Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

THE OTHER HALF - 3

 





    Simulizi : The Other Half

    Sehemu Ya Tatu (3)







    “…haupaswi kusikia sauti hii, haupaswi kuujua ukweli huu na haupaswi kufahamu siri hii. Lakini nitakueleza. Nitakueleza dunia mbili zilizomo ndani ya dunia hii moja, nitakueleza aina ya binadamu wanaoishi kwa kuwinda binadamu kama wewe. Nitakueleza dunia ya pili ndani ya dunia hii wanayoishi binadamu hao. Nitakueleza binadamu waliowahi kuwakabili binadamu wa sampuli hiyo, na nitakueleza namna damu yao ilivyo tiririshwa.







    Haupaswi kujua kitakachosemwa na sauti hii, lakini kama umefanikiwa kuisikia sauti hii… yawezekana uko ndani ya msitu, uko mahali ambapo haupaswi kuwa na unahitaji msaada ambao haupaswi kuomba, na msaada pekee ni hii sauti unayoisikia, na hauwezi kuizuia kwa kuwa hata ukiziba masikio yako, bado utaisikia ndani ya nafsi kwa kuwa sauti hii ndio kitu pekee kinachoweza kuondoa upweke ulionao kwenye msitu uliopo. Msitu wa Ox.







    Kwa hiyo, acha nikueleze usichopaswa kukisikia… acha nikueleze kilichotokea mwaka 2038. Nikueleze kuhusu vita kati ya damu na maji, nikueleze vita ya binadamu na watoto wa Maldives. Nikueleze kuhusu muamuzi wa dunia, The 46. Nikueleze kuhusu miji iliyotwaliwa mwaka huo na nikueleze ni kafara gani tulizitoa nafsi zetu kuifanya dunia iwe namna ilivyo leo.







    Haupaswi kusikia sauti hii, haupaswi kujua historia iliyofutwa isijulikane. Lakini nitakueleza, nitakueleza kwa sababu kwangu sio historia tu, bali nimeishi kati kati ya binadamu wa upande wa pili, nusu ya pili, The Other Half.! Nimeishi kati kati ya watoto wa Anabelle 1.







    Acha nikueleze kwanini unaiskia sauti hii, na kwanini nimekuwa hai mpaka leo hii ilhali sipaswi kuwepo. Nimezaliwa miaka 56 kabla ya mwaka 2038 na leo hii unapoisikia sauti hii ni miaka 80 baada ya mwaka 2038. Na katika kipindi chote hicho cha miaka 136 mwili wangu umebakia na mwonekano wa kijana wa miaka 24!











    Haupaswi kuwepo ndani ya msitu huu, haupaswi kusikia sauti hii. Huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa hatma yako na dunia.



















    EPISODE 15



















    NDANI YA MSITU WA OX, MARYLAND – MAREKANI











    Yule binadamu wa ajabu aliyetokea kichakani alikuwa amekaza macho wakiangaliana na  Mzee Caleb kwa muda mrefu sana bila yeyeto kutingishka wala kusema chochote kile.







    Naomi, Ethan na wanajeshi wenzake walikuwa wametulia kimya kabisa na kwa tahadhari kubwa wakiwaangalia namna binadamu huyu wa ajabu na Mzee Caleb walivyokuwa wamekaziana macho.











    Kuna hali fulani hivi ilikuwa dhahiri kati ya Mzee Caleb, na huyu binadamu wa ajabu. Hali fulani kama hii sio mara yao ya kwanza wao kukutana, hali fulani ya uchungu kati kati yao, hali fulani kama ya kuoneana huruma.











    Kadiri muda ulivyokuwa unaenda binadamu yule wa ajabu ngozi yake nyeupe ya kupauka ndivyo ilivyokuwa inazidi kupauka na kuwa nyeupe zaidi. Mwili wake ukikuwa katika msisimko mpaka zile nywele mikononi mwake zilikiwa zimesimama



    Kadiri alivyokuwa amemkazia macho Mzee Caleb uso wake ulibadilika zaidi na hali ya uchungu na huruma ilikuwa dhahiri zaidi usoni mwake.











    Mzee Caleb naye alikuwa anahema kwa uchungu na huruma mpaka akawa anatetemeka.







    Wakabaki wamekazina macho hivyo kwa dakika kadhaa nyingine. Yule binadamu akaanza kutokwa na machozi machoni, hayakuwa machozi ya kawaida… ilikuwa ni damu inatoka machoni mwake katika namna ya machozi.











    “Baba! Unafanya nini hapa?” Mzee Caleb aliuliza kwa sauti ya kutetema huku naye akiwa anatokwa na machozi usoni.











    Naomi, Ethan na wanajeshi wengine wote walipigwa na butwaa. Kilichowashangaza zaidi ni neno la kwanza alilotamka Mzee Caleb, “Baba!”



    Neno hili liliwachanganya haswa, kwanza wote wanafahamu kuwa baba yake Mzee Caleb ameshafariki miaka mingi, na si hivyo tu hata kwa muonekano binadamu huyu wa ajabu alikuwa na muonekano wa ujana kuliko Mzee Caleb ambaye alikuwa ni kikongwe zaidi.







    Kwa namna yoyote ile, kama ukiamua kukadiria, basi binadamu huyu wa ajabu alikuwa hawezi kuvuka miaka 50 kwa muonekano wake.



    Mzee Caleb alikuwa na zaidi ya miaka 80, inawezekanaje amuite “baba” binadamu huyu wa ajabu ambaye anaonekana ni kijana zaidi yake?











    “Wamechukua kitabu!” Yule binadamu wa ajabu akajibu kwa sauti ya mkwaruzo kama vile amekabwa na kitu fulani kooni.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/









    “Unafanya nini hapa nimekuiliza?” Mzee Caleb akajibu kwa hasira zaidi huku machozi zaidi yanamtoka.











    “Niko hapa kukusaidia Caleb! Najua mzigo ulionao ni mkubwa na hauwezi kuubeba peke yako!” Yule binadamu wa ajabu akajibu huku anamuangalia Mzee Caleb kwa huruma.











    “Sihitaji msaada wako baba! Ulikuwa na nafasi ya kunisaidia miaka sitini iliyopita na haukufanya hivyo… sihitaji msaada wako kwa sasa!” Mzee Caleb akaongea kwa uchungu huku machozi zaidi yanamtoka.











    Yule binadamu hakujibu chochote, wakabaki wanaangaliana tu na Mzee Caleb. Damu zaidi ikatoka machoni mwake na kulowesha mashavu kama machozi yafanyavyo.











    “Caleb! Usinilaumu kwa makosa niliyoyafanya miaka sitini iliyopita… ndio maana niko hapa, najaribu kufukia makosa yangu! Najua siwezi kuondoa maumivu yote uliyoyapata moyoni mwako lakini angalau naamini naweza kufanya kitu kukufuta hata chozi moja kati ya maelfu ya machozi uliyolia kwa sababu ya nilichokifanya… niko hapa kukusaidia Caleb! Niko hapa kukushika mkono mwanangu!”







    Yule binadamu akaongea kwa hisia kali huku damu ikizidi kutiririka machoni mwake na kulowesha mashavu yake na shati lake chakavu.







    Mzee Caleb alikuwa kana kwamba anashindwa kutamka neno lolote, machozi yaliendelea tu kumtoka wakiwa wanaangaliana na binadamu huyu.







    Alipoona Mzee Caleb haongei chochote, yule binadamu akaendelea tena kuongea.











    “Wamechukua kitabu cha babu yako Caleb!”











    “Nani amekichukua?” Hatimaye Caleb alipata nguvu ya kuongea na kuuliza.











    “Sancta Cedes! Wamechukua kitabu siku mbili zilizopita… unajua kuwa Mimi na wenzangu hatuwezi kushika Book Of Codes au kuwazuia Sancta Cedes… kwa hiyo tulibaki kuwaangalia tu! Hatukuwa na uwezo wa kufanya chochote!”











    “Tunakipataje tena kitabu?”











    “Naamini mpaka muda huu inawezekana kimeshafikishwa kwa wakuu wa The 46! Namna pekee mnaweza kuwazuia kukitumia kitabu ni endapo babu yako atawasaidia!”











    Safari hii wote walijikuta wanapigwa na butwaa.







    Naomi, Ethan na wanajeshi wengine wote walikuwa wamepigwa na butwaa kwanza kwa namna Mzee Caleb na binadamu huyu wanavyoitana. Mzee Caleb anamuita baba, na huyu binadamu kuna sentesi akamuita mwanangu.







    Pia wakawa wanajiuliza alimkosea kitu gani Mzee Caleb miaka 60 iliyopita… na inawezekanaje amkosee miaka sitini iliyopita wakati huyu binadamu kwa makadirio tu alikuwa havuki miaka hamsini?







    Lakini kilichowafanya wapigwe na butwaa zaidi ni sentensi ya mwisho ambayo binadamu huyu aliiongea… kwamba namna pekee wanayoweza kuzuia The 46 wasitumie kitabu ni endapo watapata msaada kutoka kwa babu yake Caleb!



    Wakajiuliza hili linawezekana vipi ilhali wote wanajua kwamba babu yake Caleb naye amefariki miaka mingi iliyopita na walikuja mahali hapo kwa kuwa hili lilikuwa ni kaburi lake ambalo alizikwa pamoja na kitabu cha “Book Of Codes”!







    Suala hili halikuwashangaza akina Naomi pekee bali pia hata Mzee Caleb lilimshangaza.











    “Babu ananisaidiaje kuwazuia The 46 wakati ambapo amefariki miaka mingi sana na hata wewe unajua hilo!” Mzee Caleb aliongea huku anamuangalia binadamu huyu kwa macho ya udadisi.











    “Caleb, najua kuwa babu yako amefariki miaka mingi… lakini bado anaweza kukusaidia!” Yule binadamu akaongea huku anaangalia lile kaburi lililofukuliwa mbele yao huku pembeni kukiwa na mabaki ya mafuvu na mifupa ya binadamu.







    Mzee Caleb naye akajikuta anaangalia pale kwenye kaburi lililofukuliwa na ghafla akakumbuka kitu.











    “Kwenye hii mifupa yote iliyopo hapa… hakuna masalia ya babu! Hakuna fuvu lake hapa!” Mzee Caleb akaongea huku amemkazia macho yule binadamu.







    “Tuliiondoa muda mchache kabla Sancta Cedes hawajafika… tulijua tu kuwa wataitaka mifupa ya babu yako!”











    “Wanataka kuifanyia nini? Na kwanini unaswma ‘tuliondoa’? Mliondoa wewe na nani?”











    “Na jamii yangu Caleb! Siko peke yangu… nina jamii ninayoishi nayo upande huu wa pili wa maisha..”











    Mzee Caleb akakumbuka kauli ya Ethan walipoingia msituni kwamba anahisi kuna watu zaidi ya mmoja wanawafuatilia.











    Ilikuwa ni kana kwamba binadamu yule alikuwa anaisoma akili ya Mzee Caleb kuwa alikuwa anajiuliza maswali kuhusu hiyo ‘jamii yake’ anayoishi nayo ‘upande wa pili wa maisha’!







    Pasipo kumuuliza chochote kile Mzee Caleb, binadamu yule akaangakia pembeni na kutamka kwa sauti kubwa ya kujiamini







    “Njooni wanangu!!”











    Ghafla katika vichaka vilivyopo karibu ya na miti iliyofungamana wakaanza kusikia mlio kama waliousikia awali kabla ya binadamu huyu kujitokeza. Ilikuwa kana kwamba kuna wadudu wanapekua pekua majani kwenye vichaka. Kana kwamba vichaka vinatikisika, na kufumba na kufumba walikuwa wamezungukwa na binadamu wengine wa ajabu kila upande wakiwaangalia kwa macho makali ya kufanana kabisa na macho ya paka.











    Kwa haraka Ethan na wanajeshi wenzake walijipanga kwa kasi ya ajabu kutengeneza kama duara wakipeana migongo na kuinua bunduki zao kuwaelekezea viumbe hawa wa ajabu.











    “Msipige risasi!” Mzee Caleb alipga tena kelel kwa mara nyingine, “Msipige risasi!”











    Ethan akatumia umakini wake wa kijeshi na kuwahesabu kwa haraka binadamu hawa wengine waliojitokeza, walikuwa wapo thelathini na mbili na ukimjulisha na yule wa kwanza jumla wanakuwa thelathini na Tatu.











    Wote muonekano wao walikuwa wanafanana kabisa na yule binadamu wa kwanza.



    Walikuwa na ngozi nyeupe iliyopauka sana kupita kiasi. Mikononi walikuwa na manyoya mengi mno kama paka. Macho yao yalikuwa amakali kufafanana kabisa na macho ya paka na hawakuwa na kope wala nyusi machoni.











    Wote walikuwa wamevaa nguo za rangi ya khaki zilizochakaa mno kana kwamba wamezivaa bila kuziondoa mwilini kwa miongo kadhaa.







    Walikuwa wanawaangalia kwa macho makali huku wanahema taratibu kama vile chui anapovizia windo lake mbugani.











    “Hii ndio jamii yangu Caleb!” Yule binadamu wa kwanza akaongea huku akitabasamu kwa mara ya kwanza.











    Mzee Caleb akabaki ameduwaa tu asijue aseme kitu gani.



    Yule mtu hakusubiri Mzee Caleb aongee chochote kile, akatoa kama ishara fulani hivi ya mkono kwa wenzake na mara moja wenzake wengine wanne wakajitokeza wakiwa wamebeba jeneza lilichochaa sana ambalo lilikuwa linaonekana dhahiri kwamba limefukuliwa kutoka ardhini muda si mrefu.







    Mzee Caleb alijikuta anafumba mdomo kwa macho viganja vya mkono. Hili lilikuwa ni jeneza la babu yake ambalo walimzikia zaidi ta miaka sitini iliyopita.











    “Caleb, nakukabidhi mifupa ya babu yako… Sancta Cedes tayari wamechukua kitabu! Ili kuwazuia kufanya wanachokitaka namna pekee mnayoweza kufanikisha hilo ni kwa msaada wa babu yako ambaye aliyunza Book Of Codes kwa zaidi ya miaka arobaini… japokuwa amefariki lakini hayo masalia yake yanaweza kuwasaidia!” Yule binadamu akaongea kwa kumaanisha haswa wakati wenzake wakiliweka lile jeneza mbele ya Mzee Caleb.











    “Haya masalia yanatusaidiaje?” Mzee Caleb akauliza kwa mshangao.















    “Mpelekeeni Rais ambaye anajua siri iliyomo kwenye mchoro wa George Washington… atajua nana gani haya masalia yanaweza kuwasaidia kuwazuia The 46 ktumia Book of Codes!”











    “Rais hayupo, amepotea wiki ya pili hii sasa!” Kwa mara ya kwanza Naomi akaingilia mazungumzo ya Mzee Caleb na yule Binadamu.











    Yule binadamu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kama anatafakari jambo fulani, kisha akajibu.







    “Tumieni mchoro wa George Washington mtaelewa namna gani mnatumia haya masalia!”











    “Mchoro nao haupo umepotea!” Naomi akajibu tena kwa kifupi na kwa woga.















    Yule binadamu akaguka kuangaliana na wenzake kana kwamba kuna kitu fulani hivi wamekihisi.







    “Amepotea lini? Na mchoro umepotea siku gani?” Akauliza akimuangalia Naomi kwa udadisi.











    “Rais amepotea wiki tatu zilizopita na mchoro umepotea siku moja baada ya yeye kupotea!” Naomi akaongea kwa woga kana kwamba kuna kosa fulani amefanya.











    Yule binadamu akaangalia pembeni mkono wake wa kushoto ambapo alisimama mmoja wa wenzake ambaye kwa muonekano alikuwa ni mwanamke. Waliangaliana kwa karibia dakika nzima bila kusema chochote. Walikuwa kana kwamba wanawasiliana bila kusema chochote.







    Ni dhahiri sasa kwamba kuna jambo kubwa walikuwa wanalihisi baada ya kusikia taarifa hii juu ya siku ya kupotea Rais na siku ta kupotea kwa mchoro wa George Washington.







    “Mleteni!” Yule binadamu akaamuru wenzake waliopo upande wake wa kushoto.











    Naomi, Mzee Caleb, Ethan na wale wanajeshi wote wakageuka kuangalia upande huo kuona ni nini au nani huyo anayeamuliwa aletwe na kuna uhusiano gani na hii taarifa Naomi aliyompa huyu binadamu kuhusu siku ya kupotea kwa Rais na siku ya kupotea kwa mchoro.!!





    THE OTHER HALF















    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE























    ANDREWS AIR FORCE BASE – MAREKANI















    Takribani masaa mawili yalikuwa yamepita tangu kikao cha baraza la mawaziri kimalizike huko Washington.







    Makamu wa Rais alikuwa ametua na ndege mbadala ya Air Force One katika uwanja wa ndege wa wa kituo cha kijeshi  Andrews Air force Base, jimboni Maryland.



    Japokuwa Air Force One ilikuwa imezama katika bahari ya Atlantic kwa raia wa kawaida angeshangaa imekuwaje makamu wa rais bado anatumia ndege ambayo nayo ni Air Force One.











    Moja ya mambo ambayo labda hayafahamiki sana kwa umma kuhusu ndege ya Rais wa Marekani Air Force One, ni kwamba, ndege hizi ziko mbili.



    Katika muda wowote ule, ni lazima ndege hizi ziwepo zote mbili na mara nyingi huwa zote mbili zinaelekea sehemu yoyote ambayo Rais wa Marekani anakuwepo.











    Lengo kuu la kwanza la kufanya hivi ni kwa ajili ya tahadhari kama ikitokea ndege inayotumiwa na Rais kupata hitilafu na kushindwa kuruka kutoka sehemu alipo, kwa hiyo Air Force nyingine ina uwezo wa kutua na kumchukua rais ili aendelee na ratiba yake.



    Lakini sababu ya pili ya kuwa na ndege hizi mbili ni kwa sababu ya masuala ya kiusalama.



    Kwa mfano mara nyingi rais wa Marekani akitembelea nchi fulani ya kigeni, baada ya kushuka na kupokelewa na wenyeji wake na kuondoka uwanja wa ndege kuendelea na shughuli zilizompeleka huko, baada ya masaa kadhaa na mara nyingi majira ya usiku, Air Force One itaruka kuondoka uwanja wa ndege wa kurejea masaa kadhaa baadae. Jambo ambalo wengi huwa hawalifahamu ni kwamba ndege hii inayokuja kutua mara ya pili si ile Air Force One ya kwanza. Hii inakuwa ni ile nyingine. Lakini zote zinafanana kwa asilimia mia moja kwa kila kitu.











    Jambo lingine ambalo labda linafahamika na wengi lakini pia bado wengi hawalifahamu ni kuhusu sehemu inapohifadhiwa Air Force One muda ambapo Rais wa Marekani haitumii.











    Wengi wanadhani kwamba Air Force One huwa inatua White House na huwa ‘inapaki’ hapo kama ikiwa haitumiki.



    Ukweli ni kwamba katika viunga vya White House hakuna ‘air strip’ ya kutosha kwa Air force One kuweza kutua na kuruka.







    Kama ikiwa haitumiki, yaani Rais yuko ofisini Washington anaendelea na shughuki zake za kila siku, ndege ya Air Force One huwa inapaki katika uwanja wa Andrews Air force Base uliopo jimboni Maryland.



    Hii maana yake ni kwamba rais wa Marekani akitoka safari yoyote kwa kutumia Air Force One, huwa haendi moja kwa moja Washington, huwa ndege yake lazima ielekee Maryland na kutua kisha yeye aanze safari ya kwenda ofisini Washington.











    Kutoka Maryland kilipo kituo cha Andrews Air Force Base mpaka Washington, kulipo na Whitehouse kuna umbali wa kilomita thelathini na nane.



    Rais ana machaguo mawili namna gani atasafiri kutoka Andrews Air Force Base mpaka Washington.







    Anaweza kutumia gari la rais ‘president’s limousine’ maarufu kama “The Beast” akisindikizwa na magari ya Secret Services. Au anaweza kutumia ‘chopa’ ya kijeshi ya Marine One iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya Rais wa Marekani.



    Vivyo hivyo Rais akiwa anatoka Whitehouse kwenda kupanda Air Force One, anatumia The Beast au Marine One kusafiri kutoka Washington mpaka Andrews Air Force Base ilipo ndege yake ya Air Force One.















    Kwa hiyo makamu wa Rais David Logan alipotoka sehemu ya siri ambapo alikuwa amefichwa, Site SQ 1204 ndege ya Air Force One ilikuwa imekuja kutua mahali hapa Andrews Air Force Base.



    Alikuwa ametua hapa ili aweze kuelekea moja kwa moja Whitehouse ambako masaa mawili yaliyopita kikao cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeisha baada ya mabishano makali ya kuhusu muelekeo wa uongozi wa nchi.











    Waziri wa mambo ya nje ambaye alikuwa ni swahiba mkubwa wa David Logan alikuwa amependekeza kuwa, Makamu wa Rais aapishwe kuwa Rais wa nchi baada ya wiki tatu kupita bila dalili yoyote ya Rais Laura Keith kujulikana alipo.



    Mawaziri kadhaa walikuwa wanamuunga mkono kwenye hoja hii lakini kwa upande mwingine kulikuwa na mawaziri ambao walikuwa wanapinga hoja hii wakiependekeza kwamba Logan aendelee kufanya majukumu ya Rais pasipo kuapishwa awe amekaimu tu nafasi hiyo kwa kuwa hakukuwa na uthubitisho wowote ule kama Rais Laura Keith alikuwa amefariki.











    Baada ya mabishano makali hatimaye ikapigwa kura ya Mawaziri wote kuamua ni uamuzi gani ufanyike, na hatimaye waliokuwa wanaunga mkono David Logan aapishwe kuwa Rais hoja yao ikapita.











    Kwa hiyo David Logan baada ya kutua Andrews Air Force Base moja kwa moja akachukuliwa na chopa ya Marine One kuelekea Whitehouse kwa ajili ya zoezi la dharura la kuapishwa ili aweze kuwa na mamlaka kamili ya kutekeleza majukumu ya Rais wa Marekani.







     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Dakika kumi na moja baadae Marine One ilikuwa imetua katika viunga vya Whitehouse na David Logan pamoja na katibu wake Kevin waliteremka na moja kwa moja kuelekea Eastern Room ya Whitehouse ambako alikuwa anasubiriwa na mawaziri pamoja na Jaji mkuu Ralph Powel kwa ajili ya kumuapisha.











    Lakini kabla haijaingia Eastern Room ambako alikuwa anasubiriwa ilimbidi kwanza moja kwa moja aelekee Situation Room ambako alikuwa amekubaliana kuonana na Admiral Smith ili wamalizie mazungumzo yao ambayo waliyakatisha kipindi wanaongea kwa ‘Video Call’ akiwa Site SQ 1204 alikokuwa amefichwa awali.











    “Kevin! Naomba uende Eastern Room ukawakirimu mawaziri waliopo… nahitaji kuongea na Admiral tukiwa peke yetu!” Logan akaongea bila kumuangalia Katibu wake Kevin akiwa anakaribia kupanda kwenye lift kushuka ghorofa ya chini ardhini kulipo na Situation Room.











    “Sawa Mr. Vice President!” Kevin akajibu na kutaka kuanza kuondoka, lakini ikabidi ageuke tena kumuangalia Boss wake baada ya kumuona ametoa tabasamu kubwa sana. “Ni nini Muheshimiwa? Tufurahi wote basi!” Akaongea kwa utani.











    “Nimefurahi tu kuwa ndani ya dakika ishirini zijazo hautaniita tena Mr. Vice President!” Logan akaongea na kutoa tabasamu kubwa zaidi.











    “Hongera sana muheshimiwa!” Kevin akampongeza huku anasindikiza hongera zake na tabasamu kubwa.











    Logan hakusema chochote, akatabasamu tu na kubonyeza kitufe cha lift na mlango ukajifunga na kuelekea chini kabisa ya kwenye Situation Room akiwa na ulinzi was Afisa mmoja tu wa Secret Services.











    Alipofika nje ya chumba cha kukutania na Admiral Smith, akamuomba afisa was Secret Services abakie nje kwani ana mazungumzo ya faragha kubwa. Kisha akaingia ndani ya chumba ambako muda wote huu Admiral Smith alikuwa amekwisha fika na akiwa anamsubiri.











    Moyoni mwake bado alikuwa na hofu kama siri aliyokuwa ameibeba moyoni mwake kwa muda wote huu kama bado iko salama.











    “Habari Mr. Vice President?” Admiral Smith akamsalimu Logan na kusimama kwa heshima.















    “Nzuri Admiral… nasubiriwa huko juu Eastern Room kwa ajili ya kuapishwa kwa dharura kwahiyo naomba twende moja kwa moja kwenye mazungumzo yetu… ni kitu gani cha ajabu hasa maafisa wa Navy wamekikuta kwenye magofu yaliyopo huko kisiwa cha Saman?” Logan akauliza haraka haraka huku akiwa anakaa kwenye kiti mkabala na Admiral Smith.



    “Kama nilivyokueleza muheshimiwa kwamba zoezi la kuibua Air Force One kutoka chini ya bahari litachukua muda mrefu.. Kwa hiyo kwanza kabisa maafisa wa Navy wanaondoa miili ya watu waliyoikuta kwenye Air Force One.. Lakini….”











    “Ni nini wamekikuta kwenye magofu kwenye hicho kisiwa Admiral? Hayo maelezo mengine utanipa wakati mwingine!!” Logan akamkatisha Admiral kabla hajamaliza sentes, alionekana kuwa shauku yake kubwa ni kujua hicbi ambacho maafisa wa Navy walikikuta kwenye magofu ya kisiwa cha Saman na kiwashangaza.















    “Ndio nilikuwa nakuja huko muheshimiwa… mpaka sasa tunaweza kusema kwamba tumefanikiwa kuondoa miili yote iliyokuwemo ndani ya Air Force One lakini hatujafanikiwa kuona mwili wa Madam President! Lakini jambo la ajabu ni kwamba maafisa wa Navy wamekuta nguo zake kwenye hayo magofu ya kisiwa cha Saman!”











    “Nguo zake? Una maana gani kusema nguo zake? Kwamba zimekutwa nguo tupu bila mwili?”  Logan akauliza kwa mshangao mkubwa.











    “Ni bora hata ingekuwa hivyo muheshimiwa… nguo zake zimekutwa katika namna ambayo ni kama vile zimevuliwa kutoka mwilini katika hali ya kawaida na hazionyeshi dalili yoyote kama nguo hizo zimegusa maji… yaani ni kana kwamba Madam President alikuwepo hapo akavua nguo na kuzitlekeza hapo.. Kana kwamba hakuwepo kwenye ndege ilipodondoka.. Hichi ndicho kinachotuchanganya zaidi, kwa sababu Air Force One iliporuka kutoka Vatican Madam President alikuwemo ndani ya ndege na mpaka Ndege ilipopoteza muelekeo na mawasiliano bado aliwemo na tunaamini mpaka ilipodondoka alikuwemo ndani.!”







    Admiral Smith akafafanua zaidi.











    “Unataka kusema kwamba labda aliweza kuogelea kutoka baharini na kuelekea kwenye hayo magofu na kisha kuvua nguo kwa sababu fulani na kuziacha hapo?” Logan akauliza kwa sauti ya wasiwasi.











    “Hapana muheshimiwa… kama nilivyokueleza! Nguo hizo hazionyeshi dalili kuwa zimegusa maji… ni kana kwamba hakuwepo kwenye ndege na amezivua nguo mahali hapo akitokea sehemu nyingine kabisa na sio baharini ndege ilipodondoka.!”











    “Inawezekanaje hilo?” Logan akauliza kwa mshangao zaidi.











    “Ni jambo ambalo haliwezekani kabisa na ndio maana tumebaki na kitendawili mpaka sasa hatujui ni nini kinaendelea au hii ina maana gani?”











    “Au labda sio nguo zake!” Logan akajikuta anajaribu kutafuta kila aina ya ufafanuzi ili kuelewa kinachoendelea.











    “Ni nguo zake muheshimiwa… suti ya kike ya rangi ya zambarau iliyochanganya weusi kama rangi ya sare za Navy, viatu vya kike vya kisigizo cha washani… mkufu wa shanga za lulu, na hereni zake… hivi ndivyi ambavyo rais alikuwa amevaa alipotoka roma na zaidi ya hapo sehemu hiyo hiyo kulipo na nguo tumekuta POLO-TD!!” Admiral akaongea kwa kujiamini anachokisema akimuangalia Logan kwa udadisi.











    Logan alishtuka kweli kweli aliposikia kuwa maafisa wa Navy wamekuta POLO-TD sehemu walipokuta nguo za Madam President. Hii ilimaanisha kuwa hakika hizo zilikuwa ni nguo za Rais bila ubishi.



    POLO-TD (POTUS (President Of The United States) Location Tracking Device) kilikuwa ni kifaa kidogo sana chenye ukubwa wa kama ncha ya peni au penseli ambacho kinawekwa ndani ya nyama ya mkono wa kushoto wa Rais ili kuwawezesha maafisa wa Secret Services kujua alipo Rais muda wote.











    Akili ikaanza kumjia Logan, akaanza kuhisi kama kuna mtego mbele yake. Mpango wake alioupanga zaidi ya mwaka mmoja nyuma ambao aliutekeleza kwa umakini na usiri mkubwa kuanzia wiki Tatu zilizopita ambak mwanzoni aliamini umefanikiwa kwa asilimia mia, sasa alihisi labda umemuingiza kwenye mtego.











    Akaanza kujihoji ni nani labda atakuwa anamzunguka? Swahiba wake Waziri wa mambo ya nje? Au ni mshirika wake kwenye utekelezaji wa mpango huu, kampuni ya DATHMOV CONTRACTOS LLC.??















    “Muheshimiwa… muheshimiwa!! Mr. Vice President! Muheshimiwa!!”







    Admiral Smith alikuwa labda anamuita kwa takribani dakika mbili nzima, lakini Logan alikuwa hakusikia kutokana na lindi la mawazo yaliyokuwa yanatirirka kichwani mwake muda huu.











    “Nahitaji kuongea na Jaji Mkuu Ralph Powel kabla hajaniapisha!” Logan aliongea baada ya kuzinduka kutoka kwenye mawazo.











    “Uko sawa muheshimiwa?” Admiral Smith akauliza kwa udadisi akimuangalua Logan usoni.



    “Admiral! Naomba uniitie Jaji mkuu..  Nahitaji kuzingumza naye!”







    Logan akaongea huku anajiinamia kwenye meza kuficha machozi ya woga yaliyoanza kumtoka.







    THE OTHER HALF























    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE















    “…unaweza kuniona? Najua huwezi kuniona… lakini bado nataka kufanya mazungumzo, japokuwa hatuwezi kuyaita mazungumzo kwa kwa kuwa huwezi kujibu au kusema nami kama ninavyosema nawe!







    Nataka nikufahamishe juu ya tukio kubwa linaloweza kutokea duniani. Ndani ya nafsi yangu napata hisia kuwa kuna janga kubwa linaloelekea kutokea juu ya dunia.







    Japokuwa hujawahi kufanikiwa kunijibu ninachokueleza, lakini ni mara nyingi sana nimewahi kukueleza kuwa… katika maisha kila mtu anajiona shujaa katika historia yake, lakini ukweli ni kwamba hakuna shujaa, na wala hakuna mafedhuli. Sote ni binadamu tunajitahidi kufanya kile tunachoweza kusimama na kutetea kile tunachokiamini.







    Ndani ya nafsi ya kila mmoja wetu kuna ubaya na pia kuna uzuri, lakini tendo la kujitoa kuokoa maisha ya watu unaowathamini moyoni mwako ni uzuri halisi wa nafsi usio na mlingano.







    Naweza nisidumu kwa muda mrefu, najua umebakia muda mchache kabla sijaondoka duniani, lakini mzigo pekee nilionao moyoni mwangu ni kuhakikisha ninaowathamini wanendelea kuishi baada ya mimi kuondoka…”























    EPISODE 17















    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)















    Yule mnyama kama mbwa, mwenye mbawa za popo na ngozi kama ya binadamu alikuwa ametulia kimya kabisa kama ambavyo alivyojitokeza kwa mara ya kwanza. Alikuwa kana kwamba hawaoni Salim na wenzake waliosimama kwa kutengeneza duara.











    Salim na wenzake walikuwa wametulia tuli kabisa wanamuangalia yule mnyama kuona ni nini ambacho atakifanya.







    Salim alikuwa amefura kwa hasira akitafakari ni namna gani afanye kuokoa wenzake. Ndani ya nafsi yake aling’amua dhahiri kwamba mnyama huyu atawawinda mmoja mmoja mpaka awamalize wote.



    Kwahiyo ilikuwa ni eidha wachaukue hatua ya kumshinda sasa au wasubiri awawinde kama vifaranga mmoja baada ya mwingine.











    Salim akafura zaidi kwa hasira kama vile simba ambaye amejeruhiwa na mnyama ambaye anahisi hapaswi kumnynyasa. Licha ya baridi kali lilipo ndani ya Anabelle lakini kwa mara nyingine alikuwa anajisikia jasho linamtoka kutokana na lile ambalo alikuwa analifikiria kichwani mwake.



    Alichokuwa anataka kukifanya ni kumrukia huyu mnyama wa ajabu kisha waanze kukurukushana mpaka mmoja afanikiwe kumuua mwenzake. Ndani ya nafsi yake Salim alikuwa anakataa kabisa kufa kama kifaranga wa kuku. Alikuwa anaona ni bora afe akitetea uhai wake na wenzake kuliko kusubiri kiwindwa na huyu.











    Salim akiwa tayari kabisa amejiandaa kumrukia huyu mnyama ghafla katika maji ya ule mto pembeni yao waliamza kusikia kama kuna kitu kingine kinaibuka kutoka majini. Na ubaya zaidi hakikuwa kitu kimoja pekee bali vilikiwa vinasikika kama vitu viwili au vitatu vinaibuka taratibu kutoka majini kama vile mamba afanyavyo anapovizia windo lake lililo nchi kavu akitokea majini.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Salim na wenzake walihisi kama roho zinataka kuwatoka.











    “Mungu wangu! Wanaongezeka?” Magdalene akaongea kwa mshtuko na kwa sauti ya kilio ya kunong’ona.







    Hakuna yeyote kati yao aliyeweza kujibu au kujua ni nini hasa kilikuwa kinatokea. Walichokuwa wanakisikia masikioni mwao ni sauti ya viumbe ikiibuka kutoka majini.







    Kwa taabu sana kutokana na giza totoro lilipo ndani ya Anabelle, Salim akajitahidi kukaza macho kuangalia viumbe hawa waliokuwa wanaibuka na kuwahesabu. Akang’amua kuwa walikuwa ni viumbe watatu wanaibuka kutoka majini.







    Lakini kadiri viumbe hawa walivyokuwa wanaibuka kutoka majini walijikuta wanapatwa na mshangao zaidi. Viumbe hawa hawakuwa na muonekano kama huyu mnyama wa ajabu aliyepo mbele yao. Viumbe hawa walikuwa na umbo na mwonekano wa binadamu.











    “Watoto wa Maldives?” Salim akauliza kwa kunong’ona huku anahema kwa nguvu.



    Alikuwa anauliza kama viumbe hawa ni moja ya wale ambao mwenzao wamemuua pindi tu walipoingia ndani ya Anabelle.











    “Hapana! Hawa sio watoto wa Maldives… watoto wa Maldives hawatembei kama binadamu… wanatembea kwa miguu na mikono kama mbwa au paka!” Cindy akajibu kwa kunong’ona huku amekaza macho kwa wale viumbe.



    Kadiri walivyokuwa wanakaza macho ili wawaone vizuri wale viumbe ndivyo ambavyo walivyokuwa wanazidi kuwa dhahiri machoni mwao. Hakika walikuwa wanaonekana kufanana na binadamu kabisa.











    Yule mnyama wa ajabu kama mbwa mwenye mbawa za popo naye alionekana kuhisi uwepo wa binadamu hawa walioibuka kutoka kwenye maji.



    Mara moja akaanza kubadilika rangi kama awali. Rangi yake ikaanza kubadilika kutoka kwenye weupe pee kama theluji na kuanza kuwa rangi nyekundu ikiyopauka.











    Kwa kuwa hii haikuwa mara ya kwanza kwa Salim na wenzake kumuona mnyama huyu anabadili rangi namna hii, walielewa kuwa mnyama huyu amesikia harufu ya uwepo wa adui mahali hapo.







    Akina Salim walibaki wameduwaa kwa mshangao na woga wasijue yule mnyama anabadilika kwa kuhusi uwepo wa adui wao au wale binadamu wengine watatu walioibuka kutoka majini.











    Yule mnyama akageuka kwa haraka nyuma kuwatazama wale binadamu walioibuka kutoka majini, akawa kama anajiaandaa hivi kuwarukia. Mtu mmoja kati ya wale watatu akaruka kwa kasi kutoka majini mpaka nchi kavu na kumfanya yule mnyama asiruke bali ageuke tena nchi kavu.











    Baada ya yule mnyama kugeukia tena nchi kavu na wale wengine wawili wakatoka majini na kumzunguka yule mnyama kila upande.











    Salim na wenzake wakabaki wameshikwa na mshangao tu wasielewe ni nini kilikuwa kinaendelea hapa? Hawa watu wametokea wapi? Wanalengo gani hasa?











    Mmoja wapo wale watu watatu alikuwa ana kitu kama chemli hivi japokuwa ilionekana dhahiri kabisa sio chemli kama ya kawaida.



    Mwengine alikuwa amebeba kitu kama nyavu mkononi na yule wa tatu alikuwa na fimbo nene na inawaka moto sehemu ya mbele. Hata moto huu pia akina Salim walijua haukuwa wa kawaida kwa kuzingatia kwamba watu hawa walikuwa wameibuka kutoka majini lakini moto huo mbele ya hiyo fimbo haukuzimika.











    Kutokana na ile chemli iliyoshikwa na mmoja wao hii ilifanya eneo walilopo liwe na mwanga wa kitosha kabisa na kuwawezesha kuwaona vyema watu hawa.







    Watu wote wale watatu walikuwa ni wanaume, lakini walikuwa na muonekano wa ajabu. Walikuwa wevalia nguo za khaki zilizochakaa sana. Walikuwa na ngozi nyeupe sana ya kupauka kama vile si ngozi ya binadamu, na mikononi walikuwa na manyoya mengi sana ya kufanana kabisa na manyoya ya paka. Manyoya haya pia yalikuwepo mpaka masikioni ambako yalikuwa wametokeza hasa mpaka yananing’inia. Miguuni walikuwa peku peku.











    Salim, Cindy, Shafii na Magdalena wakasogea pembeni tena na kubaki kuduwaa kuangalia hiki kilichokuwa kinaendelea.











    Yule mtu mmoja aliyekuwa ameshikilia fimbo yenye moto mbele kwenye ncha alikuwa anaitumia kama kumtisha nayo yule mnyama.



    Fimbo hii ilionekana kuwa na kitu fulani chenye kuweza kumdhuru mnyama huyu kwani kila alipomtisha nayo yule mnyama alitoa sauti kali ya kilio na kurudi nyuma.







    Wale wengine wawili waliobakia walikuwa wameishikilia nyavu kama wameitegesha kumsubiria huyu mnyama anavyorudi nyuma ajitumbukize mwenyewe nyavuni.















    “Nani hawa?” Salim aliuliza huku anahema kwa nguvu wakiwa wamesimama pembeni kabisa wanaangalia hawa watu wanavyopambana na huyu mnyama.











    “Masalia ya The 46!” Cindy akajibu kwa ufupi.











    “Masalia?? Una maana gani?” Salim akauliza kwa mshangao huku bado anahema kwa nguvu.







    Cindy hakujibu chochote! Macho yake na akili yake yote alikuwa ameielekeza kuangalia namna watu hawa aliowaita ‘Masalia ya The 46’ wanavyopambana na huyu mnyama.











    “Wamempata!!” Cindy aliliouka kwa furaha akionyesha mkono upande ule ambako wale watu walikuwa wanapambana na yule mnyama.











    Watu wale walikuwa wamemuingiza yule mnyama kwenye ile nyavu na walikuwa wanamwagia kitu fulani hivi kilichokuwa kinamfanya yule mnyama apaparike pale chini kama ana kifafa.



    Yule mnyama akapaparika kwa kama dakika tatu hivi kisha akatulia kimya kabisa.











    Baada ya kutulia na kumaliza kumfunga vyema ndani ya ile nyavu mmoja wa wale watu akawageukia akina Salim.











    “Msiogope mko Salama!” Yule mtu akaongea kwa sauti ya ajabu ambayo hakuna kati yao ambao aliwahi kuisikia maisha yake yote. Alipokuwa anaongea sauti ilitoka kama vile alikuwa ananong’ona lakini sauti ilisikika sawia kabisa ikiwa na kama mwangwi hivi pindi ikitua masikioni.



    Alipoongea hivi alikuwa pia anawasogelea akina Salim pale walipo simama kwa kujikusanya kama vifaranga.











    “Nani nyinyi!” Magdalena akajikuta ameropoka kwa sauti akiongea kama vile analia.











    Yule mtu akatabasamu na kufanya meno yake yaliyochongoka kwa ncha kali yaonekane.











    “Jina langu naitwa Caleb!” Yule mtu akajibu.















    “CALEB???” Cindy akalipuka kwa sauti ya mshangao.















    “Una mfahamu?” Salim akauliza kwa mshangao zaidi.











    Si Cindy, wala yule mtu aliyejibu… walibaki tu wamekaziana macho kwa muda mrefu. Cindy alikuwa na mshangao fulani usoni mwake kana kwamba alikuwa yuko ndotoni asiamini kile kilichopo mbele yake.



    Wengine wote wakabaki wameduwaa wakiwaangalia Cindy na huyu aliyejimbulisha kama Caleb walivyokuwa wamekaziana macho.





    “…nimejikuta natumia zaidi ya nusu ya maisha yangu kujiuliza ni namna gani binadamu anapata ujasiri wa kuwa dhalimu na katili kama hivi tulivyo.

    Baadae nikajipa jukumu la kubadili mbari ya binadamu, kuwasahihisha namna walivyo.



    Ni mwaka 2038 nilipojipa kusudi hili la kuirekebisha mbari ya binadamu, na sasa unaposikia sauti hii ni zaidi ya miaka themanini imepita.



    Kutokana na yaliyotokea, kutokana dhahama kubwa iliyotokana na jukumu nililojipa, nimejikuta najiuliza na kujitathimini upya juu ya chaguzi niliyoifanya, vitu ambavyo labda ningevifanya tofauti, au labda kwa usahihi zaidi.

    Yote ni kwasababu nimejikuta napoteza usahihi na uhalisia wa mambo ambayo nilidhani ninayaelewa hapo mwanzoni.

    Ni ajabu jinsi ambavyo chaguo moja tu kwenye maisha linavyoweza kubadili kabisa hatma yako. Najikuta najiuliza, dunia ingekuwaje leo hii kama ninsingefanya chaguo nililolifanya.



    Leo hii, miaka themanini baada ya mwaka 2038, hakuna hata binadamu mmoja anayeishi maisha anayoyatamani. Japokuwa siko nanyi, lakini nafahamu kuwa kila mnapolala usiku kitu pekee mnachokiona kwenye ndoto ni kifo.



    Kuna muda ulikuwepo, japokuwa nasi tuliona kifo kila tulipofumba macho kulala, lakini walau hata kama tulikufa lakini tulikufa kwa sababu ya tunaowapenda na tunavyoviamini na kuutetea ulimwengu.



    Ndio sababu bado najiuliza kama ilikuwa sahihi kwangu kujipa jukumu ambalo nilijipa. Bado najiuliza kama ilikuwa sahihi kwangu kuacha tumaini life, kuacha duniani ipige goti, kuacha mbari ya binadamu kufutwa ulimwenguni… yote kwa sababu ya kusimamia jukumu ambalo nimejipa.



    Kuna mtu aliniuliza miaka michache iliyopita kama nimejifunza lolote kutokana na chaguo nililolifanya?



    Nilimjibu jambo ambalo liko moyoni mwangu siku zote, kwamba; “kila binadamu ni shujaa katika maisha yake! Lakini ukweli ni kwamba, hakuna shujaa katika maisha, na wala hakuna dhalimu. Sote ni binadamu tunapambana kufanya linalowezekana na kutetea tunachokiamini!”

    Imepita miaka themanini sasa tangu mwaka 2038. Najua uko mpweke juu ya dunia, na hii ndio sauti pekee unayoweza kuisikia! Najua unachofikiria, lakini unapaswa kujua kwamba, labda huu sio mwisho.!”

    RABAT, MOROCCO



    Laura Keith na Duran walikuwa wapo kwenye mojawapo ya vyumba katika lile Kasri kuu kuu lililopo kwenye msitu mnene kama kilometa tano kutoka pwani ya mji wa Rabat nchini Morocco.



    Chumba hiki kilikuwa katika ‘ghorofa’ moja kwenda chini katika Kasri hili. Licha ya taa za chemli kuwashwa ndani ya hiki chumba lakini bado kulikuwa na hali fulani ya giza na kufanya ndani ya chumba kuwa na mwanga hafifu.



    Hiki ndicho chumba ambacho Duran alikuwa anakitumia kama ofisi katika Kasri hili.

    Wote wawili walikuwa wameketi kwenye viti na katikati yao kulikiwa na meza ya kizamani sana ya kiofisi ambayo ilionekana dhahiri kwamba imekuwepo hapo kwa miongo mingi sana.

    Nyuma ya Duran kulikuwa na ‘Shelves’ ndefu zilizokwenda mpaka juu kwenye paa ambazo zote zilikuwa zimejaa vitabu vikubwa vikubwa.



    Laura Keith alikuwa amenyoosha mkono wake wa kushoto na kuuweka kuu ya meza akiwa kuna kitu mkononi mwake anajaribu kumuonyesha Duran.



    “Sikuelewi ni nini unataka nione?” Duran akaongea huku akiondoa macho yake kutoka kwenye mkono wa Laura na kumkazia macho usoni.



    “Huoni hicho kidonda kibichi?” Laura akamuuliza huku naye anamkazia macho.



    Duran akahamisha macho kutoka usoni kwa Laura na kuangalia tena kwenye mkono.



    “Nakiona Laura lakini sijui ni hasa unamaanisha!” Duran akamjibu huku anahamisha tena macho yake kutoka mkononi kwa Laura na kumkazia macho tena usoni.

    [5/5, 22:09] The Bold: “Hapo ndipo inapokaa POLO-TD! Kifaa kinachotumiwa na watu wa usalama kujua sehemu alipo Rais muda wote!” Laura akaongea huku amemkazia macho Duran.

    “Hicho kifaa kinahusiana nini na haya maongezi yetu au tunachokifanya hapa?” Duran akaongea huku akioneaka wazi kabisa kuwa alikuwa bado hajafahamu hasa muelekeo wa hoja za Laura.

    “Nadhani unakiona hakipo hapo? Kimetolewa ndio maana kimebaki kidonda!”



    “Kwahiyo?” Duran akauliza bado akiwa haelewi nini hasa muelekeo wa haya maongezi.



    “Ulisema kwamba eneo hili vifaa vya elektroniki haviwezi kufanya kazi!”



    “Laura nadhani ungeongea unachokusudia kukisema badala ya kupinda pinda kona!” Duran akaongea kwa hasira kidogo safari hii akionekana kukereka na Laura kuongea kwa mafumbo.



    Laura akainama zaidi kwenye meza ili kumsogelea kwa karibu zaidi na Duran. Akasogea mpaka nyuso zao zilipokaribiana kabisa kugusana kisha akaanza kuongea kwa hasira lakini kwa utulivu wa hali ya juu.



    “Kama vifaa vya elektroniki havifanyi kazi eneo hili kwanini umewaambia vijana wa Sancta Cedes wanitoe POLO-TD?” Laura akauliza huku amemkazia macho Duran.



    “Sijampa maagizo mtu yoyote akutoe hicho kifaa na nakuhakikishia hakukuwa na umuhimu wowote wa kufanya hivyo kwa sababu hakuna kifaa cha elektroniki kinachoweza kufanya kazi eneo hili!” Duran akajibu kwa kujiamini huku anamuangalia usoni Laura kwa udadisi.

    “Kwa hiyo kama sio Sancta Cedes walionitoa POLO-TD, ni nani amefanya hivyo?”



    Laura akauliza! Duran hakujibu chochte akawa kama anatafakari jambo fulani hivi kwa muda mrefu.



    “Uliniambia kwamba kuna kitu ulikiona kabla hatujaiodondosha Air Force One?” Hatimaye Duran akauliza.



    “Ndio! Kwa usahihi zaidi niseme ilikuwa ni muda ambao Air Force One ilikuwa inadondoka! Nahisi ilikuwa imebakia kama futi mia kadhaa tu hivi kabla ndege haijagusa maji nadhani nilikiona kisiwa cha Saman mbele yetu.” Laura aliongea huku amemkazia macho zaidi Mzee Duran.



    “Ati?? Haiwezekani!” Duran akahamaki kwa mshituko mkubwa.



    “Ndio Duran! Nimeyaona magofu ya kisiwa cha Saman kwa macho yangu kabisa mbele yetu ndege ikiwa inaelekea kuzama baharini!”



    “Hapana… itakiwa ulikuwa kwenye mshituko tu!” Duran akaongea huku ana simama kutoka kwenye kiti.

    “Kisiwa cha Saman kiko bahari ya Atlantiki ya kusini, na njia Air Force One iliyopita kutoka Vatican kuelekea Washington ni Atlantiki ya kaskazini…. Unachokisema hakiwezekani Laura!”



    “Duran! Nakueleza kile ambacho nimekiona!” Laura akajibu huku akimuangalia Duran alivyokuwa anatembea tembea mle chumbani na ule mwanga hafifu unaotoka kwenye chemli.



    “Kwa hiyo ni nini unachokihisi? Kuwa Masalia ndio walikutoa baharini kabla ya vijana wetu wa Sancta Cedes kukupata?”



    “Sijui Duran! Nilikuwa nategemea wewe ndio unipe majibu yote ya nini kimetokea! Nimepoteza fahamu tangu Air Force One idondoke mpaka masaa machache uliponizindua tena… nategemea unijibu ni nini kimetokea? Nani aliyenitoa POLO-TD?” Laura akauliza huku naye anasimama kutoka kwenye kiti.



    “Hizi nguo ulizivaa muda gani?” Duran akauliza baada ya kuacha kutembea tembea mle chumbani na kumuangalia moja kwa moja Laura.



    “Sifahamu ni muda gani! Duran nimekueleza kuwa sijui kilichotokea kuanzia muda ndege inadondoka mpaka muda mchache uliopita uliponizindua.”



    “Unataka kusema kuwa wakati ndege inadondoka haukuwa umevaa nguo hizi?” Duran akauliza kwa wasi wasi na mshangao.

    Laura akaanza kujiangalia kana kwamba ilikuwa ndio mara ya kwanza kwake kugundua zile nguo zilizoko mwilini mwake.

    Alikuwa amevalia gauni jeupe la moja kwa moja la mikono mirefu.. Shingoni na mikononi mwishoni karibu na viganja lilikuwa limedariziwa kwa urembo wa rangi ya zambarau.



    Laura akajiangalia tena na tena kana kwamba muda wote huu alikuwa hajui amevaa nini mwilini mwake.



    “Sikuvaa hivi Duran! Nilivaa suti ya kike ya kampuni ya Ralph Lauren, rangi ya zambarau iliyofifia kufanana na rangi ya Navy! Na shingoni nilikuwa na mkufu wa shanga za lulu na hereni zake… hivyo ndivyo nilivyovaa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu… nilipozinduka nikajikuta nimevaa hivi na nilijua ni vijana wako ndio wamenivalisha hizi nguo!” Laura akaongea kwa hofu kubwa akishangaa kusikia kuwa Duran hajui nguo hizo Laura amvalishwa na nani.



    “Mungu wangu! Umepita mkononi mwa masalia kabla ya kuletwa hapa!!” Duran akahamaki na kuanza kuzunguka upande wa pili wa meza pale alipokaa awali.



    “Masalia? Unamaanisha Caleb na wenzake ndio walinitoa baharini kwanza kabla ya vijana wako wa Sancta Cedes kufika?” Laura akapigwa na butwaa pia na kukaa chini kwenye kiti.



    “Ndio Laura! Nina amini Caleb na wenzake walikutia mikononi mwao kabla haujafika hapa na kabla vijana wa Sancta Cedes hawajakuleta hapa!”



    “Ina maana wanajua ushirika wangu na wewe? Na kwa nini waniachie baada ya kunitoa baharini? Na kwa nini wanibadilishe nguo? Hawatavujisha hiyo siri kama wameng’amua ushirika wangu nawe?” Laura aliuliza maswali mfululizo huku akiwa anahema kwa nguvu kwa woga kutokana na aliyoyasikia.



    “Ni mtego!” Duran akajibu kwa ufupi huku anatafuta kitu fulani pale mezani.



    “Mtego? Mtego wa nini?” Laura akauliza.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Mzee Duran hakujibu chochote akaendelea tu kutafuta kile alichokuwa anatafuta pale juu mezani.

    Hatimaye akakipata, ni kama nyundo fulani hivi ya mbao inayofanana kabisa na zile ambazo zinazotumiwa na majaji mahakamani. Akichukua na kuigonga mezani kama wafanyavyo majaji mahakamani.



    Mlango walioingilia ukafunguliwa na akaingia moja ya wale vijana wanaovaa suti nyeusi na wamenyoa upara kama walinzi ambao wanasimama milangoni na getini.



    “Niite kiongozi wa Sancta Cedes!” Duran akamueleza yule kijana wa ulinzi mara baada ya kuingia ndani.



    “Sawa mzee! Pia mchoro kutoka Vatican umewasili!” Yule kijana akajibu.



    Duran akawa anatafakari kama ameduwaa kwa dakika kadhaa hivi kama anatafakari ni kitu gani aanze kukifanya kwanza kati ya alichokuwa anakiwaza awali au hii taarifa aliyopewa muda huu.



    “Waambie wanisubiri ukumbini!” Duran akamuelekeza yule kijana.



    Yule kijana akainama kama anasujudu hivi kwa heshima kisha akageuka na kutoka nje.



    “Duran mtego gani?” Bi. Laura Keith akauliza tena.



    Duran hakujibu chochote, safari hii akageuka nyuma yake kwenye ile shelf ya vitabu na kuanza kupangua vitabu kwenye sehemu mojawapo kwenye shelf.

    Alikiwa anaondoa vitabu na kuviweka juu ya meza. Alipoondoa vitabu kama ishirini hivi pale kwenye shelf kulimuwa na kama kitasa hivi cha mlango. Akakifungua na kulikuwa na uwazi kama kidirisha kidogo sana na akapitisha mkono na kuuzungusha kama anafungua kitasa kigine kwa ndani.



    Mara ule ukuta wote wenye shelves za vitabu ukafunguka kama mlango.



    Duran akampa ishara Laura amafuate kule ndani kwenye kijichumba cha siri kilichokuwa kinaonekana baada ya ukuta kufunguliwa kama mlango.



    Walipoingia ndani kilikuwa ni kijichumba kidogo hivi cha mraba chenye urefu wa kama Mita tatu kila upande. Vitu pekee ambavyo vilikuwa kwenye chumba hiki ni majeneza matatu yenye rangi nyeusi mawili na lile lingine jeupe.



    “Naomba uingie humu!” Duran akamuonyesha Laura aingie kwenye jeneza moja wapo kati ya yale matatu lenye rangi nyeusi.



    “Kwa nini?” Laura hakamaki.



    “Laura! Nitakuja kukueleza ila kwa sasa sina muda wa kutosha.. Nimekwambia naamini huu ni mtego wa Caleb naasalia wenzake.!”



    Duran akaongea huku wamekaziana macho na Laura. Kutokana na imani kubwa Laura aliyokuwa nayo juu ya Duran hakutaka kubishana chochote. Akaingia kwenye lile jeneza jeusi ambalo Duran alikuwa amelifungua.



    “Kwa hiyo kunilaza kwenye hili jeneza kunahusiana vipi na mtego wa Masalia?” Laura akaongea akiwa amekaa Kitako ndani ya jeneza huku amenyoosha miguu.



    “Inabidi uende nyumbani ukarekebishe mambo kabla hayajaharibika… hatuwezi kufeli sasa, tumekaribia mno kupata sanduku la Pandora.! Naenda kuonana na walioleta mchoro wa George Washington kisha narudi muda si mrefu!” Duran akaongea kwa unyonge na hirima lakini akimaanisha haswa.



    Laura hakujibu chochote. Akajilaza ndani ya lile jeneza kama maiti. Duran akalifuniaka jeneza.











    NDANI YA MSITU WA OX – MARYLAND, MAREKANI



    Baada ya yule binadamu wa ajabu ambaye alikuwa anaongea na Mzee Caleb na kumuita mwanawe, kuwaamuru wenzake walio mkono wa kushoto kuwa amuru kuwa “mleteni”, wenzake wengine kama wanne hivi walikuja huku wakiwa wanaburuza kitu kama tundu au banda kama la mbwa hivi au mfugo fulani lakini lenyewe hili lilitengenezwa katika namna ambayo chini yake kulikuwa na matairi ya chuma.



    Watu hao waliliburuza banda hilo mpaka mbele ya yule mwenzao aliyeonekana kuwa kiongozi wao.

    Ndani ya hili banda kulikuwa na kiumbe wa ajabu ambao kwa kumuangalia tu mshituko ambao Naomi, Mzee Caleb, Ethan na wenzake walikaribia kudondoka na kuzirai.



    Alikuwa ni mnyama ka mbwa. Lakini alikuwa ni mkubwa zaidi mwenye kimo kama ndama. Alikuwa na mbawa zenye kufanana kabisa na mbawa za popo lakini hakuwa na nyoya au unywele hata mmoja. Rangi yake ilikuwa ni nyeupe kama theluji.



    Alikuwa amelala ndani ya lile banda kama amekufa lakini alikuwa anahema juu juu kuonyesha bado yuko hai.



    Wote walibaki wanakodoa macho wepigwa na butwaa wasiamini kile kilichopo mbele yao.



    “Ni nini hiki?” Hatimaye Naomi akapata nguvu ya kuiliza.



    “Ni mlinzi katika Anabelle!” Yule binadamu akajibu.



    “Mlinzi wa Anabelle? Mmemtoa wapi nyinyi?” Mzee Caleb akauliza kwa mshangao.



    “Tumemtoa ndani ya Anabelle, Caleb!” Yule binadamu akajibu huku anatabasamu safari hii.



    “Ina maana mna uwezo wa kuingia ndani ya mini iliyotwaliwa?” Naomi akamuuliza kwa udadisi.



    “Mara chache dirisha likijitokeza tuna uwezo wa kuingia na kutoka!”



    “Dirisha? Una maana gani?”



    “Hilo sio muhimu kwa sasa, jambo la muhimu ni huyu kiumbe mnachokiona hapa! Nahitaji muende naye na mumtunze mpaka pale tutakapo kuja kumchukua!” Yule binadamu akawaeleza kwa sauti ya kumaanisha.



    “Twende naye wapi? Ili iweje baada ya hapo!” Ethan akauliza kwa kukereka kutokana na hili jukumu analotaka kuwapa huyu binadamu.

    “Tunapaswa kuondoka hapa muda huu… muda wetu wa kukaa hapa umeisha.. Sikilizeni kwa makini! Mmetueleza kwamba mchoro wa George Washington umepotea, na rais pia amepotea… nataka muwe makini mtakaporudi huko mnakoenda na muwe macho kutazama kwa sababu kuna wakala wa The 46 atarudishwa siku yoyote kuanzia sasa… huyu mnyama nataka mumtunze sehemu ya siri, mtu yeyote zaidi yenu ya mliopo hapa aismuone! Kila baada ya siku tatu, jioni mpeni kopo moja la damu ya binadamu… msiongeze zaidi ya hapo atapata nguvu atawadhuru nasipumguze chini ya hapo atakufa! Nawasisitiza tena kuweni makini na muwe macho huko mnakorudi… kuna wakala wa The 46 anarudishwa! Caleb mwanangu… nisamahe kwa nilichokifanya miaka 60 iliyopita… nitarekebisha kila kitu!”



    Yule binadamu akaongea mfululizo wa maongezi kwa haraka haraka. Ni kana kwamba walikuwa wanatakiwa kuondoka hapo kwa haraka kwa hiyo alikuwa anahakikisha anawapa maelezo yote muhimu kwa haraka.



    Alipomaliza tu kuongea. Kulitokea sauti kama ya kunong’ona lakini ilikuwa sauti Kali sana iliyoambatana na mwangwi na ilikuwa inachoma haswa masikioni.

    Iliwabidi Mzee Caleb na wenzake wazibe masikio na kujiinamia ili kuzuia kuumia masikio na ile sauti kali.



    Ndani ya kama sekunde kumi hivi ile sauti ikapotea.

    Mzee Caleb, Naomi, Ethan na wenzake wakainua vichwa vyao na kutoa mikono masikioni.



    Yule binadamu na wenzake wote wale wapatao thelathini na mbili walikuwa wametoweka. Kilichobakia mbele yao alikuwa ni yule mnyama wa ajabu kwenye banda.



    Wote wakabaki wanaangaliana kwa mshangao na woga.

    MASAA MACHACHE YALIYOPITA

    NDANI YA ANABELLE 27

    Cindy bado alikuwa amekaziana macho na yule binadamu wa ajabu aliyeibuka kutoka kwenye maji na wenzake na kujitambulisha kwa jina la Caleb.



    “Caleb?” Cindy akauliza tena.



    “Umewahi kunisikia?” Yule binadamu wa ajabu akauliza.



    “Nimewahi kusikia kuhusu Masalia wa The 46 lakini lakini sikuwahi kuamini kama wapo!”



    “Nadhani umepata jawabu sasa!”



    “Wewe ni Caleb yupi? Baba yake Caleb au Caleb aliye hai?” Cindy akauliza.



    “Mimi ni Caleb mwenyewe, baba yake Caleb aliye hai!” Yule binadamu akajibu.

    “Alikuwa mnaelekea wapi?”



    “Tunatafuta mlango wa The 46!” Cindy akajibu kwa kifupi.



    “Huku mnakoelekea siko! Shukeni huku chini kuufuata ukingo wa mto kama kilomita 20 hivi!” Yule binadamu akawaonyesha muelekeo wanakotakiwa kwenda.



    “Asante sana Caleb kwa kutuokoa!” Cindy akashukuru.



    “Kuweni makini… bado kuna walinzi wengine wawili kwenye ukingo wa mto huko mnakoelekea… Tutaonana tena humu siku nyingine kama bado mtakuwa hai.!”



    “Siku gani?” Cindy akauliza kwa haraka.



    Lakini kabla hajajibu, kulisikika sauti kama ya kunong’ona hivi lakini ilikuwa sauti kali iliyoambatana na kama mwangwi hivi na ilikuwa kali kiasi cha kuumiza masikio.



    Cindy na wenzake wakaziba masikio na kujiinamia kupunguza maumivu ya masikio kutokana na ukali wa ile sauti.

    Kitu pekee walichokisikia baada ya hapo ni kama mshindo wa watu wakijitupa ndani ya maji pale mtoni.



    Zilipita kama sekunde kumi hivi ile sauti ikatoweka. Walipokuja kuinuka na kutoa mikono masikioni yule binadamu wa ajabu na wenzake wawili pamoja na yule mnyama wa kutisha walikuwa wametoweka mbele yao.

    Wote walibaki na wameduwaa na wamepigwa na bumbuwazi.



    “Cindy wale ni akina nani?” Salim hatimaye akauliza.



    “Yule ni Caleb, kiongozi wa Masalia ya The 46!” Cindy akajibu huku bado anaangalia mtoni walipojitupa wale watu.



    “Ndio akina nani?” Salim akauliza tena.



    “Twendeni tutafute huo mlango wa The 46 huku nikiwaeleza ni akina nani!” Cindy akajibu na wakaanza kutembea kwenye ukingo wa mto kuelekea muelekeo ambao yule binadamu wa ajabu alipowaelekeza.









    YALIPO MAKAZI YA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI (WASHINGTON D.C, NAVAL OBSERVATORY)

    Kuna siku ambayo tangu asubuhi kunavyo anza kukucha unajua itakuwa siku ya namna gani, unaweza kuona dhahiri kabisa labda itakuwa ni siku ya kufurahi, au siku ya kutimiza ndoto, au siku ya kufanikisha ulichokuwa unakitamani kwa muda mrefu.



    Lakini pia hata siku ambayo kuna damu itamwagika unaweza kuiona dhahiri kabisa tangu asubuhi kunavyokucha.

    Ndege wa asubuhi unawasikia sawia zaidi jinsi wanavyoimba kuliko siku zote. Ukiwasha birika ya kuchemsha chai unaweza kusikia kwa sawia zaidi mlio wake hafifu wa mluzi pale maji yakichemka. Utulivu mkubwa ndani ya nafsi unakuwa dhahiri kiasi kwamba unaogofya na kuweza kukufanya unatamani utoke ndani ya nafsi yako. Kila mtu anaogopa kelele za uchungu au kelele za kukera.

    Lakini hakuna kitu kinachoogofya juu ya dunia kushinda ukimya. Ukitembea usiku kwenye mtaa mtupu, usio na mtu hata mmoja barabarani, ukisikia kelele labda za radio au watu hata wakiwa wanagombana, ndani ya nafsi yako unajisikia amani. Kwa kuwa unajua hauko peke yako.



    Lakini ukitembea kwenye usiku kwenye mtaa ulio tupu, na kukiwa na ukimya kiasi kwamba unaweza kusikia hata panya akiwa anatembea, hakuna hisia ya kuogopa kuzidi ukimya wa namna hii. Ndio sababu ukiwa gizani kwenye mtaa wenye kimya kikuu namna hii unatamani ungelikuwa unaweza upae na kufika unakokwenda ndani ya sekunde.



    Hakuna kitu cha kuogofya kuzidi ukimya, kwa sababu ukimya unaashiria upweke, na upweke ndio hofu kuu ya binadamu.



    Hivi ndivyo ambavyo siku ambayo damu itamwagika inavyoanza, haijalishi hata ukifungulia redio au runinga mpaka sauti ya mwisho lakini ndani ya nafsi yako unasikia ukimya mkuu wa kuogofya.

    Vitu ambavyo katika siku za kawaida haukuwa ukivisikia au akili yako kuvinga’amua, siku hii unavisikia kwa dhahiri kabisa kana kwamba ni mara yako ya kwanza. Sauti za ndege wa asubuhi wakiimba, maji ya bomba la kuogea bafuni, mluzi wa birika la kuchemsha chai, pumzi unayoivuta ndani na inavyotoka nje. Vyote unavisikia kwa usahihi kabisa. Kila sauti ambayo haikuwahi kuitilia maanani, katika siku hii inakuwa dhahiri masikioni mwako kutokana na ukimya mkuu wa kuogofya uliopo ndani ya nafsi yako.



    Hivi ndivyo ambavyo siku ya David Logan, Rais Mpya wa Marekani aliyeapishwa siku tatu zilizopita ilivyoanza.



    Baada ya kumaliza kufanya mazoezi na kuoga na kisha kijiandaa kwa ajili ya kuanza siku ya kazi, akafanya kitu ambacho huwa anafanya kila siku ambapo anakuwa anajisikia hisia kama hii aliyokuwa anajisikia leo.



    Ilikuwa ni takribani saa kumi na mbili kasoro robo ambapo David Logan alielekea kwenye “basement” ya nyumba yake. Basement hii ilikuwa inatumiwa kama chumba cha stoo kwenye nyumba hii.



    Ukishafika humu ndani ya basement mkono wa kushoto kulikuwa na maboksi ya vitu mbali mbali vimepangwa. Pembeni ya maboksi haya kulikuwa na baisikeli ya mtoto wa kama miaka 10 au 12 hivi. Hii ilokuwa ni baisikeli ya mtoto wake wa kike anayeitwa Natalie.



    Macho ya Logan yalipotua kwenye hii baisikeli aliiangalia kwa muda mrefu sana na kwa huzuni sana kutokana na kumbukumbu ya huzuni iliyokuwa inamjia kichwani kutokana na kuiona baisikeli hii.



    Katikati ya basement kulikuwa na meza ya mchezo wa “table tennis”. Meza hii iko hapa siku zote lakini leo hii alijikuta anaiangalia kwa uchungu kama ambavyo ameiangalia ile baisikeli ya mtoto wake Natalie.

    Kwa uchungu na huzuni akajikuta Meza hii inamrejeshea kumbukumbu za mke wake Latisha.

    Logan akajikuta anaikodolea macho ile meza kwa karibuni dakika tano nzima kana kwamba anajiona yeye upande mmoja wa meza na mkewe Latisha upande mwingine wakicheza mchezo huo waliokuwa wakiupenda kuucheza pamoja. Akajikuta uchungu uliochanganyika na furaha unaujaza moyo wake.







    Logan akajikuta anatabasamu na kugeukia upande wa kushoto wa hii basement.



    Upande huu wa kushoto kulikiwa na kabati tupu la vitabu. Kabati lilikuwa na vumbi kiasi kutokana na kutowekewa kitu chochote kwa muda mrefu.



    Logana akalisogeza kabati pembeni na mbele yake ukutani kulikuwa na ‘keypad’ kama ya kufungua ‘safe’ ikiwa na vitufe kadhaa.

    Logan akabofya vitufe kadhaa kuingiza neno la siri na kisha kuvuta kitasa kidogo kama kitasa cha mlango kilichokuwa pembeni ya ‘keypad’ hiyo.

    Ukafunguka mlango wenye ukubwa saizi ya kati lakini unaotosha mtu kuingia ndani. Logan akaingia ndani ya kijimlango hiki na kutokea ndani ya kijichumba kidogo cha saizi ya kati.



    Kijichumba hiki kidogo kilikiwa nadhifu mno kilichopakwa rangi ya kijivu chumba kizima. Vitu pekee ndani ya chumba hiki vilikuwa kabati dogo la kioo lilipo upande wa kulia ukiingia ndani ya hiki kijichumba. Pia kulikuwa na kiti ch a kukaa cha kiofisi kilichopo upande mwingine wa chumba na mbele yake kulikuwa na cemera iliyo kwenye kwenye stendi.

    Logan akafunga mlango na akatembea moja kwa moja na kwenda kuketi kwenye kile kiti kilicho mbele ya camera.

    Baada ya kuketi na kurekebisha vizuri shati lake akawasha camera na kuanza kujirekodi akiongea.







    “…Novemvber 13, 2038. Ujumbe namba 15 kwa Mwanangu Natalie Logan na vizazi vijavyo..”







    Akanyamaza na kukohoa kidogo kuweka sauti yake sawia kisha akaendelea.

    “……nimejikuta natumia zaidi ya nusu ya maisha yangu kujiuliza ni namna gani binadamu anapata ujasiri wa kuwa dhalimu na katili kama hivi tulivyo.



    Baadae nikajipa jukumu la kubadili mbari ya binadamu, kuwasahihisha namna walivyo.



    Ni mwaka 2038 nilipojipa kusudi hili la kuirekebisha mbari ya binadamu, na sasa unaposikia sauti hii ni zaidi ya miaka themanini imepita.







    Kutokana na yaliyotokea, kutokana dhahama kubwa iliyotokana na jukumu nililojipa, nimejikuta najiuliza na kujitathimini upya juu ya chaguzi niliyoifanya, vitu ambavyo labda ningevifanya tofauti, au labda kwa usahihi zaidi.



    Yote ni kwasababu nimejikuta napoteza usahihi na uhalisia wa mambo ambayo nilidhani ninayaelewa hapo mwanzoni.

    Ni ajabu jinsi ambavyo chaguo moja tu kwenye maisha linavyoweza kubadili kabisa hatma yako. Najikuta najiuliza, dunia ingekuwaje leo hii kama ninsingefanya chaguo nililolifanya.







    Leo hii, miaka themanini baada ya mwaka 2038, hakuna hata binadamu mmoja anayeishi maisha anayoyatamani. Japokuwa siko nanyi, lakini nafahamu kuwa kila mnapolala usiku kitu pekee mnachokiona kwenye ndoto ni kifo.







    Kuna muda ulikuwepo, japokuwa nasi tuliona kifo kila tulipofumba macho kulala, lakini walau hata kama tulikufa lakini tulikufa kwa sababu ya tunaowapenda na tunavyoviamini na kuutetea ulimwengu.







    Ndio sababu bado najiuliza kama ilikuwa sahihi kwangu kujipa jukumu ambalo nilijipa. Bado najiuliza kama ilikuwa sahihi kwangu kuacha tumaini life, kuacha duniani ipige goti, kuacha mbari ya binadamu kufutwa ulimwenguni… yote kwa sababu ya kusimamia jukumu ambalo nimejipa.







    Kuna mtu aliniuliza miaka michache iliyopita kama nimejifunza lolote kutokana na chaguo nililolifanya?







    Nilimjibu jambo ambalo liko moyoni mwangu siku zote, kwamba; “kila binadamu ni shujaa katika maisha yake! Lakini ukweli ni kwamba, hakuna shujaa katika maisha, na wala hakuna dhalimu. Sote ni binadamu tunapambana kufanya linalowezekana na kutetea tunachokiamini!”

    Imepita miaka themanini sasa tangu mwaka 2038. Najua uko mpweke juu ya dunia, na hii ndio sauti pekee unayoweza kuisikia! Najua unachofikiria, lakini unapaswa kujua kwamba, labda huu sio mwisho.!”

    Akamaliza… akashusha pumzi ndefu! Kisha akazima Camera na kunuka kwenye kiti na kuelekea kufunga mlango na kutoka basement kuelekea juu ya nyumba.







    “…Mr. President! Habari ya asubuhi? Nimekusubiri muda mrefu sana hapa… uko sawa muheshimiwa?” Kevin, katibu wa Rais Logan akauliza maswali mfululizo.



    “Niko sawa Kevin.! Habari ya asubuhi?” Logan akajibu kwa kujiamini huku anaelekea kupeana mikono na Kevin.



    Pale sebuleni kulikuwa na maafisa wa Secret Service karibia kumi na tano waliokuwa wamesimama kona mbali mbali nao wakimsubiri Rais Logan.

    “Niko salama Mr. President! Tunahitaji kuelekea Whitehouse mara moja muda huu, Admiral Smith anahitaji kukupa muhtasari wa suala muhimu.!” Kevin akaongea haraka haraka huku anachukua mkoba wa Logan ambao ulikuwa juu ya Sofa.

    Logan hakujibu chochote! Moja kwa moja akaanza kutembea kuelekea nje huku maafisa usalama wakiwa wamemznguka kila upande.



    Uzuri ni kwamba katibu wake Kevin alikuwa amedumu naye kwa miaka mingi tangu angalu Seneta, kwa hiyo alikuwa anamfahamu vizuri bosi wake muda gani yuko sawa na muda gani hayuko sawa na anapaswa ampe nafasi ya kuwa peke yake.

    Kwa hiyo walipoingia kwenye gari na msafara kuanza kuelekea Whitehouse Kevin akakaa kimya kabisa na kumuacha bosi wake aendelee kuwaza na kuwazua kilichopo kichwani mwake.



    Logan alikuwa ameketi kwenye gari huku macho yanatazama nje akionekana dhahiri kwamba mawazo yake yalikuwa mbali sana kuna kitu kinachomsumbua rohoni alikuwa anakitafakari.



    Kichwani mwake Logan alikuwa anawaza wazo moja tu kuhusu siri kubwa iliyokuwa ndani ya moyo wake. Alikuwa anawaza na kutafakari kama alichokifanya wiki tatu zilizopita kilikuwa ni sahihi. Akawaza pia kama kuna usaliti umetokea kwa washirika wake waliomsaidia kutekeleza mpango huo, Waziri wa Mambo ya nje na kampuni ya DathMov Contractors.



    Akawaza pia kuhusu maneno aliyomwambia jaji mkuu kabla hajamuapisha kama ilikuwa sahihi kumwambia meneno yale au iko siku maneno yake yatakuja kumgharimu.



    Aliwaza pia kuhusu hiki kitu cha dharura ambacho Kevin amueleza na kuwataka waende Whitehouse mara moja ili wapewe maelezo na Admiral Smith. Logan presha ilikuwa inampanda siku hizi kila aliposikia kuwa Admiral Smith anataka kuongea naye. Admiral amekuwa akimpa habari mbaya mfululizo kwa siku za karibuni.



    Logan akawaza na kuwazua. Alipokuja kuzinduka kwenye mawazo yake tayari walikuwa wamefika Whitehouse. Jambo la kwanza Logan kuligundua ilikuwa ni familia ya Rais aliyepita Laura Keith ambayo Jana wakati anaondoka kutoka ofisini, aliwaacha wako na pirika pirika ya kuhama ili waweze kumpisha yeye na mwenza wake wahamie rasmi Whitehouse. Lakini Leo hii baada ya kufika hapa Whitehouse hakuona pirika pirika yoyote, kulikuwa na utulivu mkubwa na ndani ya ghorofa ya juu ya Whitehouse ambako ndiko Rais anapaswa kuishi na familia yake, akaona bado familia ya Laura bado ipo.



    Akamgeukia Kevin ambaye alikuwa amekaa mbele yake ndani ya Presidential Limousine,



    “Kevin! Nadhani familia ya Laura walikuwa wanatakiwa kuhama mpaka sasa, sivyo? Imekuwaje?” Logan akauliza huku anaonyesha kidole juu ghorofani kwenye makazi ya Rais na familia yake.



    “Nitafuatilia Mr. President kwanini hawajaondoka mpaka muda huu?” Kevin akajibu huku anaandika kwenye PDA ya tablet mkononi mwake.

    Baada ya wote kushuka kwenye gari wakaelekea moja kwa moja mpaka situation room ambako walielezwa kuwa Admiral Smith anawasubiri.

    “Habari ya asubuhi?” Logan akamsalimu Admiral mara tu alipoibgia ndani ya situation room.



    “Nzuri muheshimiwa!” Admiral akaitikia Salamu huku anapiga saluti na kisha kuketi mara baada ya Logan kuwa ameketi.



    Logan hakutaka kukatakata kona, akaenda moja kwa moja kwenye suala lilipo mezani.



    “Admiral! Kuna lipi jipya asubuhi yote hii?”

    “Mr. President nina taarifa muhimu mno na nilitaka wewe uzipate kabla ya mtu yeyote yule!” Admiral akauongea akiwa na uoga kidogo.



    “Ni nini admiral?” Logan akauliza huku amemkazia macho.

    “Mr. President… tumefanikiwa kumpata Madam President Laura Keith!!!” Admiral akaongea huku anatazama chini kukwepesha macho yake na Logan.



    “Ati???” Logan akahamaki mpaka akasimama wima.

    “Ndio Mr. President! Amepatikana Leo usiku kwenye pwani ya visiwa vya Caribbean!”

    Logan akahisi kama dunia nzima inapasuka vipande vipande na anamezwa ndani yake.



    Ilibidi akae chini ili asidondoke kwa mshituko.





    THE OTHER HALF

    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE

    EPISODE 20











    SIKU YA PILI







    Ni sauti iliyofifia ikigugumia kwa uchungu ndio pekee ilikuwa inasikika kwa mbali sana katika ghala kubwa lenye kiza totoro ambalo lilikuwa na taa moja tu ambayo ilikuwa inajitahidi kuangaza.



    Japokuwa giza lilikuwa ni kubwa mno huku kukiwa na mwanga hafifu tu ndani ya ghala, lakini pua zilikuwa na uwezo kabisa wa kusikia harufu ya damu. Damu ambayo ilikuwa imetuama chini sakafuni na kutengeneza kidimbwi kidogo kama vile kisima kilichojaa mchanga na kufanya maji yabaki juu juu tu pekee.



    Harufu ya damu haikuwa inaogofya kama ambavyo ilikuwa inaogofya sauti hii hafifu ya kugugumia kwa uchungu.

    Haikuwa dhahiri sana ni nini hasa ambacho sauti hii hafifu iliyokuwa inalalama kwa uchungu ilikuwa inatamka. Maneno pekee ambayo labda yalikuwa yanaweza kusikia yalikuwa ni “…natalie…”, ambayo yalikuwa yanasikika yakitamkwa na sauti hii hafifu kana kwamba yanatamkwa na mtu aliyeshikwa na kwikwi.



    ” na…ta…li..e”



    Sauti iligugumia kwa uchungu huku ikirudia tena na tena ilichokuwa ikitamka.



    Harufu ya damu mbichi ilikuwa imetapakaa kwenye ghala hili kubwa kiasi kwamba mtu ungeliweza kufikiria labda alikuwa ndani ya mto au kisima kinachotiririsha mifereji ya damu mbichi ya binadamu.



    Katikati kabisa ya ghala hili kubwa ambapo ndipo taa ndogo ya ‘balbu’ ilikuwa inawaka kwa mwanga hafifu wa njano, kulikuwa na mnyororo uliofungwa kutoka juu ya paa la ghala kwa kuning’inizwa.

    Mnyororo huu uliokuwa unaning’inia haukuning’inizwa hivi hivo tu, bali kuna binadamu aliyefungwa na mnyororo huu.



    Mtu huyu alikuwa amefungwa katika namna ambayo alikuwa amesimama na mnyororo umefungwa mikononi mwake na mikono kuvutwa juu ya kichwa. Namna ambayo alikuwa amesimamishwa ilikuwa ni kusimama kwa maumivu makubwa kwa sababu ule myororo aliofungwa mikononi ulikuwa umekazwa kwa kuvutwa juu mpaka kufikia hatua ambayo alikuwa kama amesimama kwa kuchechemea na vidole. Yawezekana labda ni kucha tu ndizo ambazo zilikuwa zimegusa sakafu, lakini mwili wote ulikuwa unaning’inia kwa nyororo iliyofungwa mikononi na kuning’inia angani.



    Mwili wake mweupe wa kizungu ulikuwa umechoka kwa maumivu na ngozi ilikuwa imebadilika na kuwa nyekundu kabisa kana kwamba alikuwa amewekwa juani kutwa nzima. Kutokana na kuning’inizwa vile angani kwa muda mrefu huku kucha tu zikiwa vimegusa sakafuni, mikono yote ilikuwa imekufa ganzi na hakuwa anahisi chochote kile kuanzia mabegani kuelekea mikononi, ilikuwa ni kana kwamba mikono imekatika tayari.



    Tumboni na kifuani alikuwa na vidonda vikubwa ambavyo viliambatana na michirizi mikubwa ya damu.

    Kichwa chake ambacho alikuwa amekiinamisha kama amelala kilifanya majeraha aliyonayo mdomoni yasionekane vyema lakini ikisababisha damu nyingi kuvuja kutoka mdomoni.

    Damu ilionekana kwamba ilikuwa imevuja kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua kwamba ilianza kutoka damu nzito iliyokuwa inanata kama udenda. Hii ilifanya mdomoni kwake kuwe na kama ‘uzi’ mwekundu wa damu unaoning’ninia.



    Mwili wake haukuwa na hata kipande kimoja cha nguo, alikuwa uchi wa mnyama kama alivyozaliwa na hii ilifanya majeraha yaliyopo mgongoni mwake, kifuani na tumboni yaonekane vyema na kuogofya zaidi hata kuyatazama.



    Pamoja na mtu huyu aliyeninginizwa hivi na majeraha mwili mzima ndani ya ghala hili, pembeni yake kulikuwa na mtu mwingine, mzee aliyevalia suti nyeusi tii kabisa na akiwa amenyoa upara ambaye alikuwa kwenye kiti cha chuma anavuta kiko huku anatazama mwenzake aliyening’inizwa kana kwamba anafurahia kumuona katika hali hii.



    Lakini si mzee huyu tu pekee aliyekuwemo kwenye ghala hili. Bali pia kulikuwa na kijana ambaye yeye alikuwa amesimama mikono yake imeloa damu, naye alikuwa amevaa suti nyeusi huku kichwani amenyoa upara naye kama yule mzee pembeni yake aliyekaa kwenye kiti anavuta kiko.







    Yule mzee akainuka kutoka kwenye kiti, mkononi alikuwa ameshikilia chupa ndogo ambayo ndani yake ilikuwa imejaa aina fulani ya pombe kali. Baada ya kuinuka moja kwa moja akamsogelea yule mtu aliyening’inizwa kwa nyororo na kisha kumwagia kifuani ile pombe, akimwagia katika namna ya kummiminia kama vile bomba linatiririsha maji.



    Maumivu ambayo alikuwa ameyapata baada ya kumwagiwa pombe hii kali hayakuwa na mfano, lakini mwili wake wote ulikuwa umeishiwa nguvu kabisa kwa hiyo hata alipojaribu kulia cha uchungu kutokana na kumwagiwa pombe sauti haikutoka kabisa, aliishia kufungua mdomo kwa nguvu na kugugumia kana kwamba mtu anayezama kwenye maji akiwa ameanza kukosa pumzi.



    “Amka David!! Sitaki ulale… hii shughuli ndio kwanza imeanza!”



    Mzee Duran aliongea huku anaelekea kukaa tena kwenye kiti ambacho alikuwa amekaa awali.

    Huyu alikuwa ni mzee Duran, kiongozi wa sasa wa jumuiya ya THE 46 na ndiye yeye ambaye siku chache zilizopita alikuwa anaongoza kikao na wemzake kule Rabat, nchini Morocco. Ndiye yeye pia ambaye baada ya mazungumzo yake na Madam President Laura Keith wakiwa ofisini kwake kwenye jumba la ajabu kule Rabat, alimuweka Lauara kwenye jeneza na kumueleza kuwa anatakiwa kurudi ili akarekebishe jambo Fulani kabla halija haribika kabisa.



    Na huyu aliyekuwa anaongea naye, huyu ambaye ening’inizwa katikati ya ghala kwa nyororo alikuwa ni David Logan, makamu wa Rais wa Marekani ambaye wiki moja tu iliyopita alikuwa ameapishwa kuwa Rais wa Marekani.



    Masaa machache tu yaliyopita Logan alikuwa zake Whitehouse, akitekeleza majukumu kama kiongozi wa nchi. Amefikaje katika hali hii?? Ni swali ambalo ni la kusisimua sana ambalo hata David Logam mwenyewe ambaye japokuwa nusu ya ufahamu wake alikuwa ajitambui kutokana na maumivu makali iliyokuwa anayasikia mpaka kufika wakati ambao sasa alikuwa mwili mzima umekufa ganzi, lakini bado kwa ufahamu kidogo ambao bado alikuwa nao, alipofikiria namna ambavyo alifikia hatua hii, hakuamini macho yake na akili yake. Kama hiki ambacho alikuwa anakikumbuka kilikuwa ni halisi na si maluwe luwe ya maumivu, hii ilimfanya ajikute anaanza kukata tamaa kabisa kama kuna uwezekano wowote wa kusitisha miji kutwaliwa duniani na kugezwa kuwa Anabelle.



    “David!! Nakuiliza tena na safari hii usiponijibu kitakachofuata hautakuja kumsimuliza mtu yeyote mpaka unaingia kaburini!”



    Duran akaongea huku anainuka tena na kumsogelea Logan pale aliponing’inizwa.



    “David!! Kwanini ulifahamu kinachofanywa na Laura na ukaruhusu akifanye?? Ulikuwa na maslahi gani? Unafahamu nini kingine kuhusu The 46?”

    Duran aliuliza maswali mfululizo huku anamtazama Logan ambaye uso wake alikuwa ameuinamisha akionekana dhahiri kabisa kwamba nusu ya ufahamu wake haukuwepo.

    “Na…ta…li..e..!!”



    Ndio maneno pekee ambayo David alikuwa anayatamka tena na tena.



    Duran akionekana kukereka akageuka kumuangalia yule kijana aliyevalia kama yeye suti nyeusi na upara, huku mikono yake imelowa damu.



    “Endelea..!!” Duran akamuamuru yule kijana kisha yeye akaenda kuketi kwenye kiti pale alipoketi awali na kuendelea kuvuta kiko.

    Pale sakafuni pembeni ya yule kijana kulikuwa na kama kisanduku cha bati ambacho kimejaa vitu mbali mbali vya ajabu na vingine vya kutisha. Kulikuwa na mikasi, kimsumeno kidogo, visu, ‘prize’, sindano, na vitu vingine ambavyo havikuwa hata na majina yanayojulikana. Baadhi ya vifaa hivi vilikuwa vimelowa damu mbichi, hii ikimaanisha kuwa vimetumika mwilini mwa David Logan muda si mrefu.



    Baada ya kijana huyu kupewa amri na Mzee Duran kuwa aendelee na zoezi lake, akainama mpaka kwenye kisanduku hili cha bati na kuchukua kitu kirefu na chembamba kama ‘spoku’.



    Baada ya kuichukua akamsogelea Logan pale aliponinginizwa huku akiwa anatabasamu.

    “Maumivu ambayo utayasikia muda mchache ujao, haujawahi kuyasikia wala kuyafikiria maisha yako yote kwamba yanawezekana binadamu kusikia maumivu kiasi hicho!” Yule kijana akaongea huku anatoa tabasamu la kifedhuli.







    Kwa kutumia mikono wake wa kushoto akashikilia uume wa David Logan ambaye yuko uchi kabisa kama alivyozaliwa, kisha mkono wa kulia akashikilia ile spoku nyembamba sana.



    Akachukua spoku na kuanza kuingiza katika tundu la juu ya kichwa cha uume taratibu huku anaizungusha zungusha ili iingie vyema.

    Maumivu ambayo David Logan alikuwa anayapata kutokana ma spoku hii kuingizwa kwenye uume wake yalikuwa makubwa yasiyomithirika kiasi kwamba mpaka yakamfanya zimuondoe kwenye ‘usingizi’ wake na nusu kuzirai na kujikuta ghafla anapiga mayowe ya maumivu huku anapaparika kama vile kuku aliyekanyagwa shingo ili achinjwe.



    Kelele hizi za uchungu hazikumfanya kijana huku akatize zoezi lake la kumuingiza Logan spoku uumeni, aliendelea hivyo kiasi kwamba mpaka katibia nusu nzima ya spoku ilikuwa imezama ndani ya uume kwa kupitia tundimu la kukojolea.



    Alipohakikisha kuwa imezama vya kutosha, ndipo akaanza kuitoa taratibu huku anaizungusha zungusha tena kama awali.

    Maumivu ambayo Logan aliyasikia muda huu yalikuwa ni makubwa maradufu kuliko hata muda ambao spoku ilipokuwa inaingizwa ndani kwenye uume. Logan alipiga yowe kubwa la maumivu kuwa sauti ya juu mpaka mapafu aliyasikia yanataka kupasuka.



    Spoku ilipotoka yote alijikuta anahema kwa nguvu huku jasho likimtoka na kuchanganyika na damu ambayo ilikuwa imetapakaa mwilini mwake kote.

    Alihema kwa nguvu jasho na damu zikimiminika takribani dakika kumi nzima.



    “David!! Kwanini ulifahamu kinachofanywa na Laura na ukaruhusu akifanye?? Ulikuwa na maslahi gani? Unafahamu nini kingine kuhusu The 46?”



    Duran alikuwa ameinuka tena na amesimama mbele ya David na kumuuliza tena swali lile kama ambavyo alimuuliza awali.

    “Na…ta…li….e…!” David aligugumia maumivu ksa uchungu huku akimungunya tena jina la mtoto wake Natalie.

    “Endelea.!!” Duran akamuamuru tena yule kijana anendelee na zoezi lake.



    “Mzee! Nahisi anajaribu kukujibu!” Yule jamaa akaongea huku anakaza macho yake midomoni kwa David Logan.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Nini?” Duran akauliza huku anageuka kabla hajakaa kwenye kiti chake pale pembeni yao.



    “Natalie!! Hili jina analolitamka kila mara… Nadhani ndio jibu analojaribu kukupa kila muda ukimuuliza swali!” Yule kijana akaongea kwa shauku huku anamuangalia boss wake.



    “Natalie?? Natalie ni jina la mtoto wake!” Duran akajibu na kuuliza huku akamsogelea tena David.

    “David?? Natalie ndio amekufanya ufahamu kilichokuwa kinafanywa na Laura au Natalie ndio mwenye majibu?”



    Mzee Duran akaongea huku anainamisha uso wake ili uwe kwenye usawa mmoja na uso wa David ulioinamishwa kutokana na kuchoka.



    Lakini safari hii David alipoulizwa swali hili na Mzee Duran, hakujibu chochote na wala hakumungunya tena jina la mwanaye kama alivyokuwa anafanya awali.



    “David? Natalie ndio jibu?” Mzee Duran akauliza tena.



    Sijui Logan alipata wapi nguvu mwilini, lakini aliinua uso wake na kumtazama Duran moja kwa moja usoni na kwa haraka akamtemea mate usoni.



    Duran akaruka nyuma kidogo lakini mate yote yalikuwa yamempata usoni. Akatoa kitambaa chake cha jasho kutoka kwenye mfuko wa ndani wa koti la suti na kujifuta uso mate hayo yaliyokuwa yamechanganyika na damu na kufanya kuwa mekundu kabisa.

    “Nadhani tumepata kwa kuanzia!! Natalie..” Duran akaongea huku anatoa tabasamu la kifedhuli na kumuangalia Duran.



    Baada ya hapo akageuka na kumuangalia yule kijana wake mtesahi.



    “Nahitaji Natalie apatikane popote alipo na ndani ya masaa kumi na mbili yajayo awe amekishwa hapa mbele yangu!” Duran akatoa amri kwa yule kijana mtesaji.











    MASAA 72 YALIYOPITA (TAREHE 20 DESEMBA 2038)



    Mpaka kufikia siku ya leo desemba 20, mwaka 2038 tayari zilikuwa zimepita takribani siku 734 tangu kutokea kwa Anabelle 1 (nchi ya Maldives).



    Wiki mbili tu zulizopita dubuani kote kulikuwa na Anabelle 29 pekee, ambapo kati ya hizo, Anabelle mbili zilikuwa ni mji wa Dar es salaam na Ruangwa nchini Tanzania.



    Lakini mpaka leo hii tayari kulikuwa na jumla ya Anabelle 78 duniani kote na jambo ambalo lilikuwa linawatisha zaidi serikali ya Marekani ni mji mmoja ndani ya nchi ya Marekani kutwaliwa…. Mji wa Minnesota, ambao ulitwaliwa na kufanywa kuwa Anabelle 76.



    Rais mpya wa Marekani, David Logan pamoja na Jaji mkuu Raph Powell, na mwanasheria mkuu Jerome Kings walikualiwa katika Oval Office kwenye viunga vya white house kujadili ni nini hasa walikuwa wanatakiwa kufanya baada ya kupokea kwa taarifa kuhusu kuoatikana kwa Bi. Laura Keith kwenye pwani ya visiwa vya Carriabeans.



    Logan alikuwa anapaswa kumaliza kikao hili mapema ili hatimaye aweze kuelekea Situation Room ambako alikuwa anasubiriwa na Mkurugenzi wa CIA, FBI na Mshauri wa Masuala ya Usalama pamoja na Mwenyekiti wa Joint Chiefs of Staff ili wampe taarifa ya juhudi zinazoendelea ili kunusuru Wamarekani kwenye miji mingine wasiweze kupotea ndani ya Anabelle kama ambavyo ilitokea Minnesota.



    Kitendawili kikubwa ambacho kilikuwa kinaumiza vichwa vyao ilikuwa ni namna gani wanatakiwa kupata suluhu ya changamoto iliyoko mbele yao ambapo ilikuwa ni kana kwamba nchi ilikuwa na Marais wawili kwa wakati mmoja.



    David Logan alikuwa ameapishwa siku moja iliyopita kutokana na kupotea kwa takribani wiki tatu kwa Rais Laura Keith mara baada ya Air Force One kudondoka katika bahari ya Atlantic ikitokea Vatican.



    Baada ya vikosi vya Navy kumtafuta baharini kwa takribani wiki tatu bila mafanikio, hatimaye wote wakaamini kuwa Madam President, Laura Keith alikuwa amefariki kama ambavyo ilivyopatikana miili ya wengine wote waliokuwemo kwenye Air Force One. Hii ndio sababu ya David Logan kuapishwa siku moja iliyopita na kumfanya kuwa Rais kutoka kwenye cheo cha Makamu was Rais.



    Lakini kabla hata ya Massa 48 kupita, ndipo ambapo wanapokea taarifa kwamba, mwili wa Laura Keith umepatikana kwenye pwani ya visiwa vya Carribeans.

    “…kwa hiyo tunafanyaje?” Logan akauliza huku anamuangalia Mwanasheria mkuu ambaye tangu maongezi haya yameanza alikuwa amekaa kimya tu aliwasikiliza Logan na Jaji miu Raph Powell.



    “…sidhani kama kuna mbadala.!! Nchi haiwezi kuwa na Marais wawili kwa wakati mmoja… samahani Mr. President lakini nadhani unatakiwa uache uongozi kwa Laura!” Mwanasheria mkuu Jerome Kings akaongea kwa kumaanisha huku amemkazia macho Logan.



    “Pia sielewi kwa nini mpaka sasa habari ya kupatikana kwa Rais akiwa hai imefanywa kuwa siri namna… nadhani raia wa Marekani wanapaswa kufahamu hili.!”

    Logan hakusema chochote, akamuangalia Jaji Raph Powell kumpa ishara kama aeleze kuhusu kitu fulani.



    Raph Powell akakohoa kidogo kuweka sauti sawa na kisha kujiweka vizuri kwenye kiti alipokaa na kisha kuanza kuongea.



    “Jorome! Kuna vitu kadhaa muhimu nadhani inapaswa kuvifahamu ili nawe labda uelewe kwa nini taarifa hii ya kupatikana kwa Laura tunaifanya siri na kwa nini pia tunasita Laura kurejea tena kwa haraka kwenye nafasi ya kuongoza nchi.!”

    “Nitafurahi mkinifafanulia kinachoendelea!” Mwanasheria mkuu Jerome Kings alijibu kwa sauti ambayo iliashiria kama vile alikuwa anahisi kulikuwa na ‘mchezo mchafu’ umepangwa na Logan pamoja na Jaji Raph Powell.



    “Nadhani Mr. President ni vyema ukieleza wewe mwenyewe!” Ralph akongea huku amemkazia macho Logan.







    “Sawa kabisa!” Logan akaitikia huku anajiweka sawa kwenye kiti.

    “Takribani miezi sita iliyopita nilipenyezewa taarifa muhimu na nyeti sana kutoka kwa watu Fulani hivi… taarifa hii mwanzoni nilihisi kama zilikuwa ni mbinu chafu tu dhidi ya Rais lakini baada ya kuzifanyia kazi nikaanza kuona kuwa zilikuwa na mashiko..!” Logan akaanza kujieleza.



    “Taarifa gani? Na ni nani walikupa hiyo taarifa?” Jerome Kings akauliza huku anamuangalia Logan kwa mashaka.

    “Walionipenyezea taarifa walikuwa ni DATHMOV CONTRACTORS, na kuhusu taarifa ilihusu nini ndio nataka kuwaeleza hapa!”

    “Dathmov?? Kampuni hii ya masuala ya ulinzi??” Jerome Kings akahamaki.



    “Naam! Ndiyo yenyewe!” Logan akajibu huku amemkazia macho Jerome Kings akijua fika kabisa ni nini kibaendelea kichwani mwake na ni nini ambacho alitaka kukisema.

    “Mr. President, nadhani unafahamu uhasama uliopo kati ya Dathmov na Laura… sidhani kama ni sahihi kutilia maanani neno lolote linalosemwa na upande mmoja dhidi ya mwingine.!”



    “Hata Mimi mwanzoni niliwaza kama hiki unachonieleza wewe sasa hivi… kwamba labda kampuni ya Dathmov wanataka kunitumia ili kutengeneza skandali ya uzushi dhidi ya Laura… lakini baada ya kuwasikiliza shutuma zao nikajikuta najiuliza ni nini kitatokea iwapo shutuma hizu zitakuwa ni za kweli?”



    “Kitu gani ambacho walikueleza?” Mwanasheria mkuu akauliza huku amemkazia macho Logan.

    “Uchaguzi mkuu wa mwaka 2036! Kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya Democrats… nadhani unakumbuka jinsi ambavyo Laura alikuwa anaburuza mkia kati ya wagombea watatu tuliobakia tukiwa tunaelekea mkutano mkuu wa chama kumtangaza atakayepeperusha bendera ya Democrats… Unakumbuka kuwa nilikuwa naongoza kwa kura za jumla lakini Laura alikuwa anaongoza zaidi katika sera za masuala ya Ulinzi na Sera ya nchi za nje… lakini nadhani kama ambavyo unakumbuka kuwa suala la muhimu zaidi katika uchaguzi ule lilikuwa ni suala la Uchumi… na katika hilo nilikuwa naongoza kuwazidi wagombea wengine wote waliobaki na kila chambuzi ya siasa ilikuwa inanitabiria ushindi kuwa nitapeperusha bendera ya chama cha Democrats.. Lakini mwishoni tukiwa tumebakiza miezi miwili kufikia mkutano mkuu ndipo likatokea lile balaa la Maldives na miji kuanza kutwaliwa kila kona ya dunia na hii ikasababisha muelekeo wa uchaguzi wa Marekani kuhama kutoka Uchumi kuwa suala la muhimu zaidi linaloangaliwa na wananchi na badala yake suala la usalama ndilo likageuka suala la muhimu zaidi… na ndipo hapa ambapo nyota ya Laura ikang’ara na hatimaye kupata baraka ya chama kupeperusha bendera Democrats na licha ya uadui wetu mkubwa wa kisiasa akaniteua mimi kuwa mgombea mwenza ili kuvuta kura zaidi za waliokuwa wananiunga mkono kipindi chote cha mchakato wa kura za maoni.! Sijui tuko wote pamoja mpaka hapo?”



    Logan akanyamaza kidogo kumuangalia Jerome.

    “Mr. President nafahamu yote haya uliyonieleza… bado nasubiri kusikia jambo jipya ambalo silifahamu.” Jerome Kings akajibu kwa sauti ya kiburi kidogo.

    “Suala ambalo hulifahamu ni kwamba mwezi mmoja kabla ya tukio la wavuvi kuokota chupa baharini ambayo ilisababisha kizaa zaa chote cha miji kugeuzwa Anabelle… Laura alisafiri kwa siri mpaka nchini Morocco kwenye mji wa Rabat.. Kampuni ya Dathmov kwa kutumia majasusi wao waliweza kufuatilia nyendo za Laura akiwa Rabat na wakafanikiwa kumpiga Picha kadhaa..”



    Logan akanyamza kidogo na kufungua bahasha iliyopo juu ya meza na kutoa picha ndani yake na kosha kumkabidhi Jerome.



    “Unaona hao vijana waliovalia suti nyeusi na kunyoa upara?”



    Logan akamuinyesha kwa kidole Jerome kiti ambacho alikuwa anataka akione kwenye zile picha. Picha ilikuwa inamuonyesha Laura Keith muda wa usiku akiwa anashuka kwenye gari kwenye jengo fulani kama hoteli hivi huku kukiwa na kijana aliyevalia suti nyeusi na kunyoa Upara akiwa anamfungulia mlango.







    Picha nyingine ilimuonyesha Laura akiwa sehemu fulani sokoni kwenye watu wengi sana mfano kama ‘kariakoo’ hivi na Laura alikuwa amevalia hijab huku anaongea na simu… nyuma yake kama mita kumi hivi na mbele yake kama mita tano hivi kulikuwa na vijana waliovalia suti nyeusi na kunyoa upara.

    “Ndio Mr. President nawaona.!” Jerome akajibu huku bado macho yake akiwa amekodoa kwenye zile picha mikononi mwake.

    “Dathmov wanaamini kuwa hao vijana ni walinzi binafsi wa mtu anayeitwa DURAN!”



    Logan akaongea huku anamuangalia Jerome kwa uchunguzi ili kuona muitikio wake kama amewagu kulisikia hili jina.

    “Duran??” Jerome akauliza usoni akionyesha dalili kuwa hakuwa anafahamu Duran ni nani.

    “Baada ya kupwa hizi taarifa na Dathmov, japokuwa nilijua kuwa walikuwa wanataka kutengeneza skandali dhidi ya hasimu wao Laura, lakini sikutaka kuzipuuza… nikaanza kuzifanyia kazi! Nilikuja kugundua kuwa Duran ni kiongozi wa jumuiya ya siri inayojiita The 46.!”



    “The 46??” Jerome akauliza tena kwa kifupu tu.



    “..hawa ni watu ambao wanaamini kuwa wao ndio wanawezesha dunia iendelee kuwepo na kwa karbe kadhaa sasa wamejitoa maisha yao yote kutafuta mahali lilipo sanduku la Pandora.!”



    “Hahaha! Mr. President sidhani kama unaamini hizi hadithi kuhusu Pandora… tafadhali sana sitegemei tuongee kuhusu mambo ya kufikirika!” Jerome akaangua kicheko mara baada ya kumsikia Logan anaanza kuongea kuhusu Sanduku la Pandora.

    “Jerome! Najua mtu unahitaji kuwa mwendawazimu kiasi gani mpaka kuamini simulizi kuhusu Pandora… lakini kwa kuzingatia kinachoendelea duniani… miji kutwaliwa katika mazingira ya kutatanisha… naicha akili yangi wazi kupokea wazo lolote lile haijalishi ni la kufikirika au la kiwendawazimu kiasi gani!”



    Logan aliongea akiwa serious mpaka akamfanya Jerome asikie aibu na aondoe tabasamu la kicheko usoni mwake.

    “Naelewa Mr. President… kwa hiyo hii ina maana gani?” Jerome akauliza.



    “Sitaki kutoa hitimisho kuwa hii ina maana gani… lakini inatia shaka kidogo kumuona Laura anaenda Morocco kukutana na kiongozi wa jumuiya ya usiri mkubwa na miezi miwili baadae mauza uza yanaanza kutokea Duniani na hatimaye anashinda urais.. Binafsi inanitia mashaka sana..!”



    “Nakuelewa kabisa unachonieleza Mr. President… najiuliza tu ulichukua hatua gani baada ya kubaini yote haya?”



    “Sikuchukua hatua yoyote… nilichofanya ni kufuatilia kwa makini tu ili nijue mwisho wa yote haya itakuwa ni nini!” Logan alidanganya safari hii, au tuseme alisema ukweli nusu kwa sababu kuna vitu alivifanya baada ya kugundua masuala yote haya kuhusu Laura. Kuna vitu alivifanya ambavyo akikumbuka anahisi kama moyo wake unataka kupasuka na vingine alikuwa bado anajutia ni kwanini alivifanya.

    “Jerome! Hizi ndizo sababu ambazo zimetufanya tukutane hapa… sisi watu watatu tu, kabla ya Logan kuonana na baraza la mawaziri ili ufahamu kinachoendelea nyuma ya pazia na tutafakari nini cha kufanya kuhusu Laura.. Mimi binafsi siku ya kumuapisha kabla hatujafanya zoezi hilo aliniita situation room na kunieleza yote haya. Alitaka ushauri wangu kuwa kama ni sahihi yeye kushika madaraka huku akiwa na taarifa nyeti kama hizi ambazo hawezi kumueleza mtu yeyeto yule, pia alitaka kujua kama itakuwa sahihi kwake kushika madaraka huku akiwa amemfanyia upelelezi binafsi wa siri Madam President, na pengine ulikuwa ni upelelezi ulio kinyume na sheria. Hoja yangu Mimi ilikuwa ni moja tu, kwamba nchi haiwezi kukaa bila Rais. Kwa hiyo nikamuapisha… sasa tunahitaji pia ushuri wako ukiwa kama mwanasheria mkuu wa serikali na mtu pekee mwenye mamlaka ya kikatiba kumkamata, au kumshtaki au kumuweka kizuizini Rais wa Marekani… tushauri Jerome, tunafanya nini juu ya Laura?”



    Jaji Ralph Powell hatimaye naye aliongea baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

    Mwanasheria mkuu, Jerome Kings akajikuta anapata kigugumizi. Alijikuta anashindwa kusema chochote kila na kuinamisha kichwa chini kutafakari.

    [5/21, 20:15] The Bold: Wakati wao wanatafakari wafanye nini, Logan kichwani mwake alikuwa anatafakari kama alikuwa anafanya kiti sahihi kuendelea kubaki na siri kubwa zaidi moyoni mwake. Juu suala aliloligundua kuhusu makuzi na utoto wa Laura Keith, kuhusu suala la muhimu na la siri kubwa kuhusu baba yake mzazi Laura.

    Alijikuta anajiuliza mara mbili mbili kama alikuwa sahihi pia kuwaficha wenzake kuhusu ukweli unaoujua ni namna gani mchoro wa George Washington uliondolewa kutokea Whitehouse.

    Lakini suala la hatari zaidi, alikuwa anajiuliza kama ilikuwa sahihi kwake kuendelea kuficha siri kubwa ya kwa nini nguo za Laura Keith ziliokotwa na Navy katika kisiwa cha Saman na yeye mwenyewe Laura Kuokotwa pwani ya visiwa vya Carribeans.



    Muda ni fumbo kubwa zaidi katika maisha ya mwanadamu, laiti kama tungefahamu kesho basi kesho basi kuna vitu vingi tunavyovifanya leo, tungevifanya kwa tofauti.



    Laiti Rais David Logan angelifahamu mateso yaliyokuwa yanamsubiri masaa 72 kutokea sasa, kamwe asibgethubutu kubaki na siri hizi moyoni mwake.





    MASAA 48 YALIYOPITA (OVAL OFFICE, WHITE HOUSE – WASHINGTON D.C)

    “David hatuwezi kuwa na Marais wawili kwa wakati mmoja.!”



    “Nafahamu nafahamu! Najua vizuri sana, lakini ninachotaka ukione ni hatari ya Laura kurudi tena kwenye uongozi.!”



    “David! Hilo lilikuwa ni jukumu la mwanasheria mkuu kufanya maamuzi, kama ameona hakuna uthibitisho wa kutosha au hakuna hoja imara kumchukulia hatua Laura sidhani kama kuna la zaidi la kufanya zaidi ya kumuacha Laura aendelee na majukumu yake. Ukiendelea kushikilia huu msimamo nadhani watu wataanza kukuona una uroho wa madaraka!”



    “Najua watu watakachofiri… na sitaki kukataa kuwa nina utamani urais, lakini tamaa yangu ya Urais haizidi matamanio yangu ya kuiona Marekani iko salama.!”



    “David, kama ni kweli unatamani kuiona Marekani iko salama, nakushauri uachane na kung’ang’ania hili suala na badala yake uwekeze akili yako kwenye tishio kubwa zaidi linalotukabili hivi sasa… miji kutwaliwa na Dunua nzima kuwa katika tishio la kugeuzwa Anabelle!”

    David Logan na rafiki yake wa muda mrefu Seneta Steven Lopez ambaye pia ni Waziri wa mambo ya nje wa nchi, walikuwa ofisini ambako David alimuita rafiki yake huyo kumueleza namna ambavyo jana yake, mwanasheria mkuu wa serikali Jerome Kings alikataa kumchukulia Laura Keith hatua yoyote licha ya tahadhali zote alizompa na kumueleza wasiwasi alionao endapo Laura atarejea tena kwenye wadhifa wake.



    Wazo ambalo David alikuwa amelipata ilikuwa ni kujaribu kumshawishi Seneta Steven Lopez kukubali kumuunga mkono ili afanye ushawishi wa kupeleka muswada bunge la Congress ili liendeshe “Special Hearings” na hatimaye kumtia hatiani Laura kwa kosa la kushrikiana na maadui wa Marekani na hatimaye yeye aendelee kushikilia wadhifa huo wa urais ambao mpaka muda huu alikiwa amekaimu.



    Seneta Steven Lopez alikuwa anaona kama huu ni wendawazimu kuendeleza vita za kisiasa wakati ambao dunia ilikuwa inakaribia yote kugeuzwa kuwa Anabelle.

    Kitu ambacho wote walikuwa hawakifahamu ni ilikuwa namna gani urais wa Laura Keith na matukio yanayoendelea duniani vilikuwa vinahusiana.



    David alikuwa anatamani awaeleze kile anachokijua. Alikuwa anatamani awaeleze kuhusu baba yake Laura na kile ambacho amekigundua. Alikuwa anatamani awaeleze kuhusu maana ya kupatikana kwa nguo za Laura kwenye kisiwa cha Saman, lakini moyoni mwake alikuwa anasita.

    “Si busara kuweka karata zote mezani kwa mara moja!” Hivyo ndivyo ambavyo David alikuwa anajifariji moyoni, bila kujua kuwa masaa 48 tu kutoka sasa, siri hizi zitakuja kumtia katika mateso mazito ambayo hakuna binadamu ambaye anaweza kudhani yapo duniani.



    Baada ya mazungumzo haya na swahiba wake Seneta Steven Lopez, waliagana pasipo David Logan kumpa ahadi yoyote ile kuhusu yapi hasa ni maamuzi ambayo atayachukua. Alichokifanya ni kumueleza tu kwamba anahitaji kutafakari zaidi.



    Lakini uhalisia si kwamba David alikuwa anahitaji kutafakari, bali alikuwa anataka kufikiri zaidi ni namna gani ataweza kufanikisha azma yake ya kuhakikisha anaendelea kubakia kwenye nafasi ya urais na anamdhibiti Laura kisheria na ikiwezekana amuwajibishe kwa makosa ya jinai au uhaini.

    Mpaka sasa alikuwa ameshindwa kumshawishi Mwanasheria mkuu wa serikali kumuunga mkono kwenye suala hilo, lakini pia alikuwa ameshindwa kumshawishi swahiba wake Seneta Steven Lopez mtu kwenye ushawishi mkubwa ndani ya baraza la mawaziri na kwenye siasa za Marekani.



    Chaguo pekee ambalo alikuwa analiona limebaki mbele yake ilikuwa ni kuangalia ni namna gani ambavyo ataweza kulazimisha suala hilo lijadiliwe katika baraza la mawaziri au katika bunge la wawakilishi (House of Representatives).



    Akiwa amejiinamia hivyo anatafakari mara mlango wa ofisi yake ukagongwa taratibu na kisha kufunguliwa nusu na katibu wake Kevin akachungulia.



    “Naweza kuingia Muheshimiwa?” Kevin akauliza huku anamuangalia Logan kwa macho ya udadisi.



    “Ingia Kevin!” Logan akajibu huku anazuga anaandika vitu fulani kwenye makabrasha juu meza.



    “Mheshimiwa Rais! Nina habari mbaya kidogo..” Kevin akaongea kama ana kigugumizi amemkazia macho Logan.

    “Habari gani?” Logan akaacha kuandika na kuinua uso kumuangalia Kevin.



    “Miji mingine miwili imetwaliwa ndani ya ardhi ya Marekani… New Jersey na Delaware.!” Kevin akaongea kwa kifupi huku amemtumbulia macho Logan.

    “Dear God.!!” Logan akajishika kichwa na kujiinamia kwa uchungu.



    Kuna muda mtu unakuwa unatarajia habari mbaya kwamba lazima itakuja, lakini kuna utofauti wa kuitarajia habari mbaya na habari hiyo ikikufikia kwa uhalisia wenyewe.

    Habari hii ya miji kutwakiwa sio kwamba tu ilikuwa mbaya kutokana na kutishia uwepo wa taifa la Marekani na uliwengu, bali pia ilikuwa mbaya kwa David Logan binafsi kutokana na mipango yake ambayo alikuwa anaipabga kichwani.



    Na si hivyo tu lakini pia David Logan alikuwa naiona hatari kubwa zaidi ambayo ilikuwa mbele yao ambayo watu wengine wote walikuwa hawaioni.



    Licha ya kwamba kila mtu alikuwa na hofu kubwa kutokana na miji zaidi kutwaliwa nchini Marekani, lakini yawezekana hakuna mtu ambaye alikuwa analiona suala hilo katika namna ambavyo David alikuwa analiona.

    Watu wengine waliona miji inatwaliwa kama sehemu nyingine duniani kote. Lakini David Logan alijua hii ilikuwa ni ishara ya nini hasa.



    Akakumbuka tena suala la nguo za Laura kukutwa kisiwa cha Saman na pia akakumbuka alichokigundua juu ya baba yake Laura. Alikuwa anatamani aeleze kila kitu kuhusu siri hii kubwa, lakini aliendelea kuufariji moyo wake, “si busara kueweka karata zote mezani kwa wakati mmoja!”



    Aliendelea kujifariji na kuitunza siri hiyo kwenye sakafu kabisa ya moyo wake, pasipo kujua kwamba siri hii, siku mbili zijazo itamfanya ajisikie kana kwamba amepelekwa kuzimu na itakaribia kuughalimu ulimwengu wote.





    SIKU MOJA ILIYOPITA (MASAA 24 YALIYOPITA)











    ANNAPOLIS, MARYLAND

    Msitu wa Ox ambao Mzee Caleb na wenzake walienda hauko mbali sana na mji wa Annapolis ambako ndiko mzee Caleb anaishi. Sehemu zote hizi mbili, yaani msitu wa Ox na mji wa Annapolis ziko ndani ya jimbo la Maryland.



    Hata hapo Annapolis, mzee Caleb hakuwa anaishi mjini katikati, bali alikuwa anaishi kwenye kitongoji kidogo nje kidogo ya mji sehemu iliyojitenga kidogo ikipakana na mashamba makubwa yaliyotelekezwa miaka mingi na upande mwingine ikipakana na kijimsitu fulani hivi.



    Nyumba yake kwa muonekano tu ilikuwa inaashiria kuwa nyumba hiyo imerithiwa kutoka vizazi kadhaa vilivyopita katika ukoo wa akina Caleb.



    Lakini nyumba hii pia ilikuwa ilikuwa na muonekano unaoashiria kwamba ilikuwa ni nyumba ya hadhi ya juu katika miaka hiyo ya zamani ambapo ilikuwa imejengwa.



    Ilikuwa ni nyumba aina ya ‘bungalow’, ambayo ilikuwa na vyumba juu na chini.



    Japokuwa nyumba haikiwa chafu, au kuu kuu au kuchoka lakini ilionyesha dhahiri kwamba ilijengwa miaka mingi sana iliyopita.

    Baadae Caleb aliwaelza kuwa nyumba hii ilijengwa na Baba wa Babu yake ambaye enzi hizo alikuwa ni seneta wa eneo hilo wanaloishi.

    Baadae nyumba hii ikarithishwa kwa babu yake, na baadae baba yake na sasa iko chini yake.

    Mzee Caleb, Naomi, Ethan na wenzake walikuwa wamewasili hapa toka jana usiku waliwa na kiumbe kile cha ajabu ambacho walikabidhiwa kule msituni na kuelezwa kuwa wakitunze.



    Kiumbe cha ajabu, mbwa mwenye mbawa kama popo, rangi nyeupe kama theluji na asiye na unyoya hata mmoja walikuwa wamemuhifadhi kwenye nyumba chini kwenye ‘basement’.

    Leo hii asubuhi walikuwa wameamka na wamekusanyika wote sebuleni wakipata kifungia kinywa huku wanajadili ni nini hasa cha kufanya.







    “Tunapata wapi damu?” Naomi akawauliza wenzake huku ameshikilia kikombe cha kahawa.

    “Kumbukumbu yangu inanieleza kwamba amesema tumpe huyo mnyama damu kila baada ya siku tatu!” Ethan akajibu.



    “Kesho kutwa inatimia siku ya tatu nadhani tunapaswa kuwa na mkakati unaoeleweka ni namna gani tutapata damu kopo moja kila baada ya siku tatu..? Na sielewi aliposema kopo moja alikuwa ana maanisha kiwango gani?” Naomi akawakodolea macho wenzake.

    “Ni lita moja… kwenye familia yetu tangu tuko watoto mzee wetu alikuwa na kopo lake la lita ambalo alikuwa naweka maziwa… kwahiyo alikuwa akikutuma kitu na kukueleza kiwe kopo moja, alikuwa anamaanisha Lita moja!” Caleb akasaidia kujibu swali la Naomi.

    “Na kabla hatujazungumza mengine zaidi… nadhani mzee ungetueleza ni nini kinaendelea hapa?? Kwa nini yule binadamu kule msituni alikuwa anakuita ‘mwanangu’?” Ethan akauliza huku amemkazia macho Mzee Caleb.

    Ulipita ukimya wa dakika kadhaa wote wakiwa wametulia bila kutibgishika. Swali la Ethan kila mmoja alikuwa anajitahidi kuepuka kuliuliza tangu jana walipotoka msituni lakini pia kila mmoja alikuwa anatamani kujua ni nini kilikuwa kinaendelea kati ya Caleb na yule binadamu wa ajabu msituni. Kwa nini alikuwa anamuita mwanangu kila muda?



    Mzee Caleb alikuwa emejiinamia anaangalia kikombe cha kahawa kilichopo juu ya meza mbele yake. Alikuwa anaonekana mawazo yake yako mbali mno. Kuna kitu alikuwa anakiwaza na kilikuwa kinamuumiza moyo mno. Alikuwa kama vile ametoneshwa kidonda.



    “Kuna umuhimu wa kujibu haya maswali sasa hivi?” Mzee Caleb alijibu huku bado uso ameinama chini anatazama kile kikombe cha kahawa mezani.



    “Mzee hatuwezi kufanya hili suala kwa ufanisi tukiwa na maswali kichwani… nina maswali mengi sana nahitaji kufahamu… mfano hapo nje karibu na hii nyumba nimeona makaburi matatu ambayo yameondolea vibao vya maandishi juu nadhani ili kujaribu kuficha yasigundulike kuwa ni makaburi… nahitaji kujua pia ni makaburi ya nini na kwanini unayaficha yasijulikane…”



    Ethan aliongea huku ameuvaa haswa uhusika wa fani yake ya mwanajeshi wa weledi. Aliongea bila kupepesa macha wala kutafuna maneno. Alikuwa anamaanisha hasa kile anachokiongea.

    “Naelewa kuwa mna maswali mengi na mnahitaji majibu… ninachowaeleza ni kwamba kuna ulazima wowote wa kuyaongea haya sasa hivi??” Mzee Caleb aliongea huku safari hii naye akiwa ameinua uso akimuangalua Ethan.

    “Hamdhani kwamba labda tungetumia muda huu kujadili kuhusu wakala wa The 46 ambaye tumeambiwa kule msituni kwamba anarudishwa?”



    “Mzee tutafika kote huko… tuanze na masuala yanapaswa kuanzwa kwanza… tueleze ukweli yule ni nani? Au labda nirahisishe zaidi wewe ni nani?” Ethan aliongea sauti inayopenya mpaka kwenye moyo ambayo ilidhihirisha kabisa kuwa alikuwa na mashaka makubwa na ukweli na uhalisia wa Mzee Caleb.

    Ethan alikuwa ni Mwanajeshi Komando wa weledi wa juu kabisa. Alikuwa na uwezo mzuri sana wa kumsoma mtu, kwa hiyo pale anapokuwa ana mashaka na mtu fulani basi kuna sababu ya msingi kabisa.

    Hii ilimtia hofu pia Naomi na kufanya asisimke kwa woga mpaka vinyweleo vikasimama.



    Wote wakabakia wanpiga jicho la udadisi na mashaka Mzee Caleb ambaye alikuwa amerejea kuinamisha uso kuangalia kikombe cha kahawa pale juu ya meza.



    Ukimya mkuu ukarejea tena pale sebuleni. Kila mmoja akisubiri jibu la Mzee Caleb. Yule binadamu wa ajabu msituni ni nani? Kwanini anamuita “mwanangu”? Baba yake Caleb si alishafariki? Makaburi pale nje ya nyumba ni ya nani? Na kwa nini yemefichwa?



    Ukimya auliendelea kuwa mkubwa zaidi. Mzee Caleb bado alikuwa amejiinamia akionekana kuwa mbali sana kimawazo.



    Ukimya huu ulikatishwa na simu ya Naomi kuanza kuita ghafla.



    “Samahani… samahani.!” Naomi aliomba radhu huku anachukua simu na kuiweka sikioni.

    “Hallo… hallooo… Mr. President… halloooo… uko sawa muheshimiwa?? Ndio nakusikia… ndio…. Tuko naye hapa muheshimiwa…. Ndio tuko naye… ndio… ndio…. Haiwezekani Mr. President… hapana… hapana… ndio, ndio Mr. President… unahakika Mr. President… ndio… ndio… una hakika muheshimiwa??”



    Naomi akakata simu huku anatetemeka.







    Alikuwa kana kwamba amepatwa na bumbuwazi la maisha… alikuwa amekata simu lakini bado ameishikilia mkononi huku ametumbua macho anawaangalia wenzake bila kusema neno lolote mdomo amechama wazi.



    “Nini?” Ethan akauliza akiwa na mshituko mkubwa.



    Mshangao uliokuwa usoni kwa Naomi ulikuwa unatisha.



    “White House imevamiwa muda huu… watu wa usalama wanahaha kumtorosha Rais… amenipigia simu kwa taabu sana hapa akitaka kufahamh kama wote tupo kama ambavyo tuliondoka kule Site namna SQ 1204.!”



    Naomi aliongea huku ameganda kama sanamu. Simu bado ameshikili mkononj vile vile bila kuiweka chini na huku bado akiwa amekodoa macho kama vile ameona jini.



    “Kwanini Rais atupigie simu kutaka kujua kama tuko wote badala aelekeze akili yake kuokoa maisha yake?”

    Ethan aliuliza huku anaanza kuinuka. Kuna kitu alianza kukihisi.



    “Ni kwasababu ya hicho kikosi kilichovamia white house!” Naomi akaongea tena bila kutingishika kama sanamu.



    “Kimefanyaje?” Ethan akauliza tena huku safari hii akisogea mbali na meza kabisa.

    “Anasema kikosi kilichovakia Ikulu kimeongozwa na Mzee Caleb!” Naomi hatimaye aakapasua jipu.

    Wote walihisi kama wanachanganyikiwa. Huu alikuwa ni utani au ni nini kinaendelea?

    Inawezekanaje Rais aseme wameviwa Whitehouse muda huu na kikosi kinachoongozwa na Caleb ilhali wako naye hapa muda huu?

    Wote waliinuka wanahema na kusogea pembeni ya meza.



    Mzee Caleb mwenyewe alikuwa hajashituka wala kushangaa. Bado alikuwa amejiinamia anaangalia kikombe cha kahawa pale juu ya meza.

    “Hii vita ni ya tofauti na kuna siri nyingi hampaswi kuzijua… siku yoyote tunaweza kuupoteza ulimwengu… msiogope… kaeni chini niwaeleze ni nini kinaendelea!”



    Hatimaye mzee Caleb akaongea. Aliongea kwa utulivu mno bila hata kutingishika au kuinua uso kuwatazama.



    Naomi na wenzake walijikuta wanashikwa na hofu zaidi na kuanza kuhema kana kwamba walikuwa wanakimbia marathon.



    Naomi akapiga moyo konde na kuwa wa kwanza kukaa tena kwenye kiti pale mezani misha wenzake wakafuata.











    CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI, MONDULI ARUSHA – TANZANIA.



    Tayari ulikuwa umepita mwezi mzima tangu mji wa Daer es Saalam kutwaliwa na Kugeuzwa Anabelle 27. Kwa maana hii pia tayari umepita mwezi mzima tangu Rais wa Jamuhuri ya Muungao wa Tanzania, Muheshimiwa Zuberi Z. Miraji kuhamishwa kutoka Ikulu ya Dar es salaam na kupelekwa Arusha shemu ya siri ndani ya eneo la chuo cha Kijeshi cha Monduli.



    Mahali hapa pa siri ambapo alikuwa amefichwa kijeshi palikuwa panajulikana kama PEMR-03 ikimaanisha Presidential Emergency Millityary Residency, site namba tatu. Hili ni moja kati ya sehemu kadhaa za kimkakati ndani ya nchi ambazo jeshi la JWTZ zinazitunza kwa siri kubwa kwa ajili ya dharura kama hii ambapo Rais anatakiwa kufichwa kutokana na hatari iliyoko mbele yake.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Katika site hii namba tatu iliyopo ndani ya chuo hiki cha kijeshi cha Monduli, sehemu hii ya siri ilikuwa imejengwa upande wa kaskazini mwa chuo, mbele kidogo ya majengo ya utawala karibu na msitu unaopakana na jengo kubwa la wastani ambalo linatumika kama stoo chuoni hapo. Ndani ya stoo hii ndimo ambapo kuna ‘entrence’ ya mlango sakafuni ambao unakuwezesha kuingia chini kwenye makazi haya ya siri ya dharura maalumu kwa ajili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.



    Sehemu hii iliyoko chini ardhini ilijengwa kama nyumba ya kuishi familia nzima. Kulikuwa na vyumba vitatu vya kulala na chumba kingine cha nne kilitumika kama chumba cha kuhifadhi vitu muhimu kama vile vyakula na madawa. Katika vyumba hivi vya kulala kimoja kilitumiwa na Rais pamoja na mkewe Nasma Miraji na chumba kingine kilitumiwa na mtoto wao wa kiume wa miaka 26 aliyeitwa Wangwe Miraji na chumba kilichobakia kilitumiwa na mtoto wao wa kike Faraja Miraji.



    Johonson Dilunga, kiongozi wa kitenngo maalumu cha ulinzi wa Rais ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa (Presidential Protection Unit) pamoja na vijana wake wapatao 26 walikuwa wanatumia sebule na wengine wakiwa juu kwenye lile jengo la stoo la chuo hiki cha Monduli.



    Japokuwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wote waliokolewa kwa pamoja lakini kwa sababu za kimkakati za kiusalama walikuwa wamewekwa kwenye makazi tofauti.



    Makamu wa Rais January Nchimbi alikuwa amehifadhiwa kwenye jengo linalo milikiwa na Idara ya Usalama wa Taifa lililopo mtaa wa Njiro, wakati ambapo Waziri mkuu Halima Bulaya alikuwa amehifadhiwa kwenye jumba kubwa la siri la Idara ya Usalama wa Tiafa lililojitenga na makazi ya watu wengine lililopo mtaa wa Daraja mbili.







    Kwa muda wa mwezi mzima uliopita hali ya hatari ilikuwa imetangazwa nchi nzima, serikali ikiwataka wananchi wachukue tahadhari ya kuokoa maisha yao pale ikitokea dalili ya mji kutwaliwa imeonekana katika eneo walilopo na ambapo dalili kuu ilikuwa ni tetemeko hafifu kupita na sauti kubwa yenye kishindo kusikika kama vile mlio wa tarumbeta au parapanda.



    Kwa mwezi mmoja pia uliopita tayari miji mkingine miwli ilikuwa imetwaliwa kuongeza na ile miwili ya kwanza. Miji hii mingine ilikuwa ni Dodoma na Tabora. Kwa maana hii ilifanya sasa kuwe na miji minne ambayo imetwaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania, yaani Ruangwa, Dar es salaam, Dodoma na Tabora.



    Hofu ilikua imetanda kila kona ya nchi, kila mahali kulikuwa na pirika pirika za watu kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine bila hata kufahamu huko wanakoelekea kuko salama kiasi gani na ni kuda gani kabla nako hakujatwaliwa. Ilikuwa imefikia hatua ambayo serikali ilikuwa imezidiwa uwezo wake wa kuwasaidia kuwaokoa wananchi wake kwa sababu mtihani mkubwa walikuwa hawajui wawaokoa na kuwapeleka wapi. Mfano, mji wa Dodoma ulipotwaliwa na kugeuzwa Anabelle, serikali ilijitahidi kuokoa wananchi wengi iwezavyo na kuwapeleka Tabora. Lakini wiki moja baadae mji wa Tabora nao ukatwaliwa na kugeuzwa Anabelle na wananchi wote waliokuwemo ndani yake walipotea. Kwa hiyo ilikuwa ni dhahiri kabisa kwamba haikuwa na maana kutumia rasilimali nyingi na muda kuhamisha wananchi bila kujua usalama wa kule ambako walikuwa wanawapeleka.



    Laini pia serikali nao ka upande wao walikuwa kwenye sintofahamu kubwa, hofu kuu waliyokuwa nayo ilikuwa ni nana gani hasa watamlinda Rais na viongozi wenzake waandamizi kwa uhakika zaidi kwani hata hapo ambapo wamefichwa muda huu hakuna ambaye alikuwa anajua ni muda gani ulikuwa umebakia kabla ya miji hiyo nayo kutwaliwa.



    Hii ndio sababu iliyopelekea kikao adhimu cha siku ya leo kati ya Rais Zuberi Z. Miraji, Makamu wa Rais January Nchimbi, Waziri Mkuu Halima Bulaya, Mkuu wa Majeshi, CDF Henry Kaizirege na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Titus Mollel.



    Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wa Tiafa wote walikuwa Monduli pamoja na Rais, lakini Waziri Mkuu na Makamu wa Rais walijumuika kwennye kikao kwa njia ya “video call” kutoka sehemu walizopo, yaani Njiro na Daraja Mbili.



    “…kwa hiyo ni miji 126 mpaka sasa?” Mheshimiwa Rais Zuberi Miraji aliluza.



    “ndio Muheshimiwa Rais… miji 126 mpaka sasa imetwaliwa Duniani kote.!” CDF Henry Kaizirege akamjibu Rais.



    “…this is getting out of hand!!” Rais alilalamika na kujiinamia.



    “…ni kweli kabisa muheshimiwa huo ndio uhalisia… kasi ya miji kutwaliwa sasa imekuwa ‘exponential’…. Kila kukicha inaogezeka zaidi… mwanzoni wenzetu wa Marekani walikadiria kwamba labda itachukua miaka mitatu kwa dunia yote kutwaliwa lakini kwa kasi hii tunayoiona sasa nadhani tukiendelea hivi ndani ya mwezi mmoja au miwili ijayo hatutakuwa na dunia hii tulioyonayo sasa!” CDF Kaizirege aliongezea.



    “na situation ya Marekani ikoje mpaka sasa?” Rais akauliza tena



    “nako miji miwili imetwaliwa mpaka saa.” Akajibu Titus Mollel, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.



    “nafahamu kuwa miji imetwaliwa… nataka kujua vipi wamepiga hatua yoyote kuhusu kuelewa suala hili? Vipi wanaendelea kutupa ushirikiano? Vipi kuhusu Rais Laura? Na kadhalika na kadhalika… mambo kama hayo!!” Rais akaonge kwa ukali kidogo.



    “samahani muheshimiwa nilikuwa sijakuelewa…” Titus Mollel akomba radhi na kisha kunyamaza kidogo na kukohoa ili kuweka sauti sawa kisha akaendelea, “Kwa taarifa rasmi kutoka Washington zinaeleza kuwa Rais Laura Keith bado hajapatikaba… lakini kwa siku za hivi karibuni Washington kumekuwa na mwenendo wa kutia mashaka kidogo… mfano Rais mpya David Logan hajaonekana hadharani kwa siku tatu sasa… bado hatujajua sababu kubwa hasa ni nini lakini kuna minong’ono kwamba kunaweza kuwa na kupishana mawazo kati ya viongozi wa juu wa Marekani  kuhusu ya uhalali wa malaka ya David Logan na vitu vinavyofanana na hivyo… muheshimiwa Rais, kuhusu ushirikiano wanaotupa kwa sasa umepunguwa mno, nadhani hii inatokana labda pia na changamoto ambao wao wenyewe pia wako nayo, yaani miji kuanza kutwaliwa kwenye ardhi yao na pia rais wao kupotea kwenye nmazingira ya kutatanisha… lakini pia ndege yao ya kivita F-15 waliyoituma mwezi mmoja uliopitra kuja kumchukua mwanasansi wao Dr. Cindy bado iko kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi Morogoro haijaondoka wakidai kuwa wamepewa amri ya kutorusha ndege pasipo Dr. Cindy kuwa ndani yake, kwamba ni lazima waondoke naye… tulishuriana na CDF hapa na tukakubaliana kwamba ndege ile iendelee kukaa pale kwa kadiri watakavyotaka, lakini hatutawaruhsu kuirusha sehemu yoyote ile ndani ya ardhi ya Tanzania na wao wenyewe hatutawaruhusu kutoka nje ya eneo la jeshi.!” Mkurugenzi wa TISS, Titus Mollel akafafanua kwa kirefu.



    “Ok! Vizuri sana… nadhani inatosha kwa sasa… labda kama kuna lolote kutoka kwenu… Makamu wa Rais, Waziri Mkuu..!” Rais aliongea na kutazama ‘sreen’ zilizopo mbele yao zilizokua zinawaonyesha makamu wa Rais na Waziri Mkuu kutoka huko walipo.



    “Mheshimiwa Rais… bado nina jambo lingine!” Titus akadakia kabla Makamu wa Rais au Waziri mkuu hawajasema chochote.



    “kitu gani?” Rais akageuka kumuangalia.











    “…ni kuhusu Anabelle 27! Dar es Salaam!”



    “Nakusikiliza Titus!” Rais akaongea huku anamuangalia Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa kwa shauku na udadisi mkubwa.



    Titus akageuka kidogo na kumuangalia CDF Henry Kaizirege. CDF akampa ishara kama anamuitikia kwa kichwa hivi, na baada ya hapo Titus akavuta mkoba wake akliokuja nao na kuanza kutoa makabrasha.



    “…mheshiwa Rais mara baada ya DR. Cindy na wenzake kuingia ndani ya Anabelle 27 na kupotelea humo, tukaunda timu ya dharura kuwafuatilia humo wakati wa mchana. Kama ujuavyo kwamba muda wa mchana kabla ya kufika saa kumi jioni hakuna madhara yoyote yale ukiingia ndani ya Anabelle. Kwa hiyo hii timu ambayo tuliiunda walikuwa wanaingia ndani ya Anabelle muda wa mchana na kuanza kufanya  ufuatiliaji kwa kadiri ambavyo walikuwa wanaweza. Sababu kuu ya kutufanya kuchukua uamuzi huu wa kuunda hii timu ni kwamba, tulihisi kuwa Dr. Cindy na wenzake wanajua kitu fulani ambacho sisi labda bado hatukifahamu… kwa sababu haiwezekani wataalamu kama wao wajipoteze kwa makusudi ndani ya Anabelle… tulihisi kwamba lazima kutakuwa na jambo fulani nyuma yake.” Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Titus Mollel akaanza kueleza.



    “endelea Mkurugenzi.!!” Rais Zuberi Miraji akaongea tena kwa shauku.



    “kwa muda wa mwezi mzima timu hii imefanya uchunguzi ndani ya Anabelle 27 bila mafanikio yoyote au kuona jambo lolote tofauti na Anabelle nyinginezo. Lakini siku tatu zilizopita walikuata na kitu cha tofauti sana ambacho nahisi kinaweza kutupa mwanga kidogo huko mbeleni tunakoelekea.!”



    “Waliona nini?” Rais aliuliza safari hii kwa shauku zaidi.







    Titus akaingiza tena mkono wake kwenye mkoba na kuanza kutoa picha fulani ambazo zimechapwa kwenye karatasi kubwa za saizi ya A4. Akazichukua zile picha na kuziweka mbele ya Rais mezani na kisha kuanza  kumpa maelezo.



    “hiki ndicho walichokiona Muheshimiwa… chupa ambayo imewekwa karatasi ndani yake!! Chupa yenyewe tumeipeleka kwenye kituo cha utafiti Ifakara… tulipoifungua hii chupa na kutoa karatasi iliyopo ndani yake, mara tulipoona maneno yaliyoandikwa na kulingannisha na mwandiko tukagundua kwamba huu ni aliyeandika hii karatasi ni Dr. Cindy.!”



    “ameandika nini?”



    “Samahani Muheshimwa… kabla sijakueleza kilichoandikwa kwenye hiyo karatasi niruhusu nikupe tena maelezo machache.!”



    “Sawa nakusikiliza Mkurugenzi.!” Rais aliitikia kwa shauku tena huku anajigeuza kukaa sawia pale kwenye kiti alipoketi.



    “baada ya kubaini kwamba muandiko wa kwenye karatasi uliyoikuta kwenye chupa ni mwandiko wa Cindy, tukawasiliana na wamarekani wale ambao wamekuja na ndege ya jeshi iliyoko kule Morogoro kuona kama wanafahamu chochote… hatukuwaonyesha karatasi au kilichoandikwa lakini tuliwapa maelezo tumeipataje na hiyo chupa ilikuwa na nini.!”



    “Waliwajibu nini?” Rais akauliza kwa udadisi na shauku.



    “hawakupa jibu papo hapo… waliwasiliana na wenzao na siku mbili zilizopita badala ya kutupa jawabu wakaanza kutushinikiza kwamba tuwakabidhi hiyo chupa pamoja na jaratasi iliyomo ndani yake!” Titus Mollel akaongea.



    “naamini hamjawapa hiyo chupa, right?” Rais akuliza kwa uso unaokaribia kushikwa na hasira.



    “hapana Muheshimia Rais! Hatujawapa chup wala karatasi… tulichokifanya ni kuwatega kwamba kama wanataka chupa kwanza kabisa watueleze ukweli kuhusu hiyo chupa!”



    “walikubali?”



    “Walitusumbua sana lakini mwishowe wakatupa ukweli… kwamba chupa ile ndiyo ile ambayo iliokotwa na wavuvi mnchini Maldives miaka miwili iliyopita na kwamba DR. Cindy aliichukua bila ruhusa kutoka kwenye maabara ya Akiolojia chuo kikuu cha Stanford anakofanyia kazi… lakini ajabu ni kwamba walitueleza kuwa karatasi ambayo ilikuwa ndani ya hiyo chupa ilikuwa na maandishi ya kiitalianoa au kilatini cha kale sana kiasi kwamba mpaka sasa hawajaweza kuelewa hasa maandishi ya le yana maana gani… lakini sisi timu yetu ilipookota hii chupa ndani yake ilikuwa na karatasi yenye maandishi ya kiingereza tena kwa kadiri tulivyousoma na kuuchunguza ule mwandiko tuna uhakika kwa asimili mia moja kwamba ni Cindy aliyeandika!” Titus akaeleza kwa kirefu.



    “Kwahiyo unajaribu kutueleza kwamba Cindy na wenzake wamebadili karatasi halisi ambayo ilikuwa ndani ya chupa hiyo na kuweka karatasi nyingine ambayo kwa namna fulani hatimaye chupa ikaokotwa nah ii timu ya uchunguzi mliyounda?” Makamu wa Rais January Nchinbi hatimaye aliuliza swali baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu tangu maongezi yameanza.



    “Mmefahamu labda ni kwanini Dr. Cindy amefanya hivyo? Kubadili hizo karatasi?” Waziri Mkuu Halima Bulaya naye akazinduka kutoka kwenye ukimya wake tangu mazungumzo yaanze na kuuliza swali.



    “Hapana Muheshimiwa Makamu wa Rais… hilo hatujafahamu bado.. Bado hatujajua ni kwanini amebadili karatasi?” Titus akajibu.



    “Swali la msingi hapa ni kwa namna gani hii chupa imepatikana ilhali Cindy na wenzake wamepotea ndani ya Anabelle takribani mwezi mzima? Wao wenyewe wako wapi?” Rais Zuberi Miraji naye akadakia na kuiliza swali.



    “Muhishimiwa Rais hilo bado tunalifanyia kazi… hata sisi tumeshindwa kufahamu ni namna gani hii chupa imeweza kuonekana mwezi mmoja baadae lakini Cindy na wenzake hawajaweza kuonekana!”



    “Unadhani bado wako hai?” Makamu wa Rais January akauliza tena.



    “Sidhani kama watakuwa hai.… lakini kama nilivyosema hatuna uhakika wa nini hasa kinaendelea… kwa hiyo ningekuwa na jibu la uhakika zaidi kwamba hawako hai endapo kama tungeokota miili yao!” Titus akajibu tena.



    “Hebu tafadhali tusipoteze muda hapa… Kipindi Dar es Salaam inatwaliwa takribani watu milioni Tatu walibaki ndani yake… Je kuna mwili hata mmoja tumeupata? Hapana… na hakujawahi kupatikana mwili wowote dunia nzima tangu miji ianze kutwaliwa… watu wanapotelea kusikojulikana.. Kwa hiyo nadhani ni sahihi tukikubali kwamba Cindy na wenzake hatunao tena. Wametutoka tayari… nadhani ninachohitaji kujijua zaidi ni nini hasa kimeandikwa kwenye hiyo Karatasi?”  Rais aliongea kwa haraka na kumaliza kwa swali ambalo lilikuwa kwenye vichwa vya viongozi wenzake wote, yaani Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.



    Titus Mollel akaingiza tena mkono wake taratibu ndani ya mkoba wake na kutoa karatasi ndogo ambayo imevingirishwa au waweza kusema imejaladiwa kwenye karatasi nyingine ya plastiki.



    Ndani ya karatasi hii ya plastiki ilikuwa inaonekana karatasi nyingine ya kawaida ambayo ilionekana kama vile imechanwa kutoka kwenye daftari au diary na mtu kuandika akiwa na haraka sana kutokana na jinsi mwandiko ulivyo vurugika.



    Karatasi hii ilisomeka hivi;



    “Ni masaa 16 tangu tuingie ndani ya Anabelle 27… wote tuko salama isipokuwa Kanali ameuwawa na kiumbe cha ajabu. Tumefanikiwa kufika nje ya mlango wa The 46. Ndani ya masaa manne yajayo Tunahitaji detail #127 kushoto mwa mchoro wa George Washington ili tuweze kufanikisha azma yetu na kutoka tukiwa hai.

    Pia mikononi mwetu tunazo nguo za za Madam President Laura Keith, kidani chake cha shingoni, hereni, bangili, pete ya ndoa na POLO-TD.

    Tumeonywa pia kuwa wakala wa The 46, amerejea duniani. W7. W7. W7”



    Ujumbe ukaishia hapo.



    Ulitawala ukimya wa kama dakika kumi nzima kila mmoja akichakata kichwani mwake kile ambacho alikuwa amekisoma.



    “The 46 ni kitu gani? Na detail #127 ni nini?” Baada ya kimya kirefu hatimaye Rais akauliza huku amemkazia macho Titus.



    “Mheshiwa Rais hata sisi tupo gizani… hatufahamu The 46 ni kitu gani, wala detail #127, wala maneno ya mwishoni W7, W7, W7… kwa ujumla hatujaelewa maana nzima ya huu ujumbe! Kitu pekee tulichoelewa ni kwamba uliandikwa takribani masaa 16 tangu waingie ndani ya Anabelle 27 na walikuwa wanahitaji wapewe hicho wanachokitaka ndani ya masaa manne ili watimize walichokifuata na watoke wakiwa hai. Mheshimiwa huu ni mwezi sasa umepita, kwa hiyo kwa lugha nyingine… Cindy, Salim, Shafii, Magdalena na Kanali… wamefia ndani ya Anabelle 27”



    Titus akaongea kwa hisia. Ukimwa mwingine wa karibia dakika tano nzima ukatawala tena.



    “Lakini pia wameeleza kuwa mikononi mwao wana nguo za Madam President Laura Keith na vitu vyake vingine… inawezekana vipi hii? Air force One ilidondoka Bahari ya Atlantic… inawezekanaje vitu vyake viokotwe ndani ya Anabelle 27 Afrika?” Makamu wa Rais January Nchimbi kauliza kwa hisia kubwa.



    “Nadhani tunapaswa kuwapa hii taarifa Serikali ya Marekani… hasa hasa kuhusu hivi vitu vya Laura Keith!” Rais akongea huku amekunja uso.



    “Niwie radhi lakini sidhani kama ni wazo sahihi Muheshimiwa Rais!” Titus akapinga lakini akiongea kwa heshima kubwa.



    “Kwa nini?” Rais akauliza kwa kifupi huku amekunja ndita.



    “Kila nikisoma hii kauli iliyoandikwa hapa “wakala wa The 46? amerudishwa duniani… sielewi hasa wanamaanisha nini lakini naona kama ni onyo Fulani… nadhani tuwe makini na kila hatua tunayochukua!” Titus akajieleza tena kwa heshima kubwa na unyenyekevu.



    “Unadhani serikali ya Marekani wakija kujua tulikiwa na taarifa nyeti kama hii kuhusu kupatikana kwa vitu vya rais wao alafu hatukuwaeleza… unadhani watatuelewaje?” Rais akamuiliza Titus kwa hasira.



    “Nilikuwa natoa angalizo tu Muheshimiwa Rais!” Titus akajibu kwa unyonge.



    Rais Zuberi Miraji hakumjibu wala kumsemesha kingine chochote Titus, akageuka tu kumuangalia CDF Henry Kaizirege na kumpa agizo.



    “Piga simu Washington… waambie nahitaji kuongea na Rais haraka sana.!” Rais akaamuru.



    “Sawa Muheshimiwa!” CDF Kaizirege akainuka na kupiga saluti na kisha kuelekea meza iliyopo pembeni yao ambayo ilikiwa na vifaa vya mawasiliano.





    THE OTHER HALF











    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE











    EPISODE 23











    NDANI YA ANABELLE 27

    “Unahisi yamepita masaa mangapi mpaka sasa?”



    “Nadhani saa moja, au saa moja na nusu lakini kwa namna yoyote haiwezi kuwa zaidi ya masaa mawili!”



    “Walikiwa wanatakiwa kutupa majibu mpaka muda huu.”



    “Kabisa! Nina wasiwasi kama hata ujumbe wenyewe wameupata? Na sidhani kama hata tulichokifanya kimefanikiwa..!”



    “Tufanye kile tunachoweza tu kukifanya Salim! Hatupaswi kukata tamaa wala kujilaumu.”



    “Nakuelewa Cindy, lakini wasiwasi wangu ni kama tutafanikisha hili suala ndani ya wakati na kama nitaweza kumuokoa mke wangu na mwanangu Basra!”



    “Pole Salim! Tuombe Mungu tufanikishe kwa wakati!”



    Cindy na Salim pamoja na wenzao ambao walikiwa ndani ya Anabelle walikuwa wejigawa katika makundi mawili.



    Cindy na Salim walikuwa wamejipa jukumu gumu la kutafuta namna ya kuwasiliana na ulimwengu wa nje ili kuomba msaada kufanikisha hatua waliyokuwa wefikia.

    Shafii na Magdalena walikuwa wamepewa kazi ya kulinda mlango wa The 46.



    Takribani kama masaa sita yaliyopita waliponusurika kuuwawa na yule mnyama wa ajabu baada ya kuokolewa na binadamu wa ajabu walioibuka kutoka majini namoja kujitambulisha kama ‘Caleb’ na kisha kuondoka na mnyama yule lakini kabla hawajaondoka wakiwaelekeza njia ya kuifuata ili kuufikia mlango wa The 46.

    Kwa masaa yote haya sita Cindy, Salim, Shafii na Magdalena walikuwa wanafanya kazi hii nzito ya kuutafuta huo mlango mpaka wakafanikiwa kuupata.

    Miji wa Dar es Salaam ambao sasa tayari ulikuwa Anabelle 27 ulikuwa unabadilika zaidi na kuanza kuwa kama unavurugika tofauti na namna ambavyo walikuwa wanaukumbuka kabla haujatwaliwa.



    Walipoelekezwa na yule binadamu wa ajabu kwamba waelekee upande wa kaskazini kufuata mto, alikiwa anamaanisha kwamba kutoka pale walipo ambapo kabla mji kutwaliwa ndipo ilikuwa eneo la ubungo, walitakiwa waelekee kufuata mto ambao awali ilikuwa ni barabara ya Sam Nujoma na waende mbele kufuata maeneo ambayo awali kulikuwa ni Mwenge na kadhalika.

    Salim na wenzake walifuata muelekeo huu walioelekezwa na yule binadamu.



    Walitembea kwa takribani masaa mawili pasipo kukutana na jengo hata moja kama ambavyo walikuwa wanaukumbuka mji wa Dar es Salaam namna ambavyo ulikuwa.

    Baada ya kama masaa mawili hivi ndipo ambapo walikuwatana na msitu mkubwa wa miti isiyokuwa na majani wala matawi mengi. Yaani ilikuwa ni miti kabisa lakini haikuwa na matawi mengi kama ambavyo mti unapaswa kuwa na miti hii yote hakukuwa hata na mti mmoja ambao ulikuwa na jani hata moja lakin miti ilikuwa ni mingi kweli kweli kiasi kwamba ulikuwa kama msitu kabisa.



    Mahali hapa Cindy aliwaeleza wenzake kwa kadiri alivyosoma na anavyokumbuka kichwani mwake ujuzi wake wa akiolojia ni kwamba ilikuwa ni sehemu ya Makutano ya Watoto wa Anabelle 1 (Maldives) na Wanachama wawakilishi wa The 46.

    Yaani kwamba, kwa nadharia ambayo Cindy alikuwa anaiamini, aliamini watoto wa ajabu wenye manyoya ambao waliozaliwa miaka miwili iliyopita nchini Maldives ndio hao ambao kwa msaada wa kikundi cha The 46 walikuwa wanatwaa miji duniani.



    Cindy aliamini kwamba watoto wale waliozaliwa Maldives hawakuwa na uwezo wa kuishi katika mazingira ya ulimwengu wa kawaida na kwa kuzingatia kuwa waligeuka kuwa viumbe wa ajabu namna hiyo baada ya chupa iliyokuwemo kwenye sanduku la Pandora kufunguliwa, basi walikuwa wanataka kuirejesha dunia yote katika namna ambavyo dunia ilikiwa maelfu ya miaka iliyopita kipindi ambacho Mungu wa Kigiriki Zeus alimuumba mwanamke wa kwanza, Pandora na kumuweka katika mji wa Anabelle wa kipindi hicho.







    Licha ya ufafanuzi wote huu lakini Cindy alishindwa kuwajibu wenzake swali moja muhimu… kama miaka elfu iliyopita baada ya Zeus alimuumba Pandora na kumuweka kwenye mji wa Anabelle, je ni nini kilitokea duniani mpaka kuifanya dunia kubadilika na kuwa hivi ilivyo leo hii mpaka kuwafanya watoto wa Maldives kutaka kuibadili tena kuwa namna ambavyo ilikuwa awali, Yaani ulimwengu mzima kuwa Anabelle?



    Kitu pekee ambacho Cindy aliweza kuwaeleleza ni kwamba hili suala kabla ya kutokea hakukuwa na mtu ambaye aliamini simulizi kuhusu Pandora, zilikuwa ni hadithi za kufikirika, ni mpaka sasa baada ya dunia kuanza kubadilishwa kuwa Anabelle ndipo ambapo wanaakiolojia wameanza kuamini juu ya historia kuhusu Pandora, Sanduku alilopewa na Zeus pamoja mji wa Anabelle.



    Swali lingine ambalo Salim alimuuliza Cindy lilikuwa ni kutaka kufahamu kwa nini jumuiya ya siri ya The 46 walikuwa wanasaidia watoto wa Maldives kuibadili dunia kurejea tena kuwa Anabelle ya maelfu ya miaka iliyopita.

    Cindy pia hakuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu swali hili. Alichowaeleza wenzake kwamba, kwa kadiri anavyofahamu historia ya siri ya jumuiya ya The 46, kikundi hiki ndicho ambacho kinaifanya dunia iendelee kuwepo. Ni wao ndio wanaopambana kila siku na matishio yasiyoonekana ya kuidhuru dunia. Ndio wao ambao wanatimiza majukumu ambayo binadamu wengine hatuyajui ili tu kuitetea dunia. Kwa hiyo kitendo cha kuwepo kwa dalili ya jumuiya ya The 46 kusaidia watoto wa Maldives kuibadili dunia kuwa Anabelle ilikuwa ni suala linalochanganya akili. Cindy aliamini kuwa kuna suala aliko sawa ndani ya jumuiya ya The 46, kuna kitu kitakuwa kimetokea.



    Cindy akaendelea kuwaeleza wenzake kuhusu eneo hilo ambalo walikuwa wamesimama, msitu mnene wa mito isiyo na majani. Akawaeleza kwamba kama nadharia yake iko sahihi basi hapa walipo ndio eneo ambalo mawakala wa The 46 wanakutana na watoto wa Maldives. Na kama yuko sahihi kuhusu eneo hili kwamba ndipo ambapo The 46 wanakutana na watoto wa Maldives, basi hapa ndipo ambapo Mlango wa The 46 ulipo. Mlango huu ndio ambao unatumiwa na mawakala wa The 46 kuingia ndani ya Anabelle kutokea duniani.



    Cindy aliwaongoza wenzake kwa makini kukagua eneo hili. Kwanza kabisa akatoa chupa ambayo aliweka damu ya yule kiumbe wa ajabu, binadamu mwenye kufanana na paka kwa muonekano na kutembea kwakwe kwa kutumia miguu na mikono, mmoja wa watoto wa Maldives ambaaye walimuua mwanzoni kabisa mara tu baada ya kuingia ndani ya Anabelle.

    Akatoa kichupa hiki alichohifadhi ile damu ambayo haikuwa nyekundu kama damu ya binadamu wa kawaida, bali ilikuwa na unjano wa kufifia na ilikuwa nzito zaidi. Pia akatoa na ile ngozi aliyomchuna kiumbe yule, mtoto wa Maldives. Ngozi hii alimpatia Magdalena aishikilie.



    Kisha akawaamuru wenzake wote wachovye vidole kwenye kile kikopo chenye damu na kujipaka mwilini kama vile ambavyo huwa wanapaka mafuta.



    Baada ya kumaliza zoezi hili ndipo akawaruhusu wenzake wote na yeye mwenyewe waanze kukagua ule msitu wa miti isiyo na majani.

    Aliwaeleza kuwa japokuwa walikuwa hawaoni mjongeo wowote kwenye ule msitu lakini alikuwa na uhakika kuwa kulikuwa na walinzi kila kona. Kwa hiyo lengo la kupaka ile damu ilikuwa ni kufanya harufu yao ya ubinadamu isiweze kuhisiwa na pua za viumbe vinavyolinda mahala hapo.



    Jambo lingine la muhimu pia, aliwapa tahadhari wenzake kuwa watembee kwa uangalifu mkubwa na wasivunje mti au hata tawi moja la mti. Aliwaeleza kwamba anaamini kuwa kukifanyika kitu chochote cha tofauti mahali hapo kama mti kuvunjika au tawi basi moja kwa moja walinzi wa mahali hapo wataamka na maisha yao yanaweza kuishia hapo hapo kama ilivyotokea kwa mwenzao Kanali.







    Cindy na wenzake wakaanza kukagua ule msitu hatua kwa hatua.

    Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa anajua labda mlango wa The 46 unafananaje.

    Ilifika muda mpaka wakakaribia kukata tamaa na waache kukagua msitu huo wasonge mbele ma safari yao, labda hapa siko kwenye mlango wa The 46, lakini ghafla kitu cha ajabu kikatokea.



    Mahala fulani mbele yao chini ardhini walisikia kuna sauti inatoka kama mtu anayegonga mlango mzito wa chuma.

    Namna ambavyo mlango huu ulikuwa unagongwa ilikuwa tofauti kidogo. Mara ya kwanza waliposikia sauti mtu anagonga walisikia kitu hicho chenye mlio kama chuma kikigongwa mara tatu kisha kukapita ukimya. Baada ya hapo wakasikia tena umegongwa mara tatu nyingine na kisha ukapita ukimya mwingine. Na kisha wakasikia mlio wa kugonga mara tatu kwa safari nyingine ya tatu na kisha ukimya mwingine ukatawala.

    Ghafla tu kufumba na kufumbua wakasikia kuna kitu kinakuja kwa kasi ya ajabu kinakimbia kama mbwa au simba. Walipoangalia kwa makini waligundua alikiwa ni moja ya binadamu wa ajabu, mtoto wa Maldives anakuja kwa kasi anakimbia kwa mikono na miguu kama mbwa kuelekea pale sauti ya kugonga gonga ilipokuwa inatokea.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Baada ya yule kiumbe kufika sehemu ile ambayo sauti ilikuwa inatokea, akafukua chini kidogo na kisha wakamuona kuna kitu kama msukani anazungusha.

    Ghafla ukatokea mwanga mkali unamulika kutoka chini ardhini kama vile tochi au taa yenye mwanga mkali. Lakini tofauti ni kwamba huu haukuwa mwanga wa tochi au mwanga wa taa, ilikuwa dhahiri kabisa kwamba huu ulikuwa ni mwanga wa jua. Yaani ilikuwa ni kana kwamba upo kwenye chumba chenye giza kubwa wakati wa mchana alafu mtu afungue dirisha.



    Baada ya mwanga huu mkali kupiga kutokea pale chini ardhini yule kiumbe wa ajabu, mtoto wa Maldives akaondoka kwa kumbia vile vile kama ambavyo alikuwa amekuja.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog