Search This Blog

Friday 18 November 2022

PASIPOTI YA GAIDI 'THE RETURN OF KAMANDA AMATA' - 1

 








IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE



*********************************************************************************



Simulizi : Pasipoti Ya Gaidi 'The Return Of Kamanda Amata'

Sehemu Ya Kwanza (1)





1

IKULU – DAR ES SALAAM

Saa 10:30 alfajiri



WAKATI GIZA LA USIKU likijiandaa kutoweka na kuipisha nuru ya asubuhi, miti yote ilikuwa imetulia kimya kana kwamba kuna aliyeiambia ifanye hivyo. Ni Tausi mmoja mmoja aliyekuwa akilia tena kwa nyakati tofauti; hawakuwa na zamu ya kufanya hivyo isipokuwa ilitokea tu. Hekaheka katika jengo hilo la Makao Makuu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa kubwa. Vijana wa jeshi la polisi, kikosi maalum cha kutuliza ghasia FFU, kilikuwepo kikiwa kimejiweka tayari kwa lolote. Vijana wa Jeshi la Wananchi waliovalia kombati zao za mabakamabaka nao walikuwa wamezunguka jengo zima kuanzia juu hadi chini, kila mmoja akionekana kutingwa na shughuli inayompasa kufanya kwa muda huo.



Gari za wagonjwa kutoka Jeshi la Wananchi na zile za hospitali za serikali zilikuwa zikifanya kazi ya kubeba majeruhi na maiti zilizokutwa ndani ya jengo hilo, hekaheka.

Msemaji wa Ikulu alikuwa kasimama katikati ya ukumbi mkubwa ndani ya jengo hilo, alikuwa kimya bila kusema lolote, macho yake yalijawa na machozi, midomo yake ilitetema bila kutoa neno.

“Samahani Mzee!” sauti ilitokea nyuma yake, alishtuka kama mtu aliyekutana na Israel mtoa roho, aligeuka na kumtazama kijana aliyemwita kwa mtindo huo, lakini alijikuta anashindwa hata kuitikia ile salamu au kuuliza anamwitia nini badala yake alimfuata yule kijana pindi alipoondoka eneo lile. Moja kwa moja walifika kwenye ukumbi mdogo ambao ulikuwa na watu wasiozidi sita, yaani wale wenye vyeo vya juu vya dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi, pamoja nao kulikuwa na wasaidizi wengine ambao ni maofisa wachache wa Ikulu.



“Kama mnavyoona, maofisa kadhaa na wafanyakazi wa Ikulu wameuawa,” Makamu wa Rais aliliambia jopo, “Kilichotokea hapa hakieleweki, hakuna anayejua nini kimetokea, ila mke wa Rais yaani First Lady ametoweka, nafikiri, kwa uwazi kabisa kuwa huu ni uvamizi lakini sijui ni nani au siwezi kuhusisha na kikundi gani kwani uchunguzi ndio kwanza umeanza,” akatulia kimya bila kusema lolote.



“Bila shaka, inawezekana walidhamiria kumteka au kumdhuru Rais, walipoona hayupo basi wameondoka na mkewe, First Lady. Kumbukeni, Ikulu ya Tanzania ni kati ya majengo machache duniani yanayolindwa kwa mitambo ya hali ya juu na wanausalama waliokomaa kwenye fani yao, lakini kama tumevamiwa, bila shaka waliyovamia ni kundi lenye weledi wa juu zaidi katika medani hii ya usalama,” Waziri wa ulinzi aliongezea na wajumbe wote wakatikisa vichwa.

“Tumepoteza vijana wetu makini kabisa ambao hata miezi sita hawajamaliza tangu watoke mafunzoni. Rais hana budi kukatisha ziara yake, lazima arudi nyumbani kwani hali hii si ya kuvumilika, tunategemea neno la mwisho kutoka kwake,” Makamu akalieleza baraza na wote wakaunga mkono.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Mheshimiwa Makamu wa Rais, naomba utoe tamko la wazi juu ya hali hii maana Watanzania wanasubiri kwa hamu, tusipoangalia waandishi wa magazeti kama kawaida yao wataanza kutoa habari zisizothibitishwa,” Msemaji wa Ikulu alimwambia Makamu wa Rais.

“Ok, naomba ieleweke hivi, Ikulu imevamiwa na kundi la kigaidi, walinzi kadhaa wameuawa na bado kuna hali ya sintofahamu. Vyombo vya usalama viko katika harakati za kuhakikisha vinategua kitendawili hiki ndani ya saa chache. Tunaomba wananchi kuwa watulivu na pia kutoa taarifa polisi pindi unapoona mtu unayemhofia katika maeneo yenu,” Makamu wa Rais akazungumza na wakati huo tayari katibu alikuwa ameishaiandika kwenye mashine, ikasainiwa akakabidhiwa huyo bwana, Msemaji wa Ikulu ili kuwafikishia wanahabari waliofika alfajiri hiyo katika ukumbi mdogo wa maelezo ulio ndani ya jengo hilo.



***



Ikulu ilikuwa haiingiliki mpaka uwe na kibali maalumu, vijana wa Jeshi la Wananchi waliegesha magari yao upande wa baharini na mengine mawili upande wa hospitali ya Ocean Road na nyingine zilisimama karibu na Ofisi ya Hazina. Barabara ya Magogoni ilifungwa haikuruhusiwa gari wala mtembea kwa miguu kupita eneo lile. Juu angani helkopta ya jeshi na polisi zilikuwa zikifanya doria zikishirikiana na zile za Jeshi la Wananchi.

Kwa ujumla jiji la Dar es salaam lilikuwa katika misukosuko ya hapa na pale. Majira ya saa sita mchana barabara kubwa na ya muhimu zaidi katika jiji hilo ilifungwa kwa muda, ile inayotoka uwanja wa ndege kuelekea mjini. Ving’ora vikasikika na gari kama saba hivi zilipita kwa kasi ya ajabu kuelekea mjini. Na dakika kumi na mbili tua gari hizo ziliingia katika lango kuu la Ikulu na kuegeshwa mahala pake wakati tayari Mkuu wa nchi alikuwa amekwishashuka na kuingia ndani ya jengo hilo, moja kwa moja akiwa na walinzi wake alipitiliza na kuteremka ngazi iliyompeleka katika chumba maalum ambacho hufanyia mikutano yake ya siri kilichopewa jina la ‘Kilimanjaro Square’.



“Nimesikitishwa na kilichotokea, hii haiwezekaniki kuivumilia, ni uvamizi,” Rais aling’aka huku akizunguka chumba badala ya kuketi chini. Watu watano waliokuwa naye ndani ya chumba hicho walibaki kimya kabisa. Mkuu wa nchi akarudi na kuketi mezani kwake, akakamata kalamu yake na kutaka kuandika kitu lakini mkono ulikuwa mzito.

“Tulikuwa tunakusubiri wewe Mheshimiwa Rais ili utoe neno lako vijana waingie kazini mara moja,” Makamu wa Rais alitamka.

“Oh! Shiiit, Come on, hii ni Cold War! Let me say Cold War, na ntaipigana mpaka mwisho. Mtu kukuvamia ndani ya chumba chako na kumchukua mkeo ni matusi, matusi yasiyovumilika!” akang’aka huku akisimama wima kwa hasira, “Ni jengo gani au taasisi gani Afrika ina ulinzi mkali na makini kama hili jengo hapa? Hakuna, ninyi mnajua na dunia inajua. Sasa hawa waliokuja na kufanikiwa kufanya madhara haya ina maana wamejuaje njia za kuingia humu na njia za kutokea kama si hujuma?” aliendelea kung’aka kwa sauti. Kisha akatulia kidogo huku kijasho kikimtiririka, mwili wake ulimtetemeka kama mtu asikiaye baridi kali. Akasimama na kutazamana na Mkuu wa Majeshi “Nataka vijana wako waliobobea kweye michezo hii wahakikishe wanampata First Lady ndani ya saas12.



“Umesomeka Amiri Jeshi Mkuu,” akajibu Mkuu wa majeshi na kusimama akatoa saluti ya utii.

“Na ninyi wengine muwe katika kazi zenu za kawaida lakini nyote muangaze macho katika sakata hilo,” akatoa maagizo kwa viongozi wa vikosi vingine. Nao wakaitikia wito huo na kila mmoja akaondoka katika jengo hilo lililotukuka. Ni dakika hiyohiyo tu ambapo ule ukumbi ulikuwa na watu wawili tu yaani Rais na Makamu wake.

“Inaniuma sana Mheshimiwa!” Rais alimwambia makamu wake huku mikono yake ikiwa haitulii sehemu moja.

“Mimi pia, ukizingatia tumepoteza vijana wenye ujuzi wa hali ya juu sana katika maswala ya usalama,” makamu naye alijibu.

“Nina uhakika kwa vijana wetu hawa wa JW, hao wahalifu watapatikana tu,” Rais akajibu.

“Sawasawa kabisa, lakini unafikiri wao peke yao wataweza kulibaini kundi hilo lililofanya kadhia hii?”

“Kwa nini unasema hivyo?”

“Kwa sababu kutokana taaluma yao nahisi kama kazi hii inaweza kuwa ngumu,” makamu alikazia.

“Hapana! Hata mimi nilikuwa mwanajeshi, najua, tuna idara ya upelelezi ya jeshi, na kutokana na uzito wa jambo hili, wao ndio watu muafaka.” Akameza mate kisha akaendelea, “Unajua hawa lazima wapambane na mtu anayelingana nao kwa sababu bila shaka ni magaidi sasa gaidi ni levo nyingine, lazima apambane na mtu wa levo yake na hao si wengine ni vijana wa jeshi,”



Mheshimiwa Rais alamwelekeza makamu wake juu ya mpango huo. Kikao cha wawili hao kilipomalizika, Makamu wa Rais akaondoka na kumwacha mkuu wake peke yake ndani ya ofisi hiyo. Kitendo tu cha Makamu wa Rais kutoka na kumwacha mheshimiwa peke yake, simu ya mezani ilianza kuita kwa nguvu na fujo. Mheshimiwa Rais akaingalia kwa tuo kabla hajaamua kama ainyanyue na kuisikiliza au aiache, lakini tatizo ni kwamba hakujua simu hiyo ilikuwa inahusu nini au inamhusu nani. Na mara nyingi simu ya chumba hicho ikiita basi huwa kunakuwa na jambo zito la kiofisi. Kwa mkono wa kitetemeshi aliukwanyua mkono wa simu ile na kuiweka sikioni bila kuongea lolote.

“Usijaribu kuchukua hatua yoyote kwa kumtafuta mkeo, tunajua unampenda na ndiyo maana tumemchukua, lakini ujue sisi tunachokitaka si fedha wala hatuna ugomvi na wewe. Tunahitaji jambo moja tu, toa amri ya kuondoa majesji yako ya kulinda amani katika Kusini mwa nchi ya Ngoko. Ukilitekeleza hilo, mkeo utampata, na husipotekeleza tutateka na watu wa familia yako waliobakia, na wewe utakuwa wa mwisho…”

“Ninyi ni nani? Enh! Ni nani?” alikatisha simu ile na kurusha swali ambalo halikujibiwa na simu ile ikakatika. Rais alibaki amesimama bila kufanya lolote huku simu ile bado ikiwa sikioni, akili ilipomrudia akateremsha mkono taratibu na kuipachika mahala pake. Akajitupa kitini nacho kikampokea bila hiyana huku kikinesanesa. Mlango wa chumba hicho uliwaka taa ya kijani kwa ndani, akabonyeza swichi iliyo chini ya meza na kijiluninga kidogo kikaonesha mtu aliye upande wa pili.



“Chakula kipo mezani Mkuu!” akakribishwa lakini alipojitafakari aliona hata njaa hana, akanyanyuka na kutoka nje ya chumba hicho ambapo mlinsi wake namba moja kutoka idara ya Usalama wa Taifa alimpokea na kumwongoza kuelekea katika ukumbi wa chakula. Ndani ya ukumbi huo kulikuwa na watu watatu tu ambao daima alipenda kula nao, hawa ni watu wa karibu sana nay eye, yaani watoto wake, mmoja wa kike na mwingine wa kiume. Aliwaangalia watoto wake lakini alijikuta anashindwa kula chakula kile, badala yake aliamua kuondoka na kurudi ofisini, mara hii aliingia ofisi yake ya kawaida, akamwita katibu wake na kumwomba amwitie mkuu wa usalama wa Ikulu.

“Pole kwa kupoteza vijana wako!” alimpa pole.

“Siwezi kupoa mpaka nipate ukweli wa hili,” yule mkuu wa usalama alijibu huku chozi likimdondoka.

“Umefika Olduvai?” akamwuliza.

“Ndiyo mkuu!”

“Hakuna madhara yoyote?”

“Hakuna mkuu, kule hawajafika kabisa,” yule mkuu wa usalama akampa jibu lililomfanya yule Rais kutabasamu kwa mbali.

“Sikiliza Othman, hili swala si dogo, ni gumu, nimetoa kazi kwa vijana wa JW walikamilishe, lakini nataka na wewe hapa unifanyie uchunguzi juu ya hili, hawa jamaa wamewezaje kuingia hapa ndani pasi na kuonekana?” rais alionesha wasiwasi wa wazi.

“Mheshimiwa Rais! Hicho kitu kinanishangaza mpaka sasa, bado naumiza kichwa kujua ni vipi hawa watu wameweza kuipenya hii ngome ya chuma, sipati jibu. Nafikiri inabidi tuwashirikishe wanaintelijensia wa juu kabisa katika hii Nyanja,” Othman, mkuu wa usalama Ikulu alimweleza rais.



“Usemalo ni sahihi, je unataka tukodi vyombo vya nje?” akamwuliza mara baada ya kuiinua uso wake.

“Inapobidi hatuna budi kufanya hivyo,”

Mkuu wan chi akajiinamia tena kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama Othman.

“Sikia Othman, ina maana sisi vyombo vyetu vimeshindwa? Ni mapema mno kuomba msaada kutoka mataifa ya nje, ngoja tushindwe kabsa hapo hatutakuwa na budi lakini si sasa,” akamwambia.

“Ngoja nikwambie kitu, mimi kama mwanausalama nakueleza tu hili swala linaweza kuwa gumu sisi kulitatua, kwa sababu hatujui nini na nini kimetukwamisha katika kugundua hao majahili. Isitoshe pamoja na ulinzi mkali wa jengo hili ndio maana unaona vijana wetu wamekufa na kuumia, wavamizi hao wameingia moja kwa moja mpaka ndani ya nyumba yako ilipo ndani ya Ikulu hii, hili si la kawaida na halijawahi kutokea popote katika karne hii,” Othamn akaongea kwa uchungu sana.

Maneno haya yaliifinya akili ya rais kwa muda huo, akatafakari jambo, akamtazama Othman, “Othman, kati ya vijana wangu wachache ninaoheshimu mawazo yao, wewe ni mmojawapo ndio maana nilikutoa kule ubalozini kukurudisha hapa Ikulu, sawa nitalifanyia kazi leo hii, asante,” rais akamshukuru Othman, wakaagana.



***



KUSINI MWA NCHI YA NGOKO



MVUA KUBWA ILIKUWA IKINYESHA wanajeshi wa majeshi ya kulianda amani kutoka Tanzania walikuwa wamejificha katika msitu huo mnene, wakiwa wamegawana makundi ya askari ishirini ishirini na kuuzungukla mzitu huo unaokaliwa na waasi wa X65. Waasi hao waliouvamia msitu ho miaka kadhaa nyuma walikuwa sugu na hawakutaka kuondoka kabisa kwa kuwa waliteka migodi ya dhahabu na almasi kwa manufaa yao na waliowatuma.

Uamuzi wa Tanzania kutoa batalioni moja ya wapiganaji wake mahiri wa Jeshi la Wananchi ulitokana na ombi la Umoja wan chi za Afrika ili kukomesha kabisa uasi huo uliokuwa ukikiuka haki za binadamu kwa watu waishio katika maeneo hayo. Mara kadhaa majeshi ya kujitolea yalikwenda huko lakini yalikutana na waasi wenye silaha nzito za kivita hivyo kupelekea kushindwa na kurudi nyumbani bila kutimiza azma yao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya muda mrefu wa kuwaacha waasi hao, maafikiano ya amani yalishindikana kwa njia ya kidiplomasia kati ya viongozi wa Afrika na kiongozi wa wassi hao wa X65 waliokuwa wakipigana vita ya gorilla. Vikao vilikaliwa miji mbalimbali ya Afrika lakini ilikuwa ngumu kufikia muafaka, waasi hao hawakutaka kabisa kuuachia msitu huo.



“Hawa jamaa si wa kuwaonea huruma hata kidogo!” mmoja wa wanajeshi aliyekuwa katika ficho lake huko msituni aliwaambia wenzake.

“Ila inaonekana sio tu waasi bali ni wanajeshi waasi kwa maana wanajua vyema mbinu za kivita.

“Yeah ni kweli, maana kila tunapowazunguka nao wanakuwa makini, na kila tufanyalo inaonekana kama wanalijua,” askari mwingine wa mstari wa mbele alimjibu mwenzake huku akiweka bunduki yake sawia kifuani pake maana mapambano yangelipuka wakati wowote.

“Kumbukeni wenzetu wameshindwa kazi hii na sisi tumeaminiwa kuifanikisha,” kiongozi wao akawaambia.

“Aaaa sisi ni jeshi imara la Tanzania, hawatuwezi, tunawapanga wadunguaji kisha tunamaliza kazi, hawa waasi ni kuwafutilia mbali tu, aliongea mwanajeshi mwingine aliyekuwa amebeba redio kubwa mgongoni mwake.

“Chonjo wasiliana na makundi mengine waambie karibu tunaingia kijiji cha Mpumbutu, hapo lazima tuzunguke kijiji kwa maana hatujui, labda wapo hapo” kiongozi wa kundi akampa maagizo mtaalamu huyo wa redio aliyejulikana kwa jina la Chonjo.





***



Kutoka katika makundi mengine yote walipata taarifa ile ya redio kupitia vyombo vyao vya kisasa kabisa ambavyo kila mmoja aliweza kusikia kwa wakati wake na aliweza kuongea na mwenzake. Askari wale wakajiweka vyema kila mmoja akaiweka tayari bunduki yake kubwa (assault rifle) aina ya M4 Carbine kifuani tayari kwa uvamizi. Bunduki hii wanajeshi wote walipewa katika operesheni hiyo ukiachana na hiyo bunduki kila mmoja alikuwa na bastola mbili zenye nguvu kwa operesheni za dharula, mabomu ya kutupa kwa mkono ‘fragmentantion granade’, mabomu ya kutoa moshi ‘smoke granade’ kwa ajili ya kumchanganya adui. Zaidi ya hapo kila kundi lilikuwa na mtu mwenye LPG, ‘anti-tank weapon’, silaha ya kujitwisha begani inayotumika kuvunja vizuizi wakati wa operesheni. Kwa ujumla vijana hawa walitimia kila idara.



Kutoka katika maficho walipita chini kwa chini kwenye vichaka vinene kwa minajiri ya kuzunguka kile kijiji cha Mpumbutu, wengine wakaenda mlimani na wengine upande wa chini. Iliwachukua kama dakika ishirini na tano kuzingira kijiji hicho ambacho mara nyingi waasi walipenda kujificha humo. Kisha askari wawili walijitoa chambo kuingia kijijini ili kuwafanya waasi hao kujitokeza kirahisi.



Katika moja ya vichaka kulilala watu wawili waliojifunga nyasi kavu na mbichi migongoni na kichwani kiasi kwamba wakilala kifudifudi huwezi kutambua kama ni binadamu, hawa walikuwa ni wadunguaji kitaaluma walikuwa na bunduki kubwa ya kudungulia ‘Heavy Sniper Rifle’ M82A1. Walijificha kimya kwenye kichaka kilicho juu ya kilima huku kwa chini wakikiona kile kijiji.



KIJIJI CHA MPUMBUTU



Shughuli za wanakijiji ziliendelea kama kawaida, watu walikuwa wakijpatia huduma ndogondogo katika maduka na vigenge, wengine wakipata vinywaji na kulewa ili kujisahaulisha shida zao. Pembezoni mwa kijiji hicho, ukimaliza tu nyumba za wenyeji kulikuwapo na nyumba nyingine kubwa tu, nyumba hiyo ilikuwa ya tajiri mmoja mfanyabiashara aliyeuawa na waasi na kisha wao kuichukua na kuifanya maskani yao kila waingiapo kijijini hapo. Hakuna mtu aliyekuwa akiisogelea nyumba hiyo kwa kuhofia kuuawa. Waasi waliitumia zaidi ya kazi hiyo, waliitumia kama dangulo, pale mkubwa wa waasi anapojisikia ashki ya kufanya ngono vibaraka wake walikwenda kijijini na kukamata mwanamke yoyote na kumleta humo ndani. Endapo atakataa aliuawa hadharani, hali hii iliwafanya watu wawafungia mabinti na wake zao ndani na wengine hata kukikimbia kijiji hicho.



“Hiki ndiyo kijiji cha Mpumbutu, wananchi wake hufanyiwa vitendo vya uzazalishwaji na hutendwa kinyume na haki za binadamu, serikali ya Ngoko kama haiyaoni haya, tunataka kusafisha waasi kwa mashambulizi ya kimbunga, na si wananchi, hakikisha risasi yako inampiga muasi na shabaha yako isikosee,” sauti ya kiongozi wa vikosi vya ukombozi ilisikika sikioni mwa kila mmoja.



Benson Boko aliweka jicho lake katika lensi ya bunduki lake kutoka pale alipojificha na kuchungulia, akiangalia lile jumba waliloelekezwa kwenye ramani na kisha taratibu alielekeza kwenye vijia na njia zinazopita katikati ya kijiji hicho. Akaondoa jicho na kuangalia saa yake, ilikuwa yapata saa 12 jioni. Bado si wanakijiji wala waasi waliokuwa wakijua kuwa wamezingirwa, muda ulikuwa haujafika wa kufanya kazi yao.



***



Bensoir Banginyana alikuwa juu ya kiti chake akipendacho huku wasichana wawili warembo walikuwa wakimkanda mwili wake. Kinywani mwake kulikuwa na siga kubwa kila akipiga pafu mbili hulitoa na kukung’uta jivu kibwetani.

Mlango mkubwa wa mbele wa jumba hilo la kifahari ulifunguliwa ghafla na kijana mmoja aliyevalia kijeshi akasimama mbele ya Bensoir Banginyana, akapiga saluti na kutulia kiutulivu wa kiaskari.

“Mkuu nahisi tuna wageni katika himaya yetu,” yule askari akaongea kwa ukakamavu bila hata kutikisika.

“Nani aliyekwambia mpiganaji huwa anahisi, sema vizuri, sema kitu chenye uhakika na si kuhisi,” Bensoir akang’aka na kuinuka pale kitini huku akiwasukuma pembeni wale wasichana, akavuta jaketi lake la kijeshi na kulivaa, “Mmeona nini?” akauliza.

“Kuna sura mbili ngeni hapa kijijini zimeingia, kwa jinsi walivyo ni kama majasusi wanaopeleleza kitu fulani,” akajibu.

“Mmewaweka jichoni au ndiyo mmewaacha tu kama kawaida yenu?”

“Wako jichoni mkuu,”

“Waleteni sasa hivi tugawane nyama!”



Dakika tano baadae vijana wawili waliingizwa katika ile sebule kubwa ya Bensoir, wakaamuriwa wapige magoti. Miili yao walikuwa wameifunika kwa makoti marefu ya mvua, lakini miguu yao ilionekana dhahiri kuwa wamevaa buti za kisasa za jeshi.

“Ha! ha! ha! ha! Wenzenu waliotangulia walisalimu amri kwenye msitu huu wa shetani ninyi mmekuja sio, sasa tutawachinja na video yenu ataiona rais wenu.” Akakohoa kidogo, “ wavueni hayo makoti,” akaamuru.

Baada ya kuvuliwa makoti walibaki na kombati zao za kijeshi, kwenye mabega yao kulipachikwa kibaka cha mstatili kilichoonesha bendera ya Umoja wa Mataifa.

“Tuwaambie mara ngapi pumbavu ninyi? Sasa wakuu wenu wamewasaliti, kwa kuwa wanajua wazi maafikiano yetu na wao,” Bensoir akawaeleza. Wale askari wawili walikuwa wamejiinamia huku mikono yao ikiwa imefungwa kwa nyuma.

“Mnatoka wapi?” akawauliza lakini hawakujibu. “Kuna ujeuri huwa hausaidii, maana mjibu, msijibu lazima niwaue tu”.

Teke moja la kushtukiza lilitua shavuni mwa kijana mmoja akamgonga mwenzake na wote wawili wakaanguka chini sakafuni.



“Nipe bastola yangu,” akamwambia askari mwingine aliyekuwa akilinda sebuleni hapo. Akiwa anapokea bastola hiyo akasikia kishindo kizito kutokea nje, akahamaki kidogo.

“Nini hicho? Hebu angalia nje,” akimalizia kusema hayo akasikia kishindo kinginie upande wa pili na kingine tena, mara taa zikazimika giza likatawala mle ndani.

“Ambush !!!” akanong’ona na kila askari wake akachukua kona yake, wakawasahau wale wawili pale chini.



***



“Nimeshaangusha watatu, eneo liko salama mnaweza kuingia,” yule mdunguaji alisema kwenye kile chombo chao cha mawasiliano. Kutoka kule milimani vijana kama ishirini waliteremka kutoka pande tofauti kwa mwendo ambao huwezi kuwagundua hata siku moja, waliikaribia ile nyumba na kujificha kimya kwenye vichaka vidogo mita chache tu kabla ya lile jumba. Walishuhudia wale jamaa waliokuwa wakilinda jumba hilo kutokea upande wa juu wakidunguliwa kwa ustadi kabisa kilichofuatia ni kufuata amri ile ya wadunguaji kuwa sasa wanaweza kuvamia jumba hilo.



Kutokana na mafunzo waliyoyapata vijana wale waliivamia ile nyumba kwa mtindo ambao uliwashangaza adui zao, walikuwa wakiingia kwa mstari na kila walipofika kwenye kona yule wa kwanza alibaki pale na kuwapa ishara wa nyuma yake kuwa wapite na kusonga mbele. Mmajibizano ya risasi yalipamba moto ndani ya jumba hilo, iliwapa taabu sana wale waasi kuwadhibiti hao wanajeshi kutokana na giza lililokuwako ndani humo. Vijana wa jeshi JWTZ chini ya mwamvuli wa UN walikuwa ngangari, ndaani ya vifaa vyao vilivyokaa machoni badala ya miwani ambavyo vilikuwa vikiwawezesha kuona vizuri gizani.

Walihakikisha hawapotezi risasi hata moja kwani kila moja ilianguka na mtu, wengine waliwasaidia wale wenzao huku wengine wakiendelea na msako wa chumba kwa chumba.

“Vipi?” mmoja alimuuliza mwenzake baada ya kumuona anakuja sebuleni.

“Hayupo?” akajibu. Askari wote walikutana sebuleni mwa jumba hilo lakini walimkosa Colonel Bensoir Banginyana.

“Kakimbilia wapi mwanaharamu huyu?” kiongozi wa ile platuni aliuliza wenzake.

“Hatujamwona, walinzi wake wote na askari wa nyumbani tumewaangusha.” Yule askari akajibu kisha dakika hiyo wote wakaiacha ile nyumba pweke baada kusikia kikirikikiri za watu huko nje.



“Marc weka wapangaji ndani ya nyumba,” amri ikatoka kwa kiongozi. Marc akapachika mikono katika mifuko ya mkanda mkubwa aliouvaa na kutoa mabomu matatu madogomadogo lakini yaliyokuwa yakitumia saa, akayapachika sehemu tatu tofauti na kisha kuiacha ile nyumba huku nyuma yake risasi zikirindima kumfukuza, lakini bahati nzuri alikuwa amekwishakwea ukuta na kujitupa upande wa pili na risasi za waasi waliovamia nyumba hiyo zikachimba ukuta.

“Move around!! move around!!” ilisikika sauti iliyokuwa ikiwapa amri wale waasi kuzunguka nyuma ya nyumba.

“Comander!” Mark akaita huku akimwangalia mkubwa wake hatua kama mia mbili mbali na ile nyumba.

Kutoka pale walipo walishuhudia mlipuko mkubwa ukiitawanya ile nyumba vipande vipande, mbao na vitu kama hivyo vikiruka hewani na kutawanyika kila upande..

“Sangalamanda mchuzi wa dagaa!” yule commander wa kikosi akatoa tusi la ajabu huku akiwasha sigara yake na kuipachika kinywani.

“Return to zero! Return to zero!” maelekezo yalisikika kutoka katika chombo cha kila mmoja na wote wakaondoka eneo hilo kwa njia ya siri, wakajificha tena msituni huku wakisikiliza matokeo ya operesheni yao hiyo.



MWAKA MMOJA ULIOPITA

Ikulu ya Dar es salaam



MKUTANO WA WATU WANNE ulifanyika katika ofisi ya Rais wa Tanzania ndani ya jengo la Ikulu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) mwenyekiti wa kamati ya usalama ya umoja huo, mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Amirijeshi Mkuu wa Tanzania walikutana asubuhi hiyo kwa kikao kizito.

“Tunaelekea kushindwa na waasi hawa!” yule Katibu wa AU aliwaambia wajumbe, “Kwa sababu majeshi kutoa SADC yameelemewa na waasi, hapa hatuna jinsi tumeona ikiwezekan nchi yako itusaidie jeshi lako japo Batalioni moja nina uhakika na vijana wako,” akamwambia rais wa Tanzania ambaye ndiye alikuwa Amri Jeshi Mkuu, akamkabidhi na waraka wa kiofisi wa ombi hilo.

“Nalijua hilo!” rais akajibu, “kama majeshi ya muungano ya SADC yanaelekea kushindwa, mimi jeshi langu ni moja tu litaweza?” akaongeza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Oh, Sikia Mheshimiwa, wale waasi wapo msituni wanapigana vita ya ardhini, tulipokaa na kuchambua tumeona katika Afrika ni Tanzania yenye jeshi linaloweza vita hiyo tena kwa weledi mkubwa. Tumerejea vita ya Uganda, tumerejea ukombozi wa kisiwa cha Anzuan kule Comoro alkadhalika jeshi lako ndiyo limekuwa mwalimu mzuri wa mazoezi ya vita hii katika ukanda wa Afrika na hata nje ya Afrika, Ufaransa walikuja hapa kubadilishana uzoefu, India na nchi nyingine. Kiukweli tumeona jeshi lako litamaliza hii kazi,” akamaliza kusema na kuketi kitini.

“Nimekusikia na waraka huu tulishaupata, sasa kuna mambo ambayo tuliyazungumza” akampa waraka mwingine kutoka upande wa Tanzania, “bunge lilikubaliana hayo, kama yatatekelezwa sisi hatuna tabu. Opersheni yetu haitakuwa ya kulinda amani, sisi tunaenda kusafisha waasi, na lazima waondoke ndani ya kipindi kifupi,” akamaliza kusema.

Mwafaka ukafikiwa, na JWTZ wakapewa kazi chini ya kofia ya AU kutimiza kazi hiyo, miezi miwili baadae, batalioni moja ya wanajeshi wa miguu (Infantry) waliondoka Dar es salaam kueleke huko katika nchi ya Ngoko.



UPANDE MWINGINE WA AFRIKA



NDANI YA JENGO MOJA refu sana ambalo kwa juu kabisa lina kitu kama kisahani cha chai kinachojizungusha kwenye mhimili wake walikutana watu watatu waliotofautiana hata kimaumbile. Mwenye mwili mdogo kuliko wote ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikao hicho kisicho rasmi lakini wenyewe walikiita cha dharula. Majadiliano makubwa yalikuwa ni kusimamisha mtazamo wao na kuufanya kuwa kinyume na matakwa ya wengine.

“Huyu jamaa anatuharibia! Sisi tumeshweka msimamo wetu wa siri na mataifa mengi yanajua hata Rais wa Ngoko mwenyewe anajua hilo. Ina maana wao hawashangai kwa nini jeshi la Ngoko halifiki kule Kusini mwa nchi yao? Sasa huyu ni nani hata yeye kama yeye atoe jeshi la nchi yake tu kupambana na wale vijana wa X65?” yule kiongozi wao aliyekuwa na kauli yenye nguvu akawaambia wajumbe wake hao wawili juu ya swala hilo.

“Mimi nilipinga sana muswada huo pale Addis Ababba, kwa kuwa nilijua madhara yake, lakini nchi nyingi zikang’ang’ania tu, ikapita kauli ya ‘wengi wape’, basi, lakini sijui tufanyeje Comrade!” mwingine alichangia.



“Hakuna jinsi huyu lazima tumkomeshe, nilifanya hila mpaka nchi yangu ikaingia katika umoja wenu huu lengo langu mimi nataka nitawale hapa pote, na ninaweza kwa sababu nina akili japo nina mwili mdogo, we unafikiri pesa itatoka wapi? Lazima tuchukue madini kule Ngoko kwa nguvu tuwauzie huko dunia ya kwanza ili nipate pesa ya kuweka watu wangu. Ninyi nyote nimewaweka madarakani kasoro hawa wawili hawa, na huyu mwingine ananivuruga kabisa yaani,” yule Kiongozi aliongea mpaka akaona miwani nzito haimtoshi.

“Comrade, hapa ni mapinduzi tu, mi nakuaminia sana wewe, kama uliwatungua wale kipindi kile ukachukua nchi utawashindwaje hawa wawili?” akaongea mjumbe aliyevaa pama kichwani mwake. Wote hawa watatu walikuwa ni marais kutoka nchi tatu tofauti, walijitenga na kufanya mambo yao katika umoja wao usiotambulika popote.

“Msijali, wajumbe tukutane kikao kama hiki wiki tatu zijazo nitawajuza nini nimefikiria kufanya juu ya hili,” akamaliza. Kikao kikaahirishwa na wale wajumbe kila mmoja akaondoka kuelekea atokako.



2

UJERUMANI MASHARIKI



KAMANDA AMATA kama alivyojulikana, aliteremka kwenye gari ya kifahari aina ya BMW X5 liling’aa kwa rangi ya kimetaliki, ilimfikisha katika jengo hilo kubwa ambalo kwa juu liliandikwa kwa maandishi makubwa na ya kupendeza yaliyosomeka IN DIAMOND WE TRUST. Kwa hatua za haraka haraka alitembea kuelekea jengo hilo, zaidi ya suti ya gharama aliyoivaa mkononi mwake alikuwa na briefcase kubwa na ya kitajiri sana, kiatu chake kilionekana wazi kuwa hakijawahi kukanyaga udongo tangu kinunuliwe. Pamoja naye aliongozana na mwanamama mtu mzima, Theresia Schurman, aliyekuwa ni mmoja wa maajenti wa kampuni hiyo iliyokuwa ikisifika kwa ununuaji wa madini hayo ya almasi.

“Karibu sana!” alikaribishwa ndani ya ofisi nadhifu sana, akiwa na yule mama waliongoza mpaka kwenye mlango mwingine mdogo ambako walifunguliwa na kuingia ndani ya ofisi hiyo. Kulikuwa na mtu mmoja wa makamo, si mnene sana lakini alikuwa na nyama za kutosha. Juu ya meza yake kulikuwa na jina lake lililochongwa vyema kwa mwandiko mlalo, Stephen Mc Donald.



“Mc Donald kama tulivyoongea kwenye simu, huyu ni Mr. Spark kutoka Afrika yeye ni mfanyabiashara wa madini na anapenda kufanya kazi na sisi,” yule mama akamaliza na bwana Stephen akanyanyuka na kumpa mkono Mr. Spark kisha wakaketi.

“Ndiyo Mr. Spark!” akaanzisha mazungumzo.

“Yeah, kama alivyokwambia Bi. Theresia Schurmann, natokea Afrika, mimi ni mnunuzi na muuzaji wa madini haya na dhahabu pia, lakini kuja kwangu ni kutafuta masoko ya almasi hii mpya, sijui kama umepata kuiona kabla,” Mr Spark akazungumza na kufungua ile briefcase yake akampa huyo bwana kipande cha almasi. Mc Donald akakichukua na kukitazama kwa makini sana, akaonekana kama kapatwa mshituko hivi lakini baadae akakaa sawa.

“Unasema almasi hii umeitoa wapi?” Mc Donald akauliza.

“Inatoka Afrika, mimi ni biashara ya kukusanya madini haya, na nimefanya kazi na makampuni mbalimbali, safari hii nikapenda kuja kwenye kampuni yako…” Kamanda Amata au Mr Spark kwa jina la kificho alimwambia yule bwana ambaye sasa alikuwa kachuku kitu kama koleo na kubana kile kipande cha ng’walu, akikiangalia kwenye mwanga wa taa.

“Unajua kwa nini nakuuliza umeipata wapi?”





“Najua; ni kwa sababu unataka ujue kitu bora kama hiki kinatoka wapi, ni Afrika tu mzee, hakuna kwingine duniani,” Amata akamjibu huku akikunja nne na kujiweka sawa .

“Mr Spark! Hii sampuli haiuzwi wala haifanyiwi biashara yoyote kwa sababu ni ‘conflict diamond’, hata uende kwa nani Ulaya hii hawezi kununua,” akameza mate na kisha akanywa maji kidogo, uso wa Mc Donald ulionekana kutona kwa matone madogomadogo ya jasho, “Huwa tunaogopa sana watu wanaokuja na hii sampuli ya almasi,” akamalizia.

“McDonald, hii ni almasi ghali sana, kwa nini hamuitaki?”

“Sio hatuitaki, labda ninachoweza kukusaidi ni kukukutanisha na mtu anayeweza kufanya biashara ya sampuli hii na wewe,” Mc Donald akamweleza Amata.



“Ok, wazo zuri, basi kama utanikutanisha naye, itakuwa vyema name nitakupa sampuli ingine labda hiyo utaikubali,”

“Bila shaka!” akakohoa kidogo kwa sababu alionekana kuathiriwa sana na tumbaku, “Nitakupigia simu mara baada ya kumpata mtu huyo,” akamalizia na kuagana na Amata.

Conflict Diamond, Kamanda Amata akawaza wakati akiwa ndani ya gari hiyo kuelekea hotelini kwake ndani ya jiji hilo la Berlin. Kichwani mwake hakuwa na shaka na bishara hiyo anayojaribu kuifanya na nchi hizo za Ulaya kwani hata yeye anajua kuwa inalipa. Baada ya kupita mitaa kadhaa yenye mabarabara ya kutisha kwa uzuri aliwasili katika hoteli aliyofikia, Paradox Hotel.



T S A MAKAO MAKUUhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



CHIBA WA CHIBA alikuwa ametingwa kwenye kompyuta zake akiangalia mambo mbalimbali katika mtandao, akifuatilia hiki na kile huku kwenye luninga kadhaa akitazama mienendo ya jiji la Dar es salaam sehemu nyeti nyeti kwa ajili ya usalama. Mlango ukafunguliwa na Madam S akaingia huku mkononi akiwa na kikombe cha kahawa.

“Bibi kweli umezeeka, jua lote hili na kahawa?” Chiba akaanza kumchokoza.

“Hivi hata humu ndani kuna jua? Na hilo air conditioner uliloliwasha unategeme nini, hata hivyo hiki ni kinywaji kama vinywaji vingine,” akajibu huku akivuta kiti na kuketi, jicho lake likipita kwenye zile luninga.

“Hivi ilikuwaje tukio la majuzi lile kutukia ilhali tuna vifaa kama hivi kwa usalama?” akauliza Madam.

“Hivi unawajua magaidi au unawasikia? Usijiulize imekuwaje au imewezekanaje, kuna watu hata wakiamua kwenda kukiiba kiti cha enzi kule mbinguni wanaweza, sasa sembuse hapa kwetu?” Chiba akajibu huku akigeuza kile kiti na kukigeuzia kwa Madam.

“Hapo unafanya nini?” akamwuliza.

“Aaah nilikuwa nachambua habari za watu tishio Afrika zaidi zaidi huyu kiongozi wa X65 ndiye ambaye namsoma zaidi na kuchukua vitu fulani Fulani,” Chiba akajibu huku akiurudi tena kwenye kompyuta yake.



“Enhe, nani mwingine uliyemdadavua?”

“Wengi, kuna Joseph Konyi naye nilikuwa namcheki hapa, kuna huyu kiongozi wa Al-Shabab na hawa Boko Haram wote nilikuwa nawapitia ila nimestak zaidi kwa huyu Bensoir Banginyana kwa sababu yeye ni hot cake,” akaeleza.

“Enhe nini kipya zaidi ya kuwa kiongozi wa juu wa X65?” Madam akazidi kuhoji.

“Eh, madam una maswali ka’ mtoto wa miaka minne! Bensoir Banginyana ni mzaliwa wan chi ya Nduruta, amesoma na kukulia huko Ngoko miaka mingi nyuma, baadae wazazi wake wakarudi Nduruta pamoja naye na kuanza maisha mapya. Huyu bwana alijinga na jeshi miaka ya 1985 na kwa sababu ya elimu yake alipata cheo cha juu sana cha Kanali akiwa na umri mdogo. Ameliongoza jeshi la Ndyryta kwenye operesheni mbalimbali na zote zimefanikiwa. Alikwenda USA kwa kujifunza zaidi maswala ya Military Intelligency kwa miaka minne, inasemekana alishiriki katika moja ya operersheni kubwa iliyofanywa na jeshi la Marekani katika jangwa la Afghanistan lakini hawajasema hapa ni operersheni gani…”

“We unasoma katika mtandao gani hizo habari mbona kwenye weekpedia hayo hayajaandikwa?” Madam S alimkatisha Chiba.



“Madam S! Mkuu wa TSA, mimi kuwa TSA 2 haikuwa makosa na ni wewe mwenyewe uliona nafaa au siyo. Hapa nimevunja codes za mtandao wa CIA, nimechukua faili kisha nimerudisha kama ilivyo. Hili tunaliweza watu wachache sana duniani, hapa ningekaa na code yao kwa dakika tatu tu wangegundua na wangejua ni wapi imevunjwa hiyo code, lakini nilijiandaa nikafanya kwa kasi ya ajabu bahati nzuri nikalipata, nikachukua faili hilo tu basi…”

“Umelipakua au?” Madam akamkatisha tena.

“Kama kawaida!”

“Endelea!”

“Bensoir Banginyana alirudi na kuendelea na wajibu wake katika jeshi la nchi yake kama awali. Baada ya mapinduzi ndipo huyu kanali alipohasi jeshi na kuingia msituni, huko aliwafundisha vijana kadhaa na kuanzisha kikundi kidogo cha uasi kilichosumbua sana nchi ya Nduruta. Faili hili linasema kwamba Banginyana aliongoza mapinduzi ya pili ya kumtoa Rais Sabinus wa Nduruta na kumtangaza Brigedia Kadanse Sebutunva kuwa rais na ndye huyu mbabe mpaka sasa, hataki kuachia madaraka…”

“Doh, hiyo habari mpya kabisaaa, niliwahi kufikiri lakini kwa kuwa sikuona haja ya kumfikiri mtu huyo. Sasa hapo kuna vitu vinanichanganya Chiba,” akasigeza kiti chake mpaka pale kwenye kompyuta ya Chiba, “kwa nini baada ya mapinduzi kufanikiwa na kumweka madarakani huyo Sebutunva yeye ameingia tena msituni?” akauliza.



“Sasa hapa ndipo pa kufanyia kazi kwa sababu mchunguzi kasema tu kuwa ‘miezi michache baadae Banginyana na vijana wake wakarudi msituni…’ hii taarifa imeishia hivyo, sasa hapa mawili, kama kuna mtu alikuwa anachunguza taarifa hii basi aliuawa bila shaka au kwa nini aliacha? Mi najua CIA aking’ang’ania kitu hata kama ni miaka mia atakimaliza tu” Chiba akamaliza.

“Ndiyo imeishia hapo?”

“Yes Sir!” akajibu.

“Na we kaka yako Amata anakuharibu. Haya hebu tafuta ‘Black Page’ angalia mwaka huo ni nani aliingia kwenye hiyo kurasa nyeusi CIA,” Madam akamwambia Chiba.

Chiba akafunga lile faili kutoka katika mtandao nyeti wa usalama ambao umeunganisha karibu mashirika mengi ya kijasusi ikiwamo TSA.

“Yeah ni watu watatu tu! Mmoja Amerika kwa ugonjwa wa kansa, mwingine Afghanistan haijaandika alipigwa risasi na nani, ila imeandikwa tu alishambuliwa kwa risasi ndani ya gari yake, na huyu niiii… ok… ok huyu ni Afrika katika mlipuko uliotokea katika hoteli ya Kijelos katika mji mdogo wa Ntukuta…”

“…katika nchi ya Ndurata, sivyo?” Madam akadakia na kumalizia. Chiba alibaki akitikisa kichwa juu chini huku akisukuma kiti chake nyuma.



“Blamack Laideoff…” Chiba akataja jina hilo.

“Alikufa katika hoteli ya Kijelos, mwaka 1998 kwa bomu lililotegwa katika mkoba wa mwanamke aliyekuwa naye chumbani humo…” Madam S alieleza habari nyingi sana juu ya mtu huyo na zote hizo zilitoka kichwani hakuwa anasoma popote.

“Ebo! Madam umemeza mafaili, unatisha!” akampa sifa inayomstahili. Madam S akanyanyuka na kuchukua rimoti akawasha televisheni iliyokuwa imebandikwa ukutani. Aliitazama saa yake ilikuwa ni saa saba mchana.

‘…vikosi hivyo vya jeshi la Umoja wa Mataifa viliivamia kambi hiyo jioni ya jana na kuisambaratisha, lakini taarifa zinasema kuwa kiongozi wa waasi hao kanali Bensoir Banginyana hajapatikana.’

Ilikuwa sauti ya Charles Hilal ikitoa taarifa hiyo kupitia kituo cha BBC . Chiba na Madam S walikuwa macho kodo wakikodolea luninga hiyo.

“Dah! Kumbe wamemkosa!” Chiba akashangaa.

“Wamemkosa, unajua yule jamaa ni mpiganaji huwezi kumpata kilaini namna hiyo,” Madam S aliongezea huku akivuta kiti na kuketi.



“Kamanda lini anatua?” Chiba akauliza.

“Aaaa Kamanda anafanya biashara ya madini huko Ujerumani, hawezi kurudi mpaka apate mteja na soko la kudumu,” Madam akaeleza, “Vipi umemmiss?” akauliza.

“Hii ishu ya Ikulu inanitia uchungu sana, yaani tumedharaulika kiasi hiki? Tuingie kazini Mama tufunge mchezo,” Chiba alisema.

“Sikia Chiba, haya mambo hayana haja kuyashobokea, kazi wamepewa MI, nafikiri watafanya vizuri kwa sababu ni levo yao, siyo yetu. Unapenda sana mateso ee? Mi kwangu naona ni poa tu maana saa hizi vichwa vingekuwa vinatuzunguka, tunakimbizana huku na kule,” madam alieleza wakati huo akiuelekea mlango tayari kwa kuondoka.

“Ngoja nikwambie Madam, MI wao moja kwa moja wataanza kuwasaka hao jamaa, lakini watasahau kuchunguza hao watu wameingiaje Ikulu, kwa sababu ukichunguza wameingiaje ndipo utajua ni akaina nani, kwa mtazamo wangu mimi asilimia 60, adui yuko miongozi mwetu, na huyu adui si rahisi kumpata kama akili yako haifanyi kazi sawasawa,” Chiba akaunguruma huku akipigapiga meza yake kwa ngumi hafifu. Madam S alisimama mlangoni akimsikiliza Chiba kwa makini.



“Unachosema ni sahihi kabisa, lakini kila watu wana mbinu zao, sisi TSA tuna mbinu zetu na wao kama MI wana mbinu zao, hivyo nafikiri wataweza si unaona wanavyofanya vizuri kule Ngoko,” madam alimwambia Chiba.

“Ina maana Ngoko MI wamekwenda?”

“Chiba, Chiba, uko wapi wewe? Wakati majeshi ya SADC yamekwenda tuliombwa kupeleka baadhi ya wanajeshi katika kuunda jeshi hilo, kilichofanyika waliochanguliwa wote ni Military Intelligency, walikuwa wane, wakaenda kule lakini lengo lilikuwa pia wakafanye uchunguzi wa kujua hawa waasi wamejipanga vipi, kwa hiyo lilipokuja swala hili imekuwa rahisi kwani ramani yote ya Kusini mwa Ngoko tunayo,” Madam alieleza huku akifungua mlango tayari kutoka nje.

“Aisee!” Chiba akapiga kofi la mshangao, “Hii ndiyo nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania. Na hao waasi watauona moto, wamuulize Nduli Idd Amin Dada atawaambia kwa nini alikimbilia Saudia,” akamaliza na kugeuza kiti chake kuendelea na kazi zake.



***

UJERUMANI MASHARIKI



SIMU YA KAMANDA AMATA ikaita kwa vurugu pale ndani ya kijikapu kidogo kilichokuwa katika stuli ndogo pembeni tu mwa kitanda. Juu ya kitanda hicho kikubwa chenye kila aina ya starehe, Amata Ric alikuwa na mwanadada mrembo wakipeana raha za dunia.

“You are so sweet buddy!” mrembo alitoa sifa kwa Amata baada ya kushughulikiwa ipasavyo.

“Mmm kawaida tu,” akajibu huku mkono wake ukikifikia kile kikapu na kuinyakuwa ile simu, akaitazama kwenye kioo na kukunja sura kidogo, akatoka pale kitandani na kumwacha Precious akiwa anagalagala.

“Yes Sir!” akaitikia ile simu.

“Bwana Spark, yule mtu niliyekwambia anasema mnaweza kuonana leo jioni saa kumi ofisini kwake,” ilikuwa sauti ya Mc Donald iliyoongea Kijerumani safi.

“Ok, niko tayari, labda ni saa ngapi na ninakwendaje?” Amata akauliza.

“Nimewapa kadi yako ya biashara, watakupigia na kukujulisha jinsi gani mtaonana,” Mac Donald akamaliza.

“Ok, asante!” Amata akakta simu. Akavuta hatua chache na kuiweka ile mezani kisha akarudi kitandani na kumkumbatia yule binti wa kizungu, Precious Nancy Heibelghen, ndimi zao zikakutana na shughuli hiyuo ikaanza upya kwa amau nyingine. Wakiwa katikati ya mchezo ambapo kila mmoja alijikuta kwenye sayari yake anayoijua yeye, simu ile ya Amata ikaita tena kwa fujo, akataka kuipuuzia lakini akakumbuka kitu, akainyakuwa na kutazama, ilikuwa ‘private call’.



“Yes, hello!”

“Unaongea na Jirack Peterson, nusu saa ijayo kutoka sasa, teremka hapo nje ya hoteli yako, utamwona mtu mmoja mwenye nywele ndefu akisoma gazeti huku kaegemea gari aina ya Jeep Cherokee nyeusi, mfuate umwombe sigara, yeye atakuonesha kiberiti. Mfuate akulete tufanye biashara,” ile simu ikakatika.

Mwili wa Kamanda Amata ukasisimka kwa ujumbe huo, akakurupuka na kuliendea dirisha, akachukua darubini yake ndogo na kutazama nje lakini hakuona jipya. Akaingia bafuni na kujiswafi.

“Wapi unaenda mya black dog, uje tuendelee,” Precious aliendelea kumbembeleza Amata.

“Kuna kazi kidogo, tuonane jioni nitakupigia simu,” Amata akajibu wakati akijitupia koti lake mwilini, akavaa saa yake yenye uwezo wa kufanya mambo mengi, kunasa sauti kupiga picha. Ndani ya saa hiyo kulikuwa na bomu dogo lenye ukubwa wa kidonge cha pirton, chini yake kulikuwa na kijibomba kidogo ambaco kwa kutumia nguvu ya mkono kama utabetua kiganja kuja juu, kinatoa risasi ndogo kama kishale na sumu yake inaweza kukuua kwa dakika tatu tu, akaivaa na kuifunga. Kisha akachukua briefcase yake na kutoka taratibu huku akimwacha yule mwanamke bado akiwa bafuni.



Nje ya hoteli hiyo, shughuli mbalimbali zilikuwa zikiendelea, maji yaliyokuwa yakiruka huku na huko yaliwafanya watoto kufurahia hali hiyo, akavuta hatua chache na kumwona yule mtu kama alivyoelekezwa, akamwendea.

“Sigara tafadhali,” akamwambia, na yule mtu akamtazama Amata kisha akaingiza mkono mfukoni akatoa kiberiti cha gesi na kukiwasha, alipozima alifungua mlango wa ile Jeep na kumtaka Amata kuingia ndani, akafanya hivyo na mlango ukafungungwa.

“Mr. Spark, utanisamehe kwa hili, hutakiwi kujua mwenyeji wako anapatikana wapi,” yule jamaa akamvalisha sox nyeusi na kuuficha uso wako, watu wengine wawili zaidi wakaingia upande huu na huu naye akawa katikati.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





“Mr. Spark, utanisamehe kwa hili, hutakiwi kujua mwenyeji wako anapatikana wapi,” yule jamaa akamvalisha sox nyeusi na kuuficha uso wako, watu wengine wawili zaidi wakaingia upande huu na huu naye akawa katikati.

Gari iliendeshwa kwa takribani nusu saa mpaka ilipoegeshwa kwenye moja ya majumba makubwa nay a kifahari sana nje kabisa na mjini. Amata akahisi kuwa wamesimama getini kisha akjua kuwa gari imeegeshwa ndani ya kitu kama chumba kutokana na muungurumo wake kuwa na mwangwi, akilini mwake alikuwa akihesabu kona zote walizokuwa wakipind naye akapata kona tatu na alijaribu kuhesabu kila kona moja na nyingine walitembea dakika ngapi na kumbukumbu hiyi yote akaiweka kichwani. Akatshushwa garini na kushikwa mkono mpaka ndani kabisa, akahisi kaingizwa kwenye lifti kwani alihisi ile hali ya chombo hicho kikiwa kinaelekea juu. Wakamtoa na kumwongiza chumba kingine kisha akakalishwa kitini. Ukimya ukatawala ile sox bado ilikuwa kichwani mwake kabla ya kuondolewa na mtu aliyekuwa mbele yake.



Amata akafikicha macho na kujiweka sawa, akamtazama watu wawili walio mbele yake, mmoja alikuwa ameketi kitini na mwingine alikuwa amesimama ndani ya suti ya gharama sana, zaidi ya hapo ule ukumbi ulikuwa mkubwa sana usio na kitu ndani yake.

“Mr. Spark, karibu sana,” ilsikika sauti ya tule bwana aliyekuwa ameketi kitini, uso wake ulionekana ni mtu wa makamo huku madevu aliyoyafuga yalikizunguka kinywa chake, alikuwa ndani ya vazi la kawaida lakini ukiliangalia utajua tu gharama ya vazi hilo unaweza kununulia gari moja ya wagonjwa.

“Asante sana Mr…”

“Jirack Peterson!” akadakia na kumalizia yeye mwenyewe.

“Nina dakika kumi tu za kuzungumza, sasa twende kwenye lililotukutanisha,” yule bwana akamwambia Amata. Amata akafungua briefcase yake na kutoa sampuli moja ya alamasi akampatia yule bwana, naye akaipokea na kuwasha kijitochi chake kidogo, akaiangalia kwa makini, kisha akaiweka mezani na kutikisa kichwa.

“Hii ni sampuli hadimu sana, umeipata wapi?” akauliza.

“Mimi ni mfanya biashara, sampuli hii nimepata huko kwetu Afrika katika, katika machimbo ya Bagon,” akajibu.

“Bagon, Bagon, ha! Ha! Ha! Naijua sana sehemu hiyo. Sawa, mimi niko tayari kufanya biashara na wewe, lakini sijajua biashara yetu mi na wewe tunafanyaje. Kwa sababu hapa ninafanya biashara na watu wengi sana, biashara za cash, na pia zile za kubadilishana vitu, unanipa almasi name nakupa ndege,” Jirack alieleza. Amata akameza mate baada ya kuona koo limemkauka, akainua na glass ya maji akajijiminia kinywani.

“Sawa nimekuelewa bwana Jirack, nina mzigo huo na mwingine huu hapa,” Amata akatoa sampuli nyingine akampa. Jirack akaichuykua na kufanya vilevile, akaiangalia na kubaki kakodoa macho.



“Na hii, umepata wapi? Maana ni almasi hadimu sana, nina mtu mmoja tu anayeniuzian kutoka Afrika nay eye mgodi wa almasi hii ni wake,” Jirack akaeleza huku akiiweka mezani ile sampuli.

“Ni nani huwa anakuletea na anasema mgodi huo ni wake?” Amata akeleza.

“Aaa Mr. Spark biashara hizi zina usiri mkubwa sana, siwezi kukueleza juu ya mteja wangu, na wala simwezi kumweleza mwingine juu yako. Kitu ambacho tutafanya mimi na wewe, kwanza tuiache hii sampuli ya pili, na tufanye biashara ya hii sampuli ya kwanza. Kwa sababu hii sampuli ya pili inaweza kuleta matatizo,” Jirack akaeleza.

“Sawa Mr. Jirack, kwa kifupi sampuli hii ya pili nimeepata huko Afrika, Magharibi mwa Tanzania, kuna machimbo makubwa ya almasi,” Amata akaeleza.

“Ok, tutaizungumza hilo. Sasa hiyo sampuli ya kwanza ya Bagon niko tayari kufanya kazi na wewe, je utaileta mwenyewe au nitume vijana wangu waje kuichukua kadiri ya biashara yetu?”

“Utakaponipigia simu tutapanga biashara nzima,” Amata akamwambia Jirack. Vijana watatu wakatokezea mbele yake kupitia milango tofauti. Na mara hiyo mwanadada mmoja alitokea katika ukumbi ule mkubwa na moja kwa moja alimfikia Mr. Jirack na kumnong’oneza jambo. Kamanda Amata akaikutanisha mikono yake na sekunde hiyo hiyo alipiga picha takribani ishirini za yule mwanamke kwa kutumia saa yake pasi na mtu yeyote kujua. Wale vijana wakamfunika lile sox na kuondoka naye kwa mtindo uleule.



***



Kamanda Amata alitulia chumbani kwake peke yake, akaivua ile saa na kuchukuwa waya wa USB akaunganisha kisha akauchomeka kwenye simu yake kubwa na kupakua zile picha pamoja na sauti ya mazungumzo aliyokuwa akiirekodi kati yake na Mc Donald na kati yake na Jirack Peterson, alipohakikisha zimeingia zote sawasawa, akazituma kwa Chiba moja kwa moja ili kuhakikisha kila kitu kipo salama, kishapo akaweka vitu vyake vizuri tayari kwa kazi ya pili ya kibiashara.

Usiku wa siku hiyo ukamkuta Kamanda Amata ndani ya Cassino la kisasa katika moja ya hoteli kubwa hapo Berlini. Akiwa katikati ya kaunta akiendelea kupata kinywaji chake Couvosier alihisi kuguswa begani, alipogeuka akagongana macho na mwanadada aliyevalia gauni refu la kumetameta. Amata alimtazama mwanamke huyo, sura yake kama aliijua lakini hakukumbuka wapi ameiona.

“Habari ya jioni!” yule mwanamke akamsalimu Amata.

“Nzuri, u mwanmke mrembo sana,” akamsifia na kumwangalia kutoka juu mpaka chini, mkono wake mmoja ukampapasa kalio.

“Tafadhali, sio wa aina hiyo,” aksindikiza na sonyo refu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Oh samahani sana kwa hilo, karibu sana unatumia kinywaji gani?” akamwuliza lakini yule mwanamke hakujibu lolote badala yake alikuwa akimwangalia Amata bila hata ya kupepesa macho. Amata akashusha kinywaji chake na kumwangalia yule mwanadada wakati huohuo nyuma yake akahisi kushikwa mbavuni alipogeuka akutana na Precious Nancy.



“Yes my queen!” akamsalimu kwa namna hiyo, huku akimpa bilauri iliyo tupu na kummiminia kinywaji.

“Mr Spark!” yule mwanamke wa kwanza akaita kwa sauti ya upole.

“Sema mrembo, maana naona unaniangalia tu bila kusema lolote,”

“Nakupenda, u kijana mzuri mtanashati,” kisha akamwangalia tena kwa makini, “Njoo nje nina shida na wewe!” akaondoka.

Kamanda Amata akageuka kwa Precious Nancy, akamtazama kwa jicho la mahaba.

“Nisubiri mpenzi!” akamwambia.

“Mpenzi wako nani, unafikiri mi naweza kushare mapenzi na mwanamke mwingine! Na tunakwenda wote hukohuko,” Precious akawa mkali mpaka watu waliokuwa jirani kwenye kaunta ile walibaki kuwatazama. Kamanda Amata akaondoka na kukatisha katika makundi ya watu waliokuwa kwenye burudani mbalimbali, akatoka mlango mkubwa na kumkuta yule mwanamke akiwa amesimama ngazini.

“Jina lako tafadhali,” Amata akamwambia akiwa kasimama nyuma yake.

“Haina haja ya kujua jina langu, nimetoroka kuja kukwambia jambo moja tu…”

“Umetoroka wapi? Mbona sikuelewi. Kwanza we ni nani?” Amata akang’aka huku akimshika began a kumgeuza, mara hii wakawa wanatazamana. Yule mwanamke akateremka ngazi mpaka kwenye maegesho ya cassino hiyo, Amata naye akamfuata hukohuko.



“Sikia, wewe si Mr. Spark, wewe ni Amata Ric, taarifa zako zimefika katika mtandao wa baba yangu, na najua nini kitafuata kwani wao hawana mchezo katika kazi yao. Wewe ni spy umegundulika, nakuomba uondoke haraka sana kwani hata mimi nitakuwa mashakani ikigundulika nimekwambia hili,” yule mwanamke alipomaliza kusema hayo, akaondoka zake na kuingia kwenye moja ya gari za kifahari zilizokuwa zimeegeshwa hapo na kuondoka nayo.

“Shiiiiiit!” akajisemea kwa sauti ndogo huku akibana meno yake, akageuka kurudi kule kwenye casino, alipogeuka tu akagongana kikumbo na Precious Nancy. Kamanda haukuongea kitu isipokuwa kumwangalia tu mrembo yule mwenye macho ya buluu, alikuwa mazungu haswa!

“Hey my buddy! Vipi?” akaongea kwa lugha ya kiingereza.

“Fine fine,” akavuta mkono na kurudi naye ndani, mara hii akaenda kujiunga na kundi la wacheza kamali kwenye mchezo aina ya Poker.



3



BENSOIR BANGINYANA aliketi na makamanda wake wa juu kabisa katika kikosi chake cha X65. Hakuna ambaye aliruhusiwa kuongea mbele ya kanali huyo. Hakuna asiyemjua kwa ukatilia wake pindi tu unapombishia jambo ambalo yeye anaamini likiwa hivyo ndipo mafanikio yatakuja.

“Jamani hapa tuna jeshi lililojipanga haswa! Lazima tuwe makini na kila mmoja apange watu wake vyema!” aliwaambia makamanda wake waliokuwa wamemzunguka, “Tayari wameisambaratisha ngome yetu ya Mpumbutu, na najua ni wale vijana wawili watakuwa walifanya uchunguzi kuijua ilipo au watu wa Mpumbutu wamewaonesha,” akaongeza.

“Mkuu, nina uhakika watu wa Mpumbutu watakuwa wamewaonesha kambi ilipo, na kama ni huvyo, tupe ruhusa tukawafunze adabu,” kamanda mmoja akasema na wazo lake likaiutikiwa na Banginyana.

“Lakini tukumbuke kulinda migodi yetu, hii ndiyo migodi inayotoa almasi yenye thamani sana duniani, ni vipi kama watu hawa wakiivamia si tutakosa kila kitu!” kamanda mwingine akadakiaza maneno.

Banginyana akaonesha ishara ya kuwa wote wanyamaze, na walipotulia akainua simu yake ya mezani na kupiga mahala Fulani.



“Mkuu wa wakuu, ni jeshi gani lililopo huku msituni linatusumbua hivi, yaani ni kama mashetani kwa sababu ukiwasaka hawaonekanai walipo, wamesambaratisha ngome ya Mpumbutu na sasa nina wasiwasi wasije kufika migodini kule Lugombesi maana si mbali kutokam hapa…” aliongea kwenye simu.

“Kwanini mnashindwa kuwakabili nanyi ni magorilla mliobobea? Kanali Banginyana, uwezo wako wa upiganaji unauficha wapi?...” sauti ya upande wa pili ikamwambia. Ukimya ukatawala kati ya watu hao kisha Banginyana akajibu.

“Sikia Mkuu wa wakuu, kiukweli hapa tunahitaji silaha za kisasa sana kuweza kuwakabili hawa wendawazimu, tukiwa na silaha kama zao tutawadhibiti vyema na tutafutilia mbali uwepo wao, kwanza ni nani aliyewatuma wakati kila mmoja tuna mkataba naye?”

“Sikiliza Banginyana, hilo usiliwaze, hao wanajeshi sio wa Umoja wa Mataifa, ni kutoka Jeshi la Tanzania. Sasa naomba uje huku Nduruta ili tuweke mambo sawa, askari wote waambie wahakikishe ulinzi wa eneo,” ile sauti ya upande wa pili ikamwelekeza, kisha simu ikakatika.

Banginyana akawaangalia watu wake, “Sikilizeni, nakwenda Nduruta nitarudi ndani ya saa kumi tu, hivyo hakikisheni usalama wa eneo nyeti, na kikosi kimoja kiende Mpumbutu kikawatie adabu watu wa pale,” akamaliza kusema na kunyanyuka, vijana wake akampigia saluti za ukakamavu wakati kanali huyo akitoka ndani ya jengo hilo huku mlinzi wake akimsindikiza.



NDURUTA



KATIKA MAKAO MAKUU ya nchi ya Nduruta, kikao cha watu wawili tu kilikuwa kikiendelea. Rais wa Nduruta Brigedia Kadanse Sebutunva na Kanali Bensoir Banginyana walikutana kwenye chumba Fulani ndani ya jengo hilo, Banginyana aliingia hapo kwa siri na hakuna hata mtu mmoja aliyembaini.

“Mkuu, tunahitaji silaha nzito sana!” Banginyana akamwambia Rais Sebutunva.

“Usijali, wiki hii natakiwa nipeleke madini kule kwa wale matajiri wetu ili waendelee kutupatia pesa kwa ajili ya operesheni hii, unajua nchi yetu sasa hivi ni tajiri sana japokuwa ni kanchi kadogo tofauti na hiyo Tanzania inayojidai kimbelembele. Kwanza swala la huko Tanzania niachie mimi, najua cha kufanya na mpaka watakapokuja kugundua tayari nitakuwa nimeshawamaliza the! the! the! the!” rais aliongea na kuangusha cheko.

“Mimi nilifikiri tufanye juu chini tuwazibe midomo!”

“Aaaaaaa! Hawazibiki, kwanza Rais wao ni jeuri si unajua kuwa alikuwa mwanajeshi pia hivyo ana ile jeuri ya kijeshi ijapokuwa yeye aliishia kwenye vyeo vya chinichini. Mimi ni Brigedia na kule Tanzania nimeshapandikiza watu wangu katika kila idara nyeti, hivyo ile nchi yote iko hapa. Lakini nayamezea mate sana madini yao, yaani ipo siku nitayatia mkononi,” Rais Sebutunva akamwambia Banginyana.



“Sasa mkuu wa wakuu, unajua ile ndoto yako ya kuinua himaya yako ya Paramado itatimia kama tukiyapata na haya machimbo ya huko Tanzania. Kama vipi tugawe wale gorilla wengine waende huku wakavamie na kuanza kazi kama tulivyofanya huko Mpumbutu,” Banginyana alipendekeza.

“Aaaaah! Banginyana, hiyo siyo mbinu hata kidogo. Katika swala la usalama Tanzania usiiguse, wale inabidi kuwavamia kidiplomasia tu, kuweka mapandikizi yetu kama ambavyo nimefanya. Tutayapata yale madini kwa kuwekeza na wao kuwaminya, lakinikwa kutumia mtutu pale sahau, usione wapole vile, wabaya sana wale. Tuyaache hayo! Kesho kutwa mzigo wa almasi unatakiwa uende Amerika na Ulaya kwa wale wateja wetu, yule mteja wa Ujerumani atatupatia silaha za kisasa badala ya pesa, hizo zikija ndiyo utakuwa mwisho wa hao wanaojiita wanajeshi wa nini sijui, kwa hiyo kapange watu wako waweke ulinzi. Wewe utatakiwa uende mwenyewe Ujerumani ili ukaone vifaa vinavyofaa kwa kazi yetu ya msituni, nazani nimeeleweka sivyo?” Rais Sebutunva alimaliza, wakakubaliana na kuweka mipango sawa, kisha banginyana akarudi msituni kwa njia ileile ailiyokuja nayo.



DAR ES SALAAM



RAIS WA TANZANIA, mheshimiwa Robert Sekawa alikuwa kimya akisikiliza taarifa za kiintelijensia kutoka kwa kiongozi wa kitengo cha MI kutoka Jeshi la Wananchi.

“Tafiti zetu zinaonesha kuwa watu waliovamia hapa na kufanya unyama ule ni watu kutoka Nduruta kwa kuwa mpaka sasa ni rais wa nchi hiyo ambaye hatuna uhusino mzuri kidiplomasia,” yule kijana aliyevaa kombati zilizochafuka kwa vyeo alikuwa akimwambia rais Sekawa. Umakini wa rais huyo katika kusikiliza ulimkumbusha ile simu aliyopigiwa siku tatu zilizopita.

“Umenikumbusha! Hilo usemalo lina ukweli, juzi nilipigiwa simu na watu nisiowajua wakidai kuwa nisichukue hatua yoyote ya kumtafuta mke wangu isipokuwa niondoe majeshi kule Kusini mwa Ngoko,” rais akaeleza.

“Nafikiri hapo utathibitisha uchunguzi wetu wa awali, kwa hiyo bila shaka Nduruta ndiyo adui yetu mkubwa,” yule mwanajeshi kijana akaeleza.

“Ok, bila shaka hawa waasi kule Kusini mwa Ngoko ni watu wake, au ninyi mnaonaje?” akauliza.

“Kwa simu uliyopigiwa mheshimiwa ambayo sasa inabidi tuifanyie kazi kabla hatujasema ndiyo au hapana. Kama hiyo simu tukiipata na kuisikia upya bila shaka tutasema ndiyo wale waasi ni watu wake,” yule kijana aliongeza. Rais Robert Sekawa alikunja sura na kuonekana kuwa na hasira za wazi kabisa.



“Endeleeni kuchunguza na mkibaini ni wao waliyofanya haya, lazima tuwavamie kijeshi na tutahakikisha tunafagia takataka zote, asanteni sana. Mkuu wa majeshi naomba uwaongezee nguvu vijana kule Kusini mwa Ngoko kwa kuwapelekea silaha nzito, naona sasa kazi inaanza,” rais Sekawa akamaliza na kuwapa mikono kisha wakaagana naye akabaki peke yake ofisini. Macho yake yalionekana wazi kushikwa na hasira ya wazi, alivuta moja ya faili lake na kulipekua pekua kurasa hii na ile, akashika ukurasa fulani na kuutazama vizuri. Juu kabisa ya ukurasa huo kuliandikwa The DEAD Line kisha ukapigiwa mstari mwekundu pale chini, akasoma kurasa ile na kuchukua kalamu yake, akataka kuandika kitu fulani, alipoanza tu mlango wake ukafunguliwa, akalifunga lile faili na kuliweka kwenye sefu ya chini kabisa akalifungia humo.

“Mheshimiwa kuna ugeni unakusubili kama ilivyo ratiba yako ya leo!” kiongozi wa usalama wa rais alimpa taarifa hiyo na kumruhusu kupita mlangoni. Katika sebue kubwa iliyopangwa samani zake vyema na nyingine zilionekana kuwa ni mpya ambazo ziliwekwa badala ya zile nyingine kuvunjika. Wale wageni walisimama mara tu walipomuona kiongozi huyo akiingia katika sebule hiyo pana akiongozana na watu wengine wawili akiwamo katibu na mwandishi wake. Wakasimama na kupeana mikono huku wakimpa pole kwa kila lililotokea, wageni hao walikuwa maofisa wakubwa wa kibalozi. Mmoja alikuwa ni balozi kutoka Umoja wan chi za Ulaya akisindikizwa na msaidizi wake, lengo na madhumuni ya safari yao ilikuwa ni kutoa salamu za pole kwa serikali ya Tanzania baada ya tukio hilo lililoitwa la kigaidi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Pamoja na hayo yote, tuliona tukupe msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nje, tulifikiri FBI wangekusaidia sana katika hili,” yule balozi alimwambia Rais Sekawa.

“Nashukuru, lakini ni mapema mno kuamua hilo, vyombo vyetu viko kazini na vinaendelea vyema kabisa katika kazi zao,” alijibu. Mazungumzo mengine yakaendelea na kukubaliana kuwa itakapofika muda wa kuhitaji msaada huo basi wangewapa taarifa hiyo. Lakini hata hivyo ofisi ya balozi huyo iliaahidi kuleta wanausalama kadhaa kwa ajili ya uchunguzi wa hapa na pale. Ijapokuwa ilikuwa ngumu kwa serikali kukubali lakini libidi kuwa hivyo.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog