Search This Blog

Friday 18 November 2022

MKONO WA CHUMA - 5

 






Simulizi : Mkono Wa Chuma

Sehemu Ya Tano (5)





"sijamtorosha mtuhumiwa" Sajenti Minja alijibu tena jibu lile lile,



"inasikitisha sana, Yaani bado unaendelea na msimamo wako ule ule?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"naomba unirudishe selo, maana kati sitobadili jibu langu, kwa sababu ndilo jibu la ukweli, na nyinyi hamuwezi kubadili msimamo wenu, kwa kuwa hamniamini tena" Sajenti Minja aliongea na kumuangalia mkuu wake,



"kabla sijakurudisha selo, ningependa kukufahamisha kuwa, hiki kitendo cha kipuuzi ulichokifanya cha kumtorosha yule mwanamke, kinaweza kupelekea mimi kufukuzwa kazi, pia kinaweza kupelekea wewe kufungwa na kukosa kazi" Mkuu wa polisi aliongea kwa uchungu,



"kama nitapoteza kazi na kufungwa kwa ajili ya ukweli wangu, ni sawa tu, ila siwezi kubadili kauli yangu" Sajenti Minja aliongea na kumfanya mkuu wake apige ngumi kwa hasira juu ya meza,



"afandee" Mkuu wa polisi aliita kwa sauti kubwa,



"naam afande" Askari aliyemleta Sajenti Minja aliitikia nje ya mlango huku akiingia ndani ya ofisi ya mkuu wa polisi,



"mrudishe selo huyu" Mkuu wa polisi aliongea na kisha yule Askari akamuinua Sajenti Minja na kumpeleka selo, Sajenti Minja akaingia selo na kwenda kukaa katika chumba kimoja kilichokuwa na harufu kali, kilikuwa jirani na choo, alikuwa akitafakari nini hatma yake, hasira ziliongezeka zaidi kila alipomfikiria BQ,



"nife mimi afe yeye, labda nisitoke humu" Sajenti Minja aliongea huku akiilalia mikono yake ambaye aliigemeza katika magoti, aliamua kulala huku akiwa amekaa.



Wakati Sajenti Minja akiwa katika hali hiyo, mkuu wa polisi yeye bado alikuwa na mawazo mengi, ikiwemo atazizuia vipi zile habari za Sajenti Minja kumtorosha mtuhumiwa zisifike kwa Rais, je zikifika yeye mkuu wa polisi kazi ndio itakuwa basi tena? au atashushwa cheo na kupelekwa mkoa mwingine?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo mkuu wa polisi alikuwa anajiuliza. Akajikuna kidevu, akakumbuka kuwa kati ya waandishi wa habari waliokuwepo pale usiku huu waliokuwa wakimsubiri Sajenti Minja na mtuhumiwa, alikuwepo muandishi wa habari mmoja maarufu sana wa moja kati ya vyombo vya habari vinavyoaminika sana nchini. Mkuu wa polisi akapanga kumtumia huyo muandishi wa habari, alichopanga ni kutoa hata rushwa ili mradi tu gazeti litalotoka siku inayofuata kutoa habari ambayo haitomchafua Sajenti Minja, alijua endapo Sajenti Minja angechafuliwa tu, wa kwanza kuwajibika atakuwa yeye mwenyewe mkuu wa polisi.



Mkuu wa polisi akawa anapeleka mkono wake ili aichukue simu yake mezani na kumpigia huyo muandishi wa habari, ila kabla mkono wake haujaishika simu, simu ilianza kuita, mkuu wa polisi akarusha mkono kwa mshtuko baada ya kuona jina la mpigaji, alikuwa ni Rais, mkuu wa polisi akahisi hofu kuu moyoni, jasho likaanza kumtoka ilihali ndani Kuna kiyoyozi cha kutosha.



Akaipokea ile simu kwa mashaka,



"ndio mkuu" Mkuu wa polisi aliongea mara baada ya kupokea simu,



"ulisema jina la kijana wako uliyempa kazi ya kuifuatilia hii kesi ya yule mwanamke muuaji, anaitwa Sajenti Minja?" Rais aliuliza kupitia simu,



"ndio mkuu" Mkuu wa polisi alijibu huku amepiga saluti, utadhani anayeongea nae katoka simu anamuona,



"huyo kijana wako imekuwaje tena amemtorosha muarifu?" Rais aliuliza na kusubiri jibu kutoka kwa mkuu wa polisi,



"hata mimi nimeshindwa kuelewa, ila huyu kijana tumemuweka selo" Mkuu wa polisi aliongea huku akitetemeka,



"huyo kijana namuhitaji hapa ikulu" Rais aliongea,



"sawa mkuu, namleta sasa hivi" Mkuu wa polisi aliongea,



"hapana, sihitaji umlete, nitatuma mtu aje amchukue" Rais aliongea,



"sawa mkuu" Mkuu wa polisi alijibu,



"wewe bado nakujadili, ila kaa ukijua umekalia kuti kavu" Rais aliongea,



"ila mheshimiwa, mimi sija..." Mkuu wa polisi alitaka kujitetea, ila simu ikakatwa, mkuu wa polisi akabaki akiitazama simu tu kwa hasira,



"nimekalia kuti kavu, kuti kavu?" Mkuu wa polisi alijiuliza huku akiangalia kiti alichokalia, kisha akainuka na kuzunguka zunguka mule ofisini kwake, akarudi akakaa, alimlaani sana Sajenti Minja kwa kumuharibia kazi, zaidi mkuu wa polisi akajuta kwa kumuamini Sajenti Minja na kumpa kazi ya kumtafuta mtuhumiwa.



Kufikia hapo alifuata wazo lake la kumpigia muandishi wa habari, maana tayari Rais alishapata taarifa ya Sajenti Minja kumtorosha mtuhumiwa.



**************



Asubuhi ya leo Rais alikuwa anajiandaa kwenda kuongea na waandishi wa habari, alisimama mbele ya kioo huku msichana mmoja akimpaka vipodozi usoni, na pembeni alikuwepo Ray Charles akifuatilia kila hatua.



Baada ya muda mchache maandalizi yalikuwa yameshakamilika, Rais akavaa koti lake la suti,



"wewe utanisubiri hapa" Rais alimwambia Ray Charles aliyekuwa amesimama,



"sawa" Ray Charles alijibu kisha Rais akatoka nje ya ofisi na yule msichana, wakawa wanaelekea katika chumba cha mikutano.



Rais alitembea mpaka katika mlango wa kuingilia, alimkuta bodyguard wake akimsubiri, wakaongozana mpaka katika chumba cha mikutano.



Rais alipoingia ndani ya chumba cha mikutano, watu wote wakasimama, Rais akaenda moja kwa moja katika sehemu ya kutolea hutuba na kusimama, ukapigwa wimbo wa Taifa.



Baada ya wimbo wa Taifa kuisha, Rais aliwasalimia wageni waalikwa, kisha akaendelea,



"Leo mnaweza kushangaaa na kuulizana vipi, mbona ametuita ikulu, kuna nini?, kifupi hakuna kitu kigeni sana msichokijua ambacho nitakieleza hapa.



Leo nimekuja na mambo mawili tu, kwa kuanza ningependa kuanza na jeshi letu la polisi. Jeshi letu la polisi limeoza, limeoza kabisa, hasa hasa hapa katika makao makuu ya polisi, inashangaza sana kuona mtu anaua viongozi wa serikali, alafu huyo mtu yupo hapa hapa mkoani na hakamatwi, ni upuuzi uliokithiri, au jeshi la polisi linashirikiana na waarifu? Sio polisi wote, ila Kuna baadhi wenye mamlaka watakuwa wanashirikiana na waarifu, yaliyotokea jana si mmeyasikia? Kijana mdogo tu wa polisi, mwenye cheo cha usajenti, ameenda katika nyumba ya mtu na akamkuta mtuhumiwa yule mwanamke muuaji, akamkamata vizuri tu, ila akataka kuondoka na mtuhumiwa akiwa yeye peke yake, akawatoa wenzake ndani ya gari, kwa kuwa wenzake hawana vyeo, wakakubali amri ya Sajenti wao. Sasa cha kushangaza huyo Sajenti akafika kituoni bila mtuhumiwa" Rais aliongea na kucheka,



"sio nacheka labda nafurahi, hapana, hii inasikitisha sana, yaani Sajenti wa polisi unashirikiana na mtuhumiwa? Huyo Sajenti amemtorosha mtuhumiwa, watu wakubwa na vyeo vyao walikuwa wanamsubiri Sajenti anampeleka mtuhumiwa, Sajenti akashuka peke yake, upumbavu wa kimataifa huu, yaani mtu anashuka kwa kujiamini na kusema mtuhumiwa ametoroka? Wakubwa zake wakamuweka ndani, ila sidhani kama kumuweka ndani inatosha, ni lazima achukuliwe hatua zaidi, maana huyo ni muhasi, hatufai, ni lazima awajibike kwa matendo yake ya kisaliti" Rais aliongea na kunywa maji kidogo, kisha akaendelea,



"jeshi la polisi nitalipa nafasi nyingine ya kurekebisha makosa yake, na wizara husika, yaani wizara ya ulinzi, nayo lazima ihusike na hii kashfa ya jeshi la polisi, kwa kuwa jeshi la polisi liko chini ya wizara, kwa hiyo basi, endapo endapo jeshi la polisi litashindwa kufanya kazi yake tena, nitaifumua wizara ya ulinzi mpaka jeshi lote la polisi makao makuu.

Hilo la kwanza nimemaliza. La pili ni kuhusu wizara yetu ya katiba na sheria, haina waziri kwa muda mrefu, nilikuwa najaribu kumtafuta mtu ambaye ataweza kuendana na wizara hiyo. Na nimeshampata, kwa leo nitampa ubunge wa kuteuliwa, naomba bwana Said Tambala asimame" Rais aliongea na kisha akasimama yule bwana waliyekuwa nae ikulu siku chache zilizopita,



"huyu bwana kuanzia sasa ni mbunge, ataenda kuapishwa bungeni, kisha nitampa uwaziri.



Nataka watu waende na kasi ninayoitaka mimi, sitaki kiongozi mzembe kabisa, viongozi wazembe mbadilike, maana fagio ninalokuja nalo sio la kawaida.

Sina mengi zaidi kwa leo, ni hayo tu" Rais alimaliza na kisha watu wakampigia makofi, Rais akatoka sehemu ya kutolea hutuba, na kwenda kuwapa mkono baadhi ya wageni na kupiga nao picha, kwa maana hiyo mkutano ulikuwa umemalizika rasmi.



*************http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



BQ hali ya kizunguzungu iliyomuanza siku chache zilizopita ilikuwa bado inamsumbua, ilizidi zaidi kiasi kwamba kwa siku alikuwa anazimia zaidi ya mara moja, hiyo ilikuwa ni hatari sana kwa ajili ya usalama wake.



Asubuhi ya leo aliamua kuingia katika maduka ya madawa kuitafuta dawa ambayo alitakiwa aitumie kwa muda huku akisubiri dawa nyingine kutoka urusi.



Asubuhi hiyo Askari walikuwa wamezagaa barabarani mara baada ya hutuba ya Rais, waliweka msako mkali ndani ya jiji, ila BQ alivaa Dela refu na miwani mipana, kichwani alifunga kiremba cha ki-nigeria, alibadilika muonekano, maana alipishana na Askari kadhaa na hawajamtilia shaka.



BQ akaingia katika duka kubwa la madawa ya binadamu, akaulizia dawa anayoitaka, akaambiwa ipo, akatajiwa na kiasi cha pesa, akatoa.



Wakati muhudumu akizitoa dawa katika shelves na kuziweka katika bahasha ndogo nyeupe, BQ alianza kuhisi kizunguzungu, kikazidi na akaanguka chini vibaya, akapoteza fahamu, wahudumu wa mule na wateja wakapata taharuki, mteja mmoja akatoka mbio kwenda nje kusogeza gari yake, Ile kasi aliyotoka nayo mteja ndio iliwashtua polisi wachache waliopo maeneo yale, polisi wawili wakaingia ndani ya lile duka la madawa, wakakuta baadhi ya watu wamemzunguka mwanamke akiwa amelala,



"Kuna nini?" Askari moja aliuliza huku akimsogelea yule mwanamke,



"ameanguka tu ghafla" Mhudumu mmoja alijibu, na kumfanya yule Askari asogee karibu zaidi ya BQ ambaye kiremba chake kilimvuka baada ya kuanguka, yule Askari akashtuka, akamuita mwenzie kwa ishara, yule Askari mwingine akasogea, kisha wakijadiliana kwa muda, mmoja kati yao akatoa simu na kuangalia picha kadhaa,



"ndio yeye" Askari mmoja aliongea, kisha wakapiga simu, baada ya dakika tano gari ya polisi ilisimama nje ya duka lile, wakambeba BQ na kutoka nae mpaka katika gari na kumlaza katika bodi ya gari, kisha mkono wake mmoja wakaufunga pingu na upande mwingine wa pingu wakaufunga katika chuma ya gari, gari ikaondolewa kwa kasi,



"tumefanikiwa kupata mkuu" Askari mmoja aliongea katika simu huky akitabasamu.



Ndani ya duka la madawa waliwaacha watu wakishangaa lile tukio huku wasijue kinachoendelea....





Polisi waliendelesha gari kwa kasi sana, breki ya kwanza ilikuwa kituoni, wakashuka na wengine wakaizunguka gari, kisha mkuu wa polisi akatoka ndani na kwenda kushuhudia hilo tukio ambalo hajategemea, yaani mtuhumiwa kukamatwa kirahisi rahisi hivyo, eti amedondoka tu dukani alafu akakamatwa? Hiyo kwa mkuu wa polisi ilikuwa si tu habari ya kushangaza, ilikuwa ni habari ya kushangaza zaidi.



Mkuu wa polisi akajongea mpaka katika gari na kumshangaa mwanamke yule aliyekuwa amelala huku akiwa hana fahamu, mkuu wa polisi akatabasamu, kisha akapanda juu ya gari na kwenda kumgusa kabisa, maana kwa matukio aliyoyafanya yule dada, mkuu wa polisi hakuwahi kabisa kuamini kama huyu dada ni mtu, alihisi huenda ni jini.



"alaaaaah, kumbe ni mlemavu, hana mkono mmoja?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akikanyaga kanyaga kile kipisi cha mkono wa BQ,



"Sasa ndio ameanguka na kufa, na nyie mlivyo waoga mpaka maiti mkaifunga pingu" Mkuu wa polisi aliongea kwa ujasiri huku akiwacheka vijana wake,



"hajafa huyo, amezimia tu" Askari mmoja alijibu na kumfanya mkuu wa polisi arudi nyuma ghafla mpaka akapamia ukingo wa bodi ya gari na kuanguka kutoka juu ya gari mpaka chini, ila vijana wake walimuwahi na kumdaka, akawa anahema juu juu,



"Sasa mbona hamjaniambia tangu mwanzo kama kazimia, mmeniacha mpaka nimemsogelea, angeamka je?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa hasira,



"amefungwa pingu, hasingeweza kufanya kitu" Askari mmoja alijibu,



"amezimia muda gani mpaka sasa?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"imeshapita dakika kumi" Askari alijibu,



"mpelekeni hospital, hapa anaweza akatufia" Mkuu wa polisi aliongea na kufanya vijana wake waingie katika gari,



"muweke ulinzi wa kutosha, mpigeni pingu kila sehemu" Mkuu wa polisi aliongea huku akiingia ndani kifua mbele, aliona tayari amemfurahisha Rais, mtuhumiwa ameshampata.



Gari ya polisi iliyombeba BQ, uliondoka na mwendo ule ule iliyokuja nao, tena safari hii na king'ora walipiga na kufanya magari mengine yakae pembeni.



Gari ilifika hospitali na kusimama, kisha wakamshusha BQ na kuingia ndani huku wakiwa wamembeba wenyewe. Walielekea mpaka eneo la mapokezi,



"mpelekeni wodi ya watu maalum, huyu ni mtu maalum" Askari aliongea bila hata kuwapa salamu,



"mmepita kwa daktari lakini, au mmeamua tu kusema apelekwe wodi maalum?" Dada wa mapokezi aliuliza,



"unatuuliza hata huoni sisi ni wakina nani?" Askari aliuliza kwa hasira,



"kila sehemu kuna utaratibu wake, hapa sio polisi, ni hospitali" Dada wa mapokezi alijibu huku nae akionekana hapendi dharau,



"Dada huyu ni mtuhumiwa hatari, hatakiwi kuwekwa wodi iliyo na watu wengine, anatakiwa kuwa katika wodi maalum ambayo Askari watakuwa na nafasi ya kukaa na kumlinda" Askari mwingine aliongea kistaharabu,



"sawa kaka yangu, ila hapa Kuna utaratibu wake, huyo anatakiwa kupimwa kwanza, alafu ndio apelekwe katika hiyo wodi mnayoitaka" Dada wa mapokezi aliongea huku akiwa ameshusha jazba kidogo,



"sawa, utaratibu ukoje?" Askari yule aliuliza,



"nendeni pale chumba cha vipimo, achekiwe kisha atapelekwa wodini, huyu mwanamke inaonekana ana hali mbaya, hamuwezi kumpeleka wodini tu, je akienda kufa uko?" Dada wa mapokezi aliuliza,



"kwa hiyo tumpeleke chumba cha vipimo?" Yule Askari aliuliza,



"mpelekeni tu, ila mlitakiwa muanzie kwa daktari" Dada wa mapokezi aliongea na kufanya Askari wote waliokuja pale hospital waanze kuelekea chumba cha vipimo,



"aisee nyie, sasa mnaendaje wote?" Dada wa mapokezi aliuliza kwa mshangao,



"inabidi twende wote, maana huyu dada ni hatari sana" Askari alijibu,



"jamani si amefungwa pingu huyo? Askari msijitie aibu kwa kweli, yaani wanaume karibia saba mnamlinda mwanamke mmoja aliyefungwa pingu?" Dada wa mapokezi aliuliza huku akishindwa kuzuia tabasamu lake KS dharau. Ikawabidi polisi wajadiliane kwa muda, na mwisho wote wakabaki mapokezi, katika chumba cha vipimo akaingia yule Askari mbishi kuliko wote.



BQ alilazwa kitandani na kisha daktari akaingia katika chumba kile cha vipimo, kwa haraka haraka tu, daktari aliweza kuliona lile jeraha la BQ la kichwani, alijua huenda hilo ndilo lililofanya dada huyo apoteze fahamu, lakini pia daktari alitaka kumfanyia vipimo vingine, kama vya presha na kisukari.



Daktari akavaa mipira mikononi, kisha akachukua kifaa cha kupimia presha,



"naomba usubiri hapo nje" Dokta alimwambia yule Askari aliyekuwa ndani,



"siwezi kuondoka na kumuacha mtuhumiwa" Askari alijibu,



"kaka, ethics zangu haziruhusu nichukue vipimo vya mgonjwa huku mtu hasiye na undugu au uhusiano wowote na mgonjwa akiwa ndani" Daktari aliongea huku akiwa anamuangalia yule polisi,



"hata mimi maadili yangu ya kazi hayaruhusu kukaa mbali na mtuhumiwa" Askari alijibu na kukaa katika kiti kidogo ndani ya chumba kile,



"ni bora nimuache mgonjwa, kuliko kumfanyia vipimo huku nikiwa nimesimamiwa" Daktari aliongea huku akivua mipira mkononi,



"maadili yangu ya kazi yananiruhusu kukukamata wewe endapo utakuwa kinyume na amri za polisi. Mpime au na wewe tukutie pingu" Askari aliongea huku akisimama,



"hiyo haiwezekani" Daktari aliongea kwa jeuri akitoka nje, Askari akasimama na kumzuia, mkwaruzano ukaanza ndani, Askari wa nje wakasikia, mmoja akaingia katika kile chumba,



"Kuna nini kwani?" Askari aliyeingia aliuliza,



"huyo mwenzio anataka kunifundisha kazi, wakati mimi nafanya kutokana na maadili ya kazi yangu" Daktari aliongea,



"huyu anataka nitoke nje ili amfanyie vipimo mtuhumiwa, sasa mimi nimegoma, ndio anataka kuondoka" Askari mbishi aliongea,



"sawa, ebu tutoke tumuache daktari afanye kazi yake, hapa tukibishana na wajuzi wa mambo, hakuna kitachoendelea, tutapoteza muda tu" Yule Askari aliyeingia alimshawishi mwenzake ambaye alikubali kukaa nje na kisha daktari akaendelea na vipimo.



Baada ya dakika ishirini, daktari aliwaita wauguzi na kumuweka BQ katika kitanda cha matairi, wakaanza kumsukuma kuelekea katika wodi maalum.

Askari walikuwa wanatembea nyuma ya kitanda kile kinachosukumwa na wauguzi. Walifika katika wodi na kumuweka kitandani BQ, kisha Askari yule mbishi akamfunga BQ pingu ya mkono akaambatanisha na chuma ya kitanda, kisha akaona haitoshi, akamfunga pingu ya mguu na kuambatanisha na chuma ya kitanda, kisha akatabasamu,



"mhhm jamani!! " Muuguzi mmoja aliguna baada ya kuona hicho kitendo,



"maadili yenu ya kazi yaishie uko uko katika vyumba vya vipimo, huku ni maadili ya kipolisi tu" Askari mbishi aliongea kwa ukali na kufanya wauguzi watoke mule wodini bila kuongeza neno.



******************



Rais anaonekana amekaa katika kiti akitazama mlango mmoja wa chuma, nyuma yake walikuwa vijana waliobeba machela, na Rais mkononi alikuwa akiangalia simu sehemu ya saa, yaani alikuwa akihesabu dakika, na muda huo ilikuwa sekunde ya hamsini na nne, mlango ukafunguka, akatoka Ray Charles, hapo Rais akatabasamu huku akipiga makofi,



"safi sana, leo umetumia dakika chache sana" Rais aliongea huku akitabasamu, lakini Ray Charles hakujibu kitu,



"hey nyie, nendeni mkatoe uchafu" Rais aliongea huku akiwatizama wale vijana waliokuwa nyuma yake, wale vijana haraka wakaingia katika kile chumba chenye mlango wa chuma na kutoka na pandikizi la baba waliolibeba katika machela, alikuwa ameshakufa na kichwa chake kilionekana kupondeka pondeka vibaya sana, kama kimetwangwa na chuma.



"Leo umetumia sekunde hamsini na nne tu, inaonesha umeimarika sana, tofauti na yule mtu wa mwisho, yule mtu wa mwisho ulitumia dakika moja na sekunde nne, safi sana Ray" Rais aliongea huku akimpiga piga mgongoni Ray Charles ambaye alikuwa kimya.



Kipindi hicho wale vijana wengine walikuwa wakiuweka ule mwili wa yule mtu katika kiroba, kisha wakakifunga vizuri,



"huyo mtamtoa usiku na mtaenda kumtupa baharini, kuna mwenzake mwingine atakuja huku kufa usiku, mtawajumuisha wote. Haya nendeni nje" Rais aliongea huku akisimama katika kiti chake na yeye akaelekea nje.



Hiyo ni tabia ya Rais, uwa anawatafuta wale watu shupavu au wenye uwezo wa kupambana na kisha uwaleta wapambane na Ray Charles ili kumuamrisha zaidi katika uwezo wa kupigana, kwa maana Ray bado alikuwa mzito mzito, kwa hiyo hapo alikuwa anamjengea kasi Ray Charles.



Vijana wengi waliokuwa wakipotea mitaani bila taarifa, mara nyingi waliokotwa asubuhi katika bahari huku wakiwa ndani ya magunia, hakuna aliyejua nani anayeua vijana hao, hiyo ilikuwa ni siri ya wachache tu.



Rais alivyotoka nje, aliwakuta wale vijana wakiwa pale,



"jioni ndio muda wa kazi, mnatakiwa mvamie na mumtoroshe yule bwana, nataka mission ionekane ya kutoroshwa, ili baadae watu wasiangaike kumtafuta, wajue amejificha" Rais aliongea huku akiwatazama vijana kwa zamu, ambao walitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na Rais,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"kila kitu kinaenda kwa mipango, afe yule kibaraka, kisha tutamtafuta mwenzake" Rais aliongea na kuondoka, nyuma yake alikuwa Ray Charles.



*************



Mida ya saa kumi jioni, Sajenti Minja bado alikuwa yupo selo, hii ilikuwa ni siku ya tatu mfululizo, hakujua hatma yake. Hapo aliambiwa siku inayofuata atapelekwa magereza, kwa maana kukaa selo mwisho ni siku tatu, kitu kingine kilichomshangaza Sajenti Minja ni kuwa hakuna hata mtu aliyeenda kumuona, Iwe Sajenti Minja au Edward Sambo, hakujua sababu.

Sajenti Minja akiwa amekaa hapo chini na baadae ya watu wengine, alisikia kelele zikitokea nje, mule ndani ya selo wote wakapata taharuki mara baada ya kusikia milio ya risasi, watu wote selo wakakimbilia vyumbani, maana walihisi hali ya hatari.

Mara wakasikia mlango wa selo ukifunguliwa, kisha wakaingia watu wawili waliokuwa na silaha, na nyuso zao walizifunika kwa vitambaa vyeusi, waliacha wazi eneo la macho tu.



Wale watu wakaanza kuingia kila chumba na kukagua, kuna mtu walikuwa wanamtafuta. Walipofika katika chumba alichokuwepo Sajenti Minja, mmoja kati ya watu wale akamsogelea na kumkumbatia,



"tumekuja kukuokoa, maana leo ilikuwa siku yako ya kufa, tumetumwa na jeshi la ulinzi" Yule mtu aliongea na kumrushia Sajenti Minja bunduki, Sajenti Minja akaidaka, kisha wakaanza kutoka huku wale watuhumiwa wengine wa selo wakishangaa tu.



Sajenti Minja alitoka na wale watu mpaka nje, ambapo alikuta Askari kadhaa wakiwa chini ya ulinzi, Sajenti Minja alienda na kuingia ndani ya gari, kisha wale watu wengine wakaingia, na gari ikaondoka kwa kasi.



Baada ya gari kupotea kabisa katika eneo la polisi, wale vijana wakatoa vitambaa usoni, hakuna hata mmoja Sajenti Minja aliyemjua, wote walikuwa watu wageni kwake.



Gari iliendelea kutembea bila mtu yoyote kuongea, ubaya hata Sajenti Minja hakujua wanapoelekea, kwa maana alikaa upande wa nyuma wa gari na hakukuwa na vioo.



Baada ya muda mfupi gari ikasimama,



"tunakuomba tukuzibe macho boss, kwa maana hutakiwi kujua upo wapi mpaka baadae" Kijana mmoja aliongea jua heshima mbele ya Sajenti Minja,



"kwa hiyo mtaniziba macho mpaka kesho?" Sajenti Minja aliuliza kwa wasiwasi,



"hapana, ukishaingia ndani tu unafunguliwa kitambaa, usiogope mkuu kwa maana mwili wote tutakucha huru, ila macho ndio tutaziba" Kijana aliongea huku akitabasamu, Sajenti Minja akakubali. Sajenti Minja akafungwa kitambaa na kutelemka, alitembea kwa muda mchache mpaka akahisi ameingizwa katika chumba, akasikia mlango ukifungwa, kisha akafunguliwa kitambaa usoni, akajikuta yupo ndani ya chumba kizuri sana.



"nenda kaoge na ukitoka uko utakuta chakula safi" Yule kijana aliongea, kisha Sajenti Minja akaingia bafuni kuoga huku akijiuliza kwanini jeshi limsaidie, au limejua hana hatia? na kwanini aletwe katika chumba hicho kizuri, kwanini wasingempeleka kambini?.



Sajenti Minja alijiuliza huku akioga. Baada ya dakika kumi, Sajenti Minja alitoka bafuni na kukuta amewekewa kitandani suruali ya mazoezi na mezani Kuna chakula cha kutosha, akakimbilia mezani na kuanza kula, maana hakuwa amekula muda mrefu sana. Alikifakamia chakula kwa haraka. Alitumia muda mchache tu, kisha akaenda mlangoni na kufunga mlango, akarudi mezani akanywa maji, kisha akajitupia kitandani, usingizi ukampitia, akalala kama amekufa, maana ni muda mrefu aliukosa usingizi.



Sauti ya mlango kugongwa ndio ilimuondoa usingizini, akakurupuka na kuangalia saa, ilikuwa saa mbili na nusu usiku, akakumbuka alilala kwenye saa kumi na moja hivi.



Mlango ukagongwa kwa nguvu zaidi, Sajenti Minja akainuka na kuvaa suruali ile mpya aliyoletewa, kisha akainuka na kwenda kufungua mlango, atakutana na binti,



"unaitwa" Binti aliongea bila salamu, Sajenti Minja hakujali, akatoka huku akimfuata huyo binti, walitembea huku Sajenti Minja akiyaangalia mazingira ya eneo hilo, walitembea na kukatiza eneo moja, kutoka kwenye jengo moja na kwenda jengo lingine, Sajenti Minja akashtuka, alilijua vizuri hilo eneo, lilikuwa eneo la ikulu, ila hakusema kitu, akaendelea kumfuata yule dada.



Safari yao iliishia katika eneo kama ukumbi, na mbele kulikuwa na chumba kingine chenye mlango wa chuma, Sajenti Minja akaambiwa asubiri hapo.



Baada ya muda akaingia Rais, Sajenti Minja akashangaa zaidi, akajiuliza anataka kupandishwa cheo au anataka kupewa ulinzi wa Rais?

Raia akasogea na kukaa katika kiti ambacho kiliangalia ule mlango wa chuma, kisha akaitoa saa yake, wala hukutaka kuongea sana,



"fungueni mlango" Rais aliongea kwa sauti kisha vijana wanne wakaingia pale, Sajenti Minja aliwatambua, ni wale walioenda kumtorosha kituo cha polisi.



Vijana wakaingia na kwenda kuufungua kidogo ule mlango,



"ingia pale, ukitoka tutaongea" Rais alimwambia Sajenti Minja, kisha Sajenti Minja akawa anaelekea katika ule mlango huku akijiuliza Kuna nini?



Aliufikia mlango na kuingia, akastaajabu mara baada ya kumkuta Ray Charles ndani, Sajenti Minja akataka kutoka, ila mlango ukajifunga,



"unatakiwa upambane ili ujiokoe, wewe ni msaliti, unashirikiana na yule mwanamke muuaji na ndio maana ulimtorosha" Sauti ya Rais ilisikika kupitia spika za mule ndani ya chumba. Sajenti Minja sasa ndio akajua maisha yake yako hatarini zaidi kuliko alivyokuwa selo.



Wakati Sajenti Minja akiwaza hayo, Ray Charles alikuwa akimsogelea taratibu huku kichwa chake kikiwa kinataka kumaliza kazi haraka ili akapate sifa kwa Rais, sekunde kumi zilikuwa zimeshakatika tangu Sajenti Minja aingie mule ndani.



Rais alikuwa akihesabu huku akitabasamu, ilipofika sekunde ya thelathini, mlango ulifunguliwa, akatoka Ray Charles na nyuma yake alionekana Sajenti Minja akiwa amelala na mwili umepondwa pondwa vibaya, Damu zilienea chumba kizima.



"hii nzuri, umetumia muda mchache zaidi" Rais aliongea huku akitabasamu na kipindi hicho wale vijana wengine waliingia na kuuchukua mwili wa Sajenti Minja, wakautoa pale,



"ebu ngojeni, amekufa?" Rais aliuliza huku akiinuka,



"tayari mkuu" Kijana mmoja alijibu,



"malizia kabisa ili tupate uhakika" Rais aliongea kisha yule kijana akatoa bastola na kumpiga risasi nyingi Sajenti Minja,



"basi" Rais aliongea na kuelekea nje.



Ndani wale vijana waliuingiza mwili wa Sajenti Minja katika gunia, kisha wakautoa na ule mwili mwingine wa yule pandikizi la baba aliyeuawa mchana, wakaipeleka katika buti za gari, kisha wakaondoka na yale magari, miili wakaenda kuitupa baharini kwenye kina kirefu cha maji.



Habari ya Sajenti Minja ikaishia hapo....







Wale vijana baada ya kuitupa miili ya Sajenti Minja na yule pandikizi la mtu, wale vijana walikuwa wakijirudisha huku kila mtu akiwa kimya, hakuna aliyeongea. Gari yao ilienda mpaka ikakaribia ikulu, kijana mmoja akaguna,



"nini wewe" Mwenzake aliyekaa nae siti ya nyuma akauliza,



"aisee sikioni kitambulisho changu, nna wasiwasi kitakuwa katika gunia la ile maiti ya pili, maana nakumbuka wakati naiweka ile maiti katika gunia, kitambulisho kilikuwa katika mfuko wa shati" Yule kijana aliongea,



"Bob huu uzembe, twendeni tu ndani, labda kitakuwa ndani tu" Dereva wa ile gari aliongea, alionekana kuchoka,



"Sasa tukishaingia ndani alafu ikaonekana kitambulisho sina? unataka niuawe ndani kwa sababu ya uzembe?" Yule jamaa aliuliza,



"kweli, sio poa mwenzetu akiuawa, bora turudi tukaangalie katika yale magunia ya maiti" Kijana mwingine alimuunga mkono,



"Sasa tufike tena kule, tuanze kuingia kwenye maji tulowane, tufungue gunia,..dah" Dereva wa ile gari aliongea kwa kulalamika,



"nyie twendeni tu, tukifika uko mimi mwenyewe nitaingia na kufungua gunia" Yule kijana aliongea,



"poa bwana, ila Dizonga huu ni usumbufu mshkaji wangu" Dereva aliongea na kutaja jina la yule mwenzake aliyesahau kitambulisho,



"kusahau si kupo tu, kwani Kuna mtu hajawahi kusahau hapa?" Mwingine nae aliongea baada ya kuona kama Dizonga analaumiwa.



Dereva akageuza gari na kuanza karudi huku akionekana kukasirika.



" ebu simama nikachukue dawa, mtoto wangu anasumbuliwa na mafua" Dizonga aliongea baada ya kuona duka la dawa,



"Dizonga unazingua mshkaji wangu, tunazidi tu kuchelewa" Dereva alilalamika huku akisimamisha gari,



"tusamehane" Dizonga aliongea huku akitelemka katika gari, akakimbia kuelekea kwenye duka la madawa na kuwaacha wenzake wakimtazama tu,



"Dizonga anazingua sana" Yule jamaa aliyekaa nyuma aliongea,



"wewe si ulikuwa unamtetea?" Dereva aliongea kwa jazba,



"lazima nimtetee, sisi ni timu, wewe unafikiri Rais angejua kuwa Dizonga kapoteza kitambulisho, unadhani angemuacha hai?" Yule jamaa wa nyuma aliuliza,



"aaagh, kazingua tu" Dereva aliongea na kipindi hicho Dizonga alikuwa akiingia katika gari.



'"samahanini nimechelewa kidogo" Dizonga aliongea Ila hakuna aliyemjibu, Dereva akaondoa gari.



Walifika baharini na kuegesha gari yao, kisha wakashuka na kuelekea eneo ambalo waliipeleka ile miili.



Walifika lile eneo, kisha Dizonga akavua viatu,



"nyie nisubirini hapa, ngoja niingie mwenyewe" Dizonga aliongea huku akiingia katika maji,



"Sasa mbona umeingia na nguo?" Mwenzake mmoja aliuliza,



"nikisema nivue nitachekelewa, miili yenyewe inaonekana kwa mbali" Dizonga alijibu huku akitembea katika yale maji yanayomfikia kiunoni. Alitembea mpaka alipofika katika maji ya shingo, akajitupa na kuanza kuogelea kuelekea miili ilipo, aliwaacha wenzake wakimuangalia tu.



Wenzake waliendelea kukaa ufukweni pale, baada ya dakika ishirini, Dizonga alionekana akirudi huku akivuta gunia lenye mwili wa Sajenti Minja. Alisogea mpaka ufukweni, kisha akachana lile gunia na kuutoa mwili wa Sajenti Minja, alafu akalichana lile gunia na kutafuta kitambulisho chake, akafanikiwa kukipata, akatabasamu kisha akausukumia majini mwili wa Sajenti Minja.



"tuondokeni sasa" Dereva aliongea,



"hakuna cha kusubiri" Dizonga alijibu huku akizivua nguo zake zilizokuwa zimelowana, akazitia katika mfuko wa nylon kisha ule mfuko akauingiza katika begi lake la mgongoni, kisha yeye akaingia katika gari akiwa mtupu,



"tembeza moto bab" Dizonga aliongea kisha Dereva akaondoa gari kwa fujo.



****************



Ndani ya chumba cha hospitali, BQ fahamu zilimrejea, uwa hakurupuki fahamu zinapomrejea, uwa anaendelea kufunga macho huku masikio na pua vikifanya kazi ya kutambua eneo husika. BQ alivuta harufu ya dawa, akakumbuka mara ya Mwisho alikuwa duka la madawa, lakini masikio yake bado hayajasikia chochote, kulikuwa na hali ya utulivu sana.



BQ taratibu akafungua macho, akajikuta yupo amelala kwenye kitanda kilichokuwa na mashuka meupe, na pembeni akaona Kuna chuma la drip, hapo akahisi mkono wake ndio umeunganishwa na ile drip iliyokuwa inang'inia katika lile chuma. BQ akageuza shingo ili kuhakikisha, ila alitangulia kuiona pingu, akashtuka, tayari aligundua yupo chini ya ulinzi.



BQ akataka kujivuta ili akae, akahisi miguu mizito, akanyanyua shingo na kuona miguu yote imefungwa pingu, akachoka kabisa, yaani walimuweza haswa.



akajaribu kuivuta miguu kwa nguvu, lakini hakufanikiwa kufungua, ni kelele tu zilisikika baada ya chuma ya pingu kusuguana na chuma ya kitanda, BQ akatoa tusi la nguoni, na muda huo alisikia hatua za mtu akisogea mlangoni mwa chumba alichopo, BQ akajilaza haraka na kufunga macho tena, akajifanya amezimia.



Zile hatua zilizidi kusogea na kisha mlango ukafunguliwa, akaingia Askari, akatupa macho kila pembe ya kila chumba, kisha akasogea mpaka dirishani na kufungua, akatoa kichwa na kutazama nje, akaingiza kichwa ndani na kufunga dirisha,



"vipi, mbona unakagua hivyo?" Askari mwingine aliingia na kumuuliza yule Askari anayekagua katika ile wodi aliyolazwa BQ,



"nimesikia kama mtu anagonga vyuma humu ndani" Askari wa hawali aliongea na kumfanya mwenzake acheke,



"wee jamaa wewe, itakuwa usingizi unakusumbua, maana nasikia leo umekesha hospital hapa" Askari mwingine aliongea huku akiendelea kucheka,



"sidhani kama ni usingizi, nimesikia kabisa kwa macho yangu" Yule Askari aliongea,



"si unaona sasa, umesikia kwa macho yako? Sio masikio" Askari mwenzake aliuliza na kucheka,



"aya bwana, ndio umekuja kunipokea?" Askari wa hawali aliuliza,



"ndio, nenda kapumzike bwana, maana Kuna muda mtu akiwa na usingizi mwingi hata akili inapungua" Mwenzake aliongea na kuendelea kucheka,



"sawa kaka, acha mimi niende" Askari wa hawali aliongea huku akitoka nje, mwenzake akamfuata na wakafunga mlango na kutoka nje, BQ akafungua macho, akaangaza macho wodi yote,



"mtihani huu" BQ aliongea peke yake na kutikisa kichwa kwa masikitiko.



Akatupia macho kwenye chupa ya drip, akaona ndio kwanza ipo nusu, pia alihisi kiu ya maji na hukutaka kuomba msaada wa kuyapata hayo maji. Wakati akiwa bado hajui cha kufanya, alisikia hatua za mtu zaidi ya mmoja zikisogelea mlango wa wodi aliyokuwepo, BQ akafunga macho na kujikausha, kisha mlango ukafunguliwa, alikuwa mkuu wa polisi na watu wengine akiwepo daktari, wakaingia na kukizunguka kitanda,



"vipi maendeleo yake lakini?" Mkuu wa polisi alimuuliza daktari,



"bado sioni unafuu, nilitegemea atapata fahamu leo, ila naona imeshindikana" Daktari alijibu,



"ni nini umegundua kinamsumbua mpaka kapoteza fahamu muda mrefu hivi?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"ni jeraha la kichwani, bado bichi sana, yaani hilo jeraha hajapona kabisa, sasa linapoanza kumuuma humletea maumivu ya kichwa na kusababisha kupoteza fahamu" Daktari aliongea huku akisoma katika kijitabu chake,



"kwa hiyo dawa yake ni nini?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"kwa sasa hakuna dawa ya moja kwa moja, ila ninachofanya ni kumchoma sindano za kukausha kidonda hicho, na kingine kipo upande wake wa kushoto, na vyote ni vidonda vya risasi" Daktari aliongea na kumuangalia mkuu wa polisi,



"ataamka tu, safari hii lazima afungwe" Mkuu wa polisi aliongea huku akielekea nje, na wengine wakamfuata. Walipotoka tu, BQ akazidi kujiona yupo hatarini, uwa na roho ngumu, ila siku hiyo machozi yalimtoka, hakuwa na msaada kutoka kwa mtu yoyote.



**********



Siku ya leo Rais alikuwa kufuatilia habari, alijaza magazeti mengi katika meza yake, na kila gazeti alikuwa ameshalipitia, ila Kuna habari mbili tu zilionesha kumfurahisha, habari ya kwanza ni ile ya kukamatwa BQ, na habari ya pili ni ile iliyoonesha Sajenti Minja ametoroshwa kituo cha polisi.



Aliifurahi sana kwa maana aliona kazi yake dhidi ya watu wanaomsumbua inaisha kirahisi sana, kwa maana BQ tayari yupo mikononi mwa polisi, kwa hiyo suala la kumuua ni mipango midogo midogo tu.



Kitu kingine alichokipenda ni kuona kuwa amewaaminisha watu kuwa Sajenti Minja ametoroshwa na watu wakaamini, ila ukweli aliujua yeye na watu wake, kuwa Sajenti Minja tayari ameshakufa.



"Ray" Rais aliita na kwa haraka mlango wa kuingilia ofisini ukafunguliwa, akaingia Ray Charles aliyekuwa amevaa shati nyeusi na suruali ya kitambaa,



" nimepata wazo, nataka tushirikiane. Nataka ukamuue yule dada kule hospitali, usifanye makosa tena, endapo utashindwa tena kumuua, mwanao nitamuua" Rais aliongea huku akitabasamu,



"hakuna shida, ila uwa nakosa raha kwenye mambo kama haya unaishirikisha familia yangu" Ray Charles aliongea kwa utulivu,



"Ray, inabidi sasa familia yako niingize, kwa maana naona ufanisi wako umepungua Ray" Rais aliongea huku akiinuka na kumpiga piga mgongo Ray Charles, ambaye alikaa kimya,



"na kama nitakuta polisi, niue wote?" Ray Charles aliuliza,



"kweli umeuliza swali zuri, nitaongea na mkuu wa polisi" Rais aliongea,



"sawa, na nitaenda muda gani kutekeleza hilo agizo?" Ray Charles aliuliza,



"kesho kabla jua halijaonekana, nataka roho ya BQ iwe haipo" Rais aliongea,



"sawa mkuu" Ray Charles alijibu,



"nisubiri nje hapo" Rais aliongea na kisha Ray Charles akatoka nje. Rais akachukua simu yake na kumpigia mkuu wa polisi,



"naam mkuu" Mkuu wa polisi aliongea baada ya kupokea simu,



"naona sasa mmekuwa wepesi mpaka waarifu wanakuja kutorosha watu wao kituoni?" Rais aliuliza,



"hapana mkuu" Mkuu wa polisi alijibu,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"ni nini sasa kinaendelea kiasi kwamba mmedharaulika kiasi hicho? muarifu kuja kumtorosha mtu kituoni" Rais aliongea,



"hata mimi sielewi, nadhani kutakuwa na polisi wanashirikiana na waarifu" Mkuu wa polisi aliongea,



"huyo Minja aliyetoroshwa wewe ndiye ulimpendekeza aisimamie na kumtafuta yule mwanamke muuaji. Unataka kuniambia ulikuwa hujui uhusiano uliopo kati ya Sajenti Minja na yule mwanamke muuaji?" Rais aliuliza,



"sikuwa nafahamu kitu mkuu" Mkuu wa polisi alijibu,



"kifupi sina imani na nyinyi tena, kwa hiyo sasa, naomba uondoe polisi wako wote katoka ile hospital ambayo yupo yule mwanamke muuaji, maana mnaweza kumtorosha tena na kudanganya ametoroka mwenyewe" Rais aliongea kwa mamlaka,



"kwa hiyo mkuu kama kutakuwa hakuna polisi hata mmoja, si itakuwa hatari zaidi na kuwa rahisi kwa mtuhumiwa kutoroka?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"unaniuliza sasa?, wewe kama nani?" Rais aliuliza,



"sawa sawa mkuu, nitafanya kama ulivyoagiza" Mkuu wa polisi aliongea kwa upole,



"kuanzia sasa hivi, ondoa Askari wote, nitapeleka watu makini zaidi kumlinda yule mwanamke, kwanza nilikuambiaga umuue kabisa, ila wewe unaendelea kumlea" Rais aliongea kwa hasira,



"ni kweli mkuu, ila nilikuwa nasubiri nafasi ya kufanya hivyo" Mkuu wa polisi alijitetea,



"pumbavu, unazidi kunikera tu, wewe nitakushusha cheo na sitokuamisha mkoa" Rais aliongea na kukata simu, akamuacha mkuu wa polisi akiangalia simu yake tu,



"dah" Mkuu wa polisi alishusha pumzi na kusikitika, kisha akapiga simu hospitali na kuwataka Askari wote waondoke eneo hilo, Askari waliishangaa hiyo amri, ila hakuna aliyehoji, hawakufundishwa kuhoji amri za wakubwa, walifundishwa kutii tu.



************



Mida ya saa tatu usiku, Ray Charles alikuwa kwenye korido za hospital akielekea katika wodi aliyolazwa BQ, haikuwa tabu sana usiku ule mtu kuonekana katika korido, kwa sababu ni wodi maalum kwa hiyo mpaka mtu aingie mule, ujue amekaguliwa vya kutosha.



Ray Charles alitembea kwa mwendo wa taratibu, alionekana hana haraka. Alitembea mpaka ilipo wodi ya BQ. Wakati huo BQ alikuwa bado anajaribu kufanya jaribio la kufungua pingu, ila hakufanikiwa. BQ alisikia hatua za mtu akisogea mlangoni, BQ akafunga macho na kuendelea kujifanya amepoteza fahamu.



Ray Charles akaingia na kumkuta BQ akiwa amefunga macho, Ray Charles akafunga mlango kwa ndani, kisha akasogea dirishani na kufunga madirisha, kisha akashusha pazia. Akarudi mpaka kitandani na kumuangalia BQ aliyekuwa amelala, Ray Charles akainua mkono wake na akauangalia, kisha akavua gloves na kubaki uhalisia wake, yaani mkono wake wa chuma ulibaki wazi. Ray Charles akanyanyua mguu wa BQ wenye pingu na kuutizama, kisha akapiga ngumi ile pingu, pingu ikaachia, BQ akawa haelewi kinachoendelea, alijiuliza huyo aliyeingia ni polisi au daktari? Lakini hakuwa na jibu, na wala hakuwa na mpango wa kufungua macho.



Ray Charles akasogea mpaka kilipo kichwa cha BQ kisha akachomoa drip na mipira mingine iliyokuwa inamsaidia BQ kupumua. Kisha Ray Charles akakinyanyua kichwa cha BQ na kukilaza juu ya chuma ya kitanda, alichotaka kufanya ni kupiga ngumi kichwa cha BQ na kumpasua kabisa.



Ray Charles akakiweka vizuri kichwa cha BQ juu ya chuma ya kitanda, kisha akavuta ngumi kali sana kuishusha juu ya kichwa cha BQ......









Kile kitendo cha Ray Charles kumuweka kichwa kwenye chuma, kilisababisha BQ ajiulize ni huduma gani hiyo mpya anataka kupewa, pia hata mikono iliyobeba kichwa chake ilikuwa migumu, haikuwa mikono ya kawaida.



Kwa hiyo sasa wakati kichwa cha BQ kikiwa juu ya ile chuma, Ray Charles akajiandaa na kuachia ngumi kali kuelekea katika kichwa cha BQ, BQ ghafla akafungua macho, ndipo akashtuka kuona ngumi ikija usoni, BQ akakwepesha kichwa, Ile ngumi ya Ray Charles ilipiga chuma ya kitanda mpaka ikakatika. BQ akajivuta na kujiinua, maana tayari pingu ya mguuni ilikuwa imeshakatwa na Ray Charles, ilibaki ya mkononi tu.



Ray Charles yeye alishangaa baada ya BQ kuikwepa ngumi ile, maana alijua BQ hana fahamu, ila bado Ray Charles alikuwa na nafasi nyingine ya kummaliza BQ, kwa BQ alikuwa na pingu mkononi. Ray Charles akamfuata BQ, BQ akaona Kuna haja ya kujitetea, BQ akachomoa drip, kisha ile chuma ya drip akamrushia Ray Charles, Ray Charles akaidaka, bado akawa anamsogelea BQ, BQ akaruka upande wa pili wa kitanda na kisha akainama, alipoinuka akaamka mzima mzima na kitanda, akamvaa Ray Charles, Ray Charles akajikuta anasukumwa kurudi nyuma, Ray Charles akakimata kitanda, kisha akakiinua juu kikiwa na BQ, alafu akakipigiza chini, BQ akadondoka, akauona mkasi, akachukua na kwa utaalam wa hali ya juu akafungua pingu ya mkononi kwa kutumia miguu na mkasi, akawa huru sasa, BQ akasimama na kutabasamu, akakisogeza kitanda pembeni na kusogea karibu kabisa na Ray Charles,



"Leo umepotea njia, sio kama ulivyoniotea mwanzo na risasi" BQ aliongea na kukunja vizuri gauni la hospitali.



Ray Charles alibaki kimya akimuangalia tu, BQ akakunja ngumi ya mkono mmoja,



"Sasa sogea" BQ aliongea na kujitayarisha kwa pambano, Ray Charles akaanza kumsogelea taratibu, BQ akamtisha, ila Ray uwa hatishiki. BQ kuona hivyo, akapiga hatua moja nyuma BQ kisha akarusha teke kali lililotua katika kichwa cha Ray Charles, Ray Charles akayumba, akakasirika kwa kupigwa lile teke,



"we mwepesi tu, ila uwa unanikutaga sipo vizuri kiafya" BQ aliongea huku akicheka na kuzidi kumuongezea hasira Ray Charles, Ray Charles akaing'uka mikono kama anatoa uchafu, kisha akakunja ngumi sasa, BQ akajiandaa na mkono wake mmoja.



Ray Charles alirusha ngumi za haraka haraka kama ishirini hivi, BQ alijikuta anarudi nyuma mpaka akaenda kugota kwenye kioo, maana hakuwa na uwezo wa kupangua zile ngumi, endapo angezuia ngumi hata moja tu, angevunjika mkono.



BQ akawa anahema kwa haraka haraka, yaani pale ndio ilikuwa mwisho, hana pa kukimbilia tena,



"one two, one two" Ray Charles aliongea huku akiruka ruka na akirusha rusha ngumi kama mpiga masumbwi, BQ alipata uoga wa ghafla,



"Tuendelee sasa" Ray Charles aliongea na kumfuata BQ kwa kasi, kisha Ray Charles akapiga ngumi mbili za haraka kulenga kichwa cha BQ, BQ akainama, zile ngumi zikapasua kioo dirishani, Ray Charles hakujali hilo, yeye alitaka kuua tu. Ray Charles akasogea tena na kuachia ngumi nyingine kali zaidi, BQ akainama kisha akakamata miguu ya Ray Charles na kujaribu kumbeba, alishindwa. Akaamua amsukume tu,



"ngoja kwanza" BQ aliongea huku akihema,



"ebu nipe hayo maji" BQ aliongea huku akimnyooshea kidole nyuma ya Ray Charles, Ray Charles akafanya makosa kugeuka, BQ akavuta fire extinguisher iloyopo ukutani na kumpiga nayo kichwani, Ray Charles akapepesuka, BQ akapiga tena, kisha akampulizia usoni, Ray akawa haoni mbele kutokana na ile gesi ya fire extinguisher. Ray Charles akajifuta macho na kuweza kuona vyema tena, ila cha ajabu hakukuta mtu, akachungulia dirishani, akamuona BQ akikimbia kwa nje, tayari BQ alishatokea dirishani muda mrefu tu.



"shit" Ray Charles aliongea kwa hasira na kisha akajitupa dirishani kwenye lile jengo la ghorofa moja. Ray Charles akatua juu ya gari ndogo, mpaka ile gari ikabonyea kutokana na uzito wa Ray Charles.



Ray Charles akarukia chini na kuanza kukimbia kuelekea mahali BQ alipokimbilia. Ray Charles alikimbia kwa muda kidogo ila hakufanikiwa kumpata BQ, Ray Charles akapiga ngumi mti kwa hasira, kisha akawa anaondoka pole pole mara baada ya kashindwa tena kumuua BQ.



Aliumia sana kumkosa BQ, maana aliambiwa endapo atashindwa kumuua BQ, basi mtoto wake atakuwa matatizoni. Ray Charles alikosa raha, maana aliijua vyema roho ya Rais.



Ray Charles akaondoka zake, kitu ambacho hakujua ni kuwa ile njia anayoondoka nayo, ndio hiyo hiyo aliyoondoka nayo BQ.



**************



Tom alikuwa na siku kadhaa hajamuona Sajenti Minja, hata alipopiga simu, simu ya Sajenti Minja ilikuwa haipatikani.



Tom alikuwa yupo kwenye jumba moja la kubeti, alikuwa akiangalia michezo ya mbio za mbwa na farasi. Baada ya nusu saa Tom aliinuka na kuanza kuondoka, alitoka nje na kupiga hatua mbili tatu, akasimama ili asubiri gari ipite ili avuke barabara, ila gari aliyokuwa akiisubiri ipite ilisimama mbele yake jirani kabisa na yeye, kisha Dereva wa ile gari akashusha kioo,



"Habari yako kaka?" Dereva wa ile gari alimsalimia Tom,



"aaagh nzuri tu, vipi?" Tom alijibu kwa kigugumizi huku akimtazama yule Dereva ambaye alikuwa ni mama mtu mzima kidogo,



"safi, naomba uninulie gazeti hapo, maana nguo niliyovaa nashindwa hata kutelemka katika gari" Yule mama aliongea huku akimpatia noti elfu moja Tom,



"gazeti gani?" Tom aliuliza huku akiipokea ile pesa,



"leta udaku spesho" Mama alijibu huku akitabasamu. Tom akasogea mpaka sehemu iliyo na gazeti na kununua hilo gazeti, ila aliona gazeti moja la siasa likiwa na picha ya Sajenti Minja,



"SAJENTI WA POLISI ALIVYOTOROSHWA NA WAARIFU WENZAKE" hicho ndio kichwa cha habari kilichoandikwa juu ya gazeti lile,



"nipe na hili" Tom aliongea huku akitoa pesa yake mfukoni na kupewa lile gazeti la siasa, Tom akaweka mfukoni gazeti lake, kisha akampelekea yule mama wa kwenye gari gazeti lake la udaku.



Tom baada ya kumpa yule mwanamke gazeti, Tom alivuka barabara na kuanza kuelekea nyumbani, njia nzima alitamani asome gazeti, aliona kama anachelewa kufika, ila nafsi ilimzuia, Tom akaona ni bora akalisomee nyumbani tu huku akiwa ametulia.



Tom alikaza mwendo mpaka nyumbani, akamkuta mpenzi wake akikatakata spinach, Tom akavua shati na kukaa kitandani, akatoa gazeti mfukoni na kuanza kupitia ile habari inayomuhusu Sajenti Minja, aliipitia yote huku jasho jembamba likimchuruzika asomapo kila aya,



"mwenzetu leo vipi?" Mpenzi wake alimuuliza baada ya kuwa kumtazama Tom muda mrefu,



"kwani vipi?" Tom nae aliuliza huku akimkata jicho mpenzi wake,



"umekuja tu wangu wangu hata huongei, unaanza kusoma mgazeti, jasho linakutoka, kwanza sijawahi ona ukinunua gazeti, sijui leo imekuaje?" Mpenzi wake aliuliza huku akiinuka katika kochi,



"Sajenti Minja kafukuzwa kazi, pia alitoroka kituoni baada ya kukamatwa kwa kushirikiana na yule dada muuaji ambaye yeye ndio aliyefanya mpaka leo sina kazi" Tom alimwambia Mpenzi wake,



"huyo Sajenti Minja ndio nani?" Mpenzi wa Tom alihoji,



"we nawe kichwa chako kama cha bata, hakitunzagi kumbukumbu, humjui Sajenti Minja? si yule rafiki yangu polisi" Tom alijibu,



"khaaa, kumbe ndio yule? Sasa ni kweli uwa anashirikiana na huyo mwanamke muuaji?" Mpenzi wake aliuliza,



"hapana kwa kweli, hii haiwezekani kabisa, hapo walimuonea " Tom aliongea kwa masikitiko,



"Sasa nani aliyemtorosha polisi kama hana uhusiano na waarifu?" Mpenzi wake aliuliza,



"inawezekana ametoroshwa kweli, ila sio na waarifu, itakuwa mipango yake tu, kwa maana yule ni komando, kama ni waarifu wamemtorosha Sajenti Minja, kwanini hao waarifu hawajaenda kumtorosha hospital yule dada muuaji?, maana ni mwenzao" Tom aliuliza,..



"Sasa unanihoji mimi kwani mimi najua kitu? Ngoja niende gengeni kuchukua nyanya, maana nikikaa hapa nitahojiwa weee, kama mimi ndio tageti Minja, sijui sadent Minja!" Mpenzi wake aliongea huku akielekea nje na kumuacha Tom akiwa anairudia kuisoma ile habari.



"kwanini atoroshwe Sajenti Minja, tena ndani ya kituo kikuu cha polisi wenye silaha za kutosha? Kwanini hasitoroshwe yule dada muuaji ambaye yupo tu hospital na ulinzi wa kule hospital ni wa kawaida tu" Tom alijiuliza huku akijikuna kidevu,



"huu mchezo huu" Tom aliongea mwenyewe na kujilaza kitandani.



**************



Ray Charles alikuwa bado anatembea huku akiwaza namna ya kumdanganya Rais kuhusu BQ. Ray Charles alitembea na giza lile huku akiwa amevurugwa akili kabisa, hakujua ni kipi atakutana nacho endapo atafika kwa Rais.



Ray Charles aliendelea na mwendo mpaka akatokea sehemu moja iliyochangamka kidogo, ila aliona Kuna sehemu watu wamezunguka na kutengeneza duara, yaani kama kulikuwa na tukio wanalishuhudia, Ray Charles akapuuza, sio mtu ambaye anapenda sana kujuchanganya na watu,



"Yule atakuwa ametoroka hospital, si huoni hata zile nguo ni za hospital kabisa?"



"atakuwa mwendawazimu yule, haiwezekani mtu mwenye akili timamu atoroke hospital, alafu mwanamke?" Haya ni maongezi ya wazee wawili waliokuwa wakipishana na Ray Charles, hawa wazee walikuwa wakitoka katika lile eneo ambalo kulikuwa na kundi lake watu wakiangalia kitu.



Yale maneno yalimshawishi Ray Charles aende kuona katika lile kundi Kuna nini? maana hata yeye ametoka kumkimbiza mwanamke aliyevaa nguo za hospitali, Ray Charles akajikuta ameshawishika kuingia katika lile kundi la watu ili kuona ni kipi kinajili hapo.



Ray Charles alijinyepenyeza na hatimae akatokea mbele kabisa ya watu, hapo ndipo alipoweza kumuona BQ akiwa amelala chini, alipoteza fahamu tena, Ray Charles akatabasamu, akataka kutoa bastola yake, ila akaona anaweza kuleta tafrani katika eneo hilo watu wengi.



Ray Charles akafikiri kwa muda na kisha akamsogelea karibu kabisa BQ, akamshika shavuni kama anampima homa, kisha Ray Charles akambeba BQ juu juu,



"unamjua huyo?" Kijana mmoja alimuuliza Ray Charles, lakini Ray Charles hakutaka kujibu, alipenya mpaka akatoka katika lile kundi la watu, akasimamisha Baja na kuingia na BQ,



"nipeleke maeneo ya ikulu" Ray Charles alimwambia Dereva bajaj kisha Dereva akaondoa bajaj, Ray Charles akamlaza BQ mapajani mwake, Ray Charles akatabasamu.



Bajaj ilitembea mpaka maeneo ya ikulu,



"simamisha hapa" Ray Charles alimuamrisha dereva Bajaj ambaye alitii, kisha Ray Charles akatelemka na kumlipa Dereva Bajaj, kisha Ray Charles akambeba BQ na kutembea nae kwa mwendo mfupi, kisha akaingia nae Ikulu.



Ray Charles alipitiliza moja kwa moja mpaka katika kile chumba chao alichomuulia Sajenti Minja.



Alifika na kumtupa BQ chini, kisha akampigia simu Rais na kumpa taarifa. Baada ya dakika kumi Rais aliingia mule, kwanza alivyomuona BQ, Rais alijikuta akitoa tabasamu la ushindi,



"kwisha habari yake" Rais aliongea na kutabasamu, kisha akachomoa bastola kiunoni kwa Ray Charles, akamuelekezea BQ kichwani......





"ujanja mfukoni, haya ebu niue sasa" Rais aliongea huku akimshikisha bastola BQ, lakini ndio hivyo tena, BQ hakuwa na fahamu.



"Ray kwanini umemleta, si ungemuua uko uko hospital?" Rais aliuliza huku akimuangalia Ray, hakujua kuwa Ray alishashindwa kumuua BQ, na alitorokwa ndani ya jengo la hospital, ila alimpata tena BQ kwa bahati tu.



"ni bora tungeipata mikataba kwanza ndipo tumuue, vinginevyo kama Ile mikataba itakuwa amempa mwanasheria au kaiweka sehemu, inaweza ikaja kutusumbua baadae hata kama huyu mwanamke atakuwa amekufa" Ray Charles alijibu,



"eti eee? Kwa Ray hiyo tunafanyaje sasa?" Rais aliuliza,

"huyu ni kumtafutia chumba na kumuacha mpaka fahamu zimrejee, alafu tutambana atuoneshe mikataba ilipo, tukiipata ndio tunamuua" Ray Charles aliongea,



"safi kabisa, je hospital hukukuta upinzani wowote?" Rais aliuliza,



"hapana" Ray Charles alijibu,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sawa, huyu mpeleke katika vyumba vya nyumba ya nyuma, uko utamfungia katika chumba kimoja, nadhani utarudi kumuona tena kesho ili tujue hali yake" Rais aliongea huku akiondoka na kumuacha Ray Charles akiwa amesimama pembeni ya mwili wa BQ.



Rais alivyotoka tu, Ray Charles akambeba BQ na kutoka nae katika kile chumba cha kifo, na kumpeleka katika nyumba nyingine iliyokuwa upande wa nyuma katika eneo lile la ikulu. Alivyomfikisha alimtupa chini, BQ akadondokea katika lile jeraha lake la kichwani na kufanya damu zianze kutoka, Ray Charles hakujali, akatoka nje na kufunga mlango, kisha akaondoka zake.



******************



Edward Sambo alikuwa sebuleni kwake akipitia habari tofauti tofauti katika magazeti, alisikia mtu akigonga mlango,



"nani?" Edward Sambo aliuliza kwa uoga, alikuwa hajiamini kabisa tangu BQ amvamie mara mbili,



"mimi mlinzi" Mgonga hodi alijibu,



"unataka nini?" Edward Sambo aliuliza,.



"Kuna mgeni wako" Mlinzi alijibu,



"anaitwa nani?" Edward Sambo aliuliza kwa wasiwasi,



"Tom, Thomas Anthony" Mlinzi alijibu na kufanya Edward Sambo ashangae, maana ni muda sana hajawahi kukutana na Tom, na pia hawakuwa na mazoea sana, sasa alijiuliza Tom amefuata nini hapo?



"mruhusu aingie, ila mkagueni sana" Edward Sambo aliongea kisha yule mlinzi akarudi getini.



Baada ya muda Tom aliingia sebuleni kwa Edward Sambo, akamkuta Edward Sambo akisoma gazeti. Tom akaelekea moja kwa moja kukaa kwenye kochi,



"shikamoo mzee" Tom alimsalimia Edward Sambo,



"marahaba kijana, za siku?" Edward Sambo alimuuliza Tom,



"nzuri kwa kweli, ingawa kuna mitihani ya hapa na pale, Ila tunapambana" Tom alijibu huku akitabasamu,



"kweli kabisa, karibu sana, nikuketee kinywaji gani?" Edward Sambo aliuliza huku akisimama,



"hapana, nashukuru mzee" Tom aliongea na kumfanya Edward Sambo arudi kukaa katika kochi,



"umekujaje kujaje leo, umekuja kuchimba mambo yako au umekuja kuniona tu?" Edward Sambo aliuliza na kumfanya Tom atabasamu,



"nimekuja kujua ukweli kuhusu Sajenti Minja kumtorosha mtuhumiwa, maana habari zinadai alikuwa hapa mara ya Mwisho kabla hajaondoka na mtuhumiwa" Tom aliongea na kumuangalia Edward Sambo,



"Kijana yaliyokukuta katika ufuatiliaji wako wa lile sakata la memory card bado umeyasahau? au unapenda tu kujitaftia matatizo mengine?" Edward Sambo aliongea huku akivua miwani,



"mimi sijaja kufuatilia habari yoyote, nafanya uchunguzi wangu kuhusu Sajenti Minja. Sajenti Minja amekuwa kama ndugu kwangu, na wewe ni mtu wake wa karibu siku nyingi sana" Tom aliongea na kutabasamu,



"Sasa unataka kuchunguza nini? Umeambiwa Minja ametoroshwa na wenzake, wenzake wakina nani? polisi? wanajeshi? Jibu litakuwa hapana, polisi wala mwanajeshi hawezi kumtorosha Minja, ila ni waarifu. Je kwanini waarifu wamtoroshe Minja? Kwa sababu ni mwenzao. Jibu ni rahisi tu" Edward Sambo aliongea,



"ni ngumu kuaminika kuwa Sajenti Minja ni muarifu, hainiingii akilini" Tom aliongea,



"endapo ungeona yale mazingira aliyoondoka nayo Minja huku akiwa na muarifu, na namna alivyokataa kuongozana na Askari wengine, basi usingekataa hiki nilichokueleza" Edward Sambo aliongea,



"sawa, huenda ni kweli, ila sijawahi kuhisi Waka kuona dalili kuwa Kuna uhusiano wowote kati ya Sajenti Minja na yule mwanamke muuaji" Tom aliongea,



"hivi unamjua yule mwanamke?" Edward Sambo alimuuliza Tom,



"nimeshawahi kuonana nae sana tu kabla hajaanza kufanya mauaji hapa mjini, maana alianzia katika wilaya niliyokuwa nafanyia kazi hapo awali" Tom alijibu,



"unamjua vizuri? Jibu ndio au hapana, hayo maelezo mengine ya nini sasa" Edward Sambo aliongea kwa ukali



"hapana, simjui" Tom alijibu,



"wewe si ulifuatilia kwa karibu sakata la memory card, kwanini unasema humjui yule mwanamke?" Edward Sambo aliuliza,



"inawezekana nimemsahau" Tom alijibu na kumfanya Edward Sambo acheke,

"ukija siku nyingine, nitakukumbusha" Edward Sambo aliongea,



"kwa hiyo huyu mwanamke ni zao la memory card?" Tom aliuliza huku akijaribu kuvuta kumbukumbu, ila kila kumbukumbu anayoivuta kuhusu mwanamke wa katika lile sakata, picha iliyokuwa ikimjia ni ya BQ, ila sasa anachojua yeye ni kuwa BQ alishakufa siku nyingi tu, huyu hawezi kuwa BQ kwa maana hata sura ni tofauti, huyu mwanamke wa sasa hivi havutii, ana majeraha usoni na isitoshe hana mkono mmoja.



"ndio, huyu mwanamke ni zao la memory card, kwa hiyo hapa kinachoendelea ni mambo yale yale ya memory card, huyu mwanamke and mikataba ambayo alisaini na Tammy Semmy, mikataba ya umiliki majengo, ila sasa serikali inamtambua Tammy Semmy ni muarifu, kwa hiyo mikataba yote aliyoingia na watu au nchi yoyote, hiyo mikataba ni batili, ila kwa sheria za kimataifa, hiyo ni Mikataba halali kabisa" Edward Sambo aliongea,



"kwa hiyo yule mwanamke ana haki?" Tom aliuliza,



"ndio, ila hatakiwi kuishi, kizazi chote kilichoisumbua nchi katika sakata la memory card, ni lazima kipotee, ibaki historia tu" Edward Sambo aliongea,



"duh, sawa mzee" Tom aliongea,



"ila si unajua hata yule mwanamke muuaji nae alikamatwa?" Edward Sambo aliuliza,



"ndio, ila nimesikia pia jana usiku alitoroshwa" Tom aliongea,



"ndio hivyo, sasa umeshajiuliza mtu aliyekuwa amezimia ametoshwaje?, polisi hawakuwepo, je walikuwa wapi? kama habari zinasema hakukuwa na Askari hata mmoja eneo lile la wodi, je nani aliwaondoa Askari pale? Kijana Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia" Edward Sambo aliongea na kutikisa kichwa,



"kweli, hayo maswali nilijiuliza sana, ila sikupata jibu, ila pia nikahisi huenda hospital watakuwa na camera zilizoshika hayo matukio" Tom aliongea,



"una akili sana, ila sasa kwanini hospital wapo kimya Mpaka muda huu?" Edward Sambo aliuliza,



"hapo ndio sijajua sasa" Tom alijibu,



"mimi ni mmoja wa watu wachache sana waliobahatika kuona video za lile tukio, kuna rafiki yangu yupo mule ndani, ni daktari, alinirushia kwa ufupi ile video. Ila hata polisi hawajaiona, na kwa maelezo ya ndani kabisa ya hospital, yanadai wamezuiwa wasiongee chochote, wajifanye hawajui chochote" Edward Sambo aliongea,



"ni nini kilitokea sasa?" Tom aliuliza,



"Kuna mtu aliingia ndani ya hospital usiku, akaingia na kuanza kupambana na yule dada, alafu kumbe yule mwanamke muuaji hakuwa amezimia, alikuwa amezinduka muda tu, madaktari wenyewe waligundua hilo baada ya kurudia rudia kutazama zile video. Basi yule mtu alipambana na yule mwanamke, ila yule mwanamke alipata upenyo, akatorokea dirishani, mpaka sasa hivi haijulikani alipokimbilia" Edward Sambo aliongea,



"Sasa kwanini serikali inaficha hii kitu?" Tom aliuliza,



"mimi nadhani Kuna mawili, la kwanza kulinda heshima ya polisi, kwa maana haiwezekani polisi wasiwepo eneo la tukio la kumlinda yule mwanamke muuaji. Pili, inawezekana hili tukio la huyu mwanamke kutoroka lilipangwa na viongozi wa serikali, au kwa kuongeza, inawezekana pia huyu mwanamke alitakiwa auawe bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria" Edward Sambo aliongea,



"hiyo video unayo hapo, video ya huyo mtu aliyekuwa akipambana na yule mwanamke muuaji?" Tom aliuliza,



"ndio, ninayo. Unataka kuiona?" Edward Sambo alimuuliza Tom,



"ipo, nitakurushia, ila hutakiwi kumuonesha mtu, endapo utamuonesha mtu na ikasambaa, ujue hakuna atayesalimika kati yetu" Edward Sambo aliongea,



"kuhusu hilo, usijali" Tom aliongea na kisha Edward Sambo akamrushia ile video. Wakaongea na mengine kwa masaa kadhaa, baadae Tom akaaga na kuondoka, huku akiwa na shauku ya kuiona ile video aliyorushiwa na Edward Sambo.



Tom aliondoka na kufika nyumbani kwake, alipofika cha kwanza alifungua ile video na kuanza kuangalia, alishtuka alipogundua kuwa yule mtu ni Ray Charles,



"ni nani huyu, na kwanini anafanya hivi?" Tom alijiuliza huku akishangaa namna BQ anavyokwepa zile ngumi za Ray Charles.



"nataka kumuona tena huyu mtu" Tom aliongea, huku akiingia Facebook, kisha akaipost ile video ya Ray Charles akipambana na BQ, hakuandika neno lolote, alitaka wahusika wenyewe wamtafute, ila aliamini ni ngumu sana watu kujua anapoishi, maana ni uswahilini, tena ndani ndani.



Muda ulizidi kwenda huku ile video ikizidi kusambaa mtandaoni, ingawa Tom hakuandika neno lolote, ila tayari ilishajulikana ile video ni ya mwanamke muuaji jinsi alivyotoroka hospital, ila yule mtu wa pili ambaye ni Ray Charles, hakuna aliyemjua.



Masaa yalizidi kusogea tu, mara Tom akaona simu yake ikiita, alipoangalia jina la mpigaji, alikuwa ni Edward Sambo, Tom hukupokea ile simu, alijua Edward Sambo hana la kumuuliza zaidi ya kuuliza kwa nini amepost ile video? Tom akaitupa simu pembeni na kulala, muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa saa tano usiku.



Tom akapitiwa usingizi na kulala.



Usiku mnene Tom alishtuka, alisikia kama mtu anajaribu kuvunja mlango wa chumba, Tom akawasha taa na kumuangalia mpenzi wake ambaye muda huo hakuwa na habari, alikuwa anakoroma tu kutokana na usingizi.



Tom akazidi kupata hofu, akataka kupiga kelele, ila akaona hapana, akaona inawezekana ni kibaka tu, Tom akazima taa na kubeba chuma moja nw kusimama nalo mlangoni, alichotaka kufanya ni kumpiga huyo mwizi endapo ataingia ndani.



Mlango uliendelea kuchokonolewa kitasa bila mafanikio yoyote, mwisho alisikia kama mtu ametupa kitu kama kisu au bisibisi chini, Tom akaamini kuwa huenda huyo mwizi ameshindwa kufungua kitasa.



Wakati Tom akiwa na imani hiyo, alisikia kishindo kikubwa kikifuatia na mlango kufunguka, mtu akasimama mlangoni, Tom hakuweza kumjua kutokana na giza, alichofanya Tom ni kunyanyua chuma chake na kukishusha kwa nguvu katika kifua cha yule mtu, ukatoka ukelele mkali wa chuma kugongana na chuma, Tom akashtuka na kuwasha taa, hakuamini macho yake kwa alichokiona, alikuwa ni Ray Charles akiwa amesimama mlangoni huku macho yake yakiwa yameiva kwa wekundu, hasira zilikuwa zimemtawala...







Baada ya Ray Charles kuvua gloves, akamtazama BQ kwa dakika,



"mikataba ipo wapi?" Ray Charles alimuuliza BQ, ila bahati mbaya BQ hakuwa na fahamu, alikuwa amelala tu, Damu zilikuwa zikimtoka katika jeraha lake baada ya kutupwa chini na Ray Charles hapo hawali.



"ngoja kwanza" Ray Charles aliongea na kutoka nje, hapo akamkuta Rais akiwa na Dizonga na vijana wengine wakiongea mambo mawili matatu,



"kazi imeisha?" Rais alimuuliza Ray Charles,



"bado" Ray Charles alijibu kwa upole,



"Kwanini Ray, au unampenda huyu mwanamke?" Rais aliuliza,



"Kuna wazo nimepata, tunaweza kujadiliana kidogo?" Ray Charles aliuliza,



"tujadiliane hapa au ndani?" Rais aliuliza,



"tuingie ndani" Ray Charles na kutangulia kuingia ndani, Rais alikuja kwa nyuma na kumtupia jicho BQ,



"Ray bwana, kumbe ulishaanza kumuadhibu, kwanini umeacha sasa?" Rais aliongea huku akicheka kwa dhiaka,



"Kuna kitu nimefikiria mkuu, mimi bado sijataka tumuue huyu, endapo tunamuua na mikataba haijapatikana, inaweza kufanya usiwe na amani katika utawala wako, tena amani itapotea zaidi endapo mikataba itakuwa mikononi kwa wapinzani, wanaweza kuleta kashfa itakayokufanya uachie madaraka" Ray Charles aliongea na kuangalia chini,



"hiyo haiwezekani, wananchi waandamane niachie madaraka? haiwezekani, nitawamaliza vibaya mno" Rais aliongea kwa jazba,



"pia hata jeshi linaweza kukuondoa madarakani endapo utakiuka haki za wanadamu" Ray Charles aliendelea kuongea,



"Ray hiyo ndio point uliyoniitia baada ya kushindwa kumuua huyu mwanamke?" Rais aliuliza kwa ukali,



"hapana, point niliyokuitia ni kwamba hatupaswi kumuua huyu mwanamke mpaka aamke na tupate mikataba" Ray Charles aliongea,



"anaamka vipi sasa na tumeshindwa kupata suluhisho la kumuamsha?" Rais aliendelea kuuliza kwa jazba,



"mimi suluhisho nadhani nimelipata, ingawa linaweza kusaidia au kutosaidia, ila ni vyema tujaribu" Ray Charles aliongea na kumkazia jicho Rais,



"sema sasa, haya mambo ya kuongea nusunusu ni kupoteza muda Ray" Rais aliongea huku jazba bado zikiwa zimemtawala,



"Kuna yule Dokta wa kizungu ambaye yupo gerezani anakabiliwa na kesi ya kumsaidia mtuhumiwa, yule Dokta ni bora tumfanyie mpango tu atolewe, alafu tumchukue ili aje kumtibu huyu mwanamke" Ray Charles aliongea na kumuangalia Rais.



Rais akafikiria kwa muda, alihisi hilo ni wazo zuri sana,



"ni wazo zuri Ray, hapo ndio umeongea point, sio mwanzo ulikuwa unabwabwaja tu utumbo" Rais aliongea huku akimpiga piga bega Ray Charles,



"Sasa naomba hiyo kazi ya kwenda kumtorosha unipe mimi" Ray Charles aliongea,



"hapana Ray, nipe muda wa kufikiri kwanza ili nipate njia sahihi ya kumtwaa yule Dokta, tusije kufanya makosa kama tuliyoyafanya hospitali kipindi unaenda kumchukua huyu mwanamke" Rais aliongea kwa sauti tulivu,



"sitofanya makosa, nipe hiyo nafasi" Ray Charles alisihi,



"hapana Ray, nipe muda wa kufikiri kwanza, hilo wazo lako ni zuri sana" Rais aliongea,



"Mkuu huyu mwanamke endapo siku ya leo itaisha na ataendelea kuwa hivi na chakula hapati, anaweza kufa" Rais Charles aliongea,



"Ray acha ubishani, nimekwambia nipe muda. Unataka niongeeje ili nieleweke?" Rais aliuliza,



"sawa" Ray Charles alijibu,



"funga mlango na tutoke nje" Rais aliongea na kisha Ray Charles akatoka nje huku Rais akiwa nyuma yake. Walipotoka nje, Ray Charles alifunga mlango kisha akafuata uelekeo alioendea Rais.



***************



Mkuu wa polisi bado kichwa kilikuwa kinamuuma, yaani lile tukio la hospital, hasa hasa kumuona tena Ray Charles, yaani ni tukio ambalo hakuwa analiamini kabisa,



"kumbe Minja alikuwa hatua moja mbele yangu. Nakumbuka aliwahi kunambia kuwa kipindi kile yule mwanamke muuaji alivyopigwa risasi, alipigwa na Ray Charles, ila nikamuona Minja mpumbavu, nilihisi anakurupuka tu" Mkuu wa polisi alikuwa akiwaza mwenyewe,



"Sasa Kuna nini kati ya huyu mwanamke na Ray Charles??" Mkuu wa polisi alijiuliza,



"nimekumbuka, kulikuwa na kesi hapa ya kijana mmoja kudai kutekwa na Ray Charles, nayo niliipuuza, ngoja niangalie sasa" Mkuu wa polisi aliwaza na kuchukua simu yake, kisha akapiga namba ya kaunta, simu iliita kidogo tu na kupokelewa,



"naam mkuu" Polisi aliyepo kaunta aliitika baada ya kupokea simu,



"nitafutie kabrasha moja la kesi ya utekaji, jina la mtuhumiwa ni Ray Charles, alafu niletee ofisini kwangu" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa mkuu" Askari aliyepo kaunta alijibu kisha mkuu wa polisi akakata simu, akawa anangojea hilo file la kesi.



Baada ya nusu saa mlango wa ofisi ya mkuu wa polisi uligongwa,



"ingia" Mkuu wa polisi aliongea kisha mlango ukafunguliwa na akaingia Askari mmoja aliyekuwa na makabrasha mkononi, yule Askari baada ya kuingia akapiga saluti, kisha akamkabidhi mkuu wa polisi yake makabrasha aliyoyashika mkononi, kisha yule Askari akageuka kikakamavu na kuondoka ndani ya ofisi ya mkuu wa polisi.



Mkuu wa polisi akasoma jalada la juu ya lile kabrasha, kisha akafungua ndani na kuanza kusoma maelezo yalioyoandikwa, aliyarudia kusoma mara mbili, kisha akakutana na jina la mtoa tuhuma, alikuwa ni Thomas Anthony ambaye anadai alitekwa na Ray Charles, kisha akasababishiwa maumivu ya mwili kwa kupigwa.



Na uzuri ni kuwa namba ya simu ya Tom aliiacha katika lile kabrasha, huo ukawa msaada mwingine kwa mkuu wa polisi, yaani ilimrahisishia kazi mkuu wa polisi, ilikuwa rahisi zaidi kumpata Tom.



***********



Tom alizinduka saa moja jioni na kujikuta yupo hospital amezungushiwa bandeji kichwani, pembeni alikuwa mpenzi wake,



"ha!!! Tom umeamka?" Mpenzi wake aliuliza kwa mshangao, na muda huo Tom alikuwa akiangaza macho yake kushoto na kulia, akijaribu kuyasoma mazingira ya mule ndani,



"ngoja nikamuite daktari" Mpenzi wake aliongea huku akiinuka kitandani,



"ngoja, nani kanileta hapa?" Tom aliuliza huku akijitahidi kukaa,



"majirani tu, toka saa kumi alfajili mpaka sasa hivi ulikuwa umezimia, ulikuwa unakufa Tom" Mpenzi waliongea na kumfanya Tom aanze kuvuta kumbukumbu, hapo ndipo alikumbuka kilichomtokea,



"wewe hujaumia?" Tom alimuuliza mpenzi wake,



"hapana, nipo poa tu" Mpenzi wake alijibu,



"ilikuwa hatari sana" Tom aliongea na kusikitika,



"kwani yule kaka aliyetuvamia ulimfanya nini? Mbona alionekana kama Kuna kitu anakuonya?" Mpenzi wake aliuliza,



"Yule ndiye yule aliyenitekaga kipindi kile nikaja kuokolewa na Sajenti Minja" Tom aliongea,



"ila wewe Tom usikute ulianza kumchokonoa wewe, haiwezekani mtu aje tu atuvamie usiku" mpenzi wake aliongea,



"umeshaanza, yaani wewe imani yako siku zote ni kwamba kila tukio linalonikuta, basi mimi ndio uwa mchokozi" Tom aliongea kwa hasira,



"mimi nakujua wewe, sio mgeni wa matukio yako" Mpenzi wake Tom aliongea na wakati huo simu ya Tom ilikuwa ikiita,



"allow" Mpenzi wake alipokea, kwa maana simu ilikuwa mikononi kwake,



"hujambo?" Sauti ya upande wa pili iliuliza,



"sijambo, shikamoo" Mpenzi wa Tom aliamkia baada ya kugundua anaongea na mtu aliyemzidi umri,



"marahaba, hii ni namba yako au umepokea tu" Sauti ya upande wa pili iliuliza, ikabidi mpenzi wa Tom ampe simu Tom,



"nani? " Tom alimuuliza mpenzi wake,



"sijui, ongea nae" Mpenzi wake alijibu.



"naam" Tom aliongea,



"wewe ndio Thomas Anthony?" Sauti ya upande wa pili iliuliza,



"ndio" Tom alijibu,



"unaweza kufika kituo cha polisi leo?" Sauti ya upande wa pili iliuliza,



"Kuna nini?" Tom aliuliza,



"wewe si umeshawahi kuleta kesi ya kutekwa na kuteswa hapa kituoni?" Sauti ilihoji na kumfanya Tom afikirie kidogo,



"ndio, ni mimi" Tom alijibu,



"uje sasa kituoni, kuna maswali machache nataka nikuulize" Sauti iliongea,



"mimi nipo hospital, nimelazwa, usiku wa kuamkia leo Ray Charles alinivamia na kutaka kuniua" Tom aliongea kwa jazba,



"tena? sawa nakuja hapo, hospital gani" Sauti ya upande wa pili iliuliza,



"siwezi kukutajia hospital niliyopo, kwa sababu sikuamini" Tom aliongea,



"mimi ni mkuu wa polisi wa mkoa, niamini tu" Sauti ya upande wa pili ilijibu na kufanya Tom kufikiria kwa muda kidogo,



"sawa, nipo hospital ya mkoa" Tom alijibu



"sawa, nakuja" Mkuu wa polisi aliongea na kukata simu,



"afadhali nimempata huyu kijana, hii itakuwa ni kazi rahisi sana kupata angalau mwanga kuhusu Ray Charles, na leo tena alimvamia eti!!" Mkuu wa polisi aliongea na kuvua miwani yake, akasikia simu yake ikiita, alipotupia macho katika kioo cha simu yake, akakuta anaepiga ni Rais, akapokea haraka,.



"ndio mkuu" Mkuu wa polisi aliongea kwa sauti tulivu,



"nasikia yule mwanamke muuaji alitoroshwa hospitali?" Rais aliuliza,



"ndio mkuu, ila aliyemtorosha nimeshamtambua" Mkuu wa polisi alijikuta anaongea kwa uoga ili aonekane ni mchapa kazi,



"ni nani huyo?" Rais aliuliza huku akipata hofu,



"Kuna mtu mmoja namuhisi, anaitwa Ray Charles" Mkuu wa polisi aliongea na kufanya moyo wa Rais upige kwa kasi zaidi,



"unamuhisi? kwa hiyo unafanya kazi kwa kuhisi bila kuwa na uhakika?" Rais aliuliza kwa sauti Kali,



"Kuna video niliichukua hospitali inayoonesha hilo tukio, pia Kuna kesi mbili tatu zipo hapa kituoni zinazomuhusu huyo mtu, ya kwanza ni ile inayofanana na hii, kwamba aliwahi kumpiga risasi yule mwanamke muuaji, na ya pili ni kuwa Kuna kijana alishawahi kumteka na kumjeruhi, na usiku wa kuamkia leo alimvamia nyumbani kwake na kumpiga, huyo kijana yupo hospital ya mkoa amelazwa, nataka niende baadae nikamuhoji" Mkuu wa polisi aliongea na kushangaa simu ikikikatwa,



"sijui hajapenda maongezi yangu" Mkuu wa polisi aliongea na kuiweka simu mezani.



Kwa upande wa Rais alionekana ana gadhabu sana kusikia zile habari kutoka kwa mkuu wa polisi. Rais akapiga simu kwa vijana wake wanne, haraka sana wakawa wamefika katika ofisi ya Rais,



"Ray kawa mpumbavu sana, nilijua amemuua Tom kumbe hajamuua!!, sasa basi, Nyie wanne, nataka mpange mpango wa dakika kumi wa kuingia katika hospital ya mkoa na mkammalize Tom, kwa maana ameshakuwa kikwazo sasa, endapo mkuu wa polisi ataenda kumuhoji, basi Ray atakuwa muarifu anayetafutwa" Rais aliongea kwa jazba,



"picha yake ipo?" Dizonga aliuliza,



"ninayo " Kijana mwingine alijibu,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sawa, twendeni, tukifika, mimi nitakaa upande wa ndani wa geti, jirani na mlinzi, alafu Oppy utakuwa nje katika gari, Ally na Tod mtaingia ndani, msimuue ndani ya hospital, maana kuna camera, isije ikawa umeme kama aliofanya Ray" Dizonga aliwapanga wenzake,



"kwa hiyo mtafanyaje?" Rais aliuliza,



"huyu tutafanya kama tunamtorosha, alafu tutakuja nae huku, kummaliza" Dizonga aliongea,



"wazo zuri D, fanyeni hivyo" Rais aliongea,



"na pale hospital itabidi tutoke nae kirafiki, au tuvae kinyago usoni ili camera zisinase nyuso zetu" Dizonga aliongea,



"sio lazima vinyago, hata makoti yenye kofia yanaweza kuwa msaada" Kijana mwingine aliongea,



"tutatumia makoti tu" Mwingine aliunga mkono,



"sawa, nendeni sasa" Rais aliongea na kisha vijana wakajiandaa na kuingia katika gari, safari ya kwenda hospitali ikaanza.



Walitumia muda mfupi kufika hospital, Dizonga akashuka na kuongea na simu kwa muda mfupi, kisha akarudi ndani ya gari na kukuta wenzake wakimaliza kuchora ramani ya mipango yao,



"wewe Dizonga utakaa hapa getini kwa ndani, Oppy utakuwa katika gari nje, hakikisha gari imewaka muda wote, alafu mimi na ally tunaingia wodi hadi wodi kumtafuta huyo maiti mtarajiwa" Kijana mmoja aliongea na kisha wakapeana tano wote kama ishara ya kukubaliana kwa kile wanachofanya. Wakatelemka na kufanya kama walivyopanga.



**********



Tom alikuwa amekaa kitandani akimsubiri mkuu wa polisi muda huo, alikuwa akichezea simu yake, ghafla mlango ukafunguliwa, akaingia Dizonga akiwa na koti lenye kofia kubwa, Tom alishtuka kwa maana sura ya Dizonga ilionesha imekuja kishari tu, Tom akataka kumuuliza yeye ni nani, lakini hakupata muda huo, kwani Dizonga aliruka na kutua juu ya kitanda, kisha akamkaba Tom mpaka akapoteza fahamu, kisha akatoka nae huku akiwa anamsukuma na toroli ya wagonjwa, koridoni alipishana na mkuu wa polisi akielekea katika wanapotoka wao, Dizonga akatabasamu baada ya kupishana na mkuu wa polisi,



"kwisha kazi" Dizonga aliongea wakati akimtoa Tom nje, Tom ambaye hakuwa anajitambua wakati huo......





Dizonga alikisukuma kile kiti cha matairi mpaka nyuma ya hospital, kisha akachomoa bastola na kumuelekezea Tom usoni, kisha akatoa kichupa kidogo cha dawa kumpulizia Tom puani, Tom akazinduka na kuanza kupiga chafya mfululizo, ubongo ulipokaa sawa ndipo akagundua Kuna mtu mbele yake amemshikia bastola, Tom akashtuka na kutulia,



"nisikilize kwa umakini sana, mimi ni mbaya nimetumwa kukudhuru, ila nadhani muda wa kukudhuru bado haujafika, sasa tafuta njia yoyote huku nyuma ya hospitali, na utoroke, usikae tena mazingira ya huku hospital, na usimuamini mtu yeyote" Dizonga alimwambia Tom,



"wewe ndio mkuu wa polisi uliyenipigia simu?" Tom aliuliza kwa hofu,



"hapana, mimi sio mkuu wa polisi, wala sina uhusiano na mkuu wa polisi, ila mtu aliyefanya tupajue hapa ni mkuu wa polisi" Dizonga aliongea huku akirudishia bastola kiunoni,



"sawa, nashukuru kwa wema wako" Tom aliongea huku akiwa hamuamini kabisa mtu aliye mbele yake, alijua ndio wale wale wakina Ray Charles,



"kaka ondoka, usije ukafia humu, na usipite geti la mbele, kwa maana utanikuta tena mimi na sitokuonesha tena huruma kama ninaokuonesha sasa hivi" Dizonga aliongea na kuanza kurudi geti kubwa la mbele, alitembea kwa umakini mkubwa ili wenzake walioingia ndani ya wodi wasigundue kama aliondoka katika eneo alilopangiwa.



Dizonga alifika getini na kutoa simu yake, kisha akampigia mtu aliyemsevu kama "X soldier"



"kaka mkubwa" Dizonga aliongea baada ya mtu wa upande wa pili kupokea simu,



"niambie" Sauti ya upande wa pili iliyoonekana kama ya mtu mzee sana ilijibu,



"dogo nimemsaidia na kumpa mwanga namna ya kuondoka, akizembea atakuwa ametaka mwenyewe kujiua" Dizonga aliongea,



"sawa, umefanya vyema sana" Sauti ya upande wa pili iliongea,



"sawa, baadae basi" Dizonga aliongea,



"haya, kazi njema" Sauti ya upande wa pili ulijibu na kukata simu.



Dizonga akaendelea kuhesabu dakika tu huku akiwasubiri wenzake watoke wodini, aliwasubiri muda mrefu na hakuna kilichotokea. Mission walitakiwa waifanye ndani ya dakika kumi, lakini tayari dakika ishirini na tano zilikuwa zimeshakatika.



Dakika tano baadae, Dizonga alimshuhudia mkuu wa polisi akitoka ndani ya jengo la hospital huku akiwa na daktari, kuna kitu walikuwa wanaongea, waliongea kwa dakika mbili kisha wakaagana, mkuu wa polisi akaingia katika gari yake na kuondoka. Dizonga akamshuhudia daktari akija pale getini alipokuwepo, kisha akaingia katika kibanda cha mlinzi,



"Kuweni makini sana na watu wanaotoka ndani, inasemekana kuna mgonjwa ametoroka au ametoroshwa, bado tunafuatilia" Daktari aliongea na mlinzi ndani, ila Dizonga alisikia yale maelezo,



"sisi kazi yetu ni kufungua geti kwa ajili ya kuingia na kutoka magari, na kuruhusu watu kuingia kuona wagonjwa kwa muda sahihi, hilo suala la wagonjwa kutoroka ni jukumu la ulinzi wa ndani ya jengo" Mlinzi alisikika akijibu,



"sawa, ngoja ukweli ujulikane, walinzi wote mtashikwa, ndipo utajua nani mwenye jukumu la ndani au nje" Daktari aliongea huku akitoka nje ya kibanda cha walinzi, kisha mlinzi nae akatoka na kuangaza kushoto na kulia, Dizonga akajifanya kama anaongea na simu. Mlinzi alivyorudi ndani, Dizonga akarudisha simu mfukoni, na muda huo wale wenzake waliokuwa ndani ya jengo la hospital, walikuwa wakitoka nje huku nyuso zao zikionesha hazina furaha hata kidogo.



Dizonga akatangulia kutoka ndani na kuingia ndani ya gari, akamkuta mwenzao ambaye ni Dereva nae akishangaa



"mbona mmetumia muda mrefu" Dereva aliuliza,



"walioingia ndani ya jengo ndio wamechelewesha mchezo" Dizonga alijibu,



"wako wapi?" Dereva aliuliza,



"wanakuja" Dizonga alijibu na kipindi hicho wale wenzao wawili walikuwa wakitoka ndani ya geti la hospitali na moja kwa moja wakaingia katika gari,,



"vipi, imeshindikana?" Dizonga aliuliza,



"jamaa hatujamkuta katika ile wodi" Mmoja alijibu,



"Sasa si mngekagua mpaka vyooni" Dereva aliuliza,



"tumefanya hivyo na ndio maana tumechelewa" Mwingine alijibu,



"hospitali yote mmeamua?" Dizonga aliuliza,



"mzeebaba, tumekagua kila eneo na ndio tumetumia muda mrefu ndani, labda tukuulize wewe uliyesimama getini, hukumuona huyo dogo hakitoka? " Mmoja kati ya wale watu waliokuwa na mission ya ndani waliuliza,



"hakuna kitu kama hicho, mpaka gari ya mkuu wa polisi niliiona ilivyoingia na muda wa kutoka niliiona, aliingia ndani ya gari peke yake" Dizonga alijibu,



"huenda basi aliruhusiwa" Dereva aliongea,



"kama aliruhusiwa, mkuu wa polisi alifuata nini pale hospitali?" Dizonga aliuliza,



"Yule jamaa ameshakoswa koswa kuuawa mara mbili, naona hajiamini sasa hivi, kila anapokaa atakuwa anajichunga mwenyewe" Jamaa mwingine aliongea,



"tuondokeni sasa" Dereva aliongea,



"Rais tunaenda kumuambia nini" Mmoja kati yao aliuliza,



"tutamwambia ukweli tu, hakuna haja ya kumficha" Dizonga aliongea,



"sawa" Dereva aliongea na kuondoa gari.



***************



Siku iliyofuata saa mbili asubuhi, wale vijana wanne wa rais walikuwa katika ofisi ya Rais, mbele ya Rais,



"kwa hiyo mpaka mnaondoka hospital hamkuweza kugundua Tom yupo wapi?" Rais aliuliza huku akiandika andika katika karatasi zake mezani,



"ndio, huenda aliruhusiwa mapema kabla sisi hatujaingia pale" Kijana mmoja alijibu,



"au tuamini tu huyu dogo ana ngekewa, maana nyie mmekosa, pia Ray ndio hataki kabisa kumuua" Rais aliongea huku akiendelea kuandika,



"naamini endapo tutajua alipo kwa mara nyingine, hatutofanya kosa tena" Dizonga aliongea kwa utulivu,



"nani kajibu hivyo" Rais aliuliza huku akiwa bado anaandika,



"mimi, Dizonga" Dizonga alijibu huku mapigo ya moyo yakiongezeka,



"ooh, D, Sasa Kuna kazi moja nataka uifanye wewe. Hivi mmefuatilia na kujua kesi ya yule Dokta Smith inaendaje?" Rais aliuliza na kuinua kichwa,



"Leo inasikilizwa kwa mara mwisho, alafu watapanga siku ya hukumu" Kijana mmoja alijibu,



"tumechelewa, maana si itasikilizwa saa nne?" Rais aliongea na kumtazama yule kijana aliyejibu,



"ni saa kumi jioni" Kijana alijibu,



"basi sawa, sasa Dizonga itabidi uende ukaongee na Dokta Smith kabla ya hiyo saa kumi, mwambie unamsaidia kumtoa, ila kwa sharti moja tu, akusaidie kumtibu mgonjwa wako, sitaki ajue kama mimi nipo nyuma ya haya,



"sawa, je ataamini vipi mimi naweza kumtoa?" Dizonga aliuliza,



"akiuliza swali kama hilo, mwambie hata jioni hatoitwa mahakamani, badala yake muda wa yeye kuwa mahakamani, ndio muda ambao mkuu wa gereza atamtoa nje""Rais aliongea,



"sawa mkuu, je niende muda gani?" Dizonga aliuliza,



"Sasa hivi, rudi kwako na ukavae suti, huende kama mtu mwenye pesa, usiende kihuni huni, anaweza akagoma kukuamini,



"sawa mkuu" Dizonga alijibu,



"utaondoka na gari ya serikali, utachagua yoyote hapo nje, na Dereva nitakupatia" Rais aliongea,



"sawa mkuu" Dizonga alijibu na kisha akaaga, akatoka mpaka nje na kuchagua gari moja ya serikali iliyokuwepo ndani ya uzio wa Ikulu, kisha akaingia na baada ya dakika tano dereva akaja na kuingia, wakasalimiana na kisha Dizonga akamuelekeza anapoenda.



***********



Dokta Smith alikuwa amekaa ndani ya gereza huku mwili wake ukionekana umepungua tofauti na hapo hawali, ila hakuonekana mtu mwenye mawazo, alikuwa akiongea na kutaniana na wafungwa mbalimbali. Askari magereza akasimama mbele yake,



"Dokta Kuna mgeni wako" Askari magereza aliongea na kumfanya Dokta Smith ashangae, kwa maana tangu amehamishiwa gerezani hakuwahi kutembelewa,



"nani" Dokta Smith aliuliza,



"mimi hata simjui, ila inawezekana ni viongozi wa serikali, maana hata gari yake ina namba za serikali" Askari magereza aliongea na kufanya Dokta Smith ashangae zaidi, yaani kusikia kuwa huyo mgeni ni kiongozi wa serikali,



"sawa, twende" Dokta Smith aliongea na kisha akatangulizwa mbele na Askari akakaa kwa nyuma.



Walitembea na wakaingia katika ofisi moja ndani ya gereza, hapo Dokta Smith akazidi kushangaa zaidi, baada ya mlango wa ofisi kufunguliwa, Dokta Smith akamkuta ndani kijana mtanashati ndani ya suti bei mbaya, na mdomoni alikuwa na sigara kubwa kama wanazovutaga majambazi katika sinema za kizungu, alikuwa ni Dizonga.



Dokta Smith akabaki anatoa macho tu,



"kaa hapo, uongee nae" Askari magereza aliongea kisha akatoka nje, akamuacha Dokta Smith ndani akijiuliza huyu mtu ni nani na anataka nini,



"samahani, hii sigara huenda inakukera" Dizonga aliongea na kuitupa ile sigara chini, kisha akaikanyaga,



"hapana usijali" Dokta Smith aliongea na kutabasamu,.



"samahani sana kwa huu uvamizi wa ghafla, ila nimekuja hapa nataka nikusaidie, alafu na wewe unisaidie" Dizonga aliongea na kumuangalia Dokta Smith,



"wewe unanisaidiaje, Na mimi nakusaidiaje?" Dokta Smith aliuliza kwa umakini,



"mimi nitakupa msaada mdogo tu, wa kukutoa humu na kufuta kesi yako" Dizonga aliongea,



"na mimi nitakusaidiaje?" Dokta Smith aliuliza,



"msaada wako kwangu, ni kuwa mimi nina mgonjwa nahitaji unisaidie kumtibu, maana ana siku ya tatu leo hajaenda hospital" Dizonga aliongea



"kwanini hamumpeleki hospital?" Dokta Smith alihoji,.

"endapo utakubali kunisaidia, basi utajua sababu pindi utakapomuona mgonjwa mwenyewe" Dizonga aliongea,



"sawa, mimi nitakusaidia, nitajaribu kumtibu" Dokta Smith aliongea na kumfanya Dizonga atabasamu,



"sawa, acha niende, ila jiandae, baadae nakuja kukuchukua" Dizonga aliongea,



"itawezekama vipi wakati leo ni siku ya kusikiliza kesi yangu?" Dokta Smith aliuliza,



"muda huo unaotakiwa usikilize kesi, ndio muda ambao utaachiwa huru, jiamini Dokta" Dizonga aliongea huku akiinuka katika kiti na kumuacha Dokta Smith akimuangalia tu.



"baadae dokta" Dizonga aliongea huku akitoka nje na kupishana na Askari magereza akiingia ndani ya ile ofisi aliyetoka.



Dizonga alitembea kwa mbwembwe kama mtu mwenye wadhifa serikalini, alitembea na kuingia katika gari, kisha Dereva akaiondoa gari eneo lile la magereza.



*************



Mishale ya saa tisa unusu wakati wafungwa wakiitwa majina ili wapelekwe mahakamani, jina la Dokta Smith halikuitwa, hapo akaanza kuamini maneno ya mgeni aliyemtembelea nyakati za asubuhi.



Baada ya wafungwa walioitwa kuondoka na basi na kupelekwa mahakamani, akaja Askari magereza na kumuita Dokta Smith, akampeleka mpaka ofisi ya mkuu wa gereza, kisha akaonana na mkuu wa gereza, wakaongea mambo mawili matatu kuhusu uhuru atakaopewa, kisha Dokta Smith akaruhusiwa kutoka gerezan.



Alivyotoka tu nje ya mlango wa gereza, alimkuta Dizonga akimsubiri ndani ya gari, Dokta Smith akaenda moja kwa moja kuingia katika gari ile ya serikali,



"pole sana kwa maisha ya gerezani" Dizonga alimwambia Dokta Smith,



"asante" Dokta Smith aliongea,



"tunapitia kwanza duka la nguo, alafu kwa mgonjwa husika utaonana nae jioni" Dizonga aliongea,



"sawa" Dokta Smith alijibu.



Dereva aliendesha mpaka katikati ya mji katika maduka ya nguo na kisha akasimamisha gari nje ya duka kubwa la nguo,



"wewe ondoka tu, kazi yako imeshaisha" Dizonga alimwambia yule Dereva wa gari la serikali,



"sawa" Dereva alijibu na kisha Dizonga na Dokta Smith wakatelemka katika gari na kuingia katika duka la nguo.



Wakati Dokta Smith akichagua za kuvaa, Dizonga alikuwa anaongea na simu, alipigiwa na Rais,



"ndio mkuu" Dizonga aliongea,



"mpo wapi?" Rais aliuliza,



"tupo kwenye maduka ya nguo" Dizonga alijibu,



"Sasa itabidi uzunguke nae kwanza mpaka jioni, kwa maana huyu mwanamke tunataka kumuhamishia nyumbani kwa Ray Charles, ili huyo Dokta hasigundue kama nipo nyuma ya haya yote" Rais aliongea,



"kutokana na hali ya huyo dada si bora mngemuhamisha sasa hivi ili Dokta akaanze matibabu?" Dizonga aliuliza kwa unyenyekevu,



"ni kweli D, ila muda Kuna ugeni kutoka nje upo ikulu hapa, kwa hiyo upo ulinzi wa aina mbalimbali, kuna Kuna walinzi wa huu ugeni, na Kuna ulinzi wa kimataifa, ila tuna maongezi ya saa moja tu, yakiisha utajulishwa" Rais aliongea,



"sawa mkuu" Dizonga aliongea na Rais akakata simu.



Dizonga akakaa huku akifikiria atampeleka wapi Dokta Smith kwa muda huo, wazo likamjia,



"Dokta tayari umemaliza kuchagua?" Dizonga alimuuliza Dokta Smith,



"ndio mheshimiwa" Dokta Smith alijibu na kumfanya Dizonga atabasamu,



"twende sasa" Dizonga aliongea na kutangulia nje, kisha Dokta Smith alimfuata kwa nyuma.



Dizonga akakodi taxi, aliamua arudi nyumbani kwake huku akiwa na Dokta Smith, kwa maana nyumbani Dizonga alikuwa na mgonjwa wake.



Taxi ilitembea mpaka nje ya nyumba ya kifahari ambayo Dizonga ndipo alipokuwa anaishi, ni nyumba aliyopewa zawadi na Rais. Taxi ilisimama kisha Dizonga akatelemka na kumlipa Dereva taxi.



Dizonga akaingia ndani huku Dokta Smith akimfuata, walifika sebuleni na Dokta Smith akasalimiana na familia ya Dizonga, mke na watoto wawili wa kike,



"mgonjwa anaendeleaje" Dizonga alimuuliza mke wake,



"bado, mpeleke hospital, atatufia ndani" Mke wake aliongea kwa huruma,



"nimekuja na Dokta leo, atamtibu tu" Dizonga alijibu,



"Dokta Smith twende huku" Dizonga aliongea na kupiga hatua kuelekea upande wa vyumbani huku Dokta Smith akiwa nyuma yake.



Walienda na kuingia katika chumba kimoja cha mwisho kabisa, kilikuwa na ukubwa wa stoo,



"Karibu Dokta" Dizonga alimkaribisha dokta Smith huku akifungua mlango,



"asante" Dokta Smith alijibu huku macho yake yakimtazama mwanaume aliyekuwa amelala huku mgongo ukiwa juu na majeraha kadhaa yalionekana mgongoni mwake,



"X soldier, leo nimekuletea daktari" Dizonga aliongea huku akikaa pembeni ya yule mgonjwa,



"Daktari kutoka wapi?" Yule mgonjwa aliuliza huku akijigeuza ili amuone daktari. Mgonjwa alipojigeuza ndipo Dokta Smith nae akaweza kumuona vizuri mgonjwa mwenyewe, mgonjwa mwenyewe akatabasamu, tabasamu lake bado halikuzuia kuonesha maumivu aliyokuwa nayo,



"Karibu Dokta" Mgonjwa aliongea,



"asante, pole kwa kuumwa" Dokta Smith aliongea huku akimtazama mgonjwa yule ambaye hakuwa na jicho moja la upande wa kushoto, naam, yaani alikuwa chongo........



Nadhani mimi nimeshamjua mgonjwa, sijui nyinyi wasomaji wangu.





"nini tatizo?" Dokta Smith aliuliza huku akimtazama yule mgonjwa,



"huyu alivunjwa vunjwa kila kiungo cha mwili, sasa mimi nimemtibu vilivyokuwa vinawezekana, ila Kuna vilivyonishinda" Dizonga alijibu,



"na wewe ni Dokta?" Dokta Smith alimuuza Dizonga,



"ndio, mimi ni Dokta, tena Dokta mzuri sana wa jeshi" Dizonga alijibu,



"umeegemea katika matibabu ya nini na nini?" Dokta Smith alimuuliza Dizonga,



"moyo zaidi" Dizonga alijibu,



"Sasa ilikuwaje ukaacha utabibu na kuwa kiongoz wa serikali?" Dokta Smith aliuliza,



"mzee endelea kuwa na mimi, utajua mengi sana, ila kifupi mimi sio Mfanyakazi wa serikali, ila niliamua kujifanya vile ili nikupate, kuna mtu mkubwa zaidi ya serikali ndio alinituma nije nikufuate" Dizonga aliongea maneno mengi na kufanya Dokta Smith ashtuke,



"lengo la kufanya yote haya ni nini?" Dokta Smith aliuliza,



"utajua tu zinavyozidi kwenda, kwanza ebu anza kumuangalia mgonjwa wangu" Dizonga aliongea na kumfanya Dokta Smith atikise kichwa tu, kisha akaanza kumuangalia X soldier kwa kumshika shika baadhi ya maeneo mwilini, na kugundua Kuna sehemu za mwili zimevunjija, hasa mguu wa kulia, ila maeneo ya mbavu na kichwa kulikuwa na maumivu tu.



"hayo maumivu ya kichwa, ni vyema tukamcheki kwenye X ray" Dokta Smith aliongea,



"huyu jamaa hawezi kutoka nje, hatakiwi kuonekana" Dizonga aliongea,



"Sasa tutajuaje tatizo lake?" Dokta Smith aliuliza,



"Dizonga, ni bora nipelekwe tu hospital, kuendelea kujificha humu naweza kufa" Sajenti Minja aliongea,



"na kwanini unajificha?" Dokta Smith aliuliza,



"taratibu utajua tu, si tupo wote kila siku?" Dizonga alimwambia Dokta Smith,



"yasije kuwa kama yale yaliyonikuta msituni, natibu mtuhumiwa alafu nakuja kupewa kesi nzito" Dokta Smith aliongea,



"hata usijali Dokta, mtu aliyekutoa gerezani ni zaidi ya sheria, yaani yeye ndio anayeziamrisha sheria, ana uwezo wa kumgeuza mtuhumiwa na kuwa hana tuhuma" Dizonga aliongea,



"Sasa kama ni hivyo, mbona mgonjwa wake huyu anaogopa kwenda hospitali wakati mtu wake ana nguvu za namna hiyo?" Dokta Smith aliuliza,



"huyu sio mgonjwa ambaye amefanya umeachiwa, yupo, yupo utamuona" Dizonga aliongea na kuzidi kumchanganya Dokta Smith,



"Sasa kama yupo, kwanini usingenipeleka moja kwa moja kwa huyo mgonjwa?" Dokta Smith aliuliza,



"huyo mgonjwa hawezi kumuona hovyo, kila kitu kina taratibu zake, hapa nasubiri kupigiwa simu ili nikupeleke kwa huyo mgonjwa" Dizonga aliongea na kuzidi kumvuruga Dokta Smith,



"lakini hata mimi ni mgonjwa" Sajenti Minja aliongea,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"ndio, ila sasa ili utibiwe, tunatakiwa tujue tatizo kwa undani, ili tatizo lijulikane, ni lazima uende hospital" Dokta Smith aliongea kwa upole,



"sawa, kesho nitaenda hospital, maana nimechoka kukaa kitandani kila siku" Sajenti Minja aliongea,



"X soldier sasa hospital utaendaje, huoni ni kujipa mitihani tu" Dizonga aliongea,



"nitaenda tu, hata ukunikatalia kunipeleka, nitaenda hata kwa kutambaa" Sajenti Minja aliongea na kipindi hicho simu ya Dizonga ilikuwa ikiita, akaipokea,



"nambie" Dizonga aliongea baada ya kuipokea simu



"tayari tumeshampeleka yule mwanamke kwa Ray, sasa unaweza kumpeleka Dokta" Sauti ya upande wa pili iliongea,



"sawa" Dizonga aliongea na kukata simu, kisha akamgeukia Dokta Smith,



"twende sasa uko sehemu husika, na tukifika hutakiwi kuzungumza chochote kuhusu huyu mgonjwa wangu hapa" Dizonga alimuonya Dokta Smith,



"nitafanya hivyo" Dokta Smith alijibu,



"X soldier baadae, acha nimpeleke Dokta" Dizonga alimwambia Sajenti Minja,



"poa D" Sajenti Minja aliongea,



"Kijana, jitahidi uende hospital, alafu nitajua nianze wapi kukutibu" Dokta Smith aliongea,



"usijali, nitaenda kesho" Sajenti Minja aliongea,



"sawa, ugua pole" Dokta Smith aliongea huku akitoka na Dizonga, wakamuacha Sajenti Minja akiwa anajigeuza kitandani.



Walitoka mpaka nje, Dizonga akachukua gari yake na kisha Dokta Smith akaingia upande wa pili wa gari, siti za mbele, Dizonga akaondoa gari.



"huyu unaemuita X soldier alipata matatizo gani, maana haiwezekani mtu aumie mwili mzima, hata ajali hakuna ya namna hiyo, hiyo labda kwa mwizi ndio inaweza kutokea, kwa sababu wananchi wakianza kumpiga mwizi hawachagui pa kupiga, wanapiga kila sehemu" Dokta Smith aliongea,



"huyo alitakiwa afe, yaani kipigo alichopewa kilikuwa kipigo cha kifo, alipoteza fahamu siku tatu" Dizonga aliongea,



"kwanini alipigwa?" Dokta Smith aliuliza,



"ni mambo ya kijinga tu, utayajua mbele siku zinavyozidi kwenda" Dizonga aliongea,



"na imekuwaje amepona wakati tangu amepigwa hujawahi kumpeleka hospitali, na hapo ulisema alizimia siku tatu?" Dokta Smith aliuliza kwa mshangao,



"huyu jamaa alipigwa na kufungwa kwenye gunia, kisha akatupwa baharini, na kati ya watu walioshiriki kumtupa baharini, mimi nilikuwepo, ila sasa huyu jamaa mimi nilikuwa namfahamu juu juu tu, kwa kuwa huyu ni mwanajeshi, kwa hiyo baada ya kupigwa na kutupwa baharini, mimi nilienda duka la dawa na kununua dawa na bomba la sindano, kisha nikawaambia wenzanu nimesahau kitambulisho katika gunia tulipomuweka huyu mtu, kwa hiyo tukarudi baharini na mimi mwenyewe ndio niliingia baharini kwenda kuutoa mwili wa huyu jamaa na uko uko nilimchoma sindano ya kushtua mapigo ya moyo, wenzangu hawakuweza kugundua kitu kwa kuwa nilikuwa mbali sana na nchi kavu, kwa hiyo nilifanya kila kitu kwa utaratibu sahihi. Baada ya kumchoma sindano, mapigo ya moyo yalianza kupiga, basi nikambeba na kumpeleka nchi kavu, kisha ndipo nikajifanya kufungua gunia alilofungwa na kutoa kitambulisho changu, nikauacha mwili nchi kavu, kisha tukarudi kwa mkubwa aliyetutuma, tukarudisha report kwa mkuu, baada ya hapo tukatawanyika, ndipo niliporudi baharini na kumchukua huyo X soldier na kumpeleka nyumbani kwangu, kisha nikampigia mkuu mmoja wa jeshi na kumueleza kuhusu habari za huyu jamaa kutaka kuuawa, akanambia niendelee kumuhifadhi huku nikiendelea kumchunguza, kwa maana alikuwa na tuhuma za kumtorosha muarifu, mpaka sasa hakuna aliyethibitisha hilo" Dizonga aliongea,



"kwa hiyo X soldier ni Mfanyakazi wa jeshi, na wewe ni Mfanyakazi wa jeshi. Jeshi lipi sasa, la polisi au la ulinzi na usalama?" Dokta Smith aliuliza,



"hilo hupaswi kujua" Dizonga alijibu,



"sawa, je na huyo mgonjwa mwingine ninayeenda kumtibu, nae amevunjwa kama X soldier?" Dokta Smith aliuliza na kumfanya Dizonga amtazame,



"huyo ugonjwa wake ni tofauti, ila pia hatibiwi kwa nia njema" Dizonga aliongea,



"kwanini unasema hivyo?" Dokta Smith aliuliza,



"huyo anatakiwa atibiwe ili afe" Dizonga aliongea,



"bado sijakuelewa" Dokta Smith aliongea huku akimgeukia Dizonga,



"hujaelewa nini sasa?" Dizonga aliuliza,



"kuwa anatibiwa ili afe, yaani kivipi?" Dokta Smith aliuliza,



"huwezi kunielewa kwa kuwa tunazungumza lugha moja ila vichwa vyetu vinajenga picha tofauti" Dizonga aliendelea kuongea,



"unaongea mafumbo sana" Dokta Smith aliongea,



"sio mafumbo, ninachoongea ni ukweli halisi, ngoja ufike tuendapo na uzoee mazingira, huenda utajua ninachoongea leo, maana ukishazoea mazingira ya pale, huenda tukawa tunajenga picha moja na kuongea lugha moja" Dizonga aliongea na kumfanya Dokta Smith akae kimya tu,



"ila endapo nitamkuta mgonjwa yupo katika hali kama ya X soldier, hapo ndipo nitaamini unyama upo" Dokta Smith aliongea,



"hivi pale X soldier unamuona ana hali mbaya? Je ungemkuta ndio nimetoka kumuokoa, si ungelia kabisa wewe" Dizonga aliongea na kukohoa,



"tusiishi kwa mazoea, mimi ninachokushauri, ni vyema utumie mbinu yoyote ile, uhakikishe X soldier anafika hospital kufanyiwa X Ray, vinginevyo unaweza kumsababishia ulemavu usiokuwa na maana, kwa maana ule mguu ambao umevunjika, eneo ulipovunjikia ni pabaya sana, sasa kwa umri wa X soldier, mifupa yake haikui tena, endapo utamchelewesha zaidi, mnaweza shangaa mnampoteza.



"kuhusu hilo nitalifanyia kazi" Dizonga aliongea huku akisimamisha gari mbele ya geti la nyumba ya Ray Charles,



"ndio hapa?" Dokta Smith aliuliza na kipindi hicho Dizonga alikuwa akipiga honi mfululizo, baada ya muda geti likafunguliwa, Ray Charles akasimama mlangoni, akamkata jicho kali Dizonga,



"mambo vipi Ray?" Dizonga alimsalimia Ray,



"unajua mimi sipendi kelele, hizo upigie kwako, ukifika hapa simama getini na ungoje ufunguliwe, haina haja ya kupiga honi au kugonga geti" Ray Charles aliongea kwa hasira, Dizonga akatabasamu tu na kuingiza gari ndani ya uzio. Walipofika ndani ya geti, Dizonga akazima gari na kisha wakatelemka, wakawa wanamngoja Ray afunge geti. Ray alimaliza kufunga geti na kuwapita huku akiingia ndani ya nyumba yake, Dizonga nae akaamua kumfuata kwa nyuma huku wakiambatana na Ray Charles. Ray Charles alitembea mpaka katika chumba kimoja na kufungua mlango,



"Dokta ingia" Ray Charles aliongea kisha Dokta Smith akampita dizonga na kuingia ndani, Dizonga nae akawa anataka kuingia, Ray Charles akamzuia kwa kumuwekea mkono kifuani,



"wewe ulitakiwa uishie nje ya geti, ndio kazi yako iliishia pale, hukupaswa kuingia humu" Ray Charles aliongea na kumsukuma Dizonga, Dizonga akatabasamu na kuondoka huku akitikisa kichwa kwa masikitiko.



Dokta Smith alipoingia akapigwa na butwaa kumuona mgonjwa mwenyewe ni BQ,



"siwezi kumtibu huyu, maana huyu ndio amesababisha nikawa gerezani" Dokta Smith aliongea,



"ila huyu huyu ndio amefanya uwe huru tena" Ray Charles aliongea,



"unachotakiwa kufanya ni kutii amri, mimi sio mtu salama kwako, kwa hiyo usinilazimishe nikuoneshe upande wangu mbaya" Ray Charles aliongea na kumfanya Dokta Smith awe mpole.



Dokta Smith akamsogelea BQ na kumpima joto, akashtuka, sura yake ikahamaki,



"nipishe kidogo" Dokta Smith aliongea huku akihema haraka haraka, alikuwa na hofu mno, Ray Charles akaondoka na kwenda kukaa sebuleni.



Dokta Smith akafungua begi lake na kutoa vipimo kadhaa, akaanza kumpima BQ, ila kila kipimo alichokuwa anampima BQ, kilikuwa kinagoma, kinaleta majibu yasiyoridhisha, Dokta Smith akaamua amfunue macho BQ kwa kidole, akakuta macho yameshakuwa meupe, Dokta Smith akaanza kulia,



"kwisha kabisa, ni unyama huu" Dokta Smith aliongea huku akilia kwa uchungu, Ray Charles akasikia kilio cha Dokta Smith, akaja haraka ndani,



"Kuna nini?" Rav Charles aliuliza,



"mmenileta nitibu mtu au nifufue mtu?" Dokta Smith aliuliza kwa uchungu huku akilia, Ray Charles akamsogelea BQ na kumuangalia kwa umakini,



"unamaanisha amekufa?" Ray Charles alimuuliza Dokta Smith,



"muda sana" Dokta Smith alijibu huku akiendelea kulia,



"basi, hakuna hasara, jiandae nikurudishe gerezani" Ray Charles aliongea huku akitoka katika kile chumba....







Kilio cha Dokta Smith, kilimfikia Dizonga aliyekuwepo nje, ilimbidi aingie ndani, akakutana na Ray Charles,



"unaenda wapi?" Ray Charles aliuliza huku akisimama,



"Dokta Smith analilia nini?" Dizonga aliuliza,



"Dizonga si nilishakuambia kazi yako iliishia getini, kinachoendelea ndani hakikuhusu tena" Ray Charles aliongea huku akimtazama Dizonga,



"sawa" Dizonga alijibu kinyonge na kuanza a kuondoka, ila alikuwa anataka sana kujua kinachomliza Dokta Smith, ila hakubahatika kujua, Dizonga alitoka nje na kukaa ndani ya uzio huku akiwa ameegemea gari yake, Ray Charles nae akaja,



"unaweza kuondoka tu, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa hapa, sasa hivi sitoongea tena na mdomo" Ray Charles alimwambia Dizonga, Dizonga akaona isiwe tabu, akaingia ndani ya gari na kuondoka zake.



Ray Charles akarudi mpaka katika chumba alichokuwepo Dokta Smith, na kumkuta akimgeuza geuza BQ,



"naweza kumchukua nikamuhifadhi sehemu nyingine?" Ray Charles alimuuliza Dokta Smith,



"wapi? hospital?" Dokta Smith aliuliza,



"hospital? Amekufa nimpeleke hospital akafanye nini?" Ray Charles aliuliza,



"ngoja nijaribu kumtibu tu" Dokta Smith aliongea,



"kumtibu? Kutibu mtu aliyekufa?, acha upuuzi mzee, tunapotezeana muda ujue" Ray Charles aliuliza kwa mshangao,



"ngoja nikueleweshe, niliposema amekufa ni kwa sababu Kuna dawa moja tu ya kumtibu huyu, na inatakiwa ipatikane ndani ya masaa sita kuanzia sasa, na hiyo dawa inaweza kupatikana China, marekani au Israel. Kwa maana hiyo ni ngumu kupatikana, kwa hiyo huyu masaa machache sana ya kuishi" Dokta Smith aliongea kwa huzuni,



"kumbe wewe mzee ni mwendawazimu, ulikuwa unalia nini wakati mtu bado hajafa? Subiri masaa sita yafike ndio ulie" Ray Charles aliongea na kumtazama BQ,



"sawa, mimi naomba uniachie huru niondoke, kwa maana hata nikitumia ujuzi gani, sitoweza kuokoa maisha ya huyu dada bila ya hiyo dawa" Dokta Smith aliongea,



"uondoke? Kuondoka huwezi mzee, mpaka tujue hatma ya huyu mwanamke" Ray Charles aliongea,



"bila hiyo dawa, hakuna hatma nyingine zaidi ya kifo, Nyie mlimuweka ndani siku zote bila hata ya kumpa chakula, mlikuwa mnategemea nini?" Dokta Smith aliongea kwa ukali na kufanya Ray Charles atabasamu,



"huyo dawa inaitwaje?" Ray Charles aliuliza,



"tremols" Dokta Smith alijibu,



"Sasa hivi ni saa ngapi? " Ray Charles aliuliza na kumfanya Dokta Smith atazame saa yake,



" saa moja kasoro robo" Dokta Smith alijibu,



"kwa maana hiyo mpaka Ikifika saa saba usiku, huyu mwanamke anatakiwa awe ameipata hiyo dawa?" Ray Charles aliuliza,



"ndio, lakini haipatikani, na ukisena uagize kutoka nje, haiwezi kufika ndani ya hayo masaa" Dokta Smith aliongea,



"ngoja nikajaribu kuzunguka hospitali, naweza kubahatisha" Ray Charles aliongea na kumfanya Dokta Smith amuangalie tu,



"hapa nchini hazipo" Dokta Smith aliongea,



"uwa sijafunzwa kukata tamaa, ngoja nikajaribu" Ray Charles aliongea huku akitoka nje, akaingia chumbani kwake na kuchukua funguo ya gari, kisha akarudi mpaka katika chumba alichokuwepo Dokta Smith na BQ, akakifunga kwa nje na kuondoka zake, aliamua kwenda kujaribu kutafuta dawa, ingawa aliambiwa hazipatikani.



**************



Tom alikuwa kama amechanganyikiwa, sasa alianza kuona mambo ni ya moto, alishaanza kuogopa baada ya kutekwa na kisha mtekaji kumuachia na kumwambia akimbie.



Tom alivyokuwa upande wa nyuma ya hospitali, ndipo alipohisi simu yake ikiita, alipoangalia jina la mpigaji, alikuta ni ile namba ya mkuu wa polisi, Tom hakupokea wala hakutaka simu, ila aliirudisha mfukoni ikiwa vile vile, kisha Tom akarudi taratibu mpaka maeneo ya wodi aliyolazwa, alikaa kwa mbali sana, ndipo aliposhuhudia vijana wawili wa makamo yake wenye makoti ya kofia wakiingia katika ile wodi, baada ya dakika akawaona wale vijana wakitoka huku wakiwa wamehamaki, wakaanza kuingia kila wodi, hapo ndipo akajua kweli alikuwa akitafutwa, Tom akaanza kuondoka , alihisi huenda mkuu wa polisi anahusika na huu mchezo wa yeye kutaka kukamatwa.



Tom alirudi mpaka upande wa nyuma wa hospital, na kupanda ukutani, kisha akarukia nje, akaanza kukimbia kuelekea nyumbani kwa mpenzi wake, alikimbia akachoka, maana kumbuka Tom ni lazy. Tom akasimamisha boda, akapanda na kumpa Dereva maelekezo ni wapi ampeleke.



Boda boda akaondoa pikipiki kwa kasi. Baada ya dakika tano pikipiki ilikuwa mlangoni katika chumba anaichoishi mpenzi wake Tom, bahati nzuri walimkuta na yeye amebeba kikapu kidogo, alikuwa anataka kutoka,



"wewe umeruhusiwa? Mimi ndio nilikuwa nakuletea chakula hivyo" Mpenzi wake Tom aliongea huku akimshangaa Tom,



"una buku jero hapo?" Tom alimuuliza mpenzi wake,



"nina elfu mbili" Mpenzi wake alijibu huku bado akimshangaa Tom,



"mpe hiyo hiyi" Tom aliongea na kisha mpenzi wake akafungua pochi yake, na kutoa noti ya elfu mbili, akampa Dereva bodaboda, dereva akaipokea nw kumrudishia mia tano, kisha Dereva akaondoka,



"vipi mwenzetu, mbona hima hima?" Mpenzi wake alimuuliza,



"tuingie ndani kwanza" Tom aliongea huku akitangulia kuingia ndani,



"wewe leo upo tofauti sana, au kile kipigo cha yule baba kimekutia wendawazimu?" Mpenzi wake aliuliza huku nae akimfuata Tom, akaingia mpaka ndani na kumkuta Tom akiwa amesimama,



"enhe, nambie" Mpenzi wake alianza kumuongelesha,



"tunatakiwa tuhame hapa, vinginevyo nitakufa, kuna watu wananiwinda, wanataka waniue" Tom aliongea huku akihema haraka haraka,

"haka mwenzangu, wewe hama tu, mimi siwezi kuondoka hapa" Mpenzi wake aliongea huku akimshangaa Tom,



"kwa hiyo lile balaa la usiku wa kuamkia leo unajifanya hukuliona? hujaona nilivyopigwa mpaka nikazimia? na mbaya zaidi Kuna watu wengine walikuja kunitafuta hospital na walitaka kuniua, hao watu ni tofauti na yule mtu aliyenivamia usiku" Tom aliongea na mpenzi wake akashtuka,



"lakini umewafanya nini wewe? Mbona unapenda kujiweka mashakani?" Mpenzi wake aliuliza,



"Mama, tuondoke, hayo maswali tutayajua mbele ya safari" Tom aliongea,



" tunaenda wapi sasa?" Mpenzi wake aliuliza,



"twende tukakae Lodge kwa muda, alafu tutatafuta chumba"" Tom aliongea,



"una pesa sasa?" Mpenzi wake aliuliza,



"ipo, mshahara wangu bado unaingia katika account yangu ya bank, nitautumia huo huo" Tom aliongea,



"sawa, kesho asubuhi tutaondoka" Mpenzi wa Tom aliongea,



"pumbavu kabisa, tuondoke sasa hivi tukalale uko, hiyo kesho tutarudi kuhamisha nguo tu" Tom aliongea kwa hasira,



"jamani!!!, na vyombo je?" Mpenzi wake aliuliza,



"bwana, kama unataka kufa, endelea kubaki hapa, mimi acha niondoke" Tom aliongea kwa hasira huku akiondoka,



"nisubiri sasa angalau nibebe nguo mbili tu" Mpenzi wake aliongea kwa kulalamika,



"wewe unaudhi, hujui tu" Tom aliongea huku akisimama mlangoni,



"jamani, yamekuwa hayo tena?" Mpenzi wake Tom aliongea huku akifungua kabati na kutoa nguo chache na kuziweka katika begi.



**************



Dizonga baada ya kuondoka nyumbani kwa Ray Charles, alirudi nyumbani kwake, alipofika alioga na kisha akaenda mezani na kupakua chakula.



"mgonjwa ulimpelekea chakula?" Dizonga aliuliza,



"ndio" Mke wake alijibu,



"sawa, ngoja nikakae nae, nina maongezi nae kidogo" Dizonga aliongea huku akibeba chakula chake, na kuelekea moja kwa moja katika chumba alichokuwepo Sajenti Minja,



"X soldier vipi?" Dizonga aliongea huku akikaa kitanda karibu na Sajenti Minja,



"poa ndugu" Sajenti Minja alijibu,



"umeuona yule Dokta, nimetoka kumtoa gerezani leo kwa oda ya Rais, kuna mgonjwa anatakiwa akamtibu" Dizonga aliongea,



"huyu Dokta si ndo yule Dokta Smith, alishikwa baada ya kupatikana na hatia ya kumtibu yule mwanamke muuaji?" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio huyo huyo, kumbe upo makini?" Dizonga aliuliza,



"ni mgonjwa yupi anaenda kumtibu, kiasi kwamba akatolewa magereza bila kusomewa hukumu yake?" Sajenti Minja aliuliza,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"huyo mgonjwa hata mimi simjui" Dizonga alijibu, hakutaka kumuweka wazi Sajenti Minja,



"atakuwa ni ndugu wa Rais tu" Sajenti Minja aliongea,



"itakuwa hivyo. sasa X soldier, nimeongea na daktari mmoja ambaye ni rafiki yangu, amesema nikupeleke usiku ukafanyiwe vipimo vya X Ray, maana Dokta Smith leo amenisisitiza sana ufanyiwe vipimo ili kesho aanze kusimamia matibabu yako" Dizonga aliongea,



"vipi mazingira ya hiyo hospital unayotaka kunipeleka? hakuna unoko wowote?" Sajenti Minja aliuliza,



"sikutaka kumwambia kuwa mgonjwa ninayempeleka ni mtu anayetafutwa, maana ningemwambia hivyo inaweza kuwa sio salama kwetu, watu hawaaminiki siku hizi" Dizonga aliongea,



"ni kweli, ila hakushangaa uliposema mgonjwa wako utampeleka usiku?" Sajenti Minja aliuliza,



"alishangaa, ila nilimwambia nafanya hivyo kwa kuwa mgonjwa anatoka safarini, na anaingia usiku" Dizonga alijibu,



"sawa, tunaenda saa ngapi?" Sajenti Minja aliuliza,



"kwenye saa tano hivi, sasa hivi ni saa mbili kasoro" Dizonga aliongea huku akitazama saa katika simu yake,



"sawa ndugu yangu" Sajenti Minja aliongea,



"poa, acha nikaongee na wife, muda ukifika nitakuja" Dizonga aliongea huku akiinuka,



"sawa" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama Dizonga aliyekuwa akitoka nje.



************



Mishale ya saa tano na dakika tatu, Dizonga alikuwa anaegesha gari ndani ya uzio wa hospital, kisha Dizonga akatelemka na kuzunguka upande wa pili, akamtoa Sajenti Minja na kumsaidia kutembea, waliingia mpaka ndani ya jengo la hospital na kuelekea moja kwa moja katika ofisi ya daktari aliyeongea na Dizonga,



"Karibu, umechelewa kama dakika tano hivi, usingekunikuta kwa maana nilidhani hutokuja tena, sema tu Kuna rafiki yangu amenipigia simu, amesema anakuja kuchukua dawa" Daktari aliongea,



"samahani kwa kuchelewa, si unajua gari zinazotoka mikoani uwa haziingii kwa muda?" Dizonga aliongea na kisha Sajenti Minja akamsapoti kwa kuchezesha kichwa chake kwa kukipandisha na kukishusha,



"mimi nadhani twendeni moja kwa moja katika vipimo, si ni x-ray tu?" Daktari aliuliza,



"ndio, ni x-ray tu" Dizonga alijibu, kisha daktari akavuta kiti cha matairi na kumtaka Sajenti Minja akae, Sajenti Minja alivyokaa, Dizonga akaanza kusukuma kiti cha matairi kumfuata daktari



Safari yao iliishia ndani ya chumba kikubwa ambacho kilikuwa na nafasi ndogo ya kupumzika mgonjwa baada ya vipimo, na pia kulikuwa na chumba kidogo chenye machine za kisasa za x-ray.



"muingize ndani ya chumba" Daktari aliongea huku akiingia katika kile chumba chenye machine za x-ray, Dizonga akaingia na Sajenti Minja,



"muweke juu ya hiki kitanda" Daktari aliongea na kisha Dizonga akambeba Sajenti Minja na kumuweka juu ya kitanda kile kilichozungukwa na vifaa vya kisasa kabisa,



"tutoke nje sasa" Daktari aliongea kisha Dizonga akatangulia kutoka, daktari akafuatia, chumba kile wakakifunga, kisha daktari akahamia katika computer,



"ni x-ray ya mwili mzima?" Daktari aliuliza,



"ndio" Dizonga alijibu,



"sawa " Daktari aliongea kisha akabonyeza bonyeza computer, kile chumba alichokuwepo Sajenti Minja kikatoa mwanga mwekundu kwa sekunde thelathini, kisha ule mwanga ukazima,



"ingia umtoe" Daktari aliongea na Dizonga akaingia katika kile chumba na kumtoa Sajenti Minja,



"funua mashuka na umuingize humo, kuna kitanda cha kupumzikia, kwa maana mwanga wa x-ray sio mzuri, anatakiwa apumzike kama dakika kumi hivi" Daktari aliongea, kisha Sajenti Minja akaingia katika kile chumba kilichofunikwa na mashuka, akakuta Kuna kitanda kidogo, akamlaza Sajenti Minja, Dizonga akarudi kwa daktari aliyekuwa bize na computer,



"alipata ajali huyu?" Daktari aliuliza,



"alipigwa na wenzake, sijui walizurumiana" Dizonga aliongea na kipindi hicho simu ya daktari ilikuwa ikiita, akatabasamu na kupokea,



"njoo kwenye chumba cha x-ray, acha uboya wakati maelekezo nilishakupa" Daktari aliongea na kukata simu, akaendelea kutabasamu,



"unasema alipigwa?" Daktari aliuliza huku akimuangalia Dizonga,



"ndio, wenzake walimchangia" Dizonga aliongea,



"khaaa, walikuwa wanampa kipigo cha aina gani? maana dah!!" Daktari aliongea huku akitazama computer na sura aliikunja aliikunja, na muda huo mlango wa mule ndani ulifunguliwa, akaingia Ray Charles, hapo Dizonga kidogo akimbie, maana hakutegemea kukutana na mtu huyo,



"dawa zikwapi wewe mwendawazimu?" Ray Charles aliuliza huku akimtazama daktari ambaye alikuwa akitabasamu tu,



"subiri basi, usiniendeshe mdogo wangu" Daktari aliongea Kwa utani na kumfanya Ray atabasamu,



"ujue nina mgonjwa anatakiwa apate hizo dawa haraka, yaani apate kabla ya saa saba, sasa hivi ni saa sita na dakika kumi" Ray Charles aliongea huku akiweka msisitizo,



"subiri nikakuletee, ningojee hapa hapa" Daktari aliongea huku akiinuka katika kiti na kutoka nje, akamuacha ndani Ray Charles na Dizonga ambaye alikuwa na wasiwasi muda wote,



"vipi sasa hivi upo huku, una mgonjwa?" Ray Charles alimuuliza Dizonga,



"ndio, ndio ninae. Vipi mgonjwa wenu anaendeleaje?" Dizonga aliamua kubadili mada,



"ndio hizi dawa nimemfuatia hapa, hali yake sio nzuri" Ray Charles alijibu na kipindi hicho yule Daktari alikuwa akirudi na mfuko mdogo uliojaa dawa.



"shika vizuri, zifiche kweli kweli, maana hizi dawa uwa hazitolewi kawaida" Daktari aliongea huku akimpatia Ray Charles ule mfuko wa dawa,



"sawa, wewe endelea na kazi, nitakuona kesho kama dawa zitafanya kazi" Ray Charles aliongea,



"sawa, mimi kuna mgonjwa namuangalia hapa, aisee kaumia umia mifupa mpaka inatisha" Daktari aliongea na kumfanya Ray Charles asogee katika computer na yeye akatazama, hapo Dizonga alikuwa na hofu kuu, moyoni alimlaumu Daktari kwa kulopoka,



"Yupo hai au amekufa?" Ray Charles aliuliza huku akitazama computer,



"Yupo hai, yupo katika chumba cha mashuka umo" Daktari aliongea na kufanya Dizonga sasa Jasho lianze kumtoka,



"Dizonga, ni ndugu yako?" Ray Charles alimuuliza Dizonga ambaye hata sura ilionesha wasiwasi,



"ndugu yake huyo, ndio kamleta hapa" Daktari alijibu na kumfanya Dizonga amtukanie tusi la nguoni, ila alimtukania moyoni,



"naweza kumuona?" Ray Charles alimuuliza Dizonga,



"muangalie tu" Daktari alijibu tena kabla hata Dizonga hajajibu,



"muache apumzike, utakuja kumuona kesho home " Dizonga alijibu,



"ndugu yako ni ndugu yetu, ngoja nimuone ili siku nyingine nisimpite barabarani" Ray Charles aliongea na kwenda kufungua mashuka ya kile chumba, akamkuta Sajenti Minja akiwa amelala kitandani.



Dizonga alitoka nje kabisa, alijua ndani kumeshaharibika.......



______________



Uzuri alimkuta Sajenti Minja akiwa amelalia tumbo, kisogo na mgongo ndio vitu pekee ambavyo Ray Charles aliviona,



"pole sana" Ray Charles alimwambia Sajenti Minja,



"asante" Sajenti Minja alijibu huku akitetemeka, maana alishamtambua kuwa huyo ni Ray Charles, kwa maana aliyasikia maongezi yao yote yeye na daktari. Simu ya Ray Charles ikaanza kuita, Ray Charles akatoka mule katika kile chumba,



"Hoya, kesho" Raa Charles alimwambia daktari huku akitoka nje na bado simu yake ilikuwa inaita,



"hey" Ray Charles aliongea baada ya kupokea simu,



"hiyo dawa umepata au bado?" Sauti ya upande wa pili iliuliza na kufanya Ray Charles aitoe simu sikioni na kuangalia namba ya mpigaji,



"naongea na nani?" Ray Charles aliuliza,



"Dokta Smith" Sauti ya upande wa pili ilijibu,



"namba yangu umeipata wapi?" Ray Charles aliuliza,



"dawa umepata?" Dokta Smith aliuliza bila kujibu swali la Ray, Ray Charles akakata simu na kuiweka mfukoni, akaelekea kwenye gari yake na kuingia, akaitoa gari kwa mwendo wa wastani, akatoka mpaka nje ya geti la hospital, akamuona Dizonga, ila Dizonga alikuwa bado hajamuona Ray Charles. Dizonga alishtuka gari ikisimama mbele yake,



"mi naondoka, ila kuhusu matibabu ya mgonjwa wako, usimlipe kitu daktari, nitamlipa mimi" Ray Charles aliongea na muda huo Dizonga alikuwa anajiuliza huyu Ray Charles amemtambua Sajenti Minja au hajamtambua,



"wewe mbona umezubaa?" Ray Charles alimstua Dizonga,



"umeonana nae lakini, umemuona jinsi alivyo?" Dizonga aliuliza,



"nimemuona, ila alikuwa amelala" Ray Charles aliongea,



"sura umeiona?" Dizonga aliuliza,



"hapana, kwani vipi?" Ray Charles aliuliza,



"tumefanana sana, ni kaka yangu" Dizonga aliongea,



"poa, acha mimi niwahi" Ray Charles aliongea na kuiondoa gari kwa kasi sana. Dizonga akabaki amesimama huku akiwa ahamini kama ni kweli Ray Charles hajamuona Sajenti Minja.



Dizonga akatoa simu yake ili ampigie Sajenti Minja, ila kabla hajampigia, simu yake ilianza kuita, alipoangalia jina la mpigaji, alikuta ni lile la yule daktari,



"sema" Dizonga aliongea baada ya kupokea simu,



"upo wapi, muda unaenda alafu unaniweka tu hapa " Daktari aliongea kwa ukali,



"nakuja, nipo nje hapa" Dizonga aliongea na kisha akakata simu, akaanza kutembea mwendo wa haraka haraka ili kuwahi wodini.



Alifika na kuingia katika kile chumba cha vipimo, akamkuta daktari ameshikilia majibu ya x-ray,



"kaka unajua usiku huu, mimi nilitakiwa niondoke mapema ila kwa ajili yako ndio maana nipo mpaka muda huu" Daktari aliongea kwa sauti ya kinyonge ila yenye hasira,



"samahani sana, nilidhani tunaweza kuchukua muda mrefu" Dizonga aliongea,



"kwani tunafanya operation mpaka tutumie muda mrefu? Majibu haya hapa, sasa utaamua mgonjwa wako atibiwe hapa, au uondoke nae" Daktari aliongea huku akimpatia Dizonga yale majibu,



"nitaondoka nae tu. Masuala ya pesa atamaliza Ray" Dizonga aliongea,



"Ray?? kwani mimi niliongea na Ray? Ray kaja amefanya mambo yake na kuondoka, sasa unasemaje huduma yako ailipie Ray?" Daktari aliuliza kwa ukali,



"basi haina shida, shilingi ngapi?" Dizonga aliuliza,



"laki tu" Daktari alijibu na kisha Dizonga akajipekua mfukoni na kutoa pesa, akampatia daktari,



"nashukuru kwa huduma yako" Dizonga aliongea huku akiingia katika kile chumba chenye mashuka na kumtoa Sajenti Minja, kisha wakatoka ndani ya jengo la hospital na kuingia katika gari, Dizonga akawasha na kuondoka.



"hivi unajua tukio lililotaka kutokea pale?" Dizonga alimuuliza Sajenti Minja,



"bwana we, yule daktari wako nae mpuuzi, yaani ningekuwa mimi mzima, ningemtwanga makofi vibaya mno" Sajenti Minja aliongea huku hasira zake zikiwa wazi kabisa,



"hivi alivyoingia ndani ni kweli hajakuona?" Dizonga aliuliza,



"si unajua pozi langu la kulala siku hizi ni sura chini kisogo juu, hiyo ilinisaidia" Sajenti Minja aliongea,



"ilikuwa hatari, ilikuwa wote tufe" Dizonga aliongea,



"mimi ningejaribu kupambana, nisingekubali kufa kirahisi hivyo" Sajenti Minja aliongea,



"ulimshindwa ukiwa mzima kabisa, sasa utamuweza vipi sasa hivi wakati hata kutembea huwezi" Dizonga aliuliza,



"ungeona wala usingeamini" Sajenti Minja aliongea,



"aisee nimeona majibu ya x-ray yako, ila nimeshindwa hata kuelewa, nimeiangalia zaidi ya mara mbili ila bado sijaelewa kitu" Dizonga aliongea,



"si ungemuuliza daktari?" Sajenti Minja aliuliza,



"mpuuzi yule, yaani amenitoka rohoni kweli, mwanajeshi gani anakuwa mbeya mbeya vile?" Dizonga alihoji,



"kwa hiyo hayo majibu ya x-ray tutajuaje kama wewe umeshindwa kuyaelewa?" Sajenti Minja aliuliza,



"nitampelekea Dokta Smith, yeye ni mtaalam zaidi" Dizonga aliongea,



"Sasa utampataje na ulisema kuwa Ray Charles alikuzuia kuonana nae tena?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapo ndipo mbinu za kijeshi zitatumika sasa" Dizonga aliongea na kutabasamu,



"nakuaminia D" Sajenti Minja aliongea,



"haya mambo ni taratibu tu X soldier, utapona" Dizonga aliongea na kuongeza sauti ya gari, safari ikaendelea huku story mbili tatu zikiwapunguzia umbali wa safari.



*****************



Baada ya kutoka hospital, Ray Charles akielekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwake, aliingiza gari ndani ya geti na kutelemka haraka haraka, akaingia mpaka katika chumba alichowafungia Dokta Smith na BQ, alivyoingia tu akampatia Dokta Smith zile dawa, Dokta Smith akazipokea na kuzitoa ndani ya mfuko, akaanza kuzikagua,



"safi, sasa kaandae uji mwepesi sana" Dokta Smith aliongea huku akiendelea kufungua zile dawa,



"mbona ndani hamna Unga wala jiko?" Ray Charles aliuliza,



"katafute, usiku huu yapo maduka mengi tu uwa yanakesha" Dokta Smith aliongea huku akivuta dawa katika bomba la sindano,



"asipoandaliwa huo uji inakuaje?" Ray Charles aliuliza,



"ni sawa na kufanya kazi bure, kwa maana hizi dawa zinanguvu sana, na hapa nampa dozi kubwa, kwa hiyo ni lazima awe na kitu tumboni, vinginevyo huyu atakufa" Dokta Smith aliongea huku akimchoma BQ sindano ya mkononi,



"sawa, ngoja nikatafute" Ray Charles aliongea na kutoka nje, kitu ambacho hakusahau ni kuwafungia kwa nje, hakutaka kabisa Dokta Smith atoke nje.



Dokta Smith hakujali kufungiwa, alichokuwa anakifukiria muda huo nikuhakikisha tu BQ anapata nafuu.



Baada ya kumchoma sindano, sasa alikuwa anataka kumfunua mdomo, ili amnyweshe dawa, ila alishindwa kumnywesha, meno ya BQ yalishikana sana, yaani mifupa ya mdomo ilikuwa imekakamaa kabisa, huo ni mtihani mwingine kwa Dokta Smith, alihitaji dawa ya kuchua ili aweze kulainisha mifupa ya mdomo wa BQ.



Dokta Smith akatoa simu yake na kumpigia tena.



"tafuta dawa yoyote ya kuchuwa na ya sindano za mifupa, kisha leta upesi" Dokta Smith aliongea baada ya Ray Charles kupokea simu,



"mbona unaagiza vitu nusunusu, unataka kumtorosha nini?" Ray Charles aliuliza kwa hasira, ila hakubahatika kupata jibu, tayari Dokta Smith alikuwa ameshakata simu muda mrefu tu mara baada ya kumaliza kutoa maagizo.



Ray Charles aliiangalia simu yake na kuiweka katika siti ya pembeni, akaanza kutafuta maduka ya madawa.



Hakupata shida sana kupata duka la dawa, aliingia katika duka la dawa na kuchukua dawa alizoagizwa, kisha akaingia katoka gari na safari ya kurudi kwake ikaanza.



Ilimchukua dakika chache kuweza kufika kwake, aliingiza gari ndani ya uzio, kisha akatereka na jiko la gesi pamoja na vitu vingine alivyoagizwa.



Aliviweka vitu sebuleni, kisha akaelekea katika chumba alichowafungia Dokta Smith na BQ, mkononi alikuwa na zile dawa alizoagizwa. Alifika mlangoni na kufungua, kisha akaingia ndani, akaziweka dawa juu ya meza,



"vitu vingine vipo wapi?" Dokta Smith aliuliza,



"vitu gani? Unataka nije na jiko na unga na masufuria huku?" Ray Charles aliuliza huku akimshangaa Dokta Smith,



"we kalete, mimi si ndio nimeagiza?" Dokta Smith aliongea huku akiendelea kuchanganya dawa zake, Ray Charles akaona isiwe tabu, akaenda mpaka sebuleni na kurudi na vitu vyote,



"kachote maji nusu sufuria, na uje uwashe jiko na bandika hayo maji" Dokta Smith aliongea huku akianza kuichuwa eneo lote la kuanzia mashavuni mpaka katika shingo ya BQ.



"unapika huo uji humu humu chumbani?" Ray Charles aliuliza,



"fanya nilivyokuagiza" Dokta Smith aliongea, Ray Charles akatoka na sufuria, akaelekea mpaka sehemu lilipo bomba, na kisha akarudi na maji, akawasha jiko na kubandika sufuria ile yenye maji.



"nipo sebuleni" Ray Charles aliongea huku akiwa anatoka nje,



"usitoke, mimi nina kazi hapa, kwa hiyo uji inabidi upike wewe, mimi siwezi kushika kazi mbili kwa wakati mmoja" Dokta Smith aliongea na kumfanya Ray Charles aendelee kubaki ndani na kusimamia matayarisho ya uji.



Ila baada ya kukaa kwa dakika tano mbele ya jiko, alianza kama kukosa amani , hiyo hali aliiona hata Dokta Smith, akawa anamuangalia Ray Charles kwa jicho la wizi, alimuona jinsi anavyopata tabu.



"ebu njoo hapa, unisaidie kumfungua mdomo huyu mwanamke" Dokta Smith alimwambia Ray Charles ambaye alisogea jirani na Dokta Smith kiasi kwamba wakagusana, Dokta Smith aliruka kidogo baada ya kuhisi kuungua alipogusana na Ray Charles,



"vipi?!" Ray Charles aliuliza huku akijitahidi hasigusane tena na Dokta Smith,



"hakuna kitu" Dokta Smith aliongea huku akipanda kitandani kabisa na kupakata kichwa cha BQ, kisha taratibu akaufunua mdomo wa BQ,



"leta huo uji, upooze kidogo tumnyweshe" Dokta Smith aliongea,



"Sasa mbona bado haujaiva?" Ray Charles aliuliza,



"leta hivo hivo, lengo langu sio uive" Dokta Smith aliongea na kisha Ray Charles akarudi jikoni, akazima jiko na kutoa sufuria jikoni, kisha akafungua dirisha na kumimina ule uji kwenye bakuli kubwa, na kuliweka dirishani ili uji upigwe na upepo.



**************



Ndani ya ofisi ya katiba na sheria, alikuwepo waziri mpya aliyeteuliwa na Rais, huyu waziri mpya jina lake no Said Tambala, alikuwa bize kupitia baadhi ya sheria za nchi na mambo mengine, ila macho yake yaligota katika sheria za mikataba, alisoma sheria ya mwaka 1957 iliyosema mkataba utakuwa hai mpaka utakapotekelezwa, bila kujali wahusika wapo hai au wamekufa, cha muhimu ni nakala original ikiwepo tu. Hiki kipengele alikirudia kukisoma zaidi ya mara mbili,



"huu ni upuuzi, lazima hii sheria ifutwe" Said Tambala aliongea na kutabasamu,



"hapa ni kumuingiza king na kisha unampoteza, kuaminiana kulishakufa zamani tu, hata biblia ina hadithi nyingi sana za usaliti, kwa hiyo suala la kusalitiana lipo enzi hadi enzi" Said Tambala aliongea na kuvuta droo katika meza yake, kisha akatoa chupa ndogo, akaimimina yote katika glass, japo aliimimina yote, ila bado haikuweza kujaza glass, alichofanya aliinuka na kwenda kwenye friji ndogo iliyokuwepo ndani ya ofisi yake na kutoa energy drink ya baridi, kisha akaimimina na yenyewe katika glass ile ile yenye pombe kali, akakaa juu ya meza na kuigida ile pombe yote,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sheria uwa zinabadilishwa ili zinufaishe wachache" Said Tambala aliongea huku akiiweka glass ya pombe mezani, kisha akainuka na maker pen mkononi, akaenda mpaka ilipo picha ya Rais, akaiweka alama ya X,



"lazima ufe" Said Tambala aliongea huku akiiangalia ile picha na pia alitabasamu....





MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog