Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

MIMI NA RAIS : THE PRESIDENT AND I - 1

 





    IMEANDIKWA NA : LELLO MMASSY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mimi Na Rais (The President And I)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    UTANGULIZI

    Naitwa Joseph Kaduma Ndani Ya Serikali Ya Nchi Ya STANZA Watu Hupenda Kuniita Joe.Nina Nusu Saa Tu Ya Kuamua Kati Ya Maisha Yangu,Familia Yangu Na Utajiri Wangu Ama Uhai Wa Rais. Rais Anaeongoza Zaidi Ya Watu Milioni 70,Mwenye Ulinzi Zaidi Ya Ma Rais Wengi Hapa Duniani Leo Hatma Ya Maisha Yangu Ipo Mikononi Mwake Na Yake Mikononi Mwangu.



    Nimwache Animalize Au Nimmalize Nibaki Salama?.Siwezi Kurudia Kosa Nililolitenda Hapo Kabla.Ni Ama Mimi Ama Rais.



    Inaendelea..

    **************************



    WITO WA RAIS

    “Baba kuna wageni wanakuulizia”, Derick kijana wa kwanza wa Joseph alimwita baba yake aliekuwa bustanini akiweka mbolea kwenye mashina ya migomba nyuma ya nyumba yake.



    “Kina nani Derick, mbona sina miadi na mtu leo?”, Joseph alimuuliza Derick huku akiendelea na shughuli na asionyeshe shauku ya taarifa ya wageni aliyopewa na mtoto wake.



    “Sijawajua ila wamekuja na magari yenye namba za blue na hazieleweki”, Derick alimjibu Joseph. “Ok, tell them I am coming” (Sawa waambie nakuja), Joseph alimjibu kijana wake. Joseph alimalizia kuweka mbolea kwenye shina moja kisha akaelekea ndani kuonana na wageni.Kwa namna Derick alivyomwelezea baba yake juu ya wale wageni tayari Joseph alishawatambua ni kina nani.



    “Meshack habari”, Joseph alimsalimia kiongozi wa msafara aliekuwa amesimama kibarazani. “Joe, habari mkuu?, Mh. Rais anakuhitaji sasa hivi lipo jambo anataka kuongea na wewe”, Meshack alimwambia Joseph huku akiwa ameweka tabasamu la bandia na akimkazia macho usoni huku amemshika mkono wa salamu.



    Joseph alibaki kimya kwa dakika kadhaa huku akiwatupia macho maafisa wengine watatu wa idara ya usalama wa taifa waliokuwa wameambatana na Meshack. “Rais ana shida gani nami Meshack?, Nilishatoka huko, alishanifukuza kwa aibu na fedheha kubwa baada ya kulitumikia taifa kwa moyo mkunjufu kwa miaka yangu 15 ya utumishi. Ameninyanyasa vya kutosha, amenifilisi na sasa nina kesi ya uhujumu uchumi. Leo amenikumbuka? Namba yangu anayo angeweza kunipigia simu.” Joe alimjibu Meshack huku akiwa amemkazia macho.



    Alikuwa akiongea kama mtu aliekuwa na uchungu mwingi moyoni. Machozi yalikuwa yakimlengalenga. Meshack alimwangalia Joe kisha “Joe, please accept his excellency’s call” (Joe, tafadhali kubali huu wito wa muheshimiwa). Meshack alimsihi Joe kwa sauti ya upole.



    “Sawa naomba mmwambie nitafika Ikulu kesho saa nne asubuhi” Joe alimjibu Meshack na kisha waliagana wakaondoka.



    Joe aliingia ndani na kumkuta kijana wake mkubwa Derick na mke wake wakiwa sebuleni kimya kama watu waliokuwa wakisubiri taarifa fulani. Alipoingia tu mke wake alimuuliza kulikoni, Joe alimweleza mke wake juu ya ule wito. “Joe, usikubali kuingia tena kwenye mtego huu. Mtu huyu ameshatunyanyasa vya kutosha. Tii wito wake lakini tafadhali usikubali kufanya nae kazi”, mke wake Joe alimsihi mumewe.



    *********************************

    Joseph Kaduma mwanadiplomasia mbobevu, balozi mstaafu wa Stanza nchini Urusi na mbobevu kwenye idara ya usalama wa taifa la Stanza ndio huyu leo anahitajika na Rais. Joseph ambae hujulikana kama Joe ni muhanga wa utawala dhalimu wa Rais Sylvester Costa, Rais aliepo madarakani kwa muhula wa tatu baada ya kuibadili katiba ili imruhusu kufanya hivyo.



    Ni balozi pekee aliefukuzwa kazi na Rais Costa na kufutiwa hadhi ya ubalozi mara baada ya kupingana nae mara tu Rais Costa alipoanzisha vuguvugu la kutaka kubadili katiba ili aendelee kubaki madarakani. Joe hakumuunga mkono, hivyo mara tu baada ya Rais Costa kushinda uchaguzi uliojawa na utata mwingi alimteua ubalozi na baada ya miezi mitatu alimrudisha nchini Stanza kumvua ubalozi na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi akihusishwa na ununuzi uliokiuka taratibu wa jengo jipya la ubalozi kule Urusi.



    Joe kwa wakati huo alishafilisiwa mali zake nyingi na nyingine nyingi kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali huku yeye akiendelea na kesi. Watoto wake wawili waliokuwa wakisoma nchini Sweden walirudishwa nchini na yeye na familia yake wote walinyang’anywa haki ya kusafiri nje ya nchi.

    Lakini wakati hayo yakimkuta ni Joseph huyu huyu kwa kutumia ujuzi wake katika masuala ya diplomasia na ushawishi aliwezesha ujenzi wa Chuo kikuu cha Kilimo nchini Stanza ambacho kinaongoza kwa bara la Africa na kilichosababisha mapinduzi makubwa ya kilimo nchini Stanza.



    Ni yeye aliesababisha ujenzi wa Bandari kubwa ya kisasa inayoliingizia taifa la Stanza robo ya GDP hivyo kuifanya chanzo cha mapato namba mbili baada ya kilimo. Bandari hii ilijengwa kwa msaada wa China, Urusi na India.



    Ni yeye aliesababisha Stanza kukubaliwa kuwa mwanachama mwalikwa wa umoja wa kiuchumi wa BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika ya Kusini) .



    Joe kama wengi serikalini walivyozoea kumwita alishiriki kwenye suluhisho la amani la Sudani ya Kusini. Isitoshe ni yeye alihusika sana kwenye kuweka mikakati iliyomwingiza Rais Sylvester Costa madarakani awamu ya kwanza na ya pili. Hakuna alieamini kama ni huyu Joe angekuja kugeukwa na Rais Costa na kuwekwa kwenye mateso makubwa na kurudishwa kwenye umaskini.

    Joe alikuwa ni mbobevu wa mambo ya usalama. Hata Rais Costa alipotaka kupinduliwa na jeshi katika mwaka wa tatu wa utawala wake wa awamu ya pili ni yeye akishirikiana na mbobevu mwenzake Stanley Macha (ambae kwa sasa ndio mkuu wa Idara ya Usala wa Taifa) walihusika sana kurudisha hali ya usalama wa nchi katika hali ya kawaida na kulituliza jeshi.Ueledi na uzalendo wa Joe kwa taifa la Stanza haukupaswa kuhojiwa.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Joe alioana na Eliza mwaka 1995, mkewe Eliza akiwa mtaalam na mbobevu katika sekta ya mabenki alifanikiwa kujijenga sana kibiashara pia. Eliza akiwa mmiliki wa makampuni matatu moja ya uzalishaji bidhaa za mabomba ya plastiki na nyingine ya uchakataji madini na moja ya usafirishaji bidhaa za kilimo nje ya nchi aliingia kwenye rekodi za kuwa kati ya wanawake 10 wenye nguvu katika taifa la Stanza.



    Mara baada ya Rais Costa kupishana na Joe kampuni zote zilifilisiwa na kutaifishwa. Joe alirudishwa kwenye umaskini ulioambatana na mateso ya kutofanya lolote la maendeleo. Alibaki kama mpweke na mtu mwenye uchungu mwingi asijue ni kwa nini Rais Costa ameamua kumfanyia yote hayo kwa yeye kuonyesha msimamo wake juu ya demokrasia.



    Alijiuliza sana kama Rais Costa hakupenda msimamo wake ilikuwa ni suala la yeye kutomteua tena ubalozi na kumwacha aendelee na Maisha yake hakukuwa na haja ya kumfanyia yote hayo anayomfanyia. Joe, alikuwa akiishi kwa uchungu mwingi.



    ************************

    Ilikuwa ni asubuhi tulivu sana kwenye viunga vya Ikulu ya Stanza iliyojengwa mwambaoni mwa bahari ya Hindi. “Ndg. Joseph karibu sana. This way Sir…”, Meshack alimkaribisha Joseph aliewasili ikulu kuitikia wito wa Rais Costa.



    Alimwelekeza kuelekea chumba ambacho ndipo Rais anakuja kuongea nae. “Habibu anaendeleaje” Joseph alimuuliza Meshack wakiwa wanatembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano. “Yupo vizuri sana, hana matata”, Meshack alijibu huku akicheka.



    Habibu ni mmoja wa vijana matunda ya Joseph katika wigo wa diplomasia. Sasa Habibu ni balozi nchini India. Ni mmoja wa vijana ambao Joe anamkubali sana. “Habibu is genius” (Habibu ana akili sana), Joe alimjibu Meshack .“Sure” (Hakika), Meshack alijibu huku akimkaribisha Joe aketi na kumsubiri Rais.

    “My friend Joseph Kaduma welcome home” (Rafiki yangu Joseph kaduma karibu nyumbani), Rais Sylvester Costa aliingia kwenye kile chumba ambacho Joe alikuwa akimsubiri huku akicheka na kumsalimia Joe kwa sauti kubwa. Alimkaribia Joe na kumpa mkono.



    “Mh. Rais”, Joe alinyanyuka na kumpa mkono wa salamu Rais Costa.



    “Unaendeleaje, kesi inatajwa lini tena?” Rais Costa alimwambia Joe huku akiketi kwenye kiti.



    “Siku utakayosema itajwe itatajwa” Joe alimjibu Rais Costa kwa ghadhabu kidogo huku akiketi.



    “Give us space gentlemen and Meshack switch them off” (Vijana tupeni nafasi kidogo na wewe Meshack zizime) Rais Costa aliwaamrisha walinzi wawili walioambatana nae watoke nje ya chumba ili azungumze na Joe na kumwambia Meshack azime vifaa vyote vinavyorekodi sauti kwenye kile chumba.

    “Joe, sahau yanayoendelea sasa kwenye familia yako Taifa linakuhitaji hasa mimi ninakuhitaji. Lipo jambo ninataka unisaidie nimejaribu watu wangu wote limekwama umebaki wewe” .Rais Costa alianza kuongea na Joe huku akimmimina Joe kahawa iliyokuwa kwenye meza kati kati yao.



    Joe akiwa amekaa kwa utulivu huku akimwangalia Rais Costa kwa macho yaliyojaa uchungu mkubwa alinyanyuka na kukaa vizuri kisha “Sylvester, sidhani kama nina la kukusaidia ama kulisaidia taifa hili mara baada ya yote niliyokwisha kufanya na kuishia kuishi maisha ninayoishi sasa. Bila kusikia hata unachotaka nikusaidie naomba niseme wazi sitaweza”. Joe alimwambia Rais Costa kwa kumwita kwa jina.



    Alikuwa akiongea kwa ghadhabu na kwa wakati ule alisahau kama Costa ni Rais bali alimwona kama mtu wa kawaida, mporaji, mnyanyasaji na asiestahili hadhi ya Urais. Hakuwa na chochote cha kupoteza zaidi ya alivyopoteza, alishapoteza kila kitu na labda kilichobaki ni yeye kupewa hukumu ya kuishia jela.



    “Joe, naweza kufuta kesi zako zote na kurudisha hadhi yako na heshima yako na vyote ulivyopoteza kwa kunisaidia hili suala langu” Rais Costa alimwambia Joe huku akikunja nne kwenye lile kochi alilokuwa amekalia.



    “Tofauti zetu tunahitaji tuzimalize leo na tuangalie mbele” Rais Costa alimalizia. Joe alimwangalia Rais Costa kwa macho yaliyojaa wekundu uliosababishwa na machozi. Aliwaza na kupata uhakika kuwa yote yaliyomtokea ni kwa sababu Rais Costa aliamua iwe hivyo.



    Aliwaza jinsi hali ile ilivyomsababishia matatizo ya kisukari na presha ya kushuka. Aliwaza jinsi alivyonyimwa kumsafirisha mama yake kwenda matibabu India kwa sababu ya amri ya Rais Costa ya kutoruhusu mtu yeyote wa familia ya Joe kutoka nje ya nchi na hivyo mama yake kufariki dunia. Joe alipatwa hasira sana.



    *********************

    “With all due respect Mr. president there is nothing to resolve between me and you. I can’t help” (Kwa heshima mheshimiwa Rais hakuna kitu cha kutatuliwa kati yetu. Siwezi kusaidia). Joe alimjibu Rais Costa huku machozi yakiwa yamechirizika mashavuni huku akinyanyuka kwenye lile kochi alilokalia tayari kwa kuondoka.



    “Bahati Mbaya sana huwezi kutoka humu ndani mpaka tumeelewana na kukubaliana. Utakapokuwa tayari kuongea na mimi mwambie Meshack aniite” .Rais Costa alimjibu Joe huku akitoka kwenye kile chumba.



    Wakati Rais Costa amefika mlangoni haraka Joe akamsimamisha “Unataka nifanye nini?” Joe alimuuliza Rais Costa.



    “Nataka nikutume Korea Kaskazini”



    “Nini!!”



    “Ndiyo” Joe na Rais Costa walijibizana. Wote walirudi kwenye makochi na kukaa.

    Joseph alikuwa tayari kumsikiliza Rais Costa, hakuona sababu ya kuendelea kupambana nae alikumbuka mafundisho waliyopewa wakiwa mafunzo ya usalama wa taifa nchini Israel kuwa unaweza kupambana na mtu yeyote lakini si aliekalia kiti cha u Rais, kupambana nae ni kujiumiza mwenyewe. Alikuwa mpole na kuwa tayari kumsikiliza.



    “Joe, nashukuru sasa tunaweza kuongea” Rais Costa alimwambia Joseph huku akiketi. “Nakusikiliza” Joe alijibu.



    “Ninahitaji nikutume Korea ya Kaskazini” Rais Costa alianza maongezi. Joe alibaki kimya akimsikiliza kisha “Mkuu kutokana na makubaliano ya umoja wa mataifa tulisaini wenyewe kutoshirikiana na taifa hili suala unalotaka kufanya litatuletea vikwazo na nchi nyingine. Lakini kwanza nijue ninahitajika kwenda kufanya nini” Joe alishauri na kuuliza.



    “Joe ninaelewa ndio maana nilitaka kutafuta mtu mahiri katika hili na hii inakuwa ni misheni nyeti na yenye usiri mkubwa. Kwa hali ilivyo tunamuhitaji Korea Kaskazini kama mshirika.



    Ninajua tuna historia na taifa hili lakini ushirikiano wetu umeyumba sana hasa baada ya kuzifutia usajili zile hospitali zao tatu walizozifunguaga hapa nchini. Ulikuwa ni uamuzi uliokosa busara lakini wenye umuhimu kwa wakati ule.



    Kwa sasa ninahitaji kuimarisha jeshi na vifaa vya vita ikiwepo rada. Ninahitaji mfumo mpya wa mawasiliano wa Ikulu na idara ya usalama wa taifa kwani tupo kwenye hatari kubwa sasa hivi hasa baada ya kukataa kuunga mkono baadhi ya sera za nchi za Magharibi hasa Ushoga.



    Unajua pia badiliko la katiba nililolifanya lililoniruhusu kugombea tena halikuwafurahisha. Usisahau tumepingwa sana kwenye huu mradi wa ufuaji madini ya Uranium mradi ambao mimi naona unatija kwetu.



    Lakini pia tulipowabana hawa wawekezaji wa sekta ya gesi tumejiongezea maadui sana, sijioni kuwa salama hata kidogo tunahitaji kupanua wigo wa marafiki.



    Mifumo yetu ya mawasiliano tunayotumia sasa ni ya kwao, jeshi letu silioni kutosha kupambana na aina za uvamizi wa kisasa. Nahitaji Korea ya kaskazini sasa kuliko kawaida”. Rais Costa alimweleza Joe kwa kituo. Joe alionekana kutulia akisikiliza na kisha alivuta pumzi kwa nguvu.

    “Mheshimiwa Rais nadhani bado tuna nafasi kubwa ya kuwatumia China, Urusi na Japan kufanikisha yote hayo uliyosema. China wana mifumo mizuri ya mawasiliano. Urusi na Japan tunaweza kuwatumia kwenye kuimarisha jeshi na kama una shaka na Israel kwa mafunzo ya kiusalama Urusi wanaweza kutusaidia hata Cuba.



    Tukiwatumia hawa hatutaleta hamaki kama tukiwatumia Korea Kaskazini.Hawa tuna mashirikiano nao mazuri sana na wapo kwenye ushindani wa kawaida na hayo mataifa mengine. Nina uzoefu nao kuliko huko Korea. Na hawa hawana shurti ya kufuata sera zao kama wa magharibi isipokuwa tu wataangalia watafaidika vipi. Nilikuwa nashauri tuwatumie hawa”. Joe alishauri.

    “Hapana. Hivi karibuni mahusiano yangu na Rais wa China sio mazuri hasa baada ya kumkatalia raia wake zaidi ya laki moja waliotaka kuingia nchini kufanya biashara ndogo ndogo.



    Sikukubali maana hawa machinga wangu ningewapeleka wapi niliahidi kuwainua kiuchumi sasa haiwezekani mpaka machinga niwaletee wachina, nilikataa.



    Urusi nae anataka amiliki asilimia 80 ya fedha zitakazotokana na uchimbaji wa mafuta kule jimbo la Kindori na sisi tubakiwe na 20%, hilo nimekataa pia na inaonekana Vijisky hajafurahia ndio maana naona kwa sasa tuende na Korea Kaskazini”, Rais Costa alimjibu Joe.



    “Lakini mheshimwa nadhani kutokukubaliana ni Sehemu ya mazungumzo na tuna nafasi ya kurudi tena mezani kuzungumza na kufikia muafaka wa sisi wote kufaidika kuliko kuwaacha na kuhamia Korea, twajuaje kama huko nako hatutakubaliana?.



    China mfano, badala ya kumkatalia ungempa nafasi ya yeye kutujengea soko kubwa la kisasa la matunda na mazao halafu umwambie unampa 60% ya umiliki na watu wake wakati 40% ichukuliwe na sisi na vijana wetu. Hapa tungekuwa tumeinua uchumi wa wakulima wa matunda na mazao lakini pia ajira na soko la nje.



    Urusi suala la mafuta pia linajadilika, lakini vipi Japan, India na Cuba?”. Joe alionekana kuzidi kusisitiza kutoungana na Korea Kaskazini.



    “Joe nimekuita hapa unisaidie kufanya ninalokuomba na sio kunishauri. Siku nikihitaji ushauri nitakwambia unishauri, kwa sasa nahitaji unisaidie maongezi na Korea.” Rais Costa alionekana kukerwa na ushauri wa Joe.



    Joseph alikaa kimya kwa dakika chache kisha “Sawa nitafanya kama utakavyoona inafaa lakini kwanza nijue nitapata nini kwa kulifanya hili” Joe alitaka kujua.

    “Kwanza kesi yako itafutwa. Nitatoa maagizo vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi yako viondolewe. Biashara zote za mke wako na mali zilizoshikiliwa na serikali utarudishiwa.



    Mke wako nitamtafutia nafasi benki kuu na Watoto wako watasoma nchi utakayoipendekeza. Joe sidhani kama kuna lingine nimelibakiza” .Rais Costa alimalizia huku akimwangalia Joe usoni. Joseph alihema kwa nguvu kisha alimshukuru Rais.



    “Nadhani Joe tusahau yaliyopita na tusaidiane kuijenga nchi. Utaniambia unahitaji nini ndani ya siku tatu ili tuanze mikakati ya namna ya kulienenda hili suala. Thank you for coming my old friend”. Rais Costa alimalizia kuongea huku akifungua mlango na kutoka huku akisindikizwa na wasaidizi wake waliokuwa wakimsubiri.



    Joe alibaki pale kwenye kochi akiwa ameinamisha kichwa chini. Alikumbuka maneno ya mke wake kuwa asikubali atakachoombwa na Rais na alikuwa hajui atakwenda kumweleza vipi Eliza. Alijipa moyo na kusimama.

    Haraka Meshack akiwa ameambatana na kijana mwingine mmoja walikuja kumwomba watoke na kwa mshangao Joe alipotoka nje alielekezwa aingine kwenye Land Cruiser V8 toleo jipya. Hakuelewa kinachoendelea.



    Alikuwa akiwaza sana nini maana ya hayo yote, kuwa Rais Costa anamuhitaji kwa ajili ya hayo tu? kuimarisha jeshi na mfumo wa mawasiliano? Kuwa ni hilo tu?hakuelewa. Wakati akiwaza hilo alijikuta tayari yupo mbele ya nyumba yake na kumkuta mkewe Eliza na Watoto wake wawili wakiwa nje huku vijana zaidi ya watano wakiwa wanatoa mabegi ya nguo nje huku askari zaidi ya sita wakiwa wameizunguka nyumba.



    “Mheshimiwa karibu, tunahitaji kuwahamisha kwa maelekezo ya Rais. Tunaelekea nyumba uliyopangiwa Endokasi Estate”. Meshack alimwambia Joe.



    Endokasi Estate ni mahali penye nyumba za serikali ni eneo analoishi Waziri mkuu na Spika wa bunge. Joe na familia yake walikuwa wanahamia huko. Joe alikuta pia Land Cruiser ingine ikiwa pale aliyoambiwa ile ni ya mke wake.



    Eliza alipomuona Joe alimfuata na kumuuliza kwa upole “Nini kinaendelea mume wangu?”. Joe kwa utaratibu alimjibu mke wake kuwa atamweleza baadae ila Rais amemtuma kazi.



    “Joe, umekuwa mume wangu kwa miaka 23 sasa sikuwahi kuacha kukubaliana nawe katika maamuzi yako. Tumepoteza vingi kwa sababu ya Rais huyu dhalimu. Tumempoteza mama, tumejichumia magonjwa tumeishi kwa dhihaka kubwa leo unaniambia Rais amekutuma?” Eliza alianza kumrushia Joe maswali mfululizo.



    “Eliza tutazungumza utaelewa” Joe alimsihi Eliza.



    “Hapana Joe ninasikitika kukwambia kuwa nimemwita mwanasheria, ninafungua jalada la talaka. Mimi si mke wako tena. Utaishi na Rais Costa” Eliza alimwambia Joe huku akiondoka kuelekea ndani ya nyumba. Joe alisimama pale asijue afanye nini.

    ************************

    Nini kitaendela katika simulizi hii ambayo ndio kwanza inaanza?.Anza kufuatana nami sasa katika mtiririko huu mzima wa kisasi,ghiliba,Kushinda na Kushindwa



    RAIS COSTA ATIKISA MUHIMILI WA MAHAKAMA.JOE AFUTIWA MASHTAKA

    “Sizya wataarifu Jaji Mkuu, Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Mwanasheria Mkuu kuwa nitawahitaji kesho saa tatu asubuhi. Waziri wa Fedha na Msajili Mkuu wa Hazina nitakuwa na kikao nao kuanzia saa saba mchana na kisha nitataka kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Viwanda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jioni saa kumi”, Rais Costa akiwa ofisini kwake alitoa maagizo kwa msaidizi wake bwana Sizya Kagonda. Nae alitii.

    Siku iliyofuata saa tatu kamili, Rais Costa aliingia kwenye chumba cha mkutano ili kukutana na Mwanasheria mkuu, Jaji mkuu na Mwendesha Mashtaka waSerikali. Aliwaeleza nia yake ya kutaka mashtaka yanayomkabili Joseph Kaduma yafutwe na hivyo alitaka ushauri namna ya kulitekeleza jambo hilo mara moja.

    “Mheshimiwa Rais, kutokana na mwenendo wa kesi ilionekana kuna matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na Joe kuifuta kesi hii itatuweka kwenye wakati mgumu kwenye kesi nyingine mbili za uhujumu uchumi zinazoendelea sasa”, Jaji mkuu Dr. Charles Kaseja alishauri. Alishauri kuwa ni vyema kesi ikaachwa iishe halafu Joe apewe nafasi ya kukata rufaa halafu ndio ikamalizikie kwenye rufaa lakini alitoa angalizo kuwa itachukua muda kidogo tofauti na ombi la Rais.

    “Kaseja kuna Ushahidi gani uliopata? Huna Ushahidi wewe zaidi ya huu mwendesha mashtaka anaojitahidi kuutengeneza. Joe hana kosa, kila jambo niliagiza mimi. Ninahitaji hii kesi isitishwe haraka iwezekanavyo”, Rais Costa alisisitiza.

    “Mheshimiwa Rais, mahakama na utaratibu wa sheria hauendi hivyo, ni vyema tungeheshimu misingi ili kutopoteza imani ya wananchi na muhimili huu”, Dr. Kaseja alisisitiza kwa nidhamu kubwa. “Yeyote mwenye kuwaza sawa na Dr. Kaseja aseme”, Rais alihoji na mwanasheria mkuu pamoja na mwendesha mashtaka wa serikali walibaki kimya, hakuna aliyethubutu kumuunga mkono Jaji Mkuu kwasababu kumuunga mkono Dr. Kaseja ni kusema unapingana na Rais. Rais Costa aliwashukuru na kuwaruhusu waondoke.

    Kama ilivyopangwa, saa saba kamili Rais Costa alikutana na Waziri wa Fedha na Msajili Mkuu wa Hazina. Aliwapa maelekezo kuwa mali za Joseph zilizotaifishwa zirudishwe mara tu kesi yake itakapofutwa. Pia, alimpa maelekezo Waziri wa Fedha kuwa Eliza, mke wa Joe aanze kutafutiwa nafasi Benki Kuu, cheo cha Mkurugenzi.

    Waziri wa Fedha alishauri kwa kuwa nafasi ya mkurugenzi wa Benki ya Kilimo ipo wazi, ni vyema Eliza akapewa nafasi hiyo kuliko kupelekwa Benki Kuu kwani ana uzoefu na biashara za kilimo hasa usafirishaji wa mazao ya Korosho, Pamba na Kahawa. Kikao cha Rais na Waziri wa Fedha hakikuwa na changamoto nyingi.

    Rais Costa ni mtu wa kwenda na muda. Ilipotimia jioni saa kumi na mbili, alikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Viwanda na wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama ilivyopangwa kwenye ratiba. Alitoa maagizo kuwa vikwazo vyote alivyowekewa Joseph vitolewe, pia alimuagiza Waziri aangalie namna ya kuanza kuviwezesha na kuvirudisha kwenye uendeshwaji viwanda vyote alivyokuwa anaendesha Eliza. Maagizo ya Rais Costa yaliafikiwa bila kuhojiwa.

    Rais alimaliza siku kwa mafanikio kwa kuonana na watu wote wanaohusika katika kutekeleza yale waliyoafikiana na Joseph isipokuwa yote yangeweza kuendelea kama tu mahakama itatoa hukumu kuwa Joe hakuhusika na uhujumu uchumi na hivyo kufutiwa mashitaka jambo ambalo Jaji Mkuu alipingana na Rais Costa na lilionekana kutofikiwa muafaka.

    ***************************************

    “Kwa mamlaka aliyopewa Mh. Rais na katiba chini ya ibara ya 57(ii)b, leo ametengua uteuzi wa aliekuwa Jaji Mkuu Dr. Charles Kaseja na kumteua ndugu Dastan Kibwana kushika wadhifa huo. Hapo kabla, Jaji Dastan Kibwana alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Aliyekuwa Jaji Mkuu Dr. Charles Kaseja atapangiwa kazi nyingine”, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, ndugu Alpha Wauwau alimalizia kutangaza kwa waandishi wa habari.

    Rais Costa si mtu aliyependa kupingwa mawazo yake. Suala la kazi aliyomtuma Joe alitaka lifanyike kwa kasi aliyoihitaji na hakutaka mtu yeyote atokee wa kukwamisha azma yake. Dr. Kaseja aliyekuwa Jaji Mkuu alionekana kutoelewa hilo na sasa aliondolewa kazini ili awekwe mtu ambaye angeweza kwenda na kasi ya Rais Costa.

    Dastan Kibwana, Jaji wa Mahakama ya Rufaa mbobezi wa sheria za biashara za kimataifa sasa alipewa dhamana ya kuwa Jaji Mkuu kwa maelezo ya kazi yake ya kwanza iwe kuhakikisha Joe anafutiwa mashtaka.

    ************************************

    “Shemeji naomba umuelewe mume wako. Ni kweli mmeshapoteza vingi, lakini je, mtavirudisha kwa kuzidi kupingana nae? Mimi naona ni muda wa kuvirudisha mlivyopoteza kwa sababu ukisema mnamkomoa nani ajuaye muda atakaokaa madarakani? Lakini huoni hali hii inawaumiza na watoto ambao hawahusiki na ugomvi wenu na Rais?

    Nadhani mume wako amefanya uamuzi wa busara kuafiki kufanya kazi na Rais. Sahau yaliyopita, msaidieni Rais kuijenga nchi” alikuwa ni Stanley Macha, Mkurugrnzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na rafiki mkubwa wa Joe akiwa anamsihi Eliza aelewe ni kwanini Joe amekubali ombi la Rais Costa.

    “Hivi shemeji kama wewe unatambua hili na kwa nafasi yako na kama kweli Joe ni rafiki yako ulishindwa nini kuongea na Costa mpaka sisi tukaingia kwenye mateso namna hii kwa muda wote huo?”, Eliza alihoji.

    “Eliza, Joe anaelewa hata hili suala la Rais kumtafuta yeye ni mimi”, Stanley alijibu kwa ufupi.

    Ilikuwa ni baada ya wiki moja tangu siku ya kwanza Joe kukutana na Rais ambapo hakuwa kwenye maelewano mazuri na mke wake Eliza. Joe ilibidi amwombe Rafiki yake Stanley aje amsaidie kumwelekeza mkewe.

    Tayari Joe alikuwa nje ya muda wa kupeleka mkakati kwa Rais Costa kama walivyokubaliana maana alitakiwa amrudie baada ya siku tatu. Joe alimwambia Rais angerudi kwake baada ya kujihakikishia mashtaka yake kufutwa. Baada ya siku mbili tangu Stanley kuongea na Eliza alionekana kuelewa. Alitulia, na sasa alikubaliana na hali kuwa ni ngumu kupambana na Rais akiwa madarakani.

    ****************************************

    Haikupita wiki Mahakama ilitoa hukumu ya kutomkuta Joseph Kaduma na hatia zozote za uhujumu uchumi. Wachambuzi wengi na magazeti ya uchambuzi waliweka mijadala kila mahali kuelezea hatua hiyo wakichambua hatua ile kuwa na msigano wa kimaslahi na kutoeleweka ukizingatia maendeleo ya kesi ilivyokuwa hapo nyuma kufutwa imekuwa ni ghafla sana.

    “Serikali imeshindwa kuleta Ushahidi pasi shaka na hivyo mahakama imemkuta Joe bila hatia. Tumeiagiza serikali na vyombo vyake kuachilia mali zote za familia ya Joseph na kumtolea vikwazo vyote iliyokuwa imeviweka dhidi yake hapo kabla”, alikuwa ni Jaji Kunambi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kutoka kutoa hukumu ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Joe.

    “Naishukuru mahakama kwa kunitendea haki. Hilo tu ndilo ninaloweza kusema” Joe aliwajibu waandishi kwa ufupi nje ya mahakama.

    “Vipi serikali ikikuhitaji uitumikie maana tunajua wewe ni mwanadiplomasia mbobevu na ni serikali hii hii ilikutia hatiani”, Seif, mwandishi kutoka gazeti la NIJUZE alimuuliza Joe.

    “Sijachoka kuitumikia serikali. Kesi yangu ni ishara kuwa serikali chini ya Rais Costa inapingana na vitendo vyovyote vya uhujumu uchumi na haibagui, yeyote anaweza kushtakiwa kama ikihisiwa anajihusisha na vitendo hivyo. Hivyo serikali ikinihitaji nitaitumikia sina ugomvi nayo”, Joe alimjibu mwandishi huku moyoni akiwa amejawa na hasira nyingi.

    Kwa siku zile tatu vyombo vya habari vyote vilijaa habari ya mwanadiplomasia Joseph Kaduma kuishinda serikali juu ya mashtaka yake ya kuhujumu uchumi.

    “Watu wanaisifia mahakama kwa kutenda haki, ni wazi wengi walikuwa wanamuhurumia Joseph” Gideon mshauri wa karibu wa Rais Costa alimwambia Rais mchana mmoja wakiwa wanakula chakula Ikulu. “I see, we have made the right move” (Naona, tumefanya jambo sahihi), Rais Costa alijibu kisha akanywa funda la mvinyo kushushia chakula.

    ***************************************

    Ilikuwa ni siku ya Alhamisi yenye mchanganyiko wa hasira na furaha baada ya hukumu. Usiku wake Joe alikuwa ametulia chumbani na mke wake Eliza maeneo ya Endokasi Estate, mahali walipopewa nyumba na serikali. Walikuwa katika hali ya utulivu na tayari baadhi ya mali zao zilianza kurudishwa na vikwazo kuondolewa.

    Hakuna aliyekuwa akiongea na mwenzake bali kila mmoja alikuwa akibubujikwa na machozi. Hawakuamini kilichotokea baada ya miaka mitatu ya kuishi kifungoni na maisha duni na ya manyanyaso makubwa, leo wanarudishwa tena.

    Eliza alianza kuelewa nguvu ya Rais na alikuwa akijuta kimoyomoyo alivyokuwa anamkatalia Joe kukubali maagizo ya Rais Costa. Alianza kuelewa kuwa njia moja tu ya kupambana na mtawala ni labda kupambana nae kinyume na sheria yaani nje ya mfumo wa vyombo vya haki vilivyopo chini ya serikali au kupambana nae ukiwa sehemu ya serikali yake ila tu omba Mungu asikugundue kitu ambacho kwa mifumo ilivyo ni ngumu sana. Angalau hali ndiyo ipo hivyo katika nchi nyingi zinazoendelea.

    Mawazo ya Eliza kutaka Joe apambane na Rais Costa yalikuwa si sahihi na yasingewafikisha popote, yangewamaliza. Alinyanyuka na kumkumbatia mume wake. “Joe, ya kale yamepita na tazama sasa yamekuwa mapya”, Eliza aliongea kwa sauti ya upole akiwa kifuani mwa Joe pale kitandani.

    “Ni kweli mke wangu. Kila jambo lina wakati wake. Kadiri niishivyo nakuahidi kila mmoja aliesababisha tukaingia kwenye hali tuliyokuwa nayo ATALIPA. Kesho nakwenda kuonana na Rais Costa tayari kuanza kutimiza majukumu aliyonituma.

    Najua Rais Costa hakunitafuta kwa ajili ya hiki alichonituma kuna kubwa nyuma ya hili, mimi ninaelewa ila ngoja nijifanye sielewi”, Joe aliongea kwa utaratibu na kumwacha Eliza akiwa na maswali mengi hasa aliposikia kuna suala la malipizi. Aliwaza mumewe anataka kufanya nini, amlipize nani, lini, kwa njia gani? Aliwaza hilo lililo nyuma ya pazia ni nini haswa? Mengi yalikuwa akilini mwake ila hakutaka kuuliza alibaki kimya.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Asubuhi ya kesho yake mishale ya saa mbili hivi Joe alikuwa tayari kuelekea Ikulu kuonana na Rais Costa ili kumpa mpango mkakati wake wa jinsi ya kulitekeleza suala la kurudisha mahusiano na Korea Kaskazini na kisha kufanya yale Rais anayoyataka wasaidiwe.

    Alivaa suti nyeusi na tai nyekundu. Alibeba kalamu yake aina ya Vintage rare carandash AK-45 moja ya kalamu ghali zaidi alizopewa zawadi na Rais Vijisky wa Urusi siku chache kabla ya kufutiwa hadhi ya ubalozi na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi na Rais Costa.

    Alijipachika na nembo ya bendera ya taifa pembeni mwa kola ya koti lake la suti. Hakika Joe alijua kuonekana nadhifu na kidiplomasia haswa. Nje ya nyumba yake, Land Cruiser V8 toleo jipya ilikuwa ikiunguruma na dereva akiwa nje ya mlango akimsubiri atoke.

    Joe alisimama mbele ya kioo akajiangalia kwa muda wa dakika kama tatu hivi. Juu ya ile meza yenye kioo kulikuwa na biblia akafungua Zaburi ya 23 akaisoma yote. “Mungu nisaidie”, Joe alimalizia na kubeba mkoba wake na kutoka tayari kwenda Ikulu kukutana na Rais.

    ***********************************





    Joe Achagua Kikosi Kazi Chake Cha Misheni Ya Korea Kaskazini. Wakutana China. Rais Costa Atuma Kijana Wa Ki Vietinam Kuwafatilia Kwa Siri.

    Korea ya Kaskazini ni taifa lililo na balozi 48 duniani kote lakini ni nchi 25 tu ndio zenye balozi zao jijini Pyongyang. Taifa hili hutegemea zaidi biashara kati yake na nchi za Uchina na India, ambapo asilimia 95 ya biashara zake za nje na uagizwaji wa ndani hufanywa baina ya nchi hizi mbili na asilimia iliyobaki kwingineko kama vile Ufilipino.

    Tangu mtawala wa nchi hiyo Kim Jong Un atangaze majaribio ya makombora ya nyuklia ya masafa marefu, Marekani na Umoja wa mataifa iliiwekea vikwazo. Pia taifa la Marekani liliwataka washirika wake kutojihusisha kibiashara na Korea Kaskazini hata hapo itakapositisha majaribio yake. Hali hii ilifanya hali ya kiuchumi ya Korea Kaskazini kudorora na hata wananchi walipotaka kudai haki zao, ukatili uliongezeka dhidi yao na udikteta ukaota mizizi, ingawa katika utambulisho rasmi wa jina la nchi hiyo ni ‘Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea’.



    Nchi nyingi za kiAfrika ziliingia kwenye wakati mgumu wa namna gani kukubaliana na Marekani na Umoja wa mataifa juu ya vikwazo walivyoweka dhidi ya Korea na wakati huohuo kuendelea kuwa na mahusiano mema na taifa hilo lenye historia kubwa ya kikomunisti na mataifa mengi ya kiAfrika.

    Mahusiano mengi kati ya Korea Kaskazini na nchi nyingi za kiAfrika hayapo kisiasa tu lakini pia kiuchumi kwani inakadiriwa kati ya mwaka 2007 na 2015 biashara iliyofanywa kati ya taifa hili na nchi za kiAfrika yafikia dola za kimarekani milioni 217.

    Korea ikilitumia shirika lake la Mansudae wametekeleza miradi kadhaa ya ujenzi katika nchi baadhi za kiAfrika lakini hasa Namibia ambapo Ikulu na Makazi ya Rais yamejengwa na Korea Kaskazini. Nchi za Uganda, Tanzania na Mozambique mwaka 2017 zilishutumiwa kuiomba Korea iwasaidie katika Nyanja za jeshi, shutuma ambazo nchi kama Tanzania ilizikana lakini Uganda walikubali na kuahidi kusitisha.

    Mbali na miradi ya ujenzi barani Afrika, Korea Kaskazini pia hufanya biashara kubwa ya silaha za kivita. Katika nchi za Eritrea, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Congo na nchi nyingine, Korea ni washirika wazuri katika biashara hiyo. Pia, ripoti ya kiuchunguzi ya Forbasi, taasisi inayoaminika kwa uchambuzi wa masuala ya usalama duniani yenye makao makuu Uskochi inasema kuwa taifa hili la Korea Kaskazini ndilo husaidia ulinzi binafsi wa Rais wa Congo kwa kutoa mafunzo, utaalamu na ufuatiliaji wa usalama wake. Taarifa ambazo serikali ya Congo inakanusha hata leo.

    Mwezi Septemba, 2017 Rais wa Marekani Chriss Donald kupitia agizo lake namba 13810 aliomba nchi zote marafiki wa Marekani kuungana nae katika kusitisha aina yoyote ya biashara na mahusiano na Korea Kaskazini kama kuunga mkono jitihada za kuhakikisha taifa hilo haliendelei na majaribio yake ya makombora ambayo Marekani ilihofia yangeachwa kuendelea, hatimaye wangefikia uwezo wa kitaalamu wa kutengeneza makombora ya nyuklia yanayoweza kusafiri masafa marefu na kufikia ardhi ya Marekani.

    Stanza, moja ya nchi barani Afrika na mshirika mkubwa wa Marekani leo inafanya jitihada wanazotaka ziwe za siri kujenga mahusiano na Korea Kaskazini. Wakati asilimia 50 ya bajeti ya Stanza ikiwa inatokana na mapato ya ndani na asilimia 50 iliyobaki ikitoka kwa nchi wahisani, Marekani pekee inachangia asilimia 20, achilia mbali fedha nyingine nyingi inazopokea kupitia mashirika ya maendeleo ya ki Marekani. Ni katika hali hiyo Rais Costa anataka kukiuka maagizo ya Marekani juu ya mashirikiano yake na Korea Kaskazini.

    Rais Sylvester Costa anataka kwenda mbali kuwaingiza kabisa watoe mafunzo, vifaa na mfumo mzima wa mawasiliano wa Serikali, Jeshi na Idara ya Usalama wa taifa la Stanza.

    ********************************

    “Mh. Rais kutokana na hayo niliyokwishaeleza, basi kwa kuwa sisi hatuna ubalozi Pyongyang wala Korea Kaskazini hawana ubalozi wao hapa kwetu ni vema tukautumia ubalozi wetu pale China kama Sehemu ya kufanyia mikakati mimi na timu yangu nitakayoipendekeza. China wana mahusiano ya karibu sana na Korea na hivyo ninaweza kuwatumia baadhi ya marafiki pale katika, kwanza kujenga mahusiano kisha ndio nitaendelea na mengine uliyoniagiza.

    Lakini nikuombe Mh. Rais kuwa wakati haya yakiendelea ni vyema usiwe na makwazo mengi kwa nchi za magharibi kwani wanaweza wakaanza kutufatilia sana kwa ukaribu na kuharibu mikakati na pia kuwekewa vikwazo vitakavyofanya hali ya uchumi wetu iwe mbaya.

    Lakini pia angalia namna ya kuzungumza na Rais wa Urusi, Kamaradi Vijisky na Rais wa China pia juu ya yale mlioshindwa kuelewana. Njia hiyo itanisaidia sana mimi kuwatumia kwenye misheni yangu hii na pindi wa magharibi watakapoanza kutuletea zengwe wao watasimama kidete nasi”, Joe aliwasilisha mapendekezo yake kwa umakini wakati akielezea mikakati yake kwa Rais Costa.

    Meza ile ilikuwa na watu watano, Rais Sylvester Costa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Ernest Nduta, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Chonge Kalumanzila, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Stanley Macha, na Joseph Kaduma.

    Mara baada ya Joe kumaliza kuongea, kila mtu alikuwa kimya na kuonekana kumuelewa vyema. Aliyekata ukimya ule alikuwa ni Rais Costa, “Joe, tutajitahidi kufanya uliyopendekeza lakini niseme mambo haya kwasasa ni siri kubwa na nimewaeleza wenzangu namna ya kuenenda. Ninajua suala hili likiwafikia Marekani na washirika wake tutakuwa kwenye wakati mgumu na ninajua watang’amua mapema sana ndio maana sitaki tushindwe”, Rais Costa alimsisitiza Joe.



    Joe aliomba timu ya watu wawili wa kusaidiana nae alimtaja Habibu Chamchua Balozi wa Stanza nchini India ambae ni kijana mpendwa wa Joe na Luteni Jenerali Pius Kihaka Mnadhimu Mkuu wa Jeshi na Mkuu wa kitengo cha Idara ya usalama wa jeshi na mmoja kati ya vijana wadogo na wasomi sana katika jeshi la wananchi wa Stanza.

    Pius Kihaka ni Rafiki mkubwa wa Joe, hawa wote; Habibu na Pius ni wanafunzi wa Joe katika chuo cha Diplomasia walipokuwa wanafanya Shahada zao za Uzamili. Joe anaamini hawa ni baadhi ya vijana wenye upeo mkubwa sana katika uwanda wa kidiplomasia, ushawishi na ushushushu. Ndio watu aliowataka kufanya nao kazi. Lakini pia alikuwa na ajenda nao nyingine nyuma ambayo hakuna mtu alieijua. Rais Costa alimkubalia na kutoa maagizo vijana hao wataarifiwe na kuwa sasa watafanya kazi kwa maelekezo ya Joe.

    Kikao kile kiliisha vyema. Joe aliridhika kuwa sasa anaweza kuanza kutimiza majukumu yake. Alipatiwa kila aina ya mahitaji na nyaraka alizohitaji ili kutekeleza kazi aliyopewa. Rais Costa alipeleka salamu za kutaka mazungumzo na Rais Kim wa Korea na kuwa ujumbe wake utaelekea huko. Rais Kim aliridhia na kutaka kujua haswa ni nini taifa kutoka Afrika tena wenye ushirika mkubwa na Marekani linataka kuzungumza. Hakika kila nchi ilijitayarisha kwa mazungumzo hayo.

    *******************************

    Habibu Chamchua, kijana mahiri katika medani za kidiplomasia, machachari katika ushushushu na sasa balozi wa Stanza nchini India alifurahishwa na taarifa kuwa anahitajika kufanya kazi na Joe. Habibu alikuwa kijana makini na aliyefanya vyema kwenye chuo cha diplomasia, alishawishiwa na Joe aingie kwenye siasa ili kushika nafasi za uongozi wa nchi.

    Ni Joe aliyempa moyo Habibu kwa kumwambia kuwa anamuona siku moja kama Rais wa Stanza. Mara baada ya Habibu kuingia kwenye siasa alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuteka nyoyo za vijana wengi wa chama tawala mpaka upinzani. Ni yeye aliewezesha kubadili hali ya kisiasa kwa wakati fulani kwa jinsi alivyoweza kujenga hoja na kujieleza.

    Katika chama tawala alionekana sana tishio na ni hapo Rais Costa ili kumpunguza nguvu aliona yafaa amtoe nchini na kumpangia ubalozi ili apotee machoni na masikioni mwa wengi. Habibu sasa anapewa jukumu la kuhakikisha Korea Kaskazini inasaidia Stanza kijeshi lakini hususani kufanya kazi na Joe, ilikuwa ni heshima kubwa kwake.

    *******************************

    Zilipita wiki mbili tangu mashtaka ya Joe dhidi ya uhujumu uchumi kufutwa na mahakama ya uhujumu uchumi na ufisadi ya Stanza. Waziri wa Fedha alimteua Elizabeth Kidampa Kaduma kuwa Mkurugenzi wa benki ya Kilimo ya Stanza. Elizabeth, mke wa Joseph Kaduma aliwasili makao makuu ya benki na kupokelewa kwa heshima kubwa. Eliza alijaa haiba na tabasamu, ni mwanamke asiejikweza mwenye uwezo mkubwa wa kusikiliza na kung’amua mambo.

    Mara baada ya kusomewa taarifa fupi ya maendeleo ya benki, alibainisha wazi kuwa vipaumbele vyake ni pamoja na kuhakikisha fedha zote zinazotengwa na serikali kwa ajili ya ruzuku zinawafikia wakulima kwa wakati na hilo hatakuwa na msamaha na mtendaji yeyote atakayezembea, lakini pili ataanzisha maghala yatakayosimamiwa na benki na kuwa mazao yote ya biashara yatapangiwa bei elekezi na mfanyabishara atapaswa kuyanunua kwa bei hiyo kutoka kwa wakulima, vinginevyo basi benki itayanunua na kuyatafutia masoko.



    Alitanabaisha benki ile ni lazima iwe msaada kwa wakulima kwa kutoa mikopo nafuu na kuhakikisha wakulima wa Stanza wananufaika. Pia, alielezea mpango wa benki kwa kushirikiana na wizara kujenga mabwawa makubwa na ya kisasa kwa ajili ya umwagiliaji katika kanda tano zinazoongoza kwa kilimo cha mazao ya biashara na chakula kwa kuanzia ili nchi itoke kwenye kutegemea mvua pekee kwa ajili ya umwagiliaji. Ilikuwa ni taarifa njema.

    *********************************

    “Kaka shikamoo”, alikuwa ni Habibu akimsalimia Joe kwa bashasha na tabasamu kubwa huku akimkumbatia ndani ya ofisi za ubalozi wa Stanza jijini Beijing China zilizopo mtaa wa Liang Ma He, Nan Lu. Ilikuwa ni faraja kubwa kwa Habibu kukutana na Joe. “Luteni Jenerali” Habibu alimwita Pius huku akionyesha ishara ya kupiga saluti kisha kumkubatia kwa kicheko kikubwa.

    Habibu alikuwa akiwalaki Joe na Luteni Jenerali Pius Kihaka waliokuwa wamewasili kutoka Stanza, yeye akiwa amewatangulia siku moja kabla akitokea India. Habibu ndio alikuwa mdogo kiumri kati ya Joe na Luteni Jenereli Pius Kihaka. Wote kwa pamoja walilakiwa na balozi Kimweri anaeiwakilisha Stanza huko China.

    Walielekea kwenye chumba walichotengewa na ubalozi maalumu kwa ajili ya vikao vyao na Joe alikuwa tayari kutoa muhtasari na mwongozo wa namna kazi itakavyofanyika. “Ni jukumu letu kuleta matokeo yanayotegemewa na Mh. Rais. Tutaingia kwenye vitabu vya historia kwa kuanzisha mahusiano na Korea Kaskazini lakini pia kwa kufanikisha kazi hii Mh. Rais aliyotutuma”, Joe alimalizia. Habibu na Pius walionekana kutikisa vichwa ishara ya kuelewa na kuafiki. Wakati Joe akiongea walikuwa wakipitia baadhi ya nyaraka Joe alizowagawia waziangalie na kuzisoma. Tayari ubalozi wa Stanza pale China ulishaanda utaratibu mzima wa Joe na wenzake kuingia Korea Kaskazini.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Baada ya maongezi yale yaliyodumu kwa masaa mawili wakiweka mikakati na nini cha kuzungumza na nani azungumze nini. Joe alipendekeza jioni wakutane mgahawa wa Cheng Lee ulio jirani na Ubalozi kwa ajili ya kupata kahawa.

    **********************************

    Ilikuwa ni habari iliyowasisimua viongozi wa taifa la Korea Kaskazini kusikia kuwa kuna taifa kutoka Afrika linataka kuanzisha mahusiano nao ukizingatia tamko na maazimio ya Marekani na Umoja wa mataifa. Rais Kim alikuwa akisubiria ujumbe kutoka Stanza kwa shauku kubwa.



    Kuonyesha shauku yake na kwa ajili ya usalama aliagiza ndege kutoka shirika la ndege la Korea Kaskazini, Air Koryo llyushin II-62M ndiyo iwabebe kwa kuwatengea siti maalum. Viongozi wa Korea walijipanga kusikia nini ujumbe kutoka Stanza utawaeleza na mashirikiano gani wanahitaji, watafaidika vipi na wamejipangaje kushindana na shinikizo kutoka nchi za Magharibi zisizowaunga mkono hasa Marekani.

    ********************************

    “Kimweri niambie kinachoendelea”, alikuwa ni Rais Sylvester Costa akiongea na balozi Kimweri aliyeko China kupitia mfumo salama wa mawasiliano ya kiserikali. “Mpaka sasa hakuna tishio lolote walilojadili ila jioni wamekubaliana kukutana mgahawa wa Cheng Lee kwa ajili ya kupata kahawa”, balozi Kimweri alimjibu Rais Costa. “Kuna mtu kule tayari? Nahitaji ufuatiliaji kwao hatua kwa hatua hasa wakiwa hapo China”, Rais Costa alisisitiza. “Ndiyo mkuu”, balozi Kimweri alijibu.

    Bila Joe na wenzake kujua Rais Costa alishaweka namna ya kufatilia kila wanaloongea Joe, Habibu na Pius. Alihakikisha vyumba vyote watakavyokuwa wanakutana vimewekewa vinasa sauti kwa siri vyenye uwezo mkubwa sana. Maongezi yao na simu zao zote zilikuwa zikirekodiwa.

    Rais Costa alikuwa akipata kila kinachoendelea kwenye maongezi ya Joe na wenzake. Japo alimwita Joe amsaidie kazi lakini hakumwamini. Alianza kupata mashaka hasa Joe alipotaka kazi ile asaidiane na Habibu na Pius watu anaowajua ni watiifu kwa Joe. Rais Costa hakutaka kupitwa na kitu hivyo tayari balozi Kimweri alishatuma mtu mgahawani kuangalia namna atakavyoweza kurekodi maongezi ya kina Joe bila wao kujua.

    Kimweri alifanya hivyo mara baada ya kuona Joe ametoka kwenye kikao na kwenda kupumzika lakini hakumualika kwenye kahawa jioni wakati yeye ndo mwenyeji wao. Aliwaza ni nini Joe alitaka kwenda kuongelea huko. Kati ya watu watiifu na vipenzi wa Rais Costa basi balozi Kimweri ni mmoja wapo.

    ***********************************

    Jioni ilifika na Joe, Habibu na Pius walitoka kwenda mgahawani. Walipofika Joe alichagua meza iliyo mwishoni mwa mgahawa ili apate kuona kila anaeingia ndani ya mgahawa na alihakikisha upande aliokaa hakuna anaeweza kingia bila yeye kumuona. Kati ya Habibu na Pius hakuna aliyekuwa anajua kinachotaka kujadiliwa pale, walidhani ni maongezi ya kawaida tu.

    Waliketi, na baada ya kumaliza kuagiza kahawa Joe alivunja ukimya. “Guys, ninyi ni vijana wangu na ninaelewa nguvu yenu. Mfano Habibu unaelewa jambo nililoongea nawe miaka mitano iliyopita lililokufanya ujiingize kwenye siasa kwa mara ya kwanza. Pius wewe pia unaelewa au sio? Huu ndio wakati wa kuanza utekelezaji, tunaenda na yote mawili ndani ya moja”, Joe alitulia na kunywa kahawa.

    Habibu na Pius walionekana ni kama watu wasioelewa Joe anazungumza kitu gani, walibaki wameshangaa wakiangaliana. Joe alikuwa akizungusha macho mgahawani kuhakikisha hakuna yeyote anakaa meza karibu yao ama hata kuwasogelea.

    Akiwa amemaliza kunywa tena kahawa kwa mara ya pili simu yake ilitoa sauti kuashiria kuna ujumbe umeingia. Alipoangalia vyema aligundua ujumbe umeingia kupitia App ya game uliosomeka “Hakikisha mdudu yeyote hakukaribii wakati wowote wa mazungumzo nje ya Ubalozi”, Joe aliposoma alivuta pumzi na kujikaza ili Habibu na Pius wasishtuke kisha akaanza kuzungusha macho kila kona hasa maeneo ya ukuta na dirisha lililo umbali mchache kutoka pale walipokaa. Alipokuwa akiangalia aliona mdudu kama nzi akiwa anawasogelea.

    Akaja akatua juu ya kichwa cha Joe kwa ukutani. Joe alishtuka sana akajikaza. Pius akawa kama kuna jambo ameshtukia akamuuliza Joe kulikoni? Joe hakujibu akamwonyeshea Pius ishara ya kuwa anyamaze, kisha akaonyesha ishara kuwa waondoke. Waliposimama na kuanza kuondoka Joe aliwasogelea wenzake na kukaa katikati yao kisha akawaambia atawaambia kilichotokea ila wasiwe na wasiwasi.

    ******************************

    Stanley Macha, mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa Stanza na Rafiki mkubwa wa Joe alikuwa akifuatilia hatua kwa hatua safari na misheni aliyotumwa Joe nchini Korea Kaskazini. Ni ukweli usiopingika Macha na Joe walikuwa ni zaidi ya marafiki, ni yeye alietengeneza mazingira misheni ya kutafuta mahusiano na Korea Kaskazini isifanikishwe na mtu yeyote katika serikali ya Rais Costa mpaka Joe aitwe.

    Ilikuwa ni ngumu kumuacha Joe peke yake hasa akijua mahusiano ya kutilia shaka aliyonayo Joe na Rais Costa. Mara baada ya Joe kukubali kutumika na Rais Costa katika misheni ya Korea Kaskazini Macha aliamua kutafuta njia ya siri ya kuwa wanawasiliana na Joe. Waliamua wote kuwekagame (mchezo wa kwenye simu) unaoitwa Clash Royale ambao wachezaji huweza kutumiana jumbe na kuwasiliana. Ili mtu mwingine kuweza kufatilia jumbe zinazotumwa humu ni lazima uwe na wewe umeweka huu mchezo kwenye simu yako ama uwaombe wamiliki wakupe.

    Lakini pia majina yanayotumika huwa sio ya halisi hivyo pia ni ngumu kujua ujumbe huu unatoka na kwenda kwa nani. Macha na Joe hutumia njia hii kuwasiliana. Macha alichelewa sana kupata taarifa juu ya mpango unaondelea juu ya Joe na wenzake unaofanywa na Rais Costa na balozi Kimweri. Hakuna anaejua alipataje hasa ukizingatia maelekezo ya Rais kwa balozi Kimweri ni ufuatiliaji wa Joe ufanywe baina yake na Kijana ambae Rais Costa alimpelekea balozi Kimweri kutoka Vietnam.

    Balozi Kimweri na yule kijana wa kiVietnam walitumia kinasa sauti mfano wa Nzi kinachoweza kuendeshwa kwa rimoti ya kwenye simu kutokea mbali. Hivyo kutokea meza ya mbele kabisa ya mgahawa kijana yule wa kiVietinam alikitoa kile kinasa sauti na kuanza kukiendesha kwa simu kama mtu aliekuwa akichat kuelekea mwisho wa mgahawa walipokuwa wamekaa Joe na wenzake.

    Macha alipopata ile taarifa alimtumia ujumbe Joe kuwa awe mwangalifu na mdudu yeyote arukae atakaesogea karibu nao. Joe aliona yule mdudu kama nzi na aligundua kilichokuwa kikiendelea. Waliondoka.





    Mazungumzo Mazito.Yawaacha Njia Panda



    “Mr. President, I respect the outstanding, long time bilateral relations our countries have enjoyed for the past 50 years. I, personally appreciate the two-way respect between you and I, but with all due respect, I will not allow your country to forcibly impose your culture on ours. We will not allow or legalize homosexuality in our country. It is against our normalcy, tradition, and culture as Africans. It is against our spiritual beliefs and the order of nature. If you have accepted it as your way of life, let it remain yours”

    (Mh. Rais ninaheshimu mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi zetu mbili katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Na binafsi, ninaheshimu pia mahusiano tuliyo nayo sisi wawili, lakini kwa heshima kubwa niseme sintoruhusu taifa lako lilazimishe mapenzi ya jinsia moja kukubalika kwenye nchi yetu. Ni kinyume cha tamaduni na desturi zetu, kinyume na imani zetu, lakini zaidi na muhimu ni kinyume na asili ya mwanadamu. Kama mmekubaliana hayo kuwa Maisha yenu, basi ibaki kuwa hivyo huko kwenu.)

    Rais Costa alikuwa akiongea na Rais wa Marekani, Chriss Donald masuala mbalimbali yanayohusu Stanza na hapo alikuwa akimjibu matakwa ya Marekani kutaka mataifa yanayopokea msaada kutoka kwao kuruhusu mahusiano ya jinsia moja (ushoga).

    “Mr. President I understand your position, but I suggest that we talk about this in the next bilateral meeting. We will need to review most of our foreign relations policy with Stanza, if at all we do not come into a mutual understanding on the matter.

    I can tell that after deliberations, your position will change, and Stanza will consider same-sex marriage as not only a private matter between two adult individuals who have chosen to love one another but also as a basic human right to associate and to form social relations. That I can guarantee”.

    (Mh. Rais naelewa msimamo wako, ingawa nashauri kuwa tulizungumzie suala hili katika mkutano ujao kati ya nchi zetu. Tutalazimika kufanya mapitio ya sera yetu ya mambo ya kigeni na Stanza, ikiwa hatutofikia maelewano kuhusu suala hili.

    Ninaweza kusema kuwa baada ya kukaa na kufikiria, msimamo wako utabadilika na Stanza itakubaliana na ndoa za jinsia moja si tu kuwa ni masuala ya faragha kati ya watu wazima wawili walioamua kupendana, bali pia kama haki ya msingi ya binadamu ya kuhusiana na kuanzisha mahusiano ya kijamii. Nakuhakikishia hilo). Rais Donald alimjibu Rais Costa kwa sauti ya kuamrisha kidogo. Rais Costa alighadhibika ila akakaa kimya.

    “Again, it is interesting Mr. President to hear that your country is intending to amend the constitution that will change the legal age to run for presidency from 40 to 55 years.

    (Nimepata taarifa kuwa Stanza inakusudia kufanya mabadiliko ya katiba yatakayofanya umri wa kisheria wa kugombea nafasi ya Urais kuwa miaka 55 tofauti na miaka 40 ya sasa). Rais Chriss Donald alimwambia Rais Costa kwa kebehi.

    “I think you are crossing the line Mr. President, Stanza is a sovereign country. It is of best interest if each of our countries is let to freely define democracy according to their local context and choose what works best for them.

    (Nafikiri unakwenda mbali Mh. Rais, Stanza ni taifa huru. Nibusara kuachia kila nchiijiamulie nini maana yademkorasia kwao kwa misingi yamuktadha na kile ambachokinafanya kazi katika nchihusika). Rais Joe nae alijibu kwakicheko cha kebehi lakinikilichojaa ghadhabu.

    “No no no. It is not my intention, nor that of the United States to interfere with your internal affairs. I raised the matter so that we can both have the same understanding of the happenings. We shall see to that too”.

    (Hapana! Hapana. Si lengo langu wala la Taifa la Marekani kuingilia masuala ya ndani ya nchi yenu. Nimelisemea suala hilo ili sote, mimi na wewe tuwe na uelewa unaofanana wa masuala yanayotokea. Tutaliangalia na hilo pia’’), Donald alimalizia.

    “It was nice time speaking with you Mr. President” (Umekuwa muda mzuri kuongea nawe Mh. Rais) Rais Costa alimuaga Rais Donald kwa hasira kidogo.

    “Pass my hello to Chairman, Mr. Kim”, (Salamu nyingi kwa Mr. Kim), Donald alimalizia na kukata simu akimwambia Rais Costa amsalimie Kim, Rais wa Korea Kaskazini.

    Rais Costa alibaki na mshangao ulioonekana waziwazi usoni mwake. Alijiuliza maswali mengi, muhimu zaidi ikiwa imekuwaje Rais Donald akamtaja Kim muda ambao Joe na wenzake wanatekeleza misheni aliyowatuma ambayo kwa wakati huo alitambua ni siri.

    “Macha wapigie simu kina Joe, nataka kufahamu wamefikia wapi. Haraka nitafutie nani amevujisha mpango huu kwa Marekani kabla hata ya Joe kukutana na Rais Kim”, Rais Costa alimwambia Stanley Macha kwa ghadhabu kisha alijiegamiza kwenye kochi na kupumua kwa nguvu. Alichanganyikiwa. Anafahamu mabavu ya Marekani katika siasa za kimataifa. Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, mataifa yaliyotofautiana na Marekani yameingia katika misukosuko mikubwa ya kiuchumi na kijamii.

    **************************************

    Ndege waliyopanda Joe na wenzake iliondoka mishale ya saa moja asubuhi kwa saa za China kuelekea Pyongyang ikitokea uwanja wa Beijing Capital International Airport. Joe na wenzake waliwekewa nafasi kwenye daraja la watu muhimu, ulikuwa ni ujumbe maalum unaosubiriwa sana na uongozi wa Korea Kaskazini. Kutoka Beijing mpaka Pyongyang ni safari ya masaa mawili hivi, hivyo mara tu baada ya ndege kutulia juu ya anga Joe aliwapa alama Habibu na Pius wasogee kwenye nafasi yake karibu. Nafasi zao zilifuatana.

    Joe aliwaambia kwa kifupi kwanini aliwaondosha pale mgahawani. Aliwaambia kuwa Rais Costa alikuwa akifatilia maongezi yao kwa kuwatumiadrone yenye umbo la Nzi ili inase maongezi yao. Pius na Habibu bado walikuwa hawajaelewa kwanini hayo yanatokea. Joe alitambua hilo na haraka alianza kuwaweka bayana, “Nadhani kati yenu hakuna anaefurahia namna Costa anaipeleka nchi, ni jukumu letu sasa kumpumzisha kwa amani na usalama”.

    “Najua mnaweza kudhani ninataka kulipa kisasi lakini nayasema haya kwa nia njema ya kizazi kijacho na ustawi wa nchi yetu ya Stanza”, Joe alikuwa akiongea kwa kunong’ona sana huku akiwakazia macho Pius na Habibu. “Ninawaambia haya kwa sababu ni ninyi mnaoweza kutekeleza hili. Ninawategemea kama vijana wangu, lakini ikiwa mtaona haya si ya msingi, basi tunaweza kuachana na mpango huu kabla hata hatujauanza. Tafakarini na tutaamua kwa pamoja uelekeo ambao ninyi mnatamani taifa letu lichukue”. Joe alimalizia na kukaa kimya kuwasikiliza.

    Baada ya sekunde kadhaa za ukimya, Habibu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuuvunja ukimya. “Joe, unachomaanisha ni kututaka tushiriki kumpindua Rais aliyepo madarakani kihalali?”. Habibu alionekana kutoelewa anachoshauri Joe. Habibu ni mtiifu kwa Joe lakini katika hili aliona ukakasi.

    “Hapana, hatumpindui, tunampumzisha kwa ustawi wa Stanza.” Joe alijibu kiufupi. “Unampumzishaje mtu kabla ya muda wake wa kukaa madarakani kihalali kuisha?”, Habibu alizidi kuuliza.

    “Muda wake kihalali uliisha 2015, nini kilitokea baada ya pale? Costa hana uhalali na nilazima ataibadili katiba na sasa nadhani Pius anafahamu, labda wewe kwa sababu upo mbali na varanda za Ikulu hujui, anataka kuhakikisha uchaguzi ujao anapandisha umri wa mtu kugombea Urais ili abakie yeye. Costa hana muda wa uhalali”. Joe alijibu huku akiwatazama usoni Habibu na Pius.

    “Joe, nimekula kiapo cha kumlinda Rais, unachoniambia hapa ni Uhaini, na ni lazima utambue nafasi yangu katika jeshi”. Luteni Jenerali Pius Kihaka alionekana kumjibu Joe huku akiwa amekunja ndita.

    “Luteni ulikula kiapo kuilinda katiba na Rais anayeitii misingi ya katiba. Utamlinda Rais pale tu akiitii katiba na si vinginevyo. Rais asiyetaka kuitii katiba, misingi ya haki na utawala bora anageuka kuwa muhalifu kama wahalifu wengine. Sasa nikuulize kiapo chako kinakuelekeza kumtii na kumlinda muhalifu?” Joe alimjibu Pius.

    “Nahitajika kumtii yeyote alieshikilia nafasi inayoitwa Rais bila kujali anafuata katiba ama vinginevyo. Hivyo ndivyo mafunzo na miiko yangu jeshini inavyoniongoza. Wananchi ndio wanatakiwa waseme huyu haifuati katiba na wamtoe kwa chaguzi za kidemokrasia lakini sio mimi. Lakini je, wewe ndio kipimo cha kuhalalisha kuwa huyu anavunja katiba ama la? Au wewe ndio wa kusema huyu hafuati haki na utawala bora ama la? Nijuavyo mimi mamlaka hayo imepewa Mahakama au angalau Bunge na sio hisia za mtu binafsi Joe” Pius alisisitiza kwa maswali mfululizo.

    “Pius, nadharia ya mgawanyo wa kimamlaka kati ya Serikali kuu, Bunge na Mahakama kiuhalisia haupo kwenye nchi zetu nyingi za kiAfrika achilia mbali Stanza. Nadharia hizo zimewekwa kwenye katiba kwa mkono mmoja na kuporwa kwa mkono mwingine. Tuliyajadili haya kwa kina sana nilipokuwa nawafundisha pale chuo cha diplomasia. Pius ulionekana kukasirishwa sana na hali hii, Habibu uliniahidi siku ukipata nafasi ya uongozi ungerekebisha haya, lakini tazama leo baada ya kuzipata nafasi mbalimbali mmesahau mara moja hii? Leo ninyi nanyi mnaona hali hii ni sawa na kunihoji maswali kana kwamba hamfahamu ukweli huu?” Joe aliongea kwa hisia kubwa na kuanza kuwapa darasa.

    Aliongea nao kwa kina na kuwapa mifano mingi ya uvunjifu wa haki za raia, unyanyasaji na uteswaji. Aliwaambia jinsi hali inavyokwenda kuwa Mbaya baada ya Rais Costa kuweka sera nyingi mbovu na kuharibu sana mahusiano na mataifa rafiki. Aliwaambia hata safari yao ile ni kwa sababu Stanza inakosa marafiki na sasa inatafuta marafiki wapya kwa nguvu.

    Aliwaeleza kinagaubaga namna mihimili miwili ya Bunge na Mahakama jinsi ilivyo ghoshiwa na Rais Costa na kuwa hakuna chochote kinaweza kuendelea ndani ya mihimili hiyo kilicho kinyume na Rais Costa hata kama kina maslahi makubwa kiasi gani na nchi ya Stanza. Aliwashangaa ni kwanini wao kwa nafasi zao inawawia vigumu kuling’amua hilo vipi kwa mtu wa kawaida.

    Aliwaambia, wao wanaweza kukataa kwa sababu wana nafasi serikalini lakini wajueakumulikaye mchana usiku atakuchoma hivyo wasishangae siku moja kugeukwa na kuingia kwenye mateso makubwa. Aliwauliza nani katika serikali ile alikuwa rafiki wa karibu na Rais Costa kuliko yeye? Na je wanajua kilichompata?



    Alimalizia kwa kuwaambia kuwa ili kutoka katika hali ile inahitajika juhudi za mmoja mmoja na sio kutegemea wengi. Wao kwa nafasi zao wapo kwenye nafasi nzuri za kuhakikisha Rais Costa anapumzishwa nje ya madaraka na marekebisho makubwa ya kimfumo,kisera na kikatiba yanafanyika kwa maslahi mapana ya wana Stanza. Joe aliongea kwa hisia, na baada ya kumaliza Habibu na Pius walionekana kuanza kuelewa.

    “Kwa hiyo kwenye mpango huu upo na nani?”, Pius alihoji. “Ni mapema sana kuwaambia. Kwanza nilitaka nipate nafasi hii kuwapa huu muhtasari na kutaka utayari wenu kisha nitawaambia wote waliopo kwenye mkakati huu” Joe alijibu.

    “Kwa hiyo jambo hili linafanikishwaje”, Habibu alihoji. “Nitawaambia, but first, let’s focus on what brought us all the way here”. Joe alijibu akikusudia kufunga ule mjadala, na kabla hajamaliza muhudumu wa ndege aliwasogelea na kuwauliza kama kuna kitu wanahitaji. Waliagiza Chai. Joe na Habibu wakarudi kukaa kila mtu akionekana kujaa mawazo. Mawazo ya jinsi gani watampumzisha Rais Costa nje ya madaraka, nani ataongoza Stanza na nini kitafuata baada ya hayo?

    *************************************

    “Sikiliza Sylvester, haya sio makubaliano yetu. Ulinitoa Canada kwa ahadi kuwa unakuja kunipa Uwaziri, umeishia kunipa Ukatibu Tawala wa jimbo tena huku kijijini, kweli? Ungeniacha Canada kule kule bwana”. Alikuwa ni mrembo, Ketina, kimada wa Rais Costa akiongea nae kwa simu kutokea Jimbo la Kichumbi alikomteua kama Katibu tawala.

    “Keti, mbona una haraka mpenzi? Hujakaa kwenye hiyo nafasi hata miezi sita unataka nikupe Uwaziri? Hatuendi hivyo mpenzi wangu. Subiri angalau umalize mwaka nitakupa Ubunge kwa kutumia nafasi zangu kwa mujibu wa katiba halafu utaanza na Unaibu Waziri”. Rais Costa alijibu kwa utaratibu na kubembeleza.

    “Nani asubiri mwaka mzima Costa? Mimi Keti au nani? Wachezee hao hao watu wako wa Stanza sio mimi. Hakuna linaloshindikana ukiamua. Wewe ni mtu mwenye nguvu kuliko wote chini ya jua la Stanza. Katiba imekupa mamlaka ya kuamua uzima na kifo cha yeyote nchi hii sembuse kunipa uwaziri mimi? Ketina alichachamaa.

    “Kwanza ndani ya siku mbili tatu hizi nitakuja Peron kuonana na wewe nimeku miss”, Ketina alimalizia kwa sauti ya upole. Alimtaarifu Rais Costa kuwa anakuja Peron mji mkuu wa Stanza ilipo Ikulu ya Rais Costa kwa ajili ya kuonana nae.

    “No, no Keti, I have pressing issues that I am dealing with right now. I will tell you when to come” (Hapana Keti, nina masuala nyeti ninayoshughulikia sasa hivi. Nitakwambia lini uje), Rais Costa nae alijibu kwa upole.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Midts of your pressing issues, you can always slot a time to hang on with your bae, aren’t you Mr. President?”. (Hata katikati ya masuala yako nyeti huwezi kukosa muda wa kukutana na mpenzi wako, au sio Mh. Rais?). Ketina aliongea kwa sauti ya kimahaba iliyomlainisha Rais Costa. “Aaa…. aaaa. Ok Keti just come”, (Aaaa…. aaaaa. Sawa Keti njoo basi). Rais Costa alijikuta anakosa kauli. “That’s my baby” (Huyo ndio mpenzi wangu), Ketina alimalizia na kukata simu.

    ***************************************

    Kwa macho na mbele ya wananchi na watendaji wa Serikali, Rais Sylvester Costa alikuwa akionekana mkali na mtu asiesogeleka. Ilikuwa ni ngumu kumwangalia machoni mara mbili akiwa anaongea na wewe. Hata watendaji wa serikali ikiwemo na mawaziri wake huongea nae wakiwa wameinamisha kichwa. Alikuwa mkali na mbabe kwelikweli.

    Ketina Nikodemas, msichana mdogo kiumri aliyekutana nae nchini Canada miaka mitatu iliyopita katika moja ya ziara zake, ndiye pekee aliyeweza kumuendesha Rais Costa jinsi alivyotaka. Ketina akiwa nchini Canada kumalizia masomo yake ya Uzamili alionana na Rais Costa na katika kumsalimia, Rais Costa alivutiwa nae na hivyo kuagiza kuonana nae Hoteli aliyofikia.

    Rais Costa alianzisha mahusiano na binti Ketina na hakika binti huyu alijua kumteka Rais. Ni katika mapenzi hayo ambapo Ketina alitaka apewe Uwaziri na hivyo Rais Costa alimrudisha nchini Stanza na kuanza kwa kumpa Ukatibu Tawala wa jimbo.

    Ketina hakufurahishwa na uteuzi huo na sasa alikuwa akimlazimisha Rais ampe Uwaziri kamili. Hakuna aliyekuwa akijua kinachoendelea nyuma ya pazia kati ya Rais Costa na Ketina isipokuwa kwa wafanyakazi wachache wa Ikulu hasa vijana wa Usalama wanaotumiwa na Rais kupanga na kuandaa mazingira ya kukutana kwao mara kwa mara sehemu mbalimbali.

    **********************************



    Joe Awasili Pyongyang. Siri Nzito Yawashtua Habibu Na Pius.



    “??? ???” seonlyanghan dongjideul (Habari za asubuhi kamaradi). Ndugu En Ki, waziri anayehusika na masuala ya kigeni wa Korea Kaskazini aliwasalimia kiKorea Joe na ujumbe wake mara tu baada ya kuwapokea uwanja wa ndege wa Pyongyang.



    “?? ??” joh-eun achim(Salama) Joe nae alijibu kiKorea huku akiwa ameshikana mkono na ndugu En wakiwa wameinamishiana vichwa. “??? ?? ?? ?????. pyeong-yang-e osin geos-eul hwan-yeonghabnida, (Karibuni Pyongyang), Waziri En aliendelea.

    “???. ??? ??? ?? ?”gomawo. uliui jeulgeoum dongji ya. (Asante sana. Ni furaha yetu kubwa sana kuwa hapa), Joe nae alijibu huku akitabasamu.



    Joe akiwa mwanadiplomasia mbobevu alielewa itifaki za mataifa mengi. Alikuwa ni mtu makini ambaye ukikutana nae unajua kabisa kuwa ameiva kwelikweli katika masuala ya mahusiano ya kimataifa, diplomasia na hata lugha za kigeni.



    Ndugu En aliwaongoza Joe na ujumbe wake mpaka kwenye magari yaliyoandaliwa kwa ajili ya msafara kuelekea Ikulu ya Pyongyang. Kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pyongyang Sunan jijini Pyongyang mpaka makazi ya Rais Kim ni mwendo wa kama dakika 40 hivi kwa gari, hivyo msafara ulianza kwa kuifuataHeeecheon Expressway.

    Yalikuwa jumla ya magari manne, la mbele likiwa linaongoza msafara, la pili alipanda Waziri En na Joe, la tatu alipanda Habibu na Pius na la nne likiwa ni la ulinzi. Wakiwa njiani, Joe alikuwa akiongea mawili matatu na En. En alikuwa ni mjuzi wa lugha nne ukiacha ya kiKorea.



    Alizungumza kwa ufasaha kiingereza, kichina, kirusi na kifilipino. Alikuwa ni mtu mwenye uelewa mkubwa sana wa masuala ya kimataifa na mwenye akili nyingi sana. Aliaminiwa na Rais Kim Jon Un wa Korea Kaskazini tangu alipoingia madarakani kurithi mikoba ya baba yake alipofariki.

    “Comrade Kim has high expectations of your visit”, (Rais Kim ana matarajio makubwa na ujio wenu huu). En alimwambia Joe huku akitabasamu kwa shauku. “Same to President Costa”, (Hata Rais Costa), Joe nae alijibu kwa ufupi. Joe alijua mbinu za mazungumzo, alijua wapi pa kuongea sana na wapi pa kuongea kwa uchache, alijua lipi la kujibu na lipi la kukaa kimya. Tangu anawasili Pyongyang kila jambo analofanya alitumia umakini mkubwa.

    Safari iliendelea huku Joe akishangaa na kustaajabu namna barabara ilivyokuwa tupu na nyeupe. Hakuona hata mtu mmoja tokea walipouacha uwanja wa ndege. Alikuwa akistaajabu na alipouliza kwa En alijibiwa hivyo ndivyo wanavyowaheshimu wageni muhimu kwa taifa. Joe hakuelewa.

    **************************************

    Ryongsong ndilo jina la makazi ya Rais Kim. Wengine hupenda kuyaita Residence No. 55 auCentral Luxury Mansionkutokana na umaridadi wake. Ni makazi yanayosemekana kulindwa na kuwa salama kuliko makazi yoyote duniani. Ukubwa wa eneo yaliyopo makazi haya ni kilometa za mraba 12 pakiwa na kila aina ya kitu kinachohitajika kwa kiongozi mkuu wa nchi.

    Wataalamu wa masuala ya ulinzi na ujasusi wanaamini kuwa askari kati ya 95,000 – 120,000 wapo maalumu kwa ajili ya kulinda eneo hili pamoja na usalama wa Rais Kim na maeneo mengine yote yalipo makazi ya familia ya Rais Kim. Wakiwa chini ya kikosi namba 963wakiongozwa na Jenerali Yun Jong-Rin, wanakifanya kikosi hiki kuwa moja ya vikosi vikubwa kabisa vya ulinzi wa Rais duniani.

    Ryongsong imezungukwa na machimbo yaliyotegwa kulipuka kama kuna mvamizi yeyote atataka kusogelea makazi haya kwa njia ya ardhi, lakini pia kuna wigo mkubwa wa umeme pamoja na vituo vingi vya ukaguzi kwenye njia ya kuingilia na kuzunguka makazi haya. Makazi haya pia yamezungukwa na vituo vya kijeshi vyenye makombora makubwa ya maangamizi na ya masafa marefu na mitambo ya kunasa chochote kinachoikaribia eneo lile bila taarifa na kuweza kutuma kombora kukisambaratisha.

    Hakuna ndege wala kifaa chochote kinachoruhusiwa kupita juu ya anga lililopo jengo hili la sivyo kitatunguliwa hapohapo. Ndani ya makazi haya, chini ya ardhi kuna Sehemu salama ya kumficha Rais ikiwa itaonekana yupo hatarini. Eneo hilo limejengwa kwa kuta za chuma kizito na zege zito lililofunikwa na madini ya leadili kuzuia nyumba hiyo kuathirika hata kwa shambulio la nyuklia.

    Lead ni moja ya madini yenye myeyuko hafifu (Low melting point), hivyo huhitajika joto la kuanzia nyuzi joto 327 ili yaweze kuyeyuka. Ni katika Sehemu hiyo Rais Kim huweza kuishi huko kwa usalama bila chochote kutoka kwa maadui kuweza kumvamia ama kumdhuru kwa miaka zaidi ya mitatu mfululizo bila kutoka, huku akiweza kutoa maelekezo ya kivita na kiutawala.

    Makazi haya pia yameunganishwa na makazi mengine ya Rais ya Changgyongau huitwa Residence No.26. Makazi haya yote yamewekewa mfumo utakaoruhusu kutumia njia iliyopo chini ya ardhi ikitokea kuna uvamizi. Pia chini ya ardhi kutokea kwenye nyumba hii kuna reli maalumu kwa ajili ya Rais tu na kitu cha kustaajabisha kwa wachambuzi wengi wa masuala ya kiusalama ya peninsula ya Korea ni kuwa reli hii ilitengenezwa kuelekea mahali kusikojulikana.

    Inadhaniwa kuwa mwisho wa reli hii hubadilikabadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika lakini lengo kuu likiwa kuhakikisha kuwa Rais na familia yake wanakuwa salama likitoea shambulio. Mbali na mambo mengine mengi ya kiulinzi na kiusalama, nyumba hii imepambwa sana kwa nakshi, taa na samani nzuri. Nje kukiwa na bustani nzuri na za maua zenye kuvutia, mito na maziwa ya bandia yaliyotengenezwa kupendezesha eneo hili. Hakika makazi haya yalivutia.

    Joe, Habibu na Pius walikuwa wanakuja kuingia hapa kwa mara ya kwanza.

    *******************************************

    “Wananchi wenzangu mlinichangua ili nilete maendeleo na maendeleo ndiyo haya. Nimesema na nimemwagiza Waziri wa Kilimo na Chakula hapa kuwa Sitaki kusikia mkulima yeyote anakatwa tozo eti ya kusafirisha mazao. Mtu hata kuuza hajauza unamkata tozo kivipi? Vibali vya kusafirisha mazao vitolewe bure kama mtu amelima mazao yake kihalali anayatoa shamba anayapeleka mjini ama mkoa fulani kuuza unamwambia alipe, sasa alipe na nini wakati hata kuuza hajauza? Tena sitataka kusikia ukiritimba katika kutolewa vibali hivi.

    Waziri upo hapa unanisikia na viongozi wengine wote hili nalifuta kuanzia leo”, Rais Costa alikuwa akiongea huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi wa Kisasampara, Jimbo la Kengwe alipokwenda kuzindua ghala kubwa za chakula za hifadhi ya Taifa.

    “Tumeanza mazungumzo na serikali ya China na tutaingia nao ubia kutujengea soko kubwa la kimataifa la matunda. Soko letu likikamilika litakuwa la kwanza kwa ukubwa bara la Afrika, hivyo vijana anzeni kujikita kuzalisha matunda. Neema inakuja!” Rais Costa aliendelea huku umati mkubwa wa watu ukimshangilia. Alikuwa ameanza utekelezaji wa ushauri aliowahi kupewa na Joe siku za nyuma namna ya kujadiliana na Rais wa China juu ya kuingiza vijana wa kichina zaidi ya laki moja kuja nchini Stanza kufanya biashara ndogondogo.

    Rais Sylvester Costa alimaliza kuhutubia na kushuka jukwaani na kusalimiana na wananchi wawili watatu kisha kuanza kutembea kuelekea kwenye zile ghala kuzikagua. Alikuwa amefuatana na mawaziri, viongozi wengine wa serikali kuu na ya Jimbo pia alikuwepo na bi. Eliza, mke wa Joseph ambae kwa wakati huo ni Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo ya Stanza. Aliingia akayakagua na kuridhika kisha msafara uliondoka kuelekea kwenye nyumba ya mapumziko ya viongozi wa kiserikali kwa ajili ya mapumziko iliyopo pale Kengwe.

    Wakiwa kwenye nyumba ya mapumziko Rais alipata chakula pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Waziri wa Fedha ambaye ndiye alikuwa Waziri wa zamu kwa wiki hiyo, Gideon, mshauri wa karibu wa Rais Costa na Eliza mke wa Joe.

    “Eliza Watoto wanaendeleaje”, Rais Costa aliuliza. “Wanaendelea vizuri Mh Rais’’, Eliza alijibu pasi kumtazama Rais usoni. “Nimeipata mikakati yako ya kuboresha ufanisi wa benki na hakika taifa lilikumisi sana”, Rais Costa aliendela kuongea huku akikata kipande cha nyama kwa uma na kisu. “Nafurahi kutoa mchango wangu kwa taifa”, Eliza alijibu kishupavu na maongezi mengine yaliendelea. Mara baada ya kumaliza kula Eliza, Waziri wa Fedha na Waziri wa Kilimo na Chakula waliaga na kuondoka kuelekea mahali walipoandaliwa kupumzika.

    “Mh. Umeona wananchi wanavyokupenda? Umesikia walivyokuwa wapiga kelele uendelee kubaki madarakani? Mimi nadhani hata tulivyobadili katiba kuruhusu miula mitatu ya utawala tuliwarahisishia kazi sana”, Gideon alikuwa akimjaza upepo Rais Costa wakiwa pale sebuleni wakisoma magazeti huku wakitazama habari kwenye runinga.



    “Ninaona hapa huyu Kibwe ameanza kupiga kelele juu ya azma yangu ya kubadili umri wa kugombea urais. Ni vyema tukamdhibiti mapema, si mtu wa kubeza, ana ushawishi mkubwa ndani na nje ya nchi. Hawa jamaa wa magharibi watatusumbua tukimwacha aliongelee ongelee”.

    Badala ya kujibu aliloambiwa na Gideon, Rais Costa yeye alimwonyesha habari katika gazeti inayomwonyesha Julius Kibwe, kiongozi kijana na machachari wa upinzani akipinga vikali tetesi za muswada wa kutaka kubadili umri wa kugombea urais uongezwe kutoka miaka 40 mpaka miaka 55.

    “Nitamshauri Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge njia nzuri ya kulipeleka hili, lakini wakati huo huo ni vema wewe ukazidi kuongeza imani na mapenzi kwa wananchi”, Gideon alimjibu Rais Costa.

    ‘’Umetoka kusema kuwa wananchi wananipenda. Hiyo Imani na mapenzi unayoshauri niongeze kwa wananchi ni kwa njia zipi?’’, Rais Costa alimuuliza Gideon akionekana wazi kuwa hajaelewa hilo lingefanyikaje kwani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, pamoja na ukandamizaji wa demokrasia na kufunga wapinzani wake, lakini alianza kuhisi umaarufu wake umeshuka na kwa namna fulani wapinzani wake kisiasa walizidi kumkalia kooni wakimtaka aheshimu haki za binadamu, Sheria na Katiba ya nchi. Aliona kama alichosema Gideon hakiingii akilini kwa hali ya sasa.



    ‘’Tengeneza tatizo kupitia viongozi wa chini yako kisha wewe jiweke mbali nalo, hakikisha kuwa linamgusa kila mmoja au watu wengi, acha watu wapige kelele, wanasiasa waongee, kisha litatue na kulaumu watu wengine aidha kwa kuwataja hadharani au hata kwa kuwataja kwa ujumla tu katika makundi yao, ikiwezekana tumbua baadhi yao. Hii itakufanya wewe uonekane usiye na hatia, tena mkombozi haswa’’, Gideon alijibu na kumfanya Rais Costa kumpa usikivu zaidi na hata kubadilisha mkao.

    “He he he he!”, Kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu, Rais Costa alicheka na kuonekana kuvutiwa na mipango ya Gideon ambayo ingemuongezea umaarufu na kupendwa. Rais Costa alipenda kusifiwa zaidi, hakutaka kusikia mtu anayemkosoa au asiyemuunga mkono. “Tatizo kama lipi kwa sasa?’’, Rais Costa alihoji kutaka kufahamu zaidi kuhusu mpango wa Gideon ambao ulishaanza kumvutia.

    “Leo umetoka kuwafurahisha wakulima, ina maana vijijini tayari umezidi kupendwa kwani tozo hizi zilikuwa ni kero. Lakini ukumbuke kwa kufanya hivi umepunguza chanzo cha mapato kwa halmashauri nyingi hivyo ni lazima tutafute pa kulipia, sasa waite Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Taifa ya Mapato na Makusanyo. Wape maagizo waanze operesheni ya kukamata wote ambao hawajalipa kodi hata kama mhusika biashara yake mtaji ni wa chini ya shilingi laki moja, alazimishwe kulipa kodi kwanza kabla hajaanza bishara kwa kukadiriwa”, Gideon alishauri na kukaa kimya huku akimtazama Rais Costa.

    “Ukweli kuna uliyosema ya msingi hasa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato lakini hili la kulipisha watu kodi hata kabla ya biashara kuanza tena hata wenye mitaji ya chini kabisa sijaliunga mkono. Halina afya kwa mwananchi wa kawaida na tunajiua kiuchumi wenyewe”, Rais Costa alionekana kutoelewa.

    Gideon alicheka sana kisha akamwambia Rais, “Hilo ndio litakuwa tatizo, na baada ya miezi mitatu hivi hadi sita ya watu kupata taabu na Mamlaka za Ukusanyaji Mapato na Kodi na kulalamika sana, utafuta huo utaratibu kwa kisingizo kuwa ni kumkandamiza mnyonge na wewe haupo kwa ajili ya kutesa wanyonge”, Gideon alimaliza.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Rais Costa alimwangalia Gideon kwa sekunde kama tatu akiwa kimya kisha aliangua kicheko kikubwa “Gideon you are a genius”, (Gideon una akili sana). Alifungua chupa ya wine na kuanza kummiminia Gideon.

    ***************************************

    Msafara wa Joe na En uliwasili kwenye makazi ya Rais wa Korea. Rais Kim alikuwa mlangoni akiwasubiri na mara baada ya kushuka walipokelewa. Joe akiwa mbele ya Habibu na Pius alifika mbele ya Rais Kim kwa heshima kubwa, akainama kidogo na kumkabidhi nembo ya Rais wa Stanza (‘The Republic of Stanza’s Presidential Seal’), kama ishara haswa ya ujumbe maalumu wa Rais wa Stanza. “Karibuni sana”, kwa mshangao mkubwa Rais Kim aliwakaribisha kina Joe kwa kutumia Kiswahili. Walikumbatiana na kuelekea chumba maalum kwa ajili ya mazungumzo ya awali na kufikisha ujumbe Rais wa Stanza aliotaka umfikie Rais Kim.



    Walifika na kuketi, Kim akiwa sambamba na En Waziri wake wa masuala ya kigeni huku kina Joe wakiwa wamepewa mkalimani waliulizana habari za hali na maendelo baina ya nchi hizo mbili. Joe alimkabidhi faili maalumu la siri alilopewa na Rais Costa lililo na barua na maelezo ya lengo la ujumbe ule. Hata hivyo maelezo yote aliyaandika Joe.

    Baada ya Rais Kim kupokea faili lile alitoa maelekezo kuwa siku ile ya kwanza wangekutana ujumbe wa Joe na ujumbe wa serikali ya Korea Kaskazini. Joe na ujumbe wake wangeeleza kila jambo lililowapeleka Korea na kisha ujumbe wa Rais Kim ungeenda kutafakari na kisha kukutana nae kutafakari kabla ya kukutana tena wote kwa makubaliano na maazimio kesho yake.

    Ilipangwa kuwa ni ugeni utakaodumu kwa siku mbili wakianza siku hiyo waliyowasili mpaka watakapoondoka. Mara baada ya kupata ratiba hiyo Joe na wenzake walielekezwa eneo la mapumziko na kuachwa hapo watatu wakiwa wamepewa kahawa kama walivyohitaji.



    Joe akiwa na wenzake aliwaambia sasa muda wa kuonyesha vipawa vyao vya majadiliano ya kimataifa umefika. Wakiwa wanajadiliana, Pius alionekana kutotulia kiakili. Suala walilokuwa wamezungumza kwenye ndege lilikuwa likimsumbua sana.



    “Upo sawa?”, Joe alimuhoji Pius. “Hapana, suala lile bado linanitafuna akili nataka kujua ni nani mwingine anafahamu”, Pius alimjibu Joe. Kwa kujua kuwa maongezi yao yaweza kuwa yanarekodiwa ndani ya makazi yale kwa kutumia vinasa sauti vyenye uwezo mkubwa ilikuwa ni lazima watumie maneno machache sana kuzungumza mambo yao au hata kwa ishara. Joe alishajua Pius anazungumzia nini, alijua anataka kujua ni nani mwingine yupo kwenye ule mpango aliowashirikisha wa kumpumzisha Rais Costa nje ya madaraka pasi yeye kutaka kwa hiari kuyaachia.

    Joe aliwaangalia Habibu na Pius usoni. Aligundua kuwa bila kuwafumbulia fumbo hilo wasingefanya vizuri kwenye mazungumzo yao kwasababu akili zao zilitekwa na mpango ambao Joe aliwashirikisha kwa kifupi. “Ok, nitawaambia ili akili zenu mzirudishe hapa. Stanley Macha ni mmoja wapo kwenye mpango huu, mwingine sitawatajia kwa sasa” Joe aliwadokeza kwa kifupi.



    Habibu na Pius walionekana kushtuka. Hawakuamini kama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa nae yupo kwenye mpango huo. “This is serious guys”, (hili suala ni nyeti). Joe aliwaambia huku akiwatazama usoni. “Tutaamini vipi kama ni kweli?”, Habibu alihoji.

    “Nitawapa namba za siri (codes). Sasa kila mtu kwa wakati wake na ikiwa umekubaliana na mpango huu kwa ustawi wa nchi yetu na kuwa mmoja kati ya watakaoleta chachu ya mabadiliko ya kweli, utamtumia Stanley hiyo namba ya siri kwa njia ya WhatsApp nae atajibu kama utakavyomwandikia, na baada ya hapo hamtaendelea na mazungumzo yoyote. Hiyo itakuwa ndio ishara kuwa nimeshawaambia na kuwa tupo pamoja”, Joe aliwaeleza.

    “Tupe hizo codes”. Habibu na Pius walijikuta wakiuliza kwa pamoja. “Ego testor”, Joe aliwajibu (Hili ni neno la kilatini lenye maana ya kuapa/kula kiapo). Haraka Pius na Habibu walitoa simu zao za mkononi kwa shauku kutaka kuhakikisha kile wanachokisikia.



    Waligundua simu zao hazinasi mtandao wowote, wapo ugenini lakini hata kama wangekua wanaweza kuwasiliana kwa wakati ule isingewezekana kwani ukikaribia tu makazi ya Rais Kim mawasiliano yote hukatika na ni mfumo wao tu maalumu wa mawasiliano ambao wanao watu wachache sana ndani ya makazi yale ndio hutumika. Walihema wote kwa pamoja na kutulia.

    ************************************





    Mazungumzo Mazito Yarindima Pyongyang. Timu Ya Joe Na Timu Ya Waziri En Zaonyeshana Ujuzi



    “Gentlemen, it’s time” (Ndugu, muda umefika), Waziri En, anayehusika na masuala ya kigeni na mahusiano ya kimataifa wa Korea Kaskazini aliingia akiwaita Joe na wenzake wamfuate.

    Huku En akitangulia, Joe alifuata na kisha Habibu na Pius. Mara baada ya wote kutoka mlango wa chumba namba 315 ulijifunga lakini ghafla Pius aligundua kuwa amesahau simu yake juu ya meza ndogo ya kahawa iliyokuwa pembeni yake. Simu ile aliitoa mara baada ya kutaka kuwasiliana na Stanley Macha ili kujiridhisha kama kweli kuna mpango wa kumpumzisha Rais Costa nje ya madaraka kabla ya muda wake kuisha. Hivyo alipokumbuka alitaka kurudi ndani ya chumba kwa haraka ili aichukue.

    “Aaaaaaaaaaaaaah”, alisikika Pius akilia kwa nguvu mara tu baada ya kugeuka na kuusogelea mlango ule wa chumba namba 315. Haraka En alitoa ishara fulani na hapo hapo walitokea askari wawili wa usalama kama upepo wa kisulisuli na kumnyakua Pius kumpeleka ambapo Joe hakupafahamika.



    “What’s going on here?” (Nini kinaendelea?), Joe aliuliza kwa mshangao huku akimwangalia En.

    “Relax, it is just a normal security measures that have been taken. He has been exposed to methylbenzene, a chemical substance that is irritants when contacted to an eye, so they have taken him to wash it out and he will join us soon. He should have told me that he was returning to the room, I would have given him security clearance. My apologies for the inconvenience”.

    (Tulia, ni utaratibu wa kawaida wa kiusalama umechukuliwa. Ameingiwa machoni na kemikali iitwayo methylbenzene, ni kemikali ambayo ikikuingia machoni inawasha sana, kwahiyo wamemchukua kwenda kumuosha na ataungana nasi muda si mrefu. Alitakiwa anitaarifu kuwa anarudi kwenye chumba ili nimuombee kibali. Samahani sana kwa usumbufu huu). Alikuwa ni Waziri En akimwelezea Joe nini kimetokea huku wakiingia kwenye chumba cha mkutano.

    ***********************************

    Jengo la makazi ya Rais Kim lilikuwa na ulinzi usio wa kawaida. Katika vyumba na korido zote kumefungwa kamera ambazo zina scan sura yako. Kila mtu aliyepo ndani ya jengo lile hupimwa nyuzi joto la mwili wake pamoja na mapigo ya moyo na sensors zilizofungwa kila kona, hivyo ni kusema joto lako likipanda ama mapigo ya moyo yakipanda ama kushuka kuliko kawaida haraka utaanza kufatiliwa nini kinaendelea kwenye mwili wako.

    Si hivyo tu, ilikuwa hairuhusiwi kuelekea popote ambapo sio eneo lako la kazi bila kutoa taarifa kwenye chumba cha usimamizi (Control room) ili wakupe ruhusa na kuzuia hatua zozote za kiusalama kuchukuliwa dhidi yako la sivyo ni lazima udhibitiwe. Hivyo ni kusema mienendo ya kila mtu ndani ya jengo lile inajulikana kwa kila hatua na kila dakika.

    Katika kila eneo kuna matundu madogo na sensors zinazofatilia lenzi ya macho ya mtu. Matundu hayo hurusha maji ya kuwasha pale tu mtu anapokatiza eneo ambalo hajapewa kibali. Maji hayo hupigwa moja kwa moja machoni kufuatana na mahali unapotazama labda uwe umeyafunga.

    Milango yote hufunguliwa kwa rimoti kutoka chumba cha usimamizi. Hivyo ni kusema kamwe huwezi muona mtu yeyote akifungua mlango wowote na milango yote haina vitasa. Kuta za jengo lile zina unene sawa na mita moja zenye kujengwa na chuma kizito na juu kuweka simenti kali. Kuta na milango yote havipitishi risasi.

    Kitendo cha En, Joe, Habibu na Pius kutoka ndani ya chumba namba 315 kilitoa taarifa chumba cha usimamizi kuwa watu hawa wametoka na wanaelekea chumba namba 441 hivyo kila hatua za kiusalama zilirudishwa kwenye chumba namba 315. Mlango ulifungwa,sensors za maji washa zilifunguliwa na za kupima joto zilifunguliwa kuonyesha kuwa eneo lile halihitaji tena kuwa na joto lolote bila taarifa.

    Kitendo cha Pius kurudi kilasensor ilimdhania ni mvamizi na haraka kuchukua hatua. Mlango ulikuwa umebana na sensor inayofata macho ilifanya kazi na kuruhusu methylbenzenekurushwa moja kwa moja machoni mwa Pius. Ni sahihi kusema kuwa Ryongsong si makazi ya kawaida.

    Wakiwa wameketi, Joe na En pamoja na wajumbe wao walimwona Pius akiingia huku akitabasamu. “This place is crazy”, (Hili eneo ni la ajabu). Pius alimnong’oneza Joe akiwa anaketi upande wa kulia kwake.

    “Gentlemen, my apologies once again, now we can start our conversation. Shall we?” (Ndugu, niwaombe radhi kwa mara nyingine tena na sasa tunaweza kuanza mazungumzo yetu. Au siyo?). Waziri En aliwaalika Joe na wenzake huku akitabasamu. “???” Hwagsilhan (Sawa), Joe alijibu kwa kiKorea.

    Wakati Upande mmoja akiwa amekaa Joe, Habibu na Pius, upande wa pili wa meza alikaa Waziri En, Jenerali Uk In ambae ni Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la Korea Kaskazini na wajumbe wengine wawili. Kikao kilianza.

    ***************************************

    “Tetesi hizi ninazozisikia za chama Tawala kinachoongozwa na Rais Costa za kutaka kubadili umri wa kumruhusu mtu kugombea Urais kutoka miaka 40 mpaka 55 sisi kama wafanya siasa mbadala tunakataa na muswada huo ukija tutaupinga kwa nguvu zote, kwanza haufai hata kuingia bungeni, vuguvugu la kutaka kuruhusu Rais agombee muhula wa tatu tena kwa kipindi kirefu zaidi ya awali lilianza hivihivi’’. Alikuwa ni ndugu Julius Kibwe kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Stanza akizungumza wakati wa mahojiano katika kipindi cha Tarumbeta la Alasiri, kipindi cha Luninga kinachorushwa na stesheni ya MULIKA.

    Akiwa ni miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye mjadala huo akiwemo na Katibu Mkuu wa chama tawala ndugu Stanslaus Kaberege. Wote walikuwa wakimulika hali ya kisiasa na Uchumi nchini Stanza.

    “Kwani shida ni nini”, Stansalaus aliuliza kwa kebehi.

    “Ndugu yangu usijitie upofu kwa sababu upo hapo kutetea maslahi ya tumbo lako. Madhara yapo wazi kabisa katika hii hatua na tunajua lengo la Rais Costa ni kutaka kuminya upinzani katika uchaguzi ujao akijua fika wengi wa viongozi wa upinzani wenye matamanio na nafasi ya Urais watakuwa hawajafikia umri huo hivyo kutaka tupate wagombea wasiojulikana na kupunguza ushindani kwake.

    Lakini la pili, hata ndani ya chama tawala na wewe mwenyewe unajua vijana wengi machachari na wenye uzoefu mkubwa wa uongozi watakuwa hawajafikia miaka 55. Vijana kama kina Habibu alioamua kuwanyamazisha kwa kuwapa ubalozi ni miongoni mwa watu aliowatoa kwenye ulingo wa kisiasa ili kupunguza upinzani dhidi yake hata ndani ya chama chenu”, Kibwe aliongea kwa msisitizo.

    “Unajua ndugu mtangazaji, hata kama tetesi hizi zina ukweli maana nikiri wazi hazijafika kwenye meza yangu, sisi kama chama tunaamini na tunatambua kuwa uRais ni taasisi nyeti inayohitaji mtu aliyetulia kiakili na aliyekomaa, hivyo sioni shida kabisa kama wabunge wakipima wakaona hili linafaa wakaliafiki”. Stanslaus aliamua kujibu kiunyonge kwa kumuelekezea majibu mtangazaji badala ya Julias Kibwe alietoa hoja.

    “Wakati nchi za wenzetu wakifikiri kupunguza umri ili kuwapa vijana nafasi ya kujiamulia hatma ya kizazi chao wewe unatetea kuongeza umri kuwapa wazee watuamulie hatma ya Maisha yetu? Hatutakubali.” Kibwe alionekana kukasirika kidogo na jibu la Stanslaus.

    “Sawa, labda kwa sababu suala hilo ni tetesi tuliache na kwasasa tuangazie uchumi na hatua za maendeleo anazochukua Rais Costa, kwako katibu”, mtangazaji alimrushia Stanslaus swali.

    “Juhudi zinaonekana. Tumeshuhudia mapinduzi makubwa ya kilimo, mapinduzi makubwa ya kibiashara katika bandari yetu. Leo tu Rais ametoka kuzindua maghala makubwa ya chakula na kutoa kodi zote sumbufu kwa wakulima achilia mbali mapinduzi makubwa yaliyotangazwa na benki ya kilimo kuwawezesha wakulima.



    Tumeshuhudia miundombinu ikitengenezwa na mambo mengine mengi. Unajua ubaya wa wapinzani kama kina Kibwe, japo tunaheshimu michango yao lakini huwa hawaoni mazuri serikali inayofanya. Inawezekana ni kwasababu tu hawalitakii mema taifa letu au wana tamaa ya madaraka badala ya kuonesha uzalendo na kuungana na serikali kuwalete wananchi masikini maendeleo”, Stanslaus alionekana kujibu kwa bashasha.

    “Miundombinu gani? Tuache kucheza na maisha ya watu. Hospitalini hakuna madawa wala madaktari, mashule hayana hata matundu ya vyoo, walimu wala madawati. Maji bado ni tatizo halafu mnasimama kusema maendeleo yanaonekana? Maendeleo ya Vitu na siyo maendeleo ya Watu ndugu Stanslaus.



    Unawezaje kujenga uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege jimbo la Nungu kisa tu ndipo Rais alipotokea wakati ungeweza kufanya uwekezaji huo maeneo ya kimkakati ambayo yangekuza biashara za ndani za utalii na usafiri wa anga wa kikanda. Tija ipo kwenye uwekezaji wa kimkakati. Sasa kiwanja kile kimegeuka eneo la Kunguru kufanyia mashindano ya kuruka badala ya ndege, ndege gani itatua kule na ili iweje?

    Mmejenga kituo kikubwa cha sayansi na teknolojia mkijinasibu mnataka Stanza iwe kitovu cha TEHAMA ukanda huu lakini mmewezaje kujenga kituo hicho huku mkijua elimu yetu bado ni tia maji tia maji? Kwanini tusingeanza kuimarisha kuanzia elimu ya msingi kuja juu hivyo kituo hiki kingekuja kuwa na manufaa?”, Kibwe alionekana kuongea mfululizo.

    “Tatizo ni moja tu, ni wewe, sio Rais”, Stanslaus alionekana kujibu tena kwa kebehi.

    “Ndio maana tutahakikisha Rais Costa harudi tena madarakani”, Julias alijibu kwa hasira tena kwa ufupi.

    “Muda wetu unakaribia kufika ukingoni, labda kwa kumalizia ningependa kujua ni kwa vipi na hasa wewe Julius umejipanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya juu ya uongozi wa nchi, na Stansalaus kwa upande wa chama tawala mmejipangaje kuhakikisha vijana wanasimama na kugombea nafasi hii?” Mtangazaji alimalizia kuuliza.

    “Kwanza, chama chetu kina uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa vijana. Tumefanya utafiti na kugundua kuwa kama uchaguzi ungefanyika leo, chama tawala kingepata asilimia 22 tu ya kura katika nafasi ya Urais. Ninachoweza kusema ni kuwa, uchaguzi mkuu ujao hakutakuwa na wizi wa kura ambao chama tawala kimezoea kufanya. Kila kura itahesabiwa.

    Tutaamkia na kulala kwenye kila kituo cha kupiga kura. Huu ni mwisho wa Costa na mabavu yake. Lakini pia tumejipanga kupigana kwa njia zozote zile kuhakikisha kuwa katiba haibadilishwi ili kuzuia wagombea vijana kuwania nafasi ya Urais. Mwambieni Costa kuwa hilo haliwezekani’’, alisema Kibwe akionekana waziwazi kujipanga haswa kwa uchaguzi mkuu ujao.

    “Sisi tumejipanga. Chama chetu ni chama tawala na kitaendelea kuwa chama tawala milele kwasababu kinapambania maslahi ya nchi yetu. Namshauri tu Kibwe na wenzake wamuunge mkono Rais Costa ili tuwaletee maendeleo wanastanza’’. Alihitimisha Stanslaus akionekana kutokuwa na wasiwasi na utawala wa Rais Costa.

    *************************************

    Mazungumzo kati ya timu ya Joe na Waziri En yalikuwa mazito na ya ndani sana.

    “I think the issue of establishing a secured communication system for Stanza should be handled by our Chinese friends who are more technologically advanced than us. Over the last few decades, China has been able to develop the best technology, second to none and they are our very good partners. We also use their technology in our communications. If that is something of interest to you, we can assist you to establish conversation with the Chinese who are also good friends with your country. So, lets put that aside and focus on the military assistance and technology”.

    (Nafikiri suala la mtandao wa mawasiliano salama tuwaachie China. Wao wana teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano na ni marafiki zetu wazuri. Kwa kipindi cha miongo michache iliyopita, wao wameweza kuendeleza teknolojia kubwa ya mawasiliano salama ambayo haina mshindani. Tunaweza kusaidia mazungumzo nao maana hata sisi tunatumia teknolojia yao. Hivyo suala hili tuliweke pembeni kwa sasa na tuangazie suala la msaada wa kijeshi na teknolojia), alikuwa ni Waziri En akiweka sawa majadiliano baada ya kuona suala la masuala ya mawasiliano ni vema wakapewa China.

    Alitoa maoni yale kwa sababu kuu mbili ambazo Joe alizing’amua lakini akamezea. Kwanza ni ukweli teknolojia ya mawasiliano wanayotumia Korea Kaskazini ni muunganiko wa teknolojia ya Uchina kwa asilimia kubwa na Urusi na yao kidogo. Lakini kiufundi, En hakutaka kuharibu wala kuleta sintofahamu kati ya taifa lake na China. China ni chanda na pete na Korea Kaskazini.

    Kwake En aliona si sawa kwa Stanza kuivuka China au kwenda kuongea na Korea kuhusu masuala ya kusimika mifumo ya mawasiliano salama na kuiacha China, ambayo ni mbobevu wa siasa za Afrika na mwekezaji mkubwa.

    En alitaka China ahusike katika mchakato huo. Korea haikutaka iwe katika sintofahamu na China hata kidogo hivyo En alionelea kwa namna moja ama nyingine hiyo iwe ni fursa kwa Korea kuiambia Rafiki yake wa karibu China kuwa kuna jambo tunataka kutekeleza Africa nchini Stanza. En alianza kutabiri mbele kurudi nyuma kwa kuelewa nguvu kubwa itakayoibuka kutoka mataifa ya magharibi mara tu mambo fulani yakianza kutekelezwa na sasa Korea ilihitaji iwe na mshirika mapema.



    Joe alikubali kuwa wajadili kwanza kuhusu rada na misaada ya kijeshi kama ilivyopendekezwa na Waziri En. Waziri En alimwambia wana uwezo wa kuwapa rada zote za kuangazia usalama wa maji, hewa na nchi kavu.

    “Comrade En, our priority is installing AN/SPF-71 generation radar’’. (Kamaradi En tungependa kupata rada kizazi cha AN/SPF-71 kama kipaumbele chetu cha kwanza), Luteni Jenerali Pius aliingilia kama eneo lake la uzoefu.

    AN/SPF-71 ni kizazi cha rada za hali ya juu zenye uwezo wa kunasa aina zote za mawimbi na kwa maeneo yote. Huitwa kwa kizungu three surfaces radar detection, huweza kunasa mawimbi ya makombora ya masafa marefu yatupwayo angani, majini na nchi kavu. Pia kizazi hiki kina mfumo wa kunasa mazungumzo na uwezo mkubwa wa kuingilia mazungumzo mengine.

    “No, that is an outdated generation, we have invented new version, TI/333-A. As our good partners, Stanza will be the first country outside Pyongyang to have such technology.’’ (Hapana, kizazi hicho ni cha zamani, tunacho kipya chaTI/333-A, kwasababu Stanza ni marafiki zetu wa kihistoria, tunaweza kuwapa kama nchi ya kwanza kuwa na teknolojia hiyo baada yetu). Jenerali Uk In Mkuu wa majeshi ya ukombozi wa Korea Kaskazini alidakia.

    Pius hakuamini kama kuna kizazi kingine cha rada chenye uwezo zaidi ya AN/SPF-71. Kizazi hiki alielezwa kina uwezo wa kunasa mawimbi ya rada nyingine mfano ya adui na kuharibu kabisa isifanye kazi tena na uwezo mkubwa wa kunasa mawimbi ya targets mbalimbali kwa wakati mmoja yaani Multi-targets sensors detection.

    “Excuse me, when did this invention happen? Because the latest generation even in the USA, China and Russia is AN/SPF-71.” (Ningependa kujua ugunduzi huu ulifanywa lini kwa sababu hata Marekani, China na Urusi kizazi chao cha mwisho ni kile cha AN/SPF-71). Pius alionekana kushangaa na kutokuamini. Kwa uchunguzi wake alijua hakuna rada zenye teknolojia ya hali ya juu zaidi ya zile za kizazi cha AN/SPF-71ambazo ndio hutumiwa na mataifa makubwa matatu ya Marekani, China na Urusi.

    “You have no idea about the military supremacy of North Korea my friend, it is the very reason why we have managed to keep our country safe over the past 50 years. We develop our technology in utmost secrecy, arguably undetected. TI/333-A is more powerful than any radar generation in this world so far. With it’s Wang-C3NKR series, you can put your three neighbor countries in range all at once. Ha ha ha”.

    (Hujui chochote kuhusu nguvu za kijeshi za Korea Kaskazini Rafiki yangu na ndiyo maana tumeweza kuifanya nchi yetu kuwa salama kwa kipindi cha miaka 50 sasa. Tunaendeleza teknolojia yetu kwa usiri mkubwa, naweza kusema bila kufahamika na washindani wetu. TI/333-A ni kizazi cha rada chanye nguvu kuliko kizazi chochote katika ulimwengu huu. Kwa kutumia toleo lake moja tu la Wang-C3NKR unaweza ukaziweka nchi zako tatu majirani kwenye uzio wako zote kwa wakati mmoja. Hahaha’’. Jenerali Uk In alimjibu Pius kwa majivuno ya kicheko.

    Pius aliendelea kuwapa maombi mengine na kutaka kujua marekebisho yatakuwaje na nani atakuwa anazisimamia. Walikubaliana kuwa wanajeshi kutoka Stanza wangeenda Korea kupata mafunzo lakini zaidi ya hayo marekebisho yote yatakuwa yakifanyika na wa Korea wenyewe.

    Maongezi yaliendelea na sasa walijadiliana misaada ya kijeshi.

    “Well, president Costa is intending to mordenize the military. We require technical trainings backed up with high mordenised military equipments”. (Sasa, Rais Costa anakusudia kuliimarisha jeshi. Katika eneo hili tunahitaji mafunzo ya kijeshi na vifaa vya kisasa kabisa), Joe alitoa maoni.

    “Mr. Joe, there is a lot of highly advanced military equipments that we can offer, but there is one which we think is more interesting and ofcourse unmatched by enemies, nucler weapons”. (Joe, kuna vifaa vingi vya kisasa vya kijeshi tunavyoweza kuwapa lakini kuna hii moja tunafikiri ni nzuri zaidi ya yote, silaha za nyuklia), Waziri En alijibu kwa haraka. Maneno ‘silaha za nyuklia’ iliwafanya Joe na wenzake waangaliane.

    “Mmmh mmmh (Joe alisafisha koo). Comrade En…I don’t think if at all, we can handle such equipments. We can talk about other military equipements, that do not include nuclear weapons”. (En, sidhani kama tupo kwenye nafasi nzuri ya kumiliki silaha za nyuklia. Tuongelee vifaa vingine ambavyo havihusishi matumizi ya nyuklia), Joe alijibu kwa haraka.

    “Are you afraid of America and her allies?”, (Mnawahofia Marekani na washirika wake?) Jenerali Uk In aliuliza.

    “No we are not, but our visit here is rather focused on acquiring a new friend without jeopardizing friendship with others. (Hapana, lakini lengo la safari yetu ni kupata Rafiki mpya bila kuathiri urafiki tulio nao na mataifa mengine), Pius alidakia.

    “You can’t have a friendship with North Korea without jeopardizing some of your other friendships even if that doesn’t include acquiring nuclear weapons from us”. (Huwezi kuwa na urafiki na Korea Kaskazini bila kuathiri urafiki na baadhi ya marafiki zako wengine hata bila kupata silaha za nyuklia kutoka kwetu), Waziri En aliwasisitizia kina Joe.

    “If we take your proposal of acquiring nuclear weapons, how will you support us against pressure from international community, particularly from America?” (Kama tukichukua wazo lenu la kuwa silaha za nyuklia kwenye taifa letu, mnatuhakikishia vipi usalama wetu wakati tutakapoanza kupata vitisho vya kimataifa hasa Marekani?) Habibu alivunja ukimya wake wa muda mrefu.

    “We should be able to ensure that Stanza remain safe against aggression of the West and so-called international community. In fact China and Russia has been secretly looking for an African country that will be able to join the East in balancing the world’s power by acquiring nuclear weapons technology. All you need to do is to escalate your relationship with China and Russia and, potentially India so that you will still be able to remain afloat if they sanction you, but security-wise you will be fine”.

    (Tutawalinda kikamilifu dhidi ya tishio lolote kwa Stanza kutoka kwa magharibi na kinachoitwa Jumuiya ya Kimataifa.Hata hivyo China na Urusi zimekuwa zikitafuta mshirika imara kutoka Afrika atakayekuwa na teknolojia ya Nyuklia ili nchi ziheshimiane duniani. Mnachotakiwa kufanya ni kuongeza mashirikiano ya kiuchumi baina yenu na China na Urusi na labda India pia ili msitetereke kutokana na vikwazo vya kiuchumi vitakavyowekwa, lakini kiusalama mtakuwa sawa kabisa), Waziri En alimjibu Habibu.



    “If I am correct, you haven't provided nuclear weapons to any country so far, we will be the first country in the world to get such a technology from you. So, you claim that you will ensure our country is safe against any aggression. Let us remind you a few things; where is Abdul Qadeer Khan, a Pakistanian nuclear scientist who was exporting nuclear technology to your country, Libya and Iran including centrifuges and consequently caught by Americans in 2004?. What did you do to assist India to clear the 2016 UN allegations that the country through her Technology Institute was giving specialized training on Space Instrumentation to one of your students that lead to the launch of Unha-3 rocket in 2012?”http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    (Kama nipo sahihi, hamjawahi kutoa silaha zozote za nyuklia kwa nchi yoyote, sisi tutakuwa taifa la kwanza duniani kupata teknolojia hiyo kutoka kwenu. Hivyo kama mnataka kutuaminisha kuwa mnaweza kutulinda, mnaweza kutuambia yupo wapi Abdul Qadeer Khan, mwanasanyansi wa nyuklia wa Pakistan aliyekuwa akiingiza teknolojia ya nyuklia hapa kwenu, Libya na Iran na hatimaye kukamatwa na Marekani mwaka 2004? Pia, mlifanya nini kusaidia India kusafisha jina lao mbele ya Umoja wa Mataifa uliotuhumu kuwa kwa kutumia chuo chao cha teknolojia walitoa mafunzo kwa mmoja wa wanafunzi wenu yaliyomsaidia akaongoza timu ya kutengeneza roketi aina yaUnha-3 mwaka 2012?). Habibu alionekana kuwa na taarifa za kutosha na aliuliza maswali mfululizo. Joe alionekana kutabasamu kwa uwezo wa vijana alioambatana nao.



    “About Abdul Khan, he is fine. If you are more interested to know what happened, we can talk to him right now. He was put under house arrest by the then General Perves Musharaf and to correct you, he was never touched by the Americans. Do you know why? I can assure you that you will be fine.

    Abdul was a double-agent, used by both Americans and UK for the same job, we managed to have him work for us while the Americans believed he was their covert asset. When they learned that he is working for us too they reacted, but we managed them.

    About India, after the UN report, what happened next? Have you heard anyone talking about it again? Mr Habibu come on, you are better than that”

    (Kuhusu Abdul Khan yupo salama na unaweza kuongea nae hata sasa kama ukitaka. Alihifadhiwa sehemu salama na aliyekuwa Jenerali Perves Musharaf na kukusahihisha tu hakuguswa na Marekani. Unajua ni kwa nini? Sasa unaweza kuelewa ninaposema tutahakikisha mpo salama.

    Abdul alikuwa akitumiwa pia na Wamarekani na Uingereza kwa kuwapa teknolojia ya nyuklia. Wakati huohuo alifanya kazi na sisi huku wao wakiamini kuwa ni mtu wao. Walipofahamu kuwa anafanya na sisi pia wakachukia na kutaka kumkamata, lakini tuliweza kuwadhibiti.

    Kuhusu India, baada ya ile tariifa ya UN ni nini kilifuata? Kuna yeyote unaemsikia akiiongelea tena. Habibu vipi bwana?). Waziri En alijibu kwa majigambo.



    “Why is it necessary that we agree with you on this matter of nuclear weapons?”, (Kwanini inaonekana ni muhimu sisi kukubaliana nanyi katika suala hili la silaha za nyuklia?), Joe alidakia baada ya ukimya kidogo.

    “Because this is one of the terms and condition of our partnership, along with others that Comrade Kim will suggest after we present our today’s deliberations’’. (Kwasababu hili ni mojawapo ya vigezo na masharti ya msaada na ushirika wetu nanyi, pamoja na mambo mengine ambayo kiongozi wetu Kamaradi Kim atatuambia baada ya kujadiliana nae, nasi tutawaambia kwanini tunahitaji hili liwe miongoni mwa mahitaji yetu), Wazir En alimjibu Joe.



    Joe aliwaangalia wenzake na ilionekana ni vyema wakapewa muda kulijadili hivyo wapumzike halafu wakutane tena baadae kuendelea na mazungumzo. Walikubaliana na kurudishwa kwenye chumba namba 315.

    Walipofika kila mmoja alipumua kwa nguvu. Kila mmoja alikaa kimya kwa dakika chache. Mazungumzo yale yalikuwa nyeti na mazito yaliyohitaji hekima kubwa. Suala la kukubali silaha za nyuklia kwenye taifa la Stanza lilikuwa kubwa. Kwanza sio jambo walilotumwa na lingeleta mtikisiko usio kawaida. Kila mmoja hakuwa tayari kuliingiza taifa la Stanza kwenye mtafakuru na robo tatu ya dunia kwa sababu tu ya kumiliki silaha hizo.



    Waliwaza hivi siku ikatokea Korea wakawasusa itakuwaje? Maswali mengi yalirindima kwenye vichwa vyao. Lakini waliwaza kama hilo ndilo hitaji namba moja la Korea Kaskazini ili waweze kuwapa msaada walioufuata sasa wao wakakataa watarudi kumwambia Rais Costa kuwa wameshindwa? Joe hakutaka kukubali kushindwa.

    Baada ya ukimya wa kama dakika tano nzima kila mmoja akiwa anamtegea mwenzake aanze kuongea Joe alivunja ukimya. “Guys come closer”, (Jamaa, sogeeni karibu). Joe aliwaita wamsogelee.

    ************************************





    Mazungumzo Yakamilika Pyongyang. Rais Costa Ndani Ya Mgogoro Na Askofu Begere





    Rais Sylvester Costa aliwasili Ikulu ya Stanza akitokea jimbo la Kengwe alipokuwa akizindua maghala ya taifa ya kuhifadhia chakula. Akiwa amesikiliza na kufuatilia vyema mahojiano kati ya Julius Kibwe na Katibu Mkuu wa chama chake tawala bwana Stanslaus alikasirika kwa jinsi Julius alivyomshambulia yeye na Serikali yake.





    Akiwa amepokelewa na Stanley Macha na viongozi wengine wakitembea kwenye korido za Ikulu huku akisindikizwa na Gideon na Waziri wa Fedha, Rais Costa alitoa maagizo; “Gideon, mtaarifu Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge kuwa kesho asubuhi anione akiwa na taarifa amefikia wapi kuhusu ule muswada wa kubadili umri wa kugombea uRais.





    Tamara wewe tutaonana mchana kesho, kuna maagizo nitakupa, uje na Mkurugenzi wako wa Mamlaka Ya Mapato na Makusanyo. Macha wewe ukiambatana na Waziri wa Polisi na Magereza mje na mpango mkakati wa namna ya kumdhibiti Julius Kibwe. Ni vyema akadhibitiwa mapema kabla hajawa tishio la kweli. Asanteni”. Rais Costa alimaliza kutoa maagizo na kuwashukuru wote waliokuwa wakitembea nae kuelekea kwenye makazi yake na kisha kuwaaga. Aidan Tamara ni Waziri wa Fedha wa Stanza.



    ***************************************





    “Tunafanyaje hapa?”. Joe alianzisha majadiliano baada ya kusogelewa kwa karibu sana na Habibu na Pius.





    “Kwa sababu hili ni moja la hitaji lao la lazima japo hatujajua kwanini lakini nadhani tukubali ili tufanikiwe. Ni lazima tukubaliane nao, hivyo tuwaambie suala la silaha za nyuklia liwe ni siri kubwa. Lakini ninajua kwa sababu wanajua tuna madini ya Uranium watataka kuzalisha baadhi ya silaha kule kule”, Habibu alidakia.





    “Habibu, hakutakuwa na siri yoyote, Marekani wakijua tuna ushirikiano na Korea ni lazima watakuja kung’amua kuwa tunazalisha silaha za kivita za kinyuklia baada ya muda na watataka ukaguzi wa wataalamu wa kimataifa kama ambavyo wamelazimisha kwa kipindi kirefu kwa Iran’’, Joe alimjibu Habibu.





    “Kwanza nadhani tuwape Korea wawe na ngome yao ya kijeshi Stanza. Hii itakuwa ngome yao ya kwanza nje ya Taifa lao. Ngome hii tuwape kwenye milima ya Usungulilo ambapo ndio tumegundua madini ya Uranium na ardhi ile iwe ni miliki halali ya Korea na hapo ndipo pawe panakaa vifaa vyote vya nyuklia. Hivyo tutamshauri Rais Costa awape haki miliki ya miaka hamsini kwa kuanzia.





    Kwa namna hii tutahakikisha kuwa hata Marekani wakisema tunamiliki silaha hizo tunakana na wakitaka kukagua tunawaruhusu. Tunafahamu kabisa hawatapata na ikiwa watapata Ushahidi wa namna yoyote katika kukagua milima ya Usungulilo, ina maana wanaingilia ardhi ya Korea jambo ambalo halitawezekana hivyo tutakuwa tumeondoa mzigo wa kesi mabegani mwetu na kuuhamishia kwa waKorea”, Pius alichangia.





    “Wataingia kwa nguvu Pius na hiyo ni vita sasa”, Joe alimwambia Pius.





    “Hawataweza labda kama wanataka vita kati yao na Korea. Korea inamiliki makombora ya masafa marefu (Intercontinental Ballistic Missiles) ambayo kwa sasa Marekani yote ipo kwenye uzio wao (within target).





    Wakati Marekani wakiwa wanamiliki Exoatmospheric Kill vehicle (EKV), teknolojia inayotumika kulipua makombora ya masafa marefu kabla ya kufikia tageti, tayari Korea hawa wana Multi-Object Kill Vehicle (MOKV) ambayo haizuii tu makombora yaliyotumwa bali pia yenyewe inazuia na wakati huohuo inatuma kombora muelekeo uleule kombora la adui lilipotokea na kwenda kuharibu chanzo. Hii ni teknolojia ya hali juu kabisa kwa sasa.





    Aidha, ndege ya kishushushu iliyozinduliwa na China yenye uwezo wa kuruka bila kunaswa na rada yoyote na uwezo mkubwa wa kupiga picha kutokea juu sana ni zao la ushirikiano wa Korea na China. Marekani hana ubavu wa kuwasumbua Korea kwasasa”, Pius alionekana kushirikisha uzoefu wa kijeshi.





    “Pius, lazima utambue kuwa kama mapigano haya yakianza ni dhahiri kuwa yanatokea katika ardhi yetu. Je, tungependa tuingie kwenye vitabu vya historia kuwa ni sisi tuliyaleta haya? na Je, haya yote yana tija gani kwa maendeleo na maisha ya watu wa Stanza au ni kukidhi tu matakwa ya Rais Costa?” Joe alionekana kuwa makini sana.





    “Joe, chagua moja urudi umwambie Rais Costa umeshindwa haya mazungumzo au ukubali tuendelee”. Pius alihoji na kusimama. Walibaki na ukimya.



    ************************************





    “Gentlemen, it’s time” (Jamaa, muda umefika), alikuwa ni Waziri En akiwaalika tena waelekee chumba namba 441 kuendelea na mazungumzo.





    Baada ya kupeana muda wa mapumziko timu ya Waziri En ilikuwa imeelekea kuonana na Rais Kim ili kumpa kinachoendelea na yeye atoe maoni yake. Ilikuwa watakapomaliza haya mazungumzo ya awamu ya pili, watapumzika mpaka kesho yake ambapo watakutana wote na Rais Kim kumalizia mazungumzo.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Joe na ujumbe wake ulikuwa ukielekea kwenye mazungumzo bila muafaka na hakuna aliekuwa anajua nini wataongea. Joe alikuwa akitembea huku akiwaza sana. Alichakata akili kuliko wakati wowote katika maisha yake, ni kama mtu aliepewa nafasi atoe hukumu kati ya mauti ama uzima. Pius na Habibu wote walikuwa wakimtegemea yeye. Waliingia na kuketi.





    “We have decided to go on and accept your terms. However, we would like to know more details about it, and whether there are any other demands as a result of your military aid to Stanza so that we can determine if we can meet them or not’’.



    (Tumeamua kukubali sharti lenu lakini tungependa kufahamu taarifa zaidi za sababu ya kutaka silaha za nyuklia ziwepo nchini kwetu, lakini pia tunapenda kujua matakwa yenu mengine ili tuweze kutathmini ikiwa tunaweza kukubali au kukataa). Joe alianzisha mazungumzo yaliyowaacha Habibu na Pius mdomo wazi.





    Waziri En alitabasamu na kisha kumweleza Joe na wenzake kuwa chanzo hasa cha kutaka wawe na silaha za nyuklia Afrika, kwanza ni kutaka kuwa na sehemu mbadala wanapozalisha silaha hizo nje ya nchini kwao kama sehemu yao kimkakati na kiulinzi.





    Lakini pili, wangependa Stanza ndiyo iwe sehemu yao ya kimkakati kupata mashirikiano mengine Afrika kwa maana ya kuzitoa woga nchi za kiAfrika kutokuwa na mahusiano nao na hivyo kuwa kama Ushahidi kuwa hakuna lolote wanaweza kufanywa na yeyote eti tu kwa sababu wana mashirikiano na taifa lao.





    Sababu ya tatu aliyotoa Waziri En ni kuwa Korea wanataka chanzo kipya cha kupata madini ya Urani ambayo ni malighafi muhimu sana kwa utengenezaji wa silaha za nyuklia. Madini hayo usafirishwaji wake ni hatari zaidi kuliko yakiwa tayari yameshatengenezewa silaha.





    Waziri En alienedelea kuwa mahitaji mengine mawili watahitaji. Kwanza, mazao ya chakula na pili wapatiwe sehemu ya mgodi wa dhahabu ili kwa kutumia shirika lao la Mansudae waweze kuchimba na kuitumia kama sehemu ya kunyanyua uchumi wao.





    Joe na wenzake walikubali kwani mazao ya chakula na madini ya dhahabu ni rasilimali ambazo zipo kwa wingi nchini Stanza. Majadiliano ya awamu ya pili hayakuwa marefu na walikubaliana na kuafikiana kukutana kesho kumalizia mazungumzo na Rais Kim.





    Waziri En akishirikiana na Ujumbe wake waliwachukua Joe na wenzake tayari kuwapeleka nyumba watakayolala usiku huo ili wakutane kesho yake. Walitembea kwenye korido kuelekea mashariki kisha waliingia kwenye lifti iliyowashusha chini ya ardhi umbali kama wa mita mia moja, kisha walitoka na kuingia kwenye treni dogo kabisa.





    Ilikuwa ni jambo la kushangaza kidogo kwa Joe. “Where are we going En?” (Tunaelekea wapi En), Joe alishindwa kuvumilia na kumuuliza Waziri En. Waziri En alicheka kidogo na kumweleza kuwa wanaelekea Kangdong Residence, moja ya makazi mengine ya Rais Kim.





    Ni umbali wa mwendo wa kama dakika 6 kwa treni ile ipitayo chini ya ardhi. Ni treni ya umeme na maalum tu kwa ajili ya Rais Kim ama ugeni wake. Katika njia (tunnel) ile Joe alishangaa jambo moja, ni kuwa ipo giza totoro na treni ile hutumia sensor tu na haina dereva.





    En alimweleza kuwa njia ile haiwezi kulipuka hata kwa bomu la nyuklia ni salama kabisa sawa na Rais Kim akiwa kwenye nyumba yake. Alimweleza pia ndani ya njia ile kama ikijulikana kuna hatari basi kunaweza kuachiliwa joto kali lenye uwezo wa kuyeyusha chuma kizito na kukigeuka uji ndani ya dakika tatu. Ilikuwa ni hatari.





    Pius alikuwa akisikiliza hayo maongezi na akilini alikiri kuwa ulinzi alio nao Rais Costa wa Stanza ni sawa na hakuna. Alitabasamu akabaki kimya.





    “You may have thought that the president of America is the most protected in the world, now you know who is. If you want to harm President Kim, he must be the last one alive in this nation’’.



    (Unaweza kufikiri kuwa Rais wa Marekani ndiye anayelindwa zaidi duniani, sasa unajua ukweli ni nani analindwa zaidi. Ukitaka kumdhuru Rais Kim, labda awe ndiye mtu wa mwisho aliyebaki hai ndani ya taifa hili). Waziri En alimalizia kwa majigambo huku wakishuka kwenye ile treni na kuingia kwenye lifti iliyowapandisha juu.





    Walitokea kwenye jengo hilo na kama kawaida kuna watu wachache sana wanaoonekana katika viunga vyake. Walipewa wana usalama wawili watakaokuwa wanawasaidia mahitaji yao. Waziri En aliwaaga, “Don’t worry today, no Methylbenzene here. Ha ha” (Msiwe na hofu, leo hakunaMethylbenzene hapa. Ha ha), En aliwatania kwa kukumbushia kilichompata Pius. Aliondoka.



    ***********************





    “Nimesema wasipewe hili eneo. Waziri hakikisha hili eneo hawalipati, tena na hata lile eneo la Kiberege walipoanza kujenga ile seminari yao wabomoe. Hamfahamu kuwa lipo karibu na mto, sehemu ambayo serikali yangu inakusudia kuweka mradi wa kuzalisha umeme?”. Alikuwa ni Rais Costa akiongea kwa hasira jioni ile huku akimfokea Waziri wake wa Ardhi, ndugu Chaurembo Chalamila Ikulu ya Stanza.





    “Mh. Rais, eneo lile la Kanisa pale Kiberege lipo mbali sana na mto na sehemu yenye maporomoko ya kuzalisha umeme na kuwa halitaathiri mradi. Lakini pia, ujenzi wa ile seminari yao ambayo ni kubwa kuliko zote nchini umekamilika kwa asilimia kubwa. Na eneo hili wanaloomba la Kilungulula kufanya mradi wa hospitali ya kisasa una manufaa kwa wananchi wa eneo lile kwani katika kanda nzima hakuna kabisa hospitali ya rufaa”, Waziri Chaurembo alimjibu Rais Costa kwa unyenyekevu mkubwa.





    “Chaurembo, sidhani kama wewe unajua manufaa ya wananchi kuliko mimi,kwa hiyo usianze kunipa darasa la manufaa ya wananchi hapa. Nimesema eneo wasipewe na ile seminari yao kule wabomoe. Kama waliuziwa eneo lile na serikali za awamu iliyopita iliyokuwa imejaa rushwa, siwezi kuacha kuwapa wananchi wangu umeme kwa sababu eti watu wajenge shule ya kusomea kusali na kupiga cheteso (cheteso ni chombo kinachotumika kufukizia ubani kwenye madhabahu ya kanisa. Mara nyingi kanisa katoliki na yale ya Orthodoxy)





    Hii nchi ina watu zaidi ya wakatoliki. Hata kama ni fidia nitatoa hela za kuwalipa ninazo ila wabomoe waondoke”, Rais Costa alisisitiza kwa hasira.





    “Sawa Mheshimiwa Rais. Nitafanyia kazi maelekezo yote mkuu”. Waziri Chaurembo alijibu huku akiwa ameinamisha kichwa na kuanza kuondoka.





    “Sasa mpelekee Askofu Begere salamu, mwambie aendelee kuhubiri sana kuhusu demokrasia, matumizi ya pesa za serikali na utawala bora. Mwambie akitaka aje agombee uRais kabisa. Mpuuzi!”, Rais Costa alionekana kughadhabika sana.





    Chaurembo alisikiliza akatabasamu na kutoka. Katika hali ile kutia neno ni kujihakikishia kufukuzwa kazi palepale. Rais Costa alifahamika zaidi kwa tabia ya kuwa na hasira za haraka.



    Alifukuza kazi watendaji asiokubaliana nao akiwa sehemu yoyote, katikati ya hotuba, kwenye mikutano ya hadhara na hata katika vikao vya kawaida tena bila kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa kweli walikosea au vinginevyo. Alifanya hivyo kutafuta umaarufu na kuonesha tu mabavu yake kama Rais.



    **************************************





    Damian Begere, Askofu Mkuu wa jimbo kuu Katoliki Peron na mwanashirika wa shirika la Wajesuiti alikuwa kwenye sintofahamu na Rais Costa. Askofu Begere ni kiongozi mwadilifu wa kanisa katoliki Stanza alitambulika sio tu Stanza bali na Afrika nzima kwa misimamo yake isiyotetereka juu ya tawala za kidhalimu, zilizokosa kufuata misingi ya utawala bora, haki za binadamu na matumizi sahihi ya pesa za umma.





    Nchini Stanza alikuwa ni mwiba kwa serikali ya Rais Costa. Ni Askofu asiyeogopa kusema mawazo au kutoa msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali. Asiemung’unya maneno tena mwenye kupenda kusema ukweli. Alijizolea umaarufu na kuheshimika miongoni mwa wananchi wengi wa Stanza. Vyombo vya habari vilipenda kumtumia kama rejeo la masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.





    Askofu Begere sio tu alikuwa na hamasa kwa wananchi wa kawaida Stanza, bali hata katika jumuiya yao ya maaskofu alikuwa na ushawishi mkubwa. Kwanza, ni kwa sababu ya umri wa utumishi katika nafasi ile, lakini pia kwasababu ya ukomavu wa mawazo yake katika masuala mtambuka ya kitaifa.



    Ilikuwa ni vigumu atoe neno halafu lije kukanushwa na Askofu mwingine yeyote hata wale wasio wakatoliki. Aliheshimika sana na viongozi wa dini ya Kikristo na hata dini nyingine.





    Ni katika muktadha huo, Askofu Begere alikuwa na uhasimu mkubwa na Rais Costa. Uhasimu ulichagizwa zaidi hasa kipindi Rais Costa alipoanza harakati za kutaka kubadili katiba iliyomruhusu kugombea tena Urais kwa awamu ya tatu. Lakini na sasa kukiwa na vuguvugu la tetesi za kuongeza umri wa kugombea Urais.





    Isitoshe, yamekuwepo matukio kadhaa ya uvunjifu wa haki za raia na demokrasia lakini lililomgusa zaidi Askofu Begere na Jumuiya nzima ya viongozi wa dini ni kusudio la serikali kufuta kabisa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. Wengi wanaamini kuwa kwa kufutwa ofisi hii, hakutokuwa na anayekagua matumizi ya fedha za umma na hivyo kutoa mwanya wa kukithiri kwa rushwa na ufisadi katika taifa la Stanza.





    Rais Costa na Askofu Begere hawakuweza kupikika chungu kimoja na sasa kwa hasira Rais Costa anatumia mamlaka yake kuhujumu miradi mbalimbali ya kanisa Katoliki anayojua ina mkono na msukumo wa Askofu Begere.



    ************************************





    Usiku wa siku ile hakuna alielala. Japo waliwekwa vyumba tofauti lakini kila mmoja alikuwa akijitahidi kuingia kwenye kichwa cha mwenzake kimawazo. Joe alikuwa akiwaza nini Habibu na Pius wanawaza kwa wakati ule na wanachukuliaje mpango aliowashirikisha .Lakini Pius nae alikuwa akiwaza na kutokuwa na hakika kama je, ni kweli Joe na mipango yake ya kumpumzisha Rais Costa ni hakika ama anapimwa?





    Habibu yeye alikuwa hawazi kupumzishwa kwa Rais Costa bali hatima nzima ya nchi yao kuanza kuzalisha silaha za kinyuklia. Kila mtu kwenye chumba chake alilala akiwa anaangalia juu. Wakiwa na mawazo yale waliendelea kustaajabu uzuri wa makazi yale ya pili ya Rais Kim. Ni katikati ya mawazo hayo walijikuta kunapambazuka bila kupata lepe la usingizi. Hawakuamini.



    ***************************************







    Rais Kim Awaaga Joe Na Ujumbe Wake. Rais Costa Akarahishwa Na Utendaji Wa Waziri Wake





    “Kinyamagoha huwa nakwazika sana na tabia ya mimi kutoa maagizo kisha nianze kufuatilia utekelezaji, ikiwa umechoka niambie nikupumzishe”. Alikuwa ni Rais Costa akiongea na Gambani Kimampala Kinyamagoha, Waziri wa Sheria na masuala ya Bunge wa Stanza.





    “Samahani mkuu”, Kinyamagoha alijibu kwa utaratibu.





    “Suala nililokupa la kuhakikisha muswada unaandaliwa wa marekebisho ya umri wa kugombea Urais umefikia wapi”, Rais Costa aliuliza.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Mkuu, suala hili nilikuwa nafikiria njia nzuri ya kulienenda bila kuathiri hali ya kisiasa ya nchi…”





    “Kinya acha ujinga”, Rais Costa aling’aka kwa hasira na kumkatiza Kinyamagoha kabla hajamaliza kujieleza.





    “Unafikiria suala hili mara tatu tatu kwanini? Hivi nchi hii nani kiongozi?’’, Rais alihoji.





    “Wewe mkuu”, Kinyamagoha alijibu.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog