyo

    Drel Fille yeye alikuwa akitafuta mlango mwingine wa kutokea mbali na ule

    tuliyoingilia mle ndani na mara akauona mlango mmoja uliyokuwa kwenye

    kona ya ofisi ile. Ulikuwa mlango wa kutokea sehemu ya nyuma ya ofisi ile

    ya posta mahali kulipokuwa na sehemu ya maliwato na stoo lakini kwa sasa

    mlango huo ulikuwa umefungwa kwa makufuli mawilimakubwa.

    Nilipomuona Drel Fille anasita kuusogelea ule mlango nikausogelea na

    kuuchunguza na wakati nikifanya hivyo tukasikia sauti ya vishindo vya watu

    wakija kwenye ile ofisi. Drel Fille aliwahi kukimbia na kwenda kuufunga ule

    mlango wa kuingilia mle ndani na wakati huo mimi nikiyavunja yale makufuli

    mawili ya mlangoni kwa risasi kisha nikamuonesha ishara Drel Fille kuwa

    mambo yalikuwa poa hivyo tuondoke zetu.

    Tuliufungua ule mlango na kutokezea sehemu ya nyuma ya ofisi ile mahali

    kulipokuwa na chumba cha maliwato,stoo na tenki kubwa la kuhifadhia maji

    huku sote tukiwa makini. Nilipanda ukuta wa uzio wa jengo lile na kuchun-

    gulia nje na hapo nikawaona baadhi ya wanajeshi wakiwa katika sare zao na

    bunduki zao mikononi wakilizunguka lile jengo na sikuweza kuona hata raia

    mmoja akirandaranda eneo lile.

    Drel Fille akiwa chini anasubiri nimpe taarifa kuhusu hali ya mambo il-

    ivyokuwa kule nje nikamwambia kuwa hali haikuwa ya usalama na hapo

    nikashuka kwenye ule ukuta na kuelekea upande mwingine ambapo nilipanda

    ukuta na kuchungulia tena nje.

    Kitendo cha kuwaona tena wanajeshi wengine upande ule nikagundua kuwa

    eneo lote la nje ya jengo lile lilikuwa limezungukwa na wanajeshi na baada ya

    kuchunguza vizuri nikagundua kuwa ni sehemu ya nyuma tu ya jengo lile ndi

    yo iliyokuwa haijazingirwa na wale wanajeshi na hali hiyo ilitokana na jengo

    lile kuwa limepakana na jengo jingine kwa upande ule.

    Bila kupoteza muda tulianza kupanda ngazi kuelekea juu ya lile tenki la

    maji. Lile tenki la maji lilikuwa juu zaidi ya ule ukuta uliyopakana na lile jen-

    go la nyuma. Ukuta huo mrefu ulikuwa na seng’enge juu yake hivyo kupitia

    tenki lile la maji mara baada ya kufika juu tuliruka juu ya seng’enge zile na

    kuangukia upande wa pili wa ukuta ule ndani ya ile nyumba ya jirani.

    Nilifurahi kuwa nyumba ile haikuwa na wenyeji kwa wakati ule hivyo mara

    baada ya kuangukia kule chini tuliambaa na ukuta ule hadi mbele ya nyumba

    ile sehemu kulipokuwa na geti kubwa. Kupitia uwazi mdogo uliokuwa kati

    ya geti na ukuta ule niliweza kuona nje. Sikuwaona wale wanajeshi na badala

    yake niliwaonabaadhi ya raia wakiharakisha kuelekea mbali na lile jengo la

    posta. Bila ya kupoteza muda nikafungua mlango mdogo wa lile geti kisha

    tukatoka na kujichanganya na wale watu tukiharakisha kulitoroka eneo lile.

    Baadhi ya watu walionekana kututilia mashakalakini walipotuona kuwa tume-

    shika hamsini zetu hakuna aliyeshughulika na sisi.

    Tulivuka barabara ya lami ya mtaa ule tukakatisha katikati ya majengo

    marefu ya ghorofa tukiharakisha kulitoweka eneo lile na wakati tukifanya

    hivyo tulipishana na magari ya jeshi mawili yaliyokuwa yakielekea kwenyeile

    ofisi ya posta. Wakati tukitembea nilimshukuru sana Drel Fille kwa kuyaokoa

    maisha yangu kule kwenye kile chumba cha meneja wa posta bwana Betrand

    Masambu. Ingawaje nilikuwa na hakika kuwa majibu ya maswali yangu men-

    gi yalikuwa yameanza kujibiwa huku mengine nikiwa na hakika kuwa yange-

    jibiwa kupitia ile bahasha ya Dr. François Tresor niliyoichukua kule posta lak-

    ini akili yangu haikuacha kufikiri.

    Nilimkumbuka Dr. Amanda Albro nikaanza kujiuliza nini nilichokuwa

    kimemsibu na kama alikuwa hai alikuwa wapi kwa wakati huu. Kwa kweli

    sikupata majibu ya maswali yangu na hapo mawazo yangu yakahamia kwa

    Niyonkuru, msichana rafiki wa marehemu Tobias Moyo na hapo nikahisi ni

    kama niliyekuwa ninahitajikakuonana naye ingawaje sikuwa na hakika kama

    bado angekuwa kwenye ile nyumba.

    Mwishowe mawazo yangu yakahamia kwa Ikirezi, msichana niliyeonana

    naye kule Kigali Casino wakati ule nilipowasili hapa jijini Kigali na tukio hilo

    likanipeleka moja kwa moja kuikumbuka Hotel des Mille Colines na hapo

    nikakikumbuka kile chumba changu kwenye hoteli hiyo wakati ule nilipofika

    hapa jijini Kigali.

    Siku nyingi zilikuwa zimepita huku nikiwa mbali na chumba hicho ingawa-

    je kwa pesa niliyolipa bado ilikuwa inaniruhusu kuendelea kukaa kwa muda

    wa wiki mbili mbele. Niliwaza huku nikishawishika kukitembelea tena chum-

    ba hicho.

    Mawazo yangu yaliporudi nilishtukia kuwa tulikuwa tumebakisha hatua

    chache kukifikia kituo cha teksi kilichokuwa mbele yetu. Nilimuuliza Drel

    Fille kuwa alikuwa ana mawazo gani akaniambia kuwa tulikuwa tukielekea

    nyumbani kwani alihitaji utulivu wa akili yake kwa wakati ule na mimi sikuwa

    na sababu ya kutoheshimu na kukubaliana na maamuzi yake. Hivyo tulikodi

    teksi moja eneo lile na safari ya kuelekea

    nyumbani ikaanza.



    #214

    MVUA KUBWA ILIKUWA IKINYESHAsambamba na upepo wa wastani

    hivyo sehemu kubwa ya jiji la Kigali kwa wakati huu ilikuwa imetawaliwa

    na hali ya baridi. Ilikuwa ni mara tu tulipofika nyumbani Drel Fille hakutaka

    tupumzikekama alivyoniambia hapo awali na badala yake kupitia ushawishi

    mkubwa aliokuwanao kama mwanamke tulijikuta tukitumbukia tena kwenye

    mtego mwingine wa mapenzi mazito ambayo yalinipelekea niweke kando shi-

    da zangu kama si kuzisahau kwa muda.

    Drel Fille alikuwa msichana mtundu sana aliyejua kucheza vizuri na hisia za

    mwanaume na kwa kweli aliniwezea sana na kunifanya nisahau mikasa yote

    niliyokumbana nayo katika harakati zangu.

    Tulianzia bafuni huko tulikokwenda kuoga ili kuipoza miili yetu na tukiwa

    huko Drel Fille alianza vitimbi vyake vya hapa na pale ambavyo kwa kweli

    sikuweza kuvivumilia na hapo tukajikuta tukipeana mapenzi motomoto.

    Baadaye tulipomaliza kuoga tuliekea chumbani na kujitupa kitandani na

    hapo kila mmoja akaendeleza ufundi wa mapenzi kwa mwenzake. Tulibinu-

    ka kila sarakasi iliyowezekana na tukafanya kila kionjo cha mapenzi ilimradi

    kuikamilisha furaha yetu na kwa kweli furaha yetu ilikamilika na kuiacha miili

    yetu ikiwa hoi kwa uchovu huku kitanda kikiwa na mengi ya kusimulia. Tuli-

    maliza ngwe ile ya mapenzi tukiwa hoi kwa uchovu.

    Sikuweza kutambua ni wakati gani usingizi ulituchukua lakini wakati nili-

    poshtuka usingizini ilikuwa ikielekea kutimia saa kumi na moja kasoro jioni.

    Nilikuwa wa kwanza kuamka toka usingizini, niliamka na kumtazama Drel

    Fille aliyekuwa bado amelala pembeni yangu. Nilimtazama Drel Fille kwa

    utulivu huku nikiutathmini vizuri uzuri wake na kwa kweli nilijisikia faraja

    sana kuwa mmiliki halali wa penzi lake.

    Wakati huu Drel Fille alikuwa amevaa chupi tu huku kifua chake kikiwa

    wazi. Shuka alilojifunika lililichora vizuri umbo lake na kunifanya nijisikie fa-

    raja sana kulitazama. Niliyatega vizuri masikio yangu na kwa mbalinilimsikia

    Drel Fille akikoroma kuashiria kuwa bado alikuwa kwenye usingizi mzito.

    Nikalitupa shuka pembeni na kuketi kwenye pembe ya kitanda huku ni-

    kivinyoosha viungo vyangu kutoa uchovu halafu nikainama uvunguni mwa

    kitanda kuichukua ile bahasha niliyoichukua kule posta. Ilikuwa bahasha nzito

    kiasi na kubwa na hali hiyo ikaniashiria kuwa ndani yake kulikuwa na kitu

    zaidi ya barua. Nilipoichukua bahasha ile niliigeuzageuza na kuichunguza na

    kwa nje hapakuwa na sehemu yoyote yenye upenyo hivyo niliamua kuichana

    kwa juu na wakati nikifanya hivyo Drel Fille alishtuka usingizini na kujigeuza

    pale kitandani.

    Ndani ya bahasha ile nilikuta bahasha nyingine ndogo iliyofungwa kwa-

    gundi kali. Nilipoichunguza bahasha ile nikagundua kuwa haikuwa na upenyo

    wowote hivyo nayo pia niliamua kuichana kwa juu na wakati nikifanya hivyo

    Drel Fille alikuwa tayari amekwisha amka kisha akasogea karibu yangu na

    kunikumbatia kwa nyuma huku shingo yake akiilaza begani kwangu. Nili-

    geuka kidogo kumtazama huku kila mmoja akionesha tabasamu usoni mwake

    ingawaje hakuna aliyemsemesha mwenzake.

    Nilimalizia kuichana bahasha ile na ndani yake nilikutana na vitu vilivyon-

    ishangaza na kunivutia. Kulikuwa na idadi ya picha kumi na moja na picha

    zote zilimuonesha Dr. François Tresor akiwa na makamanda wa jeshi la Rwan-

    da ambao miongoni mwao niliweza kuwatambua.

    Nikiwa na hakika kuwa Drel Fille alikuwa nyuma yangu akizitazama picha

    zile niliendelea kuzichunguza zile picha kwa makini moja baada ya nyingine

    na hapo nikagundua kuwa zilikuwa zimepigwa katika maeneo tofautihuku wa-

    husika wake wakionesha nyuso za furaha. Na kwa hakika picha zile zilinivutia

    kwani sana nilikuwa na hakika kuwa Dr. François Tresor alikuwa akishirikiana

    kwa namna moja au nyingine na makamanda wale wa kijeshi katika dhana ya

    maslahi fulani.

    Kila nilipomaliza kuichunguza picha moja niliigeuza nyuma na hapo niliku-

    ta orodha ya majina ya wahusika wote na eneo ambalo picha hiyo ilipigwa na

    wakati nikifanya hivyo niligundua kuwa kulikuwa na baadhi ya majina yaliy-

    ojitokeza mara nyingi zaidi na miongoni mwa majina hayo lilikuwepo jina la

    Kanali Bosco Rutaganda. Hali hiyoikaanza kunifanya nianze kujiuliza maswa-

    li mengi ambayo sikua na majibu yake ingawa ninachoweza kusema ni kuwa

    Dr. François Tresor alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Kanali Bosco Ru-

    taganda kabla ya urafiki wao kutumbukia nyongo na hatimaye kugeukana hali

    iliyopelekea Dr. François Tresor kutekwa na kuuwawa kule mapangoni.

    Nilimaliza kuzitazama picha zile huku nikiwa na hakika kuwa zingekuwa

    ushahidi tosha endapo ningeamua kuwafungulia mashtaka makamanda wale

    wa kijeshi kwenye mahakama ya makosa yajinai na haki za binadamu duniani.

    Nilimaliza kuzitazama picha zile na kuziweka kando huku nikimwacha Drel

    Fille akiendelea kuzitazama na hapo nikaanzakuzipekuwa karatasi zilizoku-

    wa pamoja na zile picha kwenye ile bahasha. Niliichukua karatasi moja mle

    ndani iliyokunjwa vizuri nikaifungua na baada ya kiufungua niligundua kuwa

    karatasi ile haikuwa barua kama nilivyodhani bali zilikuwa ni karatasi mbili

    zilizobanwa vizuri zenye maelezo fulani.

    Nilipoanza tu kuyapitia maelezo katika karatasi zile nikagundua kuwa ya-

    likuwa maelezo yaliyokuwa katika lugha ya kifaransa na kwa kuwa mimi si-

    kuwa stadi sana wa lugha hiyo nikaona ni bora nimpe Drel Fille azipitie ili

    atakapomaliza anielezee kwa ufasaha kilichoandikwa mle ndani. Drel Fille

    akazipokea zile karatasi na kuanza kuzipitia na wakati huo mimi nikiendelea

    na upekuzi wangu.

    Nilichungulia tena ndani ya bahasha ile nikaona kulikuwa na makaratasi

    mengine yaliyosalia lakini makaratasi hayo yalikuwa katika mafungu mawili.

    Fungu la kwanza lilikuwa na karatasi chache na lile la pili lilikuwa karatasi

    nyingi zaidi. Nikaamua kuanza kushughulika na lile fungu la karatasi chache

    na hapo nikazichukua na kuanza kuzipitia. Hata hivyo sikuweza kuendelea

    kwani maelezo ya kwenye karatasi zile nayo pia yalikuwa katika lugha ya

    kifaransa. Kuona vile nikamtupia Drel Fille zile karatasi na kuhamia kwenye

    lile fungu la karatasi zilizosalia.

    Zilikuwa karatasi hamsini zilizobanwa vizuri na zenye maelezo ya kuto-

    sha yaliyoandikwa kwa mkono wenye hati nzuri inayasomeka. Niliichunguza

    hatiile na haponikagundua kuwa ilikuwa ni hati ya Dr. François Tresor. Ni-

    lipokitazama kichwa cha habari kilichokuwa juu ya ukurasa wa kwanza wa

    karatasi zile nikagundua kuwa ile ilikuwa ni ripoti maalum inayoelezea hali ya

    uvunjifu wa haki za binadamu na masuala ya usalama katika nchi ya Rwanda.

    Ripoti ile ilikuwa imeandikwa na Dr. François Tresor mwenyewe akiwa na nia

    ya kuituma makao makuu ya shirika la haki za binadamu amaHuman Right

    Watch huko jijini New York, Marekani.

    Maelezo katika karatasi zile yalikuwa katika lugha ya kiingereza na si

    kifaransa kama zile karatasi za awali hivyo sikupata ugumu wowote katika

    kuyasoma maelezo yake.

    Nilianza kusoma kwa makini ukurasa mmoja baada ya mwingine na nilipo-

    maliza nilihisi kichwa changu kilikuwa kimetua mzigo mkubwa wa maswali

    yaliyokuwa yakikisumbua kichwa changu. Kwa kweli ilikuwa ni ripoti iliy-

    okuwa ikielezea kwa ujumla hali ya uvunjifu wa haki za binadamu na masuala

    ya usalama katika nchi ya Rwanda kwa ujumla.

    Katika ripoti hiyo Dr. François Tresor alikuwa ameweka viambatanisho vya

    ushahidi kama picha, video cd,audio tapes na nyaraka nyingine muhimu za

    kimaandishi. Nilishangaa kukuta kuwa miongoni mwa picha hizo zilikuwapo

    picha mbiliza Tobias Moyo, mwandishi wa habari wa nchini Tanzania ambaye

    nilikuwa nimetumwa nchini Rwanda kufuatilia juu ya kifo chake.

    Nilizitazama vizuri picha zile katika mshangao wa kipekee na picha ya

    kwanza ilimuonesha ndugu Tobias Moyo akiwa amelala katikati ya dimbwi

    la damu huku mwili wake wote ukiwa na majeraha ya mapanga. Mwili wa

    Tobias Moyo ulikuwa umelala kifudifudi pembeni ya kitanda sakafuni. Ni-

    liitazama picha ile huku kumbukumbu zangu zikirudi nyuma kwenye enzi za

    uhai wakena hapo simanzi ikanishika kabla ya kuiweka picha hiyo pembeni.

    Picha ya pili iliuonesha mwili wa Tobias Moyo ukiwa umelazwa chali huku

    ukiwa umevuliwa nguo zote. Macho yake yalikuwa wazi kama anayetazama

    kitu fulani. Uume wake ulikuwa umekatwa na kuchomekwa mdomoni na sura

    yake ilionesha kuwa alikuwa ni mtu aliyekufa katika maumivu makali sana na

    pembeni yake kitandani alikuwa ameketi mwanaume mrefu na mwenye mwili

    wenye afyanjema.

    Mwanaume huyo alikuwa amevaa sare za kijeshi na alikuwa akivuta sigara

    huku uso wake ukiwa umenawiri tabasamu la kifidhuli. Mtu huyo alikuwa

    amegeuka akiitazama maiti ya Tobias Moyo iliyokuwa imelala kwenye dimb-

    wi la damu sakafuni.

    Nilimtazama kwa makini yule mtu kwenye ile picha na taswira yake hai-

    kuniingia kabisa akilini na nilipoigeuza kwa nyuma nikakutana na jina la

    Kanali Theoneste Bagasora. Kitendo cha kuliona jina lile ikanibidi niigeuze

    tena ile picha kumtazama vizuri yule mtu huku nikianza kupata picha kamili

    kuwa kumbe Kanali Theonaste Bagasoro ndiye aliyekuwa nyuma ya mauaji na

    utekaji wote wa watu uliokuwa ukifanyika jijini Kigali.

    Nilirudia kuitazama vizuri picha ile na nilipoizoea niliirudisha ndani ya ile

    bahasha huku nikivitazama vielelezo vingine vya ushahidi vilivyokuwa ndani

    ya bahasha ile.

    Nilipomaliza kuvipitia vielelezo vyote vya ushahidi vilivyokuwa ndani ya

    bahasha ile pamoja na ile ripoti ya Dr. François Tresor nilijikuta nimepata ufa-

    hamu mzuriwa jinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea katika nchi hii.

    Sasa nilifahamu kuwa baadhi ya makamanda wa jeshi wasiokuwa waamin-

    ifu kwa serikali ya Rwanda kama Kanali Theoneste Bagasora, Bosco Ruta-

    ganda na wengine nisiowafahamu walikuwa wamepanga kufanya mapinduzi

    dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani ya rais Juvenal Habyarimana nakiini

    kikubwa cha mapinduzi hayo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kwa siri ni

    chuki ya ukabila iliyojengeka kwa muda mrefu baina ya pande mbili za mak-

    abila makubwa ya wahutu na watutsi, eti kwa kile tu kilichoonekana na kuse-

    mekana kuwa watutsi wachache katika nchi hii ndiyo waliyokuwa wakihodhi

    nafasi za juu serikalini huku wahutu ambao ni wengi wakiendelea kufanya

    kazi zachini.

    Niliikumbuka nchi yangu Tanzania ambako pia kulikuwa kumeanzishwa

    vikundi fulani vya ki-dini na watu fulani wasioitakia mema nchi hiyo huku

    wakidai wanampigania Mungu kwa kueneza chuki dhidi ya watu wa dini

    nyingine kwa kufanya mauaji ya siri kwa kutumia milipuko natindikali na

    hapo nikaona hatari inayoikabili Tanzania endapo tatizo hilo lisipotafutiwa

    ufumbuzi wa kudumu kwa kuvitokomeza kabisa vikundi hivyo pamoja na

    watu hao waliokinaishwa na tunu ya amani tuliojaliwa.

    Udini na ukabila, dhana hii ilipojengeka vizuri kichwani mwangu nikaan-

    za kulitazama bara langu la Afrika katika sura mpya kabisa huku nikijiuliza

    kwanini waafrika wengi tulikuwa watumwa wa fikra, wabinafsi na wepesi

    kutumika na watu wa nje ya bara hilo katika kugombanishwa wenyewe kwa

    wenyewe, huku nikijiuliza hivi mtu anawezaje kumchukia mtu mwingine kwa

    kigezo cha kabila lake ambalo halina athari zozote na mfumo wa maisha yake

    au kumchukia mtu kwa kigezo cha dini yake wakati dini zote zililetwa na wa-

    geni huku kila mmoja akiwa na uhuru wa kuabudu dini anayoiona inamfaa?.

    Kwa kweli hasira zilinipanda sanapale nilipokumbuka kuwa dini hizo zil

    iletwa na wageni barani Afrika huku mababu zetutayari wakiwa na dini zao

    walizokuwa wakiziabudu ambazo kimsingi zilionekana kuwasaidia kwa imani

    zao. Upumbavu gani huu tulionao waafrika? nilishikwana hasira huku nikiji-

    uliza ni nani atakayebaki milele chini ya jua hili hata ajitambe kuwauawengine

    kwa kigezo cha dini au kabila? kwa kweli nilishikwa na hasira.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Dr. François Tresor kulikuwa na mapinduzi yali-

    yokuwa yamepangwa kufanyika hapa nchini Rwanda hata hivyo ripoti hiyo

    haikueleza ni lini mapinduzi hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika ingawa

    ilionyakuwa tukio hilo halikuwa mbali sana hadi kufanyika.

    Vile vile ripoti hiyo ilieleza kuwa kulikuwa na uingizwaji kwa kificho wa

    silaha za kutekelezea mauaji dhidi ya watutsi mara baada ya mapinduzi hayo

    kufanyika. Silaha hizo baadhi yake zikiwa ni bunduki, mabomu, marungu,

    visu na idadi kubwa ya mapanga.

    Ripoti hiyo iliendelea kueleza kuwa ili kuweza kutimiza adhma hiyo ya

    mauaji kulikuwa na utaratibu uliokuwa ukifanywa kwa siri wa kuorodhesha

    majina na makazi ya raia wote wa nchi ya Rwanda wenye asili ya kabila la

    kitutsi na wale wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani ambao walikuwa

    wakishirikiana na watutsi kwa namna moja au nyingine ili wakati wa kute-

    keleza mauaji hayo iwe rahisi kuwafichua, kuwatambua na hatimaye kuwaua

    kwa urahisi.

    Ripoti hiyo iliendelea kueleza kuwa mara baada ya mpango wa mapinduzi

    hayo kutekelezwa vizuizi vingewekwa barabarani ili kuwazuia watutsi wa-

    takaojaribu kutoroka na hatimaye kuwaua kabla hawajatimiza adhma yao. Pia

    katika ripoti hiyo kulikuwa na orodha ya majina ya watu waliokuwa nyuma

    ya mpangowa mapinduzi hayo na majina hayo ni pamoja na jina la Kanali

    Theoneste Bagasora, waziri mkuu wa serikali ya mpito ndugu Jean Kamban-

    da, Kanali Bosco Rutaganda, Jean Marie Vianney Mudahinyuka a.k.a zuzu

    kama mmoja wa kiongozi wa kundi la Interahamwe, Robert Kajuga rais wa

    Interahamwe, Gitera Rwamuhuzi, Pauline Nyiramasuhuko kama waziri wa fa-

    milia na maendeleo ya wanawake na majina mengine mengi ambayo sikuweza

    kuyashika haraka kichwani.

    Ripoti ile iliendelea kueleza kuwa mara baada ya mapinduzi hayo kufan-

    yika njia zote za usafirishaji kama barabara na viwanja vya ndege na njia za

    mawasiliano kama vituo vya kurushia matangazo ya redio,runinga na ofisi za

    posta vingefungwa na badala yake ni kituo kimoja tu cha redio cha RTLM am-

    bacho ndiyo kingetumika kurusha matangazo yake kufichua mahali ambapo

    watutsi wangekuwa wamekimbilia kujificha.

    Nilimaliza kuipitia ripoti ile huku nikihisi kuwa akili yangu ilikuwa mbioni

    kuugua maradhi yasiyoeleweka. Kulikuwa na masuala mengi ya kuendelea

    kutafakari juu ya ile ripoti hata hivyo akili yangu ilikuwa imechoka sana na

    kwa mara ya kwanza nilihisi kuwa akili yangu ilikuwa mbioni kulemewa na

    wingu la hisia mbaya na hivyo kuendelea kutafakari kungenipelekea niende-

    lee kujihisi mnyonge zaidi. Hivyo nikageuka kumtazama Drel Fille aliyekuwa

    pembeni yangu akiendelea kuzipitia zile karatasi.

    “Vipi kuna chohote cha maana?

    “Ndiyo, hii ni barua ya onyo toka kwa Kanali Theoneste Bagasora akimu-

    onya Dr. François Tresor” Drel Fille aliniambia huku akinikabidhi karatasi ile.

    “Onyo la nini?

    “Alikuwa akimuonya Dr. François Tresor kuwa endapo angeendelea kumzu-

    ngusha kwa kutokumueleza ni wapi alipokuwa Jaji Makesa basi angeamua

    kumlazimisha amueleze kwa njia anazozijua yeye ikiwemo kuifichua biashara

    ya madini ya magendo iliyokuwa akifanywa kwa siri na Dr. François Tresor.

    Nilimtazama Drel Fille na kuelewa kuwa alikuwa akimaanisha alichoku-

    wa akikisema na hapo nikayakumbuka maelezo ya Dr. Amanda Albro juu ya

    mashaka aliyokuwanayo dhidi ya Dr. François Tresor kwa namna alivyokuwa

    na urafiki na baadhi ya makanda wa kijeshi na tamaa yake ya kutafuta ma-

    dini katika bara la Afrika na hapo nikawa nimepata picha kamili ya mambo

    yalivyokuwa.

    “Huu unaweza ukawa ushahidi tosha wa kuwafikisha hawa watu kwenye

    mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai” niliongea kwa utulivu huku ni-

    kitafakari.

    “Hapana shaka kabisa kuwa huu ni ushahidi unaoweza kuaminika kwa ura-

    hisi” Drel Fille aliongea huku akirudia tena kuyasoma maelezo yaliyokuwa

    katika karatasi zile.

    “Haya ni maelezo ya huyo Dr. François Tresoryakieleza mahali alipo Jaji

    Makesa” Drel Fille aliongea na hapo nikamtupia jicho kumtazama kwa ma-

    kini.

    “Mahali alipo Jaji Makesa...? nilimuuliza kwa shauku.

    “Ndiyo”

    “Huyo ni mtu muhimu sana katika kutoa ushahidi juu ya hali ya mambo

    ilivyo hapa nchini Rwanda na nimekuwa nikiwaza sana namna ya kumpata”

    “Usiniambie? Drel Fille akaniuliza kwa shauku.

    “Kweli mpenzi, hivi unadhanikwa hayo maelezo tunaweza kumpata huyo

    Jaji Makesa?”

    “Kwa kufuata maelezo haya nafikiri tunaweza kumpata” Drel Fille aliniam-

    bia na hapo nikamtazama huku uso wangu umeumba tabasamu la furaha.

    “Hebu nipe picha kamili”

    “Tazama!kwa kufuata maelekezo haya yanaeleza vizuri kila jina la barabara

    hadi kufikia kwenye mtaa wenye nyumba ambayo huyo Jaji Makesa anasadik-

    ika kujificha” Drel Fille aliniambia huku akinionesha zile karatasi.

    “Huu ndiyo mtaa ambao una nyumba aliyojificha Jaji Makesa, mtaa wa

    Gasabo nyumba namba 12” Drel Fille aliendelea kunieleza huku akinionesha

    maelezo kwenye ile karatasi.Niliichukua ile katarasi na ingawaje sikuwa mzu-

    ri sana wa lugha ya kifaransa lakini niliweza kuokota baadhi ya maneno na

    kunifanya nijenge picha fulani kichwani mwangu.

    “Nahitaji kuonana na Jaji Makesa” hatimaye nilinong’ona

    “Si rahisi sana kama unavyodhani Luteni. Jaji Mkesa anatafutwa kwa hali

    na mali kama tunavyotafutwa sisi hivyo usidhani kama itakuwa rahisi sana

    kumpata istoche una uhakika gani kuwa hadi wakati huu Jaji Makesa yupo

    kwenye nyumba hiyo?maana

    “Hakuna namna ya kujihakikishia juu ya hilo ni mpaka hapo nitakapoji-

    ridhisha kwa kumtafuta. Ondoa shaka mpenzi hatuwezi kulitatua tatizo kwa

    kulikimbia. Usiniambie kuwa mara hii tu umesahau kuwa kazi yetu ni ya nam-

    na gani” nilimwambia Drel Fille katika namna ya kumuondolea hofu. Drel

    Fille akanitazama bila kuzungumza neno na hakupenda kuendelea kupingana

    na mimi hata hivyo macho yake yalinionya na hiyo ikawa afadhali kwangu.

    Tuliendelea kujadiliana hili na lile huku kila mmoja akiyaweka wazi mawa-

    zo yake juu ya muktadha wa mambo yalivyokuwa yakiendelea nchini Rwanda

    na wakati huo mvua kali ilikuwa ikiendelea kunyesha na mvua hiyo niliiona ni

    kama iliyokuwa ikinichelewesha katika harakati zangu.



    #215

    NILIMUACHA DREL FILLE AKIWA MEZANIanaandika ripoti ya kija-

    susi kwa mkuu wake wa idara ya kijasusi nchini D.R. Congo-Kinshasa. Kuli-

    kuwa na sababu ya kwanini sikutaka kuongozana naye.Kwanza nilitaka abaki

    huku akiendelea kufanya kazi zake kwa utulivu wa hali ya juu. Pili nilikuwa na

    ratiba zangu tofauti ambazo niliona kuwa endapo kama ningeongozana naye

    kungekuwa na ugumu kiasi katika kupata majibu niliyoyahitaji.

    Wakati huu mvua ilikuwa imeacha kunyesha na kilichobaki yalikuwa ni

    manyunyu hafifu na hali ya baridi ya wastani. Nilikuwa katika mwonekano

    mpya kabisa wa suruali nyeusi ya jeans, fulana nyeusi, kofia ya rangi ya damu

    ya mzee na kotijeusi ambamo kwenye mifuko ya ndani ya koti hilo nilikuwa

    na zana zangu za kazi ikiwemo bastola yenye magazini tatu zilizojaa risasi.

    Wakati teksi ikiniacha nje ya jengo la posta katikati ya jiji la Kigali ilikuwa

    tayari imekwishatimia saa moja na dakika tano usiku. Nilimlipa dereva wa

    teksi pesa yake kisha nikashuka na kuelekea mbele ya ofisi hizo. Hizi zilikuwa

    ni ofisi nyingine za posta na si zile tulizoenda asubuhi mimi na Drel Fille.

    Nilikuwa na bahati sana kuzikuta ofisi zile zikiwawazi hivyo nikapitiliza moja

    kwa moja hadi idara ya huduma kwa mteja ambapo niliwakuta wafanyakazi

    wawili wa kiume wakiwa katika hatua za mwisho za kufunga ofisi zile kwani

    muda wa kazi ulikuwa umekwisha. Wale watu waligeuka kunitazama wakati

    nilipokuwa nikiingia mle ndani. Hapakuwa na mteja yoyote mle ndani hivyo

    nikajua hilo pengine ndiyo lililowashangaza watu wale kwani muda wa kutoa

    huduma ulikuwa umekwisha.

    Kwa kulitambua hilo nilianza kwa kuwataka ladhi watu wale huku niki-

    waomba wanisaidie huduma ya kutuma bahasha yangu jijini Dar es Salaam,

    Tanzania.Niliwaona wale wafanyakazi wawili wakisita kunihudumia na hapo

    nikaishtukia adhma yao mapema. Niliingiza mkono mfukoni na kutoa noti

    moja kishanikaiweka juu ya meza mbele ya wafanyakazi wale.

    “Tafadhali naomba msaada wenu” niliwashawishi kwa utulivu wale watu na

    hapo nikawaona wakigeuka kunizama na nilipowachunguza nikajua kuwa wa-

    likuwa wakishauriana kuhusu ile noti nami sikutaka kupoteza muda nikaingiza

    tena mkono kwenye mfuko wa koti langu na kuitoa ile bahasha ya Dr. François

    Tresor yenye vielelezo vya ushahidi juu ya hali ya uvunjifu wa amani na hali

    ya usalama nchini Rwanda.

    “Andika jina la mtu anayemtumia na namba yake ya sanduku la posta na

    eneo unalotaka bahasha hii ifike” kijana mmoja kati ya wale wawili aliniambia

    huku akinikabidhi kalamu kubwa yenye wino mweusi na bahasha kubwa ya

    kaki.Kisha nikavipokea vile vitu huku nikiichukua ile bahasha yangu na kuitia

    ndani ya ile bahasha kubwa niliyopewa na nilipomaliza kuiingiza ile bahasha

    nikaifunga vizuri kwa gundi kali iliyokuwa juu ya meza ile na kisha juu yake

    nikaandika jina langu kamili, namba ya sanduku la posta na eneo nililotaka

    bahasha ile ifike huko jijini Dar es Salaam, Tanzania.

    “Gharama ya kutuma ni kiasi gani? niliuliza.

    “Ngoja tupime uzito wake kwanza” yule kijana aliniambia huku akiichukua

    ile bahasha na kuiweka juu ya mzani mdogo uliyokuwa pembeni ya meza

    ile. Alipomaliza kuipima uzito ile bahasha akaniambia gharama yake na hapo

    nikatoa pesa mfukoni na kumlipa.

    “Itachukua muda wa siku ngapi hadi kufika?

    “Wiki moja hadi wiki moja na nusu”

    “Nitashukuru” hatimaye nilimwambia yule kijana na kumuaga huku niki-

    ondoka eneo lile. Nilitembea taratibu na kwa utulivu kuelekea nje ya ofisi

    zile huku nikiwa na hakika kuwa macho ya vijana wale wafanyakazi wa ofisi

    ile ya posta yalikuwa yakinisindikiza kwa nyuma. Moyoni nilikuwa na furaha

    kwa kuweza kuituma bahasha ile katika sanduku langu la posta jijini Dar es

    Salaam, Tanzania kwani ule ndiyo ungekuwa ushahidi pekee wa kuwafiki-

    sha Kanali Bosco Rutaganda na wenziwe mbele ya mahakama ya kimatifa ya

    uhalifu dhidi ya haki za binadamu.

    Nilitoka nje ya jengo lile la posta nikiwa na mlolongo wa mikakati kichwani

    mwangu lakini baada ya kutafakari niliibuka na uamuzi mmoja baada ya ku-

    kumbuka kuwa Kigali Casino haikuwa mbali sana na pale nilipokuwa.

    Nilikuwa nimemkumbuka Mutesi, msichana aliyekuwa akifanya kazi

    kwenye casino hiyo ingawaje tayari nilikuwa na majibu ya maswali yangu

    mengi lakini roho yangu iliendelea kunisumbua kuwanilipaswa kuonana tena

    na msichana huyo hivyo niliamua kuanza safari ya miguu kuelekea ilipo casi-

    no hiyo ambayo haikuwa mbali na eneo lile ingawaje kwa kweli sikutegemea

    kupata mapokezi yoyote ya mazuri kwani ni mimi ndiye niliyekuwa nimevun-

    ja ahadi ya kuonana naye wakati ule nilipomtaka aje Hotel des Mille Colines

    kabla sijatekwa na wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda na kupelekwa kule

    mapangoni.

    __________

    SAA YANGU YA MKONONI ilionesha kuwa zilikuwa zimesalia dakika

    chache kabla ya kutimia saa tatu usiku wakati nilipokuwa nikiingia mlango

    wa mbele wa jengo lile la ilipo Kigali Casinoyaani ndani ya Top Tower Hotel.

    Sikuwa mgeni tena wa mazingira yale hivyo nilielekea moja kwa moja hadi

    eneo la mapokezi. Tofauti na mara ile ya kwanza wakati nilipofika, wakati huu

    nilizikuta nyuso ngeni kabisa machoni mwangu za wasichana wawili waliovaa

    sare za kazi. Wote walinikaribisha kwa tabasamu zuri la kibiashara na sikuwa

    na shaka kuwa uzuri wangu ulifanikiwa kuwapumbaza kwa kiasi fulani wasi-

    chana wale na jambo hilo lilinifurahisha.

    “Habari za kazi? niliwasalimia

    “Salama” wote wakaitikia

    “Nitahitaji kufika casino”

    “Una kadi ya mwanachama? mmoja aliniuliza

    “Ni mara yangu ya kwanza” niliwadanganya.

    “Utabidi ulipe pesa ya kiingilio na utuachie kitambulisho chako”

    ‘‘Oh! sasa mtanisaidiaje na mimi nimesahau kuja na kitambulisho? nili-

    wadanganya huku nikijidai kujipekua mifukoni.

    “Bila kitambulisho tutashindwa kukusaidia kaka kwani taratibu hazituruhu-

    su kufanya hivyo” yule dada aliendelea kunitahadharisha na kwa kweli nil-

    ianza kuona ugumu wa kufanikiwa katika adhma yangu. Niligeuka kutazama

    huku na kule huku akili yangu akifanya kazi na wakati huo niliwaona baadhi

    ya watu wakiendelea kustarehe sehemu ile.

    “Naomba msaada wako dada” hatimaye nilinong’ona kwa sauti ya chini

    “Kuna mtu nahitaji kumuona ndani ya casino basi naomba ukaniite kama huto-

    jali dada yangu, nitakulipa kwa usumbufu’’

    “Taratibu hazituruhusu kaka vinginevyo tungekusaidia’’yule dada alinijibu

    na kwa kweli alikuwa akimaanisha alichokuwa akikisema na kwa mara ya

    kwanza nikaanza kuona hila zangu zilikuwa mbioni kukwama.

    Niliitazama saa yangu mkononi na kugundua kuwa zilikuwa zimesalia da-

    kika chache kabla ya kutimia saa nne usiku. Niliona muda ulikuwa ukienda

    haraka hivyo nikaanza kuwaza namna ambavyo Drel Fille angeshikwa na

    wasiwasi mara baada ya kuona ninakawia kurudi. Nikiwa nipo mbioni kuka-

    ta tamaa niligeuka tena kuwatazama wale wahudumu katika uso wa kuomba

    msaada na wakati nikifanya hivyo nilisikia sauti ya hatua za watu waliokuwa

    wakishuka ngazi za pembeni ya sehemu ile ya mapokezi kutoka ghorofa ya

    juu ilipokuwa casino.

    Nilisubiri hadi wale watu walipomaliza kushuka zile ngazi na kunipita nyu-

    ma yangu ndivyo nikageuka kuwatazama na wakati nikifanya hivyo hisia to-

    fautizilinijia. Watu wale walionipita nyuma yangu walikuwa ni mwanaume

    na mwanamke na walikuwa wakitembea kizembezembe kama walevi huku

    wamekumbatiana.

    Hawakufanikiwa kunipotea kwani mara tu nilipotoka nje ya jengo lile nili-

    waona wale watu wakielekea kwenye eneo la maegesho ya magarisehemu lili-

    pokuwa gari aina ya VolkswagenComb nyeupe. Sikutaka kupoteza muda hivyo

    haraka nikaanza kuzitupa hatua zangu kuwafuta wale watu na hapo nikagun-

    dua kuwa hisia zangu zilikuwa za kweli pale nilipomuona Mutesi wakati ali-

    posita na kugeuka nyuma akinitazama baada ya kuona nilikuwa nikiwakaribia.

    “Mutesi”nilimuita kinyonge kama nisiyejiamini wakati huo yule mwanau-

    me aliyeongozana naye akiwa tayari ameshafungua mlango wa mbele wa lile

    gari. Mutesi alisita na kunitazama na hapo tukabaki tukitazama ingawaje mimi

    nililazimisha tabasamu kuununua urafiki wetu ulioanza kuota mbawa.

    “Patrick…!’’ Mutesi aliita kwa mshangao na hapo nikajua sauti yake iliku

    wa na ulevi kiasi.

    “Ndiyo mimi mpenzi habari za siku nyingi”

    “Ulikuwa wapi mbona ulinidanganya?

    “Ni hadithi ndefu mpenzi” nilimwambia na kabla sijamaliza kuongea yule

    mwanaume aliyeongozananaye alikuja kwa hasira akamshika mkono Mute-

    si na kumvuta huku akinitupia jicho la kunionya nami sikutaka kuachana

    na Mutesi katika namna ile hivyo nilitupa hatua zangu kumsogelea na hapo

    nikapata rabsha. Ngumi moja aliyoitupa vizuri mtu yule alinipata shingoni

    na kunipelekea nipepesuke huku nikisikia maumivu makali yaliyokivuruga

    kichwa changu, nikajitahidi kujizuia bila mafanikio na hapo nikaanguka chini.

    “Kaa naye mbali kenge mkubwa weh! huyu tayari nimemlipia” yule mtu

    alinionya huku akinifuata pale chini hata hivyo nilikuwa makini kuzisoma

    nyendo zake hivyo pigo la teke alilolirusha niliwahi kuliona na kulipangua

    na hapo nikajipindua na kumchota mtama uliompaisha hewani, alipotua chini

    nikamchapa ngumi mbili kavu, moja ya shingo na nyingine ya korodani na

    hapo nikamuona akiachama mdomo kama mbwa wenye kiu kali bila kupiga

    yowe. Alipotaka kusimama nikamtandika tena kiwiko nyuma ya kichwa chake

    na hapo akaanguka chini kama gunia huku fahamu zikiwa mbali na mwili

    wake.

    Nilisimama na kumtazama mtu yule na sikuona dalili zozote za uhai usoni

    mwake na hapo nikainama na kuanza kumpekua mifukoni wakati huo Mutesi

    akiwa amesimama pembeni anatetemeka kwa hofu.

    Nilipomaliza kumpekua yule mtu nilipata bastola moja aina ya Korg na kiasi

    cha pesa za kutosha ambazo zingeniwezesha kuishi kwa muda wa siku mbili

    hadi tatu bila kuwaza. Baadaye nilimuacha yule mtu pale chini kisha nikam-

    shika mkono Mutesi nikimtaka tuondoke eneo lile lakini nilishangaa kumuona

    Mutesi akisita.

    “Tuondoke mpenzi”

    “Kwanini umempiga vile? Mutesi akaniuliza kwa hasira

    “Sikupanga kufanya vile kama asingeniletea rabsha. Hukumuona namna

    alivyonipiga wakati nilipokusogelea?

    “Kwa hiyo umemuua? Mutesi aliniuliza tena kwa hasira

    “Kama ana bahati atazinduka baada ya siku mbili” nikaamua kumtoa hofu

    Mutesibaada ya kumuona ametaharuki isivyo kawaida

    “Una maanisha nini, hivi unajua kuwa yule mtu ni nani? swali la Mutesi

    likanifanya nigeuke kumtazama usoni.

    “Simjui, kwani yeye ni nani?

    ‘‘Andre Ntegerura mmoja wa viongozi waandamizi wa Interahamwe”

    “Interahamwe? nilimuuliza Mutesi kwa mshangao kisha nikaitazama saa

    yangu mkononi na hapo nikagundua kuwa muda ulikuwa ukiyoyoma sana na

    sikutaka mtu yeyote atukute eneo lile.

    “Tuondoke Mutesi hii si sehemu salama” nilimwambia Mutesi huku ni-

    kifungua mlango na kuingia kwenye lile gari Volkswagen Comb. Nilifurahi

    kukuta funguo za gari zikiwa kwenye swichi yake hivyo nikawasha gari na

    kuliondoa sehemu ile ya maegesho na wakati huo nilimchungulia Mutesi na

    kumuona kuwa bado alikuwa akimtazama Andre Ntegerura pale chini.

    “Twende” nilimwambia Mutesi baada ya kusimama na gari kando yake.

    “Nenda tu mimi siendi kokote” Mutesi aliniambia huku akijipangusa ma-

    chozi, nikaegemea usukani huku nikimuonea huruma hata hivyo sikuwa na

    namna ya kumsaidia.

    “Muda si mefu watu watagundua kuwa mpenzi wako yupo katika hali hiyo

    na hakuna mwingine watakayemshuku kuhusika isipokuwa wewe kwani ni

    wewe ndiye uliyekuwa mtu wa mwisho kuwa naye. Hawatakuamini hata uki-

    jitetea vipi na badala yake watakuua kinyama kwaninawafahamu hivyo ni af-

    adhali tuondoke eneo hilikwani haupo salama tena’’

    “Nani atakayekuamini kwa uongo wako. Sihitaji kuongozana na wewe, nen-

    da zako kwani wewe ndiye uliyemuua na siyo mimi hivyo usidhani kuwa ha-

    watakufahamu” Mutesi alifoka kwa hasira na wakati akiongea hivyo niligeu-

    ka na kutazama kwenye lile lango la kutokea kwenye lile jengo la Top Tower

    Hotel ilipo Kigali Casino na hapo nikawaona wanaume watatu wakitoka nje

    na kuja ule upande wetu.

    “Wanakuja na muda si mrefu watajua kuwa ni wewe ndiye uliyemuua”

    nilimwambia Mutesi na hapo akageuka na kutazama kule nilipokuwa nikita-

    zama na alipowaona wale watu wanakuja akageuka kunitazama usoni huku

    akionekana kuwa ni mwenye mashaka na wakati huohuo mimi nilishaingiza

    gia tayari kuondoka eneo lile.

    “Twende Mutesi watakuua tu kwani ni lazima ufahamu kuwa hakuna mtu

    atakae yaamini maneno yako kuwa si wewe uliyemuua Andre Ntegerura”

    nilimwambia na hapo nikamuona akisogea taratibu kuukaribia mlango wa

    mbele wa gari na hapo nikawahi kumfungulia. Alipoingia ndani nikafunga

    mlango na kuwasha gari na hapo safari ikaanza tukiondoka eneo lile.

    Wakati tukiendelea na safari hakuna aliyemsemesha mwenzake na nilipo-

    geuka kumtazama Mutesi kwa jicho la wizi niligundua kuwa alikuwa katikati

    ya lindi zito la mawazo. Uso wake ulikuwa mbali kabisa na furaha na hapo

    nikajua bado alikuwa akimuwaza yule mtu niliyepambana naye kule nje ya

    casino. Kwa kuogopa kuzidi kuuharibu urafiki wetu nilinyamaza kimya huku

    nikiyahamishia mawazo yangu kwa Drel Fille, msichana niliyetokea kumpen-

    da kupita kiasi tena katika muda mfupi tu tangu tuonane.

    “Tunaenda wapi? sauti ya Mutesi ilirudiwa na uhai na kuniuliza kwa masha-

    ka

    “Mahali salama tunapoweza kujificha watu hawa wasitupate” nilimwambia

    Mutesi na hapo akageuka na kunitazama kwa mshangao

    “Wapi?

    “Hotel des Mille Colines chumbani kwangu, tunaweza kujificha humo kwa

    muda fulani wakati tukisubiri mambo yapoe’’

    “Na vipi kuhusu Andre Ntegerura?

    “Oh! sahau kuhusu yeye kwani muda si mrefu wenzake watamgundua lak-

    ini hawawezi kujua sehemu ya kutupata na wakati huo tunaweza kuwa mbali



    #260

    NIKIWA NIMEANZA KULIZOEA VIZURI JIJI LA KIGALI na baadhi ya

    vitongoji vyake niliamua kupunguza urefu wa safari kwa kuingia barabara za

    mkatohadi pale tulipotokezea kwenye barabara kuu na hapo nikaingia upande

    wa kushoto nikiifuata barabara ielekeayo Hotel des Mille Colines. Nilishukuru

    sana kuwa hapakuwa na gari lolote lililotufungia mkia kwa nyuma.

    Saa sita na robo usiku niliegesha gari nje ya viunga vya maegesho ya magari

    vya Hotel des Mille Colinesna kushuka. Wakatitukitembea kuelekea ndaniya

    hoteli ile niliweza kuhisi wanyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yakianguka

    toka angani. Mutesi alijitahidi kwendana na kasi ya hatua zangu kwani niliji-

    tahidi sana kuharakisha.

    Mhudumu mmoja wa hoteli ile alinitambua kwa haraka wakati nikiingia

    na Mutesi eneo la mapokezi huku akinionesha tabasamu la ukaribisho na si-

    kuwa na muda wa kupoteza hivyo nilipofika eneo lile la mapokezi nikaom-

    ba funguo za chumba changu na wakati mhudumu yule akinipa funguo hizo

    nikamuuliza kama kulikuwa na mtu yeyote aliyefika kuniulizia kwa muda

    wote ambapo sikuwepo. Nilimuona mhudumu yule akimtazama Mutesi na

    kutabasamu nikajua ni yeye tu ndiye aliyefika kuniulizia tangu kipindi kile ni-

    lipotekwa. Baadaye mhumu yule alinihakikishia kuwa hakuna mtu mwingine

    aliyeniulizia isipokuwa yule msichana niliyeongozana naye ambaye ni Mutesi.

    Nilizichukua funguo zilekisha nikapandisha ngazi kuelekea ghorofa ya juuki-

    lipokuwa chumba changu huku nikiwa nimeongozana na Mutesi.

    __________

    NILIFURAHI KUKUTA CHUMBA KIKIWA KISAFI na tulipoingia ndani

    nikafunga mlango wa chumba na kumkaribisha Mutesi aketi kwenye moja ya

    kochi lililokuwa mle ndani. Nilizunguka kwanza kukagua kile chumba na nili-

    poridhika na hali ya usalama nikarudi pale chumbani na kuketi kwenye kochi

    jingine lililotazama na lile aliloketi Mutesi.

    Muda haukuwa rafiki kwangu kwani nilijua hadi wakati huu Drel Fille an-

    gekuwa na wasiwasi kwa kuniona nakawia kurudi. Nilimtazama Mutesi na

    kumuona kuwa mawazo yake bado yalikuwa kwenye kumbukumbu ya tukio

    la nyuma na sikuwa na pingamizi katika fikra zake.

    “Kinywaji gani ungependa kutumia mpenzi?

    “Nashukuru, nimekunywa sana sihitaji chochote kwa sasa” Mutesi aliniam-

    bia huku ni mwenye huzuni.

    ‘‘Pole sana kwa kumpoteza mpenzi wako’’ nilimwambia huku nikiingiza

    mkono kwenye mfuko wa koti langu kisha nikaziweka zile pesa nilizozichukua

    kwa Andre Ntegerura juu ya meza fupi iliyotutenganisha.

    “Chukua’’ nilimwambia Mutesi ‘‘Zinaweza kukusaidia kwa siku mbili hadi

    tatu kabla hujamnasa mteja mwingine” Mutesi alisita kidogo akanitazama ki-

    sha akazichukua zile pesa juu ya meza na kuzitia ndani ya mfuko wa suruali

    yake ya Jeans na hapo nikaliona tabasamu hafifu likijipenyeza usoni mwake

    na hali hiyo akanipa faraja”

    “Ulikuwa wapi siku zote hizo? akaniuliza kwa shauku

    “Ni hadithi ndefu” nilimwambia huku nikianza kumsimulia mkasa wote uli-

    onikuta ingawaje kuna mambo mengine sikupenda ayafahamu na nilipomaliza

    kumsimulia hakuonesha tashishwi yoyote usoni mwake.

    “Pole sana” hatimaye aliongea pindi nilipomaliza kumsimulia

    “Na wewe je ulikuwa ukifanya nini?

    “Kutafuta mwanaume yoyote wa kunistarehesha na kunipa pesa ya kuni-

    wezesha kuishi. Hata hivyo hali imekuwa mbaya tangu tulipopoteana siku ile.

    Nimekuwa nikija hapa hotelini kukuulizia mara kwa mara na bahati mbaya

    sana hakuna aliyekuwa na taarifa zako”

    “Sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kuwa sasa mimi ni mzima

    wa afya”

    “Hata mimi nimefurahi kukuona Patrick”

    Ukimya kidogo alichukua nafasi nikiitumia nafasi hiyo kutafakari jambo

    fulani na nilipoitazama tena saa yangu mkononi nilivunja ukimya.

    “Bila shaka ulinifanyia kazi yangu”

    “Ndiyo” Mutesi alinijibu kwa kujiamini na hapo nikakohoa kidogo nikiketi

    vizuri na kutega sikio

    “Jina lakeanaitwa Bosco Rutaganda, ni kiongozi mkuwa wa kijeshi hapa

    nchini Rwanda, kabila lake ni Mhutu” Mutesi aliweka kituo huku akinitazama

    na hapo nikatambua kuwa alikuwa akinidadisi kama taarifa zile zilikuwa na

    umuhimu wowote kwangu.

    “Endelea” nilimwambia kwa utulivu.

    “Ni askari mwenye cheo cha Kanali na kiongozi wa kambi ya kijeshi ya

    Bugesera”

    “Unadhani ni kwanini alikuwa akinifuatilia? nilimuuliza Mutesi huku nikip-

    ima uzito wa swali hilo kwake.

    “Siku nne baada ya miadi yetu ya kukutana hapa hotelini kushindikana

    mmoja wa askari wa karibu wa Bosco Rutaganda alifika kule kwenye casi-

    no lakini pamoja na wasichana wote waliokuwa mle ndani chaguo lake bado

    lilikuwa kwangu. Hivyo mara baada ya kupata kinywaji aliondoka na mimi

    kuelekea nyumbani kwake kwa lengo la kustarehe lakini wakati tukiwa kati-

    kati ya starehe hiyo alikuja askari mwenzake na gari pale nyumbani kwake.

    “Ilikuwa saa ngapi?

    “Sikumbukiile ilikuwa ni saa ngapi lakini kwa kufikiri huenda ilikuwa ni

    kati ya saa saba usiku na saa nane” nilimtazama Mutesi kwa udadisi kisha

    nikampa ishara kuwa aendelee.

    “Starehe yetu ikiaishia pale kwani yule mwenyeji wangu ikabidi aende se-

    buleni kumkaribisha yule mgeni na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kuyasikia

    maongezi yao”

    “Walikuwa wakizungumza nini? nilimuuliza Mutesi kwa shauku

    “Walikuwa wakizungumza jambo fulani ambalo nahisi lilikuwa la siri na la

    hatari ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika hapa nchini. Sikuweza kusikia

    vizuri mazungumzo yao kwani chumba kile nilichokuwa kilikuwa mbali kido-

    go na sebule ile lakini miongoni mwa maongezi niliyoyasikia ni kuwa mtu

    pekee aliyekuwa amesalia alikuwa ni Jaji Makesa ambaye ni Jaji mashuhuri

    sana hapa Rwanda. Na wakati maongezi yale yakiendelea vilevile niliwasikia

    wakizungumza juu ya wao kuwa macho kufuatilia wageni wote wanaoingia

    hapa chini Rwanda”

    Mutesi aliweka kituo na kunitazama, nikatabasamu kidogo na sikuona kitu

    chochote kipya katika maongezi yake kwa kuzingatia kuwa mambo mengi

    nilikuwa tayari nayafahamu tangu nilipoanza upelelezi juu ya kifo cha Tobias

    Moyo katika nchi hii. Lakini nilipotaka kuongea nilisita baada ya kumuona

    Mutesi akifungua zipu ya mfuko wa koti lake na kutoa bahasha ndogo ya rangi

    ya kaki.

    “Hiyo ni nini?

    “Bahasha, niliiiba kutoka kwenye droo ya kitanda cha yule afisa wa jeshi

    niliyeenda kustarehe naye nyumbani kwake siku ile na nimekuwa nikitembea

    nayo kila siku. Niliichukua nikidhani kuwa huenda ndani yake kungekuwa na

    pesa wakati yeye alipokuwa akiongea na yule mgeni kule sebuleni. Hata hivyo

    niliporudi nyumbani kwangu na kuifungua niligundua kuwa haikuwa na pesa

    ilakaratasi yenye maelezo fulani ambayo yalinitia uvivu kuyasoma’’

    Niliichukua ile bahasha na kuifungua na ndani yake niliiona karatasi nyeupe

    iliyokunjwa mara tatu, nikaitoa na kuifungua kishanikaanza kuisoma. Ingawa-

    je maelezo katika karatasi ile yalikuwa katika lugha ya kifaransa ambayo mimi

    sikuwa stadi nayo hata hivyo niliweza kudonoa neno moja moja na nilipotulia

    na kuyaunganisha maneno hayo baadaye nilipata maana kamili ambayo ilizidi

    kunishtua.

    “Inaeleza nini? Mutesi aliuliza baada ya kuona hali yangu inabadilika baa-

    da ya kumaliza kuyasoma maelezo kwenye karatasi ile na kabla ya kumjibu

    nikairudisha ile karatasi ndani ya bahasha na kuitia mfukoni.

    “Kuna nini? Mutesi aliniuliza tena

    “Kinani ni nani?nilimuuliza Mutesi kwa taharuki

    “Ni jina la utani la rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana likiwa linalo-

    maanisha mtu mashuhuri au asiyeonekana kwa urahisi. Kwani kuna nini?

    “Kanali Bosco Rutaganda na wanajeshi wengine wasio waaminifu kwa ser-

    ikali wamepanga mapinduzi ya kijeshidhidi ya serikali ya nchi na tukio hilo

    limepangwa kufanyika mnamo tarehe 6 mwezi huu wa nne. Mipango yote ya

    utekelezaji wa mapinduzi hayoimeshakamilika nakilichobaki ni utekelezaji tu.

    Wamepanga kuwaua watutsi wote hapa Rwanda mara baada ya mapinduzi

    hayo kufanyika” nilimueleza Mutesi huku akili yangu ikiwa mbioni kuchan-

    ganyikiwa. Nikayazungusha macho yangu kuitazama kalenda iliyokuwa ime-

    tundikwa ukutani mle chumbani na hapo koo langu likakauka kwa hofu na

    moyo ukaanza kwenda mbio pale nilipogundua kuwa zilikuwa zimesalia siku

    mbili kabla ya mapinduzi hayo kufanyika. Mutesi alinitazama kwa hamaki

    kama kigoli aliyevunja ungo bila kujitambua.

    “Una maanisha nini? Mutesi akaniuliza kwa wasiwasi.

    “Wamepanga kuwaua watutsi wote katika nchi hii na hilo ndiyo kusudi la

    mapinduzi hayo. Unadhani kuna ukweli wowote kuhusu hili? Nilimuuliza

    Mutesi na hapo nikamuona akinikazia macho kunitazama.

    “Inawezekana kabisa kwa sababu wahutu wanatuchukia sana hivyo sishan-

    gai sana kusikia hivyo lakini sijajua kwanini wanataka kutuua?

    “Nani anayewachukia? nilimuuliza Mutesi kwa utulivu kama ambaye

    sijamsikia.

    “Wahutu ambao ni wengi katika nchi hii. Wanatuchukia sana wakidai sisi

    tunahodhi madaraka ya juu ya serikali na kumekuwa na vitendo vingi vya

    mauaji dhidi ya watutsi katika baadhi ya maeneo hapa nchini’’ nilimtazama

    Mutesi na kumuona kuwa alikuwa akitokwa na machozi na kitendo hicho ki-

    kanifanya nianze kutafakari chuki kubwa iliyojengeka baina ya makabila hayo

    mawili makubwa katika nchi hii, yaani wahutu na watutsi na hapo nikamsoge-

    lea Mutesi na kumshika mkono.

    “Usijali mpenzi bado tuna muda wa kuzuia tukio hili lisitokee” nilimwam-

    bia Mutesi katika namna ya kumfariji na hapo akainua macho yake kunitazama

    na machozi yaliyotanda katika macho yake yakanifanya nimuonee huruma.

    “Hakuna namna yoyote unayoweza kuzuia mapinduzi na mauaji hayo yali-

    yopangwa yasifanyike hapa nchini Patrick, najua unanifariji tu.Hawa watu

    watatuua tu kwani wanaamini kuwa watutsi wote tukifa wao watakaa kwa

    amani na furaha kwa kuwa wao ni wengi zaidi hapa nchini”

    Maneno ya Mutesi yakanifanya niuinue mkono wangu kuitazama saa yangu

    ya mkononi na hapo nikagundua kuwa muda ulikuwa umeenda sana. Nikam-

    kumbuka Drel Fille huku nikijaribukutengeneza picha ambayo angekuwa

    nayo baada ya kuniona nakawia kurudi.

    “Nataka kuondoka Mutesi na pengine nikakawia kurudi lakini lazima nita-

    rudi”

    “Unaenda wapi?, nakuomba twende wote Patrick huwezi kuniacha pake

    yangu humu ndani” Mutesi akataharuki.

    “Hatuwezi kuongozana Mutesi kwani ni salama zaidi ukinisubiri humu

    ndani. Nahitaji kufanya kila linalowezekana ndani yausiku huu katika ku-

    hakikisha kuwa mapinduzi haya ya kishenzi hayafanikiwi na hili ni jambo

    hatari hivyo hatuwezi kuongozana. Nakuomba uwe mvumilivu na unisubiri

    humu ndani na chochote utakachohitaji tafadhali usisitekupiga simu ofisi ya

    mapokezi utaletewa”

    “Wewe unaenda wapi?

    “Nitakwambia nitakaporudi hata hivyo usitoke nje ya chumba hiki kwani ta-

    arifa zako zinaweza kuwa zimewafikia polisi hivyo wakawa wanakutafuta na

    ukiona jambo lolote tofauti tafadhali nipigie simu kupitia namba hizi” nilimpa

    Mutesi namba ya simu ya ile nyumba niliyomuacha Drel Fille halafu bila ku-

    subiri neno lolote kwake nikamuonesha tabasamu la tumaini kisha nikafungua

    mlango wa chumba kile na kutoka nje.



    #261

    WAKATI NIKIWASHA INJINI YA GARI Volkswagen Comb kwenye mae

    gesho ya magari ya Hotel des Mille Colines hisia tofautizilinijia nilipoya-

    kumbuka maneno ya Mutesi kuwa hakuna namna yoyote ambayo ningefanya

    kuyazuia mapinduzi yaliyopangwa dhidi ya serikali na umwagaji damu ambao

    ungefanyika. Siku zote nilikumbuka kuwa nilikuwa na hisia za kweli kati-

    ka maeneo yaliyokuwa yakijirudia kichwani mwangu hata hivyo wakati huu

    nilizipuuza hisia hizo kwa kuutazama mshale wa mafuta kwenye dashibodi

    ya gari.

    Kulikuwa na mafuta ya kutosha ya kuniwezesha kufanya safari zangu bila

    wasiwasi hivyo niliyaacha maegesho yale na kuingia mitaani na wakati ni-

    kiendelea na safari nilikuwa macho kutazama kama kulikuwa na gari lolote

    lililokuwa likinifungia mkia kwa nyuma.

    Nilizunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Kigali nikitafuta mahali ambapo

    ningepata huduma ya simu ya haraka hata hivyo baadaye niliona ugumu wa

    kufanikisha zoezi hilo kwani kwa muda ule wa usiku ofisi nyingi zilikuwa

    zimefungwa.

    Nilikuwa mbioni kukata tamaa pale nilipoiona ofisi moja ya huduma za

    mawasiliano katika mtaa wa La Paixhivyo nikaegesha gari kando ya barabara

    na kushuka nikielekea kwenye ofisi zile. Kulikuwa na watu watatu ndani ya

    ofisi zile. Wahindi wawili ambao niliwatambua kuwa ni wafanyakazi wa ofisi

    zile na mwafrika mmoja ambaye mara tu nilipoingia mwafrika yule mweusi

    kama mimi aliondoka baada ya kumaliza kuhudumiwa.

    Mhindi mmoja mfupi na mnene akanikaribisha vizuri na kuniuliza shida

    yangu kwa lugha ya kifaransa, nikamwambia kuwa nilikuwa nikihitaji hudu-

    ma ya simu kwenda nchini Tanzanialakini jibu alilonipa lilinishtua sana.

    “Samahani hatuwezi kukusaidia ndugu kwani kumekuwa na tatizo la

    mawasiliano tangu alfajiri ya siku ya leo. Hakuna simu yoyote inayotoka wala

    kuingia ndani ya nchi labda kwa simu za ndani ya nchi tu”

    “Mna taarifa zozote kuwa tatizo hili litaisha saa ngapi? niliwauliza

    “Tumeambiwa tusubiri hadi hapo ukarabati wa mitambo ya mawasiliano

    utakapokamilika ndiyo watatutaarifu”

    Taarifa zile zilinishtua sana kwani sikuamini kama ilikuwa kweli kwamba

    tatizo lile la mawasiliano lilitokana na sababu za kiufundi. Hisia zangu ziliku-

    wa juu ya mapinduzi ya siri yaliyopangwa kufanyika nchini Rwanda na sasa

    niliamini kuwa mpango huo ulikuwa mbioni kutekelezwa. Nikamtazama yule

    mhindi kwa hisia tofauti na yeye akawa kama anayenisikilizia.

    “Kuna huduma moja tu iliyosalia ambayo inatoa mawasiliano nje ya nchi,

    sijui kama itakufaa? yule mhindi aliniuliza akionekana kunionea huruma.

    “Huduma gani?

    “Telegram.”

    Nilimtazama yule mhindi nikiwa na tumaini jipya lililochipua haraka moy-

    oni mwangu na muda mfupi uliofuata nilikuwa mezani nikiandika telegramu

    tatu zenye ujumbe unaofanana. Telegramu ya kwanza niliiandika kwenda ofisi

    kuu ya idara ya ujasusi nchini Tanzania. Ya pili niliiandika kwenda kwenye

    ofisi ya mkuu wa operesheni zangu za kijasusi nchini Tanzania na ya tatu na

    ya mwisho niliituma kwenda ofisi ya umoja wa mataifa pia nchini Tanzania.

    Nilipomaliza nikazituma zile telegramuzikiwa na ujumbe unaofanana wa

    kutaka hatua za haraka zichukuliwe katika kuzima mapinduzi yaliyopangwa

    kufanyika nchini Rwanda ambayo mimi sikuwa na shaka kabisa kuwa yenge-

    pelekea umwagaji mkubwa wa damu huku nikielezea kwa hisia zangu namna

    ya mambo yalivyokuwa yakiendelea nchini Rwanda.

    __________

    ILIKUWA TAYARI IMESHATIMIA SAA SITA USIKU wakati nilipozi-

    acha ofisi zile za mawasiliano zilizopo mtaa wa La Paix. Nilikuwa na hisia

    kuwa kuanzia muda ule mambo hayakuwa salama tena katika nchi ya Rwan-

    da hivyo niliendesha gari hadi makao makuu ya ofisi za msalaba mwekundu

    Quartie Matheus mtaa wa Burera. Muda ulikuwa umesonga sana na wakati

    huu jiji lote la Kigali lilikuwa limegubikwa na ukimya wenye hisia mbaya

    kwa binadamu.

    Kulikuwa na magari matano yaliyoegeshwa nje ya ofisi zile za msalaba

    mwekundu ama Red Crosswakati nilipokuwa nikiegesha gari mbele ya mlan-

    go wa kuingilia. Nikashuka na kutoa maelezo machache ya utambulisho kwa

    walinzi wa ofisi zile waliokuwa kibandani kisha nikaingia ndani ya zile ofisi

    ambapo nilikutana na mama mmoja wa kizungu na kijana mmoja mwafrika.

    Baada ya kuwasalimia nikawaeleza shida yangu kuwa nilikuwa na bahasha

    yangu niliyokuwa nikihitaji kuitumanchini Tanzania kwa njia ya gari kwani

    bahasha hiyo ilikuwa na taarifa zilizokuwa zikihitajika na ofisi yangu kwa

    haraka. Yule kijana mwafrika alishangazwa na ombi langu.

    “Kwani usiitume kwa njia ya posta? yule kijana aliniuliza

    “Inahitajika kufika mapema zaidi hivyo nimeona kuwa kwa njia ya posta

    huenda ikachukua muda wa zaidi ya wiki moja hadi mbili”

    “Tuna gari moja ambalo muda si mrefu kuanzia sasa huenda litaondoka

    kuelekea mkoani Kagera nchini Tanzania na mimi ndiyo dereva wa gari hilo.

    Nikiifikisha huko ni nani atakaeipokea?

    Nilimtazama kijana yule katika namna ya kumshukuru kisha nikaingiza

    mkono mfukoni na kuitoa ile bahasha aliyonipa Mutesi.

    “Utakapofika mkoani Kagera, Tanzania tafadhali nakuomba uitume bahasha

    hii katika posta yoyote ya karibu kwani inatakiwa ifike jijini Dar es Salaam

    mapema iwezekanavyo. Anwani iliyopo juu ya bahasha inajieleza vizuri”

    Yule kijana akionekana kuyasikiliza kwa makini maelezo yangu aliipokea

    ile bahasha na kuichunguza chunguza. Alipoigeuza akagundua kuwa niliku-

    wa nimeiambatanisha na noti mbili za faranga za kinywaranda zenye thamani

    ya elfu ishirini pesa ya kitanzania. Tabasamu alilonionesha usoni sikuwa na

    mashaka kuwa hoja yangu ilikuwa imekubalika.

    “Naitwa Gasana Twagiramungu” yule kijana aliniambia huku akinipa mko-

    no

    “Naitwa ndugu Stefen Mwakawago’’ nilimdanganya kijana yule huku niki-

    shikana naye mkono

    “Ondoa shaka bwana Stefen kwani nitakufikishia bahasha yako bila wasi-

    wasi wowote na ni matumaini yangu kuwa pindi kutakapopambazuka nitaku

    wa mjini Ngara mkoani Kagera Tanzania. Najua ofisi ya posta iliyopo wilayani

    pale ambapo nitaituma barua yako”

    “Nitashukuru sana” nilimwambia Gasana huku nikifurahi kisha nikawaaga

    wote na kutoka nje ya ofisi zile za msalaba mwekundu.

    Wakati nikiendesha gari kuelekea kule kwenye ile nyumba niliyomuacha

    Drel Fille mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani mwangu. Picha kub-

    wa iliyokuwa ikiumbika kichwani mwangu ni namna ya mambo ambavyo

    yangekuwa endapo hatua za haraka zisingechukuliwa katika kuyazuia map-

    induzi katika nchi hii.

    Ingawaje nilikuwa nimefanya jitihada za kupeleka taarifa kwa vyombo

    muhimu ambayo niliamini kuwa vingeweza kutoa msaada katika kuzima

    mapinduzi hayo hata hivyo bado nilihisi kuwa nilikuwa sijafanya jitihada

    kubwa sana kama nilivyodhani huku nikijiuliza, vipi taarifa zile nilizozitu-

    ma endapo zingechelewa ama kutofika kabisa kule nilipokusudia?. Swali hilo

    likayapeleka mawazo yangu mbele zaidi na kunifanya nijione kuwa bado ni-

    lihitajika kufanya jitihada zaidi katika kuokoa janga hili.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Katika jitihada za kuzidi kufikirimara nikakumbuka kuwa kulikuwa na

    vikosi vya kijeshi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vilivyokuwa

    nchini Rwanda vikijulikana kama UNAMIR yaani The United Nations As-

    sistance Mission for Rwandaambavyo vilikuwa vikisimamia utekelezaji wa

    makubaliano ya amani yaliyoazimiwa mkoani Arusha nchini Tanzania. Maaz-

    imio hayo yakipewa jina la Arusha Accordsmnamo tarehe 4 mwezi Agosti

    mwaka 1993 kati ya rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana na kiongozi wa

    kikundi cha kijeshi chaRPF ama Rwandese Patriotic Front, Meja Paul Kag-

    ame. Makubaliano hayo yakiitaka serikali ya rais Jevenal Habyarimana kukipa

    nafasi ya madaraka kikundi hicho cha kijeshi katika serikali yake ili kuleta

    usawa na amani ya kudumu.

    Kuvikumbuka vikosi hivyo vya UNAMIR vilivyopo nchini Rwanda hali

    hiyo ikanipa faraja kiasi kuwa angalau nilikuwa na sehemu ya kukimbilia na

    kwenda kutoa taarifa ya mpango wa mapinduzi haramu yaliyopangwa kufan-

    yika katika nchi hii.

    Niliona muda ulikuwa ukisonga sana huku bado nikiwa na mambo mengi ya

    kuyafanyia kazi kabla hakujapambazuka siku ya pili hivyo niliingia barabara

    ya mtaa wa Rèpublique nikiendesha gari kurudi nyumbani na wakati nikifanya

    hivyo mawazo yangu yalihamia kwa Drel Fille huku nikijaribu tena kuvuta

    picha hali ambayo angekuwa nayo baada ya kuniona ninakawia kurudi.



    #262

    SAA NANE KAMILI USIKU WAKATI INATIMIA nilikuwa nimebakisha

    umbali mfupi kuifikia ile nyumba niliyomuacha Drel Fille hata hivyo kwa

    kuwa nilishaanza kuhisi hali ya usalama ilikuwa tete nchini Rwanda niliamua

    kuegesha gari mbali na ile nyumba kisha nikashuka na kuanza kutembea kwa

    tahadhari na kwa mara nyingine tena nilijikuta nikizishukuru hisia zangu

    kwani nilikuwa nimebakisha hatua chahe tu kuifikia ile nyumba pale nilipoy-

    aona magari mawili ya kijeshi yakiwa yameegeshwa mbele ya nyumba ile.

    Nikachepuka na kujibanza nyuma ya mwembe mkubwa wenye giza nene

    uliokuwa jirani na nyumba ile. Taa za ndani za nyumba ile zilikuwa zime-

    washwa hivyo kutoka pale nilipokuwa nimejibanza niliweza kuwaona baadhi

    ya wanajeshi wakifanya upekuzi ndani ya nyumba ile. Moyo wangu ulishtuka

    sana na hasira zikanipanda kwani nilihisi kuwa wale wanajeshi huendawali-

    kuwa wamemkamata Drel Fille na hapo nikaanza kujilaumu kwa kuchelewa

    kurudi.

    Kwa kweli nilipandwa na hasira hata hivyo sikutaka kukubaliana na haraka

    ya mawazo yangu hivyo niliendelea kujibanza pale nyuma ya mwembe huku

    nikiendelea kutazama kwenye ile nyumba na wakati nikifanya hivyo niligun-

    dua kuwa kulikuwa na askari wengine waliokuwa wakirandaranda kuizunguka

    ile nyumba na wote walikuwa na bunduki zao mikononi.

    Nikiwa nimejibanza nyuma ya ule mwembe akili yangu ilianza kufanya

    kazi nikifikiria namna ya kumwokoa Drel Fille endapo angekuwa amekamat-

    wa na wale wanajeshi. Haukupita muda mrefu mara niliziona taa za ndani za

    ile nyumba zikizimwa kisha wale wanajeshi waliokuwa mle ndani walianza

    kutoka kupitia mlango wa mbele wa nyumba ile.

    Hali hiyo ikanifanya niyaache yale maficho yangu nyuma ya ule mwembe

    kisha nikanyata nikihamia kwenye maficho ya mti mwingine uliyokuwa jirani

    zaidi na ile nyumba, mahali ambapo ningeweza kuwaona vizuri wale watu.

    Wale wanajeshi walitoka ndani ya ile nyumba kisha wakaanza kuongozana

    wakielekea kwenye magari mawili ya kijeshi yaliyoegeshwa nje ya ile nyum-

    bana wakati wakifanya hivyo nilipata nafasi nzuri ya kuihesabu idadi yao.

    Walikuwa askari wa kijeshi ishirini na moja hata hivyo nilishtuka kuwa mi-

    ongoni mwao hapakuwa na hata mmoja aliyeelekea kufanana na mwanamke

    ambaye ningemdhania kuwa angekuwa Drel Fille. Muda mfupi uliyofuata

    magari yale yaliondoka.

    Niliendelea kujibanza pale nyuma ya mti ule hadi pale nilipojihakikishia

    kuwa hapakuwa na mtu mwingine aliyesaliaeneo lile na hapo ndiyo nikaanza

    kunyata kwa tahadhari nikielekea kwenye ile nyumba.

    Mlango wa nyuma wa nyumba ile ulikuwa wazi hivyo nilifanya jitihada

    kidogo kuusukuma kisha nikaingia ndani huku bastola yangu ikiwa mkononi

    kutuliza ukorofi wa namna yoyote ambao ungejitokeza.

    Mara baada ya kuingia mle ndani nilisimama kimya huku nikiupima utulivu

    wa mle ndani na hisia zangu zikaniambia kuwa hapakuwa na dalili za uwepo

    wa kiumbe hai yoyote mle ndani ingawaje hali hiyo haikunifanya nijiamini

    kisha nikaanza kunyata taratibu kuelekea sebuleni na nilipofika nikawasha taa.

    Vitu vyote vilikuwa vimechanguliwa na kutawanywa ovyo sakafuni. Kabati

    la vitabu lilikuwa limeangushwa chini nakupasuliwa vipandevipande. Vitabu

    vyote vilikuwa vimetawanywa sakafuni kuashiria kuwa msako na upekuzi wa

    kina ulikuwa umefanyika mle ndani. Makochi yalikuwa yamechanwachan-

    wa na foronya zake zikitawanyika sakafuni. Ile runinga ilikuwa imepasuli-

    wa vipandevipande, kalenda ilikuwa imechanwa na saa ya ukutani ilikuwa

    imevunjwa sakafuni ilimradi kila eneo lilikuwa limepekuliwa.

    Nilipoelekea chumbani nako hali ilikuwa vilevile kwani vitu vilikuwa vi

    metawanywa ovyo kila mahali na kwa kweli ulikuwa upekuzi wa kishenzi

    ulionipandisha hasira. Nilijaribu kuchunguza kamakulikuwa na viashiria vy-

    ovyote vya rabsha za kibinadamu na sikuona kiashiria chochote cha mikiki

    mikiki na hali hiyo iliniacha njia panda huku nikishindwa kuelewa kama wale

    watu walikuwa wamefanikiwa kumkamata Drel Fille au lah!

    Niliukumbuka ule uvamizi aliyofanyiwa Dr. Amanda Albro kule nyumbani

    kwakena hapo nikagundua haukutofautiana sana nahuu wa humu ndani hata

    kidogo na hapo roho iliniuma sana. Niliendelea kuzunguka mle ndani niki-

    tarajia kuona chochote cha maana hata hivyo sikufanikiwa hivyo nilizima taa

    za mle ndani na hatimaye kuiacha ile nyumba nikipitia mlango wa nyuma.

    Ijapokuwa nilitembea kwa utulivu na tahadhari ya hali ya juu wakati nikiia-

    cha ile nyumba nyuma yangu huku mara kwa mara nikigeuka kuitazama lakini

    akili yangu haikuwa na utulivu hata kidogo. Taswira za watu wote muhimu

    kwangu ambao nilikuwa nimepoteana nao tangu nilipoingia jijini Kigali zili-

    kuwa zikipita taratibu akilini mwangu na kunipa maradhi ya upweke.

    Drel Fille msichana niliyetokea kumpenda sana alikuwa ameacha jeraha

    kubwa moyoni mwangu na kila nilipokumbuka wakati tulipokuwa pamoja

    nilijihisi mnyonge sana na kwa mara ya kwanza nikajikuta nikiichukia safari

    yangu ya kijasusi nchini Rwanda. Hatimaye nikaapa kufanya chochote kulipa

    kisasi kamasehemu ya kumuenzi msichana huyo niliyetokea kumpenda isivyo

    kawaida.

    Nilirudi pale nilipoegesha gari nikafungua mlango na kuingia ndani na

    muda mfupi uliyofuata niliondoka eneo lile na wakati nikiendelea na safari

    nilijihisi kama niliyekuwa mgonjwa wa maradhi yasiyoeleweka.

    Nilikuwa na hisia kuwa pesa niliyobakiwa nayo ilikuwa mbioni kuisha na

    hali hiyo ilinipa tahadhari kubwa kuwa harakati zangu nazo zilikuwa mbioni

    kudorora kwani ni pesa ambayo ingeweza kunirahisishia pilika zangu. Fikra

    hizo zikatoa mwanya wa kuchipua kwa wazo jipya kichwani mwangu.

    Niliiacha barabara ya Mount Juruna kuingia upande wa kulia nikiifuata

    barabara ya Kiyovuna njiani nilipishana na magari machache ambayo yaliku-

    wa ni ya watu binafsi. Nilijaribu kwa kila hali kuyaweka kando mawazo juu

    ya Drel Fille kwani nilijua kuwa kuzidi kuyapa nafasi mawazo hayo yangeni-

    fanya nizidi kujisikia mnyonge. Kwa wakati huu mitaa mingi ya jiji la Kigali

    ilikuwa tulivunaisiyokuwa na msongamano wa aina yoyote na hali ya hewa

    ilikuwa tulivu na yenye baridi ya kiasi.

    Wakati nikiingia barabara ya mtaa wa Ihema nilipunguza mwendo baada ya

    kuyaona magari makubwa yakija mbele yangu. Nilikuwa na uzoefu mkubwa

    wa magari ya namna ile hivyo nilizima taa za gari haraka na kuegesha pembeni

    huku nikiyatazama magari yale kwa makini kupitia kioo cha mlangoni.

    Yalikuwa malori makubwa ya kijeshiaina ya Iveco, niliyaona vizuri mlori

    yale wakati yalipokuwa yakinipita na idadi yake yalikuwa kumi na nne na

    yote yalikuwa yamefunikwa nyuma kwa maturubai ya kijeshi katika namna ya

    kuzuia mtu yeyote kuona ndani yake.

    Niliyatazama maroli yale yalivyokuwa yakitokomea nyuma yangu huku ni-

    kihisi kutapika kwa hasira na hapo nikaegemea usukani wa gari huku mikono

    yangu ikitetemeka kwa hofu. Nilikuwa na hisia mbaya dhidi ya malori yale ya

    kijeshi yaliyonipita, hisia dhidi ya silaha ambazo zingetumika katika umwaga-

    ji damu mara tu baada ya mapinduzi yaliyopangwa kufanyika.

    Nikiwa nimeuinamia usukani wa gari nilifanya sala fupi nikimuomba Mun-

    gu aiepushie mbali nchi ya Rwanda dhidi ya janga la umwagaji damu lililoku-

    wa likielekea kuikumba nchi hii.

    Wakati nikiwasha injini ya gari na kuanza tena safari nilihisi machozi yali-

    kuwa yakishuka taratibu mashavuni mwangu. Nilishtuka sana kwani sikuwahi

    kukumbwa na hali ile hata siku moja katika harakati zangu za kijasusi, hata

    pale nilipolikaribia shimo la kifo. Niliyafuta machozi kwa mgongo wa kiganja

    changu na kuendelea na safari.

    Niliitazama saa yangu ya mkononi nikagundua kuwa ilikuwa ikielekea

    kutimia saa nane na nusu usiku na wakati huo nilikuwa nimeingia kwenye

    barabara ya mtaa wa IOua. Niliikumbuka vizuri barabara ile kwani ilikuwa ni

    ile barabara ambayo nilitekwa wakati ule nilipokuwa nikitoka nyumbani kwa

    Niyonkuru na kuelekea Hotel des Milles Colines.

    Ilikuwa barabara tulivu sana na yenye miti mirefu iliyotengeneza giza la

    kutisha ingawaje mimi binafsi sikuona kitu chochote cha kuniogopesha kwa

    wakati ule.

    Mara baada ya kuingia kwenye barabara ile nilizima taa za gari na kuende-

    sha gari taratibu huku macho yangu yakijitahidi kuizoea mandhari ile. Kum-

    bukumbu zangu bado zilikuwa timamu kichwani hivyo niliitazama miti ile mi-

    kubwa iliyokuwa kando ya barabara ile huku nikiichunguza vizuri mti mmoja

    baada ya mwingine kupitia dirishanina mwishowe nikauona ule mti niliokuwa

    nikiutafuta. Mti mkubwa aina ya mvule uliyokuwa pembeni ya kichaka hafifu

    na hapo nikaegesha gari kando ya barabara na kushuka.

    Nilikuwa nikipakumbuka vizuri mahali nilipoirushia pochi yangu ndogo ya

    mfukoni yaani wallet yenye vitambulisho vyangu vya kijasusi, kadi za benkina

    pesa kidogo. Nilienda eneo la chini ya mti ule mkubwanakuanza kupapasa-

    papasa ile sehemu nilipoirushia ile walletyangu lakini nilishangaa kutoiona

    na hapo nikaanza kuhisi huenda ingekuwa imeokotwa na mpita njia. Lakini

    nilipotuliana kufikiri vizuri nikakumbuka kuwa kulikuwa na vipindi vya mvua

    tangu wakati ule nilipotekwa na kupelekwa kule mapangoni hivyo kulikuwa

    na uwezekano mkubwa wa wallet ile kusombwa na maji ya mvua hizo. Dha-

    na hiyo ikanifanya niufuate mteremko hafifu wa mkondo wa maji uliyokuwa

    ukielekea sehemu ya chini ya eneo lile huku nikipapasa papasa chini na hati-

    maye nikaipata ile wallet ikiwa imenasa chini ya gogo.

    Ilikuwa ni wallet nzuri iliyotengenezwa kwa ngozi ya nyoka aina ya Black

    mamba isiyopitisha maji kwa urahisi hivyo nilipoifungua ndani nilikuta vitu

    vyangu vyote vikiwa salama kama hapo awalina hapo nikaitia mfukoni na

    kurudi kwenye gari na muda mfupi uliyofuata nilikuwa njiani kurudi Hotel

    des Milles Collines.



    NILIMKUTA MUTESI AKIWA HAJALALA ingawaje macho yale yalion

    esha uchovu wa kila namna. Sikuwa na shaka kuwa kurudi kwangu kulikuwa

    kumemletea faraja sana. Alikuwa amevua nguo zake zotena kubakiwa na ch-

    upi na sidiria. Nipoingia tu nilitazama juu ya meza ndogo iliyokuwa pembeni

    ya kitanda mle chumbani na hapo nikaona chupa kadhaa za pombe zilizokuwa

    tupu hivyo nikajua kuwa Mutesi alikuwa akinywa pombe tangu nilipomuacha

    peke yake mle ndani. Mara tu niliposimama Mutesi naye alisimama na kutem-

    bea kilevilevi akija kunikumbatia na hapo nikawahi kumshika kabla hajaan-

    guka chini na wakati nikifanya hivyo nikamuona akinionesha tabasamu lake

    la kilevi.

    “Ulikuwa wapi mpenzi?Mutesi aliniuliza huku akinikumbatia, nikam-

    pokonya chupa ya pombe aliyoishika mkononi na kuiweka pale mezani kisha

    nikamkokota na kwenda kumlaza kitandani.

    “Pumzika sasa inatosha mpenzi umekunywa sana pombe” nilimwambia

    Mutesi wakati nikimlaza kitandanina hapo akaangua kicheko hafifu cha kilevi.

    “Niache tu niendelee kunywa pombe Patrickkwani ni afadhali waniue niki-

    wa katika hali hii.Sitaki kuweka kumbukumbu yoyote mbaya kichwani mwan-

    gu. Sitaki kuiona damu ya ndugu zangu ikimwagika na sitaki kusikia sauti ya

    vilio vya uchungu vya ndugu zangu”

    Maneno ya Mutesi yalinishtua sanana nilipomtazama usoni ilikuwa vigu-

    mu sana kuamini kuwa maneno yale yalikuwa yakitoka kwenye kinywa chake.

    Hata hivyo sikusema nenona hapo nilimuona Mutesi alinitazama usoni kama

    mtu anayefikiria jambo fulani na kisha akageuka kutazama ukutani.

    Nilisimama huku nimejishika kiunoni nikiyatafakari yale maneno ya Mutesi

    na baadaye nikavua nguo zangu na kuelekea bafuni kuoga.

    Niliporudi kutoka bafuni nilimkuta Mutesi akiwa tayari amepitiwa na usin-

    gizi pale kitandani hivyonikamfunika vizuri kwa zile shuka za kitandani na ni-

    lipomaliza nikamshushia chandarua. Ingawa nilikuwa na uchovu wa harakati

    za kutwa nzima hata hivyo sikuwa na dalili zozote za usingizi machoni mwan-

    gu. Hisia juu ya Drel Fille, Dr. Amanda Albro, Jean Pierre Umugwaneza,

    Madame Marie Grace, Jerome Muganza, Dr. Francois Trezor na Niyonkuru

    pamoja na hali ya mambo yalivyokuwa yakienda hapa nchini Rwanda viliku-

    wa miongoni mwa vitu vilivyoninyima usingizi wa haraka.

    Nilienda kwenye jokofu lililokuwa mle chumbani nikachukua mzinga

    mmoja wa wiski aina ya Gordon na pakiti ya sigara aina ya Intore ambayo ni-

    liinunua njiani wakati nilipokuwa nikirudi pale hotelini kisha nikaenda kuketi

    kwenye kochi mle chumbani nikijipatia kinywaji taratibu na mliwazo wa siga-

    ra huku nikiendelea kutafakari kichwani.



    SAA KUMI NA MBILI NA NUSU ALFAJIRI wakati inatimia nilikuwa ta-

    yari nimeamka na kumaliza kujiandaa. Nilijihisi kupata nafuu ya msongo wa

    mawazo uliokuwa ukiniandama kwasiku mzima ya jana. Nilikuwa kiumbe

    kipya chenye mawazo mapya na fikra zenye uhai huku roho yangu ikiwa na

    dhana ya uthubutu.

    Nilimwamsha Mutesi aliyekuwa bado akiendelea kukoroma kitandani,

    akaamka kwa kujivutavuta na kwenda bafuni kuoga ili kuondoa uchovu.

    Wakati Mutesi akirudi kutoka kule bafuni nilimtazama na kugundua kuwa

    alikuwa akiona aibu kiasi kwani ile pombe aliyokunywa usiku ilikuwa imeis-

    ha kichwani. Mutesialipokuwa akijiandaa mimi nikautumia muda huo kupiga

    simu sehemu ya mapokezi nikiagiza kifungua kinywa.

    Saa moja kasoro asubuhi tulikuwa mezani mle chumbani tukipata kifungua

    kinywa kilicholetwa na mhudumu wa hoteli ile kikiwa kimeambatana na gaze-

    ti moja maarufu la nchini Rwanda.

    Wakati tukiendelea kupata taftahi nilifungua lile gazeti na kupitia vinywa

    vya habari. Ukurasa wa mbele ulikuwa na picha ya yule mtu niliyepambana

    naye jana usiku nje ya Kigali Casino akiwa amebebwa kwenye machela. Juu

    ya picha hiyo kulikuwa na maandishi makubwa ya lugha ya kifaransa yaliyo-

    someka kwa tafsiri ya lugha ya kiswahili “Kamanda wa jeshi la wananchi wa

    Rwanda auwawa na gari lake kutoweka. Polisi bado wanaendelea na msako

    wa msichana mmoja anayesadikika kuhusika na mauaji hayo’’. Niliitazama

    habari ile kwa makini kisha nikayahamishia macho yangu kwenye habari

    nyingine iliyokuwa chini ya gazeti lile.

    Ilikuwa habari picha iliyozionesha picha mbili, picha moja ya kwangu na

    nyingine ya Drel Fille na juu ya picha hizo kulikua na maandishi makubwa

    ya lugha ya kifaransa yenye tafsiri kwa lugha ya kiswahili“Watu hawa ni ha-

    tari kwa usalama wa nchi hivyo popote ukiwaona toa taarifa kwenye kituo

    chochote cha polisi cha jirani na wewe”. Nilitabasamu kidogo kwa kujiridhi

    sha kuwa angalau nilikuwa bado nikitafutwa mitaani na hapo nikalikunja lile

    gazeti na kulitia mfukoni bila kumwambia neno lolote Mutesi kwani taarifa

    zile huenda zingemshtua sana.

    Nilikuwa nimeagiza English breakfast kwani kilikuwani kifungua kinywa

    chenye taftahi nzito zaidi ya French breakfast ambayo ilikuwa na kifungua

    kinywa chepesi kwa kuzingatia kuwa jana usiku nililala bila ya kula. Ulikuwa

    ni mlo wa kiamsha kinywa wenye vipande vya mkate mzito, kahawa, juisi

    nzito ya parachichi, soseji, mayai na saladi.

    Wakati tukiendelea kupata kiamsha kinywa nilimuuliza Mutesi kama ali-

    kuwa akiufahamu mtaa wa Masaka ama Masaka Avenue na hapo akaniambia

    kuwa alikuwa akiufahamu vizuri mtaa huo kwani ulikuwa ni mtaa maarufu

    miongoni mwa mitaa iliyokuwa katika jiji la Kigali. Nilikuwa nimeamua

    kuanza harakati zangu katika nyumbanamba 16 ya mtaa huona kulikuwa na

    sababu kubwa iliyonipelekea kuanza harakati zangu katika nyumba hiyo, na

    sababu hiyo kubwa ilikuwa ni ukata wa pesa. Sikuwa na pesa ya kutosha ya

    kuendeleza harakati zangu na vilevile nilikuwa nimejitumbukiza kwenye ma-

    tumizi mengine ya gari ambalo lilihitaji mafuta ya kutosha kufanikisha mizu-

    nguko yangu, hivyo pesa ilihitajika.

    Tulimaliza kupata kiamsha kinywa na Mutesi kisha tukatoka na kufunga

    chumba na wakati tukikatisha eneo la mapokezi kuelekea nje ya hoteliile nili-

    fanya jitihada za kila namna za kuwaonesha watu kuwa mimi na Mutesi tu-

    likuwa mume na mke ingawaje nilifahamu kuwa Mutesi hakulifahamu hilo.

    Nilipenda tuonekane wapenzi tuliyoshibana mbele ya macho ya watu walio-

    tutazama kwanikwa kufanya viletungepunguza maswali vichwani mwa watu.

    Tulipofika nje ya hoteli ile tuliingia kwenye gari na safari ya kuutafuta mtaa

    wa Masaka ikaanza. Nilifurahi kuwa hapakuwa na gari lolote lililokuwa lik-

    itufungia mkia nyuma yetu wakati tulipokuwa tukiendelea na safari yetu. Tu-

    liingia mtaa huu tukatokea mtaa ule tukiendelea na safari. Mutesi alikuwa aki-

    nielekeza barabara na mimi nikawa nikiyafuata maelekezo yake kwa makini.

    Tulipoingia mtaa waRoi Baudouinnilipata wazo fulani baada ya kuliona jen-

    go la benki na hapo nikaegesha gari kwenye maegesho ya magari ya benki

    ile na kumtaka Mutesi anisubiri mle ndani ya gari. Nilikuwa na kadi mbili za

    benki ambazo zilikuwa na uwezo wa kuniruhusu kutoa pesa kwenye akaunti

    yangu kupitia benki yoyote iliyopo kwenye nchi za maziwa makuu.

    Zilikuwa ni kadi za benki ambazo hutumiwa na majasusi kutoa pesa kwenye

    benki mbalimbali zilizopo nje ya nchi husika ndani ya makubaliano maalumu

    ya nchi washirika. Kwa kuzingatia kuwa siku ile haikuwa miongoni mwa zile

    siku za kupokea mishahara kwa wafanyakazi hivyo sikukuta watu wengi ndani

    ya benki ile.

    Nilichagua foleni fupikisha nikapanga mstari na baada ya muda mfupi tu

    nilikuwa kwenye dirisha la mhudumu wa benki na kwa kuwa huduma yangu

    ilikuwa tofauti na watu wengine mhumudu yule mama wa kinywarwanda alin-

    itaka nisubiri kidogo kisha akatoka kwenye kile chumba chake cha huduma na

    kupotelea kwa nyuma huku akiwa na zile kadi zangu mbili za benki. Hivyo

    nikabaki nimeegemea pale dirishani nikimsubiri yule mama.

    Nikiwa naendelea kusubiri pale dirishani mara nilishangaa kumuona Mutesi

    akiingia mle ndani ya benki. Muonekano wake ukanitia mashaka na kunitahad-

    harisha kuwa mambo hayakuwa sawa. Nilimuona Mutesi akitazama huku na

    kule na hapo nikajisogeza mahali penye uwazi ili anione kwa urahisi na bila

    ya kufanya ishara yoyote Mutesi akaniona pale niliposimama na kunifuata.

    “Kuna nini?niliwahi kumuuliza Mutesi pindi aliponifikia.

    “Kuna wanaume wawili waliokuwa wanakufuatilia wakati ulipokuwa

    ikiingia humu ndani”

    “Wako wapi?nilimuuliza kwa shauku

    “Wamesimama pale nje mlangoni, ulipoingia tu humu ndani niliwaona

    wakipeana ishara fulani na hapo wakasimama pale mlangoni na kukuacha uin-

    gie”

    Nilimtazama Mutesi na kumuona kuwa alikuwa msichana mwerevu sana

    ingawaje hapo kabla sikuwa nimemtilia maanani sana.

    “Wakoje hao watu?

    “Kimo na maumbo yao yanaelekeana ingawa umewapita kidogo kwa ure-

    fu. Wamevaa nguo za kawaida tu za mashati na suruali na hawaelekei kuwa

    watu hatari lakini nimekuwa na wasiwasi sana pindi nilipowaona ndiyo maana

    nikaamua nije kukupasha habari”

    ‘‘Nashukuru sana Mutesi”

    Maelezo ya Mutesi yakanifanya nitabasamu kidogo kwanikwa haraka nili-

    tambua kuwa tathmini yake juu ya watu hao huenda haikuwa sahihi hata hivyo

    sikumpuuza kwani sikuwa na rafiki yoyote hapa nchini Rwanda hivyo mtu

    yeyote ambaye angeupoteza muda wake kunifuatilia niliamini kuwa asingeku-

    wa rafiki yangu. Nilimtazama tena Mutesi huku akili yangu ikianza kufanya

    kazi.

    “Unafahamu kuendesha gari vizuri?hatimaye nilimuuliza Mutesi

    “Ondoa shaka”

    “Endesha gari ukanisuburi nje ya duka la vinyago mtaa waRèpublique, si

    unapafahamu?

    “Sawa lakini usikawie sana kwani sijisikii salama sana kuwa peke yangu

    Patrick”

    “Nipe dakika ishirini”

    “Utanikuta” Mutesi aliniambia huku akiondoka taratibu

    “Kuwa mwangalifu” hatimaye nilimwambia wakati akiondoka na hapoakan-

    ionesha ishara kwa kichwa akionesha kunielewa. Nikamsindikiza kwa macho

    hadi pale alipopotea kwenye usawa wa macho yangu.

    “Patrick Zambi” sauti ya yule mama mfanyakazi wa benki ilinizindua na

    hapo nikageuka na kulisogelea tenalile dirisha dogo la huduma huku nikimta-

    zama mama yule kwa shauku.

    “Akaunti zako zote hazina pesa ndugu, tumeshindwa namna ya kukusaidia’’

    yule mama aliniambia huku akanipa zile kadi zangu za benki na bila kusita

    nikapenyeza mkono wangu na kuzipokea huku nikiwa siamini kabisa nili-

    chokisikia toka kwa yule mama, na bila shaka mama yule aliiona taharuki

    yangu kwani tangu niingie nchini Rwanda nilikuwa sijatumia kiasi chochote

    cha pesa toka kwenye akaunti zangu na vilevile nilikumbuka kuwa wakati ni-

    kiondoka jijini Dar es Salaam akaunti zangu zote zilikuwa na pesa ya kutosha.

    “Vipi hujaridhika na majibu yangu ndugu? yule mama mfanyakazi wa benki

    aliniuliza baada ya kuniona nimeganda kama sanamu.

    “Oh!hapana wala hakuna shida yoyote” nikamjibu kwa kiwewe huku ni-

    kiondoka eneo lile na wakati nikifanya vile nikawaona wanaume wawi-

    li wakiingia mle ndani ya benki na muonekano wao ulikuwa sawa na yale

    maelezo ya Mutesi.

    Mara tu watu wale walipoingia mle ndani niliwaona wakijigawa, mmoja

    akaenda upandewa kushoto na mwingine upande wa kulia na hapo wale watu

    wakaanza kusogea taratibu wakizikagua kwa siri nyuso za watu waliokuwa

    mle ndani. Kuona vile mimi nikawahi kujibanza nyuma ya nguzo moja kubwa

    na ndefu miongoni mwa nguzo mbili zilizoshikilia paa la jengo la benki ile.

    Nikiwa nimejibanza nyuma ya ile nguzo niliwatazama wale watu kwa jicho

    la wizi huku nikijihisi kuchanganyikiwa. Kulikuwa na kijana mmoja mdogo

    aliyeniona wakati nikijibanza nyuma ya ile nguzo na kuichomoa bastola yangu

    kutoka mafichoni. Nilimuona kijana yule akitaka kupiga yowe lakini niliwahi

    kumuonya kwa mtutu wa bastola yangu ambayo sasa nilikwisha ichomoa ku-

    toka mafichoni na kuikamata vema mkononi.

    Niligundua kuwa sikuwa na njia yoyote ya kujinasua mle ndani kutoka kwa

    wale watu isipokuwa kufanya shambulizi moja la kushtukiza lakini wakati

    huohuo nikiufikiria upinzani ambao ungejitokeza kupita askari walinzi wa

    benki ile pale ambapo wangeusikia mlio wa risasi zangu au majibishano ya

    risasi baina yangu na wale watu hatari waliongia mle ndani ya benki.

    Nikiwa bado nimejibanza nyuma ya ile nguzo nilimsubiri yule mtu hatari

    aliyekuwaakija upande wangu na alipobakisha hatua chache kunifikia nikam-

    fanyia shambulizi moja la nguvu na la kushtukiza kwa kuvuta kilimi cha

    bastola yangu na kuziruhusu risasi mbili kupekenya kifua chake na kuacha

    matundu mawili yanayovuja damu kwenye moyo wake.

    Ilikuwa shabaha nzuri sana kwani muda uleule nilimuona yule mtu akisom-

    bwa hewani kwa nguvu ya risasi na kutupwa sakafuni huku ile bastola aliy-

    oishikilia kwa hila mkononi mwake ikimponyoka na ilipoanguka chini risasi

    kadhaa zikafyatuka na kuchimba sakafuni na yule mtu akakata roho palepale.

    Kelele za risasi zile zikawa zimewashtua wale watu mle ndani na hapo vil-

    io na mayowe vikaanza kusikika. Watu wakaanza kukimbia ovyo huku kila

    mmoja akishika uelekeo wake hata hivyo mimi sikuwa miongoni mwao kwani

    bado niliendelea kujibanza nyuma ya ile nguzo nikimtazama kwa kificho yule

    mtu hatari mwingine aliyesalia.

    Nilimuona yule mtu akiwa amehamaki sana kama ambaye haamini kili-

    chomtokea mwenzake na wakati huo alikuwa ameitoa bastola yake toka ma-

    fichoni na kuishika vizuri mkononi bila kificho huku akijaribu kuchunguza

    kwa makini ni wapi zile risasi zilizommaliza mwenzie zilipotokea. Tukio hilo

    likanifanya nianzekuwaza kuwa huenda baada ya muda mfupi mtu yule an-

    geweza kuzitilia mashaka zile nguzo mbili kubwa mle ndani zilizoshikilia paa

    la benki na hali hiyo ikanifanya niiname chini kisha nikachepuka kwa siri na

    kwenda kujibanza nyuma ya meza kubwa iliyokuwa mle ndani.

    Muda uleule nikamuona yule mtu hatari akizisogelea zile nguzo lakini kabla

    hajazifikia akasita na kutazama upande wangu na hapo tukakutana macho kwa

    macho. Alipotaka kuinyanyua bastola yakeilianilenge akajikuta amechelewa

    kwani nilishajiandaa kwa tukio hilo hivyo haraka nikairuhusu risasi moja

    kuupasua mfupa wa bega kwenye ule mkono wake uliyoshika bastola na hapo

    ile bastola ikamponyoka mkononi huku akipiga yowe kali la taharuki. Nika-

    mchapa tena risasi mbili za magotini na bila upinzani wa namna yoyote yule

    mtu akaanguka chini na kupiga magoti kama anayeungama kwa paroko huku

    akiwa haamini macho yake. Yule mtu akabakiakinitazama kwa mshangao na

    pasipo kumchelewesha zaidinikavuta tena kilimi cha bastola yangu kuiruhusu

    risasi moja kufanya mjongeo wa nguvu. Risasi hiyo ikapenya kwenye paji lake

    usoni na kuufumua vibaya ubongo wake upande wa nyuma ya kichwa risasi

    hiyo ilikotokezea.

    Askari walinzi wa ile benki walikwishaingia mle ndani ya benki baada ya

    kuisikia ile milio ya risasi hivyo sikutaka kupoteza muda, nikairudisha bastola

    yangu mafichoni na kusimama toka nyuma ya ile meza nilikojificha na hapo

    nikaanza kutimua mbio na kujichanganya na watu wengine waliokuwa waki-

    kimbilia nje ya ile benkikwa hofu huku na mimi nikijidai kupiga mayowe.

    Nilipishana na baadhi ya wale askari pale mlangoni huku wakiwa na bun-

    duki zao mikononi hata hivyonilishukuru kuwa hakuna aliyenishtukia.Nilipo-

    toka nje ya ile benki nikavuka barabara na kuanza kutimua mbio nikielekea

    barabara ya mtaa wa pili huku nikiwa nimeongozana na watu wengine walio-

    kuwa wakitimua mbio kama mimi. Njiani nilikutana na gari moja aina ya Land

    Rover nyeupe iliyokuwa na askari wannesehemu ya nyuma na wote wakiwa

    na bunduki zao na hapo nikajua kuwa walikuwa wakielekea kuongeza nguvu

    kule benki.

    Nilipoingia mtaa wa tatu nilipunguza mwendo na hatimaye kutembea

    kabisa kama mtu mwenye hamsini zangu hata hivyo sikuacha kugeuka nyuma

    kutazama kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia nyendo zan-

    gu, sikumuona mtu yoyote na hali hiyo ikanifanya nitabasamu.





    #296

    NILIMKUTA MUTESI AKIWA ANANISUBIRI kwenye gari nje ya duka

    kubwa la vinyago mtaa Rèpubliquekama nilivyomuelekeza hata hivyo alikuwa

    ni mwenye wasiwasi mwingi. Nilipoitazama saa yangu mkononi nikagundua

    kuwa dakika kumi zilikuwa mbele ya muda wa makubaliano.

    “Vipi imekuwaje? Mutesi akaniuliza pindi nilipofungua mlango wa gari na

    kuingia ndani.

    “Nimewadhibiti vizuri ondoa shaka”

    “Nilianza kupatwa na wasiwasi nilipoona kuwa unakawia kuja, imekuwaje?

    “Wote wamekufa”

    “Wamekufa!...”

    “Endesha gari kuelekea Masaka Avenue, nyumba namba 16”

    Nilimwambia Mutesi aendeshe gari kwani sikutaka anirudishe nyuma kuja-

    dili juu ya tukio lile kwani ukurasa wake ulishafunikwa kwenye fikra zangu na

    badala yake nilihitaji kufunua kurasa nyingine haraka ili kuuhitimisha mkasa

    huu hatari wenye vimbwanga vya aina yake.

    Wakati tukiendelea na safari yale maneno ya yule mama mfanyakazi wa

    benki aliponiambia kuwa

    ‘ Akaunti zako zote hazina pesa ndugu, tumeshindwa namna ya kukusaidia’

    yalikuwa yakipenya kwenye fikra zangu na kutengeneza mjadala usiokuwa na

    mwisho.

    Nilikumbuka kuwa kabla ya kuanza safari yangu ya kijasusi kutoka jijini

    Dar es Salaamna kuja hapa jijini Kigali, Rwanda akaunti zangu zote ziliku-

    wa zimeingizwa pesa ya kutosha na idara yangu ya ujasusi ili kunirahisishia

    harakati zangu kwawakati wote ambao ningekuwa hapa nchini Rwanda.

    Hivyo jibu la yule mama lilikuwa limenichanganyasana na kwa mara nyingine

    nilianza kuhisi kuwa kulikuwa na mizengwe fulani iliyokuwa ikiendelea nyu-

    ma ya harakati zangu.

    Nikamkumbuka Brigedia Masaki Kambona, mkuu wa operesheni zangu za

    kijasusi na hapo nikameza funda kubwa la mate kwa hasira.

    “Hii ndiyo Masaka Avenue Patrick, sasa anza kuitazama hiyo nyumba nam-

    ba 16” sauti ya Mutesi iliyarudisha tena mawazo yangu mle ndani ya gari na

    hapo nikageuka na kuanza kuzitazama vizuri nyumba za mta ule.

    Ulikuwa ni mtaa wenye nyumba za kisasa na zilizojengwa katika mpangilio

    unaovutia.

    “Ile pale” Mutesi alikuwa wa kwanza kuiona nyumba tuliyokuwa tukiitafuta

    na hapo akaanza kupunguza mwendo wa gari.

    “Usisimame hapa endesha hadi mwisho wa barabara ya mtaa huu,nahitaji

    kuwa na hakika kwanza kuwa hakuna mtu anayetufuatilia”

    “Unaenda kufanya nini kwenye nyumba ile?

    “Nisubiri hapa nitatumia dakika chache tu” nilimwambia Mutesi huku ni-

    kilipuuza swali lake kishanikafungua mlango wa gari na kushuka na hapo

    nikaanza kurudi kule nyuma kwenye ile nyumba tuliyoipita.

    Wakati huu kulishapambazuka vizuri hivyo njiani nilipishana na watu wa-

    chache wakiwahi makazini. Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa dakika

    chache zilikuwa zimesalia kutimia saa tatu asubuhi. Ilikuwa ni rahisi sana kui-

    tambua nyumba namba 16 katika mtaa ule kwani ilikuwa nyumba ya kisasa

    sana pengine kupita nyumba nyingine zote za jirani lakini nilishukuru kuwa

    haikuwa na uzio.

    Ilikuwa ni ile nyumba niliyoelekezwa na Madame Marie Grace, mfanyakazi

    wa benki ya taifa ya Rwanda na mateka mwenzangu kule kwenye mapango

    ya Musanze muda mfupi kabla hajakata roho wakati tulipokuwa tukiyatoroka

    mapango yale.

    Wakati nikiifikia nyumba ile mawazo yangu yalijikuta yakimuwazia mume

    wa Madame Marie Grace, afisa wa jeshi wa kikundi cha RPF, Rwandese Pa-

    triotic Front kilichokuwa kikipigana msituni kuiondoa serikali ya rais Juvenal

    Habyarimana iliyokuwa ikisemekana kukandamiza maslahi ya watu wa kabila

    la kitutsi nchini Rwanda.

    Baada ya kufanya jitihada kidogo kitasa cha mlango wa mbele wa ile nyum-

    ba kilifyatuka na hapo nikausukuma ule mlango taratibu na kuingia ndani.

    Dalili zilinionesha kuwa hapakuwa na mtu yeyote mle ndani kwani vumbi kali

    lilikuwa limetapakaa kila mahali hivyo niliurudisha ule mlango nyuma yangu

    na kabla ya kupiga hatua nyingine mbele yangu nilisimama nikiupima utulivu

    wa mle ndani huku macho yangu yakisafiri kupeleleza mandhari.

    Sebule ilikuwa kubwa na yenye samani za kisasa yakiwemo makochi ma-

    zuri ya sofa, zulia la kupendeza sakafuni, rafu ya vitabu,seti moja ya runinga,

    sistimu ya muziki na meza kubwa ya kulia chakula yenye viti sita vilivyoizu-

    nguka meza ile katika ukumbi mdogo wa kulia chakula iliyokuwa pembeni

    ya sebule.

    Kulikuwa na picha kubwa iliyotundikwa ukutani ikimuonesha Madame

    Marie Grace, Meja Ciprian Ndukumana na mtoto wao Diane, wote wakiwa

    wamekumbatiana kwa furaha na picha hiyo ikanipa tumaini kuwa nilikuwa

    sijakosea nyumba. Niliita kidogo mle ndani nikitarajia kuwa kama kungekuwa

    na mtu yeyote mle ndani angekuja kunisikiliza na nilipoona kimya kinazidi

    nikaendelea na hatua iliyofuata.

    Nyumba ile ilikuwa na vyumba vitatu vikubwa vya kulala,sebule pana,u-

    kumbi mdogo wa kulia chakula, jiko, choo, bafu na stoo. Nilitumia muda

    mfupi tu kufanya upekuzi vyumbani. Chumba cha kwanza nilikigundua kuwa

    ndiyo alichokuwa akilala mtoto wao Diane kutokana na vitu nilivyovikuta mle

    ndani ambavyo vilielekea kufanana naye kwa namna moja au nyingine. Vitu

    kama kama nguo za kike za kitoto na viatu na nilipoendelea na upekuzi wangu

    zaidinikapata picha moja ya Diane katika sanduku la nguo aliyopiga na wana-

    funzi wenzake shuleni.

    Chumba cha pili sikuweza kukielewa vizuri kwani kilifaa kufananishwa na

    chumba cha wageni au kilichokuwa kikitumiwa na dada wa kazi kutokana na

    vitu vilivyokuwa mle ndani.

    Nilipoingia kwenye chumba kikubwa cha mwisho nilianza kuhisi harufu

    nzito ya uvundo ambayo kama siyo kujizuia ningeweza kutapika haraka. Il-

    ikuwa harufu ya uozo wa kitu fulani ambacho nilishindwa kukifahamu kwa

    haraka.Niliusukuma mlango wa chumba kile na nilipoingia ndani nikagun-

    dua kuwa kile kilikuwa ndiyo chumba kilichokuwa kikitumiwa na Madame

    Marie Grace na mumewe Meja Ciprian Ndikumana ama kwa lugha nyingine

    ningeweza kukiita Master Bedroom.

    Kilikuwa chumba kikubwa kupita vyote mle ndani chenye kitanda kipana

    cha futi sita kwa sita, zulia la kupendeza sakafuni, kabati la nguo la ukutani,

    meza ya kujipamba ama Dressing table, sistimu ndogo ya muziki na seti moja

    ya runinga. Cha ajabu kwangu ni kuwa vitu hivi vyote vilikuwa vimechanguli-

    wa ovyo na kutawanywa sakafuni katika namna ya upekuzi kama ule uliyofan-

    yika kule nyumbani kwa Dr. Amanda Albro na kwenye ile nyumba tuliyokuwa

    tukikaa mimi na Drel Fille na hapo nikajua kuwaule ulikuwa upekuzi ulio-

    fanywa na mtu au watu wa aina moja na tumaini la kupata kitu nilichokuwa

    nakikitafuta likaanza kufifia taratibu hata hivyo sikukata tamaa.

    Nilikuwa mtundu zaidi kugundua mfuko wa nailoni uliyofichwa nyuma

    ya tenki dogo la maji ya kusukumia uchafu lililokuwa kwenye maliwato ya

    chumba kile. Nilipoufungua mfuko ule ndani yake nikavikuta vitu nilivyoku-

    wa nikivihitaji, picha tatu za kifamilia lakini moja ikiwa na nyongeza ya msi-

    chana nisiyemfahamu, kitabu cha benki, cheti cha ndoa na hati ya nyumba.

    Sikuhitaji kitu kingine hivyo niliuchukua mfuko ule na kutoka nje ya kile

    chumba na wakati nikitoka nilijikuta nikipambana tena na ile harufu kali ya

    uvundo na hapo nikashawishika kuvipeleleza vile vyumba vilivyosalia vya

    choo, stoo na bafu.

    Sikuona kitu chochote katika chumba cha choo na stoo lakini nilipoufungua

    mlango wa bafu miguu yangu iliishiwa nguvu ghafla huku nikibana pua yan-

    gu kwa kiganja na kushindwa kuendelea na safari na haponikajikuta nikianza

    kuyafukuza mainzi makubwa yaliyoshtushwa na ugeni wangu.

    Maiti ya msichana ilikuwa imelala uchi sakafuni huku kichwa chake kiki-

    wa kimetenganishwa na kiwiliwili. Titi lake la kushoto lilikuwa limekatwa na

    kutupwa kwenye tundu la choo cha kukaa. Miguu yake ilikuwa imetanuliwa

    na hilo lilinijulisha kuwa msichana yule alikuwa amebakwa kinyama kabla ya

    kuuwawa.

    Baadhi ya maeneo ya mwili wake yalikuwa yameharibika vibaya kutokana

    na mwili wake kukaa siku nyingi tangu kuuwawa. Mabaki ya nguo na makadi-

    rio ya kimo chake vilinifanya nimfananishe na yule msichana niliyemuona

    kwenye ile picha ya kifamilia muda mfupi uliyopita.

    Dada wa kazi!...hisia zangu zilihitimisha hivyo na hapo nikajikuta nikitok-

    wa na machozi huku jitihada za kujizuia zikishindikana. Ilikuwa picha mbaya

    kabisa isiyopendeza kuitazama. Niliitazama maiti ile huku nikijisikia kiche-

    fuchefu na hasira. Damu nyingi ilikuwa imetapakaa sakafuni mle bafuni na juu

    ya dimbwi lile la damu niliiona chupi ya msichana yule ikielea.

    Niliishiwa na nguvu nikaegemea mlango huku machozi yakinitoka. Siku-

    weza tena kuitazama ile maiti hivyo nikatoka nje na kuufunga mlango wa kile

    chumba taratibu nikielekea nje ya nyumba ile.

    Nilimkuta Mutesi ananisubiri kwenye gari, sikutaka kumuonesha hali yoy-

    ote ya huzunina badala yake nikamwambia awashe gari na tuondoke eneo lile.

    Wakati tukiendelea na safari nilijitahidi kuitowesha taswira ya maiti ya yule

    msichana niliyemuacha kule bafuni kwa kuanzisha mazungumzo ya kawaida

    ambayo yangeniweka mbali na hisia mbaya. Mwishowe nilimtaka Mutesi

    aendeshe gari kuelekea ilipo shule ya wasichana yaSainte Anne Mariehuku

    nikimuuliza kama alikuwa akiifahamu shule hiyo. Mutesi akaniamba kuwa

    alikuwa akiifahamu hiyo shule kwani ilikuwani shule maarufu sana ya wasi-

    chana iliyokuwa ikimilikiwa na kanisa la Katoliki.

    Nilimueleza Mutesi kuwa tulikuwa tukienda kwenye shule hiyo kumchukua

    mwanafunzi aitwaye Diane hivyo mara baada ya kufika kwenye shule hiyo

    nilimtaka Mutesi ajidai kuwa yeye nindugu wa karibu wa msichana huyo na

    alikuwa amefika shuleni hapo kumchukua kwani mama yale alikuwa amezid-

    iwa na ugonjwa wa ghafla na alikuwa amepelekwa hospitali.

    Hoja yangu haikueleweka mapema kwa Mutesi hivyo alinibidi nimpe picha

    kamili ya mpango wangu huku nikitumia ushawishi wa hali ya juuna hapo

    akanielewa.

    __________

    SHULE YA SAINTE ANNE MARIE ilikuwa shule ya kisasa kabisa na yenye

    vigezo vyote vya kutoa elimu bora kama madarasa ya kisasa, ofisi za kutosha

    za walimu, maabara,viwanja bora vya michezo na mabweni.

    Tuliyakuta magari mawili yakiwa yameegeshwa nje ya shule ile katika eneo

    maalumu la maegesho, gari moja likiwa nila mkuu wa shule na jingine la

    paroko mwangalizi wa jimbo lile.

    Tulikuwa tayari tumeshakubaliana vizurina Mutesi katika kufanikisha

    mpango ule wa kumtorosha mtoto wa Madame Marie Grace katika shule ile

    hivyo tulipofika tu Mutesi alishuka kwenye gari na kuelekea kwenye jengo la

    utawala la shule ile.

    Sikutaka kuongozana naye kwani kwa kufanya hivyo tungeweza kutiliwa

    mashaka na hivyo mpango wote kuvurugika bila mafanikio. Nilikuwa nimem-

    pa Mutesi maelezo yote muhimu ambayo angeweza kuyatuma pale ambapo

    angekutana na maswali yenye utata hivyo nilibaki kwenye gari nikimsubiri

    na wakati huo nikapata nafasi nzuriya kuweza kuvichunguza vizuri vile vitu

    vilivyokuwa kwenye ule mfuko wa nailoni niliyouchukua kwenye ile nyumba

    ya Madame Marie Grace.

    __________

    NILIITAZAMA SAA YANGU YA MKONONI nikagundua kuwa dakika

    ishirini zilikuwa tayari zimetoweka tangu Mutesi aliponiacha na sikuona dalili

    zozote za yeye kurudi kwake na yule mtoto wa Madame Marie Grace na hapo

    nikaanza kuingiwa na wasiwasi.

    Muda wa nusu saa ulipokuwa mbioni kutimia wasiwasi ukazidi kunishika

    na hapo nikafyatua komea la mlango wa gari nikitaka nishuke na kuelekea

    kwenye lile jingo la utawala. Lakini kabla sijatimiza adhma yangu kupitia kioo

    cha ubavu wa gari nilimuona Mutesi akirudi huku ameongozana na msichana

    mdogo mwenye umri usiozidi miaka kumi na tano na nilipomchunguza nilim-

    tambua haraka kuwa alikuwa mtoto wa Madame Marie Grace kwani alikuwa

    amefanana sana na mama yake istoshe ile picha ya familia aliyopiga pamoja

    na wazazi wake bado ilikuwa kwenye kumbukumbu zangu.

    Niliendelea kumtazama msichana yule kupitia kioo cha ubavuni mwa gari

    na hapo huruma ikaniingia kiasi cha kutaka kunitoa machozi hata hivyo nili-

    jizuia kwani sikutaka kukutwa na hali ile.Nilipenda kuonekana kama dereva

    tu wa gari lile hivyo niliamua kujifanya dereva.

    Mutesi na Diane walipokaribia nilishuka kwenye gari na kuwafungulia

    mlango na wakati wakiingia kwenye gari Diane aliniamkia hata hivyo nilitam-

    bua kuwa kulikuwa na mashaka katika uso wake. Sikutaka kupoteza muda

    hivyo mara tu Mutesi na Diane walipoingia ndani ya gari nilifunga mlango

    wa gari nikazungua na kuinga upande wa dereva na hapo nikawasha gari na

    kuliondoa kwenye maegesho yale.

    Mutesi alikuja na kukaa kwenye siti ya pembeni yangu, Diane yeye akakaa

    nyuma na wakati tukiondoka eneo lile nililazimika kupunguza mwendo na

    sote tukawapungia mikono paroko na sister waliokuwa wametoka na kusima-

    ma nje ya jengo lile la utawala wa shule huku wakitupungia mikono kutuaga.

    Tukabadilishana tabasamu na vicheko vya kuigiza visivyo kuwa na maana

    yoyote kwangu na hapo nikakanyaga pedali ya mafuta kuongeza mwendo ku-

    lipita geti la kutokea nje la seminari ile ya wasichana.

    “Mbona mmechelewa sana?nilimuuliza Mutesi aliyekuwa pembeni yangu

    huku nikiwa na hakika kuwa Diane alikuwa hafuatilii maongezi yetu.

    “Walitaka uthibitisho hivyo nilitumia jitahadaza ziada katika kuwashawishi”

    “Diane hakukutilia mashaka?

    “Ilinibidi nitumie utundu wa maelezo yako kumuondolea wasiwasi huku

    nikijidai kuwa mimi ni ndugu wa mama yake niliyekuwanje ya nchi na niliku-

    wa nimerudi ghafla baada ya kupigiwa simu kuwa dada yangu ambaye ndiyo

    mama yake Diane anaumwa”

    “Umefanya vizuri sana Mutesi” nilimwambia Mutesi huku nikikunja kona

    kuingia mtaa mwingine na wakati huo nikipiga akili ya kumwingilia Diane ili

    asiweze kuleta matata mbele ya safari.

    Tulipokuwa tumefika mbali nilitafuta maegezo mazuri yenye utulivu kando

    ya barabara na hapo nikaegesha gari na kuanza kumsimulia Diane ukweli wa

    mambo ulivyokuwa, nikianza kumsimulia yote yaliyotokea tangu nilipokutana

    namama yake kule mapangoni hadi wakati huu.

    Nilimueleza Diane kuwa mimi nilikuwa mpelelezi kutoka nchini Tanzania

    na nilikuwa nimeenda kumchukua kule shuleni kwa lengo la kumsaidia hivyo

    hakutakiwa kuwa na hofu yoyote na mimi wala Mutesi kwani ni mama yak-

    endiye aliyenitaka nifanye vile na baadaye nilimvalisha Diane kile kidani cha

    baba yake yaani Meja Ciprian Ndikumana nilichokichukua kule hospitali.

    Katika mazingira kama yale nilifahamu kuwa ni ukweli tu ambao ungeweze

    kunisaidia katika kutengeneza msimamo wa urafiki kati yangu mimi na Diane.

    Baada ya kutumia ushawishi wa hali ya juu hatimaye Dianealinielewa vizuri

    ingawaje alilia sana baada ya kumpa taarifa za kifo cha mama na baba yake.

    Mutesi akambembeleza sana Diane na kwa kweli hali ile ilinitia huzuni sana

    nabaadaye tuliendelea na safari yetu.

    Tulirudi Hotel des Milles Collines tukaelekea chumbani ambapo tulipata

    mlo wa pamoja yaani mimi, Diane na Mutesi huku nikiendelea kumuweka

    Diane sawa na ilipofika mchana niliwaaga Mutesi na Diane na kuwaacha mle

    chumbani nikiwaahidi kurudi baadaye.



    NILIEGESHA GARI KANDO YA BARABARA ya Avenue de la Justice mk-

    abala na benki ya taifa ya Rwanda kisha nikavuka barabara kuelekea ndani ya

    benki hiyo. Kulikuwa na watu wengi ndani ya benki ile na jambo hilo lilinifu-

    rahisha kwani uwepo wa watu wachache ungewapelekea kuyavuta macho yao

    kwangu. Ilikuwa rahisi sana kuitambua ofisi ya meneja wa benki ile kutokana

    na kibao kidogo kilichoandikwa wadhifa wake kilichokuwa kimetundikwa nje

    kwenye mlango wa ofisi yake.

    Bila kupewa ruhusu niliusukuma mlango wa ofisi ile na kuingia ndani, mzee

    wa makamo mwenye umri wa miaka sitini na ushei, mfupi na mnene alikuwa

    ameketi nyuma ya meza kubwa yenye mafaili mengi na bila shaka ugeni wan-

    gu ulimshtua sana hivyo akaacha kuandika maelezo fulani kwenye kitabu kili-

    chokuwa mezani mbele yake na hapo akainua macho yake kunitazama huku

    alama ya mshangao ikiumbika usoni mwake.

    “Subiri nje ndugu huu si muda wa kuhudumia wateja, hujui utaratibu? mzee

    yule alifoka huku akionekana kuutumia vizuri wadhifa wake kama meneja wa

    benki.

    Sikurudi nyuma badala yake nikafunga ule mlango wa ofisi nyuma yangu

    kisha nikavuta kiti na kuketi mbele ya ile meza yake. Yule mzee akabaki aki-

    nitazama kwa mshangao halafu nikamuona akinyanyua mkonga wa simu ya

    mezani iliyokuwa juu ya meza yake na kuanza kubofya tarakimu falani. Nika-

    jua alikuwa akiomba msaadawa usalama na hapo nikatoa bastola yangu yenye

    kiwambo cha kuzuia sauti na kumuashiria kuwa asitishe alichokuwa akitaka

    kukifanya. Taharuki ikiwa imemnasa mzee yule akaurudisha mkonga wa simu

    mahala pake na kutulia akinitazama.

    “Unashida gani? hatimaye aliniuliza kwa utulivu na hapo nikamtupia kile

    kitabu cha benki cha Madame Marie Grace mezani kwake.

    “Unamfahamu huyu mama? nilimuuliza mzee yule huku nikimuonesha pi-

    cha iliyokuwa kwenye kile kitabu cha benki.

    “Namfahamu, ni mmoja wa wafanyakazi wangu” yule mzee akanijibu baa-

    da ya kuiona ile picha kwenye kile kitabu cha benki.

    “Ana muda gani hajafika kazini?

    “Hiyo si kazi yangu” yule mzee akanijibu kwa jeuri na kulikuwa na namna

    iliyonifanya nimuone kuwa hata yeye alikuwa miongoni mwa wafuasi wa Ka-

    nali Bosco Rutaganda.

    “Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa huwa huna utaratibu wa kuwajulia hali

    wafanyakazi wako pale unapowaona kuwa hawaji kazini?

    “Hiyo si kazi yangu nabadala yake ni wao ndiyowanapaswa kunipa taarifa

    mimi kama kuna tatizo lolote”

    “Madame Marie Grace ameuwawa na kwa mujibu wa maelezo aliyonipa

    ni kuwa hana mrithi wa mali zake aliye hai na amenipa jukumu hilo mimi

    kabla ya kufikwa na umauti. Unaweza ukadhani ni nini kilichopelekea umauti

    wake? lilikuwa swali la mtego nikitaka kuzipima hisia za mzee yule na tabia

    aliyoionesha ikaniletea majibu niliyoyahitaji kwani nilimuona akiangua kiche-

    ko cha dharau, kicheko kilichonifanya nihisi kitu chenye ncha kali kilikuwa

    kikipenya taratibu kwenye moyo wangu na kunipelekea maumivu makali ya

    hisia hata hivyo nilijitahidi kuzimudu hisia zangu.

    “Mimi ni meneja wa benki na siyo polisi, siwezi kufanya kazi mbili kwa wa-

    kati mmoja, hiyo ni kazi ya polisi na ninakutahadharisha kijana kuwa usijiingi-

    ze kwenye mambo yasiyokuhusu. Ninamfahamuvizuri mume wake na ni yeye

    ndiye mwenye dhamana ya kurithi mali za mkewe na siyo mtu mwingine”

    “Nahitaji pesa yote iliyopo kwenye akaunti yake”niliongea kwa utulivu

    huku nikikipuuza kicheko chake.

    “Hiyo haiwezekani kwani taratibu za kibenki haziruhusu kufanya hivyo,

    acha njaa zako za kipumbavukijana. Tunamuhitaji mume wake na huyo ndiye

    mlengwa wetu”

    “Una maana gani kusema hivyo, wewe na wenzako akina nani mnaomuhita-

    ji huyo mume wake?

    “Ndiyo maana nikakwambia kuwa mambo haya hayakuhusu Luteni ni bora

    ukaangalia namna ya kuinusuru roho yako kwa kurudi nchini kwako salama

    ingawaje sidhani kama hata hilo litafanikiwa kwa sasa”maneno ya meneja

    yule wa benki yakanifanya nishikwe na butwaa kwani sikuwa nimefikiria

    kuwa hata huyu meneja wa benki angekuwa na taarifa zangu. Hasira zikanis-

    hika nikasimama na kumzaba makofi ya nguvu yule mzee.

    “Fanya haraka kwani nazihitaji hazo pesa sasa hivi”nilimwambia kwa hasira

    “Unajidanganya Luteni huwezi kufanikiwa mpango wako,watu wetu ni ma-

    kini sana na watakutia mikononi kabla hujafika mbali”yule mzee aliongea kwa

    kejeli na hapo nikafyatua risasi moja kwenye paja lake, akapiga yowe kali

    hata hivyo risasi ile haikusikika kwani bastola yanguilikuwa na kiwambo cha

    kuzuia sauti.

    “Nitaendelea kwenye mguu mwingine kama utaendelea kushikilia msi-

    mamo wako”nilimtahadharisha na aliponiona ninaihamishia bastola yangu

    kwenye mguu wake mwingine akanisihi nimuache.

    “Nitakupatia pesa yote tafadhali nakuomba uniache”alilalama kwa maumi

    vu.

    “Fanya haraka vinginevyo nitalichakaza vibaya tumbo lako”

    Yule mzee alinyanyua mkonga wa simu akabofya tarakimu fulani na muda

    mfupi uliofuata simu ile ilikuwa hewani akiongea na mhasibu wa benki ile. Ni-

    likuwa makini kufuatilia alichokuwa akikizungumza na alipomaliza kuongea

    akaurudisha ule mkonga wa simu mahala pake na kisha kunitazama

    “Analeta sasa hivi” akaniambia huku akipambana na yale maumivu ya jera-

    ha la risasi kwenye mguu wake.

    “Sikiliza,wakati atakapoleta hizo pesa usioneshe kuwa kuna hali yoyote to-

    fauti humu ndani vinginevyo wote mtapoteza maisha, umenielewa?

    “Sawa” yule mzee alinijibu na hapo nikavuta kiti na kuketi vizuri mbele

    ya ile meza yake ya ofisini kama mteja halali wa benki ile na wakati huo

    yule mzee alikuwa akitetemeka kwa hofu huku damu nyingi ikiendelea kutoka

    kwenye lile jeraha la risasi mguuni mwake.

    “Wenzako wako wapi?nilimuuliza

    “Sifahamu”

    “Kwa hiyo mliamua kumuua Madame Marie Grace baada ya kumkosa

    mume wake, Meja Ciprian Ndikumana, sasa hiyo imewasaidia nini? nilim-

    uuliza yule mzee wakati tulipokuwa tukiendelea kumsubiri yule mhasibu wa

    benki alete pesa.

    “Sijui unazungumza nini, mimi sijamuua mtu yeyote” yule mzee aling’aka

    “Wenzako je?

    “Wenzangu akina nani?

    “Interahamwe”

    “Nani aliyekupa taarifa hizo? nilimuona yule mzee ameshikwa na hofu sana

    huku jasho likianza kumtoka.

    “Hakuna wa kunipa taarifa mimi huwa nazitafuta mwenyewe. Hebu niam-

    bie nini hasa kiini cha mapinduzi mliyoyapanga”

    “Hii ni nchi yetu na chochote tutakachokifanya ni kwa maslahi yetu, sisi ni

    jamii ya wengi iliyodhulumiwa haki na kukandamizana watu wachache wana-

    ohodhi madaraka makubwa ya nchi hii. Wewe hufahamu chochote kwa sababu

    ni mgeni katika nchi hii unayeingilia tu mambo kwa kujitafutia umaarufu”

    “Hiyo jamii ya wengi ni ipi na hao watu wachache ni akina nani? nilimuuli-

    za huku nikitabasamu kwa kejeli.

    “Wahutu tulio wengi tunanyanyaswa na kunyimwa nafasi za juu kwenye

    uongozi wa serikali ya nchi hii, wengi wetu ni maskini wasio na elimu ya ku-

    tosha na wakulima wasiokuwa na uelekeo mzuri wa maisha. Watutsi ni wach-

    ache sana katika nchi hii na wamejipatia madaraka na nafasi za juu serikalini,

    wengi ni wasomi na wenye maisha mazuri kwa hiyo hakuna usawa na sisi

    ndiyo tunaotaabika”

    “Kwa hiyo hicho ndiyo kiini cha mapinduzi yenu? nilimuuliza yule mzee

    hata hivyo hakunijibu hivyonikaendelea kuongea

    “Nani aliyewakataza msiende shule?,nani aliyewazuia msishike nyadhifa za

    juu serikalini kama mna elimu ya kutosha?, kwa nini msiielimishe kwanza

    jamii yenu ili ipate hizo nyadhifa za juu mnazozitaka serikalini?. Unaoneka

    na ni mtu mwenye busara nyingi na mawazo ya maana lakini sivyo ulivyo.

    Elimu na dini zililetwa na wakoloni sasa kwa nini vitu hivi vitugawe waafrika

    na kutengeneza chuki isiyo na sababu miongoni mwetu?. Udini au ukabila

    una athari gani katika mfumo wa maisha yako?, vipi leo ungezaliwa mzungu,

    mwarabu au mhindi na si mhutuwala mtutsi, ungejihalalisha vipi?, hivikwa

    nini sisi waafrika wengi wetu bado ni watumwa wa ki-fikra?, Utakapomuua

    jirani yako mtutsi wewe mhutu unayejiona upo salama utaishi kwa miaka min-

    gapi hapa duniani?.

    Nilikuwa nataka kuendelea kuongea pale nilipokatishwa na kelele za mtu

    aliyeusukuma mlango wa kuingia mle ndani na hapo nikageuka kumtazama.

    Alikuwa mhasibu wa ile benki, kijana mwenye umri unaoelekeana na wangu

    na alikuwa amebeba mfuko mkubwa wa kaki wenye nembo ya benki ile na

    hapo nikajua kuwa alikuwa amebeba zile pesa alizoagizwa na bosi wake.

    Kijana yule alipoingia akanisalimiavizurina hapo nikajua kuwa alikuwa

    hafahamu chochote kinachoendelea mle ndani. Nilipomtazama yule menejawa

    benki nikamuona kuwa alikuwa amezingatia vizuri lile onyo langu na nili-

    chokiona usoni mwake lilikuwa tabasamu la furaha ya kujilazimisha.

    “Samahani sana kwa kuchelewa mzee”yule kijana akamwambia bosi wake

    “Usijali, nashukuru, unaweza kwenda tu” meneja wa benki alimwambia

    yule kijana na hapo yule kijana akafungua mlango na kutoka akituacha wawili

    mle ndani na muda uleule nikauchukuwa ule mfuko wa pesa.

    “Hizo ndiyo pesa ulizokuwa ukizihitaji Luteni, ukipenda unaweza kuzihesa-

    bu kwa hakika zaidi”yule mzee aliniambia na hapo nikaufungua ule mfuko na

    kuchungulia ndani. Zilikuwa pesa nyingi sanaza kinyarwanda, mpya na zilizo-

    fungwa katika vibunda tofauti. Sikuwa na muda wa kuzihesabu badala yake

    nilizichunguzachunguza zile pesa na nilipoyahamisha macho yangu kumta-

    zama yule mzee nikashangaa kujikuta nikitazamana na mdomo wa bastola

    mikononi mwake.

    “Huendi kokote Luteni weka hizo pesa mezani” sauti ya yule mzee ilinionya

    huku mikono yake iliyoshika bastola ikitetemeka. Sikuwa na namna hivyo

    nikauweka mezani ule mfuko wa pesa taratibu huku nikijilaumu tena kwa ku-

    tokuwa makini.

    “Kwa hiyo mapinduzi yenu yanaanzia kwangu? nilimuuliza yule mzee huku

    nikiitazama mitetemo ya mkono wake uliyoshika bastola.

    “Geuka nyuma” yule mzee alifokana sikuwa na namna ya kukaidi amri ile

    kwani mitetemo ya mikono ya yule mzee ilinionya kuwa muda wowote in-

    geweza kuruhusu risasi kwenye ile bastola hivyo niligeuka nyuma taratibu

    huku nikijihisi kuzidiwa ujanja kirahisi. Lakini ghafla wakati nikifanya vile

    nilishangaa kuuona mlango waile ofisi ya meneja wa benki ukifunguliwa kwa

    kasi. Sikutaka kusubiri kuonani nini ambacho kingefuatia hivyo nikawahi ku-

    jitupa chini na muda huohuo nikasikia mlio wa risasi zikifyatuliwa sambamba

    na sauti ya yule mzee meneja wa benki akipiga mayowe kali.

    Nikageuka haraka kumtazama yule mzee pale kwenye kile kiti chake nyuma

    ya meza ile ya ofisini na hapo nikashikwa na taharuki. Kichwa chake kiliku-

    wa kimefumuliwa vibaya na risasi, ubongo wake ulikuwa umerushwa na kut

    awanywa ovyo ukutani, kiwiliwili chake kilikuwa kikibembea taratibu kutoka

    upande huu na kwenda upande ule kwenye kiti chake cha ofisini.Nilipogeuka

    kutazama kule mlangoni hapo nikashikwa na mshangao baada ya kumuona

    Drel Fille.

    “Polesana Luteni, pole sana mpenzi wangu, simama twende zetu watakuua

    hawa washenzi”

    “Drel… ni wewe? nilimuuliza Drel Fille kwa kiwewe.

    “Ni mimi mpenzi, tuondoke haraka kwani sehemu hii si salama, wame-

    wasambaza watu wao kila kona ya nchi hii kutusaka”

    “Drel oh!my God... ulikuwa wapi mpenzi wangu? oh!...nashukuru sana”

    “Twende mpenzi hapa siyo mahali pa kuzungumzia hayo”

    Nilisimama haraka nikauchukua ule mfuko wenye pesa pale mezani kisha

    nikasimama nikiitazama maiti ya yule mzee meneja wa benki iliyokuwa bado

    ikibembea kwenye kile kiti huku nikimsikitikia halafu nikasogea na kuichukua

    ile bastola yake mkononi.

    Tulipotoka nje ya ile ofisi ya menejawa benki nikafahamu kuwa wale watu

    mle ndani ya benki walikuwahawajashtukia kilichokuwa kinaendelea kwenye

    ile ofisi ya meneja wa benki hivyo kwa utulivu tukakatisha katikati ya mson-

    gamano ule wa watu mle ndani tukielekea nje lakini wakati huohuo kila mmo-

    ja akiwa macho kuzitazama nyendo za watu waliokuwa eneo lile.

    Tulivuka barabara na kuelekea nilipoegesha lile gari na muda mfupi baa-

    daye tulikuwa mitaani mbali na lile jengo la benki ya taifa ya Rwanda.

    “Drel... ulikuwa wapi mpenzi wangu? niligeuka na kumuuliza Drel Fille

    wakati tukiendelea na safari.

    “Nilijificha kwenye nyumba moja ya kulala wageni ya kichochoroni”

    “Mbona hukuendelea kunisubiri kwenye ile nyumba jana usiku japo nili-

    chelewa?

    “Nilipomaliza kuandika ripoti yangu ya ki-jasusi kwa mkuu wangu wa idara

    niliamua nikaitume posta huku nikiwa na hakika kuwa ningewahi kurudi kabla

    yako. Nilifanikiwa vizuri kuituma ile ripoti katika ofisi moja ya posta iliyopo

    mjinikati na kisha kurudi nyumbani lakini wakati nilipokuwa nikiikaribia ile

    nyumba nilishtuka kuyaona magari mawili ya kijeshi yakiwa yameegeshwa

    nje ya nyumba ile na hapo nikajua mambo yalikwisha haribika hivyo nikapo-

    telea mitaani”

    “Hukutaka kufuatilia kama wamenikamata au lah?

    “Nilijua kuwa upo hai tu kwani kwa muda ule wa jana usiku wakati narudi

    nyumbani nilijua kuwa ulikuwa bado hujarudi na hili gari ni la nani?

    Nilianza kumuelezea Drel Fille mambo yote yaliyojili tangu siku ile ya jana

    tulivyoachana, nikamueleza nilivyoenda Kigali Casino kuonana na Mutesi pa-

    moja na mkasa wote ulionikuta kule Kigali Casino. Nikaendelea kumueleza

    Mutesi namna nilivyompata Diane, yule mtoto wa Madame Marie Grace kule

    shule ya Sainte Anne Marie na ile maiti ya yule msichana aliyeuwawa kule

    kwenye ile nyumba ya Madame Marie Grace na mwishowe nikamuelezea

    Mutesinamna nilivyofika pale benki kuchukua pesa ya Madame Marie Grace.

    “Ulijuaje kama niko pale? hatimaye nilimuuliza Drel Fille

    “Ni kama bahati tu, unajua mimi nilienda pale benki kushukua pesa kwenye

    akaunti yangu baada ya kuona nilikuwa naelekea kuishiwa sasa nilipokuwa

    kwenye utaratibu huo ndiyo nikakuona ukiingia mle ndani na kisha nikakuona

    ukielekea kwenye ile ofisi ya meneja wa benki.

    Nilimaliza kuhudumiwa nikawa nakusibiri lakini nilishangaa kukuona un-

    akawia na hapo nikaanza kushikwa na wasiwasi. Kwanza nilimuona kijana

    mmoja akiingia kwenye ile ofisi ya meneja wa benki muda mfupi baada ya

    wewe kuingia mle ndanina hata yule kijana alipotoka wewe bado ulibaki mle

    ndani na hilo likanizidishia wasiwasi hivyo nikaona nikufatilie huku nikiwa-

    za kuwa huenda ulikuwa umekumbana na kigingi na ndiyo nikakukuta tayari

    umedhibitiwa na yule bwege”

    “Duh! hapo kweli nimeyakubali mambo yako, nakushukuru sana mpenzi

    kwa kuyaokoa tena maisha yangu na zawadi pekee nitakayokupa ni mtoto,

    tena mtoto mzuri wa kike anayefanana na mama yake hadi nywele” nilimtania

    Drel Fille huku nikiangua kicheko hafifu.

    “Siyo siri nina hamu sana na huyo mtoto mpenzi, mh! sasa baba mpelelezi

    na mama naye mpelelezi sijui huyo mtoto wetu atakuaje? Drel Fille akache-

    ka na wakati tukiendelea na maongezi nilichukua ile bahasha niliyopewa na

    Mutesi na kumpa Drel Fille ayasome maelezo yaliyokuwa kwenye ile karatasi

    ya ndani.

    “Mungu wangu…ni leo usiku?Drel Fille akang’aka kwa taharuki baada ya

    kumaliza kusoma yale maelezo kwenye ile karatasi.

    “Ni lazima tuzuie tukio hili vinginevyo kutakuwa na umwagaji damu mkub-

    wawa wa kutisha. Vipi tukienda kumuona mkuuwa vikosi vya ulinzi wa amani

    vya umoja wa mataifa vilivyopo hapa Rwanda UNAMIR au kiongozi yeyote

    mkubwa wa serikali atakayeweza kuyazuia mapinduzi haya?

    “Ni wazo zuri la kumuona huyo kiongozi waUNAMIR lakini nina mashaka

    na kuwaona viongozi wa serikali ya hapa Rwanda kwani ni lazima kwanza

    tulijue kabila lake vinginevyo tunaweza kupeleka taarifa kwa watu wanaotut-

    afuta na kuyashabikia mapinduzi hayo”

    “Mh! hapo kweli ndiyo ugumu ulipo” niliongea huku nikifikiria njia

    nyingine mbadalana wakati huo nilikuwa nikijunja kona kuingia barabara ya

    mtaa mwingine.

    “Tunaelekea wapi? Drel Fille akaniuliza

    “Hatuwezi kutembea na hizi pesa zote ni hatari hivyo nataka kuziweka

    kwenye akaunti yangu ya sirina nitazitoa wakati nitakaporudi jijini Dar es Sa-

    laam”

    “Nimeamua twende wote Dar es Salaam, nataka niache hii kazi na kuishi na

    wewe kama mume wangu, naomba uniahidi tu mpenzi”

    “Nikuahidi nini mpenzi?

    “Kuwa tangu sasa mimini mke wako wa kufa na kuzikana Venus” Drel Fille

    aliongea huku akitabasamu.

    “Nakuahidi mpenzi ondoa shaka, wewe mwenyewe si unajua kuwa bila

    wewe hata hii kazi haiendi vizuri” nilimwambia Drel Fille huku nikilifurahia

    wazo lake na tulipotazamana kila mmoja akaonesha hisia za mapenzi kwa

    mwenzake.

    __________

    NILIEGESHA GARI NJE YA TAWI MOJA LA BENKI ya eneo la maziwa

    makuu ambayo makao yake makuu yalikuwa jijini Dar es Salaam. Ni kati-

    ka benki ile ndiyo nilikuwa na akaunti yangu hivyo nikauchukua ule mfuko

    wenye pesa, nikapunguza vibunda vichache na kuviacha mle kwenye gari ki-

    sha nikashuka na ule mfuko nikielekea ndani ya ile benki. Kwa kuwa hakuku-

    wa na foleni kubwa sikukawia,muda mfupi baadaye nilirudi nikiwa nimefani-

    kiwa kuziweka zile pesa kwenye akaunti yangu.

    Ilikuwa ikielekea kutimia saa tisa alasiri hivyo niliendesha gari kuelekea

    Hotel des Mille Collines mahali ambapo tungeweza kupanga mkakati wa

    namna ya kuumalizia mkasa huu wa kutisha lakini wakati huo nikiwa tayari

    nimemtahadharisha Drel Fille dhidi ya Mutesi ili asije akaona wivu. Nilifurahi

    kuwakuta Mutesi na Diane wakiwa salama, nikawatambulisha kwa Drel Fille

    na maongezi mengine yakafuata.



    NDANI YA MUDA WA MASAA MAWILI tulikuwa tumefanikiwa kuyafikia

    maeneo yote muhimu yaliyokuwa ndani ya ratiba yetu ingawaje mafanikio

    tuliyoyapata hayakuwa ya kuridhisha. Baada ya kutoka kule Hotel des Milles

    Collines tulikuwa tumekubaliana na Drel Fille kuwa twende kwanza kule

    nyumbani kwa Niyonkuru, msichana aliyekuwa mpenzi wa marehemu Tobias

    Moyo lakini tulichokutana nacho kule kwenye ile nyumba kilituacha na si-

    manzi isiyoelezeka.

    Ilikuwa ni baada ya kugonga mlango wa nyumba ile kwa muda mrefu na ku-

    tojibiwa tukaamua kuingia ndani kwa mbinu zetu na baada ya kufanya upekuzi

    wa kina tukawa tumefanikiwa kupata kitambulisho kimoja cha afisa wa jeshi

    la Rwanda ambaye nilimhisi kuwa huenda angekuwa ndiye yule aliyekuwa

    akiishi na Niyonkuru na vilevile mwanachama wa Interahamwe.

    Ni Drel Fille ambaye alikuwa ameshtukia kuwa kulikuwa na harufu kali

    iliyokuwa ikitoka ndani ya jokofu lililokuwa mle ndani sebuleni na tulipoenda

    na kulifungua jokofu lile tulichokiona ndani yake kilitufanya tutapike.Mwili

    wa Niyonkuru ulikuwa umekatwa vipande vipande na kuhifadhiwa ndani ya

    jokofu lile huku kichwa chake kikiwa kimewekwa kwenye sehemu ya juu ya

    jokofu. Siyo mimi wala Drel Fille aliyeweza kuongea chochote juu ya tukio

    lile na baadaye tukaamua kutoka nje ya nyumba ile na kuondoka tukiwa na

    simanzi isiyoelezeka tukielekea zilipo ofisi za UNAMIR, vikosi vya kulinda

    amani vya umoja wa mataifa nchini Rwanda.

    Hoja zetu juu ya tukio la mapinduzi ya kijeshi lililokuwa limepangwa ku-

    fanyika usiku na baadhi ya viongozi wa kijeshi wasiokuwa waaminifukwa

    serikali ya rais Juvenal Habyarimana kwa misingi ya ukabila hazikuonekana

    kuchukuliwa kwa uzito wowote na badala yake tulikutana na maswali mengi

    kutoka kwa makamanda wa kijeshi wa UNAMIR. Maswali kama,sisi ni akina

    nani na tulikuwa na uhakika gani na taarifa zetu?na hata tulipotoa vielelezo

    hai tuliambiwa kuwa kwa kuwa tulishawafikishia taarifa zile, tuwaachie suala

    lile nao wangeanza kulifanyia kazi.

    Baadaye tuliondoka kwenye ofisi zile tukiwa tumekata tamaa sana na wakati

    tukiondoka kwenye ofisi zile za kijeshi za UNAMIRniliyakumbuka maneno ya

    Mutesi kuwa nilikua namfariji tu lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni vigumu

    sana kuyazuia mapinduzi yaliyopangwa kuwa yasifanyike.

    Ingawaje yalikuwa maneno ya kawaida tena yaliyozungumzwa na mtu ali-

    yelewa pombe lakini nilianza kuhisi kuwa yalikuwa na kiasi fulani cha ukweli

    ndani yake. Hata hivyo sikukata tamaa hivyonikaendesha gari hadi ilipo ofisi

    ya ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, nilipofika nikashuka na kumuacha

    Drel Fille akinisubiri kwenye gari lakini hata hivyo nilishangaa kukuta ofi-

    si zile zikiwa zimefungwa na hapo nikawauliza walinzi wa ofisi zile kama

    wangeweza kunisaidia nionane na balozi. Jibu nililopewa lilizidi kunikatisha

    tamaa, wale walinzi wakaniambia kuwa balozi alikuwa amesafiri kurudi nchi-

    ni Tanzania kikazi kwa muda wa wiki moja.

    Sikuwa na namna nyingine ya kufikisha ujumbe wangu hivyo nilirudi

    kwenye gari na kuondoka eneo lile huku nikimuelezea Drel Fille mambo

    yalivyokuwa. Nilihisi mzunguko wa damu yangu mwilini ulikuwa ukiongeze-

    ka taratibu kwa kadiri mshale wa sekunde wa saa yangu ya mkononi ulivyoku-

    wa ukiendelea na safari yake na mara kwa mara nikajikuta nikifanya sala fupi

    kuzifukuza hisia mbaya zilizokuwa zikikizengea kichwa changu.

    Kulikuwa na dakika chache zilizosalia kabla ya kutimia saa kumi na moja

    jioni na sikupenda kuitazama tena saa yangu nikihofia kuwa muda ulikuwa

    ukienda haraka kuelekea mapinduzi yale ya kishenzi.

    Wakati nikiendelea kuwaza,wazo la mtu muhimu katika kufanikisha ush-

    ahidi wangu dhidi ya wale maafisa wa kijeshi wasio waaminifu kwa seri-

    kali waliopanga kufanya mapinduzi haramu hapa nchini Rwanda likanijia

    kichwani. Mtu huyo alikuwa Jaji Makesa, mwanasheria na mwanaharakati wa

    haki za binadamu aliyekuwa akishutumiwa na baadhi ya viongozi wa serikali

    kwa kuzungumzia hali ya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Rwanda. Jaji

    Makesa angekuwa shahidi muhimu katika kufanikisha uthibitisho waushahidi

    wangu katika kuwatia hatiani wahusika wa mapinduzi yaliyopangwa kufan-

    yika.

    Nilimshirikisha Drel Fille wazo la kumtafuta Jaji Makesa huku nikimueleza

    dhamira yanguna nikafurahi sana kwa kunielewa hivyo tulibadilisha uelekeo

    wa gari tukitafuta kitongoji ambacho kulikuwa na nyumba ambayo Jaji Make-

    sa alisemekana kajificha.

    __________

    KILIKUWA KITONGOJI KILICHOKUWA KANDO YA JIJI LA KIGALI

    hivyo ilikuwa ni safari ya mwendo mrefu kidogo lakini yenye utulivu wa kiasi

    kwani wakati huu msongamano wa magari barabarani ulikuwa umepungua.

    Maelezo juu ya sehemu ilipokuwa nyumba aliyokuwa amejificha Jaji Make-

    sa bado yalikuwa yamehifadhiwa vizuri kichwani mwangu tangu nilipoyaso-

    ma kwenye zile nyaraka za Dr. Francois Tresor nilizozichukua kule posta.

    Nilikuwa wa kwanza kuiona nyumba hiyo katikati ya nyumba nyingi zilizo

    ongozana nyuma ya barabara ya mtaa ule ambao sikuweza kwa haraka kuufa-

    hamu kuwa ulikuwa na nyumba ngapi ingawaje naweza kusema kuwa nyumba

    zote za eneo lile zilikuwa za kisasa sana na nyingi zilikuwa ni za ghorofa na

    zenye uzio wa kuta ndefu na mageti makubwa mbele yake.

    Barabara ya mtaa ule ilikuwa ya lami iliyopakana na sistimu nzuri ya

    mirefeji ya maji kando yake pamoja na nguzo ndefu za taa za barabarani. Taa

    hizo wakati huu zilikuwa zikiangaza kwani kulikuwa na giza hafifu lililoletwa

    na wingu zito la mvua iliyokuwa ikijiandaa kunyesha angani.

    Nilikuwa nakaribia kusimamisha gari mbele ya geti la nyumba ile wakati

    Drel Fille aliposhtukia jambo.

    “Usisimame, endesha gari kuna watu wanatutazama”

    “Watu gani?nilimuuliza Drel Fille huku nikigeuka kumtazamana hapo

    nikamuona kuwa alikuwa akitazama juu ya nyumba ya ghorofa ya upande wa

    pili wa ile barabara kupitia dirishani

    “Kuna watu wawili kule juu ya ghorofa wote wanaonekana kutufuatilia”

    “Kwanini unadhani hivyo?nilimuuliza Drel Fille huku nikiinama vizuri ili

    niweze kuona kule juu ya ghorofa alipokuwa akitazama na hapo nikawaona

    watu wawili wanaume wakiwa wameegemea uzio wa ukuta mfupi ulioten-

    genezwa kuizunguka baraza ya ghorofa ile. Wote walikuwa wamevaa miwani

    nyeusi na makoti marefu ya mvua.

    “Kipi kinachokufanya uamini kuwa watu wale wanatutazama sisi na kwani

    usifikirie kuwa wapo kwenye mapumziko yao? nilimuuliza tena Drel Fille

    huku nikigeuka kumtazama.

    “Alikuwa mtu mmoja tu pale juu akiangalia upande huu lakini mtu yule

    alipoliona hili gari nilimuona akionesha ishara fulani kumuita mwenzake ali-

    yekuwa upande mwingine”

    “Mh! inamaana hawa watu sasa wamesambazwa kila kona?nilimuuliza Drel

    Fille kwa mshangao

    “Tunatakiwa kuwa waangalifu Luteni hawa watu wanaweza kutuua endapo

    jitihada zao za kutukamata zitashindikana”

    Niliongeza mwendo wa gari kulipita geti la nyumba ile katika namna am-

    bayo sikutaka wale watu kule juu ya ghorofa wafahamutulikuwa tukielekea

    wapi.

    “Nimepata wazo” hatimaye nilimwambia Drel Fille”

    “Wazo gani?

    “Inavyoonekana hawa watu hawafahamu hasa ni nyumba gani alikojifi-

    cha jaji Makesa na pengine wakawa wametuwekea mtego wakitaka kujua ni

    nyumba gani tutakayoingia ili watufuatilie kwa nyuma”

    “Ni kweli nawanavyoonekana ni kama wameweka mtego fulani”

    “Hebu subiri tuone” nilimwambia Drel Fille huku nikikunja kona kuingia

    mtaa mwingine lengo langu likiwa nikuwapotezea malengo wale watu.

    Nilitafuta maegesho mazuri katika mtaa ule tuliyoingia na tukawa tume-

    kubaliana na Drel Fille kuwa yeye atangulie kwenye ile nyumba halafu mimi

    ningekuja nyuma yake huku tukiachana kwa umbali fulani ili niweze kujua

    kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angemfuatilia kwa nyuma.

    Wazo langu lilionekana kukubalikana Drel Fille hivyo alitangulia kurudi

    kwenye ile nyumba tuliyoipita, nikamuacha atangulie na baada ya muda mfupi

    na mimi nilianza safari nikimfuata nyuma yake taratibu lakini huku nikijiuliza

    kama kweli Jaji Makesa bado alikuwa kwenye ile nyumba.

    Nilitokezea kwenye barabara ya ule mtaa wenye ile nyumba na hapo

    nikamuona Drel Fille kiasi cha umbali wa mita hamsini akiwa amesimama

    nje ya lile geti la ile nyumba na ingawa alifahamu kuwa nilikuwa nyuma yake

    lakini hakugeuka kunitazama na hilo lilinifurahisha.

    Nilimuona Drel Fille akigonga hodi kwenye geti la nyumba ile na nili-

    poyapeleka macho yangu kuwatazama wale watu waliokuwa juu kwenye

    ile nyumba ya ghorofa sikuwaona hivyo nikapunguza urefu wa hatua zangu.

    Haukupita muda mrefu mara nilimuona Drel Fille akiusukuma mlango mdogo

    wa geti lile na kuingia ndani na hisia zangu zilinieleza kuwa hakuwa amefun-

    guliwa ule mlango na mtu yeyote.

    Mara baada ya Drel Fille kuingia ndani ya geti lile nilisubiri kidogo muda

    upite huku nikifanya tathmini ya usalama wa eneo lile. Niliporidhika nikaanza

    kutupa hatua zangu kwa utulivu kumfuata Drel Fille na wakati huu nilianza

    kuhisi manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yakianza kuanguka toka angani.

    Nilikuwa sijafika mbali sanapale nilipowaona wanaume wawili wakitoka

    kwenye geti la ile nyumba ya jirani na hapo nikasita kuendelea na safari hivyo

    nikachepuka na kujibanza kwenye ukuta wa jirani na eneo lile. Nikiwa nime-

    jibanza sehemu ile niliweza kuwaona vizuri wale watu na hapo nikawakum-

    buka kuwa walikuwa ni wale waliokuwa kule juu ghorofa. Hata hivyo muda

    mfupi uliofuata aliongezeka mtu mwingine kutoka ndani ya lile geti ambaye

    alikuwa mgeni kabisa kwangu na kuifanya idadi yao iongezeke na kuwa wa-

    naume watatu.

    Niliwaona wale watu wakitazama huku na kule na waliporidhika kuwa

    hapakuwa na mtu yeyote aliyewaona wakavuka barabara upande wa pili na

    kupotelea ndani ya lile geti la ile nyumba aliyoingia Drel Fille.

    Nilisubiri kidogo muda upite na nilipoona kuwa hapakuwa na mtu mwingine

    aliyeongezeka nyuma yao nikaanza kuharakisha kuwafuata wale watu kwa

    nyuma.

    Nilifika kwenye lile geti nikausukuma ule mlango taratibu na kuingia ndani.

    Kulikuwa na magari matatu yaliyokuwa yameegeshwa mbele ya nyuma ile

    ya ghorofa na nilipoyatazama yote yalionekana kuwa hayakuwa yametumika

    kwa muda mrefu. Sikumuona mtu yeyote eneo lile hivyo niliichomoa bastola

    yangu toka mafichoni na kuikamata vema mkononi halafu nikachepuka na ku-

    jibanza nyuma ya gari moja miongoni mwa yale magari matatu yaliyoegeshwa

    pale nje.

    Nikiwa nimejibanza nyuma ya lile gari sikuweza kumuona mtu yeyote eneo

    lila na jambo lile lilinishangaza sana. Niliitazama nyumba ile ya ghorofa tatu

    mbele yangu huku nikihisi kuwa mtu yeyote ambaye angekuwa juu ya ghorofa

    lile angeweza kuniona kwa urahisi.

    Wakati huu mawazo yangu yalihamia kuwa Drel Fille huku nikijiuliza kuwa

    angekuwa eneo gani katika nyumba ile mbele yangu

    Niliendelea kujibanza nyuma ya lile gari huku nikilichunguza eneo lile nani-

    lipoona hali ilikuwa poa nikachepuka na kujibanza kwenye pembe ya nyumba

    ile huku nikichungulia sehemu ya nyuma ya ile nyumba.

    Nilikuwa mbioni kuhama lile eneo pale niliposika hatua za mtu akija upande

    wangu hivyo haraka nikarudi tena nyuma kujibanza huku nikifanya makadirio

    chanya. Muda mfupi baadaye yule mtu alikaribia ule usawa wangu na niliku-

    wa nimezikadiria vizuri hatua zake hivyo nilimkabili kwa pigo moja la kiwiko

    cha pua kilichoupasua mgongo wa pua yake, alipojishika puani nikamtandika

    pigo jingine la kareti shingoni lililozichukua fahamu zake.

    Sikutaka kelele za mshindo wa anguko lake zisikike hivyo niliwahi kumda-

    ka kabla hajafika chini na hapo nikamburuta na kumficha kwenye maua yaliy-

    okuwa jirani na eneo lile kisha nikaichukua bastola yake na kuitia maungoni.

    Niliendelea kujibanza kwenye lile eneo na nilipoona muda unaenda bila

    mtu mwingine kujitokezanikaamua kunyata nikiuendea mlango wa mbele wa

    nyumba ile. Nilikuta mlango ule ukiwa wazi hivyo niliingia taratibu huku ni-

    kijitahidi sauti ya hatua zangu isisikike.

    Nilitokezea kwenye eneo la sebule la nyumba ile. Ilikuwa sebule pana yenye

    samani za kisasa za kila namnana hapo nikasita kidogo nikiupima utulivu wa

    eneo lile huku nikifikiria nielekee wapi. Nikiwa mbele ya sebule ile nilijikuta

    nikitazamana ngazi zilizokuwa zikielekea ghorofa ya pili.

    Upande wa kulia kulikuwa na korido na korido hiyo nyembamba ilikuwa

    ikielekea kwenye vyumba vya ndani vya ghorofa lile na eneo la jiko lililokuwa

    na mlango wa kutokea nyuma ya ile nyumba.

    Nikaamua nianze kwanza kuvichunguza vile vyumba na jiko kabla kuelekea

    kule juu ya ghorofa lakini nilipokuwa mbioni kufanya hivyo nilisikia hatua

    mtu aliyekuwa akishuka kwenye zile ngazi.

    “Bizimugu.., Bizimungu...” nilimsikia yule mtu akiita kwa utulivu huku

    akiendelea kushuka zile ngazi na sikutaka kupoteza muda hivyo haraka nika-

    jibanza nyuma ya pazia refu lililokuwa kwenye dirisha la pale sebuleni.

    “Bizimungu.., Bizimungu.., Bizimungu” yule mtu aliendelea kuita huku

    akishuka zile ngazi na hapo nikajua kuwa alikuwa akimuita yule mwenzake

    niliyepambana naye kule nje na mtu yule alipomaliza kushuka zile ngazi

    nilimuona akisita kuendelea mbele kisha akatoa bastola toka ndani ya koti

    lake na kuishika vyema mkononi.

    Mtu yule alikuwa mrefu na mwembamba kiasi na muda mfupi uliofuata

    nilimuona yule mtu akinyata kuja upande wangu na hapo nikajua kuwa ali-

    kuwa akitaka kuelekea nje hata hivyo nilishangaa kumuona akisita baada ya

    kufika usawa wa lile dirisha na hapo moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu.

    Yule mtu sasa alikuwa akilitazama lile pazia la dirisha ambalomiminilikuwa

    nimejificha nyuma yake na hapo nikahisi kuwa huenda alikuwa ameushtukia

    uwepo wangu eneo lile. Muda mfupi uliofuata nilimuona akilisogelea lile di-

    risha na hapo wasiwasi ukazidi kunishika, nikataka nianzishe shambulizi la

    kumuwahi lakini nafsi yangu ilinionya hivyo nikaendelea kusubiri.

    Wasiwasi ukiwa umenishika mara tu mtu yule aliponikaribia pale dirishani

    nilimuona akinyanyua bastola yake mkononi na kuielekezea kwangu na hapo

    nikajua ni nini kilichokuwa kikifuatia hivyo niliwahi kujirusha chini na muda

    huo nikasikia mshindo mkubwa wa risasi juu yangu kabla ya kufuatiwa na

    sauti kali ya mpasuko wa kioo cha lile dirisha.

    Risasi nyingine iliyofuatia iliparaza kidogo kichwani mwangu na kuchimba

    ukuta na hapo nikawahi kujirusha tena pembeni lakini yule mtu alikwishani-

    fikia hivyo nikaikamata vizuri bastola yangu ili nimuwahi lakini nilishachele-

    wa kwani teke la kasi alilolirusha mtu yule liliipokonya bastola yangu mkononi

    na kuirushia mbali na hapo nikajikuta nikishangazwa na uwezo mkubwa wa

    mbinu za mapambano aliokuwa nao mtu yule.

    Mapigo mengine ya mateke yaliyofuatia niliyaona nikaanza kuyakwepa

    kwa kijiviringisha sakafuni hata hivyo yule mtu hakuniacha, akawa ananifuata

    huku akiendelea kunirushia mateke. Niliendelea kujiviringisha na nilipofika

    ukutani nilijibinua nikaukita mguu wangu mmoja ukutani kisha nikajifyatua

    hewani na kumtandika teke zito la kifuani yule mtu huku mimi nikiangukia

    upande wa pili. Yule mtu akajibamiza ukutani na ile bastola ikamponyoka

    mkononi na kabla hajaiwahi niliwahi kumfikia na kumpiga pigo moja la judo

    lakini alikuwa mwepesi kulikwepa kisha akanidaka mkono na kunitandika

    pigo la kareti mbavuni na hapo nikapiga yowe kali la maumivu huku niki-

    pepesuka na nilipokuwa mbioni kusimama nilishangaa tena nikichotwa he-

    wani mzimamzima kwa mtama wa kiufundi sana ambao ulinishangaza hata

    hivyo nilitua sakafuni kwa utulivu kama paka kwa miguu yangu miwili na

    mkono mmoja.

    Yule mtu hatari akanifuata tena lakini safari hii pigo la teke alilolirusha ni-

    liwahi kuliona nikaudaka mguu wake kisha nikajipindua na kumtandika teke

    farasi ambalo lilizikoroga vibaya korodani zake na kumfanya apige yowe

    kama mbwa mwizi. Nilitaka kumuwahi tena lakini alikuwa mwepesi kunish-

    tukia hila yangu hivyo aliwahi kurudi nyuma na hapo akasimama na kujipanga

    vizuri, nikajua kuwa kazi bado ilikuwa pevu hivyo na mimi nikasimama na

    kujipanga upya, tukabaki tukitazamana kila mmoja akimsoma mwenzake.

    Muda mfupi baadaye nilimuona yule mtu hatari akija kwa kasi pale nilipo

    nikaijua dhamira yake hivyo nilimsubiri hadi pale alipokuwa mbioni kunifikia

    na hapo nikaruka samba soti hewani huku nikimtandika pigo la teke kavu nyu-

    ma ya shingo yake lililomrusha vibaya sakafuni na kabla hajatulia vizuri na

    kujipanga mimi nilikuwa nimeshajiviringisha haraka kwa mtindo wa ki-ninja

    na nilipomfikia alikuwa ndiyo anamalizia kusimama hivyo nikajikita ukutani

    na kumchapa pigo maridadi la ki-ninja liitwalo Muay Thai shingoni mwake na

    hapo nikamvunja shingo na kumbamiza ukutani hali iliyompelekea aanguke

    chini taratibu huku damu ikimtoka puani, mdomoni na masikioni. Nikatua chi-

    ni na kumsikilizia na nilipomuona ametulia kimya nikajua alikwisha kata roho

    hivyo niliiendea ile bastola yangu kule ilipoangukia na kuikota hata hivyo

    nilipata mashaka kidogo kwani nilitegemea kumuona yule mwenzake akija

    kumsaidia lakini hali ilikuwa tofauti na nyumba yote ilikuwa kimya kabisa na

    sikuweza kusikia sauti ya kiumbe hai yeyote mle ndani. Nikashindwa kuelewa

    kuwa Drel Fille na yule mtu mwingine walikuwa wapi hata hivyo sikuona

    kama ingekuwa busara ya kumuita kwani niliamini kuwa kama angekuwa

    karibu kwa vyovyote lile varangati la pale chini lingesha mvuta.

    Niliichukuwa bastola yangu na kuanza kupanda zile ngazi kwa utulivu na

    tahadhari ya hali ya juu nikielekea ghorofa ya pili huku nimeyatega masikio

    yangu kusikia kama kulikuwa na sauti ya kiumbe chochote eneo lile.

    Nilimaliza kupanda zile ngazi na kujikuta katikati ya korido pana iliyota-

    zamana na milango ya vyumba kwa upande wa kushoto na upande wa kulia

    kulikuwa na sebule nyingine kubwa yenye samani za kisasa. Upande wa mbele

    yangu nilitazamana na ukuta mkubwa wa kioo ambao uliniwezesha kuona

    kule chini mbele ya ile nyumba bila kificho. Nilipotazama angani nikagundua

    kuwa mvua kubwa ilikuwa mbioni kunyesha muda wowote kuanzia pale.

    Nilipiga hatua chache mbele yangu kisha nikasimama katikati ya ile sebule

    huku nikiichunguza kwa makini. Ilikuwa sebule ya kisasana ya kisomi kwani

    sehemu fulani kando ya ukuta wa sebule ile kulikuwa na rafu mbili kubwa

    zilizojaa vitabu vya kila namna. Nilivitazama vitabu vile na kugundua kuwa

    vingi vilikuwa vitabu vya kisheria na hilo likanipa faraja kuwa nilikuwa sija-

    kosea nyumba kwani nyumba yoyote ya mtukama Jaji Makesa isingeshangaza

    kuviona vitabu vya namna ile.

    Upande wa kulia wa sebule ile kulikuwa na ngazi, nilizitazama ngazi zile

    nikagundua kuwa zilikuwa zikielekeaghorofa ya tatu na ya mwisho ya jengo

    lile. Nilishawishika kuanza kuzipanda ngazi zile lakini kabla sijafanya vile

    niliamua kuanza kuvichunguza vile vyumba vilivyotazama na ile korido.

    Haikuwa kazi ngumu kwani niliikuta milango ya vile vyumba ikiwa hai-

    jafungwa hivyo niliingia chumba kimoja baada ya kingine kufanya upekuzi.

    Kwa kweli hali vya vyumba vile ilinijulisha kuwa ile nyumba ilikuwa ime-

    telekezwa kwamuda mrefu bila kuwa na mwenyeji au wenyeji na hilo likaanza

    kunipa wasiwasi kama kweli Jaji Makesa bado alikuwa akiishi kwenye ile

    nyumba.

    Nilipofika chumba cha mwisho hali ilikuwa vilevile na sikuona chochote

    cha kunivutia hivyo nikaamua kurudi tena kule sebuleni na kuanza kupanda

    zile ngazi za kuelekea kwenye ile ghorofa ya mwisho.

    Nilikuwa mbioni kumaliza kupanda zile ngazi wakati nilipojikuta nikirud-

    ishwa chini kwa pigo baya la teke la kifuani. Nilirushwa vibaya na kuanza

    kuporomoka chini kwenye zile ngazi huku nikijitahidi kujizuia bila mafanikio.

    Nilifika chini ya ngazi zile nikiwa sijewezi kwa maumivu. Yule mtu alishuka

    zile ngazi kwa kasi kama upepo, akawa amenifikia pale chini na hapo nikai-

    weka vizuri bastola yangu ili nimlenge lakini nilikwishachelewa kwani teke la

    mtu yule liliipangusa bastola yangu mkononi kama mzaha. Halafu nikapigwa

    tena pigo jingine la teke la kichwa ambalo niliwahi kulikwepa kwa kuinama

    chini kidogo.

    Pigo jingine lilipokuja niliruka sarakasi nikatua pembeni lakini yule mtu

    alizidi kunifuata na safari hii sikumkawiza.

    Nilijirusha nikamkumba na hapo wote tukaanguka chini lakini yeye alikuwa

    mwepesi kunipiga kabari matata shingoni na nyingine tumboni kwa miguu

    yake katika mtindo wa judo. Nilijitahidi kufurukuta bila mafanikio kwani nili-

    kuwa nimebanwa kisawasawa huku macho yamenitoka pima na hapo nikawa

    nikirusharusha mikono huku na kule bila mafanikio na hivyo nikawa nimekata

    tamaa sana.

    Lakini ghafla nikiwa katika hali ile wazo fulani likanijia kichwani, wazo la

    kulitekenya mbavuni lile njemba na nilipofanya hivyo likajitikisa kama Kam-

    bare huku likijilegeza miguu na mikono yake kama shoga na kuangua kicheko

    na hapo nikautumia mwanya ule kujinasua.

    Nikamtandika ngumi mbili za pua zilizompelekea apige yowe kama an-

    ayebakwa huku akiniachia ile kabari aliyonitundika na hapo nikajipindua kwa

    wepesi na kukaa juu yake huku nikimshindilia ngumi za shingo mfululizo

    zilizolipasua koo lake na kumfanya azidi kupiga yowe kama mwendawazimu

    huku ile bastola aliyoishika mkononi mwake ikimponyoka.

    Bila kupoteza muda nikajipindua na kumpiga kabari ya tumbo katika mtin-

    do wa judo kwa kutumia miguu yangu huku mikono yake nikiwa nimeidhibi-

    ti kwa nyuma. Yule mtu akafurukuta bila mafanikio na hatimaye akatulia na

    hapo nikaiondoa ile kabari na kumsukuma pembeni akiwa marehemu.

    Sikutaka kupoteza muda hivyo nikasimama na kwenda kuichukua ile basto-

    la yangu kule ilipoangukia kisha nikaanza kupanda zile ngazi kwa tahadhari

    huku nikiendelea kujiuliza Drel Fille angekuwa wapi muda ule.

    Nilimaliza kuzipanda zile ngazi nikatokea kwenye korido nyingine lak-

    ini kabla sijaendelea na safari nikaiona miili ya watu wawili ikiwa imelala

    sakafuni huku damu ikiendelea kuvuja kwenye majeraha ya risasi yaliyokuwa

    kwenye miili yao, kichwani na kifuani.

    Nilishtuka sana kwani sikufikiria kama mle ndani kungekuwa na watu

    wengine zaidi ya wale watatu niliowaona wakiingia kwenye geti la nyumba

    hii muda mfupi baada ya Drel Fille kutangulia. Hata hivyo tabasamu hafifu

    liliumbika usoni mwangu pale nilipohisi kuwa ile ilikuwa kazi nzuri ya Drel

    Fille.

    Nikaanza kutembea kwa tahadhari na bastola yangu mkoni huku nikiziruka

    zile maiti na kuendelea na safari nikiifuata ile korido mbele yangu na wakati

    huo pia nikimuita Drel Fille kwa sauti ya chini hata hivyo sikumsikia akiitikia

    na hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi.

    Upande wa kushoto wa korido ile kulikuwa na vyumba hivyo nikaanza ku-

    fungua chumba kimoja baada ya kingine nikivikagua huku bastola yangu iki-

    wa mkononi tayari kufanya shambulizi.

    Vyumba vinne vya mwanzo havikuwa na kitu chochote cha maana hivyo

    niliachananavyo na kukifuata chumba cha mwisho kilichokuwa mwisho ka-

    bisa wa ile korido.

    Nilikisogelea chumba kile na kusikiliza kama kulikuwa na sauti yoyote,

    sikusikia chochote na hali hiyo ikazidi kunipa wasiwasi. Nikakishika kitasa

    cha mlango ule na kuusukuma mlango ule kwa kasi ya ajabu nikiwa nime-

    kusudia kuliwahi windo langu lakini ghafla nilishangaa kumuona Drel Fille

    akiwa amepigwa kabari matata shingoni mwake na mwanaume mmoja mrefu

    mweusi mwenye sura mbaya kama ya panya aliyekuwa nyuma yake.

    “Oh! Drel mpenzi…!” nilishikwa na taharuki

    “Tupa bastola yako chini wewe bwege” yule mtu alinionya huku kile kisu

    alichokishikilia kikiwa tayari kimeanza kutafuta njia kwenye koo la Drel Fille

    hali iliyopelekea mchirizi wa damu kushuka taratibu kifuania mwake.

    “Nimesema tupa bastola yako chini vinginevyo usije ukanilaumu” yule mtu

    alinitahadharisha

    “Una haja na mimi au bastola yangu? nilimuuliza huku nikimtazama kwa

    makini mtu yule ingawaje hali ya Drel Fille ilinionya kuwa ule haukuwa

    wakati wa kuleta mzaha.

    “Ah! unaleta masihara eh! basi subiri uone nitakachomfanya huyu malaya

    wako” yule mtu alinionya halafu muda uleule nikakiona kile kisu cha yule mtu

    kikianza tena kutafuta njia kwenye koo la Drel Fille huku Drel Fille akioneka-

    na kushikwa na hofu.

    Nikaona kitendo kile kingepelekea hali ya Drel Fille kuzidi kuwa mbaya

    hivyo nikaitupa ile bastola yangu chini lakini wakati huohuo nikiwa nimebaki-

    wa na ile bastola ya yule mtu niliyepambana naye kule chini.

    “Good boy…nilidhani ungejifanya kichwa ngumu” yule mtu aliongea huku

    akiangua kicheko cha kejeli kilichonitia hasira.

    “Tayari nimefanya kama ulivyoniagiza muachie basi huyo dada huoni aibu

    kutumia nguvu nyingi kwa kiumbe cha kike na si kwa mwanaume mwenzio?

    “Hakuna haja ya kunieleza kwani mimi sina macho, mbona unakuwa huji-

    amini Luteni utadhani umefumaniwa na mume wa mtu”

    “Sawa, basi muachie huyo dada”http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Funga mdomo wako, usinifundishe cha kufanya” yule mtu alifoka huku

    ametoa macho

    “Haya basi sema utakacho”

    “Ipige teke hiyo bastola yako uliyoitupa chini ili ije upande wangu na

    usijidanganye kufanya hila”

    “Sawa nimekuelewa” nilimwambia yule mtu huku nikifanya kama alivyo-

    niagiza hivyo nikaipiga teke ile bastola yangu ikaserereka mpaka miguuni

    mwake na hapo akaikota na kuchomeka kiunoni mwake.

    “Umefanya vizuri, mimi huwa napenda watu watiifu kama wewe”

    “Kingine…?” nilimuuliza huku nikiupima umakini wake.

    “Bahasha”

    “Bahasha gani?

    “Nipe ile bahasha uliyoichukua kule posta” yule mtu aliniambia na hapo

    nikashikwa na mshangao kidogo kwani sikuelewa habari za kule posta huyu

    mtu zilimfikiaje.

    “Mwenzako tayari ameichukua”

    “Mwenzangu nani?

    “Mimi nitamjuaje na wakati mpo wengi?

    “Unaleta ujanja eh?

    “Kwa nini hutaki kuniamini?

    “Nani akuamini, wewe ni mtu wa kuaminika wewe?, nipe ile bahasha ni-

    muachie huyu malaya wako vinginevyo wote nitawachapa risasi”

    “Ukituua sisi itakusaidia nini wakati hizo taarifa mnazozihitaji bado ham-

    jazipata” niliongea katika namna ya ushawishi na hapo nikamuona yule mtu

    akinitazama kama anayepima ukweli wa maneno yangu.

    “Bahasha iko wapi?

    “Nyumbani” hatimaye nilimdanganya

    “Nitakuamini vipi?

    “Nakuahidi”

    “Okay, bado kuna jambo moja, kwanini mmekuja kwenye hii nyumba, mna-

    tafuta nini hapa? yule mtu aliniuliza

    “Hilo ni swali letu sote na wewe”

    “Najua mmekuja kumtafuta Jaji Makesa bila shaka hilo ndiyo lililowafiki-

    sha hapa. Sasa nataka mnioneshe mahali alipo Jaji Makesa halafu mtanipa na

    hiyo bahasha kisha nitawaacha muende zenu”

    Nilimtazama yule mtu nikayapima maneno yake na hapo nikamuona kuwa

    alikuwa akitufanya sisi kama watoto wadogo tusiojua kupambanua. Lakini

    wakati akiongea sote tukasikia sauti ya mtikisiko wa kitu fulani na hapo sote

    tukageuka na kuutazama mlango wa chumba kingine mle ndani kilichokua

    upande wa kushoto wa sehemu ile. Halafu ile sauti ya mtikisiko ikatoweka na

    hapo nikajua mle ndani kulikuwa na mtu.

    “Tulieni na mtu yoyote asithubutu kusogea kwani sitomvumilia” yule mtu

    alituonya huku akiendelea kuutazama ule mlango.

    Nilimtazama Drel Fille akiwa bado amekabwa na yule mtu na hapo nikam-

    fanyia ishara kuwa ainamishe kidogo kichwa chake ili kunipa nafasi ya kuto-

    sha kuiona sura ya yule mtu nyuma yake na hapo Drel Fille akawa amenielewa

    dhamira yangu. Muda uleule ile sauti ya mtikisiko hafifu ikasikika ndani ya

    kile chumba, sauti kama ya mwanguko wa kitu kisichokuwa na uzito mkubwa.

    Yule mtu aliyemkaba Drel Fille akashtuka tena na kuutazama ule mlango wa

    kile chumba na hilo likawa kosa kubwa alilolifanya enzi za uhai wake kwani

    kwa haraka mkono wangu ulizunguka na kuichomoa ile bastola nyingine nili-

    yokuwa nimeisunda kiunoni kwa nyuma na kwa kuwa nilikuwa mlenga shaba-

    ha mzuri. Risasi mbili nilizozifyatua ziliziparaza kidogo nywele za Drel Fille

    lakini zikapekenya fuvu la yule mtu na kukifumua vibaya kichwa chake na

    hapo akarushwa na kubamizwa ukutani.

    “Luteni…, Honey…, Dear…” Drel Fille aliita.

    “Naam!...”

    “Nilikuwa nikiogopa sana mpenzi mh! umejifunzia wapi shabaha ya namna

    hiyo? Drel Fille aliniuliza kwa shauku.

    “Nilifanya makadirio mazuri hivyo nilikuwa na hakika na kazi yangu”

    “Ahsante sana mpenzi wangu loh! hili dubwana lingeniua hivi hivi” Drel

    Fille kaniambia huku akiwa tayari amesimama akiitazama maiti ya yule mtu

    huku akijipapasa papasa shingoni.

    “Vipi umeumia sana mpenzi?

    “Siyo sana, sidhani kama paniletea matatizo”

    “Pole sana mpenzi”

    “Oh! nashukuru sana kwa kuyaokoa maisha yangu”

    “Usijali Drel vipi Jaji Makesa umemuona? nilimuuliza Drel Fille na hapo

    nikasikia tena mtikisiko hafifu mle ndani ya kile chumba na hapo sote tuka

    geuka kuutazama ule mlango wa kile chumba kisha nikaanza kupiga hatua

    taratibu kuukaribia ule mlango na wakati huo Drel Fille alikuwa akizikusanya

    zile bastola, yaani ya yule mtu na ile yangu.

    Muda mfupi baadaye sote tukawa tumeufikia ule mlango na hapo tukakusan-

    ya nguvu kwa pamoja, tukarudi nyuma kidogo kisha tukauvamia kwa nguvu

    zetu zote mlango ule huku bastola zetu zikiwa mikononi tayari kufanya kazi.

    Ule mlango ukavunjika vipandevipande huku tukiangukia mle ndani kama

    magunia na hapo vumbi likatimka.

    Kilikuwa chumba kidogo lakini chenye msongamano wa vitu lakini vilevile

    kilikuwa chumba kichafu chenye harufu mbaya ya uvundo na nilipotazama

    chini niliona mabaki vya vyakula yakiwa yametelekezwa sakafuni.

    “Yule pale” Drel Fille alinong’ona na hapo nikageuka kutazama kule ali-

    pokuwa akitazama Drel Fille na mwanga hafifu wa taa ya mle ndani ukani-

    wezesha kumuona mwanaume mmoja mwenye nywele nyingi zilizotimka

    ovyo na ndevu chafu kiasi cha kumfanya aonekane kama msukule.

    Mtu yule alikuwa amevaa shati chafu, kizibao na suruali ya kitambaa na

    alikuwa amejificha chini ya meza ndogo yenye mafaili mengi juu yake.

    “Jaji…” niliita

    “Stay away from me you bastards” yule mzee alifoka huku ametoa macho

    kwa hofu.

    “We are not bastards judge, we are here to help you, you need to come with

    us, nothing to worry about judge”

    “I say stay away from me, don’t you understand or you want to see me doing

    something wrong here?

    “Something wrong…what? nilimuuliza yule mzee huku nikisita kuzidi kum-

    sogelea zaidi

    “Don’t move…” yule mtu tuliyemhisi kuwa huenda angekuwa ndiye Jaji

    Makesa alitutahadharisha huku tukiwa tayari tumekwisha simama na hapo tu-

    kamuona yule mzee akisimama pale alipokuwa amejibanza na kuanza kurudi

    nyuma taratibu na alipofika mahali kulipokuwa na kiti akaketi huku akituta-

    zama kwa wasiwasi.

    Drel Fille aligeuka kunitazama kama anayetaka kuniambia kitu fulani hata

    hivyo hakuzungumza kwani nilimuona tena akiyahamisha macho yake kum-

    tazama yule mzee na hapo nikajua kuwa tulikuwa tumezidiwa ujanja hivyo

    nikaanza kufikiria mbinu za kidemokrasia na kabla sijazungumza neno yule

    mzee akavunja ukimya,

    “Who are you? yule mzee alituuliza kwa utulivu

    “I am Luteni Venus Jaka of Tanzanian Peoples Defence Force”

    “Drel Fille de la D.R Congo, nous somme ici pour t’aider de donner votre

    temoignage á propo de la violence du troit de l’homme” Drel Fille alimwam-

    bia yule mtu akijitambulisha kuwa “Yeye ni Drel Fille kutoka jamhuri ya

    kidemokrasia ya Kongo na tulikuwa pale mimi na yeye kumsaidia Jaji Makesa

    ili akatoe ushahidi wake dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Rwan-

    da”

    Yule mzee alitulia akitutazama kwa udadisi na alipoyaondoa macho yake

    kwa Drel Fille akayahamishia kwangu huku akitikisa kichwa chake taratibu

    akionesha kutokukubaliana na maelezo yetu na hapo yule mzee akaongea kwa

    lugha ya Kiswahili,

    “Mnadhani hayo ni maelezo yatakayonifanya niwaamini?

    “Ni vugumu sana kutuamini lakini ukweli ni kwamba hicho ndiyo kilichot-

    uleta hapa” nilimwambia yule mzee na hapo nikamuona akicheka kwa kejeli.

    “Nani aliyewaambia kuwa mimi nipo hapa?

    “Ni kupitia maelezo ya Dr. Francois Tresor kwa njia ya maandishi aliy-

    oyahifadhi kwenye sanduku lake la posta na kwa bahati mbaya sana ni kuwa

    Dr. Francois Tresor sasa ni marehemu” nilimaliza kuongea na kumuacha Jaji

    Makesa akiwa katika mshtuko usioelezeka.

    “Nani aliyemuua?

    “Ameuwawa na hao watu wanaokutafuta wewe”

    “Kanali Bosco Rutaganda!...” Jaji Makesa aliongea huku akinitazama katika

    hali ya kukata tamaa huku uso wake ukiwa umesawajika

    “Nilijua tu kuwa wangemuua oh! my God”

    “Tumekuja kukuchukua Jaji kwani wewe ndiye mtu pekee wa kuaminika

    katika kutoa ushahidi”

    “Siendi kokote” Jaji Makesa alifoka kwa hasira

    “Usiwe na shaka jaji sisi ndiyo watu pekee unaoweza kutuamini kwa sasa”

    nilimwambia

    “Msijidanganye vijana mimi simuamini mtu yeyote kati yenu. Mmemuua

    mke wangu, mmewaua watoto wangu na sasa mnataka eti niwaamini kirahisi”

    Jaji Makesa aliongea kwa sauti ya kitetemeshi yenye hofu na mashaka halafu

    akasimama kwa tahadhari kisha akaanza kutembea taratibu akielekea sehemu

    moja mle ndani iliyokuwa na kabati chakavu. Alipofika akafungua droo moja

    ya kabati lile na kuchukua bastola na hapo sote tukashtuka kwa tukio lile, Drel

    Fille akataka akimbie kumuwahi lakini niliwahi kumzuia.

    “Huoni kuwa anataka kujiua?

    “Hatuwezi kumzuia” nilimwambia

    “Hapana hatuwezi kumuacha ajiue sasa hapo si kila kitu kitakuwa kimehari-

    bika? Drel Fille alinong’ona kwa jazba akionesha kutokukubaliana kabisa na

    uamuzi wangu.

    “Tumeishachelewa mpenzi na hatua moja tu utakayoitupa kumkaribia ataki-

    fumua kichwa chake ni afadhali tumuache azungumze” nimwambia Drel Fille

    na hapo akasimama huku akimtazama Jaji Makesa kwa mashaka.

    “Sasa tunafanyaje? Drel Fille aliniuliza kwa hamaki na hapo Jaji Makesa

    akavunja ukimya

    “Nimeishi ndani ya chumba hiki kwa zaidi ya miaka mitatu sasa nikiwa

    kama panya aishiye shimoni kuwakimbia paka wakubwa wenye njaa kali.

    Mimi ni panya mdogo sana na sina haki yoyote mbele ya paka wakubwa

    na wenye njaa kali ambao ni wengi katika nchi hii, na haya yote yananitokea

    kwa sababu ya ukweli wangu ulioniponza na kuipelekea roho yangu iwindwe

    usiku na mchana kama kito cha thamani sana kwa watu wenye kiu ya utajiri.

    Muda si mrefu nchi hii itatumbukia kwenye machafuko ya kihistoria yenye

    kwa Drel Fille akayahamishia kwangu huku akitikisa kichwa chake taratibu

    akionesha kutokukubaliana na maelezo yetu na hapo yule mzee akaongea kwa

    lugha ya Kiswahili,

    “Mnadhani hayo ni maelezo yatakayonifanya niwaamini?

    “Ni vugumu sana kutuamini lakini ukweli ni kwamba hicho ndiyo kilichot-

    uleta hapa” nilimwambia yule mzee na hapo nikamuona akicheka kwa kejeli.

    “Nani aliyewaambia kuwa mimi nipo hapa?

    “Ni kupitia maelezo ya Dr. Francois Tresor kwa njia ya maandishi aliy-

    oyahifadhi kwenye sanduku lake la posta na kwa bahati mbaya sana ni kuwa

    Dr. Francois Tresor sasa ni marehemu” nilimaliza kuongea na kumuacha Jaji

    Makesa akiwa katika mshtuko usioelezeka.

    “Nani aliyemuua?

    “Ameuwawa na hao watu wanaokutafuta wewe”

    “Kanali Bosco Rutaganda!...” Jaji Makesa aliongea huku akinitazama katika

    hali ya kukata tamaa huku uso wake ukiwa umesawajika

    “Nilijua tu kuwa wangemuua oh! my God”

    “Tumekuja kukuchukua Jaji kwani wewe ndiye mtu pekee wa kuaminika

    katika kutoa ushahidi”

    “Siendi kokote” Jaji Makesa alifoka kwa hasira

    “Usiwe na shaka jaji sisi ndiyo watu pekee unaoweza kutuamini kwa sasa”

    nilimwambia

    “Msijidanganye vijana mimi simuamini mtu yeyote kati yenu. Mmemuua

    mke wangu, mmewaua watoto wangu na sasa mnataka eti niwaamini kirahisi”

    Jaji Makesa aliongea kwa sauti ya kitetemeshi yenye hofu na mashaka halafu

    akasimama kwa tahadhari kisha akaanza kutembea taratibu akielekea sehemu

    moja mle ndani iliyokuwa na kabati chakavu. Alipofika akafungua droo moja

    ya kabati lile na kuchukua bastola na hapo sote tukashtuka kwa tukio lile, Drel

    Fille akataka akimbie kumuwahi lakini niliwahi kumzuia.

    “Huoni kuwa anataka kujiua?

    “Hatuwezi kumzuia” nilimwambia

    “Hapana hatuwezi kumuacha ajiue sasa hapo si kila kitu kitakuwa kimehari-

    bika? Drel Fille alinong’ona kwa jazba akionesha kutokukubaliana kabisa na

    uamuzi wangu.

    “Tumeishachelewa mpenzi na hatua moja tu utakayoitupa kumkaribia ataki-

    fumua kichwa chake ni afadhali tumuache azungumze” nimwambia Drel Fille

    na hapo akasimama huku akimtazama Jaji Makesa kwa mashaka.

    “Sasa tunafanyaje? Drel Fille aliniuliza kwa hamaki na hapo Jaji Makesa

    akavunja ukimya

    “Nimeishi ndani ya chumba hiki kwa zaidi ya miaka mitatu sasa nikiwa

    kama panya aishiye shimoni kuwakimbia paka wakubwa wenye njaa kali.

    Mimi ni panya mdogo sana na sina haki yoyote mbele ya paka wakubwa

    na wenye njaa kali ambao ni wengi katika nchi hii, na haya yote yananitokea

    kwa sababu ya ukweli wangu ulioniponza na kuipelekea roho yangu iwindwe

    usiku na mchana kama kito cha thamani sana kwa watu wenye kiu ya utajiri.

    Muda si mrefu nchi hii itatumbukia kwenye machafuko ya kihistoria yenye

    unyama usio na mfano.

    Natambua vizuri kuwa vijana mnayo dhamira ya kweli kabisa ya kuta-

    ka kuniokoa katika kadhia hii lakini si rahisi kama mnavyodhani na nyinyi

    si watu wa kwanza kujaribu kufanya hivyo” Jaji Makesa aliongea na hapo

    nikamuona akifungua droo nyingine ya lile kabati na kutoa bahasha kubwa

    ya kaki na kuitupa juu ya meza chakavu yenye vumbi iliyokuwa mle ndani.

    “Napaswa kuwaamini tu hata kama sijisikii kufanya hivyo. Kwa kipindi

    kirefu cha maisha yangu hapa duniani nimekuwa mstari wa mbele katika ku-

    tetea usawa na haki kwa binadamu wote pasipo kuegemea misingi ya ukabila,

    udini, hali za vipato vya watu au rangi zao. Hata hivyo nimegundua kuwa

    mimi ni tofauti na wenzangu na mbaya zaidi siwezi kuwalazimisha wakione

    kile ambacho ninakiona katika taifa hili.

    Ni wakati wa nyinyi kuitahadharisha dunia juu ya umwagaji damu uliopang-

    wa kufanyika katika nchi hii lakini kwangu ni afadhali kwani pindi tukio hilo

    litakapotokea mimi sitakuwepo.

    Bahasha hiyo ina majina ya wahusika waliopo nyuma mpango huo mchafu

    wa umwagaji damu na vielelezo vyote vya ushahidi vinavyoweza kutumika

    kuwatia hatiani watu hao.

    Siyo kazi rahisi lakini naamini kuwa mnaweza kuifanya. Nawatakia haraka-

    ti njema zenye mafanikio” Jaji Makesa alimaliza kuongea na tukiwa katika

    hali ile ya kutafakari maneno yake ghafla tuliomuona akiinyanyua ile bastola

    yake mkononi na kuielekeza kwenye tundu la mdomo wake na kabla hatu-

    jaamua tufanye nini Jaji Makesa alivuta kilimi cha bastola yake na tukio lile

    tuliloliona kamwe halitofutika katika fikra zetu daima.

    Kufumba na kufumbua kichwa cha Jaji Makesa kilitawanyika na ubongo

    wake ukachanguka ovyo, shingo yake ikabaki kama kichuguu na hapo kiwi-

    liwili chake kikaanguka chini na kuanza kurukaruka huku na kule na muda

    mfupi baadaye kilitulia pale chini huku kikivuja damu na ule ndiyo ukawa

    mwisho wake.

    Hofu ilitushika na hakuna aliyependa kuundelea kukaa ndani ya chumba

    kile kidogo nyenye harufu kali mfano wa pango la mwendawazimu. Hivyo

    niliichukua ile bahasha ya Jaji Makesa iliyokuwa juu ya ile meza kisha nikam-

    shika mkono Drel Fille ambaye alikuwa ameanza kulia na hapo nikamvuta

    taratibu yukielekea nje.



    #318

    SAFARI YA KURUDI HOTEL DES MILLE COLLINES ilikuwa fupi lakini

    iliyopoteza amani na utulivu wa mazingira na nafsi zetu.

    Tukiwa tumebakisha mitaa minne kabla ya kuifikia Hotel des Mille Collines

    tulipishana na kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbia kuelekea kule tu-

    lipotoka hivyo tukaamua na sisi kubadilisha uelekeo na kushika njia nyingine

    ambayo haikuwa na msongamano mkubwa wa watu. Hata hivyo hali ile ilin-

    ishangaza sana na kwa haraka sikutaka kuamini kile nilichokuwa nikikiwaza

    kichwani.

    Njiani tulipishana na magari makubwa ya jeshi yaliyokuwa yamebeba wa

    najeshi nyuma yake. Wanajeshi wale walijaribu kutusimamisha lakini sikuwa

    tayari kutii amri yao hivyo nikakanyaga mafuta na kuendesha gari kwa kasi na

    baada ya kuingia mtaa huu na kutokea ule hatimaye tukawa tumefika Hotel des

    Mille Collines. Hata hivyo idadi kubwa ya watu, wamama, vijana, watoto na

    wazee waliokuwa wakikimbilia kwenye hoteli ile ilizidi kutuchanganya zaidi.

    Nilikumbuka kuitazama saa yangu ya mkononi wakati tulipokuwa tukita-

    futa maegesho nje ya hoteli ile ambayo wakati huu ilikuwa imefurika watu

    wengi kuliko wingi wa magari.

    Ilikuwa ikielekea kutimia saa mbili usiku na sikupenda tena kuitazama saa

    ile kwani muda ule ulikuwa una maana kubwa sana kwangu na hapo hofu

    ikaniingia.

    Baada ya kupata maegesho mazuri tulishuka kwenye gari tukaelekea ndani

    ya hoteti ile na tulipofika eneo la mapokezi nikashtuka baada ya kuona mle

    ndani kulikuwa na idadi kubwa ya wazungu na watu wa kutoka bara la Asia

    kushinda jamii ya watu weusi na hali hiyo ikanifanya nimuulize mmoja wa

    wahudumu wa hoteli ile niliyekuwa nimeanza kuzoeana naye

    “Kuna nini hapa? nilimuuliza yule mhudumu kwa shauku

    “Ndege ya rais imedunguliwa wakati ilipokuwa ikijiandaa kutua uwanja

    wa ndege wa kimataifa wa Kigali” maneno ya mhudumu yule yakalipelekea

    koo langu kukauka kwa ghafla, moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na hapo

    jasho jepesi likaanza safari kwenye sehemu mbalimbali za mwili wangu.

    Drel Fille aliyekuwa pembeni yangu akiyafuatilia maongezi yale hakuhi-

    taji kuelezwa zaidi na badala yake nilimuona akijiegemeza pale mapokezi na

    kuinamisha kichwa chake chini katika hali ya kukata tamaa.

    “Nani aliyekupa taarifa hizo? nilimuuliza yule mhudumu na hapo nikamu-

    ona akinishangaa

    “Vyombo vya habari vinazungumza hivyo hata sasa ukifungua utasikia”

    “Oh! my God” nilibwatuka na yule mhudumu akanitazama kama ananye-

    nionea huruma ingawa hakuna aliyekuwa na afadhali miongoni mwetu.

    “Serikali imetoa tamko gani?

    “Kwa sasa jeshi ndiyo limeshika hatamu na tutaendelea kufahamishwa ki-

    nachoendelea”

    Niligeuka nikamtazama Drel Fille pembeni yangu kisha nikamuonesha is-

    hara kuwa tuelekee kule chumbani na muda mfupi baadaye tulikuwa tukipan-

    da ngazi kuelekea kule chumbani.

    __________

    TULIMKUTA MUTESI NA DIANE wakiwa wamejikunyata kwa hofu

    huku wakitazama runinga iliyokuwa mle ndani na wote walishtuka sana baada

    ya sisi kufungua mlango na kuingia mle ndani.

    Kulikuwa na namna fulani ya kukata tamaa katika nyuso zao. Matikuo yali-

    yokuwa yakirushwa hewani kupitia kituo kile cha runinga yaliufanya moyo

    wangu upoe kwa ghafla kama kiumbe kinachoelekea kupoteza uhai.

    Katika baadhi ya mitaa ya jiji la Kigali makundi vya vijana wenye mapanga,

    mashoka, marungu, visu, bunduki na mabomu ya kutupa kwa mkono yaliku

    wa yakirandaranda mitaani na kuwakamata watu na kuvikagua vitambulisho

    vyao, na wale waliooneka kutokukidhi vigezo waliuwawa kwa kukatwakatwa

    na mapanga mwili mzima.

    Sote tukiwa tunaendelea kutazama ile runinga tulimuona mama mmoja

    na binti yake wakifukuzwa na vijana hao na wale vijana walipowakamata

    wakaanza kuwabaka kwa zamu na hatimaye kuwaua kwa kuwatandika kwa

    marungu kichwani.

    Kufikia hapo sikuweza kuvumilia kwani Diane alikuwa akilia sana hivyo

    nikaenda kuizima ile runinga.

    “Tunahitajika kuondoka hapa muda huuhuu kabla ya mambo hayajahari-

    bika zaidi” niliwaambia Drel Fille, Mutesi na Diane na hapo wakageuka na

    kunitazama

    “Tutaondokaje wakati kila barabara imewekewa kizuizi? Drel Fille aliniuli-

    za kwa mshangao na wakati akiendelea kuongea mara tukasikia ule mlango

    wa chumba ukigongwa na hapo mimi na Drel Fille tukakimbia kujificha huku

    tukimtaka Mutesi afungue mlango na kuusikiliza ugeni ule.

    Mutesi akafanya kama tulivyomwambia na alipoufungua ule mlango me-

    neja wa hoteli ile mwanaume wa makamo alisimama mlangoni na kuongea

    “Kuna tetesi kuwa baadhi ya wanajeshi wa kikundi kinachosemekana

    kuhusika na machafuko haya cha Interahamwe wanapita kwenye nyumba za

    wageni na hoteli mbali mbali kuwatafuta watutsi ili wawauwe, na hapana sha-

    ka kuwa miongoni mwetu wapo watu wa kabila hilo.

    Uongozi wa hoteli unafanya kila jitihada za kuifanya sehemu hii iwe salama

    kwa kuomba ulinzi kwa vikosi vya walinzi wa amani wa umoja wa mataifa

    waliopo hapa nchini Rwanda UNAMIR. Hata hivyo makamanda wa kijeshi wa

    vikosi hivyo bado hawajatupa jibu la moja kwa moja.

    Ninachoweza kuwashauri kwa sasa ni kwamba kuweni makini sana na iki-

    wezekana kujificha katika sehemu salama zaidi huku mkimuomba Mungu.

    Hoteli ina mahitaji machache kufananisha na idadi ya watu iliyopo kwa sasa,

    hivyo ni vizuri mkaifahamu hali hii mapema zaidi.

    Kama wewe si raia wa Rwanda na una uthibitisho unaweza kuniona niku-

    kutanishe na balozi wako tayari kwa kukamilisha taratibu nyingine za kusafir-

    ishwa kurudi kwenu.

    Nawaomba muendelee kuwa watulivu kwani ni matumaini yangu vyombo

    vya usalama wa dunia vinafahamu kile kinachoendelea hapa Rwanda hivyo

    naamini kuwa tutapewa msaada muda si mrefu, ahsanteni!”

    Yule meneja wa hoteli alimaliza kuongea kisha akafunga mlango na

    kuelekea chumba cha pili. Ingawaje nilikuwa sijamuona wakati alipokuwa

    akizungumza lakini sauti yake ilitosha kinieleza kuwa alikuwa mbioni kuan-

    gusha chozi kwa simanzi.

    “Hatuwezi kuendelea kukaa hapa kwani hii ni sawa na kuwasubiri wauaji

    hao watufikie” niliendelea na msimamo wangu.

    “Sasa tutafanyaje? Drel Fille aliniuliza kwa mashaka

    “Tuna gari na lina mafuta ya kutosha, tunaweza kulitumia hilo kutorokea”

    “Na vizuizi vya barabarani je? Mutesi aliuliza



    SAFARI YA KURUDI HOTEL DES MILLE COLLINES ilikuwa fupi lakini

    iliyopoteza amani na utulivu wa mazingira na nafsi zetu.

    Tukiwa tumebakisha mitaa minne kabla ya kuifikia Hotel des Mille Collines

    tulipishana na kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbia kuelekea kule tu-

    lipotoka hivyo tukaamua na sisi kubadilisha uelekeo na kushika njia nyingine

    ambayo haikuwa na msongamano mkubwa wa watu. Hata hivyo hali ile ilin-

    ishangaza sana na kwa haraka sikutaka kuamini kile nilichokuwa nikikiwaza

    kichwani.

    Njiani tulipishana na magari makubwa ya jeshi yaliyokuwa yamebeba wa

    najeshi nyuma yake. Wanajeshi wale walijaribu kutusimamisha lakini sikuwa

    tayari kutii amri yao hivyo nikakanyaga mafuta na kuendesha gari kwa kasi na

    baada ya kuingia mtaa huu na kutokea ule hatimaye tukawa tumefika Hotel des

    Mille Collines. Hata hivyo idadi kubwa ya watu, wamama, vijana, watoto na

    wazee waliokuwa wakikimbilia kwenye hoteli ile ilizidi kutuchanganya zaidi.

    Nilikumbuka kuitazama saa yangu ya mkononi wakati tulipokuwa tukita-

    futa maegesho nje ya hoteli ile ambayo wakati huu ilikuwa imefurika watu

    wengi kuliko wingi wa magari.

    Ilikuwa ikielekea kutimia saa mbili usiku na sikupenda tena kuitazama saa

    ile kwani muda ule ulikuwa una maana kubwa sana kwangu na hapo hofu

    ikaniingia.

    Baada ya kupata maegesho mazuri tulishuka kwenye gari tukaelekea ndani

    ya hoteti ile na tulipofika eneo la mapokezi nikashtuka baada ya kuona mle

    ndani kulikuwa na idadi kubwa ya wazungu na watu wa kutoka bara la Asia

    kushinda jamii ya watu weusi na hali hiyo ikanifanya nimuulize mmoja wa

    wahudumu wa hoteli ile niliyekuwa nimeanza kuzoeana naye

    “Kuna nini hapa? nilimuuliza yule mhudumu kwa shauku

    “Ndege ya rais imedunguliwa wakati ilipokuwa ikijiandaa kutua uwanja

    wa ndege wa kimataifa wa Kigali” maneno ya mhudumu yule yakalipelekea

    koo langu kukauka kwa ghafla, moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na hapo

    jasho jepesi likaanza safari kwenye sehemu mbalimbali za mwili wangu.

    Drel Fille aliyekuwa pembeni yangu akiyafuatilia maongezi yale hakuhi-

    taji kuelezwa zaidi na badala yake nilimuona akijiegemeza pale mapokezi na

    kuinamisha kichwa chake chini katika hali ya kukata tamaa.

    “Nani aliyekupa taarifa hizo? nilimuuliza yule mhudumu na hapo nikamu-

    ona akinishangaa

    “Vyombo vya habari vinazungumza hivyo hata sasa ukifungua utasikia”

    “Oh! my God” nilibwatuka na yule mhudumu akanitazama kama ananye-

    nionea huruma ingawa hakuna aliyekuwa na afadhali miongoni mwetu.

    “Serikali imetoa tamko gani?

    “Kwa sasa jeshi ndiyo limeshika hatamu na tutaendelea kufahamishwa ki-

    nachoendelea”

    Niligeuka nikamtazama Drel Fille pembeni yangu kisha nikamuonesha is-

    hara kuwa tuelekee kule chumbani na muda mfupi baadaye tulikuwa tukipan-

    da ngazi kuelekea kule chumbani.

    __________

    TULIMKUTA MUTESI NA DIANE wakiwa wamejikunyata kwa hofu

    huku wakitazama runinga iliyokuwa mle ndani na wote walishtuka sana baada

    ya sisi kufungua mlango na kuingia mle ndani.

    Kulikuwa na namna fulani ya kukata tamaa katika nyuso zao. Matikuo yali-

    yokuwa yakirushwa hewani kupitia kituo kile cha runinga yaliufanya moyo

    wangu upoe kwa ghafla kama kiumbe kinachoelekea kupoteza uhai.

    Katika baadhi ya mitaa ya jiji la Kigali makundi vya vijana wenye mapanga,

    mashoka, marungu, visu, bunduki na mabomu ya kutupa kwa mkono yaliku

    wa yakirandaranda mitaani na kuwakamata watu na kuvikagua vitambulisho

    vyao, na wale waliooneka kutokukidhi vigezo waliuwawa kwa kukatwakatwa

    na mapanga mwili mzima.

    Sote tukiwa tunaendelea kutazama ile runinga tulimuona mama mmoja

    na binti yake wakifukuzwa na vijana hao na wale vijana walipowakamata

    wakaanza kuwabaka kwa zamu na hatimaye kuwaua kwa kuwatandika kwa

    marungu kichwani.

    Kufikia hapo sikuweza kuvumilia kwani Diane alikuwa akilia sana hivyo

    nikaenda kuizima ile runinga.

    “Tunahitajika kuondoka hapa muda huuhuu kabla ya mambo hayajahari-

    bika zaidi” niliwaambia Drel Fille, Mutesi na Diane na hapo wakageuka na

    kunitazama

    “Tutaondokaje wakati kila barabara imewekewa kizuizi? Drel Fille aliniuli-

    za kwa mshangao na wakati akiendelea kuongea mara tukasikia ule mlango

    wa chumba ukigongwa na hapo mimi na Drel Fille tukakimbia kujificha huku

    tukimtaka Mutesi afungue mlango na kuusikiliza ugeni ule.

    Mutesi akafanya kama tulivyomwambia na alipoufungua ule mlango me-

    neja wa hoteli ile mwanaume wa makamo alisimama mlangoni na kuongea

    “Kuna tetesi kuwa baadhi ya wanajeshi wa kikundi kinachosemekana

    kuhusika na machafuko haya cha Interahamwe wanapita kwenye nyumba za

    wageni na hoteli mbali mbali kuwatafuta watutsi ili wawauwe, na hapana sha-

    ka kuwa miongoni mwetu wapo watu wa kabila hilo.

    Uongozi wa hoteli unafanya kila jitihada za kuifanya sehemu hii iwe salama

    kwa kuomba ulinzi kwa vikosi vya walinzi wa amani wa umoja wa mataifa

    waliopo hapa nchini Rwanda UNAMIR. Hata hivyo makamanda wa kijeshi wa

    vikosi hivyo bado hawajatupa jibu la moja kwa moja.

    Ninachoweza kuwashauri kwa sasa ni kwamba kuweni makini sana na iki-

    wezekana kujificha katika sehemu salama zaidi huku mkimuomba Mungu.

    Hoteli ina mahitaji machache kufananisha na idadi ya watu iliyopo kwa sasa,

    hivyo ni vizuri mkaifahamu hali hii mapema zaidi.

    Kama wewe si raia wa Rwanda na una uthibitisho unaweza kuniona niku-

    kutanishe na balozi wako tayari kwa kukamilisha taratibu nyingine za kusafir-

    ishwa kurudi kwenu.

    Nawaomba muendelee kuwa watulivu kwani ni matumaini yangu vyombo

    vya usalama wa dunia vinafahamu kile kinachoendelea hapa Rwanda hivyo

    naamini kuwa tutapewa msaada muda si mrefu, ahsanteni!”

    Yule meneja wa hoteli alimaliza kuongea kisha akafunga mlango na

    kuelekea chumba cha pili. Ingawaje nilikuwa sijamuona wakati alipokuwa

    akizungumza lakini sauti yake ilitosha kinieleza kuwa alikuwa mbioni kuan-

    gusha chozi kwa simanzi.

    “Hatuwezi kuendelea kukaa hapa kwani hii ni sawa na kuwasubiri wauaji

    hao watufikie” niliendelea na msimamo wangu.

    “Sasa tutafanyaje? Drel Fille aliniuliza kwa mashaka

    “Tuna gari na lina mafuta ya kutosha, tunaweza kulitumia hilo kutorokea”

    “Na vizuizi vya barabarani je? Mutesi aliuliza

    “Tutajua nini cha kufanya pale tutakapokutana navyo”

    “Nyie nendeni mimi nitakisubiri hicho kifo nikiwa hapahapa” Mutesi

    aliongea katika namna ya kukata tama sana huku machozi yakimlengalenga

    “Kwa nini hutaki kuongozana na sisi? nilimuuliza

    “Mimi ni mtutsi na nina tabia zote zinazoonekana kwa macho, wataniua tu

    pindi watakaponishtukia. Nyinyi si wanyarwanda hivyo mna nafasi kubwa ya

    kuvivuka vizuizi hivyo vya barabarani pasipo kusumbuliwa”

    “Mimi pia nitabaki na Mutesi” Diane naye alidakia huku akiendelea kulia na

    hapo wote wakawa wakinitazama mle ndani. Mutesi alikuwa ameongea jambo

    lenye mantiki hata hivyo sikutaka kukubaliana naye. Nikiwa katika namna ile

    kufikiri niliisogelea ile runinga iliyokuwa mle chumbani na kuiwasha tena na

    hapo tukaona mauaji yaliyokuwa yakifanyika katika ile shule ya wasichana ya

    Sainte Anne Marie iliyokuwa ikimilikiwa na kanisa la Katoliki.

    Wanafunzi walikuwa wakitenganishwa kwa misingi ya ukabila na wale

    waliokuwa watutsi waliuwa. Halafu muda mfupi baadaye tulioneshwa mauaji

    mengine yaliyokuwa yakifanyika katika kanisa moja la Nyarubuye, nje kidogo

    ya jiji la Kigali. Nikaizima tena ile runinga na kugeuka kuwatazama wenzan-

    gu mle ndani na hapo nikatambua kuwa kila mmoja alikuwa na wazo lake

    kichwani hata hivyo sikuwa tayari kumuacha Diane kwani nilishakabidhi-

    wa na mama yake kule pangoni hivyo sikutaka damu yake idaiwe mikononi

    mwangu.

    Muda uleule nikachukua mfuko mkubwa nilioukuta mle ndani kwenye ka-

    bati la nguo kisha nikaenda na kufungua jokofu lililokuwa mle ndani. Kuliku-

    wa na vinywaji vingi na baadhi ya vyakula vya kopo, vyote nikavitia kwenye

    ule mfuko tayari kukiacha chumba kile.

    “Yeyote anayetaka kuongozana na mimi? niliwauliza tena huku nikiwa na

    hakika kuwa bastola nilizokuwa nazo zingeweza kunisaidia mbele ya safari.

    “Tunaondoka pamoja mpenzi wangu, ahadi yangu ya kuishi na wewe Tan-

    zania bado iko palepale” Drel Fille aliongea kwa kujiamini.

    “Tutaenda wote” Mutesi naye alidakia kwa sauti ya unyonge.

    “Na mimi pia” Diane naye aliongea na hivyo wote tukawa tumekubaliana

    kuwa tutaondoka kwa pamoja.

    Lakini kabla ya kuondoka mle ndani tulishikana mikono kwa pamoja na

    kufanya sala fupi ya kumuomba Mungu kuwa atuepushie na balaa lolote huko

    mbele ya safari. Baada ya sala ile ndefu tukatoka na kufunga ule mlango wa

    chumba.

    Wakati tukifika sehemu ya chini ya hoteli ile niligundua haraka kuwa idadi

    ya watu ilikuwa imeongezeka sana na kulikuwa na magari yaliyokuwa yakifi-

    ka pale hotelini kuwaleta wazungu waliokuwa wakikimbia machafuko toka

    katika vituo vyao kama seminari na hospitali. Magari hayo yalikuwa yaki-

    wabeba pia baadhi ya watu ambao walikuwa wamejeruhiwa baada ya macha-

    fuko yale kuanza.

    Kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wamepoteza viungo vyao kama

    mikono, masikio, vidole, pua hata miguu. Kwa kweli hali ilikuwa imechafuka

    sana na eneo lote lile lilikuwa limetawaliwa na vilio vya hofu.

    Kulikuwa na baadhi ya magari ya umoja wa mataifa UN yaliyokuwa ya-

    kiwasili pale hotelini. Magari hayo malori makubwa niligundua kuwa yali-

    kuwa yamekuja pale kuwachukuwa raia wa kigeni hususani wazungu wenye

    vielelezo vya ukazi.

    Kuyaona magari yale nikapata wazo, wazo la kujiunga na msafara wa magari

    yale kwa nyuma pale yatakapokua yakianza safari. Lakini kabla ya kuamua

    kujiunga kwenye mafara ule niliamua kwenda kuonana na kamanda mmoja

    wa vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani nchini Rwanda aliyekuwa

    akiongoza msafara ule, cheo na jina lake aliitwa Luteni Kanali Petit William.

    Nilipofika nikamsalimia kamanda yule wa kijeshi hata hivyo nilikutana na

    upinzani kidogo kwani mwenye shida kama yangu sikuwa mimi peke yangu.

    Nilijaribu kumuelezea shida yangu yule kamanda kuwa nilihitajia kujiunga na

    msafara wake hivyo nilimuomba anitetee pale ambapo ningekumbana na vik-

    wazo vya barabarani. Lakini kamanda yule alinikatalia katu akidai msafara wa

    magari ya UN ulikuwa ikitambulika kisheria na gari langu halikuwa kwenye

    idadi hiyo hivyo kama ningeamua kuwafuata kwa nyuma ni mimi mwenyewe

    ambaye ningewajibika kwa lolote ambalo lingetokea huko mbele ya safari.

    Sikuwa na namna hivyo nilirudi kule kwenye gari letu Volkswagen Comb,

    nikawakuta Drel Fille, Mutesi na Diane wakiwa wananisubiri na wote wali-

    kuwa wakitaka kufahamu juu ya jibu la ombi langu. Nikawaambia kuwa tuli-

    kuwa tumekataliwa hata hivyo niliwatoa hofu kuwa bado safari yetu ilikuwa

    palepale huku nikijitahidi kupambana na hofu katika nyuso zao.

    “Tunahitaji kwanza kuwa na uhakika wa barabara itakayoweza kutufikisha

    katika mpaka wa Tanzania na Rwanda” Drel Fille aliongea

    “Mimi naifahamu hiyo barabara, nimewahi kusafiri kwenda mkoani Kagera,

    Tanzania mara kwa mara’’ Mutesi alidakia na hapo wote tukageuka na kumta-

    zama tukiwa na robo ya matumaini ya safari yetu.

    Nilimtazama Diane na kumuona kuwa alikuwa na mashaka sana hata hivyo

    sikumsemesha.

    Wale wazungu waliokuwa ndani ya hoteli wakati huu walikuwa wakitoka na

    kuingia kwenye yale malori baada ya kuonesha vitambulisho vyao pamoja na

    baadhi wa wageni wengine weusi kama mimi. Askari wa UN walikuwa waki-

    wazuia watu wengine waliokuwa wakiyakaribia yale malori ambao hawakuwa

    na vibali kwa kufyatua risasi angani.

    Watu wengi walikuwa wakiendelea kumiminika kwenye ile hoteli wakikim-

    bia mapigano sehemu mbalimbali katika jiji la Kigali kwani bila shaka huenda

    pale hotelini ndiyo palionekana kuwa ndiyo sehemu pekee yenye usalama.

    Milio ya risasi ilikuwa ikisikika kwa mbali toka pale tulipokuwa na tulikuwa

    tukiona vichuguu vya milipuko na moshi ukisambaa angani jirani na hoteli ile.

    Wakati nikisubiri ule msafala uanze ili na sisi tujiunge kwa nyuma niliu-

    kumbuka balozi wa Tanzania pale nchini Rwanda, kuwa angekuwa msaada

    mkubwa katika kuifanikisha safari yetu lakini nilipokumbuka kuwa balozi wa

    ubalozi ule alikuwa amesafiri kikazi kurudi nchi Tanzania niliachana kabisa

    na fikra zile.



    #321

    SAA TATU KASORO USIKU ule msafara wa magari ya UN ulianza kuondo-

    ka pale hotelini. Kulikuwa na malori makubwa sita na magari madogo mawili

    na yote yakiwa na nembo za UN ubavuni.

    Niliwasha gari na kujiunga na msafara ule kwa nyuma na wakati nikifanya

    vile nikagundua kuwa sikuwa peke yangu kwani nyuma yangu kulikuwa na

    magari mawili mengine ya watu binafsi yaliyonifuata kwa nyuma yangu.

    Wakati tukiondoka eneo lile la Hotel des Mille Collines nilisikia vilio vya

    akina mama na watoto waliokuwa wakilia kwa kuachwa na wale askari wa UN

    bila ulinzi na hali ivileinihuzunisha sana hata hivyo sikuwa na namna yaku-

    wasaidia ingawaje niliumia sana.

    Tulitembea kwa umbali mrefu nyuma ya msafara ule wa UN na tukiwa

    tunaendelea na safari njiani niliweza kuziona maiti nyingi zikiwa zimetelekez-

    wa ovyo barabara na kuna wakati tulilazimika kukanyaga juu ya maiti hizo

    pale tulipokuta zimelundikwa barabarani.

    Kwa kweli hali ilikuwa inatisha sana na kadiri usiku ulivyokuwa ukizidi

    kuingia ndiyo mashaka nayo yalivyokuwa yakizidi kuongezeka.

    Yale malori ya UN yalikuwa yakizidi kutokomea mbele yetu na mimi siku-

    taka yaniache. Drel Fille ambaye alikuwa ameketi pembeni yangu tulikuwa

    tumekubaliana kuwa endapo kungetokea rabsha yoyote njiani awe tayari kuji-

    bu mashambulizi haraka ili lengo letu litimie. Diane alikuwa akilia na Mutesi

    alijitahidi kwa kila hali kumfariji na hali hiyo ilinipa faraja kidogo.

    Wakati tukiendelea na safari tuliona baadhi ya nyumba zikiwa zinateketea

    kwa moto huku sauti za vilio na mayowe ya hofu zikihanikiza. Nchi nzima ya

    Rwanda ilikuwa ikinuka damu na hadi pale tulipofika kuziona maiti za watu

    halikuwa jambo la kushangaza tena.

    Tulikuwa tumeziona maiti za kila aina na zenye majeraha yasiyo tazamika

    kwa urahisi na hapo nikayakumbuka maneno ya Jaji Makesa juu ya umwagaji

    damu wa kutisha uliokuwa mbioni kutokea kwenye nchi hii.

    Hali ya mambo ilivyokuwa ilikuwa imenichanganya na kunikatisha tamaa

    sana. Niliona ni kama lilikuwa tukio la kufikirika lakini haikuwa vile kwani

    lilikuwa ni tukio la kweli na lililonishangaza sana.

    __________

    TULIKUWA TUMESAFIRI umbali wa zaidi ya kilometa ishirini pale tuli-

    poyaona yale malori ya UN yakipunguza mwendo na hapo nikahisi kule mbele

    kulikuwa na rabsha.

    Akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka, nilimtazama Drel Fille pembe-

    ni yangu nikamuona kuwa alikuwa amejiandaa kwa lolote hivyo na mimi

    nikaisunda vizuri bastola yangu mafichoni tayari kwa lolote.

    Muda mfupi baadaye yale malori ya UN mbele yetu yalisimama na hapo

    tukasikia makelele ya watu wakishangilia kama wehu. Mle ndani ya gari nili-

    wasihi watu wasiwe na hofu ila wawe tayari kukabiliana na lolote.

    Haukupita muda mrefu mara niliwaona madereva wa yale malori ya UN

    wakishuka chini na hapo nikawaona vijana wenye bunduki, mapanga na

    marungu wakija kukagua kwenye yale malori.

    Ukaguzi ule ulipoisha niliwaona baadhi ya watu wakishushwa chini toka

    kwenye yale malori kisha yale malori yakaruhusiwa kuendelea na safari. Wale

    watu walioshushwa walihojiwa kidogo na kisha wakakusanywa barabarani na

    hapo kilichofanyika kilinitia simanzi sana.

    Mtu wa kwanza alikabidhiwa panga na kulazimishwa amfyeke mwenzake

    na mtu yule aliyefekwa alipokufa mwingine alikabidhiwa tena lile panga

    amuue yule muuaji wa awali. Zoezi hilo liliendelea hadi pale alipobakia mtu

    wa mwisho na yule mtu wa mwisho aliuwawa kwa risasi huku wauaji wale

    wakishangilia.

    Zoezi lile lilipomalizika wale wauaji walihamia kwetu na mimi sikutaka

    kuonesha ukaidi wa namna yoyote mbele yao kwani nilipanga kutumia akili

    zaidi kabla ya nguvu kutumika baadaye.

    Kilikuwa kikundi cha watu ishirini na nane na ishirini na sita kati yao wali-

    kuwa na silaha za jadi kama marungu, mapanga na visu na wawili waliosalia

    ambao ndiyo walioonekana kuwa ni viongozi wa kizuizi kile walikuwa na

    bunduki mikononi mwao.

    Niliwatazama watu wale wakati wakilikaribia gari letu na hapo nikapiga

    moyo konde na kumtaka Drel Fille akae tayari wa lolote.

    “Wote shukeni chini” mmoja alituamrisha kwa lugha ya kinyarwanda na

    hapo nikashusha kioo cha gari na kuwatazama. Ila kwa kuwa ilikuwa usiku

    wale watu wakawasha tochi na kuanza kutumulika mle ndani, mmoja baada ya

    mwingine na kitendo kile kilinikera sana hata hivyo sikuwa na namna.

    “Mnaenda wapi? mwingine aliuliza

    “Ngara, mkoani Kagera, Tanzania” niliwajibu

    “Nyinyi ni watanzania?

    “Ndiyo”

    “Tunataka kuona vitambulisho vyenu” kiongozi wao mmoja mwenye bun-

    duki aliongea na hapo nikatoa kitambulisho changu cha bandia toka kwenye

    wallet na kuwapa. Tule kiongozi wao alikipokea kitambulisho kile kisha aka-

    kitazamatazama na kunirudishia lakini niligundua kuwa hakuwa ameridhika.

    “Na hao wengine vitambulisho vyao viko wapi?

    “Huyu ni mke wangu, huyu ni shemeji yangu na huyu ni mtoto wetu. Vitam-

    bulisho vyao wamevisahau kwenye begi wakati tulipokuwa tukifanya haraka

    kuondoka” nilijaribu kutunga uongo na yule kamanda akacheka kwa kejeli.

    “Kwanini mlifanya haraka kuondoka? mwenzake aliuliza huku akicheka

    “Ubalozi wetu umefungwa kwa muda kwa hiyo hakuna shughuli inayoen-

    delea kwa sasa ndiyo maana nikaonelea nirudi na familia yangu nyumbani

    Tanzania”

    “Mbona hawa siyo watanzania hata wewe mwenyewe ukiwatazama tu una-

    gundua” mmoja alidakia.

    “Unatudanganya siyo eh” yule kiongozi wao aliuliza kwa hasira

    “Hapana si hivyo mnavyodhani”

    “Inyenzi...! ’’ mmoja alisikika akisema na hapo wote wakacheka

    “Wote shukeni chini” kiongozi wao mmoja aliongea kwa hasira

    Niliwatazama wale watu na nilipoona kuwa hawaelekei kunielewa nikafun-

    gua mlango wa gari na kushuka. Drel Fille aliwahi kunishika mkono akinizuia

    lakini nilimuonesha ishara kuwa asiwe na wasiwasi.

    Niliposhuka kwenye gari wale watu walinizingira wakinizongazonga na

    hapo nikaona hali ilikuwa ikielekea kuwa mbaya zaidi.

    Nikiwa pale nje niligeuka kumtazama Drel Fille na hapo akaelewa kuwa

    nilikuwa nikimaanisha nini. Sasa akili yangu yote ilikuwa kwa wale viongozi

    wao wawili wenye bunduki.

    Kwa kuzingatia kuwa nilikuwa komandoo niliyehitimu vizuri katika medani

    za mapambano ya kivita wale watu walipokuwa wakinizongazonga nilijisoge-

    za kwa hila karibu na yule kiongozi wao mmoja mwenye bunduki huku niki-

    jidai kuwasihi watuache.

    Nilipofika kwenye usawa mzuri wa kufanya mashambulizi kufumba na ku-

    fumbua nikawa nimemdhibiti yule kiongozi wao mmoja kwa kabari ya nguvu

    huku bastola yangu ikiwa kichwani mwake.

    “Wekeni silaha zenu chini kama mnapenda kumuona mwenzenu anaendelea

    kuishi” wale watu walitaharuki na muda uleule Drel Fille akamchakaza kwa

    risasi yule kiongozi wao mwingine mwenye bunduki.

    Kuona vile wale wenzake wakaanza kurudi nyuma na hapo Drel Fille

    akashuka na kuikota ile bunduki ya yule kiongozi wao aina ya AK-47. Yule

    mtu niliyemdhibiti nikamshona risasi ya kichwa na aliponguka chini nikaic-

    hukua ile bunduki yake.

    Wale vijana kuona vile wakataka kukimbia lakini hakuna aliyefika mbali

    kwani wote tuliwafyeka kwa risasi na hapo tukarudi haraka kwenye gari na

    safari ikaanza.

    Mutesi na Diane walikuwa wameshangazwa sana na tukio lile hata hivyo

    hatukuwa na muda wa kupoteza.

    Yale malori ya UN yalikuwa yameisha tuacha hivyo hatukuwa na namna

    tena badala yake Mutesi ndiyo akawa anatueleza sehemu ya kupita.

    Wakati tukiendelea na safari njiani bado tuliendelea kuziona maiti nyingi

    sana zikiwa zimetawanywa ovyo barabarani. Nilijitahidi kuzikwepa nisizikan-

    yage lakini wakati mwingine nilishindwa hivyo nikapita juu yake ingawa roho

    iliniuma sana.

    Safari iliendelea usiku mzima na kuna wakati tulilazimika kubadili njia pale

    tulipoona kuwa kulikuwa na vizuizi vya Interahamwe mbele yetu.

    Kwa mujibu wa maelezo ya Mutesi ni kuwa katika uelelekeo ule hatukuwa

    mbali sana na ulipo mpaka wa Rwanda na Tanzania na hilo lilinitia moyo sana.

    Wakati tukiendelea na safari nilianza kushawishika kumueleza Drel Fille

    juu ya mashaka niliyokuwa nayo kwa mratibu wangu wa safari za kijasusi,

    Brigedia Masaki Kambona.

    Sikufahamu haraka ni nini kilinishawishi kufanya vile lakini huenda niliona

    ni wakati sahihi wa kueleza hisia zangu.

    __________

    NAKUMBUKA KUWA ILIKUWA SAA KUMI USIKU kasoro dakika

    chache pale tulipokutana na kizuizi kingine cha Interahamwe barabarani. Na

    wakati huo tulikuwa peke yetu kwani ile yale magari mengine yaliyokuwa

    yakitufuata nyuma yetu tulikuwa tumeyaacha kule nyuma na hatukuwa tuki-

    fahamu habari zake.

    Kizuizi hiki kilikuwa kikubwa zaidi na chenye watu wengi wenye bunduki.

    Wakati tukisimamishwa nilitazama pembeni ya kizuizi kile na hapo nikao-

    na maiti nyingi zikiwa zimelundikwa kando yake. Nilikata tamaa zaidi baada

    ya kuona kulikuwa na kichwa mtu kilichokuwa kimekatwa na kuchomekwa

    kwenye mti uliokuwa pembeni yake.

    Hofu ikiwa imetushika safari hii sikutaka kushuka kwenye gari na badala

    yake nilimwambia Drel Fille ajiweke tayari kwa lolote. Niliposimamishwa

    tu viongozi wa vizuizi vile walioonekana kuwa makatili zaidi walilisogelea

    gari letu na wakati wakilisogelea walisita halafu nikamuona mmoja akim-

    nong’oneza jambo mwenzake na ile kwangu ilikuwa ishara mbaya.

    “Shukeni chini wote” kiongozi wao aliyevaa suruali ya jeshi na fulana

    nyekundu alituamrisha huku akisogea mbali na gari lile na wakati akifanya

    vile niliongeza mwanga wa taa kumulika mbele huku nikijidai natafuta mae-

    gesho mzuari, na hapo nikaziona picha zetu, mimi na Drel Fille zikiwa zi-

    mening’inizwa mbele ya kizuizi kile kama watu hatari tunaotafutwa.

    Drel Fille alikuwa ameziona picha zile hivyo alianza kunionya juu ya hatari

    ya kusimama eneo lile.

    Nilipokuwa najidai kujiandaa kusimama Drel Fille akasogeza kioo cha gari

    kwa siri na kuupenyeza mtutu wa bunduki na hapo mvua ya risasi ikaanza

    kusikika. Mimi kuona vile nikaingiza gia na kukanyaga mafuta na kwa kuwa

    mbele yetu kulikuwa na kizuizi ikanibidi nipite katikati ya kile kizuizi na kuki-

    bomoa hali iliyopelekea taa za mbele na kioo cha mbele cha gari letu kupa-

    suka.

    Sikutaka kusimama hata hivyo nikaanza kusikia tukitupiwa risasi kwa nyu-

    ma na hapo nikawaambia watu wote mle ndani ya gari walale chini.

    Risasi zile zilipasua kioo cha nyuma cha gari letu na baada ya muda gu-

    rudumu la nyuma la upande wa kushoto nalo likapasuliwa kwa risasi lakini

    sikusimama badala yake nikatia moto nikiliendesha lile gari vilevile.

    Hatukufika mbali sana pale niliposikia mshindo mkubwa wa ajabu na hapo

    nikaliona gari letu likinishinda nguvu huku likiyumbayumba ovyo. Nilijitahidi

    kulidhibiti lakini haikuwa kazi rahisi hivyo nililiona gari lile likiacha barabara

    na kuingia vichakani na hapo nikasikia watu wote mle ndani wakipiga mayowe

    ya hofu. Hata hivyo tukio lile lilikuwa nje ya uwezo wangu.

    Muda mfupi baadaye tuligonga kitu ambacho sikukitambua haraka kutoka-

    na na giza la usiku na baada ya hapo sikufahamu kilichoendelea.

    ____________

    KAMBI YA WAKIMBIZI YA BENACO wilayani Ngara, mkoani Kagera il-

    ikuwa imefurika watu waliokata tamaa sana. Wengi wao walikuwa wakimbizi

    wa kitutsi na baadhi ya wahutu wenye msimamo wa wastani.

    Drel Fille aliwasili kwenye kambi hiyo ya wakimbizi huku akiwa amembe-

    ba Luteni Venus Jaka begani na Diane akiwa anamfuata kwa nyuma.

    Ilikuwa safari ndefu ya masaa yasiyopungua saba na njiani waliongozana na

    kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbia mapigano na kuelekea kwenye

    kambi ile.

    Wapo baadhi ya wazazi ambao waliwaacha watoto wao njiani baada ya ku-

    choka kuwabeba na kuna wengine walipoteana kabisa na ndugu zao.

    Drel Fille akiwa amembeba Luteni Venus Jaka njiani alikuwa amekutana na

    Jèrome Muganza ambaye kwa haraka alipomtazama Luteni Venus Jaka alim-

    kumbuka. Hivyo akaamua kufanya hisani kwa kumsaidia Drel Fille kumbeba

    kuelekea kwenye kambi ile ya wakimbizi.

    Mutesi alikuwa amekufa kule kwenye lile gari walilolitelekeza kule porini

    kwani zile risasi zilizokuwa zikifyatuliwa nyuma yao muda mfupi kabla hawa-

    japata ile ajali, moja ilikuwa imepenya mgongoni na kupotelea kwenye moyo

    wake na jeraha hilo lilikuwa limempelekea apoteze damu nyingi na hatimaye

    kuaga dunia akiwa ndani ya lile gari.

    Mara baada ya ajali ile kutokea Drel Fille alimchukua Luteni Venus Jaka

    na kumbeba begani na kisha wakapotelea kule msituni na Diane kabla ya baa-

    daye kuja kukutana na barabara yenye wakimbizi wengi na hapo ikawa salama

    kwao. Wakajichanganya na wakimbizi wale wakielekea kambi ya wakimbizi

    ya BENACO.

    Wakati wakivuka daraja la Rusumo waliziona maiti nyingi sana zikielea juu

    ya maji ya mto ule huku zikiwa zimeharibika vibaya.

    Mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha ilikuwa ikizisomba maiti hizo

    na kuzisafirisha hadi kwenye mto Rusumo, zikiendelea mbele na safari na kwa

    hakika hali ile ilitisha.

    __________

    KAMBI YA WAKIMBIZI YA BENACO ilifurika vilio vya watu wenye ma-

    tatizo ya kila namna. Shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa la

    UNHCR lilikuwa limeweka mahema kwa ajili ya makazi ya wakimbizi hao

    kwa muda na pia kulikuwa na msaada wa kitabibu kwa watu wenye majeraha.

    Vilevile kulikuwa na msaada wa chakula na ushauri nasaha juu ya macha-

    fuko yale ingawaje mahitaji bado yalikuwa madogo ukilinganisha na idadi ya

    watu. Hivyo uharibufu wa mazingira nao uliongezeka kwa vitendo vya watu

    kukata miti ovyo kwa ajili ya kujengea nyumba na matumizi ya kuni.

    Kulikuwa na utaratibu kuwa kila mkimbizi alipaswa kujiandikisha jina lake

    na sehemu anayotoka huko nchini Rwanda kwenye kambi ile ili iwe rahisi kwa

    ndugu kutafutana.

    Mara tu walipowasili kwenye kambi ile Jèrome Muganza aliamua kujichan-

    ganya kivyake akiwaacha Drel Fille, Luteni Venus Jaka na Diane huku akidai

    kuwa kuambatana kule kungemponza kwani yeye alikuwa akitafutwa sana na

    washirika wa Interahamwe. Jèrome Muganza pia alimtaka Drel Fille amu-

    ombee msamaha kwa Luteni Venus Jaka pale ambapo afya yake ingeimarika

    kwa kumwambia kuwa alishawishika kumtoroka kule mapangoni baada ya

    kuwa na wasiwasi naye lakini baadaye alikuja kugundua kuwa alifanya ma-

    kosa.

    Mwisho wakapeana anwani za kutafuta na kisha wakaagana kila mmoja aki-

    shika hamsini zake.

    Kabla ya yote mara tu walipoingia kwenye kambi ile ya wakimbizi Drel

    Fille aliichukua ile bahasha yenye vielelezo vya ushahidi waliyoipata kwa Jaji

    Makesa na kiasi cha pesa walichokuwa nacho, kisha kwa njia za panya akavi-

    tuma vitu hivyo kwenye sanduku la posta la Luteni Venus Jaka kwenye ofisi

    za posta iliyokuwa karibu na eneno lile.

    Baadaye alimkutanisha Luteni Venus Jaka na baadhi ya maafisa wa jeshi la

    Tanzania waliokuwa wakitoa msaada kwenye kambi ile huku Luteni Venus

    Jaka akiwa bado hajitambui.

    Maafisa wale walimshukuru sana Drel Fille kwa kuyaokoa maisha ya Lu-

    teni Venus Jaka hadi kumfikisha kwao. Baadaye kwa msaada wa helikopta ya

    kijeshi Luteni Venus Jaka alisafirishwa hadi Dar es Salaam kupewa matibabu

    kwenye hospitali ya kijeshi.

    Drel Fille hakuishia pale bado aliwaeleza maafisa wale juu ya mashaka aliy-

    okuwa nayo Luteni Venus Jaka juu ya kiongozi wake wa operesheni za kijeshi

    Brigedia Masaki Kambona, na maafisa wale kuona vile wakamshukuru sana

    Drel Fille na kuamua kuongozana naye pamoja na Diane kama sehemu ya

    ushahidi wa kuaminika.

    Hivyo Drel Fille na Diane wakawa wameingia kwenye orodha watu wali-

    omsindikiza Luteni Venus Jaka hadi jijini Dar es Salaam hospitali.

    MIAKA MIWILI BAADAYE

    JOPO LA MADAKTARI WA KIJESHI lilijiridhisha kuwa Luteni Venus Jaka

    alikuwa amepona kabisa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu uitwao AMNE-

    SIA baada ya kichwa chake kuwa kimepata misukosuko mikubwa hadi ile ajali

    iliyompelekea apoteze fahamu na kumbukumbu zote

    Maelezo ya Luteni Venus Jaka yalisaidia kwa kiasi kikubwa kukamatwa

    kwa Brigedia Masaki Kambona. Na hapo ndiyo ikajulikana kuwa Brigedia

    Masaki Kambona hakuwa mtanzania ila mnyarwanda wa kabila la kihutu ali-

    yejipenyeza nchini miaka mingi iliyopita. Akajifunza vizuri lugha ya kiswahili

    na kupata elimu yake katika shule na vyuo vya Tanzania kabla ya kujiunga na

    jeshi akiaminika kuwa ni mtanzania. Hivyo basi alikuwa akiwasaidi wahutu

    wenzake katika ule mpango mchafu wa umwagaji damu kwa kuvujisha siri,

    kuwasaidia pesa na hata mbinu za kijeshi kwa siri.

    Vielelezo hivyo vikamtika hatiani Brigedia Masaki Kambona pamoja na

    ushahidi wa nyaraka alizokutwanazo baada ya kufanyiwa upekuzi wa kina

    nyumbani na ofisi kwake.

    Baadaye alihukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya uhalifu wa ki-

    vita na uvunjifu wa haki za binadamu huko The Hague nchini Uholanzi. Na

    baada ya kesi ya Brigedia Masaki Kambona kuisha, Luteni Venus Jaka akawa

    amepata picha kamili juu ya mambo yalivyokuwa, kwamba Brigedia Masaki

    Kambona hakuwa Mtanzania. Lakini vilevile kwa kuwa Luteni Venus Jaka ali-

    kuwa ndiye mpelelezi mahiri sana ambaye angeweza kutumwa nchini Rwanda

    na kurudi na majibu sahihi hivyo ulikuwa ni mpango wa Brigedia Masaki

    Kambona kummaliza Luteni Venus Jaka kabla hajaileta ripoti yake na baada

    ya hapo ukweli wa mambo usingejulikana na hivyo wahusika wa mauaji yale

    ya Rwanda wasingekamtwa.

    _________

    AKIWA NA VIELELEZO VYA KUTOSHA, jopo la mawakili wa kesi za

    mauaji ya Rwanda zilizokuwa zikisikilizwa katika mhakama ya ICTR-Inter-

    national Criminal Tribunal for Rwanda mkoani Arusha, Tanzania. Lilimtaka

    Luteni Venus Jaka kwenda kutoa ushahidi wake kwa baadhi ya washukiwa

    wa mauaji hayo waliokamatwa ambao Luteni Venus Jaka alikuwa na ushahidi

    dhidi yao.

    Mawakili hao walituma ombi hilo baaada ya kupata uthibitisho toka kwa

    madaktari kuwa Luteni Venus Jaka alikuwa amepona kabisa, mwenye afya

    njema na fahamu zake zote zilikuwa zimerudi.

    Luteni Venus Jaka alilipokea ombi hilo kwa mikono miwili akapewa tiketi

    ya ndege na kusafiri hadi mkoani Arusha ambapo alishiriki kikamilifu katika

    kutoa ushahidi wake.

    Kwa kuwa vielelezo vingi alikuwanavyo washukiwa waliingizwa hatiani

    kwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika mauaji yale.

    Akiwa ndani ya ukumbi wa mahakama ya ICTR, Luteni Venus Jaka alipata

    bahati ya kuonana na Dr. Amanda Albro lakini wakati huu daktari huyo akiwa

    kwenye kiti cha magurudumu kwani alikuwa tayari amepoteza miguu yake

    miwili na baadaye kubakwa baada ya kutekwa na wale askari wa Kanali Bosco

    Rutaganda.

    Hivyo Dr. Amanda Albro na yeye alikuwa amefika pale kwenye mahakama

    ya mauaji ya Rwanda kutoa ushahidi wake dhidi ya Marceline na Kanali Bos

    co Rutaganda baada ya kusikia kuwa walikuwa amekamatwa na wanajeshi wa

    RPF-Rwandese Patriotic Front ambao baadaye walifanikiwa kuirejesha hali

    ya amani nchini Rwanda.

    Vikosi vya jeshi la RPF vilikuwa vimeingilia kati na kutuliza machafuko

    yale nchini Rwanda na hivyo kufanya kazi nzuri ambayo kwa hakika vilistahili

    kupewa pongezi kwani huenda bila vikosi hivyo vya kijeshi machafuko yale

    yangeendelea zaidi.

    Kipindi cha mwezi mmoja cha kutoa ushahidi katika mahakama ya ICTR

    kilikuwa kimemfanya Luteni Venus Jaka ajione tena kama binadamu wa

    kawaida lakini aliyepungukiwa na kitu fulani.

    Baada ya kufikiria sana Luteni Venus Jaka akamkumbuka Drel Fille, msi-

    chana aliyetokea kumpenda sana na hapo ndiyo akajua kuwa kutokuwepo kwa

    Drel Fille ndiyo kitu pekee ambacho kilishindwa kuikamilisha furaha moyoni

    mwake.

    _________

    ILIKUWA JIONI MOJA na manyunyu ya mvua hafifu yalikuwa yakianguka

    kutoka angani sambamba na baridi ya wastani iliyokuwa mkoani Arusha.

    Luteni Venus Jaka alikuwa ndiyo amemaliza kutoa ushahidi wake wa

    mwisho kwenye mahakama ile ya ICTR, na alikuwa akitoka kwenye ukumbi

    ule kuelekea hotelini alipokuwa amefikia wakati alipokutana na mwanamke

    fulani nje ya geti la kuingilia kwenye jengo lile la mahakama.

    Alikuwa mwanamke mzuri wa ajabu, mwenye weusi wa asili na alikuwa

    amembeba mtoto mdogo wa mwaka mmoja, na pembeni ya mwanamke huyo

    alisimama binti wa makamo.

    Luteni Venus Jaka ilikuwa bado kidogo awapite watu hao pale aliposikii

    akiitwa

    “Luteni!...” alipogeuka kumtazama yule mwanamke moyo wake ukapoteza

    utulivu kabisa, hisia kali zikamchota akili huku ameachama mdomo wazi kwa

    mshangao.

    “Drel Fille...oh! my God ni wewe? Luteni Venus Jaka aliongea kwa sauti

    kubwa ya mshangao kiasi cha kuwafanya watu waliokuwa jirani na eneo lile

    wageuke kumtazama. Yule mwanamke aliyebeba mtoto hakusema kitu badala

    yake alibaki amesimama tu huku akitabasamu.

    “Drel Fille mpenzi wangu oh! siamini...”

    “Ndiyo mimi mpenzi na nimefurahi sana kukuona kuwa umepona hadi

    kunikumbuka namna hii” Drel Fille aliongea huku akitabasamu.

    “Diane...? Luteni Venus Jaka alimuita yule binti aliyesimama pembeni ya

    Drel Fille na hapo yule binti akaitika

    “Bhee!”

    “Na huyu ni nani mpenzi? Luteni Venus Jaka aliendelea kuuliza huku akim-

    tazama yule mtoto mchanga aliyebebwa na Drel Fille huku akishangaa.

    “Mtoto wako, ...mama mpelelezi na baba naye mpelelezi, sijui huyu mtoto

    atakuwaje” Drel Fille aliongea huku akiangua kicheko hafifu.

    “Yaani siamini mpenzi, mbona ilikuwa haraka sana vile?

    “Haraka lakini ilitosha kupata mtoto, sakafuni, kwenye kochi, kitandani na

    bafuni”http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Loh! safi sana, jina lake je? Luteni Venus Jaka aliuliza huku akiwa hajiwezi

    kwa furaha.

    “Tanzania” Drel Fille aliongea

    “Kwanini aitwe Tanzania mpenzi?

    “Nitakwambia?

    Halafu wote wakakumbatiana kwa furaha huku mchozi yakiwatoka

    “Twendeni” baadaye Luteni Venus Jaka aliwaambia huku akijifuta machozi

    “Wapi?

    “Hoteli niliyofikia hakika leo nina furaha sijawahi kuona”

    Muda mfupi baadaye walikuwa kwenye teksi wakielekea hotelini na njiani

    maongezi ya furaha hayakuisha baina yao.



    LA FIN - MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog