Simulizi : Tai Kwenye Mzoga
Sehemu Ya Nne (4)
“Mmejuaje kuwa ninayo hayo mengi ya kuwaambia?
“Subiri na muda si mrefu utafahamu ni kwa nini tunasema hivyo Luteni”
yule mtu aliyesimama alidakia maongezi.
“Na ndiyo maana umekaribishwa hapa uketi” yule mtu wa nyuma mwenye
sura kama anayetaka kupiga chafya alizungumza kwa sauti ya upole ingawaje
hakuonekana kuwa ni mtu wa tabia inayofanana na sauti yake. Nilisita kukaa
kwenye kile kiti lakini kila mmoja aliishtukia haraka dhamira yangu.
“Hebu keti kwenye hicho kiti Luteni, tunaweza kuokoa muda kama uta-
onesha utii” yule sura ya kifo alinitahadharisha na mimi sikuona sababu ya
kukaidi amri ile hivyo nikakisogelea kile kiti na kuketi. Mara tu nilipoketi
yule mtu mfupi alisimama kwenye lile kochi aliloketi kisha akaanza kuja pale
nilipoketi na muda ule ule nilimuona akitoa pingu mbili toka katika mifuko
ya koti lake.
“Samahani utatusamehe kidogo Luteni kwani ni kawaida yetu kuzungumza
na mtu tusiye mfahamu vizuri huku akiwa kwenye kizuizi cha pingu” yule
mtu alininong’oneza huku akiikamata mikono yangu kwa nyuma na kuifunga
pingu, alipomaliza akachukua pingu nyingine na kunifunga miguuni. Zoezi
lile halikuishia pale na kilichofuata nilimuona yule mtu akiitoa tena kamba ya
katani na alikuwa stadi sana kwa kazi ile kwani kufumba na kufumbua mwili
wangu wote ulikuwa umezungushiwa kamba iliyokazwa kikamilifu na alipo-
maliza kunifunga akanichapa makofi mawili mazito ya usoni yaliyonipelekea
niteme damu halafu yule jamaa alirudi na kuketi.
“Luteni...” yule jamaa aliyekuwa akishangilia kwa kupiga mruzi wakati ni-
lipokuwa nikishushwa kutoka kule ghorofani aliniita na hapo nikageuka na
kumtazama na wakati huu niligundua alikwisha nikaribia pale nilipokuwa.
Hofu ikapiga hodi moyoni mwangu pale nilipokumbuka kuwa mtu yule ali-
kuwa miongoni mwa wale watu waliokuwa wakinitafuta kwenye lile lori la
sukari nililokuwa nimepewa lifti kule njiani wakati nilipokuwa nikija hapa
jijini Kigali. Kwa kweli nilikata tamaa sana na kwa mara nyingine nikawa ni
kama ninayeiona hatima ya maisha yangu.
“Tunafurahi sana kuwa umerudi tena kwenye mikono yetu Luteni, na hupas-
wi kuwa na wasiwasi kwani sasa upo kwenye mikono salama” yule mtu alin-
iambia huku akitabasamu
“Tunafahamu kuwa upo hapa nchini Rwanda kwa maslahi ya taifa lako na
sisi hatushangazwi na hilo kwani hata sisi tupo hapa kwa maslahi ya watu
wetu kama ilivyo kwako”
“Sasa kwa nini mnifunge hivi kama kiumbe tishio kwenye hii dunia?
“Huwa ni utaratibu wetu wa kawaida tu Luteni sema wewe hujauzoea”
“Kwani hamuwezi kuzungumza na mimi nikiwa huru mpaka mnifunge hivi
kama mnyama au mnaniogopa?
“Nani akuogope mbweha kama wewe?, nimesema huu ni utaratibu wetu
wa kawaida tu ambao wewe hujauzoea” yule mtu aliniambia baada ya kuni-
shushia kichapo cha ngumi za kutosha mbavuni na tumboni na hapo nikapiga
yowe lakini hakuna aliyeonesha kunijali.
“Sikiliza Luteni sisi tunachohitaji kwako ni utii na nidhamu ya hali ya juu.
Na unafahamu nini maana ya utii kwani wewe ni mwanajeshi mwenye cheo
kikubwa jeshini”
“Mimi sijui unachozungumza”
“Utafahamu tu”
“Hivi ni kitu gani hasa mnachotaka kwangu? niliwauliza
“Tunaitaka bahasha yetu uliyoiiba kule msituni” yule mtu mwenye sura
kama anayetaka kutapika aliniambia.
“Bahasha ipi mliyonipa?
“Usitufanya sisi wajinga Luteni, tunataka bahasha yetu” yule mtu mfupi
manywele alisisitiza.
“Nyinyi ni watu wa ajabu sana mnanidai vipi kitu ambacho hamjanipa?,
sasa hizi kama siyo tabia za kishoga ni nini?
“Hivi unadhani sisi tunafanya utani basi subiri utatuelewa vizuri” yule mtu
mwenye kifua kipana kama Sokwe aliongea. Kilichofuata baada ya hapo ki-
likuwa ni kipigo ambacho sidhani kama niliwahi kukiona katika maisha yan-
gu kwani wale watu wote watatu kwa pamoja walianza kunishambulia kwa
ngumi na mateke. Niliwasihi sana waniache lakini hakuna aliyenisikia hivyo
bado kile kichapo kiliendelea hadi pale walipoona wenyewe kuwa hali yangu
ilikuwa ikielekea kuwa mbaya ndiyo wakasitisha huku wakihema ovyo kama
kuku wa kisasa na hadi kufikia pale nilikuwa nimetapakaa damu mwili mzima.
“Nenda kalete ndoo ya maji” yule mtu mwenye sura kama anayetaka kupiga
chafya alimwambia yule mtu mfupi mwenye manywele na muda mfupi baa
daye ndoo hiyo ya maji ilipoletwa nilimwagiwa mwilini.
“Mwacheni kwani bila shaka yupo tayari kutueleza mahali ilipo bahasha
yetu” yule mtu mwenye kifua kipana kama Sokwe aliwaambia wenzake.
“Mimi siijui hiyo bahasha mnayoizungumzia”
“Kwani bahasha uliyonayo wewe ni ipi? yule mtu mfupi mwenye manywele
aliniuliza.
“Sina bahasha yoyote” jibu langu likampelekea yule mtu mwenye sura kama
anayetaka kupiga chafya anitandike ngumi ya shavu na hapo nikapiga yowe
kali la maumivu halafu akanikaba shingoni kwa kiganja cha mkono wake wa
kulia huku akinisogelea karibu na kunitazama kwa macho yake makali kama
ya nyoka mwenye hasira. Nikawa nashindwa kuhema vizuri kutokakana na ile
kabari mbaya ya kiganja chake aliyonitundika na nilipoona haelekei kuniachia
na huku hali yangu inazidi kuwa mbaya nikatengeneza funda kubwa la mate
mdomoni na kumtemea usoni na hapo akaniachia na kunitandika ngumi moja
kavu puani.
Kwa kweli nilisikia maumivu makali sana lakini kwa upande mwingine nil-
ishukuru kuwa ile kabari iliondoshwa kooni mwangu na kunifanya niweze
kuhema tena vizuri.
“Ni afadhali uwape bahasha yao Luteni kwani hao watu hawana utani na
ukiendelea kuleta mzaha watakuua” yule mtu aliyeniteka toka kule chumbani
juu ya ghorofa alinionya huku akitabasamu.
“Mbona unaongea kama mwanamke malaya, unataka niwaambiaje ili
mnielewa kuwa sina hiyo bahasha mnayoisema? nilimwambia yule mtu huku
nikutweta kwa hasira
“Ngoja nikueleze Luteni, fahamu kuwa huwezi kuizuia mipango yetu labda
ukijitahidi sana unaweza kuichelewesha tu lakini hata hivyo kwa sasa nafasi
hiyo huna kwani hatima yako ndiyo leo lakini kama utaonesha ushirikiano na
sisi tunaweza kukufikiria. Tunachohitaji ni bahasha yetu uliyoiiba kule msituni
ili mipango yetu tuitimize haraka na kuichukua hii nchi kiulaini na hivyo kutoa
fursa kwa nguvu ya wengi kuifurahia nchi yao”
Maneno yale yalinishtua sana hasa pale nilipoyakumbuka na yale maneno
ya Kanali Bosco Rutaganda wakati nilipokuwa mateka kwenye yale mapango
ya Musanze kuwa walikuwa wakijipanga kufanya tukio kubwa kwenye nchi
hii, tukio ambalo litaipelekea dunia yote kuwatambua kuwa wao ni akina nani.
Hivyo nilipoyalinganisha maneno ya watu wale na yale ya Kanali Bosco Ru-
taganda nikaanza kuelewa kuwa wale watu walikuwa shirika moja na Kanali
Bosco Rutaganda na kwa kweli walikuwa wakimaanisha walichokuwa waki-
kisema ingawaje bado sikuweza kuelewa tukio hilo lingekuwa ni tukio gani.
“Najua mnajitahidi sana kunishawishi kwa kuniambia ukweli wa hali
yenyewe ulivyo lakini mimi sina hiyo bahasha mnayo ihitaji na wala sijawahi
kuiona” niliwaambia kwa msisitizo.
“Sasa humu ndani ulifuata nini? yule mtu mfupi manywele aliniuliza.
“Nilikuja kumuona rafiki yangu Marceline”
“Usituhadae kijinga Luteni, toka lini mimi nikawa na urafiki na wewe?
Marceline ilinikana haraka hata kabla sijamaliza kuongea
“Sishangai sana ukinikana mbele ya hawa waumezako kwani mimi na wewe
tuna mengi ya kuzungumza baada ya hapa”
“Ha ha ha wewe mwanaume acha ghiliba yaani unaleta mzaha hadi wakati
wa kuingizwa kwenye jeneza. Mimi na wewe tutazungumza nini wakati ume-
bakiwa na muda mfupi sana wa kuwepo hapa duniani au ndiyo unajifariji?
“Luteni usitupotezee muda wetu tuambie haraka bahasha yetu iko wapi”
“Hata mkiniua itawafaa nini wakati hiyo bahasha mnayoitafuta mimi sina”
niliwaambia huku nikiwatazama mmoja baada ya mwingine.
“Basi kama hutaki kutuambia hauna faida kwetu Luteni” yule mtu mwenye
kifua kipana kama Sokwe aliniambia na sikumsikia mtu yoyote akipingana na
kauli yake na hapo nikajua kuwa mwisho wangu ulikuwa umefika.
“Fanyeni kazi yenu” yule mtu aliyeniteka toka kule chumbani ghorofani
aliwaambia wale wenzake na muda uleule niliwaona wale wenzake wakin-
isogelea na hapo nikafumba macho na kuinamisha kichwa changu chini na
kilichofuata baada ya hapo sikukifahamu kwani mvua ya kipigo cha nguvu il-
ifuatia. Kipigo cha ngumi, mateke, makofi na kila kilichowezekana kufanyika
juu yangu katika kuhakikisha kuwa naionja joto ya jiwe. Nilipiga mayowe ku-
wasihi waniache lakini hakuna aliyenisikiliza kwani bado niliendelea kupokea
kichapo na muda ulivyozidi kwenda nikaanza kuona giza mbele yangu.
Nikajaribu kupiga mayowe tena lakini sauti yangu ilikuwa ni kama iliy-
okuwa ikipotelea masikioni kwangu. Kile kipigo kiliendelea na kwa mbali
nikaanza kuisikia ile simu ya mezani ikianza kuita tena pale sebuleni hata
hivyo sauti ile ni kama iliyokuwa ikififia masikioni mwangu kadiri muda
ulivyokuawa ukizidi kwenda. Muda mfupi baadaye sikuweza kusikia tena
chochote kilichokuwa kikiendelea eneo lile kwani macho yangu yalifumba
taratibu, mdomo wangu haukuweza tena kutamka neno lolote na hatimaye fa-
hamu zikanitoweka na hapo nikajihisi ni kama niliyekuwa nikielekea kwenye
sayari nyingine mpya.
#154
“AMEPATA HITILAFU KIDOGO KWENYE UBONGO na ni bahati nzuri
kuwa mmemuwahisha vinginevyo hakuna daktari yeyote ambaye angepoteza
muda wake kujishughulisha naye”
“Unadhani upo uwezekano wa kuinuka tena na kuendelea na maisha yake
ya kawaida?
“Hilo linawezekana hata hivyo atalazimika kutojishughulisha na kazi ngu-
mu ya aina yoyote kwa muda usiopungua miezi sita”
“Leo ni siku ya tatu, unataka kutuambia amebakiwa na siku ngapi hadi ku-
rudiwa na fahamu?
“Maendeleo yake ni mazuri huenda hadi kesho jioni akawa amerudiwa na
fahamu”
“Una hakika?
“Ni kutokana na maendeleo ya afya yake yanavyoonesha”
“Sikiliza daktari, wewe fanya ufanyavyo tunachotaka ni kumuona mtu huyu
anarudiwa na fahamu zake haraka iwezekanavyo na ikiwezekana iwe mapema
sana kabla ya huo muda unaosema”
“Nitajitahidi ingawaje upo uwezekano mkubwa kuwa anaweza akarudiwa
na fahamu mapema lakini hadi kuongea ikamchukua siku kadhaa”
“Hiyo si kazi yetu na ndiyo maana wewe ukaitwa daktari na sisi ni wanajes-
hi. Ukishindwa kazi tutamtafuta daktari mwingine na wewe tutajua ni wapi pa
kukupeleka”
“To hell...kama mnadhani mimi ni mtenda miujiza”
“Tutarudi saa moja usiku kufuatilia maendeleo yake” nilimsikia yule mtu
akiongea halafu kukafuatiwa na kitambo kidogo cha ukimya na hapo nikam-
sikia yule mtu aliyekuwa akiongea na yule daktari akisema,
“Sam, wewe unaweza kwenda kula halafu utarudi hapa kukaa na mgonjwa
wetu”
“Ondoa shaka Kapteni”
“Ninyi wengine twendeni” yule mtu aliongea
Muda mfupi uliofuata nilizisikia kelele za kishindo cha hatua za watu waki-
ondoka eneo lile halafu kukafuatiwa na kelele za mlango uliokuwa ukifungu-
liwa na kufungwa na muda mfupi uliofuata zile kelele zikawa zimetoweka na
kuiacha ile sehemu ikigubikwa na ukimya.
Yalikuwa ni maongezi yaliyokuwa yakiendelea baina ya daktari aliyekuwa
akinitibu na kikundi cha wanajeshi watano walivaa sare za kijeshi na bundu-
ki zao mikononi. Fahamu zilikuwa zimenirudia taratibu na kitu cha kwanza
kukisikia ni maongezi hayo na hali hiyo ikawa imenipa nafasi ya kutafakari
matukio yote yaliyopita nyuma yangu na hapo ndiyo nikakumbuka kuwa mara
ya mwisho nilikuwa nimekamatwa kule nyumbani kwa Marceline na wale
watu nisiyowafahamu. Halafu nikakumbuka namna nilivyohojiwa na watu
wale kabla ya kushushiwa kipigo cha nguvu na baada ya hapo sikuelewa kili-
choendelea.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa nilikuwa nimeletwa pale hospitalini kupati-
wa tiba baada ya kuzidiwa na kile kipigo. Nikiwa na hakika kuwa wale watu
walikwishaondoka katika chumba kile nilichoanza kikifananisha na wodi mo-
jawapo ya ile hospitali akili yangu sasa ilipata uhai mpya. Hasa nilipoanza
kulitafakari kwa kina jina la Sam ambalo nilikuwa nimelisikia likitajwa na
yule kamanda wa kijeshi aliyesemekana kuwa na cheo cha Kapteni. Na hapo
nikashindwa kuelewa kama Sam huyu aliyekuwa akizungumziwa angekuwa
ndiye yule niliyeambiwa habari zake na Rosine kuwa ndiye aliyekuwa rafiki
wa Jean Filex Akaga ambaye kwa namna nyingine yeye ndiye aliyekuwa aki-
husika na kupotea ama kuuwawa kwa huyo Jeukimyax Akaga na mpenzi wake
aitwaye Diane ambaye pia ni dada wa Rosine.
Kwa kweli sikuweza kupata majibu katika tafakari yangu na badala yake
niliyatembeza kwa siri macho yangu nikitazama upande huu na ule toka pale
kitandani nilipolala nikiyapeleleza mazingira ya mle ndani.
Nilikuwa sijakosea kwani kwa hakika chumba kile kilifaa kufananishwa
na wodi mojawapo ya hospitali kutokana na mandhari ya mle ndani. Mbele
ya kile kitanda nilicholazwa nilitazamana na dirisha kubwa ingawaje kupitia
dirisha hilo niliweza kufahamu kuwa muda ule ulikuwa ni jioni kwani giza
lilikuwa limeanza kuingia. Upande wa kushoto kwangu kulikuwa na kitanda
kingine kama kile nilicholazwa na nilipojaribu kuchunguza vizuri nikagundua
kuwa juu ya kitanda kile kulikuwa na mtu aliyelazwa akiwa ametundikiwa
dripu ya damu. Mtu huyo alikuwa amefunikwa kwa shuka safi na nyeupe za
hospitali ile na alikuwa amekonda sana na hata nilipozidi kumchunguza sikuo-
na dalili zozote za yeye kutikisika wala kujitambua.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Sikutaka kumchunguza zaidi mtu yule badala yake niliyatembeza taratibu
macho yangu na kuweka kituo kutazama juu ya shuka zile alizofunikwa yule
mgonjwa na hapo nikayaona maandishi makubwa meusi yaliyosomeka “Cen-
tre Hospitalier Universitaire de Kigali” nikajua kuwa pale nilikuwa kwenye
hospitali yenye jina lile iliyokuwa katikati ya jiji la Kigali hapa Rwanda.
Nilijaribu kuwaza namna nilivyofika mle ndani na hapo nikajua kuwa kwa
vyovyote wale watu walioondoka ndiyo wangekuwa wamenileta mle ndani.
Hadi kufikia hapo akili yangu ikaanza kufanya kazi na kwa muda mfupi tu
mawazo mengi yakawa yamepita kichwani mwangu.
Nilipoyakumbuka yale maongezi ya yule daktari na yule mwanajes-
hi mwenye cheo cha Kapteni ambaye wakati huu alikuwa ameondoka na
wale wenziwe kumbukumbu hiyo ikatosha kabisa kunieleza kuwa nilikuwa
nimeletwa pale kutibiwa na pindi hali yangu itakapotengamaa zoezi la kuho-
jiwa juu ya wapi nilipoipeleka ile bahasha na mambo mengine lingeendelea.
Na kwa mujibu wa maelezo ya yule daktari ni kuwa nilikuwa natarajiwa kuz-
induka kesho yake lakini sasa nilikuwa nimezinduka mapema kabla ya muda,
nilishukuru sana kwa hilo.
Niliyatembeza macho yangu kutazama ule upande wa kulia toka pale nili-
polazwa na hapo nikaiona meza kubwa ukutani na juu ya meza ile kulikuwa
na vifaa vichache vya hospitali kama chupa za dawa na mabomba kadhaa ya
sindano. Mbali na vifaa vile kulikuwa na beseni dogo la Aluminiamu, bunda
kubwa ya bendeji, pamba, chupa kubwa ya potassium parmanganate na mka-
si. Nilipozidi kuyatembeza zaidi macho yangu pembeni ya meza ile nikaona
kochi moja na meza fupi na nyuma yangu kulikuwa na kabati dogo la mbao.
Zaidi ya vitu vile hapakuwa na kitu kingine cha ziada mle ndani.
Nilikumbuka kuwa yule mtu aitwaye Sam ambaye ndiye aliyekuwa ameach-
iwa jukumu la kunilinda mle ndani alikuwa ametoka kwenda kula na hivyo
muda si mrefu angerudi. Hilo sikupenda litokee kwani endapo yule mtu anger-
udi uwezekano wa mimi kutoroka mle ndani ungekuwa mdogo sana.
Niliuinua mkono wangu wa kulia na kuanza kujipapasa kichwani taratibu
na hapo nikagundua kuwa nilikuwa nimefungwa bendeji kwa sehemu kubwa
kukizunguka kichwa changu. Nilipoifikia sehemu ya usoni nikagundua kuwa
uso wangu ulikuwa umeharibiwa vibaya kwa kile kipigo nilichoshushiwa na
wale watu kwani mdomo wangu ulikuwa umechanika sehemu ya chini na vi-
levile meno yangu mawili ya taya la chini upande wa kushoto yalikuwa yaki-
tikisika. Pua yangu ilikuwa imevimba na sehemu ya juu ya jicho langu la kulia
ilikuwa imechanika.
Japokuwa hapakuwa na kioo chochote cha kujitazama mle ndani lakini nili-
weza kuvuta picha ya kufikirika kuwa uso wangu ulikuwa umeharibika vibaya
japokuwa daktari alikuwa ametumia ufundi wake wa kila namna katika ku-
hakikisha kuwa sura yangu inafanana na ya binadamu wa kizazi hiki.
Niliuona muda ulikuwa ukikimbia sana isivyokawaida na bado sikuwa na
uhakika wa kutoroka mle ndani hata hivyo sikukata tamaa hivyo nikanyanyuka
pale kitandani taratibu na kuketi, na wakati nikifanya hivyo nilisikia maumivu
makali yakipenya mwilini mwangu. Kichwa nacho hakikuonesha utulivu hata
kidogo kutokana na kuzunguzungu kilichokuwa kimenishika lakini hata hivyo
nilijitahidi sana kuamka na hatiamaye kuketi juu ya kile kitanda. Nilipoketi
vizuri juu ya kile kitanda taratibu nikauinua mkono wangu wa kushoto ulioku-
wa umetundikiwa dripu iliyokuwa imening’inizwa pembeni ya kitanda juu ya
stendi maalumu ya chuma.
Ile dripu ilikuwa na kimiminika cha dawa fulani ambayo sikuweza kuifaha-
mu kwa haraka kwani nje ya dripu ile hapakuwa na maelezo yoyote hata hivyo
nilikuwa na hakika kuwa ile ingekuwa ni dawa.
Nikaugeuza vizuri mkono wangu na kuishika sindano ya dripu ile iliyokuwa
imechomekwa kwenye mshipa mmoja wa damu na kuzuiliwa kwa kipande
kidogo cha plasta. Sikuwa na muda wa kujishauri hivyo nikaibandua ile plasta
na kuichomoa ile sindano ya dripu lakini wakati nilipokuwa nikifanya vile
ghafla nilisikia ule mlango wa ile wodi ukifunguliwa. Mshituko niliyoupata
hata wewe msomaji unaweza kuvuta picha kuwa nilikuwaje lakini nilifanya
kile nilichokiweza. Katika nukta moja tu ya sekunde nilikwisha jifunika vizuri
lile shuka la kitandani kama nilivyoachwa hapo awali na ile sindano ya dripu
nikaichomeka kwenye godoro na kuifunika vizuri kwa shuka. Moyo wangu
ulikuwa ukienda mbio sana huku ukipiga kite kwa nguvu kama mtu aliye-
koswakoswa na ajali mbaya barabarani.
Mara baada ya ule mlango wa wodi kufunguliwa nilisikia kelele za ma-
gurudumu ya meza ya utabibu yakiteleza taratibu kuja ule upande wangu.
Nilipoyatega vizuri masikio yangu nikasikia kelele nyingine za viatu vyenye
visigino vya ncha kali vikiyasindikiza magurudumu yale taratibu. Ni hadi pale
mtu yule aliyeingia mle wodini alipofika pembeni ya kile kitanda changu na
hatimaye kukipita akienda kule kulipokuwa na kile kitanda kingine cha yule
mtu aliyelazwa mle ndani ndiyo hapo nikapata nafasi ya kumuona vizuri mtu
yule aliyeingia mle ndani. Alikuwa mwanamke wa kizungu aliyevalia mavazi
ya kidaktari na kifaa maalumu cha kupimia mwenendo wa mapigo ya moyo
ya mgonjwa kilichokuwa kimening’inia shingoni mwake. Mwanamke yule
mzungu alikuwa akikisukuma kitanda cha mgonjwa na juu ya kitanda kile
kulikuwa na mtu fulani aliyelala na kufunikwa shuka za hospitali ile.
__________
NILIPATA NAFASI NZURI YA KUMCHUNGUZA MTU YULE aliyeku-
wa juu ya kile kitanda kwani yule daktari mwanamke wa kizungu alikuwa
amesitisha kukisukuma kile kitanda wakati kilipofika pembeni yangu huku
akitembea taratibu kuelekea kwenye kile kitanda cha yule mgonjwa mwingine
mle ndani.
Nikiwa bado nimetulia pale kitandani niliendelea kujitahidi kwa kila hali
kuhakikisha kuwa sifanyi tukio lolote litakalompelekea daktari yule afahamu
kuwa nilikuwa nimeisharudiwa na fahamu zangu. Hata hivyo moyoni nilim-
uomba Mungu kuwa yule mtu aliyefahamika kama Sam apate dharura huko
alipokuwa na asirudi haraka mle ndani kwani endapo angewahi kurudi ninge-
hitaji miujiza ya hali ya juu kutoroka mle ndani. Hivyo akili yangu ikaanza
kufanya kazi haraka isivyokawaida.
Kwa kificho cha hali ya juu nililisogeza kidogo lile shuka nililojifunika
pembeni na hapo nikapata upenyo mdogo wa kutembeza macho juu ya kile
kitanda cha magurudumu alichoingia nacho yule daktari mwanamke wa kizu-
ngu ambacho sasa kilikuwa umbali mfupi pembeni yangu. Juu ya kitanda kile
niliweza kuliona umbo la mtu mwenye urefu kama wangu likiwa limefunikwa
kwa shuka za hospitali ile toka kichwani hadi miguuni.
Niliendelea kumchunguza mtu yule ingawaje sikuwa na hakika sana lakini
kwa muonekano wa umbo lake tu lililofichika chini ya shuka zile nilikuwa na
kila hakika kuwa mtu yule alikuwa mwanaume na katika sehemu ya kati ya
tumbo lake kulikuwa na doa kubwa la damu. Hali hiyo ikanipa mashaka kuwa
mtu yule huenda alikuwa tayari amekata roho muda mfupi uliyopita kutokana
na lile jeraha la tumboni kwani yule daktari hakuonekana kumjali.
Niliendelea kumchunguza yule mtu kwa kificho toka pale kitandani nilipo-
lala na kwa muda mfupi uliyofuata nilianza kushikwa na mshituko pale nili-
poisoma kadi maalumu ya mgonjwa iliyokuwa imetundikwa kwenye pembe
ya kitanda kile alicholazwa yule mtu. Maelezo ya kwenye kadi ile iliyoku-
wa pembeni ya kile kitanda yalieleza kuwa jina la yule mtu aliitwa Caprian
Ndikumana, kiongozi wa kijeshi mwenye cheo cha Meja katika jeshi la RPF
yaani Rwandese Patriotic Front. Chini ya maelezo hayo kulikuwa na maelezo
mengine yaliyoeleza saa, tarehe, siku, mwezi na mwaka aliyofariki mtu yule.
Ambapo kupitia maelezo yale niligundua kuwa mtu yule juu ya kile kitanda
alikuwa amefariki muda mfupi uliyopita.
Mshtuko uliyoipata akili yangu ulitokana na kumbukumbu sahihi nilizoku-
wanazo kichwani juu ya mtu yule. Fikra zangu zilikuwa zimerudi nyuma ku-
kumbuka wakati nilipokuwa nikiyatoroka yale mapango ya Musanze na hapo
nikalikumbuka jina la mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa jina
la Madame Maria Grace, mfanyakazi katika benki ya taifa ya Rwanda.
Muda mfupi kabla ya kifo chake kwa mujibu wa maelezo niliyoyapata ku-
toka kwa mwanamke huyo ni kwamba, mume wake alikuwa ni afisa wa ngazi
ya juu katika jeshi la RPF na alikuwa miongoni mwa watu hatari waliokuwa
wakitafutwa na jeshi la Kanali Bosco Rutaganda ili wauwawe. Na kutopa-
tikana kwake ndiyo ilikuwa sababu ya mkewe yaani Madame Maria Grace
kutekwa na kupelekwa katika mpango yale akilazimishwa azungumze ni wapi
alipokuwa mumewe.
Muda mfupi kabla ya kifo chake mwanamke huyo pia alikuwa amenieleza
kuwa alikuwa na mwanae pekee, binti ajulikanaye kwa jina la Daine aliyeku-
wa akisoma katika shule ya wasichana Sainte Anne Marie iliyopo jijini Ki-
gali. Vilevile alikuwa amenisisitiza kuwa endapo ningefanikiwa kuyatoroka
mapango yale salama alinitaka niende nikamchukue binti yake katika shule
hiyo na kurudi naye nchini Tanzania akiwa chini ya malezi na uangalizi wan-
gu.
Nilindelea kuyakumbuka maelezo ya mwanamke yule kuwa familia yake
ilikuwa ikiishi katika eneo moja la jiji la Kigali lijulikanalo kama Masaka Av-
enue, nyumba namba 16 na kuwa alikuwa na pesa nyingi katika akaunti yake.
Akinitaka niichukue pesa hiyo na niitumie kumlea na kumsomeshea mwanae
pindi nitakapofanikiwa kuvuka mpaka salama na kurudi nchini kwangu Tan-
zania.
Roho iliniuma sana, nikafumba macho kwa sekunde na kumeza funda kub-
wa la mate kuitowesha hasira iliyokuwa kifuani kwangu. Kwa kweli nilim-
hurumia sana Diane kwa kupoteza baba na mama yake ingawaje huyo Diane
hadi wakati huu nilikuwa simfahamu. Baada ya kifo cha Madame Maria Grace
kule pangoni nilikuwa nimeiweka ahadi moyoni kuwa ningefanya jitihada
zangu zote kuhakikisha kuwa namkutanisha Meja Caprian Ndikumana na
mwanae Diane na kumueleza yote yaliyomtokea Madame Maria Grace kule
mapangoni kabla ya kurudi Tanzania. Kwani sikuona kama lingekuwa jambo
la busara kumchukua binti huyo na kumlea wakati baba yake bado alikuwa
yupo hai. Lakini kwa sasa ndoto hiyo ilikuwa imeyeyuka haraka kama barafu
kwenye jua kali la jangwani kwani Meja Ciprian Ndikumana sasa alikuwa
marehemu juu ya kitanda kile cha jirani yangu.
Niliwaza kuwa bila ya shaka Meja Ciprian Ndikumana alikuwa amekamat-
wa na wale wanajeshi wa Kanali Bosco Rutaganda na kuuwawa pengine al-
ipokuwa katika harakati za kuitafuta familia yake. Moyo wangu ulijawa na
simanzi sana kila nilipokuwa nikimkumbuka Madame Maria Grace na hali
hiyo ikanipa roho mpya, roho ya chuma yenye ujasiri wa kuendeleza mapam-
bano bila kikomo mpaka pale ushindi utakapopatikana.
Niligeuka kutazama upande ule wenye kile kitanda alicholazwa yule mgon-
jwa mwingine na hapo nikamuona yule daktari mwanamke wa kizungu aki-
andika maelezo fulani kwenye kadi fulani aliyoishika mkononi sawa na ile
niliyoiona ikiwa imening’inizwa kwenye kile kitanda cha Meja Ciprian Nd-
ikumana. Alipomaliza kuandika alichokuwa akikiandika nilimuona daktari
yule akiining’iniza ile fomu pembeni ya kitanda cha yule mgonjwa kisha kama
anayetaka kujiridhisha na hali ya yule mgonjwa alimfunua yule mgonjwa lile
shuka alilofunikwa toka kichwani hadi kifuani kisha akaweka kituo akimta-
zama yule mgonjwa na kulikuwa na kila dalili za simanzi katika uso wake.
Baadaye nilimuona yule daktari akilishika tena lile shuka na kumfunika yule
mtu pale kitandani lakini kwa namna alivyomfunika yule mtu toka kichwani
hadi miguuni nikajua tu yule mtu alikwisha kata roho.
Yule daktari alirudi nyuma kidogo kisha akapiga ishara ya msalaba na muda
ule ule nilimuona akitoa kitambaa cha leso toka katika mfuko wa koti lake na
kuwahi kuyapangusa machozi yaliyokuwa mbioni kuyazingira macho yake
halafu akaanza kuzitupa hatua zake taratibu kuja ule upande wangu. Kabla ha-
jafanikiwa kunifikia nilikuwa tayari nimekwishajitengeza katika ile hali yangu
ya awali yaani hali ya mgonjwa aliyepoteza fahamu.
Yule daktari alipofika alisimama kando ya kitanda changu na kunitazama
kisha aliitazama ile chupa ya dripu iliyokuwa imetundikwa kwenye stendi
maalumu pembeni ya kitanda changu. Baadaye nilimuona yule daktari aki-
kisukuma kidogo kile kigurudumu cha dripu ili kuongeza kasi ya ile dawa
kuingia mwilini.
Moyo ulinienda mbio pale nilipowaza kuwa pengine yule daktari aliku-
wa akitaka kunifunua na kuutazama ule mkono niliyotundikiwa dripu lakini
nilishukuru kuwa hilo halikutokea kwani alipomaliza alinishika pembeni ya
shingo yangu na hapo nikajua kuwa alitaka kuhakikisha mzunguko wa damu
mwilini mwangu. Alipomaliza nilimuona akiondoka kwa haraka kuufuata ule
uelekeo wa mlango wa ile wodi na wakati akitembea kwa haraka vile visigino
vyenye ncha kali vya viatu vyake vilitoa mlio mkali sakafuni sambamba na
hatua zake. Muda mfupi uliyofuata nilisikia ule mlango ukifunguliwa na ku-
fungwa kisha kukafuatiwa na ukimya.
Nilitabasamu kidogo na sikutaka kupoteza muda kwani ni kama niliyehisi
kuwa nilikuwa nikimuona yule mtu aitwaye Sam akiwa amesimama nje ya ule
mlango wa kuingilia mle ndani. Nikiwa ni kama mtu aliyekufa na kufufuka
baada ya miaka mingi huku nikisikitishwa kwa kupitwa na mambo mengi,
akili yangu sasa ilianza kufanya kazi haraka kuhakikisha kuwa muda wote
niliyoupoteza naufidia haraka iwezekanavyo kabla ya yule mtu aitwaye Sam
na yule daktari wa kizungu hawajarudi huko walipokwenda.
Kwa haraka nilinyanyuka pale kitandani nilipolala kisha nikaziweka zile
shuka nilizofunikwa pembeni na hapo niliyasikia tena yale maumivu makali
yakipitia mwilini mwangu. Nikapambana na hali ile kwa kuuma meno kisha
nikaishusha miguu yangu sakafuni na kusimama. Kichwa changu kilikubwa
bado kina mawengemawenge lakini baada ya muda mfupi niliizoea hali ile
hivyo nikakisogelea kile kitanda jirani yangu kilichokuwa kimeubeba mwili
wa Meja Caprian Ndikumana. Nikimfunua shuka na kuziweka pembeni na
hapo nikapata nafasi ya kumuona vizuri.
Umri wake ulikuwa kati ya miaka arobaini na sita hadi hamsini, mwenye
urefu kama wangu na sura ya kuvutia lakini yenye kuhifadhi mambo mengi
na misukosuko ya kila namna. Shingoni alikuwa amevaa mkufu wenye kidani
cha dhahabu kilicho chongwa katika mtindo unaovutia wenye herufi mbili zin-
azosomeka MG, nikajua herufi zile mbili zilimaanisha jina la mkewe yaani
Maria Grace.
Nilikishika kidani kile nikakivuta kwa nguvu na kukikata kisha nikakitia
kwenye mfuko wa suruali yangu. Niliweka kituo nikiutazama mwili wa Meja
Ciprian Ndikumana kwa makini kama ninayeinakili vizuri taswira yake katika
ubongo wangu, taswira ya mtu aliyekufa akiwa ndani ya mavazi ya kijeshi
ambaye sikuwa na hakika ya kuonana naye tena mbele ya safari yangu.
Alikuwa mwanajeshi kwa kila idara mwenye kifua kilichojengeka vizuri,
mikono yenye misuli imara na makovu mawili ya risasi, kovu moja kwenye
kiganja chake cha mkono wa kulia na jingine pembeni ya shingo yake. Uzito
wake ulikuwa si zaidi ya kilo themanini na tano na tumboni alikuwa na jeraha
kubwa, jeraha ambalo huenda lilitokana na kisu kisichokuwa na makali kili-
chomchoma mara kadhaa, muuaji akirudia rudia kufanya hivyo hadi pale
alipokata roho.
Nilimbeba Meja Ciprian Ndikumana na kumhamishia kwenye kile kitanda
changu kisha nikamchomeka ile dripu mkononi mwake bila kujighushulisha
kutafuta mshipa wowote kwani tayari alikuwa mfu. Nilipomaliza nikamten-
geneza tengeneza na kumfunika vizuri kwa zile shuka huku nikiwa na hakika
kuwa angeendelea kufanana na mimi mpaka hapo ambapo wangemshtukia
wakati huo mimi nikiwa mbali na eneo lile.
Nilipomaliza kwa haraka nikapanda na kijilaza kwenye kile kitanda chake
kisha nikajifunika zile shuka ambazo hapo awali zilikuwa zimeufunika mwili
wake. Zile shuka zilikuwa na harafu kali ya damu hata hivyo sikuwa na njia
mbadala.
Wakati nikimalizia kujiweka sawa muda uleule nilisikia ule mlango wa
wodi ukifunguliwa na hapo nikasikia vishindo sakafuni kabla ya mlango ule
kufungwa. Sauti ya mgongano wa sakafu na viatu ukanitanabaisha kuwa dak-
tari yule mama wa kizungu alikuwa ameingia mle ndani na mwenzake. Wali-
tembea wakanipita wakielekea kwenye kile kitanda kingine alicholazwa yule
mtu ambaye sasa nilikuwa na hakika kuwa ni marehemu.
Walipokifikia kitanda kile nikasikia maongezi ya hapa na pale katika
lugha ya kifaransa, maongezi hayo muda mfupi baadaye yalikatishwa na mtu
mwingine aliyefungua mlango na kuingia mle ndani. Tukio hilo likaupelekea
moyo wangu kupoteza utulivu na ghafla nikawa nasikia kiu kali sana kinywani
huku mate mdomoni yakinikauka kwani nilihisi kuwa yule mtu aliyeingia mle
ndani angekuwa ni yule Sam.
Nikajiridhisha zaidi kuwa mtu yule aliyeingia mle ndani alikuwa ni yule
Sam baada ya kusikia sauti kavu ya soli za viatu vyake zikiisulubu sakafu ya
mle ndani. Alipoingia mle ndani akaufunga ule mlango kwa nyuma. Nikaji-
weka tayari kukabiliana naye pale amabapo angeamua kuleta rabsha. Hatua
za mtu yule aliyeingia ziliishia kati ya kile kitanda nilichomlaza Meja Ciprian
Ndikumana na hiki nilicholala mimi na hapo mapigo ya moyo wangu yakazidi
kuvurugika. Hata hivyo nilijitahidi sana kujifanya mfu pale kitandani lakini
wakati huohuo nikitamani kumuona yule mtu aliyeingia mle ndani. Kwa kwe-
li moyo wangu ulikuwa ukienda mbio isivyokawaida huku nikihofia kutokea
kwa lolote mle ndani.
Yule mtu aliyeingia mle ndani aliposimama kati ya kitanda changu na kile
kitanda nilichoulaza mwili wa Meja Ciprian Ndikumana kukafuatiwa na ki-
tambo kifupi cha ukimya na wakati huo nilijihisi ni kama niliyekaribiwa na
shetani. Japokuwa nilikuwa nimejifunika mwili mzima lakini niliweza kuihisi
hofu waliyokuwa nayo wale madaktari mle ndani.
“Que faitez vous ici à l’interieur? yule mtu aliwauliza wale madaktari kwa
lugha ya kifaransa akiwauliza “Mnafanya nini humu ndani? na sauti yake ili-
kuwa kavu na isiyokuwa na chembe yoyote ya mzaha.
“Il est mort, nous voulons que tu le transportes au morgue” mmoja wa
wale madaktari wawili alimjibu kwa woga “Amekufa tunafanya utaratibu wa
kumpeleka mochwari”
“Leisse ce travail à ton collegue, enleve ce cadavre jusqu’ à la morgue”
yule mtu aliwaambia wale madaktari akimaanisha “Hiyo kazi mwachie mwan-
zako wewe ondoa huu mzoga peleka mochwari”
“Garder un cadavre c’est un travail de communauté mon capitain”“Kuuhi-
fadhi mwili ni kazi ya ushirikiano afande” nilimsikia daktari mmoja akijibu.
“Faites ce que j’ai dis” “Fuata nilichokisema” yule mtu alifoka.
“Daccord” daktari mmoja alijibu kwa woga akimaanisha “Sawa”
Muda mfupi uliyofuata nikaanza kuhisi kile kitanda changu kikianza kusu-
kumwa taratibu huku zile kelele za magurudumu ya kitanda zikisindikizwa
na sauti kali ya mgongano wa sakafu na vile visigino vya viatu nyenye ncha
kali na hapo nikajua kuwa yule daktari alikuwa akikisukuma kitanda changu
kunipeleka mochwari huku akiamini kuwa mimi nilikuwa ndiyo ule mwili wa
Meja Ciprian Ndikumana.
Chini ya shuka zile nilizojifunika tabasamu hafifu liliuvamia uso wangu
huku nikijipongeza tena kuwa kwa mara nyingine nilikuwa nimefanikiwa
kuwazidi ujanja watu wale hatari. Haukupita muda mrefu tangu kuanza kwa
safari yetu hadi pale niliposikia kelele za ule mlango wa ile wodi ukifunguliwa
kisha kile kitanda kikasukumwa kidogo na kusimama halafu nyuma yangu
nikausikia ule mlango ikifungwa na hapo safari ilianza tena.
Ingawaje nilikuwa nimejifunika kwa zile shuka lakini nilihisi kuwa tuliku-
wa tukisafiri kwenye mojawapo ya korido za hospitali ile na wakati tukisafiri
mara kwa mara nilimsikia yule daktari aliyekuwa akikisukuma kitanda changu
akisalimia na madaktari wenzake waliokuwa wakipishana naye. Ni katika
salimiana hiyo ndiyo nilipolisikia jina la Dr. Lisa likitajwa na muda uleule
akili yangu ikaanza kufanya kazi nilipoyakumbuka maneno ya yule mzee wa
kifaransa François Trezor niliyekutana naye kule pangoni muda mfupi kabla
ya kumuona akitandikwa risasi za kichwa na wale askari wa Kanali Bosco
Rutaganda mbele ya macho yangu.
Niliyakumbuka maneno ya François Trezor kuwa endepo ningefanikiwa
kutoroka kule pangoni alinitaka nikamtafute Dr. Lisa Olivier ambaye aliku-
wa akifanya kazi kama daktari wa kujitolea au daktari asiyekuwa na mipaka
kutoka nchini ufaransa katika hospitali hii yaCentre Hospitalier Universitaire
de Kigali.
Kwa mujibu wa maelezo ya Dr. François Trezor ni kwamba mara baada
ya kuonana na Dr. Lisa ni yeye amabaye angenielekeza ni wapi ningempata
Jaji Makesa na baada ya hapo maswali yangu mengine yangeendelea kujijibu.
Ingawaje sikuweza kufahamu haraka kuwa kulikuwa na uhusiano gani kati
ya Jaji Makesa na Dr. Lisa lakini bado niliyaamini maneno yale ya François
Trezor huku nikijiuliza aliyafahamu vipi hayo yote.
Tulifika sehemu nikahisi kile kitanda nilichobebwa kilikuwa kikibadilisha
uelekeo na kushika uelekeo mwingine wa upande wa kushoto. Kwa umbali
mrefu tuliokuwa tumesafiri huku nikisukumwa juu ya kitanda kile ulinifanya
nihisi kuwa ile hospitali ilikuwa kubwa sana na yenye uwezo wa kupokea
wagonjwa wengi.
Tulipita sehemu moja nikasikia kulele za watoto wachanga wakilia nikahisi
tulikuwa karibu na wodi ya watoto baadaye kelele hizo zilitoweka na kwa
mbali nilianza kuyasikia makelele ya jenereta la hospitali ile likiunguruma na
hapo nikaanza kuhisi kuwa tulikuwa tukikaribia eneo la mochwari.
Moyo wangu ulianza tena kwenda mbio kwa hofu na kupungua kwa mwen-
do wa kile kitanda cha magurudumu nilichobebwanacho nikisukumwa iliku-
wa ishara tosha kuwa safari yetu ilikuwa ikielekea kufika ukingoni. Na siku-
weza kufahamu kuwa ingemchukua muda gani yule mtu aitwaye Sam hadi
kushtukia kuwa yule mtu aliyekuwa akimlinda kule wodini hakuwa mimi bali
maiti ya Meja Ciprian Ndikumana. Fikra hizo zikiwa zimeanza kunitawala
na kunijaza hofu moyoni na hapo nikaanza kuhisi kuwa muda ulikuwa mfupi
sana kuitekeleza mipango yangu na kama ningeendelea kujifanya mfu ju ya
kile kitanda basi muda si mrefu mambo yangeharibika.
Tulifika mahali tukasimama na hapo nikajua kuwa tulikuwa tumefika
mochwari hivyo taratibu nililisogeza lile shuka nililojifunika na kutazama
mbele yangu na hapo nikauona mlango mpana wa mbao. Juu ya mlango ule
kulikuwa na na kibao kidogo kilichoandikwa kwa maandishi meupe juu yake
neno la kifaransa Morgue lenye maana ya Mochwari.
Nilimuona yule daktari akikiacha kile kitanda na kuusogelea ule mlango na
hapo nikajua kuwa alikuwa akitaka kubonyeza kitufe chekundu cha kengele
kilichokuwa pembeni ya mlango ule. Sikutaka kupoteza muda kwani nili-
jua endapo angefanikiwa kubonyeza kitufe kile ule mlango ungefunguliwa na
hapo ningekutana na upinzani ambao sikuwa tayari kukabiliana nao hivyo bila
kuchelewa nililitupa lile shuka pembeni na kushuka kitandani.
Yule daktari aligeuka nyuma na kukitazama kile kitanda na hapo nilimuo-
na namna alivyoshikwa na mashituko wa hofu usioelezeka. Macho yalimto-
ka pima kama binadamu aliyeona kiumbe cha ajabu kabisa kuwahi kutokea
duniani. Nilimuona akihamaki sana huku akianza kutetemeka mwili mzima
kwa hofu na kwa muda mfupi tu daktari yule wa kizungu akawa ameshabadi-
lika rangi na kuwa kama papai bivu. Nilimuona akianza kurudi nyuma tarat-
ibu nikajua alikuwa akijiandaa kutimua mbio. Nilikuwa nimeifahamu haraka
dhamira yake na sikutaka kumlaumu kwani kwa mtu yoyote kama yeye an-
geweza kunidhania kuwa mimi nilikuwa mzimu.
Kilichonifurahisha zaidi ni kile kitambulisho chake cha kidaktari kilichoku-
wa kimening’inizwa kwenye sehemu ya kifuani ya koti lake upande wa kush-
oto kikiwa kimeandikwa Dr. Lisa Olivier Docteur Volontaire yaani mtu sahihi
niliyepaswa kumtafuta mara baada ya kutoroka kule mapangoni. Nilijisemea
moyoni na bila kupoteza muda niliruka toka pale kitandani na kumshika mko-
no daktari yule. Akajitahidi kufurukuta bila mafanikio kwani mikono yangu
ilikuwa imara zaidi kumzuia.
Alitaka kupiga yowe lakini nilimuwahi kumziba mdomo asipige kelele kwa
kiganja changu huku nikimsihi asiogope, nikimwambia kuwa mimi sikuwa
mfu isipokuwa nilikuwa nimefanya ujanja wa kujibadilisha kwa kuhamia
kwenye kitanda kile na ile maiti ya Meja Ciprian Ndikumana nilikuwa ni-
meihamishia kwenye kile kitanda changu kwani nilijua kuwa kwa vyovyote
wangeupeleka ule mwili wa Meja Ciprian Ndikumana kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti na hivyo nilikuwa nikitaka kuitumia nafasi hiyo kutoroka.
Nilimwambia daktari yule kwa lugha ya kifaransa cha kubabaisha na hapo
nikamuona akitingisha kichwa chake kuonesha kukubaliana na maelezo yangu
ingawaje hofu bado haikuiacha sura yake.
Wakati nikiendelea kumsihi kuwa asiwe na hofu na mimi mara nilisikia
hatua za mtu anayekimbia akija ule upande wetu na hapo nikajua kuwa mam-
bo yalikwisha haribika hivyo nikawahi kumshika mkono Dr. Lisa na kuan-
za kutimua mbio tukielekea nyuma ya jengo lile sehemu iliyokuwa na giza.
Mwanzoni Dr. Lisa alionesha kusita lakini alipoona yule mtu nyuma yetu ali-
kuwa mbioni kutokezea kwenye ile korido akabidi alegeze msimamo wake
taratibu na kuanza kunifuata na muda mfupi baadaye mwendo wetu ukawa na
uwiano sawa sote tukikimbia.
Tulipofika nyuma ya jengo lile la mochwari nikagundua kuwa hapakuwa
na taa yoyote iliyokuwa ikimulika eneo lile na kulikuwa na miti mingi iliy
otengeneza maskani ya giza zito. Nililichunguza eneo lile vizuri na kugun-
dua kuwa mazingira yale yalikuwa mageni sana kwangu na wakati nikifikiria
kuwa tushike uelekeo upi nilisikia kile kishindo cha yule mtu aliyekuwa aki-
kimbia nyuma yetu kuwa sasa kilikuwa kimetukaribia. Bila ya kusubiri nilim-
shika tena mkono Dr. Lisa na kumvutia kwenye pipa moja la taka lilikokuwa
jirani na eneo lile tukajibanza na muda ule ule nikauoma yule mtu aliyekuwa
akikimbia kuja ule usawa wetu akitokezea eneo lile na bastola yake mkononi
na hapo nikapata nafasi ya kumchunguza vizuri yule mtu.
Kama walivyo wanyarwanda wengi mtu yule alikuwa mrefu wa kimo an-
ayekaribiana na mimi hata hivyo alikuwa na mwili iliojengeka vizuri kim-
azoezi. Ingawaje alikuwa gizani lakini aligundua kuwa alikuwa miongoni
mwa wanaume wenye ushawishi mzuri katika macho ya wanawake. Alikuwa
amenyoa upara pia alikuwa amevaa suti nadhifu sana. Alifika eneo lile na
kusimama pembeni ya lile pipa la taka tulilojificha kisha akawa akitazama
tazama eneo lile na hapo nikajua alikuwa akitutafuta. Sasa nilikuwa na hakika
kuwa mtu yule ndiye yule aliyekuwa aliyefahamika kwa jina la Sam, aliyeku-
wa akinilinda kule wodini.
Kilipita kitambo cha muda yule mtu akiendelea kutazamatazama huku na
kule baadaye nilimuona akijishika kiunoni kama mtu aliyekata tamaa kisha
akageuka alipotoka na kuanza kutimua mbio kurudi kule alipotoka. Tukiwa
bado tumejibanza nyuma ya lile pipa niligeuka taratibu kumtazama Dr. Lisa
kisha nikatabasamu kidogo ingawaje yeye alionekana kama mtu aliyechang-
anyikiwa kwa namna mambo yalivyokuwa yakimtokea. Muda ule ule nikam-
shika mkono na kumtaka tuondoke eneo lile hata hivyo tofauti na matarajio
yangu Dr. Lisa alikataa.
“Niache” alifoka kwa lugha ya kifaransa
“Haupo salama dokta!” nilimwambia
“Usijali wewe nenda na usisumbuke kuhusu mimi”
“Usiwe mkaidi dokta hebu jaribu kuniamini, ukibaki hapa muda si mrefu
watakukamata na kukuua”
“Nimesema naomba uniache na wala sihitaji msaada wako” Dr. Lisa alifoka
na kuutoa mkono wake kwa nguvu na hapo nikajua kuwa alikuwa akimaanisha
alichokuwa akikisema, nikamtazama katika namna ya kukata tamaa.
“Wewe nenda sihitaji msaada wako” akasisitiza tena na hapo nikamsogelea.
“Bado hujafahamu kuwa uamuzi unaoufanya ni hatari sana dokta na wakati
atakapokuja kushtuka utakuwa umechelewa, huenda ungekubaliana na mimi
haraka endapo ungekuwa unafahamu yalimtokea mwenzako Dr. François
Tresor” nilimwambia huku nikiwa nimeanza kushikwa na hasira na wakati
nikimaliza kuongea nilimuona namna alivyotaharuki.
“Tafadhali niambie yuko wapi na umemfahamu vipi”
“Hapa si mahala pake” nilimnong’oneza huku nikiwa na hakika kuwa ma-
neno yangu yalikuwa yamebeba uzito na ushawishi wa kuaminika.
“Kwa heri” hatimaye nilimuaga na pasipo kupoteza muda nikaanza kuambaa
ambaa na ukuta wa eneo lile jirani hata hivyo sikufika mbali pale nilipouhisi
mkono laini wa kike ukinishika begani. Nilipogeuka nyuma nikamuona Dr.
Lisa
“Usiniache” alinong’ona
Tulimaliza kuambaa na ukuta ule na mwisho kulikuwa na kona. Tulipofika
hapo nilimuonesha ishara Dr. Lisa kuwa asimame na mimi nikaitumia nafasi
hiyo kulichunguza eneo lile. Wakati nikifanya hivyo nikagundua kuwa kuliku-
wa na mtu mmoja aliyekuwa akija upande ule na mtu huyo mkononi alikuwa
ameshika bastola. Nikamtahadharisha Dr. Lisa kuwa aendelee kujibanza nyu-
ma yangu huku nikifikiria mbinu za haraka za kumkabili yule mtu, haukupita
muda mrefu yule mtu akawa ameifikia ile kona tuliyojibanza na sikutaka kum-
chelewesha. Kwa kasi ya ajabu nilimtupia yule mtu pigo moja shingoni na
hapo akapiga yowe hata hivyo niliwahi kumtuliza kwa pigo jingine la tumboni
na hapo ile bastola aliyoishika ikamponyoka kisha akapepesuka na kuanguka
chini. Alijitahidi kunyanyuka lakini nilikuwa mwepesi kumfikia nikamrukia
na kumkaba koo na hapo akafurukuta kidogo na kutulia, habari yake ikawa
imeisha.
Mwanzoni nilidhani kuwa huenda yule mtu angekuwa ni yule aliyefahami-
ka kwa jina la Sam lakini nilipomchunguza nikagundua hakuwa Sam na hali
hiyo ikanitahadharisha kuwa lile eneo lilikuwa tayari limezungukwa na wale
watu hatari niliyowahisi kuwa huenda wangekuwa wafuasi wa Kanali Bos-
co Rutaganda. Nilipohakikisha kuwa yule mtu asingeweza kuamka tena pale
chini nikaiokota ile bastola yake kisha nikageuka nyuma kumtazama Dr. Lisa
na hapo nikamwona namna alivyoshikwa na woga. Pasipo kupoteza muda
nikamshika mkono na kuanza kuelekea gizani.
“Tunaenda wapi? akaniuliza kwa woga kama anayeongea na mzimu
“Tunatakiwa kutoka nje ya hospitali hii haraka iwezekanavyo kabla hawa-
jatufikia”
“Huku hakuna njia”
“Njia ipo wapi?
“Eneo hili lote limezungukwa na uzio na kama hupendi tupitie kwenye geti
la mbele la hospitali ipo njia moja ya kificho. Njia hiyo hutumiwa na wafanya-
kazi wa hospitali hii pindi wanapochelewa kazini asubuhi”
Nilitabasamu kidogo kisha nikamuuliza tena kwa kifaransa changu cha ku-
kata na shoka
“Ipo wapi hiyo njia?
Muda uleule nilimuona Dr. Lisa akianza kuongoza mbele na kunipitisha
kwenye eneo lile lenye miti yenye giza zito. Tulipoanza tu safari yetu nilim-
shauri alivue lile koti lake jeupe la kidaktari kwani lingeweza kutufichua hara-
ka mbele ya macho ya adui zetu kwa ile rangi yake nyeupe.
Tulikatisha katikati ya miti ile tukatokezea kwenye jengo la choo cha hos-
pitali ile na hapo tukaambaa na ukuta wa nyuma wa jengo lile hadi tulipolif-
ikia jengo la jiko la hospitali ile. Tulipofika hapo tukasimama kidogo baada
ya kusikia minong’ono fulani. Dr. Lisa akaniambia kuwa nisihofu kwani mi-
nong’ono ile yalikuwa ni maongezi ya wapishi wa hospitali ile waliokuwa
ndani ya lile jengo. Hivyo kwa tahadhari tukaendelea na safari yetu huku
tukiinama inama kukwepa mwanga wa taaa za eneo lile na hapo tukapenya na
kuendelea na safari.
Tulipokuwa tumefika kwenye jengo la mwisho kabla ya kuufikia uzio wa ile
hospitali ghafla niliona tukimulikwa na kurunzi yenye mwanga mkali. Liliku-
wa tukio la kushtukiza sana na hapo nikapiga yowe kumtahadharisha Dr. Lisa
kuwa alale chini lakini nilikuwa nimechelewa kwani muda ule ule nilisikia
mlio wa risasi kisha nikamuona Dr. Lisa akisombwa na kutupwa hewani huku
akipiga mayowe kwa hofu. Nikawahi kumfikia kwa wepesi wa ajabu na ali-
porudi chini akatua begani kwangu huku akiwa ametapakaa damu hata hivyo
sikumwachia na nilikuwa nimepandwa na hasira za mzuka usio na kifani.
Nikaikamata vizuri ile bastola niliyoichukuwa kwa yule mtu kisha nikageuka
haraka na kufyatua risasi kuelekea usawa wa ule mwanga wa tochi ulipokuwa
ukitokea.
Lilikuwa shambulio zuri sana miongoni mwa mashambulizi niliyowahi
kuyafanya kwani muda ule ule nilisikia sauti kali ya mtu akipiga yowe kisha
nikaiona ile kurunzi ikiruka hewani na kisha kuanguka chini. Risasi nyingine
niliyoifyatua ikaitawanya kabisa ile kurunzi na kulipekea eneo lile lote kut-
awaliwa na giza na bila kupoteza muda nikaanza kutimua mbio huku Dr. Lisa
akiwa begani mwangu, nikielekea kwenye uzio wa seng’enge wa hospitali
ile. Na wakati nikitimua mbio nyuma yangu nilisikia sauti ya vishindo vya
mbwa wikinikaribia hata hivyo sikusimama na nilipoufikia ule uzio nikaanza
kuukwea ule uzio kwa kuuparamia kwa mikono yangu huku zile seng’enge
zikinichana chana mikononi. Hata hivyo sikuhisi chochote na badala yake nili-
jiona ni kama niliyekuwa nikibembea kwenye kamba laini ya katani na kwa
muda mfupi nikawa nimefanikiwa kushuka upande wa pili wa uzio ule. Dr
Lisa aliendelea kulalamika juu ya maumivu ya bega lake hata hivyo sikuwa na
la kufanya kwani nilichohitaji haraka ilikuwa ni kutoweka eneo lile.
Nje ya uzio ule nilianza kutimua mbio tena huku nikihisi kuwa muda ule
huenda ingekuwa kati ya saa mbili na saa tatu usiku na njiani nilipishana na
watembea kwa miguu wengi waliyonipisha na kunishangaa hata hivyo hali
hiyo haikuwa na athari zozote kwangu kwani bado niliendelea kutimu mbio.
Niliupita uzio wa hospitali ile kisha mbele kidogo nilivuka barabara na waka-
ti nikifanya hivyo niligeuka kutazama nyuma na kiasi cha umbali wa kama
mita hamsini niliwaona watu wawili wakitimua mbio kunifukuza. Mtu mmoja
nilimtambua haraka kuwa alikuwa ni yule mtu aliyefahamika kwa jina la Sam
kutokana na mavazi yake na yule mtu mwingine alinichukua muda kumtam-
bua kuwa alikuwa ni yule mwenyeji wetu kule msituni ambaye hadi wakati
huu nilimfahamu kwa jina la Bolos.
Kuwaona watu wale wakinifukuza nilianza kutabiri hatari ambayo ingeku-
wa mbele yangu endapo ningeendelea kuamini kuwa mbio zangu zingenisa-
idia huku nikiwa na nyongeza ya uzito wa Dr. Lisa begani mwangu. “Lazima
nifanye kitu” nilijiambia wakati nilipokuwa nikikatisha katikati ya umati wa
watu katika eneo moja lenye msongamano wa vibanda vya biashara ndog-
ondogo. Kwa kukwepa kuyavuta macho ya watu ile bastola yangu mkononi
nikaichomeka na kuificha kiunoni na kila nilipokuwa nikizitupa hatua zangu
watu walisogea pembeni kunipisha.
Wakati nilipogeuka kutazama tena nyuma yangu Bolos na Sam walikuwa
wamenikaribia zaidi ingawaje ulikuwa usiku lakini niliweza kuziona nyuso
zao zilivyojawa na tabasamu la ushindi. Uzito wa Dr. Lisa begani kwangu
ulikuwa mbioni kunielemea na hali hiyo nilianza kuiona kuwa ni kikwazo
katika kuwatoroka watu wale. Hata hivyo sikusimama nikaendelea kutimua
mbio huku akili yangu ikifikiria namna ya kufanya. Nilikatisha katika eneo
lile lenye msongamano wa vibanda vya biashara ndogondogo na kwa kutaka
kujiridhisha kuwa ni watu wawili tu ndiyo waliokuwa wakinifukuza niliamua
kuvuka barabara iliyokatisha mbele yangu na nilipomaliza kuvuka barabara ile
nikawaona wale jamaa wawili nao wakivuka ile barabara na hapo nikawa na
hakika kuwa nilikuwa nakabiliana na watu wawili tu.
Bado niliendelea kutimua mbio nikalipita jengo la posta lililokuwa eneo lile
na mbele kidogo nilikutana na mzunguko wa barabara. Ulikuwa mzunguko wa
barabara mkubwa uliyokuwepo katika jiji la Kigali na pembeni ya mzunguko
huo kulikuwa na majengo ya ghorofa yenye maduka mbalimbali na ofisi to-
fauti chini yake. Lilikuwa ni eneo lenye msongamano wa watu na magari, ni-
lipofika eneo hilo nikawa nimepata wazo la kuwapotezea malengo wale watu
waliokuwa wakinifukuza nyuma yangu. Hivyo haraka nikaichomoa ile bastola
yangu toka mafichoni na nilipofika kwenye eneo lile lenye msongamano wa
watu nikafyatua risasi mbili hewani.
Mlio wa zile risasi ukawashtua watu waliokuwa eneo lile hivyo wakaanza
kukimbia wakitawanyika ovyo kama mzinga wa nyuki unaporushiwa jiwe.
Katika kukimbia huko baadhi ya watu wakawa wakigongana na kuanguka
ovyo wakikanyagana na mimi nikautumia mwanya huo kuingia kwenye duka
moja la Mhindi lililokuwa hatua chache upande wa kushoto wa mzunguko wa
barabara.
Lilikuwa duka la nguo za aina tofauti na ndani yake nilimkuta mama mmoja
wa kihindi ambaye bila ya shaka nilimhisi kuwa mmiliki wa duka like. Mama
yule aliponiona nikiingia mle ndani huku begani nikiwa nimembeba mwanam-
ke wa kizungu aliyetapakaa damu alihamaki sana akataka kupiga yowe lakini
niliwahi kumuonya yule mama kwa mtutu wa bastola yangu kuwa asithubutu
kupiga kelele. Moja kwa moja nikaenda kujificha nyuma ya meza kubwa iliy-
okuwa ndani ya duka lile.
Nikiwa nimejibanza pale chini niliweza kuona kule nje ya lile duka kupitia
kioo cha dirisha lililokuwa upande wa kulia wa duka lile mahali kulipotazama
na ule mzunguko wa barabara. Wale watu bado walikuwa wakikimbia ovyo
na haukupita muda mrefu mara niliwaona wale watu waliokuwa wakinifukuza
wakipita mbele ya duka lile huku wakitazama tazama huku na kule na hapo
nikajua kuwa walikuwa wakinitafuta mimi. Muda mfupi baadaye niliwaona
wale watu wakiingia ndani ya lile duka nilimojificha na vishindo vyao vikan-
ifanya nijibanze chini zaidi.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Wewe…!” yule mtu niliyemfahamu kwa jina la Sam alimwita yule mama
wa kihindi kwa lugha ya kifaransa chenye dharau ndani yake.
“Hujamwona mtu amepita hapa na mwanamke wa kizungu begani? akauliza
“Nimemuona”
“Ameelekea wapi? yule mwenzake aliuliza kwa shauku
“Upande wa kushoto wa hili jengo” yule mama wa kihindi aliongea kwa
kutetemeka.
“Una hakika?, tukigundua umetudanganya tutakurudia”
“Siwadanganyi” yule mama wa kihindi aliwahakikishia wale watu na kupi-
tia kioo cha meza ile nilimuona yule mama akisogea taratibu na kuyakanyaga
matone mawili ya damu ya Dr. Lisa yaliyokuwa yameangukia kwenye sakafu
ya mle ndani katika namna ya kuyaficha yasionekane na wale watu hatari.
Nilimuona yule mtu niliyemtambua kwa jina la Bolos akizifuatilia hatua za
yule mama kwa makini lakini nilishukuru kuwa hakugundua kilichokuwa ki-
kiendelea.
“Unaenda wapi? Bolos alishtuka na kumuuliza yule mama hata hivyo Sam
alikwisha mshika mkono na kumtaka waondoke mle ndani akihisi kama wa-
likuwa wakipoteza muda. Muda mfupi aliofuata niliwaona wale watu waki-
ondoka lakini macho makali ya Bolos yaliyosheheni kumbukumbu ya unya-
ma wa kila namna hayakubanduka kumtazama yule mama wa kihindi kiasi
cha kumfanya mama yule aanze kutetemeka kama aliyepigwa shoti kali ya
umeme. Yule mama aliendelea kutetemeka kwa hofu hadi pale wale watu wa-
lipotoweka na hapo nikamuona akishusha pumzi kwa mkupuo kama mtu aliy-
eutua mzigo mzito baada ya safari ndefu ya uchovu.
Niligeuka kumtazama Dr. Lisa kwa mara ya kwanza tangu tulipotoroka kule
hospitali na hapo nikamuona kuwa bado alikuwa akihema taratibu ingawaje
sasa alikuwa ameyafumba macho yake huku ametulia kama mfu. Risasi ile
iliyofyatuliwa ilikuwa imemlenga begani upande wa kushoto na kuacha tundu
dogo katika eneo hilo. Nikagundua kuwa hali ile mbaya aliyokuwanayo ilito-
kana na damu nyingi aliyoipoteza kwenye jeraha lile pamoja na sumu ya risasi
ambayo sasa ilikuwa akisambaa taratibu mwilini mwake. Nikamnyanyua na
kumweka begani huku ile bastola nikiichomeka kiunoni. Nilipomaliza nika-
geuka kumtazama yule mama wa kihindi na hata kabla sijazungumza naye
nilimuona akitabasamu nami nikafanya hisani kutabasamu kidogo ingawaje
nilijua kuwa tabasamu lake lilitokana na woga aliokuwanao.
“Nashukuru” nilimwambia na hapo akanijibu kwa kutikisa kichwa.
Nilitoka nje ya duka lile Dr. Lisa akiwa begani kwangu na moja kwa moja
nikaiendea teksi moja iliyokuwa imeegeshwa mbele ya duka lile na wakati
nikiendea ile teksi niligeuka kulichunguza eneo lile nikashukuru kutowaona
wale watu waliokuwa wakinitafuta ingawaje kulikuwa na watu wachache
waliokuwa wakinitazama eneo lile. Dereva wa teksi mwanaume wa miaka
thelathini, mrefu na mwembamba alitupokea kwa bashasha za kila namna na
muda mfupi baadaye tukaondoka eneo lile.
Nikiwa nimeketi siti ya nyuma ya teksi ile huku Dr. Lisa akiwa ameegemea
begani kwangu. Akili yangu ilikuwa imepoteza utulivu kabisa. Kumbukumbu
ya mikasa yote iliyonitokea nyuma yangu ilikuwa ikipita kichwani kwangu na
kunifanya nijihisi kama ninayetazama mkanda wa fulani wa filamu usiyopen-
deza. Hata hivyo nilijitahidi kwa kila hali kuyarudisha mawazo yangu mle
ndani ya gari na hapo nikakumbuka kuwa sikuwa nimemueleza yule dereva
wa teksi ni wapi alipaswa kutupeleka.
Nilikua nimeanza kushawishika kutaka kumwambia kuwa atupeleke
kwenye ile nyumba niliyofikia lakini nilijikuta nikisita kufanya hivyo pale ni-
lipofikiria suala la usalama wa nyumba ile ambao sikuwa nikiufahamu vizuri.
Halafu ghafla wazo jipya likapenya katikati ya fikra zangu, wazo la kumfanyia
upekuzi Dr. Lisa huku nikiwa na hakika kuwa dereva wa teksi ile alikuwa
tayari amekwisha zama katika umakini wa kazi yake.
Nilianza kumpekua Dr. Lisa ndani ya mifuko ya nguo zake na muda mfupi
baadaye nikawa nimekipata kile nilichokuwa nikikitafuta. Kitambulisho kido-
go cha kazi kilichokuwa na anwani ya makazi na mkungu wa funguo na muda
ule ule nikamwambia yule dereva atupeleke ilipo nyumba namba 6 Gikondo
Avenue. Dereva akaonesha kunielewa kwa kutikisa kichwa chake huku nikiwa
na imani kuwa nyumba hiyo ndiyo aliyokuwa akiishi Dr. Lisa.
Teksi ilisimama mbele ya nyumba namba 6 Gikondo Avenue huku dakika
thelathini zikiwa zimeyeyuka tangu mwanzo wa safari yetu na wakati nikishu-
ka na kumlipa dereva yule wa teksi pesa yake niligundua kuwa nilikuwa nime-
bakiwa na noti mbili tu za pesa mfukoni mwangu. Tukio hilo likanipunguzia
furaha moyoni mwangu kwani katika harakati zangu pesa kilikuwa kiungo
muhimu sana katika kinisafishia njia. Nikiwa naifikiria hali hiyo nilimchukua
Dr. Lisa na kumtupia begani na wakati nikifanya hivyo niligundua yule dereva
kuwa alikuwa akinitazama kwa udadisi sana hata hivyo sikushughulika naye
kwani kichwa changu kilikuwa kimejaa mikasa ya kila namna na yeye hakuwa
miongoni mwayo.
Nilizitupa hatua zangu kwa uangalifu kuiendea nyumba namba 6 ya mtaa
ule huku masikio yangu yakipotelewa na sauti ya muungurumo wa injini ya
teksi ile iliyokuwa ikitokomea nyuma yangu. Ingawaje sikuwa na saa yangu
mkononi niliweza kuhisi tu kuwa muda ule ulikuwa ukielekea kutimia saa nne
usiku.
Kulikuwa na magari machache yaliyokuwa yameegeshwa kando ya baraba-
ra ile. Ulikuwa ni mtaa uliokuwa kwa barabara safi, mirefeji mizuri ya maji
iliyojengewa kando yake na hata nyumba za mtaa ule zilikuwa na afya na
zilipendeza sana kutokana na ramani ya ujenzi wake wa matofali mazuri ya
kuchoma na madirisha makubwa ya vioo na paa za vigae. Nyumba zote zili-
fanana na wakati huu nyumba zote zilikuwa zikiwaka taa isipokuwa nyuma
ya Dr.Lisa.
Niliufikia mlango wa mbele wa nyumba ile na kukijaribu kitasa chake. Ule
mlango ulikuwa umefungwa hivyo nikazichukua zile funguo toka katika koti
la Dr. Lisa na baada ya kuijaribu kila funguo hatimaye funguo moja ikawa
imekubali kufungua hivyo nikaufungua ule mlango na kuingia ndani.
Kabla ya kuwasha taa ya mle ndani pua yangu ikanasa ugeni wa harufu nzu-
ri, harufu ya manukato ya kizungu na hali hiyo ikanifanya nijipongeze kuwa
sikuwa nimekosea njia. Sebule ilikuwa na seti moja ya makochi ya sofa ya
kisasa, runinga, rafu kubwa ya vitabu vya kidaktari, redio ya kisasa iliyokuwa
pembeni ya kabati kwenye kona, zulia maridadi lililokuwa sakafuni na meza
fupi ya kioo iliyokuwa katikati ya sebule ile.
Ukutani kulikuwa na picha kubwa za kuvutia baadhi zikimuonesha Dr. Lisa
akiwa na familia yake mahali fulani na nyingine zikiwa ni za mazingira tofauti
tofauti katika nchi za Afrika. Na ni katika picha hizo niliiona picha moja Dr.
Lisa akiwa pamoja na marehemu Dr. Francois Tresor, wote wakiwa na nyuso
za furaha. Nilimlaza Dr. Lisa katika kochi moja pale sebuleni huku nikiwa
na matumaini kuwa katika nyumba ya daktari kama ile nisingekosa vifaa vya
huduma ya kwanza.
#155
“JINA LANGU NAITWA GHASPARD GAHIZI…umewahi kunisikia po-
pote? aligeuka na kumuuliza msichana aliyempa lifti kiasi cha muda wa da-
kika kumi na tano zilizopita huku akiutumia muda huo kulidadisi umbo la
msichana huyo kwa macho ya wizi wizi. Uzuri wa msichana huyo mwenye
umbo la kuvutia ulikuwa kichocheo cha kwanza cha kumkubalia ombi lake la
lifti mpaka katikati ya jiji la Kigali ingawaje kama ingelikuwa ni mwanaume
asingejisumbua kupunguza hata mwendo wa gari lake aina ya Volkswagen.
“Sina hakika”
“Ghaspard Gahizi, mhariri mwandamizi wa Radio Television Libre des
Mille“RTLM”, hujawahi kunisikia nikitangaza? mwanaume huyo mrefu wa
wastani mwenye umri kati ya miaka thelathini hadi arobaini akiwa ndani ya
suti yake ya kijivu na tai nyeusi alijinadi tena kwa manjonjo huku akionekana
kutofurahishwa kwa msichana huyo aliyempa lifti kutomfahamu.
Bado alikuwa akiyachunguza mapaja ya abiria wake kwa macho ya wa-
ziwizi kisha aliyahamishia tena macho yake kuutazama mzigo wa matiti ya
wastani kifuani kwa msichana huyo kabla ya kushusha pumzi taratibu na ku-
geuka kutazama mbele huku akijaribu kuudhibiti usukani wa gari kwa mikono
yake wakati huo akipambana kuitowesha taswira tofauti za kimahaba zilizo-
anza kuumbika kichwani mwake. Hata hivyo haukupita muda mefu kabla ya
kukiri kuwa zoezi hilo lilikuwa gumu kwake pale alipoyarudisha tena macho
yake kwenye umbo la msichana huyo.
“Jina lako nani, si vibaya tukafahamiana” hatimaye aliamua kubadilisha
mada.
“Naitwa Anne marie ingawa wengi wanaonifahamu hulifupisha kwa kulii-
ta Anne” Rosine aliongea huku uso wake ukiumba tabasamu hafifu. Alikuwa
ameamua kutumia jina la Anne marie, jina ambalo aliamini lingemuweka mba-
li na kushukiwa na mtu yoyote mwenye ushirika na Kanali Bosco Rutaganda
na watu wake pindi atakapowasili jijini Kigali na kujichanganya mitaani.
Kumbukumbu ya matukio yote yaliyomtokea nyuma ilikuwa ikipenya tara
tibu katika ubongo wake na kutengeneza kitu kama mkanda wa filamu ndefu
wenye picha za matukio ya ajabu. Miongoni mwa picha za matukio hayo ni
yale matukio yote yaliyotokea katika mapango ya Musanze na ile nyumba ya
ajabu iliyojitenga kule msituni iliyokuwa ikimilikiwa na yule mtu wa ajabu
aliyefahamika kwa jila la Innocent Gahizi. Kufikia hapo ikatumbukia taswira
ya Patrick Zambi, mwanaume aliyetokea kumpenda kuliko kitu chochote dun-
iani tena kwa muda mfupi tu walionana kule msituni.
Hadi wakati huu alikuwa hafahamu hasa ni wapi mwanaume huyo mwenye
mvuto wa kipekee na moyo wa huruma usiofananishwa na mwanaume yoyote
alikuwa na yapi yaliyomsibu. Alichokuwa akikumbuka kwa mara ya mwisho
ni kuwa walikuwa pamoja yeye na Patrick wakiwa wamelala juu ya kitanda
katika mojawapo ya vyumba vya ile nyumba iliyokuwa katikati ya msitu na
aliposhtuka usingizini alikuwa ameshangazwa sana na kutokumuona Patrick
akiwa kando yake. Bila shaka Patrick alikuwa amemtoroka hivyo ndivyo hisia
zake zilivyomwambia kichwani huku akijiuliza ni kwanini mwanaume huyo
amtoroke na kumtelekeza peke yake katika mazingira ya msituni kama yale
huku akiendelea kujiuliza nini kilichompelekea afanye hivyo. Rosine alien-
delea kujiuliza huku akijaribu kuifuta taswira za matukio yote yaliyomtokea
bila mafanikio.
Aliendelea kukumbuka namna alivyoitoroka nyumba ile mapema mara baa-
da ya kushtukia kuwa alikuwa ametelekezwa mle ndani peke yake. Safari yake
ilikuwa ngumu na yenye kuhitaji ujasiri wa hali ya juu akikatisha katikati ya
misitu na mawe, mlima na mabonde kabla ya kutokezea katika barabara ya
lami ambayo ilimchukua zaidi ya mwendo wa masaa zaidi ya manne akitem-
bea kwa miguu hadi alipopata lifti hii usiku ukiwa tayari umeshaanza kuingia.
Akiwa ameketi pembeni ya dereva Rosine alijikuta akiwaza namna am-
bavyo mkuu wa idara yake ya kijasusi ambavyo angekuwa na wasiwasi baada
ya zaidi ya muda wa wiki mbili kupita kimya bila ya kusikia kutoka kwake.
Labda angeamua kumtuma mtu mwingine aje kumfuatilia na kujua yaliyomsi-
bu au pangine angekaa kimya akizidi kusubiri. Bado hakuwa na hakika inga-
waje alishaanza kupanga kuwa hii ingekuwa ni mara yake ya mwisho kufanya
kazi yake hatari ya kijasusi. Umri wake ulikuwa ukienda na alihitaji kuolewa
na kuzaa watoto na kuishi maisha ya familia. Hilo ndilo lililokuwa jambo la
kwanza kulipa kipaumbele mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa.
Alikuwa ameonana na kukutana na wanaume wa kila namna katika harakati
zake lakini ni mwanaume mmoja tu aliyetokea kuugusa moyo wake na mwa-
naume huyo alikuwa Patrick. Lakini kwa sasa uwezekano huo aliuona kuwa
ulikuwa umeanza kufifia kwani hakujua Patrick Zambi alikuwa wapi.
Akiwa amezama katika fikra hizo Rosine aligeuka na kumtazama mwenye-
ji wake aliyempa lifti baada ya yeye kuchoka kutazamwa. Uso wake ukiwa
mbali na tashwishwi yoyote mawazo yake yalianza kutengeneza majadala
mwingine mpya pale alipoanza kulitafakari vizuri jina la mwanaume yule ali-
yempa lifti ndani ya gari akijinadi kwake kwa jina la Ghaspard Gahizi, mhari-
ri mwandamizi wa Radio Libre de Mille Colline au kwa tafsiri ya lugha ya
kiswahili ikimaanisha stesheni huru ya radio na runinga ya milima elfu moja,
jina milima elfu moja ikimaanisha nchi ya Rwanda.
Rosine alizidi kuitafakari redio hiyo maarufu kwa matangazo, vipindi
mbalimbali na muziki iliyoanzishwa mwaka mmoja tu uliyopita, lakini uma-
arufu wake ulikwisha upita hata ule wa redio ya Serikali. Na sasa alikuwa
pembeni ya mhariri mwandamizi wa redio hiyo RTLM na gazeti maarufu la
nchini Rwanda liitwalo Kangura. Vilikuwa ni vyombo vya habari vilivyokuwa
vikihusishwa kwa namna moja au nyingine kuchochea uhasama wa kikabila
kati ya Wahutu na Watutsi, makabila makubwa mawili ya nchi ya Rwanda.
Baadhi ya nyimbo zilizokuwa zikipigwa sana katika stesheni ya RTLM ni zile
nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na mwanamuziki wa kabila la Kihutu aitwaye
Simon Bikindi zote kwa lugha ya kinyarwanda, moja akiitwa“Bene Sebahizi
(Watoto wa wakulima) na nyimbo nyingine iitwayo “Nanga Abahutu” nayo
pia kwa lugha ya kiswahili ikimaanisha (Nawachukia wahutu)
“Unaelekea eneo gani ukifika jijini Kigali?
“Bado sijajua ila nafikiri nikifika nitaamua kutokana na hali itakavyokuwa”
“Kwa hiyo huna mwenyeji?
“Sina”
“Sasa unawezaje kwenda sehemu ambayo huna mwenyeji?
“Kweli ni vigumu lakini nataka nikajaribu kutafuta maisha huko”
“Si rahisi kama unavyodhani na ingekuwa mapema sana ningekushauri
kwani mimi ni mwenyeji wa muda mrefu wa jiji la Kigali. Maisha si rahisi
sana kama watu wengi wanaotaka kwenda huko wanavyodhani” Ghaspard
Gahizi aliongea huku akigeuka kumtazama Rosine na wakati huohuo Rosine
aliweza kuzisoma fikra za Ghaspard Gahizi namna zilivyotafunwa na uchu
wa ngono.
“Nisingependa usumbuke Anne marie kama hutojali unaweza kukaa kwan-
gu hadi pale utakapokuwa tayari kujitegemea ingawaje mimi nisingekushauri
utafute maisha kwa utaratibu huo.
Rosine akiwa amejiandaa kupata mwaliko wa namna hiyo alitabasamu
kidogo huku akitabasamu.
“Sidhani kama itawezekana, vipi mke wako akikuona unarudi na mwanam-
ke mwingine nyumbani?
“Oh! usijali kuhusu hilo mimi nyumbani kwangu sina mke wala mtoto kwa
hiyo hakuna wa kukusumbua”
“Huoni kuwa nitakuwa nakubebesha mzigo usio kuhusu?
“Ondoa shaka kwanza tukiwa wawili upweke utapungua”
“Nitashukuru” Rosine aliongea kivivuvivu.
Kilichofuata baada ya hapo yalikuwa ni maongezi ya hapa na pale huku
kila mmoja akijaribu kumfahamu mwenzake kwa kadiri alivyoweza. Ingawaje
Rosine alijitahidi kwa kila hali kuchangia maongezi hayo lakini akili yake
ilikuwa mbali sana ikitafakari hili na lile.
Kulikuwa na jambo moja tu lililompa matumaini katika kuonana tena na
Patrick, jambo hilo lilitokana na uongo alivyomwambia Patrick Zambi ambao
alikuwa na hakikanao kuwa ulikuwa ni uongo ulioaminika bila shida.
Nyumba ya Ghaspard Gahizi ilikuwa katika eneo liitwalo Gisenyi kilometa
chache kutoka yalipo makao makuu ya ofisi za RTLM, nje kidogo ya jiji la
Kigali. Waliwasili katika nyumba hiyo katikati ya usiku huku Rosine akiwa
amepitiwa na usingizi mara mbili kabla ya kufika kwenye nyumba hiyo.
Nyumba hiyo ilikuwa miongoni mwa nyumba za kisasa kabisa katika eneo
lenye uzio mkubwa wa ukuta na geti. Ghaspard Gahizi alimkaribisha Ros-
ine katika nyumba hiyo yenye kila kionjo cha ukwasi kama samani za kisasa,
sebule na vyumba vinne vikubwa na baadaye akamuonesha chumba cha ku-
lala, jiko na vitu vingine vyote muhimu ambayo Rosine angevihitaji. Rosine
aliitathmini vizuri ile nyumba na kuridhika nayo japokuwa kulikuwa na kitu
kimoja tu ambacho kilimtia wasiwasi juu ya mwenyeji wake. Kitu hicho ki-
likuwa ni suala la Ghaspard Gahizi kutokuwa na mwanamke wa kuishi naye
huku akionekana kuwa na kila kitu nyumbani kwake.
Baada ya kuoga na kubadilisha nguo alizopewa na mwenyeji wake Rosine
aliingia jikoni na kutayarisha chakula na muda mfupi baadaye wote walikuwa
sebuleni wakipata mlo.
Kwa Ghaspard Gahizi mbele yake alimtazama Rosine kama kiumbe kutoka
sayari nyingine chenye uzuri usioelezeka. Muonekano wa Rosine kwa waka-
ti huu ulikuwa mpya kabisa na uzuri wake ulikuwa umeongezeka maradufu.
Wakati wote wa mlo Ghaspard Gahizi macho yale yalikuwa kwa Rosine na
Rosine alifahamu hilo.
“Unaishi vipi peke yako kwenye nyumba kama hii yenye kila kitu? Rosine
alivunja ukimya katikati ya mlo huku akitabasamu. Upande wa pili wa meza
mbele yake aliketi Ghaspard Gahizi akiwa ndani ya mavazi yake ya kulalia.
“Nimekua nikilifikiria suala hilo kwa kipindi kirefu na hii hali inanichosha
sana”
“Kwa nini usioe?
“Nilikuwa na mke kwa bahati mbaya sana ndoa yetu ilivunjika?
“Oh! pole sana tatizo lilikuwa nini?
“Alikuwa akinilalamikia kila mara eti mimi sina muda wa kukaa naye na
badala yake muda mwingi nilikuwa nikishinda ofisini kufanya shughuli zangu
na kurudi nyumbani usiku sana. Labda alikuwa sahihi lakini yote niliyafanya
kwa ajili yake” Gharpard aliongea huku akibetua mabega yake.
“Unatakiwa uwafahamu wanawake vizuri. Sisi ni viumbe wa ajabu sana
yaani hata kama utatafuta pesa nyingi za namna gani na kuihudumia familia
kwa kiasi gani ila kama hutakuwa na mapenzi ya karibu na mke wako hivyo
vyote vinaweza visiwe na maana kwake”
“Hilo ndilo tatizo letu wanaume lakini sasa nimejifunza”
“Lakini usijali kwani ipo siku moja mke wako atarudi tu akichoshwa na
huko alipo”
“Sidhani kama ni kweli atarudi kwani ni muda mrefu sasa umepita. Ni zaidi
ya miaka mitatu sasa na nilijaribu kumtafuta bila mafanikio”
“Pole sana” Rosine aliongea kwa sauti laini na nyepesi ya kubembeleza.
“Nashukuru sana Rosine na uwepo wako leo umenifanya niwe na furaha
sana na sipendi uondoke katika nyumba hii. Inavyoonekana ni kama tunao-
endana na hivyo ni suala la kuamua tu kuwa tuishi pamoja” Ghaspard Gahizi
aliongea huku akiumba tabasamu hafifu usoni mwake.
“Siwezi kukujibu kwa sasa, vuta subira tuone muda utakavyosema kwani
pengine mke wako akawahi kurudi”
“Nakuomba ufikirie kuhusu hilo kwani siyo siri nimechoshwa na haya mai-
sha ya upweke”
“Usijali nakuomba unipe muda wa kutafakari kwanza”
Waliendelea kuongea hili na lile wakijaribu kufahamiana zaidi lakini Rosine
alikuwa mwangalifu kujizungumzia huku akificha hili na kuongea lile. Usi-
ku ulipozidi kuingia Ghaspard Gahizi alisimama na kumuaga Rosine kuwa
anaenda kulala ili kesho awahi kwenda kazini baada ya likizo yake ya mwezi
mmoja kuisha, Rosine naye akaelekea chumbani kwake.
#157
INTERAHAMWE
SEHEMU FULANI KATIKA JENGO FULANI la ghorofa katikati ya jiji la
Kigali mkutano wa siri ulikuwa ukifanyika katika ukumbi mdogo wa wastani
wenye uwezo wa kuchukua watu wasiopungua arobaini. Mkutano huo uliku-
wa umeandaliwa na kuratibiwa kwa usiri mkubwa hivyo hata wahudhuriaji
waliaswa kufika kwa siri sana katika mkutano huo. Meza ya mbele ya ukumbi
huo viti vyake vilikuwa vimekaliwa na watu kumi na mbili na ni kiti kimoja
tu ndiyo kilikuwa wazi na mwenyeji wake ndiye aliyekuwa akisubiriwa ili
mkutano huo uanze.
Watu hao walioketi mbele ya ukumbi huo nyuma ya meza ndefu na pana,
kutoka upande wa kushoto majina na vyeo vyao yalikuwa hivi; Georges Rug-
gui mtangazaji RTLM, Hassan Ngeze mkurugenzi na mhariri wa gazeti la Kan-
gura, Ferdinand Nahimana mkurugenzi mtendaji wa RTLM, Felicien Kabuga
mkurugenzi mwandamizi na mwanzilishi wa RTLM, Jean Kambanda waziri
mkuu wa serikali ya mpito nchini Rwanda, Meja Jean Bosco Barayagwiza
mkufunzi wa kikosi maalumu cha kijeshi cha vijana kiitwacho Impuzamugam-
bi (watu wenye lengo moja) na kamanda wa kikosi maalumu cha kijeshi cha
CDR - Coalition pour la Défense de la République. Wengine waliofuata wa-
likuwa ni Kanali Bosco Rutaganda mnadhimu mkuu wa Interahamwe, Luteni
Marce Ayme mratibu wa operesheni za kijeshi wa jeshi la ufaransa linalolinda
amani nchini Rwanda ama UNAMIR (United Nations Assistance Mission for
Rwanda) Jean–Marie Vianney Mudahinyuka a.k.a zuzu, kiongozi wa propa-
ganda za Interahamwe, Robert Kajuga rais wa Interahamwe.
Waliosalia walikuwa watu wawili, mmoja akifahamika kwa jina moja la
Sam na mwingine akiitwa Bolos. Mwenyekiti wa mkutano huo Meja Jean
Bosco Barayagwiza, mwanaume mrefu na mweusi mwenye macho makubwa
na makali alikohoa kidogo na kurudia kuitazama saa yake ya mkononi huku
akionekana kuanza kukata tamaa kwa namna dakika zilivyokuwa zikiyoyoma
bila mtu wanaye msubiri kufika. Hali hiyo ilipokuwa mbioni kumchosha aka-
kisogeza kiti chake karibu na meza kisha akavikamatisha viganja vya mikono
yake akijiandaa kufungua mkutano.
Lakini kabla hajafanya hivyo muda uleule mlango wa ukumbi ulifunguliwa
kisha akaingia mtu mrefu, mwembamba na mweusi aliyevaa suti nyeusi na
shati jeupe. Mtu huyo alipoingia mle ndani watu wote waligeuka kumtazama
wakionekana kufurahishwa na ujio wake. Haukupita muda mrefu mtu huyo
aliyeingia aliwasalimia watu wote mle ndani na kisha kwenda kuketi kwenye
kile kiti kilichosalia.
“Kwa kuwa tuliyekuwa tukimsubiri amefika natangaza rasmi kuwa mkuta-
no wetu umefunguliwa” Meja Jean Bosco Barayagwiza alivunja ukimya na
kufungua mkutano huku akigeuka na kuonesha tabasamu hafifu kwa yule mtu
wa mwisho kuingia.
”Karibu sana comrade Ghaspard Gahizi” hatimaye yule mwenyekiti wa
mkutano aliongea
“Ahsante sana na naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kufika”
“Ni matumaini yangu kuwa wajumbe wote wamelipokea ombi lako kwa
mikono miwili” mwenyekiti aliendelea “Kama nilivyosema mkutano wetu ni
wa dharura na wa siri hivyo hatutatumia muda mwingi sana hapa kwa hiyo
ni vema kila mtu akatambua wajibu wake ili kazi tuliyoipanga imalizike kwa
mafanikio makubwa” akakohoa na kuendelea huku macho yake yakipita juu
ya kurasa chache za kitabu kidogo alichokitoa katika mfuko wa koti lake.
“Tunayo mambo mengi ya kuyafanyia kazi na bado muda si rafiki kwetu”
akakohoa kidogo na kuendelea na wakati huo ukumbi wote ulikuwa umet-
awaliwa na ukimya. Lakini kabla ya kuendelea aligeuka upande wa kushoto
akiwatazama watu wawili jirani yake waliokuwa wakimsikiliza kwa makini na
watu hao walikuwa ni Bolos na Sam.
“Mliniambia kuwa Luteni Venus Jaka, yule mwanamke aitwaye Drel Fille
na mfungwa mwingine moja wametoroka na sasa mnaniambia kuwa Dr. Lisa
naye ametoroka. Inavyoonekana ni kama hamtambui hatari ikatayotukabili
endapo watu hawa wasipopatikana. Tunafahamu kuwa Luteni Venus Jaka na
Drel Fille ni wapelelezi wa kiwango cha juu waliotumwa na nchi zao yaani
Tanzania na R.D Congo kuja hapa Rwanda na mpaka sasa hivi inawezeka-
na kabisa watu hawa wanaifahamu mipango yetu kwa kiasi fulani ingawaje
kadiri muda unavyokwenda ipo hatari ya ukweli wote wa mambo kuangukia
mikononi mwao. Sioni haja ya kuwaeleza kuwa ni nini kitakachotokea enda-
po siri zetu zitaangukia mikononi mwao. Sote tunafahamu madhara yake na
mara baada ya mkutano huu kuisha Sam na Bolos mtaingia mtaani kuwatafuta
watu hawa na katika mzingira yoyote yale lazima wauwawe, sitarajii makosa
mengine kutendeka.
“Sawa” wote wakaitikia huku wakitikisa vichwa.
“Mpango wetu utatekelezwa tarehe 6 mwezi wa nne muda wa jioni kama
ilivyopangwa. Tunaye mtu wetu aliyeko nchini Tanzania kwenye mkutano wa
viongozi wa nchi za maziwa makuu unaoendelea, yeye ndiye anayetutumia ta-
arifa za mambo yote yanayokwenda. Na taarifa alizotutumia ni kuwa msafara
wa Kinani (Kinani ni jina la utani la rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda
likimaanisha mtu asiyeonekana kwa lugha ya kinywaranda) utawasili uwanja
wa ndege wa Kanombe (Kigali International Airport) tarehe na muda ule ule
niliyowaambia. Hivyo ni wakati wa kuitumia nafasi hiyo bila kufanya makosa.
“Tunahitaji kufahamu kuwa ataongozana na nani katika msafara huo” Kana-
li Bosco Rutaganda aliuliza akionesha kuvutiwa na habari hizo. Swali hilo
likamfanya waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Rwanda Jean Kambanda
aingilie maongezi.
“Ninayo orodha ya watu wote katika msafara wake, ukiwatoa wahudumu
wake wachache miongoni mwao yupo mnadhimu mkuu wa jeshi la Rwanda
Deogratias Nsambimana na Kanali Elie Sagatwa mkuu wa usalama na ulinzi
wa rais”
Watu wote wakageuka kumtazama waziri Jean Kambanda.
“Hizo ni taarifa nzuri ndugu” ndugu Hassan Ngeze, mkurugenzi na mhariri
wa gazeri la Kangura aliongea.
“Mimi bado sijaelewa namna itakavyokuwa baada ya mpango huo wa ku-
muondoa Kinani na watu wake kutekelezwa? Ferdinand Nahimana aliuliza.
“Ni swali zuri na mpango wenyewe utakuwa hivi. Mara baada ya kazi hiyo
kukamilika kitakachofuatia baada ya hapo ni kuwaambia vijana wetu wa Im-
puzamugambi kuweka vizuizi kwenye barabara zote za miji” Meja Jean Bosco
Barayagwiza aliendelea kuongea huku akitabasamu baada ya kuridhishwa na
kiwango cha uchangiaji mada.
“Vizuizi vya nini? George Ruggui aliuliza.
“Vizuizi vitatusaidia kuwakamata wale maadui zetu wote watakao kuwa
wanajaribu kututoroka. Orodha ya majina yao tunayo na kila mtu miongoni
mwetu atapewa orodha hiyo kabla ya kuondoka ili aweze kuwapanga vizuri
watu wake katika eneo lake. Orodha ya majina ya watu hao wengi ni wale
viongozi wa vyama pinzani vinavyoipinga serikali ya Kinani na wale wote
waliohusika katika mchakato wa kutengeneza serikali ya mpito.
“Na vipi tutakapowakamata nini kitafanyika? Felicien Kabuga aliuliza
“Ni kifo tu, lazima wauwawe na vifo vyao viwe vya kutaabisha ili kutoa
fundisho kwa wengine. Njia nzuri ni kwa kutumia mpanga na marungu tut-
akayowapa vijana katika maeneo yetu.
“Tumeshapata fedha za kutosha toka kwa wahisani wetu” Meja Jean Bosco
Barayagwiza akaweka kituo kisha akaachia tabasamu hafifu kwa yule mfaran-
sa Luteni Mercel Ayme na yeye akafanya hisani kwa kurudisha tabasamu ki-
sha maongezi yakaendelea tena.
“Vile vile zoezi hilo litaendelea pia katika maeneo yote ya makazi ya watu.
Vijana wetu watapita kila nyumba na kuomba vitambulisho na kupitia vitam-
bulisho hivyo tutawafahamu walio wa kwetu na wale wasio wa kwetu. Wasio
wa kwetu sote tunafahamu nini cha kuwafanya”
Watu wote waligeuka kutazamana mle ndani kisha kukafuatiwa na mi-
nong’ono hafifu na minong’ono hiyo ilipopungua na hatimaye kukoma Georg
es Ruggiu akanyoosha kidole na kuuliza tena swali huku uso wake ukiwa
umeumba tabasamu la ushindi.
“Mimi ningependa kujua RTLM ina nafasi gani katika mapinduzi haya”
“Hilo ni swali muhimu sana ndiyo maana tukawataka baadhi ya ma-com-
rade wa stesheni yenu kuwepo na kushiriki kikamilifu katika mkutano huu.
Kazi ya RTLM katika kufanikisha mapinduzi haya ni kwamba mara baada ya
kumalizana na Kinani na msafara wake hapana shaka kwamba nchi itakuwa
haina kiongozi...”
“Nadhani tumemsahau waziri mkuu Bi. Agathe Uwilingiyimana kwani yeye
ndiye atakayestahili kukaimu madaraka ya rais, yeye tutamfanyaje ili katiba
isitushtaki? Jean Kambanda waziri mkuu wa serikali ya mpito aliuliza tena.
“Hilo lisiwape shida kwani nimeshaandaa kikosi maalumu kitakachomshu-
ghulikia mara tu baada ya mapinduzi kufanyika”
Wajumbe wote wakatabasamu na kukenua meno yao isipokuwa mtu mmoja
miongoni mwao, mtu huyo alikuwa Ghaspard Gahizi. Yeye alikuwa ameza-
ma katika fikra tofauti na wenzake na hisia fulani zilikuwa zikipita kichwani
mwake. Hisia juu ya Anne marie msichana aliyempa lifti usiku wa jana ali-
pokuwa akitokea kijijini kwake alipokuwa kwenye kipindi chake chote cha
likizo ya kikazi kusalimia na hatimaye kulala naye nyumbani kwake.
Alimtafakari msichana huyo na kuanza kumtoa katika kundi la wasicha-
na washamba waliokuwa wakimiminika jijini Kigali kutafuta maisha. Yeye
hakuelekea kufanana nao pamoja na mavazi yake ya kishamba aliyokuwa
ameyavaa wakati akimpa lifti siku ya jana, uongeaji wake kimtazamo ulifa-
nana kabisa na wasichana wajanja wa mjini wenye ufahamu na uelewa mkub-
wa katika masuala mbalimbali. Halafu akaanza kumfananisha msichana huyo
na huyo mpelelezi hatari kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
aliyetajwa katika mkutano huu kwa jina la Drel fille. Na hapo akaanza kujiuli-
za itakuwaje kama msichana huyo anayetajwa katika mkutano huu ndiye yule
aliyemwacha nyumbani asubuhi ya leo wakati akija humu mkutanoni?
Kwa kweli hakupenda kabisa hilo litokee kwani ingawaje walikuwa wame-
onana na msichana huyo aliyemtambua kwa jina la Annemarie kwa muda mfu-
pi tu lakini alikuwa ametokea kumpenda sana.
Kelele za makofi hafifu yaliyopigwa ukumbini mle na wajumbe wenzake
yakazikatisha fikra zake.
“RTLM nyinyi hapa ndipo kazi yenu inapokuja, mnachotakiwa ni kueneza
chuki dhidi ya watutsi wote kwani hiyo itasaidia kuwapa morali vijana wetu
wa Impuzamugambi waweze kuwatafuta watutsi wote katika maeneo yao na
kuwapa kile kinachostahili. Wakati wa mapinduzi hayo RTLM itaendelea ku-
wafichua maadui zetu wote kokote walikojificha na kuwaelekeza vijana wetu
mahali walipo.
Hebu ngoja niwaambie, katika mapinduzi yoyote huwa hapakosekani
wasaliti na usaliti wa namna yoyote malipo yake huwa ni kifo, na ni lazi-
ma tulizingatie hili. Vilevile labda ningependa niwatie moyo wa ujasiri katika
kutekeleza mapinduzi haya ili watu wetu wanaotutegemea waje kufaidika. Na
tunachoenda kukifanya ni sehemu tu ya unyama tuliyokuwa tukifanyiwa na
wenzetu na uonevu usio na mipaka wa miaka mingi. Ushahidi wa mambo
hayo tunao, mfano tarehe 21 mwezi Octoba mwaka 1993 askari wa kitutsi
walipanga mipango na hatimaye kumuua mhutu mwenzetu wakati huo akiwa
rais wa kuchaguliwa kwa uchaguzi halali wa Jamhuri ya watu wa Burundi, rais
Melchior Ndadaye. Na pia kumekuwa na mtukio mengi ya chini chini yanay-
oendeshwa kwa usiri mkubwa na watutsi katika kuhakikisha kuwa wahutu
tunaendelea kugandamizwa na kuwa chini katika kila eneo.
Kama hatutakataa aina hii ya ukandamizaji basi tuwe tayari kukubaliana
na unyanyasaji wa kila namna lakini wakati huo tukae tukijua kuwa wenzetu
hawalali kama sisi na wana umoja na mbinu chafu kuliko tunavyodhani. Sote
tunajua kuwa rais wa nchi hii ni mhutu mwenzetu lakini tunashangaa kuona
kuwa anatusaliti. Mkutano unaoendelea sasa hivi nchini Tanzania ni moja ya
mikutano mingi inayofanywa baina yake na viongozi wa Rwandese Patriotic
Front(RPF) katika kuhakikisha nchi hii inaongozwa na serikali ya mpito ita-
kayozingatia usawa kati ya wahutu na watutsi.
Napenda niwaambie kuwa huu ni mwanzo wa kampeni za watutsi katika ku-
hakikisha wanaiongoza nchi hii na kwa bahati mbaya sana Kinani hafahamu
na wala haioni hatari inayotukabili mbele yetu endapo watu hawa watapewa
nafasi katika serikali hii. Mfano mzuri mwingine tulionao ni ule wa mwezi
Octoba mwaka 1990 wakati RPF ilipofanya uvamizi wa kutaka kuiangusha
madarakani serikali ya mhutu mwenzetu rais Juvenal Habyarimana. Sote tuna-
fahamu kuwa RPF ni jeshi la wavamizi wa kitutsi ambao askari wake wengi
ni wakimbizi wa kitutsi wa Rwanda waliokimbilia nchini Uganda na kuomba
hifadhi kwa muda.
Wakati huo wote wakiwa ukimbizini wamekuwa wakijipanga kwa kufan-
ya mafunzo makali ya kijeshi na askari wa Uganda na hata wengine kupewa
nafasi za juu za kijeshi katika jeshi la Uganda kwa kile wanachokiita maan-
dalizi ya kurudi nchini Rwanda na kulipa kisasi. Kama si marafiki zetu askari
wa kifaransa kuingilia kati uvamizi huo leo hii serikali ya Kinani isingekuwa
madarakani kwani kwa bahati nzuri mapinduzi ya RPF yalizimwa na baadaye
kufuatiwa na mkutano wa makubaliano wa Arusha 1993 (Arusha Acords) kati
ya serikali ya Kinani na RPF.
Mifano ni mingi sana inayoonesha njama mbalimbali zinazofanywa na wa-
tutsi dhidi yetu na kwa bahati mbaya sana muda hauruhusu kuitaja mifano
hiyo yote hapa, lakini kwa hii mifano michache tunaweza kupata picha kamili
ya namna mambo yalivyo” Meja Jean Bosco Barayagizwa aliweka kituo huko
uso wake ukiwa tayari umepoteza nuru ya kibinadamu. Ukumbi wote ulikuwa
kimya na kila mjumbe alionekana kuingiwa vizuri na hotuba hiyo fupi isiyo
rasmi. Wajumbe wote wakakaa katika mkao wa kutafakari.
“Mpaka hapa tulipofika hatuwezi kurudi nyuma, Kinani ametusaliti watu
wake hivyo hatuoni sababu ya kumuacha, serikali yake itaangushwa na tut-
aweka utawala wetu ingawaje kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia mga-
wanyo wa madaraka utakavyokuwa. Tutawauwa “Inyenzi” wote (Inyenzi ni
neno la kinyarwanda linalomaanisha mdudu aitwaye Mende, mdudu huyo
akifananishwa na watutsi kwa jinsi walivyo na miguu mirefu kama Mende).
Wahutu wote waliooa na kuolewa na watutsi au kushirikiananoa kwa namna
moja au nyingine tutawafichua na kuwafyekelea mbali kuanzia watoto, vi-
jana mpaka wazee bila kumuacha hata mmoja, na yeyote miongoni mwetu
atakayeonekana kuwakumbatia hatutamuacha. Tunatambua kuwa miongoni
mwetu watawaficha watutsi kwa kujidai kuwa wana ubinadamu sana, watu wa
namna hiyo pia ni wasaliti hatutawaacha.
“Sauti ya Meja Jean Bosco Barayagwiza ilikuwa alitamba ukumbi mzima
na kila mjumbe alionekana kuingiwa vizuri na maneno yake. Ukumbi mzima
sasa ulikuwa kimya huku kila mmoja akivuta picha ya mambo yatakavyokuwa
kwa namna yake.
“Mimi nina wazo” Hassan Ngeze alivunja ukimya na kuwafanya wajumbe
wote ukumbini wageuke kumtazama.
“Ni kuhusu Drel Fille, Luteni Venus Jaka na Dr. Lisa. Nionavyo mimi
ni vizuri suala la kuwatafuta watu hawa likapewa uzito wa kipekee. Mimi
ningependekeza kuwa waongezewe watu zaidi katika kuwatafuta kwani nina
kila hakika kuwa bado wapo hapa jijini Kigali kwani endapo wangekuwa wa-
metoroka hapa nchini watu wetu waliopo mipakani wangeishawakamata. Ni-
juavyo mimi upo uwezekano mkubwa kuwa Dr. Lisa ndiye anayefahamu wapi
alipo Jaji Makesa, mtu ambaye ni hatari sana kwetu”
Wajumbe wote wakaunga mkono hoja hiyo hivyo ikapitishwa moja kwa
moja bila pingamizi huku Meja Jean Bosco Barayagwiza akiahidi kuongeza
watu zaidi katika kufanikisha zoezi zoezi la kukamatwa kwao.
“Na kwa kumalizia ni kwamba, wakati tunaendelea na mipango yetu kuna
baadhi ya wanausalama wa serikali wanaotufuatilia. Mpaka sasa tumeisha
wauwa watano hivyo ni vizuri kila mmoja mara baada ya kutoka hapa awe
makini na nyendo zake na mengine tutaendelea kufahamishana kadiri tutaka-
vyoona umuhimu wa kufanya hivyo”
Bila ya kusubiri maswali na maoni zaidi Meja Jean Bosco Barayagwiza
akafunga mkutano ule kisha akasimama na kuelekea ulipo ule mlango wa ku-
tokea ukumbini huku nyuma yake akifuatiwa na mjumbe mmoja baada ya
mwingine. Mkutano ukawa umefika ukomo.
__________
MUDA MFUPI MARA BAADA YA GHASPARD GAHIZI kumuaga kuwa
anaenda kazini asubuhi hii Drel Fille aliamka na kuelekea bafuni ambapo huko
hakukaa muda mrefu na alipotoka akaingia jikoni kuandaa kifungua kinywa.
Wakati akipata kifungua kinywa mawazo yake yote yalikuwa kwa Luteni
Venus Jaka ama Patrick Zambi kama alivyolizoea jina hilo, hadi wakati huu
alikuwa hafahamu Patrick alikuwa wapi. Kitu fulani kuhusu mapenzi na mwa-
naume huyo kilikuwa kimeanza kujengeka na kufikia hatua kubwa moyoni
mwake kiasi kwamba alianza kuhisi kuichukia dunia endapo huu ungekuwa
ndiyo mwisho wa kuonana kwao.
Baada ya kuvuta kumbukumbu zake taratibu akawa ameikumbuka namba
ya simu ya ile nyumba ya Jean Felix Akaga huku akiamini kuwa endapo Pat-
rick Zambi angekuwa hai na bado yupo jijini Kigali basi kwa vyovyote asin
gesita kwenda kwenye nyumba hiyo kumtafuta. Wazo hilo likamfanya aindee
simu ya mezani iliyokuwa mle ndani sebuleni na kwa muda mfupi akaipiga ile
namba na simu ikaanza kuita upande wa pili.
Mwanzoni Drel Fille alitabasamu baada ya kusikia simu ikiita upande
wa pili lakini muda mfupi baadaye taratibu tabasamu lake likafifia na hati-
maye kukoma kabisa baada ya kurudia mara kadhaa kuipiga simu hiyo bila
kupokelewa. Mwishowe akakata tamaa kabisa na kuurudisha mkonga wa simu
mahala pake kwani kutokupokelewa kwa simu hiyo kulimaanisha hakukuwa
na mtu yoyote ndani ya nyumba hiyo. Akarudia tena kupiga ile namba hata
hivyo simu haikupolewa hivyo hatimaye akakata tamaa kabisa na kusitisha
zoezi hilo.
Drel Fille akiwa amekata tamaa kabisa na matarajio ya kupokelewa kwa
simu yake upande wa pili alirudi na kuketi kwenye kochi mojawapo lililokuwa
pale sebuleni huku kengele ya wasiwasi ikianza kugonga taratibu kichwani
mwake. Akajikuta akijiambia kuwa kuendelea kukaa ndani ya nyumba hiyo
kusingemletea majibu ya maswali yake badala yake alipaswa kuondoka na
kuingia mitaani mahali ambapo aliamini kuwa majibu ya maswali yake mengi
yalikuwa yakimngoja.
Saa ya ukutani pale sebuleni ilionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa
5:00 asubuhi. Kulikuwa na muda wa masaa manne kabla ya muda wa ku-
rudi mwenyeji wake bwana Ghaspard Gahizi kutoka kazini kama alivyom-
taarifu muda wa asubuhi wakati akiondoka. Drel Fille hakupenda Ghaspard
Gahizi amkute ndani ya nyumba hiyo hata hivyo alifahamu kuwa bila ya pesa
asingeweza kufika mbali katika harakati zake. Wazo hilo likamfanya asimame
na kuelekea chumbani kwa Ghaspard Gahizi na kuanza kufanya upekuzi kama
anaweza akapata kiasi chochote cha pesa katika kufanikisha harakati zake.
Alipoifungua droo ya chini ya kabati kubwa la nguo lililokuwa chumbani
humo akakuta bahasha mbili za kaki huku moja ikiwa ametuna zaidi. Ali-
poachana ile bahasha iliyotuna akakuta noti za pesa mpya zilizofungwa vizuri
na bila kuzihesabu akazichukua pesa hizo na kuzitia mfukoni. Bahasha ya pili
haikuwa imefungwa, ilikuwa ndogo kuliko ile ya awali na ndani yake kuli-
kuwa na karatasi. Ingawaje hakuona sababu yoyote ya kutaka kuichunguza
katarasa hiyo hata hivyo Drel Fille hakuona sababu ya kuirudisha karatasi
hiyo huku tayari akiwa ameshaitoa kwenye bahasha yake, hivyo akaifungua
na kuanza kuisoma.
Ilikuwa ni wakati alipokuwa akimaliza kuisoma katarasi hiyo pale alipohisi
mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa hofu. Akarudia kuisoma karatashi hiyo
kwa mara nyingine tena huku akiwa haamini macho yake. Hofu ikiwa imem-
shika Drel Fille akaichukua karatasi ile na kuitia mfukoni kisha akasimama.
Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni kuondoka haraka sana katika nyumba
hiyo na suala la wapi angeelekea baada ya kutoka hilo angelijadili tayari akiwa
mitaani.
Drel Fille alipogeuka na kuanza kuuendea mlango wa kutoka nje ya chumba
kile hapo akajikuta akiishiwa nguvu kwa woga pale macho yake yalipojikuta
yakitazamana na mwenyeji wake Ghaspard Gahizi huku akiwa ameegemea
mlango na mikono yake ameikunjia kifuani, tabasamu lisilo na maana yoyote
likijivinjari usoni mwake.
Lilikuwa ni fumanizi la kipekee ambalo Drel Fille hakuwahi kulitarajia,
moyo wake ukapiga kite kwa nguvu huku jasho jepesi likianza kumtoka usoni.
“Mbona umerudi mapema, nilidhani ungekawia hadi saa tisa jioni kama
ulivyoniaga? akiwa hafahamu nini cha kuongea Drel Fille akauliza huku
akimtazama mwenyeji wake kwa mashaka.
“Hupendi nikiwahi kurudi nyumbani kwangu? Ghaspard Gahizi akaongea
huku akiendelea kutabasamu. Kupitia sauti hiyo Drel Fille akatambua kuwa
mambo yalikwishaharibika kwani mwenyeji wake hakuwa mwenye dalili zo-
zote za furaha kama jana na hata uso wake ulishapoteza nuru. Drel Fille aka-
bakia amesimama huku akishindwa kuelewa kuwa alikuwa ametazamwa kwa
muda gani bila kujijua.
“Unafanya nini chumbani kwangu, nilidhani ningekukuta sebuleni?
“Samahani nilikuwa natafuta sabuni, nataka kufanya usafi”
“Sabuni!,... mbona sabuni zote zipo juu ya sinki jikoni?
“Oh! nilikuwa sijaziona, basi ngoja nikachukue” Drel Fille akadanganya
huku akipiga hatua kuukaribia mlango wa chumba hata hivyo hatua moja tu
aliyoitupa mbele yake akajikuta akitazamana na 38 Semi-automatic bastola
ya Ghaspard Gahizi iliyokuwa mafichoni kwenye koti la suti yake.
“Hauendi popote Drel Fille, unadhani utaendelea kunifanya bwege kwa
kunidanganya kama mtoto”
“Nakudanganya nini?, na mimi siitwi Drel Fille jina langu ni Anne marie”
akiwa na hakika kuwa uongo wake umeishashtukiwa Drel Fille alijitahidi
kuumeza mshtuko aliokuwa nao.
“Usinidanganye wewe si Anne marie, wewe ni Drel Fille na tambua kuwa
taarifa zako zote nazifahamu. Kuanzia sasa upo chini ya ulinzi na usijaribu
kufanya hila yoyote Drel kwani sitakuvumilia. Mwenzako yuko wapi?
“Mbona sikuelewi unazungumza nini na mwenzangu nani unayemzungum-
zia?
“Usijifanye hujui, mwenzako Luteni Venus Jaka mliyetoroka naye kule
pangoni” Ghaspard Gahizi aliongea huku akiangua kicheko cha dharau. In-
gawaje Drel Fille aliendelea kujifanya hafahamu kinachoendelea lakini taarifa
hiyo ilimpa faraja kuwa angalau Patrick Zambi ambaye huenda ndiye angeku-
wa ni huyo Luteni Venus Jaka bado alikuwa hai na watu hawa hadi wakati huu
walikuwa hawafahamu mahali alipo na hapo akajikuta akitabasamu moyoni.
“Huyo Luteni Venus Jaka ni nani mbona mimi simjui na unanihusisha vipi
na yeye? wakati Drel Fille akijitetea Ghaspard Gahizi alikuwa ameyahamisha
kidogo mawazo yake kwa kuanza kulitathmini upyaumbo maridhawa la Drel
Fille lililofichika bila ya mafanikio toshelevu ndani ya blauzi yake nyeupe na
suruali ya jeans iliyolichora vizuri umbo lake lenye kubomoa ukuta wa hisia
wa moyo wowote wa mwanaume aliyekamilika.
Drel Fille alikuwa amevaa nguo hizo toka katika sanduku la nguo lililokuwa
chumbani na Gharpard Gahizi alipozichunguza nguo hizo aligundua kuwa zi-
likuwa ni zile nguo za mkewe waliyeachana. Akawa kama anayeliona umbo la
mkewe katika nguo hizo lakini wakati huu lilikuwa zuri maradufu. Drel Fille
akashtukia kinachoendelea, matiti yake makubwa ya wastani yaliyotuna vizuri
kifuani, kiuno chake chembamba na makalio yaliyoshiba minofu kikamilifu
na kuhifadhiwa na suruali nyepesi ya jeans vikaufanya moyo wa Ghaspard
Gahizi usimame kwa sekunde kama uliopigwa na ugonjwa wa kiharusi kab-
la ya kukusanya nguvu na kuanza kwenda mbio kama kiumbe kilichokoswa
koswa na ajali ya kutisha.
Uzuri wa Drel Fille ulikuwa umeongezeka maradufu kwenye macho
ya Ghaspard Gahizi hata ule mkono wake uliyoshika bastola aliyoilekeza
kwa Drel Fille ukaanza kumsaliti huku akiushusha taratibu kama asiyeona
umuhimu wa kufunya tukio lolote kwa Drel Fille.
“Hebu niambie wewe nani hasa? hatimaye Ghaspard Gahizi akaishusha
bastola yake chini na kuuliza kivivuvivu huku macho yake yakiwa juu ya ki-
fua cha Drel Fille.
“Anne marie, mara hii tu umesahau, jana ulinipa lifti ulipokuwa uki…”
“Oh! nimekumbuka”
Wakatazamana kwa muda huku kila mmoja akizipima hisia za mwenzake.
Drel Fille akatambua kuwa alikuwa hajaonwa wakati alipokuwa akizichukua
zile bahasha mbili kwenye ile droo ya kabati. Akashusha pumzi taratibu kisha
akapiga hatua polepole kumpita Ghaspard Gahizi pale mlangoni akielekea
sebuleni huku akiwa ni mwenye mashaka.
Ghaspard Gahizi akasimama kwa muda kama aliyepigwa na butwaa, uzu-
ri wa Drel Fille ulikuwa umemchanganya kwa namna ya ajabu. Hakuwahi
kuonana na kiumbe cha kike chenye uzuri wa ajabu namna ile tena kikiwa
ndani ya himaya yake.
“Hapana lazima nifanye kitu” Ghaspard Gahizi alijiambia huku akipiga hat-
ua taratibu akimfuata Drel Fille kwa nyuma.
Drel Fille alikuwa amezama katika mawazo mapya kabisa, tabia aliyoio-
na kwa Ghaspard Gahizi ilikuwa tofauti kabisa na siku ya jana wakati wa-
lipoonana kwa mara ya kwanza wakati huo Ghaspard Gahizi akionekana ni
mwanaume muungwana sana. Mabadiliko hayo yakamfanya Drel Fille ahisi
kuwa sasa alikuwa ameingia kwenye ngome ya mtu hatari zaidi na anayemfa-
hamu vizuri kuliko alivyokuwa akidhani. Drel Fille hakutaka kuamini kuwa
uongo wake ulikuwa umeaminika na kukubalika na Ghaspard Gahizi kwani
ulikuwa ni uongo mwepesi na usiokuwa na ushawishi wa kutosha unaoweza
kutungwa na mtu yeyote katika harakati za kujitetea.
Kulikuwa na kitu kimoja tu kilichompelekea Ghaspard Gahizi ampe Drel
Fille nafasi nyingine ya mwisho kabla ya kumtia mikononi na kitu hicho ki-
likuwa ni kiu ya ngono iliyokuwa ikizitafuna hisia zake. Akakumbuka nam-
na suruali yake ilivyotuna ghafla wakati alipokuwa akimtazama Drel Fille na
hapo akajikuta akitabasamu.
Drel Fille hakuwa na hakika kama nafasi ya kujiokoa kama hii ingejitokeza
tena endapo angechelewa kufanya maamuzi hivyo alipanga namna ya kum-
maliza haraka Ghaspard Gahizi kabla ya kutoweka haraka katika nyumba
hiyo. Hivyo bila papara aliamua kutulia akiisubiri nafasi hiyo.
Maneno ya Meja Jean Bosco Barayagwiza kwenye kikao kilichofanyika
muda mfupi uliyopita kuwa msaliti wa namna yoyote ambaye atahusika katika
kumficha adui kwa maslahi anayoyajua yeye basi mtu wa namna hiyo adhabu
yake ingekuwa ni kifo yakaanza kupita taratibu kichwani mwa Ghaspard Ga-
hizi na kumfanya ajihisi kuwa alikuwa akijitengenezea kifo kwa kumuhifadhi
msichana huyu mbele yake. Hata hivyo Ghaspard Gahizi hakutaka Drel Fille
ampite hivihivi ilhali yupo chini ya himaya yake hivyo akapanga kumfanyika
starehe ya namna fulani kabla ya kumkabidhi kwa Meja Bosco Barayagizwa
na jopo lake.
“Nahitaji kuongea na wewe tafadhali hebu keti kwenye kochi” Ghaspard
Gahizi alimwambia Drel Fille huku akijidai kuwa amekubaliana na uongo wa
Drel Fille, Drel Fille akasimama na kugeuka.
“Kuna nini?
“Njoo” Ghaspard Gahizi akaongea kwa kujiamini. Drel Fille akatupa hatua
zake taratibu akielekea sebuleni na alipofika akajikuta akitazamana na mtu-
tu wa bastola ya Gashpard Gahizi. Drel Fille alipomtazama Ghaspard Gahizi
usoni akaona kuwa macho ya Gashpard Gahizi yalikwisha badilika, kiu ya
ngono ilikuwa imefika ukomo katika uvumilivu wake.
“Nakujua vizuri kuwa wewe ndiye Drel Fille usidhani kuwa nimekubaliana
na uongo wako wa kitoto. Hata hivyo wewe ni mzuri Drel na hakuna mwana-
ume anayeweza kukuacha hivihivi bila ya kukugusa katika himaya yake. Anza
kuvua nguo na usijidanganye kufanya hila yoyote, kumbuka ninayo bastola
mkononi” Ghaspard Gahizi aliongea huku akiiendea simu ya mezani lakini
mtutu wa bastola yake bado ukiwa unamtazama Drel Fille. Alipoifikia ile
simu akabonyeza vitufe vya tarakimu fulani na muda mfupi baadaye alikuwa
hewani akiongea na mtu wa upande wa pili.
“Meja, watume watu wako waje hapa nyumbani kwangu kumchukua Drel
Fille, nimeshamtia mikononi” halafu maongezi kidogo yakafuatia kabla ya
kuikata simu hiyo na kuirudisha mahala pake. Ghaspard Gahizi alipogeuka
kumtazama Drel Fille akamuona kuwa tayari alikuwa ameshavua nguo zake
zote na hapo ikabaki kidogo bastola imdondoke mkononi kwa jinsi alivy-
oshangazwa na uzuri wa Drel Fille. Bila kuchelewa Ghaspard Gahizi naye
akaanza kuvua nguo zake kwa papara, akaanza kuvua koti lake la suti, tai,
shati, mkanda, suruali na kumalizia na nguo yake ya ndani ikivitupilia mbali
kisha akaanza kuzitupa hatua zake taratibu kumkaribia Drel Fille huku bastola
yake ikiwa mkononi.
“Usijali Drel wala haitochukua muda mrefu nahitaji ushirikiano wako tu na
usijidanganye kufanya hila yoyote kwani sitokuvumilia”
Drel Fille akatikisa kichwa kuonesha kukubaliana na onyo hilo. Ghaspard
Gahizi alipomfikia Drel Fille akaanza kumpapasa kwa pupa huku kiu ya ngono
ikionekana kumfika kikomo. Bila ya kuchelewa akamkokota Drel Fille hadi
kwenye kochi refu lililokuwa pale sebuleni na walipofika akamwambia Drel
Fille alale chali. Bila upinzani wowote Drel Fille akafanya kama alivyoambi-
wa akapanda kwenye kochi na kulala chali huku akitanua miguu. Mpaka hapo
Ghaspard Gahizi hakuweza kuvumilia zaidi akaanza kupanda juu ya kifua
cha Drel Fille hata hivyo bahati haikuwa kwake kwani Drel Fille aliizungusha
miguu yake nyuma ya mgongo wa Ghaspard Gahizi na kumpiga kabari ya
tumbo kwa nguvu zake zote.
Ghaspard Gahizi hakuamini kilichokuwa kikimtokea, akajitahidi kufuruku-
ta huku akitaka kufyatua risasi hata hivyo Drel Fille alikuwa mwepesi kush-
tukia tukio hilo. Hivyo kwa mkono wake wa kushoto akaubana ule mkono
wa Ghaspard Gahizi uliyoshika bastola na kuukandamizia pembeni ya kochi
na hapo risasi zilizofyatuliwa zikapoteza shabaha. Moja ikachimba chini ya
sakafu ya pale sebuleni na risasi nyingine ikaparaza juu ya meza ya chakula
iliyokuwa pale sebuleni na kupasua kioo cha dirisha.
Hata hivyo, Drel Fille alikuwa mwepesi, akaupiga ule mkono wa Ghaspard
Gahizi ulioshika bastola na bastola ikamponyoka na kuangukia sakafuni upa-
nde wa pili wa kochi halafu kwa kasi ya ajabu Drel Fille akakunja goti lake na
kuachia pigo la goti kwenye korodani za Ghaspard Gahizi na hapo Ghaspard
Gahizi akapiga yowe kali la maumivu huku akiiachia mikono ya Drel Fille
aliyokuwa ameikandamiza kwenye kochi na hilo likawa kosa kubwa kwani
muda huohuo Drel Fille akaifyatua ile kabari ya tumbo na kuihamishia shin-
goni kwa Ghaspard Gahizi.
Ilikuwa kabari matata na safari hii Ghaspard Gahizi hakuweza kufurukuta
tena, macho yakamtoka, akabakia akirusharusha mikono na miguu huku na
kule. Drel Fille akatumia nafasi hiyo kujigeuza na kukaa juu ya Ghaspard Ga-
hizi na hapo akaachia ngumi mbili zilizotua usoni mwa Ghaspard Gahizi na
kuuchakaza vibaya uso wake. Ghaspard Gahizi akapata nafasi kidogo ya ku-
furukuta na kupiga yowe kali la maumivu na wakati akifanya hivyo Drel Fille
akatumia nafasi hiyo kujirusha toka pale kwenye kochi na kuifuata ile bastola
ya Ghaspard Gahizi iliyoangukia sakafuni. Ghaspard Gahizi aliponyanyuka
akajikuta akitazamana na mtutu wa bastola hiyo.
“Usijaribu kusogea hata hatua moja nitakufyeka” Drel Fille akamuonya
Ghaspard Gahizi huku Ghaspard Gahizi akiwa aamini macho yake.
“Weka bastola chini Drel Fille mimi na wewe ni marafiki haya yote yanato-
ka wapi mpenzi?
“Tulia hapo hapo mwanaharamu mkubwa we!, haya niambie unafahamu
nini kuhusu mimi”
“Wewe na Luteni Venus Jaka ndiyo mnaoharibu mipango yetu”
“Mipango gani?
“Sijui kitu, mimi ni mtu wa kati tu na anayefahamu kila kitu ni Meja Jean
Bosco Barayagizwa”
“Meja Jean Bosco Bayaragwiza !... yeye ni nani?
“Kiongozi wetu wa Interahamwe” Ghapard Gahizi akaongea kwa hofu.
Drel Fille akaweka kituo kidogo akitafakari maneno hayo kabla ya kuendelea.
“Intarehamwe wana shida gani na mimi na huyo Luteni Venus Jaka?
“Nilivyosikia ni kuwa nyinyi mnaharibu mipango ya Interahamwe na hiyo
mipango anayeijua ni Meja Jean Bosco Barayagwiza” Ghaspard Gahizi alijite-
tea huku macho yake yakiwa kwenye mtutu wa bastola.
Drel Fille akayapima maneno ya Gharpard Gahizi na kutambua kuwa yali
kuwa yenye ukweli wa moja kwa moja na hapo akaingiza mkono mfukoni na
kuichukua ile karatasi iliyokua kwenye ile bahasha mojawapo aliyoichukua
kule chumbani kisha akaifungua na kuisoma kidogo kisha akamtazama tena
Ghaspard Gahizi.
“Mlikuwa mna mkutano gani leo? Drel Fille akauliza
“Mkutano?
“Ndiyo, barua hii inaeleza kuwa leo mlikuwa na mkutano’’ maneno ya Drel
Fille yakampelekea Ghaspard Gahizi ataharuki na kama aliyejisahau akaan-
za kupiga hatua kumkaribia Drel Fille lakini hatua hiyo haikukamilika kwani
mtutu wa bastola ya Drel Fille ukamuonya kuwa asimame.
“Jibu swali langu”
“Mimi sijui lolote” Ghaspard Gahizi akajitetea na hapo Drel Fille akairuhu-
su risasi moja kuuvunja mfupa wa mguu wa kushoto wa Ghaspard Gahizi
na hapo Ghaspard Gahizi akapiga yote kali la maumivu huku akivuja damu
nyingi kwenye jereha.
“Usinue tafadhali nitakueleza”
“Haya nieleze”
“Tarehe sita mwezi wa nne mwaka…” kabla ya Ghaspard Gahizi hajamal-
iza Drel Fille akashangaa kumuona akitupwa hewani mzima mzima huku
akipiga yowe kali la maumivu na hapo Drel Fille akajua nini kilichokuwa
kikiendelea.
Lilikuwa shambulio la risasi iliyofyatuliwa kupitia dirishani hivyo Drel
Fille akawahi kujitupa sakafuni karibu na pale alipozivua nguo zake na hapo
akazichukua na kwenda kujibanza nyuma ya kochi moja la pale sebueni.
Kwa muda mfupi Drel Fille akawa amemaliza kuzivaa zile nguo zake na
alipomtazama Ghaspard Gahizi pale alipoangukia hakuona dalili yoyote ya
kujitikisa kwake na shingo yake ilikuwa imeharibiwa vibaya kwa lile shambu-
lio la risasi. Damu nyingi ilikuwa ikiendelea kutoka kwenye lile jereha la risasi
na hapakuwa na dalili zozote za uhai katika mwili wake.
Lile shambulizi la risasi kupitia pale dirishani likawa likiendelea mle ndani
hata hivyo risasi hizo zilikuwa zikifyatuliwa ovyo bila mlengaji kuzingatia
shabaha. Hata hivyo yule mtu aliyekuwa akifyatua risasi hizo hakuonekana
badala yake ulionekana mtutu na bastola tu ukitema cheche dirishani. Drel
Fille akajilaza chini sakafuni na kumbaa taratibu akipita nyuma ya makochi
kuliendea lile dirisha na alipofika kupitia kioo cha dirisha lile kilichokuwa
wazi aliweza kumuona yule mtu aliyekuwa akifyatua risasi ovyo mle ndani.
Drel Fille akanyanyuka ghafla na kufanya shambulizi moja na bila kufanya
makosa risasi moja aliyoifyatua ikakifumua kichwa cha yule mtu na muda
huo huo ile mirindimo ya risasi ikakoma.
Bila kupoteza muda Drel Fille akasimama na kulichunguza eneo lile nje
ya ile nyumba kupitia dirishani. Hali bado ilikuwa poa na hapakuwa na dalili
yoyote ya kuwepo kwa kiumbe hai kingine nje ya nyumba ile ingawaje hali
hiyo bado haikumpelekea aamini haraka kuwa alikuwa salama.
Drel fille akaliacha lile dirisha na kwa tahadhari akakatisha pale sebuleni
akielekea jikoni na alipofika akafungua mlango wa jikoni uliyokuwa nyuma
ya nyumba ile na kutoka.
Ilikwa ni wakati Drel Fille alipokuwa akiingia barabara ya mtaa wa pili
pale alipopishana na gari aina ya Landcruiser ya jeshi ikiwa na watu wanne
ndani yake na watu wote wakiwa na silaha zao mikononi. Drel Fille akashuku-
ru Mungu kwa kuwakuta watu wengi wakiwa kwenye barabara hiyo kiasi cha
kumfanya asiweze kutambulika kirahisi. Akatabasamu kidogo huku akiongeza
hatua zake na kutokomeza mitaani.
“UNAJISIKIAJE KWA SASA? nilimuuliza kwa kifaransa changu cha
kubabaisha huku moyoni nikifurahi kwa kumuona amerudiwa na fahamu zake
vizuri.
“Wewe ni nani? Dr. Lisa akanitupia swali na kulipuuza lile langu huku ame-
shikwa na taharuki. Nikatabasamu kidogo nikijaribu kuitowesha hofu aliy-
okuwa nayo kisha nikakisogeza kiti changu nilichokikalia karibu na kitanda
chake.
“Tafadhali niambie wewe ni nani? akarudia kuniuliza huku akinitazama kwa
mshangao.
“Naitwa Luten Venus Jaka wa jeshi la wananchi wa Tanzania” nilimwambia
huku nikiendelea kutabasamu na kama ambaye hajanisikia vizuri akayakaza
macho yake kunitazama. Macho yangu yalipokutana na yake nikaweza kuuso-
ma wasiwasi aliyokuwa nao.
“Usiwe na hofu daktari upo sehemu salama na nimefurahi kukuona umer-
udiwa na fahamu baada ya lile shambulio la risasi kule hospitali” Dr. Lisa
akayazungusha macho yake na kunitazama kama awali hata hivyo nilipom-
chunguza nikatambua kuwa alikuwa akijaribu kuvuta kumbukumbu na muda
mfupi uliofuata akaachama mdomo wake wazi kwa mshangao.
“Oh my God!... ilikuwaje? akaniuliza huku akiushika na kuuvuta mkono
wangu karibu yake.
“Ni hadithi ndefu kidogo” nilimwambia huku nikianza kumsimulia taratibu
mlolongo mzima wa matukio hadi tulivyofika ndani ya nyumba hii. Nilipo-
maliza nikamuona akishusha pumzi taratibu kama aliyepumzisha fikra zake.
“Naomba maji ya kunywa” hatimaye akaniamba na hapo nikasogeza jagi
la maji lililokuwa kwenye meza pembeni ya kitanda na kumimina kwenye
bilauri kisha nikamnywesha maji taratibu hadi pale aliponiashiria kutosheka.
Alipomaliza akajisogeza vizuri na kukiegemeza kichwa chake kwenye mto
wa kitanda.
“Luteni...”
“Venus Jaka” nikamalizia.
“Hebu niambie vizuri bila kificho, unashida gani na mimi? Dr. Lisa akani-
uliza na hapo nikakohoa kidogo nikamtazama kwa uyakinifu kabla ya kuvunja
tena ukimya.
“Nahitaji unisaidie kumpata Jaji Makesa” nilimwambia kwa utulivu.
“Jaji Makesa!...unamaanisha nini mbona sikuelewi? aliniuliza kwa mshan-
gao hata hivyo niligundua kuwa maneno yake hayakumaanisha hivyo nikam-
katazama huku nikitabasamu.
“Nisingekufahamu kama nisingekutana na Dr. François Tresor” nilimwam-
bia na hapo nikamuona akinikazia macho
“Ni yeye aliyeniambia kuwa nikutafute wewe huku akinisisitiza kuwa ni
wewe ndiye utakayenisaidia kumpata Jaji Makesa na ndiyo maana nipo na
wewe muda huu” niliweka kituo huku nikimtazama Dr. Lisa
“Wewe ulimfahamu vipi Dr. François Tresor?
“Nilikutana naye ndani ya mapango ya Musanze, unayafahamu? nilimuuliza
kisha pasipo kusubiri jibu lake nikaanza kumsimulia kila kitu kilichotokea
kule mapangoni na nilipofika katika maelezo ya kuuwawa kwa Dr. François
Tresor nilimuona Dr. Lisa Oliver namna alivyohuzunika. Nikamfariji na hati-
maye nikamalizia kwa kumueleza namna nilivyofanikiwa kutoroka hadi kum-
tafuta yeye. Kwa kweli nilimuona namna alivyo kata tamaa na hapo nikajua
kuwa habari za kifo cha Dr. François Tresor zilikuwa zimemhuzunisha sana.
“Nahitaji unisaidie kumpata Jaji Makesa na ninaamini kuwa ni wewe tu
ndiye unayeweza kunisaidia”
“Unamuhitaji Jaji Makesa wa nini?
Nikiwa nimetarajia swali la namna hiyo nikatabasamu kidogo kabla ya
kuanza kuongea.
“Nipo hapa nchini Rwanda kufuatilia juu ya kifo cha mwandishi wa habari
mtanzania ndugu Tobias Moyo aliyeuwawa katika mazingira ya kutatanisha.
Ninachofanya hapa ni kutafuta ukweli wa kujiridhisha juu ya ripoti iliyotum-
wa nchini kwangu na maafisa wa usalama wa nchi ya Rwanda na katika kufan-
ya hivyo hapo ndipo uwepo wa Jaji Makesa unapohitajika. Dr. François Tresor
aliniambia kuwa Jaji Makesa anaweza kunisaidia kupata taarifa hizo kwani ni
yeye ndiye aliyekuwa akiufahamu ukweli wa mambo huku akinisisitiza kuwa
ni wewe ndiye unayeweza kunisaidia kumpata huyo Jaji Makesa”
“Wewe ni mpelelezi? Dr. Lisa aliniuliza huku akinitazama kwa mshangao.
“Unaweza kuniita hivyo kama utapenda” nilimwambia huku nikitabasamu.
“Labda ungeenda kwenye maonesho ya mitindo ya mavazi ungekuwa na
mafanikio zaidi, you look so handsome guy. Kwa nini ukaamua kuwa mpelelezi
Luteni? swali la Dr. Lisa likanifanya nitabasamu kidogo huku nikigeuka kuta-
zama dirishani na nilipoyarudisha macho yangu kwake nikamwambia.
“Nilianza kuwa mpelelezi hodari ndiyo baadaye nikawa mzuri wa sura na
kwa hiyo uzuri wangu hauna maana yoyote kwangu mbali na ile ya kuwafikia
warembo kwa urahisi” nilimuona Dr. Lisa akitabasamu kidogo na kisha ta-
basamu lake likatoweka haraka.
“Natambua sana kuwa tupo kwenye basi linaloelekea sehemu moja na tofau-
ti yetu ipo kwenye viti vya basi hilo, pengine mmoja yupo mbele na mwingine
nyuma au huyu upande huu wa basi mwingine upande ule” Dr. Lisa alivun-
ja ukimya huku uso wake ukionesha dalili zote za matumaini. Sikumuelewa
kuwa alimaanisha nini hata hivyo nilitambua kuwa alikuwa tayari kunipa ush-
irikiano.
“Tangu sasa niite Dr. Amanda Albro, mimi ni mpelelezi kama wewe na nipo
hapa nchini Rwanda kufanya kazi kama yako. Tofauti ni kwamba mimi si-
kufika hapa kutafuta majibu ya kujiridhisha juu ya ripoti iliyotumwa nchini
kwangu hata hivyo hiyo ni sehemu tu ya mambo ninayoyachunguza. Taaluma
yangu mimi ni daktari na nipo hapa nchini Rwanda chini ya tume huru ya
shirika la haki za binadamu ama Human Right Watch barani Afrika”
Nilimtazama Dr. Lisa na kutabasamu huku nikamwashiria kuwa tupo pamo-
ja hivyo aendelee kunisimulia.
“Mimi na Dr. François Tresor sote ni wapelelezi na wanajeshi wa jeshi la
Ufaransa ingawaje tuliamua kuacha kazi hiyo na kujiunga na shirila hili la haki
za binadamu lakini kila mmoja kwa wakati wake. Mwanzoni sikujua sababu
iliyompelekea Dr. François Tresor kujiunga na shirika hili la haki za binadamu
lakini kwa sasa naweza kuanza kuzihisi sababu hizo kwa umakini zaidi kuliko
hapo awali ingawaje mimi binafsi sababu iliyonifanya niache kazi na kujiunga
na shirika hili ni kwa sababu ya kuguswa sana na matatizo ya bara la Afri-
ka, kama vita vya udini na ukabila na vita vya kugombea madaraka ambavyo
kwa pamoja vimepelekea upotevu mkubwa wa maisha ya watu wasio na ha-
tia, uharibifu wa mali, milipuko ya magonjwa, uvunjifu mkubwa wa haki za
binadamu na hatimaye kupelekea hali ya umasikini uliokithiri.
Matatizo hayo kwa pamoja ndiyo yaliyonipelekea kuacha kulitumikia jeshi
la nchi yangu na kujiunga na shirika hili la haki za binadamu duniani huku ni-
kiamini kuwa pengine mchango wangu ungeweza kuleta mabadiliko na kuifa-
nya Afrika iwe sehemu salama kuishi. Hata hivyo nimegundua kuwa si rahisi
kama nilivyodhani”
“Kwanini inasema hivyo?
“Kwa kipindi changu chote hapa barani Afrika nimegundua kuwa matatizo
mengi ya nchi za bara la Afrika yanafanana vilevile yanachangiwa kwa kiasi
kikubwa na waafrika wenyewe, machache kwa kutokujua na wengi wakiwa
wanafahamu chimbuko la matatizo hayo. Kabla ya kuja hapa Rwanda niliku-
wa nchini Sierra Lione nikifuatilia namna viongozi wa nchi hiyo walivyokuwa
vinara katika kufanya biashara ya silaha na baadhi ya nchi za magharibi. Silaha
ambazo kwa upande wa pili ndiyo zinazotumika kuwaua waafrika wenyewe
kwa uroho wa madaraka. Ndiyo kisa almasi zilizokuwa zikitoka nchini Sierra
Lione zikaitwa almasi za damu kwenye soko la almasi la kimataifa kwani
damu nyingi ya raia wasio na hatia ilikuwa ikimwagika katika upatikanaji
wake. Damu za watoto wadogo wanauwawa wakitumikishwa katika vita bila
ya wao kupenda, damu ya wanawake wanaobakwa vitani na ile damu ya watu
wanaouwawa wakitumikishwa katika kuchimba almasi hizo migodini.
Nilipofika nchini Angola hali ilikuwa hivyohivyo katika mgodi wa Catoca
, Facauma na Luarica” Nilimtazama Dr. Amanda Albro ambaye sasa nilik-
wishamzoea kwa jina la Lisa Olivier na hapo nikaelewa kuwa alikuwa kiongea
katika hali ya uchungu mkubwa juu ya bara la Afrika hali iliyonifanya nihisi
kuwa nilikuwa karibu na mwafrika mwenzangu tena mzalendo wa hali ya juu.
“Mchango wako upo wapi sasa katika kuisaidia Afrika? nilimuuliza na hapo
nikamuona akishtuka na kunitazama kama mtu anayenishangaa kwa kutokuwa
mwepesi wa kumuelewa.
“Pengine usiweze kuuona mchango wangu lakini upo na ni mkubwa sana
kuliko unavyodhani. Katika nchi hizo nilizokutajia ambazo nilipata nafasi
ya kufanya kazi hapa barani Afrika nikiwa kama mjumbe wa siri wa Human
Right Watch wakati huo nikiutumia mwamvuli wa daktari wa kujitolea.
Kazi yangu imekuwa ni kufanya uchunguzi wa matukio mbalimbali ya
uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi hizo pamoja na kukusanya ushahidi
wa vielelezo vya kutosha.
Ninapopata vielelezo vya ushahidi unaojitosheleza huwa nativuma kwa siri
kwenda makao makuu ya ofisi za shirika la haki za binadamu Human Right
Watch huko New York Marekani ambapo vielelezo hivyo vya shahidi vime-
kuwa vikifanyiwa kazi”
“Kuna mafanikio yoyote ambayo yamewahi kupatikana kupitia kazi un-
ayoifanya?
“Mafanikio yapo ingawaje wakati mwingine mtu wa kawaida anaweza asi-
yaone kwa haraka lakini mimi ninayeifanya kazi hiyo nayaona. Kwa mfano
kupitia vielelezo mbalimbali vya ushahidi ninaoutuma kesi mbalimbali zime-
funguliwa dhidi ya wavunjifu hao wa haki za binadamu katika mahakama
ya kimataifa (ICJ) International Court of Justice iliyopo The Hague nchini
Uholanzi. Mfano mmojawapo ni kesi dhidi ya viongozi wa kikundi cha waa-
si cha The Revolutionary United Front(RUF) cha nchini Sierra Lione, Foday
Saybana Sankoh, Issa Hassan Sesay, Morris Kollon na Agostine Ghabo. Vion-
gozi washiriki wakubwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo
ambapo kupitia vielelezo vya ushahidi wangu viongozi hao wamefunguliwa
mashtaka na kuhukumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita kama mauaji, uba-
kaji, utumwa wa ngono, ndoa za kulazimishwa na upotevu wa amani.
Vielelezo vingine ni vile vilivyowatia hatiani viongozi wa kikundi cha waasi
cha UNITA nchini Angola, Jonas Savimbi, Isaias Samakavu na wengine kwa
tuhuma kama hizo za uhalifu wa kivita na za kuhusika na mauaji ya raia zaidi
ya 50,000 wasio na hatia.
Kwa mifano hii michache niliyokupa unaweza kupata picha ya ni kwa
namna gani kazi yangu pamoja na wenzangu ninaoshirikiana nao imekuwa
na msaada mkubwa katika jitihada za kuelekea kupatikana kwa amani katika
baadhi ya nchi za Afrika zenye machafuko” Dr. Amanda Albro aliweka kituo
na kunitazama. Kwa kweli maelezo yake yalinifurahisha sana, nikamtazama
huku nikiendelea kutabasamu huku nikufurahi kukutana na mzungu wa kwan-
za katika maisha yangu mwenye uchungu na bara la Afrika.
“Kazi yako ni nzuri sana na huna budi kupongezwa Dr. Amanda Albro”
hatimaye nilimwambia huku nikimuona ni mwanamke jasiri sana mwenye
uzalendo wa kipekee na bara la Afrika. Hata hivyo Dr. Amanda Albro ha-
kuonesha tashwishwi yoyote badala yake alitikisa kichwa tu na kutabasamu
kisha akatulia na kunitazama.
“Hebu turudi kwa Dr. François Tresor, kwa mujibu wa maelezo yako ume-
niambia kuwa mlikuwa mkifanya kazi pamoja sivyo?
“Ndiyo”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Hebu nifafanulie vizuri ulikuwa ukimaanisha nini pale uliposema kuwa
mwanzoni hukufahamu sababu zilizompelekea Dr. François Tresor aache kazi
yake ya uaskari katika jeshi la taifa la ufaransa na kujiunga na shirika la haki
za binadamu ‘Human Right Watch’ lakini kwa sasa unazihisi kwa makini saba-
bu zilizompelekea ajiunge na shirika hili, unahisi ni sababu zipi hizo?
“Kuna matukio mengi sana ambayo nikiyajumuisha kwa pamoja naanza
kupata picha tofauti inayonifanya nianze kuhisi kuwa Dr. François Tresor
hakujiunga na shirika la haki za binadamu duniani ‘Human Right Watch’
akisukumwa na sababu kama zangu isipokuwa nahisi alikuwa na nia yake to-
fauti kabisa na nia hiyo nahisi ni maslahi na kusaka utajiri kiurahisi kutoka
katika bara hili”
“Kwa vipi useme hivyo?
“Mara kwa mara nilipokuwa naye pamoja tukitafuta ushahidi au taarifa
muhimu kuhusiana na kazi yetu katika hizo nchi nilizokutajia nilikuwa ni-
kimuona Dr. François Tresor akijiimarishia urafiki zaidi na viongozi wa vi-
kundi vya waasi waliokuwa wakishughulika na biashara za madini. Hali hiyo
ilikuwa ikinitia mashaka sana na mara nyingi nilikuwa nikimuonya juu ya
ukaribu na watu hao hata hivyo alikuwa akinitoa hofu kuwa ukaribu wake na
watu hao ulikuwa ni njia rahisi ya kupata taarifa muhimu tulizokuwa tukizita-
futa.
Dr. François Tresor alikuwa ni mtu mwenye ndoto za utajiri sana. Nilim-
tambua hivyo kutokana maongezi yake na ndoto zake zilikuwa kwenye madini
kwani mara kwa mara nilikuwa nikimsikia akiyazungumzia”
“Unadhani hiyo inaweza ikiwa ni sababu iliyompelekea Dr. François Tresor
kutekwa na kupelekwa kule mapangoni nilipokutana naye?
“Inawezekana kabisa”
“Kwanini unadhani hiyo huenda ndiyo ikawa sababu?
“Wiki mbili zilizopita alikuwa ameanzisha urafiki na kamanda mmoja wa
jeshi la wananchi wa Rwanda ambaye alikuwa akija mara kwa mara kule hos-
pitali ambapo kwa pamoja walikuwa wakifanya maongezi marefu na ya siri
katika ofisi ya Dr. François Tresor na baadaye wakiondoka wote nyakati za
jioni”
“Uliwahi kusikia chochote walichokuwa wakikizungumza?
“Haikuwa rahisi kuwasikia kama unavyodhani. Kama nilivyokwambia ma-
ongezi yao walikuwa wakiyafanyia ndani ya ofisi ya Dr. François Tresor na
mimi na yeye tulikuwa hatushirikiani ofisi ingawaje nilihisi kuwa kulikuwa
na jambo fulani walilokuwa wakilipanga”
Dr. Amanda Albro alipoweka kituo nilimtazama katika namna ya kuyata-
fakari maongezi yake kabla hajakohoa kidogo na kuendelea tena
“Siku mbili baadaye nilipoonana na Dr. François Tresor muda wa asubuhi
wakati nilipokuwa nikiingia kazini nilimuona kuwa hakuwa ni mtu mwenye
furaha kama nilivyomzoea ingawaje nilipomuuliza aliniambia kuwa nisiwe na
wasiwasi. Jioni ya siku ile wakati nilipokuwa naelekea ofisini kwake kujad-
iliana masuala fulani ya kazi yetu, nilipoukaribia mlango wa ofisi yake nilim-
sikia Dr. François Tresor akiongea na simu ya mezani ya ofisini kwake na mtu
fulani aliyekuwa upande wa pili. Nahisi mtu huyo aliyekuwa akiongea naye
kwenye simu huenda alikuwa ni yule kamanda wa jeshi la wananchi wa Rwan-
da aliyekuwa akifika pale hospitali na kuonana naye mara kwa mara. Hata
hivyo maongezi yale kwenye simu hayakuwa ya kirafiki kama nilivyozoea
kuwasikia hapo siku za nyuma”
“Unaweza kuhisi walikuwa wakizungumzia nini?
“Sikuweza kuwasikia vizuri ila ni kama waliokuwa wakirushiana maneno.
Nilimsikia Dr. Francos Tresor akisisitiza kuwa hawezi kumpa kitu fulani huyo
mtu aliyekuwa akiongea naye kwenye simu mpaka na yeye apewe kitu fu-
lani alichokuwa akikihitaji kutoka kwa mtu huyo. Hata hivyo sikuweza kuhisi
kitu hicho kilikuwa kitu gani labda pengine ningeweza kusikia zaidi lakini Dr.
François Tresor aliwahi kukata simu haraka pale alipouhisi uwepo wangu nje
ya mlango ule wa ofisi yake.
Nilipoingia ndani sikutaka kumuuliza chochote kwani nilihisi kuwa
asingekuwa tayari kunieleza hivyo nikatanguliza mbele hoja yangu ingawaje
niligundua kuwa kisaikolojia Dr. François Tresor hakuwa sawa na jioni ile tu-
lipoagana ndiyo ikawa mara yangu ya mwisho kuonana naye. Sikuonana naye
tena hadi pale wewe uliponiletea taarifa za kifo chake” Dr. Amanda Albro
aliweka kituo na nilipomtazama usoni nikayaona machozi yakimlengalenga
na sura yake ilikuwa imejawa sana na huzuni. Hata hivyo kama zilivyo tabia
za wapelelezi wengi hakuyaruhusu machozi yake kumtoka.
Ukimya ulifuata nami nikifikicha macho yangu kuyapa uhai lakini wakati
huohuo nikijaribu kuitowesha taswira ya Dr. François Tresor wakati ule ali-
pokuwa akifyatuliwa risasi na kurushwa hewani kule pangoni.
Sasa kichwa changu kilikuwa mbioni kuelemewa na mawazo chungu mzi-
ma hata hivyo maelezo ya Dr. Amanda Albro yalikuwa yamenipa mwanga fu-
lani na kama ilivyokuwa kwake na mimi pia nilianza kuhisi kuwa Dr. François
Tresor hakuwa mwaminifu katika kazi yake na tamaa ya kupata utajiri kutoka
bara la Afrika ilikuwa ni dhambi iliyokuwa ukimuandama kwa muda mrefu.
“Kabla ya kifo chake Dr. François Tresor aliniambia kuwa sababu iliyom-
pelekea yeye kutekwa na kupelekwa kule mapangoni ni yeye kutaka kujua
ni nani aliyemtorosha Jaji Makesa katika wodi ya wagonjwa mahututi kule
hospitali ambapo kwa pamoja mlikuwa mkishirikiana kuyaokoa maisha ya
Jaji Makesa baada ya kufikishwa hospitalini hapo na msamaria mwema. Huku
msamaria huyo akidai kuwa aliwaokota njiani Jaji Makesa na mkewe wakiwa
wameshambuliwa vibaya na watu wasiofahamika. Ambapo mkewe alifariki
muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo”
Wakati nikimaliza kuongea nilimuona Dr. Amanda Albro alikitikisa kichwa
chake akionesha kutokukubaliana na maongezi yangu
“Huo ni uongo mkubwa kwani mimi na yeye hatukuwahi kupokea wag-
onjwa wa aina hiyo, kwanza mimi na yeye tulikuwa madaktari katika idara
tofauti kabisa. Yeye ni daktari bingwa wa mifupa na mimi ni daktari bingwa
wa magonja ya wanawake hivyo kwa pamoja hatuwezi kuingia chumba cha
wagonjwa mahututi labda itokee kitu cha kipekee sana kitakachotukutanisha.
Hivyo huo ni uongo na sijui ni kwa nini amekudanganya”
“Kwa hiyo Dr. François Tresor amenidanganya?
“Kabisa kwani huo wote ni uongo”
Niliinamisha kichwa changu na kushusha pumzi taratibu nikijaribu kui-
pumzisha akili yangu huku nikijihisi mgonjwa wa mawazo, akili yangu iliku-
wa mbioni kuchoka. Nikainua macho yangu tena na kumtazama Dr. Amanda
Albro nikiwa kama sanamu huku taratibu nikizilowanisha papi za mdono wan-
gu kwa ulimi.
“Unawaza nini? Dr. Amanda Albro akaniuliza kama mtu anioneaye huruma.
“Najaribu kutafuta sababu zilizomfanya Dr. François Tresor anidanganye,
lakini nijuavyo mimi ni kuwa mtu hawezi kujiongezea dhambi ya uongo kira-
hisi hadi pale uongo wake uonekane kuwa na maslahi fulani kwake, lakini
siwezi kufahamu ni maslahi gani wakati alikuwa na hakika kuwa maisha yake
yalikuwa yamefika ukingoni” nilijikuta nikijisemea mwenyewe.
“Usikate tamaa Luteni hebu jaribu kutulia chini na kutafakari huenda
ukapata majibu ya maswali yako” maneno ya Dr. Amanda Albro yalinifariji
na hapo nikainua tena macho na kumtazama huku nikilazimisha tabasamu
ambalo kwa hakika halikuwa kwenye nafsi yangu.
“Kimbilio pekee sasa lililobakia kwangu ni kukutana na Jaji Makesa kwani
bila shaka huyo ndiye mtu anayeweza kunitegulia kitendawili changu. Usin-
iambie kuwa hata huyo Jaji Makesa ni mtu wa kufikirika? nilimuuliza Dr.
Amanda Albro katika namna ya kuirudisha hali nzuri ya maongezi na Dr.
Amando Albro akatabasamu.
“Ondoa shaka, Jaji Makesa yupo ingawaje sidhani kama ni rahisi sana
kumpata”
“Una maana gani?
“Jaji Makesa ni mtu anayetafutwa sana hapa nchini Rwanda mimi na Dr.
François Tresor tulipata nafasi moja tu ya kuonana naye hata hivyo haikuwa
na faida sana”
“Anatafutwa na nani na kwa sababu gani? nilimuuliza Dr. Amanda Albro
na hapo nikamuona ni kama anayenishangaa kwa kumuuliza swali kama lile.
“Jaji Makesa ni jaji mashuhuri sana hapa Rwanda na umashuhuri wake
umetokana na uwezo wake mkubwa wa kuikosoa serikali katika masuala
mbalimbali pale inapoonekana kukengeuka. Pia Jaji Makesa amekuwa mstari
wa mbele katika kuwakosoa viongozi mbalimbali wa kisiasa pale wanap-
oonekana kutanguliza kwanza maslahi yao na siyo ya kitaifa.
Kwa tabia yake hiyo amejikuta akijenga uadui na pande hizo mbili laki-
ni wakati huo huo akijizolea umaarufu na kupendwa sana na wanyarwanda
wengi. Mara ya kwanza wakati tulipokuwa tukifika hapa nchini Rwanda tu-
lielekezwa kukutana na jaji Makesa kwamba yeye ndiye mtu ambaye angetupa
taarifa zote muhimu tunazozihitaji kuhusiana na mambo yanayoendelea hapa
Rwanda. Naweza kusema nafasi hiyo tuliipata mara moja tu hata hivyo haiku-
wa yenye mafanikio.
Ilikuwa jumapili ya kwanza ya mwezi Julai mwaka 1992 katika misa ya saa
03:00 asubuhi katika kanisa la Roman Catholic la Nyarubuye. Kama unavyo-
jua ilikuwa ni siku ya ibada hivyo hatukuweza kuongea naye chochote cha
maana wakati tulipokutana nje ya kanisa mwisho wa ibada hiyo. Kwa hiyo
alitupa anwani ya ofisi yake akitutaka tumuone huko siku za kazi, hata hivyo
hatukuweza kumpata.
Tumekuwa tukifika ofisini kwake na kuhudhuria kila misa kanisani katika
jitihada za kutaka kuonana naye lakini hatukuweza tena kumuona wala kupata
taarifa zake hivyo mpaka wakati huu sijui mahali alipo” Dr. Amanda Albro
aliweka kituo na kunitazama kisha akaniashiria nimpe maji ya kunywa na
wakati akinywa mimi nilikuwa nimeshazama katika kutafakari maelezo yake.
“Umeniambia wakati mlipokuwa mkifika hapa Rwanda mlielekezwa
kuonana na jaji Makesa, wewe na nani na ni nani aliyewaelekeza kuonana
naye?
“Mimi na Dr.François Tresor, maelekezo hayo tuliyapata kutoka ofisi kuu
ya Human Right Watch jijini New York Marekani” Dr. Amanda Albro alinijibu
baada ya kumaliza kugida funda la mwisho la maji na kunikabidhi bilauri.
“Kwa hiyo inavyoonekana ni kwamba Jaji Makesa alikuwa na mawasiliano
na shirika la Human Right Watch na hivyo huenda alikuwa akituma baadhi ya
nyaraka muhimu kuhusiana na hali ya uvunjivu wa haki za binadamu inayo-
endelea hapa nchini?
“Hata mimi ninaweza kusema hivyo kwani vinginevyo sioni sababu nyingine
inayoweza kumpelekea Jaji Makesa kutambulika na Human Righ Watch”
Maelezo ya Dr. Amanda Albro yalikuwa yameniingia vizuri kichwani hivyo
nikainamisha kichwa na kushusha pumzi taratibu katika namna ya kukata
tamaa. Bado safari yangu ya kijasusi nilianza kuiona ndefu kuliko nilivyo-
dhani, nikaanza kukumbuka mlolongo wote wa matukio tangu nilipofika hapa
Rwanda. Kwa kweli nilijisikia kuchoka kifikra lakini bado niliona kulikuwa
na matumaini fulani katika safari yangu hivyo nikainua tena macho yangu na
kumtazama Dr. Amanda Albro kama niliyepata uhai mpya wa fikra zangu.
“Umefikia wapi katika harakati zako? hatimaye nilimuuliza kwa utulivu
“Mpaka sasa siwezi kusema nimefanikiwa au sijafanikiwa kwani bado
naendelea na kazi yangu”
“Usijali pengine kwa kushirikiana tunaweza kufanikiwa” niliongea na ku-
weka kituo kisha nikakohoa na kuendelea
“Nahitaji unisaidie mambo mawili muhimu”
“Yapi?
“Maelezo kuhusu ilipo ofisi ya Jaji Makesa na ofisi ya Dr. François Tresor”
“Unadhani unaweza kupata chochote cha kukusaidia?...anyway unaweza
kujaribu bahati yako” Dr. Amanda Albro aliongea katika namna ya kukata
tamaa huku akijigeuza taratibu pale kitandani kuifikia droo ndogo iliyokuwa
pembeni ya kitanda kisha akafungua droo hiyo na kunipa kipande kidogo cha
karatasi kilichofanyiwa Lamination.
Nilipoipokea karatasi ile na kuitazama nikajua kuwa ilikuwa ni Business
card ya Jaji Makesa ikionesha jina lake, wadhifa wake, jina la mtaa na nyumba
yenye ofisi yake. Pia kulikuwa na anwani yake ya sanduku la posta na namba
ya simu ya mezani. Niliitazama Business card ile huku nikijaribu kuizoea ma-
choni mwangu kisha nikaitia mfukoni.
“Ofisi ya Dr. François Tresor ipo mkabala na chumba cha bohari ya madawa
ya Centre Hospitalier Universtaire Kigali hatua chache ukiipita wodi ya wag-
onjwa wa mifupa upande wa kushoto hapo utaiona”
“Ngoja nikajaribu bahati yangu dokta kwani sioni kitu cha kupoteza” nilim-
wambia Dr. Amanda Albro huku nikitabasamu na yeye akanifanyia hisani kwa
kutabasamu kidogo ingawaje tabasamu lake halikudumu sana usoni.
“Kuwa mwangalifu sana Luteni kwani Jaji Makesa sasa ni kama mzoga
unaokimbiliwa na Tai wengi na kila Tai anavutika kwa harufu yake hivyo un-
afahamu ni nini hutokea pale Tai wanapokuwa wengi kwenye mzoga mmoja”
Dr. Amanda Albro aliniambia kwa utulivu katika namna ya kunionya na mane-
no yake yaliniingia hata hivyo hayakufanikiwa kunitia woga hata chembe na
badala yake nilimtazama kwa makini kabla ya kubadili maongezi.
“Vipi kuhusu hali yako kwa sasa, unajisikiaje?
“Siyo mbaya na ninaendelea vizuri ni kichwa tu ndiyo bado kinaniuma.
Nafikiri nahitaji kupumzika zaidi”
“Vidonge vya kuua maumivu vitakufanya ujisikie vizuri zaidi na ni kwa
bahati kuwa risasi haikugusa kabisa mfupa wa paja lako. Bila shaka baada ya
siku chache utapata nafuu”
“Hizo siku chache naziona kama karne kwangu,” Dr. Amanda Albro
aliongea huku akikiruhusu kicheko hafifu.
“Usijali kwa matibabu niliyokupa hayawezi kukulaza kitandani kwa muda
mrefu”
#184
SIKU TATU ZILIPITA NIKIWA NA DR. AMANDA ALBRO katika ile
nyumba na kadiri siku moja ilivyokuwa ikiisha na kuingia siku nyingine nili-
furahi kumuona akizidi kupata nafuu. Alikuwa mwanamke wa aina yangu,
mzuri, mcheshi na mwenye utu. Umri wake wa miaka ishirini na tisa na umbo
lake la wastani viliongeza haiba katika uzuri wake. Sikupenda kuondoka na
kumuacha peke yake na vile vile hiyo pia niliiona kuwa ni nafasi nzuri ya
kupumzika na kuyatuliza mawazo yangu wakati nikijipanga namna ya kuanza
tena harakati zangu. Hivyo nilikuwa nimepata hifadhi ya muda katika nyumba
hii ndogo yenye vyumba viwili vya kulala, sebule ndogo ya wastani, chumba
cha kulia chakula, jiko, stoo, choo, bafu na banda la kuegeshea gari lililokuwa
kwa nje.
Muda huo wote tukiwa pamoja nilikuwa nimefanikiwa kwa kiasi kikub-
wa kuupalilia vizuri urafiki wetu na Dr.Amanda Albro. Tuliongea mengi
tukibadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali na katika maongezi hayo
Dr.Amanda Albro aliniambia kuwa angependa sana kufika nchini Tanzania
kwani hiyo ilikuwa ni ndoto yake tangu mwanzoni mwa safari yake katika
bara la Afrika.
Nilimkaribisha na kumuuliza kwa nini alipenda sana kuitembelea nchi ya
Tanzania na hapo akaniambia kuwa alikuwa amevutiwa na kufurahishwa
sana na tabia za watanzania chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere katika kuzisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru wake na hivyo
safari yake ya kuja nchini Tanzania ingekuwa ni nafasi nzuri kwake kuonana
na watanzania na ikibidi kumuona Mwalimu Nyerere.
Kwa kweli nilifurahi sana kusikia hivyo vilevile kupitia urafiki nilioujenga
na Dr. Amanda Albro alinionesha vielelezo mbalimbali vya harakati zake na
baadhi ya shahidi. Nikafurahi sana kukutana na mwanaharakati huyu.
Hifadhi niliyoipata katika nyumba ile pia ilikuwa na faida nyingine ya ku-
wafanya maadui zangu wanisahau kwa muda kama siyo kuwatoka kabisa ka-
tika fikra zao hadi pale ambapo ningerudi tena mitaani kufanya harakati zangu
huku harufu ya uwepo wangu ikiwa imeshatoweka.
__________
CENTRE HOSPITALIER UNIVERSITAIRE DE KIGALIhaikuwa vigumu
kuitafuta hospitali hii kubwa iliyopo katikati ya jiji la Kigali nchini Rwanda.
Niliitazama saa yangu ya mkononi niliyoinunua kwa mmoja wa wachuuzi wa
biashara ndogondogo asubuhi hii na kuridhishwa vizuri na majira yake.
Saa nne na dakika ishirini asubuhi saa hiyo ilionesha na hapo nikajua kuwa
bado nilikuwa na muda mzuri tu wa kufanya shughuli zangu. Nilijiambia huku
nikisubiri basi la daladala lililonishusha palekituoni litowekenyuma yangu
kwani sikutaka mtu yoyote ndani ya basi lile dogo la abiria aweze kuufahamu
uelekeo wangu. Siku tatu nilizojihifadhi ndani ya nyumba ya Dr. Amanda Al-
bro zilikuwa zimenipa utulivu wa kutosha wa mwili na akili. Naweza kusema
ki-saikolojia nilikuwa ni mtu mwenye afya njema kabisa. Mawazo juu ya Ros-
ine yalikuwa bado yakizitongoza fikra zangu na sikupenda hali hiyo iendelee
kwani ingeweza kunipotezea umakini katika harakati zangu.
Kulikuwa na manyunyu hafifu yaliyokuwa yakianguka taratibu kutoka an-
gani na kuifanya hali ya hewa iwe ya baridi ya kiasi. Hata hivyo hali hiyo ya
hewa ilikutana na upinzani wa koti langu jepesi la ngoziwakinifukuza kofia,
suruali ya jeans na buti ngumu za ngozi za kijeshi zilizokuwa miguuni mwan-
gu.
Nikiwa na hakika kuwa lile daladala nyuma yangu lilikwisha toweka nilinza
kutembea nikishika uelekeo wa upande wa kulia kwangu huku nikipenyeza
mkono ndani ya koti langu kuipapasa 38 automatic, bastola niliyopewa na Dr.
Amanda Albro asubuhi hii wakati nilipokuwa nikitoka kule nyumbani kwake.
Nilitabasamu taratibu baada ya kuikuta bastola hiyo bado ikiwa mahala pake
na iliyojaa risasi.
Nilipomaliza kulipita jengo refu la ghorofa la ofisi za serikali lililokuwa
upande wa kushoto kwangu mbele kidogo nikakutana na njiapanda na hapo
nikaifuata barabara ya upande wa kushoto nikiiacha ile iendayo mbele yan-
gu na ile nyingine ielekeayo upande wa kulia. Niliifuata barabara hiyo yenye
umbali usiopungua mita hamsini. Ilikuwa baraara safi ya lami iliyopakana na
majengo marefu ya ghorofa ambayo mengi yalikuwa ni ya ofisi za serikali.
Nilipofika umbali wa kama mita hamsini hivi mbele yangu nikakutana na njia
panda nyingine na hapo nikashika uelekeo wa barabara ya upande wa kulia
kwangu huku nikigeuka kutazama nyuma kama kulikuwa na mtu yoyote ali-
yekuwa akinifuatilia, sikumuona mtu yeyote hivyo hali bado ilikuwa poa.
Niliendelea kutembea huku nikilipita jengo la ofisi za wizara ya kilimo na
chakula kisha mbele kidogo nikazipita ofisi za kiwanda cha taifa ya kupiga
chapa. Nilipoupita ukuta wa ofisi hizo nikavuka barabara upande wa kushoto
kisha nikakatisha kwenye kichochoro kidogo cha watembea kwa miguu. Ni-
lipomaliza kukipita kichochoro hicho nikatokezea kwenye barabara ya mtaa
wa pili.
Ilikuwa barabara kubwa ya magari yenye pilika za kibinadamu za kila nam-
na kama biashara ndogo ndogo, idadi kubwa ya magari ya abiria yaliyoegesh-
wa kituoni kusubiri abiria, vibanda vidogo vya wauza magazeti na vitabu.
Nilivuka barabara hiyo na kabla ya kuendelea na safari yangu nilishawishika
kutazama vichwa vya habari katika magazeti yale kwa mmoja wa wachuuzi na
hapo nikajipongeza kuwa nilikuwa nimefanya uamuzi sahihi.
Magazeti matatu kati ya magazeti saba yaliyokuwa yametandazwa juu ya
kichanja cha kibanda hicho kurasa zake za mbele zilipambwa kwa picha nne.
Haikuniwia vigumu kuitambua picha yangu miongoni mwa picha zile nne. Ili-
kuwa ni picha ya kwanza kabisa katika kila gazeti kuanzia upande wa kushoto
na picha mbili zilizofuatia pia nilizitambua, moja ilikuwa ya Rosine ingawaje
chini yake kuliandikwa jina la Dre Fille na nyingine ilikuwa ni ya Dr. Amanda
Albro. Picha ya mwisho ilikuwa ngeni kabisa machoni mwangu na niliweka
kituo kuitazama kwa makini zaidi.
Ilikuwa ni picha ya mwanaume mwenye ndevu nyingi lakini zenye afya na
zilizokatiwa vizuri. Umri wake ulikuwa kati ya miaka hamsini na nane hadi
sitini na mbili na japokuwa ilikuwa ni picha tu lakini uso wake ulionekana
kuwa na mengi yaliyofichika. Kilichonivutia ni jina lililokuwa chini ya picha
hiyo likisomeka Jaji Makesa. “Mungu wangu...” nilijikuta nikijisemea moyoni
huku nikirudiakuitazama picha ile kisha nikayahamisha macho yangu kutaza-
ma kichwa cha habari kilichokuwa juu ya picha zile ambacho kilikuwa kime-
andikwa kwa lugha ya kifaransa, kichwa hicho cha habari kikisomeka kwa
herufi kubwa“CES GENS SONT TRES DANGEREUX SI VOUS LES VOYENS
DONNER DES INFORMATIONS A LA POLICE”kwa lugha ya Kiswahilitaf-
siri yake ikimaanisha“Watu hawa ni hatari sana, popote ukiwaona toa taarifa
polisi”.
Kadiri nilivyokuwa nikirudia kuyasoma maelezo yale nilihisi mapigo ya
moyo wangu yalikuwa mbioni kukiuka mwenendo wake wa kawaida uliozo-
eleka huku nikihisi damu yote mwilini ikikimbilia kichwani.
Muuza magazeti kijana wa makamo alikuwa amesitisha shughuli zake
na kunitazama katika namna ya kunidadisi, sikupenda aendelee kunitazama
hivyo nikaingiza mkono mfukoni na kutoa pesa kisha nikanunua gazeti lile na
kuliweka kwenye mfuko wa ndani wa koti langu kisha nikaendelea kuzitupa
hatua zangu na kuendelea na safari yangu nikikatisha mbele ya kituo cha da-
ladala kilichokuwa eneo lile.
Wakati nikiendelea na safari sikuacha kuyatembeza macho yangu kuzichun-
guza nyuso za watu niliyopishana nao. Nilipomaliza kukipita kituo kile cha
daladala mbele yangu nikaona bango kubwa kando ya barabara limeandik-
wa “CENTRE HOSPITALIER UNIVERSITAIRE, KIGALI” chini ya bango
hilo kulikuwa na alama ya mshale unaoelekeza upande wa kushoto. Nilipo-
lifikia bango hilo nikapinda kona upande wa kushotonikiufuata uelekeo wa
ule mshale wa chini ya bango na wakati nikiendelea kutembea kumbukumbu
juu ya barabara ile na mazingira yake ikaanza kuumbika kichwani mwangu.
Nikakumbuka siku ile wakati nilipokuwa nikikimbizwa na wale watu usiku
kutokea hospitali huku Dr. Amanda Albro akiwa begani mwangu.
__________
KULIKUWA NA MAGARI YASIYOPUNGUA kumi na mawili yaliy-
oegeshwa nje ya Centre Hospitalier Universitaire de Kigali na miongoni mwa
magari hayo mawili yalikuwa ni ya kubebea wagonjwa ama Ambulance na
gari moja likiwa ni la idara ya zima moto.
Niliyapitisha macho yangu kuyatazama majengo ya hospitali ile na hapo
nikafahamu ni kwanini ilikuwa ni hospitali kubwa iliyokuwa ikitegemewa
kwa kiasi kikubwa na wakazi wa jiji la Kigali. Majengo yake yalikuwa makub-
wa na ya ghorofa, maegesho yake ya magari yalikuwa nadhifu na yaliyopamb-
wa kwa bustani nzuri za maua na miti mirefu iliyopandwa katika mtindo wa
mistari minyoofu inayovutia.
Nilikatisha mbele ya hospitali ile nikielekea kwenye lango kuu la kuingilia
kwenye ofisi za utawala za hospitali ile na wakati nikitembea sikutaka kuamini
kuwa nilikuwa kwenye mazingira salama hivyo nilikuwa makini kuzifuatilia
nyendo za kila mtu aliyekuwa eneo lile.
Yalikuwa mazingira mageni kabisa kwangu hata hivyo nilijitahidi kutembea
kwa kujiamini kama mwenyeji wa siku nyingi wa eneo lile huku nikipita eneo
la mapokezi. Nilikuwa nimepata maelekezo ya kina toka kwa Dr. Amanda
Albro hivyo ni kama ramani yote ya hosptali ile ilikuwa kichwani mwangu.
Kulikuwa na watu wengi kiasi sehemu ya mapokezi ya hospitali ile na wen-
gi wao walionekana wagonjwa kulingana na nyuso zao huku wakiwa wameke-
ti kwenye ma-benchi yaliyokuwa eneo lile bila shaka wakisubiri huduma. Pia
kulikuwa na wanaume wawili waliokuwa wameketi kwenye benchi la nyuma
kabisa.
Nilipoingia tu watu wale wawili waliokuwa wameketi kwenye lile benchi la
nyuma waliinua macho yao kunitazama kisha kila mmoja akaendelea na ham-
sini zake na hilo lilinivuta kidogo. Sikuwa na muda wa kupoteza nikaingia
upande wa kushoto nikiwapita wagonjwa wachache walioketi kwenye benchi
la upande wangu. Watu wachache walinitazama na wengine hawakujisumbua
hata kugeuka.
Sasa nikawa nimetokezea kwenye korido pana kiasi iliyokuwa upande wa
kulia wa ile sehemu ya mapokezi iliyokuwa ikitazamana na milango kadha
wa kadha. Juu ya milango ile kulikuwa na vibao vidogo vilivyoandikwa kwa
maandishi madogo lakini yanayoonekana vizuri yakieleza aina ya ofisi na
cheo cha mhusika wa ofisi hiyo kama Daktari wa Zamu, Mganga Mkuu na
nyinginezo. Hata hivyo malengo yangu yalikuwa si kuingia ndani ya ofisi zile
wala kuonana na watu waliokuwemo ndani yake kwani sikufika pale kufuata
huduma yoyote ya kitabibu hivyo niliendelea na safari yangu nikizipita ofisi
zile kwa upande wa kulia.
Baada ya kutembea hatua kadhaa hatimaye nilikutana na korido nyingine
iliyokatisha mbele yangu. Nilimshukuru sana Dr. Amanda Albro kwa kunipa
maelekezo sahihi na kutokana na eneo lile nilitakiwa kushika uelekeo wa upa-
nde wa kulia kwangu. Hakuna mtu yeyote aliyekuwa akinifuata nyuma yangu
na hilo lilinipa faraja kiasi.
Kulikuwa na wauguzi wawili wanawake waliokuwa wakija kutoka kwenye
korido ile ya upande wa kulia na wote waligeuka kunitazama wakati nikipis-
hana nao. Wakati nikiendelea kutembea niligundua kuwa sehemu kubwa ya
eneo la chini la hospitali ile lilikuwa likitumika kwa shughuli za ki-utawala
kutokana na kuwepo kwa ofisi nyingi eneo lile.
Mbele upande wa kulia kwangu nilikutana na ngazi. Kwa mujibu wa Dr.
Amanda Albro ngazi hizo zingenifikisha ghorofa ya kwanza zilipoanzia wodi
za hospitali ile. Nilimaliza kuzipanda ngazi zile na kujikuta nikitazamana na
wodi mbalimbali kwenye korido nyingine pana iliyopakana na ukuta wa kioo
ulioniwezesha kuwaona wagonjwa waliolazwa ndani ya wodi zile.
Nikiwa nayakumbuka vizuri maelekezo ya Dr. Amanda Albro niliingia upa-
nde wa kushoto wa korido ile na safari hii nikitembea kwa tahadhari zaidi.
Kiasi cha hatua kama sita hivi upande wa kushoto kwangu kulikuwa na ngazi
zilizokuwa zikipandisha kwenda ghorofa ya juu kulipokuwa wodi nyingine.
Niliziacha ngazi zile na kuendelea mbele na safari yangu na kwa mba-
li wakati nikiendelea na safari yangu nilisikia hatua za mtu aliyekuwa aki-
shuka kwenye ngazi zile nilizoziacha nyuma yangu. Nilikuwa mwepesi sana
kujibanza nyuma ya kabati la vifaa vya usafi vya hospitali lililokuwa mbele
yangu upande wa kushoto. Nikiwa bado nimejibanza nyuma ya kabati lile
nilimuona yule mtu aliyekuwa akishuka kwenye zile ngazi.
Alikuwa mwanaume mrefu kiasi lakini hakunizidi, mweusi na mwenye
mwili uliojengeka vizuri. Alikuwa amevaa shati la kijivu na suruali nyeusi na
umri wake ulikuwa si zaidi ya miaka thelathini. Mtu yule alipomaliza kushuka
zile ngazi alisimama akitazama upande ule nilipokuwa lakini kabla hajaamua
cha kufanya nilisikia sauti ya hatua za mtu mwingine akishuka kwenye zile
ngazi na tukio hilo likamfanya yule mtu aamue kuondoka akishuka kwenye
zile ngazi za kuja kwenye floo ile niliyokuwa.
Mtu aliyeshuka kutoka ile ghorofa ya juu alikuwa daktari na nilimtambua
kwa mavazi yake ya koti refu jeupe na mashine ndogo ya kupima mapigo
ya moyo aliyoitundika shingoni kwake. Yule daktari alipomaliza kushuka zile
ngazi alielekea upande wa kulia na kwenda kushuka kwenye zile ngazi za
kuelekea ghorofa ya chini na baada ya muda mfupi ile sauti ya vishindo vya
hatua zake ikawa imetoweka kabisa
Nililiacha lile kabati la kuhifadhia vifaa vya usafi vya hospitali nilipokuwa
nimejibanza na kuanza kutembea taratibu na kwa tahadhari nikitazama upande
huu na ule na hatimaye macho yangu yalitua kwenye kibao kidogo juu ya
mlango.
Kilikuwa chumba cha wodi ya mifupa, kibao kidogo kilichokuwa juu ya
mlango ule kilieleza hivyo. Kwa mujibu wa maelezo ya Dr. Amanda Albro ni
kuwa mbele kidogo ya wodi ile upande wa kushoto ndipo ilipokuwa ofisi ya
Dr. François Tresor. Sasa nilizikaza hatua zangu na kuzitupa kwa tahadhari
nikiendelea mbele huku macho yangu yakitazama upande wa kushoto.
Hatimaye niliiona ofisi ya Dr. François Tresor, ofisi hiyo ilikuwa upande
wa kushoto mwisho wa korido fupi isiyozidi umbali wa hatua tano upande wa
kushoto. Ilikuwa ni ofisi iliyojitenga kabisa na ofisi nyingine za madaktari wa
hospitali ile na hilo lilinishangaza kidogo. Muda mfupi uliyofuata nilijikuta
umbali wa hatua moja nikitazamana na ofisi ile ya Dr. François Tresor.
Nilisimama nikisikiliza kama kulikuwa na sauti yoyote ndani ya ofisi ile,
ofisi ilikuwa kimya kama iliyokufa na hapakuwa na dalili zozote za kuwepo
kiumbe hai ndani yake hivyo niliuchukua ufunguo alionipa Dr. Amanda Albro
toka katika mfuko wa suruali yangu na kuupachika kwenye kitasa na ndani ya
muda mfupi mlango ule ukafunguka na kazi ikawa ni kuusukuma kidogo na
kuingia ndani.
Nilipoingia ndani nikaurudishia ule mlango nyuma yangu. Hakukuwa na
giza kwani taa ndani ya ofisi ile ilikuwa ikiwaka na hapo nikajua kuwa kwa
vyoyote taa ile ilikuwa imeachwa na Dr. François Tresor siku ya mwisho ali-
poondoka kwenye ofisi hii.
Harufu ya manukato ya Dr. François Tresor ndani ya ofisi ile ilipenya tara-
tibu puani mwangu na kunifanya nizidi kumkumbuka daktari yule. Hali ya
ofisi ilivyokuwa ilinieleza kuwa ile ilikuwa miongoni mwa ofisi zilizokuwa na
harakati nyingi sana katika hospitali hii.
Ukutani kulikuwa na rafu kadhaa zilizopangwa vitabu vya kidaktari na ma-
faili chungu mzima ya rekodi za wagonjwa. Pia kulikuwa na zana za kitabibu
za mfano wa viungo mbalimbali vya binadamu vilivyokuwa vimetundikwa
ukutani. Kulikuwa na kiti kimoja kikubwa na meza ya kiofisi mbele yake na
juu ya meza hiyo kulikuwa na mafaili machache, vitabu, kasha la miwani,
mhuri na kidau cha wino. Pia kulikuwa na kikombe kimoja ambacho huenda
kilikuwa kikitumika na Dr. François Tresor kunywea kahawa.
Vitu vyote hivyo vilikuwa vimetapakaa vumbi kila mahali na hali hiyo il-
inijulisha kuwa ofisi hii haikuwa imepata ugeni wa namna yoyote tangu Dr.
François Tresor alipoifunga kwa mara ya mwisho.
Niligeuka upande wa kushoto ukutani mahali kulipokuwa na kalenda kubwa
yenye picha ya hospitali ile na maelezo. Niliitazama kalenda ile kwa udadisi
na kuyasoma maelezo yaliyokuwa chini yake na hapakuwa na chochote cha
maana zaidi ya maelezo kuhusu muundo wa utawala wa hospitali ile, huduma
za matibabu zinazotolewa, idadi ya vitanda vya wagonjwa ambavyo vilikuwa
560 na idadi ya madaktari ambayo ilikuwa 50, zaidi ya hapo sikuona kitu
kingine cha maana kwangu. Mara nikawa nimekumbuka vizuri juu ya sababu
iliyonifanya nifike ndani ya ofisi hii na hapo nikaanza kufanya upekuzi.
Panya walikuwa wameanza kuweka maskani yao mle ndani na kila nilipo-
pekua faili moja panya hao waliruka na kukimbilia upande mwinge. Vumbi
lilikuwa kali mno kiasi cha kunifanya nipige chafya kila mara.
Nilimaliza kupekua mafaili yote na vitabu vilivyokuwa kwenye rafu za
ukutani bila kupata chochote cha maana zaidi ya barua za kiofisi na baadhi
ya anwani za wagonjwa hivyo nilihamishia upekuzi wangu kwenye droo tatu
zilizokuwa chini ya meza ya ofisi iliyokuwa mle ndani. Droo mbili za mwan-
zo zilikuwa wazi hivyo sikukutana na upinzani wowote wakati wa kuzifun-
gua na ndani yake kulikuwa na bahasha kadhaa, chache zilikuwa za kiofisi
na nyingine binafsi pia kulikuwa makaratasi mengine. Niliyasoma maelezo
kwenye karatasi zile na kugundua kuwa yalikuwa ni maelezo ya kitaalamu
kwenye masuala ya tiba ya mifupa zaidi ya hapo hapakuwa na kingine cha
maana hivyo nilizifunga droo zile na kuhamia ile droo ya mwisho kabisa chini
ya meza ile.
Matumaini ya kupata chochote cha maana katika droo hiyo yalikuwa mado-
go sana hata hivyo nilipoivuta droo hiyo na kuiona haifunguki matumaini hayo
yaliongezeka kidogo. Nikafanya utundu wangu binafsi na baada ya kukuru-
kakara za hapa na pale nikafanikiwa kuifungua droo ile. Hata hivyo tofauti
na zile droo za awali droo hii haikuwa na vitu vingi kama zile bahasha nyingi
na makaratasi na badala yake nilijikuta nikitazama gazeti moja la siku nyingi
lililokunjwa na kuhifadhiwa vizuri ndani ya droo hiyo. Nililitembezea macho
gazeti lile bila kupata maana yoyote kichwani mwangu hata hivyo sikuacha
kulichunguza. Nikalichukua na kulifungua huku macho yangu yakiwa makini
kufuatilia taarifa za mle ndani.
Lilikuwa moja ya gazeti maarufu sana nchini Rwanda na nilitumia muda
mfupi tu kulipitia gazeti hilo na hadi namaliza kulipitia sikuweza kuona habari
yoyote yenye kunivutia na hali hiyo ikanifanya nijihisi kuwa nilikuwa nikipo-
teza muda wangu kufanya upekuzi katika ofisi ile. Hisia hizo zikanifanya nil-
irudishe lile gazeti ndani ya ile droo lakini wakati nikifanya hivyo kitu fulani
kilitokea. Bahasha mbili zilianguka chini toka katika lile gazeti. Nikashtuka
na kuzitazama zile bahasha zilizoanguka sakafuni na tukio hilo likanifanya
nirudie tena kulipekua lile gazeti kwa makini hata hivyo sikupata kitu cho-
chote ingawaje niligundua kuwa zile bahasha zilikuwa zimewekwa kwenye
ukurasa wa mwisho wa gazeti lile ambao nilikuwa sijaupekua.
Niliinama na kuziokota zile bahasha na bahasha ya kwanza ilikuwa ndogo
kiasi na haikuwa imefungwa, nilipoipapasa nilihisi kulikuwa na kitu kidogo
kigumu ndani yake na nilipoifungua kulikuwa na funguo fulani. Niliitazama
funguo hiyo huku nikiigeuzageuza hata hivyo sikuweza kung’amua chochote
juu ya funguo ile hivyo nikairudisha kwenye ile bahasha yake na kuitia baha-
sha hiyo mfukoni mwangu.
Bahasha ya pili ilikuwa kubwa kiasi na iliyofungwa hivyo nikaichana na ku-
toa kilichokuwa ndani yake na hapo nikaona picha ndogo iliyokuwa imepigwa
kwenye mazingira fulani ambayo nisingesita kuyafananisha na mazingira ya
hoteli fulani ya kifahari. Katika picha hiyo kulikuwa na watu watatu walioketi
kwenye kochi moja kubwa la sofa nyuma ya meza fupi yenye vinywaji vya
kila namna. Miongoni mwa watu hao alikuwepo Dr. François Tresor akiwa
ameketi mwisho wa kochi hilo upande wa kushoto katika pozi la tabasamu na
sigara mkononi. Watu wengine wawili waliosalia katika picha hiyo waliku-
wa ni wanaume wenye asili ya Afrika wakiwa wamevaa sare za kijeshi huku
wametabasamu na bilauri za vinywaji mikononi.
Niliigeuza picha ile na kuitazama kwa nyuma na nyuma ya picha hiyo
kuliandikwa namba 902 na haponikaanza kuiundia hoja namba ile nikiihusisha
na hili na lile hata hivyo hakuna cha maana kilichonijia kichwani hivyo nayo
nikaitia mfukoni.
Ilikuwa ni wakati nilipokuwa nikimalizia zoezi hilo pale nilipohisi kitu cha
baridi kikinitekenya kisogo changu. Hisia za kuwa nilikuwa nimeingia tena
kwenye mikono hatari zikanijia ghafla na kabla sijaamua nifanye nini sauti
kutoka nyuma yangu ilinong’ona.
“Tulia hivyohivyo Luteni na usifanye hila yoyote kwani safari hii hutopata
bahati tena”
“Bahati ipi unayoizungumzia na wewe ni nani?
“Usijali muda si mrefu utanifahamu kwani nimekuwa nikikusubiri kwa
muda mrefu hadi nikaanza kukata tamaa nikidhani umeshatupotea hivyo nili-
pokuona leo nikafurahi sana”
“Sasa hiyo bastola kisogoni kwangu ya nini? nilimuuliza huku nikigeuka
hata hivyo sikufanikiwa kwani nilijikuta nikikabiliana na maumivu makali ya
ngumi kavu ya mbavuni na hapo nikaanza kuhema ovyo.
“Si nimekwambia utulie sasa unajitikisa nini kama shoga? ile sauti nyuma
yangu ilinionya
“Lete bastola yako”
“Mimi sina bastola…” nilimwambia na kabla sijamaliza kuongea nikapewa
kichapo kingine cha ngumi mbili za mgongo zilizonipelekea maumivu makali
yasiyoelezeka.
“Nakushauri Luteni uache kujibizana na mimi na ufuate kile ninachokuele-
za vinginevyo utaiona chungu ya mwaka” yule mtu aliniambia.
Kwa kweli nilijikuta nikihema ovyo kama niliyekuwa mbioni kuponyokwa
na uhai huku maumivu makali ya kile kipigo yakiwa yanaendelea kusambaa
taratibu mwilini mwangu. Halafu yule mtu nyuma yangu akaanza kunipekua
mwilini na hapo nikajua kuwa alikuwa akiitafuta ile bastola yangu hata hivyo
nilitabasamu kwani hata kama ningemwachia nguo zangu zote bado ingem-
chukua muda wa zaidi ya nusu saa hadi kuifikia bastola hiyo. Mara moja au
mbili nilijikuta nikiponyokwa na tusi zito mdomoni pale nilipomuona yule
mtu akinipekua kikahabakahaba kwa kunishikashika maeneo nyeti. Alipo-
maliza kunipekuwa akawa amezipata zile bahasha mbili na lile gazeti nililoli-
nunua njiani wakati nikija hapa hospitali.
“Sasa utafuata maelekezo yangu na usijidanganye kufanya hila tambua
kuwa unatakiwa ukiwa hai au mfu hivyo sina cha kupoteza”
“Nani hao wanaonitaka nikiwa hai au mfu? nilimuuliza yule mtu.
“Kamanda wetu Bosco Rutaganda uliyemtoroka kule pangoni”
“Hebu acha kunichekesha huyo kamanda wenu mbona ana mambo ya kike.
Si nilikuwa naye kule pangoni na hakunieleza chochote cha maana zaidi ya
kuchekacheka kama fisi na sasa hivi nimeondoka anajidai ananiulizia kama si
uhanithi nini hicho?.
Maneno yangu yalimkasirisha sana yule mtu na kumpelekea anirushie teke
hata hivyo safari hii nilikuwa mwepesi zaidi hivyo nikainama chini kidogo na
kuliacha pigo lile likiniparaza kidogo juu ya kichwa changu kisha nikawahi
kugeuka nikitaka kufanya shambulizi la ghafla hata hivyo yule mtu aliniwahi
na hapo nikajikuta nikitazamana na mdomo wa bastola, nikajua kuwa nili-
kuwa nimekutana na kiumbe hatari aliyekuwa akizifahamu vizuri mbinu za
mapambano.
“Ongoza mbele na sasa tunaondoka humu ndani na makubaliano yetu bado
ni yaleyale kuwa ukileta hila ya namna yoyote nautawanya ubongo wako”
“Tunaenda wapi? nilimuuliza yule mtu huku nikipata nafasi nzuri ya kum-
tazama. Nilishtuka sana nilipomkumbuka kuwa alikuwa ndiye yule mtu
nileyemfahamu kwa jina la Sam ambaye siku nne zilizopita yeye na mwen-
zake walinifukuza kutoka katika hospitali hii huku nikiwa na Dr. Amanda Al-
bro begani. Wakati huu alikuwa amevaa mavazi nadhifu ya heshima suruali,
shati na koti la suti lakini bila tai shingoni ingawaje mavazi yake hayakuen-
dana kabisa na roho yake.
“Utapafamu pindi tutakapofika” yule mtu aliniambia
“Yule mwenzako yupo wapi?
“Anafanya kazi kama hii sehemu fulani. Tafadhali sihitaji tena maswali
yako ongoza mbele na ufunge domo lako” yule mtu alinionya na niliweza
kuipima sauti yake kuwa ilikuwa mbali kabisa na mzaha hivyo nikaanza kuz-
itupa hatua zangu taratibu kuelekea mlangoni huku akili yangu sasa ikianza
kufanya kazi kwa haraka. Nilipofika nikaufungua ule mlango na kutoka nje
lakini nilipotoka tu huku nikiwa na hakika kuwa yule mtu aliyekuwa nyuma
yangu na yeye alishaufikia ule mlango nyuma yangu huku bastola yake bado
akiwa ameielekeza kwangu niliusubiri ule mkono wake uliyoshika bastola uji-
tokeze na hapo nikageuka kwa kasi na kurusha teke. Lile teke likaubamiza ule
mlango na ule mlango ukaubamiza mkono wa yule mtu uliyotangulia mbele
na bastola.
Ule mlango ulikuwa mzito na wenye mbao ngumu hivyo ulijifunga kwa
nguvu na kuubamiza vibaya mkono wa yule mtu na kuufanya aiachie ile basto-
la mkononi bila kupenda huku akipiga yowe kali la maumivu. Niliwahi kuio-
kota ile bastola haraka huku nikiwa na hakika kuwa ile sauti ya mmbamizo
wa ule mlango ilikuwa kubwa sana kiasi cha kuweza kumshtua mtu yoyote
ambaye angekuwa jirani na eneo lile hivyo nilitakiwa kufanya haraka kabla
mtu yoyote hajafika.
Nikaufungua tena ule mlango na kurudi tena mle ndani ya ile ofisi nikim-
fuata yule mtu kule alipoangukia haraka kabla hajasimama na wakati niki-
ufungua ule mlango nikapishana na kisu kilichorushwa na kunikosa kidogo
kama nisingekuwa makini. Kisu hicho kilienda na kugota kwenye mbao ya
juu ya mlango wa ile ofisi. Sam alikuwa akijibu mashambulizi kwa kunirushia
visu hata hivyo nilifanikiwa kuvikwepa nikijirusha upande huu na ule hadi
pale vilipoisha na hapo nikasimama na kumfuata pale chini. Ule mkono wake
nilioubamiza pale mlangoni ulikuwa umevunjika kiasi cha mifupa kuchomoza
nje huku damu nyingi ikitoka kwenye lile jeraha na kusambaa pale chini. Sam
alikuwa ametaharuki huku macho yamemtoka kama ambaye haamini mambo
yalivyokuwa yakimtokea kwa kipindi kifupi mle ndani.
Nilimfikia Sam na kumkwida shati kisha nikamzaba makofi mawili kumu-
weka sawa na alipotulia akajikuta akitazama na ile bastola yake yenye kiwam-
bo cha kuzuia sauti ambapo sasa ilikuwa mkononi mwangu.
“Bila shaka umeona namna mambo yanavyoweza kumbadilikia mtu kwa
sekunde tu na kumuacha na mshangao. Haya niambie mnashida gani na mimi
mpaka mnifuatefuate kila ninapoenda kama nzi wanaomfuata mtu aliyejinyea?
Sam hakujibu kitu badala yake aliendelea kunitazama kwa mshangao huku
akigugumia maumivu ya mkono wake uliyovunjika. Nikamzaba tena makofi
manne ya nguvu yaliyomfanya ateme meno mawili.
“Nakuuliza mnashida gani na mimi?
“Naomba uniache sitokufuatilia tena nakuahidi” akaongea huku akilalamika
kwa maumivu huku damu ikimtoka mdomoni na puani.
“Bado hujanijibu swali langu”
“Mimi sina shida na wewe ila ni bosi wetu, tafadhali naomba unisamehe
nakuahidi kuwa sitokufuatilia tena”
“Bosi wenu ni nani?
“Bosco Rutaganda na wenzake”
“Wana shida gani na mimi?
“Wanasema kuwa wewe ndiye unayeharibu mipango yao”
“Mipango gani ninayoiharibu?
“Mimi siifahamu” Sam alijitetea na nilipoyapima maneno yake nikajua
kuwa alikuwa akinidanganya hivyo nikaushika ule mkono wake uliyovunjika
na kuanza kuunyonga na hapo akaanza kupiga tena mayowe ya maumivu huku
akinisihi nimuache.
“Tafadhali nakuomba uniache nitakueleza kila kitu”
“Haya niambie” nilimsisitiza huku nikimuachia mkono wake.
“Wamepanga kufanya mapinduzi ya kijeshi hapa nchini na ni wewe ndiye
wanayekuhofia kuiharibu mipango yao” maneno ya Sam yakanifanya niya-
kumbuke maelezo ya Kanali Bosco Rutaganda wakati ule nilipokuwa mate-
ka kwenye yale mapango ya Musanze akiongelea juu ya tukio la mapinduzi
linalotarajiwa kufanyika katika nchi hii na hapo nikafahamu kuwa Sam aliku-
wa akimaanisha alichokizungumza.
“Kwa nini wanihofie mimi kwani mimi ni nani katika hiyo mipango yao?
nilimuuliza Sam na hapo nikamuona akisita kunieleza zaidi. Sikuwa na muda
wa kuendelea kumlazimisha badala yake nikamuuliza swali jingine.
“Nani aliyemuua Tobias Moyo? swali langu likamfanya Sam ataharuki na
kulikuwa na kitu fulani katika macho yake, kitu kilichonipelekea nizidi kum-
dadisi.
“Hukusikia nilivyokuuliza au unataka kunipotezea muda wangu ?...nani ali
yemuua Tobias Moyo?
“Sifahamu!…kweli sifahamu” Sam alinidanganya na hapo nikambadilishia
mtindo wa kipigo. Ngumi tatu nilizomtandika mbavuni zikampelekea awe na
hali mbaya zaidi akawa ni kama aliyeshikwa na kichomi cha ghafla. Macho
yakamtoka huku damu ikizidi kumtoka mdomoni na puani.
“Nitakueleza tafadhali naomba uniache…” akalalama
“Niambie”
“Ni mimi ndiye niliyemuua na ni Kanali Bosco Rutaganda ndiye aliyenia-
giza kufanya hivyo”
“Kwanini alitaka auwawe?
“Kanali Bosco Rutaganda alisema kuwa Tobias Moyo ndiye aliyekuwa
akizifahamu siri zao hivyo alistahili kufa kabla Tobias Moyo hajazivujisha
siri hizo”
Nilimtazama Sam huku nikiwa nimeshikwa na mshangao usioelezeka. Ha-
sira zilikuwa zimenishika na kadiri nilivyokuwa nikimtazama nikawa kama
ninayeliona lile tukio la mazishi ya Thobias Moyo kule kwenye makaburi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kwa hiyo wewe ndiye uliyemuua Tobias Moyo? nilimuuliza kama
ninayehitaji kujihakikishia zaidi huku nikitetemeka kwa hasira. Hata hivyo
Sam hakunijibu na badala yake akanitazama kwa hofu.
“Nini kiini cha mapinduzi yenu?
“Sifahamu chochote, kweli sifahamu”
Nilimtazama Sam huku hasira zikizidi kunishika na sikuona chochote cha
maana ambacho angenieleza zaidi hivyo nikaukandamiza mtutu wa bastola
kwenye tundu la sikio lake na risasi mbili nilizozisukuma zikakifumua vi-
baya kichwa chake na kuutawanya ubongo wake kila mahali mle ndani. Sam
akaanguka chini na kutulia huku roho yake ikiwa mbali na mwili.
Nilizichukua zile bahasha na gazeti ambazo Sam alikuwa amevichukua
kwangu muda mfupi uliyopita kisha nikavitia mfukoni na wakati nikifanya
hivyo nikasikia sauti ya hatua za mtu zikiukaribia ule mlango wa ile ofisi. Nik-
achepuka kwa kasi na kujibanza pembeni ya ule mlango huku bastola ikiwa
tayari kufanya kazi mkononi mwangu.
Ile sauti ya hatua za mtu ilikoma umbali mfupi mbele ya ule mlango wa ofisi
na nilipotazama chini kupitia uwazi mdogo uliyokuwepo baina ya ule mlango
wa ile ofisi na sakafu nikaona kivuli cha mtu. Moyo wangu ukapiga kite kwa
nguvu huku hofu ikiwa imenishika kwani nilifahamu kuwa muda wowote nili-
paswa kutarajia purukushani nyingine zenye hatari zaidi.
Nikiwa nimejibanza pembeni ya ule mlango nilisogea taratibu na kuchun-
gulia kupitia kioo kidogo kilichokuwa katikati ya mlango ule na hapo nikamu-
ona yule mtu aliyesimama mbele ya ule mlango akitoa bastola kwa tahadhari
toka kwenye koti lake na hapo nikajua kuna kitu alikuwa amekihisi ndivyo
sivyo ndani ya ile ofisi nilimokuwa. Sikubahatika kuiona sura yake ingawaje
sehemu ya mwili wake niliyoiona ilinijulisha kuwa mtu yule alikuwa mrefu
sana, mweusi kutokana na rangi ya mikono yake na mwenye mwili imara.
“Sam vipi umempata huyo bwege? nilimsikia yule mtu akiuliza kwa sauti
ya chini na alipoona hajibiwi akainama na kuchungulia mle ndani kupitia kile
kioo kifupi kilichokuwa katikati ya mlango, nikawahi kusogea pembeni ili
asinione. Yule mtu alipoona ukimya unazidi akakishika kitasa cha ule mlango
na kukizungusha taratibu. Mlango ulipofunguka akautanguliza mbele mkono
wake ulioshika bastola na hilo lilikuwa kosa kubwa alilolifanya na sikutaka
kupoteza muda.
Nikarusha teke jepesi lakini lenye shabaha nzuri kuupiga juu ule mkono
wake uliyoshika bastola. Ile bastola ikamponyoka mkononi na kupaa hewani
nami sikutaka kusubiri mpaka ile bastola itue mikononi mwangu hivyo nikai-
fuata kulekule hewani na kuidaka. Lakini yule mtu alikwisha ishtukia hila
yangu hivyo akaingia mle ndani kwa kasi ya ajabu huku akitumia nguvu zote
kunipiga kikumbo na ile bastola ikaniponyoka na kuangukia chini ya meza
iliyokuwa mle ndani huku mimi nikiangukia kwenye rafu ya mafaili iliyokuwa
upande wa kushoto ukutani mwa ile ofisi. Mafaili yote yakaanguka chini na
kutawanyika ovyo kila mahali.
Niliwahi kunyanyuka lakini yule mtu aliwahi kunichota mtama mikono yan-
gu hivyo nikarudi chini kama gunia nikiwa nimepoteza umakini halafu yule
mtu akachukua kiti cha mbao kilichokuwa mle ndani na kunitandika nacho
mgongoni.Kile kiti kikasambaratika vipandevipande na kuniachia maumivu
makali yasiyoelezeka. Nikapiga yowe kali la maumivu lakini halikuonekana
kumshtua yule mtu hata kidogo na badala yake alinikamata miguu yangu na
kuniburuta kwa kasi akinipeleka ukutani na hapo nikajua kuwa alikuwa amed-
hamiria kunibamiza ukutani kama si kunidhulumu kabisa uhai wangu.
Nikasubiri aniburute hadi nilipoifikia meza ya ofisi ya mle ndani na hapo
nikaushika mguu wa meza ile kupata mhimili kisha nikajifyatua kwa kujizun-
gusha hewani hali iliyompelekea yule mtu aniachie miguu yangu bila kupenda
huku akipepesuka. Sikutaka kusubiri zaidi nikamuwahi yule mtu kwa kum-
chota mtama wa kuzunguka chini na kwa kuwa alishapoteza umakini mtama
wangu ukamchota na kumrusha hewani na wakati alipokuwa akikaribia hatua
chini nikasimama na kumpiga kikumbo matata kilichomrusha hadi kwenye
rafu nyingine ya vitabu na mafaili iliyokuwa upande wa kulia wa ile ofisi.
Ile rafu ikapasuka vipandevipande na yale mafaili na vitabu vikatawanyika
kila mahali sakafuni, yule mtu akapiga yowe kali la maumivu hata hivyo we-
pesi wake ulinishangaza sana kwani kufumba na kufumbua nilijikuta nimee-
nea ndani ya kabari ya mikono yake iliyonikamata vema kiasi cha kunifanya
nishindwe kufurukuta, nikajaribu kujitoa bila mafanikio.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Yule mtu akaninyanyua juu na kunipigiza chini, alikuwa na nguvu za ajabu
ambazo kwa kweli zilianza kunitia hofu. Nilianguka chini kwa kishindo huku
nikihisi kuwa huenda kishindo kile kingekuwa kimesikika eneo lote la hospi-
tali ile. Nilipiga yowe kali la maumivu lakini yule mtu alianza kucheka huku
akinitukana matusi mzito ya kila namna yasiyo na idadi.
Nilipotaka kusimama aliniwahi tena na kunizoa pale sakafuni kisha akanin-
yanyua tena na kunibwaga juu ya ile meza ya ofisi na hapo ile meza ikavunjika
katikati. Nikapiga yowe la maumivu nikimsihi aniache hata hivyo hakunisikili-
za badala yake aliendelea kucheka huku akinitukana na hata kabla sijanyanyu
ka alikwisha niwahi tena kisha akaninyanyua juu ya kunipigiza ukutani. Hofu
ikanishika na matumaini ya kushinda pambano lile yakaanza kutoweka tara-
tibu kwani mwili wote ulikuwa umetawaliwa na maumivu makali na damu
ilikuwa ikinitoka puani.
Sikutaka hali ile iendelee hivyo nikawahi kuingiza mkono wangu mafichoni
na kuichukua ile bastola ya Sam yenye kiwambo cha kuzuia sauti ambayo
wakati huu nilikuwa nimeibana kwa nyuma na mkanda wa suruali. Yule mtu
alipokuwa akija tena kuninyanyua nikamrushia teke moja zito la shingo lil-
ilompelekea apepesuke kama mlevi na sikumuacha hadi atulie hivyo muda
huohuo nikaziruhusu risasi tatu kupenya kwenye moyo wake kifuani na ku-
tokezea nyuma zikiacha matundu. Yule mtu akasombwa na kurushwa ukutani
kama tope zito lililokandikwa ukutani huku akipiga yowe la hofu na alipotua
chini akatulia bila kufurukuta akiwa tayari amekata roho. Nikasimama huku
nikitweta kama niliyemaliza mbio ndefu zenye upinzani wa hali ya juu.
Bado nilikuwa nikitweta ovyo na wakati huu nilihisi kama damu yote mwil-
ini ilikuwa ikikimbilia kichwani. Nikairudisha ile bastola mafichoni huku ni-
kimtazama yule mtu kwa udadisi. Sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni
mwangu na alikuwa mrefu sana, mweusi na mwenye mwili uliojengeka vizuri
kwa mazoezi mazito. Vilevile alikuwa na muonekano wa tabia zote za kiaskari
tena mwanajeshi aliyefuzu vizuri mafunzo ya kila namna katika hali zote.
Sasa nilijua kuwa nilikuwa nikiwindwa kwa hali na mali na watu hawa ha-
tari, nikajifuta na kujitengeneza vizuri usoni na mavazi yangu na niliporidhika
kuwa nilikuwa angalau nimerudi katika muonekano wangu wa kawaida nikau-
ruka mwili wa yule mtu kisha nikafungua mlango na kutoka nje.
Nje ya ile ofisi nilikuta kundi kubwa la watu waliokuwa wakifuatilia kili-
chokuwa kikiendelea ndani ya ile ofisi na sikutaka kuendelea kuzabaa eneo
lile hivyo niliharakisha nikikatisha katikati ya kundi lile la watu waliokuwa
wakitaka kufahamu kilichokuwa kikiendelea mle ndani na wakati nikikatisha
katikati ya wale watu, wale watu walikuwa wakinipisha kwa woga kama mzi-
mu unaotembea.
Niliendelea kuharakisha na nilipolivuka lile kundi la watu nikaanza kushuka
na zile ngazi kuelekea ghorofa ya chini ya ile hospitali. Nilipomaliza kushuka
nikaingia kwenye ile korido nikawa naufuata uelekeo wa nje ya hospitali ile.
Sikufika mbali sana wakati nilipoanza kusikia vishindo vya watu wakija
nyuma yangu na nilipogeuka nyuma kutazama nikawaona wanaume wawili
wakitimua mbio kunifuata. Sikuhitaji kuwasubiri na kuwasikiliza wale watu
kuwa walikuwa na dhamira gani na mimi kwani mikononi walikuwa wame-
shika bastola.
Bila ya kupoteza muda nami nikaanza kutimua mbio kuelekea nje ya hos-
pitali ile na muda huohuo nikaanza kusikia milio ya risasi ikirindima nyuma
yangu na watu wote waliokuwa wakija mbele yangu ambao wengi walikuwa
madaktari nao kuona vile wakageuka na kuanza kutimua mbio wakivitelekeza
vitanda vya wagonjwa walivyokuwa wakivisukuma. Nami kuona vile nika-
ongeza mwendo na kuwafikia kisha nikajichanganyanao katika namna ya ku-
wapotezea shabaha wale watu waliokuwa wakinifukuza.
Wale watu walikuwa wameishtukia dhamira yangu ya kutaka kuwapotea
hivyo nao waliongeza mbio kunikaribia na walikuwa na kasi sana. Sikutaka
kuwapa nafasi hiyo hivyo nilipofika kwenye lile eneo la mapokezi mahali ku-
lipokuwa na watu wengi nikafyatua risasi mbili hewani na hapa nilishindwa
kuelewa nani alikuwa mgonjwa na nani alikuwa mzima kwani kila mmoja ali-
yekuwa eneo lile alinyanyuka na kuanza kutimua mbio akishika uelekeo wake.
Hivyo kukawa na msongamano usioelezeka na mimi nikautumia mwanya huo
kujichanganya kwenye kundi lile la watu na kupotea nikishika uelekeo wangu.
Nilitoka nje ya hospitali kupitia geti dogo lililokuwa upande wa nyuma wa
hospitali ile. Nje kulikuwa na watu wachache na miongoni mwao walikuwa
wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa kando yateksi zilizoegeshwa eneo
lile. Na wakati nikitembea njiani nilipishana na watu wengine waliokuwa
wakiingia ndani ya hospitali ile na miongoni mwao hakuna hata mmoja ali-
yeonekana kunitilia mashaka ingawaje bado nilikuwa macho kuzichunguza
sura za watu hao na mienendo yao.
Wale watu waliokuwa wakinifukuza nyuma yangu sikuwaona tena hivyo
nikajua kuwa nilikuwa nimefanikiwa kuwatoroka. Kwa kuhofia kutengene-
za chanzo kizuri cha upelelezi sikutaka kukodi teksi nje ya geti lile dogo la
hospitali hivyo nilipotoka nje tu nikajichanganya kwenye kundi la watembea
kwa miguu nikishika uelekeo wa upande wa kushoto. Sikujua uelekeo ule un-
genifikisha wapi ila nilichokuwa nimepanga ni kutoweka haraka eneo lile.
Wakati nikiharakisha kutoweka eneo lile kichwa changu kilikuwa kimet-
awaliwa na mchanganyiko wa mawazo yasiyoeleweka. Nilihisi kuwa moyo
wangu ulikuwa ukienda mbio sana huku kiu kali ikiwa imenishika kooni. Nil-
ifika mwisho wa barabara ile ya watembea kwa miguu na hapo nikakutana na
barabara nyingine kubwa ya magari iliyokatisha mbele yangu.
Kabla ya kuufuata uelekeo wa upande wa kulia wa barabara ile nikakumbu-
ka kutazama nyuma na hapo moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu. Kuliku-
wa na mtu mmoja aliyekuwa akinifuatilia kwa nyuma, ingawaje kulikuwa na
msongamano mkubwa wa watu eneo lile lakini uzoefu wa mbinu za kijasusi
niliyokuwanao ulinisaidia kuligundua hilo ingawaje sikuweza haraka kufaha-
mu kuwa mtu yule alikuwa nani na alikuwa akiharakisha sana kunikaribia.
Nilishika ule uelekeo wa upande wa kushoto huku mkono wangu ukiwa
tayari umezama mafichoni kuipapasa bastola yangu. Kwa kweli nilikuwa ni-
mechoshwa sana na hali ya kufuatiliwafuatiliwa hivyo nilichokuwa nimepan-
ga ni kufanya shambulizi la kujihami na la kushtukiza ambapo ningegeuka na
kumshindilia risasi za kutosha mtu yule bila kujali macho ya watu waliokuwa
eneo lile halafu baada ya hapo ningepotea zangu.
Lakini kabla ya kufanya hivyo niligeuka tena nyuma kumtazama yule mtu
aliyekuwa akinifuatilia nyuma yangu na hapo nikajikuta nikishikwa na mshan-
gao. Yule mtu aliyekuwa nyuma yangu hakuwepo na badala yake kiasi cha
umbali wa kama mita thelathini niliwaona wale watu waliokuwa wakinifuku-
za kule hospitali wakitimua mbio kunifuata. Sikutaka kuanza kutimua mbio
kwani kwa kufanya hivyo ningeweza kuyavuta macho ya watu waliokuwa
eneo lile hivyo niliongeza mwendo huku nikiuvizia msongamano wa magari
uongezeke zaidi barabarani na msongamano huo ulipofikia katika kiwango
cha kuniridhisha nikakatisha barabarani kwa ghafla na kuvuka upande wa pili.
Lilikuwa tukio la ghafla sana na wale watu waliokuwa wakinifukuza ha-
wakuwa wamelitarajia hata hivyo nao pia wakavuka ile barabara wakinifuata
ingawaje walikwishachelewa kwani wakati wakifanya hivyo mimi tayari nili-
kuwa nimeshajichanganya kwenye kundi kubwa la watu na kuvua kofia yangu
kiasi kwamba wale watu waliokuwa wakinifukuza walinipita bila kunitambua
wakikimbilia mbele na mimi nikageuka nyuma na kuanza kurudi kule nilipo-
toka huku nikitabasamu kwa kuwapigisha chenga ya mwili. Nilikodi teksi na
kumueleza dereva anipeleke ule mtaa wenye nyumba ya Dr. Amanda Albro.
Saa yangu ya mkononi ilinionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa tisa
alasiri wakati nilipokuwa mbele ya mlango wa nyumba ya Dr. Amanda Albro
huku nikiiacha ile teksi ikitoweka nyuma yangu. Nikiwa na furaha ya mafani-
kio ya kiasi katika harakati zangu niligonga ule mlango kwa kishindo huku ni-
kisubiri sauti ya kike inikaribishe lakini nilishangaa kuona hali ilikuwa tofauti
na hapakuwa na dalili zozote za uhai ndani yake.
Niligonga mlango na kuendelea kuita bila kusikia suati yoyote ikiniitikia
na hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi. Bila kuchelewa nikaingiza mkono
mafichoni kuichukua bastola yangu kisha nikafanya utundu kidogo na kufan-
ikiwa kukibetua kitasa cha mlango ule na mlango ulipofunguka nikausukuma
taratibu na kuingia ndani huku bastola yangu ikiwa tayari kufanya kazi.
Nilikaribishwa na mazingira shaghalabaghala ya sebule ya nyumba ile yali-
yonishangaza. Vitu vyote vilikuwa vimechanguliwa na kutawanywa ovyo.
Nilisimama nikiichunguza sebule ile huku nikijaribu kuikumbuka sebule ile
namna ilivyokuwa ikipendeza wakati nilipoiacha asubuhi.
Niliendelea kuita bila sauti ya mtu yoyote kuniitikia mle ndani na hapo
nikaanza kunyata taratibu nikielekea vyumbani huku nikikikagua chumba ki-
moja baada ya kingine. Nilifarijika sana kuvikuta vyumba vya ile nyumba
vikiwa nadhifu ingawa katika sehemu moja au mbili niliweza kubaini kuwa
zilikuwa zimefanyiwa upekuzi.
Nilimaliza kuikagua nyumba yote lakini sikumuona Dr. Amanda Albro.
Kitanda chake kilikuwa kitupu na hapakuwa na dalili zozote za uwepo wake na
nyumba yote ilikuwa imetawaliwa na ukimya. Sauti pekee iliyokuwa ikisikika
ilikuwa ni ile ya mshale wa saa ya ukutani iliyokuwa sebuleni pamoja na sauti
hafifu ya maji yaliyokuwa yakiendelea kutoka taratibu kwenye bomba la maji
lililokuwa bafuni. Hofu juu ya jambo baya kuwa huenda lilikuwa limemtokea
Dr. Amanda Albro ikawa imeanza kuniingia na hapo nikaanza kujilaumu kwa
kuondoka na kumuacha peke yake asubuhi ile.
Nikafanya upekuzi wa haraka ndani ya nyumba ile na sikuambulia kitu cho-
chote cha maana kwani nyaraka zote muhimu zilikuwa zimechukuliwa. Roho
iliniuma sana lakini sikuwa na la kufanya na hatimaye nikarudi kule sebuleni
huku nikijihisi kukata tamaa sana huku nikijihisi kuishiwa nguvu kabisa katika
harakati zangu.
Wakati nikiwa naelekea sebuleni huku nimeinamisha kichwa chini na miko-
no yangu kiunoni katika hali ya kukata tamaa macho yangu yalijikuta yakita
zamana na kitu ambacho hapo awali nilikuwa sijakiona pengine kutokana na
harakati zangu.
Kulikuwa na michirizi ya damu sakafuni na michirizi hiyo ilinivuta na
nikaanza kuifuatilia tararibu ikakatisha pale sebuleni na kuelekea mlangoni na
wakati nikifanya hivyo koo langu lilikuwa mbioni kukauka kwa hasira. Hasia
zilizokuwa zikipita kichwani mwangu ni kuwa wale watu hatari waliokuwa
wakinitafuta huenda walikuwa wameyashtukia maficho yale ya Dr. Amanda
Albro na walikuwa wamefika pale na kumtesa kabla ya kumchukua kwa ngu-
vu.
Niliyakumbuka maneno ya yule mtu wa mwisho niliyepambana naye kule
hospitali wakati nilipomuuliza kuwa mwenzake alikuwa wapi huku akinijibu
kuwa mwenzake alikuwa mahali fulani akifanya kazi kama ile yake ya kutaka
kuniteka na hapo ndiyo nikajua kazi yenyewe kwa vyovyote huenda ilikuwa ni
hii ya kumtesa na kumteka Dr. Amanda Albro. Kwa kweli roho iliniuma sana
huku hasira ikiwa imenipanda nikaegemea ule mlango wa kutokea nje huku
nikijihisi kukata tamaa sana.
Sikuwa na nguvu tena za kuendelea na harakati zangu siku ile kwani mawa-
zo yalikuwa yamenielemea sana na hisia za kuhisi kutengwa na watu ziliku-
wa nikinitafuna moyoni hivyo nilihitaji kupata kwanza mlo na baada ya hapo
ningepumzika nikijipanga kwa hatua nyingine zinazofuata. Sikutaka kuende-
lea kuweka maskani yangu kwenye nyumba ile ya Dr. Amanda Albro kwani
nilihisi pengine huenda watu wale waliomteka Dr. Amanda Albro wangeweza
kumlazimisha kuongea juu yangu na kwa kufanya hivyo wasingeona ugumu
wowote wa kurudi na kuniwekea mtego wa kuninasa.
NILIMALIZA KUPATA MLO WA JIONI katika mgahawa mdogo ulioku-
wa ukitazamana na ukumbi wa sinema wa Kigali Nightmare zikiwa zimesalia
dakika chache kutimia saa mbili usiku. Nikanunua mzinga mmoja wa mvinyo
wa Afrikoko na kutoka nje ya mgahawa ule ambapo nilikodi teksi na kumtaka
dereva anipeleke eneo la Area C ilipo ile nyumba aliyonielekeza Rosine.
Sikutaka dereva yule wa teksi anifikishe hadi nje ya nyumba ile kwa saba-
bu moja kubwa ya kutotaka kushtukiwa na mtu yoyote ambaye angekuwa
ameweka mtego wa kuninasa hivyo teksi ile alinishusha mtaa wa pili kabla
ya mtaa ule wenye ile nyumba. Nikamlipa dereva pesa yake na kuagana naye
nikimtakia usiku mwema.
Nilipohakikisha kuwa teksi ile ilikuwa imeondoka eneo lile nikaingia
kwenye uchochoro wenye giza hafifu uliyonichukua hadi mtaa ule wenye ile
nyumba ya Dr. Amanda Albro lakini kabla ya kuifikia nyumba ile nikaamua
kufanya uchunguzi wa kutaka kujiridhisha kuwa nyumba ile ilikuwa salama
na hapakuwa na mtu yoyote eneo lile.
Sikuweza kumuona mtu yoyote nje ya nyumba ile na kitendo cha kuiona
nyumba ile ikiwa na giza kiliniridhisha kuwa hapakuwa na mtu yeyote ndani
yake hivyo niliamua kuingia ndani kwa kupitia upande wa nyuma wa nyumba
ile. Nilifanikiwa kuingia kupitia dirisha dogo la jikoni lililokuwa wazi huku
nikiwa nimechukua tahadhari zote za kukwepa kumshtua kiumbe yeyote am-
baye angekuwa ameniwekea mtego mle ndani.
Nikiwa sasa naifahamu vizuri ramani ya nyumba ile mara tu nilipokiacha
chumba cha jiko nikaingia upande wa kushoto nikiifuata korido iliyokuwa
pembeni ya sebule kuelekea vyumbani.
Nilikuwa mbioni kukamilisha hatua ya pili ya safari yangu ndani ya nyum-
ba ile pale nilipohisi kitu kama chuma cha baridi kikikigusa kisogo changu
na kwa sekunde kadhaa nikasimama huku viungo vya mwili wangu vikikosa
mawasiliano mazuri kama mgonjwa wa kiharusi. Moyo wangu ukasimama
ghafla kabla ya kuanza kwenda mbio huku jasho jepesi likianza kufanya zi-
ara katika sehemu mbalimbali mwilini mwangu na hapo nikawahi kuupeleka
mkono wangu mafichoni kuichukua ile bastola yangu hata hivyo sikufanikiwa
kwani wakati nikiitoa bastola hiyo nilipigwa pigo ambalo sikuweza kulielewa
kwa haraka lilipigwa kwa mtindo gani kiasi cha kuweza kuipokonya bastola
yangu mkononi kama kifaranga cha kuku kinavyonyakuliwa na mwewe.
Ile bastola yangu ikaangukia sehemu fulani sakafuni na sikuweza kuiona ku-
tokana na giza zito lililokuwa mle ndani na yule mtu nyuma yangu hakunise-
mesha neno lolote hali iliyozidi kunitia hofu na kunichanganya. Nikaupeleka
tena mkono wangu mafichoni kuichukua ile bastola niliyopewa na Dr. Amanda
Albro ambayo sasa ilikuwa imesalia lakini kabla sijafanikisha zoezi hilo sauti
ya kilimi cha bastola kilichovutwa nyuma yangu ilipenya masikioni mwangu
na kunionya. Ikabidi nisitishe kile nilichokuwa nikitaka kukifanya na sikuwa
na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuanzisha mapambano ya ana kwa ana
katikati ya giza lile.
Nilizunguka kwa kasi ya ajabu nikitupa pigo la ngumi usawa wa shingo ya
yule mtu nyuma yangu lakini ilikuwa kazi bure kwani yule mtu alikuwa mwe-
pesi kuishtukia hila yangu hivyo pigo langu lilikata hewa bila kutoa majibu
sahihi hali iliyonipelekea nipepesuke kwa kupoteza mhimili na wakati huohuo
nikajikuta nikipokea kipigo cha ngumi mbili kavu za chapuchapu mbavuni
mwangu zilizonifanya nijihisi kutaka kutapika. Pigo jingine la teke lililorush-
wa niliwahi kulikwepa kwa kuruka hewani kwa mtindo wa samasoti na nili-
pokuwa nikitua chini nilibinuka na kuachia teke farasi.
Lilikuwa pigo zuri kwani nilimsikia yule mtu akigugumia kwa maumivu na
sikutaka kumkawiza hivyo nikamfuata katika mtindo wa kujiviringisha sakaf-
uni kama gurudumu na nilipomfikia yule mtu nikajizungusha nikimchota mta-
ma wa chini lakini aliwahi kunishtukia akanitandika teke la kifua lililonirusha
nyuma.
Niliwahi kusimama hatua moja kabla yule mtu hajanifikia na kuanza kuni-
tupia mapigo ya mfululizo. Nikajitahidi kuyakwepa mapigo yale kwa kadiri
nilivyoweza hata hivyo nilipoona hali inazidi kuniwia vigumu nikaruka he-
wani na kuganda ukutani huku mguu mmoja ukiwa umegota upande mmo-
ja wa ukuta na mguu wangu mwingine vivohivyo kwa upande mwingine wa
ukuta wa korido ile kisha nikajibetua na kuruka hewani nikitua umbali mfupi
nyuma ya yule mtu lakini wakati huohuo nikimtupia pigo moja matata la teke
mgongoni mwake na hapo yule mtu akapepesuka na kugugumia kwa maumi
vu.
Nilitua chini na kumrudia haraka yule mtu nikirusha teke jingine jepesi
lakini alikuwa mwepesi wa kulidaka na kulivuta kwa kasi na hapo nikapo-
teza mhimili nikiserereka na kwenda kujipigiza ukutani huku nikiguna kwa
maumivu makali na hapo tusi zito likiniponyoka mdomoni.
Wakati nikijiandaa kusimama yule mtu tayari alikuwa amekwishanifikia
hata hivyo sikumpa nafasi hivyo nikawahi kusimama vizuri na kumrukia ni-
kimsomba na hapo wote tukaruka hewani lakini mimi nikiwa juu ya yule mtu
na wote tukaanguka chini kwa kushindo huku mkono wangu wa kulia ukiwa
umeibana vizuri shingo ya yule mtu na ule mkono wangu wa kushoto ukim-
shindilia ngumi mbili za tumbo na hapo nikamsikia yule mtu akipiga yowe
la maumivu.
Kuna kitu kimoja kilichonishtua katika yowe la mtu yule kwani lilikuwa ni
yowe la sauti nyepesi ya kike iliyonifanya nishikwe na butwaa. Pigo la tatu
nililokuwa nikijiandaa kulitupa likaishia njiani huku nikijiuliza mtu yule ni
nani na wakati nikiwa katika hali hiyo nikajikuta nimeshaenea kwenye kabari
matata ya tumbo iliyofanywa kwa kuzungushiwa miguu nyuma ya mgongo
wangu huku nikiwa nimemlalia mtu yule kwa juu.
Nilipotaka kufurukuta nikajikuta nikitazamana na mtutu wa bastola ulio-
kuwa ukikandamizwa katikati ya paji langu usoni na hapo nikawa sina tena
ujanja. Sote kwa pamoja tukabaki tukihema ovyo na wakati tukiwa katika hali
hiyo bado nilimsikia yule mtu chini yangu akalalama kwa maumivu na sauti
yake ilikuwa nyepesi na ya kike.
Taratibu nikauondoa mkono wangu niliokuwa nimeukandamizia shingo
yake na hapo yule mtu akaanza kukohoa ovyo na sikuona tena jitihada zake za
kuendelea kunibana tumboni kwa ile kabari yake. Lakini yule mtu hakuiondoa
ile bastola yake usoni kwangu hivyo tukabaki tukitazamana ingawaje haku-
na mtu aliyeweza kumuona mwenzake kutokana na giza zito lililokuwa mle
ndani.
Hisia tofauti zikaanza kujengeka kichwani mwangu, roho ya huruma ikaan-
za kuniingia taratibu huku nikijilaumu kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya
kiumbe kile cha kike. Tukiwa bado tunaendelea kukumbatiana pale chini na
yule mtu hisia za mapenzi zilianza taratibu kuzitongoza fikra zangu. Nika-
wa nikilihisi vizuri joto la yule kiumbe aliyekuwa chini yangu kuwa lilikuwa
likipenya taratibu mwilini na kuanza kuichemsha ovyo damu yangu na hapo
moyo wangu ukaanza kunienda mbio huku nikijihisi kuishiwa nguvu taratibu.
“Maradhi gani haya? nilijiuliza kama mwehu na bila kujua sauti yangu ika-
wa imesikika na yule mtu aliyekuwa chini yangu na hapo nikaisikia sauti nye-
pesi ya kike ikiniita.
“Patrick...!” hata hivyo sikuitika nikijidai kuwa sijamsikia na hapo akarudia
tena kuita
“Ni wewe Patrick? safari hii yule mtu chini yangu aliita kwa sauti ya juu na
yenye hakika
“Drel Fille...!”
“Patrick...! Mungu wangu ni wewe?
“Ni mimi mpenzi, Drel...?
“Bhee! Patrick mbona siamini... Mungu wangu!”
“Ni mimi mpenzi loh! hata mimi siamini, ulikuwa wapi Patrick?
“Ni hadithi ndefu sana mpenzi na wewe ulikuwa wapi mbona ulinitoroka?
Drel Fille aliongea huku akianza kulia kilio cha kwikwi ya chinichini.
“Sikukutoroka mpenzi ni hadithi ndefu kama yako na sikufikiria kabi-
sa kama tungeonana tena mpenzi” niliongea huku nikijitoa taratibu kifuani
kwa Drel Fille na wakati nikifanya hivyo Drel Fille alinizuia kwa miguu yake
aliyoikutanisha nyuma ya mgongo wangu lakini akaiondoa ile bastola aliy-
oielekezea usoni kwangu.
“Tafadhali usiondoke mpenzi” Drel Fille alinong’ona kwa sauti ya kubem-
beleza.
“Kwanini mpenzi hatuwezi kukaa hivi kwa muda mrefu” nilimwambia huku
nikifanya jitihada za kujinasua toka kifuani kwake lakini mara hii pia alinizuia
huku akinivutia kifuani kwake na wakati huu niliweza kuyahisi mapigo ya
moyo wake yalivyokuwa yakienda mbio na hapo nikajua ni kitu gani alichoku-
wa akimaanisha.
“Hapana siyo sasa hivi mpenzi”
“Kwani ni kipi kinachokuzuia?
“Tunahitaji kuzungumza kwanza juu ya yaliyotusibu na istoshe hapa si
kitandani mpenzi”
“Nina kiu sana mpenzi tafadhali naomba uielewa haja yangu. Kitanda hak-
ina maana sana wakati huu”
“Lakini tuna muda wa kutosha mpenzi ya nini kuharakisha?
“Nataka sasa hivi” Drel Fille aliniambia huku sauti yake akitoka kwa hi-
sia kama mtu aliyekata tamaa na kupitia maneno yake niliweza kuisoma kiu
ya mapenzi aliyokuwanayo hivyo endapo ningeendelea kuushikilia msimamo
wangu hali ingekuwa mbaya zaidi. Hata hivyo hisia zangu hazikuwa kwenye
mapenzi hivyo nikaamua kujinasua kwa nguvu toka kifuani kwake huku ni-
kimnyanyua Drel Fille lakini sikufanikiwa kwani Drel Fille alinitandika ngu-
mi ya uso iliyonirusha nyuma na kunisababishia maumivu makali.
Nikaanguka chali sakafuni na kabla sijanyanyuka Drel alishaniparamia
kifuani kwangu kama aliyepandwa na wazimu wa mapenzi. Nikajitahidi
kumzuia lakini jitihada zangu ziligonga mwamba na kabla sijazungumza neno
ulimi wa Drel Fille ukawa umeshapenya mdomoni mwangu ukizunguka huku
na kule hivyo hata yale maneno niliyokuwa nikiyatamka hayakuweza kusikika
tena na badala yake yalisikika kama lugha ya ajabu ambayo wazungumzaji
wake huenda walikuwa hawajazaliwa
Muda uleule mikono ya Drel Fille ikaanza kufanya ziara kifuani kwangu
hali iliyonipelekea nianze kuhema ovyo. Mkono wake mmoja ukawa ukite-
remka taratibu kutoka kifuani kwangu kuelekea tumboni na baadaye kitovuni
na mkono huo ulipofika kiunoni kwangu ukaweka kituo. Sikufahamu nini kili-
chotokea lakini nilishangaa kuona suruali yangu ikiteremshwa chini taratibu
na nilipojitahidi kufurukuta Drel Fille alinizuia kwa kuzidi kunikandamiza
chini.
Ule mkono wake ukawa ukiendelea kupenya zaidi kiunoni mwangu na uli-
pofika chini nikaanza kuhisi kuwa damu yangu ilikuwa ikichemka mwilini
huku mapigo ya moyo yakinienda mbio isivyokawaida. Sikuweza kuvumilia
zaidi hivyo na mimi nikaipeleka mikono yangu na kukikamata vema kiuno
chake na hapo nikamsikia Drel Fille akihema ovyo na cha ajabu zaidi hata
yale maumivu ya ngumi yake aliyonitandika usoni sikuweza kuyasikia tena
kwa wakati huu.
Niliishika blauzi yake na kuirarua na hapo nikafurahi kukuta kuwa matiti
yake hayakuwa yamehifadhiwa na sidiria hivyo mikono yangu ikazikamata
vizuri chuchu zake na kuanza kuzitomasa tomasa na wakati nikifanya hivyo
nilimsikia Drel Fille akianza kuhangaika ovyo huku akiongea maneno yasiyo-
eleweka. Mkono wake ukanishika sehemu ambayo kwa hakika sikupenda ai-
shike mapema kiasi kile na muda mfupi uliofuata tukawa kama tulivyozaliwa
huku nguo zetu tukiwa tumezitupia kusikojulikana.
Drel Fille alikuwa juu yangu na kwa mbali nilimsikia akilalamika kwa fura-
ha huku akifurahia utundu wangu katika mapenzi huku taratibu akipanda juu
na kushuka chini lakini wakati huu akiwa mtulivu na si mwenye papara tena.
Tuliendelea kubadilishana ndimi zetu kwa zamu na kila mara furaha ilipofuri-
ka hakuna aliyejizuia kupiga kelele hafifu za furaha au kuongea maneno ya-
siyoeleweka. Drel Fille alikuwa mwanafunzi aliyehitimu vizuri katika darasa
la mapenzi na kwa kweli alifanikiwa kunisahaulisha kwa muda juu ya mikasa
yote niliyopitia.
Ilikuwa starehe ya kipekee ambayo nilikuwa sijaipata kwa muda mrefu.
Drel Fille alikuwa akitoa miguno ya hapa na pale kuashiria kuwa nilikuwa
nimemfikisha anapopataka na hakutaka kuniacha mapema kwani kila nilipoji-
tahidi kujiondoa kifuani kwake bado alining’ang’ania.
Tulitoka pale sakafuni tukahamia kwenye kochi kubwa lililokuwa pale se-
buleni huku kila mmoja akiendelea kucheza vizuri na hisia za mwenzake. Drel
Fille alikuwa msichana mtundu sana wa mapenzi na alijua kucheza vizuri na
hisia zangu. Kifua chake kikiwa juu ya kifua changu niliweza kuzisikia pumzi
zake nyepesi zikipenya pembeni ya shingo yangu alipokilaza kichwa chake na
mikono yangu ilishikilia vyema kiuno chake kilichokuwa kikipanda na kushu-
ka taratibu juu ya kiuno changu katika mjongeo ulionifanya nizidi kuchangan-
yikiwa na penzi la Drel Fille.
Tulipitiwa na usingizi juu ya kochi lile huku tukiwa hoi hatujitambui kwa
uchovu na wa kwanza kuamka alfajiri alikuwa Drel Fille. Aliamka na kuni-
acha kwenye lile kochi nikiwa bado nakoroma kwa uchovu na alipoamka
akaenda jikoni kuandaa kifungua kinywa kizito ambapo baadaye alikitenga
mezani pale sebuleni.
Alipokuja kuniamsha nilikuta tayari ameniandalia maji ya kuoga bafuni.
Sote tulikuwa tunaoneana aibu kwa kuzingatia kuwa hatukuwa na mazoea ya
muda mrefu tangu tulipofahamiana na hakuna aliyekuwa akimjua mwenzake
kwa undani zaidi ingawaje mimi sasa nilikuwa namtambua Drel Fille kama
mpelelezi kutoka nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na si yule msi-
chana mwenye majina mengi aliyonidanganya.
Nilipomaliza kuoga nilikuta tayari nimeshaandaliwa nguo za kuvaa
zilizokuwa kitandani na hapo nilichagua nguo zilizonienea vizuri na kuzivaa.
Zilikuwa ni nguo zilizokuwa katika moja ya masanduku ya nguo yaliyokuwa
mle chumbani na wakati nikijiandaa nilihisi kichwa changu kilikuwa kimepata
utulivu wa kutosha wa kuweza kuanza tena harakati zangu.
Nilimkuta Drel Fille akiwa ameketi mezani akinisubiri huku yeye pia akiwa
ameshajiandaa na kubadili zile nguo zake alizozivaa jana. Drel Fille asubuhi
hii alikuwa akionekana mzuri na mrembo kupita kiasi hali iliyonipelekea ni-
jisikie furaha moyoni kwa kushiriki penzi na msichana mzuri kama huyu.
Nywele zake alikuwa amezifunga mabutu madogo madogo, nyusi za macho
yake meupe alikuwa amezipaka wanja mweusi na kumfanya azidi kupendeza.
Kifua chake kilikuwa kimebeba mzigo wa matiti yenye ukubwa wa wastani
yaliyofunikwa kidogo kwa sidiria nyepesi. Mikono yake ya kike lakini imara
yenye vidole virefu na kucha za kuvutia alikuwa ameiegemeza juu ya meza
huku mkono wake mmoja ukikoroga sukari kwenye kikombe. Drel Fille ali-
poniona uso wake ukaumba tabasamu jepesi lililoivuruga kabisa akili yangu.
Kingo za mdomo wake ziliachana kidogo na kuyaruhusu meno yake meupe
kuonekana vizuri na hapo nikakubali vizuri moyoni kuwa Drel Fille alikuwa
msichana mzuri sana niliyewahi kukutana naye katika maisha yangu.
“Pole mpenzi wangu”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Ahsante mpenzi, kweli nimekukubalia kuwa unayamudu vizuri majukumu
ya nyumba kama mama”
“Kwa nini unasema hivyo Patrick? Drel Fille aliniuliza huku akitabasamu.
“Shughuli yote ile ya jana usiku na bado umeweza kuamka mapema na
kuandaa kifungua kinywa na kuniandalia maji. Huoni kuwa nisipokupongeza
nitakuwa sijakutendei haki mpenzi? nilimtania huku nikiangua kicheko hafifu.
“Usinichekeshe mpenzi ukizaliwa wa kike hivi ni vitu vya kawaida kabisa
yaani lazima utavizoea tu”
“Mh! kama mimi ningekuwa wa kike mbona ningeachika mapema”
“Ndiyo maana ukazaliwa wa kiume” Drel aliniambia wakati nilipokuwa ni-
kivuta kiti na kuketi pale mezani na hapo tukatazamana kidogo kabla ya kila
mmoja kuponyokwa na tabasamu halafu halafu na hali hiyo ilipokoma tukaan-
za kupata kifungua kinywa na hapo maongezi mengine yalifuatia kusindikiza
tukio hilo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment