Search This Blog

Friday 18 November 2022

MKONO WA CHUMA - 2

 






Simulizi : Mkono Wa Chuma

Sehemu Ya Pili (2)







Wakati ndani ya ofisi ya naibu waziri kukiwa na kashkash hiyo, upande wa chini Askari wengine walikuwa wakipanda kuelekea juu kwenye Ile Ile ofisi ya naibu waziri.



Askari hao wapatao watano walikuwa mbio mbio huku wakijua kabisa Kuna wenzao kadhaa wameshatangulia kwenye ofisi ya naibu waziri, Ila wao walitaka kwenda tu ilimradi waonekane mbele ya naibu waziri.



Walipofika kwenye mlango wa naibu waziri, wakasukuma kwa kujiamini kwa maana walijua wenzao wapo ndani, ni kweli waliwakuta wapo ndani, lakini hawakumkuta hata mtu mmoja akiwa mzima ndani ya chumba hicho cha ofisi,



"eeh!!!nini kimetokea???" Askari aliyekuwa wa kwanza kuingia aliuliza huku akirudi nyuma kwa uoga, lakini hukuna aliyemjibu, Askari wote sura zao zilionekana zimejaa mshangao ulioambatana na hofu kuu. Hukuna aliyejua kitu kilichoendelea kwenye ofisi Ile,



"madam nae amekufa?" Askari yule aliyeuliza swali la kwanza na hakujibiwa na wenzake, alijikuta akiuliza swali jingine mara baada ya kumuona naibu waziri akiwa amekaa na kichwa chake kikiwa kimelalia kiti na pia mkono wake aliupeleka shingoni ambako kulikuwa na kalamu iliyomuingia barabara katika sehemu ya koromeo.



Hapo Askari wote wakachanganyikiwa, wakachanganyikiwa kwa mawili, la kwanza ni kukuta wenzao wote wakiwa wamekufa, tena kwa Muda mfupi tu,, kwa maana tangu kengele ya hatari ilie mpaka Muda huo zilikuwa zimepita dakika kumi tu.



La pili lililowachanganya ni kukuta pia naibu waziri akiwa amekufa, wakaona wataonekana wazembe sana na huenda wanaweza kufukuzwa kazi,



"inawezekana mtu aliyefanya tukio hili ametokea dirishani" Askari mwingine aliongea baada ya kugundua dirisha la Ile ofisi lipo wazi. Askari yule akasogea mpaka dirishani na kuchungulia kwa nje, hakuona kitu, Askari akatoa simu ya upepo na kutoa taharifa makao makuu juu ya tukio hili la mauaji ya kutisha.



*********



Tom aliamka mapema ili kufuatulia nyendo za yule Dada kichaa, alitoka na kumuacha mpenzi wake akiandaa chai. Tom alienda moja kwa mpaka kwenye kibanda cha mama lishe kilicho nje ya Guest aliyofikia yule Dada kichaa, kisha akaagiza chapati, bahati nzuri alikuta chapati za foleni, akashukuru kukuta hivyo kwa maana alitaka kukaa hapo Muda mrefu.



Ilikuwa saa moja na nusu asubuhi, akakaa mpaka saa mbili na nusu, akapatiwa chapati zake na kulipia, akaondoka hapo kwenye chapati na kuhamia kwenye duka dogo lililokuwa maeneo hayo, lengo lake lilikuwa ni kumuona tu yule Dada kichaa,



"nipatie sukari kilo moja na iriki za mia tano" Tom aliongea huku akimpa pesa mwenye duka, Ila muda wote alijitahid kugeuza geuza shingo ili aangalie watu wanaotoka na kuingia ndani ya ile guest.



"kaka bidhaa hizi hapa" Muuza duka aliongea na kumfanya Tom amgeuzie shingo, na Wakati huo simu ya Tom ilikuwa ikiita, akaitoa mfukoni na kuangalia jina la mpigaji, akajikuta akitabasamu, akapokea,



"vipi" Tom aliongea baada ya kupokea simu,



"hizo chapati umeenda kununua au umeamua ukae kabisa upike wewe?" ilikuwa sauti ya mpenzi wake akiongea kwa ukali,



"mama kulikuwa na foleni, lakini nakuja muda si mrefu, nipo njiani" Tom alijibu kwa upole,



"kama ulikuta foleni si ungeacha oda,. Mbona upo lazy lazy hivyo?" Mpenzi wake aliendelea kung'aka,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sawa, nakuja" Tom alijibu Ila aligundua simu imeshakatwa, Tom akatabasamu, akamgeukia muuzaji,



"samahani kaka, hivi leo hujaona Dada yoyote akitoka pale guest?" Tom alimuuliza Muuza duka,



"Mbona swali lako gumu broo? Maana ni wadada wengi sana wanaoingia na kutoka pale guest" Muuza duka alijibu,



"sawa, ni Dada mmoja hivi ana mkono mmoja" Tom aliongea,



"yah, nilimuona asubuhi sana akitoka" Muuza duka alijibu,



"hujamuona akirudi?" Tom aliuliza,



"sijamuona aisee, huenda Muda mwingine nilikuwa bize sana na wateja akapita bila mimi kumuona" Muuza Duka alijibu,



"asante kaka" Tom aliongea na kuondoka huku akimuacha muuza duka akiwa na maswali kumuhusu yeye, akahisi huenda Tom ni askari mpelelezi au huenda Tom ana mahusiano yoyote na yule mwanadada.



********



Ilikuwa ni saa la pili tu tangu naibu waziri afe, habari zilienea kwa kasi sana juu ya kifo chake, watu wengi walijiuliza iliwezekana vipi mtu kuingia kwenye ofisi ya naibu waziri na kumuua, hakukuwa na ulinzi eneo hilo au?



Wananchi wengine walienda mbali zaidi kimawazo na kuhisi huenda serikali imehusika na kifo hicho, kwa maana kwa maelezo ya hawali ya polisi walidai kuwa inaonekana camera zilitolewa mule katika ofisi kabla ya tukio. Sasa Wananchi walihoji inawezekana vipi mtu wa kawaida akaweza kuingia kwenye lile jengo na kutoa camera katika ofisi ya naibu waziri na wakati kuna ulinzi wa kutosha, tena wa masaa ishirini na manne?



Wakati Wananchi wakijitwisha mzigo huo wa maswali, ndani ya ofisi kuu ya polisi kulikuwa na mtu mmoja wa makamo aliyekalia kiti kilicho nyuma ya meza kubwa, na mbele ya meza kulikuwa na viti vingine vipatavyo nane, navyo vilikaliwa na askari walioonekana wana vyeo, na sura zao hazikuwa na furaha hata kidogo.



"huu ni muendelezo, tayari matukio kama haya yameshatokea kwenye wilaya moja ya mkoa wetu, aliuawa mkuu wa wilaya na msichana mmoja aliyekuwa akimsaidia, siku chache akauawa mkuu wa mkoa, na sasa ameuawa naibu waziri. Angalieni hii chain, wameanza viongozi wa wilaya, wakafuata wa mkoa, sasa vifo vimehamia kwenye uongozi wa serikali, ameanza naibu waziri, kwa chain inavyoonekana inaelekea anaweza kufuata waziri yoyote yule, haswa haswa ninavyoona atafuata waziri wa katiba na sheria. Sasa basi, hili suala sio la kukalia kimya wala halifichiki tena, tayari habari za kifo cha naibu waziri zimesambaa nchini kote, na bahati mbaya zaidi mtuhumiwa hajulikani, camera za ofisi ya naibu waziri zinaonesha zilitolewa kabla ya tukio, pia camera za jengo zimeonesha hazijanakiri tukio lolote, kwa maana hiyo ni kwamba vifaa vya kuhifadhi kumbukumbu za camera, inaelekea vilitolewa pia. Ila watu wa mapokezi wanadai kuwa mtu wa mwisho kuingia kwenye ofisi ya naibu waziri ni mwanamke ambaye alikuwa mlemavu, yaani hakuwa na mkono mmoja, na mwanamke huyo huyo ndio aliweza kuhusishwa na matukio mengine ya mauaji niliyoyaelezea hapo hapo hawali" Mkuu wa polisi wa nchi alieleza huku wale askari wengine wakimtazama, wengine walikuwa na karatasi wakiandika yale maelezo.



"kwa maana hiyo basi, mkitoka hapa hakikisheni mnasambaza askari maeneo yote kwa ajili ya kumtafuta huyo mtuhumiwa na kuimarisha ulinzi, na mtu yoyote ambaye atahisiwa anatakiwa akamatwe mara moja, pia hakikisheni upelelezi huu unaenda chini chini na kwa siri kubwa sana, raia wa kawaida hawatakiwi kujua. Na kutokana na hili tukio la mauaji ya kutisha ya naibu waziri, imembidi waziri wa katiba na sheria asitishe ziara zake za mikoani, na jioni ya leo atakuwa hapa mkoani na ulinzi wake umeimarishwa zaidi.



Nimemaliza, je Kuna mtu ana wazo lolote?" Mkuu wa polisi aliuliza, lakini hakuna mtu aliyejibu, akavua miwani yake,



"nadhani hakuna la ziada, sasa mnachotakiwa kufanya ni kutawanyika na kwenda kutekeleza maagizo niliyoyaelezea. Nimemaliza" Mkuu wa polisi aliongea kisha watu wakatawanyika na kumuacha Mkuu wa polisi akiwa amebaki mwenyewe kwenye kile chumba cha mkutano.



Alikaa akitafakari kwa Muda mrefu, kisha akainuka na kuondoka kwenye chumba kile, akaelekea ofisini kwake, na kujibwaga kwenye kiti, kisha akavua miwani yake na kuiweka juu ya meza.



********



Wakati taarifa za kifo cha naibu waziri zikienea kwa kasi nchini kote, muuaji alikuwa amekaa mbele ya runinga iliyopo kwenye chumba alichopanga guest, alikuwa akipaka rangi kucha za vidole vyake vya miguuni, huku masikio yakiwa makini kusikiliza habari zinazorushwa.



Ila habari zote kuhusu kifo cha naibu waziri hazikuwa habari kwake, habari iliyokuwa habari kwake ni ile ya waziri wa katiba na sheria kuahirisha ziara na anarejea siku hii ya leo.



Hiyo habari ilimfanya Dada kichaa ahache kupaka kucha zake rangi na kutolea macho runinga, akajikuta akitabasamu peke yake,



"bora angeendelea tu na ziara, kuahirisha kwake ni sawa na kunifuata mimi rafiki wa Israel mtoa roho" Dada kichaa aliongea peke yake na kisha akaendelea kupaka rangi vidole vyake vya miguuni, kisha alipomaliza aliinuka na kujitupa kitandani, akatoa simu na kuitega kengele ya kumuasha kulingana na Muda anaotaka yeye.



"nitaenda kumuona Waziri, baadae usiku" Dada kichaa aliongea huku akiweka simu yake mezani, Kisha akalala usingizi mzito Bila wasiwasi wowote, yaani kama mtu ambaye hatufutwi na wala hajafanya uharifu wowote.



************http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Nyakati za jioni, giza likiwa linashamiri kwa kasi sana, Tom alikuwa maeneo ya nje ya Ile guest, alikuwa akiendelea kufanya upelelezi wake, na kitu kilichochochea zaidi Tom kuamua kumuwinda kabisa yule Dada kichaa ni zile habari za kifo cha naibu waziri, yeye Tom aliamini kabisa muuaji atakuwa huyu Dada, ingawa serikali ilikuwa bado haijasema muuaji alionekanaje wala hawakusema ni nani wanayemuhisi.



Saa zilizidi kwenda, Tom alikuwa amekaa kwenye kibanda cha kuoneshea mpira, alikuwa amekaa kwa nje. Baridi likamzidia, Tom akainuka ili aende nyumbani akavae koti. Alipoinuka na kupiga hatua mbili Tatu, aliweza kumuona mwanamke akitoka ndani ya Guest, akamuangalia kwa umakini zaidi, alikuwa ni yule Dada kichaa akiwa amebeba begi dogo mgongoni, na hapo ilikuwa yapata saa nne usiku.



Tom akaamua hasiende tena kuvaa koti, akaamua amfuatilie yule Dada kichaa.



Dada kichaa alitembea mpaka barabarani, kisha akasimama kwa muda, ikapita bajaj, akaisimamisha, akaingia na kuelekeza anapotaka kwenda, dereva bajaj akageuza bajaj na kuiondoa.



Tom alibaki Amesimama, maana hakukuwa na usafiri mwingine, akabaki amesimama huku akiitazama namna Ile bajaj ikipotea machoni mwake.



Akiwa amekata tamaa kabisa, aliiona bodaboda ikija mbele yake, akaisimamisha,



"Kuna bajaj imeelekea njia ile, naomba unisaidie kuifuatilia" Tom aliongea huku akirukia kwenye bodaboda, dereva nae hakutaka kuhoji zaidi, akaiondoa bodaboda kwa kasi kama mteja wake anavyotaka.



Walitembea kwa mwendo wa dakika tano, wakaweza kuiona ile bajaj,



"Ile, sasa tuifuatilie kwa umbali huu, usiisogelee karibu'" Tom alimwambia dereva ambaye alitii.



Waliendelea kuifuatilia kwa dakika kumi, kisha bajaj ikasimama,



"na mimi nisimame?" Dereva bodaboda aliuliza,



"nyoosha tu, uipite" Tom aliongea kwa maana alihisi wakisimama wanaweza kushtukiwa.



Bodaboda ikaipita bajaj na kwenda umbali zaidi, kisha Tom akamtaka dereva asimame, akashuka na kumlipa pesa yake, bodaboda ikaondoka.



Tom akatupia macho kwenye bajaj akaona yule Dada kichaa akashuka, Tom akatembea na kuingia kwenye kichochoro, akawa anamchungulia yule Dada kichaa.



Dada kichaa alitembea kuelekea upande ule ule wa Tom alipo, Ila alipofika ule usawa wa Tom yeye hakuingia kichochoroni, aliendelelea kufuata barabara. Tom akawa anamtazama tu.



Yule Dada kichaa akaenda moja kwa moja kugonga geti la nyumba moja ya kifahari, Kisha akawa anaongea na mlinzi baada ya geti kufunguliwa, Tom hakuweza kusikia yale maongezi kwa maana alikuwa mbali na geti.



Tom akiwa anachungulia, alimshuhudia mlinzi akilegea na kudondoka chini, akashangaa. Akiwa bado anashangaa, aliweza kumuona yule Dada kichaa akiingia ndani ya lile geti, Tom akaendelea kushangaa.



Baada ya dakika kumi za Dada kichaa kuzama ndani ya geti, Tom akaona bora nae asogee jirani na geti, akapiga hatua za haraka haraka mpaka getini, akasukuma geti kidogo na kuchungulia, akapigwa na mshangao mara baada ya kuwaona Askari wapatao kumi wakiwa wamelala chini na wengine damu zilikuwa zikiwavuja, hakuna hata mmoja aliyeonekana yupo hai.



Akaingia kwa mwendo wa hatua za taratibu zisizokuwa na vishindo vikubwa, akatembea mpaka mlangoni na kusikia sauti za watu zikiongea, akapenyeza jicho kwenye uwazi mdogo uliokuwepo hapo mlangoni, akashtuka baada ya kumuona waziri wa katiba na sheria akiwa amekaa na mbele yake alikuwepo yule Dada kichaa,



"mimi sio mkorofi, endapo mtafuata sheria na kunipa mali yangu, sitowapa tabu tena" Dada kichaa aliongea kwa kujiamini,



"hiyo mikataba unayo hapo?" Waziri aliuliza huku akionekana akitetemeka, na pembeni kulikuwa na familia yake ambayo ilikuwa imefungwa kamba,



"hapana, kwa kuwa ni mambo ya kiofisi, nitakuletea kesho mapema ofisini kwako. Kumbuka kuwa sitaki kukuta kikwazo chochote, yaani nikija, polisi wakae mbali na mimi, na chombo chochote cha usalama kisinisogelee" Dada kichaa alizungumza kwa msisitizo,



"sawa, wewe utaileta mikataba nitaiangalia. una mwanasheria?" Waziri aliuliza,



"mwanasheria wa nini wakati mikataba imeweka wazi kila kitu" Dada kichaa aliongea,



"sawa" Waziri aliongea, kisha yule Dada kichaa akasimama, akaenda mpaka eneo jirani na mlango ambalo kulikuwa na kitufe ambacho ukikibofya tu, polisi wanajua Kuna hatari, Dada kichaa akabonyeza kile kitufe,



"polisi watakuja Muda wowote, acha niondoke" Dada kichaa akaongea na kuanza kuelekea nje.



Tom alipoona yule Dada anakuja mlangoni, akachomoka kwa kasi na kujificha nyuma ya nyumba, yule Dada kichaa akatoka na kufunga kwa nje mlango wa nyumba ya waziri, kisha akakanyaga maiti kadhaa za Askari na kutoka nje ya geti.



Baada ya dakika mbili, Tom nae akaamua atoke nje, akatembea kwa tahadhari mpaka getini, akafungua geti, akakuta ndio gari ya polisi inasimama, akapata kiwewe, akarudi ndani kwa kasi,



"wewe simama" Askari waliongea kwa amri huku wakiruka kwenye gari na kumfuata Tom ndani.



Tom alivyorudi ndani ya geti, akiwa na kasi na kiwewe, alijikwaa kwenye maiti na kudondokea kichwa, akaanguka chini na macho yakawa yanakosa nguvu,



"huyu ndio kawaua awa Askari, kwanza usiku huu amefuata nini kwenye nyumba ya waziri?" Askari mmoja aliongea huku akiwa amesimama mbele ya Tom na bunduki ikiwa mkononi, Tom alitaka kujitahidi aongee ili kujinasua kwa Askari, Ila hakuwa na nguvu tena, macho yalikosa uvumilivu, yakajifunga, Tom hakuona kitu tena, aliona giza na mwili ukashindwa kufanya kazi, Tom akapoteza fahamu..........





Tom alifungua macho na kuhisi baridi kali likishambulia mwili wake, na pia alihisi maumivu ya kichwa, akavuta kumbukumbu na kukumbuka ni tukio gani alikutana nalo, sasa wasiwasi ukamuingia, akahisi kabisa atakuwa chini ya uangalizi wa polisi, akaanza kujilaumu kwa kumfuatilia yule Dada kichaa, akawaza endapo yeye ndio atashtakiwa kwa vifo vya Askari waliouawa kwenye nyumba ya waziri wa katiba na sheria, atajibu nini Wakati ni yeye ndiye aliyekutwa yupo ndani ya geti la Ile nyumba? Tom akaanza kujuta huku machozi yakimtoka, mara akasikia sauti ya gari likipita, akashtuka na kuinuka kwa haraka, akashangaa, kumbe alikuwa pembezoni mwa barabara, akapepesa macho huku hasiamini kinachomtokea,



"au polisi walinipiga risasi wakajua nimekufa? Kisha wakanitupa hapa? " Tom alijiuliza huku akijiangalia mwilini kama atajikuta na jeraha la risasi, lakini alijikuta yupo sawa tu, akajisachi mifukoni, maana alikumbuka kabla ya tukio alikuwa na pesa kidogo mfukoni, akaingiza mikono mfukoni na kuzikuta, akakumbuka pia alikuwa na simu, akaitoa mfukoni na kuiangalia, akakuta amepigiwa zaidi ya mara 50, mpigaji alikuwa ni mpenzi wake, akatabasamu, akataka ampigie ila akaghairi, akaangalia sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno, akakuta sms zaidi ya kumi, akafungua na kukuta zote zimetoka kwa mpenzi wake na alikuwa akimuuliza yupo wapi? Akairudisha simu mfukoni na kusogea mpaka barabarani, ilikuwa yapata saa kumi na moja alfajili.



Akatembea kwa dakika kadhaa, bahati nzuri ilitokea bajaj, akaisimamisha na kuingia, akamuelekeza dereva ni wapi anaenda.



Ilichukua takriban dakika kumi na tano bodaboda kufika nyumbani kwa mpenzi wa Tom, Tom akatelemka na kumlipa dereva bodaboda, bodaboda ikaondoka.



Tom akasimama kwa muda huku akifikiria atamwambia nini mpenzi wake? Wakati akitafakari, mlango ulifunguliwa, akatoka mpenzi wake,



"haya nieleze ulikuwa wapi!?"Mpenzi wake Tom aliuliza huku machozi yakiwa jirani kabisa na macho,



"ebu kwanza tuingie ndani, nitakueleza" Tom aliongea kwa kumbembeleza mpenzi wake,



"Tom tokea umekuja safari hii sikuelewi kabisa, Kama una mwanamke mwingine si uniambie?" Mpenzi wake Tom aliuliza, na safari hii alikuwa analia kabisa,



"wewe unatanguliza wivu tu, hufikirii labda nilikuwa na tatizo?" Tom aliuliza,



"tatizo gani? Ungekuwa na tatizo si ungepiga simu? Mbona hukupokea simu?" Mpenzi wake alimuuliza kwa ukali,



"bwana ngoja nilale, kukisha pambazuka vizuri tutaongea" Tom alijibu huku akiingia ndani, mpenzi wake akamfuata kwa nyuma,



"umekalia umalaya tu, kama umenichoka bora uniambie tu, maana utaniletea maradhi" Mpenzi wake alizidi kulalama Ila Tom hakutaka kuongea tena, akavua shati, akajihisi ana maumivu mgongoni, akapeleka mkono eneo alilohisi maumivu, akashtuka alipouangalia mkono wake, ulikuwa na damu za kutosha.



"ebu niangalie mgongoni" Tom aliongea huku akimpa mgongo mpenzi wake aliyekuwa amekaa kitandani.



"eh!!!!!!" mpenzi wake alishtuka baada ya kumuangalia, lilikuwa jeraha kubwa kiasi, ni kama mkwaruzo chuma au kisu,



"nini?" Tom aliuliza kwa uoga,



"kidonda kikubwa, umefanyaje?" Mpenzi wake aliuliza kwa uoga, hapo tena wivu ulipungua,



"chukua maji ya moto nisafishe, nitakusimulia pakikucha" Tom aliongea huku pia akishukuru kuwa na kidonda hicho, alipanga namna ya kumdanganya mpenzi wake, na Wakati huo mpenzi wake alichukua sufuria ndogo na kuinjika kwenye jiko la gesi, Tom akatabasamu.



*****************



Mkuu wa polisi alikuwa amekaa kwenye kiti chake ofisini akitafakari, na kilichomfanya atafakari ni asubuhi Ile kuamshwa na habari za kuuawa kwa baadhi ya Askari waliokuwa wakilinda nyumba ya waziri, lakini pia taarifa zilikuwa zikikinzana, wakati waziri wa nishati na madini akidai aliyevamia na kuua polisi ni mwanamke, Wakati polisi walioenda baada ya tukio wanadai aliyeua polisi ni mwanaume, Ila pia polisi wanadai walimdhibiti yule mwanaume waliyemkuta pale, cha ajabu akaja kuokolewa na mwanamke mwenye mikono miwili, tofauti na yule wa kwanza mwenye mkono mmoja aliyeongea na waziri.



"kwa maana hiyo wapo watatu? Mwanaume, mwanamke mwenye mkono mmoja na huyo mwanamke mwingine mzima?" Mkuu wa polisi alijiuliza mwenyewe huku mawazo yakizidi.



"hapa ni lazima apatikane mtu mmoja makini wa kufuatilia hili kasheshe" Mkuu wa polisi aliongea, kisha Akachukua miwani yake na kuipachika machoni, akatoa simu yake kwenye droo na kwenda upende wa majina na kutafuta jina analolitaka, akapiga,



"upo wapi?" Mkuu wa polisi aliuliza mara baada ya mtu wa upande wa pili kupokea simu,



"nipo ofisini mkuu" Mtu wa upande wa pili alijibu,



"njoo ofisini kwangu" Mkuu wa polisi aliongea na kukata simu, kisha akavua miwani yake na kuwasha computer yake.



Baada ya dakika mbili mlango wa ofisini kwake uligongwa, akaingia kijana mrefu kidogo na miwani mieusi machoni, kijana akapiga salute,



"kaa" Mkuu wa polisi aliongea kisha kijana akaa, Mkuu wa polisi akaendelea kubonyeza vitufe vya computer yake, kisha akashusha pumzi ndefu,



"si umesikia hii hali inayoendelea nchini? Polisi wanauawa hovyo, viongozi wa nchi wanakufa pia" Mkuu wa polisi aliongea na kutulia kidogo,



"sasa bwana, kuanzia sasa hiyo hii kazi unatakiwa kuifuatilia wewe, sijaona mtu mwingine wa kuifanya zaidi yako" Mkuu wa polisi aliongea na kumtupia jicho yule kijana aliyekuwa ametulia akisikiliza kwa umakini.



"kumbuka, unatakiwa uifuatilie kwa uangalifu na usiri mkubwa sana, nakuamini katika hilo" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa Mkuu, nitafanya kama unavyotaka" Kijana alijibu,



"leo hii saa nne asubuhi, mtuhumiwa atakuwa ofisini kwa waziri, Kuna askari kadhaa tumewaweka kwa ajili ya kumkamata huyo Dada, sasa na wewe ni vizuri ungekuwepo eneo hilo ili upate chochote" Mkuu wa polisi aliendelelea kuongea,



"Ila kwa nilivyosikia ni kuwa waziri hataki mtu yoyote wa usalama afike eneo lile" Kijana aliongea,



"ni sawa, Ila hata hao Askari wataokuwepo eneo hilo pia watakuwa wamevaa kiraia, kwa hiyo ni ngumu kugundulika" Mkuu wa polisi aliongea,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"mimi nadhani ni vyema kufuata maelekezo ya mtuhumiwa, endapo mtuhumiwa atagundua Kuna mtego, itakuwa mbaya sana kwa waziri" kijana aliongea kwa upole,



"kijana nenda kama nilivyokuagiza, sikukuita unipangie kazi wala sikukuita tujadiliane, nimekuita kukupa amri" Mkuu wa polisi aliongea,



"sawa mkuu" kijana alijibu kikakamavu kisha akageuka na kuondoka, huku nyuma Mkuu wa polisi alimuangalia huku akitafakari maneno ya yule kijana.



"litalokuwa na liwe" Mkuu wa polisi aliongea na kuipachika miwani yake machoni.



************



Ndani ya ofisi ya waziri wa katiba na sheria, alikuwa waziri peke yake, na Muda wote alikuwa na wasiwasi, alikuwa akisimama kila muda na kwenda dirishani, anachungulia nje kwa muda na kisha anarudi kukaa kwenye kiti chake na kutupia macho kwenye runinga kubwa iliyobandikwa ukutani ambayo ilionganishwa na camera zilizopo mapokezi, kwa maana hiyo kila mtu aliyeingia na kutoka ndani ya jengo, waziri alimuona.



Pia waziri alikuwa makini kuangalia watu wa usalama kama wapo ofisini kwake, hakutaka kabisa mtu wa usalama kuwepo eneo lile, alichotaka ni kuongea na yule Dada kisha aone kama ni kweli ana haki au analazimisha tu.



Waziri aliendelelea kusubiri huku Muda ukiendelea kukatika, ilianza kupotea dakika, ikafuata saa, kisha masaa. Waziri akajiuliza kwanini huyu binti hajaja, maana alisema atafika saa nne.



Waziri hakukata tamaa, aliendelelea kusubiri, mwisho saa kumi jioni ikamkuta ofisini, na huo ndio ulikuwa Muda wake wa kutoka kazini.



Akachukua koti Lake la suti alilolitundika nyuma ya kiti, kisha akalivaa, akatoka na kuhakikisha mlango wake ameufunga vizuri, alatelemka mpaka ghorofa ya chini, akakukuta gari yake ikiwa na dereva, alikuwa akisubiriwa yeye, akaingia katika gari,



"nipeleke nyumbani" waziri wa katiba na sheria aliongea na kisha dereva akaiondoa gari, nje ya geti walimpita kijana mmoja aliyekuwa amevaa miwani mieusi, huyu ndiye yule kijana aliyetumwa amtafute mtuhumiwa wa mauaji yanayotokea hovyo. Kijana baada ya kupitwa na gari ya waziri, aliangalia saa yake, kisha akatoka kwa mwendo wa kawaida, alielekea uelekeo tofauti kabisa na lilipoelekea gari la waziri.



*************



Mishale ya saba usiku, waziri bado alikuwa sebuleni akimfikiria yule Dada, na siku hiyo hakutaka kuwe na ulinzi nyumbani kwake, aliwatimua walinzi wote, na Muda huo alikuwa sebuleni, alikaa peke yake, familia ilikuwa ndani, wamelala.



Ilipofika saa nane kasoro, waziri alianza kusinzia, Ila akahisi mlango ukisukumwa, akanyanyua kichwa haraka, macho yake yakagongana na macho ya yule Dada kichaa,



"karibu, nilijua utakuja tu" Waziri aliongea huku akijiweka vizuri juu ya kiti,



"ulijua ntakuja, ulijuaje?" Dada kichaa aliuliza huku akikaa chini,



"kwa sababu asubuhi hujatokea" waziri alijibu kwa utulivu,



"kweli, ilishindikana mimi kuja uko kwa sababu ofisi yako yote ilizungukwa na watu wa usalama, kwa hiyo sikutaka kuja kwa maana ningeua tena, na mimi sipendi kuua" Dada kichaa alijibu,



"usalama!? Lakini mimi nilizuia mtu yoyote wa usalama asisogee eneo la ofisi yangu" Waziri aliongea,



"ni kweli, Ila mipango ya kuwaweka watu wa usalama, ilifanywa na Mkuu wa polisi" Dada kichaa aliongea,



"kwanini wanaingilia mambo yangu? Nilitaka nikutane mimi na wewe na wala sio wao" waziri aliongea kwa hasira,



"usijali, kama haki ipo, ipo tu" Dada kichaa aliongea,



"alafu mpo mapacha?" Waziri aliuliza,



"kwanini mheshimiwa?" Dada kichaa aliuliza,



"maana aliyekuja jana alikuwa ana mkono mmoja, Ila wewe umekuja ukiwa na mikono miwili" Waziri aliongea, ila Dada kichaa hakutaka kujibu, alitabasamu tu,



"kilichonileta hapa ni kwamba, kampe onyo Mkuu wa polisi, mwambie ahache kunifuatilia, kama ataendelea kunifuatilia, basi vijana wake wataendelea kufa kwa sababu yake, yeye asubiri tu mpaka muda wake wa kuonana na mimi utapofika, Ila akiharakisha kuonana na mimi ni sawa na kuharakisha kifo chake" Dada kichaa aliongea na kumfanya waziri akae kimya kwa muda,



"sawa, je umekuja na mikataba ili niione?" Waziri aliuliza,



"hapana, hapa sio sehemu sahihi ya kuoneshana mikataba, nitakuja nayo ofisini kwako siku yoyote" Dada kichaa alijibu,



"Hilo nalo ni jambo zuri, Ila utaingiaje ofisini kwangu ingalikuwa kuna polisi kila kona?" Waziri aliuliza,



"hakuna wa kunizuia, mimi sio mtu kama unavyodhani wewe, sipo kawaida kabisa na watu" Dada kichaa alijibu,



"jina lako unaitwa nani?" Waziri aliuliza na kumfanya yule Dada kichaa atabasamu, kisha akainama kidogo na kurudisha nyuma kichwa kwa nguvu na kufanya nywele zake ndefu zirudi nyuma, sura yake ikaonekana vizuri,



"niite BQ, jina halisi utaliona kwenye mikataba" Dada kichaa alijibu na kutulia kidogo kama mtu aliyesikia kitu, kisha akasimama,



"vipi?!" waziri akauliza,



"Kuna mtu nje" Dada kichaa aliongea,



"hakuna mtu, mbona Askari wote niliwaondoa?" Waziri aliuliza,



"mzee acha mimi niende, funga milango yako" BQ aliongea huku akielekea nje na waziri alimfuata kwa nyuma, walitoka na kuangaza, hawakuona mtu.



"mzee funga geti, mimi naondoka " BQ aliongea huku akiondoka, waziri hakutaka kuongea tena, alifunga geti na kuingia ndani.



Dada kichaa alipiga hatua chache, akahisi Kuna mtu nyuma, BQ akasimama na kugeuka, akakukuta Kuna kijana mmoja akiwa amesimama na machoni alikuwa na miwani mieusi, ni yule kijana aliyetumwa na Mkuu wa polisi.



BQ akageuka na kuendelea kutembea huku akiamini huyo kijana atakuwa anamfuatilia yeye.



"simama wewe" kijana aliongea kwa amri na kumfanya BQ asimame na kugeuka,



"Kuna tatizo?" BQ aliuliza,



"upo chini ya ulinzi" Kijana aliongea huku akimfuata BQ, hilo lilikuwa kosa kubwa, kwani wakiwa wameachana hatua mbili tu, BQ alizungusha kwa nguvu nywele zake na kupiga uso wa yule kijana, kijana akajishika kwa maumivu, pasipo kutegemea BQ aliachia ngumi kali ya mkono wa kushoto, kijana akaiona akaiepa, ile ngumi ikapiga ukuta, ukuta ukapasuka, ukatengeneza ufa, kijana akashtuka, kwa maana haikuwa ngumi ya kawaida.



Kijana akaogopa akarudi nyuma, BQ akatabasamu. Kijana akahisi huenda leo anapambana na mtu hasiye mtu. Kijana akaokota kipande cha jiwe gumu kilichokuwa chini, akamrushia kwa nguvu, BQ kwa mkono ule ule wa kushoto akapiga ngumi kile kipande cha tofali na kusambaratika. Kijana akaona atumie mbinu za ziada kumuingia, akamfuata kwa kasi, lakini iliachiwa ngumi kali tena ya mkono wa kushoto, kijana akaiona, akakwepesha kichwa kidogo, ile ngumi ikapasua kioo cha miwani cha jicho la kulia, kijana akarudi nyuma na kuvua miwani kabisa, naaam, sasa kijana alionekana vyema, jicho lake la kushoto lilikuwa limetoboka, lilionekana vizuri kabisa, alikuwa na chongo.



Naam, baada ya kumjua BQ, sasa nadhan hata anayepambana nae mtakuwa mmeshamjua...







Ndio, alikuwa ni Sajenti Minja mwenyewe, alikuwa bado anashangaa nguvu za ajabu alizokuwa nazo yule mwanamke,



"basi tatumia mkono mmoja, wa kulia, maana wa kushoto umekutisha kidogo" BQ aliongea huku akitabasamu, Sajenti Minja hakujibu, aliupeleka mkono wake pembeni ya jicho la kulia, kulikuwa na mchubuko kidogo,



"mbona hupambani tena, umepata hofu" BQ aliuliza lakini bado Sajenti Minja alikuwa ameganda tu, alikuwa anatafuta nafasi nzuri.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"basi kajipange, tutapambana siku nyingine afisa" BQ aliongea kwa dharau na kuanza kuondoka, Ila hata kabla hajapiga hatua tatu, Sajenti Minja alimfuata kwa kasi na kurusha teke kali lililokuwa likielekea kwenye mbavu za kushoto za BQ, lakini ajabu nyingine ilitokea, unaweza kasema BQ ana macho kisogoni, maana aliruka sarakasi na kufanya kichwa kiwe chini na miguu kuwa juu, kisha lile teke lililopigwa na Sajenti Minja likabahatika kuparaza nywele tu za BQ, BQ alipotua chini, Sajenti Minja alipiga ngumi tano za haraka haraka na zote zilizuiliwa kwa kutumia mkono wa kulia wa BQ, kisha kwa kutumia mkono ule ule, aliachia ngumi dhaifu iliyodakwa na Sajenti Minja, Sajenti Minja akiwa anajiandaa kuachia pigo jingine, alishtukia akitandikwa teke kali la kidevu na kumtupa chini, Sajenti Minja akaanguka chini huku akiwa amejishika kidevu chake kwa maumivu, pia alijiuliza lile teke limepitaje Wakati walikuwa umbali mfupi tu.



Wakati Sajenti Minja akiwa anajiuliza, alishtuka kumuona yule Dada akiwa hewani kumuelekea yeye, Sajenti akataka kunyanyuka ili amkwepe, Ila akateleza na kuangukia tumbo, akahisi kitu kama jiwe kikishuka mgongoni kwake, lilikuwa ni teke la BQ, kwa uzito wa teke lile, Sajenti Minja akacheua baadhi ya chakula alichokula muda wa usiku wa siku hiyo.



Sajenti Minja akiwa bado yupo chini, aliweza kumuona BQ akijiandaa kuachia pigo jingine, Sajenti kwa kasi ya ajabu, alijibetua na kutoa Unga fulani mweupe kutoka mfukoni, akaupuliza ule unga, kisha ukaenea eneo lote lile, kwa kutumia mbinu hiyo, Sajenti Minja akaruka katikati ya ule unga huku akiamini hiyo mbinu itamchanyanya yule mwanamke, Ila aliporuka alishangaa ametua na kujikuta peke yake, akageuka kwa kasi baada ya kuhisi kuna mtu kwa nyuma, Ila alipogeuka alikutana na teke kali lililotua katikati ya miguu yake, akajikuta anabana miguu kwa maumivu aliyoyapata, Sajenti Minja akiwa ameshikilia kende zake huku miguu akiwa ameibana, alishuhudia yule Dada akiiachia ngumi yake ya mkono wa kushoto kwa kasi sana kumuelekea Sajenti Minja usawa wa paji la uso, Sajenti Minja akakata tamaa kabisa, alijisemea moyoni kuwa kama ile ngumi ya mkono wa kushoto iliweza kupiga ukuta mpaka ukuta ukapata nyufa, sasa itakuwaje katika kichwa chake chenye mifupa isiyokuwa na ugumu wa ukuta?



Sajenti Minja akaamua kufunga macho tu, maana hakuwa na uhakika wowote juu ya uhai wake. Akiwa amefunga macho kwa sekunde kadhaa, hakuweza kuhisi ile ngumi ikimpiga, akafungua macho taratibu huku akiamini yule Dada atakuwa anamsubiri afungue macho ili ampige, lakini cha ajabu Sajenti Minja hakukuta mtu, akatoa mikono katikati ya miguu na kuangaza kushoto na kulia, ila pia hakuona mtu, akakimbia mpaka mbele kwenye kona, alihisi huenda yule BQ ameelekea uko, pia hakuona mtu.



"bahati yake amekimbia, ningemmaliza leo" Sajenti Minja aliongea kwa kujiamini huku akipiga hatua za kuondoka eneo hilo, hata hatua zenye hakupiga kama kawaida yake, alitembea kwa kuchechemea kutokana na maumivu aliyoyasikia.



************



Tom yeye alikuwa bize na habari za mitandao, alikutana na Ile habari ya polisi kuuawa katika nyumba ya waziri, ila kilichomvutia zaidi ni yale maneno kuwa Kuna kijana mmoja inadaiwa alikutwa kwenye hiyo nyumba ya waziri, huyo kijana alipowaona polisi alitaka kukimbia, ila alianguka na kupoteza fahamu, ila pia alikuja kuokolewa na Dada mmoja mwenye nguvu za ajabu, maana alimshika kwa mkono mmoja na kupanda nae kwenye uzio wa chuma na kupotelea gizani,



"ina maana yule Dada kichaa alinikoa mimi?" Tom aliwaza peke yake na kushangaa,



"ndio akaenda kunitupa barabarani! Ina maana ameshajua namfuatilia?" Tom aliendelelea kujiuliza. Akili yake yote ilikuwa katika hiyo habari aliyokutana nayo muda huo. Na muda huo mlango wa chumbani ulifunguliwa na mpenzi wake akaingia,



"wewe huamki leo?" Mpenzi wake alimuuliza,



"niende wapi sasa?" Tom aliuliza,



"kaoge" Mpenzi wake alijibu,



"nitaoga baadae" Tom aliongea na kuendelea kuperuzi kwenye simu, Ila mpaka kufikia hapo Tom hakuwa na raha, alifikiri kwa nini yule Dada kichaa alimsaidia na kwenda kumtupa barabarani?



Tom akainuka kitandani na kwenda kusafisha kinywa, kisha akaenda moja kwa moja kwenye lile duka linalotazama na guest aliyofikia BQ. alipofika alitoa pesa na kununua vocha, akapewa,



"eti bro, yule Dada niliyemuulizia siku ile bado yupo hapo guest?" Tom aliuliza,



"yupo, vipi bro, wewe ni polisi nini?" Muuza duka aliuliza huku akitabasamu,



"kwanini umeniuliza hivyo?" Tom nae aliuliza,



"si nakuona unavyomfuatilia yule Dada" Muuza duka alijibu,



"hapana, mimi sio polisi, Ila huyu Dada ni ndugu yangu ambaye alitoroka, sasa najaribu kumfuatilia ili nijue anataka kufanya nini" Tom aliongea,



"aaah, sawa" Muuza duka alijibu,



"poa basi, naomba umtupie sana jicho " Tom aliongea na kuondoka.



Kipindi chote ambacho Tom alikuwa akiongea na yule muuza duka, BQ alikuwa dirishani akiwa anamtazama Tom, ingawa alikuwa umbali kidogo na pia dirisha alilokuwamo lilikuwa na kioo, aliweza kuhisi kinachoongelewa kwa maana yeye hakuweza kusikia.



Baada ya Tom kuondoka dukani, BQ alitoka ndani ya Guest na kuanza kumfuatilia kwa mbali, aliweza kumfuatilia mpaka Tom alipoingia kwenye chumba cha mpenzi wake,



"Kuna muda mwingine uandishi wa habari ni umbea, yaani unafuatilia maisha ya watu na kuyaanika hadharani, shauri yako Tom" BQ aliongea mwenyewe na kugeuza, alielekea moja kwa moja mpaka dukani kwa yule kijana aliyekuwa akiongea na Tom, akamsalimia yule kijana,



"eti kaka samahani, yule kijana ulikuwa unaongea nae nini?" BQ alimuuliza muuza duka,



"yupi?" Muuza duka aliuliza huku akijifanya hajui ni kijana gani aliyeuliziwa,



"humjui eee?, endelea kuwa nae karibu, ipo siku utamsaidia kubeba maumivu" BQ aliongea na kuondoka taratibu huku akimuacha yule kijana akiyashangaa maneno ya yule Dada.



"watajijua wenyewe bhana" Kijana aliongea kwa kujiamini huku akianza kuhesabu vocha zake zilizoletwa muda mfupi uliopita.



****************



Asubuhi ya leo ilimkuta Sajenti Minja kwenye duka la miwani, alikuwa yupo makini sana kuchagua miwani,



"kaka, hii shilingi ngapi?" Sajenti Minja aliuliza huku akiioneshea kidole miwani iliyokuwa ndani kioo, Muuzaji akaitoa na kumpatia,



"laki moja na sabini" Muuzaji alijibu huku akitabasamu,



"ina nini cha ziada?" Sajenti Minja aliuliza huku akiitupia machoni mwake,



"material yake ni ghali sana, pia miwani kama hizi uwa zinavaliwa na wacheza sinema wakubwa na wanamuziki wakubwa wa duniani" Muuzaji alijibu huku akitabasamu,



"sawa, nashukuru" Sajenti Minja aliongea na kuondoka zake huku akiwa na ile miwani machoni, hakuilipia.



Muuzaji akataka kwenda kumzuia, Ila alishikwa bega na mmiliki wa duka,



"achana nae, ataleta tu" Mmiliki wa duka aliongea huku akicheka, alikuwa anafahamiana vizuri sana na Sajenti Minja.



************



Mida ya saa kumi jioni, waziri akiwa anamalizia kazi chache zilizopo juu ya meza, alisikia mlango wa ofisi yake ukigongwa,



"Ingia" Waziri aliitikia huku macho yake yakiwa makini na kazi anayoifanya.



Lakini alijua kabisa kuna mtu ameingia, ila alishangaa kuona mtu huyo haongei wala hakai, kwa maana hiyo alikuwa amesimama. Waziri akainua kichwa na kumtazama huyo mtu, alikuwa ni BQ, alikuwa akitabasamu,



"Upo bize sana leo?" BQ aliuliza huku akitabasamu, alikuwa na mkono wake mmoja ulioshikilia bahasha ya khaki iliyokuwa na mikataba,



"Karibu ukae, umepitaje uko nje wakati kuna askari kila kona?, au umeua tena?" waziri aliuliza kwa wasiwasi,



"Mbona hakukuwa na askari, na hata wale wanaokaaga pale mapokezi nimekuta ni wengine" BQ aliongea kwa kujiamini,



"Unasema kweli?" Waziri alihoji huku akisimama,



"Ndio hivyo, na ndio maana nimeingia kwa urahisi" BQ alijibu,



"Basi ni mtego" Waziri aliongea,



"Mtego?" BQ aliuliza na kipindi hicho mlango wa ofisi ya waziri ulifunguliwa na wakaingia askari wengi sana wakiwa na bunduki mikononi, wakamzunguka BQ ambaye alikuwa bado yupo kwenye mshangao kutokana na shambulio lile la ghafla,



"Mikono juu" Askari waliongea kwa amri huku mitutu ya bunduki ikimuangalia BQ ,



"Kweli ni mtego" BQ aliongea huku akitabasamu na mkono wake ulioshika bahasha, uliachia ile bahasha na alikuwa akiupeleka kwenye mfuko wa sketi yake, ila kabla mkono haujafika kwenye mfuko, alishtukia akipigwa na kitako cha bunduki kichwani, BQ akadondoka chini na damu zikawa zinamtoka puani,



"Muacheni, msimpige" Waziri aliongea kwa ukali, ila askari hawakuonekana kumsikiliza, wakamnyanyua BQ na kumfunga pingu,



"Leo umekamatika" Askari mmoja aliongea huku akimpiga kofi zito la kichwa, BQ akauma meno kwa maumivu, leo ujanja ulikuwa mfukoni.



Askari wakatoka na BQ na kumuingiza kwenye gari, waziri akabaki akishangaa, kwa maana hakutaka yule mwanamke akamatwe .....





Askari walitoka na BQ mpaka nje kwenye gari yao, wakampakia na wakaondoka nae.

Njia nzima askari walikuwa makini kwa maana walishaelezwa kuwa huyo Dada sio mtu mzuri, ana akili hatari za kupambana na pia ana nguvu nyingi.



Wakati askari wakiwa makini kupita kiasi, BQ mwenyewe alikuwa kimya huku akiwa ameinamia chini bila kujali midomo ya bunduki zaidi ya kumi ikiwa inamuangalia yeye, yeye alikuwa na mawazo yake mengi kichwani, hakuna aliyekuwa anajua yule mwanadada anawaza au anafikiria kitu gani?



Gari ya polisi iliendelea kusonga mbele huku ikiwa kwenye mwendo mkali sana. Gari ilifika kituoni na kumshusha BQ huku askari wengine wakimpiga makofi mazito ya shingo, walionesha chuki za wazi dhidi ya binti huyo, maana walimfanya adui yao baada ya BQ kuua wenzao katika siku za nyuma.



Wakamsweka selo BQ, lakini kipindi hiki BQ hakuwa na furaha, alishakata tamaa, aliona ndoto yake imekatishwa, na alihisi waziri ndio alimtegea huo mtego.



"waziri umeniweza, ila nikibahatika kutoka, nitaanza na wewe" BQ aliongea peke yake huku akiwa amejikunyata pembezoni mwa chumba cha selo.



*************



Wakati BQ akiwa na mawazo hayo juu ya waziri, huku nae waziri alikuwa anashangaa namna mkuu wa polisi alivyopuuza amri yake ya kutokuweka mtego wa kumkamata yule Dada kichaa.



Waziri akasimama na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi yake, akaweza kuuona ule mfuko wa BQ ambao aliuangusha baada ya kushikwa na polisi. Waziri akausogelea ule mfuko na kuchuchumaa, akauokota ule mfuko, kisha akaufungua na kukuta karatasi mbili zikiwa zimebanwa pamoja na pini maalum. Moja iliandikwa kiingereza na nyingine iliandikwa kiswahili, ila maneno yote hayo yalioandikwa kwa lugha mbili tofauti bado yalikuwa na maana moja, MKATABA.



Waziri akaanza kusoma zile karatasi, kila mstari aliupitia vizuri na kwa umakini, alirudia tena na tena kuisoma Ile mikataba, kwa kuwa na yeye alikuwa akiijua sharia vizuri, akajikuta akikubali kuwa ni kweli yule Dada kichaa anatakiwa kupewa maeneo yake, ni haki kupewa maeneo yake na kisha kama atakamatwa, akamatwe kwa mauaji na wala sio kwa kesi ya kudai haki yake.



Kwa kuwa ilikuwa ni jioni na ndio mida ya waziri kutoka, akaichukua ile mikataba na kuirudishia kwenye mifuko yake, kisha akavaa koti lake la suti na kuelekea nje, akaingia kwenye gari yake,



"nipeleke kituoni, kituo kikuu cha polisi mkoa" Waziri alimwambia dereva wake ambaye alimkuta ndani ya gari.



Dereva akaiondoa gari taratibu bila kuuliza kitu,



"ongeza mwendo kaka" Waziri aliongea baada ya kutoridhika na mwendo waliokuwa nao, dereva akaongeza mwendo bila kuhoji.



Walifika kituoni, Waziri akatelemka na kwenda moja kwa moja mpaka ilipo kaunta ya polisi, askari waliokuwa pale wakampa heshima,



"mkuu wenu yupo?" Waziri aliuliza,



"ndio, yupo ofisini kwake" Askari walijibu, kisha waziri akaelekea moja kwa moja mpaka katika ofisi ya mkuu wa polisi, akamkuta akiwa ndani.



Mkuu wa polisi alipomuona waziri akampa heshima yake,



"nimekuja kwa jambo moja tu, nataka umuachie yule Dada mliyemkamata ofisini kwangu" Waziri aliongea huku akiwa amesimama, hakutaka kukaa,



"kwanini mheshimiwa, yule ni muarifu" Mkuu wa polisi aliongea,



"uarifu gani alioufanya?" Waziri aliuliza,



"ameua askari, ameua viongozi wa serikali" Mkuu wa polisi alijibu,



"sio kweli, mnayemtafuta sio huyu, huyu ni mwingine" Waziri alijibu,



"kwanini mkuu? huyu ndio tuliyekuwa tunamtafuta sisi" Mkuu wa polisi aliongea,



"mbona hunielewi?? Muachieni huyo Dada, nimeshasema huyo siye anayetakiwa kutafutwa" Waziri aliongea kwa ukali,



"ni yupi sasa aliyetakiwa kukamatwa?" Mkuu wa polisi aliuliza,



"sijui, ila unatakiwa umuachie huyo Dada, kumbuka hii ni amri" Waziri aliongea,



"sawa, tutamuachia" Mkuu wa polisi alijibu,



"sio mtamuachia, Yaani Muachieni sasa hivi niondoke nae" Waziri aliongea kwa ukali,



"sawa" Mkuu wa polisi aliongea na kisha akasimama, akaanza kutoka kinyonge ofisini kwake huku waziri akimfuata kwa nyuma.



Wakatoka mpaka kaunta na kuwakuta askari kadhaa, askari wenyewe walijiuliza kwa namna mkuu wao alivyopoa muda huo, sio kawaida yake.



"mfungulieni yule mwanamke mliyemkamata ofisini kwa waziri" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama askari mmoja aliyekuwa kaunta, yule askari akataka kuuliza, ila akakumbuka kuwa kauli yoyote itokayo kwa mkubwa mkubwa wake ni amri. Yule askari akachukua funguo na kuelekea ilipo selo ya wanawake.



Baada ya dakika tano yule askari alirudi huku akiwa na BQ, BQ kwanza alishangaa kumuona waziri eneo lile, pili alijiuliza maswali mengi kuhusu waziri, swali mojawapo likiwa ni nini kilichompeleka waziri hapo?



"upo huru binti" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama BQ na kuzidi kumfanya BQ aendelee kushangaa,



"nipo huru kirahisi rahisi hivi? au kuna mtego mwingine? au wanataka waniue?" BQ alijiuliza mwenyewe, hakutoa sauti ila alijiuliza kimoyo moyo.



"twende" Waziri aliongea huku akimshika mkono BQ, wakatoka nae mpaka nje na kuingia nae kwenye gari,



"unaishi wapi ili nikupeleke?" Waziri alimuuliza BQ,



"nipeleke katikati ya mji, nitajua pa kwenda" BQ alijibu huku bado akiwa na imani kuwa yupo mtegoni.



"tuelekee uko aliposema binti" Waziri aliongea huku akimtazama dereva wake, dereva hakuongea kitu, akawasha gari na kuiondoa.



Kwa muda wa dakika tano wote walikuwa kimya, ndani ya gari hakuna mtu aliyekuwa anaongea isipokuwa radio tu.



Waziri akapeleka mkono chini, jirani na miguu yake, akachukua mfuko wa BQ ambao aliuangusha ofisini kwa waziri baada ya kukamatwa na polisi. Waziri akauokota ule mfuko na kugeuka kisha akampatia BQ,



"nimepitia hiyo mikataba, nimeona unastahili kupata haki yako, ila kitakachokukwamisha ni hizo tuhuma za mauaji" Waziri aliongea huku akigeukia mbele,



"Kuna muda inabidi uue ili kujilinda, na Kuna muda unaweza kuua ili kutia hofu watu wengine" BQ alijibu katika sauti kavu,



"sawa, mimi nitajaribu kukusaidia ili upate stahiki zako, ila na wewe jitahidi kujisaidia ili usiingie mikononi mwa polisi, sasa sijui utajisaidiaje?" Waziri aliongea kwa upole,



"cha muhimu ni haki, hayo mengine pia yatakuwa kwenye haki baada ya mimi kupewa haki ya mikataba yangu" BQ alijibu,



"sawa, acha tukuache hapa, ila kuwa muangalifu sana na nyendo zako, endapo utatiwa tena mikononi mwa polisi hakuna wa kukusaidia" Waziri aliongea huku gari yake ikisimama pembezoni mwa barabara.



"kwa maana hiyo hutaki mimi niendelee kutembea mitaani?" BQ alihoji,



"utembee ili utafute nini tena?" Waziri aliuliza kwa jazba,



"ili niendelee kupigania haki yangu, au umeridhika haki yangu kudhulumiwa?" BQ aliuliza,



"unachotakiwa kufanya ni kujificha, mambo mengine kuhusu mikataba yako nitayafuatilia mimi ili upate haki yako" Waziri aliongea huku akimaanisha kile anachoongea,



"sawa, ila sitojificha" BQ aliongea na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo za kuondoka na kumuacha waziri akimtazama tu.



"nirudishe nyumbani"" Waziri alimwambia dereva wake ambaye nae alifanya kama alivyoagizwa. Ila kitu ambacho waziri hakukijua wala BQ hakukijua ni kuwa nyuma yao kulikuwa na gari ndogo ikiwafuatilia, na ndani ya gari alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa akiwafuatilia kila hatua.



Baada ya kuona ile gari ya waziri imeondoka, yule kijana hakutaka tena kujua waziri anaelekea wapi, yeye alichokuwa anakiangalia ni wapi yule Dada kichaa anaenda, aliamua kumfuatilia.



Alihakikisha anafuatilia kila hatua iliyopigwa na BQ, na alimfuatilia kwa akili kubwa sana, hakutaka kumpoteza. Alimfuatilia mpaka BQ alipofika katika nyumba ya wageni alipopanga chumba, ubaya ni kwamba BQ hakuwa akijua kama anafuatiliwa, maana alishageuka zaidi ya mara kumi kuona kama Kuna mtu atamtilia mashaka, ila hakubahatika kuona mtu.



Baada ya yule kijana kuridhika, alitoa simu mfukoni na kupiga katika namba anayoijua yeye,



"nimeshapapata anapoishi" Kijana aliongea kwa sauti kavu,



"ni wapi?" sauti ya upande wa pili iliuliza,



"ni katika guest moja iliopo nongwa uswahilini" Kijana aliongea,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"sawa, kwa leo achana nae, ila unatakiwa uanze na waziri, ni msaliti, na wewe ni mwanajeshi na unajua msaliti anatakiwa afanywe nini?" sauti ya upande wa pili iliuliza,



"haina shida mkuu, je hiyo kazi natakiwa niifanye lini?" kijana aliuliza,



"kesho asubuhi kukicha nataka habari juu yake ndio iwe habari kuu, mimi naanza nae sasa hivi, kuna habari zitaanza kusambaa muda sio mrefu'' Sauti ya upande wa pili iliongea na kukata simu, kijana akabaki anatazama tu kioo cha simu yake, alitamani kuuliza ni habari gani itasambaa kuhusu waziri, ila alishindwa, hakuwa na mamlaka ya kumuuliza mkuu wake, mamlaka yake ni kutelekeza tu maagizo.



************



Tom akiwa yupo kitandani huku akipitia habari za kwenye mitandao, Kuna habari moja ilimshtusha na akajikuta akiguna kwa mshtuko,



"kwani vipi mwenzangu!?" Mpenzi wake aliuliza kwa mshangao huku akiendelea kujisugua kucha zake za miguuni,



"Kuna habari imenishtua hapa, eti waziri wa katiba na sheria amevuliwa uwaziri na rais" Tom aliongea huku akiendelea kushangaa,



"kwa sababu zipi?" Mpenzi wake aliuliza,



"sijui hasa, ila inasemekana eti alienda kumtoa muarifu kituoni" Tom alijibu,



"kama ni hivyo, ni sawa" Mpenzi wake alijibu na kuachana na habari hiyo, ila kwa upande wa Tom Hali ilikuwa tofauti, alishahisi kitu, alishaona huenda Kuna kitu waziri alikigundua kwa yule Dada kichaa na ndio maana akaenda kumtoa polisi, ila swali alilojiuliza Tom, ni kwanini waziri alijivika ujasili huo na kwenda kumsaidia muarifu anayeua polisi na viongozi? Tom nae akataka kulivalia njuga suala hilo, aliona Kuna kila sababu ya kuurudia uandishi wa habari.



************



Asubuhi nyingine ilifika, lakini haikufika na habari njema, Taifa liliamka na majonzi, kulikuwa na habari mbaya, kulikuwa na habari za kifo, kifo cha waziri wa katiba na sheria aliyevuliwa madaraka siku iliyipita.



Sajenti Minja aliwasili katika nyumba ya waziri huyo na kuwakuta askari kadhaa pamoja na waandishi wa habari wakiwa eneo hilo. Sajenti Minja akapitiliza mpaka sebuleni kwa waziri na kuukuta mwili wa waziri ukiwa umetundikwa juu ya ukuta huku ukiwa na matundu kadhaa ya risasi mwilini, na pembeni yake ukutani kulikuwa na maandishi yaliyoandikwa kwa damu,



"mikataba" Sajenti Minja aliyasoma yale maandishi na kuvua miwani, tayari akili zake zilishajua kuwa aliyefanya hivyo ni yule Dada kichaa ambaye ndio alisikiaga kuwa kila akifanya mauaji ndio uacha ujumbe kwa mtindo huo.



Wakati Sajenti Minja akiwaza hayo, na Tom nae alikuwa na mawazo kama hayo, Tom alikuwa nje ya nyumba ya waziri, alienda kama muandishi wa habari, na kuhusu tukio la ndani aliwasikia askari wakisimuliana nje, ndipo akaunganisha lile tukio la kifo cha waziri na namna ujumbe ulivyoachwa, akaunganisha na matukio ya nyuma ya yule Dada kichaa aliyowahi kuyashuhudia.



"sasa kama waziri alimtoa huyo Dada polisi, kwanini tena huyo Dada aje kumuua waziri?" Tom alijiuliza huku akishangaa.



***********



Ila cha kushangaza, Hali ilikuwa tofauti kabisa kwa BQ, wakati asilimia kubwa ya wananchi na viongozi wakiamini kabisa huyo Dada anahusika na kifo hicho, yeye hizo habari ndio kwanza alikuwa anazisoma katika simu yake ya mikononi kupitia mitandao, alishtuka na kuogopa, hakutegemea asubuhi angeamka na habari ya kushangaza vile, habari iliyomkatisha tamaa, kwa maana alishaanza kuamini kuwa yule waziri anaweza kumsaidia kupata haki yake.



BQ akanyong'onyea, akajilaza kitandani huku akitazama juu kwenye dari.



"hii ni safari ya DANDBEETLE (bingirisha mavi), akitoka asubuhi katika shimo lake, akirudi usiku ni lazima arudi na mzigo wa kinyesi" BQ aliongea huku akiwa anatafakari.......





BQ sasa alihisi uoga, alihisi huenda hii kesi anataka kubambikiwa yeye, hakuogopa kesi, kilichomtia uoga ni kugombanishwa na wananchi, kwa maana waziri alikuwa ni kipenzi cha wananchi, na wapo waliodhani kuwa rais aliyepo madarakani akimaliza muda wake, atayefuata ni huyo waziri aliyeuawa.



"lakini pia haiingiii akilini kudhani serikali imemuua, au huenda Kuna watu walikuwa na visasi nae, wameaumua kuutumia mwanya wa kumuua katika kipindi hiki baada ya kuenguliwa katika uwaziri?" BQ aliendelea kufikiria huku taswira ya yule waziri ikiwa kichwani kwake.



"OK, ishakuwa hivyo sasa, hapa ni kuendelea na mapambano tu" BQ aliongea na kuendelea kuperuzi habari katika mitandao.



**************



Sajenti Minja bado aliendelea kuiangalia ile maiti ya waziri huku akiwa makini zaidi,



"mkuu, gari ya hospital imefika kuuchukua mwili" Askari mmoja aliongea baada ya kuingia ndani, Sajenti Minja hakujibu kitu, aliendelea tu kuutazama mwili mpaka wahudumu wawili wa hospital walipoingia ndani huku wakiwa wamevaa makoti yao meupe na walikuwa wamebeba machela za kisasa.



Walipoingia ndani waliwasabahi baadhi ya polisi waliowakuta akiwepo Sajenti Minja pia.



"tunaweza kuubeba mwili?" Mhudumu mmoja wa hospital aliuliza huku akimtazama askari aliyekuwa jirani nae,



"eti mkuu, wanaweza kuuchukua mwili wa mheshimiwa" Yule askari aliuliza huku akimtazama Sajenti Minja,



"uchukueni" Sajenti Minja aliongea na kukaa katika kochi, kisha akatoa simu yake na kuupiga picha ule mwili, na pia akapiga picha yale maneno yaliyoandikwa kwa damu pale ukutani.



Mwili uliondolewa na sebule ikabaki na askari tu waliokuwa wakiendelea kufanya uchunguzi wao,



"familia ya mheshimiwa ipo wapi?" Sajenti Minja alimuuliza askari aliyekuwa jirani nae,



"wameondelewa, wamepelekwa sehemu nyingine" Askari alijibu,



"sawa" Sajenti Minja aliongea na kuinuka, akawa anaelekea nje, hapo mawazo yalikuwa yakimtafuna kwa kufikiri ni kwanini yule binti amuue waziri, wakati waziri alimsaidia siku iliyopita kwa kumtoa kituoni? Wakati Sajenti Minja akiwaza hayo, mbele yake kulikuwa na kundi la waandishi wa habari wakitaka kusikia ni kipi kimegundulika katika mwili wa waziri? Sajenti Minja hakutaka kuhojiwa, ila waandishi wa habari walimzonga huku wengine wakiuliza maswali ila Sajenti Minja hakutaka kujibu, ilibidi askari wengine waje wamsaidie kuzuia waandishi wa habari ili Sajenti Minja apate njia ya kupita.



Sajenti Minja alifanikiwa kupita mpaka akaingia kwenye gari yake, na kupandisha vioo vya gari juu, akashusha pumzi ndefu na kuwasha gari yake, ila kabla hajairuhusu gari yake kuondoka, alisikia mtu akigonga kioo cha gari cha mbele upande wa kushoto, Sajenti Minja akageuka na kumuona mtu akiwa na simu mkononi na kijitabu kidogo alichoshika pamoja na kalamu, Sajenti Minja akakunja ndita zake kwa hasira, alishajua ni muandishi wa habari amefanya hiyana mpaka amefikia gari yake, Sajenti Minja akaanza kuondoa gari yake, ila yule muandishi wa habari aligonga body kwa nguvu na kumfanya Sajenti Minja asimamishe gari huku akiwa na hasira, akashusha kioo ili huyo muandishi wa habari achungulie amtukane au amuonye, lakini cha ajabu badala yule muandishi achungulie, alifungua mlango na kuingia ndani ya gari, kisha akakaa na kufunga mlango na kumgeukia Sajenti Minja, Sajenti Minja akabaki na mshangao baada ya kumgundua,



"Tom umefuata nini hapa?" Sajenti Minja aliuliza huku akishangaa,



"habari, nimefuata habari kiongozi" Tom alijibu huku akitabasamu,



"umerudia kazi yako ya uandishi wa habari? Si ulikuwa unafanya kazi ofisi ya mkuu wa wilaya wewe?" Sajenti Minja aliuliza maswali mfululizo,



"ni habari ndefu sana" Tom alijibu huku akishusha pumzi,



"habari ndefu kivipi? Bado upo ofisi ya mkuu wa wilaya au ndio umeamua kugeukia tena uandishi wa habari?" Sajenti Minja aliendelea kuuliza maswali na kipindi hicho waandishi wengine wa habari walianza kulisonga gari lake,



"ondoa gari hapa kwanza, si unaona wanahabari wanavyokuzonga" Tom alimwambia Sajenti Minja,



"unaelekea wapi wewe?" Sajenti Minja alimuuliza Tom,



"popote tu uendapo, ila nina maongezi na wewe kidogo, naomba utafute sehemu unipe muda wa kuongea na wewe" Tom aliongea kwa sauti tulivu,



"usitegemee nitakwambia chochote kuhusu tukio la leo, maana nyie waandishi wa habari hampaswi kujua vitu kabla polisi hawajamaliza uchunguzi wao" Sajenti Minja aliongea kwa utani huku akitabasamu na kwa wakati huo huo alikuwa akiliondoa gari lake eneo hilo,



"sitaki unihadithie chochote, ila nataka nikupe mwanga kuhusu hiki kinachotokea" Tom aliongea na kumfanya Sajenti Minja amgeuzie uso, hakutegemea kukutana na kauli kama hiyo,



"mwanga?? unajua nini kuhusu hili tukio la leo?" Sajenti Minja alimuuliza Tom,



"twende tu braza, tutaongea tukishapata sehemu iliyotulia" Tom alijibu huku akifunua kijitabu chake kidogo alichokuwa nacho mkononi.



Sajenti Minja akaondoa gari huku akiwaza ujio wa Tom, ni kijana aliyemuamini sana kwa kipindi kifupi.



"hivi yule mtu wako wa ajabu, Sudy Bakari, umeshawahi kumuona tena?" Sajenti Minja aliuliza huku alitabasamu,



"hapana, tangu kipindi kile tulipoenda nae kule msituni na akachukuliwa na radi, sijawahi kumuona tena" Tom alijibu,



"Yule jamaa alikuwa ana mambo ya kushangaza sana, endapo binadamu tungekuwa vile dunia sijui ingekuwaje?" Sajenti Minja alihoji,



"alafu uzuri yule jamaa alikuwa mpole sana, je fikiria angekuwa mtu wa fujo ndio ingekuwaje!?" Tom aliuliza wakati Sajenti Minja akiegesha gari nje ya mgahawa.



Wakatelemka na kutafuta meza moja iliyokuwa nje ya mgahawa na iliyokuwa imejitenga kidogo, wakaenda na kukaa, muhudumu akawafuata na kuwasikiliza, wakaagiza wanachohitaji na kisha muhudumu akaenda kuwaletea.



"haya sasa niambie unachokijua kuhusu huyo Dada" Sajenti Minja aliongea na kumuangalia Tom aliyekuwa akitafakari aanzie wapi?



"kwanza kabisa unatakiwa ujue kuwa mimi nimeondoka kazini kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya huyo Dada, na mimi ndio mtu wa kwanza niliyempa nafasi ya kuonana na mkuu wa wilaya, alafu siku iliyofuata ndio akamuua" Tom aliongea na kumuangalia Sajenti Minja aliyekuwa ametega vizuri masikio.



"ulifanikiwa kujua kwanini amemuua mkuu wa wilaya?" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio, kwa maana mkuu wa wilaya alikutwa na ujumbe puani uliokuwa umeandikwa katika kikaratasi, ujumbe ulisomeka hivi "KESHO KILA MTU ATAKUWA PANAPOSTAHILI", Tom aliongea na kutulia,



"na kwanini ujumbe ulikuwa na maneno hayo?" Sajenti Minja aliendelea kuuliza,



"nadhani ni kutokana na kauli ya mkuu wa wilaya, kwa maana siku ile baada ya yule Dada kichaa kuingia ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya, hata hakukaa sana, mlango ulifunguliwa na kisha mkuu wa wilaya alimfukuza, alimwita chizi na alidai hakustahili kuwa eneo lile, yule Dada kichaa aliondoka na kupita karibu yangu, akatasamu na kuongea kuwa, KESHO KILA MTU ATAKUWA PANAPOSTAHILI, kisha akaondoka, wala sikujua anamaanisha nini? ila siku iliyofuata ndio mkuu wa wilaya alikutwa amekufa akiwa na ujumbe huo" Tom alijibu na kumfanya Sajenti Minja akitingisha kichwa kuonesha amekubaliana nae,



"lakini ulitoa taarifa polisi na ukawaeleza hicho kitu?" Sajenti Minja aliuliza,



"nilitoa taarifa hapo hapo eneo la tukio, ila yule Dada alipotea katika mazingira tata, kwa maana wakati natoa taarifa, alikuwepo mbele yangu, ila nilipoinua macho sikumuona tena, ila kwa kuwa nilitoa taarifa, polisi ilibidi waondoke na mimi, wakanihoji na nikawaeleza kila kitu, wakanitupa selo, ila baada ya siku chache walifanikiwa kumkamata yule Dada, akakataa kuhusika na kifo cha mkuu wa wilaya, na hata walipompima alama za vidole, hazikuendana na zile zilizokutwa katika mwili wa marehemu, kwa hiyo polisi wakamuachia" Tom alijibu huku akimtazama Sajenti Minja,



"kwa maana hiyo hakuwa na hatia?" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio hivyo, alafu wiki moja baadae akamuua msaidizi wa mkuu wa wilaya, kisa tu alimuita kichaa, na katika maiti ya huyo msaidizi iliyokutwa sebuleni kwake, kulikutwa na maneno ukutani yaliyosomeka kuwa chizi naye mtu" Tom aliongea,



"hapo tena alikamatwa?" Sajenti Minja aliuliza,



"alikamatwa na wakampima alama ya vidole, ila bado mambo yakawa yale yale, akaachiwa, na pia ilionekana asingekuwa na uwezo wa kuua kwa sababu ana mkono mmoja" Tom aliongea,



"ana mkono mmoja? Sasa mbona huyo tunayemtaka sisi ana mikono miwili, tena nilishawahi kukutana nae na tukapambana" Sajenti Minja aliongea kwa mshangao,



"kuhusu kuwa na mikono miwili sijui, ila labda inawezekana wapo wawili, ila aliyetolewa polisi jana na waziri, ndio huyo mwenye mkono mmoja" Tom aliongea na kumfanya Sajenti Minja atafakari kidogo,



"huenda ipo hivyo, je una picha yake?" Sajenti Minja aliuliza,



"picha sina, ila anapokaa kwa sasa napajua" Tom aliongea na kumuangalia Sajenti Minja aliyeonesha mshtuko,



"sasa si twende tukamchukue?" Sajenti Minja aliongea kwa jazba kidogo,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"kwa asubuhi hii ni ngumu kumkuta, kwa maana nimeshawahi kumfuatilia mara kadhaa na kugundua muda ambao uwa yupo, ni muda wa usiku" Tom alijibu kwa utulivu,



"hapo anapokaa ni kwao?" Sajenti Minja aliuliza,



"hapana, ni katika nyumba ya wageni, ipo katika mtaa ambao mimi naishi kwa sasa" Tom alijibu,



"sawa, basi itabidi nikupe namba yangu, alafu tutawasiliana usiku ili nije kumkamata" Sajenti Minja aliongea,



"hakuna shida, uje ukiwa umejipanga" Tom aliongea huku akiwa makini kabisa,.



"nalijua hilo" Sajenti Minja aliongea huku akikumbuka namna alivyochezea kichapo walipokutana na huyo Dada.



Baada ya kumaliza maongezi yao, waliagana na kuachana kwa mihadi ya kuwasiliana nyakati za usiku kwa ajili ya kwenda kumdhibiti yule Dada.



**************



Mishale ya saa nne usiku, anaonekana yule kijana aliyekuwa akimfuatilia BQ na Waziri katika siku iliyopita, yule kijana alikuwa katika ule mtaa ambao BQ alikuwa amefikia katika nyumba ya wageni.



Yule kijana alifika mpaka katika ile Guest na kuingia moja kwa moja mpaka ndani.



Tom yeye alikuwa katika duka ambalo uwa ananunua bidhaa zake, hilo duka linatazamana na Guest aliyofikia BQ. Tom alimuona huyo kijana akiingia, ila hakumtilia umakini sana, alihisi ni mteja wa kawaida.



Baada ya dakika kumi aliweza kumshuhudia yule kijana akitoka ndani ya ile guest, akasimama mlangoni na kaweka tai yake vizuri, kisha akaondoka na ile njia aliyokuja nayo hawali.



"atakuwa amekosa chumba huyo" Tom aliongea peke yake huku akitazama saa yake ya mkononi, alikuwa akimsubiri Sajenti Minja aliyemwambia yupo njiani anakuja.



Na kipindi hicho duka lilikuwa likifungwa, muda ulikuwa umeyoyoma sana, Tom akatoka eneo la dukani na kuelekea katika upande mwingine katika mtaa huo huo.



Baada ya robo saa, Sajenti Minja alifika mtaa huo, kwa bahati nzuri Tom alifanikiwa kuwahi kumuona, Tom akasogelea gari ya Sajenti Minja na kugonga kioo, Sajenti Minja akashusha kioo,



"ingia twende" Sajenti Minja akaongea,



"geuza gari, guest yenyewe si hiyo nyuma yako" Tom aliongea na kumfanya Sajenti Minja atabasamu, kisha akageuza gari na kulisogeza katika eneo la ile guest, akatelemka na kumsubiri Tom aliyekuwa amebakiza hatua chache kumfikia.



Tom alipomfikia, waliingia ndani ya guest na kwenda moja kwa moja mapokezi, ila hawakumkuta mtu, wakasimama kwa dakika tano, pia muhusika hakuonekana,



"atakuwa amelala nini?" Sajenti Minja aliuliza,



"sijui, ebu tujaribu kuita" Tom alijibu kisha akaanza kuita, ila pia hakukuwa na jibu,



"ebu ngoja niitie huku upande vilipo vyumba" Tom aliongea huku akielekea upande vilipo vyumba, ila kabla hajaanza kuita, aliona katika mlango wa chumba kimoja damu zikitiririka kutoka ndani, Tom akaguna,



"vipi mbona unaguna?" Sajenti Minja aliuliza huku akipata mashaka,



"damu" Tom alijibu,



"damu!!!??" Sajenti Minja alishangaa huku akielekea upande aliopo Tom, alipomfikia Tom aliweza kuona hizo damu zikiwa katika mlango wa chumba, Sajenti Minja akachomoa bastola yake kiunoni na kuanza kuusogelea ule mlango, alipoufikia akatega sikio kusikiliza kama Kuna watu, kulikuwa kimya. Sajenti Minja akashika kitasa na kusukuma mlango, alichokiona kilimfanya aogope, alikuta mwili wa mwanamke ukiwa umenyongwa kwa kutumia shuka iliyofungwa kwenye feni za juu, maarufu kama panga boy. Mwili ule ulikuwa ukining'inia na nywele ndefu za yule mwanadada ziliangukia usoni na kumziba sura, na pia huyo mwanamke hakuwa na mkono mmoja.



Na kipindi hicho Tom ndio alikuwa akiingia katika kile chumba, alijikuta akitaka kukimbia kutokana na unyama alioukuta mule ndani,



"mwanamke mwenyewe mwenye mkono mmoja uliyekuwa ukimzungumzia ndio huyu?" Sajenti Minja aliuliza na kumfanya Tom aangalie mikono ya yule Dada, akagundua ni kweli hana mkono mmoja,



"ndio, ndiye huyu" Tom alijibu huku akiutazama mwili ule uliokuwa ukining'inia huku ukivuja damu, na haukuwa na uhai.....





_____________

"sasa mbona damu zinavuja mkononi, na chini ya kitanda Kuna damu nyingine I natoka?" Sajenti Minja aliuliza huku akipiga magoti na kuchungulia chini Ya kitanda, akaguna,



"vipi?" Tom akauliza huku nae akiinama, nae akashtuka baada ya kuuona mkono wa mtu ukiwa chini ya kitanda,



"basi huu mkono ni wa huyu Dada hapa aliyetundikwa juu" Sajenti Minja aliongea baada ya kuona yule Dada damu zikiwa zinatoka katika eneo mkono ulipokatwa.



"kweli, kwanza huyu sio yule tunayemtaka, hata sura yake ni tofauti" Tom aliongea huku akiwa ameukazia sura ule mwili wa yule dada,



"huyu kauawa muda si mrefu" Sajenti Minja aliongea huku akiangalia joto la mwili la yule Dada,



" inawezekana yule Dada kichaa ndie amemuua" Tom aliongea,



"ebu njoo huku" Sajenti Minja aliongea huku akitoka nje ya kile chumba, akaelekea upande wa nyuma wa ile guest, alikuwa anaangalia kama Kuna mlango wa kutokea upande wa nyuma, lakini mlango haukuwepo, pia ile guest haikuwa na uzio.



Sajenti Minja akarudi mule ndani ya chumba huku Tom akiwa nyuma yake.



"wewe si ulikuwa nje muda mrefu?" Sajenti Minja alimuuliza Tom,



"ndio" Tom alijibu huku alijiuliza kwanini ameulizwa vile,



"Kuna mtu yoyote ulimuona akiingia hapa?" Sajenti Minja aliuliza,



"ndio, ni jamaa mmoja hivi alikuwa amevaa suruali ya kitambaa amechomekea, na pia alivaa moka" Tom alijibu,



"huyo ndio mauaji, kwa maana humu ndani hamna hata mtu mmoja, na huyu msichana ameuawa muda si mrefu" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa simu yake, kisha akawataarifu polisi juu ya tukio lililotokea katika eneo hilo.



Sajenti Minja akatoka pale chumbani na kuelekea moja ilipo kaunta ya mapokezi. Tom alikuwa akimfuata kwa nyuma.



Sajenti Minja alipofika, akapekua katika droo iliopo chini ya meza, na kutoa daftari kubwa lililokuwa na orodha ya wageni walioingia na kutoka siku hiyo, aliona jina la mgeni mmoja tu aliyetoka siku hiyo.



"sasa wewe niache, nenda nje tu, maana polisi wanaweza kukubeba endapo utaonekana ulikuwa shahidi hapa" Sajenti Minja aliongea na kisha Tom akatoka nje kwa minajili ya kuwasiliana na Sajenti Minja katika siku inayokuja.



Dakika kumi tu baada ya Tom kuondoka, gari ya polisi ilifika katika Ile guest na kuuchukua mwili wa yule mhudumu wa guest.



Polisi walifika, wakaubeba mwili na kuondoka, eneo zima lilizima kutokana na lile tukio, watu wa ule mtaa walikuwa na hofu, wale waliokuwa na tabia za kuchelewa kurudi majumbani kwao, siku hiyo waliwahi, Mtaa wote ulipoa siku hiyo.



Kipindi hayo yote yanatokea, BQ alikuwa kwa mbali akishuhudia kila hatua, baada ya gari ya polisi kuondoka, BQ akaanza kupiga hatua ndogo ndogo kuondoka eneo hilo, mkononi alikuwa na pochi yake na mgongoni alivaa begi dogo jeusi.



***************



Yule kijana aliyefanya mauaji siku iliyopita, alionekana akiingia ikulu na gari yake ya kifahari, hakuna hata mlinzi aliyeweza kumzuia usiku huo, inaelekea wote walikuwa wakimfahamu vema.



Kijana aliegesha gari yake sehemu husika na kutelemka katika gari, kwa bahati nzuri alimkuta Rais akiwa katika bustani moja wapo katika eneo la ikulu, alikuwa ameketi nyuma ya meza ya kioo na juu ya meza kulikuwa na birauri ya kioo iliyoonekana ina kinywaji na pembeni ya birauri kulikuwa na chupa moja ndefu iliyoonekana ya mvinyo wa gharama kutoka nje.



Kijana alielekea moja kwa moja mpaka alipo Rais, akamsalimia na kisha akaketi katika kiti kingine kilichopo hapo.



"hongera kwa kazi nzuri ya kifo cha waziri" Rais aliongea huku akitabasamu,



"asante" Kijana aliongea huku akitabasamu,



"ulikutana na ugumu gani ulipoingia nyumbani kwa waziri?" Rais aliuliza,



"hakukuwa na ugumu wowote, kwa maana hakukuwa na walinzi nje kwa sababu waziri alishakataa nyumba yake iwe na ulinzi tangu yule mwanamke alipoanza kwenda kwake mara kwa mara" Kijana alijibu,



"familia yake ilikuwa wapi ulipofika pale?" Rais aliuliza,



"walikuwa wamelala, nadhani mkewe alikuwa ndani, kwa hiyo sikuweza kukaa muda mrefu sana, mpaka naondoka hakuna aliyekuwa amegundua kitu" Kijana alijibu,



"safi sana, je na yule Dada umeshammaliza? maana ulisema ulikuwa na ratiba ya kwenda kummaliza usiku huu?" Rais aliendelea kuuliza,



"ndio nimetoka huko muda si mrefu, sijafanikiwa kumkuta" Kijana alijibu,



"ameondoka, amehama au alikukimbia, hujafafanua" Rais alihoji,



"imeonekana alihama mchana, nikajaribu kuulizia jina lake na namba ya simu, ila yule dada mfanyakazi wa pale imeonekana hakuwa akimuandika na wala hana kitu chochote muhimu kuhusu yule dada, sasa nikaona huo ni uzembe, nikammaliza na yeye" Kijana alijibu kwa kujiamini,



"hakukuwa na sababu ya kumuua, ila sawa" Rais alijibu.



"sasa mimi naendelea kumtafuta huyo dada popote pale" Kijana aliongea,



"sawa, ufanye haraka kwa maana sio mtu mzuri yule, muuaji anatakiwa auawe" Rais aliongea,



"sawa mkuu" Kijana alijibu.



"kapumzike sasa, mimi mwenyewe namalizia hiki kinywaji kisha naingia kulala" Rais aliongea huku akiinua chupa yake ya mvinyo na kuangalia kiasi kilichobaki.



"haya mkuu, nikutakie usiku mwema tu" Kijana aliongea huku akisimama,



"sawa kijana wangu" Rais alijibu kisha yule kijana akaelekea katika gari lake na kuondoka kwa mwendo tulivu huku Rais akimuangalia.



****************



Siku iliyofuata, Sajenti Minja alimchukua alimchukua Tom na kwenda kule katika wilaya ambayo Tom alikuwa akifanya kazi hapo hawali, walikuwa wanaenda kwa jambo moja tu, kufuatilia alama za vidole katika hospital ambayo alifanyiwa vpimo yule Dada, na mambo mengine kumuhusu yule Dada kichaa.



Walifika katika Ile wilaya na kwenda moja kwa moja katika Ile hospitali, wakafanikiwa kupata kile Wanachotaka, pia hasa Sajenti Minja alitaka kujua jina la yule Dada, akafanikiwa kujua kuwa anaitawa Maria Zyachenko. Sajenti Minja akanakili lile jina katika kijitabu chake kidogo.



"hili jina la kirusi kabisa, alafu inashangaza mwenyewe mwenye jina ni mswahili" Sajenti Minja aliongea huku akiingia katika gari lake,



"inawezekana anatumia jina la uongo, wewe unadhani angetumia jina lake la ukweli si angepatikana kirahisi, kwa maana watu wake wengi wa karibu wangemjua endapo jina lake la ukweli litatangazwa katika vyombo vya habari" Tom aliongea huku akijifunga na mkanda wa gari,



"hiyo pia inawezekana, ila mimi nitaanza kumtafutia hapa hapa katika jina hili" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha gari yake na kuiondoa.



"ila pia nadhani wapo wengi wanaofanya mauaji, kwa maana kwa namna yule Dada anavyoua ni tofauti sana na ile namna tuliyoiona pale guest, pia hata katika kifo cha waziri" Tom aliongea,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"pale guest inawezekana ameua yeye au yule mtu uliyemuona akiingia pale, ila kuhusu waziri nadhani ni yule yule mwanamke, hakuna mtu mwingine wa kumuhisi" Sajenti Minja aliongea,



"ila sidhani" Tom aliongea,



"hapo mimi nimeongea kipolisi zaidi, ila kama wewe unajua zaidi, ni vyema nikushike ili uisaidie polisi" Sajenti Minja aliongea,



"mimi sijui kitu, nilikuwa natoa maoni tu" Tom aliongea kwa kigugumizi na kumfanya Sajenti Minja atabasamu.



*************





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog