Search This Blog

Friday, 18 November 2022

MKONO WA CHUMA - 4

 






Simulizi : Mkono Wa Chuma

Sehemu Ya Nne (4)





"hivi we mzee ni mwendawazimu? yaani mtu amenishambulia juzi tu usiku alau unasema alishakufaga mtu mrefu'' Sajenti Minja aliongea ndani ya nafsi bila kutoa sauti, hakutaka kabisa kuamini maneno ya mkubwa wake huyo.



"ujue Minja kama hii kazi inakuwa ngumu kidogo kwako, ni bora useme mapema, ila mimi siamini kama kazi hii itakushinda. Ila vielelelezo unavyoniletea ndio vinapunguza imani yangu kwako" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama Sajenti Minja,



"samahani mkuu kama nitakuhudhi kwa swali langu. Hivi huyu mtu amekufa lini? jana au leo?! " Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia mkuu wake kwa mshangao,



" jana au leo? Ulianza alikufa miaka mingapi iliyopita" Mkuu wa polisi alijibu huku akikunja ndita katika paji la uso wake,



"miaka tena?, kwanza umemjuaje na alikuwa ni nani?" Sajenti Minja aliuliza,



"anaitwa Ray Charles" Mkuu wa polisi alijibu,



"alikuwa ni nani?" Sajenti Minja alimuuliza mkuu wake, ila mkuu hakutaka kuendelea na maswali muda huo,



"sihitaji maswali zaidi, wewe kaendelee na kazi zako, ila kumbuka kuwa hiyo kazi unayoifuatilia ni kwa ajili ya manufaa ya serikali yako, sasa endapo utaendelea na upuuzi huo wa kuniletea picha za watu waliokufaga miaka mingi iliyopita na kuwabebesha tuhuma, tambua kazi utaiweka ajira yako hatarini" Mkuu wa polisi aliongea na kumfanya Sajenti Minja ainuke katika kiti, hakutaka kujibu kitu, alikuwa na mshangao ulioambatana na viulizo vingi visivyokuwa na idadi. Sajenti Minja baada ya kuinuka, alitoka nje bila kuaga.



Kama Kuna siku alivurugwa, basi hiyo siku ni leo. Sajenti Minja akaingia katika gari yake na kuondoka huku akiwaza ampe taarifa Tom au akae kimya kwa muda afanye uchunguzi wake?



"kwa kuwa jina nimeshalijua, haitonisumbua?" Sajenti Minja aliongea mwenyewe huku akifikicha jicho lake ambalo ni chongo.



Ilimchukua dakika chache tu Sajenti Minja kufika katika hoteli anayoishi kwa muda huo, alishuka katika gari na kupitia funguo yake mapokezi, kisha akaelekea katika lifti.

Dakika chache tu alikuwa nje ya mlango wa chumba chake, akafungua na kuingia, alipoingia alivua shati na kulitupa katika kochi, kisha yeye akajitupa kitandani, akaitoa simu mfukoni na kuelekea katika application iliyoandikwa "GOOGLE" akabonyeza na kwenda katika sehemu iliyoandikwa "SEARCH" hapo akaandika RAY CHARLES, hilo ndilo jina aliloambiwa na mkuu wake, hilo ndio jina la yule kijana aliyemvamia siku chache nyuma.



Matokeo yaliyokuja baada ya kuandika jina lile, Ray Charles aliyeonekana ni yule mwanamumziki wa kimarekani aliyekuwa na ngozi nyeusi, yaani mmarekani mweusi, aliyezaliwa 1930, na kufariki mwezi wa sita wa mwaka 2004.



Historia ya huyo Ray Charles, ilionesha kuwa alianza kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka mitano, na alipofikisha miaka saba alikuwa kipofu kamili, yaani hakuwa na uwezo wa kuona kabisa. Na mwisho Ray Charles alikufa akiwa na miaka 73, hiyo ni mwaka 2004, na kilichomuua ni ugonjwa wa ini.



Sajenti Minja akatoka katika habari hiyo, kwa maana huyo Ray Charles mmarekani alikuwa anazifahamu habari zake, alikuwa ni mtu maarufu sana.



Akaendelea kupekua habari za watu wengine ambao wana jina hilo hilo la Ray Charles, ndipo alipokutana na kichwa cha habari "WANAJESHI WA TANZANIA WAMEKUFA BAADA KUVAMIWA NA AL SHABAB" hicho kichwa cha habari kikamvutia, kwa maana mmoja wa hao wanajeshi waliouawa, jina aliitwa Raymond Charles.



Sajenti Minja akaifungua ile habari na kuisoma kwa umakini,



"wanajeshi watatu wamekufa baada ya kukamatwa na kundi la kigaidi la AL shabab, inadaiwa wanajeshi hao walikuwa wameingia nchini Somalia kwa lengo la kwenda kumkamata na kumpeleka katika vyombo via sheria mmoja kati ya viongozi wa juu wa AL shabab, ila waligundulika na kukamatwa, kisha wakapewa mateso makali kabla hawajafa, na baadae inasemekana walipigwa risasi na kutangazwa katika vyombo vya habari huku nyuma ya miili yao wakiwa wamesimama wanamgambo wa AL shabab wakiwa wameshika bunduki na kujifunika usoni kwa kutumia vitambaa.

Majina ya wanajeshi hao, ni Luteni Said Sedan, kanali Raymond Charles, na kanali Mdendu Kidufu.



Jeshi la Tanzania limethibitisha kuwa hao ni watu wao, ila wamekanusha vikali kuwa walienda Somalia kwa ajili ya kwenda kumkamata kiongozi wa AL shabab, wanachodai wao ni kuwa wanajeshi hao walikuwa katika Jeshi la umoja wa Africa, lililokuwa Somalia kwa ajili ya kulinda amani" Habari ilisomeka hivyo, Sajenti Minja akajikuna kichwa, ila bado hakuamini huyo mtu ndio huyo aliyeambiwa amekufa au lah! Akaamua atafute na picha za hao wanajeshi, hapo ndipo alipata mshangao, kwa maana kwenye jina la Raymond Charles, ndipo kulikuwa na picha ya yule kijana anaemtafuta,



"kweli amekufa, sasa kwanini yupo hai? ni mzimu?" Sajenti Minja alijiuliza huku akiwa ameikazia macho ile picha ya yule mwanajeshi aliyekufa, ila ndio huyo huyo ambaye alitaka kumuua siku chache zilizopita.



"hii ni ngumu kukubalika, haiwezekani kwa kweli" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka kitandani, akasimama na kuvaa shati, akavua tena, alikuwa kama kachanganyikiwa,



Akaiangalia simu yake, kisha akatafuta namba ya Tom na kumpigia, simu ikaanza kuita,



"Tom vipi?" Sajenti Minja aliongea mara baada ya upande wa pili kupokea simu,



"poa bro, nambie" Tom alijibu katika hali ya uchangamfu,



"una kazi muda huu?! " Sajenti Minja aliuliza,



"nipo tu, nasoma soma habari mitandaoni" Tom alijibu,



"njoo hapa hotelini, chukua bajaj" Sajenti Minja aliongea,



"sawa bro, ila unanitisha" Tom aliongea huku akicheka kwa utani,



"njoo ili uje uogope zaidi" Sajenti Minja alijibu na kumfanya Tom aanze kupata wasiwasi wa kweli,



"Kuna nini kwani?" Tom aliuliza, safari hakuwa akicheka kama mwanzo,



"bwana njoo, utayajua huku huku" Sajenti Minja aliongea na kukata simu, kisha akajitupa kitandani, macho yakaangalia pangaboi namna linavyozunguka, ila akili haikuliwaza pangaboi hilo, akili iliwaza juu ya Ray Charles, hilo ndio jina lililomvuruga kwa wakati huo.



**************



Upande wa msituni, anaonekana Dokta Smith na yule bwana mswahili wakiwa wamekaa pembeni mwa BQ, Dokta Smith alikuwa akimnyesha dawa BQ ambaye alikuwa bado fahamu hazijamrudia, na wala kulikuwa hakuna dalili za fahamu kumrudia.



Baada ya Dokta Smith kumaliza kunywesha BQ dawa, alifungua sanduku lake na kukitoa kile kukichukua kile kichupa kilichoandikwa "POISON", yule bwana mswahili akakikumbuka kile kichupa, kuwa alishawahigi kukichukua na kufyonza dawa ile kwa sindano na kumchoma BQ.



"mbona hii dawa imepungua sana, imemwagika nini?" Dokta Smith aliuliza huku akikagua katika sanduku aone kama ile dawa imemwagika kweli, lakini hakuona kitu, Dokta Smith akapuuza, akachukua bomba la sindano na kufyonza ile dawa ya kwenye kichupa, kisha akamchoma BQ katika mkono, bwana mswahili akajifanya ameshtuka,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"wewe mbona unamchoma sindano ya sumu?" Mswahili aliuliza huku akijifanya amepaniki,



"wewe si ulikuwa unataka afe? basi acha afe" Dokta Smith aliongea huku akitabasamu, ila kitu ambacho hakukijua, ni kuwa tayari yule mswahili alishawahi kumchoma BQ ile dawa, na BQ hakufa, kwa hiyo alichokuwa akikifanya yule bwana mswahili, ni kumdadisi tu Dokta Smith bila Dokta Smith kujua kitu,



"acha ujinga wewe, yaani unamchoma mtu sindano ya sumu alafu unacheka?" Mswahili aliinuka kwa hasira sasa, hata sura yake ilionesha amepaniki,



''subiri wewe punguani, unafikiri mimi nina akili za kijinga kiasi hicho? Hii sio sumu, bado haijakamilika kuwa sumu, ili iwe sumu, ni lazima hii dawa ichanganywe na mkojo, ila bila kuchanganya na mkojo, inakuwa inaongeza joto tu mwilini" Dokta Smith aliongea huku akirudishia ile dawa katika sanduku lake,



"siamini mpaka nione matokeo yake" mswahili aliongea huku akiwa amesimama, ila kwa upande mwingine alishajua namna ya kuichanganya ile dawa na kuwa sumu.



"wewe pumbavu kweli, kwa hiyo unabishana na mimi mtaalamu wa dawa? hii ingekuwa sumu, huyu angeshakufa kitambo tu, ebu ngoja niibebe kidogo alafu tuingie msituni uone" Dokta Smith aliongea huku akifungua sanduku lake na kukitoa tena kile kichupa cha ile dawa, kisha akaipunguzia ile dawa katika kichupa kingine kidogo, kisha akachukua na bomba la sindano,



"haya, twende nikakuoneshe sasa" Dokta Smith aliongea huku akielekea nje, mswahili nae akabeba camera yake na kumfuata Dokta Smith, alidhamiria haswa kujua undani wa ile sumu.



Wakatoka na kufunga ngome yao, kisha wakaingia msituni, lengo lilikuwa ni Dokta Smith kumuonesha yule bwana mswahili kazi ya ile sumu.



Wakafanikiwa kukamata kima wawili, uwa wanamitego yao ambayo hutegea wanyama wa kitoweo chao, na pia mitego mingine uwa kwa ajili ya kukamata wanyama kwa ajili ya utafiti wao.



Dokta Smith akawasogelea wale kima huku mswahili akiangalia kwa umakini. Dokta Smith akatoa kile kichupa, kisha akatoa bomba la sindano, akafyonza dawa katika kichupa na kumchoma kima wa kwanza,



"unaona, bado kima yupo vizuri tu. Chukua hiki kichupa, kojolea kidogo tu, alafu tuangalie zoezi linalofuata" Dokta Smith aliongea huku akimpatia yule mswahili kile kichupa ili aweke mkojo wake,



"Sasa si ungekojolea hata wewe?" Mswahili aliongea huku akikichukua kile kichupa na kusogea pembeni kidogo, kisha akakojolea kidogo kile kichupa, alafu akamrudishia Dokta Smith. Dokta Smith akakipokea kisha akafyonza dawa iliyochanganywa na mkojo ambayo ipo ndani ya kile kichupa, akamchoma yule kima mwingine, sekunde mbili tu baada ya yule kima kuchomwa ile sindano, akaanza kushtuka kama ana kifafa, alifanya hivyo kwa sekunde thelathini, kisha akaanguka na kufa,



"umeona sasa, hii ndio sumu, ila kabla Haijachanganywa na mkojo inakuwa sio sumu. Kwa hiyo yule dada hawezi kufa, nilimchoma hii dawa ikiwa haina mkojo" Dokta Smith aliongea huku akimuonesha kile kichupa yule mswahili, mswahili akakikwapua kile kichupa mikononi mwa Dokta Smith,



"lete ni kusikia. Hivi kama nikitaka nimuwahi ili hasife, natakiwa nimpe dawa gani? au maziwa?" Mswahili aliuliza huku akikitia mfukoni kile kichupa,



"akishafikia hatua ya kupapalika hivo, ujue ndio basi hawezi kupona tena, ni wa kufa tu, hata aje nabii mwenye miujiza kiasi gani, hawezi kumuepusha na kifo kiumbe aliyechomwa hiyo sumu" Dokta Smith alijibu,



"duh, ni hatari sana" Mswahili aliongea huku akijipiga piga katika mfuko wake wa suruali alioweka kile kichupa cha ile sumu,



"kitupe tu, cha nini sasa?" Dokta Smith aliuliza wakati huo mswahili alijifanya hasikii, akageukia upande wa pili kabisa, na akatoa camera yake na kujifanya anapiga picha huku akitembea kuelekea mbele, Dokta Smith akatabasamu, kisha akamuachia yule ambaye alikuwa mzima, na yule aliyekufa, alimtupa, kisha akageuka kumtazama yule mswahili, akamuona kwa mbali akiendelea kupiga picha, Dokta Smith akatabasamu huku akitikisa kichwa kwa masikitiko.



Upande wa pili, huyu mswahili, hakuwa akipiga picha kama Dokta Smith anavyodhani, huyu mswahili alichokuwa akifanya ni kuzuga anapiga picha huku akitembea, lengo lake lilikuwa ni kumtoroka Dokta Smith na kurudi katika hema, ili akammalize BQ.



Baada ya dakika ishirini za kujifanya anapiga picha, alifanikiwa kumtoroka Dokta Smith, kisha akarudi mpaka katika ngome, akafungua kufuri na kufunga kwa ndani katika ile "cage" kisha akanyoosha mpaka katika hema, akaingia, akafungua sanduku na kutoa bomba la sindano, akatoa mfukoni kile kichupa cha ile dawa kilichochanganywa na mkojo, akanyonya ile dawa kwa ile sindano, kisha akamchoma BQ mkononi, kisha mswahili akainua kichwa kutazama mlangoni mara baada ya kuhisi Kuna mtu kasimama, ndipo alipokutanisha macho yake na Dokta Smith akiwa anamuangalia huku machozi yakimtoka, na muda huo BQ alianza kushtuka kama mtu mwenye kifafa, Dokta Smith akatoka nje na kukalia katika jiwe, akawa analia kwa uchungu, atafanyaje sasa na alishamwambua yule mswahili kuwa mtu akifikia katika hali ile ya kushtuka vile, hawezi kupona tena, ni lazima afe tu. Dokta Smith alilia kwa uchungu sana, wakati ndani yule mswahili alikuwa anashangaa namna BQ anavyopapalika pale chini, kwa namna alivyokuwa akipapalika, roho ya huruma ikamuingia yule mswahili, alitamani kumsaidia ila hakuwa na njia ya kutoa msaada, na kipindi hicho BQ alikuwa anatulia na mwili ukanyooka, yule mswahili akatupa lile bomba la sindano, akaanza kulia, alijilaumu kwa kile alichofanya, na upande wa nje, Dokta Smith alikuwa akilia kwa sauti nzito na uchungu mkuu, ngome iligubikwa na machozi...



TTEMBET

Yule bwana akajitupa chini kabisa, nguvu zilikuwa kama zinataka kumuishia, mara akainuka na kutoka nje, akamkuta Dokta Smith akiwa amekaa huku akilia,



"naona umetimiza hadhma yako" Dokta Smith aliongea huku akijifuta machozi, ila yule bwana mswahili alishindwa kujibu, alikuwa akilia tu.



Dokta Smith akainuka taratibu na kuingia ndani ya hema, huku machozi yakiendelea kumtoka, baada ya kuingia ndani, alifungua sanduku lake na kutoa kichupa kidogo sana kilichokuwa na dawa ya maji iliyokuwa na rangi ya ugoro pembeni iliandikwa antibiotic, kisha akamkamulia BQ mdomoni maji ya kile kichupa, alafu akamuondoa shuka mwilini na kumuacha akiwa amelala mtupu.

Alafu akachukua chupa ya maji safi, akaijaza maji aliyoyachanganya na mizizi iliyotwangwa, akamtundikia kama drip, kisha Dokta Smith akatoka nje huku akijifuta machozi, akaenda kukaa na yule mswahili,



"kile kichupa cha sumu ulichotumia kumuua huyo mwanamke umekiweka wapi?" Dokta Smith aliuliza huku akiwa na hasira,



"nisamehe sana rafiki yangu, roho inaniuma sana kufanya kitendo hiki" Mswahili aliongea huku akifuta kamasi kutokana na kilio,



"Ile sumu upo wapi?" Dokta Smith aliuliza kwa kufoka kiasi kwamba mate yakamtoka, lakini yule bwana mswahili hakujibu kitu aliendelea kulia tu.



Dokta Smith akaona kama anadharauliwa vile, akampiga yule bwana mswahili ngumi kali ya kichwani,



"Ile sumu ipo wapi?" Dokta Smith aliuliza kwa hasira huku akimkwida shati,, yule bwana Mswahili akaona ni vyema aitoe ile chupa ya sumu, akaitoa mfukoni na kumpatia Dokta Smith,



"mpumbavu wewe" Dokta Smith aliongea huku akiikwapua ile chupa, kisha akamsukuma yule Bwana Mswahili, kisha Dokta Smith akakifungua kile kichupa, akamkata jicho kali yule Mswahili, kisha akaigida dawa yote iliyokuwa katika kile kichupa. Kuona hivyo yule Mswahili akahamaki, akabaki amepigwa na bumbuwazi,



"unafanya nini wewe?" Mswahili aliuliza huku akijaribu kumpora ile dawa, ila alikuwa amechelewa, alifanikiwa kumpora ila chupa ilikuwa tupu, tayari dawa yote aliinywa Dokta Smith.



Mswahili akapiga hatua moja nyuma na kubaki akishangaa, ghafla Dokta Smith akaanza kupapalika kwa kurusha miguu huku na uko kama anakata roho, kisha akanyooka na kutulia.



Mswahili akajishika kichwa na hasiamini anachokiona, kulia alishindwa, kucheka alishindwa, alibaki mdomo wazi huku nguvu zikimuishia mwilini.



*******************



Sajenti Minja alikuwa yupo kitandani muda huo akimsubiri Tom, bado kichwa chake kilikuwa kikimuwaza yule kijana aitwaye Ray Charles, yaani alikuwa hajielewi kabisa, yaani kwanza alikuwa ahamini maelezo ya habari aliyoisoma mtandaoni kuhusu mtu yule kufa, na pia aliilalazimisha akili yake ijaribu kutofautisha kati ya picha ya mtu yule aliyesoma habari zake kwenye gazeti na mtu yule aliyemvamia siku chache zilizopita, lakini ilishindikana, kwa maana mtu ndiye yule yule mmoja.



Wakati akiwa katika tafakari nzito, alisikia mlango ukigongwa kwa nguvu, akainuka na kuchukua bastola yake, hakuwa akijiamini kabisa, alishamuogopa Ray Charles baada ya kusoma habari zake, alihisi ni mzimu au mtu hasiye wa kawaida.



Sajenti Minja alisogea mlangoni kwa umakini mkubwa, huku nako mgongaji alizidisha nguvu ya kugonga mlango. Sajenti Minja aliufikia mlango na kufungua kwa nguvu, kisha akaelekeza bastola mlangoni,



"we we we bastola hiyo!" Tom aliongea kwa uoga huku akijiziba uso wake kwa mikono, Sajenti Minja akacheka,



"we lazy kweli, yaani unaizuia risasi kwa mkono?" Sajenti Minja aliongea huku akiendelea kucheka,



"mambo gani hayo ya kutishiana bastola hivyo?" Tom aliongea kwa kulalamika huku akiingia ndani,



"sio nakutishia, najihami tu kutokana na kitu nilichokigundua leo" Sajenti Minja aliongea huku akikaa katika kochi,



"ni nini tena?" Tom aliuliza,



"si unakumbuka ule mchoro niliokuonesha siku iliyopita?" Sajenti Minja aliuliza huku akiiweka bastola yake pembeni,



"ndio, si ya yule jamaa aliyekuvamia?" Tom alijibu kwa mtindo wa kuuliza,



"swadakta, ndio huyo huyo" Sajenti Minja alijibu,



"amefanyaje sasa?" Tom aliuliza,



"Yule bwana, ni mtu aliyekufa. Yaani inasemekana amekufa muda mrefu tu" Sajenti Minja aliongea na kumtazama Tom usoni, uso wa Tom ulionekana kutaharuki kabisa,



"sijakuelewa bro" Tom aliongea huku akiwa bado kataharuki,



"ni somo gumu sana kulielewa, ila shika hii simu na uangalie hii habari" Sajenti Minja aliongea huku akimpatia Tom simu yake.



Tom akaanza kuipitia ile habari, alisoma mpaka akaimaliza, akarudia tena, akaisoma mpaka akaimaliza.



"tayari nimeimaliza, sasa hii habari inahusiana vipi na yule jamaa aliyekuvamia?" Tom aliuliza huku akitaka kumrejeshea Sajenti Minja simu,



"umeangalia na picha ya huyo mwanajeshi uliyesoma habari zake?" Sajenti Minja alimuuliza Tom huku akiwa hataki kupokea simu,



"picha zipo kwa wapi?" Tom aliuliza,



"chini kabisa ya hiyo habari" Sajenti Minja alijibu, kisha Tom akashuka mpaka chini katika ile habari, hapo ndipo alipopigwa na butwaa, ni kweli kabisa, picha ya mtu ambaye habari zake inasemekana alikufa, ndiye yule yule Tom aliyemshuhudia nyumbani kwa Sajenti Minja siku chache nyuma.



"hii haiwezekani" Tom aliongea kwa kupaniki,



"ndio imeshawezekana sasa" Sajenti Minja aliongea,



"haya mambo mbona kama ya Sudy Bakari? au amerudi?" Tom aliuliza huku akimuangalia Sajenti Minja,



"sijui, ebu chekecha kichwa ili tupate kitu" Sajenti Minja aliongea kivivu,



"Sasa mimi nitachekechaje kichwa? sijui pa kuanzia" Tom aliongea huku akiitupia kitandani simu ya Sajenti Minja,



"lazy sana wewe, hivi taaluma yako ni nini?" Sajenti Minja aliuliza huku akiinua kichwa chake kumtazama Tom,



"mimi ni muandishi wa habari" Tom alijibu huku akimtazama Sajenti Minja,

"tumia taaluma yako kupata ukweli, usikae kizembe" Sajenti Minja aliongea,



"Sasa mbona sina ajira, nitatumiaje taaluma yangu kupata ukweli? si bora Ningekuwa naandika gazeti au natangaza " Tom alijibu,



"unajua ulimwengu ni kama kijiji? Ebu tafuta maneno ya kujaribu kuchimbua hii habari ya huyu mtu, ukiyapata you jaribu kupost mtandaoni ili tuone ni nini kitafuata" Sajenti Minja alimuelekeza Tom,



"bro hukumbuki kipindi kile nilifanya hivyo kwa lile tukio la waziri wa ulinzi? nilikutana na kashkash nyingi sana. Kwa hiyo bro hilo wazo lako siliungi mikono, naogopa" Tom aliongea,



"wewe fanya kama inawezekana, nakuhakikishia, mimi na vyombo vya usalama tutakuwa nyuma yako" Sajenti Minja aliongea,



"bro usiseme hivyo, mimi najua kwa namna nilivyoteseka" Tom aliongea kwa huruma,



"mbona huniamini wewe, amini mimi nipo nyuma yako" Sajenti Minja alijaribu kumshawishi Tom,



"ujue bro wasiwasi wangu ni kama huyo mtu atajua na mimi nafuatilia mambo yao, ndo hatari itapoanzia, nadhani sasa hivi hana mpango na mimi kwa kuwa anajua simfuatilii" Tom aliongea,



"unakuwa kama mtoto wa kike bwana, watoto wa kiume uwa hatuogopi kupambana Tom" Sajenti Minja aliongea kwa kusihi,



"sawa bro, ngoja nifikirie cha kuandika" Tom aliongea kiunyonge huku akisikitika,



"huo ndio uanaume sasa, basi wewe endelea kufikiria, ngoja nikalete chakula nje" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka kitandani na kuvaa shati yake, kisha akaelekea nje na kumuacha Tom akiwa peke yake ndani.



Tom baada ya kufikiri kwa muda mchache kidogo, akaitoa simu yake mfukoni na kuingia "Facebook" akaenda katika account yake na kuandika "UNAMJUA RAYMOND CHARLES? ASKARI WA TANZANIA ALIYEKUFA MIAKA MITATU ILIYOPITA, ILA AMEONEKANA TENA AKIWA HAI. BAADA YA SIKU MBILI NITAKUJA NA HABARI KAMILI" Tom alindika na kurudia kusoma alichoandika, kisha akapost ule ujumbe, akatoka Facebook.



Baada ya dakika mbili, Sajenti Minja alirudi ndani akiwa na chipsi na soda,



"dogo umeshapata cha kuandika au bado unafikiria?" Sajenti Minja alimuuliza Tom,



"nimeshaandika na kutupia Facebook kama dakika mbili zilizopita" Tom alijibu,



"safi, safi sana, tusubiri majibu" Sajenti Minja aliongea kwa furaha huku akimpa Tom mfukn mmoja uliokuwa na chipsi na soda,



"sasa bro mimi niache niende, hizi chipsi nitaenda kula na shemeji yako" Tom aliongea huku akiinuka katika kiti,



"sawa, we wahi, chukua hii utapanda bajaj" Sajenti Minja aliongea huku akimpa Tom noti ya shilingi elfu kumi, Tom akaipokea na kuiweka mfukoni,



"ngoja nikutoe basi" Sajenti Minja aliongea huku akisimama,



"hapana, hapana, we endelea kula tu" Tom aliongea,



"sio vizuri bwana, ngoja nikufikishe hata hapo mapokezi" Sajenti Minja aliongea kwa kusihi,



"we kula bwana, kwani mimi mgeni bwana?!" Tom aliuliza na Sajenti akabaki anatabasamu,



"usiku mwema basi" Sajenti Minja alimuaga Tom,



"poa bro, na kwako pia" Tom aliongea kisha akaondoka, akatoka nje ya geti la hotel, na kuingia barabarani, safari ya kurudi kwake ilianza usiku ule, hakuchukua bajaj, aliamua atembee tu kwa kuwa hakuwa na haraka ya kuwahi kurudi.



***************



Mida Ile ile ya usiku, anaonekana Ray Charles akiwa ameegesha gari yake nyeusi pembezoni mwa barabara, na upande wa pili wa barabara kulikuwa na nyumba nzuri ya Kisasa yenye geti jeusi.



Ray Charles alikuwa akiitazama ile nyumba huku akionekana ana huzuni, alipeleka mkono wake katika picha ndogo aliyoibandika katika kioo cha gari yake, akaipapasa ile picha ambayo alionekana yeye akiwa na mwanamke mrembo, pamoja na mtoto wa kiume wa miaka minne.



Ray aliipapasa ile picha huku akiuma meno yake kwa hisia kali, wakati akiendelea kuwa katika hali hiyo, alishuhudia gari ikasimama mbele ya ile nyumba, kisha akatelemka yule mwanamke mrembo aliyekuwa katika picha ya Ray Charles, baada ya hapo yule mwanamke akasogea mlango wa nyuma na kumchukua mtoto, ambaye huyo mtoto nae yupo katika picha ya Ray Charles. Kisha ile gari ikaondoka, yule mwanamke akagonga geti, mlango ukafunguliwa, yule mwanamke akaingia ndani, Ray Charles akatabasamu, ila tabasamu halikubeba furaha.



Simu yake ikaanza kuita, akaiangalia na kupokea,.

"naam mheshimiwa" Ray Charles aliongea baada ya kupokea simu,



"wewe umeona habari zinazozagaa mitandaoni muda huu?" Rais aliuliza kwa ukali,



"hapana mheshimiwa" Ray Charles alijibu huku akijiuliza ni habari gani?



"Kuna mpumbavu mmoja amepost habari zako Facebook, na watu wengi wameonekana kuvutiwa na habari, ile, ebu ingia uitafute hiyo habari, aliyepost anaitwa Thomas Anthony" Rais aliongea na kukata simu, Ray Charles akaingia mtandaoni na kutafuta jina aliloambiwa, kweli akaikuta ile habari, akaipitia muda mfupi tu, kisha akabonyeza katika jina la huyo aliyeandika habari, shida yake ilikuwa kuiona picha tu ya huyo aliyeandika hiyo habari. Alipofungua picha, akakutana na picha za Tom, Ray Charles akatabasamu kwa hasira, maana huyu mtu anamjua, na kipindi hicho simu yake ilikuwa ikiita, aliyepiga alikuwa Rais.



"umeshaiona hiyo habari?" Rais aliuliza baada ya ray Charles kupokea simu,.

"ndio mkuu" Ray Charles alijibu,



"huyo mtu mtafute siku mbili kabla hajapost habari kamili, na umuue" Rais aliongea kwa mamlaka,



"sawa mkuu, huyu atapatikana leo hii hii" Ray charles alijibu,



"unamjua?! " Rais aliuliza,



"ndio, ni rafiki yake na yule Askari amayefuatilia kesi ya yule dada niliyemuua baharini" Ray Charles alijibu,



"basi uwa, uwa wote" Rais aliongea na kukata simu.



***********



Tom aliendelea kukata mitaa usiku ule. Akaona kama ataendelea kufuata barabara atachelewa vile, alichoamua ni kuingia njia za vichororoni. Alipita kichochoro cha kwanza, kikafuata cha pili, ila kichochoro cha tatu alipofika, alihisi kuna mtu alikuwa akija huku akikimbia, Tom akataka kujikaza asimame, ila akakumbuka mkaa huo una vibaka sana, Tom akaamua akimbie tu. Tom alipoanza kukimbia, yule mtu akaongeza kasi, Tom akakunja kona, yule mtu nae akamfuata huko huko, Tom alikimbia dakika tano tu, akachoka, akaamua asimame huku akihema kwa nguvu, vichomi vilimshika,



"sina hela, nina simu tu, hii hapa" Tom aliongea huku akihema, alishaamini huyo anayemkimbiza ni kibaka. Yule mtu akaichukua ile simu, kisha akaiwasha huku sura yake ikiwa karibu na kile kioo, hapo Tom ndipo aliiona vizuri sura ya yule mtu, alikuwa ni Ray Charles, Tom akashtuka, akaanza kukimbia tena, ila alishangaa akipigwa risasi ya bega na kutupwa chini, Tom akaanguka chali huku akihisi maumivu makali sana begani,



"wewe ndiye unayejifanya unanijua sana?" Ray Charles aliuliza huku akiwa ameelekeza mdomo wa bastola katika kichwa cha Tom,



"nisamehe, mimi nilitumwa tu" Tom aliongea huku akilia, na pembeni ya kichwa chake kulikuwa na mfuko chipsi uliopasuka baada ya kuutupa chini,



"msamaha utasaidia nini kwa jambo ambalo limeshasambaa nchi nzima?" Ray Charles aliuliza huku akiikoki bastola yake, Tom mkojo ukamtoka, Ray Charles akaruhusu risasi usawa wa kichwa cha Tom, Tom akakumbwa na giza nene kichwani, hakuona kitu tena, hisia zake hazikuwa tena duniani, mwili wake ulilegea na hakutambua tena kitu chochote kinachoendelea duniani......



Wakati Ray Charles akitenda unyama huo wa kutisha dhidi ya Tom, upande mwingine Sajenti Minja alikuwa yupo juu ya kitanda cha hoteli huku akipitia pitia ujumbe tofauti unaotumwa na wachangiaji katika post ya Tom aliyoiandika Facebook muda mchache uliopita, kitu alichokuwa anakifanya Sajenti Minja ni kumtafuta mtu mwenye comment ambayo inaweza kumpa mwanga juu ya mtu wa kuitwa ray Charles,



"hakuna hata anayejua habari zake humu, ngoja kesho kukicha, huenda tukampata mtu ambaye anaweza kunipa mwanga kiasi" Sajenti Minja aliongea huku akiiweka simu yake katika stuli iliyokuwa pembeni ya kitanda, kisha akavuta shuka na kujifunika



Kitu ambacho hakujua Sajenti Minja, ni kuwa tayari ile post Tom ilishazalisha matatizo, na kingine ambacho hakujua ni kuwa tayari muda huo Tom hakuwepo duniani.



*******************



Uko msituni, mswahili alikuwa hajui afanye nini, ilikuwa ni nusu saa tangu Dokta Smith anyooke chini, sasa mswahili akaona huo ni msala, yaani watu wawili wamekufa kwa wakati mmoja? akaona njia nzuri ya kujinasua katika msala huo, ni kubeba vitu vyake tu na kuondoka msituni hapo.



Mswahili akaingia ndani ya hema, cha ajabu akakuta BQ ametundikiwa drip, akashangaa, akamsogelea kwa karibu, kwa pembeni ya BQ kulikuwa na kile kichupa cha antibiotic ambacho Dokta Smith alimpa BQ.



Mswahili akakiokota kile kichupa na kutoka nje huku akiwa amekishika, lengo lake lilikuwa ni kwenda kumnywesha Dokta Smith, ila yule Mswahili alipotoka tu, alipigwa na butwaa nyingine, alikuta Dokta Smith akiwa anasimama, Bwana Mswahili akabaki amesimama na kumtolea macho Dokta Smith,



"Dokta Smith" Mswahili aliita,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"niletee maji ya kunywa" Dokta Smith aliongea huku akijikung'uta vumbi,



"mbona hujafa Dokta Smith?" Mswahili aliuliza huku bado akiwa amepigwa na butwaa,



"niletee maji mshenzi wewe" Dokta Smith aliongea kwa hasira huku akikaa katika jiwe,



"Mungu ni mwema" Mswahili aliongea kwa upole huku akielekea ndani, akatoka na maji katika kidumu cha lita tano, akampa Dokta Smith, Dokta Smith akakipokea kile kidumu na kuanza kugida maji, alikunywa maji mengi sana, kama lita mbili kwa wakati mmoja, kisha akashusha kile kidumu, akaanza kuhema haraka haraka,



"pale pembeni ya yule mwanamke pale ndani, kuna kichupa kidogo cha antibiotic, niletee" Dokta Smith aliongea huku akimtazama Mswahili,



"ninacho hapa" Mswahili aliongea huku akimpatia kile kichupa Dokta Smith, Dokta Smith akakipokea na kujikamulia mdomoni, kisha akakiangalia na kugundua kishakikamua mpaka kimeisha, akakitupa,



"eti jamaa, mbona umekunywa sumu na hujafa?" Mswahili aliuliza huku akikaa chini,



"kabla sijakujibu, napenda kusema wewe sio mtu mwema, na hupaswi kufuatana na daktari kama mimi" Dokta Smith aliongea na kutema mate,



"lakini jamaa hamjui tu huyu dada, lahiti ungemjua, usingethubutu kuishi nae, ni bora ukae chumba kimoja na chui kuliko huyo mwanamke" Mswahili aliongea,



"wewe una roho mbaya kuliko yeye, yaani ulijaribu kumuua mara ya kwanza kwa kumpa kile kichupa kilichoandikwa "poison" ila ulishindwa, hilo nililijua, na ndio maana leo nikakupeleka msituni na kukuelekeza namna ya kuifanya dawa ya katika kile kichupa iwe sumu, nilijua ulikuwa na lengo gani, na hata ulivyonitiroka msituni, nilijua ulichokuja kukifanya huku, nikasubiri hili hadhma yako itimie, na kweli umetimiza hadhma yako, umemnywesha" Dokta Smith akanyamaza na kuchukua kile kidumu cha maji, akagida na kukiweka tena chini, muda huo yule bwana Mswahili machozi yalikuwa yakimtoka tu.



"Ile ni sumu kweli, ila ni sumu inayotegemea mzunguko wa damu, kwa kiumbe kidogo kama kuku, kima na wengineo wadogo wadogo, hummchukua muda mchache tu kufa baada ya kuchomwa sindano yenye ile sumu, ila kwa mwanadamu na viumbe wengine wakubwa, huchukua siku tano ndipo kifo hufuata" Dokta Smith aliongea na kumeza mate,



"kwa hiyo baada ya siku tano wewe ndo unakuja?" Mswahili aliuliza kwa masikitiko,



"subiri bwege wewe, bado sijamaliza kuongea. Ukinywa hiyo sumu na ukawahi kunywa hii antibiotic niliyokunywa, basi hapo utakuwa umefanikiwa kujiepusha na kifo, na hii antibiotic unatakiwa uinywe ndani ya masaa ishirini na nne baada ya kunywa sumu, ukichelewa zaidi to hapo, ujue lazima ufe" Dokta Smith aliongea,



"afadhali, bora umewahi kuinywa hiyo antibiotic" Mswahili aliongea huku akitabasamu na kumfanya Dokta Smith amuangalie kwa sekunde chache, kisha akawa anatafakari,



"ila ndugu yangu, nimetafakari sana, nimeona ni bora mimi na wewe tusiendelee kuwa tena pamoja, huna roho ya hutu, sikuwahi kufikiria kuwa itakuja siku utakuwa na roho ya namna hii" Dokta Smith aliongea kwa sauti tulivu,



"hapana jamaa yangu, nimeshajutia makosa yangu, na pia huyu mwanamke alishawahi kufanya ukatili mkubwa ambao nimewahi kuhushihudia, pia huyu mwanamke na wenzake, wameshawahi kuninyima uhuru kwa sababu ya vitisho nk, na kwa sababu yao hao, nilifungwa jela" Mswahili aliongea kwa upole,



"kwa hiyo ukaona njia sahihi ni kumuua?"Dokta Smith aliuliza,



"ndio, ila kwa sasa sioni sababu ya kumuua, nimeamua kukusaidia kumrejesha katika hali yake" Mswahili aliongea,



"bado siyaamini maneno yako, yaani huaminiki kabisa" Dokta Smith aliongea huku akiinuka,



"naomba uniamini, alafu kama ningekuwa na nia thabiti ya kumuua, si ningemuua tu, humu ndani si Kuna ile bunduki ya kuulia wanyama, si ningetumia hiyo kwa ajili ya kumuua?" Mswahili aliuliza huku akimtazama Dokta Smith,



"uko ni kujitetea tu, ila wewe sio mtu kabisa" Dokta Smith aliongea,



"kuonesha nimedhamilia kumsaidia huyu dada, kesho nitaenda mjini kununua mahitaji ya hapa, alafu nitatafuta dawa za kisasa zaidi kwa ajili yake" Mswahili aliongea,



"utanikumbusha pia nikupe hela ukaniletee kemikali fulani kwa ajili ya kuchanganyia dawa" Dokta Smith aliongea na kuingia ndani, akamkuta BQ akiwa bado yupo katika hali yake ile ile. Dokta Smith akachukua shuka na kumfunika, kisha na yeye akaelekea pembeni ya hema na kulala, kwa upande wa nje, Mswahili alikuwa akitabasamu, tabasamu la mshangao, kwanini yule mwanamke hafi?



"sikati tamaa, lazima tu nimuondoe" Mswahili aliongea huku akisogeza mafiga ya jiko yakae vizuri.



************



Sajenti kama kawaida yake, uwa anachelewa sana kuamka kipindi anapokuwa hana sababu ya kuwahi kuamka. Sajenti Minja alipoamka, alichukua simu yake na kukuta Kuna "missed call" sipatazo saba, tena zilikuwa za namba moja ambayo ni ngeni kwa Sajenti Minja. Sajenti Minja akaipuuza na kuamua kuingia Facebook ili akaangalie labda Kuna kitu chochote kimeongezeka katika post ya Tom, akakuta ile post haipo, yaani imefutwa, Sajenti Minja akatoa macho,



"Tom muoga muoga sana, sasa kwanini ameifuta?" Sajenti Minja alijiuliza huku akiitafuta namba ya Tom katika simu yake, akaipata, akapiga, simu akaweka sikioni, ila akakutana na sauti ya kike ikimtaharifu kuwa simu anayopiga kwa sasa haipatikani, akakiangalia kioo cha simu yake, akarudia tena kupiga namba ile ile ya Tom, ila ujumbe aliokutana nao ni ule ule,



"kazima simu, huyu mtoto mpumbavu sana" Sajenti Minja aliongea peke yake huku akiinuka kitandani, kisha akaingia bafuni na kujisafisha mwili.



Alipotoka bafuni, alivaa nguo na kujitupa katoka kochi, na kuwasha runinga, ila akakumbuka kuna missed call ya namba ngeni katika simu yake, akaichukua na kukuta tena ile namba imemtafuta tena dakika mbili zilizopita, Sajenti Minja akaamua kupiga ile namba, simu ikaanza kuita,



"hallow" ilikuwa sauti laini ya kike,



"eee, habari" Sajenti Minja alisalimia,.



"nzuri, eti kaka upo na Tom uko?" Dada yule aliuliza,



"mhm hapana, kwani vipi?" Sajenti Minja aliuliza,



"Tom ni mchumba wangu, jana usiku wakati anatoka hapa, aliniaga anakuja kwako, wewe si ndio polisi Minja?" Dada aliuliza,



"ndio, ni mimi" Sajenti Minja alijibu huku wasiwasi ukimuingia,



"Sasa tangu jana amesema anakuja kwako, hajarudi mpaka muda huu. nilikupigia simu usiku ila hukupokea" Dada aliongea kwa sauti yake ya upole, ila Sajenti Minja alizidi tu kupata wasiwasi,



"hallow" Dada aliongea na kumtoa Sajenti Minja katika dimbwi la mawazo,



"upo wapi kwanza?" Sajenti Minja alimuuliza mchumba wake Tom,



"nipo nyumbani" Mchumba wake Tom alijibu,



"ok, nakuja, nakuja ingawa mtaa naujua ila nyumba siijui, nikifika ntakupigia simu unielekeze" Sajenti Minja aliongea,



"lakini hujaniambia kama upo na Tom au haupo nae?" Mchumba wake Tom aliuliza,



"nakuja, tutaongea vuzuri" Sajenti Minja aliongea,



"sawa, ila unanitisha" Mchumba wa Tom aliongea kwa uoga,



"usipate wasiwasi, nakuja" Sajenti Minja aliongea kisha mchumba wa Tom akakata simu,



"mhmmmm" Sajenti Minja aliguna, kisha akaipiga tena namba ya Tom, ila bado haikupatikana, akaamua atoke, hakupanga kwenda kwa mchumba wa Tom, aliamua aende kazini, tayari kichwa chake kilihisi huenda Tom amekutwa na jambo baya.



****************



Siku nyingine tena, yule Mswahili alikuwa mjini, hakwenda kwa lengo la kununua vitu vilivyokwisha, alikwenda kwa nia ya kutoa taarifa za BQ, hakuwa anajua kama BQ anatafutwa kwa muda huo.



"mbona Minja haipatikani tena?" Mswahili aliongea huku simu yake ikiwa sikioni, alijaribu tena na tena lakini wapi. Akaweka simu mfukoni na kwenda kununua gazeti la siasa, maana muda mrefu kidogo hakuja mjini, kwa hiyo hajui mambo mengi yaliyojili nchini. Katoka pita pita zake kusoma habari gazetini, atakutana na makala inayozungumzia mwanamke aliyefanya mauaji kwa viongozi kadhaa wa serikali, kwa jinsi mwanamke huyo alivyoelezewa, ni wazi kabisa alikuwa ni BQ. Mswahili sasa akashtuka, akaamua aende kituo cha polisi cha karibu, akawapa taarifa juu ya wapi mwanamke huyo anapatikana.



Wakaondoka Askari arobaini, maana walishapewa habari kuwa huyo Dada hafai, na hata yule Mswahili alipowaambia kuwa yule dada kule msituni hana fahamu, bado Askari walitaka kwenda vile vile wengi, na kumi kati yao wakabeba silaha za moto, safari ya msituni ikaanza, wakamuacha mkuu wao wa kituo akiwasiliana na makao makuu ya polisi kwa ajili ya kuwapa taarifa hizo njema za kupatikana kwa BQ.



**************



Ndani ya msitu, Dokta Smith alikuwa bize akiendelea kuchimba mizizi kwa ajili ya utafiti wake wa madawa, aliona kwa mbali kundi la askari likija, alidhani ni Askari wa msituni wanaendelea na doria zao, hakuwa na wasiwasi kwa maana alikuwa na vibali vya kuendelea kufanya utafiti katika eneo hilo la msitu.



Dokta Smith akaendelea kuchimba dawa, ila sasa vishindo vya miguu ya Askari wale, vilikuwa nyuma yake, akageuka, akakuta kundi kubwa la Askari wakiwa na silaha, na mbele alikuwepo bwana Mswahili akimtazama,



"huyu ndio mwenzangu, mimi na yeye ndio tulimuokota yule dada, na huyu rafiki yangu ni daktari, ndio anaangaika kumtibu" Mswahili aliongea huku akiwa amemshika bega Dokta Smith, mpaka kufikia hapo sasa, Dokta Smith alianza kuhisi ni nini kinaendelea, akatingisha kichwa kusikitika,



"Kweli umedhamiria, kweli wewe una roho, roho ya ajabu" Dokta Smith aliongea kwa masikitiko,



"hakuna haja ya kuendelea kumlinda muarifu, akamatwe tu" Mswahili aliongea kwa sauti tulivu,



"katika hali ile aliyonayo, anaenda kufa tu" Dokta Smith aliongea huku akiikusanya mizizi, kisha akawa anaelekea upande mwingine,



"ndio uko anapoenda huyo?" Askari mmoja alimuuliza yule bwana mswahili,



"hapana, ni huku" Mswahili alijibu huku akishika njia iendayo katika hema lao,



"wewe mzungu, hutakiwi kuondoka, upo chini ya ulinzi, maana ulichokuwa unafanya ni kumuhifadhi muarifu na ukijua kabisa ni kosa kufanya hivyo" Askari aliongea huku akimvuta Dokta Smith,



"ndio yamekuwa haya tena?" Dokta Smith aliuliza kwa mshangao,



"sitisha kila kitu, unatakiwa uambatane na sisi" Askari aliongea, Dokta Smith akatii amri, safari ya karudi katika cage wanayoishi Dokta Smith na Mswahili ikaanza,. Njia nzima ukimya ulitawala, wakafika nje ya cage na kufungua kufuri kubwa iliyokuwepo mlangoni, kisha wote wakaingia, wakawa wanaelekea katika hema, polisi wenye silaha wakatangulia mbele, wale wasio na silaha walilizunguka hema kwa nje kwa ajili ya kulinda usalama, kisha Mswahili akafungua mlango na kuchungulia ndani,



"Yupo?" Askari mmoja mwenye silaha aliuliza,



"ndio, ataenda wapi wakati hajitambui?" Mswahili alijibu huku akitoa kichwa nje, usoni alikuwa na tabasamu tamu la ushindi, Dokta Smith alisikitika huku akimuangalia yule bwana mswahili kwa jicho la hasira.....



"Pisha sasa" Askari mmoja aliongea huku akiingia ndani ya hema kwa fujo na kumpiga kikumbo bwana mswahili na kumfanya apepesuke.



Askari wengine wenye bunduki wakaingia ndani, ila wote walishangaa kukiwa na damu nyingi katika eneo ambalo BQ alikuwa amelala,



"mbona hamna mtu sasa, ni shuka tu" Askari mmoja aliongea huku akimtazama yule bwana mswahili aliyekuwa amesimama mlangoni, ikambidi yule bwana Mswahili aingie ndani, akasogelea mpaka pale alipolazwa BQ, akakuta kweli hakuna mtu,



"nilipokuwa mlangoni sikuona, nilipoona haya mashuka nikajua yupo tu, kwa maana ni mtu ambaye amepoteza fahamu" Mswahili aliongea,



"Sasa kama amepoteza fahamu, ameondokaje?" Askari mmoja alimuuliza yule bwana Mswahili,



"eti Dokta Smith, wewe si ndio nilikuacha naye hapa, umempeleka wapi?" Mswahili aliuliza huku akimtazama Dokta Smith,



"mimi mwenyewe nilimuacha hapa, nikaingia msituni, kwa hiyo sijui chochote" Dokta Smith alijibu huku akishangaa hilo tukio,



"ebu njooni muone huku" Askari mmoja alifunua hema kwa nyuma na kuwaita wenzake, tena hiyo sehemu alipofunulia hema, kuliona kumechanwa.



Askari wengine pamoja na bwana mswahili, na Dokta Smith wakaenda kuangalia uko walipoitwa, wakakuta Kuna michilizi ya damu iliyoelekea kwenye uzio wa cage yao, kisha Ile michilizi iliendelea nyuma ya cage na ilionesha imeelekea porini. Dokta Smith akashtuka,



"inawezekana kuna mnyama ameingia humu na kumbeba yule dada" Dokta Smith aliongea huku akionesha kuguswa sana na hilo tukio,



"usilete ujanja hapa, kama wanyama wangekuwa wanaingia katika hii cage si mngekuwa mmeliwa siku nyingi tu? Hii kesi ni yako mzee, wewe utakuwa umemtorosha tu huyo dada" Askari aliongea huku akimkata jicho Dokta Smith,



"huenda kweli, kwa maana chui uwa wanaingia ingia sana humu, ila uwa tunawadhibiti. Kwa hali ya yule mwanamke, ni ngumu kupanda hapo na kushukia upande wa pili" Mswahili aliongea,



"ebu twendeni tuifuatilie hiyo michilizi ya damu?" Askari kiongozi aliongea, kisha wote wakatoka nje ya cage na kuanza kuifuatilia ile michirizi. Walitembea kwa mwendo mrefu kidogo, mpaka katikati ya msitu, ila hawakufanikiwa kugundua kitu chochote, mwisho wa siku wakakata tamaa,



"Sasa wewe mzungu ni lazima uwe mshukiwa wa kwanza wa hii kesi" Askari kiongozi aliongea huku akimgeukia Dokta Smith,



"sawa" Dokta Smith aliongea kwa sauti tulivu,



"mfunge pingu" Askari yule akatoa amri kwa wenzake, kisha Askari mwingine akatoa pingu kiunoni na kumsogelea Dokta Smith, Dokta Smith akanyoosha mikono mbele, Askari akamfunga pingu.



"mngeamuacha tu, mimi sioni kama Kuna kosa tena, maana mwanamke mwenyewe ameshaliwa na wanyama" Mswahili aliongea kwa lengo la kumtetea Dokta Smith,



"kaliwa na wanyama? huo ushahidi unao?" Askari kiongozi aliuliza huku akimuangalia Mswahili,



"si wote tumejionea hali ilivyo ingawa mwili wake hatujauona" Mswahili aliongea,



"mfunge na huyu pingu, hawa wote lao moja, haiwezekani wakae na mtuhumiwa muda mrefu hivyo, alafu leo ndio aje kutoa taarifa" Askari yule yule aliyeonekana kuwaongoza wenzake, aliongea na kumfanya yule bwana mswahili atoe macho,

"mimi ni msamalia jamani, au mmesahau?" Mswahili aliongea huku akishangaa,



"kwa hiyo wewe umetokea Israel?" Askari kiongozi alimuhoji yule Mswahili,



"sijaelewa swali lako, unamaanisha nini?" Mswahili aliuliza,



"wewe si umesema wewe ni msamalia?" Askari kiongozi aliuliza huku akimsogelea yule bwana mswahili,



"ndio" Mswahili alijibu,



"Sasa hujui kuwa wasamalia ni makabila ya Israel, waliishi uko miaka mia saba na upuuzi kabla ya ujio wa yesu?" Askari kiongozi aliongea na kumfanya bwana mswahili atabasamu, akashtukia anapigwa kofi kali la shavu,.



"unamcheka afande sio?" Askari kiongozi aliuliza huku akimuangalia Mswahili aliyekuwa anasugua shavu lake kwa maumivu, kwa wakati huo Dokta Smith alikuwa akiangalia namna mwenzake anavyoteseka,



"funga pingu huyu, mbona mnachelewa?" Askari kiongozi aliwaambia wenzake huku yeye akisonga mbele na kumuacha Mswahili akiwa ahamini kinachotokea eneo hilo, hapo ndipo akaanza kujuta.



"Mchimba kisima, huingia mwenyewe" Dokta Smith aliongea kwa sauti ndogo wakati akipita jirani na bwana Mswahili, na kumfanya bwana yule Mswahili aangalie pembeni kwa aibu.



*****************



Anaonekana Ray Charles akiwa na soda mkononi, alikuwa akiingia katika sehemu ya kararakana yake.



Alipita mpaka katika kile chumba chake kidogo, na kwenda kusimama mbele ya kioo, akajiangalia katika kile kioo, kisha ghafla sura yake ikajenga huzuni, akatazama chini, hakuwa na moyo tena wa kuangalia taswira yake kupitia kioo. Wakati hayo yakiendelea, alisikia mtu akipiga kelele upande wa chini katika karakana, Ray Charles akaamua aelekee upande huo, kulikuwa na mlango wa chuma, akafungua na kuingia ndani, ndani alikuwepo Tom, Tom alipomuona Ray Charles, Tom akarudi nyuma na kuegemea ukuta,



"umezinduka ee?" Ray Charles alimuuliza Tom huku akikaa katika kiti kidogo kilichopo humo ndani. ila kwa upande wa Tom bado alikuwa anajiuliza imekuwaje kuwaje hajafa na alipigwa risasi ya kichwa, wakati akijiuliza hayo, tayari mkono wake ulikuwa ukipapasa kichwa kuangalia kama kuna majeraha, maana fahamu zimemrudia muda si mrefu.



"sikukupiga risasi, nilipiga chini, nadhani ulipoteza fahamu kutokana na mshtuko" Ray Charles aliongea huku akimrushia soda Tom, Tom hakuiokota, aliogopa kabisa, kwa maana hakujua yupo wapi, alichojua ni kuwa yupo na mtu mbaya tu, tena ametekwa na mtu huyo.



"mimi sio mtu mbaya, kama jana ningekuwa mtu mbaya, ningekumaliza pale pale kichochoroni" Ray Charles aliongea na kuinyoosha shingo yake, Tom akasikia namna mifupa ya Ray Charles inavyonyooka kwa kutoa ukelele.



"mpaka dakika nimeamua nikupe nafasi moja ya kuishi, ila ili uishi, itabidi useme ukweli, ukweli kuhusu zile habari ulipost Facebook, ni wapi umezipata?" Ray Charles aliongea na kumtazama Tom aliyejifanya kama haelewi alichoulizwa, na badala yake alijifanya anageuza shingo kila upande wa kila chumba, yaani kama anashangaa mazingira ya mule ndani.

Wakati Tom akiendelea kujifanya hamnazo, alihisi kitu kikitua kwa nguvu katika mbavu zake, yakafuatia maumivu makali mno, mpaka machozi yakamtoka,



"unajifanya husikii sio?" Ray Charles aliuliza baada ya kumrushia Tom kiti ambacho yeye Ray Charles alikuwa amekikalia hawali.



"sioni tabu kukuua, lakini kama nitakuua, itakuwa umetaka wewe, mimi nataka kumuua aliyekupa habari zangu" Ray Charles aliongea huku akiwa anamsogelea Tom taratibu, Tom akaona kweli huenda atateseka sana, na alivyo mlaini, anaweza kufa kabisa,



"subiri kaka, rudi nyuma nikuambie ukweli" Tom aliongea huku akiinama na mikono yake bado ilishikilia mbavu za kushoto. Kwa kauli hiyo ya Tom, Ray Charles akasimama,



"haya sema" Ray Charles aliongea huku akimtazama Tom aliyeinama,



"ni kweli nilitumwa kufanya hivyo" Tom aliongea kwa maumivu,



"na nani?" Ray Charles alihoji,



"Sajenti Minja" Tom aliongea na kukaa chini kabisa,



"yeye anajua habari zangu? au ni kipi kinamfanya anichunguze?" Ray Charles aliuliza,



"hajui kitu, alikuwa anataka kukuchunguza baada ya wewe kumuua yule dada mlemavu aliyekuwa anatakiwa na polisi,



"na jina langu alilijuaje?" Ray Charles aliuliza huku akiokota kiti na kukalia,



"Kuna habari yako ile inayosema uliuawa somalia, aliipata mtandaoni" Tom alijibu na kumtazama Ray Charles ambaye sura yake ilibadilika na kuwa na huzuni wa ghafla,



"Leo hii unaweza kunikutanisha na Sajenti Minja?" Ray Charles aliuliza huku akimtazama Tom,



"siwezi, kwa maana najua lengo lako ni kumuua" Tom aliongea,



"nitakuua ujue?!, sitaki ulete ubishi ninapokuhoji" Ray Charles aliongea kwa utulivu,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"siwezi kusema kwa kweli, unataka kuniua? niue tu" Tom aliongea maneno ya kishujaa, Ray Charles akainuka kwa hasira na kumsogelea Tom, kisha akamrushia ngumi kali kuelekea katika kichwa cha Tom, Tom akainama na kuweka mikono kichwani, lakini Ray Charles akakwepesha ngumi yake na kupiga ukuta, mpaka tofali likamomonyoka,



"sihitaji nikuue kwa ngumi, maana utakufa haraka haraka sana" Ray Charles aliongea kisha akambeba Tom mzima mzima na kumpigiza chini kwa nguvu, Tom akatoa ukelele wa maumivu, lakini Ray Charles hakuonekuonekana kujali, akaendelea na zoezi lake hilo kwa kurudia mara kadhaa, mwisho Tom akashindwa kustahimili, macho yakakosa nguvu, ubongo ukagoma kufanya kazi, Tom akapoteza fahamu tena huku damu zikimtoka puani na mdomoni kutokana na kipigo alichokipata.



***************



Tom alikuja kufungua macho baada ya masaa mengi mbele, akajitahidi kufungua macho, akafanikiwa, ila akajikuta yupo eneo tofauti na alipokuwa hawali, safari hii alijikuta yupo umbali mfupi kutoka barabarani, na kilichomjulisha hayo, ni kusikia sauti za magari yakipita kila muda. Tom akajinyoosha na kuinuka, akahisi simu yake ikiita mfukoni, akashangaa, maana simu alinyang'anywa na zilizimwa na Ray Charles, sasa imekuwaje ajikute na simu zake na zote zimewashwa,



"huenda ameniachia, alijua nimekufa" Tom aliongea, ila kitu ambacho hakujua, ni kuwa huo ulikuwa mtego, Ray Charles hakuwa mbali, alikuwa amejificha sehemu akimuangalia Tom. Ray Charles alihisi fika kuwa endapo Tom ataamka, mtu wa kwanza kumjulisha alipo ni Sajenti Minja, na kweli hicho ndicho kilichotokea.



Tom baada ya kuitoa simu yake mfukoni, alikuta anayepiga ni Sajenti Minja, Tom akapokea haraka simu,



"Tom upo wapi?" Sajenti Minja aliuliza Tom alipopokea simu,



"bro nilitekwa, nimepigwa vibaya sana, kidogo nife" Tom aliongea huku akianza kulia,



"upo wapi? jibu basi" Sajenti Minja aliuliza kwa kufoka,



"ebu ngoja nifike barabarani, nitakujulisha nilipo" Tom aliongea huku akijivuta barabarani, Sajenti Minja hakutaka kukata simu,.

"nipo njia panda ya mizinde" Tom aliongea huku akiwa amesimama kando kando ya barabara



,"Nisubiri hapo hapo, nakuja sasa hivi" Sajenti Minja alijibu na kukata simu, kisha Tom akaanza kujikagua sehemu zenye maumivu.



Kipindi chote hicho Ray Charles alikuwa akimfuatilia kwa mbali tu. Na sasa alianza kujisogeza baada ya kuhisi Tom anasuburi bajaj au bodaboda, akaona bora asikae mbali nae, wakati akijisogeza, simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kuangalia jina la mpigaji, alikuwa ni Rais,



"vipi umefanikisha mtego wako?" Rais aliuliza,.

"nipo hapa, bado namfuatilia, nadhani anangoja usafiri, kwa maana namuona kwa mbali" Ray Charles alijibu,



"kama atakuja huyo Sajenti Minja, hakikisha unamuua hapo hapo, kama hatokuja huyo Sajenti Minja, basi huyo kijana mmalize kabla hajachukua usafiri mwingine" Rais alitoa maagizo,



"sawa mkuu" Ray Charles alijibu kisha akakata simu, kisha akawa anafuatilia mwenendo wa Tom.



Tom aliendelea kukaa pale akimsubiri Sajenti Minja. Baada ya nusu saa, gari ya Sajenti Minja ilisimama alipokuwa amesimama Tom, kisha Sajenti Minja akashuka na kumsogelea Tom, akashangaa kwa namna Tom alivyochakaa vibaya,



"pole, ebu tuingie kwenye gari tuwahi hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akimshika Tom na kumsaidia kuingia katika gari, kisha na yeye akazunguka upande wa pili wa dereva na kuingia, kisha akawasha gari, alipotaka kuiondoa tu, alishuhudia mtu akiwa amesimama mbele ya gari, na mkononi alikuwa na bastola, alimuelekezea Sajenti Minja,



"huu ni mtego" Tom aliongea huku akiwa kakata tamaa,



"Ray Charles" Sajenti Minja aliongea huku akiwa amepigwa na butwaa, wakati Sajenti Minja na Tom wakiwa katika hali hiyo ya mashaka, Ray Charles yeye alikuwa akitabasamu, na muda huo alikuwa anafyatua risasi kumuelekea Sajenti Minja, Sajenti Minja alifunga tu macho, maana katika kumbukumbu zake za mafunzo ya kikomando, hakukumbuka kama aliwahi kufundishwa kuikwepa risasi iliyopigwa kwa ukaribu wa namna hiyo.........



Tom alichofanya ni kumvuta Sajenti Minja upande wake, wakasikia kioo cha gari kikipasuka kutokana na risasi kukipiga kioo kile,



"ondoa gari" Tom aliongea kwa sauti kubwa na kumfanya Sajenti Minja ainue shingo kidogo ili aione barabara, kisha akaondoa gari kwa kasi na kumgonga Ray Charles, Ray Charles akatupwa mbele ya gari kisha Sajenti Minja akaenda kumkanyaga kabisa, yaani alipitisha gari juu ya mwili wa Ray Charles, kisha Sajenti Minja akasimamisha gari na kumuangalia Ray Charles kupitia kioo cha ubavuni mwa gari (side mirror), Tom yeye alitoa shingo kuangalia kabisa,



"nimeua shahidi" Sajenti Minja aliongea kwa masikitiko, ghafla akashangaa Ray Charles ameinuka, kisha akaangaza macho kulia na kushoto, akaokota bastola yake, akawa anakimbia kuifuata gari waliyokuwepo wakina Tom na Sajenti Minja,



"ondoa gari" Tom aliongea na kisha Sajenti Minja akakanyaga mafuta na kufanya gari iondoke kwa kasi sana, huku ikisindikizwa na risasi kadhaa zilizokuwa zikirushwa na Ray Charles.



Ray Charles akasimama na kuiangalia kwa uchungu ile gari ikipotea machoni mwake, na kipindi hicho watu wachache na magari yalikuwa yamesimama yakifuatilia tukio lile. Ray Charles akatazama kushoto na kulia, kisha akaondoka mpaka mahali alipoficha gari yake, akaiwasha na kuondoka, huku akiwaza namna alivyozidiwa ujanja na Sajenti Minja na Tom.



Akawasha gari na kuliondoa kwa kasi kuelekea upande ule walipoelekea wakina Sajenti Minja, njiani akatoa simu na kumpigia simu Rais,



"hallow mheshimiwa" Ray Charles aliongea mara baada ya simu kupokelewa,



"sema Ray, mtego wako umefanikiwa?" Rais aliuliza,



"hapana, wamefanikiwa kutoroka, nipo najaribu kuwafuatilia kama nitawapata" Ray Charles alijibu,



"Ray umekuwaje? mbona siku hizi umekuwa mzembe hivyo? unawaza nn?" Rais aliuliza kwa hasira,



"mambo yatakuwa sawa tu, nisamehe kwa hilo kosa lakini" Ray Charles aliongea, lakini Rais hakujibu, alikata simu tu. Ray Charles akaipiga simu chini kwa hasira, kisha akaongeza kasi ya gari.



Ray Charles aliranda randa mitaani akiwatafuta kina Tom bila mafanikio yoyote, mwisho wa siku akaamua arudi nyumbani kwake, huku akiwa na mawazo yamemtawala, kitendo cha kumpoteza Tom kizembe kilimuumiza kichwa, aliona Rais atapoteza kumuamini, na yeye yupo kwa ajili ya Rais, ndio, sababu ya yeye kuwa hai mpaka leo, ni kwa sababu ya Rais.



*****************



Sajenti Minja alienda kuegesha gari nje ya kituo cha polisi, kisha wakatelemka haraka haraka na kuingia ndani ya kituo kile kikubwa cha mkoa,



"vipi mkuu?" Askari aliyekuwa zamu usiku huo aliuliza,



"huyu bwana amekuja kutoa taarifa, alitekwa" Sajenti Minja alijibu huku akimsogeza Tom kwa mbele, kisha yule Askari aliyekuwa kaunta akachukua daftari kubwa na peni, alikuwa anataka maelezo kutoka kwa Tom,



"aliyekuteka unamjua?" Askari aliuliza,



"kwa jina anaitwa Raymond Charles, na kwa sura namjua pia" Tom alijibu,



"unafahamu sababu ya yeye kukuteka?" Askari alimuuliza Tom,



"kwa anavyodai yeye, kuna habari niliirusha katika mtandao wa kijamii, hiyo habari ilikuwa inamuhusu yeye" Tom alijibu,



"ni habari niliyoiandaa mimi, kuna upelelezi nilikuwa nataka nifanye" Sajenti Minja aliingilia kati na kujibu,



"alivyokuteka alikupeleka wapi?" Askari alimuuliza Tom,



"nilipoteza fahamu, na fahamu ziliponirejea nilijikuta nipo katika chumba chenye kito kimoja tu, cha chuma, ila sijajua ni wapi" Tom alijbu,



"alikudhuru mwili?" Askari aliendelea kuuliza,



"kanipiga sana, yaani sana mpaka nilipoteza fahamu, kuna muda alinipiga na kile kiti cha chuma ubavuni" Tom alijbu huku akimuonesha jeraha lake la ubavuni alipopigwa na kiti na Ray Charles,



"jina unaitwa nani?" Askari alimuuliza Tom,



"Thomas Anthony" Tom alijibu,



"sawa, labda una chochote cha kuongeza?" Askari alimuuliza Tom,



"hapana" Tom alijibu huku akimtazama Sajenti Minja,



"hapana" Sajenti Minja nae alijibu, kisha Askari akampatia karatasi ambayo alimwambia ataitumia akienda hospital kufanya matibabu,



"poa poa, naomba hiyo kesi uifikishe mpaka kwa mkuu wa polisi" Sajenti Minja alimwambia yule Askari,



"kwanini ifike ngazi za Juu wakati hata hapa tunaweza kuifuatilia?" Askari alimuuliza Sajenti Minja,



"una uhakika unaweza kuifuatilia?, mimi ndiye nilitekuambia uipeleke ngazi za juu, na usiwaambie kama mimi nilikuja na mlalamikaji" Sajenti Minja alitoa maagizo kwa yule Askari, maagizo yaliyompa ukakasi yule Askari,



"kwanini unataka iwe hivyo mkuu?" Askari alimuuliza Sajenti Minja,



"kwa sababu ni sehem ya upelelezi wangu, nadhani umeridhika sasa" Sajenti Minja aliongea huku akiondoka, Tom nae akamfuata kwa nyuma bila kuongea kitu.



Wakatoka mpaka nje ya kituo,



"hii gari itabaki hapa polisi, sisi tutafute usafiri mwingine wa kukupeleka hospital" Sajenti Minja alimwambia Tom,



"sawa, ila mkuu hivi kulikuwa na sababu ya kunileta huku kuhojiwa? si ulikuwa na uwezo wa kunihoji na ukafanikisha kupata unachokitaka" Tom alimwambia Sajenti Minja,



"kila ninachokifanya kina maana, nataka nimuaminishe mkuu wa polisi kuwa huyu mtu anayeitwa Ray Charles yupo hai" Sajenti Minja aliongea,



"ataamini vipi na hajawahi kumuona?" Tom aliuliza,



"subiri na utaona, kila kitu kinaenda kwa hatua, subiri dogo na utajua ninachokiwaza" Sajenti Minja aliongea huku akisimamisha bajaj, kisha wakaingia na kumpa maelekezo dereva bajaj ni wapi wanaenda.



"ngoja nimpigie simu mchumba wako na kumwambia aje hospital" Sajenti Minja alimwambia Tom,



"kweli kabisa, maana yule mwanamke ana kisirani na wivu, anaweza kujua nilikuwa mchepukoni" Tom aliongea na wakacheka kwa pamoja.



************



Ndani ya kituo cha polisi nje ya mji, Dokta Smith na bwana mswahili walikuwa wakifikishwa kituoni,



"waweke selo" Askari kiongozi aliyetoka nao msituni aliwaamrisha wenzake,



"lakini huyu mmoja do ndiye alikuja kutoa taarifa, kwanini naye awekewe ndani?" Askari mwingine aliuliza,



"weka ndani, sitaki mabishano" Askari kiongozi aliongea kwa amri, na wakati huo mkuu wa kituo hicho kidogo alikuwa anafika eneo hilo, wakampa heshima yake,



"awa ndio waliokuwa wamemuhifadhi yule mwanamke muuaji?" Mkuu wa kituo aliuliza,



"huyu mmoja ndiye aliyeleta taarifa, huyu Mswahili, ila huyu mzungu yeye ndiye alikuwa akimlinda" Askari mmoja alijibu,



"mbona wote wana pingu sasa?" Mkuu wa kituo aliuliza,



"Hata mimi nashangaa" Askari yule yule alijibu,



"mfungueni huyo mmoja, sio mtuhumiwa huyo, huyo ni msamalia mwema, kisha msiwaingize selo, chukueni gari muwapeleke mjini, huyo mtuhumiwa na huyu msamalia mwema wote wanatakiwa mjini" Mkuu wa kituo aliongea kisha wale Askari na wakatoka nje na Dokta Smith na Mswahili, ila safari hii Mswahili alikuwa hana pingu, alikuwa sio mtuhumiwa tena.



Wakawaingiza ndani ya gari na safari ya mjini ikaanza, iliwachukua saa moja na nusu kufika mjini, kisha wakapokelewa na kundi kubwa la waandishi wa habari ambao tayari kulikuwa na taarifa zao watu awa, taarifa zilisema waliomuhifadhi mtuhumiwa wa Vifo vya viongozi wa serikali, wamekamatwa.



Baada ya Dokta Smith kushushwa katika gari, walimuingiza moja kwa moja selo, waandishi wa habari walibahatika kupata picha yake tu.



Mswahili aliachiwa, na alitakiwa aondoke ila muda wowote ataitwa na polisi kwa ajili mahojiano.



Mswahili alipotoka tu nje ya kituo, waandishi wa habari wakamzunguka na kuanza kumuhoji habari zile za BQ, wengine walimuuliza huyo dada ni mtu wa aina gani? lakini Mswahili yeye alichokuwa anaongea ni chuki tu dhidi ya BQ, na alijinasibu yeye ni msamalia mwema. baada ya waandishi wa habari kumuhoji wanavyotaka na yeye aliwapa majibu mazuri tu, na mwisho waandishi wa habari walimaliza maswali yao na kumuachia Mswahili aondoke zake.



Siku iliyofuata magazeti yalikuwa na habari mbalimbali kuhusu tukio la kuonekana kwa dada muuaji, ila bado habari zilisema alitoweka au aliliwa na mnyama asiyejulikana. Pia magazeti mengi yalitoa picha za Mswahili, na walimpamba kwa maneno yaliyomuoneaha bwana yule ana moyo wa kishujaa, na kuanzia hapo Mswahili akawa maarufu ndani ya nchi yake.



Wakati Mswahili akiwa maarufu kwa kipindi hicho, yeye Ray Charles alipata mshtuko wa mshangao, yaani mtu aliyeamini amemuua kumbe alikuwa bado anaishi? wasiwasi wake haukuwa kuishi kwa BQ, ila wasiwasi wake ulikuwa ni vipi Rais atamchukululia, maana ameshaanza kutomuami juu ya utendaji kazi wake, na msichokijua ni kuwa Ray Charles alipewa nafasi ya kuishi na Rais, vinginevyo angekuwa ameshazikwa kitambo tu, maana hapo alipo ni marehemu.



_________________

BAADA YA WIKI

__________________,



Mswahili alishakuwa maarufu kutokana na zile habari zake za kufichua sehemu alipo muuaji wa kutisha, Mswahili alikuwa amepanga nyumba mjini na kila siku asubuhi alikuwa akiongozana na Askari kwenda msituni ili waone kama waweza kupata ushahidi wowote juu ya kifo cha BQ, kisha jioni humrudisha Mswahili katika nyumba aliyopanga.



Usiku mmoja Mswahili anaonekana akirudi katika nyumba yake, alikuwa ametoka kununua chakula, alivyofika alifungua mlango na kujitupa juu ya kochi, kisha akachana mfukn wa chakula na kuanza kula taratibu huku akitazama runinga.



Alipomaliza kula aliingia bafuni kuoga, kisha akaenda chumbani kulala, uwa hakawii kupata usingizi kutokana na pilika pilika za msituni, kwa hiyo ilimchukua dakika kumi tu kupitiwa na usingizi, akapotelea ndotoni.



Alfajili ya saa kumi na moja alishtuka, ndio muda ambao huamka, alivyoamka tu, alienda bafuni kuoga na kuvaa kabisa, chumba chake kina choo na bafu humo humo. Baada ya kumaliza, alikuwa anatoka ili aende getini polisi waje wampitie waelekee msituni.



Mswahili akatoka chumbani, akapita koridoni mpaka sebuleni, akapigwa na butwaa la mwaka, alimkuta mtu amekaa katika kochi sebuleni, juu ya meza aliweka juisi iliyokuwa ndani ya glass, na mkono wake wa kushoto uliokuwa wa chuma, alikuwa ameshikilia sigara inayotoa moshi, mkono wa kulia alishikilia bastola...



"BQ??" Mswahili aliongea bila kutegemea mara baada ya kugundua kuwa yule mwanamke ni BQ,



"nambie mzee Mswahili, Edward Sambo" BQ aliongea huku akiinuka na kufanya sura yake ioneshe hasira alizonazo....



Edward Sambo akapigwa na butwaa, maana mtu aliyeamini amekufa, au mtu ambaye alifanya majaribio mengi ya kumuua, leo hii alikuwa mbele yake wakitazamana uso kwa uso,



"naona vyombo vya habari kila siku vinakuongelea wewe kama shujaa, kwa ushujaa gani uliofanya?" BQ aliuliza huku akiwa amesimama jirani kabisa na Edward Sambo ambaye alikuwa akitetemeka tu,



"sijaja kukupa onyo hapa, nimekuja kujionesha kwako kuwa bado nipo, Mungu amenipa nafasi ya tatu ya kuishi, aliniokoa nilipotaka kulipuliwa na ndege kule katika hifadhi ya wanyama, nikapona. Nafasi ya pili ni ile nilipopigwa risasi baharini, na nafasi ya tatu ni ya wewe kujaribu kuniua kwa sumu, ila bado naishi, nitakufa nikishapata haki yangu" BQ aliongea huku akiiweka bastola yake katika kichwa cha Edward Sambo,



"ondoka, polisi watakuja sasa hivi" Edward Sambo aliongea bila kutegemea,



"Polisi, polisi ndio wakina nani? mimi ni zaidi ya polisi, na uwape ujumbe, waambie kuwa ule unyama nilioufanya hawali, nitauongeza mara mbili, maana wameshindwa kuniua kwa kunitumia mwanajeshi wa kukodi" BQ aliongea huku akiikoki bastola yake, hapo Edward Sambo ushuzi ukamtoka akajikuta anabana miguu bila kutegemea.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakati BQ akiendelea kuongea na Edward Sambo, honi za gari zilisikika kutokea getini, BQ akasogea mpaka dirishani na kuchungulia, walikuwa ni polisi, BQ akarudi mpaka aliposimama Edward Sambo,



"ebu ngoja nione kama na wewe unaweza kupewa nafasi ya pili ya kuishi kama mimi, nitafanya jaribio la kukuua" BQ aliongea huku akiiweka bastola yake katika paji la uso wa Edward Sambo,



"nina mengi sana ya kuongea na wewe, ila tutaongea kama utapata nafasi ya kuishi tena" BQ aliongea huku akiikoki bastola yake na wakati huo Edward Sambo alikuwa akiomba polisi waingie ndani tu wamuokoe.



Uko nje polisi waliendelea kupiga honi,



"mbona hatoki?" Dereva wa ile gari ya polisi alimuuliza mwenzake waliyekuwa nae upande wa mbele,



"alafu sio kawaida yake, kila siku uwa tunamkuta getini anatusubiri, leo sijui imekuwaje? au alizidisha kilevi jana?" Yule Polisi mwingine alihoji,



"kwani anakunywaga yule mzee?" Polisi dereva aliuliza huku akicheka,



"anapiga vyombo huyo, tena zile pombe kali kali" Yule polisi mwingine alijibu, kisha akatoa shingo kwa dirishani na kuangalia katika upande wa nyuma wa gari ambao kulikuwa na Askari katika bodi ya gari,



"mmoja ashuke akamuangalie ndani" Askari alipaza sauti kuwaambia wenzake, wakati askari mmoja akishuka ili aingie ndani, walisikia mlio wa risasi, wote wakaruka chini na kulala, walijua kabisa mlio ule umetokea ndani ya nyumba ya Edward Sambo.



Wakiwa bado wanajipanga namna ya kuingia ndani, walisikia mlio mwingine wa risasi, Askari mmoja mwenye nyota mbili, akainua mkono na kutoa ishara watu wawili waingie ndani, kisha yule Askari mwenye nyota akasogea getini na kufungua, Askari wawili wakaingia ndani kwa mtindo wa kutambaa ardhini, kisha wale wa nje wakasubiri sekunde thelathini, hawakusikia shambulio jingine lolote. Askari yule mwenye nyota mbili akatoa ishara kuonesha Askari wengine watatu waingie ndani, Askari watatu wakasogea na kuingia ndani ya geti, kisha yule Askari akaingia na yeye, akatambaa mpaka katika mlango wa kuingilia sebuleni wa nyumba ile, akawaita vijana wake kwa ishara, wakasogea mpaka karibu yake kwa tahadhari kubwa,



"tunavamia sasa, mmoja atafungua mlango, alafu sisi tutaingia kwa kasi ndani na kutawanyika ili kumchanganya adui, sawa?" Askari mwenye nyota mbili aliuliza na wenzake wakajibu kwa kutikisa kichwa kuonesha kukubaliana nae, kisha yule Askari akahesabu kwa vidole mpaka tatu, mmoja wao akafungua mlango kwa kasi, na wengine wakarukia ndani huku silaha zikiwa mkononi, wakamkuta Edward Sambo akiwa amekaa katikati ya dimbwi la mkojo huku akihema haraka haraka,



"mzee Kuna usalama?" Askari mmoja alimuuliza, Edward Sambo akaitikia kwa kichwa kukataa,



"nini tatizo?, maana tumesikia mlio wa risasi" Askari aliuliza,



"BQ" Edward Sambo aliongea,



"ndio nini?" Askari aliuliza,



"sio ndio nini, sema ndio nani?" Edward Sambo aliongea huku akimtazama yule askari usoni,



"sawa, BQ ndio nani?" Askari aliuliza,



"Yule mwanamke muuaji tunayemtafuta" Edward Sambo alijibu na kuwafanya Askari washangae na waweke vizuri silaha zao,



"kafanyaje?" Askari aliuliza,



"ndio aliyepiga zile risasi, alinivamia" Edward Sambo alijibu



"Yupo wapi sasa" Askari aliuliza,



"atakuwa ameshaondoka, alielekea katika chumba changu, kisha kama mlisikia ule mlio wa risasi wa mara ya pili, nadhani alitumia kuvunja kioo cha dirisha, maana alipiga ile risasi akiwa ndani" Edward Sambo aliongea,



"lakini dirishani si Kuna nondo?" Askari aliuliza,



"ndio zipo, kwa hiyo inawezekana bado yupo ndani?" Edward Sambo aliuliza huku akipata nguvu ya kuamka baada ya kugundua kuwa hata kama yule mwanamke amevunja kioo, basi nondo zitamshinda,



"Twendeni" Askari mwenye nyota mbili aliwaambia wenzake huku akiongoza kuelekea katika vyumba, kulikuwa na vyumba viwili tu, kimoja uwa kinafungwa muda wote, kwa hiyo wao walienda moja kwa moja katika chumba cha Edward Sambo, wakapigwa na mshangao mara baada ya kuliona dirisha, ndio kioo kilivunjwa, ila nondo za dirisha hazikukunjwa, ila zilikatwa kabisa, tena sio na machine, inaonesha zilikunjwa kunjwa mpaka zikakatika.



"huyo mwanamke ni mwanaume?! " Askari mmoja aliuliza baada ya kuona hilo tukio,



"acha maswali ya kipumbavu" Mkubwa wake aliongea huku akisogea dirishani.



"ameshaondoka, hakika BQ bado ana uwezo mkubwa sana" Edward Sambo aliongea na kufanya Askari wamtazame,



"unamjua muda mrefu kwani?" Askari alimuuliza,



"sana, tena sana" Edward Sambo alijibu,



"twende ukatoe taarifa ya kuvamiwa kituoni, na hayo maelezo mengine utayatoa mzee wangu" Askari mwenye nyota mbili alimwambia Edward Sambo,



"ngoja nikaoge wadogo zangu, si mnaona hali niliyonayo?" Edward Sambo aliongea huku akiwaonesha eneo la mbele la suruali yake, lilikuwa limelowana mkojo.



Ilibidi polisi wamsubirie Edward Sambo aoge, safari ya msituni haikuwepo tena, maana mtu waliyekuwa wanaenda kumtafuta, waliambiwa ametoka muda sio mrefu.



Baada ya nusu saa, Edward Sambo alikuwa ameshamaliza kuoga, wakatoka pamoja mpaka nje, wakaingia katika gari, safari ya kituoni ikaanza.



Iliwachukua muda mchache tu kufika kituoni, wakatelemka na moja kwa moja walimpeleka Edward Sambo katika ofisi ya mkuu wa polisi, alitakiwa akaeleze alichokutana nacho kutoka kwa BQ.



***************



Baada ya mahojiano kati ya mkuu wa polisi na Edward Sambo kuisha, habari ya kuonekana kwa dada muuaji ilienea kwa haraka sana, safari hii mpaka jina liliwekwa wazi, jina lake halisi, Maria Zyachenko.



Mishale ya saa moja usiku, mkuu wa polisi alipigiwa simu kutoka ikulu, alihitajika na Rais kwa haraka sana.



Mkuu wa polisi alishangaa huo uito, maana tangu alivyoapishwa ndani ya ikulu, hajawahi kufika tena eneo hilo.



Mkuu wa polisi alifika mpaka Ikulu, akakaguliwa mlangoni na kuruhusiwa aingie, akaingiza gari na kuiegesha katika sehemu maalum za maegesho, kisha akatelemka na kuanza kuelekea ndani, ila alisimamishwa na mlinzi mmoja wa Ikulu, akampa heshima yake,



"mheshimiwa Rais yupo upande wa nyuma katika bustani, anakusubiri wewe, naomba nikupeleke" Mlinzi aliongea, kisha mkuu wa polisi akamfuata mpaka nyuma ya nyumba. Walimkuta Rais akiwa amevaa kaptula, laptop ilikuwa mezani, na pembeni ya laptop kulikuwa na chupa kubwa ya mvinyo, na kulikuwa na bilauri mbili, moja ilikuwa na kinywaji, inaelekea Rais alikuwa akinywa, na nyingine ilikuwa tupu.



Mkuu wa polisi alipofika karibu na Rais, alimpigia saluti,



"kaa hapo" Rais alimwambia mkuu wa polisi, na wakati huo yule mlinzi aliyemleta mkuu wa polisi alikuwa akiondoka.



Rais akachukua chupa ya mvinyo na kumimina katika ile bilauri tupu, kisha akamsogezea mkuu wa polisi, mkuu wa polisi akaipokea kwa heshima na kuigida kiasi, kisha akaishusha mezani.



"za siku bwana" Rais alimsalimia mkuu wa polisi,



"nzuri mheshimiwa" Mkuu wa polisi aliitikia kwa uoga,



"nataka kujua haya mambo wewe unayaendeshaje, maana sioni matokeo yoyote mpaka sasa?" Rais aliuliza huku akiifunga laptop yake na kumuangalia mkuu wa polisi,



"mambo gani mheshimiwa?" Mkuu wa polisi aliuliza huku mapigo ya moyo yakiongezeka kasi, maana mpaka Rais akuulize hivyo, ujue kuna jambo hujalifanya kwa ufanisi,



"Habari ya huyo mwanamke muuaji, wewe unaichukuliaje?" Rais aliuliza na kumfanya sasa mkuu wa polisi afikirie kwa muda,



"ni jambo zito kwa kweli, ila kama unavyosikia kupitia vyombo vya habari, huyu mwanamke baada ya ukimya kidogo, aligundulika alikuwa msituni, tena alikuwa na hali mbaya, tukatuma vijana waende wakamkamate uko, ila hatukufanikiwa kumpata mpaka leo tena tulivyosikia ameonekana asubuhi kwa Edward Sambo" Mkuu wa polisi alieleza,



"hii kesi nyie mnaifuatiliaje?" Rais aliuliza,



"samahani mheshimiwa, sijaelewa swali" Mkuu wa polisi aliongea kwa utulivu,



"yaani nyie kama polisi, kuna mtu yoyote mmemteua aifuatilie hii kesi au mnasubiri mletewe taarifa na wasamalia wema tu?" Rais aliuliza kisha akagida kidogo mvinyo,



"Kuna mtu maalum nilimteua aifuatilie hii kesi kwa siri" Mkuu wa polisi alijibu,



"amefikia wapi katika upelelezi wake?" Rais aliuliza,



"mmmh, kwa maelezo ya yule mpelelezi, anadai hili jambo, kuna vita nyingine ya mtu mwingine dhidi ya yule dada, na mtu ambaye anadai alimshuhudia akimpiga yule dada baharini na ikasemekana yule dada amekufa, ni Ray Charles" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama Rais, Rais akatabasamu,



"huyo kijana wako mpelelezi anaitwa nani?" Rais aliuliza huku akitabasamu,



"anaitwa Joel Minja" Mkuu wa polisi alijibu,



"mwambie awe makini sana" Rais aliongea huku akitabasamu, ila hiyo kauli haikueleweka kwa mkuu wa polisi,



"sawa mheshimiwa" Mkuu wa polisi aliongea,



"au kama vipi, nitakupigia simu, nataka nionane na huyo kijana. Siku mbili hizi nitakupigia simu,. Kingine cha ziada, ongeza ufanisi uhakikishe huyo dada anakamatwa, na ikiwezekana afe kabisa, vinginevyo hiyo nafasi uliyonayo utaiweka mashakani" Rais aliongea kwa umakini mkubwa,



"sawa mkuu" Mkuu wa polisi alijibu kinyenyekevu,



"unaweza kwenda" Rais aliongea na kisha mkuu wa polisi aliamka na kuanza kuondoka, alipopotea tu machoni kwa Rais, alitokea Ray Charles, alikuwa amejificha, hakutaka mkuu wa polisi amuone.



"inaelekea wameshajua uwepo wako katika hii kesi, ila huyu mkuu wa polisi hana uhakika na uwepo wako" Rais aliongea lakini Ray Charles hakujibu kitu.



Wakati mkuu wa polisi akitoka, alipishana na mtu mwingine ambaye alimjua kupitia vyombo vya habari tu, hakuwahi kukutana nae, hivyo walipishana kimya kimya tu.



Yule mtu alielekea moja kwa moja mpaka upande wa nyuma wa Ikulu na kwenda alipo Rais, wakasalimiana kwa bashasha, kwa kukumbatiana, kisha yule mtu akakaa katika kiti, ila yule mtu alipotupa macho nyuma ya Rais, alimuona Ray Charles, yule mtu akashtuka, Rais akaligundua hilo,



"usiogope, kwanini unaogopa?" Rais alimuuliza yule mtu,



"huyu si Ray Charles huyu" Yule mtu aliuliza huku akimuoneshea kidole Ray Charles ambaye aliangalia chini,



"ndiye yeye" Rais alijibu huku akitabasamu,



"imekuwaje kuwaje anaishi wakati alishakufa, familia ilishazika mabaki ya mwili wake?" Yule mtu aliuliza,



"unataka kujua imekuwa Ray anaishi tena?" Rais aliuliza huku akitabasamu,



"ndio, nataka kujua kwa kweli, maana huu ni muujiza" Yule bwana alijibu huku akiwa bado akimtazama Ray Charles,



"lakini hicho sicho nilichokuitia hapa?!" Rais aliongea huku akimimina mvinyo katika bilauri yake,



"ulichoniitia utaniambia baadae, nataka kujua kwanini Ray Charles yupo hai" Yule bwana aliongea,



"sawa, Ray, ebu nenda katembee kidogo" Rais aliongea huku akimgeukia Ray Charles, ambaye taratibu aligeuka na kuondoka eneo hilo, yule bwana alikuwa bado anamuangalia tu Ray Charles, hakuwahi kuamini hata siku moja kuwa Ray Charles anaishi,



"huyo utakuwa unamuona kila siku, hata usijali" Rais aliongea huku akimtazama yule bwana,



"aisee, dunia ina maajabu. Haya nieleze ilikuwaje?" Yule bwana alimuuliza Rais,



"ni story ya kusisimua kidogo'' Rais aliongea huku akiweka sura ya umakini,



"nieleze tu" Yule bwana alionesha kiu yake ya kutaka kuujua ukweli,



"sawa, ngoja nikupe ukweli, ila hakuna anayejua ukweli zaidi yangu na yeye, wewe utakuwa wa Tatu" Rais alianza namna hiyo, kisha akaendelea..



"Huyu Ray Charles sio mzimu wala sio robot " Rais aliongea na kumfanya yule bwana awe makini zaidi..........









Rais akaendelea kutoa sababu ya Ray Charles kuwa hai,



"katika ule mchakato wa kuipindua serikali ili Tammy Semmy awe Rais, wale watu ambao walikuwa kama bodyguard wa Tammy Semmy, yaani marehemu Gabby, Jimmy na BQ, walikuwa wakishafanikisha ile kazi, kila mmoja angekuwa tajiri, wasingeendelea na kazi to kumlinda Tammy Semmy, kwa maana nyingine mikataba yao ilikuwa inaisha baada ya Tammy Semmy kuchukua madaraka rasmi. Ila baada ya Tammy Semmy kuchukua madaraka, bado Gabby na Jimmy waliendelea kuwa walinzi binafsi wa Tammy Semmy, kwanini?" Rais aliuliza mwenyewe kisha akaichukua chupa ya mvinyo na kuimimina katika bilauri, ila ilionesha haina kitu, akailaza juu ya meza, kisha akaendelea,



"waliendelea kuwa walinzi wa Tammy Semmy kwa sababu mlinzi aliyetakiwa kuja kuwa anamlinda Tammy Semmy, alikodiwa na jeshi la Somalia kwa ajili ya kwenda kumuua mkuu wa kikosi cha Al shabab, alienda yeye na wenzie watatu, yaani huyo mlinzi ninayemzungumzia ni Ray Charles" Rais aliongea na kumtazama yule bwana,



"kwa hiyo ina maana ile habari iliyotolewa na al shabab juu ya kuwa watu awa walienda kuwachunguza kumbe ilikuwa habari ya kweli?" Yule bwana mwingine aliuliza huku akikaa vizuri zaidi,



"ni habari ya kweli, ila kule walienda bila serikali kujua, walienda kwa makubaliano binafsi baina ya Tommy Semmy na serikali ya Somalia. Kwa hiyo hata walipokamatwa kule, serikali yetu ilikataa kuwatambua, hivyo wale wanamgambo wakaamua kuwaua, ila baadae serikali ilidai kuwatambua ila ikadai haikuwa na taarifa zao. Ila kumbuka kabla Ray Charles hajaenda somalia, tayari aliandaliwa kuwa mlinzi wa Tammy Semmy kutokana na mafunzo maalum aliyokuwa nayo Ray Charles.



Kwa hiyo basi baada ya serikali kuwatambua, viongozi kadhaa wa serikali walienda somalia kuonana na viongozi wa Al shabab, ambapo viongozi hao walikataa kuwapa viongozi wa serikali miili ile mpaka wapewe pesa, serikali ikatoa pesa na viongozi wale wa serikali wakaichukua miili ile na kurudi nayo, ila ilionekana katika ile miili kuna miili miwili ilikuwa bado na uhai ingawa ilikuwa na matundu mengi ya risasi, serikali ikaipeleka ile hospital, ikaonekana ni lazima wafe, kulikuwa hakuna dalili za watu hao kupona, ila madaktari wakashauri labda wapelekwe nje ya nchi, Tammy Semmy akatoa pesa na miili ile ikapelekwa nje, ila mmoja kati ya wale watu alifia njiani, kwa hiyo ukabaki mwili mmoja ambao ni wa Ray Charles.



Mwili ule ulifikishwa China, baada ya kuuchunguza kwa umakini, wakagundua kuwa Ray Charles ataendelea kuishi, ila kama mfu, yaani ataishi ila hatoamka tena, ataendelea kupumua ila ubongo wake na mwili wake havitofanya kazi tena" Rais aliongea kisha akanyamaza, akachukua simu yake na kupiga simu ndani, aliagiza mvinyo mwingine.,



"hii habari inasimumua, lakini mwili wa Ray Charles si tuliuzika kabisa na tuliuaga?" Yule bwana mwingine aliuliza huku akitoa tabasamu la mshangao,



"usiwe na haraka basi, hivi nilikwambia ubongo wake na mwili havitofanya kazi tena?" Rais alimuuliza yule bwana,



"ndio" Yule bwana mwingine alijibu,



"nimekosea, ni kwamba mwili hautofanya kazi tena, ila ubongo ulikuwa ukifanya kazi kwa taratibu sana, unaweza kumuwekea soda mbele, ila akaitambua baada ya wiki.



Sasa wale wachina wakashauri wanaweza kumsaidia kwa njia mbili, ya kwanza ni kummalizia tu, yaani kumuua, na ya pili ni kumuwekea mwili wa bandia, hilo la kwanza, la pili walisema wana uwezo wa kumfunga vifaa vidogo vidogo katika kichwa chake kwa ajili ya kuusaidia mfumo wake wa ubongo kuwa na kasi ya kawaida,



Kwa kuwa Tammy Semmy alikuwa anampenda sana Ray Charles, Tammy Semmy akakubali kumtengeneza Ray Charles, kwa hiyo akakubali kuingia makubaliano ya mkataba wa kuokoa uhai wa Ray Charles, ila gharama za kumfanya Ray Charles aendelee kuwa mtu, zilikuwa kubwa, Tammy Semmy hakuwa na pesa kipindi hicho, pesa zote alizitumia katika mpango wake wa kuingia ikulu. Sasa alichokifanya Tammy Semmy ni kutoa eneo kwa wale wachina, na eneo lenyewe ndio hilo ambalo huyu mwanamke anayetusumbua kwa kuua viongozi, alipewa hilo eneo na Tammy Semmy, tena alipewa kwa mkataba na sahihi za pande mbili, wakiwemo mashahidi, ila na hao wachina tena akawapa hilo eneo, tena kwa mkataba, kwa hiyo basi ikawa Tammy Semmy ameingia mikataba miwili kwa mara moja, ubaya zaidi kuwa hiyo mikataba ililenga sehemu moja. Sasa basi ili kuwa huru, Tammy Semmy aliamua kutumia mbinu za kuua upande mmoja alioingia nao mkataba, na upande alioona utakuwa rahisi, ni upande wa BQ, kwa hiyo akamtengenezea ajali ya ndege, na zoezi likafanikiwa, kila mtu akajua BQ amekufa, mpaka leo wapo wanaoamini BQ amekufa, hata mimi niliamini hivyo, mpaka niliposikia tena habari zake. Je unajua kama BQ amerudi tena?" Rais aliuliza huku akisimama,



"hapana, kwanza mimi ni mmoja wapo ninayeamini BQ amekufa" Yule bwana mwingine alijibu,



"BQ hajafa, yule mwanamke anayeua viongozi wa serikali, ndio BQ" Rais aliongea na kumshangaza zaidi yule bwana,



"bwana wewe, mbona leo unaongea vitu vya kushangaza hivi?" Yule bwana mwingine aliuliza,



"ngoja niende kujisaidia haja ndogo, nikirudi sitoendelea na habari za BQ, nitaendelea na habari za Ray Charles, maana habari zake ndio zimeleta na haya" Rais aliongea huku akiondoka eneo hilo na kumuacha yule bwana akitoa miguno ya mshangao.



***************



Sajenti Minja asubuhi ya leo alikuwa ameamka mapema sana, alikuwa amekaa huku akiona mambo kama yanaenda nyuma na kwenda mbele, yaani mambo yalivyokuwa yanaenda hakujua kabisa, sana sana vitu vilivyomchanganya ni pamoja na watu anaowafuatilia, hawakuwa wakieleweka ni watu au majini? kwa maana akikumbuka lile tukio la kumgonga na gari Ray Charles, kisha akamkanyaga, lakini Ray Charles akaamka na akaendelea kuwashambulia, kitu cha pili kumuhusu Ray Charles ni siku ile Ray Charles alipomvamia, anakumbuka kuwa alimpiga risasi nyingi sana mwilini, lakini Ray Charles hakupata majeraha,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"hapana kwa kweli'' Sajenti Minja aliongea huku akitikisa kichwa kuonesha hakubaliani na utu wa Ray Charles,



"au mzimu? maana kufa alikufa kweli, imekuwaje anaishi?, na yule mwanamke muuaji nae ndio wale wale, yaani nilishuhudia akipigwa risasi ya kichwa, pia akazamishwa na bahari, eti leo hii anaishi? hii ni ngumu kuwezekana" Sajenti Minja aliongea na kutabasamu, yaani alikuwa kama mwendawazimu.



Kilichomtoa katika wimbi la mawazo, ni simu yake ilionesha ikiita, alipoangalia namba ya mpigaji, alikuwa ni mkuu wake wa polisi, akapokea simu haraka.



"upo wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza, siku hiyo hakuanza hata na salamu,



"bado nipo hotelini" Sajenti Minja alijibu,



"kazi imekushinda sasa unaamua kulala lala tu, hujui hela ya hoteli unayolipiwa inatoka serikalini?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa hasira na kumfanya Sajenti Minja aendelee kuduwaa,



"najua mkuu" Sajenti Minja alijibu kwa sauti ndogo,



"njoo ofisini kwangu, nakupa dakika tano tu, unatakiwa uwe mbele yangu" Mkuu wa polisi aliongea na kukata simu, Sajenti Minja akaangalia kioo cha simu yake na kumshangaa mkubwa wake kwa yale maneno yake,



"sidhani kama Kuna wema" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka katika kitanda, aliamua kuvaa nguo moja kwa moja, hakutaka kwenda kuoga kwa maana alipewa dakika chache mno, kwa hali ya kawaida tu, mwendo wa kutoka hapo hotelini mpaka katika kituo cha polisi, ni mwendo wa zaidi ya dakika kumi, sasa leo amepewa dakika tano tu.



Sajenti Minja alitoka mbio mpaka nje, akachukua boda boda iliyomfiksha mpaka kituoni, akamlimpa dereva bodaboda kisha akawa anakimbia kuelekea katika ofisi ya mkuu wa kituo, dakika tano zilishaisha muda tu.



Sajenti Minja alifika mpaka katika mlango wa mkuu wa polisi na kugonga hodi, hakujibiwa, akaamua kusukuma mlango na kuingia, akamkuta mkuu wake akiwa amekaa tu, mezani hakukuwa na kitu kama kawaida, maana Sajenti Minja alishazoea kuwa kila akija hapo ni lazima akute mkuu wake akipitia makabrasha kadhaa yenye kesi za watu.



Sajenti Minja alipokaa, ukimya ukatawala,



"upelelezi wako wa kesi ya huyo dada muuaji umepata kipi kipya?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa utulivu,



"kilichoongezeka ni yule mtu tu wa ajabu aliyempiga risasi yule dada kule baharini" Sajenti Minja aliongea kwa utulivu,



"nani huyo?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"Yule yule niliyekuambiaga, Ray Charles" Sajenti Minja aliongea na kumfanya mkuu wake akunje sura kwa hasira,



"nilishakuambiga huyo mtu alishakufa, wewe bado unakazania tu, hiyo ni dalili hii kesi inakushinda" Mkuu wa polisi aliongea kwa hasira,



"Mkuu huyu mtu yupo hai na anaishi, kama huamini nenda kaangalie kesi za hapo kaunta, kuna kesi ya mtu kutekwa na mtu huyo" Sajenti Minja aliongea, safari hii alipaza sauti hakuongea kinyonge, mkuu wake akamuangalia, maana hakutegemea ipo siku Sajenti Minja atampandishia sauti,



"sikia Minja, jana niliitwa na Rais, anafuatilia kwa karibu sana hii kesi, na anataka huyo dada auawe, sio akamatwe, vinginevyo mimi nafasi yangu ya kazi itakuwa mashakani" Mkuu wa polisi aliongea kwa huruma, hapo sasa Sajenti Minja akagundua kwanini mkuu wake amechanganyikiwa,



"kwanini auawe, akamatwe afikishwe katika vyombo vya sheria"" Sajenti Minja aliongea,



"haya ni maelezo kutoka juu, hayaitaji kupingwa wala kutiliwa shaka, yanatakiwa yatekelezwe" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa, nitajitahidi mkuu" Sajenti Minja aliongea,



"hakikisha unamtembelea Edward Sambo na unamuhoji kuhusu kitu chochote anachokijua kuhusu dada huyo" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa" Sajenti Minja alijibu,



"unaweza kuondoka, pitia hapo kaunta na uwaambie wanipe jalada la kesi la huyo mtu anayedai kutekwa na Ray Charles" Mkuu wa polisi aliongea, kisha Sajenti Minja akaondoka huku akifurahi kimoyo moyo, aliona lengo lake la kumuaminisha mkuu wa polisi juu ya uwepo wa Ray Charles, lengo linatimia.



Sajenti Minja alifika mpaka kaunta, akamkuta yule Askari aliyeandika maelezo ya Tom,

"wewe peleka kwa mkuu lile jalada la yule dogo niliyemleta wiki iliyopita, hakikisha humwambii mkuu kuwa huyo kijana nilimleta mimi" Sajenti Minja alimwambia yule Askari,



"sawa mkuu" Askari alijibu huku akipekua pekua katika madroo ya meza za pale kaunta.



Sajenti Minja akaondoka zake huku akiwaza kuwa Ikifika usiku, ataenda kuonana na Edward Sambo, sio tu kwa ajili ya kujua habari za BQ, ila pia kumsalimia kwa kuwa ni mshkaji wake wa siku nyingi, ingawa Edward Sambo ana umri mkubwa kidogo kumzidi Sajenti Minja.



****************



Muda wa saa tatu usiku, Edward Sambo akiwa sebuleni, alikuwa ana wasiwasi mwingi sana, ingawa nyumba yake siku hizi ilikuwa na ulinzi wa kutosha, kulikuwa na Askari si chini ya watano na wote wana silaha.



Kawaida muda huo Edward Sambo ni muda wake wa kuingia check chumbai kwa ajili ya kulala, ila tangu BQ amtembelee amekuwa na uoga sana, amekosa kujiamini kabisa.



Edward Sambo alizima runinga na kupiga hatua za kuelekea chumbani, ila mlango wa sebuleni uligongwa, moyo wake ukaripuka kwa hofu,



"nani?" Edward Sambo aliuliza kwa mamlaka,



"mimi Dammy" Sauti ilijibu, Dammy ni mmoja wa Askari aliyezoeana nae sana.



"nini usiku huu?" Edward Sambo aliuliza huku akionekana kutofurahishwa na huo usumbufu,



"nisaidie maji mzee wangu, leo nilisahau kununua dukani, alafu nina kiu sana" Dammy aliongea, Edward Sambo akasogea mlangoni na kufungua, mlango ulipofunguka, Dammy aliingia ndani, ila nyuma yake alikuwa BQ huku akiwa amemuwekea Dammy bastola kichwani, Edward Sambo akahisi jasho likimtoka,.



"asante afande" BQ aliongea na kumpiga na kitako cha bunduki Dammy, alimpiga kisogoni, Dammy akapoteza fahamu na kuanguka chini, yote hayo Edward Sambo alikuwa anayaangalia,



"kaa hapo, naona siku hizi unajifanya bandidu sana, yaani huniogopi kabisa, pamoja na kukutisha sana nilivyokuja hapa mara ya kwanza, lakini bado unatafuta sifa katoka vyombo vya habari kwa kutumia jina langu?" BQ aliuliza huku akimtazama Edward Sambo aliyekuwa ameganda tu,



"hajibu au?" BQ aliuliza huku akiinuka, kitu ambacho hakujua ni kuwa Edward Sambo alikuwa amepoteza fahamu muda mrefu tu tangu alipomuona, kilichokuwa kinamsaidia ni ukuta tu alioegamia,



"wewe mzee" BQ alimuita kwa hasira huku akitaka kumkunja shati, lakini Edward Sambo akaanguka kama mzigo, hapo ndipo BQ akajua mzee tayari amekata moto,



"unajifanya mwamba mbele ya vyombo vya habari, kumbe muoga tu" BQ aliongea peke yake huku akimtazama Edward Sambo aliyekuwa amepoteza fahamu, ila BQ alihisi Kuna mtu amemsimamia nyuma, BQ akageuka kwa haraka na bastola mkononi, ila kwa kasi ya ajabu sana bastola yake ilipigwa teke na kuangukia mbali, BQ akarusha ngumi ya mkono wake mmoja, maana hakuwa na mkono wake wa chuma. Ile ngumi ilidakwa na na kisha BQ alipigwa kichwa katika paji lake la uso, akarudi nyuma huku akipesusuka, kisha akanyooshewa bastola, BQ akabaki anashangaa tu, mbele yake alikuwepo Sajenti Minja huku akiwa hana sura ya mzaha kabisa.



"huyu mwanamke anatakiwa auawe, haya ni maelezo kutoka juu" Sauti ya mkuu wa polisi ilimrudia kichwani Sajenti Minja, Sajenti Minja akaikoki bastola yake, alishaamua kutekeleza maagizo kutoka juu............





Ila Sajenti Minja akashusha bastola chini, kuna kitu alikiwaza kichwani mwake, huyu mwanamke ni mara ya pili wanakutana, mara ya kwanza waliwahi kukutana nje ya nyumba ya waziri wa katiba na sheria, anakumbuka mara ya kwanza walivyokutana, yule mwanamke alikuwa na mikono miwili, tena alikuwa na nguvu za ajabu, sasa kwanini safari hii awe na mkono mmoja? Sajenti Minja akairudisha bastola katika sehemu yake, aliamua kujaribu kupigana nae ili aone ni yeye au mwingine, hapo Sajenti Minja alikuwa anacheza kamari,



"ngoja nikupe nafasi ya kujitetea, tupambane" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama BQ, BQ akaona huo ndo wakati wa kujitetea, kwanza alidharau uwezo wa Sajenti Minja, kwa maana alishawahi kupambana nae na akamshinda. BQ akafanya kama anageuka anampa mgongo Sajenti Minja, kisha kwa kasi akageuka na teke kali, Sajenti Minja akaudaka mguu wa BQ, tena aliudaka bila kutingishika wala kuumia, kisha akamsukuma BQ, BQ akadondoka chini, Sajenti Minja akapiga piga mikono yake kama anafuta vumbi.



"inuka pambana ili ushinde na ujiokoe" Sajenti Minja aliongea, ila aliona BQ akipeleka mkono sehemu bastola inapokaa, Sajenti Minja akaruka na kutua mbele ya BQ, kisha akapiga teke kali mkono wa BQ uliokuwa unachomoa bastola, basi bastola ikatupwa mbali, BQ akainuka kwa mtindo wa ajabu kabisa, na kwa kasi akamuelekea Sajenti Minja, alipomfikia alipiga ngumi nyingi mfululizo za mkono mmoja, ila zile ngumi Sajenti Minja alikuwa anazipangua kama anajipepea na mkono, yaani ngumi za BQ hazikuwa nzito kabisa, kisha Sajenti Minja akainama na kuichota miguu ya BQ, alafu akamnyanyua juu na kumtupa chini, BQ akapata maumivu,



"ni wewe kweli au mpo wawili?" Sajenti Minja aliuliza huku akimtazama kwa umakini, kipindi BQ alikuwa anavuja damu eneo la kichwani katika kidonda kilichotokana na kupigwa risasi na Ray Charles kipindi cha nyuma, kifupi BQ hakuwa vizuri, yaani aliamua kuingia mitaani kabla hajapona majeraha ya risasi, hicho ndicho kilimfanya akose nguvu na mapigo yake kuzuiwa kirahisi na Sajenti Minja.



BQ akajizoa chini, lakini bado alikuwa katika hali ya kizungu zungu. BQ akamfuata kwa kasi Sajenti Minja, kisha akasimama ghafla, hiyo mbinu ilimchanganya Sajenti Minja, kisha BQ akafanya kama anainama kuivuta miguu ya Sajenti Minja, basi Sajenti Minja yeye alikuwa na kasi mara mbili, yaani kabla BQ hajaigusa miguu ya Sajenti Minja, tayari mikono ya Sajenti Minja ilikuwa imeshafika chini, na hicho ndicho BQ alikuwa anakitaka, basi Sajenti Minja alivyoshika chini tu, BQ aliruka juu ya mgongo wa Sajenti Minja na kutua upande wa pili, kisha akaseleleka mpaka bastola yake ilipoangukia, akainama kuiokota, na kumgeukia Sajenti Minja, akamnyooshea bastola, Sajenti Minja akaanza kuilaumu nafsi yake kwa kumshawishi kupambana na huyo dada, na kipindi BQ alikuwa ameshika bastola kumuelekea Sajenti Minja, ila ile hali ya kizunguzungu ikaongezeka kwa BQ, BQ nguvu zikaanza kumuishia na giza likaanza kuongezeka machoni, BQ akaamua kufyatua risasi kumuelekea Sajenti Minja, lakini kutokana na hali yake, alijikuta shabaha ikipotea na kumkosa Sajenti Minja, kisha BQ akaanguka chini na kuzimia.



Sajenti Minja akabaki anashangaa kwa namna hilo tukio lilivyotokea kwa miujiza, yaani hakuamini kabisa kuwa yule mwanamke muuaji amemuacha.



Sajenti Minja akasogelea sehemu alipokuwa amelala BQ, akamkuta yupo katika usingizi mzito, hakuwa na fahamu, na kipindi hicho Edward Sambo ndio alikuwa anaamka, akashangaa kumkuta Sajenti Minja na pia kuona yule dada akiwa amelala chini,



"Minja vipi?" Edward Sambo aliuliza huku akisogea eneo hilo,



"safi, vipi upo salama?" Sajenti Minja aliuliza,



"nipo salama, mbona umekuja peke yako?" Edward Sambo aliuliza swali ambao Sajenti Minja hakulielewa,



"mbona umeniuliza hivyo?" Sajenti Minja aliuliza na muda huo polisi wengine watano walikuwa wanaingia,



"Kuna kengele ya hatari nimewekewa ukutani na polisi, kwamba chochote kibaya kikitokea niibonyeze hiyo kengele" Edward Sambo aliongea huku akionesha katika eneo ambalo kengele hiyo ipo, na hilo ndio eneo ambalo alisimama sana mpaka akapoteza fahamu kipindi alipovamiwa na BQ,



"sisi ndio tumekuja kwa ajili ya hiyo kengele" Askari mmoja kati ya wale watano, aliongea,



"mbona mmechelewa sana?" Sajenti Minja aliuliza kibabe,



"tulikuwa tunajua huku wapo Askari wengine" Askari alijibu,



"sawa, endeleeni kukariri matukio" Sajenti Minja aliongea huku akimbeba BQ mabegani,



"Mkuu sisi tuna gari, ungetupa tu huyo mtuhumiwa tumpeleke" Askari mmoja aliongea kwa utulivu,



"nyie ndio mmemkamata? mnajua nimeuza roho yangu kiasi gani mpaka huyu dada akawa katika hali?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwatazama, lakini wale askari walikuwa kimya, hawakuwa na cha kujibu,



"acheni upumbavu, muwe na akili ya kufikiria" Sajenti Minja aliongea huku akitoka na BQ aliyekuwa amemuweka begani, alitoka nae mpaka nje ambapo kulikuwa na gari walilokuja nalo wale polisi, alimkuta Askari mmoja akiwa amekaa upande wa dereva, Sajenti Minja akazunguka upande wa pili wa mbele na kufungua mlango, kisha akamtupia BQ,



"Mkuu mtuhumiwa hatakiwi kukaa mbele" Askari alizungumza kwa upole, Sajenti Minja hakujibu, alirudi mpaka katika mlango wa dereva,



"toka ndani ya gari" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama yule Askari,



"kwanini mkuu? Mimi si ndo dereva niliyekuja na gari hili kumkamata huyu dada muarifu?" Askari alimuuliza Sajenti Minja,



"mmekuja kumkamata ee? mbona mmechelewa? je mngemkuta huyu mzee wa humu ni marehemu tayari?" Sajenti Minja aliuliza,



"isingewezekana, maana kulikuwa na Askari wengine huku" Askari yule alijibu huku akitabasamu,



"bado mnaishi kwa kukariri tu?" Sajenti Minja aliongea huku akifungua mlango na kumvuta nje yule Askari, kisha akaingia ndani ya gari, na kipindi hicho Edward Sambo alikuwa akitoka ndani na Askari wengine ambao walikuwa wakishangaa mambo anayofanya Sajenti Minja,



"hao Askari waliopoteza fahamu wawekeni ndani ya gari" Sajenti Minja aliwaambia Askari,



"wote wamezinduka" Edward Sambo alijibu,



"nitakuja kukuona baadae, ngoja nimfikishe polisi huyu" Sajenti Minja alimwambia Edward Sambo, kisha akawasha gari na kuiondoa na kuwaacha Askari wengine wakimjadili, walihisi wamedhalilishwa.



"Muacheni, huyo ndivyo alivyo, uwa ana maamuzi ya kitata sana" Edward Sambo aliongea huku akirudi ndani na kuwaacha askari nje ya geti.



Sajenti Minja ndani ya gari aliendesha kwa mwendo wa kasi ili kuwahi kumfikisha kituoni BQ, ingawa pia alikuwa na wazo la kumpeleka hospitali, ila alihofia endapo angempeleka hospital na kisha mwanamke huyo akapata fahamu na kutoroka, basi hakuna mtu yoyote ambaye angemuelewa, kwa maana hiyo basi, Sajenti Minja aliona bora amfikishe tu polisi ili wamuone, sasa polisi wenyewe wataamua kama wampeleke hospital au wamuue,



"wao ndio wafanye maamuzi, ila mimi kuua mtuhumiwa siwezi" Sajenti Minja aliongea peke yake na kushika breki ghafla, alifika eneo la darajani na mvua zilikuwa zikinyesha, ikabidi Sajenti Minja apunguze kasi na aendeshe gari kwa umakini sana, kwa maana eneo hilo kukiwa na mvua na giza kama hilo, uwa ni hatari sana.



Sajenti Minja akaweka umakini katika barabara, na muda huo simu yake ilikuwa inaita, akaipuuza, hakutaka kuangalia hata mpigaji ni nani?

Wakati Sajenti Minja akiwa makini namna hiyo, BQ nae alikuwa akifungua macho, fahamu zilikuwa zikimrejea, alifungua macho na kuangalia mazingira aliyopo, akagundua yupo ndani ya gari, tena gari la polisi, alifanya hayo yote kwa umakini mkubwa bila hata kujitingisha. Ila BQ aliona kikwazo ni mkanda wa gari aliokuwa amefungwa, na Sajenti Minja alimfunga makusudi kwa kuwa alikuwa amezimia.



Wakati BQ akiwaza namna ya kumtoka Sajenti, aligundua wapo eneo la darajani, akaona ni eneo zuri sana, ila alihofia kujifungua mkanda kwa maana anaweza kudhibitiwa na Sajenti Minja, kwanza alishakuwa na mashaka kuhusu afya yake na kwa hali aliyonayo hasingeweza kupambana na Sajenti Minja, kingine alichoona ni hatari ni kwamba alihisi jeraha lake la kichwani likivuja damu, ni kweli damu ilikuwa ikitiririka kutoka kichwani na kushukia katika macho.



BQ akafikiria kwa sekunde chache, kisha akatabasamu, alikuwa ameshapata jibu,



"acha nijaribu" BQ aliongea kwa sauti na kumfanya Sajenti Minja ashtuke na kugeuka, hilo lilikuwa kosa, alipigwa ngumi ya shavu, kisha kwa kasi ya hatari BQ akaufungua mkanda wa gari, Sajenti Minja akaona njia nzuri kwa muda ule ni ku-lock milango yote ya gari, akafanya hivyo, kisha akapiga breki za gari, lakini alikuwa amechelewa, maana BQ aliinua miguu yake na kumpiga mateke mengi ya kichwani, Sajenti Minja alijitahidi kuzuia ila alishindwa, kisha BQ alipiga kichwa kioo cha gari, kioo kikapasuka, alafu BQ akajitupa nje ya gari, Sajenti Minja akasimamisha na kutoka huku bastola ikiwa mkononi, ila alichelewa, alikuta BQ akijirusha chini ya daraja na kuangukia katika maji, Sajenti Minja akakimbilia katika zile chuma za daraja na kumuona BQ akipiga mbizi kufuata mkondo wa maji, hapo Sajenti Minja akaona bora apige risasi tu, akalenga na kufyatua risasi nyingi mfululizo, BQ akazama chini ya maji na Sajenti Minja hakumuona tena, akakaza macho kwa dakika kadhaa ila hakumuona, akajishika kichwa huku akijilaumu, kisha akarudi ndani ya gari, na kukumbuka kuwa simu yake ilikuwa ikiita, akaangalia nani alimpigia, akakuta ni mkuu wa polisi, akaiweka simu katika siti ya pembeni, ila simu ikaanza kuita tena, na mpigaji ni yule yule mkuu wa polisi, Sajenti Minja akapokea simu,



"naam mkuu" Sajenti Minja aliongea baada ya kupokea simu,



"hongera sana, nasikia umemkamata yule dada na unakuja nae, tupo kituoni tunakusubiri hapa. Upo maeneo gani?" Mkuu wa polisi aliongea kwa furaha,



"nipo daraja la Dessa" Sajenti Minja alijibu kinyonge,

"sawa, fanya haraka basi, maana mpaka waandishi wa habari wanakusubiri shujaa wetu" Mkuu wa polisi aliongea kwa ucheshi,



"nakuja mkuu" Sajenti Minja alijibu na kisha mkuu wa polisi akakata simu, Sajenti Minja akaitupa simu yake kwa hasira, akawa anajiuliza ataenda kuwaambia nini wakubwa zake? je wataamini kuwa ni kweli yule dada ametoroka? je akiulizwa ni kwanini aliwaacha Askari wengine kwa Edward Sambo na kuondoka peke yake?



Hayo maswali yalianza kumtafuna kichwa Sajenti Minja, akaegemea usukani wa gari, ila alishtuliwa na honi za magari yaliyokuwa nyuma yake, akagundua amesimama katikati ya daraja ambapo ni barabarani, akawasha gari na kuiondoa mpaka mwisho wa daraja na kuisimamisha, bado majibu ya maswali ambayo alihisi ataulizwa, alikuwa hana jibu.



"acha niende, nitapambana uko uko" Sajenti Minja aliongea kisha akawasha gari na kuliondoa kwa mwendo wa kinyonge.



*****************



BQ alipozama wakati Sajenti Minja alipokuwa anapiga risasi, aliibuka baada ya dakika tano, alikuwa akipumua haraka haraka sana, akaendelea kuyakata maji kwa dakika tano nyingine mpaka alipoona Kuna sehemu tulivu kidogo, akaogelea mpaka ukingoni mwa lile bonde na kutoka nje, kwa kuwa ni usiku, hakuweza kulitambua eneo lile haraka haraka, ila lilionekana ni eneo lenye utulivu mkubwa sana, yaani utulivu wake ulitisha, ila BQ aliamua apumzike hapo kwa kuwa alijiamini .



BQ akaanza tena kuhisi kizunguzungu kutokana na kuogelea muda mrefu, pia kuvuja damu katika jeraha lake. BQ akasimama ili aondoke eneo hilo akidhani kuwa huenda akitembea mpaka mbele kidogo anaweza kujua yupo wapi.



BQ alipiga hatua mbili tu, Hali ya kizunguzungu ikaongezeka, akasimama ili apate muda wa kupumzika zaidi, ila alihisi kama kuna hatua za watu zikija kwa mbele yake, akajitahidi kuinua shingo, akawaona watu hao, walikuwa Askari kama wawili hivi, ingawa kulikuwa ni giza na pia BQ alikuwa na hali ya kizunguzungu, ila aliwatambua ni Askari, akili yake ikamwambia afanye kitu, akakusanya nguvu na kutaka kupiga hatua ili akimbie, ila kutokana na hali aliyonayo, na zile nguvu alizikusanya, ubongo ulishindwa kuhimili, akajikuta anapoteza nguvu na kuanguka chini, akajaribu kuinuka ila alishindwa, akajaribu tena, pia akashindwa, akaona hana ujanja, akalala chini chali, ubongo ukawa unalazimisha macho ayafunge, ila mwili ukawa unalazimisha macho yasifunge, na wale watu walikuwa wameshafika, BQ akawaangalia, hakukosea, ni Askari. Macho ya BQ yakakosa nguvu, akayafunga na kisha giza likamtawala.......







Wakati BQ akiwa bado anapambana na lile giza machoni, akaamua aulegeze mwili kwanza, hicho kilisaidia kidogo,



"huyu atakuwa mlevi mbwa au wale watu wanaoishi katika mazingira magumu" Alisikia wale watu wakimjadili,



"kweli kamanda, huoni hata nguo zake zilivyochafuka, amelowana, nywele zimekaa hovyo" Wale watu waliendelea kumjadili BQ,



"hawa ndio wanaobakwaga maeneo haya, alafu kukicha lawama tunapewa sisi watu wa usalama" Wale watu waliendelea kuongea,



"sijui amezimia au amelala, ebu jaribuni kumtingisha" Wale watu waliendelea kumuongelea BQ na kipindi hicho alikuwa akiwaza ni kweli hao watu hawajamtambua au wanaigiza,



"ebu tuwapigie simu polisi tuwape habari, usikute amekufa huyu" Wale watu waliongea na kufanya BQ ajiulize wale watu ni wakina nani? Kwanini waseme wawapigie polisi, ina maana wao sio polisi? BQ alijiuliza na mwisho akaone bora afungue macho ili awaone vizuri watu hao, kwa maana hata nguvu zilianza kumrejea.



BQ akafungua macho, kweli akakuta watu wanne wote wanamtolea macho, na wote walikuwa wamevaa gwanda, BQ akakaza macho zaidi katika giza lile na kugundua kuwa rangi ya zile gwanda zilikuwa za blue,



"sio polisi awa" BQ aliongea moyoni kisha akatoa tabasamu usoni,



"huyu sio mzima, huoni anacheka peke yake?!" wale watu waliongea huku wakimtazama BQ aliyekuwa akijiinua taratibu, kisha akasimama huku akiendelea kutabasamu,



"tumpige hata makofi, atakujaje kulala eneo la hatari hivi wakati Kuna vibao vingi vinavyotahadharisha watu kutokaa eneo hili nyakati hizi?" mmoja kati ya watu wale aliongea na kumsogelea karibu BQ, kisha akamtandika kofi kali la shavu, BQ akasimama na kumuangalia,



"umoja security guard" BQ aliongea aliposoma maneno yalioyoandikwa kati gwanda ya yule mtu, kisha BQ akatabamu na kuondoka bila kujishika hata shavu, wale wagambo wakabaki wakimtazama,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"awa wanawake wengine ni majini, yaani mnapiga halii wala hajishiki shavu, anacheka tu" Wale mgambo waliongea huku wakimtazama BQ aliyekuwa akitembea mwendo wa kupepesuka, bado alikuwa akihisi kizunguzungu.



******************



Baada ya muda Rais alirejea kutoka mariwatoni, mkononi alikuwa na chupa nyingine ya mvinyo, akakaa katika kiti,



"Habari unazonipa leo sio mchezo" Yule bwana mwingine aliongea huku akifurahi,



"dunia ina mambo mengi sana, we iangalie hivi hivi" Rais aliongea na kutabasamu,



"Tuendelee na story" Yule bwana alizungumza na kupiga funda moja la mvinyo,



"Tuendelee sasa, ila sasa nitamzungumzia Ray Charles tu" Rais aliongea na kukaa vizuri, kisha akaendelea,



"baada ya kuona ubongo wa Ray Charles haufanyi kazi kwa kasi ya kawaida, ilibidi apandikizwe kifaa cha umeme katika kichwa chake ili ubongo wake ufanye kazi kawaida, ila kifaa alichowekewa, kilifanya ubongo wake usiwe wa kawaida, akawa ana uwezo wa kufikiri mara nne zaidi ya uwezo wake aliokuwa nao hawali, kisha wakamchoma sindano za kutanua misuli ya mwili, ambazo zilimrejeshea hisia za mwili baada ya wiki, yaani akaanza kuchezesha hata viungo vya mwili, kifupi mwili wake ukawa unafanya kazi, ila hakuwa na nguvu kabisa, hata za kuinuka, hapo madaktari waliangaika nae sana kumrejesha katika nguvu zake, ila walishindwa, na mwisho wakaja na wazo la kumpachika tena vifaa vya umeme katika mwili wake, walitaka kumpachika kwa ndani ya mwili, ila ikaonekana watamchana sehemu nyingi sana za mwili, sasa wakatafuta wazo jingne, nalo ni kumvalisha chuma nyepesi ambayo itawekewa huo mfumo wa umeme, na nyaya chache zitaunganishwa katika sehemu muhimu za mwili, hilo wazo likapitishwa na Tammy Semmy. Wale wachina wakatengeneza hizo chuma kulingana na mwili wa Ray Charles, zoezi lilichukua miezi sita hili kupata kitu bora, kisha akavalishwa Ray Charles, akaweza tena kuamka na kutembea. Ila nguvu ndani ya vile vyuma ni nyingi sana, zimegawanyika katika sehemu kuu Tatu, kuna nyeusi, ambayo ni nguvu zake za kawaida, kuna kijani, ambayo ni nguvu za ziada, ambazo hutumia akienda kupambana na watu wenye silaha nzito, na pia Kuna nyekundu, hii hatujawahi kuitumia kwa kuwa inaweza kuleta athari kwake na kwa watu wote walio karibu nae, yaani uwa ile nguvu akizidishiwa, akili pia hufanya kazi nje ya uwezo wake, uwa kama chizi, anaweza hata kuua watu wote waliopo eneo hilo" Rais aliongea na kutema mate pembeni,



"kwa hiyo Ray Charles alipatiwa muda wa kuishi kwa namna hiyo?" Yule bwana mwingine aliuliza,,



"kitu kingine usichokijua ni kuwa Ray Charles ni immortal" Rais aliongea na kumuangalia yule bwana,



"immortal ni mtu wa aina gani, au ni nini?" Yule bwana mwingine aliuliza,



"mtu akishakuwa immortal, yaani uwa anaishi bila kufa, yaani hafi labda mumuaribu tu, na kuharibika ni sehemu moja tu ninayoijua mimi, yaani maisha ya Ray Charles yapo mikononi kwangu" Rais aliongea na kutabasamu,



"duh, imekuwaje wewe ndio uwe unayaendesha maisha ya Ray Charles?" Yule bwana mwingine aliuliza,



"OK, sikia. Baada ya Ray Charles kukamilika na kuwa mtu anayeweza kujongea na kufanya mambo mengine kwa ufanisi, ndipo hapo mapinduzi yakafanyika nchini, jeshi lilichukua nchi baada ya kugundulika kuwa Tammy Semmy alimuua Rais ili yeye awe Rais. na mwisho at siku Tammy Semmy aliuawa katika ndege ya RUSSIA AIRLINE, maiti yake ilikutwa ndani na ikarejeshwa nchini kwa ndege ya mizigo, hapo chama chetu kikavurugiga na mambo mengi yakatokea, mpaka jeshi lilipoamua kunipa kushika madaraka kwa muda, kisha ukafanyika uchaguzi na nikashinda moja kwa moja. Baada ya hapo serikali ya China ikanipa taarifa juu ya Ray Charles, waliniuliza wamuharibu au ninaweza kumtumia? Ikabidi nifunge safari mpaka China, nikamuona Ray Charles sasa, nilishtuka kwa kuwa hata mimi niliamini amekufa, ndipo nikaelezwa na kupewa video iliyoonesha namna ilivyokuwa mpaka Ray Charles akawa hivyo, nilichoulizwa ni kuwa nitamchukua au nitamuacha? Nikasema nitamchukua, wakaniuliza kwa lengo gani? Nikasema kwa lengo alilokuwa kuwa nalo Tammy Semmy, yaani awe mlinzi wangu binafsi. Ila pia Ray Charles aliulizwa anataka aendelee kuishi chini ya mamlaka yangu? alijibu ataishi chini ya mamlaka yangu ila sio kwa ajili yangu, alipotakiwa aifafanue hiyo kauli yake, alisema kuwa ataishi kwa ajili ya familia yake , yaani mke na mtoto wake mdogo wa miaka sita, akaenda mbele zaidi na kusema hasingekuwa na familia, hasingetaka kuendelea kuishi huku amefungiwa machuma mwilini, nimesimama Basi nikapewa maelezo jinsi ya kumtumia na namna ya kumuendesha. Baada ya hapo nikakabidhiwa nyaraka muhimu za Ray Charles na nilichofanya, ni kumuamrisha Ray Charles auwe kiwanda chote kilichomtengeneza, akaua, kisha tukaondoka. Lengo lile la kumuamrisha kuua kiwanda kazima, lilikuwa kwa ajili ya siri hii nibaki nayo peke yangu, pia nilitaka kujua uwezo wa wa Ray Charles wa kupambana.



Baada ya hapo tulirudi huku kwa kutumia ndege ya Rais, ambaye ndio mimi, niliamua kumchukua na ndege yangu moja kwa moja ili tusipate usumbufu wa kukaguliwa uwanja wa ndege, na isitoshe katika iko kiwanda kulikuwa na uwanja wa ndege, kwa hiyo ndege ilitufuata hapo hapo, tukaondoka mimi na Ray Charles, huku kila mmoja akiwaza Lake, mimi nilichokuwa nakiwaza ni familia ya Ray Charles, sijui Ray Charles alikuwa akiwaza nini? Kwa hiyo nilivyofika nchini, kwa siri kubwa niliwatuma usalama wa Taifa wamteke mtoto wa Ray Charles bila Ray mwenyewe kujua, kwa sababu nilimzuia Ray kuonana na familia yake kwa muda. Walipomteka yule mtoto, nilimpandikiza mlipuko katika kifua chake, yaani alipasuliwa yule mtoto na kuwekewa bomu dogo tu, kama punje ya harage, kisha nikawaagiza wamrudishe kwa mama yake, kisha video ya lile tukio nikaliweka katika flash, nikamuonesha Ray Charles, alitaka kupaniki, ila nilikuwa na remote ya lile bomu alilopandikizwa mwanae, nikamwambia ukinifanyia chochote kibaya, namlipua mwanao, akawa mpole, na nikamwambia kuanzia sasa utaishi kwa ajili yangu na sio kwa ajili ya familia yako, hakuleta ubishi, na ndio maana mpaka leo unaona nipo nae" Rais alimaliza kuongea,



"na yule tuliyemzika na serikali ikasema ni Ray Charles, ni nani?" Yule bwana mwingine aliuliza,



"ni mwili wa mtu tu tulimuua na kisha tukauharibu vibaya kiasi kwamba alishindwa kutambulika, familia tukawapa majibu ya uongo kutoka hospital, wakaridhika tulipowapa na fungu kubwa la rambirambi kutoka serikalini, wakakaa kimya, wakazika mwili ule" Rais alijibu na kutabasamu,



"aisee, leo umenifungua ubongo, hata sikuwahi kuhisi kitu kama hiki" Yule bwana mwingine aliongea,



"hayo mambo nayajua mimi tu, wewe ni wa pili" Rais aliongea huku akitabasamu,



"dah, haya sasa niambie ulichoniitia ndugu yangu" Yule bwana mwingine aliuliza,



"hapa nimekuita kwa ajili ya BQ, yule mwanamke muuaji anayetafutwa na polisi" Rais aliongea na kumtazama yule bwana,



"mimi tena nipambane na BQ?, Ray Charles si yupo?" Yule bwana mwingine aliuliza kwa mshangao,



"sio kupambana kwa ngumi au mateke, nataka nikupe wizara ya katiba na sheria, maana tangu ameuawa yule mjinga niliyempa ile wizara, naona mambo bado hayajakaa sawa katika wizara hiyo, nataka umdhibiti BQ na ile mikataba yake" Rais aliongea na kumtazama yule bwana mwingine,



"Sasa jamaa yangu, mimi nitamdhibiti vipi? yaani nitafanyaje?" Yule bwana mwingine aliuliza huku akimuangalia Rais,



"hujui? wewe sheria si unaijua, tumia njia zozote kumdhibiti, lengo langu ni kumpata na auawe" Rais aliongea,



"mbona unatumia nguvu kubwa kupambana na mtu anayeidai serikali? kama ana mikataba so ipitiwe kama Kuna haki apewe" Yule bwana mwingine aliongea,



"ana haki, tena asilimia themanini, ila sasa, lile eneo ambalo ndio analotaka apewe, ni eneo la serikali ambalo ilipewa ile kampuni iliyomtengeneza Ray Charles, tena walipewa kwa mkataba wa miaka kumi, wafanye chochote kisha walirudishe lile eneo kwa Tammy Semmy, sasa Tammy Semmy alishakufa, hata wale wachina wameshakufa, kwa hiyo nilichofanya ni kufungua akaunti mpya ya benki kwa kampuni ile ile ya wachina, kwa hiyo serikali inaingiza pesa za kutumia yale majengo ya wizara yaliyojengwa na wale wachina katika eneo lile, serikali iliyakodi kwa msukumo wangu mie, kisha makubaliano yalifanyika kwa kuwaleta wachina feki walioingia makubaliano na viongozi kuhusu kodi za kuweka wizara hii ya katiba na sheria, kwa hiyo basi natumia nguvu kubwa huyu mwanamke hasipate haki yake kwa sababu pale napamiliki mimi ila kwa mgongo wa kampuni hewa, yaani haipo, kwa hiyo endapo BQ atafanikiwa kupachukua, kwanza nitakosa mapato, pia serikali inaweza kuchimbua sana mmiliki wa hili jengo, nikaonekana ni mimi, hapo walipa kodi hatoweza kunielewa, yaani wananchi" Rais aliongea na kumuangalia yule bwana mwingine aliyekuwa amejishika kidevu huku akionekana kutafakari,



"wewe ni rafiki yangu sana, nimeona hii ndio njia sahihi ya wewe kutajirika na mimi kulinda mali yangu, isitoshe mimi na wewe tumejuana muda mrefu, najua hata tabia tunaendana" Rais aliendelea kumshawishi yule bwana mwingine,



"mimi nitanufaikaje hapo?" Yule bwana mwingine aliuliza,



"kodi ya lile jengo ni million mia moja hamsini kwa mwezi, kila mwezi nitakupa million ishirini na tano katika kila kodi ya mwezi, na mshahara wako kama waziri, badala ya million tano, nitakupa million kumi" Rais aliongea na kumtazama yule bwana,



"hakuna shida jamaa yangu, sasa huo uwaziri utanipaje wakati mimi sio mbunge wala sio mfanyakazi wa serikali? " Yule bwana aliuliza,



"hiyo kazi niachie mimi, kesho nakupa ubunge wa kiteuliwa, kesho kutwa unaapishwa, alafu siku inayofuata nakupa uwaziri" Rais aliongea kwa utulivu,



"haina shida jamaa yangu" Yule bwana mwingine aliongea kwa furaha,



"hizi habari usimwambie mtu hii habari, yaani nataka huu uteuzi uwe kama wa kushtukiza, hata ujifanye hujategemea kwa huu uteuzi" Rais aliongea kwa utulivu,



"Sawa mkuu" Yule bwana mwingine alijibu,



"nadhani wewe ondoka tu, haya mambo mengine yatafuata" Rais aliongea huku akisimama na kumpa mkono yule bwana mwingine, yule bwana mwingine akapokea ule mkono wa kuagana, kisha akaondoka kwa furaha, alishayaweza maisha kimzamzaa tu, aliuona utajiri mkubwa mbele yake, kiasi kwamba akawa anatabasamu kila akipiga hatua.



**************×**



Sajenti Minja alifika kituo cha polisi na ile gari ya polisi, akakuta waandishi wa habari na watu wengine pamoja na Askari wenye vyeo zaidi yake wakimsubiri kama shujaa.



Waandishi wa habari walishaanza kupiga picha gari aliyopanda Sajenti Minja, kipindi hicho Sajenti Minja alikuwa bado amekaa ndani ya gari huku akiwaza atawaambia nini wakuu wake, alikaa ndani ya gari muda mrefu mpaka watu wakapata wasiwasi. Mwisho Sajenti Minja akatelemka peke yake, watu wakawa wanangoja kama ataenda upande wa pili wa mlango wa gari ili amtemleshe mtuhumiwa, lakini ilikuwa tofauti, Sajenti Minja alienda moja kwa moja mpaka mbele ya mkuu wake ambaye bado alikuwa akishangaa hali ya Sajenti Minja,



"vipi?" Mkuu wa polisi alimuuliza Sajenti Minja,



"ametoroka" Sajenti Minja aliongea kwa sauti ya chini,



"unasemaje Minja?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"Yule mwanamke ametoroka" Sajenti Minja aliongea tena na kumfanya mkuu wake awaangalie Askari kadhaa waliokuwepo pale,



"kamateni hii mbwa na muiweke selo" Mkuu wa polisi aliongea kwa mamlaka huku Akiwatazama wale Askari, wale Askari wakamzunguka Sajenti Minja, Sajenti Minja akanyoosha mikono mbele, ishara ya kukubali kufungwa pingu, Askari wakamfunga pingu Sajenti Minja, wakaanza kumpeleka selo, kichwani Sajenti Minja alichokuwa anafikiria ni kifungo tu, kwa kosa kama lake la kuambiwa amemtorosha mtuhumiwa, lazima afungwe, hakwepeki hiyo........





Sajenti Minja akapelekwa selo na kuwaacha wakubwa zake wakijadiliana, wote walionekana kutopendezwa na kitendo cha Sajenti Minja, na wote waliamini Sajenti Minja amemtorosha yule mwanamke, ila hawakujua sababu kwanini Sajenti Minja amtoroshe yule mwanamke?.



Baada ya majadiliano ya nusu saa, wale polisi walitawanyika, kila mtu akaelekea panapo muhusu, mkuu wa polisi alirudi ofisini kwake, hukutaka kuongea hata na waandishi wa habari, kichwa chake kilishavurugika kabisa, hakikukaa sawa kwa muda huo.



Mkuu wa polisi akaingia ndani ya ofisi yake, kisha akavua kofia na kuiweka juu ya meza, akaanza kufikiri huku akizunguka mule ndani ya ofisi yake, alifanya hivyo kama dakika kumi, kisha akachukua simu na kupiga namba anayoijua yeye,



"bado upo zamu?" Mkuu wa polisi aliuliza kwa mamlaka,.



"ndio mkuu" Sauti ya upande wa pili ilijibu kwa utii,



"mlete Sajenti Minja ofisini kwangu, sasa hivi" Mkuu wa polisi aliongea kisha akakata simu, alafu akavuta kiti na kukaa, kisha akanywa maji yaliyokuwa katika chupa, na kisha akavaa kofia yake, akatulia akimsubiri Sajenti Minja.



Baada ya dakika mbili mlango wa ofisi yake uligongwa, akaingia Askari mmoja aliyemtanguliza Sajenti Minja mbele huku mikononi akiwa na pingu,



"kwa hiyo hata alipokuwa selo hamkufungua pingu?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"ndio mkuu" Askari yule alijibu,



"na nyie mkaona sawa tu mtu kuwa na pingu ndani ya selo?" Mkuu wa polisi akaendelea kuongea na kumfanya yule Askari aliyemleta Sajenti Minja atoe funguo mfukoni ili amfungue Sajenti Minja,



"muache tu, sijasema umfungue " Mkuu wa polisi aliongea na kumfanya yule kijana arudishe funguo mfukoni,



"nipishe kidogo, kuna maswali nataka nimuhoji Minja" Mkuu wa polisi aliongea na kumfanya yule Askari apige saluti na kutoka nje ya ofisi ya mkuu wa polisi, ndani akabaki Sajenti Minja na mkuu wa polisi.



Mkuu wa polisi akamuangalia Sajenti Minja kwa muda, kisha akajikooza kusafisha koo,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"kwanini umemtorosha yule mwanamke?" Mkuu wa polisi aliuliza na kumtazama Sajenti Minja,



"sijamtorosha" Sajenti Minja alijibu kwa utulivu,



"acha upumbavu Minja, umeondoka nyumbani kwa Edward Sambo ukiwa wewe na mtuhumiwa tu, hukutaka kumpakia Askari mwenzako hata mmoja, alafu unafika peke yako kituoni na kusema mtuhumiwa ametoroka, ametorokaje?, yaani atoroke mikononi kwako? hapana, sio rahisi hivyo, ni lazima utakuwa umemtorosha tu" Mkuu wa polisi aliongea na kumfanya Sajenti Minja aangalie chini huku akitafakari.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog