Search This Blog

Sunday 20 November 2022

THE OTHER HALF - 4

 





    Simulizi : The Other Half

    Sehemu Ya Nne (4)





    Cindy na wenzake wakatulia wakiwa wamejificha nyuma ya miti wakiangalia kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mbele yao.



    Kama dakika moja baada ya yule mtoto wa Maldives kuondoka pale ambapo sauti ilitoka na mwanga wa jua, ghafla binadamu wa kawaida kama walivyo wao akina Cindy aliyokea kwa kukwea kutokea ardhini. Mtu huyu alikuwa amevalia suti nyeusi na kichwani alikuwa amenyoa upara unaongaa kama umepakwa mafuta ya kupikia.

    Baada ya kukwea kutokea ardhini, alisimama aliwa na kifurishi fulani hivi amekishikilia. Hakuna na wasiwasi, alionekana dhahiri alikuwa anajua anachokifanya na hii ilikuwa ni kawaida kwake kufanya hiki anachokifanya hapa. Akakiweka pembeni juu ya ardhi kisha akaanza kurejea ardhini akishuka kama vile anashuka ngazi kwenda chini.



    Akashuka namna hiyo mpaka akapotea ardhini na mara tu baada ya kupotea ule mwanga wa jua ukapotea ghafla.



    Cindy na wenzake wakabakia wanazamana tu. Kile kifurushi alichokuja nacho yule mtu kilikuwa kimebaki pale pale juu ya ardhi. Ilionekana kwamba mtu yule kusudi lake la kuja ilikiwa ni kuleta hiki kifurushi.



    Salim pasipo kuongea chochote akaanza kutembea kuelekea pale kwenye kifurushi. Wenzake nao wakaanza kumfuata kuelekea pale pale.

    Walipolifikia tu, Cindy aliwakataza wenzake wasikiguse. Akachukua ile damu ya mtoto wa Maldives akamwagia kidogo juu ya kifurushi na kisha kuanza kukifungua. Kilikuwa ni kifurushi kimevingirishwa kwenye kitambaa kikubwa cheusi. Baada ya kukifungua walichokikuta ndani yake ilikiwa ni nguo ambayo waligundua kuwa ni suti ya kike, pia kulikuwa na hereni, bangili, kidani cha shingoni na kitu fulani kidogo sana kimewekwa kwenye kijimkebe cha pastiki.



    Cindy hakujua ni kwa nini lakini alijikuta anapata hisia kwamba amewahi kumuona mtu amevaa vitu hivi lakini hakuweza kukumbuka sawa sawa ni nani mtu huyu.

    Lakini pia macho yake yaliganda kwenye kile kidubwasha kiduchu ambacho kiko kwenye kijimkebe cha plastiki. Cindy akachukua ile chupa yao yenye kutoa mwanga wa bluu na kutumia kutazama kidubwasha hiki huku akikigeuza geuza. Baada ya kama dakika mbili hivi akaelewa ni kitu gani, kilikuwa ni POLO-TD.







    Ndipo hapa ambapo akawaeleza wenzake kuhusu kifaa hicho na kazi yake na pia akawaeleza kuwa ana hakika kuwa nguo hizo ni nguo za Bi. Laura Keith, rais wa Marekani na ndio maana alipoziona tu alihisi kuzifahamu.



    Wakiwa bado wanaendelea kujadili nguo hizo, Salim akawashitua wenzake waangalie pale pembeni ambapo yule mtu aliyeleta hicho kifurushi aliingia ardhini.



    Kulikuwa na kama mfuniko hivi wa chuma kizito wenye umbo la mstatili na ukubwa wa kama meza ya chakula, ambao juu yake kulikuwa na kama usukani hivi wa chuma wa kuzungusha.



    Juu ya mfuniko huu wa chuma kizito, kulikuwa na maandishi machakavu sana yanayosomeka kwa shida yakiwa yameandikwa kilatini QUADRAGINTA SEX (THE FORTY SIX).



    Cindy akawaeleza wenzake, “huu ndio mlango wa The 46 tuliokuwa tunautafuta…”.



    Salim akataka kuzungusha ule usukani kama ambavyo yule mtoto wa Maldives alifanya na kufungua huo mfuniko lakini Cindy akamuwahi na kumkataza. Akamueleza kuwa kuna namna maalumu ya kuzungusha usukani huo wa chuma na kufungua huo mfuniko. Kama wakikosea hajui nini kitatokea lakini ana uhakika kuwa watajutia kitakacho wakuta.

    Akawaeleza kwamba siri ya kufungua mlango huo wa The 46 iko kwenye mchoro wa George Washington, detail #127 upande wa kushoto.



    Wakiwa wanaongea haya ghafla wakasikia kuna kitu kinakuja kwa kasi sana kuelekea pale walipo



    ” nadhani watoto wa Maldives wanakuja!” Salim akawaeleza wenzake.



    Kwa haraka sana wakakimbia na kwenda kujificha tena nyuma ya miti.



    Safari hii walikuja viumbe hawa watatu. Walipofika wakaanza kutafuta tafuta ikonyesha dhahiri kuwa walikuwa wanatafuta kile kifurushi kilicholetwa. Baada ya kutafuta kama dakika mbili nzima bila kukiona wakaanza kuunguruma huku wanainua vichwa juu kama fisi afanyavyo. Walikuwa kwenyr hasira kubwa na walikuwa wameng’amua kuwa kuna kiumbe kimeingilia himaya yao.



    Wakatoka mahala pale kwa kasi ya ajabu lakini hawakuelekea mbali sana. Wakaenda mpaka mtoni na kuanza kufukua ili kuchepusha maji kuelekea kule msituni. Hawakuakuingiza maji mengi sana bali kiasi tu, lakini ghafla hali ya hewa pale msituni ikaanza kuwa tete. Baridi liliongezeka mara dufu kiasi kwamba Cindy na wenzake wakajua kabisa kwamba wako hatarini.



    Ndipo hapa ambapo wakajigawa makundi mawili. Shafii na Magdalena wakabaki mahali fulani karibu na msitu ili kuchunguza kila kinachoendelea mle ndani hasa hasa hasa ple kwenye mlango wa The 46.

    Cindy na Salim wakarudi tena walikotokea ili kutafuta masaada kutoka duniani.

    Wakiwa njiani Cindy na Salim baada ya majadiliano marefu ya namna gani wanaweza kuwasiliana na dunia, ndipo hapa wakapata wazo la kutumia ile Chupa inayowaka mwanga wa bluu ambayo inawalinda humu ndani ya Anabelle.



    Japokuwa alikuwa hataki kuwaeleza wenzake ili wasije kupaniki, lakini Cindy alifahamu fika kwamba japokuwa walikuwa wamekuwa ndani ya Annabelle kwa masaa kadhaa tu lakini huko duniani yawezekana mawiki au miezi imepita lakini wao kitu pekee walichokuwa wanakiona ndani ya Anabelle ni usiku wakisubiri kukuche. Lakini alijua wazi kwamba huko duniani kunakucha na kuwa usiku tena kila baada ya dakika kadhaa za ndani ya Anabelle.



    Ndipo hapa ambapo alipata wazo la kutumia chupa chupa hii iliyotoka kwenye sanduku la Pandi kuiweka kwenye barabara mojawapo ili huko duniani kukikucha labda wanaweza kuiona hiyo chupa kama watakuwa bado wanaendelea na utaratibu wa kukagua Anabelle.

    Cindy akachukua kalamu na kuandika;



    “Ni masaa 16 tangu tuingie ndani ya Anabelle. Wote tuko salama isipokuwa Kanali ameuwawa na kiumbe cha ajabu. Tumefanikiwa kufika nje ya mlango wa The 46. Ndani ya masaa manne yajayo tunahitaji detail #127 kushoto mwa mchoro wa George Washington ili tuweze kufamilisha azma yetu na kutoka tukiwa hai.

    Pia mikononi mwetu tunazo nguo za Madam President Laura Keith, Kidani chake ch a shingoni, hereni, pete ya ndoa na POLO-TD.

    Tumeonywa pia wakala wa The 46 amerejeshwa duniani. W7. W7. W7.”







    Huu ndio ujumbe ambao Cindy na Salim waliuweka kwenye chupa na kuiweka barabarani masaa mawili yaliyopita na waliporejea sasa hivi Chupa hawakuikuta na wakaamini kuwa watu waliopo duniani wameiona na kuichukua.



    Kilichowashangaza ni kwa nini mpaka muda huu bado walikuwa hawajajibiwa.



    “Tukiwa tunaendelea kusubiri hayo majibu nina maswali kadhaa nataka unifafanulie!” Salim akaongea huku amekaza macho kwa Cindy.



    Kabla hata hajauliza, Cindy alijua wazi kwamba Salim alikuwa anatala kujua kwa nini ameandika ndani ya masaa manne wanaweza kufa. Kwa nini ameandika wakala wa The 46 amerejeshwa duniani. Detail #127 ya mchoro wa George Washington ni nini?? W7 ilikiwa na maana gani? Na kama Salim alikuwa ni mtu mwenye kufikiri kwa uangalifu lazima alikuwa ameng’amua kuwa kuna tofauti kubwa ya muda kati ya dunia na ndani ya Anabelle.



    Cindy akashusha pumzi kwa nguvu. Yatosha sasa. Huu ulikuwa ni muda wa kuwaambia ukweli wote na kuwatoa gizani.







    THE OTHER HALF

    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE







    EPISODE 24







    MASAA 8 YALIYOPITA (WASHINGTON D.C)







    WHITEHOUSE MEDICAL UNIT







    “Madam president… madam President… Madam president!!”



    Rais Laura Keith alikuwa anaisikia kwa mbali sana sauti ya ikimuita akiwa anatoka kwenye usingizi mzito wa ‘coma’ ya karibia siku nne aliyokuwemo.

    Kwa kiasi fulani alikuwa anahisi anafahamu mahali alipo lakini pia kwa kiasi fulani usingizi wa Coma bado ulikuwa haujaondoka vizuri kichwani.



    “Madam President… Madam President…” Dominic Wallace, daktari mkuu wa kitengo cha afya cha Rais, au kama kinavyojulika “Whitehouse Medical Unit” alikuwa anajitahidi kumuamsha na kumsikiliza Laura ili kujua kama alikuwa amerudi katika ufahamu wa kawaida.



    “Niko….wapi?” Laura akatamka kwa taabu sana hatimaye.



    “Madam President! Tafadhali usijigeuze… upo Whitehouse kitengo cha afya… uko Salama!! Tafadhali bakia mtulivu.!” Dr. Wallace alikuwa anaendelea kumuondoa hofu Laura ambaye bado alikuwa kwenye bumbuwazi la usingizi wa Coma.

    Baada ya mshituko kumuisha Laura na kurudi kwenye hali ya utulivu madaktari wote wa Ikulu waliingia kwenye chumba alichokuwemo na kwa haraka na uangalifu makubwa kila mmoja alianza kuangalia mwenendo wa afya yake kupitia vifaa vya kielektroniki alivyoungamishwa navyo.



    Zoezi hili lilichukua karibia dakika kumi na tano mpaka ambapo madaktari wote walijiridhisha kuwa afya ya rais iko kwenye hali nzuri na hakuna tishio lolote la afya yake.

    “Dr. Wallace.!” Laura alimuita daktari wake wa siku zote tangu siku ambayo ameapishwa kuwa Rais mpaka siku ambayo alipotea.

    “Ndio Madam President.!” Dr. Wallace akaitikia.



    “Nahitaji kuongea na Admiral Smith.!” Laura akaongea kwa ufupi.



    “Madam President nadhani itabidi usubiri kidogo… tumefikisha habari ya wewe kuzinduka kutoka usingizini kwa Makamu wa Rais… na nadhani wako kwenye kikao muda huu wanajadili swala hili kabla hawajaja hapa kukuona.!”



    Japokuwa Laura hakujibu chochote lakini uso wake ulionyesha dhahiri kabisa kuwa habari hii ilikuwa imemshitua sana. Ingawa alikuwa anajaribu kwa kila namna kuficha mshtuko ambao alikuwa nao lakini hata Dr. Wallace aliweza kuusoma uso wa Laura.



    “Madam? Uko sawa?” Dr. Wallace aliuliza huku naye akiwa yuko kwenye mshangao kwa kumuona Laura yuko kwenye mshtuko.



    Laura bado alikuwa na mshtuko huku uso wake ameuelekeza juu kama kuna kitu fulani anafikiri au anajaribu kufanya uamuzi fulani hivi.



    “Madam President!” Dr. Wallace akaita tena, “Madam President.!”

    “Wallace niitie Kiongozi wa Maafisa wa Secret Services walioko zamu Leo!” Laura aliongea huku bado anaangalia juj kama bado anafikiria jambo au anajaribu kufanya uamuzi fulani kichwani.



    “Uko sawa mama?” Dr. Wallace aliuliza tena.



    “Wallace.!! Nimesema niitie Afisa kiongozi wa Secret Services..!!” Laura aliongea kwa ukali safari hii huku akiacha kuangalia juu na kumkazia macho Dr. Wallace.



    “Sawa Mama.!” Wallace aliongea kwa ufupi na kuanza kutoka ndani ya chumba alichomo Rais Laura Keith kwa haraka.











    ************











    Kama dakika tano baadae, Special Agent In Charge, Renaldo Gillemo alikuwa mbele ya kitanda alicholazwa Madam President Laura Keith.



    Hakuwa peke yake bali nyuma yake alikuwa ameongozana na maafisa wengine watatu.



    “Habari Madam President.!” Gillemo akamsalimia Laura.



    “Nzuri.! Habari yako Renaldo.!” Laura akaitikia Salamu.



    “Niko mzima kabisa… pole sana kwa kilichotokea Madam… na kwa niaba ya Idara nzima ya Secret Services naomba utusamehe kwa kushindwa kukulinda sawia pale tulipotakiwa kufanya hivyo na pia kushindwa kukupata na kukurejesha jyumbani salama.!” Agent Gillemo akaongea kwa heshima kubwa.



    “Usijali Renaldo, hakuna ambacho mngeweza kukifanya… ilikuwa ni ajali.!”



    “Hata hivyo naomba utusamehe Madam President.!” Gillemo akasisitiza tena.



    “Sawa Renaldo! Shukrani kwa uungwana wako… nimekuita hapa kuna suala la dharura kidogo.!” Laura akaongea huku uso ukibadilika kutoka kuwa na muonekano wa kirafiki mpaka kuwa na muonekano wa ‘kazi’.



    “Madam President… haudhani kwamba ungepumzika kidogo kabla ya kuanza kujiingiza kwenye taharuki ya kazi za ofisi na mambo mengine… Makamu wa Rais na viongozi wengine wako kwenye kikao muda huu wanapewa muhtasari kuhusu hali yako na nadhani muda si mrefu watakuja hapa kukuona.!” Gillemo akaongea kwa msisitizo na heshima.



    “Renaldo, hicho hasa ndicho ninachotaka ukizuie.!” Laura akaongea kwa msisitizo na kupaniki kidogo.



    “Nini Madam?” Renaldo akauliza kwa mashangao.



    “Makamu wa Rais, David Logan… nataka awekwe chini ya ulinzi sasa hivi bila kupoteza muda wowote ule.!” Laura akaongea kwa sauti ya mamlaka.



    “Ati? Unahakika kuhusu hili Madam President?” Gillemo akauliza kwa mshangao mkubwa sana.



    “Renaldo, umenisikia nilichokuambia?” Laura akamkazia macho Gillemo.



    “Madam! Samahani naweza kukuliza ni kwanini unataka tufanye hivyo??” Gillemo akauliza tena kwa mshangao mkubwa zaidi.



    Laura aliinuka kwa hasira na kukaa kitako pale kitandani, akasogeza uso wake karibu kabisa na uso wa Special Agent Renaldo Gillemo.



    “Hii ni amri kutoka kwa Rais wa United States Of America.! Nakuamuru umuweke chini ya Ulinzi David Logan Mara moja.!” Laura akaongea akiwa amemkazia uso Gillemo.



    “Sawa Madam President.!” Gillemo akatii amri na kugeuka nyuma.

    Baada ya kugeuka tu akaanza kuongea kwenye kinasa sauti kilichopo kwenye kiganja usawa wa mkanda wa saa ya mkononi.

    “..code 6 – sahara – oo7.! Narudia code 6 – sahara -007! Narudia code 6 – shahara – 007!”



    Gillemo akaongea kwenye ‘microphone’ kiganjani kwa kurudia rudia huku wanaondoka kwa kukimbia na wenzake aliofuatana nao.

    Sahara lilikuwa ni jina la fumbo ambalo kilikuwa linatumiaka kumtambua Makamu wa Rais David Logan katika mawasiliani ndani ya Secret Services.

    Code 6 ni tahadhali kwa maafisa wa Secret Services kwamba wanatakiwa wampe ulinzi wa dharura mtu huyo anayehusika.

    007 ilikuwa ni utambulisho wabtahadhali kwamba ulinzi atakaopewa mtu huyo uwe ni ulinzi wa kuchukuliwa kama adui au kwa umombo ndio kusema mtu huyo mi “hostile”.

    [6/3, 22:55] The Bold: Ndani ya dakika chache maafisa kadhaa wa Secret Services walikuwa wanakimbia kwenda Oval Office na wengine wakikimbia kuelekea Situation Room.



    “Nini kinaendelea?” Kevin, Katibu wa Makamu wa Rais David Logan alimuuliza Gillemo baada ya yeye na wenzake kuingia kwa kusukuma mlango kwa nguvu.



    “Makamu wa Rais yuko wapi?” Gillemo akauliza kwa hasira.



    “Gillemo nini kinaendelea?? Nimesikia code 6 imewekwa kwa Makamu wa Rais? Nini tatizo?” Kevin akauliza tena bila kujibu swali la Gillemo.

    “Ni amri kutoka kwa Rais anatakiwa kuwa chini ya ulinzi.!” Gillemo akajibu haraka haraka.



    “Ati? Kuna nini kinaendelea?” Kevin akauliza kwa mshangao.



    “Kevin nieleze kwanza yuko wapi?” Gillemo akaongea kwa hasira zaidi.



    “Ameondoka dakika kumi zilizopita na Maafisa wachache kuelekea nyumbani kwake.!” Kevin alijibu huku bado akiwa kwenye mshangao.



    Kwa akili yake iliyozoea masuala ya ushushushu na ujasusi, Gillemo alitambua wazi kwamba Makamu wa Rais David Logan alikuwa anajua kuwa anafuatiliwa na alikiwa amachukia tahadhari mapema.

    Hakutaka kupoteza muda, akaanza kuongea tena kwenye kinasa sauti mkononi mwake huku anaondoka kwa kasi yeye na wenzake kutoka Oval Office.



    “Maafisa wote narudia code – 6 sahara -007! Code 6 sahara -007. Narudia code -6 sahara 007.!!”

    Gillemo akarudia tena maelezo haya ya mafumbo kwa matumaini kuwa labda maafisa waliopo na Makamu wa Rais David Logan walikuwa hawajasikia tahadhali hiyo. Kwa hiyo alirudia kwa matumaini kuwa watasikia na hatimaye kumuweka David Logan chini ya ulinzi.



    “Agent 0012… nahitaji alaert kwa Leopards, nahitaji Assault Team iwe imefika Naval Observertory Cicre sasa hivi.!”



    Gillemo akaongezea. Hii alikuwa anaipa taarifa ofisi ya Secret Services hapo Whitehouse wawsiliane na Whitehouse Military Office (jina la fumbo “Leopards”) ili wapeleke Assault Team kwenda Naval Obsertory Circle ambako ndiko kuna makazi ya makamu wa Rais.

    Whitehouse Military Office (Leopards) ni ofisi ya jeshi (tawi) iliyopo ndani ya Whitehouse ambayo kazi yake ni kumpa taarifa au kuwa kiunganishi cha Rais na jeshi muda wote. Lakini pia ni ofisi ya kimkakati kwa Whitehouse kufanya mawasiliano na jeshi kwa haraka pale ambapo msaada wa kijeshi ilikuwa unahitajika.

    Laiti kama wangelijua kinachoendelea. Laiti wangejua hii “ngoma” wanayochezeshwa. Laiti kama wangelijua mtego mujaribu uliokuwa umetegwa. Wanasema majuto ni mjukuu.





    Dakika 10 baadae…











    Taarifa ilikuwa imetumwa Whitehouse kutoka kwa Assault Team iliyoenda Kwenye makazi ya Makamu wa Rais yaliyopk Naval Observertory Circle.



    Taarifa hii ilikuwa inaeleza kwamba, wamekuta hapo magari yote matatu ambayo yaliondoka Whitehouse na Makamu wa Rais. Magari mawili yakiwa ni ya ulinzi wa Secret Services na gari moja lilimbeba Makamu wa Rais.

    Ilionekana kwamba Makamu wa Rais aliondoka na ulinzi wa Maafisa 12 wa Secret Services.



    Taarifa hiyo ilieleza kuwa Maafisa 9 wa Secret Services walikutwa ndani ya nyumba wakiwa wameuwawa kwa kupigwa Risasi lakini Maafisa watuatu walikuwa hawajulikani walipo na pia Makamu wa Rais David Logan naye hajulikani alipo na hakukuwa na viashiria vyovyote (trail) ya kuonesha ni wapi wameenda.



    Watu wote pale Whitehouse wakabaki na mshangao na maswali lukuki kichwani.



    Makamu wa Rais yuko wapi?

    Nani ameua wale maafisa 9?

    Wengine watatu wako wapi?

    Aliwezaje kuondoka na msafara pale Whitehouse bila Secret Services wengine kujua?

    Ni nini kilikuwa kinaendelea hapa? Kwanini ameondoka??



    Wote walikuwa wanaumiza akili kufikiria ni wapi Makamu wa Rais alipo.

    Lakini Kevin kwa upande wake akaanza kupata hisia mbaya! Akaanza kuhisi kuna kitu kikubwa zaidi kimejificha nyuma ya pazia. Kuna ‘mchezo’ wamechezewa. Na alipata hisia hii baada ya wazo kupita kichwani mwake kuhusu nani alitoa amri David Logan akamatwe?? Sababu ilikuwa ni nini??





    SASA HIVI…

    “..Natalie..!” David Logan aligugumia tena kwa maumivu huku analitaja tena jina lile lile.



    Damu ilikuwa inazidi kumwagika pale chini sakafuni. Hii ulifanya harufu ya damu mbichi ya binadamu kuongezeka maradufu ndani ya lile Jengo kubwa tupu kama ghala.



     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Vidonda vyake vibichi tumboni na usoni vilizidi kutiririsha damu.

    Pale kwenye sehemu za siri alipoingizwa kitu chanye ncha kama spoku nako kulinza kuvuja damu.



    “..na…ta…li..e.!” Logan aliendelea kugugumia kwa maumivu huku anataja tena lile jina.

    “…mzee kama nilivyo kwambia nadhani anajaribu kunibu swali lako… ni nini anachokijua kuhusu The 46.!” Yule kijana mwenye upara na suti nyeusi akiwa ameloa damu ya David Logan aliongea huku anamuangalia Duran.

    “Nadhani hivyo pia! NATALIE..” Duran aliongea huku anatoa tabasamu la kifedhuli.





    THE OTHER HALF















    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE















    EPISODE 25



















    ANNAPOLIS, MARYLAND (NYUMBANI KWA MZEE CALEB)











    Naomi, Ethan, na wenzao wote walikuwa wamekaa kimya pale mezani wakimsubiri mzee Caleb awafafanulie ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Licha ya purukushani zote ambazo walipitia pamoja lakini kutokana na taarifa ambayo waliipata kupitia simu aliyopigiwa Naomi kwamba Ikulu kumevamiwa na aliyeongoza uvamizi huo alikuwa ni Caleb, hii iliwafanya wote wamtazame kwa jicho la mashaka licha ya ukweli kwamba walikuwa naye muda wote huu.







    Caleb mwenyewe alionekana alikuwa anafahamu ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Alikuwa bado amekaa kwenye meza pale uso ameinamisha anatazama chini kwenye kikombe chake cha kahawa.







    “Mnataka niwape ufafanuzi upi? Kuonekana mtu kama mimi Ikulu ilhali niko nanyi hapa? Au mnataka ufafanunuzi kwa nini yule binadamu wa ajabu porini ameniita mwanangu au niwaeleze kuhusu hayo makaburi hapo nje ya nyumba yaliyofichwa?” caleb aliuliza bila kuwaangalia huku bado anaendelea kutazama kikombe chake cha kahawa pale mezani.







    Naomi na Ethan wakatazamana bila kusema neno lolote lile. Lakini walikuwa kama wanajaribu kusomana usoni kufanya uamuzi wamueleze aanze na ufafanuzi upi.







    “Vitu vya kwanza vinatakiwa kuwa mwanzoni… tuanze na yule binadamu wa ajabu msituni aliyekuita mwanangu?” Ethan hatimaye alitoa pendekezo la ufafanuzi upi uwe wa kwanza.







    “Ni baba yangu.!! Baba yangu mzazi..!” Caleb alijibu kwa kifupi.







    Naomi na Ethan pamoja na wenzao walijikuta wanatazamana mshangao bila yeyote kuongea nenoo lolote lile.







    “samahni… unasema baba yako? Kama macho yangu yanaona sawa sawa nadhani yule kiumbe anaonekana kijana kuliko wewe..!” Naomi akauliza kwa sauti ya utulivu lakini iliyojaa mshangao.







    “Macho yako yanaona sawa sawa na naamini pia yameona vitu vingi sana ambavyo sio vya kawaida juu ya yule binadamu… kwa hiyo sidhani kama kuna jambo la kushangaza akionekana kijana kuliko mimi na bado akiwa baba yangu..!” Caleb aliongea huku bado ametazama chini.







    “Mzee nadhani ingekuwa vyema kama ungetufafanulia zaidi kuhusu hili…!” Ethan akaongezea.











    Mzee caleb alivuta pumzi ndefu ndani na kisha kuitoa nje. Kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya nusu saa akainua uso wake kutoka kwenye kutazama kikombe cha kahawa na kuwatazama.











    “Niliwaeleza kuwa babu yangu ambaye mimi nimerithi jina lake, Caleb ndiye ambaye alimpokea mke wa Rais zaidi ya miaka 150 iliyopita uvamizi ulipotokea Whitehouse na kuchomwa moto. Niliwaeleza kuwa mke wa Rais aliokoa kitu kimoja tu pale Ikulu… mchoro wa George Washington ambao huwa unakaa Eastern Room… kwa wiki moja ambayo mke wa Rais alikaa nyumbani kwa babu yangu… na hapa ninapowaeleza nyumbani kwa babu yangu namaanisha nyumba hii tuliyomo sasa hivi… kwenye wiki moja hiyo mke wa Rais alimueleza babu yangu siri nyingi sana kuhusu mchoro huu wa George Washington… sijui mnanielewa mpaka hapo?” Caleb alinyamaza kidogo ili ajiridhishe kama Naomi na Wenzake wanamuelewa kitu ambacho alikuwa anakiongelea.







    Wote wakaitikia kwa kutikisa vichwa.







    Caleb akaendelea.







    “Miaka kadhaa baadae babu yangu alifuatwa na mawakala wa kikundi kinachojiita THE 46 na kumshawishi kujiunga nao… hakuna anayejua walifanikiwa vipi kumshawishi lakini mwisho wa siku alijiunga nao na kuwa moja ya wanachama watiifu na wenye ushawishi mkubwa ndani ya kikundi hicho… mojawapo ya jukumu la msingi kabisa ambalo alipewa babu yangu ilikuwa ni kutunza kitabu cha siri cha kikundi hiki, kitabu kinachojulikana kama BOOK OF CODES ambcho ndicho hasa kilichotufanya twende kule msituni kukitafuta sababu tulipo mzika, tulimzika nacho kama ambavyo mwenyewe alikuwa ametaka kabla ya kufariki… tuko pamoja wanangu?” Caleb akauliza tena.







    Wakaitikia tena kwa Vichwa.







    Caleb akaendelea tena.







    “Mtoto wa babu yangu, yaani baba yangu mzazi… yule kiumbe ambaye tulikutana naye kule msituni, tangu akiwa kijana mdogo alikuwa anaandaliwa kuja kurithi nafasi ya baba yake ya kutunza kitabu cha BOOK OF CODES pindi babu akifariki… lakini kwa sababu ambazo hajawahi kunieleza, baada ya babu kufariki na baba yangu hatimaye kuingizwa rasmi kwenye kikundi hiki cha siri cha THE 46 kuna jambo lilitokea huko ndani ya kkundi hiki cha siri ambalo lilimfanya baba yangu kutamani kutoka huko… na akaanza harakati za kutaka kutoka huko… lakini kuna maswala kadhaa yalikuwa yanamkwamisha kutimiza azma yake hii..!” Caleb alinyazama kidogo huku kama uso wake ghafla ukiingia huzuni.







    “Ni nini kilikuwa kinamkwamisha?” Naomi aliuliza kwa upole baada ya kuona huzuni usoni kwa Caleb.







    Caleb aliinamisha tena uso mezani akitazama kikombne cha kahawa. Akavuta tena pumzi ndefu ndani na kuishusha.







    “Sababu ya kwanza ilikuwa ni mimi hapa… na sabau ya pili ni yeye mwenyewe..!! inaonekana kuwa huko kwenye jumiya ya THE 46 kuna mikataba au maagano au viapo wanapewa wakiunganishwa ambavyo vinawafanya waogope kutoka au kuenenda kinyume na matakwa ya jumuiya yao… sasa baba yangu alikuwa amekula kiapo huko kwenye jumuiya yake kuwa atakapo fariki yeye mimi ndiye ambaye nitarithi mikoba yake ya kutunza BOOK OF CODES, kwa namna fulani inaonekana ilikuwa ni lazima kiapo hiki kitimie… pia yeye mwenyewe kutokana na kiapo chake alipoingia kwenye jumuiya ya THE 46 ilionekana kwamba kulikuwa hakuna uwezekano wa kutoka huko na akabakia salama…” Caleb akanyamaza tena.







    “Ikawaje?” Ethan aliuliza huku amemkazia macho. Kutokana na uzoefu wake wa kijeshi na misukosuko mingi katika uwanja wa vita ilikuwa ni ngumu kwake kumuamini mtu kwa urahisi baada ya kumtilia mashaka.







    “ili atoke kwenye jumuiya ya THE 46 ilikuwa anatakiwa aniache mimi nirithi nafasi yake ndani ya The 46 au atafuta mbadala wangu, na yeye atoke huku akiwa tayari kukumbwa na maswahibu yoyote ambayo yatamkuta baada ya kutoka..!”







    “Kulikuwa na ugumu ganio wa kutafuta mbadala wako? Kwa nini asingetafuta tu mtu mwingine ambaye atavutiwa kuwa kwenye jumuiya hiyo?” Naomi akauliza tena kwa utulivu kama kawaiida yake.







    “Shida siyo mimi… yani sio mimi kwa maana ya huu mwili wangu… suala zima ni nafsi yangu… kama anapatikana mbadala mwingine anatakiwa awe na nafsi yangu… kwa kuwa kiapo walichoingia kuhusu mimi kuriothi nafasi yake pindi akifariki, hawakuibngia makubaliano wakilenga mwili huu na damu na nyama… wanachokitaka ni nafsi.!” Caleb aliwaeleza huku amewakazia macho.







    Wote walijikuta vinywa vimebaki wazi wakiangalia na machoni huku Caleb mwenyewe akiwa ameinamia kwenye meza anatazama kikombe chake cha kahawa. Kuna swali walikuwa wanataka kumuuliza lakini walikuwa wanashindwa wamuulizeje.



    Caleb alikuwa kama vile amesoma maswali ambayo walikuwa nayo vichwani, na akaamua kuvun ja ukimya.







    “Kuna siku nikiwa kijana mdogo, muda wa usiku nikiwa kwenye usingizi mzito baba yangu alinichukua mpaka mahala fulani msituni nikiwa sina fahamau, yaani bila kuamka… huko msituni nilikatwa kifuani na kuna kitu kiliondolewa ndani yangu ambacho sijawahi kukijua mpaka leo hii… kesho yake asubuhi nilipo amaka nilishangaa nina jeraha kubwa kifuani ambalo limeshonwa kwa nyuzi… baada ya kumlazimisha baba yangu kwa miezi kadhaa anieleze ni nini ambacho kilitokea usiku huo, ndipo kuna siku alinieleza kuwa nafsi yangu iligawanywa na nusu kubaki ndani yangu nha nyingine kupelekwa The 46. Kisha akanieleza kuwa huo ndio ulikuwa mbadala aliokuwa natakiwa kutoa kama alikuwa hataki mimi nirithi nafasi yake kama ambavyo alikuwa ameahidi huko The 46 wakati anajiunga. Nusu ya nafsi hii ambayo ilitolewa ndani yangu ndiyo ambayo ilienda kuwekwa ndani ya mtu ambaye mmepokea simu muda mfupi uliopita kuwa amevamia Makamu wa Rais David Logan akiwa na umbo na sura yangu… na hii si mara ya kwanza kutokea tukio la namna hii na kudhaniwa kuwa mimi Caleb ndiye niliyehusika… bado sifahamu masuala mengi kuhusu mtu huyo aliyewekewa nafgsi yangu lakini naamini kuwa yawezekana ana uwezo wa kimaajabu na lazima atafanya kila juhudi kunipoteza ili aipate nafsi yangu kamili.!!”







    Sebule yote ilikuwa umegubikwa na ukimya wa kuogofya wakimsikiliza Caleb akieleza masuala haya mazito ambayo yalionekana kama vile ni mambo ya kufikikirika tu. Hakuna ambaye alikuwa anaamini masikio yake kutokana na mambo mazito waliyokuwa wanayasikia kutoka kwa mzee Caleb. Ilikuwa ni kama vile mtu anakusimulia hadithi ya kutisha ukiwa ndotoni. Walikuwa hawajui kama waulize swali au wampe pole Caleb kutokana na hiki walichokisimulia.







    Wakiwa bado wako kwenye bumbuwazi hili, walishangaa kumuona Mzee Caleb anasimama na kuanza kuvua shati. Walibakia wanakodoa macho tu ili washuhudie kile ambacho kitafuata.







    Mzee Caleb alivua shati lote na kubakia kifua wazi. Katikati ya kifua chake alikuwa na jeraha kubwa sana kama mstari uliochorwa kwa chuma cha moto kuanzia juu kabisa ya kifua kunapoanzia shingo mpaka kwenye usawa wa mwisho wa kifua kunapopakana na tumbo.







    “Hii ndiyo sababu ya mzee kuniomba msamaha kule msituni… ni kitu ambacho sijawahi kumsehe…”



    Caleb aliongea kwa hisia machozi yakikaribia kumtoka huku ananoosha kidole pale kifuani kwenye mstari mkubwa wa jeraha.

    Naomi, Ethan na wenzake walikuwa wamebaki vinywa wazi huku Naomi akifunika macho yake kuogopa kuangalia muonekano wa lile kovu kubwa.



    Ulipita ukimya wa karibia dakika tano nzima Caleb akifuta machozi machoni bila kulia kwa sauti. Ilionekana dhahiri kuwa jeraha hili lilikuwa llinarejesha kumbukumbu ambazo alikuwa hapendi na hataki zijirudie kichwani mwake.



    Baada ya kutulia kidogo na machozi kuacha kumtoka, akavaa tena shati na kuendelea kuongea.



    “Yeye mwenyewe pia baba yangu hakubakia salama… baada ya kutoka kwenye jumuiya ya The 46 ni kana kwamba kuna laana walimtupia au walifanya jambo fulani kutokana na kuvunja kiapo chake cha utii kwenye jumuiya… akageuka kuwa kama mnyama kama ambavyo mmemuona… nywele zikamuota masikioni… ngozi ikapauka na kuwa nyeupe kabisa kama sufi, meno yakachomoza kuwa kama meno ya simba. Baada ya hapo akaanza kuishi msituni kama mnyama na akawakusanya wenzake ambao nao waliwahi kutoka kwenye jumuiya ya The 46 na kupewa laana… ndio wale watu 32 mliowaona wako naye Kule msituni.. Hawa ndio ambao watu wa historia na jumuiya ya The 47 wanawaita *” Masalia”*. Na lengo lao kuu kabisa la maisha walilojipa ni kuwadhibiti jumuiya ya The 46 na kukwamisha kila ambacho wanakua wanakifanya.!”

    Akainua uso na kuwatazama wenzake. Naomi, Ethan na wenzao wote walikuwa wamemkodolea macho wasiamini kile walichokuwa wanakisikia. Mzee Caleb alivuta pumizi ndefu kwa mara nyingine, kisha akainuka mezani na kuanza kuongea huku anatembea tembea.

    “Lakini laana kubwa zaidi waliyompa sio huo muonekano wa ajabu… laana kubwa zaidi ni kumfanya aishi maisha yale kama mnyama milele… sijui ni kwa muda gani anaweza kuishi lakini naamini hata miaka mia moja ijayo bado atakuwa hai… Kwa hiyo kwa kifupi hayo ndiyo maajabu ya kwanini yule kiumbe msituni aliniita mwanangu na pia kwa nini David Logan aliamini kuwa ameniona kwenye uvamizi Whitehouse! Kama hamjaridhika na maelezo yangu mnaweza kuniuliza swali.!”



    Caleb alimaliza na kukaa tena chini pale mezani huku akimimina tena kahawa kwenye kikombe.

    Naomi na wenzake walitamani waulize swali lolote lakini mshangao waliokuwa nao walikuta wanashindwa hata kupanga sentensi sawia vichwani mwao.



    “Tunafanyaje baada ya hapa?” Naomi aliuliza swali kwa sauti ya unyonge kudhihirisha mshangao ambao bado alikuwa nao ndani yake.

    “Sidhani kama kuna mtu mwingine mwenye kufahamu zaidi kuhusu kinachoendelea kwa sasa duniani kushinda mimi… Naongelea matukio ya miji kutwaliwa kimaajabu… kwa hiyo ni imani yangu kuwa The 46 watafanya kila namna ili waweze kunipoteza haraka iwezekanavyo… na nikifariki yule mtu wao ataipata nafsi yangu yote kamili na sitaki kuwaeleza mambo ya ajabu ambayo atakuwa na uwezo wa kuyafanya nafsi yake ikikamilika…”



    “Mfano mambo gani ambayo ataweza kuyafanya?” Naomi aliuliza kwa shauku kubwa.



    “Hakuna haja ya kujadili hayo kwa sasa, suala la msingi ni kujiuliza tunafanyaje kuwazuia?”



    “Na hapo unaongelea kuzuia nini? Miji isitwaliwe? Kumzuia huyu mtu aliyewekewa nafsi yako? Au kuwazuia The 46? Maana nahisi kama tunapoteza dira sasa… badala ya kutafuta suluhisho la tunafanya nini kuzuia miji isitwaliwe sasa tumegeuka kuwa wanaharakati wa kuwazuia The 46?” Ethan akauliza kwa sauti ya ukali na kukereka.



    “Vyote hivyo chanzo chake ni kimoja… kama tukiweza kuwadhibiti The 46 basi moja kwa moja tutaweza kudhibiti hali ya miji kutwaliwa… Usiniulize ni kwa namna gani lakini naamini kabisa rohoni mwangu kuwa The 46 ndio wanaratibu hiki kinachoendelea sasa duniani!” Caleb akajibu kwa ukali pia.



    “Na tulienda kule msituni kwa sababu ulitueleza tukatafute BOOK OF CODES ili tuweze kuwadhibiti wapiganaji wa SANCTA CEDES na tukiwadhibiti wao basi tutaweza kuidhibiti The 46!” Ethan akafoka tena huku anasimama.



    “Na bado hatujachelewa… BOOK OF CODES tumeshachelewa wamechukua… lakini nadhani tumepata njia mpya ya kufanya hapa, au hamuoni?”







    Caleb akawauliza huku amewakodolea macho akiwaangalia katika namna ambayo mtu unamuangalia mwenzako ambaye haoni jawabu dhahiri la fumbo linalowasumbua.



    “Njia gani?” Naomi akaukiza kwa shauku.



    “Huyu mtu mwenye nafsi yangu… kama tukiweza kumfuatilia yeye basi moja kwa moja atatupeleka mpaka kwa The 46 bila mwenyewe kujijua… tuwe kama Mbwa, tusifuate mtu, bali tufuate harufu… maana yangu kwamba The 46 ndio lengo letu, lakini huyu kiumbe mwenye nafsi yangu ndio ‘harufu’ ya kutufanikisha tuwafikie The 46!”

    Japokuwa wazo la Mzee Caleb lilikuwa linaonekana ni gumu kuliunga mkono lakini ndilo lilikuwa wazo pekee ambalo labda kwa kiwango fulani lilikuwa linatoa mwanga unaoleta walau mwanga kidogo katika wakati huu wa kiza cha hofu kilichotanda ulumwengu mzima.



    “Ethan unasemaje?” Naomi akamuuliza Ethan ambaye alikuwa kimya kwa dakika kadhaa zilizopita.



    “Nadhani twende Washington kwanza tukawajulishe wengine tumefikia wapi… pia tuwaeleze haya mawazo tuliyo nayo na kisha tusonge mbele baada ya hapo!”



    “Nadhani ni wazo zuri pia?” Naomi akaunga mkono.



    Caleb naye akaitika kwa kichwa kuunga mkono.

    Wakakubaliana kuwa kwa kuwa kutoka hapa walipo Maryland mpaka Washington ni kama mwendo saa moja tu kwa chopa, basi waite chopa ya jeshi, kisha Naomi na Ethan waelekee huko na vijana wa Ethan wabaki hapa na Mzee Caleb kwa ajili ya kumlinda. Kisha Naomi na Ethan wakifanikiwa kuwashawishi watu wa serikali huko Washington kuhushu mpango walionao, basi watarejea tena hapa nyumbani kwa mzee Caleb kupanga mkakati wa namna ya kumpata huyu mtu mwenye nafsi nusu ya Caleb na hatimaye kuwapata The 46 na mwishowe kuiepusha Dunia nzima kutwaliwa na watoto wa Maldive na kugeuzwa Anabelle.

    Ethan alipiga simu Langley, Virginia kuomba chopa ya dharura iwafuate Maryland na wakaanza kujiandaa kwa safari ya Washington.

    Mazungumzo yao yote haya, yaliwafanya wasahau kuzungumzi vitu viwili muhimu mno.

    Moja, lile kaburi la siri lilipo pale nyuma ya nyumba ya Caleb. Na pili walisahau kuzungumzia kuhusu ile kauli waliyoelezwa msituni na yule binadamu wa ajabu, baba yake Caleb, kwamba “kuna wakala wa The 46 amerejeshwa duniani”.

    Kiza kinene kilikuwa kinasubiri nafsi zao wote na ulimwengu mzima.





    THE OTHER HALF















    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE



















    EPISODE 26















    VATICAN CITY







    Kuna muda ambao unafika na ndani ya nafsi yako unahisi kabisa kuwa umeishi maisha yako yote ili kuufikia wakati huo ambao uliopo muda huo. Ukiwa katika hali hii pasina shaka kabisa ndani ya nafsi yako ukiangalia nyuma maisha yako, kila sekunde ambayo umeishi, kila dakika, kila saa na kila siku pamoja na kila kitu ambacho kimetokea katika maisha yako unakiona kabisa kimekuongoza kuufikia wakati huo uliopo.



    Si lazima wakati huu uliopo uwe wakati war aha au kufanikiwa kwa jambo fulani, lakini pia wakati huu unaweza kuwa ni jambo baya zaidi kutokea katika maisha yako na ukitazama nyuma unaona kabisa kila ambacho umekifanya, ulikifanya kujiingiza katika mtego ambao uliopo. Japokuwa utajuta kwa kusaga meno lakini dhahiri kabisa uthisi ndani ya nafsi yako kuwa hatma yako ndio ilipaswa kuwa hvi ilivyo.











    Lakini uzuri unakuja pale ambapo ukiangalia nyuma maisha yako na kuhisi kwamba kila ambacho kimetokea kimekufanya uwe katika jambo fulani la mafanikio ambalo umo sasa hivi.





    http://pseudepigraphas.blogspot.com/





    Hivi ndivyo ambavyo Father Ricardo alikuwa anajisikia siku ya leo akiwa mikononi mwake ameshikilia BOOK OF CODES. Tangu ameijua siri zaidi ya miaka thelathini iliyopita, moja ya siri kubwa zaidi duniani… aliishi maisha yake yote akiota siku moja kuiweka katika himaye yake gombo muhimu zaidi alilowahi kulifahamu, BOOK OF CODES.











    Ilikuwa imepita karibia miezi mitatu tangu apate ugeni adhimu wa wawkilishi wa kikundi cha wapiganaji wa siri wa SANCTA CEDES ambao katika makutano yao hayo aliwakabidhi mchoro wa George Washington na wao kumkabidhi kitu muhimu zaidi ambcho amekisubiria kwa maisha yake yote, BOOK OF CODES.











    Leo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa miezi mitatu iliyopita kufungua kitabu hiki. Saa ukutani hapa kwenye jengo la maktaba ya Vatican ilikuwa inaonyesha ilikuwa tayari ilikuwa imetimia saa saba usiku na kulikuwa na utulivu wa ajabu ndani ya maktaba. Huu ndio ulikuwamuda muafaka kabisa mabo Father Riacrdo alikuwa anausubiri ili kufanya kile ambacho alikuwa anapaswa kukifanya. Taa zote zilikuwa zimezimwa ndani ya maktaba na alikuwa anatumia tochi ndogo ili kuona anachokifanya.











    Moyo wake bado ulikuwa unadunda kwa kasi kubwa akiwa anakitoa kitabu kutoka katikati ya kichaka cha vitabu vingine kwenye ‘shelf’ ambayo alikiweka miezi mitatu iliyopita na kukiweka juu ya sakafu. Taratibu sana kana kwamba alikuwa anahofia kukiharibu alianza kwa kufunua kimbaa kizito cheusi ambacho kitabu kilivingirishiwa kwa juu. Mara tu baada ya kuondoa kitambaa hiki cheusi juu ya kitabu na kuona maneno BOOK OF CODES ambayo yameandikwa kwa mcharazo wa ‘gothic’ juu ya ‘cover’ la kitabu alijikuta tena kwa mara nyingine tena anaweka mkono wake kifuani juu ya moyo.







    Father Ricardo alijishika kifua akisikilizia mapigo yake ya moyo yanavyoenda mbio kwa takribani dakika tatu nzima huku amekodolea macho kitabu pale sakafuni.











    Kwa miaka zaidi ya thelathini iliyopita amesubiria wakati huu ufike, na leo hii ulikuwa umefika kwa kiasi fulani alikuwa anajihisi kama vile yuko ndotoni. Kichwani mwake alikuwa anajitahidi kutafakari namna ambavyo maisha yake yatabadilika kabisa na kuchukua muelekeo mwingine pindi tu akifungua kitabu hiki kilichopo pale sakafuni. Shauku ambayo alikuwa nayo moyoni ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba akaanza kuhisi kana kwamba kuna woga unaingia moyoni mwake kwa kujua namna ambavyo atakuwa binadamu mwingine kabisa muda mchache ujao.











    Father Ricardo akanyoosha mkono wake na kufunua kitabu pale sakafuni. Karatasi za kitabu ziliakisi kabisa umri wake wa karne kadhaa. Karatasia ambazo zilionekana dhahiri kuwa mwanzoni zilikuwa na rangi nyeupe lakini kutokana na ukongwe wa kitabu zilikuwa zimegeuka na kuwa rangi ya kahawia.











    Maandishi yake hayakuwa ya kuchapwa, yalikuwa yameandikwa kwa kalamu ya wino kwa mwandiko nadhifu kabisa na kwa muonekano wa mwandiko na umri wa kitabu iliashiriakabisa maandishi hayo yaliandikwa kwa kalamu ya wino wa kuchovya.







    Father Riacrdo akaanza kuperuzi ukurasa mmoja mmoja akiwa kama vile kuna kitu fulani haswa ndicho ambacho alikuwa anakitafuta ndani ya kurasa za kitabu hiki. Kadiri ambavyo alikuwa anaperuzi na kufunua kurasa za kitabu ndivyo ambvyo hali ya hewa ndani ya maktaba ilikuwa inabadilika.



    Hali ambayo kabla ya kufunua kitabu ilikuwa ya kawaida kabisa, ilibadilika na baridi kali lilianza kugubika chumba chote cha maktba. Japokuwa kulikuwa na giza lakini ukungu ulianza kuonekana kufunika kabisa chumba cha maktaba.











    Katika hali ya kawaida Father Ricardo angeacha kufanya hiki alichokuwa anakifanya kwa kuogopa namna ya ajabu ambavyo hali ya hewa ilikuwa inabadilika mule ndani.



    Lakini siku ya leo ilikuwa imesubiriwa na Father Ricardo kwa zaidi ya miaka thelathini na hakuwa tayari kukwamishwa na kitu chochote kile. Aliendelea kupekua kurasa za kitabu hiki kikubwa kwa haraka kutafuta alichokuwa anakilenga.











    Alipekua mpaka kufika karibu kabisa nakuraa za kati kati kabisa za kitabu ndipo alipoacha kufunua kurasa na kuanza kusoma kurasa fulani hivi mstari mmoja mmoja huku akifuatisha kwa kidole kila mstari ambao alikuwa anausoma.











    Hii ilikuwa ni kurasa namba 327 na ilikuwa na kichwa cha habari kiliandikwa kwa kilatini, “SECUNDA SEPTIMANA” (WIKI YA PILI).











    Kurasa hii ilikuwa inaeleza kitu cha ajabu sana ambacho kwa fikra ya kawaida kilionekana kitu cha kawaida mno. Ilieleza namna ambavyo mvinyo wa mfalme wa kale wa ugiriki aliyeitwa Secus ulikuwa unatengenezwa. Ilionekana wazi kuwa kwenye kurasa za nyuma ambazo Father Ricardo alizipita bila kuzisoma zilikuwa zinaeleza namna mvinyo huo unavyandaliwa katika hatua za awali na wiki la kwanza. Lakini Father Riardo alionekana wazi kuwa alichokuwa anakitaka kilikuwa katika kurasa huu ambao ulikuwa unaeleza kuhusu hatua mvinyo huo unazopitia katika wiki lake la pili la maandalizi.











    Father Ricardo akatembea kidole chake juu ya kurasa mpaka kuifikia sentesi fulani kati kati kabisa ambayo nayo iliandikwa kwa kilatini ikisema;











    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..” (mvinyo ni kama damu… kadiri inavyokaa zaidi ndivyo inavyoongeza nguvu ya kuiteka dunia)











    Father Ricardo alichukua kalamu na kipande cha karatasi kutoka kwenye mfuko wa joho lake la ukasisi na kuandika sentei hii ya kilatini herufi kwa jerufi kama amavyo ilikuwa imeandikwa kwenye kitabu hiki.











    Hali ya baridi na ukungu pale ndani ya maktaba ilikuwa imeongezeka mpaka kufikia kiasi kwamba Father Ricardo alikuwa anatetemeka kama vile amewekwa ndani ya jokofu. Alipomaliza tu kuandika sentesi hii alikifunga kitabu haraka na kukifunika tena na kile kitambaa cheusi.



    Baada ya kukifunga kitabu na kukiviringisha tena kwenye kile kitambzaa cheusi hakukirudisha kwenye ‘shelf’ kama ambavyo alikiweka miezi mitatu iliyopita. Alikishikilia sawia mkononi na kuinuka na kisha kutoka taratibu pale ndani ya maktaba.











    Alipofika nje ya maktaba akajibanza mahala fulani kwenye giza kuangalia kama hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye alikuwa anafuatilia nyendo zake. Akapepesa macho huku na huko na baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na mtu yeyote anaye mfuatilia akaanza kutembea kwa mwendo wa kasi kufuata barabara inayo elekea jengo la Basilica, kanisa kuu la hapo Vatican.











    Father Ricardo hakutaka kusubiri kukuche au asubiri kesho ifike ili kutimiza azma yake aliyokuwa ameikusudia. Alisubiri siku hii kwa zaidi ya miaka theleathini na siku ya leo alijiapiza kuwa ni lazima amalize kila kitu. Alitembea mwendo wa haraka kuelekea Basilica huku kichwani mwake akiwa anatafakari jambo moja tu, sanamu ya Mfalme daudi iliyoko ndani ya basilica ambayo ilifinyangwa na Michelangelo karne tano zilizopita.











    Dakika kumi baadae alikuwa mbele ya lango kuu la Basilica na walinzi kutokana na kumfahamu hakuna ambaye alimuhoji chochote, walimfungulia lango na kuingia.







    Mapigo ya moyo ya Father Ricardo yaliongezeka baada ya kukanyaga mguu wake ndani ya Basilica. Kila sekunde iliyokuwa inasonga mbele ndivyo ambavyo alikuwa nabakiza dakika chache zaidi kuipata hatma yake. Akakitoa tena kile kitabu kutoka mkononi mwake na kukiweka sakafuni kama ambavyo alifanya kule maktaba na kukifungua. Tofauti na namna ambavyo ilikuwa kule maktaba hali ya hewa kubadilika kwa taratibu, humu ndani ya Basilica hali ya hewa ilibadilika haraka mno. Baridi lilikuwa kali ghafla kana kwamba kanisa zima lilikuwa ndani ya jokofu kali. Ukungu ulitanda ndani ya jengo zima kama vile jengo lilikuwa limebebwa mpka juu mawinguni.











    Father Ricardo aliacha kitabu pale sakafuni kikiwa vile vile ambavyo amekifungua na taratibu akaanza kutembea kuelekea upande wa kulia wa Basilica ambao ulikuwa una sanamu ya mfalme daudi. Alitembea huku ana mung’unya taratibu yale maneno aliyoyasoma kwenye kitabu;











    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..” (mvinyo ni kama damu… kadiri inavyokaa zaidi ndivyo inavyoongeza nguvu ya kuiteka dunia)











    Kadiri alivyokuwa anaisogelea sanamu hii ya mfalme Daudi ndivyo ambavyo sanamu hii nayo ilianza kufuka moshi kama mvuke mkali wa baridi huku chini ambako ilikuwa imesimamisha kukianza kuzunguruka kuonesha kama vile kulikuwa na mfuniko wa shimo fulani pale chini.



    Father Ricardo alikaza macho yake kwenye sanamu hii huku ana mung’unya tena na tena maneno yale ya Kilatini.







    Mbele yake alikuwa amebakiza hatua kadhaa tu kuifikia hatma yake, kufikia kiu yake ya maisha, kufikia lengo kuu la maisha yake alilopambana kulipata kwa zaidi ya mika thelathini iliyopita.







    Baridi lililoambatana na ukungu lilizidi kuchachamaa ndani ya Basilica kiasi kwamba mpaka hewa ikawa kama inaganda. Lakini siku hii ya leo, hakika hakukuwa na kitu chochote ambacho kingeweza kumzuai Father Ricrado kutimiza azma yake.















    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)











    Japokuwa mwanzoni walipoingia walihisi humu ndani kulikuwa na baridi lakini safari hii ndio baridi hasa la Anabelle waliweza kulisikia. Baridi lilichoma mpaka kwenye mifupa na walianza kuhisi kama vile muda mchache ujao miili yao ingeweza kuganda.







    Ghafla radi kali zilianza kupiga angani zikiambatana na upepeo mkali mno ambao hawakuwahi kuuona tangu waingie ndani ya Anabelle. Zilikuwa ni radi kali kweli kweli zenye kishindi kiasi mpaka mlio wake zilifanya masikio yaume. Ilikuwa dhahiri kwamba kuna jambo la tofauti lilikuwa linatokea humu ndani ya Anabelle.







    “..nini kinaendelea.!” Salim alimuuliza Cindy kwa mshangao huku amejikunyata akihema kwa shiida sana kutokana na baridi kupitiliza kwa ukali.







    “tunakufa Salim.!” Cindy aliongea kwa sauti ya unyonge iliyojaa kukata tama kabisa.







    “unasemaje Cindy?” Salim aliuliza kwa woga zaidi.







    “unaelewa hizo radi ni nini?” Cindy akumuuliza.







    “hapana!”







    “imeshatimia miezi mitatu huko duniani… The 46 wanajiandaa kufanya kafara ya kwanza… tunakufa Salim… I’m so soryy niliwashawishi tuingie humu.!” Cindy aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtoka.











    Salim akiwa kwenye hofu hii kuu, kwenye kukata tama huku… kuna kitu kwa mbali sana kutoka pale walipokuwa kama mita mia moja hivi aliokiona… hakuelewa ni kitu gani hasa laki ni moyoni mwake aliamini kuwa ndani ya dakika chache hizi walizobakiza za maisha yao labda wanaweza kufanya kitu kwa faida ya watu walio waacha huko duniani.







    “Cindy… unaona ninachokiona ple mbele yetu?” Salim aliongea huku anamtingisha Cindy.







    Baridi lilikuwa limemzidia Cindy kiasi kwamba japo alikuwa hai lakini hakuweza kusema chochote wala kujitingisha, alibakia tu kumkodolea Salim.







    Sura ya mwanaye Basrat ikamjia kichwani, na sura ya mpenzi wa maisha yake, mke wake Khadija ikamjia kichwani… akajiapiza kuwa hawezi kufa bila kuziona tena sura zao. Salim akajikaza kiume na kuinuka kuelekea pale kwenye kile alichokuwa anakiangalia.









    THE OTHER HALF











    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE











    EPISODE 27















    NDANI YA ANABALLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAM)







    Baada ya Salim kuinuka kwa taabu sana kutoka pale ambapo alikuwa ameketi, taratibu akaanza kujikongoja kuelekea kule kwenye kile ambacho alikuwa anakiona mbele yake.







    Muda mchache kabla ya baridi kuwazidia walikuwa wanaelekea kwa mara nyingine tena mahala ambapo waliacha chupa ikiwa na kikaratasi ndani yake chenye maelezo kadhaa kwa lengo la kuwasiliana na ulimwengu wa nje.











    Ubaya ni kwamba Anabelle 27 ilikuwa inabadilika kwa kasi sana, kwa hiyo muda mwingi walipokuwa wanatafuta pale ambapoa awali waliicha chupa yenye maelezo ndani yake, walihisi kama vile sehemu walikuwa wanatafuta haikuwa hiyo ambayo waliacha chupa awali. Kwa hiyo walizunguka na kuzunguka sana mpka mwishowe walipozidiwa na baridi walijikuta wanakaa chini pale walipokuwa na ghafla wakaanza kuona zile radi zilizoambatana na upepo mkali sana.











    Salim akakaza mwendo kuelekea kwenye kile alichokuwa anakiona mbele yake mpaka akakikaribia mita chache tu ndipo alipogundua kwamba mng’ao ule aliokuwa nauona kwa mbali ulikuwa ni mwanga wa buluu ambao ulikuwa unafanana kabisa na mwanga ambao ile chupa ilikuwa inatoa kipindi walipokuwa nayo humu ndani ya Anabelle. Tumaini fulani likaongezeka ndani ya nafsi ya Salim na akajikuta anapata nguvu zaidi ya kutembea kwa ukakamavu kufuata ule mwanga wa buluu.







    Salim alitembea kwa haraka mpaka akaufikia ule mwanga wa buluu. Na alipoufikia hakuamini macho yake kile ambacho alikuwa nakiona mbele yake. Chupa ambayo walikuwa wanaitafuta kwa zaidi ya masaa mawili ilikuwa mbele yake chini ardhini ikiwaka kwa mwanga wa buluu kama ambavyo hufanya siku zote. Alipoitazama vizuri zaidi akagundua kuwa kulikuwa na kipande cha karatasi ndani yake.











    Salim akainama kuiokoto kwa furaha na shauku kubwa kujua ile karatasi iliyoko ndani ya chupa kama ilikuwa ni ile ile waliyoiweka wao au ilikuwa ni karatasi kutoka ulimwengu wa nje waliokuwa wanajaribu kuwasiliana nao. Kwa jinsi ambavyo alikuwa na shauku leo hii mpaka aliona chupa inang’aa kuliko siku zote. Akainama na kuiokota kutoka ardhini na kisha kuipindua ili karatai iliyoko ndani yake idondokee juu ya kiganja chake cha mkono.











    Karatasi ilipotua tu juu ya kiganja chake, akaweka chupa pembeni na kuanza kuifungua karatasi kwa haraka ili kuona ambacho kilikuwa kimeandikwa ndani yake.







    HATUJUI KAMA BADO MKO HAI AMA LA… UMEPITA MWEZI MMOJA SASA TANGU MUINGIE NDANI YA ANABELLE 27. KAMA BADO MKO HAI HAYA NI MAJIBU YA MLICHOULIZA. DETAIL #127 NI 6, 2, 1, 9. PIA TUNAWASISITIZA MLINDE MLICHOKIPATA KUHUSU MADAM PRESIDENT KULIKO CHOCHOTE KILE. X3. X3. X3.







    Japokuwa Salim hakuelewa kwa ufasaha wote kuhus hiki ambacho kilikuwa kimeandikwa hapa, lakini dhahiri kabisa hili lilikuwa ni jibu kutoka dunia ya nje ambayo walikuwa wanajaribu kuwasiliana nayo.







    Licha ya kuusikia mwili wake kama vile ulikuwa umekufa ganzi wote kutokana na baridi, lakini Salim alijikuta anapata nguvu ya ajabu na kuanza kukimbia kurudi pale ambapo alimuacha Cindy.







    “Cindy… Cindy… Cindy! Amka..”







    Salim alikuwa anamtingishga Cindy huku anamuita jina lake. Cindy alifumbua macho tu kuonyesha kuwa alikuwa anamsikia lakini alishindwa kuongea kitu chochote kile. Cindy alimuangalia tu Salim na kisha akatabasamu. Alikuwa kama vile anamfariji Salim au kutaka kumtoa hofu. Lakini uhalisia ulikuwa ni dhahiri kabisa kwa Salim, kwamba muda wowote ule kama hali haitabadilika basi angeweza kumpoteza Cindy.







    “Cindy… majibu kutoka nje!”







    Salim aliongea huku amekunjua karatasi mbele ya Cindy. Japokuwa Cindy alikuwa hawezi kuongea sawa sawa lakini mshangao ambao ulikuwa usoni mwake ulikuwa ni dhahiri kabisa .







    “ni….ni…. ki…me..to…ke..a?” Cindy aliuliza kwa taabu sana.







    “sijui ni nini kimetokea… nimeipata chupa pale mbele ikiwa na hii karatasi… nadhani ni jibu kutoka huko nje.!” Salim alijibu kwa tabasamu huku ananyoosha kidole kuelekea pale ambapo aliikota chupa.







    MASAA MAWILI YALIYOPITA (TAKRIBANI SIKU NNE DUNIANI)







    WASHINGTON D.C – MAREKANI







    Kevin, katibu mkuu kiongozi wa Makamu wa Rais David Logan alikuwa amemaliza kuongea na simu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Zuberi Z. Miraji muda mchache uliopita. Ilimbidi aongee naye yeye badala ya Rais wa Marekani kutokana na changamoto iliyokuwepo, kwamba David Logan alkuwa haonekani na Rais Laura Keith alikuwa ndio kwanza alikuwa amezinduka kutoka kwenye ‘coma’ na Kevin hakudhani kama alikuwa tayari kuanza kupokea simu zihusuzo masula mazito ya kitaifa. Lakini kiuhalisia wenyewe, si tu kwamba Kevin alikuwa anajali hali ya afya ya Bi. Laura Keith bali pia alikuwa ana wasiwasi juu ya mwenendo wa matukio yalivyotokea.







    Mpaka muda huu alikuwa anashangazwa na kitendo cha kupotea au kutekwa kwa David Logan muda mchache baada ya Rais Laura Keith kurejea kutoka kwenye kupotea baharini kwa zaidi ya wiki tatu. Lakini pia alikuwa mpaka muda huu haelewi kwa nini Bi. Laura Keith alipozinduka kutoka kwenye coma amri ya kwanza ambayo aliitoa ilikuwa ni kuamuru kukamatwa kwa Makamu wa Rais David Logan ambaye ndiye alikuwa amekaimu nafasi yake ya Urais.











    Kwa hiyo kwa kiwango kikubwa Kevin alikuwa ana kila sababu ya kutokuwa na imani na muenendo wa mambo hapo Whitehouse. Ndio maana simu ilipopigwa na kuunganishwa na ofisi ya Rais ambapo mpaka muda huo alikyekuwa anawajibika kama Rais alikuwa ni David Logan, lakini kutokana na kutokuwepo kwake ndipo simu ilipounganishwa moja kwa moja ofisini kwa Kevin, Katibu wake kiongozi. Kwa mujibu wa protokali Kevin alikuwa anatakiwa kwenda kuripoti kwa Bi. Laura Keith kwa kuwa atyari aikuwa amezinduika. Lakini kutokana na wasiwasi aliokuwa nao Kevin hakutaka kabisa Laura ajue chochote kuhusu simu hiyo kutoka Tanzania.







     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Rais wa Tanzania alikuwa amemueleza kila kitu… kuhusu chupa kuokotwa ndani ya Anabelle 27, kuhusu karatasi ambayo waliipata ndani yake kile ambacho kiliandikwa.



    Baada ya kumueleza yote hayo, Kevin alimjibu Rais Zuberi Z. Miraji kuwa asubiri baada ya muda kadhaa atampa majibu ya maswali hayo kama kwa namna moja au nyingine wataweza kung’amua mambo kadhaa.







    Kevin alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha ofisi akitafakari yale aliyoyasikia kutoka mkwa Rais Zuberi Miraji. Lililokuwa linamsumbua kichwani sio kusuhu detail #127 ya mchoro wa George Washington au neno ‘W7” mwisho wa ujumbe alioambiwa umetoka Anabelle 27. Bali kilichokuwa kinamsumbua kichwa ni yale maneno kuwa nguo za Madam President Laura Keith pamoja na POLO-TD zilikuwa zimepatikana ndani ya Anabelle 27. Alijitahidi kuchekecha akili kweli kweli lakini hakuweza kung’amua chochote kile cha kumsaidia japo kuhisi tu ni kwa nini nguo z Laura zipatikane ndani ya Anabelle? Na kulikuwa na maana gani ujumbe huo kusema kuwa kuna wakala wa The 46 amerejeshwa duniani?











    Hakukuwa na haja ya kupoteza muda zaidi. Kevin akaita chopa ya kijeshi kutoka kitengo cha 1st Helicopter Squadron cha Jeshi la nga la Marekani. Baada ya chopa kufika, moja kwa moja ikamchukua mpaka chuo kikuu cha Stanford. Aliposhuka tu kwenye chopa bila kupoteza hata dakika moja, alielekea mpaka kwenye jengo la Idara ya Akiolojia na kuonana na wahusika.







    Kiongozi wa wataalamu ambao aliwakuta hapa alkuwa anaitwa Profesa Lameck Jendar, mbobezi wa masula ya akiolojia ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya India.



    Kevin aliwaeleza kila kitu, kuhus mwenzao kuingia ndani ya Anabelle 27 na kisha ujumbe wa karatasi ambao aliutuma kutoka ndani ya Anabelle.







    “nadhani kabla ya yote nikujibu kuhusu detail #127 ya mchoro wa George Washington.!”  Profesa Jendar aliongea huku anaelekea upande fulani wa ‘shelves’ za vitabu na kwenda kuchukua likitabu limoja likubwa sana na kuja nalo pale mezani ambako walikuwa wameketi.







    ”naamini mpaka sasa utakluwa umesikia hadithi kuhusu Rais George Washington kupata sanduku la Pandora na kwenda kulificha mahali kusikojulikna na kisha kumtumia msanii kuchora picha yake yenye mafumbo mengi ambayo ukiyajua yana uwezo wa kukupeleka moja kwa moja mpka kwenye sanduku la Pandora?”

    Profesa Jendar alimuuliza Kevin.











    ”nafahamu yote hayo kuhusu mchoro wa George Washington!” Kevin alijibu kwa ufupi tu.











    ”vizuri! Sasa kwenye ule mchoro kuna jumla ya details ndogo ndogo 207 ambazo ukifahamu namna ya kuziweka pamoja na kuleta m,aana ndizo ambazo zinakupa ramani ya sehemu ilipo sanduku la Pandora. Detail namba 127 ambayo Cindy anaulizia ni mguu wa kushoto wa meza iliyo nyuma ya George Washingtoa amhala aliposimama kwenye mchoro.!” Profea Jendar aliongea huku anamuonyesha picha ya mfano wa mchoro huo pale kwenye lijikitabu ambalo amekua nalo.







    ”Sasa… detail yenyewe sio mguu wote wa kuhoto.. bali ni hizo nakshi zake… tazama hapa” Profesa aliongea huku anamuashiria Kevin kusogeza macho yake atazame kwa umakini zaidi pale ambapo alikuwa anajaribu kumuonyesha.







    Kwenye mguu wa kushoto wa nyuma ya meza aliposimama George Washington, ulikuwa na nakshi za mistari sita kutoka juu kwenda chini na kisha kabla ya kufika chini ya mguu wa meza kuna nakshi nyingine ya kama ringi au pete mbili na kisha mguu huo wa meza mwishoni umechongezka kuwa na ncha ambayo ndio inagusa chini ya Sakafu.







    ”hii detail katika akiolojia tunaisoma kama, 6 – kumaanisha hiyo mistari sita kutoka juu kwenda chini, alafu 2 – kumaanisha hizo ringi mbili kabla ya kufika mwisho, alafu 1 – kumaanisha huo mchongoko mwishoni unagusa sakafu na kisha 9 – ambayo ni jumla kuu ya detail nzima namba 127..,. kwa hiyo ukiisoma kwa pamoja inakuwa ni 6, 2, 1, 9.!” Profesa Jendar alimaliza kutoa ufafanuzi.







    Kevin alikuwa anaandika haraka haraka kwenye kijitabu chake kidogo kile ambacho Profesa Jendar alikuwa anakiongea.







    ”OK! Na vipi kuhusu nguo za Madam President Laura Keith Kupatikana ndani ya Anabelle?” Kevin aliuliza kwa msisitizo huku amemkazia macho Prefesa.







    ”hilo sina jibu sahihi?” Profesa alijibu kwa kigugumizi.







    ”Profesa tuko katika hatari ya kuupoteza ulimwengu mzima na kugeuzwa kuwa Anabelle… kwa hiyo jibu lolote lile ambalo utanipa ni bora kuliko kutokuwa na jibu lolote kabisa” Kevin aliongea kwa msisitizo.







    Profesa alikuwa kama vile anaogopa kutoa mawazo yake. Akasita sita kwa sekunde kadhaa lakini mwishowe akaamua kutoa donge lake rohoni.







    ”umenieleza kuwa, pia ujumbe umesema kuwa kuna wakala wa The 46 amerejeshwa duniani… kwa kadiri ninavyofahamu historia ya Anabelle halisi yenyewe ambayo aliishi Pandora maelfu ya miaka iliyopita… mtu yeyote yule ambaye alikuwa ameingia mkataba wa kiapo cha damu na watoto wa Pandora ambao wanafanana kabisa na wattot wa Maldives wa kizazi chetu hiki, ilikuwa ni lazima uache vitu vyako binafsi vinavyokufunga nafsi yako wao na wewe… kwa hiyo kwa maoni yangu… mwenye nguo hizo ndiye wakala ambaye amerejeshwa duniani… namna pekee ya kumdhibiti kabla hatujajua chochote cha kufanya lazima kuhakikisha kuwa ngu hizo hazipati… zibakie ndani ya Anabelle.!” Profesa aliongea mawazo yake kwa upana zaidi bila kutamka moja kwa moja kuwa alikuwa anahisi kuwa Bi. Laura Keith ndiye wakala wa The 46 ambaye amerejeshwa duniani.











    ”asante sana Profesa nimekuelewa vyma kabisa..!” Kevin alijibu kwa msisitizo kumuonyesha Profesa kuwa alikuwa ameelewa kile ambacho alikuwa amekiongea kwa fumbo.







    Haraka haraka Kevin aliinuka na kuanza kuufuata mlango ili aondoke. Lakini alipofika mlangoni kuna kitu alikumbuka. Akasimama kidogo na kugeuka nyuma.







    ”Samahani Profesa!”







    ”Bila samahani.!”







    ”huu ujumbe unaeleza kuwa wamo ndani ya Anabelle kwa masaa 16 mpaka sasa… je unadhani kuwa bado watakuwa hai mpaka sasa ukizingatia kuwa umepita mwezi mzima sasa tangu waingie ndani ya Anabelle 27?” Kevin akauliza.







    ”Kwa ninavyofahamu muda uko tofauti ndani ya Anabelle… ndani ya Anabelle kuna uwezekano wa muda kwenda haraka sana au taratibu sana kushinda huku nje duniani… ndio maana miji ikitwaliwa tu huwa inabdilika sana na kuonekana kuchakaa… kwahiyo ndio, kuna uwezekano wako hai na kama mnataka kuwajibu ni vyema mfanye hivyo haraka sana!”



    Kevin hakutaka kupoteza muda. Alitoka pale Idarani kwa haraka na kukwea kwenye chopa. Alipoingia tu ndani moja kwa moja akafungua simu na kupiga ofisini kwake Whitehouse kwa wasiaidizi wake.







    ”hallo… niunganishe haraka na Rais wa Tanzania… waambie Rais wa Marekani anataka kuzungumza naye haraka sana… its an emergency.!” Kevin aliongea mara tu baada ya simu yake kupokelewa.



















    *****







    NDANI YA ANABELLE 27







    Salim bado alikuwa ameshikilia ile karatasi aliyoitoa kutoka kwenye chupa mbele ya uso wa Cindy.







    “YES… ni… ni… ni majibu kutoka nje!” Cindy aliongea kwa taabu sana.







    ”wana maana gani?” Salim aliuliza.







    ”hatuna muda wa kutosha Salim… twende kwenye mlango wa The 46!” Cindy alijitahidi tena kuongea na kisha akafumba macho.







    Salim alimama akifikiria ni nini afanye. Wanatakiwa warudi kule ambako waliwaacha Magdalena na Shafii ambapo ni mwendo kidogo kutoka hapa. Lakini Cindy alikuwa hana nguvu ya kuongea nah ii ilimaanisha kuwa asingeweza hata kutembea. Lakini kabla ya kufumba macho alieleza kuwa wanatakiwa waelekee hapo, kwenye mlango wa The 46.







    Salim alijua wazi kabisa hili ndilo lilikuwa tumaini lao pekee kama wataka waendelee kuwa hai. Hii labda ndio inaweza kuwa mwanzo wa kupata suluhisho la kuuokoa ulimwengu kutoka kwenye janga lililo mbele yake la kugeuzwa kuwa Anabelle.







    Kwa mara nyingine tena sura ya mtoto wake Basrat na mkewe Khadija zilimjia kichwani. Akiajikuta anajiapiza tena kuwa ataziona tena kabla hajaondoka ulimwenguni.







    Nguvu za ajabu zilimjia. Uchungu na hasira vilijaza nafsi yake. Akajiapiza kuwa hawawezi kufa namna hii bila kutimiza kusudi lao.







    Akainama na kumuinua Cindy akimbeba kama mtoto mdogo na kuanza kutembea kuelekea kule ulipo mlango wa The 46 walipowaacha Shafii na Magdalena.







    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE







    EPISODE 28











    WASHINGTON D.C



    Naomi na Ethan walikuwa wamewasili kama masaa mawili yaliyopita.



    Hali ambayo walikuwa wameikuta Washington ilikuwa imewashangaza haswa.







    Kwanza walishitushwa na taarifa kuhusu kupatikana kwa Madam President Laura Keith kwenye visiwa vya Caribbean. Kwa siku zote ambazo walikuwa kwenye msitu wa Ox na baadae Nyumbani kwa Caleb, mjiji Maryland walikuwa bado hawakuipata taarifa kuhusu kupatikana kwa Laura.







    Lakini hili halikuwa limewashangaza zaidi ya taarifa ya kupotea kwa Makamu wa Rais David Logan. Na ajabu ni kwamba si Logan tu peke yake ambaye alikuwa haonekani, bali pia mpaka Katibu wake kiongozi Kevin naye alikuwa haonekani.



    Muda huu walikuwa wamekaa ofisini kwa Kevin kwenye jengo la West Wing ndani ya Whitehouse wakimsubiri Mkurugenzi wa CIA Bw. James Ruppert awaleze kwa kina ni nini hasa kilikuwa kinaendelea.







    “Mnisamehe kwa kuchelewa…!” Ruppert aliongea huku akiingia pale ofisini akiwa ameongozana na vijana kama watatu hivi.







    “Usijali.!” Naomi aliitikia huku akigeuka kumuangalia.







    Ofisi ilikuwa ni chumba fulani kikubwa cha wastani, kama muunganiko wa vyumba viwili vya kuishi. Kulikuwa na meza na kiti upande mmoja wa chumba mbele… na upande mwingine kulikuwa na viti vya sofa na meza ndogo katikati.

    Naomi na Ethan walikuwa wamekaa hapa kwenye viti vya Sofa, na pia Ruppert alipoingia na vijana wake nao walikuja kukaa hapa.



    “Nini kinaendelea?” Ethan alimuuliza Boss wake mara tu alipoketi.







    “Ni balaa tupu kila mahala… miji mingine mitatu imetwaliwa ndani ya ardhi ya Marekani… tumepokea taarifa muda si mrefu… mji wa South Dakota, North Dakota na Monatanna..!” Ruppert aliwaeleza haraka haraka.



    Ukapita ukimya wa kama nusu dakika hivi bila yeyote yule kusema neno. Dhahiri kabisa ulikuwa unaweza kuhisi woga katikati yao hata hewani pale ofisini. Woga mkubwa zaidi, hakuna ambaye alikuwa anajua ni mji gani hasa ambao ungefuata. Japokuwa hakuna ambaye alikuwa anasema chochote, lakini kila mmoja kati yao alikuwa anajiuliza itakuwaje kama Washington ndio utakuwa mji unaofuata?



    “Nini kimempata Makamu wa Rais? David Logan?” Naomi aliuliza swali na kuwazundua wenzake kutoka katika fikra za woga ambazo walikuwa nazo kichwani.



    Ruppert alifikiri kwa sekunde chache kisha akajibu.



    “Hakuna ambaye anafahamu mpaka sasa ni kitu gani hasa kimetokea… tunachojua ni kwamba aliondoka hapa Ikulu katika mazingira ya kutanisha… kwa maana ya kwamba hakuna anayefahamu aliondokaje, hata watu wa Secret Service hawajui aliwezaje kuondoka bila wao kujua… alichukua walinzi kadhaa tu na kuelekea Nyumbani kwake Naval Observatory Circle… baada ya hapo hatujui ni nini kilifuata… Tunachojua ni kwamba walinzi wengine wote wa Secret Services wameuwawa kasoro wawili tu pamoja na David Logan hawajulikani walipo!” Ruppert aliongea kwa kirefu.



    Naomi alikuwa anatamani aeleze kuwa kabla ya Makamu wa Rais David Logan kupotea kusikojulikana aliwapigia simu wakiwa Maryland na kuwaeleza kuwa amevamiwa Ikulu na mtu anayefanana na Caleb.

    Lakini Ethan alimpiga jicho Fulani hivi kumuashiria kuwa siongee chochote.







    “Na Kevin imekuwaje?” Naomi aliuliza swali lingine badala ya kuongea kile ambacho kilikuwa kichwani mwake.



    “Kevin alichukua chopa hapa ya kijeshi na kwenda nayo Stanford University… lakini alipokuwa anarejea aliwaeleza kuwa wapitie jimboni Palo Alto, California kuna mtu anahitaji kuonana naye… lakini dereva wa chopa anaeleza kuwa walipofika Palo Alto, aliingia kwenye nyumba fulani na wao wakamsubiri nje chopa ilipopaki… lakini ilipita nusu saa bila Kevin kutoka… na walipoingia ndani walikuta nyumba iko tupu bila mtu yeyote ndani yake.… ni dhahiri kuwa Kevin ametoroka kwa makusudi… lakini hatujui bado ameenda wapi au ni sababu gani imemfanya atoroke!”



    Ruppert aliongea tena kwa kirefu.



    Naomi na Ethan walianza kuhisi kama akili ilikuwa inachanganyikiwa. Kila ambacho walikuwa wanakifikiria jibu likikuwa haliji kichwani.



    “Na hiyo sio mwisho..!” Ruppert akaongea huku anawatazama.



    “Kuna lingine?” Ethan aliuliza kwa mshangao.







    “Ndio… Spika wa bunge la Wawakilishi pia hatujui alipo na si yeye peke yake! Pia Waziri wa mambo ya nje naye hatujui alipo… yani ni kama wamepotelea hewani… hatujui hata tuanzie wapi kuwatafuta!”







    “Oooohh Mungu wangu, mungu wangu! Nini tena hiki?” Naomi akajiinamia kwa uchungu.



    “Hivi mnaona kile ambacho mimi nakiona?” Ethan ghafla akaongea.



    “Nini?” Ruppert naye akuliza.



    “Wanajaribu kuondoa mtiririko wa kurithi madaraka… yaani watu wanaokubalika kikatiba kushika urais wa nchi ikitokea Rais ameshindwa kutimiza majukumu yake kwa kifo labda kwa mfano!” Ethan aliongea huku ananyanyuka kutoka kwenye sofa.



    Ilikuwa kama vile taa imewaka vichwani mwao wote.



    “Yes! Yeah… Rais akifa au asipokuwepo au akishindwa kutimiza majukumu yake, nafasi yake inakaimiwa na Makamu wa Rais, kama Makamu wa Rais hayupo basi Spika wa Bunge la Wawakilishi la Congress au Bunge la Senate… na kama hao nao hawapo basi Waziri wa mambo ya nje anashika nafasi hiyo…. Na wote hawa wepotea kusikojulika… nini kinaendelea?” Naomi aliongea huku naye akisimama kutoka kwenye sofa.



    Taa iliwaka zaidi vichwani… mwanzoni walihisi labda viongozi hao walipotea tu ili kuficha suala fulani, lakini sasa ilikuwa wazi kabisa kuna suala lilikuwa linatekelezwa kimkakati vizuri kabisa kuhakikisha kuwa uongozi wa juu wote serikalini haupo na hakuna ambaye ataweza kurithi nyadhifa ya Rais wa Marekani ikitokea Rais hayupo au hawezi kutekeleza majukumu yake!



    “Nadhani kuna jambo la msingi hapa tunashindwa kuliona!” Ruppert akawatazama wenzake kwa uso wa kung’amua fumbo.



    Naomi na Ethan hawakuitikia… walibaki kumuangalia tu wakisubiri afumbue hilo fumbo ambalo lilikuwa kichwani mwake.







    “Japokuwa hatujui kama viongozi wametoroka makusudi au wamepotezwa… lakini nadhani kwa mazingira yalivyo kuna kila sababu ya kuamini kuwa wamepotezwa… lakini kama ingelikuwa ni mimi nisingehangaika kwanza na kuwapoteza warithi wa kikatiba wa nyadhifa ya rais… ningeanza kumpoteza Rais mwenyewe….!!” Ruppert akaongea kwa fumbo huku amewakazia macho bila kumalizia sentensi.



    “Ajabu ni kwamba Rais hajaguswa!” Ethan akaongezea huku anamkazia macho Naomi.







    “Na si tu kwamba hajaguswa… bali amerejea kutoka kusikojulikana wakati wenzake wanapotea kusikojulikana!!” Naomi akaongezea.



    Wakabaki wanangaliana tu kwa mshituko. Taa kichwani iliwaka kwa mwanga angavu kabisa. Walihisi wamelifumbua fumbo ambalo walikuwa wapo gizani muda wote.







    “Ruppert nadhani kuna jambo tunapaswa kukueleza!” Naomi akaongea huku anamuangalia Ethan. Alikuwa anataka kuona kama atamapa ishara ya kumruhusu aongew au aendelee kukaa kimya. Ethan akatingisha kichwa kwa kumkubalia.



    “Kitu gani?” Ruppert akaongea huku anapepesa macho kutoka kwa Naomi mpaka kwa Ethan ana kisha kurudi tena kwa Naomi.



    “Tulivyoenda kwenye msitu wa Ox, Maryland kutafuta BOOK OF CODES kwenye kaburi la babu yake Caleb… tumekutana na vitu vingi sana ambavyo tutakueleza baadae… lakini nilichotaka kukwambia ni kwamba… tulikutana na kiumbe wa ajabu… binadamu ila ni wa ajabu kabisa sio kama mimi na wewe… ni baba yake Caleb… yeah yeah najua una maswali… nitafafanua baadae! Jambo la msingi alitueleza kuwa tuwe makini kuna wakala wa kikundi cha The 46 amerejeshwa duniani!”



    Naomi aliongea huku macho yamemtoka kweli.



    “Unamaanisha wakala wa The 46 ambao inaaminika wanaratibu matukio ya miji kutwaliwa duniani?” Ruppert akauliza.



    “Sahihi kabisa!” Ethan akajibu.







    Jibu lilikuwa dhahiri mbele yao na kwenye akili zao lakini hakuna ambaye alikuwa anaweza kuthubutu kutamka. Vichwani mwao wote, jibu moja tu lilikuwa linawajea, kwamba Madam President Laura Keith ndiye wakala wa The 46 ambaye wameonywa.



    Wakiwa bado wanatazama kwa mshangao mara ghafla walisikia mlango wa ofisi unafunguliwa bila kugongwa na kisha karibia maafisa kumi na tano wa Secret Services.







    Wote wakajikuta wamegeuka kwa pamoja kuwatazama maafisa wale wa Secret Services. Kwa kuwatazama tu nyuso zao walionekana dhahiri kabisa kwamba hawakuwa wamekuja hapo kwa nia njema. Nyuso zao zilionyesha wazi kabisa kwamba kulikuw a na jambo lingine la ziada.



    Walibakia wanatazamana karibia dakika nzima kila upande ukisubiri upande mwingine uwe wa kwanza kuongea. Alikuwa ni afisa yule yule Renaldo Gillemo ambaye awali alipewa amri ya kumkamata Makamu wa Rais David Logan.







    “Ndugu zangu… inatulazimu kuwaweka chini ya ulinzi.!” Mmoja wa maafisa wa Secret Services akaongea kwa aibu.



    “Kwa kosa lipi?” Ruppert akafoka.



    “Ni amri ya Madam President… mnapaswa kuwa chini ya ulinzi!” Gillemo aliongea bado uso wake ukowa na aibu.



    “Renaldo… ifike kipindi uanze kujiuliza kuhusu hizi amri za Madam President… mwanzoni alikwambia umkamate Makamu wa Rais, sasa hivi ituweke sisi chini ya ulinzi… umejiuliza ni nini kinaendelea? Renaldo fikiri kwa makini..!” Ruppert akaongea kwa msisitizo huku amemkazia macho.



    Japokuwa kwa kiasi fulani maneno yale yalimchoma Gillemo lakini alijikaza kiume na kuficha kabisa hisia zake.



    “Samahani sana kwa hili… Lakini napaswa kutekeleza jukumu langu! Kuanzia sasa nawaweka chini ya ulinzi kwa amri ya Rais wa Marekani.!”



    Gillemo aliongea na vijana wake wote wa Secret Services aliokuja nao waliwazunguka akina Naomi.



    Uzuri ni kwamba Naomi na wenzake walikuwa wanajua vyema protokali ya vyombo vya ulinzi. Afisa usalama anapokuweka chini ya ulinzi haupaswi kukaidi. Kitu unachotakiwa kuoingana naye ni shutuma atakazokupa…. Lakini sio amri ya kukuweka chini ya ulinzi.







    Kwa hiyo bila kubishana nao, wakatoka pale ofisini wakiwa wamezungukwa kila upande.



    Kwa kuwa Whitehouse hakuna gereza, iliwapasa maafisa hawa wa usalama kwenda kuwafungia Naomi, Ethan na Ruppert kwenye chumba kikuu kuu ambacho huwa kinatumiaka kama stoo kwenye jengo hili la West Wing ndani ya Whitehouse.







    “Renaldo… kabla haujaondoka naomba msaada wako kidogo.!” Naomi akaongea kwa upole akiwa amesimama karibu na mlango wa stoo kabla Gillemo hajaufunga.



    “Nini? Unajua sitakiwi hata kuzungumza na nyinyi?” Gillemo aliongea bila kumtazama Naomi.



    “Hey Renaldo… najua una amri ya kutuweka chini ya ulinzi lakini sisi sio wahalifu… kwa hiyo acha kusema nasi kama unasema na wahalifu fulani hivi… kumbuka unasema nasi, sisi… Naomi, National Security Advisor… Ruppert, Mkurugenzi wa CIA… Ethan, kiongozi wa timu ya weledi wa kijeshi… ni sisi! Kwa hiyo acha kusema nasi kama unasema na wahalifu fulani hivi…”



    Naomi akaongea kwa ukali kidogo huku amemkazia macho Renaldo Gillemo.

    Kidogo Gillemo akalainika na aibu ikamjaa usoni.



    “Nakusikiliza Naomi!”



    “Asante! Kuna kitu cha tofauti sana kinaendelea… sitaki kukuambia kwa kuwa hautoniamini… ninachokuomba ukiingia ndani ya Oval Office… ichunguze kadiri utakavyoweza na utaona kuna kitu hakiko sawa… kisha tafakari juu ya hicho ambacho utakiona.!” Naomi aliongea kwa kujiamini.



    “Kitu gani?” Gillemo aliuliza kwa udadisi.



    “Renaldo kama nilivyokwambia… nikikuambia hautaniamini… nataka uone mwenyewe… hakikisha unaingia ndani ya Oval Office! Ukiingia tumia ubobezi wako wote chunguza nukta kwa nukta… utaona kitu hakiko sawa… kisha tafakari!” Naomi aliongea kwa kujiamini zaidi na kisha akasogea mlangoni kumpisha Gillemo awafungie.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Gillemo alichukua kama dakika nzima kuchekecha akilini kile ambacho Naomi alikuwa amekiongea. Kisha bila kusema neno lolote lile akafunga mlango.







    “Kitu gani unataka akione ndani ya Oval Office?” Ethan aliuliza swali kwa haraka mara tu baada ya mlango kufungwa.



    “Hata sijui!!” Naomi alijibu huku anajiinamia.



    “Ati? Unasemaje?” Ethan na Ruppert waliuliza kwa pamoja.



    “Sikilizeni… Ruppert umetueleza kuwa David Logan aliondoka kinyemela hapa bila yeyote kujua… na kama alitekwa au alitoroka basi kitu hicho kilifanyika Nyumbani kwake Naval Observatory Circle… lakini sisi tukiwa Maryland alitupigia simu na kutueleza kuwa amevamiwa Ikulu na mtu anayefanana na Caleb… kwa hiyo nina imani kabisa kuna suala hapa hatujaling’amua… kuna kitu kilitokea kabla hajaondoka hapa Whitehouse ambacho nyinyi hamjakiona… hicho kitu naamnini ndicho kilimfanya atupigie simu… na naamini kilitokea akiwa ofisini Oval Office.!”







    Ethan na Ruppert walau walianza kumuelewa sasa. Hata wao kadiri walivyochakata akili zao walijikuta wanahisi kabisa kuwa. Kuna jambo lazima lilitokea ndani ya Oval Office kabla ya David Logan kupotea kiutata.







    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE







    EPISODE 29







    MANHATTAN AVENUE – ECKFORD STREET (NEW YORK)



    Makao Makuu ya Dathmov Contractors







    Ofisi ya Rodney Van Der Berg, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dathmov Contractors ilikuwa ni kubwa kukaribia vyumba vitatu au labda vinne vya kulala. Upande mmoja wa ukuta ulikuwa ni kioo kitupu ambacho kiliwezesha kuona kwa usawia na kwa upeo mkubwa jiji hili la New York kutokea hapa ghorofa ya 122 ya Dathmov Tower.



    Rodney Van Der Berg, Mmarekani mwenzi asili ya kiholanzi alikuwa amesimama uku amegeukia upande ule wenye kioo tupu akitazama nje akitafakari. Japokuwa alikuwa ni kijana wa miaka 38 tu, lakini alikuwa amefanikiwa kutengeneza himaya ya biashara ambayo ilikuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 60 na kumfanya kuwa moja ya watu wenye ukwasi mkubwa zaidi duniani.



    Kampuni yake ya Dathmov Contractors ilikuwa na matawi karibia kwenye nchi thelathini na mbili duniani. Na ilikuwa na kampuni tanzu ndogo ndogo zupatazo nane.



    Mfano kulikuwa na Dathmov Teknologies ambayo ilijikita zaidi kwenye bara la Asia ambako waliwekeza kwenye viwanda vya utengenezaji wa vifaa vinavyotumiwa na makampuni mengine kutengeneza simu.



    Barani Afrika walikuwa na Dathmov AgroLabs ambao walijikita kwenye uzalishaji wa madawa ya mashambani, utengenezaji wa mbegu za kisasa, mbolea na usindikaji wa bidhaa za kilimo.



    Barani ulaya walijikita zaidi kwenye biashara ya ujenzi na upangishaji wa majengo.







    Lakini nchini Marekani, Dathmov Contractors walijulikana zaidi kutokana na mikataba yake nono kutoka serikalini juu ya masuala ya ulinzi. Na hapa ndipo ambapo kilikuwa kitovu cha ukwasi wa Rodney Van Der Berg.

    Dathmov Contractors, walihusika na utengenezaji wa silaha, gari za kijeshi ambazo zilikuwa zinatumiwa kwenye majeshi ya Marekani. Lakini si hivyo tu, Dathmov Contractors walikuwa pia wanahusika kwenye miradi mingi ya utengenezaji wa teknolojia za siri za vyombo vya ulinzi na usalama vya Marekani.



    Kutokana na haya yote, licha ya kuwa kijana mdogo wa miaka thelathini na nane, Rodney Van Der Berg alikuwa ni moja ya watu wenye ushawishi zaidi ndani ya nchi ya Marekani.



    Mtu hauinuki tu kufikia katika mafanikio makubwa kiasi hiki hivi hivi tu, Rodney Van Der Berg amepitia mengi na kutengeneza maadui wengi mpaka kufikia hapa alipo. Lakini kitu kingine kilichomsaidia zaidi ni namna yake ya ufanyaji biashara. Mbinu na falsafa aliyokuwa anaitumia kwenye biashara zake zilimfanya aogopwe na kila mmoja kwenye sekta za biashara alizomo. Kitu pekee ambacho kilikuwa akilini mwake na alikuwa anakiona mbele yake, ilikuwa ni fedha na himaya ya kibiashara ambayo alikuwa anaitengeneza. Alikuwa haruhusu chochote kile kikae mbele yake na kuzuia malengo yake. Hata uchaguzi wa ofisi yake ulitokana na mtazamo wake na haiba yake. Ukuta wa kioo upande mmoja wa ofisi yake ambao ulimuwezesha kuona sehemu kubwa ya jiji la New York, mwenyewe alipenda kusema kwamb ilikuwa kana kwamba anaiona dunia nzima kwenye upeo wa macho yake na alitamani kuiweka kiganjani mwake.



    Falsafa zake na namna yake ya kuendesha biashara ndio ambayo ilimfanya kusigana na Laura Keith tangu kipindi akiwa Senata kabla hata ya kukwaa Urais.



    Chuki na ugomvi wao huu ndio ambao ulimfanta Rais Laura Keith mara tu baada ya kuapishwa kuanza michakato ya kusitisha mikataba yote minono ambayo Dathmov walikuwa wamepewa na serikali.



    Lakini kama ambavyo Rodney Van Der Berg aliamini katika falsafa yake, kwamba hawezi kuruhusu yeyote au chochote kumkwamisha, ndivyo ambavyo alikuwa amepanga kumdondosha Laura Keith tangu siku ambayo alikuwa ameapishwa.



    Miezi kadhaa katika kupekua pekua na kumchimba Madam President Laura Keith na kufuatilia nyendo zake zote hata zile za siri kubwa, ndipo ambapo aligundua siri kubwa iliyopo kati ya Bi. Laura Keith na jumuiya ya siri ambayo ilikuwa inajiita The 46. Siri hii ndio ambayo alimpenyezeka Makamu wa Rais David Logan, na ni siri ndio ambayo ilikuwa imemponza David Logan kutekwa na kupelekwa kusikojulikana mpaka sasa.







    Rodney Van Der Berg bado alikuwa anatazama nje akiwa amesimama pembeni ya ule ukuta wake wa kioo akitafakari jambo fulani.











    Kwenye kiti cha wageni pale ofisini mwake alikuwa ameketi Donald McLaren. Mume wa Latisha, mtaliki wa makamu wa Rais David Logan, mama wa Natalie mtoto pekee David Logan.







    Donald McLaren ni wakili wa kujitegemea hapa New York. Alimuoa Latesha, mama yake Natalie baada ya kutalikiana na David Logan miaka miwili iliyopita. Licha ya ofisi yake ya uwakili kuwa na mafanikio makubwa sana na kuwa na Wateja wazito ambao ni wafanyabiashara wakubwa, lakini leo hii kuitwa ofisini kwa nguli wa biashara Rodney Van Der Berg kulimfanya kwa kiasi fulani ajisikie kama moyo unataka kupasuka kwa hofu.



    Alikaa pale kwenye kiti akifikiria kila aina ya uwezekano wa kwanini ameitwa hapa. Labda Dathmov Contractors walikuwa wanataka msaada fulani wa kisheria, lakini hii ilikuwa haiingii akilini mwake maana Dathmov tayari wanapata huduma za kisheria kutoka kwenye moja ya kampuni bora zaidi za kisheria na kubwa na maarufu kuliko hata ofisi yake.



    Na kitu ambacho kilimshitua zaidi ni kwamba, alipigiwa simu moja kwa moja kutoka kwa Rodney Van Der Berg mwenyewe na alipofika hapa moja kwa moja alipelekwa ofisini mwake. Hili lilimsumbua sana kichwani. Rodney Van Der Berg alikuwa na wasaidizi binafsi karibia kumi labda, na kwa desturi ya watu wa hadhi yake kamwe huwa hawafanyi mawasiliano na watu wao wenyewe moja kwa moja kama sio rafiki yake wa karibu au mwanafamilia wake. Mawasiliano yao yote yanafanywa na wasaidizi wao, kila ambacho wanataka kukisema kinasemwa kupitia wasaidizi wao.



    Pia kingine kilichomshangaza zaidi ni kitendo cha kufika tu hapa kwenye ofisi za Dathmov kuitikia wito na moja kupelekwa ofisini kwa Rodney Van Der Berg.

    Rodney au ‘Ron’ kama ambavyo watu wake wa karibu wanamuita, ni aina ya watu ambao unamuona karibu kila siku kwenye runnga, unamsoma kwenye magazeti lakini kamwe haufikirii kama ipo siku unaweza kuonana naye. Inawezekana ni rahisi zaidi kuonana na Rais kuliko kuonana na ‘Ron’… Rodney Van Der Berg.



    Chochote kile ambacho alikuwa ameitiwa hapa, lazima kilikuwa ni kitu muhimu mno, na cha siri mno. Na hii ilizidi kumtisha ndani yake.







    Kabla Ron kugeuka na kutazama nje kupitia kioo, alikuwa emuuliza Donald “ni nini alikuwa anahisi kinaendelea duniani?”



    Dinald alijing’atang’ata ulimi kujaribu kueleza mawazo yake japokuwa hakuwa na point yoyote ya maana sana. Tangu alipoanza kuongea mpaka anamaliza na mpaka sasa takribani zimepita dakika tano nzima, Ron alikuwa amegeuka anazama tu nje.



    Ghalfa akageuka taratibu bila kumuangalia na kisha kwenda kuketi tena kwenye kiti chake nyuma ya meza yake kubwa ya ofisi ya kifahari.

    Baada ya kuketi wakabaki wanakodoleana macho tu. Ron alikuwa anamuangalia Donald katika namna ambayo kama alikuwa anajaribu kumdadisi fikra zake.







    “Kwa nini huwa hautaki Natalie aonane na baba yake David Logan mara kwa mara.!” Hatimaye Rodney Van Der Berg aliongea.







    Lilikuwa ni swali la kushitukiza na ambalo hakulitegemea kabisa. Hakuelewa ni kwa nini Ron alikuwa anamuuliza swali hili. Alipounganisha na swali la kwanza ambalo alimuuliza, “unahisi ni nini kinaendelea duniani” hakujua kulikuwa kunahusiana nini na hili swali ambalo alikuwa anamuuliza sasa.

    Kwanza alishangaa ni kwa namna gani mtu adhimu kama Ron afahamu kuhusu familia yake na mtoto wao Natalie. Kilichokuwa kinamshangaza sio kitendo cha Ron kupata hiyo taarifa maana kwa mtu wa hadhi yake kuwa na taarifa kama hiyo ni kitendo cha dakika tu, lakini kilichokuwa kinamshangaza ni kwa nini alikuwa anaulizia.



    Kichwani alihisi kwamba Ron alikuwa anajaribu kuzungumza mambo ya ‘kawaida’ kwanza kuhusu familia na kadhalika kabla hawajaanza kuzungumzia hasa kitu ambacho alikuwa amemuitia hapa.







    “Kwa heshima na taadhima… mkuu nisingependa kuzungumzia masuala hayo… ni binafsi mno!” Donald alimjibu Ron.



    “Nisamehe kwa kukuingilia masula yako binafsi… lakini nadhani ni muhimu ukinijibu!”



    “Kuna umuhimu gani?” Donald alishangaa.



    “Donald… sidhani kama utapungukiwa kitu kama utanijibu.!”



    Ukapita ukimya wa karibia dakika nzima. Walikuwa wanakodoleana macho tu. Donald alionyesha kukereka haswa kutokana na swali hili la Ron. Alitamani ainuke kwenye kiti na kuondoka, lakini aliamini kuwa Ron hakumuita hapa ili kuzungumzia migogoro ya ndoa yake. Kuna suala kubwa zaidi lazima alikuwa anataka kuzungumza naye, labda hii ilikuwa ni mbinu yake ya ‘kupasha moto’ maongezi kabla hajaongea lengo lake hasa la kumuita hapa.



    “OK.. Natalie ana hasira na baba yake kutokana na ule mkasa wa kujihusisha kimapenzi na sekretari wake ambako kulipelekea mpaka kutalikiana na Latisha… kwa hiyo kimsingi ni Natalie ndiye ambaye hataki kumuona baba yake, ndio maana kila mara David Logan akijaribu kuonana na Natalie huwa nazuia… ni hivyo tu! Umeridhika?” Donald aliongea kwa kukereka.







    Ron alinyamaza kwa sekunde kadhaa akitafakari, kisha akaanza kuongea.



    “Donald… unajua David Logan kwa kiasi fulani yuko kama mimi… binafsi kitu pekee kilichopo akilini mwangu na ninachokiona mbele zangu ni biashara zangu… David naye yuko hivyo, kitu pekee anachokiona mbele yake na kukijali ni madaraka… lakini kuna siri ambayo unapswa kuijua… kila kitu kigumu, haijalishi ni kigumu kiasi gani, kina pahapa pa udhaifu, pahala penye ulaini… na udhaifu wa David ni Natalie… kitu pekee ambacho nafahamu kwa hakika David anakijali kukipenda kuliko kitu chochote kile ni Natalie…!” Ron aliongea huku amemkazia macho Donald.







    “OK…ok..OK! Nimeelewa sasa… amekutuma wewe swahiba wake ili uje kunilainisha ili Mimi na Latisha tulainike amchukue Natalie… hahah kwa nini sikuliona hili tangu mwanzo!” Donald aliongea huku anainuka kwenye kiti na kufubga vyema vishikizo vyake vya koti la suti akiashiria kuwa anataka kuondoka.



    “Donald… amini kwamba hakuna mtu mwenye uwezo wa kunituma kufanya kitu fulani… Nimeongea haya kwa utashi wangu na nina sababu kwa nini nakwambia hivi.!” Ron aliongea kwa kujiamini pasipo kuinuka kwenye kiti pale ambapo alikuwa ameketi.



    “Kitu gani?” Donald alijibu kwa ushari ushari fulani hivi huku ameweka mikono mfukoni. Alikuwa amesimama katika ile namna ambayo inaashiri kwamba ‘ukiongea neno lingine la kijinga naondoka’. Ameweka mikono mfukoni huku amemkazia macho.



    “David Logan hajulikani alipo!!” Ron aliongea ghafla akiwa amekaza macho huku ameinua uso kumuangalia Donald ambaye amesimama.



    “Unasemaje??” Donald akahamaki na kutoka macho.



    “Haijatangazwa bado kwa umma, lakini suala linaloendelea Whitehouse ni kwamba, David Logan hajulikani alipo, inasemekana kwamba ametekwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake Naval Observatory Cirle.!”



    Donald alijikuta anakaa chini bila kutaka kutokana na mshituko. Alishindwa hata aseme kitu gani.



    “Kwa nini unanieleza yote haya?” Donald akauliza akiwa bado yuko kwenye taharuki.



    “Mwanzoni mwa mazungumzo yetu nilikuuliza unahisi ni nini kinaendelea duniani? Haya matukio ya kutwaliwa kwa miji… sasa ndani ya mwezi mmoja au hata labda wiki mbili kisipofanyika kitu dunia nzima inaweza kugeuzwa Anabelle… mtu pekee ambaye nina uhakika ana uwezo wa kutusaidia kupata suluhisho ni David Logan na hii ndio sababu ya yeye kutekwa! Sasa mtu pekee ambaye anaweza kutusaidia kumpata David ni Natalie..!” Ron aliongea bila hata kutabasamu. Hii ndio ilikuwa mtindo wake akiwa anajadili kitu kizito. Anaweza kuongea hata maswaa mawili bila kuonyesha chembe ya tabasamu.







    “Sikuelewi kabisa ni nini unamaanisha? Natalie anwezaje kusaidia kumpata David? Na David anawezaje kusaidia kuzia miji kutwaliwa? Na kwa nini hajafanya hivyo mida wote huu?” Donald aliongea huku ametumhua macho akionyesha dhahiri kabisa amechanganyikiwa kutokana na hii habari.







    “Ndio maana nimekuita hapa… nitakueleza kila kitu.!”



    Ron akakaa sawa kwenye kiti na kuanza kumpa maelezo.





    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE











    EPISODE 30







    VATICAN CITY







    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..” (mvinyo ni kama damu… kadiri inavyokaa zaidi ndivyo inavyoongeza nguvu ya kuiteka dunia)











    Baridi bado lilikuwa ni kali hasa ndani ya Basilica. Ukungu ulikuwa umejaa ndani kiasi kwamba ilikuwa kama vile wingu limeshuka na kujaza Basilica. Ukungu huu ulikuwa umeambatana na baridi kali kupitiliza.



    Father Ricardo bado alikuwa anaisogelea sanamu ya mfalme Daudi huku akitamka tena na tena maneno yale yale.







    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..”



    Kadiri alivyokuwa anatamka maneno haya na kuisogelea sanamu, ndivyo ambavyo sanamu inazunguka kutokea pale chini bapo imeshikiliwa.



    Sanamu hii yenye urefu wa mita tano kwenda juu inayomuonyesha Mfalme Daudi akiwa kijana na kuchongwa na moja ya wasanii maarufu zaidi kwenye historia, Michelangelo na kama ambavyo ilikuwa mtindo wa kipindi hicho sanamu hii ilikiwa imechongwa ikimuonyesha kijana Daudi akiwa bila nguo.



    Japokuwa sanamu hii tangu ichongwe kwa zaidi ya miaka 500 iliyopita ilikabidhiwa katika kanisa la Florence Cathedral ambalo mdilo kanisa kuu la dhehebu la Roman Katoliki nchini Italy na kisha baadae kuhamishiwa kuhishiwa kituo cha Galleria dell’Accademia, ambacho ndicho kituo rasmi cha utunzaji wa kazi kuu zaidi za sanaa katika historia ya dunia.



    Lakini miaka mitatu iliyopita, yaani mwaka 2035 ndipo hasa sanamu hii ilihamishiwa Vatican na kuwekwa kwenye jengo la Basilica.

    Kuna watu wachache sana ambao walijua siri halisi ya kwanini sanamu hii ilihamishwa kutoka kituo cha Galleria dell’Accademia na kuletwa Vatican. Umma ulifahamu kuwa sanamu hii ilihamishwa kutokana na Papa kuwa mpenzi mno wa kazi za Sanaa za Michelangelo na hivyo alitamani sanamu hiyo ya kihistoria itunzwe ndani ya Vatican.



    Japokuwa sanamu hii ilikuwa ni ya kupendezwa na kutengenezwa kwa ustadi mkubwa lakini kwa kiwango fulani ilikuwa inatia shaka umuhimu ambao ilikuwa inapewa. Ni dhahiri kibisa kwamba kulikuwa na uwezekano kabisa wa msanii mwingine mahiri katika kizazi hizi, mwaka huu wa 2038 kufinyanga au kuchonga sanamu nzuri kama hii au labda nzuri zaidi kupita hii. Lakini ni ajabu kwamba kwa muda wa miaka zaidi ya 500 sanamu hii bado imeendelea kupewa umuhimi wa kipekee kuliko kazi zingine karibia zote za kuchonga na kufinyanga.



    Kwa yeyote yule mwenye udadisi na kuhoji maswali kichwani angeliweza kung’amua kuwa kuna jambo la ziada juu ya sanamu hii ya Daudi. Father Ricardo alikuwa ni moja ya watu hasa wachache ambao walijua siri iliyojificha juu ya sanamu hii.



    Father Ricardo aliendela kuisogelea sanamu mpaka akaifikia karibu yake kabisa.

    Ukungu na baridi kwenye chumba ulikuwa umefikia kiwango ambacho kilikuwa kimepitiliza kabisa. Ukungu ule ulikuwa kama vile sio wingu tu bali ulikuwa kama kuna kitu kinaungua na kutoa moshi mkali. Ukungu ulikuwa umetanda ndani ya Basilica kufikia kiwango ambacho mtu akisimama mbele yako mita mbili tu usingeweza kumuona.



    Father Ricardo aliingiza mkono ndani ya joho lake na kutoka kichupa kidogo chenye ujazo kama wa robo lita hivi ambacho alikuwa amekificha muda wote huu. Chupa hii ndogo ilikuwa imejazwa kwa mvinyo na si mvinyo tu kama ulivyo mvinyo wowote bali ulikuwa ni mvinyo wa Mfalme wa kale wa ugiriki, mvinyo wa Mfalme Secus.



    Kwa zaidi ya miaka thelathini iliyopita kama ambavyo Father Ricardo alikuwa ametaabika kupata BOOK OF CODES ndivyo vivyo hivyo pia alikuwa ametaabika kupata kiasi hiki cha robo lita ya Mvinyo wa Mfalme Secus.



    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..”







    Father Ricardo alitamka maneno yale kwa uthabiti zaidi safari hii akiwa amefika mbele kabisa ya sanamu.



    Sanamu ilikuwa inaongeza kasi ya kuzunguka kadiri muda ulivyokuwa unaenda. Pale chini iliposimimashwa ilikuwa kana kwamba kulikuwa na mota ambayo ilikuwa inafanya sanamu izunguke kwa kasi kubwa namna hii.



    Father Ricardo alikuwa anaitazama huku anahema na akitetemeka kwa nguvu. Kutetemeka huku hakukuwa kwasababu ya baridi ambalo lilikuwa ndani ya Basilica bali alitetemeka kwa woga, au kwa usahihi zaidi si woga bali shauku ya kile ambacho kilikuwa kinafuata mbele yake muda mchache ujao.



    Father Ricardo alifungua mfuniko wa chupa hii ndogo yenye mvinyo na kisha kuanza kumimina mvinyo kwenye sanamu ya Mfalme Daudi ambayo ilikuwa inazunguka kwa kasi kweli kweli.



    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..”



    Father Ricardo alirudia tena kutamka yale maneno huku akiwa anamimina mvinyo kwenye sanamu.



    Kadiri ambavyo alikuwa anamimina mvinyo kwenye sanamu ndivyo ambavyo sanamu ilikuwa inamung’unyuka taratibu na udongo wake kudondoka pale chini iliposimamishwa ambapo ndipo palikuwa panafanya sanamu yote izunguke.



    Father Ricardo aliendelea kumimina mvinyo kwa taratibu huku akitamka yale maneno tena na tena. Alimimina mvinyo mpaka ilipofikia hatua ya sanamu yote kumung’unyuka kabisa na kubakia udongo mtupu pale chini panapo zunguka.



    Sanamu ambayo imekuwepo ulimwenguni kwa zaidi ya miaka mia tano na kujipatia umaarufu mkubwa na kulindwa kama mboni ya jicho hatimaye ndani ya dakika chache tu ilikuwa imepitea na kubakia udongo tu kama ambavyo imulitumiwa kifinyangwa siku ya kwanza, miaka mitano iliyopita na msanii Michelangelo.



    Pale chini ambapo sanamu ilikuwa imesimamishwa paliendelea kuzunguka vile vile huku ule udongo uliomung’unyuka ukiwa juu yake.



    Mapigo ya moyo ya Father Ricardo yaliongezeka maradufu. Hali ya kutetemeka iliongezeka zaidi. Sio kwa sababu ya baridi tu, bali ni kutokana na hatua muhimu zaidi ya hiki alichokuwa anakifanya hapa kuwadia.



    Sekunde hii, dakika hii ilikuwa imesubiriwa na Father Ricardo kwa maisha yake yote. Sio kwamba tu ndani yake alikuwa na furaha ambayo ilikuwa imepitiliza, bali pia alikuwa na shauku na pia kwa kiwango Fulani alikuwa na woga juu ya maisha yake ndani ya dakika chache zijazo. Ndani ya dakika chache tu maisha yake hayatakuwa tena kama ambavyo aliyaishi kwa muda wote tangu azaliwe.



    Kumbukumbu za utoto wake akiwa nchini kwao Mexico zikamjea kichwani. Kila aina ya kumbukumbu nzuri au ya uchungu ilimjia muda huu. Ndani ya sekunde chacje karibia kila kumbukumbu ambayo ilichangaia kumfanya awe jinsi alivyo kumfikisha wakati huu wa sasa ilirejea kichwani. Chozi la uchungu na furaha lilimtoka.







    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..” (mvinyo ni kama damu… kadiri inavyokaa zaidi ndivyo inavyoongeza nguvu ya kuiteka dunia)







    Father Ricardo alitamka kwa mara ya mara nyingine tena yale maneno na kisha kukanyaga mguu wake ndani ya ule mchanga uliomung’unyula ambao ilikuwa unazunguka. Kisha akakanyaga na mguu wa pili. Sasa alikuwa amesimama katikati ya ule mchanga huku akizunguka nao kama ambavyo ulivyokuwa ukizunguka kutokana na pale chini ambapo awali ili simama sanamu kuzunguka.







    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..” (mvinyo ni kama damu… kadiri inavyokaa zaidi ndivyo inavyoongeza nguvu ya kuiteka dunia)



    Father Ricardo alitamka maneno haya kwa mara ya mwisho na kwa nguvu zake zote huku akijimiminia kichwani kiasi kidogo kilichobakia cha mvinyo wa Mfalme Secus ambacho kilikuwa kimebakia kwenye ile chupa.



    Tone la kwanza la mvinyo ambao alijimiminia kichwani lilipotua chini kwenye ule udongo ambao ulimung’unyuka kutoka kwenye sanamu, ulianza kumpanda mwilini kana kwamba ni mti wa jamii ya mkunde unaota kwa kuzunguka tawi la mti.



    Udongo ulikuwa unampanda mwilini kwa kasi kubwa ya ajabu. Bado pale chini palikuwa panazunguka. Na kadiri ambavyo udobgo ulivyokuwa unaoanda mwilini mwa Father Ricardo ndivyo ambavyo kasi ya kuzunguka ilivyozidi.







    “Aaaaaaaaaaaaaaaahhhhhh”







    Father Ricardo alipiga ukelele mkali wa maumivu kutokana na hali ya tofauti ambayo mwili wake ulikuwa unapitia na kubadilika. Pale chini palikuwa panazunguka kwa kasi kubwa ya ajabu na kufanya mwili wa Father Ricardo nao kuzungushwa kwa kasi kubwa kama ile iliyopo pale chini alipokanyaga.



    Udongo ulimpanda mwili mzima na hatimaye kumfunika mwili wote kuanzia kichwa mpaka unyanyo.



    Udongo wote ulipomfunika mwili mzima, kasi ya kuzungushwa iliongezeka mara dufu kiasi kwamba Father Ricardo alikuwa panazunguka kwa kasi mpaka akawa haonekani sawia.



    Ghafla hali ile ya pale chini kuzunguka ilikoma ghafla na kufanya Father Ricardo arushwe kwa nguvu na kwenda kujibabiza kwa nguvu kwenye ukuta wa Basilica.



    Kishindo cha kujibamiza ukutani kilikuwa ni kikubwa kiasi kwamba mpaka ukuta wa Basilica uliweka nyufa.



    Ukungu ambao bado ulikuwa umetanda ndani ya Basilica haukuwezesha Father Ricardo kuonekana mara moja kwa urahisi kama mtu angelikuwa na azwa ya kutaka kumtazama. Lakini baada ya Father Ricardo kurushwa vile kwa ghafla ukungu ulianza kupotea kwa kasi kubwa na mandhari ya ndani ya Basilica kuanza kurejea kama ambavyo huwaga siku zote.



    Ukungu huu ulivyokuwa unapotea ndivyo ambavyo ulifanya Father Ricardo kuonekana pale ambapo alikuwa amedondokea baada ya kurushwa na kujibamiza kwenye ukuta wa Basilica.







    Ilikuwa ni ajabu lakini ndio ulikuwa uhalisia. Ilikuwa ni kitu ambacho unahitaji kukiona kwa macho ndipo uamini. Ilikuwa ni kitu ambacho kitakuja andikwa kwenye vitabu vya historia na kusomwa na vizazi vijavyo miaka elfu ijayo.



    Ule udongo ambao ulimung’unyuka na baadae kuanza kutambaa mwilini mwa Father Ricardo ulikuwa umembadili na kumgeuza kuwa sanamu ya Daudi inayoishi. Yaani Sanamu ya Daudi ya zaidi ya miaka mia tano ilikuwa imegeuka kuwa Father Ricardo na Father Ricardo alikuwa amegeuka kuwa sanamu ya Daudi. Ilikuwa ni kana kwamba roho ya Father Ricardo ilikuwa imeingia kwenye sanamu ya Mfalme Daudi na kuipa uhai.



    Alikuwa ni mfalme Daudi kijana. Japo hakuwa binadamu wa kawaida. Alikuwa na rangi ya marumaru (marble) ya aina ya kijivu iliyopauka sana. Pia urefu wake ulikuwa kama wa sanamu jinsi ambavyo ilikuwa, mita tano kwenda hewani. Kwa kifupi ilikuwa ni kwamba sanamu maarufu ya mfalme Daudi ilikuwa imepata uhai.



    Father Ricardo, au uzuri zaidi kuita sanamu ya Daudi yenye Uhai iliinuka kutoka pale sakafuni ilipodondoka na kusimama. Urefu wake wa futi tano ulikuwa unaogofya. Rangi yake ya marumaru ya kijivu iliyopauka iliogofya zaidi.



    Yeye mwenyewe aliinuka huku akijishangaa na kujiangalia angalia kama vile aamini kile ambacho kilikuwa kimetokea. Kuna utofauti mkubwa sana wa kuamini jambo Fulani na kuliona likitokea.



    “…vinum est sicut sanguis maior et maior est potententia eus..”



    Aliongea baada ya kuinuka na kusimama sawia. Akanyoosha mkono kuokota kitabu chake cha BOOK OF CODES ambacho alikiacha kikiwa kimefunuka muda wote huu.



    Mateso yote na kutaabika kote kwa zaidi ya miaka thelathini kwa ajili ya kufikia wakati huu hatimaye kulikuwa kumeitimishwa.



    Kiumbe hiki kipya kilitoa kicheko cha furaha kwa mafanikio haya. Japokuwa kilikuwa ni kicheko tu, lakini mtetemo ulioambatana nacho ilisababisha mpaka radi kutoka. Angani.







    Hatimaye kafara ya kwanza ya kukaribia kuifanya Dunia yote kuwa Anabelle ilikuwa imekamilika. Silaha mpya na hatari zaidi ya The 46 ilikuwa imezaliwa.



    Haikiwa imebakia miezi, au wiki. Bali sasa zilikuwa zimebakia siku chache tu kwa Dunia mzima kutwaliwa na kufanywa kuwa Anabelle.







    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE







    EPISODE 31











    MARYLAND, MAREKANI



    Japokuwa ilikuwa ni saa nane mchana lakini giza ambalo lilikuwa limetanda lilifanya ionekane kama vile usiku ulikuwa unataka kuingia. Halikuwa giza totoro, lakini lilikuwa ni giza la kutosha tu kufanana kabisa na giza la saa moja jioni.



    Mzee Caleb akiwa ameongozana na vijana makomando waliopo kwenye kikosi maalumu cha Ethan kutoka CIA ambao waliachwa hapa kumlinda Caleb pindi Ethan na Naomi walipoelekea Washington, walitoka nje ya nyumba ili kushangaa hiki ambacho kilikuwa kinatokea.



    Caleb alisimama katikati ya uwanja wa nyumba yake huku akiwa amezungukwa na wale vijana makomando. Mbele ya macho yao kama vile wakiwa ndotoni, mchana ulikuwa unageuka kuwa usiku. Saa nane ya mchana inageuka kuwa saa moja ya jioni.

    Giza hili lililokuwa linaingia lilikuwa limeambatana na upepo mkali na pia labda ni kwa sababu ya upepo au labda ndio kiroja kingine tu kama ambavyo mchana ulikuwa unageuka kuwa usiku, ajabu ni kwamba angani nako mawingu yalikuwa yanatembea kwa kasi kuliko kawaida yakiwa na rangi nyeusi kushinda ilivyo kawaida. Na haikuwa upepo tu au kasi ya mawingu bali pia radi kali zilisikika kwa kishindo angani.



    “Mzee nini kinatokea?” Moja ya wale vijana makomando alimuuliza Caleb akiwa amehamaki.



    Mzee Caleb alikuwa kama vile hasikii kile ambacho kilikuwa kinaulizwa. Alikuwa anageuka geuka upande huu na kisha upande huu kama vile kuna kitu alikuwa anakitafuta kule juu angani.



    Yule mnyama wa ajabu ambaye walikabidhiwa walipokuwa msituni alikuwa anapiga kelele ya ajabu kule chini kwenye basement ambako walikuwa wamemuweka. Kelele ambayo alikuwa anaitoa ilikuwa inafanana kabisa na kelele kali ya tai lakini yenye muungurumo mkali. Alikuwa anapiga kelele mfululizo kama kwamba alikuwa amekasirika au anataka kufanya shambulio.



    “Mzee nini kinaendelea…. Mzee.!” Kijana mwingine komando aliuliza kwa taharuki kubwa zaidi.



    Mzee Caleb bado aliendelea kuangalia angani akigeuka huku na huko kama vile kuna kitu anakitafuta akione juu ya anga. Alikuwa kama vile hasikii maswali ya wale vijana makomando wa Ethan.



    Kelele za yule mnyama wa ajabu zilizidi kushika kasi kule chini kwenye basement ambako alikuwa amehifadhiwa.



    “…Tunahitaji damu.!” Mzee Caleb aliongea huku anatembea kwa kasi kuelekea ndani ya nyumba yake.



    Wale vijana wote kwa pamoja wakamfuata ndani.



    “Damu.? Ya nini?” Kijana mwingine akauliza.



    “Mmesahau kule msituni tuliambiwa huyu kiumbe tumpe damu kopo moja kila baada ya siku tatu.? nadhani ana njaa… tunahitaji kumpa damu!” Mzee Caleb aliongea huku anakuna kichwa kama vile amechanganyikiwa anajaribu kufikiri jambo fulani.



    “Muacheni afe tu… tumekuuliza nini kinatokea hautujibu!” Yule kijana ambaye walipokuwa nje alikuwa anauliza nini kinatokea alibwatuka kwa hasira.



    “Huyu kiumbe ametolewa ndani ya Anabelle… kama wangelikuwa wanataka afe basi wangemuacha afe huko huko… lakini kitendo cha kumtoa huko na kumleta duniani kinanishawishi kuamini kwamba kuna umuhimu mkubwa wa huyu kiumbe… lazima tuhakikishe anaishi… tunahitaji damu sasa hivi haraka sana!” Mzee Caleb akamjibu kwa ukali.



    “Mzee nadhani haujanisikia ninachouliza… nini kinaendelea hapa? Hii ni saa nane mchana lakini ghafla kumegeuka giza na kuwa usiku… nini kinaendelea?” Yule kijana akauliza tena safari kwa ghadhabu huku akiwa amemkazia macho Mzee Caleb.



    Mzee Caleb alifumba macho na kuvuta pumzi kubwa ndani na kisha kuitoa nje. Dhahiri kabisa alionekana kwamba alikuwa hataki kuongea suala hilo kwa kuwa lilikuwa linamuogofya ndani yake.



    “Kafara.!” Mzee Caleb alitamka neno moja tu na kukaa kimya kujiinamia pale mezani baada ya wote kuingia ndani na kuketi.



    “Kafara? Kafara ya nini?” Kijana komando mwenye gadhabu muda wote akauliza tena.



    “The 46 wamefanikisha kufanya kafara ya kwanza… wamemfufua moja ya mashujaa wa kale… sijui ni nani lakini ninachojua kwamba hii ni kafara na tunaweza tusilione jua tena na siku chache zijazo ulimwengu wote unaweza kugeuzwa kuwa Anabelle.!” Mzee Caleb aliongea kwa woga mpaka sauti ilikuwa inatetema.



    Ulipita ukimya wa dakika kadhaa kila mmoja akijaribu kuchakata kichwani mwake hiki ambacho Mzee Caleb alikuwa amekisema.



    “Sielewi hiki unachokisema lakini nadhani tunapaswa kutoa taarifa hii kwa Ethan!” Mmoja wao aliongea baada ya ukimya wa dakika kadhaa.



    “Hakuna mawasiliano!” Kijana mwingine komando alidakia huku akiwa ameshikilia simu ya satelaiti mkononi.



    “Unasemaje?”



    “Hakuna mawasiliano… nimejaribu kwa mara kadhaa hakuna mawasiliano… hatuwezi kupiga wala kupokea simu!” Akaongea kwa sauti ya unyonge huku akibamiza chini simu ambayo alikuwa ameishikilia mkononi.



    “Nini kinatokea?” Wakajikuta makomando kadhaa wanauliza swali moja kwa pamoja.



    “Nimewaambia kuwa kafara imefanyika na ndani ya siku chache tu ulimwengu mzima unageuka kuwa Anabelle… hizi ni hatua za awali kuurejesha ulimwengu wote ulivyokuwa awali enzi za uhai wa Pandora mwenyewe… uasili tupu unatawala hakuna teknolojia.!” Mzee Caleb aliongea huku safari hii aliwa esimama akitembea tembea pale sebuleni.



    “Tunafanyaje? Hatuwezi kukaa tu tukishuhudia ulimwengu unatwaliwa.!” Komando mmoja akapayuka.



    “Natamani tungekuwa na kitu ambacho tunaweza kufanya… lakini nasikitika kusema kwamba The 46 wametuzidi kete, ndani ya siku chache wanaurejesha ulimwengu mzima kuwa Anabelle ya Pandora kama ambavyo ilikuwa miaka elfu kadhaa iliyopita.!” Mzee Caleb aliongea kwa kunyong’onyea huku anakaa chini kwa upole kama vile amemwagiwa maji mwilini.



    Ilikuwa inasikitisha mno kumona hata Caleb amekata tamaa. Kwa kiasi fulani Caleb ndiye ambaye alikuwa anaonekana kama tumaini kuu la kusaidia kuurejesha tena ulimwengu katika hali yake ya kawaida. Kumuona yeye anakata tamaa ilikuwa inaumiza moyo na kukatisha tamaa zaidi kuliko hata yeye mwenyewe namna vile amekata tamaa.



    “Comoooonn! Lazima kuna jambo tunaweza kufanya Mzee!” Komando mmoja alijaribu kuwatia moyo wenzake pamoja na Mzee Caleb.



    “Jambo gani… namna pekee kuukoa ulimwengu kwanza kabisa tunapaswa kuisambaratisha jumuiya ya The 46 ili kuzuia kuendelea kufanya wanachokifanya.!” Mzee Caleb akaongea.



    “Natamani utoe wazo hata kama ni la kufikirika tu… ni namna gani tunaweza sambaratisha jumuiya ya The 46?” Yule komando akaongea kwa kujiamini.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Kabla hata ya kufikiria ni namna gani tunaweza kusambaratisha jumuiya ya The 46… kumbuka kwamba hatujui hata tunawapataje!” Mzee Caleb aliongea tena kwa sauti ile ile ya kukata tamaa.



    “Lakini nakumbuka kabla ya kina Naomi na Ethan kuondoka ulitoa wazo kuhusu namna tunayoweza wapata The 46.!” Yule komando aliongea tena kudhihirisha kwamba hakuwa tayari kukata tamaa.



    “Nilisema tufuate harufu..!” Mzee Caleb aliongea kwa kifupi tu.



    Yule komando hakusema chochote. Alimkodolea macho Mzee Caleb kwa namna ambayo alimaanisha kuwa ‘nakusikiliza’. Aendelee kuongea.



    “Nilisema tufuate harufu kwa maana ya kwamba, yule kiumbe mwenye sura yangu ambaye alivamia Whitehouse… huyu ndiye ambaye nimetumia lugha ya harufu kwa sababu kama tukiweza kumfuatilia yeye basi moja kwa moja atatupeleka mpaka walipo The 46!! Lakini ubaya ni kwamba sijui hata tunampataje lakini pia uzuri ni kwamba akiwa karibu yangu kuna hali fulani hivi nakuwa naisikia na naweza kujua kuwa yuko hapo.!” Mzee Caleb akaeleza tena kwa kirefu.



    Ukimya mwingine ukatawala, kila mmoja wao akijaribu kuchanganua kile ambacho kilikuwa kinasemwa. Jambo ambalo lilikuwa linawaumiza kichwa ilikuwa ni namna gani wataweza kuanza kufuatilia nyendo za kiumbe huyo ambaye ataweza kuwafikisha walipo jumuiya ya The 46.







    Wakiwa katika ukimya huu na kitafakari ni nini hasa cha kufanya na katika kiza hiki kinene huko nje japokuwa ilikuwa ni mchana. Ghafla tu kukasikia sauti kubwa mno… muungurumo wa kama baragumu au tarumbeta nzito kiasi fulani ikifanana kabisa na honi ya treni lakini yenyewe ikiwa na uzito mkubwa zaidi na kirandana na sauti ya tarumbeta. Ilikuwa ni kama vile parapanda kuu inapigwa na papo hapo ikiambatana na tetemeko la ardhi la wastani.



    Ilikuwa ni dalili kwamba mji wa Maryland nao ulikuwa unaelekea kutwaliwa.



    Waliposikia sauti hii kuu ya kuu ya kutisha wote walisimama huku wakijishikilia kwenye viti na meza ili wasidondoke kutokana na mtetemo wa tetemelo la ardhi.



    Kama ilivyo sehemu nyingine zote duniani ambazo zilitwaliwa. Dalili hii ndio ambayo ilikuwa inaashiria kwamba ndani ya masaa sita mji huo husika ulikuwa unaenda kutwaliwa.



    “Maryland inaenda kutwaliwa.!” Mzee Caleb aliongea kwa sauti ya kigugumizi huku akiwa amejishikilia kwenye kiti kutokana na mtetemo wa ardhi.



    Vijana wa Ethan walibakia wajishikilia kwenye viti huku wamekodoa macho kwa taharuki Kubwa. Licha ya kufuzu na kuwa na weledi wa hali ya juu kwenye masuala ya kijeshi lakini kwenye hali kama hii hawakuwa na tofauti yoyote na Mzee Caleb. Hawakuwa na chochote kile ambacho wangeliweza kufanya.







    Tetemeko liliunguruma kwa muda wa kama robo saa hivi na kisha likakoma. Pia sauti ya ile kubwa na nzito kama baragumu nayo ilikoma.



    Kama ilivyo ada mji unapotwaliwa sehemu ya mwisho ya mji kutwaliwa inakuwa na nyufa kuashiria mpaka wa Anabelle na Dunia ya kawaida. Kwa hiyo Mzee Caleb na vijana wa Ethan walikuwa na masaa sita tu kuondoka kutoka hapa walipo mpaka mahala ambapo kuna nyufa hiyo ya mpaka wa Anabelle na dunia.



    “Ibabidi tuondoke sasa hivi bila kuchelewa.!” Moja wa wale makomando aliongea kwa haraka Mara tu baada ya tetemeko na sauti ya baragumu kukoma.



    “Kabla hatujaondoka nataka mnisaidie kufukua hilo kaburi hapo nje..!” Mzee Caleb akaongea ghafla tu akiwakatisha wenzake mazungumzo ya mipango wa namna ya kuondoka ndani ya mji huo wa Maryland ambao ulikuwa unaelekea kutwaliwa.



    “Umesema?” Kijana mmoja akauliza kwa mshangao.



    “Kabla kiongozi wenu Ethan kuondoka aliniuliza kuhusu kaburi hapo nje ambalo limefichwa… ni kaburi moja ambalo nilimzika mkewangu na mwanangu… niliwazika ndani ya kaburi moja… siwezi kuyaacha mabaki yao hapo kwa kuzingatia kuwa mji unaenda kutwaliwa… lazima niondoke nayo!” Mzee Caleb akaweza msimamo.



    “Kwa nini uliwazika kwenye kaburi moja kwani………” kijana mmoja akajaribu kuuliza kabla ya mwenzake kumkatiza.



    “Mzee hatuna muda wa kufanya hayo… Hatujui ni umbali gani ambao tupo mpaka kuupata mpaka wa Anabelle… tunaweza kupoteza muda kufukua mizoga huku tukihatarisha usalama wetu.!” Kijana mwingine akadakia maongezi kwa ghadhabu.



    “Chunga kinywa chako kijana… usiite mwanangu na mkewangu kuwa ni mizoga… na si wao tu kuna lingine pia!” Mzee Caleb alifoka kwa hasira.



    “Lipi?” Karibia makomando wote waliuliza kwa pamoja kwa sura ya hamaki na hasira



    “Hatuwezi kuondoka bila huyu mnyama aliyepo kwenye basement!” Mzee Caleb akaweka msimamo mwingine kwa wenzake.



    “Mzee nadhani unamsikia huyo kiumbe anavyolia muda wote na umesema anahitaji damu… sitaki damu huyo aikamue kutoka shingozi mwangi… Kama unataka kubaki huo ni uamuzi wako lakini hatuwezi kuhatarisha uhai wetu kwa sababu ya vitu tusivyovielewa… twendeni.!” Kijana yule mwenye gadhabu na ushawishi kwa wenzake akaongea na kisha kuwaamuru wenzake waondoke.



    “Samahani sana mzee lakini hatuwezi kubaki.!” Kijana mmoja muungwana alimuomba radhi Mzee Caleb na kisha kutoka nje kwa haraka kufuata wenzake ambao tayari walishatimua mbio nje.







    Ndani ya kama sekunde thelathini tu Mzee Caleb alisikia nje magari yakiwashwa na kisha kutokomea.



    Alibakia amejishika kiuno asijue ni hata aanze na lipi. Kizee cha miaka themanini na mbili. Moja alikuwa anatakiwa kuhakikisha mnyama aliyepo chini kwenye basement anapata damu isiyopungia Lita moja. Kisha baada ya hapo anatakiwa kufukua kaburi lililoko nje lenye mabaki ya mkewe na mwanae. Kisha japokuwa hakuwa na usafiri wowote alitakiwa avibebe vyote na kutoka navyo nje ya mji huu wa Maryland. Na yote haya alikiwa anatakiwa ayatimize chini ya masaa sita. Kushindwa kufanya hivi ilimaanisha kwamba Mzee Caleb angepotelea ndani ya Anabelle na kutoonekana tena milele na milele.







    Japokuwa wale vijana makomando walikimbia ili kuokoa uhai wao, lakini walishindwa kutumia busara na kujua kwamba wanayemuacha nyuma ndiye tegemeo kuu la kuokoa ulimwengu kutoka kwenye hatari ya kutwaliwa. Lakini pia mwenzao mmoja aliuliza swali zuri ambalo hawakumpa nafasi Mzee Caleb kulijibu. “Kwa nini aliwazika mkewe na mwanae kwenye kaburi moja?”. Lakini pia swali lingine la msingi zaidi ambalo walipaswa kujiuliza ni kwa nini ilikuwa ni muhimu mno kwa Mzee Caleb kuchukuaabaki yao.



    Ulimwengu umezungukwa na siri kila mahala. Hakuna chochote ambacho kiko dhahiri na kina maana kwa namna ilivyo. Lakini mtihani mkubwa zaidi ni pale unapojua baadhi ya siri hizo, mara nyingi ni salama zaidi kubaki nazo moyoni.



    Mzee Caleb alitikisa kichwa na kukiri moyoni mwake, alifanya vyema kubaki na baadhi ya siri bila kuwaeleza Ethan, Naomi na wale vijana. Akachukua sululu na kutoka nje tayari kuanza kufukua kaburi lenye masalia ya mkewe na mwanae.



    Kiza liliongezeka zaidi. Yule mnyama kwenye basement alizidisha kupiga kelele. Baridi liliongezeka zaidi kuashiria muda unayoyoma Maryland kuwa Anabelle kamili. Mzee Caleb alikuwa kwenye mtihani mzito zaidi wa maisha yake.





    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE











    EPISODE 32











    SCARSDALE – NEW YORK, MAREKANI



    “Don sidhani kama ni sahihi kumuamini huyu mtu.!”



    “Hakuna haja ya kumuamini au kumtilia shaka… tumpe nafasi tu na kuona ukweli jinsi ulivyo.!”



    “Hapana… tatizo ni kwamba sitaki kumuhusisha Natalie na kitu chochote kuhusu David… unakumbuka namna ambavyo aliteseka miaka miwili tu iliyopita.!”



    “Latisha? Unaona hiki kinachotokea duniani? Vipi kama liko jambo ambalo tunaweza kufanya ili kusaidia?”



    “Sijui nisemeje Don?”



    “Latisha! Ninachosema ni kwamba tukunjue mioyo yote na kutoa nafasi… hiwezi jua… labda anachokisema ni kweli.!”







    Donald McLaren alikuwa jikoni akisemezana na mkewe Latisha. Walikuwa wamemuacha Rodney Van Der Berg sebuleni akiwa na mtoto wao Natalie wakiwasubiri waje na jibu la kukubali au kukataa ombi la Rodney Van Der Berg.



    Muda mchache uliopita Rodney au Ron kama ambavyo rafiki zake wanamuita, alikuwa amewasili akiwa ameongozana na Donald McLaren katika maeneo haya ya Scarsdale kwenye kaunti ya Westchester jimboni New York. Hapa ndipo ambapo Donald alikuwa anaishi na mkewe Latisha na mtoto wao Natalie ambaye baba yale halisi ni Makamu wa Rais David Logan ambaye alipeana talaka na Latisha miaka miwili iliyopita.



    Kabla hawajawasili hapa walikuwa wametokea ofisini kwa Ron hapa hapa New York mtaa wa Eckford eneo la Manhattan. Wakiwa ofisini, Ron alifanikiwa kumshawishi Donald kuhusu kuruhusu Natalie asaidie juhudi za baba yake mzazi David Logan kupatikana. Kwa mujibu wa Ron, alikuwa anaamini kuwa Makamu wa Rais David Logan alikuwa etekwa na jumuiya ya siri ya The 46 kwa kuwa yeye ndiye pekee ambaye alikuwa naijua siri ya namna gani ya kuwazuia The 46 wasiendelee na juhudi za kusaidia kufanya dunia itwaliwe na kugeuzwa kuwa Anabelle.



    Ron alikuwa anadai kwamba kuna uwezekano fulani kwamba kuna siri ambayo eidha David Logan alikuwa amemueleza Natalie bila Natalie mwenyewe kujua kwa kuwa labda alimueleza kwa dhahiri au kwa fumbo l. Au labda kuna namna ambayo David Logan lazima atajaribu kuifanya siri hiyo ijulikane kwa Natalie.



    Ron aliyaamini haya kwa sababu kwamba, alimueleza Donald kuwa kwa miaka yote ambayo amemfahamu Logan, tangu akiwa kwenye bunge la Senate alikuwa ni mtu ambaye siku zote ana mpango mbadala. Siku zote ana namna fulani ya kuhakikisha kuwa kama linatokea jambo la kumdhuru basi masuala yake yote muhimu yanajulikana kwa watu mahususi ambao watachukua kijiti cha kuyatimiza.



    Kwa hiyo katika hili kuhusu siri kuu hii ambayo Ron aliamini kabisa kwamba Logan aliijua na ilikuwa ina uwezo wa kuiokoa dunia, Ron aliamini kabisa David Logan lazima kuna namna atakuwa amefanya ili siri hii pia asife nayo yeye pekee na kama kuna mtu ambaye David Logan alikuwa na uwezo wa kumuambia siri kubwa kama hii basi ni mtu pekee ambaye anampenda kuliko kitu chochote juu ya uso wa dunia na anamuamini kwa asilimia zote, mtoto wake pekee Natalie.



    Baada ya kuzungumza sana kule ofisini kwa Ron na kufanikiwa kimlainisha moyo Donald, ndipo ambapo walisafiri mpaka mitaa hii ya Scarsdale hapo hapo New York ili kufika Nyumbani kwa Donald na mkewe Latisha ili ajaribu kumshawishi naye akubali mtoto wao Natalie atumike kusaidia juhudi hizo za kumpata Makamu wa Rais David Logan au kung’amua siri iliyomponza mpaka kutekwa na watu wa The 46.



    Baada ya Latisha kuambiwa suala hili, jambo la kwanza kabisa ambalo alilifanya alimuomba mumewe Donald wakazungumze chemba. Na ndipo hapa wako jikoni wanajadili huku Latisha akionyesha kila hoja ya kwa nini inamuwia vigumu kwake kumuamini Ron na kuruhusu mwanaye Natalie atumike kwenye juhudi hizo za kumsaka David Logan au kujua kile kilichomponza mpaka atekwe.



    Jambo la kwanza alidai kuwa ilikuwa haiingia akilini mwake mtu tajiri kama Ron na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Marekani atake msaada wa mtoto Mdogo kama Natalie. Alihisi kuwa kuna jambo lingine la zaidi lilikuwa limejificha nyuma ya pazia.



    Lakini Donald aliendelea kumshawishi kuwa wasimuhukumu Ron moja kwa moja yawezekana ni kweli alikuwa na nia ya kusaidia.



    Hoja kubwa ambayo alikuwa nayo Donald ilikuwa ni kile ambacho kilikuwa kinaendelea duniani kote, sio tu miji kutwaliwa bali tukio ambalo limetokea masaa machache yaliyopita… tukio la ulimwengu mzima kugubikwa na giza japo ilikuwa ni mchana bado. Japokuwa hawakuwa wanajua kuhusu masuala ya kafara iliyotolewa na The 46 kwa kumfufua tena shujaa wa kale, lakini kwa akili ya kawaida tu wakijumlisha na kasi mpya ya miji kutwaliwa funiani hii ilitoa kila dalili kwamba hatari ya ulimwengu wote kutwaliwa kwa pamoja ilikuwa njiani.



    Kwa hiyo Donald ilikuwa inamuwia vigumu kwake kuamini kwamba katika hali kama hii ya hatari ya dunia yote kutwaliwa kwa pamoja na kufanywa kuwa Anabelle, hakuhisi kama Ron anaweza kuwa mjinga wa kuendekeza tamaa zake za uroho wa utajiri na mambo yake binafsi. Aliamini kwamba hata Ron alikuwa na hofu ya kutwaliwa pamoja ndani ya Anabelle na kuwa mwisho wake na Mali zake na utajiri wake wote.



    Baada ya kupeana hoja nzito nzito chungu mzima pale jikoni walikosimama hatimaye Latisha akalainika na kukubali kumpa nafasi Ron ya kuonyesha uaminifu wake, kumtumia Natalie kuwasaidia kumtafuta David Logan au kung’amua siri ambayo Logan alikuwa anaijua.

    Licha ya kukubali suala hili lakini Latisha alimaliza maongezi yao kwa kumwambia mumewe Donald kwamba,



    “Sawa nimekubali Donald… lakini nina sharti moja tu kama wanataka Natalie awasaidie..!”



    “Sharti gani?”



    “Twende utaona.!!” Latisha aliongea huku anageuka na kuanza kutembea kuelekea sebuleni.



    Walipofika sebuleni walishangazwa kukuta Ron na vijana wake wanaomlinda wakiwa wanahaha kuhangaila kuongea na simu huku wakiwa na nyuso za taharuki.



    “Nini kinaendelea?” Donald aliuliza kwa mshangao.



    “Mambo yanazidi kuwa magumu.!” Ron alijibu huku mkono mmoja ameziba kwenye sehemu ya kuongelea na simu.



    “Kitu gani?” Donald akauliza huku bado akiwa kwenye taharuki kubwa.



    Ron alifumba macho kwa uchungu na kuangalia juu akiwa anamalizia kuongea na simu. Jambo ambalo alikuwa ameelezwa kwenye simu lilionekana kumchoma moyo haswa. Akakata simu na kuiweka mezani.



    Nini kinaendelea?” Latisha naye akauliza kwa taharuki kama mumewe.



    “Nadhani hata hili zoezi letu la kumtafuta David Logan litakuwa gumu zaidi sasa au lisiwezekane kabisa.!” Ron aliongea kwa hasira iliyochanganyika na kukata tamaa huku anakaa chini kwenye sofa.



    “Ron! Nini kinaendelea?” Donald akauliza kwa ukali safari hii.



    “Rais amehuisha THE MARSHALL LAW.!!” Ron aliongea huku amejiinamia na kufumba mamcho kwa uchungu.







    Donald, mkewe Latisha na wote ambao walikuwepo pale sebuleni walijikuta wameganda ghafla kwa bumbuwazi kama vile wamemwagiwa maji ya baridi.



    The Marshall Law?? Inawezekanaje??



    Hilo ndilo swali ambalo kila mmoja alikuwa anajiuliza kichwani.



    Na kwa kuwa suala la Madam President Laura Keith kupatikana lilikuwa halijawekwa hadharani walikuwa wanashangaa zaidi inawezekaje hata serikali ihuishe Marshall Law??



    Hii ilikuwa na maana kwamba kuanzia muda huo, kwa mujibu wa katiba ya Marekani… baada tu ya Rais kuhuisha Marshall Law basi jeshi linashika hatamu. Nchi nzima inakuwa chini ya jeshi na amri ya jeshi huku Rais akiwa kama amiri jeshi mkuu. Hakuna raia yeyote ambaye anaruhusiwa kuonekana mtaani au kutoka nje ya nyumba yake.



    Walizoea kusoma masula ya Marshall Law kwenye vitabu vya historia tu kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe namna ambavyo Rais alihuisha Marshall Law ili kuituliza nchi. Lakini leo hii, kwenye kizazi hiki… zaidi ya miaka mia mbili baadae wanashuhudia kwa macho yao kifungu hiki katili cha katiba kikihuishwa.







    Lakini kwa namna yoyote ile kama wanataka waje kuliona tena jua likichomoza wanapaswa kumsaka na kumpata Makamu wa Rais David Logan au kung’amua siri iliyomfanya atekwe.!



    Lakini wakikanyaga tu mguu nje ya nyumba yao, kutokana na rais wa nchi kuhuisha Marshall Law, wanajeshi walikuwa wanaruhusiwa kuwatandika risasi.



    Japokuwa raia wengi wangeliona hii kama juhudi ya serikali kufanya nchi isiingie kwenye taharuki kutokana na tukio la kushangaza la mchana kugubikwa na kiza totoro na kasi ya utwaliwaji miji kuongezeka… lakini Ron moyoni mwake alihisi kabisa kulikuwa juhudi za kusudi kabisa za kuzuia juhudi zozote za kutaka kuutetea ulimwengu usigeuzwe Anabelle. Alijua kitu ambacho wengi hawakukijua. Na cha muhimu zaidi alimjua baba mzazi wa Madam President Laura Keith.





    THE OTHER HALF







    SEASON 1 – THE LEGEND OF ANABELLE







    Ulimwengu unahitaji shujaa mmoja tu. Shujaa mmoja tu anayeweza kuubeba mabegani na kuupeleka hatua inayofuata.



    Kwa miaka maelfu ambayo mwanadamu amekaa juu ya uso wa dunia ni kitu kimoja tu ambacho amekifanya kwa ufanisi. Uharibifu.

    Uharibifu wa kila alichokikuta. Uharibifu wa kila uzuri ambao uliupamba dunia. Uharibifu wa kila lililo jema. Uharibifu. Ndicho pekee ambacho binadamu amekifanya kwa ufanisi.

    Kila mwanadamu ambaye anaishi katika kizazi tulichopo ndani yake amerithi mbegu hii ya uharibifu na ndiyo anasa tunayopambana kuwa nayo.



    Ulimwengu unahitaji shujaa mmoja tu. Shujaa mmoja wa kuubeba ulimwengu na kuuvusha hatua inayofuata.



    Lakini tunafahamu gharama ya hatua hii? Tunafahamu ni nini tutakutana nacho tukifika hatua inayofuata? Tunajua ni nini kesho inahitaji kutoka leo yetu? Tunafahamu shujaa wa kutuvusha hatua hiyo?



    Pengine namna pekee ya kuuzusha ulimwengu ni kuuacha utwaliwe… pengine namna pekee ni kuacha ugeuzwe kuwa Anabelle! Pengine mwaka 2038 ndio siku ya kwanza ya kesho tunayoisubiri. Pengine watoto wa Maldives ndio kichocheo cha kuuvusha Ulimwengu wetu!







    Lakini bado… bado tunahitaji shujaa mmoja wa kutuongoza katika hatua inayofuata… iko siku tutalala na kuamka na kukuta ulimwengu wetu hauko namna ambayo tunafahamu na kuizoea.



    Tunafahamu ni nini kesho inahitaji kutoka kwetu??







    EPISODE 33















    NDANI YA ANABELLE 27 (ULIOKUWA MJI WA DAR ES SALAAM)







    Japokuwa alikuwa amechoka mno lakini Salim alijikaza na kujitutumua vivyo hivyo kumbeba Cindy begani mwake. Cindy alikuwa ametulia kimya kabisa kama vile hana ufahamu. Kama vile mwili wake hauna uhai tena, lakini kilichokuwa kinampa moyo Salim ilikuwa ni mapigo ya moyo kwa mbali ambayo alikuwa anayasikia kila akiweka mkono wake juu ya kifua cha Cindy na kila alipokiwa akimgusa mshipa wa damu shingoni.



    Walikuwa tayari wamefika kwenye eneo ambalo masaa kadhaa yaliyopita walikuwa wamewaacha Magdalena na Shafii, sehemu ambayo waligundua mlango wa The 46 na kushindwa kuufungua.



    Wenzao ambao waliwaacha hapa, Shafii na Magdalena walikuwa wamelala kwenye eneo karibu kabisa na ule mlango ardhini wakiwa hawajitambui kabisa. Kutokana na namna ambavyo walikuwa wamelala Salim aliamini kabisa baridi kali ambalo lilikuwa limewakumba liliwafanya watambae mpaka ulipo mlango ule ili labda waufungue na kuingi ili kiokoa maisha yao kutoka kwenye baridi lilipo ndani ya Anabelle lakini walishindwa kuufungua na kujikuta wakipoteza fahamu.



    Salim alimshusha Cindy kutoka begani kwake na kumlaza pembeni mwa walipolala wenzao Magdalena na Cindy. Licha ya yeye kuwa ndiye pekee ambaye alikuwa na ufahamu lakini naye alikuwa hoi kweli kweli… alikuwa anahema juu juu kama vile pumzi ilikuwa inataka kumtoka muda wowote ule.



    Akamgusa mshipa wa damu shingoni Magdalena… alisikia kwa mbali sana damu ikisukumwa na kutembea. Akageuka na kumshika mshipa wa damu Shafii… hakukuwa na ‘pulse’. Hakusikia damu ikitembea wala dakili ya moyo kupiga. Shafii hakuwa hai tena.

    Kwa hali ambayo walikuwa nayo ilikiwa ni suala la muda tu kabla ya wao nao kupoteza maisha, kwa hiyo Salim hakuwa na muda wa kupoteza kuomboleza japokuwa alisikia majonzi haswa moyoni mwake.



    Cindy ambaye walikuwa wanamtegemea awape muongozo hakuwa na fahamu ili aweze kumuongoza nini cha kufanya. Lakini Salim alikumbuka kauli ya Cindy tangu walipokanyaga tu ndani ya Anabelle, kwamba jambo la muhimu zaidi ambalo walikuwa wanatakiwa kulifanya humu ni kutafuta malango wa The 46. Na mlango waliusaka mpaka waliupata lakini walishindwa kuufungua kutokana na kutokuwa na “combination” ya herufi au namna za siri ambazo walikuwa wanatakiwa kuwanazo. Na ndipo ambao masaa machache yaliyopita waliondoka kutoka hapa yeye na Cindy kwenda kutafuta msaada kutoka duniani na kuwaacha hapa Shafii na Magdalena.



    Salim akachukua chupa ambayo waliweka ujumbe yeye na Cindy masaa kadhaa yaliyopita na kisha baadae wakakuta majibu kutoka duniani… akaichukua na kutoa tena karatasi ambayo ilikuwa ndani yake na kisha kuisoma tena,







    “HATUJUI KAMA BADO MKO HAI AMA LA… UMEPITA MWEZI MMOJA SASA TANGU MUINGIE NDANI YA ANABELLE 27. KAMA BADO MKO HAI HAYA NI MAJIBU YA MLICHOULIZA. DETAIL #127 NI 6, 2, 1, 9. PIA TUNAWASISITIZA MLINDE MLICHOKIPATA KUHUSU MADAM PRESIDENT KULIKO CHOCHOTE KILE. X3. X3. X3.”







    Japokuwa Salim hakuelewa maana kamili ya ujumbe huu ni nini lakini alikumbuaka tena mara ya kwanza walipofika hapa kwenye huu mlango na kushindwa kuufungua Cindy aliwaeleza kwamba wanahitaji detail namba 127 kutoka kwenye mchoro wa George Washington ili waweze kuufungua. Kwa hiyo kwa asilimia zote aliamini kwamba kile ambacho kimeandikwa kwenye ujumbe wa karatasi kwenye chupa kama detail #127, yaani namba 6, 2, 1 na 9 ndio detail namba 127 waliyokuwa wanahitaji kufungulia mlango huu ardhini.



    Jambo ambalo kilikuwa linamsumbua kichwani Salim ni kutokujua wakiufungua mlango huo ni nini hasa ambacho walikuwa wanatakiwa kukifanya. Hakuna muda ambao alikuwa anatamani Cindy angelikuwa na ufahamu kama sasa.



    Akageuka tena na kuwagusa wenzake wote mishipa ya damu shingoni na kusikiliza mapigo yao ya moyo… Cindy na Magdalena walikuwa na wako hai japo mapigo yao ya moyo yalisikika kwa mbali sana. Shafii hakukuwa na ubishi kwamba ni hakika alikuwa amekufa tayari na muda si mrefu yeye na wenzake wanaweza kujikuta katika hali hiyo ya kifo. Kwa kiasi fulani japo alikuwa anaweza kufikiri sawa sawa lakini alikuwa kama nusu hivi hajitambui. Alikuwa kana kwamba amelewa hivi. Alikuwa anahema juu juu kwa shida sana.



    Salim akageuka na kuangalia ule mlango ardhini na kuyasoma maandishi ya kilatini yaliyopo juu yake,



    “QUADRAGINTA SEX”







    (THE FORTY SIX)







    Ulikuwa mfuniko mkubwa wa duara wa ukubwa wa kipenyo kama mita mbili hivi. Kwa muonekano tu ulionekana dhahiri kwamba umetengenezwa kwa chuma kigumu thabiti na kizito mno. Katikati ya ule mfuniko kulikuwa na dura lingine dogo la kipenyo cha kama mita moja hivi. Duara hili dogo la katikati lilikuwa na nakshi lililofanya lionekane kama vile ni saa ya ukutani, au kwa ligha nyingine kwa kutazama haraka tu mtu angeweza kusema mfuniko huu mkubwa ardhini ulikuwa na saa ndogo katikati. Sio ndogo kwa kulinganisha na saa za kawaida ilikuwa ni ndogo kwa kuzingatia ukubwa wa mfuniko wenyewe mkubwa wa kipenyo cha mita mbili au mbilo na nusu lakini duara hili dogo la katikati la saa nalo lilikuwa kubwa wastani kutokana na kipenyo chake cha karibia mita moja.



    Nakshi ambazo zilikuwa zinafanya lile duara dogo katikati kuonekana kama saa zilikuwa ni herufi za kirumi pembezoni mwake ambazo zilipangiliwa sawa sawa kabisa na namna ambavyo zibaoangiliwa kwenye saa ya ukutani,



    I, II, III, IV, V, VI, VII, VII, IX, X, XI, XII



    Pia duara hili katikati nalo lilikuwa na mshale wa kufanana kabisa na mshale wa saa lakini tofauti tu ni kwamba wenyewe ulikuwa ni mshale mmoja tu peke yake. Mshale muda huu ulikuwa umeguzwa kuonyesha XII.



    Salim akisimama akiwa anakodolea macho mfuniko huu pale ardhini kwa karibia dakika nzima. Kichwani akikuwa anawaza ni namna gani alikuwa anatakiwa kuufungua mlango huu hapa ardhini kwa kutumia yale maelezo kutola duniani.



    Detail namna 127 tayari walikuwa nayo ambayo waliambiwa ni 6, 2, 1, 7. Lakini kitendawili kilikuja ni namna gani ambavyo walitakiwa kuzitumia ili kufungua mlango.



    Pembezoni mwa huu mfuniko kulikuwa na kama mshikio hivi. Kwa mara ya kwanza baada ya kuukodolea macho kwa muda mrefu Salim aliugusa mfuniko kwa kukanyaga katikati yake kwa miguu miwili na kisha kutembea mpaka upande wa pili ambako kulikuwa na ule mshikio pembezoni.



    Akainama na kujaribu kuinua mfuniko huu kwa kuvuta kwenda juu kutumia ule mshikio. Alivuta kwa nguvu zake zote lakini mfuniko hakutikisika hata chembe. Alikaa chini anahema kutokana na kutumia nguvu nyingi kunyanyua mfuniko ilhali alikuwa muda wote anahema juu juu kwa shida.



    Akiwa amekaa chini pale pale ghafla akasilia sauti ya ajabu kwa mbali sana inaunguruma.



    “Aaaaawwwwoooooohhhhh”



    Ulikuwa ni kama mlio wa fisi mwenye hasira lakini wenyewe ulikuwa ni wa sauti nzito zaidi. Ulilia mara moja tu na kisha hakuusikia tena. Salim akapepesa macho huku na huko lakini hakuona chochote wala mjongeo wa kiumbe. Akasimama tena nabkuanza kufikiri. Ni namna gani atumie yale maelezo kutoka duniani kufungua huu mlango ardhini.



    Akasimama na kuukodolea mlango macho kwa karibia dakika mbili nzima. Mwishoni wazo kikamjia kichwani. Labda mlango huu unafunguliwa kama namna ambavyo “safe” huwa zinafunguliwa duniani. Safe zenyewe zinafunguliwa kwa kuzungusha kishikio cha duara kufuata namba za “combination” moja baada ya nyingine. Akahisi labda ajaribu hivyo.



    Ghafla kabla hajainama kujaribu alichokuwa anakifiria akasikia tena ile sauti ya muungurumo,







    “Aaaaaaawwwwoooooohhhhh”







    Safari hii ilikuwa na kishindo zaidi, na ilionekana kuwa karibu zaidi. Pia sasa hivi sauti hiyo ilionekana ilitolewa na kiumbe zaidi ya mmoja. Labda wawili au watatu. Salim akapapasa tena macho huku na huko lakini hakuona kitu.



    Akakanyaga juu ule mfuniko lakini pembezoni mwake bila kukanyaga lile duara la katikati lenye saa. Akasoma tena yale maelezo waliyoyapata kutoka duniani,



    “HATUJUI KAMA BADO MKO HAI AMA LA… UMEPITA MWEZI MMOJA SASA TANGU MUINGIE NDANI YA ANABELLE 27. KAMA BADO MKO HAI HAYA NI MAJIBU YA MLICHOULIZA. DETAIL #127 NI 6, 2, 1, 9. PIA TUNAWASISITIZA MLINDE MLICHOKIPATA KUHUSU MADAM PRESIDENT KULIKO CHOCHOTE KILE. X3. X3. X3.”







    Alichokuwa anataka kujikumbusha ni detail namba 127 ya mchoro wa George Washington, yaani namba 6, 2, 1, 9.



    Akapiga magoti na kisha kunyoosha mkono kuelekea kwenye lile duara katikati la saa. Akahamisha mshale kutoka pale ulipo kwenye XII na kwenda VI (6).



    Alipohamisha tu, ghafla akasikia tena ule mlio wa kishindo ukilia tena.



     http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Aaaaaaawwwwooooohhhhhh”







    Sauti kali kama ya fisi mwenye hasira kali lakini ikiwa na uzito zaidi. Na sasa ilikuwa karibu zaidi kuliko alivyoisikia mara ya mwisho na safari hii aling’amua dhahiri kabisa kwamba sauti hiyo ilitoka kwa viumbe zaidi ya wawili au watatu, kwa kuisikiliza tu ilionekana ilitoka kwenye kundi la viumbe si chini ya kumi walio pamoja. Akapepesa tena macho kila upande lakini hakuona kitu.



    Akarejesha macho yake pale kwenye duara la saa kwenye mfuniko. Alikuwa anabadili uelekeo wa mshale kwa kufuata mtiririko wa namba ambazo walikuwa wamepewa kwenye ule ujumbe kutoka duniani, yaani 6, 2, 1, 9.

    Kwa hiyo safari hii akahamisha mshale kutoka kwenye VI kwenda kwenye II (2).



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog