Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KIAPO CHA JASUSI - 4

 





    Simulizi : Kiapo Cha Jasusi

    Sehemu Ya Nne (4)





    “Kuna nini darling? akauliza Dr Mboki



    “Usijali ni masuala ya kikazi” akajibu rais kwa kifupi



    “Nimesikia ukimuagiza IGP atumie kila uwezo alio nao kuhakikisha mtu huyo anapatikana.Ni nani unamtafuta kwa nguvu kubwa namna hiyo?Ni jambazi sugu? Akauliza Dr Mboki.Rais akatafakari kidogo halafu akasema



    “Ni mkuu wa gereza la Markubelo kamishna Dastan ndiye anayetafutwa”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Anatafutwa kwa kosa lipi? Akauliza Dr Mboki



    “Anatafutwa kwa mambo mawili.Kwanza kuna mauaji yamefanyika gerezani usiku wa leo na watu nane wamefariki dunia.Bado haijajulikana kama watu hao ni majambazi au walikuwa na nia nyingine ovu.Kama unavyofahamu gereza lile wanafungwa watu maalum hasa majambazi sugu,magaidi na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.Tunahisi labda watu hao walikuwa na lengo la kumtorosha mmoja wa wafungwa kama vile tunavyoona mambo kama hayo yakitokea katika magereza makubwa ya nje ya nchi.Tunataka kumuhoji Zaidi Dastan ili tufahamu watu hao ni akina nani na nini lengo lao kwani ni yeye ndiye aliyepambana nao”



    “oh kumbe ni suala dogo kama hilo?Hupaswi kuumiza kichwa Darling hiyo ni kazi ya polisi.Waachie waifanye kazi yao na wewe shughulikia masuala makubwa ya nchi.Mimi nilidhani labda kuna suala kubwa limetokea kumbe ni hilo,usiwaze sana hilo ni suala dogo sana” akasema Dr Mboki



    “Kuna jambo lingine kuhusiana na huyu Kamishna Dastan” akasema Dr Enock na kunyamza kidogo akamtazama mke wake na kusema



    “Taarifa zake hazionekani katika taarifa za watumishi wa umma”



    “Hakuna taarifa zake?Inawezekanaje?akauliza Dr Mboki



    “Hilo ndilo jambo la kushangaza.Nilimpigia simu inspekta jenerali wa magereza nikamtaka anipatie taarifa za Dastan na muda mfupi baadae akajiua kwa kujipiga risasi.Hii inazidisha udadisi zaidi kuhusiana na huyu mtu na ndiyo maana ninahitaji apatikane kwa haraka ili tujiridhishe na mtu tuliye naye na tufahamu kwa nini hakuna taarifa zake?Analipwa vipi?Ameipataje nafasi hii kubwa ya kuwa mkuu wa gereza muhimu kama Markubelo? Akauliza rais



    “Kweli hili si suala dogo lakini naviamini vyombo vya usalama vitalishugulikia na ukweli utajulikana.Lazima taarifa zake zipo yawezekana hazijatafutwa vizuri.Nakushauri kesho omba taarifa kutoka wizara zote zinazohusiana na watumishi wa umma ukianza na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.Kwa sasa tupumzike na tuviache vyombo vya usalama vifanye kazi yake” akasema Dr Mboki na kumkumbatia mume wake





    *************





    Range rover evogue rangi nyeusi ilipunguza mwendo na kuingia katika barabara iliyoelekea katika jumba kubwa la kifahari lililokuwa linawaka taa nyingi.Lilikuwa ni kasri lililopendeza mno kwa usiku huu.Nje ya jumba lile kulikuwa na walinzi wawili waliovalia sare maalum ashati meupe na suruali nyeusi na wote wakiwa na bunduki.Gari lile likasimamishwa kwa umbali wa mita kadhaa na walinzi wale wakalikagua gari lile kwa kutumia chombo maalum cha ukaguzi na halafu geti likafunguliwa gari lile likaruhusiwa kupita na kuingia ndani hadi katika maegesho.Dereva wa gari lile akamuamuru mtu aliyekaa kiti cha pembeni yake ashuke kwani walikuwa wamefika mahala walikokuwa wakielekea kisha akamuongoza wakaingia ndani wakakaribishwa sebuleni na mwanadada mrembo mwenye tabasamu la kuvutia sana.Akawakirimu vinywaji na baada ya kama dakika sita hivi akatokea mwanamama mmoja mrembo sana aliyekuwa akitembea kwa mwendo wa maringo kama vile hataki kukanyaga ardhi.Alikuwa mrefu wastani na mwenye weupe wa kung’aa.Nywele zake ndefu zenye weusi wa kung’aa zilizidisha uzuri wake.Umbo lake lilikuwa jembamba na la kuvutia.Alikuwa ni mwanamke aliyeumbwa akaumbika hasa.



    “Adam karibu sana” akasema yule mwanamama ambaye alipotabasamu uzuri wake ukaongezeka mara dufu

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Ahsante sana madam Paula ” akasema yule dereva aliyejulikana kwa jina la Adam



    “Madam Paula mgeni huyu hapa amefika salama” akasema Adam



    “Ahsante sana Adam kwa kumfikisha salama.Dastan karibu sana jisikie uko nyumbani” akasema Paula huku akitabasamu



    “Ahsante sana madam Paula” akajibu Dastan



    “Adam ahsante kwa kumfikisha mgeni wangu salama.Sasa unaweza kwenda” akasema Paula na Adam akainuka akaondoka



    “Dastan pole sana kwa safari ya usiku huu.Carmelita yuko nje ya nchi ila kesho atarejea na ameniagiza nihakikishe kwamba unakuwa salama hadi atakaporejea hapo kesho.Usihofu kuhusu usalam wako hapa ni mahala salama Zaidi ya usalama.Sitaki nikuchoshe kwa maongezi mengi naomba nikupeleke moja kwa moja katika chumba cha kulala ukapumzike hadi kesho” akasema Paula na kusimama akamuongoza Dastan hadi katik chumba kimoja kikubwa na kizuri.



    “Utalala humu chumbani.Muda wowote ukihitaji kitu chochote nijulishe kwa kunipigia simu ile pale mezani.Nimeelekezwa vile vile kwamba kuanzia sasa uzime smu yako na usitumie kifaa chochote cha mawasiliano.You are going dark from now” akasema Paula



    “Tayari nimekwisha ingia gizani muda mrefu.Ahsante Paula unaweza kwenda.I need to be alone for now” akasema Dastan na Paula akaondoka.Dastan akakaa kitandani na kuzama mawazoni



    “Hatimaye nimeimaliza kazi ambayo imenichukua muda mrefu zaidi ya nilivyotegemea.Zaidi ya miaka saba nimekuwa Tanzania nikiifanya kazi hii.Ni wakati wanbgu sasa wa kwenda kuungana na familia yangu ambao hawajaniona kwa kipindi hiki chote japo tumekuwa tukiwasiliana kwa simu na mtandao wa skype.” Akainuka akavua viatu na kingie bafuni kujimwagia maji halafu akarejea tena kitandani



    “Sikutegemea kama mwisho wa kazi yangu ungekuwa namna hii.Nilitegemea ningeimaliza kazi yangu na kupotea kama upepo lakini imekuwa tofauti kwani suala la mzee Alfredo limetibua kila kitu na sasa wanaanza kunitafuta wakitaka kufahamu mimi ni nani.Tayari wamekwisha nitilia shaka na ndiyo maana rais akamtaka Dr Isaack amtumie taarifa zangu.Sijui Dr Isaack atamueleza nini rais lakini hayo si masuala yangu.Katika mkataba wanu na wao tulikubalina kwamba wao watahakikisha wananilina na kila hatari na mwisho wahakikishe ninarejea salama nyumbani kuungana na familia yangu.Ametekeleza jukumu lake la kunitaka nimalize kazi yangu na kuondoka hivyo masuala yay eye na rais kuhusu taarifa zangu atayamaliza yeye mwenyewe.Ninachokisubiri ni kesho nimkabidhi madam Carmelita majibu ya kazi yao kisha niondoke zangu nikapumzike.Imekuwa ni kazi ndefu sana na ya hatari lakini ninashukuru nimeikamilisha vyema.Nimetengeneza marafiki wengi hapa Tanzania na nimetokea kuipenda sana hii nchi.Ina watu wakarimu na wenye upendo mkubwa” akaendelea kuwaza Dastan na taratibu kijiusingizi kikaanza kumchukua akalala







    **************







    Ni saa kumi na mbili za asubuhi,tayari mitaa ya jiji la Dar es salaam ilikwisha furika watu wakianza harakati za kuyakabili majukumu yao ya siku.Hakukuwa na taarifa zozote katika magazeti kuhusiana na mauaji ya watu nane yaliyotokea katika gereza la Markubelo.



    Ikulu jijini Dar es salaam,rais Dr Enock alitoka katika chumba cha mazoezi akaenda chumbani kwake kujiandaa kwa ajili ya kuanza majukumu yake ya siku. Akiwa chumbani simu yake ikaita alikuwa ni mkuu wa jeshi la polisi.



    “Habari za asubuhi IGP”



    “Habari nzuri mheshimiwa rais”



    “Nipe ripoti.Mmefanikiwa kumpata kamishna Dastan?akauliza Dr Enock



    “Mheshimiwa rais kwa taarifa nilizozipokea muda mfupi uliopita kutoka kwa kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam ambaye ndiye anayesimamia zoezi hilo,bado kamishna Dastan hajapatikana ila juhudi za kumtaf…….”



    “Mheshimiwa IGP” akasema Dr Enock na kumkatisha Inspekta jenerali wa polisi



    “Usiku uliniahidi kwamba haitafika asubuhi Kamishna Dastan atakuwa amepatikana lakini tayari jua limechomoza na bado hajapatikana.Hii inaonyesha huna uhakika na kazi yako”



    “Mheshimiwa rais vijana wamesambazwa kila kona kumtafuta Dastan na wamekesha wakifanya kazi hiyo ila hawajafanikiwa kumpata.Askari Zaidi wataongezwa asubuhi hii ili kuongeza nguvu katika msako.Nakuhakikishia mheshimiwa rais kwamba Dastan atapatikana.Ninakutana na makamanda wangu asubuhi ya leo na kuweka mikakati mizito namna ya kuweza kumpata”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “IGP ninakuamini sana na sina shaka na uwezo wako.Ninaomba ulifanye suala hili kuwa kipaumbele namba moja kwa siku ya leo na jeshi la polisi litumie kila aina ya uwezo lilio nao kumsaka Dastan na kumpata.Nina uhakika mkubwa kwamba yupo hapa hapa Dar es salaam kwa hiyo ufanyike msako mkali hata ikibidi kukagua nyumba hadi nyumba mimi sina tatizo ili mradi Dastan apatikane.Ulinzi uimarishwe katika sehemu zote za kuingilia na kutokea jijini Dar es salaam ili Dastan asiweze kutoka nje ya Dar es salaam.Ninataka mpaka kufika saa sita mchana siku ya leo nipate taarifa kwamba tayari Dastan amepatikana.Jeshi la polisi ni imara sana na haliwezi kushindwa na mtu mmoja.Sambaeni kila kona na mhakikishe Dastan anapatikana siku ya leo.Umenielewa IGP? Akasema rais



    “Nimekuelewa mheshimiwa rais na ninakuahdi kufuata maelekezo yako na Dastan atapatikana”akasema IGP



    “Good.Vipi kuhusiana na Dr Isaack mmefanikiwa kuipata laini yake ya simu?akauliza Dr Enock



    “Laini ya simu ya Dr Isaack imetafutwa sana lakini haijapatikana ndipo mwili wake ukafanyiwa vipimo na kuna vitu vikaonekana tumboni kama chembe chembe za plastiki na bati.Mwili ukapasuliwa na kukutwa vipande vidogo vidogo na bati dogo ambavyo vinatufanya tuamini kwamba kabla ya kujiua Dr Isaack aliitafuta laini yake ya simu na kumeza vipande vyake.”akasema IGP na kumfanya Dr Enock abaki kimya kwamuda halafu akasema



    “IGP endeleeni na msako na muhakikishe leo hii Dastan anapatikana na kama niliyoelekeza pindi akipatikana aletwe kwangu mara moja na kama kuna suala lolote litajitokeza ambalo si la kawaida nijulishe haraka sana”



    “sawa mheshimiwa rais nitafanya hivyo”



    “Good” akajibu Dr Enock na kukata simu akazama katika mawazo



    “Huyu Dastan ni mdudu wa aina gani? Kwa nini amejitokeza ghafla nakuanza kuumiza vichwa vya watu namna hii? Nini mahusiano yake na Dr Isaack ambaye alijuia mara tu nilipomtaka aniletee taarifa zake? Kwa nini ameitafuna laini yake ya simu kabla ya kujiua? Haya ni maswali ambayo endapo tukifanikiwa kuyapatia majibu tutapata picha kubwa.Kuna mambo yanaendelea hapa chini kwa chini ambayo hatuyafahamu.Ninamuamini IGP ni mtu wa kazi na nina hakika leo hii Dastan lazima atapatikana.Siamini kama jeshi la polisi wanaweza wakashindwa kumpata mtu mmoja” akawaza na kuchukua simu akampigia Noah



    “Shikamoo mzee” akasema Noah baada ya kupokea simu



    “Noah kuna lolote mmefanikiwa kulipata kuhusiana na Dastan? Akauliza Dr Enock.



    “Hapana mzee bado hatujafanikiwa kupata chochote kuhusu huyu mtu.Inashangaza kwani hakuna mahala kokote kwenye taarifa zake.Tumekesha tukifanya uchunguzi lakini mpaka sasa bado hatujapata chochote”



    Dr Enock akavuta pumzi ndefu na akafikiri kidogo na kuuliza



    “Huyu mtu ni nani?http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Mheshimiwa rais hilo ni swali ambalo hata sisi tumejiuliza Zaidi ya mara mia moja bila kupata majibu ila bado tunaendelea kulitafutia majibu.Asubuhi hii tunakutana kulijadili suala hili kwa mapana Zaidi kwani linaonekana ni suala kubwa na linahitaji uchunguzi mpana.Polisi wamefanikiwa kuipata laini ya simu ya Dr Isaack?akauliza Noah



    “Hapana hawajafanikiwa kuipata.Dr Isaack aliitafuna na kuimeza laini yake ya simu kabla ya kujiua.Hii inaonyesha kuna jambo hakutaka lijulikane.Ninachotaka mkifanye ni kupata rekodi za mawasiliano yote ya Dr Isaack ili tujue alikuwa anawasiliana na akina nani kabla ya kujiua”



    “Sawa mheshimiwa rais tutafanya hivyo.Ninaamini Dr Isaack hakujiua hivi hivi lazima ipo sababu kubwa iliyompelelkea akafanya vile.Nataka tuchunguze vile vile mahusiano yake na Dastan”



    “Good.Nitamuagiza waziri wa mambo ya ndani ya nchi aniletee taarifa za Dastan baadae leo na atakaponiletea nitawajulisha”



    “Mheshimiwa rais sina hakika kama taarifa hizo zipo.Tumepekua kila sehemu ambako tunahisi labda taarifa zake zitakuwepo lakini hatujafanikiwa kupata chochote”



    “Tusubiri kwanza tuone yawezekana akafanikiwa kuzipata kwani yeye ndiye kiongozi wa wizara hii ya mambo ya ndani ya nchi” akasema Dr Enock na kuagana na Noah







    **************





    Ibada ya kila siku asubuhi ilimalizika katika kanisa la Mt Elizabeth na Padre Thadei aliyeongoza ibada hiyo akasalimiana na waumini wachache halafu akaelekea sehemu ya kiungamishio kwa ajili ya waumini ambao walitaka kujitakasa kwa kuungama dhambi zao.Ibada hii ya asubuhi huwa inahudhuriwa na waumini wachache tu hivyo baada ya ibada kumalizika wengi waliondoka isipokuwa mwanama mmoja mweupe aliyevaa suti nyekundu iliyompendeza.Alionekana ni mwenye kujiweza sana kifedha kutokana na mavazi yake ya gharama.Akiwa ameshika kitabu chake cha sala mkononi akaelekea sehemu ya kiungamishio alikokuwapo padre Thade akaingia na kufunga mlango.



    “Hallo Mariana” akasema Padre Thadei kwa sauti ndogo sana



    “Father Thadei,anaendeleaje Anna Stella? Akauliza yule mwanamama ambaye padre Thadei alimuita kwa jina la Mariana



    “Hali yake nzuri kwa sasa na hana tatizo lolote.Vipi kuna maendeleo yoyote yamepatikana?akauliza Padre Thadei



    “Hapana.Mpaka sasa bado sijafanikiwa lakini ninaendelea na uchunguzi.Sintachoka hadi hapo ntakapohakikisha nimeipata dawa yake”



    “Jitahidi Mariana kwani jana Anna Stella amekamatwa na simu na baada ya upekuzi zimekutwa jumbe kadhaa akiwasiliana na kijana mmoja anaitwa Gidion na inaonekana wawili hawa wanaelekea katika kuanzisha mahusiano ya kimapenzi.Tumegundua huyo kijana ni mtoto wa waziri Stanley Msimbe” akasema Padre Thadei



    “Nitajitahidi Padre Thadei ila nakuomba ufanye kila linalowezekana kuhakikisha kwamba Anna hajiingizi katika masuala ya mapenzi”akasema Mariana



    “Kuna suala lingine pia” akasema Padre Thadei



    “Jana nimepigiwa simu na mkuu wa gereza la Markubelo akanieleza kwamba Dr Alfredo amefungwa pale”



    “Oh my God ! akasema Mariana na kushusha pumzi akamtazama padre Thadei kwa macho ya mshangao.Zilikuwa ni taarifa ambazo hakuwa ametegemea kuzisikia



    “Unamuamini huyo mtu aliyekupa taarifa hizo?



    “Ndiyo.Kuna ujumbe amepewa na mzee Dr Alfredo aufikishe kwangu” akasema padre Thadei na kuichomoa simu kutoka katika kanzu yake na kumuonyesha Mariana ujumbe uliotoka kwa Dastan.Mariana akausoma na kudondosha machozi



    “Mariana tafadhali fanya kila linalowezekana kuhakikisha unaonana na baba yako.Ujumbe huu ni mzito sana”akasema padre Thadei.Mariana akausoma tena halafu akamrejeshea padre Thadei simu yake



    “Ahsante sana baba Padre.Nitajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili nipate nafasi ya kumuona baba.I have to go now” akasema Mariana



    “Mariana subiri kidogo” akasema Padre Thadei



    “Nadhani unafahamu kuwa kitendo cha kufahamu mahala alipo Dr Alfredo kimetuweka katika hatari kubwa na ninaamini hata huyo mkuu wa gereza ambaye ametupa taarifa hii naye atakuwa katika hatari.Kwa kuwa tayari umekwisha upata huu ujumbe ninaufuta kabisa katika simu yangu na hata namba ya simu ya mkuu wa gereza.Hii ni kwa ajili ya usalama wetu”akasema padre Thadei na kuifuta picha ile ya ujumbe wa Dr Alfredo pamoja na namba ya simu ya Dastan



    “Ninalifahamu hilo father Thadei na nitachukua tahadhari.Uwe na siku njema” akasema Mariana na kuinuka akafungua mlango akatoka.Nje ya kiungamishio kulikuwa na watu wawili wamekaa katika kiti wakisubiri zamu yao ya kuingia.Mmoja wao alipomuona Mariana ametoka naye akasimama na kuingia.Padre Thadei hakumuona mtu aliyeingia katika kiungamisho kama ilivyo desturi ya kutomtazama usoni muungamaji.Wakati akiendelea kumuombea mara akahisi kitu cha baridi kinagusa sikio lake.Akafumbua macho kutazama nini kilimgusa akajikuta akitazamana na bastora iliyofungwa kiwambo.Padre Thadei akatetemeka.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Relax father” akasema yule jamaa kwa sauti ndogo



    “Unataka nini? Akauliza padre Thadei



    “Nina jambo moja ambalo nataka unieleze ukweli.Unamfahamu huyo mwanamke aliyetoka hapa kuungama muda si mrefu?



    Padre Thadei akasita kujibu



    “Father nakuuliza unamfahamu?



    “Ndiyo namfahamu.Anaitwa Mariana”



    “Kila siku amekuwa akija hapa kanisani asubuhi na kila ibada inapomalizika amekuwa akiingia katika chumba hiki.Kuna nini kinaendelea kati yako naye?



    “Chumba hiki ni kwa ajili ya waumini kuungama dhambi zao.Mariana ni mmoja wa waumini ambaye huja kuungama dhambi zake kila ibada inapomalizika.Ni mtu ambaye hupenda kujiweka karibu na Mungu kila siku”akajibu padre Thadei na yule jamaa akavua miwani na kumtazama kwa macho makali



    “Una hakika padre?



    “Ndiyo nina uhakika”



    “Huungama dhambi gani kila siku?



    “Kwa kawaida maungamo ni siri kati ya muumini na Mungu kupitia kwa mtumishi wake ambaye ni padre hivyo hatuwezi kutaja dhambi za mtu”



    “Father nitazame vyema! Akasema yule jamaa na padre Thadei akamtazama usoni



    “Bastora hii ina kiwambo cha risasi na ina risasi ishirini,zote zitaingia katika kichwa chako endapo hautatupa majibu tunayoyahitaji.Nieleze tafadhali ni dhambi zipi ambazo Mariana huja kuungama hapa kila siku?



    “Kwa hilo siwezi kukueleza hata kama utaniua” akasema padre Thadei na yule jamaa akausogeza mkono wake uliokuwa na saa ya mkono karibu na mdomo wake halafu akasema



    “Take him”



    Mara mlango wa chumba alimokuwamo padre Thadei ukafunguliwa akaingia mtu mmoja akiwa amevaa suti ya bluu na kumtaka padre Thadei asimame



    “Utaongozana nasi na usithubutu kupiga kelele zozote”



    “Nini hasa mnakitaka ? akauliza Pare Thadei



    “Inuka twende” akasema yule jamaa na kufunua koti akamuonyesha padre Thadei bastora.Bila ubishi padre Thadei akasimama na kutoka nje ya kile chumba akaongozana na yule jamaa.Kulikuwa na watu wengine wawili wakaungana na wale jamaa na kumuweka padre Thadei kati kati wakatoka nje ya mlango mkuu wa kanisa na walipofika kibarazani gari moja yenye vioo vyeusi ikasogea taratibu na mara kukatokea tukio la ghafla ambalo hawakuwa wamelitegemea.



    Padre Thadei aligeuka kama kima na kumpiga ngumi mmoja wa wale jamaa na kwa wepesi wa aina yake akaichomoa bastora ya yule jamaa lakini kabla hajageuka ili kuwakabili wengine tayari mvua ya risasi ilimnyeshea akaanguka chini.Watu wale baada ya kumuona padre Thadei ameangukia chini huku damu nyingi ikimtoka wakakimbia haraka katika gari lao na kuondoka kwa kasi kubwa.Watu ambao bado walikuwa eneo lile la kanisa walishuhudia kilichotokea na kupiga kelele za kuomba msaada na wengine wakapiga simu polisi.Padre Thadei akachukuliwa haraka na kukimbizwa katika hospitali ya kanisa kwa ajili ya huduma ya kwanza lakini daktari alipompima tayari alikwisha fariki.Polisi wakafika kwa haraka lakini wale jamaa walikwisha toweka kitambo.



    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Katika ukumbi mdogo wa mikutano ndani ya jengo la ofisi za gazeti la Beautiful Tanzania watu ishirini na tano walikuwa wameizunguka meza kubwa tayari kwa kikao cha dharura.Mlango ukafunguliwa na Noah akaingia akaenda kuketi mbele ilipo nafasi yake.



    “Jamani habari za asubuhi” akawasalimu na wote wakaitika



    “Nimewaiteni hapa kwa dharura kutoka na suala moja lililojitokeza ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa haraka sana.”akanyamaza kidogo akasimama na kuelekea katika runinga kubwa iliyokuwa mbele ya ukumbi ule



    “Jana usiku tumewapoteza wenzetu nane niliowatuma kwenda katika kisiwa cha Markubelo.Tulipata taarifa kwamba mkuu wa gereza la Markubelo amepewa ujumbe na Dr Alfredo aupeleke sehemu Fulani na ujumbe huo aliupeleka kwa njia ya simu.Ili kufahamu ujumbe huo aliutuma kwa nani ilitulazimu kufanya mkakati wa haraka wa kuipata simu yake na nikawatuma wenzetu nane waende huko gerezani na walipofika huko wote wakauawa.Wanne waliuawa na Dastan na wengine wanne wakauawa na askari magereza ambao walidhani watu wale walikuwa wavamivi wa gereza.Baada ya kitendo hicho kutokea tulianza kumchunguza Dastan ni nani lakini hatukufanikiwa kupata taarifa zake zozote kutoka katika orodha ya watumishi wa umma.Nilimjulisha mheshimiwa rais na akamuelekeza mkuu wa magereza ampelekee taarifa zote za kumuhusu Dastan lakini dakika chache baadae inspekta jenerali wa magereza akajiua kwa kujipiga risasi.Nilikwenda na baadhi ya wenzenu hadi eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uchunguzi lakini tukagundua kwamba laini ya simu haikuwepo katika simu yake.Kwa taarifa nilizozipata asubuhi ya leo kutoka kwa rais ni kwamba laini hiyo imekutwa tumboni.Inaonekana aliitafuna kabla ya kujiua.Hii inatupa picha kwamba kuna mambo ambayo hakutaka yajulikane kutoka katika laini ile ya simu”akanyamaza akameza mate halafu akaendelea



    “Rais alimuagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini atume kikosi kiende gereza la Markubelo usiku huo huo kumchukua Dastan lakini taarifa walizozipata baada ya kufika ni kwamba Dastan aliondoka gerezani hapo muda mfupi kabla ya kikosi hicho kuwasili na ameelekea Dar es salaam.Imefanyika jitihada kubwa usiku kucha kumsaka lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yoyote.Dastan bado hajapatikana.Inasemekana alionekana na wavuvi pwani ya Dar es salaam akiingia katika gari moja usiku na kutokomoea kusikojulikana” akanyamaza tena



    “Nimezungumza na rais asubuhi ya leo na ametoa maelekezo kwamba tuhakikishe kwa kila namna tunafahamu mahala alipo Dastan.Tunapaswa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha kwamba Dastan anapatikana.Sisi tunao uwezo mkubwa sana wa kuweza kumpata kuliko chombo kingine chochote.Hatujawahi kushindwa kitu chochote na nina Imani hata huyu Dastan lazima atatua mikononi mwetu muda si mrefu.Kazi yetu kubwa ni kufahamu mahala alipo,tunapaswa kufahamu ujumbe ule aliupeleka kwa nani na tatu tunapaswa kuchunguza kama yeye na Dr Isaack inspekta jenerali wa magereza aliyejiua wana mahusiano.Hakikisheni mnapata rekodi za mawasiliano ya mwisho ya Dr Isaack ili tujue aliwasiliana na nani na waliwasiliana kitu gani.Tulichimbe suala hili kiundani Zaidi na tupate majibu.Mheshmiwa rais anasubiri majibu kutoka kwetu.Kila mmoja aweke pembeni kazi zote na tulishughulikie kwanza jambo hili.Nataka nipate taarifa kila baada ya nusu saa.Kumbukeni lazima lengo kubwa hapa ni kumpata Dastan.Kuna yeyote mwenye swali?akauliza Noah na mmoja akanyoosha mkono



    “CT15 Jenny uliza swali lako”akasema Noah



    “Mkuu nadhani njia rahisi ya kuweza kumpata huyo Dastan ni kwa kutumia simu yake.Unazo namba zake za simu?



    “Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba Dastan alikuwa na simu ya mkononi ya ofisi ambayo ndiyo inayofahamika na ndiyo anayoitumia kwa shughuli za kiofisi lakini vile vile alikuwa na simu nyingine aliyoitumia kwa shughuli zake binafsi na mpaka sasa bado hatujafanikiwa kuipata namba hiyo.Wakati tunaendelea kuitafuta hiyo namba katika mitandao ya simu,tuchunguze kwanza kama Dastan na Dr Isaack wana mawasiliano yoyote na tutaligundua hilo kama tutachunguza mawasiliano yote ya Dr Isaack.Nahitaji mpaka saa nne,niwe tayari na jibu la kumpa rais kwani anasubiri jibu kutoka kwetu.Let us get to work”akasema Noah na wote wakatawanyika kwenda kuanza kazi waliyopewa





    *************

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Mariana alifika nyumbani kwake na kuelekea moja kwa moja chumbani akakaa kitandani na kuchukua kitambaa akajifuta machozi.



    “Finaly I know where my father is” akasema kwa sauti ndogo na kuinua kichwa akatazama juu



    “Ahsante Mungu kwa kunisaidia nimeweza kufahamu mahala aliko baba yangu.Nimemtafuta kwa muda mrefu na hatimaye leo nimefahamu mahala alikofungwa” akafuta tena machozi halafu akasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani



    “Sitakiwi kupoteza muda lazima nitafute namna ya kuonana na baba haraka sana kwani kama alivyoelekeza katika ujumbe kuwa anaumwa na anaweza akafariki muda wowote.Kuna mambo mengi ya muhimu nahitaji kuyafahamu kutoka kwake” akawaza halafu akafunua zuria na kutoa mfuniko wa kigae kukatokea shimo dogo ambalo ndani yake kulikuwa na kasiki.Akaandika namba na kasiki likafunguka akatoa simu akaiwasha na kuzitafuta namba Fulani akapiga



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog