Search This Blog

Sunday 20 November 2022

VIPEPEO WEUSI: FROM ZURICH WITH RULES - 4

 





    Simulizi : Vipepeo Weusi: From Zurich With Rules

    Sehemu Ya Nne (4)







    Nikarudi sebuleni mezani ambako kulikuwa na ile chupa ya windex niliyoikuta bafuni. Nikaitazama kwa sekunde kadhaa kisha nikakata shauri kwamba nayo niichukue. Nikafungua tena begi na kuiweka ndani.



    Sikutaka kupoteza muda, kwa haraka kabisa nikatoka chumbani humu na kushuka mpaka chini mapokezi.



    "Are you checking out, Sir?" Muhudumu wa pale mapokezi aliniuliza huku akiwa na uso wa mshangao.



    "Yes!" Nikamjibu kwa kifupi tu.



    "Sir, are you sure?" Akaniuliza tena huku akiwa na uso wa mshangao zaidi ambao alikuwa anajitahidi kuuficha. Nilikuwa naongea naye huku nikimuangalia na nikibofya bofya simu yangu. Lakini nilipoona mshangao wake pale usoni ilinibidi niache kubofya simu na kumuangalia kwa makini zaidi.



    "Is there a problem mam?" Nikamuuliza huku nimemkazia macho kwa makini zaidi.



    Nilimuona namna ambavyo alikuwa anajitahidi kuficha uso wake wa mshangao na wasiwasi. Nilianza kuhisi kama kuna kitu fulani binti huyu alikiwa anakijua ambacho kilimfanya ashangae kuona naondoka na awe na wasiwasi huo. Nikamkazia macho zaidi kwa umakini niweze kumsoma anachowaza.



    "Are you ok?" Nikamuiliza baada ya kumuona kama amepatwa na kitete hivi baada ya kujitahidi sana kuficha hisia zake usoni.



    "I am fine, thank you sir..! aah here is your bill, sign here please..!" Alijitahidi kupeleka mazungumzo kwenye muelekeo mwingine lakini bado nilikuwa nahisi wasiwasi na taharuki yake usoni.



    Kwa muda wa kama nusu sekunde tu hivi kwa haraka sana nikamuona ametupa jicho nyuma yangu, kama kuna kitu hivi alikuwa anatazama nyuma yangu lakini hakutaka nijue ni kitu gani. Kwa hiyo aliangalia kwa haraka sana na kisha kurejesha macho pale kwenye 'kaunta' ambako aliniwekea karatasi nisaini kwa sababu nilikiwa natoa fedha tasilimu.





    Nikavuta ile karatasi na kuanza kuandika. Nikajaza haraka haraka na kisha kuingiza mkono mfukoni, nikatoa hela na kumpa…



    "Keep change…"



    "Thank you sir and thank you for staying at……"



    Nikamsikia anaongea kwa mbali lakini akili yangu hata haikuwa inamsikiliza tena. Niligeuka haraka ili nione ni kitu gani hasa ambacho alikuwa ametupa jicho na kukitazama kwa haraka haraka huku akijaribu kuficha nisijue anacho kiangalia.

    Pale mapokezi mbele yake kulikuwa na eneo kubwa la kupumzika. Kulikuwa na masofa makubwa kama sita hivi ya kukaa watu wawili wawili na mawili ya kukaa watu watatu au wanne. Katikati kulikuwa na meza nadhifu ya mbao ambayo ilionekana ilikuwa ghali na adimu. Pembeni karibu na ukuta kulikuwa na 'water dispenser' pamoja na sehemu ya kahawa ambako niliona watu kama watatu hivi, wawili wakitengeneza kahawa na mmoja akichukua maji.



    Kwenye moja ya sofa kubwa kulikuwa na mama pamoja na watoto wake wawili mmoja akiwa amekaa naye kwenye sofa na mwingine amekaa sakafuni akichezea mdoli. Kwenye sofa lingine moja kulikuwa na vijana wawili wa kizungu, mmoja wa kike na wa kiume. Kutokana na walivyokuwa wanaongea kwa kudalizana daliazana ni dhahiri kabisa kwamba walikuwa ni wapenzi.

    Lakini macho yangu yaliganda kwenye sofa lingine dogo la kukaa kama watu wawili hivi lakini lilikuwa limekaliwa na mtu mmoja. Mtu huyu ndiye ambaye mara moja nilihisi kwamba yule muhudumu alikuwa amemuangalia kwa kuibia ibia kwa haraka nisijue.



    Mtu huyu ndiye alikuwa mtu mweusi kati ya wote ambao walikuwa hapa mapokezi. Au kwa usahihi zaidi niseme mimi na yeye ndio ambao tulikuwa watu weusi pekee. Alikuwa kichwani amevalia kofia nyeusi ya 'pama' pamoja na koti jeusi refu ambalo lilifika mpaka chini kidogo ya magoti. Alikuwa ameinamisha kichwa chake akisoma gazeti ambalo amelishikilia mikononi mwake katika namna ambayo nilishindwa hata kuona sura yake. Alikuwa ametulia kimya kabisa kiasi kwamba kama alikuwa haoni chochote cha zaidi pale mapokezi zaidi ya gazeti lake ambalo alikiwa ameinamisha kichwa kulisoma.

    Kwa asilimia zote nikahisi kabisa kwamba huyu ndiye ambaye yule muhudumu alikuwa anamuangalia. Nikaanza kujiuliza ni nani huyu? Au ndiye ambaye alikuwa amepekuwa chumbani kwangu na kisha kufuta alama zake za vidole kwa windex? Anataka nini?



    Lakini kabla ya huko kote swali la msingi zaidi likaninia kichwani, kwa nini huyu muhudumu alimuangalia kwa kificho? Kwa nini muhudumu huyu wa mapokezi alipata taharuki aliponiona nimekuja mapokezi 'kucheck out'? Kuna kitu gani ambacho alikuwa anakijua?

    Muhudumu huyu ndiye yule yule ambaye dakika kadhaa zilizopita niliposhuka kuja kuuliza kama wamesahau windex chumbani kwangu, ni yeye huyu ambaye nilimkuta hapa mapokezi. Kuna nini kilikuwa kinaendelea?



    Nikageuka kumtazama tena yule muhudumu. Kumbe alikuwa ameganda ananitazama muda wote huu… nilipogeuka tu na macho yetu kugongana akalazimisha tabasamu na kisha kugeuka pembeni akijifanya kuendelea na shughuli zake nyingine. Kichwani nilipata kiaisi fulani cha uhakika kwamba muhudumu huyu kuna kitu anakifahamu. Lakini sikuwa na muda zaidi wa kupoteza. Nikabeba mabegi yangu na kutoka nje ya hoteli. Nikatembea hatua kadhaa mpaka barabarani na kuita Taxi.



    "Where are we going Sir.!" Muendesha Taxi akaniuliza kwa tabasamu mara tu baada ya kupanda kwenye Taxi.



    "Just drive..!" Nikamjibu huku macho yangu yakiwa yanaangalia kwenye kioo cha gari cha kutazama nyuma.



    "What?" Dereva akauliza tena huku ananiangalia kwenye kioo kwa sura ya kukereka.



    "Hey man!! Just drive?" Nikaongea kwa kufoka.



    Niliona uso wa mshangao wa dereva akiniangalia kwenye kioo… hakusema chochote, aling'oa gari na kuanza kuendesha. Macho yangu bado yalikuwa yameganda kwenye kioo cha kutazama nyuma nikiangalia pale hotelini nilikotoka.



    Kama sekunde thelathini tu baada ya gari kuondoka pale Hotelini nikiwa bado naangalia nyuma kwa kioo, niliwaona wale vijana wawili wa kizungu waliokaa pale kwenye sofa, wa kike na wakiume ambao walionekana kama wapenzi nao walitoka hotelini haraka haraka wakasimamisha Taxi na kuanza kuja uelekeo huu huu ambao sisi tulikuwa tunaelekea.





    Official Robot: Moyo ukanilipuka, nilihisi kabisa hawa vijana wananifuatilia mimi. Nilipokuwa pale mapokezi sikuwatilia shaka yoyote bali shaka yangu ilikuwa kwa yule jamaa mweusi mwenye kofia ya 'pama' na koti refu akisoma gazeti.



    Dereva alipoendesha gari umbali wa kama dakika moja hivi nikamuamuru asimame. Nilifanya hivi ili nione ile Taxi ya wale vijana nyuma yetu itafanya nini. Ajabu nayo ikasimama kama hatua ishirini hivi kutoka pale tuliposimama sisi.



    "Sir, what's going on?" Dereva aliniuliza kwa wasiwasi.



    "Wait a little bit" niliongea huku nimegeuka nyuma nikiitazama Taxi ya wale vijana ambayo ilikuwa imesimama nyuma yetu kama umbali wa hatua ishirini. Walisimama kwa muda wa kama dakika moja hivi kisha sikujua kwa nini lakini walionekana kubadili mawazo. Nikaona Taxi yao ikiondoka na kutupita pale tuliposimama.

    Haraka haraka nikaingiza mkono mfukoni haraka haraka na kutoa noti mbili ambazo sikumbuki zilikuwa za faranga ngapi, nikamkabidhi dereva na kushuka kwenye Taxi.



    "Keep change!" Nikaongea huku nimeanza kuondoka.



    Nikatembea kwa miguu kurudi kule tuliko toka, hotelini. Sikujua ni kwa nini nilikiwa narudi, lakini akili yangu iliniambia kwamba nirudi hotelini… nilihisi kabisa kuna suala la zaidi ambalo nahitaji kuling'amua.

    Kutokana na kwamba hatukuwa tumeenda mbali sana na Taxi kwa hiyo kama baada ya dakika tano tu nilikuwa nimefika Hotelini. Nikafungua mlango wa mbele na kuingia mapokezi.



    Yule mama mwenye watoto wawili alikuwa pale pale na watoto wake. Pale kwenye kutengeneza kahawa na maji ya kunywa safari hii kulikuwa na mtu mmoja tu akitengeneza kahawa. Ajabu ni kwamba yule jamaa mweusi, mwenye kofia ya pama, na koti jeusi alikuwa amekaa pale pale na katika 'pozi' lile lile akiwa anasoma gazeti.



    Nikageuka kutazama mapokezi. Macho yangu yaligongana na ya yule muhudumu. Safari hii alishindwa kabisa kuficha mshituko wake. Alinitazama kwa mshangao mkubwa aliponiona nimeingia tena hotelini usoni akiwa na taharuki kama vile alikuwa kama vile ameona jini. Nikamkazia macho na kuanza kutembea kwa haraka kuelekea pale alipo. Kila nilivyokuwa napiga hatua ndivyo ambavyo alizidisha taharuki usoni. Akaanza kuniangalia mimi alafu anahamisha macho anamtazama yule jama mweusi mwenye kofia na koti. Ananitazama mimi, kisha yule jamaa. Tena na tena kana kwamba kuna kitu alikuwa anategemea kitokee.

    Nikaelewa kwamba hisia zangu za awali sikukosea, mwanzoni huyu muhudumu alipotazama nyuma yangu alikuwa anamuangalia jamaa huyu mweusi. Nikajiuliza tena, kama huyu jamaa ndiye wa kumtilia shaka, wale vijana wa kizungu walionifuatilia nyuma na Taxi ni akina nani?



    Nikaendelea kupiga hatua kwa haraka kuelekea pale mapokezi. Kila hatua ambayo nilikuwa napiga ndivyo ambavyo nilianza kuelewa ni nini kilikuwa kinaendelea hapa…





    Nikapiga hatua za haraka mpaka pale kwenye meza ya mapokezi.



    Yule muhudumu alikuwa ananikodolea macho kama vile ameona jini.



    "Can I help you sir?" Aliongea kwa wasiwasi huku anajitahidi kuficha wasiwasi alio nao.



    "I need a room!" Nikajikuta nimeropoka tu.



    Mpaka muda huu akili yangu ilikuwa kama vile haifanyi kazi. Nilikuwa sijui hata nifanye kitu gani hasa ukizingatia niko ugenini hapa kwenye nchi ya watu. Nilichokuwa nahisi ni sahihi kukifanya labda ni kujaribu kuwachanganya kama kuna watu wowote wale ambao walikuwa wananifuatilia wasiweze kutabiri 'next move' ambayo nitafanya. Kwa hiyo nilikuwa nafanya mambo hovyo hovyo tu.



    "Excuse me?" Yule muhudumu akaniuliza kwa mshangao zaidi.



    "Can I get a room please?" Nikamjibu kwa kujiamini kabisa.



    "No…aaah no sir we dont have one!" Akajibu kwa kigugumizi huku anaangalia nyuma yangu kila baada ya kuongea neno moja.



    Nilikuwa na hakika kabisa kwamba alikuwa anamuangalia yule jamaa aliyekaa kwenye sofa aliyevalia kofia ya pama na koti jeusi.

    Bado akili yangu ilikuwa inajaribu kupiga hesabu kwa nini muhudumu huyu kila mara alikuwa anamuangalia yule mtu. Lakini nilihisi mambo mawili. Moja, inawezekana kwamba muhudumu huyu alikuwa anajua kwamba yule jamaa ndiye ambaye aliingia chumbani kwangu na kufanya upekuzi na kisha kufuta alama za vidole kwa windex. Au pili, labda jamaa huyu alikuwa amempa onyo fulani la vitisho muhudumu huyu labda ndio maana kila sentesi ambayo alikuwa anaongea alikuwa anageuka nyuma kuhakikisha kwamba haendi kinyume na matakwa ya yule mtu.



    "What? What do you mean? How can you not have a room… I checked out like ten minutes ago!" Nikaongeakwa kukereka huku nimemkazia macho.



    "It has already been taken by another customer… am sorry sir!" Akanijibu huku anajitahidi kulazimisha tabasamu lake la 'customer care'. Lakini japokuwa alikuwa anajitajidi sana kulazimisha tabasamu, wasiwasi wake usoni ulikuwa haufichiki.



    "What? It has been taken? By who?"



    "I am sorry sir but that is non of your business!" Safari hii alinijibu kwa kujiamini walau kidogo. Hata mwenyewe nilijishtukia kwa kuuliza swali la kijinga vile. Lakini bado hasira zangu ziliiuwa hazijapoa. Kuna mchezo hapa ulikuwa unafanyika na huyu muhudumu alikuwa anaujua.



    "What the **** is going on here.!??"Nikamuuliza kwa hasira kwa kunong'ona huku nimemsogezea uso wangu kukaribia kabisa kugusana na uso wake.



    "What do you mean sir?"



    "Well lets see… for staters… who the hell is that guy you are looking at after every two seconds?"



    Tulibakia tumekaziana macho kwa muda wa karibia nusu dakika hivi. Kwa namna fulani nilianza kuona ule wasiwasi ambao nilikuwa nauona awali usoni kwa huyu muhudumu ulianza kuondoka. Sasa hivi ghafla alikuwa na hali fulani hivi ya kujiamini. Hata kile kitendo cha kuangalia nyuma yangu alipo yule jamaa kwenye sofa kila baada sekunde kadhaa sasa hivi alikuwa hafanyi hivyo tena.

    Alikuwa na uso fulani hivi wa kujiamini ambao kwa kiasi fulani ulianza kunifanya nianze kuogopa kuendelea kuongea naye hovyo hovyo.



    Nikageuka kuangalia nyuma yangu pale kwenye masofa ya wateja kupumzika. Yule jamaa mwenye koti jeusi na kofia ya pama hakuwepo!!

    Nikajikuta natabasamu mwenyewe… halikuwa tabasamu la furaha, bali tabasamu la woga na kuchanganyikiwa. Kuna jambo la ajabu sana hapa lilikuwa linaendelea. Iweje huyu muhudumu aanze kujiamini ghafla tu baada ya yule jamaa kuondoka? Alikuwa anamuogopa? Kwa nini amuogope?





    "Sir… i am going to ask you to leave!" Akaongeak kwa kujiamini zaidi nilipogeuka tena upande wake kumuangalia.



    Nikajikuta tu nimeishiwa maneno ya kuongea. Nikabaki namuangalia tu huku naye amenikazia macho. Hapepesi wala kuangalia pembeni. Kuna kitu fulani moyoni kilikuwa kinaniambia kuwa huyu dada alikuwa ni zaidi ya muhudumu. Kuna kitu fulani hivi cha ziada alikuwa. Namna ambavyo alikuwa anajiamini, namna ambavyo alikuwa anaongea kwa mamlaka, namna ambavyo alikuwa ananikazia macho bila kupepesa… kuna hisia fulani nilianzakuipata, kwamba huyu dada alikuwa ni zaidi ya "receptionist".



    "What is going on here?"



    Wote wawili tuligutushwa kutoka kwenye kukaziana macho na sauti ya mtu pembeni yetu. Alikuwa ni jamaa fulani hivi.. mzungu mtu mzima wa makamo kama katikati ya miaka ya arobaini hivi. Alikuwa amevalia suti ya kibiashara nadhifu na miwani ya macho.



    "Who are you?" Nikamuuliza kwa kiburi… bado nilikuwa na hasira kutokana na huu mchezo ambao nilikuwa nahisi ulikuwa unafanyika dhidi yangu hapa.



    "I am the Manager!" Akanijibu kwa tabasamu huku ananipa mkono.



    Nikajifanya kama vile ule mkono alionipa nilikuwa siuoni. Nikamtazama tu kwa hasira na kuanza kung'aka.



    "Ok Mr. Manager… your employee here is dening to give me a room… is that how you do business.!"



    "Is that true Erica?" Meneja akamuuliza muhudumu ambaye sasa nilijua kuwa anaitwa Erica. Alimuuliza kwa mshangao kidogo.



    "No sir that is not true… all rooms have been taken and I was trying to explain that to Mr. Ray here but he doesn't seem to understand…"



    "What…??" Yule muhudumu alikuwa anajitetea kwa boss wake lakini nilimkatisha kwa mshtuko wangu usoni na swali ambalo lilinitoka ghafla pasipo mimi mwenyewe kujua. "What".



    "Sorry sir!" Akaniuliza kwa tabasamu la kufoji.



    "What did you call me?" Nilimuuliza kwa mshangao mkubwa kama vile nimeona shetani mbele yangu. Nilikuwa siamini kile ambacho nilikuwa nafikiria kichwani mwangu. Ameniita 'Ray'??



    "I said your name… aaah you did register here earlier that your name is Rwe…ye…ma…mu Charles! Right?" Alijifanya kulisoma jina langu kwa shida kama ambavyo wazungu wote wanavyopataga shida kulitamka.



    Sikuwa naogopa yeye kulifahamu jina langu. Wala sikuwa naogopa yeye kulikumbuka jina langu kiusahihi licha ya ukweli kwamba ni ngumu mtu kukumbuka tu jina langu ukizingatia kwamba anahudumia mamia ya watu hapo mapokezi kila siku. Kilichokuwa kimeniogopesha ni yeye kuniita "Ray". Ningeelewa kama angeliniita "Rweye" labda ningesema amefupisha. Lakini sio 'Ray'. Ray ni 'nick name' ambayo wananiita watu wangu wa karibu na wale ambao nafahamiana nao vizuri. Huyu muhudumu ameijuaje?



    Nikamuangalia tena. Alikuwa ananitazama kwa jicho fulani hivi la kifedhuli. Nina hakika kabisa na yeye alikuwa amejishtukia kwamba amefanya makosa makubwa kuniita 'Ray'. Amenifanya ning'amue kwamba kuna kitu cha ziada alikuwa anakijua na alikuwa ni zaidi ya 'receptionist'.



    "Sorry sir we can…………"



    Nilimsikia kwa mbali sana yule meneja akiwa anaongea. Tayari nilikuwa nimeshageuka na kuanza kuondoka nikikaribia mlango wa kutoka nje. "Who is she? And what does she want?" Nilijiuliza maswali mwenyewe baada ya kutoka nje ya hotel.



    Kwa muda wa kama dakika nzima nilisimama tu kando ya barabara nisijue nifanye nini hasa. Nilijikuta ghafla tu naogopa hata kwenda kukaa kwenye hoteli nyingine. Nilianza tena kujilaumu huu uamuzi wangu wa kuja Zurich. Ugeni nilio nao ulikuwa unanifanya nisijue hata nielekee wapi au nifanye nini ambacho kitakuwa sahihi.

    "Mr. Ray", nilijikuta kama naisikia tena sauti ya yule muhudumu akitamka jina ambalo wananiita watu wanaonifahamu kwa uzuri na watu wangu wa karibu. Amelijuaje huyu muhudumu. Nikakumbuka tena namna ambavyo alikuwa anajiamini. Nikakumbuka tena namna ambavyo aliniangalia kwa jicho la kifedhuli baada ya kujishtukia kuwa "ameropoka" jina langu ambalo hapaswi kulijua.

    Moyo ulinilipuka.



    Baada ya kufikiria kwa karibia dakika tatu hivu hatimaye nikakata shauri. Sikujua ni kwa nini lakini kuna sehemu moja tu kwa sasa hapa Zurich ambako moyo wangu ulikuwa na amani kwenda.

    Nikasimamisha taxi na kukwea ndani.



    "Hardstrasse!" Nikamuambia dereva taxi mara tu baada ya kukwea ndani.



    Nilikuwa natamani kungekuwa na chaguo lingine la mahala kwa kwenda ambako moyo wangu ungekuwa unasikia amani, lakini hapakuwepo. Japokuwa kwenye lile jengo ninalokwenda sikujua hasa undani wale ni upi zaidi ya nyaraka zinazoonyesha kwamba ni langu kutokakwa marehemu mzee wangu, lakini walau moyo wangu ulikuwa unasikia amani kwenda.



    Kama dakika kumi na tano baadae tayari nilikuwa nimeshuka kwenye taxi na nilikuwa mbele ya mlango wa jengo.

    Namna ambavyo nilikuwa nakokota mabegi yangu usiku huu kuingia kwenye jengo ambalo limetelekezwa muda mrefu nilikuwa naonekana kama kichaa au chokoraa. Ati mimi Rweyemamu Charles, mume na baba wa mtoto… mjasiriamali, na 'kichwa' wa kutegemewa huko nyumbani Tanzania, kama kungekuwa na mtu ananiangalia sasa hivi nikiingia kwenye hili jengo pasina shaka yoyote angeamini kuwa ni chokoraa natafuta 'kambi' ya kulala usiku huu. Nijakuta natabasamu peke yangu na kukumbuka watu wote ambao nilikuwa nikiwaona wakilala kwenye mitaro au nje ya 'fremu' za maduka usiku Dar es Salaam, ni nadra sana kuwafikiria mara mbili baadaya kuwaona… mara nyingi tunadharau tu, "chokoraa hawa" kumbe yawezekana kabisa wako wenye mambo mazito ambayo yamejificha nyuma ya pazia kama leo hii 'chokoraa Ray' na hii hali yangu ninayopitia.



    Niliingia kwenye jengo na moja kwa moja nikaelekea kwenye kile chumba ambacho siku ya kwanza nilijikuta nimeamka ndani yake na baadae kutazama ule ujumbe wa video wa mzee Charles.

    Chumba kilikuwa vile vile kama ambavyo nilikiona mara ya mwisho nilivyokuwa hapa. Nikasimama huku nimejishika mikono kiukoni nikatazama huku na huko pale chumbani kujaribu kuangalia namna gani ambavyo nitalala humu ndani. Lakini kila ambavyo nilikuwa nikifikiria kulala ndivyo ambavyo usingizi ulikuwa unanikimbia.



    Kichwani wazo moja tu lilikuwa linanitesa… Erica, yule muhudumu wa pate Hotelini ni nani? Amenifahamu vipi? Na kwa nini alikuwa anaongea kwa wasiwasi sana kipindi yule mtu aliyevaa kofia ya pama na koti jeusi lakini mara tu baada ya yule mtu kuondoka alibadilika ghafla na kuwa na hali ya kujiamini kwa hali ya juu? Yule mtu mwenye kofia na koti jeusi ni nani? Vipi wale vijana wawili wa kizungu? Nao ni akina nani? Kwa nini nao walikuwa wananifuatilia?

    Hii ndio sababu ambayo ilinifanya hata niogope kwenda kukaa kwenye hoteli nyingine… kwa kiasi fulani nilianza kuwa 'paranoid'. Nilikuwa na mashaka na kila mtu ambaye alikuwa mbele yangu… kila mtu nilimuhisi kwa namna moja au nyingine alikuwa ananiwinda mimi. Kwa hakika nilikuwa nahitaji kutuliza akili ili niweze kung'amua kile ambacho kilikuwa kinaendelea na kubwa zaidi nijue hicho ninachopaswa kujua na kurudi nyumbani Tanzania.



    Siku ambayo nilipanda ndege kuja huku Zurich kwa hakika sikudhani kama kutakuja kuwa na vitendawili namna hii na endapo kama ningelijua basi kamwe nisingethubutu kufunga safari ya kuja huku. Kipindi nakuja niliamini labda nitafika tu na kukabidhiwa kama ni nyaraka au taarifa zote ambazo napaswa kuzipata hapa mara moja na kisha kurejea nyumbani. Lakini tofauti na mategemeo sasa nimegeuka kama swala kwenye msitu uliojaa simba na chui. Kila jani ambalo litatikisika nahisi ni mimi nawindwa kukamatwa.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Nikakitazama kile chumba kwa dakika kadhaa… usingizi haukuwepo kabisa.

    Nikavuta moja ya begi langu na kulifungua na kisha kutoa lundo la zile nyaraka ambazo nilizipata hapa na nyingine nilizopewa na Hudini.



    Nikapekua karatasi kwa karatasi… hakuna chochote kile ambacho nilikielewa zaidi ya mfululizo wa anuani kadhaa, namba za akaunti za benki na baadhi ya majina ya watu. Na kilichofanya kazi ya kuelewa nyaraka hizi kuwa ngumu ni namna ambavyo zilikuwa 'reducted'. Sehemu kubwa za maandishi zilikuwa zimefutwa kwa kuzibwa na wino mweusi. Nilipekua mpaka kuifikia tena ile picha ya mgahawa wa kichina. Nikaiangalia tena na tena kisha nikaendelea kutazama nyaraka zilizokuwa zinafuata baada ya picha hii. Kuna hisia fulani hivi ilikuwa inanijia nilikuwa nimeanza kujihisi kama kuna kitu mimeanza kukielewa hasa hasa nyaraka zilizofuata chini baada ya picha hii ya mgahawa wa kichina. Zilikuwa na uhusiano fulani hivi au mfanano wa baadhi ya vitu.



    Nikaanza kupekua haraka haraka nione ni nyaraka ngapi zilikuwa na huu mfanano. Nilipekua haraka haraka mpaka kufikia nyaraka ambayo macho yangu yalipotua juu yake ilinifanya nihisi moyo unalipuka kiasi kwamba kama ulikuwa unataka kuchomoka kifuani. Ilikuwa ni nyaraka ambayo juu kabisa upande wa kulia ilikuwa na picha ya 'passport'. Japokuwa ilikuwa kwenye rangi ya 'black and white' lakini macho yangu yaliona sawia kabisa ile picha na kuing'amua. Ilikuwa ni passport ya Erica, yule binti wa mapokezi pale hotelini. Chini ya picha hii kulikuwa na maandishi yalisomeka;



    IVANKA WYCLIFFE

    AFFOLTERNSTRASSE 44

    CITYPORT

    POSTFACH 8131

    8050

    ZURICH



    Chini ya anuania hii kulikuwa na maandishi mengine lakini yote yalikuwa yamefutwa kwa wino mweusi.



    Jambo ambalo lilinishitua zaidi ni kwamba anuani hii inafanana kabisa na ile anuani ambayo niliikuta kwenye bahasha ambayo nilipewa na mzee wangu ambayo niliifungua siku ile usiku nyumbani kwangu na kuwa chanzo cha mpaka mimi kusafiri kuja huku… tofauti yake ilikuwa ni moja tu… jina la kwanza la mwenye anuani. Anuani ile kutoka kwenye bahasha niliyoifungua nyumbani iliandikwa;





    HUDINI

    AFFOLTERNSTRASSE 44

    CITYPORT

    POSTFACH 8131

    8050

    ZURICH

    SWITZERLAND.



    Sikutaka kupoteza muda zaidi… nikaanza kupekua nyaraka za chini yake ili nione kama kuna mfanano zaidi na kama nitaweza kuanza kung'amua kitendawili ambacho kilikuwa kinanizunguka tangu nifike hapa Zurich.

    Lakini nikiwa naanza kupekua tu nikasikia kama mlango wa kule nje wa kuingilia ndani ya jengo umefunguliwa. Niliweza kusikia kwa usawia kabisa kutokana na ukimya mkubwa ambao ulikuwa kwenye jengo hili.



    Nikainuka haraka haraka na kutoka ndaji ya chumba. Nikatembea mpaka kufika kwenye korido ambayo inaelekea nje. Ghafla tu hapa koridoni nikakutana ana kwa ana na 'jinamizi'. Ilikuwa ni kama vile nilikuwa usingizini nimeota shetani na hatimaye kuamka na kumkuta amesimama pembeni mwa kitanda.

    Mbele yangu alikuwa amesimama Erica, yule binti wa mapokezi pale Hotelini. Mkononi ameshika bastola. Nilijikuta nainua mikono juu kabla hajasema chochote kile. Uso wake haukuonyesha mzaha hata kidogo, alikuwa anajiamini na aliniangalia moja kwa moja usoni bila kupepesa macho.



    "Give it to me!"



    Akaongea kwa sauti ya upole lakini iliyojaa mamlaka na kujiamini.



    "Give you what?" Nikaongea huku sauti inakwama kwama kama nina kigugumizi. Sikumbuki kama nimewahi kunyooshewa bastola tangu nizaliwe. Licha ya misukosuko yote niliyopitia lakini hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwa mdomo wa bastola kuwekwa mbele ya uso wangu.



    "I said give it me"



    Akaongea tena kwa ufupi tu.



    "I don't understand... give you what?"



    "I am going to ask you one last time… give me the keys!"



    Akaongea kwa hasira na 'kuikoki' bastola kwa kidole gumba.



    "What key are you……??"



    "BAAAAAAAAANNNGG..!!"



    Sikujua ni nini kilitokea lakini nilijikuta nimedondoka chini kwa kishindo kama gunia la mchele. Siku zote nilikuwa nikidhani kwamba ukipigwa risasi kuna maumivu makali unapitia… lakini sijui kama ilikuwa ni mshtuko nilioupata au nini, lakini sikusikia maumivu… kitu pekee ambacho nilikihisi ni baridi kali sana tumboni, kama vile napepewa na kipupwe… mwili ulikuwa unashindwa hata kusogea… nikiwa nimelala pale pale chini nikapeleka mkono mpaka pale tumboni nilipokuwa nahisi baridi kali… palikuwa pamelowa chapa chapa. Nikajipapasa tumbo kwa mkono na kisha kuinua mkono mpaka usoni nione. Kiganja cha mkono chote kilikuwa kimelowa damu. Kitu cha mwisho nilichokiona ilikuwa ni Erica akiniruka pale chini nilipodondoka na kuingia kule chumbani nilikoacha nyaraka. Mwili ukaniishia nguvu na macho yakafunga.







    "…jasho tunalovuja, damu inayomwagika na maumivu yote ambayo tunapitia, ili kumfanya mtu mmoja tu awe na furaha, mtu mmoja ambaye ameufanya moyo wako kuwa dhaifu na kuanguka kwenye mapenzi… kuna muda unajiuliza kama huwa anawaza, kama huwa anakaa chini na kutafakari na kushukuru kwa kafara zote ambazo umezifanya juu yake. Siku zote ambazo haukulala ili tu upate fedha za kutosha kununua gauni lake la ndoto, maumivu yote ambayo umeyavumilia kupambana na adui zake kumuweka salama, namna uhai wako uliuweka rehani ili kufanikisha maisha yenu ya ndoto, damu iliyomwagika kutetea furaha yenu. Je, huwa anakaa na kutafakari na kusikia fahari juu yako? Ubaya nikwamba kafara zote hizi unazifanya pasipo yeye kufahamu, siri ambazo nyingi utakufa nazo moyoni mwako, na siku tu ambayo utakufa siku chache baadae ataanguka tena kwenye mapenzi na mtu mwingine. Je, tukiwa kwenye maisha hayo mengine baada ya kifo, kisha tukatazama chini na kuwaona tuwapendao ambao tulitoa kafara maisha yetu kwa ajili yao, tukiwaona wakiwa na furaha mapenzini na mtu mwingine… ni nini ambacho roho zetu zitasikia? Uchungu wa kuhisi tumesalitiwa au furaha kwa kuwa tuwapendao wanaishi maisha ya furaha huku nyuma tulikowaacha?



    Labda maisha hayahitaji kutafakari sana na kujiuliza… muheshimu Mungu, mpende mkeo na tetea nchi yako. Labda tunapaswa kuishi kwa kanuni hii bila kujiuliza sana italeta matokeo gani.. tunapswa kuishi tu huku tukinuia kuacha alama kubwa duniani ambayo itatufanya tusikie fahari siku tukiwa kwenye maisha mengine baada ya kifo na kutazama nyuma duniani…"







    *****





    Tulikuwa nyumbani kwa Luke yule jamaa ambaye alikuwa na yule chokoraa ambao walinikuta kwenye lile jumba mtaa wa Hardstrasse nilipopigwa risasi.

    Luke alikuwa anakaa mtaa wa Sahilstrasse hapa hapa Zurich.



    Tayari nilikuwa nimemaliza kumsilimulia kila kitu ambacho kimenitokea mpaka kupelekea kupigwa ile risasi tumboni na wao kunikuta pale. Swali moja ambalo bado alikuwa hajanijibu ni kwa namna gani walinikuta pale? Ni nini ambacho wao kiliwapelekea kufika kwenye lile jumba?





    "…nahisi ni muhimu twende hospitali.!" Nilimueleza huku najiangakia tumboni kwenye kidonda kibichi ambako nilikuwa nimepigwa risasi.



    Kwa namna ambavyo hapa kwake kulivyo nilikuwa na mashaka kama ndio nyumbani kwake halisi au ni sehemu tu ambayo alikuwa anaitumia kwa dharura. Ilikuwa ni aina ya chumba ambacho wazungu wanaita 'studio apartment'. Yaani ni chumba kimoja kikubwa sana ambacho sehemu ya kulala, sebule na jiko vyote viko pamoja ndani ya chumba hiki hiki. Lakini sio sababu ambayo ilinipa wasi wasi kama luke alikuwa anaishi hapa au la… ni mazingira ya chumba hiki ndiyo ambayo yalikuwa ynanipa wasiwasi. Hakikuwa na runinga humu ndani, vyombo pale jikoni vilikuwa vimekaa katika namna ambayo ilionyesha wazi kabisa kwamba huwa havitumiwi mara kwa mara. Pia hata kitanda nacho kilionyesha kuwa kimetandikwa nadhifu vivyo kilivyo siku nyingi kidogo.





    "Ukienda hospitali alafu unawapa maelezo gani?" Luke alinijibu huku anaendelea kuchemsha kitu fulani pale jikoni.



    "Nitajificha hapa mpaka lini… pia hili ni tukio la kihalifu nimefanyiwa. Polisi wanapaswa kujua!" Nikamjibu.



    "Na polisi wakishajua utawaeleza ulikuwa unafanya nini pale kwenye lile jumba ulipopigwa risasi?" Luke akanijibu tena bila kugeuka akiendelea kuchemsha kitu pale jikoni.





    Kwa kiasi fulani alichokuwa anaongea kilikuwa kinaingia akilini.





    Nilifikiria mara mbili mbili. Je, niko tayari kuwaeleza polisi nimekuja hapa Zurich kufanya nini? Niko tayari kuwaeleza matukio yote ambayo yametokea mpaka kufikia hatua hiyo ya kupigwa risasi? Na je nikiwaeleza haitavuruga kile ambacho nimekuja kukifanya hapa Zurich?



    Nikahisi ili niweze kufikia lengo ambalo limenileta hapa Zurich ni vyema nikafuata ushauri wa Luke, nisiende polisi wala kuwahusisha kwenye suala hili.



    "Kwa hiyo tunafanyaje baada ya hapa?" Nikamuuliza Luke.



    "Hatua ya kwanza nadhani ni kwenda pale hotelini na kupata taarifa juu huyo binti muhudumu Erica ambaye unasema amekupiga risasi!"



    Luke alinijubu huku anakuja kukaa kwenye sofa karibu yangu na pale ambako nilikuwa nimejilaza. Alanikabidhi kikombe chenye kitu ambacho alikuwa anachemsha…



    "Kunywa hii!"



    "Ni nini?"



    "Chong Ko! Chai fulani ya majani ya kichina… inasaidia kwa ajili ya kudhibiti maumivu na msongo!"



    Nilipokea likombe na kuanza kuchwa chai hiyo yenye harufu kama miti shamba na uchungu wa wastani kama kahawa.



    "Nitahitaji kupiga simu.… sijui una simu humu?" Nilimuuliza huku nikiangaza angaza pale chumbani.



    "Unampigia nani?" Luke aliniuliza kwa mshangao.



    "Relax! Sihitaji kuwapigia polisi… nataka kupiga simu nyumbani Tanzania!"



    "Ile simu ya mezani hauwezi kupiga nje ya nchi… tumia hii simu yangu!" Luke aliongea na kurusha simu kwenye sofa ambalo nilikuwa nimejilaza na kuanzankusimama.



    "Unanipa simu yako hii vipi nikihitaji kikupigia ukiwa umeenda huko hotelini?"



    "Sitachukua muda mrefu… ndani ya nusu saa tu nitakuwa nimerudi.!" Luke aliongea huku anajifunga skafu ya kujikinga na baridi na kuanza kuondoka.



    "Ok.!" Nikamjibu kwa kifupi tu.



    Alipotoka tu nje ya mlango nikaanza kujiuliza tena na tena. Luke ana maslahi gani haswa kwenye suala hili mpaka amelivalia njuga hivi? Japokuwa amekuwa akinieleza kwa fumbo kwamba "kuna deni anayaka kuwalipa Hudini" lakini bado nilikuwa nahisi kuna jambo la zaidi. Kuna kitu kimejificha nyuma ya hili.

    Kila ambavyo nilikuwa nikiwaza ni kwa namna gani Luke na yule Jimmy chokoraa walinikuta pale kwenye lile jengo nilikuwa sipati jawabu.



    "Kuna kitu gani ambacho kimejificha?"



    Nikajiukiza peke yangu kimoyo moyo.



    Nikainamisha tena shingo kuangalia kidonda cha risasi pale tumboni. Nilikuwa nasikia maumivu kwa mbali sasa hivi. Labda na hii chai tiba niliyopewa na Luke ilikuwa imesaidia.

    Nikajikaza kiume na kujiinua kutoka pale kwenye sofa na kuanza kutembea kwa kuchechemea mpaka kwenye dirisha la hiki chumba.



    Nje kilikuwa kumepambazuka na ilikuwa asubuhi murua kabisa isiyo na mawingu. Jua lilikuwa linaangaza vyema nje. Chumba hiki cha Luke kilikuwa kwenye ghorofa ya tatu ya jengo hili tulilomo. Kwa hiyo hapa dirishani ambako nilikuwa nachungulia nilikuwa naweza kuona vyema kabisa huko nje mitaani.



    Nilijikuta nawaonea wivu watu waliokuwa wanapita pita kule chini barabarani kuwahi makazini na kwenye mihangaiko yao.

    Nilijikuta nasikia wivu na kutamani maisha yale… maisha rahisi tu, ambayo hayana siri za kufichua, hayana watu wa kuwatafuta na wala hayana jumuiya ya siri ya kupambana nayo. Ni kwa namna gani maisha hayo yanapendeza. Kuamka tu asubuhi kwenda kwenye mihangaiko na kurejea kwa familia yako.



    "Wengine hatukupata fursa ya kuchagua maisha… tumezaliwa kwenye maisha tuliyonayo!"



    Niliongea mwenyewe kwa sauti ya taratibu huku bado nikitazama nje dirishani. Hii ndio ilikuwa imani yangu siku zote. Kuna baadhi yetu hapa duniani tangu kuzaliwa hatujapata fursa ya kuchagua maisha tunayoyataka. Tumejikuta tumezaliwa tu na tuna maisha ambayo tuko nayo. Usiri, hatari, migogoro na mapambano. Sikuchagua kuzaliwa na kuwa mtoto wa Charles Bernard Kajuna.

    Lakini upande mwingine wa akili yangu ulinikosoa, kwa sababu ilikuwa ni chaguo langu kuja hapa Zurich, hakuna mtu ambaye alinilazimisha. Ni kiu yangu ya kutaka kujua, ni 'curiosity' yangu imenileta hapa.



    "Wengine hatukupata fursa ya kuchagua maisha… tumezaliwa kwenye maisha tuliyonayo!"



    Nikarudia tena ile kauli huku nikiitazama simu ambayo Luke alinipa kiganjani mwangu.



    Nikajiukiza kama nina ujasiri wa kupiga simu ambayo nilikuwa nataka kupiga. Kama nitaweza hata kuongea.



    Lakini sikuwa na jinsi. Nilijihisi kama niko msituni nimepotea. Nilijihisi kama niko mtupu nafsini mwangu. Nilijihisi kama nimepoteza ramani kabisa. Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kunifanya akili yangu ikae sawa sawa na kujihisi nina kila kitu juu ya uso wa dunia.



    Nikabofya namba kwenye simu.



    Nikaweka simu sikioni.





    "Hello.!"



    Moyo wangu ulipasuka niliposikia sauti upande wa pili wa simu. Kwa jinsi ambavyo nafsini mwangu nilikuwa mtupu na jinsi ambavyo nafsi ilikuwa imepotea… sauti hii ya upande wa pili ilipenya mpaka kwenye nafsi yangu kama vile kisu cha moto kinavyopenya kwenye siagi.





    "Hello.!" Nikajibu.





    Japokuwa sikuwa namuona lakini niliweza kuhisi mshituko wake. Hakujua kwamba ilikuwa ni simu yangu na alishituka kusikia sauti yangu.





    "Ray.!" Aliongea kwa sauti ya kinyonge kabisa kama vile anataka kuanza kulia.





    "Cheupe.!" Nilimuita huku nikijikaza na kutabasamu.



    Nilihisi pia tabasamu lake upande wa pili. Kwa miezi kadhaa ambayo tumekuwa na migogoro na Cheupe hata majina yetu ya utani tangu utoto tulikuwa hatuyatamki wala kuitana.



    "Uko wapi Ray.!" Cheupe alijikuta anashindwa aseme nini na kuniuliza swali ambalo alikuwa na jawabu lake.



    "Bado niko Zurich… mwanangu ajambo?"



    "Ajambo! We miss you please come back..!"



    Kwa jinsi ambavyo aliongea niliweza kuhisi majuto kwenye sauti yake. Nilihisi kabisa kwa namna fulani labda anajutia ni kwa namna gaji mgogoro wetu ulianza kutokana na ajira yake.



    "Nitarudi mama… kuna masuala namalizia!" Nikamjibu.





    "Hapana Ray! Nataka kesho upande ndege na kurudi…!" Cheupe aliongea kwa kumaanisha.



    "Siwezi kuondoka haraka namna hiyo kwa sababu…." Nilijishtukia na kushindwa kumaliza sentensi.



    "Kwa sababu gani Ray?" Cheupe aliuliza kwa shauku.



    "No its nothing! Kuna masuala tu namalizia..!" Nikijaribu kudanganya.



    "Hapana Ray! Kwa sababu gani? Nieleze ukweli!!"



    Wakati mwingine ndio ubaya wa mtu kukufahamu kana kwamba kiganja cha mkono wake. Cheupe alikuwa ananifahamu kama mimi mwenyewe ninavyojifahamu. Tayari alihisi kuna changamoto nilikuwa nayo.



    "Nimepata ajali… nina majeraha! Sidhani kama nitaruhusiwa kusafiri.!" Nikaongea kwa upole.



    "Majereha? Ajali? Nini kimetokea Ray?" Cheupe aliongea kwa taharuki.



    "Usijali mama… nitakuwa sawa!"



    "Hapana niambie ni nini kimetokea!"



    "Ah… mh! Nimepigwa risasi tumboni lakini…."



    Sikumalizia hata sentensi yangu nilimsikia Cheupe anaanza kulia.



    "Ray! Please come back! You are losing yourself honey… please come back.!" Cheupe aliongea kati kati ya kilio.



    Kwa mara nyingine tena ni kama kisu cha moto kilipitisha nafsini mwangu. Hakuna kitu ambacho kilikuwa kinanipasua nafsikama kumsikia mkewangu akilia. Tena akilia kwa kosa ambalo sikupaswa kukifanya. Lakini pia aliongea kitu ambacho nilikuwa nakihisi muda wote. I was loosibg myself. Mimejitumbukiza kwenye masuala mazito ambayo sasa yakikuwa yananigharimu. Nilijisikia uchungu. Nilisikia hasira. Nilijihisi kujichukia ghafla.



    "I am so sorry..!" Nilishindwa kusema chochote zaidi. Niliongea kwa kwikwi nikijizuia kulia.



    "Please come back!" Cheupe aliongea huku bado akiwa na sauti ya kilio.





    Kabla sijajibu chochote ghafla nilisikia mlango unagongwa. Ulikuwa unagongwa kitemi isivyo kawaida. Mara moja nafsi yangi ikatambua kuna jambo haliko sawa.



    "Honey! Naomba nikupigie tena baadae kidogo.." niliongea haraka haraka kwa sauti ya chini.



    "What is happening Ray!" Cheupe aliongea kwa taharuki zaidi.



    "will call you back honey!" Niliongea kwa sauti ya chini zaidi.



    "Please take care of yourself… please cone back!"



    Nilishindwa hata kujibu. Mlango ulikuwa unagongwa kwa nguvu sana na kitemi.



    "Nakupenda mkewangu…!"



    Sikusubri jibu. Nikakata simu na kusogea katikati ya chumba kusikiliza kwa makin.





    "NGO NGO NGO NGO.!!"



    Mlango uligongwa kwa nguvu zaidi.



    Ugongaji huu wa mlango ulinifanya nishikwe na hofu ya ghafla. Haukuwa ugongaji wa heri.



    "Who is this?" Nikauliza kwa sauti ya juu.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "It's the police! Open the door!"



    Sauti upande wa pili wa mlango iliongea kwa nguvu.



    Nilihisi kama vile nijirushe na kupiga mbizi sakafuni na kupotea. POLISI.!

    Wameshitukia kilichotokea? Nimekuja kukamatwa au kuna nini la hatari zaidi?



    Sikujua kama nikafungue mlango au niruke dirishani nikimbie? Lakini nitakimbiaje na hiki kidonda tumboni?



    Nikiganda kama sanamu kijasho chembamba kikinitoka ghafla.





    Nilisikia wale watu ambao walikuwa wamejitambulisha kama polisi wakigonga tena.

    Wasiwasi wangu wa kwanza ulikuwa ni kidonda tumboni kwangu, nilikuwa nawaza hawa polisi wakiniuliza kidonda hicho ni cha nini nitajibu vipi? Lakini pia wasiwasi wangu wa pili ulikuwa ni kitu gani hasa polisi hao kimewaleta haswa mahala hapa.



    Sikutaka wagonge sana mlango kwani wangeweza kuingiwa na wasiwasi. Nikijikaza kiume kwa nguvu zangu zote na ujasiri wangu wote niweze kutembea sawasawa bila kuchechemea.



    "…good morning Sir.!"



    "…morning. How can I help you?"



    Niliwasalimia lakini hawakunijibu haraka walibakia kunitumbulia macho tu kisha wakaangaliana. Walikuwa mwanaume mmoja na mwingine alikuwa ni mwanadada. Wote wawili walikuwa wamevalia suti. Nilielewa wazi kabisa walikuwa ni askari wapelelezi



    "Do you live here?" Yule mwanadada aliniuliza huku bado amenitumbulia macho.



    "No, why? Is there a problem?" Nikamuuliza.



    "I am detective Corol Lawrence and this detective Noah Johnson. We would like to ask you a few questions… can we come in?" Yule dada aliongea huku ananionyesha kitambulisho chake cha upolisi.



    "Yes, ofcourse!"



    Niliwakaribisha ndani na haraka nikaenda kuketi kwenye sofa. Sikutaka kujibaraguza kwa kufanya ukarimu wa kuwapa kahawa au kinywaji kama ilivyo desturi ya wazungu. Niliketi haraka ili maumivu tumboni yasinizidie na wakagundua kuwa nina kidonda tumboni yakaanza maswali ya jeraha hilo kimelipataje.



    "How do you know Luke Madison?" Yule mwanaume aliniuliza swali.



    "Ahn! We are friends!" Nilitoa jibu la haraka haraka.



    "Friends like how? You guys live together or….!"



    "Im am sorry detective, you are asking me all these questions but i dont why? What is happening? Why am i being interrogated?" Nikawauliza nikiwa na uso serious. Tayari nilijua kuwa kuna kitu kilikuwa hakiko sawa kwa hiyo kabla sijasema maneno mengine yoyote ambayo yangeweza kunitia matatani.



    "Well, its not an interrogation. Just some routine questions!" Yule dada aliongea huku analazimisha tabasamu.



    "There is nothing 'routine' about this. You guys have come here for a reasons! I want to know why before I answer any more questiins!"



    Niliwaona wanaangaliana na kupeana ishara fulani hivi. Kisha yule mpelelezi mwanamke akaongea.



    "Luke is dead!"



    Nilihisi kama sijasikia vizuri au labda sikumuelewa.



    "What? What did you just say?" Niliongea kwa mshituko mkubwa usoni.



    "Luke is dead?"



    Mpelelezi mwanamke, Carol alinijibu tena. Nilitamani kama vile wawe wananitania tu. Inawezekana vipi? Luke ameondoka hapa kama nusu saa tu iliyopita.



    "How? What happened?" Niliuliza nikiwa bado kwenye mshituko.



    "He was shot few minutes ago!" Akanijibu tena huku amenikazia macho nahisi akitaka kuona mwitikio wangu usoni.



    Nilijiinamia uso viganjani kwa sekunde kadhaa. Wao walidhani labda nilikuwa nasikitika kwa taarifa hii ya msiba, lakini kichwani mwangu kulikuwa na kitu kingine kabisa kinapita. Nilikuwa nawaza kama kuna uwezekano wa aliyenipiga risasi juzi usiku, Erica… kuwa ndiye huyo huyo ambaye alikuwa amempiga risasi Luke. Kuna upande fulani wa akili yangu ulikuwa unataka niwaambie maaskari hawa kuhusu tukio ambalo lilinitokea, lakini moyo wangu ulikuwa unasita kabisa kuwapa taarifa hii.



    "Where did this happen?" Nikawauliza kwa sauti ya unyonge.



    "Freacht West Street…!"



    Wakanitajia mtaa ule ule ambao kuna hotel ya Radisson Blu ambayo nilifikia nilipoingia hapa Zurich. Luke pia alipoondoka hapa tulikubaliana aende hotelini pale ili kupata taarifa juu ya yule binti muhudumu Erica ambaye alinipiga risasi.



    "Sir, if there is any information that can help us we will be happy to hear it!"



    Kichwani nikajiuliza ni kitu gani hasa niwaambie? Niwaeleze ukweli? Je, sitaingia matatizoni kwa kuwaeleza ukweli na lengo langu la kuja hapa Zurich kuvurugika? Hapana siwezi kuwaambia ukweli…



    Ilibidi nitunge uongo usio na kichwa wala miguu lakini wenye kuweza kuaminika.

    Kwanza niliwadanganya jina langu3… niliwaelezankuwa naitwa "Jimmy Adekela", asili yangu ni Nigeria lakini naishi hapa Zurich kwa mwaka wa pili sasa. Kwa hiyo sikuwaeleza ukweli kwamba mimi ni Mtanzania ambaye nimeingia hapa Zurich siku chache tu zilizopita.

    Nilijua kwa ujio wao huu wa haraka haraka hawawezi kunibana sana kwa maswali labda waseme wananikamata na kunipeleka kituoni, lakinj uzuri hawakuwa na sababu ya kunikamata. Japokuwa kama nikiwaeleza uongo na baadae wakigundua kuwa nimewadanganya lazima wanisake ili kunikamata na kunihoji ili kufahamu najua nini kuhusiana na kifo hicho cha Luke.



    Nilikata shauri kichwani mwangu niwadanganye, siwezi kuwaeleza ukweli… nikawaeleza kwamba Luke ni rafiki yangu wa muda mrefu tu na mimi nilikuwa nimekuja hapa kumtembelea jana usiku na ndio maana ilinibidi kulala hapa. Asubuhi ya leo aliniaga kwamba anatoka kwa muda mfupi tu na atarudi baada ya dakika chache lakini badala yake ni wao wamekuja kunipa taarifa kwamba amepigwa risasi.



    "…can you think of anyone who might want to kill him? Anyone… an enemy or someone who may be had a fight with a few days ago… anyone?"



    Yule mpelelezi wa kiume, Noah aliniuliza.



    "No.! I dont think if there is anyone who would want to kill Luke… he was a very good guy!" Nikadanganya tena.



    "Ok sir, we would like to talk to you again later, but thats it for now… thank you sir!"



    "No problem.!"



    "If you remember anything, please give us a call… this is my number..!"



    "Thank you!"



    Walinipatia 'business card' nikaipokea na kuiweka mfukoni. Wakafungua mlango na kuondoka.



    Nilivuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Sikuamini kama hatimaye wameondoka. Lakini huu haukuwa mwisho… hawa wanaonekana ni wapelelezi wazoefu, lazima watakuwa wamegundua kwamba kuna jambo nilikuwa naficha. Wameamua kuondoka kana kwamba hawanitilii mashala ili 'nirelax'. Hawataki niingiwe na wasiwasi kisha nikakimbia. Lazima wanaenda kuhakiki taarifa nilizowapa kabla hawajaja kunikamata rasmi wakigundua uongo niliowaeleza. Huu ulikuwa ni muda wa kufanya maamuzi ya haraka kabla sijachelewa.



    Nikafunua shati nililovaa kutazama kidonda changu ambacho kimefungwa bandeji. Kilikuwa kiko sawia.



    Nikaelekea mpaka karibu na kitanda ambako kulikuwa na mabegi yangu. Nikaanza kuyaburuza na kuondoka.



    Sikutaka kupitia mlango rasmi wa mbele ya jengo au kutumia lifti. Nikihofia ningeweza kukutana na askari wale ambao wameondoka muda huu. Au labda wameacha mtu nje kunichunguza nyendo zangu.

    Nikaburuza begi langu na kushuka ngazi taratibu kuelekea mlango wa nyuma wa dharura. Kutokana na kuhofia kutonesha kidonda tumboni ilinibidi kutembea taratibu sana na kwa tahadhari. Ilinichukua karibia dakika kumi nzima mpaka kutokea kwenye mlango wa nyuma wa dharura. Nikasogea mpaka barabarani na kuita Taxi.



    "Freacht West Street… Radisson Blu Hotel!" Nilimuelekeza dereva taxi kisha aling'oa gari na kuondoka.



    Katika ambao nilitakiwa kuwa makini kupitiliza basi ulikuwa ni huu. Nilikuwa kwenye nchi ya kigeni na tayari kulikuwa na kila dalili ya kuingia kwenye matatizo makubwa na vyombo vya usalama. Hiki kilikuwa ni kitu cha mwisho ambacho nilikuwa sitaki kitokee. Tayari nina adui asiyejulikana ambaye alikuwa ananiwinda. Sihitaji tena kuingia kwenye uadui na vyombo vya usalama.

    Pia kila nilipokuwa nafikiria hii taarifa juu ya Luke kupigwa risasi nilikuwa siishi kujiuliza kama ni yule mwanadada Erica ndiye anayehusika. Nilijikuta tu natamani kufika pale hotelini ili kujionea walau kwa macho yangu ni nini hasa ambacho kilikuwa kinaendelea.



    Kama dakika saba baadae tulikuwa tumeingia mtaa wa Freacht West. Nilimuelekeza dereva apaki gari upande wa pili wa barabara mkabala na Radisson Blu Hotel. Nilikuwa nataka kuona kile ambacho kilikuwa kinaendelea pale hotelini lakini sikutaka kufika kuhofia kutambulika na pengine kuingia kwenye matatizo zaidi. Hapa tulipopaki upande wa pili wa barabara nilikuwa naweza kuona vyema kabisa kile ambacho kilikuwa kinaendelea.



    Nje ya hoteli pembeni karibu na mlangoni, kulikuwa kumefungwa utepe wa njano wa polisi kuashiria kwamba hiyo ndiyo 'crime scene'. Ndipo mahala ambapo Luke alipigwa risasi.

    Kulikuwa na kama polisi watano hivi wenye sare ambao walikuwa eneo hili. Pia kulikuwa na watu wawili ambao walionekana ni watu wa 'forensic' mmoja akiwa anapiga picha lile eneo sakafuni na mwingine akiwa kama anapima vitu fulani hivi pale chini.



    Pembeni nje ya ule utepe kulikuwa na raia kadhaa wasiozidi kumi na tano wamesimama wakishangaa. Nilimuona moja ya askari akiwa anachukua maelezo ya meneja wa Hoteli, yule jamaa ambaye juzi alinikuta mapokezi nabishana na Erica na kunitaka niondoke.

    Nikapepesa macho yangu kutazama watu walioko pale wakishangaa. Moyo wangu ulipasuka ghafla nilipomuona moja ya watu ambao walikuwa eneo hili. Katika lile kundi la raia ambao walikuwa wamesimama wakishangaa alikuwepo yule jamaa anayevaa kofia ya 'pama'. Yule jamaa mweusi ambaye juzi hapa hotelini alikuwa ameketi kwenye moja ya sofa za pale mapokezi anasoma gazeti. Jamaa ambaye Erica alikuwa anaongea na mimi huku anamwangalia kwa kuibia ibia kana kwamba anamuhofia hivi. Ni yule jamaa alikuwepo tena mahala hapa kwenye kundi la raia wanaoshangaa.



    Tangu juzi sikuweza kumuona sura yake kutokana na kofia lake la pama. Na hata leo hii muda huu pia sikuweza kuona sura yake. Lakini nilikuwa na hakika kwa asilimia mia moja kwamba alikuwa ni yeye. Kofia yake ile ile ya pama kubwa kiasi ya rangi ya kijivu. Koti lake jeusi refu lenye kufika mpaka usawa wa magoti na kuvuka chini kidogo. Mkononi ameshikilia gazeti. Hakika sikuwa nakosea. Alikuwa ni yeye. Alikuwa anatazama kinachoendelea pale kama vile watazamaji wengine.



    "Ni nani huyu mtu?" Nilijiuliza mwenyewe kichwani.



    Nikiwa najiuliza hivu maswali kichwani… ghafla! yule jamaa akageuka na kutazima upande wetu, hapa taxi ilikopaki. Ubaya ni kwamba nilikuwa nimeshusha dirisha chini kidogo ili niweze kuona kwa usawia. Nilijikuta macho yangu na yake yanagongana. Kijasho kilianza kunitoka huku nahema kwa nguvu. Tulikaziana macho kwa takribani sekunde thelathini nzima. Sasa ndio nilipata wasaa wa kumuona vyema. Upande wa kushoto usoni alikuwa na kovu kubwa kana kwamba aliwahi kupata jeraha kubwa la kukatwa na kitu.



    "Namjua huyu jamaa.!!"



    Ndilo wazo la kwanza ambalo lilikatisha akilini mwangu. Nilikuwa na hakika kwa asilimia mia moja kwamba huyu mtu namfahamu. Nimeshawahi kumuona hapo kabla siku za nyuma kabla ya hapa hotelini. Kovu lake hili ndilo haswa lilinipa uhakika kwamba namfahamu huyu mtu. Lakini sikuweza kukumbuka ni wapi. Akili ilikiwa inashindwa kutambua ni wapi haswa niliwahi kumuona. Lakini kwa hakika kabisa kumbukumbu yangu iliniambia huyu mtu namfahamu.



    Nilimkazia macho. Sikupepesa hata kidogo japo nilikuwa nimekumbwa na woga wa ghafla moyoni mpaka jasho linanitoka.

    Taratibu nikamuona anageuka na kuendelea kushangaa kule kwenye eneo la tukio.



    Nikamuamuru dereva tuondoke.



    "Hardstrasse.!" Nikamuelekeza kwa kuelekea.



    Ndio. Hardstrasse. Ndio mahala pekee ambako kwa sasa nilihisi palikuwa sahihi kwangu kwenda. Siwezi kukaaa tena hotelini. Itakuwaje kama Polisi wakinishuku kuwa nimehusika na mauaji ya Luke na picha yangu kusambazwa? Nimewadanganya kila taarifa ambayo nimewapa. Wakigundua uongo huo wana kila sababu ya kunishuku kuhusika na mauaji hayo. Kwa hiyo nahitaji kukaa mbali na maeneo ya umma.

    Lakini huku Hardstrasse ambako tunaelekea kwenye lile jumba ndipo ambako nimepigwa risasi juzi na kuokotwa na kina Luke. Lakini uziri wake polisi walikuwa hawaifahamu hii sehemu. Kwa hiyo hata wanitafute vipi hawaezi kujua ni wapi watanipata.



    "This time I fight back.!'



    Nilijipa moyo. Kwamba ikitokea nikishambuliwa tena safari hii nitapambana.

    Huu si muda wa kujiuliza maswali tena. Nimejiuliza maswali ambayo kila muda yaninipa maswali na vitendawili vingine. Huu ni muda wa kutafuta majibu.

    Sihitaji tena kujificha mbali na adui ambaye ananiwinda. Huu ni muda wa kupambana. Kupambana mpaka nipate jawabu la kile kilichonileta hapa Zurich.



    Nilikuwa nahema kwa nguvu kana kwamba nimepandwa na maruhani. Maruhani ya ushari na kupambana. Nilijikuta hofu yote imeniondoka. Kitu pekee ambacho kilikuwa kimeujza moyo wangu sasa hivi ilikuwa ni hasira.



    "I need a gun!" Niliwaza moyoni huku bado nahema kwa nguvu.



    Nilidhamiria kupambana sasa. Nilidhamiria kupata majibu.







    Nilikiwa nimefika kwenye lile jumba mtaa wa Hardstrasse karibia masaa manne yaliyopita. Muda wote huu nilikuwa nachambua lundo la nyaraka nilizonazo. Kuanzia zile ambazo nilizipata kwenye bahasha aliyoniachia mzee wangu mpaka zile ambazo nilizipata kutoka kwa Hudini.



    Kama mara zote zilizopita, nyaraka hizi zilikuwa hazieleweki kabisa. Zilikuwa na mfululizo wa anauani pamoja na majina ya watu na namba za akaunti za benki pamoja na kumbukumbu za miamala. Wingi wa nyaraka hizi ulikuwa unanifanya nishindwe hata kuweka kipaumbele nianze kufuatilia anuani ipi, au jina lipi au anuani ipi kwanza kabla ya nyingine. Walau ingekuwa orodha yenye vitu vichache ningeweza kusema nifuatilie kitu kimoja baada ya kingine mpaka nipate jawabu. Lakini lundo hili la nyaraka na orodha ndefu namna hii ilikuwa inanifanya nishindwe kufanya maamuzi ya wapi hasa nianzie.



    Lakini nikiwa katika mkanganyiko huu kuna jambo moja ambalo nilihisi lilikuwa dhahiri mbele yangu ambalo walau nilikuwa naweza kuanza kuanzia. Ilikuwa ni ile anuani. Anuani ambayo niliikuta kwenye bahasha ambayo nilipewa na mzee wangu ikiwa na jina la Hudini lakini pia anuani hiyo hiyo nilikuja kuikuta kwenye nyaraka nikizopewa hapa Zurich ikiwa na jina picha ya Erica lakini jina tofauti la kike.



    IVANKA WYCLIFFE

    AFFOLTERNSTRASSE 44

    CITYPORT

    POSTFACH 8131

    8050

    ZURICH



    Anuani hii ilikuwa inarandana kabisa na ile ambayo nilikuta ndani ya bahasha niliyopewa na mzee wangu.





    HUDINI

    AFFOLTERNSTRASSE 44

    CITYPORT

    POSTFACH 8131

    8050

    ZURICH

    SWITZERLAND.



    Tofauti ikiwa jina la kwanza tu.



    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Nikakata shauri kichwani mwangu kwamba hii ndio anuani ambayo natakiwa kuanza nayo kwa sababu katika lundo la nyaraka hizi na orodha ya majina, akaunti, miamala na anuani zote zilizopo hapa, ni anuani hii tu ambayo mara moja iliamsha udadisi ndani yangu. Nyingine zote sikuzielewa.



    Nikachukua simu yangu na kufungua upande wa utafutaji wa ramani. Nikachagua mji wa Zurich. Nikatafuta mtaa wa Affolterntrasse 44. Nikaupata. Nikatazama umbali ulipo kutoka hapa mtaa wa Hardstrasse. Nikaona ni mwendo wa kama dakika kumi na tano hivi kwa gari.



    Nikatazama saa kwenye simu. Ilikuwa saa tisa kasoro mchana.



    Huu haukuwa muda mzuri kwangu kuzurura mitaani. Bado sijajua kama wale wapelelezi kama wameshang'amua taarifa za uongo ambazo niliwapa. Kwa hiyo sikutaka kujiweka kwenye matata kirahisi rahisi. Ni vyema nisubiri. Ndio, ni vyema nisubiri giza liingie kisha nianze kuchanja mbuga kufuatilia hii anuani.



    Nikainua shati kutazama kidonda tumboni. Bado kilikuwa kwenye hali nzuri, lakini nahitaji baada ya muda fulani kubadili bandeji kwenye hiki kidonda. Ubaya ni kwamba siwezi kwenda hospitali. Hivyo nahitaji kuchakata akili haraka nifanye nini kuhusu huduma ya kidaktari juu ya hili jeraha.



    Nilikuwa na karibia siku mbili sijapata usingizi wa uhakika. Nikakata shauri muda huu ambao nasubiria giza liingie ni vyema niutumie kupunguza lundo la usingizi nilionao kichwani.



    Nilijisogeza mpaka pembezoni mwa ukuta. Nikafungua begi langu na kutoa nguo kadhaa. Nikazikunja vyema na kuziweka sakafuni na kisha kulalia kama mto.



    Nililala chali macho nikitazama juu. Mawazo kadha wa kadha yalikuwa yanapita kichwani.

    Sikuwa salama nje mitaani kwa kuwa naweza kukumbuna na polisi ambao nilikuwa na hakika kabisa kwamba walikuwa wananitafuta muda huu. Lakini pia siko salama mahala hapa kwa kuwa ni siku mbili tu zilizopita nilipigwa risasi humu humu ndani ya hili jengo.





    Nahitaji kujilinda. Nahitaji kupambana kama nitakabiliana na hatari kwa mara nyingine. "I need a gun.!"



    Nikiwa bado nimejilaza vile nikaanza kutafakari kuhusu jengo hili. Kuna nini kwenye floor za juu? Nimekuwa nikifika hapa kwa mara kadhaa sasa lakini bado sikuwahi kupandisha floor za juu. Kuna kitu gani hasa huko juu?

    Kwa nini pia mzee Rweyemamu alinunua hili jengo? Alilinunua kutoka kwa nani? Lazima kutakuwa na sababu mahususi ya yeye au wao kununua jengo hili. Nahitaji kufahamu kwa nini.



    Nikiwa kwenye huku kuwaza na kuwazua na kujiuliza maswali usingizi ukanipitia.





    ******



    Sikuwasikia wakiingia au mlango kufunguliwa. Nilishangaa tu ghafla walikuwa mbele yangu au tuseme juu yangu kwa ufasaha zaidi.



    Nilikuwa bado nimejilaza sakafuni, wao walikuwa wamesimama wakinitazama. Walikuwa ni yule mzee wa Hudini, Erica na Luke.

    Nilijihisi kama nimeona jini nilipomuona Luke akiwa hai, mzima na salama bin salmin ananitazama.



    "Luke? You are alive?" Nikatahamaki.



    Hakujibu chochote. Alitabasamu tu. Lilikuwa ni tabasamu la kifedhuli ambalo halikuashiria kheri mbele yangu.

    Nikamuona yule mzee wa Hudini akimgeukia Erica na kumpa ishara fulani hivi kwa kumkonyeza.

    Nikamshuhudia Erica akiingiza mkono kwenye mkoba wake wa mokononi na kutoa bastola na kuninyooshea. Aliielekea usawa wa kichwa.



    Naamini alikuwa anaona uso wangu wa woga na wasiwasi na ilikuwa inampa furaha nafsini mwake. Alitabasamu huku yule mzee wa Hudini na Luke wakitoa vicheko vya kifedhuli.



    "Goodbye Ray!" Aliongea kwa sauti kali ya kunong'ona ikiashiria ukatili ulioko nafsini mwake.

    Akafyatua risasi. "BAAAANNNGGG.!!"





    "Nooooooo.!!"



    Nilishituka kutoka usingizini jasho likinitiririka kama nimemwagiwa maji. Nilikuwa nahema kwa nguvu nikitazma huku na huko. Ilikuwa ni ndoto tu lakini ilinifanya nisikie hofu kana kwamba nilichokiona kilikuwa ni kitu halisi kinanitokea.



    Nikachukua simu na kutazama muda. Ilikuwa ni saa mbili na dakika tano usiku. Nilikuwa nimelala kwa zaidi ya masaa manne.



    Nikainuka na kuanza kukushanya makaratasi yangu vyema pale safuni ambayo nilikuwa nayafanyia uchunguiz awali na kuyarejesha kwenye begi. Nikazikunja vyema zile nguo nilizozilalia na pia nazo kuzirejesha kwenye begi.



    Nikainuka na kuanza kuondoka. Ulikuwa ni muda sasa kufuatilia ile anuani mtaa wa Affolterntrasse.



    Sikujua ni kwa nini lakini kidonda tumboni kilikuwa kinaanza kuniuma. Nilikuwa nahitaji daktari wa kukitazama haraka lakini sikujua ni nini hasa napaswa kukifanya. Nikajikaza kiume na kutembea mpaka nje ya jengo mpaka barabarani.



    "Affolterntrasse 44."



    Nilimuambia dereva taxi baada ya kusimama na kukwea ndani.

    Ilituchukua karibia nusu saa nzima kufika mtaa wa Affolterntrasse tofauti na ambavyo nilikuwa nimekadiria awali.



    "Keep change.!"



    Nilimlipa dereva taxi na kushuka.



    Nilishuka upande wa pili wa barabara mkabala na nyumba yenye anuania ambayo ilikuwa imeandika kwenye zile nyaraka zangu.



    Nyumba hii ilikuwa kwenye moja ya mitaa iliyoko pembezoni kidogo mwa jiji hili la Zurich. Ni mitaa ambayo kwa umombo wanaita "suburbs". Mitaa yenye kuishi watu wenye kipato cha kati. Sio mitaa ya kitajiri sana lakini wanaishi watu wenye haueni kubwa ya kimaisha. Nyumba zake zote zilikuwa za kufanana. Zilikuwa nyumba kubwa nzuri zenye mandhari ya kuvutia.



    Zilikuwa nyumba za rangi nyeupe ambazo zilikuwa na ghorofa moja juu kila myumba. Nyumba zote zilikuwa na ukoka wa kijani kibichi ambao ulionekana kutunzwa vizuri na kukatwa kimaridadi. Kwa mbele kila nyumba ilikuwa na uzio wa mbao za urefu wa kama mita moja ambazo zilikatwa nadhifu na kupakwa rangi nyeupe yenye kurandana na rangi ya nyumba hizi.





    Jambo la haraka ambalo nililing'amua mara moja ni kwamba nyumba ambayo ilikuwa na anuani ya kwenye nyaraka yangu ndio pekee ambayo haikuwa inawaka taa ndani yake. Yaani kwamba nyumba zote nyingine zilionekana taa ndani na nje zikiwaka huku nikisikia vicheko na sauti hafifu za maongezi ya hapa na pale kuonyesha nyumba hizo wenyewe walikuwepo wakipiga soga. Lakini nyumba hii ya anuani yangu haikuwa inawaka taa wala kuonyesha dalili ya uwepo wa watu ndani yake.



    Sikutaka kupoteza muda kujiuliza maswali. Nikavuka barabara na kutembea mpaka mlangoni mwa ile nyumba.



    "Hallowwwww.!!"



    Nilibisha hodi.



    "Hallowwww… anybody home?"



    Nilibisha tena hodi bila majibu. Nikabisha tena hodi na tena na tena lakini palikuwa kimya. Hakuna mtu ambaye alijibu. Ilithibitisha nilichokuwa nakiwaza. Hakukuwa na mtu ndani ya nyumba hii?

    Nilianza kuwaza nifanye nini? Niondoke? Hapana… siwezi kuja mpaka hapa nakugeuza tu. Nifanyeje sasa?



    Uzuri au ubaya wa mitaa hii ya "suburbs" duniani kote ni namna ambavyo majirani wanavyoishi. Kila mtu anajali maisha yake. "Everyone minds his own business." Hakuna ambaye anajali nini kinaendelea kwa jirani. Hakuna kuombana 'chumvi' kama mitaa ya uswahilini. Iwe ni Masaki, Dar es Salaam au Saratoga, California au Affolterntrasse, hapa Zurich au sehemu yoyote ile yenye suburbs duniani. Ukiishi hapo tegemea maisha ya upweke kana kwamba hauna majirani.



    Siku pekee ambayo utajua una jirani ni msimu wa sikukuu jirani akikuletea 'pie' aliyoipika kwake au bakshishi nyingine kama pipi na vikolombwezo vidogo vidogo kukutakia heri ya sikukuu.



    Hii ilikuwa ni faida kwangu. Niliamini kabisa hakuna jirani ambaye alikuwa anafuatilia nyendo zangu au hata kujua kama niko hapo. Nikazunguka nyuma ya nyumba. Nikapekua pekua mpaka kupata kipande cha waya mgumu kama pini hivi. Japokuwa sikuwa hodari sana lakini nilikuwa najua namna la 'ku-pick lock' za vitasa. Nilikuwa najua nini cha kufanya.



    Nikahangaika na kitasa karibia dakika kumi nzima mpaka nilipokisikia kimefyatuka. Nikaingia ndani bila kupoteza muda. Sikutaka kuwasha taa ili nisije kuwashitua watu kama kuna yeyote ambaye alikuwa anafuatilia. Niliamua kutumia tochi ya simu yangu.



    Kwa muonekano wa haraka tu, ndani humu kulikuwa ni nadhifu mno. Vitu vikiwa vimepangika sawia. Lakini kulikuwa kunatoa taswira mbili zenye kukinzana.

    Moja kulionekana kuna watu wanaishi kwa kuwa hakukuwa na vumbi na vitu vilipangwa sawa sawa. Lakini taswira ya pili palikuwa panaonyesha dalili kinzani kwamba hakukuwa na watu wanaishi hapo. Kwa sabahu vitu vilikuwa vimepangwa kwa usahihi mno wa kupitiliza. Nyumba ambayo watu wanaishi lazima uone rapsha za hapa na pale. Labda sofa limebonyea au kuvurugika fulani… hiki kiko pale ambako hakitakiwi kuwa na kadhalika. Kuna dalili fulani hivi unaiona mahala ambako kuna binadamu anaishi. Lakini hapa palikuwa pamepangiliwa kuwa ufasaha mno.



    Nilikuwa sebuleni mwa nyumba hii nikimulika huku na huko. Sikuona kitu chochote cha kushitua au kuvutia kukidadisi. Ni mpaka mwanga wa tochi yangu ya simu ulipotua ukutani ndipo ambapo mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda mbio.



    Nikasogea karibu kutazama.



    Ukutani kulikuwa kumewekwa picha kadhaa zikiwa kwenye 'fremu' nadhifu. Lakini katika picha hizi ni picha moja ambayo ilinifanya moyo kwenda mbio. Ilikuwa ni picha ikionekana ya familia. Kulikuwa na baba, mama na watoto watatu. Watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike.



    Mwanamama sikumtambua lakini yule ambaye alikuwa anaonekana kama baba alikuwa ni jamaa yule yule mzungu ambaye yuko kwenye picha ambayo niliikuta kwenye bahasha niliyopewa na mzee wangu imeandikwa '"Strike #1" ambayo yuko mahala fulani kama bandarini kwenye makontena yeye na Rais Albert Kafumu na watu wengine. Ni mtu huyu huyu ambaye pia yuko kwenye picha ile nyingine iliyoandikwa "Strike #5" ambayo kama imepigwa mahala fulani mtaani maeneo ya ulaya au Marekani. Lakini pia ni mtu huyu huyu ambaye yuko kwenye picha niliyopewa na Hudini akiwa kwenye picha ya pamoja na baba yake Cheupe na Chuepe mwenyewe akiwa mtoto.



    Lakini kilichonishitua zaidi ni wale watoto walioko kwenye picha hii. Hasa watoto wawili… yule wa kiume mmoja na yule wa kike. Sura zao hazikuwa ngeni kwangu. Nilikuwa nzifahamu… walikuwa ni Luke aliyeniokoa siku niliyopigwa risasi na ambaye leo asubuhi ameuwawa na yule mtoto wa kike alikuwa ni Erica yule binti muhudumu wa hoteli na ambaye alinipiga risasi juzi usiku.



    Nilihisi labda macho yangu hayaoni sawa sawa. Nikayafikicha na kisha kumulika tochi yangu kwa karibu zaidi.



    Sikukosea… alikuwa ni Luke na Erica wakiwa watoto.





    Kichwani taa ikianza kuwaka. Nikaanza kung'amua hii anuani ina maana gani hasa.







    Nilikuwa tena kwenye taxi kutokea mtaa wa Affolterntrasse ambako nilienda kutazama nyumba yenye anuani ambayo ilikuwa kwenye zile nyaraka nilizonazo. Kitu pekee ambacho niliondoka nacho kwenye ile nyumba ilikuwa ni ile picha ukutani. Picha ambayo inawaonyesha yule binti Erica muhudumu wa pape hotelini lakini kwenye nyaraka zangu picha yake imeandikwa jina la Ivanka, pamoja na Luke utotoni mwao wakiwa na mtu ambaye kwenye picha yuko kwenye picha nyingine nilizonazo.



    Kuna wazo lilikuwa linanijia kichwani. Kuna taa ilianza kuwaka na kuanza





    Niliitazama tena ile picha. Nikaitazama kwa makini kweli kweli. Yes! Huyu ni Erica akiwa mtoto, na huyu ni Luke akiwa mtoto. Na huyu mwanaume ndiye huyu ambaye yuko kwenye picha nyingine tatu nilizonazo. Moja akiwa na Rais Kafumu, ya pili akiwa mahala fulani mtaani na ya tatu akiwa na cheupe na baba yake. Mtu pekee ambaye sikumtambua kwenye ile picha alikuwa ni yule mwanamke. Kwa muktadha wa mantiki na mtindo wa upigaji huu picha ilionekana kabisa ilikuwa ni picha ya familia. Ikimaanisha kwamba Erica na Luke ni mtu na dada yake. Na yule jamaa ni baba yao. Na yule mwanamke ni mama yao.



    Lakini kuna kitu ambacho kilikuwa kimenishangaza zaidi. Huyu mtu alikuwa anaonekana kana kwamba ni kijana mno kutosha kuwa mzazi wa kina Erica na Luke. Kwa sababu picha ambayo amepiga na Rais Kafumu inaonekana wazi kabisa kwamba imepigwa miaka ya hivi karibuni.



    Nikaitazama tena picha kwa makini. Naam! Taa ilikuwa inawaka zaidi… nilianza kung'amua ile anuani ilikuwa na maana gani. Nilikuwa nahitaji tu kuhakikisha kama ninachokifikiria kilikuwa sahihi.



    Nikiwa nimezama sana kwenye kutafakari ile picha mpaka sikujua kama tulikuwa tumefika tayari Haedstrasse mpaka pale dereva taxi aliponishtua na kunirejesha tena kwenye mawazo ya kawaida. Nikalipa na kushuka.



    Nilikuwa natembea taratibu kuelekea kwenye uchochoro wa jengo ambao unaenda kwenye mlango wa nyuma ya jengo ambao nimekuwa nautumia mara zote. Nilikuwa natembea taratibu ili nisitoneshe kidonda pale tumboni. Nikakumbuka tena kwamba nahitaji daktari wa kukitazama hiki kidonda kabla hakijanipa madhara zaidi.

    Nikakukumbuka tena kwamba napaswa pia kulitazama hili jengo zaidi, floor za juu kuna nini? Na pia The Board walilinunua kutoka kwa nani? Na walinunua kwa lengo lipi haswa?

    Hili napaswa kulifanya asubuhi… kwa usiku huu napaswa kupumzika na kuchekecha akili kuhusu Erica, Luke na yule jamaa wa kwenye picha.



    Nilipoufikia mlango niliukuta ukiwa umefunguliwa na kuegeshwa tu. Yaani kwamba ulionekana kuwa ulifunguliwa na kisha kurudishwa bila kufungwa tena tofauti na ambavyo niliuacha ukiwa umefungwa. Eidha kulikuwa na mtu ndani au mtu huyo aliingia na kutoka kwa haraka bila kufunga mlango.



    Kama ambavyo nilijiapiza kwamba, safari hii sikimbii… nitapambana. Ndivyo ambacho nililifanya. Nilishinda woga wote ambao nilikuwa nausikia muda huu. Nikavuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Kisha nikafungua mlango na kuingia kwa tahadhali.

    Pale koridoni kulikuwa na giza kama siku zote kwa hiyo nilitembea kwa kunyata taratibu mno ili nisimgutushe yeyote kama yuko humu ndani. Moyoni nilikuwa najilaumu sana kwa kutofanyia kazi mapema wazo la kuwa na silaha ambalo nilikuwa nalo tangu asubuhi.



    "Damn! I really need a gun!"



    Nilijilaumu moyoni huku nikinyata taratibu.



    Nikiwa nanyata hivi taratibu pale pale koridoni nikaanza kusikia sauti. Sauti ya mtu akigugumia.



    Mwanzoni nilihisi labda ni mtu yuko kwenye maumivu lakini niliposikiliza kwa makini niligundua kwamba alikuwa ni mtu analia, alikuwa analia kwa uchungu sana kiasi kwamba alikuwa inaifunda sauti ndani ili isitoke. Sauti iliashiria kwamba mtu huyo alikuwa analia kwa mida mrefu kiasi kwamba sauti ilianza kumkauka.



    Nikatoa simu yangu mfukoni taratibu na kuwasha tochi. Hamad.!! Mbele yangu alikuwa Jimmy. Yule chokoraa ambaye juzi waliniokota yeye na Luke. Alikuwa amekaa chini amejikunyata kwa kuinamisha kichwa chake kwenye magoti ambayo alikuwa ameyakunja mpaka usawa wankifua.



    Alipoona mwanga akainua kichwa chake kutazama. Usoni alikuwa amelowa machozi chapa chapa. Ule waupe wake wa kizungu ulikuwa umebadilika na kuwa mwekundu usoni kuashiria kwamba amekuwa akilia kwa muda mrefu sana.



    "Jimmy!! What's wrong?" Nilitahamaki huku naenda haraka ukutani kuwasha taa.



    "Get away from me.!!! Go away.!!" Jimmy alifoka huku analia.



    Nilibaki nimepigwa butwaa tu. Jimmy alikuwa na nini? Au amepata habari juu ya kifo cha swahiba wake Luke?



    "Look Jimmy, I am really so…"



    "You are a jinxy! You are a jinxyyy.!! Jimmy alinikatisha na kufoka kwa hasira huku bado akiwa analia.



    "Jimmy! I am sorry, I know Luke was your friend… I am really really sorry mate.!" Nilijitahidi kuongea kwa huzuni na kufariji kwa kadiri ambavyo niliweza.



    Lakini nilishangaa Jimmy anainua uso na kunitolea macho kwa mshangao. Alitoa macho kana kwamba amesikia jambo kubwa asilolijua. Aliacha kulia ghafla. Aliinua uso na kunitazama kwa mshangao mkubwa. Mpaka nilianza kuogopa kutokana na mshangao wale usoni.



    "What is it.!" Nilijitahidi kumuuliza.



    "What did you just said?" Aliniuliza huku anaanza kuninuka.



    Nilitafakari kama kwenye sentensi yangu nimeongea kitu chochote cha kukera au dhihaka? Lakini sikukiona… Jimmy alikuwa anainuka taratibu kana kwamba ni chui anajiandaa kurukia windo lake la siku.



    "Chill out mate!" Nilijitahidi kumtuliza huku nimenyoosha mkono kuashiria awe mtulivu.



    "No no no! What did you just say?"



    "I said…I am sorry for Luke's death.!"



    Mshangao usoni mwake ulikuwa mkubwa zaidi.



    "Whaaaatt! When did this happen?"



    "You dont know.?" Nilishangazwa. Ina maana hajui kwamba swahiba wake amefariki leo asubuhi? Kama hajui ni kitu gani kilikuwa kinamfanya alie kiasi hiki kama mtoto mdogo?



    "When did this happen?" Aliniuliza tena kwa taharuki.



    "Today morning… he was shot! Wait a minute… you dont know anything about this? Then why are you craying?"



    Nikamuona anainamisha tena kichwa chini kwa uchungu. Nikaanza kusikia kwikwi. Mara moja akaanza tena kulia na kukaa tena chini sakafuni.



    "You are jinxy mate! You are a jinxy!!" Jimmy alilalama huku analia pale sakafuni.



    "Jimmy! Whats going on?"



    Jimmy anasema kwamba alikuwa hajui kuhusu kifo cha Luke? Kwa nini analia? Na kwa nini kilio kimeongezeka zaidi baada ya kumuambia kuhusu kifo cha Luke?



    "Jimmy! What's going on here?" Safari hii nilifoka.



    Akainua kichwa na kunitazama cha uchungu.



    "My sister died today! She shot.!!" Alinijibu kwa kifupi huku amenikazia macho.



    Nikihisi kama jiwe zito limedondoshwa ndani ya nafsi yangu? Dada yake? Ina maana Jimmy huyu chokoraa naye ana dada? Na huyo dada naye ameuwawa leo? Tena naye kwa kupigwa risasi kama Luke?

    Lazima kutakuwa na uhusiano.



    "Your sister? Who is she… I mean am so sorry! When didi this happen?" Niljikuta napata kigugumizi nisijue ni kitu gani hasa niongee.



    "I would rather show you!" Jimmy aliongea kwa hasira huku anainuka. "Lets go!"



    "Where? To do what exactly?" Nilihamaki kwa mshangao.



    Nini kimempata Jimmy? Nimemuuliza kuhusu dada yake aliyeuwawa badala yake ananieleza kwamba ni bora alinionyesha. Anataka kunionyesha nini?



    "Do you want to know or what?" Aliniuliza bila kuniangalia akiwa amesimama kuelekea mlangoni.



    "Ofcourse I want to know but…"



    "Then lets go!"



    Hakunisubiri nimjibu au chochote… tayari alishafika mlangoni na kuufungua kutoka nje.

    Sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kumfuata japo sikujua tunaenda wapi au anataka kunionyesha nini?



    Tulifika barabarabi na kusimamisha taxi kwa mara nyingine tena.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Freacht West!" Jimmy alimueleza dereva taxi baada ya sote kukwea ndani.



    Moyo ulinipasuka. Huo ndio mtaa ambao iko hoteli ya Radisson Blu Hotel ambayo nilifikia siku nilipoingia hapa Zurich. Sikutaka kuonyesha mshangao wangu au kumuuliza Jimmy kitu chochote. Nikasubiri nione mwisho wa hii safari.



    Kwenye taxi wote tulikuwa kimya. Kila mmoja akiwaza na kuwazua lakwake kichwani.



    Nilikuwa najihisi kama vile niko kwenye "maze". Kana kwamba ni uwanda mpaka wenye mamia ya kuta na mamia ya kona kona na kukiwa na mlango mmoja tu wa kuingilia na kutokea. Ukiwa kwenye maze ukikata kona moja tu isiyo sahihi umekwisha. Utazunguka na kuzunguka ndani yake na kamwe hutouona mlango wa kutokea. Unapaswa kila kona ambayo unaipinda iwe sahihi.



    Ndivyo ambavyo nilikuwa najihisi muda huu. Kulikuwa na kona kona nyingi mno za mafumbo na kama nitakosea hata suala moja tu nitajitumbukiza gizani zaidi kuzidi hata giza nililokuwepo kabla ya kufika hapa Zurich.



    Tulienda kama mwendo wa dakika kumi na tano hivi tukiwa wote kimya kama mabubu. Taxi ilifika mpaka Freacht West. Tulikuwa kwenye 'blocks' zile zile ambazo ilipo Radisson Blu Hotel.



    "Stop here!" Jimmy alimuamuru dereva taxi.



    Gari ilipaki mkabala kabisa na Radisaon Blu Hote. Mahala pale pale ambako asubuhi ya leo nilikuja niliposikia kifo cha Luke.



    Sasa nilielewa dada yake Jimmy ni nani. Sikuwa na hata haja ya kuuliza.



    Safari hii Hoteli ilikuwa imefungwa kabisa. Pale mlangoni kulizungushiwa utepe wa njano wa polisi. Hii iliashiria kwamba mauaji hayo yalifanyika ndani ya Hoteli.



    Niligeuka na kumtazama Jimmy kwa kumkazia macho. Kichwani mawazo kadhaa yalipita. Hivi huyu Jimmy ni chokoraa kweli au ni mtu tu amepandikizwa kwa kazi maalumu hapa Zurich?



    "So Erica was your sister?" Nilimuuliza kwa hasira huku nahema.



    Hasira nilizokuwa nazo ni kwa jinsi ambavyo Jimmy muda wote tangu siku ile wameniokota pale kwenye jengo Hardstrasse alikuwa anajifanya hajui chochote kuhusu mimi au kinachoendelea.



    "Her name was Ivanka!" Jimmy alinijibu bila kuniangalia macho ameyalaza kuelekea mbele.



    Jimmy alitaja jina la yule binti ambalo pia nililiona kwenye nyaraka zikiwa na picha yake.



    Nikijikuta na hasira zaidi, kuchanganyikiwa zaidi lakini pia nikisikia hatia ndani yangu. Watu hawa wawili wameuwawa mara tu baada ya kukutana na mimi. Kwa namna fulani nilihisi kuna uhusiano wa vifo vyao na kukutana na mimi. Nilihisi ndio sababu ya Jimmy kung'aka akisema "you are a jinxy!"



    "Jimmy!" Nilimuita kwa utulivu.



    Hakugeuka. Aliendelea kukaza macho yake mbele.



    "Jimmy! Do you know who I am? I mean before we met… did you know who I was?" Nilimuuliza tena kwa sauti ya utulivu.



    "For two years she was obsessed with finding you… I knew this would bring bad luck. But she dint listen… she was too determined to find you!"



    Jimmy alinijibu kwa uchungu huku bado akiwa amekaza macho mbele.

    Kwa maneno mepesi alikuwa amekubali kuwa alikuwa ananijua kabla hata ya kuonana ile juzi pale kwenye jengo nilipopigwa risasi. Kwamba dada yake Erica, au Ivanka kwa usahihi zaidi… alikuwa na mshawasha na nadhiri ya kunipata. Kwa nini?



    Mara ya kwanza baada ya kukuta ile picha kwenye nyumba ya Affolterntrasse nilidhani kwamba Luke na Erica ndio ndugu. Lakini Jimmy anasema Erica ni dada yake? Ina maana wote watatu ni ndugu? Haiwezekani, Jimmy ameguswa zaidi na kifo cha Erica kuzidi Luke.

    Uzuri safari hii siko gizani tu peke yangu, bali niko hapa na mtu wa kunipa majibu yote haya ya maswali yangu, Jimmy.



    "Jimmy! We need to talk. I need answers.. you hear me? we need to talk… hey take us back to Hardstrasse!"



    Nilimuamuru dereva. Kuturudisha tena Hardstrasse. Jimmy hakukaidi. Nilihisi nae alikuwa amechoka kukaa na siri moyoni mwake. Alikuwa anataka hatimae atue mzigo huo alionao moyoni.



    Dereva aligeuza gari na kuanza kurejea tulikotoka.



    Tukiwa tunaondoka eneo hili. Nilitupa tena jicho pale nje ya hoteli palipozungushiwa utepe wa njano wa polisi. Inaonekana tukio lilikuwa limetokea si masaa mengi yaliyopita. Bado polisi walikuwa wanahoji watu hapa na pale. Na kulikuwa na wapita njia kadhaa kama kawaida wamesimama kushangaa na kupata 'umbea' wa kilichotokea.

    Katika mkusanyiko huu wa wapita njia wachache waliosimama kutazama, nilimuona tena yule jamaa… yule jamaa wa asubuhi, mwenye kofia ya pama ya kijivu, koti refu lenye kufika usawa wa magoti, mkononi akiwa na gazeti, Jamaa yule yule ambaye juzi usiku alikuwa ameketi kwenye sofa za mapokezi ya hoteli akisoma gazeti nilipokuwa nabishana na Erica.



    Inaonekana alikuwa anaangalia taxi yetu muda wote. Tulipoondoka nilimuona akitusindikiza kwa macho mpaka tulipopotea upeo wa macho yake.



    Nikamgeukia Jimmy.



    "Wewe mpumbavu leo una maswali mengi sana ya kunijibu!" Nilijikuta na hasira mpaka nimemsemesha kwa kiswahili nikijua kabisa hakuelewa chochote.



    Nilitamani taxi ipae na kufika haraka nianze kupata majibu kutokakwa Jimmy.









    Cheupe,



    Haijalishi ni sauti ya kinanda ama kinubi. Haijalishi kama ni sauti ya zumari ama gitaa. Ala murua inaweza kuinua roho ya binadamu, inaweza kuinua na kuitweza katika mawanda ya juu ya nguvu iliyonayo na kumpa ushujaa.

    Si lazima muda wote kusikia ala murua kwa masikio ya kawaida. Roho inapohitaji kutwezwa, inapohitaji kuinuliwa, inapohitaji kupata ushujaa… nafsi ndiyo mahala sahihi zaidi pa kusikilizia ala murua.



    Roho ikiwa imepondeka unaweza kufumba macho na kuzama nafsini kusikiliza ala murua ya kinubi. Roho yako ikowaimepondeka unaweza kukaa sakafuni ukaegemea ukuta na kufumba macho na nafsi kusikia ala murua ya zumari.



    Macho si lazima yaone mpiga gitaa. Na wala masikio si lazima yawambwe kwa mawimbi ya sauti ya kinanda. Ni nafsi ndiyo yenye kuhitaji kusikia ala hii murua.

    Fumba macho, kaa sakafuni, egemea ukuta. Acha nafsi iambae kwenye ngazi ifuatayo ya ufahamu. Iachie roho ipate ushujaa. Ushujaa unaohitaji kwa ajili ya kuikoa roho iliyopondeka. Ushujaa unahohitajika kwa ajili ya uendelevu wa mbari ya mwanadamu.



    Kila mapenzi yanahitaji ushujaa. Kila familia inahitaji shujaa. Na kila taifa linahitaji shujaa. Lakini ushujaa wahitaji utayari wa kuitoa nafsi kuwa dhabihu. Ushujaa wahitaji utayari wa kuwa kafara.

    Na pasipo kafara hakuna ushindi. Na pasipo ushindi hakuna survival.



    Uwe na moyo mkuu.



    Kwa ushujaa, unyenyekevu na upendo wa hali ya juu,



    Ndimi,



    Mumeo R.C. Kajuna





    Nilivuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Nikakunja kikaratasi chenye ujumbe huu niliouandika na kukiweka kwenye mfuko wa pembeni wa begi langu la nguo.



    "What are you writting mate?" Jimmy aliniuliza kwa udadisi.



    "Nothing!"



    Nilifunga zipu ya begi na kisha kukaa vyema kwenye kiti kilicho karibu na meza.



    Tulikuwa tumerudi kwenye jengo la mtaa wa Hardstrasse kama nusu saa hivi iliyopita.

    Safari hii hatukuwa tumekaa koridoni pale bali tuliingia kwenye lile lichumba likubwa ambalo mara ya kwanza kufika hapa nilijikutaga nikiwa nimeamka ndani yake. Chumba kile chenye mlango wa kuhitaji kuufungia kwa alama za vidole.



    Jimmy alikuwa amemaliza kunijibu maswali kadhaa ambayo nilikuwa najitaji kufahamu. Baada ya kumaliza kunieleza kile ambacho anakifahamu nilihisi kwamba watu ninaokabiliana nao hawakuwa wa kawaida. Naweza kupoteza maisha muda wowote. Ilinibidi niandke ujumbe huo kwa ajili ya Cheupe kama ikitokea chochote kibaya kikinipata na nisipate fursa ya kumueleza kile ambacho kiko moyoji mwangu.



    Jimmy alikuwa amenieleza kwamba, yeye na Erica au Ivanka kama ambavyo mwenyewe anapendelea kumuita, ni ndugu wa damu kabisa. Wazazi wao wote wawili walifariki kwa ajali ya gari kipindi wao wakiwa na umri wa miaka sita tu. Baada ya hapo yeye na dada yake walikuwa wakihama hama kuishi kwenye "foster homes" kwa karibia kipindi cha miaka minne mpaka pale ambapo dada yake alipata bahati ya kuasiliwa na familia.



    Jimmy alinieleza kwamba Ivanka aliasiliwa na familia ya Mr. Kimberly Delani ambaye ndiye yule jamaa aliyeko kwenye picha zile nyingine nilizonazo moja ikimuonyesha akiwa na Rais Albert Kafumu na nyingine akiwa na Cheupe na mzee wake. Jimmy akanieleza kwamba huyo ndiye Kimberly Delani ambaye yeye pamoja na mkewe Zarah mwenye asili ya mashariki ya kati walimuasili Ivanka.



    Jimmy alinieleza zaidi kwamba inaonekana kuwa Mr. Delani na mkewe Zarah walikuwa ni wagumba au hawakutaka kuzaa mtoto wao wenyewe maana Ivanka alipofika huko kwenye familia yao alikuta wakiwa na mtoto mwingine mkubwa zaidi ambaye walimuasili miaka mitatu nyuma. Mtoto huyu ni Luke, yule jamaa ambaye walinikota hapa pamoja siku mbili zilizopita na ambaye ameuwawa leo hii asubuhi nje ya Radisson Blu Hotel.





    #309

    Jimmy alinieleza kwamba kama miaka miwili baada ya Ivanka kuasiliwa aliona mabadiliko makubwa sana kwa dada yake. Mawasiliano yao yalipungua kabisa. Hata utamaduni wao wa kuonana walau kila mwisho wa wiki ulikoma.



    Baadae Ivank alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Zurich. Chuo hicho hicho ambacho pia Jimmy alikuwa anasoma. Nilishituka kidogo aliponieleza hili kuhusu yeye kusoma chuo



    "You went to University??" Nilimuuliza kwa mshangao.



    "Yes mate! Why… I look dumb?" Jimmy alitia utani kidogo.



    "No no! Not at all… what did you study?"



    "Medicine!" Alijibu huku anatabasamu.



    "Wooo!! No offince mate but how did you end up homeless?"



    "Long story mate! Dont wann' talk about it!"



    Fair enough! Sikutaka kumlazimisha anipe historia ya maisha yake kwa sasa. Sikutaka mwishowe aghairi hata kunipa taarifa kuhusu Ivanka na Luke. Japokuwa sasa nilielewa kwamba yeye ndiye lazima ambaye akinitibia lile jeraha la risasi juzi aliponiokota na baadae kupoteza fahamu.



    Jimmy aliendelea kunieleza kuwa hata walipokuwa hapo chuo kikuu cha Zurich, Ivanka hakutaka kabisa ukaribu nae. Ilionekana dhahiri kabisa kwamba hakutaka watu wafahamu kuwa wana undugu.



    Jimmy akanieleza kwamba kipindi hicho Ivanka yuko chuo, Luke alikuwa amejiunga na jeshi la Uswisi kitengo cha "Kommando Spezialkräfte" (Special Forces Command) akipangiwa kikosi cha Grenadier Command 1 chenye wanajeshi wasiozidi elfu tatu tu nchi nzima ya Uswisi.



    Jimmy alinieleza kwamba Delani mwenyewe hakuwa mtu wa kukaa sana pale nyumbani, mara nyingi alikuwa akisafiri nje ya nchi kibiashara.



    "What business was he into?" Nilimuuliza.



    "I dont know for sure, but I think he was some type of a banker or something.!"



    "A banker? Ok.." kichwani nukta ziliendelea kujiunga. Kwanza ile anuani. Zile picha na sasa kujua kwamba yule jamaa wa kwenye picha zote nilizonazo kwamba ni 'banker'.



    Jimmy aliendelea kunieleza.



    Aliniambia kwamba baadae yakaanza kufululiza matukio ya ajabu zaidi. Kwa mfano Ivanka aliacha chuo na kusafiri kwenda Marekani na kutokomea huko. Luke aliacha utumishi jeshini naye pia kutokomea kusikojukikana.

    Pale nyumbani kwao alibaki Zarah na Delani pekee na huku Delani mwenyewe ambaye nae pia muda mwingi analuwa yuko safarini je ya nchi kwa hiyo muda mwingi ni Zarah pekee ndiye alikuwa nyumbani.



    Jimmy alinieleza kwamba kama miaka mitatu iliyopita, Delani na mkewe zarah walisafiri na hawajahi kurejea tena mpaka leo hii.



    Ili nipate uhakika zaidi nakumbuka nilimuuliza swali,



    "Where were they living exactly?"



    "Affolterntrasse!" Jimmy alinijibu.



    Nikatingisha kichwa kwa kuitikia. Sikuhitaji kumuuliza anuani. Nilikuwa na hakika ni nyumba ile ile ambyo nilienda kuipekua masaa machache yaliyopita. Nyumba ambayo anuani yake iko kwenye nyaraka nilizonazo kutoka kwa mzew wangu.



    "So what happened next?" Nikamuuliza.



    "Two years ago… out of no where they both came back!"



    "Who?"



    "Ivanka and Luke!"



    Jimmy alijijibu. Alinieleza kwamba miaka miwili iliyopita ghafla tu Ivanka na Luke walirejea.



    Kichwani niliikumbuka kwamba miaka miwili iliyopita ndio muda ambao niliidondosha jumuiya ya The Board na mzee wangu kujipiga risasi. Nilihisi kwa hakika kabisa kulikuwa na uhusiano wa matukio haya na kile ambacho kilitokea kule nyumbani Tanzania.



    Jimmy alinieleza waliporejea walikuwa na jambo moja tu kichwani.



    Jimmy alinieleza kwamba inaonekana walikuwa wanafahamu kwamba siku hizi yeye ni chokoraa anayelala mitaani na walikuwa wanajua namna ya kumpata. Aliniambia kuwa waliporejea walimpa kazi moja kubwa. Walimuonyesha picha yangu na kumueleza kwamba kila siku anatakiwa afuatilie mahali hapa kwenye hili jengo la Hardstrasse mpaka siku atakaponiona nikiingia humu na kisha awape taarifa haraka.



    #310

    Jimmy alinieleza kwamba kazi hiyo ilikuwa ngumu na yenye kuchosha. Kila mara aliwalalamikia Ivanka na Luke kwamba amechoka na hawezi kuendelea tena. Ivanka na Luke walimtishia kwamba wataacha kumpa hela ya chakula na matunzo mengine ambayo alikuwa anayapata. Hakuwa na jinsi ilibidi aendelee tu japo kwa shingo upande.



    Ndipo hatimaye juzi, baada ya kusubiria kwa muda wa miaka miwili… alinishuhudia nikiingia ndani ya jengo hili.



    "So tell me mate… why were they obsessed with finding you?" Jimmy aliniuliza huku amenikazia macho usoni.



    Kwa muda wa dakika nzima nilikuwa natafakari nimueleze nini haswa? Nimdanganye? Au nimwambie ukweli?

    Nikimdanganya na akigundua anaweza kupoteza imani na mimi… nahitaji aendelee kuwa upande wangu. Wacha nimueleze ukweli, japo sio ukweli kamili. Ukweli hata nusu tu.



    Nilimueleza Jimmy kwamba, mzee wangu alifariki miaka miwili nyumbani Tanzania. Katika karatasi zake za wosia aliacha maagizo yenye anuani ya nyumba ya kina Ivanka na kwamba natakiwa nije kufuatilia.



    Nakumbuka aliniuliza kufuatilia nini? Nikamjibu kuwa sijui…



    "You are dumb mate. You travelled all the way up here for something you dont know..?"



    "I know it sounds stupid but that's it.!"



    Jimmy hakunijibu chochote. Alibakia tu kunikodolea machokwa mshangao.



    Kichwani niliendelea kuunganisha nukta kuhusu ile nyumba nilienda kuipekekua masaa machache yaliyopita na hizi taarifa ambazo Jimny amenipa. Hisia zangu kwamba nyumba ile ilikuwa haikaliwi na mtu zilikuwa sahihi kama alichonieleza Jimmy ni cha kweli. Kwamba Delani na Zarah wameitelekeza nyumba hiyo kwa miaka mitatu sasa. Lakini kuna kitu kilikuwa hakiniingii akilini. Nyumba ile ilikuwa safi mno na vitu vimepangiliwa sawia. Lazima kuna matunzo yanafanyika.





    "So who is taking care of the house… the one Delani and his wife left?"



    "Why do you ask that?"



    Nikamueleza kuhusu safari yangu kwenye hiyo nyumba siku ya leo masaa machache yaliyopita na nilichokiona na kusababisha wasiwasi wangu kuwa kuna mtu anaitunza.

    Nikamueleza pia kwamba niliwahi kuandika barua nikiwa Tanzania kuja kwenye anuani ya nyumba hiyo na ikajibiwa.

    Jimmy alibaki kunikodolea macho tu kwa mshangao.



    "There must be someone taking care of the house and picking up mails… and that is our lead.!" Nilimueleza.



    Jimmy alibaki ananitazama tu. Sikujua anawaza nini lakini nilihisi kabisa alikuwa anajiuliza kichwani "who is this guy". Alinitazama tu kwa karibia dakika nzima kisha hatimaye akaongea.



    "Let me take a look at that wound!"



    Nikafunua shati tumboni. Nikamuacha akifanya shughuli yake ya kidaktari. Nikaegemeza kicha ukutani. Nikafumba macho.

    Kana kwamba nilikuwa nasikia ala ya muziki kwa mbali nafsini mwangu. Ala ambayo ilikuwa inanifanya nizidi kujipa moyo kufumbua fumbo lililo mbele yangu. Kukabiliana na udhalimu mkubwa ambao nilikuwa nahisi umejificha. Japo nilihisi unaweza kugharimu uhai wangu… lakini nilijipa moyo… Kila mapenzi yanahitaji ushujaa. Kila familia inahitaji shujaa. Na kila taifa linahitaji shujaa. Lakini ushujaa wahitaji utayari wa kuitoa nafsi kuwa dhabihu. Ushujaa wahitaji utayari wa kuwa kafara.

    Na pasipo kafara hakuna ushindi. Na pasipo ushindi hakuna survival.



    Nilitamani usiku ukuche haraka nianze kufuatilia ni nani hasa anayeitunza ile nyumba na kuchukua 'mails' zinazotumwa pale.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Yalikuwa yamepita karibia masaa mawili tangu tufike hapa mimi na Jimmy. Ilikuwa ni asubuhi ya kama saa nne hivi. Siku ya leo ilikuwa na baridi haswa, kwa hiyo tulikuwa tumevalia masweta mazito na kofia ya mzula kwa ajili ya kujikinga na baridi.



    Nilikuwa nasikia auheni kubwa sana pale tumboni kwenye kidonda. Jimmy hakuwa anatania, kitendo chake cha kunikagua kidonda jana usiku na kusafisha alinidhihirishia kuwa yeye ni daktari haswa licha ya huu uchokoraa alionao sasa. Japo kila baada ya dakika kadhaa kichwani swali lile lile lilikuwa linanijia tena na tena, "huyu mtu ilikuwaje mpaka akawa chokoraa?"

    Lakini sikutaka kuwahisha mambo, nilidhamiria kusubiri mpaka wakati sahihi ukiwadia nimbabe kwa maswali mpaka anieleze ukweli wa nini hasa kilimtokea mpaka kimfanya awe na maisha haya aliyonayo sasa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog