Search This Blog

Sunday 20 November 2022

NJIA NYEMBAMBA (2) - 1

 





    IMEANDIKWA NA : STEVE MOLLEL



    *********************************************************************************



    Simulizi : Njia Nyembamba (2)

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    ILIPOISHIA





    “Ni kuhusu Guinea ama Sierra?” Kone aliuliza.

    “Ni kuhusu Sierra!” Akajibu Raisi. Hapo Kone akavutiwa zaidi. Ni kipi hicho Raisi wake alichomtolea Sierra na kumuitia pale haraka vile? Ni kipi hicho tena Raisi wake anachakusema kuhusu Sierra na si nchi yake, Guinea?



    Moyo wake ulianza tu kwenda mbio. Hakujua kwanini.



    “Kone, hili jambo ni serious sana. Na kama nilivyokuambia, ni siri sana. Hakuna kiongozi mwingine anayelijua hili isipokuwa waziri wa mambo ya nje tu.” Raisi akaweka kituo kwanza. “Kuna nchi huko ughaibuni, wanataka kuwezesha zoezi la kuiondoa Sierra madarakani.”



    Kone alihisi hilo jambo haliko sawa hata kabla Raisi hajaendelea.



    “Wamekuja na mapendekezo yao kwangu. Wao na sisi kuna mambo tunayoshea: wote kuna kitu tunahitaji ndani ya nchi ya Sierra Leone. Wamesema ya kwamba itakuwa rahisi sana kuiondoa serikali hiyo kwa kutumia mwamvuli wa utawala wa kimabavu ambao upo madarakani kwani halitasababisha maneno wala macho ya ndani kugundua nini ambacho kipo nyuma ya pazia.”

    Kukawa kimya kidogo.

    “Wewe Kone unaonaje hili kabla sijajitumbukiza mzima?”

    “Sisi kama Guinea tutafaidika vipi na huo mpango wao?” Kone aliuliza.

    “Wamesema ya kwamba kuna faida nyingi tutazipata mbali na ambazo wamezianisha.” Raisi akajibu. “Uhusiano baina yetu utaimarika, watatusaidia kiuchumi kwa kiasi kikubwa kwa misaada na mikopo yenye riba nafuu. Lakini pia tutapata yale ambayo tuliweka nayo maagano na Assessoko.”

    Kone alikuna kidevu chake akiwaza. Kichwa chake kilimpa ala za hatari. Alidadavua jambo hilo kwa sekunde kadhaa, akamtazama Raisi kwa macho ya uhakika.

    “Huu unaweza ukawa mtego hatari. Tatizo linakuja hatujui ni nini haswa malengo ya hao watu, hata kama wametuweka wazi baadhi. Endapo itagundulikana kama nasi tulikuwa pamoja nao, wanaweza wakatugeuka tukawa wahanga wakubwa. Lakini vilevile, tuna uhakika gani kama utayapata yale ambayo yalikuwa ndani ya maagano yetu? Hata pale watakapotugeuka, kumbuka hatutakuwa na mahala pa kushitaki.”

    Raisi alivuta kwanza pumzi akabinua mdomo wake. Alikuwa anawaza na kuwazua. Uso wake ulijikunja na macho yake ndani ya miwani yenye fremu nzito nyeusi yalikuwa yanazunguka huku na kule. Aliishia tu kushusha pumzi, akauliza:

    “Ila Kone ukiachana na hizo hatari, huoni kama hii ni njia nyepesi zaidi?”

    “Ila ni hatari zaidi,” akajibu Kone. “Ila kama unataka tu kulipa kisasi kwa Sierra, nakushauri uende na hiyo njia. Lakini kama unataka kupata kitu kutoka huko, nakushauri uende mwenyewe.”

    “Sawa. Basi tunakuwa tumebakiwa na chaguzi lako pekee. Natumai utalifanikisha hilo ndani ya juma moja. Endapo kama likishindikana kwa muda huo basi itanilazimu kwenda na chaguzi la nchi ya ughaibuni.”

    Walifikia makubaliano hayo. Kone alikabidhiwa pesa zaidi za kufanikisha mipango yake. Hakudumu sana hapo akaenenda nyumbani kwake baada ya kuagana na mke wa Raisi.

    Ilimchukua muda mfupi, akawa nyumbani kwake. Alionana na mkewe aliyemkaribisha kwa bashasha za mapenzi na kumkarimu chakula. Napo hakukaa muda mrefu, mwanaye akaja tokea shuleni. Alimkumbatia babaye na kumweleza namna alivyomkumbuka kabla hajaenda kula na kucheza.

    “Unakuwa bize sana, mimi na watoto tunakuhitaji pia.” Alilalama Fatma. Uso wake mpana uliokuwa ndani ya hijabu ulikuwa na sononeko. Tangu mumewe alipopewa kazi na Raisi amekuwa adimu sana nyumbani, na hata pale mara chache anapokuwepo basi hatokaa kwa muda kabla hajahepa. Jambo hilo lilimkosesha furaha Fatma, na hata kumpukutisha mwili kwa kukosa mahaba ya mumewe.

    “Unajua nini nafanya kwa sasa. Nimekuwa nikikuambia kila siku.” Alisema Kone. Sauti yake ilikuwa na kaukali ndaniye.

    “Mume wangu, najua nini unafanya na wala sihitaji kuambiwa tena. Lakini kumbuka kwamba familia ni kitu cha kwanza na si mali: nyumba, gari wala fedha!”

    Kone alisimama akavua shati lake. Alivua pia na suruali kisha akajilaza kitandani. Fatma alimjongea akalala pembeni. Hakutaka kumkwaza mumewe, alimpa tabasamu na kuweka kiganja chake mgongoni mwa mwanaume huyo.

    “Samahani kama nakukera, nakukosa mno. Natumai leo utakuwa na mimi kwa muda mrefu.”

    Macho yake yalionyesha upendo kwa ndani. Na haikumchukua muda mrefu Kone akauona upendo huo alioupokea kwa tabasamu mwanana.

    “Nitakuwepo na wewe mpenzi wangu.”

    Fatma alitabasamu akasaula nguo na kulala karibu na mumewe. Alimwelezea ni kwa namna gani alivyokuwa anamkosa akawa mpweke. Alimweleza maendeleo ya watoto na biashara zao. Wakati akifanya yote hayo mikono yake milaini ilikuwa inakanda hamu toka kwa mumewe. Kone alikuwa anarembua kwa raha: kwa namna kubwa alikuwa ‘amemisi’ huduma hizo.

    Lakini kama vile kitumbua mchangani, umoja huo ukavunjwa na muito ulioingia ndani ya simu ya Kone. Fatma alimtaka mumewe asipokee wala kusumbuka nayo lakini Kone hakuweza kuinyutia simu hiyo kwani alitumai inaweza kuwa ya muhimu sana. Alikuwa ni Rose anamtafuta, na alijikuta anatabasamu baada ya kuona jina hilo kiooni.

    “Amenitafuta.” Sauti ya Rose ilisema kwa ufupi.

    “Sawa, tutaonana baada ya muda mfupi,” akajibu Kone. Simu ilikatwa ikawekwa kando. Kone alimtazama mkewe akamkuta akiwa amefura, na akiwa anafanya jitihada za kuvaa hijabu yake.

    Alijaribu kumwelezea mkewe hali ilivyo lakini mwanamke huyo hakutaka kusikia chochote. Alichosema ni:

    “Nenda kwa Rose wako huyo.” Kisha akatoka ndani ya chumba isieleweke anaenda wapi.





    Muda wa usiku wa saa nne:



    THE GHOSTS wakiwa wamejipakia vema ndani ya gari, wamebebelea mabegi makubwa matupu na wamevalia nguo nyeusi, walishika njia kuelekea Rokel Barracks Ulsher akishikilia usukani. Kwa usiku mzima walikuwa wanapanga nini cha kufanya huko Barracks wakitumia ramani iliyochorwa vema na na Mou Farah. Walianisha mpango A, be na hata che. Walishajipanga wapi pa kuingilia na wapi pa kutokea. Wapi wapite na wapi wasipaguse. Kilichobakia ilikuwa ni kutenda tu.

    Baada ya dakika chache walifika karibu na eneo la tukio. Wanaume wote walishuka wakamwacha Ulsher ndani ya gari. Walikuwa wamebebelea bunduki ndogo na migongoni wakiwa na mabegi makubwa meusi. Wanaume hao waliposhuka Ulsher aligeuza chombo, akazima taa na injini kisha akatulia tuli sasa akiwa anangojea kupokea taarifa yoyote toka kwa wenzake.

    Amadu na wenzake walijongea karibu zaidi na Barracks. Wanaume hao walijigawa kila mtu akaenenda pande yake. Waliufikia ukuta wakapanda na kuingia ndani kwa uangalifu mkubwa. Kazi kubwa kwa wakati huo ilikuwa ni kukwepa taa kubwa ya mnara. Walifanikiwa kukwepa taa hiyo na kujiweka salama zaidi ndani ya kambi hiyo kubwa, Chui alimuua mwanajeshi aliyekuwa anaendesha taa hiyo kwa kumrushia kisu kilichomuangua na kumtuza chini. Wanajeshi watano nao waliokuwa zamu wakauwawa, mkono wa Amadu, Farah, Ussein na Mou ukihusika.

    Mpaka wanakutana mahali walipopanga ndani ya muda waliopanga, walikuwa tayari wameshawateketeza wanajeshi kumi huku kusiwe na kelele zozote. Kuwanyonga watu hao na kuwanyofoa uhai kwa kutumia visu ndiyo ilikuwa namna ya kusonga. Walifanya kwa upesi na yote hayo yalichukua chini ya dakika moja tu!

    Farah alitoa ishara kwa kutumia mikono. Wenzake walimtazama kwa umakini. Alipomaliza pasipo hata kutia neno, wakajigawa tena katika vijikundi. Mou alienda na Chui, Amadu alienda na Farah, na Ussein akaenda mwenyewe. Hatukujua wapi walielekea, tulikuja kustaajabu wakiwa mbele ya stoo ya silaha, tena tulijua uwepo wao baada ya kudondoka chini kwa mlinzi wa eneo hilo. Alikuwa tayari anavuja damu, kabla hajapiga kelele akiwa anaenda kuchukua kifo chake, Chui alimziba mdomo mpaka akaenda. Macho yake yalielekea juu akawa kimya.

    Wakati Chui akiwa anamalizana na mtu huyo, wenzake walikuwa tayari ndani wakipakuwa silaha. Walichukua za kutosha na kujaza mabegi. Lakini walipotoka ndani wapate kuondoka, mwanajeshi mmoja akawaona. Alikuwa ni mojawapo wa watu wa lindo. Salama yake kuwa hai mpaka muda ule, ilikuwa ni kukaa ndani ya kambi na si nje.

    Lakini uhai huo usidumu, ukapokonywa na risasi iliyotoka kwenye bunduki yenye kiwamba cha kumeza sauti. Alikuwa ni Amadu alimlenga. Risasi ilitoboa fuvu la mwanaume huyo na kuzama ndani. Bunduki yake aliyokuwa ameibebelea begani haikumsaidia kitu. Kwa namna tukio hilo lilivyochukua nafasi, hakupewa hata muda wa kusogeza kiungo. Alianguka chini kama mzigo. Sauti ya kishindo chake kilimshitua mwanajeshi mwingine upande mwingine, sasa ikawa wazi kuwa wakina Amadu walikuwa katika hatari ya kugundulikana.

    Yaani muda wowote!

    Walikwepa kwa kupita njia nyembamba ili wasionekane. Lakini hawakufanikiwa kuufikia ukuta, sauti ya king’ora ikawaka. Wanajeshi walifurumuka toka ndani ya makazi wakaanza kurandaranda huku na kule. Ndani ya muda mfupi waligundua mtu wa roll call alikuwa ameuwawa, mtu wa mnara alikuwa ameuwawa, mlinzi wa stoo alikuwa ameuwawa, na watu wa zamu walikuwa wameuwawa. Haraka wanajeshi walielekea kwenye stoo ya pili kudaka silaha kisha wakasambaa ndani ya kambi.

    Ila kama kuna kitu ambacho hawakuwa wanakijua ni kwamba, tayari THE GHOSTS walikuwa wamejiweka kwenye mpango be. Walikuwa wamejificha kwenye stoo hiyo hiyo ya pili wakijua fika hakuna atakayedhani watakuwa hapo. Na kweli, nani angeliwaza? Wanajeshi walifikiri wavamizi watakuwa wanahaha huku na kule kuchoropoka ndani ya kambi hiyo. Na basi huo ukawa mwanya kwa THE GHOSTS kutoka eneo hilo kwa wepesi na kudaka kuta. Walibebana wakarushiana nje. Amadu alimpa taarifa Ulsher juu ya hali hiyo kwa kubinya kitufe pembeni ya begi lake kikasafirisha taarifa mpaka kwa Ulsher kwa kulia tip tip, Ulsher akatia moto chombo na kuyoyoma.

    Baada tu ya kutua chini, THE GHOSTS walitoa vikopo vyeupe ndani ya begi lao wakawa wanamwaga mchanga wenye rangi ya njano huku wakikimbia kuelekea kusini mwa kambi. Mbwa wa wanajeshi waliwafuata, lakini baada ya kunusa mchanga ule, walidondoka chini wakafa! Wanajeshi hawakuwa na mwelekeo, sasa wakawa wanakimbia wasijue maadui wameelekea wapi.

    THE GHOSTS walifika mtoni, huko walikuwa tayari wamepanga magogo ambayo waliyatupia ndani ya maji ya mto wakaambaa nayo mpaka pale walipotimiza muda wa dakika kumi majini kisha wakatoka na kufuata barabara ambapo huko walimkuta Ulsher. Walikwea kwenye gari na kuondoka upesi.



    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Baada ya masaa kumi na mawili:





    “Amesemaje?” Aliuliza Kone. Alishindwa kuvumilia aketi kwanza ndiyo aongee. Hamu yake ya kuongea na Rose ilikuwa kubwa tangu pale alipopewa muda mchache sana na Raisi apate kutimiza malengo yao.

    “Kaa kwanza.” Rose alisema akitabasamu. Kone alivuta kiti akaketi. Macho yake yalikuwa yanamtazama Rose kwa kulowa na matamanio.

    “Amesema niende jioni hii. Atakuwa mwenyewe na ameniandalia bonge la party,” alisema Rose kwa tambo za kike.

    “Sasa hapo ndio pa kumaliza kazi, Rose,” alisema Kone. “Tusipoteze tena hii nafasi. Raisi ametupa muda mdogo sana.”

    “Njia si ile ile?”

    “Kama tulivyokubaliana yaani. Ile ile!”

    Walipeana habari hizo na sasa matumaini ya kumaliza walichokianzisha yakiwa makubwa zaidi. Waliagiza vinywaji baridi na chakula cha bei kali. Matabasamu yalituama usoni mwao. Wakiwa wanamaliza chakula chao hicho, mara ujumbe ukaingia kwenye simu ya Rose. Ulikuwa unatoka kwa Kessy, na ulisomeka:

    ‘Samahani, siwezi tena kuonana na wewe kwa leo kuna jambo limetukia’

    Rose aliachama mdomo kwa kushangazwa. Alimuonyesha Kone huo ujumbe, Kone akavunjika moyo. Alilalama kweli na hakujua nini kiliharibu tena hiyo sherehe. Ila baada ya muda mfupi kwenye mojawapo ya televisheni iliyokuwepo karibu, akapata kushuhudia taarifa ya habari: kambi ya jeshi imevamiwa na kuibiwa silaha!

    Alijikuta anatikisa kichwa chake akasonya.

    “Tutakuwa tunafanya kazi ya ubuyu kila siku. Tuwatafute hawa waasi kwanza!”









    ***





    ‘Samahani, siwezi tena kuonana na wewe kwa leo kuna jambo limetukia’



    Rose aliachama mdomo kwa kushangazwa. Alimuonyesha Kone huo ujumbe, Kone akavunjika moyo. Alilalama kweli na hakujua nini kiliharibu tena hiyo sherehe. Ila baada ya muda mfupi kwenye mojawapo ya televisheni iliyokuwepo karibu, akapata kushuhudia taarifa ya habari: kambi ya jeshi imevamiwa na kuibiwa silaha!



    Alijikuta anatikisa kichwa chake akasonya.



    “Tutakuwa tunafanya kazi ya ubuyu kila siku. Tuwatafute hawa waasi kwanza!”



    Hilo ndilo lilikuwa amuzi la busara kwa muda huo, kuwatafuta THE GHOSTS. Kone alishindwa kabisa kula wala kunywa akiwa hapo. Hakudumu tena muda mrefu kabla hajaagana na Rose kwa kumpatia kiasi fulani cha pesa kisha akaondoka zake kwenda kuweka mipango thabiti ya kuwapata watu anaowataka.



    Kichwa chake kiliamini ya kwamba akiwapata hao watu itakuwa njia rahisi na fupi kwenye kutimiza malengo huku ikiacha mikono yao safi toka kwenye umwagaji wa damu.



    Kazi yao wao itakuwa ni kuwapa THE GHOSTS silaha na pesa wauawane wana Sierra wenyewe kwa wenyewe, huku wao wakikaa pembeni na kutazama.



    Kuna kazi gani nyepesi kama hiyo kwenye kuteka nchi?



    Mawazo yake hayo yalimnyima kabisa fursa ya kumuwaza mkewe wala familia yake. Kila taswira ya familia yake ilipokuja kichwani alijipa ahueni ya kwamba amewaachia pesa ya kutosha, hivyo hakuna cha kuhofia. Yeye kama baba tayari ameshatimiza majukumu yake kwahiyo hana lawama za kutupiwa.



    Pasipo kufanya hivyo angelikosa usingizi kwasababu nafsi yake ilikuwa inamshutumu kila mara.







    ***









    Rockel Barracks, wasaa wa alasiri.





    Umati wa wanajeshi wa Sierra Leone ulikuwa umekusanyika mbele ya kiongozi wao mkuu, bwana Kessy. Kulikuwa ni tulivu mno na wanajeshi walikuwa wamejipanga kwenye mistari iliyonyooka huku wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wa hali ya juu.



    Kessy alikuwa anatembea kwenda mbele na kurudi nyuma akiwa ameshikilia bunduki ndogo mkono wake wa kulia. Sura yake ilikuwa nyeusi zaidi na iliyokunjamana.



    Alikuwa amevalia gwanda za kijeshi yenye kila aina ya cheo. Japokuwa jua lilikuwa limepoteza nguvu yake, lakini bado lilitosha kufanya vyeo hivyo ving’ae na kumetameta kwenye nguo hiyo maridadi.



    Kila mtu hapo kiwanjani alikuwa anafahamu ya kwamba Kessy alikuwa amekasirika. Hata kwa mtoto mdogo angelijua hilo. Hakutaka mtu yeyote amsogelee wala kumuongelesha.



    Hakutaka mtu yeyote asimame hata mbele yake. Alikuwa anatazama chini akisaga meno, akienda mbele tu na kurudi nyuma, tendo ambalo alikuwa amelifanya kwa muda wa dakika kumi na tano sasa pasipo kukoma.



    “Naona mmeshindwa kazi na hamna umuhimu wowote kwangu wala kwa taifa,” alisema kana kwamba hakutaka mtu yeyote amsikie, ila ghafla aligeukia umati wa wanajeshi akapaza sauti:



    “Nataka wote waliokuwa zamu ya ulinzi waje hapa mbele!”



    Walijongea mbele watu wanne tu, wengine wote walikuwa marehemu kwa kuuwawa siku ya tukio la uvamizi.



    Kessy aliwatazama watu hao akibinua mdomo wake. Macho yake yalionyesha hasira iliyochemka ndani yake.



    Hakuchukua hata muda wa kufikiria akanyanyua mkono wake uliobebelea silaha na kuwaua wote hao wanne kwa kupasua vichwa vyao na risasi.



    “Hii ndiyo dawa ya wazembe!” Alifoka. “Inawezekanaje watu ambao hawafiki hata kumi kwa idadi, wanaingia eneo lenye wanajeshi kiasi hiki wanaiba silaha na kutoka salama?”



    Hakuna aliyejibu, na pengine walidhani jibu halikuhitajika.



    Kessy alimuita mbele meja wa kambi, akamuuliza swali hilo akitaka majibu ndani ya dakika moja.



    “Nataka unielezee, ni kwa namna gani watu wanaingia humu ndani na kuiba silaha pasipo kukamatwa.”



    Meja hakuwa na majibu. Mwili wake ulikuwa unatetemeka kwakuwa alifahamu fika kifo kipo karibu naye. Na kweli hakuchukua muda mrefu akatobolewa fuvu la kichwa na risasi moto.



    “Si unaona?” Kessy alifyumu. “Ni ushenzi na uzembe!”



    Hakuishia hapo kwa meja na waliohusika na zamu, akaendelea kuua na kuua akihusisha wale walio chini ya meja, wasaidizi wake na wasaidizi wake.



    Alitengeneza dimbwi la damu akijaza maiti. Zoezi hilo la mauaji lilikuja kukoma pale tu Talib alipomtaka Kessy asifanye zaidi.



    “Isingelikuwa nimewaua hawa washenzi, ningelianza na wewe!” Kessy alimwambia Talib akiwa amekunja uso.



    “Nikisikia hao washenzi wamefanya tukio lingine tena kabla hujawakamata, kifo chako kitakuwa malipo!”



    Aliposema hayo alijiweka ndani ya gari lake, akaondoka akisindikizwa na msafara wenye magari ya kifahari.



    Alichomoa simu yake toka mfukoni akampigia mwanaume mmoja aliyemuagiza amletee wanawake wa kutosha Ikulu usiku huo. Baada ya hayo maagizo akaweka simu pembeni akiendelea kuwaza na kuwazua.



    Usiku wake ulijaa anasa kwa kunywa na kufanya mapenzi na wanawake zaidi ya watatu kwa lengo la kutafuta pumziko toka kwenye msongo wa mawazo na hasira alizokuwa nazo.



    Harufu ya pombe ilitapakaa ndani ya chumba chake kikubwa chenye samani za kila aina. Pombe ghali zilinyweka na nyama za kuokwa zililiwa mpaka basi.



    Alichoka mno, kichwa chake kilichojaa pombe na tumbo lake lililojaa nyama vilimfanya alale kama mfu. Hakuamka mpaka pale alipokuja kuamshwa apokee simu yake toka Liberia.



    Alikuwa ni kiongozi wa kundi la Le tueurs, Al Saed, akiwa anamtafuta. Alianza kumtafuta tokea jana usiku lakini hakuwa anapatikana.



    Kuna habari nzuri alikuwa anataka kumfikishia, habari ambayo hakuweza kuvumilia kukaa nayo kwa muda mrefu.



    “Umetazama televisheni yako?” Al Saed aliuliza.

    “Hapana.” Kessy akajibu kiuchovu akijaribu kuketi. Alikuwa yu mwenyewe chumbani wanawake wakiwa tayari wameondoka.



    Yalikuwa yamebakia mabaki ya chupa za vileo na foili za nyama ambayo muda si mrefu yangekuja kuondolewa na mfanyakazi wa ndani.



    “Unasubiri nini? Tizama televisheni yako.”



    Kessy aliwasha televisheni yake akaona taarifa ya habari ikionyesha yale yaliyotukia Liberia. Kundi la Le tueurs lilikuwa limeshinda vita na limetwaa dola ya nchi hiyo.



    Japokuwa watu wengi mno walikuwa wamekufa, Kessy hakuliona hilo zaidi ya ushindi wa kundi rafiki kwake. Alijikuta anatabasamu kwa kuanza siku na habari njema kama hiyo.



    “Muda si mrefu nitakutafuta,” alisema Al Saed, “Unafahamu hatuna uzoefu na mambo haya ya utawala. Tunatumai utatusaidia kwa namna kubwa.”



    Kessy aliwakubalia na aliona hiyo ni fursa nzuri ya kufanya muungano wao uwe imara. Lakini zaidi muungano huo utawafanya waweze kusaidiana kutatua matatizo yao.



    Alipokata simu, aliipatia supu kali kabla hajajiweka kwenye kibaraza cha Ikulu ambapo hapo aliendelea kutafakari juu ya tukio la kuvamiwa kwa kambi na kuibwa kwa silaha.



    Alimpigia simu Talib aje Ikulu, baada ya mfupi waziri huyo akawasili. Aliletwa na gari jeusi Lamborghini.



    “Kuna kitu wanataka kukifanya,” alisema Kessy. “Ni wazi hizo silaha walizoiba zitaenda kutumika kuunda kikundi, na mawazo yangu yananambia watakuwa wana kambi msituni ndio maana hatuwapati tuwatafutapo.”



    Walikubaliana kwenye hilo wazo. Silaha zilizokombwa zitakuwa kwenye matumizi muda si mrefu, na hao wezi watakuwa wanajiimarisha kidogokidogo huko misituni wakilenga kuipindua serikali. Hivyo hatua za haraka inabidi zichukuliwe.



    “Tuma na usambaze vikosi vya jeshi kwenye misitu yote. Wahakikishe hakuna watu huko wakiwa wanafanya lolote!” Aliamuru Kessy, “Kama tukipata uhakika hakuna watu huko basi itakuwa rahisi kuwapata kwenye makazi ya watu.”



    Talib alichukua amri hizo tayari kwenda kuzitekeleza. Lakini kabla hajaondoka, Kessy alimkumbusha alichomwambia jana:



    “Kama watu hao wakifanya tukio lolote kabla hujawakamata, basi uhai wako ndio utakuwa malipo.”



    Talib alitikisa kichwa na kuondoka.



    Ndani ya siku tatu vikosi mbalimbali vya wanajeshi vilisambazwa misituni kwa siri. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kutafuta watu na kuwamaliza.



    Waliambatana na silaha nzito na nyepesi. Walitembea huku na huko wakihakikisha hakuna wanachokiacha.



    Laiti kama wangelijua THE GHOSTS walishafahamu hayo mawazo basi wasingelihangaika. Watuhumiwa wenyewe walikuwa wametulia ndani ya nyumba yao kubwa yenye uzio mrefu wakiwa wamerilaksi.



    Walikuwa wamelenga kutofanya lolote kwa muda wa majuma kadhaa kuhakikisha kwanza usalama umetulia ndipo watayafichua makucha yao.



    Hivyo basi, wanajeshi wa Sierra walizunguka misitu yote kwa majuma matatu pasipo kupata chochote kitu.





    Jambo hilo likamnyima raha Kessy, lakini zaidi Talib ambaye roho yake ilikuwa mkononi akiomba lisitokee lolote ili aendelee kuwa na pumzi yake.



    Siku moja ndani ya juma la mwisho la tatu tangu oparesheni ya kutafuta misituni ianze, Kessy alipokea ugeni toka Liberia.



    Alikuwa ni Al Saed akija kuomba ushauri na muongozo toka kwa mwenzake huyo. Tafrija kubwa iliandaliwa kumkarimu huyo kiongozi, watu wakanywa na kula.



    Baada ya tafrija hiyo fupi, viongozi hao, Kessy na Al Saed, walikaa faragha kupeana mawili matatu.



    Ni mambo matatu makubwa ambayo Kessy alimshauri mwenzake: kwanza kutoruhusu demokrasia nchini kwake maana inachochea chuki kwenye mioyo na wananchi; pili, kuminya wizara na kupunguza uwingi wa viongozi ili pesa zisitapanywe; tatu, awe mkali ili kuwatisha na kujiweka salama dhidi ya maadui wake.



    “Kama ukiwa lelemama, litatokea kundi lingine kama lako kudai madaraka.”



    Hilo lilikuwa nyeti sana. Hakuna aliyetaka kupoteza madaraka ilhali ameyasotea kwa muda mrefu hivyo. Lakini pia Kessy hakusita kumweleza mwenzake juu ya yale yanayoendelea ndani ya nchi yake. Jinsi gani anavyosumbuliwa na vijana aliowalelea.



    “Kama unataka msaada wa aina yoyote, tupo tayari,” alisema Al Saed. “Muda wowote siku yoyote nipo tayari kukusaidia.”



    Hilo likampa faraja Kessy. Alitabasamu akatikisa kichwa na kusema:



    “Bado hawajanishinda kabisa. Natumai nitawamudu, lakini wakinipanda kichwani basi sitajiuliza mara mbili kukuomba msaada.”



    Wakaendelea na kuganga yajayo.



    “Nadhani itakuwa vema na baadae tutakapokuja kukaa vizuri, tufikirie kujipanua zaidi,” alishauri Kessy. Kwa Al Saed hilo likawa na ukakasi.



    “Unadhani itakuwa rahisi?” Aliuliza.

    “Hakuna linaloshindikana. Tukiwa pamoja hakuna atakayetuzuia,” aliamini Kessy. “Na tena tutaanza na Guinea.” Akaongezea.



    Lakini hala hala chunga jicho na kidole, walishasema washenga na wahenga.



    ***





    Wakati majuma hayo matatu yakiwa yanayoyoma wanajeshi wakiwa msituni, Kwa Kone yaliyoyoma akiwa mtaani kuwatafuta THE GHOSTS. Hakulala usingizi ukaja; alizunguka kila kona ya jiji la Freetown; aliulizia karibia kila mtu akigawa pesa kwa yeyote aliyemsaidia.



    Mchana akiwa mtaani, usiku alikuwa kwenye maklabu na madisko bado kusaka.



    Majuma matatu yalimuishia akisaka na huku akimuomba Raisi wake aendelee kumpatia muda zaidi. Wakati juma lijalo la nne likiwa katikati, juhudi zake zikazaa matunda.



    Ukiwa ni muda wa mchana, gari lake lilisimama mbele ya nyumba yenye ukuta mrefu rangi ya krimu. Alikaa hapo kwa muda wa masaa pasipo kuona dalili yoyote ya mtu. Alichoka kungoja akaamua atoke kwenye gari na kuendea geti kugonga.



    Mlinzi alifungua kidirisha cha geti akamuuliza shida yake. Aliposema ni kuonana na wenyeji, hakuruhusiwa kuingia ndani kwa madai kwamba anaowatafuta hawaishi hapo.



    Aliendelea kusubiria nje ya geti kama atamuona mtu yeyote akitoka nje, lakini hakuona kitu!



    Hali hiyo iliendelea kutokea kwa takribani siku nne asione yoyote kutoka nje ya geti. Alipoenda tena kugonga geti siku hiyo ya nne, aliruhusiwa kuingia ndani.



    Kwa siku zote hizo alizokuwa maeneo hayo ya karibu alikuwa anaonekana pasipo kujua. Kamera zilizokuwa getini zilimsoma kwanzia alipokuwa anakuja mpaka anaondoka. Mpaka anakaribishwa ndani, tayari THE GHOSTS walikuwa wamejidhihirishia usalama.



    Kone aliketi sebuleni pasipo kuona mtu yeyote. Baada ya dakika kama tatu ndio THE GHOSTS wakatoka ndani na kuungana naye sebuleni. Kone alijitambulisha kwa watu hao na kisha akaeleza namna alivyohangaika kuwatafuta kwa muda mrefu.



    Alieleza adhma yake iliyomleta pale, ya kwamba anahitaji kuwasaidia watu hao kushika madaraka ya Sierra Leone.



    Kwa kupitia nchi yake, Guinea, atawapatia silaha wanazohitaji, wanajeshi na pesa pia. Lakini yote hayo yakiwa kwenye makubaliano.



    “Makubaliano yapi?” Aliuliza Amadu.



    Kone akaeleza juu ya makubaliano yaliyowekwa baina ya marehemu Assessoko na Raisi wa Guinea hapo awali, ambayo mwishowe yalikuja kuvunjwa na Kessy.



    Amadu na wenzake wakamsikiliza kwa umakini. Alipomaliza kunena, wakamtaka mguinea huyo awape muda wa kufikiria zaidi.



    “Tutakutafuta baada ya kujadiliana.”



    Kone akaondoka. Alimpasha taarifa Raisi wake juu ya maongezi yake na THE GHOSTS, na namna alivyojawa na matumaini.



    Alitumai kabisa atazishinda nyoyo za wanakikundi kile na alimfanya Raisi wake aamini vivyo, lakini ikawa kinyume kwa namna moja ama nyingine.



    Ilipita juma moja pasipo majibu. Alirudi nyumbani kwa THE GHOSTS lakini hakuwakuta tena pale, THE GHOSTS walikuwa wameshapotea! Na hakuwa na njia yoyote ya kuwapata tena.



    Alichoka pale alipokumbuka ni kwa ugumu gani alivyowapata watu hao na kwa wepesi gani walivyopotea mbele ya macho yake.



    Aliamua kurudi Guinea kupumzika kwanza na familia yake. Mkewe, Fatma, akafurahi sana kumuona baada ya majuma kedekede. Hasira za mwanamke huyo zilikoma japokuwa zilimtesa kwa muda mrefu.



    Alimkubatia mumewe na kumkaribisha ndani. Kone alivua nguo akala na kujiweka kitandani.



    Ikiwa ni usiku, na Fatma anataka kukata kiu yake ya mwili kwa shoka, simu ya Kone inaita. Ilikuwa ni namba mpya. Kone alipokea simu hiyo akaiweka sikioni.



    “Tumejadili, na tumeafikiana kutoungana na upande wowote.” Sauti nzito ya Amadu ilivuma simuni kisha simu ikakata.





    Kone alishusha pumzi ndefu akatikisa kichwa chake. Mood yote ya tendo ya kula apple la Adamu ilikata.





    Kichwa chake kilitingwa na mawazo mzito juu ya THE GHOSTS na Raisi wake. Aliona sasa mambo yanazidi kuwa magumu na yu njia panda ndefu. Ingawa mkewe alijitahidi kwa udi na vumba kupandisha hisia zake, jogoo alikuwa likizo na aligoma kabisa kurudi kibaruani





    ***











    Kone alishusha pumzi ndefu akatikisa kichwa chake. Mood yote ya tendo ya kula apple la Adamu ilikata. Kichwa chake kilitingwa na mawazo mzito juu ya THE GHOSTS na Raisi wake.





    Aliona sasa mambo yanazidi kuwa magumu na yu njia panda ndefu. Ingawa mkewe alijitahidi kwa udi na vumba kupandisha hisia zake, jogoo wake alikuwa likizo na aligoma kabisa kurudi kibaruani.





    Fatma anakwazika sana na jambo hilo. Atakaa na kiu yake hiyo mpaka lini na ilhali analala na mwanaume kitanda kimoja? Kwa namna moja alijiona aidha hampendezi mume wake, labda havutii na amepoteza uwezo wa kumsisimua laaziz wake.



    Alisononeka na nafsiye. Mume wake alijitahidi kupooza makaa yake ya moto lakini hakufanikiwa abadani.http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    “Naomba unirejeshe nyumbani kwetu, Kone,” alisema na sauti ya juu.



    “Kwenu kufanya nini Fatma?” Kone akauliza kwa sauti ya chini. Sauti yake ilikuwa imepooza na uso wake ulionyesha kweli ameguswa na kughafirika kwa mke wake.



    “Kwetu kufanya nini?” Fatma aling’aka. “Hivi mie nimekuwa dada yako, sio?”



    “Dada yangu kivipi?”



    “Usijifanye mtoto, Kone. Kama haunipi haki yangu ya ndoa, ni bora nikaondoka niende kwetu. Kuna haja gani ya kukaa na mwanaume asiyenigusa wala asiye na hamu na mimi?”



    “Lakini Fatma mama unaelewa ni hali …”



    “Sielewi chochote, Kone. Na usidhani kama nitaelewa. Nimesema hivi, kesho nipeleke kwetu, la sivyo unipe haki yangu usiku huu mpaka n’tosheke.”



    “Sawa. Nitakupa mke wangu. Hakuna haja ya kuzozana mpaka watoto huko wasikie.”



    Kone alijitahidi kuvuta hisia ili apate kumhudumia mke wake, Fatma, lakini akashindwa. Uume haukupanda kabisa. Alijitahidi kumpapasapapasa mkewe lakini bado haikuleta mabadiliko. Hakuweza!



    Fatma aliachana na mume wake huyo akageukia upande mwingine pasipo kuongea neno lolote. Alikuwa amevimba kwa hasira. Mwili wake ulikuwa una joto, kiu na haja lakini zilishindwa kutolewa.



    Alidondosha chozi akisaga meno yake. Aliyafumba macho yake kuutafuta usingizi lakini ikamchukua muda mrefu kuupata.



    Lakini kwa upande wa Kone alilala tu upesi. Sauti yake ya kukoroma ilimfikia Fatma masikioni na kumshangaza mwanamke huyo ya kwamba mume amelala haraka vile pasipo kujutia alichotoka kufanya.



    Fatma aliishia kusonya na kuuminya mto alioulalia. Naye Mungu asimtupe, akampuzisha toka kwenye maumivu aliyokuwa nayo kwa kumpatia usingizi mzito. Alilala akikoroma kiwepesi.



    Masaa yalijongea zaidi ndani ya usiku. Kichwa cha Kone bado kilirejelea mawazo ya kazi yake na hivyo basi ndani ya muda mfupi akaanza kuota mambo ya kazini kwake.



    Alijiona yu ndani ya sebuleni kubwa iliyojazwa na sofa zenye nyama, hapo alikuwa pamoja na THE GHOSTS wakiwa wanateta mawili matatu kuhusu misheni yao ya kuupiku utawala wa Sierra Leone.



    Ilikuwa ni wakati wa asubuhi na hivyo kukawa na vikombe vya kahawa mezani basi wakawa wakiteta huku wanatia kinywaji hicho mwilini. Maongezi yalikuwa ya manafanikio makubwa na yaliishia kwa kupeana mikono ya pongezi pia ikiashiria kwamba wapo pamoja.



    Ila Pasipo kujua wakati akiwa ndotoni, Kone alikuwa anaongea kana kwamba ni kweli yupo katika mazingira hayo ya sebuleni. Maneno yake yalimfanya mkewe, bi Fatma, aamke kumtazama na kumsikiliza mume wake.



    Na pasipo kumshitua mwanaume huyo, Fatma alisikiliza mpaka mwisho kisha akaendelea na usingizi wake.



    Asubuhi na mapema Kone alipokuja kuamka, hakumkuta mwanamke kitandani. Alikuwa tayari ameshasomba nguoze na kuondoka. Alikuwa tayari ameelekea nyumbani kwao.



    Kone aliamka kurupu akapepesa nyumba nzima asione mtu. Hata watoto hawakuwepo. Alichanganyikiwa na hakujua cha kufanya kwa dakika kadhaa kabla hajaamua kupiga simu ya mkewe. Simu iliita lakini haikupokelewa. Mwishowe alichoka akashika tama.



    Alilaza kichwa chake sofani na mara akakumbuka jambo – kuwapigia simu THE GHOSTS! Haraka alitafuta ile namba iliyompigia jana yake usiku, akaiita na kuiweka simu sikioni.



    Simu haikupokelewa. Na baada ya muda mfupi ikawa haipatikani!



    Kichomi.





    ****







    Muda wa kukaa kimya ulikuwa umetosha, kwahiyo sasa THE GHOSTS walikuwa tafakurini kipi kifuate katika misheni yao. Iliwalazimu wawe waangalifu sana na hatua zao zisiache nyayo za kumwezesha adui wao kuwapata kwa urahisi.



    Walighani kadhaa ya kufanya ila kati ya hayo zito lililochomoza ni kuongeza kwanza nguvu ya kundi.



    Sauti ndogo ya televisheni iliyokuwa hapo sebuleni haikuwafanya wasisikizane. Hakuna aliyekuwa anatizama televisheni hiyo hivyo kwa muda ilikuwa pweke ikitafuta mteja wakuiunga mkono.



    Idadi ya watu sita wa THE GHOSTS kweli ilikuwa ndogo ukilinganisha na kazi kubwa waliyonayo mbele. Walihitaji watu zaidi. Lakini watu ambao wapo tayari kupambana kwa namna yoyote ile.



    Watu wenye nia ya kweli na wapo tayari kutoa sadaka uhai wao ili kuikomboa nchi yao.



    Hilo lilikuwa jema, ila shida kubwa ilikuja kwamba ni kwa namna gani watu hao watafunga vinywa vyao na kupanua vifua vyao kwa kutunza siri?



    Jambo la kutafuta watu usiowajua ni hatari maana halina uhakika mkubwa wa kufuata yale mliyokubaliana, pia pana uzito na uweusi kwenye kuchambua; utajuaje wenye dhamira ya kweli na waliotumwa humo miongoni?



    Hapo palikuwa pagumu sana. Na palifanya wengine waone si mpango sahihi.



    “Serikali inaweza kutupata kwa urahisi endapo tukifanya hivyo,” alisema Farah.



    “Ni kweli,” Mou akaunga mkono, pia akafuatiwa na Ussein na Chui.



    “Wewe unasemaje?” Amadu aliuliza akimtazama Ulsher. Wote walikuwa kimya wakimtazama mwanamke huyo mwenye uso wa utulivu. Walikuwa wanangojea jibu kwa hamu pana, macho yao yalionyesha hivyo.



    “Tunahitaji watu zaidi,” sauti ya Ulsher ikavuma juu ya sauti ya televisheni. Alienda kinyume na wenzake. Amadu alijikuta anatabasamu kana kwamba alikuwa anategemea jibu hilo.



    “Hapana, siungi mkono!” Alisema Chui akitikisa kichwa.



    “Tazama kule.” Ulsher akanyooshea kidole kwenye televisheni. Wote walitazama wakakuta taarifa ya habari ya CNN ikimuonyesha Al Saed, kiongozi wa kundi la Le tueurs la Liberia akiwa anatoa hotuba ya kwanza rasmi tangu ajiteue kuwa kiongozi wa nchi hiyo iliyopokwa kimabavu.



    Chini ya kioo cha televisheni kulikuwa kuna maandishi meusi makubwa na madogo yakiwa ni machache mazito yaliyotoholewa toka kwenye hotuba husika. Mosi, nchi ya Liberia imekata mahusiano rasmi na nchi za Ulaya na Marekani, pili: hakutaruhusiwa shughuli zozote za kidemokrasia nchini, tatu na mwisho; anatazamia siku za usoni kuonana na rafikiye, bwana Kessy, wapate kuunda umoja wao utakaokuza uchumi wa nchi zao.



    Kutokana na hicho alichoona, Ulsher aliamini wanahitaji watu zaidi kwani vita ni kubwa na adui hatokuwa mmoja. Hoja yake ikawa nzito masikioni mwa wenzake wasisite kukubali, ila sasa wakarejea kulekule kwenye mjadala wa mwazoni ambao kwa sasa Amadu aliomba akabidhiwe yeye hilo fukuto.



    “Nadhani nitatafuta njia ya kulikwepa hilo,” alisema Amadu kwa kujiamini.



    Baada ya masaa kumi na nne;



    Ilikuwa ni usiku wa saa sita. Jiji la Freetown lilikuwa limepoa kwa kuwa na magari machache barabarani. Mataa yalikuwa yanawaka huku na kule, upepo nao wa bahari ya Atlantiki ukipuliza kwa mbali.



    Gari moja, Suzuki Vitara yenye rangi bluu nyeusi, ilipunguza mwendo lamini na kukunja kona ya kushoto kuingia katikati ya mitaa ya Freetown. Ndani ya gari hilo alikuwamo mwanaume mmoja; Amadu. Mkono wake wa kulia uliojaza ulikuwa umekamatia usukani. Alishusha vioo vya mbele vya gari akawa anaangaza kandokando mwa barabara nyembamba za katikati ya jiji.



    Kuna mtu alikuwa anamtafuta. Mwendo wake wa polepole na macho yake yaliyokuwa yanaangaza yalikuwa shahidi wa hilo.



    Alizunguka kwa muda wa dakika kama kumi na tano akikaguakagua nyuso za wazururaji pasipo kupata chochote, lakini hakuchoka. Alisemea moyoni mara kwa mara:



    “Lazima nimpate … lazima nimp …”



    Alikata kona kama tano hivi akaona wanaume wawili wakiwa wanapigana. Mwanaume mmoja alikuwa amejaza mwili kwa mazoezi; tisheti nyeusi aliyokuwa ameivaa ilikuwa imembana haswa; kichwa chake kilikuwa kimejazwa rasta nyeusi ndefu kiasi. Aliyekuwa anapigana naye alikuwa yu mwembamba ila mrefu; tisheti lake kubwa rangi ya zambarau lilikuwa linampwerepweta; hata suruali yake alikuwa kaikabia kiunoni na kamba ya viatu.



    Kwa haraka Amadu alimtambua mwanaume yule mwembamba ndiye anayemtafuta. Alikuwa ni yule mwanaume mkabaji aliyewahi kumharibia zoezi lake la ukabaji huko nyuma.



    Alikuwa ni yule mkabaji aliyemwambia Amadu anafanya dhambi hiyo ili aweze kugharamia matibabu ya mama yake aliyejawa na maji kwenye figo.



    Amadu alitumai atamkuta kijana huyo mtaani, na ni kweli alikuwa sahihi. Aliweka gari pembeni akachomoa funguo na kutoka ndani kufuata eneo la mpambano.



    Mwanaume yule mwenye rasta alimtupia mwenzake chini kama kiroba cha magimbi alafu akamtazama Amadu kwa macho yaliyojaa shari.



    “Naweza nikakusaidia?” Aliuliza.



    “Ndio. Namuhitaji huyu kijana,” alijibu Amadu akimnyanyua mwanaume yule aliyetupiwa chini.



    “Hauendi naye popote mpaka pale nitakapomalizana naye!” Alihororoja Rasta.



    “Kwakuwa wewe ni nani?” Aliuliza Amadu. Alimsogeza nyuma kijana yule aliyemkomboa kisha akamsogelea Rasi.



    Rasta alifanya makosa makubwa sana kurusha ngumi. Amadu aliikwepa alafu akamkandika Rasta kichwa kizito kilichompasua pembeni ya jicho lake la kulia na kumvujisha damu.



    Rasta aliugulia maumivu yake kwa sekunde kadhaa kabla tena hajaamua kurusha turufu yake kwa ngumi za mfululizo.



    Amadu alizikwepa ngumi hizo kama mtu afanyaye mchezo kisha akakamata mkono wa Rasta na kuupeleka usoni mwa mwanaume huyo kwanguvu. Ukakita puani na kumvujisha damu, alafu akasindikizwa na teke la haja lililomnyanyua juu na kumtupia chini kwa kishindo.



    Amadu aliondoka na yule mwanaume aliyemtwaa kuendea gari na kutoka eneo lile.



    “Naomba unisamehe, braza. Sitoiba tena!” Alisema mwanaume yule aliyekuwa na Amadu garini.



    “Ina maana tokea siku ile hujaacha kuiba?” Aliuliza Amadu.



    “Nimeacha.”



    “Acha kuniongopea.”



    Kijana yule akatazama chini.



    “Siwezi kuacha braza. Sina namna nyingine ya kupata kipato cha kutunza wadogo zangu.”



    “Mama yako anaendeleaje?”



    Mara kijana yule akabubujikwa na machozi.



    “Amekufa,” alijibu. “Wiki mbili zilizopita baada ya kushindikana kufanyiwa upasuaji.”



    “Pole sana.”



    Kimya.



    “Nataka nikupe nafasi ya kubadilisha nchi hii. Upo tayari?”



    Kijana alisita. Akili yake ilimkumbusha picha za Amadu zilizobandikwa jiji zima la Freetown ya kwamba anatafutwa. Kichwani alichambua upesi na kabla hajajibu swali, aliamua kuuliza kwanza kwanini Amadu anatafutwa.



    Amadu alimjibu kiwepesi, yeye ni muasi wa serikali, kisha akarudisha swali kwa kijana huyo kama yu tayari kubadilisha hali yake na ya wenzake pia, kijana akaridhia.



    “Kuna kazi kubwa nataka ufanye,” alisema Amadu. “Kwa kupitia kazi hiyo, nitapata kujua kama kweli unanifaa au lah!”



    Waliyoyoma na barabara mpaka walipomezwa na giza. Mataa ya gari yaliyoyomezwa ndani ya umbali tusipate kuyaona tena.





    Baada ya lisaa limoja: saa saba kasoro robo.





    Ndani ya klabu ya usiku ya Aces watu walikuwa wamejaa kupata burudani, ila laiti ungelikuwa nje ya klabu hiyo pasi na shaka usingelidhani kama ndani yake kuna mziki mkubwa na makelele ya haja kwani kulikuwa kimya watu wachache wakiwa wanaongeaongea huku wakielekea ndani ya klabu hiyo ama wakiwa wamesimama.



    Wanawake waliokuwa hapo nje walikuwa wamevalia vijiguo vifupi wakiwa wamejipara haswa. Magari kadhaa yalikuwa yamepakiwa nje, ila watembea kwa miguu ndio walikuwa wengi zaidi.



    Ukilinganisha na huko nyuma, klabu hii maarufu ilikuwa imepoteza mvuto wake. Watu hawafuriki tena kama awali. Hao unawaona hapo klabuni ni wale tu wenye fedha zao, na wale ambao hawahofii sana juu ya usalama wao.



    Tangu utawala mpya ulipoingia madarakani, uchumi umedorora mno, hamna pesa. Lakini zaidi hakuna amani ya kudumu. Matukio ya mahali penye ulinzi mkubwa kama vile benki kuu na kambi ya jeshi kuvamiwa, kuliwapa watu sababu madhubuti ya kukaa ndani ya viota vyao kwa usalama zaidi.



    Ila binaadam hatufanani kama alama za vidoleni, linaeleweka hilo, hivyo wakati wengine wakiwa wamejifungia ndani, kuna wengine wenye mioyo na mifuko mipana walikuwa wameenda kutumbua. Miongoni mwao alikuwapo Talib, waziri wa ulinzi.



    Alikuwa ameongozana na jopo la watu wake watano, wanne kati yao wakiwa walinzi wamlindao japokuwa hawakuwa na silaha mkononi.



    Aliketi kwenye kitengo cha VIP, kule kusipo na usumbufu. Meza yake ilikuwa imechafuliwa na vinywaji vikali vya bei ghali. Alikuwa anakunywa na mwenzake aliyekaa kando wakipiga soga.



    “Nimeona nitumbue mwenzangu kabla sijafa,” alisema Talib na sauti ya kilevi.



    “Kwanini unasema hivyo?” Aliuliza rafiki yake kando. Naye alikuwa amebebelea glasi ndogo ilyojaa kilevi.



    “Kwanini?” Talib alitahamaki. “Mpaka sasa sijawakamata wale washenzi. Yani roho yangu ipo mkononi … endapo tu wakifanya tukio lolote, basi kwisha habari yangu.”



    “Usijali,” Rafiki akapooza jambo. “Utawakamata tu.”

    “Lini?”



    Waliendelea kuzozana mpaka pale Talib alipomuona mwanamke mrembo, mrefu mwenye shepu ya haja, akiwa anacheza mziki kwa ustadi mkubwa. Alivutiwa mno, na kichwa chake ndani ya suruali kikafanya maamuzi ya kumuwinda mwanamke yule.



    Alimuagiza rafiki yake akamuitie huyo mwanamke lakini Rafiki akamtaka Talib amtume mlinzi. Talib alikataa kumtuma mlinzi kwani hakutaka kuhatarisha usalama wake, hivyo akasisitizia Rafiki aende.



    Rafiki alikunywa fundo moja la kinywaji chake alafu akanyanyuka kwenda kutimiza agizo.



    Alimfikia mwanamke yule na kumpasha habari, ila mwanamke akakataa. Alisema ana bwana ‘ake amekuja naye na pia hataki kampani yoyote.



    Rafiki akapeleka taarifa kwa Talib. Talib alighafirika akamshutumu Rafiki ya kwamba ni mpumbavu na asiyejua kucheza na masikio ya wanawake. Aliamua kunyanyuka mwenyewe na kwenda akiwa anaongozana na walinzi wake.



    Alipomkaribia mwanamke yule anayemhitaji alimshika kalio, mwanamke akashituka na kutazama aliyemtenda. Uso kwa uso akakutana na Talib.



    Kumbe mwanamke yule alikuwa ni Rose! Talib aligundua ile sura si ngeni machoni mwake, lakini hakukumbuka ni wapi haswa alimuona huyo mhusika.



    Kabla ya yeyote hajatia neno lolote, ghafla ulisikika mlio wa risasi kisha sauti ya kuamuru.



    “Wote chinii!”







    ???









    Kabla ya yeyote hajatia neno, ghafla ulisikika mlio wa risasi kisha sauti ya kuamuru:



    “Wote chinii!”



    Kwa hofu watu walilala chini upesi. Sauti za wanawake zilisikika zikipiga yowe ila ndani ya muda mfupi zikakoma baada ya kuamriwa hivyo na mwanaume mmoja miongoni mwa watano waliokuwa wamevamia eneo hilo.



    Nyuso zao zilikuwa zimefunikwa na vinyago vyeusi na mikononi walikuwa wamebebelea bunduki ndogo na SMG. Walivalia matisheti meusi na suruali nyeusi pia.



    Walinzi wa Talib hawakuweza kufanya kitu chochote kwakuwa hawakuwa na silaha hivyo nao walikuwa wamelala chini wakitulia kulinda maisha yao.



    Wale majambazi walijigawa kwenda pande tofauti tofauti wakaanza kusachi mifuko ya watu na kubeba waleti na pochi za wanawake. Wakati tukio hilo linafanyika mziki uliwa umezimwa kukiwa kimya.



    Wanaume wale watano walikomba kila kitu wakilazimisha wahanga kutoa kila kitu cha thamani walichonacho. Pale mhanga alipokuwa mkaidi basi nguvu ilitumika kwa kupigwa mateke ama kwa kitako cha bunduki.



    Baada ya muda mfupi, mmoja wa wale majambazi alimfikia Talib. Alimpukutisha kila kitu kuanzia simu ya thamani, pete, cheni, waleti na pesa za kutosha.



    Ila kabla hajaondoka, aligundua mwanaume yule aliyemtenda ni mtu mkubwa serikalini – waziri, tena waziri wa ulinzi! Alijikuta anastaajabu lakini baada ya muda mfupi akatabasamu na kupaza sauti kuwaita wenzake wamshuhudie mtu yule.



    Wenzake wawili walisogea kushuhudia wakati wawili wakibakia kuendelea kudumisha ulinzi. Walimtazama Talib na kweli wakagundua ndiye yule waziri wa ulinzi.



    Walijikuta wanacheka na kuanza kumdhihaki. Lakini zaidi kumtuhumu juu ya serikali.



    “Nyie ndio mnafanya maisha yetu yawe magumu, mahayawani wakubwa!” Alifoka mmoja.

    “Ni bora upo humu, ngoja upate kile unachostahili,” akadakia mwengine. Alimkandika Talib mateke ya tumbo na mbavu mpaka akamcheulisha damu.



    “Inatosha. Tuondokeni sasa!” alishauri mwanaume mmoja. Walichukua ufunguo wa gari wa Talib kisha wakaondoka zao kwenda sehemu ya kupumzisha magari.



    Huko haikuwachukua hata muda mrefu kulitambua gari la waziri, jaguar nyeusi, gari ghali kuliko yote pale. Walijiweka humo ndani na kupotea kwa mwendo mkali.



    Walikimbiza gari hilo kama toy na kana kwamba vile humo ndani kulikuwa kuna magazeti, si binadamu. Ndani ya muda mfupi sio tu kwamba hawakuwa wanaonekana maeneo ya karibu, walikuwa hawaonekani kabisa!



    Polisi na wanajeshi kadhaa walifika eneo la klabu baada ya dakika kama kumi na tano. Walikuwa watu wakiwa wametawanyika.



    Talib, rafikiye na walinzi wake ndio walikuwa wanazungukazunguka mbele ya klabu. Nyuso za walinzi zilikuwa nyekundu kwa kuzabwa makofi mfululizo na Talib akiwatuhumu hawana faida na hawajui kazi yao.



    “Nawalipa bure tu hawa nguruwe!” Aling’aka. Mdomo wake ulikuwa umepasuka kwa pembeni. Hakuonekana nadhifu; suti yake ilikuwa imechafuka na haikuwa mpangilioni.



    “Nimesema hivi, leo ndio mwisho wa kazi yenu. Nahitaji watu wa kunilinda na sio kunisindikiza!”



    Akamgeukia na rafiki yake. Akamtazama na macho yanayowaka moto.



    “Na wewe kumbe ni punguani mzee kabisa! Ulishindwa kupiga simu na ulikuwepo VIP?”



    “Nisingeweza wa…”



    “Kwanini usingeweza?”



    “Walikuwa wamekuja hadi kule. Sikuwa na fursa ya kufanya kitu.”



    “Sasa nyie mna faida gani?” Aliuliza Talib akiwanyooshea mkono walinzi na rafiki yake.



    Hakuishia tu hapo alihamia pia hadi kwa polisi na wanajeshi waliofika eneo hilo kwa kuwaita wazembe na wasiofaa kazini.



    Wamechelewa kufika tukioni na hilo jambo lingeweza kugharimu maisha yake, hivyo basi kugharimu pia na taifa.



    “Sasa nasema hivi …” alisema akiwa amekunja sura. “Hao washenzi walionidhalilisha wakamatwe haraka! Wakamatwe leo hii na wanyongwe mbele ya hadhara!”



    Aliweka kituo na kuuliza:

    “Mmenielewa?”

    “Ndio, mkuu!” Akajibiwa.

    “Sasa kama hamjanielewa, mtaenda kulielewa kaburi!” alitoa kitisho hicho kisha akaondoka zake kufuata mojawapo ya gari walilokuja nalo wanajeshi. Alitekenya ufunguo, akaondoka zake peke yake.



    Baada ya masaa matano: Ni asubuhi ya saa mbili.



    Palepale kwenye eneo lao la kawaida la kukutana, mgahawa ulio karibu na fukwe ya bahari, Kone na Rose wakiwa wamewasili ndani ya muda mfupi, waliagiza juisi za parachichi na vitafunwa vyepesi.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kone alikuwa amevalia suti nyeusi isiyo na tai, kama apendavyo, huku Rose yeye akiwa amevalia gauni refu rangi ya udhurungi na viatu vyenye visigino virefu vilivyomfanya aonekane mrefu kuliko Kone, kitu ambacho si kweli.



    Baada ya kunywa mafundo kadhaa ya juisi kwa kupitia mirija mipana, Kone alijikuta anasonya kabla ya kufungua mdomo wake kuanza maongezi rasmi ya kile kilichowaleta pale.



    “Mpaka sasa simu haipokelewi,” alisema kwa sauti yenye mashiko ya huzuni. Kwa kupitia dirisha kubwa la kioo la mgahawa, alitazama mawimbi madogomadogo ya bahari yakipiga ufukweni.



    “Wananipa wakati mgumu sana,” aliendelea kulalamika. “Na muda nao ndio hivyo unazidi kuyoyoma kama upepo.”



    Rose alikunywa juisi yake mafundo mawili kabla hajang’ata sambusa yake ya nyama na kuirudisha sahanini.



    “Sasa tunafanyaje, Kone?” Aliuliza. Uso wake haukuwa na shaka hata kidogo tofauti na ule wa Kone ulioonekana kukanganyikwa. Alikuwa anatafuna kwa madaha sambusa yake mdomoni kana kwamba ni jojo.



    “Rose, inabidi ufanye jambo. Hatuwezi tukaendelea kungoja zaidi ya hapa.”



    “Najua. Jambo gani sasa tufanye?”

    “Mtafute Kessy!” Kone alipaza sauti. Alijishitukia kwa kutazama mazingira yake kama kuna mtu amemsikia. Alipoona hakuna, akaendelea kuongea. Sasa akiwa amepunguza sauti.



    “Mtafute, hakikisha unamsumbua vya kutosha. Hakikisha unaonana naye kesho ama keshokutwa.”



    Rose akanywa juisi na kung’ata sambusa yake akimtazama Kone.



    “Tukikaa kumngoja akutafute, tutakesha, na hatuna huo muda. Inawezekana hata akawa amekusahau, wewe si mwanamke pekee mrembo anayekutana naye.”



    “Hilo sio shida Kone. Lakini unajua kwamba tukimuua huyo jamaa, tutakuwa tumetangaza vita rasmi na wale waasi?”



    Ukimya ukachukua sekunde tatu.



    “Unajua walivyo vema kimapambano na namna walivyojipanga,” Rose aliendelea kudadavua. “Kwa sasa adui wao ni jamaa madarakani, kwahiyo tutakapomuondoa, sisi wakaimu ndio tutakuwa maadui.”



    “Hilo lisikupe shaka, Rose.” Kone alitikisa kichwa. “Sisi tuna nchi yetu, hapa tunakuja tu kutimiza kile kilichokuwa ndani ya mkataba. Tutakapomuua huyo jamaa basi tutapata upenyo wa kufanya yetu. Mpaka waje kuunda serikali sisi tutakuwa tumeshakwenda!”



    “Wale waasi watatuacha salama?”



    “Watatujulia wapi? Watatuonea wapi? Watatupatia wapi?”



    Rose akanywa juisi yake mpaka akaimaliza.



    “Sawa,” alijibu akipandisha bega lake la kulia. “Nitafanya hicho ulichosema.”



    “Saa ngapi? Fanya sasa hivi!” Kone alisihi. Rose alitoa simu yake kwenye pochi yake kubwa aliyokuwa ameilaza juu ya meza, akatafuta namba ya Kessy na kumpigia.



    Simu iliita lakini haikupokelewa. Rose alimtaarifu Kone. Kone akamtaka aendelee kujaribu.



    Mara tano, simu haikupata wa kuiitikia.



    “Atakuwa yupo bize,” alisema Kone. “Ni mkubwa wa nchi, ana kazi nyingi. Lakini hakikisha utamtafuta tena baadae.”



    “Sidhani kama kuna haja. Akikuta missed calls zangu atanitafuta mwenyewe.”

    “Rose, una uhakika?”

    “Asilimia zote.” Akajibu mwanamke huyo akirembua macho. Aliagiza juisi nyingine anywee sambusa yake moja iliyobakia kwenye sahani.



    Baada ya masaa nane: saa kumi ya jioni.



    “Unamwamini lakini?” Mou aliuliza. Macho yake yalikuwa yanamtazama Amadu kwa mashaka baada ya kutoka kumtazama mgeni wao aliyeletwa na mwenzao huyo.



    Amadu alimshika Mou begani akisema:

    “Niachie mimi.”



    Mou akapandisha kichwa chake kabla hajaketi kitini kuwakuta wenzake: Farah, Mou, Chui, Ussein na Ulsher waliokuwa wamejaa kwenye kiti kimoja kikubwa na kirefu.



    Ulikuwa ni wasaa wa Amadu kukabidhi majukumu kwa mgeni wao ambaye alijitambulisha hapo asubuhi kwa jina la Fredy. Ndani ya asubuhi hiyo Fredy alijieleza wapi alipotokea, familia yake, asili yake na nini alichokuwa anafanya kusogeza maisha.



    Baada ya hapo alipewa muda wa kupumzika kabla ya tena muda huu kuwekwa kati ya THE GHOSTS kwa ajili ya kupewa jukumu ambalo lilikuwa na sura ya jaribio, kama vile alivyosema Amadu.



    “Tunahitaji watu waaminifu, wasiri na wachapakazi kwa ajili ya kujiunga kwenye kundi letu.” Alifungua mjadala kwa kunena hivyo. Watu wote walikuwa wanamsikiliza, ila Fredy alifanya hilo kwa umakini zaidi.



    “Umesema tunaweza tukakuamini, si ndio?”

    “Ndio,” Fredy alijibu akitikisa kichwa.

    “Sawa, na tumetokea kukuamini hilo. Lakini nataka nikujulishe mapema kwamba, kama hauwezi kazi ni bora ukasema sasa. la sivyo ukikiuka yale tuliyokubaliana, tutakutafuta popote pale ulipo. Tutakupata, na tutakuua!”



    Baada ya maneno hayo Fredy alikabidshiwa kiasi kadhaa cha pesa kisha akapewa maelezo ya kwenda kutafuta wenzake anaowaamini wataweza kazi.



    Akiwapata basi atawapeleka mahala fulani karibu na fukwe, huko THE GHOSTS watakuja kuwatwaa.



    Hilo jambo inabidi liwe la siri mno. Hakuna yeyote anayetakiwa kujua isipokuwa hao wahusika tu. Na wale wote atakaowafuata kuwashawishi basi wawe ni watu ambao anawajua kwa undani, si mtu mgeni wala mtu ambaye anamjua kwa rasharasha.



    Awe ni mtu ambaye akiulizwa upatikanaji wake basi litakuwa ni jambo linalowezekana ndani ya muda mfupi.



    Fredy aliridhia hayo akaondoka zake. Alinyookea nyumbani kwao kwanza kuwajulia hali wadogo zake wawili walioshinda njaa siku nzima. Aliwaletea chakula alichowaachia na kisha akaenda kufanya kile alichotakiwa kufanya muda huo.



    Alienda kwa rafiki yake wa kwanza ambaye aliongea naye kwa muda wa dakika kama ishirini. Alipotoka hapo akanyooka tena na barabara kama mwendo wa kilomita moja, akagonga kwenye nyumba fulani ndogo, ambapo humo alitoka msichana mweusi aliyefunga kiremba.



    Aliongea naye kwa sekunde chache kabla msichana huyo hajaingia ndani na kisha kutoka mwanaume mfupi mwembamba. Alimvutia mwanaume huyo pembeni ya nyumba. Akahakikisha usalama kwanza na kuanza kuteta naye.



    Alitumia hapo dakika kama kumi na kitu hivi kabla hajapaena mkono na mwanaume huyo na kuondoka. Alitembea tena kwa mwendo wa nusu kilomita ndipo akakutana na nyumba nyingine ambayo hiyo hakuhitaji kuigonga mlango maana alimkuta mlengwa wake nje.



    Aliongea naye kwa dakika kama ishirini, wakapeana ‘tano’ akaondoka zake.



    Usiku ulikuwa umeanza kuchukua fursa. Mataa yaliwashwa barabarani na hata majumbani. Fredy kana kwamba hakuona giza hilo, aliendelea kutembea.



    Hata hakuwa amepumzika wala kutia chochote mdomoni. Alikazana na mwendo wake haukuwa umepungua tokea pale alipoanza hilo zoezi.



    Alimalizia nyumba kama tatu kisha akaanza safari yake ya kurudi nyumbani. Hakuhitaji kukaba siku hiyo, kukwapua wala kukesha usiku mzima mtaani kutafuta pesa kwani alikuwa nayo mkononi.



    Akilini mwake alikuwa anawafikiria wadogo zake tu na kupumzika kabla ya kuamka kesho mapemba aende fukweni.



    Akiwa anatembea zake kichwani akiwa na hizo tafakuri za familia na harakati yake changa ya mapambano, ghafla kuna mtu alitokea mbele yake na kumsimamisha.



    Alirudisha akili yake barabarani akamtazama mtu huyo, akagundua ni yule Rasta aliyekuwa anampatia kisago jana usiku. Alikuwa amevimba jicho lake la kulia hivyo kufanya uso wake utishe zaidi.



    Rasta alisukuma Fredy akimuuliza:

    “Ulidhani sitakupata?”



    Fredy hakujibu kitu. Uso wake ulijikunja akimtazama mwanaume huyo mchokonozi.



    “Nipe pesa yangu. Umenisikia?”



    Kimya.



    “Si naongea na wewe!” Rasta alimsukuma tena Fredy.

    “Nipe pesa yangu!”

    “Pesa ipi? Kama kuiba si tuliiba wote, na si nilikupa mgao wako?” Fredy alifungua kinywa chake kwa hasira.



    Rasta alinyanyua mkono wake wa kuume amtwange Fredy ngumi, ila ajabu mkono huo ulikamatwa na mwingineo kwa nyuma. Rasta aligeuka haraka kutazama, akakutana uso kwa uso na Amadu.



    “Naona bado hujajifunza,” alisema Amadu. Rasta akatabasamu kisha akatia vidole viwili mdomoni mwake kupiga mluzi. Baada ya muda mfupi wakatokea wanaume wawili waliofanana miili na Rasta.



    “Leo upo kwenye himaya yangu,” alijigamba Rasta akitabasamu.



    Amadu alimsogeza Fredy akamweka nyuma yake. Alikunja ngumi zake kubwa akitanua miguu yake kutafuta balansi.



    “Haya naomba mnipatie hayo mazoezi,” alisema Amadu. Wanaume wale watatu wakaja kwa zamu.



    Amini usiamini, hakuna aliyerusha ngumi wala teke. Amadu alipanda juu, na akiwa huko alifungua miguu yake mizito kuwashindilia mateke ya haja wanaume hao watatu waliojikuta chini ndani ya sekunde tatu tu!



    Wote walikuwa wanaugulia chini wakiwa hawajiwezi kuamka, ama tuseme wakiwa wanategeana kuamka. Amadu aliwatazama kwa huruma kisha akamuuliza Fredy ni kiasi gani anachodaiwa na Rasta.



    “Hanidai!” Fredy alijibu.

    “Basi anataka kiasi gani?”



    Fredy alijibu, Amadu akatoa kiasi hicho cha pesa na kumtupia Rasta.



    “Nisikuone tena!” Amadu alisema kisha akamshika Fredy mkono kuelekea upande wa magharibi.



    “Umefikaje hapa?” Fredy aliuliza.

    “Nilikuwa nakufuatilia tokea umetoka getini,” Amadu akajibu.



    Walitembea kidogo, wakasikia sauti ikimuita Fredy. Waligeuka nyuma wakamwona Rasta akija anachechemea huku akishikilia tumbo lake. Walimngojea mpaka mwanaume huyo akawakaribia. Walimtazama kwa hamu ya kutaka kujua wakati uso wa Rasta ukiwa rafiki.



    “Naomba unifundishe,” alisema Rasta. “Nipo na wenzangu pia.”



    Amadu alitumia sekunde mbili kuwaza. Akasema:



    “Waite mnifuate.”

















    Tuseme Mungu hakuwa upande wao, wanaume wale waliomkwapulia gari waziri Talib, hawakufika mbali wakakamatwa. Walikuwa wakifanya jaribio la kutoroka nje ya jiji la Freetown. Walikuwa ndani ya gari lile lile walilolikwapua, na aidha hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya wao kukamatwa kwa upesi pale tu walipoonekana na wanajeshi ambao walikuwa tayari wameshapashwa habari.







    Walijaribu kukimbia na gari hilo lakini hawakufanikiwa. Barabara zilizibwa wakaishia kugonga na kujijeruhi. Wanajeshi waliwatwaa na kuwatia lupango huku Talib akipashwa habari ya kwamba ‘watu’ wake wameshatiwa nguvuni. Isichukue muda mrefu, Talib akafika eneoni. Alitumia ndege ndogo ya abiria wawili.







    Alifika hapo, majambazi hao wakiwa hoi tayari kwa kichapo cha haja walichokula. Walikuwa wanavuja damu wakiwa wametepeta kama kuku wenye midondo. Hata Talib mwenyewe ilimuwia vigumu kuwatambua na kuamini kama ndio wenyewe. Aliwajongea karibu akiwa anatabasamu upande mmoja, akasema kwa kebehi:

    “Mlidhani mtafika wapi?”







    Hakuna aliyejibu. Hakuna aliyekuwa na nguvu hiyo. Hata tu kumtazama ilikuwa shughuli.







    Talib aliguna akabinjua lips zake.

    “Nataka mniambie Amadu yupo wapi!” Alifoka Talib. Aliamini sasa watu wale watakuwa wana mahusiano na THE GHOSTS na kwa namna moja anaweza akapata taarifa muhimu ya kuwapata hao mahayawani, kama vile anavyoamini.







    Aliuliza sana juu ya Amadu na wenzake lakini hakupata majibu alikuwa anayataka ama kuyategemea. Alikata tamaa, lakini pia hakutaka kuacha nafasi hiyo isimuachie harufu ya waridi. Kwa kujua ama kutokujua alijikuta anaamini majambazi wale watakuwa wametumwa na THE GHOSTS, na hata kama hawajakiri inambidi ainyonye fursa hiyo adhimu sana kwake.







    Alimpigia simu bosi wake, Kessy, akiwa anatabasamu pana usoni. Simu ilipokelewa ndani ya muda mfupi tu, Kessy akakoroma na sauti yake nzito. Inaonekana wazi mwanaume huyo hakuwa anategema taarifa yoyote nzuri toka kwa Talib. Ila baada ya Talib kutia chumvi kisichostahili, kuremba mkaa kwa kuupaka rangi, basi Kessy akakenua kwa furaha.







    “Hakikisha wanaongea!” Alisema. “Huo ndio utakuwa mwisho wao sasa.”

    Baada ya simu hiyo kukatwa, Talib aliwaagiza majambazi wale wakubali ya kwamba wao ni washirika wa wakina Amadu kama kweli wanautaka uhai wao. La sivyo siku hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho kwao duniani.







    Unajisikiaje unapoambiwa jambo hujalifanya wala hulijui? Ndivyo ilikuwa kwa majambazi hao waliokamatwa. Japokuwa hawakuwa na uwezo wa kuongea, macho yao yaliyoa uchovu wa kipigo yalikuwa kwenye butwaa. Na kama kuna swali lililokuwa linawatatiza kichwani basi ni: Amadu ni nani?







    Baada ya masaa kama matano mbele walipakiwa kwenye ‘karandinga’ wakirushiwa humo kama viroba vya mnafu. Walipelekwa moja kwa moja ikulu, huko wakapokelewa na Talib na Kessy.

    “Ndio hawa?” Kessy aliuliza.

    “Ndio wenyewe, mkuu,” Talib akajibu akiwatazama majambazi hao na macho ya kudai ahadi ile aliyowapa.

    “Wako wapi wenzenu?” Aliuliza Kessy.







    Ni majambazi wawili tu ndio walikuwa wanaonyesha dalili za uhai. Walikuwa wamelala chali wakihema kana kwamba wamekandamizwa na jokofu. Ni nguvu ya kuhema tu ndiyo walikuwa nayo, ilikuwa ni ajabu Talib na Kessy hawakuligundua hilo.







    Tungeweza sema labda walikuwa wanafanya makusudi.

    Baada ya kuona hakuna kinachoendelea, majambazi wale walirudishwa kwenye karandinga wakaenda kunyongwa hadharani tena wakihusishwa na kundi la THE GHOSTS. Talib aliamua hivyo, na hivyo Kessy. Na walikuwa wanawaaminisha watu hivyo wao walivyokuwa wanaamini.







    Miili ya majambazi hao ilining’inizwa kwenye vitanzi. Na hata hawakupapatika kutetea uhai wao, bali kungojea kifo. Ni kama vile walikuwa wamepumzishwa toka kwenye mateso ya maumivu waliyokuwa wanayapata.

    Ilipohakikishwa hawapo hai, walitolewa kwenye vitanzi wakapakizwa kwenye karandinga lililowaleta wakaenda kufanywa chakula cha mbwa wa jeshi!









    ***









    Ilikuwa ni wasaa wa jioni ya saa kumi na moja wakati mwili mzuri unaovutia wa Rose ukiwa juu ya kitanda kikubwa sita kwa sita.







    Mwanamke huyo alikuwa amelala akiwa amevalia nguo nyepesi isiyombana. Nakuambia kama usingemtazama vema basi ungejikuta unakufuru kwa kumuita malaika. Alikuwa ni yule yule Rose ila kila unapomuona anakuwa mpya kama kifo.







    Aliamka baada ya simu yake kuita kwa muziki laini. Ilikuwa mbali kidogo na yeye hivyo akanyoosha mkono kuidaka akiwa amefungua jicho moja. Alitazama nani anampigia akakuta ni Kessy! Aliamka upesi akasafisha koo lake na kupokea simu.







    “Nimekuta missed calls zako, mrembo. Kuna shida?” Sauti ya Kessy ilinguruma ndani ya simu.

    “Ndio ipo.” Rose akasema kwa sauti moja hivi tamu yenye uwezo wa kuvunja ukuta wa Berlin. “Naona hutaki kuniona kabisa,” alilalamika.

    “Hapana mama, kazi zinabana.” Kessy akaroroma kuelezea. “Ila leo nimelenga kukuona kabisa, sidhani kama nitakosa hyo fursa mpenzi.”

    “Mie ni mhanga wa kiu kwenye jangwa lako, nitakataaje?” Alisema Rose.







    Baada tu ya muda mfupi alikuwa ameshajipara na amependeza hatari akiwa amejivika gauni lililofeli kabisa kuzuia kuonekana kwa maungo yake ya kutesa macho. Pia bila kusahau kipochi chake alichoweka zana yake ya kufanyia kazi, sumu kali ya taratibu.







    Alijipulizia marashi matam akatembea kama asiyegusa chini kwenda nje ya nyumba aliyomo. Huko akakuta range rover sport nyeupe ikiwa inamsubiria. Aliingia ndani ya gari, chombo kikaondoka. Baada tu ya robo saa akawa amefika ndani ya eneo la ikulu.







    Yani ni tatizo moja tu lipo ikulu, hata kama panapendeza vipi, kile kitendo cha watu waliobebelea bunduki kutembea tembea huku na huko kinaweza kukutoa kwenye ‘mood’ kabisa. Ila hilo lilikuwa kinyume kwa Rose, yeye hakuwa na shida nalo, alitembea kwa maringo kumkuta Kessy aliyekuwa amesimama kibarazani akimtazama mwanamke huyo kwa jazo la huba.







    Walikumbatiana wakaingia ndani. Talib alikuwa naye ameketi sebuleni, na macho yake yalivyomtazama tu Rose akili yake ikamkumbusha ni wapi alionana na mwanamke huyo. Kulee klabu! Tena alimshika na kalio. Alijikuta moyo unampasuka na anahangaika kutafuta pumzi.

    Rose alimkonyeza mwanaume huyo kana kwamba hakumbuki kitu. Talib asiweze kudumu hapo akaamua kuaga.







    “Talib, yani shemeji yako ndio amekuja na wewe unaondoka?” Alisema Kessy.

    “Hapana, mkuu. Kuna kazi tu nataka nikamalizie,” alijitetea Talib.

    “Sawa. Umefanya kazi nzuri sana leo. Natumai utaendelea hivi mpaka uwakamate wale mahasidi!”

    Talib akaondoka.







    Kessy alianza kunyonyana ndimi na Rose wasahau kabisa kama wapo sebuleni. Walikuja kukumbuka hilo baadae Kessy akambeba mwanamke huyo kumpeleka chumbani. Rose asisahau mkoba wake, aliushikilia kwanguvu akaenda nao huko chumbani na kuutupia kitandani.







    Kessy alimsaula nguo zote mwanamke huyo akambakiza nguo za ndani tu. kwa papara zote, kana kwamba hajawahi onja kwa mwaka mzima, alimparamia mwanamke huyo aliyemponyoka akimpiga chenga ya mwili, akatoka kitandani.







    Kessy alimtazama mwanamke huyo kwa macho yanayoteswa na uchu mkavu. Rose alimtazama Kessy na macho yasiyojiweza, akasema kwa kupitia puani:

    “Mie wako tu usiku mzima wa leo, utanila utakavyo.”







    Rose alipomaliza kusema hivyo, alianza kuzungusha kiuno chake kwenda kushoto na kulia taratibu akicheza wimbo usiosikika. Mapaja yake mekundu yalivutia kutazama, kiuno pia na kifua chake kilichokuwa kinatikisika kipindi akitenda.







    Alifanya nguo ya ndani ya Kessy ihamie sehemu moja yote.







    Aliporejea kitandani alimfunga mikono mwanaume huyo kwa kutumia shuka, kisha akamvua nguo ya ndani, na kabla hajafanya kitu na anjoli ya Kessy aliiweka katikati ya mapaja yake ya moto na malaini akiwa amemlalia mwanaume huyo kifuani akichezea nywele zilizojaa eneo hilo.







    Kessy alijihisi anakata roho kwa kungoja. Laiti kama angelijua lile lilikuwamo kichwani mwa Rose, wala asingetubutu kuendelea kufumba macho kwa raha aliyokuwa anapata. Yani pale hata angeambiwa ahonge Sierra Leone, angekubali pasi na kinyongo.







    Rose alikuwa anasugua mapaja yake taratibu akimtazama Kessy. Ila mara kwa mara, kwa kuibia, akawa anatazama pochi yake na kuuvuta kisirisiri. Ilifikia kipindi sasa pochi ukawa upo karibu anavyotaka na ameshaufungua, na hapo ndio Kone akapewa gharika la utamu.







    Rose alizunguka kiuno chake aking’ata lips zake tamu. Kiuno kilienda kwa migandisho kisha kasi … kilitulia kama kinasusa, alafu kikaenda tena kama kinakimbizwa. Kone akaachama mdomo kwa raha.







    Mwanamke huyo alidumbukiza mkono wake ndani ya pochi akatia kidole chake ndani ya kichupa kilichokuwemo humo kabla hajatoa kidole upesi kikiwa na unga mweupe mithili ya sembe. Wakati huo alikuwa ananyonya sehemu ya chini ya sikio la Kessy huku akikisusa kiuno chake kwa kusua kama kina mafua.







    Pasipo kujua, Kessy alisogezewa kidole chenye dawa puani. Alinusa akapiga chafya. Rose alimpa pole na kuendelea kumpa mambo jambo juu ya mtambo asimpatie mwanaume huyo hata muda wa kuwaza. Walipomaliza walipumzika mpaka kesho Rose alipoondoka pasipo kujulikana adhma yake wala afya ya Kessy kuwa na mushkeli.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Rose alimpigia simu Kone akamweleza kila kitu. Walikubaliana wakutane ‘maeneo yao’ muda si mrefu. Kweli wakafanya hivyo.





    “Umehakikisha kweli?” Kone aliuliza akiwa na hamu pomoni ya kujua. Rose, mwanamke asiye na papara, akala kwanza sambusa yake akitafuna kwa madaha.







    “Huniamini au?” Aliuliza akirembua.

    “Nakuamini Rose ndio mana nikakupa hii kazi.”

    “Basi jua nimeshamaliza.”

    Kone akajikuta anatabasamu pasipo jitihada.

    “Sawa,” alisema Kone kwa uso wenye bashasha. “Pesa yako taslimu utapewa punde tu tutakapopata taarifa ya kifo chake.”

    “Sawa,” akajibu Rose akipandisha mabega yake juu. “Ila si ntapata advansi?”

    “Pasipo shaka utapata. Tukitoka tu hapa.”







    Walimalizana, Kone asipoteze muda ndani ya Sierra Leone akakwea ‘pipa’ kwenda Guinea. Huko alipanga kuonana na Raisi lakini pia vilevile kuimarisha ndoa yake kwakuwa kazi imeshakwisha sasa.







    Alienda nyumbani kwake akapumzika kwa masaa matatu kisha akajiweka kwenye gari kwenda ukweni, huko alipodhani mke wake na watoto watakuwepo. Alipoteza masaa mawili barabarani kabla hajafika mbele ya geti la saizi ya kati rangi ya udongo. Alipiga honi hapo mara mbili, geti likafunguliwa.







    Aliingia ndani akamkuta mkwewe, mama yake Fatma, pamoja na watotowe, lakini mke wake hakuwepo.

    “Ni siku ya pili sasa sijui yupo wapi?” Alilalama mkwe. “Hapatikani hewani na sijui ameenda wapi.”







    Kone akalemewa na mawazo. Aliketi akitafakuri. Aliaga watoto na mkwe wake akaondoka zake. Alizunguka kwa ‘mashoga’ zake Fatma na ndugu wote anaowajua, kote huko hakumkuta. Alijaribu kupiga simu nayo haikupatikana.







    Alichoka akarudi nyumbani kwake. Alilala akiwaza na kuwazua. Hakupata kabisa usingizi.

    “Fatma upo wapi mama?”









    ***









    Baada ya siku mbili, ikiwa ni majira ya jioni, Al Saed toka Liberia alifanya ziara kuja nchini Sierra Leone kukutana na rafiki yake, bwana Kessy.







    Kama zawadi, alibeba mvinyo mmoja wa ghali sana. Wakiwa wanakula chakula juu ya meza kubwa mno iliyojaa kila aina ya chakula ambavyo vingine hata havikuguswa, walikuwa wanateta mambo yao ya kiutawala, haswa namna ya kuimarisha ulinzi ndani ya tawala zao wasipate shurba.







    Walipomaliza kula walitembeatembea ufukweni mwa bahari huko kwenye hewa safi. Kwa mbali walinzi wao wawili walikuwa wanawafuata kuhakikisha usalama wao.







    Waliteta mengi, Kessy akiwa mshauri. Ila jipya sana lililochomoza ni maneno ya Al Saed akimtaarifu Kessy ya kwamba kuna nchi za huko ughaibuni zimemuahidi kumsaidia kwenye utawala wake, lakini wamempa masharti.







    Masharti ambayo kwa namna moja ama nyingne ndio sababu kubwa iliyomfanya aje kuomba ushauri.

    Kessy alijikuta ana hamu kubwa sana ya kujua hayo aliyokuwa anataka kuambiwa. Alimtazama Al Saed usoni akiwa amempa umakini wote. Lakini Al Saed akiwa anaongea, taratibu Kessy akaanza kupoteza uwezo wa kuona.









    Aliyafikicha macho yake akidhani atakuwa poa, lakini haikuwezekana na hali ilizidi kuwa mbaya zaidi!

    Kama haitoshi akaanza kuhisi kichwa kinauma vibaya mno. Al Saed alistaajabishwa na hilo. Walinzi walisogea karibu wakamsaidia kiongozi huyo kupata usafiri wa haraka, ‘ambulance’, akawahishwa hospitali.

    Al Saed, Talib na kiongozi mwingine wa juu walikuwepo pia eneo hilo. Walikaa wakiwa wamestaajabu ni nini kimetokea. Ulinzi wa eneo hilo ulikuwa mzito sana kiasi kwamba hakuna hata mbu aliyepita.









    Baada ya kukaa hapo kwa muda wa lisaa limoja tu, daktari alikuja kuwapa taarifa ya mgonjwa. Alimtazama Talib kisha Al Saed, akameza mate. Ni kana kwamba alikuwa anahofia kuongea. Na ni kweli kwa namna alivyokuwa anatazamwa, alikuwa ana haki ya kuogopa. Talib alikuwa ametoa macho kama nyanya mbichi wakati Al Saed akiwa amekunja uso mithili ya tambara la kikongwe.









    .***





    Baada ya kukaa hapo kwa muda wa lisaa limoja tu, daktari alikuja kuwapa taarifa ya mgonjwa. Alimtazama Talib kisha Al Saed, akameza mate. Ni kana kwamba alikuwa anahofia kuongea. Na ni kweli kwa namna alivyokuwa anatazamwa, alikuwa ana haki ya kuogopa. Talib alikuwa ametoa macho kama nyanya mbichi wakati Al Saed akiwa amekunja uso mithili ya tambara la kikongwe.









    “Nasikitika kuwaambi …”

    “Amekufa?” Talib aliwahi.

    “Hapana, hajafa.” Daktari akajibu kwa sauti ya upole. Talib alishusha pumzi akadaka kiuno chake.

    “Raisi ni aidha amekula ama amepewa sumu kali sana. Ni bahati kwake kuwa hai mpaka muda huu. Tunaweza tukauita muujiza.”









    Jambo hilo likawachanganya Talib na Al Saed kwa mawazo. Kessy amekula sumu muda gani, na hivyo basi nani kampa? Japokuwa waliteta na kuulizana sana kuhusu hilo swala hawakupata jibu wakaishia kutegemea labda Kessy atakapopata uwezo wa kufungua kinywa basi utajulikana upi ni mchele na upi ni pumba.









    Lakini zaidi ya hapo hilo swala pia likaonekana gumu baada ya muda kidogo daktari kuja na kuwapa taarifa ya kwamba hana uhakika ni kwa muda gani Kessy atakuwa kitandani mpaka aje kupata fahamu zake kwani sumu aliyotumia bado haijajulikana ni ipi ili basi wafahamu namna ya kuikabili.









    “Kwahiyo daktari unataka kusemaje?” Talib alikunja sura.

    “Mi – mie sina usemi mheshimiwa. Laki …”

    “Lakini kitu gani? … kwani wewe kazi yako ni nini? Unavyotuambia haujajua ni sumu gani sisi ndio tutajua?”

    “Tutajitahidi mheshimiwa kwa kadiri ya uwezo wetu. Tunaomba tu utupatie muda.”

    “Daktari, kaa ukijua ya kwamba; akifa nawe utazikwa naye.”









    Hilo tisho likafunga maongezi kati ya Talib na daktari aliyeondoka upesi kuelekea ndnai ya chumba maalum alipolazwa kiongozi mkuu wa nchi.

    Baada ya muda mchache mbele, Al Saed akaaga anaondoka kurudi Liberia, lakini akiahidi kuendelea kumjulia hali rafiki yake huyo aliye taabani. Talib alimsindikiza kiongozi huyo mpaka uwanja wa ndege, akaondoka zake.









    Wakati Talib akirejea kurudi hospitalini, bado kichwa chake kilikuwa kinachakata swala la Kessy. Mambo yalikuwa magumu lisilionyeshe dalili ya kung’amulika. Ila kwa namna moja ama nyingine akili ya Talib ikaanza kuelekea kwa Al Saed ya kwamba yeye ndiye anaweza kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo. Alijitahidi kukataa lakini bado akili yake ilitokea kuamini hivyo.









    Al Saed ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kessy, kwa siku zote hizo za nyuma Kessy alikuwa mzima. Al Saed alikuwa ndiye mtu wa mwisho kula na Kessy, na pia kwa mujibu wa maelezo yake, Al Saed alimletea Kessy mvinyo kama zawadi.









    Ila afanye hivyo kwasababu gani ingali hawakuwa na ugomvi wowote? Kama wangekuwa na tofauti yoyote basi Talib aliamini angekuwa anaifahamu.









    Alijitahidi kuitafuta sababu ya Al Saed kutenda hilo tendo, akakosa kabisa. Sasa basi akili yake ikawa inaamini yule ndiye mtenda lakini pia kwa wakati huohuo tena akiwa anajikosoa.









    Kufa kufaana lakini, waswahili walinena. Japokuwa Talib alikuwa kwenye rundo la mawazo, alijikuta anapata tabasamu katikati yake baada ya kujigundua ya kwamba ni yeye peke yake sasa ndiye atakaimu kiti cha uongozi wa Sierra Leone mpaka pale Kessy atakapopona. Na kama je asipopona?









    Kabla hajapata jibu alikuwa ameingia ndani ya hospitali pamoja na msafara wake. Aliendea karibu na chumba alicholazwa Kessy akaketi karibu.











    ***











    Zilipita siku tatu.









    Siku inayofuata, yaani ya nne, ilikuwa ni mahususi kwa THE GHOSTS kutoka ndani ya jiji la Freetown waende kutafuta mahali tulivu na papekee kwa ajili ya kujiandaa kama kikundi na hata pia kuongeza idadi ya watu baada ya kuona kuna haja hiyo.









    Hilo halikuwa shida, bali watatokaje nje ya jiji hilo ukizingatia wanajeshi wameambaa huko kwenye barabara, njia za maji na hata uwanja wa ndege? Mipango ilihitajika, tena mipango thabiti ya kukwepa vikwazo. Mipango itakayowawezesha kuwakwepa wanajeshi lakini kwa wakati huohuo wasafirishe silaha na wajisafirishe na wao pia.









    Hivyo basi kwa usiku mzima walipanga namna ya kutenda ili kukwepa. Asubuhi ilipodamka, gari kubwa, canter nyeupe iliyofunikwa na shuka kubwa la ngozi, lilitoka ndani ya nyumba hiyo na kushika barabara ya lami. Mwendo wake ulikuwa wa wastani na vioo vyake vilikuwa vimejiveka rangi nyeusi usiwaone waliomo ndani.









    Gari hilo lilielekea upande wa kusini wa jengo lilimotokea. Baada ya muda mfupi likaingia kwenye barabara kuu na kuanza safari ya kuelekea upande wa mashariki. Halikudumu sana katika barabara hiyo kuu, likachepuka na kwenda upande wake wa kushoto. Huko lilikaa kwa muda wa masaa matatu likafika mahala kulipokuwa na msururu wa magari yakingojea zamu ya kukaguliwa.









    Kulikuwa kuna wanajeshi sita kwa macho ya haraka. Wote walikuwa wamebebelea bunduki ndefu mikononi mwao na kwa kugawana walikuwa wanakagua magari, huyu akishika hili basi yule lile.









    Taratibu magari yalienda, na mpaka ukafikia muda ambapo Canter lilikuwa la pili kwenye msururu. Basi kutokana na ukubwa wa gari hilo na kufanya ukaguzi uwe wa kiufanisi zaidi, wanajeshi watatu walilidaka ambapo mmoja alisimama upande wa dereva wakati wengine wakiwa wanalitazama kiubavu.









    “Shukeni chini,” ilitoka amri. Alikuwa ni yule mwanaume rasta, mwanaume aliyekubali kuungana na Amadu pasipo shuruti.









    Alishuka akatia mikono yake mfukoni. Rasta zake zilikuwa zinamtekenya mabega, na uso wake haukuonyesha hofu yoyote.









    “Umebeba nini humu?” Aliuliza mwanajeshi kwa uso kakamavu.

    “Nimebeba nyama. Nawapelekea wazazi wangu kijijini,” akajibu Rasta.









    Aliamriwa aonyeshe nyama hiyo, akaenda nyuma ya gari na kufungua shuka lililofunika gari. Humo ndani kulikuwa kuna ‘dude’ kubwa rangi nyeusi lenye pembe nne. Rasta aliamriwa alifungue hilo dude kionekane kilichomo ndani. Akasita.

    “Samahani, nina aleji na nyama. Nitapata matatizo endapo nitanusa harufu hiyo.”









    Basi mwanajeshi mmoja akajitolea kwenda kutazama. Alifungua dude hilo na kukuta mfuko mweupe ukiwa umefunika nyama iliyokuwa inanukia vilivyo. Alipekua nyama hiyo asikute kitu. Waliporidhika hamna jambo, walieleka na kwa dereva wakapekua, napo hawakukuta kitu hivyo wakamruhusu Rasta aende zake. Gari likaenda.









    Ilipita kama dakika kumi na tano, mwanajeshi yule aliyepekua nyama, pamoja na yule mwenzake, wakaanza kuwashwa miili. Walijikuna kama hawana akili nzuri. Mwasho ulizidi kuongezeka sambamba na muda, sasa wakawa kama vichaa. Walipiga kelele kali na kuzua tafrani, walitokwa na vidonda kwa kujikuna wakawa wanavuja damu. Wenzao walisitisha zoezi la ukaguzi wakawajongea kuwatazama kwa bumbuwazi.









    Walitaka kufanya utaratibu wa kuwawaisha hospitali ya karibu kwa kutumia usafiri wao, lakini kabla hawajatenda hivyo wakaliona gari la wagonjwa. Na kwenye ubavu wa gari hilo kulikuwa kumeandikwa jina la hospitali iliyo karibu. Basi kwa haraka wanajeshi wakawasaidia wenzao kuingia kwenye gari la wagonjwa wapate kwenda kupata tiba. Na kwa msaada zaidi, mwanajeshi mmoja mzima, sajenti, akaongozana na wenzake.









    Hakukuwa na muda wa kukagua gari hilo la wagonjwa, wanajeshi wagonjwa walipakiwa na chombo kikaondoshwa kwa kasi kuelekea hospitali. Dereva alikuwa ni Chui akiwa sambamba na Ulsher. Walikuwa wamevalia kofia nyeupe za nailoni na miwani ya macho. Walifika mbele Ulsher akachomoa bunduki na kumtwanga yule mwanajeshi mzima kisha akatoa simu ndani ya mfuko wake na kupiga.

    “Muda ndio huu.”









    Kisha akakata alafu akampisha Ulsher ashike usukani kabla hajaenda kutwaa ‘redio koo’ na kuitumia kuwasiliana na wanajeshi waliobakia kule kwenye kitengo cha upekuzi. Aliwapa taarifa ya kwamba kuna ujio wa gari kubwa hapo, canter ya kijivu, akalitaja na namba zake za usajili. Taarifa ni kwamba gari hilo linatakiwa kupita upesi.









    Isipite muda mrefu, wanajeshi watatu waliobaki kwenye ukaguzi wakaliona gari hilo. Baada ya kujiridhisha ndilo lenyewe, gari hilo likapita wasijue ndaniye yapo mabaki ya wana THE GHOSTS.









    Canter hilo lilitembea kwenda kukutana na ambulance pamoja pia na canter nyeupe ya mwanzoni. Tayari wanajeshi wale wawili, waliokuwa wanawashwa, walishakufa kwenda kukutana na mwenzao aliyeuwawa kwa risasi. Wote walivuliwa nguo zikapuliziwa dawa kabla ya kuvaliwa na Fredy na rafiki yake Rasta, Thomas, sasa wakaonekana ni wanajeshi.









    Walijipaki wote kwenye canter ya kijivu huku sehemu ya dereva na mwenza wakiwepo wanaume hao ndani ya sare. Sehemu ya nyuma palipokuwa pamezibwa, pakawa pamehifadhi silaha na wengineo wana THE GHOSTS.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/







    Canter hiyo ilisonga kwa muda wa masaa matatu mbele kabla ya kukutana na kizuizi cha mwisho watoke ndani ya Freetown. Kwa muda wote huo Chui alikuwa anaisikiliza redio koo kwa umakini ili wapate kujua kama kuna namna yoyote mpango wao upo hatarini. Lakini mpaka wanafika kwenye kizuizi cha mwisho, walikuwa salama.









    Kwenye kizuizi hiki hakikuwawia vigumu, wanaume wale waliokuwa wameketi mahali pa dereva walitumia nguo za za jeshi vema kuwalaghai wapekuzi na kisha kwenda zao sasa nje ya Freetown. Kwenda huko msituni wapate kujikoboa kwa mafunzo, lakini pia kujiongeza.









    Kukaa ndani ya Freetown kungewanyima fursa hiyo ya ‘kujiachia’ wapendavyo. Kwa namna iliyopendeza machoni, kutumia mfumo wa MDR kwa kuketi mbali na mkono wa serikali, lakini pia karibu na raia, ulikuwa ni mpango mtamu zaidi kufikisha malengo.











    ***









    Japokuwa ilikuwa ni mchana kamili, Kone alikuwa amechoka na yu kitandani akiwa hajafanya lolote tangu asubuhi, hata kunawa uso.

    Alikuwa amejifunika shuka mpaka kiunoni. Mara moja moja bado alikuwa anafunga macho yake kwa usingizi na kisha akiyafungua tena. Ni dhahiri shairi alichelewa kulala, alafu hakuwa anatakata kulala tena.









    Alitafuta simu yake ya mkononi, akaikuta kitandani. Aliitazama kama kuna habari yoyote kwenye kioo, hakukuta. Alisonya kisha akatafuta jina la Rose aliloliita akiiweka simu sikioni. Baada ya muda mfupi simu ikapokelewa, na sauti ya kike ikanena upande wa pili.









    “Vipi umepata taarifa zozote za Kessy?” Kone aliuliza.

    “Hapana,” sauti ikamjibu.

    “Inakaribia juma sasa, Rose. Kweli ulimpatia sumu?”

    “Bila shaka.”

    “Mbona hamna majibu?”

    “Sijajua kwanini. Nitajitahidi kufuatilia.”









    Kone alikata simu akairushia mbali. Kwa namna moja aliona ulimwengu umeamua kumfanya asiwe na amani. Ni siku kadhaa sasa anawinda habari njema na hazipati, si kwa mkewe wala huko Sierra Leone. Alijiona yupo kwenye jehanamu ndogo. Aliona kana kwamba watu wa ulimwengu wamekaa kando wakifurahia anavyotaabika.









    Alijinyanyua toka kitandani alipatie tumbo lake chochote kitu. Alijiiandalia chakula cha upesi: cornflakes na maziwa, kisha akaketi mahala pa kulia chakula. Alijitahidi kula lakini alishindwa, hakuwa na hamu kabisa japokuwa alihisi njaa. Alijikuta anasogeza bakuli la chakula kando na kushika tama.









    Mke wake, bi Fatma, alitawala kichwa chake. Na hata pale alipompa ahueni, basi Kessy akachukua zamu. ‘shift’ hiyo ilimnyima raha. Alihama kila kona ya nyumba mpaka jioni ikawasili. Wakati sasa akiitafuta usiku, alikuwa sebuleni akitazama taarifa ya habari. Alitamani aone habari ya msiba wa Kessy lakini kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga, matumaini yakawa yanafifia.









    Akiwa hapo bado anakodoa, alisikia mlango wa mlango wa sebuleni unafungwa. Upesi aligeuka kutazama akamwona mke wake, bi Fatma, akiwa amevalia dera na anatembea kwa kuyumba. Alikuwa amelewa!









    Kone alisimama akamfuata mkewe akimwita jina. Fatma alimpuuza mumewe na hakutaka kuzozana juu ya hali yake. Hakusema wapi ametokea wala wapi alipokuwa siku zote hizo. Mdomo wake ulikuwa unanuka mvinyo wa bei ghali. Alikuwa mkali kama mbogo akisisitiza asiguswe.









    Hatimaye, alijifungia ndani ya chumba akimwacha mume wake mlangoni na mabumbuwazi.









    “Fatma fungua!” Kone alibamiza mlango. Macho yake yalikuwa mekundu. Uso wake ulikuwa mweusi.

    Alikaa hapo kama lisaa asifunguliwe mlango. Alimwendea mlinzi na kumuuliza juu ya ujio wa mke wake, mlinzi akamtaarifu ya kwamba aliletwa na gari kubwa, Toyota Prado nyeusi. Kone akachanganyikiwa kwa fundo la wivu.







    Alirudi ndani akaenda kubwatukia maswali yake mlangoni mwa chumba alimo Fatma, lakini hakupewa jibu lolote. Fatma alikuwa amelala na inawezekana alikuwa hata hasikii linaloendelea.







    Kone alikata tamaa akaenda zake kulala kwa matumaini ya kwamba kesho yake, pombe zikiwa zimemtoka Fatma, basi atapata majibu anayoyataka. Alijitahidi kupunguza jazba.







    Ilimchukua kama masaa matatu kitandani kuupata usingizi. Alikuja kuamka muda wa saa mbili asubuhi, kesho yake, akaendea kile chumba kilichomficha mkewe.







    Mlango ulikuwa wazi. Aliingia ndani akakuta kitanda cheupe, hakuna mtu! Alitafuta nyumba nzima asimuone mke. Alimwendea mlinzi akamuuliza, mlinzi akamhabarisha ya kwamba mwanamke huyo aliondoka kwenye majira ya saa kumi na mbili, na gari lililomleta jana ndilo limekuja kumtwaa.







    Kone alirudi ndani aking’ata kidole chake kana kwamba anataka kukitemea chini. Alimpigia simu mkwe wake kumuuliza kama mkewe yupo huko, akakanusha. Aliwapigia na rafiki wa mke wake anaowajua, nao wote wakakanusha. Hakuna aliyempatia majibu zaidi ya kusema “sifahamu”.









    ***









    Zinapita siku tano.









    Talib akiwa nyumbani kwake anamkumbuka mwanamke yule aliyekutana naye klabu ya usiku ya Aces. Anakumbuka namna alivyoshika maungo yake na namna alivyomkonyeza akiwa na Kessy, basi akajikuta anatabasamu mwenyewe kama mwehu.







    Alijikuta anatamani kumuona tena mwanamke huyo. Alijikuta ana kiu ya kutaka kumtia mikononi. Kessy alikuwa yu hoi kitandani, hivyo basi hakuna wa kuukata mkono wake mrefu unaotaka kumdaka mwanamke huyo.







    Lakini kumbuka Talib hakuwa na namba ya simu wala hawakuwa anajua makazi ya mwanamke huyo, hivyo basi ilimlazimu kufanya namna ya ziada kumpata mwanamke huyo basi amfaidi kabla Kessy hajarudi fahamuni.







    Alimtafuta dereva aliyemleta Rose ikulu siku ya mwisho kumuona mwanamke huyo, akampata. Zoezi hilo lilikuwa rahisi kwake kwasababu alikumbuka ni gari lipi lilitumika baada ya kuliona limepaki nje alipokuwa njiani kutoka ikulu siku ile. Lakini pia alikumbuka ilikuwa ni majira gani na gari lilifanya tukio gani.







    Dereva alimweleza mahali alipomtoa mwanamke yule, basi Talib akaanza kuchukua hatua. Alijiweka kwenye gari akiwa na ‘kamsafara’ ka magari matatu mpaka eneo anapoishi Rose. Alimkuta mwanamke huyo akiwa amevaa sketi fupi nyeusi na blauzi rangi ya udhurungi ikiishia juu ya kitovu. Hakika alipendeza japokuwa haikuwa dhamira.







    Talib alimsalimu na kumtaka waende mahali bora zaidi ya pale wapate kuteta. Rose alitaka kubadili nguo lakini Talib hakuweza kuvumilia, alimtaka waende vivyo hivyo kwani bado alikuwa anavutia sana.







    Walijipaki kwenye gari wakaondoka. Rose alitabasamu akimtazama Talib, Talib akajiona yu peponi kwa wasaa.







    Lakini kama angelijua ni nini Rose alikuwa anakiwaza kichwani, basi angemshusha mwanamke huyo aende zake ili apate kujinasua toka mtegoni.

    Tabasamu la Rose lilikuwa zuri mno, hata macho yake pia. Lakini roho yake, hakuna binadamu anayeiweza zaidi tu ya yule aliyemuumba.







    Tabasamu la Rose lilikuwa zuri mno, hata macho yake pia. Lakini roho yake, hakuna binadamu anayeiweza zaidi tu ya yule aliyemuumba. Ni mwanamke hatari kuwa naye karibu kwani akili yake inafikiria mara mbili ya wewe unapoishia.

    Baada ya dakika kama kumi na tano barabarani hatimaye waliwasili mbele ya nyumba kubwa yenye uzio mrefu na wanajeshi kadhaa mlangoni wakiwa wamebebelea bunduki. Geti lilifunguka lenyewe, gari likazama ndani na kuwatema Talib na Rose walioingia ndani ya jumba na kuketi sebuleni.

    Ndani ya muda mfupi, mhudumu alikuja kuwasikiliza wanahitaji chakula na vinywaji gani. Alikuwa ni mwanamke mrefu mweupe aliyevalia sare rangi nyeusi na nyeupe. Alikuwa amependeza ndani ya sare yake na pasipo shaka alionekana anajua kazi yake na namna ya kuitenda. Alitabasamu akiwa anapewa oda alizokuwa anaziandika kando. Aliomba radhi na kuondoka akiahidi ndani ya muda mfupi atakuwa amerejea.

    Ni kama vile hotelini, kumbe ni ndani ya nyumba ya mtu! Maisha yanataka nini zaidi ya hapo?

    Vililetwa vyakula vya maana kabla hata ya waliokuwa wanangoja hawajameza mate. Vinywaji navyo visiwe nyuma vikajazwa kwenye meza, tena vile vya ghali. Yani ni kana kwamba kulikuwa kuna tafrija, kumbe vyote ni vya watu wawili tu! Hawakutumia vijiko bali visu na uma.

    Wakiwa wanakula hapo kwa kunyoosha mikono huku na kule kutwaa nyama, matunda ama vinywaji basi wakawa wanateta yanayosibu kwa muda huo. Rose alikuwa wa kwanza kuyateta kuhusu hali ya afya ya Kessy. Mwanamke huyo alikuwa ana kiu ya kutaka kufahamu.

    “Bado hajapata fahamu zake. Hali yake si ya kuridhisha kwakweli,” alisema Talib akiwa anatafuna kisha akashushia na kinywaji. Rose alimsikiliza kwa hamu lakini jibu hilo halikukata kiu yake hivyo akaendelea kudadisi.

    “Kwani daktari anasemaje?”

    “Anasema inawezekana kurudi kwenye fahamu zake lakini kuna madhara makubwa atayapata. Sijui yule dhalimu alitumia sumu gani kwakweli!”

    “Ila una uhakika ni yeye, Al Saed.”

    “Hakuna mwengine zaidi yake. Yeye ndiye alikuwa wa mwisho kula na Kessy, na tena alimletea mvinyo toka Liberia.”

    Talib akajikuta anaguna.

    “Cha ajabu ni kwamba kwenye ule mvinyo hakujaonekana ishara yoyote ya sumu. Yani daktari anasema haijulikani aliitumia lini hiyo sumu, lakini wanaamini haitakuwa muda mrefu kutokana na madhara yake makubwa, na ndio hapo ninapoamini bado tu atakuwa ni Al Saed. Bado tu sijafahamu alitendaje na ni kwa nia gani.”

    Wakala kwa muda pasipo kunena. Mara Rose akazuka tena na swali:

    “Kessy akigundua tulikuwa wote itakuwa shida,” Rose alichokoza. Bado alikuwa anamchimba Talib pasipo mwanaume huyo aidha kujua ama kutokujua.

    “Hawezi akagundua,” Talib alisema kwa kujiamini.

    “Unajuaje?”

    “Kwa hali yake ile si wa leo wala wa kesho.” Talib akajibu pasio kumtazama Rose. Alikuwa anakula lakini uso wake ukionyesha hana kabisa wasi na aongealo, basi kwa namna moja ama nyingine, Rose akatabasamu. Alipendezwa na jibu hilo. Lakini kumbuka adhma yake ilikuwa ni Kessy afe na sio kulazwa kitandani, sio? Kwahiyo bado kulikuwa na haja kwa yeye kuendelea kuchanga karata zake.

    “Hivi ikitokea akafa, ikitokea lakini, itakuaje?”

    “Nitakuchukua wewe!” Talib akaropoka kisha akaangua kicheko. Rose aliishia kutabasamu kisha akanyamaza. Alijua kabisa sasa mahali alipopagusa palikuwa ni penyewe, na Talib lazima azame.

    “Au hutaki?” Talib aliuliza kwa kukejeli, lakini bado adhma yake ilikuwa nzito ndani ya kejeli hiyo.

    “Naogopa,” Rose alijibedeuza.

    “Unaogopa na nini na hatokuwepo duniani? Au hunipendi?” Talib aliuliza akimtazama mwanamke huyo kwenye paji la uso.

    Rose aliona hiyo ndiyo fursa ya kuua mbweha. Aliyaminya macho yake kana kwamba amepaliwa na aibu, akatazama chini akitabasamu tabasamu pana. Basi Talib akajikuta anahisi kifua chake kimekuwa cha baridi. Mambo si ndo’ haya? Nafsi yake iliteta.

    “Rose, unaweza ukawa na mimi?”

    Rose kimya. Aliacha kula sasa akawa anatazama vidole vyake alivyokuwa anaviminya. Ushawahi kumtongoza mwanafunzi? Basi ndivyo Rose alivyokuwa: fisi dhalimu ndani ya ngozi ya kondoo!

    “Eti mama, unaweza ukawa na mimi? Au mie so’ kama Kessy?”

    “Talib, siwezi kukujibu swali lako kwa sasa,” Rose alifunguka. Alikuwa mjawa wa aibu nzito ambayo ilimfanya Talib azidi kuwehuka.

    “Sawa, mpenzi, ila natumai nina nafasi yangu kwako. Lakini sitakulazimisha uimulike upesi hivyo n’takupa muda zaidi.”

    Rose hakujibu, alitabasamu tu. Uso wake ukawa mweupe zaidi.

    “Usihofie kitu chochote, Rose. Kila kitu kipo chini yangu kwa sasa. Hauna haja ya kumhofia yeyote yule.”

    “Kweli?” Rose aliuliza akimtazama Talib kwa macho ambayo yanaweza msimisha kunguru kula mzoga.

    “Kweli nakuambia,” Talib akaapia. Utaanzaje kukataa mbele ya macho yale tekaji?



    ***



    Ni mida ya jioni, Al Saed anakaa mbele ya ikulu, makazi yake mapya. Hakuna mtu yeyote aliyeketi naye isipokuwa bakuli kubwa lililosheheni matunda ya kila aina likiwa limejaa kwenye meza ya ukubwa wa kawaida ikisheheni kwa urembo.

    Mwanaume huyo alikuwa amevalia gauni kubwa jeupe la kitamaduni, pamoja na kofia yake. Mkono wake wa kulia ulikuwa umekamatia fimbo ndefu ya mbao ikiwa inameremeta. Kweli alionekana ni mkubwa wa nchi, haikujalisha aliingiaje madarakani, alikuwa ana muonekano wa kuvutia na wa kimadaraka.

    Alikuna kidevu chake chenye ndevu za kumwaga akitazama ukutani kitafakuri. Kichwa chake kilikuwa kimebanwa na mawazo na kwa muda huo hakuwa anataka mtu yeyote amghasi. Akiwa anatafakari, alikuwa anakuna ndevu zake, muda mwingine akipindua mdomo wake mweusi, ama kuupeleka kando na kando.

    Ndani ya kichwa chake ni ajenda mbili zilimnyima raha. Mosi, ilikuwa ni kuhusu muelekeo wa utawala wake baada ya kukutana na vikwazo toka nchi kubwa za nje. Pili, ilikuwa ni kumhusu Kessy na afya yake. Ni siku kadhaa sasa, Kessy hajaamka toka kitandani. Alikuwa anamhitaji ampatie ushauri haswa kwa muda huu anaokumbana na taabu za ‘wazungu’ kwani yeye pekee ndiye mtu aliyekuwa anarandana naye, ama tuseme marafiki.

    Akiwa hapo anajinyima kwa ajili ya mawazo, mwanaume mrefu mweusi aliyevalia nguo za kijeshi alitokea nyuma yake akasimama umbali wa kama hatua tatu kabla hajamuita Al Saed kwa taadhima.

    “Unasemaje, Man?” Aliuliza Al Saed pasipo kumtazama anayemuita.

    “Kuna ujumbe wako,” alisema mwanaume yule, kwa jina Man. Uso wake ulikuwa umejawa na makovu. Mwili wake ulikuwa kakamavu na ulioshiba mazoezi ya viungo.

    “Kutoka kwa nani?”

    “Sijajua ni nani. Amejitambulisha kwa jina la Mr. X.”

    “Mr X?”

    “Ndio.”

    “Ni ujumbe wa aina gani?”

    “Barua pepe.”

    Al Saed alitulia kwanza, kisha akajibu:

    “Sawa, nakuja.”

    Yote hayo aliyasema akiwa hamtazami Man. Alichukua kama dakika dakika tano ndio akanyanyuka kwenda kuukuta ujumbe wake. Haukuwa umefunguliwa, ilikuwa ni barua pepe ila haikuonyesha umetoka kwa nani, yani haikujulikana mtumaji ni akaunti gani!

    Al Saed alibofya ujumbe huo uliokuwa umejaa kwenye kioo cha tarakilishi yake mpakato ya kisasa kabisa. Ndani yake akakuta maneno machache, kama mistari mitatu tu:

    “Kwa usalama wako na wa wananchi wasio na hatia, tangaza taifa kuwa la kiislamu.”

    Moyo wa Al Saed ukalipuka. Alijitahidi kujibu ujumbe huo kwa kuuliza ni nani mtumaji lakini ujumbe haukufanikiwa kwenda. Kila alipotuma uligoma akapewa taarifa ya kuweka akaunti ya mtumaji kwanza. Man naye alijaribu kama atang’amua tatizo, akashindwa.

    Al Saed alirudi zake alipokuwepo mwanzoni akaketi na kuendelea kutweta kwa mawazo, sasa yakiwa yameongezwa maradufu. Aliwaza Mr X ni nani, amepataje akaunti yake ya barua pepe? Anataka nini?

    Mwishowe kichwa chake kikawa chepesi kuamua inawezekana akawa ni Odong; mwanaume mnaijeria aliyekuwa kwenye kikundi chao cha uasi, Le tueurs, mpaka pale alipokuja kujinasua toka kwenye kikundi hicho yeye pamoja na wenzake kumi na tatu baada ya kukinzana kwenye namna ya kutenga misingi ya kikundi. Odong na wenzake walitaka kikundi kiwe na mrengo na itikiadi yenye Imani kali ya kiislamu kitu ambacho Al Saed na wenzake walipinga kwakuwa taifa lao lina watu wa dini zote, na si tu huko bali hata kundini pia.

    Tangu pale walipojing’amua toka kwenye kikundi hicho cha Le tueurs, haikujulikana Odong na wenzake walielekea na wapo wapi. Al Saed alishawasahau watu hao, ila baada ya barua pepe ile sasa anawakumbuka kwa haraka mno. Lakini pia anahofia.

    Baadae usiku wa saa nne, Al Saed anaketi kikao na wanaume watatu ndai ya kajieneo kadogo ndani ya ikulu. Kikao hicho hakikuwepo ndani ya ratiba yake bali kilikuwa ni dharura, tena ikiwa imeitishwa na msimamizi wa ulinzi, Samweli, akiwa na makachero wake wawili: Bui na Tariq.

    Ilikuwa ni ajenda nyeti ya usalama. Hata kabla Samwel hajafungua mdomo, tayari Al Saed alilijua hilo. Alitulia tuli kusikiliza.http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Mkuu, kuna jambo linalotishia amani,” Samweli alitambulisha, kisha akaongezea: “Upande wa kusini mwa nchi tumepata taarifa kuna kikundi kinachojiita AMAA – Alwaqt min ajil alttaharrur. Hatujajua makazi yake ni yapi na kinaongozwa na nani, ila watu wanakiongelea. Ni cha siri mno kiasi kwama ni ngumu sana kupata taarifa zake kwa kina.”

    Haraka kichwa cha Al Saed kikarejesha mawazo kwenye ile barua pepe. Mr X ni mhusika wa hicho kikundi? Alijiuliza. Hakutaka kusema kwa wale watumishi wake juu ya ile barua pepe. Aliwaagiza wakalifanyie kazi hilo swala kwa umakini zaidi kabla halijakuwa kubwa na hatarishi zaidi.

    Alienda akanywa mvinyo wa kutosha maana ndiyo pekee iliweza kumpumzisha toka kwenye mkanda wa mawazo uliokuwa umembana.



    Masaa nane baadae, Guinea:



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog