Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KIAPO CHA JASUSI - 3

 





    Simulizi : Kiapo Cha Jasusi

    Sehemu Ya Tatu (3)







    "Nd..ndiyo mheshimiwa rais.Unahitaji taarifa zipi kuhusiana na huyu jamaa?



    "Taarifa zake zote zinazomuhusu.Nataka taarifa zake za elimu,familia n.k.Nitawatuma vijana wangu ndani ya dakika chache zijazo watakuja hapo kupata taarifa hizo" akasema Dr Enock

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Mheshimiwa rais kwa hapa sina taarifa hizo ninaomba unipe muda hadi kesho asubuhi nikakukusanyie taarifa zote za kuhusiana na Dastan"



    "Afande Isaack ninahitaji taarifa hizo ndani ya muda mfupi ujao.Ninawatuma vijana wangu sasa hivi wanakuja hapo kuja kuchukua taarifa hizo.Fanya kila uwezavyo niweze kuzipata hizo taarifa ndani ya muda mfupi ujao" akasema Dr Enock na kukata simu halafu akampigia Noah



    "Mheshimiwa rais" akasema Noah baada ya kupokea simu



    "Nimezungumza na Inspekta jenerali wa magereza na nimemtaka aniandalie taarifa zote za Dastan"



    "Ahsante sana kwa hilo mheshimiwa rais"



    "Nataka uende nyumbani kwake sasa hivi wewe mwenyewe ukazichukue taarifa hizo kwani nimemwambia nitawatuma vijana wangu kwake usiku huu .Ukizipata zichambue uone kama kuna chochote kinachoweza kukusaidia.Kitu ingine chunguzeni kwa nini taarifa hizi za Dastan hazipo katika kumbu kumbu za serikali?



    "Sawa mheshmiwa rais nitafanya hivyo na nitakujulisha kila hatua tunayochukua"



    "Noah tafadhali,hili suala la Dr Alfredo si la kufanyia mzaha hata kidogo.Hakikisha usiku huu umefahamu ujumbe ambao Dastan alipewa na Dr Alfredo ameupeleka wapi?Nataka kabla ya kufika asubuhi niwe nimepata jibu kwamba mmemfahamu mtu huyo aliyepewa ujumbe ni nani " akasema Dr Enock



    "Mheshimiwa rais tunafanya kila tuwezalo na ninakuhakikishia kwamba kabla ya mapambazuko tutakuwa tayari na taarifa zote za kuhusiana na huyo mtu" akasema Noah na kukata simu akawageukia wenzake



    "Rais amewasiliana na Inspekta jenerali wa magereza na kumtaka atupatie taarifa zote za kumuhusu Dastan.Teddy,Jeff na Santana tunakwenda kwa Inspekta jenerali wa magereza kufuatilia taarifa hizo za Dastan.Wengine mtaendelea kudukua sehemu mbali mbali ili tuweze kupata jambo lolote la kumuhusu huyu Dastan" akasema Noah kisha yeye na vijana wake wakajiandaa wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Dr Isaack Mchana



    Dakika ishirini toka Noah na wenzake waanze safari ya kuelekea kwa Dr Isaack Mchana,simu yake ikaita alikuwa ni rais,Noah akaipokea haraka haraka



    "Mheshimiwa rais" akasema Noah na kisha ukapita ukimya mdogo halafu rais akasema



    "Noah uko wapi?



    “Mheshimiwa rais ninaelekea nyumbani kwa Inspekta jenerali wa magereza kuchukua taarifa za Dastan kama ulivyoelekeza”



    “Mmefika wapi? Rais akauliza



    "Tumefika hapa katika hospitali ya Dr Tamala" akajibu Noah



    "Noah ahhmm !! rais akasita kidogo akanyamaza halafu akavuta pumzi ndefu na kusema



    "Nimepokea taarifa muda mfupi uliopita Dr Isaack amefariki dunia"



    "Amefariki dunia?!! Noah akapatwa na mstuko



    "Ndiyo"



    "Amefariki muda gani wakati muda si mrefu umetoka kuzungumza naye?



    "Nimetaarifiwa kwamba amejiua kwa kujipiga risasi ya kichwa"



    "Dah ! akasema Noah halafu kukawa kimya



    "Noah" akaita rais



    "Ninataka muwahi hapo nyumbani kwa Dr Isaack mkaichukue simu yake.Naamini kujiua kwake si kwa bahati mbaya.Kuna jambo limepeleka akaamua kujitoa uhai" akasema Dr Enock na kukata simu.



    "Kumetokea kituko kingine" akasema Noah



    "Nini kimetokea tena?Jeff akauliza



    "Mtu tunayemfuata Dr Isaack amejiua muda mfupi uliopita kwa kujipiga risasi"



    "oh my God ! akasema Teddyhttp://pseudepigraphas.blogspot.com/



    "Jeff ongeza mwendo tunapaswa kufika hapo nyumbani kwa Dr Isaack haraka kabla polisi hawajafika.Tunaihitaji simu yake" akasema Noah na Jeff aliyekuwa katika usukani akaongeza mwendo.



    "Unadhani nini sababu ya Dr Isaack kujiua? akauliza Santana huku akizifunga vizuri nywele zake kwa nyuma.



    "I think he's hidding something" akasema Noah



    "Amejiua baada ya kuombwa na rais ampe taarifa za Dastan Mwaikambile.Inaonyesha kuna kitu anakifahamu kuhusiana ana Dastan ambacho hataki kijulikane na ndiyo maana akajitoa uhai.Hii inazidi kutupa ushawishi wa kumfahamu zaidi huyu Dastan ni nani.Tukiipata simu ya Dr Isaack tutaweza kufuatilia watu ambao amekuwa akizungumza nao na tutajua ni siri gani iliyojificha.Guys tunaingia katika operesheni nyingine ambayo inaonekana itakuwa kubwa na ngumu.Tujiandae" akasema Noah









    Walifika katika nyumba za maafisa wa juu wa serikali na wakaelekea moja kwa moja katika nyumba ya kamishna jenerali wa magereza.Tayari kulikuwa na watu wengi nje ya nyumba ile na kulikuwa na magari ya polisi yakiwasha vimuli muli huku wakiwa wamezungushia utepe unaokataza watu kuingia eneo lile



    "Tumechelewa,tayari askari wamekwisha fika na hatutaweza tena kuingia ndani" akasema Noah



    "Tutaipataje simu ya Dr Isaack bila kuingia ndani?We have to get in there" akasema Santana



    "I have to call president" akasema Noah na kuchukua simu akampigia Dr Enock



    "Noah mmefanikiwa kuipata simu ya Dr Isaack? akauliza Dr Enock



    "Bado hatujafanikiwa kuipata mheshimiwa rais tumechelewa kidogo kufika na polisi tayari wametutangulia.Tunaomba msaada wako tuweze kuingia ndani na kuipata simu yake" akasema Noah



    "Noah niliwaambia muwahi kufika kabla ya polisi.Any way let me see what I can do" akasema Dr Enock na kukata simu na baada ya dakika tatu akapiga



    "Mhshimiwa rais" akasema Noah



    "Noah nimekwisha zungumza na mkuu wa kikosi kilichopo hapo na nimetoa maelekezo,nendeni atawaruhusu mtaingia ndani ya chumba ulimo mwili wa Dr Isaack mtafanya uchunguzi na kuchukua kile mnachoona kitawafaa kisha mondoke haraka" akasema Dr Enock na kwa haraka Noah na Teddy wakashuka wakajitambulisha kwa polisi kwamba wametumwa na rais na wakapelekwa katika chumba cha kulala cha Dr Isaack.Alikuwa amelala sakafuni akiwa katika dimbwi la damu.Bila kupoteza wakati Noah akamkagua Dr Isaack na kumkuta akiwa na simu mfukoni ilikuwa imezima akaiwasha lakini ikaonyesha kwamba haikuwa na laini ndani.Akaifungua na kukuta kweli hakukuwa na laini katika simu.



    "Teddy laini ya simu haipo.Tunatakiwa kuitafuta haraka" akasema Noah na kwa kusaidiana na polis wakaanza kupekua kila mahala mle chumbani bila mafanikio.Noah akatoka mle ndani akaenda mahala kusiko na watu akampigia simu rais



    "Noah mmefanikiwa kuipata simu ya Dr Isaack? akauliza rais



    "Mheshimiwa tumefanikiwa kuipata simu lakini laini ya simu haipo.Tumeitafuta sana bila mafanikio"akasema Noah na ukimya mfupi ukapita halafu Dr Enock akasema



    "Noah hili suala limekwisha chukua sura mpya.Ondokeni hapo na nitawatumia polisi kuitafuta hiyo laini na itakapopatikana wataileta moja kwa moja kwangu nami nitawapatia.Kitu ninachotaka kukifanya usiku huu ni kumpata Dastan.Ninamuagiza mkuu wa jeshi la polisi atume helkopta iende haraka sana Markubelo kwenda kumchukua Dastan na kumleta kwangu na halafu nitamkabidhi kwenu kwa mahojiano.Nitakujulisha pale atakapokuwa amefika" akasema Dr Enock na kukata simu.Noah na wenzake wakaondoka eneo lile kama walivyoamriwa na rais



    "Hili suala linaonekana si suala dogo kwani Dr Isaack ameificha laini yake ya simu makusudi ili isipatikane.Hataki mawasiliano yake na watu wake yajulikane.Kwa kiongozi kama huyu kujiua ghafla lazima ipo sababu kubwa.Tukimpata Dastan tutafahamu mengi" akasema Noah



    "Mkuu unahisi Dastan ana mahusiano na Dr Isaack? akauliza Teddy



    "Ninahisi hivyo kutokana na mazingira yenyewe ya kifo chake.Amejiua baada ya kutakiwa kuwasilisha taarifa za Dastan kwa rais.Ni wazi kuna mambo ambayo hakutaka yajulikane na akaamua kujiua.Hili ni jambo kubwa" akasema Noah



    "Mna hakika Dr Isaack kweli amejiua mwenyewe? akauliza Jeff na wote wakabaki kimya.Baada ya muda Noah akauliza



    “Unahisi labda Dr Isaack ameuliwa?



    “Ninahisi hivyo.Tusidharau pia kwamba anaweza kuwa ameuawa” akasema Jeff



    “Jeff hoja yako ni ya msingi na si ya kuipuuza lakini mimi nina uhakika mkubwa Dr Isaack amejiua mwenyewe.Mazingira yanaonyesha wazi kwamba amejimaliza na ninaamini kuna siri anaificha kuhusiana na Dastan kwani amejiua muda mfupi tu baada ya kutakiwa kuwasilisha taarifa za Dastan kwa rais.Kuna siri kubwa kwa kifo chake ngoja rais atusaidie tuweze kuipata laini yake ya simu na tufanye uchunguzi tutajua kwa nini aliamua kujiua” akasema Noah





    MARKUBELO PRISON





    Dastan Mwaikambile alikuwa amekaa kitandani na mkononi akiwa na simu yake.Alikuwa akijaribu kumpigia smu ya Padre Thadei lakini simu yake haikuwa akipatikana



    “Padre Thade hapatikani simuni.Nifanye nini? Akajiuliza halafu akatoka mle chumbani akarejea sebuleni akatazama damu iliyotapakaa



    “I think it is the time”akawaza kisha akatoka pale nyumbani akaelekea hospitali moja kwa moja katika chumba alimo Dr Alfredo,akamkuta Dr William



    “Vipi maendeleo yake? Akauliza Dastan



    “Hivyo hivyo hakuna unafuu” akajibu Dr William



    “Dr William ninakuomba unipe nafasi kidogo ninataka kuzungumza jambo na mzee Alfredo kwa dakika mbili” akasema Dastan na Dr William akatoka.Dastan akaenda kuketi katika kitanda cha Dr Alfredo na kumsemesha



    “Mzee Alfredo ni mimi Dastan” akasema Dastan.Mzee Alfredo akafumbua macho na kumtazama Dastan halafu akamuomba amsaidie kugeuka.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Unasemaje kijana usiku huu? Akauliza Dr Alfredo .Haikuwa kawaida kwa Dastan kuonekana pale hospitali usiku ule



    “Mzee Alfredo nimekuja kuzungumza nawe jambo muhimu sana” akasema Dastan na Dr Alfredo akamtazama na kuuliza



    “Ujumbe wangu niliokupa umeufikisha?



    “Ndiyo mzee nimeufikisha kwa Padre Thadei”



    “ahsante sana kijana”akasema Dr Alfredo .Dastan akamtazama na kusema



    “Mzee Dr Alfredo kuna jambo limetokea hapa gerezani usiku huu na linakuhusu pia wewe”



    “Ni jambo gani?



    “Ni kuhusiana na ule ujumbe ulionipa niupeleke kwa padre Thadei.Sikuwa na ratiba ya kwenda Dar es salaam leo hivyo nilipotoka hapa nilizitafuta namba za simu za padre Thadei nikamtumia ujumbe ule ulionipatia.Mara nyingi jioni nimalizapo majukumu yangu ya kazi hupenda sana kwenda kuvua samaki baharini.Nikiwa baharini nikafuatwa na boti yenye watu wanne waliokuwa na silaha.Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kupambana nao na kuwaua wote.Niliporejea nyumbani kwangu nikiwa sijui hili wala lile nikajikuta mikononi mwa watu wengine wanne na mmoja wa watu hao akiwa ni katibu wangu muhtasi ambaye nimefanya naye kazi na ninamuamini sana.Walichokuwa wanakitafuta kutoka kwangu ni simu yangu na nilipowaambia kwamba imeangukia katika maji ndipo yule katibu wangu muhtasi akaniamuru niwaeleze ule ujumbe ulionipatia nimeupeleka kwa nani?Kwa bahati nzuri walitokea askari magereza na kuwamaliza wote kwa risasi wakiamini ni majambazi.Baada ya tukio hilo nilichukua simu ya huyo katibu wangu muhtasi pamoja na kompyuta yake ndogo kwa lengo la kuvichunguza kujua anawasiliana na akina nani,nikaviweka vifaa hivyo kwa Dr William na kitu cha kushangaza vyote viliwaka moto kwa wakati mmoja.Mzee Alfredo haya yote yaliyotokea yamesababishwa na ujumbe ule ulionipatia.NInahisi yule katibu muhtasi wangu aliwekwa hapa gerezani maalum kwa ajili ya kukufuatilia maisha yako.Nataka uniambie mzee wangu kuna kitu gani kinachowafanya hawa jamaa wakufuatilie namna hii hadi wakaamua kuweka watu kwa siri wakuchunguze maisha yako hapa gerezani?Kwa nini hawataki uonane na mtu yeyote? Nieleze mzee wangu hata kama kuna jambo hujawahi kumueleza mtu yeyote” akasema Dastan na sura ya mzee Alfredo haikuonyesha mstuko wowote kwa yale aliyoelezwa na Dastan



    “Dastan kijana wangu una hakika padre Thadei ameupata ujumbe ule niliokupa? akauliza Dr Alfredo



    “Ndiyo mzee ameupata ule ujumbe”akajibu Dastan



    “Ahsante sana kwa hilo.Mimi nitakuambia neno moja tu” akasema Dr Alfredo na kufumba macho kwa sekudnde kadhaa halafu akafumbua na kumtazama Dastan



    “Run”



    “Unasemaje mzee Alfredo? Akauliza Dastan



    “Run away Dastan.Go far away from here.Umeshiriki siri yangu na sasa watakuandama usiku na mchana na hautakuwa salama tena.Kusanya kila unachoweza na uondoke haraka sana ,they are after you”



    “They? Who are they?Akauliza Dastan



    “Ni akina nani hao? Unaweza ukanitajia japo mmoja wao niwajue?akauliza Dastan



    “Dastan tafadhali usiendelee kupoteza muda wako hapa.Ondoka kabla hawajakukuta hapa.Sitaki upotee kijana wangu umenisaidia sana na mimi nataka kukusaidia pia na msaada wangu pekee ni kukuomba uondoke hapa.Ondoka Tanzania.Ukiendelea kukaa hapa watakutafuta kila kona hadi wahakikishe wamekupata.Ahsante sana kwa misaada yote uliyonisaidia.Hii itakuwa ni mara ya mwisho mimi na wewe kuonana.Nakutakia kile la heri.Now go !! akasema Dr Alfredo .Dastan akamtazama mzee yule usoni ni kweli alikuwa akimaanisha kile alichokisema.Akatoka nje na kukutana na Dr William



    “Dr William ……akasema Dastan lakini kabla hajasema chochote simu yake ikaita.Akamtazama Dr William halafu akasogea pembeni akaipokea



    “Hallow” akasema Dastan



    “Dastan tafadhali usilitaje jina langu kama uko na mtu karibu. It’s time to go now.Nimepigiwa simu na rais muda mfupi uliopita akanitaka nimpe taarifa zako zote na amesema anatuma watu muda si mrefu kuja kuzifuata .Dastan usipoteze tena muda kwani muda wowote wanaweza wakakufuata hapo.Kusanya kila kilicho chako na uondoke haraka sana.” akasema mtu aliyekuwa anazungumza na Dastan simuni na wote wakavuta pumzi ndefu



    “Dastan pengine haya yakawa ni mazungumzo yetu ya mwisho. Nitakapokata simu hii utakuwa ni mwisho wetu na hatutaonana tena. Please take good care of yourself” akasema mtu yule na kukata simu.Dastan akazama mawazoni ghafla.Dr William akamsogelea na kuuliza



    “Dastan is everything ok?



    “No ! akasema Dastan na kumshika mkono Dr William



    “Dr William I have to go to Dar es salaam right now.Kuna dharura imejitokeza”



    “Dastan kama ni hivyo hata mimi ninaondoka pia.Tafadhali usiondoke bila ya mimi.Sitaki tena kuendelea kukaa mahala hapa” akasema Dr William



    “Dr William hatuwezi kuondoka wote na kumuacha huyu mzee peke yake kwa wakati hu ambao maisha yake yako hatarini.Mimi kuna jambo limetokea ninakwenda kuliweka sawa halafu nitarejea kesho asubuhi.Wewe baki hapa endelea kumuangalia huyu mzee na hakikisha anakuwa salama.Yeyote atakayekuuliza kuhusu mimi waeleze nimekwenda Dar es salaam mara moja nitarejea kesho” akasema Dastan halafu akatembea kwa kasi kuelekea nyumbani kwake.Akaingia chumbani na kupiga simu sehemu Fulani akazungumza na mtu kwa dakika tano halafu akaanza kupakia vitu vyake vichache muhimu,akageuza picha moja kubwa ya maua na nyuma yake akatoa bahasha moja ya khaki akaipakia katika mkoba wake mdogo akatoka na kuelekekea katika gati ambako zimeegeshwa boti kadhaa akaagana na meja Dickson mkuu wa zamu ya usiku akamueleza kwamba anakwenda Dar es salaam kwa dharura kisha akaingia katika boti yake na kuondoka kwa kasi kubwa





    *************

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Helkopta ya jeshi la polisi ilitua katika sehemu ya kutulia ndani ya gereza la Markubelo na askari polisi watano wakashuka wanne kati yao wakiwa na silaha.Meja Dickson Kiongozi wa zamu ya ulinzi ya usiku pale gerezani akawafuata na kusalimiana na inspekta Joseph mkuu wa kikosi kile kilichokuja kutoka makao makuu halafu wakaelekea katika ofisi maalum kwa ajili ya wageni



    “Karibuni sana afande.” Akasema Meja Dickson



    “Afande tumekuja kwa dharura kuonana na mkuu wa gereza”



    “Kamishna msaidizi Dastan?



    “Ndiyo”



    “Kamishna Dastan hayupo ametoka usiku huu ameelekea Dar es salaam”



    “Amekwenda Dar es salaam? Inspekta Joseph akauliza kwa mshangao



    “Ndiyo ameondoka kama nusu saa iliyopita amesema kwamba amepata dharura.Nilimshauri aende asubuhi kwa sababu usiku huu peke yake katika bahari ni hatari sana lakini akasisitiza kwamba anatakiwa Dar es salaam usiku huu” akasema Meja Dickson



    “Una hakika amekwenda Dar es salaam?



    “Hivyo ndivyo alivyoniaga kwamba anakwenda Dar es salaam atarejea asubuhi”



    “Amebeba nini?



    “Amebeba mkoba mdogo tu” akasema Meja Dickson



    Baada ya ukimya mfupi Inspekta Joseph akasema



    “Tupeleke nyumbani kwake”



    Meja Dickson akiwa na askari wawili wakawapeleka askari wale kutoka makao makuu ya polisi nyumbani kwa mkuu wa gereza.Inspekta Joseph akwaamuru askari alioongozana nao kuufungua mlango wa nyumba ya kamishna msaidizi Dastan wakaingia ndani.Bado kulikuwa kumetapakaa damu nyingi sebuleni.Wakazunguka nyumba nzima wakikagua na halafu wakaingia katika chumba cha kulala.Kila kitu kilikuwepo mle chumbani na kitandani kulikuwa na nguo zilizowekwa zikionekana kuandaliwa maalum kwa ajili ya kuvaliwa.Hawakupata chochote cha kuwasaidia wakatoka na Inspekta Joseph akampigia simu mkuu wa jeshi la polisi akamjulisha kwamba Kamishna msaidizi Dastan hakuwepo pale gerezani amekwenda Dar es salaam



    ‘Inspekta Joseph una hakika Kamishna Dastan hayupo hapo kisiwani? Akauliza mkuu wa jeshi la polisi



    “Hayupo afande.Tumetaarifiwa na walinzi walioko zamu ya usiku kwamba Kamishna Dastan ameondoka usiku huu akidai anakwenda Dar es salaam kwa dharura.Tumepekua nyumba yake lakini kwa hali tuliyoikuta inaonyesha kwamba hatachukua muda mrefu huko alikokwenda.Nahitaji maelekezo yako afande tufanye nini? Akauliza Inspekta Joseph



    “Nipe dakika chache halafu nitakupa maelekezo” akasema Inspekta jenerali wa polisi Robert Msanzi.Mara tu alipokata simu akampigia rais Dr Enock



    “Mheshimiwa rais kuna suala limejitokeza ambalo nimeona ni vyema nikujulishe.Nimetuma kikosi cha askari katika gereza la Markubelo kama ulivyoelekeza kwenda kumchukua Kamishna Dastan na wametua hapo muda mfupi uliopita ila wamemkosa Dastan.Inasemekana ameondoka usiku huu kwa boti akielekea Dar es salaam akidai amepata dharura” akasema IGP Robert



    “IGP watu uliowatuma unawaamini?Una hakika kweli Dastan hayupo kisiwani?



    “Ninaaamini watu niliowatuma huko mheshimiwa rais.Ni kweli Dastan hayupo”



    “Kutoka hapo kisiwani hadi Dar es salaam ni muda gani kwa boti?



    “Ni chini ya dakika thelathini kwa boti ndogo mheshimiwa rais ”



    Dr Enock akafikiri kwa muda halafu akasema



    “IGP nakupa maelekezo haya.Tuma askari wafanye doria kubwa baharini kuanzia pwani ya Markubelo hadi Dar es salaam.Watumie boti na kila kifaa chenye kuweza kufanya doria baharini.Weka askari wa kutosha bandarini na Dar es salaam ambako naamini lazima Dastan atapita kama anakuja Dar es salaam.Hakikisha Dastan anapatikana usiku wa leo na akisha patikana nataka aletwe kwangu moja kwa moja kabla ya kupelekwa sehemu yoyote.”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Nitafanya hivyo mheshimiwa rais na Kamishna Dastan atapatikana usiku wa leo kama ulivyoelekeza” akasema IGP Robert



    “Ahsante sana IGP.Nasubiri taarifa kutoka kwako” akasema Dr Enock na kukata simu.



    “Huyu Dastan mbona anaanza kuniumiza kichwa changu? Kwa nini taarifa zake zikosekane? Kwa nini Dr Isaack alijiua muda mfupi baada ya kumuomba anipatie taarifa za Kamishna Dastan? Kabla ya kesho asubuhi nahitaji niwe nimepata jibu ya hiki kilichotokea na niwe nimepata muafaka kuhusiana na kamishna Dastan.Hawezi katu kushindana nami kwani nina nguvu zaidi yake.Mpaka asubuhi atakuwa amepatikana na ataeleza ni wapi ameupeleka ujumbe aliopewa na Dr Alfredo kitwe” akawaza Dr Enock na kumpigia simu Noah



    “Mheshimiwa rais” akasema Noah baada ya kupokea simu ya rais



    “Noah kuna chochote mmefanikiwa kukipata kuhusiana na Dastan hadi hivi sasa?



    “Hapana mheshimiwa rais mpaka sasa bado hatujapata taarifa zozote za kumuhusu kamishna Dastan”



    “Nimetuma timu ya askari kwenda Markubelo kumchukua Kamishna Dastan lakini nimetaarifiwa kwamba ameondoka usiku wa leo akidai anakuja Dar es salaam.Nimeagiza ifanyike doria baharini kumtafuta vile vile kuimarishwe ulinzi bandarini ili Dastan atakapojitokeza tu basi atiwe nguvuni haraka sana.Ninachotaka mkifanye wakati polisi wakiendelea na doria baharini kumtafuta ninyi tumieni kila njia kuweza kumbaini Dastan mahala alipo.Tumieni satelaiti na vyote mnavyoona vinaweza kusaidia kufahamu huyu jamaa mahala alipo na tumpate kabla haijafika asubuhi.”akasema Dr Enock



    “Sawa mheshimiwa rais tutafanya hivyo” akasema Noah na rais akakata simu.Alikuwa amesimama katika dirisha ghorofani akilitazama jiji la Dar es salaam lilivyong’aa kwa taa za kupendeza usiku huu



    “Rough day huh ! ikasema sauti kutoka nyuma yake akageuka na kukutana na mke wake aliyekuwa amejawa tabasamu huku akiwa ameshika mkononi glasi mbili za mvinyo



    “Oh ! Darling” akasema Dr Enock na mke wake akamsogelea akambusu



    “Unaonekana umezama mawazoni.Kuna tatizo lolote? Akasema Dr Mboki Mwaipula mke wa rais huku akimpa mumewe glasi iliyojaa mvinyo.



    “Matatizo hayakosekani.Mimi ni rais wa Tanzania na kila mwananchi ananitazama mimi.Natakiwa kuilinda Amani ya nchi,natakiwa kuhakikisha raia wote wamelala usingizi mzuri kwa Amani,watoto wao wanakwenda shule na wanapata huduma bora za afya,maji safi na salama bila kusahau ajira.Kuongoza nchi ni mzigo mzito”akasema Dr Enock na kunywa funda moja la kinywaji



    “Ninafahamu ugumu wa kazi yako mume wangu na ndiyo maana niko hapa kukusaidia.Muda wowote unapokuwa na tatizo lolote lile nakuomba tafadhali usiogope kunieleza.Mimi ndiye mshauri wako mkuu kabla ya hao wengine wote hawajakushauri”akasema Dr Mboki na kumbusu rais



    “ Ahsante sana my sweet angel kwa kuwa nami karibu.Pamoja na ugumu wake lakini ninaiona kazi hii ni nyepesi kwa sababu ya uwepo wako karibu yangu.Umenisaidia mno katika majukumu yangu.Ninajiona mwenye bahati sana kuwa na mwanamke kama wewe” akasema Dr Enock na kumkumbatia mkewe wakabusiana.



    “Muda wa kwenda kupumzika mume wangu.Twende chumbani tukapumzishe akili na kujianda kwa ajili ya siku mpya ya kesho”akasema Dr Mboki akamshika mkono mumwe na kumuongoza kuelekea chumbani.Akampeleka moja kwa moja kitandani na kuanza kumvua nguo na bila kupoteza muda wakazama katika bahari ya huba.



    “Kila siku ninazidi kujiona kijana kwa ajili yako kutokana na mambo unayonifanyia.Unanionyesha mapenzi mazito sana.Kila uchao ninaona kama vile nimekuoa jana” akasema Dr Enock mara tu baada ya kumaliza mzunguko mmoja



    “Ni furaha yangu kusikia hivyo mpenzi wangu.Wewe ni kitu cha thamani kubwa mno katika maisha yangu na ndiyo maana ninafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba unakuwa na furaha kila siku ili uweze kuwatumikia watanzania vyema.Kichwa chako kinapaswa kutulia na mwenye jukumu la kukituliza si mwingine bali ni mimi pekee” akasema Dr Mboki



    “Darling..” Dr Enock akataka kusema kitu lakini mara simu yake ikaita akatazama mpigaji halafu akainuka akaipokea



    “Afande IGP una taarifa zozote nzuri? Akauliza Dr Enock



    “Mheshimiwa rais,nimepokea taarifa kutoka kwa vikosi vinavyofanya doria baharini kwamba wameipata boti ambayo wanaamini ndiyo aliyoitumia Kamishna Dastan baada ya kutaarifiwa na wavuvi wa eneo la Mkukweno kuwa kuna boti imeonekana karibu na eneo lao la uvuvi.Polisi wa doria wakaenda mara moja na wakaikuta boti hiyo wakawasiliana na gereza la Markubelo nao pia wakathibitisha kwamba Kamishna Dastan hutumia boti ya aina hiyo.Hii ikatupa uhakika kwamba hiyo ni boti yake.Kwa mujibu wa wavuvi wa eneo hilo walisikia muungurumo wa boti ikielekea mahala walipo na toka ndani ya boti hiyo akashuka mtu mmoja na muda huo huo ikatokea gari na mtu yule akaenda kupanda na kutokomea kusikojulikana.Mheshimiwa rais tunaendelea na jitihada za kumtafuta na ninakuahidi kwamba Kamishna Dastan atapatikana tu.Nimesambaza askarikila sehemu kumtafuta.Hatakuwa na sehemu ya kujificha” akasema mkuu wa jeshi la polisi .

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Dr Enock akavuta pumzi ndefu na kusema



    “Afande IGP tafadhali fanya kila namna uwezavyo kumtafuta huyu jamaa.Tumia kila nguvu uliyonayo kumsaka na kuhakikisha unampata na mara tu akipatikana basi nitaarifiwe haraka sana na asipelekwe sehemu yoyote mpaka nitakapokuwa nimeonana naye”



    “Nimekuelewa mheshimiwa rais na maagizo yako yatatekelezwa” akasema IGP na rais akakata simu na kuvuta pumzi ndefu













    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog