Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KIAPO CHA JASUSI - 5

 





    Simulizi : Kiapo Cha Jasusi

    Sehemu Ya Tano (5)









    “Hallow Omar habari za huko?akasema Mariana baada ya simu yake kupokelewa



    “Habari za huku nzuri kabisa.Unaendeleaje Mariana?



    “Ninaendelea vyema.Omar nataka kuzungumza na Farhad”



    “Farhad yuko kwenye kikao hivi sasa.Nipe ujumbe nitamfikishia”



    “Omar fanya kila uwezalo kuhakikisha Farhad anapatikana nahitaji kuzungumza naye haraka ni muhimu sana”



    “Sawa ninaomba unipe dakika tano” akasema Omar na kukata simu



    “Natamani ningefanikiwa kuonana na huyo mkuu wa gereza aliyetumwa afikishe ujumbe huu kwa padre Thadei ili anieleze Zaidi kuhusiana na hali ya kiafya ya ba…..” Mariana akatolewa mawazoni baada ya mlio wa ujumbe kusikika katika simu yake ya kawaida.Akaichukua na kutazama ni ujumbe uliotumwa katika kikundi chao cha sala kupitia mtandao wa whatsapp.Ujumbe ule ukamstua sana Mariana akahisi kama mikono inamtetemeka baada ya kuusoma ujumbe ule.



    “Padre Thadei amefariki dunia?!! Akajiuliza na kwa haraka akazitafuta namba za mmoja wa wafanyakazi wa kanisa akampigia.



    “Mama Minja tafadhali naomba uniambaie kama taarifa hizi za kuhusiana na padre Thadei ni za kweli” akauliza Marianahttp://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Mariana hizi ni taarifa za kweli kabisa.Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo mara tu ibada ilipomalizika.Kuna watu walimfuata padre katika kiungamishio na kumtaka waongozane naye na walipofika nje akaanza kupambana nao na wakamshambulia kwa risasi.Padre Thadei amefariki dunia” akasema mama Minja na Mariana akajikuta ameketi kitandani.Akarudisha kumbu kumbu nyuma alipokuwa katika kiungamisho na padre Thadei.Akayakumbuka maneno ya mwisho aliyoelezwa na padre Thadei akimtaka kuchukua tahadhari kutokana na kitendo cha kufahamu mahala alikofungwa baba yake mzee Alfredo kitwe.Alikumbuka alipotoka katika kiungamishio alikutana na mtu akiingia na kulikuwa na watu wengine wawili wamekaa katika benchi wakisubiri zamu yao ya kuungama.



    “Yawezekana ni wale jamaa niliopishana nao? Sijawahi kuwaona kabis akatik aibada.Tunaohudhuria ibada za asubuhi tunafahamiana lakini wale jamaa ni mara ya kwanza kuwaona leo.Yawezekana ni wale ndio waliomuua?Akajiuliza



    “Nina hisi hivyo.” Akaendelea kuwaza na simu yake ile anayotumia kwa mawasiliano na nje ya nchi ikaita akaipokea



    “Hallow Omar.Umefanikiwa kumpata Farhad? Akauliza



    “Ndiyo nimefanikiwa kumpata.Zungumza naye” akasema Omar na baada ya sekunde kadhaa ikasikika sauti nyingine ambayo Mariana akaitambua ni sauti ya Farhad



    “Mariana nimeambiwa unahitaji kuzungumza na mimi.Una taarifa zozote unataka kunipa?akauliza Farhad



    “Ninataka kuzungumza na rais” akasema Mariana na Farhad akasikika akivuta pumzi ndefu na kuuliza



    “Unataka kuzungumza na rais?Kuna suala gani unataka kuzungumza naye?



    “Kuna suala la muhimu sana ambalo nahitaji kuzungumza naye”



    “Siku zote umekuwa ukiwasiliana nami kwa nini leo unataka kuzungumza na rais moja kwa moja?Kitu kingine fahamu kuwa rais ni mtu mkubwa sana hivyo hadi kuzungumza naye lazima kuwe na jambo zito.Nieleze ili nione kama suala lako lina uzito wa kuzungumza na rais au kama ninaweza kulifanyia kazi mimi mwenyewe” akasema Farhad.Mariana akasita kidogo halafu baada ya sekunde kadhaa akasema



    “Nimefahamu gereza alikofungwa baba yangu” ukatokea ukimya wa sekunde kadhaa halafu Farhad akauliza



    “Una hakika Mariana?



    “Ndiyo nina uhakika” akasema Mariana



    “Sawa.Naomba subiri kidogo.Usikate simu” akasema Farhad na Mariana akaendelea kusubiri.Baada ya dakika tatu ikasikika sauti ya Farhad.



    “Mariana unaweza kuzungumza na rais”



    “Habari yako Mariana.Nimeambiwa kuna jambo la maana unataka kuniambia” ikasema sauti ya Ehsan hamed rais wa Iran



    “Mtukufu rais ni kweli nina jambo ninataka kuzungumnza nawe”



    “Endelea” akasema rais Ehsan



    “Nimepata taarifa sahihi kuhusu mahala alikofungwa baba yangu Dr Alfredo kitwe.Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata ni kwamba hali yake si nzuri na anaweza akafariki muda wowote hivyo nahitaji kwenda kuonana naye haraka iwezekanavyo.Nitahitaji msaada wako katika hilo”akasema Mariana



    “Mariana taarifa ulizonipa ni njema sana hasa kwa serikali ya Iran lakini kutakuwa na tatizo katika kukusaidia uweze kuonana na baba yako kwani hatuwezi kuingilia mambo ya ndani ya nchi yako hasa kwa wakati huu ambao nchi ya Tanzania na Iran hazima mahusiano mazuri”



    “Unaweza kunisaidia Mtukufu rais Ehsan” akasema Mariana



    “Unadhani tunawezaje kukusaidia? Akauliza rais Ehsan



    “Nataka uwasilishe suala hili kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu.Kwa muda wa miaka kumi baba amefungwa gerezani na haruhusiwi kuonana na mtu yeyote na hata sisi familia yake hatukuwa tukifahamu mahala alikofungwa.Nataka umoja wa mataifa kupitia shirika lake la kutetea haki za binadamu lipige kelele kuhusu suala hili na kuishinikiza serikali ya Tanzania iruhusu Dr Alfredo aonane na familia yake.Nikifanikiwa kuingia gerezani na kuonana na baba nina hakika atanieleza mambo mengi na ya muhimu ambayo tunayahitaji sana kuyafahamu.Tumehangaika kwa muda mrefu kutafuta mahala alikofungwa baba bila mafanikio na sasa baada ya kufahamu mahala alikofungwa ni wakati wetu wa kupata majibu ya mambo yale tunayoyahitaji hivyo tusiruhusu suala hili likatuponyoka mikononi.Tufanye kila linalowezekana hadi nifanikiwe kuingia gerezani na kuonana na baba”akasema Mariana



    “Sawa nimekuelewa Mariana.Nakuomba unipe muda nione nitafanya nini.Nitakujulisha baadae hatua nitakazokuwa nimechukua,kwa sasa endele kuchukua tahadhari na kufanya uchunguzi zaidi” akasema rais Ehsan











    TEHRAN – IRAN





    Baada ya kuzungumza na Mariana simuni,rais Ehsan akamuita Farhad mkuu wa shirika la ujasusi ofisini kwake na kumueleza taarifa alizopewa na Mariana kuhusiana na kujulikana mahala alikofungwa rais wa zamani wa Tanzania Dr Alfredo Kitwe



    “Ninataka unishauri tufanye nini? Kwa muda mrefu tumemtumia Mariana kutafuta mahala alikofungwa baba yake lakini hajafanikiwa hadi leo hii.Amefungwa mahala pa siri kubwa na viongozi wa Tanzania hawakutaka aonane na mtu yeyote hata familia yake haikujua mahala alipofungwa baba yao.Tunapaswa kufanya kila tuwezalo na Mariana aweze kuonana na baba yake na nina uhakika akifanikiwa kuonana naye tutakipata kile ambacho tumekuwa tunakitafuta kwa miaka mingi.Ninataka nishauri tufanye nini ili kumsaidia Mariana aweze kuingia gerezani na kuonana na baba yake?Mariana ameshauri kwamba niwasiliane na katibu mkuu wa umoja wa mataifa nimueleze jambo hili ili kwa kupitia shirika la umoja wa mataifa la kutetea haki za binadamu basi wapaaze sauti na kuitaka serikali ya Tanzania kuruhusu familia ikamtazame mzee huyu ambaye kwa taarifa alizozipata Mariana anaweza akafariki wakati wowote.Hatupaswi kusubiri hadi afariki kwani tutakosa mambo mengi tunayohitaji kuyafahamu”akasema rais Ehsan



    “Mtukufu rais,hizi ni taarifa njema sana kwetu na hatupaswi kufanya uzembe wowote.Ushauri alioutoa Mariana kuhusu kuwasiliana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa ni mzuri lakini utachukua muda mrefu na sisi hatutaki suala hili lichukue muda mrefu.Tunahitaji mambo yaende haraka na Mariana aweze kwenda gerezani kuonana na baba yake.Ninao ushauri” akasema Farhad na kunyamaza kidogo halafu akaendelea



    “Mahusiano yetu na China yameimarika sana siku hizi kwa hiyo tutumie urafiki wetu na China kuishinikiza serikali ya Tanzania kuruhusu familia ya Dr Alfredo kwenda kumtembelea gerezani”



    “Ni wazo zuri lakini tutatumia kigezo gani kuifanya serikali ya China iishinikze serikali ya Tanzania kuruhusu familia ya Alfredo ikamtembelee gerezani?akauliza rais Ehsan



    “Ni rahisi.Kwa siku za hivi karibuni China imewakamata watu Zaidi ya mia mbili ambao wamekuwa wakijihusisha na makossa mbali mbali na hasa ya kutaka kuingiza dawa za kulevya nchini China na wengi kati ya watu hao wanatokea nchini Tanzania.Hadi sasa kuna wafungwa wengi wa kutoka Tanzania katika magereza ya China hivyo tutaiomba serikali ya China itishie kuwanyonga watanzania wote walioko China ambao wamefungwa kwa makosa ya kujaribu kuingiza madawa ya kulevya.Watu Zaidi ya mia mbili ni wengi sana na ninaamini serikali ya Tanzania haitakuwa tayari watu hawa wote wanyongwe hivyo itataka majadiliano na serikali ya China na endapo watataka majadiliano tutawataka China waombe kitu kimoja tu ambacho ni kuitaka serikali ya Tanzania kuiruhusu familia ya Alberto ikamtembelee gerezani”akasema farhad

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Ninakubaliana na mpango huo Farhad lakini China na Tanzania ni nchi marafiki wa muda mrefu toka enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili.Sina hakika kama China wanaweza wakakubali kufanya jambo kama hilo ambalo litateteresha mahusiano yake na Tanzania”akasema rais Ehsan



    “Watakubali.” Akasema Farhad



    “Una uhakika gani kama watakubali?akauliza rais Ehsan



    “Kuna watafiti nane raia wa China waliopelekwa nchini Iraq na kampuni moja kubwa kufanya utafiti wa mafuta lakini serikali ya Iraq inawashikilia kwa tuhuma za kufanya ujasusi.Juhudi za kidiplomasia zimeshindwa kuzaa matunda na watafiti hao bado wanaendelea kushikiliwa nchini Iraq na endapo watakutwa na hatia watakabiliwa na adhabu ya kifo.Mahusiano yetu na iraq kwa sasa ni mzuri hivyo tunaweza kufanya mazungumzo nao tukabadilishana wafungwa.Sisi tukawapatia wafungwa wao Zaidi ya mia moja ambao wamefungwa hapa Iran na wao wakatupatia watafiti hao nane ili tuwakabidhi kwa China.Tukitumia njia hii nina uhakika mkubwa tutafanikiwa lengo letu”akasema farhad



    “Ahsante kwa mawazo hayo mazuri Farhad.Ninakubaliana nayo na tufanye kama hivyo ulivyoshauri” akasema rais Ehsan na kuagiza atafutiwe rais wa China Cheng Zhang katika simu.Baada ya dakika tano rais wa China akapatikana akiwa ndani ya ndege yake akielekea nchini Singapore katika ziara



    “Habari yako mheshimiwa Ehsan” akasema rais Cheng baada ya kupokea simu ya rais Ehsan



    “Habari nzuri mheshimiwa rais Cheng.Samahani sana kwa usumbufu sikujua kama uko safarini”



    “Usijali Ehsan japokuwa niko safarini naelekea Singapore lakini hainizuii kuendelea kufanya kazi zangu hivyo kuwa huru”



    “Ahsante sana” akajibu Ehsan na baada ya ukimya wa sekunde kadhaa akasema



    “Cheng nimekupigia kuna jambo nataka tuzungumze”



    “Ndiyo endelea”akasema Cheng



    “Kuna raia wako nane wanashikiliwa nchini Iraq kwa tuhuma za ujasusi na kwa taarifa nilizonazo ni kwamba hivi karibuni watafikishwa mahakamani na endapo watakutwa na hatia kuna hatari watu hao wakanyongwa”



    “Ndiyo Ehsan.Ninao raia wangu ambao ni watafiti wa masuala ya mafuta wanaoshikiliwa nchini Iraq kwa tuhuma za ujasusi lakini watu hao ni watafiti na si majasusi kama inavyodaiwa.Jitihada za kidiplomasia zimeshindikana kwa sababu kuna shinikizo kubwa kutoka serikali ya Marekani kutaka watu hao waadhibiwe kama unavyofahamu kuwa mahusiano yetu na Marekani kwa sasa si mazuri.Kuna lolote unaweza kunisaidia katika suala hilo mheshimiwa rais?akauliza rais Cheng



    “Ndiyo ninaweza kukusaidia mheshimiwa Cheng.Ninao uwezo wa kuzungumza na Iraq na nikawapata watu hao wote wakarejea salama nyumbani”



    “Mheshimiwa rais ninaomba sana unisaidie katika hilo.Ni suala ambalo linanikosesha usingizi na hadi sasa tumeanza kufikiria hata kutumia njia nyingine za nguvu kuwachukua watu wetu baada ya njia za kidiplomasia kushindikana”



    “Hakuna haja ya kutumia nguvu mheshimiwa rais Cheng.Nitakusaidia kuwapata raia wako lakini na mimi kuna kitu ninakihitaji kutoka kwako”



    “Sema mheshimiwa rais unahitaji kitu gani?akauliza rais Cheng



    “Nchini mwako kuna raia zaidi ya mia mbili wa Tanzania ambao wamefungwa katika magereza mbali mbali na wengi ni kwa makosa ya kuingiza madawa ya kulevya nchini China”



    “Uko sahihi mheshimiwa rais Ehsan.Kumekuwa na idadi kubwa ya watu kutoka Afrika kukamatwa nchini China wakijaribu kuingiza dawa za kulevya na miongoni mwao wengi ni kutoka Tanzania na Nigeria.Kuna watu unawahitaji katika orodha ya waliofungwa hapa China?



    “Hapana mheshimiwa rais sihitaji mfungwa yeyote.Ninachokihitaji ni hiki.Imepita miaka kumi sasa toka aliyewahi kuwa rais wa Tanzania Dr Alfredo kitwe kufungwa maisha gerezani.Kwa muda huo wote aliokaa gerezani hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtembelea na wala haikujulikana ni gereza lipi amefungwa hadi hivi karibuni ilipogundulika mahala alipofungwa.Dr Alfredo ni mgonjwa sana na anaweza akafariki wakati wowote.Ninataka utoe kitisho kwa serikali ya Tanzania kuwa serikali ya China itawanyonga raia wote wa Tanzania waliofunga nchini mwake kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya.Taarifa hii itaistua sana serikali ya Tanzania na lazima watahitaji mazungumzo na wakija mezani wapewe sharti moja tu kwamba waruhusu Dr Alberto atembelewe na familia yake na waruhusu aende akapatiwe matibabu katika hospitali kubwa.Ni hilo tu ninalolihitaji mheshimiwa rais Cheng na kama likifanikiwa basi raia wako nane watarejea nyumbani salama salimini” akasema rais Ehsan.Rais Cheng akafikiri kidogo halafu akasema



    “Mheshimiwa rais umenipa mtihani mgumu sana.Nchi yangu na Tanzania ni marafki wa muda mrefu sana toka enzi za waasisi wa mataifa yetu haya mawili.Kitendo hicho cha kutishia kuwanyonga raia wa Tanzania waliofungwa nchini China kitavuruga mahusiano mazuri na ya muda mrefu kati ya China na Tanzania,mahusiano ambayo yamekuwa na faida sana kwa nchi zetu zote mbili”



    “Ninalifahamu hilo mheshimiwa rais Cheng lakini lengo langu si kuwaua wafungwa hao bali ni kutishia tu ili kuileta Tanzania mezani na kuishinikiza ikubali Dr Alfredo atembelewe na familia yake.Mahusiano yanaweza yakavurugika lakini baadae mambo yakatulia na mahusiano yakarejea kama kawaida.tanzania haiwezi kuwa na uadui na China hata kidogo na wakisikia suala kama hilo haraka sana watakuja mezani kujadiliana”



    “Mheshmiwa rais Ehsan kwa nini unataka Dr Alfredo atembelewe na familia yake gerezani?Suala hili lina maslahi yoyote kwa nchi ya Iran? Akauliza Cheng



    “Mheshimiwa Cheng siwezi kukuficha ni kweli kuna maslahi kwa nchi yangu katika jambo hili na ndiyo maana tuko tayari kufanya lolote linalowezekana ili kufanikisha suala hili.Je unakubaliana na suala hili?



    “Mheshimiwa rais Ehsan siwezi kukupa jibu la haraka kwa suala hili kama unavyojua ni suala pana kidogo.Nipe muda nikae na watu wangu tulijadili halafu nitakupa jibu baadae” akasema rais Cheng na kuagana na rais Ehsan kwa miadi ya kuwasiliana tena baadae.











    DAR ES SALAAM – TANZANIA





    Hali ilikuwa ya pilika pilika nyingi katika jengo zilimo ofisi za jarida la beautiful Tanzania.Katika sehemu ya chini ya jengo hili shughuli za uandaaji wa jarida zilikuwa zinaendelea kama kawaida na katika ghorofa ya juu ndiko shughuli zote za kikundi hiki cha 100 Chitas zilikuwa zinafanyika.



    Noah akiwa ofisini kwake akizungumza na simu akamuona mmoja wa wataalamu wakubwa sana wa kompyuta anayetegemewa anayeitwa Teddy jini akiwa amesimama nje, akakatisha mazungumzo yake na mtu aliyekuwa anazungmza naye na kumkaribisha Teddy ofisini.



    “Niambie Teddy kuna loote umelipata?akauliza Noah



    “Mkuu kuna jambo nimelipata na nimeona nije nikueleze mwenyewe.Hili suala si dogo kama tunavyolichukulia ni suala pana sana.Nimeingia katika rekodi za mawasiliano ya simu ya kampuni ambayo Dr Isaack alikuwa mteja wao lakini cha kushangaza hakuna rekodi zozote za mawasiliano ya Dr Isaack” akasema Teddy na kumtazama Noah



    “Hii inamaanisha nini Teddy?



    “Hii inamaanisha kwamba rekodi hizi zimefutwa kwa makusidi kabisa na waliofanya hivi walifahamu fika kwamba tunaweza kufuatilia mawasiliano ya Dr Isaack na hivyo wakafuta kila kitu ili tusiweze kufahamu Dr Isaack alikuwa anawasiliana na nani na walikuwa wanawasiliana kitu gani” akasema Teddy na Noah akaweka mikono yake kichwani akaegemea kiti chake kwa sekunde kadhaa alikuwa kimya.



    “Hili suala linaniumiza kichwa changu sana.Najaribu kumuunganisha Dastan na Dr Isaack lakini kila njia tunayotumia tunashindwa kupata majibu.Kifo cha Dr Isaack kimeacha maswali mengi ambayo lazima tuyapatie majibu.Kwa nini rakodi hizi za mawasiliano ya Dr Isaack zifutwe?Kuna kitu gani kinafichwa?Je Dr Isaack alijiua au ameuliwa?Na kwa nini kifo chake kimetokea muda mfupi tu baada ya kutakiwa kutoa taarifa kwa rais kuhusiana na Dastan?akauliza Noah



    “Maswali haya ni magumu na tungepata mwangaza endapo tungefanikiwa kupata rekodi za mawasiliano ya Dr Isaack.Tungefahamu mara ya mwisho aliwasiliana na nani na waliongea nini.Tungefahamu pia kama ana mausiano yoyote na Dastan” akasema Teddy

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Teddy hakuna namna nyingine yoyote unayoweza kufanya kupata rekodi hizo?akauliza Noah



    “Hakuna Noah.Kama kungekuwa na sehemu ningeweza kupata rekodi hizo nisingekuwa nimesimama hapa sasa hivi” akasema Teddy na Noah akainamisha kichwa akawaza kwa muda halafu akasema



    “Teddy nakufahamu linapokuja suala la udukuzi wewe ni jini,hushindwi na kitu chochote.Hakuna mtandao ambao unashindwa kuudukua hapa duniani.I beg you,go back and dig deeper.There is must be something out there about Dastan.Siamini kama umefikia mwisho.Tunakutegemea sana wewe na kama ukishindwa basi tutakuwa tumeshindwa zoezi hili kwa hiyo nenda tena kafanye kazi hii kwa mara ya pili.Rais anatutegemea sisi na anasubiri majibu kutoka kwetu.Hatujawahi kushindwa kitu chochote na hii isiwe ni mara yetu ya kwanza kushindwa.Please Teddy” akasema Noah.



    “Ok let me try but I can’t promise anything” akasema Teddy na kuinuka



    “Thank you” akasema Noah na Teddy akatoka mle ofisini



    “Kwa mara ya kwanza limetokea jambo ambalo limenichanganya na sielewi nianzie wapi.Dastan anatakiwa apatikane na sijui nitaanzia wapi kumtafuta.Juhudi zetu zote kuanzia jana usiku hazijazaa matunda.Naamini yuko hapa hapa Dar es salaam lakini yuko sehemu gani na atapatikanaje?akajiuliza na kuzunguka katika kiti chake



    “Nadhani sehemu nzuri ya kuanzia kulichunguza jambo hili ni kujiuliza swali Dastan ni nani? Kulijibu swali hili ni lazima kufahamu historia yake kwa ujumla.Ametokea wapi,amesoma wapi,ndugu zake ni akina nani,je ana mpenzi au hana?Haya ni mambo ambayo nikiyafahamu yatatusaidia kumfahamu Dastan ni nani lakini ni wapi nitazipata taarifa hizi?Ni nani atakayenisaidia kuzipata taarifa hizi? Akajiuliza



    “Nimekumbuka kitu,rais alisema kwamba atamuagiza waziri wa mambo ya ndani ya nchi ampelekee taarifa za Dastan baadae leo.Ngoja nisubiri kama taarifa hizo zitapatikana.Endapo zitakosekana basi tutatafuta namna nyingine ya kuweza kupata taarifa za Dastan lakini endapo zikipatikana zitakua zimetusaidia sana kutegua kitendawili hiki cha kuhusu Daniel ni nani” akawaza Noah.





    *************





    Mshale wa saa ya ukutani ulionyesha ni saa nne na dakika saba za asubuhi.Katika chumba kikubwa Dastan tayari alikwisha amka na kuioga kujiweka tayari kwa ajili ya kuianza siku.Saa mbili za asubuhi aligongewa mlango na Paula ambaye alimkaribisha kupata kifungua kinywa na kumtaarifu kwamba Carmelita alikuwa njiani kurejea Tanzania hivyo baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa Dastan akarejea chumbani kwake kuendelea kupumzika wakati akimsubiri Carmelita.Kichwa chake kilijawa na mawazo mengi kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele na Carmelita hatokei.Akaenda dirishani na kachungulia nje.Lilikuwa ni jumba kubwa lililotawaliwa na ukimya mkubwa.Ni milio tu ya ndege iliyosikika



    “Jumba la kifahari mno hili.Huyu mwanamama Carmelita anaonekana ni mwanamke tajiri sana. Anafanya biashara gani ya kumfanya amiliki jumba kubwa namna hii? Ukiacha hayo ameweza kugharamia operesheni kubwa iliyogharimu fedha nyingi ambayo nimeimaliza jana.Anyway hayo hayanihusu kikubwa nimemaliza kazi yao na ni wakati wangu wa kuondoka kurejea nyumbani.” akawaza huku akitabasamu kuiona mandhari nzuri ya kuvutia iliyokuwa nje



    “Nilitegemea ningeweza kumaliza kazi yangu salama na kuondoka kimya kimya lakini imekuwa tofauti kwani hivi sasa tayari nitakuwa natafutwa sana nimeelekea wapi?Kufuatia tukio lililotokea jana naamini jeshi la polisi watanihitaji kwa ajili ya maelezo zaidi na watakaponikosa wataanza kunisaka kila kona lakini hadi wakati huo sintakuwepo nchini na nitawaachia kitendawili kigumu wapi nilipo na wataamini labda nimeuawa na mwili wangu kufichwa.Ninashukuru kwamba sikuacha alama yoyote ya kuwapa nafasi ya kunipata na ninashukuru pia kwa kuweza kumsaidia mzee Alfredo na ninaamini atafanikiwa kuonana na familia yake.Ninajiuliza sana kwa nini mzee huyu anafanyiwa hivi?Adhabu aliyoipata peke yake ya kufungwa maisha haitoshi hadi watawala wamfanyie ukatili huu wa kumzuia kuonana na mtu yeyote hata familia yake?Naamini Mungu atamsaidia na ataweza tena kuonana na familia yake baada ya ujumbe ule kumfikia padre Thadei kama alivyoelekezeza Alfredo mwenyewe.” akaendela kuwaza Dastan na kutabasamu lakini mara ghafla tabasamu likapotea



    “Ni vipi endapo serikali ya Tanzania wakagundua kwamba mimi si raia wa Tanzania na nilikuwa hapa kwa sughuli maalum? Japo sinahakika sana kama wanaweza wakagundua mimi ni nani na nini ilikuwa kazi yangu hapa Tanzania lakini sitakiwi kupuuza kwani Tanzania bado ina watu mahiri sana katika uchunguzi na wanaweza wakachunguza nakufahamu mimi ni nani nimetoka wapi na nini lengo langu la kuwepo hapa Tanzania.Lakini jambo hili nitawaachia akina Carmelita ambao ndio walioratibu misheni hii watalimaliza na kuhakikisha kwamba hakuna kitakachojulikana kuhusu mimi.Nitakapoonana na Carmelita nitamsisitiza jambo hili waliwekee mkazo kwani baada ya kuondoka hapa nataka kwenda kutulia na familia yangu na kufanya mambo yangu kwa Amani.Pesa nilizozipata kutokana na misheni hii ni nyingi na zitaniwezesha kufanya mambo mengi ya maendeleo.Ninataka kuingia katika biashara na sihitaji tena kuendelea na kazi hizi za hatari.Nataka familia yangu iishi kwa Amani bila kuwa na wasi wasi kuhusu usalama wao na wangu pia.Katika kazi hizi ninajenga maadui wengi na iko siku wanaweza wakanirudi na kuitekekeza familia yangu…..”Dastan akatolewa mawazoni baada ya mlango kugongwa akainuka na kuufungua akakutana na Paula ambaye alimtaka waongozane wakaenda katika sebule kubwa iliyopambwa vizuri.



    “Madam tayari amerejea na muda si mrefu mtaonana” akasema Carmelita na Dastan akashusha pumzi.Baada ya dakika mbili akatokea Carmelita.Alikuwa amevaa suruali ya Jeans rangi nyeupe na fulana nyeusi na juu yake akavaa shati jeupe ambalo halikufungwa vifungo na kukifanya kifua chake kizuri kilichobeba matiti yaliyojaa kuonekana vyema ndani ya ile fulana nyeusi.Alikuwa amependeza sana.Dastan akasimama kwa adabu kumsalimu.Huku akitabasamu Carmelita akamfuata na kumkumbatia



    “Hello Ivan” akasema Carmelita



    “Madam Carmelita” akasema Dastan



    “Vipi maendeleo yako? Ulikuwa na usiku mzuri?Umehudumiwa vyema?carmelita akauliza maswali mfululizo



    “Ninaendelea vyema madam Carmelita.Nimeamka salama nashukuru kwa huduma nzuri niliyoipata toka nilipofika hapa.Madam Paula amenipokea na kuakikisha ninapata kila ninachokihitaji” akasema Dastan



    “Nashukuru kusikia hivyo Ivan,naomba kama hutajali twende tukazungumze bustanini” akasema Carmelita na kuinuka Dastan naye akainuka wakatoka mle sebuleni na kufuata ujia ulioelekea katika bustani nzuri iliyokuwa na miti mingi ya maua na nyasi nzuri zenye ukijani



    “Nimetaarifiwa kwamba msako mkali unafanyika hivi sasa kukutafuta kila mahala.Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya taarifa ndani ya jeshi la polisi ni kwamba jana usiku kuna kikosi kimetumwa gereza la Markubelo kwa lengo la kwenda kukuchukua kukuhoji lakini wakakukosa na yakatolewa maagizo kwamba ufanyike msako mkali baharini na bandarini na polisi wakapewa hadi asubuhi ya leo wawe wamekupata.Hukuacha kitu chochote nyuma ambacho kinaweza kuwasaidia hawa jamaa kukufahamu?



    “Usihofu madam Carmelita hakuna kitu chochote nilichokiacha nyuma. Kwa muda huu wote nilioishi pale gerezani nimekuwa makini sana na sijaacha kitu chochote. Sijawahi kupiga picha yoyote pale gerezani nikiwa na mtu au hata peke yangu na hivyo hawataweza kuipata sura yangu.Ninakuhakikishia kwamba hawataweza kunipata.Vipi kwa upande wenu hakuna tatizo lolote?akauliza Dastan



    “Ninafurahi kusikia hivyo Dastan.Kwa upande wetu hakuna tatizo lolote.Kila kitu kimekamilika.Baada tu ya kupata taarifa jana usiku kwamba unahitimisha misheni yako nikaelekeza watu wangu kuwa wahakikishe hakuna taarifa yako yoyote inabaki katika kumbukumbu za serikali.Nimehakikishiwa kwamba tayari hakuna taarifa yoyote iliyobaki zote zimekwisha ondolewa.Hakuna hata picha yako iliyobaki hivyo usiwe na wasi wasi hakuna yeyote atakayekufahamu.Hii ina maana kwamba jina la Dastan Mwaikambile tumelizika rasmi na sasa unarejea katika jina lako halisi la Ivan Dawson.Dastan Mwaikambile imebaki hewa.He never existed” akasema Carmelita na kumkaribisha Dastan katika sehemu kulikojengwa viti maalum kwa kupumzika.



    “Kabla ya Dr Isaack kukupigia simu jana usiku alinipigia kwanza mimi na akanieleza kwamba rais anahitaji taarifa zako zote.Anataka kukufahamu wewe ni nani.Ni wazi kwamba tayari wameanza kukuchunguza wakufahamu wewe ni nani.Katika mazungumzo yetu ya dakika chache alinieleza kwamba kama tayari wameanza kuwa na wasi wasi nawe watachimba Zaidi hadi wakufahamu wewe ni nani hivyo njia pekee ni kwanza kuhitimisha kazi yako pale gerezani na kuondoka haraka.Pili Dr Isaack alifanya maamuzi magumu sana ili kulifanya suala hili liendelee kuwa siri kubwa.Kwa kuwa yeye ndiye aliyekuingiza katika jeshi la magereza na akakupangia katika gereza la Markubelo lazima angehojiwa sana kuhusu wewe na hivyo akafanya maamuzi ili kuzima kabisa jitihada zote za kujaribu kukutafuta.Dr Isaack alifanya maamuzi ya kujipiga risasi.Aliponieleza kuhusu suala hili sikumkatalia na nilikubaliana naye kwani jambo hili lingemuweka sehemu mbaya sana.Naomba rasmi nikuthibitishie kwamba Dr Isaack amefariki dunia”



    “Oh my God !! akasema Dastan na kufunika uso kwa viganja vya mikonohttp://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Maamuzi aliyoyafanya Dr Isaack ni ya kishujaa sana na ilibidi afanye vile ili kutupa sisi nafasi ya kusonga mbele.Kama asingefanya vile angekamatwa na kazi hii yote liyofanyika kwa muda mrefu ingekuwa bure.Hata hivyo nilimuahidi kwamba nitaitunza familia yake.Nitawasomesha watoto wake wote hadi pale wote watakapotimiza ndoto zao zote maishani kwani hilo ndilo hasa lilikuwa lengo la baba yao.Siku zote nitamkumbuka Dr Isaack kutokana na mchango wake mkubwa katika jambo hili.”akasema Carmelita na kunyamaza akamtazama Dastan ambaye alionekana kutaka kuzungumza jambo



    “Sikuwa nimepanga kumaliza kazi yangu kwa kusababisha maafa namna hii.Nilitegemea ningemaliza kazi yangu kimya kimya na kupotea kama upepo.Lakini haya yote yaliyotokea mwishoni mwa misheni yangu yamesababishwa na rais mstaafu wa Tanzania Dr Alfredo Kitwe” akasema Dastan



    “Amefanya nini huyu Dr Alfredo?akauliza Carmelita



    “Dr Alfredo Kitwe amefungwa kifungo cha maisha pale gerezani na kwa sasa ana miaka kumi pale gerezani na yuko chini ya uangalizi mkali sana.Kwa muda huu wote wa miaka kumi hajawahi kuonana na mtu yeyote wa familia yake na limewekwa zuio kutoka ngazi za juu kwamba asiruhusiwe kutembelewa na mtu yeyote yule.Kama haitoshi kuna mtu alikuwa amewekwa pale gerezani kwa lengo la kuchunguza maisha ya Dr Alfredo.Nilipofika pale nilijenga mazoea ya kwenda kumtembelea na kumjulia hali kwani nilimkuta akiwa anaumwa umwa japo hakuwa mgonjwa sana kama alivyo sasa hivi.Mwanzo haikuwa rahisi mimi kujenga ukaribu naye kwani hakuwa akitaka kuzungumza na mtu yeyote yule lakini baadae akanizoea na tukawa marafiki.Nilitumia nafasi yangu kama mkuu wa gereza kuhakikisha anapatiwa huduma nzuri za chakula na malazi kwani huduma nilizokuta anapatiwa hazikustahili kupatiwa mzee kama yule na tena mtu aliyewahi kuwa rais wa nchi.Hali yake ilipozidi kuwa mbaya nilituma taarifa makao makuu ili kuomba kibali mzee Dr Alfredo akapatiwe matibabu nje ya gereza lakini ombi hilo likakataliwa.Jana hiyo hiyo tukapokea majibu ya sampuli za vipimo zilizotumwa katika maabara ili kufahamu kinachomsumbua mzee Alfredo na majibu yanaonyesha kwamba mzee Alfredo anasumbuliwa na saratani ya uti wa mgongo na kwa hali aliyofikia hataweza kupona tena.Jana jioni nikaenda kumtembelea na kumpa taarifa hizo ndipo aliponiomba nimsaidie jambo moja muhimu kwake kabla hajafa.Alinipa kijikaratasi Fulani chenye ujumbe akaniambia nikifikishe kwa padre mmoja anaitwa Thadei.Nilifanikiwa kumpata huyo padre katika simu na kumtumia ujumbe ule wa Dr Alfredo kitwe” akanyamaza kidogo halafu akaendelea



    “Ni kawaida yangu kila siku jioni nimalizapo shughuli zangu kwenda baharini kuvua samaki.Nikiwa baharini nikasikia muungurumo wa boti na kwa kutumia kiona mbali nikaiona boti ikija upande wangu na ndani yake kulikuwa na watu wanne na mmoja wao alikuwa amebeba silaha.Nikajua ni majambazi hivyo nikajihami nikazama baharini na baada ya muda wale jamaa wakafika na kuanza kupekua boti yangu nikaibuka na kupambana nao nikawaua wote.Niliporejea gerezani nikaelekea nyumbani na mara tu nilipoingia ndani mwangu nikawekwa chini ya ulinzi na mmoja wa watu walioniweka chini ya ulinzi ni katibu wangu muhtasi.Kikubwa walichokuwa wanakihitaji ni kumfahamu mtu niliyempatia ujumbe ule alionipa mzee Dr Alfredo kitwe.Kwa bahati nzuri askari walipata taarifa za kilichokuwa kinaendelea pale kwangu na wakafika haraka wakawaua wale jamaa wote. Dr Isaack akanipigia simu akanitaka niondoke pale gerezani haraka sana kwani kazi yangu ilikuwa imekwisha. Hivyo ndivyo ilkvyotokea jana usiku.Hata hivyo kazi yangu tayari nilikwisha ikamilisha japo nilihitaji muda kidogo wa kufuatulia mambo Fulani Fulani madogo lakini kwa asilimia tisini na tisa pointi tisa kazi yangu imekamilika.Nasikitika sana kuhusu Dr Isaack.Sikujua kama nilikuwa nazungumza naye kwa mara ya mwisho.Amekuwa ni mtu mwema sana kwangu yule mzee na amenisaidia sana katika kuifanikisha kazi yangu.Siwezi kumsahau” akasema Dastan



    “Pole na vile vile hongera sana kwa kuikamilisha kazi yako japo imechukua muda mrefu. Ilifika mahala nikakata tamaa kwamba kazi ile imeshindikana kwani nilitaka mambo yaende haraka haraka lakini ni Dr Isack aliyekuwa akinipa moyo kwamba tuvumilie na tukupe nafasi ya kutosha kuweza kuimaliza kazi yako. Haya yaliyotokea mwishoni hayana umuhimu mkubwa sana kwetu na nitayam……”



    “Madam Carmelita samahani kwa kukukatisha lakini kilichotokea jana usiku si kitu cha kupuuzia.Yote haya yaliyotokea na kusababisha uhai wa Dr Isaack ukapotea yamesababishwa na ujumbe ule niliopewa na mzee Alfredo niupeleke kwa padre Thadei.Hii inaonyesha wazi kwamba kuna jambo ambalo viongozi walioko madarakani hawataki lijulikane na ndiyo maana wanafanya kila wawezalo ili kuhakikisha kwamba mzee Dr Alfredo haonani na mtu yeyote.Hata pale gerezani wanaoruhusiwa kuonana naye ni watu wachache tu.Kuna nguvu kubwa inatumika kuhakikisha kwamba Dr Alfredo haonani na mtu yeyote.Tujiulize swali dogo mzee yule ana kitu gani ambacho kinamfanya azuiliwe kuonana na mtu yeyote?Alifanya nini hadi akafungwa maisha gerezani?akauliza Dastan



    “Kuna mauaji makubwa yalitokea wakati wa utawala wake hivyo watawala wa sasa wakamfungulia mashtaka ya mauaji na akahukumiwa kifungo cha maisha.Tuliweke pembeni suala hili na tuzungumzie misheni yetu”akasema Carmelita



    “Madam Carmelita unafahamu chochote kuhusiana na Dr Alfredo kitwe? Unaifahamu familia yake ?akauliza Dastan



    “Ninachofahamu Dr Alfredo aliwahi kuwa rais wa Tanzania na sifahamu kuhusu familia yake kwani wakati wa utawala wake nilikuwa nje ya nchi.Kwa nini umeuliza?



    “Katika ujumbe alionipa nimpe padre Thadei ameelekeza umfikie Mariana.Nilimuuliza Mariana ni nani ili kama nitamkosa padre Thadei nimtafute Mariana na kumpa ujumbe huo moja kwa moja”



    “Alijibu nini? Carmelita akauliza



    “Alijibu kwamba siwezi kumfikia Mariana kwani ni hatari kubwa kwangu. Hakunieleza ni hatari ipi.Kuna kitu kinaniwasha kutaka kumfahamu huyu mzee kiundani Zaidi.Mauaji hayo yaliyofanyika yeye ndiye aliyatekeleza?



    Carmelita hakuonekana kupendezwa na maswali ya Dastan lakini akajibu



    “Inasemekena mauaji hayo yaliyofanyika chini ya amri yake.Ivan umekwisha msaidia vya kutosha huyo mzee kufikisha ujumbe mahala kunakotakiwa na kwa msaada huo uliomsaidia umetusababishia matatizo.Tuachane naye na tujielekeze katika masuala yanayotuhusu sisi.Ninataka kupata taarifa kamili ya misheni yako” akasema Carmelita



    “Kabla sijajibu chochote naamini yale yote tuliyokubaliana katika mkataba wangu nanyi yanazingatiwa” akasema Dastan na Carmelita akatabasamu



    “Familia yako inaishi maisha mazuri,nyumba nzuri,magari ya kifahari ya kutembelea,watoto wako mapacha wanasoma katika shule bora kabisa Marekani,kwa ujumla hawafahamu nini maana ya neno shida.Wanaishi kwa raha mustarehe wakiamini baba yao unafanya kazi katika kampuni ya mafuta Tanzania na ndiye anayewapatia kila wanachokihitaji.Tayari fedha yako yote tuliyokubaliana imeingizwa katika akaunti yako ya siri na hakuna ambacho hakijashughulikiwa.Wewe mwenyewe unazungumza na mkeo mara kwa mara amewahi kukuambia kwamba ana tatizo lolote?



    “Hapana”akajibu Dastan



    “Good.Huna sababu ya kuwa na wasi wasi kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa” akasema Peniela

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Bado kuna kitu kimoja ambacho nataka nikiweke sawa”



    “Kitu gani hicho?



    “Nimemaliza kazi yenu na sitaki kuendelea na kazi nyingine yoyote.Nataka kupumzika na familia yangu”



    “Usiwe na wasiwasi Ivan.Ulikuja Tanzania kwa kazi moja tu na kwa kuwa umeimaliza basi hakutakuwa na kazi nyingine.Nipe ripoti” akasema Carmelita akionekana kuwa na shauku sana ya kutaka kufahamu kile alichonacho Dastan



    “Mathew Wilibroad Mulumbi yuko hai na amefungwa katika gereza la siri ndani ya kisiwa cha Markubelo”



    “Oh my God ! akasema Carmelita kwa sauti ndogo



    “Katika kisiwa cha Markubelo kuna gereza la siri ambamo hufungwa watu maalum tu .Ni sehemu ya mateso makubwa na mauaji.Wanapaita jehanamu ya dunia.Nilifanya uchunguzi na kugundua kwamba gereza hilo la siri linashugulikiwa na ofisi maalum iliyo chini ya rais wa Tanzania .Gereza hili ni la siri mno na hata askari na wafungwa walioko pale kisiwani hawafahamu kama kuna gereza lingine la siri.”



    “Ivan naomba unieleze kuhusu gereza hilo kwa undani.Linatumika kuwafunga watu wa aina gani?



    “This is the killing place.Ni sehemu ambayo hutumika kuwapoteza watu ambao ni hatarishi kwa nchi au wale ambao rais ataamua kuwapoteza.Ukiingia katika gereza hili hutatoka tena.Hakuna aliyewahi kuingia ndani ya gereza hili akatoka hai.Kwa Mathew kuwa hai mpaka leo ni kwa sababu bado kuna mambo wanaendelea kumuhoji na wanaamini ipo siku atasema hivyo wanaogopa kumuua.Mpaka sasa hajawahi kutamka lolote na hilo ndilo linalomfanya aendelee kupumua hadi leo lakini hali yake inasikitisha sana.Gereza hilo limejaa mateso makubwa mno”



    “Uliwezaje kuingia ndani ya gereza hilo?Mathew ulifanikiwa kuonana naye ana kwa ana?



    “Mkuu wa gereza lazima ujulishwe kinachoendelea pale kisiwani lakini hurusiwi kuhoji chochote na unatahadharishwa kwamba siku utakapotoa siri ya kuhusu uwepo wa gereza hilo unauliwa.Nilianzisha mahusiano na mmoja wa vongozi wa gereza hilo niliyemfahamu kwa jina moja tu la Irene.Alinipenda sana na kupitia kwake nilifanikiwa kuonana na Mathew”



    “Huyu Irene bado unaendelea kuwasiliana naye? Akauliza Carmelita



    “Sina mawasiliano naye yoyote na sifahamu anaishi wapi.Nilikutana naye siku moja jioni wakati nikifanya mazoezi ya kuogelea baada ya kazi na akavutiwa na mazoezi yangu tukawa tunakutana mara kwa mara kufanya mazoezi tukawa na mahusiano na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kulifahamu vyema gereza hili mahala lilipo.Irene alinieleza mambo mengi kwani tayari alikwisha zama penzini.Niliyatumia vyema mahusiano hayo nikamchimba Irene na kufahamu mahala alipo Mathew na nikafanikiwa kuonana naye japo nilitumia muda mfupi sana kuzungumza naye,nilimueleza mimi ni nani na dhumuni la kwenda kuonana naye.Amechoka mno na kudhoofika.Baada ya kujieleza mimi ni nani akaniambia maneno machache”Ngusero bridge Arusha,nguzo ya tatu” Baada ya maneno hayo akanitaka niondoke haraka.Hayo ndiyo majibu ya operesheni hii iliyochukua miaka kadhaa” akasema Dastan na ukimya ukatawala eneo lile.Baada ya muda Carmelita akauliza



    “Ngusero bridge Arusha nguzo ya tatu.Is that all you got for all the years you’ve been there?



    “Yes Madam Carmelita.That’s all I got”



    “We knew Mathew was there na tulikutuma kumtafuta na kumchimba ilitufahamu mambo mengi kutoka kwake lakini unaniletea maneno sita tu na unadai umeimaliza kazi ?Unataka niamini kwamba maneno hayo sita yamechukua miaka kadhaa kuyapata na yamegharimu mamilioni ya fedha?Hiki ni kichekesho” akasema Carmelita na kucheka kidogo



    “Madam Carmelita unadhani ni jambo rahisi kufahamu kuhusu gereza hili la siri?Niliyatoa maisha yangu katika jambo hili.Hakuna mtu ambaye hahusiki aliyewahi kuingia ndani ya hilo gereza mimi ni wa kwanza.Hakuna aliyewahi kuonana naye Zaidi yangu.Maneno hayo sita aliyonieleza ambayo unayadharau na kusema ni kichekesho yana thamani kubwa Zaidi ya mamilioni unayojutia kuyatumia katika misheni hii.Majibu yote ambayo wewe na wenzako mnayatafuta yamo katika maneno hayo sita aliyoyasema Mathew” akasema Dastan.Carmelita akainamisha kichwa akawaza kwa takribani dakika tano halafu akasema



    “You’ll have to prove to me”



    “Prove what?akauliza Dastan



    “Nataka unihakikishie kwamba maneno hayo aliyoyasema Mathew yana maana na yanaweza kunipa majibu ninayoyatafuta”akasema Carmelita



    “Sijakuelewa madam Carmelita.Una maanisha nini?



    “Unakwenda Arusha”



    “What?



    “Ndiyo.Unakwenda Arusha mahala hapo aliposema Mathew na uone kuna nini”



    “No I’m not going to Arusha.Hayakuwa makubaliano yetu.Nimeifanya kazi yenu kama tulivyokubaliana na nimewaletea majibu.Ni juu yenu kutafuta kuna nini hapo mahala alipoelekeza Mathew”akasema Dastan



    “Ivan naomba nikuweke wazi kwamba hakuna yeyote atakayekwenda Arusha Zaidi yako.Utakwenda kaika daraja hilo aliloelekeza Mathew na kuangalia kuna kitu gani utakipata.Hapa ulipofika kazi yako haijakamilika.Ili kuikamilisha kazi yako unatakiwa uende Arusha katika hilo daraja ili tujue kuna nini”akasema Carmelita na Dastan akasimama



    “Madam Carmelita you are joking!!



    “It’s not a joke Ivan”



    “Yes it is a joke.Unawezaje kuniambia niende Arusha wakati unafahamu kuwa hivi sasa ninatafutwa kwa udi na uvumba?Taarifa zangu zimesambaa nchi nzima na polisi wananitafuta.All I need now is to go home.My mission is over!! You understand me Carmelita? Akasema Dastan kwa ukali



    “Ivan kwa sasa mimi ndiye mwenye kuamua na si wewe.Utakwenda Arusha na utakaporejea ndipo utarejea nyumbani”



    Dastan akawaza kwa uda halafu akauliza



    “Unadhani nitakwenda vipi Arusha wakati ninatafutwa?



    “Usiwe na wasiwasi.Utafika Arusha salama bila tatizo na utakaporejea hapa utaondoka kurejea nyumbani na sintakusumbua tena”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Ok fine I’ll go to Arusha but this is the last thing I’ll do to you.You understand me?akauliza Dastan



    “Good.Jiandae muda si mrefu tunaondokakuelekea Arusha” akasema Carmelita



    MWISHO WA MSIMU WA KWANZA



    ENDELEA KUFUATILIA MSIMU WA PILI



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog