Simulizi : Pasipoti Ya Gaidi 'The Return Of Kamanda Amata'
Sehemu Ya Nne (4)
***
Katika ofisi ya shirika la ndege la Qatar, vijana wale walikuwa wakiongea na mhudumu kumueleza kuwa hawamwoni ndugu yao ambaye kasafiri na ndege hiyo kutokea Doha.
“Mna uhakika na hilo?” mmoja wa wafanyakazi aliwauliza.
“Ndiyo tumeongeas naye akiwa Doha,” wakajibu. Yule kijana akaisogelea kompyuta yake na kutazama orodha ya wasafiri wote waliokuwa kwenye ndege hiyo, kweli Rajana Kadah jina lake lilionekana. Yule bwana akatahayari, akawasiliana na watu waliokuja na ndege hiyo na kuanza kufanya uchunguzi.
Katika maegesho nje ya uwanja huo, Gina aliifikia gari aliyokuja nayo, alipoikaribia aliangua kicheko baada ya kuwaona Scoba na Amata wakiwa wametulia ndani yake.
“Nyie wanga nini!” aliwatania.
“Kwani we hujui njia zetu za kupita? Mbona hujaleta mizigo sasa, nenda tafadhali, mizigo yetu ina ile lebo ya siri,” Amata akamwambia na Gina akafanya hivyo. Dakika kumi baadae wote walikuwa garini kimya.
“Mnaiona gari ile pale? Ile Cruiser…” Gina aliwaonesha.
“Ndiyo, vipi?”
“Nina wasiwasi ni watu wa mapokezi, walikuja kuwapokea,” Gina akaeleza.
“Ok, basi waache waendelee kutusubiri, na sisi tuwasubiri hapa ili tuondoke wote,” Scoba akamalizi na wote wakaketi vitini kimya huku vyoo vyeusi vya gari ile vikiwa juu kabisa na kuruhusu kiyoyozi kufanya kazi yake.
***
Kubra Khaleb alifinya macho na kuyafinyua, akaondoa simu sikioni na kuikita mezani kwa kishindo kilichotawaliwa na hasira. Rajan hakuwepo ndegeni, aliwaza bila kupata jibu, haiwezekani kabisa akajipa moyo. Hapo sasa akili yake ikaanza kukubali kuwa inawezekana mtu huyo ameuawa lakini bado lilikuwa wazo tata kwa kuwa hata huyo muuaji naye hakuonekana, je hakuwapo katika ndege? Kama ndiyo basi wapi wameshuka au wamepotelea? Akajiuliza na kujiuliza.
Mara hiyo simu yake ikaanza kuita tena, akainyakuwa na kuweka sikioni, simu ilikuwa inatoka uwanja wa ndege ofisi ndogo ya shirika la ndege la Qatar. Taarifa aliyoipata haikumfurahisha ijapokuwa hakuwa na uhakika nayo kuwa ndani ya ndege kumekutwa na maiti ya mtu mwenye asili hiyo lakini hakuwa na chochote cha kumtambulisha. Kubra akawapigia vijana wake nao wakarudi kule uwanjani kuhakikisha, ndipo waliposhuhudia mwili wa Rajani ukiwa umehifadhiwa katika chumba maalum tayari kupelekwa kuhifadhiwa…
Kubra Khaleb aliipiga teke meza iliyo mbele yake na kuivunja vipande vya kutosha, uso wake ulibadilika na kuwa mwekundu, macho yake makavu na madogo sasa yalikuwa mekundu makubwa na yaliyoonesha dalili ya kutota kwa machozi, akachomo abstola yake na kupiga hewani huku akisahau kama yuko ndani, akatobo dari kwa matundu matatu yaliyo sawa, akaitupa bastola ile chini sakafuni nayo ikatawanyika vipandevipande juu ya marumaru zile za kupendeza ambazo hazikujua hata nini kinaendelea kwa bwana huyo. Akajitupa chini kitini, alizoea kuweka miguu juu ya meza, alipoipandisha akajikuta ikianguka chini. Hodi ikabishwa mlangoni na kilichofuatia ni vijana wake kuingia wakiwa wote wamechanganyikiwa kiasi Fulani.
“Haina haja ya kuniambia chochote, nina taarifa, hivi huyu jamaa anajiamini nini kutuchezea watu kama sisi? Anathubutu kumuua Rajan! Rajan! Simini kabisa, hapana , itakuwa Rajan kajiua mwenyewe, mimi ninamjua kijana wangu, nimemfundisha mwenyewe kazi hizi, anajua kuu hadi waliokufa, ana uwezo wa kuua kwa mkono wako ilhali we mwenyewe haupo eneo hilo, imekuwaje? Imekuwajeeee? nasema huyo bwana atafutwe, mkimpata mniletee hapa nimkate kidole kimoja baada ya kingine. Poteaaa!” Khaleb akaongea kwa hasira na kuwapa kazi wasiyoitaraji hao vijana wake huku yeye akiliendea jokofu na kutoa Vat 69 kwa ajili ya kupoteza mawazo ilhali anachoma maini na kupunguza muda wa kuishi.
6
MAKABURI YA KINONDONI
UKIMYA ULITAWALA kama kungekuwa na sakafu ya saruji basi ungeisikia sindano pindi tu iangukapo. Ijapokuwa kulikuwa na watu zaidi ya elfu tano katika makaburi hayo lakini ukimya ule ulitisha, ni miti iliyojaribu kuuvunja lakini bado ilikuwa na kibarua kigumu, ndege hasa Tausi waliojificha kwenye vichaka vya makaburi hayo ya vibosile waliweka sauti zao hadimu na kuipamba huzuni ya waombolezaji na kuifanya iwe na uzito zaidi mbele zao. Hakuna aliyeongea wala aliyesikika akilia.
Katika eneo hilo kulikuwa watu waiana mbalimbali, ukiacha familia za marehemu wanajeshi waliokufa huko Mpumbutu kulikuwa na wananchi wenye uchungu waliopenda nchi yao, ambao macho yao yalijawa na hasira na uchungu usio na kipimo. Viongozi wa jeshi vyama na serikali walikuwapo katika hema yao waliyoandaliwa, viongozi wa dini kadiri ya dini za marehemu wale nao walikuwako wakiwa wamevalia mavazi rasmi tayari kwa zoezi hilo la kihistoria. Kila kona ambayo ungekatiza basi ungekutana na mwanajeshi aliyevalia combart nadhifu kabisa, iliyong’ara na kofia nyeusi aina ya barret. Katikati ya makundi hayo kulikuwa na makaburi matano yaliyochimbwa na kujengwa vizuri kwa ndani na vijana wa JKT, kwa ujumla itifaki ilizingatiwa. Bendera ya taifa na ile ya JWTZ zilikuwa zikipepea kufuatia upepo uliokuwa ukitoka baharini.
Amri ya kijeshi ikatolewa, vijana wa jeshi waliojipanga katika mistari nadhifu walijiweka sawa, wakageuka upande wa barabar na kupiga mguu chini, kisha wakatulia tuli huku mikono yao ikiwa imebanwa sawia. Na raia nao wakasimama kutoka pale walipokaa.
Upande wa barabara ya Kinondoni kulionekana polisi wa usalama barabarani aikelekeza msafara wa magari kukata kulia yaani kuchukua barabara ile iingiayo katika viwanja hivyo. Msafara ule ulikuja taratibu sana huku gari zote zikiwa zimewasha taa. Mbele kabisa kulikuwa na gari iliyokuwa ikivuta mzinga na juu ya mzinga huo kulikuwa na sanduku lililofunikwa vizuri kabisa kwa bendera ya jeshi na nyuma zikafuatia gari nyingena za mtindo huohuo. Zilipofika mahala palipotakiwa ile ya kwa nza ikasimama usawa kabisa wa lango la kuingia makaburini.
Vijana wale wa jeshi wakapewa amri na baadhi yao kwa mistari ya kupendeza walitembea mwendo wa haraka kueleka pale ile gari iliposimama, walikuwa kama vijana nane hivi wakisindikizwa na wengine watatu waliokuwa na vyeo vya juu kuliko wao. Walipofika katika ile gari wakasimama, amri iliyofuata ikawapa mamlaka wale wawili wawaondoa kofia zao na kuzishika pamoja kisha wale sita wakasogea na kulitoa lile sanduku pale katika ile gari. Wakaliweka begani na kusogeaa mahala pengine walipotakiwa kungoja. Kisha ikawa hivyohivyo kwa masanduku yote matano na sasa ikatoka amri nyingine. Bendi ya jeshi kutoka JKT ikapiga wimbo wa huzuni sana kwa tarumbeta zao, wanajeshi wale waliokuwa na zile tutsi mabegani mwao walitembea sambamba kwa mwendo wa aina yake, sio wa polepole wala sio wa haraka lakini walifanya kitu cha kupendeza ili kilichoonekana kuwa na huzuni kadiri ya melodia ile ya muziki ilivyokuwa inakwenda. Baada ya kuweka kila sanduku mahala pake wale vijana waliondoka na itifaki nyingine zilifuatia, upande wa kidini walifanya ibada zao na walipomaliza jeshi liliendelea na ratiba zake kadiri ya utaratibu wao.
Miongoni mwa waombolezaji waliokuwepo mahala hapo, Madam S alikuwa kwenye mstari wa pili kutoka ule alioketi Rais Robert Sekawa, macho yake kama kawaida yalikuwa makini kuangalia huku na kule kwani alijuwa kwa kuandaliwa kiti kile pia alikuwa na jukumu la ulinzi wa nchi, kushoto na kulia kwake kulikuwa na watu mbalimbali wadau wa usalama wa nchi na viongozi wa serikali. Vijana wake walitawanyika kona mbalimbali kwani waliamini kabisa kuwa eneo kama hilo lazima wabaya wao watakuwepo, lazima anayejua siri na utaratibu wa mauaji hayo atakuwepo, kama si yeye basi hata ‘mjomba’ wake atakuwepo.
Kamanda Amata alikuwa katikati ya kundi la vijana waliokuwa wakipiga soga la mitaani, kwa jinsi alivyovaa usingemzania, shati la kawaida tena lisilo na mifuko, kofia ya cap na suruali ya jinzi iliyokatwakatwa magotini, chini alitilia makubazi ya kawaida kabisa. Katikati ya vijana wale naye aliweka ushabiki mkubwa wa stori zilizokuwa zikiendelea, wale vijana hawakujiuliza wala kushangaa kwa nini jamaa huyo kila stori waliyokuwa wakiongea aliichangia kwani alijuwa kuliko wao. Lakini pia alijaribu kuanzisha stori mbalimbali ambazo zingeweza kumwongezea kitu kichwani maana aliamini vijana wa kijiwe hujua mengi ya chini ya zuria kuliko wale wa maofisini.
“Wale jamaa makamanda ndugu yangu! Nimewashuhudia mwenyewe juzi kati wakati naenda kufata mzigo,” mmoja aliongea kwa sauti ya kiiteja.
“Aaaa Sudi ushaanza, wapi tena?” mwingine aliuliza.
“Hawa sijui mnawita wanini hawa waliopewa tenda ya ya kutengeneza barabara hiyo apo hiyo, aaaa ndugu yangu, wana mashine mle kwenye makatapila yao, sogea uone wanakumwaga mav* wale, wale wapiganaji wana biashara mbili wale. Kwani mwezi uliopita si wamepiga milioni zao kule mtaa wa kati, sio watu wale, wamejificha mle,” Sudi aliendelea kubwabwaja. Habari hii ikamvutia sana Amata, akaitazama saa yake na kuiwasha ikaanza kurekodi kila kinachoongelewa, huku na yeye akitilia chumvi hapa na pale.
“Kwa hiyo hawa wanajifanya kutengeneza barabara kumbe…” Amata akakatishwa.
“Braza mi nakwambia…” Sudi akaendelea, “sikufichi, mi huwa naiba mafuta mle, lakini majuzi hapo sikusogea, nilikuta wanapiga stori moja ikabidi mwanangu, nikunje mkia ka’ mbwa mwoga vile. Wale jamaa hawafai, wapo wakandarasi wa barabara na wakandarasi wa maisha ya watu, oh! Mengine tusiseme jamani ngoja tuwazike makamanda wetu,” akamaliza na kunyanyuka baada ya kuona vijana wa jeshi wanajipanga tayari kutoa heshima zo kwa kupiga risasi za hewani.
MPUMBUTU
WAPIGANAJI walikuwa kimywa kwenye maficho yao kuzunguka kambi kuu ya waasi huku wakisubiri wale majasusi wao waluowatuma kuja kuleta habari ili wajue wapi pa kunzia katika mashambulizi yao. Kila mmoja alikuwa na uchungu wa kulipa kisasi juu ya mauaji ya wenzao ambapo siku hiyo wapiganaji hao wote walivalia vitambaa vyeusi katika katika mikono yao ya kuume juu ya kiwiko na chini ya bega. Amri waliyopewa ni kuweka silaha chini siku hiyo kwa kuwa walijua kuwa wenzi wao ndiyo wanazikwa hivyo nao wana haki ya kuomboleza.
Waasi wa X65 walikuwa tuli kwenye mahema yao huku wengine wakiendeleaza ulinzi wa hapa na pale. Na huko katika machimbo vijana wa kazi walikuwa wakiendelea kuchimbua madini. Katika moja ya hema iliyo karibu na mlima kulionekana kuwa na shughuli kubwa zaidi na ulinzi wa hapa na pale bila kukosa watoto wa vikopo waliokuwa wamezagaa wakifanya hili au lile. Ndani ya hema hiyo kulikuwa na watu watatu, mwanajeshi mmoja aliyeitupia miguu yake mezani huku chupa ya bia aina ya Primusi ikipanda na kushuka kinywani mwake, miwani yake nyeusi iliyaficha macho katili ya mtu huyo aliyechafuka kwa vyeo anuai vya kijeshi huku gwanda lake la kijeshi alilolivaa juu lilikuwa wazi, halikufungwa vifungo vyake. Katika meza kubwa ya pembeni alikuwa amekaa kijana mwingine naye akiwa kavalia vivyo hivyo. Ukiacha hao wawili wanajeshi wa kiafrika kulikuwa na mzungu mmoja mwembaba mrefu aliyevalia suruali ya kijivu, shati la buluu na tai ndefu iliyokifikia kitovu chake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo wewe unaniamissha kuwa mnaweza kunifadhili silaha ambazo zitakidhi mahitaji? Maana ninahitaji kuuvamia mkoa mwiongine ambao una madini kama haya, na huko kote ninahitaji silaha za kutosha na za kisasa,” Yule mwanajeshi aliyechafuka kwa vyeo akamwuliza mzungu Yule, huyu alikuwa Kanali Bensoir banginyana.
“Bila shaka! Na kwa kukuonesha majaribio bosi wangu atakupatia silaha ambazo utaziona mwenyewe ubora wake,” Yule mzungu akajibu.
“Ha! Ha! Ha! Usinichekeshe we’ mtu mweupe, hapa nina mzigo mkubwa wa silaha utashuka hapa ndani ya saa tano zijazo kwani roli zilizobeba zimeshavuka mpaka. Sasa hizo zako utaniletea lini niuone huo ubora wake?” banginyana akauliza.
“Ukikubali tu nitapiga simu na mzigo utafika hapa mara moja hata kabla ya hizo saa tano unanzozizungumzia,” Yule mzungu akasisitiza kwa lugha ya Kifaransa. Banginyana akamtazama Yule kijana wake mwingine aliyekaa pale juu ya meza na kuongea naye Kiswahili ili Yule mzungu asielewe kinachojadiliwa.
“Tusitegemee mtu mmoja, kumbuka Jirack sasa hivi ana jeraha kubwa, lakini mchanganyo wa teknolojia unaweza kutuletea manufaa katika harakati zetu,” Yule mwanajeshi akajibu hoja ya Banginyana na Kanali huyo akakubaliana na ushauri wa kijana wake aliyebakia kati ya watu wake wa karibu. Akamrudia Yule mzungu na kumwambia alete hizo silaha azione.
Nusu saa ilikuwa chache sana, Land Rover Defender tatu zikaingia kambini hapo zikiwa na vijana wawili kila moja zikaegeshwa mahala pake na wale vijana wakateremka. Banginyana akatoka kutoka katika nile ofisi na kwenda kuzikagua silaha zile, allipojiridhisha na ubora wake baada ya kuona uzito wake akawaamuru vijana wake waziteremshe nao wakafanya hivyo. Kisha akamwonesha alama ya kidole kuashiria kuwa alitaka mzungu huyo amfuate, wakaingia tena ofisini na kuiketi mezani. Banginyana akawaita vijana wake wawili na kuwataka walete sanduku moja kubwa la pesa, wakaleta mawili na kuyabwaga hapo mezani.
“Hizi ni pesa na hizi ni almasi, bosi wako anataka nini?” akamwuliza Yule mzungu.
“Anataka almasi,” akajibu.
“Mpelekee hizi,” akamwonesha box moja la alluminium. Vijana wakalifungua, Yule mzungu akatazama zile almasi lakini hazikuwa zile ambazo alizifikiria.
“Angependa zile za ubora wa juu, hizi za Bagon sio sana,” Yule mzungu akaeleza.
“Sikiliza wewe, Afrika tuna ardhi moja tu, hivyo hata madini yote yanafanana, ziwe za Bagon, Mpumbutu au hata za Mwadui zote ni zilezile tu, chukua hizo umpelekee by the way umetupatia silaha kwa majaribio na sisi tunakupa almasi kama tahadhari,” banginyana akamwambia Yule mzungu huku akisimama na kumpa mkono wa kwaheri, Yule jamaa akasaidiwa lile boksi mpaka garini na kuondoka zake.
***
Joseph Rutashobya au ‘Joru’ kama ambavyo wengi walimwita, alikuwa kimya kabisa na bunduki kinywani nyuma tu ya hema hiyo. Sare ya jeshi aliyoivaa ilikuwa ni ile ya waasi. Alisikiliza kila kilichokuwa kikiongelewa mwanzo mpaka mwisho, akasubiri mahali pale bila kuondoka. Wenzake walipopita walimsalimu kijeshi na kumwacha kijana huyo akiwa bado lindoni. Kati ya ‘nyoka’ waliotumwa kuchunguza na kujua vema eneo hilo alikuwamo kijana huyu ambaye alijulikana nwa mchezo wake wa kubadilisha rangi. Alipofika tu chini ya milima yeye alitembea bila ya wasi akiwa na guo chafu mpaka jirani na kambi hiyo na kumkuta kijana anayehshsbiana nay eye akiwa lindoni pembezoni tu mwa hema hiyo. Kama kawaida alimlaghai kwa kumwomba kuwasha sigara naye akahadaika, ndipo alipompa kichapo cha kimyakimya na kumvua magwanda kabla hajayavaa yeye na kusimama eneo hilo huku Yule marehemu akiwa shimoni.
Ilipofika muda wa kubadilisha zamu aliondoka na kuingia kijana mwingine. Upande mwingine wa kambi kijana mwingine wa jeshi hilo la Umoja wa Mataifa alikuwa katika uchunguzi wake, yeye alijichanganya na wachimbaji waliokuwa wakiingia na kutoka katika mashimo huku wakiwa wamesimamaiwa na askari wenye macho ya kifo. Kwa muda aliyofanya kazi hiyo aliweza kugundua mengi sana, na jioni ilipofika alitoka na kupanda juu yam lima kule ambako wenzake aliwaacha. Joru akishirikiana na kijana huyo ndani ya mavazi ya kijeshi tena jeshi la waasi, waliingia usiku wa manane na kutega mabomu katika magari yote yaliyokuwa katika kambi hiyo, walitega kwenye mahema na kila walipoona panafaa na walipohakikisha wamekamilisha walirudi mafichoni mwao wakisubiri kuanzisha msinambe huo.
“Nawaonea huruma sana, lakini hawana budi kulipa damu za wenzetu,” Kiongozi wa kikosi aliongea kwa sauti ndogo lakini iliyosikika na wote katika vifaa maalumu vya kusikiliza.
“Sasa na tuteremke pamoja kwenda chini na wale walioteuliwa kubaki juu wafanye hivyo,” akatoa amri na wale wapiganaje kwa umahiri wa hali ya juu walianza kuteremka kuikabili kambi ile.
SHAMBA
KIKAO KIZITO KILIKUWA kikiendelea katika jumba hilo ambalo lilitumiwa na idara hiyo ya TSA, lilikuwa jumba pweke katika viunga vya Gezaulole, moja ya majumba ya kale ambayo yalikarabatiwa na kuendesha shughuli hizo za siri au kwa jina linguine ailiita ‘Safe House’.
Sauti ya makofi ilisikika, kutoka katika moja ya chumba kilichopo katika jumba hilo, makofi yale yalikuwa ni kumpongeza Gina kwa kutimiza miaka thelathini na nne. Hafla hiyo ilichukua dakika thelathini tu kisha mambo mengine yakaendelea.
“Sikutegemea kama nitakuwa nanyi tena, kwa kweli safari hii wale wadude walinibana lakini mimi ni mimi tu,” Kamanda Amata alieleza jopo la TSA lililokuwa kimya likisikiliza habari hiyo, “Scoba amefanya kazi sana kuniondoa kwa kuwa ilifika kipindi sijui na kwa hasira nilizokuwa nazo namshukuru Chiba kwa bomu alilonitengenezea safari hii ambalo lililkuwa katika kisigino cha kiatu…”
“Ukaharibu nyumba ya watu kama kawaida!” Madam S akamkatisha.
“Siyo nyumba, sema jumba nisingeriharibu lakini wale jamaa walinata kuniharibu korodani zangu, ulitegemea nifanye nini,” akaendelea.
“Sasa Jirack amekufa? Na je una uhakika kabisa kwa mba yeye ndiye aliyekuwa akisambaza hizo silaha kwa waasi?” Madam alouliza huku wengine wote wakiwa kimya kabisa.
“Bila shaka Madam S, Yule bwana ana wenzake saba, jumla yao wapo nane ndiyo wanaosababisha mapigano na vita huku Afrika. Kuna watu huko Ulaya na Amaerika Madam, hawana utu, wanatengeza masilaha mazitomazito wanayaleta huku tuendelee kuuana mi sijui Afrika tutaamka lini katika usingizi huu mzito,” Amata alieleza.
“Kwa macho yangu, na hizi ni picha za Bensoir Banginyana akiwa katika mazungumzo ya mapeano hayo ya silaha, waliponigundu wakataka kuniua lakini mi nakaua mmoja wao, najua sasa wan hasira na wanatamani kunila nyama ila nikawatoroka,” akaendelea.
“Amata, unajua nilikutuma kazi ile kwa siri sana na nashukuru kwa majibu yako, sasa hapo Chiba unaweza kuona kile ambacho tulikuwa tunakihisi tangu mwanzo, na sasa bila shaka tunapata jibu la kuwa waasi wa X65 ni watu kutoka Nduruta kama si wao wametoka hukoi basi kiongozi wao Banginyana ametoka huko na anafuata amri za Rais Sebutunva. Chiba kumbuka katika utafiti wako uligundua nini juu ya kiumbe huyu…” Madam akaongea kwa uchungu na kuwatazama vijana wake. Chiba akaeleza kwa kifupi juu ya tafiti yake katika mitandao ya usalama aliyokuwa akijaribu kuingia hasa kumtafiti huyo Banginyana na wote wakaafiki kuwa huyu ni kibaraka.
“Tumezika vijana wetu leo, na huko wamebaki najua wazi kichapo watakachoshusha kule niu heavy, tusubiri. Banginyana alitoroka katika shambulio la kwanza lakini kama litatokea la pili sidhani, labda maana hata Idd Amain alitoroka mwishoni,” Madam akamalizia.
“Ok, sasa tuendelee na mipango ya awamu ya pili katika kazi yetu ambayo Ikulu imetukabidhi tuone tunaifanya vipi, kumbuke First Lady hajulikani alipo mpaka sasa, hai au mfu hatujui,”….
Madam S alifunga hoja hiyo akaanzisha nyingine ambayo ni mwendelezo wa ileile, “Nilipoitwa na Mheshimiwa Rais, kwanza alikuulizia Amata,” akaendelea kusema, “Lakini kwa kuwa hatukujua huko uliko unarudi lini, Gina alivaa viatu vyako japo bado alikuwa hajakutana na kashkash zozote…”
“Vizuri sana inabidi aendelee ili akutane nazo kwanza kwa kuwa mimi nina kazi nyingione Madam,” Amata akasema.
“Kazi nyingine kazi gani? Hapa ndo tunapanga kazi sasa wewe una kazi gani nyingine? Usitake kuniudhi Amata,” Madam S akang’aka.
“Sikuudhi ila hii shughuli ya sasa Madam, tuna kibarua kizito, ina pande tatu tofauti, tukiwa kwenye ndege tulitumiwa mtu wa kutuua…”
“What??” sauti za watu wawili zikagongana, madam na Gina.
“Ee tulitumiwa mtu wa kutuua lakini bahati mbaya akafa yeye,” Amata akaeleza.
“Amata umefanya mauaji kwenye ndege, motto umenishinda wewe, hujui kuwa unaweza kusababisha ajali angani kwa kuwavuruga watu kwa mapigano yenu?” akang’aka huku akuliza.
“Madam, mi sio motto, hakuna aliyejua mle ndani kama mtu huyo amekufa maana kafa taratibu tena kwa starehe sana,” akaeleza huku akitabasamu, “Sasa nataka nifanye uchunguzi nijue huyu ni nani, nani alimtuma, na kama kuna uhusiano na upande huu tunaoutuhumu kwa mengi, kadiri ya pasipoti yake huyu anaitwa Rajan Kadah, sasa sijui kama hili jina ni laukweli au siyo,” Amata akatoa ile pasipoti na kuiweka mezani, akatoa na kitambulisho kingine kisha akaweka pia”.
Madam S akaichukua ile pasipoti na kuitazama kwa makini, akaigeuza geuza na kuichambua nchi zote alizotembelea mtu huyo.
“Aliwahi kutembelea Tanzania,” akasema huku akiifunga na kuiweka mezani.
“Ndiyo nataka kujua alikuja kufanya nini na nani, maana ukiangalia hapo alikuja miezi mitatu tu ilopita, hiyo ndiyo kazi nilikwambia Madam, nipe nafasi kisha yote tutayona kama yanaendana,” Amata akaongea huku akigongagonga meza ile kwa ngumi hafifu,” Amata akaongea.
“Isitoshe, kazi ya Ujerumani na tukio hili vinaoana, so, inawezekana ama kuna wenzao hapa Tanzania au kule Ujerumani au wapi, ndiyo kazi ambayo kamanda lazima animalize name nitimize jukumu langu,” Scoba alijazia. Chiba alirefusha mkono na kuchukua kile kitambulisho kwa ncha za vidole vyake akakiweka juu ya scanner kubwa ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzitambua alama mbalimbali za watu tofauti, akakilaza juu ya kioo hicho na mara hiyo kukatokea mwali Fulani uliokiangaza pale kilipo, akainua na kukigeuza tena ule mwanga ukafanya vile vile, akasubiri kidogo, usawa wa kile kitambulisho kukajichora kitu kama boksi la mstatili na kuweka mstari mrefu sana mpaka kwenye neno, identify! Akagusa kwenye neno hilo na juu ya kioo hicho kukaonekana alama za vidole zilizoshika kitambulisho kile. Katika kijiluninga kidogo, akaingiza jina lile ‘Rajan Kadah’ na kuliamuru kielektroniki kujieleza, kila alipojaribu iligoma kwa kuwa halikuoana kati ya alama za vidole na lile jina, alipoiruhusu ijieleze yenyewe kuwa ni nani mwenye alama hizo za vidole ilieleza kuwa ni Kalmat Kaslan, mzaliwa wa Khazakhistan na picha yake ikaja pale juu, hakika alikuwa ni yuleyule ambaye Amata alipambana naye kule ndegeni. Baada ya kujiridhisha na kila ambacho Chiba alikipata kwa mtandao wao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa Rajan ni nani?” Gina akadakiza swali wakati Chiba akiendele kucheza na mashine hiyo inayoweza kutambua alama mbaimbali za binadamu na kudadavua ni nani na wapi alipo kutokana na maelezo mbalimbali tunayoyajaza kwenye fomu ama za kuzasajili simu au za kuomba akaunti za benki na kadhalika. Mashine iliorodhesha watu wengi wenye jina la Rajan Kadah tena asilimia kubwa walikuwa Wahindi. Madam S akamtazama Amata na Scoba.
“Sasa yupi mlipambana naye?” akauliza na Amata akaonesha ile picha ya Kalmat, “Sasa Chiba naomba huyu jamaa kalmat ajulikane anafanyia mtandao gani wa kigaidi duniani ili tuanze kazi hii mara moja,” akatoa amri na Chiba kama kawaida yake akafunga ule mtambo na kuwasha kompyuta kubwa ambayo daima huweza kuingia kwenye mtandao wa idara yoyote ya usalama duniani kwa kutengeneza codes namba ambazo humwezesha hilo.
Baada ya hapo tafutishi za Chiba na Gina juu ya uvamizi wa Ikulu zikawekwa mezani na Amata alikuwa akisikiliza kwa makini sana kila hatua ya maelezo hayo na alipoona pana shaka akawasimamisha na kuuliza kwa makini.
“Samahani hapo! Naweza kuona kama una picha ya hiyo soili ya kiatu uliyoiona hapo ukutani?” akauliza na Gina akampatia zile picha, Amata akaziangalia kwa makini sana kisha akatikisa kichwa, “Aina hii ya buti hutumika sana Huzbekhstan,” Kamanda akaeleza huku akishusha ile picha.
“Umejuaje Kamanda?” Madam akauliza kwa mashaka.
“Unajua Madam, kila jeshi lina aina ya buti wanazotumia, sasa zile nchi zinazotegemea misaada kama yetu huwa tunatumia aina ya buti za nchi fadhili. Sasa aina hii itazame soli yake, hii soli ni ya Russia, na buti za Russia mara nyingi utawakuta nazo majeshi ya Pakistan, Huzbekhistan, Khazakistan huko sasa, kwa hiyo mtazamo wetu wa kwanza kama hawa ni magaidi basi wametokea pande hizo, mshale wa kwanza tupige huko, sasa katika maelezo ya hiyo picha ya Kalmat huyu jamaa ni mzaliwa wa Khazakhisatan, sasa unaweza kuona uhusiano wa kwanza, sasa tuangalie muunganiko wake na hawa waliovamia Ikulu uko vipi,” Amata akaeleza na kisha kuketi sawia kitini huku akiinua bilauri yake iliyojaa mvinyo na kupiga mafunda kadhaa.
Madam S akatikisa kichwa kisha akamtazama Amata, “Laiti ungekuwapo, First Lady angeshapatikana,” akamwambia.
“Hata sasa hatujachelewa…” akamalizia na kuruhusu Gina aendelee kusoma ile tafutishi yao ambayo Chiba aliiweka katika maelezo ndani ya tovuti ya TSA, tovuti siri ambayo ilikuwa miongoni mwa watu sita tu haikuunganishwa kwenye mtandao wa kimataifa yaani Wide Area Network ila huu ulikuwa ndani ya Local Area network na Chiba alitengeneza neno au namba fungushi zilizomwezesha mtu yeyote kati ya hao sita kuweza kuingia na kuweka tafutishi zake juu ya jambo fulani. Baada ya maelezo mengine marefu kutoka kwa Gina Amata akasimamisha tena maelezo na kutaka ufafanuzi.
“Nina wasiwasi hapo juu ya huo mfumo wa kamera za usalama wa Ikulu, gaidi au mvamizi atajuaje picha ya eneo lile hata aweze kuilaghai kamera na mtandao mzima wa usalama kupata picha hiyo ya uongo? Hii ni mpya, ninavyojua mimi vitu hivi vyote hulishwa ndani ya kadi maalum, kama kwenye kamera kuna kadi ambayo inahifadhi matukio achilia mbali zile mashine kule ndani, basin a wao walikuja na kadi yao ambayo imelishwa tayari picha za eneo hilo, Chioba kagundua hilo sawa kabisa lakini mi naongeza, mtu wa ufundi wa zile kamera anayehusika na kuzifanyia maintenance akamatwe,” akawaeleza na wote wakatikisa vichwa.
“Sikufikiria hilo,” Madam akasema.
“Hata mimi!” Gina akadakiza na wote wakakili hilo.
“Mi ndiyo kazi yangu jamanai mnafikili kule Cuba nilikwenda kucheza au Langley nilikwenda kutalii, nilikwenda kujifunza intelijensi nah ii ndiyo intelijensia, wewe ukisema A ipo hivi mi kichwani nitakwambia A haiwezi kuwa A pasipo kinywa na ulimi…” aliposema hayo wote wakacheka, Gina akaandika kwenye karatasi yake mtuhumiwa wa kwanza huyo fundi wa hizo kamera. Mjadala ukaendelea na mazungumzo marefu yakaja juu ya Yule mzee aliyekuwa akibishana na Chiba.
“Umesema ni mtu wa usalama? Yukoje? Kwa sababu unapoona mtu anakukatalia jambo jua kuwa kuna kitu anafahamu sasa hataki wewe ujue, huyu ni mtu wa pili, Madam, huyu naye achunguzwe kama Chiba alivyoihofu name akili yangu inamtazama yeye,” Amata alieleza, sasa alionekana kuongea kwa ukali zaidi. Baada ya maelezo yale kumalizika na mipango kuwekwa sawa sasa ukaja uamuzi wa mwisho.
“Nafikiri tumepata picha na tumejua pa kuanzia, asante Kamanda kwa uwepo wako, yaani Jirak angekuua ningemla nyama…”
“Na nilimwambi kuwa ungeenda kumnasa vibao…” kamanda akamkatisha Madam S kwa maneno yake ya utani.
“Ok, sasa ipo hivi, Gina unajua wajibu wako sijabadilisha, ila Kamanda fanya unaloona linafaa kwa sasa, Scoba utakuwa na mimi kuna kazi maalum leo, naomba tukutane ofisi ndogo kesho saa kumi n ambili jioni, asanteni na kwaherini,” Madam akamaliza kikao hicho na kila mtu akainuka tayari kwa kazi.
MPUMBUTU
USIKU WA SAA NANE waasi wote walikutana katika uwanja mdogo na kiongozi wao Kanali Bensoir Banginyana alijitokeza kati yao na wote wakaanza kupiga makofi na kuimba nyimbo za kijeshi za kusifia kundi lao na kumtukuza kiongozi wao huku wakimpa sifa za kutosha Mkuu wa Wakuu yaani Rais wa Nduruta.
“Nimewaamsha usiku huu makusudi, nyote mnajua kuwa hapa tulipo tunawindwa na majeshi ya Tanzania yakiwa chini ya mwamvuli wa UN. Hatuyaogopi na nasema tena hatuyaogopi na tutayasambaratisha kama yale mengine yaliyokuja hapa. Sisi ni wanyama wabaya kuliko wanyama wenyewe,” alipotamka hayo wale waasi wakashangilia na kupiga risasi hewani kisha wakanyamaza.
“Nawaambia hivi kwa sababu, juu hapo ya milima majeshi hayo ya adui yamezunguka hivyo sasa ni kwenda kuwasambaratisha, wanajifanya wajanja kumbe sisi ni wajanja zaidi, mafunzo mliyopewa na wale jamaa wa Khazakhistan myatumie vyema, tunatoka sasa kwenda kufagia, kama jana wamezika watano basi wiki iajyo wazike mia tano, na tuna silaha mpya kabisa kutoka Bolivia, na tuzitumie ili zijue kuwa zimeletwa zifanye kazi na si kutembeatembea migongoni na mikononi ka za Wartanzania,” kisha akachukua bastola yake na kupiga hewani mara tatu akiashiri sasa kila mmoja aanze kazi ya kusaka adui.
Juu ya milima ile vikosi vya UN vilitulia kimya kabisa kana kwamba hakukuwa na kiumbe katika msitu huo, walikuwa wakisikia hotuba yotye kupitia chombo cha Joru ambaye alikuwa katikati ya waasi hao nay eye ndiye alikuwa kiongozi wa kuanzisha mashangilio.
Joru katikati ya waasi aliikoki bundui yake kubwa tayari kuungana na waasi hao kulishambulia jeshi lake, mfukoni mwake alikuwa na chombo kidogo ambacho kiliunganisha mabomu yote yaliyotegwa kwenye yale magari, alisubiri amri tu ya kamanda wake ili afanye kazi hiyo kwa sekunde moja.
“Joru, Joru!” sauti ikaita kwenye kifaa chake kidogo alichokipachika sikioni.
“Nakupata kiongozi,” akajibu.
“Toa mkono kwenye sikio haraka, toa!!” Yule kiongozi akamkaripia Joru kwa kuwa alijua kwa kuweka kidole chake sikioni wangemgundua kuwa alikuwa katika mawasiliano na mtu mwingine.
“Unasemaje mkuu sikusikii vyema…”
“Hey, Stop, hapo ulipo simama!” sauti ikatokea nyuma yake, Joru akahisi ganzi kwani waasi wawili walikuwa wakimfuata pale alipo.
“Unaongea na nani?” mmoja akauliza kwa sauti kavu, wakamfikia na kumvua kofia.
“Ha! Bonsoli umeiona hii kofia, huyu ni nyoka, auawe!” mmoja wa wale waasi akmwambia mwenzake mara baada ya kuichukua ile kofi nyekundu lakini alipoigeuza kwa ndani ilikuwa ya buluu bahari na nembo ya majesji ya UN. Joru alipigwa konde zito, akapigwa ngwara akaanguka chini kwenye tope.
“Msaliti mkubwa, peleka kwa Banginyana akamshughulikie,” mwingine akatoa amri, Joru akainuliwa na kupewa kichapo kikali kisha akapelekwa hemani.
HOTELI-NEW AFRIKA DAR ES SALAAM
USIKU UOHUO
KUBRA KHALEB aliegesha gari nje ya hoteli hiyo na kuteremka, moja kwa moja aliingia na kupanda lifti mpaka ghorofa ya juu aliyokuwa akiitaka, akaingia na kukutana na mwenyeji wake Bwana Briston Kalangila, ndani ya chumba kilekile namba 806.
“Yes Khaleb, unaonekana leo hauna raha vipi?” akauliza.
“Jaribio limefeli, Kalmat ameuawa,” Khaleb akamwambia Briston.
“What! Hii sasa balaa, Kalmat muuaji hatari aliyeshindikanika kote tulikomtumia, lo!” Briston alisikitika, “Ni nani huyu mshenzi? Nahitaji nikutane nae uso kwa uso nimjue,” akalalam huku kijasho cha kwapa kikimchurizika.
“Mbona nasikia ni mtu wenu wa usalama huko huko?” Khaleb akauliza.
“Hapana, simjui huyo, mimi ninajua watu wote wa usalama nchi hii na nimewaweka wakuu wote wa idara za miko na wilaya, lakini huyu mtu hapana labda kama yuko MI,” akajibu.
“Hapana, hayuko MI, huyu ni TSA,” Kheleb aktoa maelekezo.
“TSA?” Briston akauliza, “Hiyo idara mii siijui hakika,”
“Basi kama ni hivyo bado hujaweka mikononi idara zote, huyu jamaa ni mtu wenu, na ninahitaji kumuua kwa mkono wangu maaha kwa upiganaji huyu atakuwa ni shida, kumbuka Kalmat ni mpiganaji mzuri sana lakini kauawa,” Khaleb akaeleza.
“Ok nimekuelewa, nitapeleleza ili nimjue kisha nitakupa mbinu za kumtia mkononi, hilo niachie mimi tuonane hapa hapa kesho muda kama huu, kama kuna taarifa nyingine tutapeana taarifa…
Kubrah Khaleb aliteremka ngazi za hoteli hiyo na kutoka nje kabisa ya jingo hilo aliingia ndani ya gari yake na kuketi nyuma ya usukani, akaiwasha na kuondoka eneo hilo huku akili yake ikiwa inakimbia mara mbili kuliko kawaida. Kichwani mwake alimfikiria huyo adui aliyemuulia swahiba wake kama ndugu yake, alitamani kama aonane naye muda huohuo ili amchakaze ikiwezekana, lakini haikuwa hivyo kwani alichokuwa anakutana nacho ni madaladala tu na watu wenye shughuli zao nyingine kabisa. Akaendelea kuifuata barabara ya Azikiwe mpaka maktaba na kukunja kona kulia na kuifuata barabar ya Bibi Titi, alipofika makutano ya Barabara tatu; ya Bibi Titi, Ohio na Ally Hassan Mwinyi, taa zilimuamuru kusimama, akatii na gari yake ilikuwa ya kwanza kabisa. Kichwa chake kilikuwa kikiwaza mengi hata taa ziliporuhusu hakuwa na habari.
“Piii piiiiih!!! Piiiiii” honi za gari za nyuma zilimshtua Kubra akakanyaga krachi na kuingiza gia namba moja kisha akaachia krachi taratibu na kukandamiza kwa mguu wake ile akselereta mara tu baada ya kushusha breki ya mkono, ile Land Cruiser ikafuata barabara ya Ally Hassan Mwinyi kwa mwendo wa kasi. Kubrah akainua simu yake na kubofya kitufe kimoja tu kisha akaiweka sikioni.
“…naomba tuonane jengini mara moja na haraka!” akasema hayo tu na kukata simu, akairudisha kwenye kidroo chake na kutoa gia namba tatu na kuweka nyingine. Dakika kumi baadaye alikuwa akikunja kona kulia kuelekea Slip way, nayo ilimchukua mpka amitaa ya Masaki, akakaunja kulia na kupiga honi kwenye moja ya majengo mapya yaliyokuwa yakiendelea kujengwa katika eneo hilo. Mlinzi wa kimasai akafungua na ile gari ikapita moja kwa moja mpka mwisho wa barabara ile, ikaingizwa chini ya jengo hilo na kuegeshwa. Punde si punde gari nyingine nne ziliingia eneo hilohilo na kusimama pembeni yake tu. Vijana wane tofauti wakateremka na kumzunguka Kubrah huku mikono yao ikiwa imeshikamanishwa vifuni mwao.
“Wote mmekuja?” akauliza huku akiwaangalia mmoja baada ya mwingine, “Nisikilizeni kwa makini, mwenzetu, ndugu yetu, kijana wetu, mpigania uhuru mwenzetu, ameuawa kwenye ndege, nataka aliyeua auawe, sina masihara hata kidogo,” akawaambia. Wale jamaa walibaki kimya wakimwangalia tu huku giza la eneo hilo chini ya jingo lisilokwisha ambalo bado liko matengezoni likiwapa shida kidogo kuonana.
“Sasa tutampata wapi huyo mtu na hatumjui?” mmoja aliuliza.
“Dakika chache baadae nitawatumia picha na mahali ambapo huyu jamaa hupenda kuonekana,” akawajibu.
“Kiongozi, na yule Malkia kule amegoma kula kabisa,” mwingine akaeleza.
“What? Anakataa kula? Mwacheni afe kwa njaa kwani si tuna undugu gani naye?”
***
Ndani ya wigo wa Ikulu, Scoba aliegesha gari yake katika amegesho yake na kuzima injini. Kamanda Amata akateremka akifuatana na Madam S, moja kwa moja wakazipanda ngazi za jingo hilo na kupokelewa na Othman, afisa Usalama wa taifa anayefanya kazi karibu kabisa na Rais, moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba ambacho walikuwa wakisubiriwa.
“Yule uliyemwulizia huyu hapa!” Madam akamwambia Rais.
“Kijana kwanza nafurahi umerudi, hapa kuna shida ngumu kutatuka kama ulivyokwisha aambiwa, nataka ufanye kazi tupate ufumbuzi haraka,” akaelezwa.
“Mheshimiwa Rais, tayari niko hatua kadhaa mbele na nakuhakikishia ndani ya saa arobaini na nane First Lady atakuwa hapa bila hata mkwaruzo wa kalamu. Lakini kuna mambo ambayo ningependa kujua kutoka kwako…”
“Sawa, sawa kijana uliza tu nitakujibu yote, ninachotaka mimi ni utatuzi wa jambo hili,” Rais akakubaliana na Amata huku Madam S akitikisa kichwa kuafikia hilo.
“Kwa nini hukwenda na mkeo katika ziara yako? Kwa maana tumezoea kuona hilo kila mara,” Amata akauliza huku kwa siri akiwa kaiwasha zimu yake na ilikuwa ikirekodi kila kitu ijapokuwa ndani ya chumba kile hakukutakiwa kurekodi kitu chochote wala kupiga picha.
“Safari hii yeye alikuwa ana mkutano na vongozi wa asasi ziziso za kiserikali, hivyo nikmwacha,” akajibu.
“Nani aliandaa mkutano huo na lini uliandaliwa?” akazidi kuchimba.
“Aaaaa huu mkutano haukuandaliwa muda mrefu ni kama wiki tatu zilizopita, that is why nikamwacha ili ashughulike na hilo lakini baada ya mkutano ule usiku wake ndiyo hayo yakatokea,” akaeleza huku akianza kusikitika.
Ukimya ukapita kati yao, hakuna aliyeongea kwa nukta kadhaa, kisha Amata akajikohoza tena na kuuvunja ukimya ule.
“Sasa Mheshimiwa, huoni kwamba aliyeandaa mkutano huo alikuwa amekula njama? Kwa nini aandae wiki tatu hizi ilhali ulikuwa na ziara ambayo ilikupasa kuondoka na mkeo?” swali hili lilimgutusha mheshimiwa.
“Unasema!” akatamka kwa mshangao.
Kamanda Amata akarudia sentensi yake ambayo iliiingia sawasawa katika masikio ya wawili hao yaani Mheshimiwa Rais na Madam S. Hali ya Mheshimiwa Rais ilikuwa kama inabadilika na kuonekana akipumua kwa nguvu.
“Hivi hili swalama linawezekana eti?” akauliza.
“Hapana, mi nilikuwa nauliza tu. Lakini mkuu labda kuna kundi unalolihisi katika hi….”
“Enheeee hapo hapo kijana umenikumbusha, nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakinitaka nisichukue hatua yoyote juu ya swala hili, ila nikitaka nimpate tena mke wangu basi niyaamuru majeshi ya Tanzania chini ya UN yarudi nyumbani,” Rais alimkatisha Amata na taarifa hiyo ilimvutia zaidi Amata na akajiweka vyema kitini.
“Unaweza kukumbuka ilipigwa lini?” akauliza.
“Siku ileile niliporudi, ndiyo nilipokea simu hiyo,” akaeleza.
“Na simu ipi kati ya hizi mezani iliyopigwa?” akauliza Amata na Mheshimiwa Rais akaonesha mara moja ni simu ipi siku hiyo ilipigwa, Hii simu imeunganishwa kutoka nje? Akajiuliza Amata, “Naomba fundi wangu aje kuichunguza kama inatoka nje au la, tukishajua hilo tu kazi imekwisha,” akaongeza kusema huku akiinua simu yake na kumpigia Chiba, akamwita afike hapo mara moja. Wakati wakimsubiri waliendelea kuongea ya hapa na pale hasa maendelea ya operesheni ile ya kijeshi inayoendelea huko Ngoko. Haikupita hata dakika kumi na tano Chiba alifikiswah katika ofisi hiyo na Yule afisa wa usalama, Othman.
“Chiba, naomba unitazamie hii simu kama laini yake inatoka nje ya hili jingo au la, hilo tu” Amata akamwambia Chiba naye mara moja akaanza kuifuatilia ile laini kuanzi pale na baada ya dakika tano alirudi na jibu kuwa laini ile ya simu ipo kwenye mfumo wa simu za ndani ‘Internal Telephone System’ ambayo simu zake upigwa toka ofisi moja kwenda nyingine ndani ya jingo moja na sin je ya hapo ingawaje unaweza kupiga au kupokea kutoka nje endapo una namba maalum ya kufanya hivyo. Kwa hiyo ina maana simu hii ilipigwa kutoka humuhumu ndani au? Amata alijiuliza.
“Chiba! Ina maana katika mfumo huu haiwezekani simu kutoka nje ikaingia?” aliuliza swalinhilo Amata baada ya Mheshimiwa Rais kuwaelekeza simu zote zilizokuwa mezani kuwa ipi anapokelea simu za mtindo gani.
“Inawezekana kwa sababu huu mfumo uziunganisha simu zote za ndani katika swichi moja inayoitwa PBX. Sasa kama unataka kupiga simu nje ya jingo hili kwa kutumia simu hii kuna namba maalumu unayoitanguliza kisha unapiga namba uitakayo na signal ile itafika kwenye swichi ya PBX kisha hiyo swichi itaitambua kuwa hiyo simu inatakiwa kutoka nje hivyo itakuunganisha na kitu kinaitwa PSTN yaani Public Switched Telephone Network nayo itafanya kazi ya kukuunganisha na unayemtaka, lakini si kila mtu anajua namba za utangulizi yaani jinsi ya kupiga kwenda nje, kwa sababu hii siri hukaa na System Administrator na wachache wanaoaminika kwa kazi maalum,” Chiba akadadavua na kuwaacha hao watatu vinywa wazi huku Mheshimiwa Rais akiwa haamini kila anachosikia.
“Kijana, unataka kuniambia kuwa hiyo simu itakuwa imepigwa kutoka humu ndani?” Rais akauliza kwa shauku.
“Siyo hivyo Mheshimiwa, simu inaweza kupigwa kutoka nje ya jingo hata Amerika na ikaingia katika mfumo huu, ina maana mtu atakuwa anajua anyempigia ni nani,” akamalizia huku akifunga kijimkoba chake. Kwa mara ya kwanza tangu wafike hapo Madam S alifungua kinywa chake.
“Chiba, nataka rekodi ya simu zote za siku ile aliporudi Mheshimiwa zilizopigwa kwenye namba hii, hii ni 603,” akamwambia.
“Sawa hakuna tabu nina uhakika itapatikana tu japo si kazi rahisi sana,” Chiba alieleza na kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, wakaagana na Mheshimiwa ili wao waendelee na kazi nyingine. Wakatoka wote watatu kayika ofisi ile nyeti, Madam S akaingia katika ofisi nyingine huku Chiba na Amata nao wakielekea kwenye ofisi ya watu wa mawasiliano, pale wakamkuta kijana mmoja mtaalamu wa Tehama akifanya hili na lile katika kompyuta zake, huku akirekodi miito yote ya simu inayoingia na sauti za kila kinachofayika hata kama siyo simu. Kwa kuaminiwa kwake, alikuwa ni yeye tu mwenye funguo za kabati ambalo kumbukumbu zile hubakia na eneo ambalo server imehifadhiwa. Walipofika wakaonesha vitambulisho halisi vya kazi na kibali walichopewa kufanya hayo yote.
Chiba akaomba kuona miito ya siku hiyo ambayo Mheshimiwa Rais aliwasili Ikulu, lakini hakutaka kuona au kusikia iliyorekodiwa, ila alihitaji kuchambua kutoka katika kompyuta kile ambacho kiliingia, Yule kijana akisaidiana na Chiba waliweza kufikia codes za miito ya siku hiyo, Chiba akaipakua na kuihifadhi katika chombo chake maalum.
“Hivi miito inayoenda Kilimanjaro Square huwa inajirekodi au la?” Chiba akamwuliza Yule kijana.
“Ndiyo ila imefungwa kwa namba maalum ambazo bila hizo huwezi kuipata, na namba hizo wanazo watu watatu tu, hata mi sina kwani pale ndiyo mambo nyeti ya Mkuu huzungumzwa au hupangwa pale,” Yule kijana akajibu. Chiba akaitazama ile media yake mkononi ambayo alikuwa amechukua zile namba za code.
“Ok, nahitaji kuzipata kama mwana usalama kwa kuwa tupo kwenye uchunguzi wa tukio hilo la uvamizi,” Chiba akaeleza na Amata akatikisa kichwa. Yule kijanaakainua simu na kupiga mahala Fulani na dakika mbili tu aliingia bwana mmoja mwenye kitambi cha wastani, lakini mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi na tambo lake lilimruhusu kuitwa giant. Yule kijana akaeleza vyema shida ya Chiba na Amata. Na Yule mtu akawatazama kwa makini sana, Chiba alimtambua mtu huyu mara moja kuwa ni Yule waliyobishana naye sana jana yake.
“Halafu wewe jana si ulikuja hapa? Nilikujibu nini?” akamwambia Chiba, Amata akawa akimwangalia mtu huyo bila usema neno.
“Tekeleza ninalotaka, niko hapa kwa amri ya Rais na siyo wewe, ingiza hizo namba hapo haraka watu tupo kazini,” Chiba akaunguruma na Yule bwana akasonya.
“Sasa hii nyie itawasaidia nini?” akawaambia huku akiingiza zile namba na lile faili ikafunguka, lilikuwa na michoro tu ajabu ajabu, Chiba akaipakua na kuweka kwenye chombo chake kisha akaaga na kuondoka. Amata alimtazama kwa makini sana Yule jamaa, akili yake ikakimbia huku na kule akamweka alama.
KAMBI YA WAASI – MPUMBUTU
JORU ALIFIKISHWA katika hema ya Banginyana, na kumkuta kiongozai huyo akiwa bado analizia mtemba wake alioubana vyema kinywani mwake.
“Huyu naye ni nani?” akuliza huku akiwa ameketi juu ya kiti na miguu yake kaitundika juu ya maeza kama kawaida. Wale askari waasi hawakujibu wakamvua Joru koti la juu la jeshi lao na ndani yake alikuwa na kombati ya jeshi la Tanzania.
“Anhaaaa, ha! Ha! Ha! Naona sasa mnamtafuta nyoka miguu, unajifanya jasusi wewe, tena nakukumbuka hata kule kijijini ni wewe ulikamatwa vivi hivi, leo huponi, mtieni adabu kwanza,” akaamuru. Joru alishikwa huku na huku na kupokea makonde mazito, mateke na mkong’oto wa aina mbalimbali, akawa hoi alipoachiwa akaanguka chini na ile swichi ya kufyatulia mabomu ikamtoa mfukoni mwake na kutu chini. Kanali Bensoir Banginyana akaiona ikiwa pale chini, macho yakamtoka pima.
“Mshenzi wewe! Yaani hii swichi ulitaka kutulipua? Ina maana … asee, mpigeni mpaka afe kisha waambie watu watafute ili bomu mpaka walipate lilipo,” aliposema hayo akaketi akiwa kalowa jasho katka uso wake, akaiweka ile swichi mezani na kuendelea kunyonya mtemba wake.
Joru alijua asipojiokoa basi itakuwa ndiyo mwisho wake kwani wenzake bado walikuwa kimywa huko nje na alishuhudia waasi wakiwa tayari wameanza msako juu ya adui zao kwa minajiri ya kuua kila wanapowakuta. Yule muasi wa mbele alirusha ngumi na Joru akainama ile ngumi ikaufikia uso wa jamaa wa nyuma akamwacha Joru na kuanguka kando. Joru alijitutumua na kuzuia teke kali kutoka kwa mwingine huku akimshuhudia Banginyana akinyanyuka na bastola mkononi, Joru aliruka hewani na kupiaga mateke mfululizo yaliyowatawanya wale jamaa huku risasi za Banginyana zikitoboia hema na kusababisha mtafaruku mkubwa. Joru alipotua moja kwa moja aliikanyaga ile swichi pale juu ya meza na kujirusha sama soti akatoka nje ya hema.
Milipuko mizito ikasikika huko nje, magari yalilipuka yakifuatiwa na mahema ya waasi, kizaazaa. Waasi wengi waliumia vibaya na milipuko hiyo iliyozunguka karibu kambi nzima. Banginyana akatahayari kwa hali hiyo, hata hakujua ni wakati gani aliziama au aliitupa sigara yake kubwa. Walinzi wake wakajiandaa umwondosha eneo hilo.
***
Kiongozi wa vikosi vya UN alipohesabu milipuko akajua tayari imemalizika akawaamuru vijana wake wateremke chini sasa ni vita ya ana kwa ana. Kambi ya waasi ilidhibitiwa kwa kipigo kikali kutoka katika kila kona, hawakupata mahala pa kutokea, maana kama ni vyombo vya usafiri vilikwishalipuliwa tayari. Moto ulizagaa huku na huko, askari wa Tanzania chini ya UN walifanya yao na kulidhibiti eneo lote kabisa kila mahala walikuwa wao huku wakiwa wamewakamata mateka kadhaa lakini Banginyana hakupatikana. Hii ilimtia hasira sana kiongozi wa vikosi vya UN.
“Ningemtia mkononi, leo tungepambana ngumi kwa ngumi,” akasema huku akiwa haamini kama kiongozi huyo wa waasi ametoroka tena kwa mara ya pili. Vijana wa JW walitanda kila kona, wakiwa wamekalia kila mahala, sasa eneo hilo lilikuwa lao. Zaidi ya kupata maumizu madogomadogo hakuna aliyepoteza maisha. Joru alijikokota na kujiweka sawa kutoka nkwenye nyasi alizokuwa ameangukia, wakati wa mapambano alijua akisimama tu angekufa hivyo alitulia kimya kama mmoja wa wafu. Akainua mikono na kusimama wima. Askari wa UN walipomwona walimwinulia bunduki zao, na kiongozi wao akawaamuru kushusha.
“Huyo ni Joru,” akawaambia. Joru akasalimiana na kamanda wa kikosi na kuonesha wazi kusikitishwa kwake juuu ya kumkosa Banginyana.
“Wamekimbilia njia hii huku bondeni, kule kuna mto mkubwa sana wa maji,” Joru akaeleza na baadhi ya askari wakateremka huko kumsaka Banginyana kwa udi na uvumba.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipita mapori na mapori lakini hawakumuona Banginyana wala kivuli chake, baada ya mwendo mrefu walisimama, katikati yam situ uliozungukwa na miti na ndege waliokuwa wakiimba nyimbo wazijuazo wao tu.
“Huyu jamaa keishatutoka tena,” mmoja wao akasema huku akiiweka vizuri bunduki yake.
“Ana bahati sana dhidi ya mkono wetu,” mwingine akadakia kisha akawaamuru wenzake kurudi. Joru alibaki kasimama nyuma wakati wenzake wakiondoka wakati wa giza nene.
“Joru twende, achana na huyo Mungu wake anampenda lakini ipo siku,” mwanajeshi mmoja akamwambia Joru naye akageuka na kuondoka mpaka kule walikowaacha wenzake.
Giza lilikuwa likiendelea kufika mwisho wakati vikosi vya JW chini ya UN vikiwa tayari vimekalia eneo lile la waasi huku baadhi yao wakiwa chini ya ulinzi, mateka na wengine wengi zaidi wakiwa tayari hawana uhai. Taarifa ya kumkosa Banginyana ilimsikitisha sana kamanda wa vikosi hivyo ambaye alimpania kwelikweli mtu huyo, alikubali tu afanyeje lakini bado moyo wake haukukata tamaa. Aliwatazama vijana wake waliokuwa tayari wamekaa kwenye kona mbalimbali za eneo lile kuanzi kwenye hema za waasi mpaka kwenye machimbo ya almasi ya Mpumbutu.
“Mnajua …” akawaambia kiongozi wa kikosi, “Banginyana hajakwenda mbali na tukimuwahi tutampata, nina uhakika atakuwa amekimbilia kule kijijini. Joru nakupa ukamanda, chukua vijana kumi na nane mnatosha kwa kazi kahakikisheni kile kijiji nacho kipo katika mikono yetu na si sjsbu huyo Banginyana atakuwa pale…”
“Tukimkuta…” Joru akamkatiza.
“Mnajua cha kufanya, nendeni,” akawaamuru. Joru akachukua vijana kumi na nane pamoja naye wote wakiwa na silaha nzito na kupotelea msituni usiku huo. Kijiji cha Mpumbutu hakikuwa mbali kutoka eneo hilo kama ukipanda na kushuka milima kadhaa ambayo ilivitenganisha kijiji na eneo hilo la machimbo. Mwendo wa saa moja tu ungeweza kuwafikisha kama wasingeizunguka milima hiyo. Kwa ari waliyokuwa nayo hiyo viijana hao walitiana moyo na kutembea kijeshi kufika katika kijiji hicho.
KIJIJI CHA MPUMBUTU
Kikosi kiliingia kijijini saa kumi na moja alfajiri, hali ya kijiji ilikuwa hai hai maana watu walikuwa nje wa,ekusanyana vikundi vikundi hasa baada ya kuona yale mashambulizi ya kule msituni. Akina mama walikusanya watoto wao na kujificha ilhali akina baba walionekana nje wakiweka ulinzi juu ya familia zao. Joru aliwapa ishara wenzake watawanyike kuzunguka eneo hilo, kisha wakateremka kijijini kila mmoja kupitia upande wake. Joru alikuwa wa kwanza kuingia kijijini, wale wanaume waliosimama vikundi walipoona wanajeshi wa UN wameingia pale walitoa ushirikiano kuonesha kila kona ambako waasi mabaki walijificha.
“Kajengo kaleeeee, wapo mle, inawezekana kabisa hata huyo mkubwa wao yupo pale, hawezi kuondoka usiku huu…” mmoja wa wazee alikuwa akimweleza Joru. Joru alilitazama lile jingo, lilikuwa jingo la kawaida ambalo nje yake lilizungukwa na ukuta, pembeni kama mita mia moja hivi kulikuwa na lile jingo waliloliangusha kwa uvamizi wiki moja iliyopita. Joru akawaita vijana wake na kuwapanga tayari kwa uvamizi, kisha akawaomba wale wanakijiji waendde mbali na eneo hilo kwani hawakujua uzito wa mapigano yatakayotokea. Wale wanakijiji wakafanya hivyo na dakika kama kumi na tano hivi utulivu ulichukua nafasi.
Baada ya vijana kujipanga tayari kwa kazi, kiongozi aliyepewa jukumu la operesheni hiyo ndogo akatoa amri ya kuvunjwa nyumba hiyo bila huruma. Mmoja wa vijana aliyekuwa kabeba RPG muda mrefu akaliweka begani sasa tayari kwa kazi. Dole lake la shahada likavuta kifyatulio kwa nyuma na grenade lililochomekwa mbele ya bunduki hilo likafyatuka. Nalo bila kukosea lilitua kwenye ukuta na kuuangusha kipande cha ukuta huo. Askari waliobaki nje tayari na bunduki zao kubwa mikononi waliingia ndani ya wigo ule. Nusu saa ya mabishano ya risasi yalitosha kuwazimishwa waasi wale. Joru alihakikisha usalama wa vijana wake waliokuwa na hasira juu ya visasi vya ndugu zao. Waasi nao japokuwa walikuwa wachache lakini walijua vyema mbinu za mapigano kwani mtafutano haukuwa mdogo. Mapigano yalikuwa ni ya kuviziana ilipooneakana muda unazidi kuyoyoma, Joru aliamuru grenade nyingine ipigwe, ikapigwa na kuangusha kipande kingine, ikapigwa nyingine na kuangusha tena sehemu kubwa ya ya ukuta wake.
“Aaaaaiiighh!” kelele ya Yule jamaa mwenye ile RPG ilisikika, Joru alipogeuka alikuta jamaa katupa ile mashine kajishika goti lake, risasi ilikuwa imevunja mfu[pa wa goti na jamaa alikuwa chini. Mwanajeshi mmoja aliyekuwa na taaluma ya uuguzi aliwahi eneo lile na wakati huohuo askari wawili wakawawekea ulinzi, Joru na waliobaki wakaivamia ile nyumba na kutembeza kipigo kisicho na huruma na kufanikiwa kuwadhibiti waasi wale. Dakika sitini za uongozi wa Joru zilisambaratisha eneo lile lakini Banginyana hakuwapo, baada ya kuwabana na kuwatesa wale waasi wakasema kuwa Kanali huyo alikwishatoroka. Wanakijiji walijitokeza na kushangilia hali hiyo maana waliona sasa wamekomboka kutoka katika mikono ya X65. Vijana wale wa jeshi wakakikalia kijiji kile na wengine zaidi wakaongezeka.
***
Taarifa ya habari kutoka BBC saa kumi na mbili asubuhi ilimkuta Kamanda Amata akiwa bado kitandani. Saa yake ilipomgutusha kumwonesha ni saa kumi na mbili, akachukua rimoti na kuwasha redio kubwa iliyo chumbani mwake.
“…Majeshi ya ukombozi ya Umoja wa Mataifa huko Mpumbutu Kusini mwa nchi ya Ngoko yameisambaratisha ngome ya waasi na kuyakalia maeneo yake, taarifa zinasema kuwa, majeshi hayo yalivamia mahali palipo na machimbo ya almasi usiku wa kuamkia leo na kusambaratisha waasi wote huku wakiteka eneo hilo na kijiji cha Mpumbutu. Wakazi wa eneo hilo wamefurahia zoezi hilo na wamelisifu jeshi hilo kwa hatua waliyoifikia, mwandishi wetu anaripoti….
…..ulikuwa usiku wa manane vikosi vya UN vilipoteremka katika kambi hiyo ya waasi na kuisambaratisha vibaya. Msemaji wa jeshi hilo Luteni Chongo Chongoli amethibitisha juu ya shambulizi hilo na kukiri kuwa kiongozi wa waasi hao Kanali Banginyana hajapatikana, lakini msako unaendelea…..”
Baada ya kumaliza kuripoti habari hiyo zilisikika sauti za wakazi wa Mpumbutu wakishangilia na kulisifu jeshi hilo kwa kuwakomboa dhidi ya X65.
“….Hii mutu hii imetutesa sana, imechukua batoto yetu na kupelekwa kwa jeshi…”
“….ilikuwa inbaka mabinti na wanamuke yetu, tunashukuru UN kwa kukomboa kipande hii…”
“…mengine yalijificha kwa fasi hii na sasa yote imekufa, ilikuwa kumi mbili na tatu…”
Kamanda Amata alisikiliza taarifa ile kwa makini sana, akamtumia ujumbe Madam S kisha akainuka kutoka kitandani na kuwasha televisheni channeli ya Al-Jazeera ambapo aliikuta habari ileile kwa picha.
Banginyana ametoroka tena? Akajiuliza na kutikisa kichwa kisha akasonya kwa hasira na kuingia maliwato kwa minajiri ya kujiandaa kwa kwenda kulijenga taifa.
NDURUTA
KANALI BENSOIR Banginyana aliketi kwa kujiinamia huku wasaidizi wake wawili wakiwa upande huu na upande ule. Dakika hiyohiyo Rais wa Nduruta Mheshimiwa Sebutunva aliingia katika chumba hicho na kuketi kwenye kiti cha mbele yake. Banginyana alisimama na kutoa saluti kisha akaketi tena.
“Nimesikitika sana,” akaanza kusema, “Imekuwaje Banginayana, mimi nakuamini wewe mpiganaji, umefanya mapinduzi hapa hakuna asiyejua weledi wako wa kivita au umezeeka?” akauliza.
“Mkuu wa Wakuu, mbinu waliyotumia wale jamaa kutuvamia hakika imeniacha kinywa wazi, maana tumekuja kushtuka tayari adui yuko ngomeni, na we unajua jeshini tunasema ‘adui mbaya ni yule aliye miongoni mwako’ hatukuwa na ujanja walituwahi kwa pigo moja tu…”
“Unasema?” akadakiza swali.
“Wametupiga kwa pigo moja tu, wamelipua magari na mashine zetu zote za kivita kwa sekunde moja tu, wakati natoa amri ya kuanza kuwasaka ni dakika na sekunde hiyohiyo wakafanya hilo,” banginyana akaeleza.
“Kwanza wamekiuka maagizo tuliyokubaliana ya UN kuwa hawakutakiwa kuwashambuli bali walitakiwa kulinda amani, na hili lazima nilifikishe kwenye baraza la usalama. Hawa Tanzania ni nani hasa, sasa watanikoma…” alisema huku akiuma meno. Wameua wapiganaji wangu! Nitaua wa kwake, akawaza na kuondoka kwenye kile chumba. Siku hiyo ilikuwa siku ngumu sana kwa Sebutunva, moyoni mwake aliona jinsi gani itamuwia ngumu kutimiza azma yake ya kukamata na kukalia nchi fulanifulani kwa nguvu. Aliwaza wapi sasa ataendelea kupata pesa za kuendesha mambo yake na kuweza kuwatawala wenzake kama alivyokuwa akifanya mwanzo. Kichwa kiliuma.
Sasa hapa, lazima nibadilishe katiba, niongeze muda wa kukaa tena madarakani ili nifikie lengo langu, akapitisha uamuzi na kuondoka zake.
Baada ya kikao hicho Banginyana aliondoka na kuelekea kusikojulikana huku wale vijana wasaidizi wakirudishwa jeshini kuendelea na majukumu mengine.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
7
MBELE YA JENGO la Wizara ya Elimu, Kamanda Amata aliegesha gari yake na kuteremka huku akifuatiwa na Chiba na Gina.
“Hapa sasa ndipo tutapata jibu kamili juu ya huo uvamizi wa Ikulu,” Kamanda akawaambia wakati wakianza kupanda ngazi kwenda ghorofa ya juu kabisa.
“Kivipi Amata?” Chiba akauliza.
“Unajua hatukuwa na muda wa kutosha pamoja nanyi lakini kuna maeneo ambayo tuliyatazama kwa jicho la pekee, mtaona,” akawaambia na wakati huo tayari wakawa juu, ghorofa ya tano, kati ya milango mingi kulikuwa na mlango mmoja ambao kwa muonekano ulikuwa haufunguliwi kabisa.
“Du!” Gina akapiga kite kwa vumbi lililokuwa katika mlango huo ambao kabla ya kuufikia kulikuwa na maboksi kadhaa yaliyojaa makabrasha na mafaili mbalimbali. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na meza moja ndogo na kiti huku mezani hapo kukiwa na kompyuta ya kizamani, karibu na dirisha hilo ambalo ukisimama kulikuwa na mashine kubwa la kupoza hewa, ukiangalia dirisha lile moja kwa moja utaona lango kuu la Ikulu na ile barabara inayoongoza mpaka mbele ya jengo lile.
“Washa airconditioner!” Gina akamwambia Amata.
“Acha ushamba, hii siyo airconditioner,” akajibu na kuiendea ile kompyuta, “Chiba washa kompyuta hiyo, utakuta picha za tarehe hiyo tuangalie nini kilijiri,” Amata akamwambia Chiba. Vumbi lilitimka juu ya kiti kile baada ya Gina kukipiga kwa kitambaa. Chiba akaketi na kuiwasha kompyuta hiyo ya IBM, nayo ilipomaliza kuwaka ikadai nywila.
“Oya, nywila hapa!” Chiba akamwambia Amata.
“Ulichokalia na unachokitazama,” Amata akajibu huku akicheka, Chiba akaelewa na kuingiza, alipobofya kitufe cha Enter, ile kompyuta ikakaa kama sekunde kumi kisha ikawaka, moja kwa moja wakafungua app inayobeba kamera hiyo. Wote watatu walikusanyika nyuma ya chombo hicho na kuangalia kile ambacho kilitukia siku hiyo.
KILICHOJIRI…
Watu kumi waliovalia mavazi meusi, wakiwa wamekamilika kwa silaha nzito, walikuwa wamejioanga katika chombo kidogo mfano wa boti, kilichofungwa juu na chini. Chombo hicho kilichiokuwa kikisafiri chini ya maji kilisogea karibu kabisa na eneo lililotakiwa.
“Hapo hapo, kila mmoja awe tayari,” mmoja wao alitoa maelekezo. Wale watu wakachukua vidubwasha vidogo mfano wa mbilimbi na kuvipachika vinywani mwao, vidubwasha vile viliweza kuwapa hewa ya oksijeni kwa dakika tano. Kisha Yule nahodha akafungua mlango wa chini ya hiyo nyambizi yao nao wakatokea huko . dakika mbili ziliwatosha kuibuki katika bomba la maji taka lililokuwa likielekea kule wanakokutaka, wa kwanza kabisa akapanda juu ya loile bomba na wapili na wa tatu kisha wote wakawa juu ya lile bomba na kuanza kutambaa kama nyoka wakiwa katika mstari mmoja. Walipokaribia ufukweni, Yule aliyetangulia akawapa ishara wenzake watulie, kisha yeye akatoka pale alipo kwa kasi na moja kwa moja alidanda juu ya ukuta wa jingo lile na kutulia katika vyuma vilivyotengeneza maua mazuri kabisa. Juu ya ule ukuta kulikuwa na kamera ya CCTV, akapachika kidole chake kwa chini na kupachua kifuniko kidogo, ndani yake kulikuwa na kadi, akaibonya nayo ikachomoka, akachukua yak wake iliyokuwa kwenye kijifuko cha plastiki akaipachika na kisha akarudisha kile kifuniko. Mfukoni mwake akatoa kitu kama simu, akachukua waya mdogo na kuupachika kwenye moja ya matundu ya simu hiyo, na waya ule akaupachika pale kwenye kamera na kitazama nini kinaonekana, aliporidhika akaurudishia ule uliokuwapo, kisha akawapa ishara wale wenzake wakati yeye katulia palepale.
Mtu wa pili akachomoka na kuufikia ule ukuta, hakupanda, akainama pale chini kama mtu anayetafuta kitufulani, my wa wa tatu akafika na kuukanyaga mgongo wa Yule wa kwanza kisha akatulia juu huku mguu wake ukining’inia, wan ne alipokuja alikanyaga mgongo wa Yule wa kwanza, akaudaka mguu wa Yule wa pili kisha aruka na kutua ndani, alipofika tu mbele yake aliona askari wawili, akainua bunduki yake iliyofungwa kifaa cha kuzuia sauti na kuwaangusha kwa risasi moja moja kila mmoja, kimya kimya waliwainua na kuwaweka mahala kisha wao wakatawanyika na wale wa mwisho wakapitiliza na kuufikia mlango mkubwa. Yule aliyekuwa na kazi ya kuilaghai ile kamera akafika na kuingiza tarakimu fungushi na kuufungua mlango huo, wote wakiwa na shotgun mikononi mwao, waliingia ndani ya jingo hilo ….
Taa kubwa iliyofungwa katika ukumbi wa kwanza katika jingo hilo ikwaka na kuwamulika watu hao, taa hii ilikuwa imeunganishwa na chanzo mbadala na zile nyingine, mmoja wa wale magaidi akailipua kwa bastola yake na wakati huohuo wana-usalama ndani ya jingo hilo walianza kutoka kwenye kona zao mbalimbali na kufanya kazi yao. Ilikuwa kizaazaa kila kona, risasi zililindima huku na kule, wale magaidi walikuwa wamevaa nguo zisizopitisha risasi tofauti na wanausalama wa Ikulu ambao walivaa nguo zao za kawaida. Kutokana na silaha nzito walizokuwa nazo wale jamaa walifanikiwa kuwadhibiti wana usalama ambao walikuwa na silaha ndogondogo. Mapigano hayo yalikuwa magumu sana kwa watu wa usalama kutokana na giza lililotanda ndani ya jingo hilo.
Ndani ya nyumba maalumu ambayo imejengwa ndani ya Ikulu, nyumba hii ambayo huishi Mheshimiwa Rais na familia yake, wanausalama walikuwa mbioni kuufungua mlango ili kumnusuru mke wa Rais, wanausalama hao wa kike walikuwa wakisaidiwa na wanaume waliokuwa na funguo bandia katika kufanya hilo.
Lakini kabla hawajafanikiwa walifikiwa na wale magaidi wakamimina risasi za kutosha na kuwaua wale wanausalama pale mlangoni kisha wakafungua mlango na kuvamia ndani ya ile nyumba, walitanda huku na huku na kukifikia chumba cha kulala ambako walimchukua mke wa Rais na kutoka nae huku wakiwa wamefunga gundi kinywani hasipige kelele.
Walipotoka nje ya nyumba hiyo walipewa maelelekezo wapi pa kutokea, mmoja wa wanausalama aliyekuwa sakafuni akivujwa damu, alikuwa akishuhudia yote hayo, alimwona mmoja wa watu wao aliyemjua kwa sura akiwaonesha njia wale wavamizi. Akakohoa ili aseme neno yule msaliti akageuka na kugundua kuwa mtu huyo hajafa, wakagongana macho.
“Ni we-we! Aaaaaaiiiiigggghhh…!” kabla hajamaliza kusema risasi moja ikamfumua kichwas naye akanyamaza kimya. Wale magaidi wakaongozwa na kuteremka chini ambko walikuta kitu kama mlango wa chuma, kufuli lake lilikuwa limeliwa na kutu, mmoja wao akalipiga risasi likafyatuka wakaingia ndani ya kitu kama bomba kubwa ambalo liliwezesha wao kupita bila taabu. Na walipofika mwisho wake wakakuta kuna maji, kila mmoja akapachika kifaa maalum cha hewa ya oxygen kinywani mwake na kingine wakamvalisha mateka wao, wakaingia majini na kuibukia baharini, huko walipiga mbizi mpaka chini ambako walikiacha kile chombo kikiwasubiri, wakaingia kupitia mlango wa siri kisha nahodha akaondoa maji chomboni na kukiondoa eneo lile.
***
REJEA CHUMBA CHA SIRI….
“Uhhhhhh!” Chiba alivuta pumzi ndefu na kuishusha, “Sasa hawa jamaa walitokea wapi? Maana hapa mlangoni sijawaona,” akauliza.
“Kwa vyovyote hawakutokea mlangoni, kuna njia nyingine ya siri ndani ya lile jingo, ziko njia tatu tofauti, sasa hawa lazima wametumia moja wapo, na kwa kuwa walikuja kutokea baharini basi wamerudi kutpiti baharini lakini kwa njia ya siri,” kamanda akawaeleza. Gina alibaki kimya kabisa bila kuongea lolote.
“Mnajua huu uvamizi inabidi tuufanyie uchunguzi wa hali ya juu sana, hebu tuonane na Madam mara moja,” Kamanda akaeleza na Chiba wakati huohuo akampigia simu Madam S nao wakamsubiri pale ndani.
Dakika tano tu zilimchukua kuwasilia katika jingo lile kwani halikuwa mbali na Ofisi Ndogo. Alipowasili walimwonesha zile picha walizokuwa wakitazama zilipkwisha nae akawatazama vijana wake.
Kamanda Amata akasogea kutoka aliposimamawakati huo na kusimama mahala pengine.
“Enhe, nipeni mpango,” Madam S alianzisha mazungumzo. Wote wakamwamngalia Amata aliyekuwa akichungulia dirishani, kisha akageuka na kuwatazama baada ya kauli ile ya Madam.
“Nahitaji turudie uchunguzi au tuone pia tafutishi za uchunguzi wa awali, hii ishu Madam ni ngumu hata ile ya ‘Olympus Has Fallen’ ilikuwa nyepesi,” akasema.
“Maswali gani?” Madam akatupa swali.
“Yeah, najua kabisa kuwa pale Ikulu kuna chumba cha kuhifadhi silaha, tena silaha za kivita, lakini sijaona kama zilitumika, sasa je ina maana wanausalama wa Ikulu hawajui silaha ziko wapi, au mwenye gunguo alikufa au ilikuwaje?” Amatab aliuliza.
“Kwa maelezo ya Othman, mtunza silaha alikutwa amekufa pale aple kwenye mlango wa chemba hiyo nyeti na hakuna silaha iliyochukuliwa,” akawaambia. Amata akatikisa kichwa kuonesha kuwa ameelewa kitu.
“Madam S, kama ni adui aliyemuua huyo bwana basi angechukua silaha, lakini kama hakuna silaha iliyochukuliwa basi huyo mtunza silaha aliyekuwa zamu kauawa na mtu wetu wenyewe, hii ni hujuma!” Amata akaongeza shaka. Kila mmoja akatikisa kichwa kuonesha kimeeleweka kitu.
“Lakini unaonaje tukikutana na watu waliofanya uchunguzi tunaweza kung’amua mambo zaidi hapa,” Gina alifunguka.
“Inspekta Simbeye alikuwapo katika lile jopo,” Chiba akaeleza.
***
Baada ya kumaliza uchunguzi wao pale chumba cha siri sasa walikutana na Inspekata Simbeye, mzee huyu aliyechoka na majukumu aliweka miwani yake vizuri na kumtazama Amata na Gina waliokuwa wameketi mbele yake.
“Yaani tatizo lako wewe Amata, ukiwa unakunywa pombe zako hunitafuti ila ukiwa na shida inayokutatiza ndiyo unanitafuta, utakua lini wewe?” Simbeye akamuuliza kwa utani.
“We mzee ukinywa bia utazirai endelea kugonga Chibuku tu!” kwa jibu hilo wote wakaangua kicheko.
“Ok tuyaache sema…” Simbeye akawaambia huku akijivuta kwa mbele na kuiegemea meza yake.
“Mzee, najua ulikuwapo katika jopo la uchucnguzi wa tukio lililotukia pale Ikulu wiki ileee…”
“Ndiyo!” akajibu.
“Sasa nina wasiwasi kuwa kati ya watu wetu waliouawa, watakuwa wameuawa na wasaliti, yaani ndani kwa ndani…”
“Kwa nini.mbona sisi hatuliona hilo?” Simbeye akauliza.
“Fikiria, mtunza silaha aliuawa sivyo?” Kamanda akauliza.
“Ndiyo, tena palepale kwenye chemba ya silaha,” akajibu Inspekta.
“Aliuawa kwa mikono au kwa risasi?” Gina akauliza.
“Risasi,” Simbeye akajibu. Amata akatikisa kichwa.
“Mlikusanya maganda yote ya risasi?” Amata akauliza.
“Tena yote hatukubakisha hata moja, wale jamaa walitumia risasi themanini na moja kufanya shambulizi lile,” Simbeye akajibu.
“Naweza kuona maganda yake au mmeshayatupa…”
“Huwa situpi vitu kama hivyo Amata, wao walishatupa lakini mimi nimeyachukua na kuyahifadhi,” akavuta droo na kiuwapatia ule mfuko wenye maganda ya risasi, hakika yalikuwa maganda themanini na moja.
“Simbeye… sasa jibu hili hapa!” Amata akasema na wote wakakodoa macho. Maganda haya sabini na tisa ni Heavy Shotgun, mtoto wa AK-47, ina maana hawa magaidi walitumia silaha hii haribifu kabisa kwa uvamizi huu, na nina wasiwasi sasa haya maganda mawili ambayo si yah ii silaha si ya hawa magaidi. Moja umesema mmelipata kwa huyo kijana mtunza stoo ya silaha, na la pili je?” Amata akaeleza na kisha akahoji.
“La pili; mlangoni mwa nyumba ya Mheshimiwa,” Simbeye akajibu.
“Inspekta Simbeye, kwa uzoefu wako wa kipolisi na ukachero unakubali kuwa risasi hizi zote ni za hao magaidi? Sabini na tisa zinafanana na mbili tu hazifanani, maana hizi mbili ni Mgnum 22,” Amata akaonesha wasiwasi wake.
Simbeye alibaki kimya, akavua miwani yake na kuiweka mezani akamkazia macho kijana huyo shababi na mrembo wake Gina waliokuwa kimya wakisubiri jibu la mzee huyo. Akajikuna kichwani na kufikicha masikio yake.
“Amata, Kamanda Amata, unanipa fikra mpya ya kuweza kufikiria mambo amabayo nilikwishayaweka kando, hilo unalosema linawezekana tena kwa asilimia sitini, na lazima lifanyiwe kazi,” Simbeye akajibu huku akikusanya yale maganda na kuyarudisha kwenye ule mfuko, Amata akachukua yale mawili yenye utata na kuyatia mfukoni.
“Vipi?” Gina akauliza.
“Naenda kumkamata muuaji na huyu ndiye mwenye jibu la nini kilitukia. Na nitamkamata leo hiihii,” Amata akaongea kwa hasira. Wakaagana na kuondoka zao huku wakimuacha Simbeye akiwa hoi kwa mawazo.
***
“Amata! Hivi hii akili ya haraka unaipata wapi?” Gina akauliza wakati akiondoa gari pale kituo cha polisi cha kati na kuelekea mjini.
“Ukishakuwa katika kazi hizi inabidi uwe na akili ya juu sana, hata wewe baadaye utajikuta unakuwa hivyo,” Amata akaeleza, na wakati huo simu yake ikaita, daima simu hii ikiita alijua ni kutoka kwa Madam au mtu yeyote wa TSA kwa kuwa haikuwa simu ya kawaida.
“…yes Madam!” akaitika, “…ndiyo, tupo hatua moja kutoka katika ufumbuzi wa hii kitu, na naamini leo hii utafurahi huku hauamini (…) sawa Madam,” akamaliza kuongea na simu ile, akaikata na kuiweka mahala pake.
“Twende ofisi ya Kinondoni tukamwone Hosea,” Amata akamwambia Gina, na mara hiyo akawasha indiketa na kuisha barabara ya Samora akakunja kulia kuchukua ile ya Ohio na kuongoza mpaka barabara ya Hali Hassan Mwinyi. Nusu saa baadae walikua tayari katika jingo la ofisi za Usalama wa Taifa, Kinondoni. Jingo hilo lililoonekana kama limetelekezwa kwa nje, ndani kulikuwa na mambo mengi sana yaliyokuwa yakiendelea, mambo ya kiusalama. Wakazipanda ngazi na kuingianndani ya jingo hilo, moja kwa moja wakaongozwa mpaka ofisi ya mkuu huyo wa idara nyeti ya Usalama wa Taifa. Huyu bwana ndiye alikuwa na cheo cha juu kabisa katika kitengo hiki.
“Karibu sana bwana Amata, ni muda mrefu hujafika katika ofisi yangu najua utakuwa unahitaji msaada tu hakuna linguine,” Hosea alimwambia Amata huku wakipeana mikono.
“Bila shaka,” Amata akajibu huku akiketi.
“Ndiyo bwana!”
“Ndiyo, Bwana Hosea, nimekuja kweli nahitaji msaada, silaha zangu zimeibwa nyumbani mkuu unisamehe sana, na sasa sina silaha kabisa unisaidie,” akamwambia kwa kumzunguka.
“Hivi Amata mpaka unaibiwa silaha ulikuwa wapi?” Hosea akauliza.
“Mkuu, sikuwa nyumbani na wamevunja kitasa wamechukua zote. Nimeogopa kumwambia Selina najua maswali yatakuwa mengi, nitazirudisha naazima kwa sasa tu,” akamweleza. Hosea akatulia kimya akifikiria jambo kisha akatuliza mikono yake mezani.
“Kwa sababu ni wewe, nitakupa lakini saa sabini na mbili uwe umezirudisha,”
“Sawa, halafu kama una Magnum 22, ingenifaa sana,” Amata akasema. Dakika kumi zilizofuata akachukuliwa mpaka kwenye chumba maalum cha silaha, kule alikuwa na kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kutunza ghala hiyo ya silaha kwa ajili ya watu wa usalama.
“Magnun 22, hii hapa,” yule kijana akamwambia Amata huku akimkabidhi kikasha chenye silaha hiyo.
“Hii ndiyo silaha bwana, nani mwingine anayo kama hii? Najua wengi hawaipendi,” Amata akadodosa.
“Aaaa sikumbuki ngoja nitacheki kwenye kumbukumbu lakini ni kama wawili au watatu ndiyo maana unaziona zipo za kutosha maana siku hizi wengi hawataki hizi,” yule kijana aliendelea kuongea huku akimpa na risasi za bastola hiyo, kisha wakafuatana mpaka kwenye ofisi ndogo ambayo kulikuwa na kabrasha kadhaa mezani na kompyuta ndogo, ofisi hii ndiyo aliyokuwa akiitumia yule kijana kuweka kumbukumbu zake.
“Du, tuna watu kama kumi na mbili hivi wanaotumia silaha hiyo kiofisi ambao wamechukulia hapa,” yule kijana akamweleza Amata na kisha akataja namba za wale watu, hakuwajua kwa majina kwa kuwa ilikuwa ni siri za kiofisi. Kamanda Amata alikuwa akirekodi mazungumzo yote na kijana huyo alipojiridhisha akaagana naye na kuondoka kisha akapita ofisini kwa Mkurugenzi bwana Hosea na kuagana naye huku akitakiwa kuirudisha silaha hiyo ndani ya saa sabini na mbili.
“Umepata unachotaka?” Gina akauliza.
“Bila shaka!” akajibu na kutoa ile bastola mpya kabisa na kumweleza Gina mbinu aliyoitumia kupata anachotaka, “Hapa nina namba za wafanyakazi kumi na mbili wa idara ya Usalama wa Taifa, nitazichambua kujua nani ni nani na yuko wapi, najua katika hili yupo ambaye bundi litamfia na huyo ndiye tutaanza naye!” akaongeza kujibu huku Gina akiicaha barabara ya Kinondoni na kukamata ile ya Hali Hassan Mwinyi kuelekea mjini.
OFISI NDOGO
KATIKA OFISI hiyo ndogo ambayo Madam S aliitumia kama ofisi yake ya kazi, alikutana tena na vijana wake majira ya mchana. Kamanda Amata aliwasimulia yote aliyoyafanya huko alikotoka. Akampa Madam ile sauti iliyorekodiwa kati yake na yule kijana kule Kinondoni.
“Nahitaji kuzitambua hizo namba moja baada ya nyingine,” Amata akamwambia Madam S, katika idara ya usalama Madam S alaikuwa na nywila iliyomwezesha kuingia kwenye mtandao wa Usalama wa Taifa. Madam S akabofya kitufe Fulani uvunguni ma meza hiyo na juu ya ile meza pakafunguka na kujiinua kompyuta ya ukubwa wa wastani ikasimama mbele yake na kuwaka.
“Msije huku tafadhali!” akawaambia na wote wakatulia walipo. Amadam S alitaja namba moja moja na jina la mtu husika, huku Chiba akiendelea kuingiza majina hayo katika mtandao wake wa utambuzi. Jina namba 301 ambalo katika orodha hiyo lilikuwa la mwisho kabisa, lilimstua Chiba.
“Madam! Namba 301…” akamwambia wakati picha ya mtu huyo imejitokeza pale juu na taarifa zake zote…
Chiba akahamaki kwa sauti.
“What!? Gina njoo hapa haraka…” Gina akawahi pale alipo Chiba na kutazama kwenye ile kompyuta, macho yakamtoka.
“Nini nyie? Mbona hivyo?” Amata akauliza huku akigeuza kiti chake kutoka kwa madam na kukutana uso kwa uso na picha ile.
Briston Kalangila, mwajiriwa wa serikali ya Tanzania tangu mwaka 1990 katika kitengo cha Usalama wa Taifa. Kabila Muha mwenye uchanyiko wa baba wa Kiha na mama mwenye asili ya Nduruta. Amepata elimu yake huko Nduruta na kisha kuja kumalizia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kabla ya kujiunga na Idara ya Uhamiaji na baadae kuingia Usalama wa Taifa, namba ya utambulisho wake wa kikazi ni TNS 301.
“Mimi nilisema huyu ana shida, nilishamhisi tangu siku ya kwanza nilipokutana naye!” Chiba akaeleza na Gina akaunga mkono. Amata akaitazama ile picha.
“Unamjua vyema?” Madam akamwuliza Amata.
“Namjua vizuri ila nilikuwa sijui kama ni yeye,” akamgeukia Madam, “ Madam S, huyu ni mtuhumiwa wetu namba moja na sasa hivi lazima ashughulikiwe, katika maganda ya risasi themanini na moja maganda mawili ni ya huyu Briston, Briston ameua wanausalama wetu wawili na lazima achunguzwe,” Amata akasema.
Madam S akajishika kichwa na kukitikisa kisha akawatazama vijana wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa nimeelewa, nimeelewa mengi sana vijana, mmenifungua macho na akili, sasa nimeelewa kitu,” Madam S akafunga kompyuta yake nayo ikarudi pale mezani na meza ile ikawa ya kawaida, akainuka na kuliendea jokofu akachukua pombe kali na kujanayo mezani na bilauri kadhaa akawamiminia vijana wake kwenye bilauri hizo huku akionekana wazi kuwa na hasira zisizojificha. Kamanda Amata akainuka pale kitini na kumwendea Madam pale dirishani aliposimama baada ya kuwamiminia kinywaji kile.
“Madam S, nakufahamu vyema kabisa miaka yote tuliyokaa pamoja, hebu niambie ni nini umekielewa hapo?” akauliza.
“Sikia Amata, kama TSN 301 Kalangila ameshiriki katika njama hii na ye kumbuka ni chotara wa Kitanzania na Kinduruta, basi hapa kuna mengi, hii njama ni ya wengi, lazima kuna mapandikizi mengi, mengi sana tena katika idara mbalimbali za serikali; jeshini, polisi, bungeni. Serikali inabidi kuwa makini hawa watu wa mchanganyiko wa damu si wa kuwapa vipaumbele kwenye vitengo nyeti hasa vya usalama kama hivi, wapo wengi sasa naanza kuwajua mmoja baada ya mwingine. Nahitaji kuonana na Rais…” akatoka na kumwacha Amata pale akaiendea meza yake na kuinua simu.
“Subiri Madam! Ngoja tumshughulikie huyu 301 kisha utafanya hiyo process, tafadhali,” Amata akamwambia Madam. Kisha akarudi kwa Chiba na Gina.
“Ok, jioni hii ni siku ya kumnasa Kalangila Briston, na hiyo kazi itafanywa nasi sote,” akawaambia.
***
Briston Kalangila alitoka taratibu na gari yake katika geti la Ikulu, akateremka barabara ya Magogoni na kukunja kulia pale katika soko la samaki na kupandisha kuelekea Posta. Moja kwa moja mpaka barabara ya Maktaba kisha akaegesha gari yake Hoteli ya New Afrika, akateremka na kushusha miwani yake huku akiangalia huko na huko.
Gina alitulia kimya katika tax ya Scoba akimwona mtu huyo aliyemfuatilia tangu pale Ikulu bila yeye kujua, akamtazama, akiingia ndani ya hoteli hiyo ya kimataifa. Gina akataka kushuka ile aelekee kule, lakini Scoba akamzuia.
“Usiende, subiri kidogo,” Scoba akamzuia, Gina akatulia lakini wakati huo tayari damu yake ilikuwa ikichemka. Nukta hiyo hiyo Land Cruiser moja ikaingia katika hoteli ile na kuegeshwa nje tu. Kijana mmoja aliyeshupaa misuli akateremka, Gina akamkodolea jicho. Nani Yule? Akajiuliza. Kwa kamera yake ndogo akachukua picha ya mtu huyo kisha wakatulia ndani ya gari ile. Nusu saa baadae Yule jamaa mfupi akatoka, Gina akachukua kamera yake na kuchukua picha kadhaa.
“Fuata hiyo gari,” akamwambia Scoba, naye akaingiza gari barabarani na kuifuata ile Cruiser. Mpaka Masaki ilipoingia katika yale majengo ambayo bado yalikuwa kwenye ujenzi. Picha zote Gina akazihifadhi vyema katika kamera yake, kisha taratibu wakaondoa gari yao na kuchukua barabara ya kwenda Cocobeach kisha moja kwa moja wakapita tena mbele ya Hoteli New Africa lakini hawakuiona gari ya Briston.
“Ameondoka” Gina akanong’ona huku Scoba akipita bila kusimama, akazunguka mzunguko wa askari na kuchukua barabara ya Samora kurudi Ofisi Ndogo.
CASINO LAS VEGAS
DAR ES SALAAM
Briston alipotoka pale New Africa moja kwa moja alielekea katika Casino kubwa ya Las Vegas kwenye makutano ya barabara ya Hali Hassan Mwinyi na ile inayoelekea Ocean Road. Ndani ya Casino ile jioni hiyo tayari watu walianza kumiminika kwa starehe mbalimbali. Miongoni mwa waliokuwa wakiingia, Briston Kalangila alikuwa mmoja wapo akiwa sasa ndani ya suruali ya jinzi ya bei mbaya na fulana ya pundamilia iliyomkaa sawasawa, tambo lake kubwa lilimfanya aonekane kama mnyanyua vitu vizito. Mkono mmoja mfukoni na mwingine ukining’inia alivuta hatua na kupishana na warembo kadhaa waliokuwa ndani humo wakiuza na kujiuza. Ndani ya casino hiyo muda huo wa saa kumi na moja ya nje kule tayri ulikuwa usiku kwani mataa ya rangi rangi yalikuwa yakipishana kuupendezesha, gizale lilikuwa dhahir shahir. Akajivuta mpaka kwenya meza moja ya duara iliyokuwa na viti vine na katikati ya meza hiyo kulikuwa na mchezo wa ‘gurudumi la bahati’, haukupita muda aliongezeaka mtu mwingine naye alionekana kujaa mwili, walishahabiana kwa nukta chache kana kwamba walikuwa mapacha, naye akaketi palepale, huyu alikuwa maji ya kunde ukiachana na ukubwa wa mwili wake alikuwa na sura ndefu kiasi yenye pua nyembamba.
Kamanda Amata alikuwa mmoja kati ya wateja wa casino hiyo jioni hiyo, baada ya kuingia nyuma kidogo ya Briston, aliketi kaunta akipata kinywaji na kumtanabahi kila aingiaye na atokaye, kutokana na ile sehemu aliyoketi aliweza kuona hayo yote. Alimwona anyemtaka, Briston. Yule ni nani? Akajiuliza baada ya kumuona huyo aliyeongezeka, akapiga funda moja la kinywaji, kisha akashusha ile bilauri na kuendelea kuangalia upande ule kwa chati. Baadae zaidi akaja mtu mwingine kati yao, huyu alikuwa wa kawaida tu lakini alikuwa mrefu, mwembamba, aliketi kati yao, wakawa watatu. Katika meza hiyo kulionekana kuwa na mazungumzo mazito yaliyoleta shida ya muafaka. Yote hayo Amata alikuwa akiyatengeneza kadiri anavyoona hali ya waliyonayo watu hao. Alijitahidi kupata japo pizza za hao wengine lakini alishindwa kutokana na nyendo za watu ndani humo na pia. Akainua simu yake kubwa na kuandika ujumbe mfupi kwa Chiba akimtaka kuwapo nje ya casino hiyo haraka iwezekanavyo na kumwelekeza watu ambao anataka awajue ni akina nani.
Baada ya dakika kama arobaini na tano hivi, wale jamaa walionekana kumaliza mazungumzo yao, akatoka Yule mwembamba na kwenda zake huku Briston na Yule mwingine wakibakia. ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.
Chiba aliwasili nje ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.
“…mrefu, mwembamba, kava kofia ya pama,”
ujumbe uliingia kwenye kifaa cha Chiba kilichopachikwa sikioni kwa ufundi kabisa, akaendelea kufuta gari yake mara hii upande wa nyuma ili apate nafasi ya kumwona mtu huyo. Lengo lake lilifanikiwa, alimwona mtu huyo akitoka ndani ya jengo hilo, akasimama ngazini na kuwasha sigara yake. Wakati huo Chiba alikuwa nyuma ya gari yake, akafanikiwa kupata picha ya mtu huyo kwa simu yake kubwa nay a kisasa. Picha tofauti kama kumi hivi mpaka kijana huyo alipokuwa akipanda gari yake na kuondoka, kilichomwacha Chiba kinywa wazi ni gari iliyokuja kumchukua, ilikuwa na namba za kibalozi. Namba zile Chiba alizitambua mara moja kuwa ni namba za ubalozi wa nchi ya Nduruta. Akatikisa kichwa na kisha akaendelea na shughuli yake. Mara akapokea ujumbe mwingine uliyomtaka kummulika anayetoka.
“…Anata tambo kubwa kava suti kijani juu mpaka chini,”
ujumbe ulitoka ka Kamanda Amata. Mtu Yule alijitokeza nje, akapitiliza na kuteremka zile ngazi mpaka chini kabisa, na kuingia kwenye gari oja ya kisasa. Chiba alikamata picha zote alizozihitaji na kuzihifadhi kadiri alivyotaka, alipohakikisha zote amezipata, akaingia ndani ya gari yake na kujifungia kimya. akisubiri
***
Baada ya wale watu kuondoka, Briston alibaki peke yake pale mezani, Kamanda Amata akateremka taratibu na kumwendea palepale alipo, akavuta kiti na kuketi. Briston akamtazama kijana huyu mwenye macho maangavu yanayoonesha kila aina ya udadisi.
“Mbona wajikaribisha mwenyewe, kijana huna adabu…”
“Haina haja ya kukuzungusha, naitwa Amata Ric au wengi huniita Kamanda Amata bila shaka umelisikia jina hili na kama la basi ndiyo mimi mbele yako,” Amata akamwambia Briston. Briston akajiweka sawa kitini na kumwangalia tena kijana huyu.
“Nikusaidie nini Kamanda sijui kidudu gani sijui, huna kinywaji?” akamwuliza kwa kejeli.
“Sina haja ya kinywaji maana ni vingi nyumbani kwangu. Briston Kalangila TNS 301,” Amata alipotamka namba ya kazi ya huyo mtu, Bristoni alihisi akili kumpaa kwa sababu raia wa kawaida hawajui namba hizo.
“U-u-mesema unaitwa nani?” akauliza tena, sasa kwa makini zaidi. Amata akaondoa miwani yake usoni, akabandua mustachi mzuzu wake bandia nay ale masharafa akabaki wa kawaida. Briston akashusha pumzi ndefu, “Umekuja kwa heri au kwa shari?” akauliza kwa hofu iliyoonekana wazi.
“Sijaja kwa shari, ni kwa heri tu maana wakati mwingine huwa tunapenda kufanya kazi katika mazingira kama haya, wanausalama saba na zaidi wameuawa ndani ya jingo la Ikulu na mke wa Rais ametekwa na wewe ulikuwapo lakini hukufanya lolote hili ndilo limenileta kutaka kujua,” Amata akamchokoza bila kumyumbisha.
“Hivi we una wazimu? Wale jamaa walivyovamia pale ulikuwepo, unajua waliingia na silaha gani au zenye uzito gani?”
“Mzee, hukuwa mtu wa kushindwa kuzuia uvamizi ule kwa jinsi unavyojua kuorganize watu, kumbuka Rais aliyepita alikuweka kwenye kitengo cha runners kwa sababu ya weledi wako wa kupanga na kutengeneza mambo,” Amata akaendelea.
“Narudia tena, unajua silaha walizokuwa nazo na uzito wake, ulitaka wote tufe halafu nini kitokee? Si ushukuru hao saba sijui wangapi waliokufa, kama huna la kuongea nitokee hapa!” akaongea huku jazba ikipanda.
“Najua, walikuwa na Assault Shotgun, shambulizi lao walitumia risasi sabini na tisa tu lakini zilizopatikana ni themanini na moja...”
“Kwa hiyo hizo mbili zimetoka wapi?” Bristona akadakiza swali.
“Ndiyo hicho nataka unijuze, risasi mbili ni za bastola ya Magnum 22 na katika katia ya wanausalama wanaomiliki silaha hiyo mmojawapo ni wewe, na ambaye upo pale Ikulu muda mwingi. Moja imeokotwa kwenye mlango wa chumba cha silaha pamoja na maiti ya mtunza stoo hiyo, na nyingine imeokotwa kwenye mlango wa kuingilia katika apartment ya Rais, ina maana katia ya watu wetu waliouawa, wewe kwa mkono wako umeuwa wawili, na ni hao nimekutajia…” Amata alieleza bila kusitasita na kumfanya Briston afure kwa hasira, macho yake yalibadilika.
Briston alikumbuka matukio hayo yakamrudiarudia kwenye kumbukumbu zake wakati huo, alijaribu kupingana nayo lakini ilishindikana, “Hivi umetumwa?” akauliza.
“Ndiyo,”
“Na nani?” akauliza.
“Na mama yako!” Amata akamjibu huku akirusharusha yale maganda ya risasi katika kiganja chake cha mkono, kisha akayatia mfukoni na kunyanyuka, “Kazi njema Briston kalangila,” akamuaga naye akatoka eneo lile…
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Briston Kalangila, alimtyazama kijana Yule akiondoka pale mezani kwake kwa mwendo wa mikogo, akajichanganya na wateja wengine mpaka alipoishia kaunta. Kwa hasira akapiga ngumi mezani na kisha akainua simu yake na kuongea machache alipomaliza akatulia tuli, mara hii kile kinywaji kilikuwa hakipiti shingoni, mishipa ya kichwa ilimdinda na kijasgho chembembe kilitiririka ijapokuwa mashine za nguvu za kupoza hewa zilikuwa zikiwajibika kufanya hivyo.
“Yes boss!” sauti ya kike ikasikika mbele ya Kalangila, akainua uso wake na kumtazama binti huyo, mwembaba wa wastani mrefu mwenye shingo nyembamba, sura ndefu, meno yake meupe yalipangiliwa vyema na Malaika aliyesadifu kinywa hicho.
“Sikia Lulu, fanya unaloweza, umtie mkononi huyu mtu naujua ubembe wako hawezi kuchomoka kwani hakuna mwanaume ngangari mbele ya mwanamke mrembo labda awe hanithi,” muda huohuo akamtumia picha ya Amata kwenye simu na kumwacha Yule binti aende zake. Briston akanyanyuka na kutoka kwenye ile casino kuelekea nje.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment