Search This Blog

Sunday 20 November 2022

VIPEPEO WEUSI: FROM ZURICH WITH RULES - 2

 





    Simulizi : Vipepeo Weusi: From Zurich With Rules

    Sehemu Ya Pili (2)









    Sikuamini kuwa Cheupe anaweza kutamka sentensi ya namna hii baada ya mambo yote tuliyopitia pamoja tangu utoto na leo ni watu wazima. Nikajikuta naingia katika msongo wa mawazo ya kuwaza na kuwazua kwanini Cheupe ametamka sentensi hii. Katika kuwaza kwangu huko na kuwazua ndipo ambapo ukafika muda nikaanza kuhisi labda kuna ukweli katika maneno aliyoyaongea, labda kuna ukweli kwamba najali hisia zangu tu bila kuzingatia hisia za wengine.







    Katika kujilaumu kwangu huku kuhusu kotojali hisia za wengine, ndipo nikajikuta nawaza kuhusu bahasha ambayo nilipewa na baba yangu kule Dodoma. Nikajikuta Napata wazo kwamba yawezekana nilikuwa sitaki kuifungua bahasha hii kutokana na ubinafsi wangu kama ulivyosemwa na Cheupe kwamba najali hisia zangu tu. Kwa nini sijali hisia za baba yangu mzazi ambaye kauli yake ya mwisho kabla ya kufariki ilikuwa ni kuniomba niende Zurich kwa kufuata maelezo yaliyomo ndani ya bahasha?







    Nakumbuka niliinuka kitandani na kumuacha Cheupe akiwa amelala fofofo usingizi wa hasira, nikaelekea kwenye chumba kidogo pembeni ya chumba chetu cha kulala ambacho nakitumia kama ofisi ya nyumbani na kufungua droo ya meza ambayo nilihifadhi ile bahasha niliyopewa na mzee wangu.







    Nakumbuka ilinichukua kama dakika kumi na tano nzima nikitafakari kama niifungue ama la. Baada kusita sita sana, hatimaye nikaifungua.!!







    Ndani ya ile bahasha kulikuwa na na ratasi tatu zenye maandishi ya kuchapwa. Pamoja na karatasi hizi tatu pia kulikuwa na picha mbili za mnato. Macho yangu kwanza moja kwa moja yalitua juu ya picha hizi mbili. Zilionekana kama vile ni picha ambazo zilipigwa kwa siri mno na mtu ambaye alikuwa amejificha mno kuogopa kugundulika. Juu ya picha hii kulikuwa na maandishi yaliyoandikwa kwa mkono kwa kalamu ya wino ambayo yalikuwa yanasomeka “STRIKE #1”.





    Picha ilikuwa inaonekana imepigwa usiku kwenye eneo fulani ambalo kwa haraka haraka ningeweza kusema bandarini kutokana na makontena mengi yaliyokuwa yanaonekana pichani. Pia picha ilionyesha watu wanne ambao walionekana dhahiri kabisa walikuwa mahala hapo walipo kuwa kwa kificho mno kuepuka kuonekana. Kwa kutazama kwa haraka haraka nilihisi kabisa kutokana na namna walivyokuwa wamesimama watu hawa wanne… watu wawili walionekana walikuwa ni walinzi wa mmoja wapo wa watu wale wawili waliosalia.



    Nikaitazama ile picha tena na tena… lakini kila ambavyo niliendelea kuitazama akili yangu ilikuwa inaniambia kuwa moja ya wale watu wawili alikuwa ni Rais Albert Kafumu. Nilikuwa najitahidi kuitazama ile picha kwa makini zaidi nikijifariji akilini mwangu kuwa labda macho yangu yalikuwa yananidanganya tu, laniki haikujalisha niliangalia picha ile mara ngapi… jibu moja tu lilikuwa linajijenga akilini tena na tena kuwa yule alikuwa ni Rais albert Kafumu, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.







    Yule mwenzake ambaye alionekana kuongea naye, sura yake haikujificha lakini bahati mbaya kumbukumbu zangu zilikuwa zinaniambia kuwa sijawahi kumuona yule mtu, nilikuwa simfahamu.







    Picha ya pili juu yake nayo ilikuwa imeandikwa kwa mkono kwa kalamu ya wino, “STRIKE #5”.







    Nikajikuta napekua pekua tena ile bahasha na kuikumg’uta labda kuna picha ilikuwa imebakia ndani yake lakini hakukuwa na chochote. Nilikuwa najiuliza kwa nini picha hii nyingine iandikwe “STRIKE #5” badala ya kuandikwa ‘strike #2’?? Nikahisi labda kulikuwa na maana ambayo nitaielewa nikianza kusoma zile karatasi tatu ambazo nazo nimezikuta ndani ya bahasha.







    Katika hii picha ambayo imeandikwa “STRIKE #5” nayo kama picha ya kwanza ilionekana kupigwa kwa siri kubwa na kwa kujificha ficha sana. Picha ilikuwa inawaonyesha watu wanne wakiwa wamesimama mahala fulani kwa umma, mtaani, pembezoni mwa barabara yenye msongamano wa watu wengi sana… lakini mandhari yalionyesha kabisa mta huu haukuwa Africa, ulikuwa ni mtaa mahala fulani Ulaya au Marekani.







    Pich hii haikuwa na kitu chochote kile cha ajabu ambacho mtu kinaweza kukutia mashaka kama ile picha ya kwanza. Watu hawa wanne ambao wote walikuwa wamevalia suti, walikuwa wanaonekana wanaongea kwa kujiamini bila kificho hapa waliposimama kwenye msongamano wa watu wengi tena mchana wa jua kali kabisa. Baada ya kuiangalia tena picha hii kwa mara kadhaa ndipo nikagundua kuwa moja ya watu wale wanne ni yule mtu ambaye nilishindwa kumtambua katika picha ile ya kwanza na mtu ninaye amini ni Rais Albert Kafumu.







    Nikaziweka zile picha pembeni na kuchukua zile karatasi tatu.







    Karatasi ya kwanza ilionekana kama vile ilikuwa ni barua ambayo iliandikwa lakini haikutumwa kwenda kwa muhusika.







    Barua ilikuwa na maneno machache sana. Upande wa kulia ilikuwa na anuani ya posta ambayo iliandikwa;







    HUDINI



    AFFOLTERNSTRASSE 44



    CITYPORT



    POSTFACH 8131



    8050



    ZURICH



    SWITZERLAND.







    Anuania hii ilikuwa imeandikwa upande wa kulia mwa karatasi kama ambavyo barua za kiofisi huandikwa.



    Kama mistari miwili hivi chini, kati kati mwa karatasi kulikuwa kumeandikwa neno moja tu la kifaransa, “REMPLACEMENT” yaani ikimaanisha “Replacement” kwa umombo au “Mbadala” kwa Kiswahili. Kulikuwa na neno hilo tu basi bila neno linguine lolote lile baada ya hapo. Baada ya kuisoma ile karatasi tena na tena nikahisi labda huyo “Hudini” ilikuwa labda ni ofisi au kampuni fulani hivi.







    Nikaiweka pembeni na kuchukua karatasi nyingine.







    Karatasi hii ilikuwa na maneno machache zaidi, katikati ya karatasi kulikuwa kumeandikwa;







    “DECEMBER 19



    7712/LH. A+. A+.



    CITIBANK. ZURICH”







    Nilikodoa macho tu bila kujua ni kitu gani hasa ambacho maandishi haya mafupi yalikuwa yana maanisha.



    Nikaweka pembeni pia hii karatasi na kuchukua karatasi ya mwisho ile ya tatu.







    Karatasi hii yenyewe ilikuwa na orodha ya vitu vitano ambavyo sikuweza kuvielewa kwa muda huu na mpaka sasa leo hii nilikuwa bado sijavielewa. Kulikuwa kumeorodheshwa majina ya sehemu yakiwa na namba mbele yake.





    1. UPANGA 3639



    2. DODOMA 2488



    3. MINESSOTA 126455



    4. ZURICH 7712



    5. MUMBAY 10033







    Kwa hiyo kwa ujumla ile bahasha ambayo baba yangu alinikabidhi kabla ya kufariki, bahasha ambayo ilionekana aliitunza kwa moyo wake wote na ilikuwa na siri kubwa, hivi ndivyo vitu ambavyo vilikuwa ndani yake. Picha mbili za mnato na karatasi tatu zenye maandishi ya kuchapwa ambayo mpaka sasa hakuna hata moja ambayo niliweza kung’amua maana yake.







    Nakumbuka nilikaa pale kwenye chumba changu cha ofisi ya nyumbani kuanzia muda huo wa saa saba mpaka karibia na saa tisa usiku nikitafakari ni nini hasa vitu hivi vilikuwa vinamaanisha. Nilijikuta akili yangu imejikita zaidi kwenye ile picha iliyopigwa kwa kificho sehemu yenye makontena ikimuonyesha Rais Albert Kafumu na mtu ambaye sikuweza kumtambua pamoja na wale wengine wawili ambao walionekana kama walinzi wa Rais. Roho yangu ilikuwa haitulii kabisa kila ambapo nilikuwa naiangalia hii picha. Kwa mazingira ya picha ile ilionekana dhahiri kuwa kulikuwa na suala nyeti sana ambalo lilikuwa likijadiliwa na kwa namna moja aua nyingine suala hili lilimfanya Rais ashindwe hata kuongea na mtu huyu ofisini kwake Ikulu.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Ilipotimia muda huu wa saa tisa usiku, nakumbuka nilirejesha zile picha na zile karatasi kama ambavyo vilikuwa mwanzoni kwenye bahasha na kisha nikaifunga bahasha na kuirejesha kwenye droo mezani. Nilirudi kitandani na kumkumbatia Cheupe wangu kwa kiasi fulani nikisahau hata kuhusu ugomvi wetu. Akili yangu ilikuwa imezama kwenye kutafakari kuhusu zile picha na karatasi ambazo nilizikuta kwenye bahasha. Nilijikuta akili yangu inapata kiu ya kutaka kujua ni nini haswa kilikuwa kinaongelewa kwenye zile karatasi na nini hasa kilikuwa nyuma ya pazia. Ndipo hapa ambapo nasema kuwa, shauku…. Curiosity… ni moja ya laana kubwa zaidi amabazo tumeumbwa nazo binadamu wote. Ilikuwa ni kana kwamba mbegu ilikuwa imepandwa kichwani mwangu na ilikuwa inamea. Haijalishi ni kwa kiasi gani kesho yake na wiki nzima baadae nilijitahidi kuilazimisha akili yangu iache kufikiri kuhusu nilichokiona kwenye bahasha ile, lakini kadiri nilivyojilazimisha kutokuwaza kuhusu ile bahasha na vilivyomo ndani yake ndivyo ambavyo shauku ya kutaka kujua iliongezeka maradufu.







    Ndipo siku moja kama wiki moja na nusu baadae nakumbuka nilikata shauri la kufanyia kazi hiki nilichokiona kwenye ile bahasha. Nilijifungia ndani ofisini kwangu nyumbani kwa masaa kadhaa niitafakari naanzaje?



    Kwa mujibu wa baba yangu siku ile Dodoma alinieleza kwamba natakiwa niende Zurich na kufuata maelezo ambayo nitayakuta ndani ya bahasha hiyo. Lakini changamoto ambayo nilikuwa nayo, nilikuwa sijaelewa chochote ambacho kilikuwa ndani ya ile bahasha aliyonipa. Kwa hiyo hata nikisema nifunge safari kuelekea Zurich nilikuwa sijui naenda kufanya nini nikifika huko. Ndipo hapa nikaamua nijaribu kitu fulani cha kijinga lakini kilikuja kuleta manufaa ya kunipa mwangu baadae kuhus suala hili.







    Nilichukua ile karatasi yenye anuani ya posta na maneno “remplacement” alafu nikaidurufu. Baada ya kuidurufu, nikachukua nakala na kuiweka kwenye bahasha nyingine niliyonunua, bahasha ya kawaida kabisa ya kutumia barua. Juu ya bahasha hii niliandika anuani ambayo ilikuwa kwenye karatasi ile, yaani;











    HUDINI



    AFFOLTERNSTRASSE 44



    CITYPORT



    POSTFACH 8131



    8050



    ZURICH



    SWITZERLAND.







    Yaani kwa maneno mengine ni kwamba nilikuwa natuma barua kwenda kwa huyo mtu au kampuni au ofisi ambayo inaitwa Hudini, na atakapoipokea ndani yake atakuta nakala ya karatasi ambayo ina anauani yake ya posta na neno moja tu “REMPLACEMENT”.







    Nikafunga bahasha hii vizuri na kwenda posta. Nikanuna stamp, nikabandika juu yake na kutuma barua yangu. Niliondoka pale posta huku natabasamu nikijicheka mimi mwenyewe huu ‘ujing’ ambao nilikuwa naufanya. Nilikuwa najicheka kwa sababu huyo mtu atakapoipokea hiyo barua hatojua imetoka kwa nani, kwa sabau sijaweka anuania yangu wala mawasiliano yotote yale. Nilituma ile nakala niliyo durufu kama ambavyo ilivyo.





    Nakumbuka zilipita kama wiki tatu hivi hivi, siku hii ilikuwa ni kama wiki moja baada ya Cheupe kujifungua. Nilikuwa natokea mjini sokoni kununua mahitaji kadhaa ya kutengeneza chakula cha mama mzazi. nikiwa nakaribia kabisa nyumbani kwetu Forest simu yangu ya mkononi iliita. Niliendelea kuendesha gari bila kuipokea, lakini nilipotupa jicho juu ya kioo cha simu nilishituka mpaka kujikuta napaki gari pembeni. Simu ilikuwa inaita lakini hakukuwa na namba yoyote ambayo ilikuwa inaonekana juu ya kioo. Niliangalia simu kwa sekunde kadhaa na kwa haraka nikakata shauri ya kuipokea.







    “do you have a pen?” sauti nzito ya kukoroma iliongea kwa lafudhi nzito ya kifaransa upande wa pili.







    “hallo.!!” Nilijikuta naongea bila kujibu swali ambalo nililisikia kabisa.







    “do you have a pen?” ile sauti nzito iliuliza tena vile vile.







    “yes… yes.. I have it!” nilijibu haraka haraka kwa kitete.







    “this is Hudini… write down… get to Zurich in twenty one days and call this number +41 44 256 56 56… call once and wait.!”







    “Hudini… who are you… hallo.. hallo… hallo!” simu ilikuwa imekatwa tayari.







    Nikatupa jicho kwenye kikaratasi nilichokuwa nimekiweka pajani huku naandika, sikumbuki haswa niliandika muda gani kwa jinsi ambavyo nilikuwa na hofu, lakini nilikuwa nimeandika kwa usahihi kabisa ile sentesi aliyokuwa ameiongea pamoja na namba za simu alizozitaja.







    Kwa mazingira yalivyoonyesha hili lilikuwa ni jibu la barua yangu ile niliyotuma wiki tatu zilizopita. Lakini nilijiuliza huyu Hudini alipataje namba yangu ya simu au alijuaje kuwa mimi ndiye niliyetuma ile barua?



    Swali hili lilinisumbua kichwani wiki nzima. Alinijuaje? Na je, nifanye nini? Nifanye uwendawazimu wa kwenda Zurich bila kujua nafauata nini aua naenda kukutana na nani?







    Kama nilivyosema kuwa, shauku… curiosity… ni moja ya laana kubwa zaidi tulizoumbwa nazo binadamu. Nilijikuta nafsi yangu inakosa raha kila nilipojishawishi kuwa niache kufuatilia suala hili. Hatimaye nikajifariji moyoni kuwa “maji nimeyavulia nguo, sharti niyaoge!”.



    Nikakamilisha taratibu zote za viza na hatimaye kusafiri mpaka hapa Zurich nilipo leo hii katika hoteli ya Radisson Blu Hotel mtaa wa Fracht West.







    Niliangalia bahasha juu ya meza ya chumba changu cha hotel tena na tena. Niliichukia bahasha hii na kuipenda pia. Bahasha hii na vilivyomo ndani ndivyo vimenileta hapa kufanya kitu ambacho eidha kitaniingiza kwenye matatizo makubwa au kunifungulia mwanga mkubwa mbele yangu.







    Nikavuta pumzi ndefu ndani na kuishusha. Huu ulikuwa ni muda sasa wa kukabiliana na ‘mashetani’ wangu. Ni muda wa kuonana na Hudini.







    Nikachukua simu yangu ya mkononi na kufanmya kama ambavyo nilielekezwa wiki tatu zilizopita… “get to Zurich in twenty one days and call this number +41 44 256 56 56.. call once and wait”.



    Sentensi hii ilinikaa kichwani na nilikuwa naikumbuka kwa ufasaha kama ambavyo nilikuwa nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa.







    Nikabofya zile namba na kubofya kitufe cha kupiga. Simu iliita kwa takribani dakika nzima bila kujibiwa mpaka ikakatika. Nilijua hii ndio sababu ya kuambiwa “call once and wait”. Nikaweka simu yangu juu ya kitanda na kusubiri kama ambavyo niliambiwa.







    Sikujua nilikuwa nasubiri nini? Mtu aje? Simu ipigwe? Au kitugani? Nilichokifanya ni kusubiri tu kama ambavyo nilielezwa… “call once and wait!”





    Nilikaa kwenye kiti na kuiangalia simu pale juu ya kitanda kwa muda wa karibia dakika kumi nzima. Kichwani nilikuwa najaribu kujiuliza kama nijaribu kupiga tena au niendelee kusubiri. Hakuna kitu ambacho kinatesa akili kuzidi mshawasha wa kusubiria simu muhimu ipigwe. Kila dakika iliyokuwa inapita nilikuwa naona kama mwaka mzima kwa jinsi ambavyo muda nilikuwa nauona unaenda taratibu sana.







    Nilisubiri kama dakika tano nyingine ndipo nikaona simu yangu inaita pale kitandani. Kama ambavyo ilikuwa siku ya kwanza, ndivyo hivyo pia ilikuwa siku hii ya nleo, simu iliita lakini hakukuwa na namba yoyote ambayo ilikuwa inaonekana juu ya kioo cha simu.







    “hallooo.!!” Nilipokea simu haraka haraka.







    “do you have a pen?” sauti nzito ya kukoroma kama ile kama ya siku ya kwanza iliongea kwa lafundhi nzito ya kifaransa.







    “aaah.. wait a second! Let me get it..!” nilitembea haraka haraka mpaka kwenye moja ya mabegi yangi na kuingiza mkono kwenye mfuko wa pembeni na kupapasa papasa mpaka nikapata kalamu, “I have it now!”







    “write down! Get out of your hotel… walk down the street for five minutes.. you will see a Chinese restaurant… the code is ‘Fox Wings’.!”







    “code name for wha….hallo…halloo..hallo..!” simu ilikatwa kama siku ya kwanza ilivyokuwa.







    Nikaikodolea simu macho kana kwamba nilikuwa namuangalia huyo aliyekuwa naongea nami. Uzuri nilikuwa na mkono mwepesi wa kuandika kwa hiyo kila ambacho alikuwa amenieleza nilikuwa nimekiandika kwenye kipande cha karatasi.







    Sikutaka kupoteza muda zaidi, nikachukua sweta na kulitupia mwilini na kisha kushuka mpaka chini ya hotel na kutoka nje kabisa. Hali ya hewa nje ilikuwa ya ubaridi wa wastani na msongamano wa watu barabarani ulikuwa umepungua kadiri usiku ulivyokuwa unakaribia.







    Nikiwa pale nje ya hotel nikajiuliza haswa ni upande gani ambao nilikuwa natakiwa kuelekea. Ile sauti kwenye simu ilinieleza tu “walk down the street”. Nikatafakari kama kwa muda wa kama sekunde ishirini hivi na hatimaye nikakata shauri kuwa niteremke kuelekea upande wa kushoto wa mtaa. Nilitembea mwendo wa dakika tano nzima kama ambavyo nilieklekezwa kwenye simu na hatimaye nikaona mgahawa wenye maandishi ya kichina upande wa pili wa barabara.







    Nilivuka barabara na kuingia ndani ya mgahawa na kuketi kama mteja mwingine yeyote wa kawaida. Ndani ya mgahawa. Wahudumu wote walikuwa ni watu wenye asili ya china na hata asilimia kubwa ya wateja niliowakuta walikuwa ni wakichina vile vile pamoja na wazungu wachache sana. Nilikuwa ni mteja pekee mwenye ngozi nyeusi humu ndani.







    Haukuwa mgahawa wa fahari sana au wa hadhi ya juu sana kama migahawa mingine ambayo nimeiona hapa Zurich. Ulikuwa ni mgahawa wa viwango vya kawaida tu japokuwa muonekano wake ulikuwa ni wa kuridhisha.







    “welcome Sir.!” Kijana muhudumu alinikaribisha huku anatabasamu baada ya kuketi. “what can I get you sir?”







    “just water please!” nilimjibu huku naangaza macho huku na huko kuangalia labda kuna dalili yoyote naweza kuiona kunisaidia hasa suala lililonileta hapa.







    Muhudumu aliitikia tu kwa kutingisha kichwa na kuanza kuondoka. Alipogeuza kisogo tu na kuanza kuondoka nilipata wazo.







    “excuse me.!” Nilimuita yule muhudumu.







    “yes sir.!” Aliniitikia na kurudi pale nilpoketi.http://pseudepigraphas.blogspot.com/







    “can I get some ‘fox wings’ please.!” Niliongea kwa kujiamini huku namuangalia usoni.







    Wazo lilinijia haraka tu kichwani kwamba labda muda huu ndio nilipaswa kutumia ile ‘code name’ niliyopewa na mtu niliyeongea naye kwenye simu kama dakika kumi zilizopita.







    Muhudumu mwanzoni alitabasamu na kuniangalia kama vile nimeongea neno la utani na alikuwa anasubri nisahihishe nilichokuwa nakisema. Lakini sikutabasamu, niliendelea tu kumkazia macho. Aliponiona niko ‘serious’ na naendelea kumtazama usoni bila kucheka wala kutabasamu, nikamuona uso wake unaanza kubadilika na kuwa na kiasi fulani hivi cha woga. Alinitumbulia macho kana kwamba alikuwa ameona jini.





    “right away sir.!” Alinijibu kwa unyenyekevu mkubwa uliopitiliza mpaka nikashindwa kuzuia mshangao wangu.







    Aliondoka huku anageuka nyuma mara kwa mara kuniangalia pale ambapo nimeketi. Akapinda kona kwenye mlango karibu na kaunta ya mgahawa na kuelekea nyuma ambako nilihisi ndiko jikoni.



    Muda ukapita kama dakika tano hivi nikawaona watu watatu wameibuka kutoka kule alikoenda na wamekuja sehemu hii ya wateja.







    “we are closed! Everyone get out please.!” Mzee mmoja wa makamo wa kichina aliongea kuwaambia wateja.







    Watu wote waliacha kula na kumuangalia huyu mzee kwa mshangao. Alionekana kwamba alikuwa ni mmoja wa wapishi huko jikoni kutokana na ‘aproni’ na kofia ya upishi aliyokuwa amevaa. Wenzake wawili alioongozana nao walikuwa ni vijana wa kichina waliovalia suti nadhifu na kwa namna fulani walionekana kama vile ni walinzi wake.







    Nilisikia wateja kadhaa wakining’unika kuwa hawajamaliza kula wengine wakionekana kuwa walikuwa hawajamaliza mazungumzo yao na manung’uniko mengine ya kila namna.







    “I said everyone get out NOW.!!”







    Yule mzee aliongea kwa sauti fulani ya ukali na ya kimamlaka zaidi kuonyesha kuwa alikuwa hatanii alichokuwa anakiongea na alikuwa anataka haswa kila mtu aliyepo hapa atoke nje sasa hivi. Nahisi wateja wote walisoma uzito wa sauti aliotumia na mara moja nikaona kila mtu anainuka haraka haraka na kuanza kuondoka.







    Kwa namna fulani ambayo sikujua ni kwa nini nilijikuta akili yangu inanishawishi kuwa watu nisitoke nje. Kwa hiyo nikasubiri tu.







    Wateja wote walikuwa wametoka nje ya mgahawa na kuondoka. Ajabu ni kwamba hata dada wa kichina ambaye nilimuona pale kwenye kaunta wakati naingia naye alikuwa ameondoka. Na sisi yeye tu, hata wahudumu wengine wote walikuwa wameondoka. Kwa hiyo pale tulibakia mimi, huyu mzee wa kichina na vijana wawili waliovalia suti ambao aliongozana nao.







    “what are you waiting for young man?” yule mzee aliniuliza huku amenikazia macho akipiga hatua za taratibu kunifuata pale ambapo nilikuwa nimeketi.







    Mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio kweli kweli na presha ilikuwa imepanda juu haswa lakini nilijitahidi kwa kila namna nisionyeshe hofu niliyokuwa naipata ndani yangu kwa muda huu.







    “I’m waiting for my ‘fox wings’.!” Nilimjibu kwa sauti thabiti kabisa pasipo kuonyesha chembe ya hofu kwenye sauti yangu.







    Yule mzee akatabasamu na kuja kukaa kwenye kiti cha upande wa pili kwenye ile meza ambayo nilikuwa nimeketi. Alipoketi alinitazama kwa takribani dakika nzima akiwa anatabasamu tu bila kuongea neno lolote lile.







    “I have been waiting for this moment my whole life… its nice to finally meet you Rweyemamu.!” Mzee aliongea kwa tabasamu la furaha huku ananipa mkono.







    “Do I know you? Who are you?” nikauliza kwa mshangao baada ya kusikia huyu mzee wa kichina ambaye ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kumuona maishani lakini alikuwa analijua jina langu kwa ufasaha kabisa.







    “aah don’t worry about me…. (anaongea kichina huku anamuangalia moja ya wale vijana aliokuja nao)..”







    Katika maneno yale ya kichina ambayo aliongea sikuweza kung’amua chochote kile lakini nilifanikiwa kusikia maneno ‘fox wings’ yakitajwa.







    Kijana mmoja kati ya wale wawili aliondoka kutoka pale ambapo tulikuwa na kwenda kule kwenye chumba cha jikoni ambako walitokea. Nikajikuta macho yangu yameganda kwenye zile suti nyeusi ambazo wale vijana walikuwa wamevaa. Kila nilipowaangalia, nilijikuta kichwani mwangu nakumbuka suti za jumuiya ya The Board namna ambavyo walipendelea wote kuvaa suti nyeusi kama hizi.



    Yule mzee alikuwa ananiangalia kwa makini sana kila kitu ambacho nilikuwa nakiangalia. Nadhani alifahamu ni nini hasa kilikuwa kinaendelea kichwani mwangu nikiwa nawatazama wale vijana. Nilpogeuza macho na kumtazama alitabasamu tu pasipo kusema neno lolote lile.







    Yule kijana aliyeondoka kwenda kwenye chumba cha jikoni alirejea akiwa na briefcase mkononi na akaliweka juu ya meza mbele ya mzee huyu wa kichina.







    “These are your fox wings.!” Yule mzee aliongea huku anatabasamu.





    Sikujibu chochote kile nikaendelea tu kumtazama.







    Akafungua ile briefcase taratibu na kisha kuanza kutoa vitu kadhaa kutoka ndani yake. Macho yangu hayakuganda kwenye vile vitu ambavyo alikuwa anavitoa bali yaliganda kwenye upande mmoja wa ndani wa ile briefcase. Ulikuwa na rangi ya zambarau ya kukoza sana na kati kati yake kulikuwa kumechorwa kichwa cha samba kwa rangi ya dhahabu. Pembezoni mwa mchoro huu wa kichwa cha simba kulikuwa na nakshi za kufanana kabisa kama na kito cha sapphire zikiwa zimezunguka mchoro huu wa kichwa cha samba.







    Mchoro huu ulinikumbusha kabisa zile pini za walizokuwa wanavaa wanachama wa The Board juu ya suti zao kwenye ukosi kukaribia usawa wa titi. Tofauti pekee ilikuwa ni zile nakshi za vito vya sapphire kuzunguka mchoro wa kichwa cha samba.







    Yule mzee hakuonekana kujali mshangao wangu aliendelea tu kutoa vifaa kadhaa kutoka kwenye lile briefcase na kuviweka juu ya meza. Alitoa mabomba mawili ya sindano, chupa ndogo ambayo nilihisi ilikuwa na ‘spirit’, pamba, mpira wa kufunga mkono, na kichupa kingine kidogo chenye kimiminika ambacho sikukijua mara moja.







    Alipomaliza kutoa ila kitu alichokihitaji alinitazama kwa mara ya kwanza uso ukiwa ‘serious’.







    “Give me your left hand!” mzee aliongea huku anachukua mpira wa kufunga mkono kama ile itumiwayo na hospitalini wakati wa kutafuta mshipa wa damu.







    Nikiangalia vile vifaa alivyoviweka pale mezani na kauli yake kwamba nimpe mkono wa kushoto, nilielewa fika kuwa alikuwa anataka kunichukua damu na lile bomba la sindano.



    Kitendo hiki kilinikumbusha siku ile ya kwanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita nilipoenda gorofa la PPF HOUSE na kutolewa damu. Ilikuwa ni kana kwamba kitu hiki kilikuwa kinataka kujirudia tena. Tofauti tu kwa sasa nilikuwa nimeisambaratisha jumuiya yote ya The Board na nilikuwa Zurich sio posta Dar es salaam.







    “what are you doing?” nilimuuliza yule mzee kwa sauti ya mshangao na mshituko.







    “I need to verify you!” yule mzee alinijibu kwa kifupi tu.







    “verify me about what?” niliuliza tena kwa mshangao mkubwa zaidi.







    “Ray, if you are not ready for this you can go back home.! Its your choice...no one is forcing you to do anything.!” Mzee aliongea kwa upole mno na ustaarabu.







    Kauli hii nayo ilinikumbusha siku ile pale PPF HOUSE nilipokuwa nasita sita kumpa mkono yule mama anitoe damu niliambiwa hivi hivi kuwa kama bado siko tayari naweza kwenda tu.







    Kama ambavyo siku ile ‘nilijilipua’ na kumpa mkono yule mama ndivyo hivyo navyo nilifanya leo hii. Bila kufikiria mara mbili mbili nilinyoosha mkono na kumpa yule mzee.







    Alinifunga mpira katikati ya mkono, kisha akapaka spirit sehemu fulani mkononi mbapo mishipa ilionekana vizuri kisha akaingiza sindano na kutoa damu ya kutosha kabisa kujaza bomba lote.



    Akaichukua ile sindano na kuirudisha ndani ya briefcase.







    Tofauti na siku ile PPF HOUSE ambayo nilitolewa damu tu lakini mzee huyu nilimuona anachukua bomba lingine la sindano na kunyonya kimiminika mabcho kilikuwa kwenye chupa ile ndogo. Nilielewa kabisa kwamba hiki kinachotokea leo ni tofauti kabisa na kile ambacho kilitokea siku ile pale PPF HOUSE na sikudhania tena kama kuna uhsuika wowote wa The Board ukizingatia kwamba jumuiya hii nilikuwa nimeisambaratisha tayari.







    Akachukua tena mkono wangu na kunichoma sindano yenye ile kimiminika nisichokijua. Kuna upande fulani wa nafsi yangu ulikuwaunaniambia kuwa nilikuwa nafanya jambo la kipuuzi kuruhusu yote haya yafanyike, lakini kila nilipo fikiria nilivyosafiri umbali wote huu ili kufika wakati huu, nilijikuta natamka tu ‘liwalo na liwe’, maji nimeyavulia nguo sharti niyaoge.







    Baada ya kunichoma sindano hii, nilimuona anakusanya kusanya vitu vyote pale mezani na kuvirudisha tena kwenye briefcase na kumpa yule kijana akaondoka nalo.







    Mwili niliusikia unaishiwa nguvu kabisa na kama kizungu zungu kikali kilikuwa kinanijia kwa kasi ya ajabu.







    “what is happening?” niliuliza kwa suati ya ulevi kama vile nimelewa pombe.





    Yule mzee hakusema chochote kile. Alitabasamu. Lakini tabasamu lake lilikuwa la kifedhuli safari hii. Kwa namna nilivyoliona halikuwa tabasamu la kheri.







    “sweet dreams Ray.!!” Mzee aliongea taratibu huku bado akiwa na lile tabasamu la kifedhuli usoni mwake.







    Aliinuka na kuondoka pale tulipo akiwa na yule kijana aliyesalia. Nilibaki peke yangu pale mgahawani. Nilijaribu kuinua miguu lakini ilikuwa kama vile imekufa ganzi. Nilishindwa kuinua hata kidole cha mkono. Ilikuwa kana kwamba ghafla mwili wote umepooza.







    Nikaanza kuona kiza mbele yangu. Macho yakawa kama vile yanapoteza nuru. Usingizi mkali wa ajabu ukaanza kuujaza ubongo wangu. Jasho lilikuwa linanitoka nikijua kuwa kuna jambo baya sana liko mbele yangu. Nilishindwa tena kuendelea kufumbua macho, taratibu yakajifunga. Na mara moja nilipoteza fahamu.







    Niliamka kichwa kikiwa kizito na kikiniuma haswa. Nilianza kupepesa macho huku na huko ili niweze kutambua ni mahali gani hasa nilikuwepo muda huu. Nilikuwa nimelala juu ya sofa kwenye lichumba likubwa au kiuhalisia haswa hapapaswi kuitwa chumba bali lilikuwa ni ghala kubwa ambalo lilikuwa linaonekana halitumiki kwa sasa.



    Nilijitahidi kujiiunua kutoka pale kwenye sofa kwa taabu kiasi kutokana na kichwa kuwa kizito na kizunguzungu kwa mbali ambacho nilikuwa nakisikia. Nilijitahidi hivyo hivyo mpka nikainuka na kukaa kitako pale sofani.







    Hili lichumba lilikuwa ni kubwa hasa, na kama ambavyo nilihisi lilikuwa ni ghala ambalo kwa sasa lilikuwa halitumiki. Pale ndani kulikuwa na hili sofa nililokalia, pia mbele yangu kulikuwa na kiti na meza vya kiofisi huku pale juu ya meza kukiwa na makororo mengi mno pamoja na kompyuta. Pembeni ya hii meza kulikuwa na kiti kingine. Taa iliyokuwa inatia mwanga kwenye lichumba hili ilikuwa inaning’inia juu kutoka darini kwa waya wake wa umeme.



    Kwa namna fulani chumba hiki kilikuwa kinanikumbusha vyumba vya mateso ambavyo nimekuwa naviona kwenye sinema za kuigiza watu wakiwa wanahojiwa huku wakipigwa na kupewa mateso ya kikatili ya kila namnaa.



    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Nilijaribu kwa uwezo wangu wote niweze kujua ni mahali gani ambapo nilikuwa lakini bado nilishindwa kung’amua. Ukizingatia ugeni wangu kwenye nchi hii ndio kabisa nilishindwa hata kuhisi tu niko mahala gani aumtaa gani. Kitu pekee nilichokuwa nakumbuka ni kile ambacho kilitokea pale kwenye mgahawa wa kichina. Nakumbuka namna ambavyo yule mzee wa kichina aliponitoa damu na kisha kunichoma sindano ya kimiminika fulani na baada ya hapo mwili uliisha nguvu na uanza kuona giza mbele yangu na kisha kupoteza fahamu.





    ”helloooooo”





    Niliita ili kujua kama kuna mtu yeyote hapa zaidi zaidi yangu.





    ”helloooooo…anybody in here??”





    Kimya!





    Nikainuka kutoka kwenye sofa na kusimama. Niliendelea kkupepesa macho kila kona ya chumba ili kuona kama kulikuwa na mtu yeyote mule ndani zaidi yangu lakini bado nilihisi upweke tu wa chumba kizima. Dhahiri kabisa hakukuwa namwingine yeyote humu zaidi yangu.



    Nikatembea kwa hatua za taratibu ili nisidondoke kutokana na kichwa bado kuwa kizito na nilikuwa nasikia kizunguzungu. Nilikwenda mpaka kwenye meza ile yenye makorokoro na kompyuta juu yake.







    Nilitazama kwa makini kila kitu ambacho kilikuwa juu ya meza lakini sikuona maana yoyote ambayo ilikuwa inajengeka kichwani au kunipa maana ya chumba hiki kwa kuangalia vitu hivi juu ya meza. Makorokoro yalikuwa mengi sana pale mezani kiasi kwamba yalikuwa kama uchafu fulani hivi. Kulikuwa na bisibisi, CD zilizovunjika, spea za simu, hard disc za kompyuta, nati za vitu nisivyovijua, na makorokoro mengine mengi kweli kweli. Nilijaribu kufikiri na kufikiri na kufikiri tena, nikijaribu kuunganisha picha, au tuseme kuunganisha matukio na haya makororkoro yaliyopo hapa na hili lichumba, labda niweze kung’amua hapa ni wapi au hiki chumba ni cha dhumuni gani lakini sikuwa Napata jawabu lolote la kuridhisha kichwani.







    Nikakaa kwenye kiti pale mezani na kuanza kutafakari. Nikatupa jicho upande mmoja wa lile lijichumba na kuona mlango. Nilitamani kuuendea ule mlango na kujaribu kuufungua labda niondoke kama hakutakuwa na mtu yeyote yule wa kunizuia lakini upande fulani wa roho yangu ulikuwa hautaki kuondoka mahali hapa mpaka nijue ni nini hasa kilikuwa kinaendelea hapa.







    Sikutaka kufikiri zaidi na kuumiza kichwa, mara moja niliinuka na kuufuata mlango ambao ulikuwa upande mmoja wa chumba hiki na kuufungua. Ajabu ni kwamba mlango ulifunguka tofauti na nilivyofikiri labda utakuwa umefungwa na kwa funguo.



    Nilipotoka nje ya mlango nilikutana na korido ndefu lakini hakukuwa na chumba kingine chochote au mlango mwingine bali ilikuwa ni korido ndefu tu. Niliifuata korido hii mpaka mwisho ambako nilikutana na mlango mwingine ambao nao nilipoufungua, ajabu nao haukuwa umefungwa. Ulifunguka bila tabu.





    Nilipofungua, nilitokea nje kabisa kwenye uchochoro katikati ya majengo mengine ya mtaa. Yaani jengo hili ambalo nilikuwa imetoka, lilikuwa ni ghorofa ambalo lilikuwa katikati ya maghorofa mengine na chumba ambacho nilikuwepo kilikuwa kipo ‘ground floor’. Nilipoangalia mbele, mwishoni kabisa wa huu uchochoro niliona unaenda kutokea kwenye barabara kuu japokuwa sikuweza kuona gari lolote likipita au watu kutembea pembezoni mwa barabara. Uchochoro pamoja na mtaa wote huu ambao uchochoro ulikuwa unaenda kutokea, ulikuwa kimya sana. Nilihisi labda tayari ilikuwa ni usiku sana maana sikujua ni kwa muda gani nilikuwa nimepoteza fahamu tangu muda ule nilipokuwa pale kwenye mgahawa wa kichina.







    Niliinua kichwa juu kulitazama hili jengo la ghorofa ambalo nilikuwa nimetoka. Lilikuwa ghorofa fulani hivi la namna ya majengo ambayo ukiyaangalia yanaonekana ni jengo la zamani sana na kuu kuu lakini linakupa picha kuwa ‘enzi zake’ lilikuwa ni moja ya majengo ya kifahari. Tofauti na maghorofa ya kisasa ambayo yanakuta za vioo kuanzia chini mpaka ghorofa ya mwisho, ghorofa hii yenyewe ilikuwa imejengwa kwa vitofali vidogo vidogo sana vya kuchoma.







    Pale mlangoni nilipotokea kulikuwa na na kijimbao fulani kidogo cha saizi ya kati ambacho kilikuwa na maandishi ya kuonyesha anuani ya jengo hilo kama ilivyo desturi ya majengo yote niliyoyaona hapa Zurich. Nikatupa jicho langu kwenye hiki kijimbao na kusoma anuani.





    HARDSTRASSE 201, 1985







    Nilielewa kuwa hapa nilipo ni mtaa wa Hardstrasse, ambao ni mtaa namba 201 na hili jengo ni jengo namba 1985. Sikujua ni kwa nini lakini nafsi yangu ilikuwa kama inakorofisha hivi kwa ndani baada ya kusoma kibao hiki kidogo cha anuani.







    Nikaanza kutembea kuufuata ule uchochoro kuelekea kule mbele ambako niliona ulikuwa unaenda kukutana na barabara kubwa. Nilitokeza mpaka barabarani. Magari machache sana yalikuwa yanapita kila baada ya dakika kadhaa na pembezoni mwa barabara sikuona watu wowote wale wakipita. Maduka mengi na biashara zilikuwa zimefungwa. Nilihisi kwa hakika kabisa huu utakuwa ni katikati ya usiku.







    Ile hali ya kukorofishika nafsini mwangu ambayo niliisikia baada ya kusoma kile kibao cha anuani iliendelea ndani yangu japo sikujua ni kwa nini nilijisikia namna ile.





    Nikaangaza macho kila upande wa mtaa kutoka pale ambako nilikuwa nimesimama kujaribu labda kuona kama kuna taxi itapita niweze kusimamisha. Mpaka muda huu nilikuwa sijajua niko mahala gani, na ukweli ni kwamba nilikuwa sina hata uhakika kama bado nilikuwa Zurich au mji mwingine ndani ya Switzerland ingawa jina la mtaa huu lilinifanya nihisi kuwa bado nilikuwa Zurich. Kwa hiyo tegemeo langu pekee la kuweza kurejea hotelini kwangu ni kupata taxi ili iweze kunipeleka.







    Nikiwa bado nimesimama pale nikiwaza na kuwazua na labda kuendelea kutumaini muda wowote taxi yaweza kutokea na kunirejesha hotelini, ghafla ‘taa’ ikawaka kichwani mwangu. Wazo la ghafla likajiumba kichwani mwangu. Nilijisikia ile hisia mtu unaipata pale ghafla unapofanya gunduzi ya kitu fulani cha siri sana kilichojificha. Ilikuwa ni ile anuani; Hardstrasse 201, 1985. Nilihisi kuwa kuna ujumbe wa siri umefichwa kwenye anuani hii. Hasa mfuatano wa hizi namba, 201,1985. Mara ya kwanza niliposoma sikugundua ni nini hasa kilikuwa kimejificha kwenye maandishi haya lakini roho yangu nilisikia haina raha. Sasa hivi nilihisi nimetambua kwa nini roho yangu ilishituka niliposoma anuani hii.







    Tarehe yangu ya kuzaliwa ni tarehe 20 Januari mwaka 1985. Au kama itaandikwa kwa namba tupu, itakuwa ni 20-1-1985, na jengo hili lilikuwa na anuani ya 201, 1985. Hii ilikuwa ni bahati mbya au? Katika majengo yote yaliyopo hapa Zurich, well kama bado niko Zurich! Lakini katika majengo yote yaliyopo hapa iweje nije kutupwa au kuletwa au kufichwa kwenye jengo lenye anuani sawa kabisa na tarehe yangu ya kuzaliwa.? Kuna ujumbe au jambo ambalo limejificha? Au ni bahati mbaya tu?





    Yawezekana ni bahati mbaya tu lakini akili yangu haikutaka kukubali kirahisi namna hii. Niliamini kabisa hapa kuna jambo la zaidi. Nikageuza na kuanza kurejea kwenye ule uchochoro. Kisha moja kwa moja niliufuata ule mlango ambao nilitokea. Niliufungua kwa haraka na kuingia ndani na kutokea kwenye ile korido ndefu.



    Moja kwa moja nikaelekea mpaka kwenye ule mlango wa lile lichumba likubwa au ghala ambalo muda mchache uliopita niliamka nikiwa ndani yake.







    Kuna kitu kuhusu chumba hiki ambacho mara ya kwanza nilikuwa sijakigundua na nilikigundua safari hii baada ya kujaribu kufungua mlango na kugoma kufunguka. Pale pembeni ya mlango kulikuwa na kama screen ndogo hivi ama ‘tablet’ iliyogandishwa ukutani usawa wa kitasa ambayo katikati ya ile screen kulikuwa na alama ya kiganja cha mkono kimechorwa. Nilielewa kuwa ili mlango huu uweze kufunguka ulikuwa unatumia teknolojia ya kusoma alama za vidole ili kuruhusu muhusika halali tu kuingia ndani ya chumba hiki. Lakini kwa kuwa nilipotoka nilitoka tu bila kipingamizi chochote cha kuthibitisha alama za vidole mlangoni, hivyo niliamini kuwa teknolojia hii ya kuthibitisha alama za vidole ilikuwa inalinda pale tu mtu akitaka kuingia ndani lakini kwenye kutoka hakukuwa na shida yoyote ile.







    Nikaanza kuchakata akili kichwani. Nifanyeje ili kuruka hiki kizingiti cha kuthibitisha hizi alama za vidole. Pale juu ya hii screen kulikuwa na kitufe kimeandikwa enter. Nikabofya hapo. Nikaona ile screen kama imewaka kwa kutoa mwanga kama vile inavyokuwa uwashapo simu ikiwa imezimwa. Sijui ni kitu gani kilinikuta kichwani lakini pasipo kufikiria mara mbili mbili nikaweka kiganja changu pale juu ya screen. Nikaona mwanga wa kijani umetokea kumaanisha kuwa alama zangu za vidole zilikuwa zinatambulika na zilikuwa sahihi na nilikuwa na ruhusa kuingia ndani ya hiki chumba.





    Moyoni nilishituka haswa, na zaidi ya kushituka nilijikuta Napata hofu zaidi. Kwanza anuani ya jengo inayofanana na tarehe yangu ya kuzaliwa. Sasa hivi alama zangu za vidole vinatambuliwa na hii teknolojia ya ulinzi hapa mlangoni? Hii inawezekanaje? Sijawahi kufika kwenye jengo hili tangu nimezaliwa, na hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika hapa, na sina uhakika nimefika fikaje hapa… alafu ati alama zangu za vidole vinatambuliwa kwa usahihi kuwa nina ruhusa ya kuingia humu?







    Sikutaka kupoteza muda zaidi kufikiri. Nikaingia ndani ya lile lijichumba.





    Nilipoingia tu ndani nikasimama katikati ya chumba na kupepesa macho kila kona ya lile lijichumba. Nilibaki najiuliza tu. Hivi kuna kitu gani hasa ndani ya chumba hiki mpaka mtu afikie hatua ya kukiwekea teknolojia ya ulinzi wa alama za vidole?





    Nilitazama lile sofa ambalo mara ya kwanza niliamka nikiwa juu yake. Nikatazama ile meza yenye makorokoro na kompyuta juu yake. Nikahisi labda kuna kitu fulani kwenye hii kompyuta.



    Nikatembea na kuifuata mpaka pale mezani na kuketi kwenye kiti. Nikainama chini kuangalia nyaya zake kama ziko sawa sawa. Niliziona zote ziko sawa na zimechomekwa kwenye chanzo cha umeme. Nikaiwasha na mara moja iliwaka. Ilikuwa ni kompyuta fulani hivi si ya kizamani sana lakini pia haikuwa ya kisasa. Ilipowaka na kuanza kuperuzi ndani yake sikupata chochote. Hakukuwa na file wala document yoyote ndani ya kompyuta hii. Ilikuwa kama vile ilikuwa ni mpya kabisa kutoka dukani.







    Nikatulia na kuegemea kiti. Nilianza kupata hisia kuwa kuna kitu fulani hivi nilikuwa siangaliia kwa umakini. Nilitulia kwa takribani dakika tatu nzima nikifikiri na huku nikipepesa macho pale chumbani kutoka kitu kimoja mpaka kingine mpaka macho yangu yaliporudi tena kwenye hii meza. Lakini safari hii yalitua kwenye kitu cha muhimu zidi ambacho nilikuwa sijakifikiria muda wote huu. Droo za hii meza. Nikaanza kuvuta droo moja moja na kuzikagua ndani yake. Droo zote mbili za mkono wa kushoto zilikuwa tupu. Nikahamia droo za mkono wa kulia. Nilipofungua tu droo ya juu kabisa nilikuta bahasha ya ukubwa wa A4. Juu yake ilikuwa imeandikwa;





    20-1-1985





    Tarehe yangu ya kuzaliwa na pia anuani ya jengo hili.





    Nilihisi kama vile mkono unatetemeka. Nikaifungua taratibu sana ile bahasha. Ndani yake nilikuta simu ya mkononi pamoja na ‘flash disk’. Nikaiweka simu pembeni. Mshituko nilioupata ulikuwa unanifanya nifanye vitu kama roboti. Taratibu. Nikiwa nimeduwaa tu usoni.





    Nikachomeka ile flash disk mahali husika kwenye kompyuta kisha nikaanza kuiperuzi ndani ya kompyuta. Flash disk hii ilikuwa na file moja tu ndani yake. Tena file la video yenye kichwa cha habari 004W01.





    Nikabofya ili kuicheza ile video.





    Sikuamini macho yangu kile ambacho nilikuwa nakiona mbele yangu. Alikuwa ni marehemu baba yangu, Mzee Charles Bernard Kajuna. Mwenyekiti wa The Board.







    ”Naitwa Charles Bernard Kajuna. Mwenyekiti wa The Board. Hii ni recording namba 004W01..”





    Alianza kwa kujitambulisha video ilipoanza tu kucheza.





    Mshituko ambao niliupata ndani yangu nilihisi kama vile dunia nzima imedondoshwa juu ya kichwa changu. Presha nilihisi imepanda na kijasho kikaanza kutoka. Nikaongeza sauti ili nisikie sawia alichokuwa anataka kukiongea.





    “Naitwa Charles Bernard Kajuna. Mwenyekiti wa The Board. Hii ni recording namba 004W01..”





    Kwenye screen ya kompyuta alikuwa ni marehemu baba yangu, mzee Charles Kajuna. Nilikuwa nimepata mshtuko makubwa hasa… lakini nilijikuta naongeza sauti ili niweze kusikia sawia kile ambacho kilikuwa kinaongelewa.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Mwanangu Rweyemamu..!”



    Mzee alianza tena kuongea kana kwamba alikuwa anaongea nami mubashara. Japokuwa ilikuwa ni ‘recording’ lakini jinsi ambavyo alikuwa anaitazama kamera iliyokuwa inamrekodi na jinsi ambavyo alikuwa anaongea ilikuwa ni kama vile alikuwa anaongea nami katika maisha hakisi akiwa mbele yangu muda huu.

    Nilijikuta nami namuangalia usoni pale kwenye screen kana kwamba ni mtu halisi.





    “Video hii imetengenezwa kwa namna ambayo itacheza mara moja tu na kisha kujifuta… hivyo ni vyema uwe na kalamu na kipande cha karatasi.!”



    Aliposema hayo akanyamaza kidogo kama vile alikuwa ananipa mida nitafute kalamu na karatasi.



    Nikaanza kuhangaika haraka haraka pale mezani nikifungua kila droo kutafuta kalamu mpaka nikaipata kwenye droo ya chini kabisa. Nikachukua ile bahasha ambayo ilikuwa imewekewa simu na flash disk na kuamua niitumie kuandika hiki ambacho kitakuwa kinazungumzwa hapa.





    “Kama leo hii unatazama ujumbe huu, ni matumaini yangu kwamba nitakuwa nimeshafariki… na labda umekuwa ukitafuta majibu ya maswali mengi kichwani au labda umefuata maelekezo yangu na hatimaye kufikia hapa na kukutana na ujumbe huu. Ujumbe huu ni mahususi kwa ajili moja kuu. Nataka uelewe kuhusu siri kuu zaidi kuhusu ulimwengu wetu na zaidi ni kuhusu nchi yako Tanzania. Na kisha ujue jukumu ulilonalo. Kama jumuiya ya The Board bado ipo na inafanya kazi nataka ubonyeze kotufe namba moja kwenye keyboard ili usikie ninacjotaka kukueleza. Pia kama kwa namna fulani jumuiya ya The Board imesambaratika, naomba ubofye kitufe namba mbili hapo kwenye keyboard. Kumbuka ujumbe huu utacheza mara moja tu na kujifuta hivyo kuwa makini na chaguzi yako.!”





    Video kwenye screen ikaganda kama vile imewekwa ‘pause’ uku sura ya marehemu baba yangu ikiwa juu ya screen imeganda sehemu ya mwisho pale alipoongea.



    “Kama The Board imesambaratika bofya kitufe namba mbili”. Nikairudia tena kichwani ile sentesi. Nikabofya kitufe namba mbili kwenye keyboard.



    Video ikafanya kama imezimika kwa kuonyesha rangi nyeusi screen yote, kisha ikaanza tena kucheza.



    “Kwa kuwa The Board imesambaratika kabisa… sababu kuu ya kukuongoza uje hadi hapa Zurich ni kukufahamisha uelewe hasa Th Board tulikuwa na lengo gani kuu na kama utakubali nataka ukishaelewe hilo lengo ulibebe wewe binafsi na kulitekeleza.!”





    Nilijikuta naanza kutamani kuzima huu ujumbe nisiendelee kuusikiliza. Huu ulikiwa ni zaidi ya uwendawazimu. Nawezaje kukubali kufanya jukumu la jumuiya ambayo nilihatarisha mpaka maisha yangu ili niisambaratishe?



    “Kuna mambo matatu tu ambayo nitakueleza katika ujumbe huu. Moja. Hili jengo ulilomo ndani yake limekodiwa kwa niaba yako kwa muda wa miaka mitatu. Si ghorofa lote, ni hapa ulipo na floor nyingine mbili kwenda juu. Kwa muda wa miaka mitatu ijayo pengine hii itakuwa ndio sehemu muhimu zaidi na salama kwako kuliko zote. Nyaraka zote kuhusu jengo hili ziko ukutani upande wa wa chumba hiki row namba tano kutoka chini. Password ni anuani ya jengo hili.!”





    “Sielewi unachoongea!!” Nilijikuta naropoka kwa nguvu kabla ya kukumbuka kwamba nasikiliza na kuangalia recording ambayo imerekodiwa labda miaka kadhaa iliyopita. Niliandika haraka haraka kile ambacho alikuwa anakiongea.





    “Mbili. Nadhani umepata simu ya mkononi ikiwa pamoja na kifaa chenye ujumbe huu unaoutazama. Ukimaliza kutazama nyaraka za jengo hili bofya ‘speed dial 1’ kwenye simu!”





    Akanyamaza tena kidogo.



    “Tatu. Recording namba mbili. Jina Charles Bernard Kajuna. OLYMPIAN KINGS. Kilala kheri Ray!”



    Ghafla video ikaacha kucheza na kuwa rangi nyuesi tu juu ya screen.





    “What the….” Nilijikuta nang’ata midomo kwa hasira.



    Sikuelewa karibia asilimia mia Themanini ya kilichokuwa nakisikiliza hapa.



    Hili suala la tatu ndio sikuelewa hata robo. “Recording namba tatu. Jina Charles Bernard Kajuna. OLYMPIAN KINGS”. Ni kitu gani alikuwa anaongea?



    Nikajaribu kucheza tena ile video. Kila nilipojaribu iliniandikia tu ” this file doesn’t ezist!”



    “Fuuuuccckk.!” Nikajikuta natoa tusi kwa nguvu na kusimama kwa hasira.



    Mkononi bado nilikuwa nimeshikilia kile kikaratasi nilichokuwa nakiandika. Nilijaribu kukipitia tena haraka haraka kile ambacho nilikuwa nimekiandika. Mwanzoni nilirudia kusoma tena na tena kile ambacho niliandika kuanzia mwishoni. Ule ujumbe namba tatu. Lakini kadiri nilivyourudia ndivyo ambavyo ulizidi kunichanganya. Ikabidi nianze kukisoma nilichoandika kuanzia mwanzoni.



    Nilipoanza kusoma kutoka mwanzoni walau nilielewa. Nilisoma tena kile ambacho mzee, ujumbe wa kwanza.



    “Moja. Hili jengo ulilomo ndani yake limekodiwa kwa niaba yako kwa muda wa miaka mitatu. Si ghorofa lote, ni hapa ulipo na floor nyingine mbili kwenda juu. Kwa muda wa miaka mitatu ijayo pengine hii itakuwa ndio sehemu muhimu zaidi na salama kwako kuliko zote. Nyaraka zote kuhusu jengo hili ziko ukutani upande wa wa chumba hiki row namba tano kutoka chini. Password ni anuani ya jengo hili.!”





    Japokuwa sikuelewa maana kamili ya ujumbe wote lakini walau nilikuwa na pa kuanzia.





    Niliikatembea mpaka kwenye ukuta wa upande wa kulia wa hiki chumba. Ulikuwa ni ukuta wa aina fulani hivi ambao umejengwa kwa matofali ya kifahati ya kuchoma.



    Sikuelewa hasa nilikuwa natakiwa kufanya nini, lakini nilikumbuka ile kauli aliyosema kwamba “row namba tano kutoka chini.!” Nikahesabu mstari kwa mstari kutoka chini sakafuni mpaka nikafika mstari wa tano wa matofali. Nilipoufikia mstari wa tano nilibaki nadokoa macho tu nisijue nifanye nini. Pamoja na maelezo haya ya ‘row namba tano’ pia nimeelezwa kuwa password ni anuani ya jengo hili. Sikujua hata ni namna gani napaswa nitumie password kwenye haya matofali.



    Nikainama na kuweka sikio langu, pengine labda kuna sauti fulani nitasikia, lakini wapi hakukuwa na chochote.

    Nikajaribu kugonga gonga kwa vidole kama napiga konzi yale matofali, mara ya kwanza sikugundua. Lakini nilipogonga gonga tena mara ya pili kama napiga konzi nilisikia sauti fulani hivi yale matofali yanatoa. Sauti kana kwamba kwa ndani kuna uwazi fulani hivi. Yaani kana kwamba nyuma ya haya matofali kulikuwa na uwazi mkubwa kama shimo au sanduku.



    Nikajaribu kusukuma haya matofali lakini hakuna ambacho kilitokea.



    Nilirudi mpaka pale juu ya meza kwenye makorokoro. Sikumbuki kama nilichukua spana au nondo, ninachokumbuka ni kwamba nilichukua kitu fulani kizito kutoka pale mezani na haraka nikaenda pale ukutani na kuanza kugonga kwa nguvu kuyaondoa yale matofali.



    Kadiri ambavyo nilikuwa nagonga na kuyaondoa matofali ndivyo ambavyo ule uwazi uliomo nyuma yake kulikuwa dhahiri.



    Nikaondoa matofali ukubwa wa eneo la kama mita moja hivi kutoka chini kwenda juu na upana.





    Mbele yangu, ndani ya ule ukuta ilikuwa imefichwa ‘vault’ ndogo ambayo ilitengenezwa kwa kufunikiwa na zege nzito ukutani.





    Sikutaka kupoteza muda… nilielewa bayana kwamba hapa ndipo ambapo ninatakiwa kutumia hiyo password ambayo ni anuani ya hili jengo.

    Nikaifungua ile vault kwa kutumia anuani;





    2-0-1-1-9-8-5





    Bila hiyana au kokoro, vault ilifunguka.



    Ndani ya vault kulikuwa na bahasha nyingine ya kaki. Nikaichukua haraka na kuifungua. Ndani yake kulikuwa na simu kama ile bahasha ya awali pamoja na makaratasi mengi sana.



    Nikaanza kupitia kwa haraka haraka yale makaratasi. Mengine sikuyaelewa kwa haraka yalikuwa yanahusu nini. Lakini baadhi niliyaelwa yalikuwa ni mkataba wa upangaji wa jengo hili.



    Kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba, makaratasi mengine, mfano haya ya upangaji wa jengo hili yalikuwa na sahihi yangu halisi kabisa.



    Sikutaka kupoteza muda. Nilichukua ile simu niliyoikuta kwenye bahasha ya kwanza na kubofya ‘speed dial 1’ kama ambavyo nilielekezwa.



    Simu iliita kwa muda wa kama dakika moja hivi kisha ikapokelewa.





    “Halloo!” Niliongea kwa tahadhali.



    “Do you have all the papers?” Sauti nzito yenye lafudhi ya kifaransa iliongea upande wa pili.



    Mara moja niling’amua kuwa huyu ndiye yule ambaye huwa namfahamu kama Hudini. Sikujua kama ni jina lake au la, lakini kichwani mwangu nilimuita Hudini.



    “Yes! I have them!” Nikamjibu.



    “Loose this phone… take the other one and take all the papers and get out of there… we will pick you up in thirty minutes!”



    “Where should I wait for…….!”



    Simu ilikatwa kabla hata sijamaliza kuuliza swali.



    Nilibaki naitazama ile simu kwa hasira kana kwamba ndio huyo Hudini mwenyewe.





    Japokuwa kadiri ambavyo hili suala lilikuwa linaenda ‘deep’ zaidi lilikuwa kinazidi kuwa la kuogofya, lakini ndani yangu nilijikuta hari ya kutaka kujua mwisho wake inakuwa kubwa zaidi.









    Karibia dakika kumi sasa zilikuwa zimepita tangu nisimame hapa barabarani. Sikuwa na uhakika kama ni hapa ambapo nilikuwa natakiwa kusubiri au nisimame. “We will pick you up in thirty minutes”, sentesi ya yule jamaa aliyeongea upande wa pili wa simu ilijirudia tena kichwani.



    Hapa ambapo nimesimama muda huu ndipo hapa hapa ambapo nilisimama mara ya kwanza kabla ya kupata wazo la fumbo kuhusu anuani ya jengo nililojikuta nimeamka ndani yake bila kujua nimefikaje na kisha kurudi tena ndani ya jengo na hatimaye kuisikiliza ile recording ya Mzee wangu Charles Bernard kajuna.



    Kwa asilimia kubwa niliamini kuwa kama kuna mahala ambako wanahitaji niwasubiri basi ni hapa barabarani, kwani ukitoka tu ndani ya lile jengo nililokuwemo moja kwa moja uchochoro wake unatokeza hapa kwenye barabara hii.



    Nilitazama tena muda kwenye ile simu ambayo niliikuta ndani ya vault, tayari ilikuwa ni saa tisa na dakika nne usiku. Barabara ilikiwa kimya kabisa. Kwa muda wote ambao nilikuwa nimesimama hapa ni kama magari mawili au matatu tu ndio ambayo niliyaona yamepita. Kulikuwa kimya kabisa pale barabarani. Hakukuwa na hata mtembea kwa miguu mmoja ambaye alipita na wala hakukuwa na dalili yoyote kwamba kunaweza kupita kiumbe yeyote yule muda huu. Nilijihisi kama ndege nimewekwa ndani ya tundu kutokana na hapa nilipokuwa nimesimama.



    Jambo la kwanza ambalo lilikuwa linanifurukuta rohoni ilikuwa ni kutokujua niko mahala gani hasa, au kwa usahihi zaidi niseme nilikuwa sijui niko upande gani wa jiji hili la Zurich. Kutokana na jina la mtaa ambalo nililisoma pale mlangoni mwa jengo “Hardstrasse” niliamini kabisa niko ndani ya Zurich lakini sikujua hasa ni upande gani wa Zurich ambao nilikuwa.



    Jiji hili nilikuwa nalielewa vyema zaidi nikianza kuitafuta sehemu kwa kuchukulia Uwanja wa ndege wa Zurich kama ndio ‘center’ kichwani mwangu. Hii ndio sababu pia ya kunifanya hata kuchukua chumba cha hoteli karibia kabisa na uwanja huu wa ndege.



    Rohoni mwangu sikupenda kabisa hii hali ya kutokujua niko mahala gani na dakika chache zijazo watu nisiowafahamu wanakuja kunichukua na kunipeleka mahali ambapo bado sikujua ni wapi.



    Nilijikuta napata hamu nifahamu niko wapi ili iniwezeshe kujua ni wapi hasa nitapelekwa na watu ninaowasubiri hapa hata kama kwa namna fulani watajaribu kunificha wanakonipeleka.



    Nilitazama tena saa katika simu. Ilibionyesha kuwa tayari ilikuwa ni saa tisa na dakika kumi. Kama dakika kumi na tano tu zilikuwa zimesalia kabla ya watu hao kuju kunichukua. Kichwani nilipata wazo kuwa nifanye kitu fulani kwa muda huu ukiosalia kabla ya watu hao kufika hapa.



    Simu hii niliyoikta kwenye ile vault ndogo ukutani ilikuwa ni Smartphone aina ya Samsung ya kisasa japo sikujua haraka haraka ni tolea gani. Nilifungua mpaka upande wa internet lakini kutokana na simu kuwa mpya sikuweza kupata huduma za mtandao. Lakini nilijua kuwa maeneo mengi ya Zurich yalikuwa na huduma ya Wi-Fi bure, kwa hiyo nikaanza kuranda randa pale barabarani kutoka jengo moja mpaka lingine nikijaribu kuona kama naweza kupata Wi-Fi ya bure. Kama dakika mbili baadae nilikuwa mbele ya jengo moja ambalo mara moja simu yangu ikanasa huduma ya Wi-Fi na moja kwa moja nikafungua tena ‘browser’ ili niweze kuperuzi nilichokuwa nakikusudia.



    Nikaingia kwenye ukurasa wa ‘Google Maps’ na kuandika ‘Zurich’. Mtandao ukatafuta kwa kama sekunde tatu tu kisha nikaletewa ramani yote ya Zurich kwenye screen ya simu.



    Nikaanza kuikuza ramani ili iweze kuonyesha barabara na mitaa. Baada ya ramani kuwa kubwa nikaanza kutafuta mtaa wa Hardstrasse mpaka nilipoupata. Ulikuwa upande wa pili kabisa wa mji. Yaani mahala uwanja wa ndege wa na hoteli niliyofikia vilipo ni upande mmoa wa mji na hapa Hardstrasse ni upande mwingine kabisa. Yaani ni kama ilivyo mbagala na tegeta labda kwa mfano. Mji wa Zurich umegawanywa kwenye ‘Districts’. Hoteli yangu na uwanja wa ndege vipo ndani ya ‘District 1’ wakati huu mtaa wa Hardstrasse upo kwenye ‘District 5’.



    Nikaisoma vyema tena ramani ili niweze kukariri vitu kadhaa muhimu. Kutoka hapa nilipo kurudi nyuma upande wa kusini, nitatokea ‘District 4’ na mbele yake kidogo kuna barabara kuu inayopinda kulia kuelekea mtaa wa Hohlstrasse. Ukienda mbele, kaskazini unakutana na barabara ambayo inachepuka kulia na kuzunguka kisha kurudi tena hapo Hardstrasse na nyingine inapinda kushoto kutokea kwenye taasisi ya elimu inayoitwa Toni-Areal.

    Lakini kama utanyoosha moja kwa moja kuelekea kaskazini bila kukunja kona mahala kokote pale basi utakitana na daraja linalovuka kwenye mto mkubwa na kisha kutokea kwenye eneo linaitwa Wipkingen.



    Walau nikaridhika kidogo, walau sasa nilikuwa najua niko mahala gani. Nikaondoka kutoka mbele ya jengo hili ambalo nilikuwa nimesimama ili niweze kupata Wi-Fi na kurejea pale pale barabarani amapo nilikuwa nimesimama awali. Saa kwenye simu ilikuwa inaonyesha kuwa tayari ilikuwa ni saa tisa na dakika ishirini na moja. Zilikuwa zimesalia kama dakika tano ama nne tu kabla ya hao ninaowasubiri hawajawasili hapa nilipo.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Damu ilikuwa inachemka kweli kweli nikiwa na shauku ya kuwaona hao ambao niliombiwa kuwa wanakuja hapa baada ya nusu saa. Mkononi nilikuwa nimeshikilia simu pamoja na yale makaratasi ambayo niliyapata ndani ya vault ndogo kwenye lile jengo.



    Nikiwa bado nashangaa yale makabrasha mkononi mwangu, ghafla kuna gari ilikuja kwa kasi mbele yangu na kufunga breki kwa nguvu na kusimama. Gari ilikuwa ya rangi nyeupe na ilikuwa na muundo wa aina ya gari ambazo nyimbani tanzania tumezoea kuziita ‘hiace’. Gari yote mpaka madirisha yalikuwa na rangi nyeupe. Nikiwa niko kwenye taharuki kubwa nilishuhudia watu watatu walishuka kutoka kwenye ile gari na kunifuata kwa kasi kubwa pale ambapo nilikuwa nimesimama.



    Mmoja wao bila salamu au kuniuliza chochote kile alinichukua simu na makabrasha mkononi mwangu huku mwenzake akinivesha kichwani linguo jeusi kama fuko la kitambaa ili kunifanya nisione.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog