Search This Blog

Sunday 20 November 2022

NYUMA YAKO (3) - 2

 







    Simulizi : Nyuma Yako (3)

    Sehemu Ya Pili (2)







    Ni aidha kwenye mataifa ambayo hayaungi mkono jitihada za kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ama kwenye swala la mafuta.



    Japo walighani mawazo mbalimbali wawili hawa walikubaliana kwamba bwana Ian ndiye kipande cha fumbo kinachokosekana.



    Huenda bwana huyo akawa na taarifa nyeti kwenye hili yeye kama mmoja watu waliohusika na kupeleka familia ya siri ya Raisi nchini Ujerumani.



    Hawakuwa na budi kumtafuta kwa udi na uvumba kumtia mkononi, lakini swala hilo halikuwa jepesi. Bwana huyo amekuwa ni mtu wa kuhamisha makazi na ofisi yake mara kwa mara, kama vile baada ya kila miezi kadhaa.



    Hata wafanyakazi wake baadhi hawajui ni wapi haswa alipo bwana huyu. Kitu pekee kinachowafanya waone uwepo wake ni kwa kupitia akunti zao za benki tu. Pesa inakuwa ikiingizwa kila mwisho wa mwezi.



    Kwa wale wanaofahamu makazi yake na wapi anapopatikana, walikuwa hawazidi watano.



    Yote hayo kwasababu za kiusalama.



    Hata Marietta, mpenzi wake, hakuwa hafahamu lolote kuhusu wapi anapopatikana bwana Ian.



    Kumpata iliwapasa watulie na kuja na mpango kabambe.



    “Vipi, una wazo lolote?” Danielle aliuliza akimtazama Marshall. Baada ya Marshall kufikiri kidogo akasema, “Kuna njia mbili. Moja kwa kupitia Willy na nyingine kwa kupitia Marietta.”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kisha akamalizia,



    “Lakini kote kuna changamoto.”



    Danielle akatabasamu na kusema,, “Changamoto ndiyo raha ya mchezo, Marshall.”





    **



    *SEHEMU YA 08*





    Asubuhi ya saa nne …





    “Sitasema kitu,” alibwabwaja bwana Willy akimtazama Inspekta James. Bwana huyo alikuwa amefungwa mikono na pingu iliyojishikiza mezani. Miguu yake pia ilikuwa imefungwa minyororo iliyozungushiwa kwenye kiti.



    Hakuwa na uhuru.



    Uso wake ulikuwa na majeraha, haswa upande wake wa kushoto ambapo ulikuwa na rangi ya zambarau kuonyesha amevilia damu.



    Bwana huyo tangu ameketishwa hapo kwa ajili ya mahojiano, amekuwa mkaidi haswa. Hakuna swali hata moja alilojibu, muda mwingine alimtazama tu muulizaji pasipo kufungua kinywa.



    “Nakuuliza kwa mara nyingine, kwanini ulikuwa unataka kunimaliza? Na kwanini ulikuwa unataka niachie kesi?”



    Bwana Willy akamtazama inspekta kama mdoli. Hakutia neno.



    “Ukaidi wako hautakupeleka kokote, ndugu. Na ninakuhakikishia, utasema kila kitu ambacho unakificha,” akasema James akinyanyuka. Bwana Willy akamtazama akimsindikiza na macho alafu akasema akitikisa kichwa,



    “Kamwe!”



    Inspekta akaachana naye ajiondokee lakini kabla hajaufikia mlango, Willy akamtahadharisha, “kuwa makini, inspekta. Maisha yako yako kwenye mstari.”



    Inspekta asijali sana maneno hayo, akaenda zake nje.



    Alikutana na Harold na Gerrard akawapa maagizo waende wakapekua kila kitu ambacho kipo huko, na chochote wanachoona kinaweza kuwasaidia kwenye upelelezi wao, basi wakilete mara moja kituoni.



    Baada ya Harold na Gerrard kuondoka zao, inspekta akajirusdisha kwenye ofisi yake na kutazama baadhi ya mambo ya kazi. Muda kidogo akanyanyua simu yake na kumpigia Marietta. Alitumia namba ya simu ambayo ipo kwenye kadi ya biashara ya mwanamke huyo.



    Simu ikaita mara mbili, ikapokelewa.



    “Ni inspekta James Peak hapa,”



    “Ndio, inspekta.”



    “Habari yako?”



    “Njema kabisa. Unaendeleaje?”



    “Vizuri, nashukuru. Nimeona kimya nikaona nikutafute hewani. Vipi hauna jambo la kunishirikisha?”



    Kukawa kimya.



    “Madam Marietta …?”



    “Ndio, inspekta.”



    “Una chochote cha kunishirikisha?”



    “Aahm, hapana, inspekta. Namba yako ninayo, nitakapopata jambo, usihofu nitakutafuta kama nilivyofanya awali.”



    “Kweli?”



    “Ndio, usijali.”



    “Samahani, kama hutojali. Tangu ulipotoka hapa kituoni, haujakutana na kitisho ama maneno yoyote?”



    Kukawa kimya kidogo.



    “Madam Marietta,” inspekta akaita.



    Mara tiiiiiiiii! Simu ikakata.



    Inspekta akajaribu kumpigia tena mwanamke huyo pasipo mafanikio. Alikuwa hapatikani!



    “Ana shida gani huyu?” inspekta James akajiuliza akiweka simu yake chini. Alitambua kutakuwa na tatizo na haja ndani yake ilimtuma amtafute mwanamke huyo kwa maongezi zaidi.



    Kwenye ulimwengu wa kiitelijensia, kila mtu ni mtuhumiwa, hakuna wa kuaminika kwa asilimia zote.



    Alifikiria jambo hilo la Marietta kwa muda kidogo kabla hajaachana nalo na kuendelea kupitia rekodi za bwana Willy kwenye shirika lake la kazi, FBI.



    Ripoti hizo aliziomba toka huko shirikani na pasipo tatizo, wakampatia.



    Likapita lisaa limoja akiwa anazipitia. Hakuwa anaona kama kuna jambo la kumtilisha maanani hivyo kidogo akaanza kuboreka, ila kwakuwa hana budi, akaendelea kupitia.



    Kidogo akiwa katika zoezi lake hilo, hodi ikapigwa kwenye ofisi yake na kabla hajaitikia, akaingia afisa mmoja aliyemtazama kwa kukodoa,



    “Mkuu, inabidi uone hili!”



    Upesi bwana James akanyanyuka na kuongozana na afisa huyo mpaka mahali alipokuwa amehifadhiwa bwana Willy, selo.



    Hapo aliporusha macho, akastaajabu kuona bwana huyo akiwa amelala, anavuja damu puani na mdomoni!



    “Nini kimetokea?” inspekta akauliza akizama ndani. Mapigo ya moyo ya bwana Willy yalikuwa yanasikika kwa upole mno. Macho yake yalikuwa yanarembua akihema kwa uzito.



    Basi upesi bwana huyo akanyanyuliwa na haraka akakimbiziwa kwenye gari la wagonjwa kuwahishwa hospitali. Pamoja naye, wakaongozana maafisa wawili wa polisi.



    Bwana James akiwa amepigwa na butwaa, alishika kiuno akitazama gari la wagonjwa likitokomea. Alimtazama afisa yule aliyemletea habari, akamuuliza,



    “Ni nini kimetokea?”



    Bwana huyo akamwambia anadhani Willy ametiliwa sumu kwenye chai yake.



    “Alianza kubadilika muda mfupi baada ya kunywa chai. Sikujua nini kilikuwa kinamtokea, alikuwa anagugumia na kujikunjakunja akishika tumbo. Ndani ya muda mfupi ndiyo nikamwona akiwa anatokwa damu, nikaja kukufuata!”



    “Nani aliyempatia chai!” akauliza inspekta akitoa macho.



    “Ni mimi, mkuu!” akajibu afisa. Uso wake ulikuwa umejawa na mashaka lakini pia woga. Alitoa macho yake kwa kukodoa na mdomo akiuachama.



    Inspekta akamkwida nguo yake na kumsogeza karibu.



    “Umetia nini kwenye chai?” akamuuliza akimkazia macho.



    “Sijatia kitu mkuu. Kweli nakuapia!” akasema afisa kwa woga mkuu. Alikuwa amekunja ndita jasho likimchuruza.



    “Nimetoa chai kantini nikamletea moja kwa moja baada ya kuniambia anahitaji kitu cha kupasha tumbo lake!”



    Basi inspekta akaenda mpaka jikoni napo akauliza lakini hakupata majibu. Mpishi na watu wanahudumia walikana kabisa kuhusika na jambo hilo na hata kujaribu chai ile wao wenyewe kuthibitisha kwamba haina tatizo.



    Inspekta akabaki akiduwaa.



    Aliamua kurudi ofisini na kuketi huko akitafakari. Aliona ni vema akangoja majibu ya daktari kugundua nini haswa tatizo.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Lakini uvumilivu nao ukamshinda, akanyanyuka na kujieka koti lake, moja kwa moja akaelekea hospitalini yeye mwenyewe.



    Alichukua kama lisaa kufika kutokana na foleni. Alipowasili na kujitambulisha akapewa habari kwamba bwana Willy amekwishafariki!



    Bwana huyo alifariki njiani kabla hajafika hospitalini.



    “Amefika hapa akiwa tayari ni mfu kwa kama robo saa!” alisema daktari. Alikuwa ni mwanamama mwenye makamo ya miaka thelathini na kitu hivi, macho yake madogo alikuwa ameyajaladia kwa miwani.



    “Ni nini kimemuua?” James akauliza.



    “Ni sumu kali ya kemikali!” akasema daktari kisha akajaribu kwa ufupi kumwelezea inspekta juu ya sumu hiyo. Ni mchanganyiko wa kemikali kadhaa ambazo huathiri mfumo wa hewa na wa chakula kwa muda mfupi mno!



    “Yampasa mtu mtaalamu kutengeneza kitu kama hicho!” alisema daktari na kuongeza, “miligramu moja tu inatosha kabisa kumaliza uhai wa mtu!”



    Inspekta akachoka.



    **



    “Nimekamilisha kila kitu,” alisema afisa wa polisi akiwa ananong’ona na simu. Afisa huyo alikuwa amejibana mahali na kwa kuzuia sauti isisambae, akawa ameziba mdomo kwa kiganja chake.



    Afisa huyo alikuwa ndiye yuleyule ambaye alikuja kumpasha habari inspekta juu ya hali ya bwana Willy baada ya kunywa chai!



    “Ndio, tayari amekwishakufa,” alisema bwana huyo na punde akakata simu na kutoka chooni alipokuwapo. Akachomekea vema sare yake na kuendelea na kazi zake.





    **



    “Mkuu!” sauti ilipaza kwenye simu ya inspekta James. Bwana huyo alikuwa akiongea na mtumishi wake, Harold, ambaye alimpigia akiwa kwenye mazungumzo na daktari.



    Kwasababu mazungumzo yao ni faragha, akatoka ndani ya chumba cha daktari apate kuwa huru.



    “Vipi Harold?”



    “Tumezingirwa!” Harold akabwatuka. “Tumezungukwa nje ya jengo na watu waliobebelea silaha!”



    “Serious?”



    “Ndio! Wamekuja muda si mrefu. Ni sita kwa idadi!”



    “Nakuja! Nakuja!”



    Inspekta akaweka simu mfukoni kisha akanza kukimbia kama mwehu akielekea nje ya hospitali.







    Alijipaki kwenye gari yake nga kuendesha kwa kasi sana. Lakini kama haitoshi akawataarifu na polisi wengine waliopo karibu juu ya swala la wenzake kuvamiwa wakiwa wanatekeleza kazi.



    Akakimbia haswa. Ilimchukua kama dakika ishirini tu kufika eneo la tukio lakini ajabu bado alikuwa amekawia. Alikuta wadhalimu wameshatoweka na watu wake wapo hoi sana.



    Harold alikuwa ametobolewa na risasi mbili, na kwa upande wa Gerrard yeye alikuwa amekula risasi si chini ya tano! Wote walikuwa hoi. Haikupita muda mrefu, Gerrard akafa ikiwa ni muda mfupi kabla ya gari la wagonjwa halijafika.



    Mwili wa Gerrard ulichukuliwa kwa ajili ya mahifadhi, na Harold akawahishwa hospitali baada ya kupata huduma ya kwanza upesi.



    Inspekta James alipekua makazi yale ya bwana Willy na kubaini matundu mengi ya risasi ukutani, mlangoni na madirisha ya kioo yakiwa yamevunjwavunjwa.



    Maganda ya risasi yalikuwa yametapakaa karibia kila eneo, na pia damu baadhi ya maeneo na maeneo.



    Alibaini pia makabati na madroo yalikuwa yamefunguliwa, kupekuliwa na kuachwa wazi. Akiwa amevalia glovu, alitazama kitu kimoja baada ya kingine.



    Baada ya muda mfupi wakaja watu wa ‘Forensic’ - watu wanaohusika kukusanya vielelezo vya kipelelezi, wakaanza kupekua na kukusanya kila kilicho cha muhimu.



    Kitu kikubwa ambao mabwana hao walikipata ilikuwa mabaki ya damu. Walitunza sampuli za damu na kuzipeleka maabara kwa ajili ya upembuzi zaidi.



    Mpaka yafikia majira ya jioni, tayari inspekta James alikuwa amempoteza Willy na Gerrard ikiwa yeye hajapata kitu! Siku mbaya kiasi gani?



    Alionana na mkuu wake na kumweleza kila jambo, na kwa kupitia hayo basi, ili atimize kazi yake vema, akaona kuna haja ya kuongezewa nguvu maradufu.



    Alikuwa anahitaji watu kama watano kwa ajili ya kazi.



    Kazi ambayo alikuwa anaiona yeye kichwani.



    Habari zilitapakaa kwenye vyombo vya habari vyote; redioni, runingani na zaidi mitandaoni. Mosi, kifo cha mazingara cha bwana Willy, pili mauaji ya maafisa wa polisi wakiwa wanatekeleza kazi zao juu ya kesi ya bwana Willy.



    Mambo yalikuwa yanawaka na kuunguza.



    Taifa zima la Marekani lilikuwa limezama kwenye bumbuwazi kutokana na matukio haya ya kufululiza. Watu walikuwa wanataka hitma. Walikuwa wanataka nchi yao irudi kwenye amani iliyozoeleka hapo nyuma.



    Swala hilo lilitafuna kichwa cha inspekta. Aliona mzigo huo wote upo mgongoni mwake.





    **



    Saa sita mchana …





    “Wamemuua asitoe siri!” alisema Jack akitoa macho. Marshall alikuwa anatazama tarakilishi yake mezani kwa udadisi. Alikuwa yu mtandaoni.



    “Ni ajabu, wamemuua akiwa kwenye kituo cha polisi!” Jack aliendelea kubweka. “Si bure kuna watu kila eneo. Ni kazi kwelikweli.”



    Jack aliweka kituo akamtazama Marshall.



    “Kwahiyo naongea mwenyewe hapa, sio?” akauliza akipandisha nyusi.



    “Kuna cha maana ambacho umeongea sijasikia?” Marshall akauliza pasipo kumtazama Jack, bado alikuwa bize na tarakilishi yake.



    “Marshall, usikiite usichoweza kupambana nacho!”



    “Kipi hicho?”



    “Unakijua wewe. Yani mimi kuongea kote huko we hujaona la maana?”



    “Kabisa.”



    “Marshall, nikinyamaza, utajuta.”



    “Nitanenepa maana utakuwa umeniepusha na ujinga.”



    “Aaanh!”



    “Sikia, Jack. Nipo bize hauoni? Waweza kunipa muda wa kuhema tafadhali.”



    Basi Jack akakwapua mfuko wa chocolate uliokuwepo pembeni, kwa hasira akaufungua na kuanza kumumunya. Baada ya muda kidogo, akafunggua tarakilishi yake na yeye akaanza kufanya mambo yake.



    Lakini muda kidogo, tarakilishi ya Marshall ikaanza kukonyezakonyeza. Ilifanya vivyo kwa kama dakika kisha ikazima!



    Marshall akaibamiza,



    “What the f*ck!” akalalama. Akajaribu kuiwasha tena lakini isidumu ikafanya kama awali na kuzima tena.



    Alishindwa cha kufanya. Alimtazama Jack, akamwona mwaname huyo akiwa yu bize na tarakilishi yake kana kwamba hakuwa anamwona wala kumsikia akilalama.



    Akajaribu kuchomoa tarakilishi yake toka kwenye umeme na kulazimisha kuizima kisha akangoja kwa kama dakika tano, akaiwasha tena!



    Alikuwa amekunja uso kwa hasira. Alikuwa anafanya mambo kwanguvu na kwa upesi.



    Tarakilishi iliwaka, akashusha pumzi ndefu ya ahueni, pheeeeeeww!



    Asifanye kitu, sekunde tano tu mbele, tarakilishi ikaanza kukonyeza, mara ikazima tena! Marshall akatukana akibamiza meza.



    “Jack, nini shida na hii mashine?” akauliza.



    Jack hakumjibu, badala yake akawa analiza mluzi. Hapa ndio Marshall akapata jambo kichwani -- atakuwa ni --



    “Jack, wewe ndo umefanya hivyo, sio?” akapaza kuuliza. Jack akamtazama pasipo kumjibu kisha akarudisha macho yake kwenye kioo cha tarakilishi na kuendelea kuperuzi.



    Mdomoni alikuwa analiza mluzi.



    “Jack, si naongea na wewe?”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Huoni nipo bize, ama?”



    Marshall akashindwa kujizuia kutabasamu.



    “Jack, niko serious!”



    “Sawa sawa, mimi nimekuelewa. Endelea kuwa serious na kazi yako, na mimi niko serious na kazi yangu. Kwani kuna shida?”



    “Najua ni wewe, nirekebishie basi ndugu yangu?”



    Jack hakujali, akaendelea na kazi yake. Marshall akambembeleza mpaka alipoona anyanyuka na kumfuata akimlazimisha ampatie tarakilishi yake atumie.



    Wakiwa wanazozana na kuvutana, Danielle akaingia.



    “Habari njeeeema!” mwanamke huyo alipaza sauti akiwa amenyoosha mikono yake juu. Mkono wake wa kuume ulikuwa umebebelea bahasha rangi ya kaki.



    Akiwa na furaha, akaiweka bahasha mezani, upesi Marshall akawahi kuifungua bahasha hiyo, ndani akakuta nakala za vibali.



    “Kila kitu kipo tayari sasa!” alisema Danielle. “Kuanzia kesho tutaanza kazi!”



    Marshall aliendelea kupekua kwa macho yake nakala moja baada ya nyingine. Kulikuwamo na nyaraka nne.



    “Hadi na ya gazeti?” akauliza Marshall akitazama nyaraka. Alitabasamu kwa ukubwa kabisa kisha akampongeza Danielle kwa kazi aliyofanya.



    “Lakini imekuwa ni upesi sana! Sikujua kama hili swala la gazeti lingechukua muda mfupi,” alisema Marshall.



    Danielle akatabasamu.



    “Hiyo haili muda. Haina vigezo vingi kama kibali cha kufungua taasisi ya kipelelezi. Vilevile ghushi ambazo ametengeneza Jack zimesaidia sana!”



    Baada ya kufurahia mafanikio hayo, wakaanza kujadili kuhusu matukio yaliyotokea siku hiyo. Moja ya jambo kubwa kabisa ambalo walikubaliana ni juu ya usalama wa bibie Marietta.



    Kama Willy ameweza kuuawa kwasababu ya kuficha maneno, Marietta atapona?



    Basi usiku mzima wakajadili kuhusiana na jambo hilo, na kwa kushirikiana wakaandaa habari ndefu na ya kina ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kabisa kwa ajili ya gazeti lao la kesho.



    Gazeti lao hilo wakalipa jina la MWAMBA.



    Kumaanisha mwamba waliokataa waashi, umegeuka kuwa …





    **





    Asubuhi ya saa tatu …





    “Haya hapa majibu, mkuu,” alisema afisa akiwa anamkabidhi inspekta James bahasha. Yalikuwa ni majibu ya vinasaba ambavyo vimepatikana kwenye mabaki ya damu yaliyokusanywa kwenye eneo la tukio na wataalamu - forensic experts.



    Alipotazama zaidi ndani ya bahasha akapata kuona picha za wanaume wawili.



    Wanaume ambao ni watuhumiwa wa tukio la kuwavamia maafisa na hata kusababisha kifo.





    **





    *SEHEMU YA 10*





    Baada ya kupata picha hizo, inspekta akafanya namna zikuzwe na kutandazwa mitaani kwa ajili ya msako wa watu hao wawili. Lakini katika namna ya ajabu kidogo, ilibainika kuwa watu hao ni maafisa wa USSS! - shirika linalohusika na ulinzi wa Raisi, makamu na watu wengine wakubwa na familia zao.



    Kwenye majira ya mchana, bwana James akaenda hospitali kuonana na Harold apate kumjulia hali. Alipofika huko akapata kuongea machache na mwanaume huyo kabla ya simu yake kuita mfukoni.



    Alipotazama, akaona ni Marietta!



    Basi akasonga kidogo kando apate kuongea.



    “Inspekta, naweza nikaonana na wewe?” sauti ya Marietta ilisema. Ilikuwa inatikisika ikiakisi woga. Kabla inspekta hajatia neno, Marietta akaongeza,



    “Naogopa sana. Nahisi sipo salama!”



    Inspekta akamuuliza,



    “Upo wapi muda huu?”



    “Kwangu!” Marietta akajibu.



    “Unaweza fika kituoni?”



    “Sawa.”



    Inspekta alipokata simu, akafanya namna kurudi kituoni apate kuonana na Marietta. Aliagana na Harold akimuahidi kuja tena kesho kumjulia hali.



    Basi baada ya muda mfupi akawa ameshawasili kituoni, na isichukue muda, Marietta akafika pia.



    “Nipo hatarini inspekta!” alisema Marietta kwa hofu. Uso wake ulikuwa umejikunja, mikono yake ameifumbata.



    Alifungua pochi yake akatoa gazeti na kuliweka mezani. Inspekta aliponyanyua gazeti hilo na kulitazama, akaona picha ya Marietta na habari iliyokuwa inasomeka juu,



    “MLENGWA ANAYEFUATA!”



    Alisoma jina la gazeti hilo, akaona ni MWAMBA. Basi akajipa muda kidogo kupitia gazeti hilo na habari yake.



    Akasoma namna ambavyo mwandishi alivyohariri kutabiri kuwa Marietta ndiye mtu anayefuata kuuawa sababu zikiwa yeye kuwa karibu na polisi lakini pia kuandamwa na mambo kadhaa yanayotishia usalama wake hapa karibuni.



    Inspekta alipomaliza kusoma habari hiyo, akaliweka gazeti hilo pembeni na kumtazama Marietta,



    “Una kitu cha kuniambia, madam?” akauliza.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Marietta alikuwa akitetemeka, anatazama chini. Macho yake yalikuwa mekundu akiwa anaminya lips.



    “Kwanini unajihisi upo hatarini? Ni muda wa kuongea madam, siwezi kukusaidia kama umefunga kinywa.”



    Basi baada ya Marietta kufikiria kidogo, akasema amekuwa akipokea jumbe za vitisho na anahisi kuna mtu anamfuatilia.



    “Unahisi mtu huyo ni yule ambaye alikunywesha hotelini?” inspekta akauliza.



    “Hapana, lakini kuna mahusiano naye,” Marietta akajibu na sasa kwa wazi akafunguka kwamba, anahofia taarifa alizompatia mtu yule hotelini ndizo ambazo zinamuweka kwenye hatari ya kupoteza maisha.



    “Habari gani hizo unadhani ulimpa mtu huyo kiasi cha kukuhatarisha?” akauliza inspekta. Alikuwa anamtazama Marietta machoni ingali mwanamke huyo akitazama chini.



    “Inspekta, sijui wapi pa kuanzia. Ni mlolongo mrefu sana.”



    “Usijali, nina muda wa kutosha.”



    Basi Marietta kwa woga, akaelezea yale yote anayoyafahamu. Akaelezea tangu alivyokuwa anamjua bwana Ian na namna gani ambavyo alikuwa na mahusiano naye kwa siri.



    Alieleza kila kitu, kila kitu. Sasa inspekta akapata picha kamili juu ya kinachoendelea. Kumbe bwana Willy yupo nyuma ya bwana Ian, na mabwana hao pamoja na jeshi lao ni washukiwa kuhusu kupotea kwa Raisi.



    Sasa kwanini wanataka kumuua Marshall? Inspekta akajiuliza.



    Alipofikiri kwa muda akakubaliana na akili yake kwamba huenda Marshall ana taarifa ambayo mabwana hawa hawataki ivuje.



    Lakini pia kama haitoshi, Marshall ndiye yule aliyemnywesha Marietta kisha akatokomea na habari ambazo ndizo zimechapishwa kwenye gazeti/



    Na kuhusu yale mabaki ya damu yaliyokutwa kwenye nyumba ya Jack Pyong, yalikuwa ni ya afisa wa usalama ambaye anahusika pia na genge lan. Walikuwa kwenye mapambano haya kwa muda.



    Na wale watu wote ambao Marshall anadaiwa kuuawa, watakuwa ni washirika wa bwana Ian pia vilevile!



    Alishangazwa sana na namna ambavyo habari hiyo ilivyozunguka. Kwa namna moja ama nyingine aliikuta akipata hamu sana ya kuonana na Marshall. Pengine ulimwengu sivyo vile anavyouona.



    Lakini atampatia wapi?



    Alitazama gazeti lile la MWAMBA akajikuta akipata wazo.



    “Madam, ina maana unataka kuniambia haujui kabisa mahali ambapo mumeo atakuwapo?” inspekta akamuuliza Marietta.



    “Sijui kabisa!” Marietta akaapa. “Laiti ningelikuwa najua, basi ningeshafanya jambo. Najutia sana kwa nilichokifanya kwakweli. Najiona mkosefu kabisa!”



    “Na vipi kuhusu Ian?”



    “Sijui kuhusu yeye, ila naamini atakuwa anajua. Naomba unisaidie inspekta nimwone mume wangu. Nataka nimwombe radhi kabla sijafa ama kufungwa kama ikitokea.”



    Marietta akaanza kudondosha machozi.



    “Tunawezaje kumpata Ian?” inspekta akauliza.



    “Si rahisi kumpata,” Marietta akajibu, “hana makazi maalum, anapohitaji kuonana nami huwa anakuja ofisini kwangu ama nyumbani.”



    “Vipi kuhusu mawasiliano yake?”



    “Ana namba kadhaa na barua pepe moja ninayoifahamu. Labda inaweza kusaidia.”



    Inspekta akachukua namba hizo na kuzinakili kwenye kijitabu chake.



    “Inspekta,” Marietta akaita. Alimtazama inspekta machoni na kumwambia, “kuwa makini sana, hata humu ndani kuna watu wa Ian.”



    Inspekta akamtazama Marietta kwa umakini.



    “Kifo cha Willy ni ishara tosha kuwa humu kuna maajenti wasaliti,” alimalizia Marietta.



    Hilo jambo likazama kwenye kichwa cha inspekta.





    **



    Jioni ya saa kumi na moja …





    “Changamka, hatuna muda wa kukaa hapa!” alisema jamaa mmoja aliyevalia koti la ngozi. Mkono wa kuume alikuwa amebebelea bunduki ndogo na wa kushoto kuna begi dogo.



    Alikuwa amesimama akimtazama mwenzake ambaye alikuwa anakusanyakusanya vitu kuvitia kwenye begi.



    Mwenzake huyo alikuwa amevalia sweta, suruali ya kadeti na viatu vyeusi imara vya ngozi. Walikuwa wapo kwenye haraka sana.



    Upesi walifungua mlango na kutoka ndani, wakaelekea kwenye gari na kujipaki kisha wakatimka.



    Mabwana hawa walikuwa ndiyo wale waliokuwa wakitafutwa baada ya picha zao kutandazwa mitaani kama wahusika wa mauaji ya bwana Gerrard na kujeruhiwa kwa bwana Harold.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Walinyooka na gari lao moja kwa moja mpaka kwenye makazi fulani tulivu. Humo waliketi sebuleni na baada ya muda mfupi wakaonana na bwana Ian.



    Walipoongea kidogo, Ian akatoa ishara ya kichwa, wanaume hao wakauawa kwa kumiminiwa risasi kisha wakawekwa kwenye mfuko na kuwekwa ndani ya gari kwa ajili ya kwenda kutupwa.



    Lakini kulikuwa na jambo …







    Ingali wanaume hao wawili wanaenda kutupwa, kuna gari lilikuwa linawafuata kwa nyuma, tena kwa utaratibu na tahadhari.



    Gari hilo lililokuwa linawafuata si kwamba lilianzia hapa, hapana, lilikuwapo tangu mabwana hawa wawili wanatoka zao kwenye yale makazi.



    Basi lile gari lililobebelea maiti likaenda mpaka baharini na huko wakashuka watu wawili na kutupa miili hiyo. Pasipo kutambua wakapigwa picha za mnato ambazo ziliwavuta vema.



    Wakarudi zao kwenye gari na kuhepa.



    Bado wasiwe wanajua kama wanafuatwa.



    Walilivuka gari lile lililokuwa linawafuatilia, wakaenda zao na safari yao. Kwa ushahidi zaidi, picha zingine zikapigwa mbele na nyuma ya gari hilo kukamata namba za usajili.



    “Hizo namba zingine nimekutumia, umeziona?” alisema mwanaume kwenye simu. Alikuwa ni bwana Marshall akiwa amevalia glovu nyeusi mkononi na macho yake ameyafunika na miwani meusi ya jua.



    “Ndio, nimezipata,” sauti ikamjibu kwenye simu.



    “Basi zifanyie kazi na unipe majibu upesi!” akasema Marshall na kisha akakata simu.



    Akawasha gari na kuhepa.



    **



    “Kila kitu kipo hapa,” alisema Marshall akiweka kamera mezani. Jack akaikwapua kamera na kutazama picha zilizomo. Kulikuwa na picha nyingi sana.



    “Vema!” akabwatuka, “hizi tutazitumia kwenye gazeti.”



    “Hapana, si zote,” Marshall akampa angalizo. “Kuna ambazo tutazitumia na kuna ambazo hatutazitumia mpaka pale tutakapokamilisha kazi yetu kwanza.”



    “Picha zipi hizo?” akauliza Jack. Marshall akampokonya kamera na kumwonyesha zile picha za jengo ambapo bwana Ian anapatikana. “Hili eneo linatakiwa kuwa siri mpaka pale tutakapompata ama kuwa na uhakika wa kumpata Ian.”



    Basi Jack akaziweka picha zote kwenye tarakilishi yake, alafu akamtumia Miss Danielle picha kadhaa kwa kutumia mtandao akiwa yu kwenye faragha kubwa.



    Danielle alikuwa kule kwenye ofisi ipatikanayo jijini.



    Punde aliona picha hizo na maelezo kadhaa. Akafurahishwa sana.



    Akiwa anazitengenezea picha hizo maelezo, mara mtumishi wake aliingia na kumwambia ana ugeni. Kabla hajasema jambo akarusha macho yake kwenye tarakilishi kutazama mrejesho wa kamera alizozifunga.



    Alikuwa anataka kumjua mgeni huyo ni nani.



    Basi kwa kutazama, akamwona bwana James Peak. Bwana huyo akiwa amevalia suti alikuwa amekunja miguu yake nne akingoja.



    “Anataka nini?” Danielle akajiuliza. Alifikiri kidogo kish akamtaka mtumishi wake amruhusu bwana huyo aingie ndani.



    Alipoingia, akaketi na kusalimiana na miss Danielle. Mkononi mwake alikuwa amebebelea gazeti. Hapo Danielle akajua bwana huyo alikuwa amekuja kwasababu gani.



    Inspekta aliweka gazeti mezani kisha akamtazama Danielle.



    “Nadhani una kitu cha kuniambia kuhusu gazeti hili,” akasema bwana huyo, sasa akiwa anamtazama Danielle kwa macho ya mkazo.



    “Inspekta, nilidhani nimemalizana na wewe,” akasema Danielle. Akapandisha nyusi moja na kupindisha shingo yake akimtazama inspekta, “Ile faini haikutosha?”



    Bwana James akamtazama mwanamke huyo kwa sekunde kadhaa kabla hajashusha pumzi na kutia neno, “Miss Danielle, najua una mahusiano na Marshall. Najua kabisa kuwa mnawasiliana na huenda mnafanya vitu pamoja. Na--”



    “Kwanini usinikamate?” akakejeli Danielle.



    “Sikia, Danielle, mimi sipo hapa kukuhukumu ama kukutuhumu. Nipo hapa kutazamia kama kuna uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja kwasababu ya taifa letu kwa ujumla. Waweza kufikiria kuhusu hilo?” alisema bwana James.



    “Inspekta,” akaita Danielle. “Mimi nipo hapa kila uchwao. Nipo radhi kutoa msaada wowote ule kwa ajili ya taifa langu. Hilo halina shida.”



    “Danielle, kwenye gazeti hili imeonyesha kuwa Marietta yupo kwenye hatari, na jambo hili limekuwa kweli. Kama inawezekana naomba niwe napata taarifa hizi, zitanisaidia sana.”



    “Inspekta, nadhani nimeshakuambia hapo kabla. Sijui lolote unalozungumza.”



    Basi inspekta baada ya kuona jitihada zake hazizai matunda, akanyakua gazeti na kusimama aende.



    “Utakapobadilisha mawazo, karibu sana!” alisema vivyo kisha akaenda zake. Danielle akamsindikiza kwa macho mpaka alipotoka.



    Akahamishia macho yake kwenye runnga ya kamera, akamtazama bwana huyo mpaka anaondoka kuacha jengo.





    **



    Usiku wa saa tatu …



    “Ni mapema sana,” alisema Marshall akitazama mbele. Walikuwa wawili ndani ya gari, yeye pamoja na Danielle.



    Watu hawa walikuwa wamevalia nguo nyeusi za kubana, kila mmoja amevalia kofia ya soksi kichwani. Mahali hapa ambapo wameweka kambi palikuwa pametulia sana.



    Ni kiza.



    “Hatuwezi jua yupo upande gani,” Marshall aliendelea kusema. “Ni vema tukajipa muda zaidi tukajua mienendo yake.”



    Baada ya Marshall kusema vivyo akamtazama Danielle na kumuuliza, “Au unasemaje?”



    “Nakuunga mkono,” akasema Danielle akitikisa kichwa. “Japo ana nia safi, hatujajua mdomo wake unaweza kupanuka kiasi gani.”



    Basi baada ya mazungumzo hayo mafupi kumwongelea inspekta James, Marshall akafanya namna kuwasiliana na Jack Pyong. Mwanaume huyo wa kichina alikuwa nyumbani mbele ya tarakilishi zake nne ambazo ameziunga na mtandao lakini pia akiwa amedukua mfumo wa satelaiti.



    Pembeni yake kulikuwa na kopo la bluu lenye kubebelea soda.



    “Kuna kitu huko?” akauliza Marshall.



    “Hapana,” akajibu Jack. “Bado ni kimya.”



    Ukapita kama muda wa nusu saa. Kimya kwa Jack na pia kimya kwa wakina Marshall.



    Ukimya huo usidumu zaidi, mara Marshall akaona gari jeupe aina ya van ikiwa inapita barabarani kwa mwendo wa stara. Alitilia mashaka gari hiyo. Alimshtua Danielle wote wakaitupia macho.



    “Nadhani wameshawasili!” akasema Marshall.



    “Jack ameshakupa taarifa?” Danielle akauliza. Alikuwa amesinzia kidogo wakati wakingoja.



    “Hapana, watakuwa wametumia usafiri mwingine,” akasema Marshall akiendelea kutazama van ikienda.



    Kama yalivyokuwa makisio yake, van ile ikaelekea mashariki mwao. Hapo wakashusha kofia zao na kuwa barakoa kisha Marshall akatia moto chombo na kusonga.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    **



    “Hakikisha haufanyi makosa!” alisema mwanaume ndani ya van akimwambia mwenziwe. Walikuwa watu watatu kwa idadi.



    “Najua cha kufanya,” akasema mwanaume mwingine karibu na mlango. Alikuwa amebebelea bunduki mkononi. Bunduki ambayo tayari ameshaikoki kwa ajili ya tukio.



    “Na nyie fanyeni kazi yenu,” akasema bwana huyo alafu akajiveka kinyago chenye uso wa mbuzi na ndevu zake kisha akajongea kuufuata ukuta na kuukwea.



    Tih! Akashukia kwa ndani.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog