Simulizi : Mimi Na Rais (The President And I)
Sehemu Ya Nne (4)
Jesuiti, kwa kimombo wakiitwa Jesuits au kwa maneno mengine Society
of Jesus ni moja ya mashirika makongwe sana ya mapadri. Shirika hili
likiwa limeanzishwa huko Ufaransa na Mtakatifu Ignatus wa Loyola ni
moja ya mashirika yanayoheshimika sana na lenye nguvu kwenye
kanisa katoliki.
Mathalani, hata Baba Mtakatifu Francis ni zao la shirika hili akiwa ndiye
Papa wa kwanza ambaye ni Jesuiti. Wenyewe hujiita Jeshi la Mungu la
Askari wa Nchi kavu na kwenye Maji au kizungu hujiita ‘God’s Marines’.
Labda hii imetokana na asili ya mwanzilishi wao kuwa na historia ya
jeshi.
Moja ya sifa yao nyingine ni usomi wa hali ya juu. Ni wasomi wa
kiwango cha juu sana na ndio maana wana shule nyingi duniani na vyuo
vikuu zaidi ya 189 tena vyenye hadhi za juu. Chuo kama Georgetown
huko Marekani (Georgetown University), Boston (Boston Collage), Loyola
(Loyola University), Fordham (Fordham University) na vingine vingi ni
vyuo vinavyomilikiwa na shirika hili.
Inaaminika kuwa shirika hili ndilo humtii Papa kuliko mapadri wowote
wale. Wao husema kuwa wapo tayari kufa kwa ajili ya Papa na kufanya
chochote atakachowaagiza. Kiapo hiki wanachokiita Kiapo cha nne
(Forth Vow) hutakikuta kwenye shirika lolote la mapadre wa kanisa
katoliki isipokuwa kwa wana Jesuiti. Wana mengi hawa. Itoshe tu
kusema Jesuiti ni zaidi ya watawa.
*************************
Mishale ya saa tano hivi Gideoni alikuja kuchukuliwa o?isini kwake pale
Ikulu ili akakutanishwe na Stanley Macha. Alitolewa na kuingizwa
kwenye gari siti za nyuma. Alishangaa kuona kuwa hawezi kuona nje
kwa namna yoyote ile, yaani ni kama mtu aliyeingia kwenye pipa halafu
likafunikwa kwa juu.
Ndani ya gari lile siti aliyokaa kwa juu kulining’inia kipaza sauti
ambacho aliweza kuongea na kujibiwa na waliokaa mbele. Aliuliza ni
kwanini wanamsa?irisha katika hali ile na kujibiwa kuwa sehemu
anayopelekwa ni siri na alitakiwa asijue ni eneo au nyumba gani na
kwamba ni watu maalumu tu wanaotakiwa kujua nyumba hiyo ipo
wapi.
Gideon aliposikia hivyo akaona isiwe tabu akachukua simu yake ili
awashe Google Map na angeweza kujua anapoelekea. Alishangaa kuona
mtandao ndani ya gari lile haupatikani na hata sauti za nje hazisikii
ndani.
Gari lilianza safari na Gideon aliona ujanja ni kuanza kuhesabu kona.
Alijaribu akidhani atafanikiwa lakini kuna mahali alichanganywa hadi
biashara ile ikamshinda.
“Mkuu usihesabu kona hutaweza”, alisikika dereva akimwambia Gideon
huku akicheka. Walijua ujanja ambao Gideon angeufanya.
“Huku ndipo mnapopaita Red Square?”, Gideon alihoji.
“Ilipokuwa Red square ya zamani maana tangu juzi imetoka amri Red
square imeshabadilishwa eneo. Sabinasi kabadili na bado ni siri kubwa”,
dereva alijibu.
Gideon alihisi kuishiwa nguvu. Kwa miaka yake saba akiwa Ikulu
hakuwahi kujua Red square, moja ya nyumba za siri za Idara ya Usalama
Wa Taifa Stanza ipo eneo gani. Hata Ra?iki yake kipenzi Stanley Macha
hakuwahi kumwambia.
Walitembea kwa dakika 40 na kisha Gideon alihisi kama wanaingia
shimoni ama kwenye handaki maana gari iliinama chini kwa dakika
kama tatu hivi na kisha mlango ulifunguliwa akashuka.
Eneo lile lilikuwa na taa nyingi na madirisha lakini ambayo yalikuwa
ndani ya jengo yaani usingeweza kuona anga.
Kijana mmoja alimwongoza Gideon wakiwa wanapita milango kadhaa
iliyofunguliwa kwa alama za vidole (?inger prints) mpaka mlango wa
mwisho uliofunguliwa kwa kuweka lenzi ya mboni ya jicho ya mmoja
wa wale madereva.
Waliingia ndani na Gideon alistaajabu hali aliyomkuta nayo Macha.
Stanley Macha alikuwa amechoka na mwenye maumivu makali. Alikuwa
amelazwa kwenye kitanda cha chuma akiwa amefungwa mikono, kiuno
na miguu vyote vikiwa vimefungamanishwa na kitanda kile kama vile
maiti inayotaka kwenda kuzikwa.
Mbele ya nyayo zake kuliwashwa mishumaa iliyokuwa ikiunguza nyayo
zake tartiiibu hivyo kusababisha malenge lenge makubwa. Mdomoni
alifungwa riboni ya gundi iliyomfanya asiweze kutoa sauti za kilio cha
maumivu.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Inspekta Majita alikuwa akiendesha kile wazungu wanakiita ‘enhanced
interogation’ yaani mahojiano ya mateso. Mahojiano ya namna hii
hufanyika mara baada ya jitihada za kumfanya mlengwa aongee jambo
unalotaka a?ichue zinaposhindikana.
Lakini pia kwa siku za karibuni mahojiano ya namna hiyo yamekuwa
yakipigwa vita kwani humfanya mtu kudanganya au kukubali jambo
ama kukataa hata kama si kweli ili tu ajiepushe na mateso. Kwa nchi
zilizoendelea wametengeneza mifumo na teknolojia zinazoweza
kumfanya anaehojiwa kugundulika kama anadanganya ama la bila hata
kumtesa.
Mashirika mengi ya kijasusi na ya kiuchunguzi katika nchi zilizoendelea
hutumia teknolojia inayoitwa ‘Polygraph’, almaarufu kama ‘lie detector
test’ ambacho ni kifaa maalumu kinachopima na kurekodi viashiria
mbalimbali vya kimwili kama vile msukumo wa damu, mapigo ya moyo,
upumuaji, na mienendo ya ngozi wakati ambao mtuhumiwa anaulizwa
na kujibu maswali mfululizo.
Mathalani, kuna vifaa vinavyopima mapigo ya moyo ukiwa unaongea
ukweli au uongo, vifaa vinavyopima mpepeso wa macho na njia
nyingine kama zile wazungu wanazoita ‘Logical deduction’ ambazo
hazimuumizi muhojiwa lakini humpelekea anaehoji kuujua ukweli.
Pamoja na teknolojia hizi kuwepo, bado nchi nyingi duniani ikiwamo
Stanza ziliendelea kupendelea mfumo wa zamani wa mahojiano
uliohusisha mateso kwa mlengwa hadi aseme lile anayehoji anataka
kusikia. Hali hii ilimkumba Macha, aliyekuwa bosi wa wale wanaofanya
kazi hizo. Lakini Stanley Macha akiwa mtaalaamu wa yote hayo
ilishindikana kumpata kwa lolote.
Gideon alipoingia na kumkuta Macha akiwa kwenye mateso makubwa
huku akigugumia wakati Majita akivuta sigara bila hata kumtazama
Macha alipiga kelele….
“Kwa amri ya Rais simamisha zoezi hili Majita”, Gideon alifoka huku
machozi yakikaribia kumtoka.
Majita bila hata kujibu kitu alisogea na kufungua zile kamba kisha bila
kusema na mtu alitoka nje ya kile chumba. Majita alikuwa ni kama
shetani aliejivika ng’ozi ya mtu.
Gideon alimsogelea Macha na kukosa la kutamka. Alibaki akimwangalia
na Macha hakika alikuwa akigugumia kwa uchungu wa kilio alichojikaza
kisitoke nje.
“It’s ok. I have got your back”, Gideon alinong’ona.
“Familia yangu ipo salama? Joe amekamatwa?”. Macha aliuliza haraka.
“Familia zipo salama na Joe bado hajakamatwa ila Costa ametoa amri ya
Majita kukutesa hata kifo kama hutasema chochote kuhusu mpango ule.
Hivi ninapoongea na wewe amesema pia atawatuma watu China
wakamsake Joe na popote watakapoweza kumuua basi wamuue”,
Gideon aliongea kwa haraka na yeye. Hawakuwa na muda wa kupoteza.
“Umejitahidi mpaka ku?ika hapa kuniona, umejitahidi sana. Sasa
utawasiliana na Meja Kairuki Byabato wa pale makao makuu ya Jeshi,
uki?ika mwambie ‘Sienta-Go’ ataelewa. Lakini pia Rais akikuuliza
nimekuambia nini kwa ujio wako huu mwambie ninahitaji kuongea nae.
Sio huku, Ikulu ama Idarani. Lakini niambie nani amekaimishwa
kuongoza Idara?” Macha alihoji kwa haraka.
“Sabinasi, na amepangua watu wote Ikulu. Hivi jengo hili lipo wapi
nimeshindwa kupafahamu.” Gideon alihoji.
“Majengo haya yanaitwa Red square huwa ni siri kubwa kati ya watu
wanne. Rais, Mkuu wa Idara na wale madereva wawili. Hata Inpekta
Majita hajui hapa ni wapi ameletwa kama ulivyoletwa wewe.
Sasa sidhani kama jengo hili mimi nitakuwa najua lipo wapi kwa sababu
lazima wamebadilisha na ndio utaratibu. La zamani lilikuwa mtaa wa
Khanama lakini najua mkuu mpya wa Idara akiingia cha kwanza ni
kutafuta Red square yake na madereva wake wa kuwaleta watu huku.
Huku ndiko watu huweza kutoweka na wasipatikane maisha yao yote
na watu wakadhani wamekufa kumbe wapo huku. Watu wenye taarifa
muhimu huwezi kuwaua, unawatunza lakini unawatoa kabisa kwenye
macho ya dunia na mara baada ya kujiridhisha kuwa hawana faida tena
na wewe ndio huwaua. Gideon nimekwambia kuliko uliyotakiwa
kusikiliza, muda sio Ra?iki, kaendelee na taratibu za misheni.
Ila hakikisha haukamatwi kwani mateso haya huwezi kuyastahimili
hata kwa sekunde moja”, Macha aliongea kama mzazi kwa mwanae.
“Sasa wakati nilipotaka kutoka niliona Rais Costa akisaini jalada fulani
limeandikwa Presidential Order: Order to Kill. Sikuweza soma vizuri
linahusu nini ila kulikuwa na majina na jina moja wapo ni Sylvanus
Majura, unalifahamu hili jina?”, Gideon alihoji.
“Loh, huyo ni ‘Special assassin’ wa Idara. Kwa vyovyote ni kati ya
waliotumwa kumuua Joe. Jina hilo llikuwa la kwanza ama la mwisho?”,
Macha aliuliza.
“La Mwisho”, Gideon alijibu kwa haraka.
“Basi huyo ndio kiongozi wa misheni. Sisi huandikaga kutokea chini
kwenda juu. Sasa mtaarifu Joe awe makini”, Macha alishauri.
Kabla Gideon hajaongea jambo lingine, mlango ulifunguliwa na Majita
kwa sauti ya kukoroma na yenye besi nzito alimtaka Gideon kuondoka
eneo lile.
Gideon alitoka kwa kasi akiongozwa na wale madereva na kuingia
kwenye gari lililomleta ili kuelekea Ikulu.
Ali?ika Ikulu na kukuta Rais yupo na ratiba yake ya vikao hivyo alienda
o?isini kwake na kuingia kwenye game ya Clash Royale na kuanza
kumpa Joe taarifa zote alizokusanya siku ile.
******************************
“Habibu muda wetu kukaa hapa umekwisha kesho twapaswa
kuondoka” Joe alimwambia Habibu aliyekuwa amejilaza kitandani
kwenye kile chumba.
“Tunaeleke wapi?”, Habibu alihoji.
“Sijajua bado. Najua Korea wataanza kumsumbua Rais Costa kuanzia
kesho”, Joe alijibu.
Wakiwa wanajadiliana mara mlio wa simu wa Joe uliita kuonyesha
kuwa kwenye game yake ya Clash Royale kuna ujumbe umeingia.
Alichukua na kuanza kusoma.
Alikuwa Gideon amempa taarifa na mipango yote. Alihuzunika sana
aliposikia hali ya Macha.
“Subiri niwasiliane na Meshack kuhusu huyu Sylvanus”, Joe alimjibu
Gideon.
“Kuna taarifa gani?”, Habibu alihoji.
“Tuwe makini kuna watu wametumwa kuja kunitafuta ili waniue. Bahati
nzuri wewe sio tageti wa Rais Costa. Sasa subiri niwasiliane na
Meshack”, Joe alijibu.
Joe alianza kumpigia Meshack Simu kwa njia ya WhatsApp kwenye
namba ambayo Meshack huitumia kwa kazi maalumu. Kwa kawaida
simu za WhatsApp ni salama kwasababu maongezi yake hayawezi
kudukuliwa na serikali au mashushuhu kwasababu tu zina mfumo wa
usalama wa usimbaji ?iche wa mpigaji au mtumaji ujumbe na mpokeaji,
yaani end-to-end encryption. Simu iliita na mwishowe akaipokea.
“Kaka”, Meshack aliita.
“Got an intel kuwa Sylvanus ametumwa kuja kunimaliza.
Unamfahamu?”, Joe alihoji.
“Ndiyo. He is the master of silent killing. One of the worst assasins in
Stanza, I can con?idently argue”. Meshack alionekana kuongea kwa sauti
ya taratibu.
“Now, you need to deal with him before he boards to China”, Joe
alimwambia Meshack kifupi.
“Do you mean killing him? No, that I can’t guarantee you Joe. He is a
very intelligent agent, If I poke him, I may compromise everything here.”
Meshack alijibu
“Meshack, wewe ndio ulikuwa unamlinda Rais Costa, iliwezekanaje
awekwe mtu asiye hodari kumlinda Rais? Macha ameniagiza nikwambie
‘umhandle’ Sylvanus”, Joe alimwambia Meshack.
Meshack alikaa kimya kidogo. Alitafakari ni namna gani anaweza
kumuua Sylvanus, kwanza bila yeye kuwahiwa na pili bila kujulikana.
Aliona sasa hapo ametiwa majaribuni na suala hili litaweka Maisha yake
kwenye mstari wa mauti.
“Hii ni mbwa kula mbwa kaka”, Meshack alinong’ona akijua Joe
hamsikii.
“Vyovyote utakavyoiita. Just do it” Joe wakati huu alionekana kuongoea
kwa kutoa amri. Alikata simu.
Mara baada ya Joe kukata simu alipokea ujumbe mwingine kwenye
simu yake. Aliusoma kwa makini kama vile unampa maelekezo Fulani
aliyopaswa kuyafuata kwa makini. Wakati huo Habibu alikuwa
anamuangalia kila kitu, akishangazwa na sura ya Joe iliyoonekana kuwa
na hasira mara baada ya mazungumzo yake na Meshack.
Mara baada ya Joe kusoma ujumbe ule na kumaliza, alimwambia Habibu
kuwa asimame waondoke. Habibu alitaka kutouliza, lakini akajikuta
anashindwa kuvumilia.
‘’Joe, ni nini kinaendela? umeshajua tunakwenda wapi na hatua gani
inafuata’’? Habibu aliuliza maswali mfululizo.
‘’The transfer window has just opened. Expect some new powerful
signings soon. Stanza will be turned upside down soon enough. We are
going to reclaim our country, the country that the founding fathers and
mothers fought to liberate from the yokes of colonialism. We cannot
allow to be colonized by our fellow countrymen’’.
(Dirisha la Usajili limefunguliwa. Tarajia uhamisho wa wenye nguvu hivi
karibuni. Stanza itageuzwa juu chini hivi karibuni, ingawa bila kumwaga
damu ya mtu. Lazima tuichukue nchi yetu, nchi ambayo wazee wetu
waliipigania kuondoa minyororo ya ukoloni. Hatuwezi kuruhusu
kufanyiwa ukoloni na Wanastanza wenzetu’’, Joe alimjibu Habibu kwa
mafumbo.
‘’So be it’’, Habibu hakuongezea neno bali kujibu kwa ufupi.
*************************
Stanza Mambo Ni Vululu Vululu
“Gideon, did you manage to get any intel from that grand traitor? (Gideon, umepata taarifa zozote za kiintelijensia kutoka msaliti mkuu?), Rais Sylvester Costa alimuuliza Gideon huku wakitembea kulekea ofisini kwake.
Rais Costa alikuwa kitoka kwenye kikao cha kuhabarishwa yanayojiri kwenye vyombo vya habari hususani suala la yeye kumiliki visiwa vya kitalii huko Ufilipino lilifikaje kwenye vyombo vya habari na ilikuwaje ikachapishwa bila watu wa usalama kujua na hivyo kuanza kuharibu taswira yake mbele ya wana Stanza. Alitaka kufahamu kiongozi wa upinzani, Julius Kibwe alifahamu vipi taarifa ambazo hakuwahi kumwambia hata msaidizi wake wa karibu, Bw. Gideon.
“Nimeongea kwa kina na Macha na amenipa ushirikiano wa kutosha, nadhani wazo langu lilikuwa sahihi kuwa watu kama hawa wanaona kuhojiwa na mtu kama Inspekta Majita ni kumdhalilisha. Ameniambia mpaka sasa ameteswa sana na ni kweli nimemkuta kwenye mateso makubwa.
Kimsingi Macha anasisitiza kuwa anataka kuzungumza na wewe, na ili kusema kile anachotaka anasisitiza kuwa ni vyema akaja hapa Ikulu au kule ofisi za Idara, na si nyumba za maficho za usalama.” Gideon alimjibu Rais Costa huku wakitembea wakiwa wamezungukwa na vijana wanne wa Idara ya Usalama.
“Gideon, kwa hiyo hilo ndilo alilokwambia? Sijaona cha maana hapo, anataka kuongea na mimi? Mimi huwa siongei na wasaliti, never!” Rais Costa alijibu kwa dharau.
“Mh. Rais, tumejiridhisha vipi kuwa taarifa alizotupatia Pius ni za hakika na kweli? Je, tuna hakika gani kuwa Macha au Joe hawakufanya jambo lile kwa sababu fulani? Kumbuka hawa ndio waliokusaidia kuzuia jaribio la wewe kupinduliwa na jeshi, leo wao kupanga kukupindua hainiingii akilini. Macha ameniarifu kuwa hatoniambia lolote, na wala hatosema chochote kwa maafisa wanaomtesa, alichosisitiza ni mimi nimuombee kwako ili uruhusu yeye kukuona.
Lakini pia kumbuka watu kama Macha ni watu wa usalama waliobobea katika fani yao, wapo tayari kufa kama usipofikiana nao makubaliano fulani. Macha yupo tayari kufa. Ni aidha ukubali kuonana nae ili upate kujua mambo mengine mengi ama umwache auwawe na baadae ujikute unapinduliwa na masalia yao maana mpaka sasa Idara imeshindwa kupata mawasiliano ya Macha na Joe kwa namna yoyote ile. Ipo gizani”, Gideon aliendelea kushauri kwa kumjaza upepo wa uoga Rais Costa.
Ushauri ule ulionekana kumwingia Rais Costa kidogo, alipiga hatua kama kumi hivi akiwa kimya kisha…
“Sawa Gideon nitaongea na Sabinasi aandae utaratibu nionane na Macha, Rais alimjibu Gideon huku akiwa anaingia nae ofisini kwake.
“Sawa mkuu lakini pia nashauri Inspekta Majita aache mara moja kumtesa Macha, yafaa siku unayokutana naye awe hana maumivu ili muongee vizuri lakini pia isilete picha mbaya kwa watu watakaomwona”, Gideon alishauri.
“Sawa, na hilo nitamwambia Sabinasi. Halafu Gidi, kuna suala hili la Marekani kututishia juu ya hali ya demokrasia na utawala bora nchini kwetu. Rais Chris wa Marekani ametuma waraka mrefu wenye lugha ya mabavu na kukemea. Bado nafikiria namna bora ya kumjibu. Uhusiano na Marekani ukiingia dosari zaidi ya ulivyoingia sasa inaweza ikaleta shida kubwa”. Rais Costa alimkubalia Gideon ushauri wake lakini pia akamuuliza Gideon juu ya barua aliyoipokea kutoka Ikulu ya Marekani Washington.
Barua ile iliyotoka kwa Rais Chriss Donald ilikuwa imeainisha masuala kadhaa ya yanayotokea Stanza kubwa likiwa hali ya demokrasia na utawala bora iliyoonekana kudorora kwa kasi katika kipindi kifupi. Rais Costa hakujua ajibu nini kwani huwa ni mtu wa hasira na asiyependa kupewa amri na yeyote, bali afanye anavyotaka yeye.
“Nipe nikaisome kwa utulivu kisha tutaona tunaijibu vipi Mh. Rais”. Gideon alijibu huku akisogea kuichukua ile barua.
“Sio tutaijibu vipi, wewe isome uijibu uje kunionyesha ulichoandika. Sina muda wa kupoteza kujadiliana na mataifa ya magharibi yanayokusidia kuingilia uhuru wetu. Stanza ni taifa huru’’. Rais Costa alijibu kwa hasira huku akiirusha ile barua mezani ili Gideon aichukue.
Gideon aliichukua ile barua na kutoka haraka. Alikuwa akitembea kwenye korido ile inayotoka ofisi ya Rais pale Ikulu upande wa Magharibu mwa jengo lile akielekea upande wa Kaskazini-Magharibi zilipo ofisi zake.
Tabasamu lilijaa moyoni kwasababu kuu moja, alihakikisha mateso kwa Stanley Macha yanasitishwa mara moja. Hakujua Macha anakuja kuongea nini na Rais lakini alijua Macha ni mtu mwerevu na atajua namna ya kufanya mbeleni.
“One step at a time”, Gideon alijisemea mwenyewe huku akitabasamu sana na kuingia ofisini kwake.
Wakati hayo yakiendelea, tayari familia za Joe na Macha zilishaanza kuingiwa na hofu pamoja na kufahamu asili ya kazi za wapendwa wao. Mke wa Joe ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Benki Ya Kilimo Stanza alianza kupata wasiwasi kwasababu ilikuwa kimepita kipindi kirefu tangu awasiliane na Joe, lakini pia wakati Joe anaondoka alimwarifu kuwa wasingechukua Zaidi ya wiki mbili kuwa wamerudi nyumbani.
Sasa ilikuwa zimetimia wiki tatu tangu Joe na wenzake kusafiri kwenda Korea Kaskazini kufikisha ujumbe wa Rais Costa kwa Rais Kim.
Mke wa Joe alifikiri kuwa pengine mume wake ameingia katika mgogoro na Korea na wao wakamshikilia kama ambavyo wamewashikilia watu wa mataifa mengi ambao walivunja sheria ndani ya nchi yao.
Wakati huohuo, Mke wa Stanley Macha hakuzoea mume wake asiwasiliane na familia kwa kipindi kirefu cha Zaidi ya wiki moja. Pamoja na kufahamu asili ya kazi ya mume wake kuwa anaweza akawa anasimamia misheni maalumu za usalama wa nchi, alipatwa na wasiwasi hasa kutokana na simu ya Macha kutopatikana na jumbe anazotuma kutojibiwa.
Familia hizi zote mbili zilianza kuingiwa na wasiwasi sana.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
*********************************
Kikao cha taarifa zinazoendelea kwenye vyombo vya habari kilikuwa kichungu siku hiyo. Rais aling’aka kama mbogo akiwatuhumu vijana wake kuruhusu taarifa kama ile kumfikia Kibwe na hatimaye kuchwapwa wao wakiwepo.
Aliwashangaa walikuwa wapi mpaka gazeti linasambaa mitaani. Aliwaambia alishawaagiza kweye kila chombo muhimu cha habari iwe gazeti, kituo cha luninga na radio kuwe na mtu angalau mmoja alieajiriwa mule atakayekuwa anawapa taarifa za kishushushu ya kila kilichochapwa ili kuzuia kuharibu taswira yake ama ya serikali ili wajue namna ya kulizima suala hilo haraka iwezekanavyo.
Pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini bado kuna vyombo vya Habari walishindwa kupenyeza watu wao kwasababu tu watu hawa huwa hawapenyezwi kwa lazima, bali hupitishwa katika mchakato wa kawaida wa uajiri ili wasitambulike na yeyote. Katika utawala wa Rais Costa, vyombo vya Habari vilikuwa matatani wakati wote. Vingi vilifungiwa, wahariri kutishiwa na wengine wakisimamishwa na uongozi wa vyombo vyao kwa amri kutoka Ikulu bila kukiuka miiko yoyote ya uandishi wa Habari.
Lakini pia waandishi walitekwa na kupotezwa katika mazingira ya ajabu. Lengo kuu likiwa kuwazima wasichape habari za masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali lakini pia kuwatisha waandishi wengine ili kuwaondoa katika kujikita kuandika Habari za serikali na kujikita katika masuala mengine ambayo ‘yasingechafua taswira ya serikali’. Vyombo vya Habari chini ya Rais Costa vililazimika kujifanyia ukaguzi na udhibiti wa kile wanachokichapisha au kwa kimombo inaitwa ‘’self-censorship’’ ili kuepuka dhahma ya serikali ya Rais Costa. Tasnia ya Habari haikuwa inayowavutia wanafunzi kusoma tena kama ilivyokuwa hapo awali.
Rais Costa aliendelea kuwakoromea vijana wake kwa kushindwa kuzuia habari ile pamoja na kwamba mazingira tayari yalishatengenezwa ya kuvitia hofu vyombo vya habari. Aliwaambia kuwa alishatoa agizo hilo na kuwa watu wapenyezwe kwenye kila chombo na wangelipwa kwa utaratibu maalumu, alishangaa ni kwanini mpaka muda huo agizo hilo halijatekelezwa mpaka Julius Kibwe anafanikiwa kumchafua namna ile.
Kwenye kikao kile hakuna aliyethubutu kuongea, kila mtu alikuwa kimya. Rais Costa alitoa agizo kuwa Julius Kibwe asiguswe maana kutamfanya azidi kuongea zaidi hivyo alitaka apuuzwe kwanza, lakini muhariri wa STANZA TODAY gazeti lililochapisha habari ile aitwe chemba aminywe na apewe onyo kali kutoendelea na habari ile.
****************************************
“Sabinasi, nimepata ushauri kutoka kwa Gideon kuwa tusitishe mateso anayopata Macha ili kumfanya azungumze na kuwa yupo tayari kuzungumza nikiwa nae, hivyo nakuagiza haraka Macha atolewe kule anaposhikiliwa na ahamishiwe nyumba salama, nitaonana nae huko siku nitakayoamua baadae kidogo.” Alikuwa ni Rais Costa akitoa maagizo kwa Sabinas, mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Stanza aliyechukua nafasi ya Stanley Macha.
“Lakini mkuu Macha yupo kwenye hatua ya mwisho ya uvumilivu, ata-break muda si mrefu. Tumuache Inspekta Majita amalizie kazi aliyokwishaianza. Akija kwako atakuanzishia siasa”, Sabinasi alikazia mateso kwa Macha yaendelee.
“Sabinas, do as I say. No questions!” Rasi Costa alionekana kukwazwa na ushauri wa Sabinas. Nani ana uwezo wa kupindua ushauri wa Gideon bwana? Hakuna mtu Rais Costa alikuwa akimwamini wakati ule kama Gideon.
**************************************
“Mh. Rais”, Alikuwa ni kijana wa Usalama akifungua mlango wa ofisi ya Rais Costa pale Ikulu ili kumpisha mtu aingie ndani.
“Sara, karibu nyumbani”. Rais Costa aliyekuwa ameanza kusoma makabrasha yaliyopangwa pale mezani kwake alinyanyua macho na kuona aliyeingia ni mke wake Sara.
“Baba Brian kuna nini?”, Sara mke wa Rais Costa aliuliza katika hali ya taharuki. Aliuliza kwa kumwita Rais Costa jina la mtoto wao anaeitwa Brian Sylvester Costa aliyepo nchini Denmark kimasomo.
“Let’s go home and have some conversation”, (Twende nyumbani tukaongee). Rais Costa alimjibu mke wake huku akisimama na kutoka nae kuelekea upande wa Mashariki kwenye makazi ya Rais pale Ikulu.
Wakiwa wanatoka wanakatiza korido ya mwisho ili wauache upande wa Magharibi kwenye kona ya mwisho walikutana na Gideon akiwa anatoka upande wa ofisi yake ni kama alikuwa anelekea ofisini kwa Rais Costa.
“Shemeji habari. Canada wanasemaje?”, Gideon alimsalimia Sara kwa bashasha.
“Salama tu shemeji. Canada wazima, nadhani next time nitabebana na Alicia”. Sara alimjibu Gideon kwa ucheshi. Alicia ni mke wa Gideon.
“Atafurahi sana….Mh. Rais ninatoka kidogo naelekea wizara ya Mambo ya Nje kuna jambo nikajadiliane na Katibu Mkuu kule”, Gideon alimjibu Sara na kisha kutoa taarifa kwa Rais Costa.
“Sawa si ndio kazi zako bwana. Nimeshampa maelekezo Sabinasi juu ya Macha, lakini na wewe pia usiache kushughulikia ile barua ya Rais Chriss” Rais Costa alisisitiza.
“Definitely Sir, actually ni moja kati ya agenda yangu ya kwenda wizarani” Gideon alijibu kwa nidhamu.
“Please proceed”, Rais Costa alimjibu Gideon na kuendelea na safari ya kuelekea kwenye kazi yao.
Gideon alipomuona Sara alikumbuka kuwa Sara hakurudi kwasababu kongamano lililompeleka Canada limekwisha bali ni kwa sababu Rais Costa aliagiza arudishwe baada ya kuhusishwa na mpango wa kumpindua Rais. Alianza kuwaza sana juu ya hilo suala.
Rais Costa na Sara walifika kwenye makazi yao na waliingia moja kwa moja mpaka Chumbani.
“Sara wewe ni mke wangu ninaomba uniambie lipi ninalolifanya ambalo huwa ninakukosea”, Rais Costa alianza kuuliza kwa utaratibu.
“Baba Brian mimi sikuelewi, nenda moja kwa moja kwenye lengo. Unanikosea mengi, ninafahamu umalaya unaofanya na changudoa wako Ketina, unadhani silijui lakini najua kila kinachoendelea na huyo hawara wako. Sasa ukitaka niorodheshe yote hatutafikia muafaka”. Sara alijibu kwa hasira baada ya kuona mume wake anazungumza kwa mafumbo bila uwazi.
Kitendo cha Sara kumtaja Ketina, kimada wake kilimchanganya sana Rais Costa. Yeye Rais Costa akijua uhusiano wake na Ketina ni siri kubwa alistaajabu kugundua kuwa mke wake anajua na hakuwahi kumuuliza hata siku moja.
Kitendo cha Sara kumtaja Ketina kama tungekuwa kwenye medani zetu za mijadala kinzani tungekiita opponential confusion, yaani unamvuruga mpinzani wako wa mada hata kwa kuibua suala ambalo haliendani moja kwa moja na kile kilichopo mezani. Sara hakuwa na lengo hilo, isipokuwa kwa Rais Costa hakika ilikuwa ni pigo la kwanza katika mjadala kwasababu alikosa nguvu ya kuendelea na hoja. Alianza kuamini kwamba kila siri anayofanya kuna watu wanavujisha.
“Sara suala la Ketina tuliache kwanza, taarifa za kiintelijensia tulizopokea ni kuwa unashirikiana na Macha na Joe kutaka kunitoa madarakani. Hivi kweli mama Brian unaweza kunifanyia kitendo kama hicho?”. Rais Costa aliuliza kwa upole uliopitiliza.
“Costa hebu tusichanganye hapa saa hizi, niambie ulichonirudishia Stanza kabla ya kongamano kuisha maana naona unazidi kunipandisha hasira kwa mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Hebu kuwa serious, stop acting like a little boy. Huyo Ketina umeyataka mwenyewe, sikutaka kukuuliza mimi. Umenilazimisha niseme kama uliwahi kunikosea na nimekwambia sasa unaniambia nini tena”. Sara mke wa Rais Costa aliongea mfululizo. Si kawaida yake kuongea kwa namna hiyo lakini ilimbidi.
“Suala ni kuwa kuna taarifa zisizoshaka kuwa unashiriki kwenye mpango wa kutaka kunipindua ukitumiwa na Macha na Joe.” Rais Costa alihoji, safari hii akiwa amejikaza kidogo.
“Kukupindua? Mimi nikupindue wewe? Yani kama kukupindua ningeanza kupindua ndoa yangu siku niliyothibitisha kuwa unatoka na Ketina. Sikufanya lolote leo unaniambia nataka nikupindua kutoka kwenye nafasi yako ya Urais? Hivi kama mke aweza kumpindua Rais aliyepo madarakani, sasa huyo atakuwa Rais au Rahabu?”. Sara alijibu kwa dharau.
Walianza kuzozana kila mmoja akimtupia maneno mwenzake. Rais Costa akitaka aambiwe ukweli huku Sara akimshangaa Rais Costa na kutoonesha hamuelewi hata anaongea nini. Rais Costa aliishia kubaki njiapanda kwa kutokuwa na uhakika na taarifa za mkewe kuhusika na jaribio la mapinduzi.
Alitoka kule chumbani na kuelekea sehemu anayopenda kufanyia mazoezi na kujifungia na kufikiri mambo mengi. Kwanza, alianza kufikiria kama ni kweli mkewe hahusiki ama la, lakini cha pili kuhusu mkewe kujua mahusiano yake na Ketina ni jambo lililomshtua.
****************************************
Gideon alipotoka pale hakuwa akielekea Wizara ya Mambo ya Nje kama alivyomuaga Rais Costa bali alikuwa akielekea mgahawa wa Goldern Spoon kuonana na Meja Kairuki Byabato kwa malekezo ya Macha alipomtembelea. Alihitajika kuonana nae ili mpe ile code aliyopewa ya ‘Sienta-go’. Hakuielewa ina maana gani lakini alijua watu wa usalama wana namna yao ya kuwasiliana na angeelewa.
Aliwasili pale mgahawani na alikuwa amewahi kidogo, hivyo alikaa ili kumsubiri. Meja Byabato alimtaarifu kuwa yupo karibu kufika.
Akiwa pale, mawazo ya uhusika wa Sara kwenye sakata la kutaka kumpindua Rais Costa lilimjia kwa mara nyingine na alipenda kujua ni kwa vipi. Aliona bora aingie kwenye game ya Clash royale ili awasiliane na Joe.
“Che, nipo hapa Goldern Spoon namsubiri Meja Byabato kuna code nimepewa nimpe na Tiger. Ila wakati natoka Ikulu nilipishana na Rais akiwa na mkewe Sara ambaye mlimtaja kuwa anahusika na hii misheni. Hili limekaaje? Maana sasa mnatakiwa mniweke kwenye picha kamili nijue nachezaje”. Gideon anaetumia jina la Sadam Hussein alimwandikia ujumbe Joe anayetumia jina la Che Guevara ama Che kama walivyozoea kuitana. Tiger ni jina la Macha kwenye game ile.
Ujumbe ulimfikia Joe aliekuwa akikatiza mitaa ya Beijing akiambatana na Habibu wakielekea mahali ambapo Habibu hakuwa anapafahamu mpaka wakati huo. Ujumbe ule ulimfanya Joe asimame mahali ili kuusoma. Ilikuwa ni muhimu sana Joe kusoma na kujibu kila ujumbe kwa wakati maana kuchelewa hata kidogo kunaweza kuharibu misheni nzima au hata kuhatarisha maisha yake.
“Sadam kwanza ulifanikiwa kuhakikisha Tiger anatoka kule detention?”, Joe aliandika.
“Mimi tena, ila sasa sijajua ataongea nini?” Gideon alijibu kwa kujitapa.
“Cha kuongea hicho kisikusumbue, mwachie yeye anajua”, Joe alijibu.
“Sara vipi anahusikaje?” Gideon aliuliza.
“Sara tulimtaja kwa lengo maalumu, hahusiki. Kwa kawaida kwenye misheni huwa anawekwa mtu mmoja ambaye atapoteza uelekeo wa kiuchunguzi na kuleta taharuki ikitokea mambo hayajaenda kama yalivyopangwa, huyo huitwa disturbing agent. Kimsingi Sara tunamuhitaji sana baadaye ila hatukuwa tunajua namna ya kumwingia kwahiyo tulikubaliana na Macha kumuimplicate kwenye kila maongezi na mawasiliano yetu ili aonekane anashiriki kama siku tukishtukiwa kama hivi.
Lengo ni kuhakikisha Rais Costa anachanganyikiwa na kushindwa kuunganisha nukta. Lakini sasa ndiyo wakati wewe wa kufanya hatua ya pili”, Joe alimalizia kuandika ujumbe na kuutuma.
“Hatua ya pili ipi? Ya kwanza niliifanya lini?” Gideon aliuliza.
“Unakumbuka Macha alipokwambia umtonye Sara juu ya Rais Costa kuwa na mahusiano na Ketina na kuwa umsihi asimwambie mumewe chochote?”, Joe aliuliza.
“Ndio, kwani na wewe ulikuwa unajua? Mlipanga mniframe?” Gideon alihoji.
“Ndio, hakuna kinachotokea kwa Bahati Mbaya Gideon. Sasa ile ilikuwa ni hatua ya kwanza. Sasa utatekeleza hatua ya pili. Ukirudi Ikulu hakikisha unaenda kumdodosa Sara ni kwanini amerudi mapema kabla ya Kongamano kuisha. Najua wewe ni rafiki yako na mnaelewana atakwambia shutuma atakazokuwa amepewa na mumewe.
Akikueleza wewe onyesha masikitiko yako kisha mwambie kuwa umepata fununu kuwa Rais ameamua kumzushia ili apate sababu ya kumpa talaka na amuoe rasmi Ketina. Ukimaliza kumwambia hivyo utajidai unataka kufuatilia kama chokochoko hizo za kupinduliwa ni kweli au vinginevyo na kisha utaona atakavyopokea suala hilo.
Jinsi atakavyopokea utatutaarifu ikiwa ataonekana kufurahia mumewe kupinduliwa au la. Kama ataonyesha kufurahia, taratibu tutaendelea hatua ya tatu ya kumfanya awe sehemu ya misheni kwani atakuwa ana hasira ya mumewe kutaka kumwacha kwa siri hivyo atakuwa anataka kulipiza kisasi.
Akionyesha kutokuunga mkono utamrudia mara nyingine na kumwambia hakuna mpango kama huo na utaachana nae.” Gideo alimalizia.
“Che, huu mpango mliupanga lini?”. Gideon alionekana kutoamini mpango ule ulivyosukwa.
“Sadam, hatuna muda wa kujadili hayo kwa sasa”, Joe alijibu.
“Sasa akimgusia mumewe si litakuwa balaa Joe?” Gideon alionyesha mashaka yake.
“Huwezi kushindwa kujitetea, kwanza Costa hajui kama unajua mahusiano yake na Ketina. Wewe utamkana na utamwambia wazi kuwa asipoangalia atawamaliza marafiki zake wote kwa kusikiliza maneno ya watu. Ataogopa, wewe ni mtu wa karibu wa pekee uliyebaki nae, hawezi kukutupa.” Joe alimuhakikishia Gideon.
“Sawa, naona Meja Byabato anaingia hapa nitakurudia baadae. Stay safe”. Gideon alimalizia na kutoka kwenye ile game.
“Meja, heshima yako Mkuu”. Gideon alimsalimia Meja Kairuki Byabato alipowasili eneo alilokuwa amekaa.
Meja Byabato alikuwa ni mwanajeshi katika jeshi la Stanza. Alikuwa kikosi cha anga. Akiwa ni mrefu wa futi 6, ilikuwa ni rahisi kuona utofauti wake na binadamu mwingine yoyote aliyesimama au hata kukaa karibu nae. Mikono yake ilikuwa mikubwa na iliyojaa kwasababu ya mazoezi makali ya kunyanyua uzito na muda mwingi alipendelea kuvalia makombati ya jeshi na sio nguo za kiafisa.
Alikuwa ni mmoja wa makomandoo katika jeshi la Stanza. Aliongea kwa kuunguruma na akitabasamu hutabasamu kwa shavu moja bila kuonyesha meno. Alipendelea kuvaa miwani mieusi inayoziba macho kabisa.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Gideon yeye kwa sababu ya kucheza sana Rugby nae alikuwa ni mrefu na mwenye kifua kikubwa. Gideon alikuwa mweupe wakati Meja Byabato alikuwa mweusi hadi weusi wenzake wakiwa wanamtania kuwa ni mweusi kama makaa ya mawe yanayozalishwa kwenye migodi ya Liganga na Mchuchuma huko Tanzania. Kuna wakati baadhi ya Marafiki zake walimwita kwa majina ya utani ‘’Mchuchuma au Liganga’’ na wala hakukasirika.
“Gideon”, Meja Byabato alimsalimia Gideon huku wakishikana mikono yote miwili na kutingishana.
Kwa namna walivyotingishana na jinsi miili yao ilivyo kama huna afya vizuri basi ungeweza kudondoka. Lakini wao waliwezana.
“Habari za Ikulu”, Meja alianza kwa kumuuliza Gideon walipoketi kwenye viti vyao.
“Nchi ipo salama chini yenu Meja”, Gideon alijibu kidiplomasia.
“Tell me Gidi what is it”, Meja Byabato alifungua maongezi.
“Nimetumwa na Stanley Macha nikuletee ujumbe, amenipa codes nikuletee”, Gideon alianza kumwambia Meja Byabato.
“Codes gani Gidi, na yeye yupo wapi? Meja Byabato alihoji.
“Sienta-go” Gideon alimtamkia Meja Byabato.
“What? Unafahamu mahali aliposhikiliwa? Should I trust you?” Meja Byabato alionekana kushangaa sana.
“Kwani mimi nimekwambia ameshikiliwa?” Gideon aliuliza kwa mshangao.
“Gideon, hapo Macha ameniambia mambo mengi. Labda nikuulize unafahamu nini juu ya huu mpango?” Meja alihoji.
“Mpango gani?” Gideon alijitia haelewi.
“Gidi we don’t have time to play. Save some sh*t please”, Meja Byabato aliunguruma.
“Ninafahamu vyote na ndio maana nimeweza kukufikishia taarifa hii”, Gideon alijibu.
“Sawa. Tutawasiliana acha nikafanye alichoniagiza”. Meja Byabato alijibu huku akinyanyuka pale kwenye kiti.
“Ukafanye nini Meja?” Gideon aliuliza.
“Gidi umeshatimiza majukumu yako, umefikisha kijiti, acha mimi nikikimbize. Go go and keep pampering that man, Meja alijibu huku akiingia kwenye gari lake aina ya Ford Ranger.
Gideon alibaki mdomo wazi. Aligundua kuwa suala lile ni zaidi ya yeye alivyolipa uzito, wazungu wanasema ni covert operation, yaani mpango wa siri kuu. Kila mtu ana kipande chake tena kisichofanana na wa mwenzake lakini vipande vyote vikiunda kitu kimoja.
Kumtoa Rais madarakani katika hali ya utulivu bila raia kuwa na taarifa wala kusababisha sintofahamu ilihitajika akili kubwa na mkakati wa muda mrefu uliosukwa kitaalamu na kuhusisha watu wengi tofauti na alivyowaza Gideon.
Haraka Gideon alitoka pale na kuelekea Wizara ya Mambo ya Nje kuonana na Katibu Mkuu. Hakuwa na hata la maana la kuongea nae lakini alimjua Rais Costa hachelewi kudodosa kama kweli alifika wizarani ama la.
Rais Costa ana akili yenye kuwa na wasiwasi na kila suala, muda wote hujihisi hayupo salama. Gideon alijua kula na na kipofu, alimjua bosi wake na alijua namna ya kwenda nae.
Gideon alionana na Katibu wa Kudumu wa Wizara na kumpa taarifa ya barua ya Rais wa Marekani ili pia Wizara yenye jukumu la mahusiano ya kimataifa ifahamu kinachoendelea kati ya Marekani na Stanza, lakini pia kwa ushauri wa jinsi ya kuenenda katika suala lile ili hata huko mbeleni wakipokea nchi isiwe katika misukosuko. Gideon alianza kuona picha kubwa zaidi.
***********************************
“Mh. Rais Luteni Jenerali Pius Kihaka amewasili”, alikuwa ni mmoja wa wasaidizi wa Rais akimtaarifu Costa juu ya kuwasili kwa Pius akitokea nchini China.
Ilikuwa ni jioni mishale ya saa kumi. Siku nzima ya siku hiyo tangu asubuhi baada ya Rais Costa kutupiana maneno na mkewe Sara hakutoka tena kwenye makazi yake kurudi ofisini.
“Oh, mleteni kijana wangu huku nyumbani. Ameambatana na nani?” Rais Costa aliuliza.
“Yupo na Sabinasi Paulo na Jenerali Ernest Nduta”, Yule kijana alijibu.
“Sawa waje huku mtafute na Gideon”, Rais Costa alijibu huku akielekea eneo lililoitwa Presidential Lounge. Ni eneo dogo lililojengwa kwa ajili ya Rais kupumzika na wageni wake maalumu kwenye makazi yake.
Ni eneo zuri dogo kiasi lililopangwa kiustadi na kuwekwa katika hali ya kustarehesha likiwa mbele ya bustani nzuri ya maua na mandhari ya kupendeza pale kwenye viunga vya Ikulu. Mbele yake walizunguka ndege aina ya tausi na aina mbalimbali za wanyama walioletwa Ikulu ili kuboresha mandhari.
“Hongera sana Luteni. Hakika umefanya jambo la kishujaa”. Gideon alimwambia Pius wakati wakiwa wote wanaelekea kuonana na Rais Costa. Gideon ndiyo alikuwa ameingia tu viunga vya Ikulu akitokea kwenye harakati zake.
“Sikuweza kukubali kuona ujinga Joe aliotaka kuufanya”, Pius alijibu kishujaa.
Wote walipiga hatua wakiwa waasindikizwa na vijana wa Usalama na walifika kwenye Presidential Lounge na kupokelewa na Rais Costa.
“What a courageous and brilliant young man!” Rais Costa alinyanyuka pale alipokuwa ameketi na kumlaki Pius kwa kumbatio kubwa. Wengine walikuwa wamesimama kando wakiwa wanatabasamu ishara ya kuungana na Rais kihisia katika kumlaki Pius.
Waliketi na Pius alianza kuwapa muhtasari wa safari nzima. Aliwaeleza namna walivyopokelewa kwa heshima nchini Korea Kaskazini na majadiliano yalivyokwenda.
Giden wakati wote alikuwa akisikiliza kwa makini sana mrejesho ule. Alikuwa akipata maswali mengi kichwani kwa kila hatua Pius aliyokuwa akieleza. Alikuwa anajitajidi kuunganisha nukta lakini zilikuwa zinakataa. Wengine wote walikuwa wakionekana kumwamini na kumuitikia Pius kwa kila hatua.
Katika maongezi yale Pius hakuacha kuelezea namna Joe alivyokuwa akipata taarifa fulani kwa njia isiyo ya kawaida na hivyo kubadili muelekeo wa jambo au kuondoka eneo walilopo kwa haraka.
“Lazima kuna watu walikuwa wakimpa taarifa waliopo karibu na wewe Mh. Rais”, Sabinas alidakia.
“Ni Macha, ndiyo maana nasita sana kuonana nae. Nilikusudia atumbukizwe kwenye pipa la tindikali ayeyukie humo. Sitaki hata kumuona”, Rais Costa alionekana kutibuliwa tena ghadhabu.
“Hapana Mh. Rais mimi nawaza tofauti kidogo, mimi nawaza kuwa bado ipo haja ya kuonana na Macha umsikilize. Unajua Macha alikuwa mtu mkubwa sana kwenye Idara ni vema akatuambia alikuwa akiwatumia vijana wake nani na nani ili kutekeleza azma yake hii maana lazima alikuwa na vijana.
Sasa kumteketeza Macha na kuwaacha hawa vijana ni sawa na kuteketeza mzinga wa nyuki wakati nyuki wenyewe wakiwepo, ukifanya hivyo uwe na uhakika kuwa hawa vijana wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutumiwa na mtu mwingine au wenyewe kupanga uasi”, Gideon alimalizia.
“Anyway, nitaonana na Macha”, Rais Costa alijibu.
Hakika kulikuwa na mpambano mkali kati ya Sabinasi na Gideon. Wakati Sabinas akitaka Macha amalizwe ili asipate nafasi ya kujitetea na yeye asimikwe rasmi kuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Stanza, yeye Gideon alikuwa anapambana kumwokoa mmisheni mwenzake. Kila mtu akivutia upande wake kwa ustadi mkubwa.
Gideon alizidi kuona umuhimu wa yeye kutobanduka viunga vya ikulu na kujua kila anaemkaribia Rais anataka kumwambia nini maana asipokuwepo kidogo tu aweza kuta mambo yameharibika.
“Pius, umeongelea suala la silaha za kinyuklia hili mliafiki vipi?” Jenerali Ernest Ndutta alihoji.
“Suala hili kwa ukweli nililipinga sana”, Pius alianza kujitoa kwenye hilo sakata.
Alianza kujitoa baada ya kuona sura ya Rais Costa imebadilika aliposikia suala la silaha za kinyuklia kuzalishwa Stanza. Yeye ndiye haswa alieshauri wenzake walipokuwa Korea Kaskazini kuwa wakubaliane na sharti la silaha za nyuklia lakini leo imemlazimu kukaa mbali nalo ili kuendelea kuibeba sifa ya ushujaa wake ambayo amekwishavikwa.
“Aliyesababisha na kukubaliana na Korea ni Joe, kwahiyo ni lazima tuone tunafanyaje kwa sababu Korea wameliweka hili kama sharti la muhimu sana”, Pius alimalizia.
“I see, na sasa Korea wapo tu kimya inanipa mashaka nadhani wanaweza kudhani sisi tuna dharau. Ha ha ha!”, Rais Costa aliongea kwa kucheka.
Walizungumza mengi na kisha Rais Costa aliwaomba wakutane kesho yake ili waweze kuzungumza na Rais Kim. Alimwagiza Gideon aandae majibu wawaambie nini Korea lakini alisisitiza masuala ya silaha za nyuklia hayawezi kuja Stanza, hataki kusikia. Waliondoka lakini Gideon alibaki kidogo.
“Gidi, unamuonaje Luteni Pius?”. Rais Costa alimuuliza Gideon huku akinywa juisi ya Embe iliyokuwa imemiminwa kwenye glasi pale walipoketi.
“Ninamwonaje kivipi Mkuu?”, Gideon aliuliza kwanza ili ajue ajibu vipi.
“Jenerali Ernest Nduta muda wake wa utumishi unakwisha nilitaka nimuongezee miaka miwili ili Pius akomae kidogo lakini ni kama namuona anafaa sana kwasasa kushika nafasi hiyo ya Ukuu wa Majeshi”, Rais Costa alimweleza Gideon.
Katika vitu vilivyompasua moyo na kumuudhi Gideon basi suala hilo ni namba moja. Aliwaza yani huyu huyu Pius ndio anakuwa mkuu wa majeshi? Huyu huyu msaliti mkubwa. Aliona jinsi misheni inavyozidi kuwa ngumu maana Pius anajua mambo mengi na yupo haraka sana kung’amua mambo. Alikosa ajibu nini, alikasirika sana moyoni.
“Mkuu, nilikuwa nawaza bado Pius apewe muda akomae”, Gideon alishauri.
“Akomae kitu gani Gideon?” Rais Costa alionekana kuuliza kwa mshangao.
Gideon kwa mara ya kwanza alibaki kimya hakujua atetee vipi kuzuia Pius kupewa ukuu wa majeshi.
“Sikiliza Gidi, Jenerali Nduta amelitumikia taifa hili kwa weledi sana na sasa amechoka, nimwache akapumzike. Kuna jambo linanisukuma kusema Nduta akapumzike nalo ni kitendo cha Pius kutaka kuwasiliana na yeye na kushindwa. Yani kama Macha aliweza kuzuia mawasiliano yasinifikie bila Jeshi kujua, hii ni hatari. Isingekuwa ujanja wa Pius tusingejua na labda Macha angetumia njia zozote kumnyamazisha Pius huko huko China”, Rais Costa alikazia.
“Lakini unachosema ni kweli Mkuu, sikufikiria hilo. Umefikiria kwa kiwango kikubwa sana Mh Rais, naungana na wewe. Pius mpe nafasi”, Gideon ilibidi aungane na Rais Costa bila kupenda.
Walikubaliana kuwa watamtaarifu Jenerali Nduta maamuzi hayo na aanze kumkabidhi Pius kijiti kabla ya yeye kuweka wazi kwa taifa.
Gideon alimwaga Rais na kuondoka akiwa amekata tamaa kwa mara nyingine kutokana na kubadilika kwa hali ya mambo ghafla, kwa kimombo ingeitwa ‘’twist of events’’
*******************************************
Meja Kairuki Byabato aliendsha gari lake kwa aksi ya ajabu sana. Alikuwa akiwaza mengi kichwani na aliona kama imekuwa mapema sana kwa Macha kukamatwa. Meja alikuwa ni miongoni mwa wale wanajeshi waliokuwa kwenye mpango wa mwanzo wa kutaka kumpindua Rais Costa, mpango uliozimwa na Macha na Joe.
Katika uchunguzi wa Macha alibainisha baadhi ya wakuu wa vikosi waliokuwa katika mpango ule na alihakikisha wote wamestaafishwa na kutolewa kwenye jeshi isipokuwa Meja hakumjua kwa haraka kwa wakati ule.
Ulipita kama mwaka mmoja hivi ndipo Stanley Macha alipokuja kugundua na kupata uthibitisho pasi shaka kuwa Meja Byabato alikuwa ni mmoja wao. Macha alistaajabu umaridadi wa kuficha taarifa aliokuwa nao Meja Byabato kufikia kiasi cha yeye kutojulikana kabisa kama alikuwa ni Sehemu ya misheni na wanajeshi wenzake.
Ni hapo Macha alipoamua kumfata na kuongea nae. Alimweleza kinaga ubaga kuwa anao uthibitisho pasi shaka wa uhusika wake katika jaribio la kutaka kumpindua Rais Costa lakini hatamshtaki kwa Rais.
Alimtaka Meja amweleze ni kwa nini haswa walikuwa wanampango ule wakati ule. Ni katika maongezi yale kati ya Macha na Meja Byabato yaliyowafanya wawe marafiki. Mara baada ya Joe kuleta mpango wa kutaka Rais Costa atolewe madarakani Macha aliona ni muda mzuri wa kumtumia Meja Byabato kama kiungo mshambuliaji kwenye misheni.
Meja aliendesha gari na kufika kwenye kambi yao ya jeshi. Alishuka kijasiri na kuanaza kutembea kuelekea kwenye ofisi yake. Alipofika karibu na ofisi alishangaa kuona vijana wanne wakakamavu wa kijeshi wamesimama mbele ya mlango wake wakiwa wamemkazia macho. Aliishiwa nguvu.
***************************************
Joe Amchezesha Gideon Nafasi Ya "Kiungo Namba 8" Kwenye Misheni
Wazir En baada ya kuwasiliana na Joe siku ile ilimbidi apeleke mrejesho kwa Rais Kim. Alimweleza Rais Kim kila kitu kama alivyoelezwa na Joe. Rais Kim alionekana kushangaa na kuchukizwa na kitendo cha Pius.
“?? ?? ? ??? ??? ???.” geuleon da-eum du gajileul jinhaenghae bobsida (Basi tuendelee na mpango wetu namba mbili), Rais Kim alimwambia Waziri En.
“??, ?? 2? ?? ?????. ?? ???? ???? ?? ??? ??? ??? ???” dongji, daean 2neun maeu wiheomhabnida. wil-eun apeulika jeon-yeoggwaui oegyo gwangyee yeonghyang-eul michilji moleunda (Kamaradi, mpango namba mbili ni hatari sana. Unaweza kuathiri mahusiano yetu ya kidiplomasia na bara zima la Africa). Waziri En alionyesha shaka yake.
“En ??? ???? ?? ??? ????” En wiheom-eul wanhwahaneun geos-eun dangsin-ui il-ibnida (Ni kazi yako kuzuia hizo hatari zisitokee En), Rais Kim alisisitiza.
Waziri En hakuwa na namna zaidi ya kwenda kuanza utekelezaji wa mpango namba mbili.
********************************
Baada ya Pius kuwasili Stanza jana yake na kuwapa mrejesho Rais Costa na jopo lake, waliamua sasa kuwasiliana na Korea ili Rais Costa atoe mrejesho kwa Rais Kim juu ya ugeni ule alioutuma.
Wakiwa wamekaa kwenye meza ya nusu mduara asubuhi ya saa nne kwa saa za Stanza, huku wakiitazama screen kubwa iliyopo mbele yao waliunganishwa kwenye simu ya video (Video Call) kutoka Ikulu ya Korea Kaskazini, Ryongsong.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Mr. President, it is nice to hear from you” (Mh. Rais ninafuraha kusikia kutoka kwako), Rais Kim alianza mazungumzo kwa kiingereza cha kuunga unga.
“It is my pleasure too Comrade” (Ni furaha yangu pia Kamaradi), Rais Sylvester Costa alijibu.
Rais Kim alitambulisha ujumbe aliokuwa nao kwa upande wake kuwa ni Waziri En, anaehusika na masuala ya kigeni, Mkuu wa Jeshi la Ukombozi la Korea Kaskazini pamoja na Makamanda wengine wawili wa ngazi za juu wa Jeshi la Ukombozi la Korea Kaskazini.
Kwa upande wake Rais Costa alimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Stanza Jenerali Ernest Nduta, Mshauri maalum wa Rais Gideon Kalumanzila, Mkuu wa Idara ya Usalama Wa Taifa Stanza Sabinasi Paulo na Pius Kihaka, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi na Mjumbe katika msafara ule wa Korea.
“Where is Joseph Kaduma and Habibu Chamchua?” (Wapo wapi Joseph Kaduma and Habibu Chamchua?) Rais Kim aliuliza kwa mshangao kama vile hafahamu kinachoendelea.
“They are both assigned with other tremendously important matters Mr President, but nothing to worry about. We can still proceed” (Wote nimewapa tena majukumu mengine ya muhimu Mh. Rais, lakini hakuna cha kuogofya. Tunaweza kuendelea), Rais Costa alijibu kwa haraka.
Maongezi yalianza na Rais Costa alikiri kupokea mrejesho wa mazungumzo yote. Rais pamoja na timu yake walikubaliana na matakwa yote ya Korea isipokuwa tu kuanzisha uzalishaji wa silaha za nyuklia nchini Stanza. Suala hilo lilipingwa vikali na Rais Costa na timu yake.
Rais Kim hakutaka kusisitiza kutiwa saini makubaliano kulingana na nyaraka alizopokea kwani alifahamu wazi kuwa nyaraka zote hazikufikia serikali ya Stanza na kwa kufanya hivyo ingeweza kuleta hali ya sintofahamu katika kikao kile muhimu. Hakuonesha uharaka wa kutiwa sahihi makubaliano yale.
“Mr. President, I am afraid that by not providing us with the secret location and access to uranium so that we can process nuclear in Stanza, we will not be able to support you with what you requested from us”. (Mh. Rais nina shaka kuwa bila ninyi kutupa sisi nafasi ya kujenga ngome yetu huko ya kuzalisha silaha za kinyuklia hatutaweza kuwapa msaada wowote mlioomba), Rais Kim alisisitiza.
“Mr. Presient, Pius is our top rank military commander, second in rank after the Chief of Defence Forces, he specifically advised against that being part of the deal, didn’t he? (Mh Rais, Pius ni kiongozi mkubwa katika jeshi letu, mtu wa pili kimamlaka baada ya Mkuu wa majeshi, yeye alishauri kutohusisha ujenzi wa kinu cha nyuklia Stanza kama sehemu ya makubaliano. Ama sivyo?). Gideon aliona atumie mwanya huo kuzidi kumwaribia Pius, wazungu huita ‘’reputation damage’’ mbele ya Rais Costa.
Alijua fika Pius alishiriki kuhawahamasisha wenzake wakubali nyuklia izalishwe Stanza la sivyo Joe asingekubali. Kitendo cha yeye kuja na kusema sio yeye bali ni Joe aliona ni uongo wa kujipendekeza kwa Rais Costa na hivyo swahi hilo aliliuliza makusudi ili Rais Kim ‘afunguke’ mbele ya watu wote na iwe aibu kwa Pius.Kwa vyovyote vile alikuwa hataki Pius apewe nafasi ya ukuu wa mejeshi.Aliuliza swali la kinafiki.
“We are not here to discuss who said what, but to make final decisions and move forward” (Hatuko hapa kujadili nani alisema nini bali kufanya makubaliano ya mwisho na kuendelea mbele), Waziri En alijibu.
Kikawaida na kiutawala katika mazungumzo kama yale Rais humjibu Rais na ni dharau mtu wa kawaida kumtupia swali Rais ndio maana Waziri En alidakia kujibu na sio Rais Kim.
“I propose that we use today’s meeting as a learning point of the position of both our brother countries. We should perhaps call for another bilateral meeting after discussing it in detail. What do you think gentlemen?” (Nadhani kikao cha leo tukichukulie kama kikao cha kukiri kupokea mrejesho kutoka kwenu na kujua msimamo wa nchi zetu marafiki, halafu baadae tuitishe kikao kingine baada ya kujadili kwa kina. Mnaonaje?). Jenerali Ernest Ndutta alishauri baada ya kuona hakutakuwa na muafaka.
“I would recommend that too” (Sawa, ningependekeza hilo pia) Mkuu wa Majeshi wa Korea Kaskazini alijibu.
Rais Kim na Rais Costa ambao ni wenyekiti wenza wa kikao kile walikubaliana na mapendekezo ya wakuu wao wa majeshi na kukubaliana kuahirisha kikao kile.
Mjala ulifungwa na mkutano ule uliofanyika kwenye mfumo maalumu wa kieletroniki unaotumia kioo kikubwa cha video ulifungwa.
“Suala la silaha za nyuklia hapana aisee”, Rais Costa aliongea baada ya video kukatwa.
“Ni suala nyeti”, Jenerali Ernest Nduta aliunga mkono kwa kukazia.
“Nduta, nadhani kikao hiki chafaa kukutaarifu. Kwanza niseme umehudumu taifa hili kwa juhudi, weledi na uaminifu mkubwa kwa muda wote wa utumishi wako. Najua umechoka na kuna wakati uliniomba upumzike mimi nikakulazimisha uendelee, lakini sasa hata mimi nakuonea huruma. Nimeonelea nikukubalie ombi lako la kupumzika na kumteua Pius kushika nafasi yako. Sijui hilo unalionaje?” Rais Costa aliongea kwa upole na unyonge sana.
Alikuwa akimpa taarifa Jenerali Arnest Nduta ya kutaka kumpumzisha kutoka kwenye nafasi yake ya Ukuu Wa Jeshi kama walivyojadili na kukubaliana jana yake na Gideon.
“Mh. Rais nashukuru sana. Ni kweli umri umenikimbia na kama unavyoona kadiri miaka inavyozidi kwenda changamoto ni nyingi, si sawa na ile miaka yetu. Kwa hivyo mimi sioni tatizo kabisa. Pius ni askari hodari na mwenye weledi, ataliongoza vyema jeshi letu”, Jenerali Ndutta alijibu.
“Ninafurahi kuwa umepokea suala hili kwa mtazamo chanya. Wapo wengine huwa hawapendi kustaafu utumishi wa umma kwasababu wanapenda kuendelea kutumikia’’. Nashukuru kwa utumishi wako’’, Rais Costa alimjibu.
Wote walisimama na Jenerali Ndutta kwa ukakamavu mkubwa alisimama na kupiga saluti kuashiria heshima yake kwa Rais Costa. Rais Costa naye alipokea salamu ile ya kijeshi kwa kupiga saluti na kisha kushusha mkono na kumpa Jenerali Ndutta.
Wengine wote walifuata kwa kumpa Jenerali Ndutta mkono wa heshima.
“Pius najua wewe ni kijana na bado damu inachemka, naomba alipoishia Jenerali Ndutta wewe nyoosha kwa spidi zote. Nataka jeshi la kisasa.” Rais Costa alisisitiza.
“Mh Rais!” Pius Kihaka alijibu kwa kifupi akiwa bado haamini kuwa anaukwaa Ukuu wa Majeshi bila matarajio yoyote.
Wote walikubaliana waandae mpango maalumu wa ustaafu na kuachiana madaraka ili kila kitu kiende bila mawimbi.
“Mtakapokuwa tayari mtaniambia nilitaarifu taifa”, Rais Costa aliagiza.
“Sawa Mkuu”, wote walijibu kwa pamoja.
Rais alinyanyuka na kutoka na kisha kila mmoja alitoka.
Gideon alishika korido ya kuelekea ofisini kwake, Sabinasi alitoka kabisa akielekea ofisi za Idara ya Usalama na Ndutta na Pius walitoka kurudi makao makuu ya jeshi.
***************************************
Gideon akiwa anakaribia kuingia ofisini kwake alimuona Sara, mke wa Rais Costa.
“Mmemaliza kikao? Nahitaji kumuona baba Brian”, Sara alimuuliza Gideon.
“Ndiyo shemeji, tumemaliza nadhani Mh. Rais atakuwa ameelekea ofisini kwake. Lakini mbona nimeona kwenye habari BBC kuwa kongamano linaendelea na wewe nakuona hapa?” Gideon aliuliza kinafiki.
“Shemeji acha tu, huyu Costa tatizo lake la kusikiliza maneno ya watu wengi mwisho atapotezwa” Sara alimjibu Gideon.
“Embu ingia ofisini shemeji uniambie kulikoni”, Gideon alimwingiza Sara ofisini kwake.
Gideon ni mjumbe wa bodi wa shirika la Sara mke wa Rais Costa linalojihusisha na vijana walioathirika na madawa ya kulevya. Ni kawaida Sara kuingia ofisini kwa Gideon kutaka ushauri na mambo mengine mengi ya utendaji wa shirika. Ni katika mahusiano hayo walitokea kuzoeana sana na hata kupelekea Sara na Alicia mke wa Gideon kuwa marafiki wakubwa.
“Hebu shemeji nieleze, kulikoni?” Giden alihoji huku akikaa kwenye kiti.
“Costa kanirudisha ananiambia amesikia mimi nataka kumpindua sijui, kuwa nashirikiana na Macha na Joseph. Mimi hawa watu hata ukaribu nao sina, unajua nimeshangaa sana?” Sara alianza kutiririka.
“Sasa wewe ukamwambiaje?”, Gideon alihoji.
“Nimwambie nini? Kwani mimi nataka kumpindua ili iweje? Nilimwambia kama kupindua ningepindua ndoa yetu baada ya yeye kuanzisha mahusiano na yule Malaya wake’’, Sara alijibu kwa ghadhabu.
“Mmmmmh. Unajua nini shemeji, nilivyosikia na naomba usinitaje lakini” Gideon alianza kujihami.
“Sikutaji bwana we, mbona la Ketina sikukutaja kabaki kunitolea macho tu. Niambie ehee”, Sara alijibu Kiswahili Swahili.
“Nilivyosikia ni kuwa shutuma hizi sio nini wala nini ni namna ya kukuandaa ili akutaliki amuoe Ketina. Yani anakutengezea mazingira akuache kwa kosa la kutaka kushirikiana na waliotaka kumpindua ili aoane na Ketina”, Gideon alipigilia msumari kama alivyoelekezwa na Joe.
“Unasema? Shemeji ya kweli hayo?” Sara aliuliza kwa mshangao.
“Kwani nilipokwambia juu ya Ketina shemeji yangu si ulinikatalia hivi hivi mpaka ulivyothibitisha mwenyewe? Sina sababu ya kukudanganya shemeji” Gideon aliendelea kumwaga sumu kwenye uhusiano ambao tayari ulikuwa katika hali ya kuhitaji dawa.
“Kwani huu mpango wa kumpindua ni kweli?” Sara alihoji.
“Ninavyosikia ni kweli si unaona Macha kawekwa ndani na hivi karibuni atakutana na Rais kukiri. Ila sasa kuna wengine hawajulikani bado”, Gideon alijibu.
“Laiti ningewajua ningewasaidia, huyu Costa ni mpuuzi sana. Sikuwahi kufikiria kuwa anaweza akawa na mpango wa kipumbavu namna hiyo dhidi yangu. Nimeishi nae kwa miaka 30 sasa tangu akiwa hana kitu hata mavazi na chakula alishindwa kuifadhili familia. Aniache mimi nimemkosea nini? Eti shemeji nimemkosea nini mimi? Sasa ni mimi au Ketina. Hilo nitahakikisha kwa maji au damu.” Sara alionekana mwenye ghadhabu huku machozi yakionenaka kwa mbali.
“Shemeji, shemeji, shemeji basi usilie mtu ataingia hapa iwe tatizo. Ninachokuomba usimweleze chochote kwanza wakati huu ambao hatuna Uhakika sana na taarifa zozote, mimi nitaendelea kukutaarifu kila kinachoendelea na huyu kimada wake. Lakini pia nitafuatilia kuthibitisha ikiwa ni kweli kulikuwa na jaribio la mapinduzi na nitakumegea siri nikiwa na taarifa za uhakika zaidi’’, Gideon alimjaza Sara upepo huku akimvuta taratibu katika mpango wa kumng’oa Rais Costa bila Sara yeye kujua moja kwa moja.
“Sawa Shemeji. Ila bora huu mpango ungefanikiwa. Wasipompindua wao nitampindua mimi, I swear! Siwezi kukubali kudhalilishwa hata baada ya kumlea na kumfanya Costa kuwa Costa!” Sara alijibu kwa hasira na kutoka ofisini kwa Gideon.
Gideon hakuamini mapokeo aliyoonesha Sara. Alijua ni Dhahiri kuwa ikiwa Sara angekengeuka na kumdokeza Rais Costa kuhusu mazungumzo yale basi angekuwa kwenye hatari kubwa, lakini kama angeendelea kuwa mwanamke shupavu anayemfahamu basi huu ulikuwa ni ushindi kwa kambi yao.
Alichukua simu na kuingia kwenye game ya Clash Royale na kumtaarifu Joe kila kilichotokea.
“Sadam, Tiger is a living genius”, Joe alimjibu Gideon akimsifia Macha kwani mpango mzima kuanzia ule wa Gideon kutumwa kumtonya Sara mahusiano ya Rais Costa na Ketina mpaka Joe kumtaja Sara kwenye maongezi yao yote na hivyo kumfanya anahusika ili Rais Costa aanzishe ugomvi na mkewe, mpaka Gideon kufanya alivyofanya ni mchoro makini uliochorwa na Macha kabla ya misheni kuanza.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Che, hata Tiger akifa leo nitampigia saluti nyingi sana”, Gideon nae alijibu.
“Sasa tunakaribia kumpata Sara. Huyu tutaenda nae taratibu kazi yake ipo mwishoni. Bahati Mbaya mtu pekee anayeifahamu kazi hiyo ni Tiger, hivyo hakikisha unapata nafasi ya kuonana nae kumpa hizo taarifa ili akueleze namna ya kumtumia Sara”, Joe alimalizia kuandika ujumbe na kuutuma kwa Gideon.
******************************************
Meshack aliwasili mji mkuu wa Stanza, Peron akitokea jimbo alilopangiwa kama afisa usalama baada ya kupamguliwa na Sabinas.
Aliwasili kwa ajili ya kazi moja tu kuhakikisha Sylvanus hapandi ndege kuelekea China kwa ajili ya kumuua Joe. Meshack alijua fika si rahisi Joe kumkwepa Sylvanus kwani ni muuaji hatari na mahiri lakini pia hakuwa na hakika ni kwa vipi atammudu Sylvanus, aliujua umahiri wake katika medani za kijasusi na ulinzi.
Aliwasili jijini Peron na kitu cha kwanza alichofanya ni kusubiri giza liingie. Siku aliyowasili kesho yake ndiyo haswa siku waliyokuwa wanasafiri kikosi kazi kilichotumwa kwenda kumuua Joe nchini China. Kikosi kile kilikuwa kinaondoka na ndege ya saa 12 asubuhi. Meshack alijua wazi anahitajika siyo tu kumnyamazisha Sylvanus lakini pia kuhakikisha haijulikani kama ni yeye.
Ilipotimia mishale saa tatu usiku hivi Meshack alitoka akiwa amevaa koti jeusi la baridi, raba nyeusi na jinzi nyeusi. Alivaa kofia nyeusi na shati la kijivu, na hakubeba silaha ya moto zaidi ya kisu kikali kidogo kilichokuwa na uwezo wa kujikunja na kuwa kama kiberiti. Mfukoni hakubeba kitambulisho chochote zaidi ya pesa kidogo.
Mchana wa siku hiyo Meshack alishinda akifanya mazoezi ya mikono (push ups) hivyo mikono yake ilikuwa imevimba kwa kujazia. Alibeba barakoa ya skii, hii ni aina ile kofia ambayo hufunika kichwa na uso na kuacha macho tu. Akiitunza kwenye mfuko wa koti pamoja na glavu nyembamba za kuvutika kama mpira zinazofanana na zile zinazotumika hospitalini. Meshack alitoka na kuanza kuzunguka mjini.
Meshack alijua tabia za Sylvanus. Alimjua ni mtu anayependa sana kucheza kamari kwenye mahoteli makubwa makubwa hasa Casino. Alifahamu kuwa usiku wa siku kama ile ni lazima angemkuta kwenye moja ya Casino akicheza kamari.
Japo aliifahamu hulka ile lakini alijua Sylvanus ni mtu mwenye machale, yaani haikuwa kazi rahisi kumnasa kwani ni mtu aliyesomea na kubobea katika kusoma mazingira na kukwepa kila inapowezekana. Hilo lilimpa wasiwasi Meshack.
Kama alivyowaza, Meshack aliingia New Continental Casino na alipotupa macho kwa mbali akiwa ndani ya kofia yake na miwani alimwona Sylvanus kwa mbali akicheza kamari. Kama ilivyokawaida, vile Meshack anaingia tu Sylvanus ni kama alihisi jambo akanyanyua uso na kaunza kuangaza macho.
Haraka Meshack aligeuza sura na kuangalia kaunta na kuanza kuelekea kuchukua kinywaji. Meshack alichukua kinywaji na kujibanza mahali alipohakikisha kuwa anamuona Sylvanus lakini Sylvanus hamuoni yeye.
Wakati akichukua simu ili aweze kumtaarifu Joe kuwa yupo kwenye misheni aliyomuomba hakuamini alichokisikia.
“Meshack”, mtu alimgusa bega kwa nyuma huku akiita jina lake.
Meshack alichanganyikiwa kwani aliamini kabisa kwa jinsi alivyovyaa hakuna mtu angeweza kumfahamu. Haraka Meshack alirusha macho kwenye machine ya kamari aliyokuwa anacheza Sylvanus, hakuamini, Sylvanus hakuwepo pale. Meshack aliishiwa nguvu.
*************************************
Mwinda Anapowindwa
Usiku ule pale New Continental Casino kulijaa watu wengi. Ilikuwa ni siku ya Alhamisi, siku ambayo wacheza kamari huamini ni siku yao ya bahati, hivyo watu huhudhuria kwa wingi.
Mara baada ya Meshack kumuona Sylvanus na kumkwepa alielekea upande wa kaunta na kuagiza kinywaji. Alichukua kinywaji chake na kufungua simu upande wa WhatsApp ili aweze kumwambia Joe kinachoendelea. Alishtushwa aliposikia ameguswa bega na kuitwa kwa jina wakati yeye aliamini kwa jinsi alivyovaa hakuna ambaye angeweza kumtambua.
“Meshack niaje”, jamaa aliyemgusa bega alimsalimia Meshack.
Bila kujibu huku akiwa ameshtuka sana Meshack aligeuka ili kutazama ni nani amemuita. Hakuamini macho yake alipokuta ni Sylvanus. Mwendo wa mapigo ya moyo wake yalibadilika na kuanza kwenda kasi. Ni kweli aliujua uwezo mkubwa wa Sylvanus wa kuhisi na kugundua mambo lakini hakujua kama ni uwezo uliofika kiwango kile alichokishuhudia wakati ule.
“Ah! Sylvanus, na wewe upo viwanja hivi?”, Meshack alijikaza na kujibu.
“Haya ndio mambo yangu mzee labda nikuulize wewe huku umeanza lini au kuna lead unaifatilia?” Sylanus alihoji.
Lead ni neno linalotumika kuashiria mtu anaefatiliwa kwa sababu fulani. Yaweza kuwa yeye ndiye ‘target’ ama unamfatilia ili akupeleke kwa ‘target’ lakini bila yeye kujua. Mfano, kama mtu amehisiwa kuwa anafanya utakatishaji wa fedha na kuwa hana shughuli maalumu bali anatumiwa na watu basi watu wa usalama waweza kumfatilia mtu huyo ili kujua anatumiwa na kina nani. Ufuatiliaji huu huwa wa siri na bila muhusika kujua kama anafuatiliwa.
“Hapana mzee, nimeamua kuja kupumzika tu”, Meshack alijibu kwa kujikaza.
“Si kwa mavazi hayo kaka. Ha ha ha”, Sylvanus alionekana kukomalia.
Baada ya maongezi mawili matatu Sylvanus aliondoka na kumuacha Meshack. Meshack alivuta pumzi kwa nguvu sana na kutoamini kama Sylvanus amemshtukia pale. Alianza kuhisi yamkini Sylvanus ameshajua kitu, aliingiwa na woga sana.
Siku ile ilikuwa ni lazima amuue Sylvanus kwa sababu akimuacha akapanda ndege kuelekea China kesho yake alfajiri basi Joe asingekuwa salama tena. Meshack alijua wazi kuwa Joe hawezi kukwepa mkono wa Sylavanus. Ni gwiji wa mauaji ya siri aliyewahi kutumiwa na serikali kadhaa za nchi za kiafrika kuwamaliza wapinzani wao. Hakuwa mtu mwenye huruma na hakuwahi kujali jambo lolote Zaidi ya amri aliyopewa. Hata wanausalama wenzake walimuogopa.
***********************************
Sylvanus alipomaliza kuongea na Meshack hakuridhika. Hisia zake zilimwelekeza afuatilie zaidi. Aliwaza kama kweli Meshack hajaja pale kufuatilia lead basi ni lazima kuna suala jingine amekuja kufuatilia. Anafahamu wazi kuwa si hulka ya Meshack kukaa sehemu kama zile. Lakini pia kama amekuja kufuatilia lead kwanini amesita kumwambia ni nani wakati wote ni watendaji wa idara moja na pengine angeweza kumsaidia? Maswali mengi yalimsumbua sana kichwa Sylvanus.
“Oya Nyari, hivi baada ya mkuu Sabinasi kupangua safu Meshack alimpanga kitengo gani?” Sylanus aliamua kumpigia simu Nyari na kumuuliza.
Fredrick Nyari ni mwenzake na Sylvanus, wote wapo Idara ya Usalama wa taifa Stanza kitengo cha Mauaji na Uhujumu. Tungekuwa Israel basi kitengo chao hiki kingekuwa sawa na kile cha Idara ya Ujasusi ya Israel Mossad kwenye kitengo wanachokiita Metsada ambacho kazi yao kuu kwa kiingereza wanasema Assasinations and Sabotage.
“Alimtupa jimbo la Kinyunyu. Kwani vipi mzee?”, Nyari alihoji.
“Ah, namuona New Continental hapa. Nimemuuliza ikiwa ana lead ila amekana na kusema kuwa amekuja kupumzika tu wakati mimi nafahamu haya si mambo yake kabisa. Ila poa mwanangu baadae”, Sylvanus alimaliza na kukata simu.
Hapo ndipo Sylvanus alipopata wasiwasi kamili kuwa lipo jambo Meshack amemficha. Aliamua kuanza kumfatilia amemficha jambo gani. Aliwaza iweje muda ule Meshack awe pale wakati Kinyunyu ni mbali sana na Peron, mji mkuu wa Stanza. Amefuata nini?
Alianza kumuwinda. Wawindaji walianza kuwindana.
****************************************
Meshack alianza kumtaarifu Joe jinsi alivyoshtuliwa na Sylvanus. Alimweleza wasiwasi wake kuwa misheni ile inaweza kukwama kwani sasa Sylvanus ameshajua kuwa yeye yupo pale na hiyo inamuweka kwenye wakati mgumu kufanya alilokusudia. Wao kwenye usalama husema kugundulika tu kuwa wewe ni nani kwa adui tayari kunakupunguzia asilimia 50 ya kumshinda. Alihisi kuanza kushindwa.
Meshack aliamua kumtumia Joe picha ya Sylvanus na kumwambia popote anapokuwa ahakikishe mtu huyo hayupo karibu yake. Alimsihi kuwa anapomuona tu ajihami nae mara moja maana wao walizoea kumwita Sylvanus upepo kwasababu huweza kuonekana na kutoweka kwa haraka isiyotarajiwa. Kupotea mara unapohisi kugundulika ni mbinu ya kawaida kwa majasusi wabobezi.
Alikuwa pia na uwezo mkubwa wa kufanya mauaji kwa uharaka uliopitiliza na kutoacha hata alama kidogo tu ya kutenda hivyo, na iliwawia vigumu wachunguzi kujua ni nani muhusika wa mauaji yale. Alimsihi Joe kuwa atajaribu lakini kama akishindwa basi Joe hana budi kujilinda dhidi ya Sylvanus.
*********************************
Elizabeth, mke wa Joe kwa mara ya kwanza tangu mume wake aondoke kuelekea Korea Kaskazini aliingiwa na hofu sana. Hofu hii ilijengwa kwa sababu kubwa mbili. Moja, Joe mume wake alimuaga kuwa misheni ile haitamchukua zaidi ya wiki moja ama akichelewa sana basi wiki mbili lakini mpaka siku hiyo tayari alishafikisha wiki ya tatu.
Sababu ya pili ni kuwa Joe hana utaratibu wa kukaa zaidi ya wiki moja bila kumtafuta. Yeye Elizabeth alishajaribu sana kumpigia simu Joe bila mafanikio na sasa aliamua kumpigia kwa njia ya WhatsApp. Alifanikiwa kumpata kwa mara ya kwanza.
“Dear, mnaendeleaje huko? Mbona simu yako nikipiga kawaida inakataa na wewe hunitafuti hivi kweli hujanimiss mke wako?”, Eliza alianza kudeka kwa mumewe Joe alipopokea simu yake.
“Nipo China, Costa amenipa kazi nyingine hapa ila nitarudi mke wangu. Watoto wanaendeleaje lakini?” Joe aliuliza kwa sauti ya upole.
“Wapo vizuri tu Mi Amor”, Eliza alijibu nae kwa sauti ya mahaba akimwita Joe Mi Amor, maneno ya lugha ya kihispanyola yenye maana ya mahabuba wangu.
Joe na Eliza walikuwa ni maana halisi ya watu wanaopendana. Japo umri wao ulikuwa mkubwa na tayari walishakaa kwenye ndoa kwa miaka 21 sasa lakini mapenzi yao hayajawahi kupungua. Walitofautiana na wana ndoa wengi wenye kuamini kuwa baada ya kuoana kuna mambo wanapaswa kuacha. Wao hawakuwahi kuacha mambo yaliyowafanya wapendane enzi za ujana wao.
“Derrick anaendelea na lile zoezi la kujiwekea akiba? Amekwambia mwezi huu ana mpango gani? Hakikisha anakwambia ni kitabu gani atakisoma mwezi huu cha uwekezaji lakini pia kwa sababu yupo likizo aseme anataka kwenda kutembea wapi. Utaratibu wa kukaa kucheza game tu ndani nilishakataa”, Joe alimwagiza mke wake.
“Afadhali umenikumbusha, nilishasahau. Unajua wiki hii imekuwa ngumu sana kwangu maana tulikuwa tunasimamia usambazaji wa mbolea kwa wakulima. Benki ya wakulima ndio Costa ameipa jukumu la kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati sasa hawa watendaji wanataka kunivuruga, imebidi nilale nao mbele. Ila nimemalizana nao nitafatilia hayo baba Derick.” Eliza alijibu kwa heshima ya uanamke.
Joe ni baba aliyetaka kuleta mapinduzi kwa kizazi chake. Aliamini jamii ya watu wa magharibi huanza kuwafunza na kuwakuza watoto wao katika hali ambayo humfanya mtoto ajielewe na kujiamini angali bado mdogo.
Mathalani, kusoma vitabu, kutembelea maeneo mbalimbali, kuanza kuwafundisha watoto namna ya kuweka akiba, kuwekeza, kupanga malengo na kuyatimiza ni mambo ambayo kwa jamii za kiafrika yapo nyuma sana na hivyo kumfanya mtoto mpaka anakuwa mtu mzima anajikuta amezaliwa eneo hilo na kusoma hapo hapo akapata kazi na kuoa hapo hapo. Tena hajui kuweka akiba, hajui uwekezaji na huishi bila malengo.
Kuishi bila malengo ni sawa na mtu anayeendesha gari pasi kujua anaelekea wapi. Anayekwenda bila kujua anaelekea wapi ni sawa na asiekwenda popote. Wazungu husema “If you don’t know where you’re goin, then you’re going nowhere”. Joe alikataa kizazi chake kuwa cha namna hii.
“Eliza afadhali umenipigia nilikuwa nataka kuwaambia nawapenda sana familia yangu. Umwambie Derick na mdogo wake ‘wabehave’. Dunia ipo kwa ajili yao ni kazi yao kuitawala”, Joe alionekana kama kutoa maneno ya usia kwa mkewe Eliza.
Joe alijua kabisa kama Meshack atamkosa Sylvanus usiku ule basi yeye hatammudu. Aliwaza akimbilie ubalozi wa Korea Kaskazini kujificha lakini aliona haitakuwa na maana. Alitaka kufa kiume.
“Joe hujawahi kuniaga kwa staili hii, leo kulikoni? Kwani Costa kakutuma nini kinachokupa wasiwasi namna hiyo?” Eliza alihoji.
“Hapana Eliza kwani mimi kusema nawapenda nimeanza leo?” Joe alimuhoji mkewe.
Eliza aliona asiendelee kuuliza asije akasababisha wakamaliza maongezi kwa hasira, aliamua kukaa kimya na kuagana na Joe.
Lakini kama wanavyosema wengi kuwa mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuhisi mambo yajayo kuliko mwanaume, Eliza usiku ule alisikia tumbo kumuuma mara baada ya kuongea na mume wake. Hakulala wala kupata usingizi. Alianza kuhisi hali ya hatari kumnyemelea mume wake lakini hakujua ni nini wala ni lini. Alikesha macho usiku mzima.
**********************************
Meja Byabato hakuamini alichokuwa akikishuhudia mbele yake. Wale vijana wanne waliokuwa wamesimama mbele ya mlango wa ofisi yake walikuwa wameshiba kisawasawa. Wote wakiwa wamekunja sura na kuvaa miwani meusi sawa na aliyoivaa yeye walikuwa wamesimama huku wakiwa wamepanua miguu kidogo na kuweka mikono yao nyuma.
Meja Byabato aliekuwa akitembea kwa hatua ndefu na kubwa kutokea nje ilibidi apunguze mwendo na kuanza kutembea kwa taratibu huku akiwatazama akiwaza afanye nini na wale vijana wapo pale kwa ajili gani. Aliwaza au alikuwa akifuatiliwa nini? Lakini hata kama alikuwa akifuatiliwa mbona hakuna lolote la maana aliloongea na Gideon zaidi ya kupokea ile taarifa ya siri tena kwa maneno machache? Aliwaza pia kuwa labda Gideon alitumwa kuja kumtega na kuthibitisha kuwa anahusika na mpango ule, lakini pia aliwaza kama ndivyo basi ni Macha atakuwa ameamua kumsaliti.
Wakati huo huo aliwaza isingewezekana Gideo kupata ile ‘code’ kama sio kupewa na Macha na kwa anavyomfahamu Macha asingeweza kumpa mtu asiyemwamini. Lakini alidhani labda Gideon aliaminiwa na Macha na sasa kaamua kumsaliti Macha. Hakika alijawa na maswali mengi ndani ya sekunde chache yasiyo na majibu.
Meja Byabato aliamua kutoa miwani yake na kuwatazama wale vijana kwa macho makavu akiwa amesimama kama hatua kumi hivi kutokea walipokuwa wamesimama. Byabato alikuwa ni mtu wa mazoezi kwa hivyo akiwa amesimama pale alikusanya nguvu zake zote na kujiweka tayari kwa mapambano kama wale vijana wangemwanzishia varangati. Alijisemea moyoni ni bora awe mkimbizi kuliko kudakwa kama kuku.
Vijana wale kicheo walikuwa ni wadogo sana kwa Meja Byabato hivyo alitegemea wao ndio waanze kumpa salamu. Meja aliwatambua kuwa ni vijana wake tena isitoshe wapo kwenye kikundi chake cha mazoezi ya viungo kwa hiyo na wao walikuwa wameshiba kweli kweli.
Baada ya kusimama kama sekunde kadhaa bila yeye kusema neno wala wao kusema neno ghafla walipiga saluti ya kumsalimia. Meja nae alijibu.
“Kwanini mmesimama hivyo ofisini kwangu. Kuna nini?” Meja alihoji kwa sauti ya ukali sana.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Wale askari walibaki kimya sekunde kadhaa na kisha wote kwa pamoja walimwendea Meja kwa kasi ya ajabu na kumvaa.
Meja alidaka ngumi ya mmoja wapo aliyokuwa ameirusha kwa kasi ya kimbuga na kumpiga kichwa kimoja kilichomfanya aweweseke. Wakati akimdhibiti huyu mmoja kijana mwingine alimpiga Meja ngumi moja ya juu ya sikio iliyompata kwenye mshipa wa fahamu wa kichwa na kumfanya Meja nae aanze kuweweseka.
Akiwa anaweweseka mwingine alirusha ngumi nzito iliyokuwa inamwendea Meja maeneo ya pua lakini Bahati nzuri aliiona na kuikwepa ikapiga ukuta, na kwa sababu ilikuwa na kasi kubwa na uzito mkubwa yule kijana alijikuta ametengua vidole vyote vinne vya mkono wake wa kulia. Meja alijua hilo na haraka alimchota juu na kumpigiza chini kama gunia.
Mapigano hayo yalikuwa yakienda kwa kasi sana na haraka. Meja alijua hapo hali si shwari tena, alianza kuwaza ni namna gani awatoke wale vijana wake. Tatizo lilikuwa ni moja tu vijana wale aliwafunza mapigano yeye mwenyewe na walijua mbinu zote, walikuwa warefu kama yeye na walishibwa kweli kweli.
Wakati akiwaza hayo tayari king’ora cha hatari kilishapigwa na askari pale kambini walianza kuja kuamulia maana pale ilikuwa mmoja awe maiti. Kambini pale waliwajua wale vijana na waliujua vizuri uwezo wa Meja Byabato, ilikuwa huwezi kuamulia kwa mikono bila kutumia silaha.
Haraka kijana mmoja aliminya Sehemu ya nyonga ya Meja na kumfanya achutame chini kidogo na hapo mwingine alimshushia Meja ngumi moja Sehemu ya shingo na kumfanya Meja adondoke kwa magoti. Vijana wale walidhani wamemuweza Meja, wakiwa watatu wamesimama na mmoja amelala chini hajitambui Meja alishika mguu wa mmoja na kumvuta kitendo kilichosababisha adondoke na kupiga kisogo kwenye sakafu na kulala palepale akigugumia maumivu makali, na haraka Meja alinyanyuka kwa staili ambayo wachina wanaiita Jùfeng, yaani unanyanyuka kama upepo wa kisulisuli. Alinyanyuka na kumkanyaga shingo kwa nguvu kwa buti lile la jeshi alilokuwa amevaa huku akichutama kidogo na kuwapiga wale wawili maeneo ya chembe ya moyo kwa vidole viwili vya mikono wote kwa mpigo.
Eneo la chembe ya moyo pakiingizwa kidole basi ni lazima uende chini na ndicho kilichotokea. Baada ya Meja kuona angalau wote amewadhibiti huku akiwa hoi na akitokwa damu nyingi puani alianza kukimbia kuelekea nje. Hakuna askari aliyethubutu kumzuia wote walikuwa wakimpisha na alikuwa akipita kati kati yao kwenye korido ile.
“Happy birthday Sir”, Alisikika askari mmoja kati ya wale aliokuwa akipambana nao akiita kwa nguvu.
Meja Byabato alishtuka na kusimama kisha aligeuka kwa taabu mzima mzima maana shingo ilikuwa imepigwa ngumi moja na kuteguka.
“Happy birthday mkuu”, Kijana mwingine aliekuwa akijitahidi kunyanyuka kwa taabu alipokea naye huku akijitahidi kupiga saluti, salamu maalumu ya kijeshi akitokea pale chini.
Walinyanyuka vijana wawili kati ya wale aliokuwa akipambana nao na kupiga saluti huku wakiimba wimbo wa kumpongeza Meja kuashiria kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Meja Kairuki Byabato. Askari wote waliokuwa wamekuja pale kusuluhisha walipiga saluti huku wote wakimwimbia Meja Byabato wimbo wa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa, au Watoto wa mjini wangesema ‘’Happy Birthday’’
Meja hakuamini alichokuwa akikishuhudia. Ni ukweli kuwa ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na hakuwahi kuisherehekea kwa zaidi ya mwaka wa 20 sasa. Vijana wake wale walianza kucheka huku wakimsogelea na Meja nae alianza kutabasamu kama kawaida yake kwa kubinua shavu moja tu bila hata kuonyesha jino hata moja.
Alitoa kitambaa cha mkono na kuanza kujifuta damu iliyokuwa ikimchuruzika puani.
“Meja upo vizuri”, Kijana mmoja aliekuwa akipambana na Meja Byabato alimsifia huku akimkumbatia.
“Nani aliwaza huu mpango”, Meja Byabato aliuliza kwa sauti ya kunguruma.
“Tulipanga siku nyingi na mazoezi yote uliyokuwa unatuona tunafanya wiki hii nzima ilikuwa ni kwa ajili yako, tulipanga tukuzimishe leo”. Kijana mwingine alijibu huku akimkumbatia Meja.
“Dah, sasa ningeua mtu hapo maana nilijua mnaniwashia kweli”, Meja nae alijibu kwa sauti ya maumivu.
Askari wengine waliokuwa watazamaji walimpa hongera Meja Byabato kwa kuweza kuwamudu wale askari wanne. Waliondoka na kuwaacha Meja na vijana wake.
“Tuingie ofisini kwangu mara moja”, Meja aliwaambia wale askari vijana wanne aliokuwa akipambana nao. Wote waliingia ofisini kwa Meja Byabato huku kila mmoja akijikokota kwa staili yake kutokana na eneo analosikia maumivu.
***********************************
Baada ya Meshack kuhakikisha kuwa ameshampa taarifa Joe ya kila kinachojiri kati yake na Sylvanus pale New Continetal Casino aliizima simu na kuiweka mfukoni ili sasa kuona ni namna gani atatimiza misheni ile.
Alibugia kwa mkupuo toti yake moja ya Godowns na kukaa tayari kumuwinda Sylvanus. Maskini hakujua kama na yeye alikuwa akiwindwa vile vile.
Alinyanyua kichwa na kumuona Sylvanus anacheza kamari pale kwenye ile mashine yake lakini kama baada ya dakika tatu hivi alimuona akitoka na kuelekea uelekeo wa vyooni. Meshaki hapo ndipo alipoona ni muda mzuri wa kujaribu Bahati yake. Hakujua ule ni mtego aliokuwa amewekewa na Sylvanus. Wanasema ili kumpata muhalifu lazima uwaze kama muhalifu. Sylvanus alimudu sana hili alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwaza sawa na ‘target’ wake anavyowaza ndio maana aliweza kujua kwa haraka lililo mbele yake.
Sylvanus aliingia kwenye ukumbi wa vyoo na kurudishia mlango. Casino ile ilikuwa na eneo kubwa la vyoo na ukumbi mkubwa. Uligawanywa sehemu kama msala ambapo hakukuwa na milango bali kulitengwa tu kwa kioo kidogo kisichoonyesha, halafu kukawa sasa na vyumba kwa ajili ya wale wanaotaka kujisaidia kile wazungu wanaita ‘long call’.
Tena katika ukumbi ule kulikuwa na sehemu ya kuvutia sigara na sehemu ya kujitengeneza vizuri iliyotengwa pia kwa kioo kisichoonyesha. Hakukuwa na watu wengi vyooni, ni kawaida kukuta zinapita hata dakika tano bila mtu yeyote kuingia kabisa.
Meshack aliingia akiwa amevaa zile raba zake zilizokuwa hazitoi sauti na kuanza kunyemelea kujua Sylvanus yupo wapi. Akiwa anapita mlango kwa mlango akijaribu kuugusa na kuusukuma kama unafunguka Sylvanus alikuwa akimchungulia kwa upenyo mdogo sana kutokea eneo la kuvutia sigara alilokuwa amejitega huko akimsubiri Meshack.
Sylvanus alijiridhisha kuwa kumbe Meshack alikuwa akimfatilia yeye. Kwenye mambo ya usalama huwezi kumwamini mtu, wakati wowote mwenzako aweza kutumwa kukumaliza kama ikionekana uwepo wako unakwamisha masuala ama umeanza kuwa tishio.
Sylvanus hakujua ni kwanini Meshack ametumwa kumuwinda wakati ana kazi aliyopewa na Rais Costa na safari ni kesho yake. Aliwaza huyu aliemtuma Meshack ni nani na ana dhamira gani. Alitaka kuwasiliana na mkuu wao wa Idara ndugu Sabinasi, lakini aliona bora amalizane kwanza na Meshack ndipo atoe taarifa.
Meshack alisikia kama kwenye moja ya vyumba vile vya vyoo kuna mtu ana ‘flash’ na yeye haraka alikimbilia kwenye sehemu ya haja ndogo na kujifanya anajisaidia huku akiangalia kwa kioo ni nani anatoka. Alimuoana mtu mmoja akitoka na hakuwa Sylvanus. Alishangaa kwani alikuwa na uhakika Sylvanus yupo pale ndani.
Baada ya kujiridhisha kuwa ndani ya vyumba vyote vya vyoo Sylvanus hayupo alijua lazima atakuwa eneo la kuvuta sigara akivuta sigara huko. Alitoa ile kofia maalumu inayofunika sura. Akatoa glavu na kuvaa kisha alinyoosha vizuri vidole. Alivuta pumzi kwa nguvu na kwa kuambata na kioo alianza kunyemelea kuingia kwenye ile Sehemu ya kuvutia sigara.
Sylvanus alikuwa akifuatilia kila hatua ya Meshack na hakika alikuwa amewasha sigara akawa anaivuta na kuipuliza kwa juu makusudi. Moshi ule uliokuwa ukivuma kwa juu ulimpa Ushahidi Meshack pasi shaka kuwa Sylvanus yupo kule.
Meshack alisogea taratibu mpaka akafika kwenye ukingo wa kioo kile na sasa alijipanga kuingia kwa kasi ya upepo ili kumvaa Sylvanus na kupambana nae. Alikusanya nguvu na kuhesabu kimya kimya Moja…. Mbili….
Kabla hajamaliza tatu alishtukia amevutwa kwa nguvu na kupokelewa na pigo moja eneo la chini ya mbavu lililofanya mbavu za upande wa kushoto kupanda na kubaki juu hivyo kusababisha maumivu makali yaliyomfanya ashindwe kuhema na kuishiwa nguvu.
Pigo lile lilikuwa ni la uhakika yaani lisilokwepesha matokeo. Mbavu za Meshack zilibaki kwa juu kama nguo iliyotundikwa kwenye msumari nyuma ya mlango. Alikuwa akigugumia huku amejikunja. Sylvanus alimvuta kwa ndani vizuri ili kusababisha wanaoingia chooni kutoona.
“Nimpelekee ujumbe gani Gloria”, Sylvanus alimuhoji Meshack aliyekuwa akitapatapa pale chini. Gloria ni mke wa Meshack.
Meshack hakuweza kujibu, mbavu zilibana kisawasawa. Sylvanus hakuwa mtu wa kupoteza muda haraka alivaa glavu zake na kumpindua Meshack na kuiegamiza shingo ya Meshack kwenye goti lake la kulia na kisha kumpiga kabari Meshack iliyotukuka. Kabari hii wakorea wanaiita ‘gong-gan eobs-eum’, yaani unakabwa kuhakikisha hakuna nafasi ya hewa kupita kwa namna yoyote ile.
Kwa sababu tayari Meshack alikuwa ameishiwa nguvu kwa pigo la kwanza lililosababisha mbavu za upande wa kushoto kubaki juu na kusababisha apumue kwa shida, kabari hii ilikuwa ni ya kummalizia tu. Alitapatapa kidogo sana na kisha alitulia. Uuaji wa Sylvanus ulionekana ni rahisi kwa macho lakini ukiujaribu kama si mtaalamu basi hauwezi kufanikiwa.
“Nitamjua aliekutuma”, Sylvanus alikuwa akimwambia Meshack aliyeonekena kuanza kufumba macho taratibu huku akitulia kimya bila kutapatapa tena. Sylvanus alizidi kuminya kabari ile ili kujiridhisha kuwa huo unakuwa ndio mwisho wa uhai wa Meshack.
*****************************************
Mambo Yazidi Kuwa Mazito
Ilikuwa ni asubuhi yenye utulivu katika Ikulu ya Stanza. Kila mtu akiwa anaendelea na shughuli zake kama kawaida Gideon alikuwa akikatiza kwenye korido za Ikulu huku akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Ikulu kwenye ofisi zao.
Ni kawaida kwa Gideon kuingia kwenye ofisi za baadhi ya wafanyakazi pale Ikulu hasa ya Katibu Mkuu Kiongozi na kubadilishana nae mawazo mawili matatu. Kwa kufanya hivyo, ilimsaidia Gideon kujua mambo mengi yanayoendelea ndani ya Ikulu ya Stanza isiyoisha matukio.
“Ahaaa bwana Jabir, kwema kaka yangu?”, Gideon alimsalimia Jabir Salehe, Katibu Mkuu Kiongozi akiwa amesimama mlango wa ofisi yake alipopita kumsalimia.
“Gideon, salama mdogo wangu. Tena nilitaka kukufata ofisini kwako kwa sababu Mheshimiwa aliniambia amekupa kazi ya kuandaa majibu kwa Rais Chriss, umefikia wapi asee?”
“Ndiyo hii nilikuwa naelekea ofisini kwake sasa hivi akaipitie”, Gideon alimwonyesha Jabir karatasi aliyokuwa ameishikilia mkononi.
“Hata mimi nilikuwa na hii taarifa kwa vyombo vya habari aliyoandaa Alpha ya kumteua Ketina kuwa Mbunge. Ninaendelea kuihakiki ili akaitoe kwa umma”, Jabir alimwambia Gideon huku akiisoma ile barua ya majibu ya Rais Costa kwa Rais Chriss wa Marekani aliyokuwa ameishika Gideon.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Alpha Wauwau ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
“Amemteua Ketina kuwa Mbunge kwa zile nafasi zake tano za ubwerere? Ha ha ha!”, Gideon alimwambia Jabir kwa utani. Walipenda kutaniana sana.
“Ndiyo, na baada ya uteuzi huu atakuwa amezimaliza. Lakini sijui ni nani amemshauri hivi, maana yule binti ni kituko na usikute anataka kumpa nafasi nyeti”, Jabir alimwambia Gideon huku akimalizia kusoma ile barua.
“Washauri wa Rais ni wengi bwana. Yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua ni ushauri upi auchukue upi auache”, Gideon aljibu kinafiki akijua fika ni yeye aliyemshauri Rais Costa afanye uteuzi huo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment