Simulizi : Tai Kwenye Mzoga
Sehemu Ya Tatu (3)
Sikutaka kupoteza muda tena kwani nilifahamu kuwa hii ndiyo ingekuwa
nafasi yangu ya kipekee ya kuliwahi na muda uleule nikaanza kulifyatulia
risasi mfululizo kuelekea usawa wa kichwa chake. Hakika risasi zile zililipata
kisawasawa joka lile na kufanikiwa kuifumua vibaya sehemu ya kushoto ya
kichwa chake na hapo likatoa mlio wa ajabu ulioyaumiza masikio yangu mlio
huo ukisambaa pengine katika sehemu kubwa ya pango lile huku lenyewe
likijipiga kichwa na kuutupa mkia wake huku na kule na hapo vumbi kali
likatimka mle ndani. Hata hivyo mimi sikusitisha mashambulizi yangu, nilien?delea kulimiminia risasi kukilenga kichwa chake na hapo likawa likijitahidi
kuzikwepa bila mafanikio.
Niliendelea kulifyatulia risasi mpaka hadi pale risasi ziliponiishia na hapo
nikaitupa ile bunduki ili niichukuwe bunduki nyingine lakini ilikuwa ni muda huohuo pale nilipoliona lile joka likiangukia usawa wangu, nikawahi kulikwe?pa. Lilipoanguka chini nikaiwasha ile kurunzi yangu na kulimulika lile joka
na hapo nikagundua kuwa nilikuwa nimekisambaratisha vibaya kichwa chake
kwa zile risasi.
Pale chini lilipoangukia lile joka liliendelea kujinyonganyonga kiwiliwili
chake na kwa kweli nilikuwa nimefikia kikomo cha hofu yangu. Nilihisi kuwa
jasho lilikuwa likinitoka kila mahali mwilini mwangu na mapigo ya moyo ya?likuwa yakinienda mbio isivyo kawaida, nikabaki nimesimama kama sanamu.
Hofu ikiwa imenishika sikuona sababu ya kuendelea kusubiri mle ndani
hivyo nikaanza kunyata kuelekea kwenye ule uchochoro niliyokujia na akili
yangu sasa ilikuwa ni kuondoka haraka eneo lile kabla hatari nyingine hai?janifikia. Nilifanikiwa kuufikia uchochoro ule na kabla ya kuuingia ikanibidi
nigeuke nyuma kumulika baada ya sauti nyingine ya mburuto kuanza kusikika
mle pangoni.
Nilichokiona kilinifanya nitake kuzimia, kumbe ile sauti ya mburuto iliy?okuwa ikivuma mle pangoni ilikuwa ni ya joka lingine kama lile nililopambana
nalo mle ndani na lilikuwa likija mle pangoni bila shaka kumtafuta mwezake.
Joka lile lilikuwa limechungulia kupitia tundu moja lililokuwa kwenye kona
ya ukuta wa pango lile na muda mfupi uliofuata nililiona lile joka taratibu
likianza kujipenyeza kwenye lile tundu kuingia mle pangoni.
Nilihisi kutaka kuchanganyikiwa kwani nilikuwa nimechoka sana na hivyo
nisingekuwa na uwezo wa kupambana tena na joka lingine kubwa kama lile
kwani nilihisi kuwa ule ushindi niliokuwa nikiupata ni kama ulikuwa wa baha?ti tu na nijuavyo mimi bahati haikuwa na mazoea kwa mtu mmoja.
Sikutaka kupoteza muda nikaingia kwenye ule uchochoro cha pango na
kuanza kutimua mbio bila ya kugeuka nyuma na moyo wangu ulikuwa ukien?da mbio sana. Nilipofika mwisho wa ule uchochoro nikaingia upande wa kulia
kushika njia nyingine ya pango, niliendelea kutimua mbio bila ya kuelewa
kuwa nilikuwa nikielekea wapi. Niliingia kona hii na kutokezea ile nikaiacha
njia moja na kuingia nyingine ilimradi sikutaka tena kusimama huku nikihofia
kuwa lile joka lingekuwa nyuma yangu likinifukuza.
Kwa kweli nilijihisi kichanganyikiwa na damu yote mwilini mwangu ni
kama ilikuwa imehamia usoni mwangu huku kichwa kikinigonga sana hivyo
nilihisi nguvu zilikuwa zikiniishia na bega langu la kushoto lilikuwa likiniuma
sana. Niliendelea kukimbia mpaka nilipofika eneo fulani mle pangoni, eneo
pana ambalo nilihisi kuwa huenda lingekuwa na usalama kidogo kwa mimi
kupumzika huku nikiendelea kutweta. Nikageuka nyuma kutazama hata hivyo
sikuliona tena lile joka wala kusikia sauti ya ule mburuto. Nikajisongeza na
kujiegemeza kwenye ukuta wa pango huku mapigo ya moyo wangu yakien?delea kuvurugika.
Nikiwa nimeendelea kusimama lile eneo nikaanza kuhisi miguu yangu ili?kuwa mbioni kuishiwa nguvu hivyo nikasota ukutani taratibu na kuketi chi?ni. Kwa kweli nilihisi ni kama niliyepotea njia kwenye jangwa lisilokuwa na
mwisho. Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na wale watu wengine sikuweza
kuhisi kuwa walikuwa wapi wakati huu hata hivyo uzima wangu lilikuwa suala la muhimu zaidi
#33
MUDA MFUPI SANA ULIKUWA UMEPITA nikiwa pale chini nime?pumzika wakati niliposhtushwa na sauti ya milio ya risasi iliyokuwa ikivu?ma ndani pango lile. Nilishtuka na kusimama huku nikisikiliza kwa makini
milio ile ya risasi bila ya kufahamu ilikuwa ikitokea upande gani, moyo wangu
ulianza kwenda mbio na miguu yangu ilikuwa ikinishawishi nianze kitimua
mbio ingawaje akili yangu haikukubaliana haraka na suala hilo.
Nikiwa bado nimesimama ile sehemu nilingudua kuwa ile milio ya risa?si iliyokuwa ikirindima mle pangoni sasa ilikuwa ikiongezeka sambamba na
sauti ya vishindo vya hatua za watu, nikaikamata bunduki yangu mkononi
na kujiweka tayari. Muda mfupi uliofuata niliiona taswira ya mwanamke an?ayekimbia ikijitokeza upande wa kushoto wa pango lile, nilipomtazama vizuri
mwanamke yule nikaona kuwa alikuwa ameongozana na wanaume wengine
wanne nyuma yake na wote walikuwa uchi kama walivyozaliwa na waliku?wa wakitimua mbio. Japokuwa nilikuwa sijawaona vizuri kutokana na giza la
mle ndani lakini haraka hisia zangu zilinieleza kuwa mwanamke yule huenda
alikuwa Ikirezi na wale wanaume wengine walikuwa ni miongoni mwa wale
watu waliokuwa kwenye ule msafara wakati tulipokuwa tukitoroka kule pan?goni.
Nikawaacha wanipite mbele yangu bila ya wao kuniona huku nikiendelea
kubanisha ile sehemu, moyoni nilifurahi sana kuwa nilikuwa nimekutana tena
na wenzangu japokuwa bado walikuwa hawajaniona hata hivyo idadi yao ilin?ishtua sana kwani idadi yao ilikuwa imepungua.
Wale watu walinipita na kuendelea na mbio zao nikawaacha wafike mbele
kidogo kisha na mimi nikaunga msafara ule kwa nyuma yao nikikimbia ku?wafuata. Ile milio ya risasi sasa niliisikia kuwa ilikuwa ikiongezeka nyuma
yangu na hapo nikajua kuwa wale watu mbele yangu walikuwa wakifukuzwa
na mtu au watu waliokuwa nyuma yao na bila ya shaka nilijua tu kuwa watu
hao nyuma yangu wangekuwa ni wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda.
Tulipofika mbele tukaingia kwenye njia nyingine ya pango iliyokuwa upa?nde wa kulia kwetu, ilikuwa ni njia nyembamba kiasi na yenye hewa nzito na
hapo niliwasikia wale wenzangu wakihema ovyo mara tu tulipoingia kwenye
uchochoro ule lakini hawakuonesha dalili zozote za kusimama na hakuna ali?yeshtukia uwepo wangu nyuma yao.
Ile milio ya rasasi nyuma yetu ilikuwa imetukaribia sana na nilihisi kuwa
pengine ilikuwa umbali mfupi sana nyuma yetu na nilianza kuiona hatari kuwa
endapo ingezidi kutukaribia basi baadhi ya rasasi zingeweza kutulenga. Tu?livuka uchochoro ile wa pango na kuingia uchochoro mwingine upande wa ku?shoto uliyokuwa mpana kiasi lakini wenye mawe makubwa yaliyochongoka.
Kufikia pale niliwaona wale wenzangu wakipunguza mwendo ingawaje
niligundua kuwa walikuwa wakifanya vile bila yao wao wenyewe kupenda,
nikajua kuwa huenda walikuwa wameanza kuchoka. Zile risasi sasa zilikuwa
zimetufikia karibu na zilikuwa zikitukosakosa huku nyingine zikipita juu ya vichwa vyetu. Tuliharakisha kuivuka njia ile ya pango kisha tukaingia kwenye
njia nyingine iliyokuwa upande wa kulia kwetu. Zile risasi zilikuwa zikitukosa
na hali hiyo ilikuwa imewapelekea wale wenzangu kule mbele waanze kupiga
mayowe ya hofu.
Njia ile ya pango tuliyoingia ilikuwa ikielekea sehemu ya chini ya pango lile
na nilianza kushikwa na hofu nilipoyakumbuka yale majoka makubwa niliy?okuwa nimepambana nayo ambayo mpaka sasa nilikuwa nimegundua kuwa
yalikuwa yakipendelea kuishi sehemu za chini zaidi za mapango yale mahali
penye matope yenye majimaji na popo ambao bila shaka ndiyo walikuwa ki?toweo chao kikubwa.
Kwa kweli ilikuwa ni hali ya mikikimikiki na kila mmoja alipambana kuio?koa nafsi yake. Bado tuliendelea kutimua mbio huku tukiendelea kukoswa?koswa na zile risasi zilizokuwa zikifyatuliwa nyuma bila shabaha ya maalum.
Wakati tukiendelea kukimbia nilihisi kuwa ile milio ya risasi ilikuwa imetu?karibia sana nyuma yetu na kama tungeendelea tu kukimbia vile wale watu
wangeweza kutupata kwa urahisi. Hivyo nilisimama na kugeuka na hapo
nikaanza kujibu mashambulizi na bila ya shaka nilimshtukiza sana yule mlen?gaji nyuma yetu kwani hakudhani kabisa kuwa mmoja wetu angekuwa na si?laha.
Majibishano ya risasi baina yangu na yule mlengaji aliyekuwa nyuma yetu
yalifanyika kwa umakini wa hali ya juu huku kila mmoja akionekana kumvizia
mwenzake, risasi zilizokuwa zikitupwa upande wangu zilinihangaisha sana
katika kuzikwepa nikilala chini nikijiviringisha huku na kule na kujibanza
kwenye baadhi ya kona lakini hatimaye nilifanikiwa kumpata mlengaji Yule
inagawaje sikuweza kufahamu kuwa nilimlenga eneo gani mwilini mwake la?kini kukoma kwa ile mirindimo ya risasi na sauti kubwa ya mayowe aliyopiga
yule mtu baada ya kufanikiwa kuzipenyeza risasi zangu kwenye mwili wake
hiyo ilinihakikishia kuwa tayari nilikuwa nimemlenga yule mlengaji nyuma
yetu.
Niligeuka mbele na kuanza kukimbia tena nikiwafuata wale wenzangu lak?ini wakati huo nikiwa nawaza kichwani kuwa wale watu mbele yangu huenda
wangekuwa wakijiuliza kuwa yale majibishano ya risasi yalikuwa baina ya
nani na nani. Wakati nikiendelea kukimbia nilikuwa nikimuomba Mungu kuwa
mbele yangu nisikutane na njia nyingine za pango kwani zingeweza kunichan?ganya na hatimaye kushindwa kuelewa wenzangu wameelekea uelekeo upi.
Ile njia ya pango nilishukuru kuwa haikuwa na kona nyingine hivyo nilien?delea kuifuata ikishuka sehemu ya chini ya lile pango. Wakati nikishuka chini
ya pango lile niligundua kuwa hewa ya mle ndani ilikuwa ikibadilika taratibu
kwa kutoka katika hali ya hewa nzito kwenda kwenye hali ya hewa safi na
nyepesi. Ile njia ilikuwa na utelezi mkali hivyo nilijikuta nikiteleza kuelekea
kule chini bila ya kupata nafasi ya kujitetea na hatimaye nilijikuta nimean?gukia kwenye tope zito la udongo mfanyanzi lililofanikiwa kunimeza kuanzia
miguuni hadi sehemu ya kiuno.
Nilikuwa nimetokezea kwenye pango kubwa na pana lakini lenye mwanga
wa kutosha, mwanga ule ulikuwa ukipenya kutoka juu kupitia kwenye tundu kubwa lililokuwa juu ya pango lile. Kwa kweli nilijisikia furaha sana kwani
nilikuwa na hakika kuwa sasa nilikuwa nimekaribia kutoka nje ya mapango
yale.
Japokuwa nilikuwa nimezama kwenye lile tope lakini sikuwa nimeanza ji?tihada za kujinasua badala yake nikiwa pale niliendelea kulitazama lile tundu
la juu ya pango kwa furaha sana huku nikiwa siyaamini macho yangu kuwa
nilikuwa nimefika sehemu nzuri yenye matumaini makubwa katika safari yan?gu ya kukitoroka kifo katika mpango yale. Nikiwa bado nimezama kwenye lile
tope huku nikiwa furaha ya kupita kiasi ghafla nilishtushwa kwa sauti ya kike
ikiita jina langu na hapo nikageuka kutazama upande ule ile sauti ilikotokea
na hapo furaha yangu ikaongezeka zaidi pale nilipomuona Ikirezi kwenye
kona ya pango lile akiwa na wenzake mbioni kulivuka lile tope, nyuma yake
akifuatiwa na Jean Pierre Umugwaneza na wanaume wengine wawili ambao
nilizikumbuka haraka sura zao kuwa walikuwa miongoni mwa wale mateka.
Wote waligeuka kunitazama wakionesha sura za furaha nami nikafurahi
sana huku nikianza kujinasua toka kwenye lile tope kuwafuata kwani wao
walikuwa wanakaribia ukingoni kulivuka lile tope.
__________
NILIKUWA NDIYO KWANZA NIMEFIKA NUSU TU YA SAFARI YAN?GU ya kulivuka lile tope la mle ndani ya pango nikiwafuata wale wenzangu
wakati ghafla niliposhtushwa na sauti za milio ya risasi iliyoanza kurindima
kupita lile tundu la juu ya pango na hapo nikayatupa haraka macho yangu ku?tazama kule juu ya lile tundu. Niliwaona wanajeshi watatu wakiwa wanachun?gulia kwenye lile tundu huku wote wakiwa wameielekeza mitutu ya bunduki
zao kule walipo akina Ikirezi na hapo haraka nikajua kuwa wale walikuwa ni
askari wa Kanali Bosco Rutaganda na kwa bahati nzuri walikuwa hawajanio?na.
Sikutaka kusubiri nikapiga yowe kali kuwashtua wale wenzangu mbele yan?gu nikiwataka walale chini haraka kwani walikuwa mbioni kushambuliwa.
Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu wa nyuma yake bila shaka wali?nisikia na kunielewa haraka kwani kufumba na kufumbua wakawa wamejitu?pa chini kwa wepesi wa hali ya juu. Bahati mbaya sana yule mtu wa mwisho
alikuwa amekwishachelewa kwani muda uleule nilimuona akitupwa hewani
huku akipiga yowe la maumivu, na akiwa bado yupo kule juu niliuona ubon?go wake ukisambaratika hewani kama tope jepesi lililorushwa huku kichwa
chake kikirushwa upande mwingine. Kwa kweli sikuwahi kuliona tukio baya
la kifo kama kile na bila shaka silaha kali sana ya kivita ilikuwa ikitumika na
wale wanajeshi. Risasi bado ziliendelea kurindima mle ndani.
Bila ya kupoteza muda nilianza kujibu mashambulizi toka kule chini ni?kiwashambulia wale wanajeshi waliokuwa wakichungulia kwenye lile tundu
kule juu. Shabaha ilikuwa ni miongoni mwa kigezo kilichotumika kuniingiza
kwenye mafunzo ya wanajeshi makomandoo muda mfupi baada ya kujiunga
na jeshi la wananchi wa Tanzania hivyo sikuwa na mashaka kabisa na kipaji
changu. Niliishika bunduki yangu kwa mkono wa kulia nikawa nakimbia huku niki?washambulia wale wanajeshi kule juu nikiitumia njia ile kujikinga, kusham?bulia na vilevile kulivuka lile tope lakini wakati huohuo macho yangu yak?iendelea kutazama kule juu ili nisipoteze shabaha. Mkakati wangu ukaanza
kuzaa matunda kwani risasi chache tu nilizozifyatua ziliwapata vizuri wale
wanajeshi waliokuwa wakiendelea kutushambulia kwenye lile tundu la pango
kule juu na hapo nikawaona wanajeshi wawili wakianguka kutoa kule juu hadi
chini kwenye lile tope mle ndani.
Sikuwaacha watue kwa sterehe juu lile tope hivyo nikawa nikiendelea
kuwafyatulia risasi katika namna ya kuwasindikiza hadi mwisho wa safari
yao kwenye lile tope na walipofika chini walikuwa wafu. Pamoja na hayo
mashambulizi ya risasi kutoka kule juu bado yaliendelea na safari hii rasasi
zilikuwa zikichimba umbali mfupi sana pembeni yangu. Hofu ilinishika hata
hivyo sikusimama ingawaje kukimbia juu ya tope lile jingi kulinifanya nihisi
kuwa nilikuwa nikitembea badala ya kukimbia kama nilivyokuwa nikitaka.
Zile risasi zilizokuwa zikitushambulia nilihisi ni kama zilizokuwa zikinikosa?kosa kwa bahati sana au pengine mlengaji hakuwa makini kwa shabaha.
Niliendelea kukimbia kulivuka lile tope zito huku zile risasi zikinikosakosa
na mashambulizi yale yalipozidi nilifahamu kuwa nisingeweza kufika mba?li kabla ya yule mlengaji kufanikiwa kunipata hivyo nikawa nakimbia huku
moyoni nikimuomba Mungu kuwa niponyoke kwenye kadhia ile lakini wakati
huohuo akili yangu ikiendelea kupiga mahesabu ya nini kifanyike kwa wakati
ule.
Mara nikawa nimepata wazo jipya na hapo nikasimama na kuinyanyua ile
kurunzi yangu mkononi kisha nikawasha batani ya mwanga mkali na kummu?lika yule mtu aliyekuwa akitushambulia kule juu. Mahesabu yangu yakazaa
matunda haraka kwani ule mwanga mkali wa ile kurunzi yangu ukamchang?anya yule mtu kule juu hivyo akawa amesitisha kufyatua risasi na badala yake
akawa akijikinga usoni kwa kiganja chake ili kuuzuia ule mwanga wa kurunzi
ili aweze kuniona vizuri ingawaje mimi huku chini nilikuwa nikimwona vizuri
sana na sura yake mbaya kama panya ilikuwa imejianika vizuri kwenye ule
mwanga wa kurunzi yangu.
Ilikuwa nafasi nzuri na sikutaka kuipoteza hivyo niliikamata vizuri bunduki
yangu mkononi kisha nikaiweka kwenye shabaha nzuri na nilipovuta kilimi
cha bunduki ile risasi tatu za mwisho toka kwenye mtutu wa bunduki yangu
zilifanya kile nilichokitaka. Kwanza nilimuona yule mtu akitupwa hewani juu
ya lile tundu huku akinipiga yowe kali la maumivu na yowe hilo lilipokoma
nilimuona yule mtu akianguka mle ndani mzimamzima huku kichwa chake
kikiwa kimeharibiwa vibaya na risasi zangu.
Yule mtu nilikuwa nimempata na bila ya shaka umauti ulikuwa umemfika
na wakati huohuo bunduki yangu ikiwa imeishiwa risasi hivyo niliitupa na
kuendelea kulivuka ile tope kwa haraka huku nikiwa na hakika kuwa nilikuwa
nimewaua wale wanajeshi wote waliokuwa juu ya lile tundu. Ikirenzi, Jean
Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine walipoona yale mashambulizi ya
risasi yamekoma wakasimama na kuanza kukimbia wakimaliza kulivuka lile tope huku mimi nikiwa nyuma yao.
Nilikuwa ndiyo namalizia kulivuka lile tope wakati Ikirezi aliponishtua kwa
sauti ya yowe kali la tahadhari na bila ya kuchelewa nikafahamu lile yowe
lilikuwa likimaanisha nini kwani kwa haraka nilihisi kuwa alikuwa akiiona
hatari fulani nyuma yangu hivyo nikajitupa kando lakini nilikuwa nimech?elewa kidogo kwani muda uleule nilihisi kitu fulani kikipenya ghafla kwenye
bega langu la kushoto huku kikiniachia maumivu makali mno yasiyoelezeka
halafu nikasombwa na katupwa hewani na hapo niliwasikia Ikirezi, Jean Pierre
Umugwaneza na yule mtu mwingine waliyeongozana naye wote wakipiga
mayowe ya hofu.
“Laleni chini tunashambuliwa” niliwaambia huku nikipiga makelele hata
hivyo walinielewa wakawahi kalala chini. Loh! nilisikia maumivu makali
sana begani, risasi moja ilikuwa imenipata na lile jeraha lake lilikuwa likivuja
damu. Zile risasi ziliendelea kurindima mle pangoni na pale nilipotupwa si?kushawishika kujitingisha kwani kufanya hivyo kungemfanya yule mlengaji
aweze kuniona kwa urahisi ingawaje mwili wangu wote ulikuwa umetapakaa
matope hivyo nilifahamu kuwa yule mlengaji kule juu asingeweza kuniona
kwa wepesi.
Wakati huu sikuwa na silaha yoyote nyingine zaidi ya bastola moja niliy?okuwa nimeisunda kiunoni mwangu hata hivyo sikuona kama ingekuwa ni
jambo la busara kuitumia bastola hiyo katika kuyajibu yale mashambulizi kule
juu kwani ilikuwa ni silaha ndogo sana ukiilinganisha na ile ya yule adui hivyo
ni kama ningekuwa napoteza risasi zangu bure. Zile risasi bado ziliendelea
kirindima mle ndani na pango lote lilitawaliwa na harufu ya moshi wa risasi.
Toka pale nilipokuwa nimetupwa nilianza kujivuta juu ya tope lile taratibu
kwa kutambaa huku nimelilalia tumbo langu katika mtindo wa kijeshi uitwao
crawling. Mirindimo ya zile risasi iliendelea hata hivyo mlengaji bila shaka
hakuwa fundi wa shabaha maana risasi zake zote zilikuwa zikiishilia kwenye
lile tope tu. Niliendelea kujivuta juu ya lile tope hadi nilipofika ukingoni na
hapo niligeuka kutazama kule juu, nikawaona wanajeshi wengine wanne
wakiwa wameongezeka kwenye lile tundu na wote walikuwa wakichungulia
ndani ya pango.
Wale wanajeshi wengine ni kama walifika pale juu kuongeza nguvu baada
ya kuona nimewadungua wenzao kwani haukupita muda mrefu mvua ya risasi
ilianza kushuka mle ndani ikielekezwa upande wangu na hapo nikajua kuwa
walikuwa wameniona. Niliona hatari ilikuwa ikinikaribia kwa haraka sana,
Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine walikuwa wame?shamaliza kulipata lile tope na kulivuka kabisa baada ya kuona yale masham?bulizi mengine ya risasi yakielekezwa kwao. Walipomaliza kulivuka lile tope
wakawa wamesimama wakinisubiri kwenye kona ya lile pango.
Nilijitahidi kukimbia ingawa lile tope liliendelea kunipunguza kasi wakati
huo zile risasi zikinisindikiza kwa nyuma na kunikosakosa lakini hatimaye
nilifanikiwa kulivuka lile tope na hapo safari ikaanza. Safari hii niliwataka
Ikirezi na wenzake wakae nyuma yangu na mimi ndiyo nikawa tena kiongozi
wa ule msafara huku ile kurunzi nikiwa nimeishika mkononi pamoja na ile bastola. Kulikuwa na njia nyembamba ya pango hivyo niliwaongoza wenzangu kuingia kwenye njia hiyo iliyokuwa na tope la kiasi lenye majimaji kwa chi?ni. Akili yangu yote sasa ilikuwa kuutafuta mfereji wa maji wowote ndani ya pango lile kwani nilifahamu kuwa mfereji huo ndiyo ungekuwa njia ya
kutorokea nje ya mapango haya. Tulipomaliza kuipita ile njia tukaingia kicho?choro kingine kilichokuwa mwisho wa njia ile ya pango kwa upande wa kulia,
tulipofika kwenye uchochoro ule matumaini yalianza kifufuka kwani chini
yake nilikuwa nikisikia kelele za maporomoka ya maji.
Nikasimama na kuwauliza wenzangu kama walikuwa wakijua namna ya
kuogelea, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine wakaniambia kuwa
wao walikuwa wakijua kuogelea lakini Ikirezi alikataa. Nikamwambia Ikirezi
asiwe na wasiwasi kwani itakapofika wakati wa kuogelea mimi ningemsaidia
wakati wale wengine wangekuwa wakiogelea wenyewe.
Tulikubaliana na hapo safari ikaendelea tukishuka chini kwenye ule ucho?choro wa pango, baada ya kukata kona mbili kwenda kule chini tukawa tu?mefika kwenye ule mfereji ambao hapo mwanzo nilikuwa nikiyasikia yale
maji yake yakiporomoka, ulikuwa mfereji mkubwa na wenye kina pia wenye
maji yanayosafiri kwa kasi. Nikamchukua Ikirezi na kumbeba begani huku
mikono yake akiwa ameipitisha shingoni mwangu kisha sote tukajitosa ndani
ya ule mfereji na muda huohuo Jean Pierre Umugwaneza na yule mwenzake
nao wakajitosa mferejini wakinifuata kwa nyuma.
Tofauti na ile mifereji ya maji ya hapo awali mara baada ya kujitosa kwenye
maji ya mfereji ule nilihisi kuwa maji yake yalikuwa mengi zaidi, ya baridi na
yanayosafiri kwa kasi kubwa sana. Ikirezi akiwa amenishika vizuri mgongoni
niliendelea kuyakata maji taratibu na kwa umakini huku yeye akiwa ameishi?ka ile bastola yangu na ile kurunzi akimulika mbele kwani mle ndani ya ule
mfereji bado kulikuwa na giza.
Ule mfereji wa maji ulikuwa na kona nyingi sana, tuliogelea na kuzipita
kona saba za mfereji ule na kuna baadhi ya sehemu za mfereji ule zilikuwa
nyembamba sana hivyo yale maji yalikuwa mengi na yanayosafiri kwa kasi na
kuna baadhi ya sehemu za ule mfereji zilikuwa pana na hivyo kina chake cha
maji nacho kilipungua. Lakini kwa kadiri tulivyokuwa tukiendelea na safari
yale maji ya mfereji yalikuwa yakiongezeka taratibu na yalikuwa yakianza
kubadilika rangi na kuanza kuwa mekundu, wasiwasi ulianza kunishika kuwa
huenda mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na yale maji yalikuwa yakiongezeka
kutokana na mvua hiyo.
Wakati fulani niligeuka nyuma kuwatazama wenzangu na hapo nikawaona
kuwa walikuwa makini sana kunifuatilia, kwa kweli sikuwa nikifahamu hasa
ule mfereji ungetufikisha wapi lakini bado nilikuwa na matumaini nao hata
hivyo sikupenda safari yetu iwe ndefu sana kwani nilifahamu kuwa ningecho?ka kutokana na uzito wa Ikirezi mgongoni mwangu. Mle ndani ya pango la ule
mfereji kulikuwa na popo wengi wakubwa waliokuwa wakining’inia juu ya
dari la ule mfereji, popo hao walitushambulia kila tulipokutana nao hata hivyo
waliwahi kukata tamaa na kutuacha pale walipotuona tukizidi kusonga mbele. Ulipita muda mrefu tukiendelea kuogelea bila ya kuona tumaini lolote la
kutoka nje ya mapango yale na mimi nilianza kuhisi kuchoka kutokana na uzi?to wa Ikerezi mgongoni mwangu hata hivyo sikutaka kukata tamaa japokuwa
lile bega langu lililojeruhiwa kwa risasi lilikuwa likiniuma sana huku likien?delea kuvuja damu taratibu. Muda wote huo Ikirezi ilikuwa kimya mgongoni
mwangu na nilikuwa nikiyasikia mapigo ya moyo wake namna yalivyokuwa
yakienda mbio kwa hofu.
Baada ya safari ndefu ya kuogelea hatimaye tukatokezea kwenye sehemu
pana ya pango lile yenye kutisha, sehemu hiyo ilikuwa na maji mengi yaliyo?sambaa na yenye kina kirefu, niliweza kuyahisi kutokana na nguvu ya uvutano
iliyokuwa eneo lile. Maji ya eneo lile yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa
meusi na yanayozizima kwa wingi wake na yalikuwa yakienda kasi mno kuzu?nguka eneo lile kabla ya kuendelea na safari yake kwa mbele yetu.
Nilimkumbuka mwalimu wangu wa somo la jiografia wakati alipokuwa
akitufundisha mada ya maumbo mbalimbali yatokanayo na mito ya maji
wakati nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari na hapo nikaitambua sehemu
ile kama ielekeayo kutengeneza moja ya umbo la mto liitwalo Ox-bow lake
ingawaje katikati kulikuwa na shimo kubwa na maji yale yalikuwa yakizungu?ka shimo lile kwa kasi kabla ya kuendelea na safari. Tulipofika eneo lile mimi
hofu ilinizidi kwani nilianza kuona hatari ya kuweza kutumbukia kwenye shi?mo lile endapo tusingekuwa makini na sikufahamu shimo lile lililokuwa na
nguvu za ajabu za uvutano lilikuwa likielekea wapi.
Nilijitahidi kujizuia na bila ya mafanikio tukajikuta tumeingia kwenye ule
mzunguko wa maji na hapo nilimsikia Ikirezi akipiga mayowe ya hofu mgon?goni mwangu hata hivyo nilimsihi aendelee kunishika. Sasa yale maji yalianza
kutuzungusha kwa kasi ya ajabu kando ya lile shimo na nilipogeuka nyuma
nikawaona Jean Pierre Umugwaneza na yule jamaa mwingine nao wakiwa
wameingia kwenye ule mzunguko wa maji.
Tuliendelea kuzungushwa na yale maji kandokando ya lile shimo kwa mara
kadhaa na kila nilipojitahidi kijinasua sikufanikiwa na hapo kizunguzungu kil?ianza kunishika na kusababisha kichwa kuniuma kwa ghafla huku nikijisikia
kutaka kutapika.
Wakati nikielekea kukata tamaa mara ghafla nikaona wimbi kubwa la maji
likija kutokea kule tulipotokea, nikalitazama wimbi lile na kugundua kuwa
kwa vyovyote lingeweza kuleta namna ya ukinzani na ule mkondo wa mzu?ngoko wa yale maji. Hivyo nikalitegea lile wimbi wakati linakutana na ule
mkondo wa maji na mimi muda huohuo nikawa nimezama kuingia katikati ya
lile wimbi na ule mkondo wa maji na tulipoibuka juu tukatupwa mbali kando
ya lile shimo na muda huohuo nikamuona na yule jamaa tuliyeongozana naye
akitupwa na yale maji kuja upande wetu lakini sikufanikiwa kumuona Jean
Pierre Umugwaneza na hapo wasiwasi ukanishika.
Nilipogeuka kumtazama yule jamaa ambaye sasa alikuwa pembeni yangu
uso wake ulitosha kabisa kunieleza juu ya tukio lililokuwa limetokea kwani
alikuwa amegeuka na kutazama ule upande lilipokuwa lile shimo na mimi
nilipotazama kule sikuona dalili yoyote ya kuwepo kwa mtu eneo lile na hapo nikajua kuwa Jean Pierre Umugwaneza alikwisha tumbukia kwenye lile shi?mo. Loh! huzuni ilinishika sana nikajihisi kukata tamaa kwa kumpoteza mtu
muhimu sana aliyepoteza familia yake kwa kuyaokoa maisha yangu.
Wazimu ukanishika nikakosa uvumilifu na hapo nikaanza kuogelea kuli?fuata lile shimo lakini Ikirezi akatambua haraka nilichokuwa nataka kuki?fanya hivyo akaanza kupiga makelele ya kunionya kuwa nisiende hata hivyo
nilimpuuza lakini sikufika mbali yule jamaa tuliyeongozana naye akawahi
kunishika mguu na kunisihi nisiende. Baada ya hangaika hangaika ya hapa
na pale hatimaye niliamua kumsikiliza yule jamaa hivyo nikageuka na kuanza
kuogelea taratibu nikienda pembeni ya lile shimo huku nikiwa nimejawa na
huzuni sana.
Tulipofika kule kando ya lile shimo tulitulia kidogo tukiyatazama yale maji
yaliyokuwa yakizunguka lile shimo kwa kasi huku tukitarajia kumuona tena
Jean Pierre Umugwaneza lakini haikuwa hivyo kwani hapakuwa na dalili yoy?ote ya kuonekana kwa binadamu eneo lile wakati huo yale maji ya mle pan?goni yakiendelea kuongezeka taratibu mwishowe tukaamua kuendelea mbele
za safari yetu.
Tuliendelea kuogelea mpaka tulipofika mbele mahali ambapo ule mfereji
tuliokuwa tukiogelea ulikutana na mfereji mwingine na kuunganika na hivyo
kutengeneza mfereji mmoja mkubwa kama mto wenye maji mengi yanayosa?firi kwenda mbele yetu. Tukazidi kuogelea huku tukiwa na hofu kuwa huenda
ule mto ungekuwa na maji mengi sana ambayo si ajabu sana yangetushinda
nguvu hata hivyo niliutambua haraka kuwa mto ule ulikua ni wa kipindi cha
masika tu na bila shaka kipindi cha kiangazi haukuwa na maji hata tone. Tu?lipofika mbele kidogo mara tukaanza kuona mwanga wa asili wa mawingu
ukitufikia taratibu na hapo nikajua kuwa sasa tulikuwa tumefika sehemu ya
nje ya yale mapango kwa kweli nilihisi kama nguvu mpya ikinirudia mwili
mwangu huku moyo wangu ikigubikwa na furaha isiyo na kifani.
Eneo lile lote lilikuwa limetawaliwa na sauti ya maporomoko ya maji ya
ule mto wa masika, tulipofika nje kabisa ya yale mapango nikagundua kuwa
mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na hapo nikakumbuka lile fukuto la
joto kali lililokuwa mle pangoni. Yale maji ya mto yalikuwa mengi na wakati
huu yalikuwa yakisafiri kwa kiasi na yalikuwa yakiendelea kubadilika rangi na
kuzidi kuwa mekundu kutokana na mchanganyiko wa udongo wa eneo lile na
takataka zilizokuwa zikiendelea kukokotwa na yale maji.
Mara kwa mara tulilazimika kuyakwepa mabonge makubwa ya udongo,
mawe na magogo ya miti yaliyokuwa yakikokotwa na yale maji. Ikirezi akiwa
mgongoni mwangu niliendelea kuogelea taratibu mpaka pale nilipohisi kuan?za kuchoka nikapata gogo moja kubwa lililokuwa likikokotwa na maji na hapo
nikalidandia hivyo likawa likitukokota taratibu kuufuata ule mto.
Wakati tukiendelea kuelea juu ya lile gogo niligeuka kuyatazama yale mapan?go ya Musanze ambayo sasa yalikuwa nyuma yetu nikawa kama siyaamini
macho yangu kuwa hatimaye tulikuwa nimefanikiwa kumtoroka Kanali Bosco
Rutaganda na askari wake. Niligeuka kumtazama Ikirezi nikamuona aliku?wa akitabasamu ingawaje uso wake bado ulikuwa umejawa na mashaka nami nikabaki nikitabasamu tu huku tukiendelea kuelea kwenye lile gogo taratibu
tukiyaacha yale mapango nyuma yetu. Yule jamaa tuliyeongozana naye akawa
amejilaza juu ya gogo lile huku naye akiendelea kuyatazama yale mapango
nyuma yetu huku akionekana kuzama kwenye fikra zake.
Mto ule wa masika ulikuwa ukikatisha kwenye eneo lenye miti mingi mi?kubwa na misitu mizito isiyokuwa na dalili zozote za kuishi binadamu. Ni?liitazama miti ile na kuiona kama moja ya mashihidi wangu katika safari hii
ya kukiponyoka kifo. Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha eneo lile na
usiku nao ulikuwa ukianza kuingia kwani japokuwa sikuwa na saa yangu
mkononi lakini nilihisi tu kuwa muda ule ungekuwa ni kwenye nyakati za saa
kumi na mbili jioni.
__________
MVUA KUBWA ILIKUWA IKIENDELEA KUNYESHA eneo lile na
mifereji midogomidogo ya maji iliyokuwa ikitokea sehemu za juu za milimani
ilikuwa ikitiririsha maji yake katika mto ule wa msimu na hivyo kupelekea
ongezeko kubwa la maji yenye kasi ya ajabu na sasa tulikuwa tukisukwasukwa
na maji yale yaliyokuwa yakiendelea kulikokota lile gogo tulilolidandia. Tu?lipelekwa upande huu na ule wa ule mto bila ya pingamizi lolote. Sikuwa na
shaka kuwa tulikuwa tukisafiri kwenye kina kirefu sana cha maji kutokana na
namna gogo lile kubwa tulilolidandia lilivyokuwa likielea kama bua.
Nilipoyazungusha macho yangu kutazama eneo lile nikagundua mto ule uli?kuwa umepita kwenye korongo pana na refu. Tulipokuwa katikati ya misitu ile
huku tukiendelea kusafiri taratibu niligeuka kumtazama tena Ikirezi pembeni
yangu nikamuona kuwa alikuwa ameanza kuishiwa na nguvu ya kuendelea
kulikumbatia lile gogo hivyo nikamsogelea na kumshika vizuri mkono wake
na hapo akageuka kunitazama bila ya kusema kitu. Uso wake ukawa ni kama
mtu anayetaka kucheka na kulia kwa wakati mmoja huku nikiiona hofu iliyo?fichika usoni mwake.
Yule jamaa mwingine tuliyetoroka naye yeye alikuwa amelikumbatia vizuri
lile gogo huku akitutazama. Giza la jioni lilikuwa likipiga hodi taratibu na sau?ti pekee iliyokuwa ikipenya masikioni mwangu ilikuwa ni ile sauti ya mzizimo
wa yale maji ya mto.
Tukiwa tunaendelea kusafiri juu ya lile gogo ghafla nilianza kuhisi kichwa
changu kilikuwa kizito sana nikaanza pia kuhisi kizunguzungu na wakati huo?huo nikawa nahisi kama ninayetaka kutapika. Niligeuka kulitazama lile jeraha
la risasi begani mwangu na hapo nikaona kuwa nilikuwa nimepoteza damu
nyingi sana na bila shaka kile kizunguzungu kilitokana na upotevu wa damu
hiyo.
Taratibu hofu ilianza kuniingia nikawa naanza kuiona hatari mbele yangu ya
kupoteza nguvu na hatimaye kumezwa kabisa na maji ya ule mto endapo nin?geendelea kuelea juu ya gogo lile kwa muda mrefu. Ule mto ulikuwa una kona
nyingi sana kwa kule mbele yetu na hali hiyo ilinifurahisha sana kwani zile
kona zilikuwa zikipunguza ile kasi ya maji. Hata hivyo hofu ilikuwa ikizidi
kuniingia kwani uwezo wa macho yangu kuona ulikuwa ukipungua kwa haraka sana kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda.
Niligeuka tena kumtazama Ikirezi nikawa namuona kwa mbali kama anay?enishangaa ingawaje sikufahamu kwa haraka kuwa alikuwa akinishangaa nini.
Niligeuka tena kumtazama yule jamaa tuliyeongozana naye nikamuona kuwa
naye alikuwa akinishangaa sasa nikawa kama na mimi nataka kujishangaa
mwenyewe lakini sikufahamu ningejishangaa kwa sababu zipi. Mara muda
uleule nikawa nimeanza kupoteza taswira iliyokuwa mbele yangu na hapo
nikawa naona kama ile miti ya ile misitu iliyokuwa kando ya ule mto ilikuwa
ikiongezeka urefu na ilikuwa ikinipita kwa kasi sana kurudi nyuma yangu.
Muda huohuo nikawa nikihisi kuwa nguvu zilikuwa zikianza kuniishia
mwilini na kwa mbali nilianza kuhisi pia kuwa nilikuwa nikididimia kwenye shimo kubwa na refu lenye giza zito. Hofu ikiwa imenishika nikaanza ku?fumbua mdomo ili nipige mayowe ya kuomba msaada lakini hata ile sauti ya mayowe niliyokuwa nikiipiga sikuweza kuisikia masikioni mwangu.
Mara nikawa siwezi kuona tena mbele yangu na sauti pekee niliyokuwa ni?kiisikia ni ile sauti ya mzizimo wa yale maji mengi ya mtoni na wakati nikien?delea kuwa katika hali hii ghafla nikasikia nikipigwa na kitu kizito kichwanihttp://pseudepigraphas.blogspot.com/
na baada ya hapo sikufahamu kilichoendelea.
#48
ULIKUWA NI KAMA MKANDA WA FILAMU uliyokuwa ukiendelea ndani
ya kichwa changu huku ukionesha matukio yote ya nyuma kwenye kioo ki?kubwa cha runinga ambacho kilikuwa ndani ya mawazo yangu. Nilianza kwa
kuyafumbua macho yangu taratibu huku nikikigeuza kichwa changu kutazama
upande huu na ule nikijaribu kuwaza pale nilikuwa wapi. Sauti pekee nili?yokuwa nikiisikia ni sauti ya mvua kali iliyokuwa ikianguka juu ya bati la
chumba kile.
Hakikuwa chumba kikubwa sana lakini chenye meza, kiti kimoja cha mbao
na kitanda pekee cha chuma ambacho ndiyo nilichokuwa nimekilalia juu yake.
Mwanga hafifu wa taa ya kandili iliyokuwa juu ya meza iliyokuwa jirani yan?gu iliniwezesha kuyaona madirisha ya chumba kile yaliyokuwa yamefunikwa
kwa mapazia yaliyochakaa kiasi cha kuyafanya yapepee ovyo bila ya utaratibu
unaoeleweka.
Hapakuwa na mtu yoyote mwingine ndani ya chumba kile na hali hiyo alini?pa wasiwasi kidogo pale nilipokumbuka kuwa kwa mara ya mwisho tulikuwa
watu watatu yaani mimi, Ikirezi na yule mateka mwingine huku tukiwa tunae?lea juu ya gogo kubwa lililokuwa likikokotwa kwa wepesi na maji ya mto
ule yenye kasi, yaliyochafuka na yanayotisha. Niliunyanyua mkono wangu
wa kulia na kujishika kichwani na nilipouondoa na kuutazama nilishangaa
kuuona kuwa ulikuwa umetapakaa damu ingawaje niligundua kuwa nilikuwa
nimefungwa bandeji kubwa kichwani.
Nikakunja ngumi huku hisia za ugonjwa zikipenya taratibu ndani ya viungo
vyangu mwilini na muda mfupi uliofuata niliendelea kulala pale kitandani huku
upepo wenye baridi nyepesi ukipenya kwenye mawazo yangu huku nikiwa
bado sijaelewa hasa ni kitu gani kilikuwa kimenitokea. Nilijaribu kunyanyuka
toka pale kitandani nilipoketi lakini nilishindwa kwani kichwa changu kili?kuwa kikiuma sana na mwili mzima nilihisi maumivu makali hivyo nilijilaza
tena pale kitandani huku nikiwa nimegeuka kuutazama mlango wa kuingilia mle ndani huku nikijiambia kuwa chochote ambacho kingetokea ingenipasa
nisubiri tu kwani afya yangu ilikuwa mbovu sana kuweza kuleta upinzani.
Nikiwa bado nautazama ule mlango mawazo mengi yalikuwa yakip?ita kichwani mwangu na kunifanya nijihisi kama kiumbe kigeni katika sa?yari mpya halafu ghafla mawazo hayo yalikatishwa na kitendo cha mlango
wa chumba kile kufunguliwa. Moyo wangu ulisimama kidogo kisha ukaan?za kwenda mbio lakini nilipomuona yule mtu aliyekuwa akiingia nilishusha
pumzi huku mapigo ya moyo wangu yakirudi katika utaratibu uliozoeleka.
Alikuwa Ikirezi na hilo lilinipa faraja kidogo, Ikerezi alikuwa amevaa shati
na suruali ya kiume ingawaje bado mavazi hayo yampendeza tu kutokana na
uzuri wake.
“Patrick...!” Ikirezi aliniita kwa furaha huku akiharakisha kuja pale kin?dani “Ninafuraha sana kukuona umerejewa na fahamu mpenzi” aliongea kwa
shauku huku tabasamu hafifu likiumbika usoni mwake. Kwa sekunde kadhaa
nilishindwa nimjibu vipi kwani wazo jipya la kuwa nilikuwa nimepoteza faha?mu lilikuwa limeanza kufanya kazi kichwani mwangu.
“Hata mimi nimefurahi” hatimaye nilimjibu katika sauti dhaifu huku nami
nikiumba tabasamu kisha nikaendelea
“Hapa ni wapi? nilimuuliza huku nikilikagua umbo lake kwa siri baada ya
yeye kuja na kuketi jirani na kitanda changu na hapo nikahisi ni kama vile
sikuwa nimewahi kumuona mwanamke mzuri katika kipindi chote cha maisha
yangu kama huyu.
“Ni hadithi ndefu Patrick, endelea kupumzika kwanza tutaongea vizuri pale
utakapopata nafuu” Ikirezi aliniambia kwa sauti tulivu huku akivitekenya vi?dole vyangu mkononi.
“Nini kilitokea kule mtoni na hapa ni wapi? nilimuuza tena huku nikiyapuu?za maneno yake na hapo Ikirezi akanikaribia na kuanza kinipapasa taratibu ki?fuani kwangu na macho yetu yalipokutana nilihisi kulikuwa na nguvu kubwa
ya uvutano katika hisia zetu.
“Kichwa chako kiligonga mara mbili kwenye jiwe kubwa wakati lile gogo
tulilolidandia lilipogonga kwenye mwamba wa mto ule”
“My God, ilikuwaje? nilimuuliza kwa shauku.
“Ulipoteza fahamu ukaliachia lile gogo lakini nilipata ujasiri wa kukuwahi
na kukudaka kabla hujachukuliwa na maji”
“Sasa uliwezaje kufanya hivyo wakati wewe hujui kuogelea?
“Nilipata ujasiri usio wa kawaida Patrick kwani nilijua ule ndiyo ungekuwa
mwisho wa maisha yako na sikupenda kukupoteza mpenzi kwani ningeumia
sana”
“Bado hajaniambia uliniokoaje” nilimwambia huku nikiviacha vidole vyake
laini vikiendelea kukitomasa kifua changu.
“Niliwahi kukushika mkono kabla ya hujachukuliwa na maji huku mko?no wangu mmoja nikiwa bado nimelishikilia lile gogo na tulipofika mbele
kidogo lile gogo lilinasa kwenye mwamba likawa haliwezi tena kwenda hivyo
nilijivuta na kupanda juu yake ndiyo nikaweza kukuvuta na wewe huku niki?saidiana na yule mwenzetu hadi tukafanikiwa kukuokoa. Hata hivyo ulikuwa ukitokwa na damu nyingi sana kutokana na majeraha uliyoyapata kichwani
baada ya kujipigiza kwenye yake mawe na sote hatukuamini kama ungeweza
kurejewa na fahamu tena”
“Kumbe hivyo ndiyo ilivyokuwa! kweli Mungu mkubwa ahsanteni sana”
nilimshukuru Ikirezi huku nikijiona ni mwenye bahati ya kipekee sana kuwa
hai mpaka wakati huu baada ya kuusikia mkasa ule
“Sasa nini kilifuatia baada ya hapo?
“Usiku ulikuwa umeingia hivyo tusingeweza kulala katika msitu ule na
wewe ukiwa katika hali kama ile hivyo ilitubidi tukubebe na kuanza kutembea
ndani ya ule msitu kutafuta sehemu yoyote ambayo tungeweza kupata msaada.
Kwa kweli ilikuwa safari ndefu sana na inayochosha kwani hatukufahamu
kama tulikuwa tukienda mbele au tukirudi nyuma katika msitu ule lakini hati?maye ndiyo tukafanikiwa kufika hapa”
“Loh! poleni sana” nilimwambia Ikirezi “...Nawashukuru sana kwa
kuyaokoa maisha yangu”
“Hupaswi kutushukuru sisi Patrick ila ni sisi ndiyo tunaostahili kukushuku?ru wewe kwa kutuokoa kwenye mapango yale”
“Oh! usijali Ikirezi hata nyinyi pia mmenisaidia sana vinginevyo wakati huu
nisingekuwa hapa hivyo si vibaya nami nikawashukuru” vidole vya Ikirezi
vilivyokuwa vikinipapasa kifuani vilinifanya nilikumbuke vizuri joto la mwili
wake wakati ule nilipokuwa nikiogelea kwenye ule mto kule pangoni wakati
yeye alipokuwa uchi amenikumbatia mgongoni mwangu.
Nilifarijika sana kwani angalau nilikuwa nimebahatika kumuona akiwa ka?tika hali ile ingawaje hisia zangu zilikuwa mbali sana na mapenzi kwa wakati
ule. Niliyazungusha tena macho yangu kumtazama kabla ya kumuuliza tena
“Yuko wapi?
“Nani? alinijibu kwa swali huku macho yake yakiweka kituo kunitazama
“Yule jamaa tuliyetoroka naye”
“Oh! kumbe sijakwambia, ameondoka na aliniambia endapo utarudiwa na
fahamu nikupe shukrani zake. Aliniamba anahitaji kufika Kigali usiku huu huu
kujua hali ya familia yake”
“Mbona hakusubiri tuondoke wote?
“Msamehe tu kwani alikuwa akitaka kujua usalama wa familia yake hasa
baada ya kupotena nayo kwa muda mrefu” Ikirezi aliongea huku akigeuka
kutazama dirishani kama mtu anayewaza jambo fulani.
Niliyaacha mawazo mengi yakipita kichwani mwangu huku nikiwaza hili
na lile. Hisia zangu ziliniambia kuwa pale sikuwa sehemu salama kama Ikirezi
ilivyodhani na sikuwa na mashaka kuwa hata yeye mwenyewe hakulifahamu
hilo kwa upande wake. Labda alikuwa akifurahi kuniona nikiwa na yeye mle
ndani lakini mimi sikuwa kabisa na mawazo hayo badala yake nilihitaji kurudi
jijini Kigali haraka iwezekanavyo kwani hadi wakati huu sikuwa nimeifikia
hata nusu ya kazi niliyotumwa na siku zilikuwa zimeenda.
Niliyakumbuka yale mapango ya Musanze, nikamkumbuka Kanali Bosco
Rutaganda ama mwanafunzi wangu wa kijeshi aliyegeuka mdudu haramu ka?tika harakati zangu na hapo nikafumba macho na kumeza funda kubwa la mate kuitowesha hasira iliyoanza kuchipua nafsini mwangu. Nikamuomba Mungu
nipone haraka ili niendelea na harakati zangu.
“Nini kiliwatokea kule pangoni hata nikakutana tena na ninyi mkiwa wach?ache? hatimaye nilimuuliza Ikirezi nikivunja ukimya.
“Tulikuwa tukishambuliwa na wale askari kadiri tulivyokuwa tukikimbia”
Ikirezi alinijibu huku akiyahamisha macho yake kutazama pembeni na hapo
nikayaona machozi yakishuka taratibu mashavuni mwake.
“Usijali mpenzi yote yamepita sasa” nilimwambia huku nikimpapasa ki?unoni na hapo akawahi kuuzuia mkono wangu ili nisiendelee kumpapasa kisha
akageuka kunitazama huku akitabasamu.
“Pumzika kwanza mpenzi” Ikerezi akaniambia nami nikabaki nikimtaza?ma tu huku nikijilaani kwa kuwa katika hali ile vinginevyo muda mfupi tu
baadaye angekuwa amenijua kuwa mimi ni mwanaume wa namna gani kwa
wasichana wazuri na warembo wa sampuli yake.
Nilijifuta uso kwa kiganja changu huku nikiendelea kuyatafakari matukio
yote yaliyonitokea tangu nilipofika hapa Rwanda na hapo sikufahamu kama
nilikuwa nimepiga hatua katika upelelezi wangu au lah! lakini nilishukuru tu
kuwa bado nilikuwa hai. Niligeuka tena kumtazama Ikirezi nikamuona kuwa
naye alikuwa amezama kwenye fikra zake, labda na yeye alikuwa akiyawaza
yale matukio yote yaliyotokea kule pangoni, hakuna aliyefahamu. Hatimaye
nikavunja tena ukimya kwa kumtupia swali
“Hapa ni wapi?
“Bado tupo msituni Patrick na bila shaka hii ni nyumba pekee katika msi?tu huu” Ikirezi aliniambia na hapo nikageuka tena kumtazama kama ambaye
sijamsikia vizuri ingawaje maelezo yake niliyapata kwa uhakika.
“Nyumba pekee hapa msituni!, una maana gani? nilimuuliza kwa hamaki
“Ndiyo hivyo kwani inavyosemekana ni kuwa nyumba hii iliachwa na ki?kundi cha madaktari Wafaransa waliokuwa wakifanya utafiti wa magonjwa ya
watoto zaidi ya miaka sita iliyopita”
“Umejuaje?
“Nimeelezwa na mwenyeji wa nyumba hii, ni mtu mkarimu sana, ametu?pokea vizuri jina lake ameniambia anaitwa Innocent Gahizi”
Nilimtazama Ikirezi na kumfananisha na wanawake wengine duniani walio?kuwa na tabia ya kupenda kuamini vitu kwa haraka hata hivyo nilifahamu
kuwa huu haukuwa wakati wa kupingana naye na kwa mara nyingine nilianza
kuhisi kuwa hatukuwa kwenye mikono salama kama Ikirezi alivyodhani.
“Anaishi peke yake humu ndani? nilimuuliza Ikirezi kwa sauti ya chini huku
nikizitazama tena zile nguo za kiume alizozivaa.
“Ndiyo, yeye ni mwindaji wa muda mrefu katika msitu huu. Ameniambia
kuwa aliigundua nyumba hii kuwa ilikuwa imetelekezwa siku moja wakati
alipokuwa kwenye harakati zake za uwindaji na tangu hapo amekuwa akifikia
humu ndani kila anapokuja kuwinda”
Nilimtazama Ikirezi na kumuona alikuwa akiniambia maelezo ambayo ali?kuwa ameyakariri vizuri na kuyaamini lakini mimi sikuwa tayari kukubaliana
nayo.Nikiwa bado naongea na Ikirezi niligundua kuwa kulikuwa na mtu aliyeku?wa amejibanza nyuma ya ule mlango wa kile chumba chetu akiyasikiliza mao?ngezi yetu hivyo nikaamua kubadilisha mada bila ya Ikirezi kujua. Mvua kub?wa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha eneo lile na kwa kiasi fulani ilifanikiwa
kunishawishi nilale lakini hilo halikuwezekana.
Nilitembeza macho yangu kuzitazama zile gwanda za kijeshi nilizozivaa na
hapo nikagundua kuwa zilikuwa mbioni kuvunda kwa ule mchanganyiko wa
jasho, maji ya kule mtoni na matope hivyo nilihitaji kubadili zile nguo lakini
kabla ya kufanya hivyo nilikuwa na swali la kumuuliza Ikirezi pale nilipozi?tafakari zile gwanda za kijeshi mwilini mwangu kuwa yule mwenyeji wetu
angeweza kuzitilia mashaka.
“Umemwambia nini kuhusu sisi?
“Mimi na wewe ni mtu na mkewe na vilevile ni askari wa jeshi la wananchi
wa Rwanda pamoja na yule mwenzetu aliyeondoka, na kuwa tulikuwa humu
msituni tukifanya mazoezi ya kijeshi bahati mbaya tukapoteana na wenzetu na
katika harakati hizo ndiyo tukashambuliwa na wanyama wakali”
Nilimtazama Ikirezi na kumuona kuwa alikuwa amejitahidi sana kudang?anya lakini nilifahamu kuwa uongo wake usingeweza kuaminika kirahisi kwa
mtu mdadisi kama alivyokuwa akidhani hata hivyo nilimpongeza kwa jitiha?da zake. Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha kwenye eneo lile la
msitu na kwa kiasi fulani mvua hiyo ilifanikiwa kunishawishi nilale lakini hilo
halikuwezekana kwani kwangu usingizi ulikuwa ni rafiki wa karibu wa kifo na
mimi sikuwa na urafiki nao.
Tulikuwa tukiendelea na maongezi yetu wakati nilipouona ule mlango
wa chumba chetu ukisukumwa taratibu na yule mtu aliyekuwa amesimama
nyuma ya mlango aliingia kimyakimya kama mzimu. Nilipotembeza macho
yangu kumtazama nikamuona mwanaume mrefu zaidi yangu na mwembamba
kama walivyo wanaume wengi wa kinyarwanda, pengine mwenye umri wa
miaka thelathini na kitu hivi lakini harakati za msituni zilikuwa zimemzoea
na kufanya aonekane kama anayekimbilia umri wa miaka hamsini tangu afike
hapa duniani.
Uso wake ulikuwa mrefu na mwembamba, mikono yake mirefu ilikuwa na
lukuki ya mishipa ya damu iliyotuna na misuli imara. Kingo za mdomo wake
zilikuwa nyeusi zilizoungua kwa moshi wa sigara na macho yake yalikuwa
makali kama ya nyoka na yenye umbo kubwa linalokaribiana na lile la mayai
ya njiwa. Kitu kimoja nilichokuwa na hakika nacho nikuwa sikuwahi kumuo?na mtu wa namna hii katika harakati zangu.
Mtu yule alikuwa amevaa kofia kubwa aina ya pama, koti refu la mvua na
suruali ya jeans iliyochakaa. Aliingia na kukatisha taratibu katikati ya chumba
kile bila ya buti zake ngumu za ngozi kutoa sauti yoyote katika sakafu ile ya
chumba yenye nyufa za kila aina. Japokuwa alikuwa akijitahidi sana kuta?basamu lakini alionekana dhahiri kuwa alikuwa akijilazimisha. Sote tuligeuka
kumtazama wakati akiingia.
Kwa kweli niliogopa sana na japokuwa mtu tule alijitahidi sana kutabasamu
lakini kulikuwa na muonekanao tofauti katika macho yake kitu ambacho kilinionya kuwa mtu yule alikuwa hatari pengine kushinda yale majoka makubwa
niliyopambana nayo kule mapangoni.
Niliendelea kumtazama yule mtu na hapo nikagundua kuwa muonekano
wake haukufanana kabisa na ule wa mwindaji kama alivyojinadi na kwa
harakaharaka nilipomchunguza niligundua kuwa alikuwa ni mtu wa kazi to?fauti na uwindaji na hivyo kazi ya uwindaji haikuwa ni sababu iliyomleta pale
msituni. Ni sababu ipi iliyomleta yule mtu pale msituni hilo lilibaki kuwa ni
swali moyoni mwangu.
“Pole sana Koplo” yule mtu aliniambia kwa sauti yake nzito na kavu yenye
mikwaruzo baada ya kufika na kusimama jirani na kile kitanda nilicholala.
“Koplo Jonas Kabale” Ikirezi alidakia na kumfafanulia. Nilikuwa mbioni
kushikwa na mshangao lakini haraka niliuyeyusha mshangao wangu usoni
kabla mtu yule hajanishtukia kwani niligundua kuwa Ikirezi alikuwa amem?danganya yule mtu kuwa jina langu ni Jonas Kabale na kile cheo cha Koplo
ni kutokana na zile gwanda za kijeshi nilizovaa ambazo zilikuwa zikionesha
cheo changu begani.
Wakati huu nilimuona Ikirezi kuwa alikuwa mwanamke mjanja sana hata
hivyo sikuongea chochote, na sikuweza kujua ni kwanini akili yangu ilikuwa
imeanza kupoteza utulivu.
“Oh! kweli uliniambia kuwa jina lake ni Koplo Jonas Kabale wa jeshi la wa?nanchi wa Rwanda” yule mtu aliongea na kumtazama Ikirezi huku akijitahidi
kuumba tabasamu la kirafiki.
“Vipi unaendeleaje ndugu? yule mtu aliniuliza huku akigeuka tena kunita?zama
“Anaendelea vizuri ila anahitaji muda wa kuendelea kupumzika zaidi”
Ikirezi alimwambia
“Nguo zake zimevunda kama utambadilisha na kumpa chakula hiyo itam?fanya ajisikie vizuri zaidi” yule mtu aliendelea kuongea akimwambia Ikirezi
“Chumbani kwangu nyuma ya mlango kuna nguo zinazoweza kumtosha nen?da kazichukue na umtayarishie chochote cha kumpa nguvu”
Nilimsikia yule mtu akimwambia Ikirezi na ingawaje alikuwa akitoa ush?auri wa maana lakini nilijihisi kushikwa na hasira kwani yule mtu alikuwa
ni kama anayemuamrisha Ikirezi tena kwa sauti ya dharau na hata Ikirezi al?ipokuwa akiondoka mle chumbani yule mtu alibaki akimtazama kwa nyuma
huku akionekana kufurahishwa na mjongeo wa umbo lake.
Nilibaki nimelala pale kitandani huku nikizisikia hatua za Ikirezi namna
zilivyokuwa zikiyoyoma kisha nikageuka kumtazama yule mtu huku nikiwa
nimeshikwa na hasira sana halafu nikashusha pumzi na kujifuta uso kwa vi?ganja vyangu na hapo nikajihisi kuwa ni kama nimekuwa mtoto kwa ghafla
sana.
Yule mtu aliendelea kumtazama Ikirezi hadi pale alipopotea kisha akaan?gua kicheko hafifu na kugeuka kunitazama pale kitandani huku uso wake uki?wa bado umeumba tabasamu lisilo na maana yoyote machoni mwangu kisha
nilimuona yule mtu akijipapasa kwenye mfuko wa koti lake na kutoa pakiti ya
sigara na hapo akaichukua moja na kuweka mdomoni kisha akaiwasha.
“Hongera sana Koplo kwa kuwa na mke mzuri” yule mtu aliongea baada
ya kuitoa sigara mdomoni “...Nakwambia ndugu yangu ni askari wachache
sana wanaojua kufanya uchaguzi mzuri wa mke mwema kama wewe. Jina lake
ni Victorie Igabire Umuhoze ama sivyo?, mkeo ana jina zuri sana” yule mtu
aliendelea kuongea na hapo nilifahamu kuwa Ikirezi alikuwa amemdanganya
kuwa jina lake ni Victorie Igabire Umuhoze.
“Kila jina lina maana yake” nilivunja ukimya na kuongea huku nikisikia
maumivu makali kichwani mwangu huku nikikwepa kuendelea na mada ile.
“Niliwahi kuwasikia watu fulani wakisema wanawake ni viumbe wa kipe?kee sana hapa duniani na wanapokuwa ndani ya nyumba kila kitu huchan?gamka” yule mtu aliendelea kuongea lakini mimi sikutaka kuendelea kujikita
kwenye maongezi yale kwani nilihisi kuwa kuna kitu fulani kilichokuwa ki?kijengeka katika fikra zake dhidi ya Ikirezi na kitu hicho hakikuwa tofauti na
uchu wa ngono.
Yule mtu aliendelea kuongea na aliponiona kuwa sina neno lolote la kuchan?gia katika maongezi yake akaamua kubadilisha mada.
“Mke wako umeniambia kuwa nyinyi ni wanajeshi wa jeshi la wananchi
wa Rwanda na mlikuwa sehemu fulani katika msitu huu mkifanya mazoezi
ya kijeshi na kwa bahati mbaya mkapoteana na wenzenu kabla ya kusham?buliwa na wanyama wakali. Lakini nimeliona jeraha la risasi begani mwako
wakati ulipoletwa umebebwa na mke wako na yule mtu mwingine, unaweza
kuniambia ilikuwaje Koplo? yule mtu aliniuliza. Haraka nikagundua kuwa lile
lilikuwa ni swali la mtego ambalo sikuwa nimelitarajia hivyo likanipokonya
ujasiri wangu kwa kiasi fulani na kupelekea koo langu kukauka kwa ghafla.
Alipoona nakawia kumjibu yule mtu alivuta kile kiti kilichokuwa pale jira?ni ya kitandani na kuketi huku akiendelea kuvuta sigara yake taratibu, kisha
akaendelea
“Mnadhani kuwa kuna namna yoyote mnayoweza kuitumia kuwajulisha
wenzenu kuwa mko hapa?
“Hakuna haja, tunashukuru tutawatafuta sisi wenyewe” nilimjibu kwa ufupi
“Lakini ninaweza kuwasaidia kama mtapenda nifanye hivyo” yule mtu al?isisitiza tena
“Hapana wala hakuna haja, kumbuka hilo ni jukumu letu sisi, yule mwen?zetu aliyeondoka atarudi kutuchukua” nilimdanganya yule mtu na hapo nil?ishtuka kuuona uso wake ulivyokuwa umepoteza nuru kwa haraka. Toka
pale nilipolala nilimuona yule mtu akigeuka kutazama dirishani lakini nili?pomchunguza vizuri nilifahamu kuwa hapakuwa na kitu chochote cha maana
alichokuwa akikitazama upande ule na hapo nikagundua kwa lile jibu langu
lilikuwa limetengeneza mtazamo tofauti kichwani mwake.
Yule mtu aliirudisha sigara yake mdomoni na kuvuta mapafu kadhaa na ali?poitoa aliupuliza moshi angani huku akiutazama kwa ufikirivu kisha akayarud?isha macho yake kunitazama halafu muda huohuo akasimama na kuniuliza
“Mwenzenu atarudi lini?
“Nilimwambia arudi hapa baada ya wiki moja” ilikuwa ni sauti ya Ikirezi
na sote tulishtuka na kugeuka kwani hakuna aliyedhani kuwa Ikirezi angerudi mapema kiasi kile na mkononi alikuwa ameshika kikombe na sahani aliyoshe?heni nyama za kukaanga. Alipofika kwenye ile meza aliyokuwa jirani yangu
akaiweka ile sahani na kile kikombe juu yake. Ikirezi alikuwa ni mwanamke
aliyefahamu kupika vizuri na haraka kwani hakuwa ametumia muda mrefu.
“Atarudi peke yake? yule mtu aligeuka na kumuuliza Ikirezi na swali hilo
likapelekea mimi na Ikirezi kutazamana kwa siri.
“Ndiyo, nilimwambia hivyo kwani sipendi wenzetu wafahamu kuwa tuko
hapa” Ikirezi aliendelea kumjibu yule mtu huku akijisogeza karibu na kitanda
changu na bila ya shaka jibu la Ikirezi lilikuwa limemfurahisha sana yule mtu
kwani nilimuona akitabasamu ingawaje sikupenda afahamu kuwa nilikuwa
nikimchunguza.
“Poleni sana lakini mnapokuwa askari hivi ni vitu vya kawaida sana kuto?kea” yule mtu aliongea tena baada ya kutoa sigara mdomoni.
“Mwanajeshi siku zote ni mtu wa mikasa tu” nilidakia na hapo nikayaona
meno yake meusi yaliyotapakaa ukungu wa moshi wa sigara yakichanua baa?da ya kuangua kicheko hafifu ambacho pengine kilimfanya aonekane kama fisi
kisha akavunja ikimya.
“Unatakiwa kula Koplo, chakula kitakupa nguvu kidogo, hiyo ni nyama ya
nyumbu na bila ya shaka huna matatizo nayo” yule mtu aliniambia huku aki?nitazama
“Nashukuru” nilimwambia
“Vizuri, mimi nahitaji kupumzika kidogo nitakwenda kuwinda utakapofika
usiku” yule mtu alituambia na bila ya kusubiri sisi kuongea chochote yule mtu
alianza kuondoka akiufuata ule mlango wa kutokea mle chumbani. Ulikuwa ni
wakati huu mtu yule alipokuwa akiondoka wakati lile koti lake refu la mvua
lenye mpasuo katikati lilipopishana na hatua zake na hapo nikafanikiwa kuuo?na mtutu wa bunduki yake aina ya Semi automatic 223 Caliber Rifle ukiwa
anachungulia chini ya koti ya koti lile.
Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu kabla ya kuhisi koo langu likikauka
na nafasi yake kuchukuliwa na ladha chungu ya kitu kama nyongo. Ile bunduki
haikuwa maalumu kwa ajili ya kuwindia wanyama ingawaje hiyo haikumaani?sha kuwa risasi zake zingeshindwa kuuondoa uhai wa mnyama yoyote.
Nilimsindikiza yule mtu kwa macho hadi pale alipofungua mlango wa kile
chumba na kutoka na hapo nikashusha pumzi na kugeuka nikimtazama Ikirezi
lakini uso wake haukunieleza kuwa alikuwa ameshtukia chochote hivyo nil?iaamua kukaa kimya. Ikirezi alinishika mkono huku uso wake ukiwa umeum?ba tabasamu na hapo akaniuliza
“Vipi unajisikiaje kwa sasa?
“Kichwa na bega bado vinaniuma na pia nasikia njaa sana?
“Amka ule, nimepata vidonge vitakavyokupunguzia maumivu” Ikirezi alin?iambia
“Umevipata wapi?
“Kule jikoni nimekuta kisanduku cha huduma ya kwanza”
Kwa msaada wa Ikirezi nilifanikiwa kunyanyuka kidogo na kukiegemeza
kichwa changu kwenye mto niliokuwa nimeugemezea ukutani pembeni ya kitanda. Wakati huu nilisikia kichwa changu kikipwita kwa maumivu kana kwamba nilikuwa nimebebeshwa mzigo mzito sana, Ikirezi akaketi juu ya kitanda pembeni yangu na kuanza kunilisha zile nyama ambazo alikuwa amezikaanga vizuri sana. Nikawa nikishushia kwa maji yaliyokuwa kwenye
kikombe kilichokuwa mezani pale jirani.
Chakula kilikuwa kitamu sana ingawaje hakikuwa kimepikwa katika mazingira yale niliyoyazoea lakini nilishiba vizuri na nilipomaliza nikameza vi?donge vya kutuliza maumivu ambavyo Ikirezi alikuwa amevishika mkononi.
Nilimaliza kula kisha nikageuka na kumbusu Ikirezi shavuni huku tabasamu
hafifu likinawiri usoni mwangu
“Ahsante sana kwa chakula mpenzi” nilimwambia Ikirezi huku nikijiege?meza vizuri pale kitandani
“Hata mimi nafurahi kukuona umekula mpenzi, usijali muda si mrefu utapa?ta nafuu na tutaondoka”
Niliyafurahia maneno ya Ikirezi kwa kunipa matumaini ingawaje bado nili?kuwa na wasiwasi na yale maneno ayasemayo kama kweli yangetimia. Nilim?uona Ikirezi akijilaza pembeni yangu huku macho yake yakitazama juu ya dari
ya kile chumba na nilipomtazama nikatambua kuwa alikuwa akiwaza jambo
fulani hata hivyo sikumsemesha kwani na mimi nilianza kuwaza yangu.
Ule wasiwasi wa kuwa hatukuwa kwenye mikono ya mtu salama ulianza
kupenya tena katika fikra zangu na wakati huu sikuwa tena na mashaka nao.
Baada ya kuwaza sana hatimaye niliazimia kuwa pindi mtu yule atakapoondo?ka muda wa usiku kwenda kuwinda ndiyo ningeutumia muda huo kuipeleleza
vizuri nyumba ile. Niliyarudisha mawazo yangu mle ndani kwa kuunyanyua
mkono wangu na kuanza kutomasa tomasa mikono ya Ikirezi na hapo nilimu?ona akigeuka kunitazama.
“Umepanga kuelekea wapi mara baada ya kufika jijini Kigali? aliniuliza
“Nimepanga kumalizia kazi niliyoianza na baada ya hapo nitarudi nchini
kwangu”
“Tanzania?
“Bila shaka, umejuaje? nilimuuliza huku mkono wangu ukiwa umehamia
kukitomasa kiuno chake hata hivyo safari hii sikupata upinzani wowote badala
yake nilimuona Ikirezi akitabasamu tu.
“Nilikusikia wakati ulipokuwa ikiongea na rafiki yako kule pangoni kuwa
wewe ni Mtanzania”
“Ndiyo mimi ni Mtanzania na nilifika hapa Rwanda kwa kazi moja muhimu
bahati mbaya sana ndiyo nikajikuta nimetumbukia kwenye masaibu haya”
nilimwambia Ikirezi huku nikiendelea kukitomasa kiuno chake, mchezo ulio?onekana kuzidi kumfurahisha. Sikupenda Ikirezi aifahamu kazi yangu.
“Kazi gani?, mfanyabiashara, mwandishi wa habari, mwana mitindo au...?
“Mojawapo kati ya hizo” nilimjibu huku nikianguka kicheko hafifu ukweli
ni kwamba sikupenda maongezi yale yaendelee lakini nilishangaa kumuona
Ikirezi akicheka na hapo nikashikwa na butwaa huku nikimshangaa kuwa ali?kuwa akicheka nini.
“Usinidanganye mpenzi, wewe si mfanyabiashara, mwandishi wa habari wala mwanamitindo”
“Sikudanganyi”
“Usidhani kama hii ni mara yangu ya kwanza kukutana na mwanaume wa
aina yako, nimekutana nao wengi ila tofauti ni moja tu uliyonayo”
“Tofauti ipi hiyo? nilimuuliza kwa shauku
“Wewe ni mzuri sana, mwanaume mwenye mvuto na bila shaka uzuri wako
unafanana na moyo wako na nimetokea kukupenda sana Patrick” Ikirezi alin?iambia huku akinipapasa kifuani.
“Sasa unadhani kazi yangu mimi ni ipi? nilimuuliza Ikirezi huku nikikum?buka namna alivyokuwa akinitazama wakati ule tulipokuwa kule pangoni.
“Sitaki kuitaja kwa sababu hata wewe hupendi niifahamu” maneno ya
Ikirezi yalinifanya nimtazame kwa makini msichana yule kana kwamba ndiyo
nilikuwa namuona kwa mara ya kwanza.
“Sasa unadhani mimi ni nani?
“Mtu fulani mwenye kazi fulani hatari iliyokuleta hapa Rwanda na si mwan?dishi wa habari, mwanamitindo wala mfanyabiashara kama unavyoendelea
kunidanganya” nilicheka kidogo kisha nikageuka vizuri kumtazama Ikirezi
“Yeyote anaweza kusema kama wewe” nilimwambia huku nikitabasamu
“Sikulaumu kwa kunidanganya kwani ni maadili ya kazi yako ndiyo yan?ayotaka ufanye hivyo”
“Kazi ipi? Nilimuuliza kwa udadisi
“Kwa mara ya kwanza tu nilipokuona nilivutiwa sana na wewe na tulipoen?delea kuzoeana nikajikuta nikiifahamu kazi yako. Wewe ni mpelelezi Patrtick
na usinidangaye”
“Nini kinachokufanya uhisi kuwa mimi ni mpelelezi?
“Wapelelezi wote wanatabia kama zako, wacheshi, wakarimu, wanahuruma
ingawaje wakati mwingine huwa wanajifanyisha ili mambo yao yafanikiwe
lakini wewe ni tofauti sana Patrick. Una huruma sana ndiyo maana nimejikuta
najitongozesha kwako kama mwanamke malaya” Ikirezi aliniambia huku aki?angua kicheko hafifu.
“Hapana wala hujakosea kwani pale moyo unapopenda huwa hauna pin?gamizi”
“Hata mimi nilikudanganya Patrick lakini nilikudanganya kama wewe
ulivyonidanganya. Jina langu ni Rosine, Rosine Nzingamasambo na wala si
Ikirezi wala Victorie” Ikirezi aliniambia huku akiendelea kukipapasa kifua
changu
“Endelea” nilimwambia huku nikitabasamu
“Dada yangu alikuwa akiitwa Diane...”
“Kwanini unasema alikuwa akiitwa Diane na yupo wapi sasa hivi? nilim?katisha
“Nasema alikuwa akiitwa Daine kwa sababu sasa hivi ni marehemu” Ikirezi
ambaye sasa nilianza kumfahamu kwa jina jipya la Rosine aliongea huku sauti
yake akipoteza ule ujasiri. Niligeuka kumtazama na hapo nikayona machozi
yakimlengalenga machoni, nikafahamu kuwa alikuwa kwenye kumbukumbu
mbaya ya mambo yaliyopita.
“Pole sana Rosine nini kilitokea? nilimbembeleza taratibu na hapo akageu?ka kunitazama kisha akayapangusa machozi kwa vidole vyake kabla ya ku?endelea.
“Tulizaliwa wawili tu katika familia yetu yaani mimi na dada yangu Diane,
tumelelewa katika malezi ya mzazi mmoja yaani mama yetu tangu tulipokuwa
wadogo hivyo hatukuwahi kumuona baba yetu ambaye sasa namuita mwana?haramu”
“Kwanini? nilimuuliza kwa shauku
“Mama yetu alibakwa na mmoja wa askari wa kitutsi katika mkoa mmoja
wa huko kaskazini mashariki mwa Rwanda eneo lililopakana na nchi ya Jam?huri ya Kidemokrasia ya Congo wakati eneo hilo lilipokuwa na machafuko ya
vita ya kikabila. Kwa mujibu wa kumbukumbu ambayo kamwe haikunitoka
kichwani mama alifanyiwa unyama huo wakati akiwa na umri wa miaka kumi
na nne tu huku baba na mama yake wakiuwawa na vita ilipoisha ilimuacha
mama yetu akiwa mjamzito.
Baada ya muda kufika hatimaye alijifungua watoto mapacha yaani mimi na
dada yangu. Tulionekana watoto wazuri na warembo katika macho ya watu
lakini machoni kwa mama yetu ambaye alikuwa akiifahamu siri ya kupatika?na kwetu alikuwa na hasira sana kila alipokuwa akitutazama. Bila ya shaka
alikuwa akijisikia aibu na fedheha sana kila alipolikumbuka tukio la kubakwa
kwake mbele ya jamii ile iliyomzunguka.
Tulipotimiza umri wa miaka kumi na mbili mama alituambia kuwa
uvumilivu ulikuwa umemshinda na hakuwa tayari kuendelea kufedheheka
kwa kigezo kuwa tulikuwa tukifanana na baba yetu kwani japokuwa alikuwa
amemwingilia kimwili siku moja tu lakini alikuwa akiikumbuka vizuri sura
yake, kwa hiyo usiku mmoja aliamua kujinyonga” Rosine aliweka kituo huku
huzuni ikionekana kumzidi nguvu na hapo akaanza kulia kwa sauti a chini
chini.
Mimi nilikuwa na hisia kama zake hata hivyo sikumbuki ni lini niliwahi
kulia katika kukuwa kwangu badala yake nilimeza funda kubwa la mate kuji?weka sawa nikamsogeza Rosine karibu yangu huku kichwa chake kikilala juu
ya mapaja yangu na hapo nikaanza kumfuta machozi huku nikimbembeleza
kuwa asilie kwani yale yalishapita. Ilikuwa ni kazi ngumu kidogo lakini hati?maye alinisikia na kunyamaza kisha muda ulipita kidogo kabla ya kuendelea
“Baada ya kumzika mama tulipokonywa ardhi yetu kwani kwa mila na des?turi za eneo lile mwanamke hakupaswa kumiliki ardhi kwa hiyo hatukuwa
na kitu tena hivyo tuliamua kuondoka eneo lile na kuja kutafuta maisha jijini
Kigali kwa kuwa tulikuwa tukisikia maisha yalikuwa mazuri sana huko Kigali.
Lakini tulipofika jijini Kigali haikutuchukua muda mrefu kugundua kuwa hali
ya maisha ilikuwa mbaya sana kwa mtu yoyote asiye na kazi kuweza kuyamu?du maisha katika eneo lile”
“Sasa ilikuwaje? nilimuuliza huku nikiyatomasa matiti yake taratibu
“Maisha yalikuwa magumu sana tukila kwa taabu na kulala stendi za mabasi
kwa muda wa mwaka mmoja na nusu lakini pamoja na hayo hatukuwa tayari
kurudi nyuma.Tukiwa tunaendelea na maisha ya namna ile usiku mmoja dada yangu akapa?ta mwanaume wa kabila la kitutsi. Alikuwa mrefu, mwembaba, mweusi wa
wastani na mzuri sana katika macho ya mwanamke yoyote yule na alionekana
kuwa ni mtu mwenye kipato cha kuaminika. Mwanaume yule alimwambia
dada yangu Diane kuwa anampenda na alikuwa akimtaka wakaishi wote kama
mume na mke.
Nilimuonya dada yangu kuwa asiambatane naye kwa kuwa bado sote tuli?kuwa tukimkumbuka mama yetu na mkasa wa kubakwa kwake na mwanaume
wa kitutsi lakini haikuwa rahisi kumshawishi dada kwa kuegemea kwenye
kigezo hicho istoshe aliniambia kuwa yeye hakuwa tayari kuishi katika maisha
magumu tuliyokuwa tukiishi huku tayari akiwa amempata mwanaume mzuri
mwenye kipato aliyekuwa tayari kuishi naye. Hata hivyo baadaye nilitambua
kuwa dada yangu Diane si pesa tu iliyokuwa imemshawishi kumkubali mwa?naume yule bali alikuwa amempenda sana Jean Felix Akaga.
Jean Felix Akaga alituchukua kwenye gari lake usiku ule na kutupeleka
kwenye mgahawa mmoja uliopo katikati ya jiji la Kigali ambako alitununulia
chakula cha bei ya ghali ambacho hatukuwahi kula katika maisha yetu. Siku
ile na sisi tulijiona tumethaminiwa sana tukashushia mlo kwa vinywaji vya
aina aina. Tulipotosheka akatuchukua kwenye gari lake mpaka nyumbani
kwake huko Block C nyumba namba 11 katika nyumba za shirika la nyum?ba la taifa huko Amahoro. Tulipofika alitukaribisha ndani kwake. Ilikuwa ni
nyumba yenye aina ya samani za kisasa na vitu vya kifahari ambavyo tulizoea
kuviona kwenye sinema.
Nilikuwa nikiogopa sana lakini dada yangu alinitia moyo kuwa nisiwe na
hofu kwani ile ilikuwa karata yetu turufu ya kuupiga teke umasikini.
Jean Felix Akaga alikuwa ni mwanamume wa umri wa miaka ishirini na
nane wakati huo na alituambia kuwa hakuwa na mke wala rafiki wa kike kwani
ndiyo alikuwa anaanza maisha na hivyo tangu siku ile akawa shemeji yangu.
Mimi nikilala katika chumba kimoja cha mle ndani peke yangu na yeye akilala
na dada yangu kwenye chumba kingine kikubwa cha mle ndani” Rosine ali?weka kituo akimeza funda la mate halafu akageuka kunitazama ili kujiridhisha
kama nilikuwa bado nikimsikiliza au lah!. Hata hivyo tabasamu hafifu lilium?bika usoni mwake pale macho yetu yalipokutana. Kwangu lilikuwa ni simulizi
fupi ambalo lilinivutia sana na kunipa hisia za kipekee katikati ya msitu wa
kutisha kama ule lakini sikuweza kuliamini kwa asilimia zote.
Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha sambamba na upepo mwe?pesi uliokuwa ukipenya madirishani mwa ile nyumba katikati ya msitu ule.
Nilijisogeza jirani na meza iliyokuwa pembeni ya kitanda na kuishika ile taa
ya kandili iliyokuwa ikimulika mle ndani kisha nikaitikisa kidogo kuichun?guza kama bado ilikuwa na mafuta ya kutosha. Bado ilikuwa na mafuta ki?asi hivyo niliirudisha tena mezani na kujisogeza vizuri pale kitandani kisha
nikamwambia Rosine aendelee kunisumulia.
“Ule ndiyo ulikuwa mwanzo wa maisha mazuri kwetu, tulikula na kunywa
tulichotaka, tulivaa mavazi ya kisasa na kwenda kustarehe kokote tulipojisikia.
Jean Felix Akaga alitupenda sana na zaidi alimpenda sana dada yangu Diane na nilimuona kuwa alikuwa na wivu sana kwa Diane hivyo kila wakati alim?papatikia Diane na alikuwa tayari kumtimizia chochote alichokitaka. Lakini
wakati huo wote tulikuwa hatuifahamu vizuri kazi yake na kila tulipomuuliza
hakuwa tayari kutuambia huku akituambia kuwa maadili ya kazi yake haya?kumruhusu kutuambia kazi anayoifanya na mradi tulikuwa tukila na kunywa
bila ya matatizo yoyote haikuwa na haja ya kufahamu mambo mengine.
Jean Felix Akaga alikuwa ni mtu wa marafiki wengi sana wa kike kwa wak?iume wa rika tofauti. Marafiki hao walikuwa wakifika pale nyumbani mara
kwa mara na kila walipofika walitumia muda mrefu na Jean Felix Akaga ku?jadili mambo fulani waliyoyajua wenyewe. Na watu wote waliokuwa wakifi?ka pale nyumbani walikuwa na tabia zinazofanana, wacheshi, wakarimu na
marafiki wazuri kama alivyokuwa Jean Felix Akaga. Lakini baada ya kufanya
uchunguzi kwa muda mrefu tulikuja kugundua kuwa Jean Felix Akaga ali?kuwa mpelelezi katika idara maalum ya usalama wa serikali ya Rwanda na
ndiyo maana kwa tabia zile za marafiki zake haikunichukua muda kukugundua
wewe kuwa ni mpelelezi kwani tabia zenu zinafanana”
“Ni uchunguzi gani mlioufanya hadi mkajiridhisha kuwa huyo Jean Felix
Akaga alikuwa ni mmoja wa wapelelezi katika idara ya usalama wa taifa ya
hapa Rwanda?
“Alikuwa mtu wa safari nyingi sana na za ghafla na siku zote alikuwa na
marafiki tofauti. Siku moja dada yangu alikuwa akifanya usafi chumbani
kwake akaiona bastola chini ya godoro. Sote tulishikwa na wasiwasi sana
kwani tulianza kuhisi kuwa Jean Felix Akaga alikuwa akijishughulisha na vi?tendo vya uhalifu.
Jioni ile aliporudi kutoka kazini dada alimtaka amueleza juu ya bastola ile
kuwepo chini ya godoro na hapo Jean Felix Akaga ikabidi amueleze dada kuwa
yeye alikuwa ni mpelelezi katika idara ya usalama wa taifa kwenye kitengo
maalum kinachosimamia usalama wa rais huku akimuonya dada yangu kuwa
asiitoe siri ile kwa mtu yoyote kwani endapo ingekuja kujulikana sisi wote
pamoja na yeye tungekuwa matatani. Lakini nafikiri kuwa alikuwa akisema
ukweli kwani nakumbuka hata watu alikuwa akikutana nao wengi niliwafaha?mu kuwa walikuwa ni viongozi waliokuwa na madaraka makubwa serikalini”
Kufikia hapo Rosine akaweka kituo, nikamuona ni kama anayefikiria kitu
falani nami nikatumia nafasi hiyo nikayapumzisha mawazo yangu kwa muda
na hapo nikageuka kutazama dirishani ingawaje bado akili yangu haikuweza
kujitenga na lile simulizi la Rosine.
Ukimya ukawa umechukua nafasi mle ndani na hapo nikawa nikiisikia ile
mvua kubwa ikiendelea kunyesha juu ya paa la nyumba ile. Mawazo mengi
yakawa yanapita kichwani mwangu na ile taswira ya yule mtu mwenyeji wetu
ikawa ni kama inayonijia na kuondoka na wala haikunivutia hata kidogo. Nili?poona ukimya unaendelea kushika hatamu nikageuka tena kumtazama Rosine.
“Unaweza kuwakumbuka baadhi ya hao watu waliokuwa wakifika hapo
nyumbani kuonana na huyo Jean Felix Akaga? nilimuuliza Rosine kama nam?na ya kumfanya aendelee kusimulia kwani nilikuwa nimeanza kuchoshwa na
upweke wa mle ndani.
“Pale nyumbani walikuwa wakija watu wengi wa aina tufauti kama
nilivyokueleza na wengine niliwaona mara moja tu na sikuwaona tena baada
ya hapo hivyo ni vigumu kuwambukuka labda kama itokee nionane nao tena.
Ila yupo mmoja ninayemkumbuka kwa jina moja la Sam kwani mara nyingi
nilikuwa nikimsikia Jean Felix Akaga akimuita hivyo”
“Huyo Sam ni nani?
“Rafiki wa Jean Felix Akaga na bila shaka walikuwa wakifanya kazi pamoja
kwani mara nyingi alikuwa akimpitia pale nyumbani. Huyu Sam namkumbu?ka vizuri kwani ndiye aliyepelekea kutokea kwa taarifa za kusikitisha usiku
ule ambazo kamwe sitazisahau”
“Taarifa gani?
“Jioni ile dada na Jean Felix Akaga waliniomba tutoke wote na kwenda
kupata mlo katika mgahawa mmoja uliokuwa mjini wakidai walikuwa wa?mealikwa na huyo Sam lakini mimi sikuungana nao kwani nilikuwa sijisikii
vizuri hivyo waliniacha na kuondoka mimi nikaelekea kulala. Ilipofika saa
nane usiku nikashtushwa na sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlango wa
mbele wa nyumba ile.
Nilishikwa na wasiwasi sana kwani nilikumbuka kuwa mpaka muda ule
dada na Jean Felix Akaga walikuwa bado hawajarudi. Nikaamka na kwenda
kufungua mlango hata hivyo nilishangaa kukuta mgongaji hakuwa dada wala
Jean Felix Akaga kama nilivyotarajia bali alikuwa ni msichana wa miaka kati
ya ishirini na tano hadi ishirini na nane hivi, mrefu na mwembamba. Japoku?wa ulikuwa usiku lakini mwanga hafifu wa taa ya sebuleni uliweza kuufichua
vizuri uzuri wa msichana yule.
Alikuwa msichana mzuri ambaye kamwe sikuwahi kumuona katika pitapita
zangu. Baada ya kusalimiana naye akaniambia kuwa alikuwa amekuja kuni?pa taarifa ya ajali mbaya iliyotokea barabara moja iendayo mjini ikilihusisha
gari moja lililokuwa na mwanaume na mwanamke ambao vitambulisho vyao
vilijieleza kuwa walikuwa wakiishi nyumba ile. Hivyo yule msichana aliku?wa amekuja kunipa taarifa ili niende nikawatambue watu wale. Kwa kweli
niliziamini taarifa zile huku nikijihisi kutaka kuchanganyikiwa ingawaje yule
msichana alijitahidi sana kunituliza”
“Nilijiandaa haraka nikatoka na kuongozana na yule msichana tukielekea
hospitali kuu ya Kigali kwani yule msichana alikuwa ameniambia kuwa huko
ndiko walikokuwa wamepelekwa hao majeruhi.
Tulipotoka tukaingia kwenye gari lake dogo aina ya Toyota Carina ambayo
alikuwa amekujanayo pale nyumbani. Tulipoingia kwenye gari lile safari ya
kuelekea huko hospitalini ikaanza hata hivyo hatukufika mbali pale niliposh?tukia napigwa kabari kwa nyuma kisha nikahisi kitu kama sindano ndogo na
nyembamba ikipenya haraka shingoni mwangu na baada ya hapo sikufahamu
kilichoendelea na nilipozinduka nikajikuta mle ndani ya pango” Rosine ali?maliza kusimulia huku akiniacha katikati ya lindi la mawazo mengine ma?pya huku kwa mbali nikianza kuhisi kuwa pengine simulizi lile fupi lilikuwa
lina maana fulani katika safari yangu ya kijasusi, ingawaje nilipozidi kufikiri
sikuweza kuhusisha moja kwa moja na harakati zangu na vilevile sikutaka kuyaamini haraka maelezo yale. Lakini angalau mpaka sasa nilijihisi nilikuwa
na watu fulani niliokuwa nikiwafahamu tangu nifike katika nchi hii na lile jina
la Sam likiwa limeongezeka katika orodha hiyo.
Nikashusha pumzi taratibu huku nikiyapa utulivu mawazo yangu wakati
huo nikimuomba Mungu kuwa nipone haraka ili nikavitegue vitendawili vyote
kichwani mwangu. Nikiwa naendelea kufikiri Rosine akanikatisha kwa kuniita
“Patrick!, wewe ni mpelelezi?
“Ndiyo mimi ni mpelelezi” niliamua kumjibu bila kupindisha maneno na
pasipo kuujutia uamuzi wangu na jibu langu likamfanya Rosine ashikwe na
butwaa kana kwamba hakusikia nilichokitamka
“Umekuja kupeleleza nini hapa Rwanda?
“Bado sijajua mpenzi ila nafikiri napaswa kuendelea kukaa hapa Rwanda
kwa muda fulani kabla ya kurudi nchini kwangu Tanzania”
“Nani atakayekuamini kwa maneno yako Patrick? mimi binafsi sikuamini.
Najua unanificha pengine hupendi nifahamu kuwa ni kitu gani kilichokuleta
hapa nchini Rwanda lakini hapaswi kunificha mpenzi kwani mimi na wewe ni
kitu kimoja sana”
“Sidhani kama hapa ni sehemu husika ya kuzungumzia hilo mpenzi, usijali
bado tuna muda wa kutosha”
“Labda pengine hutaki kuniambia kwa sababu sina umuhimu wowote katika
masuala yako” Rosine alinijibu kwa sauti ya kinyonge huku akibetua mabega
yake.
“Hilo wala lisikusumbue mpenzi wakati utakapofika nitakusimulia mkasa
wote na pengine ukawa ni mkasa mzuri sana kwani utakuwa umekamilika”
nilimwambia Rosine huku nikiendelea kuyatomasa taratibu matiti yake na
kwa mbali nilianza kumsikia akianza kuhema juu juu. Ukimya ukafuatia baina
yetu na wakati huo nilimuona Rosine akiishika mikono yangu kama anayetaka
kuitoa ili nisiendelee kuyatomasa matiti yake lakini hakuitoa na badala yake
nilimuona akijinyonganyonga taratibu pale kitandani.
“Patrick!”
“Naam”
“Nimetokea kukupenda sana Patrick usiniache popote utakapokwenda, sina
ndugu yoyote sasa na kuona wewe kama ndugu yangu pekee katika hii dunia”
Rosine aliniambia katika sauti nyepesi ya kike inayobembeleza.
“Vipi kuhusu mume na mtoto wako mchanga uliyemuacha ndani ya kabati
kule nyumbani? nilimuuliza huku nikiyakumbuka vizuri maelezo yake wakati
ule tulipokuwa kule pangoni na hapo nikamuona akiangua kicheko hafifu.
“Usinichekeshe mpenzi yaani kumbe uliniamini? Rosine aliongea huku aki?angua kicheko hafifu
“Sasa kwanini ulinidanganya? nilimuuliza kwa hasira kidogo.
“Nilipokuona kwa mara ya kwanza kule pangoni nilifahamu kuwa ulikuwa
mwanaume wa kazi na usingekubali kufa mle pangoni kama kondoo na nili?pojaribu kuchukunguza nyendo zako kwa muda mfupi tu nikafahamu kuwa
ulikuwa ukipiga mahesabu ya kutoroka”
“Lakini bado hujaniambia ni kipi hasa kilichokupelekea unidanganye kuwa una mtoto mchanga uliyemuacha nyumbani kabatini? nilimuuliza.
“Oh yes! unajua matendo yako tu mle pangoni yalinijulisha kuwa wewe
ni mtu mwenye utu na huruma sana hivyo nikajua endapo ningekudanganya
kuwa nilikuwa na mtoto mchanga niliyemuacha nyumbani kwangu kabatini
usingeweza kuniacha mle pangoni pale ambapo ungepata nafasi ya kutoro?ka na kweli hivyo si ndivyo ilivyokuwa” Rosine aliniambia huku akiangua
kicheko
“Kweli wewe ni msichana mjanja sana hivi unajua mpaka sasa nilikuwa
nikiamini kuwa una mtoto mchanga uliyemuacha kabatini na muda wote tu?lipokuwa kule pangoni nilikuwa nikiwaza nikusaidieje” nilimwambia Rosine
huku bado nikiutafakari ujanja wake, kweli alikuwa msichana mjanja sana
kwa kuweza kunihadaa kiasi kile.
“Wanaume wenye huruma siku zote wanaamini haraka maneno ya wana?wake” Rosine aliniambia huku akitabasamu.
“Nakupenda sana Patrick”
“Hata mimi nakupenda” nilimwambia na hapo akaishika mikono yangu na
kuanza kuipapasa taratibu kitendo hicho kikaanza kuamsha hisia za mapenzi
mwilini mwangu na hapo nikaanza kuhema bila utaratibu maalum. Mikono
yake laini na yenye joto ikaifanya damu yangu mwilini ianze kuchemka, moyo
nao ukaanza kunienda mbio huku hisia za mapenzi zikizidi kunilevya. Hata
hivyo katika hali ile ya udhaifu niliyokuwa nayo sikuweza kufanya chochote
kwani nilikuwa kama nyuki wa mashineni ambaye hurukaruka kwenye pumba
bila ya kumdhuru mchukuaji.
Kichwa bado kilikuwa kikiniuma na bado nilikuwa nakijihisi kizunguzun?gu. Katika safari zangu zote za kijasusi moja ya kanuni zangu ilikuwa ni ku?jitenga na wanawake huku nifahamu kuwa mara nyingi mapenzi uharibu kazi
lakini kwa mara ya kwanza mbele ya msichana huyu mzuri ajabu nilijikuta
nikianza kuipuuza dhana hiyo na kujiona nilikuwa nikikosea sana na pengine
dhana hiyo haikuwa ikifaa kuelekezwa kwa msichana kama huyu.
Nilikumbuka kuwa nilikuwa nimemdanyanga Jean Pierre Umugwaneza na
Jerome Muganza kule pangoni kuwa nilikuwa na mke na watoto lakini ukweli
ni kuwa sikuwa na mke wala mtoto na hiyo ilitokana na kuwa mimi nilikuwa
ni mtu wa safari nyingi za kikazi hivyo kuwa na mke niliona ni kama ningeku?wa simtendei haki mwanamke huyo pale endapo ningekuwa nikiondoka na
kumuacha kwa muda mrefu akikaa nyumbani peke yake na istoshe nilikuwa
sijampata hasa msichana wa aina yangu.
Nikaanza kuwaza maisha yangekuwaje endapo ningekuwa na mke kama
Rosine na watoto wetu, nikawa kama ninayeiona familia yetu namna ilivyo
na upendo, amani na furaha na hali hiyo ikanifanya nianze kutabasamu kama
mwehu. Hata hivyo tabasamu hilo liliyeyuka upesi pale nilipoanza kufikiria
safari iliyokuwa mbele yangu.
Niliyakatisha mawazo yangu baada kuhisi kuwa mikono ya Rosine ilikuwa
imeacha kunipapasa, nilipomtazama nikagundua kuwa alikuwa akipitiwa na
usingizi na hapo nikamsogeza vizuri na kumlaza pembeni yangu huku akiwa
tayari ameanza kukoroma kwa uchovu, nami nikajilaza pembeni nikikiegemeza kichwa changu kwenye mto wa kitanda.
Sikuweza kufahamu kuwa ule ulikuwa muda gani lakini nilikuwa na hakika
kuwa ilikuwa ikielekea usiku wa manane, mvua ilikuwa imepungua kidogo
na sasa kulikuwa na upepo mkali kiasi uliokuwa ukipenya dirishani bila ya
pingamizi na kuupelekea ule mwanga wa taa ya kandili iliyokuwa mle ndani
juu ya meza pembeni ya kitanda kuchezacheza.
Nilipowaza kuwa ingekuwa rahisi kwa mtu yeyote aliyeko nje kutuona
kupitia ule mwanga wa taa ya kandili mle ndani nikaamua kuisogeza ile taa
karibu yangu na kuizima. Giza likachukua nafasi mle ndani huku Rosine aki?wa amelala pembeni yangu na hapo nikajihisi ni kama tuliyekuwa kwenye
fungate katikati ya msitu wa kutisha usiokuwa na mwanzo wala mwisho na
viumbe pekee tukiwa ni sisi tu.
__________
JAPOKUWA NILIKUWA NA UCHOVU mwingi na maumivu makali
kichwani na begani lakini sikuthubutu kulala kwani usingizi ulikuwa mbali na
mimi vilevile nilijitahadharisha kuwa katika mazingira yasiyoeleweka kama
yale kulala ilikuwa ni sawa na kuikaribisha hatari. Niliamini kuwa ningeweza
kukaa usiku mzima bila ya kulala wala kusinzia hata mara moja huku nik?iendelea kayapangilia vizuri mawazo yangu kichwani juu ya safari yangu ya
kijasusi kwani nilikuwa na uzoefu huo.
Wakati fulani nilipokuwa katikati ya misitu ya Ikweta nchini Uganda waka?ti huo majeshi ya Tanzania yalipokuwa yakipigana na majeshi ya nduli Iddi
Amin Dada katika vita ya Kagera mimi nikiwa kama mdunguaji niliyekuwa
nikishika zamu ya usiku, nililazimika kujificha pasipo kutikisika hata kido?go juu ya mti mrefu wenye kichaka cha matawi makubwa usiku kucha bila
ya kulala huku muda wote macho yangu yakiwa makini kutazama ongezeko
lolote la kitu au kiumbe katika usawa wa macho yangu na wakati huohuo
bunduki yangu nikiwa nimeitega vizuri kwenye tawi la mti na radio yangu
ya upepo ikiwa mkononi. Ilikuwa ni kazi ya kuchosha sana inayohitaji moyo
wa uvumilivu kukabiliana na mvua, upepo mkali, baridi kama siyo majoka
makubwa ya msituni yaliyokuwa yakimangamanga.
Rekodi yangu ya shabaha ilikuwa bado inaridhisha na mara chache sana adui
alifanikiwa kunitoroka mara baada ya kumona nikiwa katika maficho yangu
kwani nilikuwa stadi sana katika kulenga shabaha kwa vitu vinavyotembea au
kukimbia. Niliwakumbuka makomandoo wanne wa jeshi la Iddi Amin Dada
ambao niliwachakaza vibaya kwa risasi mmoja baada ya mwingine bila ya
wao kujua usiku mmoja wakati walipokuwa wakiinyemelea kambi yetu tara?tibu kuja kuipeleleza.
Nikiwa juu ya mti mmoja mrefu ilinichukua muda mfupi sana kwa msaada
wa darubini yangu ya kijeshi yenye nguvu aina ya Galilean niliweza kugun?dua kuwa vichaka vinne vilivyokuwa zaidi ya umbali wa mita mia tatu mbele
yangu vilikuwa vikihama taratibu na kusimama katika uwiano wa hatua tano
kila baada ya muda mfupi kuikaribi kambi yetu. Kama desturi ya komandoo
aliyefuzu vizuri katika medani ya vita ya msituni nilichukua muda mfupi tu kugundua kuwa vile havikuwa vichaka bali ni maadui wanne waliojipamba
vizuri kwa majani na matawi ya miti ili askari wetu yeyote awaamini kuwa
vile vilikuwa ni vichaka vya miti ya porini.
Nikiwa nimewashtukia maadui wale nikaanza kuwapunguza mmoja baada
ya mwingine kwa bunduki yangu yenye kiwambo cha kuzuia sauti huku niki?anza na yule wa nyuma na hatimaye kuwamaliza wote.
Niligeuka tena kumtazama Rosine aliyekuwa pembeni yangu nikamuona
kuwa tayari alikuwa amezama kwenye usingizi mzito wa kisawasawa na kwa
mbali niliendelea kuisikia mikoromo yake hafifu ya usingizi ingawaje sauti
hiyo ya mikoromo iliendelea kuingiliana na ile sauti ya manyunyu ya mvua
iliyokuwa ikiendelea kuanguka katika msitu ule. Msitu wote ulikuwa umegu?bikwa na ukimya wa kipekee na wala sikuweza kukisia kuwa muda ule uliku?wa saa ngapi.
Nilikuwa nikielekea kutongozwa na usingizi hafifu wakati niliposhtushwa
na makelele ya bawaba kavu za mlango uliokuwa ukifunguliwa. Nilishtuka
na kuyatega vizuri masikio yangu huku macho yangu yakisafiri kutazama ule
mlango wa kuingia mle chumbani. Sikuona mjongeo wa kitu chochote eneo
lile ingawaje moyo wangu ulikuwa tayari umepoteza utulivu ukienda mbio
kwa hofu na huku nikihisi baridi nyepesi ikisafiri nyuma ya shingo yangu.
Ghafla zile kelele za bawaba za mlango uliokuwa ukifunguliwa zilikoma
na hapo nikajua ulikuwa ni mlango mwingine wa mle ndani ya ile nyumba
uliokuwa ukifunguliwa. Hali hiyo ikanipelekea nimkumbuke yule mwenyeji
wetu huku nikiwaza kuwa huenda alikuwa akitoka kwani alikuwa alimetu?ambia kuwa angeamka usiku ule ili aende kuwinda. Bado nilikuwa simwamini
na nilikuwa na mashaka naye hivyo zile dalili za usingizi nyemelezi zilini?toweka kabisa na sasa nikawa naanza kuwaza namna ya kujihami endapo yule
mtu angetufanyia uvamizi wa namna yoyote mle ndani ingawaje nilihisi mwili
wangu kuwa bado ulikuwa dhaifu kutoka na yale majeraha mwilini.
Nikiwa nimeyatega vizuri masikio yangu mara baada ya makelele ya ule
mlango uliokuwa ukifunguliwa kukoma nilianza kuzisikia hatua ya mtu ali?yekuwa akitembea taratibu na kwa tahadhari kuukaribia mlango wa chumba
chetu. Moyo wangu ukasimama kidogo kwa sekunde kadhaa kisha ukaanza
kwenda mbio na hapo nikaanza kushawishika kuwa nimwamshe Rosine ali?yekuwa bado akiendelea kuuchapa usingizi kando yangu pale kitandani kwa
kadiri zile hatua za yule mtu zilivyokuwa zikisogea kuukaribia ule mlango wa
chumba chetu.
Akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka nikifikiria nini cha kufanya endapo
tungekuwa tukivamiwa na wakati nikiendelea kujipanga lile wazo la kumwam?sha Rosine nikajikuta nikiweka kando baada ya kuliona kuwa lisingekuwa
na tija sana kwani endapo ningemwamsha kwa kumshtua uzingizini pengine
angeamka akiwa na hofu kubwa zaidi yangu au pengine angepatwa na msh?tuko wa kipekee ambao ungeweza kumshtua na yule mtu na hivyo kuharibu
mikakati yangu ya namna ya kujihami hivyo namna pekee iliyobaki ilikuwa
ni kusubiri kwanza.
Muda mfupi baadaye ile sauti ya hatua za mtu anayetembea ziliishilia umbali mfupi nje ya chumba chetu kisha kukafuatiwa na ukimya na hali hiyo ikazidi kuniongezea hofu na hofu yangu hasa ilizidishwa na ile hali ya udhai?fu wa mwili wangu wa kuwa tayari kukabiliana na umbushi yoyote ambayo ingejitokeza mle ndani. Wakati nikiwa naendelea kuwaza mara niliuona ule
mlango wa kile chumba chetu ukisukumwa taratibu katika ufundi wa kipekee
ili kuuzuia usitoe sauti. Kufumba na kufumbua nikawa nimejilaza chali pale kitandani nikijidai kupitiwa na usingizi.Mlango wa chumba ulipofunguliwa nilimuona mtu mrefu akiingia mle ndani taratibu na kwa tahadhari ya hali ya juu kama mtu anayekwepa kumshitua mtu
yoyote mle ndani na hapo nikagundua kuwa alikuwa ni yule mwenyeji wetu
na ile bunduki yake wakati huu alikuwa ameining’iniza begani na mkononi
alikuwa ameshika panga lililonolewa vizuri kiasi cha kulifanya lionekane kwa mng’aro wa kipekee katikati ya giza la mle ndani. Wasiwasi ukanishika sana kwani sikuweza kuelewa kuwa yule mtu alikuwa na malengo gani na lile pan?ga mkononi hata hivyo niliendelea kutulia pale kitandani huku nikiendelea kumtazama kwa siri yule mtu.
Mara baada ya yule mtu kuingia mle ndani alisimama pale mlangoni aki?tutazama pale kitandani tulipolala na wakati akiendelea kututazama nilihisi ni kama aliyekuwa akiyaona mapigo ya moyo wangu na wasiwasi niliokuwa nao, kwa kweli sikuweza kufahamu kuwa mtu yule alikuwa akitaka kutufanya nini.
Yule mtu aliendelea kusimama kwa kitambo pale mlangoni huku akituzama
kisha nikamuona akilichomoa lile panga ndani ya koti lake refu. Kitendo kile
kikanifanya nizidi kushikwa na wasiwasi.
Kilipita kitambo kifupi yule mtu akiendelea kututazama pale kitandani ki?sha akageuka na kuondoka na hapo nikazisikia hatua zake zikiyoyoma taratibu
kabla ya kuusikia ule mlango wa chumba chetu ukifungwa. Muda mfupi ulio?fuata nilisikia tena mlango mwingine wa ile nyumba ukifunguliwa na kufung?wa halafu sikusikia tena ile sauti ya hatua za yule mtu wala hisia za uwepo
wa kiumbe chochote mle ndani zaidi yetu. Nikajua kuwa yule mtu alikuwa
ametoka nje.
Nikiwa nimelala pale kitandani huku hofu imenitawala nilisubiri muda upite
kidogo ili nijihakikishie kuwa yule mtu asingeweza kurudi tena kisha nikaanza
kushuka pale kitandani taratibu nikikwepa kumshtua Rosine aliyekuwa bado
akiendelea kuuchapa usingizi pale kitandani. Wakati nikisimama nilisikia
maumivu makali sana kichwani nikawa nahisi kama ninayetaka kutapika huku
damu yangu yote mwilini ni kama iliyokuwa ikikimbilia kichwani hali iliy?onipelekea nihisi kizunguzungu.
Ukweli ni kwamba afya yangu bado ilikuwa hairidhishi hata hivyo sikurudi
tena pale kitandani badala yake nilikiacha kile kitanda na kusimama na hapo
nusura nipige mwereka kwa kizunguzungu lakini niliwahi kujizuia nisianguke
chini kwa kushika ukuta wa chumba kile. Niliendelea kusimama pale ukutani
hadi pale nilipoona kichwa changu kimeanza kupata utulivu wa kiasi ndiyo
nikaanza kuzitupa hatua zangu dhaifu taratibu kuelekea mahali lilipokuwa
dirisha la chumba kile. Niligundua kuwa mwili wangu bado ulikuwa dhaifu
na hivyo kutembea isingekuwa kazi rahisi kwani mpaka kufika pale dirishani nilikuwa nimechoka sana.
Nikiwa pale dirishani nililisogeza lile pazia pembeni ili niweze kutazma
nje. Nje ya upande ule wa dirisha lilikuwa ni eneo lililozungukwa kwa vicha?ka na miti mikubwa na mirefu iliyotengeneza vivuli vikubwa vinavyotisha.
Mazingira yenyewe yalijieleza kuwa hayakuwa rafiki kwa binadamu ingawaje
kulikuwa na kila dalili kuwa binadamu fulani waliwahi kuishi eneo lile wakati
fulani huko nyuma. Yalikuwa ni mazingira mapya kabisa kwangu na yasiyofa?nana na kokote nilikowahi kupita. Nyasi zilikuwa zimeota hadi pale dirishani.
Nikiwa bado nimesimama pale dirishani macho yangu yalitumia muda mfupi
kulizoea lile giza la nje na wakati huohuo yakifanyakazi ya ziada kulichungu?za eneo lile.
Mvua ilikuwa imepungua sana na kwa mbali manyunyu hafifu yalisikika
yakianguka juu ya paa la nyumba ile. Upepo ulikuwa umeongezeka na kuyafa?nya matawi ya miti ile mikubwa mle msituni kuyumbishwa kila mara na hata
zile sauti kali za radi wakati huu zilikuwa zimepungua sana ingawaje ule
mwanga wa radi ulikuwa ikiendelea kumulika mara kwa mara mle msituni.
Muda kidogo ulikuwa umepita tangu yule mwenyeji wetu alipotoka nje
wakati mwanga mkali wa radi ulipomulika kwa ghafla na kulifanya eneo lile
lote la msitu ligeuke mchana kwa muda. Nikiwa bado nimesimama pale di?rishani nikitazama nje ule mwanga wa radi ukanifanya niweze kuona vizuri
mbele yangu na nilichokiona kilinishtua.
Niliwaona watu sita waliokuwa wamesimama nje ya mti mmoja mkubwa
uliokuwa mbele yangu usawa wa dirisha lile kati ya ile miti mikubwa min?gi iliyoizunguka ile nyumba. Sikuwa na mashaka kuwa wale watu walikuwa
ni wanajeshi kutokana na mavazi ya makoti marefu ya kijeshi waliyoyavaa
kujikinga na mvua na wote walikuwa na bunduki zao begani. Nilishtuka na
kujihisi ni kama niliyepigwa na maradhi ya kiharusi kwa muda mfupi kwani
sasa nilijua safari hii ndiyo ungekuwa mwisho wangu wa kuwakimbia wale
wanajeshi kama wangeshtukia kuwa mimi nilikuwa pale.
Nilifahamu fika kuwa mwili wangu bado ulikuwa dhaifu kukabiliana na
purukushani yoyote kwa wakati ule. Nilikuwa bado nikifikiria nini cha ku?fanya wakati nilipomuona mtu fulani akitoka katika usawa wa ile nyumba
tuliyokuwepo na kukatisha kichakani kuwaendea wale wanajeshi sita walio?kuwa wamesimama chini ya ule mti mkubwa nje ya ile nyumba. Nikajua kwa
vyovyote mtu yule alikuwa ni yule mwenyeji wetu na hapo nikahisi koo langu
likikauka ghafla pale nilipoanza kuhisi kuwa huenda yule mwenyeji wetu ali?kuwa amepanga kutuuza kwa wale wanajeshi.
Hisia hizo kadiri zilivyokuwa zikiendelea kupenya kwenye moyo wangu
zikanipelekea nianze kushikwa na kihoro na hapo nikageuka haraka kumtaza?ma Rosine pale kitandani alipolala. Nikamuona kuwa bado alikuwa akiende?lea kuuchapa usingizi. Sasa nilichokuwa nikikifikiria ilikuwa ni kumwamsha
Rosine ili tutoroke kabla ya wale wanajeshi hawajatufikia.
Lakini kabla sijafanya hivyo niligeuka tena kutazama kwenye ule mti am?bapo wale wanajeshi walikuwa wamesimama chini yake na kuwafanya wa?onekane kama vichungu virefu vya porini vilivyotelekezwa na mchwa. Lakini safari hii ule mwanga wa radi haukurudi kwa haraka hivyo nililazimika kuu?subiri ili niweze kuona tena chini ya mti ule. Kilipita kitambo kifupi nikiende?lea kusubiri pale na ule mwanga wa radi ulipomulika kwa mara nyingine tena
vile vichuguu vilikwisha toweka eneo lile.
__________
KWA SEKUNDE KADHAA NILIBAKI NIMESIMAMA PALE DIRISH?ANI huku nikijiuliza kuwa yale matukio niliyokuwa nikiyaona yalikuwa halisi
au lilikuwa ni jinamizi lililokuwa likizitongoza fikra zangu. Hisia zilizokuwa
zimejengeka kichwani mwangu ni kuwa yule mwenyeji wetu tuliyemfahamu
kwa jina la Innocent Gahizi sasa alikuwa akipanga njama za kutuuza kwa wale
askari wa Kanali Bosco Rutaganda hivyo endapo tungeendelea kuzubaa mle
ndani ingekuwa ni sawa na kutoa nafasi ya biashara hiyo kufanyika kwa uhuru
na mipango ya hali ya juu na kupelekea tukamatwe kiulaini huku tukiwa tume?kumbatiana pale kitandani. Hisia zangu zilinieleza kuwa muda wa kuendelea
kukaa mle ndani ulikuwa umekwisha hivyo safari ya kutoka kwenye ile nyum?ba ilikuwa ni lazima ifanyike usiku uleule mapema iwezekanavyo.
Nikiwa tayari nimeshapitisha wazo la kutoroka kwenye ile nyumba usiku
ule nilisubiri kidogo mwanga wa radi umulike tena pale chini ya ule mti wa?lipokuwepo wale wanajeshi sita ili nijiridhishe kuwa hawakuwepo kisha nik?ageuka na kuanza kuelekea kilipo kile kitanda alicholala Rosine. Rosine bado
alikuwa akiendelea kuuchapa usingizi na nilipomtazama nilimhurumia sana
kwani nilifahamu fika kuwa starehe ya usingizi wake ilikuwa mbioni kuo?ta mbawa na sehemu yake ingefuatiwa na mikikimikiki ya ukimbiaji katika
mapori, vichana na misitu. Safari ambayo mpaka sasa sikuifahamu mwisho
wake ungekuwaje.
Lakini kabla sijakifikia kile kitanda na kumwamsha Rosine nilikumbuka
kuwa kuna kitu kimoja muhimu nilichokihitaji kabla ya kuitoroka nyumba ile.
Niliona kuwa ilikuwa ni muhimu kufanya upekuzi katika nyumba ile kabla
hatujatoroka na kilichokuwa kikinisukuma kutaka kufanya hivyo ni kutokana
na tabia zisizoeleweka za yule mwenyeji wetu. Usiku ukiwa tayari umeshamiri
sauti pekee zilizokuwa zikisikika katika msitu ule zilikuwa ni sauti za bundi
zilizokuwa zikihanikiza huku na kule na kwa kiasi fulani zilinitia hofu lakini
nafsi yangu ilizidi kuniononya kuwa hatima yangu ingetokana na maamuzi
yangu ya haraka.
Wakati nilipokifikia kile kitanda nilipata wazo jipya kuwa nisimwamshe
kwanza Rosine na badala yake ningefanya hivyo baada ya kumaliza kufan?ya upekuzi mle ndani. Hivyo nilimwacha Rosine akiwa anaendelea kuuchapa
usingizi pale kitandani kisha taratibu nikakatisha katikati ya kile chumba ni?kiliendea dirisha jingine la upande wa pili wa chumba kile ambapo nilipofi?ka nililisogeza pazia na kuchungulia ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na mtu
yoyote upande ule. Hali bado ilikuwa tulivu na ule mwanga wa radi ulikuwa
ukiendelea kumulika kwa nyakati tofauti katika msitu ule sambamba na upepo
wa hapa na pale.
Nililirudishia lile pazia pale dirishani kisha nikageuka na kuufuata ule mlango wa kuingilia mle chumbani ambapo niliufungua taratibu kwa ufundi wa
hali ya juu ili usipige kelele. Upande wa pili nikatokezea kwenye chumba
kingine ambacho kwa haraka nilipokitazama nilikifananisha na sebule isiy?okuwa na kitu chochote zaidi ya kochi moja la mbao lisilokuwa na foronya,
mtungi mmoja wa gesi uliokuwa kwenye kona ambapo nilipoufikia na kuu?tikisa niligunduwa kuwa haukuwa na gesi, na kabati moja kuukuu lililokuwa
pembeni ya mlango wa kutokea nje.
Upande wa kushoto sebule ile ilitazamana na milango miwili mikubwa ya
mbao na nilipogeuka kuitazama milango ile kwa makini nikagundua kuwa
mlango mmoja ulikuwa umefunguliwa kidogo, nikahisi kuwa huenda ule un?gekuwa ni mlango wa kile chumba alichokuwa amelala yule mwenyeji wetu.
Kwenye pembeni ya chumba kile kilichokuwa wazi nilipotazama vizuri niku?gundua kuwa kulikuwa na korido ielekeayo upande wa kushoto.
Nilianza kunyata nikiifuata ile korido huku nikijaribu kulizoea giza la mle
ndani. Mwisho wa korido ile nilikutana na mlango uliofungwa, nilipoufikia
nilisimama na kusikiliza kama kulikuwa na sauti ya kiumbe chochote ndani
ya chumba kile. Sikusikia chochote hivyo hali bado ilikuwa tulivu na salama
na hapo nikashika kitasa cha mlango ule na kuusukuma. Mlango ulifunguka
bila ubishi wowote hivyo nikaingia taratibu huku nikiyaandaa macho yangu
kukabiliana na giza la mle ndani lakini hali ilikuwa tofauti.
Mle ndani ya kile chumba kulikuwa na dirisha upande wa kulia ambalo
wakati ule lilikuwa wazi hivyo ule mwanga wa radi kule nje ulikuwa ukipenya
bila ya pingamizi na kupitia mwanga ule nikapata nafasi ya kuona mle ndani.
Mle ndani kulikuwa na vyumba viwili, chumba kimoja kilikuwa upande wa
mbele kikitazamana na ule mlango wa kuingilia.
Nilisimama nikikitazama chumba kile ambacho sasa nilikigundua kuwa ki?likuwa chumba kilichotumika kama jiko kwani mle ndani niliiona mitungi
mingine miwili ya gesi inayofanana na ule niliouona kule sebuleni. Pia kuliku?wa na karo la kuoshea vyombo pamoja na kabati la fomeka lililotengenezwa
vizuri ukutani.
Juu ya kabati lile nilikiona kisanduku kidogo cha huduma ya kwanza kili?chokuwa kikimetameta kutokana na ile alama nyeupe ya msalaba juu ya ki?sanduku hicho kuakisi vizuri gizani. Nilisimama nikayapitisha macho yangu
katika chumba kile nikichunguza kila kitu kilichokuwa mle ndani ambacho
kwa hakika kilifanana na jiko lile. Madirisha mawili ya chumba kile yaliku?wa wazi na niliweza kuusikia upepo mkali ukipenya kwenye madirisha yale
kuingia mle ndani.
Nikiwa nafahamu kuwa muda haukuwa rafiki sana kwangu nilimalizia kwa
kuyapitisha haraka macho yangu katika chumba kile na kukiacha baada ya
kukiona kuwa kisingekuwa na kitu chochote cha maana kwangu. Nilikifuata
kile chumba kingine cha pembeni kilichokuwa kiasi cha umbali wa hatua nne
upande wa kulia kwangu. Wakati nikikiendea kile chumba nikajikuta nikim?kumbuka Rosine kuwa endapo angeamka na kujikuta peke yake kule chumba?ni angekuwa katika hali gani.
Niliufikia mlango wa chumba kile kingine na kuusukuma taratibu na kwa
KEVIN e. MPONDA TAI KWENYE MZOGA I 167
tahadhari, mlango ulipofunguka niliweza kuona mle ndani kupitia mwanga
hafifu wa radi uliokuwa ukipenya kupitia dirisha dogo la chumba kile. Kili?kuwa chumba kidogo na nilipokichunguza vizuri niligundua kuwa kilikuwa ni
chumba cha maliwato hivyo sikuendelea kupoteza muda wangu, nikakiacha
kile chumba na kuuendea ule mlango wa kutokea nje.
Wakati nilipoufungua ule mlango wa kutokea kwenye lile korido mwanga
mkali wa radi ulipenya madirisha na kumulika mle ndani na hivyo kulifanya
eneo lile ligeuke mchana kwa muda. Moyo wangu ulipiga kite kwa nguvu
na hofu ilinishika pale nilipomkumbuka yule mwenyeji wetu, sikuweza kujua
kuwa angerudi baada ya muda gani huko alipokwenda lakini sikutaka atukute
mle ndani kwani nilikuwa na hakika kuwa huo ndiyo ungekuwa mwisho wetu.
Nilipomaliza kuipita ile korido nikawa nimerudi na kutokezea tena kule se?buleni na hapo nilisimama kidogo na kuutazama ule mlango wa chumba chetu
ambacho nilikuwa nimemwacha Rosine akiwa amelala. Ule mlango ulikuwa
vilevile na sikusikia wala kuona dalili zozote za kuamka kwa Rosine hivyo
niliendelea na harakati zangu. Sasa nilibakisha kufanya upekuzi katika vile
vyumba viwili vilivyotazamana na ile sebule ambapo kile chumba kimoja ki?likuwa wazi.
Moyo wangu ulianza tena kwenda mbio wakati nilipokuwa nikikikaribia
chumba kile kilichoelekea kuwa cha yule mwenyeji wetu ambaye hadi wakati
huu nilikuwa na hakika kuwa lile jina la Inoccent Gahizi alikuwa amejipachika
tu kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.
Mlango wa chumba kile ulikuwa wazi hivyo nilifanya jitihada kidogo za
kuusukuma kisha nikaingia ndani. Kwa muda mfupi tu baada ya kuingia mle
ndani pua yangu ilijikuta ikikabiliana na harufu kali ya moshi wa sigara ulio?onekana kukizoea kwa muda mrefu chumba kile pamoja na harufu ya jasho la
mwanaume iliyosambaa mle ndani.
Nilisimama kidogo nikiyatembeza macho yangu mle ndani ya kile chum?ba, kilikuwa chumba kikubwa cha wastani chenye godoro kubwa lililolazwa
sakafuni na pembeni ya godoro lile kulikuwa na kibakuli cha majivu ya sigara
ambacho kilikuwa kimejaa majivu hayo na vipisi vingi vya sigara.
Niliendelea kulitazama eneo lile na kuona chupa mbili za pombe kali ziliz?oisha zikiwa zimetelekezwa kwenye kona ya chumba kile. Mbali na hayo ku?likuwa na nguo zilizokuwa zimening’inizwa nyuma ya mlango wa chumba
kile zaidi ya hapo chumba kile hakikuwa na kitu kingine chochote cha maana.
Niliupisha utulivu kichwani mwangu huku nikijihisi kujichosha kwa kufanya
upekuzi usiokuwa na tija yoyote.
Sasa nilikuwa nimebakisha kufanya upekuzi katika chumba kimoja tu kati?ka nyumba ile na chumba hicho ndiyo kile cha jirani kilichokuwa kimefung?wa. Lakini kabla ya kutoka mle ndani kwenye kona ya chumba kile niliona
jozi moja ya viatu vya ngozi ambayo vilinivutia kwani zile buti zangu mgu?uni zilikuwa mbioni kuvunda kwa unyevunyevu wa yale maji ya kule mtoni
wakati ule tulipokuwa tukitoroka kule mapangoni hivyo nikaamua nichague
kwanza nguo zilizonitosha kutoka katika zile nguo zilizoning’inizwa nyuma
ya ule mlango wa kile chumba.
Nilipata fulana moja ya rangi ya kijani na suruali moja nyeusi ya kadeti
na zile nguo zilionekana kunitosha vizuri kwa kuwa yule mwenyeji wetu tu?lielekea kulingana kwa umbo. Zile nguo nyingine nilizokuwa nimezivaa hapo
awali nilizivua na kuzitelekeza kisha nikavaa zile nguo nyingine na nilipomal?iza nikavaa na zile buti za ngozi ambazo nazo zilinienea vizuri na kunifanya
nijione nimekamilika kuanza safari muda wowote.
Sasa nilikuwa tayari kukiacha kile chumba huku nikiwa sijapata chochote
cha maana lakini kabla ya kufanya hivyo nikakumbuka kuwa kulikuwa na seh?emu moja ambayo nilikuwa sijaifanyia upekuzi. Sehemu hiyo ilikuwa ni chini
ya lile godoro la mle ndani. Hivyo nililisogelea lile godoro na kulinyanyua na
hapo niliviona vitu viwili vilivyonivutia na kunifanya kwa mara ya kwanza
nijipongeze kwa udadisi wangu.
Kulikuwa na bahasha ndogo ya kaki iliyotuna kiasi na pembeni ya bahasha
hiyo kulikuwa na bastola, bila ya kupoteza muda niliinama nikaichukua ile
bahasha na kuitia mfukoni. Nilipoichunguza ile bastola nikaitambua kuwa ili?kuwa ni bastola aina ya 25 Revolver na ilikuwa imejazwa risasi.
Niliitazama tena ile bastola na kuiona kama tumaini langu pekee ambalo lin?genisaidia mbele ya safari kwani sikuwa na silaha nyingine yoyote tangu mara
ya mwisho nilipojipigiza kichwa kule mtoni na fahamu kunipotea. Bila ya
kupoteza muda nikaupandisha mguu mmoja wa suruali yangu na kuichomeka
ile bastola mguuni kisha nikalirudisha lile godoro mahala pake na hapo nikaf?ungua mlango wa kile chumba na kutoka nje.
Chumba kilichofuata kilikuwa hatua chache jirani ya kile cha awali na waka?ti nikikikaribia kile chumba nilihisi mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakien?da mbio sana hata hivyo bado nilikuwa nikihitajika kufanya upelelezi ndani ya
nyumba kile. Mlango wa kile chumba cha pili ulikuwa imara na kimya kama
uliokufa na hali hiyo ilinipa hisia kuwa haukuwa mlango uliokuwa ukifungwa
na kufunguliwa mara kwa mara kwani hata kitasa chake nilipokishika kiliku?wa kimetapakaa vumbi kila mahali.
Nilipojaribu kuusukuma ule mlango niligundua kuwa ulikuwa umefungwa
na jambo hilo likanikosesha furaha kiasi kwani sikujua kuwa ningetumia muda
gani kuufungua mlango ule hata hivyo sikuwa na namna yoyote ya kuendelea
kusubiri kwani muda haukuwa rafiki kwangu.
Nilizunguka mle ndani na kufanikiwa kupata kipande kidogo cha nyaya ng?umu ambacho nilirudi nacho pale mlangoni na kuanza kuchokoa kile kitasa
na ndani ya muda mfupi tu kile kitasa kilifyatuka na hapo nikausukuma ule
mlango. Haikuwa kazi rahisi kwani ule mlango ulikuwa mgumu kutokana na
kutofunguliwa mara kwa mara hata hivyo kwa jitihada zangu hatimaye nili?fanikiwa kuusukuma na kuingia ndani.
Chumba kilikuwa na giza na chenye hewa nzito na madirisha yake yote
yalikuwa yamefungwa. Mara baada ya kuingia mle ndani nilisimama pale
mlangoni nikijaribu kulizoea lile giza la mle ndani ambalo hata hivyo nilikub?ali kuwa lilikuwa giza lisilozoeleka kwa urahisi kisha nikaufunga ule mlango
nyuma yangu. Nilipotulia na kuchunguza vizuri hakuna chochote nilichokiona
mbele yangu na mara moja au mbili nilizisikia kelele za panya waliokuwa wakihangaika ovyo kuukimbia ugeni wangu. Moyo wangu ulikuwa ukienda
mbio na hata miguu yangu nilihisi ilikuwa mizito kuruhusu hatua zangu ku?endelea mbele.
Kabla ya kuendelea mbele zaidi nilisimama kidogo kuusikiliza utulivu wa
mle ndani na hapo nikagundua kuwa zile kelele za wale panya waliokuwa
wakikimbia huku na kule sasa zilikuwa zimefikia ukomo, pengine walikuwa
wamejibanza mahala fulani wakinitazama kwa udadisi. Wakati huu mawazo
juu ya Rosine niliyemuacha kule chumbani yalipita tena kichwani mwangu na
hapo nikaanza kuhisi kuwa nilikuwa nikifanya makosa kwa kutomshtua na ku?mueleza kuwa alitakiwa akae tayari, vipi angeshtuka na kutoniona mle ndani,
ni hisia gani angekuwa nazo?. Nilijiuliza bila kupata majibu na hali hiyo ika?nipelekea kuharakisha udadisi wangu japokuwa kwa giza zito lililokuwa mle
ndani nilifahamu kuwa isingekuwa kazi rahisi kama nilivyodhani.
Niliunyanyua mguu wangu nikitupa hatua taratibu kuelekea mbele na kwa
tahadhari niliipeleka mikono yangu huku na kule nikipapasa. Nilipoyatega
vizuri masikio yangu mle ndani wakati huu niligundua kuwa chumba kile kili?kuwa kimegubikwa na ukimya zaidi na sauti pekee iliyokuwa ikipenya masiki?oni mwangu ilikuwa ni sauti kavu ya hatua zangu sakafuni. Ni kama niliyeku?wa nikitembea kuelekea nisikokufahamu kwani giza la mle ndani lilikuwa zito
mno hata hivyo kwa kuwa nilikuwa jasusi na komandoo niliyekubuhu vizuri
katika medani hizo niliiruhusu milango yangu ya fahamu kuanza kufanya kazi,
macho yangu yalitazama mbele yakijaribu kutengeneza hisia ya picha yoyote
mbele yangu.
Mikono yangu iliendelea kupapasa huku pua yangu ikijitahidi kunusa waka?ti huo ngozi yangu mwilini ikifanya kazi moja tu ya kuhisi mabadiliko yoy?ote ya hali ya hewa ya mle ndani na sasa nilikuwa nikitembea taratibu kama
ninayeogopa kukanyaga ardhi. Kwa muda mrefu nilijikuta nikipambana na
hisia mbaya moyoni mwangu kila nilipoyakumbuka yale majoka niliyokuwa
nikipambana nayo kule kwenye yale mapango ya Musanze. Hata hivyo kwa
kiasi fulani hisia hizo nilifanikiwa kuzifukuza nikautuliza mtima wangu inga?waje hofu bado haikuniacha.
Nilikuwa nimesafiri umbali wa hatua tano na zaidi katika chumba kile pale
nilipojigonga kwenye kitu fulani mbele yangu. Moyo wangu ukalipuka ghafla
kwa hofu hata hivyo nilijitahidi kutulia huku mapigo yangu ya moyo bado
yakienda mbio. Baada ya kusimama na kutulia sikuweza kusikia sauti ya kitu
chochote zaidi ya mapigo yangu ya moyo yaliyokuwa yakiniponyoka kiny?wani bila pingamizi, hatimaye nikairuhusu mikono yangu kuanza kupapasa
kile kitu nilichojigonga.
Hisia za haraka zilizoumbika kichwani mwangu ni kuwa nilikuwa nime?jigonga kwenye kiti na baada ya udadisi zaidi nikagundua kiti kile kilikuwa
kimeizunguka meza ndefu iliyokuwa mle ndani. Nikaendelea kuzitupa hatua
zangu taratibu nikiufuata usawa ule wa kile kiti na mbele kidogo nikagundua
kuwa kulikuwa na viti vingine vilivyopangwa pembeni kuizunguka ile meza.
Nilipomaliza kuzunguka huku nikipapasa nikagundua kuwa nilikuwa nime?papasa idadi ya viti kumi na mbili katika meza moja ndefu ya ofisini, viti vitano vikitazamana na vingine vitano kwa upande wa pili na viti viwili vilivyosa?lia kimoja kilikuwa mwanzo wa meza na kingine mwisho wa meza ile katika
mtindo wa kutazamana. Nilipoendelea kupapasa juu ya meza ile niligundua
kuwa hapakuwa na kitu chochote isipokuwa taa moja ya kandili na kiberiti
kimoja kulichokuwa kimehifadhiwa pembeni yake.
Nilisimama nikitafakari huku nikishindwa kuelewa meza ile yenye viti
kumi na mbili iliwekwa mle ndani kwa ajili gani. Ilikuwa ni meza inayofanana
kwa kila namna na meza zitumikazo kwenye mikutano mikubwa ya kiofisi
hivyo ile ilimaanisha kuwa kulikuwa na mikutano iliyokuwa ikifanyika ndani
ya chumba kile, na mikutano hiyo ilikuwa na siri gani hadi ifanyike katika
nyumba hii pekee iliyopo katikati ya msitu kama huu?. Nilijiuliza maswali
mengi kichwani mwangu na hakuna hata moja nilililoweza kulijibu.
Moyo wangu ulikuwa ukienda mbio sana isivyokawaida huku nikimeza
mate kulainisha koo langu lililokuwa mbioni kukauka kwa hofu. Nilikuwa
naendelea kupambana na hisia mbaya za mle ndani na fikra zangu zilikuwa
zikienda mbali sana na kwa mara ya kwanza nilihisi kama niliyekuwa mgeni
katika sayari mpya isiyokuwa na binadamu yoyote. Na kama si manyunyu
makali ya mvua kubwa iliyoanza ghafla kuanguka juu ya paa la nyumba ile
ningekuwa nikiendelea kutokomea katika sayari hiyo bila kujielewa.
Mawazo yangu yaliporudi mle ndani nikagundua kuwa nilikuwa nikitawa?liwa na hisia zaidi kuliko uhalisi wa mambo yalivyokuwa hivyo nikaamua
kuendelea zaidi na udadasi wangu. Nikaiacha ile meza nikiutafuta ukuta wa
kile chumba na baada ya kupapasa papasa nikawa nimeupata. Sasa nikawa ni?kiambaa na ukuta ule huku nikijaribu kuchunguza kama kulikuwa na chumba
chochote kingine kilichopakana na chumba kile.
Nilikuwa nimepapasa kiasi cha kukata tamaa pale mkono wangu ulipo?fanikiwa kukishika kitasa cha mlango, nilipozidi kupapasa nikagundua kuwa
mlango ule ulikuwa mfupi tofauti na ule wa mwanzo yaani hata kama ningeu?fungua namna ya kuingia ningelazimika kuinama kwanza.
Nilikuwa nikijiandaa kuusukuma mlango ule mfupi ili niingie mle ndani
ya kile chumba wakati nilipojikuta ghafla nikisita kufanya hivyo. Hisia mbaya
zilikuwa zimenijia kwa haraka sana kiasi kwamba niliuhisi moyo wangu kama
uliokuwa umesimama kwa sekunde kadhaa huku baridi nyepesi ikipenya
mgongoni sambamba na mikono yangu kuanza kutetemeka. Nilifahamu kuwa
huu haukuwa uwongo bali hisia za kweli ingawaje ukweli huo sikuwa na haki?ka nao.
Miguu yangu ilijikuta ikishindwa kuendelea mbele hivyo nikabaki nimesi?mama huku hofu imenitawala. Kwa hisia sizizo rasmi niliweza kuhisi kuwa ki?asi cha umbali wa hatua chache nyuma yangu kulikuwa na kiumbe kilichoku?wa kimesimama kikinitazama na hapo niligeuka taratibu nikitazama kule
nyuma huku nikipiga mahesabu juu ya muda ambao ningeutumia kuichomoa
bastola yangu toka mguuni nilipoisunda. Nilikuwa sahihi lakini sikufanikiwa
kwani muda uleule sauti kavu yenye hakika ilinionya
“Tulia hivyo hivyo Bolos huu ndiyo mwisho wako” ilikuwa ni sauti iliy?onionya kwa hakika na iliyokuwa mbali na mzaha huku ikiniacha katikati ya mduwao. Nilikuwa sahihi kabisa kwa kuhisi kuwa nyuma yangu kulikuwa na
kiumbe hai, binadamu ambaye ndiye huyu sasa anayeniita mimi Bolos bila ya
kufanya utafiti wa kutosha.
Sauti ya mtu yule ilikuwa ngeni kabisa masikioni mwangu na hata hai?kuelekea kufanana kwa namna moja au nyingine na ile ya mwenyeji wetu hali
iliyozidi kunitia mashaka, hata hivyo sikuwa na namna ikanibidi nitii amri ile
kama nilivyoambiwa. Hivyo nikasitisha zoezi la kuichukua ile bastola yangu
kule mafichoni mguuni na badala yake nikasimama bila kusema neno.
“Nakuonya kuwa mkononi mwangu ninayo bastola yenye uchu hivyo sitos?ita kuitumia endapo utajidangaya kufanya hila yoyote Bolos” yule mtu alien?delea kuniambia. Kwa kweli nilijihisi kuchanganyikiwa kwani akili yangu
ilikuwa bado hata haijamaliza kutulia tangu nilipofanikiwa kuyatoroka yale
mapango ya Musanze. Na sasa nilijiona ni kama niliyekuwa nimekimbilia aina
nyingine ya kifo tena kisichoeleweka mwanzo wake wala mwisho wake.
Mimi sikuwa nikiitwa Bolos ila nilifahamu kuwa hapa nilikuwa nikifanan?ishwa na huyo Bolos nisiyemjua ambaye bila shaka alikuwa akitafutwa na
kusakwa kwa udi na uvumba na mtu huyu nyuma yangu.
Nilimkumbuka yule mwenyeji wetu tuliyemkuta katika nyumba hii aliyejii?ta kwa jina la Innocent Gahizi na hapo nikamfananisha na huyo Bolos ambaye
sasa nilikuwa nikifananishwa naye. Hofu ikaniingia kwani sikujua huyo Bolos
alikuwa akitafutwa kwa sababu gani huku nikijiuliza mtu huyu nyuma yan?gu alikuwa ameingiaje mle ndani. Lakini nilipozidi kufikiri nikaikumbuka ile
mvua wakati ilipoanza tena kuanguka kwa fujo kwenye paa la nyumba hii na
hapo nikajikuta nikitabasamu.
Sasa nilifahamu kuwa bila shaka mtu huyu huenda angekuwa ameingia
mle ndani sambamba na zile kelele za mvua akikwepa nisiweze kuzisikia zile
kelele za mlango.
“Mimi siyo Bolos,” nilijitetea.
“Usijidanganye Bolos, kwa taarifa yako mipango yenu yote tunaifahamu na
kwa bahati mbaya sana hamtafanikiwa kwani huu ndiyo mwisho wako”
“Mipango gani, mbona sikuelewi? nimekwambia mimi siyo huyo Bolos un?ayemtafuta” niliongea kwa hasira.
“Hakuna mtuhumiwa anayekubali kosa mahakamani hivyo sishangai sana
namna unavyojitahidi kujitetea. Wenzako wako wapi? yule mtu nyuma yangu
alisisitiza na kwa kweli nilibaki njia panda nikishindwa kuelewa nifanye nini
ili mtu yule nyuma yangu anielewe huku nikiwa na hakika kuwa mtutu wa
bastola yake ulikuwa ukinitazama gizani.
“Wenzako wako wapi? yule mtu aliniuliza tena
“Niko peke yangu” nilimjibu huku nikijiuliza kama lile lingekuwa jibu sa?hihi au lah! lakini kabla ya kupata jibu nikashangaa kusikia sauti ya kicheko
cha kejeli nyuma yangu.
“Najua umekula kiapo kuwa ikitokea umekamatwa usiongee chochote laki?ni usijali kwani nitaanza kwanza na wewe halafu nitaendelea kujibanza humu
ndani hadi hapo wenzako watakaporudi na hapo nitawamaliza kiulaini na mi?pango yenu iliyosalia mtaenda kuifanyia kuzimu dhidi ya shetani ambaye hata yeye naamini kuwa atawashtukia mapema sana kwa jinsi mlivyo mabwege”
yule mtu aliendelea kuniambia na niliweza kuisoma vizuri sauti yake kuwa
ilikuwa mbali na mzaha. Haukuwa utani kwani nilizijua vizuri sauti zilizom?aanisha na sauti ile ilikuwa miongoni mwazo.
Nilijua kuwa kulikuwa na siku ambayo ningekufa lakini miongoni mwa aina
ya kifo nilichokuwa nikikichukia kilikuwa ni kifo cha gizani bila kupata nafasi
ya kuitazama sura ya muuaji wangu walau katika dakika ya mwisho ya kukata
kwangu roho. Hivyo akili yangu ilianza kufanya kazi haraka nikifikiria namna
ya kuiokoa roho yangu.
“Kwa hiyo hutaki kuniambia kuwa wenzako wako wapi? yule mtu aliniuliza
na hisia zangu zikanionya kuwa alikuwa akijiandaa kunishindilia risasi hivyo
nikaona nikiendelea kuzubaa yule mtu angeniua na hapo nikaamua kuununua
muda huku nikifikiria nini cha kufanya nijiokoe.
“Sawa! basi nitakueleza mahali walipo wenzangu ila kwa sharti moja tu”
nikamdanganya.
“Sharti gani? yule mtu akaniuliza na swali hilo likanifurahisha kwa
kuichelewesha roho yangu isiuache mwili.
“Nitakueleza mahali walipo wenzangu ila nakuomba usiniue”
“Ha ha ha kwanini nisikuue Bolos, hufahamu kuwa wewe na wenzako ni
virusi hatari sana vinavyotaka kuambukiza watu maradhi yasiyotibika kwa
muda mrefu katika nchi hii. Na kama maradhi hayo yakitibika basi yataacha
makovu kwenye mioyo ya vizazi hadi vizazi. Hivyo ni lazima mfe kwani ham?na uchaguzi”
Kilichofuata baada ya pale ni mimi kufumba macho na kusali kwani nilifa?hamu kuwa siku yangu ilikuwa imefika na akili yangu ilikuwa ukingoni ka?tika katika kufikiria njia ya kijinasua katika kadhia ile. Lakini ghafla nikiwa
nimefumba macho niliusikia ule mlango wa kuingilia kwenye kile chumba
ukifunguliwa kwa kasi ya ajabu.
Mimi nikiwa wa kwanza kuliona tukio lile nilifahamu nini ambacho kinge?fuatia baada ya pale hivyo niliwahi kujitupa chini na muda uleule nikasikia
risasi zikirindima mle ndani sambamba na sauti ya yowe kali. Yule mtu hatari
akasombwa hewani na kutupwa karibu yangu pale chini nilipolala na muda
uleule nikaanza kuhisi kitu kama kimiminika kizito kikiuzingira mkono wan?gu, nikajua ile ilikuwa ni damu ya yule mtu hatari aliyekuwa amenifumania
mle ndani. Sikuhitaji kuthibitishiwa kuwa yule mtu alikwisha kata roho.
Zile risasi ziliendelea kurindima mle ndani zikifyatuliwa bila malengo, hali
ilikuwa tete sana nikajua endapo ningeendelea kujilaza pale chini zile risasi
zingefanikiwa kuyatambua maficho yangu na kuniangamiza kwani yule mlen?gaji alikuwa kama mwenye wazimu akifyatua risasi ovyo.
Sikutaka kuendelea kusubiri hivyo nikaanza kutambaa nikiufuata ule mlan?go mfupi huku nikizikwepa zile risasi. Nilipoufikia ule mlango nikausukuma
kwa kichwa na sikupata pingamizi lolote na nilifurahi sana kuukuta mlango
ule haujafungwa hivyo nikajitoma ndani na kuufunga kwa nyuma.
Nikiwa tayari nimetokezea kwenye kile chumba kingine nilijibanza pembe?ni ya ule mlango huku nikitafakari cha kufanya, kilikuwa chumba kidogo zaidi kuliko kile nilichotoka. Nilijisogeza pembeni ya mlango ule kisha nikajiege?meza ukutani huku nikitweta kwa hofu. Nikiwa nimejibanza pale chini bado
niliendelea kuzisikia zile risasi zikirindima kwenye kile chumba nilichotoka.
Nilipoyatega vizuri masikio yangu nikagundua kuwa ile sauti ya zile risasi
ilikuwa ikiusogelea ule mlango wa kile chumba nilichoingia. Nikajua kuwa
muda si mrefu yale maficho yangu yangefichuliwa hivyo nikajilaza chini na
kuanza kutafuta upenyo wowote wa kutokea.
Katika hangaika hangaika ya hapa na pale nikawa nimejikwaa sehemu fu?lani na kutokana na giza zito lililokuwa mle ndani sikuweza kufahamu hasa
nilikuwa nimejikwaa kwenye nini lakini nilipofanya udadisi nikagundua kuwa
nilikuwa nimejikwaa kwenye kitu fulani mfano wa bomba la chuma. Nilipo?papasa papasa nikagundua bomba lile lilikuwa limefunikwa kwa kitu mfano
wa turubai na hapo nikafunua lile turubai.
Ingawaje nilikuwa sioni kutokana na giza zito la mle ndani lakini niliweza
kuhisi kwa usahihi kabisa. Lile bomba la chuma lilikuwa ni mtutu wa mzinga
maalumu unaotumika kudungulia ndege angani, kwa kuwa nilikuwa nazifa?hamu vizuri silaha nyingi za kijeshi haikuniwia vigumu kuuelewa mzinga ule
hata hivyo sikuweza kufahamu kwa haraka kuwa ulikuwa mle ndani kwa sa?babu gani.
Muda haukurusu kuendelea kufanya utafiti zaidi kwani ile milio ya risasi
sasa ilikuwa imeufikia ule mlango wa kile chumba na kutokana na sauti ya
zile risasi niliweza kuhisi kuwa yule mtu alikuwa na silaha nzito na hatari
hivyo nilianza kuhaha mle ndani nikitafuta pa kutokea. Sehemu ya kwanza
niliyofikiria kukimbilia ilikuwa dirishani hata hivyo giza la mle ndani lilikuwa
zito kwangu kuweza kuona mbele hivyo nikaanza kuzunguka zunguka mle
ndani nikitafuta sehemu lilipo dirisha. Bahati ikawa upande wangu, nikafan?ikiwa kulipata dirisha hata hivyo dirisha lile lilikuwa limefungwa kwa vitasa
maalumu.
Sikutaka kuleta ufundi zaidi hivyo nilirudi nyuma hatua chache na kisha
nikalivamia lile dirisha kwa kasi ya ajabu huku nikiitanguliza miguu yangu.
Lilikuwa dirisha chakavu la mbao hivyo nilipita nalo hadi nje likiwa vipande
vipande.
Kule nje niliangukia chini katikati ya kichaka chenye nyasi ndefu zilizolowa?na chapachapa kwa mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Nikawahi
kuichomoa bastola yangu toka mafichoni na kuishika vizuri mkononi kisha
nikajiviringisha na kwenda kubana kwenye kona ya nyumba ile sehemu il?iyokuwa na kichaka kingine kizito cha nyasi ndefu. Mambo yote nilikuwa
nakiyaona kama tamthilia kwa jinsi yalivyokuwa yakienda.
Nikiwa bado nimejibanza pale kwenye ile kona niliweza kuzisikia kelele
za mbwa waliokuwa wakibweka upande wa pili wa nyumba ile na tukio hilo
likaniongezea ziada nyingine katika fikra zangu kwani sasa nilikuwa na hakika
kuwa yule mtu aliyenishambulia kule chumbani hakuwa pake yake na kwa
maana nyingine ningekuwa najidanganya sana kudhani kuwa ningeweza kuli?toroka eneo lile kirahisi rahisi.
Sasa nilichokuwa nikipanga ni kwenda kumuokoa Rosine kwenye kile chumba mapema na haraka iwezekanavyo na baada ya hapo tungetoroka zetu.
Toka pale nilipojificha kwenye kona ya ile nyumba nilichungulia upande wa
kushoto nikakiona kile chumba tulichokuwa tumelala na Rosine lakini siku?weza kuhisi dalili zozote za purukushani mle ndani ingawaje nilikuwa na kila
hakika kuwa kwa vyovyote Rosine angekuwa tayari amekwishashtuka toka
usingizini kutokana na zile kelele za risasi zilizokuwa zikifyatuliwa ovyo na
yule mtu.
Niliendelea kujibanza kwenye lile eneo lenye kichaka cha nyasi huku nik?iusoma utulivu wa eneo lile na wakati huo mvua ikiendelea kunyesha. Nili?poridhika kuwa hali ilikuwa tulivu nikaanza taratibu kunyata kuelekea kwenye
kile chumba nilichomuacha Rosine kwa mwendo wa kuinama huku bastola
yangu ikiwa mkononi tayari kufanya kazi. Zile sauti za wale mbwa waliokuwa
wakibweka sasa zilikuwa zimekoma na tukio hilo lilinipa wasiwasi hata hivyo
sikuwa na muda zaidi wa kutafiti kwani nilichokuwa nikikifikiria sasa ilikuwa
ni kumwokoa Rosine na kisha tutoroke haraka eneo lile.
Upande wangu wa kulia nilitazamana na msitu mkubwa wenye miti mi?kubwa na mirefu ya miaka mingi yenye matawi makubwa yalichomoza kila
upande. Wakati nikinyata kuelekea kwenye kile chumba niligeuka kuutaza?ma ule msitu huku nikikumbuka namna msitu kama ule ambavyo ungekuwa
maficho mazuri kwa mdunguaji katika uwanja wa kivita. Tafsiri hiyo ikanipa
hisia mbaya zilizonifanya nianze kuhisi ni kama niliyekuwa nikitazamwa na
mdunguaji mmoja aliyejificha kwenye tawi la mti mmoja katika msitu ule. Ku?tokana na hisia hizo ikanibidi niende kwa mwendo wa kuchepuka na kuhama
hama katika mtindo wa zig zag nikinuia kumkosesha shabaha mdunguaji huyo
kama angekuwepo.
Nilikuwa nipo mbioni kukikaribia kile chumba nilichomuacha Rosine
wakati niliposhtushwa na kuyumba kwa nyasi ndefu zilizokuwa mbele yangu.
Nikasimama na kuinama chini huku macho yangu yakitazama kwenye zile
nyasi mbele yangu. Zile nyasi ziliendelea kuchezacheza na zilipotulia taswira
isiyoonekana vizuri ya kiumbe fulani ilijitokeza umbali mfupi mbele yangu.
Kile kiumbe kilisimama kwa ghafla sana nacho ni kama kilichokuwa kikisita
kuendelea na safari yake.
Kwa muonekano usio rasmi nilivuta hisia kuwa yule alikuwa mnyama wa
porini aliyekuwa katika ziara zake. Niliishika vizuri bastola yangu huku niki?piga mahesabu ya kumshindilia risasi mnyama yule endapo angetaka kunifa?nyia ukorofi. Hata hivyo wazo la matumizi ya risasi nilijikuta nikiachana nalo
kwani mlio wa risasi ingeweza kumshtua mtu yoyote aliyekuwa jirani na eneo
lile na hiyo ingekuwa ni sawa na kumuonesha adui mahali nilipo.
Tulibaki tukitazamana na yule mnyama na hapo nikajua kuwa huenda na
yeye alikuwa akipanga namna ya kunishambulia. Wakati tukiendelea kuta?zamana mara mwanga mkali wa radi ukamulika eneo lile na kuufanya siku ule
kuwa mchana kwa muda. Mwanga ule ukawa umeniwezesha vizuri kumuona
yule mnyama mbele yangu.
Alikuwa mbwa mkubwa mwenye uchu na windo lake na alikuwa amesi?mama mbele yangu akinitazama. Nilipomchunguza vizuri nikagundua kuwa hakuwa mbwa mjinga kama walivyokuwa mbwa wengi wa mitaani wasiojua
wajibu wao. Alikuwa mbwa mkubwa na mwenye misuli iliyoshiba vizuri an?ayetambua wajibu wake kama mlinzi hodari. Mbwa yule mkubwa ajabu na
mkali nilimuhisi kuwa alikuwa miongoni mwa wale mbwa waliokuwa wakib?weka. Nilijaribu kumuhadaa kwa kumfanyika ishara fulani ili anipe upenyo
lakini hakuwa mbwa wa kudanganyika badala yake alitulia akinitazama kwa
kunivizia huku akiuchezeshachezesha mkia wake na tukio hilo likanifanya ni?pige hatua moja nikinyata kurudi nyuma.
Hilo lilikuwa kosa kwani yule mbwa aliigundua haraka hila yangu na hivyo
kufumba na kufumbua alinirukia na kinipiga kumbo la nguvu lililonipeleka
chini bila ya kupenda huku nikiwa siamini macho yangu na umbo lake liliku?wa kubwa kama la simba dume mwenye njaa kali. Sikupata muda wa kufu?rukuta kwani yule mbwa aliniwahi na kunikalia kifuani huku miguu yake ya
mbele yenye nguvu akiitumia kukikandamiza chini kifua changu. Lilikuwa ni
shambulizi la kushtukiza na nisilolitarajia na vilevile nilijikuta nikimshangaa
mbwa yule kwani pamoja na shambulizi lile alilonifanyia bado hakufungua
mdomo wake kubweka hata mara moja.
Nilijitahidi kufurukuta kwa kila namna lakini yule mbwa alikuwa hodari wa
kunidhibiti kiasi kwamba juhudi zangu hazikuzaa matunda na hapo nikajiona
kama mwanamke aliyejilaza kitandani tayari kwa tendo la ndoa. Hii niliio?na kuwa ilikuwa ni hatari nyingine ya kipekee ambayo endapo nisingefanya
maamuzi ya haraka nisingepata hata nafasi ya kujilaumu. Niliipima nguvu ya
mbwa yule na kuiona kuwa ilikuwa imeegemea zaidi kwenye miguu yake ya
mbele na hilo likanifurahisha. Hivyo nikakusanya nguvu za kutosha miguuni
kisha nikaibetua ile miguu ya nyuma ya yule mbwa hivyo nikamchota yule
mbwa hewani nikimtupia mbele yangu katika mtindo wa sarakasi ya judo hata
hivyo sikuiachia ile miguu yake ya mbele ili kumpotezea uhimili.
Yule mbwa alipotua chini mimi niliwahi kujipindua nikamrukia kabla ya
yeye hajasimama na hapo nikamtia kabari ambayo kamwe asingekuja kuisa?hau katika maisha kwani ilikuwa kabari matata ya kufunga kazi isiyoruhusu
hata hewa chafu kutoka kooni mwake. Yule mbwa alijitahidi kufurukuta bila
mafanikio nami sikumwachia, akatupatupa miguu na mkia wake huku na kule
lakini ilikuwa kazi bure kwani hakuwa na nguvu ya kukabiliana na kabari yan?gu badala yake alifurukuta kidogo na kutulia mwili wake ukiwa mbali na uhai.
Nilimwacha yule mbwa na kumtupa pembeni huku nikitweta na muda uleule
nikaiokota bastola yangu pale chini na kusimama nikiyatembeza macho yan?gu huku na kule ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na kiumbe chochote kingine
eneo lile. Niliporidhika nikaanza kuendelea mbele na safari yangu safari hii
nikiwa makini zaidi.
Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha eneo lile la msitu lakini
cha ajabu kwa wakati huu mvua hiyo nilikuwa siisikii tena kwani akili yangu
yote sasa ilikuwa kwa Rosine. Nilikifikia kile chumba nilichomuacha Rosine
na hapo nikajibanza dirishani nikisikiliza kama kulikuwa purukushani zozote.
Sikusikia chochote mle ndani na hapo wasiwasi ukaanza kunishika, nikajaribu
kumuita Rosine kwa sauti ya chini pale dirishani hata hivyo sikusikia sauti
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
yoyote ikiniitikia mle ndani na hapo wasiwasi ukazidi kuniingia.
Nikaamua kujisogeza vizuri pale dirishani na kuchungulia mle ndani na
kwa msaada wa ule mwanga wa radi uliokuwa ikimulika mara kwa mara pale
msituni nilifanikiwa kuona mle ndani ya kile chumba na mara hii nilihisi bari?di kali ikipenya kichwani wangu. Hakukuwa na mtu yoyote juu ya kitanda
kile wala dalili zozote za kuwepo kwa mtu mle ndani na hapo nikarudia tena
kumuita Rosine hata hivyo hakuna sauti yoyote iliyoniitikia zaidi ya kusikia
mwangwi wa sauti yangu ikipenya ndani ya nyumba ile na kusambaa.
Niliduwaa nikitazama mle ndani ya chumba kupitia pale dirishani huku
nikishindwa kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea. Hisia za mapenzi juu ya
Rosine zilikuwa zimefufuka upya moyoni mwangu na kuanza kuitafuna nafsi
yangu taratibu. Hali hiyo ikapelekea kufufuka upya kwa hasira moyoni mwan?gu kwani sikuwa tayari kuondoka eneo lile bila ya Rosine. Akili yangu ikaanza
kufanya kazi kwa haraka huku mawazo mengi yakipita kichwani na miongoni
mwa mawazo hayo ni kuwa hisia zangu ziliegemea katika mtazamo wa kuwa
huenda Rosine alikuwa ametekwa na watu wale.
Lakini nilipozidi kufikiri nikaona ingekuwa vizuri zaidi nijithibitishie hilo
kwa kuingia tena ndani ya nyumba ile huku nikiamini huenda ningemuona
Rosine mle ndani akiwa amejibanza sehemu fulani baada ya kuamka na ku?toniona.
Wazo hilo lilipitishwa haraka kichwani mwangu na hapo nikaanza kulifa?nyia kazi. Nilipolichunguza vizuri lile dirisha nikagundua kuwa kulikuwa na
kipande kidogo cha ubao kilicholiwa na mchwa na hivyo kuacha tundu dogo
linalotosha kupitisha mkono ili niweze kufungua komeo la dirisha lile. Hilo
lilinipa faraja kidogo hivyo nikapitisha mkono kwenye lile tundu na kuanza
kulifungua lile dirisha. Nilikuwa ndiyo kwanza naanza kufungua komeo la
dirisha lile pale nilipohisi kitu cha baridi kikinigusa nyuma ya kichwa changu.
Kwa sekunde chache niliduwaa kama niliyepigwa shoti ya umeme huku
jasho jepesi likianza kushuka usoni na hapo mapigo ya moyo wangu yakawa
yamevurugika kabisa.
“Tulia hivyo hivyo wewe mwanaharamu na ukijitikisa tu nitakifumua
kichwa chako” sauti kutoka nyuma yangu ilinionya.
“Wewe ni nani?
“Usijali kwani muda si mrefu utanifahamu, weka mikono yako juu”
Kwa kweli nilijihisi kuchanganyikiwa pale nilipowaza kuwa mara hii tena
nilikuwa nikirudi kwenye mikono ya watu wale hatari. Tukio hilo liliniuma
sana hata hivyo sikuwa na jinsi hivyo ikanibidi nitii ile amri toka nyuma yangu
huku nikiinyanyua mikono yangu juu.
“Sasa utafuata kile nitachokwambia na usijidanganye kufanya utundu wa
namna yoyote kwani sitokuvumilia”
“Sawa” nilimjibu
“Tulia hivyo hivyo” yule mtu aliniambia tena kisha akaanza kunipekua
mwilini huku mkono wake mmoja ukiwa bado umeielekeza bastola yake kiso?goni kwangu. Alimaliza kunipekuwa na kuichukua ile bastola yangu lakini
nilishukuru kuwa hakuwa ameiona ile bahasha niliyoichukua kule
“Haya tembea mbele mwanaharamu mkubwa we!”
“Tunaelekea wapi? nilimuuliza nikijifanya sielewi somo.
“Fuata ninachosema, mimi huwa sipendi maswali maswali, umenielewa?
“Nimekuelewa”
Safari yetu ikawa imeanza huku mimi nikiwa nimetangulia mbele mikono
yangu juu na wakati huo bastola ya yule mtu nyuma yangu ikiendelea kuni?kuna kuna kisogoni. Hasira zilinishika kwa kuingia tena mikononi mwa adui
hata hivyo nilifahamu kuwa maamuzi yoyote ya kukurupuka kwa kipindi kile
yasingekuwa na tija yoyote na badala yake nilitakiwa kusubiri kwanza hadi
hapo muda muafaka utakapowadia.
Tulikizunguka kile chumba na kutokezea upande wa mbele wa ile nyumba
na wakati wote huo nilikuwa nikiutafiti udhaifu wa yule mtu.
“Simama” yule mtu aliniamrisha wakati tulipofika kwenye kona ya mbele
ya ile nyumba na hapo nikasimama huku macho yangu yakizunguka kulichun?guza eneo lile kama kulikuwa watu au mtu yoyote. Sikuweza kumwona mtu
yoyote ingawaje hali hiyo haikunishawishi niamini kuwa yule mtu alikuwa
peke yake eneo lile.
“Wenzako wako wapi? nilimuuliza yule mtu na safari hii niliambulia kutan?dikwa ngumi mbili nzito na kavu mgongoni.
“Sikukwambia wewe kuwa mimi huwa sipendi maswali? yule mtu alifoka
baada ya kunishushia kile kipigo.
Nilibaki nikigugumia kwa maumivu kwani zile ngumi zilinifanya nijihi?si kama niliyepigwa kwa mawe na wakati nikiendelea kugugumia maumi?vu niliutumia muda huo kugeuka kwa hila kumtazama yule mtu nikiangalia
kama kulikuwa kuna namna ya kumshambulia. Alikuwa ni mtu mfupi kiasi
lakini mwenye mwili ulioshiba vizuri na alikuwa amevaa gwanda za jeshi zin?azofanana na wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda niliyowatoroka kule
mapangoni. Nikaanza kupata imani kuwa huenda huyu mtu alikuwa miongoni
mwao na muda huohuo nikamsikia yule mtu akipiga mruzi kali kwenda upa?nde mwingine wa ule msitu. Huu ulikuwa muda mzuri niliokuwa nikiusubiri
tangu nilipokamatwa mateka na mtu yule.
Niligeuka haraka na kwa kasi ya ajabu nikatupa ngumi mbili kavu na imara
nilizoziita trouble shooting ambazo zililivuruga na kulipasua vibaya koo la
mtu yule na hapo nilimuona yule mtu akihamaki na kujishika kooni. Nikam?badilishia mtindo na kumtandika mapigo mengine mawili ya kareti kwenye
chembe ya moyo na hapo akapiga yowe kali la maumivu lakini niliwahi kum?fumba mdomo na kwa mapigo yale nilikuwa na kila hakika kuwa asingeweza
kuamka tena, hivyo alianguka chini kama gunia na kutulia huku mikono yake
ikiwa bado imelishikilia koo lake.
Bila kupoteza muda nikaichukua ile bastola yake hivyo nikawa na bastola
mbili pamoja na ile ya kwangu niliyoiba kule chumbani. Nilitulia tena kwa
muda nikiusoma utulivu wa eneo lile na kwa kweli niliona kuwa muda uli?kuwa ukikimbia sana na hadi wakati huu hakuna chochote cha maana nili?chokuwa nimekifanya. Akili yangu ilirudi tena kumfikiria Rosine na sikuweza
kuelewa alipoelekea hata hivyo nilikuwa na imani kuwa uwezekano wa yeye
kuwepo mle ndani ya ile nyumba bado ulikuwa mkubwa.
Kwa mara nyingine tena niliusoma utulivu wa eneo lile nikaona bado hali
ilikuwa tulivu ingawaje bado niliamini kuwa yule mtu hakuwa peke yake eneo
lile. Nikakumbuka namna yule mtu niliyemuua pale chini alivyopiga mruzi
kali upande mwingine wa ule msitu. Nikajua kwa vyovyote kulikuwa na wen?zake upande ule wa msitu na alikuwa akipiga mruzi kuwajulisha hao wenzake
kuwa alikwisha nipata.
Niligeuka upande wa kushoto na kuliona dirisha moja la sebule ya ile nyum?ba na kwa kuzingatia kuwa ilikuwa nyumba ya siku nyingi iliyotelekezwa bila
kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara madirisha yake yalikuwa dhaifu sana.
Hivyo nililiendea lile dirisha na kuvunja mbao mbili zilizoniwezesha kupata
nafasi na kama kule awali nikaingiza mkono na kufungua komeo la dirisha
lile. Kwa muda mfupi nikawa nimefanikiwa kulifungua dirisha lile na hapo
nikapenya na kuingia mle ndani.
Giza la mle ndani lilikuwa zito sana lakini macho yangu yalikuwa yame?kwishaanza kulizoea hata hivyo sikuweza kuhisi uwepo wa mtu yoyote mle
ndani. Nikaanza kutembea kwa kunyata nikiingia kila chumba cha ile nyumba
huku nikimuita Rosine kwa sauti ya chini lakini yenye uhakika wa kupen?ya masikioni mwa mtu yoyote ambaye angekuwa mle ndani. Sauti yangu ni
kama iliyokuwa ikinirudia masikioni hivyo nikajiona ni kama ninayejiambia
mwenyewe.
Niliendelea kumuita Rosine mle ndani bila mafanikio na matumaini ya
kumpata yakawa yakipunguwa. Kwa kweli nilikata tamaa sana huku nikihisi
kutaka kuchanganyikiwa. Sikujua ni nini kilikuwa kimemtokea Rosine, msi?chana niliyetokea kumpenda sana katika safari yangu ya kijasusi hapa nchini
Rwanda. Na sikupenda mwisho wetu na Rosine uishie vile kwani moyo wangu
ulikuwa umetokea kumpenda sana msichana yule. Mwishowe nilisimama na
kuegemea ukuta mle ndani huku nikiwa nimekata tamaa sana.
Niliona jitihada zangu za kuonana tena na Rosine zilikuwa ukingoni bila ya
mafanikio, nikarudia tena kumuita lakini ni mwangwi wa sauti yangu ndiyo
uliyokuwa ukipenya ndani ya nyumba ile na kusikika na hakukuwa na dalili
yoyote ya uwepo wa Rosine.
Roho iliniuma sana na sikuweza kujua ni kwa nini nilitokea kumpenda
sana msichana yule tena katika kipindi kigumu kama hiki. Nilifirikia ni wapi
ambapo ningemtafuta lakini sikuona tumaini lolote kwani ile sehemu niliy?okuwa ilikuwa katikati ya msitu mzito wenye miti mikubwa na ya kila aina
isiyojulikana mwanzo wala mwisho mwisho wake. Vilevile sikuwa na mazoea
yoyote na eneo lile na kila kitu kwangu kilikuwa kigeni. Katika hali kama
hii nilijua kuwa ningepoteza muda wangu kuendelea kumtafuta mtu nisiye?jua ameelekea wapi. Labda Rosine aliamua kunitoroka au labda alitekwa na
mmoja wa watu wale?, haya yalikuwa miongoni mwa maswali niliyojiuliza
kichwani bila kupata majibu.
Niliamua kurudi tena kule kwenye kile chumba nilichomuacha Rosine na
kwa mara nyingine tena nimuita lakini chumba kilikuwa kimya na hata yale
madirisha yote yalikuwa yamefungwa vilevile kama yalivyokuwa mwanzo.Nikabaki nimeegemea ukuta wa chumba kile nikiwa nimekata tamaa sana
__________
KELELE ZA MBWA WALIOKUWA WAKIBWEKA nje ya nyumba ile
zilizirudisha fikra zangu mle ndani, nikashtuka na kutega sikio. Nilikuwa sa?hihi kabisa kwani sauti za mbwa wale wakati huu zilikuwa zikiikaribia ile
nyumba. Niliingiwa na hofu sana, nikasogea na kutazama nje kupitia upenyo
wa dirisha moja la chumba kile. Mwanga wa radi ulipomulika uliwafichua
watu tisa waliovaa mavazi ya kijeshi na bunduki zao mikononi waliokuwa
wakiisogelea ile nyumba. Loh! safari hii nikajua tayari nimekamatika hivyo
niliinyanyua bastola yangu mkononi na kuanza kupapasa katika namna ya ku?jipa matumaini kuwa endapo ingetokea nimeshindwa kuwatoroka watu wale
risasi moja tu ya kichwani ingetosha kuupumzisha mwili wangu badala ya
kukubali kukamatwa tena na kurudishwa kwenye mapango yale.
Nikiwa nimejibanza pale dirishani huku nikifikiria cha kufanya mara
nilizisikia zile kelele za mbwa wanaobweka zikiwa zimekaribia upande ule wa
lile dirisha la sebuleni nililolitumia kuingilia mle ndani. Nikajua mbwa wale
walikwisha tambua harufu yangu na sasa walikwisha tambua kuwa mimi nipo
mle ndani. Niliukumbuka ule mruzi uliyopigwa na yule mtu niliyepambana
naye na hapo nikajua kuwa ile ilikuwa ni ishara ya kuwaita wenzake ambao
bila shaka ndiyo hawa waliokuwa nje ya nyumba hii.
Wale mbwa waliendelea kubweka na muda mfupi uliyofuata nilisikia mlan?go wa mbele wa ile nyumba ukigongwa na hapo moyo wangu ukapiga kite
kwa hofu kwa kadili mgongaji aliyokuwa akigonga hodi mlangoni. Zile hodi
hatimaye zilikoma pengine baada ya mgongaji kuona hafunguliwi na hapo
nikaanza kusikia minong’ono halafu muda uleule nikasikia kitasa cha mlango
ule kikichokolewa, nikajua kuwa sasa wale watu walikuwa wakifanya jitihada
za kuingia mle ndani.
Hali hiyo ikanifanya nianze kunyata taratibu na kuenda kuufunga ule mlan?go wa kile chumba nilichokuwa kwani nilifahamu kuwa muda si mrefu wale
watu wangefanikiwa kuingia mle ndani. Na kwa vyovyote mara baada ya wale
watu kuingia mle ndani na kumaliza kufanya msako katika vyumba mle ndani
wangeshtukia kuwa chumba kile nilichokuwa ndiyo chumba pekee ambacho
kimefungwa na kwa maana hiyo wote wangeelekeza juhudi zao katika kuvun?ja mlango wa chumba na kwa kufanya hivyo wangenipa nafasi ya kutoroka
kiulaini wakati wao wakiendelea kushughulika na mlango.
Nilirudi tena pale dirishani na kuanza ufundi wangu na baada ya kitambo
kifupi nikasikia ule mlango wa sebuleni ukifunguliwa kwa pupa halafu kukaf?uatiwa na vishindo vya watu wakiingia na mbwa mle ndani. Nililichokoa lile
dirisha kwa pupa hadi nikafanikiwa kiondoa komeo lake lililoshika kutu am?balo lilianza kuniwekea kauzibe. Nikawa naendelea na purukushani zile mara
nikasikia sauti nzito na kali ya mbwa wakiubwekea ule mlango wa chumba
changu ambao sasa nilikuwa nimeufunga kwa ndani. Kelele zile za mbwa
zikaniashiria kuwa walikuwa ni mbwa wanaotisha kwa maumbo makubwa na
wenye hasira.
Kelele za mbwa wale waliokuwa wakiubwekea ule mlango wa chumba
changu zikachanganyika na kelele za kuchokolewa kwa kitasa cha mlango wa
kile chumba. Hadi wakati huu sikutaka kusubiri tena hivyo nikaanza kulivuta
lile dirisha kwa papara na baada ya jitihada za hapa na pale hatimaye nikafan?ikiwa kuzinyofoa shata zake lakini nikakutana na kizuizi kingine cha nondo
za dirisha lile. Japokuwa zilikuwa nondo za muda mrefu lakini zilikuwa imara
kama ndiyo kwanza zilikuwa zimetoka kiwandani. Nikauchomeka mguu wan?gu kwenye zile nondo za chini huku nikiusukuma kwa nguvu zangu zote hala?fu ile nondo ya juu yake nikawa naivuta kwa mikono yangu yote miwili.
Ilikuwa ni kazi ngumu na inayochosha lakini sikuwa na chaguo mbele ya
zile kelele za wale mbwa hivyo nilijikuta nikilifanya zoezi lile kwa weledi
wa hali ya juu na kwa nguvu zangu zote na hatimaye nikafanikiwa kuzipinda
zile nondo na kupata nafasi ya kupenyeza kichwa na kifua changu. Sikuwa
na muda tena wa kupoteza na hapo hapo nikatanguliza kichwa changu kupita
kwenye nondo zile halafu kikafuatia kifua na lilipopita tumbo langu nikamali?zia na miguu na hapo nikaangukia kwa nje ya dirisha lile huku nikihema ovyo
kama ninayefukuzwa.
Nilipoanguka tu nje ya lile dirisha kule nyuma yangu nikasikia ule mlan?go wa kile chumba nilichotoka ukifunguliwa kwa pupa kisha kukafuatiwa na
sauti ya vishindo vya watu wakiingia mle ndani huku wameongozana na wale
mbwa. Toka pale nilipoangukia nje ya dirisha lile nililala chini kisha nikaanza kutambaa kuelekea upande mwingine wa nyuma ile. Sikuwa nimefika mbali wakati niliposikia wale mbwa wakibweka pale diris?hani ndani ya kile chumba nilichotoka, nilipogeuka nyuma kutazama nikawa?ona wale mbwa wakijitahidi kupitisha vichwa vyao kwenye ule uwazi bila ma?fanikio huku wakiendelea kubweka kwa hasira halafu muda mfupi uliofuata
wale mbwa wakaacha kubweka baada ya kupewa amri hiyo na bosi wao hivyo
wakarudisha vichwa vyao ndani, na muda uleule niliuona mwanga mkali wa
kurunzi ukianza kumulika mulika eneo lile.
Nilijibanza kwenye kichaka cha nyasi wakati mwanga ule uliponifikia, nikauruhusu unipite kisha nikasimama na kuanza kutimua mbio kuelekea
kule msituni. Muda mfupi uliofuata nikawa nimepotelea ndani ya ule msitu mkubwa wa pale jirani ulioshonana kwa miti mikubwa ya kila namna. Wakati
nikiendelea kutimua mbio niliweza kuipata vizuri ile mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha usiku ule.
__________
MWENDO WANGU WA KUKIMBIA haukuwa wa kubabaisha kwani nilitimua mbio kadiri nilivyoweza huku nikiupangua msitu na vichaka, ma?bonde na milima, nikiendelea na safari yangu nisiyoifahamu mwisho wake.
Nilipowakumbuka wale mbwa nikajua kuwa muda si mrefu wangekuwa nyu?ma yangu wakinusa nyayo zangu kunifuatilia lakini hilo halikunipa mashaka
kwani nilikwisha pambana vita vingi na vya hatari katika misitu ya aina to?fauti.Kitendo cha kulitoroka eneo lile bila kuwa na Rosine kiliniuma sana huku nikijihisi kupungukiwa na mtu wa karibu sana niliyetokea kumpenda katika
namna ya ajabu na isiyoelezeka. Hata hivyo sikuwa na jinsi kwani mazingira
yalijieleza na usalama wa roho yangu lilikuwa jambo la kwanza zaidi ya yote.
Japokuwa sikuwa na saa yangu mkononi lakini niliweza kukadiria tu kuwa
nilikuwa nimekimbia zaidi ya muda wa saa moja bila kupumzika katika misitu
ile bila ya kujua kuwa nilikuwa nikielekea wapi. Hata hivyo niendelee kutimua
mbio tu kwani nilikuwa na hakika kuwa kule nyuma yangu nilikuwa niki?fuatiliwa. Kitu pekee nilichokuwa nikikihofia ni juu ya kukutana na wanyama
wakali katika misitu ile lakini nilipokumbuka kuwa nilikuwa na bastola mbili
tena zilizojaa risasi nilipata faraha kidogo.
Baada ya mwendo mrefu wa kukimbia mle msituni hatimaye nilianza kuhisi
kuchoka, kichwa kilianza kuniuma na nikaanza kuhisi kichefuchefu. Nilikuwa
nimekimbia urefu wa maili nyingi katika misitu ile na kuna wakati niliwakuru?pusha wanyama wa mwituni waliokuwa wamelala sehemu fulani mle msituni
wakati nikipita.
Baada ya mwendo mrefu wa kukimbia hatimaye nilijikuta nimetokezea
kwenye eneo fulani la msitu mzito wenye miti mikubwa mirefu na vichaka
vya kuogopesha. Katika msitu ule niligundua kuwa kulikuwa na mfereji wa
maji uliokuwa ukielekea sehemu ya chini ya msitu ule. Nilipofika pale nikaan?za kuufuatilia ule mfereji.
Ulikuwa ni mfereji mdogo uliokuwa ukitiririsha maji yake kutoka sehemu
za juu za msitu ule na baada ya kuufuatilia vizuri mfereji ule hatimaye nikawa
nimeuona mfereji ule mbele yangu ukikatisha katikati ya mawe makubwa ya
msitu ule. Nilipoufikia ule mfereji niliinama na kuanza kunywa maji nikitumia
viganja vya mikono yangu. Kadiri maji yalivyokuwa yakipenya kooni nili?sikia faraja ya kipekee iliyonipa nguvu mpya. Nilikunywa maji ya kutosha na
mengine nikanawa kichwani kukipoza kichwa changu na hapo nikawa nahisi
auheni.
Moyo wangu bado ulikuwa ukienda mbio kutokana na ile safari ndefu ya
kukimbia mle msituni hivyo nilitafuta sehemu nzuri kando ya mfereji ule ma?hali kulipokuwa na upepo mwanana na hapo nikaketi huku nikiegemea jiwe
kubwa lililokuwa eneo lile. Nikiwa nimeliegemea lile jiwe nilihisi ni kama
niliyetua mzigo mzito uliyokuwa umenielemea.
Mawazo mengi yakawa yakipita kichwani mwangu huku yakitengeneza
muunganiko wa matukio yote tangu siku ya kwanza nilipofika nchini Rwanda.
Matukio yote niliyaona kama tamthilia ya kutunga lakini yenye ukweli ndani
yake. Ukweli ni kwamba ujasusi ilikuwa ni kazi ninayoipenda sana lakini kwa
hapa nchini Rwanda nilianza kuziona dalili za ujasusi huo kutaka kunitokea
puani huku kazi niliyotumwa nikiwa hata bado sijaifikia nusu yake.
Nikiwa bado nimeegemea lile jiwe niliendelea kuwaza huku nikiunganisha
tukio moja na jingine katika namna ya kutengeneza mkasa unaoleta maana
fulani kichwani mwangu. Hata hivyo niligundua kuwa maswali mengi nili?yokuwa nayo hayakuwa na majibu ya moja kwa moja hivyo nikakipumzisha
kichwa changu kwa kuanza kumuwaza Rosine na hapo nikaona faraja kidogo
kuwa angalau nilibahatika kuonana na msichana mzuri na mrembo wa kinyarwanda
aliyefanikiwa kupiga mhuri wa mapenzi moyoni mwangu katika sa?fari yangu hii ya kijasusi yenye changamoto za kipekee. Loh! furaha ilioje
kuwa na mrembo kama yule, nilijisemea moyoni huku nikitabasamu lakini
hata hivyo niligundua kuwa furaha yangu ilikuwa haijakamilika kwani wakati
huu sikuwa na Rosine na hapo nikajikuta nikimuombea Rosine kuwa huko
alipo Mungu amuepushie mbali na kadhia yoyote mbaya.
Sikuweza kujua ni kwa vipi nilipitiwa na usingizi mzito wa mazongezonge
nikiwa nimeegemea jiwe lile ila kilichonishtua ni sauti ya ajabu ya mvumo
usioeleweka iliyokuwa ikipenya masikioni mwangu katika msitu ule. Nikash?tuka na kufumbua macho yangu taratibu nikiyazungusha upande huu na ule
bila kujitikisa huku mkono wangu wa kulia ukiipapasa vema bastola yangu,
“Mungu wangu! nini hiki tena?” nilijiuliza huku nikivipa uhai viungo vyangu
mwilini. Macho yangu yakajikuta yakiweka kituo kutazama juu ya mti mkub?wa aina ya mvule uliokuwa kiasi cha umbali wa mita kama kumi hivi mbele
yangu.
Kwanza nilisikia kelele za mbawa za ndege wengi waliokuwa wakiukimbia
mti ule na kitendo hicho kikanishtua sana wakati nilipoyainua macho yangu
kutazama juu ya mti ule. Mvua ilikuwa imeacha kunyesha wakati huu na anga
lote lilikuwa limetulia likianza kupata ugeni wa mwanga hafifu wa mbalam?wezi hata hivyo sikuweza kukisia kuwa muda ule ulikuwa saa ngapi. Macho
yangu yaliweka kituo yakitazama juu ya mti ule na hapo nikahisi baridi nye?pesi ya hofu ikipenya mwilini mwangu na kunipokonya hata nguvu kidogo
za kuweza kusimama. Nikabaki nimeegemea jiwe lile huku nikishindwa hata
kujitikisa kwa hofu.
Joka kubwa jeusi linalomeremeta lilikuwa likishuka toka juu ya mti ule,
ukubwa wa joka lile sikuwahi kuusoma hata vitabuni. Kumbuka kuwa hadi
wakati huu nilikuwa nimeshapambana na majoka yenye ukubwa wa kila aina
kwenye mapango ya Musanze lakini miongoni mwayo hakukuwa na hata
mmoja lililolingana na joka hili lililokuwa likishuka kwenye ule mti mbele
yangu.
Kichwa cha joka lile kilikuwa na upanga mfano wa ule wa jogoo, macho
yake yalikuwa makali na yanayowaka kama ya simba. Joka lile la kutisha lili?kuwa likiteleza taratibu kushuka chini ya mti ule na kuufanya mti ule utikisike
pamoja na ardhi yote ya eneo lile. Kwa kweli niliogopa sana kwani sikuwahi
kukumbwa na hofu ya namna ile katika maisha yangu. Wakati lile joka likishu?ka kitendo hicho kiliambatana na upepo mkali uliovuma eneo lile na kuzifanya
nyasi zote zilale chini.
Hadi kichwa cha joka lile kinafika chini ya ule mti mrefu sehemu ya mkia
wake ilikuwa bado haijaonekana. Muda mfupi uliofuata nikaliona joka lile
likija upande wangu pale nilipokaa, sikuweza kuhimili kuendelea kulitazama
kwani hofu ilikuwa imenifika kikomo na nguvu zilikuwa zimeniishia kabisa
kwa hofu hivyo niliinamisha kichwa changu na kuanza kusali nikimuomba
Mungu aipokee roho yangu bila pingamizi. Nilipomaliza tu sala yangu fupi
yenye ushawishi wa kila namna niliusikia upepo mkali ukinifikia eneo lile na
hapo nikakunja miguu yangu na kujikunyata.
Nikiwa na hesabu sekunde chache tu kusubiri joka lile linimeze mzimamzi?ma nilishangaa kuona muda unaenda bila ya chochote kutokea na hali hiyo
ikanipelekea nifumbue macho kutazama mbele yangu. Loh! lile joka lilikuwa
tayari limenifikia ila cha ajabu halikuniona, likapita juu yangu na kunifunika
kwa tumbo lake. Nilisikia harufu mbaya sana iliyonifanya nijihisi kutaka ku?tapika, tumbo lote la lile joka lilipita juu ya kichwa changu ikabidi niinamishe
kichwa na kujikinga kwa mikono.
Lile joka liliendelea kupita juu yangu na niliendelea kusubiri kwa muda
mrefu kwani lilikuwa refu sana, urefu ambao sikuwahi kuuona kwa nyoka wa
aina yoyote tangu nizaliwe. Ule upepo mkali bado uliendelea kuvuma eneo
lile. Nikaendelea kujikunyata kwenye lile jiwe hadi lile joka lilipomaliza kupi?ta. Hata lile joka lilipomaliza kupita sikutaka hata kujitikisa badala yake nika?subiri muda kidogo upite ndiyo nikayafumbua tena macho yangu.
Nilipoitazama mikono yangu ile sehemu niliyojikinga na tumbo la joka lile
ilikuwa imechunika sana kiasi cha kutengeneza vidonda vikubwa vya michu?buko vinavyotoa damu. Tusi zito likaniponyoka mdomoni hata hivyo bado
sikuamini kama nilikuwa nimesalimika na joka lile. Nikageuka na kujisogeza
pembeni ya lile jiwe kutazama kule lile joka linapelekea. Kwa kweli lilikuwa
ni joka la aina yake duniani, ile sehemu lile joka lilikopita miti na majani yote
vilikuwa vimelala chini kama njia ya nyasi iliyofyekwa. Ile sauti ya mvumo
wa upepo mkali sasa ilikuwa ikipotelea kule bondeni lile joka lilipokuwa lik?ielekea.
Nilivuta pumzi kwa wingi na kuzishusha taratibu huku nikijihisi kuwa
mwenye bahati sana katika maisha yangu. Sikujua nilipata wapi nguvu ili?yonifanya niweze kunyanyuka na kusogea kwenye ule mfereji mdogo na
hapo nikanywa mafunda kadhaa ya maji kwa pupa nikitumia viganja vyangu,
nikanawa maji mengine kichwani na usoni kurudisha uchangamfu wa mwili
na akili yangu hata hivyo nilikuwa bado nikitetemeka.
Ni wakati nilipokuwa nikiendelea kunawa pale nilishtushwa na sauti ya
mlio wa risasi ukitokea upande ule lile joka lilipoeleka. Nikashtuka na ku?jibanza kwa chini huku nikiusikiliza vizuri ule mlio wa risasi. Kwanza mlio wa
zile risasi ulianza kusikika kwa mbali lakini kadiri muda ulivyokuwa ukizidi
kwenda ndivyo ile sauti ya mirindimo ya risasi ulivyozidi kusikika. Niliyatega
vizuri masikio yangu na hapo nikasikia sauti nyingine ya makelele ya mbwa
waliokuwa wakilia kiwogawoga kule msituni lile joka lilipoelekea.
Wale mbwa waliendelea kulia kwa woga na ile milio ya risasi ikaende?lea kurindima halafu baada ya kitambo kifupi zile kelele za wale mbwa na
zile risasi zilikoma na msitu wote ukawa kimya. Kwa kweli niliona ni kama
mauzauza yalikuwa yakitokea kwenye msitu ule hivyo nikabaki nimeduwaa
nikishindwa kuelewa nini cha kufanya. Lakini muda mfupi uliofuata ule mdu?wao wangu ulikatishwa na sauti ya ajabu kama ile ya mwanzo kisha kukafua?tiwa na upepo mkali uliovuma kwa kasi ya ajabu katika msitu ule. Ulikuwa
upepo kama ule wa mwanzo na hapo nikafahamu maana yake kwani muda
uleule niliiona ile miti na majani yaliyokuwa mbele yangu vikilala chini na
haraka nikajua kuwa lile joka lilikuwa likirudi kwenye ule mti.
Sikutaka kuendelea kusubiri kwani nilifahamu fika kuwa bahati kama ile ya
awali isingenitokea tena hivyo nikainama chini na kuanza kukimbia kuelekea
upande mwingine wa bonde la ule msitu. Hata hivyo ile kasi ya ule upepo mka?li ilinifikia na kuniyumbisha na hapo nikawahi kuchagua mti mmoja mkubwa
uliokuwa jirani yangu na kujikinga dhidi ya upepo ule huku nikichungulia
kutazama kule nyuma lile joka lilikotokea.
Nilikuwa sahihi kabisa kwani lile joka lilikuwa likirudi kwenye ule mti am?bao bila shaka ndiyo yalikuwa maskani yake. Wakati lile joka likipita lile eneo
lote la ardhi lilikuwa likitikisika kwa kishindo na lilipoufikia ule mti likaanza
kuupanda na hapo ndipo nilipopata nafasi nzuri ya kuliona joka lile. Lilikuwa
joka kubwa sana linalotisha na mara tu lilipoanza kuupanda ule mti, ule mti
ukaanza kutikisika na kuangusha majani yake.
Niliendelea kujibanza nyuma ya ule mti huku nikitazama na kilichungu?za vizuri lile joka na hapo nikajua kuwa lilikuwa limemeza kitu kutokana na
namna ya tumbo lake lilivyotuna na hapo nikajikuta nikitabasamu kwa mara
ya kwanza katika msitu ule kwani nilifahamu kuwa lile joka lilikuwa limewa?meza wale mbwa waliokuwa wakibweka kule chini na bila shaka na wale watu
waliokuwa wakifyatua risasi ambao niliamini kuwa walikuwa wakililenga lile
joka kwani nilipolichunguza vizuri lile joka nikaliona kuwa lilikuwa na majer?aha yanayovuja damu katika baadhi ya sehemu za mwili wake.
Nilishusha pumzi huku nikimshukuru Mungu kwa kuniepusha kwa mara
nyingine na hatari ile. Nilipoendelea kilichunguza lile joka nikagundua kuwa
lilikuwa ni joka aina ya chatu wanaopendelea kuishi kwenye miamba mikub?wa na miti mirefu ama kwa lugha ya kiingereza wakifahamika kama African
Rock Python. Tabia zote za nyoka aina ya chatu nilikuwa nikizifahamu na
mojawapo ilikuwa ni ile ya kupenda kumeza mbwa na aina hii ya nyoka huwa
na uwezo mkubwa wa kuvuta na kuhisi harufu ya mbwa katika himaya yao na
mara nyingi mbwa wanapowaona chatu wa namna hii hata kama hao mbwa
ni wakali kiasi gani hufyata mkia na kujipeleka wenyewe kwa nyoka hawa.
Kwa mara nyingine nikawa nimesalimika kwani sasa nilifahamu kuwa wale
mbwa waliokuwa wakibweka kule chini ndiyo huenda walikuwa wale mbwa
wa wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda waliotuvamia kwenye ile nyumba
kule msituni ambao sasa nilikuwa nimefanikiwa kuwatoroka na hivyo waliku?wa wakinifuatilia kwa nyuma na wale askari. Na kama lile joka lisingeshtukia
uwepo wa wale mbwa na wale askari kule chini hiyo ilimaanisha kuwa huenda
lingenimeza pale kwenye lile jiwe nililojipumzisha huku nikiwa usingizini.
Niliendelea kulitazama lile joka likikwea juu ya ule mti huku nikiwa nime?jibanza nyuma ya ule mti na lilipomaliza kuukwea ule mti lile eneo lote lili?tulia na hata ule upepo uliokuwa ukivuma eneo lile ulitoweka na hiyo ndiyo
ikawa salama kwangu. Kwa uangalifu na tahadhari ya hali ya juu niliuacha ule
mti kisha nikaanza kushuka kwenye bonde la msitu ule taratibu huku moyo
ukienda mbio isivyo kawaida.
Nilipofika eneo la chini la lile bonde la ule msitu nilijihisi kuwa angalau
nilikuwa sehemu salama hivyo nikaanza kutimua mbio nitoka kwenye msitu
ule mzito na kuingia kwenye sehemu nyingine ya bondeni zaidi Iliyokuwa tambarare yenye msitu wenye miti yenye ukubwa wa wastani. Mwanga wa
mbalamwezi uliokuwa umeanza kujitokeza usiku ule ulinifanya nijihisi kama
ninayeonekana vizuri kutoka angani katika msitu ule huku nikiendelea kitimua
mbio na bastola yangu mkononi.
#75
MIALE YA JUA LA ALFAJIRI ILIPENYA kupitia uwazi mdogo uliopatikana
baina ya jani moja na jingine na hivyo kuanza kuyapa uhai macho yangu.
Nilishtuka toka usingizini na kabla sijayafumbua macho vizuri masikio yangu
yakapata ugeni mwingine wa nyimbo tofauti za ndege wa msituni. Nilifum-
bua macho yangu taratibu na kuanza kutazama na hapo nikakumbuka namna
nilivyoukwea mti huu mrefu usiku wa jana baada ya kukimbia zaidi ya mwen-
do wa masaa matatu tangu nilipoliona joka lile kubwa la kutisha kule msituni.
Baada ya kukimbia umbali mrefu usiku ule nilikuwa nimechoka sana na
nisingeweza kuendelea na safari yangu hivyo niliamua kuutafuta mti mmoja
mrefu ulioonekana salama zaidi katika eneo lile kisha nikaukwea na nilipofika
juu ya mti ule nikatafuta tawi zuri pacha na kulala nikisubiri pindi kutakapo-
pambazuka niendelee na safari yangu. Nilichokuwa nikikihitaji mara baada
ya kupambazuka ilikuwa ni kutafuta namna yoyote itakayoweza kunifikisha
jijini Kigali kwani nikiwa huko ndiyo ningeweza kuendelea na harakati zangu.
Alfajiri hii niliamka na nguvu mpya huku nikiwa najihisi nipo salama zaidi
ingawaje bado sikuweza kufahamu pale nilikuwa wapi kwani bado nilikuwa
katika msitu nisioujua mwanzo wala mwisho wake. Niliamka na kujinyoosha
viungo vyangu na hapo nikaanza kuhisi njaa kali tumboni. Nikiwa bado nipo
juu ya mti ule niliweza kuiona vizuri nchi ya Rwanda na namna misitu yake
ilivyoshonana na kustawi vizuri katika namna ya kupendeza. Kweli bara la
Afrika tulikuwa tumebarikiwa sana kwa rasilimali za kutosha kama misitu,
mito, madini mbalimbali, maziwa makubwa, mbuga na hata wanyama na vi-
umbe adimu wasiopatikana kwingineko duniani. Lakini bado lilikuwa ni jam-
bo la kushangaza sana kuwa maendeleo ya nchi zetu ni madogo sana pamoja
na rasilimali hizo tulizojaliwa huku viongozi wetu wakijitapa kuwa tunapiga
hatua.
Nikiwa pale juu ya ule mti nilitazama huku na kule bila kuona dalili yoyote
ya kuwepo makazi ya binadamu eneo lile na hali hiyo ikanitahadharisha kuwa
kwa vyovyote bado ningehitajika tena kutembea umbali mrefu sana kabla ya
kukutana na makazi yoyote ya wenyeji mahali ambapo ningeweza kupata
msaada wa kuelekea jijini Kigali ambako hadi wakati huu sikujua jiji hilo lil-
ikuwa upande gani toka pale nilipokuwa. Sikuona sababu ya kuendelea kukaa
pale juu ya ule mti hivyo niliamua kushuka chini na kuanza tena safari yangu,
safari nyingine ya msituni iliyojaa tumaini jipya la kufika jiji la Kigali nikiwa
salama salimini na baadaye kuanza tena harakati zangu.
__________
NILIKUWA NIMETEMBEA KWA MUDA WA KUKADIRIKA usiopun-
gua masaa mawili huku nikiwa najihisi kuchoka sana bila ya kuona dalili zo-
zote za uwepo wa makazi ya binadamu katika safari yangu. Mara mbili au
tatu nilijikuta nikikutana na wanyamapori katika maeneo fulani mle msituni
ambapo niliwakwepa na kuendelea mbele na safari yangu. Nilifika sehemu
fulani yenye vichaka hafifu na hapo nikawa nimechoka sana kwani kichwa ki-
likuwa kikiniuma pengine ni kutokana na njaa kali niliyokuwa nayo tumboni.
Kwa kweli sikuwa na nguvu zaidi za kuendelea na safari hivyo niliamua kuta-
futa sehemu salama chini ya mti mmoja mkubwa uliokuwa eneo lile na hapo
nikaamua kuketi nikipumzika huku nikiutumia muda huo kupanga mbinu
nyingine za kujiokoa toka katika hali ile.
Nikiwa bado nimepumzika chini ya mti ule ghafla kwa mbali niliweza
kusikia sauti ya mvumo wa kitu fulani, kwa kweli hofu ilinishika sana hasa
nilipolikumbuka lile joka kubwa nililoliona kule msituni ambalo kabla ya
kuliona lilikuwa limetanguliwa na sauti ya mvumo wa ajabu na kisha kufuati-
wa na upepo mkali. Nilisimama na kuyatega vizuri masikio yangu nikisikiliza
sauti ile ya mvumo kwa makini na hapo nikagundua kuwa sauti ile ya mvu-
mo niliyokuwa nikiisikia wakati huu haikuelekea kufanana na ile sauti ya lile
joka nililoliona kule msituni lakini vilevile sauti ile pia haikuwa ngeni sana
masikioni mwangu ingawaje bado sikuwa na hakika nayo sana. Niliendelea
kuisikiliza sauti ile ya mvumo kwa makini na hatimaye nikaamua kuanza sa-
fari taratibu nikielekea upande ule ile sauti ilipokuwa ikisikika.
Kiasi cha umbali wa kama maili moja hivi nikawa nimetokezea kwenye
eneo fulani tambarare lisilokuwa na miti mirefu wala vichaka vya kutisha. Ni-
lipopenya kwenye vichaka vile mbele yangu nilifurahi sana kuiona barabara.
Ilikuwa barabara ya lami na kwa kweli nilifurahi sana kwani kupitia barabara
ile nilijua kuwa kwa vyovyote ingeweza kunifikisha jijini Kigali au katika mji
wowote wa karibu sehemu ambapo ingekuwa rahisi kwangu kupata usafari wa
kuelekea jijini Kigali, mji mkuu wa nchi ya Rwanda.
Nilisogea kando ya barabara ile na kujibanza kichakani. Kwa mtazamo wa
haraka nilipoichunguza vizuri barabara ile nikagundua kuwa haikuwa baraba-
ra iliyokuwa na pilikapilika sana na kama ingekuwa ni kule nchini Tanzania
ningeweza kuifananisha barabara hii na ile barabara ya kutoka Chalinzehadi
Segera au ile barabara ya kutoka eneo la Makambakohadi Songea mjini.
Kwa muda mrefu nikiwa nimejibanza pale kichakani kando ya ile barabara
yalikuwa yamepita magari matatu, gari moja dogo na mawili yakiwa ni malori makubwa ya shirika linalohusika kuhudumia wakimbizi duniani liitwalo UN-
HCR (Commissaire des Nations Unies pour les Réfugiés) Niliyatambua malori
yale kutokana na nembo kubwa iliyokuwa ubavuni mwa malori yale yenye
maandishi makubwa yaliyoandikwa UNHCR.
Sasa niliweza kuelewa kuwa sauti ile ya ule mvumo niliyokuwa nikiisikia
kule kule msituni muda mfupi uliyopita wakati nilipokuwa nimeketi chini ya
ule mti ilikuwa ni sauti ya injini ya gari. Hata hivyo sikuweza kuelewa kuwa ni
upande upi ungekuwa sahihi kunifikisha jijini Kigali japokuwa yale malori ya
shirika la misaada la wakimbizi duniani yalikuwa yemenipa maarifa kidogo.
Nilikumbuka kuwa nchi ya jirani na Rwanda yaani jamhuri ya kidemokra-
sia ya Kongo hapo kabla ikiitwa Zaire ilikuwa katika mgogoro mkubwa wa
vita vya wenyewe kwa wenyewe. Waasi wa nchi hiyo walikuwa wakipigana
vita ya msituni kuiondoa serikali iliyokuwa madarakani ya rais Mobutu Sese
seko Kuku Ngbendu wa Za Banga. Mapigano hayo yalikuwa yamefikia hat-
ua mbaya ya kupelekea maelfu ya raia wa nchi hiyo kuyakimbia makazi yao
na hivyo kupelekea janga kubwa la njaa na umaskini uliokithiri huku mamia
ya raia wa nchi hiyo waliokuwa wakiyakimbia mapigano hayo wakipoteza
maisha kwa vita na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na homa ya
matumbo.
Hivyo kwa haraka niliweza kuhisia kuwa huenda malori yale ya UNHCR
yalikuwa yakipeleka misaada ya kibinadamu kwa raia wa nchi hiyo baada ya
umoja wa mataifa kupata taarifa za machafuko hayo. Kwa dhana hii iliyoum-
bika kichwani mwangu niliona kuwa nisingekuwa sahihi kuufuata uelekeo ule
wa yale malori ya UNHCR yalipokuwa yakielekea badala yake nikaona ni
heri ningeushika ule uelekeo wa yale malori yalipokuwa yakitokea ambako
niliamini kwa vyovyote ndiyo ungekuwa uelekeo sahihi wa kuelekea jijini
Kigali japokuwa sikuwa na hakika sana.
Nilikiacha kile kichaka nilichojibanza kando ya ile barabara na kuingia
barabarani nikishika ule uelekeo wa yale malori yalipokuwa yakitokea huku
nikiwa na matumaini ya kupata lifti kwa msamaria mwema yoyote ingawaje
kila nilipofikiria niliona kulikuwa ugumu wa kupata msaada wa namna hiyo
katika mazingira kama yale kwani mtu yoyote angeweza kunitilia mashaka
kwa kuniona nikiwa peke yangu katika mazingira yale hata hivyo sikutaka
kujikatisha tamaa.
Sasa nilikuwa nikitembea kandokando ya ile barabara kuufuata ule uelekeo
niliouona kuwa ungenifikisha jijini Kigali na wakati nikitembea nilikuwa
makini kila mara kutazama gari lolote lililokuwa likitokea nyuma na mbele
yangu. Na pale nilipohisi kuwa nilikuwa na mashaka na gari fulani lililokuwa
likija nilichepuka haraka na kuingia kichakani kujificha na gari hilo lilipop-
ita nilirudi barabarani na kuendelea na safari yangu. Yale malori makubwa
ya UNHCR yalikuwa yakinipita kuelekea uelekeo ule nilikotoka na yaliku-
wa mengi kwa kadiri nilivyoyahesabu na yalikuwa yakisindikizwa kwa ulinzi
mkali wa askari wa umoja wa mataifa waliovaa sare maalumu.
Baada ya safari ndefu ya kutembea kando ya barabara ile nilianza kukata
tamaa ya kupata lifti kwani kila gari lililokuwa likija nilijitahidi kulipungia mkono kulisimamisha lakini lilinipita bila ya kusimama na wale madereva
waliosimama walinisikiliza kidogo na bila kunisemesha wakatia mwendo na
kuendelea na safari zao. Kwa kweli nilikata tamaa sana lakini sikuwa na nam-
na hivyo bado niliendelea kutembea nikiwa na tumaini hafifu sana la kupata
lifti.
Tambua kuwa tatizo kwangu halikuwa kutembea ila kutembea nikiwa na
njaa kali tumboni kwani kadiri muda ulivyokuwa ukienda hali yangu ilikuwa
ikizidi kuwa mbaya. Ilifika wakati nilikuwa nimechoka sana na hapo nikatam-
bua kuwa nisingeweza kuendelea na safari yangu nikiwa katika hali ile hivyo
nikapanga kuwa ningetembea mbele kidogo na kutafuta mti uliokuwa kando
ya barabara na kujilaza huku nikisubiri lolote la kutokea litokee kwani hadi
wakati huu nilikuwa nimetembea muda wa zaidi ya masaa matatu.
Nilikuwa nipo mbioni kukata tamaa pale nilipokiona kibao fulani kidogo
kando ya barabara. Nilikitazama kibao kile nikayasoma maelezo yake vizuri.
Japokuwa maelezo yale yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kifaransa lak-
ini niliweza kuyaelewa kuwa yalikuwa yakielekeza kuwa baada ya mwendo
wa kilometa kumi mbele yangu kulikuwa na mgawanyiko wa barabara. Na kutokana na alama ya barabarani iliyokuwa kwenye kile kibao barabara moja
ilikuwa ikichepuka kuelekea upande wa kushoto kuelekea kwenye mji fulani na nyingine ilikuwa imechepuka upande wa kulia kuelekea jijini la Kigali, na
katika sehemu hiyo ya mgawanyiko wa hizo barabara kulikuwa na mji mdogo.
Nilirudia kuyasoma maelezo kwenye kibao kile cha barabarani huku nikijisikia
kufarijika sana na hapo nikajikuta nikipata nguvu mpya ya kuendelea
na safari yangu hadi sehemu hiyo yenye huo mgawanyiko wa hizo barabara.
__________
NILIFIKA KATIKA MJI ULE NIKIWA HOI TAABANI kwa uchovu lakini
nilifurahi sana. Ulikuwa ni mji mdogo wa barabarani uliyochangamka kiasi
ukipambwa kwa mandhari ya vibanda vidogovidogo vya biashara vilivyoku-
wa kandokando ya barabara ile vikitumika na wenyeji wa eneo lile kuuzia
nyama pori za kila aina. Vilevile kulikuwa na baa mbili tatu na ni katika baa
hizo ndimo wale madereva wa yale magari ya masafa marefu walikoweka
kituo kidogo wakipata vyakula na vinywaji kabla ya kuendelea na safari zao.
Nilipofika pale niliyakuta baadhi ya yale malori makubwa ya shirika la
misaada kwa wakimbizi ama UNHCR yakiwa yameegeshwa kandokando
ya barabara kuelekea uelekeo ule nilikotokea. Vilevile kulikuwa na malori
mengine tofauti na mgari ya kawaida ya watu binafsi hasa wazungu na baadhi
ya magari hayo yalikuwa yakielekea ule uelekeo wa jiji la Kigali kutokana na
namna yalivyoegeshwa.
Hakuna mtu yeyote aliyeonekana kushughulika na mimi wakati nilipokuwa
nikiingia katika mji ule mdogo. Zile bastola nilikuwa nimezificha maungoni
mwangu ili mtu yoyote wa eneo lile asinitilie mashaka. Ilinichukuwa muda
mfupi tu kuweza kujichanganya na watu wa eneo lile bila ya mtu yoyote kunit-
ilia mashaka ingawaje nilikuwa makini sana kuichunguza kila sura ya mtu iliyok-
uwa ikikatisha mbele yangu huku nikijaribu kuifananisha sura hiyo na wale
askari wa Kanali Bosco Rutaganda. Lugha kubwa zilizokuwa zikizungumzwa
na watu wa mji ule zilikuwa ni lugha ya kinyarwanda na kifaransa na jamii
ya watu wachache waliosalia walikuwa wakizungumza lugha ya kiingereza
kibovu.
Nilizunguka eneo lile nikiyachunguza mazingira ya pale lakini vilevile ni-
kiwa natafuta namna ya kuniwezesha kufika jijini Kigali ingawaje mfukoni
sikuwa na hata shilingi. Njaa ilikuwa ikiniuma sana lakini cha ajabu baada
ya kuingia kwenye mji huu furaha niliyokuwa nayo ilinifanya nisahau ile
njaa yangu kwa muda. Kwa kuwa mahali pale palikuwa ni kituo muhimu
cha kupumzikia madereva nilijua kuwa nisingeshindwa kuwapata madere-
va wanaotokea nchini kwangu Tanzania kwani nilifahamu kuwa watanzania
mwenzangu wangeweza kunisaidia kwa wepesi zaidi kuliko madereva wa
nchi nyingine.
Baada ya zunguka zunguka ya hapa na pale katika mji ule mdogo nikawa
nimefanikiwa kuyaona malori mawili makubwa yenye sahani ya namba za
usajili za nchini Tanzania yakiwa yameegeshwa katika namna ya kuelekea
jijini Kigali. Nilipoyachunguza vizuri malori yale nikagundua kuwa yalikuwa
yamebeba mifuko ya sukari na yalikuwa yamefunikwa kwa maturubai makub-
wa yaliyoandikwa kwa maandishi makubwa MTIBWA SUGAR COMPANY
LIMITED-TANZANIA chini ya maandishi hayo kulikuwa na anwani ya kiwan-
da, namba ya simu na sanduku la posta.
Nilifurahi sana na hata kabla sijayaendea malori yale nilianza kuhisi kuwa
nilikuwa nimekutana na ndugu zangu. Nikalisogelea lori moja kati ya yale
malori mawili na kusimama kando yake huku nikisubiri mtu yoyote ambaye
angekuja kwenye lori lile ambaye angeonekana kuwa mhusika nimueleze shi-
da yangu.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Haikuwa hivyo hadi pale yalipofika majira ya mchana ndiyo nikawaona
watu wawili wakitoka kwenye baa moja ya jirani na eneo lile na kuliendea
lile lori nililokuwa nimesimama jirani nalo. Mmoja miongoni mwa watu wale
alikuwa mwanaume mtu mzima kiasi mwenye umri kati ya miaka arobaini
na nane hadi hamsini na mbili kwa mwonekano na mwenye kifua kilichotuna
misuli imara ambapo nilipomchunguza vizuri nilimhisi kuwa huenda ndiye
angekuwa dereva wa lile lori. Yule mtu mwingine alikuwa kijana mdogo tu
wa miaka ya ishirini na mwanzoni lakini mrefu na mwenye umbo lililokomaa
sana tofuati na umri wake. Nikaamua kumfuata yule mtu aliyeonekana kuwa
ni dereva wa lile lori wakati alipokuwa akijiandaa kufungua mlango wa lori
lile.
“Habari za kazi mzee” nilimsalimia mzee yule huku nikiumba tabasamu la
kirafiki usoni na hapo akageuka na kunitazama kwa mshangao bila kuzung-
umza neno.
“Salama” hatimaye aliitikia huku bado akiwa kwenye mduwao.
“Naitwa Martin Tesha, mimi ni dereva wa basi la kampuni ya Tawaqal
liendalo nchini D.R Congo, kwa bahati mbaya tumeharibikiwa na basi letu
wakati tulipoanza safari asubuhi ya leo tukitokea hapa Rwanda kwenda huko
D.R Congo. Nimeona ninyi ni watanzania na madereva wenzangu hivyo huenda
mkanipa msaada. Nataka nifike jijini Kigali nikawasiliane na meneja wa
kampuni yangu aliyeko jijini Dar es Salaam niangalie kama nitaweza kupe-
wa msaada wa basi jingine” nilimdanganya yule mzee na bila shaka uwongo
wangu ulielekea kumkolea mzee yule kwani taratibu nilianza kumuona aki-
tabasamu na wakati nikiongea naye nilimuona yule kijana aliyeelekea kuwa
utingo wa lori lile alikuwa amesogea pale dirishani kunisikiliza.
“Oh! poleni sana, kwa dereva yoyote wa masafa marefu lazima ayafahamu
matatizo ya barabarani, mmeharibikiwa wapi? yule mzee aliniuliza kwa kun-
ishtukiza kwani nilikuwa sijajiandaa kwa swali la namna ile hivyo nikaituliza
akili yangu na kufikiria kidogo.
“Eneo moja la porini sipajui panaitwaje ila si mbali sana, ni kama mwendo
wa maili arobaini kutoka hapa” nilidanganya na hapo yule mzee akanitazama
kwa udadisi kabla ya kuniuliza tena
“Una kitambulisho cha kazi? lilikuwa swali jingine la mtego lililofanikiwa
kuniyumbisha na kunifanya nianze kukata tamaa ya kupata msaada wa lif-
ti. Nikajidai kujipekuapekua mifukoni kama mjinga huku nikijua fika kuwa
hakuna ninachokitafuta kwani mimi sikuwa dereva wa basi la Tawaqalingawa-
je nilikuwa nikifahamu kuwa baadhi ya mabasi ya kampuni ya usafarishaji ya
Tawaqal yalikuwa yakifanya safari zake kutoka jijini Dar es Salaam kwenda
mji wa Lubumbashi nchini Congo.
“Oh! nitakuwa nimekisahau ndani ya basi, loh! kweli nimefanya haraka
sana” nilidanganya
“Sasa dereva mkubwa kama wewe unasahau vipi kitambulisho, huoni kuwa
hilo linaweza kuwa ni tatizo?. Kwanza si unafahamu kuwa sheria za barabara-
ni haziruhusu kuzidisha watu kwenye magari ya namna hii?. Ni afadhali kido-
go ingekuwa usiku lakini wakati wa mchana askari wa barabarani wa nchi hii
ni mwiba mchungu sana hasa kwa wale madereva wa nchi za jirani. Vilevile
uaminifu siku hizi hakuna, unaweza ukamsaidia mtu kumbe ndiyo umembeba
nyoka mwenye sumu kali ukashangaa njiani amekugeuka. Siku hizi vitendo
vya utekaji na uporaji wa magari barabarani vimeshamiri” yule mzee alin-
iambia na maelezo yake yalikuwa sahihi kabisa ingawaje kwangu hayakuwa
mahali pake kwani nilichokuwa nikikihitaji ni kufika jijini Kigali na baada ya
hapo kila mtu angefuata hamsini zake.
“Ni kweli mzee hata hivyo najilaumu sana kwa haraka nilizozifanya hadi
nikasahau kuchukua kitambulisho na hata leseni yangu. Tafadhali naomba
mnisaidie ndugu zangu” niliongea huku nikimshawishi mzee yule kwa macho.
“Ingia ndani” hatimaye aliniambia
“Nashukuru sana” nilimwambia yule mzee huku nikifungua mlango na
kuingia ndani ya kibini ya lile lori. Mle ndani nilisalimiana na yule kijana ali-
yeonekana kuwa utingo wa lile lori kisha nikapita na kukaa nyuma ya ile siti
ya dereva mahali kulipokuwa na kitanda kidogo cha kupumzikia.
“Sasa kijana kila tutakapowaona askari wa vizuizi barabarani itabidi ujifiche
usionekane vinginevyo ukigundulika utatutia matatizoni na kutupelekea tulipe
faini ya pesa nyingi sana”
“Ondoa shaka mzee wangu” nilimwambia yule dereva huku nikiyafurahia
sana maelezo yake kwani kwa maana nyingine sikutaka kuonekana na askari
yoyote wa barabarani kwani mpaka sasa nilikuwa simwamini mtu yoyote.
Nilikuwa kama Mbogo aliyejeruhiwa na sikutaka tena mzaha na mtu yoyote
ambaye angeniwekea uzibe kwenye safari yangu hii ya kijasusi.
Injini ya lori iliwashwa na safari ikaanza huku kila mmoja akionekana kuza-
ma katika fikira zake. Mimi binafsi nilikuwa nikijaribu kuunganisha matukio
yoyote yaliyonitokea tangu nilipoingia nchini Rwanda. Kwa kweli mlolon-
go wa matukio ulikuwa mrefu sana na kulikuwa na mwanya mdogo sana wa
uhusiano wa tukio moja hadi jingine na hali hiyo ilizidi kukikoroga kichwa
changu hata hivyo niliamini majibu ya maswali yangu wengi yaliyokuwa ya-
kiiyumbisha akili yangu ningeweza kuyapata nikifika jijini Kigali.
Safari iliendelea na mle ndani ya lori nikawa nimefanikiwa kuwashawishi
yule dereva na utingo wake kuchangia maongezi yangu ambayo kwa kiasi
kikubwa walionekana kuyapenda. Hivyo baada ya muda mfupi tu tukawa tu-
mezoeana vizuri mle ndani kiasi cha kutaniana kirafiki na kuongea mambo
mengi yaihusuyo nchi yetu ya Tanzania kama siasa, utani wa makabila, tama-
duni zetu na mambo ya uchumi. Na kama zilivyo tabia za Watanzania wengi
kupenda undugu, urafiki na ukarimu yule dereva na utingo wakanikaribisha
chakula hivyo nikala na kushiba vizuri huku nikisukumia kwa maji ya kunywa
yaliyokuwa kwenye galoni iliyokuwa pembeni ya ile siti ya dereva.
Kwa kweli nilijisikia nipo nyumbani Tanzania tena ni kama niliyekuwa
nimekutana na ndugu zangu wa karibu sana niliyopoteana nao kwa muda mre-
fu. Maongezi ya hapa na pale yakaendelea baina yetu mle ndani huku kila
mmoja akicheka kwa kadiri alivyojisikia. Muda mfupi baadaye nilipitiwa na
usingizi na kilichofuata sikukifahamu.
__________
SIKUJUA TULIKUWA TUMESAFIRI UMBALI GANI tangu safari yetu
ilipoanza ila kilichonishtua usingizini ni baada ya kuhisi kuwa lile lori nililo-
panda lilikuwa likipunguza mwendo. Nikashtuka usingizini na kufumbua ma-
cho huku nikiwatazama wale wenyeji wangu na hapo nikagundua kuwa wote
walikuwa wameyaelekeza macho yao kuvitazama vioo vikubwa vya ubavuni
mwa lori lile ama side mirror kama watu wengi walivyozoea kuviita.
Utingo wale lile lori alikuwa akitazama kioo cha upande wa kushoto karibu
na dirisha alipokaa na yule dereva naye akitazama kioo cha upande wake.
Nikajikuta nikishikwa na wasiwasi juu ya tukio lile la dereva na utingo wake
kuvitazama vile vioo vya ubavu wa lile lori kwa makini hivyo nami nikainama
taratibu nikikitazama kile kioo cha upande wa dereva ambacho kilikuwa kari-
bu zaidi na pale nilipoketi.
“Vipi kuna tatizo? niliwauliza dereva na yule utingo baada ya kuhisi sioni
vizuri kupitia kile kioo na hapo wote wakashtuka na kugeuka kidogo wakinita-
zama na hapo nikajua kuwa bila shaka walikuwa wakihisi kuwa bado nilikuwa
nimelala na hawakuwa wakijua kuwa tayari nilikuwa nimeshtuka toka uzin-
gizini. Hata hivyo dereva yule na utingo wake hawakuongea neno badala yake
niligundua haraka kuwa sura zao zilikuwa na mashaka. Bila kupoteza muda
niliwaona tena yule dereva na utingo wake wakirudia tena kutazama kwenye
vile vioo na hapo yule dereva akavunja ukimya.
“Nahisi kuna gari linatufuatilia nyuma yetu” yule dereva aliniambia na hapo
nikahisi kuwa kwa kiasi fulani alikuwa ameanza kuwa na wasiwasi na mimi na
hali hiyo ikanipelekea nijihisi ni kama niliyemwagiwa maji baridi usingizini.
“Una hakika gani? nilimuuliza yule dereva huku nikisogea karibu zaidi ku-
litazama lile gari kupita kile kioo cha ubavu wa dereva.
“Ni zaidi ya umbali wa kilometa kumi tangu nilipolishtukia lile gari kuwa
linatufuatilia” utingo wa lile lori alidakia, nikageuka kumtazama kwa makini
na hapo nikajua kuwa alikuwa na hakika na alichokuwa akikizungumza.
“Kila ninapo ongeza mwendo lile gari nalo huongeza na ninapopunguza
mwendo nalo hufanya hivyo hivyo” dereva aliongea na maneno yake niliyao-
na ni kama yanayonilenga mimi.
“Hebu ongeza mwendo” nilimwambia huku macho yangu yakitazama kwa
makini kwenye kile kioo. Dereva akanisikia na muda ule ule akaingiza gia na
kukanyaga pedali ya mafuta na hapo lori likaanza kutimua mbio.
“Hebu tazama” yule dereva aliniambia na nilipochunguza vizuri nikaliona
gari dogo aina ya Nissan Patrol lenye rangi ya kijeshi nyuma yetu likiwa nalo
linaongeza mwendo kutufuata nyuma yetu. Wasiwasi ukaniingia pale nilipo-
kumbuka kuwa gari kama hili lilikuwa ni kama lile lililokuwa likinifuatilia
siku ya kwanza tu nilipoingia jijini Kigali nikitokea Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa kweli nilianza kushikwa na wasiwasi kwani kwa vyovyote nilifahamu
kuwa aliyekuwa akifuatiliwa pale ni mimi na si dereva wala utingo wa hili lori.
Nikapiga mahesabu ya haraka huku nikishindwa kuelewa nini cha kufanya.
“Bila shaka umejionea mwenyewe bwana” dereva aliniambia
“Nimeona, sasa ninyi mnadhani hilo gari linashida gani na sisi?
“Tutajua vipi, sisi wenyewe tumeshikwa na wasiwasi kama wewe”
“Au labda ni watekaji? niliwauliza na hapo nikamuona yule dereva na utin-
go wake wakigeuka kunitazama.
“Labda…” utingo alinong’ona huku akionesha wasiwasi.
“Sasa tutafanyaje? dereva aliuliza huku akionekana tayari keshaingiwa na
hofu.
“Ipo namna ya kufanya hebu ongeza mwendo kwanza” nilimwambia yule
dereva huku akili yangu ikiwa imeanza kufunguka.
“Itasaidia nini bwana, huoni kuwa hata wao wataongeza mwendo kama sisi?
“Nataka tuwe na hakika kuwa ni kweli tunafuatiliwa” maneno yangu yali-
kuwa na tija kidogo kwani nilimuona yule dereva akiongeza mwendo tena na
alipofanya hivyo tu nililiona lile gari nyuma yetu nalo likitimua mbio kutu-
karibia. Sasa nikawa na hakika kabisa kuwa gari lile dogo nyuma yetu lilikuwa
likitufuatilia na hapo nikageuka kuwatazama yule dereva na utingo wake.
“Hamna silaha yoyote humu ndani? niliwauliza
“Mh! hatuna silaha ya maana humu ndani, tuna nondo na panga tu, unadhani
linaweza likawa ni gari la watekaji? yule utingo aliniuliza na kwa kweli siku-
wa na jibu la kumwambia na badala yake nikabaki kimya nikiendelea kulitaza-
ma lile gari dogo namna lilivyokuwa likitukaribia kwa kasi isiyo ya kawaida.
Ghafla muda uleule nikaliona lile gari nyuma yetu likiongeza mwendo na
kutupita, nikawahi kuegemea nyuma kwenye ile siti yangu nikijibanza ili
yeyote aliyekuwa kwenye lile gari asinione lakini niliweza kuwaona wale
watu waliokuwa mle ndani ya lile gari.
Ndani ya lile gari kulikuwa na jumla ya watu wanne yaani dereva wa lile
gari na mtu mwingine aliyekaa siti ya pembeni yake na kwenye ile siti ya
nyuma iliyofuata kulikwa na watu wengine wawili hivyo kukamilisha idadi
ya watu wanne ndani ya gari lile na wote wakiwa wamevaa sare za kijeshi.
Lile gari lilipokuwa likitupita yule mtu wa mbele aliyeketi pembeni ya dereva
alitoa mkono dirishani akimuashiria dereva wetu asimame.
Nilimtazama dereva wetu nikamuona kuwa alikuwa ameielewa vizuri ishara
ile lakini hakuelekea kutaka kusimama kwani ndiyo kwanza nilimuona akiin-
giza gia kuongeza mwendo huku akilisogelea lile gari dogo kama anayeku-
sudia kuligonga ubavuni ili lipinduke. Hata hivyo dereva wa lile gari dogo
alikuwa mwepesi kuelewa kitendo kile hivyo akamkwepa dereva wetu kwa
kuongeza mwendo wa gari lake zaidi na muda huohuo nikasikia mlio wa risasi
zikivurumishwa kulenga ile kibini ya lori letu. Vilio vya hofu vikasikika mle
ndani, dereva na utingo wake wakahamanika kwa hofu lakini mimi sikuwa na
hofu yoyote kwani risasi nilishazizoea.
“Inameni chini” nilipaza sauti na wote mle ndani wakanisikia na kuinama
chini. Lile lori letu likapoteza mwelekeo na kuanza kuyumbayumba lakini
dereva wetu alikuwa makini kulidhibiti. Akawahi kukanyaga breki na hapo
lile lori likaanza kuserereka na kuacha barabara likiingia porini na hatimaye
likasimama huku injini yake ikiendelea kuunguruma. Eneo lote la mahali pale
likawa limetawaliwa na harufu kali ya msuguano wa lami na magurudumu ya
lile lori.
Nilikuwa wa kwanza kunyanyua kichwa changu na kutazama kule mbele
barabarani na hapo nikaliona lile gari dogo Nissan Patrol lililokuwa likitupita
likiwa limesimama hatua chache mbele yetu na wale watu waliokuwa mle
ndani tayari walikuwa wameshuka wakiwa kwenye sare zao za kijesni na bun-
duki zao mkononi.
Niliwatazama wale watu mbele yetu na sura ya mtu mmoja miongoni mwao
haikuwa ngeni sana machoni kwangu na nilipoyatuliza vizuri mawazo yan-
gu nilimkumbuka vizuri mtu yule. Alikuwa ni yule mwenyeji wetu katika ile
nyumba ya kule porini aliyejitambulisha kwetu kwa jina la Innocent Gahizi,
mwindaji katika msitu ule. Kumbukumbu ya sura yake ilikuwa bado imehi-
fadhiwa vizuri kichwani kwangu na wakati huu nilishangaa kumuona mtu yule
akiwa amevaa sare za kijeshi.
Nilijitazama na kukumbuka kuwa nguo zote nilizovaa mwilini zilikuwa zake
kwani nilikuwa nimeziiba kwenye kile chumba chake ndani ya ile nyumba
kule msituni. Nikajua endapo angeniona lingekuwa fumanizi la aibu lisiloku-
wa na nafasi ya kujitetea. Nikiwa bado nimejibanza huku nikiwatazama wale
watu mbele yetu mara niliwaona wakianza kuja pale liliposimama lori letu.
“Wanakuja” yule kijana utingo wa lori alinong’ona baada ya kuchungulia
mbele.
“Sasa tunafanyaje? dereva aliuliza kwa mashaka
“Nyie shukeni na muwasikilize, hawawezi kuwadhuru lakini msiseme kuwa
kuna mtu yoyote mliyemchukua humu ndani” niliwasisitiza.
“Jiandae kutusaidia bwana kwani huenda wakatushambulia” yule dereva
aligeuka na kuniambia kwa sauti ya kunong’ona akinitahadharisha kisha yeye
na yule utingo wakafungua milango na kushuka. Niliwahi kumshika yule dere-
va mkono wakati akifungua ule mlango na kushuka, nikamwambia
“Nakutahadharisha kuwa usizungumze kuwa mimi nipo humu ndani kwani
wakijua hivyo mjue hata nyinyi hamtokuwa salama” yule dereva akageuka
kunitazama usoni kama mtu aliyeshangazwa na maneno yangu kisha akautoa
mkono wake kwa pupa halafu akafungua mlango na kushuka chini.
Mimi nikiwa nimebaki mle ndani peke yangu sikutaka kusubiri. Nyuma ya
ile kibini ya lori kulikuwa na mlango mdogo wa dharura ama emergence door
hivyo nikasogeza pazia dogo lililokuwa pale kwenye ule mlango kisha nikau-
sukuma ule mlango na hapo ukawa umefunguka kwa nyuma. Bila ya kupoteza
muda nikajipenyeza kwenye ule mlango wa dharura na baada ya muda mfu-
pi nikawa nimetokezea upande wa nyuma wa ile kibini na kuangukia juu ya
gunia la mkaa lililokuwa eneo lile.
Kwa haraka nikasimama na kuliruka lile gunia la mkaa kisha nikakanyaga
kwenye tenki la mafuta la lile lori halafu nikapanda juu na kujitupia ndani ya
tela la lile lori lililosheheni mifuko ya sukari na hapo nikajipenyeza kwenye
kona ya lile tela na kujifunika kwa ile mifuko ya sukari, lakini kulikuwa na
uwazi mdogo ulioniwezesha kuona kule mbele kwenye ile kibini.
Baada ya kitambo kifupi nikawaona wale watu waliovaa zile sare za kijeshi
wakizungumza na dereva na yule utingo wake katika lugha ya ukali kama
wanaowafokea. Kisha niliwaona wale watu kama wanaowataka yule dereva
na utingo wake kuwa wawape kitu fulani ambacho yule dereva na utingo ha-
wakuwanacho kwa pale chini, hivyo wote kwa pamoja wakaanza kuongozana
wakija kwenye kibini ya lile lori.
Wakati lile tukio likiendelea niliwaona watu wawili miongoni mwa wale
watu wanne waliovaa sare za kijeshi wakichepuka na kuja kulizunguka lile
tela la lori kwa nyuma. Wale watu wakaanza kuinama inama wakilikagua lile
lori nami ikabidi nijiweke tayari kwa lolote. Yule mtu mmoja ambaye nilim-
kumbuka kuwa ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu kule msituni akawa amebakia
na yule dereva wa lori na yule utingo wake na hapo akaichomoa bastola toka
kiunoni mwake na kumtaka yule dereva atangulie kuingia ndani ya ile kibini
ya lori na yule utingo asimame pale chini. Hapo nikajua yule mtu alitaka ku-
fanya upekuzi mle ndani ya ile kibini. Yule dereva wa lori akafungua mlango
wa kuingia ndani ya kibini akifuatiwa kwa nyuma na yule mtu niliyemfahamu
kama mwenyeji wetu wa kule msituni.
Ukapita muda wa kama dakika kumi bila ya yule dereva wa lori wala yule
mtu aliyeingia naye mle ndani kutoka kwenye ile kibini. Baadaye nilimuona
yule dereva wa lori akitangulia kushuka huku nyuma yake akifuatiwa na yule
mtu hatari. Wote walipomaliza kushuka chini nikamsikia yule mtu akiwauliza
yule dereva na utingo wake kwa pamoja
#117
“Mna hakika kuwa hamkumchukua mtu yoyote njiani?
“Hatujamchukua mtu yoyote kwani tunajua hata sheria za barabarani haz-
ituruhusu kufanya hivyo” yule dereva akaongea kwa msisitizo huku akioneka-
na kuwa mwenye mashaka.
Wale askari waliochepuka kuja kukagua nyuma ya lile tela walipekua kila
mahali huku wakifunua turubai lililokuwa limefunika ile mifuko ya sukari
hata hivyo hawakuwa watundu katika kufanya upekuzi hivyo hawakuyagun-
dua maficho yangu. Baadaye niliwaona wakiondoka na kuelekea kule mbele
na sikuweza kuwaona tena kwani walikuwa wamehamia upande mwingine.
Mimi niliendelea kujibanza mle ndani ya lile tela nikisikilizia huku bastola
yangu ikiwa tayari mkononi.
Haukupita muda mrefu mara niliwaona yule dereva wa lori na utingo wake
wakiingia ndani ya ile kibini ya lori kisha milango ikafungwa na haukupita
muda mrefu baada ya pale nikaanza kuisikia injini ya lile lori ikianza kuungu-
ruma. Muda mfupi baadaye lile lori lilianza kuondoka na kuingia tena baraba-
rani na hapo safari ikaanza tena.
Niliendelea kujibanza mle ndani ya tela hadi pale nilipohisi kuwa tuliku-
wa tumesafiri umbali mrefu wa safari yetu ndiyo nikaanza kutoka mle ndani
nikielekea kwenye ile kibini huku nikiwa makini kutazama nyuma kama lile
gari Nissan Patrol lilikuwa bado likitufuatilia. Sikuliona tena lile gari na hali
ile ilinipa furaha sana. Nilipofika kwenye ile kabini nikasimama juu ya lile
gunia la mkaa huku nikiufungua ule mlango mdogo wa dharura na baada ya
muda mfupi nikawa nimefanikiwa kurudi mle ndani ya kibini na kukaa ma-
hali pangu. Macho yenye hofu na mashaka ya utingo na yule dereva wa lori
yalinipokea bila kusema neno kisha yakageuka na kutazama mbele na hapo
nikafahamu kuwa ile hali ya urafiki ilishatoweka mle ndani na isingekuwa
rahisi kuirudisha haraka.
“Wale watu ni kama waliokuwa wakikutafuta wewe bwana kwani una shida
gani? yule dereva aliniuliza huku akionekana mwenye mashaka na mimi.
“Nilitarajia hivyo” nilimwambia yule dereva na jibu langu bila shaka lili-
washtua wote na hivyo kuwapelekea wageuke tena kunitazama kwa tuo kisha
wakageuka tena kutazama mbele.
“Kwa sababu gani unasema hivyo bwana? yule utingo aliniuliza
“Unajua kabla ya kuharibikiwa na basi letu kuna kituo kimoja cha njiani
nilisimamishwa na askari wa barabarani na hawakunikuta na kosa lolote hata
hivyo walikataa kuniruhusu eti mpaka niwape kitu kidogo. Sikuwapa pesa
yoyote na kwa hasira nikawasha gari na kuondoka nikiendelea na safari hivyo
nilijua tu askari wale wangenifuatilia. Nahisi watakuwa wameambiwa na wale
abiria kuwa mimi nimeelekea jijini Kigali kutafuta msaada hivyo wakaona
wanifuatilie na kunibana huku huku njiani wakiamini kuwa kwa vyovyote nina
pesa. Nimemkumbuka yule askari uliyeingia naye humu ndani kuwa alikuwa
miongoni mwa wale askari walionisimamisha kule njiani” nilimaliza kuongea
huku nikiupima uzito wa uwongo wangu kama ungekuwa rahisi kukubalika
hata hivyo sikuona kama uwongo wangu uliwaingia yule dereva na utingo
wake kwani nilikuwa ni kama ninayejiongelesha mwenyewe.
“Wanasema wewe ni mtu hatari unayesakwa kile pembe ya hii nchi” yule
utingo alidakia
“Toka lini mtu anayekataa kutoa rushwa akawa ni mtu hatari katika nchi?,
achana nao wale wana njaa zao. Ni kawaida kwa askari wa barabaani wa nchi
hii kudai rushwa hususani kwa madereva wasio wazawa” nilijaribu kujitetea
huku nikifahamu kuwa sikuwa na hoja ya msingi ya kujitetea lakini kukaa
kimya sikuona kama ingefaa, hata hivyo hakuna aliyeunga mkono utetezi
wangu.
“Ulikuwa umejificha wapi ?, nilikuwa na wasiwasi sana wakati yule askari
alipotaka kuingia humu ndani ili ajiridhishe kuwa hakukuwa na mtu tuliyem-
chukua” yule dereva aliniuuliza akiingiza gia na kukanyaga mafuta.
“Nilijua tu kuwa kwa vyovyote wale watu wangetaka kujiridhisha kwa ku-
fanya upekuzi humu ndani ndiyo maana niliwahi kutoka kwa kupitia mlango
wa dharura wa hii kibini na kwenda kujificha nyuma kwenye tela huku nikiji-
funika kwa ile mifuko ya sukari”
Niliendelea kuongea na wakati huu pia si utingo wala yule dereva aliyeo-
nekana kuvutiwa na maelezo yangu na hapo ukimya ukachukua nafasi yake
na mimi sikupenda tuendelee na maongezi yale. Niligeuka kutazama dirishani
nikaona kuwa kulikuwa na wingu zito limetanda angani na hapo nikajua kuwa
muda si mrefu mvua kubwa ingeanza kunyesha. Safari iliendelea na lile lori
lilikuwa likitimua mbio sana.
Mle ndani hakuna aliyekuwa na hamu ya maongezi yangu tena na mimi
nilipenda tuwahi kufika jijini Kigali ili kila mtu ashike hamsini zake. Nilitaka
kuuliza kuwa muda gani ungekuwa umesalia kabla ya kufika jijini Kigali la-
kini nilisita kufanya hivyo kwani huenda swali langu lingenifanya nionekane
kuwa sikuwa dereva niliyeifahamu vizuri barabara ile hivyo niliegemea siti
yangu vizuri nikawa nikitazama nje huku usingizi ukiwa mbali na mimi.
WALINISHUSHA PEMBENI YA KITUO kikubwa cha kujazia mafuta kili-
chokuwa katikati ya jiji la Kigali ikiwa tayari imekwishatimia saa kumi na
mbili jioni. Manyuyu hafifu ya mvua yalikuwa bado yakianguka toka angani
na giza nalo lilikuwa mbioni kushika hatamu. Niliwashukuru sana yule dereva
na utingo wa lile lori huku nikiwaahidi kuwa ningewatafuta baada ya kurudi
nchini Tanzania, na wakati nikiwaaga niliziona nyuso zao zikirudiwa na fura-
ha iliyotoweka kwa muda mrefu. Hapo nikajua furaha yao ilikuwa si kwa kwa
sababu walitaka tuonane tena hapo baadaye ila ni kwa sababu hawakupenda
kuwa na mimi na hilo halikunipa shida kwani mpaka pale walikuwa wameni-
saidia sana na sikuwa nahitaji msaada wao tena.
Baada ya kushuka kwenye lile lori na kuagana na yule dereva na utingo
wake nilisimama kando ya barabara ile nikiliacha lile lori likitoweka mbele
yangu kisha nikavuka barabara nikiwa mwenye tumaini jipya katika harakati
zangu. Sasa nilikuwa nimefika jijini Kigali.
Nikiwa na hakika kuwa hakuna mtu yeyote eneo lile aliyekuwa akizifuatilia
nyendo zangu tangu niliposhuka kwenye lile lori nilivuka barabara nyingine
upande wa kushoto na hapo nikaingia kwenye njia ya watembea kwa miguu.
Sikufahamu hasa ni wapi nilipaswa kuelekea ambapo ningeweza kutuliza
kwanza fikra zangu na kujipanga vizuri kabla ya kuanza tena harakati zangu
hata hivyo niliamini kuwa ingekuwa rahisi kupata jibu la swali hilo huku niki-
wa bado natembea kuliko nikiwa bado nimesimama eno lile.
Wakati nikiendelea kutembea nilijikuta nikifikiria kurudi kule chumbani
kwangu Hotel des Mille Colline hata hivyo nilipozidi kufikiria nilijikuta niki-
liweka wazo hilo kando kwanza kwani niliamini kuwa wale watu walioniteka
hadi wakati huu wangekuwa wakifahamu kila kitu kuhusu mimi ikiwemo ho-
teli niliyofikia na hata namba ya chumba changu na kwa kuwa nilikuwa nime-
watoroka kwa vyovyote sehemu ya kwanza ambayo wangenisubiri ingekuwa
ni kule chumbani kwangu hotelini. Hivyo sikuona kama ningekuwa nikifanya
uamuzi sahihi endapo ningeamua kufikia kule hotelini.
Nilifikiria niende kule Kigali Casino nikaonane na Mutesi hata hivyo wazo
hilo nalo pia sikuliona kuwa kama lingekuwa muafaka kwa kipindi kile hasa
nilipoanza kuhisi kuwa upo uwezekano kuwa huenda nisingemkuta Mutesi
wakati ule kwani nilikuwa sizifahamu vizuri ratiba zake na vilevile sikuwa na
hata pesa kidogo mfukoni ambayo ingeniwezesha kununua mzinga mmoja wa
pombe ambao ungetumika kuyasindikiza maongezi yetu. Hivyo wazo hilo pia
nililiweka kando huku nikifikiria mpango mwingine mzuri zaidi.
Wakati nikiendelea kufikiria nikajikuta nikiyakumbuka maelezo ya Ros-
ine wakati ule tulipokuwa pamoja kule kwenye ili nyumba katikati ya msitu.
Nikiwa nayakumbuka vizuri maelezo yake Rosine kuwa yeye na dada yake
aliyekuwa akiitwa Diane walikuwa wakiishi kwenye nyumba moja miongoni
mwa nyumba za shirika la nyumba la taifa la Rwanda eneo liitwalo Block C
nyumba namba 11 na nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mume wa dada
yake aitwaye Jean Felix Akaga. Pia nilikumbuka kuwa huyo Diane na huyo
mumewe Jean Felix Akaga walikuwa wameuwawa hivyo katika familia hiyo
mtu pekee aliyesalia alikuwa Rosine. Na hadi wakati huu nilikuwa sifahamu
kuwa Rosine alikuwa wapi tangu tulipopoteana kule msituni, huenda angeku-
wa ametekwa na kuuwawa au labda angekuwa ametoroka, sikufahamu.
Kwa tathmini hiyo niliona kuwa sehemu salama ya kukimbilia kwanza in-
gekuwa ni huko Block C nyumba namba 11 na uamuzi wangu ukanipa faraja
kiasi huku nikiamini kuwa kama Rosine angekuwa amepata nafasi nzuri ku-
toroka toka kwa wale watu hatari kule msituni basi sehemu ya kwanza ambayo
angefikia ingekuwa ni kwenye hiyo nyumba. Na kwa maana nyingine hiyo
ingekuwa sehemu nzuri ya kuonana naye kwa mara nyingine huku tukiwa ni
wenye furaha na amani na mambo mengine yote yangefuatia baada ya hapo.
Mpango huu ukanipelekea nitabasamu na kuingiza mkono mmoja mfukoni
mwa suruali na sasa kilichobaki ilikuwa ni kupeleleza na kulijua hilo eneo la
Block C na sehemu ilipo nyumba namba11.
Niligeuka nyuma kutazama nikaona hakuna mtu yeyote aliyekuwa akini-
fuatilia kwani kila mtu alionekana kupita na hamsini zake hivyo nikaendelea
kufarijika huku nikizitupa hatua zangu ndefu kuifuata ile barabara ya watem-
bea kwa miguu. Nilifika mbele kidogo sehemu kulipokuwa na jengo dogo
la shirika la posta na hapo nikakunja kona na kuifuata barabara iyelekeayo
upande kushoto huku nikifurahishwa na namna jiji la Kigali lilivyojengwa
kwa mpangilio unaovutia. Kwa wakati huu kila sehemu ya jiji ilionekana
kuchangamka na watu walionekana kukusanyika katika baadhi ya sehemu
za starehe. Biashara ndogo ndogo za barabarani zilikuwa zikiendelea kama
kawaida na hata maduka makubwa yalikuwa wazi huku yamerembwa kwa
mabango makubwa ya taa za aina tofauti zinazopendeza. Jiji la Kigali lilikuwa
limechangamka na pilikapilika za watu zilikuwa mbioni kushamiri.
Niliendelea kutembea katika barabara ile huku nikipishana na watu wa aina
tofauti hata hivyo nilikuwa makini sana kuzichinguza nyuso za watu nili-
opishana nao. Nilipofika mwisho wa barabara ile nikawa nimetokezea kwenye
kituo cha mabasi madogo yanayoelekea maeneo tufauti ya jiji la Kigali. Ku
likuwa na kundi kubwa la abiria waliokuwa wakisubiri usafiri wa kuelekea
maeneo yao. Kufikia hapo nikakumbuka kuwa sikuwa na pesa yoyote mfukoni
na pia nilikuwa silifahamu hilo eneo la Block C lilikuwa wapi toka pale nili-
pokuwa.
Nilifika sehemu fulani na kusimama pale kwenye kituo cha mabasi madogo
huku nikijaribu kumtafuta mtu wa kumuuliza ambaye angekuwa tayari ku-
nielekeza. Baada ya kuchunguza chunguza nikawa nimemuona mzee moja
aliyeonekana kuwa muungwana na mwenye ufahamu mzuri wa jiji la Kigali
hivyo nikaaza kumsogelea lakini kabla sijamfikia nikapata wazo jingine baada
ya teksi fulani kuja na kusimama pembeni yangu.
Dereva wa teksi ile alikuwa kijana wa miaka ishirini na kitu hivi, aliposim-
amisha teksi pembeni yangu akatoa kichwa dirishani na kuniuliza kwa lugha
ya kinyarwada
“Amakuru? sikuweza kumjibu kwani nilikuwa siifahamu lugha ya kinyar-
wanda ingawaje nilikuwa nimehisi kuwa alikuwa akiniuliza “Habari za saa
hizi”. Nikamtumbulia macho kijana yule na nilipomuona kuwa hanielewi
nikaongea kwa lugha yangu mama ya kiswahili.
“Nipeleke eneo liitwalo Block C, unapafahamu?
“Ugiyehe? akaniuliza kwa kinyarwanda yaani “Unaenda wapi?” kama am-
baye hajanisikia vizuri.
“Block C” nikarudia kusema kwa sauti ya juu kidogo yenye msisitizo.
“Uri umushyits? akaniuliza akimaanisha “Wewe ni mgeni hapa?”
“Block C” nikasisitiza huku nikimwona ananichanganya na kinyarwanda
chake.
“Uri u mtanzania? akaniuliza tena yaani akimaanisha “Wewe ni mtanzania?”
“Ndiyo” nikamjibu “Nataka unipeleke eneo liitwalo Block C” nilimwambia
tena huku nikianza kukata tamaa.
“Ufite kibazoki? yule dereva wa teksi akatabasamu na kuniuliza tena
akimaanisha “Unashida gani?” Sikumjibu tena yule dereva wa teksi kwani
nilianza kumuona ni kama anayenipotezea muda wangu hivyo nikaacha kum-
tazama na kugeuka nikitazama upande mwingine huku nikijaribu kuchunguza
kama kulikuwa na teksi nyingine jirani na pale. Yule dereva wa teksi akawa
ameishtukia dhamira yangu hivyo haraka akapenyeza mkono wake kwa nyu-
ma na kufyatua kabari ya mlango.
“Ingia ndani my friend” yule kijana akaniambia kwa kiswanglish cha kin-
yarwanda, sikutaka kujivunga kwani sikupenda kuendelea kupoteza muda pale
na kuvuta macho ya watu. Nikafungua mlango na kuingia nyuma ya ile teksi
na muda uleule ile teksi ikaanza safari ikielekea sehemu ya kutokea magari ya
kituo kile cha mabasi madogo.
Tulipotoka nje ya kituo kile cha mabasi madogo tukaingia barabara ya
upande wa kulia na muda mfupi baadaye tukawa tukiuacha mtaa mmoja na
kuingia mwingine tukiendelea na safari yetu na mimi sikusahau wajibu wangu
hivyo kila mara nikawa nikigeuka nyuma kutazama kama kulikuwa na gari
lolote lililokuwa likitufungia mkia. Safari ilikuwa poa kwani sikuweza kuliona
gari lolote likitufungia mkia nyuma yetu na hivyo safari yetu iliendelea
Tuliwasili eneo la Block C dakika tano zikiwa mbele ya nusu saa kwa muji-
bu wa majira ya saa iliyokuwa kwenye dashibodi mle ndani ya gari. Tulikuwa
ndiyo tunaiingia eneo la Block C wakati nilipomtaka dereva asimame kando
ya barabara ile sehemu kulipokuwa na giza lilofanywa kwa vivuli vya miti ya
barabarani na teksi iliposimama tu nikafungua mlango na kushuka.
“Pesa yangu vipi ndugu? yule dereva aliniuliza kwa mshangao baada ya
kuniona nikishuka bila kumlipa. Sikumjibu badala yake nikaingiza mkono
wangu mfukoni na nilipoutoa nilikuwa nimeshika bastola, yule dereva alipoo-
na vile akawa naye ameshtuka na kunitazama kwa woga. Nikamsogelea karibu
na kumgusagusa shavuni kwa mtutu wa ile bastola na hapo akazidi kutetemeka
kwa hofu.
“Siku moja moja jifunze kujitolea”nilimuonya.
“Sawa ndugu” akanijibu kwa kihoro kama anayepigania roho yake usiuache
mwili.
“Potea!” nikamwambia na muda uleule akatia moto gari na kutokomea
mbele yangu. Nilitabasamu kidogo kisha nikairudisha bastola yangu mfukoni
na kupotelea kwenye vivuli vya miti iliyokuwa eneo lile na muda mfupi baa-
daye nikawa nimetokezea kwenye barabara ya mtaa wa pili.
Kulikuwa na bango kubwa katika barabara ile na bango hilo lilikuwa na
maandishi yaliyoandikwa kwa lugha ya kifaransa yakisomeka “Bien venu au
rendroir C” yaani “Karibu eneo la Block C” na hapo nikatabasamu taratibu
baada ya kuwa na hakika kuwa nilikuwa sijapotea. Sikuwa mgeni sana wa
lugha ya kifaransa kwani nilikuwa nimesoma kwenye shule ya sekondari ya
Milambo iliyopo mkoani Tabora nchini Tanzania. Shule hiyo ilikuwa ni mion-
goni mwa shule chache za serikali zilizokuwa zikifundisha somo la lugha ya
kifaransa nchini Tanzania ukiachilia mbali zile shule za watu binafsi ambazo
kwa idadi zilikuwa chache sana.
__________
ENEO LA BLOCK C LILIKUWA MIONGONI mwa maeneo yenye makazi
ya kisasa kabisa jijini Kigali, nyumba zake zilijengwa kwa mpangilio unaovu-
tia na barabara za lami zenye nguzo za taa pembeni. Wakatinikitembea katika
barabara ya mtaa ule nilihisi kama niliyekuwa nikionekana kwenye nyumba za
jirani hata hivyo suala hilo halikuyumbisha msimamo wangu.
Macho yangu yalizunguka kutazama kila nyumba ya mtaa ule na hadi nafika
mwisho wa ule mtaa geti la nyumba hiyo lilikuwa limeandikwa kwa lugha ya
kifaransa “Maison numero dix” yaani nyumba namba kumi, nikajua nyumba
namba kumi na moja ingekuwa ipo nyuma ya nyumba ile katika mtaa unao-
fuata. Hivyo nilikatisha kwenye uchochoro kuingia mtaa wa nyuma na safari
hii sikuhangaika kwani nyumba namba kumi na moja ilikuwa mbele. Hata
hivyo nilishangaa kuiona kuwa ilikuwa ni nyumba pekee eneo lile isiyokuwa
na uzio pia taa zake zilikuwa zimezimwa lakini hilo halikunishangaza kwani
nilifahamu kuwa wenyeji wa nyumba ile hawakuwepo.
Nilipofika nilizunguka nyumba ile nikaichunguza kama kulikuwa na dalili
za uwepo wa kiumbe chochote mle ndani. Niliporidhika kuwa mle ndani haku
wa na mtu yoyote nikazunguka nyuma na kuingia ndani kwa kupitia dirisha
la jikoni baada ya kukiharibu kitasa chake. Niliingia sehemu ya jikoni nika-
tokezea katika sebule ndogo yenye chumba cha kulia chakula pembeni yake.
Ile nyumba ilikuwa na samani za kisasa na hali hiyo ilinifahamisha kuwa
Jean Felix Akaga, mpelelezi wa kikosi maalumu kilichikuwa kikishughulika
na usalama wa rais wa Rwanda alikuwa ni mtu mwenye kipato cha kudhirisha.
IIikuwa ni nyumba yenye vyumba vitatu vya kulala, choo, maliwato, sebule
na sehemu ya jiko. Kwa muda mfupi nikawa nimeyazoea manzingira ya mle
ndani na kuridhika na usalama wake na hapo nikavua fulana yangu na kuitupa
sakafuni kisha nikaelekea vyumbani.
Nilianza kufanya upekuzi kwenye ile nyumba mle ndani na katika chumba
cha pili niligundua mle ndimo alimokuwa akiishi Rosine kwani mle ndani
nilifanikiwa kupata picha yake na zaidi ya hapo hapakuwa na kitu kingine cha
maana isipokuwa kabati moja liliyokuwa na nguo na lukuki ya vipodozi vya
kila namna. Chumba cha tatu na cha mwisho nilipowasha taa niligundua hara-
ka kuwa huenda kingekuwa ni chumba alichokuwa akiishi Jean Felix Akaga
na Diane. Ndani ya chumba kile sakafuni kulikuwa na zulia maridadi, kitanda
kipana na kizuri, makabati mawili ya nguo, seti moja ya runinga, meza ya
kusomea na kochi moja kubwa la sofa.
Niliyazungusha macho yangu mle ndani nikaziona picha mbili zilizokuwa
zimetundikwa ukutani, picha ya mwanamke na ya mwanaume. Nilianza kwa
kuitazama ile picha ya yule mwanamke na sikutaka kujiuliza kuwa yule aliku-
wa Diane yaani dada wa Rosine kwa namna walivyofanana. Kwa kweli Diane
alikuwa mzuri sana kama aliyokuwa mdogo wake, tabasamu lililochomoza
usoni mwake lilinifanya nijihisi ni kama ninayetazamana naye pale ukutani.
Niliitazama vizuri ile picha ya yule mwanaume nikaona ni kama niliyelinga-
na naye kwa umri, alikuwa amevaa suti nadhifu ya kijivu, shati jeupe na tai
shingoni.
Alikuwa mwanaume mwenye mvuto katika macho ya mwanamke yoyote
na sikuwa na mashaka kuwa ile picha ilikuwa ya Jean Felix Akaga. Kabla ya
kuendelea na udadisi zaidi niliyasogelea yale makabati na kulifungua mojawa-
po. Ndani ya kabati lile niliziona nguo za kiume zilizopangwa kwa unadhifu,
nilitabasamu kidogo baada ya kufikiria kuwa nilikuwa nimepata nguo za kuba-
dilisha. Nilisogea karibu na kioo cha kabati lile nikajitazama na kuridhika kwa
namna nywele na ndevu zangu zilivyokuwa na kuubadilisha kidogo ule mu-
onekano wangu wa wakati nilipokuwa nikiingia hapa jijini Kigali.
Kwa kitambo kidogo nilisimama mbele ya kioo kile nikijitazama bila akili
yangu kuwepo pale kwani mawazo juu ya Rosine yalikuwa yakianza kupita
upya kichwani mwangu na wakati huu nilianza kuhisi kupungukiwa na kitu
moyoni mwangu. Sijui ni kwanini nilikuwa nimetokea kumpenda sana Rosine
ingawa hapo nyuma niliwahi kukutana na wasichana wazuri wa kila sampuli
katika nchi tofauti tofauti nilizowahi kufika wakati nilipokuwa katika harakati
zangu za kijasusi.
Nilikumbuka wakati ule nilipokuwa na Rosine katika ile nyumba ya ma-
ficho kule msituni nikiwa nimelala juu ya kitanda kimoja na mrembo huyo
huku akiniruhusu kukitomasa tomasa kiuno chake na kuzifikicha chuchu zake
kifuani bila pingamizi lolote. Loh! kwa kweli hisia juu ya Rosine zilikuwa
zikinitafuna moyoni na sasa nilikuwa ndani ya nyumba hii bila yeye. Roho
iliniuma sana kwani sikufahamu kama Rosine alikuwa hai au mfu, na kama
alikuwa hai alikuwa wapi kwa wakati huu. Kwa kweli nilihisi upungufu wa
kitu fulani katika nafsi yangu.
Kwa muda wote ambao ningeendelea kuwepo nchini Rwanda nilikuwa
nimeazimia kuwa nyumba hii ingekuwa maskani yangu kwani sikuona sababu
ya kuingia gharama za kukaa kule hotelini, tena katika sehemu nisiyokuwa na
hakika ya usalama wake. Kitu cha kwanza nilichofikiria ilikuwa ni kuoga na
kubadilisha zile nguo zangu mwilini ambazo mpaka sasa zilikuwa chafu na
zinazonuka jasho. Hivyo nilivua nguo nikajifunga taulo nililolichukuwa mle
kabatini na kuingia bafuni.
Muda mfupi baadaye nilitoka bafuni na kujiandaa vizuri nikiwa na nguo
mpya na safi mwilini, nilipomaliza nilielekea kule jikoni na kufungua jokofu
lililokuwa na vyakula lakini vingi vikiwa vya kutoka kwenye maduka makub-
wa ya kisasa ama super market. Nikachukua pakiti mbili za soseji ya ng’ombe,
mayonaizi, vinega na karoti. Kulikuwa na trei moja ya mayai juu ya kabati la
vyombo lililokuwa mle jikoni hivyo nilichukuwa mayai mawili na kwa pamo-
ja nikatengeneza mlo kupitia jiko la gesi lilokuwa pale jikoni.
Ilikuwa imetimia saa nne kasoro usiku wakati nilipokuwa nimeketi mezani
kula. Nilijipatia mlo na kushiba vizuri kisha nikasukumia kwa mzinga mmoja
wa mvinyo mwekundu uliokuwa kwenye kabati la vinywaji lililokuwa mle
ndani pale sebuleni na wakati huo nilikuwa nimewasha runinga kubwa iliy-
okuwa pale ndani sebuleni nikitafuta stesheni inayorusha habari za nchi ya
Rwanda. Niligundua kuwa stesheni nyingi zilizokuwa zikipatikana kwenye
ile runinga zilikuwa zikirusha matangazo yake kwa lugha ya kifaransa huku
baadhi ya stesheni chache zikirusha matangazo yake kwa lugha ya kinyar-
wanda.
Hakukuwa na habari yeyote ya maana iliyonivutia katika stesheni niliyoi-
fungua isipokuwa stesheni moja tu iliyokuwa ikirusha habari kuwa rais wa
Rwanda Juvenal Habyarimana alikuwa amesafiri kwenda nchini Tanzania ku-
kutana na marais wengine wa nchi za ukanda wa maziwa makuu kuzungum-
zia masuala mbalimbali likiwemo suala la amani ya kudumu katika nchi ya
Rwanda na Burundi na masuala mengine ya kiuchumi. Taarifa zile ziliendelea
kueleza kuwa katika msafara huo wa rais kwenye ndege yake Falcon 50 Jet
angeambatana na mkuu wake wa majeshi Deogratias Nsabimana na mkuu wa
usalama wa rais Kanali Elie Sagatwa.
Nilipoitafakari taarifa ile nikajikuta nikifurahi kwa namna viongozi wetu
wa Afrika walivyokuwa wakishirikiana kama ndugu wa familia moja katika
kuziletea maendeleo nchi zao. Kisha vikafuatia vipindi vingine vya runinga
ambavyo havikuonekana kunivutia hivyo niliamua kuizima ile runinga pale
sebuleni. Nilihisi kuwa akili yangu ilikuwa imepata utulivu wa kutosha wa
kuweza kutafakari hili na lile na kutengeneza hoja zenye msingi na wakati nili-
pokuwa nikitafakari nikaikumbuka ile bahasha ya kaki niliyoichukua chini ya
godoro kwenye kile chumba cha mwenyeji wetu ndani ya ile nyumba iliyoku-
wa kule katikati ya ule msitu. Wazo hilo likanifanya ninyanyuke na kuelekea
kule chumbani nilipoiacha ile suruali yangu niliyotokanayo kule msituni am-
bamo ile bahasha ilikuwa ndani ya mfuko wa suruali hiyo.
Muda mfupi baadaye nikawa nimerudi na ile bahasha pale sebuleni na hapo
nikaketi kwenye kochi. Kabla ya kuifungua ile bahasha niliyapitisha macho
yangu nikiichunguza kwa juu hata hivyo sikufanikiwa kuona kitu chochote
mle ndani kwani ile bahasha ilifungwa kwa gundi kali na karatasi yake hai-
kuruhusu macho yangu kupenya na kuona ndani. Hivyo nikaichana ile baha-
sha kwa juu na kuchungulia ndani na hapo nikaiona karatasi yenye rangi ya
samawati. Mwanzoni nilipoichunguza ile karatasi haikuwa na maana yoyote
kwangu kwani sikuweza kuona chochote kilichoandikwa kwenye karatasi ile.
Hata hivyo mimi sikuwa mshamba wa karatasi za namna ile hasa pale nili-
pofikiria kuwa hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye angetumbuki-
za karatasi isiyo na kitu ndani ya bahasha na kuifunga kwa gundi kali namna
ile.
Baada ya kuigeuzageuza ile karatasi na kuichunguza vizuri nikajikuta niki-
tabasamu. Ilikuwa ni aina fulani ya karatasi inayotumiwa sana na majasusi ka-
tika kupashana habari. Karatasi ambayo ili kuweza kuyasoma maelezo ndani
yake nilihitajika niwe na kalamu ya grafati. Kupitia kalamu hiyo ningeilaza
ile karatasi juu ya meza au juu ya kitu chochote kilichonyooka vizuri halafu
baada ya hapo ningeanza kuichorachora ile karatasi huku nikiwa nimeilaza
kalamu hiyo ya grafiti katika pembe isiyozidi nyuzi ishirini na tano ili niweze
kupata taswira nzuri ya kilichoandikwa ndani ya karatasi husika. Kwa kawaida
karatasi ya namna hii zinapotumwa kwa mhusika hutumwa pamoja na kalamu
yake maalumu.
Kwa kulikumbuka hili nilizidi kuifungua ile bahasha na muda si marefu
kweli nikaiona kalamu ndogo ya grafiti iliyochongwa vizuri. Niliichukua ile
kalamu kisha nikachukua kitabu fulani kilichokuwa kwenye rafu pale sebuleni
na juu ya kitabu hicho nikailaza ile karatasi kisha nikaanza kuichorachora ile
karatasi kwa ule wino wa ile kalamu ya grafiti.
Mwanzoni nilidhani kuwa ile karatasi ingekuwa na mchoro fulani wa siri
ambao zingehitajika jitahada za kipekee katika kuutafsiri ili kuweza kuuele-
wa maana yake kwani mara nyingi karatasi za namna hii hutumika kupeleka
ujumbe kwa njia ya mchoro. Lakini kadiri nilivyokuwa nikizidi kuichorachora
karatasi ile nikawa naanza kuona herufi, nilipozidi kuchora zaidi herufi zile
zilianza kuunganika na kutengeneza sentensi fulani.
Niliendelea kuichora ile karatasi hadi mwisho na nilipomaliza nikaona mu-
unganiko wa sentensi kamili inayoleta maana ingawaje sentensi hiyo haikuwa
na maana kamili kwangu. Sentensi yote kwenye karatasi ile ilikuwa imeandik-
wa kwa lugha ya kifaransa ikisomeka,
“Mecred recontre avec elle en Halfmoon bar à 22:00hrs avant de nous com-
mencer, chaque chose est soyez bien”
Kwa kutuumia karatasi ileile nikaigeuza nyuma na kuanza kutafsiri neno
moja baada ya jingine kwa lugha yangu ya kiswahili na nilipomaliza nikawa
nimepata tafsiri kamili ya maneno yale ambayo yalimaanisha kuwa,
“Jumatano onana naye ndani ya Halfmoon bar saa nne usiku kabla hatu-
jaanza. Kila kitu kipo tayari”
Nilipomaliza kusoma sentensi hiyo moyo ulikuwa ukinienda mbio sana
na sikuweza kufahamu ni kwanini hali ile ilikuwa ikinitokea. Niliendelea
kuichunguza chunguza tena ile karatasi hata hivyo sikuweza kuliona jina la
mwandishi wala mtumiwaji wa ujumbe ule. Ila kwa kuwa nilikuwa nime-
ichukua ile bahasha toka chumbani kwa yule mwenyeji wetu aliyejinadi kwa
jina la Innocent Gahizi kwenye ile nyumba kule msituni hivyo niliamini kwa
vyovyote mtumiwaji angekuwa ni yeye.
Niliendelea kutafakari ujumbe ule kwenye ile karatasi bila kupata maana
yoyote kamili inayonipa picha ya nini kilichokuwa kikiendelea. Nilitembe-
za macho yangu kuitazama kalenda iliyokuwa imetundikwa pale sebuleni na
hapo moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu kwani siku ile ilikuwa ni siku ya
jumatano kwa mujibu wa kalenda ile ilivyoonesha, yaani siku ambayo ujumbe
ule ilikusudiwa kufanyiwa kazi. Nikageuka kuitazama saa ya ukutani pale se-
buleni, tayari ilikwisha timia saa tatu na robo usiku hivyo zilikuwa zimesalia
dakika arobaini na tano tu kutimia saa nne usiku muda wa miadi.
Nikavuta pumzi nyingi na kuitoa taratibu huku nikianza kuhisi kuwa kuliku-
wa na hatari kubwa iliyo kuwa mbele yangu endapo ningeamua kujitumbukiza
katika mkasa huu usioeleweka. Hata hivyo kulikuwa na kitu kilichokuwa kiki-
nisukuma moyoni kuwa nisimame na kuanza kuitafuta Halfmoon Bar. Kingine
kilichonisukuma kutaka kufuatilia mkasa huu ni pale nilipowaza kuwa kwa
vyovyote mtu aliyekusudiwa kuupata ujumbe huu hadi wakati huu alikuwa
bado hajausoma na kuuelewa maana yake kwani mimi ndiye niliyekuwa mtu
wa kwanza.
Hivyo nilikuwa na hakika kuwa ndani ya hiyo Halfmoon Bar huo muda wa
saa nne usiku kungekuwa na mtu fulani anayemsubiri huyo mtu mwingine am-
baye bila shaka mtu huyo anayesubiriwa ndiye huyo ambaye ujumbe huu uli-
kusudiwa kwake. Na kwa kuwa mhusika huyo alikuwa bado hajaupata ujumbe
huu asingeweza kufika kwenye miadi na badala yake mimi ndiyo ningeitumia
nafasi hiyo. Niliendelea kuwaza nikapiga moyo konde na kusimama. Akili
yangu yote sasa ilikuwa ni wapi ambapo ningeipata hiyo Halfmoon Bar hapa
jijini Kigali.
#118
NILIIACHA NYUMBA ILE NIKIWA NIMEZIMA TAA zote na kuweka
kila kitu mahali pake kama nilivyokuta. Mbali na hayo pia nilikuwa nime-
andika ujumbe mfupi kwenye karatasi ndogo niliyoiweka chini ya sabuni ya
kuogea bafuni. Karatasi hiyo ikimuuleza Rosine kuwa kama angefika mle
ndani ajue kuwa mimi pia nilikuwa pale kwenye ile nyumba hivyo aendelee
kunisubiri. Vilevile nilikuwa nimechukua namba ya simu ya ile nyumba ili
ikitokea kuwa endapo ningechelewe niweze kupiga simu kuuliza kama Ros-
ine angekuwa amefika. Sikujua ni kwanini nilisukumwa kuichukua namba ya
simu ya nyumba ile lakini bado nilikuwa na imani kuwa ningeonana tena na
Rosine kabla ya kifo changu hapa duniani.
Nilikuwa na kiasi kidogo cha pesa nilizozichukua toka katika droo ya kabati
kwenye kile chumba nilichohisi kuwa huenda walikuwa wakiishi dada yake
Rosine yaani Diane na mumewe ambaye sasa nilikuwa nikimfahamu kwa jina
Jean Felix Akaga. Wakati nikiiacha ile nyumba na kuingia mtaa wa pili nilir-
idhika na muonekano wangu mpya wa mavazi ya kawaida usioweza kuyavuta
macho ya mtu yoyote. Nywele na ndevu zangu zilikuwa zimekua kiasi cha
kuweza kuubadilisha muenekano wangu mbele ya macho ya mtu yoyote anay-
enifahamu na kofia niliyokuwa nimeivaa nilikuwa na hakika kuwa mtu yeyote
asingenigundua kirahisi.
Nilitembea kwa muda wa zaidi ya dakika kumi kutoka barabara ya mtaa wa
kwanza hadi ile ya mtaa wa pili kisha nilikunja kona kuelekea upande wa kulia
na mwisho wa barabara hiyo nikachepuka kuingia upande wa kushoto mah-
ali kulipokuwa na kichochoro kidogo chenye giza hafifu. Wakati nikitembea
niliweza kuziona baadhi ya nyumba zikiwaka taa kwa ndani kuashiria kuwa
wenyeji wa nyumba hizo walikuwa bado hawajalala.
Kichochoro nilichoingia kilinichukua hadi upande wa pili kulipokuwa na
barabara kubwa ya lami na nilipofika kwenye barabara hiyo niligundua kuwa
muda ulikuwa umesonga kutokana na uchache wa magari katika barabara ile.
Hali hiyo ilinitahadharisha kuwa ingekuwa vigumu kidogo kupata usafiri wa
mabasi ya umma wa kunifikisha maeneo ya katikati ya jiji ambapo niliami-
ni kuwa hiyo Halfmoon bar ingekuwa rahisi kujulikana. Hata hivyo sikukata
tamaa hivyo nilivuka barabara ile na kuanza kutembea kandokando nikiufuata
ule uelekeo wa barabara inayoelekea katikati ya jiji la Kigali.
Baada ya mwendo mfupi wa miguu nikawa nimefika eneo moja lililokuwa
na bar fulani kando ya barabara. Nje ya bar hiyo kulikuwa na teksi chache
zilizoegeshwa hivyo niliiendea taksi moja iliyokuwa imejitenga kidogo na
eneo lile. Dereva wa teksi ile alinipokea kwa bahasha zote na kunifungulia
mlango.
“Nipeleke ilipo Halfmoon bar? nilimwambia yule dereva bila kudadisi
kuwa alikuwa akielewa lugha ya kiswahili au lah!. Dereva ayatuliza macho
yake kama anayefikiria jambo kisha akatamka
“Sina hakika sana kama naifahamu hiyo bar lakini hilo jina siyo geni ma-
sikioni mwangu, nahisi hiyo bar ipo katikati ya jiji sehemu fulani, twende
tutauliza hatuwezi kupotea” yule dereva aliniambia katika lugha ya kiswahili
chenye lafudhi ya kikongomani, nikajua alikuwa ni mtu mwenye asili ya nchi
ya Congo. Hapakuwa na maongezi tena baina yetu wakati teksi ile ilipokuwa
akiymtia maegesho yake na kuingia barabarani kuufuata uelekeo wa mjini.
__________
TEKSI ILISIMAMA KIASI CHA UMBALI WA HATUA ISHIRINI kab-
la ya ilipo Halfmoon Bar eneo la Remera jijini Kigali. Wakati nilipoitupia
macho saa ndogo iliyokuwa kwenye dashibodi ya gari mle ndani nilifurahi
kuona kuwa zilikua zimesalia dakika kumi na mbili kabla ya kutimia saa nne
usiku. Moyoni nilimshukuru sana yule dereva wa teksi kwa kuwa mjanja wa
kuvijua vitongoji vingi vya jiji la Kigali. Hadi kufikia mtaa ule tulishavipita
vitongoji vingi vya jiji la Kigali kama vile Nyamirambo, Kicukiro, Kacyiru,
Kwa Rubangura, Nyabugogo, Jali, Nyarutama na vinginevyo vingi. Na tuli-
kuwa tumetumia muda mfupi mno kutokana na dereva yule kuwa na ufahamu
mzuri wa maeneo yale na vichochoro vyake. Ni katika kuulizauliza hatimaye
tukaelekezwa na mtu mmoja aliyekuwa akiifahamu vizuri Bar ile.
Nilimlipa dereva wa teksi pesa yake nikamshukuru na kushuka huku nikii-
acha teksi ile ikipotelea mitaani. Mtaa ule ulikuwa upo miongoni mwa mitaa
iliyokuwa ikithaminiwa vizuri na Meya wa jiji la Kigali. Ulikuwa ni mtaa
uliochangamka na wenye afya njema kama barabara pana ya lami iliyokatisha
katikati ya majengo marefu ya ghorofa, migahawa ya kisasa, maduka ya nguo
na ofisi za benki.
Halfmoon Bar ilikuwa kando ya jengo la benki ya taifa ya Rwanda hivyo
nilitembea nikalipita jengo lile la benki na kuelekea ilipo Bar ile na wakati
nikiikaribia ile Bar niliyaona magari mawili madogo yakiwa yameegeshwa
nje ya Bar hiyo. Sikuwa na shaka yoyote kuwa Halfmoon Bar ilikuwa ipo
kwenye orodha ya Bar za kisasa kabisa zilizokuwa jijini Kigali kutokana na
muonekano wake wa nje. Bango kubwa lenye maandishi yanayowaka taa
yakisomeka “Halfmoon Bar–Bien venu”-neno la kifaransa lenye maana ya
“Karibu Halfmoon Bar” liliamsha hisia mpya moyoni mwangu kuwa niliku-
wa nimefika eneo sahihi kabisa.
Wakati nilipokuwa nukiusukuma mlango na kuingia ndani ya Halfmoon
Bar nilipishana na watu wawili wapenzi, mwanamke na mwanaume waki-
wa wamekumbatiana viunoni. Niligeuka kidogo nikawatazama na hapo nik-
agundua kuwa walikuwa wamelewa sana kutokana mwendo wao wa kuyum-
bayumba na harufu kali ya pombe iliyopenya toka vinywani mwao baada ya
jaribio lao la kunisalimia kilevilevi kutofanikiwa vizuri.
Niliingia mle ndani ya Bar huku nikiuacha mlango ukijifunga taratibu nyu-
ma yangu na hapo nikajikuta nikitazamana na macho ya mhudumu mmoja
wa Bar ile aliyekuwa amesimama pembeni ya kaunta ya vinywaji. Sikupenda
kuonesha ugeni wa namna yeyote mle ndani hivyo nilichagua meza moja iliy-
okuwa nyuma ya mlango na kuketi. Mhudumu alipokuja nikamuagiza aniletee
kinywaji baridi kisicho na kilevi na wakati akiondoka nikapata wasaha mzuri
wa kuyatembeza taratibu macho yangu mle ndani.
Ile bar ilikuwa ya kisasa sana na yenye meza kumi na mbili kila meza moja
ikizungukwa na viti vitano vya mbao aina ya mkangazi. Ndani ya Bar ile
upande wa kulia kulikuwa na ukumbi mdogo wa muziki uliotenganishwa na
sehemu hii niliyokaa kwa pazia kubwa lililotengenezwa kwa simbi nyingi za
baharini zilizotungwa kamba nyembamba katikati. Taa za rangi tofauti zili-
kuwa zikimulika mle ndani na muziki laini wa rumba ya kilingala uliokuwa
ukitumbuiza taratibu.
Katika sehemu ile niliyokaa hapakuwa na watu wengi kwani ni meza saba
tu ndiyo zilizokuwa na wateja ambao wengi wao walionekana kuwa wapenzi
na meza mbili tu ndiyo zilionekana kukaliwa na mtu mmoja mmoja, zaidi ya
hapo sikuona sura yoyote ya kuitilia mashaka mle ndani.
Niliyazungusha macho yangu tena kwenye kuta za Bar ile nikitarajia kuiona
saa ya ukutani lakini sikufanikiwa kwani hakukuwa na saa yoyote mle ndani
na hali hiyo ikanifanya niikumbuke ile saa yangu ya mkononi iliyochukuliwa
na wale wanajeshi wa Kanali Basco Rutaganda kule mapangoni. Nilikilaani
sana kitendo kile kwani miongoni mwa vitu nilivyokuwa nikivijali sana katika
maisha yangu basi muda ulikuwa miongoni mwavyo. Hivyo nilibaki nimetulia
pale kwenye ile meza huku nikitafakari hili na lile hata hivyo niliendelea kuji-
fariji kuwa bado nilikuwa ndani ya ule muda wa miadi.
Mawazo yangu yakakatishwa na sinia dogo lililowekwa mbele yangu juu ya
meza likiwa na chupa moja ya kinywaji na bilauri moja ndefu. Mhudumu yule
akatabasamu kidogo na kunifungulia kinywaji
“Are you waiting for someone? yule mhudumu aliniuliza kwa lugha ya kiin-
gereza
“No” nikamjibu na kabla hajaondoka nikawahi kutumbukiza mkono mfu-
koni na kuchukua noti moja kisha nikampa kama malipo ya kinywaji kile.
Yule mhudumu aliipokea ile noti ya fedha ya kinyarwanda huku akionesha
kila dalili za kutaka kuendeleza maongezi na mimi lakini nilijitahidi kwa kila
namna kumkwepa kwani maongezi yangeweza kunoga na kunipotezea umak-
ini wa kazi yangu. Hivyo yule mhudumu alipoona kuwa sielekei kutengeneza
urafiki naye akachukua lile sinia la vinywaji na kuondoka zake na hapo mimi
nikamimina kinywaji kile kwenye bilauri na kuanza kunywa taratibu huku
macho yangu yakiweka kituo kwenye ule mlango kutazama kila mtu aliyeku-
wa akiingia ndani ya Bar ile.
Alikuwa ni mtu wa tano kuingia nyuma ya watu wanne waliotangulia kuingia
mle ndani tangu mimi nilipoingia ndani ya Bar ile wakati nilipoyazungusha
macho yangu na kumtazama msichana mzuri na mrembo ajabu aliyeongeza
idadi ya wasichana wachahe niliyowahi kuwaona katika harakati zangu. Msi-
chana yule alikuwa amevaa suruali nyeusi ya jeans iliyolichora vema umbo
lake la msichana wa kiafrika mwenye kiuno chembamba, mzigo wa makalio
ya wastani unaopendeza kwa mtazamaji na mapaja yenye minofu ya kutosha.
Matiti yake madogo yasiyokuwa na uwiano mzuri na umbo lake yalihifadhi-
wa vyema kifuani mwake kwa blauzi nyepesi na nyeupe iliyozionesha vizuri
chuchu zake nyeusi zilizotuna. Mkufu wake unaometameta uliizunguka vizuri
shingo yake ndefu na nyembamba ukipotelea katikati ya matiti yake. Mkufu
huo ulinishtua na kunifanya nimtazame usoni yule mrembo ambaye sasa nil-
ianza kuhisi kuwa hakuwa mgeni sana machoni mwangu. Nikajitahidi kukum-
buka sehemu nilipowahi kumuona hata hivyo akili yangu ilishindwa kuniletea
majibu ya haraka.
Mara baada ya kuingia ndani ya ile Bar yule msichana alisimama na
kuyatembeza macho yake taratibu kutazama kila meza iliyokuwa mle ndani na
wakati alipogeuka upande wangu mimi niliwahi kuishusha kofia yangu chini
kisha nikaikamata bilauri ya kinywaji na kugida mafunda kadhaa nikikiacha
kinywaji kile kikiteleza taratibu kooni mwangu kama mtu ambaye nimezama
katika hamsini zangu. Nilipoinua kichwa tena kumtazama yule mrembo ali-
kuwa tayari amegeukia upande mwingine wa Bar ile na hapo ndiyo nikapata
nafasi nzuri ya kuendelea kumchunguza. Miwani nyeusi aliyoivaa ikaninyima
nafasi nzuri ya kumdadisi ingawaje mara hii pia moyo wangu ulipiga kite kwa
nguvu ukunikumbusha kuwa sura yake haikuwa ngeni sana kwangu.
“Ni wapi vile nimemuona huyu mrembo? nilinong’ona kama bwege na
wakati huu zile kumbukumbu chache zilizosalia kichwani mwangu kuhusu
yeye ziliyeyuka kabisa na kuniacha katika mduwao wa kizembe. Nywele zake
halisi za kipilipili alikuwa amezikata katika mtindo wa kipekee kwa msichana
wa kiafrika uitwao Low cut ambao kwa kweli mtindo ule ulikuwa amezidi
kuupalilia uzuri wake wa urefu wa wastani, huku pochi yake nzuri ya ngozi
ikiongeza zaida katika mwonekano wake.
Kama mtu aliyeitarajia ishara fulani kutoka kwa mmoja wa watu walioke-
ti mle ukumbini hilo halikutokea na kwa namna moja au nyingine hali hiyo
ilionekana kumshangaza sana. Hisia tofauti zikaanza kuumbika kichwani
mwangu kuwa mtu niliyekuwa nikimsubiri huenda angekuwa ndiye yule mr-
embo aliyeingia.
Yule mrembo aliendelea kutazamatazama huku na kule mle ndani na ali-
poona kuwa kila mtu alikuwa akiendelea na hamsini zake akachagua meza
moja ya jirani na kuketi. Mhudumu alikuja na kumsikiliza na muda mfupi
baadaye niliona akipelekewa kinywaji lakini sikutaka kuamini kuwa kinywaji
kile ndiyo kitu kilichokuwa kimemleta ndani ya ile Bar. Wakati yule mrem-
bo akijipatia kinywaji taratibu nilimuona mara kwa mara akinyanyua mkono
wake kuitazama saa yake ya mkononi na kisha akigeuka na kutazama katika
ule mlango wa kuingia mle ndani ya ile Bar huku akionekana mwenye haraka
na wasiwasi.
Kulikuwa na watu waliokuwa wakiendelea kuingia mle ndani ya Bar na
vilevile walikuwepo pia watu wengine walioonekana kutosheka na starehe
zao na hivyo kuamua kuondoka, na suala hilo halikuonekana kutiliwa maanani
hata kidogo na mrembo yule. Badala yake aliendelea kuitazama saa yake ya
mkononi na baadaye kutazama pale mlangoni mara kwa mara.
Ulipita muda mrefu yule mrembo akiendelea na zoezi hilo na nilianza kuhisi
kuwa alikuwa mbioni kukata tamaa na hali ile. Mwishowe nilimuona akisi-
mama kisha akaelekea pale kaunta na wakati akielekea kaunta aliyatembeza
tena macho yake kuwatazama watu waliokuwa mle ukumbini. Muda mfupi
baadaye nilimuona akirudi kutoka kule kaunta huku akiufuata ule uelekeo wa
mlango wa kutokea na hapo nikatambua kuwa alitoka kule kaunta kulipa bili
ya kinywaji na sasa alikuwa akiondoka. Nikapata nafasi nyingine nzuri ya
kumchunguza wakati akitembea kuelekea nje na bado hisia zangu ziliendelea
kunieleza kuwa hakuwa mtu mgeni machoni mwangu.
Nilimalizia funda la mwisho la kinywaji kilichosalia kwenye bilauri yan-
gu na nilipoiweka bilauri ile mezani nikasogeza kiti nyuma na kusimama na
hapo nikaanza kuufuata ule mlango wa kutokea nje. Yule msichana mrembo
alikwishatoka nje na sikutaka aniache mbali sana hivyo nilipotoka tu nje nik-
agundua kuwa usiku ulikuwa umeshamiri. Kulikuwa na giza zito lililoashiria
kuwa mvua ilikuwa mbioni kunyesha tena hata hivyo kwa msaada wa taa za
barabarani zilizokuwa kando ya barabara kwenye nguzo ndefu, giza lile zito
liligeuka mchana kwa baadhi ya sehemu.
Nilishangaa kutomuona yule msichana pale nje hivyo nikawahi kuvuka
barabara upande wa pili uliotazamana na ile Bar na hapo nikumuona. Yule
mrembo alikuwa akitembea haraka haraka katika mtindo wa mashindano ya
urembo yaani Catwalk na sasa alikuwa ameshalipita lile jengo la benki ya taifa
la Rwanda. Nilimuona mara kwa mara akigeuka nyuma kutazama na mimi si-
kutaka kupoteza muda hivyo kwa haraka nikavuka tena ile barabara na kuanza
kumfuatilia kwa nyuma lakini katika namna ambayo nilikuwa na hakika kuwa
asingeweza kunishtukia. Alikuwa akijua namna ya kutembea haraka na aliku-
wa mwangalifu sana katika nyendo zake lakini hakuwa zaidi yangu. Alikuwa
zaidi ya umbali wa mita thelathini mbele yangu, umbali mzuri ulionifanya
niweze kujificha haraka kila alipokuwa akijiandaa kugeuka nyuma.
Alipofika mwisho wa barabara ya mtaa ule akaingia upande wa kulia akii-
fuata barabara nyingine ya lami iliyokatisha katikati ya mtaa mwingine wenye
maduka mengi ya nguo na baadhi ya sehemu nyingine za starehe. Alipofika
karibu na jengo la ukumbi wa sinema akasimama kidogo na kugeuka tena nyu-
ma akitazama katika namna ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na mtu yoyote
aliyekuwa akimfuatilia nyuma yake.
Aliporidhika kuwa hakukuwa na mtu nyuma yake akavuka barabara upa-
nde wa pili na wakati akifanya hivyo ghafla nililiona gari dogo aina ya Volvo
likiacha maegesho ya ukumbi ule wa sinema uliokuwa pale jirani na kuufuata
ule uelekeo wa yule msichana mrembo alipokuwa. Gari lile lilienda kusimama
hatua chache pembeni ya yule msichana mrembo na hapo nikaelewa ni nini
kilichokuwa kikiendelea mbele yangu. Lile gari liliposimama tu yule msicha-
na akafungua mlango wa nyuma na kuingia ndani na hapo safari ikaanza lile
gari likiufuata uelekeo wa barabara iendayo kando ya mji.
Lilikuwa tukio ambalo sikulitarajia na lilikuwa limeniacha katika mduwao
usioelezeka huku nikihisi kuwa nilikuwa nimezidiwa ujanja hata hivyo sikuta-
ka kukubaliana mapema na hali ile hivyo nikaharakisha kuyaendea maegesho
ya magari ya ule ukumbi wa sinema. Nilimkuta dereva mmoja wa teksi akiwa
tayari kwani alikuwa ameniona tangu nilipokuwa mbali nikiharakisha kuja
eneo lile.
Nilipoifikia teksi ile nikafungua mlango wa nyumba na kuingia na kabla
yule dereva hajaniuliza uelekeo wangu nikamwambia aifuate ile gari aina ya
Volvo iliyoondoka pale kwenye yale maegesho muda mfupi uliyopita. Dereva
yule alinielewa na bila shaka kumbukumbu ya uelekeo wa lile gari ilikuwa
bado ipo vizuri kichwani mwake kwani muda uleule akayaacha yale maegesho
na kuingia barabarani akiufuata ule uelekeo wa lile gari. Na wakati tukiondoka
eneo lile nilimuonya yule dereva kuwa awe mwangalifu ili watu waliokuwa
ndani ya lile gari mbele yetu wasiweze kutushtukia kuwa tunawafuatilia.
Muda mfupi baada ya safari yetu kuanza nikagundua kuwa nilikuwa nimem-
pata dereva mjanja na mwerevu anayevitambua vizuri vitongoji na vichochoro
vya jiji la Kigali. Nilifahamu hivyo baada ya kumuona akiiacha ile barabara
niliyoiona ile gari aina ya Volvo ikielekea kisha akakunja kona kuingia upande
wa kushoto. Nikataka kumuuliza ni kwanini alikuwa akifanya vile na wakati
nikijiandaa kumuuliza tukawa tumikwisha tokezea upande wa pili wa mtaa
mwingine katika barabara iliyokatisha katikati ya majengo marefu ya ghorofa.
Tulipofika kwenye mtaa huo yule dereva akakatisha tena kwenye barabara
hafifu iliyoonekana kutotumika sana. Barabara hiyo ilikatisha katika ya kituo
kidogo cha kujazia mafuta halafu mbele kidogo tukachepuka upande wa kulia
wa barabara hiyo ikituchukua moja kwa moja hadi mbele ya jengo la ofisi za
wizara ya mambo ya ndani ya nchini Rwanda. Tukawa kama tunaotaka kuto-
kezea mbele ya jengo hilo lakini tulipokuwa tukilikaribia dereva alichepuka
tena upande wa kushoto na barabara hiyo ikatuchukua muda mfupi tu kuto-
kezea mbele ya barabara nyingine ya lami ielekeayo kando ya mji, na wakati
tukikaribia kuifikia barabara hiyo mara tukaiona ile gari aina ya Volvo iliyom-
chukua yule msichana ikikatisha mbele yetu.
Nikashangaa sana na kumuuliza yule dereva kuwa alijuaje kama gari lile
Volvo lingetokezea maeneo yale. Dereva alitabasamu kidogo na kuniambia
kuwa barabara ile iliyopita lile gari aina Volvo haikuwa na sehemu nyingine ya
kukatishia. Ilikuwa ni barabara ya moja kwa moja hivyo yule dereva alikuwa
na hakika kuwa angekuja kukutana na lile gari sehemu ile. Yule dereva alipun-
guza mwendo akisubiri lile gari lipite kisha akaiingia kwenye ile barabara na
kulifungia mkia kwa nyuma.
Tulikuwa tumesafiri umbali wa maili kama tatu tukiliacha jiji la Kigali nyu-
ma yetu wakati tulipoliona lile gari mbele yetu likiwasha taa kuashiria kuwa
lilikuwa linataka kukata kona kuingia upande wa kulia. Nikamtaka yule dere-
va wa teksi apunguze mwendo na hapo tukaliona lile gari mbele yetu likiingia
upande wa kulia kuifuata barabara chakavu ya lami yenye mashimo mashimo.
Barabara ile ilipakana na vichaka na mapori ya hapa na pale hali iliyopelekea
barabara ile itawaliwe na giza nene. Tukio lile likanipelekea nimwambie dere-
va wangu kuwa azime taa za gari na kuendesha taratibu kulifuata lile gari.
Lile gari mbele yetu liliendelea kusafiri kwenye barabara ile yenye mashi-
mo na madimbwi ya mji na dereva wangu alikuwa makini sana kulifuatilia.
Baada ya umbali mfupi kiasi mara tuliliona tena lile gari likipunguza mwendo
na hatimaye kukata kona likiingia upande wa kushoto. Kiasi cha umbali wa
hatua hamsini mbele yetu lile gari lilipunguza mwendo na hatimaye kusimama
mbele ya geti kubwa jekundu lililoshikiliwa na kuta ndefu zilizojengwa kuizu-
nguka nyumba ya ghorofa tatu.
Tukiwa tumesimama umbali mfupi toka pale lilipokuwa lile gari mbele yetu
nilimwambia dereva wangu azime injini ya gari. Dereva alikuwa mwepesi ku-
nielewa akafanya kama nilivyomwagiza na hapo nikamuuliza kuwa ni pesa
kiasi gani alikuwa akinidai kama malipo ya umbali wa kutoka kule nilikom-
kodi. Yule dereva akaniambia kiasi cha pesa na bila kupoteza muda nikamlipa
na kumzidishia kidogo nikijenga uaminifu kwake. Akazipokea zile pesa na
kunishukuru huku nikimtaka ageuze gari lake na aende akanisubiri kule kando
ya barabara ile ya lami kabla ya kuchepuka na kuingia kwenye barabara hii ya
vumbi iliyotufikisha pale.
Nilikuwa nimemuahidi dereva yule kuwa ningerudi baada ya muda wa
nusu saa na kuwa endapo angeona muda huo umepita bila ya mimi kutokea
basi alikuwa huru kuondoka. Sote tulisubiri mpaka pale lile gari mbele yetu
liingie ndani ya ile nyumba na haukupita muda mrefu dereva wa lile gari
mbele yetu alipiga honi na muda mfupi baadaye tuliliona lile geti la ile nyum-
ba likifunguliwa na lile gari likaingia ndani. Ingawaje ulikuwa usiku lakini lile
geti lilipokuwa likifunguliwa ili kuliruhusu lile gari aina ya Volvo kuingia nili-
pata nafasi ya kuona mle ndani ya lile geti. Ilikuwa nyumba ya kisasa yenye
mazingira mazuri ya kuvutia ingawaje kitendo cha kufungwa haraka kwa geti
lile mara baada ya lile gari kuingia ndani kuliniacha katikati ya udadisi wangu.
Kwa kuhofia kukutwa eneo lile nilishuka haraka nikiiacha ile teksi ikigeuza
na kurudi kule tulipotoka. Moyo wangu ulikuwa ukienda mbio sana na si-
kuweza kuhisi nini ambacho kingenitokea mbele yangu hata hivyo hilo ha-
likunizuia kuendelea na harakati zangu. Mara baada ya kushuka kwenye ile
teksi nilianza kutembea taratibu kuifuata ile nyumba amabayo lile gari Volvo
lilipoingia huku nikiwa tayari nimeishika bastola yangu mkononi.
Ile nyumba ya ghorofa ilikuwa imezungukwa na miti mirefu na mikubwa
na wakati nikitembea niliweza kuzisikia sauti za ndege toka juu ya miti hiyo.
Nilijiuliza ni kwanini nyumba ile ilikuwa imejengwa mafichoni katika eneo
lililojitenga na makazi ya watu kama lile na sikuweza kupata majibu. Niligeu-
ka kutazama nyuma na pembeni yangu na sikuweza kumuona mtu yoyote eneo
lile ingawaje mwanga wa taa kubwa zilizopandwa juu ya ukuta wa ile nyumba
uliniwezesha kwa kiasi fulani kuyasoma mazingira ya eneo lile. Niliendelea
kutembea kwa tahadhari nikielekea mbele ya lile geti huku nikitazama huku
na kule kuutathmini usalama wa eneo lile.
Hatua tatu tu nilizoziputa mbele yangu kulikaribia geti la nyumba ile nil-
ishtukia kuwa kulikuwa na kamera mbili zilizokuwa zimepandwa juu ya geti
lile zenye uwezo wa kunasa picha ya kitu chochote mbele ya jengo lile. Kwa
kushtukia hilo nikachepuka na kupotelea gizani kwenye mti mkubwa uliyoku-
wa jirani na geti lile. Kupitia giza lililofanywa na matawi ya miti iliyoizunguka
ile nyumba niliweza kuzunguka taratibu kwa nje nikiuchunguza ukuta mrefu
uliyoizunguka ile nyumba.
Ulikuwa ni ukuta mrefu na wenye seng’enge maalumu juu yake inazomzuia
mtu yoyote kupenya kwa urahisi endapo mtu huyo angefanikiwa kufika juu ya
ukuta huo, na kwa kweli hali hiyo ilinikatisha tamaa juu ya namna ya kuingia
ndani ya nyumba ile. Niliendelea kuzunguka huku nikiuchunguza ule ukuta na
nilipoona kuwa hapakuwa na mwanya wowote wa kuniruhusu kuingia ndani
ya nyumba ile nikapata wazo jipya.
Niliichunguza ile miti mirefu na mikubwa iliyoizunguka ile nyumba nikiwa
nimepata wazo lenye tija baada ya kugundua kuwa baadhi ya matawi ya ile
miti yalikuwa yameinga ndani ya ule ukuta mrefu wa ile nyumba. Hali ile ika-
nipa faraja kiasi kwani nilianza kupata tumaini la kuyatumia matawi yale ku-
penya na kuingia mle ndani ya ile nyumba. Wazo hilo likanifanya nianze tena
kuizunguka ile nyumba na baada ya muda mfupi nikagundua kuwa kulikuwa
na mti mmoja ulioonekana kuwa rahisi kidogo kuupanda nyuma ya nyumba
ile. Nilipoufikia ule mti nilichunguza usalama wa eneo lile na niliporidhika
kuwa hali ilikuwa poa nikaanza kuukwea ule mti.
Haikuwa kazi ngumu kuukwea mti wa namna ile kwangu kwani tayari nil-
ishawahi kukwea miti mingi ya namna ile katika harakati zangu za kijasusi pia
mafunzo mengi ya kijeshi niliyowahi kuyapitia yalikuwa yamenifunza vizuri
namna rahisi zaidi ya kukwea mti kwa muda mfupi. Hivyo kwa muda mfupi
nikawa nimefanikiwa kuukwea ule mti lakini katika namna isiyoweza kukish-
tua kiumbe chochote ambacho kingekuwa eneo lile.
Nilipofika juu ya ule mti nilichagua tawi moja zuri lililoning’inia ndani ya
ukuta wa ile nyumba lakini kabla sijafanya maamuzi ya kulitumia tawi lile
nilitulia kwanza pale juu nikiichanguza vizuri ile nyuma na mazingira yake. Il-
ikuwa ni nyumba ya ghorofa ya kifahari sana iliyozungukwa kwa bustani nzuri
ya maua na nyasi zilizokatiwa vizuri. Nikiwa pale juu ya mti niliweza kuliona
lile gari aina ya Volvo nililokuwa nikilifuatilia toka kule Halfmoon Bar pia
kulikuwa na magari mengine mawili. Gari moja aina ya Nissan Patrol nyeupe
na gari nyingine aina ya Benz. Magari yale yote yalikuwa yameegeshwa mbele
ya nyumba ile chini ya banda maalumu la kuegeshea magari.
Niligundua kuwa pia kulikuwa na walinzi waliokuwa wakilinda eneo lile na
wote walikuwa na bunduki zao mikononi huku wakipeana zamu kuzunguka
ile nyumba. Mbali na hayo niligundua pia vyumba viwili vilikuwa vikiwaka
taa katika ghorofa ya juu ya nyumba ile kwani ule mti nilioukwea urefu wake
ulilingana na kimo cha ghorofa ile ya juu. Tofauti na hapo hapakuwa na kitu
kingine cha ziada.
Nikiwa nimejiridhisha na uchunguzi wangu nilijilaza juu ya tawi lile na
kuanza kusota kwa tumbo taratibu nikishuka kuelekea mle ndani ya ule ukuta.
Tawi lile refu lilikuwa limeelekea katika chumba kimoja cha ghorofa lile na
chumba hicho kilikuwa miongoni mwa vile vyumba viwili vilivyokuwa viki-
waka taa. Hata hivyo sikuweza kuona chochote ndani ya kile chumba kutoka-
na na pazia zito lililokuwa dirishani.
Nikiwa juu ya tawi lile niliendelea kusota kwa tumbo kuelekea ule uelekeo
wa lile dirisha la kile chumba kilichokuwa kikiwaka taa na wakati huo wote
bastola yangu ilikuwa mkononi tayari kufanya shambulizi lolote na macho
yangu yalikuwa yakijitahidi kuzunguka huku na kule kujaribu kuchunguza
kama kulikuwa na mtu yoyote mwingine eneo lile kwani wale walinzi wote
walikuwa wamesimama mbele ya ile nyumba kwa wakati huu.
Wakati nikiwa nimefika nusu ya lile tawi nililazimika kusitisha kwa muda
mjongeo wangu baada ya kusika sauti fulani ikitokea kwenye pembe ya ile
nyumba. Nikatulia kimya juu ya tawi lile huku nikiyatembeza macho yangu
kutazama upande ule ile sauti ilipotokea. Nilipoyatuliza vizuri macho yangu
nikamuona mlinzi mmoja akiwa na mbwa. Nilimtazama mlinzi yule nikagun-
dua kuwa hawakuwa na hisia zozote za uwepo wangu eneo lile, na bunduki
yake alikuwa ameining’iniza begani huku mkono wake mwingine akiwa ume-
shikilia sigara. Yule mbwa aliyeongozana naye alikuwa akimrukiarukia na
yule mlinzi hakuonekana kushughulika naye.
Nikiwa nimejibanza pale juu ya lile tawi nilimuona yule mlinzi akisogea
taratibu kuja usawa ule niliokuwepo na alionekana kwa kila namna kuzama
katika starehe yake ya kuvuta sigara. Yule mlinzi aliendelea kuzitupa hatua
zake taratibu mpaka alipofika chini ya usawa wa lile tawi ndiyo akasimama na
kugeuka akitazama kule nyuma kabla ya kuirudisha tena sigara yake mdomoni
akivuta taratibu kisha kipisi cha sigara kilichosalia akakitupa chini na kukizima
kwa kiatu chake. Baadaye nilimuona yule mlinzi akiinama na kuanza kumpa-
pasa yule mbwa shingoni. Nikiwa nimejibanza juu ya tawi lile nilianza kuhisi
kuanza kuchoka kulikumbatia lile tawi hivyo nilianza kuhisi kuwa endapo hali
ile ingeendelea vile nisingeweza kuhimili zaidi hivyo nilianza kufikiria namna
ya kumfanyia shambulizi la kushtukiza yule mlinzi.
Lakini wakati nikijipanga kufanya hivyo nilimuona yule mlinzi pale chini
akianza kuondoka pamoja na yule mbwa wake na tukio hilo likanipa faraja
kidogo. Nilimsubiri yule mlinzi hadi pale alipokunja kona na kupotelea mbele
ya ile nyumba na hapo ndiyo nikaanza kuendelea na safari yangu. Nilipofika
mwisho wa lile tawi nikaning’inia kwenye bomba moja lililokuwa likitumika
kupitishia maji ya mvua toka sehemu ya juu ya paa la ghorofa lile. Kwa ku-
tumia bomba lile nikajivuta kwa mikono yangu hadi pale nilipoufikia ukuta
wa ile nyumba sehemu kulipokuwa na nafasi kidogo ya kujishikiza.
Nilipofika pale nikaanza kuambaa na ule ukuta taratibu kwa uangalifu hadi
pale nilipokifikia kile chumba kilichokuwa kikiwaka taa. Nikiwa kwenye di-
risha la chumba hicho niliweza kuona ndani kupitia uwazi mdogo ulioachwa
na pazia na wakati huu macho yangu yalijikuta yakiweka kituo kwenye umbo
zuri la msichana fulani aliyekuwa ndani ya kile chumba. Nilipomchunguza
vizuri msichana yule nikagundua kuwa alikuwa ni yule msichana mrembo
niliyemwona kule Halfmoon Bar, na wakati huu alikuwa amevua nguo zake
zote na kubaki kama alivyozaliwa. Nilimtazama msichana yule akiwa katika
muonekano mpya kabisa wenye kuvuta hisia zangu na wakati huu yule msi-
chana hakuwa na ile miwani nyeusi machoni kama kipindi kile nilipomuona
kule Halfmoon Bar.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Ni katika mtazamo huo mpya nikajikuta nikikumbuka kitu fulani na kuki-
kumbuka kitu hicho kikanipelekeanianze kuhisi kuwa damu yangu ilikuwa
ikaanza kuchemka mwilini huku nikiachama mdomo kwa mshangao. Msicha-
na yule aliyekuwa mbele yangu sasa nilikuwa na kila hakika kuwa alikuwa
ni yule msichana niliyeonana naye kule uwanja wa ndege wa Kigali nikim-
fahamu kwa jina la Marceline wakati nilipokuwa nikifika hapa nchini Rwan-
da. Kwa kweli nilishtuka sana na kwa namna moja au nyingine hisia tofauti
zikaanza kuumbika upya kichwani mwangu. Kwa kweli nilijisikia kuchang-
anyikiwa pale nilipoikumbuka ile barua yenye ujumbe wa siri niliyoiiba kule
chumbani katika ile nyumba ya maficho kule msituni.
“Mercelina...” nilijikuta nikitamka jina lile bila kujielewa na kama aliye-
shtuka baada ya kulisikia jina lake likitamkwa nilimuona Marceline akigeuka
kutazama pale dirishani nilipokuwa na hapo nikajihisi ni kama niliyepigwa
shoti kali ya umeme na kuacha moyo wangu ukiwa umesimama kwa sekunde
kadhaa kama mfu. Ingawaje nilikuwa na kila hakika kuwa pamoja na Marce-
line kutazama pale dirishani lakini alikuwa hanioni lakini bado akili yangu
ilishindwa kabisa kukubaliana na tukio lile. Nikayasimamisha macho yangu
kukabiliana naye huku nikiwa na ujasiri wa kipekee kabisa, hata hivyo aliku
wa hanioni.
Uzuri wake ulikuwa umechangia kwa kiasi kikubwa kuniduwaza mbele ya
dirisha lile. Nilianza kwa kukitathmini kifua chake kilichobeba matiti mado-
go yanayofanana na umbo lake yenye chuchu ndogo zilizosimama. Kitovu
chake kilichotumbukia ndani na kuacha kishimo kidogo tumboni kiliungana
na mstari hafifu ulioshuka chini na kupotelea katikati ya mapaja yake huku
ukikiacha kiuno chake laini kikicheza taratibu kwa kadiri alivyokuwa akijari-
bu kupiga hatua moja mbele yake.
Nilimuona Marceline ni kama aliyekuwa akija pale dirishani halafu mara
nilimuona akikunja kona kuelekea upande wa kushoto na hapo nikagun-
dua kuwa alikuwa akielekea kujitazama kwenye kioo kikubwa kilichokuwa
kwenye kabati la nguo pembeni ya kitanda mle chumbani. Na wakati akitem-
bea kuelekea kwenye lile kabati niliweza kuliona umbo lake vizuri na kwa
haraka sana niliweza kukubali moyoni kuwa sikuwahi kumuona mwanamke
mwenye umbo linalotamanisha na kuziteka haraka hisia za mwanaume kama
yeye.
Kiuno chake chembamba kilicheza taratibu pande huu na ule sambamba na
mtikisiko wa makalio yake laini yaliyopishana taratibu wakati akizitupa hatua
zake. Alipofika kwenye lile kabati alisimama kwenye kile kioo na kujishika
kiunoni akijitazama kwa kujizungusha zungusha na baadaye alipandisha juu
mikono yake na kuanza kujitomasa tomasa matiti yake. Hata hivyo nilipom-
chunguza usoni niligundua kuwa hakuwa na furaha.
Simu iliyoanza kuita sebuleni ilimshtua Marceline na kumpelekea aache ku-
jitazama kwenye kile kioo na hapo akafungua lile kabati haraka na kuanza ku-
chagua nguo. Muda mfupi baadaye nilimuona akivaa bikini kisha akavaa suru-
ali nyepesi ya jeans na fulana nyeusi na alipomaliza akaharakisha kuelekea
kule sebuleni simu ilipokuwa ikiita.
Wakati Marceline akikiacha kile chumba kuelekea kule simu ilipokuwa
ikiita nikawa nimepata wazo la kuingia mle ndani ya ile nyumba kupitia diri-
sha la chumba kile. Hivyo bila ya kupoteza muda nilifungua kioo cha dirisha
lile baada ya kupata upenyo mdogo wa kupenyeza mkono na kufyatua komeo
la dirisha na muda mfupi baadaye nikafanikiwa kuingia ndani ya kile chum-
ba. Niliyazungusha macho yangu mle ndani na hapakuwa na chochote cha
kunivutia hivyo sikutaka kupoteza muda kwani nilikuwa na kila hakika kuwa
mwenyeji wa chumba kile angerudi muda si mrefu mara baada ya kumaliza
maongezi yake kwenye ile simu.
Ile simu iliendelea kuita na muda mfupi baadaye niliisikia ikipokelewa.
Niliusukuma mlango wa kile chumba taratibu na kutoka nje na hapo nika-
jikuta nimetokezea kwenye korido pana iliyokuwa na uzio mfupi wa vyuma
vilivyopindwa katika mtindo wa kupendeza. Uzio huo ulikuwa pembeni ya
ngazi zilizokuwa zikishuka sehemu ya chini ya ghorofa lile. Nilitazama upa-
nde wa kushoto kwangu nikaviona vyumba viwili vikiwa vimefungwa mbele
yangu na mbele ya vyumba hivyo kulikuwa na ukumbi mpana nilioufananisha
na sebule ya juu ya ghorofa lile.
Katika ukumbi ule kulikuwa na seti mbili za makochi ya sofa, meza pana ya
fomeka na seti moja ya runinga vilevile kulikuwa na kabati kubwa lililoshe-
heni vinywaji vya aina tofauti kwenye kona ya ukumbi ule. Nilitazama katika
ukumbi ule na sikumuona mtu yoyote hivyo nikajua kuwa Marceline alikuwa
ameshuka sehemu ya chini ya jengo lile ambapo sasa nilikuwa na hakika kuwa
simu ile ndipo ilipokuwa ikiita. Sauti ya maongezi ya kwenye ile simu ikanifa-
nya niukaribie ule uzio wa zile ngazi za kushuka kule chini na hapo nikaanza
kupiga hatua zangu taratibu nikinyata kushuka zile ngazi.
Nilikuwa nimefika nusu ya safari yangu pale nilipotupa macho yangu upa-
nde wa kulia na kupata picha nzuri ya sebule pana ya kifahari iliyokuwa seh-
emu ya chini ya ghorofa lile. Sebule ile ilipambwa kwa zulia la kifahari la
rangi nyekundu, seti tatu za makochi ya kisasa ya sofa yaliyozunguka meza
fupi za vioo, mapazia marefu dirishani, jokofu kubwa lililokuwa pembeni ya
kaunta kubwa ya vinywaji, seti moja ya runinga iliyokuwa mbele ya sebule ile
na sistimu moja ya muziki.
Niliyazungusha macho yangu upande wa kushoto na hapo nilimuona Marce-
line akiwa ameketi kwenye kochi moja lililokuwa jirani na meza iliyokuwa
na simu juu yake. Alikuwa ameketi kwa utulivu huku mkonga wa simu hiyo
ukiwa sambamba na mdomo wa sikio lake. Mwonekano wake usoni ulikuwa
na kila dalili za mashaka na wasiwasi ambao bila shaka ulitokana na taarifa za
upande wa pili wa simu ile.
Toka pale nilipokuwa nimesimama niliweza kuyasikia maongezi baina yake
na mtu wa pili kwenye simu ile hata hivyo sikuweza kuambulia kitu kutokana
na maongezi hayo kutumia lugha ya kinyarwanda ambayo mimi sikuifaha-
mu. Katika maongezi yale kuliibuka mabishano na mabishano hayo yalipozidi
nilimuona Marceline akikata simu na kuirudisha mahala pake kisha akasima-
ma na kuanza kuufuata uelekeo wa zile ngazi ili apande na kuja kule juu.
Alikuwa hajapiga hata hatua mbili katika safari yake pale ile simu ya mezani
ilipoanza kuita tena pale mezani. Marceline aligeuka na kuitazama ile simu ki-
sha tusi zito likamponyoka huku akionekana kuwa hana mpango wa kuipokea
tena na badala yake aligeuka na kuzitupa hatua zake kwa haraka akiendelea
na safari yake.
Niliwahi kurudi kule juu kabla ya Marceline hajaanza kupanda zile ngazi
na hapo nikaingia kwenye kile chumba nilichotoka na kujibanza nyuma ya
mlango nikimsubiri. Muda mfupi uliofuata niliouna ule mlango wa kile chum-
ba ukisukumwa kwa pupa na kisha Marceline akaingia na kwenda kujitupa
kitandani. Niliyatega vizuri masikio yangu na kuzisikia zile kelele za ile simu
ikiendelea kuita kule sebuleni na muda si mrefu ile simu iliacha kuita.
Marceline alikuwa amejilaza kifudifudi pale kitandani huku akihema kwa
hasira kama mtu aliyegombana na mwenzake na bila ya kupoteza muda nili-
jitoa kule nyuma ya mlango mafichoni na kuanza kumsogelea taratibu pale
kitandani. Na kama aliyehisi uwepo wa kiumbe kingine mle ndani Marceline
akashtuka na kugeuka na macho yetu yalipokutana akashikwa na taharuki am-
bayo sikumbuki kama niliwahi kuiona kwenye sura ya kiumbe chochote hapa
duniani.
“Wewe ni nani na unafanya nini humu ndani? aliniuliza kwa mshangao huku
uso wake umejawa na hofu.
“Patrick Zambi, mara hii tu umenisahau Marceline?
“Toka nje sasa hivi kabla sijakuitia walinzi’’
“Hebu keti tuzungumze mpenzi uite walinzi wa nini? nilimwambia kwa utu-
livu huku nikitabasamu na taharuki aliyokuwanayo usoni ni kama mwanamke
aliyefumaniwa na mume wa mtu. Nilipomtazama usoni nikaisoma akili yake
namna ilivyokuwa ikifanya kazi na kufumba na kufumbua Marceline akajitu-
pa upande wa pili wa kile kitanda huku mkono wake mmoja ukipotelea chini
ya mto mmoja wa kuegemea uliokuwa pale kitandani na alipoutoa ulikuwa
umeshika bastola.
Hata hivyo hakupata muda wa kuitumia ile bastola kwani kwa wapesi wa
ajabu niliipangua kwa teke jepesi lililoitupa ile bastola chini ya kabati. Marce-
line alikuwa hodari kuliko nilivyomdhania na pigo moja alilotupa la kareti
ilibakia kidogo liitengue shingo yangu kama nisingekuwa makini kulikwe-
pa. Akalitupa pigo lingine la teke lililolenga korodani zangu lakini niliwahi
kuliona nikalidaka na kulizungusha katika namna ya kulipoteza shabaha.
Ulikuwa ni mtindo hatari sana wa mapambano ya ana kwa ana uliotumika
kwa mashambulizi ya namna ile kwani Marceline alizunguka hewani kama pia
na kutua juu ya kile kitanda akiwa hajielewi. Nikamfuata lakini wakati huu
aliniwahi na kwa wepesi wa ajabu akarusha pigo moja la teke lililotua bila
pingamizi tumboni mwangu na kunitupa ukutani nikiwa na maumivu makali
sana.
Nilishikwa na mshangao sana kwani sikuamini kuwa msichana yule an-
gekuwa ni yule Marceline niliyemuona kule uwanja wa ndege wa Kigali seh-
emu ya mapokezi ya wasafiri akiwa na haiba nzuri ya kazi yake na tabasamu
la kibiashara. Wakati nikijiandaa kusimama Marceline aliniwahi hata hivyo
nilikuwa makini zaidi kwani pigo la teke jingine alilolirusha nililiona na hapo
nikatumia jitihada kidogo kuinama chini nikiliacha pigo lile likipita hewani
na kukikosa kidogo kichwa changu. Na kabla teke lile halijafika mwisho wa
safari yake niliwahi kujibetua na hapo nilimtandika Marceline mapigo mawili
ya ngumi kavu za mgongo na hapo nikamsikia akipiga yowe kali la maumivu
huku akipepesuka kama mlevi.
Sikutaka kumsubiri hivyo kabla hajasimama nikamtandika pigo jingine la
teke la mgongoni na wakati huu sikutaka kumchukulia tena kama msichana
wa kawaida kwani dhana iliyoanza kujengeka kichwani mwangu ni kuwa nili-
kuwa nikipambana na msichana hatari na si yule Marceline niliyemuona kule
kiwanja cha ndege cha Kigali.
Mapigo niliyomtandika Marceline yalikuwa madhubuti na yenye uhakika
kwani pamoja na jitihada zake za kujizuia hakufanikiwa badala yake alien-
da kujipigiza kwenye kile kioo cha kabati. Kile kioo kikavunjika na kum-
chanachana Marcelina mikononi na usoni huku akipiga yowe la hofu na kisha
kuanguka chini. Alipotaka kusimama nilikuwa tayari nimekwisha muwahi
hivyo alijikuta akitazamana na mtutu wa bastola yangu wenye uchu na roho
yake.
“Sikupenda tufikishane huku Marceline tambua kuwa ni wewe ndiye uli
yenipelekea nifanye haya yote mpenzi”
“Si umepania kuniua basi endelea na kwa bahati mbaya sana hujui mtu un-
ayemfanyia hivi ni nani”
“Mimi sina lengo la kukuua Marceline na kama ningetaka kufanya hivyo
ningefanya tangu kipindi kile ulipokuwa uchi ukijishikashika matiti na kiuno
chako mbele ya kioo cha kabati humu ndani” nilimwambia Marceline na hapo
nilimuona akitaharuki na kunitazama kwa mshangao kisha akageuka kutaza-
ma upande ule wenye lile dirisha la kile chumba huku uso wake ukiwa tayari
umesawajika.
“Umeniambia kuwa kwa bahati mbaya nakufanyia haya yote pasipo kuku-
jua kuwa wewe ni nani. Kwani wewe ni nani mimi mbona nakutambua kama
Marceline” nilimuuliza
“Ungekuwa na shida ya kinifahamu usingenifanyia haya uliyonifanyia”
“Basi naomba unisamehe mpenzi”
“Wewe niue tu nadhani hicho ndicho kilichokuleta humu ndani” Marceline
alifoka kwa hasira.
“Marceline!...” nilimuita kwa upole na utulivu huku nikimshika begani
kama mpenzi wangu wa siku nyingi. Kwa kweli nilikuwa hodari sana wa ku-
cheza na hisi za viumbe wa sampuli ile kwani Marceline aligeuka taratibu na
kunitazama pasipo kuonesha ukaidi wa aina yoyote.
“Nimetumwa” hatimaye nilimwambia kwa utulivu huku mtutu wa bastola
yangu bado ukiwa unamtazama.
“Umetumwa nini na nani? Marceline aligeuka tena na kunitazama huku
ameshikwa na mshangao.
“Nimetumwa na Bolos!”
Marceline alishikwa na mshangao huku akinitazama kwa hofu akionekana
kuchanganyikiwa na maelezo yangu.
“Bolos amekutuma wewe!...kwa nini asije mwenyewe? Marceline alinuliza
huku akionekana kuzidi kustaajabu.
“Amepata dharura” nilimjibu kwa utulivu huku moyoni nikitabasamu kwani
kitendo cha yeye kunisikiliza zilikuwa dalili nzuri sana kwangu “...Leo usiku
ana kikao cha dharura na wageni muhimu hivyo ndiyo alivyoniambia na kuni-
taka nifike kwako na kuchukua taarifa ulizonazo” nilimdanganya Marceline
na nilipomtazama usoni nilimuona jinsi alivyozidi kuchanganyikiwa na kwa
dalili nilizoziona kwake niligundua haraka kuwa Marceline alikuwa mwana-
funzi mzuri wa kijasusi.
“Taarifa zipi na wewe ni nani mpaka akutume?
Nilitabasamu kidogo ingawaje tabasamu langu halikutokana na furaha bali
mlolongo wa maswali mengi yasiyokuwa na majibu kichwani mwangu.
“Mimi ni rafiki wa Bolos vilevile unaweza kuniita Patrick Zambi, mwandi-
shi wa habari wa kujitegemea kutoka nchini Tanzania. Bila ya shaka sasa ume-
nikumbuka” nilimwambia Marceline huku nikiivua ile kofia yangu kichwani
taratibu na kutabasamu kidogo kabla ya kuirudisha tena kichwani” hofu nili-
yoiona usoni kwa Marceline mimi mwenyewe naijua. Akabaki ameachama
mdomo wake kwa mshango kama anayetaka kuzungumza neno fulani ambalo
hakuwa na nguvu ya kutosha kuliongea.
“Bila shaka sasa umenikumbuka vizuri” nilizungumza taratibu huku niki-
tabasamu. Marceline alijitahidi tena kuzungumza neno lakini hata hivyo sauti
yake ilikuwa hafifu sana na yenye kila dalili za woga hivyo akaishia kumu-
munya maneno kama mtoto anayejifunza kuongea. Nilipomuona anakawia
kunijibu nikaendelea,
“Mimi na wewe ni kitu kimoja Marceline bahati mbaya sana hatuna muda
wa kutosha wa kukaa na kufahamiana na hii ni kutokana na usiri wa mipango
yenyewe ulivyo. Ninachohitaji sasa ni hizo taarifa nilizoagizwa kwako na Bo-
los kwani ni lazima nionane naye usiku huu kabla hakuja pambazuka halafu
baada ya hapo mimi na wewe tutapanga namna ya kuonana kwa nafasi yetu
mpenzi” nilimdanganya Marceline huku nikijiuliza kama uongo wangu uliku-
wa na ushawishi wowote kichwani mwake.
“Nani mpenzi wako? Marceline alinikana “Mimi sina taarifa zozote za kuk-
upa”
“Hebu tulia kwanza mpenzi hivi unadhani ninaweza kupoteza muda wangu
bure kwa kufuatilia kitu nisicho na hakika nacho?. Unazo taarifa Marceline na
taarifa hizo zinatakiwa kwa haraka sana kuliko unavyodhani. Hakuna haja ya
kupoteza muda kwani nahitaji kurudi usiku huu huu kabla ya hakujapamba-
zuka” Marceline aliinua macho yake kunitazama na hapo nilipata nafasi tena
kuuona uso wake namna ulivyoharibiwa na kile kioo cha kabati kisha akayak-
wepesha macho yake pembeni akitazama upande mwingine wa kile chumba.
Nilikuwa na imani sasa kuwa Marceline alikuwa akijiandaa kuniambia
kitu fulani hali iliyonipelekea nitabasamu kidogo huku nikijitahidi kum-
shawishi kwa macho yangu anieleze hicho kitu. Nikiwa nimeanza kujiandaa
kumsikia Marceline ghafla nilishangaa kumuona Marceline akianza kuangua
kicheko, alinitazama usoni kama mwehu kisha akaendelea kuangua kicheko.
Kwa kweli nilistaajabu sana kwani sikuweza kukufahamu kuwa Marceline
alikuwa akicheka nini.
“Huna ujanja Luteni Venus Jaka, unadhani na safari hii pia utafanikiwa ku-
toroka kwa kunihadaa kitoto kama hivi?. Pole sana mpenzi kwani mwisho
wako sasa umefika” Merceline aliendelea kuongea huku akicheka. Kwa kwe-
li nilishindwa kumuelewa vizuri Marceline kuwa alikuwa akimaanisha nini
kusema vile. Wakati Marceline akiendelea kucheka vile nikamuona akiangalia
nyuma yangu ikabidi na mimi nigeuke kutazama kule alipokuwa akitazama na
hapo ndiyo nikajua kwa nini alikuwa akicheka vile.
“Tupa bastola yako chini Luteni” sauti nzito ya kiume yenye amri ilinion-
ya toka nyuma yangu na kwa kweli nilihisi kuchanganyikiwa na kwa mara
nyingine nilianza kuona kuwa roho yangu haikuwa kwenye mikono salama
tena. Kipande cha mwanaume mrefu na mweusi aliyevaa gwanda za kijeshi
alikuwa amesimama nyuma yangu na mtutu wa bastola yake mkononi ukini-
tazama tayari kufanya kazi. Sura ya mtu yule ilikuwa ngeni kabisa machoni
ya mwangu na alikuwa na mwili uliojengeka vizuri kwa mazoezi na hata
alipotabasamu bado tabasamu lake lilimfanya aonekane kama mtu aliyetaka
kupiga chafya.
#153
“Tulifahamu tu Luteni kuwa hii ingekuwa sehemu yako ya kwanza kukim-
bilia baada ya kuiiba ile bahasha yetu na ulivyo na kichwa cha panzi umesh-
indwa hata kuushtukia mtego hafifu kama huu” yule mtu alinisimanga na
kweli maneno yake yalipenya moyoni mwangu na kuamsha hasira. Hata hivyo
nilikuwa mwerevu kujizuia kuleta purukushani ya namna yoyote kwani ile
bastola nyuma yangu ni kama iliyokuwa ikinionya. Bila ubishi niliiachia tara-
tibu ile bastola yangu mkononi na yule jamaa akawahi kuikwapua na kui-
chomeka kiunoni mwake.
“Pole sana Marceline” yule mtu nyuma yangu aligeuka na kumwambia
Marceline kisha akageuka tena kunitazama.
“Wewe mwanaharamu unawezaje kutumia nguvu kiasi hiki kupambana na
mwanamke?,...okay! basi leo nitakuonesha” yule mtu aliniambia na wakati
alipokuwa akijiandaa kunitandika ngumi ghafla ile simu ya sebuleni ilianza
kuita tena. Sote tulishtuka ila hakuna aliyeonekana kunipa mwanya na badala
yake yule mtu aligeuka tena kumtazama Marceline huku akimuonesha ishara
fulani kwa kichwa kuwa asimame pale alipoketi na aende akaipokee ile simu.
Marceline alisimama na kabla hajaondoka alinitandika ngumi mbili za uso na
tukio lile lilionekana kumfurahisha sana yule mtu hadi kiasi cha kutabasamu.
Marceline alipoondoka mle ndani tukawa tumebakia watu wawili.
“Hivi mmejuaje kuwa mimi nipo hapa? nilimuuliza yule mtu nikitaka kuu-
soma umakini wake.
“Shut up your mouth!...” yule mtu alifoka na muda uleule nikashtukia ni-
kitandikwa ngumi kavu mgongoni na maumivu niliyoyasikia mwenyewe nay-
ajua.
“Mimi huwa sina kawaida ya kuzungumza na watu wa sampuli yako. Tulia
na uyajibu vizuri maswali yangu na usilete hila yoyote kwani nakuhakikishia
kuwa hakuna kiumbe yeyote msumbufu aliyewahi kuponyoka kwenye miko-
no yangu” yule mtu alinionya, nikataka kumjibu lakini haraka nilisita pale
nilipokumbuka kile kichapo alichonipa.
“Nyoosha mikono yako juu na sasa utaongoza mbele kuelekea sebuleni, tu-
meelewana?
“Tumeelewana!”
Muda uleule safari ya kuelekea sebuleni ikaanza huku mimi nikiwa
nimetangulia mbele na wakati tukielekea kule sebuleni yule mtu nyuma yangu
alinionya kuwa nisilete ujanja wowote kwani asingekuwa tayari kunivumilia.
Tulitoka nje ya chumba kile tukaanza kushuka zile ngazi kuelekea kule chini
sebuleni na wakati nikishuka zile ngazi nilimuona Marceline akiwa anaongea
na simu kwenye ile meza ya simu pale sebuleni. Lakini safari hii nilishikwa
na mshtuko pale nilipowaona wanaume wengine wawili wakiwa wameketi
kwenye makochi pale sebuleni. Wanaume wale walikuwa na sura za kazi na
cha ajabu hawakuonesha tashwishwi yoyote ya uwepo wangu kana kwamba
walikuwa ni watu niliozoeana nao kwa muda mrefu. Tumaini la kutoka salama
eneo lile likaanza kuyeyuka taratibu mara nilipowaona wale watu wakiachia
tabasamu hafifu kwenye nyuso zao.
“Vizuri sana komredi” mtu mmoja miongoni mwa wale watu pale sebule
ni aliongea akimpongeza yule jamaa nyuma yangu huku akisimama na kupi-
ga mruzi mwepesi na hapo nikaweza kumtathmini vizuri mtu yule. Alikuwa
mrefu wa wastani mwenye kifua kikubwa na mikono imara, mavazi yake ya
suruali nyeusi ya kadeti na shati zito la rangi ya samawati vilinieleza kuwa
alikuwa mtu wa kazi na hata macho yake tulipotazamana niliyaogopa kwani
hayakuonesha dalili zozote za kutoa msamaha kwa maisha ya binadamu. Yule
mtu mwingine alikuwa mfupi kiasi lakini mwenye ndevu na nywele nyingi
kichwani tofauti na mwenzake, yeye hakusimama wala kufanya mjongeo wa
aina yoyote badala yake alitabasamu kidogo aliponitazama na tabasamu lake
likafifia na kutoweka baraka usoni kisha sura yake ikavaa muonekano mpya
na wa tofauti unaotisha.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Wakati tukiifikia ile sebule Marceline alikuwa tayari amemaliza kuongea na
ile simu na hivyo wote wakawa wamegeuka na kunikodolea macho. Katikati
ya sebule ile nilikiona kiti kimoja kikiwa kimetengwa, nilikitazama vizuri kiti
kile na katika yale mazingira nikajua kuwa kwa vyovyote kilikuwa kikinihusu
ingawaje kilikuwa ni kiti cha kawaida kabisa tena cha mbao kilichochukuliwa
kutoka miongoni mwa vile viti vilivyokuwa vimeizunguka meza ya chakula
pale sebuleni.
“Kaa kwenye kiti Luteni bila shaka sasa unayo mengi ya kutueleza”
“Niwaeleze kuhusu nini? nilikaa kwenye kile kiti huku nikiwauliza.
“Tunayo mengi tu tunayohitaji kuyasikia kutoka kwako na nimatumaini
yetu kuwa majibu yote sasa utakuwa nayo” yule mtu mwenye sura ya kifo
aliniambia.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment