Search This Blog

Sunday 20 November 2022

THE OTHER HALF - 2

 





    Simulizi : The Other Half

    Sehemu Ya Pili (2)













    “Ni bora hata tungekuwa tunazeeka haraka pekee.. Lakini ubaya ni kwamba ubongo wetu unaweza kuchanganyikiwa katika kung’amua uhalisia wa muda kiasi kwamba unaweza kupata shinikizo na kitu kibaya zaidi kikatokea.!” Cindy akajibu huku anageuka na kuanza kutembea.







    Na wenzake nao wakamfuata.











    “Kitu kibaya?? Kama kipi?” Kanali akauliza.











    Magdalena akadakia na kujibu.







    “Kanali, nadhani wote tunafahamu kuwa muda ni tofauti, yaani interval baina ya matukio mawili… na ubongo wetu una uwezo wa kuhisi hii interval na pia hii inaathiri fiziolojia ya mwili na mfumo…  kwa kuwa tumezaliwa kwenye Dunia ya kawaida ubongo wetu tayari umeweka namna ambayo unahisi interval hizi na kuoanisha na fiziolljia na mabadilikk ya mfumo wa mwili… kwahiyo tukiwa humu kwa kuwa muda unaenda kasi zaidi maana yake pia kutakuwa na mabadiliko ya kimwili ya kasi zaidi, mfano kuzeeka… lakini ubongo wetu haujawahi kuhisi inter



    [22:28, 4/8/2017] ?+255 718 096 811?: interval za humu kwa kuwa hatunazaliwa humu… hii unaweza kusababisha ubongo kupata msongo na shinikizo kwa kutumia oksojeni nyingi zaidi na glucose nyingi zaidi ili kuhimili hali hii mpya ya intervals na mabadiliko ya fiziolojia… sasa hii ndio itatuletea balaaa… ubongo unaweza kufeli muda wowote.!”











    Magdalena akawaeleza wenzake kitaalamu kabisa na kwa umahiri wa hali ya juu. Cindy akaitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubali maelezo aliyoyatoa.











    “Kwahiyo tunatakiwa tufanye tulichokuja kukifanya haraka sana” Cindy akaongea huku anazidi kutembea kwa haraka na wenzake wakimfuata.











    “Na haujatuambia mpaka sasa ni nini hasa tunatakiwa kukifanya humu?” Salim akauliza.











    “Kitu cha kwanza kabisa tunatakiwa kutafuta mlango wa kikundi cha watu wanaojiita The 46” Cindy akajibu kwa kifupi.











    “Ndio kina nani hao?” Salim akauliza kwa shahuku.





    THE OTHER HALF











    SEASON 1 – LEGEND OF ANABELLE



















    “…wazo! Yaani ‘idea’, ndio kirusi kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Ubongo unapopata wazo, na wazo hilo likichipua ndani yako kamwe huwezi kulitoa akilini. Wazo lolote baya au zuri likipata nafasi ya kuchipua kwenye ubongo, wazo hilo litakutesa na hautapata raha mpaka pale siku utakapolitimiliza.







    Ukitaka kumjenga binadamu, mpe wazo… kisha lichochee hili wazo lichipue ndani yake. Wazo dogo kiasi cha punje ya mchanga Lina uwezo wa kukua na kubadili ulimwengu. Ni wazo dogo lililochipua ndilo lilisababisha mwanafizikia Newton kuvumbua nguvu za uvutano na hivyo kuwa mwanzo wa msingi wa sayansi ya fizikia. Ni wazo dogo lililochipua, ndilo lililo mfanya Steve Jobs kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa teknohama.







    Unahitaji wazo dogo tu, kisha unalichochea lichipue, kisha unaweza kabisa kuubadili ulimwengu.











    Pia ukitaka kumuangamiza binadamu, mpandikizie wazo hasi. Kisha lichochee likue. Wazo hili likimea, linakuwa baya kama kirusi ambacho hawezi kulitoa akilini mwake. Huitaji bunduki wala upanga, kitu pekee unachohitaji kumuangamiza binadamu na ulimwengu, ni wazo dogo tu lililo hasi.!











    EPISODE 8







    Book Of Codes























    MAHALI FULANI PA SIRI JIMBONI VIRGINIA, MAREKANI















    Makamu wa Rais David Logan alikuwa anasikia sauti kwa mbali zikimuita kumuamsha. Alikuwa hajafahamu bado yuko wapi au alikuwa amepoteza fahamu kwa muda gani. Kitu pekee ambacho alikuwa anakikumbuka ulikuwa mlipuko baada ya kuingia kwenye gari alipotoka chuo Kikuu cha Stanford.











    “Mr. Vice President! Mheshimiwa… mheshimiwa unanisikia??”











    Logan alisikia kwa mbali hii sauti inamuita na kumuuliza kwa kurudia rudia. Pia aligundua kuwa mtu huyu alikuwa ameshika kijitochi kidogo cha kidaktari mkononi mwake anamfunua macho na kumuangalia kwa kummulika na tochi.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    “Mr. Vice President… mheshimiwa? Unanisikia mheshimiwa?” Ile sauti ikaendelea kumuita.











    “Niko wapi hapa?” Makamu wa Rais David Logan akajibu kwa sauti ya chini huku akiugulia maumivu aliyokuwa anayasikia mgongoni.







    Kitu pekee ambacho alikuwa anakikumbuka ulikuwa ni mlipuko mkubwa baada ya kupanda kwenye gari na msafara kuanza kuondoka. Baada ya hapo alikuwa hakumbuki tena ni nini kilitokea.











    “Niko wapi hapa?” Logan akauliza tena.











    “Mr. Vice President upo site namba SQ1204 Virginia!” Yule mtu aliyekuwa anamuamsha akaongea.











    “Kuna maana gani kunileta hapa?” Logan akajibu huku anaamka kutoka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa.











    Site namba SQ1204 ni moja kati ya maeneo ya siri 41 ambayo Rais wa Marekani anaweza kufichwa endapo kuna tishio kubwa juu ya maisha yake.



    Kitendo cha yeye kuletwa mahali hapa ilimaanisha kwamba kulikuwa na hali ya hatari hasa juu ya maisha ya Makamu wa Rais.











    “Mr. Vice President… tumekuleta hapa kwa kuwa nadhani umefahamu shambulio lililotokea wakati tunatoka Chuo Kikuu cha Stanford. Kutokana na udharura wa hali iliyopo hatiwezi kukurudisha Ikulu sasa hivi… tunaamini sehemu salama zaidi ya wewe kuwepo ni hapa!” Yule mtu ambaye baada ya Logan kuinuka akagundua kuwa alikuwa ni afisa wa Secret Service.







    Alikuwa amelazwa kwenye chumba fulani hivi chenye milango ya vioo na chumba kilikuwa na muonekano kama chumba cha hospitali.



    Alipoangalia ng’ambo ya chumba hiki, kulikuwa na chumba kingine ambacho kinafanana kabisa na hiki na kwenye chumba hicho kingine alikuwa amelazwa Mzee Caleb.











    Logan akashituka kidogo na kuanza kusimama huku anavaa vizuri koti lake la suti.







    “Mheshimiwa nadhani ungendelea kupumzika kidogo!” Yule ofisa wa Secret Service akaongea huku anajaribu kumlaza tena Logan kitandani.











    “Kijana… nashukuru kwa kujali, lakini niko sawa na nina nchi inayohitaji niiongoze… kwahiyo tafadhali sana siwezi kulala” Logan akaongea kwa kujiamini huku anavaa vyema koti lake la suti na kuanza kutoka kwenye kile chumba.











    Akatoka huku yule afisa wa Secret Service pamoja na wengine waliokuwa wamesimama mlangoni nao wakimfuata.











    “Wengine wako wapi? Rupert na Naomi?” Logan akauliza.











    “Wako salama mheshimiwa… wako chumba cha kupumzika masuala wanaongea na maafisa wengine wa usalama.!” Afisa wa Secret service akajibu.











    “Nahitaji kuungana nao!” Logan akaamuru.











    Maafisa wa Secret Service wakamuongoza moja kwa moja mpaka kwenye chumba fulani kama sebule hivi ambapo aliwakuta Mwanamama Naomi Cole mshauri wa Rais kuhusi Usalama na James Ruppert Mkurugenzi wa CIA wakiwa wamezungukwa na maafisa wengine wa usalama wakiwa wanajadili suala fulani hivi.











    Baada ya Makamu wa Rais Logan Kuingia wote wakasimama na baada ya yeye kuketi wote nao wakaketi.











    Naomi na Ruppert walikuwa pamoja na Logan kipindi shambulio linatokea Stanford lakini walikuwa kwenye gari tofauti.



    Yaani Logan na Naomi walipanda gari moja na Ruppert na Mzee Caleb walipanda gari lingine kwenye msafara.











    Kwa hiyo kitendo cha Logan na Mzee Caleb kuumia mpaka kupoteza fahamu hii ilimaanisha kuwa magari yote hayo mawili kwenye msafara yalishambuliwa. Lakini ajabu ni kwamba, Naomi na Ruppert hawakuwa na majeraha yoyote na walionekana wako salama salimini.











    “Nini kinaendelea?” Logan akauliza kwa uso wa kuchanganyikiwa mara baada ya kuketi.











    “Tumeshambuliwa mkuu.. Mara tu baada ya kutoka Stanford!” Ruppert akaanza kueleza.











    “Mmefahamu kwa nini tumeshambuliwa au ni nani ametekeleza hili shambulizi?”











    “Hatujafahamu hasa ni nani amefanya hili shambulizi lakini dalili inaonyesha kwamba waliofanya shambulizi walikuwa wanamlenga Mzee Caleb!” Naomi akaongezea.











    “Kwa nini mnaamini kuwa alilengwa Mzee Caleb?” Logan akauliza kwa mshituko.











    “Mr. Vice President… taarifa tulizozipata mpaka sasa kutoka FBI inaonyesha kwamba kombora lilirushwa kutoka ghorofa ya kirani na msafara ulipokuwa na Kombora hili lililengwa kwenda kwenye gari ambalo nilipanda mimi Mzee Caleb… gari ambayo mlipanda wewe na Naomi lilipinduka kutokana na nguvu ya mlipuko tu lakini silo ambalo lililengwa.!” Ruppert akaeleza.











    “Na kwa nini uhisi walimlenga Caleb na sio wewe Mkurugenzi wa CIA?” Logan akauliza.











    “Mheshimiwa ni kwasababu baada ya mlipuko kutokea na mambo kuvurugika kulitokea jaribio la watu wasiojulikana kumteka Mzee Caleb… Bahati nzuri maafisa wa Secret Service waliwahi kuwadhibiti na kumuua mmoja na mwingine alitoroka japo alijeruhiwa.!” Ruppert akafafanua zaidi.















    “Na maiti ya huyo mmoja aliyeuwawa tuko nayo hapo nadhani ni vyema ukiiona!” Naomi akaongezea.











    Baada ya Naomi kusema hayo wote wakainuka na kuelekea upande ule ambao kulikuwa na vile vyumba vya milango ya vioo vyenye mandhari ya hospitali.



    Hapa kulikuwa na vyumba vitano, chumba kimoja ndicho kile ambacho alilazwa Makamu wa Rais Logan, chumba kinachofuata alikuwa amelazwa Mzee Caleb na vyumba viwili vilivyofuatia vilikuwa tupu na chumba cha mwisho cha tano ndicho ulilazwa mwili wa huyo mtu aliyeuwawa na Secret Service.











    Mwana usalama mmoja akafungua mlango baada ya kufika nje ya mlango, kisha wakaingia ndani ya chumba.











    Juu ya kitanda pale chumbani ulikuwa umelazwa mwili wa mwanaume mwenye kuonekana kama mwenye miaka kati kati ya thelathini hivi.



    Mwili wake ulikuwa umejengeka hasa kimazoezi na alionekana alikuwa mkakamavu hasa. Alikuwa na majeraha mawili ya risasi kifuani.











    “Mr. Vice President kuna kitu nataka ukione!” Ruppert akaongea huku anazunguka upande wa pili wa ile maiti.







    Ruppert akanyoosha mkono wake na kuipindua shingo ya yule maiti ili kuonyesha sehemu ya nyuma ya shingo yake.







    Alikuwa na tatoo kubwa imeandikwa,















    ‘SANCTA CEDES’























    “Ni nini hii?” Makamu wa Rais David Logan akauliza.











    “Hatujajua hasa ni nani huyu mtu na mwenzake aliyekimbia. Lakini tunachokifahamu ni kwamba lengo lao la kushambulia msafara ilikuwa ni ili waweze kumteka Mzee Caleb.!” Ruppert akajibu.















    Kabala hawajaongea zaidi, kupitia ile milango ya vioo wakamuona  kuna afisa wa Secret Service alikuwa anakuja mbio kuja kwenye chumba walichopo.















    “Mzee Caleb ameamka!” Yule afisa aliyekuwa anakuja huku anakimbia aliongea baada ya kufika kwenye chumba walichopo Logan na Wenzake.











    Wote kwa pamoja wakatoka nje ya chumba kwa haraka kuelekea kile chumba cha pili ambacho alikuwa amelazwa Mzee Caleb.











    Walipoingia walikuta kuna daktari ambaye pia ni afisa usalama alikuwa anampa maelezo Mzee Caleb Kuhusu nini kimetokea na wako mahali gani hapo.











    “Unajisikiaje Mzee?” Logan akamsalimu mara tu daktari aliposogea pembeni.











    “Kizungu zungu tu bado kwa mbali!” Mzee Caleb akaongea huku akakaa vizuri kitandani kwa kuninginiza miguu.











    “Daktari amekueleza kama shambulio lilikuwa linakulenga wewe?” Ruppert akamuuliza.











    “Mimi?” Mzee Caleb akaongea kwa mshtuko mkubwa hasa.











    “Ndio, wewe Mzee! Shambulio zima lilipangwa ili waweze kukudhuru au kukuteka wewe!” Ruppert akaongezea.











    “Ni akina nani hao?” Mzee Caleb akauliza.











    “Tumefanikiwa kumuua mmoja wao, mwingine au wengine maana hatujui wako wangapi walifanikiwa kukimbia!” Ruppert akaeleza tena.











    Mzee Caleb hakusema chochote akabaki amejiinamia tu kama kuna kitu fulani anatafakari.











    “Unaweza kufahamu kwa nini walikulenga wewe Mzee?” Logan akauliza.











    “Hapana… sijui hata hao watu ni akina nani!” Mzee Caleb akajibu huku bado amejiinamia.











    “Mmoja tuliyemuua shingoni ana tatoo imeandikwa ‘Sancta Sedes’! Unaweza kujua lolote kuhusu hilo?” Naomi ambaye alikuwa amekaa kimya muda wote huu akaongea hatimaye.











    Mzee Caleb akainua kichwa ghafla kwa haraka baada ya Naomi kutaja ‘Sancta Cedes’.











    “Umesema tatoo imeandikwaje?” Mzee Caleb akauliza tena kwa mshangao mkubwa zaidi.











    “Sancta Cedes” Naomi akajibu.











    “Mungu wangu!” Mzee Caleb akajiinamia kwa woga.











    Wote wakatazamana kwa pamoja kisha wakamuangalia Mzee Caleb.











    “Nini Mzee! Unafahamu nini kuhusu Sancta Cedes?” Logan akamuuliza.











    “The Holy Chair” Mzee Caleb akajibu kwa sauti ya chini huku bado amejiinamia.











    “Umesemaje Mzee?” Ruppert akauliza kana kwamba hakusikia.











    “Sancta Cedes! Ni The Holy Chair!” Akaongea huku anainua uso.















    “The holy chair?? Una maana gani?” Makamu wa Rais Logan akauliza kwa mshangao.















    *”Vatican!”* Naomi akadakia na kujibu kwa kifupi.











    “Ati nini?” Logan akauliza kwa mshangao mkubwa.











    “Makazi ya Papa wa Kanisa au kwa maneno mengine mamlaka aliyonayo, yaani Vatican… ndiye pia inaitwa ‘The Holy Chair’.” Naomi akafafanua zaidi.http://pseudepigraphas.blogspot.com/











    “Vatican??” Logan akashikwa na bumbuwazi alishindwa afikiri vipi kitafsiri maana ya hii anachokisikia au aoanishe vipi na matukio yanayoendelea duniani.



    “Vatican wanahusika vipi na hawa watekaji?” Hatimaye Makamu wa Rais akajikuta anauliza.











    “Unauliza swali ambalo sio sahihi Mr. Vice President! Swali sio Vatican wanahusika vipi na hawa watu… swali la msingi zaidi ni namna gani hawa wapiganaji wa kuzimu wameweza kurudi juu ya uso wa dunia?” Mzee Caleb akaongea huku anainuka kutoka kitandani.











    “Una maana gani kuwa wapiganaji wa kuzimu?” Safari hii ni Ruppert akauliza swali.











    “Kikundi cha Sancta Cedes, mara ya mwisho kuwepo duniani ilikuwa ni mwaka 1490… baada ya hapo wapiganaji wake wote waliteketezwa kwa amri ya Papa kutoka Vatican ingawa ni Vatican hiyo hiyo ililiunda karibia miaka 150 nyuma kabla ya siku hii UA kukiteketeza”







    Mzee Caleb aliongea huku anavaa koti kana kwamba anataka kuondoka.











    “Wanataka nini hasa?” Naomi akamuuliza Mzee Caleb.











    “Sifahamu… hata mimi niko gizani kama wewe lakini nina kila sababu ya kuamini kuna mahusiano fulani na matukio ya miji kutwaliwa na kugeuzwa Anabelle!” Mzee Caleb akajibu.











    “Tunafanyaje kukabiliana nao kama wako wengi wengine?” Naomi akauliza tena.











    “Sina jibu la hilo pia! Lakini nadhani naweza kujua tuanzie wapi!”











    “Wapi?”











    “Book of Codes” Mzee Caleb akajibu kwa ufupi.











    “Ni kitu gani?” Logan akadakia na kuuliza swali.











    “Nahitaji kwenda Maryland sasa hivi” Mzee Caleb hakujibu swali badala yake akatoa amri.











    “Mzee huwezi kuondoka hapa… tuko eneo la siri ambalo linatumika kumuhifadhi Rais na Makamu wa Rais wakati wa hatari kubwa dhidi ya maisha yake… hatuwezi kutoka humu mpaka tupewe taarifa ya tathimini huko nje kwamba hali mi shwari!” Ruppert akaeleza.











    “Sio lazima Mr. Vice President au nyinyi mfuatane nami… naweza kwenda mwenyewe.!” Mzee Caleb akaongea huku anaaza kuondoka.











    “Huwezi kwenda mwenyewe Mzee muda mchache uliopita wamejaribu kukuteka! Hauko salama tena huko nje” Naomi akamuonya Mzee Caleb.











    “Mpeni ulinzi!” Logan akaongea kwa kukereka haswa.











    “Mr. Vice President, hawa watu waliotuvamia ni wahuni… naomba ruhusa yako nimpe ulonzi wa ‘wahuni’ Mzee Caleb ili wakakabiline wahuni kwa wahuni kama wakijaribu tena kumteka Caleb.” Ruppert akaongea kwa hasira akimuangalia Makamu wa Rais Logan.







    “OK! Nimeruhusu!” Logan akajibu kwa kifupi huku akienda kukaa kwenye kiti pembeni ya kitanda mule ndani.











    Ruppert akatoa simu na kubofya bofya namba na kisha akapiga simu makao makuu ya CIA, Langley Idara maalumu ya SAD (Special Activities Division).











    “Namuomba Ethan na kikosi chake mara moja!” Ruppert akaongea mara baada ya simu kupokelewa.



    THE OTHER HALF















    SEASON 1 – LEGEND OF ANABELLE























    “…mara zote linapotokea jambo ulimwenguni au katika maisha binafsi, watu wanatulia na kusibiri. Kusubiri muda sahihi wa kufanya maamuzi, muda sahihi wa kuipata fursa, muda sahihi wa kutatua changamoto… lakini uhalisia ni kwamba hakuna muda sahihi katika maisha, hakuna muda sahihi ambao fursa itajitokeza, hakuna muda sahihi ambao utafaa kufanya maamuzi. Unatakiwa kuutengeneza muda sahihi, kutengeneza muda sahihi na kuitengeneza fursa, kutengeneza muda sahihi na kuchukua maamuzi. Huu ndio mtazamo na fikra za watu walioubadilisha ulimwengu zilivyokuwa. Hawasubiri fursa, hawasubiri muda sahihi. Wanatengeneza muda sahihi. Wanatengeneza fursa. Wanafanya maamuzi, hata pale ambapo dalili zote zinashawishi wasifanye maamuzi.!











    …hii ndio sababu kwanini unatakiwa kutokuridhika na kung’ang’ania kile tu unachokijua… ukiendelea kujua kile tu unachokijua, ufahamu wako haupanuki. Ukiendelea kufanya pekee kile ulicho na ustadi nacho, maarifa yako hayaongezeki. Ili tuwe na ulimwengu ulio bora, kila siku tunapaswa kufanya gunduzi na kujifunza vitu vipya. Kuna maarifa ambayo kwa sasa ulimwengu unaweza kudhani hauyahitaji, lakini ipo siku ndiyo yatakayo kuwa na tija ya kuuokoa ulimwengu.







    Ulimwengu, na watu wote tuliomo ndani yake. Tunatakiwa kuwa tayari muda wowote.











    Ipo siku ambayo tutaiona si muda sahihi, siku ambayo haina fursa dhahiri, na ndiyo siku hii ambayo maarifa haya yatatuinua kutengeneza fursa, kutengeneza muda sahihi na kuukokoa ulimwengu kutoka mikononi mwa watoto wa Anabelle 1 (Maldives)…”











    EPISOSE 9







    Book of Codes































    ROME, VATICAN CITY











    Giza kinene kilichoshiba hasa kilikuwa kinaashiria labda tayari ilikuwa ni saa Tisa usiku.







    Watu sita waliokuwa wamevalia majoho meusi walikuwa wamesimama katikati ya eneo la wazi la mji wa Vatican linalojulikana kama Saint Peter’s Square.











    Namna walivyokuwa wamevaa, ilikuwa ni katika namna ambayo ilifanana kabisa na wale watu wa Rabat, Morocco.



    Majoho meusi, miguuni wako pekupeku wakionekana wazi kabisa kuwa wametembea umbali mrefu sana. Pia shingoni walikuwa na tatoo iliyosomeka “SANCTA CEDES”.



    Tofauti na wale watu wa Rabat, Morocco hawa hawakuwa wamebeba sanduku, walikuwa mikono mitupu japokuwa mmoja wao alionekana amebeba kitu mikononi alichokivingirisha na kitambaa cheusi.











    Kwa idadi pia walikuwa sawa kabisa na wale wa Morocco, nao hawa walikuwa watu sita.







    Pembeni yao pale waliposimama zilikuwa zimelezwa maiti nne za askari wa ulinzi wa hapa Vatican wakiwa wanaonekana wamekatwa shingo kwa kisu.











    Watu hawa sita wenye majoho meusi walikuwa wamesimama katika namna ambayo kama walikuwa wanatafakari ni wapi waelekee japokuwa walikuwa kimya hawajadili chochote kile.











    Sehemu hii ilikuwa katika namna ambayo, ukifika katikati kabisa ya mji wa Vatican, unakuwa upo eneo hili linaitwa Saint Peter’s Square. Hilo eneo ni kama ’round about’ kubwa sana ambayo unaweza hata kufanyika mkutano wa hadhara. Kutoka hapa unaweza kuelekea kulia ambako unakitana na mageti makubwa yanayo kupeleka ndani ya ofisi za Papa pamoja na kanisa kuu la hapa maarufu kama Basilica (Saint Peter’s Basilica). Alafu upande wa pili kunaakazi yenyewe (apartments) ambazo ndimo Papa anaishi.











    Lakini pia kutoka hapa Saint Peter’s Square unaweza kuelekea barabara ya mkono wa kushoto ambayo inakupeleka moja kwa moja kwenye maktaba na makumbusho maalumu ya Vatican yanayojulikana kama ’16 Chapel’.



    Huku ndiko hasa ambako walikuwa wanataka kuelekea.







    Yule mmoja wao hawa watu sita ambaye alibeba kitu alicbokifunika kwa kitambaa akaanza kutembea kuelekea huku mkono wa kushoto njia inayoelekea 16 chapel ambako kuna maktaba na makumbusho.



    Baada ya yeye kuongoza kuelekea njia hii na wenzake wote nao wakamfuata kuelekea huko.











    Giza lilikuwa nene hasa kutokana na huu usiku wa manane. Lakini watu hawa walitembea kwa ufasaha kana kwamba maisha yao yote wamekuwa wakiishi kwenye giza totoro la namna hii.







    Walipofika kwenye geti lenye kuruhusu kuingia ’16 Chapel’ yule aliyebeba kitu alichokivingirisha akagonga geti mara tatu, kisha akatulia. Akarudia kugonga tena mara tatu, akatulia, kisha akagonga tena mara tatu kwa awu nyingine ya tatu na kisha akaacha kugonga geti.











    Akasimama kimya kabisa na wenzake kama maroboti walisubiri. Wakasubiri kama dakika mbili hivi na mara kidirisha kidogo sana kwenye geti chenye ukubwa wa kama kiganja cha mkono na umbo la mraba kikafunguliwa.











    “Wageni wa nani?” Sauti kutoka kwenye kile kidirisha ikauliza.











    “Father Ricardo.!” Mmoja wa wale watu akajibu.











    Geti likafunguliwa haraka haraka na kwa tahadhari kana kwamba mfunguaji hakutaka kusikika kama anafungua geti.











    Baada ya geti kufunguliwa wale watu wakaingia.











    “Father Ricardo!” Yule aliyefungua geti akajitambulisha huku ananyoosha mkono wa salamu. Alikuwa ni mtu mzima wa kupata umri kama miaka 54 hadi 56 hivi, na muonekano wake na lafudhi yake ilionyesha alikuwa ni mtu wa Hispania.











    “Sancta Cedes!” Mmoja wa wale watu akajibu kwa kujitambulisha pasipo kushikana mkono wa salamu ulionyooshwa na father Ricardo.







    Father Ricardo hakutaka kupoteza muda zaidi, haraka sana na kwa tahadhari kubwa akawaongoza kuingia ndani ya Makumbusho ya ’16 Chapel’ kwa kupitia mlango wa nyuma wa Makumbusho.











    Huu ulikuwa ni usiku wa manane, kupata saa tisa usiku, kwa hiyo makumbusho yalikuwa tupu kabisa. Watu pekee ambao walikuwa humu kwa sasa alikuwa ni Father Ricardo na hawa watu sita.











    “Nadhani tukabidhiane haraka kabla sijaanza kutafutwa!” Father Ricardo akaongea kwa sauti ya chini.







    Ndani ya makumbusho kulikuwa na kama taa moja tu imewashwa upande Fulani, kwahiyo kulikuwa na mwanga hafifu lakini ulitosha kuona vyema.











    Mmoja wa wale watu sita, yule ambaye alikuwa amebeba kitu alichokivingirisha na kitambaa cheusi akapiga goti moja sakafunu na kuweka chini kile kitu alichokuwa amekishika mikononi na kuanza kufungua kitambaa alichokivingirisha.



    Akafungua kile kitambaa cheusi chote, na ndani yake kulikuwa na kitabu chenye ukubwa wa saizi ya kati, kama ukubwa wa laptop.



    Kulikuwa kitabu kinene, kikiwa na ukurasa mgumu wa nje kama gome. Juu ya kurasa ya nje ya kitabu hiki kilikuwa kinamaandishi yameandikwa kwa herufi kubwa kwa mwandiko aina ya ‘gothic’ na maandishi haya yalisomeka,















    BOOK OF CODES











    Father Ricardo akaweka mkono kifuani kwake kana kwamba ahamini kile alichokuwa anakiona. Akaipiga ishara ya msalaba kama mara tatu hivi. Akapiga mgoti chini na kunyoosha mikono kama anataka kukiinua kile kitabu.







    “Tafadhali” Father Ricardo akamuambia yule mtu ambaye alikuwa amepiga goti moja sakafuni.







    Yule mtu akasimama. Father Ricardo akakainuua kitabu na kukikumbatia kifuani kana kwamba mtoto anayempenda mno. Akakibusu kitabu mara kadhaa kisha akainuka.



    Haraka akatembea kuelekea upande wa pili wa Jengo ambako kulikuwa na ‘shelves’ za vitabu.







    Akatumia takribani dakika kumi kutafuta tafuta kutoka shelve moja kwenda nyingine kana kwamba kuna sehemu anaitafuta kwenye ile shelves.



    Alipoiona akachomeka kitabu hiki katikati ya vitabu vingine na kisha kurejea upande ambao walikuwa wamesimama wale.











    “Kipo sahihi!” Mmoja wa wale watu akamuuliza Father Ricardo.











    “Sahihi kabisa… mbarikiwe sana wanangu!” Father Ricardo akawashukuru.







    “Sasa nadhani utukabidhi mzigo wetu!” Yule mtu akaongea tena.











    “Bila shaka!” Father Ricardo akajibu na kuanza kuwaongoza kutoka ndani ya makumbusho kupitia mlango wa nyuma kama walivyoingia.







    Lakini kabla hawajatoka kabisa. Pembeni ya ukuta kulikuwa na simu ya mezani. Father Ricardo akainua simu na kubofya. Kisha akaweka sikioni.











    “Nipe taarifa!” Father Ricardo akaongea.











    “Papa amelala bando!” Sauti ikaongea upande wa pili wa simu.











    “Nakuja nao Basilica… sitaki usumbufu wa walinzi!”











    “Usiwe na shaka kuhusu hilo.” Sauti upande wa pili ikajibu.











    Baada ya hapo wakatoka makumbusho ya ’16 chapel’ na kwa umakini mkubwa Father Ricardo akafungua geti lisipige kelele na wakatoka na kuanza kuifuata njia inayoelekea Saint Peter’s Square.





    THE OTHER HALF















    SEASON 1 – LEGEND OF ANABELLE



















    “…yawezekana uko gizani muda huu, yawezekana ulimwengu mzima kwa sasa ukopweke bila binadamu juu yake kwa sababu sidhani kama kuna yeyote katika kizazi chetu ambaye alisalimika, sidhani kama kuna yeyote alibaki. Kama unausoma ujumbe huu, ina maana kwamba si chini ya miaka hamsini tayari imekwisha pita. Labda unatamani upate majibu ya nini kilitokea katika kizazi chetu, ni nini kilisababisha mpaka tukaupoteza ulimwengu kwa watoto wa Anabelle 1. Yawezekana ujumbe huu unaousoma ndio ushuhuda pekee uliobakia juu ya nini kilitokea duniani.







    Natamani nikueleze ni nini kilitokea, nikueleze dunia ilikopitia, nikueleze kipindi ambacho kila usiku tulipolala tulichokuwa tunakitarajia ni kifo si ndoto.



    Natamani nikueleze maamuzi yote ambayo dunia tuliyafanya lakini tulitakiwa kuyafanya tofauti.







    Kama unasoma ujumbe huu, inaamisha upo mpweke peke yako ulimwenguni miaka hamsini kutoka siku hii ya leo nilipouandika. Sitaki ujiulize kama tulishinda au tulishindwa… tumepambana kiasi kwamba nafsi yangu haikimbuki tena ladha ya ushindi ina tofauti gani na ladha ya kushindwa. Nataka nikueleze wewe ni nani? Na sisi tulikuwa akina nani na ni jinsi gani tulikikabili kifo na kupambana kutetea tulichokiamini..!”























    EPISODE 10







    Book of Codes

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





















    MARYLAND, MAREKANI











    Mzee Caleb akiwa ameongozana na wanajeshi wanane waliovalia sare maalumu, kombati nyeusi za kivita walikuwa wanashuka kwenye kiwanja kidogo cha ndege kwenye jimbo la Maryland eneo linaloitwa Oxon Hill.











    Kama nusu saa iliyopita walikuwa wetoka Site namba SQ1204 jimboni Virginia alikofichwa Makamu wa Rais David Logan na wasaidizi wake.



    Mzee Caleb aliondoka kwa kuwaeleza kuwa wanahitaji kitu alichokiita “Book Of Codes” ili waweze kukabiliana wa kikundi cha watu wanaojiita “Sancta Cedes” ambao mmoja wao aliuwawa katika jaribio la kumteka yeye Mzee Caleb. Pia akawaeleza kuwa ili kufanikisha kupata Book of Codes ilikuwa ni lazima waende jimboni Maryland.







    Pamoja naye pia alikuwepo mwana mama Naomi Cole, mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya ulinzi (National Security Advisor).



    Kwa hiyo jumla walikuwa watu kumi, Mzee Caleb mwenyewe, bibie Naomi na kikosi cha wanajeshi wanane.











    Kikosi hiki cha wanajeshi wanane kilikuwa ni moja ya vikosi vya weledi wa juu kabisa nchini Marekani kikiwa chini ya idara ya SAD ndani ya shirika la ujasusi la CIA.



    Kiongozi wa kikosi hiki aliyeitwa Ethan pamoja na wenzake wote saba kabla ya kujiunga na CIA walikuwa ni Navy SEALs katika jeshi la Wanamaji nchini Marekani. Kwa mfano Ethan yeye binafsi ana uzoefu wa kupigana vita katika vikosi maalumu vya jeshi la Marekani nchini Iraq, Somalia, Libya na Afghanistan.







    Kikosi hiki cha Ethan na wenzake, kilikuwa kinafichwa kwenye nyaraka za CIA kiasi kwamba kilikuwa kama hakipo na hakitambuliki. Hata serikalini ni watu wa ngazi za juu pekee ndio walikuwa wenye kujua juu ya uwepo wa kikosi hiki.







    Ni kikosi hiki ndicho ambacho kiliwasaidia waasi wa NTC nchini Libya mwaka 2011 kumkamata na kumuua Kanali Muammar Gaddafi mjini Sirte.



    Ni kikosi hiki ambacho kilihusika katika kuingia katika nchi isiyoingilika ya Korea Kaskazini na kumuokoa mwanasayansi wa nyuklia wa kimarekani aliyekuwa ametekwa huko na utawala wa Rais Kim.







    Kikosi hiki kilifanya kazi bila kuruhusu kikwazo chochote mbele yake, sio sheria au kanuni zozote. Kitu pekee walichokuwa wanakiona mbele yao ni ketekeleza ‘assignment’ wanayotumwa. Hii ndio sababu ya Ruppert, Mkurugenzi wa CIA kupendekeza kikosi cha Ethan na wenzake kuwalinda Mzee Caleb na bibie Naomi katika Safari yao ya kwenda Maryland kutafuta ‘Book of Codes’.











    Walikuwa wanashuka kwenye ‘Private Jet’ aina ya Gulfstream ambayo inatumiwa na kikosi hiki cha Ethan na wenzake katika shughuli zao. Ili kuficha usiri was Ethan na wenzake  ndege hii ilikuwa imesajiliwa kama mali ya Kampuni ya Van Lee ambayo ilikuwa ni kandarasi ya serikali katika biashara za masuala ya ulinzi (Defense Contractor).











    Eneo hili la Oxon Hill jimboni Maryland lilikuwa ni kamji kadogo kama ‘kijijini’ ambapo sehemu kubwa ilikuwa ni msitu mnene unaojulikana na wakazi wa hapo kwa kifupi tu kama Ox.











    “Bado hujanieleza kuhusu hii ‘book of codes’.” Naomi akamuuliza Mzee Caleb wakiwa wameshashuka kwenye ndege na sasa wako kwenye gari wanaelekea mahali fulani nje ya mji wa Oxon Hill.











    “Niliwaeleza kuhusu babu yangu, ambaye alimsaidia Mke wa rais na kumuhifadhi pamoja na mchoro wa George Washington… Nadhani unakumbuka?”











    “Nakumbuka kabisa!” Naomi akajibu.











    “Sasa kipindi Niko mtoto mara kadhaa kama kila Mara moja kwa mwaka niliwahi kumshuhudia babu yangu akifukua kitabu kutoka ardhini pembeni ya nyumba yake na kisha anatumia karibu wiki mzima kukisoma na kuandika vitu fulani hivi… nilikuwa namshuhudia anafanya hivi kwa miaka mingi sana, kila mwaka lazima afukue pembeni ya nyumba yake na kutoa hiki kitabu… kuna siku nikiwa kijana wa kama miaka 17 nikamuuliza… ni kwamba nilikuwa nikimuiliza tangu utotoni kuhusu hiki anachokifanya lakini hakuwahi kunijibu… ila siku hii aliamua kunijibu.!”











    “Alikujibu nini?” Naomi akauliza kwa shauku kubwa.











    “Alinieleza hadithi nyingi sana… lakini moja wapo ya hadithi hizo ilihusu kikundi cha wapiganaji cha kale kinachoitwa ‘Sancta Cedes’. Akanieleza kuhusu namna ambavyo kiliundwa zaidi ya karne kumi na tano zilizopita na namna ambavyo kilikiuja kupotezwa duniani kwa amri ya Papa kutoka Vatican. Kitabu hiki kilikuwa kinahusu siri nyingi kuhusu Sancta Cedes na siri nyingine nyingi duniani… na babu yangu alikuwa anaamini kuwa ipo siku Sancta Cedes watarudi tena juu ya uso wa Dunia na watakaporudi ulimwengu mzima wataubadilisha..!” Mzee Caleb aliongea kwa hisia huku macho akiwa ameyakaza kutazama mbele moja kwa moja kama anavuta hisia kukumbuka ilivyo kuwa enzi hizo na babu yake.















    “Babu yako alikitoa wapi hiki kitabu?” Naomi akauliza.











    “Hakuwa anayejua na hakuna ambaye aliwahi kumwambia alikipata wapi. Mtoto wake, yaani baba yangu aliwahi kutueleza kuwa tangu wiki ile ambayo babu yetu alimuhifadhi mke wa rais baada ya hapo alibadilika mno, alianza kuwa mtu wa siri siri sana na mara kadhaa alikuwa anaondoka nyumbani hata wiki mbili akieleza kuwa anaenda kwenye ‘kongamano’ lakini hakuna aliyekuwa anajua ni kongamani gani au lilihusu nini. Baadae miaka mingi baada ya babu kufariki baba aliwahi kutueleza kuwa anaamini babu yetu kipindi cha uhai wake alikuwa amejiunga na kikundi cha siri sana kinachoitwa *”The 46?* na ndio ambao walimpa hiki kitabu.!”







    Mzee Caleb akaeleza.











    “The 46? Kama nimewahi kusikia hiki kitu lakini kumbukumbu hainijii vizuri! Ni akina nani hasa?” Naomi alikuwa anahisi kuchanganyikiwa kwa hizi taarifa.















    “Oooooh! Sidhani hata hicho kitu kama ni kweli kipo, hicho kikundi cha ‘The 46’! Naona ni kama kitu cha kusadikika… kwa maelezo ambayo Mzee wetu alitueleza ni kwamba… duniania miaka yote lazima kuwe na watu 46 ambao ndio ‘wanaubeba’ ulimwengu uendelee kuwepo… yaani watu hawa ndio wenye kujua siri kuu zaidi za Dunia na wao wana uwezo wa kuungamiza au kuuacha uendelee kuwepo. Yaani dunia kwao ni kama yai walilolishika mkononi, wanauwezo wa kuliachia likadondoka na kupasuka au wakaacha libaki mkononi mwao na kuishi…. Sijui ni nini kilimfanya mzee aamini babu alijiunga na The 46 au hii hadithi aliipata wapi, hayo sikupata kuyajua mpaka leo hii!”











    Ukimwa wa karibia dakika tano ulipita kila mmoja akijaribu kutafakari yale maelezo ambayo walikuwa wameyaongea. Kwa Mzee Caleb habari hii haikuwa mpya kwake lakini kwa miaka yote amekuwa akiamini mambo haya kama hadithi za kusadikika na hii ndio sababu ya mshangao wake kwani hakuwa kuamini kwamba siku moja mambo haya aliyokuwa anasimuliwa tangu utoto wake na sasa ni kikongwe ati hayakuwa hadithi tu bali ni vitu halisi kabisa.











    Kwa upande wa Naomi alikuwa anajihisi kama yuko ndotoni. Ndoto mbaya ambayo unatamani mtu aje kukuamsha na kurudi katika maisha halisi. Mambo ambayo hakuwa kudhani angeweza kuyaamini hata siku moja leo hii yanakuwa dhahiri mbele ya macho yake. Miji inatwaliwa kimazingara na katika hali za kutatanisha na kugeuzwa Anabelle. Hadithi za kusadikika za Pandora zinajidhihirisha duniani, mchoro wa George Washington ati una siri inayoweza kuikoa Dunia, kikundi cha wapiganaji walipotea dunia ni zaidi ya karne kumi na tano leo wameibuka tena. Na zaidi ya hapo sasa wako safarini kuelekea mahali asikokujua ili kitafuta kitabu, kitabu kinachoweza kuwasaidia kuunusuru ulimwengu.







    Naomi alitamani aamke kutoka kwenye ndoto hii mbaya. Huu hauwezi kuwa uhalisia. Dunia haiwezi kupotea namna hii.















    “Kwa hiyo tunaelekea wapi?” Naomi akauliza kama anaamka kutoka kwenye lindi la mawazo.











    “Tunaenda ndani ya msitu wa Ox.!” Mzee Caleb akajibu kwa kifupi.











    “Msitu wa Ox? Kufanya nini?”











    “Kuchukua ‘Book of Codes’.”











    “Kiko msituni? Si umesema alikuwa nacho babu yako? Nilitegemea unacho Nyumbani?” Naomi akauliza kwa mshangao.











    “Kati kati ya msitu wa Ox kuna makaburi ya familia yetu… babu yangu alikuwa anadai kuwa wazee wake walizikwa ndani ya msitu huu ingawa binafsi sikuwahi kuona kaburi lolote… kwa hiyo kwenye wosia wake, babu yangu aliamuru kwamba atakapozikwa anataka azikwe kati kati ya huu msitu na pamoja na mwili wake anataka azikwe na kitabu chake cha ‘Book of Codes’! Na alipofariki tulifanya hivyo. Kwa hiyo Book Of codes iko ndani ya kaburi lake.” Mzee Caleb akaeleza.











    Msafara wao ilikuwa na magari matatu. Waliendesha kwa takribani nusu saa mzima mpaka kufika nje kabisa ya mji wa Oxon Hill mpaka kufikia unapoanzia msitu wa Ox.







    Ajabu ya mji huu ilikuwa ni kwamba, mji ulikuwa ni mkubwa sana lakini sehemu kubwa ya mji ulikuwa ni msitu huu mnene.



    Idadi ya watu katika mji huu ilikuwa ni chini ya watu elfu mbili na wengi wao walikuwa ni vikongwe.











    Kuna siri kuhusu mji huu ambayo Mzee Caleb kwa makusudi kabisa hakuwaeleza wenzake. Kwamba idadi ya watu kwenye mji huu ilikuwa inapungua siku baada ya siku kutokana na watu kuhama mji kwasababu ya mauza uza ya msitu huu wa Ox.







    Ilikuwa inaaminika kwamba watu waliokuwa wanaingia kufanya ‘camping’ au matembezi wakijisahau na kufika kati kati ya msitu walikuwa wanapotea na hawaonekani tena.



    Si hivyo tu lakini pia kulikuwa na matukio mengi ya watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha mjini hapa Oxon Hill.







    Wakazi wa mji huu walikuwa na imani kwamba msitu wa Ox ‘unakula’ watu na ndio maana siku baada ya siku ulikuwa unaongezeka mpaka kukaribia kufika kwenye makazi ya watu.







    Kwa wakazi wa mji huu ilikuwa ni kama mwiko kabisa kuingia ndani ya huu msitu. Na hata wale ‘vichwa’ ngumu waliokuwa wanaingia msituni kufanya camping au matembezi, walikuwa hawathubutu kufika kati kati ya msitu.











    Siri hii kuhusu huu msitu Mzee Caleb kwa makusudi kabisa aliwaficha wenzake.











    Msafara ulikuwa umefika upande wa magharibi wa msitu. Ethan na makomando wenzake walikuwa wanalizia kuandaa silaha zao na kujaza risasi kwenye bunduki zao ambazo hata kwa muonekano tu zilikuwa zinatisha.



    Walikuwa wamefungua masanduku kadhaa kama briefcase na wanachukua vitu kadhaa vya kijeshi ambavyo walihisi watavihitaji kama ikitokea wakishambuliwa.











    “Kwa hiyo hilo kaburi liko wapi tukiingia ndani ya msitu?” Ethan akauliza.















    “Lipo kati kati ya msitu!” Mzee Caleb akajibu kwa kifupi.







    “Unakumbuka sehemu yenyewe hasa?” Ethan akauliza tena ili apate uhakika zaidi.











    “Sijafika humo kwa miaka mingi, lakini kuna alama kadhaa tuliziweka ili tuweze kufika kaburi lilipo ikitokea tunataka kwenda hapo!”











    “OK! Let’s go..” Ethan akaamuru katika mtindo wa kijeshi.











    Walitembea katika mtindo ambao Naomi na Mzee Caleb walikuwa kati kati wakiwa wamezungukwa na Ethan na vijana wake pande zote.



    Makomando hao masikioni walikuwa na vinyaya vya mawasiliano na mkononi wameshikilia mabunduki ya kutisha kidole kikiwa kwenye “trigger” tayari kushambulia sekunde yeyote ikitokea hatari.



    Walikuwa wanatembea haraka lakini kwa tahadhari kubwa sana.











    Walitembea kwa takribani robo saa ndani ya msitu, Ethan akaongea kwa kunong’ona.











    “Kaeni macho, kaeni macho, kaeni macho!” Akarudia mara tatu.











    “Kaeni macho! Kuna mtu anatufuatilia… msigeuke wala kuonyesha dalili yoyote kama mnajua tunafuatiliwa.!”







    Ethan akaongea kwa kunong’ona lakini kwa umakini na ufasaha kuhakikisha wenzake wanamaikia na kuelewa.











    Wote wakafanya kama ambavyo Ethan alieleza. Japokuwa ndani ya nafsi walipata hofu kubwa lakini hawakuonyesha kushtuka, wakaendelea kutembea haraka haraka.











    Baada ya kutembea kama nusu saa hivi Mzee Caleb akasimama na kuufuata mti fulani. Akaushika shika magome yake kama kuna kitu anakitafuta. Kisha akarudi walipo wenzake.











    “Tunakaribia!” Mzee Caleb akaongea baada ya kurudi waliposimama wenzake.











    “Ulikuwa unaangalia nini?” Naomi akamuuliza.











    “Niliwaeleza kuwa kuna alama tuliziweka ili kujua muelekeo kaburi lilipo.!”











    “OK! Kwa hiyo kuna alama gani pale? Naona mti tu wa kawaida hauna alama yoyote ile?”











    “Usijali!” Mzee Caleb akauliza na wakaendelea tena kutembea.















    “Naamini sasa tunafuatiliwa zaidi ya mtu mmoja! Msishtule wala kuonyesha tunajua..” Ethan akaongea tena kwa kunong’ona.











    Msitu ulikuwa mnene kiasi kwamba ndani yake hata mwanga ulikuwa haupenyi vizuri. Hii ilisababisha kuwe na giza fulani hivi kama giza la saa moja jioni lenye mwanga hafifu kwa mbali.











    Wakatembea kwa dakika nyingine kama arobaini hivi huku kila mara Mzee Caleb akisimama na kugusa miti kuangalia ‘alama’ kama walikuwa wanaelekea njia sahihi.







    Dakika kama kumi baadae wakatokea eneo fulani la wazi lenye miti michache likiwa na muonekano kama miaka mingi sana huku nyuma kulikuwa na nyumba mahali hapo.











    “Mungu wanguuuu.!!” Mzee Caleb akalipuka kwa mshangao na kuanza kukimbia kuelekea eneo hilo la wazi.







    “Nini Mzee!!” Naomi, Ethan na makomando wake nao wakakimbia kuelekea kwa Mzee Caleb.











    “Kaburi limefukuliwa!” Mzee Caleb alisimama akiwa anahema mbele ya shimo pale kwenye eneo la wazi.



    “Kuna mtu ametuwahi.! Amefukua kaburi na kuchukua Book of codes!” Mzee Caleb akaongea huku anahema karibia aanze kulia.







    Pembeni ya shimo hili lililofukuliwa na likionekana halijafikuliwa siku nyingi, kulikuwa na masalia ya maiti, mifupa na mafuvu.











    “Ulisema hapa mmemzika babu yenu? Hii mifupa sio ya binadamu mmoja!” Ethan akaongea na kuuliza.







     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Wote wakakodoa macho pale chini pembeni ya kaburi lililofukuliwa kulikuwa na mifupa na mafuvu ya watu watatu.











    “Na hapa hakuna masalia ya babu yangu? Sioni fuvu la babu yangu!” Caleb akaongea huku ameziba mdomo kwa kiganja cha mkono kwa mshangao.











    “Kwanini unasema hakuna fuvu la babu yako?” Naomi akauliza.











    “Ssssshhhhhhhiii”







    Kabla Mzee Caleb hajajibu swali la Naomi Ethan akawaamuru wanyamaze.







    “Wako hapa” Ethan akaongea kwa kunong’ona.







    “Nani?” Naomi akauliza kwa kunong’ona pia.











    “Waliokuwa wanatufuatilia.!” Ethan akajibu.











    Wote wakabaki kimya kwa sekunde kadhaa. Mara ghafla wakaanza kusikia sauti kama mtu anapekua majani kwenye kichaka kilichopo mbele yao kama umbali wa mita tano hivi.







    Makomando wote kwa pamoja wakaelekeza bunduki zao kwenye kichaka hiki huku vidole kwenye trigger.







    Kufumba na kufumbua, kutoka kwenye kile kichaka ghafla akatokea mtu wa ajabu ambaye hawajapata kumuona.







    Alikuwa ni mwanaume wa makamo, mwenye mwili wa wastani. Alikuwa amevalia shati na suruali ya khaki zilizo chakaa mno.







    Utofauti wake mkubwa ulikuwa ni manyoya mikononi mwake. Alikuwa ni binadamu kabisa lakini mikononi alikuwa naanyoya mengi mno kupitiliza. Pia masikioni alikuwa naanyoya mengine yametokeza.







    Pia alikuwa na ngozi ya ajabu hasa. Ngozi yake nyeupe ya kizungu ilikuwa imepauka kupitiliza kiasi kwamba mpaka kuiangalia ilikuwa inatisha.







    Macho yake makali ambayo hayakuwa na nyusi wala kope alikuwa ameyakaza kuelekea kwa Mzee Caleb.











    “Nilijua utakuja tena Caleb!” Yule mtu akaongea kwa sauti ya ajabu kama ananong’ona lakini inasikika sawia kabisa na sauti ilikuwa inapenya masikioni kama kisu.



    Alipoongea meno yake ya ajabu yaliyochongoka na yenye rangi ya njano yalionekana kwa usawia zaidi.











    “Msimpige risasi!” Mzee Caleb akaongea kwa nguvu.





    THE OTHER HALF











    SEASON 1 – LEGEND OF ANABELLE











    “…kuna udhalimu mwingi mno duniani kiasi kwamba inakufanya mtu ujiulize tumefikaje hapa? Tumefikaje katika hatua ambayo binadamu ndiye amekuwa mnyama hatari zaidi juu ya uso wa dunia? Pengine hii ndio sababu ya watoto wa Anabelle 1 (Maldives) kutaka kuipoka Dunia kutoka mikononi mwetu… pengine hiki kinachoendelea duniani, miji kutwaliwa na kugeuzwa Anabelle ni matokeo ya udhalimu wa mwanadamu uliokithiri kwa miaka mingi!



    Mara zote watu hujiuliza, ni nini hasa unaweza kufanya ili uweze kuwa bora kwenye Dunia ya namna hii? Unawezaje kuukataa udhalimu uliopo duniani na kuleta tumaini na ubora katika mbari yetu ya binadamu?

    Ukweli ni kwamba, unahitaji kitu kimoja tu au mtu mmoja tu ambaye unampenda au anuekujali haswa na mwenye uwezo wa kukufanya uuone ulimwengu katika mtazamo chanya… mtu mmoja tu ambaye atakuwa na maana kubwa zaidi kwenye maisha na ukiwa naye katika maishani anakubadili na kutamani kuwa bora kila siku. Mtu mmoja unayempenda kwa dhati kiasi kwamba ndiye anakuwa kiunganishi chako kwa ulimwengu uliobaki.!!







    Lakini jambo kuna jambo la kuogkfya zaidi…. ni nini hasa kitatokea kama tayari unaye mtu huyu maishani mwako alafu ghafla tu akaondoka katika maisha yako milele? What do you become?”











    EPISODE 11

    MAHALI FULANI PA SIRI JIMBONI VIRGINIA MAREKANI (SITE NAMBA SQ1204)











    Makamu wa Rais David Logan bado alikuwa anarudia rudia kichwani mwake maneno aliyoambiwa na Kevin yule Katibu Kiongozi wake (Chief of Staff). Maneno hayo kila sekunde yalikuwa yanajirudia kichwani mwake, “Airforce One imeonekana!”



    Kwa namna moja au nyingine hii ilikuwa ni habari mbaya kwake. Sio tu kwamba alianza kuogopa ndani ya nafsi yake bali pia alianza kusikia hasira. Akaanza kuhisi huu unaweza kuwa ni mwanzo wa kuvuja kwa siri kubwa aliyokuwa nayo moyoni mwake, siri ambayo inapaswa kubakia kwake tu mpaka siku anaingia kaburini. Kuvuja kwa siri hii sio tu kwamba utakuwa mwisho wake, bali pia itazua sekeseke kubwa sana katika taifa la Marekani.

    “Mr. Vice President..!!” Kevin akamuita Logan ambaye alikuwa amezama kwenye lindi la mawazo.

    “Kevin.!!” Logan akazinduka kutoka kwenye dimbwi la mawazo kana kwamba amezinduka usingizini.

    “Mwenyekiti wa Joint Chief of Staff yuko mubashara anaomba kuongea nawe akupe maelezo zaidi.!” Keith akaongea kwa tahadhari fulani kama vile ameng’amua namna ambavyo taarifa hii ya kupatikana Airfoce One imemshitua boss wake.

    “OK! Wanaweza kuniunganisha naye tuongee!” Makamu wa Rais Logan akaongea huku anainuka na kufunga vuzuri kishikizo cha koti lake la suti.

    “Sawa Muheshimiwa… lakini… aaahh… uko sawa kweli muheshimiwa?” Keith akauliza kwa udadisi.

    “Kwa nini unauliza?” Logan akajibu huku anageuka kumuangalia Keith kwa udadisi pia.

    “Hapana muheshimiwa nimehisi tu kama hauko sawa!” Keith akajibu huku anaondoka karibu na Logan na kwenda mpaka katikati ya sebule ambako kulikuwa na vijana wa Secret Service wanaunganisha vifaa ili Makamu wa Rais Logan afanye maongezi mubashara ya kuonana ana kwa ana kupitia “Video Call” na Mwenyekiti wa Joint Chiefs of Staff aliyeko Whitehouse muda huo.







    Baada ya kama dakika tano hivi mitambo ilikuwa imekaa sawa na Logan alikuwa ameketi mbele ya ‘screen’ akionana ana kwa ana na Admiral Smith ambaye alikuwa Whitehouse.

    “Habari ya Jioni Muheshimiwa?” Admiral Smith akafungua maongezi.

    “Nzuri tu Admiral.!”



    “Mr. Vice President kabla sijaanza kukupa taarifa yangu kuhusu tulichokipata huko bahari ya Atlantic… naomba nikushauri kuhusu taarifa niliyopokea kutoka ofisi ya Secret Services!” Admiral Smith akaongea akiwa serious kiasi.



    “Taarifa gani admiral?” Logan akauliza kwa mshangao.



    “Nimepata taarifa kuwa unawashinikiza Secret Services utoke hapo site SQ 1204 na kurejea Whitehouse?”

    “Yeah ni kweli.! Sikiliza Admiral nafurahi namna ambavyo mnajali usalama wangu, lakini ni muhimu pia wananchi wakajua kuwa Rais wao yuko salama ili kuepusha kuzua taharuki na kuanza kuenea uvumi wa uongo!” Logan akaongea akiwa na hasira kwa mbali katika sauti yake huku akijisahau na kujiita ‘Rais’ badala ya ‘Makamu wa Rais’.



    “Mr. Vice President, bado hatuna uhakika juu ya usalama wako na kwa sasa tusingependa umma ufahamu mahali ulipo, hivyo nasisitiza uendelee kubaki mahali ulipo… pia tuko tunashauriana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu aweze kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa uko salama pasipo kueleza mahali ulipo!”

    “Admiral wananchi wanahitaji kuniona niko salama na nizungumze nao sio kupewa taarifa na watu wwngine kitu kinachoweza kuzua mashaka zaidi kuwa kama niko salama kwanini nitolewe taarifa na mtu mwingine?” Logan akaongea huku hasira sasa ikiwa dhahiri katika sauti yake.



    “Labda tufanye utaratibu uhutubie taifa ukiwa hapo hapo SQ 1204!” Admiral akapendekeza.



    “Jesus Christ!! Nadhani hunielewi Admiral… tuache hili kwanza… twende kwenye masuala muhimu zaidi… nipe taarifa kuhusu kilichotokea huko baharini.!” Logan akaona ni bora akwepeshe maongezi haya. Alikuwa anatamani aongee ukweli kwanini anatamani atoke sehemu hii ya siri walikomficha kwa usalama wake. Alitamani amueleze Admiral Smith na watu wa Secret Services ukweli kwanini atoke hapa. Alikuwa anahitaji kwenda kurekebisha jambo la hatari alilolifanya kabla siri haijagundulika. Taarifa hii ya kupatikana Air Force One ilikuwa ni moja ya habari mbaya zaidi kusikia maishani mwake.



    “Sawa Mr. Vice President!” Admiral akaanza kutoa taarifa kuhusu kilichopatikana huko bahari ya Atlantic. “Muheshimiwa kama unavyofahamu kuwa kwa wiki tatu sasa, jeshi la Navy limeelekeza nguvu nyingi huko bahari ya Atlantic ili kuweza kuona kama tunaweza kufanya chochote ili kuipata Air Force One kama imedondoka huko iliwa na Madam President!”



    “Nafahamu Admiral!”



    “Sasa siku Tatu zilizopota, tuliweza kupata Picha za satellite zikionyesha mabaki ya ndege kwenye Kisiwa kinatwa Saman, ndani ndani kabisa ya bahari ya Atlantic…. Kisiwa hiki hakikaliwi na watu wowote.. Ikatubidi tutume boti kwenda kuyachunguza mabaki hayo… na wanajeshi wa Navy walipoyafikia na kuyakagua walikuwa na imani kubwa kuwa yatakuwa ni mabaki ya Air Force One! Kwahiyo ikabidi kuanzia juzi tuanze kufanya ukaguzi chini ya bahari kuanzia hapa Kisiwa cha Saman na hatimaye leo asubuhi tukapata mafanikio.!”







    Admiral akanyamaza kidogo kumeza mate na kumpa nafasi Logan aweze kuchekecha kichwani hiyo taarifa.

    Logan hakusema chochote wala kuuliza swali au hata kutingishika pale kwenye kiti. Taarifa hii kadiri ilivyokuwa inawasilishwa kwake ndivyo ambavyo ilikuwa inamfanya presha izidi kupanda nafsini mwake.



    “Mr. Vice President, leo asubuhi maafisa wa jeshi la Navy walifanikiwa kuiona Air Force One imetuama chini kabisa ya bahari pembezoni mwa kisiwa hiki cha Saman..” Admiral Smith akaweka tena ‘nukta’ kidogo.



    “Madam President au mwili wake vimepatikana?” Logan akajikuta anauliza bila kujijua kana kwamba anaongea yuko ndotoni.



    “Ni mapema sana kusema chochote kuhusu hilo… hivi tunavyoongea Navy wako wanafanya juhudi za kuondoa miili yote iliyomo ndani ya Air Force One ili zoezi la utambuzi lianze huku wakiwa wanafanya juhudi za kuibua Air Force One kutoka chini ya bahari.… lakini kuna jambo lingine muheshimiwa!” Admiral akaongea sentesi ya mwisho kwa kukaza sauti kuashiria hilo ‘jambo’ lingine ni suala serious haswa.



    Logan akaanza kuhisi kama mkojo unataka kumtoka. Kichwani ndani ya sekunde aliwaza zaidi ya mambo elfu ambayo yanaweza kutamkwa na Admiral Smith kuhusu hilo ‘jambo’ lingine. Alikuwa tayari kupata taarifa yoyote ile mbaya lakini aliomba kimoyo moyo taarifa hiyo katu isiweze kuhusiana na siri aliyonayo moyoni mwake.



    “Jambo gani Admiral?” Logan akauliza huku akijikaza kuzuia woga alionao ndani yake usijionyeshe kwenye sauti yake.



    “Kwenye kisiwa hiki cha Saman tumekuta magofu ya jengo kubwa la kale ambalo Navy wameshindwa kung’amua ni namna gani limekuwepo hapo?”

    “Nini? Umenambia awali kuwa kisiwa hiki hakina watu wanaoishi?” Logan akahamaki.

    “Ni kweli Mr. Vice President… hakuna mtu anayeishi kwenye hiki Kisiwa ndio maana hata Navy wameshangaa kukuta magofu ya Jengo… lakini Muheshimiwa kitu cha kushangaza zaidi sio haya magofu ya majengo bali ni kilichokutwa kwenye majengo hayo..!” Admiral akaongea akiwa amekaza Sauti zaidi.



    Logan presha ilipanda zaidi mpaka akaanza kuhisi anaweza kupoteza fahamu muda wowote ule.



    “Ni nini wamekikuta kwenye hayo magofu?” Hatimaye akajikaza na kuuliza.











    RABAT, MOROCCO

    Mwili wa Rais. Laura Keith bado ilikuwa umelala pale juu ya meza katikati ya chumba hiki cha ajabu ambapo pale mezani kila upande waliketi wale watu ambao walionekana vingozi wa wenzao wote waliopo ambao walikuwa wameketi kwenye viti kwenye kila upande wa ile meza na jumla yao yote wakiwa 46.

    Yule Mzee aliyeketi mbele kabisa ya meza akiwa amevalia suti nyesi na kichwani amenyoa upara, akavuta bakuli lingine ambalo lilikuwa pembezoni mwa meza na kulisogeza karibu yake.

    Ndani ya bakuli kulikuwa na kimiminika kama maji hivi yenye rangi ya njano iliyofifia kiasi na ndani yale kulikuwa na sponji (sponge) limelowekwa.

    Yule Mzee akalivabua lile sponji likiwa limelowana yale maji maji ya njano na kulielekeza juu ya uso wa Rais Laura Keith aliyekuwa amelazwa pale juu ya meza bila ufahamu. Mkono wake ulipofika juu ya uso wa Laura akalikamua sponji na yale maji ya njano njano yakamiminika juu ya uso wa Laura.

    Ghafla, kwa kasi ya ajabu Laura alikurupuka kwa ajabu na kuzinduka kutoka kwenye kuzimia na kukaa kitako juu ya meza akiwa anahema kwa nguvu kana kwamba ametoka kukimbia umbali mrefu sana.

    Akaanza kupepesa macho huku na huko akishangaa pale alipo na aliokuwa anawaona mbele yake huku bado akiwa anaheama kwa nguvu.



    “Karibu tena upande wa pili Laura!!” Yule Mzee akaongea huku anatabasamu.

    Laura akageuka kumuangalia yule Mzee. Alimkazia macho na kumuangalia kwa mshangao mkubwa kwa sekunde kadhaa na taratibu akaanza kuhema kawaida na kuonyesha dalili kama vile alikuwa anajua yuko wapi.

    “Asante Duran!!” Laura akaongea huku bado anamtazama yule Mzee.

    Yule mzee hakujibu kitu, akatingisha kichwa tu kuitikia huku akiwa anatabasamu tena.









    “…kama dunia ingelikuwa na uwezo wa kuongea unahisi nini ingetamka? Je, ingetamka kuhusu mabilioni ya damu za binadamu zilizomwagika juu yake? Au ingetamka kuhusu kanuni za kale ambazo zimekuwepo kwa maelfu ya miaka na baadae tukaanza kuzipuuza na kupelekea kutugharimu? Au labda ingetamka kuhusu kosa ambalo ulimwengu mzima tulilifanya mwaka 2036?..”











    EPISODE 12



    Book of Codes

    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)

    Cindy, Salim, Magdalena, Shafii na Kanali walikuwa wamekaribia kabisa eneo ambalo wote waliamini kwamba ilikuwa ni mitaa ya ubungo kabla ya mji wa Dar es Salaam kutwaliwa na kugeuzwa kuwa Anabelle.



    Ajabu ni kwamba japokuwa bado kulikuwa na giza nene lakini waliweza kugundua kwamba kulikuwa mto ulikuwa unatiririsha maji sehemu ambayo wote waliamini kuwa hapo mwanzo kulikuwa na barabara ya Mandela.

    “Hayo ni maji au masikio yangu yana matege?” Shafii akauliza kwa utani lakini akimaanisha.

    “Hii haiko sawa! Hapa kulikuwa na barabara ya Mandela!!” Salim akaongezea.

    “Ni mto wa maji au kitu gani?” Kanali akaongea huku anasogea karibu na walipokuwa wanasikia kwa lengo la kitaka kuhakikisha kama kweli ulikuwa ni mto.



    “No no no nooooooo!!” Cindy akapiga kelele huku anamkimbilia Kanali aliyekuwa tayari ameinama na kumzuia asiingize mkono kugusa maji ya mto.



    Kanali akaruka pembeni baada ya kuona Cindy anamkimbilia na kumuinua asiguse maji. Lakini alikuwa amechelewa kiasi ncha za vidole vyake vilikuwa vimegusa maji kiasi na kuloa.

    “Nini shida??? Kwanini umenikataza nisiguse maji?” Kanali akauliza huku anahema akiwa anainuka kutoka pale chini alipodondokea.



    “Umeyagusa maji?” Cindy akauliza. Japo kuwa walikuwa gizani lakini kanali aliweza kuhisi namna ambavyo Cindy alikuwa ametoa macho kwa kuogopa.

    “Kidogo sana! Ncha za vidole tu ndio zimegusa!” Kanali akajibu huku kiasi fulani anatetemeka.



    “Mungu wangu.!!” Cindy akahamaki mpaka ikambidi akae chini.

    “Nini? Nini shida?” Salim akauliza kwa kuhamaki.

    “Mnaona hii chupa ninayoishikilia muda wote huu tukiwa tunatembea!” Cindy akawauliza huku anainyanyua ile chupa ambayo muda wote wakiwa wanatembea anakuwa anaishika mkononi kama tochi na inakuwa inang’aa kwa rangi ya buluu.

    “Imefanyaje?” Magdalena akauliza.

    “Hii chupa huu mwanga unaotoka wa bluu ndio unatusaidia tusionekane na hawa viumbe walioko ndani ya hii Anabelle..!!” Cindy alaongea kwa kifupi na kunyamaza kidogo, kisha akaendelea “hiyo ndiyo namna ya kwanza ambayo wanatumia kuwinda wanachokitaka… wanafuata kivuli cha windo lao wanalolilenga.!”

    “Kivuli?? Na giza hili kivuli kitokee wapi? Wanakionaje?” Magdalena akauliza.

    “Macho yao hayaoni kama yako wewe au macho yangu.. Wanaona tofauti kabisa?” Cindy akaongea kwa sauti ya unyonge akiwa bado amekaa pale chini.



    “Wanaonaje? Tofauti yao na sisi katika kuona ni ipi?” Shafii akauliza haraka haraka.

    “Hebu subirini kwanza… umesema hii ya kuona ndio njia mojawapo wanayotumia kuwinda walengwa wao, si ndivyo? Je, njia nyingine ni ipi na kwanini umeshituka sana baada ya kanali kusema vidole vyake vimegusa maji?” Salim akauliza maswali kadhaa mfululizo kwa pamoja.

    “Njia ya pili ni kunusa… wanafuata harufu! Mnakumbuka pale tulipovuka mpaka wa kutoka duniani kuingia humu ndani ya Anabelle nikaishika hii chupa na tukatembea kwa dakika kadhaa bila kushambuliwa… pale mwanzoni walikuwa hawawezi kutuona na ndio maana tukawa Salama… lakini baada ya hapo nadhani wakang’amua kuwa kuna harufu ya binadamu wameingia ndani ya himaya yao. Ndipo pale yule kiumbe akatushambulia na tukafanikiwa kumuua..” Cindy akanyamaza kidogo.

    “OK! Nadhani nimekuelewa mpaka hapo lakini bado haujaeleza kwanini umeshituka Kanali alipogusa maji na vidole..!” Salim akauliza tena.

    “Najua.!! Niwakumbishe tena kwanini nilimchuna ngozi yule kiumbe… ngozi yake tunaweza kuihitaji baadae kama kutakuwa na ulazima na mtaona kama uhitaji huo utatokea… lakini pia ngozi hii inasaidia kuzuia harufu yetu isisikike… kila tunapokuwa tunaenda hawa viumbe wakivuta harufu watasikia harufu hii ya ngozi ya mwenzao lakini hawatasikia harufu yetu na namna hiyo tunakuwa Salama pasipo kushambuliwa tena… au niseme tulikuwa salama kabla ya Kanali kugusa haya maji?” Cindy akaongea huku anajiinua kutoka pale chini alipoketi.



    “Kwahiyo sasa hivi wanaweza kusikia harufu yetu?” Kanali akauliza.

    “Hapana kanali, hawawezi kusikia harufu ‘yetu’! Wanaweza kusikia harufu ‘yako’ kuanzia sasa..!!” Cindy akaongea kwa msisitizo.







    “Unasemaje? Kivipi?” Kanali akajibu huku mapigo ya moyo yameongezeka na kuanza kuhema juu juu.

    “Nadhani umenisikia kanali… kuanzia sasa wanauwezo wa kusikia harufu yako na kukuwinda!”







    “Kwanini waweze kunusa harufu yangu tu pekee?”

    “Unaona huo mto kanali? Unafahamu hapa tulipo ni wapi?” Cindy akamuuliza kanali ambaye alikuwa ameanza kuchanganyikiwa kwa woga.

    “Ndio! Nadhani haya ni maeneo ya Ubungo na nadhani wote tunafahamu kuwa hakukuwa na mto hapa!” Kanali akajibu huku bado akiwa akili haijamkaa sawa.

    “Yes! Hakukuwa na mto hapo.. Huu wameutengeneza baada ya Dar es Salaam kutwaliwa na uhalisia haya mnayoyaona hapa si maji kama maji mengine mnayoyajua… mji ukitwaliwa kwa kadiri ninavyofahamu ni kwamba lazima kutengenezwe mto kama huu ambao watoto wote wachanga wanahifadhiwa baada ya kuzaliwa… humu ndimo kizazi kipya cha watoto wa Anabelle wanalelewa..” Cindy akaongea huku anapepesa macho huku na huko kama vile kuna kitu anatafuta au anategemea kitokee.



    Wenzake wote nao wakaanza kupepesa macho kufuata muelekea wasijue hata ni nini ambacho Cindy alikuwa anaangalia.

    “Kwahiyo nini kilichosababisha mpaka waanze kusikia harufu yangu?” Kanali akauliza kwa kunong’oa bila hata mwenyewe kujua kwanini ananong’ona.

    “Kanali! Nimewaambia haya sio maji ya kawaida kama unavyoyaona… humu wanalelewa watoto wote wanaozaliwa ndani ya Anabelle… sina majibu yote kwanini lakini ninachojua maji haya yanaondoa kinga yoyote ambayo unakuwa umejiwekea ili using’amuliwe na viumbe vya humu… kwa hiyo nakusisitiza tena kuwa wameanza kunusa harufu yako… Wanajua kuna binadamu humu ndani.!” Cindy akaongea huku sasa hivi akiwa amekaza macho sehemu moja ng’ambo ya mto.

    Wengine wote wakajikuta wamebaki kimya wakiwa nao wamekaza macho kuelekea kule ambako Cindy alikuwa anaangalia.

    Ghafla wakasikia kishindo kwenye maji kama mtu au kitu kimejitupa kuingia mtoni.

    Kelele hizo za kishindo cha kujitupa majibu zilidumu kwa kama sekunde tano tu kisha kukawa kimya tena.

    Cindy akaanza kurudi nyuma taratibu huku anawarudisha pia wenzake kwa mikono yake kama anawakinga warudi nyuma.

    “Kanali kaa nyuma yangu!” Cindy akaongea kwa kunong’ona.



    Kanali bila kujiuliza mara mbili mbili akarudi nyuma na kujiweka mgongoni mwa Cindy.

    “Wote nataka tumzunguke kanali kila upande… kila upande wa kanali kuwe na mtu.!” Cindy akaongea huku anainua na kuiweka mbele yake ile chupa aliyokuwa nayo tangu mwanzo wa safari yao.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Wengine wote wakasimama kumzunguka Kanali. Lengo la kufanya hivi ilikuwa ni kijaribu kumlinda Kanali dhidi ya hicho kitu walichokisikia kinajitupa ndani ya maji.

    Kama ambavyo Cindy alikuwa ameeleza kuwa kwa sasa viumbe hawa walikuwa na uwezo wa kunusa harufu ya kanali na kumwinda. Lakini wengine wote bado walikuwa Salama na walikuwa hawawezi kuwindwa na viumbe vya humu kwa kunusa harufu zao. Kwahiyo lengo la kumvunguka kila upande ilikuwa ni kujaribu kumkinga viumbe wa humu wasiweze kumuona au kunusa harufu yake na kumdhuru.

    Wakiwa wamemzunguka kila upande, wakaanza kusikia sauti ya kitu kikiwa kinatoka ndani ya maji kwenye ule mto uliopo mbele yao. Kitu hicho kilikuwa kinatoka taratibu kwa tahadhari kubwa kama vile kilikuwa kinataka kisisikike sauti yake.

    “Turudi nyuma taratibu kwa pamoja.!” Cindy akawaamuru wenzake kwa kunong’ona.



    Wote wakaanza kurudi nyuma taratibu kwa pamoja kwa mwendo wa kunyata kwa tahadhari kubwa.

    Giza lililokuwa limetanda liliwafanya washindwe kung’amua ni nini au kitu gani kilichokuwa kinaibuka kutoka majini kwenye mto.



    “Ni nini? Mtoto wa Maldives?” Shafii akauliza kwa sauti ya chini sana ya kunong’ona. Alikuwa anauliza kama kiumbe hicho kilichokuwa kinatoka majini kinafanana na kile ambacho walikuwa wamekiua masaa kadhaa yaliyopita.

    “Natamani angekuwa mtoto wa Maldives, lakini sidhani… huyu ni mlinzi wa watoto wanaohifadhiwa humu kwenye maji, nadhani amesikia harufu ya kanali!” Cindy akajibu kwa kunong’ona zaidi kushinda alivyo nong’ona Shafii.



    Wakiwa wanazidi kurudi nyuma taratibu wakaanza kuhisi kama mile kiumbe kilichokuwa kinatoka ndani ya maji kimesimama mbele yao.

    Japo giza lilikuwa ni nene sana lakini macho yao yalikuwa yameanza kuzoea hali hiyo na hivyo kwa kiasi fulani walikuwa wanaona japo kiduchu kilichopo mbele yao.



    Kiumbe kilichokuwa kimesimama mbele yao ni dhahiri kabisa hakikuwa kiumbe kile ambacho kinafanana na wanadamu ambacho walikiua masaa machache yaliyopita. Kwa kuwa kiumbe hiki kilikuwa kimetulia pasipo kujongea mbele yao walishindwa kung’amua hasa kilikuwa ni kiumbe cha namna gani.

    “Simameni!” Cindy akawaamuru wenzake wasendelee kurudi kinyume nyume kama vile walivyokuwa wanafanya.

    “Unasemaje? Huoni hicho kilichopo mbele yetu?” Salim akang’aka kwa sauti ya chini.

    “Mnakumbuka niliwaambia kuwa jambo la kwanza humu tunatakiwa kutafuta mlango wa kikundi wanachojiita The 46? Sasa huu muelekeo tunaolelekea sio.!”

    “Tunatakiwa twende mwelekeo gani?” Salim akauliza.

    “Huku mbele.!” Cindy akawaonyesha wenzake upande ambao yule kiumbe alikuwa amesimama. Kiumbe huyo alikuwa amesimama kama mita kumi kutoka pale walipo.

    “Umechacganyikiwa Cindy? Hicho kiumbe mbele yetu hukioni?” Salim akafoka kwa staili ile ile ya kunong’ona.

    “Huyu kiumbe ametoka majini baada ya kusikia harufu ya kanali… lakini hivi jinsi tulivyo mzunguka kanali hana uwezo wa kunusa harufu yake tena, kwa hiyo tunaweza kumpita pale mbele bila yeye kujua endapo tutakaa mkao huu huu wa mduara kumzunguka kanali.”

    “Na unajuaje kama huko unakosema ndio mlango wa The 46 ulipo?” Salim akahoji.

    “Salim, sina muda wa kuanza kujieleza kama tuko darasani… niamini huku tunakoenda siko, inapaswa twende upande huu ninaowaeleza.!” Cindy akasisitiza zaidi.

    “OK! OK OK!” Salim akaitikia kwa hofu huku anahema.

    “OK! Sasa twende kwa staili hii hii kama tulivyokuwa tunarudi nyuma… duara la kumzunguka kanali libaki hivi hivi.!” Cindy akatia tahadhari.

    Wote kwa pamoja wakaanza kuelekea mbele kwa hatua za taratibu kwa mwendo wa tahadhari kubwa sana.

    Wakatumia takribani dakika mbili nzima kutembea huku kwa tahadhari kutoka pale waliposimama mpaka kufika pale yule kiumbe aliposimama.



    Walipomfikia karibu ndio wakapata fursa ya kumuona kwa usahihi zaidi yule kiumbe kutokana na mwanga uliokuwa unatoka kwenye chupa aliyoishikilia Cindy.

    Kiumbe huyu alikuwa anafanana kabisa na mbwa lakini alikuwa na kimo kirefu zaidi. Alikuwa na urefu wa kama kimo cha ndama wa ng’ombe. Kiumbe huyu licha ya kuwa na muonekano wa kufanana na mbwa lakini hakuwa na hata nywele au nyoya kwenye ngozi yake. Alikuwa na ngozi ya kufanana kabisa na ngozi ya binadamu ambayo haina kinyweleo au nyoya hata moja.



    Lakini jambo la ajabu zaidi kiumbe huyu mwenye kufanana na mbwa alikuwa na mbawa. Mbawa zake zilifanana kabisa na mbawa za popo kwa maana ya kwamba nayo hayakuwa na nyoya hata moja.

    Pia rangi ya kiumbe huyu ilikuwa ya tofauti mno. Alikuwa na rangi nyeupe kabisa ya kung’aa kama weupe wa sufi au theluji.



    Kitendo cha kumuangalia tu kiumbe huyu alikuwa anatisha haswa kiasi kwamba unaweza kuzirai ghafla.



    Wote walijikuta wanatetemeka baada ya kumuona kiumbe huyu. Kiumbe mwenyewe alikuwa ametulia kimya kabisa akionyesha dhahiri kabisa alikuwa hajui kama kuna watu mbele yake.

    Wakiwa wanatembea namna ile ile kwa hatua za tahadhari wakipita mbele ya huyu kiumbe, ghalfa Shafii akakanyaga kitu kama jiwe ardhini na akajikuta anadondoka na kuharibu ule mduara waliokuwa wameutengeneza kumzunguka Kanali.



    Kitendo cha ule mduara kuvurugika na Kanali kuwa ‘exposed’, ghafla yule kiumbe alitoa mlio mkali kama mlio wa mbwa aliyepigwa na jiwe mbavuni lakini mlio wake ulikuwa na kishindo zaidi na haukuwa mlio wa maumivu au woga bali ulikuwa ni mlio wa hasira.



    Kiumbe huyo akakaza macho yake moja kwa moja walipokuwa wamesimama akina Cindy na kuanza kuwafuata akiwa anaunguruma na rangi yake nyeupe ikianza kubadilika na kuwa rangi nyekundu iliyopauka.

    Hakuna muda ambao kifo kinakuwa dhahiri mbele yako kama muda huu ambao Cindy na wenzake ulikuwa unawakabili….





    “..katika kipindi cha miaka bilioni 4.5 ambayo dunia imekuwepo, tumefanikiwa kuijaza kwa idadi ya watu bilioni 7.5 ambao tunaishi juu ya eneo nchi kavu la dunia lenye ukubwa wa kilometa za mraba milioni 149 pekee.



    Maisha yetu juu ya dunia yamegubikwa na siri kubwa sana katika kila nyanja na kila upande. Kuna siri kubwa ni namna gani viumbe wengi wanapotea na juu ya uso wa dunia lakini binadamu ndio kiumbe pekee ambaye kila siku tunaongeza mamlaka yetu ya kutawala dunia juu ya viumbe wengine.

    Wanasema unapokuwa na mamlaka makubwa, pia unakuwa na majukumu makubwa zaidi. Lakini mbari yetu ya binadamu hatukujua hili au labda tulijisahau. Ni mpaka tulipofika mwaka 2038 ndipo tulipojua kosa kubwa tulilolifanya kwa kutotimiza jukumu kubwa tulilonalo ambalo linaletwa na mamlaka makubwa tuliyo nayo juu ya dunia kuzidi viumbe wengine wote.

    Au labda tulishindwa kutambua jukumu hili kubwa kwasababu ilikuwa ni siri kubwa tuliyofichwa. Siri ambayo watu pekee wenye kuifahamu ni kikundi cha watu wanaojiita “The 46”! Ambao bila wao wanaamini dunia haiwezi kuendelea kuwepo.

    Lakini hatuwezi kujitetea kwamba ilikuwa ni siri, kwa sababu uhalisia ni kwamba hakuna siri hata moja duniani. Yes, hakuna siri. Unatakiwa ujue tu ni wapi kwa kutazama na wapi kwa kutafuta ili kung’amua.











    EPISODE 13





    VATICAN CITY, ROME











    Father Ricardo alikuwa anatembea kwa tahadhari kubwa kama ananyata kutoka katika Jengo la Basilica, ambalo ndilo kanisa kuu la hapo Vatican.

    Mkononi alikuwa ameshikilia kitu kama karatasi ndefu sana iliyovingirishwa kwa mviringo na kufanya kuwa kama amebeba fimbo nene au gongo la mti.

    Karatasi hiyo ilikuwa imeviringishwa kwa kufunikwa na kitambaa cheusi kwa juu.

    Alipotoka kwenye Jengo la Basilica moja kwa moja alikuwa anaelekea eneo la wazi la St. Peters Square ambako wale watu sita walikuwa wanamsubiri.

    Tayari ilikuwa inakaribia saa tisa usiku.



    “Inabidi muondoke sasa hivi.!” Father Ricardo akaongea haraka huku anawakabidhi kile alichokibeba.

    Wale watu hawakujibu chochote kile, mmoja wao akapokea ule mzigo alioubeba Father Ricardo na kuanza kuufungua.

    “Mnanisikia? Mnatakiwa muondoke muda huu.!” Father Ricardo akongea tena kwa msisitizo mkubwa.

    Wale watu sita walikuwa ni kana kwamba hawamsikii. Baada ya kupokea ule mzigo aliowapa walisogea pembeni kidogo mpaka mahala fulani kwenye mwanga hafifu wa taa ya ukutani.

    Yule ambaye alipokea ile karatasi kutoka kwa Father Ricardo akapigwa goti moja chini na kuanza kuifungua ile karatasi na kuitandaza pale chini.

    Wote sita walikuwa wanaonekana kwamba wana shauku kubwa sana kuhusu karatasi hii ambayo mwenzao alikuwa anaifungua.

    Macho yao yote yalikuwa yanatazama pale chini kwa shauku kubwa mno na kiasi fulani walikuwa kama wanashindwa hata kusubiri mwenzao amalize kuifungua ile karatasi.



    Yule mmoja aliyepiga goti akaifungua karatasi yote na hatimaye akaitandaza pale juu ardhini.

    Baada ya kuitandaza na wote kutazama macho yao karatasi hii walijikuta wanaweka mikononi kifuani na wengine kinywani kwa mshangao. Walikuwa hawaamini kile ambacho walikuwa wanakiona kwenye ile karatasi.

    Sio kwamba hawakutegemea kuona hiki wanachokiona muda huu, bali ilikuwa ni mshtuko wa uhalisia wa kukipata kile ulichokitafuta kwa muda mrefu sana. Kuna tofauti kubwa ya kuamini kuwa unaweza kupata kitu fulani, na hisia halisi unayoipata baada ya kupata kitu hicho.

    Mbele ya macho yao, pale chini ilikuwa ni karatasi, lakini si karatasi kama karatasi ya kawaida, ilikuwa ni karatasi nzito na ngumu kama turubai au ngozi. Au kwa uhalisia zaidi yapaswa kuitwa ni kipande cha turubai lakini lililo laini uso wake wa juu kama karatasi.

    Ilikuwa na urefu wa hesabu ya haraka haraka kama mita mbili hivi na upana wa kama mita moja.

    Lakini kilichowashitua watu hawa sio ukubwa wa hii karatasi, bali ni kile kilicho juu yake.

    Walihisi kama wako ndotoni, kwa kuwa mbele yao, pale chini walikuwa wanauangalia mchoro wa GEORGE WASHINGTON.!



    Mchoro ambao wiki tatu zilizopoita ulikuwa umeibiwa kutoka Whitehouse ya Marekani. Na ni mchoro huu ndio ambao umebeba siri nzito juu ya mahali ambapo Sanduku la PANDORA linaweza kupatikana.

    “Ni halisi au replica?” Mmoja wao akauliza kama ule mchoro ulikuwa ni ule wenyewe halisi au ni mchoro mwingine tu uliochorwa ili kuigiza ule mchoro halisi wa George Washington. Kutoamini kwake huku kote kulitokana na uhalisia kwamba bado alikuwa anahisi yuko ndotoni. Haikuwa rahisi kwao kuamini kwamba hatimaye wamekipata kitu ambacho wepigana miaka mingi sana kukiweka kwenye milki yao.

    “Ni halisi! Tazama hapa!” Yule aliyepiga goti pale chini akawahakikishia wenzake kwamba kile kilichopo mbele yao kilikuwa ni halisi na wala hawakuwa ndotoni.

    Aliongea huku ananyoosha kidole mahali fulani pembeni kwenye kona ya mchoro akitaka wenzake waone kitu fulani ili nao wajiridhishe nafsi zao kwamba huu mchoro ndio wenyewe hasa halisi waliokuwa wanautafuta.

    [4/25, 20:21] The Bold: Wote wale wengine watano wakainama kidogo ili kuona kwa ufasaha sehemu hii ambayo mwenzao alikuwa anawaonyesha.



    Ilikuwa ni sehemu ya pembeni kabisa ya mchoro ambayo jinsi ambavyo ilichorwa ilikuwa ni meza pekee imetokea, mguu mmoja wa meza ili kuwa sahihi zaidi. Chini ya meza hii iliyotokea kama nusu au robo tu kulikuwa na vitabu kadhaa ambavyo vilikuwa na maandishi fulani hivi ambayo mtu huyu mmoja aliyepiga goti ndipo ambapo alikuwa anawaonyesha wenzake.

    Alichokuwa anawaonyesha wenzake ili waweze kujua uhalisi wa mchoro huu ni wa pekee ndio walikuwa wanakijua.

    Mchoro wote kwa ujumla wake, ulimuonyesha Rais wa kwanza wa Taifa la Marekani, George Washington akiwa amesimama. Mkono mmoja wa kulia alikuwa ameunyoosha mbele au pembeni kutokana na mtu utakavyoona au kutafsiri… mkono wa kushoto alikuwa ameshikilia kitu kama fimbo japokuwa kiuhalisi kulikuwa ni sime lililowekwa kwenye kihifadhio chake.

    Nyumba yake kulikuwa na nguzo mbili za jengo ambazo zilikuwa zimezuia kidogo kwa kiasi fulani muonekano wa mawingu ynayoonekana kwa mbali angani nje ya jengo ambalo George awashington alikuwepo.



    Na nguzo nyingine ya Tatu inaonekana kiduchu mwishoni mwachoro mkono wa kushoto. Pia kulikuwa na kiti nadhifu nyuma yake. Pia kulikuwa na meza ambayo ilitokea kama nusu tu, ambayo ni mguu mmoja tu wa meza ulikuwa unaonekana na kipande kidogo cha juu ya meza kilikuwa kinaonekana na juu yale kuliwa na kalamu ya kizamani pamoja na bakuli ya wino wa kuandikia.

    Huu ndio mchoro ambao ulikuwa unabeba siri kubwa juu ya sehemu ambayo Sanduku la Pandora lilipokuwa limefichwa. Huu ndio mchoro ambao ulikuwa unabeba hatma ya dunia. Ni mchoro huu ambao kama ukitua katika mikonono Salama unaweza kutumika kusaidia kuikoa dunia kutoka katika janga la miji yao kutwaliwa na viumbe wa ajabu, watoto wa Anabelle 01, lakini mchoro huu ukitua kwenye mikono ya watu wasio sahihi unaweza kusaidia kuangamiza kabisa na kuifuta mbari ya binadamu kutoka kwenye uso wa dunia.

    Wale watu sita bado walikuwa wamepigwa na butwaa vinywa vikiwa wazi, na mikono kifuani. Walikuwa wanaona kilichopo mbele yao lakini walikuwa bado hawaamini. Walikuwa hawaamini kama hatimaye wanauweka kwenye milki yao mchoro huu ambao wameusaka sana kwa miongo kadhaa.



    “Mnanisikia? Mnatakiwa muondoke haraka sana.!” Father Ricardo akawashitua kutoka kwenye bumbuwazi lao la furaha.



    “Tuliambiwa kuwa unaweza kutupa hifadhi ya walau siku moja kabla hatujarejea Rabat, Morocco!” Yule mmoja aliyepiga goti moja chini aliongea huku anakunja tena ule mchoro na kuufunika na kile kitambaa cheusi.

    “Ningewapatia hifadhi hata wiki nzima lakini sio kabla ya kuua walinzi wa Baba mtakatifu?” Father Ricardo akaongea kwa kukereka.



    Wale watu wakabaki na mshangao.



    “Miili yao imegundulika?” Wakauliza.

    “Sio kwamba tu miili yao imegundulika, bali muda huu nilivyotoka ndani ya Basilica nimeacha Papa anaenda kuamshwa juu ya tukio hilo la miili ya walinzi wake kukutwa wamechinjwa… kwahiyo kama mnataka mtoke hapa Salama na huo mchoro mliofuata ni vyema muondoke sasa hivi bila kuchelewa.!”

    Watu hao sita wakaangaliana na kisha kupena ishara fulani hivi.

    “Sawa! Nadhani unakumbuka kuwa hauruhusiwi kufanya chochote kuhusu BOOK OF CODES kabla haujapewa ruhusa kutoka…..” Mmoja wao akaeleza lakini kabla hajamaliza Father Ricardo alimkatisha.

    “Ndio ndio! Nafahamu masharti yote… nadhani muanze kundoka sasa kabla wote hatujaingia matatani.!” Father Ricardo akaongea huku anapepesa macho huku na huko.



    Mmoja wa wale watu ambaye aliushikilia ule mchoro, akafunua ile nguo nyeusi aliyoivaa kama kanzu ambayo kiunoni wamejifunga na mshipi wa kamba, kisha akaubana ule mchoro kwa ndani kiunoni.

    [4/25, 20:21] The Bold: Baada ya hapo wakatoa ishara kama ya kuibamisha vichwa hivi kuelekea alipo father Ricardo kuonyesha heshima yao na shukrani kwa kufanikisha walichoenda kukifanya hapa na pia kumuaga.

    “Msalimieni sana Duran! Nategemea kusikia kutoka kwake karibuni!”

    Wale watu wakainamisha vichwa tena kama kukubali kile alichokisema, kisha wakageuka kwa na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi.



    RABAT, MOROCCO.



    “Tafadhalo keti Laura!” Yule Mzee ambaye Rais Laura Keith alimsalimia na kumita kwa jina la Duran aliongea akimuonyesha kiti kimojawapo ambacho kiko wazi pale mezani ili Laura aweze kuketi.



    Bi. Laura Keith ambaye bado alikuwa juu ya meza ambapo alikuwa awali amelazwa juu yake bila kujitambua.



    Alipoanza kushuka watu wote ambao walikuwa ndani ya lile hall walisimama kwa heshima kubwa.

    Akashuka taratibu na kwenda kukaa kwenye kiti pale mezani kilicho karibu kabisa Mzee Duran. Baada ya kuketi watu wote wengine nao wakaketi.

    Mzee Duran akasimama tena na kuanza kuongea.

    “Kaka zangu na dada zangu! Ndugu zangu wa jumuiya ya The 46! Niliwaeleza awali kwamba umefika wakati wa sisi kulipiza kisasi, umefika wakati wa sisi kuirudisha haki yetu ambayo ilipokwa kutoka mikononi mwetu… umefikia wakati wa kuirudisha dunia katika asili yake… kwa karne nyingi sana, tumepuuzwa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha.. Hatiwezi kusahau udhalimu tuliofanyiwa, hatiwezi kusahau usaliti tuliofanyiwa..!”

    Akanyamaza kidogo na kumuangalia Bi. Laura Keith.

    “Dada yetu Laura amefanikisha kufikisha mchoro wa George Washington Vatican… kama kila kitu kitaenda vile ambavyo tumepanga ndani ya wiki moja vijana wetu wa Sancta Cedes wataufikisha hapa mchoro huo hapa Rabat… ndani ya wiki moja nyingine tuna uwezo wa kulipata Sanduku la Pandora…. Na wiki moja nyingine itakayofuata tunairidisha dunia namna inavyotakiwa iwe…. Yaani ndani ya wiki Tatu zijazo tunaibadili dunia nzima kuwa Anabelle…. Kwa hiyo dada zangu na kama zangu, ndugu zangu wa jumuiya ya The 46 nahitaji muende sasa mkatimize jukumu lenu lililobakia, siku Tatu zijazo kila mmoja wetu arejee hapa akiwa na bilauri moja ya mvinyo wa Zeus! Nawatakia kilala kheri na mafanikio mema kwenye kutekeleza jukumu hili… nategemea kuwaona tena hapa baada ya siku Tatu..!”

    Alipomaliza kuongea maneno hayo, watu wote wakainuka na kisha kuanza kuondoka kwa kupitia ule mlango wa mbele wa kuingilia.

    Yeye mwenyewe Mzee Duran, Bi. Laura Keith na watu wengine kama watatu hivi hawakutoka nje, bali walianza kutembea kuelekea ndani zaidi ya Kasri hilo ambalo kulikuwa na kama vyumba vya kuishi au mabweni.

    “Duran.!” Bi. Laura akamkatisha kwa kuongea kwa sauti ya chini ili kuonyesha kutomvunjia heshima.

    Mzee Duran akageuka kumuangalia bila kusema chochote.

    “Kuna jambo nahitaji kukueleza kuhusu nilichokiona kabla hamjaidondosha Airforce One!” Laura akaongea kwa kunong’ona ili wale wengine wasisikie.

    “Nifuate ofisini kwangu!” Mzee Duran aliongea kwa mshtuko, huku akipiga hatua za haraka kuelekea ndani ndani zaidi mwa Kasri ambako kulikuwa na vyumba zaidi lakini kwenye giza totoro.  





    “..kesho inataka nini kutoka kwangu? Nafanyaje pale sauti pekee ninayoisikia kichwani mwangu ni neno “subiri”? Hata nikiamua kusubiri siwezi kuepuka kesho isifike, ni lazima kutakucha na itanipasa kupambana na mashetani yanayonisubiri huko kesho!



    Kesho itakapofika, nikijitoa muhanga nafsi yangu kuokoa kitu pekee chenye thamani kwenye maisha yangu, mtu ninayetamani aishi kuliko nafsi yangu! Je, usiku akienda kulala atakumbuka kafara yangu? Je, ulimwengu utakumbuka ushujaa wangu?

    Ni siku ngapi atalala akikimbuka kafara yangu kabla ya kusahau?



    Nashindwa kuiondoa sauti ninayoisikia kichwani mwangu, kadiri ninavyojitahidi kutoisikiliza ndivyo sauti inavyokuwa kubwa zaidi kichwani mwangu, sauti ya neno moja tu “subiri”!



    Ni mahali gani ambapo natakiwa kuchora mstari wa kusubiri, na muda gani natakiwa kusonga mbele?

    Nahisi kama nimejifungia kwenye dunia ya peke yangu… nahofia hata kuinua mguu kukanyaga hatua moja mbele, kwa kuhofia naweza kuharakisha kesho ikafika haraka, na naogopa pale itakapofika kwa kuwa kichwani mwangu bado sijapata jawabu… kesho inataka nini kutoka kwangu?.”















    EPISODE 14











    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)

    Yule mnyama wa ajabu alikuwa anawasogelea kwa hatua za taratibu lakini akitoa muungurumo mkali sana. Rangi yake nyekundu ya kupauka iliyogeuka kutoka nyeupe ya theluji, ilizidi kuwa nyekundu zaidi kadiri alivyowasogelea na kuunguruma.

    Shafii ambaye alikuwa amedondoka ardhini mara ya kwanza alikuwa ameshainuka na wakakaa tena katika umbo la duara.



    Waliofanikiwa tu kukaa tena kwenye duara yule mnyama akasimama na kuacha kuwasogelea. Lakini ajabu ni kwamba alizidi kuwa mwekundu na shingoni akaanza kufura kama vile kuna kitu kimemkaba au kama nyoka anavyokusanya sumu kabla ya kuitema.

    Ndani ya Anabelle kulikuwa na baridi kubwa sana lakini ajabu ni kwamba Cindy na wenzake walianza kuhisi kama jasho linawatiririka ndani ya masweta na makoti yao kutokana na wote waliokuwa wanausikia muda ule.

    Yule kiumbe akawa kama anachuchumaa hivi, kisha kwa kasi ya ajabu akajifyatua na kuruka juu na kupotea kabisa katika upeo wao wa macho.

    “Ameondoka?” Magdalena akauliza kwa sauti ya woga akiwa ananong’ona.



    “Sidhani!” Cindy akajibu huku anapepesa macho huku na huko.

    Japokuwa yule mnyama alikuwa ametoweka ghafla lakini kulikuwa na hali Fulani hivi kama vile walikuwa wanauhisi uwepo wake pale walipo. Walikuwa na woga uliofanya mwili usisimke mpaka nywele na vinyweleo visimame.

    “Nadhani itakuwa vyema kama….”

    “Ssssssshhhhh!!” Cindy akamnyamazisha Magdalena kama hajaliza alichokuwa anataka kukiongea.

    “Nini?” Magdalena akauliza.

    “Sikilizeni hiyo sauti!” Cindy akaongea huku anageuza sikio lake moja kuelekea juu hewani.

    Kulikuwa na sauti kama vile mlio was birika la umeme la kuchemsha chai mlio ambao huwa linatoa pale ambapo maji yakichemka. Mlio wa mluzi hafifu wenye kusikika kwa mbali sana.

    Wote wakasikiliza kwa kuelekeza sikio moja juu lakini kila ambavyo walivyojaribu kutazama ili wawia vigumu kung’amua chochote kutokana na giza la ajabu ambalo limetanda ndani ya Anabelle.



    Walikuwa bado wamekaa katika mfumo ambao walikuwa wameweka duara na Kanali yuko kati kati ya duara nyuma ya mgongo was Cindy.



    Kadiri ambavyo sekunde zilivyokuwa zinaenda ndivyo ambavyo mlio huo wa mluzi hafifu ulivyozidi kuwa dhahiri na kusikika kwa usawia zaidi. Kadiri ambavyo ulikiwa ukisikika kwa sawia zaidi ndivyo ambavyo ulibadilika na kusikika kama mlio wa kitu kinachoenda kwa kasi sana kukinzana na upepo.







    Mlio ulikuwa unasikika kama vile mkuki uliotupwa hewani au kama treni lisilotoa kelele likiwa kwenye mwendo kasi wa juu kabisa likikata mawimbi ya upepo.

    Ikawa dhahiri kwamba mlio huo ulikuwa ni sauti ya kitu kinachoshuka kutoka hewani kwa kasi kubwa.

    Salim akapata akili, akang’amua ni nini kilikuwa kinatokea…

    “No no no no nooooo!! Kanali lala chiniiiii..!!” Salim akapiga kelele kubwa kumtahadharisha kanali.

    Lakini kabla kanali hajafanya lolote, kuna sauti kama ya tai mwenye hasira au aliyejeruhiwa ilisikika kwa nguvu na kasi ya ajabu na kufumba na kufumbua yule kiumbe ambaye alikuwa amepotea ghafla machoni mwao alikuwa juu yao anashuka kwa kasi kama mwewe anavyoshuka kuchukua kifaranga cha Kuku. Kabla hawajapata akili ya kufanya lolote walishtuka kwa kasi ya ajabu Kanali amenyakuliwa na yule mnyama na akajitupa naye kwa kishibdo kikubwa kwenye ule mto uliopo pembeni yao.

    Ili kasi na msukumo wa upepo uliosababishwa na yule kiumbe kushuka kwa kasi ulifanya wote wadodondoke chini.

    Kishindo cha yule mnyama alichojirusha nacho majini akiwa amembeba kanali kilisababisha maji mengi kuruka kutoka mtoni na kufika nchi kavu.



    Wakiwa wanahema kwa woga na nusu kama wamechanganyikiwa wakanyanyuka kutoka kila mmoja alipodondokea na kuanza kujikagua kama yulo salama.



    “Nini kimetokea??” Shafii akauliza huku anahema anageuka geuka kila upande kama amechanganyikiwa.

    Hakuna aliyejibu, kila mmoja alikuwa katika mshtuko.

    Cindy aligeuka pembeni yake akamuona Salim anavua buti miguuni.



    “Unataka kufanya nini?” Cindy akamuuliza Salim kwa mshangao.

    “Napiga mbizi mtoni!” Salim akajibu huku kweli akijiandaa kujitumbukiza mtoni.

    “Hapana Salim!” Cindy ilibidi amrukie kumzuia asijitose mtoni.

    “Hatuwezi tena kumsaidia… tumeshampoteza kanali! Tafadhali usifanye tukupoteze na wewe!” Cindy akafoka huku amemng’ang’ania Salim kiunoni.

    “Hapana hatuwezi kumuacha apotee hivi hivi bila kufanya chochote!”Salim akafoka kwa sauti ya kutetemeka kama anataka kulia.

    ” Salim nisikilize! Ukijitosa humo ndani ya mto hautoki tena… tumempoteza kanali! Usifamye maamuzi ya kijinga!” Cindy akamng’ang’ania zaidi Salim kiunoni asijitose mtoni.



    Ilibidi Shafii naye ajikaze kiume kumsadia Cindy kumshikilia Salim asijitose mtoni.

    Kwa pamoja ikabidi wamdondoshe chini na kumbana asifanye mushkeli wowote.

    “Salim, Salim! Tafadhali usifanye maamuzi ya kijinga… wote tunatamani kumsaidia kanali lakini hakuna anayejua hapa kilichomo ndani ya huo mto… hebu msikilize Cindy!” Shafii akaongea kwa sauti ya majonzi kujaribu kufanya Salim afikiri sawa sawa kuhusu alichokuwa anataka kukifanya.

    Hatimaye Salim akatulia, akainuka na kukaa kitako pale chini anahema kama mbwa kwa hasira.



    “OK! OK OK OK!” Ndio maneno pekee ambavyo Salim alijikuta ameweza kuyatamka huku bado akiwa anahema kwa hasira.

    Wakiwa bado wanamtuliza Salim asifanye maamuzi yoyote ya kijinga ambayo yatawagharimu, pembeni yao wakamsikia Magdalena analia kwa kwi kwi sauti ya chini kabisa.

    “Magdalena! Magdalena!” Cindy akamuita Magdalena lakini hakuitika.



    Kilio chake kilikuwa kinaogopesha kwa kuwa alikuwa analia katika namna ambayo ilionyesha dhahiri kuwa kilio chake hakikuwa kilio cha kumlilia Kanali, bali lilikuwa jambo lingine kabisa.



    Wote wakajikuta wanaacha kumtuliza Salim na kumgeukia Magdalena ambaye alikuwa amekaa chini amejiinamia magotini analia kwa kwi kwi.



    “Magdalena!” Salim akamuita huku anainuka kutoka pale chini walipomdondosha na kumfuata pale Magdalena alipokaa na kujiinamia analia.

    “Magdalena! Kuna nini?” Salim alimuuliza huku amepiga magoti mbele ya Magdalena alipokaa na kujiinamia.

    Magdalena alishindwa kuongea chochote, akainua tu kiganja cha mkono na kumuonyesha Salim.



    “Maji ya mto yamenirukia!” Magdalena akaongea huku kilio kinazidi.

    Wote wakaelewa sasa ni nini kilikuwa kinamliza Magdalena. Kumbe yule mnyama alipojirusha mtoni baada ya kumnyakua Kanali, kile kishindo cha kujitupa mtoni maji yaliruka na kiasi fulani cha maji yalidondoka kiganjani mwa Magdalena.











    Hii ilimaanisha kwamba kuanzia sasa viumbe waliomo ndani ya Anabelle walikuwa na uwezo wa kunusa harufu ya Magdalena na kumuona na kuna uwezekano wa kumpata kilichompata Kanali.

    Salim alijikuta anashindwa kuongea chochote kile, akamkumbatia kwa nguvu Magdalena kwa uchungu.

    Alijisikia uchungu sio tu kwa sababu sasa kulikuwa na uwezekano wa Magdalena kumkuta kilichomkuta Kanali, bali pia alijisikia hatia moyoni mwake kwa kuwa bila yeye kuingia ndani ya Anabelle basi Magdalena asingeliingia humu ndani.

    Magdalena ameingia humu ndani ya Anabelle kutokana na mapenzi aliyonayo kwa Salim.

    Salim ameingia humu ndani ya Anabelle kwa matumaini kwamba labda anaweza kuikoa familia yake, mtoto wake Basrat na mkewe Khadija, na Magdalena alimfuata Salim alipoingia humu kutokana na kushindwa kushuhudia mwanaume anayempenda akiingia humu na yeye abaki nje bila kujua ni nini kitampata humu.

    Hii ndio ilimfanya Salim ajisikie hatia moyoni mwake endapo jambo lolote baya likimpata Magdalena.

    Akamkumbatia kwa nguvu zaidi.



    “Nakuahidi siwezi kuruhusu wakuchukue!” Salim akaongea kwa hasira na kujiamini japokuwa hakujua ni nini hasa atakifanya.

    “Umesikia Magdalena? Siwezi kuruhusu wakuchukue!” Akamkumbatia kwa nguvu zaidi.

    Wakiwa wamekumbatiana hivyo, mara wakamsikia Cindy anawaita kwa sauti ya chini sana ya kunong’ona.

    “Salim!”



    Salim akageuka haraka upande ambao Cindy alikuwa anamuita.

    “Amerudi tena! Tayari amenusa harufu ya Magdalena!” Cindy akaongea kwa woga kwa sauti ya chini sana.

    Wote wakajikuta wamesimama na kujikusanya pamoja kama vifaranga vya Kuku vilivyohisi mwewe yuko juu yao angani na hakuna mbawa za mama yao kujificha.



    Bado walikuwa hawajamuona yule kiumbe lakini mpaka sasa walikuwa wameng’amua hisia ambayo walikuwa wanaipata yule mnyama akiwa karibu.

    Nywele zilikuwa zinasimama, vinyweleo vinasimama, na kiwango cha baridi kinaongezeka maradufu.

    Wakiwa wamejikusanya vile kama vifaranga vya Kuku wakipepesa macho wasijue mnyama huyo atatokea wapi, mara mbele yao mtoni kama ilivyokuwa awali, wakaanza kusikia yule mnyama taratibu sana anatoka kwenye maji.

    Alikuwa anatoka taratibu sana kwa tahadhari kubwa kama vile mamba afanyavyo ili kufanya windo lake asisikie sauti ya yeye akiwa anatoka majini.

    Wote wakakaza macho yao mtoni sehemu ambayo walikuwa wanasikia yule kiumbe anatoka.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kama ilivyokuwa awali, ndani ya kama nusu dakika mbele yao alikuwa amesimama tena yule kiumbe mwenye umbo kama la mbwa, lakini mkubwa kuliko ndama wa ng’ombe na mwenye mabawa ya kufanana na popo na hana nyoya hata moja mwili wake wote na licha ya kwamba alipoondoka baada ya kumnyakua kanali alikuwa amebadilika na kuwa rangi nyekundu lakini Safari hii alikuwa amerejea tena kwenye rangi yake nyeupe kama theluji au sufi.

    “Cindy nipe hiyo chupa!” Salim akaamuru apewe ile chupa ambayo muda wote wakitembea Cindy huwa anaibeba kwa kuiweka mbele yao kama tochi huku iking’aa kwa rangi ya buluu.



    Cindy akamkabidhi ile chupa.

    “Tengenezeni tena duara! Magdalena kama nyuma yangu” Salim akawaamuru watengeneze duara kama mwanzo kumzunguka Magdalena ambaye yeye kwa sasa harufu yake ilikuwa inaweza kunuswa na hawa viumbe.

    “Sitaki mtu anishike tena! Niacheni nifanye ninachotaka kufanya..!” Salim akaongea kwa hasira mpaka sauti inatetemeka.

    “Unataka kufanya nini Salim!” Magdalena akauliza woga ukisikika kabisa kwenye sauti yake.

    “Subiri utaona! Hatuwezi kuacha hawa mashetani watuwinde kama vifaranga vya Kuku!” Salim akajibu kwa kujiamini.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog