Simulizi : The Other Half
Sehemu Ya Tano (5)
“Aaaaaaawwwwoooooohhhhhh.!”
Alipohamisha tu mshale alisikia tena ule ukelele wa ajabu sauti ya kama fisi aliyejeruhiwa akilia kwa hasira lakini akiunguruma kama uzito wa sauti ya simba. Safari hii alipousikia sauti hiyo ilikuwa kwa mbali sana ardhi ilikuwa inatingishika. Kwa mbali sana, kwamba kama ukiweka glasi ya maji hautaona galasi yenyewe ikitingishika lakini utaona maji yaliyomo ndani yake yakicheza na kutengeneza mawimbi.
Akahamisha mshale kutoka kwenye II kwenda kwenye I (1).
Alikuwa kama vile ameamsha mizimu iliyolala. Alielewa ni kwanini alikuwa anasikia sauti ile ya ajabu huku ikisogea karibu kila hatua.
Japokuwa kulikuwa na giza, lakini macho yake yalikuwa yamezoea giza kiasi cha kumuwezesha kuona kama mita mia tatu kutoka pale alipo kwenye mlango ardhini, kulikuwa na kundi la binadamu wa ajabu watoto wa Maldives si chini ya thelathini wakikimbia kwa kasi ya ajabu na kwa hasira kubwa kuja pale alipo. Walikuwa wanakimbia kwa mutumia miguu na mikono kama wanyama. Manyoya yao ya paka yanayofunika mwili wao yalikuwa yamesimama kwa hasira. Giza lilifanya macho yao yaliyogeuka mekundu kama kibatari yaonekane sawia na Salim mita hizi mia tatu alizopo kutoka kundi hili linalomjia la watoto wa Maldives.
Kwa kasi waliyokuwa wanakuja nayo, dhahiri ndani ya sekunde chache sana watakuwa wamefikia hapa alipo na kumrarua rarua au kumfanya chochote ambacho alikuwa hakijui.
Alielewa kwamba kitendo chake cha kuugusa ule mlango ndicho kilichosababisha yote haya na kuwaasha watoto wa Maldives waliyokuwa.
Bado alikuwa na tarakimu moja imesalia kuhamisha mshale wa duara la saa kwenda kwenye IX. Lakini pia hakuwa na hakika kama kubadili kwake huku mshale kwa mtiririko huj alikuwa sahihi au la. Na kama alikuwa sahihi mlango huo ardhini ukifunguka afanye nini na atakutana na nini akifungua mlango huo. Na je, ataweza kufanikisha yote hayo na kuokoa si nafsi yake tu bali na wenzake Cindy na Magdalena waliopoteza fahamu?
Akageuka tena kuwaangalia kundi la binadamu wa ajabu watoto wa Maldives ambao sasa walikuwa kama mita mia hamsini tu kutoka alipo, wakija kwa kukimbia kwa sauti ya ajabu na kwa hasira kama kundi la nyati. Manyoya yao ya paka yalikuwa yamesimama, macho yaliwaka kama kibatari huku wanatoa mlio mkali wa hasira,
“Aaaaaaawwwwoooooohhhhh..!!”
THE OTHER HALF
SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE
Ilipoishia Episode 33
Kwa kasi waliyokuwa wanakuja nayo, dhahiri ndani ya sekunde chache sana watakuwa wamefikia hapa alipo na kumrarua rarua au kumfanya chochote ambacho alikuwa hakijui.
Alielewa kwamba kitendo chake cha kuugusa ule mlango ndicho kilichosababisha yote haya na kuwaasha watoto wa Maldives waliyokuwa.
Bado alikuwa na tarakimu moja imesalia kuhamisha mshale wa duara la saa kwenda kwenye IX. Lakini pia hakuwa na hakika kama kubadili kwake huku mshale kwa mtiririko huj alikuwa sahihi au la. Na kama alikuwa sahihi mlango huo ardhini ukifunguka afanye nini na atakutana na nini akifungua mlango huo. Na je, ataweza kufanikisha yote hayo na kuokoa si nafsi yake tu bali na wenzake Cindy na Magdalena waliopoteza fahamu?
Akageuka tena kuwaangalia kundi la binadamu wa ajabu watoto wa Maldives ambao sasa walikuwa kama mita mia hamsini tu kutoka alipo, wakija kwa kukimbia kwa sauti ya ajabu na kwa hasira kama kundi la nyati. Manyoya yao ya paka yalikuwa yamesimama, macho yaliwaka kama kibatari huku wanatoa mlio mkali wa hasira,
“Aaaaaaawwwwoooooohhhhh..!!”
EPISODE 34
Vishindo vya mbio za lile kundi la binadamu wa ajabu, watoto wa Maldives vilikuwa vinasikia ardhini kama vile tetemeko linalokuja kutokea mbali hivi. Walikuwa wanakuja huku wanaendelea kulia kwa hasira kwa sauti zao kali na za kuogofya.
Salim hakuwa na muda wa kufikiri wala kujiuliza uliza mara mbili mbili. Akanyoosha mkono wake na kuhamisha mshale kutoka pale ulipo kwenye I na kuupeleka kwenye namba IX. Mshale ulipotua tu kwenye IX ulisikika mlionl mkali wa kama chuma hivi kinachokatika kutokea pale ardhini kwenye ule mfuniko au kitu kilichokuwa kimeshikizwa kwa kukazwa kwa nguvu kimejiachia kwa ndani,
“Taaaaaaaaaaaaaaaaa”
Ilikuwa kana kwamba kulikuwa na kitu fulani kwa kwa ndani kilikatika au kuachia kwa nguvu. Salim alinyoosha mkono wake mpaka upande ambao ulikuwa na kama mshikio hivi. Kwa nguvu zake zote alizonazo alijitutumua kuinua mfuniko ardhini.
Mungu si Athumani, alichokuwa anakiwaza kichwani kuhusu kuingiza zile namba kwa kusogeza mshale kilikiwuwa sahihi. Mfuniko ukafunuka kutoka pale juu ya ardhi. Mwanga mkali wa kama jua ukapia juu angani kama vile mwale wa tochi kutokea ndani ya ardhi aliyoifunua. Mwanga ule mkali ulifanya ionekane dhahiri kabisa tofauti ya Anabelle na dunia. Ilikuwa kana kwamba mwanga huo unapiga kutokea duniani. Pale walipo ndani ya Anabelle kote kulikuwa na kiza kikuu lakini juu ya ardhi aliyofunua mfuniko kulipiga mwanga mkali kutengeneza mstari wa nuru kama vile mtu anamulika tochi yenye nguvu kubwa kutoka ndani ya ardhi pale alipofunua.
Kwa haraka kama ndani ya robo sekunde tu Salim alichungulia pale alipofunua ardhini panapotoa ule mwanga mkali. Kilikuwa kama kisima, japo si kisima kama kilivyo kisima kingine. Lilikuwa ni shimo lenye maji meupe, masafi, ‘clear’ yenye kuonekana kwa uzuri kabisa. Ilikuwa kana kwamba, muonekano ulivyo unapopiga mbizi baharini au ziwani wakati wa mchana wa jua kali kabisa na hakuna hata wingu moja angani. Namna unavyoyaona maji kutokea chini ulikopiga mbizi, unaweza kuliona jua kabisa kutoka ndani ya maji. Maji yanaonekan meupe au bila rangi lakini yakiwa na ubuluu kwa mbali. Hivyo ndivyo ambavyo Salim aliona maji yaliyomo ndani ya shimo alipofunua mfuniko pale ardhini.
“Aaaaawwwwwwooooohhh”
Kishindo cha sauti safari hii kilikuwa kikali zaidi baada ya Salim kufunua ule mfuniko. Salim alikisikia kishindo cha sauti na zile mbio za wale binadamu wa ajabu zikiwa zimekaribia kama mita ishirini au thelathini tu kutoka pale alipo. Ndani ya chini ya sekunde kumi tu watakuwa wamefika hapa alipo na kumrarua rarua. Tumaini lake lote lilikuwa ni kukuta njia kama akifunua pale ardhini. Lakini amekuta shimo, tena shimo lililojaa maji, kama maji ya bahari ya kina kirefu yakitoa mwanga mkali.
Hakukuwa na muda zaidi wa kupoteza au kujiuliza mara mbili mbili. Ulikuwa ni muda wa kuhatarisha maisha ili kuokoa maisha.
Kishindo cha mbio za kundi la watoto wa Maldives safari hii kilikuwa karibu na kufanya ardhi itikisike kama vile kuna tetemeko la ardhi linapiata. Zile sauti zao za vilio vya ajabu zilikuwa kali kiasi kwamba mpaka masikio yalikuwa yanauma kuzikia na kuziba kabisa. Walikuwa karibu kiasi kwamba Salim aliweza mpaka kusikia harufu yao ambayo miili yao yenye manyoya waliyokuwa wanatoa. Kama harufu ya unyevunyevu wa kitu kilichokaa sana ndani ya maji machafu.
Wenzake wote Cindy na Magdalena bado walikuwa hawana ufahamu huku Shafii akiwa amepoteza maisha tayari. Salim akamvuta Magdalena na kumtupia ndani ya shimo na kisha akafanya hivyo haraka haraka kumvuta Cindy na kurusha shimoni. Kisha akashikilia ule mfuniko na kujirusha yeye mwenyewe pia shimoni. Mfuniko alioushikilia uliishia kujibamiza juu ya ardhi na kujifunga tena kama ulivyokuwa awali huku yeye akitupwa ndani ya shimo la maji.
“Baaaaaannnnggg.!!”
Salim alisikia sauti ya vitu vikijibamiza juu ya mfuniko upande wa pili baada ya kudondokea majini mle shimoni. Walikuwa watoto wa Maldives. Kama angelichelewa hata nusu sekunde tu, muda huu yeye na wenzake wote wangekuwa wameraruliwa na kufanywa mboaga kama sio mlo wa jioni.
Kuna hali mpya Salim alikiwa anajisikia mara baada ya kujitupa ndani ya maji. Hakuwa anasikia tena baridi kama ambavyo alikuwa anasikia ndani ya Anabelle. Ilikuwa kana kwamba yuko ndani ya ziwa au ndani ya bahari kwenye ulimwengu wa kawaida amepiga mbizi. Pia alijihisi nguvu za mwili zinaanza kurudi. Ile hali ya kuchoka mno aliyokuwa anasikia ilianza kuondoka.
Akaangaza macho huku na huko ndani ya maji. Akawaona wenzake Cindy na Magdalena wakiwa bado hawana ufahamu. Akaogolea na kuwashika wote wawili kama vile amewakumbatia kwa mkono mmoja. Mkono mwingine akautumia kuogelea.
Salim akatumia umahiri wake wote kuogelea kufuata ule mwanga unakotokea. Ilikuwa kama vile anaogelea kutoka kwenye kina kirefu cha bahari kurudi juu ya maji. Kanuni za “gravity” zilikuwa kana kwamba hazifanyi kazi tena au labda akili ya Salim ilikuwa imechanganyikiwa.
Kule walikotoka alifunua mfuniko na kujirusha ndani ya shimo na kupiga mbizi. Katika hali ya kawaida ilimaanisha kwamba alipiga mbizi kwenda chini. Lakini sasa hivi kila ambavyo alikuwa anaogelea kufuata ule mwanga kama mwanga wa jua alijiona dhahiri kabisa anaogelea kutoka chini ya bahari kwenda juu ya maji.
Kutokana na mauza uza yaliyokuwa yanaendelea na ambayo Salim alikuwa ameyashuhudia, alikuwa na kila sababu ya kuamini kwamba walikuwa wamefanikiwa kutoka ndani ya Anabelle 27 na sasa wako kwenye bahari mahala fulani duniani.
Salim aliogelea kwa kitumia mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa amewashikilia wenzake. Aliogolea kuufuata ule mwanga uliokuwa juu yao. Mwanga ambao ulikuwa unaonekana kama mwanga wa jua. Salim aliogelea na kuogelea. Kwa kiasi fulani walikuwa wameanza kuufikia ulw mwanga lakini mwili wa Salim uliianza kuishiwa nguvu. Akiba yake ya oksijeni ndani ya mapafu iliaanza kuisha. Japo alikuwa analiona jua kabisa liko karibu juu yao kumaanisha kwamba walikuwa wanakaribia kuibuka juu ya maji lakini mwili wa Salim alikuwa umeishiwa nguvu kabisa. Macho yakaanza kuwa mazito na hata mikono ikaanza kuishiwa nguvu kuogelea.
Salim alijitahidi kuilazimisha mikono yake kuogelea, lakini mwili haukuwa na nguvu na macho yalikuwa yamelegea na yanakaribia kufumba. Hata ule mkono mwingine ambao alikuwa amewashikilia wenzake nao uliishiwa nguvu na alikuwa amewaachia.
Walikuwa wamebakisha mita chache tu waibuke juu ya maji. Lakini oksijeni Ilikuwa imeisha mapafuni mwa Salim. Mwili wote ukalegea. Macho yakafumba. Salim akapoteza fahamu kama wenzake Cindy na Magdalena.
NCHINI MAREKANI
Hali ya kiza cha ghafla kilichoikumba dunia nzima bado ilikuwepo. Japo bado ilikuwa ni mchana lakini ile hali ya giza, kama la saa moja jioni bado ilikuwepo.
Mitaa yote marekani ilikuwa kimya kabisa. Biashara na ofisi zote zilikuwa zimefungwa. Hakukuwa na gari zozote barabarani ambazo zilikuwa zinatembea mahala kokote.
Marshall Law ilikuwa imeanza kutekelezwa. Rais Laura Keith masaa machache yaliyopita alikuwa ametangaza kuhuisha “Marshall Law”! Kwamba jeshi la Marekani linashika hatamu na yeye akiwa kama amiri jeshi Mkuu. Alikuwa ametangaza hali ya hatari nchi nzima. Hakuna raia yeyote ambaye alikuwa anaruhusiwa kutoka nje ya nyumba yake.
Yeyote ambaye angeonekana nje ya nyumba yake au mtaani jeshi lilikuwa na ruhusa ya kumtandika risasi.
Mitaani, kila mahala kulikuwa na magari ya kijeshi yanaranda randa kufanya Patrol. Maafisa wa ‘National Guard of The United States’ walikuwa wamemwagwa kila kona ili kiwadhibitk wowote ambao watakiuka agizo hilo.
Nchi yote ilikuwa kimya kabisa. Na giza ambalo lilikuwa limetanda lilifanya kimya hiki kuwa cha kuogofya. Mitaani sauti pekee zilizokuwa zinasikika zilikuwa ni sauti za mbwa wakibweka au kufukuzana na paka wakicheza. Hakukuwa na sauti ya binadamu. Kila mtu na familia yake walikuwa wamejifungia kimya kabisa ndani.
Ajabu ni kwamba hata mawasiliano ya simu nchi nzima yalikuwa yamekatwa. Ziliachwa ‘special channels’ tu kwa ajili ya mawasiliano ya kijeshi.
Serikali haikuishia hapo tu, televisheni zote zilifungiwa kurusha matangazo. Zilikuwa kana kwamba zimedukuliwa. Kila ambapo mtu angefungulia televisheni yake kitu pekee ambacho alikuwa anakutana nacho ilikuwa ni Madam President Laura Keith akiwa anatoa hotuba kuhusu hali ya dharura aliyoitangaza. Ilikuwa ni hotuba ya dakika tano ambayo ilikuwa inajirudia ikiisha. Inajirudia tena na tena.
“…wataalamu wetu wa masuala ya usalama na sayansi wanajitahidi kadiri ya uwezo wao kuelewa na hatimaye kutatua hii changamoto tuliyonayo. Hali hii ya miji kutwaliwa na sasa ulimwengu mzima kufunikwa na giza. Hivyo basi tukiwa tunaendelea na juhudi hizi nawaomba raia wote mbakie kwenye hali ya utulivu majumbani kwenu. Nimetoa agizo la kutangaza hali ya hatari nchi zima na Congress wameridhia pendekezo langu la kuhuisha Marshall law. Jeshi linashika hatamu kuanzia sasa. Na wanaruhusu ya kumpiga risasi raia yeyeto ambaye ataonekana nje ya nyumba yake au mitaani. Nawaasa tena raia wote tuwe watulivu na tusifanye hali hii ya ngumu tunayopitia kuwa ngumu zaidi. Huu ndio wakati wetu wa kushikamana kuliko kipindi chochote kile. Mungu awabariki sana. Mungu inariki United States of America.!
Kilikuwa ni sehemu ya kipande cha ujumbe wa dakika tano ambao ulikuwa inajirudia kwenye redio na televisheni zote muda wote na wakati wowote ukifungulia redio yako au televisheni.
NCHINI TANZANIA
Nchi yote ilikuwa kimya kabisa. Hii ilikiwa ni moja ya nchi ambayo ilikuwa na miji mingi iliyotwaliwa. Ruangwa ilikuwa imetwaliwa, Dar es Salaam ilikuwa imetwaliwa, Tabora imetwaliwa, Singida imetwaliwa, na Dodoma ilikuwa imetwaliwa.
Kama ambavyo ilikuwa duniani kote, nako giza lilikuwa limetamda japo bado ilikiwa mchana.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pia alikuwa ametangaza hali ya hatari nchi nzima. Hakuna raia ambaye alikuwa anaruhusiwa kuonekana mitaani. Kila raia alitakiwa kuwa ndani ya nyumba yake muda wote.
Mawasiliano ya simu yalikatwa nchi nzima isipokuwa ‘special channels’ kwa ajili ya mawasiliano ya kijeshi.
Televisheni na redio zote kila ambavyo ungewasha muda wowote ule kulikuwa na ujumbe unaojirudia rudia wa Rais Zuberi Z. Miraji akiwaasa Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambacho ulimwengu unapitia.
Ujumbe huu ulirekodia jijini Arusha ambako Rais alikuwa amefichwa kwa dharura ndani ya Chuo cha Kijeshi cha Monduli katika makazi ya dharura namba Tatu ya Rais (Presidential Emergency Military Residence – PEMR-03).
NCHINI INDIA
Ilikuwa kama vile Armageddon! Vita ya mwisho ya dunia… fujo kila mahali. Maduka yakivamiwa, nyumba zikivunjwa na kuibwa, wanawake wakibakwa.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Kitendo cha ulimwengu mzima kukumbwa na giza la ghafla na hatimaye serikali ya India kutangaza hali ya hatari ilikiwa ni kana kwamba waliwasha moto wa uhalifu na watu kuonyesha hasira walizonazo.
Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, serikali ikaingiza vikosi vya jeshi mitaani. Yalikuwa ni mapambano, na si mapambano tu bali ilikuwa ni vita. Raia dhidi ya raia, na papo japo raia dhadi ya jeshi. Raia wenyewe kwa wenyewe walivamiana madukani na majumbani na kuibiana na papo hapo raia walishambuliana na wanajeshi na kuuwana.
Ndani ya muda mchache tu, nchi nzima ya India ilikuwa kama vile inavunjika vipande vipande.
Mtaa wa Scarsdale, New York – Marekani
Kwa kuzingatia agizo la Rais wa Marekani Bi. Laura Keith kuhusu raia wote kutotoka nje, mtaa wote ulikuwa kimya kabisa. Giza lilifanya ukimya huu kuwa si wa kawaida.
Gari ya kijeshi ya National Guard ilikuwa nje ya nyumba wanayoishi familia ya Donald McLaren na mkewe Latisha pamoja na mtoto wao Natalie. Lakini leo hij ndani walikuwa na ule ugeni wa Bilionea Rodney Van Der Berg na wasaidizi wake ambao walikuja kumuomba Natalie asaidie kwenye juhudi zao za kumsaka Makamu wa Rais David Logan ambaye ametekwa na kupelekwa kusikojulikana.
Kutoka ndani ya gari hii ya kijeshi, walishuka maafisa wawili waliovalia sare zao za kijeshi huku mikononi wamebeba silaha nzito na moja kwa moja kwenda kugonga mlango wa nyumba ya Bw. Donald McLaren.
Vidole vyao wanajeshi hawa vilikuwa kwenye ‘triger’! Tayari kwa kufyatua risasi.
THE OTHER HALF
SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE
EPISODE 35
MARYLAND – MAREKANI
Yalikuwa yamepita masaa karibia mawili tangu tetemeko dogo lipite katika mji Maryland kuashiria kwamba mji huo nao ulikiwa unatwaliwa ndani ya masaa sita ambayo ya kwa sasa yalikuwa yalikuwa yamebaki masaa manne tu. Mzee Caleb alikuwa amechoka hoi akiwa pembeni ya kaburi nyuma ya nyumba yake alilokuwa analifukua. Licha ya uzee wake alikuwa amejikakamua kufa na kupona na kufukua mfululizo kwa masaa mawili mpaka sasa alikuwa ameifikia masalia ya mifupa ya mkewe na mwanaye.
Akaingia tena ndani ya shimo na kuanza kuitoa mifupa kwa utaratibu kabisa.
Kwanza alianza kutoa mifupa ya mkewe Suzanne. Kama kungelikuwa na mwana akiolojia angelisema kwamba mifupa hiyo ni ya mwanamke mwenye umri kati ya miaka thelathini na tano mpaka arobaini. Na hakika ilikuwa hivyo, kaburi hili lilichimbwa na Caleb takribani miaka arobaini iliyopita na kufukia maiti za mkewe na mwanaye.
Alipo maliza kuondoa kaburini mifupa ya mkewe akaanza kuondoa mifupa ya mtoto wake Clinton. Mwana akiolojia angelikueleza kwamba mifupa hiyo ilionekana kabisa kuwa ilikuwa na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na tisa hadi ishirini na tatu.
Mzee Caleb alimaliza kutoa mifupa yote kaburini. Pembeni yake alikuwa ameandaa mifuko miwili meusi ya plastiki. Alichukua mifupa ya mkewe Suzanne na kuiweka kwenye mfuko mmoja, kisha akachukua mifupa mtoto wake Clinton akaiweka kwenye mfuko mwingine. Lakini mafuvu ya vichwa vyote viwili hakuyaweka ndani ya mifuko. Aliyashikilia mkononi na mkono mwingine akashikilia ile mifuko miwili na kurejea ndani.
Alipoingia ndani ya nyumba, ile mifuko ya plastiki miwili yenye mifupa akaiweka sakafuni na yale mafuvu ya kichwa akayaweka juu ya meza. Akaingia chumbani na baada ya muda mfupi akarejea sebuleni mkononi akiwa ameshikilia nyundo kubwa.
Akachukia fuvu moja baada ya lingine na kuyaponda ponda kwa ustadi mkubwa.
Alianza kuponda fuvu la mkewe Suzanne. Aliliponda ponda taratibu mpaka likawa unga unga kabisa. Kisha akachukua chupa fulani tupu ya ukubwa wa wastani na kuweka ule unga unga uliotokana na fuvu la mkewe Suzanne. Baada ya hapo akaponda ponda fuvu la mtoto wake Clinton mpaka nalo likawa katika hali ya unga unga hivi na kisha unga unga huo akauweka kwenye chupa nyingine nayo ya ukubwa wa wastani.
Alipomaliza chupa zote mbili alizihifadhi kwenye mkoba fulani wa ngozi wa kiofisi, mkuu kuu wa fasheni ya kizamani.
Akaweka juu ya meza pale sebuleni ile mifuko miwili yenye mifupa ya mkewe na mwanaye pamoja na mkoba wenye chupa zenye unga wa mafuvu ya mwanaye na mkewe.
Akatupa jicho kwenye saa ya ukutani. Tayari alikuwa ametumia takribani saa nyingine moja. Kwa hiyo jumla alikuwa ametumia masaa matatu, kuchimba kaburi na kuondoa mifupa pamoja na kuponda ponda haya mafuvu mpaka kupata unga unga. Alikuwa amebakiza masaa matatu tu mengine kutoka kwenye mji huu wa Maryland kabla haujatwaliwa na kugeuzwa Anabelle.
Akashuka ngazi kuelekea chini kwenye basement ambako walikuwa wamemficha yule mnyama wa ajabu waliyepewa kule msituni na baba yake.
Akateremka ngazi haraka haraka mpaka chini kwenye basement. Mnyama alikuwa bado yuko kwenye kile kitundu chake kama namna ambavyo walikabidhiwa na baba yake msituni.
Mzee Caleb alisimama na kumuangalia tena huyu kiumbe. Tangu litokee lile tukio la ulimwengu mzima kukumbwa na giza ghafla mnyama huyu alikuwa ameacha kulia tofauti na ilivyokuwa mwanzoni. Na alikuwa amekaa katika namna fulani akiwa kama amelala usingizi na kutanua mbawa zake kujifunika umbo lake. Caleb alikumbuka sawia kabisa muonekano wa mnyama huyu siku ile wakipokabidhiwa msituni. Kimo chake kama ndama wa ng’ombe lakini muonekano wake wa kufanana kabisa na mbwa na akiwa na mbawa kama popo huku mwili mzima ukiwa laini bila hata chembe ya nyoya.
Aliikumbuka rangi yake nyeupe iliyopitiliza kama theluji lakini sasa rangi hiyo ikiwa imebadilika na mnyama huyu mwili wake ulikuwa mwekundu kabisa.
Caleb alikuwa amebakiwa na masaa matatu tu anatakiwa kutoka ndani ya mji wa Maryland kabla haujatwaliwa. Lakini alikuwa hawezi kuondoka bila mnyama huyu. Walipokabidhiwa mnyama huyu wa ajabu kule msitu wa Ox waliambiwa kuwa wamtunze mpaka siku ambayo baba yake na wenzake wa masalia ya The 46 watakapo muhitaji. Kwa hiyo kwa namma yeyote ile Caleb hakuwa tayari kumuacha kiumbe huyu hapa. Lakini mtihani wa pili ulikuja kwamba mnyama huyu alikuwa na njaa. Waliambiwa kwamba kila baada ya siku tatu wampatie mnyama huyu lita moja ya damu. Siku tatu zilikuwa zimepita na walikuwa hawajampa damu hata tone.
Kwa kawaida basement huwa inatumika kama stoo kwa ajili ya kuhifadhi makorokoro ya kila aina. Mzee Caleb akaanza kupekua kila upande humu kwenye basement kutafuta kitu.
Akapekua na kupekua mpaka alipopata alichokuwa anakitafuta. Mpira fulani hivi mwembamba. Mpira mwembaba wa kufanana kabisa na mipira inayotumiwa kuunganishwa kwenye ‘dripu’ na kisha kuingia kwenye mshipa wa damu wa mtu.
Baada ya hapo akakitafuta kisu kilipo mpaka nacho akakipata.
Wazo ambalo lilikuwa kichwani mwake lilikuwa wazo la kiwendawazimu na la hatari.
Caleb alikuwa anataka kutoa Lita moja hiyo ya damu kutoka mwilini mwake. Alikuwa anataka kujitoboa na kisha kuingiza mpira huo kwenye mshipa wa damu kisha aanze kuitoa damu na kuiweka kwenye chupa mpaka ifikie Lita moja.
Lilikuwa ni wazo la kiwendawazimu kwa sababu alikuwa anataka kujitoboa kwa kutumia kisu na kisha kuingiza mpira huu mwembamba. Kitendo hiki kingeweza kusababisha damu kumwagika hovyo na kuhatarisha maisha yake. Lakini pia lilikuwa ni wazo la hatari kwa sababu kwa mzee wa umri wake wa miaka themanini na mbili kitendo cha kujitoa damu lita moja mara moja kwa mkupuo ilikuwa ni hatari kwa maisha yake.
Lakini Caleb hakuwa na jinsi. Hakuwa na suluhisho lingine hakukuwa na mtu mwingine wa kumsaidia hapa zaidi yake. Wale vijana wa Ethan makomando wa SAD ya CIA walikuwa wamekimbia na kumtelekeza hapa peke yake. Alikuwa hawezi kuondoka hapa Maryland bila kiumbe huyu wa ajabu na alikuwa hawezi kuondoka naye bila kumlisha lita moja ya damu kama ambavyo alikuwa ameagizwa na baba yake.
Ilikuwa ni lazima kuhatarisha maisha ili kuokoa maisha na kutimiza kusudi ambalo alikuwa nalo moyoni.
Hakuna asiye ogopa kifo hata awe shujaa wa namna gani. Caleb alikuwa anajua kabisa kwamba hiki anachotaka kukifanya kingeweza kabisa kuhatarisha maisha yake na kupoteza uhai. Alikuwa ana hema kwa nguvu kila ambavyo alifikiria kwamba kama atakosea hata kiduchu tu hiki ambacho anataka kukifanya basi huu unaweza kuwa mwisho wake. Akajipa ujasiri, akajitutumua, akajikaza kiume na kuelekeza kisu kwenye mshipa wa damu.
Lakini ghafla kabla kisu hakijatua juu ya mkono na kujitoboa akasikia mlio wa gari linasimama juu nje ya nyumba yake. Caleb akashusha pumzi kwa nguvu. Ilikuwa ni kana kwamba anataka kujitia kitanzi na ghafla mtu ametokea na kumsimamisha kufanya hivyo. Akashusha tena pumzi kwa nguvu. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka.
Akajisogeza mpaka kwenye ukuta wa upande mmoja wa basement ambao kwa juu kabisa ulikuwa na kijidirisha kinachoonyesha nje ya nyumba uwanjani. Hakuamini macho yake kile ambacho alikuwa anakiona. Gari mbili za wale vijana wa Ethan makomando wa SAD ya CIA zilikuwa zimepaki mbele ya nyumba yake na vijana wale wale ambao walimkimbia hapa masaa matatu yaliyopita walikuwa wanashuka kwenye zile gari na kuingia ndani ya nyumba.
“Hawa vijana wamechanganyikiwa nini?” Mzee Caleb aling’aka mwenyewe.
Akageuka na kuanza kupanda ngazi kutoka kwenye basement kurejea juu kwenye nyumba sebuleni.
Aliwakuta vijana wote wale saba wako pale sebuleni. Ajabu alipotokea tu sebuleni walikuwa wamemkodolea macho kama wameona jini hivi.
“Mmesahau nini?” Mzee Caleb aliwauliza kwa hasira.
Vijana hawakujibu. Bado walikuwa wanamshangaa tu. Akajaribu kufuata uelekeo wa macho yao ajue ni nini hasa walikuwa wanakishangaa. Walikuwa wanaangalia mikononi mwake mkono huu akiwa ameshikia kisu na mkono huu akiwa ameshikilia ule mpira ambao alikuwa anataka kujitoa damu.
“Mnashangaa nini? Haiwahusu…!!” Caleb kwa kukereka akaweka juu ya meza kile kisu na mpira.
“Ulikuwa unataka kufanya nini mzee?” Yule komando muongeaji sana akauliza huku anamuangalia kwa jicho la udadisi.
“Nimewauliza swali ninyi kwanza… mmesahau nini mpaka mnarudi?” Caleb akaongea kwa ukali.
“Tumekwisha mzee!” Komando mwingine akadakia.
“Nini?” Mzee Caleb akukiza tena kwa hasira vile vile.
“Tumekwisha mzee… hatuwezi kutoka ndani ya huu mji.! Haijalishi tunafanyaje huu ndio mwisho wetu!”
Yule komando akaongea huku wanakaa chini kwenye viti. Kwa kuwasoma tu sura zao ilionesha dhahiri kabisa kuwa walikuwa wamekata tamaa. Nyuso zilikuwa zimesawajika kabisa na hawakuwa na nuru yoyote ya matumaini inayoweza kuonekana ukiwaangalia. Walikaa chini kwenye viti kwa unyonge na kukata tamaa.
“Kwa nini haiwezekani kutoka ndani ya Maryland?” Caleb akawauliza safari hii kwa utulivu bila ukali.
Wale vijana wakaangaliana kama kuulizana ni nani atoe maelezo. Walikuwa wamekata tamaa kiasi kwamba walikuwa hawataki hata kuongelea sababu ya kuwakatisha tamaa. Lakini hatimaye mmoja wao akaamua atoe maelezo.
“Mzee tulipondoka hapa ili tubidi tuondoke kuelekea magharibi… tusingeweza kwenda kaskazini, kusini au mashariki kwa sababu upande wa kaskazini na mashariki tunapakana na mji wa Baltimore ambao tayari wote tunafahamu kuwa umekwisha twaliwa na kugeuzwa kuwa Anabelle karibia wiki sasa imepita… lakini pia upande wa kusini tumepaka na mji wa Annapolis ambao nao tayari umetwaliwa siku moja ile ile ulipotwaliwa mji wa Baltimore… kwa hiyo sehemu pekee ya kwenda ni upande wa magharibi ambako tumepakana na Washington na hapo ndiko kwenye mtihani mzee.!!”
Yule kijana komando alieoeza na kuiweka nukta kidogo.
“Mtihani wa nini? Nipe maelezo kamili kijana.!” Mzee Caleb aliuliza kwa shauku. Hasira zake zote zilikuwa zimeyeyuka na sasa alikuwa amebakiwa na taharuki tu moyoni.
“Tumekaa porini hapa bila mawasiliano hatujui kinachoendelea huko nje… kumbe masaa machache baada ya hali hii ya giza kulikumba dunia ghafla Rais amehuisha Marshall Law nchi nzima…jeshi limechukua hatamu na hakuna raia yeyote anayeruhusiwa kutoka nje ya nyumba yake na ukionekana nje unatandikwa risasi… na kutokana na tetemeko lilitokea Maryland kuashiria kwamba mji unaelekea kutwaliwa, mamia ya maafisa wa National Guard wamewekwa mpakani mwa mji wa Maryland na Washington. Lengo ni kwanza kutekeleza agizo hilo la rais la Marshall Law na pili kuzuia watu kutoka Maryland kuingia Washington… nadhani sote tunafahamu unyeti wa mji wa Washington. Wanaogopa wakiruhusu maelfu ya watu kutoka Maryland kuingia Washington kwa mkupuo mji wa Washington unaweza kuingia kwenye taharuki ya machafuko.! Kwa hiyo hakuna uwezekano wowote wa mtu kuvuka mpaka wa Maryland kuingia Washington… huko tulikotoka karibia na mpaka wa Maryland na Washington tumekutana na mamia ya maiti zenye matundu ya risasi walizopigwa na maafisa wa National Guard. Walikuwa wanajitahidi kulazimisha kuingia Washington.!! Kwa hiyo mzee tuna machaguo mawili tu hapa… twende kusini, kaskazini au mashariki kwenye miji ya Annapolis na Baltimore ambayo tayari imetwaliwa na kufanywa Anabelle au tusubiri hapa hapa ndani ya chini ya masaa matatu yajayo tutwaliwe pamoja na mji wa Maryland ukiwa unageuzwa kuwa Anabelle na tupotelee ndani yake na uwe mwisho wa maisha yetu… ndio maana nakwambia Mzee Caleb huu ni mwisho wetu.!”
Kijana komando alieleza kwa ufasaha na kwa kirefu. Mzee Caleb alikuwa mpaka anatetemeka aliposikia maelezo haya. Ilikuwa kama vile amepigwa na nyundo kichwani. Kijasho chembamba kilimtoka zaidi. Sentesi ya yule kijana komando ilikuwa inajirudia kichwani mwake. “Mzee Caleb huu ndio mwisho wetu.!!”
Mzee Caleb alijikuta anakaa chini bila kujijua kutokana na kukata tamaa baada ya kuzikia habari hii.
Salim aliogelea kwa kitumia mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa amewashikilia wenzake. Aliogolea kuufuata ule mwanga uliokuwa juu yao. Mwanga ambao ulikuwa unaonekana kama mwanga wa jua. Salim aliogelea na kuogelea. Kwa kiasi fulani walikuwa wameanza kuufikia ulw mwanga lakini mwili wa Salim uliianza kuishiwa nguvu. Akiba yake ya oksijeni ndani ya mapafu iliaanza kuisha. Japo alikuwa analiona jua kabisa liko karibu juu yao kumaanisha kwamba walikuwa wanakaribia kuibuka juu ya maji lakini mwili wa Salim alikuwa umeishiwa nguvu kabisa. Macho yakaanza kuwa mazito na hata mikono ikaanza kuishiwa nguvu kuogelea.
Salim alijitahidi kuilazimisha mikono yake kuogelea, lakini mwili haukuwa na nguvu na macho yalikuwa yamelegea na yanakaribia kufumba. Hata ule mkono mwingine ambao alikuwa amewashikilia wenzake nao uliishiwa nguvu na alikuwa amewaachia.
Walikuwa wamebakisha mita chache tu waibuke juu ya maji. Lakini oksijeni Ilikuwa imeisha mapafuni mwa Salim. Mwili wote ukalegea. Macho yakafumba. Salim akapoteza fahamu kama wenzake Cindy na Magdalena.
EPISODE 36
Mahala fulani kwenye Pwani ya bahari
Wakwanza kuamka alikuwa ni Magdalena… hakujua ni kwa namna gani walifika hapo walipo lakini alimka akiwa kwenye pwani ya bahari huku mawimbi yakimpiga pale mchangani kila yalikuwa yakija na kuondoka.
Aliamka kwa kishindo huku akikohoa na kutapita maji.
Aliendelea kutapika maji huku akiinuka na kukaa kitako akiangaza macho huku na huko. Alijitahidi kuvuta kumbukumbu hapo alipo ni wapi au walau amefikaje lakini kumbukumbu hazikuja. Kitu pekee ambacho alikuwa anakumbuka ni kwamba mara ya mwisho alipokuwa na ufahamu wake alikuwa ndani ya Anabelle 27 pembeni ya mlango wa The 46 ardhini.
Japokuwa alidhani kwamba labda bado wako ndani ya Anabelle kutokana na kigiza cha jioni kilichopo mahala hapa alipo amka lakini hali ya hewa ilikuwa inamshangaza. Hakukuwa na baridi kali kama ambavyo alikuwa amezoea ndani ya Anabelle. Pia hakukuwa na hewa nzito yenye ukungu kama ambavyo ilikuwa ndani ya Anabelle. Lakini kiza kilikuwepo.
Magdalena akapepesa macho huku na huko kutazama pale pwani alipo. Upande wake wa kulia kwa mbali kama mita ishirini kutoka pale alipo aliona kama kivuli cha mtu amelala mchangani.
Magdalena akainuka kwa kujikongoja kama mlevi na kusimama. Kichwani alikuwa anasikia kizunguzungu kwa mbali. Akainuka na kutembea kwa kujikaza kukifuata kile kivuli cha mtu ambacho kilikuwa kimelala mchangani. Kila ambavyo alikuwa anakisogelea ndivyo ambavyo kivuli kilikuwa kinazidi kuwa dhahiri machoni mwake. Kilikiwa ni kivuli cha mwonekano wa mtu mwanaume, mrefu wa wastani nguo zake zikiwa zimeloa maji kama za kwake kuashiria naye aliletwa na mawimbi ya bahari. Akakaza macho huku anamsogelea, aling’amua kwamba alikuwa ni Salim.
Magdalena licha ya kizungu zungu ambacho alikuwa nacho alikimbia mbio mpaka pale ambapo Salim alikuwa amelala bila ufahamu.
“Salim… Salim… Salim.!!” Magdalena alimuita Salim huku anamtikisa aamke.
“Salim! Salim.!!” Aliita kwa nguvu zaidi na kumtikisa kwa nguvu zaidi. Salim hakuamka wala kufumbua macho.
Akiwa amekazana kumita Salim kwa nguvu hivi, ghafla alisikia kama umbali wa mita tano kutoka pale alipo mtu anakohoa.
“Koh koh koh koh.!”
Alimsikia mtu anakohoa huku akitoa sauti kama vile anatapika.
Magdalena akageuka na kukaza macho kuelekea kule ambako alikuwa anasikia sauti inatokea. Aliona kivuli cha mtu amekaa. Akakaza macho zaidi kuangalia kama anaweza kutambua ni nani.
“Cindy!” Magdalena akabahatisha.
“Magdalena!” Yule mtu akaitika.
“Niko hapa Cindy… Salim bado amepoteza fahamu!” Magdalena akaongea kwa taharuki.
Cindy akainuka kutoka pale alipo na kutimua mbio mpaka pale ambapo walikuwepo Magdalena na Salim.
“Yuko hai.!” Cindy aliongea baada ya kufika na mara moja kuweka mkono wake kwenye msipa wa damu shingoni mwa Salim.
Cindy akamfungua nguo Salim eneo la shingoni ili aweze kuhema kwa uzuri na aweze kumpa huduma ya kwanza ya kumzindua.
Akaanza kumpa pumzi kwa kumpuliza mdomoni mwake na kisha kumkandamiza kifuani na kuachia. Anampulizia pumzi mdomoni kwa kutumia mdomo huku amembana na kisha kumkandamiza mfululizo kifuani mara kadhaa na kuachia.
Akarudia hivyo tena na tena mpaka ambapo Salim alianza kukohoa na kutapika maji.
“Nini… nini…nini!” Salim aliamka kwa kuweweseka huku anaongea maneno ambayo hata hayaeleweki.
“Tulia Salim upo Salam… mimi Cindy na Magdalena.!” Cindy alimtuliza huku anamsaidia kumnyanyua akae kitako.
“Tuko wapi hapa?” Salim aliuliza huku amewatolea macho.
Wote watatu waliangaliana pasipo yeyote kati yao kujibu kitu. Hakuna yeyote ambaye alikuwa anajua ni mahala gani ambapo walikuwa.
“Mara ya mwisho nakumbuka nilikuwa nimejilaza karibu na mlango wa The 46 na kupoteza fahamu… sikumbuki kingine chochote baada ya hapo.!” Magdalena akajieleza.
“Mimi nakumbuka ulikuwa unanieleza kuhusu ujumbe ulioupata ndani ya Chupa… sikumbuki lingine lolote!” Cindy naye akajieleza.
“Oooh afadhali!” Salim alihema kama vile amesikia habari njema.
“Nini?” Magdalena na Cindy waliuliza swali kwa pamoja.
“Tumerejea Duniani!” Salim aliwajibu kwa kifupi.
Cindy na Magdalena waliangaliana huku wametumbua macho na kisha kugeuka tena kumuangalia Salim kwa mshangao.
“Unataka kusema uliweza kufungua mlango wa The 46?” Cindy akauliza kwa mshangao mkubwa.
“Ndio! Niliufungua na kuwatoa wote…!” Salim alijibu.
Alipotamka neno “wote”, ghafla tu Cindy na Magdalena wakakumbuka jambo ambalo walipaswa kulikumbuka muda wote huu.
“Shafii yuko wapi? Tulikuwa wote pale mlipotuacha karibu na mlango wa The 46!” Cindy aliuliza huku amemlazia macho Salim.
Salim alijiinamia tu chini asiqeze hata kutoa jibu lolote.
“Salim! Shafii yuko wapi?” Magdalena aliuliza huku safari hii sauti inatetema kama vile anaelekea kulia.
“Shafii hatunae tena… nilipofika pale tulipowaacha karibu na mlango wa The 46 nilikukuta wewe umepoteza fahamu lakini Shafii alikuwa ameshakata roho tayari.
Wote walijiinamia chini huku Magdalena akilia kwa kwikwi akijizuai sauti isitoke.
Hii haikuwa huzuni tu Bali lilikuwa pia ni pigo kubwa kwao. Kwanza alikuwa Kanali ambaye walimpoteza kando kando ya mto ndani ya Anabelle baada ya kunyakuliwa na mnyama wa ajabu na kuzama naye ndani ya mto na tangu hapo hawajamuona tena Kanali. Sasa Shafii.
“Mwili wake uko wapi?” Magdalena akauliza huku bado akilia kwa kwikwi.
“Sikuweza kuutoa ndani ya Anabelle!” Salim alijibu huku amejiinamia.
“Unasemaje? Unawezaje kumuacha…..” Magdalena alianza kufoka kabla ya kukatishwa na Cindy.
“Hebu nyamaza Magdalena… tayari tunapitia kipindi kigumu tusitake kufanya mambo kuwa magumu zaidi kwa kulaumiana… kila mtu atylize munkari na tujadili sasa tunafanya nini!” Cindy aliongea kwa ukali kumnyamazisha Magdalena ambaye alikuwa anataka kuanza kulalama kama ilivyo kawaida yake.
Ulipita ukimya wa kama dakika mbili nzima bila yeyote yule kusema neno. Wote walikuwa wamejiinamia chini kuwaza na kuwazua. Kuomboleza na kujiuliza wanafanya nini kutokea hapa.
“OK! Nashukuru kwa utulivu wenu..” Cindy aliongea kwa utani ili kuondoa msongo kwenye muda huu wa huzuni. “Salim uliwezaje kufungua mlango? Ulipata wapi detail namba 127 ya mchoro wa George Washington?” Cindy alimuuliza Salim.
Salim alionekana kuwa mbali kimawazo kiasi kwamba alikuwa kana kwamba hasikii kile ambacho Cindy alikuwa anamuuliza.
“Salim!” Cindy alimuita kwa sauti ya juu zaidi kama vile amshitue Salim kutoka kwenye maawazo ambayo alikuwa nayo.
“Unasemaje?” Salim alijibu huku amekunja uso kuashiria kukereka na jinsi ambavyo Cindy alimuita kwa sauti kubwa.
“Nimekuuliza ulipata wapi detail namba 127 ya mchoro wa George Washington?” Cindy akauliza tena.
“Una maana gani kuniukiza hivi? Hukumbuki kabla haujapoteza fahamu nilikusomea ujumbe nilioutoa kwenye chupa kutoka duniani?” Salim aliuliza huku akimshangaa Cindy kwa kumuuliza swali la namna hiyo.
“Sikumbuki chochote… ujumbe alikuwa umeandikwaje?” Cindy aliuliza huku amemkazia macho.
“Huo ujumbe ndio ambao ndani yake waliandika hiyo detail kwamba ni 6, 1, 9.” Salim akajibu kwa ufupi tu.
“Hapana! Kujua ujumbe wote ulikuwa unasemaje?” Cindy aliuliza huku anamuangalia Salim kwa shahuku.
“Cindy acha kuniumiza kichwa ujumbe ulikuwa mrefu… cha muhimu tumepita kwenye mlango wa The 46.. Sidhani kama haya ni ya muhimu!” Salim alijibu huku anajiinamia tena kurejea kwenye lindi lake la mawazo.
“Nisikilieze Salim.. Ni muhimu sana sana! Nahitaji kujua ujumbe wote ulikuwa unasemaje?” Cindy aliongea kwa msisitizo mpaka akamshika mabega Salim na kuongea nae huku nyuso zao karibia zigusane.
Salim aliona namna ambavyo Cindy alikuwa ‘serious’ ndipo ambapo alianza kujizoa zoa kifikra na kuvuta hisia kukumbuka kile ambacho kilikuwa kimeandikwa kwenye ujumbe.
“Aaannh! Ulikuwa umeandikwa aannhh kitu kama hizo details na kuhusu nguo za rais Laura na tumekaa muda gani… aaannh aisee sikumbuki kabisa!” Salim aliongea huku anakuna kichwa.
“Salim kumbuka… ni lazima ukumbuke! Ni lazima ukumbuke Salim” Cindy akimtikisa mabega zaidi kusiaitiza hoja yake kwamba ni muhimu mno kwa salim kukumbuka ujumbe huo.
Salim alianza kuvuta hisia na kukaa kimya karibia dakika mbili nzima. Akuvuta hisia haswa.
“Ndio… nadhani nimekumbuka!” Aliongea huku anainuka kusimama.
“Ulikuwa unasemaje?” Cindy aliuliza kwa shauku kubwa zaidi.
“HATUJUI KAMA BADO MKO HAI AMA LA… UMEPITA MWEZI MMOJA SASA TANGU MUINGIE NDANI YA ANABELLE 27. KAMA BADO MKO HAI HAYA NI MAJIBU YA MLICHOULIZA. DETAIL #127 NI 6, 2, 1, 9. PIA TUNAWASISITIZA MLINDE MLICHOKIPATA KUHUSU MADAM PRESIDENT KULIKO CHOCHOTE KILE. X3. X3. X3.”
Salim akamueleza Cindy kwa ufasaha kabisa nukta kwa nukta.
Wote watatu wakiwa wamesimama, Cindy alianza kugeuka geuka kama vile kuna kitu alikuwa anakitafuta.
“Nini Cindy?” Magdalena hatimaye akaongea.
“Nguo za Madam President na vitu vyake vingine viko wapi?” Cindy aliuliza huku amemkodolea macho Salim.
“Sikufanikiwa kutokanazo!” Salim alimjibu huku anajiinamia.
Mshituko ambao ulikuwa usoni mwa Cindy ilikuwa kana kwamba ameona jini au kusikia taarifa mbaya zaidi maishani mwake.
“Mungu wangu, Mungu wangu! Tumekwesha!!” Cindy alihamaki.
“Nini Cindy?” Salim akamuuliza huku amemkazia macho.
“Ile chupa iko wapi?” Cindy aliuliza bila kujibu swali la Salim.
“Sijafanikiwa kutoka nayo pia!” Salim alijibu kwa ukali safari akikumbuka namna ambavyo waliponea chupu chupu kularuriwa na binadamu wa ajabu watoto wa Maldives ndani ya Anabelle na yeye kufanikiwa kuwaokoa wenzake wote lakini sasa alijihisi kana kwamba walikuwa wanamuona mzembe kwa kuacha vitu walivyokuwa wanauliza.
Lakini Cindy hakuwa anamlaumu Salim bali mshituko aliokuwa nao ulitokana na kile ambacho alikijua kitafuata kutokana na wao kukosa kuwa na vitu hivyo.
Cindy aliendelea kugeuka huku na huko pale kwenye mchanga wa bahari walipo.
“Cindy ni nini?” Salim aliuliza.
“Nifuateni!” Cindy aliongea kwa kifupi huku alianza kutembea kutoka pale kwenye pwani kuelekea kwenye msitu ambao ulikuwa unaonekana kwa mbali mbele yao.
Walitembea kama dakika kumi na tano hivi bila Cindy kuongea chochote. Wakipoukaribia ule msitu ukiwa kama mita ishirini hivi mbele yao Cindy alianza kutembea kwa kuambaa ambaa na pwani bila kuingia ndani ya msitu. Alikuwa anatembea huku macho yako chini kama vile kuna kitu alikuwa anakitafuta ardhini. Wenzake walikuwa wanamfuata nyuma wasijue hata ni nini ambacho Cindy alikuwa anakitafuta ardhini.
Walitembea hivyo kwa kuambaa ambaa na pwani kwa muda wa kama dakika kumi hivi mpaka walipofika mahala ambapo Cindy aliwaamuru wenzake wasimame.
“Simameni hapo hapo!” Cindy aliongea kwa ghafla.
“Ni nini?” Salim na Magdalena waliuliza kwa pamoja.
“Angalieni!” Cindy aliwaonyesha kidole chini ardhini.
Kulikuwa na pea kama sita hivi za nyayo za binadamu zilizokanyaga chini na kuaacha alama. Pea mbili zilikuwa zimeachana katikati nafasi ya kama mita moja hivi huku mbele yake kuliwa na pea nyingine ikiwa na nafasi kama hizi katikati.
Mbele na nyuma ya pea hizi nne kuliwa na pea nyingine moja moja.
Kwa muda ambao walikaa ndani ya Anabelle Salim na Magdalena walijikuta wanashituka isivyo kawaida kuona nyayo za binadamu ardhini.
“Akina nani hawa?” Magdalena akauliza.
“Sijui… lakini kwa namna ambavyo hizi nyayo zimekaa ardhini inaonyesha walikuwa wamebeba kitu… kitu kama sanduku kubwa lenye pande nne kila upande ukiwa na mtu mmoja na na mbele alitangilia kiongozi wa msafara na nyuma kukiwa na mtu mmoja kulibda waliobeba sanduku.!”
Salim aliongea kwa kutumia uzoefu wake wa ujasusi aliojifunza ndani ya idara ya usalama wa Taifa. Aliongea huku anawaonyesha nyayo jinsi zilivyojipanga pale ardhini.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Walibeba jeneza!” Cindy aliropoka na kufanya wenzake wamtumbulie macho kwa mshangao.
“Kwa nini unasema hivyo?” Magdalena akauliza kwa taharuki kubwa.
Cindy alianza tena kugeuka huku na huko huku akipepesa macho kama vile anajaribu kupata uhakika wa alichokuwa anataka kukisema kabla hajatamka.
“Naam! Walibeba jeneza… mnajua kwa nini?” Cindy aliwauliza wenzake huku anatabasamu. Alikuwa tabasamu la furaha, lilikuwa ni tabasamu la woga na kukata tamaa.
Hakuna ambaye alimjibu Cindy… wote walibaki wanatetemeka baada ya kuona tabasamu la woga la Cindy. Walijua hakuwa na habari njema.
Kuna macho huwa yanamtoka mtu akiwa na woga na kuna macho huwa mtu anayakodoa kama vile amemuona shetani. Lakini hakuna macho ya kuogofya kama mtu aliyekodoa kama vile ameona kifo mbele yake.
Salim, Cindy na Magdalena walitazamana kwa woga huku wamekodoa macho wakikona dhahiri kabisa mbele yao harufu na taswira ya kifo.
“Walibeba jeneza…” Cindy alirudia tena huku anatabasamu kwa woga akipepesa macho kutazama huku na huko.
“Tuko ndani ya ardhi ya Himaya ya The 46… tuko kwenye pwani ya Rabat, Morocco.!!”
Previously…
Mzee Caleb anamaliza kufukua mabaki ya mifupa ya mkewe Suzanne na mwanaye Clinton kutoka kwenye kaburi lililopo nyuma ya nyumba yake. Mifupa mingine yote anaiweka kwenye mifuko miwili ya plastiki huku mafuvu ya vichwa akiyasaga na kuweka unga wake kwenye chupa mbili.
Akiwa anajiandaa kujitoa damu ili ampe kiumbe wa ajabu waliyepewa kwenye msitu wa Ox, vijana makomando waliomkimbia masaa kadhaa nyuma wanarejea na kumpa taarifa kuwa maafisa wa National Guard wametanda kwenye mpaka wa Maryland na jimbo la Washington na hawaruhusu mtu yeyote kuvuka.
Hawawezi kwenda kusini, kaskazini wala mashariki kwa kuwa huko wanapakana na miji ya Baltimore na Annapolis ambayo tayari imekwisha twaliwa. Chaguo pekee walilo nalo ni kubakia hapo watwaliwe pamoja na mji wao wa Maryland au waende Baltimore na Annapolis ambayo tayari imeshafanywa kuwa Anabelle.!
Episode 37
"Kurudi nyuma ndio kwenda mbele.!"
"Una maana gani mzee?"
"I say backwards is the only way forward!" Mzee Caleb aliongea huku anainuka kutoka pale sakafuni alipokuwa ameketi kutokana na kupigwa bumbuwazi kwa taarifa aliyopewa.
"Nimekusiki ndio maana nimekuuliza una maana gani?" Moja ya vijana wa Ethan aliuliza tena.
"Tunahitaji kurudi msituni tena.!!" Mzee Caleb aliongea huku anachukua tena mpira mwembamba na kisu na kuanza kushuka ngazi kwenda chini kwenye 'basement' ya nyumba.
Vijana wote saba wa Ethan nao waliinuka na kuanza kumfuata kule chini ambako alikuwa anaelekea.
"Kufanya nini ndani ya msitu?" Komando mwingine akauliza kwa kuhamaki.
"Kama kuna lolote la kutuokoa nadhani Masalia, mzee wangu na wenzake ndio pekee wanaweza kujua tufanye kitu gani! Na kama hakuna cha kufanya basi ni bora tutwaliwe tukiwa pamoja nao lakini….."
Mzee Caleb aliongea alafu akasita kumalizia sentesi yake.
"Lakini nini?" Kijana mwingine akauliza kwa woga.
"Lakini sina hakika kama tutawapata ndani ya msitu… Masalia wanahama hama muda wote kulingana na malengo yao… kwa hiyo tunachokwenda kufanya ni kubahatisha.!"
Hakuna ambaye aliuliza swali au kusema chochote kile. Ilionekana kwamba bahati haikuwa upande wao hata kidogo. Ilikuwa kama vile kila mti waliokuwa wanajaribu kuuparamia ulikuwa unateleza.
Walishuka na ngazi mpaka chini kwenye basement. Japokuwa ndani ya basement kulikuwa kuchafu, utando wa buibui kila mahala na makorokoro kibao lakini kutokana na utofauti wa yule kiumbe wa ajabu alikuwa ndiye kitu cha kwanza macho kukiona ukiingia tu ndani ya basement. Rangi nyekundu iliyotokea mwilini mwake ilikuwa imekooza zaidi na ilionekana kuendelea kukooza taratibu kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Bado alikuwa kama vile amelala usingizi ndani ya kile kitundu alichofungiwa.
"Unataka kufanya nini mzee?" Yule komando muongeaji sana akamuuliza Mzee Caleb huku anamtazama kwa macho ya udadisi.
"Tunahitaji kumpa damu huyu kiumbe kama tulivyoambiwa msituni.!" Mzee Caleb alijibu macho yake akimtazama yule kiumbe wa ajabu.
"Kwa hiyo unataka kutoa lita moja ya damu mwilini mwako?" Alimuuliza huku anatabasamu kifedhili kama 'anamuinjoi' hivi.
"Tunahitaji kumpa damu huyu kiumbe!" Mzee Caleb alirejea tena jibu lake huku akikwepesha macho na kumuangalia tena yule kiumbe pale tunduni.
"Frank! Nenda kwenye sanduku la huduma ya kwanza lete vifaa tunavyohitaji kutoa damu!" Komando muongeaji sana alimuagiza mwenzake.
Labda ilikuwa ni moja ya maadili yao ya kazi kwa sababu hii ilikuwa ni mara ya kwanza tangu kiongozi wao Ethan aondoke Caleb kuwasikia wanaitana kwa majina. Muda wote huu ambao walikuwa wote, mtu pekee ambaye Mzee Caleb alimfahamu jina alikuwa ni kiongozi wao Ethan ambaye hakuwepo hapa muda huu.
Yule kijana alikuwa kama vile amekisoma kile ambacho Mzee Caleb alikuwa anakiwaza kichwani.
"Jina langu ni Walker, huyu ni Justin, huyu Mickie, huyu Thabeet, huyu Rex, yule pale Saimon na aliyeondoka nadhani umesikia jina lake, Frank.!!" Yule komando muongeaji, Walker alijitambulisha na kuwatambulisha wenzake wote wengine sita waliosalia.
Yule komando, Frank aliyekwenda kuchukua vifaa vya kutolea damu alirejea mkononi akiwa na mipira kadhaa ya kutoa damu na vifaa vingine.
Hakuna komando ambaye aliongea neno lolote, lakini makomando watano kila mmoja alichukua seti ya vifaa na kukaa chini. Walker ambaye alionekana kama ndiye kiongozi wao baada ya Ethan kuondoka akaanza kuwachomeka mipira kwenye mishipa ya damu mmoja baada ya mwingine kwa ustadi kama ambavyo madaktari wafanyavyo.
Zilipita kama dakika ishirini na tano au thelathini za ukimya kila mtu akiwaza na kuwazua kichwani mwake kuwasubiria wenzao watano wanaotoa damu itimie kiwango kile ambacho walikuwa wanakihitaji.
Wote walikaa kimya kabisa wakionekana kila mmoja kuwa mbali kimawazo. Muda ulikuwa unayoyoma haswa. Walikuwa na labda Massa mawili tu kabla Maryland haijatwaliwa kuwa Anabelle. Tumaini la kuokoka kutokana katika uwezekano huu wa kutwaliwa pamoja na mji wa Maryland lilikuwa dogo mno. Japokuwa walikuwa wanajitahidi kufanya juhudi kadhaa kujiokoa lakini kwa namna Fulani kila mmoja wao alikuwa anajua ni nini kilikuwa mbele yao, kutwaliwa ndani ya Anabelle na kupotelea kusikojulikana.
"Nadhani imetosha.!" Walker alivunja ukimya na kuwazindua wenzake kutokana kwenye 'usingizi' wa mawazo wa takribani dakika theleathini. "Tupime hiyo damu tuone tuna kiwango gani!"
Makomando wote watano kila mmoja akajitoa mpira mkononi kwenye mshipa wa damu na kukandamiza kwa pamba mahala ambapo walichomeka sindano kuingia mshipani na kisha Walker kuchukua vipakiti vya plastiki vyenye damu kutoka kwa makomando wale watano na kuanza kuipima kwa kuweka kwenye chupa ambayo alikuwa nayo Mzee Caleb.
"Lita moja na…na… na kama robo hivi.!" Walker aliongea huku anamtazama Caleb kwa tabasamu la utani.
Chupa iliyoletwa na Caleb ilijaa yote mpaka juu shingoni na bado kipakiti kimoja cha damu kilibakia. Hii ilimaanisha kwamba walikuwa na lita moja na ushei, ambayo Walker alikisia kuwa ni Lita moja na robo.
"Sikumbuki kama Mzee wako kule msituni alieleza ni namna gani tunampatia hii damu… naamini sio kumnywesha mdomoni kama mtoto mchanga.!" Walker aliongea tena huku anatabasamu.
Mzee Caleb hakujibu chochote. Aliichukua chupa iliyojaa damu kutoka mkononi kwa Walker. Alipoishikilia mkononi alihisi kabisa joto ambalo lilikuwa linatoka kwenye damu. Alihisi kabisa uhai wa binadamu uliomo ndani ya hiyo chupa. Kwa kiasi fulani ilikuwa inaogofya kushikili chupa kubwa ya ujazo huo wa lita moja ikiwa imejaa damu ya binadamu ambayo bado ilikuwa ya moto kabisa kutoka kwenye mwili wa mtu. Chupa ilikuwa ndefu wastani wa kama urefu wa chupa ya soda lakini ilikuwa pana kiasi cha kurandana kabisa na upana wa bilauli ndogo.
Mzee Caleb alishikilia chupa mkononi akitafakari ni nini hasa afanye. Haikuwa busara kufungua kitundu na kuingia ndani ili kujaribu kumnywesha damu mdomoni mnyama huyu wa ajabu kwani hakuna ambaye alikuwa anajua mnyama huyu akipata damu ni nini ambacho kingetokea.
Mzee Caleb akachovya kidole kimoja kwenye damu. Mwili ulimsisika alipoingiza kidole chake kwenye dimbwi hilo la lita moja ya damu iliyo ya moto bado. Akachovya kidole na kutoa kisha akasogea karibu na kitundu cha yule mnyama na kukung'uta mara kadhaa ya damu juu ya mnyama huyu.
Matone kadhaa ya damu yalidondoka juu ya ngozi laini ya mnyama huyu ambayo sasa ilikuwa na rangi nyekundu iliyoiva haswa kiasi kwamba hata tone la damu lilipodondoka juu yake lilikuwa halionekani sawia ni wapi lilikuwa limedondokea.
Kuna kitu fulani hivi Caleb alikiona juu ya ngozi ya mnyama japo hakuwa na hakika sana. Akachovya tena kidole kwenye bilauli ya damu na kunyunyiza tena matone kadhaa ya damu juu ya mnyama huyu wa ajabu.
Naam, haikuwa anakosea wala kuona vibaya. Sehemu ambayo matone ya tamu ilikuwa inadondoka ilikuwa inabadilika na kuwa ya rangi nyeupe.
Mzee Caleb akasogea karibu zaidi na kitundu cha mnyama na kupenyeza ndani mkononi wake alioshikilia bilauli ya damu na kuimimina damu yote juu ya mnyama huyu.
#540
Damu ilikuwa inamwagika juu ya mnyama huyu lakini ajabu ni kwamba alikuwa alowi. Yaani kama kwamba alikuwa anamimina maji kwenye sponji. Damu ilikuwa haimlowanishi kiumbe huyu badala yake ilionekana kufyonzwa ndani ya mwili wake.
Baada ya Caleb kumaliza kumimina damu yote, taratibu rangi ya ngozi ya mnyama huyu ilianza kubadilika na kuanza kurejea mwenye weupe.
Mzee Caleb na wenzake walikaa pembeni kushuhudia viroja hivi vilivyokuwa vinatokea mbele ya macho yao. Ndani ya kama dakika tano hivi rangi ile nyekundu iliyokolea ya ngozi ya huyu mnyama iligeuka na kuwa rangi nyeupe kabisa, nyeupe sana kufanana kabisa na weupe wa sufi au theluji. Hata mnyama mwenye japo hakuamka kabisa lakini alionekana kuhema.
"Nadhani tumefanikiwa au tumeongeze tena mpaka aamke l?" Walker aliongea.
"Hapana! Tuliambiwa lita moja ya damu itamfanya asife lakini pia hatoweza kuamka na kuleta madhara… tukiongeza hata damu kidogo nyingine tunaweza kujutia kufanya hivyo… nadhani mpaka hapa tumefanikisha!" Caleb akajibu.
"Kwa hiyo kifuatacho?" Walker akauliza tena.
"Tunaelekea msitu wa Ox!!" Caleb akajibu.
"Ooooh!! Mungu tu anajua kiasi gani nachukia ndani ya ule msitu natamani kungekuwa na wazo lingine!" Walker akaongea akiwa amekereka.
"Backwards is the only way forward! Mbebeni huyu mnyama twende, tuna chini ya Massa mawili kabla Maryland haijatwakiwa!" Caleb aliongea huku anaanza kuondoka kwenye basement kuzifuata ngazi zinazoelekea juu.
Lakini ghafla…..
"Oooh! Oooh! Oooh.. Aaah.!!"
Mzee Caleb alidondoka chini kwenye ngazi huku amejishika kifuani akiwa kama analalamika mauvimu.
"Mzee nini.!?" Walker na wenzake wawili walimbilia na kumuokota kutoka chini kwenye sakafu alikokuwa anagala gala na kumkalisha kitako.
"Imekuwaje mzee?" Walker akamuuliza tena huku amemtumbulia macho.
"Nipelekeni sebuleni! Njooni na huyo mnyama…" Mzee Caleb aliongea kwa taabu sana huku bado amejishika kifuani.
Walker na wenzake wawili wakambeba Caleb kuelekea juu sebuleni huku wenzao wanne waliosalia wakibeba kile kitundu chenye mnyama ndani yake.
"Vipi mzee? Mshituko wa moyo?" Walker aliuliza walipofika sebuleni.
"Hapana!" Caleb alijibu kwa shida sana.
"Ni nini kumbe?"
"Mnakumbuka niliwaeleza kuwa nilipokuwa mdogo mzee wangu aliwahi kunipeleka msituni ambako nilitolewa nusu ya nafsi yangu na kupewa mtu mwingine?" Mzee Caleb aliongea huku akiwa anahema juu juu.
"Ndio ndio! Umetueleza hapa kabla Ethan na Naomi hajaondoka kwamba mtu huyo ndiye ambaye alivamia Whitehouse na Makamu wa Rais David Logan kudhani ni wewe.!!" Walker alimjibu kwa haraka haraka.
"Naam! Niliwaeleza kwamba tunapaswa kumfuatilia yeye ili tuweze kuwapata The 46 na dalili ya kumpata yeye niliwaambia kuwa kuna hali huwa najisikia ndani yangu…"
"Ndio ndio mzee!"
"Ndio hali hii ninayojisikia sasa… yuko maeneo haya! Tulipanga tumtafute ila anaonekana ametutafuta yeye… kuna kitu kibaya anataka kukifanya… yuko karibu kabisa na hapa ndio maana najisikia namna hii ndani yangu!" Mzee Caleb aliongea akionekana kuwa kwenye maumivu makali akiendelea kuhema kwa shida sana.
Makomando hawakusubiri Caleb aseme neno lingine lolote lile, kila mmoja alikamata bunduki yake huku kidole kikiwa kwenye 'triger' tayari kwa kushambulia muda wowote ule. Kwa haraka na weledi waligawana kila mmoja akienda dirisha la upande fulani wa nyumba na kuchungulia nje kudadisi kama wanaweza kumona mtu huyo.
"Kwa hiyo tunafanyaje sasa mzee?" Walker ambaye alikuwa amebaki na Mzee Caleb pale alipo alimuuliza kwa kunong'ona.
"Backwards is the only way forward! Twendeni msitu wa Ox!" Mzee Caleb akajibu.
Walker akawapa wenzake maelekezo kwa ishara za vidole kuashiria kwamba wanatakiwa waondoke hapo haraka.
Safari hii Walker peke yake alimbeba Mzee Caleb kama vile amembeba mtoto mdogo mikononi, huku wenzake wanne wakibeba Kitundu chenye yule mnyama na wawili waliobakia wakitoa ulinzi kwa wenzao kwa kukaa pande zote mbili wakipepesa macho huku na huko kuhakikisha hawashambuliwi kwa kushitukizwa.
Walipanda kwenye magari kwa haraka huku, gari la kwanza wakipanda makomando wawili na nyuma kuweka tundu lenye yule mnyama. Gari la pili walipanda komando mmoja akiwa anaendesha kwenye usukani na siti za nyuma walikaa Walker na Mzee Caleb. Na gari la Tatu lilifuatia nyuma likiwa na makomando wawili.
Mzee Caleb bado alikuwa anaugulia maumivu kifuani. Walikuwa wamebakiwa na kama lisaa limoja na nusu kabla ya Maryland kutwaliwa.
Gari ziliendeshwa kwa spidi kubwa ajabu kama vile roketi lakini ajabu ni kwamba bado Mzee Caleb aliendelea kuugulia ile hali aliyokuwa anaisikia kifuani kumaanisha kwamba mtu huyo mwenye nafsi yake bado alikuwa anawafuatilia.
"Inawezekanaje hii? Huyo mtu ana kasi ya namna gani kukimbizana na gari mwenye spidi kubwa hivi?" Walker alihamaki.
"Si binadamu wa kawaida… au umewahi kusikia binadamu mwenye nafsi nusu?" Mzee Caleb aliongea.
"Anataka nini kwetu?" Walker akauliza.
"Mambo mawili… kwanza naamini amejua tunaelekea Ox na anataka kutuzuia… na pili anahitaji nafsi yangu nusu iliyobaki ili awe nayo kamili… kuna vitu anatakiwa kufanya na hawezi mpaka nafsi yote kamili iwemo ndani yake!"
"Vitu gani?"
Mzee Caleb hakujibu kitu bali alikuwa ameduwaa ametoa macho anatazama nje barabarani.
Pembezoni mwa barabara kulikuwa na msongamano mkubwa sana wa miti, na ndani yake alionekana mtu au kwa usahihi zaidi tuseme kivuli cha mtu. Mtu huyu hakuonekana hata kiganja cha mkono au ukucha. Alikuwa amevalia vazi zito jeusi tii kama kaniki ambalo lilimfunika kuanzia kichwani mpaka vidole vya mguu. Mahala pekee ambalo alikuwa anaonekana ilikuwa ni usoni ambako alikuwa anaonekana kwa mbali sana kutokana na vazi hilo kufunika kichwa. Alikuwa na uso wa ajabu wenye ngozi yenye mabaka kama chatu na macho mekundu ambayo yalikuwa yanawaka kama taa.
Mtu huyu alikuwa anakimbia kwa kasi isiyo ya kawaida. Japokuwa Makomando walikuwa wanaziendesha gari kwa spidi ya juu kabisa ya kiwendawazimu lakini mtu huyu alikuwa anakimbia kwa kasi hiyo hiyo bila kuachwa nyuma huku manguo yake meusi aliyojitanda mwili mzima yakipepea kutokana na upepo.
"Ni yeye?" Mzee Caleb alijibu huku bado amekodoa macho nje.
"Nani?" Walker akauliza.
"Ni yeye! Niliyewaeleza kuwa ana nusu ya nafsi yangu… ni yeye huyu!"
"Umesema kuna jambo wanataka kufanya haliwezekani mpaka mtu huyu awe na nafsi yako kamili! Ni kitu gani?" Walker akauliza kwa shauku.
"The 46 wanajiandaa kufanya kafara ya pili.!!" Mzee Caleb alijibu kwa sauti ya kutetema kwa woga huku bado akiangalia nje kwa binadamu yule mwenye nusu ya nafsi yake.
Previously….
Rais was Marekani Bi. Laura Keith amehuisha Marshall Law nchi nzima baada ya dunia kukumbwa na giza la kabla muda wa mchna na giza kutoonyesha dalili yoyote ya kukoma. Chini ya sheria hii hakuna raia yeye ambaye anaruhusiwa kutoka nje au kuonekana mtaani. Maafisa wa vikosi vya kijeshi vya National Guard wamemwaga mtaani kote.
Hii inakuwa ni bahati mbaya kubwa kwa Bilionea Rodney Van Der Berg ambaye alikuwa nyumbani kwa familia ya Bw. Donald McLaren na mkewe Latisha ili kuomba mtoto wao Natalie awasaidie kumtafuta David Logan ambaye alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.
Lakini kuna gari la jeshi limefika nje ya nyumba ya Familia ya Donald McLaren na maafisa wawili wa National Guard walikuwa wameshuka huku wameshikilia mitutu ya bunduki na kwenda kugonga mlangoni.
EPISODE 38
Scarsdale, New York - Marekani
Mlango wa nyumba ya familia ya Bw. Donald McLaren ulifunguliwa na maafisa wa jeshi kuingia ndani.
"Habari.!" Afisa mmoja alisalimia.
Donald, mkewe Latisha, mtoto wao Natalie, Ron pamoja na walinzi wake, wote walikuwa kama vile hawajaisikia salamu walibakia wamewatumbulia macho tu.
"Gari iko tayari?" Ron aliwauliza wale wanajeshi.
"Iko tayari Mkuu?" Mwanajeshi mmoja akajibu.
"Nisubirini nje nakuja!" Ron aliwajibu kwa kifupi tu.
Wanajeshi wale wawili walitoka nje. Donald na mkewe walibakia wameduwaa wakishangaa ni nini kilikuwa kinaendelea.
"Nahitaji kwenda na Natalie sasa hivi bila kuchelewa!" Ron aligeuka nyuma kuwaangalia Donald na mkewe na kuwaeleza.
"Kwanza naomba utueleze ni nini kinaendelea hapa? Kwa nini hawa wanajeshi wakuletee gari?" Latisha aliongea akiwa na mshangao.
"Donald, Latisha! Sidhani kama ni jambo la kushangaza kwa mtu wa kaliba yangu kuweza kupata 'favour' za namna hii… labda tu niseme kwa ufupi kila kitu kina bei yake duniani… mmeridhika? Naweza kwenda na Natalie sasa?" Ron aliongea huku anatabasamu wa majivuno.
"Siwezi kukukabidhi binti yangu bila mimi mwenyewe kuwepo! Kama unahitaji kwenda na Natalie basi lazima na mimi niwepo" Latisha kaweka msimamo.
"Na siwezi kuacha binti yangu na mke wangu waondoke bila uwepo wangu! Lazima na mimi niwepo!" Donald nae akalipuka ghafla na kuweka msimamo kama wa mkewe.
"Hey, hey, hey! Samahani natamani tungeenda wote hata na ukoo wenu mzima… tatizo ni kwamba nadhani mnajua kuna Marshall Law na hakuna gari ya kiraia inayoruhusiwa barabarani… tumefanikiwa kupata gari moja tu ya kutusafirisha, kwa hiyo kama ni kwenda basi mchague ni nani ambaye ataenda kati yako na mkeo hatuwezi kutosha wote ndani ya gari!"
Hakukuwa na ubishi kwamba kama ni kwenda basi Latisha ndiye ambaye alitakiwa kwenda kwa kuwa yeye ndiye alikuwa mama mzazi na Donald alikiwa baba mlezi tu kwa Natalie.
Baada ya kukumbatiana na kufarijiana, Latisha na mwanaye Natalie wakiongozana na Ron pamoja na mlinzi wake mmoja waliondoka.
Ndani ya gari siti za mbele walikaa wale wanajeshi wawili ambao walikuja na ile gari na siti mbili za nyuma Ron, mlinzi wake, Latisha na Natalie walibanana kwa pamoja.
"Tunaelekea wapi bwana mkubwa?" Mwanajeshi ambaye alikuwa kwenye usukani aliuliza.
"Naval Observatory Circle… nyumbani kwa Makamu wa Rais!" Ron alijibu.
Natasha alitamani kumuuliza Ron kwa nini wanaenda nyumbani kwa mumewe wa zamanai wakati amewaeleza muda mchache uliopita kwamba ametekwa lakini hakuthubutu kuuliza swali lolote ambalo alihisi la siri kubwa mbele ya hawa wanajeshi wa National Guard.
Ilikuwa safari ndefu ya karibia masaa manne na nusu. Mpaka muda ambao walikuwa wanawasili ilikuwa tayari yapata karibia saa nne usiku lakini kutokana na giza lililokuwepo tangu mchana hakukuwa na tofauti yeyote ya muda ambayo ilihitaji kuitilia maanani.
Jengo la nyumba ya Makamu wa Rais lilikuwa limezungushiwa utepe wa njano wa polisi kutokana na tukio la mauaji ya maafisa wa Secret Services mahali hapo siku chache nyuma lakini ajabu ni kwamba kulikuwa na askari wawili tu wa kawaida ambao walikuwa wanalinda. Labda ni kwa sababu ya nchi kuwa kwenye wakati mgumu ndio maana vyombo vya ulinzi haviku havikuona umuhimu wowote wa kutumia rasilimali kubwa kulinda jengo tupu badala ya kulinda mitaani ambako kulikuwa na taharuki.
Wale wanajeshi wawili waliokwenda nao waliwasaidia kuwapitisha kwenye kizuizi cha polisi kwa kuongea na askari wale wawili ambao walikuwa wanalinda mahali hapa na moja kwa moja wakaingia ndani ya eneo hili la Makazi ya Naval Observatory Circle.
"Maagizo yetu yalikuwa kukupeleka mahala unakohitaji tu bwana mkubwa nadhani tumefanya hivyo na itakuwa sahihi tukirejea kwenye jukumu letu huko mitaani.!" Moja ya wale wanajeshi akaongea.
"Nahsukuru sana na amfikishieni Meja Lewis shukrani zangu!" Ron akashukuru na kupena mikono na wale wanajeshi.
Wanajeshi wakakwea kweye gari yao na kuondoka wakiwaacha hapa nje ya jumba la Makamu wa Rais.
"Unawaacha waondoke tukimaliza tunachofanya hapa tunatejea vipi nyumbani?" Latisha akamuiliza Ron.
"Usijali kuhusu hilo...!" Ron alijibu kwa kujiamini huku wakitembea kuufuata mlango wa nyumba.
Kutokana na nyumba kuwa tupu na tukio ambalo lilikuwa limetokea, hakuna mlango wowote ambao ulikuwa umefungwa.
Waliingia ndani kwenye sebule kubwa ya nakshi za fanicha za thamani lakini za enzi za "kikoloni". Japokuwa vitu hapa sebuleni hasa fanicha kuwa za enzi zilizopita lakini uthamani wake wa hali ya juu ulifanya sebule iwe nzuri na ya kuvutia kabisa.
Walitumia kama dakika kumi nzima kushangaa shangaa na kudadisi pale sebuleni. Wote wanne, yaani Ron, mlinzi wake, Latisha na Natalie kila mmoja alitumia muda wake kutazama sebule na kudadisi kadiri ambavyo alikuwa anaweza. Kila moja mara alishika picha Fulani akaiacha, mara ashangae Picha za viongozi wa zamani wa taifa, mara ashangao sanamu za kuchongwa na kufinyanga… ili mradi tu ilikuwa kudadisi japokuwa hata walichokuwa wanakidadisi hawakukijua. Japokuwa hapa ndani kulikuwa kunapendeza lakini bado sehemu kadhaa bado zilikuwa zimetapakaa damu kutokana na tukio la mauaji wa siku chache zilizopita.
"Ron! Tunafanya nini hapa?" Latisha aliuliza kwa kukereka baada ya kuchoka kushangaa na kudadisi bila kujua hata ni nini ambacho alipaswa kudadisi.
"Siwezi kusema ni nini hasa tunapaswa kuangalia lakini nina hakika kuwa kuna namna fulani ambayo David atakuwa ameacha usia kwa mtoto wake Natalie.! Tunachotakiwa kukifanya ni kuangalia kitu chochote kile ambacho kitawasha taa vichwani mwetu na kutufungulia njia ya kuijua siri ambayo David alikuwa anaifahamu.!"
"Bado sielewi ni kwa nini una uhakika asilimia mia kuwa David atakuwa ameacha ujumbe kwa ajili ya Natalie... OK, vyovyote vile tuendelee na hiki unchokifikiri.!" Latisha aliongea kwa kukereka huku anageuka kuendelea kushangaa shangaa tena.
Hakuwa amekosea, Rodney Van Der Berg alikuwa hasemi ukweli wote. Alichokuwa anakisema kilikuwa ni nusu tu ya ukweli wote anaoujua kuhusu David na kwa nini ana uhakika kuwa kuna ujumbe kwa ajili Natalie. Lakini alikuwa na sababu kwa nini hakutaka kusema ukweli wote. Alikuwa na sababu ya kifedhuli kabisa.
"Natalie baba yako alikuwa mtu 'busy' sana… ni namna gani mlikuwa mnatumia muda wenu pamoja pindi akipata muda mchache wa kuwa nawe?" Ron alimuuliza Natalie ambaye alikuwa busy kushangaa kinyago fulani kwa kuchingwa hapo sebuleni.
"Anh! Mara nyingi tulikuwa tunacheza table tenisi… yeye ndiye aliyenifundisha na kunifanya nipende table tennis mpaka sasa!" Natalie alijibu bila kugeuka akiendelea kushangaa shangaa tu.
"Mlikuwa mnacheza wapi hiyo table tennis?" Ron aliuliza kwa shahuku kubwa safari hii.
"Chini kwenye basement.!" Natalie alijibu tena kawaida tu akiendelea kushangaa shangaa.
Lakini kuna taa iliwaka kichwani kwa Ron.
"Twendeni!" Ron aliongea kwa haraka na kuanza kutembea kwa pupa.
"Wapi?" Natalie akauliza.
"Chini kwenye basement!" Ron aliongea bila kugeuka kwa sauti ya uroho huku tayari akiwa amepiga hatua kadhaa kuelekea kwenye mlango ambao kwa ndani chini ulikuwa na ngazi za kushuka chini kwenye basement.
Natalie, Latisha na mlinzi wa Ron walifuata nyuma nao kwa kasi wakishangaa shahuku hii ya ghafla ya Ron.
"…labda baada ya yote haya tutaishi kuiona siku nyingine, tutaishi kuona tena jua likichomoza. Labda iko siku tutaishi tena kushuhudia ulimwengu ukiamka kutoka jaani.
Kuna mahala tupo. Kila nafsi. Ulimwengu mzima. Kuna mahala tupo na tumekuwa kama gonjwa. Gonjwa ambalo tumedhamiria kulihamisha mpaka sayari nyingine. Labda jina zuri si ugonjwa, bali ni ulevi.
Ulevi ndio laana kubwa zaidi iliyo juu ya dunia. Ulevi wa uharibifu. Kiu ya kuharibu kwa minajili ya kujipambanua kuboresha. Ni ulevi tu.
Ndio maana kila mahala ambako tulipewa msitu, tumerejesha jangwa. Kila mahala ambako kulikuwa na chemi chemi tumepafanya kame, na kila mahala ambako tulipewa utajiri tumepafukarisha kwa kutupwa.
Dunia si sehemu ya kwanza kuwa na uhai. Yawezekana uhai ulikuwepo enzi za kale sayari ya Mirihi au labda Sayari Mshtarii. Pengine hata Zohali palikuwa na uhai. Lakini baada ya miaka elfu elfu uhai ulikoma japo zenyewe sayari bado zingalipo hata sasa. Hazikukubali zenyewe kufutika ili kuendekeza ulevi wa viumbe hai vilivyomo.
Baada ya miaka elfu elfu mingine, Dunia inapita katika mkondo huo. Ardhi inakataa na kupambana kupinga ulevi uliotamalaki hapa kwetu. Ulevi wa uharibifu. Labda mwaka huu au labda mwakani. Lakini ni dhahiri kwamba Dunia nzima ikiisha kufanywa Anabelle uhai utakoma. Na Dunia itabaki pweke kama Sayari Utaridi ama Zuhura.
Kifo ndicho kinakipa thamani Uhai. Kutokuwa nacho ndiko kunatoa thamani ya kuwa nacho.
Kabla ya kupatwa ni lazima kupotea.
Labda baada ya miaka mia au labda miaka elfu. Labda iko siku tutaishi tena. Labda iko siku uhai utarejea tena.
Kama ilivyotokea Sayari ya Utaridi, Zuhura, Mirihi na Zohali miaka elfu elfu iliyopita ndicho hicho kinapaswa kutokea duniani. Ni lazima ulimwengu wote utwaliwe na kugeuzwa Annabelle…"
MARYLAND, MAREKANI
Mzee Caleb alikuwa ameshikilia kifua na anahema kwa nguvu haswa. Hata wale vijana makomando ambao walikuwa naye walikuwa wameanza kupata wasiwasi kama Mzee Caleb atakuwa nao akiwa hai kwa muda mchache ujao.
"Mzee bado unajisikia vibaya? Simuoni yule mtu?" Walker aliongea huku anamshikilia sawia Mzee Caleb pale alipo kwenye gari.
Yule binadamu wa ajabu, kiumbe ambaye Mzee Caleb aliwaeleza kwamba ana nusu ya nafsi yake alikuwa haonekani tena katika upeo wa macho yao. Walikuwa wamefika pahala ambako ndiko kulikuwa kubatumia kama njia ya kuingilia msituni. Kwa muda wote tangu watoke nyumbani kwa Mzee Caleb mtu huyo alikuwa anakimbia kwa kasi sawa sawa na magari walivyokuwa wakiyaendesha. Lakini ajabu kwamba walipofika hapa kwenye eneo la kuingia msituni hawakumuona tena.
Lakini Mzee Caleb bado alikuwa anasikia maumivu kifuani kwake kuashiria kwamba bado mtu huyo alikuwa karibu yao.
"Ni…mtego!" Mzee Caleb aliongea kwa taabu sana.
"Mtego gani?" Walker akamuuliza.
"Hataki tumuone kwa makusudi lakini bado yuko hapa hapa ndio maana najisikia hivi… nadhani anatala tuingie ndani ya msitu ili atumalize huko huko!"
"Kwa hiyo tunafanyaje?" Walker aliuliza kwa mshangao na woga.
"Kama nilivyosema, 'backwards is the only way forward!' Lazima tuingie tena ndani ya msitu!" Mzee Caleb akamjibu.
Hakukuwa na muda wa mjadala au mabishano tena. Walikuwa wamebakiwa sasa na kama saa moja pekee kabla ya mji wa Maryland kutwaliwa. Kwa hiyo kama kuingia ndani ya msitu ndilo lilikuwa tumaini pekee la kubakia hai basi hakukuwa na muda wa kujadili.
[03/02, 16:00] Nifah: Baada ya wote kwenye magari matatu kupeana ishara fulani wakashuka kwa pamoja. Kama ambavyo walitoka kule nyumbani kwa Mzee Caleb ndivyo ambavyo pia waliingia ndani ya msitu.
Makomando wanne walibeba tundu lenye yule mnyama wa ajabu. Walker alimbeba Mzee Caleb mikononi kama vile amebeba kitoto kichanga. Na makomando wawili waliobakia mmoja alitangulia mbele na mwingine nyuma kuhakikisha kuwa wako salama. Lakini pia hawakusahau ile mifupa ya familia ya Mzee Caleb. Mfuko mmoja wa plastiki uliojaa mifupa na chupa mbili zilizojaa unga wa mafuvu ya kichwa.
Taratibu na kwa umakini mkubwa wakaanza kuingia ndani ya msitu wa Ox. Walifuata njia ile ile ambayo walikuja nayo mara ya kwanza wakiwa na Naomi na Ethan.
Kila ambavyo walikuwa wanatembea baada ya kila dakika kadhaa, pembezoni mwao mwa njia waliyokuwa wanapita, mbali kidogo kwenye miti iliyoshonana walikuwa wakiona kama kivuli cha mtu kinapita kwa kasi na kisha kupotea. Yule kiumbe wa ajabu, binadamu mwenye nusu ya nafsi ya Mzee Caleb.
Kila ambavyo kivuli hicho kilipokuwa kikipita kwa kasi na wao kuongeza umakini wao maradufu wakidhani kwamba labda huo ndio ulikuwa wakati ambao kiumbe huyo atawavamia lakini ajabu ni kwamba hakufanya hivyo. Alipita kwa kasi kama kivuli kwenye miti miti na kisha kupotea. Baada ya dakika kadhaa anapita tena na kupotea. Vivyo hivyo.
"Wa…lker..!" Mzee Caleb alinong'ona kwa taabu akiwa amebebwa mikononi mwa Walker kama katoto kadogo.
Walker hakujibu chochote, aliinamisha tu sikio lake na kumsikiliza. Muda huu walikuwa wameacha kutembea taratibu. Walikuwa wanatembea kwa kasi karibia na kukimbia. Ulikuwa umebaki muda mchache sana, kama dakika arobaini tu kabla ya mji wa Maryland kutwaliwa.
"Unajua huyo kiumbe anachokifanya?" Mzee Caleb alijikaza na kuuliza kwa kutamka sentensi sawia.
Walker akatibgisha kichwa kuashiria kuwa hakujua ni nini kiumbe huyo anakifanya.
"Anataka kututumia tumuongoze mpaka tunapoenda kisha ndio atimize azma yake!"
Japokuwa Walker alishituka ndani ya nafsi lakini alijitahidi asionyeshe mshituko wake wazi wazi. Aliendelea kutembea haraka huku amembeba Mzee Caleb mikononi.
"Naomba chupa yenye unga wa mifupa ya fuvu la kichwa na damu iliyobakia"
Bila kuongea chochote kile Walker alimgeukia mwenzake aliye nyuma yao akiwapa ulinzi na kumuamuru kumpa chupa yenye unga wa mifupa na kifuko cha plastiki kilichosalia damu ambayo waliitoa walipokuwa nyumbani kwa Mzee Caleb.
Walker akachukua vyote viwili, chupa ya unga na kifuko cha damu na kumkabidhi Mzee Caleb.
Safari iliendelea. Muda huu walijongea kama wanakimbia kabisa, nusu saa tu ilikuwa mbele yao kabla ya Maryland kutwaliwa na kuwa Anabelle.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Baada ya kukimbia kwa takribani dakika tano nyingine hatimaye walitokea pale walipokuwa wanaenda. Mahala ambako kulikuwa na kaburi la babu yake Caleb.
Siku tatu zilizopita walipofika mahala hapa kwa lengo la kutafuta Book Of Codes walikuwa kaburi limefukuliwa na mifupa ya zaidi ya binadamu mmoja imetapakaa lakini kitabu hakipo na waling'amua kuwa kikundi cha waoiganaji wa 'Sacta Cedes' walikuwa wamewawahi na kuchukua kitabu. Lakini leo hii walipofika ajabu ni kwamba walikuta lile kaburi limefukiwa na hakukuwa na mfupa wowote ule uliozagaa juu ya ardhi.
Wakiwa wanashangaa hiki walichokikuta hapa, ghafla walihisi kuna kitu kimesimama mbele yao kwenye vichaka, pembeni ya kaburi kwenye miti iliyosongana. Kivuli cha mtu.
Alikuwa ni kiumbe yule mwenye nusu ya nafsi ya Mzee Caleb ambaye alikuwa anawafuatilia tangu watoke nyumbani kwake. Kama ambavyo mzee Caleb alikuwa amehisi, kiumbe huyu kabla hajawadhuru alikuwa anataka ajue akina Caleb walikuwa wanaelekea wapi na labda kwa nini. Na hatimaye alijua… mahala hapa! Kaburini kwa babu yake Caleb. Na alijua fika kwa nini walikuwa wekimbilia hapa.
Binadamu yule wa ajabu taratibu akaanza kitoka kwenye miti na vichaka, kule ambako kulikuwa kunamfanya aonekane kama kivuli gizani. Alitoka nankupiga hatua za taratibu kuelekea pale Kaburini ambako Mzee Caleb na wenzake walikuwa wamesimama.
Walker na makomando wenzake wakainua bunduki zao.
"Msipige risasi.!" Mzee Caleb aliongea kwa taratibu.
Yule kiumbe akazidi kusogea karibu zaidi. Nguo zake nyeusi tii kama kaniki zilizomfunika kuanzia unyayo wa mguu hadi kichwani zilimfanya hata uso wake uonekane kwa shiida sana. Lakini kadiri ambavyo alikuwa anawasogelea ndivyo ambavyo Mzee Caleb, Walker na wenzake walizidi kumuona uso wake wa dhahiri.
Alipiga hatua za taratibu mpaka kufika pale Kaburini na kusimama umbali wa kama tano tu kutoka pale ambapo Caleb na wenzake walikuwa wamesimama. Alipofikia umbali huu ndipo ambapo waliweza kumuona sawia usoni.
Alikuwa na sura sawa sawa kabisa na sura ya Mzee Caleb. Walikuwa wanafanana kabisa kama mapacha. Pia naye alikuwa na sura ya kizee kama Caleb lakini mwili wake ukionekana mkakamavu na wenye nguvu kushinda hata wale makomando ambao alikuwa nao Mzee Caleb. Lakini licha ya kufanana huku, ngozi ya kiumbe huyu usoni alikuwa na mabaka kama mabaka ya chatu au kenge. Pia macho yake yalikuwa ya rangi ya kahawaia iliyofifia sana na mboni nyekundu ambazo rangi yale ilikolea kufanya kuwa kama mwali wa moto. Mwili mzima ulikuwa umefunikwa na manguo hayo myeusi. Ni uso pekee ndio ambao alikuwa anaonekana.
"Hello Caleb.! Nimeisubiria siku ya leo kwa muda wa zaidi ya miaka arobaini.!" Aliongea binadamu huyu wa ajabu kwa sauti nzito ya kukwaruza sana. Aliongea huku anatabasamu kifedhuli na meno yake marefu yaliyochongoka haswa kuchungulia nje.
EPISODE 40
"Giza…. Giza nene ndio kitu cha kwanza ninachokumbuka, kulikuwa na giza nene, kulikuwa na baridi kali... Nilijawa woga! Kadiri ambavyo niliitamani kesho ndivyo ambavyo kesho ilizidi kuwa mbali kuzidi Jana… Jana ilikuwa inaonekana karibu zaidi na yenye kuwezekana kushinda kesho… imekuwa muda mrefu sana kiasi kwamba siwezi kuona tafouti ya uhalisia na maluweluwe… kitu pekee kilicho halisi kwangu ni giza nene na baridi Kali.!"
"Unakumbuka jina lako?" Akamuuliza tena.
Hakujibu moja kwa moja badala yake alijiinamia chini kwa dakika kadhaa. Haikuwa dhahiri kama alikuwa hajaelewa swali au labda alikuwa anafikiri au kujaribu kukumbuka.
Lakini kukumbuka nini? Jina lake?
"Jina langu?" Akainua kichwa chake na kuuliza swali badala ya kutoa jibu.
"Ndio jina lako… unalifahamu?" Akamuuliza tena.
"Nimekuwa mpweke kwa muda mrefu mno kiasi kwamba sikumbuki hata jina langu..." Akajibu akiwa amejiinamia tena kwa huzuni na uchungu.
Ilikuwa inaumiza moyo kumuona namna hii katika hali hii. Akiwa amechanganyikiwa kiasi hiki, kana kwamba uhalisia haukuwa na maana tena kwake.
Cindy akachuchumaa ili awe kwenye usawa mmoja wa uso kati yao.
"Unakumbuka nini?" Cindy alimuuliza kwa sauti ya taratibu ya uchungu.
Akajiinamia chini tena kukwepesha macho yake na Cindy. Sijui ilikuwa ni woga, aibu au alikuwa anatafakari tena. Lakini alijiinamia chini kwa uchungu na huzuni kubwa.
"Nakumbuka maumivu… maumivu yaliyodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko nilivyovuta pumzi… mpaka muda huu nashangazwa hata imekuwaje bado niko hai, lakini naamini maumivu yale ndiyo yaliyofanya niupe uhai wangu thamani… kuna muda nilitamani kuukatisha uhai wangu alimradi tu maumivu yakome… kuna muda nilihisi kabisa siwezi kwenda mbele… kwa hiyo binti yangu hakuna ninachokikumbuka zaidi ya maumivu, maumivu makali na kiza kinene, baridi kali na woga.!"
Kumbukumbu hii ya maumivu japo haikumfanya akumbuke chochote cha maana lakini zilimrejeshea kumbukumbu ya maumivu aliyopitia, kumbukumbu ambayo alijitahidi kuiweka nyuma ya ubongo wake na kamwe asiitafakari.
Cindy akainua mikono yake taratibu na kumshika usoni. Uchungu ambao Cindy alikuwa anausikia moyoni mwake ulisababisha mpaka chozi limdondoke.
Akamshika kwa hisia kali uso wake na kumuangalia kwa mkazo ndani ya macho yake akiwa anabubujikwa na machozi.
"Wewe ni imara kuliko unavyodhani, kama usingali kuwa imara basi tusingekukuta hapa leo hii… Japo haukumbuki chochote lakini naomba uniamini hiki ninachokieleza… Jina lako unaitwa David Logan na wewe ni makamu wangu wa Rais nyumbani, Makamu wa Rais wa taifa la Marekani.!" Cindy akaongea kwa uchungu akitokwa machozi mapaka anatetemeka.
David Logan, Makamu wa Rais wa Marekani alikuwa chini sakafuni ameketi akiwa uchi kabisa amekondeana kiasi kwamba mpaka uso wake ulikuwa umebadilika. Alikuwa amedhohofu haswa. Mwili wake ulikuwa umejawa na makovu ya majeraha kila mahala kutokana na mateso ya muda mrefu ambayo alikuwa amepitia.
Alimkazia macho Cindy kwa mshangao kama vile alikuwa haamini au haelewi ni nini hasa alikuwa anamueleza.
"David Logan.? David Logan.? Hilo ndilo jina langu? Uhn David Logan.!!" Aliongea kwa kurudia rudia huku machozi yakimtoka taratibu na kutiririka mashavuni.
"Ndio… jina lako unaitwa David Logan na wewe ni Makamu wa Rais wa taifa Marekani… sijui umefika vipi hapa au nini kimetokea lakini nahitaji ujitahidi kukumbuka kwa nini umeletwa hapa? Kwa nini ulikuwa unateswa?"
"Kwa nini unataka kujua?" David Logan aliuliza kwa kushangaa kidogo.
"Ulimwengu mzima uko katika tishio la kuangamia na jibu lako wewe linaweza kuwa hatua ya kuepukana na tishio hilo!"
"Uhn nani? Mimi?" Logan aliongea kwa kujidharau kwa kujiona hakuwa anastahili kuwa na umuhimu wowote ule wa kuwa tegemeo la kuokoa ulimwengu kutoka kwenye kuangamia.
"Tishio gani? Jibu gani unataka?" Akauliza akiwa bado kama haamini kile ambacho alikuwa anaelezwa.
"Muheshimiwa sitaki kukuchanganya zaidi ya hivi ulivyo sasa… naomba ujaribu kukumbuka chochote kile, umefikaje hapa? Waliokuleta walikuuliza nini? Jitahidi kukumbuka Muheshimiwa!" Cindy alimuuliza kwa msisitizo.
Ubaya zaidi pia walikuwa hawajui kuwa David Logan alitekwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake Naval Observatory Circle kwani lilipotokea tukio hili wao walikuwa tayari wako ndani ya Anabelle 27 (Dar es Salaam).
"Kwa nini wamemuacha hapa? Wao wenyewe wako wapi? Huu sio mtego?" Salim akauliza.
"Inawezekana! Sijui…" Cindy alijibu kwa kitete.
"Wana sababu gani kumuacha hapa? Kwa nini wasiende naye? Kama walihisi hawamuhitaji kwa nini wasimuue? Kwa nini wamuache hapa? Wenyewe wameenda wapi? Nina hisia mbaya Cindy..!!" Salim aliongea kwa wasiwasi huku anatamaza huku na huko pale chumbani kana kwamba muda wowote wenye Kasri lao wanaweza kutokea muda wowote ule.
"Ngoja tujaribu tena kupata majibu!"
Cindy aliongea huku wanaondoka kutoka pembeni ya chumba walipokuwa wanateta na kurejea pale alipo Logan na Magdalena.
"Kuna mafanikio yoyote?" Cindy alimuuliza Magdalena huku akamshika bega kuashiria kuwa asogee pembeni ili yeye aendelee.
"Hakuna kitu! Jaribu bahati yako…" Magdalena aliongea huku anasogea pembeni.
Cindy akachuchumaa tena ili awe usawa mmoja wa macho na Logan kisha akaanza tena maongezi.
"Muheshimiwa natamani sana ukumbuke kitu chochote kile… hata kama ni kidogo kiasi gani?" Cindy aliongea kwa msisitizo huku akimuangalia kwa huruma.
"Giza…. Giza nene ndio kitu cha kwanza ninachokumbuka, kulikuwa na giza nene, kulikuwa na baridi kali... Nilijawa woga! Kadiri ambavyo niliitamani kesho ndivyo ambavyo kesho ilizidi kuwa mbali kuzidi Jana… Jana ilikuwa inaonekana karibu zaidi na yenye kuwekzekana kishinda kesho… imekuwa muda mrefu sana kiasi kwamba siwezi kuona tafouti ya uhalisia na maluweluwe… kitu pekee kilicho halisi kwangu ni giza nene na baridi Kali.!"
Logan alijibu kwa kutamaka maneno yale yale ambayo aliyatamka awali. Neno kwa neno, sentensi kwa sentesi.
Wote walishituka kana kwamba wamesikia sauti ya jini au mzimu. Hawakuamini macho yao kile ambacho waliking'amua ghafla.
"He has been hypnotized…" (Amepumbazwa) Salim na Cindy waliongea kwa pamoja mshituko mkubwa.
"Nini?" Magdalena akauliza kwa mshangao.
"Wamempumbaza ufahamu wake na kumpandikizia maneno kwa kumkaririsha… hypnosis!" Salim aliongea kwa woga.
"Hapa ni sawa kama vile tunaongea na roboti tu!" Cindy akaongezea.
"Kama wamempampumbaza na kumpandikiza maneno ya kuongea hamdhani kwamba walijua kuwa tutakuja hapa? Hamdhani kuwa huu ni mtego? Na je ni kitu gani kingine wamempandikizia?" Magdalena aliongea kwa woga.
Wote watatu macho yao yakatua kwa David Logan. Ajabu ni kwamba David Logan ambaye muda mchache uliopita alikuwa analia na kujiinamia lakini safari hii aliwatazama kwa kuwakazia macho kwa hasira huku anasimama kutoka pale sakafuni ambako alikuwa ameketi.
"Nahisi nimeanza kuelewa nini kinaendelea!" Salim aliongea huku anawarudisha wenzake nyuma kwa tahadhari mbali na David Logan.
"…je tunafahamu wapi tunapaswa kuwa? Wapi ni nyumbani kwetu katika universe? Na kama kweli tunafahamu kwanini siku zote hatufanyi chochote? Lazima kuna jambo la zaidi katika maisha… jambo la zaidi ya kula na kulala, zaidi ya kuoa na kuolewa, zaidi ya fedha, zaidi ya nyumba, zaidi ya anasa zote tunazotamani!! Lazima kuna jambo la zaidi.. mwanadamu anaishi umri chini ya miaka 100. Hii ni sawa na punje ya mchanga ukilinganisha na zaidi ya miaka bilioni 4 ambayo dunia yetu imekuwepo. Kwa lugha nyingine maisha ya binadamu juu ya uso wa dunia ni kama punje ya mchanga iliyodondoshwa katikati ya bahari. Negligible.!!
Swali ni namna gani tunaweza kufanya maisha yetu haya mafupi duniani na kuwa kama 'iceberg' baharini badala ya punje ya mchanga? Tunawezaje kukumbukwa hata baada ya miaka elfu toka sasa uhai wetu unapokoma?
Lazima kuna la zaidi katika maisha… there must be more to this life, a place to belong and a purpose for us all.!!"
Ndani ya msitu wa Ox - Maryland, Marekani
Yule binadamu wa ajabu alikuwa anapiga hatua za taratibu sana huku akiwasogolea waliposimama Mzee Caleb na wenzake.
Alikuwa na muonekano sawa kabisa na Mzee Caleb. Walifanana sura, kimo na hata umri wao ulionekana kufanana. Yule binadamu wa ajabu naye pia alikuwa na hali ya uzee kama Caleb, tofauti tu ni kwamba mwili wake ulikuwa kakamavu zaidi. Alikuwa imara zaidi na mkakamavu kushinda hata wale makomando wa CIA akina Walker ambao walikuwa pamoja na Caleb.
Walker na wenzake bado walikuwa wameshikilia bunduki zao kuelekea alipo yule binadamu wa ajabu lakini macho yao yalikuwa yakipepesa kutoka kwa Mzee Caleb kwenda kwa yule binadamu na kisha kurudi tena kwa Caleb. Walikuwa wameduwaa kutoka na mfanano huu wa Mzee Caleb na yule binadamu.
Japokuwa binadamu huyu alikuwa amefanana na Caleb kwa sura na kimo, lakini haikuwa rahisi kumtazama kwa dakika nzima mfululizo pasipo kutazama pembeni kutokana na namna alivyokuwa anaogofya.
Alikuwa amejitanda nguo nyeusi kama shuka mwili mzima na kuacha kichwa pekee pamoja na vidole vya mikono. Ngozi yake nyeupe ya uzungu ilikuwa imebadilika na kuwa rangi fulani nyeusi iliyochanganya na ukijani kwa mbali. Pia ngozi ya kiumbe huyu usoni alikuwa na mabaka kama mabaka ya chatu au kenge. Pia macho yake yalikuwa ya rangi ya kahawaia iliyofifia sana na mboni nyekundu ambazo rangi yale ilikolea kufanya kuwa kama mwali wa moto. Mwili mzima ulikuwa umefunikwa na manguo hayo myeusi. Ni uso pekee ndio ambao alikuwa anaonekana
Alikuwa na nywele nyeusi kabisa tii za urefu wa wastani ambazo zilikiwa zimelala kichwani mwake kama vile vimeloa maji au zimelambwa na mbwa.
Kucha zake za vidole zilikuwa ndefu kiasi kwamba labda yumkini hakuwa kuzikata tangu ameliona jua.
Namna ambavyo alikuwa anawatazama kwa kujiamini na kusogea tarataibu, alikuwa anaogopesha kiasi cha kutosha kabisa kumfanya mtu atokwe haja bila kujijua.
"..nimeisubiri siki ya leo kwa kipindi kirefu sana Caleb.!" Yule binadamu aliongea huku anatembea taratibu shuka lake lile kama kaniki likiburuza chini kwenye majani makavu.
"…msipige risasi!!" Mzee Caleb aliwasisitiza tena huku akiwa amemkazia macho yule binadamu.
Mzee Caleb akachukua mfuko ambao ulikuwa na zile chupa zenye unga wa mifupa ya mafuvu ambayo alifukua nyuma ya nyumba yake kisha akaanza kuumwaga kuzunguka pale ambapo walikuwa wamesimama yeye na wenzake.
Yule binadamu hakuonekana na haraka. Alikuwa anajiamini kabisa na alichokuwa anakifanya. Akabakia anamuangalia Mzee Caleb kwa dharau namna anavyomwaga ule unga kutengeneza duara kuwazunguka.
"…unafanya nini Caleb?" Walker akamuuliza Caleb kwa kunong'ona.
"Hawezi kuingia ndani ya hili duara la huu unga wa mifupa ya mafuvu ninao umwaga!" Caleb akamjibu.
"Mbona anatabasamu na wala hana wasiwasi wa kukuzuia ulipokuwa unamwaga huo unga?" Walker akauliza tena kwa udadisi zaidi.
"Anahisi tunajisumbua tu kwa kuwa muda wowote kutoka sasa Maryland itatwaliwa… sijui tumebakiwa na muda gani kabla Maryland kugeuka Anabelle?"
"Tuna chini ya dakika kumi!" Komando mwingine akajibu kwa sauti ya chini ya kunong'ona.
Yule binadamu aliendelea kutembea taratibu mpaka kufika kwenye kingo za duara la unga wa mifupa ya fuvu ambalo lilochorwa na Caleb. Alipofika hapo kwa mara ya kwanza kabisa akatabasamu.
Alikuwa na meno marefu ambayo yalikuwa kwenye ncha kama yamesagika na kutengeneza ukungu fulani wa rangi nyeusi ya damu.
"Unahisi hiki unachokifanya kitawasaidia kwa muda gani Caleb? Muda mchache ujao Maryland inakiwa chini ya himaya yetu… Maryland inageuka Anabelle!! Unahisi hiki unachokifanya kinawasaidia nini?" Yule binadamu aliongea huku anatoa tabasamu la kifedhuli.
"Yuko sahihi?" Walker aliuliza kwa woga.
"Nadhani japo sina uhakika. Lakini nahisi Maryland ikigeuka kuwa Anabelle huu unga wa mifupa hauna nguvu yoyote tena kumzuia asiingie ndani ya hilo duara tulilolizungushia kujikinga..!"
"Kwa nini huu unga una uwezo wa kumzuia asivuke?" Walker akauliza tena.
"Walker mwanangu hatuko darasani hapa… huu sio muda sahihi wa kuniuliza haya maswali… tusubiri baada ya hizo dakika kumi tuone kitakachotokea.!"
"Paaaaaaaaaaaaaaggghhhh.!!"
Radi kali zilikuwa zinapiga mfululizo huku giza likianza kutanda taratibu na hali ya baridi kuanza kuwa kubwa zaidi. Dalili tosha kwamba muda wowote ule Maryland inageuka kuwa Anabelle.
Yule binadamu bado alikuwa amewakazia macho huku anatabasamu kifedhuli akiwa amesimama kwenye kingo za lile duara. Alionekana dhahiri kabisa nafsi yake ilikuwa inabirudika na namna macho ya akina Caleb, Walker na wenzao yalivyojawa na hofu pamoja na woga kutokana na namna ambavyo walijua ni dhahama gani inayowasubiri mbele yao dakika kadhaa zijazo.
"Mpango wako ni nini kutuleta huku msituni?" Walker aliuliza kwa sauti ya woga.
"Masalia… baba yangu na wale wenzake ambao tulionana nao juzi ndio pekee ambao wanajua namna ya kuingia na kutoka ndani ya Anabelle. Kama wakirejea hapa tena na kutukuta labda wanaweza kutusaidia.!" Mzee Caleb alimjibu Walker pasipo kumtazama. Macho yake alikuwa ameyakaza muda wote kuelekea kwa yule binadamu.
"Umesema wakirejea?? Wakirejea lini? Labda tumebakiwa na dakika tatu au labda tano… wanarejea muda gani?" Walker aliuliza kwa hasira zilozochanganyika woga mkubwa zaidi.
"Sijui ni muda gani watarejea?" Mzee Caleb alijibu tena pasipo kumtazama.
"Tufanye nini?" Walker alizidi kuchanganyikiwa.
"Labda tusali sala zetu za mwisho!!" Safari hii Mzee Caleb alimjibu Walker na kugeuka kumtazama usoni.
Walitazamana kwa sekunde kadhaa huku Walker akionyesha macho ya wasiwasi wa kifo huku Mzee Caleb akionyesha macho ya kumaanisha kile ambacho alikuwa amekisema.
"Kuna mwenye kiberiti?" Mzee Caleb akavunja ukimya ambao ulikuwa umetawala ghafla mara baada ya kuwaambia wasali sala za mwisho.
Mmoja wa makomando akaingiza mkono mfukoni na kumpa kiberiti cha sigara.
"Unataka kufanya nini?" Kama kawaida Walker aliuliza tena badala ya kusubiri kuona nini Mzee Caleb anakitaka kufanya.
Mzee Caleb hakujibu chochote safari hii. Aliinama chini na kuwasha kiberiti na kisha kukielekeza pale chini kwenye mduara ambao alikuwa amemwaga unga wa mifupa ya fuvu kuwazunguka.
Ule unga ulianza kuwaka taratibu na baadae ukashika kasi wote ukiwa unaungua na kutengeneza moto wa duara kuwazunguka Mzee Caleb na wenzake kama namna ambavyo alikuwa ameumwaga.
Unga uliwaka huku unatoa harufu fulani kali kama nyama iliyooza ambayo ilikuwa inaungua kwa moto.
"Unafanya nini Caleb?" Walker aliuliza tena kwa mara nyingine.
Mzee Caleb alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kumjibu.
"Hiyo harufu inayotoka kwenye hiyo mifupa nataka baba yangu aisikie kwa haraka popote alipo. Kama ambavyo mbwa hawezi kusahau harufu ya bwana wake mtunzaji ndivyo ambavyo naamini baba yangu japo si binadamu yule wa kawaida lakini hawezi kusahau harufu hii… mifupa ya mjukuu wake na mkwe wake…" Mzee Caleb alijibu bila kumuangalia Walker. Alikuwa amerejea kumkazia macho yule binadamu wa ajabu.
"Kwa nini haukifanya hivi muda wote?" Walker akarejea na swali lingine.
"Sina hakika kama baba na wenzake Masalia watasikia harufu hii muda gani na kuja ndani ya wakati… kama ningeliwasha moto huu unga mapema na wasingetokea basi huyu kiumbe mbele yetu angekuwa ameshatugeuza asusa muda mwingi sana… maana naamini huu moto hauwezi kuwaka zaidi ya dakika tano… nimewasha sasa hivi kwa kuwa hatuna chaguo lingine… sekunde yeyote kutoka sasa Maryland inageuzwa Anabelle na hakuna cha kumzuia huyu kiumbe mbele yetu… kwa hiyo hakuna haja ya kuendelea kusubiri bila kutupa kete yetu ya mwisho!" Mzee Caleb alieleza kwa sauti thabiti kabisa.
Yule bibadamu mbele yao kwenye kingo za duara hakusogea hata hatua moja wala kutikisika baada ya moto ule kuwashwa. Aliendelea kutabasamu zaidi huku amekaza macho kwa Mzee Caleb akionekana kuwa na hakika kabisa kuwa Mzee Caleb na wenzake hakuna namna ambayo wangeweza kuokoka leo hii kutoka kwenye mikono yake.
"Paaaaaaaaaaaaaggggghhhhh"
Radi zililia kwa kishindo zaidi na kwa mfululizo zaidi huku kiza kikigubika anga na baridi likibadilika ghafla na kuwa kama vile wako kwenye ziwa la maji ya barafu tupu.
Ni dhahiri kwamba Maryland ilikuwa inageuka sasa kuwa Anabelle. Labda ilikuwa imebakia chini ya dakika moja pekee au labda sekende kadhaa tu kabla ya Maryland kuwa rasmi Anabelle mpya.
Mzee Caleb na wenzake wakaanza kusikia mabadiliko kwenye miili yao. Kama vile walikuwa wanapatwa na kizunguzungu kilichokuwa kinawafanya wasione vyema, kama vile pumzi haiji sawa sawa.
"PAAAAAAAAAAAGGGHH.!!"
Radi kubwa zaidi ya kishindo ilipiga. Kizunguzungu kikaongezeka. Uwezo wa kuona mbele ukapungua. Pumzi ikaanza kuwa nzito na miili ikaanza kuishiwa nguvu na kulegea.
"Its over Caleb!! Nimeisubiri hii siku kwa muda mrefu sana… its over!!" Yule binadamu akaongea kifedhuli huku anapiga hatua kujiandaa kuvuka lile duara walilopo akina Caleb ambalo lilikuwa linamzuia asiweke kuwafikia muda wote huu.
Lakini kabla hajaingia ndani ya duara, kabla Maryland haijawa Anabelle rasmi. Zikiwa zimebakia kama sekunde kumi tu au labda tano. Wote wakaanza kusikia sauti masikioni mwao. Kama sauti ya watu wananong'ona, kama sauti ya watu kupekua kwenye vichaka. Sauti kama ile ile ambayo Mzee Caleb na wenzake waliisikia hapa siki tatu zilizopita walipokuja kutafuta Book Of Codes. Sauti ya kuashiria kuwasili kwa Masalia. Baba yake Mzee Caleb na wanachama wenzake.
Yule binadamubwa ajabu alionekana kushituka na kuanza kugeuka huku na huko ili ajue kama ni kweli Masalia wamewasili au la. Kwa mara ya kwanza sura yake ya kutisha ilionyesha woga. Woga wa kuhofia Masalia, baba yake Mzee Caleb na wenzake.
Mzee Caleb, Walker na wenzao pia walisikia sauti hii masikioni mwao ya ujio wa masalia… lakini miili ilikuwa imishiwa nguvu kabisa wasiweze hata kutabasamu au kutazama kushuhudia kama ni kweli walikuwa Masalia wamewasili. Muda pia ulikuwa umeisha, Maryland ilikuwa inageuka rasmi kuwa Anabelle mpya.
"PAAAAAAAGGGGHH.!!" Kishindo kikuu cha radi kama tetemeko la ardhi kilisikika mara moja na ya mwisho. Mji wa Maryland ulikiwa umegeuka rasmi na kuwa Anabelle.
[04/01, 20:22] Official Robot: Mzee Caleb, Walker na wenzao hawakuhisi pumzi tena na wala hawakuweza kuona mbele, ilikuwa ni kiza kitupu machoni mwao… miili iliishiwa nguvu na wote kwa pamoja wakadondoka ardhini.
Lakini wakiwa wanadondoka japokuwa walikuwa na ufahamu nusu tu, Mzee Caleb alihisi kama kuna mikono ya mtu japo ilikuwa ya baridi mno… alihisi kuna mikono ya mtu imemgusa na kumdaka.!!
Mwili wake wote ukasisimka kwa hofu kutokana na kutokujua kama amedakwa na Masalia au yule binadamu mbele yao ndio alikuwa amemtia mikononi??
Sio mara moja au mara mbili, bali mara mia kadhaa nimewahi kuuliza na kujiuliza, "..kesho inataka nini kutoka kwangu? Nafanyaje pale sauti pekee ninayoisikia kichwani mwangu ni neno “subiri”? Hata nikiamua kusubiri siwezi kuepuka kesho isifike, ni lazima kutakucha na itanipasa kupambana na mashetani yanayonisubiri huko kesho!
Kesho itakapofika, nikijitoa muhanga nafsi yangu kuokoa kitu pekee chenye thamani kwenye maisha yangu, mtu ninayetamani aishi kuliko nafsi yangu! Je, usiku akienda kulala atakumbuka kafara yangu? Je, ulimwengu utakumbuka ushujaa wangu?
Ni siku ngapi atalala akikimbuka kafara yangu kabla ya kusahau?
Nashindwa kuiondoa sauti ninayoisikia kichwani mwangu, kadiri ninavyojitahidi kutoisikiliza ndivyo sauti inavyokuwa kubwa zaidi kichwani mwangu, sauti ya neno moja tu “subiri”!
Ni mahali gani ambapo natakiwa kuchora mstari wa kusubiri, na muda gani natakiwa kusonga mbele?
Nahisi kama nimejifungia kwenye dunia ya peke yangu… nahofia hata kuinua mguu kukanyaga hatua moja mbele, kwa kuhofia naweza kuharakisha kesho ikafika haraka, na naogopa pale itakapofika kwa kuwa kichwani mwangu bado sijapata jawabu… kesho inataka nini kutoka kwangu?.”
EPISODE 42
Ron alikuwa anatembea haraka haraka kuufuata mlango uliokuwa unaelekea chini kwenye basement ya nyumba hiyo baada ya Natalie kusema kwamba yeye na baba yake Logan walikuwa wakipendelea sana kucheza tabke tennis kila muda ambako baba yake hakuwa kazini. Latisha na mwanaye walikuwa wanafuata nyuma wakitembea haraka haraka karibia na kukimbia.
Ron alifika mpaka kwenye mlango na kuufungua. Ukifungua mlango tu unakutana na ngazi zinazoshuka chini kwenye basement yenyewe. Kabla hajaanza kushuka chini kwanza kabisa Ron alipapasa ukutani mkono wake wa kushoto na kuwasha taa ya kule chini kwenye basement na kisha ndipo alianza kushuka ngazi hizi huku nyuma yake akifuatiwa na Latisha na mtoto wake Natalie.
Ukiingia humu ndani ya basement mkono wa kushoto kulikuwa na maboksi ya vitu mbali mbali vimepangwa. Pembeni ya maboksi haya kulikuwa na baisikeli ya mtoto wa kama miaka 10 au 12 hivi. Hii ilikuwa ni baisikeli ya Natalie kipindi wanaishi wote na baba yake kabla ya ndoa ya Latisha na David Logan kusambaratika.
Macho ya Natalie na mama yake Latisha yalipotua kwenye hii baisikeli waliiangalia kwa muda mrefu sana na kwa huzuni sana kutokana na kumbukumbu ya huzuni iliyokuwa inawajia kichwani kutokana na kuiona baisikeli hii. Japokuwa ndoa ya Latisha na Logan ilikuwa imevunjika na sasa Latisha yuko kwenye ndoa nyingine na mumewe Donald McLaren lakini hakukuwa na ubishi kwamba Logan ndiye alikuwa mpenzi wa maisha wa Latisha. Kuona baisikeli hii kulirejesha tena kumbukumbu zote za furaha kipindi familia yao iko imara. Alikumbuka namna ambavyo katika siku za kwanza za kununuliwa kwa baisikeli hiyo walivyokuwa wakimshikilia Natalie baisikeli apande na kisha kumshikia tena akiwa anajifunza kuiendesha.
Kumbukumbu hizi haizikuwa zimemteka tu Latisha pekee bali pia hata Natalie. Japokuwa moyoni mwake alikuwa amejawa na kinyongo dhidi ya baba yake lakini ukubwa wa upendo ambao alikuwanao juu ya baba yake ulikuwa ni mkubwa mno. Baada ya kuitazama baisikeli hii ndipo ambapo alijua ni kwa kiasi gani alikuwa amemkosa baba yake.
Wote wawili Natalie na mama yake Latisha kwa mbali machozi yalikuwa yakiwalenga lenga baada ya kumbukumbu hizi kuwajia upya kichwani na ukweli uliopo kwamba mtu huyu wanayempenda haswa alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana na kuna uwezekano wasimuone tena.
Katikati ya basement kulikuwa na meza ya mchezo wa “table tennis”.
Macho ya Natalie yaliganda kwenye meza hii kwa muda mrefu zaidi. Machozi ambayo mwanzoni yalikuwa yakimlenga lenga sasa hivi yalianza kutirika taratibu shavuni mwake. Meza hii ina kumbukumbu nyingi za furaha kati yake na baba yake. David Logan kutokana na majukumu yake ya kiserikali pamoja na matamanio yake ya kutaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi siku moja ilimfanye awe 'busy' kweli kweli.
Upande huu wa kushoto kulikuwa na kabati tupu la vitabu. Kabati lilikuwa na vumbi kiasi kutokana na kutowekewa kitu chochote kwa muda mrefu.
Ron alisogelea kabati na kuanza kuingalia kwa makini zaidi. Alihisi kwamba kulikuwa na kitu cha ziada kuhusu hii kabati japo hakuweza kung'amua mara moja ni kitu gani.
"Kwa hiyo nini kinaendelea baada ya hapa??" Latisha aliuliza huku bado akiwa amemkumbatia Natalie. Wote wawili walikuwa wameacha kulia muda huu.
"Sijui kwa kweli… hisia zangu zilikiwa zinaniambia kuwa kama kuna siri Logan alikuwa anataka kuificha kwa ajili ya Natalie basi lazima siri hiyo itakuwa humu kwenye basement. Sijui tunafanyaje baada ya hapa…" Ron aliongea huku anageuka huku na huko pale kwenye basement.
Hakukuwa na kitu chochote kingine hapa kwenye basement zaidi ya yale maboksi mkono wa kulia, table tennis katikati na hili kabati mkono wa kushoto.
"Hakuna stori yoyote au kitu fulani kuhusu hili kabati.!!" Ron aliwauliza Latisha na Natalie akitarajia labda kuna historia fulani nyuma ya kabati hili kama ilivyo kwa ile ya table tennis katikati ya chumba.
"Hapana…" Latisha akajibu.
"Hapana… ndio kwanza naliona leo hilo kabati" Natalie akaongezea.
"Aaaaarrrrggghhh.!" Ron akajikuta anakereka mwenyewe kwa kuhisi kama amegonga mwamba na hisia zake hazikuwa sahihi.
Akaisogelea tena hii kabati. Akaiangalia tena kwa makini. Akaangalia pale chini sakafuni ilikosimama. Akaona kitu.
Hii kabati ilikuwa kama imesogezwa hivi. Yaani, kutokana na hii basement kutotumika mara kwa mara ilipelekea chini kuwe na vumbi. Na siku zote kitu kikiwa kwenye sakafu yenye vumbi kwa muda mrefu na baadae kusogezwa hata ukirejesha tena kama ambavyo kilikuwa awali bado kuna alama fulani inabaki pale chini sakafuni kwenye vumbi kuonyesha hiki kitu kilisogezwa hapa na kisha kurejeshwa tena. Hicho ndicho ambacho Ron alikiona.
Akalisogelea karibu zaidi kabati hili na kisha kulisogeza kutoka pale lilipo. Nyuma ya kabati kulikuwa na mlango mdogo uliofichwa na pembeni ya kitasa chake kulikuwa na 'keypad' ambayo ilikuwa inawaka rangi nyekundu.
Ron aligeuka kuwatazama Latisha na Natalie huku akitoa tabasamu kubwa kama vile mtoto mdogo amekuta boksi la lolipop chumbani kwake.
"Got you Logan… nilijua tu siri zako zitakuwa hapa kwenye basement.!!" Ron aliongea kwa mbwembwe huku akijaribu kufungua mlango kwa kitasa. Haukufunguka. Ilionekana dhahiri kwamba ilikuwa inahitajika kuingiza neno la siri kwenye keypad pale pembeni kabla ili kufungua mlango.
"C'mooon Logan, mbona unafanya maisha yetu yawe magumu hivi??" Ron alikereka tena baada ya kuona hicho kizingiti kingine kizito zaidi cha neno la siri.
Latisha na Natalie pia wakasogea mpaka pale mlangoni.
"Una hisia kali sana Ron… lakini unajuaje kama humu ndio kuna hizo siri tunazohitaji?" Latisha akauliza baada ya kufika pale mlangoni.
"Latisha sababu pekee ya mtu kuwa na chumba cha siri kwenye basement ni kwa kuwa ana siri nzito ambazo anahitaji kuziweka salama… kwa hiyo labda mnisaidie tu kukisia neno la siri!" Ron akajibu
"Sina hata 'idea'.!" Latisha akajibu haraka huku anatikisa kichwa.
Wakaanza kukisia kwa kujaribu kila kitu ambacho walihisi inaweza kuwa neno la siri sahihi. Wakajaribu mwaka wa kuzaliwa wa Logan lakini ikakataa halikuwa neno la siri sahihi. Wajaribu tarehe ya kuzaliwa ya Natalie, wakajaribu tarehe ya kuzaliwa na Latisha. Vyote vikakataa. Wakajaribu tarehe ya harusi kati ya Logan na Latisha, ikakataa. Wakajaribu tarehe waliyotalikiana, nayo ikakataa.
"Dah hapa tumegonga mwamba.!" Natalie alivuta pumzi ndefu na kuishusha.
"Lazima kuna kitu mtakuwa mnakijua na ndio litakuwa neno la siri jitahidini kukumbuka… c'mon guys!" Ron aliongea kwa pupa akijitahidi kuwatia hari wasikate tamaa.
"Hizo tulizojaribu ndio zilikuwa namba pekee ambazo nahisi labda angetumia kama neno la siri kama alikiwa anahitaji Natalie asipate shida kukumbuka.!" Latisha aliongea kwa kukata tamaa.
Lakini Latisha aliposema sentesi ya "kama alikuwa anahitaji Natalie asipate shida kukumbuka" kuna taa ikawaka kichwani kwa Ron.
Lakini kila ambako alikiwa anapata muda wa kupumzika alikuwa anatumia muda huo mwingi kucheza table tennis na mwanaye Natalie. Walikuwa wakicheza na wakichoka wanakaa chini hapo kwenye basement na 'kupeana stori'. Logan akimsimulia mwanaye visa vyake vya ujana na utoto na huku Natalie naye akimpa 'umbea' wa shuleni kwao na marafiki zake. Meza hii ilikuwa ni alama kubwa ya urafiki kati ya Natalie na baba yake Logan.
Natalie aliiangalia kwa muda mrefu huku machozi yakimtoka hasa hasa akikumbuka ukweli kwamba baba yake hayupo tena na kuna uwezekano wasipate tena nafasi ya kucheza mchezo huo pamoja.
"Seven nil, twelve five" Natalie aliongea kwa kwikwi ya kilio huku machozi yakimtoka.
"Naam.!!" Ron alijibu kwa mshituko na kugeuka kumuangalia Natalie.
"Seven nil, twelve five.!" Natalie aliongea tena kwa kwikwi ya kilio huku akijiziba uso kwa viganja vya mikono na kuangua kilio kikubwa zaidi.
Latisha akasogea taratibu na kumkumbtia Natalie huku naye machozi yakimtoka lakini pasipo kutoa kilio cha sauti.
"Sssssshh nyamaza mama sssshhh.!!" Natalie alimkumbatia mwanaye na kumbembeleza.
"Sijakuelewa Natale, 'Seven nil twelve five' ina maana gani?" Ron aliuliza kwa macho ya udadisi huku akiwasogelea pale waliposimama Natalie na Latisha.
"Hayo ndio yalikuwa matokeo yetu ya mwisho mimi na baba… 'seven nil, twelve five'!!" Natalie aliongea huku kwikwi ya kilio ikiwa imepungua kidogo safari hii.
Ron na Latisha wote walibaki kimya bila kusema chochote wakimuangalia Natalie kuashiria kwamba walikuwa wanataka kusikia zaidi.
Natalie akaendelea…
"Siku hiyo nilikuwa nimetoka shuleni na msongo mkubwa sana wa mawazo… nilikuwa nimegombana na rafiki yangu kipenzi kabisa. Nilivyorudi nyumbani nikajifungia chumbani sikutaka kuongea na mtu yeyote yule wala kuonana na mtu au kula chakula. Jioni baba alirudi nakumbuka alikuwa anajiandaa alikuwa na safari ya kwenda Washington siku hiyo. Alipofika nyumbani akaelezwa kwamba nilikuwa nimejifungia chumbani siku nzima sitaki kula wala kuonana na mtu. Kwa hiyo akaja mpaka nje ya chumba changu na kuanza kunigongea. Aligonga kama dakika tano nzima sikujibu wala kufungua mlango. Akavua tai yake na kukaa chini nje ya mlango wangu akaniambia kuwa hatoenda safari yake mpaka aone nimetabasamu, kwa hiyo atakesha hapo hapo nje ya mlango. Hata baada ya kusema haya sikufungua mlango au kumjibu. Akaanza kinihadithia 'stori' za utoto wake na jinsi ambavyo na yeye utotoni aliwahi kugombana na rafiki yake kipenzi utotoni. Akaanza kunihadithia visa walivyokuwa wanafanyiana ili kulipiziana kisasi. Kuna muda alihadithia visa ambavyo nilishindwa kujizuia nikaanza kucheka. Huyo ndio alikuwa baba yangu, alikuwa anajua hisia zangu na namna gani anaweza kunirejeshea tabasamu. Nikafungua mlango na baba akaingi na kunikumbatia na kunieleza kuwa haijalishi nitagombana na marafiki wangapi lakini yeye atakuwa na mimi siku zote. Akanichukua na tukashuka chini kwenye basement na kuanza kucheza table tennis. Tulicheza michezo miwili. Mchezo wa kwanza nilimfunga 'Seven nil' na mchezo wa pili nikamfunga 'twelve five'. Nadhani aliniacha nishinde makusudi, lakini majonzi yangu yote yaliondoka na akasafiri kwenda washington na kuniacha nikiwa na tabasamu. Tulikuwa kila mara tukiongea kwenye simu namtania "seven nil, twelve five' na alijiapiza kuwa akirudi lazima michezo yote miwili anifunge saba bila. Lakini hatukuwahi kucheza tena, kwani akiwa huko washington ndio ikaibuka skendali ya kujihusisha kimapenzi na sekretali wake na wiki kadhaa baadae wakatalikiana na mama. Kwa hiyo mpaka leo hii siwezi kuondoa kichwani matokeo ya mchezo wetu wa mwisho, 'seven nil, twelve five'.!"
Natalie akamaliza kueleza na kuanza tena kulia huku akilala kifuani kwa mama yake. Latisha alimkumbatia tena kwa uchungu machozi yakimtoka bila kutoa sauti ya kilio.
Wote wawili katika muda huu ndipo ambapo walijewa na hisia zilizowakumbusha ni kwa kiasi gani wanampenda Logan licha ya mambo yote mabaya ambayo alikuwa ameyafanya na kusababisha familia yao kusambaratika. Ni katika wakati kama huu ndipo ambapo unafahamu ni kwa kiaisi gani unampenda mtu pindi tu ukimpoteza.
Wakati Natalie na Latisha wamekumbatiana na kubembelezana, Ron aligeuka na kuendelea kudadisi kila kona ya hiyo basement.
"Natalie mwanzoni ulipoona table tennis ulikuwa unasema nini? 'nil twelve…' nini tena?" Ron aliuliza kwa udadisi.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"Matokeo yetu ya mwisho ya table tenis, 'Seven nil, twelve five'.!" Natalie akajibu akitoa macho naye kama taa imewaka kichwani.
Ron akageuka mlangoni haraka haraka na kuingiza tarakimu hizo kwenye keypad, 7-0-1-2-5.
Aliponingiza tu ile keypad ikabadilika rangi kutoka nyekundu na kuwa kijani.
"Yeeeessss.!!" Ron alishangilia.
Haraka haraka akshika kitasa na kufungua mlango. Mlango ulifunguka na mbele yao kulikuwa na kijichumba kidogo.
Kijichumba hiki kidogo kilikiwa nadhifu mno kilichopakwa rangi ya kijivu chumba kizima. Vitu pekee ndani ya chumba hiki vilikuwa kabati dogo la kioo lilipo upande wa kulia ukiingia ndani ya hiki kijichumba, kabati ambalo ndani yake kulikuwa na kitu kimoja tu, kompyuta mpakato.
Pia kulikuwa na kiti cha kukaa cha kiofisi kilichopo upande mwingine wa chumba na mbele yake kulikuwa na kamera iliyo kwenye kwenye stendi yake ya kurekodia.
Hatimaye siri ambayo walikuwa wanaitafuta kwa udi na uvumba ilikuwa mbele yao ndani ya chumba hiki. Siri ambayo ilisababisha Logan kutekwa na watu wasiojulikana. Siri ambayo waliamini inaweza kuuokoa ulimwengu kutoka kwenye kugeuzwa kuwa Anabelle. Siri ambayo kikundi cha siri cha The 46 wanailinda kwa maisha yao yote. Siri hiyo waliamini hatimaye wameifikia ndani ya chumba hiki.
Mara kadhaa ulimwengu umewahi kufikia katika mstari wa mwisho kabisa ambao kama ungevuka mstari huu basi ndio ungekuwa mwisho wa ustaarabu ambao binadamu amepambana maelfu ya miaka kuujenga. Katika vitabu vya kale tunaelezwa kuwa ulimwengu uliwahi kufika kwenye mstari huu kipindi cha Nuhu. Lakini pia ulimwengu ulifika tena kwenye mstari huu kwenye karne ya 7 AD na pia karne ya 16 AD.
Lakini katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukiufikia mstari huu kwa mara nyingi ndani ya muda mchache. Ndani ya miaka mia moja pekee iliyopita tumefikia mstari huu mara mbili. Mara ya kwanza ilikuwa 1914 - 1945 na mara ya pili ilikuwa mwaka 1939 - 1945.
Kabla ya hapa zilikuwa zinapita karne kadhaa au hata maelfu kadhaa ya miaka kabla ya kuufikia mstari huu tena. Lakini ni ajabu kwamba kwa kipindo cha miaka mia moja pekee tumefikia mstari huu mara mbili. Pangine hii ilikuwa ni dalili. Dalili ya kile ambacho kitafuata. Dalili ya kitakachotokea mwaka 2038. Dalili ya ulimwengu mzima siku moja kugeika kuwa Anabelle.
Rabat, Morocco
Wote watatu walikuwa wamesimama kwa tahadhali wakiwa wamemkodolea macho Logan pale ambako alikuwa amesimama. Kutokana na alivyo uchi wa mnyama na hasira ambazo alikuwa nazo usoni, Logan alikuwa anaonekana kama vile mnyama.
Cindy, Salim na Magdalena walikuwa wanapiga hatua za taratibu sana kurudi nyuma mlangoni, Logan naye alikuwa anapiga hatua za taratibu kuwafuata. Walikuwa wamekaziana macho kama wanataka kurukiana.
"Jina lako ni Logan. Wewe ni Makamu wa Rais wa taifa la Marekani na sisi sio adui zako.!" Cindy aliongea kwa tahadhali huku yeye na wenzake wakiendelea kurudi nyuma.
Logan hakuongea chochote kile, hasira usoni mwake zilizidi kuwa dhahiri zaidi. Alikuwa amepandwa na hasira kiasi kwamba mpaka mwili ulikuwa unatetemeka.
Salim kutokana na uzoefu wake wa masuala ya intelijensia na mambo ya ulinzi alijua ni nini ambacho kilikuwa kinafuata. Wakati wenzake wakirudi nyuma yeye akabakia kama hatua mbili hivi mbele yao. Akawa kama ngao ya wenzake.
"Salim? Unafanya nini?" Magdalena aliongea kwa mshituko baada ya kuona Salim akiwa amebaki mbele na harudi tena nyuma pamoja nao.
"Eidha tumdhuru au atudhuru… siko tayari kufa kirahisi hivi.." Salim aliongea huku akiwa amemkazia macho Logan ambaye walokuwa wamesogeleana kubakia kama hatua tano tu kati yao.
"Hapana Salim! Tafadhali…."
"Magdalena! kaa kimya!!" Salim aliongea kwa ukali kumnyamazisha Magdalena asiendelee kuongea.
Zilikuwa zimebakia kama hatua tatu tu sasa kutoka mahala ambako alisimama Salim na alipo Logan.
Logan alikuwa kama amepandwa na 'mzuka'. Alikuwa anatetemeka mpaka meno yanagongana. Alikuwa na hasira haswa. Alitumbua macho kumtazama Salim. Salim naye alimkazia macho bila kutingishika hata kidogo.
Ghafla Logan akaruka kama mnyama kumvamia Salim. Salim alionekana dhahiri kwamba alikuwa anatarajia Logan angefanya hivyo, alimkinga kwa mikono yake miwili ili asimvae mwilini na kisha akamsukuma kwa nguvu na Logan kuanguka kwa kishindo sakafuni. Akiwa sakafuni anapaparika ili ajiinue na kugeuka, Salim alimrukia mgongoni na kuanza kumshindilia ngumi mfululizo.
Ilikuwa ni kana kwamba kuangalia mchezo wa watu wanaopanda ng'ombe dume mgongoni na kuanza kuruka ruka nao.
Salim alikuwa juu ya mgongo wa Logan akimshindilia ngumi. Logan alikuwa anaruka ruka na kupaparika ili kujinusuru.
"Noooo Salim! Nooo..!" Magdalena na Cindy walikuwa wanapiga kelele kwa pamoja kumsihi Salim asiendelee na shambulizi hilo ili wote wawili asije mmoja wao kudhulika.
"Ole wako ufanye ujinga mwingine!"
Cindy akatoa mkwara.
"Nini kinaendelea?" Salim akauliza.
"Ameanza kukumbuka… anakumbuka jina la mwanaye Natalie… ndilo ananong'ona hapo muda woye huu!" Cindy akamfafanulia.
Cindy akachuchumaa chini kumkaribia Logan pale sakafuni alipokuwa amejikunyata. Kisha akanyoosha mkono na kumgusa taratibu mgongoni.
Logan alifyatuka kama vile alikuwa ameguswa na nyoka. Akasogea pembeni kabisa ukutani.
Kwa mara ya kwanza tangu adondoke pale sakafuni aliinua uso na kuwatazama. Uso wake sasa hivi ulikuwa umejawa na woga na si hasira tena. Alikuwa anawatazama kwa macho ya woga kiasi kwamba ilikuwa inaumiza moyo. Ilikuwa inapasua moyo kumuona mtu muhimu na mwenye nguvu kubwa duniani kama Logan katika hali hii, akiwa uchi wa mnyama, damu zinamvuja huku amejawa na woga na wasiwasi usoni.
"Hey! Its ok… hatuko hapa kukudhuru, sisi ni marafiki kabisa kwako… tafadhali usiogope.! Cindy aliongea kwa sauti ya upole na taratibu sana ili kumtoa hofu Logan.
Logan bado alikuwa anawaangalia kwa mshangao na hofu kana kwamba ndio kwanza amewaona.
"Mheshimiwa tafadhali kama unaweza kukumbuka chochote namna gani ulifika hapa, nani alikuleta na ni maswali gani ambayo walikuuliza… chochote unachoweza kukumbuka muheshimiwa kitakuwa na msaada mkubwa sana.!" Cindy aliongea kwa upole na kubembeleza.
Logan aliwatumbulia macho tu. Lakini safari hii alikuwa anawaangalia kwa 'upeo wa kupitiliza'. Yaani alikuwa anawatazama lakini kama vile akili yake ilikuwa mbali inatafakari. Kama vile anaangalia kitu kilichombali sana kuzidi akina Cindy walio mbele yake.
"Natalie..!" Logan alitamka tena jina la mwanaye. Safari hii alilitamka sawia bila kunong'ona. Alilitamka huku machozi yakiwa yanamlenga lenga.
"Natalie amefanyaje muheshimiwa?" Cindy akauliza.
"Namuhitaji Natalie.!" Logan aliongea kwa upole huku anamtazama Cindy.
"Muheshimiwa nina wasiwasi hilo halitowezekana kwa sasa." Cindy alijibu.
"Kwa nini?"
"Natalie yuko nyumbani Marekani… hapa tulipo ni Rabat, Morocco!" Cindy alimfafanulia.
"Rabat!" Logan alihamaki.
"Ndio muheshimiwa… tuko Rabat."
"No no nooo!! Haiwezekani.." Logan alitaharuki huku anaanza kujikongoja na kuinuka.
"Haiwezekani nini muheshimiwa?" Cindy aliuliza kwa mshangao kidogo.
"Haiwezekani kuwa Rabat!! No no nooo haiwezekani…" Logan aliongea kwa kuchanganyikiwa huku anashika kichwa na kuanza kutembea tembea pale chumbani.
Salim alikuwa amekuja na nguo fulani hivi kama shuka jeusi, akampatia Logan ili aweze kujisitiri.
"Muheshimiwa kwa nini unasema haiwezekani kuwa Rabat?" Cindy aliuliza tena kwa udadisi.
"Walisema kuwa makao makuu yako jangwa la Nevada." Logan aliongea huku amejiinamia chini kama amechanganyikiwa na habari hizi za kwamba wapo Rabat, Morocco.
"Makao makuu ya nini? Nani hao waliosema?" Cindy aliuliza kwa mshangao mkubwa.
Wote mle ndani ghafla walikumbwa na mshtuko baada ya kumsikia Logan akisema kwamba, "Walisema kuwa makao makuu yako jangwa la Nevada!"
Wakati wao wakimshangaa, naye Logan aliinua uso na kuwashangaa. Dhahiri kwamba alikuwa anawashangaa kwa kushindwa kuelewa kile ambacho alikisema. Alikuwa anawaangalia kwa uso fulani hivi wa mashaka. Inaonekana kwamba alisema kile alichokisema kwa kuamini kwamba akina Cindy wataelewa. Kitendo cha akina Cindy kutoelewa kulimfanya awaangalie kwa mashaka na mshangao.
"Who are you guys?" Logan aliwauliza huku anawaangalia kwa mashaka.
"We are the good guys… please stay calm!" Cindy alijitajidi kumtoa hofu.
"I asked who are you!" Logan aliuliza kwa sauti ya ukali kidogo na kumaanisha.
"Ok ok muheshimiwa.! Mimi naitwa Cindy, raia wa Marekani na ni mwana akiolojia… huyu hapa anaitwa Salim ni afisa usalama kutoa TISS nchini Tanzania… na huyu hapa anaitwa Magdalena ni mwana baiolojia kutoka chuko kikuu cha Kenyatta nchini Kenya… tumepitia mambo mengi sana ila kwa kifupi tuliingia kwenye Anabelle 27 ambao ulikuwa ni mji wa Dar es Salaam nchini Tanzania kufanya utafiti… baadae tukafanikiwa kutoka na kujikuta tuko pwani ya hapa Rabat Morocco na baadae baada ya kufuatilia nyayo pale kwenye mchanga wa pwani
Lakini Salim alikuwa kana kwamba na yeye amepandwa na shetani. Aliendelea kumtandika Logan ngumi mfululizo kama vile alikuwa asikii vilio vya akija Cindy wakimsihi.
Ghafla damu zikaanza kutapakaa pale sakafuni. Logan alikuwa ameanza kuvuja damu usoni kutokana na kipigo kikali ambacho kilikuwa kinaendelea pia damu ilikuwa inatoka na mwilini ambako alikiwa na majeraha makubwa ambayo alikuwa nayo tangu wamemkuta hapo kutokana na kuteswa na watu ambao walikuwa wamemteka. kutokana na kipigo kikali ambacho kilikuwa kinaendelea. Damu zilikuwa zinamwagika haswa. Logan licha ya akili zake kuchezewa na kuwa na hasira kama mnyama lakini alionekana kushindwa kumudu umahiri wa mwana usalama Salim. Au labda aliwahiwa au kuzidiwa ujanja.
"Salim utamuua!! Hapanaaaaa Salim… Saliiiimmm…"
Cindy ana Magdaelena waliendelea kupiga kelele kumsihi Salim asiendelee kushusha kipigo.
Magdalena ilimbidi ajitose na kumrukia Salim mgongoni. Maana yake sasa mgongoni kwa Logan kulikuwa na Salim pamoja na Magdalena. Kutokana na uzito wote watatu wakadondoka chini Sakafuni. Magdalena alimng'ang'ania Salim kama vile wapigana mieleka wanavyokabana kabali. Alimshikilia kwa nguvu zake zote huku akimnasua kutoka kwa Logan.
"Stop it Salim… please stop!" Magdalena aliongea kwa uchungu karibia na kulia.
Hatimaye alifanikiwa kuwaachanisha. Salim alikuwa anahema kama mbwa. Logan alilala chini kwa maumivu akiwa amejikunyata kama katoto kadogo.
"Nimekwambia sisi sio adui zako… tuko hapa kwa ajili ya kusaidia… kwa hiyo tuambie nini kimetokea hapa la sivyo…" Salim alikuwa anaongea kwa hasira huku anahema kama mbwa.
"Toka nje Salim… toka nje.." Cindy alifoka.
Ilibidi Magdalena amkokote Salim mpaka nje ili kumuweka mbali na Logan.
"Tafadhali Salim… kuwa mtulivu, unachokifanya akisaidii chochote zaidi ya kuongeza mkanganyiko!" Magdalena alimsihi Salim baada ya wote kutoka nje ya chumba kile walichomuacha Cindy na Logan.
"Alikuwa anataka kutuvamia na kuturarua… unataka kusema hakuona usoni mwake? Nisingemvamia kwanza tungekuwa chakula chake leo..!"
Salim aliongea kwa pupa huku bado anahema kama mbwa. Dhahiri kabisa akili yake bado ililiwa haijatulia.
"Tafadhali kaa hapa na usubiri!" Magdalena alimuamuru kama vile alikiwa anaongea na mtoto mdogo.
Magdalena alimuacha Salim hapo nje ya chumba na kurudi tena ndani.
"Nahisi akili yake imeanza kukaa sawa kiasi." Cindy akaongea mara tu baada ya Magdalena kurudi ndani.
"Nani? Salim? Bado anahema tu kama mbwa utadhani ameingiwa na shetani rohoni.!" Magdalena akajibu.
"Hapana Magdalena… namuongelea Logan! Naona akili zinaanza kumrejea taratibu. Kipigo kimesaidia ah" Cindy akafafanua huku akimalizia na sentesi ya utani na kumkonyeza Magdalena.
"Kwa nini unasema akili zimeanza kurudi?" Magdalena aliuliza kwa shauku kubwa.
"Msikilize..!"
"Na…na…nat… na… nat!"
Loga alikuwa amejikunyata sakafuni kama mtoto huku ananong'ona kitu fulani.
"Sielewi anachokisema!" Magdalena akaongea kwa kukata tamaa.
"Msikilize kwa umakini."
Magdalena ilimbidi mpaka apige magoti chini ili kuinamisha kichwa karibu na Logan na kutega sikio asikie kile ambacho Logan alikuwa anakizungumza.
"Na…na…nat…natalie… natalie!" Logan alinong'ona.
"Natalie??" Magdalena aliinuka na kumuuliza Cindy kwa mshangao.
"Yes Natalie! Ni jina la mtoto wake, mwanaye wa pekee." Cindy akajibu huku usoni akiwa na tabasamu la matumanini.
"Ameanza kukumbuka?" Magdaleba akauliza kwa shauku.
"Yes.! Naamini ameanza kukumbuka sasa… kama amekumbuka jina la mwanaye nahisi kumbukumbu zimeanza kurejea kichwani. "Muite Salim!"
"Wa nini? Aisije akafanya uninga mwingine."
"Hapana muite… anapaswa kujua hili."
Magdalena akatoka nje kwa haraka na kama baada ya dakika moja akarejea akiwa ameongozana na Salim wakitemvea kwa haraka na shauku.
"Inaonekana ngumi zangu zimesaidia kumtikisa ubongo!" Salim akaongea kwa utani mara tu baada ya kuingia ndani.
"Unasema mliingia ndani ya Anabelle?? Hakuna ambaye amewahi kuingia ndani ya Anabelle na kutoka." Logan aliwauliza kiudadisi.
"Ni kisa kirefu muheshimiwa.!" Cindy hakutaka kuanza kusimulia maswahibu ambayo walikuwa wamepitia mpaka kufika hapo.
"Una uhakika tuko Morocco?" Logan alimuuliza Cindy.
"Nina hakika kwa asilimia mia moja muheshimiwa kwamba hapa ni Rabat, Morocco."
Logan akajiinamia tena kama anatafakari hivi.
"Kwa nini walisema makao makuu yako jangwani Nevada?" Logan aliongea peke yake huku bado akiwa amejiinamia.
"Nani Muheshimiwa aliyesema makao makuu yako jangwani Nevada? Makao makuu ya nini?" Cindy akauliza tena kwa udadisi zaidi.
"Twendeni niwaonyeshe kitu.."
Logan aliongea na kuanza kutoka nje ya chumba huku Cindy na wenzake wakimfuatia nyuma kwa shauku kubwa.
NAVAL OBSERVATORY CIRCLE - YALIPO MAKAZI WA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI
Wote watatu walikuwa wameingia ndani ya kichumba kile kidogo. Ron, Latisha na Natalie.
Kijichumba hiki kidogo kilikiwa nadhifu mno kilichopakwa rangi ya kijivu chumba kizima. Vitu pekee ndani ya chumba hiki vilikuwa kabati dogo la kioo lilipo upande wa kulia ukiingia ndani ya hiki kijichumba, kabati ambalo ndani yake kulikuwa na kitu kimoja tu, kompyuta mpakato.
Pia kulikuwa na kiti cha kukaa cha kiofisi kilichopo upande mwingine wa chumba na mbele yake kulikuwa na kamera iliyo kwenye kwenye stendi yake ya kurekodia.
Japokuwa ndani ya kichumba kile kulikuwa na vitu kadhaa lakini wote macho yao yalitua kwenye ile kompyuta mpakato ambayo ilikuwa ndani ya kikabati kile kodogo cha kioo.
"What happened to you Logan… what where you doing here?" Latisha aliongea kwa masikitiko kuonyesha maumivu ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
Ilikuwa inamuuma moyo kuona kwamba mtu aliyempenda sana, mtu mchangamfu, mwenye kupenda urafiki na watu, mwenye kupenda kwenda 'out' kila siku ati kumbe alikuwa na kijichumba cha siri cha namna hii. Kijichumba ambacho kamera iliyopo hapa inaonyesha alikuwa akijirekodi jumbe za siri ili kweka kumbukumbu.
Latisha aliumia moyo akijiuliza ni nini kilitokea au nini ambacho mume wake huyo wa zamani alikijua na kumbadili Logan kuwa mtu wa namna hii.
"Nadhani tutazame humu.!"
Wote waligutushwa kutoka kwenye mawazo na sauti ya Natalie ambaye tayari alikuwa ameshikilia laptop mkononi kutoka kwenye kile kijikabati.
"Wow! Hutaki kupoteza muda… hebu tuone." Ron aliongea na kuchukua laptop kutoka mkononi mwa Natalie na kuiweka juu ya kiti.
Akaifunua kwa haraka na kisha kuiwasha. Uzuri haikuwa na neno la siri, kuonyesga dhahiri kwamba Logan alitaka mtu atakayeipata kuona kilichomo ndani yake.
Baada ya Laptop kuwaka, juu yake kwenye uwanja wa 'desktop' kulikuwa na mafaili kadhaa… kama kumi hivi au zaidi. Yote yalikuwa na tarehe tofauti. Ron akabofya faili la kwanza ambalo lilikuwa juu kabisa kushoto mwanzoni. Ndani ya file kulikuwa na 'Video'. Ron akaibofya video na ikaanza kucheza.
Kwenye screen alitokea Logan… alikuwa anaangalia mbele moja kwa moja. Inaonekana kipindi alipokuwa anajirekodi kichwani mwake hakuwa anaiwaza kamera iliyo mbele yake bali alikuwa anamuwaza huyo ambaye ataenda kuitazama video hii. Alikuwa anamuwaza mwanaye wa pekee, Natalie.
Aliangalia mbele kwa muda mrefu sana bila kusema chochote. Machozi kama yalianza kumlenga lenga hivi. Natalie ambaye alikuwa akiangalia na kina Ron na Mama yake, tayari machozi yalikuwa yana tiririka shavuni.
Ilikuwa dhahiri kwamba Logan alikuwa anataka kuongea lakini alikuwa anshindwa kupata nguvu ya kusema kile ambacho alikuwa anataka kukisema. Akajiinamia kidogo hivi na kupeleza mkono wake machoni kuzuia yale machozi yaliyokuwa yanataka kudondoka. Kisha akainua uso na kutazama mbele tena na kisha kuanza kuongea.
"Mwanangu… kama unatazama ujumbe huu naamini uko mpweke hapo ulipo. Uko mpweke nafsini mwako. Labda kitu pekee kilichobakia cha kukufariji ni ujumbe huu. Sijui kama kuna yeyote aliyesalimika duniani. Sijui kama tumeshinda au tumeshindwa. Sijui. Kwa mambo niliyoyaona na yale ambayo naamini yatatokea nashindwa hata kupata maana halisi ya ushindi au ladha yake. Vyovyote vile lakini naamini huu ni mwisho wa ustaarabu wa dunia uliyokuwa unaijua. Sitaki kukuacha na maswali baba yako alikiwa ni mtu wa namna gani, na sitaki ubaki na maswali ni namna gani dunia imefikia hapa… kwa hiyo wacha nikueleze sisi tulikuwa ni akina nani… na wacha nikueleze wewe ni nani.! Na la msingi zaidi, wacha nikueleze ni namna gani nimepambana."
EPISODE 44
Maneno ambayo Naomi alikuwa amemueleza Renaldo Gillemo yalikuwa kama vile yametiwa gundi kwenye akili yake.
Renaldo Gillemo amekuwa afisa wa Secret Services kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na miwili sasa, na miaka mitatu iliyopita alipandishwa cheo kuwa ASAI (Advance Special Agent Incharge) akiwa na jukumu la kuongoza kikosi cha maafisa wanaomlinda Rais. Katika kipindi chote hiki hakuwahi kukaidi wala kutilia mashaka amri hata moja kutoka kwa Rais. Lakini siku tatu zilizopita tangu kurejea kwa Madam President Laura Keith kumemfanya aanze kuwa na mashaka na amri ambazo amekuwa akipewa.
Kwanza kabisa, mara tu baada ya Rais Laura kuzinduka kutoka kwenye hali ya kuzimia ya karibia siku tatu toka aokotwe pwani ya visiwa vya Carribeans, amri ya kwanza ambayo aliitoa iliiuwa ni kutaka makamu wake wa Rais, David Logan awekwe chini ya ulinzi bila kutoa sababu yoyote ya msingi.
Siku tatu zilizopita Madam President aliamuru tena Naomi cole ambaye ni National Security Advisor, James Ruppert ambaye ni Mkurugenzi wa CIA na Ethan kiongozi wa kikosi cha weledi cha kijeshi kilicho chini ya SAD ndani ya CIA, aliamuru wote wawekwe chini ya ulinzi. Kwa kuwa White House hakukuwa na mahabusu, iliwabidi wawafungie Naomi na wenzake kwenye moja ya vyumba vikuu kuu ambacho hutumika kama moja ya stoo ya vifaa vya usafi.
*"Kuna kitu kinaendelea Renaldo… ukiingia ndani ya Oval Office jaribu kuchunguza kwa weledi wako lazima utagundua kitu.!"*
Maneno ya Naomi yalikuwa yanajirudia tena kichwani mwa Renaldo.
Kwa hakika kabisa kuna kitu alikuwa anahisi hakiko sawa. Lakini upande fulani wa akili yake ulikuwa unasita kufanya lolote lile. Labda ni mazoea aliyojijengea kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili ya utumishi wake kama afisa wa Secret Services ndio ulikuwa unamfanya kusita kufanya kitu ambacho alihisi kinaweza kuwa kinyume na matakwa ya Rais. "Lakini hakuna maana ya kutimiza matakwa ya Rais kama matwaka hayo yanatishia usalama wa nchi ambayo niliapa kuilinda." Renaldo alijieleza mwenyewe kimoyo moyo.
Ndani ya White House karibu na jengo la West Wing kuna nyumba ya ukubwa wa wastani. Nyumba hii ndio ambayo inatumiwa kwa ajili ya mapumziko ya maafisa wa "Advance Team" za kumlinda Rais na Makamu wa Rais. Hapa ndipo ambapo wanapumzika na kulala kama hawako kwenye 'shift' ya ulinzi kwenye jengo analoishi Rais ndani ya Whitehouse ambalo linajulikana kama 'Excutive Mansion'.
Muda huu wakati anatafakari haya, Renaldo Gillemo alikuwa bafuni kwenye nyumba hii ya mapumziko ya Maafisa wa Secret Services ndaji ya Whitehouse.
Licha ya hizi amari ambazo Madam President Laura Keith alikuwa anazitoa lakini suala lingine ambalo lilikuwa linamtatiza zaidi rohoni Renaldo ni kitendo cha kupotea katika Mazingira ya kutatanisha si Makamu wa Rais tu bali pia Waziri wa Mambo ya Nje na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Congress. Hawa wote walikuwa kwenye mtiririko wa kupokea madaraka kama ikitokea Rais hayupo au anaonekana hana uwezo wa kutimiza majukumu yake sawa sawa.
Wote hawa wamepotea mara tu baada ya Madam President Laura Keith kupatikana katika mazingira ya kutatanisha kabisa. "Kuna kitu hakiko sawa kwa hakika kabisa". Renaldo aliiambia tena nafsi yake.
"Kuna kitu kinaendelea Renaldo… ukiingia ndani ya Oval Office jaribu kuchunguza kwa weledi wako lazima utagundua kitu.!"
Renaldo akakumbuka tena maneno ambayo aliambiwa na Naomi kabla hajawafungia kule stoo.
Renaldo alimaliza kuoga na kisha kuvalia suti yake kama ilivyo ada. Ilikuwa inakaribia saa tano na nusu usiku. Akaweka silaha yake kiuoni ndani ya koti la suti na kisha kutoka nje kuelekea ilipo Oval Office.
"Habari ya jioni?"
"Nzuri mkuu habari yako?"
"Salama.!"
Renaldo alisalimiana na maafisa ambao walikuwa nje ya Oval Office na kisha kuwapita kuelekea ndani. Kutokana na cheo chake, ambapo yeye hasa ndiye alikuwa kama mlinzi mkuu wa Rais na kiongozi wa 'advance team' ya maafisa wenzake hii ilimpa ruhusa ya kuingia kwenye ofisi ya Rais au kwenye makazi yake jengo la Excutive Mansion bila kuulizwa swali lolote lile na mtu yeyote.
Kwa hiyo Renaldo aliwapita wale maafisa wenzake na moja kwa moja kuingia ndani ya Oval Office.
*"Kuna kitu kinaendelea Renaldo… ukiingia ndani ya Oval Office jaribu kuchunguza kwa weledi wako lazima utagundua kitu.!"*
Kauli ya Naomi ikajirudia tena kichwani mwake mara tu baada ya kiingia ndani ya ofisi hii ya mkuu wa nchi.
Mbele yake moja kwa moja kutoka mlangoni ikiingia ilikuwa ni 'Roulette table', meza ya kihistoria ya kiofisi ambayo imetumiwa na marais wengi wa Marekani. Meza ambayo nchi ya Marekani ilipata kama zawadi kutoka kwa Malkia wa Uingereza kipindi ambapo walimaliza msuguano wao wa kidiplomasia na kijeshi karne kadhaa zilizopita.
Meza ilikuwa imekaa maridhawa kabisa na kiti chake. Katikati ya ofisi hii kubwa kulikuwa na meza kubwa ya kioo na masofa makubwa mawili kila upande kwa ajili ya wageni wa Rais. Upande mmoja wa ukuta kulikuwa na kabati ya vitabu na upande mwingine wa ukuta kulikuwa na picha za michoro kadhaa muhimu.
Kwa haraka haraka Renaldo alishindwa aanzie wapi kutafuta na atafute nini. Nafsini mwake aliamini kabisa ile kauli ya Naomi kwamba kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia. Lakini Naomi hakumueleza ni kitu gani. Naomi alikuwa anataka Renaldo avumbue ukweli yeye mwenyewe ili uwe na maana zaidi kwake na kuchukua hatua.
Naomi alikuwa amemficha ukweli kwamba kabla ya Makamu wa Rais David Logan kupotea kusikojulikana na ikisemekana kwamba amepotea au kutekwa akiwa nyumbani kwake eneo la Naval Observatory Circle, lakini uhalisia ni kwamba, wao wakiwa Maryland nyumbani kwa Mzee Caleb aliwapigia simu kuwajulisha kwamba amevamiwa hapo Whitehouse na mtu ambaye anafanana kabisa na Mzee Caleb.
Lakini watu wa Secret Services walidai kwamba hawajui ni namna gani Logan aliondoka hapo Whitehouse bila wao kujua.
Kwa hiyo kulikuwa na utata mkubwa sana juu ya taarifa hizi mbili… inakuwaje Logan aseme amevamiwa hapo Whitehouse na Secret Services wasijue. Anawezaje pia kutoka nje ya Whitehouse na wao wasijue? Na je ni wapi hasa ambako Logan alitekwa? Nyumbani kwake Naval Observatory Circle au hapa Whitehouse? Ubaya ni kwamba ndani ya Oval Office hakuna kamera zozote zile zilizotegwa. Hii ilifanyika ili kumpa Rais faragha pale anapoteleleza majukumu yake. Tahadhali pekee ambayo imewekwa ni sehemu kadhaa ndani ya ofisi hii, ikiwepo meza yake ya ofisi, sehemu kadhaa ukutani, kwenye taa kadhaa na hata baadhi ya kalamu zake… anaweza kubofya kama ikitokea kwamba yuko hatarini na anahitaji maafisa Secret Services wafike haraka.
Naomi hakumueleza Renaldo masuala yote haya na wasiwasi wake huu. Alijua kua hata Renaldo licha ya kutii amri za Madam President Laura Keith lakini lazima naye atakuwa na wasiwasi wake moyoni kwamba kuna suala la siri ambalo limejificha nyuma ya pazia. Ndio maana akamwambia suala moja tu, "Kuna kitu kinaendelea Renaldo… ukiingia ndani ya Oval Office jaribu kuchunguza kwa weledi wako lazima utagundua kitu.!"
Renaldo akaangaza macho huku na huko… akili yake bado ilikuwa haijang'amua mi kitu gani hasa anatafuta au ni nini hasa ambacho alikuwa anatakiwa kukiwekea mkazo.
Kwahiyo aliangaza macho kila mahala kwa makini. Alitazama meza ya kioo pale kati kati ya ofisi. Akatazama masofa. Akatazama michoro iliyoning'inizwa ukutani. Akatazama kabati ya vitabu iliyopo kulia kwake. Kote hakukuwa na kitu chochote cha tofauti au kushtusha.
Akageuza shingo kutazama meza ya ofisi…. Lakini subiri.!!!
Kabla ya kugeuka akili yake kama ilikuwa imemtamkia kwa sauti kichwani "subiri". Kuna kitu alihisi. Kitu katika kabati ya vitabu. Kuna kitu hakikuwa sawa, au labda tuseme alihisi hakiko sawa.
Kabati hili lilikuwa la muundo wa kama 'shelves' za maktaba na ilikuwa na ghorofa/shelves saba ambazo zilikuwa na matabu makubwa makubwa sana. Kwa hiyo licha ya shelves hizi kuwa saba tu ilifanya kabati hii kuwa ndefu karibia na kufika mwisho wa ukuta kwa juu.
Kuna kitu ambacho Renaldo alikihisi kuwa hakiko sahihi. Vitabu katika shelves zote vilipangwa wima vimesimama. Lakini vitabu kwenye shelves mbili za mwisho vilikuwa vimepangwa kwa malalo, yaani kitabu kimoja kimeegemea kingine na kingine kimeegemea kingine mpaka mwisho.
Renaldo ameingia ofisi hii mara nyingi kiasi kwamba anaifahamu kama ambavyo anafahamu kiganja chake cha mkono. Na moja ya sifa kubwa ya kuwa afisa bora wa usalama ni kuzingatia "details" hata kama ni ndogo kiaisi gani. Renaldo alikumbuka kabisa kichwani mwake kwamba hajawahi kuona vitabu kwenye kabati hii vikiwa vimepangwa kwa mtindo wa mlalo. Alikumbuka kwa hakika kabisa kuwa vitabu kwenye shelves zote huwa vinapangwa kwenye mtindo wa kusimama wima.
Alihisi labda kuna mtu alipangua vitabu hivi na kuvirudhisha tena lakini hakukumbuka kuwa havipangwagi kwa malalo. Au labda alikuwa na haraka sana ya kurejesha vitabu hivyo kwenye shelves na akakosea kuvipanga wima akama ambavyo alivikuta.
Renaldo akatulia kidogo kusikiliza kama hakukuwa na mjongea wowote wa mtu kuelekea hapo Oval office. Alipojiridhisha kuwa bado yuko mwenyewe tu, akapiga magoti sakafuni na kuanza kupangua kitabu kimoja kimoja kutoka kwenye zile shelves mbili za mwisho ambazo zilipangwa kwa mlalo.
Akaondoa kitabu kimoja kimoja kwa umakini wa hali ya juu sana.
Aliondoa vitabu vyote kwenye shelve ya mwisho lakini hakukuwa na kitu chochote kile cha ajabu au kutia shaka. Akahamia shelf ya juu yake. Baada ya kuondoa vitabu kadhaa na kufika katikati, alipoondoa vitabu kama vitatu hivi vingine alishtuka kukuta kuna chupa ilikuwa imefichwa nyuma yake.
Ilikuwa chupa ya 'glass' yenye rangi ya kahawia iliyo kolea sana kufanana kabisa na chupa za maabara ambazo hutumika kuhifadhi kemikali. Chupa hii haikuwa na maandishi yeyote yale zaidi za herufi nne tu zilizoandikwa na mkono kwenye kikaratasi nakugandishwa juu ya chupa hiyo.
*'H2O2'*
"H2O2… hii ni Hydrogen Peroxide.!" Renaldo aliongea peke yake kwa sauti ya chini.
Alijikuta moyoni ameshtuka mno ghafla. Hydogen Peroxide ina matumizi mengi, lakini kutokana na kazi yake ya masuala ya ulinzi na usalama kuna kazi moja kuu ya hydrogen peroxide ambayo aliijua zaidi. Hydrogen peroxide inatumiwa na wahalifu kujisafisha au kusafisha eneo ili kupoteza ushahidi baada ya kutekeleza tukio la mauaji.
Moyo ukaanza kumuenda mbio na kijasho chembamba kikianza kutiririka. Akaanza kupangua vitabu vilivyobakia kwenye ile shelf kwa pupa safari hii. Alipofikia kitabu cha mwisho na kukiinua akakutana na karatasi ambayo ilikunjwa na kuwekwa chini yake.
Akaikunja haraka haraka na kisha kuanza kuisoma… ilikuwa na maneno machache tu;
#1. 5847, San Filipe, Suite 2600
Huston, Texas 77057
#2. 8 ft X 5 ft
#3. Nov 7, 20…………
Sentensi hii ya mwisho ilikuwa haijamaliziwa… ilikuwa kana kwamba aliyeandika alikosa muda wa kuimalizia na alikuwa na haraka sana hivyo akaacha kuendelea kuandika na kuikunja karatasi hiyo na kuificha.
Jasho lilikuwa linamtoka Renaldo. Japokuwa hakuelewa ni nini maandishi haya yalikuwa yanamaanisha lakini alihisi kama moyo ulikuwa unataka kupasula kwa woga. Alifikiria ni nani aliyeweka hii karatai?? Kwa nini aifiche?? Kwa nini sentesi ya mwisho haikumaliziwa?? Alikuwa anaharakaya nini? Alikuwa anamuogopa nani?? Na je hii Hydrogen Peroxide ya nini hapa?? Je kuna damu gani ilimwagika humu Oval Office??
Akiwa anaemdelea kutafakari hivi akasikia sauti ya viatu nje ya ofisi kuna matu anatembea anapiga hatua kuja uelekeo huo wa Ofisini.!
Renaldo jasho lilitoka kweli kweli, moyo ukienda kasi alihisi kama vile kifo kiko mbele ya macho yake wanatazamana…
EPISODE 45
Mlango wa oval office ukagongwa mara moja na kisha kufunguliwa.
Renaldo alisimama haraka haraka baada ya mlango kufunguliwa.
"Kila kitu kiko sawa chief?" Alikuwa ni moja wa maafisa wa Secret Services.
"Kila kitu kiko sawa kabisa!" Renaldo alijibu huku anazuga kwa kufunua makatasi anbayo aliyaokota chini na kuyashika mkononi.
"Nimesikia kama kuna purukushani hivi humu kwa dakika kadhaa.." yule afisa aliongea tena huku macho yake yakiwa kwenye vitabu pale chini ambavyo Renaldo alikuwa amevipangua.
"Kila kitu kiko sawa… yametokea matukio mengi leo kwa hiyo nahakikisha kama ofisi iko salama kabla ya Madam President kuanza kuitumia." Renaldo aliongea tena bila kumuangalia yule ofisa. Bado alikuwa anazuga kupekua makaratasi ambayo alikuwa ameyashika mkononi kwa kujiamini.
"Ok! Naomba kama naweza kujumuika nawe nikusaidie?" Yule afisa akaongea.
"Hapana! Nitamudu tu mwenyewe usijali.!"
Yule afisa akaganda anamtazama Renaldo kwa karibia nusu dakika nzima. Renaldo kutokana na uzoefu wake alifahamu kabisa kwamba hii haikiwa dalili nzuri. Kuna jambo ambalo lilikiwa linaendelea kichwani mwa yule afisa.
"Samahani… una jambo lingine?" Renaldo akamuuliza.
"Hapana chief… uwe na usiki mwema!"
Yule afisa akaaga na kuondoka. Renaldo alihisi kabisa kulikuwa na kitu cha ziada juu ya ujio wa huyu afisa wa Secret Services. Hakuja tu hivi hivi.
Akasimama katikati ya ofisi na kuanza kuwaza na kuwazua. Ni kitu gani hasa ambacho kilikuwa kimetokea hapa ofisini siku ambayo Makamu wa rais David Logan alipopotea? Ni nani ambaye alificha ule ujumbe wa karatasi na ile chupa yenye Hydrogen Peroxide?
Na je hii Hydrogen Peroxide ilitumika kufanya nini humu ofisini?
Hakutaka kupoteza muda zaidi. Akaondoka kutoka hapa Oval Office na moja kwa moja kuanza kuelekea kwehye chumba ambacho waliwafungia Naomi, Rupert na Ethan.
"Kuna shida!" Lilikuwa ndilo neno la kwanzaRenaldo kulitamka mara tu baadaya kuingia kwenye kile chumba cha stoo walichofungiwa akina Naomi.
"Nini?" Naomi aliuliza kwa shauku huku wakisogea karibu na pale ambapo Renaldo alikuwa amesimama.
"Kuna yeyote hapa kati yenu ambaye anaweza kunieleza nini maana ya hii karatasi?"
Renaldo aliongea huku anaitoa ile karatasi aliyoipata Oval Office kutoka mfukoni mwa suruali.
#1. 5847, San Filipe, Suite 2600
Huston, Texas 77057
#2. 8 ft X 5 ft
#3. Nov 7, 20…………
Ujumbe ulikuwa unasomeka kwenye kipande cha karatasi ambacho alikishikilia mkononi.
"Ni nini?" Rupert akauliza.
"Nilikuwa natarajia kuwa mnaweza kunipa jawabu?"
"Tunawezaje kukupa jawabu bila kufahamu ujumbe umetoka wapi au unahusu nini?" Rupert akajibu kwa hasira kidogo.
Mpaka sasa Renaldo alikuwa moyoni anahisi kabisa kuna jambo ambalo halikuwa sawa pale Whitehouse. Lakini kutokana na uzoefu wake wa masuala ya usalama haikuwa rahisi kwake kutoa tu taarifa fulani reja reja huku akihisi kabisa kuna uwezekano wa taarifa hiyo kuwa ni nyeti.
"Ok! Samahani kwa kuwauliza.." Akaongea na kuanza kugeuka kutoka nje ya stoo.
"Renaldo…Renaldo…!!" Naomi akamkimbilia na kumzuia asiondoke.
"Hivi ni mara ngapi unataka nikwambie hili suala… licha ya kwamba mmetufungia humu ndani lakini kumbuka kuwa mimi ni National Security Advisor na yule pale ni Mkurugenzi wa CIA na yule pale Ethan ni moja ya komando bora zaidi kwenye hii ardhi ya Marekani… kwahiyo hebu acha huu upuuzi wa kutuweka gizani namna hii? Tueleze hiyo karatasi inahusu nini?" Naomi alifoka.
"Kwanza kabisa pia unapaswa kukumbuka kuwa nimewaweka chini ya ulinzi hapa kwa amri ya Rais wa nchi ambaye ndiye amiri jeshi mkuu… pili ni kwa nia njema kabisa nimekuja kuwaonyesha hii karatasi na inaonekana kabisa hamfahamu inahusu nini? Kwa hiyo sioni sababu ya kusema kingine chochote.." Renaldo aliongea kwa kujiamini na kutaka kugeuka tena ili aondoke.
"Nafahamu kitu!" Naomi aliongea kuchokoza mjadala.
"Kitu gani?" Renaldo aligeuka na kuonekana kuhairisha nia yake ya kuondoka pale stoo.
"Huo mwandiko… ni mwandiko wa David Logan.!"
Renaldo akaiinua ile karatasi usawa wa uso wake ili kuitazama vyema.
"Damn it! Kwa nini sikung'amua hili?" Renaldo akang'ata midomo yake kwa kujilaumu kwa namna gani ameshindwa kuona suala jepesi kama hilo kwa mtu wa kaliba na wadhifa wake.
"Si hilo tu… kuna lingine nafahamu kuhusu hiyo karatasi.!" Naomi aliiongea tena safari hii kwa madaha huku anaelekea upande mmoja wa kile chumba na kwenda kukaa kwenye kiti. Alikuwa anajua kabisa amefanikiwa 'kumbananisha' Renaldo kwenye kona.
"Kitu gani kingine?" Renaldo aliuliza kwa shauku kubwa.
"No! Nishakwambia vya kutosha na mimi… tueleze kwanza hii karatasi inahusu nini kabla sijakwambia chochote kingine?" Naomi aliongea kwa msisitizo.
"Hauwezi kunipa masharti ya kunipa taarifa kuhusu usalama wa Taifa… kumbuka unaongea na afisa wa Secret Services na maslahi yangu ni kumlinda na Rais, makamu wa Rais na maslahi yao kwahiyo nakuamuru unipe hiyo taarifa sasa hivi!" Renaldo alijitahidi kuongea kwa kujitutumua japo alikuwa anajua fika kwamba alikuwa amebananishwa kwenye kona.
"Kumbuka pia unaongea na National Security Advisor na ni maslahi yangu ya kwanza kuhakikisha kuwa nchi yangu iko salama... kwa hiyo kama unataka taarifa niliyo nayo kwanza nieleze hiyo karatasi inahusu nini?" Naomi naye alijitutumua mpaka akainuka kutoka kwenye kiti na kusimama.
Wakabaki wanaangalia wamekaziana macho kwa dakia nzima. Kama vile paka wanaotaka kuraruana.
"Renaldo! Sote tuko timu moja hapa, sisi na wewe… najua inafahamu kwamba kuna kitu hakiko sawa na kuna kitu Madam President Laura Keith anakificha. Wote tunataka kuhakikisha taifa hili liko salama. Kwa hiyo badala ya kutunishiana misuli hapa tunaweza kuzungumza pamoja na kuisaidia nchi.!" Rupert akaongea kwa sauti ya busara huku amemshika bega Renaldo.
Renaldo akaonekana kupoa kidogo.
"Ok! Wacha niwaeleze…"
Akawaeleza namna ambavyo alikata shauri kwenda kutazama Oval Office kwa umakini kama ambavyo Naomi alikuwa amesisitiza. Akawaeleza ni namna gani ambavyo aligundua kwamba mistari miwili ya mwisho ya vitabu kwenye 'shelves' vilikuwa vimepangwa tofauti na ilivyo kawaida. Akawaeleza namna ambavyo alianza kupekua vitabu kwenye shelves hizo na hatimaye kukuta chupa ya Hydrogen Peroxide na kipande hicho cha karatasi.
"Inaonekana Logan alikua anaandika haraka haraka… alikuwa na hofu ya jambo fulani hivi... swali ni jambo gani ambalo alikuwa anahofia na kwa nini alikuwa anandika maelezo haya?" Rupert akachokoza mjadala.
"Naomi umesema kwamba kuna kitu kingine unafahamu kuhusu haya maelezo kwenye hii karatasi… kitu gani?" Renaldo akakumbushia kitu ambacho Naomi aliongea awali.
"Ndio! Hiyo anuani, 5847, San Filipe, Suite 2600
Huston, Texas 77057 … ni anuani ya nyumba ya baba yake Madam President Laura Keith jimboni Texas!!" Naomi akajibu.
Ukapita ukimya wa kama dakika nzima. Kila mmoja akiwa anajaribu kuwaza na kuwazua kichwani. Kuna uhusiano gani? Kwa nini Logana kama yeye ndiye kweli aliandika hii karatasi… hiyo anuania aliiandika kwa sababu gani?
"Nadhani tunapaswa kwenda kwenye hiyo anuani huko Huston, Texas kuangalia kuna nini?" Rupert akapendekeza.
"Muende wapi? Mko chini ya ulinzi kwa amri ya Rais wa nchi. Hata kama nikiwaruhusu mimi mtoke mnadhani maafisa wengine watakubali mtoke nje ya Whitehouse? Na msisahau kuwa Rais ametangaza Marshal Law… tunafikaje Texas ilhali jeshi limeamuriwa lisiruhusu mtu yeyote kuonekana mtaani?" Renaldo aliongea mfululizo.
Naomi akazungusha macho kudharau kile ambacho Renaldo alikuwa anakiongea. "Renaldo wewe ndio boss hawa maafisa wote hapa Whitehouse... ukiamua unaweza kututoa humu ndani... kuhusu huko nje hakuna mwanajeshi ambaye anaweza kutuzuia tusiende tunakotaka… tukiwaonyesha vitambulisho tu hakuna mahala ambako tutazuiwa."
"Nadhani hayutakiwi kwenda Texas!" Ethan ambaye alikuwa amekaa kimya muda wote hatimaye akaongea.
Wote wakageuka kumuangalia.
"Una maana gani?" Naomi akamuuliza.
Wote walikuwa na shauku ya kusikia maoni ya Ethan. Kwa wote ambao walikuwa hapa, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na uzoefu wa 'field' na mikiki mikiki kukaribia hata nusu ya komando jasusi Ethan.
"Umesema kuwa nyuma ya vitabu pia ulikuta Hydrogen Peroxide, si ndio?" Ethan akamuuliza Renaldo.
"Ndio. Sahihi kabisa.." Renaldo akajibu.
"Wote hapa tunafahamu kazi kuu ya kwanza ya Hydrogen Peroxide ni nini katika matukio ya kihalifu na ujasusi… watu wanaitumia kusafisha damu iliyomwagika eneo la tukio na kwenye mwili au nguo!!" Ethan akaeleza.
"Ndio tunafahamu!" Akina Naomi wakaitikia kwa pamoja.
"Renaldo umetueleza kwamba hakuna mtu anayejua ni saa ngapi au namna gani Makamu wa Rais David Logan alitoka ndani ya Whitehouse... mlichokuja kusikia tu ni maiti za maafisa wa Secret Services nyumbaji kwake Naval Observatory Circle huku yeye mwenyewe akiwa hajikani alipo.?"
"Ndio ni sahihi kabisa.!"
"Vipi kama nikikikueleza kwamba maafisa wale wa Secret Services waliuwawa ndani ya Oval Office na hii Hydrogen Peroxide ilitumika kusafisha damu isionekane? Na kwa kuwa huwezi kuacha maiti ndani ya Oval Office kwa sababu ituzua kizaa zaa kikubwa, baada ya hapo maiti zao pamoja na Logan zikasafirishwa mpaka nyumbani kwa Makamu wa Rais David Logan kule Naval Observatory Circle?" Ethan alieleza kwa kujiamini.
Wote nao taa zikaanza kuwaka vichwani mwao. Lakini bado kulikuwa na maswali mengi na sintofahamu.
"Haiwezekani mtu aingie ndani ya Whitehouse... afanye mauaji ya walinzi wa Makamu wa Rais na kisha asafirishe maiti bila sisi kufahamu!" Renaldo akaongea kwa mashaka.
"Ni kweli haiwezekani… lakini inawezekana kama waliotekeleza hayo walikuwa tayari ndani ya Whitehouse!" Ethan akaongea kwa fumbo.
"Unataka kusema kuna maafisa wa Secret Services wamehusika kwenye hili?" Renaldo aliongea huku akianza kupandwa na hasira.
"Inaonekana iko hivyo!" Ethan akajibu kwa kifupi.
"Haiwezekani!!" Renaldo aliongea kwa jazba.
"Inawezekana kabisa Renaldo…" Naomi akaingilia kati, "na hiyo ndio namna pekee yenye mashiko na mantiki kueleza ni nini kilitokea… swali la msingi la kujiuliza ni kwa nini walipeleka maiti kule Naval Observatory Circle nyumbani kwa Makamu wa Rais David Logan?"
"Nadhani kuna kitu walikuwa wanakita…" Rupert naye akachangia. "Nina kila sababu ya kuamini kuwa Logan hawakumuua pale Oval Office. Nahisi kipindi hao wahusika wanapambana na walinzi wake ndio yeye aliandika hioi kikaratasi… naamini baada ya hapo wakamchukua akiwa hai na kuna kitu walikuwa wanataka Logan awaonyeshe na kitu hicho kipo Naval Observatory Circle.!"
"Kabisa! Inaingia akilini.." Ethan akakubaliana na wazo la boss wake Rupert. "Swali ni je Logan aliwaonyesha hicho kitu? Na ni kitu gani? Na kuna njia moja tu ya kufahamu jawabu kama walikiona au hawakukiona na ni nini hicho kitu…"
"Njia gani?" Renaldo aliuliza kwa shauku.
"Inabidi utusaidie kufika Naval Observatory Circle sasa hivi!!" Ethan aliongea huku amemkazia macho Renaldo.
EPISODE 46
Ron, Latisha na Nicole walikuwa wameitolea macho screen ya laptop kusikiliza na kuangalia kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Kwa namna fulani ilikuwa inahuzunisha na kuogopesha kuwa katika hali ambayo walikuwa nayo muda huu.
Wao kuketi na kitazama video ambayo Logan alikuwa ameirekodi siku ambazo hazijulikani zilizopita ilikuwa ni kana kwamba walikuwa wanatazama ujumbe wa mwisho wa mtu kabla ya kujiua au kana kwamba ilikuwa ni kutazama ujumbe wa mwisho wa mtu ambaye alikuwa amejitoa muhanga.
Wote walikuwa kimya kabisa lakini woga, uchungu na wasiwasi ambao walikuwa nao ulikuwa unaweza kuhisiwa hata ukiingia tu kwenye chumba.
Latisha na mwanaye Nicole walikuwa wanaangalia kwa uso ambao ulikuwa unaakisi kabisa kile ambacho kilikuwa mioyoni mwao, wasiwasi na woga wa kumpoteza mtu ambaye walikuwa wanampenda kwa mioyo yao yote mpaka kwenye mifupa yao. Ron yeye alikuwa anaangalia kwa shauku kubwa na umakini.
Kama kuna swali ambalo wote walikuwa hawajajiuliza ni kwa nini Ron alikuwa bega kwa bega na wao kutaka kutatua hatari hii ambayo ilikuwa imeikumba ulimwengu. Mpaka muda huu ni Ron pekee ndiye ambaye alikuwa anajua ni kitu gani gasa ambacho alikuwa amekilenga moyoni mwake.
"….naamini uko mpweke mwanangu muda huu. Na kama unasikiliza ujumbe huu maana yake kwamba nimeshafairiki muda mwingi na pengine ujumbe huu ndio kitu pekee cha kukufariji. Hakuna haja ya kujiuliza ni kitu gani hasa kimetokea ulimwenguni. Na hakuna haja ya kutafuta jawabu. Haja yangu kubwa ni kutaka uwe salama mwanangu.."
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Ujumbe wa video ulikuwa unaongea pale kwenye laptop.
"…Nicole! Unakumbuka mara yetu ya mwisho kusafiri tulienda wapi? Basi nahitaji ufike mahala hapo. Pamoja na ujumbe huu ambao unautazama, nadhani unaweza kuona files nyingine kadhaa. Tofauti na ujumbe huu files zilizosalia zote utahitaji neno la siri ili kuzifungua. Kwa hiyo nahitaji ufike mahala ambako tulienda mara ya mwisho mimi na wewe kisha utapata maelezo yaliyosalia. Nahitaji uwe salama mwanangu. Fika hapo haraka uwezavyo.!"
Ujumbe ukaishia hapo.
Haraka haraka Ron akajaribu kufungua files nyingine ambazo zilikuwa zimesalia lakini hakukuwa na mafanikio yoyote. Kila file ambayo alijaribu kuifungua ilikuwa inahitaji neno la siri ili iweze kufunguliwa.
"Daaammmnnn it!" Ron akainuka kwa hasira kutoka pale ambako alikuwa ameketi.
"Nadhani amefanya hivyo kwa sababu za kiusalama." Latisha akaongea huku naye anasimama.
"Sababu gani za kiusalama?" Ron akaulizankwa hasira.
"Namaanisha hii sababu ya kuweka maneno ya siri na kutaka kuyapata kutoka mahala kwengine amefanya hivyo kwa sababu za kiusalama. Vuta picha ingekuwaje kama ni mtu mwingine angepata fursa ya kugundua chumba hiki cha siri na kuona hizi recordings kabla yetu? Nadhani alichukua tahadhali mapema ili kulinda hicho ambacho kipo kwenye jumbe hizi.!" Latisha aliongea kwa msisitizo.
"Tahadhali gani? Kutuhangaisha kila sehemu kama vichaa?" Ron akaendelea kufoka tena kwa hasira.
"Tahadhali ya kuhakikisha kama isingelikuwa sisi… namaanisha Nicole na mimi! Kama isingelikuwa Nicole na mimk basi mtu mwingine asiweze kujua kilichomo ndani ya hizi files kwa sababu asingeweza kujua ni wapi ambapo tulisafiri mara ya mwisho kwa pamoja!" Latisha akaendelea kujieleza.
"Na ni wapi ambako mlisafiri kwa pamoja?"
"Ilikuwa miezi kama mitatu kabla hatujatalikiana… tulisafiri pamoja kwenda Bahamas. Nadhani ndiko huko ambako anamaanisha."
"Whaaaat?? Bahamas… tunafikaje Bahamas?" Ron akang'aka kwa hasira zaidi.
"Sijui lakini ndiko ambako tulienda kwa mara ya mwisho kama familia." Latisha alijibu huku amejiinamia kutokana na kujua fika kutowezekana kwa huko ambako wanatakiwa kwenda.
"Tunafikaje Bahamas na hii Marshall Law iliyotangazwa na Rais? Umeona ni namna gani imetuwia vigumu kufika hapa kutoka New York. Kama kusafiri tu ndani ya nchi imekuwa mtihani hivi, tunawezaje kutoka nje ya nchi?"
Swali la Ron lilibakia tu 'linaning'inia hewani'. Hakuna ambaye alikuwa na jawabu au hata pendekezo la nini wafanye mpaka kufika huko Bahamas. National Guard ilikuwa imemwagwa mchi nzima. Wanajeshi walikuwa na ruhusa ya kumpiga risasi yeyote yule ambaye angeonekana mtaani. Iliwachukua kiwango kikubwa cha ushawishi alionao Ron pamoja na rasilimali fedha zake kwa wao kuweza kufika hapa Washington kutokea jijini New York wanakoishi. Kwa hiyo taarifa hii kwamba inawapasa wafike Bahamas ilikuwa ni taarifa ya kukatisha tamaa kabisa.
"Safari ya mwisho haikuwa Bahmas.!!" Nicole ambaye alikuwa kimya muda wote hatimaye akaongea.
"Naam.!" Ron akageuka kwa shauku kumtazama.
"Safari ya mwisho hatukwenda Bahamas!" Nicole akaongea tena.
"Una maana gani Nicole. Safari ya mwisho sote tulisafiri pamoja mpaka Bahamas… mimi, wewe na baba yako. Ilikuwa miezi mitatu kabla hatujatengana.!" Latisha akaongea kwa mshangao, akishangaa kwa nini binti yake anasema kile ambacho alikuwa anakisema ilhali alikuwa na uhakika kabisa kuwa safari yao ya mwisho kama familia walisafiri kwenda Bahamas.
"Mama… hiyo ilikuwa ni safari yetu ya mwisho kama familia lakini haikuwa safari yetu ya mwisho mimi na baba… kuna sehemu tulienda mimi na yeye!" Nicole aliongea huku amewakazia macho.
Wote walijawa na shauku. Lakini Ron ndiye ambaye alikuwa na shauku zaidi. Uso wa Latisha ulikuwa na woga kuzidi shauku ambaye alikuwa nayo moyoni. Alikuwa hafahamu safari hiyo ya mwisho ya mwanaye Nicole na baba yake.
"Mlienda wapi Nicole?" Latisha aliuliza kwa mshangao na woga.
"BAAAAAAAAAAANG.!"
Zilikuwa ni kelele za ghafla za mlango wa kuingilia chini kwenye basement walipo ulikuwa umefunguliwa kwa kishindo cha kuvunjwa.
Ghafla zilisikika hatua za haraka haraka za watu ambao walikuwa wanateremka ngazi za basement kwa kasi kubwa.
Kwa haraka sana Ron, Nicole na Latisha walitoka kutoka kwenye kile kijichumba cha siri na kusimama katikati ya basement kuona ni nani ambao walikuwa wamewavamia.
"Msisogee hata hatua moja.!!!" Amri ilitoka huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki.
Walikuwa ni Naomi, Rupert, Ethan pamoja na Renaldo ndio ambao walikuwa wameingia hapa kwa kishindo hivyo.
Baada ya wote kutazamana sawia hatimaye wakatambuana. Hakuna ambaye alikuwa hamtambua Latisha mke wa zamani wa Makamu wa Rais David Logan na mwanaye Nicole. Pia hakuna ambaye alikuwa hamtambui mfanya biashara maarufu Rodney Van Derberg.
"Mnafanya nini hapa?" Naomi ambaye ndiye pekee hakuwa na bunduki aliuliza kwa mshangao.
"Tuwaulize nyinyi mnafanya nini hapa?" Ron naye aliuliza swali kwa mshangao.
Si lazima kuwa Nabii ili kuweza kuona nyakati zijazo na wala si lazima kuwa mtume ili kuwa wakala wa habari njema. Kuna jambo au kitu au kiumbe kilicho juu ya sisi wote, si Mungu kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi. Lakini kiko kiumbe ambacho kilipata kuwepo kabla hata ya mito, maziwa, bahari na hata jua kupata kuwepo. Mwenye werevu wa kujua siri zote kuu juu ya ardhi. Mwenye uhai usiokoma kwa maelfu na maelfu ya miaka. Mwenye kujidhihirisha katikati yetu kama binadamu mara kadhaa katika umbo la uanadamu. Mwanzilishi wa starehe, anasa tangu mwanzo wa ustaarabu wa dunia.
Pengine ndiye ambaye alijidhihirisha akiwa katika hali ya ubinadamu kupitia mashujaa wa historia kama Mfalme Alexander, au shujaa wa vita kama Archilles. Pengine alijidhihirisha tena katila sura ya wanataaluma kama Leonardo Da Vinci au mwanamapinduzi wa kimuziki kama Morzart.
Hakuna anayejua, lakini kiko kiumbe cha hali ya juu zaidi yetu. Kiumbe ambacho kina uhai usio koma. Kiumbe ambacho kimewahi kukutana ana kwa ana na Zeus, Mungu wa Kigiriki. Kiumbe ambacho kimewahi kufanya jaribio la kumuoa Hera, Mungu mkuu wa miungu yote ya kike ya kale. Kiumbe ambacho kimewahi kukabiliana na kutunishiana misuli na Hades, mungu wa vita na mungu wa ulimwengu wa giza.
Hakuna kitabu cha imani ambacho kimethubutu kumzungumzia kiumbe huyu na vitabu vya kihistoria ni vile vitabu vya siri pekee ambavyo vimethubutu kutia mkono kumdhihirisha.
Mara ya mwisho alijidhihirisha katika karne ya 16 akiishi katikati yetu. Kwa zaidi ya karne tano hakuna mwanahistoria ya giza ambaye amefanikiwa kunasa walau dalili ya uwepo wake katikati yetu. Lakini ni tukio moja tu, tukio ambalo limetokea mwaka 2038 ndilo ambalo liliamsha uwepo wake kutoka chini kabisa ya vilindi vya bahari na hatimaye kwa mara ya kwanza kuonekana dalili ya uwepo wake katikati yetu. Tukio la kufunguliwa kwa chupa kutoka katika sanduku la Pandora.
Kalamu hii ikawe ushuhuda wa yale ambayo yametokea, yanatokea na yatakuja kutokea siku chache za usoni.
******
Mawimbi ya bahari yalikuwa yanapiga kwa nguvu kiasi na kuwasukuma akina Mzee Caleb na wenzake ambao walikuwa wamelala pembezoni mwa bahari mchangani bila kujitambua.
Kadiri ambavyo mawimbi yalivyokuwa yanapiga na kuwasukuma ndivyo ambavyo yalikuwa kama yanawatikisa ili kuwaamsha warudi katika ufahamu.
"Koh koh koh koh..!!"
Walker ndiye alikuwa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake wote. Alijitahidi kusimama japo bado alikuwa anatapika na kichwani ana kizungu zungu.
Pale mchangani walikuwa wamelala wenzake wengine makomando sita pamoja na Mzee Caleb.
"Mzee mzee mzee! Mzee Caleb.!"
Walker alimkimbilia kwanza mzee Caleb ambaye alikuwa amelala pembeni yake huku akiwa hajitambui.
Alitumia karibia dakika nzima kumtikisa mpaka Mzee Caleb alipoamka na kupata ufahamu.
"Koh koh… tuko wapi.!?" Mzee Caleb alimka huku anahema kwa nguvu na kukohoa mfululizo.
Kabla Walker hajajibu, makomando wenzake nao walikuwa wameamka tayari. Silaha ambazo walikuwa nazo awali walipokuwa wanaingia msitu wa Ox kule Maryland hawakuwa nazo tena. Wala yale mabegi ya mgongoni ya kijeshi hawakuwa nayo tena.
"Nini kimetokea?" Mmoja wa wale vijana makomando akauliza.
Walisimama pale kwenye pwani wakiangaza macho huku na huko. Mara ya mwisho walipokuwa na fahamu zao walikuwa ndani ya msitu wa Ox na wakikuwa wanakaribia kushambuliwa na kuraruriwa vipande vipande na binadamu wa ajabu ambaye alikuwa anawafuatilia.
#683
Mbele yao kulikuwa na bahari ambayo ilienda mbali kuzidi hata upeo wa macho yao. Nyuma yao pale pwani kama mita ishirini hivi kutoka pale ambako walikuwa wamesimama kulikuwa na msitu mnene.
"Mzee unafahamu tuko mahali gani hapa?" Walker alimuuliza mzee Caleb ambaye naye alikuwa anageuka geuka kupepesa macho kupatazama vyema pale walipo.
"Sifahamu tuko mahala gani.!" Mzee Caleb alijibu huku anaemdele kugeuka geuka kutazama yale mandhari yanayowazunguka.
"Kuna kitu hapa!" Mmoja wa makomando aliwaita akiwa amesimama kama mita kumu kutoka wenzake walipo.
Kwa haraka wote wakatembea kwenda pale ambapo mwenzao alikuwepo.
"Kuna nyayo za binadamu hapa!" Yule komando akawaonyesha wenzake walipofika pale alipo.
Pale ambapo alikuwa amesimama mchangani kulikuwa na nyayo kadhaa za binadamu ambazo zilionekana zilikuwa za watu ambao walikuwa wametembea kutoka hapo pwani kuelekea kwenye ule msitu ambao ulikuwa mbele yao.
"Ni akina nani hawa?" Mmoja wa makomando akauliza.
"Unauliza swali ambalo sio sahihi… hatuwezi kujua ni akina nani… lakini tunapaswa kujiuliza walichokuwa wanakifanya… tazama hapa!" Walker alijibu huku akiwaonyesha kitu fulani kwenye zile nyayo pale mchangani.
"Hizi ni seti za nyayo za watu zaidi ya nane au kumi kabisa… tazama hapa… hizi ni seti za watu wanne ambao wanaonekana walikuwa wamebeba kitu chenye pande nne"
"Kabisa… tazama hapa mbele inaonekana kuna mtu mmoja alitangulia na nyuma mtu mwingine.…" komando mwingine naye akaongeza.
"Walibeba kitu kama jeneza… lakini tazama hapa!" Walker akawaonyesha tena kitu fulanipale mchangani. "Kuna seti nyingine za nyayo ambazo zinaongozana na hizi lakini zimejitenga kidogo! Inaonekana walikuwa kama wasindikizaji.!"
"Au walikuwa wanafuatilia nyayo hizo nyingine kama sisi tunavyofanya!" Mzee Caleb alichangia kwakutoa wazo mbadala.
"Umewaza vyeama kabisa mzee… labda walikuwa nao wanafuatilia nyayo hizi zingine kama sisi.." Walker akaunga mkono wazo la Mzee Caleb.
Wakazitazama zile nyayo pale mchangani kwa umakini kwa dakika kadhaa na hatimaye wakakata shauri kuzifuatilia.
Walizifuatilia zile nyayo mpaka kuingia ndani kabisa ya msitu. Kama dakika ishirini hivi baadae, mbele yao umbali kama wa mita thelathini hivi kulikuwa na Kasri kuu kuu sana. Kama kasri la kifalme la miaka ya zamani mno. Kutokana na hali ya giza giza ambayo ilikuwepo pale walipo ilifanya wajihisi kama vile wako kwenye ulimwengu mwingine kabisa, ulimwengu wa kale wa kama karne kadhaa nyuma japo ilikuwa ni karne ya ishirini na moja mwaka 2038. Kasri hilo ambalo halikuwa na umeme au hali yoyote ya usasa, kwenye kuta zake zilikuwa zimening'inizwa chemli za mafuta ya taa kwa ajili ya kutoa mwangaza wa kasri hilo.
"Ni nini hiki?" Mmoja wa makomando aliuliza.
"Kuna njia moja tu ya kufahamu… tuingine ndani yake!" Walker akajibu huku akiwa amekaza macho yake kuelekea Kasri lilipo.
"Kama kuna ulinzi?" Mmoja wa wale makomando akauliza.
Swali lake hasa lilikuwa halimaanishi hasa wasi wasi wao kama kulikuwa na ulinzi wa kuzuia kuingia bali swali hilo lilikuwa linaakisi hofu waliyonayo kwamba labda walikuwa wanakabiliana na kitu cha tofauti kabisa ambacho hawawezi hata kupambana nacho kwa ujuzi na umahiri wao wa kijeshi.
"Tazameni.!" Mzee Caleb aliwagutusha kutoka kwenye mjadala wao na kuwaonyesga kidole kuelekea kule lilipo Kasri.
Kwenye geti lake kuu kuu, kulikuwa na watu wanatoka nje. Mzee Caleb, Walker na wenzake wakarudi nyuma kidogo na kujibanza nyuma ya mti huku wakichungulia kutazama wale ambao walikuwa wanatoka nje ya lile Kasri.
Walikuwa ni watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili. Kati yao, watu wawili, mwanamke na mwanaume walikuwa ni watu weusi na wawili wengine mwanamke na mwanaume walikuwa ni wazungu.
#684
"Hivi mnaona kile ambacho mimi nakiona?" Walker aliwauliza wenzake kwa kunong'ona lakini sauti yake ikionyesha kabisa taharuki ambayo alikuwa nayo.
Wote wakakodoa macho kutazama pale kwenye geti ili kung'amua kile ambacho Walker alikuwa anakiona.
"Mungu wangu, simani macho yangu.!!" Mzee Caleb akajishika mkono kifuani kwenye moyo kutokana na taharuki.
"Ndio Mzee… yule ni Vice President David Logan!!"
Walker aliongea huku wote wakiwa wamemkazia macho mwanaume wa kizungu ambaye alikuwa ameongozana na wale watu wengije watatu wakitoka ndani ya geti la lile Kasri.
"Tunafanyaje?" Moja ya makomando wale aliuliza.
"Yule ni Makamu wa Rais wa nchi yetu… ni lazima tuhakikishe kama yuko salama!" Walker aliongea huku bado akiwatazama wale watu ambao walikuwa wanatoka kwenye geti na David Logan.
"Lakini haonekani kama yuko kwenye hatari… anaonekana yuko hapa kwa hiari yake kabisa.!" Mzee Caleb akaongea.
"Ni jukumu langu kama afisa wa Ulinzi wa nchi yangu kuhakikisha yuko salama… lets go!" Walker ambaye ndiye alikuwa kamanda wa wenzake kwa sasa hakutaka kujadili zaidi… aliamuru wote wamfuate.
Walitembea kwa tahadhali kubwa kuwafuata wale watu pale getini.
"Kuweni tayari kwa lolote!" Walker aliwataahadhalisha wenzake kuwa macho ikitokea wakishambuliwa kwa ghafla.
Kadiri ambavyo walikuwa wanawasogelea kutoka msituni ndivyo ambavyo pia wale watu waliongozana na Logan na pamoja na Logan mwenyewe walisimama na kuanza kutazama msituni.
Yule mwanaume mmoja mweusi aliye pamoja na kina Logan alionekana kuwaonyeke ishara ya kidole mdomoni kwamba wanyamaze wasiongee kwa kuwa kuna kitu anakisikia msituni.
Ghafla… kufumba na kufumbua. Walker na wenzake waliruka kutoka msituni na kuwazunguka Logan na wenzake.
"Muweke salama Vice President!!" Walker aliamuru.
Mmoja ya mwanajeshi mwenzake alimnyakua David Logan kwa kasi na kumtenganisha na wale watu watatu ambao alikuwa nao.
Yule jamaa mweusi ambaye alikuwa na Logan aliruka kiustadi na kuanza kupambana na akina Walker. Alionekana dhahiri kuwa alikuwa ana uwezo mkubwa wa mapambano ya ngumi lakini kutokana na kuzidiwa wingi alidhibitiwa mara moja na wanajeshi wa Walker.
"Niko salama, niko salama… hawa ni watu wema waacheni… niko salama!" David Logan alisisitiza.
Aligundua kuwa hao walikuwa ni vijana kutoka kwenye moja ya vyombo vya Ulinzi nchini Marekani.
"Una hakika uko salama Mr. Vice President?" Walker aliuliza kwa msisitizo huku wanakukuruka kumdhibiti yule jamaa mweusi.
"Nimesema waacheni!" David Logan aliongea kwa mamlaka safari hii kwa kutoa amri.
Wakamuachia yule jamaa mweusi ambaye walimdhibiti kwa kumgandamiza chini kwenye mchanga.
Jamaa mweusi aliyeachiwa na akina Walker walikuwa bado wanaangaliana kwa hasira wote wakisubiri Logan aseme kitu kuweka mambo sawa.
"Uko salama Mr. Vice President?" Walker aliuliza tena kwa mara nyingine.
"Niko salama kabisa… mmefikaje hapa?" Logan akauliza kwa mshangao.
"Ni hadithi ndefu sana… labda utueleze wewe umefikaje hapa?" Walker alijibu swali kwa swali.
Wakiwa wanasuburi maelezo, macho ya Logan na Mzee Caleb yakagongana na Logan akamtambua.
"Mzee Caleb…! Ulisikia kiiichotokea Whitehouse?" Logan akauliza akikumbusha tukio lilitokea ambapo alivamiwa na mtu mwenye kufanana kabisa na Caleb.
"Nilisikia Muheshimiwa na nimewapa hawa maelezo ni nini kinaendelea… nitakueleza na wewe pia!" Mzee Caleb akaeleza kwa kifupi tu.
"Vipi mlifanikiwa kupata kile kitabu aaahh Book of… Book of…"
"BOOK OF CODES!" Mzee Caleb akamsadia David Logan kukumbuka.
Mara ya mwisho Logan na Mzee Caleb kukutana, ilikuwa ni pale ambapo Mzee Caleb alipelekwa Whitehouse na Mkurugenzi wa CIA Bw. James Rupert ili kueleza siri iliyomo ndani ya mchoro wa George Washington unaokaa Estern Room ya hapo Whitehouse. Kisha wakaondoka kwa pamoja mpaka Chuko Kikuu cha Stanford ambako walienda kutazama chupa ambayo iliokotwa huko Maldives na kufunguliwa na kuanzisha kizaa zaa cha miji kutwaliwa duniani. Japo waliikosa chupa hiyo kwa maelezo kwanba imeibiwa na mmoja wa wataalaku wa Idara ya Akiolojia ya chuo hicho ambaye amesafiri kwenda nchini Tanzania.
Kisha wakaondoka kutoka chuoni hapo kwa msafara wa pamoja ambao ulishambuliwa na watu wa ajabu ambao baadae walikuja kugundulika ni wapiganaji wa kikundi cha siri cha Sancta Cedes.
Ndipo hapa ambapo Mzee Caleb alitoa pendekezo la kwenda Maryland kwenye msitu wa Ox kwenye kaburi la babu yake ambako walifukia kitabu cha siri kinachoitwa BOOK OF CODES ili waweze kupambana na kikundi hicho cha siri cha Sancta Cedes.
Makamu wa Rais akatoa ruhusu mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. James Rupert ampatie Caleb na Naomi kikosi cha siri cha kijeshi cha CIA kinachoongozwa na Ethan kiongozana na Caleb na Naomi kwenye msitu wa Ox huko Marylanda.
"Ethan na Naomi wako wapi?" Logan akamuuliza Mzee Caleb baada ya kuunganisha nukta kwamba wanajeshi hao walio pamoja na Caleb watakuwa ni vijana wa Ethan.
"Walirudi Washington baada ya kupata taarifa kuwa umevamiwa Whitehouse!" Walker akajibu.
"Kwa hiyo mnamaanisha kwamba walienda Whitehouse?" Logan aliuliza kwa taharuki kiasi.
"Ndio Mr. Vice President." Walker akajibu.
"Damnt it! Lazima yule mwanamke atakuwa amewatia nguvuni!" David Logan aliongea kwa hasira huku amejishika kichwa.
"Mwanamke gani?" Wakajikuta wote wote wameuliza kwa pamoja.
"Madam President Laura Keith.!" Logan akajibu.
Wote wakashikwa na mshangao ghafla. Hawakuwa wanajua kile ambacho kilikuwa kinaendelea nyumbani Marekani.
"Nitawaeleza.!" David Logan akajibu tena kwa kifupi tu.
"Sawa Mr. Vice President… lakini hatujui tuko mahala gani hapa na ni muhimu tukijua nini kimetokea mpaka umefika hapa..!" Walker akauliza tena.
"Tupo Rabat, Morocco!" Cindy akajibu
"Samahani sikuwatambulisha… huyu ni Dr. Cindy Wheaton… Mzee Caleb yule mtaalamu wa Akiolojia ambaye tukiambiwa pale Stanford ameondoka na chupa ya Maldives na kwenda nayo Tanzania ndiye huyu… huyu hapa anaitwa Magdalena ni mtaalamu wa Biolojia kutoka Kenyatta University na huyu hapa ni Salim, Afisa ya Idara ya Usalama nchini Tanzania.!" Logan alifanya utambulisho wa haraka haraka.
Mzee Caleb, Walker na wenzake walibakia wametumbua macho tu kama wamechanganyikiwa. Walikuwa wanajiuliza ni namna gani Makamu wa Rais David Logan siku kama moja au mbili nyuma alikuwa Whitehouse amevamiwa na watu wasiojulikana kwa mujibu wa taarifa waliyoipata na sasa hivi yuko hapa na watu kutoka Tanzania na Kenya. Ulikuwa ni mkanganyiko mkubwa vichwani mwao.
"Mr. Vice President nadhani unaweza kuhisi ni namna gani tumechanganyikiwa vichwani mwetu!" Walker akaongea tena.
"Nafahamu… lakini hatuna muda wa kupoteza! Tunapaswa kufika sehemu haraka sana!"
"Sehemu gani?"
"Tunapswa kutafuta Hekalu la Mungu Zeus lilipo hapa Rabat!" Logan aliongea huku anaanza kutembea.
Sio Mzee Caleb, Walker na wanajeshi wenzake pekee ambao walishtuka bali pia hata Cindy, Magdalena na Salim. Walipotoka ndani ambako walimkuta kama amechanganyikiwa na baadae akili zake kukaa sawa baada ya kipigo kutoka kwa Salim, hakuwaeleza wanaenda wapi bali aliwaambia tu wamfuate. Sasa hivi ndio walijua kuwa wanatakiwa kwenda kwenye hekalu la Mungu Zeus. Kwa mtaalamu wa akiolojia kama Cindy alishituka zaidi kwa maana alifahamu fika ni namna gani suala hilo haliwezekani. Kwa sababu moja Hekalu la Zeus lilikuwepo yapata miaka elfu thalathini iliyopita na pili kwa mujibu wa historia hakuna binadamu ambaye amewahi kukanyaga mguu ndani ya hekalu hilo zaidi ya miungi kumi na mbili ya Kigiriki.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
"Hekalu la Zeus!" Cindy alirudia kichwani huku akiongozana na wenzake kumfuata David Logan.
MWISHO WA SEASON 1
ENDELEA KUFUATILIA SEASON 2
THE END...
0 comments:
Post a Comment