Simulizi : Mimi Na Rais (The President And I)
Sehemu Ya Pili (2)
“Bungeni Spika ni chama gani, na chama gani kina wabunge wengi”? Costa alihoji.
“Chama cha Ukombozi Stanza Mh. Rais” Kinyamagoha alijibu kwa upole.
Rais Costa aliendelea kuhoji kwa ghadhabu na kuonesha ukubwa wake ndani ya taifa la Stanza.
“Nani Mwenyekiti wa hicho chama Kinya?”, Rais Costa aliuliza.
“Ni wewe muheshimiwa”, Kinyamagoha alijibu tena kwa kutetemeka. Alishahisi kuwa Rais angeweza kumvua nafasi yake wakati uleule.
“Sasa wewe unavyoniambia unalitafakari hili una maanisha nini? Hii ni ishara tosha kuwa wewe ndio hutaki. Haya toka”, Rais Costa alimfukuza Kinyamagoha atoke.
“Mh. Rais nilikuwa naomba…….”, “Nimesema toka”, Rais Costa alimkatiza Kinyamagoha kwa hasira. Kinyamagoha aliondoka.
Rais Costa alibaki kimya akiwa amevimba kwa hasira kwa dakika kadhaa.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Mh. Rais nina wazo”, Gideon mshauri na mpambe wa karibu wa Rais alidakia. Rais Costa alimwangalia Gideon machoni kuashiria kuwa anamsikiliza anachotaka kumwambia. Gideoni alijua haswa pa kujipatia sifa mbele ya Rais Costa. Alikuwa ni kama mkoba wake, hakumwacha kila alipoelekea. Alimwamini sana.
“Kuna watu wengi wenye uwezo sana wa kukusaidia hii kazi”, Gideon alianza kumshauri Rais.
“Kama nani”, Rais Costa alihoji.
“Yule binti, Katibu tawala wa Jimbo la Kichumbi, anaitwa Ketina nadhani angeweza sana kukusaidia hapa. Kwanza ni msomi wa sheria na ni mchapakazi kwelikweli”, Gideoni alimaliza.
Rais Costa alionekana kushtuka kusikia ushauri ule hasa ukizingatia Ketina ni kimada wake na alifanya siri kubwa watu wasijue. Alianza kuhisi kuwa Gideoni ameshajua nini? Ukweli ni kuwa Gideon alikuwa akicheza na akili ya Rais Costa. Alishapenyezewa taarifa na mmoja wa vijana wa usalama wanaotumiwa na Rais Costa kuwakutanisha na Ketina na hivyo Gideon aliamua atumie nafasi hiyo kuzidi kujipendekeza kwa Rais Costa.
“Ketina bado hajakomaa. Atapata tabu kwenye kufanya lobbying ya wabunge, pia hajajua mambo mengi ya kiutawala. Ngoja akomae kwanza”, Rais costa alimjibu Gideon kiutu uzima.
“Kwani ni nani Rais? Spika wa bunge ni chama gani na chama gani kina wabunge wengi ndani ya bunge? Nani mwenyekiti wa chama hicho?” Gideoni alirudia maswali yote ambayo Rais Costa alimuhoji Kinyamagoha. Baada ya maswali hayo Rais Costa alibaki kimya.
“Sawa nipe muda”, Rais Costa alimjibu Gideon kwa ufupi.
**************************************
Mchana wa siku hiyo Rais Costa alikutana na Waziri wake wa Fedha ndugu Aidan Tamara akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato na Makusanyo ya Taifa.
Aliwapa maagizo kuwa sasa waanze kukusanya kodi kwa nguvu. Wahahakikishe kila mtu anayefanya chochote kinachomwingizia kipato analipa kodi. Haijalishi ndio anaanza ama biashara imeshakua, kama anaanza alipe kodi kwanza ndio aanzishe biashara. Alitaka kodi kwa nguvu na kuwawekea lengo kubwa la makusanyo kuliko kawaida.
Katika kikao kile hakuna aliehoji, wote waliitikia na kuahidi utii na utekelezaji. Waliondoka.
Gideon alifurahi na kumwambia Rais sasa ategemee kilio kila kona ya nchi, asubirie kwa miezi michache kisha ajitokeze kukemea na kuagiza utaratibu mpya wa ukusanywaji wa kodi. Ni kwa namna hiyo atakuwa ametengeneza tatizo na kulitatua na hivyo kuzidi kupendwa na wananchi na kumwimbia nyimbo za ‘atawale milele’
Jioni, Macha aliingia akiwa ameambatana na Waziri wa Polisi na Magereza.
“Mnajua nilichowaitia right?’’ Rais Costa alikuwa amechoka na hakutaka kupoteza muda.
“Ndio Mkuu. Mimi nadhani tumpoteze kabisa huyu kijana”, Kirondori Rugara, Waziri wa Polisi na Magereza alijibu kwa pupa.
Rais Costa alikuwa akiwauliza wamefikia wapi na mpango alioagiza wa kuhakikisha kijana na kiongozi mkuu wa chama cha upinzani ndugu Julius Kibwe anadhibitiwa kwani anaonekana ataleta kelele nyingi kwenye muswada anaotaka upelekwe bungeni wa yeye kubadilisha umri wa kugombea uRais kutoka miaka 40 mpaka kuwa miaka 55.
“Tumpoteze vipi Kirondori? Acha kuwaza kama kichaa bwana”, Stanley Macha alijikuta akimkatiza kirondori kwa hasira.
Macha akiwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa alikuwa katika mipango ya siri na Joe. Lakini aliifanya katika weledi uliokithiri. Alichukizwa na jibu la Kirondori kuwa Julius Kibwe apotezwe. Kupotezwa ina maana auawe. Hakuwa tayari, hakutaka. Alijua fika Kirondori alijibu vile ili kujipendekeza kwa Rais na si vinginevyo.
“Mh. Rais mimi nilikuwa nawaza tofauti kwa sababu tukianza mambo ya kupotezana hapa tutawapoteza wangapi? Suala hili mbona ni dogo sana na huyu bado hajafikia kuwa tishio la kupoteza uhai wake.
Halafu nafikiri hawa jamaa wa magharibi wanatufuatilia kila hatua na wanajua kinachoendelea, kumpoteza kwa namna yoyote ile ni kukaribisha kufuatiliwa na kubughudhiwa na mataifa ya magharibi kila siku. Tusije kuishia kupunguza wahisani kabla bajeti yetu haijajitegemea kikamilifu’’, Macha alianza kuelezea kwa utofauti jinsi ya kukabiliana na Kibwe badala ya kummaliza kama ilivyoshauriwa.
‘’Ninafikiri kuwa kwasababu chama hiki hakina wabunge wengi, wabunge 100 kati ya 500 ni wachahe sana na hivyo sehemu kubwa ya mapato yao hutegemea misaada ya wahisani na hasa matajiri wawili wakubwa hapa nchini, ninapendekeza tuwabane hawa matajiri wakate pesa zao kwake.
Hatua hii itampunguza nguvu ya kuendesha chama chake na pia safari zake mikoani zitapungua. Hatua ya pili, tuongee na wamiliki wawili wa hivi vituo vya redio kuzuia mahojiano nae ama habari zake kuziandika katika hali ambayo hazitakuwa na hamasa. Hii ni njia rahisi sana ya kumpunguza nguvu”, Stanley Macha alishauri.
“Unajua ana wafuasi wangapi kwenye mitandao yake ya kijamii au unasema tu?”, Kirondori alihoji kwa haraka.
“Ulishawahi lini kuona Stanza watu wakafuatilia mambo kwa umakini huko kwenye mitandao? Kule wanapiga kelele tu yanaishia kule, Stanza mitandao ya kijamii bado haijawa tishio, wanapiga kelele tu.
Hata hivyo hao wafuasi ni wa hapa mjini hawana madhara hata kidogo. Mh. Rais hii kazi niachie mimi nitamdhibiti bila madhara kabisa. Labda Kirondori awe anamshikilia kila mara na kumpeleka mahakamani kwa kauli zake ama vikao visivyo halali, awe anashinda mahakamani Januari mpaka Disemba na kukosa muda wa kupambana na serikali. Wananchi watamsahau tu”, Macha alimalizia.
Rais Costa alionekana kukubaliana na Macha kwanza kwasababu ya uaminifu alionao kwake katika kuhakikisha usalama wake lakini pia kwa njia aliyopendekeza ambayo haitakuwa na utata hata kwa jumuiya za kimataifa. Kikao kilimalizika.
************************************
Siku ile ilikuwa ni ya msisimko mkubwa kwa Joe na wenzake. Ni siku ambayo walikuwa wanakutana na Rais Kim mwenyewe na ndipo hapo Rais Kim angesaini hati ya kukubali ama kukataa maombi yao na wao kundoka nayo kuelekea Stanza. Ilikuwa ni siku ya ama warudi Stanza kishujaa au kiunyonge. Joe alipenda la kwanza. Asingependa kabisa arudi na majibu kuwa imeshindikana.
Timu aliyoongozana nayo haikumuangusha, ilikuwa ni ya vijana Hodari kwelikweli. Katika mawazo yake wakiwa wanaelekea Upande wa mashariki mwa makazi namba 55, makazi rasmi ya Rais Kim na upande ambao ndio hasa zilipo ofisi zake, moyo wa Joe ulijawa furaha sana. Alijiona mshindi na mtu aliefikia Kilele cha mafanikio katika Nyanja ya kidiplomasia. Walifika wakaingia na Rais Kim akawapokea.
“???? ?? ?????? ?? ?????. ??? ????? ???? ???????. ?? ? ??? ??? ?? ??? ??? ?? ? ??? ? ??? ?????. ?? ? ??. En? ????? ?? ?? ?? ?? ? ????”
himdeuljiman joh-eun tolon-eulhaessdaneun mal-eul deul-eossseubnida. geos-eun ijeongpyoija yeogsajeog-in iyagiyeossseubnida. chuga hal naeyong-i eobsjiman modeun bubun-i uliga dong-ui han bubun-e seo issneunji hwag-inhabsida. neomu jal haess-eo. Eneun ap-euloganeun gil-e daehae gyesog yeonlag hal geos-ibnida.
(Nimetaarifiwa kuwa mlikuwa na majadiliano magumu lakini mazuri. Majadiliano haya ni ya kihistoria na muhimu sana kwa pande zote mbili. Tunachotakiwa kuhakikisha ni kila upande kuona namna gani unakidhi matakwa ya mwenzake vyema. Hivyo niwatakieni heri na En ataendelea kuwasiliana nanyi kwa yote yanayofuata). Rais Kim alimaliza kuongea huku akimalizia kuweka sahihi kwenye nyaraka zile ziliandikwa vyema kabisa yote waliyojadiliana na kukubaliana kati ya ujumbe wa Joe na Waziri En.
“Thank you, Mr. President,” (Asante Mh. Rais), baada ya kupata tafsiri Joe alishukuru.
Ilikuwa ni hatua kubwa sana katika utumishi wa Joe. Habibu na Pius walionekana kutabasamu kwa kulifanikisha jambo lile. Kila mmoja alikuwa na mchango mkubwa katika makubaliano yale.
Joe asingekubali vifaa vya nyuklia vitengenezwe Stanza kama sio Pius kuwashirikisha nguvu ya Korea Kaskazini kijeshi na kuwahakikishia kuwa watalindwa. Habibu nae taarifa zake na umakini na uhodari wa kuhoji masuala uliwafungua macho kwa namna fulani Pius na Joe. Yeye Joe kama kiungo mchezeshaji alikuwa na kazi moja tu ya kuchuja na kuamua. Hakika walipongezana na baada ya dakika kadhaa waliagana na Rais Kim ili waondoke.
Wakiwa wanatoka jambo moja lilimshangaza Joe alivutwa nyuma na kurudishwa ndani ya ofisi alimokuwa Rais Kim na wenzake kubakia nje.
“If president Costa declines our offer, I will want you to make it happen in one way or another. Can I count on you? (Kama Rais Costa akikataa matakwa yetu nitakuhitaji wewe uyafanikishe kwa njia moja au nyingine. Naweza kukutegemea?). Rais Kim alimwambia Joe.
Joe alikosa la kujibu alipozungusha macho alikuta watu wote waliokuwa pale ofisini mwa Rais Kim wanamtazama yeye.
“Can I?” (Ninaweza kukutegemea?), Rais Kim alihoji tena. Joe hakujua ajibu nini.
*****************************************
“Kimweri, umeshapata nafasi ya kuwasiliana na kina Joe?”, Rais Costa alimuliza Kimweri balozi wa Stanza huko Beijing China.
“Hapana Mkuu lakini kutokana na ratiba watawasili leo saa kumi na moja jioni na ndege ya Air Koryo ile ile waliyoondoka nayo”. Kimweri alimjibu Rais Costa walipokuwa kwenye mazungumzo yao ya kufuatilia ujumbe wa Joe na wenzake.
Rais Costa alikuwa akimtumia Kimweri kufuatilia mazungumzo ya Joe na wenzake pindi wanapokuwa kwenye ardhi ya China. Alijua fika yapo watakayokuwa wanazungumza na japo hawezi yapata yote lakini machache yanaweza kumsaidia kuunganisha nukta na kujua kama Joe hana mpango mwingine ambao hauna maslahi mema kwake.
“Yule kijana umeshampanga hapo kiwanjani? Nataka wakati huu isishindikane”, Rais Costa alisisitiza.
“Sawa Mtukufu Rais”, Kimweri alijibu kwa kuinamisha kichwa japo yeye yupo China na Rais Costa yupo Stanza.
Kijana wa kiVietinam alishawekwa tayari kufatilia mienendo yote ya Joe na wenzake. Wakati huu wakitumia teknolojia ya MCC3G-R Voice ampliefier.
Hii ni teknolojia ya hali ya juu kabisa kutoka Vietnam ambayo mtu huweza kurekodiwa mazungumzo yake kwa anayerekodi kukaa mbali na kuweza kuelekeza kifaa hicho mahali anayerokodiwa alipo, kisha kifaa hicho huweza kuweka uzio wa mawimbi sauti katika eneo litakaloamuliwa na anaetaka kurekodi. Baada ya hapo chochote kitakachozungumzwa ndani ya uzio ule uliowekwa kitanaswa kutokea mbali na kisha sauti ile kukuzwa.
Kinachofanyika ni kuwa mtu yule anayerekodiwa akitembea ama kuhama ni shurti kifaa kile kigeuzwe ili mtu anayerekodiwa abakie ndani ya uzio. Ubora zaidi wa kifaa hiki ni kuwa hata kama mtu yupo ndani ya jengo ama yupo ndani ya uzio, bado sauti itanaswa na cha zaidi ni kuwa unaweza kuzipa sauti majina. Mfano, kama una hakika sauti hii ni ya mtu fulani basi unaipa jina na kuhifadhi ndani ya hiki kifaa.
Ikitokea siku yoyote unataka kunasa Sauti ya huyo mtu kama yupo ndani ya jengo hivyo haonekani na una hakika kama yupo basi utakachotakiwa kufanya ni kutengeneza uzio kisha kuanza kunasa sauti za watu walioko huko ndani. Kama huyo mtu yupo na akazungumza basi kifaa kile kitakupa ishara kuwa huyu anaezungumza ni mtu fulani kutokana na lile jina ulilotumia kuhifadhia.
Teknolojia hii haihitaji mtu kutuma kifaa chochote kuwasogelea wale unaotakiwa kuwarekodi unachotakiwa kujua ni wapo eneo gani tu basi na kisha kukaa umbali usiozidi mita 500 kutokea mahali walipo.
Wakati huu Rais Costa alihakikisha hawakosi kuwasikia kina Joe. Alishapanga pia kijana huyo aje Stanza kumfatilia Joe kwa miezi sita mfululizo ndipo amwamini.
************************************
“Ulirudi kuongea nini na Rais Kim Joe?”, Alikuwa ni Pius akimuuliza Joe kwa kumnong’oneza mara tu alipotoka kwenye ofisi ya Rais Kim aliporudishwa mara ya pili.
“Nitawaambia Pius”, Joe aijibu kifupi.
Walitembea kwenye korido za Ryongsong wakiongozwa na Waziri En Ki. Walitoka na kuingia kwenye magari yaliyoandaliwa kuwapeleka uwanja wa ndege.
Wakiwa ndani ya magari huku viongozi wengine wa Korea wakiwa wamesimama kwenye varanda kubwa mbele ya jengo lile maridadi walipiga ishara ya saluti kuonyesha kuwaaga wageni wao kutoka Stanza. Joe na wenzake nao walifanya hivyo na msafara ulianza safari.
Jinsi walivyokaa ni vile vile kama walivyokuja. Gari moja akiwa Waziri En na Joe, gari la pili alipanda Habibu na Pius. Magari mawili yaliyobaki la mbele na nyuma yalikuwa ni ya ulinzi na usindikizaji tu.
“Habibu, Joe alirudi kuambiwa nini?”, Pius alimuuliza Habibu.
“Sasa mimi nitajuaje Pius?” Habibu alijibu kiufupi.
“Tumekuja wote kama ujumbe mmoja kwa nini alirudishwa mwenyewe? Huoni kama kuna jambo tunafichwa hapa Habibu?” Pius alihoji tena. Alihoji huku akijikuna kidevu na kuangalia dirishani upande wake badala ya kumwangalia Habibu.
“Pius kwani ulipomuuliza Joe pale si alisema atatuambia? Sasa wewe haraka ya nini? Au umeanza kuwa na mashaka nae?” Habibu alimuuliza Pius. Pius alikaa kimya.
Msafara uliwasili uwanja wa ndege Sunan Pyongyang. Waziri En aliwaongoza kina Joe moja kwa mmoja mpaka kwenye ndege ndogo iitwayo Chammae-5. Hii ni moja ya ndege wanazotumia viongozi tu wa serikali ya Korea Kaskazini kwa safari maalumu. Ipo kwenye mnyororo wa ndege maalum za Rais Kim ikiongozwa na ile ya Chammae-1 ambayo ndio haswa ndege ya Rais Kim. Ndege hizi ni zao la ndege za kisovieti za Jetliner Ilyushin Il-62M.
Walipofika waliagana na kuingia kwenye ndege. Pius na Habibu walionekana kushangaa heshima ile kubwa waliyopewa. Walikuwa wakijua wanarudi na ile ndege waliokuja nayo na kumbe sivyo wanarudishwa na moja ya ndege maalum za Rais. Joe alikuwa mkimya na ndege iliacha ardhi.
Wakiwa angani Pius alikuwa wa kwanza kuuliza kulikoni na nini Joe aliongea na Rais baada ya kurudishwa ndani na wao kuachwa nje.
“Pius, kwanza lazima utambue mimi ni kiongozi wako katika msafara huu sawa kijana? Hivyo kuna mambo naweza ambiwa kwa msisitizo mimi kama kiongozi.
Kimsingi Rais Kim alitaka kunishukuru tena kwa niaba yenu kwa mazungumzo mazuri tuliyoyafanya. Amewapongeza ninyi na kusema ni hazina ya taifa la Stanza na hivyo amenishauri kuhakikisha Rais Costa anawathamini.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Pius, umeonyesha uwezo mkubwa sana wa masuala ya usalama na ameshangaa kuwa tuna vijana maridadi namna hii. Habibu, Waziri En mwenyewe amekiri kuwa una uelewa mpana na alinitania kuniambia kwanini kijana kama wewe usiwe Katibu mkuu wa Umoja wa Taifa badala ya wale waliokaa pale kuitumikia Marekani. Wamefurahi sana”.
Joe alimaliza kuwataarifu na kumfanya Habibu atabasamu na kujisikia vizuri sana. Kwa upande wa Pius alitabasamu kinafiki. Kwa taaluma yake ya usalama alisoma uso wa Joe kwa umakini na alitambua kuna maneno yamefichwa ambayo alitambua wazi Joe hatataka kumwambia. Alikwazika sana.
“Ndege hii itatua uwanja ule wa Kimataifa wa Beiijing tuliopandia wakati tunakuja ama uwanja tofauti?” Pius alihoji.
“Uwanja tofauti. Sasa hivi tutatua uwanja mdogo wa Shenyang kisha Korea wametuandalia usafiri kutupeleka kwenye ubalozi wetu”, Joe alijibu. Jibu hili lilizidi kumwacha Pius mwenye maswali.
Pius kwa taaluma yake ya usalama na intelijensia alikwiva kwelikweli. Alijua kusoma mwisho kutokea mwanzo, ilikuwa ni vigumu sana kumkwepa hasa akitaka kujua jambo na alijua kuunganisha nukta kwelikweli. Labda hiyo ndiyo sifa iliyomfanya aaminiwe na kupewa nafasi kubwa kabisa jeshini kama ile ya Unadhimu na Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia cha Jeshi la watu wa Stanza.
“Kwa hiyo vipi kuhusu balozi Kimweri ana taarifa? Maana atakuwa na yeye ameandaa utaratibu wa kutupokea kule uwaja mwingine”, Pius alihoji.
“Tukifika tutamtaarifu” Joe alijibu kiufupi.
“Joe mbali ya shauku ya kutaka kufika na kumtumia Macha yale maneno ya siri, sasa tuambie nani mwingine anahusika na mipango hii itatekelezwaje. Yaani nataka nipate picha kamili”, Habibu alidakia mazungumzo.
“Haya sasa nitawaambia mpango mzima na niseme tu baada ya kuongea hapa tutapofika China hatutazungumza lolote mpaka tutakapofika Stanza. Na hata tukifika kule tutakuwa tukiendelea na utekelezaji na mazungumzo mengine tukiwa wote yaani mimi na ninyi Macha na huyu nitakaewatajia hapa tutayafanya kwa maelekezo maalum.
Nirudie, ninaamini hapa ni Sehemu salama maana tunatakiwa tuwe waangalifu kwa sababu najua tunafatiliwa.” Joe aliwaweka sawa kwanza.
Habibu na Pius walikaa kwa shauku kusubiri ni nini wangeambiwa kuhusu mpango ule mahsusi.
************************
Rais Costa Uso Kwa Uso Na Askofu Begere.Pius Atoweka Uwanja Wa Ndege Shenyang
“Mh.Rais, Askofu Begere ameomba miadi na wewe aje akuone”, Alikuwa ni Chaurembo Chalamila, Waziri wa Ardhi akimtaarifu Rais Costa juu ya ombi la Askofu Damian Begere kuomba kuonana nae kwa mazungumzo.
Kwa haraka Rais aliamini kuwa Begere anakuja kujisalimisha kwake na kuacha kumshambulia yeye na serikali yake. Rais Costa alifurahi ingawa alificha hilo usoni mwake.
“Anataka kuniambia nini? Au anataka kunihubiria na mimi kuhusu utawala bora?”. Rais Costa alijibu kwa dharau huku akiendelea kusoma makabrasha yaliyokuwa mezani kwake.
“Hapana anataka kujadiliana na wewe masuala mbalimbali hasa yanayohusu miradi yake ambayo umeikwamisha”, Waziri Chaurembo alijibu.
“Ha ha ha ha! Kwahivyo sasa ndio anatambua kuwa Rais wa nchi hii ni mimi na sio yeye? Mwambie sawa aje tujadiliane kesho saa nne asubuhi”, Rais Costa alimjibu Waziri Chaurembo.
************************************
Ilikuwa siku ya Jumatano, ilipofika saa nne kamili asubuhi tayari Rais Costa alikuwa ofisini kwake akisubiria kuja kuitwa ili akaonane na Askofu Begere. Aliendelea kusoma taarifa mbalimbali anazowekewa mezani na watu wa usalama na wasaidizi wake.
Rais Costa alikuwa akipenda sana kusoma taarifa. Ilikuwa ni ngumu awekewe taarifa na aache kuisoma. Katika vitu watu wa Ikulu wanaheshimu ni taarifa wanazoweka mezani kwa Rais. Ilikuwa ni rahisi sana mtu kupenyeza jambo lake. Ni kuhakikisha tu linafika kwenye meza ya Rais basi ni lazima angelisoma na kulifuatilia.
Akiwa anaendelea kusoma huku akinywa Kahawa mlango ulifunguliwa na kwa mshangao yeye akijua anaitwa ili aelekee chumba cha kukutania na askofu Begere badala yake aliingia Ketina.
“Mh. Rais Shikamoo”, Ketina, kimada wa Rais alisalimia kwa adabu ya kinafiki ili wasaidizi waliopo nje ya ofisi ya Rais wasielewe kinachoendelea.
“Ketina umekuja kufanya nini?” Rais Costa alihoji akiwa amestaajabu ujio ule bila mwaliko.
“Mh. Rais mimi si mteule wako? Katibu tawala wa Jimbo au? Nimeleta taarifa kwa boss wangu”, Ketina nae alijibu huku akiketi kwenye kiti kilicho mbele ya meza ya Rais.
“Nina kikao sasa na ‘Bishop’ Begere, utanisubiri pale eneo la wageni mpaka nikitoka”. Rais Costa alimwambia Ketina.
“Bishop ndio atasubiri sio mimi”, Ketina alianza kuonesha ukaidi kama kawaida yake.
Wakati wakijibizana mara aliingia tena msaidizi na kumtaarifu Rais Costa kuwa Askofu Begere yupo tayari kuonana nae. Rais Costa alianza kutoka na kumwacha Ketina pale ofisini kwake akiwa amekaa.
Rais alipotoka tu waliingia vijana wawili wa usalama na kumwomba Ketina atoke. Ketina alianza kuleta ukaidi kwa kuwauliza wanamjua yeye ni nani? Vijana wale walimsihi kwa mara nyingine atoke na kuwa ofisi ile haitakiwi iwe na mtu yeyote ndani kama Rais hayupo. Ketina aliendelea kuonesha kiburi na kujiamini kwakuwa tu alikuwa na mahusiano zaidi ya yale ya kikazi na Rais Costa. Wanausalama si watu wa kuwafanyia mzaha wakati mwingine, kufumba na kufumbua pasi kuamini Ketina alijikuta yupo chumba asichokifahamu pale Ikulu.
Ketina alipigwa shoti na kifaa cha umeme wanachokuwa nacho vijana wa usalama na kunyakuliwa mzobe mzobe kama mwewe anavyochukua kifaranga cha kuku na kuwekwa kwenye chumba maalumu cha uangalizi. Ketina aliposhtuka alianza kupiga kelele kwa nguvu pasi kuelewa kuwa chumba kile hakipitishi sauti hata desibeli moja. Aliachwa huko adabu imshike kwanza.
***************************************
“Mhashamu Baba Askofu, Tumsifu Yesu Kristu”, Rais Costa alimsalimia Askofu Begere kwa heshima huku akiibusu pete ya kiaskofu iliyopo kidoleni mwa askofu. Kiumri askofu Begere alikuwa ni mkubwa kwa Rais Costa. Wakati Rais Costa akiwa na miaka 56 askofu Begere alikuwa na miaka 73.
“Milele amina Mh. Rais”, Askofu Begere alijibu na wote waliketi. Mazungumzo yalianza.
“………Miradi hii ndiyo nilitaka kuitumia kama kilele cha utumishi wangu nitakapotimiza miaka 75 na kustaafu, na sasa nimebakiza miaka 2 tu. Nimeshamwandikia Baba Mtakatifu barua ya azma yangu ya kustaafu uaskofu na kupumzika, sasa miradi hii kukwama inaniumiza sana.” Askofu Begere aliongea kwa huruma kubwa.
“Mhashamu Baba Askofu, kwanza nikiri kanisa limekuwa na mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Hata mimi nimesoma seminari ya kanisa hadi kidato cha sita. Lakini unachofanya wewe na kanisa kwa serikali yangu sioni kama ni sawa. Unanichonganisha na wananchi. Hivi siku ikitokea kutokana na msukumo wenu wananchi wakachukua hatua kwa kufanyia kazi unayohubiri, nchi ikakosa utulivu utaona raha gani?” Rais Costa alimweleza Askofu Begere, japo alikuwa akiongea kwa nidhamu lakini alitoa ya moyoni.
“Hayo tunayohubiri ni wajibu wetu. Kama tusiposimamia haki na usawa, utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za umma na utii wa sheria na katiba ya nchi ni nani mwingine tumtarajie atasimamia? Nani atakemea? Kwani kuna la uongo ama la uchochezi tulilohubiri?”, Askofu Begere alionekana kutoelewa.
“Mh. Baba askofu kazi hizo zote ulizosema zina vyombo vyake vya kusimamia. Tuna Mahakama, Bunge, Mamlaka ya Makusanyo ya Taifa, Ofisi za wakaguzi wa hesabu n.k. Sidhani kama ni kazi yenu kukemea hayo. Kazi yenu ninyi na hata mimi nilijifunza seminari ni kuwaleta watu kwa Yesu Kristu. Hicho ndicho kipimo chenu baba askofu. Nisahihishe kama nimeongea uongo. Sasa ukisema ni kazi yenu kukemea inamaana na sisi tuiambie mahakama ianze kuhubiri Injili? Na bunge lianze kubatiza?” Rais Costa alianza kuongea kwa kuonyesha ghadhabu.
“Mh. Rais nadhani mbali ya mimi kuwa askofu lakini pia ni raia kama raia wengine na ninazo haki kikatiba kukemea pale ninapoona mambo hayaendi sawa” Askofu Begere alijibu kwa upole.
“Ndio ukemee kwa kutumia membari?” Rais Costa alimuuliza askofu Begere kwa ufupi sana.
“Je hayo ninayokemea sio haki? Ninasingizia?” Askofu Begere nae alihoji.
“Sasa kama unachohubiri ni haki, wewe kilichokuleta hapa ni nini Mhashamu?”, Rais Costa alionekana kutofurahishwa na majibu ya askofu Begere.
Baada ya kimya cha muda mchache huku wakitazamana, Askofu Begere aliuvunja ukimya “Sawa nimekuelewa Mh.Rais. Nimekuelewa unaamaanisha nini” alimwambia Rais Costa.
“Nashukuru sana Mhashamu Baba Askofu. Amani ya Kristu iwe nasi sote. Peleka salamu zangu kwa Baraza zima la maaskofu. Mnafanya mambo mengi makubwa kwa Taifa hili”, Rais Costa alikuwa akimwambia askofu Begere huku akiwa amesimama akishikana nae mkono.
“Nitawasalimia Mh. Rais”, Askofu Begere alijibu na kisha Rais Costa alitoka na kumwacha askofu bado ameketi.
Maongezi yalikuwa mafupi sana na ya moja kwa moja. Katika lugha ya wenzetu, Askofu Begere alionekana ameshafungwa mdomo ‘once and for all’, yaani si matarajio ya yeyote kwa Askofu kuendelea kuikosoa serikali ya Rais Costa. Angalau hivyo ndivyo Rais na wapambe wake waliamini baada ya mazungumzo hayo. Kwa mtizamo wa haraka wa mazungumzo yale, ilionekana wazi Askofu Begere amekubali kushindwa ili kutoharibu maendeleo ya miradi ambayo ingempa heshima ndani ya Kanisa na hata kwa taifa baada ya kustaafu kwake.
**********************************
“Guys, mtu mwingine ambae yupo kwenye mpango huu ni Bi. Sara, yaani mke wa Rais Costa. Kama mjuavyo hawapo nae vizuri na yeye kuna mambo hakubaliani nayo hivyo ametuunga mkono katika mkakati huu. Bi. Sara atatusaidia sana mbeleni, kwasasa nisielezee kwa undani ila ni kiungo muhimu sana kuliko mnavyoweza kuelewa.
Sasa basi, maswali kuwa nchi itaongozwa na nani niseme tu kuwa Habibu jitayarishe kuwa Rais wa Stanza. Pius utakuwa Mkuu wa Majeshi. Stanley atabaki palepale kwenye nafasi yake na mimi nitakaa nje ya mfumo.
Habibu unafahamu Rais Costa alikuondoa Stanza kwasababu ya nguvu uliyonayo kisiasa hivyo tutakurudisha ukaingie kwenye siasa kwa mwaka huu mmoja urudishe tena nguvu yako, wewe ni kijana pekee unayeweza kupambana na Julius Kibwe kwa hoja na kuleta kuaminiwa na kupata ufuasi mkubwa.
Stanley atabaki pale pale, the guy is more than a perfect match for that position. Habibu ukiingia utamteua Pius kuwa Mkuu wa Majeshi, naamini kwa njia hii nchi itakuwa kwenye mikono salama.
Tulichokubaliana na kula kiapo na Macha ni kuwa tunayafanya haya ili kurudisha Misingi ya Utawala bora, Demokrasia, Haki na kuleta maendeleo kwa wanastanza wote bila kujali ukanda wanaotokea, dini, itikadi za kisiasa na madaraja mengine ya kijamii.
Katiba yenye misingi bora ipo, ingawa inakiukwa kila mara kwa kutumia mabavu. Katika Stanza mpya inayofuata misingi ya utawala bora na misingi ya sheria, tunataka yeyote atakayekiuka mara tu baada ya kushika madaraka anawajibishwa, tunataka nchi ya watu wanaofurahia uhuru wao. Maendeleo bila uhuru ni ukoloni.
Sasa hatua gani tutaanza nazo? Kwanza tukifika nitatengeneza mazingira Habibu utolewe ubalozini aidha kwa kufukuzwa ama kwa kigezo cha kupangiwa majukumu mengine. Hili tutalifanya kitaalamu mimi na Macha ili lisiharibureputation yako lakini likupe nafasi wewe ya kurudi mtaani na kuanza kufanya siasa. Tutahakikisha Rais Costa hakugusi. Mipango mingine nyeti tutaambizana tukifika Stanza”, Joe alimalizia maelekezo yake kwa kirefu huku akiwatazama usoni.
Pius na Habibu walimeza mate, walijikuta wote wameshika bilauri ya maji na kunywa maji kushusha mshangao wao, hawakuamini jinsi mpango ule ulivyosukwa kitaalamu na kuwahusisha watu ambao hawakudhaniwa na mtu yeyote. Hawakuwahi kufikiri kuwa jambo hilo lingewezekana.
“Rais Costa mkishamtoa anakwenda wapi? Kwanini nguvu tunayotaka kuitumia kumtoa isitumike kuhakikisha miswada yake haipiti na kuwa uchaguzi ujao hashindi maana kama tunaweza kumtoa kwa nguvu kabla hata ya muda wake kuisha tunashindwaje kuhakikisha muda wake ukiisha hashindi tena?”, Pius alihoji.
“Kwa kutumia njia hiyo, ni rahisi kugundulika mapema na wapambe wake na kukutoa kwenye malengo. Unafahamu namna mambo yalivyo Stanza na ndiyo sababu tunataka kumtoa kwa kumshtukiza bila yeye kujipanga. Sasa swali mnalotaka kuniuliza kuwa yupo Makamu wa Rais, sijui na Waziri Mkuu ambao kama Rais akiwa hawezi kutimiza majukumu yake hao ndio hutakiwa kuchukua nafasi hiyo na sasa Habibu ataingiaje ingiaje hapo. Niwajibu tu kuwa hayo tunayafahamu na tutaambizana kadiri muda unavyosogea”Joe aliwaacha tena kina Pius na Habibu njiapanda.
Pius aliumiza akili, aliona kabisa mpango huu ni wa kumdhuru Rais Costa na yeye hakutaka litokee. Kiapo chake kilimtesa, alijiona siyo askari kabisa kwa kumsikiliza Joe. Aliwaza jambo kichwani ila akakaa kimya. Alitaka kwanza ajiridhishe kama kweli Macha anazo hizi taarifa ama ni tantalila za Joe tu. Alitaka atume kwanza yale maneno ya siri yajibiwe na Macha ndio aamue la kufanya.
*****************************************
Yule kijana wa kiVietinam aliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa Beijing tayari kunasa maongezi ya kina Joe na wenzake. Alishajitega kwa namna ambayo kina Joe tangu wakiwa pale angeambatana nao bila wao kumjua na kunasa maongezi yao kutokea mbali.
Aliona ndege ya shirika la Korea Kaskazini, Air Koryo ikitua na alikaa tayari kufanya kazi aliyotumwa. Alistaajabu alipogundua kuwa kwenye ndege ile kina Joe hawakuwepo. Aliwasiliana na balozi Kimweri kumpa taarifa. Balozi alionekana kushangaa na haraka aliamua kuwasiliana na Ubalozi wa Korea Kaskazini pale China kuulizia kulikoni, alitaka kufahamu kwanini raia wake hawaonekani kama walivyopanga. Alijibiwa tu kiufupi kuwa Joe na Ujumbe wake wapo salama salimini na watawasili Ubalozini ndani ya muda mfupi.
************************************
Joe, mbali ya umaridadi wake katika masuala ya diplomasia lakini pia yu maridadi katika ujasusi kama sehemu ya msomo yake aliyosomea nchini Urusi miaka ya 1970 wakati nchi ya Stanza ikiwa na mahusiano thabiti na lililokuwa taifa la Umoja wa Kijamaa wa Jamhuri za Kisovieti (The Union of Soviet Socialist Republics)
Ni yeye aliporudishwa ndani kwa mazungumzo ya siri na Rais Kim akiwa peke yake, mbali na mambo mengine ya siri aliyoongea naye alimuomba usafiri wa tofauti kurudi China. Alijua Rais Costa anafuatilia nyendo zao na hivyo alitaka kumpiga chenga ili wapate wasaa wa kuongea na kina Pius na Habibu kwa kirefu.
Katika mambo walikubaliana japo ndani ya muda mfupi, Rais Kim alikubali moja ya ndege zakeChammae-5 iwabebe kina joe na kuwarudisha China. Joe alimwomba Rais Kim kuwa safari hiyo iwe ni ya kimya na Balozi Kimweri ashangae tu wamefika bila kujua utaratibu ulikuwaje. Pia alimwambia Rais Kim kuwa yeye atamwambia Rais Costa kuwa walipewa ndege ile kwa heshima kubwa ya undugu wanaoanza kuujenga baina ya mataifa yao mawili hivyo hakutakuwa na sintofahamu.
Hicho ndicho kilichotokea na sasa kwa mara nyingine tena, Rais Costa na Balozi Kimweri wanapigwa chenga ya mwili na gwiji Joseph Kaduma.
**********************************
Mara baada ya kuwasili uwanja mdogo wa ndege Shenyang simu za Joe na wenzake zilianza kushika mtandao tena. Tayari walikuwa na mipangilio iliyoruhusu watumie mtandao wa simu wakiwa China,(roaming) za China hivyo WhatsApp na mitandao mingine iliweza kufanya kazi vyema.
Kila mmoja kwa shauku kubwa alimtumia ujumbe Stanley Macha wenye yale maneno ya siri ego testor. Ndani ya dakika tatu hivi alienza kujibiwa alikuwa ni Habibu “Ego testor”, Ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa Macha uliingia. Habibu alitabasamu kwa mshangao asiamini kuwa kumbe mpango ule ni hakika na kweli.
“Ego testor”, Ujumbe uliingia kwa Pius pia. Pius alishangaa na kuzungusha macho huku na huku na alipoona si Habibu wala Joe anayemtazama alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Joe na Habibu walipiga hatua kwa haraka wakijua Pius yupo nyuma anawafuata. Joe nae alikuwa anatembea huku akiwa WhatsApp akitumiana jumbe na Stanley Macha kwani tangu waingie Korea hawakuwa wamewasiliana. Macha alimwambia Joe kuwa ni punde tu ametoka kuwajibu kina Pius na Habibu yale maneno ya siri.
Macha alimuuliza kama ana hakika vijana wake wamemuelewa? Joe alijibu ndio huku akicheka na alinyanyua kichwa ili awatazame kina Habibu wana sura gani baada ya kujibiwa na Macha. Alistaajabu kutomuona Pius. Alisimama.
“Habibu Pius yupo wapi?”, Joe alimuuliza Habibu aliyekuwa nae ameinamisha kichwa akituma jumbe kwa WhatsApp. Habibu nae alisimamisha shingo na kushangaa kutomuona Pius.
“Macha, we have a problem. Pius is missing” (Macha tuna tatizo. Pius haonekani). Joe alimwandikia Macha ujumbe huo kwa haraka huku mapigo yake ya moyo yakizidi kuongezeka kasi kila sekunde moja inapopita. Alianza kutoka jasho japo palikuwa na baridi kali.
*************************************
Kikulacho Ki Nguoni Mwako
“Mwambieni yule binti aje sasa ofisini”, Rais Costa alitoa agizo kwa mmoja wa wasaidizi wake kuwa Ketina aitwe ofisini kwake. Alitoa maagizo hayo huku akiingia ofisini kwake akitokea kuongea na askofu Begere.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Kimweri, sijasikia kuhusu kina Joe. Kwa ratiba uliyonipa wanahitajika wawe wameshafika Beijing na Joe kuwasiliana nami. Nahitaji kusikia kutoka kwao kabla sijawasiliana na Mr. Kim”. Rais Costa alikuwa akiongea na simu huku akiketi kwenye kiti chake ofisi yake maalum pale Ikulu.
“Mh. Rais unachosema ni kweli lakini ni kuwa hawakuja na ndege niliotarajia waje nayo. Nimewasiliana na ubalozi wa Korea hapa China ambao ndio nashirikiana nao na wameniambia Joe wanakuja na ndege nyingine na kuwa wapo salama na ndani ya muda mfupi ujao watawasili hapa ubalozini”, Balozi Kimweri alimjibu Rais Costa.
“Sawa. Keep me posted”, (endelea kunijuza mambo yatakavyoendelea), Rais Costa alijibu kwa ufupi.
Rais Costa aliweka simu yake chini na kuhema kwa nguvu. Pamoja na madhaifu yake, nae ana akili fulani kama ya kunguru, yaani huhisi mambo na wakati wote hujiona hayupo salama hasa vitu vinapokwenda kinyume na matarajio yake hata kidogo tu.
Ilikuwa ni kawaida sana kufukuza mtu anapochelewa hata nusu dakika kutoka kwenye ule muda waliokubaliana kukutana. Huona kama kuchelewa kwako ni kwasababu fulani. Kwa ufupi ni mtu wa tahadhari iliyopitiliza.
Ni hulka hiyo ambayo Watoto wa mjini huiita ‘machale’ ndiyo humfanya salama, na ni hulka hiyo pia ilimsaidia kugundua mapema zaidi na katika hatua za awali sana jaribio la jeshi kutaka kumpindua kwenye awamu yake ya pili ya utawala. Hivyo kwake hii ni njia ya kumuweka salama.
“Meshack, niitie Macha mara moja”, Rais Costa aliagiza Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Stanza bwana Stanley Macha aitwe ofisini kwake. Wakati akimaliza kutoa maagizo hayo Ketina aliingia akiwa macho yamevimba na nywele kichwani zimevurugika.
“Nini tena?”, Rais Costa aliuliza kwa mshangao kwa jinsi alivyouona muonekano wa Ketina.
“Waulize hao vijana wako wamenifanyia nini”, Ketina alijibu kwa hasira na kupayuka.
“Sasa ongea kwa adabu. Unapaswa kuelewa upo ofisi ya nani hapa Keti”, Rais Costa alionekana nae kughadhibika kidogo.
“Adabu gani Costa? We si uliniacha hapa ili hawa vijana wako wanidhalilishe?”, Ketina alijibu nae kwa sauti ya juu.
Wakati Rais Costa akitaka kumjibu Ketina ghafla aliingia Meshack na kumtaarifu kuwa Stanley Macha amemuomba radhi kidogo atachelewa kufika kwani kuna taarifa ameipata kutoka Beijing China ambayo anaifanyia kazi hivyo ampe muda.
Rais Costa hapo hapo alinyanyua simu na kwa kutumia mtandao salama wa mawasiliano alimpigia Macha.
“Macha, tell me what’s going on”, (Macha niambie nini kinaendelea), Rais Costa alimuuliza Macha swali la moja kwa moja.
“Mkuu, Pius haonekani. Amewatoka wenzake katika mazingira ya kutatanisha”, Stanley Macha alijibu nae moja kwa moja.
“Amewatoka wapi? Kwani kina Joe wapo wapi? Wamefikaje China bila utaratibu Kimweri anaoufahamu na kwanini Joe awasiliane na wewe kabla yangu?”, Rais Costa aliuliza maswali mfululizo kwa kupaniki.
Stanley Macha aligundua kosa, kuwa Joe hakuwa amewasili na ndege ambayo balozi Kimweri anaifahamu na kuwa hakuwa Ubalozini mpaka muda ule. Lakini kosa la pili, kiutaratibu Joe alitakiwa kwanza awasiliane na Rais Costa kwani ndiye mkuu wa nchi na ndiye aliemtuma. Ilikuwa ni kosa kubwa sana kiutawala Joe kuongea na Stanley Macha kabla ya Rais.
“Mkuu umenipa kazi ya kuhakikisha wewe upo salama na taifa lipo salama. Ni kazi yangu ninayoifanya kwa moyo wote na naifanya usiku na mchana. Mimi kwa kutumia vyombo vya ulinzi na kikosi ulichonipa na nilichokula kiapo kukiongoza nilihakikisha namfuatilia Joe kila pahala na ni mimi niliegundua kuwa wamewasili China katika njia ambayo sio tuliyotegemea na nikachukua hatua kumuuliza Joe kulikoni na ndipo nilipogundua Pius hayupo na wenzake.
Mh. Rais nakuomba radhi kama nimekukwaza kwa kulifanya hili.” Stanley Macha alijitahidi kumjibu Rais kwa kumzunguka na kumtoa kwenye lengo. Rais Costa alionekana kukubali majibu ya Macha na yalimwongezea Imani nae.
“Macha nakuomba hapa ofisini kwangu sasa hivi nahitaji ufanye ufuatiliaji wa nini kinaendelea ukiwa hapa. Njoo na timu yako”, Rais Costa alimalizia. Alimtaka Macha afike haraka Ikulu.
“Kwahiyo unaniona mimi kinyago hapa sio?”, Ketina alimuuliza Rais Costa mara tu baada ya Rais Costa kumaliza kuongea na Macha kwa simu.
Wakati Ketina akiwa anauliza swali lake hilo, Rais Costa hakuwa anamsikiliza bali alikuwa akipiga simu nyingine kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Ernest Nduta, wanajeshi wengi walizoea Kumuita Jemedari Mshua kwa aina ya maisha aliyoishi.
“Ernest, umewasiliana na Kijana wako Pius? Costa aliuliza.
“Hapana Mkuu, kuna tatizo?”, Jenerali Nduta aliuliza.
“Just find his whereabouts” (Mtafute yupo wapi), Rais Costa alijibu kiufupi na kukata simu na kuanza kupiga simu nyingine.
“Macha umefika wapi? Connect me with Joe, I can’t get hold of him” (Macha umefika wapi? Niunganishe na Joe mimi, nashindwa kumpata). Rais Costa alitoa maagizo huku akiwa amesimama akizunguka zunguka meza yake pale ofisini.
Macha alimpigia Joe simu na kumuunganisha na Rais.
“Joe, this is totally unethical. Mimi natakiwa nipate tabu kuwasiliana na wewe? Mimi ndio natakiwa nikutafute wewe? Wewe siku hizi bosi wako ni Stanley? Upo wapi? Nini kinaendelea kwa Pius? Yupo wapi? Mmefikaje China, kwanini hata Kimweri hajui mmeingiaje China? Hii inapaswa kuwa siri?” Rais Costa aliuliza kwa ghadhabu sana tena mfululizo.
“Salamu Mh. Rais. Kwanza niombe radhi kwa haya yanayotokea lakini yametokea kwa sababu ya heshima kubwa Rais Kim aliyotupatia kwa niaba yako na sisi tulishindwa kuikataa. Tumewasili China na ndege namba tano ya Rais Kim mkuu ndio maana unaona ni kama hakuna coordination nzuri na ubalozi wetu hapa China….”, Joe alianza kujieleza kwa utaratibu sana huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi.
“Joe, it’s ok Pius yupo wapi? Ninaambiwa hamjui halipo. Hili linawezekanaje?” Rais Costa alikatisha maongezi ya Joe yaliyoonyesha kumwingia kwa kiasi fulani na kumpa Tumaini lakini suala la Pius bado lilimsumbua.
“Nimetoa taarifa kwa Macha ili anisaide kufatilia kupitia mtandao wao wa usalama kwa kusaidiana na China, najua ndani ya muda mchache tu watajua nini kimetokea. Wameanza kufatilia kamera za hapa uwanja mdogo wa ndege kuonyesha ameelekea wapi”, Joe alijibu kwa ufupi.
“Macha nakusubiri sasa hivi”, Rais Costa aliongea kwenye simu kwa ufupi na kuikata.
“Kwa hiyo mimi hapa ni kinyago?”, Ketina aliekuwa ameketi pale ofisini kwa Rais aliuliza tena.
Rais Costa hakumjibu, aliminya kikengele kidogo kilicho chini ya meza yake kwenye kona na haraka waliingia vijana wawili wa usalama katika hali ya tahadhari na kumvaa Ketina na kumpiga shoti ya umeme kwa kifaa maalum kijulikanacho kitaalam kama compact stun gunswanachotembea nacho na alipopoteza fahamu Rais Costa aliwaagiza wamtoe mbele ya macho yake na kisha aliketi kwenye kiti.
Maskini binti Ketina alijua muda wote ni wa mahaba kwa Rais Costa, hakujua kwa muda ule Costa alikuwa kwenye shinikizo kubwa la kiakili juu ya kutoonekana kwa Pius katika hali ya kutatanisha na kuwa alihitaji majibu.
Pius ni mnadhimu mkuu wa Jeshi, kitendo cha yeye kupotea katika mazingira tata pale uwanja wa ndege tena baada ya kutoka safari nyeti kama ile kilimwacha na maswali mengi sana. Akili yake ya ‘kunguru’haikutulia
***********************************
Kwenye meza ya Rais Costa kwa chini kidogo tu upande anaokaa yeye huwa kuna kitufe kidogo sana cha alamu. Kwa sababu ofisi ya Rais imetengenezwa katika hali ambayo haitoi sauti na huwezi kusikia nini kinaongelewa ndani, kitufe kile kimewekwa kwa ajili ya usalama wa Rais.
Mgeni akiingia ofisini pale na kwasababu watu wa usalama wanabaki kwa nje na hivyo ikatokea kwa sababu yoyote ile Rais akahisi mgeni wake anahatarisha usalama wake, basi kwa siri atabonyeza kile kitufe na alamu itaita kwa nje na watu wa usalama wataingia moja kwa moja kumuokoa Rais.
Kitufe kile ni alama ya Rais kusema nipo hatarini na kuwa watu wa usalama hawaingii katika hali ya kuja kuuliza nini kinaendelea bali huingia katika hali ya kuja kumuokoa Rais na hivyo yule mgeni aliyeko ndani ya ofisi ya Rais huvamiwa moja kwa moja na kudhibitiwa na ndicho kilichotokea kwa Ketina.
Kwa kawaida mgeni kabla ya kuingia kwenye ofisi ya Rais Costa hukaguliwa sana na hupewa maelekezo ya namna ya kukaa kwenye meza ya Rais, kuwa wakati wote mikono yote miwili hutakiwa kukaa juu ya meza na kama unaingia na namna yoyote ya kifurushi basi japo kitakuwa kimekaguliwa sana lakini utatakiwa kukiweka juu ya meza pia kwa maana kuwa hutatakiwa uiname kunyanyua kitu chochote kutokea chini.
Zaidi ya hapo wakati mgeni anaingia huingizwa na mtu wa usalama na mtu wa usalama hatatoka mpaka umemaliza kusalimiana na Rais na Rais ameshakaa upande wake wa meza na wewe umeshaketi ndio mtu wa usalama atatoka nje. na sasa ikitokea mgeni unafanya miondoko yoyote ya mikono basi Rais nae hutakiwa ahamishe mkono wake na kuuelekeza kwenye kitufe kwa tahadhari.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Kwa hasira alizozipata Rais Costa kwa usumbufu wa Ketina na kilichokuwa kikiendelea China aliamua amtoe Ketina kama muhalifu. Atashughulika nae baadae. Nchi kwanza mahaba baadae.
**************************************
Katika watu ambao akili zao zinakimbia kwa kasi ya ajabu basi Stanley Macha ni mmoja wapo. Jasusi huyu akili zake zilikuwa si za kawaida.
Baada ya Joe kumpa taarifa zile za kutokomea kwa Pius huku akijua fika Joe alishampa mpango wote, basi haraka alijua nini Pius anataka kufanya.
Pius ni kijana aliye na maamuzi ya haraka tena asiyeweza kuvumilia mambo pale anapokuwa hajakubaliana nayo na kuwa yana athari kwa taifa. Si mara ya kwanza.
Macha alimjua Pius kuwa tayari ameshaujua mpango na kuwa hatavumilia hata afike Stanza, atataka kutoa taarifa kwa Rais. Alijua ametoweka ili alete taarifa kwa Rais, na sasa hata yeye Macha hayupo salama tena.
Mara tu baada ya Joe kumpa taarifa ile alimsihi Joe awe mtulivu na aelekee ubalozini yeye na Habibu kama walivyopanga na amwachie yeye kudili na Pius. Alimwagiza Joe amsihi Habibu awe na utulivu na kuwa asihofu kila kitu kitakuwa sawa.
Joe alimwamini Macha sana katika mambo mengi lakini katika hili hakika hakumwamini. Alimwitikia tu ila moyoni alijua mwisho wao umefika. Alijua ilikuwa ni ngumu kumfanya Pius asimfikie Rais na kumpa taarifa, ni ngumu. Ungeweza kuchelewesha tu ila sio kufanya Rais asijue.
Macha alizidi kumuhakikishia kuwa atulie na asikimbie kwani kufanya hivyo sio tu kutamuhakikishia kuwa mkimbizi wa daima bali familia yake itaingia kwenye tabu kubwa maisha yao yote. Joe alikubali kwa shingo upande.
Habibu alikuwa hana la kufanya alikuwa akimwangalia Joe kwa macho ya kutia huruma sana, ni kama mtu aliekuwa akijisema ‘najuta kukufahamu Joe’, maana alijua Pius ni lazima atamtaja na kusema kuwa yeye anahusika na amekubaliana na Joe.
“Nilijua tu hatutafika popote na mpango huu”, Ndiyo maneno ya mwisho Habibu aliyoweza kusema na alikaa kimya kuanzia hapo. Joe hakumjibu.
********************************
Pius baada ya kuwatoka kina Joe, hakwenda mbali. Alikimbilia chooni mulemule ndani ya uwanja. Kwake yeye aliona kabisa Rais Costa yupo hatarini na alitaka kumtaarifu akae katika hali ya tahadhari na Stanley Macha. Alidhani yale aliyoambiwa na Joe ni juu juu tu na kuwa kuna mpango wa ziada.
Hakuwa tayari na hakukubali Rais adhurike mbele ya macho yake. Kama yale yangetokea kazi yake ingekuwa nini basi? Hakukubali, kiapo chake cha kumlinda Rais kilimtesa sana.
Wakati akijitahidi kumpigia simu Rais simu ilikuwa ikiita lakini haipokelewi. Aliamua kumpigia Meshack kijana wa karibu wa usalama wa Rais nayo pia iliita bila kupokelewa. Pius alijaribu kumpigia bosi wake yaani mkuu wa Majeshi lakini pia simu haikupokelewa. Alishangaa.
Hakujua kuwa Stanley Macha mara baada tu ya Joe kumtaarifu kuwa Pius haonekani haraka alimwagiza kijana wake pale idara ya usalama wa taifa afanye mpango wa kitaalamu katika teknolojia ya mawasiliano unaoitwa ‘Connection scrambling’, yaani mtandao wa simu wa namba mahsusi zilizochaguliwa unavurugwa, ikiwa na maana kuwa simu zote zinazoingia kwenye namba hizo kutokea namba ya Pius basi yeye Pius atasikia zinaita lakini kihalisia huku kwa muhusika zinakuwa hazijafika na muhusika hatajua kama anapigiwa simu.
Vilevile ili kununua muda wa kuweza kukabiliana na Pius, aliagiza tena simu zote za watu ambao anajua watakuwa target ya Pius basi wakitaka kumpigia Pius wasimpate hewani, hii kitaalamu waliita ‘Connection proof’, halafu simu za wote ambao alihisi watakuwa tageti wa Pius alihakikisha hazitaingiza simu yoyote ambayo inatokea China, hii waliita ‘Connection blocking’.
Kwa kifupi Macha alifanya kila kinachowezekana kwa wakati huo kuhakikisha kuwa taarifa zozote hazifiki Stanza kutoka kwa Pius kabla hawajamdhibiti.
Macha alifanya yote haya kupitia kijana wake mbobezi wa masuala ya mitandao ya simu aliyeitwa Daudi Kigosi. Daudi ni kijana wa usalama wa taifa na mtii kwa Macha. Yeye yupo makao makuu ya Idara hiyo na wakati wote wa maongezi ya Macha na Rais Costa yeye ndiyo alikuwa akiunganisha.
Hata kitendo cha Macha kuomba kuchelewa kidogo ikulu ilikuwa ni ili ahakikishe anamwachia Daudi malekezo sawia na kupata muda wa kutosha kujua nini atafanya.
**********************************
“Salehe habari”, Pius alimsalimia Salehe kijana wa ngazi ndogo kabisa pale makao makuu ya jeshi lakini alieingia nae jeshini mwaka mmoja.
Salehe alikuwa akipatana sana na Pius. Macha hakuwahi kudhani kama Salehe anaweza kuwa tageti wa Pius hivyo katika namba alizoagiza zifanyiwe michakato ya kitaalam na kijana wake Daudi namba ya Salehe haikumjia akilini.
“Mkuu”, Salehe alisalimia kwa kupiga saluti japo alikuwa Stanza na Pius alikuwa China. Salehe alistaajabu kuona Pius anampigia simu. Pius kwa Salehe kwa nafasi za vyeo ni sawa na mbingu na ardhi.
“Salehe fanya unaloweza hakikisha unamfikia Jenerali na kumpa hii simu niongee nae sawa?”, Pius alimwagiza Salehe kwa ufupi sana.
Alifanya hivyo mara baada ya kuona simu yake haipokelewi na yeyote aliekuja kwenye akili yake alietaka kuwasiliana nae hata mke wake hata dereva wake. Hakika Macha alimuweza lakini sasa yeye alimuweza zaidi. Hakuna aliyejua kama Pius anaweza kuwa na namba ya simu ya mtu kama Salehe.
“Mkuu nitamfikiaje Jenerali? Mimi ni mdogo sana”. Salehe alijibu kwa kutetemeka. Ilikuwa ni ajabu, yani ni kitu asichowahi kuwaza na alijua angepata maswali mengi sana.
“Salehe usikate hii simu nenda ofisini kwa Jenerali na atakaekuuliza mpe simu nitampa maelekezo mpaka utamfikia Jenerali”, Pius alimwagiza.
Salehe alianza kutembea kwa kutetemeka kuelekea ofisi ya Mkuu wa Majeshi na kama alivyowaza alikuwa akizuiwa kuwa anataka kuonana nae kuna shida gani na kwanini asiwasiliane na kiongozi wake. Katika vizingiti vyote hivyo kitu Salehe alikuwa akifanya ni kuwapa simu na kila aliesikia sauti ya Pius alipiga saluti na kumruhusu kupita.
Ili kumuona mkuu wa majeshi Stanza ilikupasa upite milango sio chini ya mitatu ya wasaidizi wake. Ilikuwa si jambo jepesi. Pius akiwa Mnadhimu Mkuu wa jeshi ni mtu wa pili kicheo kutokea kwa mkuu wa majeshi. Kila aliesikia ile simu alistaajabu inakuwaje na kwanini na ilibidi msaidizi mmoja amchukue Salehe moja kwa moja mpaka kwa mkuu wa majeshi Jenerali Ernest Nduta.
“Mkuu Salehe ana simu ya Pius, anaomba akupe uongee nae”. Msaidi alitoa taarifa huku akiwa amesimama kikakamavu mbele ya mkuu wa majeshi. Mkuu wa Majeshi alionekana kustaajabu.
“Tumekuwa tukimtafuta Pius bila mafanikio imekuwaje? Embu nipe”, Jenerali Ernest Nduta aliuliza kwa mshangao na kuchukua ile simu na kusikiliza.
“Mkuu salamu. Naomba upakue programu tumishi ya WhatsApp kwenye simu yako tafadhali”, Pius aliongea moja kwa moja.
“Pius, nini kinaendelea?”, Jenerali Ernest Nduta alihoji kwa mshangao mkubwa.
“Mkuu sina muda mrefu sajili namba yako binafsi WhatsApp sasa hivi”, Pius alijibu kiufupi sana.
Jenerali Nduta hapo hapo alimpa msaidizi wake simu yake na kumpa maelekezo kuwa amsaidie kuweka programu ya WhatsApp kwenye simu yake. Hakuwa mtu wa mitandao ya kijamii hata kidogo, yani hata WhatsApp hakuwa anajua ni kitu gani. Ni mtu mhafidhina kwelikweli.
Wakiwa wanaendelea kuweka programu ya WhatsApp kwenye simu binafsi ya Jenerali huku akiwa amebaki na butwaa nini kinaendelea ghafla aliingia Meja Kotira. Meja Kotira ni mkuu wa mawasilino ya kiintelijensia katika idara ya intelijensia ya jeshi inayoongozwa na Pius. Aliingia katika hali isiyo ya kawaida.
“Mkuu tumegundua kuna mchujo wa simu unaendelea kwa baadhi ya watu wa jeshini na wewe ukiwemo pamoja na Ikulu. Mchujo huo ni baada ya kuona mkingamo na mwingiliano wa mawimbi kutoka kwenye mtambo wa mawasiliano wa idara ya Usalama wa Taifa.
Mchujo mkubwa umefanywa kwenye namba ya Luteni Jenerali Pius na simu zote zinazotoka China zilizojaribu kuingia kwenye hawa watu zilizuiwa”. Meja Kotira alieleza huku akitweta.
“Meja usiondoke…… asee tayari ushaweka hiyo makitu yenu?”, Jenerali alimsihi Meja asitoke huku akimuuliza msaidizi wake kama ameshamaliza kuweka hiyo programu ya WhatsApp. Alionekana kupagawa kidogo.
Yule msaidizi alimjibu kuwa tayari na Jenerali alimwambia amtumie ujumbe Pius kisha ampe yeye hiyo simu. Yule msaidizi alifanya hivyo na kumpa simu Jenerali na alimwamuru atoke nje na kumwacha na Meja Kotira.
“Kotira kuna mambo hayapo sawa”, Jenerali alimwambia Kotira huku akisubiri aone majibu ya Pius.
**************************
Wakati wote kijana wa Macha, Daudi Kigosi alikuwa akicheza na mawasiliano.
“Mkuu, tunaweza kukawa na tatizo kidogo. Nimefanya ‘phone triangulation’, nimegundua kuna simu kutoka China imeingia kwenye namba mojawapo pale makao makuu ya jeshi. Sio kati ya zile namba tulizoziainisha lakini naona hapa ilikaa hewani kwa dakika kama kumi hivi”, Daudi alimpigia simu Macha aliekuwa tayari kwenye korido za Ikulu kuingia kwenye ofisi ya Rais.
Phone tringuation ni namna unaweza kufanya uchakatuaji na uchambuzi wa simu zinazoingia mahali fulani na kuweza kujua imetoka wapi au umbali gani na kama kuna teknolojia ya juu uweza kusikia mpaka nini kiliongelewa.
Kuna simu zaidi ya mamilioni zinazokuwa hewani lakini kama mtu anafanya phone triangulationanaweza kuchagua anataka achuje simu zinazotoka wapi kwenda wapi au zinazoongea neno gani kama neno la umuhimu kwa mchujaji ambalo kitaalamu huliita ‘lead word’. Yaani kwa teknolojia hii unaweza kuchagua uchuje simu zote zilizopo hewani zinazotokea jimbo fulani au zinazotaja neno Rais n.k
Baada ya kusikia taarifa ile Macha aliishiwa nguvu. Alisimama katikati ya korido pale Ikulu.
**********************************
Baada ya kuhakikisha simu zote za Pius zinazuiwa Macha kwa kutumia nafasi yake aliwasiliana na uongozi wa kiwanja cha ndege Shenyang na kuwapa maelekezo yote na kuwaomba wafatilie.
Wakishirikiana na Joe na kijana mmoja kutoka ubalozi wa Korea Kaskazini pale China walianza kuangalia kamera kuwa Pius yupo wapi na walimuona yupo chooni. Walielekea moja kwa moja chooni kwani Joe aliwaambia kuwa yule ana taarifa nyeti na kuwa aliwatoka bila kuaga.
Walifika chooni na baada ya kugonga sana Pius alifungua na kuanza kutazamana na Joe.
“Pius unataka kufanya nini”, Joe aliuliza kwa sauti ya upole. Pius alibaki anamtazama.
“It’s too late Joe” (Umechelewa sana Joe), Pius alijibu kwa sauti ya kisaliti.
Kabla Joe hajaongea neno lolote aliona simu inaita na alipoangalia alikuwa ni Stanley Macha.
“Joe, we are cornered. Pius betrayed us. As I am speaking to you, I am in the middle of four security agents in the state house, they are approaching to arrest me. I think Pius managed to leak the info. See you Joe.” (Joe tumeshikwa. Pius ametusaliti. Hapa ninapozungumza nipo katikati ya vijana wa usalama wane, wananikaribia kuniweka chini ya ulinzi. Nadhani Pius amefanikiwa kupenyeza taarifa. Tutaonana Joe). Macha alionekana kuongea kwa huzuni sana.
“Do something Macha. Please!” (fanya jambo Macha tafadhali). Joe alionekana kuchanganyikiwa.
“Hakuna mnaloweza kufanya kaka. Nimemtumia Jenerali maongezi yetu yote”, Pius alionekana kujibu kwa kujiamini.
*********************************
Katika msafara ule, Pius ndiye alikuwa na kinasa sauti kilichokuwa na mfano wa kalamu. Kinasa sauti kile kina uwezo wa kuhifadhi maongezi kwa uwezo wa Terabyte 1japo ni kidogo sana.
Kinasa sauti kile hakikuwa siri na hata walipokuwa Korea walikiweka wazi na kuwa maongezi yote na majadiliano Rais Costa alitaka kuyasikia na hivyo wakati wote wa maongezi kalamu ile ilikuwa ikirekodi.
Ulikuwa unaweza kusoma dakika na kujua maongezi fulani yalizungumzwa katika dakika fulani kwa hivyo ukaweza kupeleka mbele ama nyuma na kusikiliza.
Ni kinasa sauti kile wakati wakiwa wanazungumza mambo yao ya siri na hasa Joe alipoanza kuwapa mpango wa kumpumzisha Rais Costa, yeye Pius alikuwa akikiwasha na kurekodi kwa siri. Hakuna aliyekuwa na shaka na Pius wala kuwaza kuwa anaweza kufanya jambo lile.
Baada ya Pius kuhakikisha Jenereali Nduta yupo kwenye WhatsApp alikuwa akisogeza mbele mazungumzo mpaka kwenye zile dakika alizozikariri kuwa ndipo walikuwa wakizungumza juu ya mkakati wa kumpumzisha Rais Costa basi alishikilia kitufe cha kurekodia sauti kwenye simu yake na kuiweka karibu na kile kinasa sauti na kila neno lilirekodiwa na simu na kumtumia Jenerali kama Ushahidi.
Pia alituma screenshot za yale maneno ya siri ya ‘ego testor’ kama ushahidi kuwa Macha anahusika. Ni rahisi kusema kama ni kusaliti tu basi Pius alisaliti wenzake kwa mikono na miguu yani mzima mzima.
Haikujulikana ni kwanini Pius alikuwa akimpenda Rais Costa kiasi cha kumsaliti mtu kama Joe. Ilibaki ni fumbo kubwa.
Baada ya kupata Ushahidi ule kutoka kwa Pius, Jenerali Nduta haraka alimtaarifu Rais kumuweka chini ya Ulinzi Stanley Macha na sasa vijana wa Usalama wa Taifa pale Ikulu walikuwa wakitekeleza amri hiyo. Macha alikuwa hana ujanja.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
**************************************
“Macha, atleast we have tried” (Macha, angalau tumejaribu). Joe alimwambia Macha kwa simu kwa huzuni sana na kukata tamaa kuwa sasa hawana pa kutokea lakini angalau wamejaribu kutaka kutekeleza mpango wao walioona una manufaa kwa taifa.
“Yes Joe, we have tried. Goodluck friend” (Ni kweli Joe, tumejaribu. Nakutakia kila la heri Rafiki yangu) Macha alijibu na kabla hajamaliza vijana walishamfikia na kwa heshima kubwa kwa sababu yule ni bosi wao walimwambia kwa adabu….
“Kwa malekezo ya Rais wa Jamuhuri ya watu wa Stanza, naomba unikabidhi beji yako na kuanzia sasa upo chini ya ulinzi”, Meshack alimwambia bosi wake Stanley Macha.
“It’s ok kid, do your work” (Sawa, fanya kazi yako), Stanley Macha alimjibu Meshack kwa unyonge huku akimkabidhi beji na bastola anayotembea nayo.
****************************************
Joe na Habibu walibaki katika ardhi ya China huku wakiwa wamechanganyikiwa. Hawakuweza kuelekea ubalozini kwasababu waliamini kuwa taarifa zitakuwa zimeshawafikia.
Hali ya kutokujua pa kuanzia iliwakumba wote wawili. Joe alifikiri zaidi kuhusu familia yake aliyoiacha Stanza na namna ambavyo ilishaanza kuneemeka na msamaha wa Rais Costa na ni nini kingetokea.
Yeye Habibu alifikiri zaidi kuhusu kuharibu Maisha yake ya kitaaluma kwani ubalozi ni heshima ambayo kama ukiitumikia vyema basi haiondoki tena maishani mwako. Na kwa matukio ya siku moja tu, ameshapoteza hadhi ya ubalozi na uelekeo wa Maisha yake kwa ujumla upo mashakani.
Habibu na Joe waliangaliana kwa macho ya kukata tamaa pasi na kuongea suala lolote.
Muhudumu wa pale uwanja wa ndege aliwatazama bila kuelewa jambo lililokuwa linaotokea. Kwa mara nyingine wote walimuangalia Pius ambaye alionekana kuwa upande wa mawazo ya Joe safari nzima kumbe ni shushushu. Kwakuwa ni ardhi ya ugenini, Pius asingeweza kuwakamata au kufanya jambo lolote.
Ghafla, kama mtu aliyegutuka kutoka usingizini, Joe alimtizama Habibu machoni na kumwambia kwa sauti ya taratibu iliyoanza kuwa tulivu baada ya hofu kutanda, ‘’nina wazo, huu ndiyo mwanzo. Yajayo ni zaidi ya yaliyopita’’, Joe alisema.
“Unamaanisha nini Joe? Kila kitu kimeshaharibika hapa. Maisha yetu ni sawa na yamefikia mwisho” Habibu aliongea kwa sauti ya mtetemo kama mtu anaetaka kulia lakini anajikaza kume.
“No one has a problem with the first mile of a journey, even an infant could do fine for a while. But it isn’t the start that matters. It is the finish line’’ Joe aliendelea kuongea katika lugha ya kimombo kilichonyooka, na wakati huu alimnukuu mwanafalsafaJulien Smith.
Joe alianza kusogea kwa kuondoka huku Habibu akimfuata. Alizungumza kwa utaratibu na umakini na kusema ‘’It’s never over, it’s not over, not just yet. At best, it’s just paused for a moment. Pull up your socks boy and get ready to get started’’, Joe alimaliza na kumwacha Habibu akindelea kushangaa Joe anamaanisha nini?
Joe aliendelea kupiga hatua huku moyoni akimuwaza rafiki yake mpendwa Stanley Macha atakuwa katika hali gani ndani ya mikono ya Rais Sylvester Costa.
Stanza Mambo Ni "Tetema"
“Tunaelekea wapi Joe”, Habibu alimuuliza Joe baada ya kuona wanakatiza mitaa ya Shenyang bila kuongea neno.
“Just follow me boy” (We nifuate tu dogo), Joe alijibu kiufupi ila kwa kujiamini.
“Kaka, sikufikiri hata siku moja kama maisha yangu yatakuja kuharibika ndani ya siku chache namna hii. Nilipoambiwa ninafanya kazi na wewe niliona ni heshima kubwa na nilifurahi sana lakini ukweli kwa sasa ninajuta sana.
Natamani hata wakati ule ulipokuwa unatuambia ule mpango ningetia hata neno la kukataa leo ningelitumia kama utetezi mbele ya Rais. Sasa nilibaki kimya naonekana na mimi nimeridhia”, Habibu alijiongelesha huku wakitembea.
Joe ndiye aliyekuwa ametangulia mbele na Habibu akifuata kwa nyuma.
“Kwani hukuridhia?”, Joe alihoji kwa ufupi sana.
Jibu hilo lilizidi kumtia wazimu Habibu, chuki ya ukweli ilianza kujengeka dhidi ya Joe. Aliwaza kuwa inawezekana Joe hajali lile lililotokea ambalo limemuharibia maisha kama yeye alivyoharibu yake miaka michache iliyopita.
Wakati Joe akiwa anapiga hatua kwa kasi yeye Habibu alisimama na kumwacha Joe kama hatua tatu hivi kisha akamwita.
“Joe. Nashukuru kwa yote uliyonifunza na kufanya nawe pamoja. Naelekea kujisalimisha ubalozini. I can no longer handle this”, Habibu alimalizia.
Joe aliposikia hivyo alisimama na kugeuka, alimwangalia Habibu kwa muda kama wa dakika moja kisha alipiga hatua kumsogelea na alimfikia karibu.
“Habibu, wewe ni Rais mtarajiwa wa Stanza. You need to be as strong as the president should be. We are almost there Habibu, this is just a shortfall on the process, but it should not stop us.
You’re a traitor to Costa either way, whether you return, or you follow me, pull up your socks, wipe the dusts and continue with the mission. You are as good as dead in Costa’s hands, that you know.’’
Joe aliendelea kumuasa Habibu kwa namna aliyoona ingepunguza hofu na kukata tamaa kulikoanza kushamiri machoni mwake.
‘’Sisi ndio wa kuikomboa Stanza, sisi ndio wa kujitolea kuifanya Stanza iwe vile watu wanafikiria iwe. Tumebeba matumaini yao na ya vizazi vijavyo” Joe aliendelea.
“I need you to put in your mind that you are not the only one hurting, my family is in Stanza, but the cause we are both fighting for is bigger than I, it is bigger than you and I combined. It is also more important than family and career, it is the future of our country and the next generations. Some sacrifices must be made.”
(Nahitaji uelewe kuwa si wewe pekee unaumia, familia yangu ipo Stanza. Lakini kile tunachokipigania ni kikubwa kuliko mimi, kuliko wewe na mimi pamoja, ni kikubwa kuliko familia na hata kazi yako. Hii ndiyo baadae ya taifa letu na vizazi vijavyo. Ni lazima kujitoa muhanga), Joe aliendelea kumsisitiza Habibu
‘’Na wewe ni lazima usimame kujua nini ulikuwa ukikipigania toka ukiwa chuoni. Umepata nafasi ya kukifanya kuwa kweli kwanini unaogopa?”, Joe alikuwa akiongea na Habibu huku amemkazia macho na kumgusa kwa kidole kifuani. Aliongea kwa kuchanganya lugha kuonyesha msisitizo.
“Joe, I didn’t plan my career to end up miserably like this brother. I am…I am…”, Habibu alishindwa kumalizia na kuanza kulia. Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa huyo anaelia ni balozi wa Stanza nchini India. Usingeamini.
Joe alipoona vile hakika huzuni ilimwingia, aliona kabisa amemwingiza kijana wake kwenye misheni ambayo haikuwa saizi yake. Alijiona amefanya kosa sana kuamini ustahimilivu wa mambo alio nao yeye na Macha ni sawa na hawa vijana. Alielewa hisia za Habibu na alijua kweli amemwingiza mahali pagumu.
“Habibu, I will help you out of this and you will be free”, Joe alimwambia Habibu aliyekuwa amejifunika na kitambaa cha jasho ili wapita njia wasijue kama analia.
“Mtuhumiwa wa kesi ya uhaini anawezaje kumsaidia mwenzake?”, Habibu alihoji bila kutoa kitambaa usoni.
“Nifuate. Kwa sasa sio salama sana kurudi ubalozini, acha kwanza nipige simu mbili tatu. Sawa?”, Joe alimjibu Habibu.
“Sawa kaka”, Habibu alijibu kama mtoto mdogo. Hakika kama kuingizwa choo cha kike basi hapa aliingizwa cha vikongwe kabisa.
********************************************
Mara baada ya Pius kuachwa pale uwanja wa ndege na Joe na Habibu kuondoka, baada ya muda alishtuka na kujikuta amekaa juu ya choo amelala.
Hakuelewa, alijipapasa na kukuta kila kitu anacho isipokuwa Simu aliyokuwa akitumia pamoja na kile kinasa sauti alichokuwa amerekodia mazungumzo yote ya safari nzima ya Korea Kaskazini ikiwepo na majadiliano yote.
Alisimama na alipotaka kutoka aligundua amefungiwa mlango kwa nje. Aligonga sana na hatimaye mtu mmoja alieingia maliwatoni alimfungulia. Alianza utaratibu wa namna gani atafika ubalozini.
**********************************************
Joe na Habibu waliambatana na mlinzi mmoja wa kichina wa pale uwanjani pamoja na afisa mmoja wa usalama wa ubalozi wa Korea pale China aliekuwa amekuja kuwapokea kina Joe.
Baada ya Pius kutokomea katika hali isiyotarajiwa pale kiwanjani haraka yule afisa wa usalama wa ubalozi wa Korea aliyetumwa kuwapokea kina Joe alishafanya mawasiliano na Ubalozi na kuwapa taarifa kuwa kuna mambo hayapo sawa.
Ni Ubalozi wa Korea uliofanya mawasiliano na uongozi wa ulinzi wa uwanja wa Shenyang ili kumsaidia Joe kumtafuta Pius kwa kutumia kamera za CCTV. Ni yeye baada ya kushuhudia sintofahamu kati ya Joe na Pius, Joe alimwomba ahakikishe anampatia simu na kile kinasa sauti alichokuwa nacho Habibu.
Kwa kutumia ‘style’ ya mapigo wakorea wanaiita jug-eun yaani kifo cha uzima basi yule afisa wa usalama alifanikiwa kumzimisha Pius katika hali ya utaratibu kabisa na kumfanya apoteze fahamu na kisha kuchukua simu na kile kinasa sauti na kumkabidhi Joe.
Jug-eun ni aina ya mapigo ambayo ni ya ufundi wa hali ya juu. Mtu aweza kukusogelea karibu hata katikati ya kusanyiko la watu halafu akakupa hilo pigo moja kimya kimya ukaishia kupoteza fahamu bila hata kutoa mlio. Akishakupiga anakushika hapo hapo na kukuegemeza kwenye bega lake na kuanza kutembea na wewe kama mtu anaemsaidia mgonjwa na hakuna atakaeweza kugundua kama umepoteza fahamu.
Ni pigo hilo Pius alipigwa eneo la shingo kwa nyuma na aligutuka baada ya dakika 15. Wakati pigo hilo likitokea na vitu kuchukuliwa watu waliopo kwenye control room ya kamera za CCTV walifanikiwa kukata kipande cha tukio lile na kisha kuunganisha baada ya tukio kwisha bila kuonyesha mpishano wa sekunde hata moja. Walilifanya hili kitaalamu wakiongozwa na afisa kutoka ubalozi wa Korea aliejulikana kama Sam Si.
Baada ya tukio lile afisa wa usalama wa Ubalozi wa Korea akiwa hajui kwa nini Joe ameomba yafanyike yote yaliyofanyika alidhani wangeambatana nae Ubalozi kwao kisha aelekee ubalozi wa Stanza pale Beijing lakini Joe aliomba aachwe aende anapopajua yeye na kisha atawasiliana nao.
http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Alimsihi sana asiseme lolote lililotukia ili kutoleta hali ya taharuki. Joe hakutaka ijulikane kwa Korea kuwa alikuwa na mpango wa kumtoa Rais Costa madarakani kabla ya muda. Aliona ni mapema sana Rais Kim kumjua kiundani namna ile.
***************************************
“Franco-Domino-Chi”, Ni maneno Stanley Macha aliyomnong’oneza Meshack wakati Meshack akichukua beji yake na bastola.
“Aye Sir”, Meshack alijibu kwa sauti ya chini sana sikioni mwa Stanley Macha isiyoruhusu mtu yeyote kusikia.
Vijana wengine watatu wa usalama wakiwa wamesimama hatua kama tatu kutoka walipokuwa Macha na Meshack walimwongoza Macha kuelekea ofisi ya Rais Sylvester Costa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment