Simulizi : Pasipoti Ya Gaidi 'Double Agent'
Sehemu Ya Tatu (3)
“Unanitania au?” akauliza yule dereva huku akiweka gari pembeni, “Ok, ngoja nikupeleke ukajionee mwenyewe pale hakuna cha asubuhi kama hivi wala jioni, ni kutumbua tu, we acha bwana!” akaeleza huku akirudisha gari barabarani na kurudi uelekeo wa barabara ya Himo. Mwendo mfupi tu walikuwa eneo hilo.
“Sasa, ukipita getini, kisha ile kaunta kuna mlango mwingine utauona umeandikwa VIP, ingia hapo,” akamwelekeza.
“Poa, egesha gari unisubiri,” akamwambia na kisha yeye akavuta hatua mpaka kwenye ile kaunta.
“Nipe bia, baridi kabisa,” akamwambia mtu wa kaunta.
“Bia gani?”
“Safari lager, bia ya wanaume wenye dira,” akamwambia huku akivuta stuli na kuketi, alipopewa ile bia, akapiga tarumbeta na yote ikaishia tumboni bila kushusha chini ile chupa. Yule mwanadada akabaki akimwangalia tu, akateremka na kuuelkea ule mlango, akausukuma na kuingia. Watu wawili, wanaume wenye nguvu wakamzui kwa vifua vyao.
“Vipi? Mbona unavamia tu sehemu za watu,” wale jamaa wakamwuliza.
“Nyie, sehemu za watu mnazijua…? Nataka kumwona boss wenu, Abiseilim,” akawaambia na wale jamaa wakashtuka.
Mmoja wao akachukua kifaa maalumu na kuwasiliana na walinzi walio ndani ya himaya hiyo, kwa maana hakuna mtu aliyewahi kuja kumuuliza kwa jina hilo, huyu alionekana kuwa ni wa kwanza.
“Nenda, ingia tu hapo!” akaruhusiwa na kuingia ndani ya ukumbi huo ambao ulipamba na maandishi yale yale. Huku haikujulikana kama ni usiku au mchana au asubuhi, watu walikula starehe. Walikunywa na kutafuna, walicheza kamali kwa kuwekeana dau kubwakubwa. Amata alihisi kuguswa mgongoni, alipogeuka alikutana uso kwa uso na kijana aliyeshiba akiwa ndani ya suti safi na domo la bastola likigusa mbavu za Amata.
“Twende, ongoza, ukileta vi-vurugu vyako nakumaliza, asiyehusika akiingia humu huwa hatoki,” akaambiwa. Kamanda Amata akatii na kuongoza kwa kila alichoelekezwa. Juu ya ghorofa ndogo ndani ya jingo hilo, alifikishwa katika sebule kubwa yenye kila kitu. Hapo alikutana na mwenyeji wake.
“Yes, Mr. Kamanda!” yule mtu akasema.
“Kamanda Amata, unstoppable,” akamalizia.
“This time you will be stoped,”
“Never!” Abiseilima akajibu.
“Kubrah Khaleb, kwenye sura ya Abiseilim, ulititoroka, sasa tumekuja hapa hapa, huwezi kutukimbia sisi, tuna miguu mirefu kuliko ya shetani,” Amata akamwambia.
“Aaaaha! ha! ha! Hebu mtieni disprin kwanza kisha tumpasue kende zake,” akawaamuru vijana wake waliokuja kumvamia Amata. Kama kuna makosa ambayo watajuta kuyafanya ni hilo. Amata alirusha ngumi ya kulia ikapata yule jamaa wa kushoto, akabonyea chini na kupeleka mapigo matatu ya karate, yaliyowatawanya wale jamaa wote wa nne, akachomoa bastola na kubiringisha chini huku akifyatua kwa shabaha iliyonenepa, wawili chali wakipiga mayowe ya kifo.
“Msimpe nafasi kabisa,” Kubrah alipia kelele. Amata alichomoka kutoa alipo, akaruka hewani na miguu yake ikazunguka kiufundi , wale jamaa wakajikuta chini chali. TSA 1alipotua chini kwa miguu yake miwili, alimshuhudia Kubrah akibofya swichi ya usalama ili kuomba msaada. Akachomo bastola yake na kufumu kidole cha Kubrah kilichokuwa milimita chache kabla ya kubofya kinobu hicho.
“Aaaaaaiiigh!” akapiga kelele na kujishika katika kidole chake. Amata aliinuka ili amwahi mtu huyo lakini alivutwa suruali na yule jamaa aliyeanguka. Amata akakosa stamina na kuanguka. Akaona akipoteza nafasi atamalizwa, aligeuka chali na kupiga chini kisigino, mbele ya kiatu chake kikachomoka kisu kwa kasi, na yule jamaa wa pili alikuwa akija kumvamia kwa juu aakakutana nacho. Kile kisu kilitua shingoni mwake na kudidimia kwenye koromeo. Akajiinua na kugeuka alipo Kubrah, hakumwona. Akaiwahi bastola yake iliyokuwa chini na kummaliza yule jamaa pale sakafuni, sebule ikawa kimya!....
Akaiwahi bastola yake iliyokuwa chini na kummaliza yule jamaa pale sakafuni, sebule ikawa kimya! Akaibofya kitufe cha pembeni na magazini ikachomoka kutoka mahali pake, ikadondoka chini, akachukua nyinginena kuipachika mara moja, akaondoa usalama na chuma kikatumbukia mahali pake tayari kwa kazi. Siondoki bila roho yako, akawaza huku akivuta hatua za kimya kimya kuuende mlango aliohisi Kubrah kaingia ndani yake, hii ni operesheni kimbunga, akajisemea. Mara nyuma yake akasikia mlango ukafunguliwa kwa fujo, akauwahi ule mlango na kuufungua kisha akajificha nyuma yake.
“Aaaaaah wameuawa!” mmoja akapiga kelele.
“Mamaaaaa! Msakeni muuaji mummalize haraka,” kiongozi wao akawaamuru wakachomoa bastola zao wakaanza kusaka hapa na pale ndani ya sebule hiyo. Kutoka upande ule wa ndani wa ile korido, Kamanda Amata, akatoa mfukoni kitu kama golori na kuirusha kwenye ngazi zilizokuwa zikiteremka chini. Jamaa wawili wakakimbilia mle ndani, wa kwanza akaingia na wa pili pia kisha wakatulia na kunyata taratibu kuteremka zile ngazi bila kujua kuwa mwenzao kwacheza shere. Amata akapiga mruzi na yule jamaa wa nyuma akageuka. Kutoka pale alipo aliruka na kutua kifuani mwa huyo mtu, wakaanguka katika miisho ya ngazi na kumpamia yule aliyetangulia mbele.
“Chidi, vipi wewe!” akapiga kelele, akiwa pale chini, alijigeuza kutazama akakutana na konde zito la usoni, akarudi chini. Chidi akanyanyuka haraka, “Yuko hukuuuuuu!” akapi kelele lakini akakatizwa na dhoruba ya vipigo iliyomchakaza. Milio ya risasi ikasikika na Amata akachumpa na kutua kwenye mlango wa vioo, ukavunjika na yeye kujikuta ndani. Akachomoa bastola na kumlenga huyo aliyemkuta nyuma ndani ya chumba hicho.
“Ha! Ha! Haaaaa umeingia kwenye domo la mamba, weka batola yako chini ama la namuu ahuyu mwanamke!” Kubrah Kaleb akamwambia Amata huku akiwa kamshika mwanamke na kumweke mbele yake na kabala ya kono lake ikiwa imezunguka shingo ya kiumbe huyo mtamu na mkono mwingine akiwa kaipachika bastola katika sikio lake huyo dada.
“Hata ukimuu mi simjui, kwa hiyo hana faida kwangu wala hasara kwa Taifa langu,” Amata akajibu.
“Humjui huyu ee? Sawasawa, basio huyu ni bwege kama wewe aliyetoka kwao kuja kufanya umbea umbea kama huo wako wa kutoka Dar kuja huku, sasa wote mtaishia hapa,” Kubra akamwambia Amata, “Weka silaha yako chini nyang’au wewe!” sauti ikatoka nyuma yake. Amata akaiweka silaha hiyo chini.
“We mikono kisogoni,” akaamuriwa tena. Kama kuna kauli alikuwa akiisubiri basi ilikuwa hiyo, akainua mikono yake na kuiweka kisogoni lakini nyuma ya shingo yake alikuwa amefadhi visu viwili vidogo ambavyo haikuwa rahisi kuvigundua alichomoa kimoja na kwa kasi ya ajabu, akamrushia Kubrah, na Kubra kwa kiwewe, akaiondoa bastola kumlenga Amata, Amata akachumpa kando na ile risasi ikamfumua yule jamaa wa nyuma yake, ikambwaga kando akiwa hana uhai. Kubrah akamsukuma yule mwanamke na kumwangusha pembeni, akamwendea Amata kwa kasi kisha akajirusha hewani katika mtindo wa kishaolin. TSA 1 akarudi nyuma na alipoona kubra anatua yeye ndiyo akaenda hewani kwa sarakasi maridadi na guu lake likatua kifuani kwa Kubrah, kisha kwa haraka akajigeuza na kumpa teke lingine maridadi lililopiga shavu la mtu huyo na kumbingirisha kando, alipotaka kuiwahi bastola ya Amata pale chini alichelewa, Amata alitua nyuma yake na kuukamata ukosi wa shati akiwa kamuweka katikati ya miguu yake. Alimwinua na kumpigiza chini, mwamba wa pua ukavunjika.
“Hata ungeenda nje ya nchi ningekufuata hukohuko!” akamwambia huku akimpigiza tena mara tatu zaidi. Kubraha alikuwa akigugumia tu, akajigeuza na kupeleka shambulia ambalo lililenga kutua kwenye korodani za Amata akawahi na kudaka ule mkono, akageuka na o na kuuvunja vibaya.
“Aaaaaaih! Mkono wanguuu!” akapiga kelele za maumivu.
“Nani kamuua Hamadou?” akauliza huku akiendelea kuzungusha ule mkono na kijana huyo asiye na utaifa kwa jinsi alivyo, aliyejificha kwa jina la Abiseilim alikuwa akipiga kelele tu. Lakini kwa bahati mbaya kilichokuwa kikiendelea huko ndani, waliokuwa ukumbini wote hawakukijua kutokana na uzito wa vioo vya kwenye milango, starehe zao zilizendelea na anasa zao zilishika hatamu.
“Aliye-kwa-kwa-mbia mi nam-jua n’ani? Aaaaaiiigh?” akagiga kelele na Amata akalegeza mkono. Kubraha akaona hana jinsi ila kujitetea kwa nafasi ya mwisho, akatumia mkono mmoja kupiga sehemu ya ndani ya goti la Amata, ambayo kwa nguvu na kasi ya pigo lile sis ajabu angevunja kabisa goti hilo lakini wepesi wa Amata ndiyoi uliyomwaokoa, kwani kwakuona pigo hilo, aliru hewani na kupiga samba lile pigo likapita patu, na alipotua akamaliza kazi kwa kutu goti lake kwenye kolomeo la Kubra.
“Oooohhhh!” akatoa yowe la mwisho na kukodoa macho, kisha taratibu akalegea. Amata akampekua mifukoni mtu huyo, akatoa simu ya mkononi akaitia mfukoni mwake, kisha akainuka kuondoka, alipogeuka hakumwona yule msichana. Jini? Akajiuliza.
Akatoaka taratibu baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa kwake, akavuta dirisha la alluminium na kujitupa nje akavuta hatua na kuzunguka hata kutokea upande wa pili wa jumba hilo, upande wa barabarani. Akatembea taratibu kama mtu ambaye hajafanya uharibifu wowote. Nje ya baa ile alishangazwa kukuta gari za polisi zikiwa zimewasha vimulivimuli vyake na askari kadhaa wakiwa pale, akapita taratibu na mara macho yakagongana na yule polisi wa kike, aliyemtia adabu usiku uliopita. Akamwangalia lakini hakufanya lolote, akaiendea ile tax katika maegesho ambayo karibu yake ilikuwa na askari kadhaa wameizunguka, alipoikaribia akasimama ghafla, alipoangalia ndani akakuta yule dereva ameuawa, amevunjwa shingo.
“Upo chini ya ulinzi!” sauti ya polisi ikamwambia.
“Nani na kwa lipi? Hivi hapa nani wa kumuweka chini ya ulinzi mwenzie?” akawauliza, wakanyamaza. Yule WP akawa anakuja taratibu upande huo.
“Ah! Huyu ni jambazi tia pingu kabisa, hakuna maswali. Na leo tumekukamata na kidhibiti kabisa,” akamwambia. Na kijana mwingine akaja na pingu tayari kumfunga.
Amata akavuta hatua kuondoka.
“Unajifanya uelewi au? Simama hapo, mpekueni ana bastola huyo ni jambazi mkubwa kabisa halafu sio wa hapa huyu,” yule mwanamke aliendelea kulalama. Kwa pale alionekana yeye ndiye mwenye amri.
“Kwa hiyo majambazi wa hapa wote mnawajua siyo, ila hamuwakamati kwa kuwa mnagawana nyara, sasa na wewe upo chini ya ulinzi,” akawambia na yule askari akawa amefura kwa hasira.
“Mpekuweni haraka nasema!” wakaanza kumpekua na kutoa bastola mbili wakampa yule mwanamama, “Si manona, mi jambazi nalijua, hili tuliliweka selo kimama chake kikaja kulitoa, mnaringia pesa? Hii ni serikali…”
“Ungekuwa unajua majambazi, ungekamata jambazi,” Amata akamkatisha wakatia huo yule kijana aliyekua akimsachi akatoa kitambulisho kidogo mfukoni mwake, akakitupia jicho, na kukunja sura, akaikunjua na kuonekana kama anatetemeka hivi.
“Na we Msuya nini? Umeona bangi?” akauliza yule WP. Msuya akampa kile kitambulisho huyo mawanmke alipokitupia jicho akatamani ajikojolee lakini akashinda kufanyaje, akajikuta mdogo sana kama punje ya haradali. Akamwemwesa midomo yake lakini asiweze kutoa neno.
ACP JAFARI MAKONO, kilisomeka hivyo, huku chini kukiwa na namba za kipolisi. Amata akakinyakuwa mkononi mwa yule WP, akakirudisha mfukoni.
“Utaniambia majambazi wote unaowaju na kwa nini hauwakamati,” Amata akamwambia huku akiondoka na kuvuka barabara kisha akachukua tax na kupotea.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
“Amata aliwasili katika mgahawa wa City Link na kuingia ndani ya gari yake, katika usukani alikuta kuna stika ndogo, akaipachua na kuisoma.
Transit Motel, Dar es salaam, Uwanja wa ndege, saa 10 jioni. Baada ya kukisoma akakitia mfukoni na kuwasha gari yake akaigeuza na kuondoka zake mpaka hoteli ndogo ya Kundayo ambako aliwekeza makazi ya muda lakini alijua sasa muda wa makazi hayo umekwisha. Akateremka na haraka akaingia chumbani na kumkuta mwanmke mwanamama mtu mzima akiwa chumbani humo lakini kageukia upande wa dirisha na kumpa mgongo Amata. Madam S! akawaza na yule mwanamke akageuka. Amata akachomoa bastola haraka.
“No! Im your boss!” akamwambia.
“Boss wangu haongei lugha ya kitumwa,” Amata akaeleza huku domo la bastola likiwa limetazama kule.
“Kama we ni bosi wangu kweli jibu swali hili…. Nitajie state of living….”
“State of living? Kwa nini kuniuliza swali la kitoto hivyo ilhali wajua boss wako ni mwanaitelijensia anayeweza kukujibu maswali magumua kabisa…”
“Kilichotokea pale, yule mama alishuhudia ganda la risasi likifyatuka kutoka juu ya Beretta na kuanguka chini Ngwe-nge-le!
Na yule mwanamke akenda chini bila ubishi. Amata akinua simu yake na kupiga namba ya Madam S, mara akasikia mlio wa simu ukilia ndani ya chumba kile, alipopepesa macho akakuta simu ile katika kiganja cha mkono wa mwanamke huyo, akapagawa, akamwahi pale chini na kumtazama sura.
“Madaaaaaaaaammmmmm!!!!!!!!” akapiga kelele na kuangua kilio cha uchungu na hasira…
***
Jiji la Arusha lilishikwa na mzizimo hasa baada ya taarifa ya mauaji yaliyofanyika Mererani Junction. Kila mtu alitahayari. Katika eneo la nje ya baa hiyo watu walijaa, waandishi wa habari walisambaa wakichukua picha hii na ile. Polisi walifanya kazi ya ziada kutawanya watu.
Yule mwanamke polisi (WP) alikuwa kama amelowa kwa mvua jinsi alivyokosa raha, tangu Kamanda Amata aondoke mahali pale alijifungia ndani ya gari na kutulia kimya akitoa amri kwa redio yake.
Polisi walivamia ile Mererani, wakaingia ndani na kukuta starehe za ngono na ulevi zikiendelea, wakakamata kila waliyemuona, wakaingia ndani kabisa na kukutana na maiti takribani nane hapa na pale na mwisho wakaikuta ile ya Abiseilim ikiwa imelala peke yake. Wakazipiga picha na kufanya upekuzi wa kina katika nyumba ile kwenye kila chumba walichokijua na baadi ya vyumba walikutana na carton za cocaine, heroine, mandrax na madawa mengine mengi. Silaha za aina mabalimbali na mavazi ya kipolisi, kijeshi, JKT na vifaa vingi vya upiganaji…
Na yule mwanamke akenda chini bila ubishi. Amata akinua simu yake na kupiga namba ya Madam S, mara akasikia mlio wa simu ukilia ndani ya chumba kile, alipopepesa macho akakuta simu ile katika kiganja cha mkono wa mwanamke huyo, akapagawa, akamwahi pale chini na kumtazama sura.
“Madaaaaaaaaammmmmm!!!!!!!!” akapiga kelele na kuangua kilio cha uchungu na hasira…
Kwa macho yake RPC wa mkoa wa Arusha alishuhudia hayo yote baada ya kuitwa eneo hilo na Mkuu wa upelelezi wa mkoa.
“Muuaji wa hawa watu mnaweza kumuhisi? Maana kuua ni kuua tu hata ukiua jambazi sheria bado itakuandama kwa kuwa umeua. Sasa lazima atafutwe na akamatwe kwa sababu uuaji huu ni wa kivita au kijambazi kabisa.
“Afande, hapa alikuja kijana mmoja tukaona kitambulisho chake ni afisa wa polisi ACP Jafari Makono, na ameondoka. Nahisi mauaji hayo atakuwa kayafanya yeye,” yule mwanake alieleza kwa upole.
“Huyo sio polisi, polisi yoyote akija kwa operesheni kubwa kama hii lazima mimi nipate taarifa, lakini sina kwa nini?” RPC alifoka, akainua simu yake na kupiga Makao Makuu Dar es salaam akaulizia kuhusu mtu huyo, jibu alilolipata lilikuwa tofauti na alilolitarajia.
“Hatuna ofisa wa jina hilo kwenye hicho cheo, na wala hatujatuma mtu yeyote kuja huko,” akajibiwa. RPC alijikuta anavimba kwa hasira, akamgeukia yule WP ambaye ndiye anayeongoza ile oparesheni. Yule mwanamke kwa habari ile akapata nguvu upya kabisa.
“Nilijua tu afande, yule jamaa ndiye tuliyemkamata juzi akaja kutolewa na mama yake anayejifanya anajua sheria na kututosha na vijipesa vyake,” akaeleza.
“N kwa nini mlimwachia wakati mnajua tunawahitaji watu kama hao? Hapa kwa vyovyote amekuja kulipiza kisasi, hizi biashara za madawa ndivyo zilivyo, ukidhulumu mwenzio naye anakuja kukumaliza,” RPC akaeleza huku akilielekea gari lake. Alipoketi kitini akamwita yule Mkuu wa upelelezi, “Sikia, namtaka huyo mtu ama hao watu, hakikisha unapekuwa kila hoteli na kila lodge na kila gesti mpaka mumlete kwangu nawapa saa sita tu muwe mmemkamata au kujua fununu zake,” akamaliza na kufunga mlango.
“Timamu afande!” yule Mkuu wa upelelezi akajibu na kupiga saluti.
***
Kamanda Amata akatulia kimya kwa muda, akainyakuwa ile simu na kuitazama, akatabasamu.
“Shit!” akang’aka, akamuendea huyo marehemu na kumgeuza sura yake, akagundua kuwa si mwanamke na pia alikuwa amevaa sura ya bandia. Akainuka taratibu na kuchukua kilicho chake, akapita mapokezi na kuaga kuwa anaondoka na atarudi siku iliyofuata hivyo chumba chake kisibuguziwe. Wakakubali na kuchukua funguo, Amata akaingia garini na kuondoka zake mpaka Ikulu ndogo, akaingia ndani na katika chumba kilekile akakutana na Madam S.
“Simu yako ikowapi?” akamuuliza. Madam akaiweka simu mezani.
“Na hii ni ya nani?” akamuwekea ile nyingine aliyoichukua kwa marehemu. Mwenye simu hii alinipa wakati mgumu sana lakini nimemuua, maana alivaa nguo yako hiyohiyo uliyovaa, alikuwa na simu hii na alikuwa ni wewe. Nikamuuliza swali letu la msingi, state of living akaanza kunambia kuwa namuuliza swali la kitoto. Ijapokuwa ulikuwa wewe lakini nilikumbuka ulivyoniambia kuwa State of living ni Living of state, kinyume cha hapo niue nami nikafanya hivyo, ulivyoikosea kujibu nikakufumua kichwa, baadae nikapiga simu yako ikaita ile ya yule mtu, nilichanganyikiwa lakini nikasema basi. Kwa kuwa hiyo ni kanuni yetu sisi watano ya kuji-difense kilichotokea nika-offense, lakini nilifumba macho,” akaeleza ilivyokuwa.
“Pole sana mi niko hapa na kama hao watu wameanza kuchukua sura zetu inabidi kuwa makini. Nipe ripoti…”
“Nimeangusha ngome nzima, Abiseilim ndiye Kubrah, nimshamtoa roho na watu wake kama nane hivi wote marehemu, nimewaacha polisi tu wakihangaika na mizoga yao,” akaeleza.
“Amata kila siku nakwambia kitu hichohicho hawa watu wakati mwingine tuwapate wakiwa na pumzi zao lakini we mtoto huelewi una nini?”
“Nina kanuni mbili tu, defensive na offensive, sasa ndizo huwa nazitumia na nilifundishwa kule chuoni kwetu,” akajibu.
“Haya, umeshinda, umepata tafutishi gani?” akmwuliza.
“Simu tu! Vingine wataviupata polisi sio mimi, ila cha msingi ni kuwa huyo uliyekutana naye uwanja wa ndege ndiye muuaji na amekwisha ondoka. Inanibidi nitue Maputo kumsaka,” akaeleza.
“Maputo Mozambique?” akauliza Madam.
“Yes, Mozambique, alipotoka hapa amekimbilia huko, na huyu si mwingine ni Benzilahagi, hapa alitumia jina la Ludovique Pereira,” akaeleza.
Madam S akatikisa kichwa kuionesha kumkubali kamanda Amata,
“Ndiyo maana nakupenda!” akamwambia.
“Nipo gado,” akajibu Amata huku akiipekuwa ile simu ya marehemu na kupakua faili zote za msingi akazitia ndani ya kompyuta yake ndogo.
Madam S akainua simu na kupiga mahali anakokujua yeye, akaomba ndege ya haraka kufika Arusha, na alipokata akiweka simu na kumtazama Amata.
“Saa moja ijayo, Auric Air itakuwa hapa, mara moja ufike Dar na pale Air Tanzania watakufikisha Maputo bila shaka!” Amata akamwambia.
“Asante Boss!” akajibu na kuinuka, “Oh! Nimesahau, yule dereva tax ameuawa,” akamwambia.
“Nani kamuua?”
“Kiukweli sijui, nilimwacha nje kwa maana alinifikisha hapo alipomchukua yule mteja. Nilipomaliza kazi yangu nikatoka nje na kukuta amevunjwa shingo, wale polisi wako wale wakataka kunikamata tena…”
“Ukawafanya nini…”
“Wakanipekua na kunikuta na kitambulisho bandia cha ACP Jafari Makono…”
“Hah! Hah! Hah! Hah!” Madam S akacheka sana, watakoma mama zao kudadeki,” Madam S akamalizia kicheko, “Najua tu watapiga simu Makao Makuu…”
“Simbeye atacheka mpaka aanguke,” Amata akamalizia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
4
“Uwe mwangaifu Amata, nakutegemea sana, si mimi peke yangu bali hata Mheshimiwa anajua nini unafanya kwa sasa, na amesema yale maoni yako atayafanyia kazi. Angalia sana wanawake wa Mozambique, ukijilegeza wataiteka roho yako inyauke kama mti. Fanya kazi hakikisha huyo anayeitwa Benzilahagi apne uchungu wa maisha, usimuue, mkamate ila akibisha mlipue,” Madam S akasema hayo akiwa amesimama wima wakitazamana na kijna huyo. Kutokana na Amata kumzoea mwanamama huyo alijua daima kuwa akikupa maagizo huku kasimama ujue hapo hataki ufanye mchezo, anataka kazi.
Amata akapiga saluti, “Yes Sir!”. Madam S akasonya.
“Ondoa mkia wako hapa!” akamwamuru, na Amata akatoka katika sebule ile lakini kabla hajamaliza mlango.
“Kamanda Amata…” Madam akaita, naye akasimama na kugeuka, “Come back alive!” akamwambia akimaanisha arudi akiwa hai.
***
TRANSIT MOTEL – DAR ES SALAAM
AMATA RIC aliwasili katika motel hiyo muda wa jioni kama saa kumi hivi, ndege yake ilitakiowa kuondoka saa mbili usiku. Kwa usafiri wa tax alifika eneo hilo, akashuka na kuiacha ile tax ikiondoka, akavuka geti na kukunja kulia akasukuma lango uliomfikisha katika baa ndogo lakini yenye utulivu wa hali ya juu. Akiwa anajivuta kuelekea kaunta alisikia mtu anakohoa nyuma yake, akageuka na kumwona mzee aliyevaa koti la khaki na kofia kubwa la pama kichwani mwake akiwa kajiinamia na mezani alipokaa kuna chupa kubwa ya maji. Akarudi na kuketi katika kiti cha mbele yake, akaletewa kinywaji, Safari bia baridi, na yule mhudumu alipoondoka, Amata alimtazama mzee huyo.
“Hongera kwa kazi uliyoifanya Mererani Junction,” yule mzee aliongea kwa sauti ya kukwaruza huku akikohoa mara kwa mara, Amata alijaribu kumtazama mzee huyo lakini hakumgundua kwa kuwa pozi lake alilokaa na kofia ile iliuficha uso wake.
“Asante, lakini wewe ni nani?” akauliza Amata.
“Aaaaah hunijui, mimi ni yuleyule tulikutana Moshono, na ndiye nilikuletea ile miwani kule hotelini Kundayo,” akaeleza.
“Na unajuaje hizi misheni zangu?” akamwuliza.
“Sikiliza kijana, kabla hujatua unyanyo wako mahali mi nilishafika, daima kipi utafanya mimi najua, lakini siwezi kujitokeza hadharani ila najua ninavyofanya ili wewe na watu wako mfanikiwe, TSA hamko sita tu, wapo na wengine ambao wewe huwajui lakini wao wanakujua,” maneno hayo ya yule mzee yalimwingia, hakutaka kuuliza sana alitulia kimya tu na yule mzee akaendelea.
“Kule unakokwenda, ukitaka ufanikiwe, usijioneshe kiurahisi, tumia akili zako zilizokufanya uajiriwe kitengo hiki, intelijensia, bila hiyo utayakosa maisha. Acha papara, wala usijenge uhusiano na mtu, uwe kivyako lakini hakikisha unakuwa Double Agent, ingia katika himaya yao, jifanye mmoja na wao, kisha wageuke kumaliza kazi utakapoona pamekuwa sawa, asante,” yule mzee akamaliza. Amata akainua bia yake na kuinywa yote kwa mara moja. Alipomaliza akaaga na kuondoka huku kichwani bado akijiuliza maswali mengi juu ya mzee huyo aliyekuwa kama mzuka katika kazi zake maana alihesabu kuwa kazi hii kamtokea mara mbili na kazi ile ya Hujuma alimtoke tane kule Somalia. Anyway, maadam hana madhara, akaondoka eneo hilo, safari hii hakutumia usafiri wowote zaidi ya miguu yake, kwani kutoka katika Motel hiyo mpaka kufika Uwanja wa Ndege ilikuwa ni mwendo wa dakika thelathini tu.
NDURUTA
RAIS SEBUTUNVA alipatwa na mshtuko mwingine uliomnyong’onyesha moyo wake baada ya kusiki kifo cha Kubrah. Jasho jembamba lilimwagika kutola kwenye vishina vya nywele zake zilizochanganyika kati ya nyeupe na nyeusi. Aliikuna pua yake, akasimama kisha akakaa tena. Watu wangu wanaisha, huyu jamaa ameamua kuwasafisha, akawaza huku akifunga faili lililokuwa mezani kwake. Mmoja kamfunga kule Tanzania, na nina wasiwasi sana itakuwaje kama atatoa siri ya huu mpango, akazidi kuwaza na kuwazua pasi na kupata jibu. Lazima nifanye kitu, nani huyu muuaji anayeweza kuvunja ngome yangu namna hii, tena kirahisi hivi, jinsi nilivyoficha watu wangu yeye anawezaje kuwagundua? Hapana ipo namna na lazima nifanye uchunguzi, akapitisha uamuzi na kutoka pale alipokaa, akahama na kuufunga mlango akimpita katibu wake na kuingia ofisi nyingine ndani ya jengo hilohilo la Ikulu.
Alipoketi akainua simu yake na kuongea na mtu fulani akitaka aonane naye usiku huohuo maana kulikuwa na kazi ngumu ya kufanya. Akatulia kimya huku macgo yake yakionekana kutona chozi kwa mbali.
Baada ya saa nne…
Jeep Cherokee iliegeshwa kando ya jumba la kifahari lililowekwa Ulinzi wa kutosha, wanajeshi wenye bunduki kubwa kubwa wakiwa pamoja na vijana wa polisi walizunguka kasri hilo, kasri la kupendeza.
Mwanaume mmoja, mwenye umbo la miraba minne, mweusi anayeonekana kuwa katili tangu ndani ya mboni za macho yake, aliweka mguu katika ardhi ya eneo hilo. Saluti zaikamwagika kutoka kwa wale vijana wanaolinda eneo hilo. Akavuta hatua na kuongozwa ndani ya hilo kasri. Alivaa suti, wengi huiita Kaunda Suti ambayo ilimkaa vyema kabisa na kulisanifu umbo hilo katika ubora wake.
Kanali Beinsoir Banginyana alikaribishwa katika chumba kidogo cha jumba hilo ambako alimkuta mwenyeji wake, Rais wa Nduruta, Mh. Sebutunva akiwa anamsubiri kwa shauku.
“Yes Boss, kuna mission nyingine?” akauliza mara tu baada ya kutupia salamu ya utii kwa rais huyo mwembamba, mrefu mwenye pua ndefu.
“Ndiyo, lakini sasa haitafanana na ile ya Mpumbutu…”
“Kivipi?” Akamkatisha.
“Na pia nahisi tu utaifurahia kwa jinsi ilivyo ndogo, ya dakika mbili tu lakini utakuwa umeokoa himaya nzima ya Kerebu Empire, iliyopo na inayokuja. Unajua mipango yetu ilivyo, unaju jinsi ilivyovurugwa kuanzia Ujerumani, ikaja Mpumbutu na kule Tanzania. Hawa jamaa wanataka kujionesha kuwa ni vidume wa Afrika katika medani za upelelezi,” akamweleza Banginyana.
“Hapo bado umeniacha kwenye mataa mkuu,” akaonesha shaka yake wazi wazi.
“Bensoir, unajua kuwa baada ya kusambaratishwa ule mpango wetu wa Mpumbutu, Ilikuwa tumuoneshe jeuri yule jamaa…”
“Ndiyo!”
“Lakini ilishindikana, mtu wetu tuliyempandikiza, akakamatwa na yuko jela hadi sasa, kama bado yupo hai…”
“Lakini si unajua nani hakukamatwa?”
“Ndiyo, Benzilahagi alitoroka, na wenzake wawili wale,” akaeleza.
“Yeah yule tuliyemkodi kutoka Yemen, alitorokea Arusha kwa kuwa pale nilimweka kwa shughuli maalum, na Benzilahagi alikuwa Arusha na katekeleza vyema ule mpango wentu namba nne…”
“Na amefanikiwa kuondoka?” akauliza kanali yule.
“Ndiyo, ameondoka na ameelekea mafichoni kama kawaida, kanipa taarifa kuwa yuko salama,” akakohoa kidogo na kuchukua kitambaa chake akafikicha macho na kukiweka kando, kisha akaendelea, “ Sasa yule jamaa wa Yemen wakamshtukia, ameuawa leo hii na vijana wengine nane waliokuwa wakimzunguka muda wote kwa usalama…”
“What? Ni yule mwanamke aliyemuua?” Banginyana akang’aka kwa hamaki huku akisimama.
“Sasa hapo ndipo pana utata, kwa sababu wote wamekufa, nani atanambia ukweli kuwa muuaji ni nani, na ndipo ninapochanganyikiwa,” akatikisa kichwa.
“Mmmmmm, sasa nahisi damu inachemka, lakini nitakwambia kitu…”
“Nambie Kanali…”
“Kuniambia mwanamke yule kaweza kufanya mauaji hayo, nakataa, kuna kiumbe pale Tanzania ni hatari sana, kama ni nyoka sijui yule nimpe jina gani labda swila. Huyu kiumbe ndiye aliyemuua Kyamapaso kule Ujerumani,” kauli hii ilimfanya Sebuntunva kushtuka na kujishika kifuani.
“Enhe…”
“Huyu jamaa ndiye aliyemkamata Briston siku ile pale chimbo, ni hatari, huyu anaweza kufanya hili lakini si huyu mwanamke,” akajiweka kochini kisha kidole chake kikabonyeza shavu lake na macho yake akalitumbulia paa.
“Sasa, kanali, unafikiri hatoweza kuzifuata nyayo za Benzilahagi na kujua alipo?” akauliza Rais.
“Huo ndiyo mtihani, njia pekee ni kumdhibiti huyu kenge mbaya kabisa mwenye sumu mpaka kwenye maneno yake…” Banginyana aliongea kwa uchungu na hasira, “Namtaka,” aliongeza huku akiuma meno.
“Sasa tupange mkakati, kwa vyovyote kama kafika kwa Kubra basi atafika na kwa Benzilahagi halafu tutajilaumu mara mbili kwa kutochukua hadhari juu yake, tufanye mpango…”
“Upi?” Banginyana akadakiza swali na kuikata kauli ya Sebutunva.
“Tumpoteze Benzilahagi kwa muda wakati tukimtega huyo kenge kila kona,” Rais Sebutunva aliweka mpango mahsusi pamoja na Kanali Banginyana, mpango huo ukapita na hatua za utekelezaji zikawekwa vyema.
“Nina hamu sana nimtie mkononi kiumbe huyu… na nitamnyonga kwa kono langu hili,” akainua mkono wake huku akisimama tayari kuondoka, “Mkuu mpango huu wa Benzilahagi ukikamilika nitakwambia hapo ndipo nitakwenda kumsaka mwenyewe kwa udi na uvumba. Naomba niende na nitakupa jibu kesho au keshokutwa,” akamaliza na kuagana na Rais huyo, akaondoka zake.
***
…Maringo binti Maringo,
nitakukumbuuka daima,
Kwenye vitabu vya kumbukumbu,
mateso mateso nitaandika.
Baba Kawasaki alinikanya,
hapa mjini nenda polepole,
Utavamia walanguzi wa mapenziiii
waikaange roho yako iny….
“Samahani, sijui kinywaji gani utapenda kutumia?” sauti nyororo ya mhudumu wa ndege ya Air Tanzania, ilimkatisha kutoka katika burudani tamu ya muziki ule wa Msondo uliokuwa ukisikika kutoka katika spika ndogo zilizofungwa kitaalamu ndani ya ndege hiyo. Kamanda Amata alikuwa safarini kuelekea Maputo ili kukamilisha kile alichotumwa na serikali yake.
“Asante sana, naweza kupata kinywaji kitamu kama sura yako?” akauliza na yule dada akatabasamu, tabasamu lilioutikisa moyo wa rijali huyo.
“Umejuaje kama nina uso mtamu?” akuliza yule dada.
“Aaaa macho imeona dada… waitwa nani?” akaanza ubembe wake kwa mtoto wa watu.
“Tusa…, Tusajigwe!” akajibu.
“Tusajigwe, jina zuri sana, naomba safari baridi tafadhali,” akamwambia na yule mwanadada mrembo aliyevalia suruali ya kijani cha mgomba, blauzi ya cream na kitambaa shingoni mwake kilichoandikwa Air Tanzania The wings of Kilimanjaro akampatia kinywaji hicho na kisha akasukuma kile kitorori chake na kuondoka.
Amata akamsindikiza kwa jicho la huba kisha akakumbuka jambo, akaingiza mkono katika koti lake kwa ndani na kutoa simu Sonny Ericson Touch Screen. Ilikuwa simu ya kisasa sana yenye mambo mengi sana kuliko simu nyingine. Akaiwasha na kuigusa hapa na pale, akachungulia kwenye box la ujumbe mfupi na kupitia jumbe hizo.
“For the great job you have done, meet Mr. Pampula Colonha ata Airport, and he will take you somewhere for moment…”
Ujumbe uliishia hapo, ukimtaka Bwana Benzilahagi baada ya kazi kubwa aliyoifanya, akutane na Bwana pampula Colonha pale uwanja wa ndege ili akamhifadhi sehemu. Kamanda Amata aliusoma mara kwa mara ujumbe huo ili kuweza kuujenga kichwani mwake.
Mr. Pampula Colonha, akawaza na kisha akaendelea kupekua na nyingine nyingine.
“Mr Bocca will meet you, he is at The Quiety Corner Guest house, he has something to give you and then yu will know where to send it…. But everything is as usually”
Ujumbe mwingine ulimaliza ukiwa unampa taarifa mtu huyo kuwa atakutana na Bwana Bocca akabidhiwe mzigo na yeye atajua wapi pa kuutuma lakini kila kitu ni kama kawaida. Akaandika kichwani mwake mambo matatu ya kuanzia.
Mr. Pampula Colonha, Mr. Bocca na The Quiety Corner Guest House, kutoka hapa nitajua ramani ya wapi muuaji wangu alipo, Madam anamtaka hai, sijui kama itawezekana akawaza huku akiipitia ile simu kila kikabrasha na kukuta mengine mengi asiyo fahamu ikiwamo biashara haramu ya Madawa ya kulevya, pembe za ndovu na ile ya Almasi, wamejidhatiti kweli kuhakikisha wanaimarisha utawala wao, mxiuuuuuiy serikali ya Dodoma itawafunga vinywa, akamaliza na kuitia mfukoni ile simu, mara hii ikiwa imezimwa. Akachukua bia yake na kukuta ubaridi umepungua.
“Aaaa nini tena hii lo!” akajikuta akiongea peke yake, akimiminia kichwani yote tarumbeta na kurudisha ile chupa mahali pake. Pembeni yake aliketi mwanamama wa wakamo kama miaka hamsini au sitini hivi.
“Kijana unywaji gani wa bia huo?” akauliza.
“Aaaa kwetu Kongo huu ndiyo unywaji mama,” akamjibu.
“Kwani we Mkongomani?” yule mama akauliza kwa Kiswahili kilichojaa lafudhi ya Ki-msumbiji.
“Yeah, mimi ni Mkongoman natokea Katanga,” akaeleza.
“Sasa unaenda wapi?”
“Oooh mama, si unajua ile mambo ya Congo, muziki na madanse kila kwenye pembe ya dunia,” Amata akjibu na kujigiza lafudhi ya Ki-kongo. Yule mama akamtazama Amata vizuri na kupambana na mikufu miwili ya dhahabu tupu iliyokuwa ikining’inia shingoni mwake, suti safi nyeupe ilimpendezesha kijana huyo, akashusha macho miguuni na kukuta na ‘nchomoyo’ yaani kile kiatu cha kuchongoka, kilichosheheni mng’aro wa uliotaka kutoboa macho ya mama huyo.
“…Mabibi na Mabwana, ndege yetu ya Air Tanzania, Boeing 737 inatarajia kutua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mavalane, Maputo Msumbiji. Hivyo wote mnaombwa kufunga mikanda na mtulie kwenye siti zenu. Asante kwa kutumia usafiri wa shirika letu na karibuni tena…”
Sauti nyembaba tamu ya Tusajigwe ilisikika kupitia spika zilezile zilizokuwa zikitoa muziki ule laini wa Kitanzania. Kila amtu akajianda kwa mtuo huo, wengine wakipiga ishara ya msalaba na wengine wakiomba miungu yao wanaoijua wao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
Kamanda Amata aliteremka wa mwisho katika ndege hiyo, akatembea kuwafuata abiria wenzake kule wanakoelkea wakiongozwa na mhudumu wa ndege hiyo mpaka katika mlango mmoja wa kioo ambao juu yake ulibandikwa kibao kilichosomeka ‘38’. Pale walijipanga sehemu na kusubiri mizigo yao iteremshwe na kufikishwa hapo kwa mashine maalumu kwa kazi hiyo.
Dakika kumi natano baadae alikuwa ameshalipata begi lake na taratibu akaiendea meza ya watu wa ukaguzi wa pasipoti na mambo mengine. Hapo akamkuta mwanadada, mrefu wa wastani aliyejazia vyema mwili wake, kwa haraka haraka alionekana anapenda kula sana kwa pembeni yake tu kulikuwa na kopo la ‘springle’, akainyakuwa ile pasipoti na kuisoma nchi miliki.
“We ni Mkongoman?” akauliza kwa lugha ya kireno.
“Ndiyo!” akajibu huku akiipachika vyema miwani yake usoni. Yule mwanadada akamtazama na kuanza kuipekua ile pasipoti, kurasa zote zilikuwa zimejaa mihuri ya nchi mbalimbali, mpaka akashangaa, akamtazama tena bila kummaliza.
“Unafanya kazi gani?” akauliza tena. Amata hakujibu akamtazama na kutazama watu walio nyuma yake katika foleni. Sasa haya maswali gani wakati pasipoti anayo? Akajiuliza.
“Mwanamuziki,” akajibu na kunyamaza kimya. Yule mwanadada akaendelea kugonga mihuri yake, kisdha akachukua kalamu na kuweka saini, akarudisha ile pasipoti.
“Muziki utakuwa wapi? Mi napenda sana muziki rafiki yangu, wewe itabidi uwe rafiki yangu,” yule mwanadada akamwambia Amata huku akimkabidhi pasipoti yake.
“Usijali, tutakuwa na show saa tatu usiku wa kesho, karibu sana,” Amata akajibu na kumpa kadi ya biashara.
“Wapi?”
“The Quiety Corner,” akamjibu huku akiondoka zake na kutoka nje ya uwanja huo.
Usiku ulikuwa mnene sana, hakukuwa na watu wengi nje ya uwanja huo isipokuwa wachache tu waliokuja kwa kazi za kupokea ndugu au wafanyakazi wa idara zao. Amata akawapita watu wote na kufika katika eneo ambalo halikuwa na watu kabisa, akasimama huku begi lake likiwa chini. Sekunde kadhaa mtu mmoja wa makamu alisimama kariu yake na kujikohoza.
“Mkh! Mkh! Mkh!” kisha akiweka mikono yake mfukoni, na kuondoka kuelekea katika maegesho. Alipofika aliegemea gari moja ya kisasa sana, Audi, nyeupe metaliki. Amata alitua begi lake na ghafla akachomoa bastola, kabla hajamwambia lolote mtu huyo, akawahi kuomba utulivu.
“Easy, easy kijana!” akamwambia na Amata akarudisha bastola yake kwani alielekezwa hivyo. Kisha wote wawili wakaingia katika gari hiyo na kuondoka zao. Safari ya kilomita moja na mita mia nne iliwafikisha katika nyumba ya wageni ya kawaida kabisa, siyo nzuri sana wala mbaya sana. Moringa Guest House, ilisomeka hivyo kwenye kibao cha mbao kilichokuwa katika njia panda ya barabara ya Vladimir Lenin, wakakunja kona kushoto na kuingia kwenye hoteli hiyo.
“Moya Mampasi!” akamwambia mhudumu wa mapokezi, akamwonesha chumba na Amata akakiendea na kuingia ndani. Ilikuwa chumba cha kawaida tu, kitanda kimoja kikubwa kilichotandikwa shuka jeupe na mito ya kulalai ya rangi hiyohiyo. Busati la nguvu na gharama liliificha sakafu hiyo, kabla hajafanya lolote mlango wake ukagongwa, akatazama nyuma na kuchomoa bastola yake, akauendea mlango na kuufungua. Sura ya mwanamke mrembo ikamtazama kwa tabasamu, Amata akamwangalia kuanzia utosini mpaka miguuni.
“Bem-vindo menina!” karibu msichana, akamwambia binti huyo huku akimpa tabasamu la nguvu alilohisi kummaliza nguvu mwanadada huyo. Kwa nguo alizovaa alijua wazi kuwa ni mhudumu wa nyumba hiyo ya wageni kwani katika pindo la mfuko wake wa koti paliandikwa ‘Moringa GH’.
“Muito obrigado! aqui estão o envelope,” yule mwanadada akamwambia Amata, akimaanisha kuwa ana bahasha yake. Amata akanyosha mkono na kuipokea, akaigeuzageuza na kuitupa kitandani.
“Obrigada! Existe algo mais ?” akimaanisha kama kuna lingine zaidi.
Baada ya mazungumzo machache yule mwanadada aliondoka na Amata akabaki peke yake, akaichana ile bahasha na ndani yake kulikuwa na kijitabu kidogo na funguo ya gari. Juu ya kitabu kile kulikuwa na picha ya gari moja nzuri sana kwa mwonekanao wa nje, nyeusi inayong’aa. Akapekua ndani yake na kukuta kadi moja ya kielektroniki yenye tarakimu fulani fulani juu yake. Akiwa katika kupekua bahasha hiyo ikaanguka kadi nyingine ndogo ya biashara.
Akavitupia kitandani na kuvua koti lake kisha akaelekea maliwato kuoga na kurudi kujipumzisha.
*****
Asubuhi ya siku iliyofuata aliamka mapema sana na kuingia gym iliyokuwa ndani ya nyumba hiyo ya wageni. Ilimchukua saa tatu za kufanya mazoezi hayo makali ya viungo.
“Hongera kwa mazoezi!” sauti ya kike ilisikika kutoka nyuma yake, akageuka na kukutana macho na mwanamama wa kizungu wa kadiri ya miaka sitini au sabini hivi naye akiwa katika amshine mojawapo akifanya mazoezi mepesi, “Unaonekana u mgeni hapa?” akauliza.
“Kwa nini unaniuliza hivyo?” akajibu kwa swali huku akichukua taulo lake na kujifuta jasho.
“Kwa sababu sijawahi kukuona kabisa,” yule mama akaeleza.
“Yeah, nimefika jana usiku,”
“Oh! Bom!” akamsifu, “Una body nzuri ya mazoezi...”
Kamanda Amata akatabasamu tu, akachukua chupa yake ya maji na kunywa ya kutosha.
“Karibu sana nyumbani kwangu, mimi ni mjane ninaishi peke yangu, watoto wangu wapo Ureno,” akamwambia. Amata akasukuti kama sekunde mbili tatu hivi.
“Asante sana, nitafika,” akajibu kisha akachukua kadi ya biashara ya mama huyo na kutoka zake pale gym kurudi chumbani huku akisindikizwa na macho ya mwanamama huyo.
Baada ya kupata kifungua kinywa, alitoka katika nyumba hiyo majira ya saa nne hivi na kuelekea katika maegesho ya hoteli hyo ndogo, akachukua simu yake na kuandika zile namba zilizokuwa katika ile kadi aliyoipata kwenye ile bahasha, alipomaliza akabofya ‘ok’ na mara gari moja ya kisasa ikawaka taa na kuanza kuunguruma. Amata akaikaribia na kuitazama kwa mbali. Ilikuwa gari ndogo, fupi iliyo chinichini sana, tairi zake za sports ziliifanya kupendeza zaidi.
“Kilimanjaro XT II” alisoma andishi la chuma lililondikwa kwa ufundi nyuma ya gari hiyo. Akafungua mlango na kuingia, akaketi kitini.
“Funga mlango tafadhali,” sauti ilisikia kutoka katika vipaaza sauti vya siri vilivyofungwa ndani yake.
“karibu Kilimanjaro XT II, gari ya kisasa kabisa iliyotengenezwa Tanzania, ni gari bora kuliko zote Afrika. Bonyeza batani nyekundu katika usukani ili kujisajili kama dereva wa gari hii...” ile sauti ikampa maelekezo, akabonyeza hiyo batani, na pale juu ya usukani pakafunguka, kijiluninga kidogo kikajitokeza.
“Tamka jina lako mbele ya luninga hiyo...” akafanya hivyo.
“Weka kidole gumba ili tupate alama za kidole chako...” akafanya hivyo.
“Sasa, wewe ni dereva wa gari hii na si mwingine, yeyote atakayethubutu kukaa juu ya kiti hicho hatopata muda wa kujuta... asante na karibu tena, kumbuka kutamka jina lako kila unapoketi kwenye kiti cha dereva kinyume na hapo injini haitafanya kazi,” ikamaliza. Na Kamanda Amata akashusha pumzi, akafungua dashboard na kuchungulia ndani yake, kulikuwa na bastola tu na magazine yake pembeni, akainyakua na kuiweka sawa kisha akaibana katika kizibao chake, akachukua simu yake na kufungua hapa na pale kwenye google map, akaandika
starting point ... Moringa guest House - destiny... The Quiety Corner guest house.
Simu ile ikamletea ramani ya Maputo na kuonesha nji anayotakiwa kupita ili kufika eneo hilo. Akaondoa gari yake maegeshoni na kuikamata barabara ya Vladimir Lenin kama alivyoelekezwa na GPS yake. Msukumo wa injini ya gari hiyo ulimfanya Amata kupata mzuka wa kwenda kasi na kuangalia alama za barabarani.
Dakika kama ishirini hivi aliifikia hoteli hiyo ndogo iliyojengwa katika viunga vya jiji hilo lililotawaliwa na Mreno miaka mingi nyuma na wenyeji wake kutawaliwa na lugha hiyo ya kireno huku Kiswahili wakibabiababia kwa mbali. Kilimanjaro XT II ilzimwa injini na kutulia palepale ilipoegeshwa huku kijana huyo akiteremka na kuielekea nyumba hiyo tulivu ya wageni. Kama lilivyo jina lake, The Quiety na kweli ilikuwa kimya mno, miti na uoto wa asili uliizunguka kila upande.
Nyuma ya meza kubwa iliyotengenezwa kwa mbao safi na kushikanishwa na ukuta kulikuwa na mwanadada wa Ki-macua, aliyevutia kwa sura akiandika hiki na kile.
“Habari yako mrembo!” akasalimia.
“Nzuri sijui wewe,” akaitikia na kuacha kuandika yale makabrasha yake, “Naweza kukusaidia?” akaongeza swali.
“Yeah, naweza kumuona bwana Bocca?”
“Bila shaka, pita hapa na moja kwa moja nyumba yake ipo paleee unapoona minazi minazi hivi,” akamwelekeza.
“Asante sana,” akaitika na kupita katika ujia huo aliooneshwa na kuvuta hatua za uhakika kuielekea nyumba hiyo ambayo ilikuwa imejengwa mbali kidogo na mapokezi. Akiwa njiani kabla hajafika kwenye ile nyumba akakutana na vijana wawili waliokuwa wamesimama kando ya minazi ambao ilikuwa ni vigumu kuwaona kama hukuwa na macho zaidi ya mawili.
“Stop!” wakamsimamisha naye akasimama, “Unakwenda wapi?” mmoja akauliza.
“Nakwenda kumwona bwana Bocca,” akajibu.
“Una miadi naye?”
“Hapana ila nataka kuongea naye biashara,” akajibu. Wale jamaa wakaongea kireno kisha wakawasiliana na watu wa ndani, Amata akaruhusiwa kuingia katika nyumba hiyo. Kwa nje ilionekana ya kawaida sana, iliyoezekwa kwa makuti ya mnazi na kuta zake zilikuwa za mawe ya matumbawe. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na samani za kila aina, mzee mmoja mtu mzima aliketi katika kochi moja kubwa la vono, huku mapajani kwake akiwa amembeba paka mwenye manyoya meupe na marefu. Mzee huyo alikuwa na nywele ndefu alizozibana nyuma ya kisogo chake.
“Karibu sana kijana!” yule mzee akamkaribisha na kumwonesha mahali pa kuketi, lakini Amata kama hajaona maelekezo yale, akaketi katika kiti kingine, “Naitwa Mr. Bocca, nikusaidie nini?” akuliza.
“Naitwa Moya Mampasi, raia wa Congo DR!” akajibu kisha akashusha pumzi na kuiweka vyema ile mikufu yake pale shingoni, “Nafikiri sijakosea, maana nilidhamiria kuja kwako bwana Bo...”
“Subiri kwanza!” yule mzee akamkatisha na macho yake akayapeleka kwenye luninga ndogo iliyokuwa pembeni tu ya meza yake.
“Oh! Shit! Akang’aka na kupiga ngumi mezani, akamweka paka wake chini na yule paka akaondoka. Yule mzee akabonya kitufe fulani chini ya meza hiyo na vijana watano wenye silaha wakaingia sebuleni.
“Mchukueni huyu mumuhifadhi kisha nitamwitaji baadae, tumevamiwa!” akawaambia na wale vijana wakamvamia Amata.
“Tulieni!” akawaambia, “Kuna nini Mr. Bocca?” akamuuliza yule mzee.
“We mpumbavu, hapa mambo yameharibika wafuate hao haraka,” akapiga kelele yule bwana huku akiwaamuru kwa mikono wa mchukue Amata.
“Mnakosea... subirini,” kabla hajamaliza kusema zilisikika risasi zikipiga ule mlango, Amata akruka na kuwasukuma wale jamaa wote wakaenda chini na zile risasi zikachimba ukuta. Akamnyamg’anya mmoja wao shotgun aliyokuwa nayo mkononi na kumwaga njugu kiufundi, wale jamaa wote wakaenda chini. Akanyanyuka kutoka pale na kusimama wima, mbele yake alisimama kijana mwingine mwenye silaha kutoka kundi la wale adui, alipojaribu kufyatua risasi alikutana na teka mahiri lililomyumbisha, kabla hajakaa sawa, makonde matatu ya maana yalitua mashavuni mwake na kumwacha hoi.
Yule bwana akajitahidi kujitetea, alirusha konde la kwanza, Amata akaepa, la pili vilevile, la tatu Amata akalidaka na kuunyonga mkono kisha akamzabua konde la tumboni.
“Aaaaaiiigh!” akapiga yowe la uchungu, Amata akamwacha na kumrukia teke lingine kali, akaenda chini.
“Stop!” Bocca akapiga kelele, Amata akamwacha yule jamaa hoi akitema damu.
“Oh! Good, nani kakutuma?” Bocca akamuuliza yule jamaa huku kamdidimiza domo la bastola kinywani.
“Pereire, katutuma Pereira!” yule jamaa akasema.
“Mchukueni huyu muwekeni stoo, nitaongea naye vyema,” akawaambia vijana wake kisha akamtazama Amata, akatikisa kichwa “Wewe ni mpiganaji mzuri sana... hah! Hah! Hah!” akacheka huku akimpigapiga begani na kuwaangalia wale marehemu pale chini, kisha akamtazama tena Amata, “Sikia, nitahitaji sana msaada wako, na nitakupa pesa nyingi,” Bocca akamwambia Amata, na wakati huo tayari vijana walikuwa wamefika na kuondoa zile maiti huku wengine wakisafisha kwa mashine zuria hilo....
Amata akaketi kitini, yule mzee akaliendea jokofu na kuja na kinywaji kikali, mkononi akiwa na bilauri mbili, akaziweka mezani na kumimina.
“Cheers kwa afya!” akasema huku akigonganisha bilauri yake na ile ya Amata, “Unajua kijana mimi naitwa Bocca, ukisikia Bocca hapa Maputo ndiyo mimi, hakuna asiyenijua na siishi kwa kujificha. Mimi ni mfanya biashara na hawa vijana waliokuja kuvamia hapa wametumwa na mfanyabiashara mwenzangu...”
“Kwa nni kawatuma?” Amata akamkatisha kwa swali.
“Aaaaa unajua hizi biashara zetu bwana hazina uaminifu hata siku moja, mkiudhiana kidogo tu basi, mauaji au kupeana ulemavu ni kama kununua gazeti na kusoma,” akasogeza uso wake karibu na wa Amata, “Ila wewe ni mpiganaji mzuri sana, hapa nina wapiganaji lakini we jamaa ni noma!” akamwambia.
“Sasa Mr. Bocca, hujaniuliza hata kitu gani kimenileta kwako,” Amata akamweleza.
“Oh! Ha! Ha! Ha! Ni kweli asee, unajua umenifurahisha kwa mengi ndo maana, nambie Bwana Mo...”
“Moya Mampasi,” Amata akamalizia.
Amata akajikohoza kidogo kisha akamtupia jicho mzee huyo, “Nahitaji kazi...”
“Ishia hapohapo! Kazi umepata, tena wewe nitakuweka kwenye kitengo changu nyeti kabisa cha kukutana na wateja wangu, lakini kwa kuanza kuna kazi moja ya kufanya ambayo nilikuwa naihairisha siku nyingi sana,” akamwambia.
“Obligado!” Amata akashukuru.
“Nitakupeleka shamba, lakini utakachokiona huko ukische hukohuko, ukitoa siri sintojali we ni nani, nitakuua,” akamwambia huku akiichukua bastola yake na kuipachika kiunoni. Wakafuatana na kutoka nje kwa upande wa nyuma, huko walikutana na wale jamaa wakizifukia zile maiti, mwili wa Amata aliingiwa na ganzi kwa kitendo hicho walichokuwa wakikifanya vijana hao, lakini alijipa nguvu.
“Usitazame hayo, huku kwetu ni maisha ya kawaida kabisa, tangu nimekuja huku kibiashara hiyo ni kazi inatokea japokuwa ni mara moja kwa miaka,” akaeleza.
“Ina maana wewe si mwenyeji wa hapa?”
“Hapana, ni raia tu lakini mzaliwa wa Nduruta, hapa tunapiga hela tu,” akajibu swali huku wakiingia kwenye gari, Toyota Lexus na kuondoka zao.
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mwendo mrefu walifika nje kabisa ya mji wa Maputo, kando ya barabara ya kuelkea Afrika Kusini walikunja kushoto na kuingia porini. ‘Bocca Estate’ kibao kilichoning’inia getini kilisomeka, walipokaribi tua, lile geti likafunguka na wao wakaingia ndani ya shamba hilo kubwa na kupita kama kilomita mbili ndani ambapo walikuta nyumba moja ya kawaida tu. Bocca akaegesha gari hapo na wale vijana wake nao wakaegesha pembeni yake, wakateremka na kuelekea mlango wa bati uliosimikwa kwenye nyumba hiyo mbovu. Akausukuma na kuingia ndani. Ilikuwa kama stoo yenye makorokoro mengi sana, mmoja wa le vijana akaenda kwenye meza moja kubwa na kubonyeza swich iliwekwa pembeni yake ile meza ikahama kutoka pale ilipo na kusogea kando, chini yake pakafunguka mlango ulioelekea chini na kuruhusu ngazi kuonekana, wakazifuata na kufika chini kabisa ya banda hilo chakavu. Harufu nzuri ya mawaridi ilizifikia pua za Amata, akavuta pumzi ndefu na kutulia.
“Karibu sana bwana Moya,” Bocca akamkaribisha kijana huyo kisha wakaingia ndani zaidi na huko Amata alijikuta kwenye kitu ambacho hakukielewa kama ni ghala au kiwanda, kwani kulikuwa na marobota na mashine kadhaa. Vijana wachache sana walikuwa humo ndani wakifanya kazi hii na ile.
“Hapa ndiyo shamba, mzigo wote ukitoka Mexico, Blazil au Colombia hufika hapa ukiwa ghafi kisha tunauchakata wenyewe na kuupanga katika madaraja kadiri ya sehemu unaotakiwa kwenda,” akaeleza huku wakipita huku na kule.
“Lakini Boss hii biashara siyo hatari sana mbele ya serikali?” Amata akauliza.
“Ah! Ha! Ha! Ha! Ha! Haaaaaa.... Serikali kitu gani Moya! Hii dunia inaendeshwa kwa pesa, tunafanya kazi zetu kwa uhuru tu si kwamba hawajui, wanajua vyema lakini wana kamisheni yao lazima wafunge vinywa,” akaeleza wakati akimpitisha kona mbalimbali na kumwonesha vitengo, kisha wakaingia kwenye moja ya ofisi kubwa na ya kisasa wakaketi wawili tu na kuwaacha wale vijana wengine nje.
“Sasa sikia, kazi ya kwanza ninayotaka kukupa ni hii,” akaweka picha kama tatu hivi mezani, Amata akazifuta na kuziangalia kwa umakini.
“Huyu ni nani?” akauliza.
“Usiwe na haraka, nitakueleza,” akakohoa huku akitoa kabrasha fulani, “Sikia huyo bwana anaitwa Drotone La Peruz, ni raia wa Mexico lakini mara nyingi huja hapa Mozambique. Huyu bwana ameniharibia biashara zangu sana mara kadhaa ameteka watu wangu na kuwatesa ili wamwambie mi nafanya nini, na alidiriki kuiteka ndege yangu iliyokuwa na mzigo mkubwa sana, sasa nimejaribu sana kumpa hukumu ya kumstahili yaani kifo, lakini huyu jamaa ni kinyonga, ananizidi maarifa kila wakati. Nataka umshughulikie, nitakulipa pesa iliyotakata nje ya mshahara wako,” akaeleza.
“Hiyo kazi imepita, itafanyika,” Amata akajibu.
“Unaweza kunambi itachukua muda gani?” Bocca akauliza.
“Husijali Boss, maadam umenipa kazi, we hesabu ushindi, mimi ndiyo Moya Mampasi, huwa sikosei na sijawahi kukosea...”
“Aaaaa ha ha ha najua, leo nimeona kazi ulivyoifanya kwa sekunde kadhaa tu. Sasan huyu bwana anakaa kisiwani, na hicho kisiwa kinaitwa La Peruz kama jina lake, kipo jirani sana na Madagascar, ana uwezo wa kuona kila kitu kinachosogelea kisiwa hicho kiwe cha hatari au cha heri,” akazidi kumdadavulia.
“Hata akiishi mbinguni atapatikana tu na roho yake nitakuletea,” Amata akampa moyo tajiri huyo.
“Kwa kweli kama kuna mtu atanifanya nife haraka basi ni huyu, keishamaliza watu wangu kama kumi hivi tena wale wapiganaji hodari kabisa,” Bocca akaeleza huku akifikicha macho yake kana kwamba yana pilipili ndani yake.
“Na huyo mwingine ni nani?” akauliza Amata.
“Huyu? Aaaaa tumalize huyo kwanza kisha nitakupa habari ya huyu,” Bocca akajibu.
“We nipe inawezekana nikawamaliza pamoja kwa njia nzuri tu isiyo na maumivu,” Amata akasema huku akinyoosha mkono kwa minajiri akabidhiwe zile picha. Kati ya zile picha alizokabidhiwa mara ya pili moja ilikuwa ya mwanamke na hii ilimshtua moyo kidogo, mwanamke huyo ndiye yule aliyekuwa naye gym asubuhi aliyemwalika nyumbani kwake.
“Oh, nipe hiyo ya huyo mwanamke, huyu hana tatizo ni mteja wangu tu,” akaomba na Amata akamkabidhi ile picha.
“Sikiliza...”
“Enhe!”
“Huyo bwana ni rafiki sana na La Peruz, huyu bwana ananikwamisha sana mipango yangu na ndiye anayepeleka siri zangu kule kwa huyo kibopa...”
“Anaishi wapi?”
“Beira, Krusse Gomes namba 129,” akamwelekeza.
“Sawa, kazi imeisha mpaka hapo, cha kufanya we niwezeshe kila idara, nipe saa sabini na mbili tu, utapata matokeo ya ajabu kabisa,” Amata akamsadikisha.
“Sure?! Yaani saa sabini na mbili?”
“Ndiyo na si ajabu zikawa nyingi, si ni kwenda na kumuua tu au kuna lingine?”
“Hakuna lingine, ni kumuua tu, ila mwambie nani kakutuma,” Bocca akatoa ufafanuzi.
“Sawa hamna tabu,”
Bocca akageukia kwenye kompyuta ya ke na kuandika andika vitu fulani, baada ya dakika kama kumi hivi alikuwa keshakamilisha. Walitoka na kukutana na wale vijana wengine na safari ya kurudi mjini ikaanza.
***
Saa nne usiku ilimkuta Kamanda Amata ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa malane tayari kwa safari ya Beira. Mwenyeji wake Mr. Bocca alikuwa kamwandalia kila kitu ili kuhakikisha kazi yake inakamilika. Amata aliamua kwa akili yote kuifanya kazi hiyo kwa Umakini ili aweze kupata na mengine mengi huku akiwa anamsaka adui yake, Benzilahagi aliyejificha kwa jina la Ludovique Pereira. Kutokana na hilo na jinsi alivyopewa mbinu na mtu yule asiyemjua, alijiingiza kwenye genge la wauza dawa za kulevya maarufu hapo Mozambique, lililokuwa likiongozwa na Bocca. Alijua kwa vyovyote ipoi siku atakutana na Benzilahagi au Ludovique wa bandia.
Bocca keshakuwa mtu wangu, bado Pampula Colonha, nitamjua tu, hawa sina shida nao, mimi ni Benzilahagi tu, aliwaza wakati akifunga mkanda wa kiti cha ndege hiyo tayari kwa safari.
5
KANALI BENSOIR BANGINYANA alikanyaga ardhi ya Maputo dakika chache tu baada ya Amata kuruka na ndege ya LAM Mozambique Airlines. Kanali huyo alitua katika mji huo kwa kazi moja tu ya kumsaka na kumuua Amata ili kufisha juhudi hizo. Moyoni mwake alikuwa na uchungu wa wazi kabisa juu ya mtu huyo, aliapa kumtoa roho pindi tu akimtia machoni kwani hakutaka hata kumpa nukta moja ya kujitetea kwani alikwishaaswa juu ya uwezo mkubwa wa fikra na maamuzi ya haraka ya mpiganaji huyo.
Katika uwanja huo alipokelewa na vijana waliotumwa na mwenyeji wake, na moja kwa moja alifikishwa Calanga Beach Resort.
“Boss atakukuta hapa baadae!” akaambiwa naye akachukua mzigo wake na kuingia katika resort hiyo iliyo kando kabisa na bahari ya Hindi.
Usiku huohuo mwenyeji wake alifika kumsalimu, hakuwa mwingine isipokuwa Mr. Bocca, tajiri muuza unga asiyekamatika.
“Ndiyo Kanali, karibu sana Maputo ule maisha kidogo,” Bocca akamwambia Banginyana.
“Sintokula maisha mpaka nikamilishe kazi moja tu iliyonileta,” akamwambia.
“Usiwe na wasiwasi, mimi ndiye niujuaye mji huu kila kona kila anayeingia lazima nijue, hivyo utampata tu, na kwa jinsi ninavytomsikia mtu huyo, usimpe nafasi ya kujitetea mara mbili, ndivyo wasemavyo…”
“Yaani we acha tu, nahisi yule si binadamu wa kawaida, lakini nitamwonesha kazi,” banginyana akajipa imani.
“Ushawahi kupambana naye?”
“Hapana, ila nimemwona na namjua kwa sura, nilikutana naye Ujerumani na ndiye aliyemuua yule kijana uliyenipa…”
“Aaaaah kumbe! Hafai kuishi,” Bocca akajibu.
“Ok, tuliache hilo, Ludovique yuko wapi?” Banginyana akauliza.
“Ludovique amehifadhiwa na bwana Pampula Colonha,”
“Wapi?”
“Kisiwani,” akajibiwa. Banginyana akashusha pumzi ndefu na kutulia, kisha akamtazama mtu huyo anayeongea naye.
“Sikia, Rais Sebetunva amenituma kazi moja tu niliyokwambia, lazima tuzifute nyayo zaote za huyu anayetuharibia mambo naye ni Mtanzania,” akaeleza.
“Usijali, kazi ikiwa ngumu unambie nina kijana mmoja mzuri sana amaye hata sasa nimemtuma huko La Peruz akanifanyie kazi moja inayoninyima usingizi,” Bocca akaeleza.
“Sawa kabisa, kwa nini nisimhitaji kama kazi ikiwa nzito? Nitakwambia.
***
“We tulia hapa mpaka boss wako atakapotoa amri nyingine,” Colonha alimwambia Ludovique Pereira.
“Usijali, kazi yangu nimeimaliza vyema,”
“Kazi gani?”
“Kazi gani! Si ya kumuua Hamadou,” akaeleza.
“Ok! Nimekupata, lakini licha ya kuua hawa watu mpango ukoje hasa?” Colonha akauliza.
“Sikia Colonha! Mpaka sasa mpango wetu umepata vikwazo na tumefaulu kwa asilimia kama 49 hivi. Mkuu wa wakuu Mheshimiwa Sebutunva hawezi kukubaliana na hilo, hivyo tu,efuatilia nyendo zote kujua sakata lilianzia wapi na kuhakikisha tunawamaliza wale wotea ama waliosema na kutoa amri au waliotekeleza. Tunawafuta kisha tunaanza upya, unajaua? Shujaa akiona shimo lazima arudi nyuma na kuliruka,” Benzilahagi akaeleza.
“Nimekuelewa sana,”
“Sasa tuna kikwazo hiki…. Kimoja, kama unavyojua jeshi la Tanzania lilizima mbip zetu kule Mpumbutu, Shushushu wao mahiri akagundua mbinu chafu za uingizaji silaha kule msituni, akamuua mmoja wa vijana mahiri wa kikosi chetu kulekule Ujerumani na kutia moto himaya ya Bwana Jirack, aliporudi Tanzania akaingia kwenye sakata hili, kiukweli anatutoa jasho…”
“Kwa hiyo unawasiwasi naye?” Colonha akauliza.
“Comrade! Nimemuua Hamadou nimeondoka Tanzania na kuja huku, nyuma yangu baada ya saa 48 Kubrah anauawa na vijana wake wote, na huo ni mkono wa huyo hayawani, Amata… wenyewe humwita Kamanda Amata,” Benzilahagi akaongeza kwa uchungu.
“Kubrah Kaleb, ninavyomjua mimi, ameuawa kirahisi hivyo?” Colonha akauliza.
“Yeah…”
“Ok, Kanali banginyana ametua usiku huu Maputo, amekuja kwa lengo moja tu…”
“Lipi?”
“Inasemekana huyo hayawani yuko hapa Maputo kwani amejua kuwa wewe uko hapa na anakusaka akumalize,” Colonha akamhabarisha Ludovique wa bandia.
“Come on! Shiiiit!” Benzilahagi akang’aka na kupiga ngumi meza ndogo iliyokuwa hapo mbele yake.
“Vipi?”
“Kazi ipo, Colonha kazi ipo, huyu mtu fanyeni liwezekanalo auawe,” akasema.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ludovique, usijali, hapa ulipo hawezi kukupata hata atumie uchawi wa kwao Ngende, isitoshe kuna mpango tumeuandaa wa kukuficha wewe usionekane duniani na mpango huo utatekelezwa muda si mrefu. Elewa kwamba TISS wanakutafuta, NIS wanakusaka na vyombo vingine vya usalama kwa kuwa uliyemuua ni mtu mkubwa sana, na bado una kazi ya kuwaua wengine wawili, hivyo tumepanga kukuficha, sisi tunajua ila wewe hujui vile tutakavyofanya, usihofu. Hata awe na mbinu gani lakini kwa hii hatokupata.”
“Asante kwa hilo Comrade,”
“Be cool!”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment