Search This Blog

Friday, 18 November 2022

MWANAMKE MWENYE JUBA JEUSI - 2

 






Simulizi : Mwanamke Mwenye Juba Jeusi

Sehemu Ya Pili (2)





Max Petito aliketi mbele ya meza kubwa ya duara akiwa anatizama televisheni yake, mbele yake kukiwa na vijana watatu wakakamavu “Nipeni ripoti” Max aliwaambia vijana wake “Man down” mmoja wao alijibu, wakatazamana usoni na kupeana ishara ya kukubaliana. Kicheko cha ushindi kikamtoka mtu mzima Max Petito, huku akifungua shampeini ya ushindi na kuwamiminia vijana wake “tusherehekee kazi ngumu imeisha, iliyobaki ni nyepesi tu, yuko wapi Rodolph?” aliuliza kwa upole, wale vijana wakatazamana tena “niliwaambia akimaliza kazi mumuue palepale, mmefanya nini?” Max aliwakaripia vijana wake “kama yuko mikononi mwa polisi si atatoa siri yote” aliwaeleza wale vijana huku akinyanyuka na kuingia ndani kwake “foolish! You are so foolish!”, alimalizia maneno yake huku akiingia ndani, kisha akageuka kuwaangalia wale vijana “hakikisheni mnaniletea habari za alipo Rodolph mara moja” aling’aka kwa hasira na kubamiza mlango wake.

Hamna la kufanya, vijana wale japokuwa ni wakakamavu na wana maumbo ya kiupiganaji hapo walijiona kweli hawakutumia akili hata kidogo. Walijinyanyua kutoka pale walipokaa na kuanza mikakati mipya ya kumpata Rodolph au habari zake.





Pilikapilika za jiji la Dar es salaam zilianza kama kawaida, foleni za magari kuingia mjini nazo zilikuwa kila mahali, joto lilofanya watu watembee wengine vifua wazi na wenye magari kutumia air condition ili mradi tu kila mtu airidhishe nafsi yake.

Muhimbili nako korido zote zilijaa watu wakienda kuwaona ndugu zao waliokuwa wakigonjeka hospitalini hapo. Ulinzi mkali uliimarishwa katika kitengo cha mifupa alipokuwa amelazwa Mh Chiwawa Chakwima, fahamu zilimrudia lakini hakupenda kuongea na mtu yeyote kwa wakati huo, alipapasa kifuani mwake mara kadhaa kana kwamba anatafuta kitu fulani kisha akatulia, alibomyeza kitufe fulani kilichounganishwa katika kitanda hicho mara muuguzi alikuja “samahani, mizigo yangu ilishushwa kwenye ndege?” alimuuliza muuguzi yule ambaye alibakia kaduwaa tu hakujua amjibu nini “ndege gani?” muuguzi yule naye alirusha swali na wote kubaki wanatazamana.



Inspekta Simbeye alishuka kutoka kwenye land Cruiser ya kipolisi akifuatana na vijana wake wakakamavu, moja kwa moja alielekea kitengo cha mifupa na kuomba kuonana na Mh Chakwima, muuguzi alimuongoza mpaka kitandani alipolala Mheshimiwa “afadhali umekuja mkuu, wale ni majambazi wameniibia kila kitu” Mh Chakwima alianza kubwabwaja “Kila kitu wameiba, nyaraka za serekali zilikuwa kwenye briefcase, zitafute haraka” alimalizia kwa kutoa amri, RPC Simbeye alishusha pumzi ndefu maana alijua kuwa hapo bado network hazijarudi sawasawa “sawa mzee tunashughulikia” kisha akanyanyuka na kutoka nje, pale nje alikutana na familia ya Mh Chakwima aliongea maneno machache na mke wa Chakwima kisha akaondoka na vijana wake.



Watu mbalimbali walipishana wodini humo kuja kumtakia hali Mh Chakwima lakini kwa wakati huo hakupenda kuongea na kila mtu.



Mke wa Mh Chakwima alishangazwa kuona rafiki kipenzi wa mume wake haonekani hospitali hapo kila alipojaribu kuipiga simu yake aliambiwa ‘not reachable’ , maswali mengi yalimjia kichwani hata kukata tamaa, kila alipomwangalia mumewe pale kitandani alivyozungukwa na mashine za kumsaidia kupumua hakuwa na amani moyoni wala hakuamini kuwa mumewe ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida, machozi yaliyochanganyika na kamasi jembamba yalimtoka mama huyu wa Kimeru mwenye uso mweupe, mrefu anyevutia hasa atembeapo, kila wakati alimuuliza muuguzi maendeleo ya afya yake aliambulia jibu moja tu ‘usijali atapona’ .



Akiwa ndani ya gari yake, Amata aliangalia watu wote wanaotoka na kuingia katika jengo lile la Muhimbili, aliingiza mkono mfuko wa shati na kutoa business card aliyoichukua kwa yule muuaji usiku uliopita na kuiangalia kwa makini “Smart Boy” ni jina pekee lililoandikwa juu ya card ile na kufuatiwa na baadhi ya namba, namba zile si ngeni sana kwa Amata moja ilikuwa ya Tanzania, nyingine ya Kenya na ya mwisho ilikuwa ya Afrika ya Kusini. Amata alipata shauku kuipiga ile ya Tanzania lakini aijiuliza hata akiipiga ataongea nini, aliirudisha simu chini akafungua droo ya gari na kutoa bahasha iliyokunjwa ambayo jana yake tu aliichukua kwa muuaji yule akaichana ndani mlikuwa na hundi ya pesa maelfu ya dola za kimarekani ‘ina maana pesa zote hizi ni kwa ajili ya kuua mtu tu’ Aamata alijiwazia kisha akatoa tabasamu pana ambalo ni nadra sana kuonekana akairudisha hundi ile mahali pake, kutokana na hundi ile ndipo alipojua kuwa muuaji yule au profesheno kama walivyomuita wenzake alikuwa ni raia wa Afrika ya kusini. Amata alijiuliza kwa nini wauaji wote wanatoka nje, Rodolph wa Congo na huyu wa afrika ya kusini hapo aliweza kuona kazi ngumu inayomkabili mbele yake.

Amata alifungua mlango wa gari taratibu huku akiiweka mawani yake myeusi vizuri usoni mwake ambayo ilimuwezesha kuona wanaokuja nyuma yake kwa viyoo vidogo vilivyofungwa pembeni kwenye miimo ya mawani hiyo. Aliweka koti lake vizuri na kurekebisa tai kisha kwa hatua za madaha alilielekea lango la wodi ya mifupa (MOI) na kuingia moja kwa moja hadi kwa muuguzi wa zamu

“Habari ya kazi dada?” alimtupia salamu huku akiitoa mawani yake usoni

“Nzuri sijui wewe?” Muuguzi yule alijibu huku akimuangalia Amata kutoka juu mpaka chini, akimuhusudu kwa jinsi alivyotulia ndani ya suti.

“nikusaidie tafadhali”

“Naweza kumuona Mh Chakwima?”

“Lakini muda umeisha, nenda dakika chache tu” muuguzi alijibu na kumuongoza alipo Mh Chakwima.

Amata alimtazama mheshimiwa jinsi alivyolala kwa utulivu wa hali ya juu, mke wake na mtoto mmoja walikuwa pembeni yake.

“Karibu kaka, karibu ukae” Mama Chakwima alimkaribisa Amata

“Mgonjwa anaendeleaje?”Amata alitupa swali kwa mama Chakwima

“Amelala kama unavyomuona” Mama Chakwima alijibu huku akitoa machozi. Amata aliingiwa na huruma hata kujikuta akilengwa na machozi.

“Mama usilie mama!” mtoto wa kike wa Mh Chakwima alimbembeleza mama yake. Amata aliumia sana kwa kitendo hiko, alijikuta akishikwa na hasira kama amuone yule aliyefanya haya amtafune nyama. Alimchukua mama Chakwima pembeni na kuzungumza naye machache

“Kabla ya tukio Mh alikushirikisha chochote au ulipata kujua lolote ambalo si zuri kati yake labda na rafiki zake?” Amata alohoji

“Hapana! Alienda tu kikazi huko Uarabuni aliporudi hali ndiyo hii, yeye haongei sasa hatujui hata nini labda angetuambia” machozi yaliendelea kumtoka mama Chakwima.

“Je unamfahamu rafiki yake wa karibu labda, ambaye mara nyingi huwa pamoja” aliendelea kuhoji

“Mume wangu hakuwa na marafiki wengi, rafiki yake mkubwa ni Bw Punde Kishime” alijibu kwa uchungu kisha akaendelea “hata hivyo sijamuona tangu jana sijui yuko wapi nikipiga simu zake hazipatikani. Amata alifahamu vizuri nyumba ya Mh Punde Kishime na hata ofisi yake, hivyo alijaribu kufikiri inakuwaje kama ni rafiki wa karibu na asitokee mpaka muda huo, kengele ya hatari kichwani mwa Amata ililia.

“Ok, shemeji usijali kila kitu kitakuwa sawa” Amata alimfariji mama Chakwima na kuondoka eneo hilo.

***



Vijana wa Max Petito walifanya kazi yao kama walivyoelekezwa na kugundua kuwa muuaji Rodolph Mampas yupo hospitali ya taifa akiwa chini ya ulinzi mkali, walijifanya kupita ili mradi tu waone mazingira yote jinsi yalivyo ili wajue jinsi ya kufanya. Walipopa tafutishi zote zamu za ulinzi, muda wa kubadilishana wa wauguzi walipeleka ripoti zote kwa Max Petito mtu mzima.

“Ok kazi nzuri vijana, nilijua Rodolph ni mjanja lakini si hivyo ha ha ha ha” Max aliongea na vijana wake huku akitoa cheko lake zito kisha akaendeleahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“sasa kama nilivyowaelekeza jinsi ya kufanya, kwa kuwa akibanwa na polisi hakika atasema kila kitu na nisingependa tufikie hapo. Maadam keshakamilisha kazi ya kumuua yule mshenzi, kewetu itakuwa ni mteremko tu.” Aliongea huku akinyanyuka mahali pale na kusimama kidogo akawatazama wale vijana

“Mchukueni Sharifa yeye anamudu kazi hiyo na hakika atakamilisha mpango, kila kitu mpatieni kama kawaida yetu” aliwaeleza vijana wake na kuingia ndani kwake ambako hakuna mtu aliyejua anachokifanya huko.



Sharifa, mwanamke mkakamavu mwenye mwili wa mazoezi anyejua michezo ya mapigano ka judo na karate alikuwa mwanamke asiye na mzaa hata kidogo alishamfanyia kazi za hatari na ngumu za kuua watu walioshindikana, alikuwa chini ya Himaya ya Max kwa malipo ya maana kwa kazi maalumu tu. Alijihusisha na mambo ya kijambazi baada ya kufukuzwa jeshini na kujikuta mtaani hana hata ujuzi wa kuchoma vitumbua. Akili yake ilishakata tamaa, pesa aliyopewa na Max ilitosha kufanya mchezo wowote wa hatari ambao utagharimu maisha yake, hakuwa tayari kutiwa mikononi mwa polisi, mara kwa mara aliwatoroka kwa ujuzi wake wa hali ya juu na ulaghai wake wa kike, sasa alikuwa kwenye mtihani mwingine mgumu ambao kwake aliuona ni mchezo mdogo sana wa dakika mbili tu na hakuna mtu ambaye angegundua anachofanya.

Akiwa ndani ya mavazi ya kiuuguzi, gauni jeupe lenye vifungo kwa mbele, saa iliyonining’inia upande wa kushoto wa kifua chake, mkononi akiwa na na chano iliyojaa vifaa kama sindano, drip na madawa mbalimbali alitoka ndani ya chumba cha kubadilishia nguo wauguzi akiwa tayari amewazimisha wauguzi waliokuwa wakitaka kukabidhiana wodi kwa vipigo vichache akiwa na uhakika kuwa watazinduka nusu saa ijayo. Kwa hatua za taratibu alipita koridoni alijifanya kuangalia mafaili mawili matatu ya wagonjwa wengine kisha kuendelea mpaka kwa Rodolph Mampas, alisimama kidogo na kushusha chano yake ya vifaa, akachukua faili la mgonjwa na kulipekua hapa na pale kisha akachukua drip na kumtundikia baada ya kuiweka sawa na kuhakikisha inaenda sawia alichukua moja ya sindano alizokuwa nazo na kuchoma drip ile kisha kumimina dawa iliyopo, wakati anachukua chano yake aondoke akakutana uso kwa uso na mganga wa zamu walitazamana kwa sekunde kisha Sharifa akaelekea chumba cha wauguzi kwa mwendo wa haraka kidogo, mganga yule alipatwa na wasiwasi kwani sura ile hajawahi kuiona alimuwahi mgonjwa lakini alikuta ameshakufa kwa sumu aliyowekewa katika drip ile

“Afande! Afande!” Mganga alimwita afande huku akimuonesha kidole kwa muuguzi bandia. Koplo Abdala kwa haraka alielewa kilichotokea alimfuata yule muuguzi bandia

“Chini ya ulinzi!” huku akimnyoshea mtutu wa Short Machine Gun, Sharifa hakupoteza muda alijirusha na kutua karibu na Koplo Abdala na kumpiga double kick zilizomfanya apepesuke na bunduki kumtoka mikononi, Sharifa alikimbia kuelekea kwenye ngazi za kushuka chini ya wodi ile, kelele zilisikika uku na huku wengine wakiita mwizi na wengine wakipiga kelele za msaada, Sharifa alisukuma watu kwenye ngazi na kuwaacha wakianguka huku na huku. Koplo Abdala alinyanyuka upesi na kukimbilia kwenye ngazi

“freeze!!!” alitoa ukelele huku akiweka sawa SMG yake, Sharifa aligeuka na bastola tayari ikiwa mkononi alifyatua risasi na kuharbu vibaya bega la kushoto la Koplo Abdala lakini kabla hajaanguka chini naye alijibu kwa kufyatua risasi iliyomkosa Sharifa na kuvunja kioo cha dirisha liliokuwa mahali hapo, Sharifa alijigeuza na kubinjuka sarakasi ili atoke kupitia dirisha hilo lakini alichelewa, risasi tatu moja ilitua katika paji la uso, ya pili ilitua moyoni na ya tatu ilitua katikati ya kifua, Sharifa alijibamiza ukutani na kuanguka chini bastola yake bado ikiwa mkononi, Koplo Abdala aligeuka kuangalia nyuma alimuoana Kamanda Amata akiwa bado na ile bastola yake mkononi ikimuelekea Sharifa, tayari ilishafanya kazi yake





“Asante kaka, angeniua huyu” Koplo Abdala alimshukuru Amata

“Usijali, pole sana” Amata alimpoza Koplo Abdala ambaye kwa wakati huo alikuwa akivuja damu katika bega lake la kushoto. Amata aliyeingia hapo kama mzimu alimfuata yule muuguzi marehemu na kumkagua hapa na pale akaichukua bastola yake na kuiweka katika mfuko maalumu. Sura haikuwa ngeni kwa Amata ila alishasahau alimuona wapi.



“Sharifa ameuawa” Bokelo, mmoja wa vijana wa Max alikuwa akimpa ripoti Max mtu mzima

“Unasema?” Max aliuliza kwa mshangao, hakuamini anachosikia, akaongeza swali

“Amekufaje?”

“Mzee hapo sasa ndipo penye utata” Bokelo aliendelea kusema “hatujui ni nani aliyemuua ili tulisikia milio ya risasi, kutokana na kanuni za kazi yetu, Sharifa ameuawa” Bokelo alimaliza. Max Petito mtu mzima alitokwa na kijasho chembamba hakujua afanye nini, hakuamini kama Sharifa kauawa kwa jinsi alivyomuamini na alivyomfanyia kazi nyingi na ngumu, lakini ukweli haukupingika kuwa Sharifa aliuawa kwa risasi iliyotoka kwenye bastola ya kiitaliano inayomilikiwa na Kamanda Amata au TSA1 kama anavyojulikana kikazi.

***



Taarifa za kutoweka Bw Punde Kishime zilimfikia Inspekta Simbeye masaa machache yaliyopita, akili ilianza kuchoka kwa mikasa ya ajabu kama hii. Inspekta Simbeye hakujua wapi kazi ile aianzie baada ya kupewa taarifa na vijana wake waiokwenda kumuona mke wake na kuchukua maelezo fulani, alijaribu kuunganisha matukio ili aifanye kuwa tukio moja lakini hakuona uhusiano wowote katika hayo, kupotea Mh Kishime, ajali ya ajabu ya Mh Chakwima na nyaraka za serekali zilizopote, jana usiku wameokota maiti ya mtu wasiyemjua lakini anasadikiwa ni jambazi katika barabara ya Makunganya, tukio liliotokea Belmont Hotel alipojaribu kuoanisha matukio hayo alihisi kuchanganyikiwa. Alichofanya ni kuweka askari wawili nyumbani kwa Bw Kishime na Bw Chakwima ili kusubiri labda wauwaji au watekaji watakuja tena katika moja ya nyumba hizi.

Mbele ya meza kubwa ya Inspekta Simbeye alisimama konstebo Salum na kumpa taarifa ya kifo cha mgonjwa wao na kujeruhiwa kwa Koplo Abdala.

“Hebu nenda halafu uje baadae” Inspekta Simbeye aliropoka bila kujua, akavuta droo yake na kutoa pakiti ya sigara, Marlboro ndiyo sigara iliyompa burudani kila akiwa katika mawazo. Aliwaza hili akawazua lile lakini aliona kazi ile ilikuwa ngumu sana na ilihitaji watu maalumu sio polisi wa kawaida. Kichwani mwake alimfikiria sana Kamanda Amata ambaye hapo nyuma alikuwa nae sambamba katika harakati kama hizi, ujuzi na umakini wake katika kucheza na mauti ilimfanya Inspekta Simbeye atoe tabasamu pana na kujifariji kuwa kazi itakwisha tu.

***



Ndani ya Garden night club, Amata alitulia kwenye kaunta akipata bia yake ya safari

Taratibu huku akingalia vijana wanavyocheza muziki wa taratibu wakiwa na wenzi wao, alikunywa safari yake ya kwanza na ya pili kwa utulivu mkubwa huku akitikisa kichwa kufuatili muziki laini uliokuwa ukiendelea katika club hiyo iliyo karibu kabisa na viwanja vya Gym Khana.

“Kaka naomba tukacheze” sauti nyororo ilimshtua Amata katika wimbi la mawazo, msichana mrembo, alisimama mbele yake akimrembulia macho na kujigeuzageuza kumshawaishi Amata, Amata macho yake yaliishia kifuani kwa dada yule ambaye alikuwa na kifua kilichojaa na matiti ya mviringo ambayo yalimfanya Amata aheme haraka haraka.

“Asante lakini sijisikii vizuri kucheza muziki, kaa hapa na mimi tunywe kidogo” Amata alijibu ombi la dada yule.

“Nipe Heineken tafadhali” yule dada aliomba kinywaji na kupatiwa, mazungumzo yakaendelea hapa na pale. Amata alipocheki saa yake ya mkononi alikuta imekuwa usiku mwingi

“Samahani dada narudi muda si mrefu” alimauaga yule dada na kumpati elfu ishirini. Amata alitoka njea na kuangaza huku na huku hakuona dalili ya mtu eneo hilo alivua kabashingo yake nyeupe na kubaki na nguo nyeusi tupu ambazo zilimficha gizani, kwa mwendo wa harakaharaka akakatiza mitaa miwili mitat na kukunja kushoto, jengo la kwanza, la pili, la tatu akatazama uku na huku kulikuwa na polisi mmoja aliyeshika bunduki lakini alipomwangalia alimuona kuwa kasinzia ‘askari wetu’ Amata alijisemea moyoni, kisha aka zunguka upande wa nyuma wa jengo hilo, kwa kutumia dampo la takata la manispaa alipanda na kujirusha ndani ya wigo wa jengo hilo na kutua kwa utaulivu kisha kutulia kama kwa sekunde kadhaa akasikia nyayo za mtu zikielekea upande huo akajibaza kwenye karibu kabisa na simtank lililopo hapo, polisi akapita karibu kabisa lakini hakujua hata kama mahali hapo kuna mtu. Amata akazunguka upande wa nyuma na kwakutumia bomba za chuma za maji machafu akakwea kuelekea juu mpaka ghorofa ya tatu, hapo akakanyaga kiukuta kinachotenganisha ghorofa moja na nyingine aktembea kwa makini mapaka katika dirisha moja kubwa akajaribu kulisukuma likakubali kumbe lilikuwa halikufungwa akilfungua na kuingia ndani, taratibu alitembea ndani yachumba hicho kilichoonekana kuwa ni jiko akasukuma mlango ukafunguka akatokea katika korido ndefu yenye zuria jekundu akapita mpaka mlango wa tatu akasoma mlangoni ‘Mr Punde Kishime’ maandishi yaliyojinyonganyonga kwa utaalamu wa hali ya juu yaliupendezesha mlango huo. Kwa utaratibu akatoa kijifunguo chake nakujaribu kukichezea kitasa hiko, hakikuleta ubishi mlango ukafunguka akaigia ndani na kurudishia kisha akazna kuangalia hapa na pale akiwa hajui hata ni nini anachokitafuta, akashika hapa akashika pale, alipoona hapati anachokitaka aliketi katika kiti cha mheshimiwa na kuvuta droo ya meza hapo alikutana na kilichomvutia, bahasha ya kaki inayofanana kabisa na ile aliyoikuta ofisini kwake. Aliichukua na kuitia mfukoni kisha kutoka katika mlango uleule, alipoufunga tu....





(...)alihisi kama kuna mtu nyuma yake, Amata alitulia tuli na kisha kugeuka taratibu lakini hakuona mtu korido yote ilikuwa na giza aligeuka pande zote hakuona kitu wala mtu, akaanza kutembea taratibu kuelekea chumba kile alichoingilia, aliambaa ambaa na ukuta na kuipita milango kadhaa, kabla hajafika mlango alioutaka akasimama ghafla, akaona kitu chenye guo jeusi kikipita kama mzuka kutoka mlango mmoja kwenda mwingine, akasita kidogo na kujiweka tayari kisha kwa tahadhari akasogea katika mlango ule kabla hajaangalia ni nini alichokiona alijikuta akipigwa pigo moja la kareti shingoni liliomfanya ayumbe kidogo na lipokua sawa alijaribu kujihami na mashambulizi hayo. Amata alishangazwa na kiumbe hiki jinsi kinavyopiga mapigo ya haraka haraka lakini Amata naye alikuwa mtundu kwa michezo kama hiyo. Amata alirudi nyuma hatua chache na kucheza judo mbili tatu ambazo zilimfanya adui yake kuchanganyikiwa kidogo na kukosa uelekeo, Amata akambadilishia zoezi, alijirusha juu na kuitanua miguu yake na kumchapa mateke mawili maridadi kabisa, lakini kabla hajatua chini alipigwa ngumi moja katika korodani zake Amata alipata maumivu makali na kudondoka chini. Kitendo hicho alikilaumu sana kwani kilimpa mwanya adui yake kumpiga mateke ya mbavu, Amata alijinyanyua na kupiga magoti, yule adui yake hapo ndipo alipofanya kosa alipimpiga teke Amata na Amata aliudaka mguu wake na kuuzungusha kwa ghafla na kushtua mifupa ya mguu ule, yule mtu alitoa mguno wa maumivu na kitendo bila kuchelewa alimpa Amata pigo la nguvu kwa kutumia mikono yake akidhamiria kumzimisha lakini Amata alipangua pigo lile kwa ufundi mkubwa, Amata aliinuka kwa haraka na kabla adui yake hajakaa tayari alichezea kareti za haraka haraka na kujikuta akishindwa kujibu mapigo. Yule mtu alijizungusha na guo lake lile jeusi ambalo lilimfanya Amata arudi nyuma kidogo ili awe tayari kwa mashambulizi lakini alijikuta akipigwa double kick zilizomyumbisha mpaka ukutani na kushuhudia mzuka ule ukipotea katika chumba fulani.



Amata alishusha pumzi ndefu, akaangalia huku na huku na kusogea katika mlango ule alipoingia mtu yule na hasimuone ‘Shetani!’ alijiwazia. Amata alibaki kapigwa na bumbuwazi hakuelewa ule ulikuwa mzuka au kitu gani, alijivuta taratibu na kuukuta mlango wa jikoni na kupitia njia aliyoingilia alitokomea gizani kwa tahadhali akijua kwa vyovyote Shetani lile litakuwa linamsubiri njiani.



4

Mh Punde Kishime, alizinduka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta peke yake katika chumba kikubwa sana akiwa amelala juu ya kitanda kikubwa chenye shuka jeupe, alipojichunguza alijikuta hata nguo alizovaa hazikuwa zile za mara ya mwisho, luninga kubwa ilikuwa ikionesha katuni za Tom na Jerry ambazo zilimfanya atabasamu kidogo. Alikitazama chumba kile hakuona kitu isipokuwa kitanda alicholalia, luninga na pembeni kulikuwa na henga iliyotundikwa suti safi ya rangi ya kijivu ikiwa ndani ya mfuko wa plastiki, Bw Kishime hakuelewa kinachoendelea, wala hakujua ni wapi alipo, mara hodi ikagongwa na mlango ulisukumwa ndani bila ruhusa ya aliyemo. Msichana mrefu mwembamba aliingia ndani mkononi akiwa na bahasha ya rangirangi, moja kwa moja alimuendea Bw Kishime na kumpatia bahasha ile. Bw Punde Kiahime aliipoke na haraka aliifungua kuona kilichoandikwa “1600 at Hillton Hotel” . Bw Kishime aliusoma ujumbe huo mfupi na kuiweka kitandani bahasha ile, aliponyanyua uso wake hakumuona yule msichana na badala yake alisikia hodi nyingine ikigongwa katika mlango huo na ukasukumwa ndani kama mwanzo, kijana wa makamo alisimama mbele yake akiwa katika suti iliyomkaa vizuri kabisa

“Good Afternoon Sir!” alimsabahi Mh kwa kiingereza safi, hapo ndipo alipogundua kuwa hayuko Tanzania, maswali mengi yalimpita kichwani.

“Im here to pick you Sir, Mr Mahmoud want to meet you” aliendelea kuongea huku akitabasamu akimaanisha kuwa Mr Mahmoud anataka kuonana na Mh Kishime.

“Ok” Mh Kishime alijibu huku akinyanyuka kuelekea maliwato.

Muda mfupi Mh Kishime alikuwa mbele ya kioo akijiangalia.

Muda si muda walikuwa kwenye chunba kingine ambacho kiliandaliwa vizuri kana kwamba kuna mkutano wa watu kadhaa lakini haikuwa hivyo. Bwa Kishime aliketi na mbele yake katika meza hiyo aliketi mtu mwingine aliyevaa mavazi ya uarabuni, Amata alimtambua kuwa ni mwanaume baada ya kuona ndevu zake ndefu, aliketi kwa kumtazama Amata.

“Karibu Oman” yule mgeni alijitambulisha. Bw Kishime liitika kwa kichwa tu huku akitaka kujua wapi alipo na nini kinaendelea.

“Naitwa Al-haj Mahmoud” alijitambulisha na kuendelea “Bila shaka ni Bw Punde Kishime” akimalizia kwa kumtaja jina mgeni wake yule.

“Kwa nini umeniteka Bw Mahmoud?” Bw Kishime alimtupia swali

“Kishime, sijakuteka, mimi sina desturi ya kuteka watu” Mahmoud alijibu

“Sasa hapa nafanya nini?” Kishime aliulizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Tulia utaelewa kila kitu na utajua hapa umefikaje, ondoa shaka Bw Ki-Kishime” Mahmoud aliongea kwa kiswahili chake chenye lafudhi ya kiarabu. Kimya kifupi kilitawala kati yao wakati ambapo Bw Mahmoud alikuwa akifungua kablasha fulani mezani pale.

“Bwana Kishime kama nilivyojitambulisha, mimi na rafiki zangu tunapenda kufanya kazi moja muhimu na wewe pamoja na rafiki yako Bw Chiwawa.” Alitulia kidogo kumeza mate na kisha akaendelea

“Kama uivyosoma katika ile barua tumekuletea ofisini kwako pale Dar es salaam, lakini hukutujibu na ndiyo maana tukakuleta huku ili tuongee ana kwa ana, wala hatuna nia mbaya na wewe ila ni nia nzuri tu na mwenyewe utaifurahia.” Alimtazama usoni na kumuona Bw Kishime akiwa katika utulivu wa hali ya juu.

Baada ya maneno haya ndipo Bw Punde Kishime alipoikumbuka barua aliyoletewa ofisini kwake na mwanamke aliyevaa vazi jeusi lenye kuonesha macho tu, alikumbuka kila kitu na ujumbe alioachiwa kwa maneno na yule mwanamke lakini yeye hakuutilia maanani



Wiki moja nyuma

Dar es salaam



“Samahani Boss, kuna mgeni wa dharula anataka kukuona” katibu wa ofisi ya Mh Punde Kishime alimueleza boss wake

“Si nilishakwambia kuwa mgeni asiye na miadi usimruhusu” Bw P. Kishime alimkaripia katibu wake japo kwa sauti ya chini

“Amesisitiza anataka kukuona kwani katoka mbali, kasema ana bahasha tu mkononi” katibu muhtasi aliongeza.



Mgeni yule aliingia ofisini kwa Bw Kishime na kujikaribisha kiti. Bw Kishime alimwangalia mgeni yule kwa makini, alikuwa amevaa baibui jeusi juu mpaka chini usoni kafunika kila kitu isipokuwa macho tu, hata kama walitazamana Bw Kishime aliona wazi kuwa bibie huyu alikuwa hamuoni.

“Karibu mrembo” Bw Kishime alimkaribisha mwanamke yule. Yule mwanamke akaingiza mkono ndani ya vazi lake na kutoa bahasha kisha kumpatia Bw Kishime. Bw Kishime aliisoma barua ile taratibu mara alikunja sura na mara alitabasamu, baada ya kumaliza akairudishia katika bahasha yake na kuitia katika droo, alijiegemeza katika kiti chake kikubwa cha kunesanesa huku mikono ikiwa kichwani, alipoishusha akajiinua na kuegemea meza yake

“We ni nani? Na unatoka wapi?” Bw Kishime alimsaili mwanamke yule

“Boss anahitaji jibu haraka. Ukishindwa atalitafuta mwenyewe” Mwanamke yule alisimama baada ya kutoa kauli hiyo.

“Barua hiyo ni yako usiiache ofcn tafadhali” yule mwanamke alimaliza na kutokomea zake nje ya ofisi hiyo. “Bw. Kishime alibaki kaegemea meza yake akitafakari. Mara simu ya mezani ikaita

“Hello!” Kishime aliita

“Bw Punde Kishime hata sisi tunahitaj shime yako, soma na utafakari juu ya ombi letu kisha utupatie jibu, kama huna jibu tutalifuata wenyewe” sauti ya upande wa pili ilijibu

“Wewe ni nani mbona sikuelewi?!” Bw Kishime alijikuta akiongea peke yake katika simu hiyo ambayo tayari ilikuwa imekatika kitambo...







Inspekta Simbeye aliinua simu yake ya mezani na kuiweka sikioni lakini bahati mbaya alisahau ni nani anyetaka kumpigia, akasonya na kuitua simu hiyo kuiweka mahali pake. Alichukua kitabu chake ca kumbukumbu na kuanza kupitia jambo moja baada ya jingine akifikiri labda lipo mojawapo litalomsaidia, ndipo alipogundua kitu, uzembe uliofanywa na vijana wake ‘kwa nini hawakufuatilia simu ile ilitoka wapi, labda tungepata kitu fulani’ aliinua tena simu yake ya mezani na kukoroga namba chache

“Ofisi ya maelezo Posta na Simu, nikusaidie nini tafadhali” sauti ya kike ilisikika upande wa pili

“Unaongea na Inspekta wa Polisi kituo cha kati... samahani naomba unijulishe simu zifuatazo zilipigwa kutoka eneo gani na kwa namba gani” Inspekta Simbeye alizitaja namba mbili tofauti na kuambiwa asubiri kidogo.

“inaonekana namba hizo zote zimepigwa kutokea Keko Mtaa wa Ngomati, nyumba namba 125X kwa Bw Ayubu Bakari” sauti ile ilimpa jibu ambalo lilimfanya Inspekta Simbeye atabasamu kidogo.

***

Nyumba ya Mzee Ayubu Bakari haikuwa ngumu kupatikana, moja kwa moja polisi waliovaa kiraia walifika eneo hilo la Keko mtaa wa Ngomati, nyumba ilikuwa wazi kulionekana tu msichana anayeosha vyombo, wote walijua mara moja ama binti yake au msichana wa kazi, walibisha hodi na kukaribishwa ndani, sebule ndogo isiyo na vitu vingi, kulikuwa na vikochi vitatu vikuukuu na kativii kamoja ka zamani, redio aina ya Philips ilikuwa ikitumbuiza wimbo wa Sikinde, ukutani kulikuwa na picha moja tu ya mwanaume, mwanamke na watoto wanne labda ilikuwa ni familia ya mzee Ayubu.

“Samahani dada, baba tumemkuta?” mmoja wa wale askari aliuliza

“Hapana mbona baba alishafariki muda mrefu” yule dada aliwajibu

“Oh! Pole sana” yule askari aligundua kuwa amekosea jinsi ya kuuliza swali lile kisha akaendelea

“Na mama je?”

“Mama yuko nyumba ya pili anasuka”

“Mwite tafadhali” aliomba yule askari.

Muda kidogo tu mama mtu mzima aliingi sebuleni pale alionekana wazi kuwa ameshtushwa na ugeni ule, alijichagulia kigoda na kuketi, kadiri ya unene aliokuwa nao makalio yake yalikifunika kigoda chote.

“Karibuni jamani sijui niwasaidie nini” mama yule aliwauliza

“Bila shaka wewe ni mke wa mzee Ayubu” yule askari aliuliza

“Mh! Mzee Ayubu...” yule mama alionekana kushangaa kidogo

“Mbona umeshtuka mama” yule askari alisaili tena

“Hapana, yaani simfahamu mtu huyo mimi mume wangu alikuwa anajulikana kama Mzee Kijiti, alipewa jina hilo kutokana na wembamba wake, lakini huyo mzee Ayubu ndiyo namsikia leo” yule mama alijibu

Wale vijana walitazamana kuonesha kuwa hata wao wanashangaa hilo.

“Mama samahani, sisi tunatokea kampuni ya simu, nia yetu ni kujua kama simu yenu bado mnaitumia au la” mwingine alidakia na kugeuza mada iliyopo.

“Aah hapa hatuna simu zaidi ya hizi za mikononi mwanangu.” Yule mama alijibu hoja ile. Hakuna cha kufanya, wale vijana waliamua kuaga na kuondoka, wakiwa nje walijadiliana hili na lile. Waliangalia angalia maeneo yale na kugundua kulikuwa na nguzo moja kuu kuu ya simu ambayo ilikuwa na nyaya zilizokatika muda mrefu, mmoja wa askari wale aliziangalia kwa umakini nyaya zile lakini hakuona kama kuna lolote la kumsaidi. Walijipakia kwenye gari yao na kuondoka,

“Hawa jamaa watata kweli!” mmoja wao aliwaeleza wenzake

“Sasa simu waliyoipiga waliipata wapi maana zile nyumba za NHC hata simu hazina” mwengine alidakia. Askari wale moja kwa moja waliamua kurudi kituoni kumfikishia taarifa ile Inspekta Simbeye.

Inspekta Simbeye hakuipokea taarifa hiyo kwa furaha ila ilimletea maswali zaidi kichwani mwake, alinyanyuka kitini na kutoka nje ya ofisi yake lakini hakujua wapi anataka kwenda.

Akiwa nje ya ofisi yake alitazama yapitayo wanaotoka na wanaoingia kituoni hapo, alipokea saluti za kutosha kutoka kwa wachini yake waliopita eneo hilo lenye shughuli nyingi. Macho yake yalitua katika gari moja nyeusi aina ya Vox iliyosimama karibu kabisa na maegesho ya gari zingine, gari ile ilikuwa inaunguruma haikuzimwa lakini ilikuwa na vioo vyeusi kabisa, Inspekta Simbeye alitulia kuitazama gari ile ambayo haikuonesha chochote kinachoendelea si kwenda mbele wala kurudi nyuma, hakuna aliyejua ni nani au ni nini kilichopo katika gari hilo. Mlango ulifunguka kwa kuvutwa nyuma mtu mmoja akashuka amevalia guo jeusi kuanzia viatu soksi, nguo hiyo iliruhusu macho tu kuonekana, aliichukua pochi yake na kuibana kwapani kisha kwa hatua za haraka haraka alizielekea ngazi za kituo cha polisi alizipanda na kumpita Inspekta Simbeye pale aliposimama na moja kwa moja aliifikia kaunta. Inspekta Simbeye alitamani kutoa amri ya kukamatwa mwanamke yule lakini aliona si wakati muafaka, kiu ilimshika kumhoji maswali angalau moja au mawili lakini roho yake ilimwambia hapana. Akaona labda anaweza kumkamata mtu asiyehusika maana mavazi haya ni mavazi heshima kwa wanawake. Alimuangalia mwanamke yule alipoanza kuteremka ngazi zile kulielekea lile gari mpaka alipoingia na kufunga mlango, mwendo wa mwanamke yule ulimtia mashaka sana Inspekta Simbeye. Gari ile iliondoka taratibu na kuchukua barabara ya railway kuelekea Kurasini, Inspekta Simbeye aliiona gari nyingine ya nyeusi ikiingia barabarani kuelekea kule ilikoelekea ile ya kwanza, ndipo alipoanza kuwa na mashaka. Taratibu alirudi ofisini kwake, alipoingia alikuta bahasha mezani kwake juu ikiwa na jina lake, aliichukua na kuifungua ndani akatoa karatasi moja ya njano, aliyasoma yote yaliyoandikwa alipomaliza alishusha pumzi ndefu na kuiweka bahasha ile katika droo la meza yake na kujiweka vizuri katika kiti chake, mara simu ya mezani ikaita, kwa shauku akainyakua na kuiweka sikioni

“Nafikiri ujumbe wetu umeupata, basi tunaomba utupatie jibu kama huwezi tutalifuata wenyewe...” kabla hajajibu simu ile ilikatika. Inspekta Simbeye alishikwa na hasira, hakuweza kuvumilia kudharauliwa namna ile, aliinyayua tena ile simu na kuipiga posta na kuuliza simu ile alitokea wapi, jibu alilopata ni lilelile Keko mtaa wa Ngomati.

***



Amata alipaki gari yake mbele ya kibanda kimoja cha chips, eneo la Temeke mwisho, akashuka na kuagiza chips mayai huku jicho lake likiangalia kule ilikosimama ile Vox, akishuhudia kila kitu kinachoendelea aliweza kumuona mwanamke yule akiteremka na vijana watatu wote wakaingia ndani ya nyumba moja ya kizamani iliyopo hapo, Amata alikaa kwenye kibenchi kidogo na wanafunzi wa sekondari waliokuwa wakila chips zao huku wakibadilishana mawazo juu ya masomo yao ya siku hiyo. Amata aliangalia nyendo zote kwa chati sana, baada ya muda mfupi gari ile iliondoka kuelekea mjini. Amata aliinuka alipokaahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“nihifadhie chips zangu nakuja” alimueleza muuza chips

Kisha akaingia kwenye ile tax nyeusi aliyoikodi na kuendelea kuifuata gari ile, alihakikisha muda wote dereva wa tax hajui kama kuna gari wanaifuata ila tu alimpa maelekezo ya hapa na pale na aliyafuata kwa ufasaha. Wakiwa katika katika mataa ya Tazara, Amata alihisi kitu cha baridi kikimgusa na kumonyeza katika moja ya mbavu zake

“Tulia hivyo hivyo! Usilete makeke ntakutoa uhai muda si mrefu” sauti ilisikika kutoka katika kiti cha nyuma. Amata alijaribu kugeuka lakini alilazimishwa kutulia vilevile.

“Dreva kata kushoto tuelekee uwanja wa ndege” dreva aliamuriwa na mtu huyo. Gari ile alikata kushoto na kuchukua Nyerere road. Amata alitulia kitini kama alivyoelekezwa, mara alihisi kitu chenye ncha kali kikipenya katika moja ya misuli yake ya shingo, muda kidogo alihisi macho yake yanakuwa mazito alijaribu kushindana na hali hiyo lakini haikuwezekana, usingizi mzito ulimchukua na hakujua tena nini kinachoendelea.



Gina alikaa ofisini bila kumuona Amata, alianza kuingiwa na wasiwasi alijaribu kupiga simu ya Amata lakini haikuwa ikipatikana kabisa, alijaribu laini zote sita lakini hakuna iliyokuwa hewani. Gina hakujua la kufanya aliangalia saa yake ya mkononi ilishatimu saa saba na nusu mchana, alitulia kidogo mezani kwake akindelea kusoma kitabu cha ke cha hadithi za mapenz. Mara kwa mara aliangalia saa kwa maana Amata alimwambia kuwa ikifika masaa manne hajarudi basi ajue kuna tatizo na apige mara moja simu fulani ambayo alimpatia namba yake. Saa zilikwenda na dakika ziliyoyoma Amata hakuonekana kurudi wala dalili zake, Gina alinyanyua simu na kuanza kubofya ile namba lakini bado roho yake ilisita akairudisha mezani simu ile. Aliinua tena nadio muda huo ambapo aligundua kua ile si simu, aliigeuzageuza huku na huku akifungua hapa na pale ilimradi tu udadisi. Aliamua kutoka ofisini kwani muda ulikuwa umeisha, alinyanyuka nakufungafunga vilivyo vyake bila kuisahau ile simu feki aliyopewa na Amata, Gina aliona kuwa Amata amefanya moja ya mizaha yake kwa kumpa toy lile la simu ‘eti nikichelewa piga namba hii’ alicheka mwenyewe huku akifungua mlango wa gari yake na kuketi nyuma ya usukani, lakini kabla hajawasha gari ile gari ile alipiga namba ile aliyopewa na Amata katika ile toy ya simu alipoweka sikioni huku akiwa anacheka alisikia sauti ya kitoto ikisema

‘Rescue! Rescue! Rescue!’ Gina alitoa ile toy sikioni na kuingalia, aliona hamna kitu kingine zaidi ya taa nyekundu zilizokuwa zikiwakawaka, akafungua droo ya gari yake na kukitumbukiza katika droo ya gari na kuondoka huku akicheka sana.

Kishindo kikubwa kilisikika katika njia panda ya mtaa wa Samora na Morogoro vumbi lilitimka na watu kutawanyika huku na kule, kelele na vilio vilisikika. Polisi wa usalama barabarani walianza kukimbilia huko katika eneo la tukio.

Mtu mmoja alioneka na akishuka katika gari aina Range rover nyeusi akiwa kavaa baibui kubwa jeusi alionekana macho tu alitembea kwa haraka kuyapita magari kama matatu hivi na kulifikia gari la Gina alipiga ngumi kioo na kuangalia ndani lakini hakuweza kuona kitu wa la mtu ndani yake, aligeuka huku na huku mara polisi mmoja alionekana kumuuliza maswali fulani lakini mtu yule aliendelea kulizunguka gari lile bila kujibu chochote na lipoendelea kumgasigasi polisi yule alionekana akianguka chini na kulala barabarani, yule mtu aliingia katika gari ile alofika nayo na kuondoka kwa kasi.





Mh Chakwima alikuwa akiandika vitu fulani katika kitabu chake cha kumbukumbu, akiwa kimya kabisa peke yake kitandani pale na akiwa amezungushiwa kitambaa maalumu kuonesha mgonjwa huyu yu mahututi. Muda mrefu ulipita akiwa anaandika na kuandika bila kuchoka.

“Mme wangu unaandika nini muda wote huo?” Mkewe alimuuliza, lakini Chakwima aliendelea kuandika tu

“Utajua baadae mpenzi, kwa sasa we tulia” Mh Chakwima alimjibu mkewe huku akiendelea kuandika, alijaza kurasa na kurasa bila kuchoka huku akinywa red bull yake taratibu.

“Samahani Mh kuna wageni wanataka kukuona” mhuguzi alimpa taarifa Mh Chakwima

“Nimekwambia waambie naumwa sana siwezi kuongea na mtu, kwani wewe hujui kazi yako!” Mh Chakwima alifoka.

Baada ya kuandika kwa muda mrefu akakiweka kitabu chake juu ya droo

“Naomba niletee koti langu la suti” alimuomba mkewe

“Mbona halipo hapa!” alijibiwa na mkewe, Mh Chakwima alionekana wazi kutaharuki kwa jibu hilo

“Lipo wapi?” alimuuliza mkewe huku akimkazia jicho

“Tulilipeleka nyumbani” alijibu kwa woga kidogo

“Ulilipekuwa na kukuta chochote?”

“Hapana” alitoa jibu kwa mumewe huku akimsogelea karibu.

“Ok, chukua gari nenda nyumbani ukaniletee lile koti sasa, na uwe makini sana kuna vitu vya kuvunjika” Mh Chakwima alimuagiza mkewe.

Mke wa Chakwima aliondoka katika viwanja vya Muhimbili kuelekea nyumbani kwake Makongo juu. Kama kwaida ya Dar es salaam foleni nyingi za barabarani, mama huyo kutokana na uhodari na uzoefu wa kuendesha katika jiji hilo, haikumchukua muda kuipata barabara ya Ally Hassan Mwinyi na kuelekea Morocco.

Mama Chakwima alikunja kona ya nyumbani kwake taratibu moyoni mwake akiwa na furaha kuona mumewe ampendaye ameamka na yuko safi isipokuwa tu mguu wake uliovunjika. Alipokaribia geti la nyumba yake alikuta gari moja aina ya Noah ya rangi nyeusi imesimama karibu kidogo ya nyumba hiyo, aliitupia jicho la haraka na kukumbuka kuwa mahali fulani alishawahi kuiona gari ile lakini wapi hakupata kukumbuka vizuri. Alipiga honi na geti lilifunguka akaingiza gari ndani moja kwa moja. Ndani ya nyumba yake hapakuwa na mtu mwingine zaidi ya mpishi na shamba boy wake aliwakuta wakiwa katika kijichumba kidogo wakiangalia TV.

“Nyie...” aliwashtua kwa muito huo

“Hiyo gari hapo nje ya nani?” aliwatupia swali na wao wakabaki wakitazamana hawakuelewa cjhochote kwani walikuwa na muda mwingi wakiangalia tamthiliya ya Secreto d’amore, wakakurupuka na kwenda nje kuangalia gari hiyo, maana si kawaida gari yoyote kupaki katika eneo lile.

Aliingia chumbani na kuelekea moja kwa moja mahali ambapo anaweka nguo ambazo anataka kupeleka kwa dobi, akalitoa koti lile na kupekua mifukoni, mfuko wa ndani alikutana na kitu kama kasha la plastiki alipotoa alijikuta ameshika CD yenye kava ya khaki, haikuwa na picha yoyote isipokuwa namba 6 iliyosomeka ‘6ies’ aliigeuza geuza kisha akaitia katika mkoba wake, akanyanyua simu yake na kupiga namba fulani kabla hajaondoka.

***

“Tunataka utueleze, una uhusiano gani na Max Petito?” baunsa mmoja limuuliza swali Amata baada ya kumpa kichapo kizito kiloichomtoa damu nyingi sana. Akiwa kafungwa katika kiti cha mbao na kuvuliwa nguo zote, Amata hakuwa na uwezo wa kufanya chochote isipokuwa kuwaangalia tu watesi wake.

“Sema! Unajifanya jeuri siyo?” baunsa yule aliongea kwa ukali hku mkononi akiwa kashika fimbo iliyotengenezwa kwa mpira na kuwekwa vitu kama miba midogomidogo.

“Subiri BIG! Ushamtesa sana tazama kabaki nyama tu, muache

Atasema tu!” mtu mwingine mwenye asili ya kizungu lakini alionekana kuchoka kimaisha alidakia. Amata ndipo alipata kujua kuwa yule baunsa mwenye mwili mkubwa jina lake ni BIG, akakumbuka kauli ya yule muuaji aliyempiga risasi kule Belmont Hotel. Amata aliwaangalia jamaa wale waliomzunguka kwa jicho la chini kwa chini akiwa kainamisha kichwa chake hku damu zikimtoka hasa sehemu za miguni na kichwani.

Watu wanne walikuwamo katika chumba kidogo alichofungwa Amata, wawili wakiwa wametulia tu viunoni mwao wakiwa na bastola zilizoning’inia na mikono yao wakiwa wameikunjia vifuani mwao, jamaa hao hawakuwa wakicheka wala kutabasamu muda wote walikuwa kimya wakiangalia kinachoendelea tu, pamoja nao kulikuwa na wengine wawili mzungu aliyejichoka ambaye sura yake ilionesha kama aliwahi kumwagiwa tindikali miaka mingi nyuma jinsi ngozi yake ilivyovutana vutana na mwingine ana mwili mkubwa mrefu, na ni baunsa kweli kweli. Amata alijaribu kutikisa mikono yake alihisi ikitikisika kwa mbali sana miguu yake ilikuwa huru kabisa, alitazamatazama hakuona kitu kingine katika chumba kile isipokuwa nguo zake zilizotundikwa kwenye msumari kutani ‘Gina, kwa nini Gina?’ Amata alijiwazia sana kwa kuwa aliona wazi kuwa maelekezo aliyompa Gina hakuyafuata sawasawa ‘bonyeza namba Gina, bonyeza, bonyeza’ alijikuta akimuhimiza Gina mawazoni tu kubonyeza kitu fulani halafu baadae alijiona kama mwehu kwa kuongea peke yake na hakuna anyemsikia. Wale jamaa baada ya kuona Amata hajibu chochote walikuwa wakiongea hili na lile kisha kufikia uamuzi.

“Blaco, hakikisha anasema akileta jeuri usisite kuitoa roho yake, hakuna hasara kwetu” BIG aliacha maagizo kwa wale vijana wawili ambao sasa walijiona wamepewa kazi waliyoisubiri kwa hamu sana, kila mmoja alijiweka vizuri tayari kumpa kipigo mateka waona kumlazimisha aseme juu ya uhusiano wake na Max Petito.

“Malizeni na huyo halafu kazi nyingine ni kumguata Max mwenyewe” BIG aliwaagiza vijana wake.

Vijana walimsogelea Amata kwa bashasha ya kuonesha uzoefu wao katika kutesa mtu, ngumi ya kwanza ilitua sawia katika shavu la Amata na kupelekea Amata kutema damu, ngumi ya pili alitua katika shavu la upande wa pili na kumfanya Amata kutoa yowe la maumivu

“Ha ha ha ha Kamanda Amata analia kama mwanamke!!!” walicheka na kugongana mikono. Mara moshi mzito ulitoka katika mfuko wa koti la Amata lililotundikwa ukutani hapo, vijana wale wakaanza kukohoa bila subira, Amata alinyanyua miguu yake na kumpiga double kiki yule jamaa aliyekuwa anampiga na kwa nafasi hiyo alisimama na kuzungusha mikono yake kupitia nyuma kuja mbele na kile kiti kilitua kichwani kwa yule jamaa wa pili ambaye wakati huo alikuwa anakuja kwa Amata, kiti kilivunjika vipande vipande na kuruhus kamba za Amata kulegea, bila kuchelewa alijiviringa chini na kuchomoa bastola ya jamaa aliyeanguka chini, kwa pigo moja la kichwa alimfanya jamaa yule kurudi chini sakafuni alipokuwa anataka kumshambulia Amata, Amata aligeka kwa haraka na kuachia risasi moja iliyochana kifua jamaa wa pili na kumtupa sakafuni damu zikiruka kila upande. Amata, bastola mkononi alijaribu kufungua kamba zile kwa meno lakini mara alisikia mlango wa pili ukitikiswa kana kwamba kuna watu wanataka kuingia ‘bila shaka walinzi’ wazo lilikuja moyoni aligeuka kule mlangoni na kupiga risasi ziolizotoboa mlango ule, alisikia miguno ya maumivu upande wa pili. Alipofanikiwa kufungua zile kamba haraka haraka alitazama kule alikoenda BIG na yule mzungu lakinin hakuona na badala yake alisiki mlio wa gari iliyotoka kwa kasi upande wa nje, alitulia kidogo na kuhakikisha usalama alipoona kimya aliva nguo zake haraka haraka, kisha kwa tahadhali kubwa alinyata kutokea upande ule walikoingilia akina BIG lakini alikuta moilango yote imefungwa, alirudi tena ndani ya chumba kile na kuuendea ule mlango alioutoboa kwa risasi akakuta kufuli lililokuwa likining’inia akalipiga risasi moja likajibu kwa kurhusu mlango ufunguke. Alijibanza kidogo kabla ya kutoka mlangoni pale alipoona kuna ukimya alitoka taratibu akitazama huku na huku, miili ya watu wawili ililala hapo chini ikiwa haina uhai ‘nice shot’ alijisemea huku akiiruka na kuendelea mbele kidogo, aliuta geti kubwa likiwa limefungwa, hakuona haja ya kugombana nalo alipanda juu ya gari moja bovu na kuruka ukuta mpaka nje ambapo alitua kwa utulivu sana na kutulia kama dakika mbili hivi kisha akaaza kutembea taratibu kuelekea barabarani ambako aliona gari zikipitapita.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alipofika barabarani hakupata shida kutambua ni wapi alipo japo kulikuwa na mwanga hafifu wa jua linalozama alitazama huku na huku na kuona duka moja linalotoa huduma za simu, halikuficha chochote kwani jina lake tu lilionesha kuwa hapo ni Gulukakwalala maeneo ya Pugu.

“Upo wapi mpenzi?” sauti ya Amata iliushtua moyo wa Gina aliyekuwa kajilaza katika kochi kubwa nyumbani kwake eneo la Kinondoni Stereo.

“Amata, po wapi wewe, mwenzio nataka kufa kwa ajili yako” Gina aliongea kwa sauti ya kiwewe.

“Sikia! Nipo mbali sana, toka hapo ulipo uje airport haraka” Amata alimueleza Gina

“Airport, Kuna nini Airport?” fanya haraka, usisahau kadi zako za benki tafadhali.

Gina alikurupuka kama kichaa na kunyanyua mkoba wake na kutoka, aliwaaga wadogo zake wawili

“Mi natoka sijui nitarudi muda gani lakini msinitafute, akija mtu mwambieni nimeenda Nairobi kikazi” wadogo zake wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume walisikiliza kwa makini muago wa dada yao.

“Hamna shida dada, safari njema” walimuaga

Gina alitembea kwa tahadhari kubwa huku bastola yake ndogo akiwa kaifutika ndani ya mtandio wa dela alilovaa lakini ndani yake alivalia suruali moja ya jeans na tshirt nyeusi, alitembea harakahakara jioni hiyo mpaka barabara ya Kawawa na kukodi bodaboda iliyomchukua kwa mwendo wa kasi kama kawaida

“Niwaishe nimechelewa ndege!” gina alimuamuru dereva bodaboda

“Husijari dada, sasa hivi tunawasili” kijana yule alijibu kwa kujiamini, akiwa hajavaa kofia ngumu wala tahadhari yoyote, kijana yule alikatisha katikati ya foleni ya magari mpaka eneo la Msimbazi centre ambapo alichepuka na kuelekea Ilala kwa kupitia vichochoroni. Dakika kumi na mbili Gina alifika Airport

“Haya dada, sema lingine” yule kijana alimueleza Gina,

“Sh’ ngapi?” Gina aliuliza

“Elfu nane tu” alijiiwa. Gina alitoa noti ya elfu kumi

“Keep change” alimwamia yule kijana. Kwa furaha sana yule kijana alimshukuru Gina, Gina alichkua namba za simu za yule kijana na kuingia eneo hilo la Airport. Alisimama karibu kabisa na duka la vitabu akijifanya anasoma kitabu hiki mara kile. Akiwa katika hali hiyo akahisi mkono wa mtu ukimshika begani

“Tulia!” sauti ilimwambia Gina...





Gina alichukua namba za simu za yule kijana na kuingia eneo hilo la Airport. Alisimama karibu kabisa na duka la vitabu akijifanya anasoma kitabu hiki mara kile. Akiwa katika hali hiyo akahisi mkono wa mtu ukimshika begani

“Tulia!” sauti ilimwambia Gina. Gina alitulia kama alivyoamuriwa na sauti hiyo

“Umekuja na gari?” Sauti ile ilimuuliza, kwa swali hilo Gina alitambua kuwa huyo ni mtu wanaefahamiana, alitazama kupitia kioo cha mlango wa duka hilo na kumuona Amata akiwa amesimama nyuma yake, lakini hakuwa katika hali ya utulivu kama kawaida yake.

“Hapana sina gari, nimekuja kwa bodaboda” Gina alimjibu Amata huku akiendelea kusoma majina ya vitabu vilivyowekwa katika meza hiyo maalum.

“Tutoke hapa tutaongea vizuri baadae” Amata alimwambia, kisha akatoka kuelekea kwenye maegesho ya magari uwanjani hapo na kufuatiwa na Gina, walifanya hivyo kana kwamba ni watu ambao hawajuani, waliiendea gari fulani iliyoegeshwa hapo, Amata alijaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa, aktoa kitu fulani kama ufunguo na kuupachika akatikisa mara mbili tatu kitasa kikatii mlango ukafunguka. Haikuwa kazi kuliwasha kwani ni kitu kidogo kwa Amata, walitoka uwanja wa ndege na kuelekea mjini, hakuna aliyemuongelesha mwenzie wote walikuwa kimya kabisa. Amata aliegesha gari mbele ya jumba moja kuukuu katika eneo la Gezaulole, waliteremka na kuliendea jumba hilo, jumba lilikuwa kimya hakuna dalili ya watu kuishi humo, miti na manyasi yalikuwa kila mahali hata milango yake haikuonekana vizuri. Amata alitumia nguvu kidogo kusukuma geti la kizamani lililokuwa hapo, kisha wote wawili wakaingia ndani na kutembea taratibu katika ujia uliokuwa ukielekea katika kibanda fulani kama choo kwa ukubwa wake, walifika na Amata akasukuma mlango

“Mbona umesimama, njoo!” Amata alimuita Gina baada ya kuona kasimama tu bila kuingia. Gina aliingia ndani ya kibanda hio na Amata akafunga mlango. Kibanda kilikuwa kidogo kwa ndani hakikuwa na kitu chochote zaidi ya makolokolo mengi palionekana palikuwa kama pakihifadhiwa vipuri tmizi vya magari. Gina hakuelewa kinachoendelea hapo na badala yake alitulia tu, Amata alichika kitu fulani na mara Gina alihisi sakafu ile ikitelemka chini taratibu, alijishika kwa pembeni akihisi kama anataka kutapika, mlango mkubwa ulikuwa mbele yao Amata aliufungua na wote wawili wakaongoza ndani, walipanda ngazi kuelekea ju na kutokea kwenye sebule kubwa sana lenye samani za kuvutia, Amata aliwasha taa na kisha akalienea jokofu lililokuwapo hapo

“Kinywaji gani utatumia?” alimuliza Gina

“Coka baridi sana” alimjibu

Amata akamchuklia Coka na eye mwenyewe akajichkulia grass moja ya Konyagi akachanganya na sprite kisha wakaketi na kunywa vinywaji vyao.

“Asante sana kwa kazi ulofanya lakini mbona ulichelewa?”Amata alimtupia swali Gina

“Asante kwa lipi?” Gina alirudisha swali lile kwa Amata

“Kile kidude nilichokupa nilikwambia ubonyeze masaa mawili endapo nitachelewa kuja kadiri ya miadi yetu, wewe umebonyeza masaa matatu na nusu baadae” alimueleza

“Amata, mi nilijua umeleta utani mwingine kama kawaida yako, nilikiangalia nikaona katoy tu kwa hiyo nilikapuuzia ila baada ya muda nikaona ngoja nifanye ulivyonielekeza” Gina alijibu

“Gina, nilijjua kabisa kuwa ninakokwenda si salama, na kweli nilitekwa na watu wasiojulikana nikapelekwa huko mlima wa Pugu, nimeteswa sana, nimepigwa sana ndiyo maana hapa unavyoniona hali yangu si nzuri najisikia maumivu na damu imevilia maeneo mbalimbali ya mwili wangu” Amata alimueleza Gina, akatulia kidogo na kisha akanyanyka akifuatiwa na Gina wakelekea chumbani. Chumba kikubwa chenye kitanda kikubwa na kochi moja, jokofu ndogo ilikuwa pembeni jirani kabisa na luninga ndogo ya kisasa, Amata alijilaza kitandani kifudifudi, Gina akatulia karibu yake

“Waliniteka, nilipokuwa kwenye tax pale makutano ya Tazara, wakanivutisha unga ambao sikuweza kustahimili nguvu yake kwani nililala na kujikuta nimekaa kwenye kiti cha mbao nikiwa sina nguo na nimefunga mikono yanhu kwa nyuma ya kiti hicho. Wamenipiga sana sikuwa na ujanja kabisa katika hilo” Amata alimueleza Gina, na Gina akamkatisha

“Kwa nini walikwa wanataka nini kwako?” Gina aliuliza

“Walkuwa wanataka majib ya barua yao, ile uliyoipokea ofisini, hilo tu” Amata alijibu

“Hilo tu, kwani bara ile ilihusu nini?” Gina aliuliza tena

“Ntakwambia usiwe na shaka” Amata alijibu

“Vua shati nikupe tiba ya maumivu yako, mimi leo ndiyo nesi wako” Gina aliyasema hayo hku akimfungua vifungo Amata ambaye sasa alijilaza chali, shati la Amata likawekwa pembeni, Gina alianza kuminyaminya kifua kipana cha Amata huku akihisi moyo unamuenda mbio, akaendelea taratibu kumpapasa kifuani, Amata alishusha pumzi ndefu na kuushika mkono wa Gina akamvutia kwake

“Nimeipenda tiba yako!” alimueleza Gina kwa kumnong’oneza sikioni, Gina alitulia tu mkono wake ukibaki kifuani kwa Amata kisha taratibu alianza tena kumminyaminya Amata maeneo ya kifua kisha akateremsha mkono wake sehemu za mbavu na tumbo, Amata alihisi kama anapigwa shoti ya umeme lakini alijituliza akisubiri kuona Gina anataka kufanya nini. Gina alifungua taratibu mkanda wa suruali ya Amata na kuulegeza, mono wa Gina aulitambaa taratibu katika maeneo yaliyofichwa vizuri na suruali hiyo, Amata alishindwa kuvumilia alimvuta Gina na kumnyonya ndimi kabla ya kuanza kumtoa dela lake alilolivaa usiku ule, mambo yakawa mambo.

***

“Wewe na Bw Chakwima mna mvuto sana na wananchi, mnaaminika sana. Sasa lengo letu lilikuwa ni kuwataka ninyi kuwa moja ya sehemu yetu, muijiunge na chama fulani cha siasa pale Tanzania, ila cha upinzani. Msijali kuondolewa kazini kama ikitokea, mkiwa ndani ya chama hiko sisi tutaoa misaada sana ya kukiimarisha kichumi, na kisera ili wananchi wakikubali hasa baada ya ninyi kuingia. Baada ya hapo katika uchaguzi mtafanya kampeni ya nguvu na hakika wananchi watawakubali matachaguliwa na kingia Ikulu ikiwa wewe au yeye mmoja Rais na mwingine makamu wake, hapo ndiyo tutakamilisha mpango wetu uliouona kwenye hiyo DVD” Bwana mmoja aliyeketi katika kiti kubwa mwenye asili ya kizungu alizungma maneno hayo na Mheshimiwa Punde Kishime aliyekuwa katulia akiwasikiliza wadau hao wakimwaga sera zao za kutaka kinunua nchi. Mh Punde Kishime aliskiliza kwa makini na moyo wake ulianza kuingia na kishawishi cha tamaa ya mapesa hayo, alianza kukumbuka sera za Bw John Momose Cheyo ‘nitawajaza mapesa’ .

Jopo lile la watu sita lilimshawishi kikamilifu Mh Kishime ambaye mwisho wake alikubaliana nao, kwa kuanzaia kazi hiyo walimuahidi kumuingizia pesa ya kutosha katika akaunti zake zilizopo ndani ya nchi na kumahidi kumfunglia nyingine nje ya nchi. Mh Punde Kishime hakuwa na la kujibu ‘utajiri umejileta wenyewe’ alijisemea mwenyewe huku akitabasamu kila wakati hata kama haikumpasa kufanya hivyo. Makubaliano yalipitishwa na utaratibu mwingine ulipangwa wa Kishime kurudi nyumbani na kujiunga na chama pinzani ili kuongoza mapinduzi dhidi ya chama tawala, alitakiwa kumshawishi Mh Chakwima ili kazi hiyo wote waifanye pamoja. Ndani ya chama hicho wapate uongozi, watawale nchi kila nyanja na hawa wengine wavune rasilimali nyuma yao huku wakiwajengea wananchi mashule na mahospitali kuwaziba midomo.





Mataifa mengi ya Afrika yaliingia katika mkumbo huu wa utawala wa kiimla, japokuwa katika mitindo tofauti, Afrika ya maghalibi tayari ilizama katika mkumbo huu wa tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali kung’ang’ania madaraka na mwishowe kusababisha vita za wenyewe kwa wenyewe ambazo ziliacha wajane, yatima na walemavu wasio na idadi. Akina mama na watoto ndilo kundi kubwa lililoteseka, vionghozi wasio na huruma wasiojua shida za wenzao walikaa juu ya viti vikubwa vilivyotengenezwa kwa masponji na kumfanya akaae asahau shida zote, huku mijico yao wakiitazamisha katia luninga kubwa kutazama nini kinaendelea juu ya nchi zao wakikenua meno yao wanapoona polisi wakiwapiga raia na kuwalundika rumande, hii ndiyo Afrika. Sasa kazi ilikuwa katika nchi moja iliyopo mashariki mwa Africa nchi iliyodumu kwa miaka mingi chini ya muungano wa nchi mbili, nchi nyingi zilishindwa kudumisha miungano yao na kusambaratika kama iliyokuwa jumuia ya kisovieti na hii yote ilitokana na roho ya umimi miongoni mwa viongozi, pengo kubwa kati ya watu wa upande huu na upande mwingine, tufanyeje!!



“Nimewasikia na nimewaelewa, lakini mnipe muda wa kufikiri na kuamua” Punde Kishime alitoa jibu hilo kwa jopo lile, wakatazamana kidogo na baadaye kukubaliana na alilosema Mh Kishime. Roho ya Mh Punde Kishime iligawanyika mara mbili, upande mmoja ukibaki na uzalendo akikumbuka alipokuwa JKT pale Makotopola wakiimba nyimbo za uzalendo, kuisifu Tanzania na kumsifu Nyerere leo hii anapewa wazo la kuisaliti na kuiuza nchi yake, je wananchi waliobaki watamtazamaje, alijiuliza na kushindwa kujijibu muda uo huo upande mwingine wa roho yake ulimshawishi kukubali jambo hilo ukimpa matumaini ya kuwa milionea mmojawapo duniani, ulimfariji kwa kumuonesha mashule makubwa ya huko Ulaya ambayo watoto wake wangesoma na hata kuishi huko punde likitokea tatizo ‘maisha si ndiyo haya’ nafsi yake ilimalizia kumshawishi



5

Miaka 30 nyuma

Jkt makutopola

Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, njia zote zilijawa na matope yaliyonata kwenye viatu vya kiaskari vya makuruta hawa watiifu waliojiunga kadiri ya mpango wa serekali ya awamu ya kwanza, kila amalizaye sekondari kabla ya kujiunga na elimu ya juu lazima apitie Jeshi la Kujenga Taifa ili afundishwe nidhamu na uzalendo juu ya taifa lake.

Kikosi cha kuruta kilipita kwa mchakamchaka kikitoka shambani

“Alisema alisema, alisema Nyerere alisema, vijana wangu wote mmelegea, masharti tuanze mchakamchaka” wimbo ulisikika ukiimbwa kwa nguvu na ari zote Kuruta mtiifu

Punde Kishime akiwa mbele kabisa kuanzisha nyimbo hizo, wakati huo haukuweza kabisa kuongea neno baya juu ya taifa lake abaki kimya badala ya kukuchapa makofi na kukuita ‘huna nidhamu’.

Punde Kishime alikutana na Chiwawa Chakwima katikamafunzo haya ya JKT huko Makutopola wote wakiwa vijana wakakamavu kutoka shule tofauti. Wakiwa huko walijifunza mambo mengi sana,ukakamavu, nidhamu, kilimo na kazi mbalimbali za mikono.

“Lazima tupiganie taifa letu!” Afande Mkoloni alitoa tamko kwa kuruta wenzake

“Ndiyoooooo” wengine walijibu kwa jazba

“Tumlenge adui!” Mkoloni aliongeza

“Ndiyoooooo” aliitikiwa tena

“Tusikubali kabisa adui avamie nchi yetu!” aliendelea kusisitiza

“Ndiyoooooo” alijibiwa

“Tumpige na tumtimue kama Nduli Amin” Kishime aliwapandisha jazba vijana wenzake ambao sasa walijawa na jazba utafikiri kweli wanaenda kumpiga Amin.

Chiwawa Chakwima alisimama kwa utulivu kabisa akiwa kasimamisha bunduki yake akitumia kitako na singe yake kutazama juu, akiwa mguu pande na kofia yake imejaa majani ili kumsaidia kujificha akilala vichakani. Aliwatazama kuruta wenzake jinsi walivyoshangilia kwa jazba lakini yeye alibaki kimya akimkumbuka marehemu baba yake aliyekufa katika vita vya Amin huko Uganda, hasira zilimjaa moyoni na alijihisi anahitaji kuipigania nchi yake kwa nguvu zote, jinsi alivyojawa na hasira endapo Amin angetokea mbele yake angeweza kumuua kifo kibaya ili kufidia damu ya baba yake aliyempenda.

“Sasa tumtafute adui” Afande mkoloni alitoa amri na mazoezi yakaendelea, kutambaa kwenye vichaka, kukwea kwenye miti na mengine mengi.

Jua liliwaka kwelikweli na kuruta hawa bado walikuwa machakani kumtafuta adui wasiyemjua wala kumuona

“Oya, Swahiba maji mshikaji, ku imenikamata sana” Punde Kishime alimuomba maji rafiki yake huyu aliyekuwa kajificha nyuma ya kamti kale kadogo, Chiwawa Chakwima akampa kibuyu chake cha maji Punde Kishime ili apate kunywa, alijisikia furaha sana kumsaidia mwananchi mwenzake, huo ndiyo uzalendo.

“Jua kali sana!” Punde Kishime alimueleza Chiwawa Chakwima

“Ndiyo, lakini tuwe wavumilivu sana, huu ndiyo uzalendo” Chakwima alimjibu

“Ni kweli Swahiba, tulilinde taifa letu, tusikubali wajanja walichezee” Punde Kishime aliongeza. Walitoka kwenye ile miti na kusogea miti ya mbele kwa mbinu za kijeshi baada ya kupewa ishara hiyo kutoka kwa mtu wa mbele.

Punde Kishime na Chiwawa Chakwima walitokea kuwa marafiki sana, kila mara walikuwa pamoja iwe michezoni au chakulani lazima wawe pamoja mapaka kuruta wenzao wakawaita ‘pacha’, mmoja akifanya kosa lazima na mwingine awe amehusika kwa namna moja au nyingine.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya mwaka mmoja kutimia, vijana hawa walimaliza mafunzo yao na sherehe kubwa ilifanyika ikihudhuriwa na mgeni rasmi Waziri wa Ulinzi. Punde Kishime alijisikia faraja sana kusimama mbele ya maelfu yale ya watu akiongoza moja ya vikosi tisa vya gwaride hilo, alijivuna kujiona kuwa sasa wnaweza kuipigania nchi yake katika lolote, kuilinda hata kufa. Muda wa kula kiapo cha utii ulifika muda ambao vijana hao walikuwa wakiusubiri kwa hamu sana, baada ya kula kiapo cha utii na kushangiliwa na maelf ya watanzania, kila mmoja lijiona kuwa sasa ana jukumu la kuwa mzalendo. Punde Kishime alibubujikwa na machozi ya uchungu akitafakari na kusema kuwa ‘sitakuwa tayari kuisaliti nchi yangu’, Chiwawa Chakwima akiwa kasimama kwa ukakamavu alihisi jukumu kubwa alilopewa na watanzania kuilinda, kulijenga taifa.

Katika baadhi ya kuruta wahitimu walipoewa zawadi mbalimbali Punde Kishime alipewa zawadi ya utii na ufanyakazi bora wakati Chakwima alipewa zawadi ya ukakamvu na uongozi bora. Wote walikuwa na furaha sana, siku hiyo walicheza, kula na kunywa vitu mbalimbali.



***



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog