Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

THE OTHER HALF - 1

 





    IMEANDIKWA NA : THE BOLD



    *********************************************************************************



    Simulizi : The Other Half

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Kwa miaka kadhaa hakuna aliyeamini kuwa itatokea. Hata dalili zote zilipoonyesha kwamba iko karibu kutokea, watu walipuuza na kuendelea na mambo mengine kana kwamba hawauoni uhalisia. Kila mtu akiamini haitotokea.

    Ndio sababu baada ya kutokea, kitu ambacho kilikuwa kimeonyesha dalili ya kutokea miaka mingi, kiliathiri kila mtu na kila nukta ya pembe ya Dunia.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Mwaka 2038: Nachingwea, Lindi



    Ilikuwa tayari inakaribia saa tisa na nusu alasiri, kikosi cha wataalamu wa masuala ya vinasaba, bailojia na mtaalamu mmoja wa akiolojia walikuwa wanajitahidi wamalize zoezi la ukusanyaji sampuli katika Anabelle mpya iliyotokea takribani wiki mbili zilizopita.



    Kama ilivyo katika Anabelle nyinginezo, joto lilikuwa juu kiasi cha sentigredi 30 za selsiasi, kimya kilikuwa ni kikubwa kana kwamba mji wote haukuwa na kiumbe hata kimoja chenye kujongea. Sauti pekee iliyokuwa inasikika ilikuwa ni sauti ya upepe uliokuwa unavuma kwa sauti kama ya mluzi hafifu masikioni na kutimua vumbi lililofunika lami na majengo.



    Majengo yote yalikuwa na muonekano mkuu kuu kana kwamba labda mji huo haujakaliwa na binadamu kwa karne kadhaa, na vumbi lilikuwa limetuama kwenye majengo na hata barabara kiasi kwamba lami ilikuwa haionekani. Vumbi hili lilikuwa jingi kiasi kwamba, ukikanyaga chini kwenye barabara ukiinua mguu unaacha alama ya kiatu chako kwa ufasaha mkubwa kabisa.



    Jambo la ajabu ni kwamba, japokuwa kulikuwa na uchakavu wote huu na vumbi lote hili linalotoa hisia kuwa labda mji umetekelezwa kwa karne nyingi, ukweli ni kwamba mji huu wiki mbili tu zilizopita ilikuwa na wakazi wapatao laki moja unusu na uliitwa Nachingwea kwa miaka yote nyuma.



    Eneo hili la mji wa Nachingwea kwa sasa ulipewa jina la  Anabelle 23 likimaanisha kwamba, eneo hili lilikuwa ni mji wa 23 duniani katika mfululizo wa kuchukuliwa kwa miji katika mazingira yenye utata na aina mpya ya viumbe wasiojulikana na kisha kupotea kwa wakazi wote, yaani population nzima iliyokuwamo kwenye miji hiyo inapotea kusikljulikana.



    Timu hii ya wataalamu ilikuwa imebakiza nusu saa tu kwa siku ya leo kukusanya sampuli kabla ya kufika saa kumi jioni muda ambao wakazi wapya wa Anabelle 23 walikuwa ‘wanaamka’.



    Wataalamu hawa wote walikuwa wamevalia nguo za ‘overall’ rangi nyeupe na usoni wakiwa wamefunika nyuso kwa vizuizi vya gesi (gas mask) kwa tahadhari ya kujikinga na uwezekano wa vimelea hatarishi ndani ya mji huu.



    Timu hii ya watu watano ilikuwa inaundwa na mtaalamu wa vinasaba Shafii Mwaisela kutoka kituo cha Utafiti cha Ifakara (Ifakara Medical Research Institute), Magdalena Odinga mtaalamu wa kemikali ya kibaiolojia (biochemist) kutoka chuo kikuu cha Kenyatta nchini kenya, Goodluck Hokororo mtaalamu wa masuala ya forensic kutoka makao makuu ya jeshi la polisi, mwanamama Dr. Cindy Wheaton mtaalamu wa akiolojia kutoka chuo kikuu cha Stanford nchini Marekani na Salim Kawambwa mchambuzi wa intelejensia za mashambulio ya kibaolojia kutoka Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania.



    Kwa dakika hizi chache zilizokuwa zimebakia walikuwa wanamalizia kwa haraka kuokota vipande vidogo vidogo vya sampuli mbali mbali na kuziweka kwenye vifuko vidogo vya plastiki ili waweze kuvifanyia uchunguzi baadae.



    “Dakika kumi na tano… Muda wa kuondoka.!” Salim Kawambwa afisa wa TISS ambaye ndiye kiongozi wa timu hii akawajulisha wenzake.



    Kabla ya saa kumi kamili walikuwa wanatakiwa wawe walau kilomita kumi na tano kutoka eneo la Anabelle kwa sababu za kiusalama. Japokuwa kwa muda huu kabla ya kutimia saa kumi jioni, mji mzima ulikuwa umezizima kwa ukimya wa kutisha lakini mara tu ikitimia saa kumi, viumbe vilivyouteka na kuubadili mji huu ‘wanaamka’.



    Baada ya Salim kutoa amri hii wote wakaweka sampuli zao kwenye vihifadhi kama brieface na kupanda kwenye gari waliyopaki pembezoni kabisa linapoishia eneo la Anabelle na kuondoka.



    Wakaendesha gari kama mwendo wa kama dakika kumi na mbili hivi mpaka eneo la karibu na msitu wa Namala, takribani kilo mita kumi na tano kutoka Anabelle 23.



    Hapa walikuwa wameweka kambi ya muda ya mahema.

    Pamoja nao mahali hapa kulikuwa na kikosi maalumu cha kijeshi ambacho kiliundwa mahususi na Amiri jeshi mkuu kwa ajili ya zoezi hili. Kikosi hiki kilipewa jina la Team 5C na kilikuwa na wanajeshi kumi na tano wa weledi wa hali ya juu.



    Baada ya kufika na wote kubadili nguo za kazi na kuvaa nguo za kawaida, wataalamu wote watano wakakusanyika kwenye hema la Salim, afisa kutoka Usalama Wa Taifa.



    “Kuna yeyote ana la kitushirikisha wengine?” Salim akafungua maongezi baada ya wote kuketi.



    “Vile tungekuwa labda tunajua nini tunatafuta.. Labda ningekuwa na cha kuongea.. Lakini tumekuwa hapa kwa siku mbili na sijui nini au niangalie wapi.. Niko nafuata maelekezo tu.!” Magdalena Odinga akaongea kwa lafudhi yake ya kikenya.



    “Naunga mkono hoja.!” Goodluck na Shafii wakajikuta wameongea kwa pamoja.



    Salim akageuka kumuangalia Dr. Cindy Wheaton..



    “Cindy.. Sote hapa tunafahamu kuhusu matukio yanayoendelea duniani kote kuhusu wakazi wa miji mbali mbali, population nzima kupotea katika mazingira ya kutatanisha… lakini lazima ufahamu kuwa baada ya tukio hili kutokea, nchi yetu imeunda hii timu kwa dharura, kwahiyo wengi hapa hawafahamu kiundani kuhusu hili suala.. Kwa faida ya wenzangu labda ungetupa maelezo ya kina ambacho wenzetu mmekifahamu mpaka sasa.!” Salim akaongea huku anamtazama Dr. Cindy Wheaton.



    “Nadhani tulikubaliana kuchukua sampuli tu na tukirudi makao makuu ndio tupeane maelezo.!” Cindy akajibu akiwa ameshangaa kidogo.



    “Cindy tumebakiza siku moja tu ya kesho.. Huwezi jua kama ukitupatia mwanga walau kidogo inaweza kusaidia vipi kwenye kukusanya sampuli kesho.!”Magdalena akadakia haraka haraka.



    ” Tupe japo kwa muhtasari tu.. Nini kinaendelea?? Hili suala limefikia vipi hapa?” Salim akaendelea kusisitiza.



    Cindy akavuta pumzi ndefu ndani na kushusha…



    “OK..!” Akaongea huku anainuka.



    Baada ya kuinuka, akageza laptop yake kuelekea upande mmoja wa hema na kuwasha projector kisha akaanza kuongea.



    “Chanzo cha haya yote kinatupeleka kwenye nchi ya Maldives mwezi May mwaka……”



    “Oohh sorry nadhani wote tunajua hiyo stori, unaweza kutueleza vitu vya kitaalamu ambavyo hatuvijui maana hilo ndilo swali letu.?” Magdalena akamkatisha Dr. Cindy kabla hajamaliza alichokuwa anakiongea.



    “Magdalena tafadhali kuwa mtulivu.. Acha Cindy aongee” Salim akaongea kwa busara na utulivu kutuliza mukali zilizoanza kuinuka.



    Dr. Cindy akamkata Magdalena jicho la hasira na kukereka, kisha akaendelea tena kuongea huku akitumia picha kwenye projector zilizokuwa zinarushwa kwenye ‘ukuta’ wa hema.



    “OK! Nilikuwa nasema kwamba chanzo kabisa cha hizi Anabelle kinatupeleka mpaka kwenye nchi ya Maldives mwaka juzi mwezi May.. Kwa kuwa mnasema mnafahamu historia hii kwahiyo sitazama ndani sana nitaenda moja kwa moja kwenye masuala ya kitaalamu..” Akanyamaza kidogo na kuwaangalia.



    “Eleza kila kitu tafadhali.. Tunaweza kupata kitu kingine kipya.!” Salim akaongea tena kwa hekima.



    “OK asante! Mwezi May mwaka juzi 2037, nchi Maldives.. Kama ambavyo wote tunafahamu kuwa Maldives ni kanchi kadogo kenye visiwa vidogo vidogo vipatavyo elfu moja mia moja tisini na mbili katika bahari ya Hindi kusini mwa bara la Asia.. Mwaka juzi 2037 mwezi huo May, wavuvi wawili alfajiri wakiwa kwenye shughuli zao wakiwa wanatoa nyavu walizotega, wakakuta samaki wengi tu, lakini pamoja na hao samaki kulikuwa na chupa ya rangi ya kahawia ambayo ilikuwa juu mdomoni imezibwa na kipande cha mti cha mviringo na ndani yale kulikuwa na kipande cha karatasi.. Sasa nadhani wote hapa mnafahamu Meldives ni nchi yenye tamaduni gani?”

    Cindy akauliza huku anawaangalia kuona ni nani labda anajua kile alichouliza.



    “Ni moja ya nchi chache ambazo serikali yake inatambua masuala ya kiroho na uchawi.” Shafii akamjibu.



    “Kabisa.. Kwahiyo kutokana na mazingira ya kupatikana hii chupa baharini na wavuvi, ikabidi ipelekwe kwa Gavana wa jimbo.. Kumbuka nimesema hapo Maldives kuna visiwa vidogo vidogo vipatavyo elfu moja mia moja tisini na mbili. Hivi visiwa vimegawanywa kwenye mafungu ishirini na sita na kila fungu moja linahesabika kuwa ni jimbo na linaongozwa na Gavana.. Sasa baada ya chupa hii kufikishwa kwa Gavana na wazee wa kimila wa Maldives kuitwa, ikaamuliwa kuwa ifunguliwe.. Kwa taarifa ambazo wenyewe watu wa Maldives wametupatia… Inasemekana kwamba, walipoifungua tu hii chupa ulitoka moshi na karatasi ya ndani ikawa kama inaungua.. Ndipo hapo wale wazee wa mila wakaamuru chupa ifungwe kuzuia moshi zaidi usitoke..”



    Cindy akanyamaza kidogo, kisha akawaangalia. Akabadili badili picha kwenye projector ukutani mpaka zilipofika picha alizokuwa anazitaka. Kisha akaendelea na maelezo.



    “Mwezi mmoja baadae ndipo masahibu yakaanza.. Akina mama wote wajawazito katika visiwa vya Maldives watoto walikuwa wanajifungua walikuwa wanatoka mwili nzima wana manyoya kama paka.! Yaani wanakuwa ni vitoto vichanga binadamu kabisa lakini mwili mzima unakuwa imefunikwa naanyoya ya paka.! Jambo la ajabu zaidi likaja, ilikuwa ikifika siku ya saba tu wale watoto wanapotea hawaonekani tena.. Yani huyu mama mzazi, siku ya saba akiamka asubuhi yule mtoto wake mchanga mwenye manyoya kama paka anakuwa hayupo.!”



    Cindy akanyamaza tena kuwatazama. Akaona jinsi walivyosisimuka na wote wakimsikiliza kwa umakini mkubwa. Akaendelea..



    “Sasa baada ya tatizo kuwa kubwa sana.. Maana kwa mwezi mmoja tu wa May walizaliwa watoto zaidi ya elfu tano wakiwa na manyoya na wote hao wakapotea.. Na mwezi wa pili vivyo hivyo.. Kwa hiyo serikali yetu ya Marekani ikaingilia kati maana tulikuwa na wasi wasi hili tatizo linaweza kuenea sehemu nyingine mbali mbali duniani.. Kwahiyo serikali ikatuma timu ya wataalamu kwenda Maldives kuchukua sampuli za damu za wakazi wake pamoja na ile chupa iliyookotwa na wavuvi.. Sampuli za damu zilivyoletwa Marekani na kufanyiwa uchunguzi tuligundua kitu cha ajabu sana.!”



    Cindy akanyamaza tena kidogo na kuwaangalia.



    “Mligundua nini?” Goodluck akauliza kwa shauku.



    “Idadi kubwa ya wanawake wa Maldives walikuwa wameambukizwa moja ya kirusi adimu na ambacho akijaonekana juu ya uso wa Dunia kwa maelfu ya miaka, Mollivirus Sibericum.!”



    Akawaangalia jinsi ambavyo wote walishtuka kwa mshangao juu ya taarifa hii.

    Akaendelea tena.



    “Nadhani wote hapa tunafahamu HERVs, Human Endogenous Viruses.. Aina ya virusi ambavyo tunaamini kuwa walikuwepo maelfu ya miaka iliyopita na kuwaathiri mababu zetu na kusababisha kuacha sampuli zao za ribonucleic acid (RNA) katika DNA zetu binadamu mpaka Leo hii.. Sasa huyu kirusi Mollivirus Siberium ambaye tulimgundua kwenye sampuli za damu za wakazi wa Maldives, ni moja wapo ya hao virusi aina ya HERVs na hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka elfu thelathini anaonekana tena juu ya uso wa Dunia.. Najua ni ngumu kuamin! Hata sisi siku ya kwanza tulipigwa na bumbuwazi kama ninyi hivi Leo!”



    Akanyamaza tena na kutoa tabasamu ambalo walikuwa la utani.



    “Mlichukua hatua gani?” Salim akauliza.



    “Serikali ikatoa kandarasi kwa kampuzi ya madawa ya CORBO BioTech itengeneze haraka iwezekanavyo chanjo ya kukidhibiti kirusi hicho kisiendelee na kisilete madhara zaidi. Na ndani ya mwezi mmoja CORBO walikuwa wamefanikiwa kupata chanjo na ikaenda kutolewa kwa raia wote Maldives.. Baada ya chanjo kutolewa.. Ile hali ya watoto kuzaliwa na manyoya ya paka ikaisha na maisha yakaendelea kama kawaida.. Lakini ilipofika mwaka jana mwezi june kila mama ambaye mototo wake mwenye manyoya ya paka alipotea mwaka juzi, mtoto huyo alirudi katika mazingira ambayo ni ya utatanishi kama walivyopotea mwaka juzi.. Jambo la ajabu ni kwamba watoto hawa japo walikuwa na umri wa mwaka mmoja lakini walikuwa wana uwezo wa kuongea!! Na walikuwa wanaongea sentesi mbili tu, ya kwanza, “Mama usiogope, nilienda safari!”, na sentesi ya pili walikuwa wanauliza, “Mama kwanini umeua ndugu zetu?”



    Cindy akanyamaza tena kidogo. Maelezo haya yalikuwa yanawafanya Salim na wenzake wasisimke mpaka vinyweleo vinasimama.



    Cindy akaendelea kutoa maelezo.



    “Kwa kadiri ya tafiti zetu tunadhani kwamba hili swali la pili ‘mama kwanini umeua ndugu zetu?’  lilikuwa na maana ya chanjo iliyofanyika nchini Maldives na kusababisha wasizaliwe tena watoto wenye manyoya.. Ndio hii tunadhania wale watoto walikuwa wanasema ndugu zao wameuwawa.!”



    Cindy akameza mate kidogo, kisha akaendelea.



    “Sasa wiki moja, yaani siku saba baada ya wale watoto kurudi ndipo likatokea tukio la kwanza la mji wa kwanza kuchukuliwa.. Ndipo ilipotokea Anabelle 01.. Siku hii ya saba, kulipokucha asubuhi, population yote ya wakazi wa Maldives walikuwa wamepotea wote hawajulikani walikoenda.. Ndani ya siku moja tu kulipokucha mji mzima ulikuwa umebadilika.. Miji ulikuwa umechakaa na vumbi kila mahali kana kwamba kwa karne kadhaa hakuna binadamu aliyeishi hapo.. Mji wote ulikuwa na ukimya uliotisha.! Ndipo hapa tukafanya kosa la kwanza tukapeleka timu ya wataalamu ndani ya Anabelle 01.. Na kosa kubwa walilolifanya ni kuingia ndani za zile nyumba na majengo.. Hakuna yeyote aliyetoka mpaka leo.. Tukapeleka timu nyingine, hawa wakaepuka kuingia ndani ya majengo.. Wakawa wanakusanya sampuli tu na uchunguzi mwingine lakini ilipotimia saa kumi jioni wakiwa ndani ya Anabelle 01 wote wakapotea na mpaka leo hawajarudi.. Kwa hiyo tukajifunza mambo mawili hapo.. Kwanza ukiwa ndani ya Anabelle, hutakiwi kuingia ndani ya Jengo lolote, na pili usikae ndani ya Anabelle mpaka kufikia saa kumi jioni.!”



    “Kitu gani kingine mme jifunza?” Shafii akauliza kwa udadisi.



    “Tumejifunza pia dalili za mji kabla ya kuchukuliwa!” Cindy akajibu kwa mkato.



    “Inakuwaje?” Shafii akauliza tena.



    “Linapita tetemeko dogo la ardhi lisilo maadhara yoyote na likiisha pita tetemeko masaa sita baadae mji unatwaliwa na hao viumbe.. Pia baada ya tetemeko, mwisho kabisa mwa mji kunatokea ufa wenye upana kama wa kama hatua moja, hii ni alama ya mpaka wa Anabelle na Dunia iliyobaki.!” Cindy akaeleza.



    “Vipi kuhusu ile chupa iliyookotwa na wavuvi mliyoichukua na kuipeleka Marekani?” Magdalena akamuuliza Cindy.



    “Tunaamini kuwa kile kirusi kilichosababisha watoto wazaliwe na manyoya kilitoka kwenye chupa hii, kwasababu baada ya kuipima maabara tumeikuta ina kiwango kikubwa sana wa hao virusi wa Mollivirus Sibericum..!” Cindy akajibu tena kwa ufupi.



    “Na ile karatasi?” Magdalena akauliza tena.



    “Sorry??”



    “Namaanisha ile karatasi ambayo ilikiwa ndani ya chupa na ilipofunguliwa kwa mara ya kwanza moshi ukatoka na karatasi kuungua!”



    “Oooh! Tuliitoa kwa vizuri tu.. Uzuri iliungua lakini bado ilikuwa imeshikana.. Ni kama ukichoma moto gazeti au karatasi ngumu alafu ikibaki imeshikana, unaweza bado hata kusoma kilichoandikwa.. Ndivyo ilivyokuwa kwenye hii karatasi.. Tuliitoa kwa uzuri tu na kunakili pembeni kilichoandikwa.. Kilikuwa kimeandikwa kilatini, lakini ni kilatini kikongwe mno kiasi kwamba mpaka sasa hatujapata tafsiri sahihi.. Ni sentesi moja tu ndio timefanikiwa kuitafsiri kwa usahihi kabisa.!”



    “Sentesi gani?” Salim na Magdalena wakajikuta wameuliza kwa pamoja kwa shauku.



    “Kichwa chake cha habari.. Kimeandikwa ‘Novus Ordo Sedorum'”



    “Novus Ordo Sedorum?? Ina maana gani?” Salim akauliza.



    “Novus Ordo Sedorum, ikimaanisha ‘The New Order Of Ages’” Cindy akajibu huku amewakazia macho.



    “The New Order Of Ages!” Salim akajikuta ameorudia sentesi kuitamka kwa mshangao.



    “Kwa hiyo hizo nilizowaeleza ndivyo vitendawili vilivyopo mbele yetu tunavyopaswa kuvitegua.. Kwa namna miji inavyochukuliwa, tunakadiria kwamba kama hali itaendelea hivi basi mpaka kufikia miaka mitatu ijayo, yaani mwaka 2041 dunia yote itakuwa imechukuliwa.. Na huo unaweza ukawa mwisho wa binadamu juu ya uso wa Dunia maana hatujui mpaka sasa miji ikishachukuliwa ni nini kinachoendelea huko ndani.!?” Cindy akaongea kwa kumaanisha huku anaweka sawa laptop yake na kuzima projector.



    Kwa dakika kadhaa hakuna ambaye aliweza kuongea. Kila mmoja alikuwa amezama kwenye mawazo akitafakari haya maelezo yote aliyoyasikia hapa. Hakika vitendawili vilivyopo mbele yao vilikuwa vinaonekana havina majawabu, lakini walipaswa wapate majawabu, na kazi iliyokuwepo mbele yao ilikuwa ni nzito lakini pia walipaswa kuubeba mzigo huo mabegani mwao.



    Wakiwa bado wanaendelea kutafakari, Mara simu ya Salim, ikaita.



    “Hallo Mkuu…nakusikia Mkuu…ndio, sawa Mkuu.. Aisee.. Mmehakiki lakini? Aisee… sawa Mkuu.. Sawa.. Nashukuru kwa taarifa Mkuu! Asante!” Kisha akakata simu.



    Baada tu ya kukata simu sura yake ilikuwa inasema kila kitu bila kuongea chochote kile. Uso wa Salim ulikuwa umejaa woga na huzuni kubwa. Ni mara chache sana kwa Afisa Nguli wa Usalama wa Taifa uso wake kuonyesha hofu kubwa kiasi hicho.



    “Hao walikuwa makao makuu wamenipigia!” Salim akaongea kwa unyonge huku anaweka simu mezani.



    “Wanasemaje?” Gooluck akauliza.



    “Wanasema tetemeko kimepita mahali.. Kuna dalili ya mji mwingine kutwaliwa masaa machache yajayo..!” Salim akaongea huku anajiinamia kuficha machozi yalikuwa yanaanza kumtoka.



    “Mji gani?” Shafii akauliza kwa woga na hofu iliyosikika mpaka kwenye sauti yake.



    “Dar es Salaam.!!” Salim akajibu bila kuwaangalia wenzake.. Sauti yake ilidhihirisha kuwa alikuwa ameanza kulia.



    Taarifa hii ikawaacha wote vinywa wazi, wasijui wasemeje au wafanyaje.



    Wakati huo huo..





    RABAT, MOROCCO



    Kuna kipindi ambacho kila mtu anakuwa amekata tamaa lazima wainuke watu wa kuibeba dunia mabegani na kuifanya isonge mbele. Lakini pia sio kila muda unapoona wameinuka watu basi wanakuwa na nia ya kuibeba mabegani, wengine wanainuka ili kuikimbia dunia wasizame nayo pale itakapozama! Kuna wengine watainuka na kuibeba mabegani mwao, lakini haimaanishi kwamba wanatapeleka mbele, wengine nia yao ya kuibeba mabegani ni ili waiinue juu zaidi ili watakapoibwaga ipasuke vipande vipande kisisalie kitu.



    Kila dunia inapozama, kila atayeyeinuka ana nia yake, na kila atayeibeba mabegani kuna mahali anapotaka kuipeleka. Mtihani mkubwa huja pale ambapo, tukiibeba dunia pamoja lakini hatukubaliani mahali kwa kuipeleka.

    Huu ulikuwa ni usiku wa karibia saa saba usiku, ndipo muda ambao watu sita, walivalia majoho marefu myeusi yenye kofia za kufunika vichwa na wakiwa hawana viatu miguuni, walikuwa wamewasili katika pwani ya Morocco na mashua wakitokea nchini Hispania kwa kuvuka bahari.



    Walikuwa wameshashusha mzigo wao mmoja tu waliokiwa nao na sasa walikuwa wameubeba na wakitokomea kutoka hapo pwani.



    Leo hii walikuwa wanatarajia kuhitimisha safari yao ya karibia miezi miwili kwa mguu, kutokea Italia, na baadae Hispania na hatimaye kuvuka bahari kwa mashua.



    Licha ya majoho yao meusi ya kufanana, na licha ya wote kufanana kwa kuwa peku peku, lakini pia walifanana alama iliyopo shingoni mwao wote ambao ilikuwa ni tatoo ya neno, ‘Sancta Sedes’.



    Mzigo wao pekee waliokuja nao ulikuwa ni sanduku kubwa mfano wa jeneza ambalo lilihitaji walau watu wanne ili kuweza kulibeba.

    Kwahiyo walikuwa wamelibeba mabegani kila upande wa sanduku mtu mmoja, na mmoja ametangulia mbele na mwingine nyuma.



    Sanduku hili kuu kuu linaloonekana la siku nyingi mno na pengine lilikuwa limefukiwa chini kwa miaka mingi, juu yake lilikuwa na maandishi yaliyofifia lakini bado yaliweza kusomeka.. Yalikuwa yameandikwa, “Novus Ordo Sedorum ” (The New World Of Ages).



    Japokuwa watu hawa walikuwa wamechoka haswa kwa safari hii ya miezi miwili, kiasi kwamba nyayo zao zilikuwa zimepasuka kiasi zilikiwa zinakaribia kutoa damu kwasababu ya kutembea umbali mrefu kwa miezi miwili mfululizo, lakini waliona faraja mbele yao, safari yao ilikuwa imefikia ukingoni, walikuwa wamebakisha kilomita tano tu kuingia mji wa Rabat.



    Ulimwengu unapozama, lazima wainuke watu wa kuubeba mabegani… lakini je wakishaubeba, ni wapi wataupeleka??





    THE OTHER HALF











    EPISODE 2











    Taarifa ya kuwa Dar es Salaam imeonyesha dalili ya kutaka kuchukuliwa baada ya tetemeko dogo la ardhi kupita na kumaanisha kuwa muda na saa yoyote ile, Dar inachukuliwa na kuwa Anabelle, hii ilikuwa ni taarifa ya kuogofya na kuvunja moyo.

    Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa nchi moyo miji yake miwili kuchukuliwa kwa mfululizo. Mpaka kufikia sasa kikichokuwa kinashuhudiwa ni kwa mji mmoja tu unatwaliwa kwenye nchi.



    Hali hii ya mji wa Nachingwea kutwaliwa wiki mbili zilizopita na papo hapo leo hii inaonekana dalili ya mji wa Dar es Salaam unaelekea kutwaliwa iliwachanganya hata wataalamu wanaochunguza na kutafiti suala hili.



    “Ndio Mkuu.. Ndio Mkuu.. Sawa… Asante sana.! Tafdhali nipe niongee naye ukifanikiwa kuwapata.! Shukrani Mkuu.” Salim alimaliza kuongea na simu na kukata.



    Alikuwa anahema juu juu kwa woga na kupaniki. Uso wote ulikuwa umesawajika kwa huzuni.



    “Wanasemaje?” Goodluck, yule polisi mtaalamu wa forensics akamuuliza Salim baada ya kukata simu.



    “Wanafanya evacuation ya mji.!” Salim akajibu huku anahema juu juu.

    Akaendelea kuongea. “Nimewashauri wafanye evacuation kuwapeleka watu mlandizi, chalinze na kuelekea Morogoro… wasiwalete watu maeneo ya Mkuranga, kwa sababu watakuwa trapped.. Watashindwa kurudi nyuma kwasababu kuna Dar es Salaam imechukuliwa na hawataweza kuja huku kusini kwa sababu Nachingwea imeshachukuliwa… Kwahiyo nimeshauri wapelekwe Mlandizi, Chalinze na kuendelea kuelekea Morogoro.!”



    Salim akaeleza huku bado anahema juu juu akiwa amepaniki haswa.



    “Aiseeee!! Huo ni mtihani mkubwa.. Hawawezi kuevacuate watu milioni tano ndani ya masaa sita.. Huu ni mtihani haswa!” Shafii akaongea mkono mmoja amejishika kiunoni na mwingine kajishika shavuni kwa unyonge.



    “Salim.!” Goodluck akamuamsha Salim kutoka kwenye lindi la mawazo.



    “Yes!” Salim akaitika akiwa kama amezinduka kutoka usingizini.



    “Kuna lingine? Naona kama kuna kingine haukisemi?” Goodluck akauliza kwa udadisi.



    “Familia yake iko Dar.!” Magdalena akadakia na kumjibia.



    “Basrat.!!” Salim akataja jina la mwanaye na kujiinamia.



    Kwa upande fulani akaanza kujilaumu na kuchukia nafsini mwake kwa kuiacha familia yake Dar na kuelekea Nachingwea, Anabelle 23 kufanya uchunguzi.

    Lakini hakuwa na namna, kama afisa wa Usalama wa Taifa hakuwa na chaguo zaidi ya kufuata amri kutoka juu.

    Lakini bado alijisikia hasira dhidi yake mwenyewe kwa kutokuwepo na familia yake kuisaidia katika kipindi hiki ambacho watakuwa wanahaha kukimbia mji wa Dar es Salaam kabla haujachukuliwa.



    Machozi yalikuwa yanakaribia kutoka kila alipokumbuka sura ya mtoto wake Basrat, binti wa miaka mitano tu.! Ni kiasi gani muda huu atakuwa analia akimuona mama yake anahaha kuokoa maisha yao?

    Akamuwaza mkewe Khadija, akawaza namna ambavyo anataabika muda huu kuokoa maisha yake na mtoto wao kabla Dar es Salaam haijageuzwa kuwa Anabelle.



    Akasikia hasira moyoni mwake! Alitakiwa kuwa na familia yake muda huu..



    Licha ya mtu wa makao makuu usalama wa Taifa kumuahidi kuwa atajitahidi kumtafuta mkewe na mtoto wake ili kuwasaidia kutoka nje ya Dar es Salaam, lakini hakuina huo uhalisia. Alivuta picha jinsi muda huu ambavyo jiji zima litakuwa kwenye taharuki, kumtafuta mkewe na mwanae Basrat na kuwapata, ni ngumu kama kuitafuta punje ya haradi iliyodondoshwa kwenye mchanga wa pwani ya bahari.



    Akasikia hasira zaidi! Akasikia woga zaidi.. Hofu ilitawala nafsi yake mpaka mwili ukatetemeka! Akafikiria namna ambavyo population nzima inapotea kusikojulikana baada ya mji kutwaliwa… alitamani apae na kutua Dar es Salaam awe shujaa kwa familia yake. Akajilaumu kwanini hayuko pembeni ya familia yake muda huu.



    “Basrat.!” Akatamka tena jina la mwanae kwa uchungu na kujifunika uso kwa viganja vya mkono.



    Wote watano bado wakiwa wameduwaa kwa taarifa hii ya dalili ya mji wa Dar es Salaam kuonyesha dalili ya kutwaliwa na kugeuka Anabelle.. Ghafla wakasikia mlio mkubwa, kama tarumbeta, au honi.. Mlio wenye kufanana na sauti ya ‘parapanda’.. Mlio mkali haswa wa sauti kama tarumbeta yenye kishindo..



    “Wuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.!!”



    Kishindo cha mlio wa tarumbeta kikasikia. Muda huo huo wakaanza kusikia tetemeko dogo la ardhi linapita pale walipo.



    “No no no no nooooooo!” Dr. Cindy Wheaton akaanza kulalamika huku kila mmoja akijishikilia asidondoke.



    “Nini kinaendelea?” Shafii, mtaalamu wa vinasaba akauliza kwa mshtuko na mshangao.



    “This can’t be.! Haiwezekani..!!” Magdalena akaongea kwa kuhamaki.



    “Nini kinatokea??” Shafii akauliza tena kwa jazba huku akijishikilia asidondoshwe na lile tetemeko.



    “Mji unachukuliwa!” Salim akajibu huku naye akiwa amejishikilia asidondoke.



    “What? Mji gani?” Shafii akauliza tena kwa sauti ya kupayuka.



    “Mji huu tuliomo.!” Salim akajibu.



    Tetemeko hili japokuwa lilikuwa dogo kwa kiwango cha mtetemo na mtikisiko, lakini lilidumu kwa taribani dakika tano nzima.



    Baada ya kama dakika hizo tano kupita.. Ile sauti la tarumbeta lenye kishindo ikaacha kusikika na tetemeko halikuwepo tena, kukawa na ukimya mkubwa na wa ajabu.

    Wataalamu wote wakabaki wanaangaliana wameganda wakiogopa kupiga hata hatua moja.



    “Kusanyeni kila kitu tunatakiwa kuondoka hapa sasa hivi.. Tuna masaa sita tu mbele yetu kabla mji huu haujatwaliwa na kugeuzwa Anabelle!” Cindy aliongea huku anakusanya vitu vyake haraka haraka.



    “Hii sio sawa! Something is wrong.. Dr. umewagi kuona hali hii? Miji mitatu kutwaliwa kwa pamoja mfululizo ndani ya nchi moja?” Magdalena akauliza huku naye anakusanya vitu vyake haraka haraka.



    “This is strange! Haijawahi kutokea kitu kama hiki.. Something is wrong?” Cindy akajibu kwa sauti ya hofu.



    “Kanali.!” Salim akamuita mwanajeshi kiongozi wa Team 5C, kile kikosi maalumu cha wanajeshi kumi na tano wanaoambatana nao kwa ajili ya ulinzi.



    “Ndio Mkuu!” Kanali akaitika na kuelekea kwenye hema waliyokuwemo wataalamu.



    “Nadhani umeona, hapa tulipo panaelekea kutwaliwa ndani ya masaa sita yajayo.. Tunahitaji kuondoka hapa sasa hivi… Kwa kuzingatia kuwa Dar nayo iko inatwaliwa pia muda huu.. Nini pendekezo lako?” Salim akamuuliza kanali.



    Kanali alikuwa amekuja na ramani mkononi. Akaiweka juu ya meza na kuanza kuwapa maelezo.



    “Sasa hivi tuko hapa.!” Akaonyesha sehemu kwenye ramani, “huu ni msitu wa Namala, kijiji cha Chienjele Wilaya ya Ruangwa.. Tupo takribani kilomita 15 kutoka Nachingwea au Anabelle 23.. Kama tukielekea upande wa Mashariki kama mwendo wa masaa matatu, tunatokea Wilaya ya Lindi mjini.. Sasa sitaki twende huku maana kama ulivyosema mbele yetu kutakuwa na Dar es Salaam ambayo inatwaliwa sasa hivi na nyuma yetu tutakiwa na Anabelle za Nachingwea na Ruangwa.. Tutakuwa ‘trapped’ hatuwezi kwenda mbele wala nyuma.. Tutabakiwa na njia pekee ya kutumia bahari ambayo sio salama kwa hali ilivyo.!”



    Kanali akanyamza kidogo kuona kama anenda sambamba na anaowapa maelekezo.

    Kisha akonyesha sehemu nyingine kwenye ramani na kuendelea na maelezo.



    “Kama tukitoka hapa tulipo kufuata barabara hii kuelekea magharibi.. Tunaweza kuizunguka Nachingwea, Anabelle 23 pasipo kuingia ndani ya mji na tukatokea Newala, na baadae tukapita mbuga ya Selous na kutokea Morogoro.. Hii ndio njia ninayopendekeza, japo ni ngumu na mbali mno lakini ni Salama zaidi.!” Kanali akamaliza kutoa maelezo.



    “Na hiyo ndiyo njia tutakayienda nayo!” Salim akamaliza mjadala.



    Kichwani mwake alikuwa anamuwaza mwanawe Basrat na mkewe Khadija.. Alikuwa tayari kufanya lolote ili mradi tu aweze kujua hatma ya familia yake na zaidi aweze kuiokoa.



    Baada ya kukusanya vitu vyao vyote na kuvipakia kwenye magari, wakiwa wanajiaandaa wao wenyewe kupanda kwenye magari waondoke, Magdalena alimfuata Salim na kumnong’oneza.



    “Nahisi Dr. Cindy kuna kitu anatuficha!”



    “Kwanini unasema hivyo?”



    “Nimehisi tu! Nina hisia Kali sana kwamba kuna kitu hataki kutuambia!”



    Magdalena akamaliza kunong’ona na kwenda kupanda kwenye gari.

    Salim akageuka kumuangalia Cindy ambaye alikuwa anahangaika kumalizia kupakia begi lake la mwisho kwenye gari.

    Akaenda kumsaidia pasipo kumsemesha chochote, kisha wakapanda kwenye gari.



    Walikuwa na masaa sita tu wakimbie kutoka hapi walipo, wapite msitu kwa msitu na kutokea Newala, na baadae wapite Mbuga ya Selous na kutokea Morogoro.



    Washing D.C, Marekani.



    Tayari zilikuwa zimepita takribani wiki mbili tangu ndege ya Rais, Air force One kupoteza mawasiliano na vyombo vya ulinzi nchini Marekani na kupotea kusikojulikana.



    Siku hii ambayo Air Force One ilipotea, Rais Laura Keith, rais wa 47 wa Marekani na Rais wa kwanza mwanamke wa Taifa hilo alikuwa anatokea Vatican kumsakimh Papa wa Kanisa Katoliki ambaye hali yake ya afya ilikuwa tete haswa.



    Akiwa njiani kurejea Marekani, walipokuwa wanapita juu ya bahari ya Atlantic ndipo ambapo Air Force One ilipoteza mawasiliano na kupotea kusikojulikana.

    Licha ya kutumia mbinu za ‘tracking’ zinazotumiwa na Jeshi la Navy kutambua sehemu ambayo Air Force One inakuwepo muda wowote ule, lakini hawakufanikiwa na jambo la ajabu zaidi wakifuatilia ‘tracker’, kifaa kinachopandikizwa ndani ya mkono wa Rais ili kujua mahali alipo muda wote, kifaa hicho kwa wiki mbili zote kilikuwa kinaonyesha kuwa Rais yuko juu ya bahari ya Atlantic, na hii ilikuwa ina maanisha kwamba Air Force One haijadondoka kama wengi walivyokuwa wanadhani, bali bado ili kuwa juu angani mahali Fulani kwenye bahari ya Atlantic.



    Licha ya Navy kutumia ndege za kivita F-16, kukagua karibia anga lote la bahari ya Atlantic kwa wiki mbili, bado hakuku onekana dalili yoyote ya uwepo wa Air Force One.



    Leo hii Makamu wa Rais David Logan alikuwa anatoka nyumbani kwake kwenye makazi maalumu ya Makamu wa Rais yaliyopo eneo linalomilikiwa na Navy, U.S. Naval Observatory ambapo nyumba ya makamu wa Rais na familia yake ipo kwenye Number One Observatory Cirle na alikuwa anaelekea White House kwa ajili ya shughuli maalumu.



    Kama majira ya saa nne asubuhi msafara wake ulikuwa umewasili White House.



    Ukiingia ndani ya White House kuna majengo kadhaa.

    Mbele yako kabisa baada ya kuingia, ndiko kuna Jengo maarufu ambalo watu wote wamezoea kuliona kwenye Picha na habari mbali mbali. Jengo hili linaitwa ‘Executive Mansio’ na ndilo ambalo Rais na familia yake anaishi.



    Pembeni yake kuna Jengo lingine kubwa pia kiasi. Hili ndilo linaitwa ‘West Wing’.



    Jengo hili ndilo kuna ofisi za Rais na ofisi muhimu zinazoendesha nchi ya Marekani.

    Jengo hili ndilo lina chumba maarufu cha ofisi kijulikanacho kama ‘Oval Office’.



    Pia kuna ‘Cabinet Room’ kwa ajili ya mikutano ya Rais na Mawaziri wake.



    Pia kuna ‘Situation Room’ ambacho ni chumba cha vikao vya siri za hali ya juu kati ya Rais na Wasaidizi wake wakuu.



    Pia kuna ‘Roosevelt Room’ ambacho kinatumiwa kwa ajili ya mikutamo ya watumishi wakuu wa Ikulu na Ofisi ya Rais.

    Pembeni ya Jengo hili la West Wing kuna Jengo lingine linaloitwa Eisenhower Executive Office, hili Jengo ndilo linatumika kama ofisi ya Makamu wa Rais wa Marekani.



    Kwahiyo baada ya Makamu wa Rais David Logan kuwasili, moja kwa moja akaelekea ofisini kwake Jengo la Eisenhower Executive Office.

    Alipoingia tu ofisini kwake, Katibu wake Kiongozi naye akaingia ofisini kumsabahi.



    “Habari ya asubuhi Mr. Vice President?” Kevin, katibu kiongozi akamsalimu Makamu wa Rais.



    Makamu wa Rais mwenyewe alikuwa amesimama dirishani anachungulia kuangalia Jengo la Executive Mansion ambalo wanaishi familia ya Rais.



    “Hivi watahama lini hawa?” Makamu wa Rais akamuuliza Kevin bila kumjibu salamu yake.



    “Nani muheshimiwa?” Kevin akauliza huku naye anasogea dirishani.



    “Familia ya Madam President.. Amepotea kwa wiki mbili sasa, najiuliza hii familia yake itakaa hapa mpaka lini kama rais akiendelea kutoonekana?”



    “Mr. Vice President ni mapema mno kuongelea suala la kuhamisha familia ya rais, hata protokali hairuhusu kuwahamisha kwa muda mfupi hivi!” Kevin akajibu huku ana uso wa mshangao kutokana na kujua kile bosi wake Makamu wa Rais alichokuwa anakiwaza.



    “Protoko, protoko! Damn it.. Mimi ndiye nafanya shughuli za rais sasa ajabu ati siruhusiwi hata kutumia Oval Office! Huu ni upuuzi.!” Makamu wa Rais akaongea kwa kukereka.



    “Haiwezi kulete Picha nzuri kwa Taifa na viongozi, utaonekana umefurahi rais kupotea na una uchu wa kumrithi.. Na narudia protokali hairuhusu kufanya hivyo mapema hivi.. Kuna taratibu za kufuata na unajua hilo!” Kevin akaongea kwa msisitizo.



    “Na hakuna ubaya wowote wa mimi kutamani kumrithi.. Hebu twende kwenye hicho kikao wanachonisubiri.!” Makamu wa Rais akaongea huku anafunga vizuri koti la suti na kuanza kuelekea mlangoni.



    Kevin hakusema chochote, akabakia tu mdomo wazi akishangaa maneno ta bosi wake.



    Wakafuatana na kutembea kuelekea Jengo la West Wing ambalo liko pembeni tu ya ofisi ya makamu wa Rais.



    Baada ya kuingia tu West Wing moja kwa moja wakaongozwa na watu wa Secret Service mpaka kwenye chumba cha vikao vya Siri, cha Situation Room.



    Walipoingia wote waliokuwemo ndani walisimama kwa heshima, na baada ya makamu wa Rais kukaa chini nao wakakaa.



    Ndani ya Situation Room, alikuwepo Mshauri Mkuu wa Rais wa masuala ya usalama (National Security Advisor) Bi. Naomi Cole , pia alikuwepo Mkurugenzi wa CIA Bw. James Rupert, na pia alikuwepo Mwenyekiti wa kamati ya Majemedari wa Majeshi (Chairman of Joint Chiefs of Staff), Admiral George Smith.



    Lakini pia pamoja nao alikuwepo mizee kimoja kikongwe sana, kwa makadirio alikuwa labda anaweza kufika hata miaka 84. Alikuwa amekaa pembeni ya Mkurugenzi wa CIA.



    Baada ya salamu wakaanza kumpa ‘briefing’ makamu wa Rais kuhusu masuala yote muhimu wakianzia na juhudi za kumtafuta Rais na Air Force One katika bahari ya Atlantic.



    Baada ya hapo wakampa briefing muhimu zaidi kuhusu muendelezo wa kutwaliwa miji duniani. Wakamueleza kuhusu miji mingine miwili mitatu iliyotwaliwa barani Africa nchini Tanzania.

    Wakamueleza pia kuna dalili miji pia ikaanza kutwaliwa nchini Marekani kwa kuzingatia kwamba tayari kuna mji umetwaliwa nchini Mexico na miji mingine miwili imetwaliwa nchini Canada.



    Pia wakamueleza kuhusu wasiwasi wao kuwa makisio yao ya awali walidhani kwamba kama hali hii ya kutwaliwa miji itaendelea basi ndani ya miaka mitatu Dunia nzima itakuwa imefanywa kuwa Anabelle, yaani imetwaliwa yote.. Lakini wakamueleza kwa jinsi kasi ya miji kutwaliwa ilivyoongezeka, hali ikiendelea hivyo ndani ya miezi sita, ulimwengu nzima utakuwa umetwaliwa.



    “Mr. Vice President ndipo hapa inatuleta katika mjadala wa mchoro wa George Washington ulioibiwa Ikulu wiki mbili zilizopita.!” Akaongea James Rupert, Mkurugenzi wa CIA.



    “Mchoro wa George Washington?? Unahusika nini na mambo mahimu tunayojadili hapa?” Makamu wa Rais akafoka.



    “Mr. Vice President nipe nafasi nieleze kidogo” Rupert akaongea kwa unyenyekevu.



    “OK! Ongea..!”



    “Nashukuru.. Nadhani wote tunafahamu kwamba wiki mbili zilizopita, siku moja tu baada ya Air Force One kupotea kwenye bahari ya Atlantic, hapa White House kulitokea upotevu wa mchoro wa kihistoria wa George Washington ambao una miaka karibia mia Tatu.. Mchoro huu umekuwa unakaa katika ‘East Room’ ya Executive Mansion! Upotevu wa mchoro huu umekuwa na utata mkubwa kwa sababu hakuna mlango uliovunjwa na Secret Service wanatuhakikishia kuwa hakukuwa na mlango wowote uliovunjwa wala ‘intruder’ aliyeonekana.!”



    Bw. Rupert akanyamaza kidogo na ‘kumeza mate’. Kisha akaendelea.



    “Kutokana na matukio mazito yanayotokea duniani kote, suala hili la kupotea mchoro huu was kihistoria kikapuuzwa na kutotiliwa maanani sana.. Lakini binafsi nilipolisikia, nikawaagiza vijana wangu kadhaa ndani ya CIA walifuatile kwa umakini mkubwa na waliniletea ripoti iliyonishangaza.. Sasa kabla sijaenda kwenye hoja yangu naomba niwape historia ambayo naaminj mnaifahamu lakini nataka niwakumbushe tu ili twende sawa.!”



    Wote wakatikisa vichwa kumuashiria kwamba aongee.

    Rupert akaendelea.



    “Mwezi August mwaka 1814 nadhani wote tunakumbuka kwamba ilitokea vita ya siku mbili kati ya Majeshi ya Marekani na Uingereza.. Majeshi ya Marekani yalikuwa yameharibu kwa mabomu bandari ya Dove nchini Canada ambayo ilikuwa chini ya Uingereza… na katika kulipa kisasi Uingereza ikavamia mji huu wa Washington na kuanza kuchoma moto majengo ya serikali.. Kipindi hiki nchi ilikuwa inaongozwa na Rais James Madison ambaye kwa siku hiyo ya uvamizi hakuwepo Washington.. Baada ya taarifa hii ya uvamizi kumfikia, akamtumia ujumbe wa siri mke wake, First lady Dolley Madison.. Kwenye ujumbe huu wa barua ya siri alimueleza kuwa akiona dalili yoyote ya Majeshi ya Uingereza kuvamia White House, asichukue kitu chochote kile, bali achukue mkoba wake wa ofisi wenye nyaraka mbali mbali na pia muhimu zaidi achukue mchoro wa George Washington uliopo ukutani..”



    Akanyamaza tena kidogo ‘kumeza mate’.

    Kisha akaendelea tena.



    “Masaa kadhaa baadae, wanajeshi wa Uingereza wakaanza kuivamia White House, na kabla hawajavunja geti kuu.. First lady Dolley Madison akafanya kama alivyoelezwa na mumewe.. Akachukua mkoba wa ofisi wenye nyaraka, pamoja na mchoro wa George Washington na kutoka navyo.! Baadae wanajeshi wa Uingereza wakavamia White House na kuichoma moto yote kabla ya moto huo kuzimwa na mvua kubwa iliyonyesha masaa kadhaa baadae.. Sasa first lady Dolley Madison alipotoroka na ule mchoro wa George Washington alikimbilia eneo linaitwa Brookville, mjini Maryland.! Na akiwa huko alipeqa hifadhi na mtu anayeitwa Caleb Bentley.. Ambaye ni babu wa huyu Mzee mnayemuona hapa.!”



    Rupert akaongea huku akimshika begani yule mzee pembeni yake.



    “Mzee karibu sasa uwaeleze kile ulichonieleza Mimi!” Rupert akamkaribisha yule mzee.



    Mzee akaanza kuongea huku mikono inatetemeka kutokana na hali yake ya ukongwe.



    “Jina langu naitwa Bentley Caleb Bentley… mjukuu wa Caleb Bentley, ambaye takribani miaka mia mbili iliyopita, babu yangu alimpa hifadhi mke wa Rais Madison kwa wiki mbili akiwa na mchoro wa muanzilishi wa taifa hili, George Washington.. Katika wiki mbili hizo babu yangu aliambiwa siri ambayo inarithishwa kutoka kwa rais mmoja mpaka mwingine, siri ambayo pia babu yangu alimrithisha babab yangu, na baba yangu kabla hajafariki akairithisha kwangu.. Siri ambayo naamini inaweza kuokoa ulimwengu kutoka katika janga hili linalotishia kufuta uwepo wa binadamu kwenye uso wa Dunia.!”



    Akanyamaza kidogo kabla ya kuendelea. Chumba kizima cha Situation Room kilikuwa na ukimya Mkuu, wote wakiwa wametega sikio kusikia neno hilo zito.





    THE OTHER HALF



















    EPISODE 3



















    Ilipoishia Episode 2











    Kikosi cha wataalamu kikiongozwa na Afisa wa Usalama wa Taifa Bw. Salim wanagundua kuwa mahali walipo (Wilaya ya Ruangwa) panakaribia kutwaliwa na kugeuka Anabelle.



    Wakati huo huo wamepewa taarifa kuwa mji wa Dar Es Salaam ndani ya masaa sita utakuwa umetwaliwa.







    Kanali wa kikosi maalumu cha Jeshi kinachowalinda amependekeza kwamba wasafiri kupitia mbuga ya Selous na kutoka Morogoro.











    Pia wakati huo huo nchini Marekani katika chumba cha Situation Room Whitehouse kuna kikao kikubwa kinaendelea kikiongozwa na makamu wa Rais David Logan akiongea na washauri wakuu wa Rais.



    Pamoja nao yupo mzee kikongwe anayeitwa Bentley Caleb Bentley aliyeletwa na Mkurugenzi wa CIA ili aweze kuwapa siri iliyopo katika mchoro wa George Washington ambao umeibiwa kama wiki mbili zilizopita siku moja baada ya Rais Laura Keith kupotea angani na Airforce One.











    Tuendelee..























    EPISODE 3















    Ipo falsafa ya miaka ya kale inayosema kwamba, nafsi yako inapokuwa na uwezo wa kuona huhitaji macho usoni mwako.



    Uwezo mkubwa zaidi binadamu alioumbwa nao si kuona au kusikia au kunusa. Nguvu kubwa zaidi iliyopo ndani ya nafsi ya binadamu ni hisia. Uwezo wa kung’amua kile ambacho hujakiona wala kukisikia.







    Pengine kama kila binadamu angetumia uwezo wake wa ndani ya nafsi, uwezo wa hisi aliyoumbwa nayo labda ulimwengu usingeweza kutwaliwa, labda leo hii kusingelikuwa na Anabelle hata moja juu ya uso wa dunia.











    Tumefikaje hapa tulipo? Dunia imefikaje hapa?







    Labda pengine sisi wote ni wakimbizi hapa duniani, iko sehemu, pako mahala pengine tunapopaswa kuwa.. Sayari nyingine, nyota nyingine.. Pengine, wamiliki halali wa dunia wameamka ili kuitwaa.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Lakini kama tunajua hapa ni kwetu kwanini hatuja fanya lolote muda wote huu. Kwanini tumeishi kama hapa si kwetu?



    Kwa karne kadhaa tumeishi juu ya dunia kana kwamba hapa sio kwetu, kana kwamba kuna mahali tunakimbilia kwenda.



    Tumeharibu, hatujaboresha



    tumeifubaza dunia, hatujaifanya upya!











    Ni nani alijua gharama ambayo ulimwengu na vilivyomo vitakuja kulipa siku ambayo wanaohisi dunia ni yao watakapo amka? Ni nani alijua siku moja dunia itatwaliwa kutoka mikononi mwa mwetu?







    Lazima kuna waliojua, lazima wapo walioitunza hii siri mioyoni mwao!







    Kwanini hawakutuonya? Kwanini walikaa kimya?



    Mwisho wa siku kila siri inapaswa kujidhihirisha ili uthamani wake wa kufanywa siri miaka yote upate kuwa bayana.!!























    Saa Kumi Alafajiri: Rabat, Morocco











    Wale watu sita, waliovalia majoho meusi na miguuni wakiwa peku peku walikuwa wamekaribia kabisa jumba la Kasri ambalo lipo kwenye msitu uliopo kama kilomita tano kutoka baharini.











    Mikono yao ilikuwa imechoka haswa, lile sanduku kama jeneza walilolibeba lilikuwa linaonekana ni zito kweli kweli.



    Katika giza hili kilichokuwa kinavuja kwenye viganja mikononi mwao haikuwa rahisi king’amua kama lilikuwa jasho ama ilikuwa damu.











    Licha ya kuchoka nyang’anyg’a lakini watu hawa walitembea imara kabisa bila kuyumba wala kupepesuka.







    Wakakaribia mpaka kwenye Kasri ndani ya msitu. Kasri hili lilikuwa limetengenezwa katika muundo wa kizamani sana lakini lilikuwa la kifahari haswa. Pia lilionekana kuwa kuu kuu ikiashiria limekuwepo msituni hapo kwa miaka mingi sana labda pengine hata Karne kadhaa.











    Kasri hili lilikuwa limezungushiwa ukuta wa mawe na mbele yake kuliwa na geti kubwa.



    Jumba hili lilikuwa linaonyesha kwamba halikuwa na kitu chochote chenye kuashiria teknolojia ya kisasa, hata umeme ulionekana kutokuwepo, kwani kwa mbali ndani ya hili jumba vilionekana chemli zikiwa zimenining’inizwa ili kutoa mwanga.











    Hawa watu walipofika mbele ya geti la hili Kasri, yule aliyetangulia mbele akagonga geti.







    Aligonga geti katika namna ambayo, aligonga mara mbili kisha akatulia. Akarudia tena mara ya pili kugonga tena mara mbili na kisha akagonga tena mara ya Tatu kwa mtindo ule ule wa kugonga mara mbili.











    Geti likafunguliwa na kijana mwenye ngozi nyeupe ya kizungu iliyopauka sana. Kijana huyu alikuwa amevalia suti nyeusi na kichwani amenyoa kipara.











    Wale watu waliobeba sanduku hawakumsemesha chochote wala kumsalimia na wala yule kijana hakuwauliza chochote.



    Wakaelekea mpaka kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya lile jumba. Hapa napo wakagonga tena kwa mtindo ule ule. Yule aliyetangilia mbele akagonga mara mbili, kisha akasubiri, akagonga tena mara mbili, akasubiri na kisha akamalizia kugonga tena vivyo hivyo kwa mara ya tatu.







    Mlango ukafunguliwa na kijana mwingine wa kizungu mwenye weupe wa kupauka sana na alikuwa amevalia suti nyuesi kama yule wa getini na kichwa amenyoa upara kabisa.











    Baada ya huyu kijana kufungua tu mlango, akatamka kwa sauti kubwa,











    *”SANCTA SEDESSSS..!”*







    Watu ambao walikuwa ndani ya jumba hilo wakionekana kama walikuwa kwenye kikao wakasimama wote kwa pamoja.











    Jumba hili lilikuwa katika namna ambayo, ukiingia tu lango kuu la kuingia ndani, unakutana na ukumbi mpana kama kanisa au msikiti. Kwa ndani juu ya paa la Jengo lilikuwa la umbo la nusu duara likiwa na michoro ya ajabu ya wanyama, binadamu, malaika na kadhalika kufanania kabisa kama Jengo la Basilika lilipo Vatican.











    Watu hawa ambao walikuwa wamesimama baada ya hawa waliokuja na sanduku kuingia, walikuwa wamekaa kwenye mtindo kama wakaavyo wabunge wa Uingereza bungeni. Upande huu kuna viti vyenye watu na upande huu kuna viti vingine vyenye watu na katikati kuna meza ya waongoza mjadala.







    Tofauti ni kwamba hawa wao meza yao iliyopo katikati ilikuwa kubwa na ndefu ambayo ila upande wa meza kulikuwa na viti vitatu walivyoketi watu na mbeleni kabisa mwisho wa meza kulikuwa na kiti kimoja alichoketi mtu aliyeonekana kama kiongozi wao na mwisho ya upande mwingine wa meza kulikuwa na kiti tupu ambacho hajakaa mtu yeyote.







    Pia kwenye vile viti vya pembeni vya kila upande, upande wa kushoto kulikuwa na viti vipatavyo 19 vyote wameketi watu na upande wa kulia kulikuwa na viti 19 vingine lakini ni viti 14 tu ambavyo walikuwa wameketi watu.











    Wale watu sita walipoingia na sanduku walilobeba, moja kwa moja wakaelekea mpaka karibu kabisa na ile meza kati kati.



    Watano kati ya wale sita wakaenda kuketi upande wa kulia kwenye vile viti vilivyowazi na mmoja wao yule ambaye alikuwa anatangulia mbele muda wote alienda kuketi kwenye kiti kimoja kilichobakia pale mezani.







    Baada ya hawa waliowasili kuketi na wengine nao wote wakakaeti.











    Kisha mzee ambaye alikuwa ameketi mbele kabisa ya meza ambaye alionekana kama kiongozi wa wote waliomo humu ndani, akiwa amevalia suti nyeusi sana na akiwa na upara kichwani, aliinuka na kuanza kuzungumza.







    “Viongoziii.!” Akawasalimia







    “Kiongoziii.!” Wakamuitikia salamu.











    Kisha akaanza kuongea.











    “Viongozi wenzangu wa *The 46*, hatimaye tumeifikia siku ya leo ambayo kwa karne kadhaa tumekuwa tukiitamani.. Siku ambayo tutaweza kurudisha kilicho chetu ambacho binadamu walitudhurumu kwa karne nyingi, siku ambayo tunaenda kuanza kuirudisha dunia kwa *The 46*”







    Akanyamaza kidogo na kuangalia kushoto kisha kulia. Kisha akaendelea.











    “Ulimwengu wote ni mchanga.!”







    Akachota mchanga uliopo kwenye bakuli pembeni yake pale mezani na kuumwaga juu ya meza. Kisha akaendelea kuongea.



    [22:54, 3/30/2017] ?+255 718 096 811?: “Ulimwengu wote ni maji!”







    Akachota maji kwa kiganja kutoka kwenye bakuli nyingine pembeni yake na kumwaga juu ya meza.











    “Ulimwengu wote ni damu”







    Akachota damu kutoka kwenye bakuli nyingine pembeni yake na kumwaga juu ya meza. Kisha akamalizia.











    “Hatuwezi kusahau, hatuwezi kusamehe udhalimu tuliofanyiwa karne zote hizi.. Leo tunarudisha kilicho chetu kwa halali, tunairudish dunia kwa *The 46*!! Mleteni hapa..” Akamalizia kuongea.











    Wale watu saba wengine walioketi pale mezani wakainuka na kwenda lilipo lile sanduku lililoletwa.











    Wakalifungua sanduku, na kutoa kilichomo ndani.



    Mzigo ambao ulikuwa umebebwa na watu wale kuileta hapa ulikuwa ni binadamu.







    Wakambeba na kumlaza juu ya meza. Kisha wakafunua shuka nyeupe aliyokuwa amefunikiwa.







    Binadamu huyu aliyeletwa kutoka maelfu ya kilomita na wale watu sita alikuwa ni *Bi. Laura Keith*, Rais wa Marekani.



    Bado alikuwa hai, japo alionekana alikuwa taabani kutokana na kupumua juu juu kwa shida sana.















    Yule mzee kikongwe kiongozi wao akatabasamu na kuwaangalia wenzake.







    THE OTHER HALF















    EPISODE 4























    “…katika maisha si lazima kufanya jambo sahihi muda wote. Muhimu zaidi ni kujitahidi kadiri uwezavyo kutimiza unaloliamini… Japokuwa ulimwengu mzima kila upande, kila bara, kila nchi imekuwa na imani yake na kujitahidi kufanya ya kwake wanayoona sahihi na hatimaye kutengeneza utengano, lakini pale ulimwengu mzima unapopambana na adui mmoja, tishio moja, na tunapolia kilio kimoja… huu ndio muda ambao ulimwengu mzima uinuka na kuwa na imani moja, huu ndio muda ambao nguvu iliyopo katika roho ya binadamu udhihirika… tunapopambana wote kwa pamoja, mwishoni mwa vita si sahihi kujiuliza kama tumeshinda au tumeshindwa, jambo la msingi zaidi ni kuhakikisha tunaacha alama juu ya uso wa dunia, ili karne kadhaa zijazo, wataokuwepo wajue sisi tulikuwa ni akina nani, na kwa ushujaa gani tulipambana kutetea Dunia..!”



























    WASHINGTON, D.C: WHITEHOUSE











    Watu wote waliokuwepo Whitehouse ndani ya Situation Room walikuwa wamebaki na mshangao baada ya kuyasikia maelezo ya mzee Caleb.



    Wate walikuwa wamepigwa na butwaa wasiamini kile ambacho walikuwa wamekisikia. Walichoelezwa kilikuwa kama kisa cha hadithi ya kusadikika ambayo haiwezekani katika maisha halisi.



    Lakini kwa kuzingatia jinsi matukio yaliyokuwa yanatokea duniani haikuwa ngumu sana kwao kuamini hiki walichoelezwa.















    Mzee Caleb alikuwa amewasimulia kisa cha zaidi ya miaka elfu kumi iliyopita. Kisa kilihusu uwepo wa kisanduku kinachoitwa Pithos ambacho kilitengenezwa na Mungu wa Kigiriki aliyeitwa Zeus.











    Hadithi hii karibu kila mtu duniani alikuwa amewahi kuisikia lakini hakuna mtu ambaye aliwahi kuiamini. Watu wote waliichukulia kama simulizi tu za kale za kusadikika. Ni mpaka dakika hii baada ya mzee Caleb kuwapa maelezo ya kutisha kuhusu simulizi hii walau kulikuwa na watu kadhaa ndani ya situation room ambao walianza kuamini uhalisia wa hadithi hiyo.















    Mzee Caleb aliwaeleza kwamba, Mungu Huyo wa Kigiriki, Zeus alikuwa amechukizwa sana na wanadamu ambao kwa kipindi hicho wote walikuwa ni wanaume. Ndipo hapa akamtengeneza mwanmke wa kwanza duniani na kumpa jina la Pandora (likimaanisha “aliyejaliwa kila kitu”). Mwanamke huyu alipewa uzuri usio kifani na ushawishi na mvuto wa kipekee kwa wanaume. Pia Mungu Zeus alimpa mwanamke huyu zawadi ya sanduku ambacho alimuamuri kamwe asikifungue. Ssanduku hiki kilikuwa kimejaa chupa ambazo Mungu Zeus alizijaza kila aina ya udhalimu na ufedhuli uliopo duniani. Na kadiri ambavyo sanduku hili litabakia limefungwa basi dunia itabakia kuwa salama pasipo kushuhudia kiwango kikubwa cha tishio, ukatili au ufedhuli.















    Akamsisitiza sharti moja muhimu, kamwe asifungie sanduku hili.















    Mzee Caleb akawaeleza kuwa baada ya kufariki kwa mwanamke Pandora, sanduku hili limekuwa likirithishwa kwa siri kubwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.







    Kwa zaidi ya miaka elfu mbili sanduku hili lilikaa sehemu ya siri nchini Ugiriki.



    Baadae katika kipindi cha utawala wa mfalme Alexander, akalipeleka sanduku hili nchini Misri ambapo lilikaa hapo kwa Karne kadhaa. Baadae yakatolea matukio na sanduku hili likaenda kuhifadhiwa nchini Israel katika hekalu la mfalme Suleiman.







    Baada ya hekalu la mfalme Suleiman kubomelewa baada ya kutamalaki kwa dola ya Rumi, sanduku hili likaenda kuhifadhiwa Vatican katika makazi ya Papa wa Kanisa Katoliki ambapo lilikaa hapo kwa karne nyingi mpaka kufikia karne ya 16 miaka ya 1550 mji wa Vatican ulipovamiwa na kubomolewa kwa kuchomwa moto Sanduku hili lilipotea na halikuwa kuonekana tena.











    Mzee Caleb akawaeleza kuwa inasemekana kwamba sanduku hili lilikuja kugunduliwa na maharamia wa kimarekani katika bahari ya Atlantiki mahali fulani baharini miaka ya 1780 na waliloligundua baada ya kulijua ni sanduku la Pandora wakaenda kumkabidhi Rais wa kwanza wa Marekani, George Washington.



    George Washington akalificha sanduku hili mahali ambapo ni yeye pekee anajua lilipo na akamtumiachoraji kuchora Picha yake na kuiwekea alama kadhaa za mafumbo ambayo yanamuwezesha mtu kung’amua Sanduku lilipo.











    Mafumbo haya ya kwenye mchoro, Rais George Washington alimrithisha siri hii Rais aliyekuja kumrithi John Adams, ambaye naye alipoondoka madarakani akamrithisha siri hii Rais aliyemfuatia Thomas Jefferson, na yeye Jafferson alipoondoka madarakani siri hii akamrithisha Rais James Madison na desturi hii ya kurithishana siri hii imeendelea hivi kwa kila Rais wa Marekani vizazi na vizazi mpaka Rais wa sasa Bi. Laura Keith.















    Chumba kizima cha Situation Room kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa mshagao na hofu kwa takribani dakika kumi nzima hakuna aliyekohoa wala kujisogeza kwenye kiti. Kila mtu alikuwa kwenye ombwe la mawazo na tafakari kuhusu hiki walichokisikia kutoka kwa mzee Caleb.















    “Kwahiyo hayo matukio yanayotokea duniani kote yanahusiana nini na Sanduku hili la Pandora au sijui Pithos… sijaelewa utofauti wake.!” Hatimaye Makamu wa Rais David Logan akavunja ukimya.















    “Majina yote mawili ni sawa tu, Jina la ‘Sanduku la Pandora’ ndilo limezoeleka katika historia, lakini Zeus mwenyewe alivyomtengeneza mwanamke Pandora na kumpa zawadi ya lile sanduku aliliita jina ‘Pithos’.! Na nikijibu swali lako sanduku hili linahusiana nini na kinachotokea sasa duniani…. Ni kwamba naamini wale wavuvi nchini Maldives waliookota ile chupa na kuifungua, ile chupa imetoka kwenye sanduku la Pandora… na haikupswa kufunguliwa.. shida imeanzia hapo.!”







    Mzee Caleb akajibu.















    “Kwahiyo unamaanisha kwamba hiyo sehemu ambayo George Washington alificha hilo sanduku imegunduliwa na sanduku halipo?”







    Akauliza Bi. Naomi Cole, mshauri wa Rais kuhusu usalama.















    “Hakuna anayeweza kujua ni nini kimetokea na kama sanduku limepota au kuondolewa sehemu iliyohifadhiwa… ila ninachoamini ni kwamba ile chupa imetoka kwenye Pithos, lile sanduku la Pandora.. Na hii inamaanisha kwamba limefunguliwa… Namna pekee tunavyoweza kujinusuru na kinachoendelea duniani kote ni kutafuta mchoro uliopotea wa George Washington ili tuweze kufika sehemu Pithos ilipo na kuirejesha kwenye hali ya kawaida..!” Mzee Caleb akaongea kwa msisitizo mkubwa.



















    “Ile chupa iliyookotwa na wavuvi kutoka Maldives iko wapi?” Jemedari George Smith akauliza.











    “Inafanyiwa utafirti Stanford University idara ya Akiolojia.!” Mkurugenzi wa CIA, James Ruppert akajibu.











    “Hii chupa ilikuwa na nini ndani yake?” Mzee Caleb akauliza.











    “Ndani ilikuwa na karatasi tu yenye maandishi ya kale mno ya kilatini… neno pekee ambalo tuliweza kulielewa kwenye hiyo karatasi ni ‘Novus Ordo Sedorum’ ikimaanisha ‘The New Order Of Ages’!” Mkurugenzi wa CIA, James Ruppert akaeleza.











    Mzee Caleb akashituka kweli kweli.











    “Kwanini hamkuiweka hii taarifa kwenye vyombo vya habari, kuhusu hiyo karatasi ni hayo maneno?” Caleb akauliza kwa mshangao mkubwa.











    “Ni ngumu kueleza umma kila kitu, taarifa nyingine muhimu ni lazima zibakie kuwa siri… vipi kwani mzee mbona umeshituka sana?” Ruppert akuliza.















    “Nahitaji kuiona hiyo karatasi.!!” Mzee Caleb akaongea kwa hofu na kupaniki huku anainuka.











    “Oooh samahani mzee! Tueleza nini unafikiria?” Makamu wa Rais akauliza.











    “Mheshimiwa, nimesema nahitaji kuiona hiyo karatasi sasa hivi!!” Mzee Caleb akaongea kwa msisitizo huku ametoa macho.















    Bila maelezo zaidi wote wakainuka na kuanza kutoka nje. Katibu Mkuu kiongozi mara moja akawajulisha watu wa Secret Service kuaandaa chopa ya Rais Marine One kwa ajili ya kuelekea Stanford University.











    Dakika kama tano baadae wote walikuwa mbele ya Marine One.











    “Mheshimiwa, sidhani kama kuna ulazima wa wewe kuongozana nasi… ni vyema ukiendelea na majukumu mengine hasa zoezi la kumtafuta Rais! Tuache sisi tuendelee na hili na kisha tukueletee mrejesho!” Ruppert akajaribu kumshawishi Makamu wa Rais abaki.















    “Acha kupoteza muda.. Let’s gooo!” Makamu wa Rais akajibu kana kwamba hajasikia kilichoongelewa na Mkurugenzi wa CIA na akaamuru wengine wote wapande kwenye chopa na kuondoka.











    Wote wakapanda, Makamu wa Rais, Mzee Caleb, Katibu Kiongozi Kevin, Bi. Naomi Cole na Mkurugenzi wa CIA James Ruppert.











     http://pseudepigraphas.blogspot.com/







    Muda si mrefu Marine One ilitua chuo Kikuu cha Stanford.











    Baada ya kuwasili, moja kwa moja wakaongozwa na Secret Service mpaka kwenye Jengo la Idara ya Akiolojia.







    Na walipofika hapa wakaongozwa moja kwa moja mpaka kwenye maabara inayotumia kuhifadhi vitu vya kale.











    Makamu wa Rais na msafara wake walipoingia ndani ya maabara hii waliwakuta wenyeji wao, wataalamu wa Akiolojia wanawasubiri, lakini ajabu ni kwamba walikuwa na hofu kubwa kwenye nyuso zao.











    Baada ya kusalimiana nao Makamu wa Rais akaanza kuongea.











    “OK! Nadhani mnafahamu kwanini tuko hapa?? Tunahitaji kuona chupa ambayo iliokotwa na wavuvi nchini Maldives na hasa hasa tunahitaji kuona karatasi ambayo ilikutwa ndani yake.!” Makamu wa Rais, David Logan akaongea.















    “Mr. Vice President nasikitika kukwambia kuwa chupa hiyo wala karatasi yake hatunayo?” Mtaalamu mmoja aliyevalia miwani kubwa ya macho akaongea kwa woga na heshima kubwa.















    “Nini??? Imeenda wapi?” Makamu wa Rais akauliza kwa hasira.















    “Chupa huwa inahifadhiwa kwenye jokofu hili hapa la chini ya sentigredi za selsiasi -18 ili ibakie kwenye hali yake ya asili… lakini leo tulivyoambiwa kuwa unakuja kwa ajili ya chupa hii.. Tulipoitoa chupa kwenye jokofu ili tuiandae upate kuiona, tukagundua kuwa chupa iliyomo ni feki.. Imebadilishwa.. Na tunaamini ni mmoja kati yetu kwenye idara ndio amefanya hilo!” Yule mtaalamu akajieleza.















    “Ni nani? Na amefanya hivyo kwa dhamira ipi?”















    “Tunaamini ni Dr. Cindy Wheaton amefanya hivi… yeye ndiye alikuwa in charge kwa chupa hii na kuongoza tafiti.!”















    “Yuko wapi?” Makamu wa Rais akauliza kwa hasira.















    “Ameenda Tanzania wiki ya Tatu hii sasa… ameenda kufanya tafiti kuna miji mitatu nchini humo imetwaliwa na kuwa Anabelle.!”















    Alipoongea sentesi hii mzee Caleb alishituka na kuishiwa nguvu mpaka kukaa chini.















    “No no no no.! Siamini kama anataka kufanya ninachokiwaza… no no.! Tafuteni mawasiliano naye haraka niseme naye!!” Mzee Caleb akaongea huku anakaa chini kwa hofu na kunyong’onyea.















    “Ni nini mzee?” Ruppert akauliza.





    THE OTHER HALF























    EPISODE 5



























    “…kila tendo ambalo tunalifanya, linatuma mawimbo ya mwitikio katika Dunia. Haijalishi tendo hili tunalolifanya ni dogo kwa kiasi gani. Pia kila neno tunalotamka lina uwezo wa kuleta athari chanya ama hasi kwa wale wanaotuzunguka. Leo hii mwanaume wa kawaida ataongea si chini ya maneno elfu saba kwa siku na mwanamke ataongea si chini ya maneno elfu ishirini. Lakini ni neno moja tu, au sentesi moja tu ina uwezo wa kubadili mwelekeo wa Dunia.!”



































    Maeneo fulani nchini Tanzania karibu na palipokuwa na mji wa Dar es Salaam











    Timu ya wataalamu iliyokuwa inaongozwa na Salim, pamoja na kikosi maalumu cha jeshi walikuwa wamesafiri zaidi ya masaa kumi kutoka katika wilaya ya Ruangwa mpaka kufika Morogoro na baadae kuelekea maeneo karibu kabisa na Chalinze.











    Kuanzia Morogoro walikopita mpaka hapa Chalinze, idadi ya watu ilikuwa ni kubwa kweli kweli na mvurugano ulikuwa mkubwa sana. Kulikuwa na purukushani nyingi sana kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wamekimbia mji wa Dar baada ya kutolewa taarifa ya mji huo kuonyesha dalili kuwa unaelekea kutwaliwa.











    Mji mzima wa Morogoro na vitongoji vyake ulokiwa umetawaliwa na purukushani na msongamano wa watu kama vile sokoni. Kelele zilitapakaa kwenye anga lote, kila kona watu walikuwa wanahaha na mabegi ya nguo na vyombo vya majumbani. Taharuki ilikuwa ni kubwa mno, kila kona unayotazama watu walikuwa wanakimbia au kutembea kwa haraka kuelekea mbali wawezavyo na mji wa Dar.











    Salim na timu ya wataalamu wenzake walikuwa wameendesha magari moja kwa moja kuelekea karibu na Chalinze ambako kulikuwa na kituo maalumu kilichokuwa kinaandikisha watu walikuwa wamefanikiwa kutoka ndani ya jiji la Dar kukimbilia Morogoro. Mpaka muda huu ambao ulikuwa unapata saa kumi na moja jioni tayari jiji la Dar lilikuwa limeshatwaliwa na kufanywa Anabelle 27. Pia Ruangwa nayo waliyokuwa wameikimbia masaa machache yaliyopita tayari nayo ilikuwa imegeuzwa Anabelle 29. Kulikuwa na mji mwingine nchini Nigeria nao ulikuwa umegeuzwa kuwa Anabelle 28.















    Lengo la Salim na wenzake kuja mpaka huku Chalinze kwenye kituo cha kuandikisha waliofanikiwa kukimbia Dar kabla ya kutwaliwa ni ili waweze kujua idadi ya watu waliobakia ndani ya Dar, lakini kwa Salim yeye hasa alikuja hapa ili kujua kama familia yake, mkewe kipenzi Khadija na roho yake, binti yake kipenzi Basrat walifanikiwa kukimbia Dar kabla haijatwaliwa.











    Kituo chenyewe ambacho kilikuwa kinaandikisha watu, kilikuwa kimewekwa kwenye jengo fulani hivi la muda lililotengenezwa kwa mahema ya kijeshi. Alafu barabarani ukawekwa uzio wa geti dogo la mlingoti wa chuma ambao ulikuwa unafunguka kwenda juu na chini ili kuruhusu watu kupita.











    Uandikishaji uliokuwa unafanyika haukuwa na kuandikisha kwenye daftari. Teknolojia ilikuwa imekua haswa mwaka huu 2038, watu walikuwa wanaandikishwa kwa mfumo wa teknohama ya kibaiolojia.



    Yaani kulikuwa na wanajeshi pale kwenye kituo cha uandishaji waliobeba vifaa fulani hivi vyenye umbo kama linalokaribia kufanana na bastola lakini kifaa chenyewe kina vikolombwezo vingi zaidi. Kifaa hiki walikiita B-punch (au B-gun).











    Chenyewe kilifanya kazi katika mtindo ambao mtu anayepita anampa mkono afisa wa jeshi mwenye kifaa hiki, kisha afisa huyo anaelekeza mdogo wa kifaa kama sindano hivi kwenye mkono wa muhusika kisha anamchoma kumpandikizia kidude kidogo kinaitwa MMA B-Chip (Miniaturized Microarrays Biological Chip).







    Kitu hiki (MMA B-chip) ambacho kinapandikizwa kwa muhusika ni kidogo mno labda chenye ukubwa wa punje mbili za mchanga. Lakini kifaa hiki kinasoma taarifa za kiafya na ‘identity’ ya muhusika na kutuma taarifa hizo kwenye system ya taarifa za serikali.











    Zoezi hili la kupandikiza kidude hiki linadumu kwa kama sekunde tano tu, kwa hiyo kwa dakika moja afisa wa jeshi anaweza kuandikisha zaidi ya watu ishirini kwa mfumo huu.











    Baada ya Salim na wenzake kufika eneo hili walipaki magari yao mahali fulani karibu na kituo hiki na kisha Salim na Kanali wa kile kikosi cha kijeshi kinacjowalinda wakaongozana kuelekea kile kituo kilipo.











    Wakaelekea moja kwa moja mpaka kwenye upande wa ofisi za kituo hiki cha uandikishaji na walipofika kanali akaomba aelekezwe aonane na afisa Mkuu wa kijeshi aliyepo kituoni hapo kama kiongozi wa hawa wanajeshi wote wanaoandikisha watu.











    Wakapelekwa moja kwa moja kwenye hema fulani kubwa lililojitenga pambeni na kuingia ndani. Humu palikuwa pameangiliwa kama ofisi ya kabisa na kulikuwa na afisa wa kijeshi Brigedia Jenerali Samson Mwambusi ambaye alikuwa anaongoza zoezi hili la kijeshi kuandikisha raia waliofanikiwa kuondoka ndani ya jiji LA Dar es Salaam.











    Baada ya kuingia ndani ya hema lake hili LA ofisi na kupeana salamu zao za kijeshi na kisha kuketi wakaanza mazungumzo.











    “Mkuu mimi ni Kanali Robert Shamte, kiongozi wa Team 5C inayowalinda wataalamu wanaofanya tafiti katika maeneo yaliyotwaliwa… huyu mwenzangu anaitwa Salim Kawambwa ni kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na ndiye kiongozi wa timu hiyo ya wataalamu.!”







    Kanali akajitambulisha na kumtambulisha Salim.











    “Nafahamu taarifa zenu kanali, tena kuna maagizo yenu hapa.!” Meja Mwambusi akaongea.











    “Maagizo gani mkuu?” Kanali akauliza.











    “Naomba niwasikilize kwanza nyinyi.!” Meja akajibu.











    “Mkuu, sisi tulikuwa na masuala machache tu kwanza kama hutojali utupe mihtasari wa zoezi zima la evacuation.!” Salim akauliza.















    “Mpaka sasa ni watu milioni tatu pekee ndio tunahakika wametoka ndani ya Dar es Salaam kabla haijatwaliwa… hii ina maana kwamba watu milioni nne waliosalia wamepotea ndani ya jiji baada ta kutwaliwa… pia nusu ya baraza la mawaziri nao wamepotea ndani ya mji… kabla jiji halijatwaliwa tulifanikiwa kumuondoa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu na nusu ya baraza la mawaziri… wamehifadhiwa Kwenye kambi ya jeshi hapo Kizuka, Ngerengere..”







    Meja akawaeleza kwa ufupi. Ukapita ukimya kama wa dakika mbili hivi.











    “Nilikuwa na ombi kidogo Meja.!” Salim akaongea kwa unyonge.











    “Ndio?”











    “Naona uwaambie vijana wako waangalie kwenye orodha ya watu waliofanikiwa kutoka kwenye jiji… waangalie kama kuna Khadija Kawambwa na Basrat Kawambwa..!” Salim akaongea kwa huzuni.











    “Ni familia yako hii?” Meja akauliza.











    “Ndio mkuu.!”















    Kisha Meja akanyanyua simu ya upepo iliyopo pale mezani na kuanza kumpa maagizo afisa anayehusika na kumbukumbu kuangalia taafifa hizo za hayo majina.







    Akasubiri kwenye simu kama dakika Tatu hivi kisha akaiweka chini.











    “Salim! Pole sana… Hatuna hayo majina kwenye orodha… kuna uwezekano hawakufanikiwa kutoka ndani ya jiji kabla ya kutwaliwa.!” Meja akaongea kwa sauti ya huzuni.











    Salim hakujibu chochote. Akajiinamia tu chini kwa uchungu.











    “Mkuu umeeleza pia kuna maagizo yetu hapa!” Kanali akahamisha maongezi na kukumbushia suala aliloongea Meja mwanzoni mwa Mazungumzo yao.











    “Ndio! Kuna maagizo yenu hapa… ni kuhusu Dr. Cindy Wheaton.!” Meja akaongea.











    Wote wakamuangalia kwa mshtuko. Hata Salim aliyekuwa amejiinamia akainua uso.











    “Amefanyaje?” Salim akauliza huku bado akiwa na sauti ya huzuni kama analia.











    “Kuna taarifa kutoka nchini kwake Marekani, kuna ndege ya kijeshi inakuja kumchukua ndani ya masaa machache yajayo.. Tunatakiwa kumsafirisha muda huu mpaka uwanja wa ndege wa kijeshi Morogoro..!”







    Meja akaongea kwa udadisi kuona akina Salim watasemaje.











    “Wamewaeleza kwanini wanataka kumrudisha haraka hivyo?” Salim akauliza.











    “Hapana hawajasema… ndio maana bosi wako wa Mkurugenzi wa Usalama anahitaji uhakikishe kabla hajaondoka ufahamu kwanini wanataka kumrudisha kwa haraka namna hiyo!”















    Kuna hisia Fulani mbaya na hasira Salim akaanza kuzipata. Akajikita anainuka kutoka kwenye kiti na kuanza kutoka nje kwa hasira.











    Hasira hizi zilikuwa zinampanda baada ya kukumbuka kauli ya Magdalena walipokuwa wanatoka Ruangwa, “nahisi kuna kitu Cindy anakijua ila anatuficha.”http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Hasira zilimpanda zaidi akifikiria kuwa familia yake, kitu pekee chanye thamani kubwa kwenye maisha yake, mkewe Khadija na mtoto wake Basrat wamebaki na kupotea ndani ya Dar baada ya kutwaliwa, lakini kuna mwenzao inawezekana anaijua siri fulani na hataki kuwaambia na sasa nchi hake wanataka kumrudisha kwao kwa dharura kiasi hiki.



    Hasira zilimpanda haswa.















    “Yuko wapi?” Salim akauliza kwa hasira mara tu baada ya yeye na kanali kurejea pale walipopaki magari na kuwaacha wenzao wengine.











    “Nani?” Magdalena akamuuliza.















    “Cindy! Yuko wapi?” Akauliza tena kwa hasira huku anatetemeka.















    “Oooohh no!! Nini kinaendelea tena? Umepata taarifa kuhusu Khadija na Basrat?” Magdalena akauliza swali lingine baada ya kujibu swali.















    “Nimeuliza Cindy yuko wapi?” Salim akauliza kwa sauti kubwa ya hasira.















    “Amechukua gari moja ameelekea Dar?” Magdalena akajibu kwa uoga.











    “Mnasemaje? Ameenda dar?? Mmemruhusu vipi? Haumjui kuwa dar imeshageuzwa kuwa Anabelle?? Huyu Cindy amechanganyikiwa?” Salim akaongea kwa kufoka huku anampa ishara Kanali wapande kwenye gari.











    Wote wakapanda kwenye magari na kwa kasi wakaanza kuelekea barabara inayoenda Dar es salaam kumuwahi Cindy wajue mpango wake kabla hajafanya kitu cha ajabu na kisha wamkamate kumpeleka Morogoro na ambako ndege ya jeshi la Marekani ilikuwa inakuja kumchukua.











    “Vipi kuhusu Khadija na Basrat?” Magdalena akamuuliza Salim kwa Upole wakiwa wanakaribia kabisa kupiga Mlandizi.















    “Hawakufanikiwa kutoka!” Salim akajibu kwa mkato akiwa serious kuzuia hisia zake asilie mbele za watu.











    Magdalena akashindwa kusema chochote kumfariji, akamuwekea tu mkono begani na kumpapasa kwa ukarimu wa kumfariji.











    Ukaribu ambao Magdalena aliujenga kwa Salim na jinsi alivyokuwa anamjali, ilitoa hisia kwa wengine labda Magdalena ana hisia fulani za kimapenzi kwa Salim. Alikuwa anamjali kupitiliza kuzidi namna ambavyo rafiki anapaswa kumjali rafiki yake.











    Dakika kumi na tano baadae walikuwa wamepita Kibaha maili moja, na kwa mbali wakaanza kuiona gari ambayo Cindy aliitumia kuondoka nayo.







    Wakaendesha mpaka pale ambapo gari ya Cindy ilikuwa imepaki. Wakashuka wote.











    “Cindy! Unafanya nini hapa?” Salim akaongea kwa hasira kuelekea aliposimama Cindy.











    “Nataka kuingia ndani ya Anabelle!” Cindy akajibu bila kumuangalia Salim.











    Akikuwa anafunga zipu ya jaketi zito alilokuwa wamemkuta analivaa.











    “Umechanganyikiwa au? Unajua kuwa ukiingia humo ndio umepotea na hautotoka kamwe?” Salim akafoka.











    “Najua!” Cindy akajibu kwa ufupi.











    “Cindy ni vyema utueleze kilichomo kichwani mwako ambacho hatukijui?”











    “Nadhani nimefahamu masuala machache ya msingi kuhusu Anabelle namna gani ya kuingia na kutoka ukiwa hai… Sina hakika na ninachokiwaza lakini nataka kujaribu.!” Cindy akaongea akiwa emaliza kufunga zipu ya jaketi na kiwaangalia.











    “Umegundua nini?” Salim akauliza kwa shauku.











    “Siwezi kukuambia labda ukiongozana na mimi kuingia!”











    “Siwezi kufanya ujinga wa kiasi hicho!” Salim akafoka.











    “Salim nikuulize kitu? Mke wako na mwanao walifanikiwa kutoka?”











    “Hapana!” Salim akajibu kwa uchungu.















    “Hiyo inamaana kwamba wako mle ndani… unaweza ukajaribu kuwasaidia au unaweza kuendelea kuwa muoga kama kunguru!” Cindy akaongea huku anaonyesha kidole kuelekea muelekea ulipo jiji la Dar, Anabelle mpya kutwaliwa.











    Mita chache kutoka waliposimama kulikuwa na ufa ardhini ulioashiria mpaka wa Anabelle na ulimwengu.















    “Cindy Siwezi kukuruhusu uingie humo… nina amari ya kukurejesha Morogoro ili upelekwe kwenu Marekani.!” Kanali akaingilia maongezi.











    Cindy akainama chini kwenye mkoba wake wa mgongoni na kutoa Chupa. Chupa ile ambayo aliichukua kutoka Chuo Kikuu cha Stanford.











     “HIKI NDICHO WANACHOHITAJI… HII CHUPA! KANALI UNAWEZA KUNIPIGA RISASI, LAKINI SIWEZI KURUDI WALA KUKUKABIDHI HII CHUPA… NAINGIA SASA NDANI YA ANABELLE, SALIM NADHANI NI VYEMA UKIONGOZANA NAMI… NADHANI NAFAHAMU NI NAMNA GANI TUNAWEZA KUTOKA SALAMA… SINA UHAKIKA… LAKINI NI VYEMA KUJARIBU KUELEWA KINACHOENDELEA NDANI YA HIZI ANABELLE BAADA YA SAA KUMI KUPITA KULIKO KUKAA TU NA KUSHUHUDIA ULIMWENGU MZIMA UNATEKETEA KWA KUTWALIWA MBELE YA MACHO YETU…”











    Cindy akaongea huku anageuka na kuanza kutembea kuelekea kwenye ule Ufa ardhini kutenganisha Anabelle na ulimwengu.















    “Shit!” Salimu akaongea kwa hasira na kuanza kutembea kumfuata Cindy.















    “Salim unafanya nini?” Magdalena akahamaki na kumshika mkono.











    “Magdalena, familia yangu iko humo ndani… kama kuna lolote naweza kufanya kuwaokoa niko tayari hata kama inahatarisha maisha yangu.!”















    “Na mimi nakuja!” Magdalena akaongea kwa hofu karibu machozi yadondoke.











    “Hakuna ulazima wa wewe kuja Magdalena!”











    “Salim! Kama unaingia humo kwenye Anabelle na mimi nakuja… na huwezi kunizuia! Nakuja” Magdalena akaongea kwa hisia huku anahema kwa hofu.















    “Yeyote anayekuja achukue jaketi zito la Baridi!” Cindy akaongea akiwa amesimama pembeni mwa ufa pale ardhini.















    Magdalena na Salim wakafungua milango ya gari na kuchukua majaketi mazito ya baridi.







    Wakashangaa kumuona kanali na Shafii yule mtaalamu wa Vinasaba nao wanachukua majaketi.











    Salim hakuongea chochote. Akatikisa kichwa tu.



    Wote wanne wakatembea mpaka pale Cindy aliposimama.











    Aliyebaki alikuwa ni Goodluck, yule afisa polisi na wanajeshi wengine waliosalia wa Team 5C.











    “Wakuu, sisi tunaingia ndani ya Anabelle… mkiona siku zinapita na tuko kimya nadhani nadhani mnafahamu nini ambacho kitakuwa kimetupata… tuombeeni kheri! Kwaherini.!”







    Kanali akaongea na Goodluck na wanajeshi amabo walikuwa wanabakia.











    Hii ilikuwa tayari inakaribia kabisa majira ya saa moja jioni. Muda huu ulimaanisha kwamba “wakazi” wa Anabelle watakuwa wameshaamka… Kwasababu muda Salama wa kuingia ndani ya Anabelle kwa binadamu ni saa kumi jioni.











    Kwahiyo, majira haya ya saa moja jioni, Cindy, Salim, Magdalena, Shafii na Kanali walivuka ule ufa wa mpaka ardhini na kuingia ndani ya Anabelle.















    Walitembea kwa takribani nusu saa nzima mpaka wakaanza kufika mwanzoni mwa mitaa na majumba ya hii Anabelle ambayo masaa machache yaliyopota ilikuwa ni jiji la Dar Es salaam.



    Kadiri walivyokuwa wanaingia ndani ya Anabelle ndivyo ambavyo baridi lilikuwa linaobgezeka.



    Majengo yote yalikuwa makuu kuu kama vile ni mji uliotelekezwa karne nyingi zilizopita. Giza lilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba walikuwa hawaoni hata barabara wanayokanyaga. Pia ukimya nao ulikuwa ni mkubwa na wa kutisha.











    Nyumba zilikuwa na mwanga fulani madirishani kana kwamba ndani kuna taa za chemli au moto umewashwa.











    Pia kadiri walivyokuwa wanaenda ndani ndani mwa mitaa ya Anabelle, ndivyo ambavyo chupa yenye karatasi ambayo Cindy aliishika mkononi ilikuwa inabadilika na kuwa rangi ya blue iliyoiva sana.











    Ghafla ule ublue wa chupa ukakolea zaidi na moshi ukaanza kutoka kwenye chupa.



    Katika zile ngumba kuu kuu za mitaa ya Anabelle, madirishani vikaanza kuonekana kwamba vivuli vya watu na sauti kama simba wengi wanaunguruma taratibu kwa sauti ya chini.















    Cindy, Salim na wenzao wakasimama ghafla kwa woga wakitazama huku na huo sauti zile za muungurumo zinapotokea.















    “Cindy, nadhani huu ndio muda sasa utueleze hizo siri zako kabla hivyo viumbe vinavyo unguruma havijatufikia.!”







    Magdalena akaongea kwa sauti ya kutetemeka kwa woga mkubwa.





    THE OTHER HALF



























    EPISODE 6























    “…upo muda ambao ukiutazama ulimwengu, ukiitazama dunia na historia yake… unajiuliza kama tumejifunza kitu chochote kutokana na yaliyotokea.! Jambo la msingi na lenye ukweli zaidi, ni kwamba japo tunapita katika magumu yaleyale yanayofanana, lakini unapofikia muda wa kuondoka hapa duniani kila mtu anakufa peke yake. Kila mmoja anaondoka katika hali ya upweke…. Lakini…. Kama yuko mtu hata mmoja tu ambaye ana maana kubwa katika maisha yako, kama yuko mtu umewahi kumuinua, kama yuko mtu walau hata mmoja ambaye atakukumbuka kila siku baada ya wewe kuondoka.… huwezi kufa kamwe…. Hata utakapoondoka duniani…. Utaendelea kuishi milele…”



























    EPISODE 6























    Ndani ya Anabelle 27 (uliokuwa mji wa Dar es Salaam)



















    Wote watano, Cindy, Salim, Kanali, Magdalena na Shafii walikuwa wamesimama wakiangalia vile vivuli vya watu vilivyokuwa kwenye zile nyumba ndani ya Anabelle.



    Baridi lilikuwa ni kali kweli kweli, na giza lilikuwa nene haswa, hii ilifanya ule mwanga ndani ya zile nyumba kuonekana kwa uzuri zaidi na kuvifanya vivuli vya watu madirishani kuwa dhahiri kabisa.











    Ule muungurumo wa sauti ya taratibu kama simba ulizidi kuwasogelea kadiri muda ulivyoenda.











    “Cindy!” Salim akaita kwa sauti ya chini ya woga. “Cindy, tutapotezwa sasa hivi!”











    “Ssssshhhh! Nyamaza.!” Cindy ananong’ona.



    “Msisogee hata hatua moja.!”







    Cindy akaongea huku akimvuta Magdalena pembeni, kwahiyo yeye na Magdalena wakawa wesimama kando kama hatua tano hivi pembeni ya Kanali, Shafii na Salim.











    “Msisogee hata hatua moja” Cindy akawasisitiza tena Salim, Shafii na Kanali.











    Ile sauti kama simba anayeunguruma taratibu ilizidi kusogea karibu. Ilifika karibu kiasi kwamba ilikuwa kama vile inatoka hatua tatu tu kutoka pale waliposimama akina Salim.







    Walikuwa wanatetemeka kiasi kwamba jasho lilikuwa linakaribia kuwatoka licha ya baridi kali lililopo ndani ya Anabelle.



    Walikuwa wanatamani kama vile mwanga utokee, giza liondoke waone hicho kinachounguruma karibu yao.







    Muungurumo wa hicho kiumbe ulikuwa kama simba kabisa, lakini ulikuwa unatoka katika sauti fulani ya chini sana hali iliyofanya kuogofya zaidi maana ilikuwa kana kwamba kiumbe hicho kimekasirika kweli kweli na lilikuwa kinajitahidi kuzuia hasira zake.











    Salim akakata jicho pembeni kumwangalia Cindy na Magdalena pale ambapo walikuwa wamesimama. Akagundua kwamba Magdalena alikuwa ameificha ile taa aliyoishika mkononi ambayo ilikuwa imegeuka rangi ya bluu. Alikuwa ameificha chupa ndani ya jaketi lake na haionekani.











    Mawazo kadhaa yakapita ndani ya kichwa cha Salim. Cindy ana mpango gani? Kwanini ameficha ile chupa? Kwanini amejitenga pembeni yeye na Magdalena?











    Ile sauti ya muungurumo sasa ilikuwa imefika miguuni mwao kabisa. Kwa jinsi ambavyo walikuwa na woga Mkuu ndani yao, walikuwa wanahofu hata kutazama chini. Lakini hata hivyo pia giza nene ambalo lilikuwa limetawala wasingeweza kuona pale chini walipokanyaga hata kama wangeliangalia.



    [22:16, 4/4/2017] ?+255 718 096 811?: Kanali, Salim na Shafii walikuwa wameganda kama masanamu.



    Shafii kutokana na uoga kumzidia kuliko kiwango, akafanya kosa moja kubwa… akainamisha kichwa na kutazama chini.



    Akakutana macho kwa macho na macho makali kama ya paka yanavyong’aa gizani.



    Kiumbe huyo akaachia ule mlio wake wa kuunguruma aliokuwa anaubana muda wote, akaachia muungurumo huo mkali kama simba na kuruka kwa kasi ya ajabu kumvamia Shafii.











    Muda huo huo kwa kasi kubwa pia ya ajabu, Cindi akatoa ile Chupa aliyoificha ndani ya koti na kumrushia yule kiumbe aliyekuwa amemrukia na kumvamia Shafii.











    Chupa ile ilipotua kwa kiumbe huyo, ghafala akamuachai Shafii na kuanza kugala gala chini na kupaparika kama vile ana kifafa.



    Cindy akakimbia na kuikota ile chupa na kuishika kwa kuining’iniza juu ya yule kiumbe.







    Chupa bado ilikuwa inang’aa kwa rangi ya bluu kwa hiyo hii ilitoa mwanga hafifu uliowasaidia kumuona kwa uzuri yule kiumbe pale chini.











    Umbo lake alikuwa ni binadamu kabisa… kama vile binadamu mwenye miaka 28 au 30.



    Lakini binadamu huyu mwili wake wote ulikuwa na manyoya ya paka. Mwili mzima mpaka usoni na viganja vya mikono alikuwa amefunikwa kwa manyoya ya paka.



    Macho yake pia yalikuwa ni ya bluu yenye kungaa kama alivyo paka. Lakini mwili wote alikuwa ni binadamu tena wa jinsia ya kiume.











    Pale chini kiumbe huyu alipokuwa amelala na kugala gala huku Cindy bado akiwa ameishikilia ile chupa juu ya huyu kiumbe, taratibu alikuwa anaanza kuvimba kwa kutumumuka na ile hali ya kupaparika ikawa inapungua kana kwamba alikuwa anakaribia kukata roho.











    “Shikilia hii chupa hivi hivi” Cindy akamkabidhi Chupa Magdalena ambaye aliishika vile vile juu ya yule kiumbe kama ambavyo Cindy alikuwa ameishika.











    “Kanali naomba kisu” Cindy akaongea na Kanali.







    Kanali alikuwa amemokodolea macho tu akionekana kama vile haelewi anachoambiwa.



    Wote watatu, Kanali, Shafii na Kanali bado walikuwa wako kwenye bumbuwazi kutokana na kile kilichotokea pale.











    “Kanali.!!” Cindy akaita kwa nguvu zaidi.











    “Naam!” Kanali akashtuka kutokana kwenye bumbuwazi na msahangao.











    “Nipe kisu!” Cindy akaongea.











    Kanali akatoa kisu kichokuwa kwenye ‘holder’ kiunoni mwake kwenye mkanda wa kombati zake za kijeshi.











    Cindi akapokea kile kisu, kisha akatoa kutoka ndani ya jaketi lake kikopo fulani chenye ukubwa wa kama robo lita. Alafu akapiga magoti na kutoboa yule kiumbe pale chini aliyekuwa ametutumka haswa mwili wake.







    Akamtoboa na kuanza kukinga damu yake kwenye kikopo. Damu iliyokuwa inatoka kwa kiumbe huyu ilikuwa ni nyekundu lakini ni nyekundu iliyopauka sana kupitiliza.



    Wenzake wote walikuwa bado wako kwenye mshangao mkubwa kwa hiyo walishindwa hata kuuliza swali ni nini kilikuwa kinaendelea hapo.











    Kikopo kikajaa na Cindy akakifunga na kukirudisha kwenye mfuko wa jaketi lake.











    “Cindy!” Salim hatimaye alitamka kutoka kwenye mshangao.











    Cindy hakuitika, akainua tu kichwa kutazama Salim. Japokuwa walikuwa kwenye kiza totoro, lakini aliweza kuona ‘kuchanganyikiwa’ kwa Salim kuliko jionyesha dhahiri usoni mwake.











    “Cindy! Nini kinaendelea hapa?” Salim aliongea huku anahema.











    “Ulikiwa ni mtego?” Cindy akaongea huku kama anatabasamu kwa mbali.











    “Mtego?? Na sisi ndio tulikuwa chambo wako?? Si ndio?” Salim akaongea kwa hasira huku bado sauti yake ikiwa na woga.











    “Usikarike sana! Tumefanikiwa, si unaona?” Cindy akatabasamu huku anaonyesha kidole kwa yule kiumbe pale chini ambaye sasa alionekana hana uhai.











    “Na hiki ni nini?” Salim akauliza akimnhooshea kidole yule kiumbe aliyelala chini.











    “Sijui nimuiteje… labda nimuite mkazi wa Anabelle. Yes, huyu ni moja ya wakazi wa Anabelle.!” Cindy akaongea huku anatimia kisu kumkata ngozi yule kiumbe pale chini lakini katika namna ambayo kama vile anamchuna ngozi.











    “Unataka kusema watu wote karibia milioni nne walishindwa kutoka ndani ya dar ndio wamegeuka kuwa namna hii?” Kanali akauliza kwa mshangao.















    “Hapana… well, labda walau mimi nadhani hapana.!”











    “Unaaana gani? Huyu ametoka wapi sasa?” Kanali akauliza tena.











    “Huyu ni moja kati ya wale watoto elfu waliozaliwa kimazingira nchini Maldives mwaka Juzi 2036! Mnakumbuka ile stori niliwaambia jinsi hii chupa ilivyolkotwa na wavuvi na kisha watoto wachanga kuzaliwa wakiwa na manyoya ya paka na baadae kupotea? Sasa huyu naamini ni moja wapo wa watoto wale!” Cindy akaongea huku anaendelea kumchuna ngozi yule kiumbe pale chini.











    Akina Salim wote wakajikuta wamegonganisha macho kwa kuangaliana kwa mshangao.











    “Amefikaje Tanzania huyu kiumbe?” Salim akauliza.











    “Hilo ndilo swala ambalo limenifanya nijitoe muhanga kuingia humu… kama wewe pia na mimi nahitaji kifahami wamewezaje kufika hapa Tanzania… na si hapa tu Tanzania… kila sehemu ambayo mji unatwaliwa naamini lazima kuna hawa viumbe… na najiuliza wanawezaje kuenea duniani kote kutokea Maldives!” Cindy akaongea huku bado anamchuna ngozi yule kiumbe.











    “Kabla hujaongea maneno mengine ya kutuchanganya zaidi… kwa hiyo watu wote ambao walibaki kwenye Anabelle wako wapi?” Shafii akauliza.















    “Hitaji lao kuu la kwanza ni wanaume… ndio maana nilipomsikia anaunguruma mimi na Maw tukajitenga pembeni.!”











    “Wanataka nini kwa wanaume?” Salim akauliza.











    “Mji ukishatwaliwa na kuwa Anabelle waliobaki ndani yake wanagawanywa sehemu mbili… sehemu moja wanaume na nyingine wanawake… wanaume wanapelekwa mahali… sehemu maalumu… naomba niite hii sehemu zizini… kwa hiyo wanapelekwa zizini kwa ajili ya shughuli maalumu!”











    “Shughuli gani?” Salim akauliza tena.











    “Wanakamuliwa damu mpaka wanakufa… nadhani umeona damu ya hawa viumbe ilivyo! Haina haemoglobin ya kutosha… kwa hiyo wanahitaji kunywa damu ili kupata haemoglobin katika damu yao waendelee kuishi.!” Cindy akaacha kidogo kumchuna ngozi yule kiumbe na kuwaangalia akina Salim, akijua fika kabisa Salim anataka kuuliza swali gani.











    “Kabla haujanijibu unafahamu vipi yote haya, naomba unieleze kuhusu wanawake… umesema watu wanaobakia kwenye Anabelle wanagawanywa sehemu mbili, wanawake na wanaume… wanaume umesema wanakamuliwa damu mpaka kufa… wanawake ni nini kinawakuta??” Salim akauliza kwa uchungu akiwambuka mkewe Khadija na mtoto wake Basrat.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/









    “Wanawake wanaishi… wanapelekwa kwenye zizi lingine! Na huko kazi yao ni kuzalishwa kila baada ya miezi sita… wanazalishwa viumbe vinavyofanana na hiki… wanazalishwa maisha yao yote mpaka watakapofariki.!”



    Cindy akajibu na kisha kuinama chini kuendelea kumchuna ngozi yule kiumbe.











    Wenzake wote walishikwa na bumbuwazi. Walitamani kuongea kitu lakini maneno yalikuwa hayatoki.











    “Unayajuaje yote haya?” Salim akauliza kwa uchungu huku chozi linatiririka shavuni mwake.











    Cindy akainua kichwa na kuwatazama.





    THE OTHER HALF























    EPISODE 7



















    “Wengi wanaamini binadamu aliumbwa na Mungu au kiumbe kingine chenye nguvu na uwezo zaidi. Wengine wanaamini kwamba binadamu ni zao la mabadiliko ya viumbe vya kale na dunia. Vyovyote, kama tuliumbwa au tilitokea tu, kitu kikubwa zaidi ambacho kiliwekwa ndani yetu ni uhuru wa kuamua, free will.! Uwezo wako wewe binafsi kuamua kufanya utakacho na kuamua muelekeo wa maisha yako. Zawadi hii tuliyopewa licha ya kuwa adhimu, lakini pia inabeba mzigo wa jukumu linalowatesa binadamu tangu kuwepo kwa ulimwengu. Uhuru wetu wa kufanya maamuzi unaweza kutupeleka katika kuikuza mbari ya binadamu au kuipoteza kabisa. Mzigo huu pia wa jukumu unagusa mtu mmoja mmoja. Ni mara ngapi ambapo nafsini mwako, uamuzi unaotaka kufanya ni kukimbia hali iliyopo lakini moyoni unafahamu inatakiwa ubaki na kupambana? Ni mara ngapi ambapo nafsini mwako uamuzi unaotaka kufanya ni kuishi katika mstari mnyoofu lakini moyoni mwako unajua kabisa unapaswa kuvunja kanuni ili upate unachokitaka??











    Uhuru wa kufanya uamuzi, free will ni Zawadi kubwa zaidi iliyowekwa ndani mwetu lakini ni mzigo mkubwa zaidi wa uwajibikaji binafsi ndani yetu na mara nyingi umekuwa ni kikwazo pale tunapotaka kusonga mbele au kupambana kutetea tunachokiamini. Mbaya zaidi ni pale tunapopambana na viumbe walio tofauti na sisi, viumbe ambao hawana hisia zetu.…. Binadamu tunajivunia ubora wa hisia, hii ni moja ya vitu ambavyo vinafanya haijalishi kutakuwa na maendeleo kiasi gani ya teknolojia, lakini kamwe roboti hawezi kufafanana na binadamu. Kwa sababu huwezi kutengeneza hisia. Hisia ni kitu tunazaliwa nacho, hakifundishwi. Hisia zote, mbaya na nzuri, hisia zote kuanzia urafiki, huruma mpaka ukatili. Ni binadamu pekee anazaliwa nazo. Lakini hisia nayo ni Zawadi na papo hapo ni kikwazo kwetu kufika tunapotaka.















    Sasa je, itakuwaje pale ambapo binadamu atatakiwa kupambana na kiumbe chenye ubora kama walionao binadamu, lakini wenyewe ni bora zaidi kwa kuwa hawana hisia. Hisia pekee waliyonayo ndani yao ni Kiu ya kutaka kuishi, yaani survival.!







    Binadamu, anawezaje kushinda vita pale anapotakiwa kushindana na viumbe wa ajabu, watotot wa Anabelle 1 (Maldives), waliozaliwa mwaka 1936.? Binadamu anawezaje kutetea haki yake ya kuendelea kuishi juu ya uso wa Dunia??











    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIPOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)











    Dr. Cindy Wheaton alikuwa amemaliza kumchuna ngozi yule kiumbe pale chini na sasa alikuwa amesimama anawaangalia wenzake huku mkononi ameshikilia ngozi ya binadamu yenye manyoya mengi kama paka.











    “Hii ngozi ya nini?” Kanali akauliza kwa mshangao.











    “No no! Kabla hajajibu hii ngozi ya nini ni vyema kwanza atuambie anajuaje mambo mengi hivi kuhusu Anabelle na vilivyomo ndani yake?” Salim akadakia kabla Cindy hajajibu swali la Kanali.











    “Salim! Huo sio muda sahihi wa kuanza kupeana mihadhara, mimi ni mtaalamu wa akiolojia kwahiyo si ajabu kujua vitu vingi.” Cindy akajibu akiwa anaikunja ile ngozi bila kumuangalia Salim.











    “Sikiliza Cindy… mke wangu na mtoto wangu wako humu ndani na watu wengine zaidi ya milioni nne… Mpaka sasa sijui ninachokifanya humu na nahitaji kujua unafahamu vipi taarifa zote hizi kuhusu Anabelle.?” Salim akauliza kwa hasira safari hii.











    Cindy akavuta pumzi kubwa ndani na kuishusha.







    “OK! Mnafahamu hili jina la Anabelle limetokea wapi?” Cindy akawauliza huku anawaangalia wenzake mmoja mmoja.











    Wote wakaangaliana huku wanatikisa vichwa.











    “Nadhani ndivyo zinavyoitwa… ndivyo ambavyo imezoeleka na kuripotiwa hivyo kwenye vyombo vya habari kwamba ” mji fulani umegeuzwa kuwa Anabelle ” Magdalena akjibu.











    “Nadhani mmewahi kusikia simulizi kuhusu Pandora, si ndivyo?” Cindy akawauliza.







    Wote wakaangaliana na kisha kutingisha vichwa.











    Cindy akaanza kuwasimulia simulizi kuhusu Pandora kama ambavyo Mzee Caleb aliwasimulia makamu wa Rais wa Marekani David Logan na timu yake kwenye situation room. Akawaeleza kila kitu kuhusu namna ambavyo mungu wa kigiriki, Zeus alivyomuumba mwanamke wa kwanza Pandora na kumpa sanduku lenye chupa zilizojazwa udhalimu wa ulimwengu na kumpa sharti la kutofungua sanduku hilo.







    Lakini hakuwaeleza chochote kuhusu mchoro wa George Washington kuhusika na sanduku hilo kwa kuwa hata yeye Cindy alikuwa haijui siri hiyo.











    “Sasa! Hii simulizi ya kale inatuambia kuwa mwanamke huyu wa kwanza Pandora aliwekwa kwenye mji wa kale unaoitwa Anabelle zaidi ya miaka elfu kumi iliyopita… ndipo hapa baada ya haya matukio ya miji kutwaliwa kuanza na tulipong’amua matukio haya kuhusiana na chupa za kwenye sanduku la Pandora… tukaibatiza jina la Anabelle miji hii inayotwaliwa.!”







    Cindy akanyamaza kidogo kumeza mate. Kisha akaendelea.











    “Sasa huu mji wa kufikirika wa Anabelle ambao Pandora aliwekwa na Mungu Zeus, ulikuwa na visa vinavyofanana kabisa na haya yanayotokea sasa duniani… watu kupotea, wanawake kuzalishwa viumbe vya ajabu na kadhalika… kwa hiyo baada ya kutafiti sana kinachoendelea duniani kwa sasa… najaribu kuoanisha na kilichotokea kwenye Anabelle halisi ambayo Pandora aliwekwa na Mungu Zeus… na ninachoamini ni kwamba hawa viumbe wanataka kuibadili dunia nzima kuwa kama mji wa dhahania wa Anabelle ambao Mungu Zeus alimuweka Pandora baada ya kumuumba…. kwa hiyo kujibu swali lako Salim, hivyo ndivyo namna gani najua yote haya.!”















    Cindy akamaliza kujieleza. Wote walikuwa wako kimya wanamuangalia tu.











    Giza bado lilikuwa kama ndio linazidi kuongezeka pale walipo. Bado kwenye madirisha ndani ya nyumba kulikuwa kuna mwanga mkali kana kwamba chemli au moto umewashwa ndani. Lakini ajabu ni kwamba vile vivuli vya watu madirishani havikuwepo tena.











    Cindy alikuwa amemaliza kuikunja ile ngozi ya yule kiumbe waliyemuua. Alikuwa ameikunja ngozi kama nguo na kumpa kanali aishike. Kisha akachukua ile chupa kutoka kwa Magdalena.











    “Tuna Masaa machache sana mbele yetu tunatakiwa tufike katikati ya mji.!”  Cindy akaongea huku anaanza kutembea kuondoka pale waliposimama.











    “Tunaenda kufanya nini katikati ya mji?” Akauliza Salim.







    Cindy hakujibu papo hapo. Akanyamaza kama anatafakari jambo fulani hivi namna gani amjibu Salim.











    “Umemuona huyo kiumbe tuliyemuua?” Cindy akamuuliza Salim huku wanatembea kuelekea mbele.







    Walikuwa wanatembea taratibu sana kwa tahadhari kubwa huku Cindy ameshikilia chupa mkononi na kuiweka mbele kama ameshika tochi.











    “Nimemuona!” Salim akajibu kwa kukereka na swali hili. Kwanini amuulize kama amemuona wakati walikuwa wote tukio likiwa linatokea.











    “Kama angekuwa binadamu wa kawaida unamkadiria angekuwa na miaka mingapi?” Cindy akamuuliza.











    “Kwenye 28 hadi 30 hivi” Salim akajibu.











    “Unakumbuka nimewaambia kuwa hawa ni watoto waliozaliwa nchini Maldives, kabla haijageuzwa kuwa Anabelle.?”











    “Ongea point yako Cindy, tunakumbuka yote hayo!” Salim akang’aka huku akijitahidi sauti yake isitoke kwa nguvu.











    “Nadhani kuna jambo la msingi hamlioni hapa… mnakumbuka hawa watoto walizaliwa mwaka gani kule Maldives?” Cindy akawauliza kwa msisitizo mkubwa akiata waone kile anachokitaka.











    “Mungu wangu!!!” Magdalena akadakia, “walizaliwa mwaka 2036, kwa hiyo mpaka sasa walitakiwa kuwa na miaka miwili tu!” Magdalena akaongea kwa mshangao na hofu.











    “Miaka miwili???” Shafii ambaye alikuwa kimya muda wote akahamaki “haya madude yanaonekana mababa mazima mnasema yana miaka miwili??”







    Ikabidi wenzake watoe kicheko cha chini chini baada ya shafii kuhamaki kuwa vile viumbe ni “mababa mazima”!











    ” kuna jambo la muhimu sana ambalo nataka mlifahamu kuhusu Anabelle!” Cindy akaongea serious baada ya vicheko kuisha.



    “Muda ndani ya Anabelle haufuati kanuni kama muda nje kwenye ulimwengu!”











    “Una maanisha nini?” Kanali akauliza.











    “Nadhani anamaanisha muda ndani ya Anabelle unaenda kwa kasi zaidi tofauti na muda nje huko ulomwenguni.!” Salim akajibu akiwa serious pia.











    “Uko sahihi kabisa” Cindy akaongea, “muda ndani ya Anabelle unaenda kasi zaidi tofauti na ulimwenguni… ndio maana unaona hawa viumbe wana miaka miwili pekee lakini wanaonekana ni watu wazima kabisa wa miaka 30!! Na hii ndio sababu kwanini mji ukishatwaliwa unaonekana umechakaa kana kwamba haujawahi kukaliwa na watu kwa karne kadhaa.. Yote hii ni athari ya muda… Unakuwa unaenda kasi zaidi ndani ya Anabelle tofauti na duniani.!”











    Cindy aliongea huku amegeuka kuwatazama wenzake. Wote walikuwa wamesimama wanamuangalia.











    “Kwa hiyo basi… Unataka kusema kwamba huu muda ambao tumekaa humu ambao nakadiria ni kama masaa mawili pekee inawezekana kabisa tumekuwa humu kwa muda zaidi ya huo?” Kanali akauliza.











    “Kabisa… hilo sio swali… hiyo ndiyo hali halisi… sisi tunahisi timekuwa humu kwa muda mchache lakini labda mwasaa mawili… lakini uhalisia ni kwamba… muda humu upo kasi zaidi kwahiyo inawezekana pengine tuko humu kwa wiki kadhaa tayari.!” Cindy aliongea huku ametoa tabasamu la huzuni.











    “Umesema kwamba ni muhimu tufahamu hili? Unaweza kuwa mahususi zaidi kutueleza kwanini tunapaswa kuzingatia tofauti ya kasi ya muda tukiwa humu ndani?”  Salim akaukiza.











    “Nadhani anamaanisha kuwa tutazeeka haraka!” Shafii akatoa jibu la kijinga tena.



     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Kutokana na msongo waliokuwa nao kutokana na taarifa hii hata vicheko havikuwatoka.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog