Simulizi : Mifupa 206
Sehemu Ya Nne (4)
“Kama ungekuwa umewahi kuniomba ushauri huwenda ningekushauri usiingie
humu ndani lakini kwa sasa nafasi hiyo huna. Huu ni mtandao mkubwa sana usioweza
kuvunjwa kwa urahisi na hivyo vijiharakati vyenu”
“Mbona unaongea kama mwoga?”
“Najua anazungumza hivyo kwa kuwa hufahamu uzito wa maneno yako ya ovyo”
Oga akafoka kwa dhihaka.
“Mbona hujaniambia kuwa mtandao wenu unahusika na nini?”
“Shut up your mouth you bastard!” Oga akafoka hata hivyo nilimpuuza na kuendelea
na maswali yangu.
“Mtandao wenu unajumuisha na viongozi wa serikali?”
“Muda wa maswali umekwisha” Oga akaniambia huku akisogeza kochi nyuma na
kusimama na nilipomchunguza nikamuona akiwa ameshika bastola yenye kiwambo
cha kuzuia sauti mkononi.
“Mbona hutaki kujibu maswali yangu. Kwani mtandao wenu unashughulika na
nini na kiongozi wenu ni nani?” nikamuuliza Oga lakini hakunijibu na badala yake
haraka nikamuona akiielekeza bastola yake kwangu. Risasi mbili alizozifyatua moja
ikachana lile kochi nililolikalia huku mimi nikiwahi kuruka pembeni. Risasi nyingine
ikachimba sakafu na hapo nikajua kuwa kweli Oga alikuwa amedhamiria kuniua.
Oga akaendelea kufyatua risasi ovyo mle ndani akinilenga lakini nilikuwa
mwepesi wa kujirusha upande huu na ule na hapo risasi moja ikanipunyua begani.
Hatari ikaanza kunikaribia kwani kila nilipojaribu kumkaribia Oga alinikwepa na
kurudi nyuma. Nilipoona hatari inazidi kunikaribia nikainua kitanda cha mle ndani
ili kujikinga na mashambulizi yale. Niliendelea kukitumia kile kitanda kuzikwepa zile
risasi na nilipopata upenyo mzuri nikajirusha upande wa pili sehemu aliposimama Oga
na kufumba na kufumbua nikawa nimefanikiwa kumfikia Oga na kumtundika kabari
matata isiyompa nafasi ya kufurukuta. Mshikemshike ule ukatupelekea tujibwage juu
ya ile meza ya kioo iliyokuwa mle ndani. Ile meza ikavunjika vipandevipande na vioo
vyake kutuchana hata hivyo kabari yangu matata haikutoka kwenye shingo ya Oga.
Tukiwa pale chini tukaendelea kugaragazana. Oga alikuwa akipigania kuichomoa
ile kibari yangu matata niliyomtundika shingoni huku akitafuta mhimili mzuri wa
kunishindilia risasi na mimi nikajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa hapati nafasi
ya kufurukuta.
Kile kitanda kilikuwa kimeangukia pembeni kikichanguka ovyo. Zile purukushani
zikaendelea pale chini na kwa kweli pale ndiyo nilipojua kuwa Oga hakuwa mwanamke
wa kuchezea kwani alikuwa na nguvu mno na maarifa ya mapigano. Katika
purukushani zile nikafanikiwa kumtandika Oga ngumi mbili za bega la ule mkono
wake ulioshika bastola. Ule mkono ukashikwa na ganzi,vidole vyake vikafunguka na
ile bastola yake ikaanguka chini na hapo nikaipiga teke na kuitupilia mbali.
Kwa kujibu mapigo Oga akanipiga kiwiko cha nguvu cha tumbo na hapo nikasikia
kichefuchefu cha ghafla huku maumivu makali yasiyo na mfano yakisambaa mwilini.
Hali ile ikanipelekea nishindwe kumdhibiti Oga vizuri hata hivyo sikumuachia. Oga
alipoona kuwa sitaki kumauchia akaanza kunikwaruza usoni kwa kucha zake ndefu na
kali. Nikawa nikiukwepesha uso wangu huku na kule bila kumuachia lakini hatimaye
alinizidi ujanja kwani mikono yake ilikuwa mirefu sana kuweza kuufikia uso wangu
bila kikwazo na hivyo zile kucha zake ndefu kunikwaruza vibaya.
Hali ile ikanipelekea niiachie ile kabari bila kupenda na hilo likawa kosa kubwa
kwani Oga akanitandika teke la nguvu la korodani. Kwa kweli nilisikia maumivu
makali yaliyonipelekea nigande kama sanamu.
Hasira za kudhihakiwa zikanivaa na hapo nikajibetua nyuma na kusimama.
Mapigo ya Oga mawili ya karate yaliponijia shingoni nikayakinga katika namna ya
kuyapunguza nguvu kisha kwa nguvu zangu zote nikapeleka ngumi moja matata na
kuuvunja mwamba wa pua yake na hapo Oga akapepesuka na kupoteza mhimili.
Sikusubiri Oga atulie hivyo nikamuwahi kwa mapigo mengine yenye malengo ya
kulitia udhaifu tumbo lake hata hivyo Oga alikuwa makini sana kuyapangua mapigo
yale kama mchezo na kunikwepa.
Nguvu nyingi nilizowekeza kwenye mapigo yale na kumkosa Oga zikanipelekea
nipepesuke kama mlevi nikikosa mhimili makini. Oga kuona vile akaruka round kick
na kunishindilia pigo jingine la teke mgongoni lililonipelekea nijibamize ukutani bila
kupenda. Hakika Oga alikuwa mpambanaji matata mwenye mwili wa kike lakini nguvu
za kiume na bila shaka alikuwa tayari kupambana na mimi mpaka tone la mwisho la
damu yake. Maumivu makali yakasambaa mgongoni mwangu.
Pigo jingine la teke lilipokuja nikawahi kuliona hivyo nikainama chini kidogo na
kulikwepa na hapo pigo lile likakata upepo bila mafanikio. Kuona vile jitahada zangu
nikazielekeza kwenye ule mguu wake mmoja sakafuni. Nikajipinda na kumchota Oga
mtama wa nguvu hewani na huwenda tukio lile lilimtia hofu kwani alipiga yowe kama
mtoto. Nikamsubiri atue lakini hayakuwa mahesabu mazuri kwani Oga alitua chini
kama paka kwa miguu yake miwili na mkono mmoja sakafuni huku akinitazama kwa
hasira.
Nilipomuwahi Oga pale chini ili nimmalize akawa ameishtukia dhamira yangu
hivyo akaanza kujiviringisha kama gurudumu la gari akienda huku na kule katika
mtindo wa Ninja. Sasa Oga akawa akinishambulia kwa hila. Akawa akinifikia haraka
na kunishambulia na kabla sijakabiliana naye vizuri anakuwa tayari ameshafika upande
wa pili wa kile chumba. Hali ile ikanipelekea nianze kuona hatari ya kupoteza pambano
lile.
Wakati nikiendelea kujihami mara wazo fulani likanijia. Sikutaka kuendelea
kuruhusu mashambulizi ya namna ile hivyo wakati Oga akinijia tena kwa kasi ya
ajabu nikalivuta shuka la kitanda cha mle ndani kisha kwa mtindo mzuri wa sarakasi
nikamrukia Oga na kumvalisha lile shuka usoni. Lilikuwa shambulizi makini la hila
lililompelekea Oga asiweze kuona na badala yake nguvu zake zote akazielekeza katika
kuliondoa lile shuka.
Oga hakufanikiwa kwani Kufumba na kufumbua akaanguka chini na hapo
mapigo matatu makini ya ngumi zangu kavu yakavunja taya lake la kushoto na
kulipasua vibaya koromeo lake na hapo Oga akapiga yowe kali huku damu nyingi
ikianza kumtoka puani na mdomoni. Nilitulia kidogo kumsubiri Oga afurukute na
nilipomuona kuwa ametulia nikalifungua lile shuka na kumtazama. Oga alikuwa tayari
wa baridi kifo kikiwa tayari kimemchukua.
Sikutaka kuendelea kupoteza muda mle ndani hivyo nikaanza kuitafuta ile bastola
yangu na nilipoipata nikaishindilia ile magazine na kuichomeka kibindoni. Halafu
nikaiokota ile bastola ya Oga na kuikamata vyema mkononi. Wakati nikiwa katika
harakati zile mara nikasikia ule mlango wa kile chumba ikigongwa kwa nje. Niliyatega
vizuri masikio yangu kusikiliza na hapo nikawa na hakika kuwa nje ya chumba kile
mlangoni kulikuwa na mtu akigonga. Mgongaji yule alikuwa makini akigonga kwa
muda na kusikilizia na alipoona kuwa hajibiwi akafungua ule mlango taratibu huku
ameitanguliza mbele bastola yake.
Niliwahi kuuona mdomo wa bastola ile ukichungulia kwani wakati ule nilikuwa
tayari nimeshajibanza nyuma ya ule mlango wa kile chumba. Nikamsubiri yule mtu
aingie mle ndani vizuri na hapo nikaubetua ule mkono wake kwa teke langu makini na
kuipelekea ile bastola imponyoke na kuruka hewani na ilipotua chini ilikuwa mikononi
mwangu.
“Tulia hivyohivyo ngedere mkubwa weh! na ukijitingisha tu nakufyeka”
nikamwambia yule mtu huku nikiufungua vizuri ule mlango wa kile chumba. Yule
mtu akataharuki sana akishangazwa na jinsi mambo yalivyotokea mle ndani huku
akishangazwa na ile maiti ya Oga pale sakafuni. Nilipomchunguza vizuri yule mtu
nikamkumbuka kuwa alikuwa ni mmoja wa wale mabaunsa walinzi wa kule Vampire
Casino walionizuia siku ile wakati nilipotaka kuingia mle ndani bila kitambulisho cha
mwanachama.
“Sogea mbele na mikono yako weka juu” nikamwambia yule mlinzi huku mdomo
wa bastola yangu mkononi ukimtazama kwa uchu. Yule mtu hakuwa na ujanja
isipokuwa kutii maagizo yangu. Hivyo akasogea mbele huku mikono yake ameiweka
juu.
“Wewe ni nani?” nikamuuliza yule mtu nikitaka kupata hakika ya maelezo yake
“Naitwa Beka Mandevu au Mbavu nene!” yule mtu akaniambia kwa woga na
nilipomchunguza nikajua kuwa jina lake bilashaka lilitokana na ukubwa wa misuli ya
umbo lake na ndevu nyingi alizokuwa nazo.
“Unafanya nini humu ndani?” nikamuuliza kwa utulivu.
“Mimi ni mlinzi tu” yule mtu akanijibu kwa hofu.
“Unalinda nini humu ndani?”
“Usalama wa watu na mali zao”
“Yule msichana aliyelala pale chini unamfahamu?” nikamuuliza yule mtu huku
nikimuonesha ile maiti ya Oga kwa bastola yangu pale chini. Yule mtu akanitazama na
kusita lakini aliponiona nikianza kumsogelea akavunja ukimya.
“Ndiyo namfahamu!”
“Unamfahamu kama nani?”
“Malkia wa humu ndani” maelezo yale yakanipelekea nimtazame yule mtu na
kumuona kama mtu aliyechanganyikiwa kwani tangu nizaliwe sikuwahi kusikia
utawala wa malkia katika nchi ya Tanzania.
“Humu ndani mnashughulika na nini?’’ nikamuuliza yule mtu huku nikimtazama
“Mimi sijui chochote,kazi yangu ni ulinzi tu’’ yule mtu akajitetea
“Nahitaji kuonana na Milla Cash ni wapi nitampata humu ndani?’’ swali langu
likampelekea yule mtu ageuke na kunitazama kwa mshangao sana kama niliyeuliza
swali lisilowezekana kuulizika.
“Milla Cash…!’’ yule mtu akaongea kama anayefikiri jambo kisha akaendelea
“Hakuna mtu yoyote humu ndani anayefahamu ni wapi anapoishi Milla Cash
isipokuwa Oga tu ambaye ndiye malkia wa humu ndani” yule mtu akaongea kwa
utulivu na maneno yake yalikuwa na hakika.
“Unaposema malkia wa humu ndani una maanisha nini?”
“Ndiye mwangalizi mkuu wa shughuli zote za humu ndani” yule mtu akaniambia
huku akiongea kwa woga.
“Na wale watu kule ukumbini wanafanya nini?” nikamuuliza yule mtu na mara hii
nilipomtazama shingoni nikaiona ile tatoo ya namba 666. Swali langu likampelekea yule
mtu anitazame tena kwa mshangao.
“Wako kwenye ibada” yule mtu akavunja ukimya na hapo nikaupisha utulivu
kichwani mwangu nikitafakari juu ya hiyo ibada kwani matendo ya mle ndani yalikuwa
yamenichanganya sana.
“Ibada ya namna gani?” nikamuuliza yule mtu hata hivyo hakunijibu na badala
yake akanitazama tu pasipo kusema kitu.
“Na wale watu waliovaa makoti meupe mle vyumbani wanafanya nini?”
“Sifahamu” yule mtu akanijibu kwa mkato
“Na wale mabinti vigoli kule vyumbani je?”
“Sijui chochote mimi ni mlinzi tu humu ndani” yule mtu akajitetea huku
akionekana dhahiri kutaka kunificha mambo fulani yaliyokuwa yakiendelea mle ndani.
“Sasa kama hufahamu kinachoendelea humu ndani unalinda nini?” nikamuuliza
yule mtu kwa hasira hata hivyo hakunijibu.
“Hili jengo linamilikiwa na nani?” nikamuuliza tena.
“Mimi sifahamu chochote!”
Ghafla wakati nikiendelea kumuhoji yule mtu mara mlango wa kile chumba
ukafunguliwa kwa kasi ya ajabu nami sikutaka kusubiri kwani nilifahamu nini ambacho
kingefuatia. Hivyo kufumba na kufumbua yule baunsa akawa ameenea vizuri kwenye
kabari yangu makini ya mkono wa kushoto huku mkono wangu wa kulia ukiwa
umeielekeza ile bastola kichwani kwake. Yule mtu kuona vile akashikwa kwa kihoro
na kuanza kuongea maneno mengi ya hofu huku akinisihi nimuachie.
Mle ndani wakaingia watu wawili warefu walionyoa vipara huku wamevaa suti
nyeusi na miwani myeusi machoni. Nilipowatazama vizuri wale watu nikagundua
kuwa masikioni mwao walikuwa wamevaa vifaa vya mawasiliano vyenye nyaya nyeusi
zilizojisokota na kupotelea kwenye kingo za makoti yao ya suti. Mmoja kati ya wale
watu nilimkumbuka haraka kuwa alikuwa miongoni mwa wale watu waliopata ajali
muda mfupi uliyopita kwenye ile Landcruiser ambaye kwa wakati ule alikuwa ndiye
pekee aliyekuwa na fahamu kabla ya kupoteza fahamu wakati nilipomnasa makofi ya
nguvu usoni.
Yule mtu sasa alikuwa akichechemea kwa mguu mmoja na hapo nikakumbuka
kuwa ulikuwa ni ule mguu wake uliyobanwa wakati wa ile ajali. Wale watu wote
mikononi walikuwa wameshika bastola ambazo haraka waliwahi kuzielekezea kwangu.
“Tupa bastola yako chini na usithubutu kufanya hila yoyote” mmoja kati ya wale
watu walioingia mle ndani kwa pupa akanionya na nilipomtazama nikagundua kuwa
alikuwa akinipigia mahesabu ya kuniondoa kwa risasi. Kwa kuishtukia hila yake yule
baunsa nikamsogeza mbele yangu vizuri na kumfanya kama ngao yangu.
“Nyinyi ndiyo ambao mtaziweka bastola zenu chini vinginevyo mtamponza huyu
ndugu yenu kama mwenzake yule pale chini aliyejidai mkaidi” nikawatahadharisha
wale watu kwa bastola yangu mkononi huku nikiwaelekeza pale chini ilipokuwa
imelala maiti ya Oga. Wale watu wakageuka na kutazama upande ule ilipolala maiti
ya Oga hata hivyo hawakuziondoa bastola zao kwangu. Walipoiona ile maiti ya Oga
wakaingiwa na taharuki.
“Nahesabu mpaka tatu nikimaliza kama bado mtakuwa mkiendelea na msimamo
wenu msije mkanilaumu” nikawatahadharisha wale watu kisha nikaanza kuhesabu.
Kuona vile kabla sijamaliza kuhesabu wale watu wakasalimu amri haraka na kuziweka
bastola zao chini.
“Very good! kwa kufanya uamuzi wa busara kwani nilidhani mngekaidi ili
mjithibitishie wenyewe ukweli wa maneno yangu. Haya rudia nyuma na kuanzia
sasa nyinyi ndiyo mtaongoza mbele tukielekea nje ya hili jengo. Nawatahadharisha
kuwa msijaribu kuleta hila yoyote kwani sitowavumilia” nikawaambia wale watu kwa
msisitizo na hawakuwa na namna zaidi ya kutii amri yangu. Hivyo wale watu wakageuka
nyuma na hapo safari ya kutoka mle ndani ikaanza huku nikiwa nimemdhibiti vilivyo
yule baunsa kwa kabari yangu matata na bastola mkononi.
Tulitembea taratibu na kwa tahadhari hadi pale tulipozifikia zile bastola mbili
za wale watu ambapo niliinama na kuziokota. Baada ya pale safari yetu ikaendelea
tena huku wale jamaa waliovaa suti wakiongoza msafara mbele yetu. Muda mfupi
uliyofuata tukawa tumetoka nje ya kile chumba na hapo tukashika uelekeo wa kurudi
kule tulikotoka na Oga hapo awali.
Tuliivuka korido ya kwanza kisha tukakunja kona na kuingia korido ya pili ambayo
kwa kumbukumbu zangu korido ile ingetupeleka hadi kwenye ule ukumbi niliyowaona
wale watu wakiwa wameketi kwenye vile viti wakimsikiliza mtoa mada mbele yao.
Kitu kilichonishangaza ni kuwa zile kelele za vilio vya watoto wachanga na
vicheko vya wanawake sikuzisikia tena wakati tulipokuwa tukitembea kwenye zile
korido za mle ndani. Wakati huu lile jengo lilikuwa limemezwa na ukimya wa aina
yake na hata tulipofika kwenye ule ukumbi wale watu niliyowaona pale awali wakati
huu hawakuwepo eneo lile. Jambo lile likanishangaza sana hata hivyo sikuwa na mtu
wa kumuuliza.
Hatimaye tukawa tumezifikia zile ngazi za kushukia mle ukumbini na kuanza
kuzipanda huku wale watu wakiwa wameongoza mbele yetu. Baada ya muda mfupi
mara tukawa tumefika juu ya zile ngazi ambapo mbele yake kulikuwa na ule mlango
wa kuingia kwenye kile chumba chenye michoro ya ajabu. Kufikia pale nikawaona
wale jamaa wakisita kuufungua ule mlango na kwa ishara fulani walizopeana kwa siri
nikajua kuwa walikuwa wamepanga kufanya hila dhidi yangu.
Wakati nikitafakari hali ile mara nikamuona yule mtu aliyekuwa akitembea kwa
kuchechemea mbele yangu akiupeleka mkono wake haraka kwenye mfuko wa koti
lake la suti. Nikajua alikuwa akiichukua bastola yake ya ziada ambayo hapo mwanzo
sikuwa nimeshtukia kama alikuwa nayo. Hata hivyo hakupata nafasi ya kuitumia
kwani alipoitoa tu nikamuwahi. Risasi moja niliyoifyatua kwa shabaha ya hali ya juu
ikakifyeka kiganja chake na ile bastola yake ikamponyoka na kuangukia kwenye uwazi
mdogo uliokuwa chini ya zile ngazi na kupotelea chini. Yule mtu akapiga yowe kali
la maumivu akirukaruka kama ndama huku ameshika kifundo cha mkono wake
kilichokuwa kikivuja damu nyingi.
“Fungua mlango au mlidhani kuwa natania!” niliongea kwa hasira huku
nikimtazama yule mwenzake kwa makini na kuzichunguza nyendo zake kwa ukaribu
zaidi. Yule mwenzake kuona vile ikabidi abonyeze vitufe fulani vilivyokuwa kando ya
ule mlango na hapo ule mlango ukafunguka.
Ule mlango ulipofunguka safari yetu ikaendelea huku wale watu wakitangulia
mbele. Lile tukio la shambulio langu la risasi lilikuwa limemuogopesha sana yule
mateka niliyemdhibiti vizuri kwa kabari yangu matata hivyo akawa akitetemeka kwa
hofu huku jasho jepesi likimtoka mwilini. Hali ile ikanifurahisha sana kwani nilikuwa
na kila hakika kuwa yule mtu alikuwa akinigwaya.
Mara tu tulipoingia kwenye kile chumba chenye michoro ya ajabu nikagundua
kuwa wale watu mbele yangu walikuwa tayari wameshaufungua ule mlango mkubwa
mweusi wa kutokea kwenye ile korido hivyo hatukuweka kituo katika kile chumba.
Wale watu mbele yangu walikuwa tayari wameshatoka kwenye kile chumba na kuingia
kwenye ile korido.
Sikutaka kutoka mzimamzima kwenye ile korido hivyo nikambana vizuri yule
mateka wangu kisha nikasogea taratibu na kuchungulia nikipeleleza usalama wa lile
eneo. Hali ya usalama katika korido ile haikuniridhisha kabisa kwani kulikuwa na watu
wapatao kama sita kwenye korido ile upande wa kushoto na wote walikuwa wamevaa
suti nyeusi huku wakiwa na bastola zao mikononi kama wale watu wawili waliotangulia
mbele kwenye msafara wetu. Hisia zikanitanabaisha kuwa wale watu walikuwa
makachero. Hisia za kuzidiwa ujanja zikaanza kunisimanga na hapo nikaanza kuiona
hatari ya kukamatwa mzimamzima endapo nisingepiga akili ya haraka ya kuutegua
mtego mle.
Wakati nikiendelea kuwaza namna ya kujinasua katika hatari ile wale watu wawili
waliokuwa mbele wakiongoza msafara wakaanza kutimua mbio wakielekea upande
wa kushoto wa ile korido walipokuwa na wale makachero wenzao. Wakati tukio lile
likifanyika mara kitu cha kushangaza kikatokea kwenye ile korido.
Kwanza nikasikia sauti kali ya mpasuka wa kioo halafu muda uleule nikamuona
yule kachero niliyemkata kiganja kwa risasi yangu akisombwa kwa nguvu za ajabu
na kutupwa hewani na alipotua chini kwenye sakafu ya ile korido kila mtu eneo lile
akashikwa na taharuki. Kiwiliwili chake kilikuwa kikirukaruka kama kuku ambaye
hajachinjwa vizuri halafu muda uleule kichwa chake kikaanguka chini na kuanza
kujiviringisha kwa kasi kikielekea upande wa kushoto wa ile korido walipokuwa wale
makachero.
Kuona vile wale makachero wakaanza kutimua mbio kwa hofu wakishuka ngazi
kuelekea ghorofa ya chini ya lile jengo. Lilikuwa tukio la kushangaza sana lililoniacha
kwenye taharuki isiyoelezeka. Eneo lote kwenye sakafu ya ile korido lilipotokea lile
tukio la kushangaza likawa limetapakaa damu.
Kwa kweli nilishtushwa sana na tukio lile hata hivyo sikumuachia yule mateka
wangu wala kutimua mbio ingawa sasa nilikuwa makini sana nikichungulia tena
kwenye ule upande niliposikia ile sauti kali ya mpasuko wa kioo kwenye ile korido.
Nilikuwa sahihi kwani kioo cha dirisha kubwa lililokuwa mwisho wa ile korido
kwenye lile jengo chote kilikuwa kimechanguliwa vibaya na kuanguka chini kwenye
sakafu ya ile korido na kutawanyika kila mahali. Nilipoupisha utulivu kichwani
mwangu haraka wazo fulani likanijia na kunitanabaisha kuwa yale hayakuwa mauzauza
isipokuwa lilikuwa tukio makini lenye uhalisia. Nilipochungulia tena kwenye ile korido
mara nikakiona kivuli cha mtu fulani kikipotelea kwenye dirisha la chumba cha jengo
lingine la ghorofa lililokuwa kando ya lile jengo letu likitenganishwa kwa barabara ya
lami. Kitendo kile kikapelekea baridi kali ya ghafla isambae taratibu moyoni mwangu.
Hisia zangu zikanitanabaisha kuwa ile ilikuwa ni kazi makini ya mdunguaji.
Hisia zile zikanipelekea nichungulie tena kwenye lile dirisha hata hivyo sikumuona
mtu yeyote na hapo nikajua kuwa mdunguaji yule hatari alikuwa tayari ameshatoweka
eneo lile. Kwa kweli sikutaka kuendelea kusubiri eneo lile kwani lile tukio lilikuwa
limenipotezea utulivu kwa kiasi kikubwa kichwani mwangu. Wale makachero
sasa walikuwa wamepotelea kwenye zile ngazi za kushukia ghorofa ya chini ya
lile jengo. Hivyo nikambana vizuri yule mateka wangu na hapo nikaanza kusota
kimgongomgongo ukutani huku yule mateka wangu nikimuweka mbele yangu kama
ngao.
Baada ya muda mfupi nikawa nimefika kwenye kile chumba cha lifti cha lile
jengo. Nikabonyeza kitufe cha lifti na chumba kile cha lifti kilipofika na mlango wake
kufunguka nikapotelea mle ndani huku yule mateka wangu nikiwa nimemdhibiti
kikamilifu. Muda mfupi mara baada ya kuingia kwenye kile chumba cha lifti tukaanza
safari ya kushuka chini ya lile jengo huku ndani ya chumba kile tukiwa wawili tu yaani
mimi na yule mateka wangu.
Mara tu kile chumba cha lifti kilipoanza kushuka chini ya lile jengo hisia zangu
zikanihamasisha kuwa nigeuke na kuangalia upande wa pili kwenye lile jengo la
ghorofa ambalo yule mdunguaji hatari alikuwa amelitumia kufanya shambulizi la
hatari kwa yule kachero wa usalama.
Katika lile jengo la ghorofa lililokuwa kando ya lile jengo letu nikakiona chumba
kingine cha lifti kilichotengenezwa kwa vioo vinavyomuwezesha mtu yeyote kuona
mle ndani bila shida yoyote. Chumba kile cha lifti sasa kilikuwa kikishuka chini ya
lile jengo. Hali ile ikanivutia na hapo nikayasimamisha macho yangu nikitazama kwa
makini ndani ya kile chumba cha lifti kilichokuwa kikishuka chini ya lile jengo.
Taswira nzuri ikajengeka machoni mwangu na tafsiri nzuri iliyofanyika katika
ubongo wangu ikanitanabaisha kuwa ndani ya kile chumba cha lifti kulikuwa na mtu.
Koo langu likakauka ghafla pale nilipogundua kuwa yule mtu aliyekuwa ndani ya
chumba kile cha lifti alikuwa ndiye yule dada aliyenitoroka kwenye lile jengo la Rupture
& Capture.
Yule dada alikuwa amevaa suruali ya jeans,viatu vyenye visigino virefu miguuni,blauzi
ya rangi ya hudhurungi na kichwani alikuwa amevaa kofia ya Sombrero na miwani
myeusi ya jua. Kama ambaye alikuwa ameshtukia kuwa nilikuwa nikimtazama naye
pia akageuka na kunitazama huku begi lake jeusi na jembamba likitengeneza kichuguu
kidogo nyuma ya mgongo wake.
Alikuwa ndiye yule mdunguaji hatari na ingawa mdunguaji yule alikuwa amevaa
miwani myeusi lakini kitendo kile cha yeye kugeuka na kutazama kwenye kile chumba
chetu cha lifti kikanipa hakika kuwa alikuwa akinitazama mimi. Nilitulia nikijaribu
kuvuta picha kuwa mdunguaji yule ungekuwa akiwaza nini juu yangu lakini hilo
lilishindikana kwani hakuna binadamu aliyejaliwa uwezo wa kutambua mwenziwe
anawaza nini. Hivyo tuliendelea kutazamana kwenye vyumba vile vya lifti vilivyokuwa
vikishuka chini ya majengo yale ya ghorofa taratibu huku mawazo mengi yakipita
kichwani mwangu. Kwa kweli nilishindwa kabisa kuelewa kwanini mdunguaji yule
hatari alikuwa akiendeleza ubabe wake kwa kuwadungua watu namna ile.
Mawazo mengi yaliyokuwa yakipita kichwani mwangu wakati tukishuka kwenye
kile chumba cha lifti ghafla yakakatishwa baada ya kile chumba cha lifti tulichopanda
kugota chini ya lile jengo kwenye ghorofa ya mwisho ama groundfloor na hapo
nikaikumbuka hatari iliyokuwa mbele yangu. Hivyo nikambana vizuri yule mateka
wangu kwa kabari matata huku bastola yangu nikiwa nimeikamata vyema mkononi.
Mlango wa kile chumba chetu cha lifti ulipofunguka sikutaka kuharakisha kutoka
nje na yule mateka wangu na badala yake nilisogea taratibu na chungulia nje ya kile
chumba cha lifti kwanza. Nikaupisha utulivu kichwani mwangu huku nikiyatembeza
macho yangu taratibu kule nje na kwa kweli hali ya usalama ya eneo lile ilinipa hadhari.
Eneo lote chini ya lile jengo lilikuwa limezingirwa na makachero wa usalama
wa taifa huku wakiwa katika suti zao nadhifu na bunduki zao mikononi. Baadhi ya
makachero wale niliwaona wakiwasiliana kupitia vinasa sauti vilivyokuwa katika kola
za makoti yao ya suti. Wale makachero walikuwa wamejipanga katika maeneo tofauti.
Wengine walikuwa kwenye vipenyo vya jengo lile na wengine walikuwa wamejibanza
kwenye kona za magari yaliyoegeshwa pale nje. Kwa hesabu ya haraka ni kuwa mitutu
ya bunduki zisizopungua kumi na tano ilikuwa imeelekezwa kwenye kile chumba cha
lifti nilipokuwa mimi na mateka wangu.
Hofu ikaanza kujenga taratibu moyoni mwangu huku nikihisi kushikwa na
kigugumizi cha kufanya maamuzi sahihi na ya haraka. Nikiwa katika hali ile nikaanza
kufikiria kuwa nirudi mle ndani kisha niiamuru ile lifti iturudishe kule juu ya lile jengo
tulipotoka mimi na mateka wangu huku nikiamini kuwa nikiwa kule ningepata wazo
zuri la kujinasua kutoka wale makachero.
Lakini baada ya kuyapa utulivu mawazo yangu wazo lile nikaliweka kando pale
nilipowaza kuwa uamuzi wa kurudi juu ya lile jengo ungeweza kuwavuta zaidi wale
makachero na hivyo kujipanga kikamilifu hali ambayo ingepunguza uwezekano
mkubwa wa kutoroka kwangu kwenye lile jengo. Hivyo njia sahihi niliyoiona ilikuwa
ni kukabiliana na wale makachero ana kwa ana huku nikiwa tayari kukabiliana na
lolote ambalo lingetokea.
Hivyo hatimaye nikamdhibiti vizuri yule mateka wangu na hapo tukaanza taratibu
kusogea tukitoka nje ya kile chumba cha lifti. Halaiki ya mashuhuda waliokuwa
wakiongezeka eneo lile ikazidi kuongeza uzito wa tukio lile tofauti na mimi nilivyokuwa
nikilichukulia. Hata hivyo roho yangu ilikuwa ni kitu cha thamani zaidi.
Kile kitendo cha mimi na yule mateka wangu kutoka nje ya kile chumba cha lifti
kikawapelekea wale makachero wazidi kujipanga. Nikaikamata vizuri bastola yangu
kiganjani huku yule mateka wangu akiwa ameenea vyema kwenye kabari yangu
matata ya shingo na hapo tukaanza kutoka nje. Tulipotoka nje kile chumba cha lifti
mara nikasikia tangazo kutoka kwenye spika ya kirushia matangazo iliyokuwa juu ya
Landcruiser moja iliyokuwa eneo lile.
“Tafadhali! tupa silaha yako chini na nyoosha mikono juu. Hii ni amri kutoka
kwa polisi vinginevyo tuna haki ya kukupiga risasi endapo utakaidi” ile sauti kutoka
kwenye ile spika ikahanikiza eneo lile na sikuwa na wasiwasi kuwa mimi ndiye
niliyekuwa mlengwa. Hata hivyo sikusalimu amri kwani ule ulikuwa ni mchezo wa
kufa na kupona.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Tupa silaha yako chini na nyoosha mikono yako juu tafadhali!” ile sauti ikaendelea
kunionya wakati nikiendelea kutembea taratibu na mateka wangu huku ile bastola
yangu mkononi nikiwa nimeielekeza kichwani kwa yule mateka wangu.
Nilipoyatembeza macho yangu tena eneo lile nikagundua kuwa wafanyakazi
waliokuwa kwenye lile jengo na watu wengine waliokuwa katika majengo ya ghorofa
yaliyokuwa jirani na pale walikuwa wametoka nje ya ofisi zao kushuhudia tukio lile
la aina yake. Akili yangu ikafanya kazi haraka kwani nilifahamu fika kuwa ukimya
usingenifaa kitu hivyo ile amri walionipa wale makechero nikaigeuzia kwao.
“Wekeni silaha zenu chini na mrudi hatua tano nyuma vinginevyo uhai wa huyu
mtu utadaiwa kwenu” nikafoka kwa hasira nikiwaambia wale watu.
“Nitahesabu mpaka tatu na mkiendelea kukaidi amri yangu msinilaumu”
nikaongea kwa sauti huku nikiwa na hakika kuwa mtu yoyote ambaye angekuwa eneo
lile angenisikia vizuri.
“Moja…” nikaanza kuhesabu “Mbili…” nilipokuwa mbioni kumaliza kuhesabu
mara nikasikia sauti nzito kutoka upande wa kushoto.
“Okay!…Okay! vijana wangu wekeni silaha zenu chini huwenda huyu mwehu ana
jambo zuri la kutuambia”
Nikageuka na kutazama upande ule ile sauti alipokuwa ikitokea na mara hii
nikamuona mwanaume mwenye umri wa kukadirika kati ya miaka arobaini hadi
arobaini na tano. Mwanaume mrefu na mweusi lakini mwenye umbo imara lililojificha
ndani ya suti yake ya rangi ya samawati. Macho makubwa na makali ya mwanaume
yule yakanitazama katika uso wake mrefu kiasi wenye pua ndefu na pana huku mdomo
wake ukizungukwa kwa ndevu zilizokatiwa vizuri kuuzunguka.
Misuli iliyokaza usoni kwa mwanaume yule ilikuwa ni ishara tosha kuwa yule mtu
alikuwa amekasirishwa sana na tulio lile. Nikamtazama yule mtu kwa makini na hapo
nikagundua kuwa mkono wake mmoja alikuwa ameutia kwenye mfuko wa suruali
yake na ule mwingine alikuwa ameshika bastola na hivyo kuyapelekea mabega yake
yanye umbo la mraba yazidi kutuna kama bondia.
“Wehu ni nyinyi mnaosababisha shughuli za watu zisiendelea kwa tukio lisilo na
maana” nikafoka kwa sauti huku taratibu nikisogea na yule mateka wangu kuelekea
kule nilipokuwa nimeegesha gari langu chini ya lile jengo.
“Okay! muachie basi huyo mateka sisi tumeshaweka silaha zetu chini” yule mtu
akafoka.
“Tupa chini bastola yako!” nikamwambia yule kachero aliyeonekana kuwa ndiye
kiongozi wao.
“Hivi mnadhani nyinyi ni watu wa kuaminika kirahisirahisi?. Nimesema wekeni
silaha zenu chini na mrudi hatua tano nyuma. Hii ni amri na siyo ombi na yeyote
atakayejaribu kuleta hila basi mjue kuwa nyinyi ndiyo mtakaowajibika na akifo cha
huyu mtu” nikawaonya wale makachero huku macho yamenitoka kwa msisitizo
katika hali ya kuhakikisha kuwa amri yangu inatekelezwa.
“Okay!...” yule kachero kuona vile akasalimu amri huku akiiweka bastola yake
chini na kitendo cha yeye kurudi nyuma baada ya kuiweka bastola yake chini na kurudi
hatua tano nyuma kikawapelekea na wale makachero wengine watii amri na kuanza
kurudi nyuma.
“Good!” nikaongea kwa msisitizo huku nikiwa napiga mahesabu ya kawaacha
wale makachero kwenye mataa. Hivyo nikayatembeza macho yangu taratibu na kwa
makini nikitazama eneo lile na kwa kufanya vile nikagundua kuwa umati wa watu eneo
lile ulikuwa umeongezeka mara mbili zaidi ya pale awali na hali ile ikanivutia sana.
Nikayapeleka macho yangu kutazama tena kule lilipokuwa gari langu na hapo
wasiwasi ukaniingia baada ya kuliona gari langu kuwa lilikuwa limetengwa kwani
yale magari mengine yaliyokuwa jirani na gari langu hapo awali hayakuwepo. Nilihisi
kuwa kulikuwa na hila fulani iliyokuwa ikitaka kuchwezwa eneo lile hata hivyo sikusita
kuendelea mbele na safari yangu huku yule mateka wangu nikiwa nimemdhibiti
kikamilifu mkononi mwangu. Nikageuka tena na kumtazama yule kachero mkubwa
na kumwambia
“Naondoka na huyu mateka wangu na asijaribu mtu yoyote kunifuata!”
nikafoka kwa sauti nikitaka kuhakikisha kuwa mtu aliyekuwa eneo lile ananisikia
vizuri. Yule kachero akanisikiliza kwa makini huku akiumba tabasamu jepesi usoni
mwake. Nilipomtazama usoni kwa haraka nikagundua kuwa kulikuwa na kitu hatari
kilichokuwa kimejificha nyuma ya tabasamu lake. Hata hivyo ule haukuwa muda wa
kuendelea kutafakari.
Muda mfupi baadaye nikawa nimelifikia gari langu kwenye yale maegesho ya magari
ya lile jengo huku kijasho chepesi kikiwa kinanitoka kwenye sehemu mbalimbali za
mwili wangu. Mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakienda mbio sana kila nilipokuwa
nikitafakari kitu ambacho kingefuatia baada ya pale. Hata ule mkono wangu ulioshika
bastola nao kwa mbali niliuhisi kuwa ulikuwa mbioni kulowana kwa jasho la hofu.
Wakati nilipokuwa nikijiandaa kufungua mlango wa gari hisia zangu
zikanitahadharisha kuwa kabla ya kufungua mlango ule nilipaswa kugeuke na kutazama
kwanza kule kwenye kile chumba cha lifti alichokuwa mdunguaji. Hivyo nikayapeleka
macho yangu haraka kutazama upande wa lile jengo la ghorofa kulipokuwa na kile
chumba cha lifti. Kwa kufanya vile macho yangu yakakutana na macho ya mdunguaji
huku akiwa amevua miwani yake na kuishika mkononi na hapo nikaweza kukiona
kilichokuwa kimefichika ndani ya macho yale. Jambo la hatari! hisia zangu zikaniambia
na hapo akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka.
Hivyo kufumba na kufumbua kwa nguvu zangu zote nikamsukuma yule mateka
wangu mbali na lile gari langu huku nikijirusha upande wa pili. Muda uleule sauti ya
kishindo kikubwa cha mlipuko ikazizima eneo lile. Nililiona lile gari langu likirushwa
hewani kama kiberiti na likiwa kule angani mlipuko mwingine mkubwa ukasikika
huku lile gari likichanguka vipandevipande. Vipande vile vitakawanyika angani na kwa
kuwa madhara yake nilikuwa nikiyafahamu vizuri hivyo nikawahi kujiviringisha na
kupotelea chini ya gari moja lililokuwa jirani na eneo lile. Nilichokisikia baada ya pale
ni kelele za hofu zikihanikiza kutoka kwa umati mkubwa wa watu waliokuwa eneo lile
kushuhudia hatima yangu.
Nikiwa chini ya lile gari niliweza kuiona miguu ya watu wengi waliokuwa wakitimua
mbio huku kila mtu akishika uelekeo wake katika hali ya kujihakikisha usalama wa
maisha yake. Sikumuhurumia mtu yeyote kwani tatizo moja la watanzania wengi ni
kupenda kushuhudia hatari hata kama mazingira ya kufanya hivyo hayaruhusu.
“Ile ilikuwa nafasi yangu pekee ya kutoweka eneo lile” niliwaza kisha nikajiviringisha
na kutokea upande wa pili wa uvungu wa lile gari. Nikiwa pale chini nilitazama kule
kwenye kile chumba cha lifti kwenye lile jengo la ghorofa lililokuwa upande wa pili
wa ile barabara. Kile chumba cha lifti kilikuwa tupu na yule mdunguaji hakuwepo.
Tukio lile likanishangaza sana na sikutaka kuendelea kujilaza pale chini na kutafakari
hivyo haraka nikasimama na kuanza kutimua mbio nikijichanganya kwenye lile kundi
la watu waliokuwa wakilikimbia eneo lile.
Kachero mmoja alikuwa ameniona wakati nikitimua mbio kulitoroka eneo lakini
hakuweza kunifikia kwani mwendo wangu ulikuwa siyo wa masihara.
Kitu kilichozidi kunifurahisha zaidi ni kuwa hata watu waliokuwa wamepanda
kwenye mabasi ya daladala yaliyokuwa yakikatisha kwenye barabara ya eneo lile nao
walivyoona vile wakaingiwa na hofu na kuanza kushuka chini wakitimua mbio huku
wengine wakitokea milangoni na wengine madirishani. Baadhi ya watu walianguka
chini wakati wakitoka kwenye daladala za eneo lile hususan akina mama na watoto.
Wakati nikiwapita wale watu na kuendelea kutimua mbio kulitoroka eneo lile
bastola yangu nilikuwa tayari nimeichimbia mafichoni. Bado nilikuwa salama na kazindiyo kwanza ilikuwa imeanza. NILIKUWA NAJIDANGANYA
#148
ILIKUWA NI SAWA NA KUJIDANGANYA kuwa nilikuwa salama kitu
ambacho sikutaka kukiamini kabisa kuwa kilikuwa kweli. Hivyo niliendelea kutimua
mbio kujiweka mbali na eneo lile lilitokea milipuko miwili mikubwa muda mfupi
uliyopita. Wakati nikiendelea kukimbia mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani
mwangu huku nikishindwa kabisa kuamini kuwa nilikuwa nimebahatika kuponyoka
kwenye tundu la kifo.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa ni kwa namna gani roho yangu ilikuwa ikitafutwa
na wale watu na vilevile niliamini kuwa kitendo cha mimi kuwatoroka wale watu
usingekuwa ndiyo mwisho wa kutafutwa kwangu. Dhana ile ikanifanya nianze kuhisi
kuwa kuanzia wakati ule nilitakiwa kuwa makini sana katika nyendo zangu. Wakati
nikiendelea kufikiri mara fikra zangu zikahamia kwa mdunguaji ambaye hadi wakati
huu alikuwa ni mtu hatari sana katika mkasa huu. Nilikumbuka siku ile yule mdunguaji
alivyomdungua yule mtu nje ya Vampire Casino na sasa tukio lile nikalihusisha na lile
tukio lililotokea muda mfupi uliyopita la namna risasi yake makini ilivyokikata vibaya
kichwa cha yule kachero kwenye lile jengo la ghorofa kulipotokea kizaazaa.
Mdunguaji alikuwa ni mtu hatari sana lakini kwa muda mfupi uliyopita alikuwa
amenifaa sana kwani vinginevyo habari yangu ingekuwa imeishia pale chini ya lile
jengo. Kwanini mdunguaji yule hatari alikuwa ameniokoa kwa kunipa ishara kuwa
nisilikaribie gari langu na yule mateka pale nje ya lile jengo?. Hilo ndiyo likawa swali
pekee lililozamisha fikra zangu kwenye msitu mzito wa mawazo huku nikiendelea
kujiuliza maswali mengine kama. Ina maana mdunguaji yule hatari aliniona wakati
nilipokuwa nikiingia kwenye lile jengo la ghorofa?. Mdunguaji yule hatari alijuaje
kuwa ningefika pale kwenye lile jengo na kitendo cha yeye kunipa ishara huku akiwa
kwenye kile chumba cha lifti kuwa nisiingie kwenye lile gari langu inamaanisha kuwa
mdunguaji yule alikuwa ameuona mchezo wote ulivyokuwa ukichezeka eneo lile
na hadi mabomu yale mazito mawili kupandwa kwa hila kwenye gari langu?. Huyu
mdunguaji ni nani na kipi kilichokuwa kikiendelea kati yake na wale watu hatari?.
Kwa kweli bado nilikuwa kwenye msitu mnene wa mawazo. Mapigo ya moyo wangu
yakiwa yameanza kupata afueni taratibu nikaanza kupunguza hatua za miguu yangu
huku nikiwa nimefika mbali na eneo lile.
Nilikuwa nimeshazipita kona tatu za mitaa ya jiji la Dar es Salaam yenye majengo
marefu ya ghorofa eneo la posta na sasa nilikuwa nimeingia kwenye kona ya nne
na kwa kweli sikuona tena umuhimu wa kitimua mbio. Nilipunguza mwendo na
hatimaye kuanza kutembea taratibu. Maongezi ya watu wengi niliyopishana nao njiani
na wale waliosimama kijiweni yalijikita zaidi katika lile tukio la milipuko ya mabomu
iliyokea muda mfupi uliopita kule chini kwenye lile jengo la ghorofa nilikotoka. Kila
mmoja alikuwa akizungumza lake hata kama ilikuwa uongo huku akijaribu kulipamba
kwa namna yake hadi wenzake wakamwamini utasema alishuhudia.
Niliwasikia baadhi ya watu wakihusisha milipuko ile na tukio la kigaidi. Watu hao
hawakuishia pale katika mazungumzo yao bali wakaenda mbele zaidi wakilihusisha
kundi la kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia kuwa ndiyo lililokuwa limehusika na
milipuko ile. Wengine wakaenda mbele zaidi wakilituhumu kundi la kigaidi la Boko
Haram la Nigeria kuwa ndiyo lililokuwa limehusika na milipuko ile. Mtu mmoja angalu
yeye akatofautiana na wenzake kwa kusema eti lile lilikuwa ni tukio la kijambazi na
majambazi hao walikuwa wamepora mamilioni ya fedha kutoka kwenye benki moja
maarufu iliyokuwa jirani na eneo lile la tukio na hivyo kujikuta wakikabiliana na
upinzani mkali kutoka kwa jeshi la polisi lililoshtukia mapema wizi huo.
Nikachukua mche mmoja wa sigara na kuutia mdomoni kisha nikajiwashia kwa
kiberiti changu cha gesi kilichokuwa mfukoni. Nilipoitoa sigara ile mdomoni taratibu
nikaupuliza moshi pembeni huku nikitabasamu baada ya kufahamu kuwa angalau
watu wale walikuwa hawafahamu vizuri kilichokuwa kimetokea. Nikaendelea na safari
huku nikivuta sigara yangu taratibu na kuufurahia uhuru ule tofauti na miji mingine
ya bara la Afrika kama Nairobi ambapo suala la uvutaji wa sigara hadharani lilikuwa
limepigwa marufuku na hivyo kutengewa maeneo maalum ya wavutaji sigara liitwalo
Smoke zone.
Njaa kali ilikuwa ikinitafuna tumboni hivyo wakati nikitembea nikawa
nikiyatembeza macho yangu huku na kule nikijaribu kutafuta kama kungekuwa na
mgahawa wowote eneo lile ili niingie na kujipatia chochote kwani tangu nilipoamka
asubuhi nilikuwa sijatia kitu chochote tumboni na nikiwa najipatia chakula hicho
ningeutumia muda huo kujipanga namna ya kuendelea mbele na harakati zangu.
Katika kufanya vile hatimaye nikauona mgahawa mmoja uliyokuwa ng’ambo ya
pili ya barabara ile niliyokuwa nikitembea ukiwa pembeni ya duka la mikate. Nilikuwa
mbioni kuvuka ile barabara ili nielekee kwenye ule mgahawa ng’ambo ya barabara
pale nilipokumbuka tena kutazama nyuma yangu.
Kwa kufanya vile ghafla moyo wangu ukaingiwa na baridi na hapo tumbo likaanza
kunisokota. Landcruiser nyeusi kama ile iliyokuwa ikinifukuza wakati wa asubuhi sasa
ilikuwa kiasi cha umbali wa mita zisizopungua hamsini nyuma yangu. Nilipolichunguza
vizuri lile gari nikagundua kuwa namba zake hazikuwa tofuati sana na zile namba
za gari lililokuwa likinifukuza asubuhi ile. Hisia za kuwa nilikuwa nikifuatiliwa tena
zikaniingia akilini na hapo tusi zito likanipanyoko mdomoni.
“Hivi hawa wapuuzi wana shida gani na mimi?. Mbona wananifuatafuata kila
mahali?. Nikajiuliza huku nikigeuka na kutuzama mbele. Sikuvuka tena ile barabara
na kwenda kwenye ule mgahawa badala yake akili yangu ikazama katika kutafakari
jiografia ya eneo lile.
Hatua chache kutoka pale nilipokuwa mbele yangu kulikuwa na barabara nyingine
iliyokatisha. Barabara hiyo kwa upande wa kushoto ilikatisha mbele ya msikiti mkubwa
wa mabaniani kisha ikapita mbele ya jengo dogo la posta na kuelekea mbele ikikatisha
katikati ya majengo marefu ya ghorofa za shirika la nyumba la taifa ikielekea kule
nilipotoka.
Barabara iliyoingia upande wa kulia ilikatisha mbele ya kituo kikubwa cha kujazia
mafuta cha BP. Mara baada ya kukivuka kituo kile cha mafuta barabara hiyo ilikatisha
mbele ya ofisi ndogo za shirika la ndege la Ethiopian Airlines ikipita mbele ya jengo
kubwa la supermarket ikielekea mbele. Mkabala na supermarket ile kulikuwa na barabara
nyingine iliyokatisha katikati ya majengo marefu ya ghorofa za shirika la nyumba la
taifa.
Kwa kiasi kikubwa majengo yale yalikuwa yakikaliwa na raia wa kitanzania
wenye asili ya bara la Asia. Ni katika majengo yale lilipokuwepo jengo moja kubwa la
ghorofa hapo zamani likitumika kama makao makuu ya ofisi za shirika la usafirishaji.
Lakini baada ya shirika hilo kufilisika na kufa sasa jengo lile lilikuwa limekodiwa na
wafanyabiashara mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam na hivyo kulipelekea jengo lile
muda wote kutawaliwa na pilikapilika za kibinadamu. Nyuma ya jengo lile kulitazamana
na kituo kikubwa cha daladala ambacho wakati wote kilikuwa hakiishiwi na abiria wa
kuelekea maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.
Kuyakumbuka vizuri mandhari yale kukanipelekea nitengeneze tabasamu jepesi
usoni mwangu pale nilipowaza kuwa endapo ningekuwa makini ningeweza kuwatia
adabu watu wale waliokuwa nyuma yangu kwenye ile Landcruiser. Hivyo bila kugeuka
nyuma nikaanza kuzitupa hatua zangu kwa haraka na kwa kufanya vile ni kama wale
watu kwenye ile Landcruiser nyuma yangu walikuwa wameishtukia dhamira yangu.
Hivyo lile gari Landcruiser nyuma yangu likaongeza mwendo na kunikaribia. Sikutaka
kuendelea kusubiri badala yake nikaanza kutimua mbio za kistaarabu na nilipogeuka
nyuma na kuliona lile gari Landcruiser likizi kunikaribia sikutaka kuendelea kuidanganya
nafsi yangu kuwa hali ilikuwa shwari. Hivyo na mimi nikaanza kuchanganya miguu na
kutimua mbio kisawasawa. Wale watu kuona vile nao wakaanza kuongeza mwendo
wa gari wakinifukuza nyuma yangu.
Niliipita ile barabara iliyokuwa ikichepuka upande wa kulia huku lengo langu
likiwa ni kutaka kuwapoteza maboya wale watu kwenye ile Landcruiser nyuma yangu.
Wale watu kuona vile nao wakaongeza mwendo wakinifuata na hilo likawa kosa
kubwa kwani haraka niligeuza na kurudi nilikotoka. Kitendo kile kikawapelekea wale
watu wababaike katika kufanya maamuzi. Tukio lile likanifurahisha sana kwani ingawa
nilikuwa na hakika kuwa wale watu walikuwa na silaha lakini kwa namna nyingine
nilifahamu kuwa wasingeweza kuzitumia silaha zao kama pendekezo lao la kwanza.
Nilikuwa na kila hakika kuwa watu wale walikuwa wametumwa kunikamata ili
wanipeleke mzimamzima wakanitapishe taarifa walizozihitaji.
Nilikatisha katikati ya kile kituo cha kujazia mafuta huku nikiendelea kutimua
mbio na nilipogeuka nyuma nikawaona wale watu nyuma yangu nao wakishuka
kwenye lile gari na kuanza kunifukuza huku wakiwa na bastola zao mikononi. Watu
waliokuwa eneo lile huwenda walishangazwa sana na tukio lile kwani makoti ya suti za
wale makachero yalikuwa yakipepea huku bastola zao wakiwa wamezikamata vyema
mikononi. Mwendo wangu haukuwa wa kubabaisha hali iliyowapelekea wale watu
wajitahidi kunikaribia bila mafanikio huku wakihema ovyo kama kuku wa kisasa na tai
zao shingoni zikipepea huku na kule zikipishana na vitambi vyao vya bia.
Nilikatisha mbele ya lile jengo lenye ofisi ndogo za shirika la ndege la Ethiopia
Airlines halafu nilipolifikia lile jengo la supermarket mmoja wa wale watu waliokuwa
wakinifukuza uvumilivu ukamshinda hivyo akafyatua risasi moja kunilenga lakini
shabaha yake ilikuwa mbovu kwani ile risasi ilipita mbali na mimi na kupasua kioo
kimoja cha mbele cha ile supermarket . Hali ile ikawapelekea watu waliokuwa kwenye
ile supermarket wapige mayowe ya hofu huku kila mmoja akitafuta kificho.
Risasi nyingine zilifuata baada ya pale lakini zote hazikufua dafu kwani nilikuwa
mahiri katika kuzikwepa na hatimaye nikachepukia kwenye barabara iliyokuwa mbele
ya ile supermarket. Mara baada ya kuingia kwenye barabara ile niligeuka tena nyuma na
kuwatazama wale watu na hapo nikagundua kuwa nilikuwa nimewaacha mbali hata
hivyo hawakuonesha kukata tamaa. Wale watu bado walikuwa wakinifukuza ingawa
sasa nilikuwa na hakika kuwa wasingeweza tena kunishambulia kwa risasi kwani
nilikuwa nimeanza kulifikia eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
Niliendelea kutimua mbio huku nikiyapita baadhi ya majengo ya ghorofa ya shirika
la nyuma la taifa nikilikaribia lile jengo kubwa la ghorofa lililokuwa likitumika kama
makao makuu ya chama cha usafirishaji kabla ya shirika hilo kufilisika na jengo lile
kutumiwa na wafanyabiashara. Wale watu waliendelea kunifukuza bila kukata tamaa.
Baada ya mbio ndefu hatimaye nikawa nimefika kwenye lile jengo la ghorofa
lililokuwa likitumiwa na wafanyabiashara. Nilipofika kwenye lile jengo nikaingia
sehemu ya chini nikishuka ngazi kuelekea kwenye maegesho ya magari ya lile jengo.
Kulikuwa na magari mengi yaliyokuwa yameegeshwa sehemu ile hata hivyo hakukuwa
na watu wengine zaidi ya mlinzi mmoja wa eneo lile aliyekuwa kwenye kibanda chake
akisikiliza redio. Mbali na pale eneo lote lile lilikuwa tulivu mno.
Nilikuwa na hakika kuwa wale makachero bado walikuwa wakinifuata nyuma
yangu hivyo mara tu nilipomaliza kushuka zile ngazi nikaingia kwenye ile sehemu
ya maegesho ya magari. Nilikuwa nimeamua kupita moja kwa moja eneo lile hadi
kwenye mlango wa kutokea upande wa pili wa maegesho yale ambapo mara baada
ya kutoka nje ningejichanganya kwenye mkusanyiko wa watu na kutokomea zangu.
Lakini nilipotafakari vizuri nikajikuta nikiliweka kando wazo lile. Sikutaka kuendelea
kumkimbia adui nisiyemjua vizuri istoshe nilikuwa nimeanza kuchoshwa na hali ile ya
kufukuzwa kama mnyama wa porini. Hivyo mara tu nilipomaliza kushuka zile ngazi
haraka nikachepuka na kujibanza nyuma ya gari moja kati ya magari mengi yaliyokuwa
eneo lile.
Nikiwa nyuma ya lile gari haukupita muda mrefu mara nikawaona wale watu
waliokuwa wakinifukuza wakianza kushuka kwenye zile ngazi kwa pupa na bastola
zao mkononi. Nikiwa pale kwenye yale maficho niliendelea kuwatazama wale watu
kwa makini. Wawili kati yao walielekea kufanana kwa maumbo na umri. Walikuwa
warefu wa haja na wenye miili iliyoneemeka kwa shibe isiyokuwa ya wasiwasi na
mazoezi ya mwili yasiyokuwa na ratiba kamili. Mmoja aliyesalia alikuwa mfupi na
imara mwenye macho makubwa na uso wa hasira
Wale watu ni kama walikuwa wameshangazwa sana na kitendo cha kutoniona eneo
lile. Mara nikawaona wale watu wakisimama na kuanza kushauriana katika maongezi
ambayo sikuweza kuyasikia vizuri na baada ya majadiliano yale mara nikawaona wawili
kati yao wakirudi kule juu walipotoka. Mmoja alikuwa ni yule mtu mfupi na mwingine
ni kati ya wale warefu wawili. Baada ya wale watu wawili kurudi kule juu walipotoka
mara nikamuona yule mwenzao aliyesalia akiikamata vizuri bastola yake mkononi na
kuanza kushuka zile ngazi.
Mara yule mtu alipomaliza kushuka zile ngazi akaanza kuyatembeza macho yake
taratibu eneo lile huku akipiga hatua zake makini akisogea ule upande niliokuwa
nimejibanza. Nikamchunguza kwa makini yule mtu na kwa tathmini ya haraka
nikafahamu kuwa yule mtu alikuwa makini sana na asiyehadaika kirahisi. Hivyo
nikaanza kujipanga vizuri namna ya kukabiliana naye pale ambapo ningehitajika
kufanya hivyo. Lakini hakufanikiwa kunifikia pale mlinzi wa eneo lile alipomuona
na kuanza kumuita kwa hadhari. Yule mtu kuona vile akawahi kuisunda bastola yake
mafichoni haraka na kugeuka nyuma akimtazama yule mlinzi.
“Vipi kaka una shinda gani?” mlinzi wa eneo lile kijana wa makamo akauliza kwa
hadhari huku akitoka kwenye kibanda chake na bunduki yake mkononi.
“Nataka kuelekea nje” yule mtu hatari akaongea kwa utulivu huku akilazimisha
tabasamu la kirafiki usoni mwake.
“Sasa mbona huulizi badala yake na unazunguka tu kwenye magari ya watu. Huku
hakuna njia bwana” yule mlinzi akafoka
“Njia iko wapi?”
“Rudi ukaulize huko ulipotoka hili ni eneo la maegesho ya magari tu”
“Oh! samahani bwana mimi sikufahamu” yule mtu hatari akajitetea huku akigeuka
na kurudi kule alipotoka. Yule mlinzi akasimama na kumtazama yule mtu huku
akimsindikiza kwa macho hadi pale yule mtu alipotokomea juu ya zile ngazi na hapo
nikamuona yule mlinzi akianza kuzungukazunguka akiyakagua magari machache ya
eneo lile kabla ya kurudi kule kibandani kwake.
Niliendelea kujibanza pale nyuma ya lile gari huku nikiupisha utulivu kichwani
mwangu hadi pale nilipokuwa na hakika kuwa hali ya mambo ilikuwa shwari eneo
lile ndiyo nikaanza kupiga hatua zangu kwa utulivu nikielekea kwenye eneo la kona
ya maegesho yale kulipokuwa mlango wa dharura. Nilipofika nikafyatua komeo la
ule mlango na kuufungua kisha nikaingia na kutokomea zangu upande wa pili wa lile
jengo kulipokuwa na pilikapilika nyingi za watu.
#150
INGAWA MUDA ULIKUWA UMEENDA SANA lakini kwa
M.D.Kunzugala,mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa suala lile halikuwa na
maana yoyote kwake kwani asingeweza kurudi nyumbani kwake na kupumzika
huku bado akiwa hajaona mafanikio yoyote katika kazi yake.
M.D.Kunzugala wakati huu alikuwa amejiegemeza kwenye kiti chake cha ofisini
chenye foronya laini huku chupa tupu kubwa ya maji ya kunywa na bilauri vikimtazama
mezani mbele yake. Chupa ya nne ya maji ilikuwa mbioni kuteketea mwilini mwake
kitu ambacho hakikuwa cha kawaida tangu alipoteuliwa na rais kushika wadhifa huu.
Kwa muda wa masaa matatu yaliyopita simu nyingi zilikuwa zimemiminika ofisini
kwake kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na vijana wake wa
kazi. Watu hao wakidodosa juu ya mafanikio yaliyokuwa yamefikiwa katika kazi yake
na wengine wakitoa ripoti kwake juu ya wapi walipokuwa wamefikia katika harakati za
kumnasa yule mtu aliyewatoroka maafisa wake chini ya jengo la ghorofa lililopo eneo
la posta kuu jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo hadi kufikia wakati huu bado alikuwa hajapokea hata simu moja
ya kuashiria kuwa kulikuwa na mwelekeo wa matumaini hali iliyompelekea mara
kwa mara aizime na kuiwasha simu yake ya mezani kwa kuhofia kuwa simu hiyo
ingempelekea ugonjwa mpya wa msukumo mkubwa wa damu mwilini.
Sulle Kiganga alikuwa bado akiongoza vijana wake kufanya msako makini katika
kona zote za jiji la Dar es Saalam katika kuhakikisha kuwa yule mtu aliyewatoroka
kwenye lile jengo la ghorofa anapatika haraka kabla hajaendelea kuendeleza maafa
zaidi. Hata hivyo uchunguzi kutoka kwa kamati yake ya usalama iliyokuwa ikiongozwa
na Sulle Kiganja ulikuwa umemletea majibu yenye kumshangaza na kuziyumbisha
vibaya fikra zake. Uchunguzi huo ulikuwa ukieleza kuwa yule mtu aliyewatoroka
maafisa wake kwenye lile jengo la ghorofa lililopo eneo la posta mchana ule alikuwa ni
komandoo na askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania aliyeacha kazi miezi michache
iliyopita akifahamika kwa jina la Chaz Siga. Hivyo kitendo cha kufahamu kuwa mtu
waliyekuwa wakishughulikanaye alikuwa ni askari komandoo kilikuwa kimezidi
kuzamisha matumaini yake ya kumtia mikononi kiulaini.
Pia kulikuwa na taarifa nyingine zilizozidi kumtia mashaka. Taarifa hizo
zikitanabaisha kuwa shambulizi dhidi ya afisa wake mmoja wa usalama aliyeuwawa
kwa risasi kwenye lile jengo la ghorofa la posta akifahamika kwa jina la Balimenya
lilikuwa limetokana na risasi kutoka kwa mtu mwingine na siyo Chaz Siga.
Dhana hiyo ikawa imeongeza hisia nyingine mbaya kwa M.D Kunzugala kuwa
adui hakuwa mmoja kama yeye na wanausalama wenzake walivyodhani hapo awali na
hali hiyo ikawa imeongeza hisia nyingine tofauti katika kushughulika na matukio ya
mauaji yaliyokuwa yakiendelea jijini Dar es Salaam.
Saa ya ukutani ofisini kwake ilikuwa ikionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa
tano usiku na kupitia madirisha ya vioo vya ofisini kwake katika jengo lile la ghorofa
M.D.Kunzugala aliweza kuyaona manyunyu ya mvua nyepesi iliyokuwa ikiendelea
kunyesha. Bado alikuwa kazini kusubiri ripoti kutoka kwa watendaji wake waliokuwa
mitaani kumsaka Chaz Siga na mtu mwingine aliyeshukiwa kufanya shambulizi la kifo
dhidi ya afisa wake wa usalama.
__________
TEKSI NILIYOIKODI ILINISHUSHA NYUMA YA JENGO LA Barracuda
Plaza mtaa wa tatu kabla ya sehemu lilipokuwa kanisa kubwa la The Last Days
Gospel Ministry . Kwa kuwa mvua ilikuwa imeanza kunyesha tena ikanibidi nitembee
kandokando ya baraza za majengo marefu ya ghorofa ya eneo lile la posta ili kujikinga
na manyunyu hayo.
Nilikuwa na hakika kuwa bado nilikuwa nikitafutwa na wale watu walionikimbiza
mchana uliopita. Hivyo wakati huu nilikuwa makini zaidi na nyendo zangu kwa
kuchunguza magari na watu wote niliyokuwa nikipishana nao barabarani.
Nilikuwa nimemaliza kikao cha siri cha masaa matatu na mzee James Risasi
katika hoteli moja iliyopo eneo la Magomeni nikimpa ripoti ya harakati zangu hadi
pale nilipofikia. Mzee James Risasi alikuwa ameipokea ripoti yangu na kuridhishwa na
hatua niliyokuwa nimefikia katika harakati zangu.
Mbali na hayo mzee James Risasi alikuwa amenipa mrejesho juu ya kile
kilichokuwa kikiendelea baada ya mkutano wa maafisa usalama uliyofanyika alfajiri
ile huku akinitahadharisha juu ya hatua zilizokuwa zimechukuliwa. Mzee James Risasi
akaendelea kunieleza kuwa tayari taarifa zangu zilikuwa zimeifikia ofisi kuu ya idara
ya usalama wa taifa na idara hiyo ilikuwa imejipanga vizuri na maafisa wake katika
kuhakikisha kuwa ninakamatwa mapema iwezekanavyo. Nilikuwa nimejipanga vizuri
na kamwe sikutaka kutoa nafasi kwa adui zangu.
Nilimaliza kuipita barabara ya mtaa wa kwanza kisha nikaingia barabara ya mtaa
wa pili na nilipoingia barabara ya mtaa wa tatu nikakumbuka kuitazama saa yangu
ya mkononi na hapo nikagundua kuwa zilikuwa zimesalia dakika chache kufika saa
sita usiku. Njiani nilipishana na jozi tofautia za wapenzi waliokuwa wakitoka kwenye
kumbi za starehe na walevi waliokuwa wakiyumba ovyo barabarani.
Nililipita jengo la benki ya maendeleo ya Afrika na nilipomaliza kuipita ofisi
ya magazeti upande wa kushoto nikaliona kanisa la The Last Days Gospel Ministry.
Niliyatazama mandhari ya kanisa lile na sehemu ya wazi ya kanisa lile upande wa
kushoto nikaliona gari moja dogo aina ya Toyota Starlet nyeupe. Kuliona gari lile
nje ya kanisa kukanipa matumaini kuwa mtu niliyekuwa nikimhitaji alikuwa bado
hajaondoka.
Niligeuka nyuma kuchunguza kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiniufatilia
na nilipoona hali bado ilikuwa shwari nikasubiri gari moja lililokuwa likija mbele yangu
lipite kisha nikavuka barabara na kuelekea kwenye lile kanisa. Nilitembea kwa utulivu
na wakati nikikaribia eneo lile nikagundua kuwa taa za ndani ya kanisa lile zilikuwa
zikiwaka. Hatimaye niliufikia mlango wa kuingia kwenye kanisa lile na kuusukuma
ndani huku nikivikagua vivuli vya miti ya mikungu vilivyokuwa nje ya kanisa lile.
Mara baada ya kuingia ndani ya kanisa lile kwa utulivu nikaurudishia ule mlango
nyuma yangu. Huwenda uwepo wangu mle ndani ya kanisa ulinifanya nijihisi kuwa
ni mwenye dhambi nyingi kwani sikuweza kukumbuka kuwa kwa mara yangu ya
mwisho kuhudhuria ibada kanisani ilikuwa lini. Viongozi wa dini ambao husema
binadamu humkumbuka Mungu nyakati za shida huwenda hawakuwa wamekosea
kwani kama isingekuwa shida sina hakika kama ningekuwa eneo lile.
Mara baada ya kuingia mle ndani nikasimama kidogo huku nikiyatazama kwa
utulivu mabenchi mengi ya kanisa yaliyopangwa katika pande mbili kushoto na kulia
yakiacha nafasi ya kupita katikati. Wakati huu mabenchi yale hayakuwa na mtu hata
mmoja na hivyo kupelekea kanisa lote litawaliwe na ukimya wa aina yake.
Kupitia madirisha makubwa ya kanisa lile ambayo baadhi yalikuwa wazi niliweza
kuyaona mapazia mepesi yakipepea kutokana na upepo hafifu uliosababishwa na
mvua iliyokuwa ikinyesha nje na upepo ule sasa ulikuwa ukiisukasuka mishumaa
michache iliyokuwa ikiwaka mbele ya madhabahu ya kanisa lile.
“Karibu sana kijana” sauti tulivu ya kizee ilisikika kutoka mbele ya madhabahu ya
kanisa lile na hapo nikashtuka kuwa kumbe mle ndani sikuwa peke yangu.
“Ahsante!” niliitikia pasipo kumuona yule mtu aliyenikaribisha huku nikianza
kutembea taratibu nikielekea mbele ya kanisa lile na baada ya kuyatembeza macho
yangu kule mbele ya kanisa nikamuona mzee mmoja akiwa ameketi kwenye kiti
nyuma ya meza fupi iliyofunikwa kwa vitambaa vyeupe vyenye alama za misalaba
iliyodariziwa vizuri huku akiwa amevaa mavazi meupe. Nilipomchunguza vizuri mzee
yule nikatambua kuwa umri wake ulikuwa ni miaka sabini na ushei. Mzee yule alikuwa
amejiegemeza vizuri kwenye kiti chake cha utukufu huku mikono yake ikiwa imeshika
Biblia ambayo haraka aliwahi kuiweka mezani baada ya kuniona.
“Shikamoo mzee!” nikamsalimia yule mzee
“Marahaba kijana karibu sana!” mzee yule akaniitikia huku akinitazama kwa
shauku.
“Ahsante sana” nikamwitikia huku nikitafuta nafasi nzuri kwenye benchi la mbele
la kanisa lile na kuketi. Yule mzee aliupisha utulivu kidogo huku akinitazama hadi
pale nilipoketi na yeye ndiyo akasimama na kuanza kutembea akija pale nilipokuwa
nimeketi. Yule mzee mchungaji wa kanisa lile aliponifikia pale nilipoketi nikasimama
na kusalimiana naye kisha wote tukaketi. Hata hivyo aliendelea kunitazama kwa
utulivu na hapo nikajua kuwa bila shaka alikuwa ameshangazwa na ugeni wangu.
“Jina langu naitwa Chaz Siga”
“Pastor Romanus Mugonzibwa” yule mzee akajitambulisha huku akinitazama
kwa makini kisha akaitoa miwani yake usoni na kufikicha macho yake kidogo na
alipomaliza akairudishia ile miwani yake machoni na kuongea
“Karibu sana nyumbani kwa Bwana”
“Nina shida Pastor au labda nisema nahitaji elimu ya kiroho” maelezo yangu
yakampelekea Pastor Romanus atabasamu kidogo na kupelekea makunyanzi ya uzee
yazidi kujitokeza usoni mwake.
“Umefanya jambo jema kuja kanisani kwani ni vijana wachache wa zama hizi
wanaoenda kwenye nyumba za ibada kutafuta elimu ya kiroho” Pastor Romanus
akakohoa kidogo kusafisha koo lake kisha akaniuliza.
“Shida gani kijana?”
“Nahitaji kufahamu kama kuna uhusiano wowote wa mambo ya kiroho na namba
666” niliongea kwa utulivu huku nikimtazama Pastor Romanus. Kilichonipelekea
kufika kwenye kanisa hili ni umaarufu alikuwanao Pastor Romanus katika kufafanua
masuala mbalimbali ya kiroho. Siku fulani za huko nyuma vipindi vyake vya ufafanuzi
wa masuala mbalimbali ya kiroho vilikuwa vikirushwa hewani na vyombo mbalimbali
vya habari vya jijini Dar es Saalm na hivyo kumjengea umaarufu mkubwa. Pastor
Romanus akanitazama kama aliyeshangazwa na shida yangu au pengine lile halikuwa
swali alilolitarajia kutoka kwangu.
“Hiyo ni namba ya chapa ya mnyama” Pastor Romanus akaongea kwa utulivu
akiweka kituo kisha akaendelea
“Kama wewe ni msomaji mzuri wa maandiko matakatifu ya Biblia huwenda
ukafahamu ninachozungumza” Pastor Romanus akaongea huku akionekana
kutafakari kisha akaniambia kwa utulivu
“Hebu subiri kidogo” kisha nikamuona Pastor Romanus akisimama na kuanza
kutembea kizeezee akielekea kwenye ile madhabahu ya kanisa na muda mfupi
iliofuata nikamuona akipotelea kwenye mlango fulani uliokuwa upande wa kushoto
wa madhabahu ile.
Niliendelea kuketi pale kwenye benchi huku nikimsubiri Pastor Romanus na
baada ya kitambo kirefu mara nikamuona akirejea na kitabu fulani kikubwa mikononi
ambacho hapo awali sikuwahi kukiona katika harakati zangu. Nilikitazama kitabu
kile mikononi mwake huku nikishangazwa na ukubwa wake. Kurasa za kitabu kile
zilikuwa chakavu mno zikiashiria kuwa kitabu kile kilikuwa kimetumika kwa miaka
mingi.
Pastor Romanus akaja na kuketi kando yangu kisha akafunua kurasa kadhaa za
kile kitabu na kuweka kituo akiyapitia maelezo fulani kama anayetafakari baadaye
nilimuona akigeuka na kunitazama.
Kwenye maandiko ya Textus receptus katika agano jipya la Biblia kitabu cha Ufunuo
wa Yohana 13:16-18 maandiko yanaihusisha namba 666 na chapa ya mnyama ama
The Beast ambaye ndiye shetani. Namba hii imeanza kusambazwa na inaendelea
kusambazwa kwa vizazi vya dunia hii vinavyoshikama na matendo ya kishetani. Lengo
kubwa hasa ni shetani kuhakikisha kuwa anaongeza idadi ya binadamu wengi zaidi
katika ufalme wake ambao atahukumiwa nao wakati utakapofika” Pastor Romanus
aliweka kituo na kukohoa kidogo na hapo nikapata swali la kumuuliza
“Kwa hiyo hao washirika wa shetani ni lazima wawe na hii chapa 666?”
“Ni utambulisho kwa watu wake ingawa maandiko yanaeleza kuwa mara baada
ya unyakuo wa wacha Mungu kufanyika chapa hii 666 itaingia kwenye matumizi
rasmi kwa walioachwa kwenye unyakuo huo ambao ndiyo washirika wa huyo shetani.
Watu hao watakaoachwa baada ya unyakuo huo ambao ni watu wa aina zote;wadogo
kwa wakubwa,matajiri kwa maskini,watumwa na walio huru watatiwa chapa katika
mikono yao ya kuume au katika vipaji vya nyuso zao ili kwamba mtu yeyote asiweze
kununua wala kuuza isipokuwa mwenye chapa hiyo tu”
“Kwa nini itakuwa hivyo?” nikamuuliza Pastor Romanus kwa utulivu.
“Maandiko yatimie lakini vilevile tambua kuwa mara baada ya unyakuo huo
wapo baadhi ya binadamu watakaoachwa ambao watashtukia kuwa wamedanganywa
na shetani. Sasa kitu kitakachowaokoa watu wa namna hiyo ni kuhakikisha kuwa
hawatiwi chapa ya huyu mnyama jambo ambalo naweza kusema siyo rahisi hata kwa
kulisikia” Pastor Romanus akaweka kituo na kuyapeleka macho yake tena kwenye
kile kitabu na hapo nikapata nafasi ya kutafakari huku nikiyakumbuka mambo yote
niliyoyaona ndani ya ule mlango mweusi kwenye lile jengo la ghorofa lililopo eneo la
posta jijini Dar es Salaam.
Mvua bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na kwa mbali niliisikia ikianguka kwenye
paa la kanisa lile huku upepo uliokuwa ukipenya kupitia madirishani ukiendelea
kuisukasuka ile mishumaa iliyokuwa ikiwaka pale madhabahuni mle kanisani.
“Huu ulimwengu sasa unaelekea wapi?” nikajiuliza huku nikitafakari na hapo
Pastor Romanus akageuka na kunitazama kwa udadisi.
“Huu ndiyo muda wa binadamu kutubu na kuacha dhambi wakimkimbilia
Mungu kwani baada ya hapa hakutakuwa na neema hii” Pastor Romanus akaongea
kwa masikitiko huku akionekana kufikiria jambo kisha akaendelea.
“Watu wa zama hizi hawamwogopi Mungu kabisa na ndiyo maana unaweza
kuwasikia baadhi ya wasanii,wanasiasa na wanamichezo wakijinadi kuwa eti wao ni
marafiki wa shetani lakini hawafahamu kuwa shetani huwa hana urafiki na kiumbe
chochote cha Mungu”
“Kwa hiyo wale watu wasiokuwa na hiyo chapa 666 ya mnyama wapo salama?”
nikauliza kwa udadisi.
“Hapana!” Pastor Romanus akaongea kwa msisitizo ”Kwanza ni lazima ufahamu
kuwa hii chapa ya mnyama ninayoizungumzia hapa siyo lazima sana ukaiona kwa
macho ikiwa imeandikwa katika hizo sehemu za miili ya wanadamu nilizozitaja hapo
awali. Lakini ukichunguza utagundua kuwa mfumo wa namna hii tayari umeanza
kutumika katika baadhi ya nchi zilizoendelea kiuchumi na baadaye mfumo huu
utasambaa dunia nzima.
Kwa mfano katika chapisho la mwandishi mmoja anayeitwa Mac Slavo wa huko
nchini Marekani amezungumzia vizuri juu ya seli ndogo zilizoanza kupandikizwa
katika miili ya binadamu huko Marekani. Teknolojia iitwayo Human-implanted microships
ambayo kwa siku za usoni itakuwa siyo jambo la kushangaza tena hapa duniani.
Ingawa maendeleo ya teknolojia katika dunia ya sasa siyo jambo la kupinga kwani
ni utabili wa maneno ya Mungu hata hivyo ni vizuri kuwa na maarifa ya kuweza
kuelewa kama maendeleo hayo yanavunja taratibu za Mungu au yapo katika makusudi
yake.
Watafiti wa maandiko matakatifu wanasema kuwa dunia hii tuliyonayo inaelekea
kwenye mfumo wa kishetani uitwao New World Order ambapo chapa 666 inatoa ishara
tosha katika utimilifu wa mifumo yote ya maisha ya binadamu ambayo imetengana na
Mungu na vilevile ipo kwenye nguvu ya msukumo mkubwa wa shetani na washirika
wake” Pastor Romanus akaweka kituo na kukohoa kidogo akilisafisha koo lake na
hapo nikageuka na kumtazama huku nikiendelea kuyatafakari maelezo yake. Kwa
kweli bado nilikuwa bado sijamuelewa vizuri.
“New World Order ni nini?” hatimaye nikamuuliza kwa udadisi.
“New world order ni Conspiracy theory au mikakati ya siri iliyoandaliwa kwa usiri
mkubwa na jamii ya wapinga Mungu na watu wenye nguvu kubwa za kishetani
ambao lengo lao kuu ni kuitawala dunia hii kwa kusimamisha utawala wa dunia
wenye serikali moja ambayo haitokuwa na uvumilivu kwa watu au vikundi vyovyote
vya watu watakaokuwa na mtazamo tofauti na wao au utawala wa kidikteta katika
sehemu zote za mfumo wa binadamu Authoritarian world government. Hivyo mataifa
yote huru ya dunia hii ama Sovereign nation-states yatamezwa na mfumo huu” Pastor
Romanus akatulia kidogo akiutumia wakati ule kuyapitia maelezo fulani kwenye kile
kitabu chake na mara hii nikajisikia faraja kuwa nilikuwa sijapoteza muda wangu kuja
pale na kutafuta msaada wake” Baada ya kitambo kifupi cha ukimya Pastor Romanus
akavunja ukimya na kuendelea.
“Mapema sana kabla ya miaka ya 1990 nadharia ya mkakati wa siri wa New World
Order ilikuwa ikifuatwa na makundi mawili makubwa ya huko Marekani. Kundi la
kwanza lilikuwa ni lile lililokuwa likipinga sheria za serikali ama Militantly anti-government
right na kundi la pili lilikuwa ni lile la Fundamentalist christianity ama kundi la wakristo
wenye msimamo mkali. Lakini sasa hata wewe ni shahidi kuwa huu msimamo mkali
unaendelea kuenea kwa kasi hata katika baadhi ya imani nyingine duniani”
“Kwa kweli nilikuwa sifahamu kabisa kuhusu haya mambo” nikaongea kwa
utulivu huku nikitafakari.
“Bado naendelea kutoa elimu hii kwa sababu watu wengi bado hawaelewi kile
kinachoendelea. Hata hivyo kizazi hiki ni kizazi cha ukaidi na hakina tofauti kabisa na
kizazi cha Nuhu. Muda uliobaki ni mfupi sana kuliko unavyodhani kabla ya mambo
haya kutimia. Amani inayoendelea kumomonyoka katika maeneo mbalimbali ya hapa
duniani ni ishara tosha.
Bado kuna mifano mingi ya kukuthibitishia juu ya hiki ninachokizingumza. Mifano
mizuri ya hizo Conspiracy theories ni ule wa End Time Conspiracy theory iliyoandikwa
na John Nelson Darby ikielezea nadharia ya New World Order kwa kuchambua vizuri
maandiko matakatifu kutoka katika vitabu vya Biblia kama kitabu cha Ezekieli,kitabu
cha Danieli na kile cha Ufunuo wa Yohana ambapo vimeelezea kwa kina kuwa watu
wengi wamemkana Mungu na kumkimbilia shetani ili wapate utajiri na nguvu za
kishetani zenye utatu usiyo wa kitakatifu. Utatu unaoundwa na shetani,mpinga kristo
na mitume wa uongo walioenea kila kona ambao lengo lao kuu bado ni lilelile la
kuitawala dunia kwa misingi ya kishetani.
Conspirancy theory nyingine ni ile ya jumuiya ya freemasonry iliyoanzishwa mwishoni
mwa karne ya 16 na mapema sana mwanzoni mwa karne ya 17. Kwa muda wa miaka
mingi jamii hii yenye mikakati ya siri ya kuitawala dunia kinyume na mipango ya
Mungu imekuwa ikishutumiwa kwa kuingiza ajenda za kisiasa katika serikali za hapa
duniani ile hatimaye dunia itawalike kwa kufuata misingi yao.
Katika miaka ya 1890 mwandishi wa kifaransa akifahamika kwa jina la Léo Taxil
aliandika msururu wa machapisho na vitabu vinavyoelezea freemasonry kama jamii ya
kishetani ikizituhumu nyumba zao za kulala wageni au Lodges kuwa zilikuwa zikitumika
kumuabudu lusifa ambaye ndiye shetani kuwa ndiye mwenye nguvu na mamlaka yote
na ndiye mjenzi mkuu wa hii dunia.
Conspiracy theory nyingine ni ile ya illuminati ambayo ni jamii nyingine yenye
mikakati ya kisiri iliyoanzishwa na profesa wa chuo kikuu akifahamika kwa jina
Adam Weishaupt tarehe moja mwezi wa tano mwaka 1776 katika eneo la Upper
Bavaria huko nchini Ujerumani. Misingi ya jamii hii ni kuamini katika uhuru wa
mawazo,liberalism,republicanism,secularism na usawa wa kijinsia huku akiwa amepata
elimu hiyo kutoka kwenye Lodges za freemasonry vitu ambavyo ni tofauti kabisa na
misingi ya Mungu.
Conspiracy theory nyingine ni ile ya itifaki ya kiyahudi ifahamikayo kwa jina la The
Protocols of the Elders of Zion iliyoandikwa nchini Urusi mwaka 1903 ikiwa na misingi
ileile ya kuitawala dunia. Vidokezo kutoka kwenye mkutano ya siri wa cabal wa baadhi
ya viongozi wa kiyahudi ambao waliamua kushirikiana na jamii ya freemasonry katika
kupanga mipango kwa niaba ya wayahudi kuitawala dunia kwa kuamini kuwa wao
ndiyo waliochaguliwa na Mungu.
Kwenye Conspirancy theory nyingine ni ile ya Round Table iliyoanzishwa kwenye
karne ya mfumo wa Imperialism katikati ya mwaka 1815 na mwaka 1914 na mzungu
mmoja aliyezaliwa Afrika ya kusini,mfanyabiashara,mchimba madini na mwanasiasa
akifahamika kwa jina la Cecil Rhodes ambapo alitengeza mkakati wa kuifanya dola ya
Uingereza kuunda serikali yenye utawala wa shirikisho ambayo itakuwa na nguvu na
kuimiliki amani ya dunia.
Katika muswada wake ulioandikwa mwaka 1877 akiwa na umri wa miaka 23 tu
Cecil Rhodes alieleza kuwa alikuwa amenuia kuimwagia pesa jamii ya siri au Secret Society
inayojulikana kama Society of the Elect ambayo ndiyo ingetekeleza malengo yake. Mwaka
1902 gazeti la New York Times liliandika kwamba kufuatia muswada wake wa mwaka
1877,Cecil Rhodes katika mwaka 1890 alitia msisitizo wa muswada wake huku akisisitiza
kuwa malengo ya jamii ya siri ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati wa taratibu
wa kushikilia utajiri wote wa dunia.
Open conspiracy theory ya mwaka 1928 iliyoandikwa na mwandishi wa Uingereza
na mwanamitazamo maarufu aitwaye H.G.Wells. Yeye aliupa nguvu na msukumo
mkubwa mfumo wa Cosmopolitanism kisha akatoa mwongozo wa mapinduzi ya dunia
na mhimili wa dunia kwa kuanzisha dunia yenye utawala wa teknolojia ya viwango vya
juu na mipango ya kiuchumi ambapo dhana hiyo ameilezea vizuri katika kitabu chake
cha mwaka 1940 kiitwacho The New World Order” Pastor Romanus akaweka kituo
kama anayetafakari na hapo nikaweka kituo nikimtazama kwa makini na kushangazwa
sana na utashi wake katika masuala yale yaliyofichika.
“Cosmopolitanism ni nini?” nilimuuliza.
“Cosmopolitanism ni nadharia ambayo inasema kuwa matabaka ya jamii zote duniani
yanatokana na jamii moja” Pastor Romanus akanijibu huku akinitazama na hapo
nikatikisa kichwa kumuonesha kuwa nimemuelewa na baada ya kukohoa kidogo
akaendelea
“Conspiracy theory nyingine ni ile ya Population Control. Wanatheolojia wa nadharia
hii wanaamini katika New World Order ambayo itaingizwa katika mfumo wa maisha
ya binadamu kwa kudhibiti ongezeko la idadi ya watu duniani ili iwe rahisi kwao
kusimamia na kudhibiti harakati za mtu mmoja mmoja. Hii ni tofauti na mipango
ya Mungu kwani ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 1:28 ambapo Mungu anawataka
binadamu wazaane na kuongezeka hapa duniani.
Kwa mujibu wa maelezo ya nadharia hii ni kuwa udhibiti wa ongezeko la idadi ya
watu utafanyika kupitia afya ya uzazi ambapo mikakati ya uzazi wa mpango ambayo
itawafanya watu wasizaane,watumie vidonge vya kuzuia mimba au utoaji wa mimba
au kupungua idadi kubwa ya watu duniani kwa majanga ya mara moja mfano mauaji
ya kimbari kwa kuanzisha vita visivyo na sababu za msingi. Kueneza magonjwa
hatari ya kuambukiza yasiyokuwa na tiba au pengine tiba zake ni za gharama sana au
kusababisha majanga ya mazingira kwa kuwa na mfumo wa kudhibiti hali ya hewa“
Pastor Romanus akaweka kituo kisha akakohoa kidogo na kunitazama kabla ya
kuendelea
“Mind Control ni conspiracy theory nyingine ambapo jamii inaituhumu
serikali,mashirikisho na vyombo vya habari kwa kuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kuwa kunakuwa na aina fulani ya umoja usiokuwa na maana kwa watu
wake na kupandikiza utamaduni wa kuogopa utawala ambao utapelekea jamii ya
kishetani iendelee kushikilia madaraka ya serikali na hivyo mfumo wa New Word Order
kujiingiza kirahisi duniani” Pastor Romanus akaweka kituo kidogo na kunitazama
kisha akaniambia
“Kijana!,pengine ukaona kama ninayekupotezea muda wako mwingi kwa
kukueleza haya yote lakini nafanya hivi kwa sababu maelezo haya ni sehemu ya majibu
ya swali lako”
“Ondoa shaka Pastor mimi nipo tayari kukusikiliza” nikaongea kwa utulivu na
hapo Pastor Romanus akatabasamu kidogo na kuyapelekea mapengo yake mawili
yaonekane vizuri bila kificho kisha tabasamu lake lilipofifia na kutoweka akaendekea
“Conspiracy theory nyingine ni ile ya Mass Survaillance. Katika nadharia hii
wanatheolojia wanaamini kuwa utawala wa New Word Order umeanza kuingizwa
duniani au utaingizwa kupitia mapinduzi makubwa ya akili za binadamu katika
masuala ya teknolojia ambayo matumizi yake yanaunganisha jamii kubwa ya watu.
Kwa mfano utumiaji wa teknolojia ya Barcode katika bidhaa za viwandani. Alama
fulani katika bidhaa zinazotumika au kusambazwa duniani mfano teknolojia ya RFID
tagging inayotumia seli ndogo zilizopandwa kwenye bidhaa. Matumizi ya mifumo
ya mikusanyiko ya taarifa mbalimbali za watu ama Database systems katika maeneo
mbalimbali” Pastor Romanus akaweka kituo tena na kunitazama kama aliyetaka
kupata hakika kuwa nilikuwa nikimsikiliza au lah!. Kitendo cha kuniona nikimtazama
kikampelekea aendelee na mada yake.
“Coup d’état ni conspiracy theory nyingine ambapo wanatheolojia wanaamini kuwa
mfumo wa kishetani wa utawala wa dunia yaani New World Order utaingizwa katika
utawala wa serikali za dunia kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali
zisizotaka kukubaliana na mfumo wa aina hii. Mara baada ya mapinduzi hayo utawala
wa kishetani utasimika viongozi wanaowataka ambao watakuwa tayari kukubaliana na
mfumo huu wa New World Order ambao dalili zinaonesha kuwa utakuwa ukisimamiwa
na jumuiya ya umoja wa mataifa.
Mifano bado ni mingi sana kwa mfano wanatheolojia katika Gradualism conspiracy
theory wao wanaamini kuwa utawala wa New World Order taratibu umeshaanza
kuingizwa katika mifumo ya utendaji ya mashirikisho makubwa ya kimatifa. Mfano
katika shirika la nchini Marekani la Federal Reserve System mwaka 1913. The League of
Nations mwaka 1919. Shirika la fedha duniani International Monetary Fund mwaka 1944.
The United Nations mwaka 1945. Benki ya dunia mwaka 1945. Shirika la afya duniani
WHO mwaka 1993. Shirika la biashara duniani WTO mwaka 1998. Umoja wa nchi za
Afrika mwaka 2002 na katika muungano wa mataifa ya kusini mwa bara la Marekani
mwaka 2008.
Mifano bado ni mingi sana ni bahati mbaya tu kuwa sina muda wa kuelezea mambo
yote kwa sasa japokuwa napenda ujue hali ya dunia hii kule inapoelekea. Nitakapopata
muda wa kutosha nitakueleza conspiracy theories nyingine za New World Order kama ile ya
Occultism,Fourth Reich,Brave New World na ile ya viumbe wa ajabu katoka sayari ya mbali
wanaotabiriwa kuja kuivamia hii dunia iitwayo Alien invansion conspirancy theory” Pastor
Romanus akamaliza kunieleza kisha akafunika ukurasa wa kile kitabu na kuupisha
utulivu huku akiangalia mbele ya lile kanisa kama anayefikiria jambo fulani.
“Lakini Pastor huoni kuwa haya mambo yamekaa katika mtazamo wa kidini?”
hatimaye nikavunja ukimya na kumuuliza.
“Hapo ndiyo ugumu wa watu kuelewa ulipo. Watu wengi hudhani kuwa kwa
kuwa mambo haya yanazungumzwa na mtu wa imani tofauti basi wao ambao hawapo
kwenye imani hiyo mambo haya hayawahusu. Hii dunia ni ya kwetu sote na janga
linapokuja huwa halichagui dini ya mtu na vilevile mambo haya yana ushahidi ingawa
bado kwa mtu asiyetaka kuelewa anaweza kuyachukulia mambo haya katika mtazamo
ya kidini. Viongozi wa dini tuliyobahatika kuyafahamu mambo haya tunakesha katika
kuwafahamisha watu lakini siyo busara kumlazimisha mtu atuelewe. Kila binadamu
atakuja kuelewa pale nafsi yake itakapokuwa tayari” Pastor Romanus akaongea kwa
masikitiko.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Wewe unavyodhani huu mfumo wa New World Order umeshaanza kujipenyeza
barani Afrika?” nilimuuliza Pastor Romanus na hapo akageuka taratibu na kunitazama
kwa mshangao kisha nikamuona akitabasamu.
“Siku zote waumini wazuri wa dini huwa hawajitangazi!” maneno ya Pastor
Romanus yakinipelekea nitabasamu kidogo na kabla sijatia neno akaendelea
“Viongozi wengi wa nchi za Afrika na kwengineko duniani wameshaukubali
mfumo huu aidha kwa kuutaka,kwa kujua au kwa kutokujua. Viongozi wa hizi nchi
zetu za Afrika wao ndiyo wako kwenye mtego mkubwa kwani kutokana na umasikini
uliokithiri katika nchi zao na tamaa za kupata utajiri mkubwa na kupenda kung’ang’ania
madarakani. Hivyo wanajikuta wakikubali kila kitu kutoka kwa viongozi wa mataifa
makubwa yaliyoendelea kiuchumi ambao ndiyo wadua wakubwa wa mfumo huu wa
New World Order.
Baadhi ya viongozi wetu wa Afrika wamekuwa kama msichana mwenye nuksi
ya kuolewa ambaye kuolewa kwake imekuwa ndoto ya kuisikilizia kwenye bomba.
Hivyo anapotokea mwanaume yoyote wa kumuoa hata kama hana vigezo vyake yeye
humkubalia tu ili ndoto yake itimie hata kama hiyo ndoa ni batili.
Kwa mfano chama cha kimataifa cha wanaume mashoga na wanawake wasagaji
kiitwacho International Gay and Lesbian Association katika taarifa zake za kongamano
la dunia kimetoa makadirio ya takwimu kwa kusema kuwa suala la ushoga angalau
limejadiliwa kwa namna tofauti katika nchi 38 za barani Afrika. Hivyo ukitoa idadi
hiyo kutoka katika jumla ya idadi ya nchi za Afrika ambazo ni 54 utagundua kuwa ni
nchi 16 tu ambazo hazijaruhusu mijadala ya ushoga na usagaji kufanyika. Na katika
majadiliano hayo nchi 13 za barani Afrika zimeonekana kuwa baadhi yao zimepitisha
sheria za kuruhusu vitendo vya ushoga na usagaji na nyingine hazikuruhusu au kutoa
tamko la kupitisha. Hivyo ukichunguza vizuri utagundua kuwa hata hizi nchi ambazo
hazikutoa tamko lolote kwa maana nyingine ni kuwa hazina shida ya moja kwa moja
na suala hili.
Taarifa za chama hicho zimeeleza kuwa angalau vitendo vya kujamiana kwa watu
wa jinsia moja bado havijatambulika rasmi kuwa ni kosa katika baadhi ya nchi za Afrika
kama Burkina Faso,Central African Republic,Chad,Republic of Congo,Côte d’Ivoire,Democratic
Republic of Congo,Gabon,Madagascar,Mali,Niger na Rwanda.
Tangu mwaka 2011 baadhi ya nchi za dunia ya kwanza zimeanza mchakato wa
kuzuia na nyingine zimepitisha sheria ambazo zinaruhusu kusitisha mgao wa pesa za
bajeti au kupunguza mgao huo kwa serikali za nchi za Afrika ambazo bado zinapingana
vikali na masuala ya ushoga na usagaji. Ingawa baadhi ya nchi hizi za Afrika zinapinga
vikali masuala ya ushoga na usagaji kwa kudai kuwa ni vitendo visivyoendana na mila
na dini za bara la Afrika.
Katika nchi za Mauritania,Sudan na kaskazini mwa nchi ya Nigeria adhabu ya
kushiriki vitendo vya ushoga na usagaji ni kifo. Katika nchi ya Uganda,Tanzania na
Sierra Leone washiriki wa vitendo vya ushoga na usagaji adhabu yake huwa ni kifungo
cha maisha. Lakini ni kweli kuwa hapa nchini kuna mtu yeyote aliyefungwa kifungo
cha maisha kwa ajili ya kushiriki vitendo vya namna hii?. Jibu unalo mwenyewe.
Katika nchi ya Afrika ya kusini katiba ya nchi hiyo kwa kiasi kikubwa inatoa mwanya
wa haki za mashoga,wasagaji na kuunga mkono ndoa za jinsia moja” Pastor Romanus
akaweka kituo kisha akakohoa kidogo kulilainisha koo lake.
“Sasa nimeanza kupata picha kamili ya mambo yalivyo,kuwa hii chapa 666 ni
mpango wa shetani na ina nafasi kubwa katika hii mikakati ya siri ya kusimamisha
serikani ya dunia yenye nguvu kubwa za kifedha na kishetani” niliongea kwa utulivu
huku nikihisi kuwa nilikuwa nimepata ufahamu mzuri wa masuala ya hii dunia. Pastor
Romanus akafurahi huku akizipangusa kingo za mdomo wake kwa ulimi kabla ya
kuongea kwa utulivu
“Idadi ya wacha Mungu katika hii dunia ni ndogo sana kama kipande cha ubao
moja kwenye safina ya Nuhu. Sisi kama watumishi wa Mungu kazi yetu ni kuwahubiria
watu waache dhambi na kumwabudu Mungu kwani yeye ndiye mwenye milki ya
vitu vyote hapa duniani na mbinguni. Baadhi ya watu wametusikia na kutuelewa na
wamebadilika kwani katika zama hizi kumuona mchawi anaacha kula nyama za watu
na kukimbilia mishkaki ni jambo la kumshukuru sana Mungu”
Niliangua kicheko hafifu na kumtazama Pastor Romanus kwa umakini na hapo
akanitupia swali
“Unaweza kuniambia hasa ni kitu gani kilichokupelekea ufunge safari kutoka
huko utokako na kuja hapa kanisani usiku huu kuuliza juu ya hiyo namba 666?” swali
la Pastor Romanus lilikuwa la kushtukiza na kwa kiasi fulani liliyahamisha mawazo
yangu kichwani hata hivyo huwenda ningemshangaa sana endapo asingeniuliza swali
lile hadi ukomo wa maongezi yetu. Hivyo niliviminyaminya vidole vyangu mikononi
huku nikitafakari kisha nikageuka na kumtazama Pastor Romanus na macho yetu
yalipokutana nikaanza kujieleza kuwa mimi na nani,nafanya kazi gani na kwanini
nilikuwa nimefika pale. Maelezo yangu yalikuwa yamenyooka na hivyo wakati
nikimalizia kutoa utambulisho wangu Pastor Romanus alinipa mkono na kunipongeza
japokuwa niliona mashaka kidogo katika uso wake.
“Wewe ni mpelelezi?” hatimaye Pastor Romanus akaniuliza huku akinitazama
usoni na kwa hakika swali lake lilinishangaza sana. Nilishikwa na mduwao kidogo na
fikra zangu zilipopata utulivu nikamjibu
“Ndiyo!,mimi ni mpelelezi” nikaongea kwa utulivu
“Nilikufahamu tangu wakati ulipokuwa anaingia humu ndani. Nimewahi kukutana
na wapelelezi mara kadhaa baadhi yao wakitaka kunipeleleza juu ya huduma yangu”
Pastor Romanus akaongea kwa utulivu huku akigeuka tena na kunitazama.
“Napeleleza juu ya kupotea kwa mpelelezi mwenzangu”
“Anaitwa nani?”
“Gabbi Masebo”
Mara tu nilipomaliza kuongea Pastor Romanus akanitazama kwa mshangao.
“Gabbi Masebo!...” Pastor Romanus akaongea kwa utulivu huku akitafakari.
“Hakuna anayefahamu Gabbi Masebo alipo. Muda mfupi baada ya kufunga ndoa
miaka kumi iliyopita alichana na mkewe na baada ya hapo Gabbi Masebo anasemekana
kutoweka kusikojulikana” nikaongea kwa utulivu huku nikiichukua ile picha ya Gabbi
Masebo kutoka mfukoni na kumuonesha Pastor Romanus. Baada ya kitambo kifupi
cha ukimya huku Pastor Romanus akiitazama ile picha mara nikamuona akigeuka na
kunitazama
“Unamfahamu?” nikawahi kumuuliza.
“Gabbi Masebo alikuwa rafiki yangu” Pastor Romanus akaongea kwa utulivu
halafu kama niliyeshtushwa na maelezo yake nikageuka haraka na kumtazama kwa
shauku. Nilimuona Pastor Romanus akiacha kuitazama ile picha mkononi mwangu na
badala yake akayahamishia macho yake kutazama mbele ya ile madhabahu ya kanisa.
Nilipomtazama vizuri nikatambua kuwa fikra zake hazikuwa pale. Mvua kubwa bado
ilikuwa ikiendelea kunyesha kwani niliweza kuisikia vizuri namna iliyokuwa ikianguka
juu ya paa la kanisa lile.
“Alikuwa akifika hapa kanisani mara kwa mara lakini hakuwahi kuniambia kuwa
yeye ni mpelelezi ingawa baadaye nilianza kuhisi kuwa alikuwa akichunguza jambo
fulani ambalo mimi sikulifahamu”
“Unafahamu kuwa alifunga ndoa?”
“Nilipata habari tu na sikumbuki habari hizo nilizipata kutoka kwa nani lakini
ndoa yake hakuifungia hapa” Pastor Romanus akaongea kwa hakika.
“Uliwahi kusikia tetesi zozote juu ya mkewe?” nilimuuliza Pastor Romanus huku
nikimtazama usoni kuyapima maelezo yake.
“Niliambiwa kuwa huyo msichana aliyemuoa alikuwa muumini wa hapa lakini
kwa sasa simkumbiki na huwenda Gabbi Masebo alikuwa akifika hapa katika harakati
za kumnasa huyo msichana japo sina hakika”
“Unadhani ni kwanini hawakufungia ndoa yao hapa kanisani kwako?”
“Sifahamu ingawa mara nyingi wasichana wengi wanapopata wanaume wa
kuolewa suala la wapi wakafungie ndoa yao huwa ni la mwanaume. Wasichana hufuata
maamuzi ya makanisa yale ambayo waume zao watarajiwa ndiyo wanapoamini na
huwenda hilo ndiyo lililotokea”
“Wewe kama kiongozi wa kanisa huwa hupewi taarifa juu ya wapi ndoa za
waumini wako zinapofungiwa?”
“Baadhi huona kuwa ni sahihi kuniambia na mimi huwaombea baraka zote lakini
wengine huamua kufanya mambo yao kimyakimya hivyo ni vigumu kufahamu”
Pastor Romanus akaongea kwa utulivu huku akiyatafakari maelezo yangu.
“Kwa hiyo mke wa Gabbi Masebo alikuwa muumini wa kanisa lako?” nilimuuliza
Pastor Romanus huku nikimtazama.
“Ni vigumu sana kumfahamu kila muumini wa hapa kanisani hususani katika jiji
lenye watu wengi kama hili la Dar es Salaam. Kama nilivyokuambia hapo awali taarifa
hizo nilizipata kwa waumini ambapo sasa siwakumbuki” Pastor Romanus akaongea
kwa msisitizo na nilipomtathmini vizuri nikatambua kuwa kulikuwa na ukweli katika
maneno yake. Nilitulia kidogo nikiupisha utulivu kichwani mwangu kwani maelezo ya
Pastor Romanus yalikuwa yametowesha ukungu kidogo katika fikra zangu.
“Nahitaji msaada wako Pastor” hatimaye nilivunja ukimya huku nikimtazama
Pastor Romanus kwa makini.
“Msaada upi?” Pastor Romanus akaniuliza kwa shauku
“Nahitaji kupata taarifa zinazojitosheleza juu ya Gabbi Masebo na huyo msichana
aliyefunga naye ndoa. Nina hisia kubwa kuwa huwenda kupotea kwa Gabbi
Masebo,msichana aliyefunganaye ndoa na hawa watu wasioeleweka kwenye lile jengo
la ghorofa la kule posta nililokuelezea hapo awali kwenye maongezi yangu kuwa kuna
uhusiano wa namna fulani”
“Sasa mimi nitakusaidiaje?” Pastor Romanus akaniuliza kwa utulivu
“Nahitaji kufahamu ni wapi hiyo ndoa ya Gabbi Masebo na huyo binti
anayesadikika kuwa alikuwa ni muumini wako ilipofungwa. Nahitaji pia unitafutie jina
la huyo msichana aliyefunga ndoa na Gabbi Masebo”
“Unadhani ni jambo rahisi?. Makanisa ni mengi sana hapa jijini Dar es Salaam”
Pastor Romanus akaongea kwa msisitizo.
“Najua siyo jambo rahisi lakini kwa uzoefu na mamlaka uliyonayo kupata taarifa
za namna hiyo naamini inawezekana” nilimwambia Pastor Romanus na hapo ukimya
ukafuatia hivyo nikajua kuwa kwa vyovyote alikuwa akitafakari ombi langu.
“Nitajaribu lakini hili siyo jambo la kukupa sana matumaini. Hata hivyo ningependa
kwanza kufahamu kwanini unazihitaji taarifa hizi” ombi la Pastor Romanus
likanipelekea nitabasamu kidogo kisha nikayafikicha macho yangu na kupiga mwayo
hafifu wa uchovu.
“Nafanya upelelezi kutaka kufahamu ukweli kama Gabbi Masebo yupo hai au
amekufa na kama amekufa nifahamu kuwa amezikwa wapi na nini chanzo cha kifo
chake”
“Baada ya kufahamu je?”
“Ndugu zake watafahamishwa na hapo kazi yangu itakuwa imefika ukomo”
niliongea kwa msisitizo na hapo Pastor Romanus akanitazama kwa makini kabla ya
kuvunja ukimya.
“Nafahamu nini kinachoendelea hata hivyo hili ni jambo hatari linaloweza
kugharimu uhai wa mtu” Pastor Romanus akaongea kwa utulivu huku maelezo
yake yakiibua shauku ya aina yake usoni mwangu hali iliyonipelekea niketi vizuri na
kumtazama kwa makini.
“Unafahamu nini?” hatimaye nikamuuliza kwa udadisi na hapo Pastor Romanus
akanitazama kwa utulivu kabla ya kuvunja ukimya.
“Nahisi lipo jambo kubwa lililofichika nyuma ya kutoweka kwa Gabbi Masebo
ambalo huwenda likawa kwa namna moja au nyingine lina maslahi makubwa kwa
serikali kama siyo baadhi ya maafisa wake”
“Kwanini unasema hivyo?” nilimuuliza Pastor Romanus kwa shauku
“Mara kwa mara nimekuwa nikiitwa na vyombo vya usalama na kuhojiwa juu
ya Gabbi Masebo kwa kigezo kuwa alikuwa muumini wangu” nilimtazama Pastor
Romanus na kuvutika na maelezo yake na hapo nikamuuliza
“Walikuwa wakikuhoji nini?”
“Kama nilikuwa nikifahamu taarifa zake zozote kuhusu yeye”
“Unadhani kwanini wanataka kufahamu alipo?”
“Kwa kweli sifahamu ingawa nahisi huwenda Gabbi Masebo alikuwa ni mtu
hatari sana kuliko nilivyokuwa nikimdhania”
“Mahojiano hayo yalianza lini?”
“Hizi siku za karibuni” Pastor Romanus akaongea kwa msisitizo
“Sasa naanza kuhisi kuwa kuna jambo fulani hatari limefichika nyuma ya Gabbi
Masebo na jambo hilo linapiganiwa kufa na kupona ili lisiweze kuwekwa hadharani.
Hata hivyo muda siyo mrefu ukweli wa mambo utafahamika” niliongea kwa hakika
huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu.
“Dar es Salaam limekuwa jiji la matukio ya ajabu sana kwa zama hizi. Kila mtu
anakimbizana na utajiri wa hii dunia na umaarufu wake na kwa kufanya hivyo watu
wengi wamejikuta wakijitumbukiza kwenye dini na ibada za kishetani ili mambo yao
yawanyookee kama wanavyodhani. Lakini mafanikio ya shetani huwa ni ya muda
mfupi sana na ya ghafla mno na yanapozimika huzimika kama mshumaa kwenye
upepo wa jangwani.
Chapa 666 uliyoiona katika hilo jengo ni kiashiria cha uwepo wa dini ya kishetani
iliyoanza kuzoa maelfu ya wanasiasa,wasanii,wanamichezo na hata baadhi ya viongozi
wakubwa wa kidini hapa jijini Dar es Salaam. Mafanikio ya watu hawa huambatana
na utoaji mkubwa wa kafara ya damu nyingi za watu wasio na hatia. Watoto wengi
wanaopotea kila kukicha hapa jijini Dar es Salaam ni sehemu ya ibada za kishetani
zinazofanyika ili kuwapa watu utajiri wa muda mfupi” Pastor Romanus alimaliza
kuongea na maelezo yake yakawa yamenizindua fikra zangu.
Niliikumbuka ile chapa 666 kwenye ule mlango wa lile jengo la ghorofa kule
posta kisha nikakumbuka zile sauti za vicheko vya wanawake na zile kelele za vilio
vya watoto wadogo waliokuwa wakilia mle ndani.Halafu nikakumbuka wale watu
waliokuwa wameketi kwenye ule ukumbi. Kwa kweli nilihisi kuishiwa nguvu hata
hivyo niliupisha utulivu kichwani mwangu.
“Nitapata vipi majibu ya kazi yangu?” hatimaye nilimuuliza Pastor Romanus
“Njoo nyumbani kwangu kesho jioni nyumba namba 14 mtaa wa Azikiwe”
“Nitashukuru sana” nilimwambia Pastor Romanus huku nikitabasamu kabla
hajavunja ukimya.
“Huwezi kupambana na shetani kama huna Mungu”
“Nahitaji msaada wako” nikamwambia Pastor Romanus na hapo nikamuona
akisimama na kunisogelea pale nilipoketi.
“Fumba macho” aliponifikia akaniambia nami nikafanya kama alivyotaka na hapo
akanifanyika sala fupi ya kuniombea ulinzi. Alipomaliza akanipa mkono wa baraka.
“Nitajitahidi kulifanyia kazi ombi lako” Pastor Romanus akaongea kwa utulivu
huku akiuweka mkono wake begani kwangu. Nilitabasamu kidogo kisha nikaingiza
mkono mfukoni kuchukua kadi yangu ndogo ya mawasiliano ambayo nilimpa Pastor
Romanus.
“Tafadhali! naomba tuwasiliane kupitia kadi hii” nikamwambia wakati akiipokea
kadi ile kisha akavuta mkono wa vazi lake mkononi na kuitazama saa yake.
“Bila shaka na muda nao umetutupa mkono” Pastor Romanus akaniambia
“Nashukuru sana kwa kunipa muda wako” nikamwambia huku nikisimama
“Tuonane kesho!”
Hatimaye tulishikana mkono na kuagana kisha nikaelekea sehemu ya mbele ya
madhabahu ya lile kanisa ambapo nilitumbukiza noti mbili za shilingi elfu kumi kwenye
kapu la sadaka kama shukrani yangu kisha nikaanza kukatisha katikati ya lile kanisa
katika uchochoro mpana uliofanywa baina ya mabenchi ya lile kanisa yaliyokuwa
upande wa kushoto na kulia. Pamoja na kelele za manyunyu ya mvua yaliyokuwa
yakianguka juu ya lile paa la kanisa hata hivyo bado niliweza kuzisikia hatua zangu
sakafuni wakati nikiyoyoma kuelekea nje ya lile kanisa huku nikiwa na hakika kuwa
macho ya Pastor Romanus yalikuwa yakinisindikiza kwa nyuma.
Mara tu nilipotoka nje ya lile kanisa nikasimama kwenye ngazi za pale mlangoni
huku nikiyapeleleza vizuri mandhari ya nje ya lile kanisa yenye vivuli vingi vya miti ya
mikungu. Hali ilikuwa tulivu kwani sikuona kitu chochote cha kukitilia mashaka. Mvua
kubwa iliyokuwa ikinyesha haikunizuia nisiendelee na safari yangu hivyo nikafyatua
kofia ya koti langu jeusi na refu la kijasusi ama Trench coat na kujifunika vizuri kichwani
kisha nikashuka ngazi nikitokomea mbali na ile kanisa.
Kutembea bila gari langu yalikuwa ni maisha mapya kabisa ambayo kwa kweli
sikuwa na budi kukabiliana nayo kwa wakati huu. Niliitazama saa yangu ya mkononi
na kugundua kuwa muda ulikuwa umesonga sana kwani ilikuwa ikielekea kutimia
saa saba na nusu usiku. Wakati huu barabara nyingi za jiji la Dar es Salaam zilikuwa
zimekaukiwa na pilika za watu na magari na hali ile ikanipelekea nijihisi kuwa ni kama
#186
niliyekuwa nikitembea kwenye sayari mpya iliyojitenga na shughuli za binadamu.
Akili yangu ilikuwa hoi taabani kutokana na matukio yote yaliyotokea tangu asubuhi
kulipopambazuka. Bado nilikuwa na jukumu kubwa mbele yangu hata hivyo kwa
wakati huu nilihitaji kwanza kupumzika ili pindi kutakapopambazuka niamke nikiwa
na nguvu mpya za kuendelea na harakati zangu.
Muda mfupi baadaye nikawa nimeingia kwenye barabara iliyokuwa ikikatisha
mbele ya kanisa lile huku nikitembea kwa utulivu kuelekea upande wa kulia. Mara
tu nilipoingia kwenye barabara ile gari moja lilinipita kwa mwendo wa taratibu hata
hivyo sikulitilia maanani. Kwa kumbukumbu sahihi zilizokuwa kichwani mwangu ni
kuwa kituo cha teksi kilikuwa barabara ya mtaa wa tatu kutoka pale nilipokuwa mbele
ya hoteli moja maarufu iliyokuwa ikitazamana na jengo la ofisi za shirika la nyumba
la taifa NHC.
Nilikuwa nimepanga kutembea hadi kwenye kituo kile na kukodi teksi ambayo
ingenipeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwangu nikapumzike. Wakati nikitembea
mara kwa mara niligeuka nyuma kutazama kama kungekuwa na gari au mtu yeyote
aliyekuwa akinifuatilia na nilipoona kuwa hali bado ilikuwa shwari nikaendelea na
safari yangu bila wasiwasi.
Nilipofika mbele ya barabara ile eneo kulipokuwa na mzunguko wa barabara
nikashika uelekeo wa upande wa kushoto nikiifuata barabara ya mtaa wa Shaaban
Robert. Mvua kubwa bado ilikuwa ikiendelea kunyesha na njiani nilipishana na
magari machache sana ambayo yalinipita kwa kasi yakiendelea na safari zao. Hivyo
ilinichukuwa muda mfupi tu kugundua kuwa binadamu pekee aliyekuwa akitembea
kwa miguu katika barabara ile nilikuwa ni mimi peke yangu na hali ile ikanipelekea
nijihisi mpweke sana.
Wakati nikitembea nikajikuta nikimkumbuka yule mdunguaji hatari. Alikuwa ni
msichana mrefu mweusi na mrembo sana kiasi kwamba hakuelekea kabisa kufanana
na ile shughuli aliyokuwa akiifanya. Kiu ya kuonana naye ana kwa ana bado ilikuwa
kwenye nafsi yangu hata hivyo niliishia kujipa matumaini tu kwani sikujua ni lini na
wapi ningekutana naye kwa mara nyingine msichana yule mrembo aliyeinusuru roho
yangu kutumbukia shimoni.
Hatimaye nikawa nimeyafikia makutano ya barabara ya mtaa wa Shaaban Robert
na ile barabara ya Samora Avenue na wakati nilipokuwa nikijiandaa kuvuka makutano
yale ili niingie kwenye barabara ya Samora Avenue ghafla mbele yangu nikashtushwa
na mwanga mkali wa taa za gari zilizowashwa ghafla kumulika pale nilipokuwa. Gari
lile lilikuwa limeegeshwa umbali mfupi kabla ya yale makutano ya barabara na hivyo
kunipelekea nisite kuendelea na safari yangu. Hivyo nikapunguza urefu wa hatua
zangu taratibu huku bado nikiutafakari ule mwanga wa taa za lile gari.
Sehemu moja ya nafsi yangu ilinitaka nigeuze na kurudi kule nilipotoka wakati
sehemu nyingine ilinitaka niendelee mbele na safari yangu. Hali ile ikaipelekea akili
yangu ipoteze mhimili wa maamuzi ya haraka na kuifanya miguu yangu iwe mizito.
Hatimaye nikapiga moyo konde na kuendelea mbele.
Sikufika mbali katika safari yangu mara nikaliona lile gari likiacha maegesho na
kuingia barabarani likifuata uelekeo wangu. Tukio lile likapelekea mapigo ya moyo
wangu yapoteze utulivu kabisa huku jasho jepesi likianza kunitoka mwilini. Haraka
nikahisi kuwa mambo hayakuwa shwari tena hivyo nikavuka barabara na kuhamia
upande wa pili na wakati nikifanya vile niliweza kuliona vizuri lile gari. Lilikuwa ni
gari aina ya Landcruiser ya rangi ya samawati. Kitendo cha mimi kuvuka barabara
kikampelekea dereva wa ile gari Landcruiser naye aongeze mwendo kuyakaribia yale
makutano ya barabara. Tukio lile likanipa hakika kuwa mtu yeyote aliyekuwa ndani ya
lile gari basi alikuwa na malengo na mimi na hivyo sikutaka kusubiri ili kupata hakika
ya hisia zangu.
Hivyo mara tu baada ya kuvuka ile barabara niliongeza mwendo wa hatua zangu
huku nikiupeleka mkono wangu mafichoni kuipapasa bastola yangu. Kwa kuwa
nilikuwa karibu zaidi nikayafikia yale makutano ya barabara mapema zaidi kabla ya
ile Landcruiser. Mara tu nilipoyafikia makutano yale nikashika uelekeo wa upande wa
kushoto nikiifuata barabara ya Samora Avenue iliyokuwa ikikatisha kando ya eneo la
makumbusho ya taifa na jumba la tamaduni ama National Museum and House of Culture
kwa upande wa kulia na eneo la Bonitanical Garden kwa upande wa kushoto.
Nikiwa tayari nimeingia kwenye barabara ile nikaongeza mwendo wa urefu
wa hatua zangu na hivyo nikawa ni kama ninayetaka kutembea na kukimbia kwa
wakati mmoja. Hata hivyo jicho langu la pembe halikuacha mara kwa mara kutazama
kilichokuwa kikiendelea nyuma yangu.
Mvua iliendelea kunyesha na wakati huu barabara ya Samora Avenue ilikuwa
imemezwa na ukimya wa aina yake kwani sikuona gari,pikipiki wala mtu yeyote mbele
yangu. Taa kutoka kwenye majengo marefu ya ghorofa yaliyokuwa jirani na barabara
ile zilimulika kikamilifu hata hivyo hazikufanikiwa kutowesha giza lote eneo lile. Ule
mwanga wa taa za gari kutoka nyuma yangu kadiri ulivyokuwa ukiongezeka ukanifanya
nianze kuhisi kuwa lile gari Landcruiser nyuma yangu lilikuwa mbioni kunifikia.
Hivyo kwa kasi ya ajabu nikaanza kutimua mbio na tukio lile likampelekea dereva
wa ile Landcruiser naye azidi kuongeza mwendo hata hivyo mbio zangu hazikuwa za
kubabaisha.
Jasho likaanza kunitoka huku akili yangu ikisumbuka kufikiria nini cha kufanya.
Baada ya muda mfupi nikawa nimelifikia lile eneo la Makumbusho na kujikuta
nikishawishika kuruka uzio wa eneo lile na kuingia ndani kama sehemu salama ya
kuwapotezea malengo wale watu waliokuwa kwenye ile gari Landcruiser iliyokuwa
ikinifukuza nyuma yangu. Hata hivyo kuzidi kutafakari kukanifanya niliweke kando
wazo lile hasa baada ya kukumbuka walinzi waliokuwa wakilinda eneo lile. Hivyo
nikaendelea kutimua mbio safari hii nikiukata upepo kama mwanariadha mzoefu wa
mbio za kimataifa.
Hata hivyo sikufika mbali sana katika safari yangu pale nilipoanza kuhisi vishindo
nyuma yangu. Niligeuka haraka kutazama kule nyuma na mara hii nikawaona mbwa
wakubwa watatu wa polisi aina ya German Shepherd wenye urefu sawa na ule wa beberu
la kisasa mwenye afya ya ziada. Mbwa hao wenye hasira walikuwa wakifukua mbio
kunikaribia na sauti za vishindo vyao barabarani ilinitahadharisha kuwa nilipaswa
kuwa makini sana. Nyuma ya wale mbwa umbali wa mita kadhaa niliwaona wanaume
watano wakikimbia kuwafuata wale mbwa kwa nyuma huku nyuso zao zikiwa
zimekingwa kwa kofia za makoti ya mvua. Wote walikuwa wameshika bunduki zao
mikononi.
Wale mbwa nyuma yangu bila shaka walikuwa na hamu sana na mimi kwani
pamoja na mbio zangu kuwa za kuaminika lakini niligundua haraka kuwa umbali
baina yangu na wao ulikuwa ukipungua kwa kasi ya ajabu katika kila nukta ya sekunde
iliyokuwa ikitoweka na hapo hofu ikaanza kuniingia. Hatimaye nikaupeleka mkono
mafichoni na kuichomoa bastola yangu huku nikiwa nimepanga kuwafyeka wale
mbwa kwa risasi kabla mabosi wao hawajanifikia. Hata hivyo nikajikuta nikisita
kufanya vile kwani sikutaka kuwa wa kwanza kuanzisha shambulizi la risasi pale
nilipokumbuka kuwa sehemu kubwa ya eneo lile ilikuwa ikilindwa kwa umakini wa
hali ya juu kutokana na kwamba eneo lile lilikuwa ofisi nyeti za serikali. Hivyo milio ya
risasi ingeweza kuwavuta walinzi wengi zaidi wa eneo lile na hapo uwezekano wangu
wa kutoka salama ungezidi kuwa mdogo.
Nilivuta pumzi ya kutosha na kuongeza mwendo huku nikikimbia katika mbio
zisizoelezeka kwa urahisi. Hata hivyo wale mbwa nyuma yangu hawakunipa nafasi ya
kuwatoroka kwani nilipogeuka nyuma kuwatazama tena nikagundua kuwa walikuwa
wamejigawa katika mikakati ya kuhakikisha wananidhibiti mapema kabla sijafika
mbali.
Mbwa mmoja alikuwa nyuma yangu upande wa kushoto. Mbwa mwingine
alikuwa nyuma yangu upande wa kulia. Yule mbwa wa mwisho alikuwa hatua chache
nyuma yangu huku wote wakiwa wamekenua meno yao makali na ndimi zao ndefu
zenye uchu zikining’inia nje.
Hatimaye nikawa nimelifikia lile eneo la Botanical Garden lililokuwa upande wa
kushoto wa ile barabara. Eneo lililokuwa na bustani ya maua na vichaka hafifu
vya miti lililozungushiwa uzio wa ukuta mfupi. Wale mbwa ni kama waliokuwa
wameishtukia mapema dhamira yangu kwani nao walikuwa wameongeza kasi zaidi
kiasi cha kuwapelekea mara kwa mara kulikosakosa pindo la koti langu lililokuwa
likipepea kama kishada nyuma yangu.
Niliufikia ule ukuta wa eneo la Botanical Garden kisha nikaudandia hata hivyo wale
mbwa walikuwa werevu sana wa kutambua hila yangu hivyo wakaniwahi. Mbwa
mmoja aliwahi kuliuma pindo la koti langu na mwingine akajirusha na kung’ang’ania
buti langu la mguu wa kushoto kwani ule mguu wangu mwingine tayari nilikuwa
nimeishafanikiwa kuupandisha juu ya ule ukuta.
Nilijitahidi kwa kila hali kujinasua kutoka kwa wale mbwa wakali lakini hilo
halikuwezekana kirahisi kwani wale mbwa walikuwa ving’ang’anizi kama ruba.
Nilipogeuka kutazama kule nyuma wale watu ambao hapo awali nilikuwa nimewaacha
mbali nao pia nikagundua kuwa walikuwa mbioni kunifikia. Mara nikamuona mmoja
wao akiielekeza bunduki yake kwangu na hapo nikajua alikuwa amenuia kunishindilia
risasi. Hivyo sikutaka kusubiri badala yake nikakusanya nguvu na kuupandisha juu ule
mguu wangu wa kushoto.
Halikuwa jambo rahisi kwani yule mbwa hakuuachia mguu wangu na badala yake
akaendelea kuning’inia kwenye buti langu na kwa mbali niliyahisi meno yake makali
yakiikaribia ngozi ya mguu wangu. Yule mbwa bado hakuniachia pamoja na jitihada
zangu zote za kujitahidi kujinasua huku yule mwenzake akiwa bado ameling’ang’ania
pindo la vazi langu.
Hofu ya kudhibitiwa kikamilifu ikaniingia na wakati nikipiga akili nyingine ya
kujinasua kwenye kadhia ile ghafla nikasikia sauti ya mlio mkali wa mfyatuko wa risasi
kisha muda uleule nikasikia unafuu mkubwa katika uzito wa mguu wangu. Haraka
nikageuka tena kutazama kule nyuma walikokuwa wale watu hatari wakinifukuza.
Wale watu sasa walikuwa wameelekezea bunduki zao kwangu na hapo nikajua kuwa
yule bwege wa awali aliyenilenga kwa kutokuwa makini alikuwa amepoteza shabaha
ya kulenga mguu wangu na badala yake akakichakaza vibaya kichwa cha yule mbwa
aliyekuwa ameng’ang’ania mguu wangu.
“You bogus!...yaani nyinyi ndiyo mafala wakubwa sijapata kuona” nikawatukana wale
watu na kabla hawajapata mhimili mzuri wa shabaha zao mimi nikawa nimeshapanda
juu ya ule ukuta. Yule mbwa aliyekuwa ameng’ang’ania pindo la koti langu alikuwa
ameliachia baada ya kushtushwa vibaya na ile sauti mbaya ya risasi.
Kufumba na kufumbua nikawa tayari nimeangukia upande wa ndani wa ule
uzio huku nyuma nikisindikizwa na mvua ya risasi zilizonipunyuapunyua kiasi cha
kutengeneza matundu kwenye ukuta wa uzio ule dhaifu.
Niliangukia chini ndani ya ule ukuta huku nikihema ovyo kisha nikajiviringisha
haraka na kujilaza majanini na hapo nikaanza kutambaa kifudifudi nikijiweka mbali
na eneo lile. Nilipofika mbele sehemu niliyoihisi kuwa salama kidogo nikasimama na
kuanza kutimua mbio nikikatisha katikati ya vichaka vya miti vya eneo lile nikielekea
upande wa pili ambapo ningeupanda ukuta mwingine wa uzio ule na kuangukia nje ya
eneo lile na baada ya hapo ningetokomea zangu mitaani.
Niliendelea kukimbia na baada ya kitambo kifupi nikawa nimeufikia ukuta
mwingine wa upande wa pili wa ule uzio. Hata hivyo wakati nilipokuwa nikijiandaa
kuukwea ukuta ule nilichokiona mbele yangu nje ya ule ukuta kikapeleka baridi nyepesi
ianze kusambaa moyoni mwangu. Kingo za mdomo wangu zikakauka ghafla huku
harufu ya msukumo mkubwa wa damu mwilini ikiyasimanga matundu ya pua yangu.
Magari matatu yanayofanana na lile gari lililokuwa likinifukuza kule nyuma muda
mfupi uliyopita sasa niliyaona yakisimama kwa fujo na mbwembwe za aina yake nje
ya ukuta ule kisha milango yake ikafunguliwa kwa pupa na hapo nikawaona watu
wenye bunduki na makoti ya mvua kama wale wa awali wakishuka haraka na kusogea
kwa tahadhari wakiuzingira ule ukuta wa lile eneo nililojibanza. Nilitulia kwa makini
nikiwatazama kwa kificho watu wale na kwa kweli hapakuwa na sehemu ya kutorokea.
Hivyo niliinama tena chini nikirudi kunyumenyume kwa tahadhari na nilipokifikia
wao akiielekeza bunduki yake kwangu na hapo nikajua alikuwa amenuia kunishindilia
risasi. Hivyo sikutaka kusubiri badala yake nikakusanya nguvu na kuupandisha juu ule
mguu wangu wa kushoto.
Halikuwa jambo rahisi kwani yule mbwa hakuuachia mguu wangu na badala yake
akaendelea kuning’inia kwenye buti langu na kwa mbali niliyahisi meno yake makali
yakiikaribia ngozi ya mguu wangu. Yule mbwa bado hakuniachia pamoja na jitihada
zangu zote za kujitahidi kujinasua huku yule mwenzake akiwa bado ameling’ang’ania
pindo la vazi langu.
Hofu ya kudhibitiwa kikamilifu ikaniingia na wakati nikipiga akili nyingine ya
kujinasua kwenye kadhia ile ghafla nikasikia sauti ya mlio mkali wa mfyatuko wa risasi
kisha muda uleule nikasikia unafuu mkubwa katika uzito wa mguu wangu. Haraka
nikageuka tena kutazama kule nyuma walikokuwa wale watu hatari wakinifukuza.
Wale watu sasa walikuwa wameelekezea bunduki zao kwangu na hapo nikajua kuwa
yule bwege wa awali aliyenilenga kwa kutokuwa makini alikuwa amepoteza shabaha
ya kulenga mguu wangu na badala yake akakichakaza vibaya kichwa cha yule mbwa
aliyekuwa ameng’ang’ania mguu wangu.
“You bogus!...yaani nyinyi ndiyo mafala wakubwa sijapata kuona” nikawatukana wale
watu na kabla hawajapata mhimili mzuri wa shabaha zao mimi nikawa nimeshapanda
juu ya ule ukuta. Yule mbwa aliyekuwa ameng’ang’ania pindo la koti langu alikuwa
ameliachia baada ya kushtushwa vibaya na ile sauti mbaya ya risasi.
Kufumba na kufumbua nikawa tayari nimeangukia upande wa ndani wa ule
uzio huku nyuma nikisindikizwa na mvua ya risasi zilizonipunyuapunyua kiasi cha
kutengeneza matundu kwenye ukuta wa uzio ule dhaifu.
Niliangukia chini ndani ya ule ukuta huku nikihema ovyo kisha nikajiviringisha
haraka na kujilaza majanini na hapo nikaanza kutambaa kifudifudi nikijiweka mbali
na eneo lile. Nilipofika mbele sehemu niliyoihisi kuwa salama kidogo nikasimama na
kuanza kutimua mbio nikikatisha katikati ya vichaka vya miti vya eneo lile nikielekea
upande wa pili ambapo ningeupanda ukuta mwingine wa uzio ule na kuangukia nje ya
eneo lile na baada ya hapo ningetokomea zangu mitaani.
Niliendelea kukimbia na baada ya kitambo kifupi nikawa nimeufikia ukuta
mwingine wa upande wa pili wa ule uzio. Hata hivyo wakati nilipokuwa nikijiandaa
kuukwea ukuta ule nilichokiona mbele yangu nje ya ule ukuta kikapeleka baridi nyepesi
ianze kusambaa moyoni mwangu. Kingo za mdomo wangu zikakauka ghafla huku
harufu ya msukumo mkubwa wa damu mwilini ikiyasimanga matundu ya pua yangu.
Magari matatu yanayofanana na lile gari lililokuwa likinifukuza kule nyuma muda
mfupi uliyopita sasa niliyaona yakisimama kwa fujo na mbwembwe za aina yake nje
ya ukuta ule kisha milango yake ikafunguliwa kwa pupa na hapo nikawaona watu
wenye bunduki na makoti ya mvua kama wale wa awali wakishuka haraka na kusogea
kwa tahadhari wakiuzingira ule ukuta wa lile eneo nililojibanza. Nilitulia kwa makini
nikiwatazama kwa kificho watu wale na kwa kweli hapakuwa na sehemu ya kutorokea.
Hivyo niliinama tena chini nikirudi kunyumenyume kwa tahadhari na nilipokifikia
wao akiielekeza bunduki yake kwangu na hapo nikajua alikuwa amenuia kunishindilia
risasi. Hivyo sikutaka kusubiri badala yake nikakusanya nguvu na kuupandisha juu ule
mguu wangu wa kushoto.
Halikuwa jambo rahisi kwani yule mbwa hakuuachia mguu wangu na badala yake
akaendelea kuning’inia kwenye buti langu na kwa mbali niliyahisi meno yake makali
yakiikaribia ngozi ya mguu wangu. Yule mbwa bado hakuniachia pamoja na jitihada
zangu zote za kujitahidi kujinasua huku yule mwenzake akiwa bado ameling’ang’ania
pindo la vazi langu.
Hofu ya kudhibitiwa kikamilifu ikaniingia na wakati nikipiga akili nyingine ya
kujinasua kwenye kadhia ile ghafla nikasikia sauti ya mlio mkali wa mfyatuko wa risasi
kisha muda uleule nikasikia unafuu mkubwa katika uzito wa mguu wangu. Haraka
nikageuka tena kutazama kule nyuma walikokuwa wale watu hatari wakinifukuza.
Wale watu sasa walikuwa wameelekezea bunduki zao kwangu na hapo nikajua kuwa
yule bwege wa awali aliyenilenga kwa kutokuwa makini alikuwa amepoteza shabaha
ya kulenga mguu wangu na badala yake akakichakaza vibaya kichwa cha yule mbwa
aliyekuwa ameng’ang’ania mguu wangu.
“You bogus!...yaani nyinyi ndiyo mafala wakubwa sijapata kuona” nikawatukana wale
watu na kabla hawajapata mhimili mzuri wa shabaha zao mimi nikawa nimeshapanda
juu ya ule ukuta. Yule mbwa aliyekuwa ameng’ang’ania pindo la koti langu alikuwa
ameliachia baada ya kushtushwa vibaya na ile sauti mbaya ya risasi.
Kufumba na kufumbua nikawa tayari nimeangukia upande wa ndani wa ule
uzio huku nyuma nikisindikizwa na mvua ya risasi zilizonipunyuapunyua kiasi cha
kutengeneza matundu kwenye ukuta wa uzio ule dhaifu.
Niliangukia chini ndani ya ule ukuta huku nikihema ovyo kisha nikajiviringisha
haraka na kujilaza majanini na hapo nikaanza kutambaa kifudifudi nikijiweka mbali
na eneo lile. Nilipofika mbele sehemu niliyoihisi kuwa salama kidogo nikasimama na
kuanza kutimua mbio nikikatisha katikati ya vichaka vya miti vya eneo lile nikielekea
upande wa pili ambapo ningeupanda ukuta mwingine wa uzio ule na kuangukia nje ya
eneo lile na baada ya hapo ningetokomea zangu mitaani.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Niliendelea kukimbia na baada ya kitambo kifupi nikawa nimeufikia ukuta
mwingine wa upande wa pili wa ule uzio. Hata hivyo wakati nilipokuwa nikijiandaa
kuukwea ukuta ule nilichokiona mbele yangu nje ya ule ukuta kikapeleka baridi nyepesi
ianze kusambaa moyoni mwangu. Kingo za mdomo wangu zikakauka ghafla huku
harufu ya msukumo mkubwa wa damu mwilini ikiyasimanga matundu ya pua yangu.
Magari matatu yanayofanana na lile gari lililokuwa likinifukuza kule nyuma muda
mfupi uliyopita sasa niliyaona yakisimama kwa fujo na mbwembwe za aina yake nje
ya ukuta ule kisha milango yake ikafunguliwa kwa pupa na hapo nikawaona watu
wenye bunduki na makoti ya mvua kama wale wa awali wakishuka haraka na kusogea
kwa tahadhari wakiuzingira ule ukuta wa lile eneo nililojibanza. Nilitulia kwa makini
nikiwatazama kwa kificho watu wale na kwa kweli hapakuwa na sehemu ya kutorokea.
Hivyo niliinama tena chini nikirudi kunyumenyume kwa tahadhari na nilipokifikia
kichaka cha miti cha karibu na eneo lile nikageuka nyuma na kuanza kutimua mbio
kuelekea upande mwingine wa ule ukuta wa lile eneo. Niliufikia ule ukuta wa upande
mwingine ndani ya muda mfupi tu na kabla ya sijaukwea nilichungulia tena na
kutazama kule nje. Mara hii nikajisikia kukata tamaa zaidi.
Kulikuwa na magari manne yaliyofanana na yale niliyoyaona muda mfupi nje ya
ukuta kule nilipotoka. Watu kama wale wa awali walikuwa wakishuka kwa pupa kutoka
kwenye yale magari huku baadhi yao wakiwa na mbwa wamewashika kwa minyororo
mikononi mwao. Kwa kweli nilijisikia kukata tamaa huku nikianza kujilaumu kwa
kujiingiza kwenye mtego ule. Nikaanza kuhisi kuwa dakika za muda wangu wa kuwa
huru sasa zilikuwa zikihesabika.
Nikiwa nimejibanza pale kwenye ukuta huku nikiendelea kuchungulia kule nje
akili yangu ilianza kufanya kazi haraka ikisumbuka katika kutafuta namna ya kujinasua
kutoka katika hatari ile ya kukamatwa. Mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani
mwangu na kwa kweli sikuweza haraka kutambua kuwa ni wazo lipi hasa nilipaswa
kulifanyia kazi kwa wakati ule. Nikajishauri kuwa niende kwenye upande ule mwingine
wa ukuta ambao ulikuwa ndiyo pekee sijaufikia. Hata hivyo niliachana na wazo lile
kwani mandhari ya eneo lile nilikuwa nikiyafahamu vizuri.
Nje ya ukuta wa upande ule kulikuwa na eneo kubwa la wazi hivyo watu wale
hatari wangeweza kuutumia vyema uwazi ule kunichapa risasi endapo ningethubutu
kujitokeza. Hivyo kwa tafsiri ya haraka niliyoiona ni kuwa uwepo wangu eneo lile sasa
ulikuwa ukitambulika vizuri na wale watu na sasa walikuwa wamelizingira lile eneo
lote katika kuhakikisha kuwa sipati nafasi ya kuwatoroka.
Kitu kilichonishangaza ni namna nguvu kubwa namna ile ilivyokuwa ikitumika
dhidi yangu kana kwamba mimi nilikuwa tishio kubwa kwenye usalama wa nchi
hii. Kwa kweli hali ile ilinishangaza sana hata hivyo ule haukuwa wakati wa kujiuliza
maswali.
Niliitazama saa yangu ya mkononi na kushangazwa juu ya namna dakika
zilivyokuwa zikiyeyuka. Nilipotazama tena kule nje mara nikauona mwanga wa taa za
ving’ora vilivyokuwa juu ya magari ya wale watu hatari namna ulivyokuwa ukijitahidi
kumulika eneo lile. Hatimaye nikayaacha yale maficho na kurudi tena kule kwenye
kichaka cha miti huku akili yangu ikiendelea kusumbuka namna ya kujinasua kutoka
katika hatari ile ya kukamatwa na wale watu. Kwa kweli niliendelea kujilaumu tena na
tena kwa kujichanganya vibaya kwenye ule mtego rahisi.
Wakati nikiendelea kuwaza mara wazo fulani likanijia akilini pale nilipokumbuka
miundombinu ya majitaka ya jiji la Dar es Salaam. Katika maeneo fulani ya jiji la Dar
es Salaam mifereji ya majitaka kuelekea kwenye bahari ya Hindi ilikuwa imejengewa
chini ya ardhi kwa kukwepa uharibifu ambao ungetokana na shughuli mbalimbali za
watu au kukwepa kutumia sehemu kubwa ya ardhi hiyo ambayo ingeweza kutumika
kwa shughuli zingine zenye manufaa zaidi. Mifereji hiyo iliyojengewa chini ya ardhi
baadhi ilikuwa ikikatisha chini ya barabara za jiji mtaani. Chini ya majengo marefu
ya ghorofa au kandokando ya barabara huku makutano ya mifereji hiyo yakiitwa
chemba. Chemba hizo zilikuwa zimejengewa vizuri kwa zege na kufunikwa kwa
mifuniko imara ya chuma.
Matumaini yangu ya kutoroka yakafufuka upya na sikutaka kuendelea kujishauri
zaidi badala yake nikaanza zoezi la kutafuta chemba hizo kama kungekuwa na yoyote
eneo lile.
Nilichukua tochi yangu ndogo ya kijasusi kutoka kwenye mfuko wa koti langu na
kwa tahadhari nikaiwasha na kuanza kumulika chini katika sehemu tofauti za eneo
lile la hifadhi ya bustani ya miti mbalimbali. Nikaanza kuzunguka upande huu na ule
nikichunguza bila mafanikio. Hali ya mtupo wa damu kwenye mishipa yangu mwilini
ukanitanabaisha kuwa mapigo ya moyo wangu yalikuwa yamepoteza utulivu katika
kiwango cha juu cha hofu.
Ingawa mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha jijini Dar es Salaam lakini ndani
ya koti langu nilihisi joto kali mno. Mikono yangu nayo ikaanza kupoteza utulivu
na nilipoitazama haraka nikagundua kuwa nayo ilikuwa imeanza kutetemeka ovyo.
Wakati nikiendelea na uchunguzi wangu kule nje ya ukuta niliweza kuzisikia kelele
za wale mbwa wakibweka. Sikutaka kujidanganya kuwa nafasi ya kuwatoroka wale
watu kupitia kwenye kuta za ule uzio bado ilikuwepo kwani hadi wakati ule nilikuwa
na hakika kuwa vichochoro na matundu yote ya uzio ule vilikuwa vimezibwa au
kuwekewa mtego wa kuninasa kiulaini.
Baada ya tafutatafuta ya hapa na pale hatimaye nikabahatika kuiona chemba
moja iliyokuwa katikati ya kichaka hafifu cha miti nyuma ya mti wa mpera. Kuiona
chemba ile matumaini yakaongezeka moyoni hivyo nikaisogelea ile chemba na kuanza
kuichunguza kwa haraka. Hata hivyo kabla sijaanza kufanya utundu wangu kupitia
uwazi mdogo uliokuwa baina ya miti iliyokuwa eneo lile niliweza kuona sehemu moja
juu ya ukuta wa uzio wa eneo lile. Wale watu hatari sasa walikuwa wakiwasaidia mbwa
wao kuwapandisha juu ya ule ukuta ili waweze kuingia ndani ya lile eneo na kuanza
kunisaka.
Sikutaka wale mbwa hatari wanifikie tena hivyo niliinama kwenye ile chemba na
mara hii nikaliona kufuli chakavu likiwa limeuzuia kikamilifu ule mfuniko wa chuma
wa ile chemba. Bila kupoteza muda nikaingiza mkono kwenye mfuko wa koti langu
na kuchukua bisbisi fupi na nene,moja ya vifaa vyangu vya kazi kisha nikaipitisha
bisbisi ile katikati ya lile kufuli na ule mfuniko wa chuma wa ile chemba. Nilipomaliza
nikaanza kuikandamiza ile bisbisi kwa chini katika mtindo wa kuharibu lile kufuli.
Lile kufuli lilikuwa la shaba imara sana kama lililofungwa tangu enzi za wakoloni hata
hivyo sikuwa na njia mbadala ya kuepukana nalo.
Nikageuka tena kutazama kwenye ule uwazi na mara hii nikawaona mbwa wawili
wakiruka na kuingia mle ndani ya ule uzio kupitia ngazi waliyowekewa na hapo hofu
ikanishika.
Baada ya kukurukakara za hapa na pale hatimaye nikafanikiwa kuifyatua ile kufuli
na kuitupa kando kisha ile bisbisi nikaichomeka kwenye kingo moja ya ule mfuniko
wa chemba na kuikandamiza chini. Ule mfuniko ukanyanyuka kidogo na hapo
nikapata uwazi wa kuingiza vidole vyangu chini yake na kuunyanyua juu. Nikauondoa
ule mfuniko wa chuma na kuusogeza pembeni. Nilichokiona baada ya kuuondoa
ule mfuniko lilikuwa ni shimo kubwa la chemba ya majitaka lenye kipenyo mraba.
Nikachukua tochi yangu na kuanza kumulika kule chini ya ile chemba. Lilikuwa
shimo refu lenye kina kisichopungua futi nane kwenda chini na mwisho wa shimo
lile kulikuwa na makutano ya mifereji miwili mikubwa iliyopishana na kutengeneza
umbo la msalaba. Kiasi kikubwa cha majitaka kilikuwa kikiendelea kutiririka kwenye
makutano ya mifereji ile.
Haraka nikaitia bastola yangu na ile bisbisi mfukoni na kubakiwa na ile tochi
ndogo yenye mwanga mkali mkononi. Kisha nikaanza kuingia ndani ya ile chemba
nikishuka chini taratibu na kwa uangalifu. Fukuto la mle ndani lilikuwa kali sana kiasi
cha kunifanya nianze kutokwa na jasho jingi mwilini. Mle ndani pembeni ya kuta za
ile chemba kulikuwa na utelezi mkali hata hivyo nilijitahidi kwa kila hali kuikaza misuli
ya miguu yangu katika namna ya kuhakikisha kuwa sitelezi na kuangukia chini ya ile
chemba kwani hiyo ingekuwa hatari zaidi.
Hatimaye nilimaliza kuingia kwenye ile chemba kisha nikausogeza ule mfuniko wa
chuma na kuifunga ile chemba kwa ndani kabla ya wale mbwa hatari hawajanifikia.
Tochi yangu ikiwa mkononi mara tu nilipoufunika ule mfuniko nilianza kushuka kule
chini taratibu nikiweka vituo hapa na pale kukwepa kuteleza vibaya.
Hatimaye nilifika kule chini ya ile chemba. Hewa ya mle ndani ilikuwa nzito
sana na yenye harufu kali ya mchanganyiko wa majitaka na maji ya mvua iliyokuwa
ikiendelea kunyesha sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Yale majitaka yalikuwa
yakitiririka kwa kasi mno na kina chake kilikuwa usawa wa mapaja yangu.
Niliachana na ule uelekeo wa yale majitaka yalipokuwa yakielekea kisha nikachukua
mfereji mmoja nikiufuata uelekeo wa yale majitaka yalipokuwa yakitokea. Ule mwanga
wa tochi yangu mkononi uliniwezesha kuona mbele yangu ingawa giza lilikuwa
zito mno na kwenye kuta za mfereji ule uliotengenezwa kwa matofari madogo ya
kuchoma kulikuwa tope zito la utelezi. Ukubwa wa mrefeji ule ulitosha kunifanya
niweze kutembea vizuri pasipo usumbufu wowote. Sikujua ule mfereji ulikuwa
ukielekea wapi hata hivyo nilikuwa na matumaini ya safari yangu.
Ni kama niliyekuwa kwenye ulimwengu mwingine kwani kule chini kulikuwa
kunatisha sana na hewa ilikuwa nzito mno. Ingawa sikutarajia kukutana na hatari
yoyote ya kibinadamu mbele yangu lakini niliikamata vyema bastola yangu mkononi.
Baada ya mwendo mrefu kidogo mara nikawa nimefika kwenye makutano mengine
ya mifereji mitano lakini juu ya makutano yale hapakuwa na chemba kama ya kule
nyuma nilikotokea.
Nguvu ya maji eneo lile ilikuwa imeongezeka kiasi cha kuifanya miguu yangu
ionekane kupwaya kila nilipokuwa nikitupa hatua zangu. Nilipofika kwenye makutano
yale ya mifereji nikasimama na kugeuka nyuma nikichunguza kama kungekuwa na
mtu yeyote aliyekuwa akinifuatilia. Hata hivyo sikuona dalili za uwepo wa kiumbe
chochote kikinifuatilia hivyo nikageuka mbele na kuyatazama yale makutano ya ile
wa magharibi hatimaye nikafika sehemu moja na kuweka kituo. Hewa ya mle ndani
ilikuwa nzito mno na yenye harafu mbaya sana. Mbali na hayo kulikuwa na joto
kali lililonifanya nijute kuvaa lile koti langu refu jeusi la kijasusi hata hivyo sikulivua.
Niliusogeza karibu mkono wangu wa kushoto kisha kikabonyeza kitufe kimoja
kilichokuwa pembeni ya saa yangu ya digital na taa ya saa ile ilipowaka nikatazama
muda. Nilikuwa nimetumia muda wa nusu saa tangu nilipoanza safari yangu kutoka
kwenye ile chemba ya kwanza hivyo nikaushusha mkono wangu na kuendelea na
safari huku nikimwomba Mungu kuwa muda mfupi mbele yangu nikutane na chemba
nyingine.
Ombi langu huwenda lilijibiwa mapema kwani baada ya mwendo mfupi tu wa
safari yangu mara nikawa nimefika kwenye chemba nyingine kubwa yenye makutano
ya mifereji minne. Mifereji miwili kati yake ikiingiza majitaka na mifereji miwili mingine
ikipokea majitaka hayo na kuyatiririsha maeneo mengine. Nilisimama na kuichunguza
vizuri chemba ile na hapo nikagundua kuwa ilikuwa safi kidogo ukilinganisha na
zile chemba nyingine nilizozipita kule nyuma. Kwenye makutano ya mifereji ya ile
chemba hakukuwa na utelezi mkubwa wala takataka nyingi badala yake kulikuwa na
matuta hafifu ya mchanga mwepesi yaliyofanywa na mtiririko wa majitaka mepesi
kutoka maeneo mbalimbali.
Nilisimama chini ya chemba ile na kumulika ule mfuniko wa chuma wa ile chemba.
Nilifurahi kwani ule mfuniko nao ulikuwa msafi na haukuwa na popo kama kwenye ile
chemba ya kule nyuma nilipotoka. Nikiwa pale chini nikayatega vizuri masikio yangu
na kwa kufanya vile kwa mbali nilisikia muungurumo wa kitu fulani kisichoeleweka.
Nikajaribu kuwaza kuwa muungurumo ule ungekuwa ukitokana na kitu gani. Baada
ya kuupisha utulivu kichwani mwangu hisia zikaniambia kuwa huwenda chemba ile
ilikuwa karibu na barabara ya magari na hivyo muungurumo ule huwenda ungeweza
kuwa ni wa injini ya gari lililokuwa likipita karibu na eneo lile. Kwa mara ya kwanza
tangu niingie ndani ya mifereji ile moyo wangu ukawa umerejewa na matumaini ya
ajabu.
Kuelekea kule juu kwenye mfuniko wa chuma wa ile chemba kulikuwa na
ngazi fupi zilizotengenezewa ukutani lakini ngazi zile hazikufika chini kabisa ya ile
chemba kwa sababu za kitaalamu walizokuwa wakizifahamu wajenzi. Hata hivyo
kwangu ilikuwa afadhali sana maana ile chemba ilikuwa tofauti kabisa na zile chemba
nilizozipita kule nyuma. Ile chemba ilikuwa pana kiasi ambacho kupanda kule juu kwa
kukanyaga mguu wangu mmoja upande mmoja wa ile chemba na mguu mwingine
upande wa pili lingekuwa zoezi gumu la kunitoa jasho.
Kwa jitihada binafsi hatimaye nikafanikiwa kuzifikia zile ngazi fupi za chuma kwa
mikono yangu kisha nikajivuta na kuipandisha miguu yangu kwenye zile ngazi halafu
kwa tahadhari ya hali ya juu nikaanza kupanda zile ngazi nikielekea kule juu kwenye
ule mfuniko wa ile chemba. Zoezi lile lilihitaji uangalifu wa hali ya juu kwani zile ngazi
zilikuwa za chuma na zilizodumu kwa muda mrefu kiasi kwamba ile hali ya hewa ya
mle ndani ilikuwa imezipelekea ngazi zile zipate kutu na kuwa dhaifu.
Hatimaye nikaufikia ule mfuniko wa ile chemba kule juu. Nilipofika kule juu
nikasimama kidogo nikiupisha utulivu kichwani mwangu kisha nikaichukua ile bisbisi
kutoka kwenye mfuko wa koti langu na kuanza uharibifu huku mara kwa mara
nikiyatega vizuri masikio yangu kunasa sauti ya kitu chochote ambacho kingekuwepo
nje ya mfuniko wa chemba ile.
Sasa nilikuwa na hakika kuwa chemba ile ilikuwa eneo fulani katikati ya barabarani
kwani mara kwa mara niliweza kusikia muungurumo wa injini za magari yaliyokuwa
yakipita juu ya ile chemba. Gurudumu la gari moja liliukanyaga ule mfuniko wakati
nilipoanza kuusogeza pembeni na hivyo kuukandamiza haraka kiasi kwamba kama
nisingekuwa mwangalifu huwenda vidole vyangu vingekuwa vimefyekwa na ukingo
wa mfuniko ule wa chuma.
Nikasubiri kidogo kujipa utulivu na nilipoona kuwa hali ilikuwa shwari
nikausukuma tena pembeni ule mfuniko wa chemba na hapo nikapanda juu kidogo
kuchungulia tena kule nje.
Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na kitendo cha kuufungua kidogo ule
mfuniko baadhi ya maji ya mvua ile yakapata upenyo wa kuingia mle ndani. Hata
hivyo sikujali badala yake nilitulia kidogo nikiitathmini hali ya mandhari ya kule nje.
Magari mawili au matatu yalipokaribia kuifikia ile chemba nilirudi ndani na kuufunika
ule mfuniko na magari yale yalipopita nikausogeza tena ule mfuniko na kuendelea na
tathmini yangu. Sasa nilikuwa na hakika kuwa ile chemba ilikuwa imejengwa katikati
ya barabara ingawa nilipojitahidi kuvuta picha nilishindwa haraka kufahamu kuwa
chemba ile ilikuwa ipo kwenye barabara ya mtaa upi wa jiji la Dar es Salaam japokuwa
nilikuwa na matumaini kuwa bado nilikuwa kwenye eneo la posta jijini Dar es Salaam.
Ni mara chache sana kwa barabara za mitaa ya jiji la Dar es Salaam kukaukiwa
kabisa na watembea kwa miguu lakini nilishangazwa sana na kitendo cha kutomuona
mtu yeyote akitembea katika barabara ile. Hata hivyo huwenda hali ile ilitokana na
mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha. Taa kutoka kwenye majengo marefu ya
ghorofa yaliyokuwa yametenganishwa na barabara ile ziliangaza barabarani hata hivyo
hazikufanikiwa kulitowesha giza lote eneo lile. Hatimaye nikausukuma ule mfuniko wa
ile chemba na nilipokuwa mbioni kuuweka kando ili nitoke mara kwa mbali nikaliona
gari moja likija usawa wa ile chemba hivyo haraka nikawahi kurudi tena mle ndani
na kujifungia. Lile gari lilipopita nikausukuma tena ule mfuniko na kuuweka kando
kisha bila kupoteza muda nikamalizia kuzipanda zile ngazi za ile chemba na kutoka
nje kisha nikaurudishia ule mfuniko wa ile chemba mahala pake huku nikiyatembeza
macho yangu kuyapeleleza mazingira yale huku nikichunguza kama kungekuwa na
mtu yoyote jirani na eneo lile akinitazama.
Hali ya mandhari yale ilikuwa tulivu hivyo haraka nikachepuka kando ya barabara
ile na kuanza kutembea kwa tahadhari. Matone mazito ya mvua kubwa iliyokuwa
ikiendelea kunyesha jijini Dar es Salaam yakanipa faraja huku mvua ile ikiendelea
kuniosha uvundo wa ile mifereji uliokuwa kwenye koti langu na kunifanya nijihisi
kama kiumbe aliyetoka kwenye safari ndefu ya kuzimu baada ya kushinda vita kubwa
ya wanyang’anyi wa roho yangu.
Nikaendelea kutembea huku mara kwa mara nikigeuka nyuma na kutazama kama
kungekuwa na mtu yoyote aliyekuwa akinifuatilia na kila nilipouona mwanga wa taa
za gari likija nyuma au mbele yangu nilichepuka na kujibanza kando ya barabara ile
hadi gari hilo lilipopita.
Ilinichukuwa muda mfupi tu kuvuta kumbukumbu sahihi kichwani mwangu
kuwa pale nilikuwa wapi kwani kupitia mandhari yale nikagundua kuwa ile ilikuwa
ni barabara ya Sokoine Drive hasa baada ya kuliona jengo la ofisi za Tanzania Buildings
Agency.
Bado sikuwa sehemu salama nilijiambia pale nilipokumbuka kuwa barabara ile ya
Sokoine Drive haikuwa mbali sana na lile eneo la Botanical Garden nilipokoswakoswa
kukamatwa na wale makachero. Hivyo nikakatisha kwenye uchochoro mmoja
ulionichukua moja kwa moja hadi nyuma ya lile jengo la Tanzania Buildings Agency.
Nyuma ya jengo lile kulikuwa na barabara ndogo ya lami ambayo sikuweza haraka
kuitambua vizuri hata hivyo niliingia kwenye barabara ile fupi nikishika uelekeo wa
upande wa kushoto huku upande wa kulia kwangu nikitazamana na majengo mengine
ya ghorofa yaliyokuwa yakitumika kama makazi ya watu na ofisi mbalimbali.
Nilipokuwa nikikaribia kufika mwisho wa barabara ile mara nikayaona magari
mawili aina ya Landcruiser kama yale niliyoyaona kule Botanical Garden muda mfupi
uliyopita yakikatisha mbele yangu. Niliwahi kujibanza nyuma ya pipa kubwa la taka na
kuyaacha magari yale yapite kisha nikajitokeza na kuendelea na safari yangu.
Nilipofika mwisho wa barabara ile nikaingia upande wa kulia nikitembea kwenye
barabara nyingine ya lami yenye giza zito zaidi lililotokana na vichaka vya matawi ya miti
iliyopandwa kando yake. Ilikuwa ni barabara ya Luthuli na kutoka pale sikuwa mbali
sana na eneo la Ikulu ya Magogoni. Sikuwa salama sana niliwaza ila angalau nilikuwa
mbali kidogo na lile eneo la Botanical Garden msako wangu ulipokuwa ukiendelea.
Vivuli vya matawi ya miti kando ya barabara ile ndiyo vikawa sehemu yangu ya
kujibanza kila nilipouona mwanga wa taa za gari kwenye barabara ile. Niliendelea
kutembea hadi pale nilipofika kwenye barabara ya Kivukoni. Kuingia kwenye barabara
ile kukanipelekea nisijisikie tena mpweke kwani kulikuwa na pilikapilika za watu ambao
haraka baadhi yao niliwatambua kuwa walikuwa wachuuzi wa samaki kwani soko la
samaki halikuwa mbali sana na eneo lile. Wengine walikuwa ni wasafiri waliokuwa
wakielekea kupanda Pantoni eneo la Feri.
Nilipoingia kwenye barabara ile ya Kivukoni nikashika uelekeo wa upande wa
kushoto kama ninayeelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam halafu nilipofika mbele
kidogo nikashika uelekeo wa upande wa kulia. Kuingia kwenye uelekeo ule kukanifanya
niione ile sanamu ya Askari Monument mbele yangu na mashine za ATM za benki
ya NBC kushoto kwangu. Nilikumbuka kuwa sikuwa na pesa ya kutosha mfukoni
hivyo nikaingia kwenye zile ATM na kuchukua kiasi cha pesa ambacho kingenisaidia
kwenye harakati zangu. Nilipotoka kwenye zile mashine za ATM nikatembea hadi
katikati ya mtaa wa Azikiwe na Sokoine Drive nje ya New Africa Hotel ambapo nilikodi
teksi.
Dereva wa teksi alikuwa mzee wa makamo mfupi na mwenye maneno mengi.
Macho yake makubwa yaliyokosa utulivu yakanitanabaisha kuwa alikuwa mwerevu
sana wa dili za jijini Dar es Salaam na vichochoro vyake. Ingawa alikuwa mfupi sana
kiasi cha kutokuona kwa urahisi mbele yake lakini uzoefu ulimlinda wakati akiiacha
barabara moja na kuingia barabara nyingine kwa mbwembwe. Nilimtathmini vizuri
dereva yule na hapo nikahisi kuwa huwenda alikuwa Mpare wa Same au Mwanga
mkoani Kilimanjaro.
“Tunaelekea wapi bosi wangu?” hatimaye yule dereva akaniuliza na hapo
nikakumbuka kuwa sikuwa nimemueleza kule ninapokwenda. Hivyo nikaingiza
mkono mfukoni na kuchukua Business card niliyopewa siku ile kule Vampire Casino
na yule mwanamke mnaijeria aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Iko–Ojo Obaje.
Nilipoichukua ile Business card nikawasha taa iliyokuwa chini ya paa la ile teksi na
kusoma maelezo yake kisha nikaizima ile taa. Dereva alikuwa amepunguza mwendo
kidogo kunisikiliza.
“Endesha gari hadi 79 Haile Selassie road eneo la Oysterbay”
“Unaenda Hotel Agent 11?” mzee yule akaniuliza huku akibadili uelekeo.
“Ndiyo” nikamwitikia huku nikigeuka kutazama nyuma.
“Oh! hoteli ya kifahari sana ile na ina mabinti warembo sijapata kuona” dereva
yule mzee akaongea na kwa kweli umri wake haukuendana na maongezi yale hata
hivyo sikumuacha mpweke.
“Umewahi kufika?” nikamuuliza
“Nimefika mara nyingi sana. Sisi madereva wa teksi hukodiwa sana na wateja wa
mahotelini na asikwambie mtu viongozi wengi wa kisiasa na baadhi ya matajiri wa
hapa jijini Dar es Salaam wanayatumia maficho yale kuchepuka na nyumba ndogo”
Nilicheka kidogo nikiyatafakari maneno ya dereva yule na kwa kweli alinipunguzia
sana upweke wa mawazo na kunisahaulisha kwa muda mkasa uliotokea nyuma
yangu. Hatimaye nikamtoa kwenye maongezi yale nikimpeleka kwenye masuala
ya siasa halafu mpira wa miguu na baadaye masuala ya mapenzi na kote alionesha
kuyamudu vyema maongezi huku akitia mbwembwe za hapa na pale. Nilipendezwa
sana na ucheshi wake na ilifika sehemu sote tukawa tumeishiwa hoja na hapo ukimya
ukachukua nafasi yake. Hali ile ikiwa inaendelea taratibu nilijiegemeza kwenye siti ya
gari huku nikipiga mwayo hafifu na kuanza kufanya tathmini ya kimyakimya ya kazi
yangu.
Hadi wakati ule nilikuwa nikiamini kuwa kama siyo serikali basi ni baadhi ya watu
katika serikali walikuwa wakifanya jitihada za juu na chini kuzizima harakati zangu na
kweli sikuweza kufahamu ni kitu gani hasa kilichokuwa kikiendelea. Nikakumbuka
mambo nilioyaona kule ndani ya ule mlango mweusi kwenye lile jengo la ghorofa
lililopo kule eneo la posta kisha nikaoanisha na yale maelezo ya Pastor Romanus.
Kufikia pale nilikuwa nimeanza kuvuta picha ya namna fulani kichwani mwangu
hata hivyo picha hiyo bado ilikuwa haijakamilika vizuri. Mawazo yangu yakahamia
kwa yule msichana kisura na mlimbwende wa aina yake yaani yule mdunguaji hatari
huku nikiwaza namna alivyoniokoa na kwa jinsi alivyokuwa akipambana na wale watu
hatari kwa namna ya kimyakimya na hapo nikajikuta nikivutiwa naye. Nilikumbuka
namna nilivyotazamana na mdunguaji yule hatari kwenye vile vyumba vya lifti kule
posta wakati tukishuka kwenye yale majengo ya ghorofa na hapo hisia juu yake
zikaanza kuziteka taratibu fikra zangu. Nikajiuliza tena mdunguaji yule hatari ni nani
na kwanini aliniokoa kutoka katika ile milipuko ya mabomu ya kutegwa kwenye gari
langu. Kisha nikaikumbuka ile milipuko ya mabomu huku nikiilinganisha na thamani
ya maisha yangu na hali ile ikanifanya nizidi kuhisi kuwa kulikuwa na siri kubwa
iliyokuwa imefichika katika mkasa huu.
Kwa mara ya kwanza nikaanza kuhisi kuwa nilikuwa nimejitumbukiza kwenye
mkasa hatari zaidi wenye siri nzito iliyofichika ndani yake. Siri ambayo gharama ya
kuitunza ililingana na thamani ya uhai wangu. Kitendo cha kuwaona wale makachero
wakiwa wamejiingiza katika mkasa huu siyo tu kwamba kitendo kile kilikuwa
kimenishtua bali pia kilikuwa kikielekea kuninyima usingizi kwani nilifahamu ugumu
ulipo katika kupambana na vyombo vya usalama vya serikali.
Nikiwa katika hali ile ya kutafakari nikaanza kufikiria namna ya kuutelekeza kando
mkasa huu na kutafuta maficho salama ambapo huko ningetulia hadi pale ambapo
ningekuwa na hakika kuwa harakati za makachero wale kunisaka mitaani zingekuwa
zimefifia hapo ndiyo ningejitokeza na kuendelea na harakati zangu. Lakini nilipozidi
kutafakari haraka sana nikaliweka kando wazo lile pale nilipokumbuka kuwa bado
nilikuwa sina taarifa za kutosha juu ya kile nilichokuwa nikikipeleleza. Hivyo sikuona
kama nilipaswa kurudi nyuma katika harakati zangu badala yake nikaona kuwa
nilitakiwa kuongeza juhudi katika kuutafuta ukweli wa mambo kwani huwenda ukweli
huo ungenipa kinga ya kifo dhidi ya wale makachero.
Nilimkumbuka tena yule mdunguaji hatari na hapo tabasamu jepesi likaniponyoka
bila hiana huku fikra zangu zikiendelea kutengeneza picha na kunifanya nijihisi
kama ninayemuona mdunguaji yule hatari akiwa mbele yangu akitabasamu na hivyo
kuyafanya meno yake meupe yenye mng’aro wa kipekee yaonekane sambamba na
vishimo vyake vidogo mashavuni vyenye kuweza kuziroga vibaya hisia zangu na hapo
nikabaki nikimuomba Mungu anikutanishe naye kwa mara nyingine.
“Tumefika bosi wangu” sauti ya yule dereva ikazirudisha tena fikra zangu mle
ndani ya teksi.
“Oh! mara hii tu” nikaongea kwa uchovu kama niliyeishiwa na hoja ya kuzungumza
na hapo dereva yule akanitazama kupitia kioo cha ndani cha gari huku akitabasamu.
“Ushasau kuwa usiku huu hakuna foleni barabarani?” mzee yule dereva akaongea
kwa msisitizo kana kwamba ile hoja aliitoa baada ya kuhisi kuwa nilikuwa nikitaka
kupingana naye kwa kuionea uchungu pesa yangu mfukoni.
Teksi ilisimama kwenye barabara ya 79 Haile Selassie eneo la Oysterbay mbele ya
Hotel Agent 11 na hapo nikaingiza mkono mfukoni na kuchukua wallet yangu ndogo
ya ngozi ya Bitis arietans-Puff adder kisha nikaifungua na kutoa noti moja ya shilingi elfu
kumi na kumpa dereva. Dereva akaipokea noti ile kwa bashasha zote na kuitia kwenye
mfuko wa mbele wa shati lake huku akitabasamu.
“Shukrani kijana” dereva yule akanishukuru huku akiupapasapapasa ule mfuko
wa shati lake.
“Ondoa shaka” nikamwambia yule mzee kwa utulivu.
“Nikufuate saa ngapi bosi wangu?” yule dereva akaniuliza huku akinitazama
kupitia kile kioo cha ndani ya gari kilichokuwa chini ya paa.
“Safari yangu inaishia hapa mzee kama nitakuhitaji zaidi nitakufata pale kituoni
kwako”
“Chukua basi namba yangu ya simu kwani huwezijua utanihitaji muda gani” yule
dereva akaning’ang’aniza na sikutaka kuendeleza upinzani hivyo nikachukua simu
yangu na kuzuga kuzinakili namba za simu yake wakati alipokuwa akinitajia katika
namna ya kutaka kumridhisha.
“Hebu nipigie niinakili namba yako” yule dereva akanisisitiza
“Simu yangu haina muda wa maongezi” nikamwambia yule dereva huku
nikifungua mlango wa teksi na kushuka. Dereva yule akageuka na kunikodolea macho
na alipoona simpatilizi akawasha gari na kugeuza akirudi kule alipotoka na hali ile
kwangu ikawa afadhali.
Mvua ilikuwa imepungua hivyo mara baada ya kushuka kwenye ile teksi
nikasimama kidogo nikiitazama Hotel Agent 11 kwa udadisi. Ilikuwa hoteli ya kisasa na
yenye hadhi kiasi kwamba mtu yeyote mwenye kipato cha wasiwasi asingejisumbua
kuulizia huduma ya malazi.
Kulikuwa na magari machache yaliyoegeshwa nje ya hoteli ile na yote yaliashiria
kuwa wamiliki wake walikuwa ni watu wa vipato vya kueleweka. Hatimaye nikaingiza
mikono kwenye mifuko ya koti langu kisha nikavuka barabara nikikatisha kwenye geti
la hoteli ile kuingia ndani. Nilipozifikia ngazi za mbele za ile hoteli nikazipanda taratibu
huku nikigeuka nyuma kutazama kama kungekuwa na mtu yoyote akinifuatilia. Hali
bado ilikuwa shwari na huwenda walinzi wa getini kwenye hoteli ile hawakutaka
kunihoji kwa kunidhania kuwa huwenda nilikuwa miongoni mwa wateja wa hoteli ile.
Kipande cha zulia maridadi cha rangi nyekundu kikanichukua kutoka eneo la
mlangoni la hoteli ile hadi sehemu ya mapokezi na wakati nikitembea nikayazungusha
macho yangu taratibu kuzikagua sura za watu waliokuwa wameketi kwenye makochi
ya sofa ya kifahari yaliyokuwa kwenye ukumbi ule. Baadhi ya watu mle ukumbini
walikuwa wakiendelea kupata vinywaji huku wengine wakionekana kuendelea na
maongezi ya hapa na pale hata hivyo Iko–Ojo Obaje hakuwepo miongoni mwao.
Mandhari ya ukumbi wa chini wa hoteli ile yalifaa kuitwa ya kistaarabu
yanayoendana na watu wakwasi wanaofahamu namna ya kutumia pesa. Madirisha
makubwa ya ukumbi ule yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu na mapana
yanayopendeza na ukutani kulikuwa kumetundikwa picha nzuri kubwa na tofauti
za kuchora zinazovutia kuzitazama bila kuchoka. Sakafuni kulitandikwa zulia zuri
linalopendeza na sehemu fulani mle ndani ukutani kulikuwa na seti mbili za runinga
zilizotundikwa kwenye pande mbili za ukutani na wakati nikitembea kwa mbali
nilisika sauti ya muziki laini uliokuwa ukirushwa kwenye spika zilizokuwa sehemu
fulani katika ukumbi ule.
“Karibu sana” kijana moja wa mapokezi akanikaribisha na nilipomchunguza
nikagundua kuwa alikuwa mwembamba wa wastani lakini mwenye sura ya ucheshi na
alikuwa amevaa sare za kazi. Suruali ya rangi ya nyeusi,shati jeupe na tai ndogo nyeusi
shingoni mwake.
“Ahsante!” nilimwitikia yule kijana huku nikigeuka na kuyatembeza tena macho
yangu kuwatazama wale watu waliokuwa mle ndani ya ukumbi. Sikumuona mtu yeyote
ninayemfahamu hivyo nikageuka tena na kumtazama yule kijana huku nikiingiza
mkono wangu mfukoni kuichukua ile kadi ndogo aliyonipa Iko-Ojo Obaje halafu
nikaitelezesha kwenye meza ya kaunta ile ya mapokezi. Yule kijana hakuichukua
ile kadi badala yake akaipitishia macho kuitazama kisha akayahamishia macho yake
kwangu.
“Nimemkuta?” nilimuuliza yule kijana mhudumu wa mapokezi.
“Wewe ni nani?”
“Mimi ni mgeni wake tafadhali naomba umpigie simu chumbani kwake
umwambie kuwa Stephen Masika amefika kumuona” nilimwambia yule kijana na
hapo akanitazama kwa mashaka kidogo kisha akanyanyua simu iliyokuwa pale mezani
pambeni yake halafu akauweka mkonga wa simu sikioni huku akibonyeza tarakimu
fulani. Ile simu ilipoanza kuita yule mhudumu akageuka na kunitazama kwa udadisi
muda mfupi uliyofuata nikamsikia akiongea kwa lugha safi ya kiingereza kisicho cha
kuungaunga na hapo nikajua kuwa alikuwa akimtaarifu Iko-Ojo Obaje kuwa mimi
nimefika. Yule kijana alipokata ile simu na kuirudishia mahala pake akageuka tena na
kunitazama.
“Chumba namba 22 ghorofa ya pili” yule kijana akaniambia kwa kisirani kama
ambaye hajapokea tip hata mmoja kutoka kwa mteja tangu kulipopambazuka.
“Ahsante!” nikamwambia yule kijana huku nikiichukua ile kadi yangu pale juu
ya meza na kuitia mfukoni kisha nikazunguka ile kaunta kuelekea sehemu ya nyuma
yake kulipokuwa na chumba cha lifti. Niliifikia ile lifti na kutokomea ndani kisha
nikabonyeza kitufe cha ghorofa pili na hapo ile lifti ikaanza kupanda juu ya lile jengo
la hoteli.
Muda mfupi uliofuata kile chumba cha lifti kikatia nanga ghorofa ya pili na hapo
mlango ukafunguka. Nilipotoka nje nikajikuta nimetokezea kwenye korido pana kiasi
inayotazamana na milango mingi ya vyumba. Mandhari ya eneo lile yalikuwa tulivu
na yenye harufu nzuri na usafi wa hali ya juu. Nilianza kutembea huku nikiyatembeza
macho yangu kutazama milango iliyokuwa ikitazamana na korido ile.
Chumba namba 22 kilikuwa baada ya kuipita milango miwili upande wa kulia.
Nilipoufikia mlango wa chumba kile nikasimama na kujikarabati kidogo mwonekano
wangu kisha nikabonyeza kitufe cha kengele kilichokuwa kando ya mlango ule. Mwito
wa kengele yangu haukusubiriwa sana kwani mlango ule ulifunguliwa mapema na
hapo macho yangu yakatulia juu ya taswira ya mlimbwende chakaramu.
Iko-Ojo Obaje alikuwa amevaa pensi nyanya fupi ya rangi nyekundu iliyoiacha
wazi sehemu kubwa ya minofu ya mapaja yake laini. Fulana yake nyepesi ya rangi
nyeupe ilikuwa na mshono wa umbo la V shingoni na hivyo kuipelekea nusu ya
shehena ya matiti yake makubwa ya wastani kubaki wazi pasipo uzio wowote wa
sidiria. Fulana ile pia ilikuwa fupi kiasi cha kuipelekea nusu ya sehemu yake ya tumbo
kubaki wazi na hivyo tumbo lake ng’avu na laini kuonekana. Miguuni alikuwa amevaa
viatu vya kuchomeka vyenye manyoya laini ya rangi ya majani makavu ya miti. Nywele
zake za rasta alikuwa amezikusanya na kuzifunga kwa nyuma kama mkia wa farasi.
Kutoka pale aliposimama niliweza kuinusa harufu nzuri ya manukato yake ya gharama
aina ya Caron’s Poivre.
Macho yake legevu yenye uchovu kiasi yalinitazama kwa huba huku tabasamu
laini likiuponyoka uso wake wenye pua ndefu kiasi na midomo laini yenye kingo pana
zilizokolea vizuri rangi nyekundu ya lipstick. Tathmini yangu ya haraka ikinieleza kuwa
Iko-Ojo Obaje alifaa kushiriki kwenye kinyang’anyiro cha mashindano ya kumtafuta
mwanawake mzuri wa asili barani Afrika,na hapo roho yangu ikapoteza utulivu kabisa.
“Karibu ndani” hatimaye Iko-Ojo Obaje akanikaribisha kwa sauti nyepesi yenye
kuulevya mtima wangu kwa lugha ya kiingereza chake fasaha.
“Ahsante sana!” nikaongea kwa utulivu huku nikiliruhusu tabasamu langu
kuchanua usoni halafu nikamkonyeza kidogo kwa furaha kisha nikaingia na kufunga
ule mlango nyuma yangu na wakati Iko-Ojo Obaje akitembea kuelekea kwenye kochi
moja kati ya makochi mawili ya sofa yaliyokuwa mle ndani hisia zangu zikamezwa
vibaya na mtikisiko wa makalio yake laini yaliyojificha ndani ya kitambaa chepesi
cha ile pensi nyanya yake bila nguo ya ndani. Kwa uzoefu mzuri niliyokuwanao kwa
wanawake wa sampuli ile kwa haraka niliweza kufahamu kuwa Iko-Ojo Obaje alikuwa
ni mwanamke wa namna gani na alikuwa akihitaji nini kwangu.
Mapenzi!...nikajiambia moyoni huku nikianza kulivua koti langu na kulitupa
sakafuni wakati huo tabasamu jepesi likiwa limejivinjari usoni mwangu. Nilipoanza
kufungua vifungo vya shati langu Iko-Ojo Obaje alikuwa tayari ameshanifikia pale
nilipokuwa na hapo akauzungusha mkono wake mmoja nyuma ya shingo yangu
taratibu huku mkono wake mwingine ukianza kufungua mkanda wa suruali yangu
ya jeans kiunoni. Nikiwa bado nimesimama pale katikati ya chumba niliweza kuzisikia
pumzi nyepesi za Iko-Ojo Obaje mbele yangu kwa namna mapigo ya moyo wake
yalivyopoteza utulivu. Nikamtazama Iko-Ojo Obaje na hapo akashindwa kabisa
kunitazama usoni badala yake akafumba macho yake legevu na kuuzamisha taratibu
ulimi wake kinywani mwangu.
Sasa tulikuwa kwenye zero distance na sikuweza kabisa kuvumilia uchokozi wa
namna ile hivyo nikaipandisha juu fulana yake na hapo mikono yangu ikaanza kufanya
ziara taratibu kwenye chuchu zake nyeusi zilizotuna katikati ya matiti yake yenye
ukubwa wa wastani kifuani mwake.
Suruali yangu alipoanguka chini nikaitupia pembeni kwa teke langu huku mkono
wangu mwingine ukiwa umekikamata vyema kiuno chake na kuanza kukipapasa
taratibu. Mkono laini wa Iko-Ojo Obaje ulipofika katikati ya mapaja yangu uvumilivu
ukanishinda huku nikihema ovyo.
#210
KOPLO TSEGA ALIENDESHA GARI LAKE taratibu kuelekea mtaa wa
Undali eneo la Upanga jijini Dar es Salaam huku mara kwa mara akivitazama
vioo vya ubavu wa gari kuchunguza kama kungekuwa na mtu yoyote
aliyekuwa akimfuatilia nyuma yake. Akagundua kuwa hakuna mtu yoyote aliyekuwa
akimfuatilia hivyo hali bado ilikuwa shwari na jambo lile likamfurahisha sana.
Mvua bado ilikuwa ikinyesha na hivyo kupelekea barabara nyingi za mitaa ya jiji
la Dar es Salaam kuwa na hali ya upweke. Saa ya ndani ya gari kwenye dashibodi
ilionesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa nane na robo usiku wakati Koplo Tsega
alipoitazama na kisha kuyatumbukiza mawazo yake kwenye tafakari nzito ya mikasa
yote iliyotokea tangu alipowasili jijini Dar es Salaam. Akaanza kukumbuka namna
siku ya kwanza alivyoanza kufuatiliwa na yule mtu asiyemfahamu wakati alipokuwa
akitoka kule Vampire Casino. Kisha akakumbuka namna vichwa vya magazeti
mbalimbali vilivyokuwa vimejikita katika kukinadi kifo cha Momba. Tukio lile lilikuwa
limemuuma sana moyoni hasa alipowaza kuwa yeye ndiye aliyekuwa sababu kubwa
ya kifo kile. Koplo Tsega akaendelea kukumbuka namna ambayo yule mtu wa ajabu
alivyomfukuza siku ile katika lile jengo la ghorofa la Rupture & Capture kabla ya kumzidi
ujanja na kumuacha solemba muda mfupi baada ya kumdungua vibaya P.J.Toddo nje
ya baraza la Vampire Casino.
Fikra zake zikatia nanga kwenye tukio lile na kuanza kuunda hoja juu ya mtu yule
ambaye kwa hakika sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni pake. Mwanzoni Koplo
Tsega alikuwa amemhusisha mtu yule moja kwa moja na kifo cha Momba kwani ni
yeye ndiye aliyekuwa amemuona siku ile alipokuwa kule juu ya jengo la biashara la
Rupture & Capture na baadaye kutoroka na teksi ya Momba na hivyo akawa ameapa
kumsaka mtu yule na kumwangamiza kama sehemu ya kulipa kisasi chake kwa
kumuua Momba.
Lakini sasa adhma hiyo alikuwa ameiweka kando mara baada ya mchana wa siku
iliyopita kumuona mwanaume yuleyule aliyekuwa akimfuatilia siku ile wakati alipokuwa
akitoka Vampire Casino na siku chache baadaye mwanaume huyo akimfukuza kwenye
lile jengo la biashara la Rupture & Capture,kumuona na yeye akifukuzwa na watu
aliyokuwa akiwawinda kwa hali na mali jijini Dar es Salaam. Kisha akakumbuka
namna alivyomuokoa yule mtu na mateka wake chini ya lile jengo la ghoroga eneo la
posta kutoka kwenye gari lake lililokuwa limetegwa milipuko na wale watu hatari. Mtu
yule ni nani na kwanini alikuwa akitaka kuangamizwa?. Akajiuliza bila kupata majibu.
Koplo Tiglsi Tsega akwenyeea kukumbuka namna risasi yake moja makini
ilivyoivunja na kuitawanya vibaya shingo ya mtu aliyeitwa Balimenya ambaye alikuwa
mkuu wa itifaki ya tume ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya nchini. Namna
Koplo Tsega alivyofahamu juu ya wapi alipokuwepo Balimenya wakati ule ilikuwa kazi
rahisi sana. Kwani kupitia nyaraka muhimu na simu ya mkononi aliyoipata nyumbani
kwa Pierre Kwizera akaweza kupata namba ya simu ya Balimenya. Koplo Tsega
akakumbuka namna alivyompigia simu Balimenya akimsihi waonane huku akijidai
kuwa na taarifa nyeti za kusaidia kumnasa muuaji waliyekuwa wakimtafuta Balimenya
na makachero wenzake. Balimenya hakuwa amepata muda wa kuitathmini vizuri sauti
ya mpigaji wa simu ile na badala yake akamtaka Koplo Tsega kuwa amfuate kwenye
lile jengo la ghorofa lililokuwepo eneo la posta kulipotokea ile milipuko.
Koplo Tsega hakupoteza mfupi kwani muda mfupi baadaye alikuwa kwenye
chumba cha jengo moja la ghorofa lililokuwa likipakanana na lile jengo la ghorofa
alilokuwepo Belimenya na makachero wenzake kama alivyomuelekeza kwenye
maongezi ya simu. Kupitia chumba kile kilichokuwa kikitazamana na korido ya lile
jengo la ghorofa alilokuwapo Balimenya na makachero wenzake,Koplo Tsega akaitega
bunduki yake ya kudungulia 338 Lapua Magnum na kumsubiri Balimenya ajitokeze
vizuri kwenye korido ya lile jengo la ghorofa la jirani.
Akiwa bado amejibanza kwenye kile chumba Koplo Tsega akajikuta akivutiwa
na watu fulani waliofika chini ya lile jengo la ghorofa alilokuwepo Balimenya na
makachero wenzake. Watu wale mara tu waliposhuka kutoka kwenye gari jeupe
aina ya Landcruiser lile gari likaondoka haraka eneo lile na hapo akawaona wale watu
walioshuka kwenye lile gari lililoondoka muda mfupi uliyopita wakiharakisha kuelekea
kwenye maegesho ya magari ya jengo lile sehemu kulipokuwa na gari dogo aina ya
Peugeot 504 huku mmoja wao akiwa amebeba mfuko mweusi uliyotuna.
Koplo Tsega akaendelea kuwatazama wale watu chini ya lile jengo la ghorofa
kupitia darubini ya bunduki yake na wale watu walipolifikia lile gari wakafungua mlango
wa dereva na kuingia ndani. Kwa kutaka kupata taswira nzuri juu ya kilichokuwa
kikiendelea kwenye lile gari waliloingia wale watu na mfuko wao mweusi,Koplo Tsega
akairekebisha vizuri darubini ya bunduki yake akiielekezea ndani ya lile gari kupitia
kioo cha ubavuni. Alichokiona ndani ya lile gari Peugeot 504 kikamshtua sana.
Wale watu walikuwa wakitega mabomu mawili makubwa kwenye lile gari na tukio
lile likawa limemshangaza sana Koplo Tsega hata hivyo alijipa uvumilivu. Muda mfupi
baadaye mara akawaona wale watu wakitoka kwenye lile gari bila ya ule mfuko mweusi
huku wakiharakisha kuelekea kwenye lile jengo la ghorofa alipokuwepo Balimenya na
makachero wenzake.
Tukio lile likawa limempelekea Koplo Tsega aisogeze tena darubini ya bunduki
yake kutazama kwenye ile korido ya lile jengo la ghorofa alipokuwa akitazama hapo
awali. Haukupita muda mrefu mara akauona mlango mweusi uliokuwa kwenye
korido ya lile jengo ukifunguliwa. Kufunguliwa kwa mlango ule kukapelekea watu
wawili watoke nje. Koplo Tsega alipowachunguza vizuri watu wale mara akamuona
Balimenya akitoka kwenye ule mlango mweusi na kuanza kutimua mbio akielekea
upande wa kushoto wa ile korido walipokuwa makachero wenzake. Koplo Tsega
hakutaka kufanya makosa hivyo shingo ya Balimenya alipoenea vizuri kwenye msalaba
wa shabaha ya darubini yake akawahi kuvuta kilimi cha bunduki yake. Balimenya
hakupata nafasi ya kufurukuta kwani risasi moja tu iliyofunga safari ikaivunja na
kuikata vibaya shingo yake kiasi kwamba wale makachero wenzake waliokuwa kwenye
ile korido wakaanza kutimua mbio wakishuka ngazi kwa taharuki.
Koplo Tsega akiwa anaendelea kuendesha gari lake akakumbuka muda mfupi
baada ya tukio lile namna alivyomuona mwanaume mwengine akiwa anatoka kwenye
ule mlango mweusi kwenye ile korido huku mtu huyo akiwa amemdhibiti mwanaume
mwingine mwenye mwili mkubwa kwa kabari makini ya mkono wake wa kushoto na
mkono wa kulia ukiwa umeielekezea bastola yake kwenye kichwa cha yule mateka.
Akiwa kwenye maficho yale Koplo Tsega akaendelea kuwatazama vizuri wanaume
wale wawili kupitia darubini kali ya bunduki yake. Muda mfupi baadaye akajikuta
akishikwa na mduwao wa aina yake baada ya kumuona na kumkumbuka vizuri yule
mtu aliyemdhibiti vizuri mateka wake kwa kabari matata na bastola mkononi kuwa
alikuwa ndiye yule mtu aliyemfukuza kwenye lile jengo la Rupture & Capture siku
chache zilizopita.
Koplo Tsega akaendelea kukumbuka namna ambayo mtu yule na mteka wake
walivyoingia kwenye chumba cha lifti ya lile jengo la ghorofa alilomdungua Balimenya
kabla ya mtu huyo na mateka wake kuanza kushuka kwa lifti chini ya ya lile jengo.
Akaendelea kukumbuka namna alivyoshtuka wakati alipomuona yule mtu na mateka
wake wakielekea kwenye lile gari Peugeot 504 lililokuwa chini ya lile jengo huku likiwa
limetegwa mabomu mawili na wale watu hatari ambao sasa alikuwa na hakika kuwa
walikuwa na ushirika mkubwa na Balimenya.
Koplo Tsega akiwa anaikumbuka ile taswira ya ile milipuko miwili mikubwa
iliyotegwa kwenye lile gari Peugeot 504 akajikuta akiishiwa nguvu pale alipokumbuka
kitu kilichotokea muda mfupi baadaye mara baada ya kumpa ishara fulani yule mtekaji
na mateka wake kuwa wasilikaribie lile gari wakati yeye bado akiwa kwenye kile
chumba cha lifti kwenye lile jengo la ghorofa la jirani na eneo lile.
Akiwa anaendelea na safari yake Koplo Tsega akajikuta akizama kwenye
tafakuri nzito juu ya yule mwanaume mtekaji ambaye siku chache zilizopita alikuwa
amefanikiwa kumkimbia kwenye lile jengo la Rupture & Capture. Kupitia mlolongo
wa matukio Koplo Tsega akawa na hakika kuwa mtu yule mtekaji hakuwa na ushirika
wowote na Balimenya na wale makachero wenzake. Hivyo kwa tafsiri nyingine ni
kuwa mtu yule mtekaji kwa namna moja au nyingine hakuwa na sababu ya kumuua
Momba na hivyo kisasi hakikufaa kuelekezwa kwake. Swali likabaki kuwa mtu yule
mtekaji ni nani na aliingiaje katika mkasa huu?. Na kama mtekaji yule hakuwa shirika
moja na Balimenya kwanini siku ile alitaka kumkamata yeye kwenye lile jengo la Rupture
& Capture muda mfupi baada ya kumdungua P.J.Toddo?. Koplo Tsega akaendelea
kujiuliza bila kupata majibu.
Hata hivyo Koplo Tsega akajikuta katikati ya mgogoro wa nafsi yake pale
alipoyakumbuka maelezo ya kutoka kwa wahudumu wa Hotel 92 Dar es Salaam
pamoja na picha zilizonaswa na kamera za usalama za hoteli ile zilizokuwa ukumbini
zikimuonesha mwanaume yule mtekaji akitoka muda mfupi baada ya ile maiti ya Sikawa
kugundulika kule chumbani kwake. Huyu mtekaji ni nani hasa katika mkasa huu?.
Koplo Tsega akaendelea kujiuliza bila kupata majibu kisha akaapa kuwa angefanya
jitihada zote katika kuufahamu ukweli wa kile kilichokuwa kikiendelea huku akiwaza
kuwa huwenda Sikawa asingeuwawa endapo angekuwa ameyafuata maelekezo yake
ya kutokufika kule chumbani kwake hadi pale ambapo angemhitaji. Kwani ilikuwa
baada ya Sikawa kufika kule chumbani siku ile na kumkosa Koplo Tsega alikuwa
amefungua mlango wa kile chumba kwa funguo aliyoichukua eneo la mapokezi na
kuingia mle chumbani akimsubiri Koplo Tsega.
Saa nane na nusu usiku ilipotimia Koplo Tsega akaegesha gari lake barabara ya
pili kutoka kule yalipokuwa maskani ya Balimenya mtaa wa Undali eneo la Upanga.
Kisha akashuka na kuanza kutembea kwa miguu akielekea kwenye maskani hayo.
Taarifa alizokuwa amezipata kupitia nyaraka za Pierre Kwizera zilikuwa zimemsaidia
kufahamu kwa wepesi zaidi jina la mtaa na nyumba aliyokuwa akiishi Balimenya.
Wakati huu wa usiku wa manane ulikuwa umepelekea sehemu kubwa ya eneo
la Upanga kugubikwa na ukimya wa aina yake. Kelele pekee zilizokuwa zikisikika
zilikuwa ni zile za mbwa waliokuwa wakibweka ndani ya mageti makubwa ya majumba
ya kifahari yaliyokuwa eneo lile.
Koplo Tsega akaendelea kutembea kwa makini huku mara kwa mara akigeuka
nyuma na kutazama kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia. Hali
bado ilikuwa tulivu hivyo alipofika kwenye jengo la ofisi ndogo za shirika la posta
akashika uelekeo wa upande wa kushoto akiingia kwenye mtaa wenye nyumba
aliyokuwa akiishi Balimenya. Ukimya wa mtaa ule ukampelekea azisikie vizuri hatua
zake zilivyokuwa zikisafiri kwa utulivu barabarani. Bastola yake ikiwa tayari mkononi
Koplo Tsega akaapa kumtia adabu mtu yeyote ambaye angeonekana kuleta kizuizi
mbele yake.
Mara tu Koplo Tsega alipomaliza kulipita lile jengo lenye ofisi ndogo za posta
mbele kidogo akalipita jengo la ofisi za TTCL kisha akaingia upande wa kushoto
kwenye kichochoro kidogo kilichokuwa baina ya uzio wa bustani ndogo ya wazi na
jengo la ghorofa la shirila la nyumba la taifa. Wakati alipokuwa akimaliza kukatisha
kwenye kichochoro kile mara akasita na kusimama baada ya kuhisi kuwa kulikuwa na
mtu kama siyo watu waliokuwa sehemu fulani kwenye bustani ile wamejibanza.
Hisia zake zikimtanabaisha hivyo Koplo Tsega akasimama kwa utulivu huku
akiyatembeza macho yake kwa makini kulikagua vizuri eneo lile la bustani. Hata
hivyo hakumuona mtu yeyote isipokuwa mvua na hisia za upepo mwepesi uliyokuwa
ukiendelea kuvuma na kuyumbisha matawi ya miti iliyokuwa eneo lile. Hatimaye
akazipuuza hisia zake na kuendelea mbele na safari yake.
Koplo Tsega akaendelea kutembea na alipokuwa mbioni kufika mwisho wa
kichochoro kile hisia kama zile za awali zakamjia tena lakini mara hii kwa namna
tofauti kidogo kwani nyuma yake akahisi ni kama vile kulikuwa na mtu fulani aliyekuwa
akimfuatilia. Hisia hizo zikampelekea achepuke na kujibanza kwenye mti mmoja
uliokuwa jirani na eneo lile huku akiwa ameikamata vema bastola yake mkononi.
Kutoka pale nyuma ya mti ule alipojibanza,Koplo Tsega akageuka taratibu na
kutazama kule nyuma alipotoka safari hii akiwa makini zaidi kuyatembeza macho
yake katika vipenyo vyote vya eneo lile. Bado hakuweza kumuona mtu yeyote na hali
ilikuwa tulivu kama ilivyokuwa mwanzo. Hata hivyo Koplo Tsega hakutaka kuridhika
mapema kuwa hali ilikuwa shwari hivyo akaendelea kujibanza nyuma ya ule mti kwa
muda mrefu zaidi huku akitarajia kumuona mtu yeyote akijitokeza.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwani hakukuwa na mtu yeyote aliyejitokeza na hali
ile ikampelekea ajione kuwa ni mwenye wasiwasi mwingi na woga usiyokuwa na
sababu za msingi. Hatimaye akaamua ayaache maficho yale na kuingia tena kwenye
kile kichochoro na wakati akitembea kuendelea na safari yake hakutaka tena kugeuka
nyuma ingawa alikuwa amejidhatiti kwa kila hali kukabiliana na hatari yoyote ambayo
ingejitokeza.
Alipofika mwisho wa uchochoro ule Koplo Tsega akaingia upande wa kulia
akitembea katikati ya uwazi mpana kidogo uliotenganisha jengo moja la ghorofa la
shirika la nyumba la taifa na uzio wa eneo la mahakama. Baada ya kutembea safari
fupi kwenye uwazi ule Koplo Tsega akawa amefika sehemu kulipokuwa na ngazi
za kuelekea juu ya lile jengo la ghorofa la shirika la nyumba la taifa kwa upande wa
kushoto. Koplo Tsega alipozifikia ngazi zile kabla ya kuanza kuzipanda akageuka tena
na kutazama nyuma. Hakumuona mtu yeyote hivyo akaanza kuzipanda zile ngazi kwa
utulivu huku akiwa ameikamata vyema bastola yake mkononi.
Usiku bado ulikuwa tulivu na wenye ukimya wa aina yake na kwa mbali sauti pekee
iliyosikika ilikuwa ni sauti ya manyunyu ya mavua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Katika ghorofa ya tatu ya jengo lile la ghorofa nyumba namba 38 ndipo yalipokuwa
maskani ya Balimenya. Koplo Tsega akajikuta akikumbuka wakati alipokuwa
akiendelea kuzipanda zile ngazi taratibu huku mara kwa mara akisimama na kusikiliza
kama kungekuwa na sauti yoyote ya hatua za mtu aliyekuwa akimfuatilia nyuma yake.
Hakusikia sauti yoyote hivyo bado hali ilikuwa tulivu.
Akaendelea kuzipanda zile ngazi na alipofika kwenye korido ya ghorofa ya pili
Koplo Tsega akasimama tena huku akiyatathmini vizuri mandhari ya eneo lile. Katika
sehemu ile hapakuwa na makazi ya watu isipokuwa ofisi za shirika fulani la mtu binafsi
kutokana na vyeo vilivyokuwa vimeandikwa kwenye baadhi ya milango iliyokuwa
kwenye korido ile na nembo za shirika hilo. Mwanga wa taa iliyokuwa kwenye korido
ile ulikuwa hafifu na hapakuwa na dalili za uwepo wa mtu yeyote eneo lile. Hivyo
hatimaye akaendelea na safari yake akipanda ngazi kuelekea ghorofa inayofuata.
Koplo Tsega alipofika ghorofa ya tatu akagundua kuwa hali ilikuwa tofauti
kidogo na zile ghorofa za chini. Kulikuwa na milango nane ya vyumba vilivyokuwa
vikitazamana na korido ile na mandhari yake yalidhihirisha kuwa eneo lile lilikuwa
likikaliwa na watu. Mlango wa nyumba namba 38 ulikuwa mwisho upande wa
kushoto wa korido ile. Koplo Tsega mara tu alipoingia kwenye korido ile akatembea
kwa utulivu huku akiyatembeza macho yake upande huu na ule. Kitendo cha kuuona
mlango wenye namba 38 upande wa kushoto kikampelekea asimame kwa utulivu nje
ya mlango ule huku akiyatega kwa makini masikio yake ili kunasa hali ya utulivu wa
eneo lile. Hali bado ilikuwa tulivu hivyo akausogelea karibu ule mlango huku akiyatega
tena masikio yake kwenye tundu la kitasa cha ule mlango. Utulivu wa ndani ya ile
nyumba ikawa ni dalili tosha kuwa mle ndani hapakuwa na mtu yoyote.
Akiwa bado ameikamata vema bastola yake mkononi Koplo Tsega akasimama na
kuyatembeza tena macho yake kwenye ile korido. Ukimya wa eneo lile ukamtanabaisha
kuwa bado alikuwa peke yake.
Hivyo hatimaye akakishika kitasa cha ule mlango wenye namba 38 juu yake na
kuusukuma taratibu. Ule mlango ulikuwa umefungwa na imara kama jiwe na hapakuwa
na njia mbadala ya kuufungua mlango ule bila ya funguo kama lengo lingekuwa ni
kutowashuta wakazi wa eneo lile. Hivyo Koplo Tiglis akaingiza mkono mfukoni na
kuchukua mkungu wa funguo malaya ambapo alianza kujaribu kuufungua ule mlango
kwa funguo moja baada ya nyingine. Alipoifikia funguo ya nne majibu yakapatikana.
Kabari ya kitasa cha mlango ule ikafyatuka na hapo akakizungusha kile kitasa taratibu
huku akiusukuma ule mlango kwa ndani. Ule mlango ukafunguka taratibu huku
mdomo wa bastola yake akiutanguliza mbele.
Mara baada ya kuingia mle ndani Koplo Tsega akaurudishia ule mlango nyuma
yake na kuwasha taa ambayo swichi yake ilikuwa nyuma ya ule mlango. Baada ya
kuyatembeza macho yake akiyatathmini kwa haraka mandhari ya mle ndani nafsi
yake ikamtanabaisha kuwa sehemu ile ilikuwa sebule ya Belimenya. Kulikuwa na
makochi makubwa manne ya sofa ya vitambaa vyeusi yanayopendeza huku yakiwa
yamepangwa katika mtindo wa kuizunguka meza fupi na nyeusi ya kioo iliyokuwa
katikati ya sebule ile.
Sehemu fulani upande wa kushoto ukutani kulikuwa na runinga kubwa na
chini yake kulikuwa na meza fupi yenye king’amuzi cha Dstv na deki moja ya DVD
iliyounganishwa na spika mbili zilizosimamishwa kando yake. Sakafuni kulikuwa
na zulia zuri la manyoya lenye rangi ya ngozi ya pundamilia na hivyo kuyapelekea
mandhari yale yapendeze sana.
Kwenye kona ya sebule ile upande wa kulia kulikuwa na jokofu kubwa la rangi ya
kijivu lenye milango miwili ya juu na chini. Pembeni ya jokofu lile kulikuwa na stuli
ndefu na juu ya stuli ile kulikuwa na feni dogo. Wakati Koplo Tsega akipiga hatua zake
kuyatathmini vizuri mandhari yale mbele yake akaliona kabati dogo lililokuwa umbali
wa hatua chache kutoka pale ulipokuwa ule mlango wa kuingilia.
Mbele ya sebule ile upande wa kulia kulikuwa na mlango wa kuelekea chumbani
na mlango ule ulikuwa umefunguliwa nusu na kuachwa wazi. Koplo Tsega alipoufikia
mlango ule akasogeza pazia pambeni na kupitia mwanga hafifu uliopenya aliweza
kuona mle ndani.
Kilikuwa chumba kikubwa chenye kitanda kipana cha futi sita kwa sita. Kitanda
hicho kilikuwa kimefunikwa vizuri kwa shuka safi zenye rangi ya hudhurungi na mito
miwili ya kuegemea. Pembeni ya kitanda kile kulikuwa na meza fupi yenye redio na taa
ndogo ya Lampshade pembeni yake.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
Kwa upande wa mbele kitanda kile kilitazamana na kabati kubwa la nguo ambalo
milango yake ilikuwa imefungwa. Kulikuwa na nguo chache za kiume zilizokuwa
zimetundikwa kwenye kining’inizo maalum cha nguo kilichokuwa ukutani. Koplo
Tsega akapiga hatua zake taratibu na kusimama kando ya kitanda kile akiyatembeza
macho yake mle ndani huku akikumbuka vizuri kuwa Balimenya alikuwa hajaoa wala
kuishi na mwanamke.
Mlango mwingine uliokuwa kwenye kona ya chumba kile kwa upande wa kushoto
ulikuwa ni wakuelekea kwenye chumba cha maliwato. Koplo Tsega alipoufikia mlango
ule na kuusukuma na hapo macho yake yakajikuta yakitazamana na sinki kubwa la
kuogea pamoja na choo cha kukaa cha marumaru kilichopakana na bomba dogo la
maji.
Koplo Tsega alipogeuka nyuma akawa akitazamana na kitanda cha mle ndani
huku akiikumbuka sehemu ya ukumbi mdogo wa kulia chakula iliyokuwa ikipakana
na sebule na jiko ambako bado alikuwa hajazikagua sehemu hizo.
Akiwa ameanza kuridhishwa na hali ya usalama wa mle ndani Koplo Tsega
akaanza kufanya upekuzi kwenye kile chumba. Chini ya godoro hakukuwa na kitu
chochote cha maana zaidi ya faili moja lenye nyaraka muhimu za ofisi ya Balimenya.
Koplo Tsega akakiacha kitanda kile na kuziendea droo mbili za ile meza fupi ya mle
chumbani ambazo nazo hazikuwa na kitu chochote cha maana.
Hatimaye jitihada zake akazihamishia kwenye lile kabati la nguo lililokuwa
likitazamana na kitanda cha mle ndani. Alipoanza upekuzi katika droo ya kwanza
akakuta bastola ndogo aina ya 25 Revolver,magazini mbili za bastola hiyo zilizojaa risasi
na kitambulisho cha kazi cha Belimenya. Ndani ya droo ya pili kulikuwa na mafaili
kadhaa yenye taarifa zinazoihusu ofisi ya Belimenya. Droo ya mwisho ya meza ile
ilikuwa imefungwa. Koplo Tsega akatia utundu wake na ndani ya muda mfupi akawa
amefanikiwa kuifyatua kabari ya droo ile na kuifungua. Mle ndani hakukuwa na kitu
kingine zaidi ya bahasha moja tu ya kaki hivyo Koplo Tsega akaichukua bahasha ile na
kuanza kuichunguza. Ilikuwa bahasha nyepesi yenye kitu mfano wa karatasi nyepesi
ndani yake na juu ya bahasha ile hakukuwa na maelezo yoyote.
Koplo Tsega akaichukua bahasha ile na kuanza kuitathmini kana kwamba ndiyo
kitu pekee alichokuwa akikihitaji. Lakini wakati akiwa anaendelea na tathmini ile hisia
zake zikamtanabaisha kuwa hatua chache nyuma yake kulikuwa na mtu aliyekuwa
akimtazama. Kuitowesha hofu iliyoanza kuzitawala hisia zake akapiga moyo konde
huku akiupisha utulivu kichwani mwake. Hakupata utulivu kwani mikono yake
ilikuwa imeanza kutetemeka huku jasho jepesi likimtoka. Hata hivyo akajihimili na
kuikamata vyema bastola yake mkononi huku akipanga kugeuka ghafla na kufanya
shambulizi la uhakika kwa mtu yoyote ambaye angekuwa nyuma yake akimvizia kwa
hila. Hata hivyo alikuwa amechelewa.
“Tupa bastola yako chini mrembo” sauti ya kiume kutoka nyuma yake ilimuonya.
“Wewe ni nani?” Koplo Tsega akauliza huku sauti yake ikionekana kupwaya.
“Wewe ni nani na umefuata nini humu ndani?” ile sauti nyuma yake ikaongea
kwa tahadhari huku ikilipuuza swali lake na Koplo Tsega alipotaka kugeuka nyuma
akajikuta akikabiliana na maumivu makali ya ngumi mbili kavu mbavuni mwake.
“Utii ni bora kuliko shuruti” yule mtu akasisitiza
Koplo Tsega akaendelea kugugumia maumivu makali yaliyokuwa yakisambaa
mwilini mwake na wakati akifanya hivyo mtu mwingine akaongezeka mle ndani
ambaye alimfikia na kuanza kumpekua kila mahali. Upekuzi ule ulipoisha ile bahasha
ya kaki na bastola yake mkononi vikawa vimechukuliwa na yule mtu.
“Geuka nyuma na mikono juu!” ile sauti nyuma yake ikamtahadharisha na Koplo
Tsega alipogeuka nyuma akajikuta akikabiliana na njemba mbili matata zikimtazama
kwa hasira. Miili ya wanaume wale ilikuwa imeshiba mazoezi ya uhakika. Mmoja
alikuwa mfupi na mwingine alikuwa mrefu ingawa tofauti ya vimo vyao haikuwa
kubwa sana. Wote walikuwa wamevaa suti nadhifu nyeusi na bastola zao mikononi.
Koplo Tsega akabaki akitazamana na wale watu kwa sekunde kadhaa bila mtu
yeyote kutia neno kisha yule mtu mrefu akamfanyia ishara fulani yule mtu mfupi na
hapo yule mtu mfupi akaondoka. Muda mfupi baadaye yule mtu mfupi akarejea na
kiti kimoja alichokichukua kutoka kwenye meza ya chakula ya mle ndani na kukiweka
kando ya kitanda kilichokuwa mle chumbani.
“Karibu uketi mrembo kwani tumeona kuwa hakuna haja tena ya kutumia nguvu
kubwa kama utakuwa tayari kutupa ushirikiano” yule mtu mfupi akaongea kwa utulivu
ingawaje sura yenye chuki bado haikutoweka usoni mwake. Koplo Tsega akajikuta
akijishauri kuwa akae kwenye kile kiti au asikae na wakati akiendelea kujishauri
akashangaa akichotwa mtama wa nguvu na yule mtu mfupi hali iliyompelekea matako
yake yatue kwa kishindo juu ya kiti kile na hapo akapiga yowe la maumivu. Koplo
Tsega alipotaka kufurukuta akatandikwa ngumi nyingine tatu mgongoni huku shingo
yake ikienea vizuri kwenye kabari matata ya yule mtu mfupi.
Kufumba na kufumbua akajikuta amefungwa kamba iliyokazwa kisawasawa
kama mnyama anayetayarishwa kuchinjwa. Mambo yote yakafanyika kimyakimya na
zoezi lile lilipokamilika zile njemba mbili zikashika pembe mbili za kile kiti na kuanza
kukiburuta kile kiti kuelekea kwenye kile chumba cha maliwato kilichokuwa kwenye
kona ya kile chumba.
“Mnanipeleka wapi nyinyi majangili?” Koplo Tsega akauliza huku ameshikwa na
hofu.
“Tunataka kukusaidia mrembo”
“Pumbavu! nani aliyewaambia kuwa nahitaji msaada wenu?” Koplo Tsega akauliza
kwa kufoka
“Hujatuomba ila tumegundua kuwa unahitaji msaada na kwa vile ndiyo kazi yetu
basi hapajaharibika neno” yule mtu mrefu akaongea kwa utulivu lakini bila kujali huku
kwa pamoja wakiendelea kumburuta Koplo Tsega kwenye kile kiti kuelekea kwenye
kile chumba cha maliwato.
Mle ndani ya kile chumba cha maliwato kulikuwa na beseni kubwa la kuogea
pembeni ya koki ya maji. Wale watu wakaendelea kumburuta Koplo Tsega hadi kando
ya lile beseni la kuogea huku akiwa bado amefungwa kwenye kile kiti. Walipofika
yule mtu mfupi akamchapa Koplo Tsega makofi kadhaa na kumsogeza kando ya lile
beseni kisha taratibu akaanza kufungulia maji kwenye lile beseni na hapo mahojiano
yakaanza.
“Wewe ni nani?” yule mtu mrefu akasogea karibu na kuanza kumhoji Koplo
Tsega kwa utulivu huku akiinama chini vizuri ili waweze kutazamana.
“Mbona siwaelewi?” Koplo Tsega akawauliza wale watu kwa hila hata hivyo
akajikuta akiambulia makofi mawili mengine ya usoni.
“Jibu swali kama ulivyoulizwa na usitupotezee muda wetu” yule mtu mfupi
akafoka huku akiisukasuka ovyo shingo ya Koplo Tsega na kumtazama kwa hasira.
“Naitwa Sama” hatimaye Koplo Tsega akaongea kinyonge akidanganya tukio
lililowapelekea wale watu watazamane kidogo kabla ya kuendelea na mahojiano.
“Umefuata nini humu ndani?” yule mtu mrefu akamuuliza Koplo Tsega kwa
utulivu.
“Mimi ni mchumba wa Balimenya” Koplo Tsega akajitetea kwa hila huku
akiyatembeza macho yake taratibu kuwatazama wale watu na alipomaliza akahitimisha
kuwa wale watu walikuwa wageni kabisa machoni mwake ingawa hakuwa na shaka
yoyote kuwa walikuwa ni maafisa usalama.
“Unadhani tunaweza kuuamini huo uongo wako dhaifu?” yule mtu mrefu akauliza
kwa utulivu.
“Mtafuteni mwenyewe mumuulize kama hamniamini” Koplo Tsega akajitetea
kwa hila huku akifahamu fika kuwa hadi kufikia pale Balimenya alikuwa mfu kwa
risasi zake makini zilizohitimisha uhai wake kwenye lile jengo la ghorofa kule maeneo
ya posta katikati ya majengo marefu ya ghorofa.
“Tangu lini msichana mrembo kama wewe ukaenda kwa mchumba wako na
bastola mkononi?” yule mtu mrefu akamuuliza Koplo Tsega kwa utulivu huku
akiigeuzageuza ile bastola ya Koplo Tsega na kuitazama mikononi mwake.
“Bastola hiyo siyo yangu” Koplo Tsega akajitetea.
“Kama siyo yako ni ya nani?” yule mtu mfupi akasogea karibu na kuuliza kwa
shauku.
“Ni ya Balimenya” Koplo Tsega akajitetea kwa hila hata hivyo uongo wake
haukufua dafu.
“Usidhani kuwa sisi ni watoto wadogo kama wewe. Tunatambua silaha zote
zinazomilikiwa na maafisa usalama wetu na hii bastola haipo miongoni mwazo” yule
mtu mfupi akafafanua
“Nyinyi ni maafisa usalama?” Koplo Tsega akauliza huku akijitia mshangao
hata hivyo hakujibiwa kitu badala yake yule mtu mfupi akautoa mfuko mweusi
wa kitambaa kutoka mfukoni mwake na kumvalisha Koplo Tsega kichwani kisha
mahojiano yakaendelea
“Tuambie vizuri wewe ni nani na umefuata nini humu ndani vinginevyo utakiona
cha mtema kuni” yule mtu mrefu akauliza kwa utulivu kama mtu ambaye hakuwa
ameyasikia yale maelezo yote yaliyotangulia.
“Nimekwisha waambia kuwa mimi naitwa Sama,mchumba wa Balimenya. Mbona
hamtaki kunielewa?” Koplo Tsega akaendelea kujitetea kwa hila hata hivyo hakuna
aliyemsemesha tena badala yake akainamishwa kwenye kile kiti alichoketi na kichwa
chake kuzamishwa kwenye yale maji ya beseni kubwa la kuogea ambalo yale maji
yaliyokuwa yakimiminika kwenye ile koki tayari yalikuwa mbioni kujaa.
Likiwa ni tukio la ghafla ambalo Koplo Tsega hakuwa amelitarajia hivyo akajikuta
akifurukuta bila mafanikio kwani wale watu waliendelea kumkandamiza kwenye yale
maji ya lile beseni kwa nguvu zao zote hadi pale walipoanza kuona kuwa alikuwa
akielekea kuishiwa nguvu ndipo wakamuachia huku akihema ovyo. Walipomuweka
sawa yule mtu mfupi akauondoa ule mfuko mweusi kichwani kwa Koplo Tsega na
kumkaba shingo kwa kiganja chake huku akimsogelea kumuuliza.
“Tuambie wewe ni nani?” Koplo Tsega hakujibu chochote badala yake akaendelea
kukohoa ovyo kwani alikuwa amepaliwa vibaya na yale maji huku macho yamemtoka
pima.
“Hatuwezi kukuua msichana mrembo kama wewe. Hata hivyo kama hautotupa
ushirikiano wa kutosha hatuna budi kufanya hivyo”
“Tuambie wewe ni nani na umefuata nini humu ndani” yule mtu mfupi akauliza
kwa msisitizo.
“Nimekwisha waeleza mbona hamtaki kunielewa?” Koplo Tsega akaendelea
kujitetea hata hivyo wale watu wakampuuza na badala yake akashtukia akivalishwa
tena ule mfuko mweusi wa nguo na kichwa chake kukandamizwa tena kwenye yale
maji ya lile beseni la kuogea huku mara hii zoezi lile likifanyika kwa muda mrefu zaidi.
Koplo Tsega akijitahidi kujitetea bila mafanikio.
Wale watu wakaendelea kumkandamiza Koplo Tsega kwenye yale maji ya beseni
la kuogea mle ndani hadi pale walipoona tena kuwa alikuwa ameanza kuishiwa nguvu
ndipo wakamuacha. Yule mtu mfupi akautoa tena ule mfuko mweusi kichwani mwa
Koplo Tsega tukio lililompelekea Koplo Tsega atapike maji mengi kwa mkupuo na
kuanza kukohoa ovyo huku macho yamemtoka.
“Msichana mrembo kama wewe haipendezi kabisa kuwa muongo. Tuambie wewe
ni nani na umefuata nini humu ndani?” yule mtu mfupi akamsogelea tena Koplo Tsega
na kumuuliza huku amemkwida shingoni hata hivyo Koplo Tsega hakuzungumza
neno badala yake aliendelea kukohoa kama aliyepaliwa huku akihema ovyo. Kitendo
cha Koplo Tsega kukaa kimya kikampelekea yule mtu mrefu amsogelee na kumchapa
kofi zito usoni kabla ya kumwambia
“Ni afadhali utuambie ukweli vinginevyo tutakuua humu ndani na kwenda
kuitelekeza maiti yako sehemu kusikojulikana”
“Sina jingine ninalolijua zaidi ya huo ukweli niliyowaambai” Koplo Tsega akaongea
kwa utulivu huku akiendelea kuhema ovyo na macho yamemtoka kwa hofu.
“Hii ndiyo nafasi pekee uliyonayo mrembo vinginevyo usidhani kuwa tutakuwa
na muda mwingine wa kukulazimisha utueleza ukweli” yule mtu mfupi akamsogelea
tena Koplo Tsega na kuishika shingo yake kwa kiganja imara cha mkono wake huku
akimvutia karibu yake na kumtazamana wakati mtutu wa bastola yake mkononi
ukiikunakuna shingo ya Koplo Tsega. Kisha taratibu yule mtu mfupi akaihamishia
bastola yake kwenye matiti ya Koplo Tsega huku akiyatekenya taratibu kwa mtutu wa
bastola yake huku tabasamu la kifedhuli likiumbika usoni mwake.
Tukio lile likampelekea Koplo Tsega ashikwe na hasira na kisha kumtemea
mate usoni yule mtu mfupi. Yule mtu mfupi kuona vile akashikwa na hasira hivyo
akasimama na kujifuta yale mate usoni kwa kiganja chake kisha akaanza kumchapa
makofi ya nguvu na ya mfululizo Koplo Tsega huku akiporomosha matusi ya kila
namna. Kipigo kile kilipozidi mwenzake akaingilia kati na kumzuia. Koplo Tsega
akapiga mayowe kwa nguvu ya kuomba msaada kabla ya kuanza kuhema ovyo huku
damu nyingi ikimtoka mdomoni na puani.
Haukupita muda mrefu mara yule mtu mrefu akasogea karibu na kuanza
kumburuta Koplo Tsega kwenye kile kiti hadi katikati ya kile chumba cha maliwato
kisha akachota yale maji kwenye lile beseni la kuogea kwa ndoo na kuanza kummwagia
Koplo Tsega pale kwenye kile kiti katika namna ya kumuweka sawa kisha akamsogelea
tena na kuendeleza mahojiano. Hali ya Koplo Tsega ikaanza kuwa mbaya na nguvu
mwilini zikaanza kumwishia taratibu. Kipigo cha nguvu kutoka kwa wale watu kikawa
kimeupelekea mdomo wake kuchanika sehemu ya chini na maumivu makali ya
mwamba wa pua yake.
“Kama hutaki kutueleza ukweli tutakuua”
“Mnanionea bure mimi sifahamu chochote” Koplo Tsega akajitetea hata hivyo
hakuna mtu aliyemsikiliza badala yake akajikuta akianza kukabiliana na kipigo cha
nguvu kutoka kwa wale watu. Kipigo chenye mchanganyiko wa ngumi,makofi na
mateke ya kila mahali. Hali ya Koplo Tsega ikazidi kuwa mbaya akawasihi wale watu
wamuache bila mafanikio. Hatimaye nguvu zikaanza kumuishia. Ile sauti ya mayowe
ya kuwasihi wale watu wamuache nayo ikaanza kufifia taratibu. Mwishowe uwezo wa
macho yake kuona nao ukaanza kupungua na mbele yake akawa akiliona wingu jepesi
la giza. Mdomo wake ukawa mzito kuongea. Mwishowe macho yamemtoka
“Msichana mrembo kama wewe haipendezi kabisa kuwa muongo. Tuambie wewe
ni nani na umefuata nini humu ndani?” yule mtu mfupi akamsogelea tena Koplo Tsega
na kumuuliza huku amemkwida shingoni hata hivyo Koplo Tsega hakuzungumza
neno badala yake aliendelea kukohoa kama aliyepaliwa huku akihema ovyo. Kitendo
cha Koplo Tsega kukaa kimya kikampelekea yule mtu mrefu amsogelee na kumchapa
kofi zito usoni kabla ya kumwambia
“Ni afadhali utuambie ukweli vinginevyo tutakuua humu ndani na kwenda
kuitelekeza maiti yako sehemu kusikojulikana”
“Sina jingine ninalolijua zaidi ya huo ukweli niliyowaambai” Koplo Tsega akaongea
kwa utulivu huku akiendelea kuhema ovyo na macho yamemtoka kwa hofu.
“Hii ndiyo nafasi pekee uliyonayo mrembo vinginevyo usidhani kuwa tutakuwa
na muda mwingine wa kukulazimisha utueleza ukweli” yule mtu mfupi akamsogelea
tena Koplo Tsega na kuishika shingo yake kwa kiganja imara cha mkono wake huku
akimvutia karibu yake na kumtazamana wakati mtutu wa bastola yake mkononi
ukiikunakuna shingo ya Koplo Tsega. Kisha taratibu yule mtu mfupi akaihamishia
bastola yake kwenye matiti ya Koplo Tsega huku akiyatekenya taratibu kwa mtutu wa
bastola yake huku tabasamu la kifedhuli likiumbika usoni mwake.
Tukio lile likampelekea Koplo Tsega ashikwe na hasira na kisha kumtemea
mate usoni yule mtu mfupi. Yule mtu mfupi kuona vile akashikwa na hasira hivyo
akasimama na kujifuta yale mate usoni kwa kiganja chake kisha akaanza kumchapa
makofi ya nguvu na ya mfululizo Koplo Tsega huku akiporomosha matusi ya kila
namna. Kipigo kile kilipozidi mwenzake akaingilia kati na kumzuia. Koplo Tsega
akapiga mayowe kwa nguvu ya kuomba msaada kabla ya kuanza kuhema ovyo huku
damu nyingi ikimtoka mdomoni na puani.
Haukupita muda mrefu mara yule mtu mrefu akasogea karibu na kuanza
kumburuta Koplo Tsega kwenye kile kiti hadi katikati ya kile chumba cha maliwato
kisha akachota yale maji kwenye lile beseni la kuogea kwa ndoo na kuanza kummwagia
Koplo Tsega pale kwenye kile kiti katika namna ya kumuweka sawa kisha akamsogelea
tena na kuendeleza mahojiano. Hali ya Koplo Tsega ikaanza kuwa mbaya na nguvu
mwilini zikaanza kumwishia taratibu. Kipigo cha nguvu kutoka kwa wale watu kikawa
kimeupelekea mdomo wake kuchanika sehemu ya chini na maumivu makali ya
mwamba wa pua yake.
“Kama hutaki kutueleza ukweli tutakuua”
“Mnanionea bure mimi sifahamu chochote” Koplo Tsega akajitetea hata hivyo
hakuna mtu aliyemsikiliza badala yake akajikuta akianza kukabiliana na kipigo cha
nguvu kutoka kwa wale watu. Kipigo chenye mchanganyiko wa ngumi,makofi na
mateke ya kila mahali. Hali ya Koplo Tsega ikazidi kuwa mbaya akawasihi wale watu
wamuache bila mafanikio. Hatimaye nguvu zikaanza kumuishia. Ile sauti ya mayowe
ya kuwasihi wale watu wamuache nayo ikaanza kufifia taratibu. Mwishowe uwezo wa
macho yake kuona nao ukaanza kupungua na mbele yake akawa akiliona wingu jepesi
la giza. Mdomo wake ukawa mzito kuongea. Mwishowe macho yakafunga taratibu taratibu na baada ya muda fahamu zikamtoka asijue kinachoendelea.
#211
FAHAMU ZILIMRUDIA Koplo Tsega sambamba na maumivu makali mwilini
yaliyompelekea ahisi kutaka kutapika. Taratibu akataka kujisogeza kutoka pale
alipokuwa ameketi hata hivyo hakufanikiwa kwani haraka akakumbuka kuwa alikuwa
amefungwa kwenye kiti na wale wanaume wawili waliomteka na kuanza kumhoji mle
ndani. Koplo Tsega akayafumbua macho yake taratibu na kuanza kuyatembeza mle
ndani na taswira iliyoumbika machoni mwake ikamtanabaisha kuwa bado alikuwa
kwenye ile nyumba ya Balimenya lakini mara hii akiwa kwenye kile chumba kikubwa
na siyo kule kwenye maliwato alipokuwa akiteswa na wale wanaume wawili.
Koplo Tsega akaendelea kuyatembeza macho yake taratibu mle ndani ya kile
chumba katika namna ya kukipeleleza na kwa kufanya vile jambo moja likamshangaza.
Wale wanaume wawili waliokuwa wakimtesa mle ndani hawakuwepo
“Wameenda wapi?”Koplo Tsega akajiuliza pasipo kupata majibu. Alipoendelea
kuchunguza mbele yake kitandani akaona pakiti ya sigara na kiberiti cha gesi. Taa ya
mle ndani ilikuwa imewashwa na juu ya meza ndogo ya mbao iliyokuwa kando ya
kitanda juu yake kulikuwa na glasi mbili na mzinga mkubwa wa kilevi kando. Utulivu
bado ulikuwa mkubwa mle ndani.
“Wale watu watakuwa wameenda wapi?”Koplo Tsega akaendelea kujiuliza pasipo
kupata majibu hata hivyo kitendo cha kuziona zile glasi na ule mzinga wa pombe
kali juu ya ile meza ndogo pembeni ya kile kitanda mle chumbani kikawa kimeibua
hoja mpya kichwani mwake kuwa huwenda wale watu walikuwa wakitumia kile kilevi
wakati walipokuwa wakimsubiri azinduke baada ya kupoteza fahamu. Ile ingekuwa
nafasi nzuri ya kutoroka mle ndani kabla ya wale watu hawajarudi Koplo Tsega
akajikuta akiwaza.
Koplo Tsega alipotulia na kuyatega vizuri masikio yake mle ndani hakusikia kitu
chochote hivyo taratibu akaanza kuzifungua zile kamba alizofungwa kwenye kile kiti.
Haikuwa kazi rahisi kwani zile kamba zilikuwa imara na zilizofungwa kwa ufundi wa
hali ya juu kiasi cha kutoruhusu mwanya wowote wa kufurukuta. Hata hivyo Koplo
Tsega akiwa ameanza kuhisi kuwa ile ndiyo ingekuwa nafasi yake pekee ya kutoroka
mle ndani hakutaka kulaza damu badala yake akaendelea haraka kuzifungua zile
kamba alizofungwa kwenye kile kiti.
Ilikuwa ni wakati Koplo Tsega alipokuwa akimalizia kujifungua zile kamba kwenye
kile kiti ule mlango ulipofunguliwa na kisha wale wanaume wawili watekaji kuingia
mle ndani kwa mwendo hafifu wa kilevilevi huku bastola zao zikiwa mikononi. Koplo
Tsega hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kutulia kwenye kile kiti na kujidai kuwa
bado alikuwa amepoteza fahamu.
Wale watu walipoingia mle ndani yule mtu mrefu akasimama pale mlangoni huku
yule mtu mfupi akielekea pale kwenye kile alipofungwa Koplo Tsega.
“Mchunguze kama amerudiwa na fahamu?” yule mtu mrefu akaongea akimpa
maelekezo yule mtu mfupi. yule mtu mfupi akaendelea kujongea taratibu hadi pale
kwenye kile kiti alipofungwa Koplo Tsega na kisha kuanza kumchunguza kwa makini
lakini kwa kuwa Koplo Tsega alikuwa bado hajaziondoa zile kamba mwilini yule mtu
mfupi hakuweza kushtukia kitu chochote.
“Bado hajarudiwa na fahamu huyu!” yule mtu mfupi akaongea kwa kujiamini
baada ya kufanya uchunguzi wa kilevilevi.
“Una hakika?” mwenzake akamuuliza
“Kama huniamini basi uje umtazame wewe mwenyewe” yule mtu mfupi akaongea
kwa jazba kidogo baada ya kuona kuwa yule mwenzake bado ana mashaka na lile jibu
lake.
“Unadhani atarudiwa na fahamu mapema?” baada ya kitambo kifupi cha ukimya
kupita yule mtu mrefu pale mlangoni akauliza.
“Daktari anaweza kuwa na jibu la hakika zaidi hata hivyo naamini kuwa atarudiwa
na fahamu muda siyo mrefu kama tutaendela kusubiri”
“Mkuu atafurahi sana pale tutakapomkabidhi huyu mrembo mikononi mwake”
yule mtu mrefu akaongea huku akitabasamu.
“Hilo siyo jambo la kuharakisha Masam japo huyu dada anaonekana ni mtu hatari
kuliko tulivyomdhania hapo awali. Si umeona mwenyewe mifukoni tumemkuta na
kitabu kidogo chenye orodha ya majina ya watu wetu wa usalama waliouwawa. Mimi
naamini kuwa huyu ndiye muuaji mwenyewe tuliyekuwa tukimtafuta na siyo yule mtu
aliyetutoroka kule posta chini ya ghorofa. Huyu dada amevamia humu ndani akiwa
na bastola mkononi hii inamaanisha kuwa alikuwa amejipanga kukabiliana na hatari
yoyote ikiwezekana hata kutoa uhai wa mtu. Huyu dada ni mtu hatari sana tusifanye
naye mzaha hata kidogo” yule mtu mfupi akaongea kwa msisitizo huku akimtazama
Koplo Tsega pale kwenye kiti.
“Kama tutambana vizuri tunaweza kupata pesa yote kupitia zile hundi tulizozikuta
mkukoni mwake”
“Tutafanya kila litakalowezekana katika kuhakikisha kuwa pesa ya kwenye hizi
hundi inaishia mikononi mwetu vinginevyo tukizipeleka kwa wakubwa tutajikuta
tukiwafaidisha wao na familia zao wakati kazi kubwa tunaifanya sisi” yule mtu mfupi
akasisitiza.
“Kuna jambo fulani linaloendelea kufuatia haya mauaji ya wanausalama wenzetu
hata hivyo naamini kuwa huyu dada atakuwa akifahamu vizuri kila kitu. Hivyo atake
asitake mara tu atakapozinduka ni lazima tumbane vizuri atueleze nini kinachoendelea”
yule mtu mrefu akaongea kwa utulivu pale mlangoni.
“Turudi zetu kule sabuleni” yule mtu mfupi akapendekeza akimshawishi
mwenzake.
“Hapana! hatuwezi kuendelea kulewa,huyu dada siyo wa kumfanyia mzaha”
“Ondoa shaka Masam hatuwezi kukaa humu ndani na kumsubiri azinduke kwa
muda wake wakati Balimenya ametuachia vinywaji vingi kwenye jokofu lake” yule
mtu mfupi akajaribu kujenga hoja huku akiangua tabasamu la kilevi kisha akamuacha
Koplo Tsega pale kwenye kiti na kuelekea kwenye mlango wa kile chumba. Alipofika
akampigapiga yule mwenzake begani katika namna ya utani kisha akafungua ule
mlango na kutoka akielekea sebuleni. Yule mtu mrefu akaendelea kusimama pale
mlangoni akimtazama Koplo Tsega kwa utulivu kama anayefikiria jambo. Hata
hivyo baada kitambo kifupi cha ukimya kupita naye ni kama aliyehisi upweke kwa
kukosa mtu wa kuzungumza naye mle ndani. Hivyo na yeye akafungua ule mlango
wa chumba na kutoka akielekea kule sebuleni na baada ya muda mfupi kile chumba
kikawa kimerudiwa na ile hali yake ya ukimya wa awali.
Koplo Tsega akiwa na hakika kuwa wale watu wameshatoka mle chumbani na
kuelekea kwenye sebule ya ile nyumba akayafumbua tena macho yake na kuanza
kuyatembeza taratibu mle ndani. Hakumuona mtu yeyote na mandhari ya mle ndani
bado yalikuwa tulivu hivyo akaendelea kujifungua zile kamba pale kwenye kile kiti na
baada ya muda mfupi akawa amemaliza zoezi lile. Mara baada ya kumaliza kujifungua
zile kamba Koplo Tsega akasimama kichovuchovu huku maumivu makali ya kile
kipigo alichokipata yakianza tena kusambaa mwilini mwake. Koplo Tsega alipojikagua
mifukoni akajua kuwa kile kitabu chake chenye orodha ya majina ya watu aliokuwa
akiwatafuta na ile bahasha yenye hundi nyingi aliyoichukua chumba kwa Meja Khalid
Makame vyote vilikuwa vimechukuliwa na wale watu waliomteka mle ndani. Hivyo
bila kupoteza muda akaichukuwa ile chupa ya mzinga wa pombe kutoka juu ya ile
meza fupi iliyokuwa kando ya kitanda cha mle ndani na kuelekea kwenye ule mlango
wa kile chumba wa kuelekea sebuleni.
Kupitia tundu dogo la funguo kwenye kitasa cha ule mlango wa kile chumba
Koplo Tsega alipochungulia aliweza kuwaona wale wanaume wawili waliomteka.
Wote walikuwa wakitazama runinga iliyokuwa pale sebuleni huku taratibu wakiendelea
kujipatia kinywaji kwenye makochi ya sofa ya pale sebuleni na bastola zao zikiwa
mikononi. Koplo Tsega hakuwa na mashaka yoyote kuwa watu wale hawakuwa
wameshtukia chochote wakati yeye alipokuwa akijifungua zile kamba kwenye kile
kiti mle chumbani. Wakati akiendelea kuwachungulia wale watu kwenye lile tundu
la funguo kwenye kitasa Koplo Tsega akajikuta akiikumbuka bastola yake namna
ambavyo ingeweza kuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na watu wale bila ya
kutumia nguvu. Hata hivyo alitambua kuwa suala lile lisingewezekana kwani ile bastola
yake ilikuwa imechukuliwa na wale watu.
Koplo Tsega akaendelea kuchungulia kwenye lile tundu la kitasa katika namna
ya kujithibitishia kuwa wale watekaji walikuwa wamezama kwenye hamsini zao na
aliporidhika na hali ile akauacha ule mlango na kuelekea kwenye kile chumba cha
bafu akipeleleza mazingira ya mle ndani. Hali ya mle ndani ilikuwa shwari hata hivyo
hakupata silaha yoyote ya kumsaidia hivyo akarudi tena kule chumbani na kuendelea
na upekuzi. Wakati akiifungua ile droo kwenye kabati akagundua kuwa hata ile bastola
iliyokuwa mle ndani nayo ilikuwa imechukuliwa na wale watu.
Ilikuwa ni wakati Koplo Tsega alipokuwa akiendelea na upekuzi mle ndani mara
ghafla akasikia sauti ya hatua za mtu akiukaribia ule mlango wa kile chumba. Haraka
Koplo Tsega akaichukua ile chupa ya mzinga wa pombe na kwenda kujibanza nyuma
ya ule mlango. Haukupita muda mrefu mara kitasa cha ule mlango wa kile chumba
kikazungushwa na ule mlango kusukumwa.
Mtu aliyeingia mle ndani alikuwa ni yule mtu mfupi huku akiwa ameitanguliza
bastola yake mbele kizembezembe. Ulikuwa ni muda mzuri kwa Koplo Tsega kufanya
shambulizi hivyo kwa kasi ya ajabu akatupa pigo moja makini la ile chupa nyuma ya
kichwa cha yule mtu mfupi. Tukio lile likasababisha sauti kali ya mpasuko wa ile chupa
na kabla yule mtu mfupi hajaanguka chini pigo jingine la teke la mkononi lililotupwa
na Koplo Tsega likaipokonya mkononi ile bastola ya yule mtu mfupi na kuitupa
hewani. Yule mtu akaanguka chini kama mzigo huku ile bastola ikitua mkononi mwa
Koplo Tsega. Yule mtu alipojitahidi kusimama haikuwezekana kwani risasi mbili za
mgongoni zikamrudisha chini na kumlaza kifudifundi huku akiwa hajitambui.
Kelele za mikikimikiki ya mle chumbani zikawa zimemshtua yule mtu mrefu kule
sebuleni hivyo haraka akasimama na kuikamata vyema bastola yake akinyata kwa
tahadhari kuusogelea ule mlango wa kile chumba. Koplo Tsega kuona vile akawahi
kujibanza nyuma ya ule mlango wa kile chumba huku akimvizia yule mtu na bastola
yake mkononi. Yule mtu akaendelea kunyata hadi pale mlangoni halafu kama aliyehisi
jambo lisilo la kawaida akasimama kwa utulivu huku akiyatega masikio yake kwa
makini kusikiliza mle ndani ya kile chumba. Hakusikia kitu chochote hata hivyo zile
kelele hafifu za zile risasi mbili kutoka kwenye bastola iliyofungwa kiwambo maalum
cha kuzuia sauti ya Koplo Tsega na zile kelele za mpasuko wa chupa mle ndani zikawa
zimemjengea tahadhari ya aina yake. Yule mtu mrefu akaendelea kusimama pale
mlangoni huku akijipa utulivu na alipoona hakuna kitu chochote kinachosikika mle
ndani akainama taratibu na kuchungulia kwenye like tundu la funguo kwenye kitasa.
Hakuona kitu chochote hivyo akasimama na kuanza kumuita mwenzake kwa sauti ya
chini yenye hofu.
“Remmy,kuna nini?” hakuna mtu aliyemjibu na hali ile ikazidi kumtia mashaka
yule mtu. Kitambo kifupi cha ukimya kikafuatia kabla ya yule mtu kuanza kumuita
tena yule mwenzake na alipoona kuwa hajibiwi akakishika kitasa cha ule mlango na
kuufungua ule mlango taratibu. Ule mlango ulipofunguka nusu yule mtu akachungulia
mle ndani hata hivyo hakuweza kumuona yule mwenzake kwani Koplo Tsega tayari
alikuwa amewahi kumburuta yule mtu na kumficha nyuma ya ule mlango. Yule mtu
mrefu akaendelea kusimama pale mlangoni huku akichunguliachungulia mle ndani
hata hivyo hakuona vizuri hivyo taratibu akaanza kunyata akiingia mle ndani na
bastola yake ikiwa tayari kufanya kazi mkononi.
Koplo Tsega akiwa tayari amejiandaa kukabiliana na yule mtu akakusanya nguvu
za kutosha na kutupa pigo makini la kareti akinuia kuiputa chini bastola ya yule mtu
mkononi. Mara hii lengo lake halikufanikiwa kwani yule mtu alikuwa makini na
mwerevu hivyo akawahi kuukwepesha kidogo mkono wake na kulipelekea pigo la
Koplo Tsega likate upepo bila mafanikio huku yule mtu akiwahi kujitupa mle ndani
sakafuni katika mtindo wa kujiviringisha kama gurudumu. Koplo Tsega alipofyatua
risasi kumlenga yule mtu,yule mtu tayari akawa ameshapotelea kwenye uvungu wa
kitanda cha mle ndani hivyo zile risasi nazo zikachana anga bila majibu.
Kimya kifupi kikafuatia mle ndani huku kila mmoja akijitahidi kumvizia mwenzake.
Yule mtu akajitokeza tena upande wa pili wa kile kitanda na kufyatua risasi hata
hivyo Koplo Tsega aliwahi kujitupa kando huku zile risasi zikimpunyua mgongoni.
Sasa kukawa na kutupiana risasi mle ndani huku kila mmoja akimvizia mwenzake
na kujificha. Majibishano ya risasi yakaendelea kurindima mle ndani na yule mtu
alipoona kuwa ameishiwa risasi akawahi kujitupa na kumkumba Koplo Tsega pale
aliposimama. Tukio lile likawapelekea wote kwa pamoja wapige mwereka na kuanguka
chini kwa kishindo. Hata hivyo yule mtu alipotaka kuwahi kusimama akajikuta tayari
kichwa chake kimeshaenea kwenye kabari matata ya miguu ya Koplo Tsega kabla ya
kukabiliana na mapigo mawili ya ngumi za uso zilizouvunja vibaya mwamba wa pua
yake. Yule mtu akapiga yowe la maumivu makali na kwa kuwa alikwishaiona hatari
ya kudhibitiwa na Koplo Tsega akakusanya nguvu na kuinuka huku akiwa amembeba
Koplo Tsega mzegamzega akipanga kwenda kumpigiza ukutani. Hata hivyo Koplo
Tsega alikuwa mjanja kuishtukia hila ile hivyo haraka akawahi kufungua ile kabari ya
miguu shingoni kwa yule mtu kisha walipofika ukutani akawahi kuikita mbele miguu
yake na kujitupa kwa nyuma huku akimchapa yule mtu kwa kiwiko cha mgongo na
yeye akirukia upande wa pili.
Yule mtu akajipigiza ukutani huku maumivu makali yakisambaa mwilini mwake
hata hivyo aliwahi kugeuka na kurudi kule nyuma kumkabili Koplo Tsega. Yule mtu
alipomfikia Koplo Tsega akatupa mapigo mawili ya ngumi usoni mwake hata hivyo
Koplo Tsega akawahi kuyapangua mapigo yale kisha akageuka na kutupa pigo moja
makini la teke la kifua lililomtupa chini yule mtu bila pingamizi lolote. Yule mtu kuona
vile akashikwa na hasira hivyo haraka akalivua koti lake la suti na kulitupa kando. Safari
hii Koplo Tsega hakufua dafu kwani wakati akifika pale chini kumkabili yule mtu
akajikuta akirudishwa kule alipotoka kwa pigo makini la teke la tumbo lililompelekea
apige yowe kali la maumivu na kabla hajatulia yule mtu tayari akawa amemfikia na
kuanza kumtupia mvua ya ngumi kila mahali. Koplo Tsega akajikuta akikabiliana na
wakati mgumu wa kuzikwepa na kuzipangua zile ngumi kwa haraka ili zisimfikie na
kuzidi kumtia udhaifu. Hata hivyo yule mtu hakumpa nafasi ya kujitetea kwani akawa
akizidisha mashambulizi zaidi na ya nguvu.
Koplo Tsega kuona vile akawahi kuinama na kumkwepa yule mtu huku akijirusha
juu ya kile kitanda na kujiviringisha akiangukia upande wa pili. Yule mtu kuona vile
akamfuata Koplo Tsega kule alipoangukia akipita juu ya kile kitanda hata hivyo
alikwishachelewa kwani wakati akifika katikati ya kile kitanda Koplo Tsega akawahi
kukibinua kile kitanda na kumrusha yule mtu kule alipotoka na hapo chaga za kile
kitanda zikavunjika. Yule mtu kuona vile akakisogeza kile kitanda pembeni na
kuchukua mbao moja ya chaga kisha akaruka karibu na kumkabili Koplo Tsega pale
alipokuwa. Alipomfikia akaanza kutupa mapigo mengi kwa kutumia ile mbao ya
chaga ya kitanda. Koplo Tsega akawa akihama kwenda upande huu na ule kuyakwepa
mapigo yale. Hata hivyo yule mtu alikuwa mjuzi wa hila hivyo akawa akimtishia Koplo
Tsega upande mmoja na kumtandika kwa ile mbao upande mwingine. Pigo moja
likampata Koplo Tsega begani na kumsababishia maumivu makali. Mapigo mengine
yaliyofuata akawa akiyapangua ingawa yalimuumiza vibaya mikononi. Pigo la mwisho
likampata vizuri mgongoni kiasi cha kuipelekea ile mbao kupasuka vipandevipande.
Koplo Tsega akapiga yowe kali la maumivu huku akipepesuka na kurudi nyuma.
Yule mtu kuona vile akazidi kumfuata Koplo Tsega haraka kumkabili hata hivyo
hakufanikiwa badala yake akajikuta akichapwa mateke mawili ya kifua yaliyomrudisha
nyuma na kumtupa kwenye kabati la mle ndani na kuvipelekea vioo vya kabari lile
kuvunjika na kuanguka chini.
Yule mtu kuona vile akazidi kushikwa na hasira hivyo akawahi kusimama na
kuanza kutimua mbio akipanga kumvaa Koplo Tsega na kuanguka naye chini. Koplo
Tsega akiwa tayari ameishtukia hila ile akamkwepa kidogo yule mtu na kumsindikiza
kwa teke lingine zito la mgongoni lililompigiza tena yule mtu ukutani. Yule mtu akiwa
tayari ameanza kuhisi dalili za kuzidiwa maarifa kwa hasira akachana shati lake na
kulitupa sakafuni huku akibakiwa na tai shingoni na singlet nyeupe kifuani kisha
haraka akasogea karibu kumkabili Koplo Tsega. Mapigo mawili ya kareti aliyotupa
moja likasababisha maumivu makali kwenye titi la kushoto la Koplo Tsega huku
jingine likitia udhaifu mkubwa kwenye shingo yake na kumpelekea apepesuke
akirudi kinyumenyume. Pigo la tatu lilipomfikia usoni akawahi kulikwepa na kisha
kuchomoka na kichwa kimoja makini kilichokongoloa meno manne ya mbele ya yule
mtu na kuusambaratisha vibaya mwamba wa pua yake na kupelekea kamasi nyepesi za
damu zianze kuchomoza taratibu kwenye matundu ya pua yake. Maumivu yale makali
yakampelekea yule mtu apige yowe kali la maumivu huku akiyumbayumba ovyo kama
bondia aliyetupiwa sumbwi zito.
Koplo Tsega kuona vile akajitupa hewani na kuzunguka kwa uhodari akitupa
mapigo mawili makini ya mateke yaliyokilevya vibaya kichwa cha yule mtu na kumtupa
tena kwenye lile kabati la mle chumbani. Lilikuwa ni pigo la funga kazi kwani yule
mtu alikipigiza vibaya kichwa chake kwenye kona ya lile kabati kabla ya kuanguka
chini na wakati akifanya vile Koplo Tsega akawa tayari amekwishajitupa sakafuni na
kuizoa ile bastola yake iliyomponyoka pale awali. Kufumba na kufumbua tayari akawa
ameishajiviringisha na kumfikia yule mtu pale alipoangukia kisha haraka akamkwida
yule mtu kwa tai yake shingoni. Hata hivyo alijikuta katikati ya mshangao kwani
tofauti na alivyotarajia mara hii Koplo Tsega alipata upinzani hafifu kwani kichwa cha
yule mtu kilikuwa kimepasuka kwa nyuma na damu ilikuwa imeanza kuvuja kutoka
kwenye lile jeraha.
“Mna shida gani na mimi?” Koplo Tsega akamuuliza yule mtu kwa hasira
huku akimkwida shingoni kwa ile tai yake. Yule mtu akajitahidi kuzungumza neno
hata hivyo halikusikika badala yake akasikika akitoa sauti hafifu ya mkoromo na
kujinyonganyonga miguu na mikono yake huku damu nyingi ikimtoka puani na
mdomoni.
“Nyinyi ni nani na mnashida gani na mimi?” Koplo Tsega akaendelea
kumuuliza yule mtu huku akizidi kumkwida shingoni kwa tai yake. Hata hivyo
yule mtu hakuzungumza kitu kwani hali yake ilikuwa imezidi kuwa mbaya sana na
hapakuonekana tumaini lolote la uzima nafsini mwake.
Koplo Tsega hakuona sababu ya kuendelea kupoteza muda hivyo akainama na
kuanza kumpekua vizuri yule mtu. Upekuzi ule ulifanyika kwa haraka na alipomaliza
akawa amepata kitambulisho cha kazi cha yule mtu kilichomtambulisha kama afisa
wa usalama,simu ya mkononi na ile bahasha yenye hundi nyingi aliyoichukua kule
nyumbani kwa Meja Khalid Makame. Vyote vikiwa kwenye mfuko wa ndani wa
koti la suti la yule mtu. Koplo Tsega Akaichukua ile bahasha na kuitia mfukoni kisha
akasimama na kumsindikiza yule mtu kwa risasi mbili za kifua zilizompelekea yule
mtu atikisike kidogo na kutulia huku roho yake ikiwa mbali na mwili.
Ndani ya muda mfupi uliofuata Koplo Tsega akawa pia amemaliza kumfanyia
upekuzi yule mtu mwingine mfupi ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuua
mle ndani. Kwenye mfuko mrefu wa koti lake la suti akakuta magazine moja ya
bastola iliyojaa risasi,kitambulisho kimoja cha kazi kikimtambulisha yule mtu kama
afisa usalama kama yule mwenzake pamoja na ile bahasha iliyokuwa kwenye droo
ya kabati la mle chumbani ambayo wale watu walikuwa wameichukua kwake wakati
walipokuwa wakimteka mle ndani. Ile bahasha ya kaki akaitia mfukoni na kuanza
kuzunguka mle ndani akiitafuta ile bastola yake sehemu ilipokuwa imeangukia wakati
ule yale mapambano yalipokuwa yakiendelea mle ndani.
Kwa namna moja au nyingine Koplo Tsega aliamini kuwa wale watu aliopambana
nao mle ndani wangekuwa wakisubiriwa kutoa ripoti juu ya nini kilichokuwa
kikiendelea juu ya kazi waliyotumwa. Hivyo ukimya wao wa muda mrefu ungeweza
kusababisha mashaka kwa huyo mtu wao aliyekuwa akisubiri kupewa ripoti kutoka
kwao na hali hiyo ingeweza kumpelekea mtu huyo kufika pale mapema iwezekanavyo.
Koplo Tsega hakutaka kukutwa tena mle ndani hivyo kila alichokifanya alikifanya kwa
haraka. Muda mfupi uliofuata akawa amemaliza kufanya upekuzi makini katika ile
nyumba ya Balimenya pasipo kupata kitu chochote kingine muhimu katika uchunguzi
wake.Hatimaye hakuona sababu ya kuendelea kupoteza muda wake zaidi mle ndani
hivyo haraka akatoka kwenye ile nyumba ya Balimenya na muda mfupi uliyofuata
alikuwa akitembea taratibu na kwa tahadhari akielekea kwenye ile barabara ya mtaa
alipoegesha gari lake. Dakika chache baadaye Koplo Tsega alikuwa mbali na ile
nyumba ya Balimenya akikatisha kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam huku mawazo
mengi yakipita kichwani mwake. Usiku bado ulikuwa mwingi.
TAARIFA ZA KUUWAWA KWA MAAFISA wengine wawili wa usalama
zilikuwa zimempelekea mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa M.D Kunzugala
kuiona kahawa aliyokuwa akiinywa imebadilika ghafla na kuwa chungu kama supu
ya mwarobaini ndani ya ofisi yake hii iliyopo juu ya jengo moja la ghorofa. Taratibu
akakishusha kikombe chake cha kahawa na kukiweka juu ya meza yake ya ofisini
huku mkono wake wa kushoto ukiwa bado umeshikilia kiwambo cha simu ya
mezani sambamba na sikio lake. Sauti ya upande wa pili wa ile simu haraka ilikuwa
imempelekea amfahamu mzungumzaji. Sulle Kiganja,kachero na mwanausalama
mwandamizi alikuwa akizungumza upande wa pili wa ile simu.
“Umejuaje?” M.D Kunzugala akauliza kwa taharuki akiendeleza maongezi yale.
“Nipo eneo la tukio Chifu” Sulle Kiganja akatanabaisha.
“Unamaanisha kuwa sasa hivi upo nyumbani kwa Balimenya?” M.D Kunzugala
akauliza kwa hakika
“Ndiyo Chifu,tumeikuta miili miwili ya maafisa wetu”
“Damn shit!,nani aliyefanya upuuzi huo?” M.D Kunzugala akauliza kwa jazba
huku akifahamu fika kuwa asingeweza kupata jibu la moja kwa moja hali iliyompelekea
aanze kulikumbuka tena jina la Chaz Siga,komandoo mstaafu wa jeshi la wananchi
wa Tanzania aliyesemekana ndiye aliyemteka mmoja wa wanausalama wake katika
lile jengo moja refu la ghorofa lililopo maeneo ya posta jijini Dar es Salaam. Hasira
zikamshika akakizoa kile kikombe cha kahawa juu ya meza na kukibamiza ukutani
kikipasuka vipande vipande na kutengeneza doa hafifu la kahawa nyeusi.
“Chifu?...” sauti ya Sulle Kiganja upande wa pili wa ile simu ikaita baada ya kitambo
kifupi cha ukimya kuzidi kuendelea.
“Una hakika gani kuwa hiyo miili ni ya watu wetu?” M.D Kunzugala akauliza
huku akijitahidi kuimeza hasira kali kifuani mwake kwa kitendo cha idara yake ya
usalama kuzidi kuchafuliwa na mauaji ya kiholela.
“Masam na Remmy ni maafisa wetu,nawatambua vizuri na ni watu wangu wa
karibu ambao wamekuwa wakifanya kazi na mimi kwa muda mrefu” Sulle Kiganja
akafafanua huku akikohoa kuiweka sauti yake sawa.
“Walikuwa wakifanya nini nyumbani kwa Balimenya?” M.D Kunzugala akauliza
kwa udadisi.
“Niliwatuma kuichunguza nyumba ya Balimenya na kuweka mtego wa kumnasa
mtu yeyote ambaye angeonekana kuinyemelea nyumba hiyo. Nadhani muuaji
aliwazidi nguvu” Sulle Kiganja akaongea kwa utulivu huku sauti yake ikipwaya baada
ya kuhisi alikuwa na sehemu ya kulaumiwa katika mauaji yale. Kitambo kifupi cha
ukimya kikapita huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye fikra fulani kisha sauti
ya M.D Kunzugala ikarudiwa tena na uhai baada ya kikohozi hafifu kusikika.
“Bado sijaridhika na utendaji wako Sulle,nadhani haupo makini. Ulishindwa
kumkamata muuaji wakati ukiwa na watu wa kutosha na makini kule posta kwenye
jengo la ghorofa na sasa unanipigia simu kunifahamisha juu ya vifo vya maafisa wangu
waliouwawa na mtu huyohuyo uliyemruhusu kutoroka”
“Samahani sana Chifu nataka kukuhakikishia hilo halitatokea tena kwani tunafanya
kila jitihada za kuhakikisha kuwa mtu aliyehusika na mauaji haya anakamatwa na sheria
kuchukuwa nafasi yake” Sulle Kiganja akajitetea huku akianza kuingiwa na hofu juu ya
hatari ya kupoteza kazi yake. Hata hivyo M.D Kunzugala akayapuuza maelezo yake na
kumtumbukizia swali jingine.
“Nani aliyekufahamisha juu ya vifo vya hao maafisa usalama nyumbani kwa
Balimenya?”
“Nilikuwa nikiwasiliana nao kwa simu tukifahamishana juu ya kile kilichokuwa
kikiendelea lakini baadaye muda mrefu ulipita pasipo kusikia chochote kutoka kwao
ndiyo ikanibidi niongozane na maafisa wengine kufuatilia nini kinachoendelea” Sulle
Kiganja akafafanua.
“Nini kinachoendelea sasa hivi?” M.D Kunzugala akauliza huku sauti yake
ikionekana kukosa utulivu.
“Nimewasambaza watu wangu kila kona ya eneo hili kwani inaonekana kuwa
mauaji haya yamefanyika muda mfupi uliyopita. Hivyo ni imani yangu kuwa hadi
kufikia wakati huu muuaji atakuwa bado hajafika mbali sana na eneo hili. Kama bahati
itakuwa kwetu huwenda huyu muuaji tukamtia mikononi mapema iwezekanavyo”
“Sikiliza Sulle…,mimi sipendi mambo ya kubahatisha. Wapange vizuri watu wako
na uhakikishe kuwa huyo muuaji anakamatwa mapema sana iwezekanavyo. Kama
wewe unavyoona mambo magumu kwako na mimi pia ni hivyohivyo. Ungekuwepo
hapa ofisini kwangu na kushuhudia simu zinazomiminika kutoka kwa wakubwa wangu
sidhani kama ungethubutu kuzungumzia masuala ya bahati katika kushughulika na
hili jambo. Nimekwambia fanya linalowezekana kuhakikisha haya mauaji hayaendelei
na mhusika anakamatwa. Nimeitwa Ikulu ninakikao cha dharura na Rais juu ya haya
mauaji yanayoendelea. Ni matumaini yangu kuwa tutakapowasiliana tena utakuwa
na taarifa zinazoeleweka na siyo hizi blah! blah! zako unazonizugia na nazo kunipa
matumaini” M.D Kunzugala akamaliza kuongea kwa jazba na kukata simu kwa hasira.
#253
MIALE YA MWANGA WA JUA LA ASUBUHI ulipenya kupitia kioo cha
dirisha la chumbani na kuyapa uhai macho yangu na hapo nikayafumbua
taratibu na kuanza kupepesa huku na kule. Hisia zangu zikanieleza kuwa
nilikuwa kwenye mazingira tofauti kabisa na yale niliyoyazoea. Hapa ni wapi? Wakati
nikiendelea kujiuliza kumbukumbu za matukio yote yaliyotokea siku ya jana ikaanza
kujitengeneza upya kichwani mwangu.
Nikaanza kukumbuka namna nilivyokutana na Pastor Romanus wa kanisa la The
Last Days Ministry na kufanya naye kikao kifupi chenye majadiliano ya kina juu ya yale
yanayoendelea katika ulimwengu huu. Nikaendelea kukumbuka namna nilivyopata
dodoso chache juu ya Gabbi Masebo na msichana aliyefunga naye ndoa ambaye
alisemekana kuwa alikuwa muumini wa kanisa lile. Kufikia hapo nikakumbuka namna
nilivyokuwa nimemuomba Pastor Romanus anitafutie taarifa zote muhimu za Gabbi
Masebo na yule msichana aliyefunga naye ndoa likiwemo jina la msichana huyo na
mahali ndoa yao ilipofungwa. Nikakumbuka namna nilivyomuachia Pastor Romanus
kadi yangu ya mawasiliano ili anifahamishe haraka pale atakapokuwa amepata taarifa
hizo. Baadaye nikakumbuka namna nilivyofanikiwa kuwatoroka wale wanausalama
kule Botanical Garden maeneo ya posta ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kutoka
kuonana na Pastor Romanus.
Sasa nilikumbuka vizuri kuwa mara baada ya kufanikiwa kuwatoroka wale watu
kwenye lile eneo la Botanical Garden maeneo ya posta nilikuwa nimekodi teksi
na kuelekea mahali ilipo Hotel Agent 11 kuonana na mwanamama wa kinaijeria
aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Iko-Ojo Obaje wakati ule nilipokutana naye
usiku ndani ya Vampire Casino. Ni dhahiri kuwa kitendo cha Iko-Ojo Obaje kunipa
mwongozo wa anwani ya kumpata kupitia ile kadi aliyonipa usiku ule kule Vampire
Casino siyo tu kilikuwa kimefungua milango wazi ya kukuza urafiki wetu lakini vilevile
nilikuwa katika nafasi nzuri kabisa ya kuugusa moyo wake.
Nilipoendelea kukumbuka nini kilichofuata baada ya kupewa mapokezi mazito
na mwanamke yule wa kinaijeria wakati nilipokifikia chumba chake mle hotelini na
kugonga hodi ndiyo nikakumbuka vizuri kuwa pale nilikuwa wapi.
Nilikuwa ndani ya chumba namba 22 cha jengo la ghorofa la Hotel Agent
11 huku mwenyeji wa chumba kile akiwa ndiye yule mama wa kinaijeria Iko-Ojo
Obaje. Nikaendelea kukumbuka namna nilivyozama kwenye mapenzi motomoto
ya mwanamama yule katika kitanda kile muda mfupi baada ya kukaribishwa vizuri
mle ndani ya kile chumba usiku wa jana. Loh! kumbukumbu ile ikanipelekea nianze
kutabasamu taratibu pale kitandani kisha pasipo kugeuka nikaupeleka mkono wangu
kwa kiumbe kile. Mara hii sikufanikiwa na jitihada zangu zikagonga mwamba. Hisia
zangu zikanieleza kuwa nilikuwa nimeachwa peke yangu pale kitandani. Moyo
wangu ukalipuka ghafla,nikatupa shuka pembeni na kuketi pale kitandani. Mara hii
nikagundua kuwa sikuwa na nguo hata moja mwilini kama nilivyozaliwa. Hata hivyo
hali ile haikunishtua sana kama kile kitendo cha kutokumuona mwenyeji wangu akiwa
pale kitandani.
Kwa sekunde kadhaa nikaendelea kuketi pale kitandani huku nikiupisha utulivu
kichwani mwangu. Nilipoyatembeza macho yangu mle ndani nikajiridhisha kuwa
mandhari ya kile chumba yalikuwa hayajabadilika. Upande wangu wa kushoto
kulikuwa na dirisha pana lililofunikwa kwa pazia refu na jepesi. Mbele ya kile kitanda
kulikuwa na runinga kubwa ukutani na pembeni ya runinga ile kulikuwa na kabati
kubwa la nguo. Nilipoyatembeza macho yangu upande wa kulia nikaona makochi
mawili ya sofa yanayotazamana na meza fupi ya mbao ya mti wa mpingo pembeni ya
chungu kikubwa chenye ua la kupandwa la asili. Juu ya meza ile kulikuwa na glasi mbili
na chupa nne tupu za pombe kali tupu kando ya kibakuli kidogo cha majivu ya sigara
chenye vipisi vingi vya sigara vilivyotelekezwa.
Hatua chache kutoka pale yalipokuwa yale makochi na ile meza kulikuwa na
mlango wa kuingilia mle chumbani na nyuma ya mlango ule nikaziona nguo zangu
zikiwa zimening’inizwa katika sehemu maalum. Mlango ule ulikuwa ukitazamana na
mlango mwingine wa kile chumba kwa upande wa pili ambao haraka nilipouchunguza
nikagundua kuwa ulikuwa ni mlango wa kuelekea sehemu ya maliwato ya kile chumba.
Kiyoyozi makini bado kilikuwa kikiendelea kusambaza hewa safi mle ndani.
Haraka nikajisogeza pembeni na kushuka kwenye kile kitanda huku nikivinyoosha
viungo vyangu mwilini kuondoa uchovu kisha nikaelekea kwenye lile kabati la nguo
mle ndani. Nilipolifungua ndani yake nikaziona nguo nyingi za kike zilizotundikwa
kwenye sehemu maalum ya kuning’inizia nguo mle ndani na chini yake kulikuwa na
sanduku dogo la nguo lililokuwa wazi. Ndani ya sanduku lile kulikuwa na nguo nzuri
za kike za bei ya ghari zilizonyooshwa na kupangwa vizuri na sehemu ya juu ya lile
sanduku kulijaa vipodozi vya kila namna.
Nilishawishika kutaka kupekua lile sanduku na kwa kufanya vile nikaviona vibunda
vya noti nyingi vya dola za kimarekani vikiwa vimepangwa kuifunika sehemu yote ya
chini ya lile sanduku chini ya nguo. Ilikuwa fedha nyingi sana kwani pamoja na kuwa
ingelinichukua muda mrefu kukaa chini kwa utulivu na kuhesabu kiasi kile cha fedha
lakini kwa tathmini yangu ya awali ilikuwa ni vigumu kidogo kwa raia wa kawaida wa
kiafrika kumiliki kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kama kile. Lakini vilevile lingekuwa
ni jambo la hatari kwa mtu kuweza kutembea na kiasi kingi cha pesa kama kile kwenye
sanduku badala ya kuweka benki ambapo ndiyo sehemu salama zaidi ya kutunzia
fedha
Niliendelea na upekuzi wangu kwenye lile sanduku na hapo nikakutana na kadi
nyingi za ATM za benki tofauti za kimataifa zenye majina tofauti ya kike na ya kiume
na pasi moja ya kimataifa ya kusafiria yenye picha ya yule mwenyeji wangu huku ikiwa
na jina la Chimamanda Okechukwu,mwanamke raia wa Nigeria iliyogongwa mihuri
mingi katika namna ya kunieleza kuwa mmiliki wa pasi ile ya kusafiria alikuwa ni
mtu wa safari nyingi za kimataifa nje ya taifa lake. Niliitazama pasi ile ya kusafiria
kwa makini huku hisia za kudanganywa zikianza kupenya taratibu nafsini mwangu.
Nilianza kuhisi kuwa Iko-Ojo Obaje alikuwa amenidanganya juu ya jina lake kutokana
na ile pasi ya kusafiria yenye jina tofauti na lile alilojitambulisha kwangu huku ikiwa
na picha yake na kwa kweli sikujua kwa nini alikuwa amefanya vile.Nilimaliza upekuzi
wangu pasipo kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya lile sanduku ingawa hisia
tofauti juu ya yule mwanamke zilikuwa zimeanza kuniingia moyoni.
Mwanzoni nilidhani kuwa Iko-Ojo Obaje huwenda angekuwa ndani ya kile
chumba cha maliwato akijifanyia usafi na kuoga hata hivyo nilipousogelea ule mlango
na kuufungua sikumuona mtu yeyote mle ndani hali iliyonipelekea niamini kuwa Iko-
Ojo Obaje hakuwepo katika mazingira yam le ndani ya kile chumba. Ameenda wapi
na amewezaje kuondoka mle ndani kimyakimya pasipo mimi kushtuka huku sote
tukiwa tumelala kitanda kimoja?. Kwa nini hakutaka kuniaga?. Niliendelea kujiuliza
bila kupata majibu ingawa kwa namna moja au nyingine niliamini kuwa asingekuwa
mbali na maeneo yale kwa vile vitu vyake vyote bado vilikuwa mle ndani pamoja na
kiasi kile kikubwa cha fedha sandukuni.
Nafsi yangu ikanionya kuwa sikutakiwa kuwa na haraka badala yake nilipaswa
kuvuta subira. Hivyo taratibu nikazitupa hatua zangu hafifu kuelekea nyuma ya ule
mlango wa kile chumba mahali nguo zangu zilipokuwa zimening’inizwa. Nilipofika
nikafanya upekuzi wa haraka wa vifaa vyangu vyote muhimu vya kazi kwenye mifuko
ya nguo zile. Kitendo cha kuikuta bastola yangu ikiwa salama kwenye mfuko wa
lile koti langu la kijasusi na vifaa vyangu vyote vya kazi kikanipa matumaini kuwa
sikupaswa kuwa mashaka sana nafsini mwangu.
Nikiwa bado nimesimama pale nyuma ya mlango nikaendelea kuyatembeza
macho yangu taratibu mle ndani na kwa kufanya vile nikaiona simu ya mezani ikiwa
juu ya stuli ndefu ya mbao iliyokuwa kando ya kitanda cha mle ndani. Wazo jipya
likawa limeumbika kichwani mwangu baada ya kuwaza kuwa ule ungekuwa ndiyo
muda mzuri wa kufanya mawasiliano na Mwasu kule ofisini kwangu ili kumueleza
mambo yote yaliyotokea na kumtoa hofu juu ya kwanini hakuniona ofisini mapema
kama ilivyokuwa kawaida yangu. Hata hivyo ni kama niliyekuwa nikibahatisha tu
kwani sikuwa na hakika ya moja kwa moja kama simu ile ilikuwa na uwezo wa kutoka
nje ya lile jengo la ile Hotel Agent 11.
Hatimaye nilifanikiwa kwani baada ya miito kadhaa simu ya upande wa pili
ikapokelewa na Mwasu hata hivyo kupitia sauti yake nikagundua ni kama mtu
aliyekuwa na wasiwasi juu jambo fulani nisilolifahamu.
“Mwasu ni mimi Chaz Siga” niliwahi kujitambulisha.
“Habari za asubuhi,upo wapi Chaz?. Nilianza kupatwa na mashaka nikidhani
jambo baya limekutokea” Mwasu akaongea kwa shauku akionesha kujali.
“Nzuri tu,ondoa shaka Mwasu mimi bado niko salama ingawa changamoto za
hapa na pale hazikosekani kama unavyojua” niliongea kwa utulivu huku nikitengeneza
sauti ya kirafiki kisha nilipokohoa kidogo kuliweka koo langu sawa Mwasu akawahi
kuniuliza.
“Vipi utakuja ofisini leo?”
“Bado sina hakika,kwani vipi,kuna mtu yeyote anashida na mimi?” nikauliza.
“Wapo ila imenibidi niwatake waniachie namba zao za simu ili utakapofika
niwapigie na kuwafahamisha kuwa umerudi”
“Umefanya vyema sana Mwasu hata hivyo ningependa nikutahadharishe kuwa
kuanzia sasa kuwa makini kwani nimeanza kuhisi hatari kubwa katika kushughulika
na huu upelelezi wa Mifupa 206”
“Una maana gani?” Mwasu akauliza kwa shauku
“Kutoweka kwa Gabbi Masebo siyo tukio jepesi kama nilivyokuwa nimelichukulia
hapo awali. Nimefikia hatua ya kuhisi kuwa kuna jambo la hatari zaidi lililofichika
nyuma ya kutoweka kwake na jambo hilo huwenda lina mtazamo mkubwa wa
kimaslahi kwa serikali au viongozi wachache wa serikalini. Hali inayonipelekea nianze
kuhisi kila hatua ninayoipiga kwenda mbele ndiyo ninavyozidi kukikaribia kifo na siyo
tamati ya haraka ya mkasa huu” niliweka kituo na hapo nikasikia sauti hafifu ya mguno
wa Mwasu kutoka upande wa pili wa ile simu.
“Kama ni hivyo kwanini usiachane nao na kurudisha kiasi cha pesa ulichokichukua
kama malipo ya awali ya kazi yenyewe. Mimi nadhani ungemuita mzee James Risasi na
kumueleza bayana kuwa hutoweza tena kuendelea na kazi yake na kumrudishia pesa
yake” Mwasu akaongea kwa msisitizo.
“Hapana Mwasu siwezi kufanya hivyo”
“Kwa nini usifanye hivyo na kazi yenyewe ni ya hatari namna hiyo?”
“Hii kazi nimeshapiganayo hatua istoshe bado ninauhitaji mkubwa pesa. Nahitaji
kukulipa mshahara lakini vilevile kodi ya pango inatusubiri na matumizi mengine
madogomadogo na nikisema hii kazi imenishinda huu utakuwa ndiyo mwanzo wa
kufukuza wateja”
“Sasa pesa yenyewe itakuwa na faida gani kama utakuwa mfu?” Mwasu akauliza
kwa jazba kwa vile alikuwa akinipenda sana,kuniheshimu na kunijali vinginevyo
angeweza hata kunitukana.
“Bado sijafikia hatua hiyo Mwasu. Hebu ngoja tuone nini kitakachofuata baada
ya hapa” nikaweka kituo kisha nikaanza kumuelezea Mwasu mlolongo wa matukio
yote yaliyotokea mpaka kufikia muda ule. Hata hivyo katika maongezi yangu nilikuwa
makini kutomtaja Iko-Ojo Obaje,mwanamke wa kinaijeria ambaye alikuwa ameniacha
mle chumbani katika mazingira yasiyoelezeka. Nilipomaliza kusimulia nikamsikia
Mwasu akitua chini pumzi nyingi kama mtu aliyeanza kuingiwa na mashaka.
“Ndiyo maana nikakusisitiza kuwa uwe makini sana kuanzia sasa” nikahitimisha.
“Nimekuelewa” hatimaye Mwasu akaongea kwa sauti tulivu.
“Bado nipo mitaani naendelea na kazi hivyo kila nitakapopata muda nitakuwa
nikikufahamisha yanayoendelea. Wewe endelea kutengeneza ripoti nzuri yenye
maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na huu mkasa wa Mifupa 206. Nitakapokuja
ofisini nitajazia vipengele vilivyosalia. Kazi njema,” niliwahi kumuaga Mwasu lakini
kabla sijamaliza akanikatisha.
“Chaz…”
“Naam! zungumza Mwasu nakusikia”
“Umepata taarifa juu ya mlipuko wa bomu uliyotokea posta?. Nasikia magaidi
wameingia jijini Dar es Salaam”
“Nani aliyekwambia?” nikamuuliza Mwasu kwa udadisi huku nikitabasamu
“Gazeti moja limeandika hivyo”
“Siyo magaidi Mwasu ni mimi” nikaongea huku nikicheka na kabla Mwasu
hajanitupia swali jingine nikawahi kukata ile simu.
Nilipogeuka nyuma Iko-Ojo Obaje alikuwa nyuma yangu kiasi cha umbali wa
hatua moja huku tabasamu jepesi likiwa limejivinjari usoni mwake. Moyo wangu
ukalipuka na kupiga kite kwa nguvu huku kijasho chepesi kikinitoka maungoni
mwangu. Nikamtazama Iko-Ojo Obaje kwa utulivu huku usoni nikilazimisha
tabasamu ingawaje sikuwa nimeona kitu chochote cha kunifanya nitabasamu mbele
yake. Hata hivyo taratibu nikafanikiwa kuumeza mshtuko ule na kuvaa tabasamu la
asili.
Iko-Ojo Obaje alikuwa amevaa suruali nyepesi nyeusi ya jeans iliyolichora
vyema umbo lake maridhawa lenye uwezo wa kuziteka hisia za mwanaume yeyote.
Miguuni alikuwa amevaa viatu virefu vyekundu vya mikanda. Kichwani nywele zake
za rasta alikuwa amezikusanya na kuzifunga kwa nyuma kama mkia wa farasi na
kumpelekea azidi kupendeza. Machoni alikuwa amevaa miwani myeusi ya jua huku
kingo za mdomo wake zikiwa zimekolea vizuri rangi nzuri nyekundu ya mdomoni.
Shingoni alikuwa amening’iniza mkufu mzuri wa Almasi uliyoizunguka shingo yake
na kupotelea katikati ya matiti yake yaliyotuna vizuri na kuhifadhiwa ndani ya sidiria
yake nyeupe na blauzi ya rangi ya damu ya mzee. Mkononi alikuwa ameshika mfuko
mzuri wa nailoni uliotuna.http://pseudepigraphas.blogspot.com/
“Ulikuwa wapi mpenzi?” nikamuuliza kwa lugha ya kiingereza huku nikiwa na
shauku ya kutaka kufahamu.
“Nilishtuka mapema sana kutoka usingizi nikaona nishuke chini ya hili jengo
nikaogelee kwenye bwawa. Niliporudi na kukuta bado hujaamka sikutaka kukusumbua
nikawa nimepata wazo la kutoka na kwenda kukununulia nguo nyingine za kubadilisha
katika duka moja lililopo katikati ya jiji” Iko-Ojo Obaje akaongea kwa utulivu huku
akiutupa ule mfuko juu ya kile kitanda na kuvua miwani yake kisha taratibu akizitupa
hatua zake na kwenda kuketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa mle ndani. Maelezo
ya Iko-Ojo Obaje yakawa yameniacha njia panda. Kwanza lilikuwa ni jambo gumu
sana nilale na mtu halafu ashtuke kutoka usingizini na kutoka kitandani pasipo
kumsikia lakini vilevile nilikuwa nimeshangazwa sana na kitendo cha Iko-Ojo Obaje
kuweza kufanya mambo yote yale aliyonisimulia pasipo mimi kushtuka usingizini mle
ndani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment