Simulizi : Mifupa 206
Sehemu Ya Pili (2)
“Nenda ukalale na mkeo huku mkifikiria mbinu mpya za kuzidi kutunyonya,
Sipendi kuua mtu asiye na hatia” Koplo Tsega akafoka na yule mhindi kuona vile
hakutaka kuendeleza mjadala badala yake akageuza na kurudi ndani kwake. Halafu
zikafuatia kelele za milango mingine ya jirani kila mtu akijitahidi kujifungia vizuri
ndani kwake.
Ilikuwa zamu ya Koplo Tsega kushikwa na mshangao kwani wakati alipomaliza
kuufunga ule mlango na kurudi pale sebuleni Guzbert Kojo hakuwepo na hapo
paridi nyepesi ikaanza kuutafuna mtima wake. Kulikuwa na michirizi ya damu kutoka
sehemu ile sebuleni kuelekea kwenye ile korido iliyopakana na vile vyumba.’Guzbert
Kojo alikuwa ametoweka wakati yeye alipokuwa akiongea na yule mhindi’ Koplo Tsega
aliwaza kisha akaikamata vema bastola yake mkononi na kuanza kuifuatilia taratibu
ile michirizi ya damu iliyokuwa ikichuruzika bila shaka kutoka kwenye lile jeraha la
kalamu jichoni mwake.
Alipotoka pale sebuleni ile michirizi ya damu ikaelekea kwenye ile korido. Koplo Tsega aliitazama kwa makini michirizi ile na sehemu fulani ukutani kulikuwa na
alama za viganja vya mikono ya mtu vilivyotapakaa damu. Koplo Tsega akatambua
kuwa alama zile za damu zilitokana na viganja vya Guzbert Kojo wakati alipoiondoa
mikono yake kwenye lile jeraha na kushika kwenye zile kuta wakati akitafuta mhimili
mzuri wa kutembea. Ile michirizi ya damu iliendelea mbele na kupotelea kwenye
mlango mmoja wa chumba. Chumba hicho kilikuwa ni kile kilichokuwa karibu na
kile chumba cha bafu.
Koplo Tsega alipofika kwenye mlango wa kile chumba alisimama kidogo na
kutega masikio yake kuupima utulivu uliokuwa mle ndani. Chumba kilikuwa kimya
kama kilichokufa na hali ile ilimshangaza sana. Baada ya kujiridhisha na tathmini yake
Koplo Tsega akakishika kitasa cha ule mlango na kukusanya nguvu za kutosha kisha
akaupiga kumbo ule mlango kwa nguvu zake zote. Ule mlango ukafunguka kwa kasi
na hapo akazama ndani huku bastola yake ikiwa tayari kufanya kazi mkononi. Koplo
Tsega alitulia kidogo akiyatembeza macho yake mle ndani hata hivyo hakukuwa na
dalili zozote za uwepo wa Guzbert Kojo mle ndani.
Hali ile ikazidi kumchanganya zaidi Koplo Tsega na hapo akatafuta swichi ya taa
ya mle chumbani na kuiwasha. Macho yake yakapumbazika kidogo na chumba kizuri
chenye samani za kifahari;kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita na pembeni ya kitanda
kile kulikuwa na meza fupi na juu ya meza ile kulikuwa na redio ndogo. Kwenye kona
moja ya chumba kile kulikuwa na jokofu dogo ambalo lilikuwa likitoa muungurumo
hafifu mle ndani. Runinga kubwa iliyounganishwa na sistimu nzuri ya muziki wa
Home theatre ilikuwa pembeni ya Dressing table ya kisasa yenye lukuki ya vipodozi
vya kiume juu yake ilitokuwa ikitazamana na kitanda cha mle ndani. Ukutuani kulikuwa
na picha nzuri za kuchorwa zilizotundikwa katika namna ya kupendeza sana. Guzbert
Kojo hakuwepo mle ndani.
Pazia jepesi lililokuwa likipepea taratibu kwenye dirisha la kile chumba bila
kikwazo chochote lilitosha kumjulisha Koplo Tsega kuwa dirisha lile lilikuwa wazi.
Hivyo akashawishika na kuanza kuzitupa hatua zake taratibu kulisogelea lile dirisha.
Alipofika pale dirishani akalisogeza lile pazia kando na kutazama. Dirisha lile kubwa
la vioo lilikuwa wazi na Koplo Tsega alipolisogelea vizuri na kutazama chini nje ya
dirisha lile mara akaona kitu mfano wa kifurushi kisichoeleweka kikiwa kule chini ya
ghorofa usawa wa lile dirisha. Baada ya kutulia na kutazama kule chini kwa makini
kifurushi kile kisichoeleweka hatimaye taswira yenye hakika ikaumbika machoni pake.
Guzbert Kojo alikuwa amejiuwa kwa kujirusha chini ya jengo lile ghorofa kupitia lile
dirisha.
Koplo Tsega aliendelea kuyatuliza macho akitazama kule chini huku akishindwa
kuamini kama Guzbert Kojo angeweza kuchukua uamuzi wa namna ile.’Guzbert
Kojo alikuwa akificha siri gani hadi akadiliki kuyakatisha maisha yake kinyama namna ile
pasipo kutoa ushirikiano?’ Koplo Tsega akajikuta akijiuliza mwenywewe pasipo kupata
maajibu. Kisha akaanza kuvuta picha namna ambavyo taarifa za kifo cha Guzbert
Kojo kitakavyowavuta watu fulani mara baada ya taarifa hizo kuwafikia watu hao.
********
Koplo Tsega aliendelea kusimama kwa kitambo huku akitazama kule chini ilipokuwa
maiti ya Guzbert Kojo na mara akaona watu wakianza kukusanyika pale chini
kushuhudia ile maiti ya Guzbert Kojo. Koplo Tsega akiwa ameanza kutahadharishwa
na ongezeko lile la mashuhuda pale chini ya lile jengo la ghorofa akairudisha bastola
yake mafichoni. Kisha akachukua pipi ya kijiti kutoka mfukoni mwake na alipomaliza
kuimenya akitia mdomoni na kuibana upande mmoja wa shavu lake huku akianza
kuinyonya taratibu na hivyo kulifanya shavu lake litune kama tumbola chura.
Muda mfupi uliofuata Koplo Tsega alikuwa akifanya upekuzi wa kina ndani ya
ile nyumba ya Guzbert Kojo. Kazi ya upekuzi wa mle ndani ilikuwa ngumu kwa vile
ilihitaji umakini wa hali ya juu katika kuzifikia sehemu zote muhimu lakini Koplo
Tsega alijitahidi kwa kila hali kufukuzana na muda. Mwishowe alimaliza upekuzi wake
pasipo kuambulia chochote cha maana. Hata ile simu ya Guzbert Kojo iliyokuwa
pale sebuleni kwenye lile kochi nayo haikuwepo,Guzbert Kojo alikuwa ameichukuwa
wakati ule Koplo Tsega alipokuwa akiongea na yule Mhindi.
Kulikuwa na kompyuta mpakato moja chini ya meza ya mle chumbani. Kompyuta
ile haikuwa imefungwa kwa neno la siri ama password hivyo Koplo Tsega baada ya
kuiwasha akaanza kupekuwa mafaili yaliyokuwa mle ndani. Mle ndani ya ile kompyuta
kulikuwa na mafaili mengi na baadhi ya mafaili yale yalikuwa na taarifa binafsi za
Guzbert Kojo ambazo hazikuhusiana na tume. Mafaili yaliyosalia yalikuwa na taarifa
za kiutendaji na ripoti kadhaa za ile tume ambazo hazikuwa na maana yoyote kwa
Koplo Tsega. Hivyo hatimaye aliifunga ile kompyuta na kuirudisha mahala pake.
Chini ya lile godoro pale kitandani kulikuwa na bastola moja aina ya Tokarev TT
na yenye magazine mbili zilizojaa risasi. Huwenda Guzbert Kojo alikuwa amesahau
uwepo wa bastola ile au labda alipatwa na kihoro na hivyo fikra zake kupoteza
umakini. Kwani vinginevyo angeweza kuitumia bastola ile katika kujihami. Koplo
Tsega akajikuta akiwaza wakati alipokuwa akiitazama bastola ile na kuirudisha mahala
pake. Katika droo za kabati la nguo lililokuwa kwenye kona moja ya kile chumba
hakukuwa na kitu chochote cha maana zaidi ya mafaili yenye nyaraka binafsi za kiofisi
za Guzbert Kojo zisizo na msaada wowote kwa Koplo Tsega.
Wakati Koplo Tsega alipokuwa akifanya upekuzi kwenye droo moja ya ile Dressing
table iliyokuwa mle chumbani mara akasikia kelele za mtu aliyekuwa akifyatua kitasa
cha mlango wa mbele wa kule sebuleni. Tukio lile likampekea Koplo Tsega amalizie
haraka upekuzi wake mle chumbani. Muda mfupi uliyofuata mara ule mlango sebuleni
ulisikika ukifunguliwa taratibu na kwa uangalifu huku mtu huyo akionekana kukwepa
kumshtua mtu yeyote ambaye angekuwa mle ndani.
Mpelelezi yoyote huongozwa na hisia zake na kwa Koplo Tsega hali hiyo haikuwa
tofauti. Hisia zake zilimueleza kuwa mgeni yule mvamizi hakuwa miongoni mwa wale
majirani wa Guzbert Kojo. Hivyo kwa vyovyote alikuwa ni mtu wa kutoka mbali
lakini mwenye malengo fulani na ziara yake ile isiyo rasmi. Hivyo aliwahi kuizima
taa ya mle ndani kisha kupitia dirisha lile la chumbani lililo kuwa wazi akaning’inia
kwenye pazia lefu la mle chumbani huku akilitumia pazia lile kama nyenzo muhimu ya kushukia chini.
Koplo Tsega alipojiachia akatua kwenye ukingo mfupi wa dirisha la chumba
cha ghorofa ya chini. Wenyeji wa chumba kile walikuwa wamelala hivyo hapakuwa
na usumbufu wa aina yoyote. Halafu kwa msaada wa bomba la maji taka lililokuwa
likitoka sehemu ya juu ya lile jengo ghorofa,Koplo Tsega akaning’inia na kuangukia
kwenye korido ya ghorofa ya chini. Kisha kutokea pale haikumchukuwa muda mrefu
kufika chini ya jengo lile la ghorofa sehemu lilipokuwa gari lake. Muda mfupi baadaye
alikuwa mbali na eneo lile akivipangua vichochoro vya jiji la Dar es Salaam.
NJAMA AKAIVUTA SIGARA YAKE taratibu na alipoitoa akaugemeza
mkono wake juu ya mgongo wa kochi huku akionekana kuzama kwenye
tafakari nzito. Halafu baada ya kitambo kifupi cha ukimya kupita akageuka
pembeni kumtazama Milla Cash aliyekuwa ameketi pembeni yake kwenye kochi huku
akionekana kufikiri jambo.
Walikuwa ndani ya chumba kimojawapo cha Vampire Casino,chumba ambacho
hutumika na Milla Cash kuwahudumia wateja wake.
“Sikujua kama mtu niliyekuwa nikiwasiliana kwenye simu ni wewe” Njama
akavunja ukimya.
“Mimi nilikufahamu mapema kwani namba yako ya simu ninayo!” Milla Cash
akaongea kwa utulivu.
“Vipi biashara yetu inaendeleaje?”
“Business is as usual my dear!” Milla Cash akaongea kuwa utulivu huku akiangua
kicheko hafifu cha kikahaba na kabla hajamalizia kicheko chake Njama akamkatisha.
“Alba Gaumo amekufa!”
“Nafahamu!,vyombo vya habari vya leo vingi vimepambwa kwa taarifa zake”
Milla Cash akaongea kwa utulivu huku akionekana mwenye masikitiko na hapo
kitambo kifupi cha ukimya kikapita kila mtu akionekana kuzama kwenye fikra zake.
“Hicho ndiyo kilichonileta hapa” hatimaye Njama akaongea kwa utulivu baada ya
kuitoa tena sigara yake mdomoni.
“Nafahamu!” Milla Cash akaongea kwa utulivu kisha akachukua sigara moja
kutoka kwenye pakiti iliyokuwa juu ya meza fupi mbele yake. Kisha akajiwashia na
kuivuta taratibu mdomoni pasipo kumtazama Njama na alipoitoa sigara ile mdomoni
akavunja tena ukimya.
“Nilikuwa naye jana usiku na sikuwaza kabisa kama asubuhi ya leo ningeamka na habari tofauti za maisha yake!”
“Ni jambo la kusikitisha sana” Njama akaongea kwa utulivu
“Polisi wana taarifa zozote?” Milla Cash akauliza huku akigeuka na kumtazama
Njama kwa udadisi.
“Mpaka sasa hatuna taarifa zozote na hatupendi polisi wajiingize kwenye suala hili
ingawa mpaka sasa bado hatujajua nini sababu ya kifo chake” Njama akaongea huku
akivigongesha vidole vyake juu ya mkono wa kochi lile.
“Taarifa nilizozisoma leo magazetini zinaeleza kuwa kifo chake kimetokana na
kugongwa na gari lakini sina hakika sana hilo” Milla Cash akaongea kwa utulivu mara
baada ya kuitoa sigara mdomoni. Gauni lake fupi lilikuwa limeyaacha wazi mapaja
yale laini na mang’avu yaliyotawaliwa na michoro mingi ya Tatoo tofauti. Matiti yake
makubwa ya wastani yalikuwa nusu wazi kwa kukosa uhifadhi wa sidiria na gauni lake
lenye umbo la V shingoni. Miguu yake mirefu mmoja aliupandisha juu ya mwingine
huku mara kwa mara akuichezesha chezesha na kukifanya kikuku chake alichokivaa
mguuni kutoa mng’aro wa kipekee. Sikio lake moja lilikuwa limetogwa hereni tatu
tofauti za madini ya Gold,Diamond na Green tomalin.
“Kwa nini unasema hivyo?”
Njama akauliza huku akigeuka na kumtama Milla Cash kwa makini. Milla Cash
akaanza kusimulia mkasa wote uliotokea jana usiku wakati alipokuwa na Alba Gaumo.
Akianzia tangu kuvamiwa kwao na yule mtu,zile kukurukakara zilizotokea mle ndani
na namna mtu yule alivyopambana na hatimaye kumzidi nguvu Alba Gaumo kabla
ya kuanza kufukuza.
“Alikuwa akihitaji nini huyo mtu?” hatimaye Njama akauliza kwa utulivu baada ya
maelezo ya Milla Cash kufika ukomo.
“Alisisitiza kuwa alitaka kuonana na Gabbi Masebo”
“Unadhani kwa nini alitaka kuonana na Gabbi Masebo?”
“Hakuna anyejua” Milla cash akaongea kwa utulivu huku akiibetua midomo yake
baada ya kuitoa sigara mdomoni.
“Huyo mtu umewahi kumuona hapo kabla?”
“Hapana”
“Kwa hiyo ni mgeni kabisa kwako?”
“Ndiyo”
“Unaweza kunielezea mwonekano wako?” Njama akauiliza kwa udadisi na
hapo Milla Cash akaanza kumuelezea mwonekano wa yule mtu. Alipomaliza Njama
akahitimisha kuwa hata yeye hakuwahi kumuona huyo mtu.
“Hofu yangu ni kuwa huwenda kukawa na mtu au watu wanaofanya uchunguzi
juu ya kupotea kwa Gabbi Masebo!” Njama akaongea kwa utulivu huku akifikiri.
“Kama watu hao wapo basi wanapoteza muda wao bure!” Milla Cash akaongea
huku akiutikisa mguu wake taratibu.
“Pamoja na hayo lakini hatupaswi kupuuza tukio hili” Njama kaongea kwa utulivu
huku akiipeleka sigara yake mdomoni.
“Hatuwezi kusema lolote kwa sasa ngoja tuone nini kitakachofuata baada ya kifo
cha Alba Gaumo” Mill a Cash akaongea huku akiitazama saa yake ya mkononi.
“Polisi wanaweza kuanza kufanya uchunguzi juu ya kifo cha Alba Gaumo na
hivyo huwenda wakakufikia. Unachotakiwa ni kukanusha jambo lolote ambalo
litakuhusisha na Alba Gaumo wakati sisi tukiendelea na uchunguzi wetu juu ya huyo
mtu”
“Msiwe na shaka juu ya hilo!” Milla cash akaongea kwa kujiamini huku akionekana
kutafakari halafu akausogeza mkono na kuitazama saa yake ya mkononi.
“Nina mteja atakayefika hapa muda si mrefu nafikiri unaweza ukaniacha sasa na
kama kutakuwa jambo lolote tofauti tutawasiliana” Milla Cash akaongea kwa utulivu
mara baada ya kuito asiga mdomoni.
“Tutaendelea kuwasiliana” Njama akaongea huku akisimama na kuyatembeza
macho yake mle ndani. Kile chumba kilifaa kufananishwa na chumba cha biashara za
kikahaba kwa namna ya picha za utupu zulizokuwa zimebandikwa kwenye kuta zake.
Mandhari ya mle ndani iliundwa kwa makochi mawili makubwa ya sofa. Kaunta
ndogo ya vinywaji vikali vya kilevi. Taa zenye mwanga hafifu za rangi tofauti. Upande
wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na pazia refu na jepesi la kitambaa mlangoni
ambalo lilikuwa limekitenganisha chumba kile na kingine. Kupitia pazia lile mtu
angeweza kuona ndani ya kile chumba kingine chenye kitanda kikubwa chenye
foronya laini. Mbele ya kitanda kile kulikuwa na kioo kikubwa cha ukutani. Na upande
wa kulia wa chumba kile kulikuwa na sehemu ya maliwato na beseni kubwa la kuogea
lenye mfumo wa mabomba mawili ya maji moto na baridi. Pembeni yake kulikuwa na
sehemu maalum iliyoning’inizwa mataulo matatu masafi huku harufu nzuri ya sabuni
ya kuogea aina ya Vatika dermoviva ikitabaruku mle ndani.
Akiwa ameridhika na taarifa alizozipata Njama aliagana na Milla Cash kisha
akaanza kutembea taratibu akielekea kwenye mlango wa kutokea wa kile chumba cha
Vampire Casino huku akiwa na hakika kuwa macho ya Milla Cash yalikuwa nyuma
yakimsindikiza.
Alipofika pale mlangoni akapishana na mwanaume mmoja raia wa kichina akiingia
mle ndani kwa uso wa furaha. Njama hakuwa na shaka kuwa mchina yule ndiye
mteja aliyekuwa akisubiriwa wa Milla Cash. Njama akasalimiana na yule mchina huku
akitoka nje ya kile chumba. Muda mfupi baadaye alikuwa akikatisha kwenye ukumbi
wa chini wa ile Casino kuelekea nje.
_____
FULGENCY KASSY ALISIMAMA kwa utulivu huku akiyatembeza macho
yake taratibu katika hali ya kutathmini kukurukakara zilizotokea kwenye sebule ile
muda mfupi uliyopita. Halafu akaanza kujilaumu kuwa ilikuwaje hadi akapishana
na tukio ile la aina yake. Hata hivyo dhana hiyo ilipoanza kujengeka vizuri kichwani
mwake akaiweka kando. Hakuwa na sehemu ya kujilaumu kwani alichofanya yeye
ilikuwa ni kuitikia wito kwa haraka kama alivyofanya.Simu ya Guzbert Kojo ilikuwa imelifukuzia mbali lepe lake la usingizi aliloanza
kutongoa. Kama isingelikuwa ni simu ya kutoka kwa Guzibert Kojo bila shaka
Fulgency Kassy angeikata simu yake kama siyo kuizima kabisa na kumuacha mpigaji
mbali na matumaini. Ukweli ni kwamba mara nyingi simu za usiku huishilia kwenye
mikasa mizito mno na hatari za kuponea chupuchupu. Hata hivyo hukuwa ameyanasa
vizuri maongezi ya Guzbert Kojo wakati alipokuwa akizungumza naye muda mfupi
uliyopita kwa njia ya simu.
Fulgency Kassy akakumbuka maneno machache aliyoyasikia kwenye simu ile
yakisema “Nimevamiwa tafadhali nahitaji msaada wako!...” maneno yale hayakufika
mwisho huku Guzbert Kojo akionekana kusukumwa na hali fulani iliyomfanya
ashindwe kumalizia kuongea kile alichokikusudia. Halafu muda mfupi baada ya
sauti ile kupotea hewani yakasikika makelele fulani kama mvumo wa upepo kabla ya
simu ile kukatika. Muda mfupi uliyofuata FulgencyKassy alikuwa kwenye gari lake
barabarani akielekea sehemu yalipokuwa makazi ya Guzbert Kojo huku kichwani
akiwa na mawazo mengi.
Mazingira ya sebule ile yalikuwa yamebeba ushahidi tosha juu ya hali ile iliyomsukuma
Guzbert Kojo kushindwa kumalizia kuongea kile alichokuwa amekikusudia. Kulikuwa
kumefanyika uvamizi. Ile sebule ni kama ilikuwa imevamiwa na nyoka mwenye sumu
kali hali iliyompelekea mwenyeji wake kuhamanika mno,akimkimbia nyoka huyo
huku na kule ili kuinusuru roho yake. Swali likabaki huyo mvamizi ni nani?,Fulgency
Kassy akajiuliza huku akiendelea kuyatembeza macho yake taratibu ndani ya sebule ile
akitathmini ukubwa wa athari. Hatimaye akaichomoa bastola yake aina ya Colt Detective
Spl kutoka kwenye mfuko wa koti lake na kuishika mkononi.
Kuukuta mlango wa mbele wa nyumba hii ukiwa umefungwa kulitengeneza
dhana mbili katika kichwa chake. Kwanza huwenda mvamizi alikuwa ametoka na
kuufunga ule mlango au pengine mvamizi huyo alikuwa amejibanza sehemu fulani
ndani ya ile nyumba. Dhana hizo zikamfanya azidi kujidhatiti huku akizitupa hatua
zake taratibu na kwa uangalifu.
Kulikuwa na michirizi mikubwa ya damu sehemu za sakafuni na mingine kwenye
baadhi ya makochi yaliyokuwa pale sebuleni na hali ile ikazidi kumpa wasiwasi. Fulgency
Kassy akatulia kidogo huku akiitafakari hali ya ukimya wa mle ndani iliyobeba tafsiri
ya kifo au uzima.“Jitokeze basi wewe mvamizi uone shughuli yangu”. Hatimaye akajikuta
akijiongelesha taratibu huku akiendelea kuyatembeza macho yake huku na kule tayari
kuinasa taswira yoyote mbele yake.
Muda mfupi baadaye Fulgency Kassy alikuwa amemaliza kufanya uchunguzi
wake kwenye ile sebule ya Guzbert Kojo pasipo kupata kitu chochote cha maana.
Ile michirizi ya damu pale sebuleni hatimaye ikamuongoza hadi kule chumbani
kwa Guzbert Kojo. Baada ya kumaliza kufanya upekuzi akajikuta akishikwa na
mshangao. Vitu vyote muhimu ambavyo alidhani huwenda mvamizi yule alikuwa
amevifuata mle ndani vilikuwepo. Vitu kama nyaraka za kiofisi,kiasi kikubwa cha pesa
iliyokuwa kwenye droo moja ya kabati la nguo mle chumbani na bastola moja yenye magazine mbili zilizojaa risasi iliyokuwa chini ya godoro kwenye kile kitanda. Akazidi
kujiuliza,Guzbert Kojo alikuwa wapi na mvamizi yule alikuwa na shida gani?,huku akiliendea
dirisha la chumba kile lililokuwa wazi.
Mara alipofikia pale dirishani Fulgence Kassy akagundua kuwa pazia moja la
dirisha lile lilikuwa limefunguliwa kutoka sehemu yake na kufungwa kwenye mhimili
wa kati wa lile dirisha. Pazia lile likitumika kama nyenzo muhimu ya kushukia chini. Ni
Mvamizi au Guzbert Kojo alikuwa amelitumia pazia lile kama nyenzo ya kutoroka?,Fulgency
Kassy akajiuliza huku akitazama chini ya lile jengo la ghorofa kupitia ule uwazi wa lile
dirisha.
Kulikuwa na kikundi cha watu wachache waliokuwa wamekizunguka kitu fulani
wakikitazama kule chini ya lile jengo. Kitu kile kilikuwa mbele kidogo usawa wa lile
dirisha la kile chumba. Fulgency Kassy akameza fundo kubwa la mate akiyadhibiti
vizuri mapigo ya mtima wake katika namna ya kuzitowesha fikra mbaya zilizoanza
kujengeka kichwani mwake.
Fulgency Kassy Aliendelea kutazama kule chini kwa kitambo kabla ya kujikuta
akiliacha lile dirisha taratibu baada ya kuona kuwa kulikuwa na ongezeko la watu
waliokuwa wakifika kukishuhudia kile kitu kisichoeleweka pale chini ya lile jengo.
Mara akawaona baadhi ya watu wale wakiinua macho yao na kutazama pale dirishani
aliposimama.
Fulgency Kassy kwa kuishtukia hali ile hakutaka kuendelea kusimama pale
dirishani kwa hofu ya kuhusishwa na tukio baya lolote ambalo lingekuwa limetoke
mle ndani. Hivyo akaliacha lile dirisha na kuelekea kwenye ule mlango wa sebuleni
ambapo aliufungua na kutoka.
Lakini kabla hajatoka mle ndani akakumbuka kuwa kulikuwa na mambo ya kufanya
kwanza. Hakutaka polisi wapate chanzo cha uchunguzi wao kama endapo kungekuwa
na jambo baya lolote lililotokea mle ndani. Hivyo alirudi tena mle ndani na kusafisha
alama za vidole vyake pamoja na kuondoa ile bastola chini ya godoro,nyaraka muhimu
za kiofisi na vitu vingine ambavyo vingeweza kuvuta upelelezi wa polisi.
Muda mfupi baadaye Fulgency Kassy alimaliza kufanya zoezi lile na wakati
alipokuwa akijiandaa kutoka mle ndani mara macho yake yakajikuta yakivutiwa na
ganda la pipi lililokuwa mle ndani sakafuni. Akainama taratibu na kuliokota ganda
lile la pipi huku akilitazama kwa makini na hapo maswali mengi yakaanza kuibuka
kichwani mwake. Alimfahamu vizuri Guzbert Kojo kuwa hakuwa na mazoea ya
kutumia viburudisho vya sampuli ile,na hapo akajiuliza kuwa lile ganda la pipi lilitoka
wapi. Kwa mwanamke au mtoto…?. Akajiuliza bila kupata majibu huku akilitia mfukoni
lile ganda la pipi kwa utafiti wa baadaye.
_____
MAHOJIANO YALIYOFANYIKA kati ya Fulgency Kassy na majirani wa
Guzbert Kojo yalikuwa yametoa taswira mpya kwa Fulgency Kassy. Mvamizi alikuwa
msichana wa makamo,mweusi,mwembamba kiasi na mrefu. Majirani wakaendelea kumueleza kuwa hawakumuona msichana huyo wakati alipokuwa akiingia wala
wakati alipokuwa akitoka kwenye ile nyumba ya Guzbert Kojo. Huku wakidai kuwa
walikuwa wameamshwa na kelele za vurumai zilizokuwa zikitokea mle ndani ambapo
walitoka nje wakitaka kufahamu kilichojiri lakini msichana yule mvamizi alikuwa
amewaonya kwa bastola yake mkononi kuwa warudi majumbani mwao.
Kutaka kufahamu kama vurumai lile lililotokea kwenye nyumba ya Guzbert
Kojo lilikuwa ni baina ya Guzbert Kojo na mpenzi wake au vinginevyo hilo liligonga
mwamba kwani wale majirani walisema kuwa hawakuwahi kumuona yule msichana
mvamizi hapo kabla.
Fulgency Kassy hakutaka kupoteza muda baada ya kuona kuwa majirani wale
hawakuwa na ziada nyingine katika maelezo yao. Hivyo akawashukuru na kuwaaga
huku akiondoka zake.
_____
CHINI YA LILE JENGO LA GHOROFA usawa wa lile dirisha la chumba cha
Guzbert Kojo wale watu walikuwa wameongezeka mara mbili zaidi ya ile idadi ya
awali. Fulgency Kassy aligundua hilo wakati alipokuwa akijipenyeza katikati ya wale
mashuhuda ili kutazama kile ambacho watu wale walikuwa wakikitazama pale chini.
Maiti ya Guzbert Kojo ilikuwa imezungukwa na watu. Kichwa chake kilikuwa
kimepasuka vibaya huku akiwa ameulalia mkono wake katika namna nyepesi yenye
tafsiri kuwa umauti ulikuwa umemfika. Jicho lake la kulia lilikuwa limeshindiliwa
kalamu ya wino na damu nyingi ilikuwa ikiendelea kuvuja na kuganda kutoka kwenye
jeraha lile.
Sehemu kubwa ya ulimi wake ilikuwa nje na nusu ya meno yake yalikuwa
yameng’oka. Mkono wake mmoja ulikuwa umevunjika na mbali na hayo maiti ile
ya Guzbert Kojo ilikuwa uchi wa mnyama hali iliyopelekea gumzo kubwa kwa
mashuhuda waliofika eneo lile huku kila mmoja akizungumza lake.
Fulgency Kassy aliendelea kuitazama maiti ile huku akishindwa kuamini taswira ile
mbele yake. Baadaye akaanza kupiga mahesabu ya umbali wa kutoka kwenye dirisha
la kile chumba cha Guzbert Kojo kule juu ghorofani hadi pale chini. Mahesabu yale
yalipokamilika kichwani mwake akalivua koti lake la mvua na kuifunika ile maiti ya
Guzbert Kojo pale chini.
Mianga ya flash za kamera za waandishi wa habari waliofika mahali pale ilipishani
kama miale ya mwanga wa radi huku kila mwandishi wa habari akijaribu kutafuta
picha nzuri zaidi ambayo ingemletea sifa ofisini kwake. Halafu kupitia maelezo ya
mashuhuda waliokuwa eneo lile Fulgency Kassy akaongeza ziada nyingine katika
dodosa zake. Kuwa muda mfupi baada ya Guzbert Kojo kuanguka kutoka kule juu
ghorofani mtu fulani alikuwa ameonekana akitoka kwenye kile chumba cha Guzbert
Kojo akipitia lile dirisha la kile chumba kwa kuning’inia kupitia lile pazia lililofungwa
pale dirishani.
Fulgency Kassy aliyasikiliza maongezi yale huku akimeza fundo kubwa la mate kuitowesha hasira kooni mwake.
“Ukimuona huyo mtu aliyetoka kupitia pale dirishani unaweza kumkumbuka?”
Fulgency Kassy akamtupia swali mzee mmoja aliyejinadi kuwa yeye ni mlinzi wa eneo
lile.
“Sikumuona vizuri kwani taa nyingi za nje za jengo hili ni mbovu”
“Unadhani kwa mwonekano tu mtu huyo alikuwa mwanamke au mwanaume?”
Fulgency Kassy akamuuliza yule mzee huku akimtazama kwa makini.
“Nahisi alikuwa mwanaume” yule mzee akaongea kwa utulivu huku watu
waliokuwa jirani yake wakionekana kuvutiwa na maelezo yake.
“Kwanini unadhani kuwa huyo mtu alikuwa mwanaume?” Fulgency Kassy
akauliza kwa udadisi zaidi.
“Hakuna mwanamke anayeweza kuning’inia namna ile!” yule mzee akaongea kwa
kujiamini na maelezo yake yakampelekea Fulgency Kassy atambue kuwa yule mzee
hakuwa amemuona vizuri yule mtu aliyetoka kupitia lile dirisha la kile chumba cha
Guzbert Kojo. Hata hivyo Fulgency Kassy akamezea kabla ya kumtupia swali jingine
yule mzee.
“Unayafahamu magari yote ya wakazi wa jengo hili?”
“Ndiyo!,wenye magari ni watu watano tu na wote magari yao yapo”
“Hakuna gari lolote lingine lililoingia na kutoka kabla na baada ya kutokea kwa
tukio hili?” Fulgecy Kassy akauliza tena na swali lile likamfanya yule mzee mlinzi
asite kuzungumza huku akionekana kufikiria jambo. Kitendo kile kikampelekea
Fulgency Kassy ashtukie kuwa sehemu kubwa ya wale mashuhuda eneo lile walikuwa
wamesogea karibu kusikiliza mahojiano yale.
“Nakumbuka kama niliiona teksi nyeupe ikiondoka muda mfupi baada ya tukio
hili lakini sikuitilia maanani kwani akili yangu ilikuwa imehamanika sana kutokana na
hili tukio” yule mlinzi alijitetea. Fulgency Kassy akatabasamu kidogo huku akimtazama
yule mlinzi. Yule mlinzi alikuwa ameanza kubabaika baada ya kuanza kuhisi hatari ya
kupoteza kibarua chake kwa kutokuwa makini. Fulgency Kassy akahitimisha kuwa
mlinzi yule alikuwa akifanya kazi kwa mazoea. Mlinzi lofa!.
“Unamfahamu huyu mtu?” hatimaye Fulgency Kassy akavunja tena ukimya na
kumuuliza yule mlinzi.
“Namfahamu,ni mkazi wa jengo hili” yule mlinzi akaongea kwa utulivu.
“Ulimuona wakati alipokuwa akirudi jioni ya leo?”
“Huyu bwana mimi huwa nakutananaye siku moja moja tena kwa bahati tu maana
sijui huwa anaondoka na kurudi saa ngapi” yule mlinzi akajitetea.
“Sasa unacholinda hapa ni katu gani kama siyo usalama wa watu na mali zao?”
Fulgency Kassy akamwambia yule mlinzi na hapo yule mlinzi akabaki kimya asijue
la kuzungumza. Halafu Fulgency Kassy akatulia kidogo akiupisha ukimya huku
akiyatembeza macho yake kuwatazama watu waliokuwa eneo lile kisha akavunja
ukimya.
“Wakati mwingine jitahidi kuwa makini na kazi yako mzee na uache kufanya kazi kwa mazoea”
Yule mzee akatikisa kichwa chake kwa utulivu huku akionekana kuipokea hoja ile
kwa makini kama sehemu ya mwisho ya lawama kwake.
Polisi tayari walikuwa wamefika eneo lile na Fulgency Kassy hakutaka kuonekana
kivutio kwa askari wale hivyo haraka akajichanganya katikati ya kundi lile la mashuhuda
na kutokomea zake.
Muda mfupi baadaye Fulgency Kassy alikuwa mbele ya lile jengo la ghorofa
akifanya uchunguzi wa mwisho wa kutazama na kutengeneza hoja ama Smart perfect
observation.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Kando ya jengo lile la ghorofa yalipokuwa maskani ya Guzbert Kojo kulikuwa na
Supermarket ndogo lakini ya kisasa yenye kuta safi za vioo. Taa za ndani ya Supermarket
ile zilikuwa zikiangaza kwenye bidhaa zilizokuwa mle ndani bila shaka kuyavuta
macho ya wapita njia wa eneo lile.
Usiku huu Supermarket ile ilikuwa imefungwa. Fulgency Kassy alipoisogelea
kuichunguza akaona kuwa kulikuwa na kamera mbili za kiusalama ama CCTV camera
zilizokuwa zimepandwa sehemu ya mbele ya ile Supermarket ili kunasa taswira za
matukio yoyote ambayo yangetokea mbele ya eneo lile.
Kwa tathmini ya haraka Fulgency Kassy akatambua kuwa kamera zile zingeweza
kunasa taswira ya tukio lolote ambalo lingetokea sehemu ya chini ya mbele ya jengo
lile la ghorofa la shirika la nyumba la taifa yalipotokea yale mauaji ya Guzbert Kojo.
Tabasamu jepesi likaivamia sura ya Fugency Kassy na hapo akakishika kidevu chake
katika namna ya kufurahia matunda mazuri ya uchunguzi wake. Kisha akaitazama saa
yake ya mkononi na kuanza kuondoka taratibu eneo lile akielekea sehemu alipokuwa
ameegesha gari lake. Usiku huu Guzbert Kojo alikuwa amekufa.
_____
KUNA VITU VIWILI VIKUBWA ambavyo watu wanavipenda sana nchini
Tanzania. Vitu hivyo ni umaarufu na pesa. Wanaume wenye pesa huwavuta
wanawake wanaowataka wakati umaarufu wa mtu huwavuta watu na vyombo vya
habari kuandika au kuzungumzia habari za mtu huyo kila kukicha hata kama habari
hizo ni za uongo.
Mpumbavu hulevywa na umaarufu huku akiifungulia pesa mlango iondoke bila
kujua. Unapokuwa na pesa watu watakufurahia na kukuchekea hata kama utakuwa
ukiwatukana watu hao huku idadi ya marafiki ikiongezeka kwa kasi ya ajabu kama
hesabu ya vifo vya watu barani Afrika.
Kama wewe ni mwanaume basi wasichana wazuri na warembo wa kila sampuli
watakuita handsome hata kama mama yako mzazi aliyekuzaa anakiri kuwa sura yako
mbaya alikuwa akiitumia kumtishia mdogo wako wakati alipokuwa akikataa kula.
Hivyo pesa ni muhimu zaidi kuwa nayo kwani pesa huleta umaarufu.
Mawazo haya yalikuwa yakipita kichwani mwangu taratibu wakati nilipokuwa
nikivipitia vichwa vya habari vya magazetini na kuliona gazeti moja maarufu la udaku likionesha picha za msanii mmoja maarufu wa muziki wa Bongo fleva akiponda raha na
wanawake warembo wa jiji la Dar es Salaam wakati huo akisadikika kudaiwa kodi ya
vyumba viwili alivyopanga eneo la uswahilini.
Vichwa vingine vya habari vya magazetini asubuhi hii vilijikita zaidi katika nadharia
za kisiasa na vyote havikunipendezea isipokuwa kichwa cha habari kilichokuwa kwenye
gazeti moja maarufu hapa nchini. Kichwa hicho cha habari kiliandikwa “MAUAJI
YAENDELEA KULITIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM”. Nikajikuta nikivutiwa
na kichwa kile cha habari,labda kwa kuwa mikasa ya vifo ni sehemu ya maisha yangu.
Hivyo nikaingiza mkono mfukoni kuchukua pesa ya kununulia gazeti lile.
Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa moja na nusu
asubuhi wakati nilipokuwa nikitembea kuliendea gari langu nililokuwa nimeliegesha
muda mfupi uliyopita hatua chache kutoka pale kilipokuwa kile kibanda cha muuza
magazeti katika kituo hiki cha daladala cha Akiba kuelekea eneo la posta kuu jijini Dar
es Salaam.
Muda mfupi baadaye nikatia gari langu moto na kuingia tena barabarani huku
nikitafuta sehemu nzuri ya kukatisha upande wa kulia ili nielekee eneo la Kisutu
ilipokuwa ofisi yangu.
Sehemu kubwa ya usiku wa kuamkia leo nilikuwa nimeitumia katika kutengeneza
hoja na kuunganisha matukio yote ya usiku uliyopita,nikianzia kule Vampire Casino
hadi kwa yule msichana dereva wa lile gari Corolla limited nyeupe niliyemtafutia kule
barabara ya mtaa wa Nkurumah usikuwa wa jana. Kwa kweli bado nilikuwa sijapata
uelekeo mzuri wa kazi yangu ingawa hisia zangu zilikuwa zimetawaliwa na viashiria tu.
Kabla ya kutoka nyumbani nilikuwa nimemtafuta mzee James Risasi kwa njia ya
simu na kumueleza pale nilipokuwa nimefikia katika kazi yangu huku nikimwahidi
kuwa upelelezi wangu ulikuwa ukielekea katika sehemu nzuri zaidi.
Asubuhi hii niliendelea kuendesha gari langu taratibu nikielekea eneo la Kisutu
ilipokuwa ofisi yangu huku nikiiacha barabara ya mtaa mmoja na kuingia barabara ya
mtaa mwingine. Lakini wakati nilipokuwa nikiendelea na safari hisia zangu zikajikuta
zikizidi kuvutwa na kile kichwa cha habari za mauaji kilichokuwa kwenye lile gazeti
nililolinunua ambalo wakati huu nilikuwa nimeliweka kwenye siti ya abiria pembeni
yangu.
Kuzidi kukiundia hoja kichwa kile cha habari kukanifanya nijikute nikipunguza
mwendo wa gari langu taratibu. Wazo la kuelekea ofisini kwangu moja kwa moja
sikuliona tena kama lilikuwa na uzito mkubwa hivyo nikatafuta sehemu nzuri katika
barabara ile na kuegesha gari langu kando ya barabara. Hakukuwa na msongamano
mkubwa wa magari eneo lile hivyo sikukutana na upinzani wa namna yoyote.
Mara nilipoegesha gari langu kando ya barabara ile nikalichukuwa lile gazeti na
kulifunua hadi ukurasa wa tatu ambapo habari ile ya mauaji ilikuwa imeelezewa kwa
kina na mwandishi wa habari wa gazeti lile.
”Mwanaume mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kuanguka
kutoka ghorofani baada ya inavyosemekana mwanaume huyo kashambuliwa na mtu asiyejulikana…”.
Niliendelea kuisoma habari ile ikiendelea kueleza namna mwanaume huyo
alivyoanguka kutoka juu ya jengo moja la ghorofa la shirika la nyumba la taifa mtaa
wa Nkurumah huku akiwa uchi wa mnyama na jeraha kubwa la kalamu ya wino
iliyoshindiliwa jichoni mwake.
Nilipomaliza kuisoma habari ile mwishoni nikakutana na habari picha ndogo
ya mwanaume mmoja akifanya mahojiano na mzee mmoja mlinzi wa eneo lile
yalipotokea yale mauaji huku waandishi wa habari wakiwa wamemzunguka. Macho
yangu yakajikuta yakivutiwa na picha ya yule mwanaume ambaye sasa nilimfananisha
na kachero ingawa mwandishi wa habari wa gazeti lile alikuwa ameshindwa kulitambua
jina na kazi yake.
Hisia zangu zikanieleza kuwa huwenda ile haikuwa habari ya kuipuuza. Hivyo
nililifunika lile gazeti na kulitupia kando yangu na hapo nikachukua simu yangu ya
mkononi na kumpigia Mwasu nikimweleza kuwa ningechelewa kufika ofisini hivyo
asiwe na shaka.
Niliitazama saa yangu ya mkononi na kuridhika na mwenendo wake na hapo
nikaliingiza tena gari langu barabarani nikielekea mtaa wa Nkurumah yalipotokea yale
mauaji.
Niliwasili mtaa wa Nkurumah ndani ya muda mfupi hasa kwa kuzingatia kuwa
nilikuwa nazifahamu vizuri barabara za mitaa mingi ya jiji la Dar es Salaam zisizokuwa
na msongamano mkubwa wa magari.
Nilitaka kufahamu ni wapi tukio lile la mauaji lilikuwa limetokea na suala hilo
lilikuwa rahisi kwangu. Kwa kupitia wenyeji wa eneo lile nilipata maelezo ya kutosha
huku nikielekezwa kwenye lile jengo la ghorofa la shirika la nyumba la taifa ambapo
tukio lile la mauaji lilikuwa limetokea.
Nilifika kwenye jengo lile la ghorofa huku nikishawishika kutaka kuelekea juu
ghorofani kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi yule marehemu lakini kitendo cha
kuwaona polisi walikarandaranda eneo lile kukanifanya niachane na wazo lile.
Baada ya kupata maelezo ya hapa na pale kutoka kwa wenyeji wa eneo lile
nikaamua kulizunguka lile jengo la ghorofa yalipotokea yale mauaji katika namna ya
kuzipa uhai fikra zangu.
Katika kufanya hivyo mara nikaiona Supermarket ndogo iliyokuwa kando ya
jengo lile la ghorofa. Kuisogelea Supermarket ile kukanifanya nizione kamera mbili
zilizopandwa mbele yake. Nilipozichunguza kamera zile nikazifahamu kuwa zilikuwa
ni kamera za kiusalama zenye nguvu kubwa ya kunasa picha za matukio katika mfumo
wa video. Hivyo kamera zile zingeweza kunasa picha yoyote mbele ya lile jengo la
ghorofa ambapo nyuma yake yalikuwa yametokea yale mauaji. Kamera zile zikanivuta.
Muda mfupi uliyofuata nilikuwa mbele ya Supermakert ile ambayo kwa wakati
huu ilikuwa tayari imefunguliwa. Nilipofika nikausukuma mlango wa kioo wa ile
Supermarket na kuingia mle ndani. Mle ndani kulikuwa na vijana wanne;wasichana
watatu wazuri na warembo na mvulana mmoja wote wakiwa wamevaa sare za kazi.Nikawasalimia wale wafanyakazi wa ile Supermarket huku wakinikabirisha vizuri kama
mteja na hali ile ilinifurahisha.
Niliupokea vizuri ukaribisho ule huku nikipiga hatua zangu taratibu kuelekea
sehemu ilipokuwa kaunta ya Supermarket ile iliyokuwa na msichana mmoja mrembo
aliyeketi nyuma ya meza fupi yenye kompyuta mbili. Kompyuta moja kwa ajili ya
kuhifadhi kumbukumbu za mahesabu ya mauzo ya mle ndani na kompyuta nyingine
ikionesha pembe mbalimbali za picha zinazonaswa na zile kamera za CCTV. Pembeni
ya kompyuta zile kukiwa na mashine ndogo ya utambulisho wa aina ya bidhaa na bei
yake iitwayo Barcode.
“Habari za kazi dada!” nilimsalimia yule dada huku wale wenzake wakiwa
wamesitisha shughuli zao kwa muda wakigeuka na kunitazama. Huwenda walikuwa
wameshangazwa kwa kutokuniona nikielekea kwenye ule upande wa bidhaa.
“Nzuri! karibu sana kaka” yule msichana aliniitikia kwa utulivu huku akinikodolea
macho yenye shauku. Nilipomchunguza vizuri nikagundua kuwa umri wake huwenda
ulikuwa ni kati ya miaka ishirini na mbili na ishirini na nne. Mwembamba na mweupe
mwenye macho mazuri na tabasamu la kibiashara. Msichana yule aliiweka simu yake
aliyokuwa akishughulika nayo juu ya meza na kuniazima uwepo wake kwa asilimia
zote.
“Asante! poleni na kazi” nilimwambia yule dada huku usoni nikiumba tabasamu
la kirafiki baada ya kuifikia vizuri ile meza ya kaunta.
“Tushapoa” yule dada aliniitikia kwa bashasha zote huku macho yake yakiweka
kituo kunitazama.
Nikiwa bado sijatulia vizuri haraka niliyatembeza macho yangu kuitazama screen
kubwa iliyokuwa kwenye pembe ya ile Supermarket mle ndani na hapo nikaziona picha
nyingi za video zilizonaswa maeneo tofauti na kamera za ile Supermarket. Katika picha
zile za video zilikuwepo picha mbili zilizonaswa katika pembe tofauti kutoka sehemu
ya mbele ya lile jengo la ghorofa mbele ya ile Supermarket. Nilitabasamu kidogo na
kuyarudisha macho yangu tena kwa yule dada wa kaunta.
“Naitwa Sajenti Manda Chegwa wa kituo cha polisi cha mjini kati” nilijitambulisha
kwa yule dada huku nikiingiza mkono mfukoni kuchukua kitambulisho changu feki
na kisha kumkabidhi yule dada.
Yule dada akakipokea kile kitambulisho na kuyasoma maelezo ya mle ndani kisha
akainua macho yake kunitazama mara hii akiwa ameshikwa na mshangao kidogo huku
macho kuyatumbua. Akiwa katika hali ile nikanyoosha mkono wangu na kukichukua
kile kitambulisho na hapo nikavunja ukimya.
“Bila shaka mnazo taarifa juu ya mauaji yaliyotokea usiku wa jana nyuma ya
lile jengo la ghorofa” nilimwambia yule dada huku nikimuonesha kwa kidole
changu lile jengo la ghorofa yalipotokea yale mauaji. Wale wenzake tayari walikuwa
wameshasogea karibu na eneo lile la kaunta na walikuwa wameyasikia maongezi
yangu hivyo wakatazama kama wanaoshauriana kwa macho kuwa wakubaliane na
hoja yangu au lah!. Hata hivyo macho yao yalikataa kudanyanya.
“Ndiyo!” hatimaye wote wakaitikia kwa pamoja huku nyuso zao zimebeba alama
za viulizo.
“Okay! nina maswali machache ambayo ningehitaji ushirikiano wenu kwani taarifa
zenu kwa namna moja au nyingine zinaweza kuwa msaada tosha katika kumnasa mtu
aliyefanya muuaji yale halafu baada ya hapo nitawaacha muendelee na kazi yenu”
niliwaambia wale wafanyakazi na hapo wakasogea karibu vizuri kunisikiliza.
“Ngoja nimpigie simu bosi wetu aje” yule dada wa kaunta akavunja ukimya na
kuongea kwa msisitizo.
“Bosi wenu alikuwepo hapa usiku wa jana wakati mlipokuwa mkifunga hii
Supermarket?” nilimuuliza yule dada huku nikimkazia macho.
“Hapana!” wenzake waliwahi kunijibu.
“Sasa bosi wako anahusikaje hapa?” nilimuuliza yule dada na hapo akajiona mjinga
kwa kutojiamini ingawa nilimhisi kuwa huwenda yeye ndiye aliyekuwa mwenye
madaraka zaidi ya wenzake kwenye Supermarket ile. Hivyo pasipo kupoteza muda
nikaanza kuwafanyia Interview.
“Mtu aliyekufa mmewahi kumuona hapa kabla?”
“Ndiyo!” wote wakaitikia na hapo nikayatembeza macho yangu kuwatazama kwa
udadisi mmoja baada ya mwingine. Kitendo kile kikampelekea yule mvulana avunje
ukimya na kufafanua zaidi.
“Tunamfahamu kama mteja ambaye alikuwa na mazoea ya kununua mahitaji
yake katika hii Supermarket” yule kijana akaongea kwa kujiamini na hapo nikageuka
na kumtazama.
“Jina lake?”
“Hatulifahamu” wote wakajibu kwa pamoja huku wakinitazama.
“Jana alifika hapa kuwanunuza?”
“Hapana! kwani ni kwa kipindi kirefu tulikuwa hatujamuona na leo asubuhi ndiyo
tukashangaa kusikia taarifa za kifo chake” yule dada wa mapokezi akanijibu huku
akionekana kuurudisha urafiki wetu.
“Nani aliyewapa taarifa hizo?” niliwauliza.
“Tumeambiwa na mlinzi wa eneo hili asubuhi wakati tulipokuwa tukifungua” yule
dada mwingine akajibu.
“Mna mazoea yoyote na huyo mlinzi kiasi cha kuweza kuwapa taarifa hizo?”
niliwauliza tena na baada ya ukimya mfupi kupita yule mvulana akanijibu.
“Huwa tunamuhifadhia vifaa vyake vya kazi humu ndani”
“Okay! hebu turudi kwa huyo marehemu. Mnafahamu kazi aliyokuwa akiifanya?”
swali langu likapeleka tena ukimya kwa wale wafanyakazi wa ile Supermarket halafu
baada ya kutamazana tena mmoja wao akavunja ukimya.
“Hatuifahamu”
Jibu lao lilinishtua kidogo na hapo nikawatazama katika namna ya kutafakari
kile walichokuwa wakikizungumza. Hali ile ikanipelekea nijiulize kama nilichokuwa
nikikipeleza pale kilikuwa sahihi au nilikuwa nikijiingiza kwenye kesi isiyonihusu.Nilitafakari kidogo kisha nikashusha pumzi taratibu na kuwatazama tena wale
wafanyakazi ile Supermarket.
“Huwa mnaacha on kamera za hii Supermarket wakati mnapofunga na kuondoka?”
niliwauliza.
“Ndiyo!” yule dada wa kaunta akawahi kuitikia.
“Naomba mniruhusu niipitie kompyuta yenu. Nataka niangalie kama nitapa
kumbukumbu ya picha yoyote ya video itakayonisaidia katika upelelezi wangu”
niliwaambia wale wafanyakazi kwa utulivu huku nikizipima hisia zao. Bahati ikaangukia
kwangu kwani sikupata upinzani wowote.
“Karibu” yule dada wa kaunta akaniruhusu.
“Ahsante! lakini naomba mniwie radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
hata hivyo nawaahidi kuwa sitotumia muda mrefu” niliwaambia
“Hakuna shida afande” yule dada akanikaribisha huku akinisogezea kiti vizuri ili
nizunguke na kuketi.
Muda mfupi uliyofuata nilikuwa nyuma ya screen kubwa ya kompyuta ya mle ndani
iliyounganishwa na ile sistimu ya kamera za ki-usalama huku tabasamu langu la asili
likiniponyoka taratibu usoni. Hata hivyo nilijitahidi kulimeza kwa kila hila.
Utundu wangu katika kucheza na kompyuta ulikuwa na kuridhisha. Mle kwenye
ile kompyuta nilijua ni wapi ningeweza kuzipata taarifa nilizozihitaji hivyo sikupoteza
muda. Nilianza kwa kuzipitia picha zote za video zilizonasawa na zile kamera za ile
Supermarket kwa muda wa wiki moja iliyopita.
Kulikuwa na mlolongo wa picha za wateja walioingia na kutoka kwenye Supermarket
ile pamoja na magari na watu waliopita nje ya ile Supermarket kwa kwa nyakati tofauti.
Picha ambazo zilikuwa za kawaida kabisa.
Nilipokuwa mbioni kukata tamaa hatimaye nikakiona kile nilichokuwa nikikitarajia.
Gari ndogo aina Corolla limited la rangi nyeupe lilinaswa na kamera zile likiingia na
kutafuta maengesho yake nje ya lile jengo la ghorofa yalipotokea yale mauaji.
Niliinama vizuri kuitazama ile picha ya video huku mara kwa mara nikiirudisha tena
nyuma ianze upya huku macho yangu yakisafiri taratibu sambamba na tukio lile.
Yule dada niliyekuwa nikimfuatilia ule usiku wa jana kutoka kule Vampire Casino
hadi kule mtaa wa Nkurumah,kupitia ile picha ya video sasa alionekana akiegesha gari
lake nje ya lile jengo la ghorofa kisha akashuka kwenye lile gari Corolla limited nyeupe
na kuanza kuelekea kwenye lile jengo la ghorofa yalipotokea yale mauaji. Tukio lile
likaupeleka moyo wangu upige kite kwa nguvu na hapo koo langu likaanza kukauka
taratibu.
Niliendelea kuirudisha nyuma ile picha ya video kwa mara kadhaa hadi pale
ilipozoeleka vizuri machoni mwangu. Mambo yote yalikuwa yakienda sawa kwani
ni kama nilikuwa nimetupa jiwe kichakani na mtu liliyempata alikuwa ameanza
kujitokeza taratibu huku akipiga yowe la maumivu.
Baada ya tukio lile kulikuwa na picha nyingine za video za magari na watembea kwa
miguu zilizonaswa na zile kamera za ile Supermarket na zote zile zilikuwa za kawaida tu. Mwishowe nikamuona tena yule msichana dereva wa lile gari jeupe Corolla limited
akitoka sehemu ya chini ya lile jengo la ghorofa na kuelekea kwenye lile gari ambapo
aliingia kuondoka eneo lile. Nilirudia kuitazama picha ile ya video mara kadhaa kisha
nikapiga hesabu zangu na kujikuta nikitabasamu.
Kwa mujibu wa kumbukumbu na mahesabu yangu ni kuwa lile tukio la mauaji
ya yule mtu lilikuwa limefanyika ndani ya ule muda wa yule dada kuwasili na gari lake
kwenye lile jengo la ghorofa na kuondoka kwake. Niliupitisha ulimi kuzilowanisha
kingo za mdomo wangu huku nikitabasamu. Muuaji amepatikana! hatimaye nilijisemea
moyoni.
Baada ya pale kila nilichoweza nilikifanya kwa haraka. Nilifahamu fika kuwa muda
siyo mrefu polisi makini wangeweza kuifikia kompyuta ile na kupata chanzo kizuri
cha upepelezi wao huku mshukiwa namba moja wa mauaji yale nikiwa mimi. Hivyo
nikazifuta kumbukumbu za picha zote zilizokuwa kwenye ile kompyuta na hapo kazi
ikawa imekwisha.
Nilisogeza kile kiti nyuma yangu na kusimama huku nikiwa nimeridhika na
uchunguzi wangu na hapo nikaliachia tabasamu langu maridhawa likizitongoza hisia
za yule dada wa pale kaunta.
“Nashukuru sana!” hatimaye nilimwambia yule dada.
“Umefanikiwa unachohitaji?” yule dada aliniuliza huku akifurahishwa na uharaka
wangu.
“Bado ila huwenda nikawa nimepata sehemu nzuri ya kuanzia” nilimwambia yule
dada huku nikiitazama saa yangu ya mkononi kisha nikavunja ukimya.
“Nafikiri sasa nipo huru kuondoka ili nikaendelee na majukumu mengine”
nilimwambia yule dada.
“Nakutakia kazi njema” yule dada akaniaga.
“Kazi njema na nyinyi na naomba niwashukuru kwa ushirikiano wenu”
nilimwambia yule dada huku nikizunguka na kutoka ile sehemu ya kaunta. Wale
wafanyakazi wengine wa ile Supermarket walikuwa mbali na eneo lile wakiendelea na
shughuli zao hivyo nikawaaga kwa kuwapungia mkono nao wakafanya vivyo hivyo.
Nilitoka nje ya Supermarket ile huku nikiwa na furaha iliyotokana na mwanzo
mzuri wa kazi yangu. Nilikuwa nimepiga hatua kwani hisia zangu zilinieleza hivyo.
Nikashika uelekeo wa upande wa kushoto wa ile Supermarket huku nikiupachika mche
wa sigara mdomoni na kujiwashia. Muda mfupi baadaye ningekuwa mbali na eneo lile
nikiendelea na harakati zangu.
_____
KAMA SIYO FOLENI YA KUCHUKIZA ya magari katika barabara nyingi za
jiji la Dar es Salaam basi huwenda Fulgency Kassy angekutana na Chaz Siga katika
Supermarket ile. Lakini kwa sasa hilo lisingewezekana kwani muda robo saa baada ya
Chaz Siga kuondoka Fulgency Kassy aliegesha gari lake nje ya Supermarket ile huku
akiwa na uhakika wa chanzo chake cha upelelezi anachokiendea. Kisha akausukuma ule mlango wa ile Supermarket na kuzama ndani huku akipiga mruzi mwepesi wa
furaha.
“Hamjambo vijana?” Fulgency Kassy akawasalimia wale wafanyakazi wa ile
Supermarket ambao walishaanza kulisahau kwa muda lile tukio lililopita muda mfupi
la kutembelewa na kachero aliyejinadi kwa jila la Sajenti Manda Chegwa wa kituo cha
polisi cha mjini kati.
“Hatujambo!” wale wafanyakazi wa ile Supermarket wakamwitikia kwa mshangao
kidogo.
“Mimi ni afisa usalama nahitaji kupitia kamera zenu kama sehemu ya uchunguzi
wa tukio la mauaji lililotokea jana usiku” Fulgency Kassy akajitambulisha huku
akimkabidhi kitambulisho chake yule dada mfanyakazi wa ile kaunta ya Supermarket.
Maelezo yake yakawapelekea wale wafanyakazi mle ndani wageuke na kumtazama
kwa mshangao.
“Kamera zimeshapitiwa na mwenzako aliyetoka hapa muda siyo mrefu” yule dada
wa kaunta akavunja ukimya huku akionekana kukasirishwa na ugeni ule.
“Mwenzangu nani?” Fulgency Kassy akauliza kwa mshangao.
“Sajenti Manda Chegwa wa kituo cha polisi cha mjini kati” maelezo ya yule dada
yakamfanya Fulgency Kassy ashikwe na mshangao huku akikichukua kitambulisho
chake juu ya ile meza na kukitia mfukoni.
“Yupoje?” hatimaye akauliza kwa wasiwasi.
“Mrefu na mweusi mwenye mwili uliyojengeka vizuri” yule dda akafafanua
“Amevaa sare za jeshi la polisi?” Fulgency Kassy akauliza.
“Hapana!”
“Sasa mmemwamini vipi kuwa yeye ni polisi?” hatimaye akauliza kwa jazba
kidogo.
“Kitambulisho chake ni kama chako” yule dada wa kaunta akafafanua na hapo
Fulgency Kassy akaduwaa kidogo kama anayetafakari jambo kabla ya kuvunja ukimya.
“Huyo mwenzangu amefanya makosa hii siyo kesi anayopaswa kuisimamia.
Tafadhali nahitaji kuzipitia kamera zenu“ Fulgency Kassy alisisitiza na hapakuwa na
mtu wa kumzuia. Hivyo akazunguka pale kaunta na muda mfupi uliyofuata alikuwa
nyuma ya screen kubwa ya ile kompyuta iliyounganishwa na ile sistimu ya zile kamera
za usalama akianza upekuzi.
Hata hivyo hakuambulia kitu chochote kwani picha zote zilizonaswa na zile
kamera zilikuwa zimefutwa na zile kamera zilikuwa zimesimamishwa kwa hila ule
unasaji wake wa picha.
Fulgency Kassy kuona vile hisia za kuzidiwa ujanja zikaanza kuutafuna mtima
wake na hapo akajihisi ni kama aliyekuwa akipoteza muda wake bure kwa kutafiti kitu
kisichokuwa na taarifa zozote. Hivyo akasimama pale kwenye kiti na kuondoka bila
ya kuaga.
_____
“MWAMBIE AINGIE NDANI” sauti ya kiume yenye mamlaka iliunguruma
ndani ya chumba kile cha ofisi ya mkuu wa kituo cha polisi cha mjini kati.
Askari wa zamu akafunga mguu kisha akapiga saluti na kugeuka nyuma akielekea
sehemu ulipokuwa mlango wa ofisi ile kuelekea nje. Muda mfupi baadaye askari yule
alirudi eneo la kaunta ya kituo kile cha polisi sehemu alipokuwa amesimama Fulgency
Kassy.
“Pita ndani mlango wa kulia mwisho wa korido” askari yule aliongea huku
akioneka kukerwa na usumbufu ule.
Mara baada ya kutoka kule Supermarket mtaa wa Nkurumah Fulgency Kassy alikuwa
ameamua kuelekea kituo cha polisi cha mjini kati kumtafuta Sajenti Manda Chegwa.
Hivyo majibu ya askari yule wa zamu yakamruhusu kuingia mle ndani ya kile kituo cha
polisi ili kuonana na mkuu wa kituo.
Mlango wa kulia mwisho wa korido ile ulikuwa umempelekea Fulgency Kassy
kuipuuza ile milango mingine ya mle ndani iliyopakana na korido pana inayotazamana
na milango sita.
Mara alipofika mwisho wa korido ile upande wa kulia akauona mlango wa ofisi ya
mkuu wa kituo kile. Kibao cha utambulisho wa cheo chake kilikuwa juu ya mlango
ule. Fulgency Kassy akajitengeneza vizuri koti lake la suti kisha akaanza kubisha hodi.
“Ingia!” sauti nzito ya kiume iliunguruma kutoka mle ndani. Fulgency Kassy
akashika kitasa na kuusukumu ule mlango kisha akaingia mle ndani.
Mzee wa makamo alikuwa ameketi kwenye kiti nyuma ya meza kubwa yenye
lukuki ya majalada,magazeti,mhuri wa ofisi,kidau cha wino na vitabu vya risiti. Juu
ya meza ile pia kulikuwa na kibao kidogo cha utambulisho wa cheo chake na jina la
O.J.Mkwaju Ngoma.
Macho makali ya mzee yule yakafunga safari kumtaza Fulgency Kassy kisha akavua
kofia yake ya kiafande na kupiga mwayo mkali wa uchovu huku akijinyoosha viungo
vyake. Kichwa chake hakikuwa na unywele hata mmoja. Mzee yule alipomaliza kupiga
mwayo akairudisha ile kofia kichwani na kuivua miwani huku akiyafikicha macho
yake. Alipomaliza akaivaa tena ile miwani na kuiegemeza mikono yake mezani.
“Karibu kijana” yule mzee akavunja ukimya huku akimtazama mgeni wake juu ya
ile miwani.
“Nashukuru mzee pole na kazi” Fulgency Kassy akaongea huku akiumba
tabasamu hafifu usoni mwake lakini uso wa yule mzee haukutetereka na badala yake
ulikunjamana kama aliyelamba ndimu.
“Tafadhali keti kijana una shida gani?” mzee yule alisisitiza na hapo Fulgency
Kassy akavuta kiti na kuketi huku akitoa kitambulisho chake cha kazi na kumpa yule
mzee.
Yule mzee mkuu wa kituo akakipokea kitambulisho kile na kukipitishia macho
kwa haraka kabla ya kukirudisha kwa Fulgency Kassy huku sasa akiwa anafahamu
kuwa alikuwa anaongea na mtu wa aina gani mbele yake.
“Karibu sana kijana bila shaka una sababu kubwa ya kutaka kuniona” hatimaye yule mzee akavunja tena ukimya.
“Nimeshakaribia!,naitwa Fulgency Kassy kama kitambulisho changu
kinavyojieleza. Nipo kwenye idara maalum ya usalama wa taifa vilevile ni mjumbe wa
tume ya udhibiti na upambanaji wa biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini”
Fulgency Kassy aliweka kituo kidogo akikohoa kulisafisha koo lake na yule mkuu wa
kituo akabaki akimtazama tu bila tashwishwi yoyote usoni mwake.
“Endelea…” mzee yule akadokeza.
“Nipo kwenye uchunguzi wa kifo cha Guzbert Kojo mwanausalama mwenzetu
aliyeuwawa usiku wa kuamkia leo mtaa wa Nkurumah. Bila shaka ofisi yako ina taarifa
za kifo chake”
“Taarifa tayari zimetufikia na tumeshaanza kuzifanyia kazi”
“Vizuri sana na hilo ndiyo lililonifikisha hapa. Ningependa nifahamu kama vijana
wako watakuwa wamefanikiwa kupata taarifa zozote muhimu kuhusiana na tukio
hilo”
“Hivi tunavyoongea vijana wangu bado wapo kazini hivyo siwezi kukusaidia kitu
chochote kwa sasa” yule mzee mkuu wa kituo kile cha polisi akaongea kwa utulivu
na hapo Fulgency Kassy akaweka kituo akifikiri jambo baada ya kuanza kuhisi kuwa
juhudi zake zilikuwa mbioni kugonga mwamba.
“Upelelezi wa kesi ya mauaji haya unafanywa na nani?” Fulgency Kassy hatimaye
akauliza.
“Vijana wangu”
“Yaani namaanisha majina na vyeo vyao”
“Taratibu za kiofisi haziniruhusu kukuweka bayana”
“Lakini marehemu alikuwa mwanausalama mwenzangu hivyo ni haki yangu
kufahamu nini kinachoendelea juu ya upeleleza wa kifo chake” Fulgency Kassy
akaongea huku akijitahidi kumshawishi mzee yule.
“Kama wewe ni mwanausalama kwanini usifanye upelelezi kivyako na badala yake
unasubiri kuzifanyia kazi taarifa zetu?” mkuu wa kituo kile cha polisi akaongea kwa
jazba. Swali lile likampelekea Fulgency Kassy ashikwe na kigugumizi cha hoja kwa
sekunde kadhaa kabla ya kuvunja tena ukimya.
“Lakini kazi ya upelelezi haina mipaka afande hata wewe inaweza ikatokea siku
moja ukahitaji taarifa fulani kutoka kwangu au kwa mtu yeyote”
Maelezo ya Fulgency Kassy yakampelekea yule mzee mkuu wa kituo kile cha polisi
atabasamu kidogo huku taratibu akivigongesha vidole vyake juu ya ile meza ya ofisini.
“Huoni kuwa hiyo ni sawa kuipeleleza polisi?” yule mzee akauliza kwa utulivu na
hapo Fulgency Kassy akaishiwa hoja badala yake akabaki akiyatembeza macho yake
mle ndani kama anayefikiri jambo fulani na hapo akawa amekumbuka kuuliza.
“Nahitaji kuonana na askari wako aitwaye Sajenti Manda Chegwa”
Mkuu wa kituo kile cha polisi akaweka macho yake kituo akimtazama Fulgency
Kassy kama mgeni asiyekuwa na maongezi ya maana. Kijana handsome mwenye elimu
nzuri iliyomtunuku idadi ya vyeo vingi vyenye mshahara mkubwa zaidi yake pamoja na miaka yake mingi ya kulitumikia jeshi la polisi huku yeye akiambulia cheo chenye
ongezeko dogo la mshahara ikiwa tayari imekwishafika jioni ya umri wake.
“Sina askari yoyote mwenye jina hilo hapa kituoni kwangu” hatimaye yule mzee
mkuu wa kituo cha polisi akaongea kwa utulivu.
“Sajenti Manda Chegwa…!” Fulgency Kassy akasisitiza akidhani mzee yule
hakumsikia vizuri.
“Bila shaka umekosea mlango kijana. Askari wangu wote nawafahamu na hakuna
askari mwenye jina la Sajenti Manda Chegwa. Rudi ukaulize vizuri huko ulipotoka”
yule mzee mkuu wa kituo cha polisi akaongea kwa jazba akionekana kukerwa na ugeni
wa Fulgency Kassy.
“Okay! nashukuru afande” Fulgency Kassy akasimama na kuaga baada ya kuhisi
kuwa hakukuwa na kitu chochote kingine ambacho angekipata kutoka kwa mkuu yule
wa kituo cha polisi.
“Kazi njema” mkuu wa kituo kile cha polisi akaongea huku akimsindikiza
Fulgency Kassy kwa macho hadi pale alipofungua mlango wa ofisi ile na kutoka nje na
hapo akashusha pumzi taratibu huku akiitikisa miguu yake. Fulgency Kassy alikuwa
amekwishatokomea mbele yake.
MIAKA KUMI ILIYOPITA
RIPOTI YA DAKTARI BINGWA wa magonjwa ya akili ama Brain disorders
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Saalam ilikuwa imetoka na kile
kinachosemekana kuwa ni majibu ya uchunguzi wa kina wa kitabibu.
Matokeo ya taarifa hizo za uchunguzi yalikuwa yamerejesha ombwe la furaha
kwa baadhi ya watu waliofika hospitalini hapo pamoja na daktari husika aliyesimamia
mchakato mzima.
Hata hivyo kwa namna moja au nyingine bado ilikuwa ni taarifa mbaya na siyo
kwa mgonjwa tu pekee lakini hata kwa jamii iliyokuwa ikimfahamu vizuri wakili
mashuhuri wa kujitegemea Advocate Makundi. Ambaye wakati huu alikuwa amelazwa
wodini huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa mikanda maalum ya
kitanda cha wagonjwa wa akili huku kumbukumbu za matukio yote ya nyuma zikiwa
zimetoweshwa katika fikra zake.
Akijivunia taaluma yake,hesabu ya umri wake duniani ilikuwa miaka hamsini na
mbili. Mwanaume mrefu,mweusi mwenye sura isiyovutia sana lakini macho yake
makubwa yaliyojificha nyuma ya miwani yake yenye lenzi kali yakiwa yamehifadhi
kumbukumbu ya taswira mbalimbali za kutisha na kufurahisha. Uso wake
mwembamba wenye pua yenye matundu makubwa na ndevu zilizotakiwa vizuri
viliongeza haiba katika mwenekano wake.
Kwa mara ya mwisho kabla ya kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi kwa wahusika
alikuwa ameingia tena kwenye chumba hiki cha wodi maalum ya siri kufuatilia
maendeleo ya mgonjwa wake. Mtu mashuhuri na wakili wa kijitegemea Advocate Mkundi.
Hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia kwenye wodi hii isipokuwa yeye na madaktari
wenzake wachache ambao walikuwa na kazi maalum za kiusalama.
Dr.Nungu alimaliza kusoma majibu ya uchunguzi wa kitabibu kutoka kwenye
kompyuta yake juu ya meza wodini mle kisha akaprint karatasi kadhaa na kuzibana
kwa pini maalum za ofisi.
“Kazi kwishnei” akajisemea moyoni huku akipiga mruzi mwepesi na hafifu
wenye kuashiria furaha ya mafanikio. Alipomaliza akakisogeza kiti chake nyuma na
kusimama halafu akaanza kupiga hatua zake taratibu kukiendea kitanda cha mgonjwa
alicholazwa Advocate Makundi.
Kupitia mashine maalum ya kupumulia itumikayo kusukuma hewa ya Oksijeni
kwa mgonjwa na kuonesha mwenendo mzima wa mapigo ya moyo wake ilimueleza
kuwa mgonjwa wake alikuwa akiendelea vizuri na endapo mambo yangeendelea vile
basi siku chache baadaye angerudiwa na fahamu na kujionea taratibu za duniani.
Kwa kutaka kujiridhisha zaidi Dr.Nungu akakivua kifaa chake cha kupimia mapigo
ya moyo ya mgonjwa kiitwacho Stetheskopu. Vishikio vya kifaa kile akavitumbukiza
masikioni kwake na kule mwishoni akakuweka juu ya kifua cha Advocate Makundi.
Alichokisikia kupitia kifaa kile kikimfanya atabasamu kama siyo kuangua kicheko
hafifu. Pasipo kupoteza muda akakichukua tena kile kifaa na kukivaa shingoni na
kule mwishoni mwa kile kifaa akakutumbukiza kwenye mfuko wa mbele wa koti
lake la kidaktari. Kisha akamfunika vizuri mgonjwa wake na kuanza safari ya taratibu
kuelekea sehemu ulipokuwa mlango wa kutokea nje ya wodi ile ya siri.
Kofia yake ya kitabibu bado ikiwa kichwani mara tu alipotoka nje ya wodi ile
Dr.Nungu akavua glovu zake nyeupe za mpira na kuzitupa kwenye ndoo ndogo ya
taka ama dustbin ya njano iliyokuwa kando ya mlango ule halafu akaanza kutembea
kwenye korido pana ya hospitali ile akielekea ofisini kwake.
“Tumekusubiri kwa muda mrefu sana hadi tukaanza kukata tamaa” sauti kutoka
nyuma ikamshtua Dr.Nungu wakati alipokuwa akiendelea kuzitupa hatua zake
zinazopwaya na hapo akageuka nyuma kumtazama yule mtu aliyekuwa akimsemesha.
Wasiwasi ukamtoweka pale alipowaona vijana watatu aliokuwa akiwafahamu nyuma
yake.
Pweza,kijana mrefu,mweusi mwenye mwili imara uliyojengeka kwa ratiba nzuri
ya mazoezi ya viungo na macho tulivu yasiyo na huruma. Fulgency Kassy,kijana wa
miaka thelathini na mbili,mrefu na mwenye mwili mkubwa na sura ya uviringo yenye
bashasha za kirafiki lakini hatari na makini. Na wa mwisho alikuwa Kombe,yeye
mfupi kidogo zaidi ya wenzake,maji ya kunde kwa rangi ya ngozi yake,mtu asiye na
maneno mengi,hatari na mwenye uso tulivu lakini asiyependa mzaha.
“Oh! kumbe ni nyinyi” Dr.Nungu akawasabahi kwa kuwapa mikono huku uso
wake ukiumba tabasamu hafifu.
“Pole na kazi dokta” Pweza akaongeza huku akimpa mkono Dr.Nungu.
“Ahsanteni sana vijana!. Kwa kweli hii kazi ya utabibu inahitaji mtu uwe na wito vinginevyo mgonjwa wa kichwa utamfanyia operesheni ya mguu na yule wa mguu
utamfanyia operesheni ya kichwa kama siyo kusahau mkasi na vifaa vingine vya
kitabibu kwenye tumbo la mgonjwa” Dr.Nungu akachangamsha maongezi huku
akiwatazama vijana wale kwa udadisi.
“Vipi kazi inaendeleaje?” Kombe akadakia.
“Twendeni ofisini kwangu hapa siyo mahala pake” Dr.Nungu akawatahadharisha
na hapo vijana wale wakatazamana kabla ya kuanza kuongozana na Dr.Nungu
wakielekea ofisini kwake.
Mwisho wa korido ile wakaingia upande wa kushoto wakiifuata korido nyingine
inayotazamana na milango ya wodi nne zilizoongozana ambazo milango yake ilikuwa
wazi na hivyo kuwaruhusu kuona mle ndani bila pingamizi. Wagonjwa waliokuwa
wakitaabika na magonjwa yao walikuwa wamepumzika vitandani huku wakingoja
hatima zao.
Wodi ya mwisho ilipakana na korido fupi na pana kwa upande wa kulia. Mara
walipoingia kwenye korido ile ofisi ya Dr.Nungu ilikuwa mwishoni ikitazamana na
korido ile na kwa upande wa kulia na kushoto ilipakana na chumba cha bohari ya
madawa,stoo ndogo ya vifaa vya usafi na sehemu ya maliwato.
“Karibuni mketi vijana” Dr.Nungu aliwakaribisha wale vijana ofisini kwake
mara baada ya kufungua mlango huku yeye akizunguka na kwenda kuketi kwenye
kiti chake nyuma ya meza pana yenye kompyuta moja,mlima wa vitabu vya elimu ya
kitabu,kibeseni kidogo cha majivu ya sigara,majalada ya wagonjwa,mhuri na kidau cha
wino.
Mandhari ya ofisi ile yalijieleza yenyewe kuwa ilifaa kuitwa ofisi ya daktari bingwa
wa magonjwa ya akili kwani ukutani kulikuwa na rafu zenye vitabu na majalada mengi
yaliyoshika vumbi. Pia kulikuwa na picha kubwa zilizotundikwa ukutani zikionesha
sehemu mbalimbali za ubongo wa binadamu pamoja na maumbo tofauti za mifano
yake.
Mara tu alipoketi Dr.Nungu akachukua pakiti ya sigara kutoka kwenye mtoto
wa meza yake na kuanza kuitembeza kwa wale wageni wake huku akimtaka kila
mmoja achukue sigara. Hata hivyo hakuna aliyechukua sigara zile huku wote wakitoa
visingizio kuwa hawakuwa na kiu nazo kwa wakati ule. Hilo halikumkatisha tamaa
Dr.Nungu badala yake akaugonga ule mdomo wa ile pakiti na sigara moja ilipojitokeza
na kuchungulia juu akainama na kuibana kwa kingo za mdomo wake. Halafu baada
ya hapo ile pakiti ya sigara akaitupia pale juu mezani na kwa msaada wa kiberiti
chake cha gesi kilichokuwa mfukoni akajiwashia ile sigara na kuanza kuivuta taratibu
huku akiyatembeza macho yake kuwatazama wale vijana kama ambaye anawasoma
mawazo yao.
“Ondoeni shaka vijana,kazi imekwisha” Dr.Nungu alipoitoa sigara yake mdomoni
akavunja ukimya. Maisha bila sigara kwake ilikuwa ni sawa na gari bila mafuta. Alikuwa
mvuta sigara mahiri kabisa ama Chain smoker na bila kuvuta sigara asingeweza kuifanya
kazi yake ya kitabibu kwa umakini,na hayo ndiyo yaliyokuwa mazoea yake.Wale vijana wakasogea karibu ili wamsikie huku kila mmoja akimtathmini kivyake.
Msomi na daktari bingwa anayevijua vyanzo tofauti vya magonjwa lakini anayateketeza
taratibu mapafu yake yasiyo na spea huku akiifungulia mlango saratani ya koo.
“Vipi hali yake?” Pweza akavunja ukimya na kuuliza.
“Anasumbuliwa na ugonjwa uitwao Amnesia. Mmewahi kuusikia popote?”
Dr.Nungu akawauliza katika namna ya kujivunia taaluma yake huku akiyatembeza
macho yake kuwatazama wale vijana moja baada ya mwingine. Wale vijana
hawakuzungumza chochote kwani Amnesia kwao ulikuwa bado ni msamiati mpya.
Ukimya wa wale vijana ukampelekea Dr. Nungu alisogeze lile kabrasha la ripoti
yake alilotokanalo kule wodini na kuliweka pale mezani mbele yake kisha akafunua
ukurasa wa kwanza na kuvunja ukimya.
“Amnesia!,huu ni ugonjwa wenye maana kwa lugha ya kiingereza ’…a without
memory’ au kwa tafsiri ya lugha ya kiswahili ni ‘…bila ya kumbukumbu’.
Huu ni ugonjwa wa binadamu kupoteza kumbukumbu. Ugonjwa huu unaweza
kusababishwa na hitilafu katika ubongo,magonjwa sugu au maumivu ya kisaikolojia.
Ugonjwa wa Amnesia pia unaweza kusababishwa kwa muda tu kutokana na
matumizi mbalimbali ya Sedatives au madawa ya kumeza ya binadamu yenye lengo la
kupunguza ufanyaji kazi wa ubongo. Kwa mfano madawa ya binadamu yenye lengo
la kuleta usingizi kwa wagonjwa wenye maumivu makali au wale wenye matatizo
ya kutopata usingizi kwa muda mrefu pamoja na yale madawa yatumikayo kwenye
shughuli za operesheni kwa wagonjwa mbalimbali ama kwa lugha ya kitaalam Surgical
Anesthesia.
Kitu cha muhimu kufahamu ni kuwa Amnesia ni ugonjwa wa upotevu wa
kumbukumbu katika ubongo wa binadamu. Upotevu huu wa kumbukumbu
unaweza ukawa ni upotevu wa kumbukumbu zote kwenye ubongo au sehemu tu ya
kumbukumbu hizo na hali hii hutegemeana na kiasi cha uharibifu kilichosababishwa
kwenye ubongo huo” Dr.Nungu akaweka kituo akikohoa kidogo kisha akautia
mche wake wa sigara mdomoni na kuuvuta taratibu huku akiyatembeza macho yake
kuwatazama wageni wake katika namna ya kufanya tathmini kama maelezo yake
yalikuwa yakiwaingia vizuri. Alipotoa sigara mdomoni akaendelea
“Kuna aina mbili za ugonjwa wa Amnesia na aina hizi mbili zinatambulika kwa
lugha ya kitaalam kama Retrograde amnesia na Anterograde amnesia.
Tukianza na Retrograde amnesia. Hii ni aina ya ugonjwa wa Amnesia ambayo
mgonjwa hushindwa kurudisha kumbukumbu ambazo zilikuwepo kabla ya tarehe
husika ya upotevu wa kumbukumbu hizo. Aina hii ya Amnesia inaweza kusababishwa
na kutokea kwa ajali mbaya au operasheni ya kitabibu kwa mgonjwa husika. Na katika
mazingira fulani ya potevu wa kumbukumbu hizo unaweza kuwa ni kwa kipindi cha
miongo kadhaa nyuma huku mtu mwingine anaweza kupoteza kumbukumbu hizo
kwa muda wa miezi michache tu” Dr.Nungu akaweka tena kituo na kuutia mche wake
wa sigara mdomoni huku akiivuta sigara hiyo kwa madaha na kuupuliza moshi wa
sigara ile akiutoa taratibu kwenye pembe ya mdomo wake. Wale vijana wakayatuliza macho yao wakimtazama lakini hakuna aliyetia neno. Dr. Nungu alipoitoa sigara yake
mdomoni akaendelea
“Anterograde ni aina ya pili ya Amnesia ambayo hutokea pale ubongo wa mtu
unaposhindwa kuhamisha kumbukumbu kutoka kwenye uhifadhi wa kumbukumbu
wa muda mfupi short-term store kwenda kwenye uhifadhi wa kumbukumbu wa muda
mrefu long-term store. Wagonjwa wengi wa aina hii ya Amnesia hawawezi kukumbuka
matukio kwa muda mrefu. Aina hizi mbili za Amnesia huwa hazitegemeani hivyo zote
zinaweza kumtokea mgonjwa kwa wakati mmoja.
Kwa watu wanaosumbuliwa na Amnesia uwezo wa kurudisha kumbukumbu
haraka bado upo na vilevile wanaweza kutengeneza kumbukumbu mpya ingawa
upungufu mkubwa wa kujifunza vitu vipya na kurudisha kumbukumbu za zamani
unatakiwa utazamwe kwa umakini sana. Wagonjwa wanaweza pia kujifunza taratibu
mpya za ujuzi.
Mbali na hayo wagonjwa wa Amnesia pia wanaweza kubakiwa na kumbukumbu
toshelevu za mambo waliyojifunza,lugha,ujuzi mwingine wa kijamii ingawa hilo
huchukua kipindi kirefu cha kujikumbusha” Dr.Nungu akaweka kituo akikohoa
kidogo mara hii akiwatazama wageni wake katika hali ya juu ya tathmini juu ya kile
alichokuwa akikiongea. Alichokiona kwenye macho ya vijana wale ni kuwa somo lake
lilikuwa limeeleweka hata hivyo akahisi kuwa alikuwa amezama sana katika maelezo
kitaalam zaidi kuliko kile walichokuwa wakitarajia kukisikia. Hivyo akapanga kubadili
mtindo wa maelezo yake.
“Advocate Makundi anasumbuliwa na ugonjwa wa Amnesia. Sasa nadhani
mmeanza kunielewa vizuri” Dr.Nungu aliweka tena kituo huku akiivuta sigara yake
taratibu lakini safari hii hakuwatazama wageni wake. Wale vijana wakatikisa vichwa
vyao kuonesha kukubaliana na kile anachokizungumza. Dr.Nungu alipoitoa sigara
mdomoni akaendelea.
“Aina ya Amnesia anayougua Advocate Makundi ni Retrograde amnesia ambayo kama
nilivyokwisha waeleza hapo awali ni kuwa mgonjwa wa aina hii huwa anashindwa
kurudisha kumbukumbu za matukio yote ya nyuma kabla ya ile tarehe ya tukio
lililopelekea kuugua Amnesia. Hivyo mgonjwa wa namna hii huwa anaweza kuwa na
kumbukumbu mpya tu zilizotengenezwa baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Retrograde amnesia mara nyingi husababishwa na Head trauma ama msongo
mbaya wa mawazo kichwani ama Brain damage. Yaani uharibifu katika ubongo hasa
katika sehemu za ubongo zilizopo pembeni ya eneo lijulikanalo kama Hippocampus.
Hippocampus ni sehemu inayohusika na upelekaji wa taarifa mpya.
Uharibifu huo katika ubongo mara nyingi husababishwa na head trauma,ajali katika
mishipa ya ubongo iitwayo Cerebrovascular stroke au kuharusi,hypoxia,encephalitis ambayo
ni mambo ya kitaalam zaidi pamoja na unywaji wa pombe wa kupita kiasi au ulevi
sugu.
Watu wanaougua Retrograde amnesia wanaweza kukumbuka maarifa ya kiujumla
kuliko maarifa maalum ama kwa lugha ya kitaalam specific knowledge. Pia ni vigumu kwa wagonjwa wa namna hii kukumbuka haraka yale matukio yaliyofanyika kwa kipindi
cha muda mfupi uliyopita. Hata hivyo kumbukumbu za matukio ya nyuma zinaweza
kurudi taratibu baada ya kipindi kirefu sana kupita.
Retrograde amnesia hata hivyo ni hali itokeayo kwa kitambo tu cha muda na siyo
hali ya kudumu. Hivyo mgonjwa anaweza kutibiwa kwa kukumbushwa taratibu
juu ya yale matukio aliyoyasahau. Hata hivyo hili ni zoezi la muda mrefu linaloweza
kuchukua masaa,siku,wiki,miezi na miaka katika kuhamisha taarifa kutoka kwenye
hippocampus kwenda kwenye eneo la uhifadhi wa kumbukumbu za kudumu liitwalo
cortex” Dr.Nungu akaweka kituo tena safari hii akiwatazama kwa makini wageni wake
huku sigara ikiendelea kuteketea kwenye pacha ya vidole vyake.
“Advocate Makundi anaugua aina hii ya Amnesia na kwa mujibu ya maelezo yangu
ya hapo awali tatizo lake linaonekana kuwa limetokana na kupigwa na kitu kizito mara
kadhaa nyuma ya kichwa chake kwenye sehemu ya ubongo wa nyuma iitwayo Medula
Oblangata” Dr.Nungu akaweka kituo na kuitia tena sigara yake mdomoni na kuivuta
taratibu huku akiuachia mwili wake ustarehe kwenye foronya laini ya kiti chake cha
ofisini. Wale vijana wakageuka na kutazamana kidogo huku wakionesha nyuso za
furaha na hapo wakageuka na kumtazama Dr.Nungu.
“Tulihitaji afe kabisa kwani hilo ndiyo lililokuwa lengo letu” Fulgency Kassy
akavunja ukimya
“Hakuna haja!” Dr.Nungu akaongea huku akitikisa kichwa chake kuonesha
kutokukubaliana na wazo lile.
“Hii ni amri ya kutoka juu” Pweza alidakia.
“Nafahamu lakini sidhani kama kuna haja ya kufanya hivyo. Advocate Makundi
kwa sasa hana kumbukumbu zozote. Ubongo wake ni sawa simu mpya isiyokuwa
na line. Atakapozinduka nitamuanzishia dozi ya pombe kali na hayo ndiyo yatakuwa
maisha yake kuhakikisha kuwa hakuna kitu anachokikumbuka yaani kama msukule”
Wale vijana wakacheka kwa furaha huku wakitikisa vichwa vyao.
“Una hakika kuwa Advocate Makundi hatoweza kurudiwa tena na fahamu zake?”
Kombe akauliza kwa utulivu.
“Kasi yangu siyo ya kubahatisha kijana na ndiyo maana ninaitwa daktari bingwa wa
magonjwa ya akili. Ninapouharibu ubongo wa binadamu huwa namaanisha uharibifu
hivyo kupona kwake labda miujiza itokee na nyinyi ni mashahidi kuwa dhambi za
binadamu wa kizazi hiki zinazidi kuifukuzia mbali miujiza ya Mungu” Dr.Nungu
akaweka kituo kisha akautia tena mche wake wa sigara mdomoni na kuuvuta taratibu.
“Mimi sina mashaka kabisa na kazi yako” Pweza akaongea kwa utulivu na
kumfanya Dr.Nungu atabasamu hali iliyoyapelekea meno yake yenye ukungu wa
moshi wa sigara kuonekana vizuri.
“Kuna kitu gani kinachoendelea nyuma ya Advocate Makundi?” hatimaye
Dr.Nungu akavunja ukimya huku akiwatazama wale vijana.
“Ni itifaki tu imezingatiwa” Fulgency Kassy akaongea huku akitabasamu.
“Una maana gani?” Dr. Nungu akauliza huku akiwatazama wale vijana mmoja baada ya mwingine.
“Huyu Advocate Makundi ni bonge la fala” Pweza naye akadakia huku akiangua
kicheko hafifu.
“Mbona siwaelewi?” Dr.Nungu akauliza huku ameshikwa na mshangao.
“Advocate Makundi anajidai mwanaharakati na amekuwa akionywa mara kadhaa
lakini ameshikilia msimamo wake. Sasa kinachomtokea sasa hivi ni stahili yake”
Kombe akaendelea
“Baadhi ya vigogo wameamua kumuazimia na hiki kinachofanyika kwa sasa ni
kumziba mdomo vinginevyo harakati zake angejikuta anazifanyia kuzimu” Pweza
akaongea kwa kujiamini.
“Amefanyaje?” Dr.Nungu akaendelea kuuliza akionekana kutoelewa kile
kinachoendelea kwa vijana wale.
“Advocate Makundi amekuwa akiisimamia kesi cha Mtenzi Binagwa bila shaka
unamkumbuka!” Fulgency Kassy akaongea kwa utulivu huku akimtazama Dr.Nungu
kwa utulivu.
“Mtenzi Binagwa!mwandishi wa habari?” Dr.Nungu akauliza
“Huyo huyo” Pweza akadakia
“Kwani imekuwaje?” Dr.Nungu akauliza kwa mshangao.
“Mtenzi Binagwa anao ushahidi wote unaoweza kuwatia vigogo hatiani na lengo
lake lilikuwa ni kufanya hivyo. Vigogo wakaamua kumfuata kimyakimya na kuongea
naye kabla hajalilipua bomu lakini kijana akashikilia msimamo wake. Hatukuwa na jinsi
zaidi ya kuyageuza mashtaka yamgeukie yeye mwenyewe. Mipango ikatengenezwa
akabambikiwa kesi ya mauaji yenye ushahidi wa kupikwa ambayo itamsotesha miaka
kumi na tano akiwa mahabusu wakati huo kigezo cha upelelezi wa kesi yake kuwa
unaendelea kitakuwa kikitumika na atakapopandishwa kizimbani hukumu yake ni
kifungo cha maisha” Fulgency Kassy alimaliza kuongea huku akiviminyaminya vidole
vyake mkononi.
“Mtenzi Binagwa kwa sasa yupo wapi?” Dr. Nungu akauliza.
“Kwenye chumba kidogo chenye kuta nne cha gereza la Segerea” Fulgency Kassy
akaongea huku akitabasamu kidogo.
“Advocate Makundi naye anaingiaje katika suala hili?”
“Advocate Makundi ni wakili wa mwandishi wa habari Mtenzi Binagwa. Sasa
baada ya Mtenzi Binagwa kufumbwa mdomo Advocate Makundi akaibuka na
kudai kuwa mteja wake ameonewa huku akiahidi kutoa vielelezo vyote juu ya kile
kilichokuwa kikiendelea na kuahidi kukata rufaa”
“Hatukuwa na namna ya kufanya zaidi ya kumuwahi Advocate Makundi kabla
hajatimiza lengo lake” Pweza akadakia.
“Sasa mmefanikiwa kupata chochote kutoka kwa Advocate Makundi?” Dr.Nungu
akauliza kwa utulivu huku akiivuta sigara yake.
“Amekataa kabisa kutupa ushirikiano hivyo tukaamua kutumia Plan B,” Kombe
akaongea huku akitabasamu.
“Basi tambueni kuwa kazi imekwisha na msiwe na wasiwasi tena” hatimaye Dr.
Nungu akaongea baada ya kuitoa sigara yake mdomoni.
“Mkuu atafurahi sana kusikia habari hizi,” Pweza akaongea huku akivigongesha
vidole vyake pale juu ya meza.
“Naomba mnifikishie salamu zangu kwake kuwa asiwe na wasiwasi kwani kazi
yangu haina mashaka,” Dr. Nungu akaongea kwa furaha kabla ya kuendelea
“Sasa nafahamu kipi kinachoendelea. Kupambana na huu mtandao ni hatari sana
na ni vigumu kufanikiwa kwani ni sawa na kuanza safari ya kulipa kisasi ambapo
msafiri hulazimika kuchimba makaburi mawili. Kaburi moja kwa ajili yake mwenyewe
na jingine kwa ajili ya adui”
Wale vijana wakaangua kicheko huku wakionekana kufurahishwa na maongezi
yale.
“Nini kinachofuata baada ya hapa?” Fulgency Kassy akauliza kwa utulivu.
“Advocate Makundi atakapozinduka nitamfahamisha mkewe aje kumchukua
kwani hakuna cha zaidi,” Dr.Nungu akaongea huku akiivuta sigara yake taratibu na
kuwafanya wale vijana watazamane kwa furaha.
Ripoti ya Dr. Nungu ilikuwa amewafurahisha sana vijana wale hivyo hatimaye
wakasimama na kuichukua ripoti ile juu ya mezani huku wakishikana mkono na
kuagana na Dr.Nungu.
“Kazi njema mkongwe” wote wakaaga.
“Kazi njema na ninyi pia” Dr. Nungu akaongea kwa utulivu.
Kisha Fulgency Kassy, Pweza na Kombe wakafungua mlango wa ofisi ile na kutoka
nje huku kila mmoja akivuta picha ni kwa namna gani ripoti ile itakavyopokelewa kwa
furaha na mkuu wao.
Dr. Nungu aliendelea kuvuta sigara nyuma ya ile meza yake ya ofisini huku
akiwatazama vijana wale wanausalama namna walivyokuwa wakitokomea mbele yake
kisha akaitundika miguu yake juu ya ile meza na kuanza kubembea taratibu kwenye
kiti chake cha ofisini.
“
ANGALAU NIMEPUNGUZA HISIA ZANGU” Koplo Tsega alijisemea
moyoni baada ya mjadala mkubwa kumalizika nafsini mwake. Matukio ya jana
usiku yalikuwa yamemuacha hoi kwa uchovu baada ya kugaragazwa na kupindwa
katika kila namna ya mkao na mwanaume shababi mfanyakazi wa hoteli ile aliyelala
naye usiku kucha.
Tangu aliposalitiwa na mpenzi wake Koplo Tsega alikuwa ameapa kutojihusisha
tena na mapenzi katika maisha yake lakini hilo lilikuwa gumu kutekelezeka. Hisia
zikakataa kabisa kukubaliana na akili yake hivyo mapenzi akayageuza na kuyafanya
kama starehe nyingine ambapo angeyatafuta na kuyafanya na mwanaume yeyote yule
ambaye angekuwa na vigezo vyake na baada ya hapo kila mtu angeshika hamsini zake.
Usiku wa jana aliporudi kwenye hoteli ile aliyofikia iliyopo nyuma ya stendi kuu ya
mabasi yaendayo kasi eneo la Ubungo Koplo Tsega aliingia kwenye eneo la mgahawa
wa hoteli na kujipatia mlo wa nguvu kisha akashushia na kinywaji baridi huku akili
yake ikitafakari matukio yaliyopita.
Akiwa kwenye mgahawa ule akajikuta akikumbuka zile kukurukakara zilizotokea
kule nyumbani kwa Guzibert Kojo huku akijaribu kuwaza ni kwa namna gani polisi
na vyombo vya habari vitakavyolichukulia tukio lile. Akiwa katikati ya tafakari ile mara
akajikuta akimkumbuka yule mtu aliyekuwa akimfuatilia usiku wa jana tangu alipotoka
kule Vampire Casino huku akijiuliza kuwa mtu yule alikuwa nani na alikuwa akihitaji
nini kutoka kwake.
Halafu mawazo yake yakatoweshwa na taswira ya kijana mzuri handsome mhudumu
wa hotelini pale. Kijana mrefu na mweusi mwenye sura nzuri,kifua kipana kiasi chenye
misuli imara na macho ya huruma huku akiwa katika sare zake za kazi akiwahudumia
wateja.
Kijana yule alipokuwa akiinama ili aondoe vyombo na kusafisha meza aliyoketi Koplo Tsega. Koplo Tsega akabahatika kukiona kifua imara cha kijana yule
kilichohifadhiwa vyema ndani ya singlet yake nyeupe. Kukiona kifua cha kijana yule
hisia za mapenzi zikaanza kuitongoza nafsi yake na kujikuta akianza kumtamani
huku manukato yenye harufu nzuri ya kijana yule yakiziteka kabisa hisia zake. Kiu ya
mapenzi ikiwa imemnasa vilivyo Koplo Tsega akaamua kuvunja ukimya.
“Pole na kazi” Koplo Tsega akamwongelesha yule kijana wakati alipokuwa
akimalizia kufuta ile meza.
“Ahsante! dada yangu” kijana yule akaitikia kwa bashasha zote za kirafiki huku
akifikiria Tip ya mteja.
“Hivi wifi yangu akikuona unafanya kazi hizi si atakasirika?” Koplo Tsega
akachombeza utani.
“Ah! wapi mwanamke gani wa nyakati hizi utakayempata kwa mshahara wa
hotelini” yule kijana akaangua kicheko hafifu huku akiendelea kufuta ile meza aliyoketi
Koplo Tsega kwenye mgahawa ule.
“Kwa hiyo hujaoa wewe?” Koplo Tsega akauliza kwa sauti ya kubembeleza.
“Hao wasichana wenyewe wa kuoa wako wapi dada yangu. Sasa hivi kila msichana
unayemgusa hapa mjini anataka maisha mazuri utasema sisi wanaume hatuyataki hayo
maisha mazuri” yule kijana akaongea huku akionekana kufurahishwa na maongezi
yale. Ukimya kidogo ukapita kisha Koplo Tsega akavunja ukimya akimuuliza yule
kijana
“Unaitwa nani?”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Mimi?” yule kijana akauliza kwa haya huku akijua fika kuwa ni yeye ndiye
aliyekuwa akiongeleshwa halafu walipotazamana akaachia tabasamu maridhawa
lililozidi kumchanganya vibaya Koplo Tsega.
“Naitwa Sikawa”
“Mh! jina lako tamu kama asali” Koplo Tsega akaongea huku akijitahidi kuilegeza
sauti yake ya kiafande.
“Acha utani dada yangu tangu lini jina la mtu likawa tamu kama asali” Sikawa
akaongea huku akiangua kicheko chake hafifu lakini kilichopeleka ujumbe kwa Koplo
Tsega kuwa yupo tayari kwa hatua inayofuata.
“Au hupendi nikusifie kuwa wewe ni mzuri?”
“Mh! hata sijui nisemeje dada yangu” Sikawa akaongea katika mazingira ya
kuruhusu urafiki kisha kitambo kifupi cha ukimya kikapita kabla ya Koplo Tsega
kuvunja tena ukimya.
“Utatoka kazini saa ngapi?”
“Saa nne usiku baada ya mwenzangu anayenipokea zamu kufika” Sikawa akaongea
kwa utulivu.
“Unaishi wapi hapa Dar es Salaam?”
“Nimepanga chumba mtaa wa mama Ngoma eneo la Mwenge” Sikawa akaongea
kwa utulivu huku akishindwa kuelewa muelekeo wa maongezi yale.
“Unaishi na nani?” Koplo Tsega akazidi kumdadisi Sikawa.
“Naishi peke yangu” Sikawa akaongea kwa utulivu huku akiutathmini uzuri wa
Koplo Tsega mbele yake.
“Usijali siku moja utampata mwenza wako. Mimi nipo chumba namba 18
ghorofa ya pili. Utakapotoka kazini kama hutojali unaweza kuja chumbani kwangu
tukabadilishana mawazo” Koplo Tsega akaongea kwa sauti ya kubembeleza kiasi cha
kuzivuruga hisia za Sikawa na kumfanya atabasamu.
“Sawa nitajitahidi” hatimaye Sikawa akaukubali mwaliko wa Koplo Tsega huku
akimaliza kufanya usafi juu ya ile meza na kuondoa vyombo kisha akaondoka na
kuelekea dirisha la jikoni.
Koplo Tsega akamsindikiza Sikawa kwa macho hadi pale alipotoweka mbele
yake huku wazimu wa mapenzi ukizitaabisha vibaya hisia zake. Kisha akasimama na
kuanza kuzitupa hatua zake za shibe kivivuvivu kuelekea chumbani kwake ghorofa
ya pili ya hoteli ile.
Tangu tukio la kifo cha Guzbert Kojo,Koplo Tsega alikuwa ameamua kutojitokeza
mitaani kwa muda wa siku mbili au zaidi huku akisubiri mambo yatulie kwanza.
_____
SAA TATU NA NUSU USIKU ILIPOTIMIA Koplo Tsega aliamka kutoka
kitandani alipokuwa amelala kwa muda wa masaa kadhaa akiupunguza uchovu.
Mawazo yake yalipotulia akamkumbuka Sikawa na hapo akageuka kuitazama saa
iliyokuwa imetundikwa ukutani mle chumbani. Muda mfupi baadaye alitarajia kuusikia
mlango wa chumba chake ukigongwa na Sikawa kuingia mle ndani. Hivyo akaamka
na kutandika kitanda chake vizuri kisha akawasha runinga iliyokuwa mle chumbani
juu ya meza fupi iliyokuwa kwenye kona na kuweka stesheni yenye muziki laini wa
kubembeleza.
Alipomaliza akapiga simu eneo la mapokezi na kuagizia mzinga mmoja wa
kinywaji kikali ambao wangeutumia kwa pamoja kusindikiza maongezi yao. Mzinga
huo wa pombe kali ulipoletwa na mmoja wa wahudumu wa hoteli ile Koplo Tsega
akaupokea na kuuweka juu ya meza fupi ya kioo iliyokuwa pembeni ya kochi moja la
sofa lililokuwa mle ndani pamoja na bilauri mbili kisha akaelekea bafuni kuoga.
Sikawa alikuwa ni kijana aliyekuwa akipapatikiwa sana na wanawake kutokana na
sura nzuri aliyokuwa nayo,umbo lake refu lenye kifua kipana kiasi,utanashati na tabia
yake ya ucheshi. Kwa vigezo hivyo wasichana warembo walimpenda na ama kwa
hakika alijua kucheza vizuri na hisia zao. Hivyo kwa haraka sana alikuwa ameitambua
shida ya Koplo Tsega na kwa kweli hakutaka bahati ile impite hivi hivi.
Uzuri wa Koplo Tsega ulikuwa umezikoroga vibaya hisia zake za mapenzi kiasi
kwamba kila wakati alijihisi ni kama alikuwa akimuona Koplo Tsega mbele yake. Kwa
tathmini yake ni kuwa wasichana wazuri na warembo wa sampuli ya Koplo Tsega
walikuwa wachache sana jijini Dar es Salaam na wengi wao walikuwa wakiwapenda
wanaume wenye pesa. Hivyo Sikawa akajiona ni kijana mwenye bahati sana kwa
kualikwa chumbani kwa Koplo Tsega. Akaendelea kufanya kazi zake kwa furaha huku mara kwa mara akipiga mruzi mwepesi mdomoni bila wafanyakazi wenzake
kufahamu kitu kilichokuwa kikiendelea wakati huo akiomba masaa yasogee mbele.
Ilipofika saa nne usiku Sikawa alikuwa nje ya mlango wa chumba namba 18 cha
hoteli ile ghorofa ya pili akigonga mlango.
“Karibu” sauti myepesi ya Koplo Tsega kutoka ndani ya chumba kile ikamfanya
Sikawa ajitengeneze vizuri. Wakati huu alikuwa amevaa nguo zake za uraiani;fulana
nyeupe,suruali nyeusi ya jeans na raba nyepesi miguuni.
Mlango wa chumba ulipofunguliwa Sikawa akajikuta akitazamana na macho laini
ya Koplo Tsega akiwa amejifunga kanga laini kifuani iliyolishika vema umbo lake
katika baadhi ya maeneo kutokana na ubichi wa mwili wake kwani ndiyo alikuwa
anatoka kuoga.
“Karibu ndani Sikawa,utanisamehe kidogo kwani ndiyo nilikuwa natoka kuoga”
Koplo Tsega akaongea kwa sauti laini ya kubembeleza huku tabasamu lake maridhawa
likielea usoni mwake.
“Oh! samahani kwa usumbufu bila shaka nimewahi sana” Sikawa akajibaraguza
huku akiingia mle ndani na wakati akifanya hivyo harufu nzuri ya sabuni ya kuogea ya
Koplo Tsega ikapenya puani mwake na kuamsha hisia mpya za mapenzi.
“Wala usijali kwani ungechelewa zaidi ya hapa ningekulaumu Sikawa” Koplo
Tsega akaongea huku akiangua kicheko hafifu na kuufunga ule mlango wa chumba.
“Ndiyo maana sikutaka kuchelewa” Sikawa akaangua kicheko chepesi cha
kistaarabu huku akielekea kuketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa mle ndani.
Koplo Tsega akiwa unaufahamu vizuri udhaifu wa wanaume mara baada ya kuufunga
mlango wa kile chumba akatembea taratibu kukizunguka kitanda cha mle ndani na
hatimaye kuketi kihasara kwenye pembe ya kile kitanda huku akiwa na hakika kuwa
macho ya Sikawa yalikuwa yakimsindikiza nyuma yake. Kisha akageuka ghafla na
kukutana na macho ya Sikawa yakimtazama. Sikawa kuona vile akashikwa na haya
huku akiyakwepesha macho yake haraka kutazama muziki uliokuwa ukirushwa
kwenye ile runinga ya mle chumbani ujasiri ukiwa umeanza kupungua.
Koplo Tsega alikuwa fundi mzuri wa kuanzisha maongezi hivyo akajikuta
akianzisha mada moja na kurukia nyingine huku macho yake mara kwa mara yakitua
juu ya kifua cha Sikawa. Sikawa naye hakuwa nyuma alimpatiliza vizuri Koplo Tsega
na pale alipohisi kuwa alikuwa mbioni kuishiwa hoja akazuga kwa kuinyanyua bilauri
ya kinywaji na kugida mafunda kadhaa huku macho yake mara kwa mara yakiutazama
mlima wa matiti ya wastani yaliyokuwa kifuani mwa Koplo Tsega.
Maongezi yao hayakuwa na hoja za maana lakini yaliendelea na kila mara Sikawa
alipojaribu kumdadisi Koplo Tsega kiundani zaidi alijikuta akiambulia patupu kama
siyo kudanganywa. Maongezi yalipoonekana kufifia muziki uliokuwa ukirushwa na
runinga ya mle chumbani ukarudisha uhai wa mandhari yale.
Hatimaye mshale wa saa ya ukutani mle chumbani ukasoma saa nane na robo usiku
na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha nje ikatengeneza kizingiti kingine kwa Sikawa
huku Koplo Tsega akionekana kufurahishwa na hali ile. Kile kilevi walichokuwa wakikitumia kikaanza taratibu kuwaondoa nishai kadiri muda ulivyokuwa ukisogea
mbele.
Hatimaye uvumilivu ukaondoka na kuwapelekea washindwe kuzidhibiti vyema
hisia zao. Sikawa akahamia pale kitandani huku akijidai anataka kuugemeza mgongo
wake baada ya kuchoka kukaa muda mrefu kwenye lile kochi la sofa mle chumbani.
Koplo Tsega naye akajifungua kanga yake kwa hila na kugeukia upande wa pili wa
kitanda huku akimpa mgongo Sikawa.
Nadharia ya somo la fizikia ya unlike charges attract each other hatimaye ikachukua
nafasi yake huku kila mmoja akiacha kuigiza. Muda mfupi uliyofuata shughuli ikaanza
pale kitandani kila mmoja akijitahidi kuonesha ufundi wa mapenzi kwa mwenzake.
Sikawa alikuwa fundi mzuri wa mapenzi aliyejua vizuri kumridhisha mwanamke
mwenye kiu ya mapenzi. Alimgeuza Koplo Tsega upande ule kisha akamkunja upande
huu halafu akamuinua hapa na kumkandamiza pale huku ndimi zao zikitekenyana
mdomoni na kutengeneza kiwango cha mwisho cha hisia za mapenzi kwenye miili
yao.
Mara ya kwanza,mara ya pili,mara ya tatu na walipofika mara ya nne walikuwa hoi
taaban hawajitambui kwa uchovu. Usingizi ukaja na kuwachukua huku kila mmoja
akiwa amelala kwa namna yake. Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha jijini Dar
es Salaam.
_____
Koplo Tsega ALIKUWA wa kwanza kuamka kutoka usingizini. Kitendo
cha kuuona mkono wa kiume juu ya titi lake kifuani kukamfanya amkumbuke
Sikawa,mhudumu wa hoteli ile aliyelala naye jana usiku.
Sikawa alikuwa hajitambui kwa uchovu na alikuwa akiachia sauti ya mkoromo
hafifu kinywani mwake huku miguu na mikono yake ameisambaza ovyo pale
kitandani.
Koplo Tsega akageuka na kumtazama Sikawa kwa makini pale kitandani huku
nafsi yake ikimsuta kwa kitendo cha kujirahisisha na hatimaye kugawa penzi lake
kwa kijana yule mhudumu wa hoteli. Hata hivyo kwa upande mwingine hakutaka
kujilaumu sana. Penzi zito la Sikawa lilikuwa limefanikiwa kukata kiu yake ya mapenzi
ya muda mrefu tangu alipoachana na mpenzi wake mara ya mwisho.
Koplo Tsega aliendelea kumtazama Sikawa pale kitandani huku uso wake
ukiumba tabasamu laini la shukrani. Mikiki mikiki ya usiku pale kitandani ilikuwa
imemuacha na uchovu wa aina yake. Kila kiungo cha mwilini alipojaribu kukisogeza
kilikuwa kikilalamika. Sikawa alikuwa ameitosheleza vizuri haja yake katika kila eneo
la mapenzi. Hata hivyo hisia mpya zilipomjia juu ya sababu iliyomrudisha jijini Dar
es Salaam zikamfanya aanze kuyapuuza matukio yote waliyoyafanya usiku yeye na
Sikawa.
Koplo Tsega akatupa shuka pembeni na kushuka kitandani. Kioo kikubwa
cha kabati lililokuwa mle ndani ukutani kikamfanya asimame kidogo na kuanzakujitathmini.
Macho yake makubwa bado yalikuwa legevu kwa uchovu,matiti yake madogo ya
wastani yalisimama wima kifuani pamoja na misukosuko ya Sikawa iliyoyapitia wakati
wa usiku. Kiuno chake chembamba kilichofuatiwa na mzigo wa wastani wa makalio
yake imara yaliyoshikiliwa na mihimili thabiti ya misuli ya mapaja yake yaliyonona
vikamfanya ajizungushe mbele ya kioo cha lile kabati huku akijitazama.
Matokeo ya tathmini yake kupitia taswira iliyojengeka kwenye kioo kile cha kabati
yakampelekea Koplo Tsega ajiridhishe kuwa bado alikuwa kwenye soko la uzuri kama
walivyokuwa wasichana wengine wa mijini.
Hatimaye Koplo Tsega akavinyoosha viungo vyake mwilini kwa mazoezi mepesi
kisha akaelekea maliwatoni huko ambako alimaliza haja zake zote pamoja na kuoga.
Koplo Tsega aliporudi kutoka maliwatoni akavaa bukta yake nyepesi na blauzi
yake mchinjo kisha akaelekea pale kitandani na kumwamsha Sikawa.
Sikawa alishtuka kutoka usingizini huku akiwa mwingi wa uchovu. Haraka
akayapeleka macho yake kuitazama saa ya ukutani iliyokuwa mle chumbani. Ilikuwa
ikielekea kutimia saa mbili asubuhi lakini alipokumbuka kuwa alikuwa na zamu
ya usiku ya kuingia kazini hakujipa haraka na badala yake akageuka pembeni yake
na kumtazama Koplo Tsega kwa macho yenye haya kidogo lakini yasiyojali kitu
chochote huku akitabasamu. Sikawa alitamani sana kuwa wangeendelea kulala mle
chumbani na kuendeleza starehe hata hivyo macho ya Koplo Tsega yalimuonya kuwa
hilo lisingewezekana tena kwa wakati ule.
“Umeamka saa ngapi?” Sikawa akavunja ukimya huku akitabasamu.
“Muda siyo mrefu”
“Mh! usingizi wa leo ulikuwa mzito kama wa Pono!” Sikawa akaongea huku
akivinyoosha viungo vyake mwilini na kuzipa uhai fikra zake pale kitandani.
“Mimi ndiyo hata sikumbuki kuwa ni wakati gani nilipitiwa na usingizi mpenzi”
Koplo Tsega akaongea kwa sauti nyepesi kisha walipotazamana usoni kila mmoja
akatabasamu kabla ya Koplo Tsega kuvunja ukimya.
“Amka ukaoge kumeshapambazuka”
“Asubuhi yote hii kwani tunakimbilia wapi?” Sikawa akauliza kichovuchovu.
“Huingii kazini leo?” Koplo Tsega akamuuliza Sikawa akiutazama mchoro wa
umbo la Sikawa ndani ya lile shuka la kitandani.
“Leo nina zamu ya usiku” Sikawa akajitetea.
“Hata hivyo kumeshapambazuka”
“Lakini mimi sina haraka!”
“Mimi nina haraka” Koplo Tsega akaongea kwa msisitizo huku hisia za mapenzi
zikiwa mbali naye.
“Sasa nani kakuzuia?’’ Sikawa akaongea kwa jazba akichukia kushurutishwa.
“Umeshasahau kuwa hapa siyo kwako!” Koplo Tsega akafoka.
“Lakini si ni wewe mwenyewe ndiye uliyeniita humu ndani?” Sikawa akauliza kwa
mshangao.
“Ndiyo! lakini ilikuwa jana siyo leo”
“Kwa hiyo haja yako ilikuwa ni ngono tu?”
“Pigia mstari” Koplo Tsega akaongea kwa jazba huku akihisi kuanza kukereka.
“Sasa kwanini hukuniambia mapema ili nijue?”
“Hata kama ungejua kwani ungekataa?”
“Sikiliza wewe dada…” Sikawa akaanza kujitetea hata hivyo alikatishwa.
“Nashukuru sana kwa penzi lako lakini muda wa starehe umeisha. Inuka
ukajiandae uondoke” Koplo Tsega akaongea huku haraka akiliondoa shuka mwilini
kwa Sikawa na hapo Sikawa akabaki akimshangaa kwa hasira.
“Sasa kama hutaki wanaume ilikuwaje ukajitongozesha kwangu?” Sikawa
akaongea kwa jazba.
“Nilikujua kuwa wewe ni malaya mwenzangu” Koplo Tsega akaongea kwa
msisitizo.
“Malaya ni wewe au mimi?” Sikawa akauliza kwa mshangao
“Simama ujiandae uende mpenzi malumbano hayatakusaidia kitu” Koplo
Tsega akaongea katika namna ya kupuuza hoja za Sikawa kwani alikuwa ameanza
kuwachukia tena wanaume baada ya kumkumbuka Kiango. Kiango alikuwa mpenzi
wake wa muda mrefu na mwanaume aliyemkabidhi moyo wake wote lakini siku moja
akaambulia kumfumania bila kificho akiivuruga amri ya sita na rafiki yake wa karibu.
“Hivi wewe malaya una wazimu?” Sikawa akauliza kwa hasira lakini kabla
hajamalizia kuongea ngumi mbili za korodani pale kitandani zikamfanya atulie kwa
sekunde kadhaa huku ameachama mdomo wake kama anayeimba wimbo wa taifa.
“Tafadhali! usiniite malaya wewe mpuuzi” Koplo Tsega akamuonya Sikawa huku
Sikawa akiendelea kugugumia kwa maumivu makali pale kitandani. Sikawa alipotaka
kufurukuta akatulizwa pale kitandani kama mtoto mdogo huku akishindwa kuamini
ubabe na nguvu za ajabu za msichana yule mbele yake. Hatimaye Sikawa akaacha
upinzani hivyo akaamka pale kitandani na kuelekea maliwatoni ambapo alimaliza haja
zake na kuoga ndani ya muda mfupi.
Aliporudi mle chumbani akamkuta Koplo Tsega akiwa amerejewa na utulivu
na bashasha zote za kirafiki huku akishindwa kumuelewa vizuri mwenyeji wake.
Walipotazamana tena wote wakajikuta wakitabasamu.
“Nisamehe mpenzi wangu” Koplo Tsega akaongea kwa sauti ya kubembeleza na
yenye urafiki ndani yake.
“Usijali lakini umeniumiza sana!” Sikawa akaongea kivivuvivu huku donge la
hasira limemnasa kooni.
“Pole mpenzi lakini nilitaka uamke mapema” Koplo Tsega akajitetea huku
akizunguka na kumkumbatia Sikawa kwa nyuma na hapo wote wakaondoa tofauti
zao huku wakitabasamu.
“Unajisikiaje kwa sasa?” Koplo Tsega akamuuliza Sikawa huku akiupeleka mkono
kuzishika korodani zake. Sikawa akiwa ameshtukia hali ile akajitoa mikononi mwa
Koplo Tsega haraka huku akiangua kicheko cha kimahaba.
KEVIN e. MPONDA
“Please don’t touch them,they are still very hot” Sikawa akaongea kwa ujivuni huku
akianza kuvaa nguo zake na hapo wote wakacheka.
“Mwenge unakaa sehemu gani?” Koplo Tsega akavunja ukimya.
“Mtaa wa mama Ngoma nyumba namba 11” Sikawa akaongea huku akiendelea
kuvaa nguo zake.
“Nikija kukutembelea kuna shida yoyote?” Koplo Tsega akauliza huku akiumba
tabasamu usoni.
“Shaka ondoa mpenzi” Sikawa akaongea kwa furaha.
“Naomba namba yako ya simu”
Sikawa hakusita badala yake akaanza kuitaja namba yake ya simu taratibu katika
namna ya kuhakikisha kuwa Koplo Tsega anazinakili namba zile bila usumbufu.
“Mchana utakuwa na ratiba gani?” Sikawa akauliza
“Bado sijafahamu ila huwenda nikawa na mizunguko ya hapa na pale” Koplo
Tsega akaongea kwa utulivu huku akifikiria jambo.
“Basi tutawasiliana mpenzi” Sikawa akaongea baada ya kumaliza kujiandaa.
“Ondoa shaka ila usije humu ndani hadi tuwasiliane kwanza”
“Kama jana?”
Sikawa akachombeza utani huku akielekea sehemu ulipokuwa mlango wa
kile chumba. Alipofika akaufungua ule mlango na kabla hajatoka nje akageuka na
kumkonyeza Koplo Tsega kimahaba kisha akatoka nje ya kile chumba na kutokomea
zake.
_____
MUDA MFUPI BAADA YA SIKAWA kuondoka mle chumbani Koplo Tsega
akaichukua ile kamera yake kutoka kwenye begi lake lililokuwa chini ya uvungu wa
kile kitanda na kuanza kufanya mapitio makini ya zile picha alizopiga usiku wa jana
nje ya Vampire Casino.
Ile kamera aina ya Toymaster ilikuwa imenasa picha nne safi na zenye ubora
wa kuaminika. Katika zile picha nne zilizokuwa kwenye ile kamera picha mbili
zilimuonesha msichana mmoja aliyevaa gauni fupi akishuka kutoka kwenye gari refu
na jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van huku akiwa ameongozana na wapambe
wawili waliovaa suti nadhifu kuificha miili yao imara iliyojengeka vema.
Picha nyingine mbili zilizosalia zilimuonesha msichana yule akisalimiana na
mwanaume mwingine aliyevaa suti nadhifu huku wale wapambe wakiwa wamesimama
kando yake.
Koplo Tsega akaendelea kuzitazama zile picha moja baada ya nyingine kwa utulivu
huku akijaribu kurudisha kumbukumbu zake. Muda mfupi uliyofuata baridi nyepesi
ikaanza kuusimanga mtima wake pale alipogundua kuwa msichana yule kwenye zile
picha ndiye yule aliyemuona kwenye habari picha za magazeti fulani huko siku za
nyuma.
Koplo Tsega akaendelea kukumbuka namna picha zile za magazetini zilivyokuwa zikimuonesha msichana yule wakati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
J.K.Nyerere huku akiwa ameongozana na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa serikali
kuelekea nchi fulani ya ughaibuni katika safari ya kikazi ya kiongozi huyo.
Koplo Tsega akaendelea kukumbuka tena namna ambavyo habari za msichana
yule zilivyovuma huko siku za nyuma baada ya picha zake za ngono na mfanyabiashara
mmoja maarufu wa jijini Dar es Salaam kusambazwa mitandaoni kama rasimu ya
katiba mpya.
Koplo Tsega akajikuta akimkumbuka mwandishi wa habari aliyefahamika kwa
jina la Mtenzi Binagwa ambaye baadaye alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya
kusemekana kuwa ndiye yeye aliyehusika katika kuzipiga picha hizo na kuzieneza
mitandaoni.
Koplo Tsega akajikuta akizikumbuka picha hizo za utupu namna zilivyolitikisa jiji
la Dar es Salaam kwa muda wa wiki kadhaa na kupamba vichwa vya habari magazetini.
Kabla ya kwenda nchini D.R Congo Koplo Tsega akakumbuka kuwa yeye na
Sajenti Chacha Marwa walikuwa katika hatua za mwisho kabisa za kuonana na meneja
wa Vampire Casino baada ya kuhisi kuwa katika casino ile kulikuwa na mambo fulani
ya chinichini yaliyokuwa yakiendelea. Lakini walijikuta wakipigwa chenga na uongozi
wa casino ile mara kwa mara na walipokuwa wakijiandaa kutumia njia mbadala ndiyo
wakapokea wito wa kujumuishwa kwao kwenye mpango wa amani ya kudumu nchini
D.R Congo.
Akili yake ikiwa imezama kwenye tafakuri nzito Koplo Tsega akajikuta akipiga
mwayo mwepesi wa uchovu huku akiendelea kuzitumbulia macho zile picha za
kwenye ile kamera.
#46
SASA NILIKUWA NA HAKIKA KUWA yule mtu aliyekufa kwa kuanguka
kutoka juu ya lile jengo la ghorofa la shirika la nyumba la taifa kule mtaa wa
Nkurumah,kuwa kifo chake kilikuwa na mahusiano ya namna fulani na yule
msichana niliyekuwa nikimfuatilia usiku wa jana kutoka kule Vampire Casino. Ingawaje
hadi hapa nilipofikia tukio lile bado lilikuwa halina uhusiano wowote wa kile
nilichokuwa nikiendelea kukichunguza.
Niliendelea kuwaza wakati nilipokuwa nikiegesha gari langu kwenye viunga
vya maegesho ya magari vya Vampire Casino baada ya kutoka kwenye ile nyumba
alipoingia yule msichana usiku wa jana kule mtaa wa Nkurumah na kumkosa. Nilikuwa
nimepitisha msako wa kina kwenye ile nyumba na hatimaye kuja na hitimisho moja
kuwa ile myumba ilikuwa ikikaliwa na mwanaume askari wa jeshi la wananchi wa
Tanzania baada ya kuiona picha yake uliyovunjika mle ndani ya ile nyumba sebuleni
sakafuni na sare za jeshi zilizokuwa kabatini chumbani kwake. Bado sikuweza
kumtambua yule msichana kuwa alikuwa nani hata hivyo niliampa kumfuatilia.
Niliegesha gari langu na nilipoitazama saa yangu ya mkononi nikagundua
kuwa dakika chache zilikuwa zimetoweka tangu ilipotimia saa nne asubuhi. Magari
yaliyoegeshwa mbele ya Vampire Casino hayakuwa mengi na miongoni mwa magari
hayo zilikuwepo teksi za abiria.
Kabla ya kushuka kwenye gari niliyatembeza macho yangu tena nikitathmini hali
ya mandhari yale kisha nikafungua mlango na kushuka nikielekea sehemu ya mlango
wa mbele wa casino ile kulipokuwa na ofisi ya mapokezi na huduma kwa mteja.
Kwa namna nyingine nilifurahi sana kwa kutowaona wale mabaunsa wa mlangoni
waliyonichachafya usiku wa jana wakati nilipokuwa nikitaka kuingia ndani ya casino
ile na badala yake msichana mzuri na mrembo akanipokea kwa bashasha zote huku
akiniweka kwenye kundi la Status conscious customer kutokana na mwonekano wangu nadhifu wenye sura ya kirafiki.
‘Kumbe wasichana warembo bado wapo duniani’ nilijisemea moyoni wakati nikilifikia lile
dawati la mapokezi mbele yangu lililomwifadhi msichana mlimbwende mwenye kila
kionjo cha uzuri.
“Karibu kaka” dada yule alinikaribisha kwa bashasha zote.
“Ahsante sana pole na kazi” nilimwambia huku nikiumba tabasamu la kirafiki
usoni mwangu.
“Nishapoa” dada yule aliongea kwa sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni huku
tabasamu lake usoni likikataa kwenda likizo.
“Tafadhali! naomba nikusikilize” hatimaye yule dada alivunja ukimya baada ya
kuniona nikiendelea kumkodolea macho ya mshangao uliotokana na uzuri wake.
Kabla ya kumjibu yule dada nikageuka nyuma kutazama kule kwenye maegesho
ya magari ya ile casino baada ya kuona gari dogo aina ya Nissan March likiingia eneo lile
na kutafuta maegesho. Kitendo cha kuwaona mwanamke na mwanaume wakishuka
kwenye gari lile kikanifanya niyarudishe macho yangu kumtazama tena yule dada
mbele yangu.
“Nahitaji kuwa mwanachama wa casino” nilimwambia yule dada kwa utulivu huku
tukitazamana.
“Oh! karibu sana na ondoa shaka kaka” yule dada aliniambia huku akivuta
mtoto wa meza yake na kuchukua karatasi fulani na kuziweka juu ya ile meza mbele
yangu. Niliposogea karibu na kuzitazama vizuri karatasi zile nikagundua kuwa
zilikuwa ni fomu kwa ajili ya usajili wa uanachama wa casino ile. Fomu zile zilikuwa
na vitu kama;nembo kubwa ya ile casino,anwani zake zote kama namba za simu za
uongozi,namba za nukushi,tovuti na barua pepe. Chini ya fomu zile kulikuwa na
sehemu za kujaza taarifa ya mtu anayeomba uanachama.
“Jaza taarifa zako humo ndani” yule dada akaniambia huku akinipa kalamu ya
wino.
“Naomba unijazie wewe mimi sijui kusoma wala kuandika” nilimwambia yule
dada nikichombeza utani huku nikimrudishia zile fomu. Tukio lile likampelekea
yule dada anitazame kwa mshangao hata hivyo macho yetu yalipokutana kila mmoja
akajikuta akitabasamu.
Yule dada akaipokea ile fomu na muda mfupi uliyofuata akaanza kuniuliza taarifa
zangu na kila nilipomjibu akawa akinijazia taarifa zile za uongo kwenye ile fomu.
Baada ya muda mfupi tukawa tumemaliza zoezi lile.
“Bado ada ya mwanachama” yule dada akaniambia huku akimalizia kujaza taarifa
zangu kwenye ile fomu.
‘‘Ada ni pesa kiasi gani?” nilimuuliza yule dada na aliponiambia nikatumbukiza
mkono mfukoni kuchukua wallet yangu kisha nikachukua kiasi cha pesa nilizopaswa
kulipa kutoka kwenye wallet ile na kumkabidhi yule dada.
Taratibu za ule usajili zilipokamilika nikakabidhiwa kadi ndogo ya utambulisho
wangu ambayo ningekuwa nikiitumia kuingia kwenye casino. Niliipokea kadi ile na kuitia mfukoni huku nikifurahi kufanikiwa kwa zoezi lile ndani ya muda mfupi.
Hatimaye nikaagana na yule dada na kuelekea sehemu nilipoegesha gari langu
kwenye yale maegesho ya ile casino.
Muda mfupi baadaye niliyaacha maegesho yale na kurudi ofisini kwangu ambapo
asubuhi ile nilikuwa nimemwacha Mwasu akiendelea kuandaa ripoti ya upelelezi wa
mkasa wa MIFUPA 206.
_____
KITENDO CHA KUEGESHA GARI LANGU chakavu aina ya Peugeot 504 toleo
la zamani katikati ya magari mawili ya kifahari na kisasa katika viunga vya maegesho
ya magari vya Vampire Casino usiku huu kilinifanya nijihisi mnyonge wa kipato.
Ningeweza kutafuta sehemu nyingine katika maegesho haya ambayo ingeendana na
hadhi ya gari langu lakini kwa wakati huu nilifahamu kuwa hilo lisingewezekana.
Magari mengi yaliyoegeshwa kwenye eneo lile bila shaka yangeweza kwendana na
thamani ya kiinua mgongo cha wakurugenzi wa kampuni kubwa za hapa nchini na
mgeni yeyote kutoka nje ya Tanzania ambaye ingekuwa ndiyo mara yake ya kwanza
kufika eneo lile huwenda angeshangazwa sana na ile kauli ya kuwa Tanzania ni nchi
masikini.
Eneo la maegesho yale lilikuwa mbioni kufulika magari ya kifahari hata hivyo hali
ile haikunitia mshawasha wowote badala yake nikautia mche wa sigara mdomoni na
kuiwasha huku nikiendelea kutathmini hali ya mandhari yake.
Niligeuka na kuitazama saa ndogo ya gari iliyokuwa kwenye dashibodi na saa ile
ilionesha kuwa dakika chache zilikuwa zimetokomea baada ya kutimia saa mbili usiku.
Nikajishauri kuwa nishuke na kuelekea ndani ya casino ile au niendelee kukaa mle
ndani ya gari huku nikilisubiri lile gari refu na jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van
lililombeba yule mlimbwende wa jana liwasili eneo lile.
Hata hivyo baada ya kufikiri kwa kitambo lile wazo la kulisubiri lile gari refu na
jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van lifike eneo lile hatimaye nikaliweka kando
kwani sikutaka kutengeneza aina yoyote ya kivutio eneo lile.
Hatimaye nikaichukua bastola yangu na kuichimbia kwenye maficho mazuri mle
ndani ya gari kisha nikafungua mlango na kushuka. Kupitia kitabu kidogo chenye
maelekezo ya taratibu zinazopaswa kuzingatiwa na mwanachama wa casino ile
ambacho nilikuwa nimepewa na yule dada aliyenisajili kuwa mwanachama wa casino ile
asubuhi iliyopita. Nilikuwa nimekumbuka kuwa kuingia na silaha mle ndani ya casino
lilikuwa ni jambo lililokatazwa kwa herufi kubwa. Hivyo sikutaka kujiingiza matatani
kwa kuikiuka sheria ile na ndiyo kisa nikaamua kuiacha bastola yangu mle ndani ya
gari.
Nililisubiri gari moja lililokuwa likija ule upande wangu linipite kisha nikavuka
eneo lile na kuanza kutembea taratibu nikielekea kwenye ule mlango wa mbele wa
casino.
Nilifika eneo la mbele la casino ile na kuanza kupanda ngazi zilizokuwa eneo lile na mara tu nilipomaliza kuzipanda ngazi zile njemba mbili matata,mabaunsa wa
mlangoni pale zikajitokeza kunikabili. Niliwatazama mabaunsa wale waliokuwa tayari
kukabiliana na aina yoyote ya ukorofi wangu na hapo nikafurahishwa na utendaji
wao. Hivyo pasipo kupoteza muda nikazama mfukoni kuichukua ile kadi yangu ya
utambulisho wa mwanachama wa casino ile na kuwaonesha. Zile njemba kuona vile
zikanywea na kufungua njia zikiniruhusu niendelee na safari yangu.
Niliirudisha ile kadi yangu mfukoni kisha nikaendelea na safari yangu na baada ya
muda mfupi nikawa nimeufikia ule mlango wa mbele wa vioo wa ile casino ambapo
niliusukuma na kuzama ndani huku nikiwa na hakika kuwa macho ya njemba zile
mbili zenye nguvu za kipigo yalikuwa yakinisindikiza nyuma yangu.
Sasa nilikuwa nimeingia ndani ya Vampire Casino kisima cha starehe chenye bidhaa
zote za kishetani.
Wakati nikipiga hatua zangu kuendelea na safari mle ndani ya ile casino nikajikuta
nikijiuliza kama bado nilikuwa jijini Dar es Salaam au nilikuwa kwenye jiji lingine
mashuhuri duniani. Kwani kwa namna moja au nyingine nilikuwa nimeshangazwa
sana na mambo niliyoanza kuyaona mle ndani.
Kwa tathmini yangu ya haraka ni kuwa idadi kubwa ya watu waliokuwa
mle ndani ya ile casino walikuwa ni watu wa kutoka mataifa yenye afya kiuchumi
kama;wazungu,wachina,waarabu na wahindi. Idadi ndogo ya watu waliosalia mle
ndani walikuwa ni watu weusi kama mimi.
Katika korido fupi na pana niliyoingia niliziona jozi kadhaa za wapenzi wakiwa
wamekumbatiana wakinyonyana ndimi na kufanya matendo mengine ya kishetani.
Nilipowatazama watu wale nikagundua kuwa wanaume walikuwa wa rika tofauti
wadogo kwa wakubwa lakini wale wasichana walikuwa ni mabinti wadogo sana kwa
umri huku wakiwa wamevaa nguo fupi nusu uchi na mienge ya sigara mikononi
mwao.
Hata hivyo watu wale hawakuonekana kushtushwa sana na ugeni wangu mle
ndani badala yake walionekana kuendelea na hamsini zao. Wasichana wawili wadogo
walinisogelea na kujaribu kuniwekea ukuta njiani wakijaribu bahati zao lakini mwendo
na sura yangu viliwaonya hivyo wakawahi kunipa mgongo huku wakiachia misonyo
ya hasira.
Hatimaye nikawa nimetokezea kwenye ukumbi mpana na ndani ya ukumbi ule
kulikuwa na taa za aina tofauti zikimulika huku na kule katika namna ya kupokezana.
Upande wa kushoto wa ukumbi ule kulikuwa na makochi ya sofa yaliyopangwa katika
namna ya kuzizunguka meza fupi za vioo zilizokuwa katikati. Pia kulikuwa na meza
na viti vya kisasa ambavyo baadhi yake vilikuwa vimekaliwa na watu huku juu ya meza
hizo kukiwa na aina tofauti za vinywaji.
Sehemu ya katikati casino ile ndipo palipokuwa pakifanyika mambo ya ajabu.
Wasichana wawili wenye maumbo mazuri ya mvuto wa ngono walikuwa wamevaa
chupi nyekundu za bikini zenye mikanda myembamba zilizokuwa zimeacha wazi
baadhi ya sehemu nyeti za miili yao.
Wasichana wale walikuwa wakinyonyana ndimi na kushikana sehemu zao nyeti
katika namna ya kuwapandisha ashki wanaume waliokuwa wakiwatazama. Wasichana
wale walikuwa juu ya jukwaa dogo la umbo duara lililokuwa likimulikwa kwa mwanga
mkali wa taa tofauti zilizokuwa sehemu ya juu ya eneo lile.
Katika jukwaa lile kulikuwa na bomba moja refu lililokuwa limeshikiliwa na
sehemu ya juu ya paa la ile casino huku sehemu ya chini ya bomba lile ikiwa imejikita
katikati ya lile jukwaa la umbo duara.
Wasichana wale juu ya lile jukwaa walikuwa wakilitumia bomba lile kucheza
muziki uliokuwa ukipigwa mle ndani kwa kujibinua binua katika mitindo tofauti huku
wakizishika nyeti zao. Kwa kufanya watu wengi wa mle ndani walitulia wakiwatazama
wasichana wale katika namna ya kuhamasika na matendo ya ngono
Niliyatembeza macho yangu mle ndani na upande wa kulia wa ule ukumbi
sehemu kulipokuwa na giza hafifu nikaona kuwa kulikuwa na makochi ya sofa na
baadhi ya makochi yale yalikuwa yamekaliwa na watu. Niliutazama vizuri upande
ule na hapo nikawaona baadhi ya mabinti wadogo wakiwa uchi wa mnyama huku
baadhi yao wakiwa wamevaa sketi fupi bila nguo za ndani. Wasichana wale baadhi
yao walikuwa wamepakatwa na wanaume wadogo kwa wakubwa na nilipochunguza
vizuri nikagundua kuwa walikuwa wakifanya ngono na wanaume wale bila wasiwasi
wowote kama sodoma na gomola. Kwa kweli niliwahurumia sana wabinti wale wadogo
lakini sikuwa na namna ya kufanya.
Niligeuka na kutazama mbele ya ukumbi ule na hapo nikaona kaunta kubwa ya
vinywaji ikiwa na wahudumu waliovaa sare. Baadhi ya wahudumu wale walikuwa
wakipishana huku na kule na masinia yao mikononi kupeleka vinywaji kwa wateja na
kuchukua chupa za vinywaji zilizokwisha tumika.
Nilitembea nikikatisha kando ya ukumbi ule wa casino na nilipofika sehemu
fulani upande wa kushoto nikaona ukumbi mwingine mkubwa. Ndani ya ukumbi
ule kulikuwa na mashine nyingi za kamari zilizopangwa katika mtindo unaovutia.
Nilisimama na kutazama eneo lile na hapo nikawaona baadhi ya watu wakiwa
wanaendelea kucheza kamari katika mashine zile.
Upande wa kulia wa ukumbi ule kulikuwa na milango mitatu iliyoongozana.
Katika ile milango mitatu milango miwili ilifanana kwa ukubwa lakini ule mlango
mmoja wenyewe ulikuwa tofauti na mkubwa. Juu ya mlango ule kulikuwa na
maandishi makubwa yakisomeka Bulk transaction Only . maelezo yale yakanitanabaisha
kuwa ndani ya mlango ule kulikuwa na chumba kilichokuwa kikitumiwa cha wacheza
kamari wenye pesa nyingi. Katika ile milango miwili iliyolingana juu yake kulikuwa
na vibandiko vyenye kuelekeza sehemu za maliwato kwa wanaume na wanawake.
Muziki laini uliokuwa ukipigwa kupitia spika fulani zilizokuwa mle ndani uliwaacha
watu katika viwango vya juu vya starehe zao.
Hatimaye nikaendelea na safari yangu nikielekea kwenye eneo la ile kaunta
ya vinywaji ambapo baada ya kufika ningetafuta sehemu nzuri ya kuketi ambayo
ingeniwezesha kuona vizuri kitu chochote ambacho kingekuwa kikiendelea mle ukumbuni. Hata hivyo wakati nikiendelea kutembea mle ndani nikagundua kuwa
kulikuwa na wanaume wawili waliokaa nyuma ya ule ukumbi ambao walikuwa
wakinitazama kwa makini sana.
Nilifika pale kaunta kisha nikavuta stuli moja ndefu na kupanda juu. Watu
wachache waliokuwa kwenye kaunta ile wakijipatia kinywaji wakageuka kunitazama
kidogo kabla ya kuendelea na hamsini zao.
Mhudumu wa kaunta ile mwanaume mrefu mweusi mwenye mwili uliojengeka
vizuri na sura ya ucheshi akiwa amevaa suruali nyeusi,shati jeupe na tai ndogo nyeusi
shingoni alinisogelea haraka na kunisikiliza haja yangu.
“Leapfrog cocktail baridi tafadhali!” nilimwambia mhudumu yule huku nikigeuka
kutazama kule nyuma ya ule ukumbi sehemu walipokuwa wamekaa wale wanaume
wawili. Sikuwaona wale watu hata hivyo hali ile haikunitia mashaka.
Muda mfupi baadaye yule mhudumu wa ile kaunta alinisogezea bilauri ya
kinywaji baridi cha Leapfrog cocktail yenye mrija mrefu na karatasi nyeupe ya tishu
iliyozungushiwa kwa nje.
Niliisogeza bilauri ile karibu yangu na kupitia mrija ule nikavuta funda moja la
kinywaji kile kikali na kukiacha kikiteremka taratibu kifuani kwangu na kutengeneza
starehe ya aina yake.
Kabla ya kuja kwenye casino hii nilikuwa nimetoka mtaa wa Nkurumah kwenye ile
nyumba huku nikitarajia kumuona tena yule msichana niliyemfuatilia kutoka Vampire
Casino usiku wa jana. Hata hivyo juhudi zangu zilikuwa zimegonga mwamba.
Nilikuwa nimejibanza kwa muda mrefu mle ndani ya ile nyumba huku nikimsubiri
yule msichana arudi lakini kitendo cha kuyaona masaa mengi yakitoweka bila msichana
yule kujitokeza nikaamua kutoka nje ya nyumba ile na kuendelea na hamsini zangu
huku nikipanga kurudi tena baadaye.
Bado akili yangu ilikuwa ikiendelea kusumbuka katika kutaka kufahamu kuwa
msichana yule alikuwa nani na kwani alihusika katika kifo cha yule mtu kule ghorofani
mtaa wa Nkurumah. Hata hivyo bado nilijipa matumaini kuwa hatimaye ukweli wa
mambo ungejulikana.
Mara kadhaa nilijikuta nikishawishika kutaka kuwasaidia polisi juu ya muuaji yule
kwani hadi wakati huu ushahidi nilikuwanao ingawa haukuwa wa moja kwa moja.
Lakini nilijikuta nikiachana na mpango hule pale nilipoanza kuhisi kuwa huwenda
msichana yule alikuwa akihusika kwa namna fulani na kile nilichokuwa nikikipeleleza.
Nilivuta tena funda moja la kinywaji kuupoza mtima wangu huku nikiyatembeza
tena macho yangu mle ukumbini. Kutoka pale nilipoketi niliweza kuziona ngazi
upande wa kushoto wa ukumbi ule zilizokuwa zikielekea ghorofa ya juu. Tukio lile
likanipelekea nianze kuhisi kuwa kule ghorofani ngazi zile zilipokuwa zikielekea
kulikuwa na shughuli nyingine za casino ile zilizokuwa zikiendelea. Nilipotazama vizuri
upande ule wenye zile ngazi mara nikakiona kibao kingine kidogo chenye maandishi
ya V.I.P hall and accommodation na hapo nikajua kuwa kule juu kulikuwa na ukumbi
mkubwa wa starehe na sehemu za kulala zilizokuwa zikitumika na watu wa daraja la juu. Kwa kweli ule ulikuwa ni uwekezaji wa aina yake. Niliendelea kuyatembeza
macho yangu mle ndani huku nikivuta sigara yangu taratibu mdomoni.
Niliitazama tena saa yangu ya mkononi kisha nikavuta funda jingine la kinywaji.
Bado kulikuwa na muda mfupi wa kusubiri kabla ya Milla Cash hajaingia mle ndani na
hicho ndiyo nilichokuwa nikikisubiri.
“Vipi hujisikii upweke?” mwanamke mmoja aliyeketi jirani yangu pale kaunta
aliniuliza kwa lugha safi ya kiingereza pengine baada ya kushochwa na ukimya wangu.
Mwanamke yule alikuwa amevaa suruali nyeusi ya jeans na blauzi nyepesi ya rangi ya
cream chafu. Katika vidole vya mkono wake alikuwa amevaa pete mbili za madini ya
Tanzanite na Almasi nyeupe. Nywele zake za rasta alikuwa amezizungusha na kuzifunga
kichwani kwa kitambaa cha rangi nyeusi. Mara nilipotulia na kumsikiliza vizuri yule
mama nikagundua kuwa namna ya matamshi ya kiingereza chake alifaa kufananishwa
na raia wa kutoka nchini Nigeria.
Mwanamke yule alikuwa akivuta sigara ya brand ya kifahari na juu ya meza ile ya
kaunta mbele yake alikuwa na kinywaji baridi cha Cocktail aina ya Manhattan. Kwa
tathmini yangu ya haraka nikahitimisha kuwa mwanamke yule alikuwa ni mtu mwenye
kipato cha kueleweka.
“Nilidhani unahitaji utulivu kidogo bibie” nilimwambia mwanamke yule kwa
lugha yangu safi ya kiingereza kisicho cha kubabaisha huku nikigeuka kumtazama na
kutabasamu.
“Kwa nini unapenda Cocktail ya Manhattan?” nilimchokoza mwanamke yule huku
nikimtupia macho ya udadisi.
“Ni kama wewe unavyopenda Cocktail ya Leapfrog” mwanamke yule aliongea huku
akitabasamu kisha akaendelea
“Hapo zamani nilikuwa mpenzi wa Cocktail aina ya Leapfrog,Negroni naSpritz lakini
nilijikuta nikiachana nazo baada ya kupata company nzuri ya wanywaji wa Manhattan
Cocktail. Hata hivyo sizichukii ingawa kwa sasa sizipendelei sana” mwanamke yule
aliongea huku akiitia sigara yake mdomoni.
Nilimtazama kwa udadisi mwanamke yule na hapo nikagundua kuwa alikuwa
akionekana kuzimudu vizuri starehe za dunia kwa namna yake.
“Mimi huwa ni mpenzi wa Manhattan Cocktail ingawa siyo mnywaji wa mara kwa
mara” niliongea kwa utulivu na baada ya kitambo kifupi cha ukimya nikaendelea.
“Lafudhi yako inaonesha kuwa wewe siyo mwenyeji waTanzania”
“Mimi ni raia wa Nigeria lakini maskani yangu kwa sasa yapo Capetown nchini
Afrika ya kusini” mwanamke yule aliniambia kwa utulivu huku akivuta funda la
kinywaji chake pale juu ya kaunta.
“Umekuja hapa Dar es Salaam kwa safari ya kikazi?” nilimuuliza yule mwanamke
huku taratibu kisha nikaipeleka sigara yangu mdomoni.
“Hapana! nipo hapa Dar es Salaama kwa ajili ya mapumziko mafupi ya likizo
yangu” yule mwanamke akaniambia huku akinitazama na hapo nikapata nafasi ya
kuiona vizuri sura yake.Alikuwa mwanamke wa makamo umri wake huwenda ulikuwa kati ya miaka
ishirini na nane na thelathini na mbili. Macho yake imara yenye nguvu makubwa na
legevu kiasi yalikuwa na kila kitu mwanaume alichopenda kukiona. Tulitazamana
na macho yetu yalipokutana kila mmoja akatabasamu na hapo haraka nikajua kuwa
alikuwa ni mwanamke wa aina yangu.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Kwa nini ukaichagua Dar es Salaam kama sehemu ya mapumziko ya likizo
yako badala ya miji mingine ya Afrika mashariki kama Nairobi,Kigali,Bujumbura au
Kampala?” nilimuuliza mwanamke yule baada kuvuta funda la kinywaji.
“Nimewahi kufika huko kote lakini mtindo wa maisha ya hapa jijini Dar es Salaam
naweza kusema umenivutia sana” mwanamke yule aliongea huku akitabasamu na
hapo uzuri wake ukajitokeza.
“Kwa vipi?” nikamuuliza.
“Watanzania ni watu wakarimu mno!” yule mwanamke aliongea huku akiangua
kicheko hafifu kilichoniacha njia panda na hapo nikashindwa kuelewa kama kweli sisi
watanzania tulikuwa wakarimu kiasi cha kusifiwa na wageni au tulikuwa waoga katika
kufanya maamuzi ya msingi.
Nilipozikumbuka kashfa mbali mbali zilizokuwa zikiibuka nchini Tanzania kila
kukicha kama;EPA,Richmond,Escrow,kusafirishwa kwa wanyama wetu kwenye ndege kwenda
nchi za nje,kauli za viongozi wakwapuaji wa mamilioni ya pesa zetu bila huruma,chokochoko
za itikadi za kidini,mauaji ya wapigania haki na usawa na ubabe wa vingozi wetu,nikabaki
nikimeza funda kubwa la mate kuitowesha hasira yangu kifuani.
“Karibu sana!” hatimaye niliongea huku nikitabasamu.
“Ahsante!” yule mwanamke akaitikia huku akivuta funda la kinywaji.
Nilivuta funda moja la kinywaji kisha nikayatembeza macho yangu mle ukumbini
kabla ya kuyarudisha kwa yule mwanamke na hapo nikamuuliza huku nikimtazama
usoni.
“Jina lako?”
“Iko–ojo Obaje” mwanamke yule aliongea huku akiitia sigara yake mdomoni na
alipoitoa akaupuliza moshi wake pembeni kisha akaisogeza ile bilauri yake ya kinywaji
na kuvuta mafunda kadhaa kisha akageuka tena na kunitazama.
“Na wewe je?” akaniuliza.
“Naitwa Stephen Masika” nikamdanganya
“Wewe ni mwenyeji wa hapa Dar es Salaam?”
“Ndiyo! nimezaliwa na kukulia hapa”
“Oh! vizuri sana bila shaka sasa nitakuwa nimepata mwenyeji wa kufikia hapa jijini
Dar es Salaam” mwanamke yule akaongea huku akiangua kicheko hafifu cha furaha
nami nikaungana naye kwa kutabasamu kidogo kisha nikavunja ukimya.
“Umekuja na familia yako?” nilimuuliza lakini nikashangaa kumuona akitabasamu
na hatimaye kuangua kicheko.
“Mimi sina familia wala sijaolewa” mwanamke yule aliongea huku akiitia sigara
yake mdomoni huku kicheko chake kikiwa bado hakijafika tamati.
“Kwanini mwanamke mzuri kama wewe hujaolewa na umri wako unakuruhusu?”
nilimuuliza.
“Wanaume wanataka wake zao wawe ni watu wa kukaa nyumbani,wawafulie nguo
zao na kuwapigia pasi,wawapikie vyakula vitamu na kuwazalia watoto. Mimi najiona
kuwa siyo mwanamke wa aina hiyo” yule mwanamke akaongea baada ya kuitua bilauri
yake ya kinywaji pale juu ya kaunta na hapo nikamtazama huku nikimlinganisha na
maneno yake.
“Huna mpango wa kupata mtoto?” nikamuuliza na kuitia sigara yangu mdomoni
huku nikapambana na taswira ya matiti yake yaliyokuwa nusu wazi kifuani mwake.
Harufu nzuri ya manukato yake ikazipumbaza kwa muda hisia zangu. Hata hivyo
nilishangaa kumuona akitabasamu.
“Hujui kuwa mtoto ni sawa na mume wa pili. Itabidi umlishe,umfulie
nguo,umuogeshe,umpeleke hospitali,umpeleke shule. Kwa kweli nawahurumia sana
wanawake wenzangu”
“Mh! basi wewe utakuwa mwanamke wa aina yake” nilimwambia yule mwanamke
huku nikiipeleka bilauri ya kinywaji mdomoni na wakati nikifanya vile mara nikajikuta
nikivutiwa na tatoo iliyokuwa shingoni mwake. Mchoraji wa tatoo ile bila shaka alikuwa
fundi stadi mno ingawa hata hivyo tatoo ile haikunivutia hata kidogo.
Ilikuwa ni tatoo ya kichwa cha nyoka mwenye sumu kali huku akiwa ameachama
kinywa chake wazi na ulimi wake mrefu wenye pacha mbili ukiwa nje. Nikiwa
nimeduwaa kuitazama ile tatoo yule mwanamke ni kama ambaye hakuvutiwa na angalia
yangu hivyo aligeuka katika namna ya kunifanya nisiweze kuiona vizuri ile tattoo. Kwa
kutaka kumpa uhuru zaidi nikatumbukiza hoja mpya.
“Hapa Dar es Salaam umefikia wapi?” nilimuuliza yule mwanamke na hapo
nikamuona akiupeleka mkono wake kwenye pochi yake ndogo ya mkononi.
Alipoifungua ile pochi akatoa kadi ndogo na kunipa. Niliipokea ile kadi na kuitazama
kwa makini. Ilikuwa ni kadi ndogo yenye maelezo ya namba ya chumba cha hoteli
moja ya kifahari iliyopo jijini Dar es Salaam na chini ya kadi ile kulikuwa na namba
za simu.
“Ukipata nafasi unaweza kuja kunitembelea kwani bado nina siku kadhaa za kukaa
hapa jijini Dar es Salaam” yule mwanamke akaniambia huku akivuta tena funda la
kinywaji pale kaunta.
“Ninaweza kukutembelea wakati gani?” nilimuuliza na baada ya kufikiria kidogo
akaniambia
“Muda wowote utakapopata nafasi”
“Nashukuru sana,nitajitahidi” niliichukua ile kadi na kuitia mfukoni na wakati
nikifanya vile macho yangu yakajikuta yakivutwa na msichana aliyekuwa akiingia mle
ndani. Nikageuka na kutazama upande ule wa ukumbi na mara nikamuona Milla Cash
akiingia mle ndani.
Mshangao kidogo ukiwa umenishika nikayapelekea macho yangu nikimtazama
msichana yule kwa udadisi na mara hii niliweza kuubaini vizuri uzuri wake. Alikuwa mwanamke mzuri mno niliyewahi kumuona katika kipindi chote cha maisha yangu.
Nikiwa na hakika kuwa pale nilipokuwa nimekaa isingekuwa rahisi kwake
kunitambua niliyapa macho yangu utulivu huku ubongo wangu ukifanya usajili makini
wa taarifa nilizokuwa nikizihitaji.
Milla Cash alikuwa akitembea kwa madaha katika ule mtindo wa catwalk huku
mwili wake ukinesa taratibu kama mtu aogopaye kukanyaga ardhi. Alikuwa amevaa
gauni jepesi na fupi la rangi nyekundu iliyoiva vizuri lenye utepe mweupe kiunoni
na kulifanya umbo lake adimu lijichore vizuri na kuamsha hisia kwa mwanaume
yeyote ambaye angethubtu kumtazama. Gauni lile fupi liliyaanika wazi mapaja yake
laini yenye minofu ya misuli. Uwazi mdogo ulioachwa na gauni lile kifuani mwake
uliyaacha wazi matiti yake makubwa ya wastani yenye chuchu imara.
Milla Cash aliendelea kutembea kwa madaha huku akiyaacha macho ya wanaume
waliokuwa mle ukumbuni yakimsindikiza kila alipozisimika chini hatua zake. Wale
walinzi wake wawili walimuwekea ngome imara ya ulinzi upande wa kulia na kushoto
huku wakiwa wameshika mabegi mikononi mwao. Nilipowachunguza walinzi wale
vizuri nikatambua kuwa walikuwa walinzi mahiri wasiokuwa na mzaha. Suti zao
nyeusi ziliwakaa vyema na miili yao ilikuwa imejengeka vizuri kuwakabili wakorofi.
Bado macho yangu yalikuwa kwa Milla Cash huku moyoni nikijiuliza kwanini
alikuwa akilindwa namna ile na kwa kweli tukio lile lilinishangaza sana. Nikautia tena
mche wangu wa sigara mdomoni huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu.
Niliendelea kumtazama Milla Cash huku nikitambua kuwa subira na uvumilivu
ndiyo silaha kubwa katika mafanikio yangu. Nilipoitoa sigara yangu mdomoni
nikaupuliza moshi pembeni kisha nikainama na kuvuta funda la kinywaji huku
nikiyatembeza macho yangu mle ukumbini.
Sasa nilimuona Milla Cash na wale wapambe wake wakipanda zile ngazi kuelekea
ile ghorofa ya juu yenye kile kibao cha V.I.P hall and Accommodation. Nikaendelea
kuwatazama hadi pale walipopotea kabisa machoni mwangu na hapo nikabaki
nikitafakari.
Baada ya kitambo kifupi kupita tangu Milla Cash na wale walinzi wake kupanda
kule ghorofani. Mara nikamuona mtu mmoja aliyekuwa ameketi pale kwenye makochi
ukumbini akisimama na kuelekea kule juu ya ghorofa. Kilipita kitambo kirefu huku
macho yangu yakiendelea kutazama juu ya zile ngazi na hatimaye nikamona yule mtu
aliyeelekea kule juu hapo awali akishuka tena zile ngazi.
Yule mtu alipofika pale chini hakurudi tena pale alipokuwa ameketi hapo awali
na badala yake aliambaa na ukuta wa ukumbi ule akielekea nje huku akiwa ameushika
mkoba mweusi wa ngozi mkononi.
Muda mfupi baada ya yule mtu wa awali kutokomea mara nikamuona mtu
mwingine akisimama kutoka pale ukumbini na kuelekea kule juu ghorofani alipotoka
yule mtu wa awali huku akiwa na mkoba mkononi. Hali ikawa kama kwa yule mtu
wa kwanza kwani baada kitambo kifupi kupita mara nilimuona yule mtu akirudi na
mkoba wake mkononi na alipomaliza kushuka zile ngazi hakurudi pale alipokuwa ameketi hapo awali badala yake nilimuona akielekea nje. Mtu wa tatu naye akafanya
vilevile kabla ya kufuatiwa na mtu mwingine. Kwa kweli hali ile ilinishangaza sana.
Niliendelea kuitazama mienendo ya watu wa mle ndani huku nikiendelea kuupisha
utulivu akilini mwangu. Hata hivyo nilishindwa kabisa kuelewa kilichokuwa kikiendelea
mle ndani. Hatimaye nikainama tena na kuvuta mafunda kadhaa ya kinywaji hadi pale
bilauri ile ilipobaki tupu.
Fikra zangu ziliporudi eneo lile nikakumbuka kuwa uchunguzi wangu ulikuwa
umeniweka mbali na maongezi ya Iko-Ojo Obaje aliyekuwa kando yangu pale kaunta.
Hivyo nikageuka na kumtazama Iko-Ojo Obaje huku nikiona aibu kwa kutokuwa
makani na uwepo wake. Yule mwanamke hakuwepo pale alipokuwa ameketi na kiti
chake kilikuwa wazi. Loh! nikaanza kujilaumu kuwa nilikuwa nimepoteza umakini kwa
kiwango cha juu huku nikijiuliza kuwa mwanamke yule angekuwa ameelekea wapi.
Hatimaye nikaitoa wallet yangu kutoka mfukoni ambapo niliifungua na kuchukua kiasi
fulani cha pesa kwa ajili ya kulipia kile kinywaji. Hata hivyo nilishangaa sana kumuona
yule mhudumu wa kaunta ya vinywaji akikataa kuipokea pesa yangu.
“Bro! umeshalipiwa” yule mhudumu wa kaunta akaniambia huku akiondoa bilauri
za vinywaji zilizokuwa pale kaunta halafu kwa kitambaa chake kidogo mfano wa taulo
alichokuwa amekining’iniza begani akaanza kufuta ile meza ya kaunta.
“Una maana gani?” nilimuuliza yule mhudumu wa kaunta kwa makini huku
nikimtazama usoni.
“Umeshalipiwa kinywaji na yule dada aliyekuwa ameketi kando yako” yule jamaa
akaniambia huku akitabasamu. Sikuwa namna hivyo nikaichukua pesa yangu pale juu
ya kaunta na kuitia mfukoni.
“Alikueleza kuwa anaelekea wapi?” nikamuulia yule mhudumu wa kaunta
“Hapana!” yule mhudumu akanijibu huku akiendelea kutabasamu na hapo
nikajua kuwa kile kitendo cha mimi kulipiwa kinywaji na yule mwanamke kilikuwa
kimemfurahisha sana. Nilimuacha yule mhudumu akiendelea kufurahi kisha nikashuka
kutoka kwenye ile stuli ndefu ya kaunta na kushika uelekeo wa upande wa kulia wa ile
kaunta nikielekea eneo la maliwato la ukumbi ule.
Wakati nikitembea kuelekea eneo la maliwato la ukumbi ule nikajikuta nikivutiwa
na ubora wa casino ile. Mikono ya mafundi ujenzi ilikuwa imeitendea haki taaluma
yao. Kila eneo la ndani ya casino ile lilivutia kulitazama na kuta zake zilikuwa safi na
zilizonyooka vizuri na kupambwa kwa nakshi tofauti za kupendeza. Mwanga wa taa za
mle ndani uliakisiwa vizuri na marumaru za kisasa zilizokuwa sakafuni na kutengeneza
mandhari nzuri inayovutia sana kutazama.
Baada ya hatua chache za safari yangu hatimaye niliingia upande wa kushoto
sehemu iliyokuwa na milango miwili. Mlango mmoja ulikuwa kwa ajili ya sehemu
ya maliwato ya wanaume na mlango mwingine ulikuwa ni kwa ajili ya sehemu ya
maliwato ya wanawake.
Nilishika kitasa cha mlango wa maliwato ya kiume kisha nikaufungua mlango ule
na kupotelea ndani. Mara baada ya kuingia mle ndani nikawa nimetokezea kwenye korido pana iliyotazama na milango kumi na mbili ya vyoo. Baadhi ya milango ile
ilikuwa wazi huku mingine ikiwa imefungwa. Hata hivyo hakukuwa na dalili za uwepo
wa mtu yoyote mle ndani. Vyoo vyote vilionekana visafi na kwenye ule ukuta wa
korido iliyokuwa ikitazamana na ile milango ya vyoo kulikuwa na kioo kipana cha
kujitazama.
Pembeni ya kioo kile kulikuwa na masinki ya ukutani kwa ajili ya haja ndogo
pamoja na mifereji midogo ya chini iliyojengewa vizuri kwa marumaru nyeupe kwa
ajili ya kukusanya maji taka na kuyasafirisha nje.
Nilichagua choo kimoja kilichokuwa mwishoni mwa ile korido kisha nikafungua
mlango na kuingia ndani. Nilitaka kwenda haja ndogo kwani kile kinywaji kilikuwa
kimekijaza vibaya kibofu changu.
Wakati nilipokuwa nikijiandaa kwenda haja ndogo mara nikaanza kuhisi kuwa mle
ndani kwenye korido ya vile vyoo kulikuwa na mtu na mtu huyo alikuwa akitembea
taratibu kuvikagua vile vyoo.
Nikiwa nimeanza kuhisi jambo baya sikutaka kumshtua mtu yule hivyo kimiminika
changu nikakitupia ukutani na hapo kikawa kikishuka chini kwa utulivu katika ukimya
wa kifo huku masikio yangu yakifanya kazi ya ziada kusikiliza hatua za mtu yule.
Hatimaye ile sauti ya hatua za yule mtu ikakoma na eneo lote la vile vyoo likawa
kimya. Niliendelea kuyatega masikio yangu na kwa kweli sikuweza kuhisi kitu chochote
eneo lile. Baada ya muda mrefu wa kusubiri hatimaye hisia zikanijia kuwa nje ya ule
mlango wa choo changu kulikuwa na mtu aliyesimama.
Hali ile ikanipelekea nikatishe haraka kile nilichokuwa nikikifanya huku nikiudhika
sana na hali ile. Niligeuka taratibu na kutazama chini ya ule mlango sehemu kulipokuwa
na uwazi mdogo kati ya ule mlango na sakafu ya kile choo. Kupitia mwanga wa taa
iliyokuwa nje ya ile korido ya vile vyoo niliweza kukiona kivuli cha miguu ya mtu na
hapo koo likanikauka ghafla. Muda mfupi uliyofuata mara nikaanza kuona kitasa cha
ule mlango kikizungushwa taratibu na hapo nikajua kuwa sikuwa salama tena.
Nikiwa bado nafikiria kitu cha kufanya ule mlango wa kile choo ulifunguliwa kwa
kasi kisha mkono uliyoshika bastola ukatangulizwa mbele. Niliwahi kuudaka mkono
ule kisha nikaupigiza ukutani kwa nguvu zangu zote na hivyo kuifanya ile bastola
ianguke chini. Hata hivyo yule mtu alikuwa makini sana hivyo akatupa ngumi mbili
zenye kasi ya upepo. Niliwahi kujibanza pembeni hivyo pigo moja la ngumi lilinikosa
na kukata hewa bila majibu.
Pigo la pili lilipotupwa nilichelewa kidogo hivyo ngumi yake makini ikaitandika
vibaya shingo yangu na kunifanya nihisi kichefuchefu huku maumivu makali
yakisambaa mwilini mwangu na kunipelekea mfadhaiko wa aina yake. Halafu
nikapokea mapigo mawili ya ngumi kavu za tumboni zilizolikoroga vibaya tumbo
langu na kunifanya nianze kuhema ovyo. Nilikuwa nimejitahidi kuyadhibiti mapigo
yale bila mafanikio kwani yule mtu alikuwa fundi sana wa mapigano.
Pigo la teke alilolirusha mtu yule huku dhahiri akioneka kudhamiria kuzitawanya
kama siyo kuzipasua vibaya korodani zangu nikalipangulia chini kwa mikono yangu imara. Tukio lile likampelekea yule mtu apoteze mhimili na kuanza kupepesuka ovyo
lakini alikuwa mwepesi sana. Akapepesuka kidogo hadi pale alipopata mhimili wa
ukuta wa kile choo na bila kusubiri akarusha pigo jingine matata la ngumi ya chembe
ya moyo.
Mara hii nilikuwa mtulivu na makini hivyo nikaipangua ngumi ile kama mchezo
huku nikiisukumia kwenye koki ya bomba la maji la mle ndani na hapo nikasikia sauti
kali ya mvunjiko wa mfupa wa mkono wa yule mtu. Yule mtu akapiga yowe kali na
kubweka kama mbwa mwizi lakini hakukata tamaa mapema.
Pigo jingine la teke alilolirusha yule mtu niliwahi kuliona hivyo nikalikwepa kwa
kusogea kidogo pembeni na hapo pigo lile la teke likapita bila shabaha na kujipigiza
ukutani. Mguu wa yule mtu ukavunjika kwenye kifundo na kumpelekea yule mtu
apige yowe kali la aina yake.
Hata hivyo yule mtu alikuwa mkaidi hivyo kwa ule mkono wake mmoja mzima
akawahi kuikota ile bastola yake mle ndani sakafuni hata hivyo alichelewa kwani
ulikuwa ni kama mchezo wa paka na nyoka. Niliwahi kumshika miguu yule mtu na
kumvuta nyuma hivyo ile bastola akawa anaiona kwa mbele yake lakini hakuweza
kuifikia.
“Wewe ni nani na una shida gani na mimi?” nikamuuliza yule mtu huku nikiwa
nimemkwida shati lake mkononi. Yule mtu akaendelea kulalama kutokana na
maumivu makali ya majeraha yake. Alikuwa mwanaume mrefu na mweusi mwenye
mwili uliojengeka vyema. Alikuwa amevaa suruali nyeupe ya jeans na fulana nyekundu
na miguuni alikuwa amevaa buti za askari. Kijana wa makamo mwenye umri wa miaka
thelathini na kitu.
“Nakuuliza bwana wewe ni nani na una shida gani?”
Yule mtu hakunijibu badala yake akaendelea kugugumia maumivu na hapo
nikamchapa makofi mawili ya nguvu usoni kumuweka sawa.
“Nakuuliza wewe una shida gani na mimi mbona tunafuatana fuatana chooni
kama mainzi?” nilimuuliza tena yule mtu na nilipomchunguza vizuri nikagundua
kuwa alikuwa miongoni mwa wale watu wawili waliokuwa wakinitazama kule nyuma
ukumbini.
“Sikufuati wewe bwana” yule mtu akaongea kwa hofu huku akilalama kwa
maumivu.
“Kwani vyoo vyote humu ndani vina watu?” nilimuuliza huku nikizidi kumkwida.
“Hapana!”
“Sasa mbona huna msimamo wewe bwege na yule mwenzako yuko wapi?”
nikamuuliza kwa hasira
“Mwenzangu yupi?” yule mtu akaniuliza huku akinitazama kwa mshangao.
“Mwenzako uliyekuwanaye kule nyuma ya ukumbi”
“Mbona sikuelewi?”
“Hivi nyinyi mna shida gani na mimi?” nilimuuliza yule mtu na kumchapa kofi
jingine usoni na hapo akalalama kwa maumivu.
“Unanionea bure tu mimi sifahamu chochote” yule mtu akazidi kulalama lakini
alikuwa ni mtu mwenye hila kwani wakati akinisemesha kumbe alikuwa akiupeleka
haraka mkono wake nyuma kiunoni mwake ili kuichukua bastola yake nyingine ya
ziada na hapo mshipa wa huruma ukanikatika.
Nilikuwa kwenye nafasi nzuri hivyo lengo lake halikufanikiwa kwani haraka
niliwahi kukipigiza kichwa chake kwenye sinki la choo cha mle ndani. Kichwa chake
kikafumuka na ubongo wake ukaruka na kutapakaa kwenye marumaru za mle ndani.
Yule mtu akahangaika kidogo kabla ya kutulia huku roho yake ikiwa mbali na mwili.
Nilimaliza kumfanyia upekuzi yule mtu pasipo kupata kitu chochote cha maana
kwake hivyo nikanawa vizuri kwenye bomba la mle ndani na nilipomaliza nikarudi na
kumalizia haja yangu kwenye kile choo.
Sikutaka mtu yoyote anikute mle ndani hivyo mara tu nilipomaliza shida zangu
nikatoka na kuufunga ule mlango wa choo halafu kwa msaada wa kalamu niliyokuwa
nayo mfukoni nikaandika kwa maandishi makubwa juu ya mlango ule wa choo kuwa.
CHOO HIKI HAKITUMIKI.
Dakika chache zilizofuata nilikuwa mbali na choo kile huku taratibu sigara yangu
ikiteketea mdomoni.
Mara hii nilijikuta nikimkumbuka tena Milla Cash na wale wapambe wake wakiwa
ubavuni. Hata hivyo macho yangu bado yaliendelea na kazi ya kutathmini sura na
mienendo ya watu waliokuwa mle ndani.
Mambo yangu sasa yalitakiwa kwenda haraka kabla ya uwepo wa yule mtu kule
chooni haujashtukiwa. Niliendelea kutembea mle ndani huku nikikatisha kando ya ile
kaunta ya vinywaji kisha nikapita pembeni ya ule ukumbi wa casino kama mwenyeji.
Sikumuona mtu yeyote akinitazama au kunifuatilia hivyo nikaamini kuwa hali ilikuwa
shwari.
Nilipofika mwisho wa ule ukumbi nikashika uelekeo wa upande wa kulia na muda
siyo mrefu nikawa nimezifikia zile ngazi na kuanza kuzipanda nikielekea kule juu.
Wakati nikiendelea kuzipanda zile ngazi njiani nikapishana na mwanaume mmoja
mwarabu akishuka zile ngazi na mkoba mweusi mkononi. Niligeuka na kumtazama
yule mwarabu huku nikiwa nimevutiwa sana na ule mkoba wake mkononi.
Ule mkoba ulikuwa ukifanana na ile mikoba ya wale watu waliokuwa wakipanda
kule juu ghorofani muda mfupi wakati ule baada ya Milla Cash kufika.
Katika zile ngazi kulikuwa na kamera mbili zilizopandwa katika namna ya kunasa
taswira za watu wanaopanda na kushuka kwenye zile ngazi. Nilizitazama kamera zile
kwa hila hata hivyo nilifurahi kuwa nilikuwa nimevaa kofia yenye kuikinga vizuri sura
yangu.
Wakati nikiendelea kuzipanda zile ngazi mawazo fulani yalikuwa yakipita kichwani
mwangu. Bado nilikuwa nikimkumbuka yule mtu niliyepambana naye kule chooni
muda mfupi uliyopita. Nilikuwa na kila hakika kuwa yule mtu alikuwa amedhamiria
kuniua. Ama kwa tafsiri nyingine ni kuwa uwepo wangu mle ndani tayari ulikuwa
ukifahamika na baadhi ya watu. Kwa kweli nilishindwa kabisa kuelewa kitu kilichokuwa kikiendelea mle ndani.
Nilipomaliza kuzipanda zile ngazi nikawa nimetokezea mbele ya korido nyingine
ya ghorofa ya pili lakini mandhari yale hayakuwa kama ya kule chini nilipotoka.
Nilisimama kidogo pale juu huku nikiyachunguza mandhari yale na hapo nikagundua
kuwa kulikuwa na korido mbili. Korido moja ilikuwa upande wa kushoto na korido
nyingine ilikuwa upande wa kulia. Korido zile zilikuwa zimelizunguka eneo kubwa
la ukumbi mwingine wa pale juu uliyofunikwa wenye umbo kubwa mfano wa koni.
Niliutazama ukumbi ule wenye kiwambo cha kuzuia sauti ama Sound proof na
haraka nikatambua kuwa mle ndani kulikuwa na mambo makubwa zaidi ya kishetani
yaliyokuwa yakiendelea. Nilirudia tena kuitazama korido ile na hapo kitu fulani
kikaanza kujengeka kichwani mwangu.
Kulikuwa na milango mingi iliyokuwa ikitazamana na zile korido na hapo mawazo
fulani yakaanza kujengeka kichwani mwangu. Milango ile mingi ilikuwa ikitazamana
na zile korido mbili kuuzunguka ule ukumbi.
Juu ya milango ile kulikuwa na namba na hapo nikawa na hisia juu ya nini
kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Nikashawishika kuisogelea ile milango lakini
kwa kuwa eneo lile lilikuwa likitazamana na zile ngazi niliona kuwa yeyote ambaye
angeniona eneo lile angeweza kunitilia mashaka hivyo niliamua kuifuata ile korido ya
upande wa kulia.
Niliendelea kutembea huku nikiitazama ile milango ya vile vyumba ambapo
kwa wakati huu niliigundua kuwa yote ilikuwa ikifanana kwa mwonekano. Wakati
nikiendelea na safari yangu taswira ya yule msichana Milla Cash ikawa ikiendelea
kuumbika taratibu kichwani mwangu. Tatizo ni kuwa sikuweza kufahamu kuwa Milla
Cash alikuwa ameingia katika chumba kipi miongoni mwa vyumba vile.
Wakati nilipokuwa nikiendelea na uchunguzi wangu ghafla mlango wa chumba
kilichokuwa kikifuatia mbele yangu ulifunguliwa kisha mwanaume mmoja mwarabu
alitoka nje ya chumba kile na kunipita pasipo kunipa salamu huku marashi yake makali
yakiitesa pua yangu.
Niligeuka na kumtazama Mwarabu yule na hapo nikagundua kuwa mkononi
alikuwa ameshika mfuko mweusi uliyofanana na ile mifuko ya wale watu wa awali.
Kwa kweli nilishangazwa sana na hali ile hata hvyo niliendelea kumtazama mwarabu
yule hadi pale alipopotea kwenye zile ngazi za kushukia kule chini nilipotoka kisha
nikayarudisha tena macho yangu kuutazama ule mlango wa kile chumba ambacho
muda mfupi uliyopita yule mwanaume mwarabu alikuwa ametoka mle ndani.
Hatimaye nikazitupa hatua zangu kwa utulivu nikiuendea ule mlango wa kile
chumba huku nikitazama huku na kule kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa
akinitazama. Nilipofika nikakishika kitasa cha ule mlango na kuusukuma taratibu. Ule
mlango haukuwa umefungwa hivyo ulifunguka taratibu bila pingamizi lolote na hapo
nikaingia mle ndani na kuufunga kwa nyuma.
Nikiwa sasa nimeingia mle ndani ya kile chumba niliweza kuinusa vizuri ile harufu
kali ya yale marashi ya yule mwarabu aliyetoka mle ndani muda mfupi uliyopita.
Nilipomaliza kuzipanda zile ngazi nikawa nimetokezea mbele ya korido nyingine
ya ghorofa ya pili lakini mandhari yale hayakuwa kama ya kule chini nilipotoka.
Nilisimama kidogo pale juu huku nikiyachunguza mandhari yale na hapo nikagundua
kuwa kulikuwa na korido mbili. Korido moja ilikuwa upande wa kushoto na korido
nyingine ilikuwa upande wa kulia. Korido zile zilikuwa zimelizunguka eneo kubwa
la ukumbi mwingine wa pale juu uliyofunikwa wenye umbo kubwa mfano wa koni.
Niliutazama ukumbi ule wenye kiwambo cha kuzuia sauti ama Sound proof na
haraka nikatambua kuwa mle ndani kulikuwa na mambo makubwa zaidi ya kishetani
yaliyokuwa yakiendelea. Nilirudia tena kuitazama korido ile na hapo kitu fulani
kikaanza kujengeka kichwani mwangu.
Kulikuwa na milango mingi iliyokuwa ikitazamana na zile korido na hapo mawazo
fulani yakaanza kujengeka kichwani mwangu. Milango ile mingi ilikuwa ikitazamana
na zile korido mbili kuuzunguka ule ukumbi.
Juu ya milango ile kulikuwa na namba na hapo nikawa na hisia juu ya nini
kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Nikashawishika kuisogelea ile milango lakini
kwa kuwa eneo lile lilikuwa likitazamana na zile ngazi niliona kuwa yeyote ambaye
angeniona eneo lile angeweza kunitilia mashaka hivyo niliamua kuifuata ile korido ya
upande wa kulia.
Niliendelea kutembea huku nikiitazama ile milango ya vile vyumba ambapo
kwa wakati huu niliigundua kuwa yote ilikuwa ikifanana kwa mwonekano. Wakati
nikiendelea na safari yangu taswira ya yule msichana Milla Cash ikawa ikiendelea
kuumbika taratibu kichwani mwangu. Tatizo ni kuwa sikuweza kufahamu kuwa Milla
Cash alikuwa ameingia katika chumba kipi miongoni mwa vyumba vile.
Wakati nilipokuwa nikiendelea na uchunguzi wangu ghafla mlango wa chumba
kilichokuwa kikifuatia mbele yangu ulifunguliwa kisha mwanaume mmoja mwarabu
alitoka nje ya chumba kile na kunipita pasipo kunipa salamu huku marashi yake makali
yakiitesa pua yangu.
Niligeuka na kumtazama Mwarabu yule na hapo nikagundua kuwa mkononi
alikuwa ameshika mfuko mweusi uliyofanana na ile mifuko ya wale watu wa awali.
Kwa kweli nilishangazwa sana na hali ile hata hvyo niliendelea kumtazama mwarabu
yule hadi pale alipopotea kwenye zile ngazi za kushukia kule chini nilipotoka kisha
nikayarudisha tena macho yangu kuutazama ule mlango wa kile chumba ambacho
muda mfupi uliyopita yule mwanaume mwarabu alikuwa ametoka mle ndani.
Hatimaye nikazitupa hatua zangu kwa utulivu nikiuendea ule mlango wa kile
chumba huku nikitazama huku na kule kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa
akinitazama. Nilipofika nikakishika kitasa cha ule mlango na kuusukuma taratibu. Ule
mlango haukuwa umefungwa hivyo ulifunguka taratibu bila pingamizi lolote na hapo
nikaingia mle ndani na kuufunga kwa nyuma.
Nikiwa sasa nimeingia mle ndani ya kile chumba niliweza kuinusa vizuri ile harufu
kali ya yale marashi ya yule mwarabu aliyetoka mle ndani muda mfupi uliyopita. Hata hivyo harufu ile ilikuwa imechanganyikana na harufu ya moshi wa sigara za kifahari
na marashi mengine ya kike. Hisia zikaniambia kuwa huwenda mle ndani kulikuwa na
mtu mwingine ambaye sikuweza kumfahamu mapema.
Nilisimama nikikichunguza chumba kile na mbele yangu nikaliona pazia jepesi la
kamba nyembamba zilizotungwa simbi za baharini. Kupitia uwazi mdogo uliyokuwa
baina ya zile kamba niliweza kuona mle ndani ya lile pazia.
Nyuma ya pazia lile kulikuwa na chumba kikubwa chenye makochi makubwa ya
sofa za kisasa kilichokuwa kikimulikwa kwa mwanga hafifu wa taa za rangi tofauti za
kupendeza na sehemu fulani katika chumba kile sauti ya muziki laini ilikuwa ikisikika.
Nilizitupa hatua zangu taratibu kulisogelea lile pazia na nilipolifikia nikalisogeza
pembeni kuchungulia mle ndani na hapo nikaiona taswira kamili ya mandhari ya kile
chumba.
Mbali na yale makochi ya sofa niliyoyaona pale awali mle ndani pia kulikuwa na
meza pana ya kioo na juu ya meza ile kulikuwa na bilauri mbili na chupa nne za
kinywaji cha kilevi aina ya Russian Standard. Chupa tatu miongoni mwa zile chupa
nne zilikuwa tupu. Pembeni ya chupa zile kulikuwa na kibeseni kidogo cha majivu ya
sigara chenye umbo mfano wa kifaranga cha bata na ndani yake kulikuwa na kipisi
kidogo cha sigara kilichokuwa kikiteketea.
Niliyatembeza macho yangu mle ndani na sehemu fulani kwenye kona ya chumba
kile kulikuwa na simu ya mezani juu ya meza ndogo yenye ua jekundu. Upande
wa kulia wa chumba kile kulikuwa na runinga kubwa ukutani na katika runinga ile
kulikuwa na filamu ya ngono iliyokuwa ikioneshwa lakini hapakuwa na mtu kwenye
kile chumba ambacho sasa nilianza kukifananisha na sebule ya aina yake. Pembeni
ya seti ile ya runinga kulikuwa na jokofu jembamba na refu lenye kuta za vioo zenye
kumuwezesha mtu yeyote kuona mle ndani ambapo kulikuwa na lukuki ya chupa za
vinywaji.
Chumba chote kilikuwa kimefunikwa kwa zulia zuri la manyoya laini lililodariziwa
kwa maua mazuri ya rangi tofauti za kuvutia. Nilisimama nikiyatazama mandhari yale
huku nikiendelea kushangazwa na uwekezaji ule wa aina yake.
Upande wa kushoto wa chumba kile kulikuwa na mlango. Mlango ule sasa ulikuwa
wazi ukitenganishwa na chumba kile cha sebule kwa pazia jepesi linalomwezesha mtu
yoyote kuona mle ndani ya kile chumba kwa shida.
Adha ya hali ya joto kali la jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepelekwa likizo na
kiyoyozi makini kilichokuwa kikisambaza hewa ya baridi nyepesi isiyokinaisha.
Nilizitupa hatua zangu taratibu kukiendea kile chumba kilichokuwa upande wa
kushoto na mara hii nilijikuta nikivutiwa na kitu.
Katika kochi moja lililokuwa pale sebuleni nililiona vazi la kike aina ya sidiria
ya rangi ya pinki. Nilipoendelea kusogea mbele kidogo chini ya sakafuni usawa wa
kuelekea kwenye kile chumba nikaiona chupi ya bikini ya rangi nyekundu. Hatimaye
nikausogelea ule mlango na kulisogeza lile pazia nikichungulia mle ndani.
Msichana mzuri alikuwa amelala ndani ya beseni kubwa la kuogea huku baadhi ya sehemu za mwili wake kama magoti na mikono zikionekana bila kificho. Msichana
yule mzuri alikuwa amelala mle ndani ya lile beseni huku sehemu zake nyingine za
mwili wake zikishindwa kuonekana vizuri kutokana na mapovu ya sabuni nzuri ya
kunukia yaliyokuwa yametanda juu ya maji yale.
Kifua chake laini chenye mzigo wa matiti yenye ukubwa wa wastani yaliongeza
chachu nyingine katika uzuri wake. Msichana yule alikuwa amejilaza chali akitazama
juu huku kichwa chake chenye nywele ndefu,nyeusi na laini akiwa amekiegemeza
sehemu ya mbele kwenye ukingo wa lile beseni la kuogea. Mkono wake mmoja alikuwa
ameukunja na kuuegemeza upande wa kushoto kwenye lile beseni huku kiganja cha
mkono huo kikipotelea ndani ya lile povu la sabuni. Mkono wake mwingine ulikuwa
umeibana sigara katika pacha ya vidole vyake huku mkono huo ukibembea taratibu
nje ya beseni lile.
Mwanzoni nilidhani kuwa huwenda msichana yule alikuwa mfu kwa namna
alivyokuwa ameyatuliza macho yake kutazama juu kwenye dari ya chumba kile lakini
kitendo cha kumuona akiupeleka tena mkono wake mdomoni kuivuta ile sigara
kikanihakikishia kuwa msichana yule alikuwa hai na hapo nikatabasamu kidogo.
“Naomba unaniruhusu niingie mrembo” nilivunja ukimya na hali ile ikampelekea
msichana yule mrembo ashtuke na kugeuka akinitazama pale nilipokuwa nimesimama
huku akiwa ameshikwa na mshangao. Msichana yule aliendelea kunitazama kwa
mshangao halafu taratibu akalegeza uso wake na hapo tabasamu la kibiashara
likaumbika usoni mwake.
“Ondoa shaka unakaribishwa” msichana yule akaniambia huku akifanya jitihada
kidogo za kukaa vizuri kwenye lile beseni na hapo nikapata nafasi nzuri ya kuziona
chuchu zake imara zilizoupumbaza kwa muda mtima wangu.
Nilipoingia mle ndani nikaweza kuona vizuri mandhari ya kile chumba. Kilikuwa
chumba kipana chenye seti nyingine ya runinga pana ukutani na makochi ya sofa ya
ngozi nyeusi. Upande wa kulia kulikuwa na kioo kikubwa cha kujitazama na chini ya
kioo kile kulikuwa na chupa za mafuta mazuri ya kunukia pamoja na sabuni tofauti za
kuogea huku pembeni yake kukiwa kumening’inizwa mataulo mawili meupe. Sakafu
ya chumba kile kilichofaa kifananishwa na bafu la kisasa ilitengenezwa kwa marumaru
zenye rangi tofauti za kuvutia.
Niliyatembeza kwa utulivu macho yangu mle ndani na upande wa kushoto wa
chumba kile kulikuwa na sehemu ya kukaa iliyokuwa imetengenezwa kwa foronya
laini. Ile runinga ya kile chumba ilikuwa ikionesha filamu ya ngono kama ya kule
sebuleni na hapo nikajua runinga zote mbili za mle ndani zilikuwa zimeungwanishwa
na king’amuzi kimoja.
“Ahsante!” niliitikia kwa utulivu kisha taratibu nikapita na kwenda kukaa kwenye
ile sehemu yenye foronya laini huku nikiendelea kuyapeleleza mandhari yale.
“Yule rafiki yako ameenda wapi?” nilimuuliza yule msichana huku akiendelea
kunitazama.
“Rafiki yangu yupi?” yule msichana akaniuliza kwa mshangao.
“Mwarabu aliyetoka humu ndani muda mfupi uliopita!”
“Oh! sahau kuhusu yeye,huduma yake tayari imekwisha” msichana yule aliongea
kwa bashasha zote za kirafiki huku akiumba tabasamu usoni na nilipomchunguza
nikatambua alikuwa amelewa kidogo.
“Biashara inakwendaje?” nilimuuliza msichana yule huku nikimtazama.
“Dola mia moja kwa muda wa saa moja na huduma yangu utaifurahia” yule
msichana akaongea huku akiangua kicheko hafifu na hapo nikagundua kuwa alikuwa
akijitahidi kutengeneza mazingira ya kirafiki kama maadili ya kazi yake yalivyokuwa
yakimtaka. Kazi ya kuuza mwili wake.
“Haipungui?” nilimuuliza huku nikitabasamu hata hivyo umri wake mdogo
ukapeleka simanzi moyoni mwangu.
“Bei zetu ni nafuu sana ukifananisha na maeneo mengine hapa jijini Dar es
Salaam” msichana yule akaongea kwa kujiamini baada ya kuitoa sigara yake mdomoni
na nilipomchunguza nikagundua umri wake haukuwa zaidi ya miaka kumi na sita.
“Hakuna mkopo?” nilimuuliza yule msichana huku nikitumbukiza utani.
“Kama unataka mkopo nenda Pride au Faidika huko utapewa kwa masharti
nafuu” akaniambia kwa hasira huku akihisi kuwa nilikuwa nikitaka kuleta dharau
na kazi yake. Nilimtazama msichana yule huku nikimuonea huruma kwa namna
alivyokuwa mwathirika wa biashara ile ya ngono huku akiwa na umri mdogo ingawa
yeye mwenyewe hakuonekana kujali kitu.
“Dola mia moja ni pesa ndogo sana kwa mwanaume anayejua nini maana ya
starehe” yule msichana akaniambia huku taratibu akiipeleka mdomoni ile sigara
iliyokuwa mkononi mwake na kuanza kuivuta pasipo kunitazama. Alipoitoa akageuka
na kutabasamu huku akiniambia
“Napenda sana wanaume weusi wenye nguvu na warefu kama wewe” msichana
yule mdogo akaongea na hapo nikaanza kuilaani dunia kwa namna ilivyoharibika
namna ile. Hata hivyo nilitabasamu kidogo kuununua urafiki.
“Kwa nini?” nilimuuliza huku nikitabasamu.
“Huwa wananiacha nikiwa nimeridhika” yule msichana akaongea kwa sauti ya
mahaba.
“Jina langu naitwa Stephen Masika!” nilivunja tena ukimya.
“Mimi naitwa Zera”
“Jina lako tamu sana masikioni mwangu” niliongea kwa utulivu huku nikimtazama
msichana yule.
“Mh! kila mwanamume anaongea hivyo utasema mmeambizana” yule msichana
akaongea hukua akiipeleka sigara yake mdomoni na kuivuta taratibu.
“Unatumia kilevi gani?” hatimaye akaniuliza baada yakuitoa ile sigara mdomoni.
“Oh! usijali mrembo kilevi kwa sasa hapana!”
“Kwa nini?” akaniuliza kwa mshangao kidogo.
“Nina dozi ya Malaria” nilimwambia huku nikitabasamu na hapo akazidi kunikata
jicho kwa mshangao.
“Sasa kama unaumwa malaria unafanya nini humu ndani?. Si ungeenda hospitali
ya Ocean Road,Muhimbili au TMJ badala ya kuja hapa?”
“Kwani wagonjwa hatuna haki ya kununua huduma hii?” nilimuuliza kwa utulivu
huku nikimtathmini vizuri msichana yule.
“Nenda kauguze ugonjwa kwanza usije ukanifia kitandani” yule msichana
akaongea kwa dhihaka na hapo nikaingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda cha
shilingi laki moja na kumrushia pale kwenye lile beseni la kuogea. Yule msichana
ambaye sasa nilimfahamu kwa jina la Zera akakidaka kibunda kile cha pesa kama
mbwa mwenye njaa adakavyo mfupa aliorushiwa kisha akaanza kuzihesabu zile noti
chapuchapu kwa vidole vyake virefu kama mashine ya ATM huku ile sigara yake
akiwa ameibana kwenye pembe ya mdomo wake. Alipomaliza kuzihesabu zile noti
akageuka na kunitazama kwa shauku kama atarajiaye maelekezo juu ya zile pesa.
Alipoona kuwa nakawia kuongea akavunja ukimya
“Nimesema dola mia moja ya kimarekani siyo shilingi laki moja ya kitanzania?”
Zera akaongea huku akinitazama kwa udadisi.
“Vuta subira mrembo haraka ya nini?” nilimwambia yule msichana hata hivyo
hakusema neno badala yake nilimuona akianza kutoka kwenye lile beseni la kuogea
na mara hii mapigo yangu ya moyo yakasimama huku akili yangu ikishindwa kufanya
kazi kwa sekunde kadhaa.
Uzuri wake ama kwa hakika ulikuwa umefanikiwa kuzichukua mateka hisia zangu.
Pamoja na kuwa niliwahi kukutana na wasichana wengi warembo na wazuri katika
harakati zangu lakini Zera alikuwa ni matokeo ya kazi bora kabisa ya mfinyanzi.
Alikuwa mrefu lakini nilimzidi kwa sentimita chache za hisabati. Nywele zake
ndefu laini na nyeusi ziliteleza taratibu kutoka kwenye yale maji ya povu la sabuni
kama samaki aina ya kambare kwenye tope jepesi la udongo mfinyanzi. Niliendelea
kumkodolea macho Zera na hapo nikamuona akizikamua maji zile nywele zake kwa
viganja vya mikono yake katika namna ya kuzichuja maji kistaarabu.
Macho yake makubwa meupe na legevu yalizungumza kuwa alikuwa tayari kwa
kazi. Pua yake ndefu na nyembamba na midomo yake yenye kingo laini na pana
viliutanabaisha vizuri uzuri wa sura yake nyembamba kiasi yenye mvuto wa kipekee
kuwahi kutokea duniani.
Matiti yake yaliyosimama wima yenye chuchu nyeusi katikati yalitikisika kidogo
wakati alipokuwa akiutua mguu wake wenye kikuku sakafuni mara baada ya kutoka
kwenye lile beseni la kuogea huku akiwa uchi bila ya nguo yoyote ya kujisitiri maungoni
mwake.
Zera aliposimama mwili wangu ukashikwa na ganzi na akili yangu ikayumba na
kupoteza uelekeo kama bondia aliyeshambuliwa kwa pigo la konde la nguvu kichwani
kutoka kwa mpinzani wake. Kiuno chake chembamba chenye aina tofauti za shanga
kilikuwa kimechongwa vizuri kuushikilia mzingo wa makalio yake usiokinaisha
kuutazama. Kitovuni alikuwa ametoga kipini kimoja cha dhahabu. Niliendelea
kumkodolea macho na hapo nikayaona yale mapovu ya sabuni nzuri ya kunukia kutoka kwenye lile beseni la kuogea mle ndani yakichuruzika taratibu na kutengeneza
ziada nyingine katika uzuri wake wa kustaajabisha.
Mikono yake mirefu,laini na yenye kucha ndefu zenye rangi ya kuvutia aliipeleka
kiunoni mwake na kujishikashika kisha akajitikisha kidogo katika namna ya kuzidi
kuzitaabisha vibaya hisia zangu ambazo tayari zilikuwa mahututi.
Zera alipoanza kutembea taratibu akinifuata pale nilipokuwa nimeketi mitetemo
ya mapaja yake laini na mang’avu yenye misuli imara yakaupelekea ule mzigo wake wa
makalio makubwa na laini uanze kuweweseka kama mshumaa unaopulizwa na upepo
mkali wa baharini.
Taswira ile mbele yangu ikanipelekea nianze kuhisi kuwa nilikuwa nimepotea njia
na hatimaye kujitumbukiza kwenye kiumbe kile kilichohitimu vizuri katika kucheza
na hisia za wanaume.
Zera alitembea taratibu na hatimaye kuketi pembeni yangu. Nilipogeuka
kumtazama mkono wake mmoja tayari ulikuwa umepenya ndani ya fulana yangu na
kuanza kufanya ziara ya taratibu tumboni na kifuani mwangu. Tukio lile likanifanya
nijihisi kama niliyepigwa na shoti kali ya umeme. Muda mfupi badaye nikaanza kuhisi
kuwa endepo ningeendelea kuiruhusu hali ile basi mawasiliano ya ubongo na kazi za
viungo vyangu mwilini yangekatika. Hivyo nikajitahidi kujinasua kwa jitihada zangu
zote.
“Subiri kidogo mpenzi” nilinong’ona taratibu kando ya sikio lake hata hivyo Zera
hakutaka kunisikia badala yake akaendelea kunipapasa maungoni mwangu.
“Mpenzi…!” nilimuita huku nikifanya jitihada za kujinasua mikononi mwake bila
mafanikio. Kufumba na kufumbua ulimi wake laini ulikuwa kwenye tundu la sikio
langu huku ukisababisha kiwango kikubwa cha hisia kuwahi kunitokoea mwilini.
Sikutaka kuendelea kuiruhusu zaidi hali ile hivyo hatimaye nikaamua kutumia nguvu
katika kujinasua mikononi mwake. Jitihada zangu zikafua dafu kwani hatimaye
nikafanikiwa kumshinda shetani na vishawishi vyake.
Zera akaondoa mikono yake haraka maungoni mwangu na kunikata jicho lenye
chuki na hasira halafu akanisukuma kando kiasi kwamba kama nisingekuwa makini
ningeweza kupiga mwereka mbaya.
“Wewe ni mwandishi wa habari?” hatimaye Zera akaniuliza kwa hasira.
“Habari zipi mpya huyo mwandishi wa habari anaweza kuzitafuta humu ndani
bibie?” nilimuuliza Zera huku nikijitahidi kuurudisha urafiki wetu ulionza kuingia
nyufa.
“Sasa umefuata nini humu ndani?” Zera akaniuliza kwa jazba.
“Tafadhali! hebu keti kwanza unisikilize mpenzi” nilimwambia Zera ambaye
wakati huu alikuwa tayari amesimama kwa hasira huku akinikata jicho.
“Sitokurudishia pesa zako” hatimaye Zera akavunja ukimya baada ya kitambo
kirefu cha ukimya kupita mle ndani huku tukitazamana.
“Ondoa shaka!” nilimwambia na hapo Zera akanitazama kwa mshangao na kuketi
taratibu kando yangu.
“Zungumza shida yako” hatimaye akaniuliza kwa sauti tulivu ya upole.
“Nitachukua dakika chache za muda wako” nilimwambia huku nikigeuka na
kumtaza wakati huo mkono wangu ukifanya ziara fupi kwenye sehemu za mapaja
yake.
“Zungumza!” akaniambia huku akiendelea kunitazama na hapo nikaichukua
ile sigara mkononi mwake na kuivuta mapafu kadhaa kisha nikamrudishia huku
nikiupuliza moshi taratibu katika namna ya kuipa utulivu akili yangu kisha nikavunja
ukimya
“Nahitaji kuonana na Milla Cash bila shaka unaweza kunisaidia kumpata”
nilimwambia Zera huku nikimtazama usoni na nilichokiona machoni mwake ni
mshangao wa hali ya juu.
“Hicho ndiyo kilichokuleta humu ndani?” hatimaye Zera akaniuliza kwa utulivu
huku akiutikisa mguu wake uliokuwa juu ya mwingine huku macho yake yakitazama
mbali na eneo lile kama mtu anayetafakari kitu.
“Nahitaji msaada wako” nilimwambia kwa utulivu.
“Sasa utamuuliziaje Milla Cash wakati upo na mimi. Huoni kuwa unanivunjia
heshima?” Zera aliongea kwa hasira kidogo lakini sauti yake bado ilikuwa na utulivu na
hapo nikacheka moyoni huku nikijiuliza kahaba kama yule ni heshima gani aliyokuwa
akiizungumzia.
“Sina maana hiyo mpenzi” nilimwambia kwa utulivu.
“Unadhani Milla Cash ni msichana mzuri na mrembo zaidi yangu?” Zera akaniuliza
na swali lake likanifanya nifahamu kuwa alikuwa akihisi wivu kwa kumuulizia Milla
Cash na siyo yeye na hapo nikatabasamu kidogo
“Ungekuwa hujathubutu kuzigaragaza vibaya hisia zangu huwenda ningekubaliana
na maneno yako” nilimwambia huku nikiangua kicheko hafifu cha kirafiki.
Zera akatabasamu kidogo huku akiipeleka sigara yake mdomoni. Nilipomtazama
usoni nikagundua kuwa maneno yangu yalikuwa yameukosha vizuri moyo wake.
Nijuavyo mimi ni kuwa ukitaka mwanamke akusikilize basi anza kwa kumsifia juu ya
uzuri wake lakini Zera alistahili sifa.
“Nina shida naye binafsi”hatimaye niliongea kwa utulivu
“Shida gani?”
“Binafsi”
“Sasa si ungemuulizia kule mapokezi badala ya kuja kwangu?”
“Nilihisi kuwa huwenda nisingepata ushirikiano wa kutosha” nilimwambia Zera
huku nikimtazama usoni.
“Wewe ni Njagu?” Zera aliniuliza kwa utulivu huku akigeuka na kunitazama na
hapo nikajua kuwa alitaka kufahamu kama mimi nilikuwa askari polisi au lah!
“Kwanini unaniuliza hivyo?” nilimuuliza kwa udadisi.
“Unaonekana kama polisi na sisi humu ndani polisi hatuwataki” maneno ya Zera
yakawa yamenivuta na hapo nikageuka na kumtazama kwa makini.
“Mimi siyo polisi lakini kwa nini hamuwapendi polisi na wakati wao ndiyo wanaolinda usalama wenu?” nilimuuliza Zera na hapo nikamuona akiupisha utulivu
kichwani mwake. Kitendo kile cha kuchelewa kunijibu kikanifanya nihisi kuwa
alikuwa akijipanga namna ya kukwepa kunieleza ukweli wa jambo fulani la mle ndani
ambalo mimi sikulifahamu.
“Polisi huwa wanatusumbua mara kwa mara wakidai biashara yetu ni kinyume na
sheria za nchi na wakati baadhi yao ni wateja wetu wa kuaminika”
Nilimsikiliza Zera pasipo kutia neno lolote badala yake nikatabasamu kidogo huku
nikifahamu fika kuwa lile halikuwa jibu sahihi la swali nililomuuliza huku mashaka
juu ya kilichokuwa kikiendelea ndani ya casino ile yakizidi kuniingia. Nilitulia kidogo
nikiikumbuka ile mifuko myeusi niliyowaona nayo wale watu mle ndani ya casino na
hapo akili yangu ikapoteza kabisa utulivu.
“Milla Cash yupo chumba namba ngapi humu ndani?” nilimtupia swali Zera
nikinuia kumrudisha kwenye msingi wa maongezi yetu. Zera aligeuka tena na
kunitazama kisha akaongea kwa utulivu baada ya kuitoa sigara mdomoni.
“Hakuna mtu yeyote miongoni mwetu anayefahamu. Humu ndani kuna idadi ya
vyumba vipatavyo sitini na nane na kila mmoja ana chumba chake kama unionavyo
mimi humu ndani na mbaya zaidi wengine hatufahamiani”
“Kwa nini msifahamiane?” nilimuuliza Zera kwa udadisi.
“Huwa tunaingia humu ndani kwa zamu. Kuna wanaoingia asubuhi saa mbili
asubuhi na kutoka saa mbili usiku na tupo wale tunaoingia saa mbili usiku na kutoka
saa mbili asubuhi ya siku inayofuata. Hivyo katika mazingira kama hayo unaweza
kuona mwenyewe kuwa ni kwa nini inakuwa vigumu kufahamiana miongoni mwetu”
Zera aliongea huku akiipeleka sigara yake mdomoni na hapo nikageuka na kumtazama
tena kwa udadisi. Kwa mara nyingine tena nafsi yangu ikajikuta ikiridhika kuwa Zera
alikuwa miongoni mwa wasichana wachache wazuri sana kawahi kuonekana kwenye
sayari hii. Niliupisha tena utulivu kichwani mwangu huku nikianza kuhisi ugumu wa
kazi iliyokuwa mbele yangu.
Wakati nikizama katika tafakuri ile mawazo juu ya yule mtu aliyenivamia kule
chooni yakaanza kuchipua upya katika fikra zangu huku nikijiuliza kuwa kwanini mtu
yule alitaka kuniua. Ina maana kuna watu waliokuwa wakifahamu sababu ya uwepo
wangu mle ndani?. Watu hao walifahamu vipi na nani aliyewaambia?. Nikaendelea
kujiuliza bila kupata majibu.
Nikajikuta nikizikumbuka pia sheria za casino ile kwenye kile kitabu kidogo
nilichopewa na yule binti asubuhi ile. Mojawapo ya sheria zile ni kuwa hakuna mtu
aliyekuwa akiruhusiwa kuingia na silaha mle ndani. Swali likabaki kuwa yule mtu
aliyenishambulia kule chooni aliwezaje kuingia na bastola humu ndani ya casino?.
Niliendelea kujiuliza bila kupata majibu huku mbele yangu nikihisi bado kulikuwa na
kiza kinene katika kuyapatia uvumbuzi maswali yangu.
Niliuinua mkono wangu na kuitazama saa yangu ya mkononi na hapo nikaridhika
na mwenendo wa majira yake. Baada ya muda mfupi ile maiti ya yule mtu kule chooni
ingeshtukiwa na sikutaka suala hilo litokee huku mimi nikiwa bado nipo mle ndani ya casino. Hivyo nikageuka kumtazama Zera kwa tabasamu langu la kichokozi.
“Wasichana wote wa humu ndani wanaofanya kazi kama yako huwekewa ulinzi
kama ilivyo kwa Milla Cash?” nilimuuliza Zera huku nikimtazama machoni. Zera
akanitazama kama anayefikiria jambo fulani na alipoitoa sigara mdomoni na kuupuliza
moshi pembeni akaongea kwa utulivu pasipo kunitazama.
“Hapana!”
“Wewe huwa unafikaje hapa casino?”
“Huwa tunapitiwa na basi dogo la hii casino kutoka majumbani mwetu tunapoishi”
Jibu la Zera likanifanya nimkumbuke Milla Cash na lile gari jeusi linalomleta
casino nyakati za usiku aina ya Texas Laghorn Tailgate Van na hapo hoja fulani ikaanza
kujengeka kichwani huku nikijiuliza ni kwa nini yeye peke yake ndiye aliyekuwa
akiletwa na gari lile pale casino. Bado jibu sikulipata hivyo nikayaacha mawazo yangu
yakielea hewani pasipo kupata mhimili mzuri wa hoja.
Nilipomtazama Zera pale pembeni yangu nikahisi kuwa huwenda alikuwa
akijiuliza maswali kadhaa juu ya uwepo wangu mle ndani.
“Unamuhitaji Milla Cash?” hatimaye Zera akaniuliza kwa utulivu huku macho
yake yakizitazama kuta za kile chumba.
“Ndiyo! nitafurahi sana endapo utanisaidia kuonana naye” nilimwambia Zera kwa
utulivu.
“Sifahamu mahali anapoishi hapa jijini Dar es Salaam hata hivyo bado ninaweza
kukusaidia mahali utakapoweza kuonana naye ingawa utalazimika kuwa na subira
kidogo” Zera alimaliza kuongea kisha akaipeleka sigara yake mdomoni. Niligeuka na
kumtazama Zera huku moyo wangu ukiwa umeanza kupata matumaini.
“Kweli?” nilimuuliza Zera kwa kutaka kuhakikisha maneno yake.
“Nakuahidi ondoa shaka kaka hata hivyo itabidi unilipe kwani ni kazi ya hatari“
Zera akaongea kwa msisitizo.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Hatari iko wapi?” nilimuuliza Zera kwa shauku.
“Siwezi kukueleza chochote ila utakapofanikiwa kuonana na Milla Cash utamuuliza
swali hilo” Zera akaniambia kwa utulivu huku akionekana kutokuwa tayari kunieleza
chochote juu ya hatari hiyo nami sikutaka kumlazimisha.
“Utanitoza pesa kiasi gani?” hatimaye nikamuuliza
“Shilingi laki mbili” Zera akatamka haraka kama aliyekwisha kupanga kiwango
kile cha pesa hapo kabla.
“Usijali fanya kazi yangu pesa yako nitakulipa. Unadhani hadi lini utakuwa
umeikamilisha?” nilimuuliza Zera na baada ya kufikiria kidogo akanijibu.
“Mpaka kesho jioni kabla ya kuja hapa huwenda kazi yako tayari nikawa
nimeikamilisha”
“Nitafurahi sana” niliongea huku nikiingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda
kingine cha pesa zenye thamani ya shilingi laki moja kisha nikampa Zera.
“Chukua pesa hii kama malipo ya awali ya kazi yangu” nikamwambia.
“Wala usihofu kazi yako nitaifanya” Zera akaniambia huku akizihesabu zile noti na alipomaliza akageuka na kunitazama
“Wapi tutakutana?” hatimaye akaniuliza.
“Hapa hapa kesho usiku muda na wakati kama huu” nilimwambia huku nikiumba
tabasamu.
“Hapana!” Zera akakataa na kunikazia macho
“Vipi kutakuwa na shida yoyote?” nilimuuliza Zera kwa mshangao.
“Hii ni sehemu ya kazi na kazi yako haihusiani na hapa” Zera akaniambia kwa
utulivu huku akinikata jicho la kunionya juu ya kuleta mazoea na kazi yake. Ukimya
ukapita kidogo huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu kisha nikamuuliza tena
Zera.
“Mmiliki wa hii casino ni nani?”
Swali langu bila shaka lilimshangaza sana Zera na hapo akageuka na kunitazama
kabla ya kuangua kicheko cha kikahaba.
“Vipi unataka kuinunua?”
“Hapana! nilipenda tu kufahamu” nilimwambia Zera kwa utulivu huku
nikitabasamu.
“Hakuna anayemfahamu mmiliki wa casino hii kaka” Zera akaniambia huku
akiendelea kucheka na nilipoyatafakari maneno yake nikagundua kuwa alikuwa
akizungumza ukweli.
“Kwa hiyo tutakutana wapi?” Zera alipomaliza kucheka akaniuliza kwa utulivu.
Nilitulia kidogo nikifikiria juu ya sehemu ya kukutana halafu nilipokuwa mbioni kutoa
jibu ghafla nikapata wazo na hapo nikaichukua wallet yangu kutoka kwenye mfuko wa
suruali yangu na kuifungua. Nikatoa kadi ndogo ya biashara ama business card yenye
kila kitu feki kama;jina la kampuni,tovuti,barua pepe,jengo na mtaa wa kampuni hiyo
inapopatikana pamoja na nukushi isipokuwa namba ya simu tu ambayo ilikuwa mpya
kabisa ambapo nilimpa Zera.
“Utanipigia simu pale utakapokuwa umekamilisha kazi yangu” nilimwambia
Zera na hapo akaipokea ile kadi na kuitazama kwa makini huku wasifu wangu batili
wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kukata na kusafisha madini ukiwa umeanza
kumzuzua. Zera alirudia kusoma wasifu wangu kwenye ile kadi huku akinitazama.
“Unaishi wapi hapa jijini Dar es Salaam?” nilimuuliza Zera.
“Naishi eneo la Kinondoni B mtaa wa Ukutavuka. Ukifika eneo la Biafra kituo cha
Kanisani unaingia upande wa kushoto ukiifuata barabara ya mtaa wa Bolingonanga halafu
mbele kidogo upande wa kushoto unaingia barabara ya mtaa wa Isere. Hutosafiri
sana na barabara ya mtaa huo mbele kidogo utakutana na barabara nyingine ya lami
inayoingia upande wa kulia kwako. Hiyo ndiyo barabara ya mtaa wa Ukutavuka.
Huwezi kupotea kwani kuna kibao cha barabara kinachoelekeza jina la mtaa huo.
Ukifika kwenye huo mtaa niulizie kwa jina la Zera utanipata kwani kila mtu wa mtaa
huo ananifahamu.
“Unaishi nyumba namba ngapi ya mtaa huo?” nilimkatisha Zera.
“Naishi nyumba namba 12 ina geti jekundu kwa mbele na ina tazamana na duka kubwa la madawa lenye jina la MM Pharmacy”
Mojawapo ya kigezo kilichotumika kunitunuku nishani ya juu ya masuala ya
upelelezi ni wepesi wa akili yangu katika kunasa na kuhifadhi taarifa za namna yoyote
kwa muda mrefu. Hivyo maelezo ya Zera nilikuwa nimeyanasa vyema kichwani.
Niligeuka na kumtazama Zera huku nikiyapapasa mapaja yake kisha nikatazama
muda kwenye saa yangu ya mkononi. Sikuwa na kitu kingine cha kufanya mle ndani
hivyo nikawa nimeamua kuondoka lakini wakati nikiwa kwenye hali ile mara simu
ya mezani iliyokuwa kule kwenye kile chumba cha awali ikaanza kuita. Mwito wa
simu ile ukamshuta Zera na hapo akageuka na kunitazama kwa mashaka kabla ya
kusimama haraka na kuelekea kule kwenye kile chumba kuipokea ile simu. Wasiwasi
niliouona machoni mwa Zera ukanisukuma na mimi kusimama na kumfuata Zera
kule kwenye kile chumba. Hivyo wakati Zera akiipokea ile simu mimi nilikuwa kando
yake nikimsikiliza.
“Haloo!” sauti ya upande wa pili iliita.
“Haloo nakusikia zungumza” Zera akaongea kwa utulivu huku akinitazama.
“Bila shaka naongea na chumba namba 26,sivyo?” ile sauti ya upande wa pili
iliuliza na niliweza kuihisi sauti ile kuwa ilikuwa ya kiume.
“Ndiyo chumba namba 26 hapa zungumza nakusikia” Zera akasisitiza.
“Kuna mwanaume yoyote chumbani kwako?” ile sauti ya upande wa pili iliuza tena
na niliweza kuisikia kwa mbali kutoka pale Zera aliposimama. Swali lile likamfanya
Zera ageuke na kunitazama kwa mashaka lakini niliwahi kumuonya kwa kumfanyia
ishara ya kukataa. Zera alikuwa mwepesi kunielewa.
“Hakuna mtu yoyote” hatimaye Zera akaongea kwa utulivu kwenye ile simu
“Una hakika?” ile sauti ya upande wa pili wa simu ikauliza kwa msisitizo
“Ndiyo! mteja wangu wa mwisho alikuwa ni yule mwarabu na naye ameshatoka”
“Okay! mwanaume yeyote atakayeingia chumbani kwako kuanzia sasa utanijulisha”
“Sawa!” Zera akaitikia kwa utulivu na ile simu upande wa pili ilipokatwa Zera
akairudisha mahala pake na hapo akageuka na kunitazama kwa wasiwasi.
“Mbona kama wanakuuliza wewe?” Zera akaniuliza huku uso wake ukionesha
mashaka,
“Bila shaka!” nikamjibu Zera huku nikifikiria uongo wa kumwambia utakao
karibiana na ukweli kwani endapo ningekataa kuwa siyo mimi niliyekuwa nikiuliziwa
kwenye ile simu Zera angeanza kuingiwa na mashaka na mimi.
“Sasa kwa nini ukanikataza nisiitikie?” Zera akaniuliza kwa mshangao.
“Kuna rafiki yangu nimekutana naye humu ndani sasa ananing’ang’ania na
anataka kunichomoa pesa ndiyo ikabidi nimtoroke nikamwambia kuwa nakuja huku
vyumbani kutafuta mrembo wa kustarehe naye. Sasa naona jamaa kapatwa na mashaka
baada ya kuona sipatikani kwenye simu kwani simu yangu nimeizima” niliongea huku
nikijichekesha mbele ya Zera katika namna ya kumzuga ingawa akilini nilishaanza
kuhisi kuwa huwenda ile maiti ya yule mtu kule chooni ilikwisha gundulika.
“Kama ni hivyo basi una haki ya kumkimbia” Zera akaongea kwa utulivu na nilipomtazama usoni nikafurahi kuwa angalau nilikuwa nimefanikiwa kumlainisha
hata hivyo sikutaka kuendelea kukaa mle ndani. Huku nikifahamu kuwa baada ya
muda mfupi polisi wangefika pale kwenye casino na kuanza uchunguzi wao nikaamua
kuagana na Zera kisha nikaelekea mlangoni ambapo niliufungua na kutoka nje.
Nilikuwa nimejiandaa kwa hali yoyote hivyo mara tu nilipotoka nje ya kile chumba
cha Zera niliigeuza kofia yangu nyuma kisha nikachukua miwani mfukoni na kuivaa
huku nikiharakisha kuelekea kwenye zile ngazi za kushukua ukumbi wa chini wa
casino. Lakini kabla sijashuka nilitazama kule chini kwenye ule ukumbi wa casino na hali
ya mambo haikuniruhusu kutimiza adhma yangu.
Watu wote mle ukumbini walikuwa wakielekea kule nyuma kwenye lile eneo la
maliwato ya casino na baadhi ya wanawake walikuwa wakilia. Nikajua ile maiti ya mtu
niliyepambana naye kule chooni ilikuwa tayari imegundulika na baadhi ya mabaunsa
wa casino ile walikuwa wakihaha haku na kule kumtafuta mtu aliyehusika na mauaji
yale.
Sikushuka tena kule chini ya ule ukumbi wa casino na badala yake nikashika uelekeo
wa kule nilikotoka nikitafuta njia nyingine mbadala ya kutokea nje ya jengo lile pasipo
kupitia kwenye ule mlango mkubwa wa mbele wa ile casino. Nilitembea kwa haraka
huku macho yangu yakizunguka huku na kule kutafuta sehemu ya kutokea.
Hatimaye nikakutana na milango miwili iliyokuwa upande wa kulia. Nilipoichunguza
milango ile nikagundua kuwa ilikuwa ni milango ya vyoo kama vile vya ule ukumbi wa
chini. Choo cha kiume na cha kike. Bila kupoteza muda nikaufungua ule mlango wa
choo cha kiume na kuzama ndani. Mandhari ya mle ndani hayakutofautiana kabisa na
vile vyoo vya kule chini kwenye ule ukumbi wa casino.
Nikaanza kuzunguka mle ndani nikitafuta sehemu ya kutokea nje lakini nilishindwa
kwani mle ndani hapakuwa na upenyo wa namna yoyote na kila sehemu ilikuwa
imezibwa kwa kuta nene. Sehemu ya juu ya dari ya kile choo ilikuwa imefunikwa kwa
ukuta wa zege kwa ajili ya sakafu ya ghorofa inayofuata. Nikiwa nimeridhika kuwa
nisingeweza kuitimiza adhma yangu ya kutoka nje ya lile jengo la casino kwa kupitia
mle ndani sikutaka kupoteza muda mle ndani. hivyo nikafungua mlango wa kile choo
na kutoka nje.
Mara tu nilipotoka nje ya kile choo nikawaona wanaume wawili mabaunsa wa
ile casino wakija upande wangu. Sikutaka wale mabaunsa wanifikie hivyo nikashika
uelekeo wa upande wa kushoto nikiharakisha kwenda mbele huku macho yangu
yakitazama huku na kule nikiendelea kutafuta sehemu ya kutokea. Hata hivyo kabla
sijafanikiwa wale mabaunsa walikwishanifikia na kunitahadharisha.
“Oyaa! braza hebu simama” baunsa mmoja alinionya hata hivyo niliendelea na
safari yangu huku nikijidai sijamsikia.
“Oyaa! vipi unajidai hutusikii au ndiyo unaleta kiburi?” mwenzake akasisitiza.
Haraka nikatazama kule mbele yangu na bado sikuona matumaini ya kutoka mle
ndani kwa hila hivyo ikanibidi nipunguze mwendo na kugeuka nyuma.
“Vipi mnaniongelesha mimi?” niligeuka na kuwauliza.
“Sasa unadhani tunamwambia nani mwingine kama siyo wewe!” mmoja akafoka
huku akiongeza hatua zake kunikaribia.
“Mimi siitwi wewe bwana hebu tumieni majina ya heshima basi” niliwaambia wale
mabaunsa huku nikizipima vizuri hatua zao kadiri walivyokuwa wakizidi kunikaribia.
“Huku unaelekea wapi?” mmoja aliniuliza pindi waliponifikia.
“Kwani nyinyi mnaenda wapi?” nikawarudishia lile swali.
“Oyaa mbona unajitia kiburi hebu jibu ulivyoulizwa” mwenzake akadakia huku
akizidi kunisogelea.
“Mna shida gani na mimi hadi mniulize mahali ninapoelekea wakati mnaniona
bado nipo humu ndani ya casino?” niliwauliza huku nikawatazama wale mabaunsa.
Miili yao ilikuwa mikubwa iliyotuna na yenye misuli iliyokaza na kugawanyika vizuri
kwa mazoezi makali yenye ratiba inayozingatiwa vizuri. Nguo walizovaa;fulana nyeupe
na suruali nyeusi za jeans hazikufanikiwa kuificha miili yao.
“Geuka nyuma na tunaenda na wewe” baunsa mmoja alinionya baada ya
uvumilivu wake kuonekana kufika kikomo na hapo kwa pamoja nikaanza kuwaona
wakinisogelea pale niliposimama.
”Niende wapi na nyinyi kwani mmekuja na mimi humu ndani?” niliwauliza kwa
jazba za kuchelewesha na hapo baunsa mmoja akawahi kunishika kwa nyuma na
kunikwida na kutokana na ukubwa wa mwili wake nikawa nimeenea vizuri kwenye
kabari matata ya mkono wake wenye nguvu.
“Mnanipeleka wapi nyie mabwege?” niliwauliza kwa hasira huku nikijitahidi
kufurukuta.
“Agh! sisi mabwege siyo eh! basi subiri uone kazi yetu” yule baunsa aliyenikwida
akaongea kwa hasira huku akizidi kunibana kwa nguvu kisha akamwambia mwenzake.
“Oyaa! Kibusta atatusumbua sana huyu fala hebu mlegeze kidogo”
Sikuelewa maana ya maneno yale hadi pale nilipoziona ngumi mbili za nguvu na za
chapuchapu zikitua tumboni mwangu na kunisababishia maumivu makali yasiyoweza
kusimulika huku nikianza kuhisi kichefuchefu. Tumbo lango lilikuwa limekorogeka
vibaya na kwa mbali ladha chungu ya nyongo ikaanza kutembea kwenye ulimi wangu
na hapo nikaanza kuifikiria roho yangu.
Ngumi nyingine zilipotupwa niliikaza vizuri misuli ya tumbo langu kukabiliana
na maumivu yake hata hivyo kuendelea kuruhusu kichapo cha namna ile tumboni
nilitambua kuwa kingezidi kuidhoofisha afya yangu. Hivyo nilikusanya nguvu za
kutosha kisha nikajipinda na kumtandika kichwa cha nguvu yule baunsa aliyenishika
nyuma yangu na hapo nikasikia kelele za yowe kali la maumivu. Yule baunsa akaniachia
mwenyewe bila kupenda. Kile kichwa nilichomtandika kilikuwa kimeupasua na
kuusaga vibaya mwamba wa pua yake huku sehemu ya mbele ya mdomo wake
ikichanika na kuvuja damu. Wale mabaunsa walikuwa na nguvu za ajabu lakini
walikuwa hawafahamu mbinu za mapigano hivyo hawakuweza kufua dafu mbele
yangu.
Wakati yule baunsa mwingine niliyemtandika kichwa akijishika usoni kuugulia maumivu yule mwenzake akasogea haraka kunikabili huku akirusha ngumi moja
ambayo niliiona mapema nikainama kidogo na kuikwepa kisha nikamtandika ngumi
moja ya nguvu mbavuni. Yule baunsa akapiga yowe kali la maumivu na kubweka kama
mbwa na kabla hajatulia vizuri nikamsindikiza na teke zito la mgongoni lililompekea
ajibamize vibaya kwenye ukuta wa ile korido na hapo tusi zito likamponyoka. Alipotaka
kugeuka nikamzaba ngumi kavu mbili za shingo zilizompotezea mawasiliano na
ubongo na hapo akaangua chini na kutulia.
Yule mwenzake niliyekuwa nimemtandika kichwa pale awali akaanza kunifuata
kwa hasira. Aliponifikia akarusha teke lakini nilikua makini kuishtukia dhamira yake
hivyo nikawahi kujitupa pale chini huku nikiliacha lile teke lake likikata hewa bila
mafanikio. Ilikuwa nafasi nzuri kwangu hivyo nikajizungusha na kumchota mtama
wa aina yake na hapo yule baunsa akapaa hewani mzobemzobe alipotua chini akatulia
kimya huku fahamu zikiwa mbali na nafsi yake.
Nikayumbayumba hadi pale nilipopata mhimili mzuri wa ukuta wa ile korido na
hapo nikajiegemeza huku nikihema ovyo kuirudisha pumzi mwilini mwangu. Yale
madubwana mawili yalikuwa yamelala pale chini sakafuni huku yakiwa hayajitambui.
Nikiwa bado nimeegemea ule ukuta huku nikiendelea kuhema ovyo mara nikasikia
sauti ya hatua za mtu mwingine akija upande ule. Sikutaka kusubiri hivyo nikaanza
tena kuharakisha nikielekea kule mbele ya ile korido ingawa sikuweza kufahamu kuwa
nilikuwa nikielekea wapi. Hatimaye bahati ikaangukia kwangu kwani mbele kidogo ya
korido ile upande wa kulia nikaziona ngazi nyembamba zinazoelekea sehemu ya juu
ya lile jengo la casino. Chini ya ngazi zile kulikuwa na mlango mdogo kwenye chumba
kidogo kisichoeleweka ujenzi wake. Ingawa sikuwa na utaalam wowote katika masuala
ya ujenzi lakini kuiona sehemu ile nikakumbuka kitu.
Kilikuwa chumba kidogo chenye Mainswitch ya umeme wa lile jengo lote la
casino. Ufundi umeme ulikuwa miongoni mwa fani zangu hivyo niliufungua ule
mlango mdogo wa kile chumba kisha nikaanza kufanya utundu wangu. Kufumba na
kufumbua jengo lote la ile casino likagubikwa na giza zito na hapo kazi iliyosalia ikawa
rahisi sana kwangu.
Haraka nikarudi kule chini kwenye ule ukumbi wa casino na kwa kuwa hakuna
mtu yeyote aliyeweza kuniona kutokana na giza la mle ndani hivyo ikawa rahisi sana
kwangu kujichanganya kwenye kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbilia mlango
wa kutokea nje ya ile casino huku wengi wao wakiwa ni wanawake waliokuwa wakipiga
makelele ya hofu.
Kwa uzoefu niliokuwanao nilifahamu fika kuwa jengo kama lile lisingekosa
jenereta kubwa la kusambaza umeme pale inapotekea kuwa ule umeme wa gridi ya
taifa umekatika. Hata hivyo nilikuwa na hakika kuwa kutokana na ukorofi niliyoufanya
kwenye kile chumba cha umeme wa jengo lile la casino hata jenereta hilo lisingeweza
kufua dafu.
Hapakuwa na namna ya kuwazuia watu wasitoke nje ya lile jengo la casino kwa
kuzingatia kuwa usalama wa watu lilikuwa zingatio la kwanza katika biashara za namna ile. Hivyo nikajichanganya katika kundi lile kubwa la watu waliokuwa wakikimbia
ovyo kwenda nje huku tabasamu maridhawa likifanya ziara usoni mwangu.
Kitu kilichozidi kuwachanganya watu ni kuwa majengo yote ya jirani na lile jengo
la ile casino yalikuwa na umeme. Hali ile ikampelekea kila mmoja aanze kuongea lake.
Baadhi ya watu niliwasikia wakiwashuku magaidia kuwa walikuwa wakihusika na
lile tukio la kifo cha yule mtu kwenye ile casino na baadaye kukatika kwa umeme.
Wengine nikawasikia wakiilaani miundo mbinu ya umeme wa jengo lile kuwa ilikuwa
mibovu tangu siku nyingi bila kubadilishwa.
Wengine nikawasikia wakidai kuwa umeme wa lile jengo la casino ulikuwa
umezimwa makusudi ili kufanikisha mpango wa mauji ya watu uliyoanza kutekelezwa
mle ndani. Ili mradi kila mtu alikuwa huru kuzungumza vile alivyojisikia lakini ukweli
wa mambo niliufahamu mimi.
Nje ya lile jengo la casino kila mtu aliharakisha kuliendea gari lake na wale wasiokuwa
na magari wao waliekea kwenye geti la kutokea nje ya eneo lile la casino kisha kila
mmoja akashika uelekeo wake.
Nililifikia gari langu nikafungua mlango na kuingia ndani kisha nikaipekua bastola
yangu na kuridhika kuwa bado ilikuwa kwenye maficho yake salama. Niliwaza kuwa
kuondoka kwangu eneo lile mapema kungeweza kutengeneza chanzo kizuri cha
upelelezi wa tukio lile la mauaji kwenye ile casino. Hivyo niliendelea kusubiri mle ndani
ya gari na baada ya magari manne kunitangulia kuondoka kwenye yale maegesho
na mimi ndiyo nikaunga mkia nyuma yao huku mche wa sigara ukiteketea taratibu
mdomoni mwangu.
Usiku ulikuwa mbioni kushamiri na kwa mbali manyunyu hafifu ya mvua yalianza
kuanguka kutoka angani nami nikayaondoa mbele yangu kwa kuwasha wiper za kioo
cha mbele cha gari langu. Mvua za masika bado zilikuwa zikiendelea kunyesha sehemu
mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
_____
MUDA MFUPI BAADAYE mafundi umeme kutoka kitengo cha dharura cha
shirika la umeme la Tanesco walikuwa ndani ya lile jengo la Vampire Casino wakifanya
kazi waliyoitiwa.
Kwa weledi wao na maarifa ya masuala ya umeme waliyokuwa nayo wakamtoa
hofu meneja wa casino ile mwanaume mrefu na mwembamba aliyeshindwa kabisa
kuitowesha hasira yake usoni tangu kugundulika kwa yale mauaji kule chooni na
hatimaye kukatika kwa umeme katika lile jengo la casino.
Mafundi wale wa umeme wakamuweka bayana meneja wa casino ile kwa kumueleza
kuwa tatizo lile la kukatika kwa umeme kwenye lile jengo la casino lilikuwa limetokana
na fyuzi chache muhimu zilizochomolewa kutoka kwenye Mainswitch iliyokuwa
ikisambaza umeme kwenye lile jengo la casino. Huku wakisisitiza kuwa hakukuwa na
uharibifu wowote uliokuwa umetokea katika miundo mbinu ya umeme wa lile jengo.
Hatimaye wakarudishia zile fyuzi na hapo umeme wa lile jengo ukawaka.
Wakati wale mafundi umeme wa kitengo cha dharura kutoka Tanesco wakiondoka
kwenye lile jengo la casino baada ya kukamilisha kazi yao mlangoni wakapishina na yule
mkuu wa kituo cha polisi cha mjini kati ASP O.J.Mkwaju Ngoma akiwa ameongozana
na askari wake watatu vijana wa kazi huku wote wakiwa wamevaa sare zao za polisi.
Taarifa za mtu aliyeuwawa katika choo cha Vampire Casino zilikuwa zimeifikia ofisi
yake kupitia simu ya mlinzi mmoja wa casino ambaye hakupenda kujitambulisha jina
lake. Askari wale walipoingia ndani ya casino wakafahamiana na baadhi ya uongozi wa
casino ile kisha wakaelekea moja kwa moja hadi kwenye eneo la tukio.
Kulikuwa na watu wachache waliosalia wakiitazama ile maiti ya yule mtu aliyeuwawa
kwenye kile choo cha casino. Miongoni mwa watu hao walikuwa ni wafanyakazi wa ile
casino ambao walikuwa wakimsikiliza kwa makini kijana mmoja ambaye alijinadi kuwa
yeye ndiye aliyekuwa shuhuda wa kwanza kulishtukia tukio lile la mauaji. Kijana yule
akaacha kusimulia mara baada ya kumuona ASP O.J.Mkwaju Ngoma akiingia eneo
lile huku ameongozana na askari wake.
“Poleni sana jamani!” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akasimama na kuisalimia
kadamnasi ile.
“Tumeshapoa Afande” wote wakaitikia na hapo ASP O.J.Mkwaju Ngoma akaanza
kujitambulisha.
“Sisi ni askari tunaotokea kituo cha polisi cha mjini kati. Tafadhali! tunaomba
mtupishe kidogo tufanye kazi yetu. Hata hivyo tungeomba maelezo machache kama
kutakuwa na shuhuda yeyote mwenye taarifa za kutusaidia” ASP O.J.Mkwaju Ngoma
alimaliza kuongea kisha akachezesha sharubu zake na kujivika tabasamu la kirafiki.
Wale mashuhuda kuona vile wote wakageuka na kumtazama yule kijana aliyekuwa
mstari wa mbele akiwasimulia namna alivyokuwa wa kwanza kuishtukia ile maiti ya
yule mtu pale chooni na hiyo ikiwa ishara nzuri kwa ASP O.J.Mkwaju Ngoma kupata
kupata sehemu ya kuanzia mahojiano yake. Hivyo akageuka na kumtazana yule kijana
aliyekuwa akitazamwa na wale watu eneo lile huku akitengeneza tabasamu hafifu
usoni mwake.
“Ulikuwepo hapa wakati mauaji haya yalipofanyika?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma
akauliza huku akimtazama kijana yule kwa makini.
“Sikuwepo ila nilikuwa shuhudua wa kwanza kuishtukia maiti hii” yule kijana
akaongea kwa kujiamini na hapo askari mmoja miongoni mwa wale watatu akasogea
na kuanza kuchukua maelezo yake.
“Nyinyi wengine mnaweza kwenda ili mtupe uhuru wa kufanya kazi yetu” ASP
O.J.Mkwaju Ngoma akawataka wale mashuhuda wengine waondoke eneo lile na
wakati wale watu wakiondoka akawaambia
“Naomba mtuitie na meneja wa hii casino”
Wakati wale mashuhuda wakitawanyika wale askari polisi wawili waliosalia
wao walikuwa wakishughulika na kuufungua ule mlango wa kile choo kwani wale
mashuhuda walikuwa wameitazama ile maiti ya yule mtu kwa kuchungulia kwa juu
kupitia choo cha jirani.Ule mlango ulipofunguka askari wote wakasogea karibu na kuitazama ile maiti
ya yule mtu. Kichwa cha ile maiti kilikuwa kimepasuka vibaya baada ya kubamizwa
kwenye sinki la choo cha mle ndani na hivyo kupelekea ubongo wake na damu nyingi
kutapakaa eneo lile huku mguu na mkono wake mmoja ukiwa umevunjika.
“Jina lako?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza yule kijana huku yule askari
wake pembeni akiendelea kuchukua yale maelezo. Baada ya yule kijana kujitambulisha
mahojiano yakaendelea.
“Wewe ni mteja au mfanyakazi wa hii casino?”
“Mfanyakazi”
“Kazi yako?”
“Kusafisha vyoo vya hii casino” yule kijana akaendelea kutoa maelezo huku akianza
kuingiwa na woga wa kuhojiwa na polisi.
“Ilikuwa majira ya saa ngapi wakati ulipoishtukia maiti ya huyu mtu?”
“Kati ya saa tatu na nusu na saa nne kasoro usiku huu”
“Ilikuwaje?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza yule kijana huku akimkazia
macho.
“Mimi kazi yangu ni kusafisha vyoo vyote vya hii casino hivyo mara kwa mara huwa
napita kufanya usafi. Sasa wakati naingia humu ndani kusafisha ndiyo nikashtuka
baada ya kuona damu nyingi ikitoka na kusambaa chini ya huu mlango wa choo” yule
kijana akamaliza kuongea huku akizitazama nyuso za wale askari.
“Sasa ulihisi nini baada ya kuiona hii damu?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza
yule kijana huku akiyapeleka macho yake tena kuitazama ile maiti.
“Nilihisi jambo la hatari ndiyo nikatoka kwenda kuwaita wenzangu” yule kijana
akajibu kwa woga.
“Relax kijana wangu!” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamwambia yule kijana huku
akimpigapiga mabegani baada ya kumuona akianza kuongea kwa woga.
“Wakati ukiingia humu ndani hukumkuta au kupishana na mtu yeyote akitoka?”
“Hapana!”
ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamtazama tena yule kijana kwa uyakinifu kisha
akayahamisha macho yake tena kuitazama ile maiti ya yule mtu pale chini kabla ya
kuuliza tena.
“Hiki choo ni kibovu?”
“Hapana!” yule kijana akajibu kwa kujiamini.
“Una hakika?”
“Kabisa!,humu ndani ya hii casino hatuna choo kibovu na kama kingekuwepo
ningekuwa tayari nimekiripoti kwenye uongozi”
“Sasa nani aliyeandika hapa kuwa CHOO HIKI HAKITUMIKI?”
“Hata mimi pia nashangaa” yule kijana akaongea huku akionesha kutofahamu
kabisa kilichokuwa kikiendelea juu ya maelezo yake kwenye ule mlango wa kile choo.
Kikafuatia kitambo kifupi cha ukimya huku yule askari mwingine akiendelea kuandika
maelezo ya kile walichokishuhudia pale chooni.Baada ya hapo kukafuatiwa na mahojiano mengine ya hapa na pale kisha yule
kijana akaruhusiwa aondoke ili akaendelee na kazi zake huku akisisitizwa kuwa awe
tayati kutoa ushirikiano kwa polisi pale atakapohitajika kufanya hivyo. Yule kijana
akaondoka.
Muda mfupi baada ya yule kijana kuondoka eneo lile ASP O.J.Mkwanju Ngoma
na vijana wake wakaanza kazi ya kuchukua vipimo vyote muhimu vya upelelezi eneo
lile.
Wakati ASP O.J.Mkwanju Ngoma na askari wake wakiwa wanaendelea na kazi
yao meneja wa casino ile akawa tayari amefika eneo lile huku akiwa ameongozana na
vijana watatu ambao miongoni mwao ASP O.J.Mkwaju Ngoma alimtambua mmoja.
Akajiuliza ni wapi alikutana na kijana yule na baada ya kufikiri kwa muda akakumbuka
na hapo mshangao ukamshika. Hata hivyo akajitahidi kuumeza mshtuko wake.
“Habari za kazi Afande?” mtu mmoja miongoni mwa wale watu wanne akamsalimia
ASP O.J.Mkwaju Ngoma huku uso wake ukishindwa kuonesha tashwishwi yoyote.
“Nzuri! wewe ndiye meneja wa hii casino?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akauliza
huku akimtazama yule mtu.
“Ndiyo!”
“Nahitaji kufanya mahojiano na wewe kufuatia hili tukio la mauaji” ASP
O.J.Mkwaju Ngoma akaongea kwa utulivu huku akimtazama meneja wa ile
casino,manaume mrefu na mweusi mwenye umri wa miaka arobaini na ushei.
“Mimi siyo msemaji wa hii casino” yule meneja wa casino akaongea huku akionekana
kukasirishwa na uwepo wa askari eneo lile.
“Wewe si ndiye meneja wa hii casino?” ASP akauliza huku akishindwa kumuelewa
vizuri yule mtu.
“Ndiyo! lakini kuzungumzia masuala ya hapa siyo kazi yangu” yule mtu akasisitiza
kwa kiswahili chake chenye kasoro na hapo ASP O.J.Mkwaju Ngoma akatulia kidogo
akimtazama yule mtu katika namna ya kushangazwa na maelezo yake.
“Sasa msemaji wa hii casino ni nani?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma hatimaye akauliza
kwa udadisi.
“Yupo likizo!”
Jibu la mkato la yule meneja wa casino likazidi kumchanganya ASP O.J.Mkwaju
Ngoma na wale askari wake na hapo wakatazamana kwa muda huku ukimya ukichukua
nafasi. Ukimya ule ulipokuwa mbioni kushika hatamu kijana mmoja miongoni mwa
wale vijana watatu waliofika eneo lile huku wakiwa wameongozana na yule meneja wa
casino akavunja ukimya huku akipiga hatua kusogea mbele
“Mzee unanikumbuka?” yule kijana akauliza huku akitabasamu na ASP
O.J.Mkwaju Ngoma alipomtazama haraka akamkumbuka vizuri yule kijana. Alikuwa
ni Fulgency Kassy,yule kijana aliyekuja ofisini kwake kule kituo cha polisi cha mjini
kati akiulizia taarifa za upelelezi za kifo cha Guzbert Kojo kilichotokea kule mtaa wa
Nkurumah siku ya jana. Vijana wengine wawili waliosalia mmoja alikuwa Pweza na
yule mwingine alikuwa Kombe.
“Ndiyo nakukumba” ASP O.J.Mkwaju Ngoma hatimaye akaongea huku akili
yake ikisumbuka kutafuta sababu ya swali lile.
“Naomba hilo faili lenu lenye maelezo halafu wachukue askari wako mwondoke
eneo hili kwani hii kesi haiwahusu” Fulgency Kassy akaongea huku usoni akitabasamu
na wenzake nao wakafanya vilevile huku mikono yao wakiwa wameikunjia vifuani
mwao. Hata hivyo yule meneja wa ile casino hakuonesha kushtushwa hata chembe na
yale maneno ya Fulgency Kassy,tukio ambalo liliwastaajabisha sana ASP O.J.Mkwaju
Ngoma na askari wake.
“Mnaonekana kuwa mna ajenda yenu binafsi,sivyo?”ASP O.J.Mkwaju Ngoma
akaongea kwa jazba huku akiwakata jicho la hasira wale vijana.
“Hupaswi kulalamika Afande hiki tunachokifanya ni kukurahisishia kazi wewe
na askari wako. Huoni kuwa umri wako haukuruhusu kujishughulisha na masuala
magumu kama haya!” Pweza akadakia.
“Nyinyi vijana hamna mamlaka yoyote ya kunielekeza kitu cha kufanya na
mkiendelea na hiyo tabia yenu ya kunifuatafuata nitawafahamisha kwanini nilipewa
jina la Mkwaju Ngoma” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akafoka kwa hasira lakini wakati
akifanya hivyo Fulgency Kassy alikuwa akimalizia kibonyeza kitufe cha tarakimu ya
mwisho kwenye simu yake kisha akaiweka simu yake sikoni. Ile simu ilipopokelewa
upande wa pili Fulgency Kassy akaongea kidogo kabla ya kuitoa sikioni mwake na
kumpa ASP O.J.Mkwaju Ngoma huku akiendelea kutabasamu.
“Afande zungumza na huyu mtu badala ya kuendelea kushikilia msimamo wako
usiyo na maana” Fulgency Kassy akaongea kwa ujivuni na hapo ASP O.J.Mkwaju
Ngoma akaipokea ile simu na kuiweka sikioni na baada ya mazungumzo mafupi na
mtu wa upande wa pili wa ile simu akatoa ile simu sikioni na kuirudisha kwa Fulgency
Kassy huku uso wake ukiwa umetahayari. Kisha akameza funda kubwa la mate
kuitowesha hasira iliyonasa kwenye koo lake kabla ya kuwageukia wale askari wake
na kuwaambia.
“Twendeni” wale askari wakiwa wameshajiweka tayari kusubiri jibu la namna ile
wakaacha kile walichokuwa wakikifanya. Yule askari aliyekuwa akiandika yale maelezo
ya awali ya lile tukio la mauaji ya yule mtu akamkabidhi Fulgency Kassy lile faili lenye
maelezo kisha wale askari wote kwa pamoja wakaanza kuondoka huku wameinamisha
vichwa vyao chini kama kondoo.
Taarifa juu ya mauaji yalitokea kwenye kile choo cha Vampire Casino zilikuwa
zimewafikia Fulgnecy Kassy,Pweza na Kombe kutoka kwa afisa mmoja wa usalama
wa ngazi ya juu serikalini mara baada ya afisa huyo kupokea simu kutoka kwa meneja
wa casino.
Mara baada ya ASP O.J.Mkwaju Ngoma na wale askari wake kuondoka Fulgency
Kassy akageuka na kumtazama meneja wa casino ile kabla kumuuliza.
“Una mfahamu huyu mtu aliyeuwawa?”
“Ndiyo!” yule meneja akaitikia huku akionekana kuanza kuchoshwa na mchokato
wa matukio yote yaliyokuwa yakitokea mle ndani ya casino.
“Unamfahamu vipi?”
“Ni mmoja wa walinzi wangu wa hapa casino”
“Una sababu yoyote unayodhani huwenda ikawa imepelekea kifo chake?” Pweza
akauliza huku akiziokota bastola mbili juu ya dimbwi la damu mle chooni ambapo
alipoanza kuzikagua akagundua kuwa zote zilikuwa zimejaa risasi.
“Taarifa nilizozipata kwa walinzi wenzake wa humu ndani ni kuwa yeye alikuwa
akimfuatilia huyo mtu aliyemuua baada ya kumtilia mashaka mtu huyo wakati
alipoingia kwenye hii casino. Sasa sijafahamu kipi kilichotokea hadi mlinzi wangu
akauwawa” meneja wa casino akaongea kwa masikitiko.
Kombe akaisogelea ile maiti ya yule mlinzi na kuanza kuifanyia uchunguzi kwa
ukaribu na baada ya muda mfupi akaja na hoja.
“Yeyote aliyehusika katika kumuua huyu mlinzi ni mtu mzoefu katika mapambano”
“Kwa nini?” Fulgency Kassy akauliza huku akiyapeleka macho yake kuitazama ile
maiti ya yule mlinzi pale chini.
“Inavyoonekana ni kuwa kulitokea patashika ya mapambano makali baina ya huyu
mlinzi na huyo mtu aliyemuua lakini huyu mlinzi hakuweza kufua dafu kwa huyo
mtu ingawa huyu mlinzi anaonekana kuwa alikuwa na bastola mbili na zote zilikuwa
zimejaa risasi” Kombe akaongea huku akizigeuzageuza zile bastola na kuzikagua kwa
makini.
“Ni kweli anavyosema Kombe” Pweza akadakia ”Inavyooneakana ni kuwa huyu
mlinzi ndiye aliyemvamia huyo mtu aliyemuua lakini alishindwa kuitumia nafasi hiyo
vizuri”
Flugency Kassy akageuka na kumtazama yule meneja wa casino kabla ya kumuuliza.
“Huwa mna utaratibu kuweka kumbukumbu za watu wote wanaoingia kwenye
hii casino?”
”Ndiyo!,mtu hawezi kuingia humu ndani mpaka awe na kadi ya mwanachama wa
casino” yule meneja akafafanua
“Nani aliyekueleza kuwa huyu mlinzi alikuwa akimfuatilia huyo mtu aliyepambana
naye hadi kufikia kuzidiwa na hatimaye kuuwawa?” Fulgency Kassy akaendelea
kuyaelekeza maswali yake kwa yule meneja wa casino.
“Nimeambiwa na mlinzi mwenzake”
“Tunaweza kuonana na huyo mlinzi?” Fulgency Kassy akauliza huku akimtazama
meneja yule kwa makini.
“Ondoa shaka!” meneja wa casino akaongea kisha akaichukua simu yake ya
kiganjani na kupiga namba fulani. Baada ya pale haukupita muda mrefu kijana
mwenye umri kati ya miaka ishirini na saba hadi thelathini akaingia mle ndani huku
akiwa ameongozana na mabaunsa wawili wenye sura za huzuni. Walikuwa ni wale
mabaunsa waliopambana na Chaz Siga kule kwenye ile korido ya ghorofa ya pili na
kuambulia kupigo kibaya hadi kupoteza fahamu.
Wale mabaunsa huku wakiwa wanaona aibu mara walipofika eneo lile wakaanza
kusimulia mkasa wote uliowapata juu ya yule mtu waliyepambana naye kule kwenye gorofa ya pili ya casino. Walipomaliza kusimulia Fulgency Kassy akageuka na
kumuuliza yule mlinzi mwingine aliyeitwa kutoa maelezo.
“Maelezo ya hawa wenzako juu ya huyo mtu waliyepambana naye yanawiana na
kile ulichotoka kutueleza?”
“Ndiyo!” yule mlinzi akaongea kwa unyonge
“Yupoje huyo mtu?” Pweza akadakia.
“Alikuwa mwanaume mrefu na mweusi mweupe mwenye mwili imara na alikuwa
amevaa suruali ya jeans na fulana nyeusi na kichwani alikuwa amevaa kofia” yule mlinzi
akafafanua.
“Atakuwa ndiye huyo huyo tu” Kombe akaongea kwa sauti tulivu.
“Unadhani ni kwa nini mlimtilia mashaka huyu mtu wakati alipokuwa akiingia
humu ndani ya casino?” Fulgency Kassy akamuuliza tena yule mlinzi.
“Alikuwa mgeni na alionekana kuchunguza mambo yaliyokuwa yakiendelea
humu ndani” maelezo ya yule mlinzi yakawapelekea wote wageuke na kumtazama
yule mlinzi kwa makini huku wakitafakari.
“Mnadhani ni kwa nini huyo mtu alipanda kule juu ghorofani?” Fulgency Kassy
akawatupia swali wale mabaunsa huku akiwatazama.
“Hatufahamu” wote wakaitikia
“Mimi nafikiri kitu cha kufanya hapa ni kupitia kamera zote za humu ndani na
hapo tutamfahamu huyo mtu ni nani” Pweza akasisitiza.
“Yes! hilo ni wazo zuri kwani kupitia kamera za humu ndani tunaweza kumuona
huyo mtu aliyehusika na haya mauaji” Fulgency Kassy akaongea akiunga mkono hoja
ya Pweza huku akionekana kufurahi na kabla yule meneja wa ile casino hajaondoka
eneo lile akawahi kumtahadharisha.
“Hakikisha hakuna mtu yeyote humu ndani atakayefungua mdomo wake
kuzungumza na waandishi wa habari kwani unafahamu madhara ya kufanya hivyo”
“Ondoa shaka!” meneja wa casino akaongea kwa utulivu kisha akafungua mlango
wa kile choo na kutoka nje huku akiwa ameongozana na wale walinzi wake.
Muda mfupi uliyofuata baada ya yule meneja wa casino kutoka Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe walianza kuushughulikia mwili wa yule mlinzi wakichukua
vipimo ambavyo vingewasaidia katika uchunguzi wao. Zoezi lile lilipokamilika mwili
wa yule mlinzi wakautumbukiza ndani ya mfuko wa nailoni mkubwa na mweusi
uliokuwa na zipu ndefu. Kisha wakaisafisha ile damu iliyotapakaa pale chooni sakafuni
kama namna ya kuondoa vielelezo vyovyote kwa mtu au watu ambao wangefika eneo
lile baadaye.
Walipomaliza kazi yao majibu yaliyopatika kutoka kwenye kamera za mle ndani
na taarifa kutoka eneo la mapokezi la ile casino yalikuwa juu ya meza ya ofisi ya yule
meneja wa casino. Mshukiwa namba moja wa mauaji ya yule mtu kule chooni alikuwa
amefahamika kwa jina la Stephen Masika na hata uvaaji wake ulishabihiana na maelezo
ya walinzi wa mle ndani ya casino.
Baadhi ya kamera za ile casino zilionesha kuwa katika vipindi tofauti Stephen Masika alionekana akiwa amekaa eneo la kaunta huku akijipatia kinywaji. Kamera
hizo baadaye zilimuonesha akielekea kule sehemu ya maliwato ambapo yale mauaji
ndipo yalipokuwa yametokea.
Stephen Masika alipotoka kule sehemu ya maliwato akaonekana akipanda zile
ngazi za kule ghorofani na hatimaye kuingia chumba namba 26 ambapo humo
alikaa kwa muda na alipotoka akaonekana akipambana na wale walinzi wa casino na
hatimaye kuwadhibiti vizuri kwenye ile korido. Baada ya hapo mtu yule aliyejulikana
kwa jina la Stephen Masika haikufahamika alitoka vipi nje ya jengo lile la casino ingawa
hisia zilimuhusisha na kukatika kwa ule umeme mle ndani na huwenda alitoka kwa
kujichanganya na watu waliokuwa wakitoka nje ya casino muda mfupi baadaya ya ule
umeme kukatika.
“Nyinyi endeleeni na kazi yenu sisi tutajua nini cha kufanya” Fulgency Kassy
akamwambia meneja wa ile casino baada ya majadiliano ya hapa na pale kufika tamati
kisha wakasogeza viti vyao nyuma ya meza kubwa ya ofisini na kusimama wakiagana
na meneja wa casino ile kabla ya kutoka mle ndani. Muda mfupi baadaye walikuwa
ndani ya gari aina ya Landcruiser nyeupe na mwili wa yule mlinzi wakiupeleka mochwari
hospitali ya Muhimbili.
UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU J.K.NYERERE
asubuhi hii ulikuwa umechukua sura mpya. Baadhi ya shughuli za uwanjani
hapo zilikuwa zimesimama kwa muda ili kupisha tukio la heshima na la
kizalendo kufanyika. Baadhi ya makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la wananchi wa
Tanzania walikuwa wamefika kiwanjani pale katika mwonekano wa suti nadhifu za
kijeshi. Pia kulikuwa na wanajeshi wengine wenye madaraja ya chini ya vyeo ambao
wengi wao walielekeana kwa urefu kama siyo umri.
Wanajeshi wote walivaa vitambaa vyeusi mikononi mwao kuashiria kuwa
hawakuwa katika hali ya furaha bali walikuwa katika hali ya tanzia na huzuni ya kusubiri
kuipokea miili ya ndugu wazalendo waliopoteza maisha yao wakati wakilitumikia taifa
la Tanzania katika harakati za kijeshi chini ya mwamvuli wa MONUSCO ama umoja
wa jeshi la Afrika linalolinda amani huko nchini D.R Congo eneo la mashariki na Kivu
ya kaskazini.
Kwa upande wa viongozi wa kisiasa kulikuwa na amiri jeshi mkuu na rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi
wengine wa kisiasa akiwemo waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa. Wote wakiwa katika nyuso za masikitiko.
Kundi la mwisho lilikuwa ni lile la ndugu wafiwa jamaa na marafiki ambao walifika
kiwanjani pale kuipokea miili ya askari jeshi wazalendo watatu wa jeshi la wananchi wa
Tanzania waliokufa katika harakati za kijeshi huko nchini D.R Congo. Miongoni mwa
watu wale kulikuwa na wajane wa marehemu,watoto,wazee,ndugu,jamaa na marafiki
na wote walikuwa wamevaa mavazi meusi ya kuashiria hali ya simanzi.
Koplo Tsega akiwa miongoni mwa watu wa kundi lile alikuwa amefika kiwanjani
pale ili kushuhudia kile kinachosemekana mapokezi ya heshima ya miili mitatu ya
wanajeshi waliopoteza maisha katika harakati za kijeshi huko Kivu ya kaskazini nchini D.R Congo. Huku yeye akiwa ni mmoja wa askari jeshi hao watatu waliopoteza
maisha.
“Huu ni mkasa wa aina yake” Koplo Tsega akajikuta akijisemea moyoni huku akiwa
na hakika kuwa hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumtambua kuwa yeye ni nani
eneo lile. Makachero wa usalama wa taifa walionekana kutanda kila kona katika hali ya
kuhakikisha kuwa itifaki ya ulinzi na usalama inazingatiwa vizuri eneo lile.
Koplo Tsega akiwa amejichanganya katikati ya lile kundi la raia,ndugu,jamaa na
marafiki alikuwa akifahamu vizuri kila kitu kilichokuwa kikiendelea eneo lile. Kila
mara aliyatembeza macho yake huku na kule akizichunguza nyuso za watu mbalimbali
waliofika eneo lile huku akitarajia kuziona nyuso za watu fulani.
Mara kwa mara Koplo Tsega alijaribu kujitathmini juu ya mwonekano wake
mpya na kuridhika kuwa hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumtambua kuwa
yeye ni nani eneo lile. Alikuwa amejibadilisha katika kila eneo ambalo alihisi huwenda
lingeweza kumvuta mtu yeyote aliyekuwa akimfahamu. Akianzia mavazi hadi namna
ya utembeaji wake. Kabla ya kufika kiwanjani pale alikuwa amepitia katika duka
moja maarufu la nguo lililopo mtaa wa Kongo eneo la Kariakoo kununua mahitaji yote
muhimu ya kazi yake. Mahitaji ambayo wakati huu yalimfanya aonekana mwanamke
mstaarabu na anayejua kuyazingatia vizuri maadili ya dini yake. Mwonekano wake
mpya wa mavazi meusi ya baibui, juba, nikabu, soksi na glovu nyeusi ulikuwa amempa
nafasi nzuri ya kufanya kazi yake pasipo bugdha wala hisia zozote za kutiliwa mashaka
na mtu yeyote aliyekuwa akimfahamu eneo lile.
Kila alipokumbuka sababu iliyomfanya afike kiwanjani pale tabasamu lake hafifu
lilijivinjari usoni mwake na hapo kurasa za kitabu cha kumbukumbu za matukio yote
yaliyotokea katika msitu mnene wa Govender nchini D.R Congo zikaanza kijifunua
taratibu moja baada ya nyingine. Huku kurasa hizo zikitonesha majeraha makubwa
katika mtima wake na kupeleka simanzi iliyolifukuzia mbali tabasamu lake na
kusababisha hasira isiyoelezeka.
Koplo Tsega alikuwa amefika kiwanjani pale kushuhudia mapokezi ya mwili wake
na ile miili mingine ya askari jeshi wenzake wawili wote wakiwa wameuwawa katika
harakati za kijeshi huko D.R Congo.
Akiwa katikati ya kundi kubwa la raia waliofika kiwanjani pale Koplo Tsega
aligeuka na kuwatazama kwa siri ndugu zake waliofika kiwanjani pale akiwemo mama
yake mzazi,kaka na dada zake. Pamoja na ndugu wengine,jamaa na marafiki zake
ambao walikuwa wakiendelea kutokwa na machozi ya kuomboleza msiba wake kwa
huzuni tangu walipopata taarifa ya kifo chake.
Koplo Tiglis Tsega akaendelea kuwatazama watu wale huku moyoni akisikitika
sana kwa kuumia kwao ingawa hakuwa na namna ya kufanya katika kuhakikisha kuwa
lengo lake linatimia.
Koplo Tsega akiwa karibunao aliendelea kuwatazama ndugu zake na pale hisia za
huzuni zilipokuwa mbioni kumzidi nguvu akaacha kuwatazama na kugeuka akitazama
upande mwingine sehemu kiliposimama kikundi cha wanajeshi shupavu waliovaa suti nadhifu za heshima. Wanajeshi hao wakiwa wamejipanga vyema katika mistari miwili
minyoofu huku wakisubiri kuyapokea majeneza matatu yenye miili ya askari jeshi wa
Tanzania iliyokuwa ikiletwa na ndege kutoka huko eneo la Kivu ya kaskazini nchini
D.R Congo. Zinapofanyika operesheni za umoja wa jeshi la Africa-MONUSCO chini
ya mwamvuli wa umoja wa mataifa-UNITED NATIONS katika mpango wa kuleta
amani ya kudumu. Nchi za Tanzania,Afrika ya kusini na Malawi zikiunda jeshi hilo
lenye lengo la kuvidhibiti vikundi vyote vya waasi nchini D.R Congo na hatimaye
kuvipokonya silaha.
Koplo Tsega akajikuta akitabasamu tena pale alipokumbuka maelezo ya Guzbert
Kojo kuwa jina lake yaani yeye KopoTiglis Tsega lilikuwepo katika orodha ya majina
ya askari jeshi watatu wa Tanzania waliopoteza maisha yao katika harakati za kijeshi
huko nchini D.R Congo dhidi ya kikundi cha waasi cha M23 kinachopigana dhidi ya
majeshi ya serikali ili kuiondoa madarakani serikali ya rais Joseph Kabila.
Orodha ya majina ya wanajeshi hao watatu watanzania waliopoteza maisha katika
harakati hizo za kijeshi nchini D.R Congo yakisomeka kama ifuatavyo;Koplo Tsega
askari jeshi komandoo wa daraja la kwanza na mdunguaji mahiri kutoka kikosi cha
kijeshi namba 92 cha makamandoo hatari zaidi cha Sangasanga mkoani Morogoro.
Sajenti Chacha Marwa wa kutoka kikosi cha kijeshi namba 36 cha askari wa miguu
kambi ya Msangani wilayani Kibaha. Wa mwisho akiwa ni Meja Khalid Makame
kutoka kambi ya kijeshi namba 521 ya Chukwani huko kisiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa ratiba kamili iliyosomwa na msemaji mkuu wa masuala ya
operesheni za kijeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania,Brigedia Jenerali Mchwa
Mpaka ni kuwa ndege ya kijeshi ya jeshi la wananchi wa Tanzania aina ya Jet Fighter
302 ingetua kiwanjani pale muda wa saa nne na nusu asubuhi huku ikiwa na miili ya
wanajeshi hao watatu kutokea eneo la Kivu ya kaskazini nchini D.R Congo.
Koplo Tsega alivuta vazi lake refu na jeusi na kuitazama saa yake ya mkononi.
Mwenendo wa majira wa saa yake ukamfanya atabasamu kwani alikuwa hajachelewa
wala hajawahi sana kwa mujibu wa ratiba ile iliyosomwa muda mfupi uliyopita.
Hatimaye akaushusha chini mkono wake na kuitengeneza vizuri miwani yake myeusi
machoni katika kuhakikisha kuwa anaiona vizuri taswira ya kila kitu kilichokuwa
kikiendelea mbele yake.
Kulikuwa na muda wa robo saa zaidi wa kuendelea kusubiri kabla ya ndege
hiyo ya kijeshi iliyobeba miili ya wanajeshi hao haijatua pale kiwanjani na kupelekea
simanzi zaidi kwa watu waliofika uwanjani pale. Koplo Tsega aliendelea kuwaza huku
akiyatembeza macho yake kwenye halaiki ile ya watu yenye mchanganyiko mkubwa
wa wanausalama waliojificha katika mavazi ya kiraia ya miwani myeusi machoni mwao
na vinasa sauti vya mawasiliano vyenye nyaya nyeusi na nyembamba zilizopotelea
katika kola za makoti yao meusi ya suti.
Wakati Koplo Tsega akiendelea kuzitazama nyuso za watu kwenye kadamnasi ya
uwanjani pale macho yake makali yaliyompa daraja la juu kabisa jeshini katika medani
za shabaha yakasimama maeneno fulani yakizitazama kwa makini sura tofauti za wanausalama waliokuwa eneo lile. Kuziona sura hizo kukampelekea aachie msonyo
mwembamba wa hasira na kuhitimisha kwa tusi zito la chuki dhidi ya watu hao.
Mtu wa kwanza alikuwa Fulgency Kassy ambaye kwa wakati huu alikuwa
amesimama nyuma ya kundi la viongozi wa kisiasa waliofika kiwanjana pale. Mwingine
alikuwa Pweza ambaye yeye wakati huu alikuwa amesimama nyuma kabisa ya eneo
alilokaa amiri jeshi mkuu huku akizungumza na mwanamke fulani ambaye Koplo
Tsega hakuweza kumfahamu. Mtu wa mwisho alikuwa Kombe. Kombe alikuwa
amesimama upande wa kushoto wa eneo walilokuwako mabalozi wawakilishi wa
nchi zao hapa nchini Tanzania. Kombe alikuwa amevaa suti nadhifu nyeusi huku
macho yake yakijificha nyuma ya vioo vipana na vyeusi vya miwani ya jua sun goggles .
Njama yeye alikuwa amejitenga kando ya watu akiongea na simu nyuma ya gari moja
Landcruiser nyeupe. Wingine hakufanikiwa kuwaona.
Koplo Tsega aliendelea kuwatazama watu hao katika maeneo yao tofauti
waliosimama. Hata hivyo hakushtuka kabisa kuziona nyuso zao zikiwa na furaha
kana kwamba lile halikuwa tukio la kusikitisha kama watu wengine waliofika eneo lile
walivyokuwa wakionekana.
Nyuso za watu wale zilionekana kwa kila hali kufurahia kile kilichokuwa
kikisubiriwa kufanyika kiwanjani pale muda mfupi baadaye. Furaha katika msiba!...
Koplo Tsega akaendelea kuwaza huku akimeza funda kubwa la mate kuitowesha upya
hasira kali iliyoanza kuchipua kifuani mwake.
Kelele mbaya za ndege ya mapigano ya kijeshi aina ya Jet fighter 302 ya jeshi la
wananchi wa Tanzania zilianza kuhanikiza angani na hapo watu wote waliokuwa eneo
lile wakageuka na kuitazama ndege hiyo yenye sauti mbaya.
Muda mfupi uliyofuata ndege ile ya kijeshi yenye sauti mbaya ikatua pale kiwanjani
kwa kasi ya ajabu na mbwembwe za aina yake na kwenda kusimama kando ya kile
kikundi cha wanajeshi wa mapokezi waliojipanga katika mistari miwili minyoofu tayari
kuipokea miili ile.
Kitendo cha kutua kwa ndege ile kikawapelekea baadhi ya watu waliofika eneo
lile waanze kuangua kilio cha mayowe ya huzuni na hapo eneo lote likagubikwa na
simanzi ya aina yake.
Muda mfupi baada ya ndege ile kusimama itifaki za kijeshi zikaanza kufuatwa
katika ukimya wa aina yake. Mlango wa ndege ile ulipofunguliwa sura ya mwanaume
mrefu,mweusi na mwenye macho makali aliyevaa sare za jeshi ikachungulia kidogo
baada ya mlango wa ndege ile kufunguliwa na hatimaye mtu huyo kutoka.
Koplo Tsega akayapeleka macho yake kumtazama mwanaume yule mwenye umri
wa miaka hamsini na ushei na hapo akamkumbuka vizuri. Alikuwa ni Luteni Kanali
Ngozikavu Binamwamba. Kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi la MONUSCO ama
muungano wa vikosi vya kijeshi kutoka nchi ya Tanzania,Afrika ya kusini na Matawi
vilivyopo kwenye harakati za kuleta amani ya kudumu nchini D.R Congo huko eneo
la mashariki na Kivu ya kaskazini.
Koplo Tsega akaendelea kumtazama kwa makini kamanda yule wa kijeshi wakati alipokuwa akishuka kwenye ndege ile kikakamavu sana tofauti kabisa na umri wake
na hapo akajikuta akitabasamu baada ya kukumbuka vizuri tabia ya ucheshi na roho
nzuri ya kamanda yule. Tabia nzuri zilizokuwa zikipingana na sura yake ya kikauzu
isiyokuwa na chembe ya huruma kwa askari jeshi yeyote mzembe kazini.
Pamoja na tofauti kubwa ya vyeo baina yao lakini Koplo Tsega na Luteni
Kanali Ngozikavu Binamwamba walikuwa marafiki wazuri sana huku Koplo Tsega
akimchukulia kamanda huyo wa kijeshi kama baba yake mzazi.
Urafiki wa Koplo Tsega na Luteni Kanali Ngozikavu Binamwamba ulianza pale
kamanda huyo wa kijeshi alipokuja kufahamu na hatimaye kushangazwa na uwezo
mkubwa wa Koplo Tsega katika kulenga shabaha baada ya faili lake la utendaji wa kazi
kuifikia ofisi yake wakati jina lake lilipopendekezwa na kujumuishwa kwenye orodha
ya askari jeshi wa Tanzania waliochaguliwa kutekeleza mpango wa amani ya kudumu
nchini D.R Congo. Tangu hapo wakawa marafiki wa chanda na pete kama ilivyokuwa
kwa baba na binti yake mpendwa.
Lakini wakati huu Koplo Tsega alimtazama Luteni Kanali Ngozikavu
Binamwamba katika mtazamo tofauti kabisa huku akijaribu kuvuta picha ya simanzi
ambayo kamanda yule wa kijeshi aliipata tangu pale alipopewa taarifa za kifo chake.
Koplo Tsega akajikuta akiwaza.
Mara baada ya Luteni Kanali Ngozikavu Binamwamba kushuka kwenye ile ndege
ya kijeshi huku akiwa ameongozana na maafisa wengine watano wa ngazi za juu
jeshini,majeneza matatu ya miili ya wanajeshi wa Tanzania yaliyofunikwa kwa bendera
ya taifa yakaanza kushushwa taratibu na kile kikundi cha askari jeshi wa mapokezi ya
heshima.
Majeneza yale yakapokewa kwa heshima zote na kile kikundi cha wanajeshi
waliokuwa wamejipanga katika mistari miwili minyoofu huku wakiacha nafasi ndogo
kati ya mstari na mstari. Nafasi ambayo ilichukuliwa na yale majeneza ambayo
wanajeshi wale waliyabeba mabegani mwao huku wakitembea kwa mwendo wa pole
kama itifaki za jeshi zilivyowataka.
Tukio lile likaambatana na kuhanikiza kwa sauti za vilio vya huzuni ya aina
yake kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki wa marehemu waliofika kiwanjani pale.
Wanajeshi wale wa mapokezi ya heshima wakaendelea kutembea mwendo wa pole
hadi walipoyafikisha majeneza yale ya askari wazalendo na kuyaweka mbele ya jukwaa
la amiri jeshi mkuu.
Bendi ya jeshi ilipomaliza kazi yake amiri jeshi mkuu akasimama na kuwasalimia
watu wote waliofika eneo lile huku akiwafariji wafiwa. Baada ya hapo akaanza kusoma
hutoba fupi lakini yenye ujumbe mzito kwa watu wenye mapenzi mema na wazalendo
wa nchi ya Tanzania. Huku akimalizia kwa kusoma wasifu wa wapiganaji wale ambao
miili yao sasa ilikuwa imefunikwa kwa bendera ya taifa.
Koplo Tsega akasikiliza kwa makini hotuba ile ya amiri jeshi mkuu wakati alipokuwa
akisoma wasifu wake kama ilivyokuwa kwa wale marehemu wengine wapiganaji. Hata
hivyo akajikuta akiuchukia wasifu ule pale alipohisi kuwa kila kilichokuwa kikisomwa hakikuwa sahihi na baadhi ya ukweli ulikuwa umefichwa. Hatimaye wasifu ule
ukamalizia kwa kusema
“Koplo Tsega! mpiganaji huyu hodari ameacha pengo kubwa jeshini lisiloweza kuzibika kwa
urahisi na kamwe hatutoacha kumkumbuka na kuuenzi mchango wake. Mungu na azilaze pema
peponi roho za mashujaa hawa wazalendo.
Wakati amiri jeshi mkuu akimalizia kusoma wasifu wa wapiganaji wale Koplo Tsega
alikuwa akiyatembeza macho yake kuwatazama wale watu aliokuwa akiwatazama pale
awali. Katika kufanya vile akagundua kuwa nyuso za watu wale zilikuwa na furaha
sana kana kwamba ule msiba haukuwa na maana yoyote kwao. Akasikitika sana na
kuzidi kuwalaani.
Hotuba ile ya amiri jeshi mkuu ilipofika kikomo taratibu nyingine za kijeshi
zikaanza kufuatwa ikifutiwa na watu waliofika eneo lile kuanza kutoa heshima zao
za mwisho.
Wakati wa kuaga ile miili majeneza mawili hayakufunuliwa. Jeneza la Meja Khalid
Makame lenyewe halikufunuliwa kwa kufuata taratibu za kidini na lile la Koplo Tsega
kwa kigezo kuwa mwili wake ulikuwa umeharibika sana. Hivyo ni jeneza la Sajenti
Chacha Marwa tu ndiyo lililofunuliwa kiwanjani pale na watu kuweza kutoa heshima
zao za mwisho.
Koplo Tsega akaendelea kutazama namna ambavyo mambo yalivyokuwa
yakiendelea eneo lile huku akitabasamu. Labda kitendo cha mtu kuhudhuria mazishi
yake mwenyewe,kusikia wasifu wake ukisomwa mbele ya halaiki ya watu na hatimaye
kuuaga mwili wake mwenyewe lilikuwa ni tukio la kwanza kuwahi kumtokea binadamu
duniani.
Amiri jeshi mkuu alikuwa wa kwanza kapita mbele ya majeneza ya wapiganaji wale
kutoa heshima zake za mwisho huku akiwa amefuatana na baadhi ya viongozi wake
wa juu serikalini. Kisha likafuata kundi la mabalozi wawakilishi na wageni wengine
wa kitaifa. Ndugu,jamaa na marafiki likawa kundi la mwisho kupita na kutoa heshima
zao.
Koplo Tsega alisimama kwa mbali huku akiwatazama watu wote waliokuwa
wakipita mbele ya yale majeneza kutoa heshima zao za mwisho. Simanzi ikamuingia
pale alipomuona mama yake mzazi na ndugu zake wakiwa hawajiwezi kwa kilio na
hivyo kusaidiwa na ndugu na marafiki wa karibu. Hali ile ikamtia huzuni kubwa Koplo
Tsega na kumpelekea ageuke na kutazama pembeni ili kuyazuia machozi yake.
Katika mstari ule wa watu waliokuwa wakipita mbele ya yale majeneza ili kutoa
heshima zao za mwisho kwa marehemu. Koplo Tsega pia aliweza kuwaona Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe wakiwa wameongozana wakipita kutoa heshima zao
kando ya yale majeneza. Walipolifikia jeneza lake Koplo Tsega akawaona Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe wakipeana ishara fulani na kusimama kidogo kando ya
jeneza lile wakilitazama kwa tabasamu la chinichini kabla ya kuendelea mbele.
Koplo Tsega akajikuta akitabasamu pale alipokumbuka kuwa jeneza lake halikuwa
limefunuliwa kwa kile kinachosemekana kuwa mwili wake ulikuwa ameharibika vibaya. Hivyo watu wale wakaishilia kuitazama picha yake ya kijeshi iliyokuwa imewekwa juu
ya jeneza lile. Lilikuwa ni tukio la kushangaza sana ambalo lilimuacha Koplo Tsega
akiendelea kutabasamu pale alipokuwa amesimama.
Zoezi lile la kuiaga miili ya marehemu lilipofika tamati lile jeneza lenye mwili wa
Meja Khalid Makame likabebwa na wale wanajeshi wa mapokezi na kurudishwa tena
kwenye ile ndege ya kijeshi tayari kwa kupelekwa nyumbani kwake huko kisiwani
Zanzibar kwa ajili ya mazishi. Yale majeneza mawili yaliyosalia yakabebwa na wanajeshi
na kuingizwa kwenye malori mawili ya kijeshi kisha baadhi ya wanajeshi wakapanda
huku wakifuatiwa na ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu tayari kusafirishwa.
Mwili wa Sajenti Chacha Marwa ulikuwa ukisafirishwa na kupelekwa kijijini kwao
Nyasicha wilaya ya Tarime mkoani Mara. Kwa vile mwili wa Koplo Tsega ulikuwa
unasemekana kuharibika vibaya hivyo ndugu wa marehemu walikuwa wamekubaliana
kuwa mazishi yake yangefanyikia katika makaburi ya Mwananyamala jioni ile ile mara
tu baada ya kutoka pale kiwanjani.
Koplo Tsega akaendelea kuwatazama ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa
wakipanda lori lile la kijeshi lililoubeba mwili wake. Watu walikuwa wengi sana na
hali ile ikampa faraja kidogo kuwa angalau kulikuwa na watu waliokuwa wameguswa
na kifo chake. Msafara wa lile lori la kijeshi lililoubeba mwili wake kuelekea makaburi
ya Mwananyamala ulipoanza Koplo Tsega naye akaingia kwenye gari lake na kuunga
msafara kwa nyuma.
Kulikuwa na magari mengi sana yaliyokuwa yakiusindikiza mwili wake makaburini.
Baadhi ya magari yale akayakumbuka kuwa yalikuwa ni ya marafiki zake wa kazini na
mitaani na mengine yalikuwa ya ndugu zake waliokuwa wakiendelea kulia.
Koplo Tsega akiwa nyuma ya msafara ule wa mazishi ndani ya gari lake lenye vioo
tinted mara akaliona gari dogo aina ya Nissan Skyline jeusi likimpita kwa kasi na kwenda
kuunga msafara nyuma ya lile lori la jeshi lililobeba mwili wake. Kitendo cha kuliona
gari lile kikamjulisha kuwa Fulgency Kassy,Pweza Kombe na wanausalama wengine
walikuwa wamejigawa katika misiba ile bila shaka kufuatilia hadi chepe la mwisho la
udongo kwenye kaburi. Vioo vya lile gari jeusi lililompita havikuwa tinted hivyo ilikuwa
rahisi sana kumuona Pweza akiwa nyuma ya usukani wa gari hilo.
_____
SAA TISA KAMILI ALASIRI msafara wa mazishi ya Koplo Tsega ulihitimisha
safari yake katika makaburi ya Mwananyamala eneo la Kinondoni jijini Dar es
Salaam. Lori lile liliposimama jeneza lenye mwili wa Koplo Tsega likashushwa chini
na wanajeshi huku ndugu jamaa na marafiki wakishindwa tena kujizuia na kujikuta
wakiangua kilio kisichoelezeka.
Koplo Tsega akiwa nyuma ya msafara ule mara alipofika kwenye makaburi
yale akaegesha gari lake mbali kidogo na eneo lile la makaburini kisha akashuka na
kujichanganya kwenye kundi la watu waliofika eneo lile na kuelekea kule makaburini.
Idadi ya watu waliofika eneo lile la makaburini ilikuwa imeongezeka zaidi ukifananisha na kule kwenye kile kiwanja cha ndege walipotoka.
Macho ya Koplo Tsega yakasumbuka kidogo yakitazama huku na kule eneo lile
kabla ya kumuona Pweza akiwa amesimama hatua chache kando ya shimo la kaburi
katika mwonekano wa suti yake nadhifu nyeusi huku akiwa amevaa miwani ya jua.
Koplo Tsega akatembea taratibu akielekea kwenye eneo lile la maziko na
wakati akifanya hivyo mara akamuona mama yake mzazi akiwa hoi kwa kulia huku
ameshikiliwa na wanajeshi wawili wanawake ambao haraka aliwatambua kuwa
walikuwa ni Koplo Salma na Sajenti Kiege,marafiki zake wa kazini.
Kaka yake alikuwa amesimama upande wa kushoto wa lile shimo la kaburi huku
mara kwa mara akijifuta machozi kwa kitambaa chake cha leso alichokuwa amekishika
mkononi. Pembeni yake alikuwa amesimama Dan,rafiki wa kaka yake wa siku nyingi.
Dada zake wawili Loth na Tsion walikuwa wamepoteza fahamu mara mbili kabla ya
kukimbizwa hospitali.
Mara baada ya jeneza la Koplo Tsega kushushwa na kusogezwa karibu na lile
kaburi watu wote eneo lile wakaombwa kutulia na hapo mchungaji wa kanisa akaanza
kutoa neno fupi la kuwafariji wafiwa huku akiwataka watu wote waliofika eneo lile
kutubu dhambi zao na kumrudia Mungu. Huku mchungaji huyo akiyafananisha
maisha ya mwanadamu na saa ya ukutani isiyojulikana muda wa kusimama kwake.
Mchungaji yule alipomaliza kutoa neno lake fupi kwa watu waliofika eneo lile
taratibu za mazishi ya kijeshi zikafuatia na hapo vilio vikaanza kusikika tena huku
ndugu jamaa na marafiki wakipata nafasi ya kutupia udongo ndani ya kaburi lile kama
sehemu ya kuhitimisha safari ya mwisho ya Koplo Tsega hapa duniani.
Pweza alikuwa miongoni mwa watu waliotupia udongo kwenye kaburi lile mara
baada ya jeneza la Koplo Tsega kuteremshwa mle shimoni kwa kamba na wanajeshi
waliokuwa eneo lile. Ushiriki wa Pweza ulikuwa wa kiwango cha juu kupita hata na
ndugu wa karibu wa marehemu na marafiki waliofika eneo lile huku yeye akitupia
machepe mengi zaidi ya udongo yasiyo na idadi. Pweza alipomaliza kutupia udongo
kwenye kaburi akamsogelea mama wa Koplo Tsega na kumpa mkono wa pole.
Saa kumi na moja na nusu jioni ilipotimia mazishi ya mdunguaji hatari Koplo
Tsega yakawa yamefikia ukomo huku wanajeshi wenzake wakifyatua risasi kadhaa
hewani kuhitimisha safari ya wenzao.
Kwa kuwa wingu zito la mvua lilikuwa limetanda angani hivyo mara tu mazishi
yale yalipofika tamati watu wakaanza kutawanyika haraka kuikwepa mvua ile kubwa
iliyokuwa ikijiandaa kunyesha. Pweza alikuwa miongoni mwa watu wale kwani
mara tu baada ya mazishi yale kuisha akaelekea sehemu alipoegesha gari lake kisha
akafungua mlango kuingia ndani. Muda mfupi uliyofuata simu yake ya kiganjani
ilikuwa hewani ikitafuta mtandao na simu hiyo alipopokelewa upande wa pili Pweza
hakusita kuonesha furaha yake.
“Kazi kwisha mkuu!” Pweza akaongea huku akiangua kicheko hafifu.
“Vipi mazishi yake?” sauti ile upande wa pili wa simu ikauliza.
“Watu ni wengi sana kama Kanumba” Pweza akaongea huku akishindwa kuificha furaha yake.
“Una hakika kuwa umefika hadi makaburini?” ile sauti ya upande wa pili ikauliza
tena.
“Hivi ninavyozungumza na wewe bado nipo eneo la makaburi ya Mwananyamala
na amini usiamini huwenda mimi nikawa mtu wa kwanza kwa kutupia idadi kubwa ya
machepe mengi ya udongo kwenye kaburi lake”
“Waandishi wa habari walikuwepo?” ile sauti ikauliza tena
“Walikuwepo lakini hawana madhara”
“Safi sana! njoo na picha za tukio zima unitoe shaka. Sitaki yale mambo ya Daudi
Balali” yule mtu akasisitiza huku akiangua kicheko hafifu.
“Sawa mkuu!” Pweza akaitika kwa mashaka kidogo baada ya kukumbuka
kuwa alikuwa hajachukua kielelezo chochote cha ushahidi wa mazishi yale. Kwa
kulikumbuka suala hilo Pweza akafungua dashibodi ya gari na kuchukua kamera
yake ndogo ya digital yenye nguvu za ajabu katika uchukuaji wa picha kisha akafungua
mlango wa gari na kushuka akielekea kule makaburini.
Manyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yameanza kuanguka kutoka angani
yakampelekea Pweza aharakishe hatua zake huku akililaani giza hafifu lililokuwa
limeanza kuingia. Pweza alikuwa akiikumbuka vizuri sehemu lilipokuwa lile kaburi la
Koplo Tsega ambaye mazishi yake yalikuwa yamefanyika muda mfupi uliyopita. Watu
wote walikuwa wametawanyika eneo lile hivyo eneo lote la makaburi yale lilikuwa
limemezwa na ukimya wa kipekee.
Wakati Pweza alipokuwa akilifikia kaburi la Koplo Tsega mara kitu fulani
kikawa kimemvutia. Pembeni ya kaburi lile alikuwa amesimama mwanamke fulani.
Mwanamke huyo mwembamba kiasi na mrefu mwenye umbo la kuvutia alikuwa
amevaa miwani myeusi machoni na mwili mzima alikuwa amejifunika mavazi meusi
hivyo mtu yeyote asingeweza kumtambua kwa urahisi. Mwanamke huyo alikuwa
amesimama kwa heshima zote akilitazama lile kaburi kama mtu aliyekuwa kwenye
hisia kali za kumpoteza mpendwa wake.
“Habari yako dada?” Pweza aliwahi kumsalimia yule mwanamke hata hivyo
hakujibiwa badala yake yule mwanamke akageuka na kumtazama Pweza kisha
akatingisha kichwa chake akiitikia ile salamu.
“Kifo chake kimetugusa wengi!” Pweza akaendelea kuongea bila kujibiwa huku
akishangazwa na uwepo wa mwanamke yule peke yake katika mazingira kama yale.
Yule mwanamke aliyesimama kando ya lile kaburi alikuwa ni Koplo Tsega. Mara
baada ya mazishi yale kufika tamati na watu wote kutawanyika Koplo Tsega alikuwa
ameitumia nafasi ile kuomboleza na kutoa heshima zake za mwisho kwa rafiki yake
mpendwa na mpiganaji hodari wa jeshi la wananchi wa D.R Congo,Private Gina
Yhombi-Opango Makiadi codename Lovebird. Ambaye mwili wake ndiyo uliyokuwa
ndani ya lile jeneza ingawa hadi wakati huu watu walikuwa wakiamini kuwa ule
mwili uliokuwa ndani ya lile jeneza kutoka D.R Congo ulikuwa ni wa Koplo Tsega
komandoo na mdunguaji hatari wa jeshi la wananchi wa Tanzania.Koplo Tsega akakumbuka namna alivyobadili gwanda zake na kumvalisha Lovebird
kule msituni nchini D.R Congo na hivyo kuwafanya watu waamini kuwa mwili ule
uliyokuwa ndani ya lile jeneza ulikuwa ni wa Koplo Tsega.
Makosa makubwa bila shaka yalikuwa yamefanyika katika kufanya utambuzi
makini wa ule mwili. Mtu yoyote aliyekuwa wa kwanza kuiona maiti ya Lovebird kule
msituni bila shaka hakutaka kufanya uchunguzi mara mbili kwani mwili wa Lovebird
ulikuwa na magwanda ya kijeshi yenye utambulisho wa Koplo Tsega na beji ya taifa la
Tanzania. Hivyo hatimaye mahesabu yalikuwa yamekaa vizuri.
Koplo Tsega aligeuka tena kumtazama yule mtu aliyemsemesha pale makaburini
na kitendo cha kumuona tena Pweza eneo lile moyo wake ukamlipuka ghafla hata
hivyo akajitahidi kwa kila hali kuumeza mshtuko. Koplo Tsega hakusema neno lolote
kwa kukwepa sauti yake kushtukiwa na Pweza badala yake akauinua mkono wake
kidogo na kupunga hewani akiashiria kuwa alikuwa kwenye majonzi ya hali ya juu
huku akishindwa kuelewa ni kwa nini Pweza alikuwa amerudi tena pale kaburini baada
ya watu wote kutawanyika.
Wakati Koplo Tsega akitafakari mara akakumbuka kuwa bastola yake ilikuwa ndani
ya pochi yake ndogo ya mkononi na hapo akaanza kupiga mahesabu ya haraka ya
namna ya kuifikia bastola ile na kumzimisha Pweza pale pale kaburini kabla hajabadili
mawazo na kuondoka. Koplo Tsega akavuta pumzi taratibu huku akimtazama Pweza
kwa jicho la pembe. Pweza akamtazama kidogo yule mwanamke kisha akachukua
kamera ndogo ya digital kutoka mfukoni na kuanza kulizunguka lile kaburi taratibu
katika namna ya kupata picha tofauti za kaburi lile. Pweza akalifanya zoezi lile kwa
muda mfupi sana na hivyo kumnyima nafasi nzuri Koplo Tsega kuifikia bastola yake
mafichoni.
“Pole sana dada yangu Mungu na akutie nguvu. Koplo Tsega alikuwa mtu
muhimu sana kwetu lakini kwa sasa hatunaye tena. Sisi tulimpenda lakini Mungu
amempenda zaidi” Pweza akaongea huku akiitia mfukoni ile kamera yake. Koplo
Tsega akageuka kidogo na kumtazama Pweza kisha akatingisha tena kichwa chake
akionesha kukubaliana na hoja ile.
Koplo Tsega akiwa anamvizia Pweza ageuke ili apate nafasi nzuri ya kutimiza
lengo lake akajikuta akighairi kufanya hivyo baada ya kuliona kundi kubwa la vijana
waliotoka mpirani wakikatisha pale makaburini. Hivyo ikabidi awasubiri kwanza vijana
wale wapite eneo lile lakini wakati akifanya hivyo Pweza akamuaga kwa kumpungia
mkono huku akielekea sehemu alipoegesha gari lake mbali na eneo lile. Koplo Tsega
hakuwa na jinsi hivyo ikabidi na yeye ampungie mkono Pweza akimuaga huku kooni
akiwa ameshikwa na donge la hasira.
Wakati wale vijana wakimaliza kukatisha kwenye lile eneo la makaburi Pweza
alikuwa amekwishatoweka eneo lile. Koplo Tsega akabaki amesimama pale makaburini
huku akililaani tukio lile. Mvua iliyoonza kunyesha hatimaye ikamfanya aondoke
taratibu eneo lile akielekea sehemu alipoegesha gari lake. Muda mfupi uliyofuata
alikuwa mbali na eneo lile.
#59
FUKUTO KALI LA JOTO LA JIJI LA DAR ES SALAAM likampelekea Zera
aendelee kufurahia maji baridi yaliyokuwa yakitiririka kwenye bomba la bafuni
kwake nyuma ya kioo kikubwa cha kujitazama. Muda wowote baada ya pale
mvua kubwa ingeweza kunyesha na hiyo ingekuwa nafuu kubwa kwa wakazi wa jiji
la Dar es Salaam. Zera akageuka tena na kujitazama kwenye kioo kikubwa cha mle
bafuni na hapo tabasamu jepesi likapita usoni mwake. Kwa mara nyingine taswira ya
umbo lake zuri ilikuwa imefufua upya hisia zake.
Kupitia taswira iliyofanyika kwenye kioo kile Zera akafurahishwa na michirizi
ya maji ya bomba yaliyokuwa yakichuruzika taratibu mwilini mwake. Michirizi hiyo
ya maji ikianzia kichwani halafu mabegani na kisha kifuani ikiziburudisha chuchu
zake laini halafu ikaendelea kushuka chini sehemu ya kiunoni mapajani na kumalizia
miguuni. Zera alijifahamu kuwa alikuwa msichana mzuri sana na kamwe hakuchoka
kujitazama kwenye kioo kila alipopata nafasi hiyo.
Kama kungelikuwa na kazi nyingine yenye kipato chenye afya Zera alikuwa tayari
kuacha kazi ya kujiuza mwili wake kwa wanaume kule Vampire Casino ili aendelee
kuulinda uzuri wake kwa miaka mingi zaidi huku akifurahishwa na kuweweseka kwa
nyoyo za mwanaume kila wamwonapo. Lakini suala hilo hadi wakati huu lilikuwa
limeshindikana kabisa. Pamoja na uzuri aliokuwa nao lakini kazi nyingi zenye
mishahara mikubwa jijini Dar es Salaam ziliwahitaji wasomi mwenye elimu za vyuo
vikuu wakati yeye alikuwa ameishia elimu ya darasa la saba huko kijijini kwao mkoani
Singida.
Kama ilivyokuwa kwa vijana wengi wenye kupenda maisha mazuri ya haraka Zera
hatimaye akatoroka nyumbani kwao kijijini na kukimbilia jijini Dar es Salaam baada
ya kushawishiwa na marafiki waliokuwa wakirudi mara kwa mara kijijini kwao na hali
nzuri za maisha.
Alipofika jijini Dar es Salaam Zera akagundua kuwa hali ya maisha ilikuwa tofauti
kabisa na vile alivyokuwa akifikiri. Marafiki zake wote walikuwa wakiendesha maisha
kwa kujiuza miili yao katika sehemu za starehe na kumbi mbali mbali za za starehe
jijini Dar es Salaam. Zera akawalaani kwa vitendo vile na kukataa kuambatana nao.
Lakini halikuwa jambo rahisi kwani huduma zote muhimu kama chakula,malazi na
matibabu alikuwa akiwategemea wao.
Marafiki hatimaye wakamchoka na hivyo maisha yakazidi kumuwia magumu.
Ukali wa maisha ya jiji la Dar es Salaam bila kazi bila ndugu ukamshinikiza Zera
na hapo taratibu akaanza kuambatana na marafiki kwenye biashara yao ya ukahaba
huku akijifunza mbinu mpya na vichochoro vya jiji la Dar es Salaam. Baada ya miezi
michache kupita Zera akageuka na kuwa kahaba mashuhuri huku wateja wake
wakubwa wakiwa ni wanaume wenye vipato vya juu.
Tangu alipoanza kufanya biashara ya ukahaba jijini Dar es Salaam alikiri kuwa
hakuwahi kukutana na mwanaume yoyote aliyetokea kuugusa moyo wake kama
ilivyokuwa kwa Stephen Masika. Yule mwanaume aliyeonana naye kule Vempire
casino usiku wa jana. Uzuri wa Stephen Masika,ucheshi na utanashati wake vilikuwa
vimempelekea Zera usiku mzima ajikute akiweweseka kitandani kumuwaza
mwanaume yule utasema hakuwahi kulala na mwanaume yoyote.
Zera alipoamka asubuhi akaanza kufanya ile kazi aliyopewa na Stephen Masika ya
kupeleleza mahali alikokuwa akiishi Milla Cash. Kazi ilikuwa rahisi tu kwani ilipofika
saa nne asubuhi Zera alikuwa amepata taarifa zote muhimu kupitia kwa marafiki zake
aliyoongea nao kwa njia ya simu.
Muda wa masaa machache baadaye Zera alikuwa amepanga kumpigia simu
Stephen Masika na kumtaka waonane ili aweze kumpa taarifa alizozipata.
Kumbukumbu ya taswira ya Stephen Masika ikiwa inaendelea kuzitongoza fikra
zake Zera akajikuta akizidi kumpenda mwanaume huyo aliyeonekana mkwasi na
mzuri wa aina yake kuwahi kumuona jijini Dar es Salaam.
Zera alipomaliza kuoga akafungua mlango wa bafu na kutoka nje akielekea
chumbani kwake huku akiwa amejifunga taulo kiunoni katika nyumba ile aliyopanga
yenye vyumba viwili vya kulala,sebule na jiko.
Simu iliyoanza kuita ikamkumbusha Zera kuwa kabla ya kwenda kuoga alikuwa
ameiacha simu yake kwenye kochi sebuleni. Hivyo akaelekea kule sebuleni simu ile
ilipokuwa ikiita. Mara alipoichukua simu ile na kuitazama akashangaa kuiona namba
mpya ikiita hata hivyo Zera hakusita kuipokea simu ile huku maswali mengi yakipita
kichwani mwake.
“Hujambo mpenzi?” sauti nzito ya kiume iliongea kwa utulivu upande wa pili
wa simu ile. Zera akaituliza akili yake huku akijaribu kuitathmini sauti ile hata hivyo
ilikuwa sauti ngeni kabisa masikioni mwake.
“Sijambo nani mwenzangu?” hatimaye Zera akauliza kwa utulivu.
“Nahitaji kuonana na wewe mrembo” ile sauti ya mtu wa upande wa pili wa simu
ikaongea kwa utulivu ikilipuuza swali la Zera.
“Naongea na nani?” Zera akauliza tena
“Mteja wako”
“Mteja wangu nani?”
“Usijali Zera utanikumbuka utakaponiona. Chungulia nje utaliona gari jeusi.
Nimemtuma dereva wangu aje kukuchukua mimi utanikuta ufukwe wa Coco beach” ile
sauti ya upande wa pili wa simu ikazungumza kwa utulivu. Zera akaisikiliza sauti ile kwa
makini huku akisogea dirishani na kusogeza pazia akitazama nje kupitia uwazi mdogo
ulikuwa baina ya geti la nyumba ile na ukuta. Kwa kufanya hivyo Zera akaliona gari
dogo jeusi limesimama mbele ya geti lile.
“Sikiliza kaka mimi siwezi kuja kwa mtu nisiyemfahamu istoshe nakaribia kuingia
kazini” Zera akaongea kwa tahadhari.
“Kazi gani unayoiwahi mrembo tofauti na hii ninayokuitia yenye malipo mazuri
au hutaki tufurahi pamoja mpenzi. Ningekuwa nataka kukupotezea muda wako
nisingemtuma dereva wangu akufuate nyumbani” ile sauti ya upande wa pili iliongea
na hapo Zera akasogeza tena lile pazia dirishani na kutazama nje. Lile gari jeusi bado
lilikuwepo.
“Kuna mtu nahitaji kuonana naye jioni hii hivyo nahisi huwenda nikachelewa
nikija huko”
“Usijali dereva wangu atakurudisha mapema zaidi” ile sauti kwenye simu
ikaendelea kusisitiza.
Zera akatulia kidogo akitafakari kisha akachukua karatasi na kalamu vilivyokuwa
chini ya meza ndogo iliyokuwa pale sebuleni na kuanza kuandika jina la hoteli yenye
ufukwe aliyotajwa na mtu yule kwenye simu kama sehemu ya kumbukumbu baada ya
simu ile kukatwa.
Muda mfupi baada ya simu ile kukatwa Zera alikuwa chumbani kwake akijiandaa
huku mawazo mwengi yakipita kichwani mwake. Alipomaliza akatoka nje na kufunga
mlango. Lile gari jeusi bado lilikuwa nje ya geti la ile nyumba na Zera alipofika dereva
wa gari akamfungulia mlango na kumtaka aingie.
Dereva wa gari lile alikuwa kijana mrefu kiasi mwenye mwili imara huku akiwa
amevaa suti nadhifu ya rangi ya kijivu. Dereva yule akamtazama Zera kwa makini
wakati akiingia kwenye gari huku tabasamu jepesi likipita usoni mwake. Mlango wa
gari ulipofungwa safari ikaanza. Dereva wa gari lile alikuwa Pweza na wakati huu
alikuwa akifurahi namna mambo yalivyokuwa yakienda.
Gari lilipoingia barabara ya Morocco likashika uelekeo wa upande kulia kama
linaloelekea eneo la Magomeni lakini baada ya safari ya kitambo kifupi gari hilo
likakunja kona upande wa kutosho likiifuata barabara ya Kinondoni. Wakati safari
ikiendelea Zera alikuwa akimtaza Pweza huku mawazo mengi yakipita kichwani
mwake. Pweza hakuzungumza kitu chochote badala yake aliendelea kuendesha gari
huku mara kwa mara akirekebisha redio ya gari iliyokuwa mle ndani.
Baada ya safari ndefu wakajikuta wametokezea katika makutano ya barabara ya
Kinondoni na ile barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Walipofika kwenye makutano yale
Pweza akaingia upande wa kulia halafu baada ya safari fupi akakunja kona kuingia
upande wa kushoto akiifuata barabara ta Kenyatta drive. Walipoingia kwenye barabara
ile wakawa wakiiona bahari ya Hindi kwa upande wa kulia halafu walipofika mbele
kidogo wakaingia barabara ya Toure drive huku bahari ya Hindi wakiendelea kuiona
upande wa kulia kwa baadhi ya maeneo.
Mandhari ya bahari ya Hindi kwa wakati huu yalikuwa yakivutia sana. Upepo
mwanana wa bahari ulivuma na kupelekea starehe ya aina yake kwa msafiri wa
barabara ile ya Toure drive. Meli ndogo na kubwa zilionekana kutia nanga katika
baadhi ya maeneo huku majengo marefu ya hoteli na majumba makubwa ya kifahari
yakichomoza katikati ya vichaka vya miti ya fukwe ya bahari.
Pweza akiwa anafahamu vizuri wapi walipokuwa wakielekea aliendelea kuingiza
gia na kukanyaga mafuta. Baada ya muda wakawa wamefika eneo fulani lisilokuwa
na makazi ya watu huku barabara ile ikikatisha katikati ya msitu wa miti ya mikoko.
Walipofika eneo lile Pweza akapunguza mwendo na kukata kona kuingia upande wa
kulia sehemu kulipokuwa na njia hafifu ya nyasi iliyoonekana kutelekezwa kwa muda
mrefu bila kutumika.
Zera akashtukia baada ya kuona gari lile likishika uelekeo ule kwani kulikuwa na
kila dalili kuwa kule mbele hapakuwa na hoteli wala makazi ya watu na hali ile ikazidi
kumpa mashaka zaidi.
“Huku tunaelekea wapi?” Zera akauliza kwa mashaka
“Usihofu tumekaribia kufika” Pweza akaongea huku akionekana kulipuuza swali
la Zera.
“Lakini ufukwe wa Coco beach haupo huku?” Zera akazidi kuongea huku wasiwasi
ukianza kumuingia.
“Subiri na baada ya muda mfupi utaona” Pweza akasisitiza huku akizidi kushuka
na ile barabara hafifu ya nyasi.
Muda mfupi baadaye gari lile lilikwenda na kusimama katikati ya kichaka hafifu
cha miti ya mikoko na hapo Pweza akafungua mlango wa gari na kushuka. Wakati
akilizunguka lile gari upande wa pili akatumia fursa ile kuichomoa bastola yake Glock
32 kutoka kwenye koti lake la suti. Alipoufikia ule mlango wa nyuma wa gari alipoketi
Zera akaufungua huku bastola yake ikiwa mkononi. Mlango ulipofunguka Zera
akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola na hapo moyo wake ukamlipuka kwa
hofu.
“Shuka chini tumefika” Pweza akaongea lakini Zera akashtuka kuwa sauti ya
Pweza ilikuwa haina urafiki.
“Unataka kunifanya nini?” Zera akauliza kwa hofu huku akihisi hatari mbele yake.
“Bado hatujafika,sehemu ya safari yetu iliyobaki tutaimaliza kwa miguu” Pweza
akaongea kwa utulivu.
“Sishuki!...” Zera akaongea kwa hofu na kabla hajamalizia Pweza akamrukia na
kumzaba makofi mawili ya nguvu yaliyompelekea Zera ajihisi kuchanganyikiwa huku
akitema damu kisha Pweza akamshika mkono na kumvuta nje
“Sikiliza wewe kahaba! kuanzia sasa utafuata kile nitakachokueleza na usithubutu
kuleta hila yoyote kwani tambua kuwa sitokuvumilia. Ongeza mbele!” Pweza akafoka
huku amemkwida Zera kwa nyuma na bastola yake mkononi. Safari ya kushuka eneo
la chini la ile fukwe ikaanza huku Zera akitangulia mbele na pale alipotaka kuleta
upinzani akajikuta akikabiliana na kipigo.
Waliendelea kushuka kule chini na baada ya muda mfupi wakawa wametokezea
kwenye ufukwe mpana wa bahari ya Hindi. Ulikuwa ni mwendelezo wa ufukwe
mrefu wa bahari lakini usiokuwa na dalili za uwepo wa kiumbe hai chochote eneo lile
mbali na wanaume wawili ambao waliwakuta wakiwasuburi kule chini. Wanaume hao
walikuwa ni Fulgency Kassy na Kombe. Zera kuwaona watu wale kukazidi kumtia
hofu.
Pweza, Fulgency Kassy na Kombe walikuwa wameshirikiana katika kusuka
mpango mzuri wa kumnasa Zera mara tu baada ya kutoka kule Vampire Casino usiku
wa jana. Namba za simu ya Zera walikuwa wamezipata kupitia kwa yule meneja wa
Vampire Casino.
Kulikuwa na umbali mrefu kutoka kule ilipokuwa hoteli ya kifahari ambayo hapo
awali Zera alipopigiwa simu alikuwa ameahidiwa na yule mtu kuwa wangeonana
kwenye hoteli ile. Lakini katika ufukwe huu uliojitenga hapakuwa na dalili zozote
za uwepo wa mtu mwingine zaidi ya wale watu hatari na wala fukwe yenyewe
haikuonekana kufanyika shughuli zozote za kibinadamu. Kitendo cha Zera kumuona
Kombe akiwa ametundika chepe begani kikazidi kumwogopesha na hapo machozi
yakaanza kumtoka.
“Mfunge kamba hatuna muda wa kupoteza hapa” Flugency Kassy akamwambia
Kombe na hapo Kombe akaweka chepe lake pembeni na kumshika Zera. Zoezi la
kumfunga kamba Zera likafanyika kwa muda mfupi huku Zera akifungwa mikono
na miguu kama mnyama anayetayarishwa kuchinjwa na pale alipoleta ukorofi
akajikuta akiambulia kipigo cha nguvu. Kombe alipomaliza kumfunga kamba Zera
akamnyanyua Zera kama gunia na kujitwisha begani halafu wote wakaanza kutembea
taratibu wakielekea upande wa kulia wa fukwe ile. Baada ya hatua chache za safari
ile wakawa wametokezea kwenye sehemu nyingine ya fukwe iliyopakana na kichaka
kizito cha miti ya mikoko.
“Mshushe chini“ Fulgency Kassy akamwambia Kombe na hapo Kombe
akambwaga Zera chini kama gunia. Zera akapiga yowe kali la maumivu lakini hakuna
mtu aliyeonekana kumjali.
“Sikiliza wewe kahaba hivi unafahamu kwanini upo hapa?” Fulgency Kassy
akafoka huku akikiinua kichwa cha Zera ili waweze kutazamana vizuri
“Mnataka nini kwangu nyinyi wauaji?” Zera akaongea kwa hasira na hapo
Fulgency Kassy akamchapa kofi zito usoni.
“Funga mdomo wako wewe kahaba”
“Niueni tu si ndiyo mlivyopanga!” Zera akaongea kwa kinyonge huku damu
nyingi ikimtoka mdomoni baada ya kuchapwa makofi ya nguvu mfululizo.
“Tuambie huyu mtu anayeitwa Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani
wakati alipokuja kuonana na wewe kule Vampire Casino?” swali la Fulgency Kassy
likampelekea Zera ashikwe na mshangao.
“Mimi sielewi mnazungumza nini!” Zera akaongea kwa kulalama
“Tunajua kuwa unamfahamu ndiyo maana tukakuleta hapa. Kama utatupa
ushirikiano wa kutosha tutakurudisha nyumbani kwako ukiwa salama lakini kama
utaendelea na msimamo wako tutakulazimisha utuambie kwa namna nyingine
ambayo ni hatari zaidi” Fulgency Kassy akaongea kwa hasira.
“Kweli mimi sifahamu chochote” Zera akaongea kinyonge huku akimkumbuka
yule mwanaume aliyeonana naye usiku wa jana kwenye kile chumba kule Vampire
Casino aliyejitambulisha kwa jina la Stephen Masika.
“Tunataka utueleze vizuri kuhusu yule mtu uliyeonana naye jana usiku kule casino.
Mtu yule ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani?” Kombe akaongea kwa msisitizo.
“Tuambie na usithubutu kutuficha kwani yule mtu ni hatari na ndiye aliyehusika
na kifo cha yule mlinzi kule casino” Pweza akasisitiza.
“Nyinyi ni akina nani?’ badala ya kuwajibu Zera akawauliza huku akiyatembeza
macho yake kuwatazama na hapo wote wakatabasamu kwa hasira.
“Askari wa usalama” Fulgency Kassy kaongea kivivuvivu huku akitazama
pembeni.
“Sasa kama nyinyi ni askari mbona hapa siyo kituo cha polisi?” Zera akauiliza kwa
mashaka.
“Hilo siyo kazi yako wewe jibu swali uliloulizwa” Pweza akaongea kwa hasira.
“Mimi sijui chochote” Zera akaongea kwa utulivu. Fulgency Kassy hakusema
neno badala yake akamgeuki Kombe na kumwambia
“Hebu mueleweshe vizuri huyu kahaba naona bado hajatuelewa”
Maelezo yale yakaambatana na kichapo cha nguvu huku Zera akishindiliwa
makonde na makofi mazito ya Kombe na Pweza kila mahali. Hali yake ilipoanza kuwa
mbaya Fulgency Kassy akaingilia kati na kuwataka wasitishe.
“Hebu mwacheni huwenda sasa yupo tayari kutueleza” Kombe na Pweza
wakaacha kumshushia kipigo Zera na hapo Fulgency Kassy akamsogelea Zera na
kuinama karibu yake akianza kuongea kwa utulivu.
“Unajua ni kwanini tumekuleta kwenye hii fukwe. Hapa ni sehemu tulivu zaidi
tunapoweza kukuua pasipo mtu yeyote kufahamu wala sauti yako kusikika hivyo
usijidanganye kuwa msimamo wako utakusaidia. Hebu tuambie Stephen Masika ni
nani na alikuwa na shida gani mle ndani casino?”
“Mteja wangu” Zera akaongea kwa unyonge huku macho yamemtoka kwa hofu
“Mteja wako!...” Pweza akadakia ”Sasa mbona hukutuambia mapema tulipoanza
kukuuliza”
“Unaweza kutueleza ni kwa nini ulipopigiwa simu usiku ule kuulizwa kama
ulikuwa na mwanaume yeyote chumbani kwako ulikataa kusema ukweli?” Pweza
akauliza kwa hasira.
“Tuambie huyu mtu anayeitwa Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani
wakati alipokuja kuonana na wewe kule Vampire Casino?” swali la Fulgency Kassy
likampelekea Zera ashikwe na mshangao.
“Mimi sielewi mnazungumza nini!” Zera akaongea kwa kulalama
“Tunajua kuwa unamfahamu ndiyo maana tukakuleta hapa. Kama utatupa
ushirikiano wa kutosha tutakurudisha nyumbani kwako ukiwa salama lakini kama
utaendelea na msimamo wako tutakulazimisha utuambie kwa namna nyingine
ambayo ni hatari zaidi” Fulgency Kassy akaongea kwa hasira.
“Kweli mimi sifahamu chochote” Zera akaongea kinyonge huku akimkumbuka
yule mwanaume aliyeonana naye usiku wa jana kwenye kile chumba kule Vampire
Casino aliyejitambulisha kwa jina la Stephen Masika.
“Tunataka utueleze vizuri kuhusu yule mtu uliyeonana naye jana usiku kule casino.
Mtu yule ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani?” Kombe akaongea kwa msisitizo.
“Tuambie na usithubutu kutuficha kwani yule mtu ni hatari na ndiye aliyehusika
na kifo cha yule mlinzi kule casino” Pweza akasisitiza.
“Nyinyi ni akina nani?’ badala ya kuwajibu Zera akawauliza huku akiyatembeza
macho yake kuwatazama na hapo wote wakatabasamu kwa hasira.
“Askari wa usalama” Fulgency Kassy kaongea kivivuvivu huku akitazama
pembeni.
“Sasa kama nyinyi ni askari mbona hapa siyo kituo cha polisi?” Zera akauiliza kwa
mashaka.
“Hilo siyo kazi yako wewe jibu swali uliloulizwa” Pweza akaongea kwa hasira.
“Mimi sijui chochote” Zera akaongea kwa utulivu. Fulgency Kassy hakusema
neno badala yake akamgeuki Kombe na kumwambia
“Hebu mueleweshe vizuri huyu kahaba naona bado hajatuelewa”
Maelezo yale yakaambatana na kichapo cha nguvu huku Zera akishindiliwa
makonde na makofi mazito ya Kombe na Pweza kila mahali. Hali yake ilipoanza kuwa
mbaya Fulgency Kassy akaingilia kati na kuwataka wasitishe.
“Hebu mwacheni huwenda sasa yupo tayari kutueleza” Kombe na Pweza
wakaacha kumshushia kipigo Zera na hapo Fulgency Kassy akamsogelea Zera na
kuinama karibu yake akianza kuongea kwa utulivu.
“Unajua ni kwanini tumekuleta kwenye hii fukwe. Hapa ni sehemu tulivu zaidi
tunapoweza kukuua pasipo mtu yeyote kufahamu wala sauti yako kusikika hivyo
usijidanganye kuwa msimamo wako utakusaidia. Hebu tuambie Stephen Masika ni
nani na alikuwa na shida gani mle ndani casino?”
“Mteja wangu” Zera akaongea kwa unyonge huku macho yamemtoka kwa hofu
“Mteja wako!...” Pweza akadakia ”Sasa mbona hukutuambia mapema tulipoanza
kukuuliza”
“Unaweza kutueleza ni kwa nini ulipopigiwa simu usiku ule kuulizwa kama
ulikuwa na mwanaume yeyote chumbani kwako ulikataa kusema ukweli?” Pweza
akauliza kwa hasira
“Tuambie huyu Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani”
Fugency Kassy akauliza huku akionekana kuanza kuchoshwa na hali ile.
“Alikuwa mteja wangu!” Zera akaongea kinyonge.
“Kwa nini ulificha pale ulipoulizwa?” Kombe akauliza lakini Zera hakuwa na jibu.
Fulgency Kassy akamtazama Zera kwa hasira kisha akageuka na kuwatazama
Pweza na Kombe kabla ya kuwaambia.
“Hebu mshughulikieni vizuri hadi atueleze”
Kichapo cha nguvu kikafuata huku Kombe na Pweza wakimshushia Zera kipigo
cha aina yake cha mateke,ngumi na makofi mazito. Hali ya Zera ikazidi kuwa mbaya
hata hivyo hakuna aliyemuonea huruma. Kipigo kile kilipozidi Fulgency Kassy
akaingilia kati tena na kuwaambia.
“Mwacheni”
“Tueleze wewe malaya usitupotezee muda wetu” Fulgency Kassy akaongea kwa
hasira huku akiinama na kumtazama Zera usoni kisha akaendelea
“Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani?”
Zera akamtazama Fulgency Kassy kwa utulivu kisha akageuka na kuwatazama
Kombe na Pweza pembeni yake huku akionekana kukata tamaa sana. Kipigo kile
kilikuwa kimechanganya na kumpelekea maumivu makali mwilini huku akilia.
Mdomo wake ulikuwa umechanika,meno yake mawili yalikuwa yamevunjika na jicho
lake lilikuwa limeanza kuvimba na kuvilia damu.
“Alikuwa akitaka kuonana na Milla Cash” hatimaye Zera akaongea kwa shida na
hapo wote wakatazamana kabla ya Pweza kuuliza
“Kwa nini alitaka kuonana na Milla Cash?” Pweza akauliza.
“Alisema kuwa alikuwa na shida naye binafsi ambayo mimi sikupaswa kuifahamu”
Zera akaendelea kuongea.
“Kwa nini hakusema mapema wakati tulipoanza kukuuliza?” Kombe akadakia na
hapo Zera akabaki kimya akitazama chini.
“Wewe ukamwambiaje?” Fulgency Kassy akauliza.
“Nilimwambia akamuulizie Milla Cash kwenye ofisi ya mapokezi ya casino”
“Alipotoka chumbani kwako alikwambia anaelekea wapi?” Pweza akauliza
“Eneo la mapokezi la casino kumuulizia Milla Cash” Zera akaongea kwa woga
“Mlipanga tena kuonana wapi?” Fulgency Kassy akauliza na hapo Zera akatulia
tena kidogo huku akifikiria kuwa azungumze ukweli au adanganye lakini alipokumbuka
hatari ya kushushiwa kipigo zaidi akaongea ukweli.
“Alinipata business card ”http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Iko wapi?” Fulgency Kassy akauliza huku uso wake ukionesha matumaini.
“Ndani ya pochi yangu” Zera akaongea kinyonge huku Kombe akiichukua pochi
yake na alipoifungua ndani akakuta pakiti mbili za mipira ya kondomu za kiume,noti
mbili za shilingi elfu kumi na business card ndogo. Akaichukua ile business card na hapo
wote wakasogea karibu na kuanza kusoma maelezo yaliyokuwa kwenye business card
ile. Taarifa zilizokuwa kwenye business card ile zilijitosheleza na hapo Fulgency Kassy
akamtazama Pweza pembeni yake na kumpa ishara fulani ambayo haraka Pweza
aliielewa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment