Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

TAI KWENYE MZOGA - 1

 






    IMEANDIKWA NA : KEVIN E. MPONDA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Tai Kwenye Mzoga

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    KIGALI INTERNATIONAL AIRPORT, RWANDA.

    Jumamosi saa 12:45 jioni mwezi Machi, 1994.

    NILIKUWA MTU WA TATU katika mstari wa foleni yangu kabla ya kulifikia

    dirisha dogo lenye kuta za vioo mbele yangu lililomuhifadhi mkaguzi wa pasi

    za kusafiria. Msichana mrembo na mtanashati, msichana mzuri wa kinyar?wanda akionekana kuyazingatia vizuri maadili ya kazi yake kwa kutabasamu

    mbele ya abiria waliowasili jioni hii. Sikupenda kumlaumu msichana huyu

    pindi aliponitupia jicho na kujikuta akishikwa na shauku ya kutaka kuni?hudumia japokuwa zamu yangu ilikuwa bado haijafika, kwani mbele yangu

    walinitangulia wazee wawili, mwanamke na mwanamume, bibi na bwana,

    pengine walitoka kwenye maadhimisho ya fungate ya ndoa yao waliyoifunga

    zaidi ya miaka arobaini iliyopita.

    Naam, sikushtuka kwani nilifahamu fika kuwa nilikuwa nimependeza sana

    istoshe nilikuwa miongoni mwa vijana wenye mvuto kwenye macho ya wasi?chana warembo kama msichana huyu mbele yangu. Kwa mtazamo wa nje

    mtu yeyote asingesita kunifananisha na kijana anayejipenda, msanii wa muz?iki ama muigizaji wa filamu au mwanamitindo wa mavazi ya kiume. Lakini

    ukweli ni kwamba kazi yangu ilikuwa ni ya hatari mno na wala haikuelekea

    walau chembe tu kufanana na kazi hizo.

    Suti yangu ya bei ya ghali nyeusi aina ya Kenzo, shati langu jeupe, saa yangu

    ya mkononi ya madini ya dhahabu aina ya Alpha GMT-Dead Ringer, sanduku

    langu jeusi mkononi, kofia yangu kichwani aina ya pama na manukato ya gha?rama niliyojipulizia yanayolingana na mshahara wa kima cha chini wa mfa?nyakazi mmoja wa serikali, vilikuwa vimechangia kuunogesha uzuri wangu.

    Nilikuwa miongoni mwa abiria waliotua kiwanjani hapo kwa ndege ya shiri?ka la ndege la Rwanda ama Rwandair kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania.Wakati nikilifikia lile dirisha lenye yule msichana mrembo mkaguzi wa pasi

    za kusafiria, baada ya wale wazee wawili waliokuwa mbele yangu kumaliza

    kuhudumiwa na kuondoka, niliweza pia kubaini kuwa nilikuwa nikitazam?wa na wasichana wengine warembo, wakaguzi wa pasi za kusafiria walikuwa

    kwenye vibanda vya jirani. Nikajikuta nikifurahi moyoni huku nikijidai sifa?hamu kinachoendelea eneo lile.

    Nilipolifikia lile dirisha la kioo mbele yangu alilokuwa yule msichana mr?embo, nikaingiza mkono mfukoni kuchukua pasi yangu ya kusafiria kisha

    nikaipenyeza kwenye tundu dogo la kioo mbele yangu kumpa yule msichana.

    Alipoipokea nikaiegemeza mikono yangu juu ya sakafu ya kipande kidogo

    cha ubao mfupi kilichokuwa mbele ya dirisha lile huku nikiinama kidogo ili

    niweze kuliona vizuri tabasamu la msichana yule. Macho yetu yalipogongana

    kila mmoja alijikuta akitabasamu na hapo nikajikuta nikivutiwa vizuri na uzuri

    wake.

    “Hujambo miss Rwanda” nikamtania msichana yule hata hivyo hakuitikia

    badala yake alizidi kutabasamu tu huku akiikagua pasi yangu ya kusafiria.

    “Patrick Zambi…” nilimsikia akilitamka jina langu taratibu pasipo kunita?zama

    “Hilo ndiyo jina langu vipi umewahi kulisikia popote? nilimuuliza huku

    nikitabasamu

    “Akina Patrick wako wengi sana hapa Rwanda isipokuwa hili jina la Zambi

    mh! kusema ukweli sijawahi kulisikia popote” msichana yule mrembo alin?iongelesha kwa lugha ya kiswahili sanifu huku ameinama akiandika maelezo

    fulani kwenye pasi yangu.

    “Wewe ni Mtanzania? akaniuliza huku akiendelea na kazi yake, nikajua

    alipenda tu kunisikia kwani vibali vyangu vya kusafiria ambayo wakati huu

    alikuwa navyo yeye vilikuwa vikieleza wazi kabisa.

    “Ndiyo”

    “Kabila lako?

    “Mtanzania” nikamjibu

    “Mbona hapa imeandikwa kuwa wewe ni Mpogolo?

    Swali hilo likanifanya niinue macho yangu kumtazama vizuri msichana

    yule kwani sikuelewa maana ya swali lake istoshe kabila langu na taarifa zan?gu zote zilikuwa kwenye pasi yangu ya kusafiria, nikabaki nimeshikwa na

    mduwao.

    “Oh! samahani mrembo nilishasahau kabila langu, siye kwetu Tanzania

    makabila yapo zaidi ya mia moja na ishirini na si ajabu hivi leo kuna kabila

    jingine jipya linaundwa, sasa utaliacha lipi ulikumbuke lipi. Ndiyo maana

    nikakwambia mimi kabila langu Mtanzania”

    Msichana yule mrembo hakujibu kitu badala yake aliendelea kutabasamu.

    Akamalizia kugonga mhuri kwenye pasi yangu ya kusafiri kisha akazungusha

    kiti chake hadi ilipokuwa kompyuta yake ya mezani halafu akaanza kubonye?za vitufe fulani kwenye keyboard na hapo nikajua alikuwa akiingiza taarifa

    zangu.

    “Jina lako? nikamuuliza kwa sauti ya chini ili majirani wasisikie na kunishuku kuwa nilikuwa kwenye harakati za kumtongoza. Swali langu lika?onekana kuzidi kumfurahisha mrembo yule, akatabasamu kidogo kiasi cha

    kuyafanya meno yake meupe kuonekana na hapo nikaviona vishimo vidogo

    vya mashavu yake.

    “Umesema? akaniuliza na hapo nikajua tu alipenda nirudie swali langu.

    “Hujaniambia jina lako mrembo mbona langu nimekutajia” nikamuuliza

    huku nikikikagua kifua chake kilichobeba matiti ya wastani yaliyotenganish?wa na mkufu mzuri wa dhahabu na hapo shughuli za mwili wangu zikasimama

    kwa sekunde.

    “Mh! wacha uongo wako Patrick nyinyi watanzania kwa maneno nimesha?wazoea kila sehemu mnapenda urafiki na utani tu. Jina lako hukunitajia bali

    nimeliona mwenyewe kwenye pasi yako ya kusafiria” msichana yule aliongea

    kwa sauti laini ya kubembeleza huku akiangua kicheko hafifu na mimi nikaji?kuta nikifarijika kwa kulitaja jina langu kwa usahihi utasema mwalimu wangu

    wa darasa.

    “Oh! basi nakuomba unisamehe mrembo kwa kusema uongo anyway…

    napenda tu kulifahamu jina lako”

    “Marceline”

    Akalitamka kwa ghafla hata hivyo masikio yangu yalikuwa yamejitayarisha

    kwa tukio hilo, nikalinasa.

    “Marceline! mh! jina lako tamu kama asali” nikanong’ona na hapo akash?indwa kujizuia na kujikuta akicheka.

    “Usinichekeshe Patrick mwishowe nitajisahau kuwa nipo kazini” Marceline

    akaongea kwa sauti ya chini huku akiangua kicheko hafifu.

    “Basi nakuahidi kuwa sitorudia tena kukukosea mrembo” nilimwambia la?kini hata nilipomwambia hivyo yeye akaendelea kucheka tu na kicheko chake

    kilipokoma akaniuliza.

    “Pasi yako ya kusafiria inaonesha kuwa wewe ni mwandishi wa habari

    sivyo?

    “Ndiyo! mimi ni mwandishi wa habari lakini wa kujitegemea, nazunguka

    nchi za Afrika Mashariki kusaka habari na leo nimeonelea nije hapa nchini

    Rwanda hususani hapa jijini Kigali kwani sijawahi kufika nchi hii” nilimjibu

    msichana yule huku nikimtazama. Akayahamisha macho yake toka kwenye

    kioo cha kompyuta yake na kugeuka kunitazama kidogo bila kusema neno ki?sha akayarudisha macho yake tena kwenye kioo cha kompyuta lakini uso wake

    haukuonesha tashwishwi yoyote na hapo moyo wangu ukapiga kite.

    “Utafikia hoteli gani? swali lake likanifanya nipumbazike kidogo huku

    nikamtazama kabla ya kumjibu.

    “Bado sijapanga ni wapi nitafikia ila itakuwa ni hapa hapa jijini Kigali”

    “Hotelini siyo?

    “Bila shaka”

    “Chukua namba yangu tuwasiliane hoteli yoyote utakayofikia nifahamishe

    pengine tukaonana” Marceline aliongea huku akiipenyeza kwenye lile tundu

    la kioo kadi ndogo ya kibiashara ama Business card aliyoitoa toka kwenye

    faili moja lililokuwa juu ya meza yake huku akijitahidi kutokuonesha namna yoyote ya kuyavuta macho ya watu waliokuwa wakimtazama. Nikiwa nimei?fahamu vizuri hali hiyo nami nikapitisha haraka mkono wangu kupokea ile

    kadi na kuitia ndani ya mfuko wa koti langu la suti.

    Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu nilipomtazama Marceline na kugun?dua kuwa uso wake ulikwishabadilika na kuwa mbali na mzaha. Muda huo

    huo akawa amemaliza kuingiza taarifa zangu kwenye kompyuta yake kisha

    akakusanya vibali vyangu vyote vya kusafiria vilivyokuwa juu ya meza yake

    na kuvipinyeza dirishani, mimi nikavipokea na kuvitia kwenye mfuko wa

    koti langu mpaka pale nilipovifikisha ndani na kuhakikisha kuwa vilikuwa

    vimeungana na ile kadi aliyonipa aliyonipa awali. Nikashusha pumzi kwa mk?upuo na kumeza funda kubwa la mate.

    “Ahsante Marceline” nikamshukuru huku nikinyakua sanduku langu tayari

    kondoka.

    “Asante na wewe Patrick karibu sana Rwanda” Marceline akanijibu huku

    akianza kumuhudumia mtu aliyekuwa nyuma yangu, mimi nikageuka na

    kuanza kuondoka huku nikiwa na maswali mengi kichwani.

    Wakati nikitembea kuelekea nje ya uwanja ule wa ndege nilikuwa na kila

    hakika kuwa macho ya Marceline yalikuwa yakinisindikiza kwa nyuma hata

    hivyo sikugeuka kutaka kuthibitisha hilo. Sasa nilikuwa nimeingia rasmi jijini

    Kigali.

    Nipofika nje nilipokelewa na dereva mmoja wa teksi, kijana wa makamo

    ya miaka ishirini na sita hadi na nane aliyeonekana kunisomea ramani hara?ka kabla ya wenzake. Nikamwacha abebe sanduku langu huku nikiwapuuza

    madereva wengine wa teksi wa eneo lile waliokuwa wakiniita. Wengine kwa

    lugha ya kiswahili kibovu, wengine kwa kifaransa na wengine hata sikuzifa?hamu lugha walizokuwa wakizizungumza.

    Teksi ya yule kijana aliyenipokea sanduku langu ilikuwa karibu hivyo tu?lipofika akafungua buti ya gari na kuliweka lile sanduku na mimi nikafungua

    mlango wa nyuma na kuingia. Alipomaliza kuhifadhi sanduku langu kule nyu?ma kwenye buti ya gari akaja na kufungua mlango wa dereva, muda huo huo

    safari ikaanza. Teksi ikaacha maegesho ya kiwanjani pale na kuingia mitaani.

    “Unaelekea wapi bosi wangu? yule kijana aligeuka na kuniuliza kwa lugha

    ya kiswahili chenye lafudhi ya kinyarwanda wakati tulipokuwa tukiyaacha

    maegesho yale na hapo nikawa nimekumbuka kuwa sikuwa nimemwambia

    uelekeo.

    “Unaifahamu hoteli yoyote yenye hadhi nzuri iliyopo hapa mjini? nikamu?uliza.

    “Kigali ni miongoni mwa majiji yanayokuwa kwa kasi sana barani Afrika

    hivyo hoteli ni nyingi sana ni juu yako wewe mwenyewe kuchagua. Kuna

    Kigali Serena Hotel, ipo Boulevard de la Revolution, Manor Hotel Kigali ipo

    Nyarutama, Umobano Hotel ipo Boulevard de L’umuganda, Lemigo Hotel

    ipo Kimihurura, Golden Hills Hotel ipo Avenue Ntaruka huko Kiyovu, Top

    Tower Kigali ipo Boulevard de Umuganda, Stipp Hotel yenyewe ipo Rue de

    Masaka. Pia kuna Royale Villa’s Hotel, Hotel des Mille Collines yenyewe ipo

    Avenue de Republique, Kigali 1322. Hizo ni baadhi tu nyingine majina yake

    yamenitoka kidogo”

    “Nipeleke ilipo Hotel des Mille Collines jina lake nimelipenda” nilimwam?bia baada ya kufikiria kidogo na kufanya uchaguzi. Maana halisi ya Hotel des

    Mille Collines ikimaanisha hoteli ya milima elfu moja kwa lugha ya kifaransa.

    “Hotel des Mille Collines ni hoteli nzuri ya kifahari kama una pesa za kuto?sha utaifurahia, haipo kando sana ya mji na ina huduma zote za kisasa” kijana

    yule dereva aliongea kisha kukafuatiwa na ukimya kidogo wakati huo mawa?zo juu ya Marceline yakianza kupita taratibu katika ubongo huku nikijiuliza

    maswali kama, Kwa nini Marceline alitaka tuonane mpaka akanipa business

    card yake?, ni kweli kuwa alikuwa amebabaika na utanashati wangu au kuli?kuwa na jambo jingine?. Nikajiuliza hata hivyo sikutaka kuamini kuwa mimi

    ningekuwa mwanaume wa kwanza hapa duniani kumbabaisha Marceline kwa

    uzuri, sikutaka kabisa kuamini hivyo. Pengine kulikuwa na jambo alilotaka

    tuzungumze? lakini tutazungumza nini ilhali ndiyo kwanza tulikuwa tume?onana tena kwa mara ya kwanza?. Niliendelea kujiuliza na nikiwa katikati ya

    fikra hizo sauti ya dereva ikanirudisha mle ndani.

    “Wewe ni Mtanzania?

    “Endesha gari hadi Hotel des Milles Collines” nilimkatisha dereva yule kau?li akabaki kimya.

    __________

    TULIKUWA TUMESHAZIPITA kona tano za mitaa wakati nilipoukum?buka wajibu wangu. Toka katika siti ile ya nyuma niliyoketi nilikizungusha

    kichwa changu taratibu kutazama nyuma bila kumshtua dereva na hapo mwili

    wangu ukajikuta ukiingiwa na baridi ya ghafla. Moyo ukaanza kupiga kite kwa

    nguvu huku mwenendo wa mapigo yake ukiaanza kwenda katika utaratibu

    usiozoeleka, koo langu nalo likaanza kukaukiwa na mate. Gari aina ya Nissan

    Patrol yenye watu wawili mbele ilikuwa imetufungia mkia kwa nyuma huku

    nikishindwa kujua mahali ilipotokea.

    Niligeuka na kumtazama kwa udadisi dereva wangu wa hapo nikajua aliku?wa hafahamu kilichokuwa kikiendelea, nikageuka tena kutazama kule nyuma.

    Ile gari Nissan Patrol ilikuwa nyuma yetu kiasi cha umbali wa mita hamsini

    hivi, kilichozidi kunitia hofu ni kuwa gari lile lilikuwa ni gari la jeshi wa wa?nanchi wa Rwanda. Niliweza kuligundua kupitia namba zake hata hivyo nili?gundua kuwa dereva wa gari hilo alikuwa bado mwanafunzi katika kufuatilia

    windo. Nikapenyeza mkono wangu na kuzima taa ya ndani ya gari iliyokuwa

    chini ya paa la teksi ile na hapo dereva akamaka

    “Kwanini unazima taa? dereva akauliza na kugeka kunitazama hata hivyo

    akanikuta nikitazama mbele huku nikiwa tayari nimeisha lipigia hesabu tukio

    lile kuwa lingefuatia baada ya mimi kuzima taa ya mle ndani hivyo hakubaini

    chochote.

    “Mwanga wake unanisumbua”

    Jibu langu likamfanya dereva asiulize tena wala kugeuka nyuma. Nikata?basamu kidogo na kugeuka nyuma tena kulitazama lile gari. Kwa vyovyote

    nilikuwa na hakika kuwa kitendo cha mimi kuzima ile taa ndani ya gari kingetosha kabisa kuwafahamisha wale watu kwenye lile gari nyuma yetu kuwa

    nilikuwa nimeishawashtukia hila yao hata hivyo hilo halikunipa shida. Macho

    yangu sasa yaliweza kuona vizuri kule nyuma. Nikafanikiwa tena kuziona

    vizuri namba za lile gari huku nikijiuliza kuwa watu wale ni akina nani na

    kwanini wanifuatilie. Wemeshutukia nini kwangu mpaka wanifungie mkia au

    waliniona wakati nikiongea na Marcelina, au ni Marcelina ndiyo aliyowatuma

    lakini ili iweje?. Nilijiuliza bila kupata majibu na hapo nikaanza kushikwa na

    wasiwasi.

    Nikageuka kutazama mbele huku nikajitahidi kulisahau gari lile kwa muda,

    nikaipa utulivu akili yangu ianze kufanya kazi. Tayari muda wa dakika takrib?ani ishirini ulikwisha yeyuka tangu tulipotoka kule uwanja wa ndege, nili?gundua hivyo baada ya kuitazama saa yangu ya mkononi iliyoonesha vizuri

    kupitia vishale vyake vilivyokuwa vikimetameta. Kwa mahesabu ya haraka

    nikajua zilikuwa zimebaki dakika chache kufika ilipo Hotel des Milles Collin?es. Sikutaka kuendelea kufuatiliwa hadi hotelini hapo pia sikutaka watu wale

    wafahamu ni wapi nilipokuwa nikielekea. Nikapanga kubadilisha mwelekeo.

    “Unayo mafuta ya kutosha kwenye gari? nilimuuliza yule dereva

    “Yapo mafuta ya kutosha tunaweza kuzunguka jiji la Kigali mpaka asubuhi

    bila kusimama” dereva alizungumza kwa mbwembwe bila kujua kusudi la

    swali langu hata hivyo jibu lake likanifanya nitabasamu kidogo.

    “Ingia barabara ya kushoto hapo mbele” nilimwambia yule dereva lengo

    langu likiwa ni kupata uhakika kuwa wale watu waliokuwa kwenye lile gari

    nyuma yetu walikuwa wakitufuatilia au walikuwa na hamsini zao. Dereva

    akafanya kama nilivyomuagiza hivyo tulipofika kwenye ile barabara iliy?ochepuka upande wa kushoto akakunja kona kuingia barabarani hiyo. Ilikuwa

    ni barabara inayokatisha katika mtaa mmoja tulivu mno uliopo katikati ya ma?jengo marefu ya ghorofa yaliyokuwa na maduka ya kisasa kwa chini ambayo

    wakati huu yalikuwa yamefungwa ingawaje bidhaa zilikuwa ndani ya maduka

    hayo baadhi ziliweza kuonekana kwa msaada wa taa zilizokuwa zikimulika

    mle ndani kupitia kuta safi za milango na madirisha ya vioo. Utulivu wa mtaa

    ule ukanifanya niikumbuke mitaa ya jiji la Dar es Salaam ambayo usiku na

    mchana haikukaukiwa na pilikapilika za watu na magari.

    Tulipoingia kwenye barabara ya mtaa ule nikageuka tena kulitazama lile

    gari kwa nyuma, nikafarijika kutoliona likiwa limefungia mkia na hapo nika?geuka tena mbele kumtazama dereva kama kulikuwa na chochote alichokuwa

    amekishtukia, nikagundua bado alikuwa hafahamu chochote. Hali hiyo ikazidi

    kunipa furaja kwani sikutaka afahamu kuwa tulikuwa tukifuatiliwa kwani hilo

    lingemtia mashaka juu yangu.

    Kimya kikawa kimechukua nafasi baina yangu na dereva nikautumia muda

    huo kuyazungusha macho yangu kutazama huku na kule nikijaribu kuuzoea

    mtaa ule na wakati nikifanya hivyo nikaona vitu viwili muhimu ambayo vin?genifanya nisiweza kuusahau kirahisi mtaa ule.

    Kitu cha kwanza kulikua na ofisi kubwa inashughulika na uazimishaji wa

    magari, juu ya ofisi hizo kukiwa na bango kubwa lililosomeka Kigali Cars

    Rentals Services. Kitu kingine kulikuwa na duka la silaha lililokuwa upande wa kulia wa mtaa ule likiwa limezungushiwa uzio wa ukuta mfupi wa vyuma.

    Juu ya duka lile kulikuwa na bango kubwa la maandishi lililosomeka Rwanda

    Arms Association .

    Tulikuwa tupo mbioni kufika mwisho wa barabara ya mtaa ule pale nilipo?geuka tena kutazama nyuma, na hapo moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu

    kama niliyepigwa konde zito kichwa bila kutarajia. Lile gari Nissan patrol

    lililokuwa limetufungia mkia hapo awali sasa lilikuwa mita chache nyuma

    yetu, loh! nikashtuka sana.

    “Ingia barabara ya upande wa kulia” nikamwambia dereva bila kuchungu?za kama eneo lile tulilokuwa lilikuwa na barabara inayochepuka upande wa

    kulia au lah!. Dereva akapunguza mwendo na kueguka kunitazama akionesha

    kuchanganywa na maelezo yangu.

    “Wewe ni mgeni hapa Kigali na inaelekea hujui vizuri mitaa ya jiji hili.

    Hakuna barabara zinazokatisha katikati ya mitaa huwa ni hadi mwisho wa

    mtaa ndiyo utakutana na barabara nyingine” Dereva alinifafanulia.

    “Sawa! basi ukifika mwisho wa mtaa huu fuata barabara ya upande wa

    kulia”

    “Kwani tunaelekea wapi bosi? hii si barabara ya kuelekea Hotel des Mille

    Collines, huku tunazunguka mno”

    “Hatuelekei tena Hotel des Mille Collines kuna mtu nahitaji kuonana naye

    kwanza kabla ya kuelekea huko” nilimdanganya dereva huku nikiwa nafikiria

    cha kufanya endapo lile gari lililokuwa nyuma yetu lingeonekana kuzidi ku?tufuatilia.

    “Oh! kumbe umebadili mawazo, si ungeniambia ni wapi tunapoelekea

    sasa? dereva aliuliza kwa jazba.

    “Fuata maelekezo yangu nitakulipa pesa yako au kama hutaki nishuke hapa

    hapa nitafute teksi nyingine”

    “Sawa basi usijali bosi wangu mteja kwangu ni mfalme wewe sema popote

    nitakupeleka”

    “Ingia upande wa kulia hapo mbele”

    Dereva akafanya kama nilivyomwagiza tulipo mwisho wa barabara ya mtaa

    ule kulikuwa na barabara nyingine inayokatisha kwa mbele hivyo akachepuka

    na kuifuata barabara hiyo upande ule wa kulia. Muda mfupi baada ya kuingia

    barabara hiyo nikagueka tena nyuma kuitazama ile gari Nissan Patrol iliy?okuwa imetufungia mkia kwa nyuma. Bado ilikuwa ikitufuatilia na mara hii

    niliiona ikichepuka na kufuata uelekeo wetu na hapo nikawa na uhakika kuwa

    bado nilikuwa nikifuatiliwa na watu wale.

    “Sasa ni lazima nipange mkakati wa kuwapoteza” nilijisemea moyoni. Baa?da ya kuwaza na kuwazua mwishowe nikapata wazo, wazo hilo likanifanya

    nisiendelea kumficha dereva wangu, kwani kumficha kungenipelekea wakati

    mgumu sana wa kuwapotea watu wale na njia pekee ilikuwa ni kuanzisha

    maongezi ya kirafiki.

    “Bwana hatufahamiani majina ndugu yangu” nilimwambia dereva “Pengine

    nikakuhitaji kwa kipindi kingine nitakachokuwa hapa Kigali ili unichukue

    kwenye safari zangu kwani mimi huwa sipendi sana kubadili dereva”

    Nilizungumza katika lugha ya kirafiki nikafanikiwa kumhadaa dereva yule

    kiasi cha kumfanya akenue meno yake.

    “Mimi naitwa Jean Pierre Umugwaneza kabila langu ni Mtutsi, nimezaliwa

    na kukulia hapahapa Kigali hivyo vitongoji vyote vya jiji hili navifahamu.

    Wewe ni Mtanzania siyo? aliniuliza kwa furaha.

    “Ndiyo, mimi ni Mtanzania na hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa

    Rwanda” nilimwambia huku nikigeuka tena kutazama nyuma. Lile gari bado

    lilikuwa linatufuatilia.

    “Mimi nilijua tu kuwa wewe ni mtanzania wakati nilipokusikia ukizung?umza, karibu sana Rwanda. Watanzania ni ndugu zetu wa kwanza, nyie ni

    watu wacheshi na wakarimu mno, nimewahi kuwabeba wateja wengi wa ki?tanzania wanaoingia hapa nchini. Nilipofuatilia nikagundua ninyi watanzania

    tabia zenu wote karibu zinafanana. Mnazoeana na watu haraka, wacheshi na

    marafiki wazuri mnao ujua utu”

    Dereva yule alizungumza kwa furaha na mimi nikajikuta nikifurahi kwa

    watanzania kufahamika kuwa na sifa njema hata mbali ya mipaka ya nchi yetu.

    “Hujaniambia jina lako bwana” dereva alihitimisha kwa kuniuliza

    “Patrick Zambi” nilimwambia.

    “Karibu sana Patrick mimi ninauzoefu mzuri na hili jiji na vitongoji vyake.

    Kama nilivyokwisha kukuambia hivyo muda wowote utakapohitaji msaada

    nione mimi” dereva alijitapa “Wewe ni mfanya biashara? dereva aliniuliza

    pale alipoona kimya kinazidi.

    “Hapana mimi ni mwadishi wa habari wa kujitegemea na nimekuja hapa

    kutafuta habari”

    Haraka niliweza kubaini namna jibu langu lilivyomshtua dereva yule aka?inua macho yake na kunitazama kupitia kioo cha ndani ya gari kilichokuwa

    juu mbele yake.

    Wakati huo tulikuwa tumetokezea kwenye barabara nyingine inayopita

    kandokando ya jiji la Kigali.

    “Na wewe ni mwandishi wa habari? Aliniuliza kama ambaye hakulisikia

    vizuri jibu langu.

    “Ndiyo! mbona umeshtuka hivyo? nilimuuliza kwa udadisi zaidi.

    “Ni kweli nimeshtuka sana pale uliponiambia kuwa wewe ni mwandishi wa

    habari tena kutoka Tanzania”

    “Cha ajabu ni kipi?

    “Bila shaka umekuja kuchukua nafasi ya yule mwenzako aliyeuwawa wiki

    mbili zilizopita sivyo?

    “Mwenzangu nani? nilimuuliza kwa shauku.

    “Si yule Tobias Moyo, Mtanzania na mwandishi wa habari kama wewe ali?yeuwawa wiki mbili zilizopita kule Amahoro!”

    “Loh! Tobias Moyo ndiyo namfahama ni mwandishi wa habari wa gazeti la

    Afrika Mashariki, ameuwawa! nani aliyekwambia habari hizo? nilijidai ku?hanamika kana kwamba taarifa zile zilikuwa ngeni kwangu.

    “Siyo kuambiwa tu nimemuona kwa macho yangu. Mara nyingi alikuwa

    akinikodi mimi katika safari zake hapa jijini hata siku ya kifo chake ni mimi niliyemrudisha nyumbani kwake na asubuhi yake nilishtuka sana kusikia To?bias Moyo ameuwawa”

    “Umenishtua sana kwa taarifa hizi kumbe Tobias Moyo ameuwawa? ni nani

    aliyemuua?

    “Nani anayefahamu! na mpaka sasa wauaji hawajatangazwa kukamatwa

    japokuwa serikali inaendelea na uchunguzi. Baadhi ya watu wanasema ali?kuwa akitembea na mke wa mtu kwa siri hivyo mwenye mke aliposhtukia

    ndiyo akamfanyia unyama huo. Maiti yake ilikuwa haitazamiki mara mbili

    kwa namna ilivyochabangwa vibaya kwa mapanga”

    Nilimsikiliza dereva yule vizuri na nikajua kuwa alikuwa amezama kwenye

    fikra za simanzi. “Umesema kuwa usiku wa kifo chake ni wewe uliyemrudisha

    nyumbani?

    “Ndiyo! ulikuwa ni usiku wa saa sita aliponipigia simu niende nikawa?chukue huko Magda Cata”

    “Magda Cata ni wapi?

    “Magda Cata ni mgahawa mzuri na maarufu upo kando ya hili jiji”

    “Ukawachukue yeye na nani?

    “Niyonkuru”

    “Niyonkuru ni nani? nilimuuliza huku nikigeuka nyuma kulitazama lile gari

    nikaliona bado lilikuwa nyuma yetu likitufuatilia.

    “Niyonkuru ni rafiki wa kike wa Tobias Moyo, ndiye niliekuwa nikimuona

    nae mara kwa mara katika safari zake”

    “Umeonana na huyo Nyunkuru hivi karibuni baada ya kifo cha Tobias

    Moyo?

    “Hapana na hata simu yake haipatikani ila nahisi atakuwa nyumbani kwake”

    “Anaishi wapi?

    “Avenue Gikondo nyumba namba 5 si mbali sana kutoka hapa”

    Nilizihifadhi vizuri taarifa zile kichwani huku nikitafakari kisha nikavunja

    tena ukimya

    “Kwa hiyo siku hiyo ulimpeleka huyo Niyonkuru nyumbani kwake halafu

    baada ya hapo ndiyo ukampeleka Tobias Moyo nyumbani kwake?

    “Hivyo ndivyo ilivyokuwa na kabla ya hapo Tobias alimsisitiza Niyonku?ru kuwa waende wote wakalale kwake lakini Niyonkuru hakukubaliana nae

    hivyo tulimpeleka kwanza yeye”

    Maelezo ya dereva yule yalinifanya nijisikie furaha kwa kupata taarifa

    nilizizohitaji pasipo kutumia jitihada kubwa. “Angalau nilikuwa na sehemu

    ya kuanzia” nilijisemea moyoni na wakati huo tulikuwa tumekwishaanza kuli?acha jiji la Kigali nyuma yetu na hapo nikangundua kuwa tulikuwa tukienda

    bila uelekeo maalumu na lile gari lililotufungia mkia nyuma yetu halikuoneka?na kutupa mwanya wa kutoroka. Na hapo nikavuja ukimya

    “Kuna ukumbi wowote wa starehe wa hapa karibu unaoufahamu?

    “Kumbi ni nyingi mno ila kwa sasa nyingi zitakuwa zimefurika watu” dere?va alinijibu huku akijaribu kufikiria

    “Labda nikupeleke Casino Kigali si mbali sana kutoka hapa. Ipo mtaa wa

    Umuganda, ni sehemu nzuri ya kustarehe yenye warembo wa kinyarwanda wa kila namna”

    Nilicheka kidogo huku nikiivutia picha Casino hiyo

    “Sawa basi nipeleke nataka nikajionee mwenyewe”

    Nilimwambia yule dereva na muda huohuo dereva akachepuka kuifuata

    barabara ya upande wa kushoto. Niligeuka tena kutazama nyuma bado nika?liona lile gari Nissan Patrol likiwa bado linatufuatilia na hapo nikatabasamu

    huku nikijisemea moyoni “Dawa yenu ipo jikoni”.

    Baada ya muda mfupi kupita tukawa tumefikia mtaa wa Umuganda ilipo

    Casino Kigali, teksi ikaenda na kusimama mbele ya jengo refu la Top Tower

    Hotel. Dereva akageuka nyuma kunitazama na hapo nikapata nafasi nzuri ya

    kuiona sura yake nyembamba na ndefu yenye bashasha za kirafiki.

    “Umefika bosi Casino Kigali ipo ndani ya hii Top Tower Hotel” yule dereva

    aliongea katika tumaini la kulipwa ujira wake.

    “Nashukuru sana bwana Jean Pirre Umugwaneza” niliongea kwa kulitamka

    vizuri jina lake na hapo nikamwona akitabasamu.

    “Unanidai pesa kiasi gani? nilimkatisha

    “Faranga arobaini za kinyarwanda” aliniambia huku akitazama mbele ili

    nisipate nafasi ya kumuomba anipunguzie. Sikuhitaji kupunguziwa nikatoa

    pochi yangu iliyokuwa na fedha za ki nyarwanda ambazo nilizibadilisha ni?lipokuwa jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari yangu. nikahesabu pesa

    alizohitaji na kumpa. Hata hivyo japokuwa zile pesa zilizidi hakunirudishia

    akidhani nimejisahau.

    “Nenda na sanduku langu Hotel des Milles Collines ukaniwekee chumba

    pesa zitakazobaki ni zawadi yako, mimi nitakuja huko baadaye”

    Nilimwabia Jean Piere Umugwaneza na hapo nikamuona akitabasamu.

    Nilikuwa nimempa pesa nyingi kama namna ya kujenga uaminifu kwake.

    Nilikumbuka sanduku langu lililokuwa kwenye buti nyuma ya gari lake na

    kujiridhisha kuwa hapakuwa na kitu chochote cha maana ndani yake zaidi

    ya kamera yangu kubwa ya kiuandishi wa habari aina ya Olympus na nguo

    chache. Vitu ambavyo hata kama angeamua kupotea navyo visingekuwa na

    maana sana kwangu. Kisha ni kataka anipe namba zake za simu ili niweze

    kumpigia pale nitakapomhitaji na aliponipa nikazihifadhi kwenye mfuko wa

    shati langu.

    “Unakaa wapi?

    “Avanue de la Justice nyumba namba 13”

    “Sawa Jean nakuomba uwe makini kuanzia sasa. Kuna gari lililokuwa

    likitufuatilia kwa nyuma tangu tulipokuwa tukitoka kule uwanja wa ndege”

    nilimwambia na hapo akashtuka na kunitazama kwa taharuki kama aliyekabwa

    na lundo la viazi kooni.

    “Gari!, gari gani?

    “Geuka nyuma”

    Nilimwambia na alipogeuka nyuma akaliona lile gari Nissan Patrol lil?ilokuwa likitufuatilia kwa nyuma wakati huu lilikuwa limeegeshwa hatua

    chache nyuma yetu kando ya barabara.

    “Nimeliona!” akanijibu huku akishusha pumzi taratibu. Nilimhurumia sana Jean kwa namna uso wake ulivyokuwa umehamanika na kujawa na mashaka.

    “Umejuaje kama gari lile lilikuwa likitufuatilia sisi?

    “Vichochoro vyote tulivyopita lilikuwa nyuma yetu”

    “Kwanini hukuniambia mapema?

    “Ungefanya nini endapo ningekwambia?

    Nilimuuliza na hapo akashindwa kunijibu, akabakia akinitazama tu kwa

    mshangao.

    “Lile ni gari la jeshi la wananchi Rwanda kwa nini watufuatilie sisi?

    Aliniuliza huku akirudia kulitazama tena lile gari kwa nyuma.

    “Mimi na wewe hatujui hata hivyo ni mimi ndiye ninaefuatiliwa na si wewe”

    “Kwa sababu gani? akaniuliza huku ameachama mdomo kwa hofu.

    “Kwa sasa sifahamu ila wewe fanya kama nilivyokuagiza na chochote kita?kachotokea tutawasiliana kesho asubuhi”

    Nilimwambia kisha nikafungua mlango wa gari na kutoka nikimuacha ka?tikati ya taharuki.Nilipotoka sikulitazama tena lile gari Nissan Patrol lililoku?wa limeegezwa nyuma yetu kando ya barabara ile kwani kwa kufanya hivyo

    ningezidi kuwashtua wale jamaa na mimi sikutaka kufanya hivyo. Nikaanza

    kwa haraka kuelekea mlango wa mbele wa Top Tower Hotel na muda huo huo

    nikamsika Jean akiwasha gari na kuondoka nyuma yangu.

    Niliendelea kuharakisha nikielekea ndani ya Top Tower Hotel huku nikiwa

    na hakika kuwa watu wale waliokuwa wakinifuatilia wasingeweza kwa urahi?si kutambua ni wapi ambapo nimefikia.

    Nilipofika katika mlango wa kuingilia ndani ya hoteli ile nilisimama na

    kugeuka nikalitazama tene lile gari Nissan Patrol lililokuwa limeegeshwa

    nyuma yetu. Mara nikaona mlango wa mbele ukifunguliwa kisha mtu fulani

    akashuka. Mtu huyo aliposhuka alitazama huku na kule kisha akaanza ku?harakisha kuja upande wangu. Mimi nikatabasamu kidogo kisha nikaendelea

    na safari yangu kuingia ndani ya hoteli. Mara tu nilipoingia ndani ya hoteli ile

    niligundua kuwa nilikuwa nimeingia kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

    __________

    ILIKUWA NI HOTELI YA HADHI YA JUU yenye nafasi ya kutosha ya

    ukumbi mpana chini yake, ukumbi huo ulikuwa na seti nane za makochi ya

    sofa yaliyopangwa katika mtindo wa kila seti moja kuzunguka meza moja

    ya mahogani katikati. Sakafu yake ilifunikwa kwa zulia maridadi la kifaha?ri lenye rangi nyekundu ya kupendeza. Mwanga wa taa zilizokuwa zikimu?lika ukumbuni mle ulikuwa hafifu na wenye kupendeza. Madirisha yalikuwa

    makubwa na ya vioo yalifunikwa kwa mapazia marefu.

    Kupitia spika zilizokuwa kwenye maeneo fulani ya ukumbi ule nilisikia

    muziki laini wa kupendeza ukipigwa. Seti zote za makochi ya mle ndani zili?kuwa zimekaliwa na watu tofauti tofauti, wageni kwa wazelendo waliokuwa

    wakiendelea na maongezi yao ya hapa na pale huku wakitazama runinga pana

    zilizounganishwa na chaneli mbalimbali za Dstv zilizokuwa zimetundikwa

    ukutani ukumbini mle.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kipande mstatili cha zulia jekundu lililoanzia mlangoni kilinichukua hadi sehemu ya mapokezi ya hoteli ile. Vijana wawili waliovaa sare safi za hoteli

    ile, suti za rangi ya samawati, mashati meupe, tai nyeusi na glovu nyeupe

    mikononi walinikaribisha kwa kuzingatia vigezo vyote vya maadili ya kazi

    yao huku nyuso zao zikiumba tabasamu.

    “Nahitaji kuingia Casino” bila kupoteza muda nikaitanguliza mbele hoja

    yangu.

    “Ghorofa ya pili utaona mlango mpana upande wa kushoto juu yake kuna

    kibao kidogo kimeandikwa Kigali Casino Inn ndiyo humo”

    Kijana mmoja akanielekeza huku akinionesha tabasamu lake na mimi nikaf?anya fadhila kidogo kwa kuruhusu tabasamu langu hafifu.

    “Kwenda huko juu naingilia upande upi? niliuliza.

    “Oh! kumbe wewe ni mgeni na bila shaka ni mara yako ya kwanza kuja hapa

    sivyo? mwenzake akaniuliza na hapo nikatikisa kichwa kuonesha kukubaliana

    na maneno yake.

    “Unapaswa kulipia hapa kwanza halafu utapewa tiketi ya kuingilia ambayo

    utaionesha kwa mtu wa mlangoni mwa Casino. Kwenda juu unapitia upande

    wa kushoto kwako mbele utaona ngazi, pembeni yake kuna chumba cha lifti

    na hapo utachagua utumimi njia gani kati ya hizo”

    “Kiingilio cha Casino ni pesa kiasi gani?

    “Ni dola kumi za kimarekani lakini ukipenda unaweza kulipa katika Faran?ga za kinyarwanda, Euro,GB pounds, South Afrika Rands na pia tunakubali

    kwa malipo ya Visa card kama utapenda kulipa wa njia hiyo”

    Sikupenda kupoteza muda huku nikijua kuwa wale watu waliokuwa wak?inifuatilia muda mfupi tu wangekuwa pale hivyo nikaingiza mkono mfukoni

    kuichukua waleti yangu ya ngozi ya black mamba na haraka nikahesabu faran?ga za kinyarwanda kiasi cha pesa kinacholingana na dola kumi za kimarekani

    kisha nikazipitisha dirishani. Wakati huo niligeuka tena kutazama nyuma

    yangu kuhakisha kama yule jamaa aliyekuwa akinifuatilia alikwishaingia mle

    ndani ya ukumbi. Nikafarijika kutomuona yule mtu hata hivyo nilijua kuwa

    alikuwa mbioni kuingia.

    Mhudumu aliponipa tiketi nikaipokea na kutia mfukoni kisha nikaanza

    kutembea nikiufuata ule upande wa kushoto kama nilivyoelekezwa. Hatua

    chache nilizotembea upande wa kushoto nakaziona ngazi za kuelekeza seh?emu ya juu ya hoteli ile pembeni yake kukiwa na chumba cha cha lifti. Kwa

    kupenda uhuru zaidi nikaiacha lifti na kushika ile njia ya ngazi na kuanza

    kupanda juu.

    Wakati nikimalizia kuzipanda ngazi zile ili niingie ile ghorofa ya pili yenye

    casino kule chini nilipotoka niliweza kusikia sauti ya hatua za mtu mwingine

    aliyekuwa akipanda zile ngazi kwa pupa. Nikaharakisha kutembea katikati ya

    korido iliyokuwa kwenye ghorofa ile ya pili huku macho yangu yakiikagua

    milango yote iliyokuwa upande wa kushoto kwangu. Nilipoufikia mlango wa

    tatu nikaona kibao kidogo juu ya mlango huo chenye maandishi yaliyochong?wa vizuri na kupakwa rangi nyeupe yakisomeka Kigali Cassino Inn. Bila

    kupoteza muda nikakishika kitasa cha mlango ule na kukisukuma kwa ndani

    na hapo nikajikuta nikikabiliana na nyuso mbili matata za mabaunsa wa mlangoni, vijana wawili weusi walionyoa vipara, miili yao mikubwa iliyojengeka

    kimazoezi ikishindwa kujificha katika makoti meusi ya suti na suruali za jeans

    walizovaa. Mmoja akiwa amesimama upande huu wa mlango mwingine ule.

    Nilipofungua mlango tu wote waligeuka kunitazama bila kuzungumza

    neno na mimi nikachukua tiketi yangu toka mfukoni na kuwaonesha. Mmoja

    alipoiona akanifanyia ishara kwa kichwa kuwa niingie. Nikaingia ndani na

    kuusikia mlango ule ukifungwa nyuma yangu.

    Wakati nikitembea mle ndani huku nikitazama huku na kule nilijikuta niki?yakumbuka maneno ya Jean Perre Umugwaneza kuwa Casino Kigali ilikuwa

    kitovu cha wasichana warembo wa kinyarwanda wa kila namna. Ni kweli ali?kuwa hajakosea kusema vile kwani ni kama dunia yote ya wasichana warem?bo ilikuwa imehamia mle ndani na hakika sikuwahi kufikiria kama Rwanda

    ingekuwa na hazina ya walimbwende kiasi kile.

    Kwa haraka niliweza kubaini kuwa idadi ya wasichana katika casino ile ili?kuwa ni zaidi ya wanaume na pia kulikuwa na idadi kubwa ya wageni wenye

    asili ya bara la Asia, Marekani na Ulaya. Meza zote za ukumbini mle zilikuwa

    zimekaliwa na watu, mabibi na mabwana na juu ya meza hizo kulikuwa na

    lukuki ya vinywaji vya aina aina. Midundo ya muziki uliokuwa ukipigwa mle

    ndani ilikuwa juu sana kiasi cha kuwafanya watu wasiweze kusikilizana lakini

    cha ajabu zaidi hakuna aliyeonekana kukereka na na hali hiyo.

    Muziki huo ulikuwa kichezwa na wasichana wawili warembo waliovaa biki?ni tu ndani ya chumba kidogo chenye za vioo kilichokuwa katikati ya ukumbi

    wa casino ile. Mmoja kati ya wasichana hao alikuwa ameshika mjeledi mwe?pesi aliokuwa akimchapanao mwenzake matakoni na vichapo hivyo vikienda

    sambamba na midundo ya muziki wa mle ukimbini. Wasichana hao waligeuka

    kutazama wakati walipoona mlango wa kuingia ukumbini mle ukifunguliwa

    halafu wakageuka kuendelea na hamsini zao huku wakinyonyana ndimi na

    kushikana sehemu nyeti jambo hilo lilinishangaza sana.

    Nilijitahidi kupishana na watu waliokuwa wamesimama wakicheza muziki

    mle ndani na niligundua kuwa baadhi ya watu hao walikuwa wamelewa.

    Upande wa kushoto wa ukumbi ule nikaona mlango juu ya mlango huo

    kuliandikwa Gambling Hall, nikajua kuwa kile kilikuwa ni chumba cha ku?cheza kamari. Nilipotazama upande wa kulia nikauona mlango wa chum?ba kingine umeandikwa V.I.P Hall na hapo nikatambua kuwa kile kilikuwa

    chumba cha watu wa hadhi ya juu. Nilitazama mbele yangu nikaiona kaunta

    kubwa ya vinywaji ndani yake kulikuwa na mwanaume mmoja mwenye asili

    ya Asia aliyevaa suti nadhifu ya hudhurungi na tai ndogo nyeupe ya shingo?ni, kichwani alikuwa amenyoa upara na kuzikatia vizuri ndevu zake. Alikuwa

    akiwahudumia wateja katika kaunta hiyo. Nikaelekea pale kaunta nilipofika

    nikajipandisha juu ya stuli ndefu iliyokuwa eneo lile na hapo nikajikuta niki?tazamana na yule mhudumu.

    “African cocktail please” nilimwambia mhudumu huku nikiwa nimeupa

    mgongo ukumbi huku hisia zangu zote zilikuwa katika ule mlango wa kuingil?ia ukimbini mle aliokuwa nyuma yangu. Muda mfupi baadaye bilauri ndefu ya

    kinywaji baridi cha African cocktail yenye mrija mrefu ilikuwa mbele yangu huku imezungushiwa karatasi nyeupe ya tishu na kipande kidogo cha limao

    kikiwa kinaning’inia juu kwenye ukingo ya bilauri hiyo. Wakati nilipokuwa

    najiandaa kupata kinywaji hicho nikashtushwa na busu zito shavuni mwangu

    upande wa kulia, nilipogeuka nikamuona msichana mrefu na mrembo wa kin?yarwanda huku ameliachia tabasamu lake bila kificho.

    Nilipomtazama vizuri nikajua msichana yule alikuwa miongoni mwa wale

    wasichana wawili waliovaa bikini waliokuwa wakicheza muziki ndani ya kile

    chumba cha kuta za vioo kilichokuwa katikati ya ukumbi wa ile Casino dakika

    chache zilizopita. Wakati huu binti huyu mlimbwende alikuwa amavaa sketi

    fupi ya jeans iliyoyaweka wazi mapaja yake laini na mang’avu huku matiti

    yake makubwa ya wastani yaliyochorwa tatoo ya alama za nyayo za paka ya?kiwa nusu wazi kifuani mwake. Niliduwaa kwa dakika chache nikimkodolea

    macho msichana yule mwenye kila sifa za urembo huku nikijiuliza kwa nini

    asingetafuta bwana mwenye pesa na kuolewa nae badala ya kumdandiadandia

    kila mwanamume aingiaye kwenye Casino. Hata hivyo nilitabasamu tu.

    “Jina lako? nilimuuliza

    “Mutesi” alinijibu huku akitabasamu ijapokuwa jina lake halikuwa na maa?na yoyote kwangu.

    “Ni mara yako ya kwanza kuingia humu ndani eh? aliniuliza

    “Bila ya shaka”

    “Nilikutambua tu ulipoingia kuwa u mgeni wa humu ndani. Watu wote am?bao huwa wanakuja hapa hawafanyi kama wewe”

    “Niligeuka na kuvuta funda moja la African cocktail kwenye mrija kisha

    nikamgeukia msichana yule huku nikitabasamu.

    “Watu ambao wanakuja humu ndani kwani huwa wanafanyaje? nilimuuliza

    “Hawashangai shangai kama wewe”

    Maneno yake yakanifanya niangue kicheko hafifu

    “kweli?

    “Nipo humu ndani ya Casino zaidi ya miaka sita sasa hivyo tabia zote za

    wageni nazifahamu”

    “Kweli umekuwa mzoefu sana panda juu uketi, ni kinywaji gani ungependa

    kutumua? Nilimuuliza na hapo nikaliona tabasamu likichanua usoni mwake na

    bila kusita akasogeza stuli nyingine ndefu iliyokuwa pembeni yangu na kuketi.

    Nilizungusha jicho langu la siri kuangalia watu mle ukumbini na hapo nika?gundua kuwa karibu watu wote mle ndani walikuwa wemegeuka kunitazama,

    sikuwatilia maanani.

    “Chupa moja ya Four Cousins baridi”

    Mutesi alimwambia yule mhudumu wa kaunta. Mhudumu akampa mzinga

    mmoja wa mvinyo baridi aina ya Four Cousins na bilauri ndefu iliyozungushi?wa katarasi nyeupe ya tishu. Mutesi akamimina mvinyo ule mkali kwenye

    bilauri na kuyafakamia mafunda kadhaa kabla ya kuiweka juu ya meza na

    wakati huo akili yangu ilikuwa akimsubiri kwa hamu yule mtu aliyekuwa

    akinifuatilia huku nikijiuliza ni kitu gani kingekuwa kimemchelewesha kuja

    ukumbini mle.

    “Wewe ni Mtanzania? akaniuliza baada ya kuweka ile bilauri mezani

    “Ndiyo, umenijuaje?

    “Namna unavyoongea kiswahili chako na jinsi usivyomuoga kwani watan?zania wengi wapo hivyo” Mutesi aliendelea kuongea kisha akavuta tena funda

    moja la kinywakaji alipoiweka ile bilauri mezani akageuka kunitazama

    “Jina lako nani?

    “Patrick Zambi” nikamwambia huku nikikumbuka kuwa hii ilikuwa ni mara

    yangu ya tatu kulitaja jina hili kwa watu watatu tofauti tangu nilipoingia jijini

    Kigali hapa Rwanda. Hata hivyo sikuona taabu yoyote katika kurudia kulita?mka vizuri jina hili la bandia.

    “Hilo ni jina zuri sana, nimelipenda” aliniambia “Wewe ni mwanaume wa

    kwanza kuugusa vizuri moyo wangu Patrick” aliendelea kuongea huku akani?tongoza kwa macho yake legevu.

    “Nitaamini vipi maneno yako? nilimuuliza huku nikitabasamu na bila shaka

    sikuwa mwanaume wa kwanza kuambiwa maneno yale.

    “Wewe ni mzuri na unavutia sana ni hivyo tu basi”

    “Wewe ni mwanamke wa pili kuniambia hivyo mama yangu akiwa wa

    kwanza lakini hata wewe ni msichana mrembo na bila shaka unalifahamu hilo”

    “Sijui, labda!”

    Mutesi alijibalaguza kisha akageuka kunitazama

    “Umekuja kufanya nini hapa Rwanda na utakaa kwa muda gani?

    “Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, hiyo ndiyo kazi yangu ila

    sina hakika kwa sasa kuwa nitakaa hapa kwa muda gani”

    “Kwa hiyo wewe pia ni mwandishi wa habari? alinuliza kwa taharuki

    “Haswa! hiyo ndiyo kazi yangu”

    “Hujasikia habari za mwandishi wa habari Mtanzania aliyeuwawa hivi kari?buni huko Amahoro?, hizo ndizo habari zinazovuma mitaani kwa sasa”

    “Unamfahamu huyo mwandishi wa habari? nilimkatisha

    “Anaitwa Tobias Moyo, namfahamu vizuri kwani alikuwa akija hapa na msi?chana wake aitwae Niyonkuru, lakini yeye hakuwa rafiki mzuri kama wewe”

    “Kwa nini?

    “Hakuwa anapenda kuongea na msichana yoyote humu ndani, huyo Niyon?kuru kwake ndiye aliekuwa mtu wake wa maana zaidi”

    Niligeuka nikamtazama Mutesi usoni huku nikiyapima maneno yake hala?fu nikatabasamu kidogo na kuitoa pochi yangu mfukoni. Nikahesabu kiasi cha

    pesa nilichopaswa kulipa bili yangu na nilipomaliza nikamuita yule mhudu?mu karibu yangu kulipia vinywaji. Nilipomaliza nikachukua pesa nyingine na

    kumpa Mutesi.

    “Ahsante” aliniambia pindi alipozipokea

    “Umemuona yule mtu aliyeingia sasa hivi humu ukumbini?

    Nilimuuliza na hapo akageuka nyuma kuutazama mlango ule wa kuingilia

    Casino. Yule mtu aliyekuwa akinifuatilia alikuwa tayari ameingia mle ndani

    na nilikuwa nimeyazungusha macho yangu haraka kumtazama.

    “Ndiyo nimemuona” Mutesi alinong’ona taratibu huku akigeuka kunitaza?ma kwa shauku

    “Nahitaji taarifa zake nitakupa pesa zaidi” nilimwambia na hapo akageuka

    tena kumtazama yule mtu aliyeingia mle ndani halafu akageuka tena kunitazama.

    “Nipe muda” jibu la Mutesi likanifanya nifurahi kwani sikuwa nimefikiria

    kuwa angenipa jibu zuri tena mapema kiasi kile.

    “Namba yako ya simu? nilimuuliza huku nikishuka kwenye stuli ile ndefu

    ya kaunta niliyoketi.

    “Sina simu mimi”

    “Sasa tutawasiliana vipi?

    “Labda nikupe ya hapa Casino ukipiga utanipata”

    “Sawa, fanya hivyo basi”

    Nilimwambia na muda uleule akanitajia namba za simu za mle Casino na

    mimi nikazinakili hata hivyo niligundua kuwa alikuwa ni mtu mwenye masha?ka na mimi kwa kiasi fulani.

    “Nitakupigia nikufahamishe mahali tutakapoweza kuonana” nilimwambia

    huku akiwa bado ananitazama kwa udadisi.

    “Kuna njia yoyote ya kutoka humu ndani mbali na ule mlango wa kuingil?ia? nilimuuliza huku nikiwa nimegeuka kumtazama tena yule mtu aliyeingia.

    Alikuwa ni manaume mrefu na imara, mweusi anayechezea umri kati ya

    miaka thelathini na nne hadi thelathini na sita. Kwa mtazamo wa haraka nik?agundua kuwa alikuwa na tabia zote za kiaskari na sasa alikuwa akitazama

    tazama mle ukumbini.

    “Ipo njia moja inayotumiwa na wafanyakazi wa humu ndani yenyewe ipo

    nyuma ya choo cha humu ndani lakini kwa sasa imefungwa ni mpaka wakati

    wanapokuja wafanyakazi wengine kupokea zamu ndiyo hutumika”

    “Chooni ni wapi? nilimuuliza bila kupoteza muda

    “Mwisho wa kaunta upande wa kulia utaona mlango” Mutesi aliniambia

    huku akinitazama kwa mashaka.

    “Usiku mwema” nilimvuta Mutesi na kumngong’oneza “Naomba unifanyie

    kazi yangu” na wakati nikimnong’oneza niliweza kubaini namna alivyofariji?ka na harufu nzuri ya manukato yangu.

    “Usiku mwema na wewe pia” hatimaye aliitikia na hapo nikajitoa upesi

    mabegani mwake na kuushika uelekeo wa mwisho wa ile kaunta. Nilipofika

    nikakunja kona kulia na hapo nikajikuta nikitazamana na mlango wa maliwa?to, nikaufunga mlango ule na kupotelea ndani huku nikiwa na hakika kuwa

    mtu yule aliyekuwa akinifuatilia alikuwa bado hajaniona.

    __________

    MARA BAADA YA KUINGIA MLE NDANI nilikutana na milango mingine

    miwili mmoja upande wa kushoto ulioandikwa Gents toilet na mwingine upa?nde wa kulia ulioandikwa Ladies toilet, katikati korido inayotenganisha milan?go hiyo. Nikaifuata karido hiyo huko nikitembea kwa tahadhari.

    Mwisho wa korido ile fupi upande wa kushoto nikaona kichochoro kidogo

    chenye giza hafifu, nikataza huku na kule na sikuona upenyo mwingine tofauti

    na kile kichochoro hivyo nikazitupa hatua zangu kwa uangalifu nikikifuata

    kichochoro kile. Nilipofika mwisho wa kile kichochoro mbele yangu nikauo?na mlango mwingine. Ulikuwa mlango wa mbao mkubwa kiasi uliozuiwa na mlango mwingine wa grill kwa nje wenye makomeo mawili makubwa juu na

    chini. Makomeo hayo yaliyofungwa kikamilifu na makufuli imara ya Solex.

    Sikutaka kupoteza muda hivyo nikageuka nyuma kusikiliza kama kulikuwa

    na mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia, sikusikia sauti yoyote hivyo nikain?giza mkono kwenye mfuko wa koti langu la suti na kuchukua mkungu wa

    funguo malaya. Nikaanza kizifungua zile kufuli na nilipoifikia funguo ya tatu

    ikanipa jibu sahihi, zile kufuli zikafunguka na hapo nikajikuta nakikabiliana

    na ule mlango wa ndani wa mbao ambapo nilipoujaribu nikagundua kuwa

    haukuwa umefungwa hivyo nikausukuma na hapo nikajikuta nimetokezea

    kwenye chumba kidogo chenye ngazi zinazoelekea chini. Kabla ya kushuka

    kwenye ngazi zile nikaamua kuifunga kwanza ile milango nyuma yangu kama

    nilivyoikuta halafu nikaanza kushuka chini taratibu huku masikio yangu yote

    yakiwa tayari kunasa sauti za mjongeo wa kitu chochote.

    Nilizishuka ngazi zile kwa wepesi na tahadhari ya hali ya juu nikikwepa

    kumshtua mtu yeyote wa karibu. Nilipofika chini nikajikuta nimetokezea

    kwenye chumba cha chini cha maliwato kilichofanana na mazingira kama yale

    ya awali hata hivyo nilibaini kuwa kulikuwa na mlango mmoja ulioongezeka

    tofauti na kule juu. Mlango huo ulikuwa wazi hivyo nikazitupa hatua zangu

    kwa uangalifu nikiufuata mlango ule na hapo nikajikuta nimetokezea upande

    wa nyuma wa Top Tower Hotel ambako niliweza kuona mabwawa makubwa

    matatu ya kuogelea yaliyozungukwa na viti vyenye miavuli kandoni mwake.

    Kulikuwa na watu kiasi eneo lile wengi wao walikuwa wageni kutoka nje ya

    bara la Afrika hivyo nikajichanganya miongoni mwao na kuendelea na safari

    yangu.

    Giza la miti iliyokuwa imepandwa eneo lile kuizunguka hoteli lilinificha

    vizuri na kunifanyanisionekane na kutiliwa mashaka na mtu yeyote. Nili?poridhika kuwa hakuna aliyekuwa akinitazama nilichepuka chini ya miti ile

    kwenda kwenye ukuta wa hoteli. Nikafanikiwa kuufikia ukuta ule ambapo

    kwa mbinu zangu za kijasusi nilifanikiwa kuupanda ukuta ule kama ninayeru?ka mfereji mdogo wa maji machafu uliopo kichochoroni. Muda mfupi baadaye

    nikaangukia upande wa pili nje ya ukuta na hapo nikaanza kutembea nikiam?baa na ukutana huo kuifuata barabara.

    Nikiwa bado naitafuta barabara niliyatupa macho yangu kutazama kule

    mbele ya ile hoteli na hapo nikaliona lile gari Nissan Patrol lililokuwa likini?fuatilia mimi na Jean Perre Umugwaneza hapo awali likiwa bado limeegeshwa

    mbele ya hoteli. Tabasamu hafifu likaniponyoka na ili kutaka kulimudu vizuri

    tabasamu langu nikaupachika mche mmoja wa sigara ya Kingsize toka kwenye

    pakiti iliyokuwa mfukoni mwa shati langu. Nikauacha mche huo wa sigara

    ukiteketea taratibu mdomoni mwangu.

    Nilipofika mbele kidogo nikauacha ukuta ule wa hoteli nyuma yangu na

    kushika barabara moja ya mtaa iliyopakana na jengo la Kigali Business Cen?ter kwa upande wa kulia. Niligeuka nyuma kutazama kama kulikuwa na mtu

    yeyote aliyekuwa akinifuatilia hata hivyo sikumuona mtu yeyote hivyo nil?iendelea na safari yangu nikilipita jengo la posta upande wa kushoto. Nili?pofika kwenye mzunguko wa barabara ya MTN nikasimama nikivizia teksi. Magari mengi yalinipita bila ya kusimama japokuwa nilijitahidi kuyasimami?sha mwishowe nikabahatika kupata teksi iliyokuja na kusimama mbele yangu.

    Nikaingia ndani na kumtaka dereva anipeleke ilipo Hotel des Mille Collines,

    Avenue de L’Armee. Kigali 1322.

    Dereva wa teksi aliyenichukua alikuwa ni mzee mwenye umri wa miaka

    hamsini na kitu, mrefu mwembamba na mtu asiye na maneno mengi. Aligeuka

    kidogo na kunitazama wakati nilipokuwa nikiingia ndani ya teksi ile na kuketi

    siti ya nyuma na hapo safari ikaanza. Wakati wote wa safari yetu kuelekea Ho?tel Des Mille Collines dereva yule mzee alionekana kuendesha gari kwa ma?kini huku akiyafuatilia kwa makini maongezi yaliyokuwa akirushwa kwenye

    redio ya gari ambayo mimi sikuyaelewa ingawaje hata hivyo nilihisi kuwa

    yalikuwa yakirushwa kwa lugha ya kinyarwanda.

    Kwa mara ya kwanza sasa nikaanza kuhisi kuwa nilikuwa kwenye jiji tofau?ti tena mbali katika nchi ya ugenini katika jiji la Kigali lenye baridi na si lile

    jiji nilililolizoe la Dar es Salaam lenye joto kali la kukerehesha. Barabara za

    jiji hili zilikuwa zimepangiliwa vizuri mno na makazi ya watu nayo yalipende?keza kwa mpangilio unaovutia. Jiji lilikuwa limepangika vizuri na katika mtin?do wa kupunguza foleni mitaani na maeneo mengi ya wazi yalipambwa kwa

    bustani za maua tofauti ya kupendeza huku sheria za usafi zikionekana kuzin?gatiwa kila mahali. Maeneo yote wakati huu yalikuwa kijani kibichi kutokana

    na mvua za masika zilizokuwa zikiendelea kunyesha nchi nzima.

    Nikiwa nimeegemea siti ya nyuma niliyazungusha macho yangu kicho?vuchovu na kunipelekea muda fulani niyumbeyumbe kama mlevi huku ni?kipinga mihayo. Nilikumbuka kuwa nilikuwa sijapata mlo tangu nilipowasili

    hata hivyo uchovu niliokuwanao ulizidi hamu ya chakula. Mawazo yalipoanza

    kupita kichwani mwangu sikuweza kukumbuka namna usingizi ulinivyonizidi

    ujanja na kunichukua, nikabaki nimejiegemeza kwenye siti huku mdomo wazi

    nikitoa mkoromo hafifu kinywani mwangu. Dereva wa teksi alinishtua toka

    usigizini kwa kusema

    “Tumefika bosi” na hapo nikashtuka na kugeuka nikitazama nje upande

    wangu wa kulia. Nikagundua kuwa tulikuwa tumekwishafika Hotel des Mille

    Collines baada ya kuliona bango la hoteli hiyo likiwaka taa kwa nje na hapo

    nikamlipa dereva pesa yake.

    “Jitahidi upumzike bwana unaonekana umechoka sana” dereva yule

    aliongea wakati alipokuwa akipokea pesa, sikumjibu neno badala yake nikaf?ungua mlango wa gari na kutoka.

    “Usiku mwema”

    “Na wewe pia” mzee yule akaitikia huku akiwasha teksi na kuondoka. Si?kugeuka nyuma wala kumpungia mkono badala yake niliharakisha kuelekea

    ndani ya Hotel des Mille collines. Mara baada ya kuingia hotelini mle nili?gundua haraka kuwa ilikuwa hoteli ya kisasa zaidi na yenye vigezo vya hali

    ya juu na huduma za kisasa kutokana na mandhari yake. Nikaelekea moja kwa

    moja hadi mapokezi ambako nijilitambulisha kwa mhudumu mmoja mwana?mke wa makamo mrefu wa wastani aliyevaa sare zake nadhifu. Nikamuuliza

    kama kulikuwa mtu yeyote aliyefika hoteli pale kuniwekea nafasi ya chumba.

    “Wewe ndiye Patrick Zambi? aliniuliza kwa lugha ya kiingereza na hapo

    nilijikuta nikimkumbuka Jean Pierre Umugwaneza kwa kulishika vizuri jina

    langu.

    “Ndiyo”

    “Chumba namba 43 ghorofa ya tatu hata hivyo kuna taarifa unatakiwa kuja?za kwenye kitabu cha wageni”

    Yule mhudumu aliniamba huku akichukua kitabu cha wageni kilichokuwa

    juu ya meza pale mapokezi na kukipenyeza dirishani akinipa.

    “Soma na ujaze hapa”

    Akanionesha sehemu ya kujaza kwenye kitabu kile huku akanipa kalamu.

    Nikajaza taarifa zangu zote zilizohitajika kisha nikachukua funguo ya chumba

    na kuelekea kwenye chumba changu.

    Chumba namba 43 cha Hotel des Milles Collines kilikuwa upande wa diris?hani ghorofa ya tatu. Nilifika nikafungua mlango na kuingia ndani, nilifurahi

    sana kukuta begi langu likiwa mle ndani. Jean Pierre Umugwaneza alikuwa

    amefanya kama nilivyomuagiza hivyo nilifurahi sana nikaliendea begi langu

    na kulifungua. Nilishukuru kukuta vitu vyangu vyote vikiwa salama.

    Chumba kilikuwa cha kisasa chenye vitu vyote muhimu kama seti moja

    ya runinga, kitanda kikubwa, jokofu dogo, kabati la nguo la ukutani, simu ya

    mezani, kiyoyozi, seti mbili za makochi ya sofa na meza ndogo. Nilienda dir?ishani nikasogeza pazia na kutazama nje. Jiji la Kigali sasa lilikuwa likioneka?na vizuri na kupendeza kutokana na taa za barabara za mitaa kuangaza kila

    mahali usiku huu, hata hivyo niligundua kuwa kulikuwa na utulivu mkubwa

    katika barabara hizo ikiwemo barabara iliyopita nje ya hoteli ile kwa upande

    wa chumba changu, hali hiyo ikanipelekea nikumbuke kuitazama saa yangu

    mkononi.

    Nikagundua kuwa muda ulikuwa umesonga sana kwani ilikuwa tayari ime?kwisha timia saa saba na nusu usiku. Niliendelea kusimama pale dirishani ba?adaye nikaamua kurudishia lile pazia vizuri pale dirishani kisha nikavua nguo

    zangu na kuelekea bafuni kuoga. Niliporudi nikazima taa na kujitupa kitandani

    nikiwa hoi taabani na haukupita muda mrefu usingizi ukanichukua.

    __________

    NILIKUWA KICHAKANI pembeni ya mto mkubwa uliokatisha katika?ti ya msitu ule mnene wa kutisha, nilikuwa nimelala ukingoni mwa mto ule

    huku nusu ya miguu yangu ikiwa imeingia mtoni. Pembeni yangu alikuwa

    amelala mbwa mkubwa na mkali ambaye kwa sasa tulikuwa marafiki baada

    ya kukutana katika msitu huu kila mmoja akiwa na shida zake. Wote tuliku?wa tumepitiwa na usingizi mzito ingawaje mimi nilikuwa bado nikiyasikia

    makele ya maji mengi yaliyokuwa yakisafiri katika mto ule sambamba na sauti

    za ndege wa porini waliokuwa wakijiimbia nyimbo zisizopendeza kuzisikia.

    Halafu ghafla kelele zile zote zilikoma kwani kulikuwa na kitu fulani kikubwa

    kilichokuwa kikielea angani katika msitu ule ambacho kilikuwa kimetokeza

    kwa ghafla sana hali iliyowapelekea wale ndege wa msituni kuacha kuimba na

    kubaki mtini wakikitazama kile kitu angani na mimi nikageuka kukitazama. Mara ghafla nikakiona kile kitu cha ajabu angani kikianza kuanguka kwa

    kasi kuja ardhini na muda mfupi baadaye nilisikia mshindo mkubwa ardhini

    kiasi cha umbali wa nusu maili kutoka sehemu tulipokuwa na yule mbwa.

    Mshindo ule wa ajabu ukanishtua sana na yule mbwa aliyekuwa pembeni yan?gu akaanza kubweka kwa hasira kama aliyekatishwa usingizi wake na zile

    kelele za anguko la kile kitu kule mbali msituni. Hata hivyo nilipogeuka kum?tazama yule mbwa nikagundua kuwa hakuwa akiutazama uelekeo wa kile kitu

    kilipoangukia kule mbali msituni. Nilishanga kumuona mbwa yule akitazama

    angani nami ikabidi nigeuke kutazama kule angani alipokuwa akitazama na

    hapo nikashangaa kumuona ndege mkubwa ajulikanaye kama Tai akizunguka

    angani taratibu mle msituni huku mbawa zake zikiwa zimetengeneza kivuli

    kikubwa ardhini kisichoendana na ukubwa wa umbo lake.

    Tai huyo alikuwa juu sana angani kiasi cha urefu wa kilometa moja mbele

    yetu katika usawa wa mto ule. Nikataka nisimame ili niweze kumuona vizuri

    ndege yule wa ajabu hata hivyo ni wakati huu nilipogundua kuwa miguu yan?gu yote miwili ilikuwa ikielea kwenye ule mto. Nikageuka kuutazama ule

    mto na hapo nikashikwa na butwaa kuona yale maji ya mto hayakuwa maji

    kama nilivyodhani bali ilikuwa damu. Sikufahamu damu ile ilikuwa ikitoka

    wapi na ya kiumbe gani hata hivyo ilikuwa nyingi sana tena ikisafiri taratibu

    katika mto ule. “Nini hiki? nilijiuliza huku nikiitoa miguu yangu toka katika

    mto ule wa ajabu halafu muda uleule nikageuka kumtazama yule Tai aliyeku?wa akizunguka angani, sikumuona hata hivyo yule mbwa aliyekuwa pembeni

    yangu alikuwa bado akiendelea kubweka. Nikageuka kumtazama na kumuona

    kuwa wakati huu alikuwa hatazami tena kule alikokuwa akitazama hapo awali

    badala yake alikuwa akitazama katika usawa ule wa mto.

    Mbwa yule aliponiona nimesimama akageuka kunitazama kisha akanione?sha ishara kuwa nimfuate halafu pasipo kuhakikisha kuwa nilikuwa nimem?uelewa au lah! akaanza kutembea akiufuata ule uelekeo aliokuwa akiutazama

    hapo awali. Sikuwa na chaguo hivyo ikabidi nami nianze kumfuata taratibu

    mbwa yule kwani sikuwa tayari kupoteana na rafiki yule pekee katika msitu

    ule wa kutisha.

    Tulitembea taratibu kandokando ya mto ule tukiendelea na safari yetu huku

    yule mbwa akiwa mbele na mimi nyuma yake. Muda wote mimi nilikuwa ni?kiitaza ile damu nyingi iliyokuwa ikisafiri kwenye ule mto kando yetu, moyo

    ulikuwa ikienda mbio sana na hofu ilikuwa imenishika.

    Kiasi cha umbali wa kama kilometa tatu mbele yetu tukawa tumefika

    mwisho wa safari yetu chini ya mti mkubwa uliokuwa kando ya mto ule eneo

    lile la msituni. Mbele yetu tukamuona yule Tai akiwa ametua chini. Nilipomta?zama vizuri nikagundua kuwa alikuwa akila kwa kuunyofoa mzoga wa mnya?ma aliyekuwa amelala eneo lile. Mzoga huo ulikuwa ukitoa harufu mbaya isi?yoelezeka lakini harufu hiyo mbaya haikuonekana kuwa ni kikwazo chochote

    kwa Tai yule badala yake Tai yule mkubwa wa ajabu aligeuka na kututazama

    kidogo kisha akaendelea kula mzoga ule.

    Yule mbwa akaanza kumbwekea yule Tai hata hivyo yule Tai hakuonesha

    kushtushwa na kelele za yule mbwa hata kidogo, ikabidi nisogee karibu zaidi kumtazama Taiyule kuwa alikuwa akila mzoga gani. Loh! nilishtuka sana na

    kushikwa na hofu, moyo ukaanza kunienda mbio, nikajikuta nikianza kute?temeka. Yule Tai alikuwa akila mzoga wa binadamu mwanamke aliyekuwa

    amelala pale chini ya mti. Nipochunguza vizuri nikagundua kuwa yule Tai ali?kuwa ameuopoa mzoga ule toka ndani ya ule mto wenye damu na sasa alikuwa

    ameuweka chini ya mti kivulini akijipatia mlo, nikashikwa na hasira sana.

    Nilikuwa mbioni kumfukuza Tai yule wa ajabu wakati niliposhtuka usin?gizizni na kujikutana nikihema ovyo. Nilikuwa nikitetemeka mwili mzima

    huku hofu imenishika na jasho likinitoka mwilini. Nikalitupa shuka pembeni

    na kuketi kitandani. Niligeuka kuyatazama mazingira ya chumba kile huku

    nikifarijika kuwa bado nilikuwa katika chumba namba 43 cha Hotel Des milles

    Collines na si kule kwenye msitu wa ajabu kama ilivyokuwa ndotoni. “Ndoto

    gani hii?” nilijiuliza huku nikishindwa kuamini.

    Nikashuka kitandani na kuliendea lile jokofu la mle chumbani ambapo nil?ilifungua na kuchukua mzinga mmoja wa mvinyo mkali wa Afrikoko kisha

    nikatoa kizibo chake na kupiga mafunda kadhaa kwa mkupuo. Mvinyo huo

    mkali ulienda na kukwangua kila kitu tumboni nikahisi njaa kali na hapo nika?kumbuka kuwa sikuwa nimetia chakula chochote tumboni tangu nilipoingia

    jijini Kigali jana usiku.





    MIALE HAFIFU YA JUA LA ASUBUHI ilikuwa akipenya dirishani na kuki?fanya chumba hiki kizidi kuwa na nuru, saa kubwa ya ukutani chumbani mle

    ilionesha kuwa zilikuwa zimesalia dakika chache kutimia saa nne asubuhi.

    Nikagundua kuwa nilikuwa nimelala kwa muda mrefu ingawaje bado nili?kuwa nahisi uchovu mwilini hata hivyo sikuwa tayari kurudi tena kitandani.

    Nikavua nguo zangu za kulalia kisha nikavaa taulo na kuelekea bafuni kujim?wagia maji, niliporudi nikaanza kujiandaa tayari kwa mizunguko ya siku ile.

    Nilipokuwa namalizia kujiandaa nikasikia mlango wa chumba changu uki?gongwa, aina ya ugongaji ikanijulisha kuwa alikuwa ni ya mtu anayenifahamu

    hivyo nikaenda kufungua mlango. Msichana mrembo mhudumu wa hoteli ile

    alinisalimia kwa tabasamu maridhawa huku mkononi akiwa ameshika sinia

    lenye kifungua kinywa cha taftahi za kila aina. Nilimpokea na kumshukuru

    kisha nikarudi chumbani na kuketi nikifungua kinywa.

    Ni wakati huu nilipomkumbuka Jean Pierre Umugwaneza yule kijana

    dereva wa teksi aliyenichukua toka uwanja wa ndege wa Kigali jana usiku.

    Nikataka nimpigie simu ili aje kunichukua lakini kabla sijafanya hivyo nika?ona ni bora nimpigie simu kwanza Mutesi, yule msichana niliyekutana naye

    kule Kigali Casino usiku wa jana ili nimuulize kama alipata taarifa zozote

    kuhusiana na yule mtu aliyekuwa akinifuatilia. Nikachukua ile simu ya meza?ni mle chumbani na kuipakata mapajani, namba za simu za Casino Kigali

    alizonipa Mutesi nilikuwa bado nazikumbuka kichwani hivyo nikabonyeza

    tarakimu zake na muda mfupi aliofuata simu ile alikuwa hewani ikiita.

    “Haloo nani mwenzangu? sau?ti ya kiume upande wa pili iliniuliza baada ya kupokea simu ile

    ”Mimi ni Patrick Zambi tafadhali naomba kuongea na Mutesi”

    “Patrick Zambi! wa wapi?

    “Wewe mwambie Mutesi kuwa Patrick Zambi anahitaji kuongea naye,

    ananifahamu”

    “Subiri kidogo” ile sauti ya upande wa pili ilizungumza kisha ikatoweka

    hewani huku mimi nikibaki nimeushikilia mkonga wa simu. Baada ya kitambo

    kifupi kupita nikasikia simu ile ikirudiwa na uhai

    “Haloo” sauti ya kike iliita nikajua ilikuwa sauti ya Mutesi

    “Ni mimi Patrick Zambi vipi Mutesi habari za toka jana?

    “Oh! Patrick habari za asubuhi mimi ni mzima wa afya”

    “Mimi pia sijambo nilikuwa nabahatisha tu kukupigia nilidhani pengine

    nisingekupata”

    “Ungenipata tu mimi huwa naingia kazini saa mbili asubuhi na kutoka saa

    saba usiku kila siku”

    “Oh! pole sana kazi inachosha hiyo”

    “Ndiyo hivyo nitafanyaje na mimi sina elimu, vipi upo wapi sasa hivi?

    “Chumba namba 43 Hotel des Mille Collines lakini ndiyo najiandaa kutoka

    muda si mrefu. Vipi ulifanikiwa kuifanya ile kazi niliyokutuma?

    “Ndiyo! wewe andaa malipo yangu tu”

    “Nashukuru sana Mutesi ondoa shaka nitakulipa pesa yako kama tu?livyokubaliana. Tunaweza kuoanana leo hii baadaye?

    “Mimi nipo kazini labda ungeniambia hiyo baadaye ya saa ngapi na tuna?onana wapi ili nipange namna ya kuaga hapa ofisini”

    “Saa kumi jioni utaweza kuja hapo chumbani kwangu?

    Nilimuliza Mutesi na hapo kukafuatiwa na ukimya kidogo nikajua alikuwa

    akiitafakari hoja yangu”

    “Sawa nitajitahidi nije ingawa sitokaa muda mrefu”

    “Nitashukuru sana kukuona Mutesi”http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Usijali!”

    “Mutesi!” Nilimuita.

    “Bhee!”

    “Hakikisha hakuna mtu mwingine anaefahamu maongezi yetu”

    “Ondoa shaka, kazi njema tutaonana baadaye”

    Mutesi akaniaga na hata kabla sijaitikia kwa kheri yake niliisikia ile simu

    ikikatwa upande wa pili nikabaki na tabasamu la matumaini usoni. Muda ule

    ule nikaamua kumpiga Jean Pierre Umugwaneza nikimtaka aje kunichukua

    pale hotelini na kunipeleka kwenye mizunguko yangu, hata hivyo muda mfupi

    baada ya kuipiga simu ile tumaini la kumpata likayeyuka moyoni mwangu

    kwani simu yake ilikuwa haipatikani hewani. Nikarudia mara nyingi zaidi kui?piga simu ile bila ya mafanikio.

    Ilikuwa ni simu ambayo niliitarajia kuwa ingepokelewa haraka hasa kwa

    kufikiria kuwa nilikuwa nimejenga urafiki mzuri na kijana yule kwa kumlipa

    pesa nyingi jana usiku hivyo sikuona sababu ya yeye kutopatikana siku ya leo.

    Jambo hili likanitia wasiwasi kidogo nikarudi tena kuipiga ile namba ya simu

    bila mafanikio.

    Niliirudisha ile simu mahali pake nikamalizia kifungua kinywa nilicholete?wa na yule dada mhudumu wa hoteli kisha nikachukua begi langu dogo la

    kiuandishi wa habari nililolitoa kwenye lile sanduku langu ambalo ndani yake

    nilikuwa nimeihifadhi ile kamera yangu aina ya Olympus ya kuchukulia picha za matukio.

    Muonekano wa buti zangu ngumu za general lather, suruali ya jeans ili?yonikaa vema na shati langu jeusi la kadeti nililolitangulizia fulana nyeupe

    kwa ndani na saa yangu ya mkononi, asubuhi hii vilinibadilisha muonekano

    wangu. Nikiwa nimeridhika na muonekano wangu nikafungua mlango wa

    chumba kile na kutoka.

    `Nilipofika sehemu ya chini ya hoteli ile nilielekea sehemu ya

    mapokezi ambako niliacha ufunguo wa chumba changu kwa mhudumu nili?yemkuta huku nikamtaka ampe funguo hizo mgeni wangu pale ambapo ange?fika pale hotelini wakati mimi nikiwa bado sijarudi. Nilipotoka nje ya hoteli

    nikaamua kukodi teksi.

    “Nipeleke lilipo jengo lenye ofisi za Kigali Cars Rental Services” nilim?wambia dereva wa teksi

    “Ofisi hizo zipo Avenue de lac Muhaz bosi” dereva alinifafanulia

    “Huko huko”

    Nilimwambia dereva huku nikifahamu kuwa nilichokihitaji hakikuwa jina

    la mtaa huo isipokuwa ofisi zile za ukodishaji wa magari.

    “Unahitaji kukodi gari?

    Yule dereva alinisemesha hata hivyo nililipuuza swali lake kwani wakati

    huo akili yangu ilikuwa imeanza kufanya kazi niliyoizoea tangu nijiunge na

    harakati hizi za kijasusi. Kazi inayonitaka muda wote niwe macho huku ni?kiyachunguza magari au watu ninaoongozana nao pale ninapokuwa kwenye

    safari zangu.

    Hata hivyo asubuhi hii ya kwanza kwangu katika jiji hili la Kigali ilielekea

    kunipokea vizuri kwani baada ya umbali fulani tuliosafiri nilijiridhisha kuwa

    hakukuwa na gari, mtu au watu waliokuwa wakinifuatilia kwani sikuona gari

    lolote likitufungia mkia nyuma yetu kama ilivyokuwa jana usiku.

    Wakati nilipoyarudisha mawazo yangu ndani ya teksi ile nikagunuda kuwa

    tulishafika kwenye mtaa wa ilipokuwa ofisi za Kigali Cars Rental Services

    hivyo nikamlipa dereva pesa yake na kushuka nikiicha teksi ile ikitokomea

    mitaani.

    __________

    AVENUE DE LAC MUHAZ ulikuwa ni mtaa wenye afya kwa barabara pana

    na safi, majengo yaliyojengwa kwa kupangiliwa vizuri na hata maduka ya

    mtaa ule yalikuwa ya kisasa na yanayouza bidhaa za gharama. Niligundua

    kuwa ule ulikuwa ni mtaa wenye maduka mengi yaliyomilikiwa na raia wa

    kigeni wenye asili ya Asia.

    Mkoba wangu wa kamera ukining’inia begani nilisubiri gari lililokuwa lik?ija kwenye barabara ya mtaa ule lipite mbele yangu kisha nikavuka barabara

    nikielekea zilipo ofisi zile za kukodisha magari za Kigali Cars Rentals Ser?vices. Ndani ya ofisi hizo niliwakuta watu wanne, waafrika watatu na mzun?gu mmoja aliyeonekana kuwa na shida kama yangu. Nikasubiri mzungu yule

    amalize kuhudumiwa ndiyo ikafuata zamu yangu

    “Nahitaji kukodi gari” Nilimwambia jamaa mmoja kati ya wahusika wawili wa ofisi ile alieoneka?na yupo tayari kunihudumia. Bila kuongea neno akanisukumia kitabu kikubwa

    kilichokuwa pale juu ya meza.

    “Angalia aina ya gari unalotaka, muda wa kukaa nalo na kiasi cha pesa utak?achotakiwa kulipa” Nilikipokea kitabu kile na kuanza kupekua kurasa zake.

    Kilikuwa ni kitabu kilichokuwa na orodha ya magari yote yaliyokuwa yakiko?dishwa na ofisi zile, ndani ya kitabu kile niliona muda wa kukodi gari na kiasi

    cha pesa kilichopaswa kulipwa kulingana na aina ya gari ambalo lingeazimwa.

    Nilichagua gari aina ya Jeep Cherokee iliyokuwa na uwezo wa kuchukua

    watu watano, wawili mbele na watatu nyuma, na pia yenye four wheels pow?er. Niliamua kuchagua gari hii kwa kigezo kimoja tu kikubwa kuwa kipindi

    hiki kilikuwa ni cha majira ya mvua hivyo kuepuka adha ya kunasa kwenye

    matope Jeep ndiyo gari pekee ambayo ingeweza purukushani zote.

    Nikakodi gari lile kwa muda wa siku ishirini, muda ambao niliamini kuwa

    tayari ningekuwa nimemaliza harakati zangu katika jiji lile la Kigali, Rwan?da. Kwa kuwa nilikuwa mgeni nilitakiwa kuacha pasi yangu ya kusafiria na

    kutoa anwani ya hoteli niliyofikia, bila kupoteza muda nikafanya taratibu zote

    kama ilivyostahili. Malipo ya kukodi gari lile nikayafanya kwa kadi ya VISA

    iliyokuwa kwenye waleti yangu na baada ya kukabidhi kadi yangu ya VISA

    nilitakiwa kusubiri katika viti vya wateja vilivyokuwa pale ndani ofisini ili

    taratibu za kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yangu kwenda kwenye

    akaunti ya ofisi zile zikamilishwe na mhasibu wao. Niliketi na kusubiri tara?tibu zile zifanywe huku nikiutumia muda ule kuipeleleza ofisi ile. Haikuwa

    ofisi yenye msongamano mkubwa wa wateja hata hivyo ilionekana kuwa ni

    ofisi iliyokuwa ikifanya biashara ya kuaminika kutokana na muonekano wa

    wateja wakwasi waliokuwa wakiingia ndani ya ofisi ile.

    Nikiwa bado naendelea kusubiri pale kwenye kiti mawazo juu ya Jean Pierre

    Umugwaneza yakaanza kuzitongoza fikra zangu, wasiwasi ulikuwa umeanza

    kuniingia kuwa huenda Jean Pierre Umugwaneza alikuwa amekumbwa na

    jambo baya usiku ule wa jana mara baada ya kutoka kule hotelini kuniwekea

    chumba. Mawazo yangu yakakatishwa pale nilipomuona yule mfanyakazi wa

    ofisi zile aliyekuwa akinihudumia akinifanyia ishara ya kuniita. Nikasimama

    na kumfuata.

    “Taratibu zimekamilika ndugu ila kuna masharti machache ambayo wewe

    kama mteja unatakiwa kuyafahamu”

    “Ondoa shaka” nilimwambia huku nikimtazama.

    “Hutaruhusiwa kuvuka na gari letu nje ya mipaka ya nchi hii, uharibi?fu wowote utakaofanyika kwenye gari wakati ukiwa nalo ni wewe ndiye

    utakayewajibika kwa gharama za matengenezo. Huruhusiwi kumuazima gari

    mtu mwingine na gharama za mafuta ni juu yako, pia kampuni haitahusika na

    malipo ya faini yoyote ya uvunjifu wa sheria za barabarani zitakazofanywa na

    wewe. Na kama ikitokea dharura yoyote itakayoingiliana na matumizi ya gari

    letu utawasiliana na ofisi yetu kwa ufafanuzi zaidi. Bila shaka taratibu hizi

    zimeeleweka vizuri ndugu?

    Yule mtu aliniuliza nikamwambia nimezielewa vizuri taratibu zile na wala asiwe na shaka na mimi.

    “Vizuri, naomba unifuate” yule mtu aliniambia

    Tuliingia kwenye mlango uliokuwa upande wa kushoto wa ofisi ile na hapo

    tukatokezea kwenye korido iliyotuchukua hadi nyuma ya jengo lile sehemu

    iliyotumika kuhifadhia magari mbalimbali ya kampuni ile. Nikaliona lile gari

    aina Jeep nililolihitaji, lilikuwa limeegeshwa karibu na geti la kutokea nje ya

    eneo lile. Yule jamaa akanikabidhi funguo za gari na kunitakia kazi njema.

    Nilimshukuru kisha nikaifuata ile Jeep, nilipoifikia nikafungua mlango na

    kuingia ndani na kuiwasha. Mlinzi wa eneo lile alinifungulia geti na kuni?pungia mkono wakati nikitoka nami nikampungia mkono.

    __________

    GARI NILILOKODI LILIKUWA na mafuta ya kutosha hivyo nilitia moto

    na kuzunguka nikielekea lilipo lile duka la silaha jirani katika mtaa ule, nili?pofika nikaegesha gari kando ya barabara kisha nikashuka na kuelekea ndani

    ya ofisi zile. Mbali na askari wawili waliokuwa na bunduki zao mikononi

    ambao walikuwa wakilinda nje ya ofisi zile, ndani ya ofisi niliwakuta askari

    wangine watatu waliovaa sare za suti nadhifu za kiaskari. Nilipoingia askari

    mmoja aliyekuwa ameketi mbele ya meza ya ofisi ile alinikaribisha vizuri na

    kunitaka niketi kwenye kiti kilichokuwa mbele yake.

    “Habari za kazi” nilimsalimia katika lugha ya kiingereza

    “Salama ndugu, karibu sana nikusaidie nini? Askari yule mrefu na mkakam?avu mwenye macho makubwa aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.

    “Nahitaji kununua silaha sijui taratibu zake zikoje?

    “Wewe ni raia wa Rwanda?

    “Hapana”

    “Hatuuzi silaha kwa raia wa kigeni ndugu hii si genge la viazi sokoni”

    “Ninashida sana ndugu nahitaji msaada wako”

    Nilimwambia askari yule na hapo nikamuona jinsi alivyobadilika na kuni?tupia macho ya mshangao.

    “Shida gani?, kuua au kuwinda? Aliuza huku akivikamatisha vidole vyake

    vikakamavu juu ya meza ya mbele yake.

    “Vyote ikibidi” nilimjibu huku nikimtazama usoni.

    “Bila shaka wewe ni mwendawazimu, afadhali usimame na kuondoka hapa

    siyo hospitali ya vichaa ndugu. Hatuuzi silaha kwa wendawazimu” askari yule

    alifoka akionekana kuanza kukasirishwa na maongezi yangu.

    “Nahitaji kulijinda afande mimi ni mfanyabiashara, silaha yangu nimeisa?hau nchini kwangu wakati nilipokuwa nikija hapa Rwanda”

    “We ni mfanyabiashara wa kutoka nchi gani?

    “Tanzania”

    “Wewe ni Mtanzania? askari yule aliniuliza kama ambaye hajanisikia vizu?ri, nikajibu kwa kukitisa kichwa huku nikiendelea kutabasamu.

    “Mtanzania na silaha wapi na wapi ndugu, Congo, Somali na Sudani nao

    wasemeje?

    Askari yule aliongea huku akiwa haoneshi tumaini lolote la kutaka kunisaidia na hapo nikachomoa waleti yangu na kuhesabu kiasi fulani cha pesa

    nilipomaliza nikazitupia juu ya meza yake huku nikiwa na hakika kuwa wale

    wenzake hawatuoni.

    “Tafadhali nisaidie afande” nilinong’ona na hapo nilimuona yule askari

    mbele yangu akipitisha mkono wake kuzichukua zile pesa

    “Pesa hizi ni za nini?

    “Nahitaji msaada wako afande, tafadhali nisaidie nahitaji silaha” nilim?wambia yule askari huku nikimshawishi kwa macho na hapo akinitazama kwa

    udadisi kisha aliyahamisha macho yake kuwatazama wale wenzake na alipoy?arudisha macho yake kwangu alinong’ona

    “Sikiliza ndugu sheria za nchi hii hazituruhusu sisi kumuuzia silaha raia wa

    kigeni, lakini kwa kuwa unaonekana unashida sana na silaha naweza kuku?saidia kwa njia moja tu. Tunazo silaha mbalimbali hapa ambazo tunazikamata

    toka wa waasi wanaoipinga serikali ya nchi hii, ninaweza kukuuzia moja ila

    haitofuata utaratibu wa kisheria katika kuimiliki. Kwa hiyo endapo ikitokea

    umeingianayo hatiani sisi hatutohusika”

    “Ondoa shaka” nilimwambia na hapo akanitazama tena kabla ya kuniuliza.

    “Jina lako nani na utakuwa hapa Rwanda kwa muda gani?

    “Naitwa Patrick Zambi, kama nilivyokueleza hapo awali mimi ni mfany?abiashara wa kitanzania nipo hapa Rwanda kukutana na wafanyabiashara

    wenzangu wa Afrika Mashariki katika harakati za kuongeza ushirikiano wa

    kibiashara katika nchi za maziwa makuu ama common market. Nitakuwa hapa

    Rwanda kwa muda wa wiki mbili kabla kurudi nchini kwangu”

    “Karibu sana ndugu Patrick, sisi kama wanyarwanda tunafurahia ushiriki?ano huo na ndugu zetu watanzania. Ninyi mmekuwa marafiki wetu wazuri”

    askari yule aliongea huku akivuta kiti nyuma yake na kusimama.

    “Nifuate” aliniambia na hapo nikasimama na kuanza kumfuata. Tuliingia

    kwenye chumba kidogo kilichokuwa upande wa kulia na ofisi zile na hapo

    nilikuta silaha za kila aina zikiwa zimehifadhiwa katika sehemu maalumu

    ukutani. Yule askari alifungua kabati kubwa lililokuwa upande wa kushoto wa

    chumba kile na hapo nikaziona bastola za kila namna. Nilipozitazama silaha

    zile nikagundua nyingi zilikuwa ni silaha za kutoka nchini Urusi.

    Baada ya kuchaguachagua nikaipata bastola niliyoizoea kuitumia, bastola

    aina ya Colt 45 yenye uwezo wa kubeba risasi zenye kipenyo cha milimita

    9.01 pia yenye nguvu ya mfyatuko wa risasi 235 na uzito wa risasi wa gramu

    7.45. Niliipenda bastola ile kwa kuwa ilikuwa nyepesi na yenye nguvu.

    Askari yule aliponitajia bei yake haikunishtua kwani nilikuwa nimejiandaa

    kwa kiasi kile cha pesa hivyo nilihesabu kiasi kile cha pesa na kumpa halafu

    nikaongeza kiasi kingine kwa ajili ya maboksi mawili ya rasasi. Tulipomaliza?na vizuri tuliagana na askari yule nikatoka nje ya ofisi ile nikielekea sehemu

    nilipoegesha gari ambapo niliingia ndani nikatia moto na kuondoka.



    MCHANA ULE jua hafifu lilichomoza kidogo kuipa likizo ya muda mfupi

    mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha toka alfajiri. Mitaa mingi ya jiji la Kigali

    ilikuwa imerejewa na uhai, watu walikuwa ni wengi wakiendelea na shughu?lizao za kila siku halikadhalika magari nayo vilevile. Niliitazama saa yangu

    ya mkononi na kugundua kuwa dakika chache zilikuwa zimepita baada ya

    kutimia saa sita mchana hivyo nilikuwa nimesaliwa na muda wa masaa matatu

    na zaidi ya nusu saa kabla ya kukuta na Mutesi kule chumbani kwangu Hotel

    Des Mille Collines, niliwaza. Muda bado ulikuwa ukinitosha kufanya mizun?guko yangu mingine mjini.

    Kwa kuzingatia kuwa hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika nchini

    Rwanda na hasa katika jiji hili la Kigali niliona hii ilikuwa nafasi nzuri kuli?peleleza vizuri jiji la Kigali na maeneo yake yote muhimu. Kwa kuwa sikuwa

    na mwenyeji wa karibu wa kumuuliza nilishuka kwenye duka moja kubwa la

    vitabu lililokuwa katikati ya jiji na kununua ramani ndogo lakini inayoonesha

    barabara zote kuu, mitaa na vitongoji vyote vya jiji la Kigali na nchi yote ya

    Rwanda kwa ujumla, kwani kupitia ramani ile ningeweza kuzifikia sehemu

    zote muhimu bila kumuuliza mtu yeyote.

    Nilizungukia vitongoji vyote muhimu vya jiji la Kigali kwa muda wa masaa

    mawili tu na wakati nikizunguka niliweza kuziona ofisi za balozi za Afrika

    mashariki ikiwemo ofisi ya balozi wa Tanzania. Niliweza pia kuziona ofisi za

    mamlaka ya mapato ya Rwanda, ofisi za wizara ya mambo ya nje na ushiriki?ano wa kimataifa na ofisi ya wizara ya elimu ya nchi ya Rwanda, zote zikiwa

    pembeni ya mzunguko wa barabara eneo la Kimihurura. Pia niliona jengo kub?wa la hosteli ya vijana wa Rwanda lililokuwa pembeni ya barabara ya Boule?vard de l’umuganda, mbele ya barabara hiyo upande wa kushoto niliona jengo

    la wizara ya haki ya nchi ya Rwanda lililokuwa na bango kubwa mita chache

    kando ya barabara kuu kuelekea lilipo jengo lile lililoandikwa Ministere de la

    justice pembeni yake kukiwa na jengo lingine kubwa la bunge.Saa nane mchana wakati inatimia ilinikuta nikiwa kwenye mzunguko wa

    barabara ya Kimihurura hivyo nikaamua kisitisha ziara zangu kwa siku ile.

    Ile ramani yangu ndogo ya nchi ya Rwanda niliyoinunua nilikuwa nimeiban?dika kwenye kofia ya kuzuia jua iliyokuwa ikining’inia kwenye siti ya dereva

    chini ya paa la gari. Nilipofika kwenye mzunguko wa barabara ya Kimihurura

    niliingia barabara ya upande wa kulia. Barabara hiyo niliitambua kwa jina

    la barabara ya Kibungo. Kwa mujibu wa ramani ile niliyoinunua barabara

    ile ya Kibungo kwa mbele kidogo iliungana na barabara nyingine iliyokuwa

    ikielekea mpakani mwa Rwanda na Tanzania ijulikanayo kama barabara ya

    Kayonza-Rusumo.

    Baada ya kutembea umbali wa kilometa chache mbele yangu nilikutana na

    mzunguko mwingine wa barabara ambapo niliiacha barabara inayoelekea upa?nde wa kushoto kwangu eneo la Amahoro. Nikaiacha barabara nyingine mbele

    yangu inayoelekea hospitali ya Kanombe ambapo niliitambua hospitali hiyo

    kupitia maelekezo kwenye bango kubwa lililokuwa pembeni ya mzunguko

    wa barabara ile, bango hilo likiwa na maandishi makubwa yaliyosomeka Vers

    Hospital Militaire Kanombe. Nilipofika hapo nikakunja kona upande wa kulia

    na kuingia barabara nyingine inayoitwa Pue du lac Ruhondo, niliposafiri um?bali mfupi mbele yangu barabara ile niliyoingia ilikuja na kuungana na baraba?ra nyingine iliyoitwa Boulevard de l’Oua halafu nilipoendelea mbele kidogo

    nikakutana na mzunguko mwingine wa barabara niliyoufahamu kwa jina la

    Rwandex. Nikauzunguka mzunguko ule nikiiacha barabara inayoelekea eneo

    la Zion Temple upande wa kushoto na kuendelea mbele zaidi.

    Kiasi cha urefu wa kama kilometa mbili mbele yangu nikawa nimeifikia

    barabara ya Avenue Gikondo hapo nikapunguza mwendo wa gari na kutem?bea taratibu huku macho yangu yakitazama mara kwa mara kwenye vioo vya

    ubavu wa gari ili kujua kama nyuma yangu kulikua na gari lolote lililokuwa

    limenifungia mkia. Sikuona gari lolote la kulishuku kwani magari yote nyuma

    yangu yalionekana kuwa katika safari zake za kawaida.

    __________

    AVENUE GIKONDO ulikuwa ni mtaa wenye mpangilio mzuri wa makazi

    ya watu katika eneo lile na sehemu yake kubwa ilikuwa na nyumba za kisasa

    zilizozingatia ujenzi wa anwani za makazi. Niliyakumbuka maelezo ya Jean

    Pierre Umugwaneza kuwa Niyonkuru, msichana aliyekuwa rafiki kipenzi wa

    mwandishi Tobias Moyo kutoka nchini Tanzania alikuwa akiishi nyumba nam?ba 5 eneo la lile. Hivyo niliyapita maduka makubwa ya kitongoji kile, nikapita

    klabu moja ya pombe aliyokuwa pembeni mwa stendi ya mabasi madogo ya

    abiria halafu nikalipita jengo dogo la posta la kitongoji kile na kuingia katika

    barabara kuu ya Gikondo iliyokatisha katikati ya makazi ya watu. Baada ya

    zungukazunguka ya hapa na pale kupeleleza nikawa nimeiona nyumba namba

    5 mwisho wa mtaa ule.

    Ilikuwa nyumba iliyozungushiwa uzio wa ukuta mrefu na geti jekundu

    mbele yake ingawaje geti hilo lilionekana kuchakaa. Nilisimamisha gari kan?do ya barabara nikilitazama geti lile halafu nikazitazama nyumba za jirani za eneo lile ambazo zilionesha uhai wa kuwako na wenyeji wake kutokana

    na nguo zilizokuwa zimeanikwa nje ya nyumba zile kwenye kamba pamoja

    na watoto wadogo waliokuwa wakichezecheza mbele ya nyumba zile. Ni?liitazama namba 5 ilivyochorwa vizuri kwa maandishi makubwa meupe juu

    ya geti lile jekundu nikajiridhisha kuwa nilikuwa sijapotea njia hivyo nikatia

    moto gari mpaka mwisho wa barabara ya mtaa ule ambako niliingia upande

    wa kulia, mbele kidogo nikaegesha gari kando ya barabara kisha nikashuka na

    kuanza kutembea kwa miguu nikirudi kwenye ile nyumba namba 5. Kulikuwa

    na watu waliokuwa wakipita katika barabara ile hata hivyo hakuna hata mmoja

    aliyeonekana kuvutika na safari yangu hivyo niliendelea kutembea taratibu.

    Nilipofika kwenye lile geti jekundu la nyumba namba 5 nikasimama na

    kuanza kugonga hodi taratibu huku nikitazama nyuma yangu ng’ambo ya ile

    barabara kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akinitazama kupitia vioo

    vya madirisha vya nyumba zile ambavyo havikuniruhusu kuona ndani. Baada

    ya kugonga geti lile kwa muda mrefu bila kujibiwa sikuona sababu ya ku?endelea kugonga kwa kuhisi kuwa nilikuwa nikipoteza muda wangu hivyo

    nikaingiza mkono mfukoni kupapasa mkungu wa funguo zangu malaya. Ni?lipoupata nikauchukua na kuchagua funguo iliyoendana na kitasa kidogo cha

    geti lile na muda mfupi uliofuata mlango ule ukafunguka.

    Kabla ya kuingia ndani niligeuka kutazama tena nyuma yangu nilipojiridhi?sha kuwa hakuna mtu yeyote aliyekuwa akinitazama nikausukuma mlango ule

    na kuingia ndani huku taratibu nikiurudishia vizuri ule mlango nyuma yangu.

    Mara tu nilipoingia mle ndani nilisimama nikachunguza vizuri mazingira ya

    nyumba ile. Kulikuwa na miti miwili mikubwa ya mimimbe, mti mmoja uliku?wa mbele ya nyumba iliyokuwa mle ndani na mti mwingine ulikuwa ubavuni

    mwa nyumba ile.

    Chini ya mti wa mwembe uliokuwa mbele ya nyumba ile kulikuwa na gari

    dogo aina ya Peugeot 504 lililoegeshwa, nililichunguza gari lile nikagundua

    kuwa lilikuwa mahali pale kwa muda mrefu bila ya kutumika kwa namna lil?ivyokuwa limefunikwa na majani mengi ya mti ule wa mwembe yaliyokuwa

    yemezagaa kila sehemu ya eneo lile. Eneo lote la nyumba ile lilikuwa chafu

    kana kwamba hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiishi eneo lile, majani

    yalikuwa yameota ovyo kuzunguka nyumba hata maua yaliyopandwa kuizu?nguka nyumba ile hayakuwa yamekatiwa. Katika nyaya za kuanikia nguo

    zilizokuwa ubavuni mwa nyumba ile nilibahatika kuiona sare moja ya kijeshi

    ikiwa imetundikwa, mashaka yakaniingia kidogo juu ya mwonekano wa sare

    ya kijeshi katika mazingira kama yale. Nikaanza kutembea taratibu kuelekea

    ulipo mlango wa mbele wa nyumba ile huku nikiendelea kulichunguza eneo

    lile.

    Kulikuwa na kochi moja refu sehemu ya mbele ya nyumba ile, mito ya kochi

    lile ilikuwa imeshika vumbi mno. Nilisimama kulitazama kochi lile lisiloone?sha dalili yoyote ya kukaliwa na watu kwa siku za karibuni halafu nikaya?hamishia macho yangu kutazama sakafuni na hapo niliziona alama za soli

    ya kiatu, zilikuwa alama za buti za kijeshi kulingana na michoro ya matope

    yaliyokauka yaliyoachwa na viatu hivyo. Nilitulia nikiipa utulivu akili yangu kisha nikaanza kubisha hodi kwenye mlango wa mbele wa nyumba ile. Kama

    ilivyokuwa kule getini hapa napo nilibisha hodi kwa muda mrefu bila maji?bu, baada ya kurudiarudia zoezi lile nikaanza kujiandaa kutumia njia nyingine

    mbadala.

    Ilikuwa ni wakati nilipokuwa nikiingiza mkono mfukoni kuchukua zile fun?guo zangu malaya wakati niliposikia sauti ya hatua za mtu akiukaribia mlango

    ule kwa ndani, nikautoa mkono wangu mfukoni na kujiandaa kukabiliana na

    tukio lolote ambalo lingejitokeza. Mara nikasikia kitasa cha mlango kikizun?gushwa kisha muda huohuo mlango ule ulifunguliwa na hapo nikajikuta niki?shikwa na butwaa baada ya kumuona msichana kisura wa kinyarwanda akiwa

    amesimama hatua moja mbele yangu huku amevaa vazi pekee la khanga moja

    lililoyasitiri maungo yake ukiachilia mbali ile nguo yake ya ndani ambayo

    iliyachora vema makalio yake.

    “Karibu ndani” aliniambia kwa lugha ya kinyarwanda sikumuelewa hata

    hivyo nilibaki nikimtazama huku tabasamu langu likilitongoza umbo lake.

    “Get in please” hatimaye akaniambia kwa lugha ya kiingereza na hapo

    nikamuelewa ingawaje nilipomtazama vizuri usoni nikagundua kuwa ta?basamu lake halikuendana na hali aliyokuwa nayo. Nikabaki nikijiuliza ni aina

    gani ya mwanamke anayeweza kumfungulia mlango mgeni asiyemjua huku

    akiwa amevaa vazi la khanga moja tu nyepesi na nguo ya ndani?. Yule msi?chana akageuka na kuanza kutembea taratibu, nilimtazama kwa nyuma huku

    mapigo ya moyo wangu yakienda mbio kwa kupewa mtihani huu wa somo

    ambalo sikufuzu vizuri.

    Nikaona ni hakika kuwa hapa nilikuwa nyumbani kwa Niyonkuru, rafiki

    wa mwandishi Tobias Moyo hivyo niliamua kujiheshimu mbele ya msichana

    huyu mzuri na mrembo wa kinyarwanda ambaye nilikuwa na hakika kuwa

    sikuwahi kumuona msichana mzuri katika maisha yangu kama yeye. Nilim?kumbuka Tobias Moyo na kumpongeza kwa kuitupa vema ndoana yake hadi

    kumnasa msichana huyu mrembo mbele yangu. Nikapiga moyo konde na kuz?ifukuza hisia mbaya zilizoanza kujengeka kichwani mwangu. Nikiwa naende?lea kumtazama kwa nyuma nilizitupa hatua zangu taratibu na kwa tahadhari

    nikimfuata msichana yule mbele yangu.

    Tuliuacha ukuta wa ukumbi wa kulia chakula wa nyumba ile uliokuwa upa?nde wa kulia tukaifuata korido fupi mbele yetu. Katikati ya korido ile upande

    wa kulia kulikuwa na mlango, tulipoingia ndani ya mlango ule tukawa tume?tokezea kwenye sebule pana. Ilikuwa sebule ya kisasa yenye samani za kuvu?tia kama makochi makubwa mazuri ya sofa, zulia la rangi ya kijivu sakafuni,

    runinga ya kisasa, sistimu ya muziki. Jokofu la vinywaji lilikuwa kwenye kona

    ukutani pamoja na kabati pana la vyombo vya dongo vilivyopangwa kwa un?adhifu mkubwa. Madirisha mapana ya sebule ile yalikuwa yamefunikwa kwa

    mapazia meupe marefu na mepesi yaliyokuwa yakipitisha upepo murua pale

    sebuleni. Katika nyumba hii yenye ghorofa moja niligundua kuwa sakafu nzi?ma ya chini ya ghorofa lile ilikuwa ikitumika kama sebule, upande wa kushoto

    wa sebule ile kulikuwa ngazi za kuelekea ghorofa ya juu, sakafu ya ngazi zile

    ilikuwa imefunikwa na muendelezo wa lile zulia la sebuleni. Tulipofika katika sebule ile yule msichana mwenyeji wangu alinikaribisha

    niketi katika moja ya kochi lililokuwa pale sebuleni.

    “Karibu uketi!”

    “Ahsante” nilimjibu huku nikichagua kochi moja na kuketi

    “Samahani utanisubiri kidogo naenda kubadilisha nguo”

    Msichana yule aliniambia na kabla ya sijamjibu akazifuata zile ngazi na

    kuanza kupanda akielekea juu

    “Bila samahani” nilimjibu huku nikigeuka kumtazama na hapo nikayaona

    mapaja yake laini ya yalivyokuwa yakitikisika taratibu kwa kadiri alivyokuwa

    akizitupa hatua zake kupanda zile ngazi. Niliendelea kumtazama msichana

    yule hadi pale alipopotea machoni kwangu na hapo nikayarudisha mawazo

    na akili yangu ndani ya sebule ile na wakati huo niliweza kuzisikia hatua za

    msichana yule zilivyokuwa zikiyoyoma.

    Kulikuwa na magazeti machache yaliyokuwa chini ya meza fupi iliyokuwa

    pale sebuleni, nikachukua gazeti moja na kuanza kulipitishia macho ingawaje

    halikuwa taarifa zozote za maana kwangu kwani lugha iliyokuwa imetumika

    katika gazeti hilo ilikuwa ni ya kinyarwanda na mimi nilikuwa siifahamu

    hivyo hatimaye nililirudisha gazeti lile mahala pake nikabaki nikiidadisi se?bule ile huku nikiendelea kumsubiri mwenyeji wangu. Nilipoitazama saa yan?gu ya mkononi nikagundua kuwa dakika chache zilikuwa zimesalia kutimia

    saa kumi jioni muda wa miadi yangu na Mutesi, nikapanga kuwa ningetumia

    muda wa saa moja tu katika mahojiano na mwenyeji wangu na baada ya hapo

    ningeondoka kumuwahi Mutesi kule hotelini.

    Nililitazama kabati kubwa lililokuwa pale sebuleni na kulidadisi na hapo

    nikagundua kuwa kabati lile lilikuwa na droo sita chini yake, nikazitazama

    droo zile na kuanza kuvuta picha kama niliyekuwa nikiona vitu vilivyokuwa

    ndani yake ambavyo pengine vingenisaidia katika harakati zangu za kijasusi.

    Nikiwa bado nimeketi pale kwenye kochi nikaanza kushawishika kusimama

    na kuliendea lile kabati hata hivyo nilisita pale nilipowaza kuwa ningejite?teaje endapo ningekutwa na mwenyeji wangu nikipekua zile droo. Hali hiyo

    ikanipelekea niachane na mpango huo hasa baada ya kuwaza kuwa pengine

    ningepewa ushirikiano wa kutosha na mwenyeji wangu hivyo upekuzi ule wa

    siri niliotaka kuufanya usingekuwa na maana.

    Hivyo niliacha kulitazama kabati lile na kuanza kuyatembeza macho yangu

    mle ndani. Wakati nikiendelea na zoezi lile mara nikawa nimekiona kitu kimo?ja kilichonishtua na kunigusa zaidi moyoni. Pembeni ya mlango wa kuingilia

    sebuleni mle kulikuwa na jozi moja ya buti za jeshi. Nilizitazama buti zile toka

    pale nilipoketi na kuona beji ndogo zilizokuwa zimeshonewa kwenye ukosi

    wa buti zile, beji hizo zilikuwa zimeandikwa Rwandese Armed Force yaani

    kwa kifupi RAF, hali hiyo ikimaanisha kuwa buti zile zilikuwa ni za jeshi la

    wananchi wa Rwanda. Buti zile za jeshi zikanifanya niikumbuke na ile sare

    ya jeshi niliyoiona nje ya nyumba ikiwa imeanikwa wakati ule nilipokuwa

    nikiingia humu ndani.

    Ikajengeka dhana kichwani kwangu kuwa mle ndani hakuwa yule msichana

    peke yake ila kulikuwa na mwanaume tena mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Rwanda aliyekuwa anaishi na msichana yule. Nikaanza kujiuliza kwamba

    hali hii ilikuwa kabla au baada ya Tobias Moyo kuuwawa wiki mbili zilizopi?ta?, ni msichana wa namna gani ambaye angekuwa na roho nyepesi ya kuan?gukia mikononi mwa mwanaume mwingine baada ya mpenzi wake kuuwawa

    wiki mbili tu zilizopita? Au msichana huyu mrembo alikuwa akiwatumikia

    mabwana wawili kwa siri yaani marehemu Tobia Moyo na mwanaume huyu

    mwenye buti hizi za jeshi bila ya wao kujua?. Niliendelea kujiuliza bila kupata

    majibu na hatimaye macho yangu yakaweka kituo juu ya kibakuli kidogo ya

    majivu ya sigara kilichokuwa juu ya meza ile fupi mbele yangu. Muda uleule

    mara nikasikia sauti ya hatua za mtu akishuka kwenye zile ngazi za ghorofani

    na hapo nikajua kuwa alikuwa ni yule msichana niliyemdhania kuwa ndiye

    Niyonkuru kuwa alikuwa akishuka zile ngazi ingawaje sikuwa na hakika sana

    kama alikuwa mwenyewe.

    Niligeuka kuzitazama zile ngazi na hapo nikamuona yule msichana

    mwenyeji wangu akishuka zile ngazi nikashtushwa sana na ongezeko la uzuri

    wake. Alikuwa amevaa kaptura fupi ya jeans na blauzi ya rangi ya hudhurungi

    iliyompendeza sana, nywele zake ndefu alikuwa amezichana na kuzibana kwa

    nyuma, shingoni alining’iniza kidani cha kifuu kilichochongwa katika umbo

    la ramani ya Afrika, miguuni alivaa makobazi ya mikanda ya ngozi.

    “Samahani sana kwa kukuweka” aliniambia pindi alipokuwa akiketi

    “Oh! wala usihofu mbona hujaniweka sana” nilimwambia huku nikiumba

    tabasamu hafifu usoni mwangu hata kabla hajaketi vizuri akakumbuka kuni?uliza.

    “Sahamani ungependa kutumia kinywaji gani?

    “Scotch baridi ningefurahi zaidi” nilimwamba na hapo akanyanyuka na ku?liendea lile jokofu ililokuwa kwenye pembe ya sebule. Muda mfupi ulipopita

    alirudi akiwa na mzinga mkubwa wa Scotch na bilauri mbili ambazo aliziweka

    mezani na kumimina kinywaji kile

    “Karibu”

    “Ahsante” nilimshukuru kisha nikanyakua ile bilauri na kipiga mafunda

    mawili kisha nikairudisha bilauri ile mezani na hapo tukabaki tukitazamana

    kwa kitambo kifupi kabla ya yeye kuvunja ukimya

    “Sasa nafikiri tunaweza kuongea, sijui wewe ni nani mwenzangu na unashi?da gani? aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.

    “Jina langu naitwa Patrick Zambi” nilianza kuongea “Bila shaka umewahi

    kulisikia jina langu”

    na hapo nikamuona msichana yule kisura akitingisha kichwa kuonesha ku?kataa.

    “Sikumbuki kama nimewahi kusikia jila la namna hiyo” aliniambia kwa

    utulivu.

    “Sikushangai sana ukisema hivyo na pengine hii ikawa mara yangu ya

    kwanza kuonana na wewe. Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea ku?toka nchini Tanzania” niliendelea kuongea huku nikiinyakuwa tena ile bilauri

    mezani na kugida funda moja na wakati huo niliweza kuuona mshtuko usoni

    mwa msichana yule.

    “Kwa hiyo unataka nikusaidie nini? aliniuliza kwa taharuki huku ile sura

    yale ya kirafiki ikitoweka.

    “Ni matumaini yangu kuwa wewe ndiye Niyonkuru” nilimuuliza.

    “Hata kama huyo Niyonkuru ni mimi wewe una shida gani? aliniuliza kwa

    hasira nami muda huohuo nikaingiza mkono mfukoni nilipourudisha mezani

    nilikuwa nimeshika picha.

    Ilikuwa ni picha ya marehemu Tobias Moyo niliyopewa na ofisi ya idara

    yangu ya kijasusi jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari. Nilipoitupa pi?cha ile mezani yule msichana ambaye bila shaka nilihisi kuwa ndiye aliyeku?wa Niyonkuru aliyatupa haraka macho yake kuitazama ile picha mezani kisha

    haraka nilimuona akiyakwepesha macho yake na kutazama pembeni. Nikaic?hukua ile picha na kuirudisha mfukoni huku nikimtazama na hapo nikaona si?manzi ilivyomshika, machozi yalikuwa yameanza kumtoka taratibu, akainama

    chini na kuyapangusa kwa vidole vyake.

    “Pole sana Niyonkuru, nafahamu ni majonzi kiasi gani uliyonayo baada

    ya kumpoteza rafiki yako kipenzi Tobias Moyo. Mimi pia nimesikitika sana

    ndiyo maana leo hii nipo hapa” nilimwambia huku huzuni nami imenishika,

    akafuta machozi na kugeuka kunitazama

    “Umejuaje kuwa mimi ndiye Niyonkuru na ni nani aliyekuelekeza hapa?

    “Ungekuwa wewe si Niyonkuru nilitegemea kuwa ungekataa mapema

    wakati nilipokuita hata hivyo ondoa shaka kwani marehemu Tobias Moyo ali?wahi kunidokeza juu ya mahusiano yenu tulipokutana hapa Rwanda miaka

    miwili iliyopita” nilimdanganya.

    “Mbona mimi hakuwahi kuniambia habari zako hata siku moja, nitakuamini

    vipi?

    “Nafikiri hakupenda kukuweka bayana kuhusu mimi na hiyo ni tabia yake

    ninayoifahamu ya kutowaweka karibu marafiki zake kwa mpenzi wake, saba?bu kubwa ni wivu wa kuhofia kupinduliwa” nilimwambia huku nikiyakumbu?ka maneno ya Mutesi aliyoniambia kule Casino Kigali kuwa Tobias Moyo

    hakuwa rafiki sana wa watu na hapo Niyonkuru akabaki akinitazama kabla ya

    kuuliza tena kwa sauti ya upole

    “Ulipafahamu vipi hapa?

    “Tobias Moyo aliwahi kunieleza kuhusu mahali hapa unapoishi hivyo hai?kuniwia vigumu kupafahamu”

    Niyonkuru alinisikiliza kwa makini halafu akashusha pumzi kwa mkupuo

    huku akiwa kama anayefikiria jambo fulani, baada ya kufikicha macho yake

    akaniuliza tena

    “Sasa unataka nikusaidie nini? akaniuliza kwa sauti ya chini kama ambaye

    hakutaka mtu fulani aliyekuwa maeneo yale asikie maongezi yetu. Mara hii

    niliweza kumuhisi kuwa alikuwa mwingi wa wasiwasi na alikuwa akiongea

    kwa woga. Hali hiyo ikanishtua ingawaje nilijitahidi sana kuuzuia mshtuko

    wangu.

    “Ninaamini kuwa serikali ya Tanzania na Rwanda zinashirikiana kikamilifu

    kuwasaka watu wote waliohusika na kifo cha Tobias Moyo hata hivyo sina

    hakika sana kama watafanikiwa kwani wauaji ni lazima wawe ni watu waliojipanga na wanaozifahamu nyendo za maafisa wa usalama wa serikali hizi mbili,

    hali inayowapa mwanya rahisi wa kutokomea. Hicho ndicho kilichonipelekea

    mimi kufika hapa nikitaka kujua kuwa pengine ukawa na tetesi zozote zilo?pelekea kifo cha Tobias Moyo, kwa kuzingatia kuwa wewe ulikuwa mtu wake

    wa karibu. Na kupitia tetesi hizo pengine tukafahamu ni nani aliyehusika”

    Nilimaliza kuongea kisha nikainyakua tena ile bilauri mezani na kuvuta fun?da moja kisha ni kairudisha mezani huku nikimtazama Niyonkuru.

    “Mimi sina chochote cha kukusaidia” alinijibu kwa mkato na hapo nikash?tuka, nilipomtazama nikamuona kuwa alikuwa akitazama kule juu ya ngazi za

    kuelekea ghorofani katika namna kuibia ibia ingawaje alijitahidi sana kuificha

    hali ile.

    Hii ilikuwa ni ishara nyingine muhimu niliyoweza kuishtukia haraka hivyo

    sikuwa na mashaka tena kuwa kule juu ya ghorofa kulikuwa na mtu ambaye

    bila shaka mtu huyo angekuwa ndiye yule mwenye suruali na buti za jeshi

    zilizokuwa pale sebuleni. Nikahisi kuwa mtu huyo wakati ule alikuwa ame?banisha juu ya zile ngazi akiyasikiliza maongezi yetu hali hiyo ikanijulisha

    kuwa pengine ile ingekuwa ni sababu iliyomfanya Niyonkuru kuongea kwa

    sauti ile ya chini.

    “Nafahamu kuwa pengine ikawa si rahisi sana kwako kufahamu sababu ili?yopelekea kifo cha Tobias Moyo ila naamini kuwa ukitulia vizuri na kufikiria

    unaweza kuwa na hisia ya jambo fulani ambalo huenda likawa ndiyo moja ya

    sababu ya kifo chake na hapo ikatusaidia kuwanasa wahusika” nilizungumza

    kwa sauti ya chini huku nikikwepa maongezi yetu yasisikike.

    “Ni kweli kuwa Tobias Moyo alikuwa rafiki yangu lakini hiyo haiwezi kuwa

    sababu ya mimi kufahamu chanzo cha kifo chake” Niyonkuru alinijibu kwa

    msisitizo

    “Sawa! lakini hebu kumbuka vizuri unaweza kuniambia kuwa ni watu gani

    aliokuwa akiwataja sana katika maongezi yake? nilimuuliza huku moyoni

    nikijuliza kama bado alikuwa akinichukulia kama mwandishi wa habari wa

    kujitegemea kama nilivyojinadi kwake.

    “Alikuwa akikutana na watu mbalimbali kutegemeana na kazi yake”

    “Miongoni mwao hakuna hata mmoja aliyekuwa akipenda kumuongelea

    sana?

    “Kwa kweli sikumbuki”

    Jibu la Niyonkuru likanifanya nisitishe mohojianonae nibaki nikimtazama

    ingawaje yeye aliendelea kuyakwepesha macho yake pembeni yasikutane na

    yangu na kwa hali ile nikajua kuwa Niyonkuru alikuwa akinificha jambo fu?lani ambalo nisingeweza kumlazimisha aniweke bayana kwa wakati ule.

    “Mimi nilikuwa miongoni mwa watu walioupokea mwili wa Tobias Moyo

    wakati ulipowasili kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam wiki mbili zilizopita

    na pia nilikuwa miongoni mwa watu walitoa heshima zao za mwisho kabla ya

    maziko kufanyika kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam. Mion?goni mwa watu niliyowatarajia kuwaona siku ile wa kwanza ulikuwa ni wewe,

    ilikuaje hakuweza kufika?

    “Niliumizwa sana na kifo chake, nisingeweza kustahimili kusafiri mpaka

    Dar es Salaam msibani”

    “Pole sana”

    Nilimpa pole huku nikifahamu fika kuwa nilikuwa nikidanganywa, hakunii?tikia hivyo nikayazungusha macho yangu pale sebuleni huku nikianza kuona

    kuwa jitihada zangu zilikuwa mbioni kugonga mwamba.

    “Nafikiri huna swali jingine? Niyonkuru alinikatisha wakati nilipokuwa ni?kiendelea kufikiri.

    “Nina swali, usiku ule wa kifo cha Tobias Moyo inavyosemekana ni kuwa

    Tobias Moyo alikusisitiza sana kuwa muende mkalale wote nyumbani kwake

    lakini ukamkatalia, unaweza kuniambia ni kwa nini hukutaka kumsikiliza

    ombi lake? swali langu likamshtua Niyonkuru na kumfanya anitazame usoni

    “Nani aliyekupa habari hizo?

    “Marehemu”

    Jibu langu likampelekea Niyonkuru kuzidi kutaharuki kisha nikasimama

    na wakati nikisimama nikasikia kelele hafifu za mjongeo wa mtu aliyekuwa

    kule juu kwenye ngazi akisikiliza maongezi yetu hata hivyo nikajidai sikusikia

    chochote.

    “Nashukuru kwa kinywaji shemeji”

    “Uliingiaje humu ndani wakati geti lilikuwa limefungwa? aliniuliza kwa

    taharuki kana kwamba ndiyo nilikuwa nimeingia muda ule.

    “Limefungwa vipi mbona nilipolisukuma lilikuwa wazi? nilimdanganya na

    hapo nikachukua kalamu na karatasi toka mfukoni kisha nikaandika namba za

    simu za chumba changu kule hotelini na kumpa.

    “Nitakuwa hapa jijini Kigali kwa muda wa wiki mbili ningependa tuonane,

    namba zangu ni hizo” nilimwambia huku nikinyoosha mkono kumpa karatasi

    ile yenye namba za simu. Baada ya kusita kidogo akaipokea ile karatasi na

    kuificha kwenye sidiria yake huku akitupa jicho la wizi kutazama kule juu ya

    ngazi.

    “Ni matumaini yangu kuwa tutaonana tena hivi karibuni, nashukuru sana

    kwa ukaribisho wako siku njema” nilimuaga.

    “Karibu tena” alinijibu huku akisimama pale kwenye kochi tayari kunis?indikiza. Tulirudi kupitia ile njia tuliongilia na tulipofika mlangoni tulipeana

    mikono na kuagana. Nilitoka nje ya nyumba ile huku nikiuacha mlango wa

    mbele wa ile nyumba ukifungwa nyuma yangu. Mara tu nilipotoka nje sikuon?doka na badala yake nilipiga hatua chache mbele yangu kisha nikageuka nikin?yata taratibu kurudi tena pale mlangoni. Nilipofika nikabanisha na kusikiliza

    mle ndani na hapo nikaisikia sauti ya kiume ikiuliza

    “Ameondoka?

    “Ndiyo” nikamsikia Niyonkuru akijibu

    “Una uhakika? ile sauti ya kiume iliuliza kwa msisitizo kiasi cha kunifan?ya nitabasamu kwani sasa nilikuwa na hakika kuwa mle ndani kulikuwa na

    mwanaume ingawaje sikuweza kuelewa kwanini hakutaka niutambue uwepo

    wake. Hatimaye niliamua kuondoka zangu lakini nikiwa na maswali mengi

    kichwani.

    Baada ya kutoka nje ya geti la nyumba ile nilitembea nikiifuata baraba?ra ya mtaa ule mpaka mwisho ambapo nilikunja kona kuelekea nilipoegesha lile gari langu. Nilipofika nikafungua mlango na kuingia ndani na hapo safari

    ikaanza huku nikiendelea na zoezi la kuyachunguza magari yote niliyoongo?zana nayo barabarani kupitia vioo vya ubavu wa gari. Hata hivyo sikuona gari

    lolote la kulitilia mashaka ingawaje sikusitisha zoezi lile.

    __________

    NILIPOIFYATUA ILE KOFIA YA JUA iliyokua juu ya kiti changu cha

    dereva na kuitazama tena ile ramani ya jiji la Kigali niliyokuwa nimeibandika

    juu yake, niliona kuwa ningekuwa nikizunguka na kupoteza muda wangu bure

    endapo ningeamua kurudi na njia ile niliyoipita awali hivyo kwa kuokoa muda

    nilipofika kwenye ule mzunguko wa barabara ya Rwandex nikabidili uelekeo.

    Nikaiacha ile barabara Pue de lac Ruhondo nikaishika barabara ya kushoto

    kwangu iitwayo Boulevard de l’Oua ambayo mbele yake ingekuja kukutana

    na barabara nyingine inayotoka eneo la Nyarugenge na nyingine ya Avenue de

    lack Muhaz katika makutano ya barabara ambayo ningeyapita na kuendelea

    mbele nikiifuata barabara ya Boulevard de l’Oua kuelekea Hotel Des Milles

    Collines.

    Wakati nikiendelea na safari mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani

    mwangu juu ya Niyonkuru na yule mwanaume aliyekuwa akiishi naye mle

    ndani. Kwa kila hakika nilijua kwa Niyonkuru alikuwa amenificha jambo fu?lani pengine kutokana na shinikizo la yule mtu aliyekuwa mle ndani kwake.

    Mtu yule alikuwa nani na kwa nini Niyonkuru alionekana kumuogopa? niji?uliza huku nikikataa kabisa kukubali kuwa ule ndiyo ulikuwa mwisho wa ma?hojiano yangu na Niyonkuru. Kwa vyovyote vile nilijua tu kuwa Niyonkuru

    alikuwa na taarifa muhimu juu ya Tobias Moyo ambazo hakuwa tayari kunipa

    kutokana na sababu alizozijua yeye mwenyewe.

    Nilirudia tena kuitazama saa yangu ya mkononi nikaona kuwa dakika

    chache zilikuwa zimepita tangu ilipotimia saa tisa alasiri, nikajiambia kuwa

    bado nilikuwa na muda wa kutosha wa kuniwezesha kuwahi na kuonana na

    Mutesi kule chumbani kwangu Hotel Des Milles Collines hivyo sikuona saba?bu ya kukimbia. Nikapunguza mwendo wa gari na kuanza kutembea taratibu

    huku macho yangu mara kwa mara yakirudia kuvitazama vioo vya mbele vya

    ubavu wa gari ili kuchunguza kama kulikuwa na gari lolote lililokuwa likini?fungia mkia nyuma yangu. Hali bado ilikuwa tulivu.

    Nilikuwa tayari nimekwishasafiri umbali wa zaidi ya kilometa moja kati?ka barabara ile iliyokatisha msituni wakati nilipokiona kuzuizi cha barabara

    mbele yangu. Nikashtuka kwani hakikuwa kizuizi rasmi kama vile vinavyo?tumiwa na askari wa barabarani wa nchi yoyote bali kizuizi kile kilifanywahttp://pseudepigraphas.blogspot.com/

    kwa mawe makubwa matano yaliyopangwa katika mstari mnyoofu kuziba

    barabara ile. Wasiwasi ukaniingia kwa kuzingatia kuwa sheria za barabarani

    nilikuwa nikizifahamu vizuri kuwa eneo lile halikufaa kuwekewa kizuizi cha

    namna yoyote. Kwanza lilikuwa eneo la porini lisilokuwa na makazi yoyote ya

    binadamu na pili kizuizi kile hakikufanywa na askari wa usalama barabarani

    wa jeshi la polisi la Rwanda kwani sare zao nilikuwa nikizifahamu vizuri. Ku?likuwa na askari wa watatu wa jeshi la wananchi wa Rwanda yaani Rwandese Armed Force wote wakiwa na bunduki zao zilizokuwa zimening’inia begani.

    Mwanajeshi mmoja alisimama upande wa kushoto wa barabara na mwingine

    upande wa kulia na watatu alisimama katikati ya barabara akinionesha ishara

    kwa mkono wake kuwa nisimame. Sikuona gari lolote lililokuwa limesima?mishwa eneo lile hali hiyo ikazidi kunitia mashaka zaidi hata hivyo sikuona

    namna yoyote ya kugeuza gari haraka eneo lile na kuwakimbia wale watu

    kwani kwa kufanya hivyo nilifahamu kuwa nisingefanikiwa kufika mbali

    kwani wale watu wangeweza kuyafyatulia risasi magurudumu ya gari langu

    na kunikamata kiulaini, istoshe sikufahamu hasa walikuwa na lengo gani,

    pengine walikuwa wakimtafuta mtu wao na siyo mimi.

    Nilijipa moyo na kupunguza mwendo huku nikiwa nimechukua tahadhari za

    kila namna. Nilichukua bastola yangu Colt 45 niliyokuwa nimeisunda kiunoni

    kwa nyuma na kuichomeka eneo fulani mafichoni chini ya kiti kile cha dereva

    nilichokikalia. Sikutaka watu wale wanikute na silaha yoyote kwani kwa ku?fanya hivyo ingenipelekea matatizo zaidi japo nilifahamu fika kuwa nilikuwa

    nikielekea kukabiliana na hatari mbele yangu.

    Nilipunguza mwendo na kusimama umbali wa mita kama tano kabla ya kili?po kizuizi kile huku mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio. Askari mmoja

    aliyekuwa amesimama upande wa kulia pembeni ya kizuizi kile alinifuata kwa

    tahadhari mno nikabaki nikimtazama.

    “Ndagamunu!” aliniambia katika lugha ya kinyarwanda ambayo kwa kweli

    sikufahau alikuwa akimaanisha nini, nikabaki nikimtumbulia macho tu.

    “Don’t you understand?Please i need papers, ...identity” alirudia kuniambia

    huku akionesha hasira kwa kutomuelewa mapema na hapo nikawa nimefaha?mu kuwa alikuwa anahitaji kitambulisho changu. Nikachukua kitambulisho

    changu cha bandia toka katika mfuko wa shati na kumpa, akakipokea na kuan?za kukipekuwa akisoma maelezo yaliyokuwa kwenye kitambulisho kile kisha

    akanyanyua macho yake kunitazama

    “Wewe ni mtanzania? akaniuliza hata hivyo nilipomtazama nilijua alikuwa

    na kitu kingine alichokuwa akikifikiria kichwani na si swala la mimi kuwa

    mtanzania au raia wa nchi nyingine yoyote.

    “Taarifa zangu zote si zipo kwenye kitambulisho hicho afande? nilimjibu

    kwa hasira baada ya kuanza kuchoshwa na swali lake lisilokuwa na kichwa

    wala miguu na hapo nilimwona yule askari mwingine aliyekuwa amesimama

    upande wa kushoto wa kile kuzuizi akisogea pale tulipo.

    “Kazi yako inakutambulisha kuwa wewe ni mwandishi wa habari wa ku?jitegemea kutoka Tanzania, unadhani ni habari zipi unazozitafuta hapa Rwan?da? askari yule aliniuliza kwa kejeli na hapo nilimwona akichukua kitambu?lisho changu na kukitia kwenye mfuko wa gwanda lake la jeshi. Nikaanza

    kuhisi kuwa hatari ilikuwa ikininyemelea taratibu hata hivyo nafsi yangu ilin?ionya kuwa nisilete ukorofi wa namna yoyote.

    “Waandishi wa habari huwa hatuna mipaka ya maeneo katika ufanyaji kazi

    wetu ilimradi tusivunje sheria za nchi husika. Mwandishi wa habari wa Tanza?nia anaweza kufanya kazi nchini Rwanda, Burundi, Uganda, Congo au kokote

    kule barani Afrika na mwandishi wa habari wa Rwanda vilevile anaweza kufanya kazi nchini Congo, Burundi, Uganda au Somalia na kwengineko ili mradi

    aheshimu sheria za nchi husika” nilimjibu kwa jeuri.

    “Nani aliyekuambia kuwa Rwanda haina waandishi wa habari wa kutosha

    mpaka wewe uje kuwasaidia? yule askari akaniuliza kwa dharau huku akinita?zama katika uso wa kiafande uliozoea amri na mamlaka.

    “Kwa hiyo mnanifukuza nchini kwenu siyo? nilimuuliza.

    “Vifaa vyako vya kazi viko wapi? akaniuliza huku akionesha kulipuuza

    swali langu

    “Hivi hapa” nilimwambia huku nikiushika ule mkoba wangu wenye kamera

    ya kiuandishi wa habari aina ya Olympus

    “Nipe” akaniamrisha, na hapo nikageuka na kumtazama huku hasira zi?menishika hata hivyo nilijionya juu ya kuleta ukorofi wa namna yoyote. Nika?chukua ule mkoba na kumkabidhi akaupokea na kuufungua kisha akaichukua

    ile kamera na kuanza kuichunguzachunguza ingawaje nilipomdadisi niligun?dua kuwa lengo lake halikuwa kwenye ile kamera

    “Unatoka wapi? yule mwenzake alikuwa amekwisha tufikia akaniuliza aki?wa amesimama upande wa kushoto kwenye dirisha la mbele

    “Natokea mitaani afande kutafuta habari”

    “Shuka chini”

    “Umesema?

    “Shuka chini, hujanisikia?

    “Mimi? nikamuuliza nikijaribu kumbabaisha na muda uleule akaingi?za mkono dirishani na kufyatua kitasa cha mlango kisha akafungua mlango

    wa gari na kuikoki bunduki yake AK-47 akiziruhusu risasi kadhaa kuingia

    kwenye chemba hali iliyoupelekea moyo wangu kupiga kite kwa nguvu pale

    nilipozisikia risasi zile zikigota.

    “Okay, okay, okay afande nashuka” nilimwambia askari yule na hapo nika?jizoazoa taratibu nikishuka. Sasa nikafahamu kuwa askari wale hawakuwa na

    lengo la mtu mwingine yeyote isipokuwa mimi huku nikijiuliza kuwa wali?juaje kama ningepita barabara ile au kulikuwa na vizuizi vingi walivyokuwa

    wamevitega kwenye barabara za mitaani kunikamata? nilijiuliza kimoyomoyo

    huku nikiikumbuka ile gari Nissan Patrol ya jeshi la Rwanda iliyokuwa iki?nifungia mkia jana usiku huku nikijiuliza kama watu hawa wangekuwa ndiyo

    wale waliokuwa wakinifuatilia ile jana. Wanahitaji nini kutoka kwangu? nili?jiuliza.

    Wakati nikishuka nilikumbuka kutazama saa yangu ya mkononi nikagundua

    ilikuwa ikielekea kutimia saa tisa na nusu, muda wa nusu saa tu ulikuwa ume?salia kabla ya kukutana na Mutesi kule Hotel Des Milles Collines. Nikajikuta

    nikimuwaza Mutesi kuwa angechukua maamuzi gani mara baada ya kufika

    hotelini kule na kunikosa na hapo nikajikuta nikimkumbuka Niyonkuru na

    yule mwanaume aliyekuwa mle ndani ambaye bila shaka alikuwa mwanajeshi

    wa jeshi la wananchi wa Rwanda. Sasa nilianza kuwahusisha watu hawa na

    yule mwanajeshi.

    Niliposhuka chini yule askari wa mwanzo akaniparamia na kunigeuza niuta?zame ule upande wa gari langu, nilipogeuka akaichukua mikono yangu na kuigemeza kwenye bodi la gari kisha akaanza kunipekua akianzia chini mpaka

    kifuani.

    “Huu ndiyo utaratibu mnaoutumia kuwakaribisha wageni kwenye nchi

    yenu? nilimuuliza yule askari aliyekuwa amenikandamiza kwenye bodi ya

    gari huku akiendelea kunipekua maungoni bila haya utadhani mimi mkewe.

    “Funga mdomo wako na muda si mrefu utatufahamu kuwa sisi ni nani”

    alinijibu huku akichukua ile waleti yangu toka katika mfuko wa nyuma na

    suruali yangu na kuitia mfukoni mwake.

    “Kwani nyie ni akina nani na mbona mnachukua vitu vyangu kiubabeubabe

    bila kunieleza kosa langu? niliwauliza nikitaka kununua muda. Akili yangu

    ilianza kufanya kazi haraka nikipanga namna ya kujinasua toka mikononi

    mwa watu wale hatari wakati huo nikiwaza hatima yangu ingekuwaje endapo

    ningekubali kutekwa na watu wale.

    Mimi ni jasusi niliyehitimu vizuri na nilikuwa na hakika kuwa watu hawa

    walikuwa wakinifahamu mimi kama jasusi na si yule Patrick Zambi mwan?dishi wa habari wa kujitegemea kutoka nchini Tanzania kama nilivyokuwa

    nikipenda watu wanifahamu tangu nilipoingia hapa nchini Rwanda. Ujasusi

    ni mzuri sana na mtamu mno hasa pale unapofanikiwa kutimiza lengo lako na

    kurudi nchini kwako salama lakini ikitokea umekamatwa majuto yake huwa

    hayaelezeki kwani adhabu yake huwa ni kifo na mbaya zaidi ni juu ya adui

    yako kuamua yeye mwenyewe kuwa kifo chako kiwe cha namna gani. Hali

    hiyo ikazidi kuisukuma akili yangu izidi kufikiria namna ya kujinasua.

    Kwanza nilijilegeza kabisa na kujionesha kuwa nilikuwa nimebwana kisa?wasawa na yule askari ili aniamini kuwa nilikuwa siwezi kufanya purukushani

    ya namna yoyote. Yule askari wakati akiendelea kunipekua niligeuka kuwata?zama wale askari wengine wawili ambao kwa sasa walikuwa wamenikarib?ia kiasi cha umbali wa hatua mbili huku wakimtazama mwenzao aliyekuwa

    akiendelea kunipekua. Niliwatazama askari wale na kugundua kuwa bunduki

    zao walikuwa wamezishika kihasarahasara ingawaje walionekana tayari kun?ishambulia muda wowote pale ambapo ningethubutu kufurukuta.

    Kwa mara ya kwanza nilianza kuhisi kuwa akili yangu ilikuwa imeshikwa

    na ganzi pale nilipowaza kuwa ni kitu gani kingefuatia pale ambapo jarib?io langu la kujinasua toka mikononi mwa watu wale hatari lingeshindikana.

    Hata hivyo bado nilipiga moyo konde huku nikijiambia ni lazima nijiokoe

    vinginevyo ningekufa kama kondoo. Yule askari sasa alikuwa akinipapasa

    makalio na kiuno bila haya nikabana pumzi kwa hasira na kukusanya nguvu.

    “Mnataka nini kwangu? niliwauliza tena baada ya kuona hakuna anaeongea.

    “Tunakupeleka sehemu nzuri utakayojionea mwenyewe kwa macho yako

    na bila shaka utapiga picha na kuandika habari unazozihitaji za matukio yote

    muhimu. Huoni kuwa tutakuwa tumekurahisishia kazi yako ya uandishi wa

    habari wa kujitegemea na siyo kuzungukazunguka hovyo mitaani kama ufa?nyavyo sasa? askari yule alinijibu kwa dharau huku akindelea kunipapasa

    maungoni.

    “Sasa ndiyo mpaka mnikabe namna hii halafu kwa nini msinisikilize

    mwenyewe kama ninahaja na hizo habari zenu au lah?

    “Tulia tunakusaidia we bwege, tiba nyingine huwa zina maumivu kidogo”

    yule askari aliyekuwa akiendelea kunipekua iliniambia kwa dharau na wakati

    huo mikono yake ilikuwa inakaribia mabegani mwangu. Japokuwa nilifany?iwa upekuzi wa harakaharaka ila kila sehemu aliyokuwa akinigusa yule askari

    nilikuwa nasikia maumivu makali mno, vidole vyake vilikuwa vimekomaa na

    vigumu mno mithili ya vipande vidogo vya mbao ya mninga.

    Sasa muda niliokuwa nikiusubiri ulikuwa umewadia, mikono ya yule askari

    aliyekuwa akinipekua ambaye alikuwa akilingana urefu na mimi sasa ilikuwa

    mabegani mwangu sambamba na usawa wa shingo yake. Niligeuka kuwataza?ma wale wenzake nikawaona kuwa walikuwa wemezama katika kumwangalia

    mwenzao. Nilimsubiri yule askari aliyekuwa akinipekua wakati akinyanyuka

    nyuma yangu na hapo nikageuka haraka na kumpiga kiwiko cha nguvu mdo?moni, nikamvunja taya lake na kumng’oa meno manne palepale bila ganzi

    huku akipiga yowe kali la maumivu na kupepesuka. Nikageuka na kuudaka

    mkono wake wa kulia halafu nikaushushia pigo jingine la kiwiko cha chini na

    hapo nikausikia mfupa wa mkono wake ukitoa sauti kali ya mvunjiko kama

    buti la askari linapokanyaga kijiti kikavu cha tawi la mwembe. Yule askari

    akipiga tena yowe na bunduki yake iliyokuwa begani ikamteleza na kuanguka

    chini.

    Kilikuwa kitendo cha haraka sana kiasi kwamba wale wenzake wakawa

    kama wameshikwa na butwaa, fahamu zao zilipowarudia vizuri walinikama?ta haraka na kunielekezea mitutu ya bunduki zao kwangu. Hata hivyo wa?likwisha chelewa kwani tukio hilo nilikuwa nimeshalipigia mahesabu hivyo

    wakati huo nilikuwa nimeishamuwahi yule askari niliyemshambulia na kumt?uliza kifuani kwangu kwa kabari matata iliyoruhusu kiasi kidogo cha hewa

    kupenya kwenye koo lake.

    “Wekeni silaha zenu chini” niliwaambia wale wanzake wakati huo nikiwa

    nimeshaichomoa bastola ya askari yule niliyemdhibiti toka kiunoni mwake

    kwa mkono wangu wa kulia na kuielekezea kichwani mwake. Wale wenzake

    kuona vile wakawa wameduwaa huku nikijuafika kuwa wasingeweza kujibu

    mashambulizi kipumbavu kwani yule mwenzao nilikuwa nimemweka mbele

    yangu kama ngao hivyo wakabaki wameshikwa na butwaa wasijue cha kufa?nya.

    “Nimesema wekeni silaha zenu chini vinginevyo huyu mwenzenu atakwen?da na maji” niliwafokea hata hivyo hakuna aliyeweka bunduki yake chini.

    Nilipowatazama kwa haraka nikatambua kila mmoja alikuwa akipiga mahes?abu ya namna ya kunidhibiti. Sikutaka kupoteza muda hivyo kufumba na

    kufumbua niliuondoa ule mkono wangu ulioshika bastola toka kichwani mwa

    yule mateka wangu na kuielekezea kwa askari mmoja kati ya wale wawili

    mbele yangu na hapo nikavuta kilimi cha bastola na kuziruhusu risasi mbili

    kwa shabaha makini kuupekenya moyo wa askari yule na kumtupa hewani al?ipotua chini sikutaka kuifahamu habari yake kwani nilikuwa na hakika kuwa

    hakuwa hai tena.

    Niliirudisha tena bastola na kuilekezea kichwa kwa yule mateka wangu. Yule

    askari aliyesalia akashikwa na hofu kwa kumuona mwenzake amesombwa he?wani na risasi zangu hivyo akafyatua risasi toka kwenye bunduki yake AK-47 bila shabaha nzuri akikusudia kunilenga, nikawahi haraka kuiondoa bastola

    yangu toka kichwani mwa yule mateka kisha nikamsukuma na kumlengesha

    usawa wa zile risasi za adui huku mimi nikiwahi kujitupa chini. Muda ule ule

    nikasikia sauti kali ya yowe la maumivu halafu nikamuona yule mateka wan?gu akitupwa hewani sambamba na michirizi mirefu ya damu ikipaa hewani.

    Risasi zile zilikuwa zimekifumua vibaya kifua chake na alipotua chini alitulia

    kimya, yule mwenzake aliyemlenga akabaki akipiga yowe la taharuki akiwa

    haamini kilichotokea.

    Sikutaka kumsubiri nikajiviringisha pale chini majanini nilipokaa sawa

    nikakivuta tena kilimi cha bastola yangu mkononi, safari hii pia sikufanya

    makosa jicho langu la kushoto nikiwa nimelifumba vizuri nilikiona kichwa

    cha mtu yule kikiwa kimeenea vizuri kwenye usawa wa jicho langu la kulia

    na bila ya kuchelewa nikavuta kilimi cha bastola yangu kwa mara nyingine na

    muda huo huo nilikiona kichwa cha askari yule kikitawanyika hewani huku

    yeye akirushwa mzobemzobe na kutupwa kichakani. Kwa sekunde kadhaa

    mimi nilibaki nimelala pale chini majanini bila kufanya mjongeo wa namna

    yoyote huku macho yangu yakisafiri kulichunguza eneo lile kama macho ya

    kinyonga.

    Nilipoona hali ni tulivu nikanyanyuka taratibu na kwa mwendo wa kuinama

    nikaanza kuelekea kule ilipokuwa ile maiti ya yule mateka wangu aliyekuwa

    akinipekua. Nilipomfikia nikampekua haraka na kuchukua vile vitu vyangu

    aliyonipora na kuviweka mfukoni mwake lakini wakati nikiendelea na zoezi

    lile ghafla nikaanza kusikia milio ya risasi zikivurumishwa pale nilipokuwa

    ikabidi niwahi kujitupa na kulala chini pembeni ya maiti ya yule askari. Zile

    risasi ziliendelea kuvurumishwa hovyo huku nyingine zikipita umbali mfupi

    tu juu yangu huku risasi nyingine zikitua karibu yangu na kuchimba udongo

    wa mahali pale hivyo muda mfupi tu uliofuata eneo lile likawa limefunikwa

    kwa vumbi la udongo mwekundu.

    Sikuwa na namna ya kujiepusha na shambilio lile na safari hii nilifahmu

    kuwa sikuwa na ujanja tena kwani nilikuwa nimejianika eneo la wazi na adui

    aliyekuwa akinishambulia nilihisi alikuwa akiniona vizuri pengine hadi mapi?go ya moyo wangu hivyo mjongeo wowote ambao ningeufanya tafsiri yale

    ilikuwa ni kifo.

    Hofu ikanishika sana mwisho wangu nikawa kama ninaeuona ukinikarib?ia, nikaichukua ile maiti ya yule askari aliyekua amelala pale chini pembeni

    yangu na kuifanya kama ngao ya kujikinga na zile risasi. Sikutaka kukamatwa

    nikiwa na vile vitambulisho vyangu kwani kwa kufanya hivyo ingekuwa rahisi

    kunifahamu kuwa mimi ni nani hivyo niliichukua ile waleti yangu iliyokuwa

    na kitambulisho, pesa kidogo na kadi za benki mbalimbali ambazo nilikuwa

    nimezichukua muda mfupi uliopita toka katika mfuko wa suruali wa yule

    mateka wangu kisha nikairusha ile waleti katika shina la mti mkubwa wa

    mvule uliokuwa pale jirani na barabara.

    Muda mfupi uliofuata zile risasi zilikoma huku mimi nikiwa bado nimelala

    pale chini na hapo nikawaona wanajeshi sita wa jeshi wa jeshi la Rwanda

    wakitoka kule vichakani na bunduki zao zikiwa zimetulia vizuri mikononi tayari kunishambulia endapo ningejidai kuleta ujuzi.

    “Tupa silaha yako chini na utulie hivyo hivyo ukijidai kuleta namna yoyote

    ya ujanja hatutokuvumilia” nilisikia sauti ya mmoja wao akinionya toka nyu?ma yangu hofu ya kukamatwa mzima mzima sasa ikawa imenishika.

    Nikawa najishauri kuwa nijipige risasi kabla hawajanifikia na kunikama?ta hata hivyo nafsi yangu ilisita kwani hiyo ingekua hatua ya mwisho baada

    ya mbinu zote za kujiokoa kuonekana kugonga mwamba. Nikashusha pumzi

    taratibu na kutii amri ile huku niikatupa chini ile bastola iliyokuwa mkononi

    mwangu wakati huo nikiomba muujiza mwingine utokee niponyoke kwenye

    hatari ile iliyonikabili.

    Niliendelea kutulia pale chini na muda mfupi uliofuata nikaliona buti la jeshi

    likinikanyaga sikioni na kunigeuza taratibu, nilipogeuka nikatupa macho ku?muangalia aliyekuwa akinikanyaga na hapo nilijikuta nikitazama na kipande

    cha mtu, mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Rwanda ama Rwandese Armed

    Force, mweusi na mrefu mwenye sura mbaya yenye kovu kubwa upande wa

    kushoto wa jicho lake, kovu lililotokana pengine na ajali fulani ya kuungua

    na moto kwani hata baadhi ya nywele zake za upande wa kushoto wa kichwa

    chake hazikuwepo.

    Mwanajeshi yule mkononi alikuwa na bunduki aina ya M-16 ambayo mtutu

    wake aliuelekezea pale chini nilipolala. Muda mfupi uliofuata wenzake nao

    wakawa wamefika pale nilipokuwa na kunizunguka. Yule jamaa akanikand?amiza pale chini kwa kiatu chake na hapo nikasikia maumivu makali sana siki?oni kisha akanitemea mate usoni kwa hasira, nikataka kusimama hata hivyo

    sikufanikiwa kwani nilipigwa buti moja la kichwa na kulala tena pale chini

    nikihisi kizunguzungu.

    Nikakusanya tena nguvu na kutaka kusimama na hapo vidole vyangu

    vikakanyagwa na buti za askari wale huku wakivisaga ardhini. Muda uleule

    nilimuona askari mmoja akianza kunifunga kamba miguu na mikononi kati?ka mtindo wa kukusanya miguu na mikono kwa pamoja kama mnyama wa

    porini. Kamba zile ngumu zilivutwa na kukazwa miguu na mikononi nikawa

    nimefungwa kama ng’ombe tayari kupelekwa machinjioni. Nilisikia maumivu

    makali sana na nilipolalamika askari mmoja alinizaba makofi ya nguvu yaliy?onipelekea nione maruerue mbele yangu.

    Halafu muda ule ule nikashangaa nikinyanyuliwa na kubebwa mzobemzobe

    kupelekwa kwenye lile gari nililokuja nalo, mlango wa nyuma ulipofunguli?wa nikatupwa kule nyuma kama gunia la mihogo na hapo nikasikia maumivu

    makali na kupiga yowe hata hivyo yowe langu lilinyamazishwa kwa kofi zito

    nililotandikwa mgongoni na mmoja wa wale wanajeshi.

    Halafu muda uleule wale wanajeshi wakazunguka na kuingia ndani ya gari

    mbele wakaa watu wawili na wengine wakakaa ile siti iliyofuatia kwa nyuma

    mimi nikabebwa na kuwekwa katikati huku mtutu wa bastola ukizitekenya

    mbavu zangu. Hakuna aliyenisemesha na muda uleule safari ikawa imeanza

    bila ya kujua tulikuwa tukielekea wapi ingawaje nilihisi tulikuwa tukielekea

    uelekeo wa mbali na mji sehemu ambayo mimi bado sikufahamu. Wakati

    tukiendelea na safari nilinyanyua kichwa kutazama nje hata hivyo sikuweza kuona vizuri kwani bado macho yangu yalikuwa na maruerue kutokana na lile

    kofi zito nililozabwa usoni.

    “Mnanipeleka wapi nyinyi mashoga? niliwauliza hata hivyo hakuna ali?yenijibu na hapo nikaanza kushikwa na wasiwasi.

    “Eti nyie malaya mbona mmevuta midomo kama mnagombea bwana, niji?buni basi huku manipeleka wapi sasa? niliwauliza tena nikiwapandisha hasira

    hata hivyo bado hakuna aliyenijibu wala kunisemesha.

    “Hivi nyinyi mna akili kweli au ni wendawazimu mbona hamnijibu? niliwa?uliza tena na hakuna aliyenijibu badala yake nilishangaa nikipigwa kichwani

    na kitu kizito kama kitako cha bunduki na muda uleule nikaanza kujihisi

    mzito, kizunguzungu kikanishika, nikafumbua mdomo ili niongee hata hivyo

    sikufanikiwa kwani sauti yangu ni kama iliyokuwa ikinirudia mwenyewe ma?sikioni.

    Ghafla nikaanza kuhisi mdomo wangu nao ulikuwa ukielekea kuwa mzi?to na hapo nikaanza kuona giza mbele yangu. Kufumba na kufumbua nika?valishwa kitu kama mfuko mweusi kichwani na wakati nilipokua nikijitahidi

    kupambana na kitendo kile nikashtukizwa tena na pigo jingine kama lile la

    awali nyuma ya kichwa changu na hapo nikalegea na kufumba macho taratibu

    na kilichofuata sikukifahamu





    FAHAMU ZILIPONIRUDIA nilijikuta nimeketi kwenye kiti huku miguu na

    mikono yangu imefungwa kamba ndani ya chumba kilichofanana na pango

    dogo. Nilikua nimevuliwa nguo zote na kubaki uchi wa mnyama, baridi kali il?ikuwa ikinitafuna mwilini na nilipojaribu kufumbua macho kwa shida sikuwe?za kuona kitu chochote mbele yangu kwani nilikua bado nimefunikwa na ule

    mfuko mweusi. Hisia zangu zilinieleza kuwa mle ndani kulikuwa na watu hata

    hivyo sikuweza kuwaona kutokana na kichwa changu kufunikwa. Ni kama

    watu wale walinihisi kuwa nilikua nimerudiwa na fahamu kwani nilisikia sauti

    nzito ya kiume ikitoa amri mbele yangu.

    “Muondoe kitambaa anarejewa na fahamu huyo” muda uleule mara ni?kasikia sauti ya hatua za mtu ikinijia kwa nyuma, moyo ukaanza kunienda

    mbio huku nikijiuliza pale nilikuwa wapi, nikifanya nini na watu wale wali?osemeshana walikua ni akina nani.

    Ile sauti ya hatua za yule mtu ilikuja na kuishia kando yangu na hapo ni?kasikia ule mfuko mweusi niliokuwa nimefunikwa kichwani ukivutwa kwa

    juu na hapo nikabaki nikitumbua macho huku nikihisi kizunguzungu kikipita

    kichwani mwangu. Nikaanza kuzungusha macho yangu mle pangoni na hapo

    nikawaona watu wanne mle ndani, watatu walikua wameketi kwenye viti nyu?ma ya meza kubwa iliyokuwa mbele yao huku juu ya meza hiyo kukiwa na

    taa moja ya kandili iliyokua imewashwa na kutoa mwanga hafifu na sehemu

    nyingine zote za chumba kile zilikuwa na giza.

    Niliwatazama wale watu mbele yangu na sikuweza kumtambua hata mmo?ja wao, zilikuwa sura ngeni kabisa na miongoni mwao hakuwepo hata mmoja

    kati ya wale wanajeshi walioniteka kule porini. Hata hivyo walikuwa ni maaf?isa wa ngazi za juu wa jeshi la wananchi wa Rwanda, niliwatambua kutokana

    na mavazi yao ya kiafisa wa jeshi kwa namna yalivyokuwa yamechafuka vyeo

    vya kila namna isipokuwa mmoja wao ambaye alionekana kuwa ni mwanajes?hi mwenye cheo cha chini sana yaani kuruta ambaye ndiye aliyekuwa akitu?mikishwa mle ndani. Wakati nikiendelea kutafakari ile hali ya mle ndani nikajikuta nikimwagi?wa maji ya baridi kichwani na yule askari mwenye cheo cha kuruta na hapo

    nikawaona wale maafisa wa jeshi mbele yangu wakitabasamu. Wakaniacha

    nijitikisetikise kuyaondoa yale maji usoni mwangu kwani nilikuwa nimefung?wa na nilipotulia afisa yule alieketi mbele yangu katikati ya wenzake akaanza

    kunisemesha baada ya kunywa funda moja la kahawa iliyokuwa kwenye ki?kombe juu ya meza ile mbele yake. Uso wake haukuonesha hata chembe ya

    mzaha.

    “Una bahati sana kuwa mpaka sasa upo hai tena bila ya kutuhonga chochote

    ndugu Patrick Zambi ingawa mimi nitaendelea kukuita Luteni Venus Jaka,

    mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania”

    Nilishtuka sana kusikia jina langu halisi likitajwa na afisa yule wa jeshi,

    moyo wangu ukawa kama uliopigwa shoti kali ya umeme wenye nguvu za

    ajabu hali iliyonifanya nijihisi kama niliyeugua maradhi ya kiharusi. Kwa

    sekunde kadhaa nilihisi akili yangu ilikuwa imevurugika kabisa, nilipotulia

    nikabaki nikimtazama afisa yule kwa makini huku kurasa za kitabu changu

    cha kumbukumbu zikianza kufunuka moja baada ya nyingine kichwani. Muda

    mfupi baadaye nilijikuta nikishusha pumzi taratibu na kuishiwa nguvu, nikaa?chama mdogo wazi kwa mshangao kwani sikuamini macho yangu.

    “Kanali Bosco Rutaganda...” nilijikuta nikinong’ona kwa sauti ya chini

    huku nikishindwa kuamini macho yangu. Ukweli ni kwamba mara ya mwisho

    kuonana na kanali Bosco Rutaganda ilikuwa ni miaka minne iliyopita mkoani

    Arusha Tanzania katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Tanzania Military

    Academy (T.M.A) Monduli. Wakati huo mimi nikiwa ni mmoja wa wakufunzi

    wa chuo hicho kwa wanafunzi waliokuwa wakisomea mafunzo ya uafisa wa

    jeshi kutoka nchi kumi na moja za bara la Afrika. Nchi hizo zikiwemo D.R

    Congo, Kenya, Malawi, Uganda, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Tanza?nia, Djibout, Burundi na Rwanda. Naam! sasa nilimkumbuka vizuri kanali

    Bosco Rutaganda kipindi hicho akiwa miongoni mwa wanafunzi wangu, na

    hapa nilimtazama akiwa katika suti yake nadhifu iliyokitambulisha vizuri cheo

    chake cha kanali.

    “Luteni Venus Jaka! kweli milima haikutani lakini binadamu tunakutana na

    bahati mbaya sana ni kuwa maisha huwa yanabadilikabadilika ndiyo maana

    leo upo uchi mbele yangu kama mchawi. Niliposikia kuwa ni wewe ndiye

    uliyetumwa hapa Rwanda nilijikuta nikifurahi sana kwani nilijua hii ndiyo

    ingekuwa nafasi nzuri ya kuonana kwetu tangu tulipopoteana miaka minne

    iliyopita rafiki yangu”

    “Mbona sikuelewi unachoongea” nilimkatisha kwa hasira “Nyinyi ni akina

    nani na mnashida gani na mimi?

    “Usijidanganye kuwa nimekusahau Luteni hukumbuki kuwa miaka minne

    iliyopita ulishiriki kikamilifu katika jopo la maafisa wa kijeshi kutoa hukumu

    dhidi yangu nchini Tanzania. Eti kuwa nifukuzwe kwenye mafunzo yale ya

    kijeshi kisha nikamatwe na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kwa kuwa ni?likuwa kwenye orodha ya watu waliokuwa wakipanga njama ya kumpindua

    Rais wa Rwanda.Mlijitahidi sana lakini bahati mbaya hamkufanikiwa kwani nilikuwa mjanja

    zaidi yenu nikawaacha kwenye mataa, viongozi wa kijeshi wa jeshi la Rwanda

    wanaufahamu vizuri mchango wangu katika nchi hii, nawashukuru tu kwa

    kuwa hawakunitupa na ndiyo maana hadi leo hii bado nipo jeshini naitumikia

    nchi yangu nikiisubiri ile siku ya mapinduzi ya kweli na bila shaka dunia

    itafahamu nini kinachoendelea katika nchi hii” Kanali Bosco Rutaganda alizu?ngumza kwa hisia huku akinitazama.

    “Mbona unaongea kama unayetaka kulia kanali?, ni mapinduzi ya namna

    gani hayo ambayo utaweza kuyafanya mtu mwoga kama wewe unayejificha

    kwenye pango hili kama Popo?

    “Ndiyo maana sikupenda uuwawe mapema kwani ningeweza kufanya hivyo

    ila niliamua kuichelewesha safari yako ya kifo nikitaka siku ile ya mapinduzi

    ikukute ukiwa hai, ujionee mwenyewe mambo yatakavyokuwa halafu baada

    ya hapo nitajua namna ya kukufanya”

    “Ni mapinduzi gani hayo unayozungumzia?

    “Mapinduzi ya kuwarudishia uhuru wazawa wa nchi hii, uhuru wao waliop?okonywa na kupewa kundi dogo la watu wachache ambao kimsingi wao ni

    wavamizi tu”

    “Mimi sikuelewi ni uhuru gani huo unaouzungumzia. Ninavyofahamu ni

    kuwa nchi zote za Afrika zimekwisha pata uhuru wake toka kwa wakoloni sasa

    huo uhuru unaozungumzia wewe ni upi?

    Nilimuuliza Kanali Bosco Rutaganda na hapo nikamuona yeye na wale

    wenziwe wakicheka, sikufahamu kitu kilichokuwa kikiwachekesha nikabaki

    nikiwatazama kwa hasira. Kanali Bosco Rutaganda akachukua kile kikombe

    cha kahawa pale mezani na kunywa mafunda kadhaa alipokirudisha mezani

    aliendelea

    “Nani aliyekudanganya kuwa nchi zote za Afrika zimepata uhuru Luteni?,

    kama zimepata uhuru mbona bado haziwezi kujiendesha zenyewe?, huo un?aosema wewe si uhuru bali ni kubadilisha aina nyingine ya mfumo wa ukoloni

    na mbaya zaidi wakoloni wa sasa ni waafrika kama sisi wanaozijua vizuri

    shida za nchi hizi”

    “Mbona sikuelewi Bosco kwa nini usiniweke wazi badala yake unajionge?lesha kama baamedi aliyenunuliwa bia na basha wake” nilimuuliza Kanali

    Bosco Rutaganda huku nikimtazama kwa hasira hata hivyo sikumuona kama

    alikuwa akifanya jitihada zozote za kutaka kujibu swali langu badala yake

    nilimuona akigongeshagongesha vidole vyake juu ya meza huku akinitazama

    bila kuzungumza neno kisha akavunja ukimya

    “Tuambie Luteni ni kitu gani kilichokuleta hapa Rwanda? aliniuliza huku

    chuki ikionekana dhahiri machoni mwake.

    “Kwani mimi siruhusiwi kuingia hapa Rwanda? nilimuuliza huku nikimta?zama.

    “Jibu swali kama ulivyoulizwa siyo unauliza swali” yule kamanda aliyeku?wa upande wa kulia wa Kanali Bosco Rutaganda alinifokea.

    “Nilikuja kutembea”

    “Kwa nini ukajiita Patrick Zambi wakati wewe ni Luteni Venus Jaka?

    kwanini hukutaka kutumia jina lako?

    “Tatizo ni mimi kuwa na majina mawili au tatizo ni mimi kuja hapa Rwan?da? Niliuliza na hapo nikamuona Kanali Bosco Rutaganda akimtazama

    yule askari kuruta aliekuwa karibu yangu. Muda uleule nikaanza kupewa

    mkong’oto wa nguvu wa makofi ya kichwani na ngumi za tumbo, kwa kweli

    nilisikia maumivu makali sana na damu ikaanza kunitoka puani na mdomoni.

    Yule askari hakuacha kunishushia kibano na alikuwa akifanya kwa sifa ili ku?waridhisha wakubwa zake. Walipoona kichapo kile kimenikolea wakamwam?bia yule askari aniache.

    Kwa kweli askari yule alikuwa amebobea katika kutoa mkong’oto maana

    kichapo kile kiliniingia sana nikachanika mdomoni na kutapakaa damu mwili

    mzima. Aliponiacha nikabaki nikihema hovyo na hapo nilimuona Kanali Bo?sco Rutaganda akikichukua tena kile kikombe cha kahawa mezani na kuvuta

    funda moja alipokirudisha mezani alibaki akitabasamu.

    “Hata kama ukiendelea kutuficha tunajua kwa hakika kuwa umetumwa

    hapa Rwanda na kwa taarifa yako habari zako tulizipata mapema sana Lu?teni” Kanali Bosco Rutaganda aliendelea kuongea na hapo nikainua macho

    kumtazama, nikagundua kuwa alikuwa akimaanisha alichokua akikisema.

    Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu “Ina maana nilikuwa nimeuzwa!” nili?jisemea moyoni huku nikiwaza ni nani ambaye angeweza kutoa taarifa zangu

    kwa watu hawa na hapo nikajikuta nikumkumbuka Brigedia Masaki Kambona

    ambaye ndiye aliyekuwa mratibu mkuu wa safari zangu za kijasusi kutoka

    jijini Dar es Salaam. Hata hivyo akili yangu ilishindwa kabisa kumuhusisha

    na sakata hili kwani Bregedia Masaki Kambona alikuwa si tu bosi wangu

    mwenye cheo kikubwa cha kijeshi ila pia rafiki yangu wa karibu sana pamoja

    na utofauti mkubwa wa vyeo uliotutenganisha.

    Vilevile sikuona sababu yoyote ya yeye kuniuza kwani hapakuwa na sababu

    yoyote ambayo ingempelekea kufanya hivyo, istoshe hii haikuwa operesheni

    yangu ya kwanza ya kijasusi kuifanya nikiwa chini yake. Kwa kweli nilijisikia

    kuishiwa nguvu huku nikijihisi kuchanganyikiwa na kukata tamaa.

    “Nani aliyewapa taarifa zangu? niliwauliza hatimaye na hapo wakaanza

    tena kuangua kicheko cha kejeli, nikabaki nikiwatazama huku hasira zimeni?panda. Nilijitahidi kufurukuta pale kwenye kiti bila mafanikio badala yake

    nilitulizwa na ngumi mbili za puani toka kwa yule askari kuruta aliyekuwa

    amesimama pembeni yangu. Nikapiga yowe la maumivu huku damu ikianza

    kunitoka puani, nikawa najisikia kutaka kutapika.

    “Tulia wewe kenge” yule askari Kuruta alinionya na hapo nikakumbuka

    kuitazama ile saa yangu ya mkononi hata hivyo nilijikuta nikikata tamaa pale

    nilipokumbuka kuwa nilikua uchi na vitu vyangu vyote nilikuwa nimevuli?wa. Giza zito la mle ndani halikuweza kabisa kunifanya niweze kukisia kuwa

    muda ule ulikuwa ni saa ngapi hivyo nilijikuta nikimkumbuka Mutesi huku

    nikijiuliza kuwa angefanya nini endapo angefika kule Hotel des Mille Collin?es na kunikosa?, na vipi kama ingetokea Niyonkuru angenitafuta kupitia zile

    namba za simu nilizompa na kunikosa?. Bila shaka ningekuwa nimepoteza

    hatua muhimu sana katika harakati zangu.

    Loh! Kwa nini nilikubali kukamatwa na watu hawa hatari na hapa ni wapi?

    nitabahatika kweli kutoka nikiwa salama? niliendelea kujiuliza bila kupa?ta majibu. Halafu wakati nilipokua nikiendelea kuwaza wazo la Jean Pierre

    Umugwaneza likatumbukia katika fikra zangu, Jean Pierre Umugwaneza

    alikuwa wapi na kipi kilikuwa kimemsibu hadi asiweze kupatikana kwenye

    simu? mpaka kufikia hapa nilijihisi kuchanganyikiwa.

    “Luteni!” Kanali Bosco Rutaganda aliniita na hapo nikayakatisha mawazo

    yangu na kuinua macho kumtazama.

    “Wewe ni kiongozi mkubwa wa jeshi na bila shaka unafahamu vizuri hu?kumu aipatayo mtu pale anapokamatwa akifanya shughuli za kijasusi katika

    nchi nyingine tena mbaya zaidi kwa manufaa ya nchi yake” aliniuliza na hapo

    nikabaki nikimtazama katika hali ya kukata tamaa.

    “Adhabu yake huwa ni kifo. Kifo tu ndiyo malipo stahili ya kazi kama hiyo

    na bila shaka uliingia hapa nchini Rwanda ukiwa unaifahamu vizuri adhabu

    hiyo” Kanali Bosco Rutaganda aliendelea kuongea huku akimalizia kunywa

    funda la mwisho la kahawa iliyobakia kwenye kile kikombe mezani halafu

    akasimama na hapo niliwaona wale wenzake nao wakisimama.

    “Endelea kufikiria nini cha kutueleza vizuri tukakuelewa ili tutakapokutana

    tena uwe na majibu yaliyonyooka” Kanali Bosco Rutaganda akaniambia kisha

    akageuka tena na kumtazama yule askari Kuruta aliyekua amesimama pembe?ni yangu na hapo hofu ikaniingia kwani nilikuwa nafahamu ni tukio gani am?balo lingefuatia. Mara ghafla nikasikia kitu kizito kikinipiga nyuma ya kichwa

    changu, nikapiga yowe kali la maumivu hata hivyo ni kama sauti ile ya yowe

    nilikua nikiisikia peke yangu mle ndani kwani hakuna aliyeshtuka.

    Muda uleule nikaanza kuona giza huku viungo vyangu mwilini vikiishiwa

    nguvu, macho yangu yakafumba na sikusikia tena kilichokuwa kikiendelea,

    fahamu zikanitoka.

    _________

    NILIPOFUMBUA MACHO nilihisi maumivu makali sana nyuma ya

    kichwa na mgongoni kwangu, mikono yangu ilikuwa bado imefungwa hivyo

    sikuweza hata kupapasa eneo lile ambalo wakati huu lilikuwa limeshatawa?liwa na giza zito. Niliyatega vizuri masikio yangu lakini hata hivyo sikuwe?za kusikia sauti ya kitu chochote eneo lile hata pale nilipoituliza vizuri akili

    yangu. Hata hivyo nilikumbuka kuwa fahamu zilikuwa zimenitoka baada ya

    kupigwa na kitu kizito mara tu sehemu ya kwanza ya mahojiano yangu na

    Kanali Bosco Rutaganda ilipomalizika kwenye lile pango dogo na baada ya

    hapo sikufahamu kilichoendela.

    Fahamu ziliponirudia vizuri nilihisi maumivu ya mgongoni yaliyokuwa ya?kiongezeka kadiri muda ulivyokuwa ukienda, nilipotuliza vizuri akili yangu

    nikashtuka kuwa nilikuwa nikiburutwa katika sakafu ya eneo lile. Miguu yan?gu ilikuwa imefungwa minyororo na mvutaji alikuwa mbele yangu akiendelea

    kuniburuza hivyo nikaelewa kuwa yale maumivu ya mgongo yalitokana na

    machibuko niliokuwa nikiyapata katokana na kule kuburuzwa. Nilijitahidi ku?jitetea bila mafanikio kwani yule mvutaji bado alikuwa akiendelea kuburuta minyororo ile iliyonifunga miguuni.

    Matundu ya pua yangu yaliweza kupitisha harufu mbaya ya uvundo iliyoku?wa eneo lile hali iliyonifanya nijisikie kutaka kutapika hata hivyo sikuweza

    kutapika kwani tumboni hakukuwa na kitu chochote. Nilihisi njaa kali sana,

    njaa iliyoambatana na hali ya homa pengine kutokana na ile baridi kali ya mle

    ndani. Maumivu ya mgongo yalikuwa makali mno kiasi kwamba nilianza

    kuhisi kuwa nilikuwa nikichubuka nyama zangu za mgongoni kutokana na

    mburuzo ule sakafuni.

    Mara ghafla tulisimama eneo fulani ambalo nilisikia ukimya wa kupita ki?asi halafu mara nikasikia kelele za kitu kama funguo zilizokuwa zikifungua

    kwenye kitasa mlangoni huku mfunguaji akionekana kutokuwa na uhakika

    wa funguo halisi. Muda uleule mara nikaona mlango fulani wa eneo lile uki?funguliwa na hapo nikaona mwanga hafifu toka ndani ya mlango ule ukipenya

    nje, muda huohuo nikasikia kelele za minong’ono hafifu toka ndani ya chum?ba kile. Hofu ilinishika sana kwani sikufahamu watu wale walikuwa ni akina

    nani.

    Yule mtu aliyekuwa akiniburuta sasa alikuwa amesimama pale mlangoni

    akitazama mle ndani ya kile chumba. Nilipomtazama kwa makini mtu yule

    nikamkumbuka kuwa alikuwa ni yule askari kuruta aliekuwa kule pangoni

    na wale maafisa wengine wa jeshi la Rwanda akiwemo Kanali Bosco Ruta?ganda. Japokuwa sikuweza kumuona vizuri lakini nilimtambua kutokana na

    umbo lake, urefu na magwanda ya jeshi aliyoyavaa. Alipomaliza kutazama

    mle ndani ya kile chumba akageuka kunitazama na hapo nikahisi kama nili?yekuwa nikitazamwa na mnyama mkali mwenye njaa. Muda uleule yule mtu

    akaishika ile minyororo na kuanza kunivutia pale aliposimama, nilipomfikia

    akanifungua ile minyororo miguuni na kunisimamisha huku akinitazama na

    kuangua kicheko hafifu cha dharau.

    “Wewe ndiye Luteni? Luteni nani sijui huko, Luteni gani unakuwa na tabia

    za kishogashoga za kuingilia mambo yasiyokuhusu. Utakaa humu ndani na

    wenzako mpaka hapo hukumu yako itakaposomwa” yule Kuruta aliniambia

    kwa dharau na muda uleule nami nikakusanya mate mdomoni na kumtemea

    usoni.

    Akanitazama kwa hasira usoni kisha kwa kutumia kitambaa cha gwanda

    lake mkononi akajifuta yale mate na hapo akageuka na kuanza kinishushia

    kichapo cha nguvu cha ngumi na mateke ya tumbo. Nilihisi maumivu makali

    mno ambayo sikuwahi kuyasikia hapo kabla. Aliporidhika na kichapo ali?chonitandika akanisukumiza ndani ya chumba kile kwa pigo la teke la mgon?goni. Nikaingia ndani mzimamzima na kuanguka chini kisha nilisikia ule

    mlango ukifungwa nyuma yangu.

    __________

    NIKIWA NIMEKATA TAMAA sana pale chini niliinua macho yangu kuta?zama mbele yangu, mwanga hafifu wa taa ndogo ya kandili iliyokuwa katikati

    ya chumba kile mfano wa pango kama lile la awali uliniwezesha kuwaona

    watu waliokuwa mle ndani na hapo nilishikwa na mshangao nikisikitishwa na afya za watu wale kwani walikuwa wamekondeana sana kiasi cha sehemu za

    mifupa ya miili yao kuchomoza. Walikuwa wamekonda haswa hata vichwa

    vyao vilionekana kama mafuvu, meno yao yalichomoza nje na macho yao ya?likuwa yameingia ndani ya vishimo na kuwafanya watishe sana kuwatazama.

    Harufu kali ya uvundo iliyokuwa mle ndani ilinifanya nijihisi kutaka ku?tapika. Mbaya zaidi watu wale walichanganywa kwa pamoja wanawake kwa

    wanaume wote wakiwa uchi “Balaa gani hili? nilijisemea. Wakati nikiende?lea kutazama mle ndani mara nikasikia mkono wa mtu ukinigusa begani na

    hapo nikageuka taratibu kumtazama yule mtu aliyenigusa. Nilishangaa sana

    nilipomwona Jean Pierre Umugwaneza nyuma yangu na hapo tukabaki tukita?zamana kwa mshangao.

    “Pole sana Patrick” Jean Pierre Umugwaneza aliniambia huku akinisaidia

    kuninyanyua pale chini, niliposimama niliendelea kumtazama nikishindwa

    kuamini macho yangu.

    “Jean... ni wewe?” nilimuuliza.

    “Ni mimi, sikutegemea kukuona humu ndani Patrick imekuaje? aliniuliza

    kwa mshangao.

    “Ni hadithi ndefu Jean hata mimi sikutarajia kukuona hapa, nilikuwa na hi?sia mbaya nikidhani pengine ulikuwa umeuwawa baada ya kukutafuta kwenye

    simu na kukukosa”

    “Oh! Patrick nilijua tu kuwa ungenitafuta lakini waliwahi kunikamata hivyo

    nikabaki nikimwomba Mungu atukutanishe tena” Jean aliendelea kuongea

    huku machozi yakimtelemka mashavuni, nikampigapiga kidogo kifuani kum?tia moyo.

    “Usijali Jean tupo pamoja, sisi ni marafiki sasa lazima tuimalize safari yetu

    pamoja kama tulivyoianza” nilimwambia na hapo nikaiona sura yake ikirud?iwa na tumaini, akanivuta na kunikumbatia kwa sekunde kadhaa kabla ya

    kuniachia kisha niligeuka kuwatazama wale watu wengine waliokuwa mle

    pangoni.

    Wote walikuwa wakitutazama na baadhi walikuwa wakilia. Nilisimama

    taratibu nikiwatazama watu wale ambao walikuwa wa rika tofauti wanawake

    kwa wanaume wote wakiwa uchi bila ya nguo kama mimi. Aibu aliniingia hata

    hivyo sikuona sababu ya kuziba utupu wangu kwani watu wote mle ndani ni

    kama tulifanana tu ingawaje nilihuzunishwa sana na baadhi yao kwani afya

    zao zikionekana kudhoofika sana.

    Harufu mbaya ya uvundo ilikuwa imesambaa kila kona mle ndani na cha

    kustaajabisha sikumuona hata mmoja miongoni mwa watu wale aliyeonekana

    kutaabishwa na harufu ile mbaya. Nikageuka kutazama sehemu za wazi iliy?oonekana kutengwa na wale watu mle ndani na hapo nilishtuka sana kuuona

    mwili wa mtu fulani ukiwa umelala sakafuni sehemu ile.

    Nikapiga hatua taratibu kuuendea ule mwili na nilipoufikia nilishtuka kuwa

    ile ilikuwa ni maiti ya mwanamke yenye majeraha ya kutisha. Mwili wa mwa?namke yule ulikuwa umeanza kuharibika na baadhi ya nyama za mwili wake

    zilikuwa zimeanza kupukutika. Macho yake yaliingia ndani na kuacha vishi?mo, mifupa ya mashavuni ilikuwa imechomoza nje na mdomo wake ulikuwa wazi huku amekenua meno. “Mungu wangu!” nilijisemea huku nikiuziba

    mdomo na pua yangu kwa kiganja changu kupambana na harufu ile kali ya

    uvundo.

    Nilisimama nikiitazama maiti ile iliyokuwa imeharibika vibaya pale chi?ni huku ikitoa harufu mbaya na hapo nikajua kwa nini watu wale mle ndani

    walikuwa wamejitenga na kujikusanya sehemu moja ingawaje lile pango lili?kuwa dogo na lisilokuwa na hata tundu dogo la kupitishia hewa safi. Ile mai?ti ilikuwa ikitoa funza wakubwa waliokuwa wakisambaa kuizunguka. “Loh!

    unyama gani huu binadamu anaweza kumfanyia mwenzake? Nilijisemea huku

    machozi yakinilengalenga nikachuchumaa chini na kuanza kuangua kilio hafi?fu hata hivyo Jean alinifuata akaninyanyua na kunirudisha taratibu kule tuli?pokuwa mwanzo, sikupenda tena kugeuka na kutazama upande ule ilipokuwa

    imelala ile maiti.

    Pango lilikuwa dogo kulingana na idadi ya watu waliokuwa mle ndani hali

    iliyopelekea ongezeko kubwa la joto. Niligeuka kulichunguza pango lile dogo

    na kwenye kona moja nikaona galoni ya kijeshi, juu ya galoni ile kulikuwa na

    kikombe na hapo nikajua kuwa galoni ile ilikuwa na maji ya kunywa.

    Jean akanitambulisha kwa watu wote waliokuwa mle ndani na alipomal?iza akaanza kuwatambulisha wale watu kwangu. Nikawapa pole wale watu

    na kuwatia moyo kisha tulitafuta eneo la pembeni ya ukuta wa pango lile na

    kuketi. Ile njaa na yale maumivu makali niliyokuwa nikiyasikia hapo awali

    yalikwishatoweka kutokana na ile hali niliyokutana nayo mle ndani. Baada ya

    kutulia chini na kuanza kumchunguza kila mtu mle ndani niligundua kuwa ni

    watu watano tu ndiyo tuliokuwa na afya nzuri, yaani mimi, Jean, mzee mmoja

    wa makamo, msichana mmoja na kijana mmoja.

    Tulipoketi nilimtaka Jean anisimulie masaibu yaliyomkuta mpaka mimi

    kumkuta mle pangoni akiwa mateka. Jean alianza kunielezea namna alivyote?kwa, kuwa mara baada ya kuniwekea nafasi ya chumba kule Hotel Des Milles

    Collines aliamua kurudi nyumbani kwake Avenue de la Justice nyumba namba

    13 kupumzika kwa vile siku ile alikuwa amepata pesa ya kutosha hivyo hakuo?na sababu ya kurudi tena kule uwanja wa ndege wa Kigali kusubiri tena abiria

    usiku ule. Akaendelea kunisimulia kuwa mara baada ya kufika na kuegesha

    taksi yake nje ya nyumba aliingia ndani ambapo alipokelewa vizuri na mkewe

    huku mtoto wao akiwa tayari amekwisha lala. Akaniambia kwa vile alikuwa

    na uchovu sana aliamua kwenda kwanza bafuni kuoga alipotoka alirudi meza?ni na kula ambapo baadaye alipomaliza alielekea chumbani kulala. Ikawa

    ilipofika saa tisa usiku ndipo aliposhtuliwa usingizini na mkewe akimwambia

    kuwa mlango wa mbele wa nyumba yao ulikuwa ukigongwa.

    “Nilishtushwa sana na ugongaji ule kwani mgongaji alikuwa akigonga

    mlango kwa fujo mno, si kutaka kabisa kumfungulia nikwamwambia mke

    wangu tumpuuze mgongaji hata hivyo haikuwa rahisi kwani tusingeweza ku?lala tena. Mgongaji aliendelea kugonga kwa fujo hali iliyomfanya mtoto wetu

    atoke chumbani kwake na kukimbilia chumbani kwetu akiogopa. Makalele ya

    mgongaji yalipozidi mke wangu alinishawishi nikafungue mlango nimsikilize

    mgongaji akidhani pengine alikuwa ni mmoja wa majirani zetu aliyepatwa na shida.

    Nilipingana sana na hoja ya mke wangu hata hivyo baadaye nilizidiwa na

    kelele za mgongaji hivyo nikaamua nikamfungulie na kumsikiliza ili kuon?doa kelele zile. Loh!...” Jean alishindwa kuendelea kunisimulia badala yake

    machozi yalianza kumtoka na ili kujihimili akainama chini na kuanza kuchor?achora sakafuni. Nilimtazama na kumuonea huruma sana huku nikifahamu fika

    kuwa maelezo ambayo yangefuatia baada ya pale yasingependeza kuyasikia.

    “Pole sana Jean, nafahamu..., nafahamu...” nilimpigapiga mgongoni huku

    nami nikijizuia nisitokwe na machozi.

    “Nini kilifuatia baada ya hapo? nilimuuliza baada ya kitambo kifupi cha

    ukimya kupita na hapo akageuka na kunitazama uso wake ukiwa umesawajika

    huku machozi yakimtoka kama mtoto mdogo. Akarudia tena kutazama chi?ni huku akichorachora sakafuni, nilimpigapiga mgongoni kumtia moyo kisha

    nikamuacha kidogo aweze kutulia. Alipotulia aliendelea

    “Nilipofungua mlango nikawaona wanajeshi wawili wakiwa na bunduki

    zao mikononi, nilitaka kuwahi kufunga mlango hata hivyo nilichelewa. Askari

    mmoja aliupiga teke mlango ule mlango ukafunguka na hapo askari wale

    wakaingia ndani, nikajitahidi kuwazuia hata hivyo sikufanikiwa kwani askari

    mmoja alinipiga korodani zangu kwa kitako cha bunduki yake. Nikapiga yowe

    kali la maumivu hali iliyowapelekea mke wangu na mtoto waje kuniangalia

    lakini...” Jean alishindwa tena kuendelea kunisimulia na safari hii akaangua

    kilio hafifu. Nikamwacha alie kidogo kupunguza simanzi aliyokuwanayo baa?daye alipotulia nikambembeleza nikimshawishi aendelea kunisimulia.

    “Niliwauliza wale wanajeshi kuwa walikuwa na shida gani hadi wani?vamimi vile, wakasema niwapeleke sehemu nilipompeleka abiria niliekuwa

    nimembeba ambaye ni wewe. Sikutaka kuwaeleza mahali ulipokuwa kwani

    nilijua kulikuwa na jambo la hatari”

    “Sasa uliwaambiaje?

    “Walipozidi kunibana nikawaambia mimi nilikushusha nje ya Top Tower

    Hotel ukanilipa pesa yangu nami nikaondoka na baada ya hapo sikufaha?mu ulipoelekea. Niliwaambia vile nikiamini kuwa mpaka wao kunipeleleza

    hadi kunifuata pale nyumbani walikua tayari wamekukosa na kama muda ule

    wangeamua kurudi tena kule Top Tower Hotel niliamini kuwa wasingekuku?ta kwani ulikuwa ukifahamu fika kuwa ulikuwa ukifuatiliwa hivyo niliamini

    kuwa wasingekupata” Maelezo ya Jean yalinifanya nimshangae kwa namna

    alivyokuwa mwelevu.

    “Sasa ikawaje baada ya hapo? nilimuuliza tena na hapo akageuka kunita?zama huku machozi yakimlengalenga tena ingawaje alifanikiwa kuyadhibiti,

    akajifuta machozi kwa kiganja chake na kutazama tena chini na hapo alianza

    tena kusimulia.

    “Hawakutaka kunielewa, wakang’ang’ania tu msimamo wao kuwa lazima

    niwaonesha ulipo huku wakinionya kuwa endapo ningeendelea kushikilia

    msimamo wangu wangenionesha cha mtema kuni. Mimi bado niliendelea ku?shikilia msimamo wangu wa kuwa sijui mahali ulipokuwa na kuwa mawasilia?no yangu na wewe yalimalizika pale nilipokushusha nje ya Top Tower Hotel na baada ya hapo sikujua ulipoelekea. Walipoona kuwa naendelea na msimamo

    wangu hawakutaka tena kunilazimisha, wakawashika mke wangu na mtoto”

    kufikia hapa Jean alianza tena kulia, nikamwambia ajikaze kiume huku tarati?bu nikimpigapiga tena mgongoni.

    “Nini kilichoendelea niambie Jean?

    “Walimuua mtoto wangu kwa kumfyatulia risasi mbele ya macho yangu

    mimi nikiwa siwezi kutoa msaada wowote kwani nilikuwa nimepigwa sana

    kiasi cha kushindwa kusimama”

    “Pole sana Jean” nilimfariji huku nami nikitokwa na machoni kwa huzuni,

    Jean akafuta machozi na kuendelea

    “Mke wangu walimbaka palepale sebuleni kwenye kochi na walipomaliza

    wakamuua kwa risasi. Nilishindwa kuvumilia na nafikiri nilipoteza fahamu

    kwani baada ya pale sikuona kilichoendelea na nilipozinduka nilijikuta ndani

    ya pango hili na mpaka sasa sijui hatima yangu” Jean alimaliza kunisimulia

    huku akigeuka kunitazama nikajua alikuwa akisubiri na mimi nimsimulie

    mkasa wangu. Nikamtazama huku nikamuonea huruma kwa namna alivyo?jitolea kupoteza mke na mtoto wake ili ayaokoe maisha yangu. Kwa kweli

    sikuwahi kuona upendo wa namna ile na sijui ningemlipa nini kama sehemu

    ya shukrani yangu.

    Nilimsubiri atulie na hapo nikaanza kumsimulia mkasa wangu huku ni?kiamua kumueleza wazi kuwa mimi sikuwa nikiitwa Patrick Zambi kama

    nilivyojitambulisha kwake hapo awali. Bali mimi nilikuwa mwanajeshi ko?mandoo na mpelelezi kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania na nilikuwa na

    cheo cha Luteni na jina langu halisi lilikuwa Venus Jaka na nilikuwa nime?kuja pale Kigali Rwanda kuchunguza juu ya kifo cha mwandishi wa habari

    wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda na vilevile mwandishi wa habari wa

    gazeti la Afrika mashariki aitwae Tobias Moyo aliyeuwawa katika mazingira

    ya kutatanisha.

    Nimlimsihi asimueleze mtu yeyote mwingine kuwa mimi ni nani ili kama

    ingetokea mimi ningekufa mle ndani na yeye akabahatika kuachiwa huru au

    kutoroka aende akatoe taarifa kwenye ofisi za ubalozi wangu ijapokuwa ni?likuwa nikikiuka maadili ya kazi yangu kwa kumueleza kuwa mimi ni nani.

    Hata hivyo sikuona sababu ya kumficha kwa kuzingatia kuwa sikuwa na tu?maini lolote la kutoka salama mle ndani istoshe alikwishapoteza mke na mtoto

    wake ili kuyaokoa maisha yangu.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Vilevile niliwaza kuwa kama nisingepata muujiza wa kutoroka mle pangoni

    nilifahamu fika kuwa adhabu iliyokuwa ikinisubiri ilikuwa ni kifo tu kwani

    Kanali Bosco Rutaganda alikuwa tayari amenifahamisha kuhusu hilo. Hivyo

    kwa kuzingatia haya yote sikuona kama nilikuwa nikifanya makosa kumuele?za Jean Pierre Umugwaneza kuwa mimi ni nani. Nikampa namba yangu ya

    simu na anwani ya posta ya mtu ambaye angewasiliana nae aliyeko nchini

    Tanzania na kumjulisha yaliyonikuta endapo mimi ningeuwawa na yeye Jean

    kufanikiwa kutoka salama mle pangoni.

    Baada ya hapo nilianza kumueleza Jean mambo yalivyokuwa mpaka mimi kufikishwa mle pangoni. Jean alistaajabu sana akabaki akinitazama kwa

    mshangao, mshangao wa kukutana na komandoo mzoefu kwenye uwanja wa

    mapambano ndani ya pango lile nikiwa mbali kabisa na ule mwonekano wan?gu wa awali wa suti ya ghali aina ya Kenzo, kofia yangu nadhifu aina ya pama,

    saa ya dhahabu mkononi aina ya Alpha GMT-Dead Ringer, sunduku langu

    mkononi na yale marashi yangu ya gharama niliyojipulizia yenye harufu nzuri,

    thamani yake ikilingana na mshahara mmoja wa kima cha chini wa mfanya?kazi wa serikali, huku nikijibatiza kwa jina la Patrick Zambi, mwandishi wa

    habari wa kujitegemea.

    “Loh! kweli sikudhani kabisa kuwa wewe ni mwanajeshi tena komandoo”

    Jean aliniambia mara tu nilipomaliza kumsimulia mkasa wangu nikabaki ni?kitabasamu tu huku akili yangu ikiwa mbioni kuanza kufanya kazi nyingine.

    Kazi ya kuanza kufikiri namna ya kutoroka mle pangoni ingawaje sikuona

    matumaini yoyote kwani mlango wa pango lile ulikuwa wa chuma nao uliku?wa ikifungwa kwa nje na zaidi ya hapo hapakuwa na dirisha lolote isipokuwa

    uwazi mdogo uliokuwa chini ya mlango ule ambao ulitumika kupitisha hewa

    kidogo iliyotuwezesha kuishi mle ndani.

    Niliyazungusha macho yangu kukipeleleza vizuri kile chumba kidogo cha

    pango na hapo nikajikuta nikipoteza tumaini la kutoka mle ndani salama. Nil?igeuka kumtazama Jean nikamuona kuwa alikuwa amezama katika simanzi na

    hapo nikajua kuwa alikuwa akiiwaza familia yake kisha nikaanza kumtazama

    kila mtu aliyekuwa mle ndani. Wanawake waliyakwepesha macho yao pale

    nilipowatazama, bila shaka waliona aibu namna walivyokuwa uchi bila nguo

    yoyote ya kujisitiri. Hasira zilinishika huku nikiulaani uvunjifu huu mkubwa

    na udhalilishaji wa haki za binadamu.

    “Hapa ni wapi? niligeuka na kumuuliza Jean aliyekuwa ameegemea ukuta

    pembeni yangu.

    “Sipajui wala sijawahi kufika ila nafahamu kuwa bado tupo Rwanda na si

    nchi yoyote ya jirani”

    “Unaweza kufahamu huu ni muda wa saa ngapi?

    “Nani anaefahamu? pango lote hili ni giza si mchana si usiku kweli hii ni

    sehemu hatari”

    “Wale askari huwa wanabadilishana zamu kuja humu ndani? nilimuuliza

    Jean huku nikimtazama

    “Siwezi kujua, kama nilivyokueleza kuwa mimi fahamu ziliponirudia nili?jikuta nipo humu ndani nikiwa sifahamu nimefikajefikaje” Jean alinijibu na

    wakati huo nilimuona kijana mmoja aliekuwa jirani yetu akijisogeza pale tu?lipokaa huku akionekana kutaka kujiunga na maongezi yetu. Jean akazung?umzanae kwa lugha ya kinyarwanda ambayo mimi nilikuwa siifahamu kabisa

    kisha nilimuona yule kijana akigeuka kunitazama na hapo nikasikia Jean aki?niambia.

    “Muulize huyu anasema anayafahamu vizuri mapango haya” nikageuka

    kumtazama vizuri yule kijana na hata kabla sijamsemesha akafungua mao?ngezi

    “Habari yako” alinisalimia huku akinipa mkono na hapo nikajua kuwa Jean alikuwa amemwambia kuwa mimi ni mtanzania na nilikuwa siifahamu lugha

    ya kinyarwanda.

    “Nzuri” nilimjibu na kushikana nae mkono.

    “Nimeambiwa na huyu bwana kuwa wewe ni Mtanzania”

    “Ndiyo, nimekuja hapa Rwanda kikazi bahati mbaya nimejikuta humu”

    “Pole sana, mimi nimewahi kukaa Dar es Salaam”

    “Dar es Salaam! ulikuwa ukifanya nini? nilimuuliza huku nikimtazama

    “Nimesoma chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati nilipokuwa nikichukua

    shahada yangu ya pili ya Akiolojia na wakati nikisoma nilikuwa nimepanga

    chumba eneo la Kijitonyama” yule kijana aliniambia na hapo tumaini dogo

    lilifufuka moyoni mwangu. Kusikia kijana yule alikuwa amesomea Akiolo?jia yaani taaluma ya mambo ya kale na ugunduzi wa vitu kama mapango na

    utamaduni na hapo nikajua kuwa kwa vyovyote angeweza kuwa na msaada

    kwangu.

    “Mimi naishi Tegeta ndipo nilipojenga”

    “Umeoa? yule kijana aliniuliza huku nikishindwa kuelewa dhamuni la swali

    lake

    “Sijaoa ila naishi na mwanamke nimezaanae mtoto mmoja” nilimdanganya

    “Hongera na afadhali yako wewe umeoa na una mtoto mimi ndiyo nilikuwa

    nikijiandaa kufunga ndoa ndiyo haya yakanikuta sasa siitamani tena hiyo ndoa

    na endapo nikifanikiwa kutoka nikiwa hai humu ndani nitaitoroka hii nchi”

    “Kwa nini? nilimuuliza

    “Hakuna haki!, mimi ni mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti la hapa

    Rwanda liitwalo République ukweli wangu ndiyo ulioniponza na sasa nipo

    humu pangoni nasubiri kifo tu” kijana yule aliongea kwa majuto na nilipomta?zama nikauona uso wake namna ulivyokata tamaa

    “Jina lako nani? nilimuuliza

    “Jérome Muganza”

    “Unaweza kufahamu hapo tulipo ni wapi?

    “Napafahamu, nimefanya kazi miaka minne ndani ya mapango haya kama

    mtunzaji mkuu hifadhi ya mapango yote ya hapa nchini Rwanda na vivutio

    vingine vya kale kabla ya kuacha kazi hiyo na kujiunga na gezeti la Répub?lique nikiwa kama mwandishi wa habari na mhariri mkuu. Haya ni mapan?go ya Musanze yapo jimbo la kaskazini mwa nchi ya Rwanda ama Northern

    Province” Jérome Muganza aliniambia na maelezo yake yakanifanya nigeuke

    na kuketi vizuri nikimsikiliza.

    “Kwa hiyo hapa tupo Northern Province?

    “Bila shaka hata hivyo si mbali sana na jiji la Kigali”

    “Mapango haya yapoje?

    “Una maana gani? aliniuliza

    “Yaani namna yalivyo, njia zake, ukubwa wa eneo lake na endapo kuna

    makazi yoyote ya watu eneo la jirani”

    “Oh! sasa nimekuelewa, haya ni mapango yanayotokana na miamba mikub?wa ya kivolkano iitwayo Cenozoic, mfano kuna mwamba wa Manjari wenye

    urefu wa zaidi ya mita moja na nusu na mwingine uitwao Nyiraghina wenye urefu wa mita moja.

    Jumla ya mapango yaliyogunduliwa eneo hili yapo hamsini na mbili na

    yenye jumla ya njia zenye urefu wa kilometa kumi na tano. Lakini hili bila

    shaka ni pango la Musanze, urefu wake ni kilometa mbili kwa njia zake za

    chini. Njia hizo zimepita juu ya matabaka ya uji wa volkano ulioganda kwa

    zaidi ya miaka sitini iliyopita. Matabaka hayo sasa yametengeneza bonde kub?wa mbele ya mapango haya liitwalo Albertine Rift Valley. Mapango haya yana

    njia za kuingilia zipatazo thelathini na moja lakini mengine sehemu zake juu

    zimemong’onyoka, haya ni mapango marefu zaidi kwa hapa Rwanda na yana?patikana popo wakubwa wenye midomo mirefu na wakali na nyoka wakubwa

    aina ya chatu.

    Bado watafiti wanaendelea kuyachunguza vizuri mapango haya ili kuyain?giza kwenye vivutio rasmi vya utalii vya hapa Rwanda.

    “Kuna makazi yoyote ya watu karibu na mapango haya? nilimuuliza

    “Yapo, kiasi cha urefu wa maili zaidi ya kumi mashariki mwa mapango

    haya” Jérome Muganza aliniambia na hapo nikajikuta nikianza kuwawaza

    chatu na hao popo wakali waliosemekana kuwapo ndani ya mapango haya.

    Nilimtazama Je’rome Muganza huku nikifarijika kwa maelezo yake.

    “Umesema ulikuwa ukifanya kazi kwenye gazeti la République la hapa

    Rwanda kama mhariri na ukaniambia kuwa ukweli wako ndiyo uliokuponza,

    ni ukweli gani huo? nilimuuliza huku nikimtazama.

    “Ndiyo, hata sasa hiyo ndiyo kazi yangu na hilo gazeti la République mmi?liki wake ni mimi. Baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu kidogo mimi

    nikiwa kama mtunzaji wa mwangalizi mkuu wa hifadhi za mapango yote ya

    hapa Rwanda hatimaye niliomba kustaafu mapema kabla ya umri wangu.

    Nilipolipwa mafao yangu nikaamua kuanzisha hilo gazeti lengo lake kubwa

    likiwa ni kuionya serikali juu ya hali tete ya amani katika nchi hii na hali ya

    kisiasa ilivyo kwa ujumla. Naweza kusema nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa

    kwani gazeti hilo liliondokea kupendwa sana hapa nchini na hata mauzo yake

    yalikuwa ya kuridhisha na hii ilitokana na gazeti langu kujikita zaidi katika

    kuzungumzia ukweli juu ya mambo yanayoisibu nchi hii”

    “Unaweza kuniambia kuwa ni sababu gani hasa iliyopelekea wewe kuka?matwa na kuletwa humu ndani? nilimuuliza

    “Ni kutokana na ukweli wa gazeti langu, nahisi nilikuwa nikiyagusa maslahi

    ya baadhi ya viongozi wakubwa wa kisiasa wa hapa nchini. Kabla ya kuka?matwa niliwahi kupewa vitisho vya hapa na pale juu ya kugusa maslahi ya vi?ongozi hao, nilitoa taarifa kwenye vyombo vya usalama lakini sikuona juhudi

    zozote za vyombo hivyo vya usalama katika kuzifanyia kazi taarifa zangu”

    “Umesema habari zako zilikuwa zikigusa maslahi ya baadhi ya viongozi,

    kwa vipi?

    “Wiki mbili zilizopita nilichapisha habari iliyokuwa ikieleza juu ya matukio

    ya mauji ya chini chini yaliyokuwa yakiendelea sehemu mbalimbali hapa

    nchini. Katika habari hiyo niliandika juu ya majina ya washukiwa wakuu wa

    mauaji hayo huku nikiishauri serikali iingilie kati hali hiyo kwani maisha ya

    watu wasio na hatia yalikuwa yakipotea kila kukicha. Habari ile ilipokelewa vizuri na wasomaji wengi hasa kwa kuwa ilikuwa

    ikiongelea hali halisi ya hapa nchini hata hivyo siyo wote ambao walifura?hia ukweli ule kwani siku mbili tu baada ya kuchapisha habari ile nilianza

    kupokea vitisho kutoka kwa watu nisiowajua. Nikatoa taarifa kwenye vyombo

    vya usalama juu ya vitisho hivyo ila sikupata msaada wowote kwani ni kama

    taarifa zangu ziliishia kwenye mafaili yao.

    Ilikuwa ni baada ya muda wa siku nne kupita tangu nilipochapisha habari

    zile gazetini ndiyo nilipokutana na mkasa huu ulionifikisha humu ndani nikiwa

    sina fahamu” Jérome Muganza aliweka kituo kidogo akimeza funda la mate

    nami nikavuta pumzi kubwa na kuishusha taratibu kisha nikageuka pembeni

    yangu kumtazama Jean Pierre Umugwaneza ambaye nae alikuwa akiyasikiliza

    kwa makini maongezi yale halafu nikarudia tena kumtazama Jérome Mugan?za na hapo akaendelea

    “Ndiyo nakumbuka kuwa ilikuwa imetimia saa tano na nusu usiku na niliku?wa ni mtu wa mwisho kufunga ofisi yangu iliyopo Masaka Avenue katikati ya

    jiji la Kigali ambako nilikuwa nimemaliza kuhariri habari ambazo zingetoka

    kwenye gazeti la asubuhi inayofuata. Baada ya kumaliza kuhariri nilizipele?ka habari zile chumba cha pili tayari kuchapishwa na mara baada ya kutoka

    na kufunga ofisi ile nilihisi uchovu mwilini hivyo sikuona sababu ya kuanza

    mizunguko mingine, nikaamua kuwasha gari langu na kuelekea nyumbani ku?pumzika.

    Wakati nilipokuwa njiani kuelekea nyumbani ndipo nilipopigiwa simu na

    mtu nisiyemfahamu akiniambia kuwa kulikuwa na tukio la mauaji lililokuwa

    limetokea muda ule kwenye jengo moja la shirika la nyumba la hapa Rwanda

    lililokuwa katikati ya jiji la Kigali. Nilikuwa nimechoka mno kwa wakati ule

    na sikupenda kujishughulisha na kitu chochote zaidi ya kwenda kupumzika la?kini nilijikuta nikihisi habari zile huenda zingekuwa na umuhimu wake kama

    ningeweza kuziwahi na kuzitoa kwenye gazeti la asubuhi ya siku iliyofuata

    hivyo hatimaye niliamua kubadilisha uelekeo na kuelekea mjini ilipo nyumba

    ile.

    Sikufika mbali sana wakati nilipogundua kuwa nyuma yangu kulikuwa na

    gari fulani lililokuwa likinifuatilia, nilishikwa na wasiwasi sana nikaamua

    kupiga simu polisi lakini simu ile iliita muda mrefu bila kupokelewa na ili?popokelewa hakuna aliyenipa msaada. Lile gari nyuma yangu lilinifikia na

    kunisimamisha kwa mbele, nakumbuka walishuka watu sita kwenye gari lile

    wakiwa na mapanga mikononi. Wakanishusha kwenye gari langu na kuanza

    kunipiga bila ya kuniambia chochote, nilisikia maumivu makali sana nikawasi?hi waniache lakini hakuna aliyenisikiliza. Maumivu ya kipigo kile yalikuwa

    makali mno hivyo nikapoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nipo ndani

    ya pango hili” J’erome Muganza alimalizia simulizi lile fupi huku akionesha

    kusikitika sana.

    “Pole sana” nilimtia moyo

    “Ahsante”

    “Sasa nini hatima yetu humu ndani? Jean aliuliza huku akionekana mwenye

    hofu.

    “Watatuua tu, mmoja baada ya mwingine na inavyosemekana ni kuwa sisi si

    watu wa kwanza kufichwa ndani ya mapango haya. Nilikuja kufahamu kuwa

    wapigania haki wengi wa nchi hii waliokuwa wakipotea katika mazingira ya

    kutatanisha walikuwa wakitekwa na kuletwa hapa kabla ya baadaye kuuwawa

    na taarifa zao kupotelea kusikojulikana” Jérome Muganza alikuwa akiongea

    huku akionekana kuwa ni mwenye hakika na maelezo yake.

    Sote tulibaki tukimtazama Jérome Muganza huku kila mmoja akitafakari

    lake moyoni. Nilifahamu sasakuwa nilikuwa nimetumbukia kwenye shimo la

    kifo na kujinasua kwake isingekuwa kazi rahisi. Niliyazungusha macho yangu

    kulitazama tena lile pango ambalo sasa lilionekana kama kaburi la kuzikia

    watu hai na sikuona tumaini lolote la kutoka mle ndani nikiwa hai na hapo

    nikayarudisha macho yangu kumtazama tena Jérome Muganza.

    “Sasa tumewekwa humu ndani nini hatima yetu? niliuliza katika namna ya

    kukata tamaa.

    “Huwa wanakuja kumchukua mtu mmoja baada ya mwingine wakidai wa?naenda kufanya nae mahojiano lakini pindi mtu huyo anapochukuliwa hatu?muoni akirudi tena na hicho ndiyo kitu kinachonifanya niamini kuwa watu hao

    huwa wanaenda kuuwawa” Jérome aliendelea kutueleza.

    “Ulituambia kuwa wapigania haki za binadamu wengi katika nchi hii wali?osemekana kupotea katika mazingira ya kutatanisha ulikuja kugundua kuwa

    walikuwa wakitekwa na kuletwa humu kabla ya baadaye kuuwawa, umejuaje?

    nilimuuliza.

    “Ni kupitia uchunguzi nilioufanya ndani ya pango hili mara tu baada ya

    kujikuta nipo humu ndani”

    “Uchunguzi upi huo? Jean aliuliza na hapo nilimuona Jérome Muganza aki?geuka kutazama sehemu fulani ya ukutani mle pangoni. Wote tukawa tume?geuka kutazama kule alipokuwa akitazama Jérome Muganza

    “Pale kuna majina ya watu ninaowafahamu ambao hapo siku za nyuma wal?itoweka katika mazingira ya kutatanisha na hakuna aliyekuwa akifahamu taar?ifa zao. Nilikuja kufahamu kuwa watu hao walitekwa na kuletwa humu baada

    ya kukuta majina yao yameandikwa ndani ya pango hili na nina kila hakika ni

    wao wenyewe ndiyo walioandika majina yale”

    Huku tukiwa tumeshikwa na mshangao wote tuligeuka vizuri na kuanza

    kutazama kwa makini pale ukutani na hapo tukayaona majina mbalimbali

    ya watu yakiwa yameandikwa pale ukutani. J’erome Muganza alituonesha

    baadhi ya majina ya watu aliokuwa akiwafahamu na hata wengine ambao wa?liwahi kuwa marafiki zake wa karibu. Miongoni mwa majina yale lilikuwepo

    jina la Théoneste Egide ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la haki

    za binadamu duniani yaani Human Right Watch nchini Rwanda na alikuwa

    ametoweka katika mazingira ya kutatanisha sana zaidi ya miaka mitatu iliyo?pita wakati alipokuwa akiingoza tume ya kuchunguza vifo vya watu ishirini

    na moja waliouwawa kwa kukatwa mapanga katika eneo moja nchini Rwanda

    liitwalo Nyarugenge.

    Miongoni mwa majina yale pia lilikuwepo jina la mama Magdeline Muka?sano aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanawake cha nchini Rwanda ambaye nae pia ilisadikika kuwa alikuwa ametoweka mi?aka miwili iliyopita wakati usiku mmoja alipokuwa akirudi nyumbnai kutoka

    ofisini kwake na baadaye gari lake lilikutwa eneo fulani porini likiwa lime?telekezwa na baadhi ya matundu ya risasi yaligundulika katika mlango mmoja

    wa gari hilo.

    Nilimuuliza Jérome Muganza kuwa ni sababu gani aliyokuwa akiidhani

    kuwa pengine ilikuwa imepelekea kutekwa na kuuwawa kwa mama Magde?line Mukasano naye akaniambia kuwa kifo chake kilitokana na harakati zake

    za kupigania haki na kutetea wanyonge kwa njia ya uhandishi wa habari kama

    yeye, na pia katika maelezo yake Jérome Muganza alitueleza kuwa mama

    Magdeline Mukasano alikuwa na urafiki sana na jaji mmoja maarufu nchini

    Rwanda aliyekuwa akijulikana kwa jina la Jaji Makesa ambaye naye alitowe?ka muda mfupi baada ya kupotea kwa mama Magdaline Mukasano.

    Jérome aliendelea kutueleza kuwa alikuwa ametarajia pia kuliona jina la Jaji

    Makesa katika orodha ile ya majina yaliyoandikwa katika ukuta ule wa pango

    lile kwa kuwa alikuwa akiamini kuwa hata jaji Makesa nae alikuwa ametweka

    lakini alishangaa sana kuona katika orodha ile ya majina jina la Jaji Makesa

    halikuwepo.

    Mimi na Jean Pierre Umugwaneza tulikuwa kama tulioshikwa na bumbu?wazi wakati tulipokuwa tukiyasikiliza maelezo ya Jérome Muganza mle pan?goni. Kila mtu akajikuta amezama katika fikra fulani juu ya maelezo yale hata

    hivyo nilipomtazama Jean niligundua namna alivyokuwa na hofu na hata uso

    wake ulijieleza.

    Nilijihisi kuanza kuyazoea mazingira ya mle ndani ingawaje hata mimi

    nilikuwa na wasiwasi mwingi juu ya hatima ya maisha yangu na wale watu

    waliokuwa mle ndani. Nikayahamishia tena macho yangu kuyasoma yale ma?jina yaliyokuwa yameandikwa kwenye ule ukuta wa pango. Yalikuwa ni zaidi

    ya majina ya watu thelatini na baadhi ya majina yale yalikuwa ni ya watu

    mashuhuri sana niliowahi kuwasikia wa nchini Rwanda. Majina mengine ha?yakuwa na maana sana kwangu hata hivyo majina yote niliyapa heshima kwa

    kufa kishujaa katika harakati za kutetea haki za binaadamu na usawa na vile?vile kuwasaidia wanyonge sambamba na kuwakosoa baadhi ya viongozi wa

    serikali.

    Nikiwa naamini sasa kuwa yule majina ya watu yaliyoandikwa mle pangoni

    sasa watu hao walikuwa marehemu nikajikuta na mimi nikipata hisia za kuan?dika jina langu na kuwashawishi wengine kujiandika katika orodha ile huku

    nikiamini kuwa hata kama watu wote tungekufa mle ndani ipo siku moja dunia

    ingekuja kuufahamu kweli wa mambo kupitia orodha ya majina yetu.

    Kwa kweli lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwa namna majina yale

    yalivyokuwa yameandikwa kwa kuchongwa kiustadi katika ukuta wa mwam?ba mgumu wa pango lile. Nikajikuta nikiwaza kuwa bila ya shaka ilimchukua

    mtu mmoja kwa zaidi ya siku mbili hadi kufanikiwa kuandika jina lake katika

    ukuta ule kwa kutumia kipande cha ncha kali ya jiwe lililochongoka. Nilimta?zama Jérome Muganza na kumuona kuwa alikuwa ni mtu msomi na mwelevu

    sana hadi kuweza kupeleleza na kugundua orodha ile ya majina yaliyoandikwa mle ukutani. Kwa kweli nilipoyatazama yale majina nilijisikia faraja sana

    kuwa hatukuwa peke yetu kwani japokuwa watu wale walikwishakufa lakini

    nilikuwa ni kama ninaewaona huku nyuso zao zikiwa zimejawa na tumaini la

    kufa kishujaa. Nikiwa naendelea kuiwaza hali ile nikaanza kuhisi kuwa mbegu

    ya ujasiri ilikuwa ikianza kuchipua taratibu moyoni mwangu huku nikijiapia

    kuwa kabla ya kifo changu ingefaa na mimi kufanya kitendo tofauti cha ujasiri

    ili nife nikiwa na amani moyoni.

    Bila shaka muda ulikuwa umesonga sana ingawaje sikuweza kufahamu

    wakati ule ulikuwa ni muda wa saa ngapi kutokana na giza zito lililokuwa

    limetanda mle pangoni. Niligeuka kumtazama Jérome Muganza pembeni

    yangu nikagundua kuwa alikuwa ameanza kusinzia ingawaje nilimuona kuwa

    alikuwa akijitahidi sana kupambana na hali ile ya usingizi. Nikageuka kumta?zama Jean Pierre Umugwaneza ambaye naye alikuwa ameketi pembeni yangu

    na hapo nikagundua kuwa japokuwa nae alionekana kunitazama lakini macho

    yake hayakuonesha mjongeo wa namna yoyote.

    Alikuwa ameachama mdomo wazi na sauti hafifu ya mkoromo wa uchovu

    ilikuwa ikipenya kinywani mwake. Kichwa chake kiliegemea bega lake upa?nde wa kushoto huku yeye mwenyewe akiwa ameegemea ule ukuta wa pango.

    Sikutaka kuendelea kuwasemesha nikawaacha waendelee kupumzika na hapo

    nikayazungusha tena macho yangu kutazama mle pangoni, nikagundua kuwa

    watu wote mle ndani walikuwa wamelala.

    Baadhi ya wanawake walikuwa wamelala pale sakafuni pasipo kuonesha ji?tihada zozote za kuficha tupu zao, baadhi yao walikuwa na majeraha makubwa

    katika sehemu zao za matiti, migongoni, tumboni na kwenye makalio. Roho

    iliniuma sana nilipoyatazama majeraha yao na kuanza kuvuta picha juu ya

    mateso waliopitia kabla ya kuletwa mle pangoni.

    Wote walikuwa wamejilaza sakafuni kila mmoja akiwa amelala katika

    namna yake aliyodhani ingemfaa bila ya kujali mbu wakali waliokuwa mle

    pangoni. Wengi walikuwa ni wanawake warefu wenye maumbo na sura nzuri

    za kuyavutia macho ya mwanaume yoyote kuwatazama, na kutokana na mu?onekano wao sikuwa na shaka kuwa wengi wao walitoka katika mazingira ya

    ukwasi kama siyo kwenye kazi zenye vipato vya kuridhisha.

    Niliwatazama wote mmoja baada ya mwingine kwa zamu huku nikiwaza

    hatima yangu mle pangoni na wakati nilipokuwa nikiendelea na zoezi hilo

    ghafla nilijikuta nikitazamana na msichana mmoja mrembo aliyekuwa ame?jikunyata katikati ya kundi lile la wanawake waliolala pale chini sakafuni.

    Macho yangu yalipogongana na macho ya msichana yule nikagundua kuwa

    hata yeye alikuwa akinitaza kwa muda mrefu. Niligundua pia kuwa yeye ndiye

    aliyekuwa mwanamke pekee aliyekuwa bado hajalala mle pangoni hadi waka?ti huu. Nilishangaa kumuona msichana yule akitabasamu usoni pindi macho

    yetu yalipogongana na japokuwa tabasamu lake lilichanua vizuri usoni lakini

    niligundua kuwa tabasamu lile halikufanikiwa kuitowesha sura yake ya hofu

    na mashaka iliyokuwa nyuma ya tabasamu lile.

    Sura ya mashaka yenye alama za mifereji ya machozi yaliyokauka baada ya

    kulia kwa muda mrefu bila matumaini. Nilibaki nikimtazama msichana yule mrembo kwa muda mrefu huku nikiwa nimepumbazika kwa uzuri wake na

    hapo nikajikuta nikizisahau kwa muda shida zote za mle pangoni. Msichana

    yule alikuwa mzuri sana, mrefu na mweusi mwenye nywele nyeusi na laini

    ingawaje nywele hizo zilikuwa zimesukwa mabutu.

    Alikuwa ameketi chini kwenye sakafu ya pango lile huku ameikunja miguu

    yake kifuani katika mtindo wa kujikunyata, mikono yake alikuwa ameigemeza

    juu ya magoti yake. Nilipomchunguza niligundua kuwa alikuwa ameishiwa

    nguvu kwa kulia muda mrefu.

    “Kwanini hulali mrembo? nilimuuliza huku nikiendelea kulimudu tabasamu

    langu. Hakunijibu kitu badala yake alitikisa kichwa chake upande huu na ule

    kuonesha kukataa kisha aliinama chini na hapo nikayaona machozi yakianza

    safari ya kushuka kwenye mashavu yake. Huzuni ilinishika moyoni wakati

    nilipokuwa nikiendelea kumtazama nami nikajikuta nikipambana kuyazuia

    machozi yasinitoke.

    “Jina lako nani? nilijikaza nikamuuliza tena na hapo akanyanyua macho

    yake kunitazama, tulitazamana tena huku nikipumbazika kwa uzuri wake.

    “Ikirezi” hatimaye alinijibu kwa upole

    “Ikirezi!” nilirudia kulitamka jina lake “Lina maana gani jina lako?

    “Sifahamu mimi nilipewa tu na wazazi wangu”

    “Una muda gani tangu uletwe humu ndani ya pango hili?

    “Wiki moja na siku mbili”

    “Pole sana” nilimfariji kwa sauti ya upole na hapo akatikisa kichwa akio?nesha kuikubali pole yangu pasipo kuzungumza kisha ukimya kidogo ukapita

    kabla hajaniuliza

    “Unaitwa nani?

    “Naitwa Patrick Zambi, mimi ni Mtanzania”

    “Mtanzania? alionesha mshangao kidogo “Imekuwaje ukaletwa humu

    ndani?

    “Ni kama wewe tu bila shaka hukupenda kuwepo humu ndani ila imetokea

    tu na ukajikuta umeletwa humu ndani” niliongea huku nikimtazama.

    “Una ndugu yako yoyote anaefahamu kuwa wewe upo humu ndani? alini?uliza

    “Hapana, sikupata nafasi ya kumueleza yoyote kwani kutekwa kwangu ku?likuwa ni kwa ghafla sana”

    Ikirezi alinitazama kwa kitambo kifupi kama mtu anayetafakari jambo fu?lani kisha akavunja ukimya

    “Unadhani kuna uwezekano wowote wa kutoroka ndani ya pango hili?

    “Mh! bado sioni tumaini lolote kwa sasa labda itokee miujiza” nilimwambia

    Ikirezi huku nikijaribu kuyasoma mawazo yake na hapo nilimuona namna

    alivyokata tamaa kwa ghafla.

    “Kama sitofanikiwa kutoroka humu pangoni ndani ya muda wa wiki moja

    kuanzia sasa nitauwawa” Ikirezi aliniambia huku machozi hafifu yakianza

    tena kumtoka.

    “Nani aliyekuambia kuwa utauwawa? nilimuuliza kwa udadisi.

    “Watakuja kunichukua nikahojiwe kwani zamu yangu imekaribia na najua tu kuwa mara baada ya mahojiano hayo nitauwawa kwa sababu hakuna mtu

    hata mmoja aliyechukuliwa humu ndani kwa mahojiano hayo na baadaye ku?rudishwa. Wote wanaochukuliwa humu ndani huwa hawarudi”

    “Wanataka kukuhoji kuhusu nini na kipi kilichopelekea wewe kuletwa

    humu ndani?

    “Wanataka niwaeleze mahali alipo mume wangu”

    Nilimtazama msichana yule huku nikikilaani sana kitendo hicho cha yeye

    kuolewa na mwanaume mwingine na siyo mimi kwani ukweli ni kwamba

    nilishaanza kumpenda ingawaje mapenzi yetu yasingekuwa na maana yoyote

    ndani ya shimo hili la kifo.

    “Mume wako amefanya nini hadi wamtafute?

    “Kwa kweli mpaka muda huu sifahamu”

    “Mume wako yuko wapi? nilimuuliza na hapo nikamuona namna alivyoni?tazama kwa jicho la hasira.

    “Sifahamu na hata kama ningekuwa nafahamu sehemu alipo nisingekuele?za” akanijibu kwa hasira.

    “Kwanini unasema hivyo huoni kuwa sisi sote humu ndani ni mateka na

    pengine tukasaidiana kwa namna moja au nyingine endapo tukafanikiwa ku?toka humu ndani salama”

    “Lakini si umeniambia kuwa uwezekano wa kutoroka humu ndani ni mdogo

    na labda itokee miujiza sasa ni vipi unipe matumaini hewa?

    “Ni kweli lakini sikusema kwamba miujiza imeisha” nilimwambia na hapo

    nikaona tabasamu hafifu likiumbika usoni mwake.

    “Unadhani kuna uwezekano wa kutoroka humu ndani kabla ya muda wa

    wiki moja haujatimia? aliniuliza

    “Sina hakika ila itategemeana na hali ilivyo”

    “Itategemeana na nini?

    “Hali yenyewe itakavyokuwa mfano namna ya ulinzi ulivyo eneo hili na

    kama hiyo nafasi ya kutoroka itapatikana” nilimwambia huku nikijaribu

    kuyatafakari mawazo yake. Kitambo cha ukimya kilipita huku kila mmoja

    akionekana kutafakari, ukimya huo ulipokuwa mbioni kushika hatamu nikaan?zisha tena maongezi

    “Mume wako anafanya kazi gani? nilimuuliza na hapo akanitazama tena

    kabla ya kunijibu

    “Ni afisa wa jeshi la wananchi wa Rwanda”

    “Ana cheo gani?

    “Meja”

    “Anaitwa meja nani?

    “Meja Faustine Bagasora”

    “Mumeo aliwahi kukueleza juu ya hali yoyote ya kutoelewana na mtu au

    watu fulani hapo kabla?

    “Hakuwahi kunieleza chochote ingawaje hizi siku za karibuni nilimuona

    akiwa ni mwenye wasiwasi na mashaka”

    “Kwa vipi?

    “Alikuwa akirudi usiku wa manane na haikuwa kawaida ya mume wangu”

    Ikirezi aliongea huku akijizuia asitokwe na machozi.

    “Ulipokuwa ukimuuliza alikuwa akisemaje?

    “Hakutaka kunieleza chochote ingawaje nilifahamu kuwa hakuwa katika

    hali ya kawaida”

    “Pole sana” nilimfariji huku nikimtamza “Sasa ilikuwaje mpaka ukaletwa

    humu ndani? nilimuuliza na hapo alinitazama kisha akayapangusa machozi

    na kuendelea

    “Ilikuwa usiku wa saa mbili pale simu ya sebuleni ilipoanza kuita, nili?poipokea simu ile ndiyo nilipogundua kuwa nilikuwa nikiongea na mume

    wangu. Alikuwa ni mtu anaeongea kwa wasiwasi na kwa haraka sana kama

    mtu anayekimbizwa na hatari”

    “Alikuambiaje?

    “Aliniambia kuwa alikuwa kwenye hatari”

    “Hatari gani?

    “Hakuweza kunieleza ni jambo gani badala yake alinitaka nijiandae haraka

    na nichukue vitu vyote muhimu vikiwemo nguo na pesa zote ambazo tuliku?wa tumezihifadhi pale nyumbani na kisha nimchukue mtoto wetu mchanga

    halafu niondoke na gari mpaka mzunguko wa barabara wa katikati ya jiji la

    Kigali ambapo ningemkuta akinisubiri”

    “Alikwambia baada ya hapo mngeenda wapi?

    “Rusumo, mpakani mwa Tanzania na Rwanda na baada ya hapo tungevuka

    mpaka na kuingia nchini Tanzania”

    “Ulimuuliza ni kwa sababu gani alilazimika kufanya vile”

    “Hakutaka kunieleza badala yake alinisisitiza tu kuwa nifanye haraka sana

    kwani kulikuwa na hatari mbele yetu” Ikirezi aliendelea kunielezea na safari

    hii machozi yakimtoka.

    “Pole sana jipe moyo” nilimfariji kisha nikamuacha atulie kabla ya kumu?uliza tena

    “Sasa ilikuwaje?

    “Nilifanya kama alivyoniagiza mume wangu lakini bahati mbaya sikufan?ikiwa”

    “Nini kilitokea?

    Nilikuwa nipo mbioni kumalizia kupanga nguo kwenye sanduku toka

    kwenye kabati lililokuwa chumbani wakati niliposikia mlango wa mbele wa

    nyumba ukigongwa usike ule. Wasiwasi ulinishika sana nikaanza kuhisi hatari

    ikinikaribia nikaacha kupanga nguo huku nikijishauri nimchukue mtoto wan?gu mchanga na kutoroka kupitia mlango wa nyuma wa nyumba hata hivyo

    nilijikuta nikipingana na wazo lile pale nilipofikiria kuwa kama wengekuwa

    wameizunguka ile nyumba wangeweza kunikamata tu”

    “Sasa ulifanyaje?http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Sikuwa na jinsi kwani nilifahamu kuwa kama watu wale wangekuwa na

    nia mbaya wangenikamata tu hivyo nilimchukua mtoto wangu na kumficha

    kabatini, nikamuacha na chupa ya maziwa” Ikirezi akafuta machozi na kuen?delea “Mlango wa mbele wa nyumba ulivunjwa kabla ya mimi sijaufikia na

    hapo nililiona kundi la wanajeshi wakiingia, walipoingia ndani wakaniuliza kama mume wangu alikuwa mle ndani nikawaambia alikuwa bado hajarudi

    kutoka kazini. Wakaniuliza kama mle ndani nilikuwa peke yangu nikawajibu

    ndiyo hata hivyo hawakuniamini wakaanza kufanya upekuzi mle ndani na nin?achoshukuru ni kuwa hawakulifikia lile kabati nililomficha mwanangu”





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog