Search This Blog

Friday 18 November 2022

SALA YA SARAH - 4





Simulizi : Sala Ya Sarah

Sehemu Ya Nne (4)





Sarah fahamu zilimrudia saa kumi alfajili, alipofungua macho akajitahidi kupambana na giza la mule ndani, akahisi maumivu makali mgongoni, akakumbuka mateso aliyokuwa anapewa na Trigger ndo yamemuachia maumivu hayo, akataka kupiga hatua, miguu ikawa inaelea, akakumbuka tena alining'nizwa, kitu kingine kilichomshangaza ni kujikuta amefunikwa na nguo kifuani wakati fulana yake ilichanwa na Trigger, akiwa anawaza hayo, alisikia sauti ya mtu akikohoa, tena kikohozi kikavu kabisa, Sarah akageuka shingo ila hakuona mtu kutokana na giza kushamiri ndani ya chumba kile.



Sarah nae akajikoholesha huku akiamini huenda huyo mtu aliyekohoa hawali anaweza kumuongelesha,



"mama umeahamka?" Sauti iliuliza kutoka katika ya giza, sauti hiyo ilionesha imetoka kwa mtu aliyechoka sana,



"ndio, wewe nani?" Sarah aliuliza huku akijifanya amechoka sana, yule mtu hakujibu, badala yake akaenda moja kwa moja sehemu switch ilipo na kuwasha taa, Sarah hakuamini macho yake, alikuwa ni babu yake, alikuwa amechoka sana, Sarah akataka kuuliza kitu ila nafsi ikamzuia akajikuta ameshangaa tu,



"mama hawa watu ni wabaya sana, umewafanya nini mpaka wakakuleta hapa?" babu yake Sarah aliuliza huku akionekana kutomkumbuka kabisa Sarah,



"Mimi sikuwafanya kitu, wamenikamata tu na kunileta huku" Sarah aliongea huku akishangaa hali ya babu yake, huruma ilimjaa,



"pole sana mama, sijui hata kama utqtoka mzima, juzi juzi tu alikuja msichana wa makamo yako, wamempiga wakamvunja miguu yote, wakaenda kumtupa na Sidhani kama yupo hai tena" Babu yake Sarah aliongea kwa huruma na kumfanya Sarah ajue anaezungumziwa ni Dokta Pendo, hapo roho ikamcheza kuhusu hali aliyomuacha nayo Dokta Pendo,



"na wewe kwanini wamekukamata?" Sarah alimuuliza babu yake utasema hajui kweli,



"Mimi wamenikamata kwa ajili ya mjukuu wangu, sasa sijui wanamdai na hawajui alipo au kuna sababu nyingine" babu yake Sarah alijibu na kumfanya Sarah machozi yamtoke,



"sasa mbona hawajakufunga kamba, upo huru alafu unashindwa kutoroka?" Sarah alimuuliza babu yake,



"hata nikitoroka nitapita wapi? Mlango umefungwa kwa nje, na uko nje kuna ulinzi mkali sana" Babu yake Sarah alijibu,



"ndio maana wamekuacha huru, wanajua huwezi fanya kitu" Sarah aliongea kwa upole,



"sijaachwa huru mama, mimi nafungiwa humu, ila kuna upenyo hapa chini uwa napita, humu ninapofungiwa ni padogo sana, ukilala lazima ujikunje sana na uamkapo mwili wote uwa unauma, kwa hiyo mimi nikifungiwa humu uwa natoka usiku sana nalala hapa mpaka panapokucha, kisha narudi humu kwenye kibanda changu" Babu yake Sarah aliongea huku akiwa anamuoneshea Sarah kakibanda kadogo kama cha mbwa,



"kwa hiyo hawajuagi kama unatoka usiku?" Sarah alimuuliza,



"hawajui, siku wakijua watanimaliza" babu yake Sarah alijibu,.



Baada ya hapo waliendelea kuongea mpaka palipokucha, kisha babu yake Sarah akarudi kibandani kwake, Sarah roho ilikuwa inamuuma sana, baada ya babu yake kuingia kibandani, Sarah alilia sana, aliona mateso yote yanayomkuta babu yake, basi chanzo ni yeye,



"mchuma janga hula na wakwao" Sarah aliongea kwa sauti ndogo huku machozi yakitiririka mashavuni mwake.



Sasa muda ukiwa umeenda tangu Sarah aongee na babu yake, mlango ulifunguliwa na Trigger akaingia huku akivuta sigara,



"za asubuhi?" Trigger aliongea kwa kejeli huku akimsogelea Sarah,



"nzuri, karibu tena" Sarah alijibu huku akitabasamu na kumfanya Trigger achoke kabisa, aliamini atamkuta Sarah kwenye hali mbaya sana,



"leo sitokupiga, na kama nitakupiga sitotumia mnyororo kama jana, leo nitatumia njia nyingine" Trigger aliongea huku akiitoa bastola yake na kuitazama,



"huamuzi ni wako, niko himayani kwako, fanya chochote utachojisikia" Sarah alijibu huku akiendelea kutabasamu,



"leo sitokupiga, ila nina maswali machache unatakiwa uyajibu" Trigger aliongea huku akivuta kiti na kukaa mbele ya Sarah,



"uliza" Sarah alijibu,



"endapo tutakuua, itakuwa tumekosea?"Trigger aliuliza,



"kuuawa vitani sio kosa kisheria, na hii iliyo kati yetu ni vita, siogopi kufa na wala sitojuta kufa" Sarah alijibu huku akitabasamu,



"unajua hata kifo cha wazazi wako ni vita, sasa nashangaa wewe unavyotaka kulipa kisasi wakati unajua kuwa kufa vitani ni ushujaa" Trigger aliongea huku akimtazama Sarah,



"vita ni mapambano ya majibizano kutoka pande husika, sasa ile haikua hivyo, mlichofanya nyinyi ni uonevu, kwa maana mlimshambulia mtu ambaye hakuwa akiwashambulia, na mtawajibika kwa hilo" Sarah aliongea huku akiwa amemkazia macho Trigger,



"tutawajibika??? nani atatuwajibisha wakati wewe unafia huku?" Trigger aliuliza kwa madaha,



"kama hutoniua muda huu, kamwe hutopata nafasi ya kuniua tena" Sarah aliongea kwa kujiamini kabisa,



"nitakuua muda ninaotaka, usinipangie" Trigger aliongea huku akinyanyuka katika kiti,



"nisipokupangia muda wa kukuua, basi jiandae kupangiwa muda wa kufa wewe" Sarah aliongea na kufanya Trigger aangushe kicheko kikubwa sana,



"wewe mtoto mpumbavu sana, yaani umedhibitiwa hivyo bado unajiamini?" Trigger aliongea huku akiendelea kucheka,



"endelea kujidanganya" Sarah aliongea,



"nilitaka nisikupe chakula leo, ila nitaagiza uletewe jioni, umenifurahisha sana ndio maana nitakuletea chakula, Trigger aliongea huku akielekea nje, alipofika mlangoni akageuka,



"uwa unapenda chakula gani?" Trigger aliuliza huku akitabasamu,



"nahitaji maji tu, na glucose" Sarah aliongea na kumfanya Trigger azidi kucheka,



"glucose???? Unataka upate nguvu??" Trigger aliongea kwa kejeli huku akitoka nje na kumuacha Sarah akitabasamu tu.



Baada ya nzima ya Trigger kuondoka, Sarah alitupia macho kwenye kile kibanda alichoingia babu yake,



"we mzee" Sarah aliita kwa sauti ya chini,



"nakusikia" Babu yake alijibu,



"toka uko, njoo mara moja" Sarah alimuita yule mzee, babu akaja,



"binti nimesikia maongezi yenu yote, inaelekea mnajuana sana" Babu yake aliuliza kwa uoga,



"nisaidie kitu, ebu nifungue hizo kamba miguuni" Sarah Alimwambia babu yake,



"mama unataka kufanyaje, usije ukaniponza na mimi nikafa" babu yake Sarah aliongea kwa uoga,



"mzee nifungue, acha uoga" Sarah Alimwambia babu yake,



"mama mimi siwezi" Babu yake alijibu hivyo ingawa alikuwa na uwezo wa kumfungua,



"mzee huna watoto? Toka jana nimefungwa miguu inaning'inia, hunionei huruma" Sarah alimuuliza kwa upole,



"sawa nitakufungua miguu, lakini si bado utakuwa unaning'inia tu, mikono ndio ipo juu" Babu yake aliongea,



"nifungue hivyo hivyo tu ili damu ipite vizuri" Sarah alimuomba babu yake, babu aliendelea kuleta mgomo ila mwisho alikubali kumfungua Sarah miguu, Sarah alivyofunguliwa miguu, akaivuta miguu juu mpaka kwenye mikono na kujifungua kamba mikononi, akawa huru, kipindi chote babu yake alipigwa na mshangao kwa maana hakuwahi kuona kitendo kama hicho kabla.



"rudi bandani mzee, hapa hapakufai tena" Sarah aliongea huku akijifuta damu mgongoni mwake.



****************/*****



Sajenti Minja kutwa nzima alishinda na mawazo, ila pia kuna wazo baya lilimjia, alianza kumuhisi Sarah vibaya, na kitu kilichopelekea hiyo ni gari la Sarah, alianza kulitilia mashaka kutokana na kufanana na gari la mwanamke anayemtafuta,



"mara nyingi namba halisi ya gari hukaa kwenye vioo vya gari husika, lazima nikalichunguze lile gari la Sarah" Sajenti Minja aliwaza,



"na kwanini tokea amepotea Dokta Pendo na Sarah nae haonekani na hata simu yake haipatikani, kwanini nisianze kumchunguza na yeye?" Sajenti Minja aliendelea kujiuliza.



Kisha akatoa simu yake na kujaribu kupiga namba ya Sarah, ikawa haipatikani, akajaribu tena na tena lakini jibu likawa ni lile lile, akajaribu kupiga namba ya Dokta Pendo alikadhalika ikawa haipatikani pia, Sajenti Minja akapiga meza kwa hasira.



Nyakati za usiku zilipofika, Sajenti Minja alichukua gari yake na kuelekea moja kwa moja kwa Sarah, alipofika aliegesha gari nje na kisha yeye akaenda getini, akakuta mlango umefungwa kama alivyouacha siku iliyopita, Sajenti akaruka ukuta na kuingia ndani, alipoingia tu kitu cha kwanza alichofanya ni kuangalia namba za gari ya range Rover ya Sarah, akazikuta ni zile zile alizozizoea, na hata alipoangalia kwenye kioo zilikuwa zinarandana na za plate.



Sajenti Minja akaridhika, akaamua aingie ndani, alipofika sebuleni aliikuta kama alivyoiacha siku iliyopita, kila kitu kilikuwa vile vile,



"huyu mwanamke yupo kweli?" Sajenti Minja alijiuliza huku akipepesa macho mule sebuleni.



Mwisho akaanza kuita jina la Sarah, aliita kwa zaidi ya mara tatu hakupata jibu, kitu ambacho hakukijua ni kuwa muda huo Dokta Pendo alikuwa chumbani kwa Sarah na alikuwa ameshapoteza fahamu tangu siku iliyopita.



Sajenti Minja akiwa pale sebuleni akaamua aondoke zake, alipozima taa ya sebuleni akaona kuna sehemu kuna mwanga, yaani taa zinawaka, Sajenti Minja hakudhani kama kuna kitu au mtu, ila aliamua aende hiyo sehemu, kitu ambacho hakukijua ni kuwa hapo anapoelekea ni chumbani kwa Sarah, na mbaya zaidi Dokta Pendo yupo humo.



Sajenti Minja alienda moja kwa moja mpaka mlangoni, akapiga hodi mara mbili lakini hodi yake haikuitikiwa, akaamua kushika kitasa cha mlango na kuusukuma mlango, mlango ukafunguka.







"stop" Sajenti Minja alisikia sauti ikitokea nyuma yake na kufanya ahache kuingia ndani na kugeuka nyuma, akakutana na Sarah akiwa amevaa koti kubwa la kiume na nyuma ya Sarah alikuwepo babu yake, Sajenti Minja akajifanya anashangaa,



"sasa hata sijui nikuite mwizi au nani?" Sarah aliongea huku akiwa amejishika kiuno na huku akiwa na wasiwasi kuwa huenda Sajenti Minja amegundua uwepo wa Dokta Pendo ndani ya chumba,



"ujue nimeamua kuja huku baada ya wewe kutopatikana hewani tokea jana, nikahisi huenda una matatizo" Sajenti Minja alijitetea,



"kweli, tulikuwa na tatizo baba" Babu yake Sarah alidakia na kumfanya Sarah amzuie kwa kumuwekea kidole mdomoni,



"ningoje hapo" Sarah Alimwambia Sajenti Minja huku akimshika mkono babu yake na kumpeleka kwenye chumba kimoja ambacho alikifanya cha dharura,



"hapa ndio chumbani kwako, choo kile pale, oga na ukimaliza nisubiri humu humu nitakuletea chakula, alafu kitu kingine, usiwe unaongea ongea matatizo yetu kwa watu usiowajua" Sarah alimpa onyo babu yake,



"lakini mama mimi nina kwangu, kwanini usinipeleke kwangu?" babu yake Sarah aliongea,



"hivi unanijua mimi?" Sarah alimuuliza babu yake,



"sikujui, mimi nakuona msamalia mwema tu uliyeniokoa" Babu yake Sarah alijibu,



"ukishaoga na kula, nitakujulisha" Sarah aliongea na kutoka zake nje na kumkuta Sajenti Minja akiwa amekaa juu ya kochi akimngojea,



"hata nambie kwa nini umeingia kwangu bila ruhusa yangu?" Sarah alimuuliza Sajenti Minja,



"kama nilivyolwambia hawali, nilipata hofu baada ya wewe kutopatikana hewani" Sajenti Minja aliongea,



"hapa kwangu pako salama, ndio maana uwa nafunga geti tu, alafu ndani naacha mlango wazi, sasa wewe ukaingia na kuanza kupekua pekua droo zangu, tatizo ni nini? au kujuana kidogo unataka kuleta mazoea?" Sarah aliuliza huku akionekana hajafurahishwa na vitendo vya Sarah na wakati huo Sajenti Minja nae akawa anajiuliza Sarah amejuaje kama droo zimeguswa wakati tokea amerudi hajakaa hapo sebuleni,



"nisamehe Sarah, je unaweza kuniambia ulikuwa wapi siku mbili hizi?" Sajenti Minja aliuliza,



"nilikuwa kijijini, nilimfuata babu yangu alikuwa na matatizo ndio nilienda kumuangalia" Sarah alijibu huku akimuomba Mungu amuondoe Sajenti Minja pale ili yeye aende akaangalie hali yake,



"sawa, nilipata mashaka kidogo, nikadhani waliomteka Dokta Pendo ndio wamekuteka wewe" Sajenti Minja aliongea,



"Mimi nipo salama, muda huu naomba uniache tu nilale, tutaongea siku nyingine afande" Sarah aliongea kivivu,



"hujasikia habari yoyote kuhusu Dokta Pendo?" Sajenti Minja aliuliza huku akinyanyuka,



"Mimi nilikuwa kijijini ndugu yangu, hata simu niliacha mjini, sasa hizo habari nitazisikia wapi?" Sarah aliuliza huku akiwa anamuangalia Sajenti Minja,



"sawa, mimi naenda, ila kuwa muangalifu sana" Sajenti Minja aliongea huku akipiga hatua za kuondoka,



"ngoja nikutoe" Sarah aliongea huku akamfuata Sajenti Minja, lengo lake ni kumtoa haraka haraka tu,



"vua hilo koti, huoni joto, koti lenyewe ka kiume, sijui la babu yako?" Sajenti Minja alimtania Sarah huku wakitoka nje,



"ili mradi linanisitiri" Sarah alijibu huku akitabasamu, kisha wakatoka nje na Sajenti Minja akaingia kwenye gari lake na akaondoka.



Baada ya Sajenti Minja kuondoka, Sarah alirudi sebuleni mbio na kuvua koti, mgongo wote ulikuwa na vidonda kutokana na kutandikwa sana na Trigger, Sarah hakujali hilo, akakimbia moja kwa moja mpaka chumbani kwake,



"yesu wangu" Sarah aliongea baada ya kumuona Dokta Pendo akiwa hajitambui, Sarah hakujua kama Dokta Pendo amekufa au yupo hai, Sarah akakimbia mpaka jirani na dokta Pendo, kisha akamfungua vifungo vya blauzi yake na kuweka sikio kwenye kifua cha Dokta Pendo, aliweka kwa sekunde kadhaa kisha akakimbilia sanduku dogo lililokuwa chini ya kabati hapo chumbani, akatoa chupa mbili za dawa, akazichanganya na kuota chupa ya drip, akaweka ule mchanganyiko wa dawa na kisha akaweka na maji na kumtundikia Dokta Pendo.



Baada ya hapo akaelekea jikoni na kuanza kuandaa uji, baada ya dakika tatu tu uji ulikuwa tayari, Sarah akaupoza na kuwa vuguvugu, kisha akarudi chumbani kwake na kukuiinua kichwa cha Dokta Pendo, akakipakata, kisha akauminya mdomo wa Dokta Pendo na kuufanya ukae wazi, Sarah akaanza kumnywesha uji Dokta Pendo, alimmiminia vikombe viwili, kisha alimaliza aliangalia tena mapigo ya moyo ya Dokta Pendo, akaona yameaongezeka kidogo tofauti na hawali, Sarah akapata tumaini, akatoka chumbani kwake na kwenda jikoni kuandaa chakula chake na babu yake, hakutaka kujali kabisa juu ya vidonda alivyokuwa navyo mgongoni.



*****************



Trigger alikuwa amechanganyikiwa baada ya kufika kambini usiku huu na kuambiwa Sarah ameua karibia vijana wote na ametoroka na babu yake, Trigger baada ya kupewa ujumbe huo na Kijana mmoja ambaye alikuwa hai ila hakuwa katika nzuri baada ya kupigwa risasi maeneo tofauti mwilini mwake.



Trigger alivyopokea habari hiyo, akatoa bastola na kummaliza kijana yule,



"kwanini wewe ubakie wakati nawe ni mzembe kama wenzako waliokufa" Trigger aliongea huku akiirudishia bastola yake katika sehemu husika.



Trigger akatoka kwa hasira eneo hilo na kuelekea moja kwa moja hospitali, alimkuta Harry akiwa pamoja na vin, akawasalimia



"Harry njoo tuongeee kidogo" Trigger aliongea huku akiondoka na kumfanya Harry amfuate,



"kuna nini?" Harry aliuliza baada ya kufika nje,



"Sarah ametoroka, ameua vijana wote" Trigger aliongea huku hasira zikiwa zimemtawala,



"katorokaje" Harry aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa kabisa,



"hakuna anayeyajua, mbaya zaidi ametoroka na babu yake" Trigger aliongea huku akiangalia chini,



"sasa tujiandae kwa lolote, maana huyo babu yake alikuwa kama ngao yetu, kama amemuokoa basi tujiandae kwa lolote" Harry aliongea kwa upole, tena alipoa kweli.



"Mimi nadhani huu ndio muda wa kumshirikisha Vin" Trigger alitoa ushauri,



"nadhani, twende ndani" Harry alijibu huku akipiga hatua za kuondoka na Trigger akamfuata.



Waliweza kufika mpaka sehemu alipokuwa amekaa Vin, nao wakakaa,



"Boss kuna tatizo kidogo na ndio maana tulikuacha" Harry aliongea huku akiwa hana furaha,



"matatizo gani?" Vin aliuliza huku akionekana kutotilia maanani hayo matatizo,



"juzi tulimkamata Sarah, alikuja kuvamia kambi ambayo uwa wanakaa wafanyakazi wa baba yako, tulivyomkamata tukamfunga ndani ya chumba ili tupate muda mzuri tukueleze" Harry aliongea kisha akameza mate,



"mngeniambia nije nimchune, ila bado sijakuelewa, nitaongea nae baadae" Vin aliongea kwa hasira,



"umechelewa boss, hapa Trigger ameniletea habari kuwa Sarah ameua vijana wote na ametotoka" Harry alitoa taharifa iliyomfanya Vin ashangae,



"hao vijana ni wa kike au wa kiume? Na walikuwa wangapi?" Vin aliuliza kwa taharuki,



"vijana walikuwa zaidi ya ishirini na wote walikuwa wanaume" Trigger alijibu,



"huyo Sarah hatokuwa mtu wa kawaida, kama sio mtu mwenye mafunzo ya jeshi, basi atakuwa anatumia nguvu za giza. Wanaume ishirini?!?" Vin aliongea huku mshangao ukiwa wazi machoni mwake,



"ndio hivyo boss" Harry alijibu kinyonge,



"ila mlipomkamata mlitakiwa mniambie mapema, au mngepeleka taharifa polisi" Vin aliongea,



"Polisi????? polisi hapana, kwa anavyotutesa tukimkamata tutamalizana nae wenyewe" Harry alijibu huku akimaanisha anachokiongea,



"sio jambo jema, anatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya usalama" Vin aliongea,



"anatakiwa kumalizwa na si kufikishwa kwenye vyombo vya usalama, hivyo ndivyo baba yako alisema" Harry aliongea,



"kama mzee alisema hivyo, basi anajuana nae" Vin aliongea huku akiwa amegundua kitu,



"sisi hilo hatulijui" Harry alijibu,



"basi nitammaliza mimi kwa niaba ya baba" Vin aliongea akiwa hatanii.



****************

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

BAADA YA WIKI.



Harry akiwa ofisini kwake alipokea simu iliyopigwa kwa namba ngeni,



"hi...." ilikuwa ni sauti ya Sarah iliyomfanya Harry ahisi tumbo limejaa gesi,



"unataka nini?" Harry aliuliza kijeuri huku akiwa anaficha hofu aliyokuwa nayo,



"unakumbuka ahadi uliyonipa? ulisema endapo nitafanikiwa kutoka kule kambini kwenu mliponifunga, utanusaidia kesi yangu?" Sarah aliuliza na kufanya Harry azidi kuogopa,



"acha ujinga, ninawezaje kukusaidia wakati na mimi ni mtuhumiwa?" Harry aliuliza,



"hutaki?? Jiandae kupoteza mtu mmoja mmoja kwenye familia yako, sitowaua kwa sababu ya wewe kukataa kunisaidia, nitawaua kwa sababu ya wewe umekataa kutimiza ahadi" Sarah aliongea kwa sauti tulivu,



"ngoja Sarah, nimekubali, jioni tukutane tuongee" Harry aliongea kwa upole,



"wapi?" Sarah aliuliza,



"ufukweni" Harry alijibu,



"saa ngapi?" Sarah aliuliza,



"saa kumi na mbili jioni" Harry alijibu,



"ok poa, kazi njema" Sarah aliongea kisha akakata simu. Harry mawazo ya hofu yakaanza kumtafuna, Harry akatoa simu yake na kumpigia Vin, kutokana na hofu aliyokuwa nayo alijikuta anamueleza Vin kila kitu walichoongea na Sarah kuhusu kukutana kwao, ilikuwa ni habari njema sana kwa Vin.



***********



Mishale ya saa jioni, Sarah akiwa kwenye suruali ya jeans iliyomkaa vyema, alifika eneo la ufukweni na kuwasiliana na Harry ambaye alimuelekeza ni wapi alipo. Sarah akapiga hatua za madaha mpaka katika eneo alilokaa Harry, halikuwa eneo zuri, lilikuwa ni eneo la juu mwishoni na chini kulikuwa na bahari.



Sarah alivyofika alimsalimu huku akitabasamu, ila hata kabla maongezi hayajaanza, Vin nae alitokea na kuja kukaa pale pale, Sarah alipomtupia jicho mapigo ya moyo yakaanza kumwenda mbio, na wakati huo hiyo hali ilimkuta Vin.



"Sarah huyu ni Vin, mtoto wa Taita" Harry aliongea huku akitabasamu na kumfanya Sarah astahajabu, maana kabla hajakutana nae hilo jina alishalisikia,



"lakini hausiki kwenye kikao chetu" Sarah aliongea, alikuwa amepaniki,



"Mimi sihusiki, ila nimekuja ili uniambie baba yangu alikufanya nini mpaka umfanyie vile?" Vin aliuliza kwa sauti ya upole,



"kwanini hujaniuliza yeye alinifanya nini mpaka nikaamua kumfanya vile?" Sarah nae aliuliza kwa hasira,



"haya niambie alikufanya nini?" Vin akauliza,



.



"kwa kuwa nimekufundisha kuuliza hilo swali, basi tukikutana siku nyingine hilo ndio liwe swali la kwanza, alafu Harry leo umenikosea kwa mara nyingine tena, huu ndio mwisho wa kukubembeleza" Sarah aliongea kwa hasira huku akisimama aondoke, Vin akamshika mkono kwa nguvu,



"Baba yangu amekufanyia nini mpaka umefanya ateseke vile?" Vin aliuliza huku machozi yakimjaa machoni,



"Mimi sikutaka ateseke vile, mimi nilitaka kumuua ili asiteseke, lakini nashangaa kwa nini hajafa?" Sarah aliongea kwa jeuri huku akijaribu kujinasua mikononi mwa Vin, Vin akamkata Sarah kofi kali la shavu,



"unajua uchungu niliokuwa nao mpaka unanijibu hivyo?" Vin alifoka kwa hasira huku akisimama,



"unanipiga kwa ajili ya yule nguruwe ambaye ni baba yako???, siku akipata fahamu muulize kuhusu mimi, atakujibu" Sarah aliongea kwa hasira na kumsukuma Vin,



"malaya mkubwa, unamuita baba yangu nguruwe?" Vin hasira ziliongezeka, akataka kumpiga kofi jingine, Sarah akaudaka mkono wa Vin, kisha Sarah akataka kutoa bastola ili amtishe Vin, Vin kuona hivyo akatoa bastola yake haraka hata kabla ya Sarah hajatoa yake, kisha bila mtu yoyote kutarajia, Vin akamfyatulia risasi Sarah ya kifua, Sarah akaganda huku asiamini kinachotokea, akiwa ameganda vile vile, Vin akafyatua risasi ya pili iliyopiga paja la Sarah, Sarah akadondoka kutoka ukingoni mpaka chini kwenye maji



"kazi nzuri, umeua" Harry aliongea huku wakiondoka na vin.



Uko chini kwenye bahari, watu waliokuwa hapo walijaa wakiushangaa mwili wa Sarah uliokuwa ukielea juu ya maji...........







Mwili wa Sarah ulielea kwa muda wa nusu dakika na watu wakaanza kujaa wakiuzunguka, ghafla bila kutegemea Sarah alifungua macho na kukuta kundi la watu likimtazama, Sarah akakurupuka na kuanza kupiga hatua huku akiuvuta mguu wake, alikuwa ameumia baada ya lile shambulio la risasi. Sarah aliendelea kujivuta huku akiwa amelowa mwili mzima, akajikuta mpaka kwenye gari yake, Range Rover nyeusi na kuingia huku kundi la watu wakimfuatilia na wakishangaa mtu aliyepigwa risasi amewezaje kusimama? Sarah baada ya kuingia kwenye gari yake, aliwasha na kuiondoa kwa kasi, akuwa na furaha kabisa kwa kitendo alichofanyiwa na Harry, hiyo siku Sarah alikuwa na hasira kupita maelezo, njia nzima alikuwa anamuwaza huyo mtu aliyetambulishwa kama mtoto wa Taita, na pia aliwaza usaliti aliofanyiwa na Harry.



"Harry una hali mbaya" Sarah aliongea peke yake huku akikanyaga mafuta ya gari.



**************************



Sajenti Minja aliweza kufika eneo la tukio ambalo mwanamke alipigwa risasi, ila bahati mbaya alikuta mtu aliyepigwa risasi amekimbia na waliompiga risasi wamekimbia.



"sasa huyo mwanamke aliyepigwa risasi amewezaje kukimbia?" Sajenti Minja alimuuliza dada mmoja ambaye ndiye alikuwa shuhuda wa tukio,



"amenyanyuka na ameondoka huku akiuvuta mguu wake na kuingia kwenye gari" Dada alitoa maelezo,



"kwa ulivyomuona, hiyo risasi amepigwa eneo gani?" Sajenti Minja aliuliza,



"itakuwa mguuni kwenye paja, maana ndio alikuwa amepashika" Dada shuhuda aliongea,



"ulisema alivyoinuka alienda kwenye gari lake, hilo gari uliweza kulitambua" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio, ni Range Rover Sport nyeusi" Dada shuhuda alijibu na kumfanya Sajenti Minja acheke,



"namba zake ulifanikiwa kuzinakiri?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, sikuwa na akili ya kuwahi kukariri namba, nilikuwa na mshangao kwa kitendo cha mtu aliyepigwa risasi kuamka na kutembea" Dada shuhuda alijibu,



"je, waliompiga risasi huyo dada uliwaona?" Sajenti Minja aliuliza,



"sikubahatika kuwaona kwa kuwa tukio lilitokea juu na huyo dada akaanguka kutoka kule juu na kufikia kwenye maji" Dada shuhuda alijibu huku akionesha kidole eneo la juu,



"ahaa, kumbe aliporomoka kutoka kule?" Sajenti Minja aliuliza huku akimtazama eneo la juu,



"nilibahatika kuchukua video wakati huyo dada amelala hapo chini" Dada shuhuda aliongea huku akibonyeza simu yake na kumfanya Sajenti Minja ajongee ili aweze kumuona huyo dada ambaye alikuwa akimtafuta kwa muda mrefu, ile video ilimuonesha Sarah akiwa amelala akielekea juu ya maji ila sura ilikuwa chini, alafu video ikaishia hapo hapo.



"sasa mbona fupi, hakuna inayomuonesha uso?" Sajenti Minja aliuliza huku akionekana kukereka,



"simu yangu iliisha charge, hata hapa unapoiona inaweza kuzimika muda wowote" Dada shuhuda aliongea huku akizima data kwenye simu yake,



"nirushie hiyo video" Sajenti Minja aliongea huku nae akitoa simu yake mfukoni na kisha akarushiwa ile video fupi.



Baada ya kumaliza kuchukua ile video, Sajenti Minja alienda mpaka eneo la juu ambapo inasemekana huyo mwanamke alipigwa risasi eneo hilo.



Alimkuta mdada mmoja ambaye inaonekana alikuwa muhudumu hapo, Sajenti Minja akamsalimia,



"Mimi ni polisi, unaweza kuniambia hilo tukio la kupigwa mwanamke risasi lilikuwa?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kujitambulisha,



"Mimi kwa kweli nilikuwa bize na mambo yangu, ghafla nikasikia watu wanapiga kelele huku wengine wakikimbia, ndipo nilipoangaza macho nikaona kwenye meza moja wamekaa wanaume wawili na mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesimama huku akiwa ameganda, muda huo huo tena mwanaume mmoja yule aliyeshika bastola akamfyatulia risasi yule mwanamke, ilimpata pajani, yule mwanamke akaangukia chini, kisha wale wanaume wakasimama na kuondoka" Muhudumu alitoa maelezo yake,



"kati yao unamjua yoyote?" Sajenti Minja aliuliza,



"siwajui kwa kweli, ila kama nitabahatika kuwaona tena, nitawatambua" Muhudumu aliongea,



"na huyo mwanamke nae ukioneshwa unaweza kumtambua?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, mwanamke alinipa mgongo, sikuweza kuiona sura yake" Muhudumu alijibu,



"nashukuru, ila inatakiwa ufunge huduma kwa sasa" Sajenti Minja alimwambia Muhudumu,



"ndicho ninachokifanya kwa sasa na ndio maana hujakuta mteja" Muhudumu alijibu na kumfanya Sajenti Minja aelekee zake nje.



Alichofanya Sajenti Minja aliondoka moja kwa moja mpaka kwenye mamlaka ya mapato na kuomba aonane na mkurugenzi, akaoneshwa ofisi na kwenda. Alipofika aliingia moja kwa kwa mkurugenzi na kumkuta akiwa anajiandaa kutoka,



"vipi bwana, wamekuruhusu vipi kuingia wakati ni muda wa kutoka huu?" Mkurugenzi aliuliza huku akivaa koti lake la suti,



"nina shida muhimu, naomba unipe kama dakika tano hivi" Sajenti Minja aliongea huku akikaa kwenye kiti,



.



"sina muda kijana, uje kesho" Mkurugenzi aliongea huku akimuinua Sajenti Minja,



"sijaja kwa tatizo binafsi, nimekuja kiserikali" Sajenti Minja aliongea na kutoa kitambulisho na kukiweka mezani na kumfanya yule mkurugenzi atulie kidogo,



"ooh kumbe umekuja kitaifa?, ungesema mapema" Mkurugenzi aliongea huku akivuta kiti na kukaa,



"usijali boss" Sajenti Minja aliongea,



"kuna tatizo gani?" Mkurugenzi aliuliza huku akivua miwani,



"naomba unitazamie gari aina ya Range Rover Sport zipo ngapi zilizosajiliwa hapa nchini?" Sajenti Minja aliuliza na kumfanya mkurugenzi ashangae,



"sasa hilo tatizo si ungelimaliza huko chini?" Mkurugenzi aliuliza,



"nina sababu zangu za kuja huku, sasa nisaidie tu" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu, na kumfanya mkurugenzi avute computer yake na kuanza kubofya bofya, baada ya dakika tano akamgeukia Sajenti Minja,



"Range Rover tulizozisajili ni kumi na mbili, ila tulizosajili mwaka huu ni mbili, moja ni ya mwanamke anayeitwa Sarah Isack na nyingine ni mzee mmoja wa kiarabu, ila ya huyo mzee sasa hivi haipo, alishaondoka nchini na aliondoka na gari yake" Mkurugenzi aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja,



"hiyo ya huyo mwanamke namba zake ni hizi?" Sajenti Minja aliuliza huku akimpatia mkurugenzi karatasi yenye namba za gari la Sarah, mkurugenzi akaangalia na kisha akarudisha macho kwenye computer,



"hakika ndio yenyewe" Mkurugenzi aliongea huku akimrudishia karatasi Sajenti Minja,



"na hii namba ya nani, nani anaimiliki?" Sajenti Minja aliuliza huku akimpatia karatasi ile yenye namba ya siri ya Sarah anayoitumiaga Sarah kipindi anapoenda kufanya tukio. Mkurugenzi akaichukua ile namba na kuiingiza kwenye computer, akabofya bofya vitufe vya computer kisha akawa anasubiri kwa muda,



"hiyo namba haijasajiliwa, ilifutwa usijili wake, ila hakuna sababu yoyote iliyoandikwa kama chanzo cha kufuta hiyo namba" Mkurugenzi alitoa jibu,



"ilikuwa inamilikiwa na nani?" Sajenti Minja aliuliza,



"hakuna record nyingine zaidi ya hiyo niliyokuambia" Mkurugenzi aliongea huku akimgeuzia computer Sajenti Minja ili nae ajionee,



"basi hiyo namba inafanya kazi, tena inatumiwa na mtu anayefanya uharifu" Sajenti Minja aliongea huku akiirudisha computer usawa wa uso wa mkurugenzi,



"sasa hiyo kazi ya kupeleleza ni yenu, hapa msaada wetu umeishia hapo" Mkurugenzi alijibu,



"nashukuru, ila nitarudi tena nikihitaji msaada wako" Sajenti Minja aliongea huku akimpa mkono wa shukran,



"usijali, karibu tena" Mkurugenzi aliongea huku akiweka vitu vyote vizuri juu ya meza.



Sajenti Minja akaelea nje na kuingia ndani ya gari,



"kwa maana hiyo gari ambayo imesajaliwa na ipo ni moja tu, ya Sarah. Au kuna mtu yupo karibu yake uwa anatumia na uwa anabandika namba battle?" Sajenti Minja alijiuliza huku akiwasha gari na kuliondoa,



"sasa bora nimfuatilie Sarah, huenda kuna kitu anakijua, natakiwa niende nae kwa akili sana" Sajenti Minja aliongea huku akiingia ndani ya mgahawa, muda ulikuwa umeenda sana.



Sajenti Minja aliingia mgahawani na kula, alipomaliza akaenda nyumbani, hakuwa na cha kufanya muda huo, akaona bora aende kumuona Sarah huku akiamini kama ni kweli yeye ndiye aliyepigwa bastola, basi lazima amkute na majeraha, Sajenti Minja akatabasamu, akaingia chumbani na kuvaa kaptula fupi na fulana, na juu akavaa koti.



Akatoka na safari ya kwenda kwa Sarah ikaanza, njia nzima alikuwa anawaza kama kweli Sarah atakuwa mtuhumiwa, atamfanyaje?



"sharia itafuata mkondo tu" Sajenti Minja aliongea huku akiwa makini na barabara.



Mishale ya saa mbili na nusu Sajenti Minja alikuwa akiegesha gari yake nje ya nyumba ya Sarah, baada ya hapo akatelemka na kuingia moja kwa moja mpaka mlango wa sebuleni na kupiga hodi, sauti ya kiume toka ndani ikaitikia kisha Sajenti Minja akaingia,



"shikamoo babu" Sajenti Minja alimsalima babu yake Sarah aliyekuwepo sebuleni huku akitazama runinga,



"marhabaa kijana, karibu" Babu yake Sarah aliitikia kichangafu huku kikombe cha kahawa kikiwa mbele yake,



"naona umeshapazoea hapa" Sajenti Minja aliongea huku akikaa juu ya sofa,



"tena sana, Unaona nilivyojitanua" Babu yake Sarah aliongea huku akicheka,



"naona aisee, vipi huyu bibie nimemkuta?" Sajenti Minja alimuulizia Sarah,



"yupo, yupo ndani uko" Babu yake Sarah alijibu na kisha akapaza sauti kumuita Sarah, baada ya sekunde chache Sarah alitokezea sebuleni huku akitembea kwa kuuvuta mguu wake kama umeumia, Sajenti Minja akapata mshtuko ila hakuonesha wazi mshtuko wake,



"karibu afande" Sarah aliongea huku akijitupa juu ya sofa,



"huo mguu vipi?" Sajenti Minja aliuliza,



"nadhani umeteguka" Sarah alijibu,



"babu naomba utupishe kidogo" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia babu yake Sarah,



"kwanini?" Sarah aliuliza,



"babu tupishe muda mchache tu utarudi" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado anamtazama babu yake Sarah,



"kwanini aende?" Sarah aliuliza huku akiwa hamuelewi Sajenti Minja,



"kuna mambo muhimu nataka nikuulize" Sajenti Minja alijibu,



"babu nenda, nitakuita" Sarah Alimwambia babu yake na kisha babu akasimama na kuondoka zake huku akiwa na wasiwasi.



"jioni leo ulikuwa ufukweni?" Sajenti Minja aliuliza na kufanya Sarah apate mshtuko, akahisi Sajenti Minja amemgundua,



"leo nimeshinda nyumbani tu" Sarah alidanganya,



"sasa naongea kama askari na wala sio Joel Minja. Toa hiyo khanga uliyoivaa" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa bastola na kumfanya Sarah apate hofu zaidi, Sarah alijua kabisa Sajenti Minja amejua kuwa Sarah yeye alipigwa risasi pajani,



"unataka nikuvulie nguo afande, unataka kunifanya nini?" Sarah aliuliza huku akijifanya ana hasira,



"Sarah fuata amri nikiyokupa, vinginevyo tutaonana wabaya" Sajenti Minja aliongea na kufanya Sarah azidi kupata hofu,



"sheria ndio inasema nimvulie nguo afande?" Sarah aliuliza kwa ukali huku akiwa amesimama,



"toa khanga hiyo, kuna kitu nataka niangalie pajani kwako" Sajenti Minja aliongea kwa ukali huku nae akisimama, Sarah akaona leo kazi anayo,



"sitoi khanga na wala siogopi bastola yako" Sarah aliongea huku akigeuka na kuanza kuondoka huku akiuvuta mguu wake na pia akiamini amefanikisha kumtoka Sajenti Minja,



"unaongea na serikali kama unaongea na bwana wako" Sajenti Minja aliongea kwa hasira huku akiivuta khanga ya Sarah, khanga ikadondoka na Sarah akabaki na kaptula fupi sana iliyoacha kwa asilimia kubwa mapaja yake wazi, kisha Sajenti Minja akamgeuza Sarah kwa kasi wakawa wamegeukiana, macho ya Sajenti Minja yakakimbilia kwenye mapaja ya Sarah kuangalia eneo alilopigwa risasi...........





Sajenti Minja hakuona kidonda wala dalili yoyote ya kidonda mapajani kwa Sarah, Sajenti Minja akapatwa na bumbuwazi,



"umeridhika sasa? Au niondoe na hii kaptula?" Sarah aliuliza kwa hasira huku akifungua kifungo cha juu cha kaptula yake,



"basi, usifanye hivyo" Sajenti Minja aliongea huku akiokota khanga ya Sarah na kumfunga kiunoni,



"haya nakuomba uondoke nyumbani kwangu" Sarah aliongea kwa hasira,



"usichukulie hasira, tujadili kidogo hili jambo" Sajenti Minja aliongea kwa upole huku akiwa amesimama mbele ya Sarah,



"sihitaji kujadili kitu na wewe, we ondoka tu nyumbani kwangu, mimi nilikuchukulia rafiki kumbe mwenzangu unanipeleleza?" Sarah aliongea huku hasira zikiwa bado zinamuandama,



"no Sarah, ebu Kaa tuongee" Sajenti Minja alijaribu kumshawaishi Sarah,



"sihitaji kukaa na wewe, ondoka officer, nahitaji kulala" Sarah aliendelea kupayuka,



"sawa, nisamehe Kama nimekukwaza" Sajenti Minja aliongea kwa upole,



"nimeshakusamehe, wewe nenda tu" Sarah aliongea huku akimfungua mlango,



"sawa, mbaki Salama" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka kwenye kochi na kuelekea nje,



"tubaki salama au tusibaki salama hiyo haikuhusu officer, ni mambo ya familia yangu" Sarah aliongea huku akielekea nje kufunga geti, wakati akiwa ndani alisikia gari ya Sajenti Minja ikiondoka nje,



"aisee nilijisahu vibaya, kumbe huyu panya ananifuatilia?" Sarah alijiuliza mwenyewe huku akiingia ndani, alipitiliza mpaka chumbani kwake,



"shoga ulikuwa unaongea na nani?" Dokta Pendo aliuliza,



"bwana wangu" Sarah alijibu huku akiogopa kusema ni Sajenti Minja kwa sababu alifahamu fika kuwa Dokta Pendo anajuana na Sajenti Minja,



"hii mpya, mbona sijawahi kumuona kabla?" Dokta Pendo aliuliza huku akicheka,



"utamjua tu, sema na wewe ni mbeya shoga yangu" Sarah aliongea huku akicheka,



"kwa mwanamke umbea ni sana bibi wewe" Dokta Pendo aliongea na kufanya wote wacheke,



"bado wiki tatu uondoe hayo mahogo miguuni, usijali utapuyanga kutafuta umbea mji mzima" Sarah aliongea,



"Alafu uliniambia kuwa utanisimulia hadithi ya maisha yako, lakini sioni ukifanya hivyo" Dokta Pendo aliongea,



"unataka nikwambie ili unitangazie umbea? Usijali shoga yangu, ngoja upone nitakuambia kila kitu" Sarah aliongea,



"nipone haraka niupate huo umbea" Dokta Pendo aliongea na kucheka,



"usijali, acha niende sebuleni nikaangalie movies" Sarah aliongea,



"si uangalizie hapa hapa jamani?" Dokta Pendo aliuliza,



"nitakupiga kelele bure wakati kihalisia hutakiwi kupigiwa kelele, unahitaji utulivu" Sarah aliongea huku akielekea sebuleni.



Sarah alipofika sebuleni, aliwasha lap top yake na kuingiza moderm kisha akaenda sehemu ya Google kisha akaenda sehemu ya "search" na kuandika JOEL MINJA, kisha yakatokea majina mengi, akaelekea kwenye jina ambalo analolijua yeye, "SAJENTI JOEL MINJA" akabonyeza kwenye jina na kuanza kuangalia wasifu wa Sajenti Minja, akaelekea kwenye masuala ya kazi, akakuta kesi nyingi tu za utata ambazo Sajenti Minja alizifuatilia na kufanikisha, kesi iliyomshangaza zaidi Sarah ni kesi ya "FUMBO LA UTAMBUZI" ambayo ilionekana aliifuatilia kwa muda mfupi sana na akaweza kuwakamata wahusika.



Kufika hapo Sarah akajikuna kichwa,



"kumbe ni mtu anayeaminika na serikali?" Sarah alijiuliza na kuendelea kupekua wasifu wa Sajenti Minja. Baada ya kuridhika, Sarah alifunga lap top yake na kuelekea kwenye chumba chake cha siri, akaingia na kukuta bullet proof zake zikiwa zimezagaa chini, akaziokota na kuziangalia,



"mmeniokoa leo" Sarah aliongea huku akiichukua bullet proof moja iliyokaa kama tight na kuiweka kwenye kabati, kisha akarudi sebuleni na kuendelea kuangalia runinga.



*******************



Siku iliyofuata, Nyakati za usiku, Harry na vin walikuwa Vin hotel wakipata kinywaji, walikuwa wametoka hospitali kumuangalia Taita,



"Ujue Vin nipo kwenye hali mbaya sana, najua lazima Sarah atakuwa ananiwinda muda huu, anasubiri wakati ufike tu ili anishambulie" Harry aliongea, alikuwa na wasiwasi mkubwa sana,



"ujue nimegundua yule mwanamke sio wakawaida, huenda ana mafunzo maalum, yaani nimempiga risasi mbili na hajafa, itakuwa alivaa bullet proof" Vin aliongea huku akiwa na soda mkononi,



"bullet proof mpaka miguuni?" Harry aliuliza,



"mguuni nitakuwa nimempiga, si umesikia baadhi ya watu walisema aliondoka huku akiuvuta mguu?" Vin aliuliza,



"ila mbona ulivyompiga hakutoka damu? Ina maana hana damu?" Harry aliendelea kuuliza,



"ila inawezekana ni kweli alivaa bullet proof ya miguuni, hiyo tabia inafanywa sana na wanajeshi wa uingereza" Vin aliongea,



"kwa hiyo unataka kusema Sarah ni mwanajeshi wa uingereza?" Harry aliuliza kwa hamaki,



"sijasema hivyo, nilichosema ni kuwa hizo tabia za kuvaa bullet proof mpaka miguuni ni tabia za jeshi la uingereza" Vin aliongea,



"huenda Sarah ni mwanajeshi kweli, maana wakati akiwa mtoto alipelekwa kuishi uingereza" Harry aliongea huku akiwa anaangalia chini,



"kwa hiyo kumbe unamjua vizuri Sarah, yaani unajua mpaka habari zake za utoto?" Vin aliuliza huku akishangaa,



"hapana, nimelopoka tu" Harry alijibu huku akijichekesha,



"ukinificha itakuwa hunisaidii, Baba yangu atazidi kuumia" Vin aliongea,



"usiwe na haraka, ngoja baba yako apate fahamu, naimani atakueleza kila kitu" Harry aliongea huku akimtazama Vin,



"na Sarah uliniambia alitaka umsaidie katika kesi yake, je ni kesi ipi hiyo?" Vin aliuliza,



"hajaniweka wazi, nadhani alitaka kuniweka wazi jana tulipokutana pale" Harry aliongea,



"kuna kitu mnanificha, basi acha nikalale, tutaonana kesho" Vin aliongea huku akiinuka,



"sawa boss, acha na mimi nijirudishe nyumbani, nikifika nitakujulisha, maana si unajua naweza kuvamiwa" Harry aliongea huku nae akinyanyuka,



"si umemuweka Trigger akufuatilie kwa mbali, nina imani yupo makini" Vin aliongea,



"Trigger mwenyewe bangi tupu yule, hata simuamini" Harry aliongea na kufanya wacheke, kisha Harry akaelekea kwenye gari yake na kuingia, kisha akaiondoa.



Harry alivyoondoa tu gari, gari nyingine ndogo ikaondoka kuifuata gari ya Harry, ilikuwa ni gari inayoendeshwa na Sarah, baada ya hapo gari nyingine ikaondoka kuzifuata hizo gari nyingine, hiyo gari ya tatu ilikuwa inaendeshwa na Trigger.



Baada ya dakika mbili Trigger aliitilia mashaka gari ndogo iliyokuwa inaifuatilia gari ya Harry, Trigger akaongeza mwendo ili kuisogelea kwa jirani hiyo gari aliyoihisi vibaya.



Huku nae Sarah alipata wasiwasi baada ya kugundua kuna gari inamfuatilia kwa muda mrefu, Sarah akaamua kuiacha njia ambayo gari ya Harry ilikuwa inaelekea, Sarah akabadili njia, na kwa upande wa Trigger akaona ni bora aendelee kuifuata hiyo gari kwa maana aliziamini sana imani zake.



Sarah alizidi kujiuliza huyu ni nani anayemfuata? Sarah akaongeza mwendo wa gari, na Trigger nae akaongeza mwendo wa gari.



Sarah akaendesha gari na kuegesha mbele ya nyumba moja ambayo haikuwa na muonekano wa watu kuishi, kisha akaingia ndani, nyumba haikuwa na geti.



Trigger yeye alivyofika hakuegesha gari hapo, alienda kuegesha mbele kidogo, kisha akashuka na kurudi mpaka kwenye ile nyumba na kuangaza, kisha akauendea mlango wa sebuleni na kuusukuma kisha akatanguliza bastola mbele, alivyoingia akazungusha macho sebule yote hakuona mtu, akawa anaelekea kwenye korido ya vyumbani, ila ghafla alishtukia mkono wake ukipigwa na chuma kizito, akaangusha bastola chini,



"hatimaye tumekutana tena baada ya siku chache, sema leo tumekutana kwenye hali tofauti, leo mwenyeji ni mimi" Sarah aliongea kwa dharau huku akiwa ameiweka bastola yake usawa wa kichwa cha Trigger aliyekuwa ameshika mkono wake mmoja huku akiugulia maumivu baada ya kupigwa na chuma.



"geuza, rudi nje mista" Sarah aliongea na kumfanya Trigger ageuze na kuanza kuelekea nje, walipofika nje Sarah akamuamuru Trigger asimame,



"twende nyuma ya nyumba" Sarah aliongea na kumfanya Trigger ashangae



"ebu ngoja tuongee kidogo" Trigger aliongea huku akiwa amesimama, Sarah akatoa kisu na kumchana mara mbili mgongoni,



"hutakiwi kuongea bila ruhusa yangu" Sarah aliongea huku akimuangalia Trigger alivyoukunja mgongo kutokana na maumivu aliyoyapata,



"songa mbele mbwa wa boss" Sarah aliongea huku alimtandika Trigger teke la mgongo, Trigger akajikuta anasonga mbele bila kubisha tena. Walipofika nyuma ya nyumba walikuta kuna ngazi ikiwa imeegeshwa ukutani,



"panda ngazi" Sarah alimuamrisha Trigger ambaye alitii huku akijuta kumfuatilia Sarah usiku ule.



Walipanda mpaka juu, Sarah nyuma, Trigger mbele, walipofika juu hakukuwa na bati kulikuwa na zege tu na pia kulikuwa na viti viwili vilivyoizunguka ile meza.



"Kaa kwenye kiti hapo, hivi viti niliviandaa kwa ajili yangu na Harry, ila sio mbaya, maana kilichotokea ni mtego wa perege kukamata kambale, sio mbaya, wote ni samaki na wanaliwa" Sarah aliongea kwa dharau huku akicheka, Trigger alikuwa kimya huku akikaa kwenye kiti,



"unakumbuka mara ya mwisho nilikuambia uniue ila ukakataa? sasa leo zamu yangu kukuua" Sarah aliongea na Kumtazama Trigger aliyekuwa anatokwa na jasho licha ya hali ya hewa kutawaliwa na baridi.



"nilisikia wewe ni mtaalam sana wa kuchezea silaha za moto, leo nitakufundisha namna nzuri ya kucheza nazo" Sarah aliongea huku akivua bullet proof mwilini mwake na kumfanya Trigger ashangae,



Baada ya kuvua bullet proof, Sarah alipomaliza kutoa bullet proof, akachomoa bastola nyingine na kuitoa risasi zote na kuiweka juu ya meza mbele ya Trigger, kisha na yeye Sarah akatoa risasi kwenye bastola yake, baada ya hapo Sarah akaondoa bullet proof zote mwilini mwake, muda wote huo Trigger hakutambua lengo la Sarah ni nini?.



Baada ya hapo Sarah akaingiza mkono mfukoni na kutoa risasi mbili, moja akaiweka mezani upande wake, na risasi nyingine akaiweka upande wa Trigger pembeni ya bastola aliyomuwekea Trigger, kisha akaitoa stop watch na kuitega sekunde thelathini,



"ikifika sekunde sifuri tunatakiwa kuwahi hizo bastola mezani na kuzitia hiyo risasi, alafu atakayewahi atampiga mwenzake eneo lolote analotaka, mimi nitakupiga kichwani, maana siku yako ya kifo ni leo" Sarah aliongea kwa kejeli na sasa Trigger alishajua lengo la Sarah, Trigger akaachia tabasamu moja baya sana, tabasamu la dharau.



Sekunde zilizidi kuhesabu tu kutoka juu kwenda chini, ilipofika sekunde ya sifuri tu, Sarah kwa kasi ya ajabu akaiwahi bastola yake na kuijaza risasi haraka, alipotaka kuinyanyua ili amfyatulie risasi Trigger, Sarah ndipo aliposhtuka, alikuta tayari mdomo wa bastola ya Trigger upo usawa wa kichwa chake, Sarah akainuka kwa kasi ili akimbie, lakini alichelewa tayari, wakati akiinuka ndio muda huo Trigger alifyatua risasi iliyompiga Sarah na kumtupa mbali............. Sarah akawa yupo chini huku damu ikiwa imejaa kichwani eneo la kisogoni........







Kichwa chote cha Sarah kilitapakaa damu aliyokuwa ameilalia, sio kwamba alikuwa amepigwa risasi ya kichwa, lah! alipigwa risasi ya bega baada ya kuinuka kwa kasi, lengo la Trigger lilikuwa ni kufumua kichwa cha Sarah, ila baada ya Sarah kuinuka kwa kasi, ile risasi ilipiga bega la Sarah na kumfanya Sarah aanguke chini huku akivuja damu, na ile damu iliyokuwa inavuja kwa wingi ilitapakaa eneo lile na kumfanya Sarah ailalie damu yake na kichwa chake chote kikatapakaa damu.



Baada ya Sarah kuanguka kutokana na pigo la risasi, Sarah akainuka na kuwahi kuokota bastola yake ili ammalize Trigger, lakini alikuta Trigger hayupo muda tu, alishasepa kitambo eneo, Sarah akajikuta anajitukana matusi ya nguoni kwa kufanya uzembe wa kutokummaliza Trigger mapema bila kufanya nae mashindano, Sarah akaenda upande ngazi ilipo ili atelemke, akakuta ngazi imeangushwa chini, Sarah akachoka kabisa, ila akarudi nyuma hatua kadhaa na kwenda mbio mpaka ukingoni kwenye ukuta na kuruka mpaka chini, akahisi maumivu kwenye mkono wake uliopigwa risasi, kisha akaondoka mpaka nje ya nyumba, akaangaza angaza kuona kama ataliona gari la Trigger, lakini hakuiona, akaingia kwenye gari yake na kuiondoa kwa kasi kuwahi nyumbani kwake, ilibidi atumie mwendo wa kasi kwa kuwa alihofu anaweza kupata tatizo kubwa endapo hiyo risasi itaendelea kukaa mwilini mwake. alitumia mkono mmoja tu kuendeshea gari yake.



Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani, hakukuta mtu sebuleni, Sarah akapitiliza mpaka kwenye chumba chake cha siri na kuvua fulana, akaenda kwenye sehemu lilipo box lake la huduma ya kwanza, akatoa kisu na mikasi kadhaa, akaenda kukaa mbele ya kioo kikubwa na kisha akaanza kutoa risasi, ingawa alisikia maumivu ila alijitahidi mpaka akafanikisha, alafu akachukua dawa ya maji na kumwagia eneo la jeraha, kisha akaweka pamba na kujifunga bandeji begani, baada ya hapo alitoka na kwenda zake chumbani kwake, alimkuta Dokta Pendo amelala usingizi mzito, Sarah akabadili nguo na kuvaa za kulalia kisha akaingia ndani ya shuka na Kulala.



*****************



.



Trigger alivyompiga risasi Sarah, aliamua kukimbia baada ya kujua Sarah hajafa na kitu kingine ni kuwa Sarah alikuwa jirani na bastola, Trigger hakuona kitu cha kufanya, aliamua kukimbia, alishuka kwenye ngazi na kuitoa ngazi kisha akakimbia mpaka eneo la nje na kuchukua gari yake na kuondoka kwa kasi,



Alipofika kwake alichukua simu na kumtaharifu Harry kila kitu kilichotokea, Harry alishangaa sana, ila alimlaumu Trigger kwanini hakumuua Sarah!? Trigger alijitetea ila ilikuwa ngumu kwa Harry kumuelewa.



"huyu mpuuzi kweli, mbona yeye hakuwahi kumpiga hata ngumi, kazi kulaumu wenzake tu" Trigger aliongea baada ya Harry kukata simu, kisha Trigger akaingia chumbani kwake.



****************



Siku iliyofuata, nyakati za asubuhi, Harry aliamua kumtafuta Aisha, wakakutana kwenye mgahawa waliozoea kukutana,



"Aisha mimi sikuelewi, yaani sijui unachokifanya, hela umekula na Sarah anazidi kunisumbua tu" Harry aliongea kwa kulalamika,



"bado namfuatlia, tena kwa ukaribu sana, hata jana nilikuwa namfuatilia usiku ule wakati akikufuatilia, ila Trigger aliingilia nikaamua kuachana nae, uwa sipendi kuingiliwa kwenye mipango yangu" Aisha aliongea,



"alaah, kumbe ulikuwa unamfuatilia? basi endapo ungeendelea kumfuatilia ungemuua jana, maana Trigger alifanikiwa kumpiga mpaka risasi ila hajamuua" Harry aliongea,



"kwani ni lazima nianze kumuua Sarah? Taita nae si anatakiwa afe? Kwanini nisiangalie ni yupi anaweza kuwa mwepesi kuuawa kwa muda huu?" Aisha aliuliza,



"wote wanatakiwa kufa, fanya uwezavyo ila wote wafe" Harry aliongea,



"sawa, basi niachie hiyo kazi mimi" Aisha aliongea kwa kujiamini,



"sawa, cha muhimu uharakishe kutekeleza hayo yote" Harry aliweka msisitizo,



"nikupe muda gani wa utekelezaji?" Harry aliuliza,



"nimeshakuambia niachie mimi hiyo kazi, kwa hiyo hayo masuala ya utekelezaji yanahitaji mipango yangu, wewe subiri tu taharifa" Aisha alijibu,



"sawa, ila jua maisha yangu yako hatarini" Harry aliongea kwa hofu,



"hata ya kwangu pia, wewe unadhani huyo Sarah endapo nitamuendea hovyo na kunidhibiti, ataniacha?" Aisha aliuliza huku kamtumbulia macho Harry,



"sawa, fanya uwezavyo, na mimi nitafanya niwezavyo" Harry aliongea kwa upole,



"poa, acha nikuache" Aisha aliongea huku akiinuka katika kiti,



"haya" Harry alijibu huku akimuangalia namna Aisha anavyoondoka.



Baada ya dakika tano za Aisha kuondoka, Harry alimpigia simu Tekso, huyu ndiyo yule bwana wa mkuu wa technology katika mamlaka ya Taita. Ilimchukua dakika kumi tu za Tekso kufika, aliongozana na Trigger, walipofika waliagiza chai na kuendelea na maongezi,



"hivi Tekso huwezi kutengeneza bomu dogo lakini lenye mlipuko wa kuleta athari ndani ya umbali wa mita mita tano?" Harry aliuliza huku akimuangalia Tekso,



"udogo wa hilo bomu ni upi unaouzungumzia wewe? Ni kama kiazi mviringo au kama kizibo cha soda?" Tekso aliuliza kwa kujiamini,



"nadhani tupate yenye mlingano na kifungo cha koti la suti" Harry alijibu,



"hiyo inawezekana, nipe wiki moja na pia andaa pesa kidogo kwa ajili ya kununulia vifaa" Tekso aliongea,



"hilo bomu la kazi gani?" Trigger aliuliza,



"nataka ninunue nguo maalum na nitamshawishi Aisha awe anazivaa, na pia kifungo kimoja kitawekwa kinasa sauti ili niweze kumfuatilia" Harry alijibu,



"humuamini tena Aisha?" Trigger aliuliza,



"nahisi nina dalili hizo" Harry alijibu,



"ulimfahamia wapi?" Trigger aliuliza,



"nilikutana nae Congo, alikuwa anatumiwa kama jasus na majeshi ya waasi" Harry alijibu,



.



"mzee mimi niwaache" Tekso aliongea huku akiifunga laptop yake juu ya meza, Tekso kijana mwenye nywele nyingi zisizojua kitana wala chanuo ndani ya muda mrefu,



"umekuja na gari?" Harry alimuuliza,



"hapana, huyu bwana alinipa lift" Tekso aliongea huku akiwa amemshika bega Trigger



"unaenda wapi sasa muda huu?" Trigger alimuuliza,



"kufanya utaratibu wa kutengeneza huo mlipuko" Tekso alijibu,



"sawa, ngoja twende wote, maana sina kazi muda huu" Trigger aliongea huku nae akiinuka, alimfuata Tekso na kumuacha Harry akiwa amekaa pale pale mgahawani.



******************



BAADA YA MWEZI.



Siku hii ya leo, babu yake Sarah alikuwa hana raha kabisa, alikuwa yupo sebuleni na dokta Pendo wakitazamana runinga, Sarah yeye alikuwa yupo kazini.



Na kwa Nyakati hizi hali ya Dokta Pendo ilikuwa njema kiasi kwa maana hakuwa na bandeji ngumu miguuni, tayari zilishatolewa na siku hizi Dokta Pendo alikuwa anafanyishwa mazoezi machache ya kutembea kwa ajili ya kumuweka vizuri miguu yake,



"mzee mbona leo haupo sawa, una nini?" Dokta Pendo alimuuliza babu yake Sarah,



"nipo sawa, hivi ni wapi ulikutana wapi na huyu mwenzako, au alikuweka? Kwa maana mimi nimeanza kukuona wiki iliyopita tu na nikashangaa kuambiwa eti ulikuwepo kabla yangu" Babu yake Sarah aliuliza,



"Mimi ni rafiki yake tu, nipo muda mrefu tangu nimevunjika miguu" Dokta Pendo alijibu,



"ujue binti kuwa muwazi, huyu mwenzako mimi simuamini kabisa, kwanza tulikutana kama mateka, sijajua huyu mwanamke ni nani?" babu yake Sarah aliendelea kuongea,



"kwanza mzee umewaza nini mpaka uongee hivyo?" Dokta Pendo aliuliza huku akitabasamu,



"wewe binti kuwa muwazi, wewe ulitekwa hospitali na Mpaka leo vyombo vya usalama vinakutafuta, usibishe kuhusu hilo" Babu yake Sarah aliongea huku akitupa juu ya meza gazeti lenye habari za kutekwa Dokta Pendo na picha yake, Dokta Pendo akaishiwa pozi,



"ndio ni kweli huyu aliniteka, je unataka kunisaidia?" Dokta Pendo aliuliza kwa utulivu,



"tayari nimeshakusaidia" Babu yake Sarah aliongea huku akiwa hatanii,



"umenisaidiaje sasa, mbona mzee sikuelewi?" Dokta Pendo aliuliza huku akishangaa, ila kabla babu yake Sarah hajajibu, Sarah aliingia huku akitabasamu,



"aisee nimechelewa kidogo, ngoja nibadili nguo haraka twende mazoezini" Sarah aliongea kwa furaha,



"Mimi nilishajikatia tamaa ya kwenda uko mazoezini" Dokta Pendo alijibu huku akitabasamu,



"lakini kwema hapa?" Sarah aliuliza huku akielekea chumbani na kuwaacha hapo sebuleni.



"haya babu nielezee, umenisaidiaje sasa?" Dokta Pendo aliuliza huku akimuangalia babu yake Sarah,



"subiri utaona" Babu yake Sarah aliongea huku akitabasamu na kumfanya Dokta Pendo akae kimya tu, kwa maana hakuelewa kitu.



Baada ya nusu saa Sarah aliweza kutoka chumbani huku akiwa amevaa nguo za mazoezi na kwenda moja kwa moja kwenye friji na kuchukua juisi, akaimiminia kwenye kikombe na kuinywa kwa haraka,



"kuna habari gani mpya?" Sarah aliuliza huku akitabasamu



"hakuna mpya, habari ni zile zile" Babu alijibu huku akijichekesha,



"mmekula mmeshiba?" Sarah aliuliza huku akiendelea kutabasamu,



"tumeshiba mama, ila mama mpaka leo hajawahi kuniambia ni lini utanipeleka kwangu, maana naishi na wewe hata sikujui" Babu aliuliza kwa sauti kavu,



"tatizo nini mzee, si unakula na unalala vizuri tu, hayo masuala ya kujuana yatakuja mbele ya safari" Sarah aliongea huku akiweka utani,



"usiseme hivyo binti, kama suala la kula hata kwangu ningekula na Kulala vizuri tu" Babu aliongea kwa kujiamini,



"mzee usijifanye huna shida, mzee wewe toka amekufa mwanao Isack na maisha yako yalibadilika na kuwa mabaya sana" Sarah alitoa kauli iliyomshangaza babu yake,



"Isack, wewe umejuaje hayo yote?" Babu yake alimuuliza,



"Pendo twendezetu matizi, mzee anazingua" Sarah alipuuza swali la babu yake na kisha akamuongelesha Dokta Pendo,



"mjibu mzee kwanza" Dokta Pendo aliongea huku akicheka,



"twende bwana, ipo siku atapata majibu" Sarah aliongea huku akimsaidia Dokta Pendo kunyanyuka,



"ipo siku ee? Au utanijibia kituoni?" Babu yake Sarah aliuliza kama utani ila alikuwa amedhamilia,



"mzee leo husomeki ujue, umeonja nini?" Dokta Pendo aliuliza kwa utani,



"twende shoga, kwani alitoka leo?" Sarah alimuuliza Dokta Pendo huku wakitoka kwenye mlango wa sebuleni



"alitoka kuanzia asubuhi, amerudi muda sio mrefu" Dokta Pendo alijibu,



"alikuambia alipoenda?" Sarah aliuliza,



"hajaniambia, ila nahisi itakuwa alienda mjini, maana alirudi na gazeti ambalo lina picha yangu inaonesha nimepotea na natafutwa" Dokta Pendo aliongea na kisha akacheka,



"huyu mzee kichaa, ngoja nikirudi niongee nae, maana alivyo na akili finyu anaweza kwenda kutoa taharifa polisi, na hivi wametangaza na donge nono" Sarah aliongea huku akiushika mguu wa Sarah na kuuvusha kwenye geti.



"Sarah" Dokta Pendo aliita baada ya geti kufunguliwa,



"sema shoga" Sarah alijibu huku macho yake yakiwa bize kuuvusha mguu wa Dokta Pendo uliobakia ndani ya chuma cha geti,



"Sarah" Dokta Pendo aliita tena huku macho yakiwa mbele,



"unaniita, nahitika ila hata huongei" Sarah aliongea huku akirudishia geti, kisha akageuza shingo yake kuangalia mbele, kidogo aanguke kwa kitu alichokiona, walikuwa polisi zaidi ya kumi na wote walikuwa na silaha na walizinyoosha kuelekea sehemu aliposimama Sarah na dokta Pendo,



"wewe mtekaji weka mikono juu" Polisi mmoja aliyeonekana kiongozi aliongea huku akiwa amemkazia macho Sarah, Sarah akajikuta akiinua mikono juu huku na hakiwa hataki kuamini kama lile tukio ni la kweli kwa maana limetokea ghafla sana, alilazimisha iwe ndoto lakini haikuwezekana, Sarah maji yalizidi Unga. ........







Sarah akaamua atii amri ya polisi huku akishangaa hao polisi wamepajuaje nyumbani kwake?



"mfungeni pingu huyu muharifu" Kiongozi wa kikosi kile cha polisi alitoa amri ambayo askari wawili walimsogelea Sarah na kuchukua mikono yake na kuifunga pingu.



"naombeni muda kidogo niingie ndani nikaache maagizo" Sarah aliongea kwa huruma huku akimuangalia kiongozi wa kikosi kile cha polisi, ila kabla kiongozi yule hajatoa jibu, babu yake Sarah alitoka ndani huku akiwa kifua wazi na kujongea eneo ambalo Sarah na kiongozi wa polisi walikuwa wamesimama pamoja, Sarah alitegemea babu yake ameenda eneo lile kwa ajili yake, lakini cha kushangaza alishuhudia tukio lililomfungua ubongo, alimshuhudia babu yake akipeana mkono na yule kiongozi wa polisi,



"kazi nzuri mzee, tunamshukuru kwa taharifa yako iliyosaidia kumkamata muharifu" Kiongozi wa polisi aliongea kwa tabasamu pana,



"usijali kiongozi, sisi raia wema lazima tufichue maovu" Babu yake Sarah aliongea huku akitabasamu,



"mzee kumbe ni wewe ndio umeniletea polisi?" Sarah aliuliza huku akimuangalia babu yake,



"mpelekeni bwana, ananipigia kelele" Babu yake Sarah aliongea huku akigeuka nyuma,



"mzee mzigo wako uje uchukue kesho asubuhi, pale pale kituoni ulipotoa taharifa" Kiongozi wa kikosi kile cha polisi alimwambia babu yake Sarah,



"usijali, nitafika hiyo kesho mapema" Babu yake Sarah aliongea huku akirudi zake ndani ya geti.



Wale polisi walimpakia Sarah ndani ya gari huku Sarah akiwa na mawazo dhidi ya babu yake ingawa hakutaka kujenga chuki dhidi yake. Baada ya Sarah kupakiwa ndani ya gari, kupitia kwenye kioo cha gari aliweza kushuhudia Dokta Pendo nae akipakiwa kwenye gari nyingine, alimshuhudia Dokta Pendo akiwa na furaha huku akiongea na baadhi ya askari waliokuwa wanamsaidia kupanda gari. Sarah akawa anajitahidi kuangalia uso wa Dokta Pendo ili ajaribu kumsoma hisia zake, lakini haikuwezekana kwa maana muda wote macho ya Dokta Pendo yalikuwa makini na askari aliokuwa anaongea nao na alionekana akiongea kwa furaha huku akicheka, na hata Dokta Pendo alimpomtazama Sarah, wakikutanisha macho yao Dokta Pendo aliyakwapesha macho yake kwa haraka sana.



Safari iliishia ndani ya kituo cha polisi na Sarah akawekwa lupango. Dokta Pendo alipelekwa moja kwa moja katika ofisi na kuambiwa amsubiri mpelelezi ambaye atakuja kumfanyia mahojiano, lakini hiyo ofisi tayari Dokta Pendo aliijua vizuri hii ofisi, alikumbuka kuwa hii ni mara yake ya pili kuingia ofisini hapo, alijua fika kuwa ofisi hiyo ni ya Sajenti Minja.



Dokta Pendo akiwa amekaa akizungusha macho ndani ya ofisi ile, aliweza kushuhudia mlango ukifunguliwa na aliingia Sajenti Minja, Dokta Pendo akaachia tabasamu laini na kumfanya Sajenti Minja nae atabasamu huku akiwa anashangaa namna Dokta Pendo alivyonenepa. Sajenti Minja akampa mkono Dokta Pendo kisha akaenda kukaa kwenye kiti,



"kwanza pole" Sajenti Minja aliongea kwa utulivu,



"pole ya nini?" Dokta Pendo aliuliza huku akijifanya kushangaa,



"ya kutekwa, au unaona hilo sio tatizo?" Sajenti Minja aliuliza huku akijifanya kutabasamu,



"nani alitekwa??? Wewe unavyodhani Sarah anaweza kuniteka mimi?" Dokta Pendo aliuliza huku akijifanya kushangaa na kumshangaza zaidi Sajenti Minja,



"ndio alikuteka, alikuchukuaje hospitali bila taharifa na kwanini hakuwai kuniambia wewe ulipo ingalikuwa nimeshawahi kufika mara kadhaa nyumbani kwake?" Sajenti Minja aliuliza kwa ukali baada ya kuona kama Dokta Pendo anataka kumtetea Sarah,



"Mimi ndio nilimwambia aniondoe hospitali na mimi ndiye nilimwambia asimwambie mtu yoyote ni wapi nilipo" Dokta Pendo alijibu kwa kujiamini,



"usimtetee Sarah, unamteteaje mtu ambaye amehatarisha maisha yako?" Sajenti Minja aliongea kwa jazba,



"amehatarisha maisha yangu? Kivipi amehatarisha maisha yangu wakati alikuwa akinihudumia kwa kila kitu, ningekuwa kwenye matatizo ningenenepa hivi?" Dokta Pendo alihoji,



"ila inafikia kipindi unatakiwa uwe mkweli Pendo" Sajenti Minja aliongea huku akiwa amepunguza jazba,



"ukweli gani unaoutaka?" Dokta Pendo aliuliza,



"Sarah sio mtu mzuri, nisaidie kuthibitisha hilo" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Dokta Pendo,



"siwezi kuthibitisha kwa kuwa sijawahi kuuona ubaya wake" Dokta Pendo aliongea huku akicheka,



"sasa alikutoroshaje hospitali na camera zisiweze kuona hilo tukio, si ina maana alizichezea camera, na kama alizichezea, basi hiyo ina maana kuwa yule mwanamke ni muharifu mzoefu" Sajenti Minja aliongea huku akiwa na hasira,



"wewe hujui kitu, usiwe unaongea vitu kwa hisia tu. Sarah hayupo kama unavyomfikiria na siku ile mimi ndio nilimwambia aniondoe hospitali baada ya kuwaona wale watu walioniteka na kunivunja miguu wakiwa wanazunguka zunguka eneo lile, sasa labda huenda wale watu ndio walioharibu camera ili wafanye tukio eneo lile" Dokta Pendo aliongea na kumfanya Sajenti Minja ashushe pumzi ndefu,



"Mimi naona hatutaelewana hapa, ebu ngoja nikupeleke nyumbani ukapumzike, nitakuhoji kesho" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka kwenye kiti,



"nyumbani wapi?" Dokta Pendo aliuliza kwa mshangao,



"nyumbani kwako" Sajenti Minja alijibu huku akimshangaa,



"nyumbani siwezi kurudi, sio eneo salama kwangu, ninapotaka kwenda ni kwa Sarah tu, hapo ndipo palipo na usalama kwa muda huu" Dokta Pendo alizidi kumvuruga Sajenti Minja,



"sasa hata nikikupekeka kwa Sarah, nani atakuhudumia?" Sajenti Minja aliuliza,



"sasa hata ukinipeleka kwangu nani atanihudumia?" Dokta Pendo aliuliza,



"sasa unatakaje?" Sajenti Minja aliuliza,



"muacheni Sarah, kwa maana yeye ndiye mtu pekee anayeniangalia kwa ukaribu" Dokta Pendo alijibu na kumfanya Sajenti Minja akune kidevu chake,



"ni ngumu kumuacha Sarah kwa kuwa ni mtuhumiwa" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amesimama,



"mtuhumiwa wa nini? Kama kuondoka hospitali ni mimi ndiye nilietaka, kama hilo ni kosa, basi nikamatwe mimi" Dokta Pendo aliongea,



"basi ngoja nikupeleke hotelini, Sarah tutamuachia baadae, tunataka kumfanyia mahojiano" Sajenti Minja aliongea kwa lengo la kumfanya Dokta Pendo akubali kuondoka,



"naweza kuonana nae muda huu?" Dokta Pendo aliuliza,



"hapana, mtaonana baada ya mahojiano" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama Dokta Pendo,



"sawa, naomba msifanye kitu chochote" Dokta Pendo aliongea kwa msisitizo,



"usijali kuhusu hilo, twende nikupeleke hotelini utakaa mpaka jioni Sarah atapokuja" Sajenti Minja aliongea huku akimsaidia Dokta Pendo kumtoa kumpeleka nje, walipofika alimuingiza ndani ya gari na kumpeleka hotel iliyo karibu na kituo cha polisi na kumuacha Dokta Pendo hapo.



********************



Habari ya kukamatwa kwa Sarah ilimfikia Harry, akaamua awaite watu wake, Trigger, strategic, Tekso na Aisha.



"Sarah yupo kituo cha polisi, nimesikia amekamatwa kutokana na lile tukio la kumteka mtu hospitali" Harry aliongea,



"ni jambo zuri, au wewe mkuu unasemaje?" Trigger aliuliza,



"hivi hatuwezi kummalizia pale pale kituoni?" Harry aliuliza,



"inawezekana, kama tutatumia bomu kulipua kituo chote" Tekso aliongea huku akiwa bize kobonyeza lap top yake,



"sasa hapo mtaua mpaka wasiohusika, angalieni njia nyingine tofauti na hiyo ya kulipua" Aisha alitoa ushauri,



"basi tufanye kitu kimoja, Aisha unaweza kuingia ndani mule na kumtorosha Sarah?" Strategic aliuliza na kufanya wenzake wamshangae,



"una lengo gani?" Harry alimuuliza Strategic,



"kama tutafanikiwa kumtoa Sarah mikononi mwa polisi, itakuwa rahisi kumuangamiza akiwa chini yetu" Strategic aliongea,



"je Aisha unaweza kufanya hiyo kazi ya kumtorosha Sarah mikononi mwa polisi?" Harry alimuuliza Aisha,



"inawezekana, ila inahitaji akili sana, kwa hiyo kwa leo haiwezekani mpaka tutengeneze mipango" Aisha aliongea,



"hii kitu inahitajika ifanyike leo, tutakusaidia, nitakupa nguo yenye mawasiliano ambayo tutakuwa tunawasiliana" Tekso aliongea na kisha akamuangalia Harry, na Harry nae akamuangalia Tekso, kuna kitu kinaendelea kati ya hawa watu wawili,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sawa" Aisha alikubali kisha Tekso akanyanyuka na kuingia kwenye chumba kimoja na kurudi na kizibao, au wengi wamezoea kukiita kijamba koti, kisha akakitupa juu ya meza mbele ya Aisha,



"usiku ukienda kuvamia kituo cha polisi, utavaa hiki kikoti juu ya nguo yako, kineunganishwa na mawasiliano, nitakuwa eneo la polisi kukupa maelekezo" Tekso aliongea huku akikaa kwenye kiti, Aisha akakichukua kile kikoti na kuanza kukikagua, kilikuwa na vufungo vitatu vyenye rangi tofauti,



"hiki kifungo cha juu mbona kikubwa alafu kizito?" Aisha aliuliza baada ya kupata hofu,



"hicho kina camera, njia zote utazopita mimi nitakuwa naziona" Tekso alijibu, lakini ukweli ni kwamba kile kifungo kilikuwa na bomu,



"na hivi vifungo vingine vina nini?" Aisha aliuliza,



"kimoja cha katikati kina kinasa sauti, ila hicho cha chini hakina kitu, ni urembo tu" Tekso aliongea,



"naweza kuondoka na hili koti?" Aisha aliuliza huku akiendelea kulikagua,



"hapana, ikifika muda wa kazi utakuja kulichukua" Tekso alijibu,



"kwanini iwe hivyo?" Aisha aliuliza huku akimuangalia Tekso kwa jicho la udadisi,



"chukua nenda nalo" Harry alijibu baada ya kumuona Tekso akibabaika kutoa jibu,



"beba tu, haina shida" Tekso aliongea huku akitabasamu,



"nadhani tukutane saa mbili usiku, Vin hatakiwi kujulishwa huu mpango, mpaka ufanikiwe ndio tutamjulisha" Harry aliongea huku akiinuka kwenye kiti,



"vipi nikupeleke au una usafiri" Trigger alimuuliza Aisha,



"nipeleke", Aisha alijibu huku akiinuka kisha akatoka huku ameongozana na Trigger, ndani wakabaki Harry na Tekso na Strategic,



"sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kumpa Aisha nguo yenye bomu wakati anaenda kumdhibiti Sarah?" Strategic aliuliza,



"Mimi simuamini kabisa, nitatumia mwanya watapokuwa karibu na Sarah wakati wakitoroka, hapo nitalipua bomu, maana hatuna uwezo wa kumfunga Sarah bomu, acha tumtumie Aisha kama mtego" Harry aliongea huku akimuangalia Tekso,



"hatutofanya kosa kipindi hiki, remote ya Bomu nitakuwa nayo mimi" Tekso aliongea huku akiioneha remote ndogo iliyokuwa kwenye mfuko wake wa shati.



***********************



Mishale ya saa nne usiku, ndani ya gari alikuwepo Harry na Trigger waliokuwa siti ya mbele na siti ya nyuma walikuwepo Aisha na Tekso.



Walikuwa wanaelekea maeneo ya kituo cha polisi kwenda kumtorosha Sarah.



Na kwa upande wa kituo cha polisi Sarah alikuwa amewekwa juu ya kiti huku akiwa pembeni yake amekaa Sajenti Minja na askari mwingine ambaye walikuwa walikuwa wanamuhoji Sarah,



"je tukisema una hatia ya kumteka mgonjwa na kumtorosha ndani ya hospitali, utakubali?" Sajenti Minja alimuuliza Sarah, lakini Sarah hakujibu,



"huyu tumpige kidogo ili alainike, la sivyo atatusumbua sana" Askari mwingine aliekuwepo hapo aliongea kwa hasira,



"muache kwanza" Sajenti Minja aliongea huku akimsogelea jirani Sarah,



"sasa mtu gani tunamuuliza maswali muda wote na wala hajibu?" Askari mwingine alihoji huku akiona Sajenti Minja anamlea sana Sarah,



"Sarah, kesho itabidi upelekwe mahakamani, acha tufanye una hatia na una kesi ya kujibu" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama Sarah, ila Sarah hakujibu,



"mpige hata kofi" Askari aliongea huku akionekana kutamani sana kumuhadhibu Sarah,



"mpige" Sajenti Minja alimruhusu yule askari, yule askari akawa anamfuata Sarah kwa hasira, ila kabla hajamfikia wakasikia mlio wa bunduki nje ya ofisi, Sajenti Minja na mwenzake wakatizamana,



"kuna nini" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa hategemei jibu,



"nipo mimi" Aisha aliongea huku akiingia kwa fujo ndani ya ile ofisi na kufanya watu wote kuchanganyikiwa, Aisha alikuwa na bastola mbili mikononi,



"nipeni huyo mwanamke kwa amani au nipeni kwa kumwaga damu" Aisha aliongea huku bastola akiwa amewaelekezea Sajenti Minja na mwenzie,



"wewe ni nani unayetutisha polisi?" Askari mwingine aliuliza huku akimtazama Aisha, ila Aisha hakujibu alimfyatulia yule askari risasi ya kifua, akadondoka na kufa pale pale,



"mfungue huyo demu, au hujanielewa bado?" Aisha alimuuliza Sajenti Minja huku akitabasamu, wakati huo Sarah alikuwa ahamini ni kwa nini Aisha amekuja kumuokoa?



Sajenti Minja akamsogelea Sarah na kuanza kumuondoa pingu mkononi, kisha alipomaliza, Sarah akasimama,



"Sarah mfunge pingu huyo polisi" Aisha alitoa amri, Sarah akachukua mikono ya Sajenti Minja na kuifunga,



"nifuate" Aisha aliongea na Sarah akawa anamfuata kwa nyuma, njiani alipishana na askari kadhaa wakiwa wamefumgwa kamba na wengine wakiwa wamekufa, Sarah akawa anajiuliza hiyo shughuli yote amefanya Aisha?



Walifanikiwa kutoka mpaka nje, kisha Aisha akamshika mkono Sarah na kuanza kukimbia nae, walikimbia mpaka kwenye daraja walilokubaliana na wenzake, muda wote Tekso alikuwa juu ya jengo moja refu akiwasiliana na Harry huku akimuangalia Aisha,



"mkuu, wameshafika darajani" Tekso aliongea kupitia kifaa maalum, aliongea na Harry,



"walipue" Harry aliongea na kisha Tekso akatoa remote yake ndogo na kuishika mkononi, akatabasamu.



Harry Trigger walikuwa ndani ya gari wakimsubiri Tekso amalize kazi ili waondoke. Wakiwa hapo ukasikika mlipuko mkubwa mpaka gari yao ikatingishika, Harry akatabasamu na kisha akashusha kioo cha gari,



"good job" Harry aliongea huku akitabasamu, kwa maana kazi ilikuwa imeisha rasmi..............





Baada ya hapo, Harry na Trigger wakiwa ndani ya gari wakimsubiri Tekso, walikaa muda kidogo bila Tekso kutokea,



"atakuwa ameondoka nini?" Trigger aliuliza baada ya kusubiri kwa muda,



"na kwanini aondoke bila kutupa taharifa?" Harry aliuliza,



"si mlikuwa mnawasiliana lakini, muulize" Trigger aliongea,



"baada ya mlipuko mawasiliano yalikatika" Harry alijibu,



"tunapotezeana muda tu hapa" Trigger aliongea huku akiwasha gari,



"pita njia ya kule darajani tukashuhudie miili ya mabinti" Harry alimwambia Trigger,



"tutasikia kwenye taharifa ya habari" Trigger alijibu huku akigeuza gari, hakupita njia ya darajani, alipita njia tofauti kabisa na ile aliyoitaka Harry.



**************



Aisha na Sarah walivyotoka kituoni kwa polisi, walikimbilia mpaka darajani kwa chini, walivyofika Aisha akaangalia kwenye jengo moja refu, kisha akawa anavua kile kikoti alichopewa na Tekso, cha ajabu kile kikoti hakikuwa na kifungo cha juu kile kikubwa, wakati akivua kile kikoti Tekso alimuona kupitia darubini, alichofanya Tekso ni kubonyeza remote ya kulipua bomu kabla, baada ya hapo kikasikika kishindo kikubwa,



"suicide mission" Aisha aliongea huku akitazama juu ya jengo ambapo alikuwepo Tekso, kulikuwa kunawaka moto, kwa maana hiyo Tekso alijilipua mwenyewe, Sarah alikuwa akishangaa tu namna Aisha alivyokuwa anatabasamu,



"Hilo bomu ulitega wewe?" Sarah alimuuliza Aisha,



"wale washenzi walinitegea mimi kwenye kifungo kimoja cha hili koti, ila wakati tupo ndani ya gari nilikitoa kifungo bila wao kujua na kukipachika kwenye nywele ndefu za Tekso, sasa amejilipua yeye huku akijua ananilipua mimi" Aisha aliongea huku akiendelea kutabasamu,



"ni wenzako lakini, kwanini watake kukuua?" Sarah aliuliza,



"sio wenzangu, walinikodi tu nikuue wewe, sasa walivyoona nachelewa wakajua labda mimi na wewe ni kitu kimoja, wakanitegea bomu ili nikiwa na wewe ndio walipue" Aisha aliongea huku akikaa juu ya jiwe,



"kwanini wasingetulipua ndani ya kituo cha polisi!?" Sarah aliuliza,



"hawakutaka watu wengi wafe" Aisha alijibu,



"sasa pale bomu lilipolipukia si ni hotelini, sasa ndio wamekufa watu wengi zaidi?" Sarah aliuliza,



"sio kosa langu" Aisha alijibu,



"nyie wote wapuuzi, hamjui mnachokifanya, mmeua watu wengi kwa ajili ya ujinga wenu" Sarah aliongea kwa hasira huku akiondoka,



"sema asante sasa kwa kukutoa polisi na kukuepusha na mlipuko wa bomu" Aisha aliongea huku akicheka akimuangalia Sarah anavyoondoka,



"hata usingenitoa polisi, ningetoka mwenyewe katika muda niliotaka" Sarah aliongea huku akisimama na kumgeukia Aisha,



"nitakufumua malaya wewe" Aisha aliongea kwa utani huku akimnyooshea bunduki Sarah,



"piga, nimeshapigwa risasi nyingi tu" Sarah aliongea kwa jeuri kisha akageuka na kuondoka na kumuacha Aisha akitabasamu huku akitingisha kichwa chake.



Baada ya hapo Aisha alinyanyuka na kuondoka zake, alikuwa na hasira sana juu ya Harry, na wala hakutaka kumpigia simu ili amwambie bado yupo hai, alichofanya Aisha alielekea moja kwa moja nyumbani kwake, alipofika aliingia ndani na kuelekea moja kwa moja bafuni, akaondoa nguo zote na kuingia ndani ya sink, akafunga macho,



"Harry sitaki vita na wewe, ila ikinibidi nitafanya utakavyo, very easy kudili na wewe, huna mbinu hujui kupambana na wala hajui lolote kuhusu technology, unachojua ni sheria tu" Aisha aliongea huku povu la jakuzi likiwa limemmeza na kumuacha kichwa tu, tena sehemu ya uso.



*********************



Sajenti Minja akiwa amefungwa kamba na akiwa anamuangalia mwenzake ambaye alikuwa tayari marehemu tayari baada ya kupigwa risasi na Aisha.



Sajenti Minja akiwa anaangalia namna ya kujiokoa alishuhudia mtu akiingia ndani, alikuwa askari,



"hii hatari, pole kiongozi" Askari aliyeingia aliongea huku akimfungua Sajenti Minja,



"asante, uko nje kuko salama?" Sajenti Minja aliuliza,



"hakuna usalama kwa kweli, kuna askari wamepigwa, wengine wapo kwenye hali mbaya" Askari alijibu,



"mshike huyu miguuni mimi nimshike mikononi tumbebe tumpele hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akiishika mikono ya yule askari ambaye alikuwa amekufa. Wakambeba mpaka nje, koridoni alipishana na askari kadhaa wakiwa na majeraha na wengine wakipeana pole, wengine waliangua kilio baada ya kuuona mwili wa mwenzao ukibebwa na kupelekwa kwenye gari.



Sajenti Minja wakati akiendelea kuwasaidia kuwabeba majeruhi wengine, alipigiwa simu na mkubwa wake,



"upo wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza baada ya Sajenti Minja kupokea simu,



"nipo kituoni, tulivamiwa" Sajenti Minja alijibu kwa utulivu,



"mmevamiwa? na nani?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa mshangao,



"kuna mwanamke alituvamia na kumchukua yule mtuhumiwa tuliyekuwa tumemkamata kwa kesi ya kumteka na kumtorosha mgonjwa hospitali" Sajenti Minja alijibu,



"kuna uharibifu wowote umefanyika?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"ameua mtu askari mmoja na wengine kama nane wamejeruhiwa" Sajenti Minja aliongea,



"waandishi wa habari wamefika?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa wasiwasi,



"hapana" Sajenti Minja alijibu,



"hakikisheni hakuna mtu yoyote tofauti na nyie atakayejua hilo tukio, msimwambie mtu yoyote" Mkuu wa polisi aliongea kwa mamlaka,



"hakuna shida mkuu" Sajenti Minja aliongea kinyenyekevu,



"ila hicho sio nilichokupigia, sababu ya mimi kukupigia simu ni kutaka uende hoteli ya Rock Hill, kuna mlipuko umetokea muda sio mrefu" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa mkuu, naenda sasa hivi" Sajenti Minja aliongea,



"sawa, mimi nakuja hapo kituoni muda sio mrefu" Mkuu wa polisi aliongea kisha akakata simu.



"huu usiku wa leo wa ajabu sana" Sajenti Minja aliongea kisha akachukua gari yake na kuondoka kwenda kwenye hotel ya Rock Hill, haikuwa mbali na kituo cha polisi, ilikuwa ni jirani tu.



Baada ya muda mfupi Sajenti Minja aliweza kufika kwenye jengo la hotel na kukuta kikosi cha zima moto kikiwajibika katika kufanya kazi husika, bahati nzuri alikuta zimamoto wako kwenye hatua za mwisho za kuzima moto huo, Sajenti Minja akasogelea kundi la watu ambao walikuwa wamevaa Sare, alihisi ni wafanyakazi wa hotel ile,



"nyie ni wahusika?" Sajenti Minja aliuliza baada ya salamu,



"ndio" walijibu,



"Mimi ni askari, nani alikuwa zamu leo?" Sajenti Minja aliuliza,



"wote unaotuona hapa tulikuwa zamu leo" msichana mmoja alijibu,



"aliyekuwa msimamizi mkuu ni yupi?" Sajenti Minja aliuliza,



"ni mimi" Yule msichana akajibu tena,



"nifuate" Sajenti Minja aliongea kisha yule binti akamfuata, safari yao ikaishia mbele ya watu wa kikosi cha zima moto, wakasalimiana na Sajenti Minja, ni mtu ambaye wanamfahamu,



"sasa naombeni mtupeleke kule juu kwa kutumia winch lenu, kuna ukaguzi nataka kuufanya" Sajenti Minja aliongea kisha wale mabwana wa kikosi cha zimamoto wakafanya kama Sajenti Minja alivyotoka.



Wakafika mpaka eneo la juu kabisa ambapo sehemu ndogo ilikuwa imeharibika vibaya, walipofika juu waliweza kukuta mwili wa mtu ukiwa umeungua vibaya na mbaya zaidi baadhi ya vipande vya mwili wa huyo mtu vilikuwa vimetawanywa vibaya, yule binti ambaye ndiye msimamizi wa ile hotel ilimbidi aanze kulia kwa maana hajawahi kukutana na tukio la kutisha namna ile, ilibidi vijana kadhaa wa kikosi cha zima moto wamfariji.



Sajenti Minja katika kukagua kagua mwili ule, aliweza kuokota mkufu wa shaba uliokuwa na kidani kilichokuwa na herufi "S", Sajenti Minja akachukua kama ushahidi na kuweka ndani ya mfuko wa nylon, kisha akamgeukia yule binti ambaye ndiye msimamizi wa ile hotel,



"hiki chumba alipanga nani?" Sajenti Minja aliuliza,



"ni kijana mmoja, aliingia usiku huu" binti yule alijibu,



"jina lake nani?" Sajenti Minja aliuliza,



"jina tulikuwa bado hatujaandika kwa maana alitaka kwanza aangalie kama hiki chumba kitamfaa" Binti alijibu na kumfanya Sajenti Minja akunje uso kwa mshangao,



"huo utaratibu gani mnampa chumba mtu alafu jina mnamuandika baadae?" Sajenti Minja aliuliza,



"hotel yetu ina utaratibu huo" Binti alijibu, kisha Sajenti Minja akainama chini na kuokota kitu, ilikuwa ni saa,



"tushusheni chini, nimemaliza" Sajenti Minja aliongea na kisha wale vijana wa zimamoto wakatekeleza agizo la Sajenti Minja, wakamshusha chini akiwa pamoja na yule binti.



Walipofika chini, Sajenti Minja alikutana na waandishi habari ambao walimuhoji maswali machache na kisha akayajibu kwa namna anavyojua yeye, kisha akaingia kwenye gari yake na kuiwasha,



"leo mambo hayajaenda nitakavyo, ngoja nikamuone Dokta Pendo" Sajenti Minja aliongea huku akiwa ameegemea staring ya gari lake, kisha akanyanyua sura yake na kuondoa gari, ilikuwa safari ya kwenda hotelini, kwenda kumuona Dokta Pendo.



**********************



Baada ya Sarah kuachana na Aisha, Sarah hakuwaza kitu kingine, alichowaza muda huo ni hali ya Dokta Pendo, wala hakutaka kuwaza kuwa Dokta Pendo alijibu nini alipokuwa akihojiwa, aliamini tu kuwa Dokta Pendo ni mtu mwema kwake, kwa sababu ameshamsaidia kwenye hali nyingi tete.



Sarah akatembea mpaka kwenye eneo moja lililokuwa na watu wengi wakifanya shughuli mbalimbali usiku ule, alienda moja kwa moja kwenye duka dogo ambalo lilionekana likifanya biashara ya kuchajisha simu, aligundua kutokana na tangazo lililokuwa limebandikwa nje.



"naweza kupata huduma ya kupiga simu?" Sarah aliongea baada ya kumsalimia muuzaji,



"hapana, hatuna huduma hiyo" Muuzaji alijibu na kumfanya Sarah ashike kichwa kwa mawazo,



"naomba unisaidie, nitanunua vocha" Sarah aliongea kwa huruma,



"inaelekea una shida sana, tumia, ongea haraka maana salio linakata muda sio mrefu, nna sekunde ishirini tu" Muuzaji aliongea huku akimpa Sarah simu,



"sekunde ishirini ni nyingi sana" Sarah aliongea huku akiipokea ile simu, kisha akaandika namba ya Dokta Pendo, aliihifadhi kichwani, baada ya kuandika akapiga, simu ikaanza kuita,



"hallow" Dokta Pendo alipokea,



"Mimi Sarah, upo wapi?" Sarah aliuliza,



"nipo hotelini, njoo shoga yangu" Dokta Pendo aliongea kwa furaha,



"hotel gani shoga" Sarah aliuliza kisha Dokta Pendo akamuelekeza, Sarah akairudisha simu ya watu na kushukuru, kisha akaanza kutembea mdogo mdogo kwenda kwenye hiyo hotel aliyoelekezwa na dokta Pendo, hakuwa na pesa muda huo, pesa yote aliiacha kaunta ya polisi.



Sarah alifanikiwa kufika sehemu ya mapokezi ya hotel na kumuulizia mwenyeji wake, akapelekwa mpaka chumba alichopo Dokta Pendo, alipofika wakakumbatiana kwa furaha,



"kaoge kwanza shoga" Dokta Pendo alimwambia mwenzake,



"kwani ninanuka shoga?" Sarah aliuliza huku akicheka,



"kukaa selo ni mkosi, nenda kaoge na uzitupe hizo nguo" Dokta Pendo aliongea,



"nikizitupa nitavaa nini shoga?" Sarah aliuliza huku akielekea bafuni,



"tutajua baadae" Dokta Pendo aliongea wakati Sarah akiingia bafuni.



Baada ya dakika kumi na tano Sarah alikuwa amemaliza kuoga na alikuwa yupo kitandani amekaa na dokta Pendo,



"umetokaje polisi? Sajenti Minja amekuachia?" Dokta Pendo aliuliza,



"nina njaa kwanza, natakiwa nile alafu tutaongea baadae" Sarah aliongea,



"ngoja niwapige simu wahudumu, utakula chakula gani?" Dokta Pendo aliuliza,



"chai, alafu wali na samaki" Sarah alijibu,



"shoga unapenda chai wewe" Dokta Pendo aliongea huku akitabasamu kisha akachukua simu na kuwapigia wahudumu, akawaagiza wampelekee chakula.



"wakati tukiwa tunasubiri chakula, haya niambie umetokaje polisi?" Dokta Pendo aliuliza,



"Aisha, yule mwanamke wa kikosi cha Taita ndio aliyekuja kunitorosha" Sarah aliongea na kumfanya Dokta Pendo ashangae,



"kwanini Aisha, kwani mnajuana?" Dokta Pendo aliuliza kwa mshangao,



"sijui kitu shoga yangu, mimi mwenyewe bado najiuliza ingawa alinipa sababu" Sarah alijibu,



"sababu gani?" Dokta Pendo aliuliza,



"eti Aisha alitegewa bomu bila yeye kujua, wakataka aje kunitorosha, alafu ndio wamlipue tukiwa nae" Sarah alijibu na kipindi hicho mlango ulikuwa ukigongwa,



"chakula hicho kimekuja, kamfungulie" Dokta Pendo aliongea na kisha Sarah akainuka, akaenda mpaka mlangoni na kufungua mlango, mlango ulivyofunguka kidogo akimbie, alikutana na Sajenti Minja ambaye alikuja kumuangalia Dokta Pendo,



"wewe mpumbavu kumbe umekimbilia huku?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa amesimama mlangoni anamuangalia Sarah.........



**********ITAENDELEA**********



the Legend?

 Thanks

Quote

Reply

Report

Thanks Reactions:Kazetela, rip faza_nelly, marybaby and 7 others

the_legend

The_legend

JF-Expert Member

Joined Jan 14, 2019

 1,225  2,000

Mar 10, 2019

Add bookmark

#334

RIWAYA : SALA YA SARAH



MTUNZI : ALEX KILEO



SEHEMU YA AROBAINI NA TISA



ENDELEA..................



Sarah akawa anarudi nyuma huku akiwa anajiuliza afanye kitu cha kushtukiza au akae kimya na kujifanya mjinga?



Sajenti Minja akaingia ndani na kufunga mlango, kipindi hicho chote Dokta Pendo alikuwa akiangalia tu,



"ebu Kaa hapa shoga yangu" Dokta Pendo aliongea huku akiwa anaoneshea eneo la jirani na alipo yeye, Sarah akasogea na kukaa pembeni ya Dokta Pendo, aliamua kutulia tu,



"mwenzako yupo wapi?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa bado amesimama,



"yule sio mwenzangu, hata mimi simjui" Sarah alijibu,



"aisee safari hii utaozea jela, yaani mnavamia kituo na kuua askari?" Sajenti Minja aliuliza,



"huyo mwenzako anayeuliziwa ni yupi?" Dokta Pendo aliuliza huku akimuangalia Sarah,



"eti Aisha" Sarah alijibu huku akiwa na hofu,



"sasa Sarah na Aisha wapi na wapi? Mbona unatuchanganyia habari wewe?" Dokta Pendo aliongea kwa mshangao huku akimuangalia Sajenti Minja,



"muulize mwenyewe aseme ni kweli alitoroshwa na huyo mwanamke au ametoroka mwenyewe?" Sajenti Minja aliuliza,



"ebu fungua mlango huo, kuna mtu anagonga mlango" Dokta Pendo alimwambia Sajenti Minja aliyekuwa amesimama mlangoni, kisha Sajenti Minja akageuka na kufungua mlango, alikutana na muhudumu aliyekuwa amebeba chakula,



"kilete hapa" Sarah aliongea huku akikaa vizuri, yule Muhudumu akaisogeza meza iliyokuwa pembeni na kumsogezea Sarah, kisha akaweka chakula juu ya meza, alafu akaondoka zake,



"kula shoga yangu, najua una njaa sana" Dokta Pendo aliongea huku akimpiga piga Sarah mgongoni,



"we Sarah si nimekuuliza? Kama yule mwanamke humjui ni kwa nini amekutorosha?" Sajenti Minja aliuliza huku akiuzuia mkono wa Sarah uliokuwa unapeleka chakula kinywani,



"khaa jamani!!!! kula ni ibada sasa kwa nini unasumbua mwenzio?" Dokta Pendo aliuliza kwa huruma,



"wewe unataka kujua nini?" Sarah aliuliza kwa hasira huku akikitupa kijiko cha chakula,



"yule mwanamke ni nani kwako?" Sajenti Minja aliuliza,



"yule mwanamke ndiye aliyemteka Dokta Pendo na kumvunja miguu, yule mwanamke ameshawahi kutaka kunichinja mara mbili, na yule mwanamke ndiye yule uliyeniokoa kule Vin hotel aliyetaka kunidhuru. Una jingine?" Sarah aliuliza kwa hasira,



"kwanini sasa amekuja kukuokoa?" Sajenti Minja aliuliza,



"hakuja kuniokoa kama unavyosema, alikuja kunichukua ili akanidhuru" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja acheke kwa dhihaka, yaani aliona anadanganywa,



"sasa mbona upo hapa ukiwa mzima na hujadhurika?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kumaliza kucheka,



"hujasikia mlio wa bomu jirani na ofisi yenu?" Sarah aliuliza na kumfanya Sajenti Minja atege vizuri masikio yake,



"basi lile bomu lilitakiwa liniondoe mimi na yule mwanamke, yaani alitegewa yule mwanamke" Sarah aliongea,



"sasa kwanini akalipuka mtu mwingine?" Sajenti Minja aliuliza,



"yule ndiye aliyetega bomu, ila yule mwanamke aliyekuja pale polisi aligundua mapema ametegewa bomu, akatumia maarifa kumpachika lile lile bomu yule mtu aliyelipukiwa" Sarah aliongea na kumfanya Sajenti Minja apate mwanga,



"na kwanini watake kukuua wewe, una tatizo nao?" Sajenti Minja aliuliza,



"sina tatizo, labda wao wana tatizo na mimi" Sarah alijibu,



"maliza kula twende kituoni, utakuwa na mengi sana ya kunieleza" Sajenti Minja aliongea huku akikaa chini,



"wewe mtu vipi? Wewe unadhani kituoni kuzuri kule? wewe muhoji hapa hapa bwana" Dokta Pendo aliongea kwa ukali huku akimuangalia Sajenti Minja kwa jicho kali,



"wewe mbona unamtetea sana Sarah?" Sajenti Minja aliuliza kwa ukali,



"sioni kosa lake, mlimkamata kwa kudai ameniteka, mlivyonihoji nikakanusha hilo jambo, haya sasa hivi mnataka kumzushia kesi kubwa zaidi, eti ameshirikiana na mwenzie kumuua askari, hamna hata haya?" Dokta Pendo aliongea na kumfanya Sajenti Minja acheke,



"sasa wswe unatakaje?" Sajenti Minja aliuliza,



"Mimi huyu ni kama kijakazi wangu, ananiogesha na kunifanyia usafi wote unaohitajika, sasa ukimchukua huyu kwa kesi ya kumsingizia, utaniogesha wewe? Nikienda msalani utanisafisha?" Dokta Pendo aliuliza huku akiwa amemshikia kiuno Sajenti Minja,



"sawa yaishe, je mnaweza kunisaidia kumpata huyo Aisha?" Sajenti Minja aliuliza,



"tutampata wapi na sisi hatujui anapokaa" Dokta Pendo alijibu,



"Sarah nakuacha kwa sababu ya Dokta Pendo, sasa ninachokuomba usirudi kwako mpaka nikupe taharifa, maana ni lazima askari waende kukagua au kukuwinda maeneo ya kule kwako" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Sarah,



"yaani nakosa uhuru kwa jambo ambalo sijalifanya?" Sarah aliuliza huku akisikitika,



"bwana wewe shukuru tu, bora uishi kwa kujificha kuliko kuishi mule selo" Dokta Pendo aliongea huku akijilaza,



"sasa mimi ninaondoka, nitarudi kesho kuwaambia kinachoendelea uko kituoni" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka,



"sawa baba" Dokta Pendo alijibu,



"haya, mbaki Salama" Sajenti Minja aliongea huku akitoka nje,



"asante, na wewe pia" Dokta Pendo alijibu Wakati Sajenti Minja akifunga mlango.



"asante shoga, maana mmh" Sarah aliongea huku akiwa ahamini kama Sajenti Minja amemuacha,



"usijali shoga, tutaongea kesho, acha nilale maana nimechoka kweli" Dokta Pendo aliongea,



"sawa, mimi mwenyewe nikimaliza tu kula nalala" Sarah aliongea huku akiendelea kula.



**************************



.



Asubuhi hii bado Harry hakuweza kupata habari yoyote kuhusu Tekso, na kila alipojaribu kupiga namba yake ikawa hazipatikani. Harry akiwa ofisini kwake alishuhudia simu yake ikipokea ujumbe mfupi wa maneno, alipotazama jina la mtu aliyetuma huo ujumbe, kidogo ashtuke, aliona jina la Aisha, Harry akaichukua simu yake na kuufungua huo ujumbe,



"ulidhani nitakufa?" ujumbe uliandikwa hivyo na kumfanya sasa Harry achanganyikiwe, hakutegemea kabisa kusikia leo hii Aisha yupo hai. Harry akajaribu kupiga namba ya Aisha ili ampoze, ila siku iliita bila kupokelewa, akajaribu tena na tena ila hali ikawa ile ile, na mwisho kabisa simu ya Aisha ikawa haipatikani,



"huyu hajafa kweli au kuna mtu ananichezea?" Harry alijiuliza huku akirudia kuusoma ule ujumbe uliotumwa na Aisha, akajikuta anatabasamu mwenyewe.



Na muda huo huo akaingia Trigger, ujio haukuwa wa kawaida ule, aliingia akihema juu juu na kumfanya Harry amtolee macho,



"nina habari ya kushangaza sana" Trigger aliongea huku akikaa kwenye kiti,



"Mimi niliyonayo inashangaza zaidi" Harry aliongea kwa utulivu huku akimuangalia Trigger,



"wewe unayo ipi?" Trigger aliuliza,



"Aisha hajafa, yupo hai" Harry aliongea na kufanya Trigger amtumbulie macho,



"basi habari hiyo na habari yangu zinafanana" Trigger aliongea huku akijifuta jasho,



"wewe habari uliyonayo ni ipi?" Harry aliuliza,



"Tekso ndiye aliyelipuliwa bomu ile jana usiku" Trigger aliongea na kumfanya Harry ajishike mdomo,



"wewe nani kakwambia?" Harry aliuliza,



"angalia taharifa za habari, ile chini na saa anayovaa ndio vilivyokutwa baada ya kupekua eneo la mlipuko" Trigger aliongea na kumfanya Harry wasiwasi umuongezeke,



"mbona nakiona kifo changu" Harry aliongea kwa uoga huku akitetemeka,



"unasema?" Trigger alimuuliza baada ya kuhisi hamuelewi,



"hamna, Taita anaendeleaje?" Harry aliamua kubadili mada,



"ametolewa leo kwenye chumba cha watu mahututi, amepelekwa wodi ya kawaida" Trigger alijibu na kumfanya Harry ashtuke, maana muda wote wakati Taita yupo mahututi, Harry alikuwa anaomba Taita afe tu kwa maana alikuwa anamnyima amani,



"jambo jema, nitaenda baadae kumuona" Harry aliongea kinyoge huku mawazo yakiwa yamemtawala,



"sasa mimi naondoka, nilikuletea tu hiyo habari" Trigger aliongea huku akinyanyuka,



"na kuhusu Tekso tunafanyaje" Harry aliuliza,



"ndio naenda kufuatilia, then niwataharifu ndugu zake" Trigger alijibu,



"sawa, fanya hivyo" Harry aliongea na kumuacha Trigger akiondoka.



"sasa si bora nimuue Taita kwa mikono yangu mwenyewe, nitaishi vipi sasa, nataka kuwa huru" Harry aliongea huku akijikuna nywele zake,



"lazima niue, nimuue ninaemuweza, Aisha simuwezi, Sarah simuwezi, Taita nitajaribu" Harry aliongea peke yake huku akiinuka kwenye kiti.



*******************



Asubuhi sana Sarah aliwahi kudamka, akamuamsha na dokta Pendo,



"sasa acha mimi nyumbani mara moja, natakiwa nibadili nguo niende kazini, leo kuna mkataba itabidi niusaini mimi kama mkurugenzi mkuu wa kampuni" Sarah aliongea huku akimuangalia Dokta Pendo,



"sasa kwani lazima uende nyumbani? Nguo si unanunua mjini unabadilishia dukani?" Dokta Pendo aliuliza,



"yaani kwenda nyumbani lazima niende tu, kwanza nafuata kadi ya kutolea pesa, kwa maana hapa sina hela, pili kuna baadhi ya nyaraka natakiwa nizifuate, zipo nyumbani" Sarah aliongea,



"hapo siwezi kukuzuia, sasa usingetoka jana usiku, hiyo mikataba ingesainiwa na nani uko ofisini kwako?" Dokta Pendo aliuliza,



"lazima ningetoka, tayari nilikuwa na mipango yangu kichwani" Sarah aliongea huku akicheka,



"poa bwana, kuwa muangalifu, hutakiwi kujionesha sana mtaani, si unajua bado unatafutwa?" Dokta Pendo alimtahadharisha Sarah,



"usijali shoga yangu, nitawahi kurudi nije nikusaidie kukuogesha" Sarah aliongea huku akisimama,



"sawa shoga yangu" Dokta Pendo aliongea,



"haya, kwaheri" Sarah aliongea huku akimbusu Dokta Pendo kwenye paji la uso, kisha akatoka zake.



Alitembea mpaka nje ya jengo la hotel, akachukua bajaj iliyomfikisha nyumbani kwake, kisha akaingia ndani na kuchukua pesa, akamlipa dereva wa bajaji na kisha dereva wa bajaj akaondoka zake, Sarah akarudi ndani, akampita babu yake sebuleni, babu alikuwa akiangalia TV, ila alivyoomuona Sarah babu alipatwa na hofu, aliogopa.



Sarah akapitiliza chumbani kwake bila kuongea kitu, kisha akaingia bafuni kuoga.



Huku sebuleni babu akataka kutoka kukimbia, ila alipojaribu kufungua mlango ila mlango haukufunguka, babu hofu ikaongezeka, babu akachukua simu yake ili awapigie simu polisi, akakuta mtandao hamna, Sarah alizuia mawasiliano yote yanayoingia na kutoka ndani ya nyumba yake.



Babu yake Sarah akaona hali ngumu, akamkimbilia chumbani kwake na kujifungia, Sarah alikuwa anayoona yote kwenye runinga ndogo iliyopo bafuni kwake, alikuwa ametega camera kila sehemu ya nyumba yake.



Sarah alivyomaliza kuoga alitoka bafuni na kuvaa nguo zake, kisha akafungua kabati na kutoa nyaraka kadhaa, akazikagua na kuzirudisha kwenye bahasha ya kaki, kisha akatoka mpaka sebuleni na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha babu yake, alitumia funguo kufungua na kumkuta babu yake akiwa amejikunyata kitandani,



"chukua hii, utatumia kwa ajili ya kununua chakula" Sarah aliongea huku akitupa noti mbili za elfu kumi kwenye sakafu, kisha Sarah akawa anatoka nje, alivyofungua tu geti ili atoe gari, alishtuka akikamatwa mkono,



"wewe ndio umeua askari na kutoroka kituoni?" Sauti iliongea huku akiivuta mikono ya Sarah, Sarah alipotupa jicho kumuangalia huyo mtu, akakuta ni askari wakiwa watano wakiwa wamemzunguka na mmoja ndiyo huyo alikuwa amemshika mkono.............................



Sarah akawa anarudi nyuma huku akiwa anajiuliza afanye kitu cha kushtukiza au akae kimya na kujifanya mjinga?



Sajenti Minja akaingia ndani na kufunga mlango, kipindi hicho chote Dokta Pendo alikuwa akiangalia tu,



"ebu Kaa hapa shoga yangu" Dokta Pendo aliongea huku akiwa anaoneshea eneo la jirani na alipo yeye, Sarah akasogea na kukaa pembeni ya Dokta Pendo, aliamua kutulia tu,



"mwenzako yupo wapi?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa bado amesimama,



"yule sio mwenzangu, hata mimi simjui" Sarah alijibu,



"aisee safari hii utaozea jela, yaani mnavamia kituo na kuua askari?" Sajenti Minja aliuliza,



"huyo mwenzako anayeuliziwa ni yupi?" Dokta Pendo aliuliza huku akimuangalia Sarah,



"eti Aisha" Sarah alijibu huku akiwa na hofu,



"sasa Sarah na Aisha wapi na wapi? Mbona unatuchanganyia habari wewe?" Dokta Pendo aliongea kwa mshangao huku akimuangalia Sajenti Minja,



"muulize mwenyewe aseme ni kweli alitoroshwa na huyo mwanamke au ametoroka mwenyewe?" Sajenti Minja aliuliza,



"ebu fungua mlango huo, kuna mtu anagonga mlango" Dokta Pendo alimwambia Sajenti Minja aliyekuwa amesimama mlangoni, kisha Sajenti Minja akageuka na kufungua mlango, alikutana na muhudumu aliyekuwa amebeba chakula,



"kilete hapa" Sarah aliongea huku akikaa vizuri, yule Muhudumu akaisogeza meza iliyokuwa pembeni na kumsogezea Sarah, kisha akaweka chakula juu ya meza, alafu akaondoka zake,



"kula shoga yangu, najua una njaa sana" Dokta Pendo aliongea huku akimpiga piga Sarah mgongoni,



"we Sarah si nimekuuliza? Kama yule mwanamke humjui ni kwa nini amekutorosha?" Sajenti Minja aliuliza huku akiuzuia mkono wa Sarah uliokuwa unapeleka chakula kinywani,



"khaa jamani!!!! kula ni ibada sasa kwa nini unasumbua mwenzio?" Dokta Pendo aliuliza kwa huruma,



"wewe unataka kujua nini?" Sarah aliuliza kwa hasira huku akikitupa kijiko cha chakula,



"yule mwanamke ni nani kwako?" Sajenti Minja aliuliza,



"yule mwanamke ndiye aliyemteka Dokta Pendo na kumvunja miguu, yule mwanamke ameshawahi kutaka kunichinja mara mbili, na yule mwanamke ndiye yule uliyeniokoa kule Vin hotel aliyetaka kunidhuru. Una jingine?" Sarah aliuliza kwa hasira,



"kwanini sasa amekuja kukuokoa?" Sajenti Minja aliuliza,



"hakuja kuniokoa kama unavyosema, alikuja kunichukua ili akanidhuru" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja acheke kwa dhihaka, yaani aliona anadanganywa,



"sasa mbona upo hapa ukiwa mzima na hujadhurika?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kumaliza kucheka,



"hujasikia mlio wa bomu jirani na ofisi yenu?" Sarah aliuliza na kumfanya Sajenti Minja atege vizuri masikio yake,



"basi lile bomu lilitakiwa liniondoe mimi na yule mwanamke, yaani alitegewa yule mwanamke" Sarah aliongea,



"sasa kwanini akalipuka mtu mwingine?" Sajenti Minja aliuliza,



"yule ndiye aliyetega bomu, ila yule mwanamke aliyekuja pale polisi aligundua mapema ametegewa bomu, akatumia maarifa kumpachika lile lile bomu yule mtu aliyelipukiwa" Sarah aliongea na kumfanya Sajenti Minja apate mwanga,



"na kwanini watake kukuua wewe, una tatizo nao?" Sajenti Minja aliuliza,



"sina tatizo, labda wao wana tatizo na mimi" Sarah alijibu,



"maliza kula twende kituoni, utakuwa na mengi sana ya kunieleza" Sajenti Minja aliongea huku akikaa chini,



"wewe mtu vipi? Wewe unadhani kituoni kuzuri kule? wewe muhoji hapa hapa bwana" Dokta Pendo aliongea kwa ukali huku akimuangalia Sajenti Minja kwa jicho kali,



"wewe mbona unamtetea sana Sarah?" Sajenti Minja aliuliza kwa ukali,



"sioni kosa lake, mlimkamata kwa kudai ameniteka, mlivyonihoji nikakanusha hilo jambo, haya sasa hivi mnataka kumzushia kesi kubwa zaidi, eti ameshirikiana na mwenzie kumuua askari, hamna hata haya?" Dokta Pendo aliongea na kumfanya Sajenti Minja acheke,



"sasa wswe unatakaje?" Sajenti Minja aliuliza,



"Mimi huyu ni kama kijakazi wangu, ananiogesha na kunifanyia usafi wote unaohitajika, sasa ukimchukua huyu kwa kesi ya kumsingizia, utaniogesha wewe? Nikienda msalani utanisafisha?" Dokta Pendo aliuliza huku akiwa amemshikia kiuno Sajenti Minja,



"sawa yaishe, je mnaweza kunisaidia kumpata huyo Aisha?" Sajenti Minja aliuliza,



"tutampata wapi na sisi hatujui anapokaa" Dokta Pendo alijibu,



"Sarah nakuacha kwa sababu ya Dokta Pendo, sasa ninachokuomba usirudi kwako mpaka nikupe taharifa, maana ni lazima askari waende kukagua au kukuwinda maeneo ya kule kwako" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Sarah,



"yaani nakosa uhuru kwa jambo ambalo sijalifanya?" Sarah aliuliza huku akisikitika,



"bwana wewe shukuru tu, bora uishi kwa kujificha kuliko kuishi mule selo" Dokta Pendo aliongea huku akijilaza,



"sasa mimi ninaondoka, nitarudi kesho kuwaambia kinachoendelea uko kituoni" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka,



"sawa baba" Dokta Pendo alijibu,



"haya, mbaki Salama" Sajenti Minja aliongea huku akitoka nje,



"asante, na wewe pia" Dokta Pendo alijibu Wakati Sajenti Minja akifunga mlango.



"asante shoga, maana mmh" Sarah aliongea huku akiwa ahamini kama Sajenti Minja amemuacha,



"usijali shoga, tutaongea kesho, acha nilale maana nimechoka kweli" Dokta Pendo aliongea,



"sawa, mimi mwenyewe nikimaliza tu kula nalala" Sarah aliongea huku akiendelea kula.



**************************



.



Asubuhi hii bado Harry hakuweza kupata habari yoyote kuhusu Tekso, na kila alipojaribu kupiga namba yake ikawa hazipatikani. Harry akiwa ofisini kwake alishuhudia simu yake ikipokea ujumbe mfupi wa maneno, alipotazama jina la mtu aliyetuma huo ujumbe, kidogo ashtuke, aliona jina la Aisha, Harry akaichukua simu yake na kuufungua huo ujumbe,



"ulidhani nitakufa?" ujumbe uliandikwa hivyo na kumfanya sasa Harry achanganyikiwe, hakutegemea kabisa kusikia leo hii Aisha yupo hai. Harry akajaribu kupiga namba ya Aisha ili ampoze, ila siku iliita bila kupokelewa, akajaribu tena na tena ila hali ikawa ile ile, na mwisho kabisa simu ya Aisha ikawa haipatikani,



"huyu hajafa kweli au kuna mtu ananichezea?" Harry alijiuliza huku akirudia kuusoma ule ujumbe uliotumwa na Aisha, akajikuta anatabasamu mwenyewe.



Na muda huo huo akaingia Trigger, ujio haukuwa wa kawaida ule, aliingia akihema juu juu na kumfanya Harry amtolee macho,



"nina habari ya kushangaza sana" Trigger aliongea huku akikaa kwenye kiti,



"Mimi niliyonayo inashangaza zaidi" Harry aliongea kwa utulivu huku akimuangalia Trigger,



"wewe unayo ipi?" Trigger aliuliza,



"Aisha hajafa, yupo hai" Harry aliongea na kufanya Trigger amtumbulie macho,



"basi habari hiyo na habari yangu zinafanana" Trigger aliongea huku akijifuta jasho,



"wewe habari uliyonayo ni ipi?" Harry aliuliza,



"Tekso ndiye aliyelipuliwa bomu ile jana usiku" Trigger aliongea na kumfanya Harry ajishike mdomo,



"wewe nani kakwambia?" Harry aliuliza,



"angalia taharifa za habari, ile chini na saa anayovaa ndio vilivyokutwa baada ya kupekua eneo la mlipuko" Trigger aliongea na kumfanya Harry wasiwasi umuongezeke,



"mbona nakiona kifo changu" Harry aliongea kwa uoga huku akitetemeka,



"unasema?" Trigger alimuuliza baada ya kuhisi hamuelewi,



"hamna, Taita anaendeleaje?" Harry aliamua kubadili mada,



"ametolewa leo kwenye chumba cha watu mahututi, amepelekwa wodi ya kawaida" Trigger alijibu na kumfanya Harry ashtuke, maana muda wote wakati Taita yupo mahututi, Harry alikuwa anaomba Taita afe tu kwa maana alikuwa anamnyima amani,



"jambo jema, nitaenda baadae kumuona" Harry aliongea kinyoge huku mawazo yakiwa yamemtawala,



"sasa mimi naondoka, nilikuletea tu hiyo habari" Trigger aliongea huku akinyanyuka,



"na kuhusu Tekso tunafanyaje" Harry aliuliza,



"ndio naenda kufuatilia, then niwataharifu ndugu zake" Trigger alijibu,



"sawa, fanya hivyo" Harry aliongea na kumuacha Trigger akiondoka.



"sasa si bora nimuue Taita kwa mikono yangu mwenyewe, nitaishi vipi sasa, nataka kuwa huru" Harry aliongea huku akijikuna nywele zake,



"lazima niue, nimuue ninaemuweza, Aisha simuwezi, Sarah simuwezi, Taita nitajaribu" Harry aliongea peke yake huku akiinuka kwenye kiti.



*******************



Asubuhi sana Sarah aliwahi kudamka, akamuamsha na dokta Pendo,



"sasa acha mimi nyumbani mara moja, natakiwa nibadili nguo niende kazini, leo kuna mkataba itabidi niusaini mimi kama mkurugenzi mkuu wa kampuni" Sarah aliongea huku akimuangalia Dokta Pendo,



"sasa kwani lazima uende nyumbani? Nguo si unanunua mjini unabadilishia dukani?" Dokta Pendo aliuliza,



"yaani kwenda nyumbani lazima niende tu, kwanza nafuata kadi ya kutolea pesa, kwa maana hapa sina hela, pili kuna baadhi ya nyaraka natakiwa nizifuate, zipo nyumbani" Sarah aliongea,



"hapo siwezi kukuzuia, sasa usingetoka jana usiku, hiyo mikataba ingesainiwa na nani uko ofisini kwako?" Dokta Pendo aliuliza,



"lazima ningetoka, tayari nilikuwa na mipango yangu kichwani" Sarah aliongea huku akicheka,



"poa bwana, kuwa muangalifu, hutakiwi kujionesha sana mtaani, si unajua bado unatafutwa?" Dokta Pendo alimtahadharisha Sarah,



"usijali shoga yangu, nitawahi kurudi nije nikusaidie kukuogesha" Sarah aliongea huku akisimama,



"sawa shoga yangu" Dokta Pendo aliongea,



"haya, kwaheri" Sarah aliongea huku akimbusu Dokta Pendo kwenye paji la uso, kisha akatoka zake.



Alitembea mpaka nje ya jengo la hotel, akachukua bajaj iliyomfikisha nyumbani kwake, kisha akaingia ndani na kuchukua pesa, akamlipa dereva wa bajaji na kisha dereva wa bajaj akaondoka zake, Sarah akarudi ndani, akampita babu yake sebuleni, babu alikuwa akiangalia TV, ila alivyoomuona Sarah babu alipatwa na hofu, aliogopa.



Sarah akapitiliza chumbani kwake bila kuongea kitu, kisha akaingia bafuni kuoga.



Huku sebuleni babu akataka kutoka kukimbia, ila alipojaribu kufungua mlango ila mlango haukufunguka, babu hofu ikaongezeka, babu akachukua simu yake ili awapigie simu polisi, akakuta mtandao hamna, Sarah alizuia mawasiliano yote yanayoingia na kutoka ndani ya nyumba yake.



Babu yake Sarah akaona hali ngumu, akamkimbilia chumbani kwake na kujifungia, Sarah alikuwa anayoona yote kwenye runinga ndogo iliyopo bafuni kwake, alikuwa ametega camera kila sehemu ya nyumba yake.



Sarah alivyomaliza kuoga alitoka bafuni na kuvaa nguo zake, kisha akafungua kabati na kutoa nyaraka kadhaa, akazikagua na kuzirudisha kwenye bahasha ya kaki, kisha akatoka mpaka sebuleni na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha babu yake, alitumia funguo kufungua na kumkuta babu yake akiwa amejikunyata kitandani,



"chukua hii, utatumia kwa ajili ya kununua chakula" Sarah aliongea huku akitupa noti mbili za elfu kumi kwenye sakafu, kisha Sarah akawa anatoka nje, alivyofungua tu geti ili atoe gari, alishtuka akikamatwa mkono,



"wewe ndio umeua askari na kutoroka kituoni?" Sauti iliongea huku akiivuta mikono ya Sarah, Sarah alipotupa jicho kumuangalia huyo mtu, akakuta ni askari wakiwa watano wakiwa wamemzunguka na mmoja ndiyo huyo alikuwa amemshika mkono.............................

Sarah akaona sasa kama akifanya uzembe anaweza kukosa kusaini mikataba ya kampuni yake,



"nitaenda mwenyewe, usinifunge pingu" Sarah aliongea huku akiivuta mikono yake kutoka kwa askari yule aliyemshika,



"wewe mwanamke usitupangie cha kufanya, usitufundishe kazi wewe" Askari yule aliongea huku akiivuta mikono ya Sarah na kutaka kuifunga pingu,



"usimfunge pingu, pingu ya nini wakati tupo sita hapa, alafu tumuhofie mwanamke mmoja tu?" Askari mwingine Aliuliza na kumfanya mwenzake asitishe zoezi la kumfunga Sarah pingu, na hicho ndicho kitu Sarah alikihitaji,



"songa mbele" Yule askari aliyetaka kumfunga Sarah pingu aliongea huku akimsukuma Sarah mgongoni, Sarah hakukasirika, badala yake alifurahi, alitembea hatua ndogo ndogo huku akiivuta sketi yake juu taratibu huku akizidi kuisogelea gari ya polisi, Sarah akainama na kuishika sketi eneo la mpasuo na kuvuta kidogo na kufanya mpasuo kuongezeka kidogo, kisha Sarah akatumia mwanya wa askari kushangaa anachofanya, Sarah akamvuta askari wa nyuma na kumpiga ngumi ya koromeo, yule askari akaangukia chini na kuanza kugala gala chini huku amejishika koo, askari mmoja akatoa bastola haraka, Sarah alikuwa na kasi zaidi ya haraka ya huyo askari, Sarah akaruka juu na kutua mbele ya askari yule, kisha akaudaka mkono wa yule askari na kisha akaupiga ngumi kwenye kiwiko, mkono wa yule askari ukastuka na kuiacha ile bastola, Sarah akaidaka na kisha akaachia teke lililompeleka yule askari chini, wale askari wengine wakataka na wao kutoa bastola,



"mi nawaua, mtu akichomoa tu silaha mi ninammaliza" Sarah aliongea huku akiwaelekezea bastola, wale askari wakawa wamesimama huku mikono yao ikiwa inataka kuelekea kwenye silaha zao.



Askari mmoja akataka kupuuza agizo la Sarah, akachomoa bastola yake, Sarah akamfyatulia risasi ya mkono iliyoondoka na kidole chake, yule askari akapiga ukelele wa maumivu huku akiwa ahamini kitendo kilichotokea,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"tupeni bastola chini" Sarah aliongea huku akiwaangalia, askari wakatii agizo na kuzirusha zile silaha mbele ya Sarah, Sarah akaziokota na kuziweka kwenye mkoba wake, kisha akapiga risasi tairi za mbele za gari waliyokuja nayo polisi, kisha akaingia kwenye gari yake na kuiwasha,



"nitakuja mwenyewe kituoni" Sarah aliongea huku akiwatizama polisi kisha akawasha gari na kuliondoa kwa kasi na kumuacha babu yake akichungulia getini huku akiwa anashangaa kitendo wanachofanyiwa polisi.



****************



Sajenti Minja alikuwa na dokta Pendo, alienda kumjulia hali na pia alienda kumjulisha Sarah kuwa kuna askari wataenda kwake asubuhi,



"Sarah yupo wapi?" Sajenti Minja aliuliza,



"Sarah ameenda kwake, anadai anatakiwa aende kazini kuna kazi muhimu" Dokta Pendo alijibu,



"aisee, atakuwa ameshakamatwa, kuna askari wametumwa kwenda kumkamata" Sajenti Minja aliongea huku akiwa hana tumaini,



"nenda basi kamsaidie" Dokta Pendo aliongea huku akiwa anataka kulia,



"Mimi nitamsaidiaje sasa?" Sajenti Minja aliuliza,



"nenda, au ngoja nimpigie simu" Dokta Pendo aliongea huku akibonyeza simu yake,



"simu yake ipo polisi, au ana namba nyingine?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia Dokta Pendo,



"dah, sasa tunafanyaje?" Dokta Pendo aliuliza huku akiwa amekata tamaa, na kipindi hicho simu ya Sajenti Minja ilikuwa ikiita,



"bosi huyo ananipigia, sijui kuna nini?" Sajenti Minja aliuliza huku akiiangalia simu yake,



"naam mkuu" Sajenti Minja aliongea baada ya kupokea simu,



"upo wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"nipo njiani naelekea kituoni" Sajenti Minja alijibu,



"unapajua kwa yule dada aliyetoroshwa jana kituoni?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"ndio napajua" Sajenti Minja alijibu,



"nenda haraka" Mkuu wa polisi alitoa amri na Sajenti Minja hakutaka kuhoji zaidi, alijua lazima kuna tukio limetokea ambalo ni tofauti.



"Sarah kuna kitu kimetokea nyumbani kwake" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka,



"atakuwa amekamatwa eee?" Dokta Pendo aliuliza kwa wasiwasi,



"sijajua, nimeambiwa tu niende" Sajenti Minja aliongea,



"ebu nenda, alafu unijulishe" Dokta Pendo aliongea huku akiwa bado na wasiwasi.



Sajenti Minja akatoka na kuelekea nje, kisha akaingia kwenye gari na akashika uelekeo unaenda nyumbani kwa Sarah, njia yote alikuwa anawaza kuna tukio gani gani limetokea uko.



Sajenti Minja ilimchukua dakika chache kufika nyumbani kwa Sarah, alikuta hali ya kushangaza sana, alikuta askari wakiwa wamekaa na kila mtu akionekana mwenye maumivu, ila mwenye maumivu zaidi alikuwa ni yule aloyetolewa kidole kwa ajili ya risasi,



"ingieni kwenye gari" Sajenti aliongea huku akiwaangalia wale askari ambao baadhi yao walijitahidi kumpigia saluti ila hakutaka kujali.



Baada ya wale askari kuingia ndani, Sajenti Minja akili yake ikamwambia ashuke ili aingie ndani kwa Sarah, alitelemka katika gari na kwenda mpaka ndani kwa Sarah, akamkuta babu yake Sarah akiwa sebuleni akiangaika kupiga simu bila mafanikio,



"mzee kuna usalama?" Sajenti Minja aliuliza,



"usalama utoke wapi? Rafiki yako amewapiga askari hapo nje" Babu yake Sarah aliongea na kumfanya Sajenti Minja ashtuke,



"rafiki yangu? Rafiki yangu gani?" Sajenti Minja aliuliza,



"Sarah" Babu yake Sarah alijibu,



"Sarah ndio amewapiga wanaume watano? Na mwingine kampiga risasi?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa ahamini,



"unashangaa nini? Yule si mwanamke wa kawaida, hafai kabisa" Babu yake Sarah alizidi kutoa maelezo yaliyozidi kumvuruga Sajenti Minja,



"twende kituoni ukanieleze vizuri" Sajenti Minja aliongea,



"kituoni tena? Maelezo si ninakupa hapa hapa?" babu yake Sarah aliongea,



"si unajua kuna wagonjwa ndani ya gari? Twende ili niwapitishe wagonjwa hospitali alafu niwaache hapo, alafu mimi na wewe tunaenda polisi" Sajenti Minja aliongea,



"sawa, twende" Babu yake Sarah aliongea na kisha akawa anaelekea nje huku Sajenti Minja akija kwa nyuma.



Wakatoka mpaka nje na kuingia ndani ya gari, kisha Sajenti Minja akawasha gari na kuliondoa huku wagonjwa wakiwa nyuma wakiugulia maumivu.



*******************



Harry aliamua kuelekea hospitali, alichukua gari yake na safari ikaishia kwenye geti la hospitali, akaegesha gari na kuingia mpaka ndani, akamkuta Vin akiwa na Taita wakiongea huku Vin akiwa na furaha,



"oooh Harry, vipi ndugu yangu" Taita aliongea kwa furaha alipomuona Harry,



"safi, aisee Mungu mkubwa, leo hii unaongea vizuri hivyo?" Harry aliongea huku akijilazimisha kuwa na furaha,



"yule malaya alitaka kuniua, ila ameshindwa, sasa mimi naenda kummaliza" Taita aliongea na kufanya Vin atege vizuri masikio,



"tuachane nae, mimi nadhani tusimfuatilie tena" Harry aliongea,



"Harry bado unao uoga? Mimi nilidhani kwa kilichonikuta utapata hasira na kupanga mashambulizi, kumbe mwenzangu unarudi nyuma?" Taita aliuliza kwa mshangao,



"Mimi nahisi natakiwa nitoke ili familia yangu iwe salama" Harry aliongea kwa utulivu,



"narudia tena Harry, endapo utasaliti hii safari tuliyoianza, ni lazima nikuue, sihitaji tena maelezo" Taita aliongea kwa ukali,



"kwani baba, huyo binti una tatizo nae gani?" Vin aliuliza huku akimuangalia Taita,



"ni mtu mbaya sana, hafai kabisa, nitakueleza baadae" Taita aliongea huku akimshika mkono Vin,



"aisee, nitarudi baadae" Harry aliongea huku akipiga hatua za kuondoka, hakuwa na raha kabisa,



"umekasirika kwa nilichokwambia? Hakuna budi mzee, pambana, ulishachagua kuwa upande wangu tangu tunaanza kazi hii, leo hii unataka kukimbia kwa kuwa yule mjusi wa kipindi kile amekuwa mamba?" Taita aliongea na kucheka, Harry hakutaka kujibu, badala yake aliendelea kutembea kuelekea nje.



"Baba ebu kuwa, muwazi, Sarah na wewe ugomvi wenu chanzo chake nini?" Vin aliuliza,



"nitakwambia mwanangu, ila kwa sasa unachotakiwa kufanya ni kunilinda mpaka nitoke hospitali" Taita aliongea Kwa upendo na mwanae,



"utaniambia lini sasa?" Vin aliuliza kwa ghadhabu,



"si unaona bado nipo hospitali? Nikitoka hospitali nitakusimulia kila kitu tukiwa nyumbani" Taita aliongea kwa kubembeleza huku akiwa na mwanae huyo,



"sawa bwana" Vin alijibu kinyonge huku akikaa pembeni ya baba yake huyo ambaye ni baba feki.



*******************



Nyakati za usiku Harry alifika hospitali na hakukuta mtu zaidi ya Taita, Harry akamsalimia Taita kisha akavuta kiti na kukaa,



"unaendeleaje?" Harry alimuuliza Taita,



"naendelea vizuri, ila nguvu ndio bado hazijarejea vyema" Taita alijibu,



"sasa, unajua tangu umepoteza fahamu kuna mambo mengi yametokea ikiwemo kumpoteza mtu wetu wa technology, Tekso, na tulipofikia inaelekea hakuna atayebaki, njia ya kumzuia Sarah ni kwenda kumfungulia kesi tu" Harry aliongea kwa utulivu na kumfanya Taita acheke,



"sasa hivi ndio mwisho wake, na vin ndio atakayemaliza huu mchezo, nataka amuue dada yake" Taita aliongea kwa kujiamini,



"Vin tayari kishawahi kumpiga risasi mbili na Sarah hakufa" Harry aliongea na kumfanya Taita ashtuke,



"kumbe wameshakutana?" Taita aliuliza,



"ndio, niliwakutanisha" Harry alijibu,



"umewaambia wao ni ndugu?" Taita aliuliza,



"hapana" Harry alijibu,



"safi sana, ngoja nitoke hapa tukaendeleze mapambano" Taita aliongea,



"Mimi hayo mapambano sitoendeleza, bora nikimbie niwaache" Harry aliongea,



"kukimbia huwezi, lazima nitakukamata na kukuua tu Harry, labda kama una njia nyingine ya kuniepuka" Taita aliongea kwa jeuri,



"njia ipo" Harry alijibu,



"ipi?" Taita aliuliza,



"lazima mmoja wenu afe, kati yako au Sarah" Harry aliongea huku akiangalia chini,



"hilo ndio jibu, najua kuniua mimi huwezi, sasa ni lazima umuue Sarah" Taita aliongea,



"kumuua Sarah nimeshindwa ingawa nimejaribu sana, sasa kwa kuwa nimeshindwa kumuua Sarah, ni bora nimuue wewe" Harry aliongea huku akiitoa bastola yake na kumuelekezea Taita,



"ni kweli au unanitania?" Taita aliuliza huku akijivuta ili akae vizuri kitandani,



"nipo hapa kwa ajili ya kutetea uhuru wangu na familia yangu, nimechoka kuishi kama mtumwa" Harry aliongea huku machozi yakimtoka,



"sasa endapo utaniua mimi, ndio Sarah atakusamehe?" Taita aliuliza huku akimtazama akimuangalia Harry,



"hatonisamehe ila nitaweza kukimbia na kwenda kujificha popote duniani" Harry aliongea kwa uchungu,



"sawa, niue" Taita aliongea na ghafla akashtukia akipigwa risasi ya kifuani na kutoa jicho kumuangalia Harry huku akiwa ahamini kama kweli amepigwa risasi na kipindi hicho Harry nae akiwa anashangaa ni wapi hiyo risasi maana yeye hakufyatua hiyo risasi,



"yaani nyani niliyemuokota porini na kumpa matunzo bora mpaka akawa mtu, leo hii unaniua?" Taita aliuliza huku akimuangalia Harry na kipindi hicho mkono wa Taita ulikuwa kifuani kwake akijishika jeraha la risasi na damu zilianza kuenea, kitu ambacho Taita hakujua ni kwamba ile risasi haikufyatuliwa na Harry,



"ila mimi...... " Harry alitaka ajitetee na kueleza kuwa hajampiga yeye, ila kabla hajaanza kumuelewesha Taita, mlango wa wodi ulifunguliwa na Vin akaingia na kumkuta Harry akiwa amemuelekezea bastola Taita, Vin akastuka na kipindi hicho risasi nyingine ikapigwa na kupiga bega la Taita, Vin akachukia sasa, akajua ni Harry amedhamiria kumuua baba yake na kipindi hicho Harry mshangao ukaongezeka na asijue ni nani anayefyatua hizo risasi.....................



"unataka kumuua baba yangu?" Vin aliuliza huku akimfuata Harry kwa hasira, Harry kuona hivyo kwa haraka sana akamgeuzia bastola Vin, Vin hakujali, akawa anazidi kumsogelea Harry, ghafla pasipo kutegemea, Vin alipigwa risasi ya bega, haikuingia ila ilimpalaza tu, ingawa ilimpalaza ila maumivu yalimpata, Vin akaanguka chini na kujishika bega lake kwa maumivu aliyoyapata, Harry kuona hivyo akazidi kushangaa iweje watu wanapigwa risasi wakati yeye hajafyatua risasi hata moja? Wakati akijiuliza hivyo, akili nyingine ilimwambia akimbie eneo hilo kwa kuwa sio eneo salama kwake, Harry akamtupia macho Vin na kumuona akinyanyuka, Harry akatumia mwanya huo kukimbilia nje, Vin kuona hivyo nae akakurupuka na kutoka zake nje mbio kwenda kuona kama atamuwahi Harry, lakini hakumpata, ikambidi apige kelele na baadhi ya watu wakamzunguka,



"msaada, Dokta anaitajika aende wodi namba Saba, kuna mgonjwa amevamiwa" Vin aliongea na kufanya watu watoe taharifa kwa madaktari, daktari mmoja akakimbilia wodi namba saba, Vin nae akawa anamfuata kwa nyuma,



"subiri hapo hapo" Daktari mwingine alimzuia Vin kuingia wodini, ikambidi asubiri pale nje ya mlango, baada ya dakika moja mlango ulifunguliwa na wakatoka madaktari wawili wakiwa wanakisukuma kitanda cha Taita,



"mnampeleka wapi?" Vin aliuliza huku akitaka kuzuia kitanda,



"usijali Vin, nipo salama, naenda theater kutolewa risasi" Taita aliongea huku akitabasamu,



"sawa baba, nitangoja hapa hapa" Vin aliongea,



"Dokta, mchukueni huyu mkamtibie hapo begani, hamuoni akivuja damu" Taita alimwambia madaktari na hapo Vin akagundua kuwa nae amejeruhiwa,



"nae amepigwa risasi?" Daktari aliuliza,



""imenipalaza tu" Vin alijibu,



"twende na wewe ukawekewe dawa na kufungwa bandeji hapo begani" Daktari aliongea na kumfanya Vin awafuate kwa nyuma huku akiwa amejishika bega lake.



*******************



Kwenye ghorofa ndefu pembeni ya hospitali, kulikuwa na mwanamke mrembo akiiweka bunduki yake kwenye begi refu mfano wa begi la gitaa. Bunduki yake ilikuwa ndefu na nyuma iliandikwa M24, rifle. Ni bunduki maalum za wadunguaji zinazotumiwa sana na wanajeshi wa marekani na Israel.



Mwanamke yule baada ya kuiweka bunduki yake kwenye begi, alibeba begi na kulivaa mgongoni, akaitoa miwani yake machoni na kutoa leso kisha akafuta jasho, alikuwa ni Aisha.



"mission complete, tunaenda kupanga mission ya pili sasa" Aisha aliongea peke yake huku akitelemka kwenye ngazi ya lile ghorofa ambalo halijakamilika.



Aisha huyu ndiye aliyempiga risasi Taita na vin, Aisha alikuwa na lengo la kumtengenezea uadui Harry dhidi ya Taita. Aisha alijua kabisa kuwa Harry anataka kumuua Taita, kitu alichokuwa akikifamya Aisha ni kumfuatilia Harry kila aendapo hospitali, aliamini ipo siku Harry atatoa bastola kwa lengo la kutisha Taita, ila hakuwa na imani kama Harry anaweza kumfyatulia mtu risasi, aliijua roho ya Harry haina ujasiri, alijua roho ya Harry imejaa uoga, wasiwasi na hofu kubwa pindi inapokabiliwa na jambo zito. Ndio maana alipoona Harry amemshikia Taita, aliona hiyo ndiyo njia bora ya kumuharibia Harry. Na hata Aisha alipomlenga Taita, alijua anamlenga sehemu gani, alipiga zile sehemu ambazo alijua haziwezi kumletea matatizo ya kupoteza maisha, alipiga sehemu ambazo hazina madhara zaidi ya vidonda tu vya muda mfupi.



Baada ya tukio hilo, Aisha alitelemka mpaka chini ya ghorofa na kuingia kwenye vichochoro kadhaa na kupotelea mitaani, ndivyo alivyo binti huyu, uwa hapendi kabisa kupanda magari, uwa anaamini anapotembea kwa miguu, uwa anaona vitu vingi tofauti mtaani ambavyo humpatia elimu tofauti.



********************



Sajenti Minja aliwapitisha wagonjwa Hospital na kisha akaelekea moja kwa moja hotelini alipo Dokta Pendo, hakwenda kituo cha polisi kama alivyomuahidi babu yake Sarah,



"sasa huku ndio kituoni?" Babu yake Sarah aliuliza,



"shuka mzee, twende tukamuone Dokta Pendo, yupo hapa" Sajenti Minja aliongea huku akimfungulia mlango babu yake Sarah, mzee akashuka na kisha akaanza kumfuata Sajenti Minja ambaye alikuwa akielekea kwenye lift kwa ajili ya kupanda ghorofa za juu.



Walifika mpaka kwenye mlango wa Dokta Pendo, wakagonga hodi, Dokta Pendo akaitikia kutoka ndani, Sajenti Minja akasukuma mlango na kuingia mpaka ndani huku akiwa ameongozana na babu yake Sarah,



"wewe mzee ndio punguani kabisa, yaani wewe kumbe uliyemchongea Sarah polisi, wewe unadhani polisi ni sehemu nzuri?" Dokta Pendo alibwata mara tu baada ya kumuona babu yake Sarah, na kumfanya mzee yule apate mshangao wa kushambuliwa kwa maneno namna ile,



"acha upumbavu binti, nimekusaidia alafu unanigombeza?'" Babu yake Sarah aliuliza kwa mshangao,



"sijatekwa mimi, ningekuwa nimetekwa si ningekuwa naomba watu msaada kipindi tulipokuwa tunaenda kufanya mazoezi?" Dokta Pendo aliuliza kwa ukali,



"kijana eee, twende kituoni kama tulivyokubaliana, kunileta hapa ni kosa kisheria, ni sawa na kuniteka" Babu yake Sarah aliongea kwa kujiamini,



"Kaa hapo, hata hapa ni polisi pia" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama babu,



"guest unapaita polisi, huoni unadhalilisha jeshi?" Babu yake Sarah aliuliza,



"mzee una wasiwasi gani wakati hapa kuna camera kila sehemu, moja, mbili, ya tatu ile pale mlangoni" Sajenti Minja aliongea huku akizihesabu camera zilizokuwa ndani ya kile chumba na kumfanya mzee atulie kidogo,



"haya, unasemaje sasa, sitaki huyu binti aingilie lakini, hapa ni mimi na wewe tu" Babu yake Sarah aliongea huku akikaa katika kiti kilichopo ndani ya chumba kile,



"sawa, je wewe na Sarah mmejuana vipi?" Sajenti Minja alimuuliza babu yake Sarah,



"yule mpumbavu tulikutana nae kwenye chumba kimoja hivi, mimi nilikuwa nimetekwa, na yeye pia alikuwa ametekwa na alipigwa usiku kucha, ilipofika kesho yake, mimi nilimuonea huruma, kwa kuwa mimi nilifungiwa ndani ya Chemba moja mule mule kwenye chumba alichofungiwa huyu mpumbavu, mimi nilikuwa na uwezo wa kutoka kwenye hiyo chemba na kurudi bila mtu yoyote kujua, sasa ndipo nilipomsaidia kwa kumfungua kamba" Babu yake Sarah aliongea,



"Alafu ikawaje?" Sajenti Minja akauliza,



"huwezi amini, baada ya kumfungua, tulikaa masaa mawili ndani ya chumba kile, kuna kijana akaingia kutuletea chakula, bwana wee, yule mwanamke alimpiga yule kijana, baada ya hapo tulitoka nje, na kila tuliyekutana nae alipigwa vibaya, tena na wengine nahisi walikufa kabisa, ndio akanipeleka kwake, na nakumbuka siku ile tunaingia kwake tu, ndio tukakutana na wewe ukitaka kuingia chumbani kwake" Babu alitoa maelezo na kumfanya Sajenti Minja aikumbuke hiyo siku,



"wewe kwanini ulitekwa?" Sajenti Minja aliuliza,



"Mimi sijui, walikuja nyumbani kwangu usiku na kuniteka mimi na mwanangu, baada ya hapo walinipiga risasi nikapoteza fahamu, nilipozinduka nilijikuta nipo sehemu hata siijui na nilikuwa na bandeji kwenye majeraha, baadae sana nikasikia na nyumba yangu ilichomwa moto na waarifu" Babu yake Sarah aliongea na kufanya Sajenti Minja akuimbuke ile kesi ya mzee kutekwa na nyumba ya huyo mzee ikachomwa moto, akakumbuka kuwa siku ya kwanza kwenda kwenye hiyo nyumba iliyoungua moto, alikutana na mwanamke ambaye walipambana nae na kisha huyo mwanamke akakimbia.



Wakati Sajenti Minja aliwaza hayo, ndio wakati huo Dokta Pendo akakumbuka kuwa ni kweli kuwa kipindi anatekwa kwa mara ya kwanza na Trigger, alipelekwa kumtibia huyo mzee, na akakumbuka kuwa Sarah alishawahi kumwambia kuwa yule mzee ni babu yake,



"wewe mzee kweli humjui huyu mwanamke aliyekusaidia kukuokoa ulipotekwa?" Dokta Pendo aliuliza kwa mshangao huku akimuangalia yule mzee,



"simjui kabisa, ningekuwa namjua si ningesema?" Babu yake Sarah aliuliza,



"wewe mzee nimekukumbuka? Na mimi hunijui?" Dokta Pendo aliuliza huku akiwa amemkazia macho babu yake Sarah,.



"sikujui" Babu yake alijibu,



"mzee unawafahamu kwa sura watu waliokuteka?" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio, nawafahamu, yupo mwanaume mmoja katili sana, amejichora chora mwili mzima, alafu yupo mwanamke mmoja katika hilo kundi ambaye anakujaga mara moja moja, mara ya mwisho kushuhudia ni siku moja ambapo kuna binti mmoja alitekwa na kupigwa vibaya, alivunjwa miguu yote na kisha akafa, ndipo wakashauriana wakamtupe" Babu yake Sarah aliongea na kufanya Dokta Pendo ajue ni yeye ndiye aliyetekwa na kupigwa vibaya,



"mwambie mzee atupishe, kuna kitu nataka tuongee" Dokta Pendo alimwambia Sajenti Minja,



"ongea tu, unamuogopa mzee?" Sajenti Minja aliuliza,.



"mwambie aondoke, kuna kitu nataka kukuambia kuhusu Sarah" Dokta Pendo aliongea na kumfanya Sajenti Minja ashtuke,



"mzee chukua nauli, nenda nyumbani, nitakuja baadae" Sajenti Minja aliongea huku akimpatia pesa babu yake Sarah,



"huyu anamjua vizuri tu, ila anamfichia madhambi yake tu" Babu yake Sarah aliongea huku akielekea nje.



"haya niambie, ni kipi unakijua kuhusu Sarah?" Sajenti Minja aliuliza,



"huyu mzee unaemuona, ni babu yake Sarah kabisa, yaani ni baba wa baba yake na Sarah" Dokta Pendo alitoa taharifa iliyomshtua Sajenti Minja,



"sasa mbona huyu mzee haoneshi kumjua Sarah?" Sajenti Minja aliuliza,



"sikia, mara ya kwanza wakati mimi nimetekwa, nilitekwa kwa ajili ya kumtibu mtu aliyepigwa risasi, sura niliyoikuta ya huyo mtu ni hii ya huyu mzee, ila pia mara ya kwanza nakutana na Sarah, alinifuata nyumbani kwangu, alijua mimi na wale watekaji tunashirikiana kwa kuwa alimfuatilia mtekaji mmoja na akamuona akiwa na mimi, tena siku hiyo huyo mtekaji alikuwa akinitoa kumtibu huyo babu na kunirudisha hospitali. Sasa usiku ndipo Sarah alinivamia na kunieleza kila kitu kuhusu huyu mzee, aliniambia maneno mengi tu kuhusu huyu mzee na pia akisema huyu mzee ndio mtu pekee anayemthamini aliyebaki duniani. Basi mimi nilimsaidia kwa kumuingiza ndani ya ngome ya watekaji, ila hakufanikiwa kumuokoa babu yake" Dokta Pendo aliongea na kumfanya Sajenti Minja aunganishe matukio, Sajenti Minja akawaza na kugundua kuwa, kama huyu mzee ni babu yake Sarah, basi ile nyumba iliyoungua zamani ambayo ni ya mtoto wa huyo mzee, basi huyo mtoto ndiye baba yake Sarah, na huyo baba yake Sarah ndiye alimuoa dada yake Taita.



"kwa hiyo Sarah na Taita ni mtu na mjomba wake?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia Dokta Pendo na kumfanya Dokta Pendo ashangae,



"kivipi?" Dokta Pendo aliuliza huku moyoni mwake akijua fika kuwa Sarah na Taita ni mtu na adui yake.



"Sarah ana kitu cha kunieleza, kuna kitu anaficha" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka kwenye kiti,



"Sarah na Taita? aisee unanivuruga wakati tulikuwa tunaongea vizuri" Dokta Pendo aliongea huku akiwa kweli amevurugwa baada ya kuambiwa kuwa Sarah na Taita ni ndugu,



"tangu umemjua Sarah ameshawahi kukuonesha ndugu yake mwingine tofauti na huyu mzee?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, mbona hata mimi hawajui ndugu zangu?" Dokta Pendo aliuliza,



"Sarah unajua anafanya kazi gani?" Sajenti Minja aliuliza,



"ana kampuni inayosafirisha mzigo inayoingia na kutoka nchini" Dokta Pendo alijibu,



"alishawahi kukusimulia makuzi yake, au habari za wazazi wake?" Sajenti Minja aliendelea kuuliza,



"hapana, ila alisema atanisimulia akipata muda kwa maana sio hadithi ya kuvutia" Dokta Pendo alijibu,



"nitarudi baadae" Sajenti Minja aliongea huku akiondoka,



"njoo unieleweshe basi" Dokta Pendo aliongea wakati Sajenti Minja akiondoka, lakini Sajenti Minja alipuuza na kuondoka zake huku kichwa chake kikianza kupata mwanga fulani juu ya kesi anayoifuatilia...........





Sajenti Minja aliamua kumrudia babu yake Sarah, aliona kupitia huyo mzee anaweza kupata kitu kingine cha ziada, Sajenti Minja alitelemka mpaka chini ya jengo na kuingia kwenye gari lake, akawasha na kutaka kuliondoa, ila alisikia mtu akigonga kioo cha upande wa pili, akamtupia jicho na kukuta ni yule mzee, babu yake Sarah,



"ingia ndani ya gari, nilikuwa nakufuata" Sajenti Minja aliongea huku akishusha kioo cha gari, Babu yake Sarah akafungua mlango na kuingia ndani ya gari,



"kuna nini tena? Mbona unanistua?" Babu yake Sarah aliuliza huku akirudishia mlango wa gari,



"kuna maswali nilisahau kukuuliza" Sajenti Minja aliongea huku akizima gari, aliamua amuulizie hapo hapo,



"uliza, tena hapa nitakujibu vizuri kwa kuwa kule juu yule mwanamke alikuwa anaingilia sana mahojiano" Babu yake Sarah aliongea,



"mzee uliposema kwamba ulitekwa na nyumba yako ikachomwa moto, kuna kesi kama hiyo ilitokea miaka kumi na tisa iliyopita, kuna bwana mmoja anaitwa Isack, aliteketezwa yeye na familia yake, na walikufa wote akabaki mtoto mmoja mdogo wa kike,. Je huyo mtu una uhusiano nae gani?" Sajenti Minja aliongea na kumfanya babu yake Sarah apoe kidogo, akatulia kwa sekunde kadhaa,



"huyo mtu unayemzungumzia ni mwanangu, alichomwa akiwa ndani ya nyumba, aliteketezwa yeye na familia yake" Babu yake Sarah aliongea kwa upole,



"hujawahi kufuatilia kituo cha polisi na kuhoji juu ya upelelezi wa hiyo kesi unaendelea au lah!? Au ulishakubaliana na matokeo?" Sajenti Minja aliuliza,



"kipindi cha mwanzo baada ya tukio, kulikuwa na polisi ambaye alikuwa akifuatilia na alikuwa anajitahidi sana kuniambia kila hatua anayopiga, ila kwa bahati mbaya, yule polisi nae alikufa baadae hospitali wakati akijitahidi kumlinda huyo binti wa mwanangu ambaye alikuwa amesalimika" Babu yake Sarah alijibu,



"huyo binti yupo wapi sasa hivi?" Sajenti Minja aliuliza,



"yupo uingereza, aliondoka akiwa mdogo sana na sasa hivi ni muajiriwa wa uko, nadhani hata uraia amechukua wa uko" Babu yake Sarah alijibu,



"mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa lini?" Sajenti Minja aliuliza,



"muda kidogo, kabla sijatekwa" Babu yake Sarah alijibu,



"jina lake unalikumbuka?" Sajenti Minja aliuliza,



"nitalisahau vipi wakati alipewa jina la marehemu mke wangu. Binti anaitwa Sarah, Sarah isack" Babu alijibu na kumfanya Sajenti Minja akubaliane na hisia zake, sasa Sajenti Minja alishajua kuwa Sarah mwenyewe anaezungumziwa ni huyo Sarah ambaye babu anamponda kila siku na kumuita mtekaji,



"huyo Sarah ukimuona utamjua?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, ni muda sana sijamuona, miaka kumi na tisa ni mingi sana" Babu yake Sarah alijibu na kufanya Sajenti Minja ajiulize kwanini Sarah anamficha ukweli babu yake?,



"na Taita Unamjua?" Sajenti Minja aliuliza,



"namjua vizuri, mwanangu ambaye ni baba yake Sarah alimuoa mdogo wake Taita" Babu yake Sarah alijibu,



"je, kulikuwa na ugomvi wowote kati ya Taita na Dada yake?" Sajenti Minja aliuliza swali lililomfanya babu ashangae,



"Mimi nitajuaje sasa? Hayo ni mambo yao" Babu yake Sarah alijibu kwa mshangao,



"sawa mzee, nashukuru kwa majibu yako" Sajenti Minja aliongea,



"sasa nipeleke basi nyumbani" Babu yake Sarah aliongea,



"nyumba yako si imeungua mzee?" Sajenti Minja aliuliza kwa hamaki,



"kwa yule mtekaji ndio nyumbani, maana sina sehemu nyingine" Babu yake Sarah aliongea na kumfanya Sajenti Minja acheke,



"wewe mzee ni mtu wa ajabu sana, yaani mtu anakuifadhi lakini bado unamchongea polisi?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa bado anacheka,



"sasa unataka nifiche maovu?" Babu yake Sarah aliuliza,



"endelea kufichua, ila kuwa muangalifu" Sajenti Minja aliongea huku akiindoa gari yake na kuiingiza barabarani.



**********************



Vin alikuwa pembeni ya kitanda cha baba yake, hali ya baba yake haikuwa mbaya kwa maana Aisha alipiga sehemu ambazo hazina madhara sana.



"mzee samahani, ningependa unipe habari za Sarah, maana haiwezekani Harry amuogope kiasi hicho mpaka atake kukuua" Vin aliongea huku akimtazama Taita,



"unataka kujua ukweli kuhusu Sarah?" Taita aliuliza huku akitabasamu,



"ndio, atakuwa ana sababu ya kufanya hivyo, sio mwendawazimu yule kiasi kwamba atake kuua watu hovyo" Vin aliongea kwa kujiamini,



"Sarah ni mtu anayenituhumu kuwa nimemuulia wazazi wake, sasa anataka kulipa kisasi" Taita aliongea na kumfanya Vin ashangae,



"ni kweli uliua wazazi wake?" Vin aliuliza,



"hapana, hata mimi sijui ni kitu gani kiliwaua, ila mama yake ni ndugu yangu, alikuwa ni mtoto wa baba yangu mdogo" Taita aliongea na kumzidishia maswali Vin,



"sasa si bora ufanye mpango wa kumfikisha mahakamani?" Vin aliuliza,



"mahakamani? Haiwezekani, ukae ukijua kuwa mama yako aliuliwa na Sarah, hicho ndicho kinachofanya nishindwe kumpeleka mahakamani, nataka na mimi nilipe kisasi" Taita aliamua kumdanganya Vin ili amtie hasira, na kweli Vin alipata hasira baada ya kusikia kuwa mama yake aliuliwa na Sarah,



"sasa kama ni hivyo, basi naomba hiyo kazi ya kumuua Sarah niifanye mimi" Vin aliongea kwa hasira huku akiwa amekunja ngumi, Taita akageukia upande wa pili na kucheka, aliamini kuwa ameshaanza kumjaza chuki dhidi ya dada yake,



"ukifanya hivyo, hakika hata nikifa, nitakufa kifo cha amani, nilikuwa nampenda sana mke wangu" Taita aliongea kwa huzuni na kufanya Vin azidi kupata uchungu, na kipindi hicho Trigger alikuwa akiingia ndani ya wodi,



"salama hapa?" Trigger aliuliza huku akiwatizama kwa zamu,



"uzima haupo, mwenzako amefanya kitu cha ajabu sana, amenipiga risasi mbili na kisha akampiga Vin risasi moja ya bega" Taita alijibu kwa ukali,



"nani aliyefanya hivyo!?" Trigger aliuliza huku akishangaa,



"Harry, namuhitaji Harry, fanya kila uwezacho kumleta Harry hapa, nahitaji akiwa mzima ili nimuue mwenyewe" Taita aliongea kwa hasira na kumfanya Trigger ashangae zaidi, hakuamini anachokisikia,



"Harry huyu huyu?" Trigger aliuliza kwa mshangao



"fanya nilichokugiza, maswali tutaulizana ukishamleta" Taita aliongea na kufanya Trigger atii amri, Trigger akapiga hatua za kuanza kuondoka, ila ghafla akageuka,



"umesema nimlete hapa? Utamuua hapa hapa?" Trigger aliuliza huku akimuangalia Taita,



"Trigger umri umeenda ujue, acha bangi mdogo wangu, sasa hapa nitamuuaje? Mpeleke kule kambini" Taita aliongea na kumfanya Trigger aondoke zake huku akitabasamu,



"Harry umenyea shuka kipindi cha baridi" Trigger aliongea peke yake huku akitabasamu na pia akitingisha kichwa chake kwa masikitiko.



********************



Sarah alivyotoka kazini, aliamua kupitia katika hotel aliyokuwepo Dokta Pendo, aliingia moja kwa moja mpaka chumbani na kumkuta Dokta Pendo akiwa ameinamia kitandani akiwa na mawazo sana,



"shoga vipi, unamuwaza nani?" Sarah alimuuliza huku akitabasamu, Dokta Pendo akainua kichwa chake na kumkuta Sarah akimuangalia,



"umeingia muda gani?" Dokta Pendo aliuliza huku akijilazimisha kutabasamu,



"sasa hivi tu, vipi umekula?" Sarah aliuliza,



"tayari, nasikia umewapiga polisi asubuhi, Minja alikuwa anakutafuta" Dokta Pendo aliongea kwa utulivu,



"nitaenda kujisalimisha baadae, sasa wangenikamata si ningeshindwa kusaini mikataba, alafu ningeonekana mswahili" Sarah alijitetea,



"umekula lakini?" Dokta Pendo aliuliza,



"bado, nikifika nyumbani nitapika" Sarah alijibu,



"hivi shoga, kumbe Taita ni mjomba wako?" Dokta Pendo aliuliza swali la ghafla lililomstua Sarah,



"nani amekuambia?" Sarah aliuliza kwa mshtuko,



"Minja, Minja alikuja na babu yako, alikuwa akimuhoji na mwisho wa mahojiano tukagundua yule mzee ni babu yako, na pia Taita ni mjomba wako, je ni kweli?" Dokta Pendo aliuliza, ila Sarah hakujibu na badala yake aliinamisha tu kichwa chini bila kujibu,



"na yule mzee amenijua mimi ni nani?" Sarah alimuuliza Dokta Pendo,



"hapana, mzee hajakujua bado" Dokta Pendo aliuliza,



"nadhani wakati umefika, nahitajika kuvua gamba na kubaki na ngozi yangu halisi" Sarah aliongea kwa sauti ya chini ila iliyomfikia vyema Dokta Pendo,



"unamaanisha nini!?" Dokta Pendo aliuliza na kumfanya Sarah ashtuke, maana hakutegemea kama sauti yake ingemfikia Dokta Pendo,



"tunaweza kwenda nyumbani mara moja?" Sarah aliuliza,



"kufanya nini?" Dokta Pendo aliuliza,



"nahitaji kujitambulisha mbele yako na yule mzee, sihitaji kujificha tena" Sarah aliongea kwa sauti tulivu,



"sawa, twende" Dokta Pendo aliongea baada ya yeye mwenyewe kupata shahuku ya kutaka kumjua vizuri Sarah.



Sarah akamsaidia Dokta Pendo na kutelemka nae mpaka chini na wakaingia ndani ya gari, Sarah akawasha gari yake na safari ya kuelekea kwake ikaanza.



Baada ya muda mfupi waliweza kufika nyumbani kwa Sarah, Sarah akatelemka na kufungua geti, kisha akarudi kwenye gari na kuliingiza ndani ya geti, akarudi na kurudishia geti, kisha akamshusha Dokta Pendo na kumuingiza ndani, walimkuta mzee akiwa amekaa sebuleni kifua wazi akitazama runinga, Sarah akamkalisha Dokta Pendo kwenye kiti, kisha yeye akaelekea chumbani kwake, hawakumsemesha kabisa mzee.



Mzee akanyanyuka taratibu na kuelekea nje, alivyofika nje ya geti, mzee akatoa simu na kupiga, alikuwa anawapigia polisi, tena hakupanga kabisa kumpigia Sajenti Minja, aliona hawezi kumkamata Sarah.



Baada ya kumaliza kupiga simu polisi na kuwafahamisha kuwa Sarah yupo pale muda huo, mzee alirudi ndani na kujitupa juu ya kochi bila kumsemesha neno lolote Dokta Pendo.



Baada ya muda Sarah alirudi sebuleni akitokea chumbani, mkononi alikuwa na picha chache za zamani. Sarah akajitupa juu ya kochi na kumsalimia babu yake, kisha akamtupia zile picha mbele yake juu ya meza, mzee akamuangalia Sarah,



"chukua hizo picha uziangalie, labda kuna mtu unaweza kumfahamu" Sarah aliongea huku akimuangalia babu yake, mzee akaokota zile picha na kuanza kuziangalia, akawa anastuka kila anapoangalia picha moja, aliziangalia zote mpaka akazimaliza,



""hizi picha umezitoa wapi?" Babu yake Sarah aliuliza,



"ni za kwangu, na hiyo ndiyo familia yangu, yaani baba yangu, mama yangu na mdogo wangu" Sarah aliongea na kumfanya mzee ashtuke zaidi,



"wewe binti wewe?" Babu yake aliongea huku akitetemeka,



"naitwa Sarah, Sarah Isack" Sarah aliongea na kujitambulisha rasmi kwa babu yake, babu yake akapigwa na bumbuwazi, akainuka kama mshale na kwenda sehemu alipokaa Sarah, akaushika mkono wa Sarah na kugeuza kwa nyuma, akaangalia kwa sekunde kadhaa kisha akamkumbatia Sarah,



"ni kweli, wewe ni Sarah mjukuu wangu, kwa nini ulikaa kimya muda wote huo? Umesababisha nakuchukulia kama muharifu" Babu yake Sarah aliongea kwa huzuni huku akiwa bado amemkumbata Sarah na kipindi hicho akiwa anajiuliza ni kipi babu yake alichokiangalia nyuma ya mkono,



"mzee mbona umemuangalia nyuma ya mkono, kuna nini?!" Dokta Pendo aliuliza,



"kwenye ukoo wetu uwa tunawapaka dawa za asili ambazo uwa zinakuwa kama doa jeusi juu ya kiwiko, wa kwanza anawekwa doa moja na wa pili anawekwa madoa mawili, yaani madoa yanawekwa kwa idadi" Babu yake Sarah aliongea na kumfanya Sarah agundue hicho kitu, maana hilo doa alikuwa analionaga ila alijua limetokea lenyewe tu.



"sasa babu kuna kitu nataka nikuambie, familia yangu haikuungua kwa bahati mbaya, ni Taita ndiye aliyechoma moto nyumba yetu huku baba na mama wakiwa wamefungwa kamba, mimi na sebastian(vin) tulitolewa nje ila baadae nilirudidhwa ndani na kuachwa kisha moto ukawashwa, Sebastian aliondoka na taita. Na mimi nilipona kwenye moto kwa sababu mfanyakazi wa ndani aliniokoa ila yeye alikufa" Sarah aliongea huku akilia na kipindi hicho sasa babu yake na dokta Pendo wakabaki midomo wazi baada ya kusikia kuwa muhusika mkuu ni Taita, na hapo Dokta Pendo ndiye akaelewa ni kwanini Sarah anadili na Taita tu.



"kumbe Taita ndiye muuaji?" Babu yake Sarah aliuliza,



"ila hili jambo msimwambie mtu yoyote, nataka kulimaliza mwenyewe" Sarah aliongea na kumfanya babu yake ashangae,



"na hata ulivyotekwa na kuchomewa nyumba yako, walikuwa wakinitafuta mimi, walidhani wakikuteka wewe, basi watanipata kwa urahisi" Sarah aliongea huku akiwa anatoka machozi na kipindi hicho polisi zaidi ya hamsini walikuwa wameizunguka nyumba ya Sarah baada ya kuarifiwa na babu yake Sarah.



"wote mliopo ndani tunaomba mjisalimishe, msipofanya hivyo itatubidi tutumie nguvu kubwa kuwashurutisha" Sauti ya tangazo kutoka nje ilisikika, walikuwa ni polisi. Sarah akanyanyuka haraka na kuchungulia dirishani na kuona askari kibao, akikimbilia upande wa nyuma napo akakuta askari wengi wakiwa wameizunguka nyumba, Sarah akarudi sebuleni na kujitupa kwenye kochi, alikuwa amekata tamaa, hakuwa na uwezo wa kupambana na askari zaidi ya hamsini. Kipindi hicho babu machozi yalikuwa yakimtoka na kujiona ana hatia,



"ni kosa langu, mimi ndiye niliyeita polisi" Babu yake Sarah aliongea huku akilia na kujilaumu mwenyewe, na wakati huo polisi wapatao kumi wakiwa na silaha mkononi walikuwa wameshavuka geti na walikuwa wakiuendea mlango wa kuingilia sebuleni kwa sarah, sura zao zilionesha kuwa na hasira nyingi sana juu ya mtu wanayemtafuta kwa maana alihaibisha jeshi la polisi kwa kuwapiga na kuwajeruhi askari wenzao kadhaa nyakati za asubuhi.........



Askari walizidi kusogelea mlango wa sebule ya Sarah huku mikononi wakiwa silaha nzito. Ila kabla hawajaufikia mlango, mlango ulifunguliwa na akatoka babu yake Sarah na kutembea kuelekea getini,



"Mikono juu" Askari mmoja aliongea kwa amri ila babu yake Sarah hakuonesha kujali, alizidi kupiga hatua kuelekea getini,



"weka mikono juu mzee, ina maana husikii?" Yule Askari aliuliza ila safari hii aliipaza sauti yake huku akiamini atamuogopesha mzee yule, ila wala yule mzee hajateteleka, alizidi kupiga hatua kulisogelea geti. Askari yule akaona anafanyiwa dharau kubwa sana, ikambidi atoke kasi kumuelekea mzee, alipofika alimpiga kikumbo na yule mzee akaanguka chini, kisha yule askari akamgeuza yule mzee tumbo chini, mgongo juu na akaichukua mikono ya yule mzee na kuifunga pingu, kisha akamnyanyua,



"wewe si unajifanya jeuri" Askari aliuliza huku akimsukuma yule mzee na kutoka nae nje ya geti,



"sasa wewe vipi? Mbona mmemkamata msamalia mwema?" Polisi ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa polisi aliuliza na kumfanya yule askari aliyemshika mzee ashangae,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"ametoka ndani, tumempa amri amekataa kutii" Askari aliongea,



"huyu ndiye aliyetupigia simu na kutupa taharifa za kuwepo muharifu hapa, alafu sio mara moja, mara zote huyu ndiye anayetupa taharifa za muharifu" Kiongozi wa kikosi kile aliongea na kumfanya babu yake Sarah asikie uchungu kwa mara ya kwanza juu ya kauli ile, kwa kuwa aliijua alikuwa anamchoma mjukuu wake,



"mfungue pingu hiyo" Kiongozi wa kikosi alitoa amri kisha askari akatii na kumfungua pingu mzee,



"mmechelewa mbona, yule binti ameshaondoka tayari" Babu yake Sarah aliongea huku akimuangalia kiongozi wa kikosi kile,



"dah, ameelekea upande gani?" Kiongozi wa kikosi aliuliza,



"sijui, kwa kuwa mimi nilikuwa ndani, sikuweza kujua ameelekea uelekeo gani?" Babu yake Sarah alijibu na kumfanya kipindi hicho Sajenti Minja alikuwa anafika, askari wote wakampigia saluti akiwemo kiongozi wa kikosi kile cha polisi.



"mmefanikiwa kumkamata?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama jirani na babu yake Sarah,



"mzee anadai ameshaondoka" Kiongozi wa kikosi alijibu,



"hawa wazembe sana, nimewapigia simu muda mrefu ila ndio wamekuja sasa hivi, sijui wanamuogopa yule mwanamke?" Babu yake Sarah aliongea huku akijifanya amekasirika,



"Dokta Pendo yupo ndani?" Sajenti Minja alimuuliza babu yake Sarah,



"ndio, yupo" Babu yake Sarah alijibu,



"chukua kikosi chako na uondoke, mmeshakosea, mnapopigiwa simu mnatakiwa mfike kwa wakati" Sajenti Minja aliongea kwa amri kwa maana alihisi kama Dokta Pendo yupo ndani, basi hata Sarah atakuwa ndani.



Baada ya Sajenti Minja kutoa amri, wale askari walijilusanya na kuondoka zao huku baadhi ya askari wakilalamika chini chini kwa kitendo cha Sajenti Minja cha kuingilia kazi yao na mwisho akawafukuza bila kuwapa uhuru wa kufanya upekuzi kwenye nyumba ya Sarah.



Sajenti Minja alisimama mlangoni pale getini mpaka alipohakikisha gari ya polisi imepotea machoni mwake, kisha Sajenti Minja akaingia moja kwa moja mpaka sebuleni na kumkuta Sarah na dokta Pendo wakiwa wamekaa, kwanza wote walishtuka mara baada ya mlango kifunguliwa.



"vipi, upo salama?" Sajenti Minja aliuliza huku akichuchumaa kwenye miguu ya Dokta Pendo na wakati huo babu yake Sarah nae alikuwa akiingia ndani,



"ndio umekuja kumkamata Sarah?" Dokta Pendo aliuliza huku akimuangalia Sajenti Minja,



"wameshaondoka" Babu yake Sarah alijibu,



"kwanini ulimchukua Dokta Pendo hotelini bila kunipa taharifa?" Sajenti Minja aliuliza huku akimgeukia Sarah ambaye muda wote alikuwa kimya kwa maana alikata tamaa mara baada ya polisi kuizunguka nyumba yake, na aliamua atulie tu sebuleni huku akisubiri litakalomkuta, kwa hiyo babu yake aliposema askari wameondoka, ulikuwa muujuza mkubwa sana kwa Sarah.



"wewe si nimekuuliza? Unaniletea kiburi" Sajenti Minja aliuliza kwa hasira huku akimtazama Sarah,



"taratibu basi, kwani yeye kumchukua Dokta Pendo hotelini kuna ubaya gani, hawa si ni marafiki? au wewe unataka kuvunja ushoga wao?" Babu yake Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja ashtuke, hakutegemea kama yule mzee anaweza kumtetea Sarah, Sajenti Minja akamgeukia mzee huku sura yake ikionesha mshangao wa wazi,



"siongei na wewe mzee, alafu leo mbona unamtetea sana Sarah, si alikuwa adui yako huyu, nasikia hata hawa askari niliowafukuza uliwaita wewe?" Sajenti Minja aliuliza huku akicheka na Dokta Pendo nae alikuwa akicheka ila kwa kujificha jificha,



"bwana wewe, binadamu tumeumbwa kukosea" Babu yake Sarah alijibu huku akiwa anaangalia chini,



"sasa Sarah itabidi twende kituoni, kwani ile kesi bado inaendelea na pia kumbuka kuwa una kesi nyingine ya mauaji, siku ile unatoroshwa kuna askari alikuwa" Sajenti Minja aliongea,



"na wewe nawe, kila kitu polisi, yaani kitu kidogo polisi, utadhani ulizaliwa uko?" Dokta Pendo aliongea huku akionekana hajapenda maongezi ya Sajenti Minja,



"hata mimi anamiudhi, Sarah mjukuu wangu uwe unachagua marafiki, sasa huyu mtu umemtoa wapi?" Babu yake Sarah huku akiwa anamuangalia Sajenti Minja kwa hasira na kumfanya Sajenti Minja acheke,



"Sarah huyu mzee ni babu yako, sitaki unijibu hilo, ila ninachokifanya kujua ni kuwa je, Taita ni mjomba wako?" Sajenti Minja aliuliza huku akimtazama Sarah,



"sio mjomba wake" Babu yake Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja amuangalie,



.



"mzee kumbuka wewe ndiye uliyeniambia kuwa mwanao alimuoa dada yake Taita, na mwanao ndiye baba yake Sarah, sasa kwa nini unakanusha swali langu, au hujui kuwa huyu Sarah ndiye yule mjukuu wako anayeishi uingereza?" Sajenti Minja alimuuliza babu yake Sarah huku akijua kuwa babu yake Sarah atashangaa,



"ndio unanitambulisha au? Mbona najua muda mrefu tu kuwa huyu ni mjukuu wangu" Babu yake Sarah alijibu na kumfanya Dokta Pendo aangue kicheko,



"mzee miyeyusho kweli. Sarah hujanijibu, Taita ni mjomba wako?" Sajenti Minja alirudia swali lake,



"ndio, ni mjomba wangu?" Sarah alijibu, Sajenti Minja akatingisha kichwa kukubaliaba na Sarah,



"kuna kitu kimoja unanificha, wewe ni mpiganaji mzuri sana, wa ngumi na mtumiaji mzuri sana wa silaha, je haya mafunzo umeyapata wapi?" Sajenti Minja aliuliza na kumfanya Sarah ashushe pumzi nzito,



"Mimi ni mwanajeshi" Sarah alitoa jibu lililomshangaza kila mtu ndani mule,



"wa kambi gani?" Sajenti Minja aliuliza huku akificha mshangao wake,



"sio wa hapa, mimi ni raia wa uingereza" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja akumbuke kitu, alikumbuka let lile tukio la kupambana na mwanamke ndani ya ile nyumba iliyoungua na akakumbuka zile risasi mbili alizoziokota na kuzifanyia uchunguzi na kugundua kuwa zinatumiwa na jeshi la uingereza,



"kuna matukio mengi sana umeyafanya, yakiwemo ya utekaji, je ni vibaya nikikutia hatiani?" Sajenti Minja aliuliza,



"na wewe nawe unaona sifa kuwatia watu ndani" Dokta Pendo aliongea,



"nyie kaeni kimya, hapa ni mimi na Sarah tu" Sajenti Minja aliongea kwa ukali na kufanya Dokta Pendo atulie,



"unataka kuniweka hatiani? Ni sawa, ila naomba muda kidogo" Sarah aliongea kwa kujiamini,



"muda? Muda wa nini, unatakiwa uondoke na mimi muda huu" Sajenti Minja aliongea,



"ngoja nikuambie kitu, yaani wewe hapo ulipo, huwezi kunifanya chochote hata nikiamua kutokwenda polisi, na nilivyokuomba muda nimetumia busara tu, kwa hiyo niache nikamilishe mambo yangu kwanza" Sarah alijibu,



"unatupangia kazi sio, kumbuka hapa sio uingereza" Sajenti Minja aliongea,



"angalia chini ya meza" Sarah aliongea na kumfanya Sajenti Minja achungulie chini ya meza, na kipindi hicho babu yake Sarah nae alitaka kuchungulia ila Sarah alimzuia.



Sajenti Minja alipochungulia aliona mabomu mawili chini ya meza, Sajenti Minja akarudi taratibu kwenye kiti,



"ningekuwa mkorofi, ni muda sana ungekuwa umeshakufa, eidha kwa ulichokiona chini ya meza, au siku ile ulipotuona na dokta Pendo kwa mara ya kwanza, maana nilikushambulia ukapoteza fahamu, ila nikakuacha, elewa sipo hapa kumdhuru mtu, nipo hapa kudili na wanyama" Sarah aliongea ila Sajenti Minja alikuwa na wasiwasi kutokana na alichokiona,



"naomba niondoke" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka,



"afadhali, nenda tu baba" Babu yake Sarah aliongea ila Sajenti Minja hakuongea kitu, Sajenti Minja akaondoka huku akitafakari neno ka Sarah alilosema anadili na wanyama.



"kwani uko chini ya meza kuna nini, mbona Minja alivyochungulia amekuwa mpole?" Dokta Pendo aliuliza,



"chungulia" Sarah aliongea huku akitabasamu na kumfanya babu yake achungulie, kidogo akimbie,



"hayana madhara, nimeweka kutisha watu tu" Sarah aliongea huku akiinuka katika kiti,



"shoga nirudishe hotelini" Dokta Pendo aliongea,



"nitakurudisha jioni, ngoja tule tushibe, nitakurudisha jioni ninapoenda kumalizana na Harry" Sarah aliongea huku akipotelea chumbani.



*******************



Mishale ya usiku, Trigger na Vin walikuwa ndani ya geti la Harry, na chini alikuwa mlinzi wa geti ambaye kwa muonekano wa haraka ilionekana amepoteza maisha au amepoteza fahamu,



"twende ndani, huyu tayari" Vin aliongea huku wakielekea ndani, walipofika hawakugonga hodi, wakasukuma mlango na kuingia, wakamkuta mke wa Harry akiwa na watoto wake,



"vipi shem, mbona unatutisha kwa namna ulivyoingia?" Mke wa Harry aliongea huku akitabasamu,



"jamaa tumemkuta?" Trigger aliuliza bila kujibu swali la mke wa Harry,



"ametoka, aliniambia anaweza asirudi leo" mke wa Harry alijibu,



"alikwambia anapoenda?" Vin aliuliza,





"hapana, kwani vipi? mbona mnanitisha?" mke wa Harry aliuliza,



"Harry amemuua Taita, kwa hiyo anatafutwa" Vin aliongea huku akimtazama mke wa Harry ambaye alikuwa amekamata mdomo kwa mshtuko,



"tupo hapa kulipa kisasi" Trigger aliongea na kumshangaza zaidi mke wa Harry,



"kivipi?" Mke wa Harry aliuliza huku machozi yakimtoka,



"maliza mchezo, Harry atakuwa amekimbia nchini tayari" Vin aliongea kwa sauti ndogo iliyomfikia vyema Trigger, Trigger akachomoa bastola yake na kuwamiminia risasi familia ya Harry, hakuna aliyebaki hai, wote walikufa,



"sasa wewe wahi Kiwanja cha ndege ukaangalie kama utamuona Harry, acha mimi niendelee kusubiri hapa, huenda atarudi" Vin alimwambia Trigger,



"poa mkuu" Trigger aliongea kisha akatoka zake nje na kuondoka zake.



Kipindi Trigger anaondoka, ndicho kipindi Sarah alikuwa anaingia ndani kwa kupitia ukuta, alivyotua tu ndani akaangaza macho na kuweza kuuona mwili wa mlinzi ukiwa umelala, Sarah akajua kuna uvamizi ulifanyika muda uliopita, Sarah akapata wasiwasi huku akiamini huenda ni Aisha ndio mvamizi.



Sarah akaufikia mlango wa sebuleni na kuingia, ila alichokiona ndicho kilichomstua, aliikuta miili ya watu ikiwa imelala na imetapakaa damu, macho ya Sarah yaliangukia kwenye mwili wa mtoto mdogo wa kike, kipenzi chake,



"princess!!" Sarah aliongea huku akiukimbilia mwili ya yule mtoto, alipoufikia akaubeba na kuutingisha huku akilia, alikuwa na uchungu sana, alilia huku akiamini huu mchezo umefanywa na Aisha,



"umekuja kumuua Harry au umekuja kumtuma?" Vin aliingia pale sebuleni huku akiongea maneno hayo na kumfanya Sarah ashtuke,



"ni nani aliyemuua huyu mtoto?" Sarah aliuliza kanakwamba hakuona maiti nyingine hapo sebuleni,



"na wewe unamfuata uko alipo muda si mrefu" Vin aliongea huku akiichomoa bastola yake na kufanya Sarah aamini kuwa huyu ndiye aliyefanya mauaji hayo, Sarah akachomoa kisu na kumrushia Vin, Vin akayumba kidogo kwa lengo la kukikwepa kile kisu, Vin alipokaa sawa alishuhudia teke kali likiupiga mkono wake na kufanya aiangushe bastola yake. Vin akagundua kuwa kiumbe anayepambana nae ana kasi ya ajabu sana. Vin akaamua kutumia mbinu za kujiami, yaani awe anapigana huku anarudi nyuma, Sarah akaligundua hilo, kwa kasi ile ile Sarah aliruka teke jingine kali, Vin akapiga hatua moja nyuma na Sarah akamkosa, Sarah akatua mbele ya Vin, Vin akaachia ngumi kali, Sarah akaidaka kisha Sarah nae akaachia ngumi kali, ikampata Vin usoni, Vin akaanza kuona nyota nyota, Sarah akatumia mwanya huo na kumpiga ngumi nyingi za haraka haraka, Vin akaenda chini,



Vin akajiinua na sarakasi nyepesi, akaokota pasi iliyokuwa hapo sebuleni na kumtupia Sarah, Sarah akakwepa, Vin akachukua king'amuzi na kumrushia Sarah, Sarah akainama, alipoinuka akakutana na ngumi ya Vin ikiwa imemlenga uso, Sarah akaidaka na kuunyongorota mkono wa Vin na kumfanya Sarah awe nyuma ya Vin huku akiwa ameushika mkono wa Vin kwa nyuma,



"nakuua mshenzi wewe ili kuilipa damu ya huyu malaika uliyemuua bila ya sababu" Sarah aliongea kwa hasira huku akiichomoa bastola yake, Vin alikuwa hana la kufanya, alibanwa vibaya sana.



Wakati Sarah akiwa amemshika namna ile Vin, Sarah kuna kitu alikiona kwenye mkono wa Vin, kilimshtua Sarah, aliona madoa mawili meusi kwenye mkono au Vin, tena yapo eneo lile lile kama lililopo doa lake, Sarah akajikuta amepoteza ujasiri wa kumfyatulia risasi Vin,



"Sebastian" Sarah aliita huku akimuachia Vin, Vin akashanga, ila hakutaka kujali Sarah anachofanya, Vin akamtupia ngumi nzito Sarah, Sarah hakuizuia ingawa alikuwa na uwezo wa kujikinga, ngumi ile ikatua kwenye pua ya Sarah, Vin akarusha ngumi nyingine, Sarah akamdaka mkono,



"Sebastian mimi ni dada yako, usinipige" Sarah aliongea kwa upole huku akimuachia mkono Vin, Vin akaona Sarah kama amechanganyikiwa, Vin akarusha teke na Sarah akaudaka mguu wa Vin na kumsukuma chini, Vin akadondoka



"Mimi ni dada yako, tusipigane" Sarah aliongea kwa ukali ila Vin hakuna alichojua, Vin akainuka na meza ya kioo na kumtupia Sarah, Sarah akakwepa na sasa Sarah akaamua aondoke, aliona akiendelea kukaa pale, Vin atamjeruhi na yeye hakutaka kupigana na mdogo wake.



"nitakutafuta Seba" Sarah aliongea na kisha akaanza kuondoka kwa mwendo wa taratibu bila hata kuangalia nyuma, alivurugwa akili kwa kumgundua mdogo wake.



Wakati Sarah akiondoka bila wasiwasi wowote, Vin aliimkimbilia bastola yake na kuiokota, aliamini muda huo ndio muda wa kutekeleza ahadi aliyompa baba yake (Taita).



Wakiwa wameachana umbali wa hatua kumi tu, Vin alimnyooshea Sarah bastola, ubaya Sarah hakuwa na habari na alikuwa akiendelea kutembea tu kuelekea nje.



Vin akatoa tabasamu la ushindi, hakujua anayetaka kumuua ni dada yake, Vin akiwa amelenga usawa wa kichwa cha Sarah, Vin alimfyatulia Sarah risasi, na kisha Sarah akaanguka chini................



Sarah hakuanguka chini, ila alijitupa chini baada ya kumuona mtu akija kwa mbele yake katika mlango wa sebuleni huku akiwa ameelekeza bunduki ndani, huyo mtu ambaye ni mlinzi wa nyumba ya Harry ndiye aliyefyatua hiyo risasi, Sarah akaiona na kujitupa chini, na kitendo kile cha yule mlinzi kumfyatulia risasi Sarah, kilifanya shabaha ya Vin iyumbe na vin akajikuta mkono umemtetemeka na kufyatua risasi bila malengo na kumkosa Sarah. Vin baada ya kumkosa Sarah kutokana na kusikia mlio mwingine wa risasi, alijikuta nae akijitupa nyuma ya kochi na kujificha.



Sarah alipojitupa chini, alibiringita huku risasi zikimfuata mpaka kwenye kochi jingine, Sarah alipofika nyuma ya kochi akageuka na kufyatua risasi iliyovunja taa, sebuleni kukawa giza. Kila mtu sasa akakaa kimya wakitegeana nani ataanza kutoka ili awe ndio chambo.



Sarah akaingiza mkono mfukoni na kutoa sarafu, akairusha katikati ya sebule, sarafu ilipotua chini tu, zilipigwa risasi mfululizo kutoka kwa mlinzi na Vin, risasi zote zilielekea sehemu sarafu ilipo, Sarah akatabasamu na kujua ni wapi walipo maadui zake. Sarah akasogeza kochi alilokuwa amekaa kwa nyuma, akasikia risasi zikipiga lile kochi, ila aliona zote zikitoka kwa mlinzi, kwa upande wa Vin alisikia bastola ikifyatuliwa ila haikutoa risasi, Sarah akajua kuwa Vin amemaliza risasi, sasa akaamua kuwa makini na mlinzi tu.



Sarah kwa kasi ya ajabu aliinuka nyuma ya kochi na kupiga risasi mfululizo kuelekea mlangoni, akasikia mlinzi akipiga kelele na kisha akasikia kishindo cha mtu kuanguka. Sarah akatoka mpaka nje na kumkuta mlinzi akiwa anagalagala huku ameushika mkono wake na gobole lake likiwa pembeni. Sarah akamsogelea na kuliokota lile gobole na kulitupa mbali na mlinzi,



"pole" Sarah aliongea kwa huruma huku akimuangalia mlinzi ambaye hakujibu kitu zaidi ya kulia kwa maumivu.



Sarah akarudi mpaka kwenye mlango wa sebuleni na kuchungulia,



"fanya uondoke haraka kabla polisi hawajafika, huyu mlinzi hawezi kutumia bunduki tena" Sarah aliongea kwa sauti kubwa kiasi iliyomfikia Vin, kisha kwa njia ile ile aliyokuja nayo ndio njia ile ile aliyoondoka nayo, alipitia ukuta na kuondoka zake huku akiwa bado anamfikiria Vin kutokana na zile alama alizoziona nyuma ya mkono wa Vin.



Huku nae Vin alitoka nyuma ya kochi kwa tahadhari, hakutaka kuamini maneno ya Sarah kuwa eneo lile lipo salama. Vin alitoka kwa uangalifu mkubwa mpaka alipomuona mlinzi akiwa chini analia na mkono ukiwa umejaa dumu.



Vin akatoka kwa kukimbia mpaka nje ya geti na kuingia kwenye gari lake, akaliondoa kwa kasi huku nae akijiuliza yule mwanamke ni nani? Na kwanini amuite Sebastian? Na kwa nini hajamuua wakati alikuwa na uwezo wa kumuua? na kwanini amuite mdogo wake.



Vin alijiuliza, hakutaka kupuuza lile tukio, alipanga kulifuatilia.



*******************



Harry alirejea nyumbani kwake, aliingia getini na kukuta mlinzi hayupo, alipotupia macho kwenye madirisha ya sebuleni, aliona giza, kwa maana hiyo taa zilikuwa zimezimwa, Harry akapata wasiwasi kidogo. Akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye mlango wa sebuleni huku mapigo ya moyo yakipiga kwa kasi, Harry akazidi kupiga hatua kuelekea mlangoni, ila kabla hajaufikia mlango, alimuona mlinzi akiwa amelala chini huku akilia na ameushika mkono wake ukiwa umejaa damu, hapo Harry alizidi kupata hofu juu ya kilichotokea,



"kuna nini kimetokea?" Harry alimuuliza mlinzi,



"Trigger alikuja na kunifunga kamba, sijui hata nini kimetokea huko ndani, maana wakati nataka kuingia nimepigwa risasi ya mkono na mwanamke na kisha amekimbia" Mlinzi alitoa maelezo yaliyomchanganya Harry,



"Mimi sikuelewi, huyo mwanamke alikuja na Trigger?" Harry aliuliza kwa wasiwasi huku akijiuliza huyo mwanamke ni nani ambaye alikuja na Trigger?



"Trigger alikuja na yule Jamaa mrefu mweusi ambaye anapenda kuvaa suti, huyu mwanamke sijajua hata muda alioingia" Mlinzi aliongea ila bado Harry hakumuelewa, alichoelewa ni huyo jamaa anayependa kuvaa suti, alijua ni Vin, hapo utumbo wa Harry ukacheza akahisi tumbo limemvuruga,. Hakutaka tena kumsikiliza mlinzi, aliamua aingie mwenyewe ndani ili aone kilichotokea,. Alipoingia ndani alipeleka mkono kwenye switch ya ukutani ili awashe taa ya sebuleni, ila aligundua switch ipo "on" yaani imewashwa, akaamua awashe tochi ya simu yake, tochi ilipowaka alijikuta akiumulika mwili wa mwanamke ukiwa umelala sebuleni, akashtuka na kummulika usoni yule mwanamke, akajikuta nguvu zinataka kumuishia, alikuwa ni mke wake na alikuwa na jeraha risasi kubwa kwenye paji la uso,



"Jane, jane, janet" Harry alimuita mke wake huku akimsogelea, ila kabla hajamfikia alijikwaa kwenye mwili wa mtoto na kujikuta akadondoka chini, akauangalia ule mwili na kugundua ni wa mtoto wake wa kiume, Harry akatoa chozi la uchungu,



"Harrison, Harrison, Princess yupo wapi?" Harry aliuliza huku akiwa ameukumbatia mwili wa mwanae wa kiume aitwae Harrison.



Harry alilia sana huku akiwa ameukumbatia mwili huo wa mwanae ambaye nae alikuwa na jeraha la risasi kwenye paji lake la uso,



"princess yupo wapi?" Harry alilia huku kamasi zikimtoka, ubaya ni kuwa hayo maswali alikuwa akiziuliza maiti, Harry akainuka na simu yake mkononi, akauona mguu wa mtoto ukiwa nyuma ya kochi, Harry akakimbilia na kumkuta mwanae princess akiwa amelala huku macho yakiwa wazi, Harry,



"nisameheni wanangu, mmehukumiwa kwa makosa ya baba yenu" Harry aliongea kwa uchungu huku akilia, alilia sana, mwisho akaamka na kusimama, akacheka, hakikuwa kicheko cha furaha,



"maisha yangu yote ndani ya dunia kumbe nilipangiwa kufanywa hivi?" Harry alijiuliza huku akicheka,



"ila sikupangiwa, inawezekana nilijipangia kuishi hivi" Harry aliongea kisha akacheka na kuanza kutoka nje huku akicheka na machozi yakimtoka,



"umeshapiga simu polisi?" Mlinzi alimuuliza,



"polisi!!?" Harry aliuliza kisha akacheka, na kumfanya mlinzi ahisi bosi wake amechanganyikiwa,



"wataharifu polisi" Mlinzi aliongea huku akiwa anamtazama Harry,



"wakija ndio watarudisha uhai wa familia yangu?" Harry aliuliza huku akimtupia simu mlinzi, kisha Harry akaelekea nje ya geti na kuondoka zake huku akicheka na kumuacha mlinzi akishangaa tu. Baada ya Harry kuondoka, mlinzi akaiokota simu na kupiga namba za msaada kituo cha polisi kuwataharifu juu ya tukio lililotokea.



***************



Sajenti Minja alifika kwenye nyumba ya Harry akiwa ameambatana na askari kadhaa pamoja na waandishi wa habari.



Sajenti Minja alipofika kwanza aliingia ndani na kukagua maiti kwa kutumia tochi walizoenda nazo, baada ya hapo wakatoa nafasi kwa wapiga picha wachukue picha.



Baada ya hapo miili ilipakiwa kwenye gari na kupelekwa kwenye kuhifadhiwa hospitali. Sajenti Minja aliondoka na mlinzi wa Harry kwenda kumuhoji.



Walifika kituoni na kisha Sajenti Minja akamuongoza mlinzi mpaka ofisini kwake na kumkaribisha kiti, kisha akammiminia kahawa kwenye kikombe kilichopo juu ya meza,



"ni nini kilitokea kabla ya mauaji?" Sajenti Minja alianza na hilo swali,



"swali sijalielewa" Mlinzi alijibu,



"ooh sawa, je unatambua ya kuwa wewe ni muhusika wa kwanza wa yale mauaji?" Sajenti Minja alibadili swali,



"hapana, mimi sihusiki kwa lolote na ndio maana niliwapigia simu" Mlinzi alijibu kwa uoga,



"kama wewe uhusiki, je unaweza kututajia muhusika?" Sajenti Minja aliuliza,



"sitokuwa na uhakika, ila kuna rafiki yake Harry aliingia na kunipiga nikapoteza fahamu, huyo ndiyo namuhisi ni muhusika, aliingia ndani na mwenzake" Mlinzi alijibu,



"anaitwa nani?" Sajenti Minja aliuliza tena,



"Trigger, namfahamu kwa jina hilo, ila yule mwenzake aliyeongozana nae simjui jina, namjua sura tu" Mlinzi alijibu,



"baada ya wao kuingia ndani ni nini kilifuata?" Sajenti Minja aliuliza,



"kwa kuwa nilipoteza fahamu sikujua kilichotokea, ila fahamu ziliponirejea niliamua niingie sebuleni na nikamkuta yule kijana aliyeingia na Trigger, alikuwa na mwanamke ndani" Mlinzi alijibu,



"Alafu?" Sajenti Minja aliuliza



"nilijaribu kuwashambulia ila walitumia akili, walivunja taa za sebuleni na kisha wakatumia mbinu hiyo kunishambulia na kunipiga mkono" Mlinzi alijibu,



"huyo mwanamke ulifanikiwa kumuona sura yake?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, kwa maana macho aliyaacha wazi, ila Kuanzia puani kushuka chini alijiziba na kitambaa". Mlinzi aliongea na kumfanya Sajenti Minja atambue kuwa mwanamke huyo ni Sarah, kwa maana wamekutana mara kadhaa akiwa amejifunga hivyo.



"Baba wa familia amepata taharifa?" Sajenti Minja aliuliza,



"alikuja na ameona kilichotokea, ila ameondoka akiwa anacheka, itakuwa amechanganyikiwa" Mlinzi aliongea na kumfanya Sajenti Minja ashangae,



"anacheka? Hajasema kitu chochote?" Sajenti Minja aliuliza,



"kwa muonekano wa haraka ilionekana amechanganyikiwa, hakuwa katika hali nzuri" Mlinzi aliongea,



"umejaribu kumpigia simu?" Sajenti Minja aliuliza,



"simu niliotumia kuwapigia ni simu yake, alinipa baada ya kumwambia awapigie nyinyi, kwa maana hiyo uko alipo hana simu" Mlinzi aliongea kwa utulivu,



"sawa mzee, itabidi uende hospitali, alafu urudi ulale kituoni" Sajenti Minja alimwambia mlinzi,



"kituoni tena, ila mimi sina kosa" Mlinzi aliongea kwa kulalamika,



"haimaanishi una kosa, ila tunafanya hivyo kwa ajili ya usalama wako" Sajenti Minja aliongea kisha akamuita askari ambaye alimpa maagizo ya kumpeleka mlinzi hospitali na baada ya matibabu arudishwe selo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya askari yule kutoka na mlinzi, Sajenti Minja alibaki peke yake ofisini,



"Sarah ameiangamiza familia ya huyu bwana, kwanini?" Sajenti Minja alijiuliza,



"na huyo Trigger ni nani?" Sajenti Minja aliendelea kujiuliza bila kupata jibu, mwisho akaamua aondoke aende Kulala ili apumzishe akili.



Sajenti Minja akatoka na kuingia kwenye gari yake na kuiondoa kwa mwendo wa wastani.



********************



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog