Search This Blog

Friday 18 November 2022

MWANAMKE MWENYE JUBA JEUSI - 1

 












IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE



*********************************************************************************



Simulizi : Mwanamke Mwenye Juba Jeusi

Sehemu Ya Kwanza (1)





Usiku ule hali haikuwa nzuri sana kwa Bw. Punde Kishime, kwa kuwa tangu alipoingia ofisini kwake asubuhi na kukuta barua ya vitisho mezani, barua hiyo iliyoonekana kuletwa kwa mkono tu haikuwa na anuani yoyote ndani yake, alipomuuliza sekretari wake alijibiwa tu kuwa barua hiyo ilikuwa imepenyezwa chini ya mlango hivyo aliiokota na kuiweka mezani.

Akiwa amejilaza juu ya sofa kubwa sebuleni kwake jioni ile, Bw. Punde Kishime aligubikwa na mawazo mazito ambayo yalimtoa kijasho chembamba, maswali aliyojiuliza hayakuwa na majibu kabisa. Mke wake, Bi Sheiza alimkaribisha chakula cha jioni lakini hakuwa hata na hamu ya kula alihisi kuwa ameshiba japo alikuwa na masaa kama ishirini na nne bila kula, woga, hofu, maswali yasiyo na majibu vyote vilichukua nafasi kubwa kichwani mwake hata alipokunywa maji kiu haikumuisha kabisa. Alibaki sebuleni hapo akitazama TV hata wote walipoenda kulala.

Mara simu yake ya mezani iliita, mshtuko alioupata haukuwa wa kawaida alihisi mwili kufa ganzi na kuchoka ghafla, taratibu alijinyanyua kutoka katika sofa lile na kuelekea mezani kuichukua simu hiyo

“Hallo… halo… haloooo” aliita lakini simu ile haikujibiwa, akairudisha kwenye kikalio chake na kuegemea meza kwa mikono yake miwili, hakujua afanye nini, aondoke aiache familia? Haiwezekani! Asafirishe familia abaki peke yake? hamna uamuzi! Alitoka pale na kujitupa kochini akiwa hajui la kufanya. Akapata wazo bora aondoke na familia yake usiku ule, lakini aende wapi? Hajui!

Kabla hajakata shauri simu yake ikaita tena, mara hii ilipokelewa na sauti ya kike



“nahisi barua yangu umeipata! kaa tayari katika siku mbili hizi nitachukua mzigo wangu, rafiki yako kipenzi Bw. Chiwawa Chakwima nimeshamalizana naye, nenda kamtembelee atakupa salamu zangu!”simu ikakatika, kabla hata Bw Kishime hajaongea.

Bw. Kishime alibaki haelewi kinachoendelea, ‘nani huyu!?’ Alikosa jibu. Alitoka nje na kuingia kwenye gari yake aina ya Toyota Harrier, gari hii alipewa zawadi na rafiki yake mmoja kutoka Thailand alipokwenda kumtembelea, aliingia na kutia moto injini ikakubali, alipiga rivas taratibu na kukunja kona, kwa mwendo wa kasi aliondoka kuelekea Masaki, akiwa barabarani aliendesha gari kama kichaa, aliiacha barabara ya Old Bagamoyo na kuchukua ya Namanga kupitia ubalozi wa USA, akiwa haelewi chochote alikunja kona kali kushoto mpaka tairi zikapiga kelele, alipofika katika mataa ya st Peter akakuta lori la takataka limeziba njia, akapiga honi nyingi lakini lori lile halikutaka hata kusogea, akaamua kushuka kwenda kumfuata dereva, alipoiacha gari yake tu mbele yake walitokea watu wawili wakiwa na shortgun mkononihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ha ha ha ha Bw. Punde Kishime, mtu mkubwa! Kwa nini unadanganyika kitoto hivyo? Yaani wewe hujui kama rafiki yako Bw. Chiwawa yuko kikazi Saudia?” mmoja wao alisema. Hapo ndipo Bw. Punde akakumbuka kuwa ni kweli rafiki yake Bw. Chiwawa amesafiri, alijiona mpumbavu sana.

“Ninyi ni nani? Na mnataka nini?” aliwauliza,

“ha ha ha ha … utatujua taratibu lakini sisi ni wajumbe tu, mama ametutuma kwako…” mwingine alijibu kwa sauti nzito huku wakipiga hatua za taratibu kumsogelea. Ghafla alihisi kitu kizito kimempiga kisogoni akaanguka katika lami.



***

Riyadh International Airport-Saudi arabia



Boeing 747-400 Jumbo Jet ya shirika la ndege la Uingereza ilikunja tairi zake kumi na nane na kuiacha ardhi ya Saudi arabia na kukata anga kuelekea Africa ya Mashariki, Bw. Chiwawa Chakwima alitulia vizuri kabisa katika kiti chake ndani ya VIP coach, mawazo, akili na moyo wake vilikuwa vikiwaza nyumbani Tanzania, pembeni yake aliketi msichana mrembo nywele zake ndefu zilifika mpaka katika viwiko vyake, macho yake ya mviringo yalimfanya Bw. Chiwawa ashindwe kuangalia mbele, alipogeuka tena kumwangalia msichana yule aliinua mguu na kukunja nne, Bw. Chiwawa akaingiza mkono katika katika mfuko wa shati akatoa business card akampatia, mrembo yule akaipokea na kuihifadhi. Mara mhudumu wa ndege ile alipita na kusimama karibu na Bw Chiwawa, akaingiza mkono katika trey ya chini akatoa bahasha ndogo ya khaki akampatia, Bw. Chiwawa akaipokea akataka kuifungua roho yake ikasita kidogo, akaitia kwenye mfuko wake wa ndani wa koti, alipogeuka kumwangalia yule mhudumu hakumuona alikuwa keshaondoka, akaingiza mkono mfukoni aitoe lakini akasita kwa mara nyingine! Akatulia kwenye kiti chake akitafakari hili na lile, alipoangalia saa yake ilitimu saa tisa alfajiri alipata faraja kwani alijua masaa matatu yajayo atakuwa nyumbani Tanzania. Mara alipata shauku ya kuona ndani ya bahasha ile kulikuwa na nini, akaitoa na kuifungua huku moyo ukimwenda mbio, alipoichana alikuta kijikaratasi kidogo kilichosomeka ‘watch the movie’ akatoa tabasamu iliyofuatiwa na kicheko cha chini chini, akaona ni upuuzi tu labda haikuwa yake mtu mkubwa kama yeye ambaye ana matarajio makubwa katika nchi yake pia ni kigogo mwenye nafasi nyeti serikalini, akavuta glass yake iliyojaa ‘covousier’ pombe aliyoipenda sana. Mhudumu wa ndege alipita tena sasa alikuwa mwingine akasimama pembeni na kutoa CD.



“Do you like to watch movie?” akauliza mhudumu huku akiiweka cd ile katika kijimeza kidogo mbele ya Bw. Chiwawa. Akaichukua akaigeuzageuza kisha akaitoa kashani na kutumbukiza kwenye kifaa maalumu cha kufanyia kazi hiyo, akanyanyua visikilizio akatia kichwani ili apate kusikia kilichomo, akaitazama yote kwa makini kisha akaitoa na kuirudisha kashani, akaiweka juu ya kijimeza kile akashusha pumzi kwa nguvu huku kijasho chembamba kikimtoka! Shughuli nzito. Akachukua ile cd na kuitia katika koti lake kisha akatulia kitini. Alipiga funda lingine la pombe yake huku akitafakari kwa makini. Akiwa katika wimbi la mawazo alishtuliwa na sauti nyororo ya mhudumu kutoka katika vipaaza sauti vya ndege hiyo kuwa wote wafunge mikanda, akajiweka tayari kwa shauku kufika nyumbani baada ya wiki mbili alizokuwa nazo huko katika nchi za kiarabu.

Boeing Jumbo Jet ilikanyaga ardhi ya Dar es salaam yapata saa kumi na mbili kamili asubuhi, abiria wote waliteremka na Bw. Chiwawa alipokelewa na kuongozwa moja kwa moja VIP. Akiwa ndani ya chumba cha VIP alikutana na watu mbalimbali waliokuwa wakimsubiri, baada ya hapo walikuwa tayari kuondoka uwanjani hapo, walitoka nje na kuingia kwenye gari maalumu kwani alitakiwa kufika Ikulu moja kwa moja kuonana na Rais kwanza. Msafara wa gari tatu uliondoka airport na kuchukua barabara ya Nyerere kueleke mjini kati.



Msafara uliendelea kwa mwendo wa wastani mbele ukitanguliwa na Hyundai ya polisi ikifuatiwa na BMW nyeusi ambayo ndio hasa ilimbeba Bw. Chiwawa na nyuma yao kulifuatiwa na Toyota Prado VX nayo nyeusi metallic, msafara ulipita kwa mwendo wa taratibu katika njia panda ya Tazara na kuongeza kasi kuelekea mjini, walipofika njia panda ya Chang’ombe kitu wasichotegemea kilitokea, gari moja iliyokuwa ikielekea Magomeni kutokea Chang’ombe iliingia kwa kasi barabarani na kukatisha katikati ya msafara na kuigonga ubavuni BMW na kuisukuma pembeni, ile gari ya polisi ilisimama na kupiga rivas kabla ya kufika eneo la tukio polisi wale walisuka na bastola mkononi kuelekea eneo la ajali, vijana watatu walishuka kwa kasi kutoka katika gari ile iliyosbabisha ajali kuelekea ile BMW kabla hawajafika mmoja wao alipaishwa juu tayari kifua chake kilifunuliwa vibaya na risasi kutoka kwa polisi mmoja, kabla hawajatahamaki vijana wale walijikuta na wakati mgumu kidogo, polisi mmoja alifyatua risasi kumuelekea kijana wa pili lakini shabaha haikuwa nzuri kijana yule alijiviringa chini na kutoa shortgun kwenye koti lake na kupiga risasi ovyo zilizowatawanya askari wale yule wa tatu akafika katika BMW na kupiga ngumi kioo cha abiria wa nyuma ambako alikaa Bw. Chiwawa na kuinyayua briefcase ya Bw. Chiwawa, aliondoka kwa kukimbia na kumuacha mwenzake ambaye alipotaka kunyanyuka alipigwa risasi ya mguuni nakuanguka chini. Yule aliyebeba briefcase alipoona yuko matatani alikimbilia kwenye gari na gari ile ailigeuzwa`kwa mtindo wa hatari kuelekea Gongo la mboto.



Polisi waliendelea kuifukuza bila mafanikio.

Bw. Chiwawa hali yake haikuwa mbaya ila alikimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu. Ulinzi wa kutosha uliwekwa nje na ndani ya hospitali hiyo kila aliyeingia kumuona Bw Chiwawa alifanyiwa ukaguzi wa kina.



****

Dhaka-Banghladesh



Kikao kizito kiliendelea huko Dhaka katika nchi ya Banghladesh katika hotel ya Nyota tano ya Hilton, hoja ilikuwa ngumu

“Tumekosea!” mmoja wa wajumbe aling’aka “ilitakiwa ile DVD alipomaliza tu kuangalia ichukuliwe sasa tumechelewa.” Aliongeza Bw Mahmoud Bashir

“Kwani ni nani alikuwa safarini?” mjumbe mwingine aliuliza

“Safarini tulimtuma mpiganaji namba 3 Bw Boniface Mc Field” alijibu mwanamama pekee aliyekuwa katika kikao hicho

“Inabidi tuwe makini sana, sasa cha kufanya ni kuhakikisha hiyo DVD inapatikana kabla haijaonekana na mtu mwingine” aliongeza mkuu wa kikao hicho Bw James Washington.

Kikao kiliendele na hoja nzito nzito zilijadiliwa, kuu ikiwa ni jinsi ya kupenyeza utawala wao katika taifa la Tanzania, kuwanunua wanasiasa maarufu na kuwapa pesa ili kujiweka vizuri katika uchaguzi ujao kushinda halafu wao kupitia viongozi hao kujinufaisha kwa rasilimali nyingi zilizopo nchini. Kutokana na hilo kamati iliundwa ya matajiri wakubwa kutoka pande mbalimbali za sayari hii. Tayari walikuwa wameshafanya hivyo katika nchi mbalimbali za Africa ambazo nyingi mpaka sasa zimeingia kwenye machafuko makubwa, mauaji ya kimbari na hata kupoteza thamani za utu kwa kupitisha miswada isiyostahili. Lakini jicho lao kubwa lilielekea katika nchi moja yenye utajiri mkubwa Africa ambayo bado ilikuwa na utawala imara usiotetereka, usioyumbishwa na mtu au taifa lolote liwe tajiri kifedha au kwa nguvu za kijeshi. Lakini kutoka na uchu wa kujilimbikizia mali kwa viongozi nchi hiyo basi na hawa jamaa wanaojiita ‘The SIXs’ ambao wana mtandao mkubwa duniani na wamejijenga katika nchi nyingi waliona sasa wanaweza kuingia katika nchi hii ambayo tayari kuna watu wapenda mali wawatumie ili kufanikisha lengo lao.



Kikao kilifungwa na kila mmoja alirudi katika shughuli zake za kawaida wakiwa wamekubaliana kukutana kwa kikao cha tatu uko huko Dar es salaam baada ya siku chache ili wakamilishe lengo lao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

****



Mwanza City



Amata Ga Imba aliendelea kula raha na mrembo wake Sundi, aliyekutana naye katika klabu ya usiku ya Sukuma Night Club ambako alienda usiku iliopita. Wakiwa kitandani wakifurahia maisha asubuhi ile huku wakiangalia TV ya taifa mara alisikia habari iliyomshtua na kumfanya kutoka kitandani na kuketi kuangalia



“...tukio hilo lililotokea asubuhi hii katika makutano ya barabara ya Nyerere na Kawawa kwenye mataa ya Chang’ombe, lilihusisha gari mbili mojawapo ikiwa ya Mh. Chiwawa Chakwima.Watu hao wasiojulikana ambao walivalia soksi nyeusi usoni waliivamia gari ya Mh Chakwima na kupora briefcase na kutokomea nayo, polisi waliokuwa eneo hilo walifanikiwa kulipiga risasi jambazi mojawapo na kulitia mbaroni, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na Mh Chakwima yuko hospitalini kwa matibabu...”



Amata Ga imaba alipigwa na butwaa lakini hakutaka kuonesha hali hiyo kwa mrembo yule aliyekuwa naye asubuhi ile, alijinyanyua na kutaka kuelekea kibarazani, yule mrembo alimuwahi na kumvutia kitandani

“Unaenda wapi mpenzi mi nakuhitaji hapa!” alijisemesha kwa sauti ya kubana pua na kumpa Amata busu la kinywani, bila kujali waliendelea kupeana mahaba mazito, mara mlango uligongwa lakini wawili hawa waliendelea na malavidavi yao wakiwa kwenye kilele cha mahaba, mlango uligongwa tena, Sundi alitaka kwenda kuufungua lakini Amata alimzuia kwa kumbana barabara, mara ya tatu mlango uligongwa na kimya kikachukua nafasi yake, moja kwa moja Amata alielekeza macho yake chini ya mlango na kuona bahasha ya kaki iliyopenyezwa hapo, akaamka na kuifuata akaichukua na kuifungua ndani akakuta simu ya maneno Telegram



“rudi nyumbani haraka mama ni mgonjwa mahututi anakuhitaji Tena Sana Aisee.”



Amata alishaelewa mara moja ujumbe huo maneno yaliyokaziwa kwa herufi kubwa ndiyo yaliyomfanya ajue simu ile ilitoka wapi... “Tena Sana Aisee” ... simu yoyote iliyomaliziwa na maneno hayo ilikuwa ni ya haraka na yenye uzito mkubwa. Amata aliiweka karatasi ile mezani na kuingia bafuni haraka akaoga na kuendelea na maandalizi ya chapchap, ndani ya dakika kumi alikuwa ameshajikamilisha akiwa ndani ya suti ya buluu na tai yake iliyomkaa vizuri

“mbona hivo dia kumetokea nini?...” Sundi aliuliza, Amata alimrushia ile karatasi kitandani

“Ha! Ina maana unaenda Dar sasa? Pole mpenzi, mpe pole mzaa chema” Sundi alisema hayo baada ya kuisoma simu ile ambayo yeye hakuielewa hata kidogo. Amata alifungua walet na kumpatia noti nyekundu tano, akachukua briefcase yake tayari kwa safari

“Mpenzi! Asante kwa kampani ngoja niwahi nyumbani nitarudi baada ya siku chache tumalizie raha zetu” akamwachia na busu nene na kutoka chumbani.

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania Boeing ilikuwa tayari kuondoka lakini kutoka na na ujumbe walioupata ilibidi wasubiri kidogo, Amata alifika uwanja wa ndege na moja kwa moja akachukua usafiri... hakuna maswali! Ndege iliiacha ardhi ya Mwanza na kukata anga kuelekea Dar yapata saa mbili na nusu asubuhi. Muziki laini wa congo ulikuwa ukisikika katika chombo cha kusikilizia muziki katika ndege hiyo, akiwa kwenye wimbi la mawazo kupanga na kuoangua kwa kuwa alijua anachoitiwa ni kitu gani, muziki ule pia ulimrudisha mbali sana aliamkumbuka rafiki yake wa shule ya msingi Bw Namoto Arap Manda ambaye kwa wakati huo naye alikuwa na majukumu mazito katika Taifa.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es salaama alikuwa akisubiriwa, mara moja aliingia katika gari na kuelekea mjini... kazi imeanza!





Ndani ya ofisi ile nadhifu kabisa Amata anakutana na katibu muhtasi wa Mkuu,

“Amata karibu sana, karibu nyumbani mkuu anakusubiri ingia, ingia!” Katibu muhtasi wa mkuu alimkaribisha Amata na kumruhusu kuingia ndani moja kwa moja. Ndani ya ofisi alimkuta Bw. Charles Machura akiwa amesimama kimya huku mkono mmoja umeshika pazia na macho yake yote mawili yakiwa dirishani kuangalia vipitavyo, alionekana ni mtu mwenye mawazo mengi

“Bw Machura!” Amata aliita na kumpa mkono. Bw Machura aligeuka na kupokea salamu ile ya mkono na kumuonesha kiti akae.

“Amata nashukuru umerudi maana tuna kazi ngumu, nimeletewa taarifa toka ofisi ya waziri wa mambo ya ndani na amesema ukifika tu tufuatane kule kwa ajili ya kikao kifupi. Nafikiri tusichelewe twende mara moja” Bw Machura alimwambia Amata, mara moja walitoka na kumuaga Secretary.

Wakiwa ndani ya gari ndogo, hakuna liyeongea si Bw Machura wala Amata, dereva aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida na baada ya muda mfupi waliwasili wizara ya mambo ya ndani.

“Karibuni sana!” Mh waziri aliwakaribisha na moja kwa moja wakaingia kwenye ofisi ya ndani, kule walikutana na waziri wa ulinzi, mkuu wa makosa ya jinai DCI, mkuu wa polisi IGP, wote walionekana wakiwa katika mjadala ambao ulikosa majibu, Amata na Bw Machura waliingia na kukaribishwa.

“Karibuni sana!” Mh waziri wa ulinzi aliwakaribisha na wote wakaketi vitini, Amata aliketi kimya akiwasikiliza wazee hao wakibishana kwa mambo mengi, lakini moja kwa moja alielewa ni kitu gani ambacho walikuwa wakizungumzia. DCI alivuta droo ya karibu na kutoa faili moja ya kaki ambayo ilifungwa kwa mkanda wa karatasi nyeupe na juu yake limeandikwa kwa mashine ya chapa ya kizamani ‘SIRI NZITO’, Amata alipokea faili hilo na kulifungua alikutana na picha mbalimbali zilizopigwa muda si mrefu, za ajali ya Bw Chiwawa na picha zingine mbalimbali ambazo ainahusiana na tukio hilo na kuisoma taarifa yote iliyoandikwa humo ambayo ilimshangaza sana Amata kwa jinsi ilivyochukuliwa kwa wepesi namna hiyo. Akashusha pumzi nzito na kuweka faili lile mezani kisha akatikisa kichwa chake kuonesha kuwa ameelwa

“Kijana taifa limeona ni wewe unayeweza kuifanya kazi hii kwa muda uliopangwa, kwa hiyo tumekaa na kukuchagua kufuatilia mpaka mwisho na kujua kila kitu kilichojiri katika hili, serekali iko tayari kukupa msaada wowote ambao utahitaji katika kazi hii. Natumaini nimeeleweka” waziri wa mambo ya ndani alimueleza Amata kwa msisitizo.

“Sawa Mheshimiwa naahidi kuifanya kazi hii kwa utiifu” Amata akajibu na kunyanyuka kitini na kusimama kwa ukakamavu kuonesha nidhamu ya kipolisi kisha kutoka nje ya ofisi.

“Kuna bahasha yako Amata” sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni ya secretary wa ofisi ya wizara ya mambo ya ndani alimueleza Amata na kumpatia bahasha ya khaki.

“Asante mrembo!” Amata alijibu na kumbania jicho yule dada akamuacha akitabasamu tu. Amata aliingia kwenye lift ya ghorofa hiyo na kuteremka, akaingiza mkono ndani ya bahasha hiyo ndogo na kutoa funguo ya gari alipoigeuzageuza alikuta maandishi yaliyosomeka ‘Land Rover’ alipuuzia kwa kuwa alijua daima gari kama hizo ni kubwa sana kwa kazi yake, akiwa kwenye maegesho ya magari hakulijua gari hilo akaminya ile switch ambayo imeambatanishwa na funguo ile mara akasikia mlio wa alarm ukitoka katika Land Rover moja aina ya Freelander, Amata akatikisa kichwa kuonesha kuwa amekubaliana na gari aliyopewa kwa kazi hiyo, alifungua mlango na kuingia ndani kisha akjifungia kwa tahadhari kubwa. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Gari ile ilikuwa mpya kabisa akaanza kuikagua hapa na pale, alipovuta droo ndogo katika dash board ya gari hiyo alikuta bastola moja ndogo ya kitaliano BERETTA MODELLO 418 na kikasha cha risasi zake pembeni, kisha akachukua bahasha iliyopo hapo ndani ilikuwa na taslim sh milioni tatu na ujumbe mfupi uliosema kwa ‘kwa matumizi ya kazi yako tu’ pembeni palikuwa na laini ya simu aliichukua na kuigeuzageuza kisha akairudisha ilipokuwepo, akawasha gari ile na kuondoka kwa kasi, alichukua barabara ya Ohio na kuiacha kuingia barabara ya Bibi Titi, kwa mwendo wa kasi aliendesha kuifuata barabara ya Nkurumah na dakika chahe akawa tayari amefika alipopataka. Njia panda ya Chang’ombe ambapo masaa matatu yaliyopita palitokea ajali yenye utata iliyotaka kuchukua maisha ya Bw Chiwawa Chakwima, alisimamisha gari yake kwa mbali kidogo kwenye kituo cha mafuta akavua koti lake na tai na kuviweka katika siti ya nyuma ili aonekane mtu wa kawaida tu pale, kisha akachukua camera yake kubwa na kitambulisho cha shirika la magazeti la serekali, taratibu akavuta hatua kuelekea eneo latukio ambapo gari ya Bw Chiwawa ilikuwa ndio inaondolewa, alipiga picha chache na kufanya mahojiano na watu wachache, aliporidhika na aliyoyapata akaanza kuondoka taratibu, lakini kitu kimoja kilimfanya asimamae kidogo, alipokuwa anapita eneo ambalo gari ile ya Bw Chiwawa ilipoanguka aliona kitu cha kupendeza kinametameta aliinama na kujifanya anachukua picha kisha akakiokota na kurudi katika gari yake, aliingia na kukaa nyuma ya usukani, alikingalia vizuri kile alichokiokota, ilikuwa ni beji ndogo nyeupe yenye nembo ya kichwa cha ndege, akakiangalia na kukiweka mfukoni alijua tu ni moja ya vitu alivyokuwanavyo Bw chiwawa. Akawasha gari na kuondoka kuelekea ofisini kwake. Aliegesha gari yake mbele ya jengo refu mtaa wa Samora na kuteremka, alipita kwenye njia ndefu iliyo ndani ya jengo hilo kabla ya kuchuku lift iliyompeleka ghorofa ya tatu, huku akili yake ikipitisha mambo mengi na kuyachambua haraka haraka lipi lakufanyia kazi na lipi siyo ailijikuta milango ya lift ile ikifunguka mbele yake na kumsubiri atoke ndani ya lift ile, akafanya hivyo na kuendelea kutembea harakaharaka huku akiiweka tai yake vizuri, aligonga mlango na kujisukumia ndani “karibu Boss!” Gina, msichana mrembo mwenye macho ya kibuluu alimkaribisha Amata na kumsaidia kuvua koti kabla ya kulitundika katika moja ya vitundikio vilivyo ndani ya ofisi hiyo nadhifu. Amata aliitikia salamu hiyo na kufungua mlango wa pili uliyotengenezwa kwa kioo kizuri chenye maua ya kupendeza ambacho kinaruhusu mtu wa upande wa ndani kumuona wa nje lakini sivyo kwa mtu wa nje, aliketi juu ya kiti chake kizuri na nadhifu, akipepesa macho katika mafaili machache yaliyokuwa mezani hapo kwa muda ule, mara mlango ulifunguliwa na yule dada akaingia ndani akiwa na bahasha ya kaki mkononi mwake, akampatia, Amata akaipokea na kuanza kuichana kuona kilichopo ndani

“Nini tena Gina?” alimtupia swali

“Ni barua ililetwa hapa asubuhi ya leo nilipofika tu” Gina alijibu. Amata alipitisha macho haraka haraka kuisoma huku akikunja ndita zake na kuonesha umakini mara tabasamu, akaiweka katika droo na kumtupia swali Gina

“Aliyeleta ulimuona?” kisha akatuliza macho yake kwa msichana yule.

“Ndiyo Boss!” alijibu lakini alikatishwa na Amata ... “kila siku nakwambia usiniite Boss! Niite kaka, humu hakuna Boss wote ni wafanyakazi” alimaliza.

“Aliyeleta yuko yukoje hujawahi kumuona kabla ?” Amata aliuliza tena.

“Sijawahi kumuona lakini hata hivyo nisingemjua kwa jinsi alivyovaa” alijibu

“alivaaje?” Amata alimkatisha “ alivaa baibui kubwa na kufunika mwili wote alionekena macho tu” Gina alijibu, “ok Gina! Nimerudi kwa dharula tu kwa ajili ya barua hii, Asante, umekunywa chai? Au kama kawaida yako!” alimuuliza na kumtania pia maana alikuwa anamjua kuwa si mpenzi wa chai, na kwa kuwa alimzoea sana kama mdogo wake hakuwa na woga wa kumtania msichana yule mrembo wa kuvutia ambaye alimuweka pale kama sekretari lakini alikuwa WP mkakamavu, mzuri kimatendo na heshima.

***

Gina, msichana wa miaka ishirini na nane, mtoto wa sita kati ya kumi wa mzee Komba Zingazinga wa huko Mahilo kijiji kilicho kandokando ya barabara ya kwenda Tunduru mkoani Ruvuma, alijiunga na jeshi la polisi baada tu ya kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Jangwani na kufaulu kwa alama nzuri tu. Alihitimu mafunzo ya upolisi huko katika chuo cha polisi Kilimanjaro au CCP kama kinavyojulikana na kazi yake ya kwanza alipangiwa Dar es salaam katika kikosi cha kutuliza ghasia ambako alifanya kazi kwa miaka mitatu akiwa sambamba na wanaume wengi katika kituo hicho wakiwa katika kutuliza ghasia mbalimbali huko mjini na ilifanya bila kuogopa aliipenda kazi yake, baada ya miaka hiyo aliomba nafasi ya kwenda kusoma bila kikwazo jeshi lilimruhusu na akijiunga chuo kikuucha Mlimani Dsm na kushukua digrii yake ya sheria, aliporudi kazini baada ya muda akapata nyota ya kwanza na kufuatiwa na yapili ndani ya miezi mitatu tu na hii ilifuatia kutokana na jinsi alivyowadhibiti majambazi saba yaliyodhamiria kutoweka na Milioni mia nne mali ya benki ya watu ‘People’s Bank’ iliyopo katikati ya jiji, kwa ustadi na wepesi aliyonao aliweza kutumia vizuri bunduki ya mmoja wa majambazi ao hao ambao yalikuwa yakipora hela katika benki hiyo, Gina akiwa kama mteja katika nguo za kiraia waliamuliwa kulala chini wote na kutii amri hiyo, akiwa pale chini katulia kimya alipepesa macho yake kwa ustadi mkubwa na kujaribu kupiga mahesabu kuona nini anaweza kufanya yeye kama mwenye dhamana ya kulinda watanzania na mali zao, roho ilimuuma sana hasa pale alipoona walinzi wa benki hiyo wamewekwa chini ya ulinzi ndani katika kona moja hivi, na mara watatu wao wakatoka ndani ya zile kaunta na sanduku la chuma ambalo ndio kwanza lilikuwa limeingizwa ndani ya benki hiyo. Watatu wakiwa nje kati yao mmoja akiwa garini akisubiri nyuma ya usukani wawili walisimama kwenye ngazi katika pande tofauti na mikono yao ikiwa ndani ya makoti yao kila mmoja mmoja aliyekuwa ndani katika ukumbi mkubwa wa benki hiyo alikuwa na short gun iliyokatwa kitako ikiwa na magazine mbili, moja iliyowekwa vizuri katika binduki ile na nyingine imefungiwa mpira wa manati katika hiyo, kwa waliyoingia ndani wawili walikuwa na bastola na yule wa tatu aliyeongoza msafara alikua na SMG ila huyu alikuwa amevaa nguo zinazofanana na za wale walinzi wa kampuni. Gina alitulia kimya pale chini na kutazama kwa uficho walivyojipanga, kila mtu akiwa tuli katika sakafu ile ya vigae nadhifu, pembeni yake kulikuwa na mama mmoja na mwanae mdogo wa kama miaka miwili hivi kutokana na hali hile mtoto yule alianza kulia hapo muda uo huo ndio hasa Gina ailiuombea utokee, yule jambazi akasogea kuona sauti hiyo ilitoka wapi alipopita kama umbali wa robo mita karibu na Gina, alijikuta akipaa hewani kwa mtama uliopigwa kiustadi sana na WP huyu, jamaa alidondoka chali na bunduki ile ikajifyatua nakupasua vyoo vilivofanya kaunta ile kupendeza. Gina aliuzungusha mguu wake wa kulia kwa ustadi akiwa amelala chali na kuutuza juu ya koromeo la jambazi yule, yule jambasi alipiga yowe la tabu Gina alijiinua kisarakasi na kuruka sarmasoti ya kitoto ya kutangunguliza kichwa akainyakua ile bunduki iliyodondoka sentimeta chache moja kwa moja alipiga goti moja na kulenga sawia mmoja wa majambazi wale walio kwenye ngazi alipaishwa juu na kutupwa barabarani chali uhai ukamuacha, WP Gina alijitupa upande wa pila wa ukumbi ule sasa aliiona vizuri ile Nissan Patrol pamoja GX 100 ambazo ziliingia pale pamoja, wale waliobeba lile sanduku wakalitupia ndani ya GX100 na yule mwenye SMG akaanza kupiga risasi hewani kuwatawanya watu eneo lile, wakiwa wote wameshaingia katika magari yao ile GX100 ilipiga norinda moja maridadi kuingia barabarani, Gina hakukubali hali ile alijirusha kwa nguvu na kutokea kwenye moja ya dirisha la vioo na kudondokea nje alilenga vizuri na mara short gun ikacheua ‘nice shot’ risasi ilimpata dereva na gari ikayumba na kuacha njia nkugonga gari la maji taka, kwa haraka alikuwa ameshafika eneo ilipo ile GX 100 kabla hajajiweka vizuri ile Nissan Patrol ilipita jirani na kudhamiria kumgonga lakini Gina alijirusha pembeni kwa sarakasi maridadi, alipotua chini alitereza na kuanguka bunduki ikamtoka mikononi aliwaona wale jamaa wakitoka na lile sanduku kuielekea Nissan Patrol, kitendo cha haraka aliona kuifikia bunduki itampotezea malengo aliokota jiwe kubwa kiasi na kulilrusha kwa ustadi mojakwamoja likampiaga kisogoni jambazi mmoja na kumpeleka chini huku kisogo chake kikitoa damu nyingi, aliiwahi ile short gun kabla hajaiokota mguu mzito ukamkanyaga mkono, bila kuchelewa akauma meno mguu ule jamaa akauondoa kwa haraka akiwa hajakaa sawa alimpiga teke la nyuma ya magoti jamaa akapiga magoti akamdaka mkono na kuuzungusha jamaa akaachia bastola Gina akaiokota na alipoainua kichwa aliiona ile Nissan Patrol ikiingia barabara kuu aliachia risasi moja na kupasua mpira wa nyuma akanyanyuka kuikimbilia jamaa huyu akamshika mguu Gina aligeuka na kumfyatulia risasi ya kichwa na kutimua ubongo ovyo ovyo, Mungu si Athumani askari wa usalama barabarani akafika eneo lile na pikipiki lake kubwa, Gina akaokota ile short gun kwa kasi ya ajabu akamfikia yule trafick polisi

“kimbiza ile Nissan Patrol afande haraka!!! Akiwa tayari amekaa katika pikipiki lile kubwa askari yule aliingia barabarani kwa ustadi na kuendesha ile pikipiki kama ailvyofundishwa jeshini sekunde kama thelathini hivi walikuwa wakiipita ile Nissan na kwa ustadi mkubwa WP Gina aliinua bastola kwa mkono wake wa kushoto na kugeuka nyuma shabaha yake maridhawa ilichana moyo wa dereva na kufanya kioo chote cha mbele kupasuka vibaya alishuka na kuwaweka chini ya ulinzi wale wawili walobaki.

“Shenzy nyie! Watu wanafanya kazi usiku na mchana nyie mnataka kuchukua pesa kiulaini hivi!” Gina aliwafokea akiwa amewaelekezea ile shortgun sasa, mara walifika polisi kutoka kituo kidogo cha Lumumba na kuwatia pingu na kuwalundika selo.



Ushujaa wa WP huyu ulisikika Tanzania yote ndani ya muda mfupi. Usiku uliyofuata ndipo Amata alipomuona kupitia televisheni ya taifa TVT na kusikia kuwa jeshi la polisi limempandisha cheo ngazi mbili juu, yaani sasa atakuwa na nyota tatu. Na benki ambayo aliiokolea pesa zao ilimzawadia milioni ishirini fedha za kitanzania na gari ya kutembelea.

‘Hakika huyu ni WP shujaa!! Amata alijisemea moyoni huku akitabasamu. Ndipo alipoanza chokochoko kumtafuta akapata taarifa kuwa yuko tena masomoni anashukua digrii ya pili ya sheria na hapo ndipo alipomnasa na kujenga urafiki naye mpaka baadaye kumuweka ofisini kwake kama sekretari akimdanganya kuwa yeye ni mfanyabiashara mbalimbali, huku akimpa nafasi ya kwenda darasani kusoma hasa nyakati za mchana.



Amata alimuona dada huyu na kuvutiwa naye pale alipomsindikiza IGP kuhitimisha mafunzo ya askari polisi huko Moshi na katika sherehe hizo walionesha michezo mabalimbali juu ya mambo waliyojifunza, Amata alishuhudia Gina alivyokuwa akipiga karate, judo na kuchezea bunduki kwa umakini na ustadi wa hali ya juu sana kuliko wenzake, na ndipo hapo alipomkariri sura yake na kujiwekea ahadi ... ipo siku... Aliendendelea kumfuatilia katika kila kitu mpaka kitengo gani alipangiwa na wapi ili mradi tu asimpoteze kwa kuwa aliona ipo siku atamuhitaji. Hata jeshi la polisi lilipoamua kumuweka Amata katika kitengo maalum cha TSA ambacho kinaundwa na watu wasiozidi kumi na hata wenyewe pia hawajuani sawasawa kwani kila mmoja wao alitupwa katika mazingira tofauti na mwingine, wakiwa sambamba na Usalama wa taifa, kikosi hiki kinachojihusisha na upelelezi wa mikasa yenye utata ambayo inahitaji intelegensia ya hali ya juu ambayo kwa polisi au wapelelezi wa kawaida sio rahisi kuipatia ufumbuzi mikasa inayoingiza pelelezi za kimataifa waliamua kumpangia ofisi yake nje na maeneo ya kipolisi ili isiwe rahisi kueleweka na kumfanyia kitu kama majungu na kuonekana kafukuzwa kazi na kisha kuanzisha ofisi hii ambayo alikodi moja ya vyumba katika jengo refu liliopo mtaa wa Samora karibu kabisa na ofisi za TRA, ndipo alipojikuta anahitaji mtu wa kuwa ofisini kumsaidia na hapo ndipo alipomkumbuka Gina, lakini angempataje hakujua na aanzie wapi pia hakujua.



****

Amata akiwa juu ya kiti chake cha kuzungukazunguka alishika hiki mara kile hakujua hasa ni nini alitakiwa kufanya, akili yake bado ilikuwa haijakaa sawa, alifungua faili hili mara lile ndipo alikumbuka kuwa ameacha faili alilopewa na waheshimiwa ndani ya gari, alinyanyua simu yake na kukoroga tarakimu kama tatu hivi, simu ilipokewa upande wa pili “Nenda pale chini kwenye parking yetu pembeni ya gari yako kuna freelander imepaki fungua uniletee faili tafadhali” alimpa maagizo Gina kisha yeye akawasha tv yake ndogo na kuangali kilichojiri duniani.

Faili lilikuwa mezani kama alivyoagiza, aliperuzi kurasa moja baada ya nyingine na kusoma kwa umakini akizungushia miduara sehemu kadhaa. Alipokwisha kusoma alinyanyua simu yake na kubonyeza tarakimu fulanifulani kisha kuitegesha sikioni, “Hallo! Ee mkuu heshima yako” Amata aliitikia simu na kutoa salamu

“Ndiyo kijana nakusikia” upande wa pili ulijibu

“Afande naweza kukuona afande, nna shida muhimu” Amata aliomba

“Hamna shida kijana karibu utanikuta”alijibiwa

Amata alinyanyuka na kuweka faili lile ndani ya droo na kuifunga vizuri kwa funguo maalumu, alimuaga Gina kuchukua lifti kushuka chini, alielekea katika maegesho ya tax maana hakuona vizuri kutumia gari yake wakati ule.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Dakika chache alikuwa mbele ya kituo cha polisi cha kati, alikwea ngazi kwa kukimbia alipita moja kwa moja kuelekea kwa mkuu hakuna aliyemzuia badala yake wote walisimama kwa ukakamavu kuonesha heshima.

“Karibu kijana, karibu kiti” alikaribishwa. Na baada ya kusalute kwa mkuu Amata aliketi kiti cha wakitazamana uso isipokuwa walitenganishwa kwa kibao kidogo mezani kilichosomeka RPC M. Simbeye kwa mwandiko uliolala vizuri.

“Ndiyo kijana!” Mh alianzisha mjadala, walizungumza mengi sana juu ya tukio lile

“Afande, hili jukumu sio dogo na nashukuru umekuja, tuone cha kufanya” Mh alimueleza Amata.

“Ndiyo afande, hata mimi nahitaji sana msaada wa vijana wako inapobidi! Umesema mmoja wa majambazi mmemshikilia siyo!?” Amata aliuliza

“Ndiyo, ila kutokana na majeraha ya risasi walizotupiana na vijana wetu yupo Muhimbili chini ya ulinzi mkali” Mh alijibu

“Ila ningependa kuonana na Mh Chakwima mwenyewe kwa mazungumzo kidogo” Amata alieleza

“Mh Chakwima mpaka sasa hawezi hata kuongea amekata kauli kabisa, cjui hata tufanyeje kwa hilo” Mh alimueleza Amata. Amata aliinua mkono wake wakushoto na kuangalia saa yake ya motima iliyomuonesha kuwa ni saa saba mchana.

“Afande! Samahani kwa hili, nina ombi...” Amata alimuomba Mh “Sema kijana!”

:Naweza kuonana na kijana yoyote aliyekuwepo katika mapambano na majambazi hayo?” Amata alitoa ombi lake

“Bila shaka kijana!” Mh alijibu na mara kuanza kuzungusha namba fulani katika simu yake ile ya kizamani na kuweka kisemeo mdomoni karibu nakinywa chake “Afande, mwambie konstebo Stani afike ofcn mara moja” amri ilitolewa na haikupita sekude hata arobaini kijana mdogo anayekadiriwa umri wa mika ishirini na saba aliiangia na kupiga mguu chini kwa ukakamavu huku kasimama bila kutikisika. “Konstebo stani! Unayemuona hapo kitini ni bw Amata, ana mazungumzo kidogo na wewe” Mh alimueleza kijana yule. Baada ya mazungumzo mafupi na kijana yule, Amata aliaga na kutoka akifuatana na konstebo Stani, walipofika nje ya jengo waliagana, lakini kabla hajaondoka eneo hilo Amata alikumbuka kitu “Samahani konstebo!” Amata aliita “bila samahani” alijibu konstebo “kule Muhimbili ni nani aliyepewa jukumu la ulinzi?” Amata aliuliza, “yupo koplo Abdalla” konstebo alijibu.

Amata alirudi taratibu mpaka kule alipoegesha gari yake na kuiwasha kuelekea Muhimbili.

Ilikuwa ni muda wa kuona wagonjwa hivyo kwake haikuwa ngumu kujipenyeza kwa watu ili kupata anachotaka, akiwa kwenye korido za muhimbili kuelekea katika wodi mojawapo alikuwa akifuatana na watu wengi wa aina mbalimbali, moyo wake ulikuwa haumtulii kabisa, aliingia wodini mle na kuangaza angaza huku na kule, alipita kutoka eneo moja na lingine, mwishoni alikutana na askari mmoja aliyeoneka yuko kazini hasa na begani mwake alikuwa na V mbili ‘bila shaka, koplo Abdala’ alijiwazia. Alimsogelea na kumnong’oneza kitu. “Karibu afande!... jamaa kaingizwa chumba cha upasuaji kutolewa risasi” koplo Abdala alimueleza Amata. “Tangu mmefika hajaongea chochote?” Amata aliuliza “hapana afande amekuwa kimya tu” koplo Abdala alijibu. “Chochote mlichomkuta nacho afande?” Amata aliuliza “pakti la sigara, kadi za benki na kitambaa cha makamasi” Afande Abdala alijibu kwa umakini “Vimehifadhiwa wapi?”Amata aliuliza tena. “Vimewekwa pale kitandani pamoja na nguo zake zingine Afande” Afande Abdala alijibu akiwa amesimama kiukakamavu kabisa, taratibu Amata alikielekea kitanda kile na kuanza kupekua nguo zile hakuona kitu kingine zaidi ya pakiti lile la sigara, akaliangalia na kulirudishia tena kwenye nguo zile na kutoka, alipofika karibu na mrango wa kutoka wodini akasita kidogo akarudi tena pale kitandani “Vipi mkuu?” Afande Abdala aliuliza “kuna kitu nimesahau pale!” Amata alijibu na kuelekea moja kwa moja katika kitanda kile na kuichukua ile pakti ya sigara akatoa sigara moja baada ya nyingine kisha akatoa lile jaribosi la ndani, pale akakuta kumeandikwa namba tatu za simu, Amata akaona hapa sasa atapata mwanga wa wapi aendelee, akainama na kuangalia uvunguni akawa kama anachukua kitu fulani hivi, alipoinuka alirudisha lile pakti na kuondoka mahali pale, muda wote huu wagonjwa wachache waliopokuwepo wodini mle walitulia tu hamna aliyejali nini kinaendelea. Moyo wake ulitabasamu kidogo akamsogelea afande Abdala “ Afande, naomba umwangalie mgonjwa vizuri nitakutafuta pindi natapokuhitaji, sawa?” Amata alitoa amri “Sawa mkuu” Afande Abdala alijibu kwa ukakamavu wa kipolisi.

Akiwa ndani ya Freelander yake Amata alizisoma kwa makini namba zile na kujaribu kuzitambua ni za akina nani kwa njia zote alizotumia lakini hakuweza kupata jibu. Aliwasha gari yake na kuondoka taratibu kuliacha eneo la Muhimbili, huku akili bado ikimuenda mbio hakujua kisa hiki inabidi akianzie wapi.





Aliegesha gari yake tena mbele ya kituo cha polisi kati na moja kwa moja aliiendea kaunta na kukutana na Konstebo Stani “samahani konstebo” alimtangulizia samahani kabla ya kusema alichotaka “bila samahani afande, nipo kwa ajili yako” konstebo Stani alijibu huku akiwa kasimama kiukakamavu kabisa. “ok! Katika vitu mlivyopata kwa yule jambazi aliyeko hospitali kuna nini na nini?” Amata aliuliza, “kuna simu moja, bastola na kisu cha kukunja” Konstebo Stani alimwambia Amata huku akivitoa vitu vile ndani ya droo maalum vikiwa kwenye mfuko wa plastiki, Amata aliuchukua mfuko ule akaomba gloves na kuvaa kisha akaufungua na kutoa simu iliyopo humo, akaigeuzageuza na kuifungua kwa nyuma kisha akairudishia, akiwasha, simu ile ikakubali bila tabu akaishika kiganjani akiiangalia kwa makini simu ile kana kwamba kuna kitu anachokisubiri, punde si punde alichokitegemea kikatokea simu ile ilitoa mngurumo wa kutikisika na picha ya bahasha ikatua juu yake, Amata akafungua ujumbe ule huku akiwa na kihoro cha kutaka kujua kilichomo humo ...

“Chole street 20 105 1500, Max Petito” Amata aliusoma ujumbe huo na kunakili namba hiyo ya simu maana katika kitabu cha namba ya simu ile hakukuwa na namba hata moja, baada ya kunakili alijipigia kwa kutumia simu ile kisha akarudisha kila kitu kwa Konstebo Stani ”asante afande!” alishukuru na kurudi kwenye gari yake, alitazama saa yake ilikuwa tayari saa tisa kasoro robo, alijiuliza afanyaje lakini hakupata jibu la haraka, alifungua maji yake ya Ndanda na kunywa chupa nzima kwa muda mfupi. Akachukua simu yake na kuandika ujumbe ule kisha akautuma kwenye simu yake ya ofisini, aliutazama ujumbe ule na mara hii akagundua kuwa haueleweki, hauna maana lakini kichwani mwake alijua wazi kwamba hawa si watu wajinga hata kidogo, na kama kuna kitu walikuwa wanataka basi labda walipanga wakutane huko Chole Street, lakini tarakimu zilizofuata hapo hazikumletea picha halisi au maana ya kitu fulani, aliendelea kuzungusha akili na alipogundua kuwa muda ulikuwa unaenda akawasha gari yake na kuondoka kwa kasi kuelekea mtaa wa Chole. Aliegesha gari yake mbele ya jengo kubwa jeupe lenye ghorofa tatu, Amata, alitoka garini na kuweka vizuri tai yake kisha akachukua bastola yake na kuihifadhi vyema ‘bila shaka sijakosea, mtaa wa Chole plot namba 20, nafikiri maana ni hii’ alijisemea mwenyewe na kuvuta hatua chache kulielekea geti, alibonyeza kitufe na kusubiri kidogo, geti lilifunguka lenyewe Amata akajitoma ndani kwa uangalifu, hakukuwa na mlinzi wa aina yoyote mahali pale alinyanyua mkono wake na kuangalia saa ilitimu saa tisa kamili mchana, alipotaka kushusha mkono wake akijikuta anaurudisha tena machoni kuangalia kioo cha saa ile kilichomuonesha tarakimu 15:00 akatikisa kichwa kwa kugundua kuwa ile 1500 ilikuwa ni saa ‘sijachelewa’ alijisemea na kusonga mbele huku mkono mmoja kaufutika ndani ya koti, aliufikia mlango mkubwa nao ulikuwa umefungwa akabonyeza kitufe mara ukafunguliwa akaingia ndani, palikuwa na ukumbi mkubwa wenye zuria mororo na taa za mwanga hafifu sana, alisimama katikati ya ukumbi ule mara mlango mwingine ukafunguliwa wakatokea vijana wawili wakakamavu waliovalia suti nyeusi nadhifu kabisa. Walipomfikia Amata mmoja wao akamsachi na kutoa ile bastola akamkabidhi mwenzake “clean” alimwambia mwenzake huku akimpatia ile bastola “good, code number tafadhali” yule wa pili alimuuliza Amata, katika nyumba hii unapoingia lazima uipewe code namba Amata aliduwaa kama sekunde tano kwa kuwa hakujua code number gani waitakayo, kazi! Haraka sana alitumia akili yake ya kipelelezi na kutaja namba iliyobaki katika meseji ile huku hakiwa hana uhakika na namba hiyo ilimradi liwalo na liwe “mia na tano!” alitamka huku akitazamana na watu wale, yule aliyeuliza akatoa ishara ya kichwa kwa mwenzie kuwa ampeleke, kumbe alikuwa amepatia namba ile, Amata alimfuata yule kijana, wakapita kwenye korido ndefu kidogo kisha akampandisha ngazi mpaka ghorofa ya kwanza wakafuata korido nyingine nayo ni ndefu pia, kwenye korido hii Amata alikutana na wasichana wa aina mbalimbali wakienda na kurudi lakini hawakuwa wakiongea. Amata alifikishwa kwenye mlango mwingine alipouangalia uliandikwa namba 105 akabidhiwa kwa msichana mmoja mrembo, amata alimwangalia kwa haraka msichana yule kutoka juu mpaka chini “password tafadhali” msichana yule alimwambia Amata, Amata alizungusha akili haraka haraka na kutumia meseji ileile aliyoipokea, nini kilibaki? “Max Petito” Amata alijibu huku akitabasamu, na mara akakaribishwa ndani na dada yule. Amata aliketi kwenye kochi kubwa la vono nyuma yake walisimama wasichana wawili na pembeni yake chini kwenye zuria waliketi wasichana warembo kama sita hivi. Muda si mrefu aliingia mzee wa makamo akisindikizwa na vijana wawili wakakamavu kabisa waliovalia suti nyeusi kama wale wa kwanza, mzee wa makamo akaketi kwenye kochi lililotazamana na alilokaa Amata, akakunja nne na kumkazia macho Amata “karibu kijana, eee Rodolph Mampass” mzee wa makamo alimkaribisha Amata na kumtaja kwa jina lile, Amata aligundua haraka kuwa lile ni jina la yule jambazi aliye hospitali, kumbe hawakuwa wanafahamiana tangu mwanzo, hii ilimpa ujasiri Amata, harakaharaka amata aligundua kuwa jina lile ni la watu wa Congo alibadili kiswahili kidogo kujifanya yeye ni mkongo “Ee Papaa nimekuya itika sms yenye nimepata” Amata alijibu huku akiangalia kwa makini pande zote za nyumba ile. “Ok! Time is tissue, nataka nikupe kazi moja kijana” mzee wa makamo alimueleza Amata huku akikunja sura na kuendelea “kazi ngumu lakini yenye thamani kubwa” akamtazama Amata tena kwa mara ya pili “nataka ukaue, ukatoe roho kiburi ya jirani yetu” mzee wa makamo akatulia kidogo na kuingiza mkono mfukoni akatoa kidude kidogo kama redio na kumpa Amata, Amata akakipokea na kukitia mfukoni, kisha mzee wa makamo akamkabidhi Amata Briefcase nyeusi ikiwa wazi ndani yake kulikuwa na binduki kubwa ya kudungulia aina ya M107.50 Calliber Long Range ambayo ilikuwa vipande vipande, Amata aliiangalia mashine ile ya kimarekani akaitambua mara moja model hii ya mwaka 2002, bunduki lisilo na masihara hata kidogo linapoteguliwa triger yake, kubwa lenye uzito wa takriban kilo 12 likiwa bila risasi, lenye uwezo wa kudungua umbali wa mita 1829 karibu kilomita mbili, si mchezo. “Rodolph!!!” sauti ilimgutusha Amata katika uduwanzi ule wa kulishangaa bunduki lile “ee Papaa nalikuwa natia machoni hii mashine yenye umenipa” Amata alijibu kwa kiswahili kile cha kikongo “Shot and leave it there!” Mzee wa makamo alimpa maagizo Amata kisha akatoka na kuingia mlango ule aliyotokea.

Mwanamke mmoja akanyanyuka na kufunga briefcase ile akamkabidhi Amata na kumuongoza nje, mara hii hawakupita katika coridor zile bali walitokea mlango wa nyuma, alipofika chini akakabidhiwa bastola yake na wale walinzi akatoka getini na kuangalia huku na huku kisha akaingia katika gari yake na kuiweka ile briefcase kwa usalama, akawasha gari yake na kuelekea mjini, hakuwa anajua ni nani amuue ni wapi yupo mbaya zaidi hakujua hata kwa nini auawe. Amata alikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu kichwani mwake mara simu yake iliita alinyanyua na kukuta meseji nyingine “your ear in your pocket!” mara moja akakumbuka kidude kile alichokabidhiwa akakitoa na kukipachika sikioni na mara tu sauti ikasikika kutoka katika kidude hiko



“Mr Rodolph, tunahitaji roho ya mtu mmoja ili tufanikishe mipango yetu, leo saa tatu usiku atakuwa ukumbi wa juu katika hotel ya Belmont mkabala na posta mpya, usiwe na shaka sight yako tumeiandaa juu ya jengo la extelecom, ukifika usiulize chukua lift panda juu, maelekezo mengine utayakuta huko, asante”



Amata alitoa kidubwasha kile sikioni na kukirudisha mfukoni, akatoa simu yake na kumpigia katibu wake “Hello, hello Gina!!” aliita, “Yes nakusikia kaka (...) sijafunga ofisi bado nakusubiri” upande wa pili Gina alijibu “mimi sintorudi ofisini naomba tukutane kesho kama nitakuhitaji nitakujulisha” kisha akakata simu na kuitupia kitini, nakuongeza kasi kuchukua barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuelekea daraja la Salender moja kwa moja alinyoosha mpaka karibu na mataa ya ubalozi wa Ufaransa na kukunja kushoto kuelekea Kinondoni, kitambo kidogo aliiacha barabara hiyo nakukunja kushoto kuchukua njia ya vumbi. Geti lilifunguliwa na mlinzi wa kimasai Amata akaingia na kuipaki gari yake “rafiki! Jambo” Amata alimsalimu mlinzi wake na kuuendea mlango wake wa mbele na kuikgia ndani, alisimama kidogo kuangali huku na huko na kuona kila kitu salama, moja kwa moja aliliendea jokofu lililopo jikoni na kutoa chupa moja ya grants akajimiminia kidogo, huku akilegeza tai yake akaendelea kunywa polepole.



Baada ya kuoga na kupumzika kidogo, Amata aliitazama saa yake ya ukutani ilitimu saa moja na nusu jioni alijinyanyua na kujiweka tayari, akavalia suruali yake ya jeans nyeusi iliyoambatana na tshirt pullneck nyeusi kichwani akajitupia mzula mweusi, mguuni buti nyeusi ilikaa vizuri kama ime shonewa hapo, pole pole alifungua kabati lake na kufyatoa moja ya droo zake za siri na kuchukua bastola moja iliyofiti katika mikanda yake myeusi iliyomkaa vizuri kifuani mwake, alichukua begi moja la mgongoni na kuviweka vipande vile vya lile bunduki kubwa na kulivaa mgongoni. BMW pikipiki kubwa ya kijerumani ilikuwa tayari ikisubiri kazi hii, kik moja Amata alitoka getini kwa kasi na kuelekea barabara ya Kinondoni mpaka na kuikuta barabara ya Kawawa alisimama kidogo kana kwamba anasubiri kitu fulani. Nissan March ilipaki pembeni yake kioo cha kushoto kikateremka taratibu “Hey dear” sauti nyororo ya Gina ilipita masikioni mwa Amata “Belmont Hotel restaurant, saa tatu kamili” Amata alitoa sentens hiyo ambayo ilimfikia Gina sawia kabisa na kioo kile cha kushoto kilipanda kama kilivyokuwa.





Belmont Hotel



Watu waliujaza ukumbi maalumu wa chakula katika hotel ile ya kimataifa ya Belmont iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam, wazungu, waafrika, wahindi, waarabu na wengine wengi, walio katika safari zao za kibiashara, kikazi, starehe hata wale walioiba wake za watu nao walijumuika katika ukumbi huu wa juu kabisa uliofunikwa kwa paa maalum lililotengenezwa kwa ustadi kwa kutumia nyasi kuonesha jinsi ya kudumisha utamaduni wetu. Siku hii maalum ilikuwa kwa wageni wote waliokuwa katika hotel hiyo kuhudhuria cocktail party iliyoandaliwa maalum na mmiliki wa hotel hiyo. Kila mtu wake kwa waume walikuwa wakibadilishana mawazo huku wakiwa na glass zao mikononi mwao kila mtu na kinywaji alichokipenda.

Nissan march ilipunguza mwendo na kuendeshwa kwa mwendo wa polepole mbele y ajengo la posta mpya kisha kuongeza mwendo kidogo na kuzunguka mzunguko wa picha ya askari kurudi maktaba, haikufika mbali ilikunja kushoto na kusimama mbele ya jengo la NMB. Gina binti Komba Zingazinga alishuka kutoka gari ile na kwa mwendo wa madaha alielekea mbele ya hotel ile na kupokelewa na walinzi kisha kuongozwa moja kwa moja kwenye lift za ghorofa hiyo na kuelekea juu.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

***

Miili ya watu watatu wenye sare za kampuni fulani ya ulinzi ililala pa si na uhai katika sakafu ya terrazo ya jengo la posta na simu, Amata alivuta hatua taratibu kuelekea mlango mkuu hakutaka kujiuliza nani kafanya kazi ile, akiwa bastola mkononi alitazama huku na huko na kubonyeza kitufe kabla ya kuingia ndani ya lifti ile, moja kwa moja juu kabisa ya jengo lile alijibanza pembezoni mwa tenki kubwa la maji na kuangalia huku na huko, usalama kwanza! Alishusha begi lake na kuanza kuunganisha bunduki lile kubwa na alipolimaliza alilijaza risasi zipatazo sita kisha kwa kunyata aliuelekea ukingo wa paa la jengo hilo huku akiielekea hotel ya Belmont, kwa mbali aliona nyendo nyingi nyingi katika ukumbi ule, alijilaza chini na kulitegesha vizuri domo la bunduki ile kisha jicho lake ndani ya kiona mbali kilichofungwa vizuri katika bunduki ile aliweza kuona vizuri sana kila mtu na kila kitu kilichopo ndani ya ukumbi ule uliopo takriban mita mia nane hivi kutoka alipo Amata. Aliweza kumuona Gina akiwa katika pozi huku akiwa na glass yake mkononi akikifurahia kinywaji chake akionekana kutazama saa yake mara kwa mara kana kwamba ana mihadi na mtu fulani mahali hapo. Amata alipachika kidubwasha kile cha sikioni na kutulia akisubiri maelekezo ‘kwa nini wamuue?’ alijiuliza kila wakati lakini hakupata jibu. “shati jeupe koti jeusi, pembeni ya mwanamke mwenye nguo nyekundu” sauti ilisikika kutoka katika kidubwasha kile, Amata aliangalia na kumuona mtu huyo kupitia kiona mbali kile alimwangalia kwa makini mtu yule mwenye asili ya kizungu, mrefu mwenye tambo la kimazoezi hasa ‘kwa nini wamuue?’ swali lilijirudia mara kwa mara, Amata aliendelea kutalii kuangalia wote waliomo mle ndani lakini hakuweza kuwatambua wengine, alirudisha jicho lake kwa mzungu yule lakini hakumuona tena mahali pale, alizungusha darubini lake huku na huku katika ukumbi ule hakumuona mtu yule, mara aliona vurugu kidogo katika ukumbi ule hapo aligundua kuwa kuna jambo limetokea akiwa katika kutahamaki alishuhudia mtu akishuka kwa kasi kwa kutumia nyaya za umeme bila kuchelewa Amata alizungusha bunduki lake na kuvuta triger, M107 ikabanja na kuuvunja mkono wa kiumbe yule, Amata alimshuhudia akianguka chini naye bila kuchelewa alinyanyuka na kujirusha kutoka ghorofa ya kumi na sita ya jengo lile na kufyatua mwamvuli wake maalum uliomshusha chini taratibu. Bila kuchelewa aliuvua mwamvuli ule akiwa na bastola yake mkononi alikimbilia moja kwa moja eneo lile aliloangukia mtu yule alijibanza kwenye moja ya gari iliyoegesha eneo hilo na ailipochungulia kwa kupitia uvungu wa gari hiyo alimuona mtu yule akijinyanyu kutoka pale alipoangukia, Amata alipita chini ya gari hiyo na sekunde chache alikuwa ameshamfikia. Mtu yule kabla hajatahamaki alipigwa ngwala maridadi kabisa iliyompeleka chini, pigo lingine la kareti lilitua nyuma ya shingo yake na kumfanya kupoteza kumbukumbu kidogo. Amata alisikia sauti za watu wakija upande ule “kadondokea wapi?” “labda huku” waliulizana na kujibishana, Amata kwa haraka alimvuta mtu yule na kujificha nyuma ya kibanda cha kuuzia kanda za muziki katika eneo hilo, alitulia nae kimya kabisa. Watu wale walikuwa wanne walipita na kuangalia eneo lile “ ni hapa si unaona damu hizi, atakuwa ameondoka si unajua yule ni profesheno” mmoja wao alisema “nani alipiga?” mwingine aliuliza “sijui labda watakuwa polisi” mwingine alijibu “tuondokeni haraka atatukuta maskani” mwingine alitoa amri, gari moja salon nyeusi ilipaki hapo na watu wale waliingia na kuondoka kwa kasi.

Amata alimlaza chini mateka wake “Uko wapi Rodlph?” sauti ilitoka katika kile kidubwasha cha sikioni, Amata hakujibu alikichukua kidubwasha kile na kukitia mfukoni, aliangalia huku na huku ukimya ulitawala eneo lile, alimwamsha mateka wake kwa kutumia kifaa maalum chenye shoti ya umeme “Aa aa aa nani wewe? Nani wewe?” alilalamika yule mtu pale chini, Amata alimziba mdomo ka nguvu asitoe sauti “tulia! Unijibu maswali yangu” Amata alimueleza kwa upole mtu yule, “ unamfanyia kazi nani?” Amata alimuuliza mtu yule huku akikikunja kidole cha mkono wa mtu yule “mi sijui, sijui kabisa, mi natumwa tu” alijibu kwa kulalamika “nani anakutuma?” Amata aliuliza tena huku akikikunja kile kidole na maumivu yake yalikua makali sana kwa mtu yule “BIG” alijibu mara moja “BIG?” Amata akauliza tena huku akiwa anaangalia pembeni, alipoona kimya akageuka kumwangalia mtu yule akakuta akitokwa na povu mdomoni, Amata alisonya kwa hasira, kwa haraka alimsachi mtu yule na kutoa business card na kuitia mfukoni, simu ndogo na bahasha moja akavitia mfukoni, akauvuta mwili wa marehemu yule mpaka barabarani na kumuacha hapo kisha yeye kutokomea gizani. Simu yake iliita kwa kujitikisa alipoisoma “upo wapi kaka?” Amata alijua kabisa meseji ile ni ya Gina “Posta mpya dada” alijibu kwa haraka na kuondoka eneo lile, polisi walishafika na kutanda eneo hilo kujua nini kimejiri.

Mbele ya stendi ya daladala ya posta mpya tax ilisimama na mlango ukafunguliwa, Amata Ga Imba alishuka akiwa na koti mkononi mwake shati jeupe na tai nyeusi iliyomkaa vyema, hatua chache mbele alikutana na Gina, Amata alimshika mkono na kuelekea Belmont Hotel “No! Usiende” Gina alimvuta mkono Amata na kumuweka kifuani “Bro huko hakufai” Gina alimuambia Amata “kuna nini?” Amata alimuuliza Gina “Kuna mauaji, subiri kidogo” Gina alijibu na kumuomba Amata.

Ambulance iliyombeba majeruhi ilishaikamata barabara ya Morogoro kuelekea Muhimbili, George Mc Field alitazama uku na huku na kuona jinsi wahudumu wale walivyozubaa ndani ya ambulance ile alijinyanyua na kujirusha huku miguu yake kaichanua na kumtandika kila mmoja teke la mguu wake, kisha akafungua mlango wa na kujirusha nje kwa ustadi kabisa na kuiacha gari ile ikienda peke yake, kitendo bila kuchelewa, alivuka barabara kuja upande wa DIT kisha pale akachuku tax haraka kurudi mjini “Billicanas tafadhali” alimwambia dreva tax kwa kiswahili chake cha kubabaisha, alivua shati lake na kubaki na tshirt nyeusi, akiwa pale katika siti ya nyuma ya tax ile ailiweza kuchomoa risasi tatu zilizotua usawa wa kifua chake lakini kwa kuwa alivaa nguo maalum ya kuzuia risasi hazikuweza kumzuru.

Polisi walifanya doria na mbwa usiku ule na kufanikiwa khttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/upata maiti ya yule muuaji waliikagua na kuipakia katia land cruiser yao na kuelekea Muhimbili.



***



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog