Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KIAPO CHA JASUSI - 2

 





    Simulizi : Kiapo Cha Jasusi

    Sehemu Ya Pili (2)







    "Kwa nini mnaitaji simu yangu?



    "Usituulize maswali.Tuonyeshe haraka iliko simu yako! akafoka yule jamaa



    "Simu yangu imepotea majini" akasema Dastan.Yule jamaa akavua kofia aliyotumia kujifunika usoni akamsogelea



    "Ndugu ninakuonya kwa mara ya mwisho usithubutu kucheza na sisis.Simu yako iko wapi?



    "Simu yangu imepotelea majini.Nilivamiwa na watu nikiwa katika uvuv..........." kabla hajamaliza kuzungumza akanaswa kibao kikali sana akaanguka chini na damu ikaanza kumtoka mdomoni.Yule jamaa akamfuata pale chini na kumuwekea bastora kichwani



    "Where is your phone!!Nitakuua kama usiponionyesha simu yako ilipo! akasema yule jamaa akiwa ameigandamiza bastora kichwani kwa Dastan



    "Sina simu !! akasema Dastan na yule jamaa akampiga pigo kali kwa kutumia kitako cha bastora na ukaonekana mchirizi wa damu kichwani kwa Dastan.Mmoja wa wale watu waliokuwamo mle ndani akavua kofia yake aliyotumia kujificha uso na kumfuata yule jamaa aliyekuwa anamuhoji Dastan



    "Chris unataka kufanya nini?Unadhani ukimuua huyu tutapaje taarifa muhimu?Tunamuhitaji sana akiwa hai!!



    "Joyce !! Dastan aliyekuwa amelala sakafuni akivuja damu akastuka baada ya kuisikia sauti ya Joyce katibu wake muhtasi.Akajitahidi kuinua kichwa na kufumbua macho ili amuone vizuri



    "Joyce ?!! akasema Dastan



    "oh my Gosh !! akasema Joyce kwa mstuko



    "Joy...." akasema Dastan na Joyce akamfuata na kumtanbdika teke la mbavuni



    "Shut up !! akasema na kumuinamia



    "Dastan nataka nikusaidie hivyo naomba unieleze ukweli.Simu yako iko wapi?



    "Joyce kwa nini unafanya hivi?Who are you?akauliza Dastan



    "Stop asking question!! Nijibu haraka sana!! akasema Joyce



    "Sikujua kama wewe ni shetani namna hii.Nakuhakikishia ukiniacha hai lazima nikuue!! akasema Dastan.



    "Ulipewa ujumbe na Dr Alfredo kitwe.Nani uliyempatia ujumbe ule? Nijibu tafadhali" akasema Joyce



    "Shetani wewe !! akasema Dastan na Joyce akamtandika teke la tumbo



    "Aaaagghhh!!! Dastan akagugumia kwa maumivu makali.



    "Dastan tafadhali usilifanye suala hili kuwa gumu.Nijibu ili tukuache hur...." Joyce hakumaliza sentensi yake ikasikika milio ya risasi mfululizo na wale jamaa wote wakaanguka chini.









    "Dastan ! ikaita sauti ya Dr William huku akiuondoa mwili wa Joyce ulioamuangukia Dastan.Haraka haraka akafunguliwa pingu



    “Are you ok Dastan? Akauliza Dr William



    “Yes I’m ok” akajibu Dastan



    "Pole sana Dastan.Wamekuumiza sana hawa jamaa" akasema Dr William akianza kumganga Dastan jeraha la kichwani.Mle ndani kulikuwa na askari magereza wapatao saba wakiwa na bunduki.



    "Ahsanteni sana kwa kuniokoa.Kama msingewahi hawa jamaa wangeniua" akasema Dastan



    "Ni akina nani hawa watu?Wana mahusiano na wale jamaa uliowaua kule baharini?Joyce naye ana mahusiano gani na hawa jamaa? akauliza Dr William



    "Nimeshangaa mno kumuona Joyce akiwa na hawa jamaa.Sikutegemea kabisa.Inabidi ufanyike uchunguzi wa kina kuwafahamu hawa jamaa ni akina nani na nini lengo lao?Wamewezaje kuingia hapa gerezani?akasema Dastan na kuinuka akatoa maelekezo kwa askari halafu akaomba simu ya Dr william akapiga makao makuu akawaeleza kilichotokea na kuwataka watume askari haraka kufanya uchunguzi wa tukio lile.



    "Ulifahamuje kama niko mikononi mwa wale jamaa? akauliza Dastan wakati akiwa katika hospitali ya gereza akipatiwa matibabu Zaidi ya majeraha aliyoyapata

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Nilitaarifiwa kuhusu kuwepo kwa mtu aliyepoteza maisha nikaambiwa kwamba wewe ndiye uliyemleta.Nikataka nipate ufafanuzi zaidi nikapiga simu yako haikupokelewa nikaamua kukufuata nyumbani kwako nilipofika nikachungulia na kuona wale jamaa wakiwa wamekuweka chini ndipo nikaenda kuwachukua askari ambao walifika na kuwaua wale jamaa wote.Nimeogopa sana Dastan.Nini hasa kinachoendelea?walikuwa wanataka nini wale jamaa? akauliza Dr william



    "Dr William naomba iwe siri yako lakini hiki kilichotokea jioni ya leo kina mahusiano na mzee Alfredo"



    "Dr Alfredo anahusika?akauliza Dr William



    "Mzee Dr Alfredo alinipa ujumbe niupeleke sehemu fulani na nilifanikiwa kuufikisha ujumbe huo kwa muhusika.Nikiwa baharini nikivua nikasikia muungurumo wa boti nikachukua kiona mbali na kutazama nikaona boti inaelekea upande ule niliokuwepo kwa kasi kubwa na nilipowachunguza vyema nikaona wana silaha nikazama majini na walipofika katika boti yangu wakaanza kupekua ndipo nilipoibuka na kuwashambulia nikawaua.Niliporejea hapa nikaenda nyumbani kwangu na ndipo nilipovamiwa na wale jamaa.Kikubwa walichokuwa wanakitaka ni simu yangu ili wajue ujumbe ule alionipa Dr Alfredo nilimpatia nani?Siku zote nimemuamini sana Joyce kumbe ni nyoka mwenye sumu kali.Alikuwa ananichunguza ninachokifanya na ndiye aliyegundua kwamba nimepewa ujumbe na Dr Alfredo kitwe."



    "Ujumbe huo ulisemaje na uliupeleka kwa nani?Kwa nini wanamfuatilia mzee Alfredo hadi gerezani? akauliza Dr William.Dastan akafikiri kwa muda na kusema



    "Dr William,kuna jambo kubwa linaloendelea hapa ambalo hatulifahamu kuhusiana na huyu mzee.Hebu unganisha picha hizi.Amefungwa maisha na amezuiliwa kuonana na mtu yeyote na kwa muda wa miaka kumi amekuwa akiishi katika upweke mkubwa sana.Hivi sasa mzee huyu anaumwa na ni haki ya kila mfungwa kupata matibabu stahiki lakini wamegoma kabisa kutoa kibali cha kwenda kumtibu nje ya gereza.Kwa nini hawataki mzee huyu aonane na mtu yeyote? Baada ya tukio hili la leo ninaanza kuamini mzee huyu yuko katika hatari kubwa.Naanza kuamini wamezuia kibali kisitolewe akatibiwe nje ya gereza ili afariki bila kuonana na na mtu yeyote.Nina wasiwasi baada ya tukio la leo wanaweza hata wakamuua ili kumzuia asizungumze chochote na mtu yeyote"



    "Unachokisema Dastan ni kitu cha kweli .Inaonekana mzee huyu ana kitu ambacho hawa wakubwa hawataki kijulikane ndiyo maana wanamfanyia hivi.Kuhusu kumuua hata mimi nakubaliana nawe wanaweza wakamuua muda wowote.Unashauri nini Dastan?



    "We have to help him.Lakini......" akasema Dastan na kunyamza baada ya kukumbuka kitu.



    "Joyce amekuwa katibu wangu muhtasi toka nilipofika hapa gerezani.Nimemuamini sana na hata siku moja sikuwahi kuwa na wasi wasi naye hata kidogo.Sikuwahi kufikiri kama anaweza akashiriki katika tukio kama hili la leo.Ninaamini yeye ndiye aliyegundua kuhusu mimi kupewa karatasi na mzee Alfredo na akanisikia nikizungumza na mtu simuni japo hakufahamu ni nani niliyekuwa nazungumza naye.Je amefahamuje kama nilipewa ujumbe na mzee Alfredo? Je amewekwa hapa kunichunguza?Kama ndiyo nani kamtuma?Watu wale aliokuwa nao ni akina nani?akauliza Dastan



    "Dastan maswali hayo yangeweza kupatiwa majibu sahihi na mwenyewe Joyce lakini amekwisha kufa na nina wasiwasi inaweza kuwa vigumu kupata majibu"akasema Dr William



    "Twende nyumbani kwa Joyce kabla wapelelezi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi hawajawasili" akasema Dastan wakatoka pale hospitali na kuelekea nyumbani kwa Dastan.Bado askari magereza walikuwa wanaendelea kulinda nyumba ile wakisubiri kikosi cha wapelelezi wafike kutoka Dar es salaam.Dastan akamuita pembeni Stanslaus mmoja wa wakuu wa ulinzi pale gerezani



    "Mmewapekua hawa jamaa kuna kitu chochote mmekipata toka kwao?



    "Tumewapekua na tumekuta vitu vichache kama fedha,simu na bangi"



    "Vipi kuhusu Joyce mmempekua pia?



    "Ndiyo tumempekua na tumemkuta na simu pekee"



    "Good.Naiomba hiyo simu ya Joyce" akasema Dastan na Stanslaus akampatia simu ile ya Joyce kisha Dastan akamtaka waongozane hadi nyumbani kwa Joyce akajaribu kuufungua mlango lakini ulikuwa umefungwa.Joyce alikuwa akiishi peke yake.Dastan akawaomba wamsubiri akaenda nyumbani kwake na baada ya muda akarejea akiwa na funguo tatu akajaribisha wa kwanza ukagoma ,akachomeka wa pili akaunyonga na kitasa kikafunguka wakaingia ndani,wakawasha taa na kisha Dastan akaanza kupekua.



    "Mkuu kitu gani unakitafuta humu tukusaidie? akauliza Stanslaus



    "I'm looking for something" akasema Dastan na kuelekea katika chumba cha kulala cha Joyce.Mlango haukuwa umefungwa akaingia ndani akawasha taa na kuikuta kompyuta mpakato iko mezani.Wakati akiendelea kupekua pekua Stanslaus akamfuata chumbani na kumjulisha kuwa wapelelezi kutoka makao makuu ya polisi Dar es salaam wamewasili na wanahitaji kumuona.Akampatia Dr William ile kompyuta na simu ya Joyce.



    "Mtu yeyote asijue kama vitu hivi ninavyo mimi.Sawa? akasema Dastan na Dr William akatoka akaelekea nyumbani kwake kwenda kuficha vile vifaa.Dastan akaenda kukutana na timu ile ya wapelelezi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi.Aliwaeleza kila kitu kilichotokea toka alipovamiwa na watu baharini alikoenda kuvua na alivyovamiwa pale nyumbani lakini hakuwaeleza kuhusu ujumbe ule aliopewa na Dr Alfredo kitwe



    "Pole sana Dastan.Unahisi hawa jamaa kwa nini walikuwa wanaitaka simu yako?akauliza Kamishna Daniel Manguzi aliyeongoza timu ile ya wapelelezi



    "Sifahamu Kamishna kwa nini walihitaji simu yangu.Kwa bahati mbaya simu yenyewe iliangukia majini wakati nikipambana na wale jamaa walionifuata baharini"



    "Vipi kuhusu huyu katibu wako muhtasi bi Joyce unaweza ukamuelezeaje?



    "Nimefanya naye kazi kwa miaka kadhaa na sikuwahi kuona tatizo lolote kwake.Ni mchapa kazi mzuri sana na muaminifu.Nimeshangaa leo kumuona akiwa na hawa jamaa.Ni vigumu kuamini"



    "Hukuwahi kuhisi kitu cha tofauti kutoka kwake?



    "Hapana.Joyce ni mtu ambaye anapendwa na kila mtu hapa kutokana na uhodari na uchapakazi wake.Ni mcheshi na anazungumza na kila mtu"

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Tunaweza kwenda nyumbani kwake kuchunguza?akasema kamishna kisha wakaongozana hadi nyumbani kwa Joyce na upekuzi ukaanza



    "Joyce hakuwa na simu? akauliza Kamishna Daniel



    "Alipopekuliwa hajakutwa na simu yoyote"akasema Dastan



    "Hii inashangaza….." akasema Kamishna Daniel akafikiri kidogo na kuuliza



    "Hana mume au mtu yeyote anayeishi naye hapa?



    "Hapana.Joyce anaishi peke yake ila siku za mwisho wa wiki huondoka na kurudi jumatatu asubuhi.Huaga kuwa anakwenda Dar es salaam kupumzika"



    "Hutumia usafiri gani kuja na kuondoka hapa gerezani siku za mwisho wa wiki?



    "Hutumia boti binafsi ambayo huja kumchukua na kisha kumrudisha jumatatu asubuhi kwa ajili ya kazi"



    "Kuna mtu yeyote anayefahamu makazi yake yalipo jijini Dar es salaam?



    "Mimi sifahamu,nitawauliza wenzangu kama kuna yeyote anayefahamu makazi ya Joyce"



    "Sawa.Itabidi tumfanyie uchunguzi wa kina huyu Joyce kwani anaonekana ndiye aliyewasaidia wale jamaa kuweza kuingia hapa na kufanya yale waliyoyafanya.Gereza hili ni gereza lenye ulinzi mkali mno kutokana na aina ya watu wanaofungwa hapa na ili watu wale waweze kuingia lazima wamepata msaada wa mtu kutoka ndani.Tutaondoka na miili ya marehemu na kesho wapelelezi wataendelea kulichunguza jambo hili.Jitahidi hadi kufika asubuhi uwe umefanikiwa kujua mahala anakoishi Joyce itatusaidia sana katika uchunguzi wetu"



    "Nitajitahidi Kamishna"



    "Ahsante kwa ushirikiano wako na kwa mara nyingine ninakupa pole sana kwa yote yaliyotokea.Nakuhakikishia kwamba wale wote walioshiriki katika jambo hili watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria."



    "Ahsante sana Kamishna" akasema Dastan na kuagana na Kamishna Daniel ambaye alienda kuungana na vijana wake wakaipakia miili ya wale marehemu na kuondoka.Dastan akarejea nyumbani kwake ambako kulikuwa kumetapakaa damu.



    "Ama kweli dunia ina maajabu makubwa.Sikutegemea kabisa kama Joyce angeweza kuwa hivi.Sikuwahi kuhisi chochote kibaya kuhusu yeye na nilimuamini sana pengine kupita watu wote hapa gerezani lakini kumbe mwenzangu alikuwa na mambo yakeya siri.Inawezekana alikuwa ananichunguza kwa muda mrefu mambo yangu lakini kwa bahati nzuri licha ya kumuamini sikuwahi kumshirikisha katika jambo langu lolote nje ya shughuli za kiofisi.Nina hakika hafamu kitu chochote kuhusu mimi.Laiti kama ningeng'amua mapema kwamba yuko hivi ningekwisha muondoa kitambo sana lakini anajua sana kujificha.Naamini Joyce ndiye aliyewekwa hapa gerezani kumchunguza Dr Alfredo kwani aliniuliza mahala nilikopeleka ujumbe ule niliopewa na Dr Alfredo.Kwa nini wanamfuatilia kiasi hiki hata huku gerezani ?Kwa nini hawataki aonane na mtu yeyote?Kuna kitu wanaogopa kitajulikana?Sasa naamini chanzo cha haya yote yaliyotokea leo ni Dr Alfredo kitwe.Kuna kitu gani hapa kinachoendelea kuhusiana na huyu mzee?I have to find out " akawaza Dastan na kutoka akaenda katika maua mahala alikoificha ile pochi yake iliyokuwa na simu akaichukua halafu akaenda sehemu fulani kulikotulia ambako hakukuwa na mtu akampigia simu Padre Thadei



    "Mr Dastan.Habari za usiku huu?akasema Padre Thade baada ya kupokea simu



    "Habari si nzuri padre. Kuna tatizo limetokea usiku huu hapa gerezani"



    "Tatizo gani Mr Dastan?



    "Kuna watu wamenifuata wakiwa wamejihami kwa silaha na walihitaji kujua ujumbe niliopewa na mzee Alberto nilimpa nani? Nimepambana nao na kwa bahati nikafanikiwa kuwadhibiti" akasema Dastan na Padre Thadei akasikika akishusha pumzi



    "Pole sana Dastan kwa haya yaliyokutokea.Wamefahamuje kama ulipewa ujumbe na Dr Alfredo kitwe?akauliza padre Thadei



    "Sielewi wamefahamu vipi lakini kuna mtu ambaye ninahisi amewekwa hapa kumchunguza Dr Alfredo na alifahamu kuhusu mimi kupewa ujumbe ule na mzee Alfredo.Huyu ni katibu wangu muhtsasi ambaye naye pia ameuawa.Huyu nilikuwa namuamini sana na alkikuwa anaingia ofisini kwangu muda wowote hata wakati sipo.Nadhani alisikia mazungumzo yangu nawe lakini hana uhakika nilikuwa nazungumza na nani na ndiyo maana walikuwa wanahitaji kuipata simu yangu ili wachunguze ni nani niliyekuwa nazungumza naye ambaye nilimpa ujumbe ule wa Dr Alfredo kitwe.Padre Thade ,ninaomba nikuweke wazi kwamba kwa hili lililotokea leo,linanifanya niamini kwamba mzee Dr Alfredo yuko katika hatari kubwa.Watu wanamfuatilia kwa karibu sana na hawataki aonane na mtu yeyote.Unaonekana una ukaribu na mzee huyu je kuna chochote unachofahamu kwa nini watu hawa hawataki Dr Alfredo aonane na mtu yeyote?Kitu gani wanakiogopa?



    " Dastan hata mimi sielewi chochote kuhusiana na kinachoendelea kwa mzee huyu.Kinachotakiwa kwa sasa ni kutafuta watu ambao huyo katibu wako muhtasi anashirikiana nao.Unatakiwa kufahamu nani waliomtuma hivyo jitahidi uweze kuipata simu yake au kifaa kingine chochote anachotumia kuwasiliana"akasema padre Thadei



    "Tayari nimefanikiwa kuipata simu yake pamoja na kompyuta ndogo"



    "Good.Sasa nitakuo................" Kabla padre Thadei hajamaliza sentensi yake kikasikika king'ora cha kuashiria moto.Dastan akastuka akageuka na kuona moshi mwingi unatoka katika nyumba za watumishi.



    "Padre Thadei I'll call you back" akasema Dastan na kukata simu akakimbia kuelekea kule ulikokuwa unatoka moshi mkubwa.Ilikuwa ni nyumbani kwa Dr William.Tayari askari walikuwa wanaendelea na jitihada za kuuzima moto uliokuwa unawaka katika chumba cha kulala cha Dr William.Dastan akaungana na wenzake na wakafanikiwa kuuzima ule moto.Baada ya kuuzima akamfuata Dr William aliyekuwa anatetemeka kwa woga



    "Dr William are you ok?



    "I'm ok Dastan.I'm ok" akajibu



    Dastan akamshika mkono wakaenda katika ofisi ya Dr William



    "Relax Dr William.Take a deep breath" akasema Dastan



    "Nini chanzo cha moto ule Dr William?akauliza Dastan



    "Dastan kuna mambo yametokea ya ajabu ambayo sikuyategemea kabisa"



    "Kumetokea nini? Dastan akauliza



    "Nilipofika chumbani nikaiwasha ile kompyuta ya Joyce ili niangalie kilichokuwemo ndani,nikaipitia kidogo na kukuta miziki mingi nikaiweka pembeni na kwenda kuoga kisha nikarejea chumbani nikijiandaa kuja kwako mara ghafla nikasikia mlipuko.Simu na kompyuta ya Joyce vyote vikaanza kuwaka moto kwa wakati mmoja.Kwa bahati mbaya vyote vilikuwa juu ya godoro na kwa mstuko nilioupata nikakimbia nje ndipo moto uliposhika godoro na kuanza kusambaa"

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Oh my God ! someone hacked the batteries" akawaza Dastan halafu akamtaka Dr William watoke wakakimbia hadi nyumbani kwa Dr William,tayari moto ulikiwsha zimwa ,wakaingia chumbani na Dastan akaishika ile kompyuta ya Joyce iliyowaka moto akaitazama



    "Vifaa hivi vimeungua vibaya sana hata hivyo nitajitahidi nione kama nitaweza kupata chochote japo vimeungua" akawaza Dastan na kuichukua ile kompyuta na simu na kumtaka Dr William amfuate



    "Dr William naomba nikuweke wazi kwamba vifaa vile havikuwaka kwa bahati mbaya,vimelipuliwa makusudi ili tusiweze kujua kilichokuwemo ndani yake.Ipo teknolojia ya kuweza kuingia katika mfumo wa betri na kuilipua simu au kompyuta hata kama iko mbali.Hawakutaka tuchunguze na kujua kilichomo ndani.Hii inatupa picha kwamba watu anaoshirikiana nao ni watu wajuzi sana wenye kila aina ya mbinu na uwezo.Mambo kama haya hufanywa na majasusi wa hali ya juu sana"



    "My God! akasema Dr William huku sura yake ikionyesha woga mkubwa



    "Liko jambo linaloendelea hapa ambalo ni kubwa" akasema Dastan



    "Dastan kesho itanilazimu niondoke nikapumzike kwani mambo yaliyotokea leo yameniogopesha sana"



    "Hutakiwi kuogopa Dr William.I need yor help" akasema Dastan



    "My help? akauliza Dr William



    "Dr William nakuhitaji unisaidie kumuokoa mzee Dr Alfredo kitwe.Maisha yake yako hatarini.Tayari tunafahamu kutokana na ugonjwa wake hana maisha marefu lakini tusiwape nafasi hawa watu ya kutaka kumuua.Tumsaidie mzee huyu afe kifo cha staha na heshima.Anastahili heshima hii kwa kazi kubwa aliyowahi kuifanya ya kulitumikia taifa kwa miaka kumi.Kama ni makosa kila mwanadamu anakosea hivyo tusimuhukumu kwa mambo aliyoyafanya wakati wa utawala wake.I need you in this brother" akasema Dastan



    "Dastan ninakuheshimu sana na hata mimi ninamuonea huruma mzee Dr Alfredo lakini kwa watu hawa ambao wameweza hata kulipua simu wakiwa mbali siwezi kujihusisha na lolote linalohusiana na huyu mzee.Sitaki kuingia katika mapambano na hawa jamaa.Nimenusurika kifo leo hivyo kesho asubuhi na mapema nitaondoka na boti linalokwenda mjini nataka nikatulize kwanza akili yangu" akasema Dr William



    "Ninakuelewa Dr William lakini ninakuomba ndugu yangu tusimuache mzee huyu.Mimi na wewe ndio pekee tunaofahamu hatari inayomkabili huyu mzee.I need you William" akasema Dastan na Dr William akainamisha kichwa akawaza kwa muda halafu akasema



    "Unahitaji nifanye nini Dastan?Nikusaidie kitu gani?



    "Wakati ninatafuta namna ya kufanya,nataka uende ukakae na yule mzee na usiondoke hadi nitakapokuambia vile vile usiruhusu mtu yeyote asiye daktari kuingia katika chumba cha mzee Alfredo"akasema Dastan na Dr William akamtazama kwa muda halafu akasema



    "Sawa Dastan.Nitafanya hivi kwa heshima yako ila ninarudia tena kukujulisha kuwa kesho asubuhi na mapema nitaondoka kuelekea mjini.Nimepaogopa sana mahala hapa" akasema Dr William



    "Usijali Dr William" akasema Dastan na kuelekea nyumbani kwake.Akachukua simu na kumpigia padre Thadei lakini simu yake haikupatikana tena.Akajaribu tena zaidi ya mara mbili lakini simu haikuwa ikipatikana.









    OFISI ZA JARIDA BEAUTIFUL TANZANIA - DAR ES SALAAM

    Beautiful Tanzania ni jarida la kila mwezi lililojizolea umaarufu mkubwa kutokana na mkusanyiko wa habari nyingi za kuvutia zilizotokea nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mzima.Ni jarida lenye kuandikwa kwa lugha ya kiingereza na lenye kusomwa na watu wengi ndani nan je ya nchi



    Licha ya kuwa jarida pendwa Tanzania,hakuna aliyefahamu siri iliyokuwepo nyuma ya jarida hili.Jarida hili lilikuwa chini ya umiliki wa kikundi cha 100CHITAS. Wafanyakazi wa jarida hili walikuwa ni watu waliopata mafunzo makubwa ya ujasusi nje ya nchi na walitumia jarida hili kama mwavuli wa kufunika shughuli wanazozifanya kwa kujifanya ni waandishi wa habari.



    Katika chumba kidogo cha mikutano kilicho ghorofa ya tatu katika jengo ziliko ofisi za jarida hili watu kumi walikuwa katika kikao cha dharura



    "Ndugu zangu tumelazimika kukutana hapa kwa dharura kufuatia taarifa za kustusha zilizotufikia usiku huu" akasema mtu mmoja mwenye mwili uliojengeka vyema,akavua kofia na kuiweka mezani



    "Tulipata taarifa kutoka kwa mwenzetu Chita73 kutoka gereza la Markubelo ambaye alitujulisha kwamba mzee Alfredo ambaye tumekuwa tukimchunguza kwa muda mrefu amempa ujumbe fulani katika karatasi mkuu wa gereza kamishan msaidizi Dastan na kumtaka aupeleke sehemu Fulani na ujumbe huo ulisomeka hivi



    "I'm dyind.I have few days left.Meet me before I die"



    "Hatujafahamu bado ujumbe huo Dastan ameupeleka kwa nani na hivyo tulihitaji kuipata simu yake ambayo aliitumia kuupeleka ujumbe huo lakini kumetokea kitu cha kustusha sana.Tumepoteza wenzetu nane jioni ya leo ambao niliwatuma kwenda kufuatilia suala hili.Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata kutoka ndani ya jeshi la polisi ni kwamba wenzetu wanne walimfuata Dastan baharini alikokuwa anavua samaki lakini Dastan akiwa peke yake aliweza kupambana nao na kuwaua wote kwa risasi.Aliporudi nyumbani alikuta Joyce na wengine Chita40,23,na 37 wakimsubiri.Walimtia nguvuni lakini wakatokea askari magereza wenye silaha wakadhani wale ni wavamizi na kuwashambulia kwa risasi wakawaua wote .Hili ni pigo kubwa sana ambalo hatujawahi kulipata" akanyamaza na kuwatazama wenzake halafu akaendelea



    "Hii ni mara ya kwanza tunapata pigo kubwa namna hii.Hatujawahi kupoteza watu wetu wengi namna hii kwa mara moja.Kwa sasa taratibu zinaendelea ili tuweze kuipata miili hiyo ya wenzetu na tuisitiri.Ninaendelea kulifuatilia jambo hili kwa karibu sana lakini wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili kuna kazi ambayo lazima ifanyike kwa haraka sana.Tunatakiwa kufahamu nani alipewa ujumbe na Dastan? Tutafanikiwa kulifahamu hili kwa kumchunguza Dastan.Kwa sasa baada ya kilichomtokea leo haitakuwa rahisi sana kumpata hivyo tunatakiwa kutafuta namna nyingine ya kumfanya atueleze mahala alikoupeleka ujumbe ule.Njia pekee ya kuweza kupata taarifa kutoka kwake kirahisi ni kwa kuitumia familia yake.Nataka Dastan achunguzwe tumfahamu chimbuko lake.Tujue wazazi wake wako wapi na kama ana watoto wako wapi?Tukimpata mtoto wake hata mmoja tutafanikiwa kupata kile tunachokihitaji.Ingieni kila mahali,dukueni kila taarifa inayomuhusu Dastan na baada ya saa moja nataka niwe nimepata taarifa kuhusiana na huyu mtu halafu nitatoa maelekezo mengine" akasema Noah Mwamba mkurugenzi mkuu wa jarida la Beautiful Tanzania ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kikundi hatari cha 100Chitas.Wote wakatoka mle katika kile chumba cha mikutano na Noah akaelekea ofisini kwake alikuwa na mawazo mengi sana



    "Hatujawahi kupoteza watu wengi namna hii kwa wakati mmoja.Hili ni pigo kubwa mno tumelipata.Rais anaweza akahoji kulikoni watu wote hawa wakauawa kirahisi namna hii ili hali ni watu wenye mafunzo ya hali ya juu.Jambo hili linaweza kumfanya akakosa Imani nami jambo ambalo sitaki litokee”akatoa sigara akawasha na kuanza kuvuta



    "Huyu Dastan ni nani hata akaweza kupambana na watu wanne wenye mafunzo ya hali ya juu akafanikiwa kuwamaliza?Ameweza hata kumuua Sam?Sikuwahi kumtuma Sam kazi yoyote akashindwa kuifanikisha.Imeniumiza sana kwani ni mtu niliyekuwa namtegemea mno katika kazi nyingi na hakuwahi kuniangusha hata mara moja.Huyu Dastan amejipalia makaa kwani maisha yake yatakuwa magumu sana kuanzia sasa na atajuta kuzaliwa.Ngoja nisubiri kwanza taarifa za kumuhusu Dastan ili nifanye kila linalowezekana usiku huu Dastan apatikane na tufahamu ujumbe ule aliopewa na Dr Alfredo ameupeleka wapi? Tukifanikiwa kujua mahala na mtu aliyepewa ujumbe ule inaweza ikasaidia katik akutoa maelezo kwa rais”akaendelea kuwaza Noah Mwamba huku akivuta sigara na kupuliza moshi mwingi

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    BAADA YA SAA MOJA



    Noah Mwamba au Chita01 alikutana tena na watu wake aliowapa kazi ya kumchunguza Dastan baada ya saa moja kupita.



    "Nadhani lile zoezi letu limekamilika.Nataka taarifa tafadhali.Teddy Jini tuanzie kwako,niambie umepata nini kuhusu Dastan? Akauliza Noah na kuelekeza macho yake kwa mwadada Teddy ambaye wanamuita Jini kutokana na uwezo wake mkubwa wa udukuaji.Teddy na wenzake wakatazamana.Noah akahisi kitu



    "Mr Noah kuna tatizo limejitokeza” akasema Teddy na kunyamaza akamtazama Noah



    “Kuna tatizo gani Teddy? Akauliza Noah



    “Hakuna taarifa zozote za kumuhusu huyu jamaa Dastan Mwaikambile" akasema Teddy Jini



    "Unamaanisha nini Teddy?



    "Mkuu nimejaribu kutafuta taarifa za Dastan lakini sijafanikiwa kuzipata.Hakuna taarifa zake zozote seemu yoyote"akasema Teddy



    "What? Noa akashangaa



    “Hilo haliwezekani kutokea.Huyu ni mtumishi wa umma na lazima taarifa zake zote ziwepo.Huwezi kuajiriwa katika utumishi wa umma bila serikali kuwa na taarfa zako zote.Search again...."akasema Noah



    "Mkuu hata mimi pia na wenzangu tumeshangazwa sana na jambo hili na ili kujiridhisha nikarudia tena na tena kukagua lakini hakuna taarifa zozote za kumuhusu Kamishan msaidizi Dastan Mwaikambile katika taarifa za wafanyakazi wa serikali.Jina hilop halipo katika orodha ya watumishi wa umma" akasema Teddy na Noah akavuta pumzi ndefu



    "Imewezekanaje? akauliza tena na wote wakabaki kimya.Hakuna aliyekuwa na jibu.Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kuzikosa taarifa za kamishna msaidizi wa magereza Dastan Mwaikambile katika taarifa za watumishi wa umma



    "Ni mara ya kwanza Teddy unaniambia kwamba umeshindwa kuzipata taarifa za mtu.Ninajiuliza yawezekana labda Dastan anatumia jina lingine tofauti na hili tunalolifahamu la Dastan Mwaikambile?akauliza Noah



    "Hapana mkuu jina lake ni hilo hilo.Kuna sehemu nimeona katika orodha ya viongozi wa taasisi zilizo ndani ya wizara ya mambo ya ndani jina la Dastan Mwaikambile lipo na ameorodheshwa kama mkuu wa gereza la Markubelo na hii inatuthibitishia kwamba wizara ya mambo ya ndanoi inamfahamu na hadi kupewa cheo cha Kamishna lazima wanazo taarifa zake zote.Kinachoshangaza ni kwamba hakuna taarifa zozote zinazoonyesha elimu yake,sehemu alizowahi kufany akazi kabla ya kuwa mkuu wa gereza la Markubelo na vile vile ,hakuna taarifa zozote binafsi"akasema Teddy bingwa wa udukuzi



    "Hii inashangaza sana.Ninaanza kufikiria yawezekana mtu huyu akawa ni hewa" akasema Noah



    "Hapana mkuu.Dastan si hewa.Ni halisi yupo na ni mtumishi wa umma.Ninaamini kabisa lazima wizara ya mambo ya ndani wanazo taarifa za kuhusu Dastan.Haiwezekani wasiwe na taarifa za mtumishi wao tena anayesimamia gereza kubwa kama Markubelo.Lazima taarifa zake zipo mahala fulani and we have to find them.I think you have to inform president and ask for help.Yeye anaweza akawaamuru wakuu wa wizara hii ya mambo ya ndani wampelekee taarifa za Dastan" akasema Teddy.Noah akatikisa kichwa kukubaliana na wazo la Teddy akachukua simu akampigia rais



    "Noah whats going on?Nimesikia kuna mauaji yametokea katika gereza la Markubelo.Unahusika?akauliza Dr Enock rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania



    "Mheshimiwa rais ni kweli tunahusika na hicho ulichokisikia kimetokea.Nilituma vijana wangu waende kupata taarifa kutoka kwa mkuu wa gereza Dastan kuhusiana na ule ujumbe aliopewa na Dr Alfredo lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia na watu wangu wote niliowatuma wakapoteza maisha"



    "Hii imetokeaje?Wameauawa vipi? akauliza Dr Enock kwa sauti ya mshangao



    "Nilitaarifiwa kwamba Dastan alikuwa baharini akivua na watu wanne wakaamua kumfuata huko huko baharini na hatuelewi nini kilitokea huko lakini watu wangu wote waliuawa.Nina hakika waliuawa na Dastan.Aliporejea nyumbani alikutana na watu wangu wengine waliokuwa wamejificha nyumbani kwake ambao walimuweka mikononi lakini kabla hajasema chochote wakatokea askari magereza na kudhani wale jamaa ni majambazi wakawashambulia kwa risasai wakawaua wote akiwemo Joyce ambaye amekuwa mtu wetu ndani ya gereza la Markubelo na ndiye mahsusi kwa ajili ya kumchunguza mzee Alfredo"akasema Noah



    "Dah ! hili ni pigo kubwa sana,haijawahi kutokea watu nane wakauawa kwa pamoja.Chita imejaa vijana wenye uwezo mkubwa sana imekuwaje wakaweza kuuawa kirahisi namna hii?hawakuwa wamechukua tahadhari yoyote?akauliza Dr Enock



    "Mheshimiwa rais hata sisi hapa imetushangaza pia kwani watu niliowatuma kule walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa"



    "Kwa hiyo mmechukua hatua gani hadi hivi sasa?Nini unafikiria kukifanya?



    "Baada ya kupata taarifa za kilichotokea tulipata ushawishi wa kumchunguza kwanza huyu Dastan ni nani na amewezaje kuwaua watu wanne akiwa peke yake?Vile vile tulitaka kumfahamu kiundani ili tuone namna tutakavyofanya ili aweze kutueleza Dr Alfredo alimtuma aupeleke wapi ule ujumbe.Tulianza kwa kutafuta taarifa zake tukiwa na lengo la kuishikilia familia yake lakini kwa bahati mbaya hakuna taarifa zozote za kuhusiana naye"



    "Sijakuelewa Noah unamaanisha kitu gani unaposema hakuna taarifa za kuhusiana na Dastan?akauliza rais



    "Mheshimiwa rais tumejaribu kuingia katika mitandao ya wizara zote zenye kuhifadhi taarifa za watumishi wa umma lakini hatujafanikiwa kupata taarifa za kumuhusu Dastan Mwaikambile mkuu wa gerezala markubelo ndiyo maana nimekupigia ili kupata msaada wako"



    Dr Enock akavuta pumzi ndefu halafu akauliza



    "Noah hicho unachokisema si kitu cha kweli.Nimewawezesha muweze kuingia katika mtandao wa serikali na kupata taarifa zozote zile ambazo mnazihitaji na taarifa zote za watumishi wa umma zipo katika kumbu kumbu za wizara ya mambo ya ndani na vile vile katika wizara ya utumishi n ahata hazina nao wana kumbu kumbu zote za watumishi wa umma hivyo si kweli kwamba taarifa zake hazipo.Yawezekana Dastan anatumia jina lingine tofauti"akasema



    "Hata sisi tulihisi hivyo lakini baada ya kuchimba Zaidi tukagundua kwamba wizara ya mambo ya ndani wanamtambua Dastan kama mkuu wa gereza la Markubelo lakini cha ajabu hakuna taarifa zozote za kuhusiana naye kama vile uraia,taarifa za elimu ,familia n.k."



    "Hii ni habari mpya tena.Inawezekanaje tukawa na mtumishi serikalini tena mwenye cheo kikubwa lakini hatuna taarifa zake? akauliza rais



    "Mheshimiwa rais kuna mtu moja ambaye tunadhani anaweza akatupa majibu kuhusiana na Dastan ambaye ni Inspekta jenerali wa magereza.Huyu ndiye aliyemteua Dastan kuwa mkuu wa gereza la Markubelo hivyo naamini lazima anamfahamu vyema hadi akamteua kushika nafasi hiyo"akasema Noah



    "Uko sahihi Noah ngoja nimpigie simu na nimtake anipe taarifa zote za Dastan" akasema Dr Enock na kukata simu akazitafuta namba za Inspekta jenerali wa Magereza akapiga.Simu ikaita na kupokelewa haraka



    "Hallo mheshimiwa rais" akasema Dr Isaack Mchana

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    "Afande Isaack,habari za usiku huu?



    "Nzuri kabisa mheshimiwa rais" akajibu Isaack



    "Afande Isaack ninahitaji msaada wako."



    "Ninakusikia mheshimiwa rais"



    "Ahsante.Ninahitaji kupata taarifa zinazomuhusu mkuu wa gereza la Markubelo Dastan Mwaikambile"akasema Dr Enock halafu ukapita ukimya mfupi



    "Afande Isaack" akaita rais



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog