Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

NYUMA YAKO (4) - 4

 





    Simulizi : Nyuma Yako (4)

    Sehemu Ya Nne (4)







    Walipoondoka naye akawasha gari yake na kutimka. Basi baada ya muda kidogo Mahmoud na wenzake wakawa wamezama ndani kwa tahadhari. Kama walivyotaraji, wakawekwa chini ya ulinzi na watu kumi waliokuwa wamebebelea bunduki kisha wakalazimishwa kunyamaa na kusalimisha silaha zao.



    Walipofungwa, Abdulaziz akatokea akiwa anatabasamu pana. Akawatuhumu watu hao kwa ujinga na kudanganyika kiurahisi.



    “Sikutaraji kama kazi hii ingekuwa nyepesi kiasi hiki,” akasema Abdulaziz kwa dhihaka. “Nalijua ningetumia rasilimali nyingi na muda. Kumbe ningejichosha tu!”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Aliposema hayo akamjongea Kelly na kumtazama kwa ukaribu. Alimshika mashavu mwanamke huyo na kumweleza;



    “Samahani sana. Ulichagua upande usio sahihi! Ningalikusamehe ila umekawia sana kwa sasa.”



    Pua ya Kelly ilikuwa inanusa mkono wa Abdulaziz. Mwanamke huyo alihisi harufu kali kiasi kwamba akalazimisha kuchoropoa kichwa chake toka kwenye mkono katili wa Abdulaziz. Alikuwa anahisi kutapika. Mkono ulikuwa unanuka damu!



    Abdulaziz akadhihaki kila mmoja na mudawe kisha akaamuru watu hao wafungiwe ndani kwani hana haraka ya kuwamaliza. Huenda akapata matumizi yao hapo mbeleni.



    Basi Mahmoud na wenzake wakatupiwa ndani ya chumba chenye mwanga hafifu. Madirisha madogo yalikuwa juu kabisa yakipitisha mwanga wa jua kwa kubagua.



    Mara Marietta akamuuliza Kelly, “Vipi, umefanikiwa?”



    “Ndio,” Kelly akajibu akitikisa kichwa. “Kila neno lake nimelirekodi vema.”



    Kiunoni mwa mwanamke huyo kulikuwa na kifaa kidogo kilichokuwa kinanasa sauti.



    “Sasa wale watakuja muda gani?” akauliza Mahmoud. Kidogo alikuwa ana shaka. Alijiuliza kama mule chumbani mtakuwa ndo hatma yao, lakini tofauti kabisa na yeye, Marietta alikuwa amejawa na imani. Hakuona haja ya kuhofia. Yeye alikuwa anajua wakina Marshall wata--



    Mara wakasikia kishindo.



    Huko nje wanaume walikuwa wameshadondoshwa kimyakimya. Tayari Marshall na Danielle walikuwa wameshafika ndani ya eneo na kufanya kazi kwa ustadi. Walikuwa wamelenga kufanya kila kitu ndani ya ukimya lakini ndani muda mfupi mpango wao huo ukafeli, iliwabidi watumie risasi kuwafyatulia baadhi ya walinzi waliokuwapo mbali haswa baada ya kuonekana.



    Risasi zilitupwa haswa, Marshall na Danielle wakitumia ujuzi wao wa kijeshi wakakakwepa na kuwalenga walengwa kwa ufasaha. Ndani ya muda mfupi wakawa wameshikilia eneo hilo kwa ukubwa. Walikuwa wameshawamaliza maadui zao kwa kiasi kikubwa.



    Basi wakasonga zaidi lakini kwa tahadhari sana. Bunduki zao zilikuwa zimebanwa vema mkononi na macho yao yamekodoa kuangaza.



    “Mkuu, twende upesi! Tumezidiwa!” alikuwa ni mwanajeshi akimsihi bwana Abdulaziz aliyekuwapo ndani. Mwanajeshi huyo alikuwa ametokea nje hivyo anajua hali halisi. Kidogo bwana Abdulaziz akasita. Hakuamini kama ameshindwa. Alikuwa anaona kuondoka hapo ni kujidhalili na kujishusha.



    Basi akiwa ametingwa na hasira, akakwapua bunduki yake na kunyanyuka aende kuwamaliza wakina Mahmoud kabla hawajakombolewa.



    “Watawakuta wenzao wakiwa maiti!” akafoka akikoki silaha, lakini hakukuwa salama huko anapoenda. Kufikia kile chumba ingempasa apite mahali ambapo pangehatarisha maisha yake kama akionekana na adui.



    Mmoja wa wajakazi wake akamtahadharisha kuhusu hilo. Hakutaka kusikia. Akarusha mguu wake kujiendea. Alipofika mahali pa wazi akatambua ni ngumu kukatiza hapo baada ya risasi mbili kutupwa aliponyoosha mguu.



    “Shit!”



    Alijaribu kutazama punde risasi ikapunyua ukuta, upesi akajirudi. Hakuwa na uhakika maadui walikuwa wangapi. Basi upesi akawarudia watu wake na kuwataka watimke upesi.



    **



    “Mko salama!” Marshall aliuliza akiwa anamfungua Mahmoud kamba. Danielle naye akainama kuwasaidia wengineo. Wote walikuwa salama.



    “Mmemdhibiti Abdul?” Mahmoud akauliza.



    “Hapana,” Marshall akamjibu, “Amefanikiwa kutoroka!”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Basi wakatoka hapo na kutokomea. Ndani ya masaa manne, wakitumia msaada wa maelezo toka kwa Jack Pyong, wakafanikiwa kumtia mikononi bwana Ramadan. Bwana huyo alikuwa anatorokea nchi jirani kujinusuru na kikombe cha kifo cha Aziz.



    Pamoja naye ilikuwa familia yake: mke na watoto wawili.



    “Sikufanya kwa kusudi!” akalia Ramadan. “Nisingefanya anachotaka basi anegeimaliza kabisa familia yangu. Sikuwa na namna nyingine. Niwieni radhi sana!”



    Wakamtoa shaka. Hawakuwa na haja ya kumdhuru bali kumtumia. Kifo chake kisingewapa manufaa yoyote yale. Lakini zaidi walimsihi kwamba akifanya kazi kwa moyo wote basi hatolazimika kukimbia nchi, jina lake litakuwa safi kwa mdhalimu kuwekwa bayana.



    “Unadhani itawezekana?” alikuwa ana mashaka. “Upande wote wa kabila lake sasa unamuunga mkono. Baba yake yu hoi kitandani na ndugu zake wengine hawana ushawishi kama ilivyokuwa kwake na kaka yake, Aziz.”



    “Itawezekana,” akasema Danielle. “Hakuna lisilowezekana. Cha muhimu ni kujua wapi tutampata Abdulaziz. Nadhani unaweza kutusaidia kwenye hilo.”



    “Bila shaka,” Ramadan akatikisa kichwa. “Nina huo uzoefu, najua karibia kila mahali ambapo kila kiongozi hufika ama kukaa.”



    “Basi itakuwa vema,” Marshall akahitimisha kabla hawajaichukua familia ya bwana Ramadan na kutimka.



    **



    Saa kumi na mbili jioni …



    “Unaweza ukaingia sasa,” alisema daktari punde baada ya kutoka ndani ya chumba. Hapo mulikuwa ni kasri kubwa ya mfalme. Daktari huyu bingwa wa magonjwa ya moyo alikuwapo hapa kwa muda akilipwa pesa ndefu kuzuia kifo cha mfalme wa Morocco. Ni kwa kitambo sasa yu hapa.



    Basi baada ya kauli hiyo, Abdulaziz akaamka toka kitini nje na kuzama ndani kwenda kukutana na baba yake aliyekuwa amejilaza kwenye kitanda cha kifo. Mzee huyo akiwa hapo hakuwa anaona tena thamani ya uongozi wake wala pesa yake. Alikuwa mwenyewe.



    Kitu pekee sasa anachokipigania kikiwa ni pumzi yake tu na vinginevyo. Ufalme wake haukuwa na msaada kwa wakati huo. Si pesa wala nafasi yake serikalini ingeweza kumrejesha kwenye afya yake isipokuwa Mungu peke yake aliyemuumba.



    Basi Abdulaziz akaketi pembeni ya kitanda na kumshika baba yake mkono wa kuume.



    “Baba,” akaita kwa sauti ya wastani. Kidogo baba akafungua macho yake kwa mbali kumtazama mwanaye. Mzee huyo alikuwa ameelemewa na mipira mwilini. Mdomo wake mkavu ulikuwa wazi. Kwa kumtazama tu ungelibaini hakuwa anasumbuliwa na moyo pekee, kuna mengine. Lakini hayo mengine yakiwa yamesababishwa ama kuchochewa na hili la moyo kwanza.



    “Abdul…” baba akaita kwa mbali na kisha akajaribu kutabasamu. Sauti yake ilikuwa kavu. Alikuwa akitumia nguvu nyingi kuongea, lakini pia alikuwa na furaha kumwona mwanaye pembeni yake. Hakuona tabu kujitutumua.



    “Abdul, kaka zako wanaendeleaje?” akauliza akijaribu kutabasamu. Abdul akamshika vema mkono wa baba yake na kunyamaza kwanza kwa kama sekunde nne. Alikuwa anawaza namna ya kujibu. Baada ya kupiga moyo konde akamweleza baba yake kwamba Aziz hayuko sawa.



    Hadhani kama anaweza kubeba majukumu ya kuwa mfalme hapo siku za usoni.



    Kidogo taarifa hiyo ikamshtua baba. Alikamata mkono wa Abdul kwanguvu kisha akahangaika kusema kwamba Aziz ndiye anayetakiwa kuwa mfalme. Ni yeye ndiye mwenye baraka naye hata kama akifa siku hiyo.



    “Vipi kama Aziz akifa?” Abdul akauliza. Macho yake yalikuwa makavu kumtazama baba yake.



    “Basi atatwaa Ilham,” baba akajibu kisha akauachia mkono wa Aziz. Aliona uchu ndani ya macho ya mtotowe. Akalia moyoni. “Abdul, hauwezi kuwa mfalme. Bado haujajiandaa,” baba akakoroma. Abdul asiseme jambo akanyanyuka zake na kwenda.



    Baba akatiririsha chozi. Kidogo kifaa cha kusomea mapigo yake ya moyo kikaanza kwenda mrama.



    Abdul alikaa nje ya chumba akitafakari. Muda si mrefu akampigia simu mmoja wa majamaa wake ndani ya jeshi kwa jina Masoud Saleh. Bwana huyo hakuwa mbali na alipo na Abdul, alikuwa tu chini ya jengo pamoja na wenzake hivyo upesi akaitikia wito. Alikuwa ni mwanaume mwenye mwili mrefu uliojaa. Alikuwa amevalia kombati na koti kwa juu.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Basi wakajadiliana na bwana huyo kwa muda wa kama nusu saa kabla Abdulaziz hajatikisa kichwa na kuchukua hatua kurejea tena ndani ya chumba alimo baba yake, lakini kabla hajafika daktari akamzuiza.



    “Hali yake sio nzuri. Ngoja kidogo!”



    Abdul hakutaka kungoja. Alimsukumia daktari pembeni akazama ndani. Alimkuta baba yake akiwa anavuja jasho, anatazama kwa kurembua kwa udhaifu.



    Akaita,



    “Baba.”



    Baba yake akamwazima macho na masikio.





    **



    Saa mbili usiku …





    Gari lilikuwa linaenda kwa kasi. Ndani yake upande wa dirishani kwenye viti vya nyuma Abdul alikuwa ameketi akiwa ameegemea dirisha. Alikuwa ana mawazo kichwani. Pembeni yake alikuwa ameketi bwana Masoud Saleh, mara kadhaa bwana huyo alikuwa akimtazama Abdul kisha asitie neno.



    Nyuma yao kulikuwa na magari mawili na mbele pia magari mawili yakiwaongoza.



    Baada ya muda kidogo, Abdul akamuuliza Masoud, “Sasa tunafanyaje?”



    “Tumeshafanya kila kinachotakiwa kufanywa kwa sasa. Wadugu wote wapo korokoroni, pia na jamal. Ni kitendi cha kungoja muda tu.”



    “Mpaka saa ngapi??”



    “Sidhani kama mfalme atachukua muda. Mambo haya yatakuwa makubwa kuliko uwezo wa moyo wake,” Masoud aliposema vivyo kukawa kimya kidogo.



    “Lakini lile tulilolifanya ni jema zaidi,” akasema bwana Masoud. “Kumwambia mfalme kwamba Wamarekani wamevamia nchi na kummaliza Aziz kutamfanya akupe ruhusa ya kuongoza jeshi zima. Hiyo ni habari njema kwetu.”



    “Vipi kama akawapa ruhusa wengineo? Kama vile Ilham?”



    “Atawapaje na wapo korokoroni? Amna chaguo lolote isipokuwa wewe tu.”



    Kukawa tena kimya. Abdul alibiduabidua lips zake akiwaza. Wakasonga na safari yao lakini wasidumu muda mrefu tangu wakomeshe maongezi yao wakastaajabu gari imesimama.



    “Kuna nini?” Abdul akawahi kuuliza.



    “Kuna gari kwa mbele limeharibika!” dereva akajibu. Ni punde tu alikuwa amepokea taarifa hiyo toka kwa dereva wa gari ya mbele kabisa.



    Wakasimama hapo kwa kama sekunde kumi.



    Kidogo mlio wa risasi ukita mara nne!





    ***





    “Lala chini!” Masoud akamwamuru Abdul kwa usalama wake kisha mwanaume huyo akatoka kwenda kutazama usalama. Hakukuwa na kitu tena bali ukimya. Wanajeshi walikuwa wametapakaa barabarani wakiwa na tahadhari.



    Masoud aliposonga akabaini kuna miili miwili ikiwa imelala chini. Ilikuwa pia ni ya wanajeshi.



    “Walikuwa wamelenga kutushambulia!” akasema mwanaume mmoja na kuongezea, “Wamekiwshakimbia.”



    Basi Masoud akaikagua miili ile marehemu kisha akarejea kwenye gari na kumwambia Abdul kuwa ni watu wa upande wa pili wa jeshi. Watu wa kabila la mama yake na Azizi.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Hawawezi kufanikiwa,” akasema Masoud. “Wapo wachache ukilinganisha nasi.” lakini Abdul alikuwa na tembe za hofu. Safari nzima sasa mawazo yake yakawa yamekengeukia huko.



    **



    “Upo sawa?” Marietta alimuuliza Kelly. Walikuwa wameketi ndani ya gari, van nyeusi, kwa pamoja na wenzao. Kelly alikuwa anajihisi vibaya. Tumbo lake halikuwa vema.



    “Kama kuna shida basi na twende ukapate huduma,” Mahmoud akapendekeza.



    “Hapana,” Kelly akajibu. “Nipo sawa tu.”



    Basi wakaachana na swala hilo na kuanza kuwekeza kwenye swala lililokuwa limewaleta eneo hilo. Upande wao wa kushoto kwa umbali wa kama kilomita mbili na nusu kulikuwa na jengo kubwa lililokuwa linasadikika kumhifadhi bwana Abdul kwa mujibu wa taarifa za Ramadan.



    Kama kawaida wakajiveka vinyago vya kuzuia gesi yenye sumu kisha watu wanne; Marshall, Marietta Kelly na Danielle, wakashuka na kuendea eneo la tukio. Baada ya kama dakika kumi, Abdul aliyekuwemo ndan ya jengo hilo akiwa anakunywa kahawa na kupitia kijitabu, akafikiwa na kijakazi wake.



    “Tayari,” kijakazi akasema kisha akaendaze. Basi kidogo Abdul akasimama na kujiveka nguo ya kwenda kuogea na kuzama ndani ya bafu. Ilikuwa ni bafu kubwa lenye hadhi yake. Bafu la kukusahaulisha mawazo.



    Akajiweka kwneye jakuzi na kutulia humo mwili wake ukiwa unakandwa na maji vuguvugu. Hakuwa na haraka, alikuwa akiwaza na kuwazua mambo yake mbalimbali kichwani. Alikuwa anaiwazia kesho yake. Aliamini ni siku kubwa ambayo anatakiwa kupata ‘the best out of it’.



    Baada ya kama dakika tano, Abdul akasikia mlio wa king’ora. Alishtuka. Upesi alitoka ndani ya jakuzi na kukimbilia kutwaa nguo kujisitiri. Napo ni muda mfupi akaja kijakazi na kumwambia Abdul kwamba wapo chini ya uvamizi.



    Basi haraka Abdul akapiga simu kwa Masoud punde tu alipotoka ndani ya bafu. Ilikuwa ni sekunde isifike dakika. Asimalize matamshi akamwona kijakazi wake akidondoka chini kana kwamba kiroba cha chumvi. Alikuwa tayari ameshavuta sumu ya kutosha.



    Naye muda si mrefu akaanza kuhisi maumivu ya kichwa na mwili umekuwa mzito. Akashika ukuta akisonga kwenda chumbani. Hatua ya kwanza, pili, tatu magoti yakarojeka, akachuchumaa. Akaendelea kusonga tena lakini asifike mbali, akadondoka chini.



    Macho yakawa mazito.



    Kwa mbali akasikia mlango ukifunguliwa na sauti ikasema, “yupo huku!” baada ya hapo hakusikia kitu kingine tena. Hakujua kilichoendelea baada ya hapo.



    Baada ya nusu saa…





    “Tazama kila eneo! Kila eneoo!” alifoka Masoud. Walikuwa wameshafika eneo la tukio pamoja na wafuasi wake kama mia moja kwa mahesabu ya macho. Wote hao walikuwa wamebebelea bunduki mikononi. Hao wakaanza kusaka na kukagua, ndani ya muda mfupi wakabaini karibia ya jumba zima lilikuwa limeathiriwa na hewa ya sumu, watu wametapakaa chini kana kwamba kuku walioathiriwa na janga la ugonjwa wa mlipuko.



    Lakini zaidi Abdul hakuwapo.



    Basi Masoud akaamuru watu wote aliokuja nao wasambae na kupeleka taarifa za kufanya msako mkubwa wa karibia kila eneo ndani ya nchi. Mipaka pia ifungwe na njia za kwenye maji zilindwe kwa hali ya juu.



    Bwana huyo alikuwa na uwezo mkubwa maana sasa jeshi lote lilikuwa mikononi mwake kungoja amri isipokuwa tu wale wachache ambao ni waasi, hivyo amri yake ikabebwa na kuanza kutekelezwa mara moja. Barabara zikaanza kufungwa na wanajeshi wakaanza kusambaa mitaani.



    **

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kichwa bado kilikuwa ni kizito. Alikuwa anahisi kama shingo yake imeelemewa kila anapojaribu kukinyanyua. Akiwa anapambana na kuumudu mwili wake akatambua ya kuwa yu kwenye gari inatembea. Alifungua macho yake taratibu na kuangaza, hakuwa anaona kitu isipokuwa maruweruwe tu.



    Aliyaminya macho yake kwanguvu mara kadhaa na kisha akatazama tena na tena. Kila alipokuwa anafanya vivyo angalau akawa anaupata unafuu, maruweruwe yalipungua lakini bado hakuwa anaona kitu! Akagundua mbele yake kulikuwa kuna kitu kilichokuwa kimemziba.



    Alikuwa yu nyuma kabisa na kiti cha nyuma ndicho ambacho kimemziba asione mbele. Akajaribu kujing’amua hapo akabaini alikuwa amefungwa miguu na mikono. Akapigapiga gari na kujibaraguza, hakuwa anaweza kuongea maana alikuwa amefumbwa mdomo kwa seal tape kubwa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog