Search This Blog

Friday 18 November 2022

SALA YA SARAH - 1

 








IMEANDIKWA NA : ALEX KILEO



*********************************************************************************



Simulizi : Sala Ya Sarah

Sehemu Ya Kwanza (1)





Ni nyakati za alasiri jua likiwa bado halijapoa ukali wake na baadhi ya watu wakiwa katika pilika pilika za kujitafutia riziki zao kwa ajili ya kuendesha maisha yao katikati ya jiji.



Ndani ya hoteli moja kubwa na maarufu hapa mjini kulikuwa na kikao kidogo kinaendelea kati ya watu wawili, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja, hawa watu ni ndugu, mtu na Dada yake, yaani mtoto wa mkubwa na mtoto wa mdogo.



Mwanaume anaitwa Denis Michael Dege alimaarufu alikuwa anaitwa Taita, na mwanamke anaitwa Mage Stewart Dege, ndani ya kikao kuna kitu kilikuwa kinajadiliwa, walikuwa wanajadili mirathi ambayo iliachwa na baba zao ambao walikuwa ni ndugu wa baba na mama mmoja, baba zao walishafariki na wakaacha mali nyingi ambazo walizirithi kutoka kwa baba yao.



Bahati nzuri asilimia kubwa ya mali walikuwa wameshagawana, walichokuwa wanajadili ni nyumba mbili tu ambazo zilikuwa katikati ya mji.



"Nimeshapata Mteja wa nyumba moja ile ya ghorofa" Taita aliongea kisha akagida maji yaliyokuwa katika glass,



"Anatoa shilingi ngapi?" Magreth aliuliza huku akimuangalia usoni Taita,



"Bilioni moja" Taita alijibu,



"Hapana, hiyo haitoshi, kwa sehemu ilipo ile nyumba ni bilioni mbili, nilifuatilia wizara ya ardhi na makazi na bei niliyoambiwa ni hiyo, hata wewe unajua hilo" Magreth aliongea huku akiendelea kumuangalia kaka yake huyo,



"Nilijua tu ni lazima ulete kikwazo, kwani kuna ubaya gani tukiuza hiyo nyumba bilioni moja? kwani uliijenga wewe?" Taita aliuliza kwa hasira



"Unadhani aliyeijenga angekubali kuuza kwa bei hiyo?" Magreth aliuliza huku sura yake ikiwa imejaa ujeuri,



"Kwanza unatakiwa kujua wewe ni mwanamke tu, hata tulivyogawana mali za hawali nilifanya ubinadamu tu, kihalisia wewe hutakiwi kupata kitu, mimi ndio mrithi wa mali zote" Taita aliongea na kutoa cheko la dharau,



"Mpuuzi wewe usilete mambo ya kizamani, dunia ya leo ni haki tu kwa wote" Magreth aliongea kwa hasira,



"Ebu acha ukorofi Mage, ujue Nina shida na hela?" Taita aliongea huku akitabasamu,



"Una shida gani wewe, kila kitu unacho, una majumba una hela na una vitega uchumi vya kila aina" Magreth aliongea kwa kufoka,



"Basi toa uamuzi, nyumba iuzwe au isiuzwe kwa bei hiyo?" Taita aliuliza,



"Nyumba haiuzwi kwa bei hiyo" Magreth alijibu,



"Alafu yule mume wako ndiyo anaekushauri ujinga, yaani mkikaa hamna cha maana mnachojadili zaidi ya hizi mali, tafuteni za kwenu" Taita aliongea kwa dharau, uwa hakasirikagi huyu bwana mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, uwa anatabasamu muda wote.



"Hatujaja kuongelea familia yangu hapa, tukisema tuongelee familia basi tuanze na wewe usiye na mtoto na bado una mke na mmeoana miaka saba iliyopita" Magreth aliongea kwa hasira,



"Nadhani tumemaliza, nyumba nitaiuza kwa hiyo pesa na nitakuletea milioni mia tano, kama utazikataa nitazichukua zote" Taita aliongea na kunywa maji tena,



"Sheria zipo" Magreth aliongea kwa hasira,



"Mwisho wa majadiliano, hati zote ninazo mimi" Taita aliongea na kunyanyuka kisha akaanza kuondoka na kumuacha Dada ake akimuangalia tu mpaka alipotoka kwenye ule mlango wa hoteli ambao ulikuwa wa vioo, Taita alitoka na kuingia kwenye gari la kifahari na kuondoka zake.



Magreth aliendelea kukaa kwa muda pale hotelini huku akionekana mwenye hasira, Dada huyu ana miaka ishirini na nane tu.



Baada ya kukaa kwa muda alinyanyuka na kutoka nje ya ile hoteli na kuingia kwenye gari lake dogo la kawaida na kuondoka zake kurudi nyumbani kwake.



Magreth ni mfanyakazi wa serikali katika wizara ya madini, ana cheo cha juu kiasi, ameolewa na ana watoto wawili, wa kwanza ni wa kike anaitwa Sarah, ana miaka mitano na wa pili anaitwa Sebastian, ana miaka mitatu tu.



Magreth alirudi kwake na kuingia mpaka sebuleni, akalakiwa na mwanaye mkubwa aitwae Sarah na kumkumbatia mama yake kisha akamsalimia,



"Shuleni leo mmefundishwa nini mwanangu?" Magreth alimuuliza Sarah,



"Kusoma na kuandika" Sarah alijibu,



"Hakuna homework leo?" Magreth alimuuliza mwanae,



"Ipo" Sarah alijibu,



"Umeshakula?" Magreth aliuliza,



"Tayari mama, nimeshiba" Sarah alijibu,



"Haya, nenda mezani ukafanye homework yako" Magreth aliongea kisha akaenda moja kwa moja kwenye kochi na kumbusu mume wake aliyekuwa amekaa hapo juu ya kochi, huyu bwana anaitwa Isack Senga, ni mlemavu wa miguu, hana miguu yote miwili, ilikatwa baada ya kupata ajali ya gari.



Magreth alimfikia mume wake na kumbusu kwenye paji la uso,



"Taita anasemaje?" Isack aliuliza,



"Anataka kuuza ile nyumba ya ghorofa kwa lazima" Magreth alijibu huku akikaa kwenye kochi,



"Sio habari mbaya, anataka kuuza shilingi ngapi?" Isack aliuliza,



"Bilioni moja, aisee hiyo bei ni ya nyumba za kawaida katika eneo lile, na sio za ghorofa" Magreth alijibu,



"Kwa hiyo bei inakuwa sio sawa. Muafaka gani mmefikia?" Isack aliuliza,



"Hakuna muafaka, alichoamua ni kuuza kwa nguvu, kesho nitaongea na mwanasheria wangu" Magreth aliongea,



"Fanya hivyo, maana yule ndugu yako hana nia nzuri" Isack aliongea,



"Umeshakula mume wangu?" Magreth alimuuliza mumewe,



"Hapana, nilikuwa nakusubiri" Isack alijibu,



"Ngoja nikaoge basi" Magreth aliongea na kunyanyuka akaelekea chumbani na kumuacha mume wake akimuangalia huku akitabasamu.



Ndivyo ilivyo nyumba hii, upendo umetawala kila kona, utafikiri wameoana juzi au jana.



Baada ya saa nzima Magreth alitoka chumbani huku akiwa ameshaoga na amevaa nguo za nyumbani. Akaelekea moja kwa moja jikoni na kuchukua chakula ambacho kilikuwa kimeshaandaliwa na msichana na kazi, akakipeleka mezani na kuanza kula na mume wake huku wakiongea mawili matatu ya kifamilia.



___________

USIKU

____________



Yapata kama mida ya saa nne na nusu usiku, watoto na Dada wa kazi wakiwa tayari wamekwishalala, Magreth na Isack walikuwa wapo sebuleni wakiangalia runinga, kipindi cha dini, wakiwa wamekolea kwenye imani walisikia mlango wa mbele wa nyumba yao ukigongwa, haikuwa ajabu kwao kugongewa mlango muda huo, maana hiyo hali walishaizoea kutokana na misaada wanayotoaga kwa majirani zao, kwa hiyo usiku kama huo kupokea ugeni ukiitaji msaada ni kawaida.



Magreth akasimama na kwenda moja kwa moja kufungua mlango, alipotoa kichwa nje alikutana na mdomo wa bastola iliyokuwa imeshikwa na kijana mweupe aliyekuwa amejichora tatoo karibu mwili wake wote,



"Bila kelele wala usumbufu rudi ndani" Kijana aliongea na kumfanya Magreth ageuke taratibu na kurudi ndani na yule kijana akaingia huku bastola ikiwa mkononi, Isack alipoona hivyo nae akashtuka, hakuwa na cha kufanya maana hakuwa na miguu.



"Vipi unataka kukimbia? Kimbia mi sitokupiga risasi" Kijena mwenye tatoo aliongea kwa dhihaka huku akitabasamu, kisha akaikagua ile nyumba kwa macho kuyazungusha sebule nzima, alipolizika akapiga mluzi kwa nguvu na kufanya Magreth na Isack waendelee kushangaa bila kujua lengo la yule kijana.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sekunde kadhaa tu baada ya ule mluzi, walishangaa kuona sebule ikivamiwa na vijana kama kumi na nyuma yao alikuwepo Taita huku akiwa ameshika makabrasha na sigara yake kubwa mdomoni na pia aliongozana na kijana mwingine nadhifu aliyevaa suti nyeusi,



"Dada mage, ni vizuri nimewakuta wote wawili maana mtatoa jibu sahihi" Taita aliongea na kujiweka kwenye kochi,



"Wewe shetani unadiriki kuniteka ndani ya nyumba yangu?" Magreth aliongea kwa uchungu huku akimuangalia Taita,



"Sijaja kujadili utekaji, nimekuja na mwanasheria wangu huyu hapa, nahitaji upige sahihi ili kuidhinisha nyumba kuuzwa" Taita aliongea huku akimuangalia yule kijana nadhifu waliyeingia nae,



"Ndio upuuzi uliokuleta huo? usitegee nitafanya hivyo" Margret aliongea kwa hasira,



"Kama ni suala la nyumba, ngoja kesho kukuche ili dada yako nae aje na mwanasheria wake ili mfikie makubaliano" Isack aliongea na Taita akamuangalia kwa jicho Kali, kisha akampa ishara yule kijana mwenye tatoo na yule kijana akakafyatua risasi iliyomkuta Isack mkono wa kushoto begani na kufanya atoe ukelele na Magreth akamkumbatia,



"Shiiiiiii hupaswi kuingilia kesi ya mali zangu na dada yangu, unatakiwa ukae kimya, nitakuondoa na mikono yako ubaki na kiwili wili tu" Taita aliongea huku akimuangalia Isack aliyekuwa Analia kwa uchungu,



"Jamani fanyeni haya, ila sitaki wanangu ndani wajue kinachoendelea" Isack aliongea huku akilia,



"Kumbe na watoto wapo?, Trigger kawalete wajomba zangu" Taita aliongea kisha yule Jamaa mwenye tatoo akaelekea vyumbani na kuanza kuwatafuta watoto, baada ya muda alirudi na watoto wawili na dada wa kazi,



"Shikamoo anko" Sarah alimuamkia Taita, masikini hakujua hata kinachoendelea,



"Marhaba, njoo anko" Taita alijibu huku akitabasamu na kumpakata Sarah na mdogo wake,



"Magreth saini wanachotaka, cha muhimu watoto wetu wabaki Salama" Isack alimwambia mkewe ambaye hakupinga, aliomba makabrasha na kusaini panapotakiwa,



"Safi sana" Taita aliongea huku akipiga makofi,



"Kinachofuata" Trigger aliuliza huku akimuangalia Taita,



"Funga kamba hao mbwa" Taita aliongea huku akisimama na alikuwa amewabeba Sarah na mdogo wake,



"Si tayari nimefanya utakacho? Kamba nifungwe za nini sasa?" Magret aliuliza lakini hakujibiwa, vijana walimfunga kamba yeye, mume wake na msichana wa kazi, kisha wakawatia vitambaa mdomoni ili wasipige kelele.



Taita akatoka nje akiwa na watoto,



"Tunafanyaje boss?"Trigger akiuliza, trigger ni yule kijana mwenye tatoo,



"Choma moto nyumba, wanatakiwa wafe" Taita aliongea huku akielekea kwenye gari na watoto,



"Tajiri eeh, huyu mtoto wa kike ni mkubwa, ana akili na anajua kinachoendelea, nae hatakiwi kuishi" Wakili alimshauri Taita,



"Kweli kabisa, kwanza atakuja kuwa msumbufu kama mama yake" Taita aliongea kisha akafungua mlango wa gari na kumtupa chini Sarah, Sarah akaanza kulia,



"Kitanzi, huyu nae kamtupe ndani, achomwe moto" Taita aliongea na kisha kijana wake mmoja aitwae kitanzi akambeba na kwenda kumtupa Sarah ndani, kisha milango yote ikafungwa kwa nje, nyumba ikamwagiwa mafuta na kuwashwa moto, nyumba yote ikashika moto,



"Tupotee" Taita alimwambia dereva wake na kisha gari ikaanza kuondoka taratibu na magari mengine waliyokuja nayo yakafuata...........



Ndani ya nyumba moto ulizidi kupamba, Sarah hakuwa na uwezo wa kufanya chochote kwa maana alikuwa mdogo, hakuweza hata kusaidia kuwafungua wazazi wake kuwafungua kamba zilikuwa zimeshika miili yao. Binti wa kazi nae alikuwa ndani ila alijaribu kuwafungua zile kamba na ilishindikana, kila alipojaribu hakufanikiwa kutokana na zile kamba kufungwa kwa ustadi wa hali ya juu, hata binti wa kazi alipojaribu kwenda jikoni kuchukua kisu, ilishindikana kwa sababu huku moto ulishashika jiko lote kutokana na mtungi wa gesi kupasuka na kulipuka,



"Dada, fanya chochote uwezacho kumtoa Sarah nje, jaribu kutumia njia yoyote ili mtoke nae" Magreth aliongea huku akilia, alishakata tamaa,



"Mama ngoja nijaribu kuwafungua tena" Dada wa kazi aliongea huku nae akilia,



"Toka nje, mtoe na mtoto" Isack aliongea kwa ukali huku machozi yakimtoka, Dada wa kazi alimbeba Sarah na kuanza kuangalia njia nzuri ya kutoka, alichoamua ni kupanda juu ya ghorofa, Dada wa kazi alipanda ghorofani huku akikimbia na Sarah alikuwa mikononi mwake, alikimbia mpaka juu na kuelekea dirishani, alipofika dirishani alifungua kioo na kumshika Sarah kwa kumning'iniza huku akijishauri amtupe chini, ila alihofia huyo mtoto anaweza kupoteza maisha kama ataanguka vibaya, au anaweza kuvunjika viungo na kipindi hicho Sarah alikuwa analia sana, wakati akiendelea kuwaza hayo, tayari sehemu ya nyumba ilianza kuporomoka na tayari moto ulikuwa umeshaanza kuenea juu ya ghorofa.



Wakati binti wa kazi akiwa anajishauri dirishani, huku mtoto akiwa amemning'iniza kwa nje, tofari lilitoka juu na kumponda kichwani dada wa kazi, na yule Dada alijikuta anamuachia Sarah na kuangukia chini umbali wa ghorofa moja, yule dada aliinguka na kupoteza fahamu ungali moto ukiendelea kushika eneo lote la ghorofa la juu.



Sarah aliangukia miguu na kupepesuka na kudondokea kisogo, akanyanyuka lakini alikuwa akihisi kizungu zungu, akajitahidi kusimama akimbie, akaanza kukimbia huku akikipesuka, alijitahidi kukimbia mita hamsini tu, akajikuta ameanguka na akapoteza fahamu, hakujua tena kilichoendelea.



*************************



Asubuhi kulikucha huku vyombo vya habari vikitangaza juu ya nyumba kuungua na watu wote waliomo ndani walitangazwa wamekufa isipokuwa mtoto mmoja mdogo ambaye hali yake haikuwa nzuri na kipindi hicho alikuwa mahututi.



Hii habari ilimkuta Taita akiwa mbele ya runinga yake huku akiwa amevaa pajama ya kulalia na mezani kulikuwa na chupa ya mvinyo na kiti cha pembeni yake alikuwa amekaa yule Jamaa mweupe mwenye tatoo mwili mzima pamoja na yule jamaa aliyetambulishwa kama mwanasheria.



Huyu Jamaa mweupe mwenye kipara na tatoo mwili mzima ndiye mlinzi wa Taita, ni mtu mmoja anaemuamini sana katika masuala ya kutumia silaha za moto, ni kijana aliyeacha kazi ya jeshi baada kwenda kinyume na sheria za jeshi, jina lake ni Malick Tasi, ila hapa anatumia jina la Trigger, jina la kifyatulio risasi, ni jina alilopewa tangu akiwa jeshini, jina hili alipewa kutokana na utumiaji wake wa silaha za moto, ni mtu mbaya sana ambaye akikunyooshea bastola kwa nia ya kukudhuru, uwa harudishi chini mpaka akupate, na lazima akupate hata kama ukiwa umbali mrefe, ili mradi tu bastola iwe na uwezo wa kurusha risasi kwa kiwango kinachotakiwa, ulevi wake ni wanawake tu.



Wa pili ni huyu mwanasheria, anaitwa Harry Denui, ni mhitimu wa chuo kikuu cha maarufu uko nchini uingereza, ana shahada mbili za sheria, na walijuana na Taita baada ya mwanasheria huyu kusimamia kesi yenye utata mkubwa na upande wa huyu bwana ulishinda, ni mtu maarufu sana hapa nchini na umaarufu wake umetokana na kushinda kwa asilimia kubwa katika kesi anazozisimamia.



Leo walikutana asubuhi kwa ajili ya kupanga namna Taita atavyoweza kukusanya haki zote za dada yake ambaye ndiye Magreth na muda huu alikuwa hayupo tena duniani.



"Tatizo lililopo ni ambalo ndio kikwazo ni yule binti kama ataendelea kuwa hai" Harry aliongea na kumtupia jicho Taita,



"Lakini Trigger ulikosea, ulivyomtupia ndani yule malaya mtoto, ungemfunga na kamba kabisa" Taita alijaribu kumtupia lawama kijana wake,



"Hapana, kwa kuwa moto ulishaanza kupamba ndani ya nyumba, kama angesema amfunge kamba yule mtoto, ni lazima amgeshindwa kutokana na ule moto kuwa mkali" Harry alimtetea Trigger,



"Basi yamepita, tusilaumiane. Je si inawezekana kummaliza yule mtoto pale pale hospitali?" Taita aliuliza huku akimuangalia Trigger,



"Inawezekana boss, ni kazi ndogo tu" Trigger alijibu,



"Basi mimi nitaenda hospitali kumuangalia kama mjomba wake, nikishatoka tu unatakiwa ufanye kazi hiyo" Taita aliongea,



"Je na yule mdogo wake uliyemchukua jana, una mpango gani nae?" Harry alimuuliza Taita,



"Yule mtoto nitamfanya awe mtoto wangu, si unajua sina mtoto na vizuri katoto chenyewe ni kadogo, hakana akili, kwa hiyo nitamlea kama mwanangu na hata akiwa mkubwa hatojua lolote" Taita aliongea kwa kujiamini,



"Unakosea, hawa watoto kuna kumbukumbu ndogo uwa wanakuwa nazo, kwa hiyo atakapokuwa mkubwa anaweza akajua ukweli" Harry alimshauri Taita,



"Kwa hiyo nimuue?" Taita aliuliza,



"Hapana, unatakiwa uende hospitali umpeleke akachomwe sindano ya kufuta kumbukumbu zake zote kichwani, yaani ubongo wake uanze upya, hapo itakuwa rahisi kumfanya utakavyo" Harry alimshauri Taita,



"Hilo ni wazo zuri, wazo safi kabisa" Trigger alimuunga mkono Harry,



"Basi sawa, inabidi hili litekelezwe mapema sana" Taita aliongea,



"Haraka iwezekanavyo" Harry alijibu,



"Sasa ngoja nijitayarishe ili niende hospitali nikamuangalie huyo Malaya mtoto" Taita aliongea huku akinyanyuka na kuingia chumbani kwake.



*******************



Ndani ya jengo liliteketea kwa moto, alikuwepo askari mmoja akikagua kagua ili kuangalia anaweza kupata kitu kitakachompa mwanga wa kujua hili tukio ni mipango au ni bahati mbaya, lakini kwenye pekua yake hakuweza kupata chochote zaidi ya picha ya familia iliyoungua upande wa chini na kufanya miguu ya wahusika isionekane, akatoa miwani mieusi machoni na kuiangalia kwa muda na kuiona namna ilivyokuwa imejaa vumbi, akaipulizia pumzi ya mdomo na kuifuta kwa kutumia kitambaa cheupe kilichokuwa mfukoni kwake.



Akapiga hatua za kutoka kwenye lile jengo na kuelekea kwenye gari yake ndogo na kuingia, akawasha gari na kufungulia mziki laini na kuliondoa gari kwa mwendo wa haraka.



Hii kesi alishahisi ni kuna mtu kuteketea kwa hii nyumba, maana majirani walisema muda mchache kabla nyumba haijaungua walisikia magari yakiondoka eneo hilo, na pia katika maiti zilizokutwa hakukuwa na maiti ya mtoto mdogo wa kiume hakionekana, kwa maana hiyo huyo mtoto huenda amechukuliwa au huenda hakuwepo? na kama hakuwepo atakuwa ameenda wapi na nani?. Hayo ni baadhi ya maswali aliyojiuliza mpelelezi huyo.



Safari yake iliishia nje ya hospitali ya kifahari ya binafsi, akaegesha gari lake na kwenda moja kwa moja kwenye mlango wa wodi moja na kusimama mlangoni, aliamua kusimama mlangoni baada ya kuona madaktari wakimpatia huduma mgonjwa aliyemuhitaji, ambaye ni mtoto Sarah.



Baada ya muda madaktari waliondoka na ndani akabaki daktari mmoja, mpelelezi akaingia,



"Karibu, mtoto huyu hapa amezinduka" Daktari aliongea, inaelekea wanajuana,



"Hakuna mtu aliyekuja kumuangalia?" Mpelelezi aliuliza,



"walikuja wafanyakazi wa wizara anayofanyia kazi mama yake" Daktari alijibu,



"Wamesemaje" Mpelelezi aliuliza,



"Hakuna, kwanza kipindi wanakuja bado mtoto alikuwa hajazinduka" Daktari alijibu,



"Ameongea tokea amezinduka?" Mpelelezi aliuliza,



"Hapana" Daktari alijibu na kipindi hiki ndipo Taita alikuwa anaingia wodini, alikuwa peke yake.



Alipoingia kwanza alishtuka kumuona Sarah akiwa amezinduka, akapata wasiwasi,



"Sarah unakumbuka jana nini kilitokea" Mpelelezi aliuliza na kumfanya Sarah amuangalie Taita, hapo sasa mapigo ya moyo ya Taita yakawa yanapishana bila mpangilio, yule mpelelezi akavua miwani na kumuangalia Taita kwa jicho kali.......





"Unamjua huyu?" Mpelelezi alimuuliza Sarah huku akimuangalia Taita, Sarah akakataa kwa kuyumbisha kichwa kushoto na kulia,



"Hana kumbukumbu vizuri, kuna baadhi ya vitu na watu hawakumbuki, nadhani aliangukia kisogo" Daktari aliongea huku akitabasamu,



"Bosi umekuja kumuona mtoto?" Mpelelezi aliuliza huku akimtupia jicho Taita,



"Ndio, ni Mjomba wangu kabisa huyu, mama yake ni mdogo wangu" Taita aliongea huku akitabasamu,



"Wewe ndio Taita? Nilikuwa nakutafuta. Naitwa Simon Frank, ila wewe niite Sai" Mpelelezi aliongea huku akivaa miwani yake na kumpa mkono Taita,



"Nashukuru kukufahamu, je kwanini unanitafuta?" Taita aliuliza,



"Mimi ndiye niliyepewa kazi ya kupeleleza juu ya moto ulioteketeza familia ya dada yako" Sajenti Minja alijibu,



"Si ni moto tu wa kawaida, inawezekana ni itirafu ya umeme, au labda unadhani nini?" Taita aliuliza huku wasiwasi ukimrudia tena, maana hakutegemea habari kama ile,



"Kwa maelezo ya majirani, inawezekana kabisa ile nyumba ilichomwa na watu" Mpelelezi yule aliongea na kufanya Taita ashtuke wazi,



"Hao watu wamepatikana?" Taita aliuliza,



"Bado, nadhani tutaongea zaidi kwa muda mwingine, hili eneo sio rafiki na maongezi yetu" Mpelelezi aliongea,



"Sawa afisa" Taita alijibu huku akishukuru kwa hayo maongezi kusitishwa,



"Sasa muheshimiwa huyu mtoto atabaki hapa kwa siku moja zaidi ili tuangalie hali yake" Daktari aliongea huku akimuangalia Taita,



"Sawa, nitakuja kumchukua nikaishi nae kwangu" Taita alijibu,



"Sawa, ila kuna mtu nae amesema atamchukua huyu mtoto ili akaishi nae" Daktari aliongea,



"Ni nani huyo mtu? mimi ndio nitakaa nae" Taita aliongea kwa ukali kidogo,



"Usipate shida, kesho uje umchukue, kwa maana wewe ni kama mwanao huyu" Daktari aliongea huku akitabasamu,



"Gharama za Huduma uliyompatia ni shilongi ngapi?" Taita aliuliza,



"Zimeshalipwa" Daktari alijibu,



"Ni nani huyo aliyelipa?" Taita aliuliza,



"Huyo mtu ambaye amesema atamchukua huyu mtoto" Daktari alijibu,



"Sawa, mimi natoka, akija tu huyo mtu umwambie akuachie namba zake ili tuwasiliane" Taita aliongea kisha akaondoka bila hata ya kuaga.



"Huyu Jamaa anaonekana mbabe mbabe sana" Mpelelezi aliongea huku akimuangalia Daktari,



"Huyu ndivyo alivyo, ila ni tajiri sana huyu, ana pesa chafu" Daktari alimuambia Mpelelezi,



"Haya bwana, acha mimi nirudi ofisini, ila unatakiwa umbadilishe huyu mtoto, mpeleke kwenye wodi nyingine" Mpelelezi alimshauri Daktari,



"Kwanini?" Daktari aliuliza,



"Mazingira ya vifo vya familia yake inaonekana wameuawa, nina wasiwasi kuwa huenda watu waliofanya hivyo wanaweza kurudi hapa kummalizia huyu mtoto"Mpelelezi aliendelea kumshauri daktari,



"Kweli aisee, basi inabidi utoke nae na kumpeleka wodi namba 543, ipo ghorofa ya juu kabisa, mimi nakuja" Daktari aliongea na kisha Sajenti Mpelelezi akambeba Sarah na kwenda nae nje ya wodi, Kisha akaingia kwenye lift na kupanda nae juu mpaka katika wodi aliyoelekezwa na Daktari, alipofika alimshusha Sarah na kumuweka juu ya kitanda,



"Nikuletee nini to too?" Mpelelezi alimuuliza Sarah, ila Sarah alijibu kwa kutingisha kichwa kwa ishara ya kukataa,



"Nitakuletea juisi baadae, lala mtoto mzuri" Mpelelezi aliongea huku akimlaza kitandani Sarah na kumfunika shuka zito, kisha Mpelelezi yule akatoka na kwenda zake ofisini kwake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

*******************



Taita alivyotoka ndani ya wodi, alienda moja kwa moja mpaka alipoegesha gari lake na kuingia ndani ya gari ambapo alikuwa Harry na Trigger,



"Trigger nenda kamalize kazi, utatukuta nyumbani" Taita aliongea,



"Wodi namba ngapi?" Trigger aliuliza huku akiitoa bastola yake ilikuwa chini ya kiti cha gari,



"Bastola ya nini tena, yule unamvunja tu shingo, mbona anashingo laini tu, alafu nenda kwa akili kwa maana kuna askari na daktari" Taita alitoa angalizo,



"Sawa mkuu" Trigger aliongea na kushuka ndani ya gari, akaanza kuelekea wodini, ndani ya gari akabaki Taita na Harry.



"Mtoto hajanikumbuka, Daktari anadai kuwa kuna baadhi ya kumbukumbu amepoteza" Taita alimwambia Harry huku akiwasha gari lake,



"Ila zitarudi, kumbukumbu za hivyo hazipoteagi Mara moja" Harry alijibu,



"Acha Trigger akammalize" Taita aliongea,



"Alafu suala la msiba linakuaje?" Harry aliuliza,



"Huu msiba utafanyika kwa wazazi wa ndugu wa mume, walinipigia asubuhi na kuniomba wachukue miili ya watu wote wawili" Taita alijibu,



"Hawajamuulizia mtoto mdogo wa kiume?" Harry aliuliza,



"Wanajua ameteketea na moto mpaka amekuwa majivu, ila kuna askari niliyemkuta ndani ya wodi, huyo anaweza kuwa kikwazo kwetu" Taita aliongea,



"Inabidi afe" Harry aliongea,



"Itabid iwe hivyo, ngoja Tri arudi nimpe hiyo mission" Taita aliongea huku akiliingiza gari lake ndani ya uzio wa nyumba yake.



"Msibani tunaenda muda gani?" Harry aliuliza,



"Nitaenda hata usiku" Taita alijibu,



"Hapo ndipo unakosea, ujue wewe ndio ndugu wa karibu kabisa wa Dada yako, unatakiwa ufike mapema ili mawazo juu ya maziko mkapange pamoja, hata Kama usipotia neno basi uwepo wako unaweza kuleta hisia nzuri kwa watu wanaojua uhusiano wenu" Harry aliongea huku akimtazama Taita,



"Muda huu nilitaka nimpeleke mtoto akachomwe sindano ya kupoteza kumbukumbu" Taita aliongea huku akiingia ndani na Harry akamfuata kwa nyuma,



"Lakini hiyo ya mtoto haina haraka sana, tutaifanya hata baada ya kumalizika msiba" Harry aliendelea kumshauri Taita,



"Lakini haya mambo ya msiba ni kama hayanihusu" Taita aliongea kijinga huku akigeuka,



"Hapo unakosea boss, inabidi twende kule msibani, usipoenda watu wanaweza kuhisi vibaya, na kama ulivyosema kuna askari wameanza kifuatilia lile tukio, itakuwa hatari upande wetu" Harry aliongea,



"Basi nimekuelewa, sasa kitu kingine ni huyu mtoto, sitaki ahishi hapa, mke wangu naijua roho yake, anaweza kumfanya kitu kibaya" Taita aliongea,



"Hilo ni sala zuri, twende kwanza msibani alafu tukirudi tutapanga" Harry aliongea,



"Haina shida, ngoja nikabadili nguo" Taita aliongea huku akielekea chumbani kwake.



**************



Trigger aliingia ndani ya hospital na kuanza kutembea koridoni huku akisoma namba za wodi katika kila mlango. Aliendelea kutembea kwa mwendo huo mpaka alipofika kwenye wodi namba nne, alisukuma mlango na kuingia, akukuta kitandani hakuna mtu, ila alimkuta daktari akikusanya vitu vyake, nadhani alikuwa anajiandaa kuondoka,



"Habari dokta, nilikuja kumuangalia mgonjwa wangu, ni mtoto mdogo wa kike, anaitwa Sarah" Trigger aliuliza huku akimuangalia Daktari,



"Wewe ni nani yake?" Daktari alimuuliza,



"Ni mdogo wa baba yake" Trigger alijibu,



"Oooh ni baba yake mdogo? mtoto tulimuamisha, yupo wodi namba 543" Daktari alijibu,



"Ipo upande gani hiyo wodi?" Trigger aliuliza,



"Nenda ghorofa ya mwisho juu, utaulizia uko" Daktari aliongea na Trigger akatoka wodini na kuelekea kwenye lifti, akapanda mpaka katika ghorofa aliyoelekezwa. Wakati anatoka ndani ya lifti, akakutana na mpelelezi,



"Samahani mista, eti wodi namba 543 ipo upande gani?" Trigger aliuliza na kufanya mpelelezi atie shaka kidogo,



"Wewe ni mgeni humu?" Mpelelezi aliuliza,



"Hujakosea, nipo hapa kumuona mtoto wa kaka yangu" Trigger aliongea,



"Elekea na hii korido mpaka kule mwisho, ingia kushoto wodi ya pili upande wa kulia" Mpelelezi alielekeza na kuingia ndani ya lifti.



Trigger akafuata maelekezo na kwenda moja kwa moja mpaka sehemu husika, alipofika alisukuma mlango na kumkuta Sarah akiwa amelala huku amefunikwa shuka zito mwilini.



Trigger akamsogelea kwa tahadhari na kumfikia, Sarah akafungua macho na kukutana na sura ya Trigger, uzuri ni kuwa alimkumbuka, Sarah akaanza kupiga kelele, Trigger akamuwahi na kumziba mdomo kwa mkono mmoja,



"Sssssssshiiii" Trigger aliongea huku akiwa ameweka kidole chake cha shaada kwenye midomo yake, alikuwa anatoa ishara ya kutaka Sarah ahache kelele, lakini Sarah aliendelea kukuruka pale kitandani, Trigger akajiona kama anapoteza muda, akachukua mikono yake na kuikamata shingo ya Sarah, Trigger akaongeza nguvu mikononi ili atimize lengo lake, alidhamiria kummaliza huyu malaika hasiye na hatia......







"Mwachie mtoto na ugeuke taratibu bila usumbufu wowote" Sauti ilisikika na Trigger akaisikia vyema masikioni make, Trigger akamuachia Sarah na kugeuka huku akitabasamu na kukutanisha macho yake na mtu aliemuelekeza wodi muda mfupi uliopita, alikuwa ni yule mpelelezi na mkononi alikuwa na bastola, na muda huo huo mtoto Sarah alitoka kitandani na kukimbilia nyuma ya mpelelezi,



"Shida nini tena, mbona kuna amani tu" Trigger aliongea huku mikono ikiwa juu



"Unamjua huyu?" Mpelelezi alimuuliza Sarah,



"Ndio" Sarah alijibu,



"Kwanini asinijue wakati mimi ni baba yake mdogo?" Trigger aliuliza huku akitabasamu,



"Ni baba mdogo kweli?" Mpelelezi alimuuliza Sarah,



"Sio, huyu alikuja jana usiku nyumbani" Sarah alijibu na ubongo wa mpelelezi ukafanya kazi haraka, akahisi kabisa huyu huenda anahusika na tukio la moto,



"Nenda nje, mtafute dokta yoyote ukakae nae" Mpelelezi aliongea na kumfanya Sarah atoke mbio mbio ndani ya wodi,



"Unataka kufanya nini sasa?" Trigger aliuliza huku tabasamu likiwa bado limemkaa,



"Upo chini ya ulinzi, hutakiwi kufanya chochote, geuka nyuma na uweke mikono nyuma ya kichwa" Mpelelezi aliongea kwa amri,



"Chini ya ulinzi kivipi? Kwanza angalia kidole chako ulivyokiweka kwenye kifyatulio, hakiko sawa na nikiamua kukufanya lolote naweza" Trigger aliongea kwa dharau na kufanya mpelelezi atupie jicho kidole kilichokuwepo kwenye trigger, ilo ndilo lilikuwa kosa lake, Trigger alituka juu na kuipiga teke ile bastola, bastola ikaseleleka mpaka mlangoni, kisha kwa ufundi wa hali ya juu akaachia ngumi Kali iliyotua sawia kwenye mdomo wa mpelelezi, mpelelezi akaenda chini na kutema damu, Trigger akaona hiyo ndio nafasi ya kuiwahi bastola, wakati anaanza kukimbia, mpelelezi akamdaka mguu na kumvuta, Trigger akaenda chini na kisha akarusha teke lingine lililomkuta shingoni mpelelezi, mpelelezi akamuachia, Trigger haraka akasimama na kwenda kuichukua ile bastola na kumuelekezea mpelelezi,



"Nyanyuka" Trigger alimwambia, mpelelezi akatii huku mikono ikiwa juu,



"Unachofanya unadhani ni sahihi?" Mpelelezi alimuuliza Trigger huku mikono ikiwa juu,



"Usahihi wa mtu upo kulingana na akiwazacho" Trigger alijibu huku akitabasamu,



"Sawa, shusha silaha chini" Mpelelezi alimwambia Trigger,



"Daima Trigger akimnyooshea mtu silaha uwa haishushi silaha chini mpaka risasi itoke" Trigger aliongea na safari hii hakuwa na tabasamu tena,



"Unamaanisha nini?" Mpelelezi aliuliza lakini hakupewa jibu, Trigger alifyatua risasi ilienda moja kwa moja katika kichwa cha mpelelezi, mpelelezi akarushwa mpaka dirishani, dirisha likapasuka vioo na mpelelezi akatokea dirishani mpaka chini, aliporomoka umbali wa ghorofa saba.



"Maana yangu ni hiyo" Trigger aliongea kisha akaitupia chini ya kitanda ile bastola na kisha akatoka ndani huku akikimbia. Alijiunga na watu wengine waliokuwa wanakimbia baada ya kusikia mlio ule wa bastola, Trigger akajichanganya nao na kuanza kukimbia kama na yeye ni mmoja wao vile, njiani wakati akishuka ghorofani alipishana na askari kadhaa wenye silaha wakipandisha juu.



Trigger alikimbia mpaka chini na kwenda eneo lile lile alipoanguakia yule mpelelezi, watu walishalizunguka eneo lile, Trigger akajisogeza na kupangua watu wawili watatu na kufanikiwa kuweza kumuona mpelelezi yule, alikuwa sio mtu tena, ulikuwa ni mwili tu usio na nafsi, yaani tayari mpelelezi alikuwa ni marehemu, Trigger akatoa tabasamu dogo na kisha akaanza kupangua watu ili aweze kutoka, aliwapangua na kutoka kwenye lile kundi la watu, akaanza kuelekea nje ya geti, alitoka nje ya geti la hospitali na kusimamisha usafiri, akapanda na kupelekwa moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Taita.



Alimkuta Taita akiwa anajiandaa na safari ya kwenda msibani,



"Nadhani umemaliza kazi" Taita aliongea huku akifungua mlango wa gari lake,



"Misheni imefeli" Trigger aliongea kwa sauti tulivu na kufanya Taita ashtuke na asitishe mpango wa kufungua mlango wa gari,



"Kipi kilichokufanya ukashindwa?" Taita aliuliza kwa ukali,



"Wakati natekeleza mpango alitokea askari mwenye silaha, ndio alinikwamisha" Trigger alijibu,



"Oooh shit, alafu nini kikafuata mpaka umerudi Salama?" Taita aliendelea na maswali,



"Nilimdhibiti yule askari, nikamuua ndipo nikafanikiwa kukimbia" Trigger alijibu,



"Safi, je mtoto hukumuona tena?" Taita alihoji,



"Sijabahatika kumuona tena, nadhani alienda kujiweka sehemu Salama zaidi" Trigger alijibu,



"Sawa, mimi naelekea msibani, nadhani wewe unapaswa kurudi kule hospital ili ukaendelee kufuatilia nyendo za mtoto" Taita aliongea huku akiingia ndani ya gari,



"Sawa, Harry yupo wapi?" Trigger aliuliza,



"Nitamkuta mbele uko, kuna sehemu ameenda" Taita alijibu,



"Safari hii inabidi niende na gari ili niwe huru zaidi" Trigger aliongea na kufanya Taita ajisachi na kutoa ufunguo wa gari na kumkabidhi Trigger,



"Chukua ile harrier nyeusi, ipo hapo mtaa wa nyuma inaoshwa, kuna tatizo jingine?" Taita aliuliza,



"Hakuna, kama litatokea tutawasiliana" Trigger aliongea kisha Taita akawasha gari na kuliondoa taratibu na kupotea eneo hilo na kumuacha Trigger akimtazama.



Taita aliendesha gari mpaka mtaa unafuatia na kumkuta harry akimsubiri hapo, akampakia kwenye gari na kisha wakaanza safari ya kwenda msibani.



Ndani ya gari Taita alimueleza Harry kila kitu kuhusu Trigger kutofanikisha mpango wa kumuua Sarah na kisha akamueleza ni kitu gani amemuagiza akakifanye.



"Hili jambo la kummaliza linatakiwa liwe la haraka, maana yule mtoto ni mkubwa na anajua kila kitu kilichotokea kuhusu wazazi wake" Harry aliongea,



"Ila nitafanikisha tu, maana nikishamchukua na kuishi nae ndipo nitamuua kirahisi" Taita aliongea,



"Hiyo usiiwaze, anaweza kutuchoma hata kabla hujamchukua, wewe fikiria kama aliweza kumtambua Trigger anashindwa vipi kukutambua wewe?" Harry aliuliza,



"Madaktari wamesema kumbukumbu zake haziko sawa" Taita aliongea,



"Upuuzi mtupu, kama kumbukumbu zake hazipo sawa amemtambuaje Trigger, ni ujinga kuendelea kufikiria hivyo" Harry aliongea huku akionekana kutofurahishwa na mawazo ya boss wake,



"Ebu ngoja tukitoka uko msibani tutapanga vizuri" Taita aliongea kwa utulivu,



"Mmh sawa" Harry aliishia kuguna tu kisha ukimya ukatawala.



Gari lilitembea kwa mwendo mrefu na atimae lilifika eneo lenye msiba. Taita aliposhuka tu, wanawake ambao walikuwa wakifahamu uhusiano wake na magreth wakaanza kuangusha kilio upya, yaani utasema wamepokea habari hizo muda huu.



"Broo unatakiwa uingie ndani moja kwa moja" Kijana mmoja aliongea sikioni kwa Taita, inaelekea huyu kijana ni ndugu wa Isack ambaye ni baba yake Sarah.



Taita akaelekea moja kwa moja sehemu aliyotakiwa na kuingia ndani ambapo aliwakuta wazazi wa Isack na ndugu wengine, Taita akawasalimia na kuoneshwa sehemu ya kukaa,



"Mbona umechelewa mwanangu?" Baba Isack alimuuliza,



"Asubuhi niliamkia hospitali ili nikamuangalie Sarah hali yake ipoje" Taita akajitetea,



"Vizuri, anaendeleaje mjukuu wangu?"Baba Isack aliuliza,



"Mzima kabisa, kesho anaweza kuruhusiwa, nitamchukua na kuishi nae" Taita alijibu,



"Na yule mwingine mdogo yeye ndio ameteketea kabisa kawa majivu" Baba isack aliongea kwa uchungu,



"Dah, ni mipango ya Mungu" Taita alijibu,



"Sasa hapa sisi tumeshapanga maziko, tumeamua kupanga mapema baada ya kukusubiri muda mrefu na hukutokea, kwa hiyo hapa tunachongoja kutoka kwako ni kuridhia na kubariki mipango yetu" Baba Isack alizungumza na kumtupia jicho Taita,.



"Mmepanga yafanyike lini?" Taita aliuliza,



"Leo hii saa kumi" Baba Isack alijibu,



"Kwanini tusimsubiri mtoto aruhusiwe hospitali hili naye ashiriki maziko ya wazazi wake?" Taita aliuliza,



"Hata sisi tulitaka iwe hivyo, ila kwa jinsi ile miili ilivyoharibika, ni ngumu sana kuacha mpaka kesho" Baba Isack alijibu



"Sawa, mimi nimeridhia" Taita aliongea kwa upole,



"Nashukuru sana kijana wangu, nadhani cha muhimu ni kwenda tu monchwari kuisafisha miili ili mpaka saa saba iwe imefika hapa na mipango ya kuaga miili ianze" Baba Isack alizungumza na watu kadhaa wakamuunga mkono, kisha wakatoka baadhi ya ndugu wa marehemu wakiambatana na Taita na wakaelekea hospitali kwa ajili ya kuitayarisha miili ya marehemu.



*********************



Trigger alikuwa ameegesha gari lake ndani ya uzio wa hospitali huku akijaribu kuyasoma mazingira ya pale vizuri. Wakati akiwa bado anapiga hesabu zake ndipo alipomuona daktari akiwa ameongozana na Sarah na mwanaume wa makamo ambaye ni Mzungu. Trigger akayaweka macho yake umakini mkubwa, akaweza kuona daktari akitoa maelezo kwa yule Mzee wa kizungu, ila Trigger hakuweza kusikia neno lolote kwa kuwa alikuwa mbali kidogo.



Trigger aliendelea kushuhudia daktari akiongea na yule Mzee Mzungu na kisha akaona wakipeana mikono, alafu yule Mzee wa kizungu akaondoka huku akiwa ameongozana na Sarah na kuingia kwenye gari moja la kifahari, kisha ile gari ikaondoka kwa mwendo wa taratibu.



Baada ya lile gari kutoka nje ya geti, Trigger nae aliondoa gari lake na kuanza kuifuata ile gari huku akiwa anaangalia namna ya kupanga mashambulizi ya kummaliza Sarah.



Zile gari ziliendelea kufuatana huku zikiwa zimeachana umbali kidogo, walipofika eneo ambalo kulikuwa na pori kidogo, Trigger akaongeza mwendo na kuipita kabisa ile gari ya Mzee wa kizungu, tena akaiacha mbali kiasi kwamba hakuiona, alifanya hivyo makusudi baada ya kutengeneza mipango yake.



Trigger alienda na kusimamisha gari pembeni ya barabara, akashuka na kuanza kusubiri. Baada ya dakika tano ilitokea ile gari ya Mzee wa kizungu na Trigger akajifanya kama anatengeneza gari lake, yaani aliigiza gari lake limeharibika.



Gari la Mzee wa kizungu lilipomkaribia Trigger akalipiga mkono na likasimama pembeni ya barabara, Trigger akatazama kioo cha mbele kwa jicho la chini ili aone watu waliomo ndani ya gari, akamuona ni yule Mzee wa kizungu na Sarah tu, akajikuta anatabasamu na kuishusha kofia yake chini zaidi ili Sarah asimtambue.



Trigger akawa anasogea katika gari ya yule Mzee wa kizungu,



"Samahani Mzee gari yangu imeniharibikia, naomba msaada" Trigger aliongea huku akiwa amesimama katika dirisha la gari.



"Unataka msaada gani sasa?" Mzee wa kizungu aliuliza,



"Nataka maji, nahisi rejeta imeisha maji" Trigger aliongea huku mkono wake ukianza kuivuta bastola ndogo iliyopo kiunoni upande wa nyuma, Trigger mtu mbaya alidhamiria kuua, na kawaida yake ni kwamba akikunyooshea bastola uwa haishushi mpaka itoe risasi.......





"Rejeta imechemka sio?" Mzee wa kizungu aliuliza huku akifungua mlango wa gari na kipindi hicho hicho kulikuwa na gari ya polisi ikija eneo hilo na kufanya Trigger ahache kufanya alichotaka,



"Ngoja nikupe maji kijana, uwa natembea na maji ya kutosha" Mzee wa kizungu aliongea huku akifungua mlango wa nyuma wa gari na kuchukua chupa moja ya maji ya dukani na kumpatia Trigger na kipindi hicho lile gari la polisi lilikuja na kusimama hapo hapo.



"Vipi Mzee kuna usalama?" Polisi mmoja aliuliza huku akimtazama yule Mzee wa kizungu,



"Hapa kuko Salama, huonekani siku hizi" Mzee wa kizungu alijibu na kuonesha kuwa anafahamiana sana na yule polisi,



"Hili eneo sio zuri, tulidhani umepata tatizo mheshimiwa" Polisi yule alizungumza,



"Msipate shida, nilikuwa namsaidia kijana maji, gari yake imemuhishia maji, hata hivyo nimemaliza tayari" Mzee wa kizungu aliongea huku akiingia kwenye gari lake na kisha akaagana na polisi na kuliondoa gari taratibu, na polisi nao hawakuwa na kitu cha ziada, nao wakaondoa gari lao na kufuata uelekeo ule ule alioenda nao yule Mzee wa kizungu.



Akabaki Trigger akiwa ameinamia injini ya gari lake huku pia akiwatizama polisi kwa jicho la chini chini wakati polisi hao wakiondoka.



"Mbona amenitoka kipumbavu hivi?" Trigger alijiuliza huku akifunga boneti ya gari lake na kuifungua ile chupa ya maji na kunywa yale maji mpaka yalipofika nusu chupa, akauendea mlango wa gari na kuufungua kisha akaingia, akawasha gari na kutulia huku akionekana kuna kitu anafikiria,



"Bado nina nafasi, ngoja nijaribu kuifuata njia aliyoondoka nayo, naweza kumuona" Trigger aliongea peke yake kisha akaiingiza gari barabarani na kuishika ile njia aliyoelekea yule Mzee wa kizungu.



Baada ya dakika tano Trigger aliweza kuliona kwa mbali gari la yule Mzee wa kizungu, Trigger akaongeza mwendo na kulisogelea ingawa sio kwa karibu sana.



Na pia trigger alishindwa kufanya kitu eneo hilo kutokana na eneo kuwa na watu na pia msongamano wa magari tofauti na lile eneo la kichakani ambalo alishindwa kutimiza adhma yake.



Trigger aliendelea kulifuatilia lile gari huku sasa dhamira yake ikimtuma kuwa huenda yule Mzee wa kizungu anaenda nyumbani kwake, akapanga atamfanyia shambulio Sarah endapo hiyo gari itasimama nje ya nyumba ya huyo mzee wa kizungu.



Trigger akaishuhudia ile gari ikikunja kushoto ambapo barabara haikuwa na lami, na yeye Trigger akakunja kisha ile gari ikanyooka na njia ile mpaka katika nyumba moja ambayo magari yalikuwa yameegeshwa mengi nje ya ile nyumba na pia kulionekana watu wamejaa, ni eneo ambao kulionekana na msiba. Kitu kilichomshtua Trigger ni kuikuta na gari ya Taita, hapo sasa akajua kuwa ametokezea msibani, nyumbani kwa baba yake Isack ambaye ndiye babu yake na Sarah.



."Huyu mtoto ana nini?" Trigger alijiuliza kwa hasira huku akiuma meno baada ya kumkosa Sarah kwa Mara nyingine tena.



Na wakati huo Sarah alikuwa anashushwa kwenye gari na yule Mzee wa kizungu, Sarah alipotelemka tu na vilio vya kinamama vikaanza upya, kila mmoja alilia kwa uchungu huku wakimtazama Sarah, bahati mbaya Sarah wala hakuonekana kujali, sijui ni kutokana na utoto wake au alihisi uchungu ila hakujua namna ya kuufikisha kwa hadhira.



Trigger hakuwa na sababu ya kutoka eneo hilo, aliona bora aendelee kuwepo na isitoshe aliliona gari la bosi wake hapo, akaamini kabisa Taita atakuwepo hapo. Trigger akatelemka ndani ya gari na kwenda kuliegemea gari la Taita huku akiitoa simu yake mfukoni na kuanza kuicheza game.



*******************



Mzee wa kizungu aliposhuka na Sarah alielekea moja kwa moja kwa moja ndani ambapo aliwakuta watu wengine wapo huko baada ya kutoka kuichukua miili ya marehemu hospitali. Mzee wa kizungu alipofika aliwasalimia na kukaa juu ya kochi.



Huyu Mzee anaitwa Mark McFadden, ni boss wa Isack ambaye ni baba yake Sarah, ni mtu aliyekuwa anampenda sana Isack kutokana na utendaji wake wa kazi, na hata Isack alipokatika miguu kutokana na ajali aliyopata wakati akiwa katika shughuli za kikazi, bado aliendelea kupokea mshahara wake ingawa alikuwa haendi tena kazini, na huyu Mzee alikuwa karibu sana na familia ya marehemu Isack na kila mwisho wa wiki alikuwa anajumuika na familia hii. Mark ni raia wa uingereza na familia yake ipo huko, hapa Tanzania kuweka tu tawi la kampuni yake ambayo inajihusisha na mambo ya kusafirisha mizigo kutoka nchi mbalimbali.



Baada ya Mark kukaa, Sarah alikimbilia kwa babu yake, na muda wote alikuwa anamtupia jicho Taita, na kila wakikutanisha macho na Mjomba wake huyo, Sarah alikimbilia mgongoni kwa babu yake, hiyo hali ilizidi kumuongezea hofu Taita, ila uzuri ni kuwa hakuna aliyeona kitu kilichokuwa kinaendelea isipokuwa Mark pekee ambaye muda wote macho yake yalikuwa kwa Sarah.



"Na huyu ni nani?" Taita aliuliza huku akimuangalia Mark,



"Huyu ndiye bosi wa Isack baba yake Sarah" Baba Isack alijibu,



"Naitwa Mark" Mark aliongea na kunyanyuka na kewnda kumpa mkono Taita,



"Sawa" Taita alijibu huku nae akipeana mikono na Mark.



"Nadhani sasa ni wakati wa kuitoa miili ya marehemu ili watu waage tayari kwa maziko" Baba Isack aliongea,



"Waage vipi tena? Mzee huoni miili ilivyoharibika vile kwa moto?, mi naona tukazike tu" Mdogo ake Isack aliongea,



"Kweli, mimi nadhani ikazikwe tu, ile miili haifai watu waione, maana inatisha sana" Taita aliunga mkono,



"Basi sawa, nadhani mkawaambie watu wajitayarishe uko nje, baada ya dakika kumi tutaelekea kuipumzisha miili ya wapendwa wetu" Baba Isack aliongea na kisha Mzee mmoja wa makamo akaelekea nje kuyafikisha maneno hayo kwa watu waliohudhuria hapo msibani.



Baada ya robo saa majeneza yalitolewa nje na kupakiwa katika gari, safari ya kwenda kuwapumzisha ikaanza.



Makaburi haya kuwa mbali sana, iliwachukua dakika tano kufika makaburini na shughuli nyingine za maziko zikaanza, wapo waliozimia baada ya kushuhudia majeneza yale yakifukiwa na udongo na wapo waliolia sana, basi ilikuwa ni huzuni mkubwa miongoni mwa ndugu, Jamaa na marafiki.



Baada ya muda mrefu kidogo ule msafara ulikuwa umeshamaliza kuwazika wapendwa wao na sasa walikuwa wanarudi nyumbani, iliwachukua chache kufika nyumbani na baadhi ya watu walitawanyika baada ya maziko, kwa hiyo walibaki watu wachache tofauti na mwanzo.



Ndani ya nyumba walikuwepo ndugu na watu wa karibu wa familia, kulikuwa na majadiliano,



"Jamani najua dunia ya sasa hivi ilivyo ya pilika pilika ni ngumu sana kama tukisema tusubiri mpaka siku ya tatu ndio tujadili hili suala, naona tujadili muda huu tukiwa tumekamalika hapa, tujadili mustakali wa Sarah pamoja na mali zake" Baba Isack aliongea na kuwatazama wanandugu,



"Suala la Sarah lisikuumize kichwa, nitaishi nae mimi" Taita aliongea kwa kujiamini,



"Huyu mtoto tayari anatakiwa nisafiri nae niende nae uingereza, kabla baba yake hajafa tulishaongea nae hilo na akakubali na hivi ninavyoongea na nyinyi tayari tulishamuombea nafasi ya masomo na amekubaliwa, baadhi ya fomu tumeshajaza na gharama pia nimetumia, jumatatu anatakiwa asafiri kwa ajili ya hilo" Mark aliongea kwa unyenyekevu,



"Hilo haliwezekani, kwanza unaongea kama nani? wewe sio ndugu ni rafiki tu wa familia" Taita aliongea kwa jazba,



"Ila ameongea jambo zuri, suala la masomo ni kitu vizuri, mimi ningeshauri umkubalie tu aende uko uingereza akasome" Baba Isack aliongea kwa kusihi huku akimuangalia Sarah,



"Swali ni kwamba yeye amchukue Sarah kama nani?" Taita aliuliza kwa ukali,



"Basi silazimishi kumchukua, kama mnaona ni sawa kubaki nae haya" Mark aliongea huku akilazimisha tabasamu,



"Ila shemeji, ni bora mtoto aende kusoma uko uingereza, si unajua elimu za wenzetu zipo juu kidogo" Mdogo wake Isack aliongea,



"Kwani shemeji mimi siwezi kumsomesha huyu mtoto uingereza?" Taita aliuliza huku akimtazama shemeji yake huyo,



"Sikuwa na maana hiyo, ila kama inawezekana kumsomesha uko sawa" Mdogo wake Isack aliongea kwa upole,



"Sawa tunefikia makubaliano kuhusu hilo, mtoto ataondoka na Mjomba wake. Je na vipi kuhusu mali za marehemu mama yake?" Baba Isack aliuliza huku akimtazama Taita,



"Zipo zote, uzuri ni kwamba kila kitu kupo wazi na uzuri zaidi ni kwamba mwanasheria wa mama yake nae ana ushahidi" Taita aliongea huku akitabasamu,



"Sawa, tutaongea na mwanasheria wa mama yake" Baba Isack aliongea,



"Na vipi kuhusu Mali zake, ambazo zimeachwa na wazazi wake kwa ujumla?" Taita aliuliza,



"Zipo Salama, na makabrasha yote yenye kuelezea mali ziliachwa na familia yake, ninayo" Mark aliongea huku akiweka mkoba ulioonekana una makaratasi,



"Huu mkoba utabaki hapa" Baba Isack aliongea huku akiuangalia ule mkoba,



"Huu nimeuleta ili mkae nao" Mark aliongea huku akitabasamu,



"Sasa nadhani vya muhimu vyote tumevimaliza, kikao kiishe na hivyo vilivyobaki tutaongea siku nyingine" Baba Isack aliongea,



"Sawa, naomba niondoke sasa" Taita aliongea huku akisimama,



"Nenda na mwanao, au unamuacha kwanza nikae nae?" Baba Isack aliongea huku akitabasamu,



"Naenda nae" Taita aliongea na kumuita Sarah, cha ajabu Sarah alimkataa kabisa, yaani kila Taita alipomuita, Sarah alikimbilia nyuma ya mgongo wa babu yake. Walimbeleza na wakatumia ukali lakini mtoto alikataa, Taita akatumia ubabe akambeba, Sarah alipiga kelele ikabidi babu yake amwambie Taita amuache,



"Utakuja kumchukua kesho" Baba Isack aliongea baada ya Sarah kushushwa na kukimbilia mapajani kwa Mark,



"Sawa" Taita aliongea na kuondoka huku akijilaumu kumkosa Sarah, Taita akaenda nje na kukutana na wenzake kisha wakaondoka.



Mark nae akaona aondoke, ila Sarah akawa anamlilia, mwisho wakamruhusu aende nae kwa makubaliano ya kumrudisha siku itakayofuta ambayo itakuwa jumapili.



Mark akaondoka na Sarah.



*****************



Siku iliyofuata ambayo ilikuwa ni jumapili, Mark alienda kanisani huku akiambatana na Sarah, uzuri ni kuwa siku hiyo hata Taita na wenzake walikuwa wamehudhuria kanisani hapo.



Wakati misa ikiwa mwishoni, ni kawaida kwa kanisa hilo itoe nafasi kwa mzee mmoja, kijana mmoja na mtoto mmoja kwa ajili ya kwenda mbele na kusali kwa niaba ya wenzake.



Alianza Mzee akaomba, akafuata kijana na nafasi ya mwisho ilimuangukia Sarah, Sarah alienda mbele ya kanisa na kuwekewa kipaza sauti mdomoni, kisha akawaomba waumini wafumbe macho, kisha kwa hisia na sauti ya kawaida kabisa, Sarah alisema,



"Mungu naomba niwe mkubwa, na niwe nawaka kama moto" Sarah alipomaliza kusema hivyo alirudisha kipaza sauti na kuacha waumini wakishangaa na wengine walicheka kabisa, ila Taita peke yake aliyekaa kiti cha mbele ndiyo alionekana ameguswa na hiyo sala ya Sarah..........







Taita aliinuka katika kiti hata kabla misa haijsisha na kuelekea nje, alipofika aliingia katika gari lake na kuchukua simu na kumpigia Trigger,



" uko upande gani?" Taita aliuliza baada ya simu kupokelewa,



"Niko nje ya uzio wa kanisa" Trigger alijibu,



"Njoo kwenye gari yangu" Taita aliongea kisha akakata simu.



Baada ya dakika Trigger alikuwa ndani ya gari ya Taita,



"Aisee yule Mzee wa kizungu yupo kanisani na Sarah, sasa itabidi umfuatiliea na ujue anapokaa" Taita aliongea,



"Yupo na Sarah kivipi wakati ulisema jana mlikubaliana Sarah abaki kwa babu yake?" Trigger aliuliza,



"Hilo limenishangaza, wewe fanya nilichokuagiza na mimi nitalifuatilia hilo" Taita aliongea na wakati huo na waumini wengine walianza kutoka ibadani ikiwa na maana misa imekwisha.



Taita aliweza kumshuhudia Mark akitoka ndani ya kabisa huku akiwa amemshika mkono Sarah na kuelekea kwenye gari la kifahari lilikuwa limeegeshwa eneo husika na kisha lile gari likatoka taratibu huku Taita akiliangalia,



"Imekuaje yule Mzungu yupo na Sarah?" Harry aliuliza huku akiingia ndani ya gari,



"Wamenigeuka wale wazee wapuuzi sana, ebu twende uko" Taita aliongea kisha akawasha gari na safari ilipangwa iishie kwa baba isack.



Iliwachukua takribani dakika kumi kufika nyumbani kwa Baba Isack, na bahati nzuri waliweza kuikuta na gari ya Mark ikiwa imeegeshwa nje ya ile nyumba.



"Nisubiri, nakuja" Taita aliongea na kutelemka katika gari kisha akaelekea ndani huku akionekana mwenye hasira.



Aliingia moja kwa moja sebuleni na kuwakuta baadhi ya ndugu wa marehemu Isack wakiwa wamekaa, Taita akawasalimia na kisha akakaa kwenye kochi,



"Sasa Mzee wangu imekuwaje huyu Mzungu amchukue Sarah? jana tulikubaliana nini au mmenigeuka?" Taita aliuliza maswali mfululizo huku akimtazama Baba Isack,



"Mwanangu bora umuache mtoto aende kusoma uko, kwa maana huyu bwana Mark amekuja na mikataba aliyoingia na baba Sarah kuhusu huyo mtoto na pia gharama alizotumia ni kubwa katika kushughulikia hiyo safari na shule atakayoenda kusoma uko" Baba Isack aliongea kwa upole,



"Kwa hiyo mmeuza mtoto?" Taita aliuliza,



"Hapana hajauzwa, ila baada ya masomo atarudi na utakaa nae kama unavyotaka" Mark alijibu,



"Kwani gharama ulizotumia ni shilingi ngapi?" Taita aliuliza huku akimuangalia Mark,



"Milioni mia hamsini tu" Mark alijibu,



"Nitazilipa" Taita alijibu,



"Sioni sababu ya kuingia hasara kuzilipa, muache akasome tu" Baba Isack alijibu,



"Kwa hiyo mpo upande wa huyu Mzungu?" Taita alihoji,



"Tupo upande wa mtoto, tunataka awe na maisha mazuri" Baba Isack alijibu,



"K wangu hatokuwa na maisha mazuri?" Taita aliuliza,



"Sijamaanisha hivyo, ila mimi kama babu nimependekeza mtoto akasome uko uingereza" Baba Isack aliongea na kufanya Taita ainuke na kuondoka kwa hasira na kuwaacha watu wakimshangaa.



Taita alitoka mpaka katika gari yake na kumkuta Trigger akiwa na Harry,



"Mtoto anatakiwa aende uingereza, tena safari ni kesho" Taita aliongea baada ya kuingia katika gari,



"Na wewe umekubali?" Harry aliuliza,



"Nimepinga ila watu wote ndani wanataka mtoto aende akasome uko" Taita alijibu kinyonge,



"Huyu Mzee wa kizungu anatakiwa afe leo, yeye na Sarah" Harry aliongea,



"Wanakufaje sasa?" Taita aliuliza,



"Trigger hakikisha unamfuatilia huyu Mzungu kila hatua leo mpaka upajue kwake na kisha usiku utaenda kummaliza, ni lazima atakuwa na Sarah tu" Harry aliongea,



"Hilo jambo ni zuri, ebu Trigger fanya hivyo" Taita aliongea,



"Sawa bosi" Trigger alijibu,



"Sasa sisi acha tuondoke, wewe endelea kumfuatilia huyu mzungu" Taita aliongea kisha akawasha gari na kuondoka.



Trigger aliendelea kuwepo maeneo yale, alisubiri kwa muda saa nzima na ndipo alipoweza kumuona Mark akitoka ndani huku akiwa na Sarah, walipotoka walielekea moja kwa moja katika gari na kuingia kisha wakaondoka.



Trigger akasubiri sekunde kadhaa kisha nae akaingia katika gari yake na kuanza kushika uelekeo ule ule ilipoelekea gari ya Mark.



Kwa mbali aliweza kuiona gari ya Mark. Trigger akapunguza mwendo na kuanza kuifuatilia kwa mbali ile gari ya Mark. Walitembea hivyo kwa dakika nyingi mpaka ile gari ya mark ilipoenda kuingia katika nyumba moja ndogo ila ya kisasa.



Trigger akasimamisha gari kwa mbali na kuanza kuangalia lile geti la nyumba ile na pia alikuwa anajaribu kuona kama atajua idadi ya watu wa mule ndani, kwa maana mpaka hapo alikuwa ameshajua idadi ya watu watatu ambao ni Mark, Sarah na mlinzi wa getini.



Trigger akiwa bado yupo pale akisoma mazingira, aliweza kuna gari jingine dogo la rangi nyeusi likiingia ndani ya ile nyumba, Trigger ikaendelea kusubiri, alipanga kujua kila kitu kwa muda huo ili usiku akija aje huku akiwa anajua pa kuanzia na pa kumalizia.



Baada ya masaa mawili Trigger aliweza kuna geti la ile nyumba likifunguliwa na akaiona ile gari ndogo nyeusi ikitoka na kusimama nje ya geti kisha Mark akatoka ndani ya geti na kuongea kidogo na yule dereva wa gari ambaye alikuwa ni kijana wa kizungu kisha wakaagana na ile gari ikaondoka na Mark akabaki peke yake kisha akarudi ndani na kurudishia geti.



Trigger ikaendelea kukaa pale mpaka giza lilipoanza kuingia na yeye akawa amepata kitu akitakacho, akawasha gari na kuondoka huku akijiaminisha kuwa ndani ya nyumba ile wapo watu watatu tu, ambao ni mlinzi, Mark na Sarah.



Trigger alirudi mpaka nyumbani kwa Taita na kuwakuta Taita na harry wamekaa katika bustani huku wakinywa kahawa,



"Umefanikisha?" Taita alimuuliza Trigger,



"Nimefanikisha kujua anapokaa na nimeweza kuangalia mazingira ya pale na nimeona panaingilika kirahisi tu" Trigger alijibu,



"Hakuna mlinzi hapo anapokaa?" Harry aliuliza,



"Yupo security guard mmoja tu pale getini, najua jinsi kumuingilia" Trigger alijibu,



"Inabidi hii mission ifanyike usiku wa leo" Taita aliongea,



"Tena naenda saa mbili tu" Trigger aliongea,



"Saa mbili mbona mapema?" Taita aliuliza,

.



"Ukienda usiku sana unaweza kufanya mlinzi aingie wasiwasi, inabidi niwahi ili niingie kama mgeni" Trigger alijibu,



"Utaenda peke yako au nikupe vijana wa kukuongezea nguvu?" Taita aliuliza,



"Mwenyewe tu, watu watatu hawawezi kunishinda" Trigger alijibu huku akitabasamu,



"Basi sawa, nenda kajiandae na hakikisha gari ni nzima na ina mafuta ya kutosha" Taita aliongea,



"Sawa" Trigger aliongea na kisha akaondoka zake na kuwaacha Taita na Harry wakimuangalia,



"Hili Jamaa ni jembe sana, mchezo ya kuua linaiweza sana" Harry aliongea wakati Trigger akiondoka,



"Sijui kama atafanikiwa leo, maana huyu mtoto kumuua imekuwa ngumu" Taita aliongea kivivu huku akijikuna kitambi chake.



********************



Mishale ya saa mbili usiku ilimkuta Trigger akiwa anajongea kwenye nyumba ya mark, alipofika aligonga geti na mlinzi akafungua,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Habari yako bwana" Trigger alitoa salamu,



"Safi, nikusaidie nini?" Mlinzi aliuliza huku akimuangalia Trigger,



"Nataka nionane na boss" Trigger aliongea kwa upole,



"Una mihadi nae?" Mlinzi aliuliza,



"Ndio" Trigger alijibu huku akitabasamu,



"Ngoja nikamuulize. Unaitwa nani kwanza?" Mlinzi aliuliza,



"Mr Danny" Trigger alijibu na mlinzi akawa anaelekea ndani, ila kosa alilofanya mlinzi ni kuacha mlango wa geti ukiwa wazi,



Baada ya sekunde chache mlinzi alirudi getini na kukuta hamna mtu, akatoka nje ya geti ili kuangalia, na ndipo hapo hapo Trigger akatoka haraka kwenye kibanda cha mlinzi na kuingia sebeleni kwa Mark, akamkuta Mark akitazama runinga, Trigger akafunga mlango kwa ndani na kuchomoa bastola na kumuelekezea Mark, na muda huo huo vikasikika vishindo vya mtu akija katika mlango wa mbele,



"Boss" Sauti ya mlinzi ilisikika ikiita na Trigger akampa ishara Mark akimtaka aitike,



"Sema" Mark aliitika,



"Mtu mwenye ameondoka" Sauti ya mlinzi iliongea,



"Sawa, kuwa makini getini hapo, usiruhusu mtu kuingia" Mark alijibu,



'Sawa boss" Mlinzi alijibu na vikasikika vishindo vyake akielekea getini.



"Boss nimekuja kwa jambo moja tu, namtaka Sarah" Trigger aliongea huku akiwa amemkazia macho Mark,



"Mmewaua wazazi wake na bado mnaitaka roho yake" Mark aliongea huku akimtazama Trigger,



"Sijaja kujadiliana hapa" Trigger aliongea kwa jeuri,



"Mimi najua kila kitu, Sarah ameniambia yote" Mark aliongea kwa lengo la kumuogopesha Trigger,



"Unajua kila kitu eee? Kama nini unachokijua?" Trigger aliuliza huku akitabasamu,



"Wewe ni kibaraka tu wa Taita, nyie ndiyo mlimchoma Isack na familia yake ndani na mkamuiba mtoto wake mdogo wa kiume, Sarah anajua vyote na msidhani ni mdogo kiasi kwamba ashindwe kuwajua" Mark aliongea huku akimtupia jicho Trigger,



"Kweli unajua kila kitu, nimeridhika" Trigger aliongea na kutabasamu,



"Hakuna cha kuficha, najua kila kitu, siri zenu zote" Mark aliongea,



"Sawa unajua kila kitu, ila hujui kitu kimoja tu" Trigger aliongea na kuacha kutabasamu,



"Nini nisichokijua?" Mark aliuliza,



"Hujui kifo" Trigger aliongea na kukaza macho,



"Unamaanisha nini?" Mark alihoji huku hofu ikimshika, lakini Trigger wala hakuongea kitu, akairuhusu risasi utoke katika bastola yake na kwenda kumpiga Mark katika kichwa, Mark akafa pale pale,



"Hiyo ndiyo maana yangu" Trigger alijibu na wakati huo huo huko nje vilisikika vishindo vya mlinzi akija mbio baada ya kusikia mlio wa bunduki, kwa mawazo ya Trigger alijua mlinzi hawezi kuingia ndani kwa kuwa mlango umefungwa.



Trigger akaiweka bastola kiunoni na alikuwa anataka sasa kuanza kupekua ile nyumba amtafute Sarah, lakini ghafla alishtuka mlango umefunguliwa na mlinzi alikuwa amesimama mbele ya Trigger huku akiwa amemuelekezea bunduki,



"Weka Mikono juu muuaji wewe" Mlinzi alimwambiaTrigger huku akimuangalia boss wake Mark aliyekuwa amekaa juu ya kochi huku mwili ukiwa bila roho.......







."Mpuuzi wewe, nyie ndio majambazi mnaotafutwa na serikali, tupa silaha chini na uweke mikono juu" Mlinzi aliongea huku kamnyooshea Trigger bunduki, Trigger akatupa bastola pembeni na kuweka mikono juu huku akitabasamu,



"Hiyo bunduki yako ni nzito sana, ina kilo sita na hujaibeba vizuri" Trigger alimwambia mlinzi huku akitabasamu,



"Muuaji wewe, yaani unatabasamu huku umeua?" Mlinzi aliongea kwa hasira,



"Bosi wako hajafa huyo, hii bastola yangu haiui, inaleta tu usingizi" Trigger aliongea huku akitabasamu na kufanya mlinzi asogee jirani na mark ambaye alikuwa hatua mbili tu toka alipokuwa amesimama Trigger, ilo lilikuwa kosa kubwa sana.



Mlinzi akamtingisha Mark ila Mark hakuonekana ana uhai tena,



"Umeua wewe" Mlinzi aliongea,



"Mgeuze kisogoni uone kama ana damu, maana ukimpiga risasi lazima utoboe mpaka kisogo" Trigger aliendelea kuongea na tabasamu halikumdondoka. Mlinzi akamgeuza na kumuangalia Mark kisogoni, Trigger akatumia mwanya huo wa na kuipiga teke ile bunduki ya mlinzi na ikadondoka, kisha hakapiga hatua moja na kurusha teke Kali lililompata shingoni yule mlinzi na kuanguka chini, na kwa haraka sana Trigger akaokota bastola yake,



"Zamu yangu sasa kukuuliza, mtoto Sarah yupo wapi?" Trigger aliuliza huku bastola ikimuelekea mlinzi,



"Sarah hayupo, alichukuliwa jioni na ndugu yake Mark" Mlinzi alijibu huku akitetemeka,



"Huyo ndugu yake Mark anakaa wapi?"Trigger alihoji,



"Sijui kwa kweli?" Mlinzi alijibu,



"Kwanini hujui wakati wewe ni mlinzi wa hapa?" Trigger aliuliza,



"Sijui kitu boss wangu" Mlinzi aliongea,



"Sawa, je humu ndani wanaishi watu wangapi?" Trigger aliuliza,



"Anaishi Mark peke yake" Mlinzi alijibu kwa hofu,



"Unaogopa nini sasa, au hii bastola niliyoishika?" Trigger aliuliza kisha akaitupa ile bastola mbele ya mlinzi, alafu akaokota bunduki ya mlinzi na kisha akawa anaelekea sehemu vilipo vyumba.



Mlinzi akaona hiyo ni nafasi yake, kwa kitendo cha haraka sana mlinzi aliiokota ile bastola na kumuelekezea Trigger ambaye alikuwa akielekea sehemu vyumba vilipo,



"Simama hapo ulipo na tupa silaha chini" Mlinzi aliongea kwa mamlaka na kufanya Trigger asimame, kisha akageuka taratibu,



"Mimi nilivyokushikia silaha sikukuua, nilikupa nafasi ya kuishi" Trigger aliongea huku akitabasamu,



"Acha kelele, nitakufumua miguu hiyo" Mlinzi aliongea kwa hasira,



"Sawa nifumue, ila ukishindwa nitakufumua mimi" Trigger aliongea kwa kujiamini na kumnyooshea bunduki mlinzi, Mlinzi akafyatua risasi ila hazikutoka, akajaribu tena na hali ikawa vile vile,



"Sikuwa mjinga kukutupia bastola, niliitoa risasi" Trigger aliongea huku akitabasamu na kisha akamuelekezea bunduki yule mlinzi, na hakuwa na cha kupoteza, akamfyatulia risasi zilipiga bega la mlinzi na kisha mlinzi akatupwa na kutua chini kama mzigo, akalala na kutulia kimya,



"Pumzika hapo, nikitoka ndio nitakuua" Trigger aliongea na yule mlinzi aliyekuwa amelala pale chini huku akiwa hana fahamu.



Trigger akaelekea upande wa vyumbani na kuanza kumtafuta Sarah kila chumba, lakini hakufanikiwa kumpata, akaanza kupekua pekua makaratasi ili apate chochote kitakachoweza kumpa uelekeo wa wapi Sarah alipo lakini alikosa.



Trigger akatoka vyumbani kwa hasira na kurudi sebuleni ambapo alimkuta Mlinzi akiwa bado amelala bila fahamu, Trigger akaikota bastola yake na kuipachika mahali husika, kisha akamuangalia yule mlinzi kwa sekunde kadhaa huku bunduki ikiwa mkononi, mwisho akaamua aitupe chini ile bunduki ya mlinzi na kisha akatoka zake nje huku akitembea kwa hatua za haraka haraka, alitembea kwa mwendo huo mpaka alipofika sehemu alipoegesha gari yake, akapanda na kuondoa gari lake kwa mwendo wa taratibu utasema hajatoka kuua vile.



Aliendesha gari mpaka nyumbani kwa Taita na kufunguliwa geti kisha akaingiza gari ndani,



"Bosi yupo?" Trigger alimuuliza mlinzi wa geti,



"Yupo ndani" Mlinzi alijibu na Taita akashika uelekeo wa kuingia ndani.



Alipofika sebuleni alimkuta Taita akiwa amekaa na yule mtoto mdogo wa kiume ambaye ni mdogo wake Sarah,



"Vipi umefanikisha?" Taita aliuliza hata kabla Trigger hajakaa,



"Mark amekufa" Trigger alijibu huku akikaa,



"Sarah je?" Taita aliuliza kwa umakini,



"Sarah sijamkuta, kwa maelezo ya mlinzi nimegundua kuwa Sarah aliondolewa eneo lile jioni, na haijulikani alipo" Trigger alijibu kinyonge,



"Huyu mtoto ana nini? kila siku tunamkosa tu, au atakuwa kwa babu yake?" Taita alihoji kwa hasira,



"Sijui kwa kweli" Trigger alijibu,



"Ila ulivyoondoka kwa Mark umeacha hali Salama, hakuna jirani aliyegundua kitu?" Taita aliuliza,



"Kupo Salama, kuna mlinzi tu nimemuacha amepoteza fahamu" Trigger alijibu,



"Hawezi kuleta shida kama Sarah?" Taita aliuliza,



"Hawezi, kwanza ni ngumu sana kuniona" Trigger alijibu,



"Sawa, basi wewe nenda kapumzike tu, masuala mengine tutaongea siku inayofuata" Taita aliongea,



"Sawa" Trigger alijibu na kuanza kuelekea nje, alitembea mpaka kwenye gari aliyokuja nayo na kufungua mlango kisha akaiwasha, baada ya hapo akaiondoa taratibu.



*******************



Mishale ya saa kumi na mbili asubuhi ilimkuta Sarah akiwa uwanja wa ndege huku akiwa ameambatana na msichana mmoja aliyekuwa anatabasamu kila wakati.



Baada ya kukaguliwa mizigo ya Sarah, Sarah aliingia ndani ya ndege na yule mwanamke alikwenda kukaa eneo la wageni pale kiwanja cha ndege, lengo lake likiwa ni kuhakikisha Sarah ameondoka na yeye ndio atoke pale uwanja wa ndege.



Baada ya nusu saa ndege ile kubwa iliyokuwa ina maandishi ubavuni yaliyosomeka "BRITISH AIRLINE" ilipaa na kuiacha ardhi ya Tanzania na ikawa angani, yule mwanamke aliyekuja na Sarah akatabasamu baada ya ile ndege kumpotea machoni mwake, kisha akaelekea nje alipoegesha gari lake na kuingia, akatoa simu yake na kutafuta namba anayoitaka na kubonyeza kitufe cha kupigia simu, baada ya sekunde kadhaa simu aliyoipiga ikapokelewa,



"Hey Mark habari?" Mwanamke aliongea kwa bashasha,



"Samahani huongei na Mark unaongea na polisi, Mark amepata matatizo" Sauti ya upande wa pili alijibu na kumfanya mwanamke ashtuke,



"Matatizo gani?, yeye yupo wapi?" Mwanamke aliuliza maswali mfululizo,



"Njoo polisi hapa, kituo cha kati utapata taharifa zote" Sauti alijibu na kisha yule mwanamke akakata simu na kuwasha gari kisha akaiondoa kwa kasi, alikuwa kama amechanganyikiwa mwanamke huyu wa kizungu.



Aliendesha gari mpaka nje ya kituo cha polisi na kushuka, kwa mwendo wa haraka akaenda mpaka pale kaunta na kusimama,



"Namuulizia Mark, Mzee wa kizungu" Mwanamke aliongea kwa pupa,



"Wewe ndio ulipiga simu yake muda mchache uliopita?" Polisi aliyekuwepo kaunta aliuliza,



"Ndio mimi" Mwanamke alijibu,



"Panda ngazi hapo, kaingie ofisi namba 13" Polisi alitoa maelekezo na yule mwanamke akafuata huku wasiwasi ukimuongezeka.



Alipofika kwenye mlango namba 13 akagonga na kukaribishwa, akaingia na kupewa ruhusa ya kukaa kwenye kiti, na mbele yake alikuwepo mwanaume wa makamo aliyekaa nyuma ya kibao kilichoandikwa "RPC" yaani Region Police Commissioner, kwa lugha yetu tunaita mkuu wa police,



"Karibu" Mkuu wa polisi aliongea huku akiwa anamuangalia,



"Namuulizia Mark" Mwanamke aliongea,



"Mark......Mark.....ndio nani?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akionekana kutojua kitu,



"Mzee wa kizungu, nilipiga siku yake asubuhi nikaambiwa yupo hapa" Mwanamke aliongea kwa hasira baada ya kuhisi anazungushwa tu,



"Oooh, ni nani yako yule Mzee?" Mkuu wa polisi aliuliza baada ya kukumbuka,



"Ni binamu yangu" Mkuu wa polisi akachukua karatasi na kuanza kuandika,



"Unaitwa nani?" Mkuu wa polisi alimuhoji,



"Emilly David" Mwanamke alijibu,



"Sasa Emily kuna shida kubwa imetoka, Mark alivamiwa jana usiku na muda huu yupo hospitali" Mkuu wa polisi aliongea huku akijaribu kumficha kuhusu kifo cha Mark,



"Ameumizwa?" Emily aliuliza kwa hamaki,



"Nitakupa vijana wangu uongozane nao, ukamuangalie" Mkuu wa polisi aliongea,



"Sawa" Emily alijibu na kisha mkuu wa polisi akapiga simu na baada ya muda wakaingia askari watatu,



"Mpelekeni hospitali mkamuangalie yule Mzee wa kizungu aliyevamiwa jana" Mkuu wa polisi alitoa agizo na kisha Emily na wale askari wakatoka na kuelekea nje, wakapanda gari na safari ya hospital ikaanza.



Haikuwachukua muda wakawa wamefika hospitali na moja kwa moja wakaelekea monchwari, hapo ndipo Emily alichanganyikiwa kabisa.



**"*************



Asubuhi hii ndiyo ilikuwa siku ya kwenda kumfuta kumbukumbu mdogo wake Sarah, Taita na wenzake walikuwa nje ya jengo la hospital wakimsubiri Daktari waliyekubaliana nae kufanya huo mpango, wakiwa wamesimama pale walishuhudia gari la polisi likisimama jirani nao, na kisha wakatelemka askari wawili wakiwa na mtu mmoja aliyekuwa ameshika bega lake na likionekana limejaa damu, ndipo Trigger alipomuangalia yule mtu, akagundua ni yule mlinzi aliyemjeruhi siku iliyopita, na kwa bahati mbaya yule mlinzi akamtupia jicho Trigger, yule mlinzi akashtuka...............







"Kaza mwendo, unashangaa nini wewe?" Askari mmoja aliongea huku akimsukuma yule mlinzi,



"Subirini basi niwaambie" Mlinzi aliongea huku akiwa bado anamtizama Trigger,



"Nenda wewe, utuambie nini sasa" Askari aliongea kisha akamsukuma tena yule mlinzi,



"Usinisukume sasa" Mlinzi aliongea kwa hamaki baada ya kuona anaonewa,



"Unabishana na serikali?" Askari aliuliza ila hakutaka kujibiwa na badala yake akampiga mtama yule mlinzi na kisha akamuinua kwa kumshika kibindoni na kumuingiza ndani ya jengo la hospitali.



Kipindi chote Trigger alikuwa makini kufuatilia lile tukio, ila hakuweza kusikia maneno waliyokuwa wakiongea kati ya wale askari na yule mlinzi, ila aliamini kuna kitu kisicho cha kawaida kilikuwa kitaendelea.



"Hapa hapafai, ngoja niwaache" Trigger aliongea kwa sauti ndogo sikioni kwa Taita,



"Kuna nini?" Taita aliuliza huku akiangaza angaza macho yake eneo lile,



"Tutaongea baadae" Trigger alijibu huku akianza kuondoka kwa kupiga hatua za haraka haraka kuelekea nje ya geti na kuwaacha Taita na harry wakimtazama tu mwenzao huyo.



***************



Mlinzi aliingizwa ndani ya hospitali juu juu na Askari huku akiwa anajitahidi kupambana na Askari wasimshike kidhalilishaji vile, ila kabla hawajaingia eneo husika, Askari waliwaona wenzao wakija eneo lile huku wakiwa wameongozana na mwanamke wa kizungu aliyekuwa anafuta machozi.



Wale Askari walipowafikia walisalimiana,



"Madam" Mlinzi aliita baada ya kunyanyua uso wake na kumuona Emily yule mwanamke wa kizungu,



"Sengu, ni nini kimetokea mpaka Mark akauawa?" Emilly aliuliza huku akionekana ana uchungu sana,



"Madame tulivamiwa jana usiku, na hapa unaponiona nimepigwa risasi ya bega" Mlinzi aliongea kwa huzuni,



"Wamechukua nini sasa baada ya kuvamia, au walikuwa wanaitaka roho ya Mark tu?" Emily aliuliza na kushindwa kujizuia kulia,



"Mvamizi alikuwa anamtaka Sarah, maana alimuulizia na alikuwa anataka kujua alipo muda ule" Mlinzi alijibu,



"Ulimtambua kwa sura huyo mvamizi? au alivaa kitu usoni?" Emily aliuliza huku akijifuta machozi,



"Ni sura ngeni, ila nimemuona hapo nje, nilipotaka kuwaambia hawa Askari badala ya kunisikiliza wananipiga" Mlinzi aliongea huku akimuangalia yule Askari aliyempiga mtama muda mchache uliopita na aligundua jinsi Askari huyo alivyotamalaki,



"Twende ukatuoneshe" Askari huyo aliongea huku akitangulia kupiga hatua na wenzake wakamfuata kwa nyuma huku wakionekana wana hamu ya kumuona huyo muuaji.



Walitoka mpaka nje na Mlinzi alielekea moja kwa moja mpaka pale aliposimama Trigger na wenzake, ila cha ajabu hawakumkuta Trigger,



"Tuambie yupo wapi hapa?" Askari aliuliza huku akimtazama mlinzi na kufanya Taita na Harry washtuke,



"Alikuwepo hapa, amesimama ni hawa" Mlinzi aliongea kwa kujiamini,



"Eti waheshimiwa huyo mtu ambaye inasemekana mlisimama nae ameenda wapi?" Askari aliuliza huku akiwatazama kwa zamu,



"Sijui, kwani huyo ni nani kwetu? mbona mnakuja kwa vitisho namna hiyo?" Taita aliuliza huku mikono ameiweka mfukoni,



"Kwa hiyo mlisimama na mtu ambaye hamumjui?" Askari aliuliza kwa hasira,



"Unauliza vitu gani wewe? unajua hapa wamesimama watu wangapi? na si kila aliesimama tunamjua, hii ni hospitali ya serikali kwa hiyo watu wengi wanakuja hapa na wanasimama popote wanapojisikia" Taita alijibu,



"Kwa hiyo huyo mtu hamumfahamu? hilo ndilo lilikuwa swali langu" Askari aliuliza,



"Hatumjui" Harry alijibu baada ya kumuona Taita amepaniki,



"Sawa tunashukuru waheshimiwa" Askari aliongea kisha akamkamata mkono mlinzi na kumpeleka ndani kupatiwa matibabu na kuwaacha Taita na Harry wakiwaangalia.



"Itakuwa ni Trigger tu, ndo maana alikimbia haraka" Harry aliongea huku akitabasamu,



"Itakuwa ni ile ishu ya kifo cha Mark, maana aliniambia kuwa hakumuua mlinzi" Taita aliongea,



"Trigger amekuwa mzembe siku hizi, au ndio amekuwa mzoefu?" Harry aliuliza,



"Kazi ya hatari inahitaji umakini, siku hizi anakurupuka tu, yaani anajiamini mpaka anataka kuharibu kazi" Taita aliongea huku akionekana kutoridhika na utendaji wa kazi wa Trigger na muda huo Daktari waliyemfuata alikuwa anafika eneo hilo,



"Nimewaweka sana ee, poleni" Daktari aliongea huku akitabasamu,



"Usijali, haya tuambie sasa" Taita aliongea,



"Mipango tayari, sasa twendeni ndani" Daktari aliongea huku akitangulia na nyuma alifuatwa na Harry na Taita ambaye alikuwa amembeba mtoto ambaye ni mdogo wake Sarah.



Waliingia mpaka katika chumba kidogo ambacho kilionekana ni cha siri ila kilijaa vifaa vyote vya vipimo na dawa tofauti,



"karibuni sana, hiki ni chumba maalum cha magendo" Daktari aliongea huku akitabasamu,



"Asante" Harry na Taita walijibu,



"Sasa hatua ya kwanza nitamchoma mtoto sindano ya usingizi, alafu nitamchoma na sindano nyingine mbili shingoni ambazo zitaharibu mfumo wa mawasiliano, alafu nitampeleka wodini, anaweza kukaa wiki nzima bila fahamu" Daktari aliongea na kumuangalia Taita,



"Akae hata mwezi, ila cha muhimu ni kumbukumbu zote zimpotee" Taita alijibu,



"Zitampotea tu, tena itakuwa rahisi maana ni mdogo sana, ana umri gani?" Daktari aliuliza,



"Miaka minne" Taita alijibu,.



"Sawa, nyie nendeni nje, ngoja nimshughulikie" Daktari aliongea huku akimchukua mtoto,



"Na malipo si tutakupa tukiwa nje?" Taita aliuliza,



"Nipeni hapa hapa, kiasi cha hawali, kilichobaki si tumekubaliana mtanipa baada ya kazi" Daktari aliongea,



"Sawa" Taita aliongea kisha akaingiza mkono ndani ya koti la suti na kutoka na kibunda cha pesa, akamkabidhi Daktari,



"Milioni tatu hizi?" Daktari aliuliza huku akitabasamu,



"Zihesabu" Taita aliongea,



"Nakuamini, hizo milioni mbili zilizobaki ndo kama tulivyokubaliana" Daktari aliongea,



"Wewe usijali kuhusu pesa, Fanya kazi tu" Harry aliongea baada ya ukimya wa muda Mrefu,



"Sawa waheshimiwa, kaningojeni nje" Daktari aliongea



"Itachukua muda gani hii hatua ya hawali?" Taita aliuliza,



"Mhmmm mhmmm nusu saa hizi, au chini ya hapo, haiwezi kuzidi dakika thelathini" Daktari alijibu huku akiitazama saa yake ya mkononi,



"Okey, kazi njema" Taita alijibu kisha wakaondoka na Harry na kumuacha Daktari akimlaza Mdogo wake Sarah katika kitanda kidogo kilichopo chumbani hapo.



********************



Mishale ya saa tatu na dakika zake usiku, ndio ndege aliyopanda Sarah ilikuwa inatua katika ardhi ya uingereza kwenye jiji la London, baada ya dakika kumi mlango wa ndege ulifunguliwa na Sarah akawa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kutelemka, alikuwa chini ya uangalizi wa muhudumu wa kike wa ndege ambaye alikabidhiwa na Emily.



Sarah alipelekwa mpaka eneo wanalokaa watu wanaousubiri wageni wao, hapo ndipo walipomkuta kijana mmoja wa kizungu akiwa amebeba bango liliandikwa jina la Sarah, yule muhudumu akampeleka Sarah mpaka mwa kijana yule, kisha yule kijana akatoa shukrani kwa yule muhudumu na baada ya hapo yule kijana akimshika mkono Sarah na kutoka nae eneo la nje ya uwanja wa ndege, wakaelekea kwenye gari ambayo alikuja nayo yule kijana na wakaingia humo, safari ya makazi mapya ikaanza, ndani ya gari ukimya ulitawala,



"Mbona umepoa hivyo, au kwa kuwa Mark ameuawa?" Sarah aliuliza baada ya muda kidogo na kumfanya yule kijana ashtuke, kwa maana yule kijana aliambiwa mtoto huyo hajui chochote kuhusu kifo cha Mark na wala hasimpe taharifa hizo za kifo.

Sasa Sarah amejuaje?







"Nani amekuambia jambo hilo?" Kijana wa kizungu aliuliza,



"Kuna mtu tulipakana nae kwenye siti niliyokaa, niliona hiyo habari kupitia simu yake" Sarah alijibu,



"Sawa, una umri gani?" Kijana wa kizungu aliuliza,



"Miaka sita" Sarah alijibu,



"Nilisikia familia yako iliteketea katika moto?, samahani lakini kama hili swali limekuumiza" Kijana wa kizungu aliongea,



"Baba na mama ndio waliteketea kwa moto" Sarah alijibu katika hali ya utulivu,



"Nilisikia na mdogo wako pia aliteketea" Kijana wa kizungu aliuliza huku akisimamisha gari mbele ya nyumba yenye geti jeusi na kupiga honi,



"Mdogo wangu hajafa, yupo, yupo hai" Sarah alitoa jibu jingine tata,



"Alishakufa bwana, yupo wapi unaposema wewe?" Kijana wa kizungu aliuliza huku akiingiza gari ndani ya geti,



"Napajua alipo, wakati ukifika kila mtu atajua ukweli" Sarah aliongea huku akitelemka kwenye gari baada ya yule kijana kumfungulia mlango,



" je huo wakati utafika lini?" Kijana wa kizungu aliuliza,



"Sijui, na sipendi kuulizwa zaidi" Sarah alijibu,



"Haya tumefika, hapa ndio nyumbani" Kijana wa kizungu aliongea huku akitelemsha begi la Sarah lililokuwepo katika buti la gari, lakini pia kijana was kizungu alijiuliza sana juu ya uwezo was Sarah katika kuongea.



Waliingia mpaka ndani na kukuta sebule kubwa ambayo ilikuwa na kochi za sofa na runinga iliyokuwa inaonesha,



"Kaa hapo, ngoja nikamuite anko" Kijana wa kizungu aliongea huku akielekea sehemu ya vyumbani, baada ya muda alirejea huku nyuma yake akifuatwa na Mzungu mwingine aliyevaa fulana nyeusi na chini alikuwa na suruali ya jeshi,



"Naitwa John, karibu sana Sarah" Mzungu alijitambulisha mbele ya Sarah huku akitabasamu,



"Nani amekuambia jina Langu?" Sarah aliuliza kitoto,



"Mimi nakujua, wewe ndio hunijui mimi" John alijibu huku akitabasamu,



"Hapa ni kwako?" Sarah aliuliza tena,



"Ndio, hapa ni kwangu" John alijibu huku akielekea kwenye friji,



"Wewe ni mwanajeshi? Mbona umevaa suruali ya jeshi?" Sarah aliuliza maswali mfululizo,



"Ndio, kwani na wewe unapenda jeshi?" John aliuliza huku akirudi kutoka kwenye friji na mkononi alibeba maziwa na kumpatia Sarah,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ndio, nataka kuwa mwanajeshi au muhubiri, sitaki kusoma" Sarah aliongea na kufanya wale wazungu wamshangae,



"Kwanini unasema hivyo Sarah? Si unajua kilichokuleta huku ni shule?" John aliuliza,



"Mimi nataka kuwa tu mwanajeshi kama wewe" Sarah aliongea,



"Basi soma, ukiwa mkubwa utakuwa mwanajeshi" John aliongea kwa upole,



"Au pale kambini kwenu si ipo shule?, akasomee pale" Kijana wa kizungu alimshauri John,



"Sasa kuna gharama ambazo zilitangulizwa kwenye ile shule ambayo ndio anatakiwa akasome" John aliongea,



"Kaongee nao tu, ni vizuri kumpatia mtoto kila anachokitaka" Kijana wa kizungu aliendelea kumshauri,



"Sawa, itabidi kesho niende kuongea nao" John alikubaliana na ushauri,



"Sarah twende nikupeleke chumbani kwako, alafu uoge na upumzike" Kijana wa kizungu aliongea huku akibeba begi la Sarah na kuelekea vyumbani huku Sarah akimfuata kwa nyuma.



Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya Sarah ndani ya uingereza.



********†***********



Nchini Tanzania ndani ya hospitali kubwa binafsi, katika wodi moja alikuwepo Taita na harry pembeni ya kitanda alicholala Sebastian ambaye ndiye mdogo wake Sarah.



Baada ya muda alikuja Daktari,



"Kazi yenu tayari imeisha, mnaweza mkamchukua mtoto wenu" Daktari aliongea,



"Kwa hiyo hapa kila kitu kinaanza upya, hajui lolote, hata jina lake halijui?" Taita aliuliza,



"Kila kitu, yaani ni mpya huyo" Daktari alijibu,



"Sawa, tunashukuru" Taita aliongea huku akimbeba Sebastian kisha wakaagana na Daktari na kutoka mpaka nje ya hospitali na kuingia ndani ya gari waliyokuja nalo.



"Harry tunafanyaje sasa, sitaki huyu mtoto aishi nyumbani kwangu, si unajua mke wangu alivyo mkorofi?" Taita aliuliza kwa upole,



"Huyu inabidi umpeleke shule za kijeshi, tena za mbali kabisa, wewe si unataka huyu aje kuwa mrithi wako?" Harry aliongea,



"Ndio, ni wazo zuri, basi ngoja akakae kwako wiki chache wakati tunashughulikia hilo jambo" Taita aliongea,



"Kwangu?? hapana, akakae tu kwako, si wiki tu, mchakato wa kupata kila kitu kuhusu usafiri ni wiki tu, kwani unataka umpeleke nchi gani?" Harry aliuliza,



"Nadhani marekani, kule ndio itakuwa rahisi kuingia jeshini, maana nataka na uraia achukue wa uko" Taita alijibu,



"Ana umri gani?" Harry aliuliza,



"Miaka minne" Taita alijibu,



"Sawa kabisa, kupewa uraia inawezekana" Harry aliongea,



"Jina inabidi abadilishwe, nitamuita Vin, kuanzia leo hilo ndio jina lake" Taita aliongea na kufanya Harry atabasamu.



Wakaondoka eneo la hospitali na kurudi nyumbani kwa Taita, baada ya hapo wakaanza kushughulikia mpango wa kumsafirisha Vin.



Baada ya wiki Vin alifanikiwa kusafirishwa na alipewa mtu wa kumuangalia na kumsimamia kwa kila kitu. Huo ndio ukawa mwanzo wa Vin katika safari ya maisha yake, aliweza kufika Marekani na huko mipango ilienda kama ilivyopangwa, Vin akaanza shule ya jeshi, alisoma mpaka akamaliza elimu ya kati, kisha akajiunga na jeshi la marekani, akapata alama za juu katika mafunzo, akateuliwa kwenda kujifunza zaidi nje ya marekani, nako akapata alama ya juu, aliporejea marekani akapandishwa cheo, na muda wote alikuwa anawasiliana na Taita, ndiye aliyemtambua kuwa ni baba yake wa damu, na Taita alikuwa anaenda marekani kila apatapo muda na kumkumbusha Vin kuwa anatakiwa arudi Tanzania alinde Mali zake, yaani Mali za Taita ambaye alijua ndiye baba yake.



Ilikuwa ngumu kumshawishi Vin kuhusu jambo hilo, Vin hakutaka kabisa kusikia suala hilo, na tayari aliambiwa huku hana ndugu, yeye alizaliwa peke yake na mama yake alishakufa, aliuawa na watu wabaya, basi Vin hakuona umuhimu wa kurudi Tanzania kwa kuwa baba yake alikuwa anaonana nae kila anapomuhitaji.



Ndio maisha ya Vin yakawa hivyo, hapo Taita akaona alitumia muda mrefu kumuandaa Vin kwa ajili ya kumfanyisha kazi za kishenzi, alafu leo hii vin hataki kurudi kumtumikia, Taita hakuwa na la kufanya, maana alimpenda sana Vin, na Vin alimpenda sana Taita, tena alimpenda zaidi ya Taita anavyompenda.



*******************



BAADA YA MIAKA KUMI NA TISA.



Ndani ya uwanja wa ndege anatoka msichana mwembamba ndani ya jengo la uwanja wa ndege, huku akivuta begi kubwa la nguo na chini alivaa suruali ya jeans nyeusi iliyombana na kufanya umbo lake lijichore vizuri, baada ya kutoka nje alisimama kwa muda na kuiangalia anga kwa muda kisha akatabasamu huku machozi yakimtoka, akajifuta na kitambaa.



Akapiga hatua chache na kuelekea sehemu zilipoegeshwa taxi na kuingia,



"Habari yako" Dereva taxi akamsalimia yule Dada,



"Ni nzuri, nipeleke hotel yoyote kubwa ya karibu na hapa" Dada alijibu kwa lafudhi ya kigeni,



"Ya nyota ngapi?" Dereva taxi aliuliza,



"Si chini ya tatu, ila isiwe na msongamano wa watu" Dada alijibu,



"Poa" Dereva taxi alijibu kisha akawasha gari na kuliondoa kwa mwendo wa taratibu mpaka katika jengo moja la hotel na kuisimamisha gari, kisha akatelemka na kumfungulia mlango yule Dada, kisha yule Dada akatelemka na begi lake na kumlipa pesa dereva taxi, na akachukua namba ya simu ya dereva taxi, kisha wakaagana na yule Dada akaelekea mapikezi na kumsalimia Dada wa mapokezi,



"Naweza kupata chumba" Dada alimuuliza muhudumu,



"Vipo, karibu" Dada wa mapokezi alijibu,



"Napendaga vyumba vilivyo ghorofa ya juu kabisa" Dada aliongea huku akitabasamu,



"Vipo, hata usijali" Dada wa mapokezi aliongea huku nae pia akitabasamu,



"Haya, nipe funguo" Dada mgeni aliongea,



"Jina unaitwa nani?" Dada wa mapokezi aliuliza huku akibofya computer iliyokuwepo mbele yake,



"Andika Sarah, Sarah Isack" Dada alijibu huku akitabasamu...





"Sarah Isack" Dada wa mapokezi aliandika hilo jina huku akirudia kulitamka, kisha akamuelekeza Sarah namna ya kukifikia chumba na Sarah akaondoka zake taratibu na kuingia ndani ya lifti huku akiwa analivuta begi lake taratibu.



Alipoingia kwenye lifti alibonyeza vitufe vilivyopo pembeni ya mlango wa lifti na kisha lifti ikaanza kupanda juu, ilipanda mpaka ghorofa ya mwisho na kisha ikasimama na mlango ukafunguka, Sarah akatoka na kuelekea upande wa kushoto huku akiwa makini kuzisoma namba zilizopo katika kila mlango wa chumba anachopita, baada ya muda alikifikia chumba anachotakiwa akae, akaingiza funguo ndani ya tundu na kisha akaizungusha ile funguo, mlango ukafunguka, Sarah akaingia na kuanza kuangaza ndani ya kile chumba kwa nusu dakika, kisha akaurudishia mlango na kuelekea dirishani, akafungua vioo vya dirisha na kwa Mara ya kwanza akauona mji vizuri, mji aliouacha miaka kumi na Tisa iliyopita,



"Karibu tena Africa" Sarah aliongea peke yake kisha akatabasamu na kuvifunga vioo vya dirisha, kisha akavua suruali yake na kuchukua taulo, akaelekea mariwatoni kujiswafi mwili wake.



***************



Taita wa nyakati hizi utu uzima ulikuwa umemfikia, alikuwa na miaka takribani hamsini na kipindi hiki pesa ilikuwa ni rafiki yake mkubwa, alikuwa yupo karibu sana na serikali kutokana na misaada aliyokuwa anaisaidia serikali na pia alikuwa ni muarifu wa kuuza vitu haramu au vya magendo.



Taita alikuwa anaingiza dawa za kulevya nchini, Taita alikuwa ana kikundi kinajihusisha na ujambazi mkubwa hapa nchini na pia Taita alikuwa na makampuni makubwa makubwa aliyokuwa anayatumia kama njia ya kuficha maovu yake.



Katika kikundi chake kilikuwa vile vile, Harry kama mwanasheria wake ingawa na umri ulikuwa umeenda, na yeye pia alikuwa na fedha za kutosha kutokana na utajiri wa Taita.



Trigger alikuwepo, yeye ndiye alikuwa kiongozi wa vikundi vyote vya uharifu vilivyokuwa vinamilikiwa na Taita, ila safari hii waliongezeka vijana wengine watatu hatari, alikuwepo Sostenes, huyu alikuwa ni msomi aliyebobea katika masuala ya teknolojia, kila mawasiliano na vitu vyote vinahusu teknolojia huyu ndiye alikuwa mratibu na jina la utani aliitwa Tekso, yaani Tek ilisimama kama Teknolojia na So ilisimama kama sostenes ambao ndio jina lake.



Wa pili aliitwa Dula, huyu alisomea masuala ya mbinu na mipango katika kufanikisha jambo, kwa hiyo mipango yao yote ilikuwa inamtegemea huyu mtu, na sifa yake kuu ni kupenda kukaa peke yake muda Mrefu na wenzake wanapenda kumuita strategic, sijui wana maana gani?



Na wa tatu ni Toisa, huyu ni mjanja mjanja tu, hutumiwa sana kwenda kufanya upelelezi kipindi genge hili likiwa linataka kuvamia sehemu, na uzuri wa hawa watu ni kuwa wote walikuwa mafundi wa mapigano na shughuli za magendo walizifanya wote, iwe kusambaza madawa au kuvamia bank basi wote walishika mitutu na kutekeleza kazi chini ya kiongozi wao Trigger.



Hata mke wa Taita alikuwa ameshafiriki kutokana na saratani ya kizazi, kwa hiyo muda huu Taita alikuwa anaishi mwenyewe na mfanyakazi wa ndani kwa ajili ya kumfanyia kazi na kumpikia.



*************



Mida ya saa kumi jioni Sarah alimpigia simu dereva taxi na kumuita, baada ya dakika tano taxi ilikuwa imeshafika nje ya hoteli, Sarah akatelemka ghorofani na kwenda mpaka nje, kisha akaingia ndani ya ile taxi,



"Nipeleke mbezi, mbezi shamba" Sarah aliongea huku akijifunga mkanda wa gari, dereva akaiondoa gari,



"Wewe ni mwenyeji wa huku?" Dereva taxi alimuuliza Sarah,



"Kidogo, nimeshawahi kuishi hapa" Sarah alijibu huku akitabamu,



"Kwa hiyo ulikuwa nje ya nchi kwa ajili ya masomo?" Dereva taxi aliuliza,



"Uko ndipo ninapoishi kwa sasa, nilihama hapa zamani sana" Sarah alijibu,



"Vipi maisha ya uko nje?" Dereva taxi aliuliza,



"Uko maisha kawaida tu" Sarah alijibu,



"Sasa huku mbezi unaenda kwa nani?, au una ndugu?" Dereva taxi aliuliza,



"Hapana, naenda kuangalia kiwanja, kuna mtu anataka kuniuzia" Sara aliongea,



"Kule ni pazuri, pametulia na isitoshe kama hutaki kujenga unapafanya shamba" Dereva taxi aliongea,



"Ebu simamisha hapa, nadhani tumefika" Sarah aliongea na gari ikasimama, kisha Sarah akatelemka na kuiangalia hotel moja kubwa sana, ya ghorofa iliyokuwa inavutia, Sarah aliangalia kwa muda na kisha huzuni ukamjaa moyoni, eneo ambalo ipo hiyo hotel, ndiyo eneo ambao nyumba yao ilikuwepo, ndipo ambapo wazazi wake walichomwa ndani ya nyumba hiyo. Hiyo hotel ilikuwa inaitwa VIN hotel.



Sarah aliendelea kuangalia kwa dakika kadhaa kisha akarudi ndani ya gari,



"Mbona umeiangalia na kuishia nje?" Dereva taxi aliuliza,



"Kuna mtu nilikuwa namuangalia, nadhani hayupo maana gari yake siioni" Sarah aliongea,



"Mpigie simu" Dereva taxi alimshauri Sarah,



"Simu nimeiacha kule hotelini" Sarah alidanganya,



"Nipe namba yake nikusaidie kupiga" Dereva taxi aliongea huku akiitoa simu yake mfukoni,



"Namba yake sijaikariri, acha tu nirudi hotelini, waswahili hawajui kwenda na ahadi" Sarah aliongea na dereva Taxi akawasha gari na kuiondoa,



"Basi bahati mbaya, utamrudia baadae?" Dereva taxi aliuliza,



"Hapana, hii hotel ya nani?" Sarah aliuliza,



"Ile ni ya boss mmoja anaitwa Taita, na jina la hiyo hotel ni jina la mwanae, yupo marekani uko" Dereva taxi alitoa jibu lililoshtua moyo wa Sarah,



"Taita ndio amekuwa na pesa mpaka amejenga hoteli kubwa hivyo?" Sarah alijikuta anauliza bila kutegemea,



"Unamjua Taita kwani?" Dereva taxi aliuliza,



"Namsikiaga tu, toka nipo uingereza nasikia habari zake, sikudhani ana utajiri mkubwa kiasi hicho" Sarah alijibu,



"Ni tajiri mkubwa sana, anaisaidia mpaka serikali" Dereva taxi aliongea,



"Ana biashara gani nyingine tofauti na hotel?" Sarah aliuliza,



"Nyingi sana, anauza magari, ana mashamba makubwa na pia kuna habari anajihusisha na madawa ya kulevya" Dereva taxi alijibu,



"Uliniambia ana mtoto yupo marekani?" Sarah aliuliza,



"Ndio, anaitwa Vin" Dereva taxi alijibu,



"Aisee huyo mtu tajiri sana, anakaa wapi?" Sarah aliuliza,



"Anaishi osterbay, si unajua ndipo matajitiri wanapoishi huko" Dereva taxi alijibu,



"Itabidi nimtafute nifanye nae kazi, unaweza kunielekeza mtaa anaoishi?" Sarah aliuliza,



"Siujui kwa kweli, ila unaweza kutafuta namba zake, kaziweka tu mitandaoni kwa ajili ya biashara" Dereva taxi alijibu huku akiegesha gari nje ya jengo la hotel aliyofikia Sarah,



"Nashukuru kaka" Sarah aliongea huku akimkabidhi ujira wake dereva taxi na kisha akatelemka katika gari, akaingia ndani, alipofika alijitupa kitandani na kuanza kutafakari namna Taita alivyoidhurumu nyumba yao na kufungua hotel hiyo kubwa, ila swali alilojiuliza huyo mtoto wa Taita ni yupi? Mbona hakuwai kumuona kabla? Ila akapuuzia tu na akili yake akaiweka katika kutafuta ukweli wa wapi alipo mdogo wake aitwae Sebastian.



Baada ya muda Sarah alichukua simu yake na kutafuta jina la Vin hotel katika sehemu ya Google, alipoipata akaingia upande wa mawasiliano na kuongea nao kwa muda, alikuwa anaomba namba ya Taita, ilikuwa ngumu kupata ila alijitahidi kubembeleza mpaka akapewa.



Akaichukua ile namba na kuiingiza sehemu ya kutafutia ni wapi mwenye hiyo namba yupo muda huo, simu ikaonesha yupo osterbay, akatabasamu, akabadili nguo na kutoka nje, akaita bajaj na kumuelekeza ni wapi pa kwenda, bajaj ikaondoka mpaka katika duka linalouza Zawadi, Sarah akaingia na kuchukua Zawadi anayoijua yeye na kuiingiza katika box dogo na kumwambia dereva bajaj ampeleke osterbay.



Baada ya dakika kumi na tano, Bajaj ilikuwa imesimama nje ya nyumba kubwa yenye geti, Sarah akatelemka na kwenda getini, akabonyeza kengele, mlinzi akafungua geti,



"Habari yako?" Sarah alimsalimia mlinzi,



"Nzuri, karibu" Mlinzi aliongea,



"Mwenye nyumba nimemkuta?" Sarah aliuliza,



"Ametoka kidogo" Mlinzi alitoa jibu na kumfanya Sarah afikirie kidogo,



"Sawa, basi akija utampatia huu mzigo" Sarah aliongea huku akimkabidhi mlinzi mfuko wa nylon ambao ndani kulikuwa na lile box la zawadi alilolinunua,



"Nimwambie umetoka kwa nani?" Mlinzi aliuliza huku akiupokea,



"Mwambie umetoka umetoka marekani, kwa mwanae" Sarah alijibu,



"Umetoka kwa vini kumbe, saw a binti" Mlinzi alijibu na kisha Sarah akaingia kwenye bajaj na kuondoka huku akitabasamu.



***************



Taita alirudi nusu saa tu baada ya Sarah kuondoka, aliingiza gari ndani ya nyumba, na kisha mlinzi akamkabidhi ule mfuko,



"Umetoka Wapi huu?" Taita aliuliza,



"Kuna binti ameuleta, anasema umetoka marekani kwa vin" Mlinzi alijibu,



"Ooh kumbe vin ameniletea" Taita aliongea kwa furaha huku akiupokea na kuingia nao ndani, alipofika aliuweka mezani na kuufungua, akakuta box, akalichana, alichoona kilichopo ndani akajikuta anashangaa, tena mshangao sio wa kitoto.......









" ni nini hiki Vin anafanya?" Taita alijiuliza mwenyewe baada ya kukuta keki ndogo ndani ya lile box, akalifunga box na kutoka mpaka getini kwa mlinzi,



"Huyo binti aliyeleta mzigo alikutajia jina lake?" Taita alimuuliza mlinzi,



"Hapana" Mlinzi alijibu na kumfanya Taita amuangalie kwa muda,



"Kuwa makini sana" Taita aliongea huku akielekea ndani, machale yalianza kumcheza, aliingia chumbani kwake kisha akawasiliana na Vin ili kujua kama kweli ametuma lile box, lakini Vin alikataa na alidai hajui chochote kuhusu hilo box, Taita akakata simu na kuhisi huenda kuna mtu anamchezea akili, akawaza ingekuaje kama hilo box lingekuwa na Bomu?



"Huyu mlinzi nae mpumbavu" Taita aliongea peke yake huku akipanda kitandani na kujilaza kitandani.



*************



Sarah alirudi hotelini na kuingia chumbani kwake, akajitupa juu ya kochi na kutabasamu peke yake,



"Pale ni rahisi sana kuingia, mlinzi mwenyewe mmoja na pia ni rahisi sana kupenyeza kitu chochote cha hatari" Sarah aliongea mwenyewe na kuendelea kutabasamu, kisha akaiendea simu ya mezani na kuipiga, aliongea na wahudumu wa hotelini, alikuwa anahitaji chakula cha jioni muda huo.



Baada ya dakika kumi mlango wa chumbani kwake uligongwa na akaingia muhudumu huku akisukuma meza ya matairi iliyokuwa na chakula,



"Asante mrembo" Sarah aliongea wakati chakula chake kikiwekwa juu ya meza,



"Hutumii kilevi chochote?" Muhudumu alimuuliza Sarah,



"Hapana, uwa natumia mara moja moja. Kwanini umeniuliza hivyo?" Sarah aliuliza,



"Mara nyingi watu wanaoagiza chakula cha jioni hapa hotelini kwetu uwa wanapewa na kilevi cha ofa wanachohitaji, sasa nashangaa wakati naweka chakula chako hapa mezani sioni kilevi" Muhudumu alijibu,



"Sikutaka kuagiza, ila ipo siku nitaagiza" Sarah aliongea huku akicheka,



"Sawa, nakutakia mlo mwema na jioni njema" Muhudumu aliongea huku akiondoka,



"Shukrani, kazi njema" Sarah aliongea na kuiendea meza ya chakula na kisha akakifunua, akanawa mikono na kuanza kula.



Baada ya muda alimaliza kula na kuingia bafuni kuoga, alipomaliza alirudi na kujitupa kitandani. Siku yake iliisha hivyo.



***************



Asubuhi na mapema Sarah aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kutoka, akampigia simu dereva taxi na kumuhitaji, baada ya muda dereva taxi aliwasili na Sarah akatoka ndani na kuingia kwenye taxi,



"Za tangu jana?" Sarah alimsalimia dereva taxi,



"Nzuri, leo wapi boss wangu?" Dereva taxi aliuliza,



"Nipeleke kinondoni makaburini" Sarah aliongea,



"Sawa boss" Dereva taxi alijibu na kisha akaiondoa gari taratibu kuelekea uko.



"Sijui itakuwa imebadilika hiyo kino?" Sarah aliuliza,



"Kwani tunapoelekea ni pale pale kwenye makaburi au eneo lingine?" Dereva taxi aliuliza,



"Naenda makaburini" Sarah alijibu,



"Kuna ndugu yako amezikwa pale" Dereva taxi aliuliza,



"Wazazi wangu wamezikiwa pale" Sarah alijibu,



"Ooh pole sana, wamezikwa sehemu moja?" Dereva taxi aliuliza,



"Hapana, wamezikwa sehemu tofauti ila eneo moja" Sarah alijibu na ukimya ukatawala.



Gari ilitembea mpaka makaburuni na kisha dereva akaiegesha nje ya uzio wa makaburi na Sarah akatelemka huku akiwa na maua makubwa mawili na mataji mawili, akatembea mpaka eneo la ndani la makaburi na kuanza kuangaza angaza sehemu yalipo makaburi ya wazazi wake, aliangaza kwa dakika kadhaa na kuyaona, yalikuwa yameshaanza kubomoka, ilionekana yalikaa muda Mrefu bila kufanyiwa matengenezo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Sarah akayasogelea na kuyaangalia kwa muda, kisha akaweka maua kwenye kila kaburi na yale mataji akayaweka kwenye ile misalaba ya makaburi, kipindi hicho machozi yalikuwa yanamtoka, uchungu wa kuondokewa na wazazi ulimjaa na pia moyoni alisikitika wazazi wake kufa kifo cha kikatili tena kilichosababishwa na mtu ambaye ni wa karibu kwao.



Sarah alipomaliza kuweka mataji, alirudi hatua mbili nyuma, akatoa kitambaa na kujifuta machozi, kisha akapiga magoti katikati ya makaburi yale na kufumba macho,



"Baba na mama yangu, nadhani wakati wangu wa kulipa kile mlichofanyiwa umefika, nadhani wakati wa kuwapa furaha angalau kwa kiasi kidogo ni wakati huu ambao ninao sasa, naamini mtanipa ruhusa ya kulipa ubaya kwa ubaya.



"Mwenyezi Mungu nipe moyo wa moto, moyo wa kumuunguza kila aliye mbaya juu yangu" Sarah alimaliza kusali na kufungua macho yake, kisha akasimama na kupangusa magoti yake, akaelekea mpaka kwenye taxi,



"Hatuwezi pata mafundi ujenzi hapa?" Sarah alimuuliza dereva taxi,



"Ebu ngoja nikamuulize mlinzi wa hapa" Dereva taxi alijibu huku akitelemka na kuelekea kwenye kibanda kidogo kilichopo pembezoni mwa uzio wa makaburi.



Dereva taxi alipofika kwenye hicho kibanda alimkuta mzee akiwa amekaa huku akivuta goso, goso ni tumbaku iliyonyongorotewa kwenye karatasi na kuwa kama sigara,



"Shikamoo Mzee" Dereva taxi alimsalimia yule Mzee,



"Marahaba" Mlinzi aliitikia,



"Babu eti hapa ni eneo gani naweza kupata mafundi, nataka nirekebishe kaburi" Dereva taxi aliuliza na kisha mlinzi akamuelekeza sehemu mafundi wanapopatikana. Dereva taxi akamshukuru mlinzi na kuondoka zake.



Dereva taxi alipomfikia Sarah alimueleza alivyoelekezwa na mlinzi, Sarah akiongozana na dereva taxi waliambatana kwa miguu mpaka sehemu walipo mafundi, hapakuwa mbali na ndio maana waliacha gari.



Waliwakuta mafundi na kisha wakawachukua mpaka eneo la makaburi yanayotakiwa kukarabatiwa, mafundi wakapiga hesabu za tofali na saruji, Sarah akatoa pesa ya tofali na muda huo tofali zikaenda kununuliwa, tofali zilipokamilika, mafundi wakaanza kujengea makaburi ya Isack na mke wake, kipindi chote Sarah alikuwa hapo akifuatilia kila hatua.



Mafundi walitumia saa moja kukamilisha ile kazi, kisha wakalipwa pesa yao na kuondoka zao huku wakimsisitiza Sarah kuwa kesho akumbuke kumwagia maji yale makaburi kwa ajili ya kufanya ukuta uwe imara, Sarah akawakubalia.



Sarah na dereva wakarudi ndani ya gari,



"Wapi boss?" Dereva taxi akauliza,



"Nirudishe hotelini" Sarah akajibu na kisha dereva taxi akawasha gari na kuliondoa kistaharabu, safari ya kumrudisha Sarah hotelini ilianza.



*****************



Asubuhi mishale ya saa mbili, Baba Isack ambaye ni babu yake Sarah alionekana makaburini huku akiwa na mwanae, kitu kilichowashangaza ni kukuta maua juu ya makaburi na pia kukuta makaburi yakiwa yamekarabatiwa vizuri,



"Ni nani aliyejengea, au Taita?" Babu yake Sarah alimuuliza mwanae,



"Sasa mimi nitajuaje baba?, mpigie simu umuulize" Mwanae alijibu kwa mshangao,



"Ila Taita sijui, maana sidhani kama alishawahi kuja hapa toka tumewazika hawa, labda kwa kuwa amekuwa mtu mzima na busara zinaanza kumuingia" Babu Sarah aliongea huku akimtazama mwanae,



"Ebu mpigie umuulize, tuache kuishi kwa hisia" Mwanae aliongea na kisha babu Sarah akaitoa simu mfukoni na kumpigia Taita na kumuuliza kama ni yeye ndiye aliyejengea makaburi, kwanza Taita alishtuka lakini alikanusha na akaahidi kufika hapo muda mfupi ujao.



************



Asubuhi hii Sarah aliamka mida ya saa tatu na kukumbuka kuwa anahitajika kufika eneo la makaburini kwa ajili ya kumwagilizia tofali zilizojengwa siku iliyopita, akaoga na kumpigia siku dereva wake kwa ajili ya kwenda makaburini.



***************



Taita aliwasili makaburini saa nne kasoro na alikuwa na Harry na Trigger, walipofika walielekea moja kwa moja mpaka kwenye makaburi husika na kumkuta babu yake Sarah na mwanae, wakawasalimia,



"Kwa hiyo mzee nyie wenyewe hamjui aliyejengea?" Taita aliuliza huku akishangaa,



"Sisi tulijua ni wewe na ndio maana tulikupigia simu" Babu yake Sarah alijibu na kufanya Taita afikiri kidogo,



"Ebu nifuateni" Taita aliongea huku akielekea kwenye kibanda cha mlinzi, alipofika walimkuta yule Mzee ambaye ni mlinzi, wakampa salamu,



"Eti ndugu ni nani aliyeyajengea yale makaburi mawili?" Taita aliuliza huku akiyaoneshea kwa kidole yale makaburi,



"Ni kijana mmoja wa kiume na wa kike, walikuja jana na kujengea hayo makaburi" Mlinzi alijibu,



"Wapoje wapoje?, au walijitambulishaje?" Babu yake Sarah aliuliza kwa shauku,



"Hawajajitambulisha kwa kweli" Mlinzi alijibu,



"Mzee ulitakiwa uwaulize, wewe si ndio mwenye mamlaka hapa?" Taita aliuliza huku akimuangalia mlinzi, na wakati huo ile taxi anayoitumia Sarah ilikuwa ikiegeshwa nje ya uzio wa makaburini,



"Bora aisee, tena watu wenyewe wale pale kwenye ile gari" Mlinzi aliongea huku akiioneshea kidole ile taxi na kufanya watu wote waitolee macho na kuangalia ni wakina nani wataoshuka, ukafunguliwa mlango wa dereva akatelemka dereva, na kufanya wakina Taita wamtolee macho bila kumjua, na wakati huo mlango wa abiria ulikuwa ukifunguliwa, hapo kila mmoja akatupa karata yake kuona huyo atayeshuka watamtambua au lah????







Alishuka kijana mmoja ambaye hakuwa nadhifu, alishuka na kuelekea upande wa nyuma wa gari na kufungua buti kisha akatelemsha madumu mawili makubwa ya maji na kufunga buti, kisha wakaongea na dereva taxi na dereva taxi akaanza kuelekea sehemu yalipo makaburi ya wazazi wa Sarah na nyuma alifuatwa na yule kijana huku akiwa amebeba yale madumu ya maji.



Walifika mpaka yalipo makaburi na kisha yule kijana akaanza kumwagia maji yale matofali yaliyojengwa siku iliyopita.



Taita na wenzake wakasogea mpaka alipo dereva taxi na yule kijana,



"Habari zenu vijana?" Taita alisalimia,



"Salama, shikamooni" Dereva taxi alijibu kwa heshima baada ya kumtambua Taita,



"Marahaba, mbona mnalimwagia maji kaburi letu?" Taita aliuliza kwa sauti tulivu,



"Hili ni lenu? mimi nimeagizwa tu nilimwagie tu baada ya kujengwa jana" Dereva taxi alijibu,



"Nani amewaagiza wanangu?" Babu Sarah aliuliza huku akistaajabu,



"Ni msichana fulani hivi, uwa anaikodi gari yangu mara kwa mara ndio tumetokea kuzoeana" Dereva taxi alijibu kistaharabu,



"Anaitwa nani na anaishi wapi?" Taita aliuliza,



"Jina lake sikubahatika kulijua, ila anaishi hotelini kule mjini" Dereva taxi alijibu,



"Kwani Sarah amerudi?" Taita aliuliza huku akimgeukia babu yake Sarah,



"Sarah hajarudi, na jana tuliongea nae na amesema hawezi kuja hivi karibuni" Babu Sarah alijibu,



"Unaweza kutupeleka hiyo hotel anayoishi huyo binti?" Taita alimuuliza dereva taxi,



"Haina shida, twendeni" Dereva taxi alijibu na kisha akatoa hela kumlipa yule kijana aliyeenda nae pale, ni kijana alimkodi kwa ajili ya kumwagia ule ukuta wa makaburi, baada ya hapo dereva taxi alienda na kuingia kwenye gari lake ambapo pia kwenye hilo gari alipanda babu Sarah na mwanae na gari la pili alikuwepo Taita ambaye alikuwa na Harry.



Safari ilianza kwa mwendo wa wastani huku gari zile zikiongozana kistaharabu na kila mmoja alikuwa anawaza lake, wakati Taita, Harry na Babu Sarah wakiwa na shauku ya kumuona huyo binti, lakini dereva taxi yeye alichokuwa anakiwaza ni kuwa leo huyo binti atapata bahati ya kukutana na Taita, tajiri mkubwa Tanzania na aliamini yule binti atafurahi kwa maana alishamwambia ana wazo la kufanya biashara na Taita.



Dereva taxi alisimamisha gari nje ya hotel ambayo anaishi Sarah na kisha gari ya Taita ikapaki nyuma ya taxi na wote wakashuka kisha dereva taxi akatoa simu yake mfukokoni Ili ampigie Sarah na kumtaharifu juu ya ugeni huo, cha ajabu namba ya Sarah hakuikuta, akajaribu kuangalia namba alizowasiliana nazo siku hiyo, lakini bado namba hakuiona, akapata mfadhaiko kidogo,



"Vipi, hapatikani?" Babu Sarah alimuuliza dereva taxi,



"Namba yake siioni, sijui nimeifuta bila kujua" Dereva taxi alijibu,



"Ebu twendeni ndani" Taita aliongea huku akianza kupiga hatua na wenzake wakamfuata kwa nyuma, akiwepo na dereva taxi pia, walifika mpaka mapokezi na kumkuta muhudumu wa pale aliyekuwa amekaa, wakamsalimia kwa upole,



"Samahani, yule Dada ambaye uwa naondoka nae hapa nimemkuta?" Dereva taxi aliuliza,



"Ameondoka muda sio Mrefu" Dada wa mapokezi alijibu baada ya kumuelewa dereva taxi,



"Ila atarudi, si ndio?" Taita akauliza,



"Yaani ameondoka moja kwa moja, amerudisha na funguo" Dada wa mapokezi alijibu,



"Unaweza kutusaidia jina lake?" Taita aliuliza,



"Jina lake silijui" Dada wa mapokezi alijibu,



"Si uangalie kwenye record zenu, au Wateja wakiingia hapa uwa hamnakiri wasifu wao?" Taita aliuliza na kumfanya yule Dada aanze kubonyeza bonyeza computer, alifanya hivyo kwa dakika mbili,



"Eeh, sioni kitu kwa kweli, hata hii mimi imenishangaza" Dada wa mapokezi aliongea kwa mshangao,



"Yaani record zake hazionekani?" Taita aliuliza,



"Yaani zimefutika zote, hii inaweza kugharimu kazi yangu" Dada wa mapokezi aliongea kwa unyonge,



"Huyu mtu ni nani?" Babu Sarah aliuliza huku akijua kabisa hakuna mwenye jibu,



"Mi naondoka inawezekana tunapoteza muda kumfuatilia mtu asiyekuwa na maana" Taita aliongea huku akielekea nje na kufanya wenzake wamfuate, walitoka mpaka nje,



"Mzee tutawasiliana, acha niwahi majukumu" Taita aliongea huku akimtazama babu Sarah,



"Mwanangu ebu tupe lifti ya kutufikisha nyumbani, maana hali ya mifuko ni tete" Babu Sarah aliongea kwa upole,



"Chukueni taxi Mzee wangu" Taita aliongea huku akitoa pesa mfukoni na kumpatia babu Sarah,



"Asante mwanangu" Babu Sarah alipokea na kuzitia mfukoni kisha wakaagana na Taita.



Taita aliingia kwenye gari yake huku akiwa na Harry,



"Huyo binti ni nani?" Taita alimuuliza Harry,



"Sasa mimi nitajuaje mkuu?" Harry alihoji huku akimshangaa bosi wake huyo,



"Ujue hivi vitu hatupaswi kuviweka kichwani sana, inawezekana huyo binti amekosea au amesahau makaburi ya ndugu zake na ameyafananisha na yale ya kwetu" Taita aliongea,



"Hiyo pia inawezekana, ila usipuuze tu, mnatakiwa mumfuatilie" Harry aliongea,



"Tutamfuatiliaje wakati hatumjui?" Taita aliuliza,



"Ila sawa, huenda uliyosema ni sawa" Harry aliongea,



"Niliyosema yapi?" Taita aliuliza,



"Hayo ya kufananisha makaburi" Harry alijibu,



"Ebu tuachane na hayo mambo. Umeshakunywa chai?" Taita alimuuliza mwenzake,



"Bado" Harry alijibu,



"Basi ngoja tupitie hotelini tukanywe" Taita aliongea,



"Ni jambo zuri" Harry aliitikia kisha Taita akakanyaga mafuta ya gari na gari ikaongeza mwendo.



*******************



Sarah alishajua kitakachotokea baada ya kujenga makaburi, alihisi kabisa kama kuna ndugu wangeenda kuangalia makaburi yale ni lazima wangepata viulizo vya maswali ya kuwa ni nani aliyeyajengea makaburi yale, kwa hiyo alichofanya ni kumtuma dereva taxi akayamwagilie, kitu ambacho hakukijua dereva taxi ni kuwa muda aliopewa pesa, kiliwekwa na kinasa sauti ambacho kilikuwa kinafikisha sauti kwa Sarah, kwa hiyo wakati dereva akiwa anahojiwa na Taita makaburuni, ndio huo muda Sarah aliosikia kuhusu watu hao kwenda hotelini hapo, alichofanya Sarah ni kubeba mabegi yake na kwenda kukabidhi funguo mapokezi na kulipia kila kitu, mkoni alikuwa na kifaa kidogo cheusi alikishika, kwa hiyo wakati yule muhudumu akijaza file la Sarah kwenye computer, kila kitu kilienda vizuri, ila kilifutika baada ya muhudumu kutoka tu kwenye file lile, naam; hivyo ndivyo Sarah alivyoucheza huo mchezo kwenye computer ya hotel hiyo na mchezo huo huo aliucheza kwenye simu ya dereva taxi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Sarah alitoka nje ya hotel na kwenda kwenye mgahawa wa kitalii uliopo mbele ya hotel hiyo, akaagiza juisi na kisha akakaa katika kiti kinachotazama mlango, mlango wenyewe ulikuwa wa kioo, kwa hiyo aliweza kupaona nje vizuri.



Aliweza kuona namna Taita alivyokuja huku akiambatana na babu yake, aliweza kusikia vyote walivyoongea, aliendelea kuwaangalia mpaka walivyoondoka, ila neno ambalo lilimuuma ni kitendo cha babu yake kumuomba pesa Taita, aliona namna babu yake alivyoisha kwa umasikini, roho ilimuuma Sarah ila hakuwa na papara. Taita alivyoondoka na kisha babu yake alivyoondoka, Sarah alitoka mgahawani hapo na kuchukua bajaji kisha akaiamuru bajaj hiyo impelekee eneo lolote la uswahilini lililo na guest.



Dereva bajaj aliondoa bajaj na kuanza kuelekea maeneo anayoyajua yeye, ilimchukua takribani dakika ishirini ndipo dereva bajaj aliposimamisha bajaj yake nje ya guest iliyochoka,



"Hapa patakufaa dada?" Dereva bajaj alimuuliza Sarah,



"Nahisi patafaa, nitelemshie begi" Sarah aliongea huku akishuka, kisha dereva bajaj akamshushia begi lake,



"Nisubiri, nataka unipeleke mahali" Sarah aliongea huku akilivuta begi lake na kuingia ndani ya guest, alifika mapokezi na kukaribishwa, akapata chumba na kuweka mizigo yake, kisha akatoka na kumwambia dada wa guest kuwa atarudi muda si Mrefu.



Akatoka nje na kupanda ndani ya bajaj,



"Nipeleke osterbay" Sarah aliongea na dereva akawasha bajaj na safari ya osterbay ikaanza chini ya maelekezo ya Sarah.



Bajaj ilifika mpaka osterbay mtaa ule ule anaoishi Taita, Sarah akashuka na kumlipa dereva bajaj pesa yake, dereva bajaj akapokea na kuondoka zake.



Sarah akapiga hatua mpaka katika nyumba ya Taita, alipofika nje ya geti akagonga geti mlinzi akafungua,



"Nimekuja tena" Sarah aliongea huku akitabasamu,



"Karibu" Mlinzi aliongea,



"Taita nimemkuta?" Sarah aliuliza,



"Ametoka" Mlinzi alijibu,



"Naomba nimsubiri" Sarah aliongea,



"Pita ndani ya geti" Mlinzi aliongea kisha Sarah akaingia ndani ya geti,



"Nyumba nzuri, kubwa" Sarah aliisifia nyumba ya Taita huku akitabasamu,



"Twende ndani" Mlinzi aliongea huku akitangulia na kumpeleka Sarah sebuleni, Mlinzi akamuita mfanyakazi wa ndani na kumkabidhisha Sarah kisha mlinzi akarudi getini.



Sarah akasalimiana na mfanyakazi wa ndani, kisha Sarah akajitambulisha yeye ni mchumba wa Vin ili kumtoa hofu yule binti, baada ya huo utambulisho, mfanyakazi wa ndani alielekea jikoni kuendelea na kazi na kumuacha Sarah akitazama runinga.



************



Taita na Harry walipotoka kupata kifungua kinywa waliamua waelekee nyumbani kwa Taita, walifika getini na kisha mlinzi akafungua geti, Taita akaingiza gari na kuiegesha kisha akashuka,



"Kuna mpya gani?" Taita aliuliza wakati alifunga mlango wa gari,



"Yule binti aliyeleta Zawadi siku ile, amekuja tena" Mlinzi alijibu na kufanya Taita amuwekee umakini,



"Ameleta nini leo?" Taita aliuliza huku akiwa amemkazia macho mlinzi,



"Leo amekuja mwenyewe tu, yupo sebuleni" Mlinzi alijibu,



"Unamuamini vipi mpaka umempeleka sebuleni?" Taita aliuliza,



"Kama ni mgeni unadhani angekaribishwa wapi?" Harry aliingilia kati,



"Sio kila mtu anaaminika" Taita alijibu huku akianza kupiga hatua za kuelekea sebuleni na pia alikuwa na shauku kubwa ya kumjua huyo binti.



Alitembea mpaka alipoufikia mlango wa sebuleni na kuufungua taratibu, baada ya kufungua akajikuta anatoa mguno wa mashaka.....





Hakukuta mtu, Taita ikabidi amuite mfanyakazi wa ndani, mfanyakazi akaja sebuleni,



"Nimeambiwa kuna mgeni, yupo wapi?" Taita aliuliza,



"Ameondoka muda si Mrefu" Mfanyakazi alijibu,



"Ameondoka?" Taita aliuliza kwa mshangao,



"Ametoka, kwani mlinzi hajakwambia?" Mfanyakazi akauliza,



"Yeye ndio ameniambia yupo ndani" Taita akajibu huku akishangaa,



"Ameshaondoka, au labda wakati akitoka mlinzi hakuwa getini" Mfanyakazi akajibu,



"Mmeongea nae nini huyo mgeni?" Taita akauliza,



"Alikuwa anataka akusalimie, ameniambia yeye ni mchumba wa Vin" Mfanyakazi akajibu,



"Ndicho hicho tu?" Taita akauliza,



"Hajaniambia kingine" Mfanyakazi akajibu,



"Sawa, kuweni makini sana na wageni, sio kila mtu unamuamini" Taita aliongea huku akielekea nje, alitoka mpaka getini kwa mlinzi,



"Vipi nifungue geti?" Mlinzi akauliza,



"Mbona ndani sijakuta mgeni, nimeambiwa ameondoka" Taita aliongea huku akimuangalia mlinzi,



"Ameondoka?" Mlinzi aliuliza,



"Unaniuliza mimi tena, ina maana wewe hukumuona wakati akiondoka?" Taita aliuliza huku hasira zikianza kumpanda,



"Kweli bosi, nimekumbuka kuwa alitoka, nisamehe nilisahau" Mlinzi aliamua kudanganya ili asionekane mzembe kazini,



"Una mawazo gani mpaka unasahau kwamba kuna mgeni ametoka?" Taita aliuliza kwa ukali,



"Nisamehe sana mkuu, nilipitiwa tu" Mlinzi aliongea huku kichwa chake kikikataa kabisa kuamini kuwa yule msichana ameondoka,



"Kuwa makini" Taita aliongea huku akielekea ndani,



"Sawa mkuu" Mlinzi alijibu huku akimtazama bosi wake anavyoondoka, Taita alivyoingia ndani tu, mlinzi akaelekea nyuma ya nyumba na kuanza kukagua usalama, alipata wasiwasi baada ya kuambiwa mgeni ameondoka wakati yeye hakumuona akipita getini.



Mlinzi baada ya kukagua upande wa nyuma na kuridhika kuwa hakuna kitu chochote kilichotokea, aliamua arudi zake getini.



"Tutakaribisha mpaka majini sasa" Mlinzi aliongea peke yake huku akikaa juu ya kiti pembeni ya geti.



*************************



Sarah alivyoenda kwa Taita, alijua kabisa Taita hayupo, alichofanya ni kwenda kusoma ramani ya ndani na pia alifanikisha kuweka vinasa sauti kwenye sehemu mbili ndani ya sebule ya Taita, na alipomaliza kuweka vinasa sauti hivyo, alimuita Dada wa kazi na kumuaga, ingawa dada wa kazi alishangaa kitendo cha Sarah kuondoka ndani ya muda mfupi, Sarah aligundua hilo na kumdanganya kuwa amepigiwa simu na anahitajika haraka ila atarudi hapo siku yoyote, Dada wa kazi hakuwa na neno, akakubali kumruhusu Sarah aende.



Wakati Sarah anafungua mlango wa sebuleni, aliweza kuna gari ikisimama nje ya geti, akahisi huenda hiyo gari ni ya Taita, alichofanya Sarah ni kutoka kwa mwendo wa haraka na kuelekea nyuma ya nyumba, uko akaangalia mazingira na kugundua anaweza kutoka nje kwa kutumia ukuta ingawa ukuta ulikuwa Mrefu kiasi, alichofanya Sarah alirudi nyuma hatua nne, kisha kwa kasi ya ajabu akauendea ukuta na kuurukia, mikono ikagusa kingo za juu za ukuta, Sarah akajivuta na kupanda juu, kisha akajitupa na kutua upande wa pili, akaangalia kushoto na kulia na hakuona mtu, akatabasamu na kuanza kutembea taratibu mpaka kwenye Barabara ya lami.



Aliendelea kutembea kwa mwendo wa madaha huku akiwa amevaa headphone kama anasikiliza muziki, kumbe alikuwa anasikiliza maongezi yote yaliyokuwa yanaendelea ndani ya sebule ya Taita.



Sarah alitembea kwa mwendo wa madaha mpaka kwenye barabara inayopitisha magari mengi, akaita bajaj na kuingia ndani na kisha akajirudisha mpaka guest ya uswailini kule alipofikia.



Akaingia ndani na kujifungia mlango na kisha akajitupia kitandani na kuanza kufikiria namna anavyopiga hatua zake katika kulipa kisasi, hakuona kama kuna hatua amekosea ila alichofurahi ni mambo kwenda kama anavyotaka yeye,



"Inafuata hatua ya usumbufu sasa" Sarah aliongea peke yake kisha akavua headphones, akasimama na kutoa nguo mwilini kisha akafungua begi lake na kutoa taulo na kujifunga, akaelekea bafuni.



Alitumia muda Mrefu kujisafi mwili, alipotoka bafuni alirudi chumbani na kutafuta suruali ilioushika mwili wake na kuivaa, kisha juu akavaa fulana nyepesi, akatoka mpaka sehemu ya mapokezi,



"Hapa ni wapi naweza kupata madalali wa nyumba?" Sarah alimuuliza Dada wa mapokezi,



"Wapo kule, shika iyo njia inayoelekea kushoto, mwisho kule utakuta kuna kijiwe cha kahawa, hapo ndipo walipo madalali wa nyumba" Dada wa mapokezi alimuelekeza Sarah,



"Nashukuru" Sarah aliongea huku akiondoka na kufuata maelekezo ya yule Dada, alienda moja kwa moja mpaka kwenye kijiwe cha kahawa na kumpata kijana mmoja, akatoka nae katikati ya kundi la watu,



"Kaka mimi natafuta nyumba" Sarah aliongea baada ya salamu,



"Nyumba au chumba?" Dalali aliuliza huku akimuangalia Sarah,



"Nataka nyumba nzima" Sarah aliongea kwa msisitizo,



"Hiyo nyumba unataka upange au unanunua kabisa?" Dalali aliendelea kuuliza,



"Nahitaji ya kununua kabisa" Sarah alijibu,



"Unataka iweje?" Dalali akatupa swali jingine,



"Nataka iwe na vyumba vitatu, kimoja kiwe master, alafu iwe na jiko, stoo, varanda na choo kingine cha ndani kwa ajili ya watu " Sarah aliongea,



"Kitapatikana, unahitaji uhamie lini?" Dalali aliuliza,



"Siku yoyote kitakapopatikana, alafu kinatakiwe kiwe nje ya mji" Sarah aliongea,



"Yaani mjini ila pembezoni, sio katikati ya mji?" Dalali aliuliza,



"Nje ya mji, hata ukipata porini ni sawa, sio lazima iwe Dar es salaam, hata nje ya Dar, ili mradi niwe jirani na Dar" Sarah alitolea ufafanuzi kauli yake,



"Nimekuelewa, nipe namba yako ya simu ili nikifanikisha kukipata, nikutaharifu" Dalali aliongea,



"Sina simu, ukitaka kunipata nenda guest moja inaitwa "SHUMBE" ipo hii barabara niliyotokea, nipo hapo muda wote, ukifika pale ulizia Sarah" Sarah aliongea,



.



"Sawa Dada, ngoja hiyo kazi niianze leo" Dalali aliongea,



"Sawa, jitahidi ukamilishe haraka" Sarah aliongea kisha wakaagana na Dalali, Sarah akarudi Guest kwenda kupumzisha akili.



Alipofika mapokezi alimkuta dada wa mapokezi,



"Vipi umempata dalali?" Dada wa mapokezi alimuuliza Sarah,



"Nimempata, nashukuru kwa msaada wako" Sarah alijibu,



"Asante kushukuru" Dada wa mapokezi alijibu,



"Naenda kupumzika, akija mtu yoyote kuniulizia, muoneshe chumba changu apitilize mpaka ndani" Sarah alimwambia dada wa mapokezi huku akiamini hakuna mtu atayekuja kumuulizia zaidi ya dalali,



"Sawa" Dada wa mapokezi alijibu na Sarah akaelekea chumbani kwake kupumzika.



*****************



Taita hakuridhika na wala hakutaka kuamini huyo msichana aliyekuja ni mchumba wa Vin, kwanza aliamini kama huyo msichana ni mchumba wa Vin, basi Vin angempa taharifa baba yake juu ya ujio wa msichana huyo.



Taita akatoa simu yake mfukoni na kumpigia mwanae huyo na kumuuliza kama ana mchumba Tanzania, lakini Vin alikataa katakata na kwanza alishangaa kusikia hivyo. Taita akakata simu na kuanza kuhisi huenda kuna adui yake katika biashara amemtuma huyo dada kumchunguza.



Taita akatoka mpaka sebuleni na kuanza kukagua kama pako Salama, katika kupekua pekua ndipo alipokiona kinasa sauti kidogo sana pembeni ya kochi, Taita akachukua simu yake na kumpigia kijana wake ambaye ni mtaalam wa teknolojia, huyo kijana anaitwa Sostenes, ila wanamuita Tekso.



Baada ya dakika kumi Tekso alifika na kuoneshwa hicho kinasa sauti, akakichunguza kisha akakizima kwa utaalam, alafu akachukua waya mmoja na kuugeuza, akaupachika kwenye kifaa chake kilichopo kama computer, hapo ndipo alipoweza kugundua huyo mtu aliyeweka hicho kinasa sauti yupo wapi muda huo,



"Tumeshampata huyu" Tekso aliongea huku akitabasamu,



"Ngoja nimuite kijana mmoja uongozane nae, mkaniletee huyo binti" Taita aliongea,



"Mwite aende mwenyewe, mimi nitakuwa hapa namuelekeza kupitia mtambo wangu" Tekso alijibu kisha Taita akamuita kijana wake mmoja aliyejaa jaa mwili.



"Kuna kazi ya ghafla imetokea" Taita alimwambia yule kijana,



"Nipo tayari, niagize mkuu" Kijana aliongea kikakamavu,



"Kuna mtu unatakiwa ukamchukue" Taita aliendelea,



"Yupo wapi?" Kijana aliuliza,



"Tekso ndio atakuwa anakuelekeza kupitia simu, mpaka hiyo sehemu alipo huyo mtu" Taita aliongea,



"Nitamjuaje kama ndiye yeye?" Kijana aliuliza,



"Ni binti, mwembamba kiasi, ukimkuta tofauti na huyo pia mchukue, inawezekana nae ni muhusika" Taita aliongea,



"Nitaenda peke yangu au nitaambatana na wenzangu?" Kijana aliuliza,



"Utaenda mwenyewe tu, chukua gari nenda" Taita aliongea na kisha kijana akapewa maelekezo mengine machache na Tekso, alafu akaondoka zake.



Kijana aliondoka huku akiwa anawasiliana na Tekso muda wote ili aweze kufika sehemu Salama.



Kijana alifanikiwa kufika hilo eneo alilopo Sarah, alifika mpaka nje ya Guest, akasimamisha gari na kuanza kupiga hesabu za kuingia ndani kama atakutana na pingamizi lolote,



Mwisho akaamua kutumia ubabe endapo kutakuwa na kikwazo chochote, kijana akashuka kwenye gari na kuingia moja kwa moja ndani ya Guest, ambapo alimkuta dada wa mapokezi akisinzia sinzia kaunta,



"Karibu kaka, unahitaji chumba?" Dada wa mapokezi alimuuliza,



"Hapana, kuna dada mmoja nimemfuata, nataka kumuona" Kijana alijibu na kumfanya dada wa mapokezi akumbuke kuwa Sarah ndiye aliyesema kuna mgeni wake atakuja kumuulizia,



"Aah yupo, nenda chumba namba nne" Dada wa mapokezi alijibu na kisha yule kijana akaenda mpaka chumba namba nne, akagonga hodi na baada ya muda mchache mlango ulifunguliwa, ulifunguliwa na Sarah mwenyewe, Sarah akapata mshtuko baada ya kukutana na sura ngeni mlangoni,



"Karibu" Sarah aliongea huku akiwa amesimama mlangoni,



"Naweza kupita ndani?" Kijana aliuliza,



"Hapana, kama una shida unaweza kuongea hapo hapo" Sarah alijibu,



"Nina shida, ila nitahitaji tuongee ndani" kijana aliongea,



"Siwezi kumkaribisha chumbani kwangu mtu nisiyemjua" Sarah aliongea huku akiwa amesimama mlangoni,



"Ebu pisha bwana" Kijana aliongea na kumsukuma Sarah na kufanya Sarah apepesuke huku akirudi nyuma, kijana akajitoma ndani kibabe.......





"Unataka nini kutoka kwangu?" Sarah aliuliza huku akionekana ana hasira,



"Sihitaji maswali, unachotakiwa kufanya ni kusikiliza amri kutoka kwangu tu" Kijana alijibu huku macho yake yakiangaza ndani ya chumba kile cha guest,



"Ndio useme sasa unachokitaka" Sarah aliongea,



"Unatakiwa uambatane na mimi mpaka sehemu ninayotaka uende. Sitaki swali jingine" Kijana aliongea,



"Sehemu gani hiyo? kwanza wewe ni nani?" Sarah aliuliza,



"Nimekwambia sitaki maswali, fanya ninachotaka" Kijana aliongea huku akimuendea Sarah,



"Sawa, naomba utoke nibadilishe nguo" Sarah aliongea,



"Badili tu, mimi siwezi kutoka, tutatoka wote" Kijana aliongea huku amemkazia macho Sarah,



"Sawa endelea kuniangalia" Sarah aliongea huku akiliendea begi lake la nguo na kulifungua, kisha akaingiza mkono, bila hata kutegemea ule mkono ulitoka na bastola na kumuelekezea yule kijana, kijana akapigwa na butwaa, maana hakutegemea kitu kama hicho,



"Kaa hapo kwenye kiti" Sarah aliongea huku akimuangalia yule kijana, kijana akatii huku akiendelea kushangaa namna mchezo ulivyombadilikia ghafla namna ile, akakiri ni uzembe mkubwa ameufanya kwa kumdharau mwanamke yule.



Sarah akamsogelea yule kijana,



"Toa earphone hizo, tupa hapo chini" Sarah aliongea na yule kijana akatii na kuitupa chini ile earphone, Sarah akaikota na kuiangalia kwa muda, kisha akaikata kata,



"Lete simu" Sarah aliongea na yule kijana akaitoa simu na kuitupa jirani na miguu yake, Sarah akaiendea akainama ili aiokote, Kijana alirusha teke lililoipiga bastola ya Sarah, kisha akarusha ngumi nyingine kumuendea Sarah, kwa ukali wa ile ngumi ilikuwa ngumu sarah kuidaka ingawa alikuwa na uwezo huo, alichofanya Sarah ni kurudi nyuma kisha akaachia teke jepesi kulenga tumbo la yule kijana, kijana akaudaka mguu wa Sarah, na hicho ndicho Sarah alichokikusudia, baada ya mguu wake kudakwa, Sarah aliruka sarakasi na kujibinua kisha ule mguu wake mwingine ukaenda kukipiga kidevu cha yule kijana, kijana akajikuta anayumba huku akirudi nyuma, Sarah akamuendea kwa kasi na kumpiga teke Kali la shingo na yule kijana akajikuta anatua chini kama mzigo huku akipambana na macho yake yaliyokuwa yanaona maluweluwe.



Sarah akarudi nyuma na kuikota bastola yake kisha akakaa kitandani huku akimuangalia yule kijana aliyekuwa ahamini kitu kilichofanywa na huyo binti muda mchache uliopita,



"Taita amekutuma si ndio?" Sarah aliuliza huku akiwa amemkazia macho,



"Hapana" Kijana alijibu huku macho yake yakipingana na jibu lake,



"Nimesikia kila mlichoongea na kila ulichoagizwa, napenda sana mtu mkweli. Ulitumwa unichukue?" Sarah aliuliza tena,



"Ndio" Kijana alijibu,



"Twende unipeleke" Sarah aliongea huku akimtazama yule kijana aliyekuwa anashangaa kujiamini kwa binti huyo,



"Nyanyuka wewe, hakuna muda wa kushangaana, ongoza mbele na usithubutu kugeuza shingo nyuma" Sarah aliongea kwa sauti kali na kumfanya Kijana asimame na kuanza kuelekea nje huku akifuatwa na Sarah.



Walipofika jirani na kaunta, Sarah akaificha bastola,



"Unatoka Bibie?" Dada wa mapokezi alimuuliza Sarah,



"Yap, nitarudi muda si mrefu" Sarah alijibu bila kugeuka na huku akisonga mbele. Walielekea moja kwa moja mpaka nje pembeni ya gari,



"Panda gari, wewe ndio dereva" Sarah aliongea na kijana akaingia upande wa dereva kisha Sarah akaingia siti za nyuma, kijana akawasha gari na kuiondoa kwa mwendo wa taratibu kulingana na maelezo ya Sarah.



Gari ilitembea kwa dakika kadhaa mpaka ilipoanza kuingia mitaa ya osterbay,



"Simamisha gari" Sarah aliongea na kijana akatii, kisha Sarah akaendelea,



"Kwa umri ulionao unaona kipi bora kati ya uhai na kifo" Sarah aliuliza,



"Uhai" kijana alijibu,



"Kuanzia sasa una machaguo mawili, chaguo la kwanza ni kufikisha ujumbe nitaokupa ili uendelee kuishi, na chaguo la pili ni kutofukisha ujumbe nitaokupa alafu ufe" Sarah aliongea kisha akameza mate,



"Nitafikisha ujumbe" Kijana aliongea kwa uoga,



"Kamwambie Taita kuwa yeye ni mpumbavu, huo ndio ujumbe unaotakiwa kuufikisha" Sarah aliongea na kukaa kimya,



"Sawa nitamwambia" Kijana aliongea,



"Hiyo ni juu yako wewe, ila matokeo yake nimeshakwambia. Ukifika nitakupa dakika tano za kumwambia, ukishindwa kumwambia ndio kifo chako kitatimia" Sarah aliongea kisha akampiga ngumi kali ya shingo yule kijana, kijana akapoteza fahamu na hakujua kitu chochote kilichoendelea.



Kijana alifungua macho na kujikuta amekaa siti ya nyuma ya gari, na alipoangalia siti ya dereva hakuona mtu, ndipo alipokurupuka na kuchungulia nje na kujikuta yupo kama nyumba ya tatu kutoka kwa Taita, Kijana akatelemka katika gari na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye geti la Taita, akaingia na kupitiliza moja mwa moja mpaka sebuleni na kumkuta Taita na vijana wengine wakiwa kama na kikao, walipomuona mwenzao walishtuka,



"Yaani tulikuwa tunaangalia namna ya kukupata, maana ulipotea ghafla mtandaoni" Tekso aliongea huku akimuangalia yule kijana,



"Aisee yule Dada sio wa kawaida" Kijana aliongea,



"Kwanini unasema hivyo?" Taita aliuliza,



"Amejipanga kupambana" Kijana alijibu huku akikikumbuka kichapo alichopigwa,



"Yupo wapi sasa?" Taita aliuliza,



"Sijui, tulikuja nae ila alinipiga na nikapoteza fahamu, niliposhtuka nikajikuta nipo peke yangu" Kijana alitoa maelezo,



"Kuna ujumbe wowote amekupa?" Taita aliuliza,



"Hapana, hapana hajanipa" Kijana alijibu, sio kwamba hakuwa na kumbukumbu kwa alichoagizwa na Sarah, ila alimuheshimu sana bosi wake kwa hiyo aliona ni dharau sana kumuita bosi wake mpumbavu na ndio maana hakutaka kumwambia.



"Lakini umejua anapokaa?" Tekso akamuuliza yule kijana,



"Ndio, anaishi guest" Kijana alijibu,



"Guest? Tukienda tutamkuta kweli?" Taita aliuliza,



"Twendeni haraka, tukimkosa tunaweza kupata mwanga wowote wa kumjua" Tekso aliongea,



"Gari ipo wapi?" Taita alimuuliza yule kijana,



"Gari ipo, ipo nyumba ya tatu kutoka hapa" Kijana alijibu



"Nyumba ya tatu kutoka hapa? Kwanini umeiegesha uko?" Taita aliuliza,



"Sio mimi, ni huyo Dada, alinipiga nikazimia ndio nikajikuta ameegesha gari hapo" Kijana alijibu,



"Kaisogeze hapa basi hiyo gari" Taita aliongea na kisha kijana akatoka kwenda kuifuata hiyo gari, alipoifikia alifungua mlango na kuingia ndani ya gari, alilikagua hilo gari kama limetegwa bomu ila hakukuta kitu, akajiridhisha kupo Salama, akawasha gari na kuisogeza mpaka nje ya geti la Taita. Akafungua mlango ili ashuke, ila akaiona simu yake iliyokuwa kwenye siti ya pembeni ikiita, akaichukua na kuangalia jina la mpigaji ila hakukuta jina isipokuwa namba tu, akabofya kitufe cha kupokelea,



"Halow" Kijana aliongea,



"Ulichagua kufikisha ujumbe niliokupa, ila umeshindwa kufikisha" Ilikuwa ni sauti ya Sarah iliyofanya kijana ajiulize kuwa huyo binti amejuaje kuwa ujumbe haujafika,



"Wewe Malaya usiniendeshe, huo ujumbe ungeupeleka mwenyewe" Kijana alijibu kibabe,.



"Umefeli, angalia chini ya kiti ulichokalia" Sarah aliongea kisha akakata simu, yule kijana akainuka na kufunua kiti, papo hapo ukatokea mlipuko mkubwa wa bomu, yaani ile gari ililipuka na yule kijana akiwa ndani ya gari, huo ndio ukawa mwisho wa yule kijana.



Kule mlipuko wa bomu uliwastua mpaka Taita na vijana wake, wakatoka sebuleni ili kuelekea getini, wakakuta geti na ukuta wake vyote vipo chini na gari aliyokuwemo yule kijana ilikuwa ikiwaka moto.



Taita akaonekana dhahiri amechanganyikiwa kutokana na lile tukio,



"Mlinzi wa geti yupo wapi?" Taita aliuliza ila hakuna mtu aliyemjibu kwa maana kutokana na watu kutojua ni wapi mlinzi alipo kwa muda huo.



Na kipindi hicho watu wengine walikuwa wakianza kujisogeza eneo la tukio, na polisi pia walifika kwa ajili ya kuja kuangalia tukio hilo.



Baada ya muda, vijana wa Taita wakaanza kutoa matofali yaliyokuwa yamezagaa hapo, ni matofali ya ukuta wa geti ulioangushwa na Bomu.



Baada ya kumaliza walinyanyua geti, chini ya geti ndipo walipomkuta mlinzi akiwa amelaliwa na geti na hakuwa na fahamu,



"Bosi mlinzi huyu hapa" kijana mmoja alimwambia Taita, Taita akasogea na kumkuta mlinzi akiwa amelala na mwili umejaa damu, bahati nzuri na gari ya hospitali ilikuwa hapo, ikambeba mlinzi na kuondoka nae.



Polisi wakachukua maelezo kidogo kwa Taita kisha nao wakaondoka zao.



Baada ya muda kidogo watu wakiwa wameshasambaa na muda huo vijana wa Taita wakiwa bize na shughuli za hapo, ndipo simu ya Taita ikaanza kuita, alipoangalia kioo cha simu akakutana na namba ngeni,



"Hallow" Taita aliongea baada ya kupokea,



"Pole kwa tukio, ila huo ni mwanzo tu, watakufa watu wengi kwa ajili yako ila mwisho ni kwamba mimi naitaka roho yako" ilikuwa ni sauti ya Sarah, iliongea maneno machache ila yalikuwa makali,



"We ni nani?" Taita aliuliza,



"Unanijua vizuri tu" Sarah alijibu na kuzidi kumchanganya Taita,



"Ningekuwa nakujua nisingekuuliza" Taita aliongea,



"Kwa hiyo unataka kuniona kwa Mara nyingine tena?" Sarah aliuliza,



"Ndio" Taita alijibu kwa shahuku,



"Geuka, nipo nyuma yako" Sarah aliongea na Taita akageuka, ndipo alipomuona msichana akiwa amesimama huku akitabasamu na sikioni alikuwa na simu aliyoishika kwa kiganja chake, alikuwa ni Sarah,



"Nahisi umeniona sasa" Sarah aliongea huku akitabasamu na kufanya Taita atoe macho.......................





Taita alipigwa na butwaa, ila ubaya ni kuwa Sarah alikuwa amesimama umbali mrefu kutoka yeye aliposimama, tena mbali sana na ilikuwa ngumu sana kuiona hata sura yake.



Taita aliendelea kumuangalia binti yule huku hasira zikimpanda taratibu,



"Nadhani umeniona, kwaheri" Sarah aliongea kisha akakata simu na kuondoka zake kwa kufuata kona iliyopo jirani na aliposimama, alifanya hivyo ili kumpoteza Taita.



Taita kuona binti huyo amepotelea kwenye kona, ndipo akili zikamjia, akamwambia Trigger atoke na gari, Trigger akatii akatoa gari ndani na kisha Taita akaingia ndani ya gari,



"Twende mpaka kwenye kona ilee" Taita aliongea kisha Trigger akaiondoa gari kwa kasi mpaka kwenye hiyo kona na kuisimamisha gari, Taita akatupa macho upande alipoelekea Sarah ili aweze kuona kama atamuona, lakini hakuona mtu kabisa upande huo,



"Twende upande huo" Taita aliongea na kisha Trigger akakunja kona kuelekea ule upande alioambiwa na Taita. Gari ilitembea kwa mwendo wa wastani kwa muda Mrefu mpaka walipotokezea sehemu iliyokuwa na pilika pilika za watu wengi, Taita akamuamuru Trigger asimamishe gari, Trigger akatii.



Taita akatelemka na kuanza kuangaza angaza kila upande ili aone kama ataabatika kumuona binti anayemtaka, lakini hakupata bahati hiyo, Taita akapiga paji lake la uso kwa hasira kisha akarudi ndani ya gari,



"Geuza gari turudi nyumbani" Taita aliongea na kisha Trigger akafuata amri ya bosi wake na kuigeuza gari na kuishika njia aliyokuja nayo.



"Kwani vipi?" Trigger alimuuliza Taita baada ya kuona kama hamuelewi vile,



"Yule binti niliyewaambieni anatufuatilia, ndio amehusika na ule mlipuko pale nyumbani" Taita aliongea huku akikuna uwaraza wake,



"Nani amekuambia?" Trigger aliuliza,



"Ndio amenipigia simu muda mfupi uliopita na kujinasibu kuwa amefanya hivyo, na cha ajabu nilimuona kwa macho yangu" Taita aliongea,



"Ungempiga risasi" Trigger aliongea kwa hamaki,



"Alikuwa mbali, ndio maana nikakwambia utoke na gari na hapa nilikuwa namfuatilia, ila bahati mbaya sijampata, sasa sijui nae alikuwa na usafiri?" Taita aliuliza bila kuwa na jibu,



"Hivi huyu mtu ni nani na kwanini afanye hivi? ni lazima tuwe makini nae, maana kwa hili shambulio inaonesha yupo upande wa hatari zaidi" Trigger aliongea,



"Inahitajika tufanye mkutano wa haraka ili tujipange, huyu mtu inaelekea anatujua vizuri" Taita aliongea wakati gari ikisimama nje ya nyumba yake,



"Tena leo hii hii, maana tukingoja mpaka kesho inaweza kuwa matatizo zaidi" Trigger aliongea,



"Leo hii, wewe wasiliana na watu muhimu wa kundi, waambie tukutane Vin hotel, saa moja jioni" Taita aliongea kisha akatelemka katika gari na kumuacha Trigger akibonyeza bonyeza vitufe vya siku yake, nadhani ndio alikuwa anajiandaa kutoa taarifa za kikao kwa wenzake.



********************



Sarah alipotoka mtaa anaohishi Taita, alirudi moja kwa moja katika guest aliyofikia, alichokiwaza muda huo ni kuwa ni lazima vijana wa Taita wataenda eneo hilo kwa kuwa walishajua ni wapi alipo kutokana na mawasiliano waliyokuwa wanayafanya na yule kijana wa kwanza.



Sarah aliwaza kuhama muda huo, na alipanga aende guest nyingine tofauti na hiyo ila iwe mafichoni kama hiyo.



Sarah akarudishia nguo zake kwenye begi kisha akakusanya kila kitu chake na akaanza kutoka nje ya chumba chake, alitoka mpaka mapokezi na kumkuta Dada wa mapokezi akisinzia,



"Dada mimi naondoka" Sarah aliongea na kumshtua yule Dada toka usingizini,



"Mbona ghafla hivyo, au tayari umepata nyumba?" Dada wa mapokezi aliuliza,



"Hapana, nahamia kwa rafiki yangu, si unajua kukaa guest kila siku ni gharama sana" Sarah alidanganya huku akitabasamu,



.



"Kweli lakini. Sawa dada, karibu tena" Dada wa mapokezi alijibu kwa huzuni,



"Hauendi kukagua hata chumba kama kipo Salama?" Sarah alimuuliza yule dada,



"Nakuhamini bwana" Dada wa mapokezi alijibu huku akitabasamu,



"Nenda kakague, ndio unaniamini ila fuata utaratibu wa kazi" Sarah alimsihi yule dada, dada wa mapokezi akaona bora aende,



"Haya ngoja nikakague, ila naamini pako Salama tu" Dada wa mapokezi aliongea huku akielekea chumbani, Sarah akatumia mwanya huo kuingiza mkono chini ya meza ya kaunta na kutoa daftari la wageni, kisha akatafuta karatasi iliyokuwa na jina lake na kuling'oa lile karatasi, kisha akarudisha daftari.



Baada ya dakika Dada wa mapokezi akarejea huku akitabasamu,



"Ndani kupo Salama, mimi nakuamini" Dada wa mapokezi aliongea huku akitabasamu,



"Sidaiwi kwa maana uwa nalipa kila asubuhi" Sarah aliongea,



"Huna deni, hilo nalijua" Dada wa mapokezi aliongea kichangamfu,



"Shika hii utakunywa soda, kwaheri" Sarah aliongea huku akimpatia noti ya elfu kumi yule dada wa kaunta,



"Asante shoga" Dada wa mapokezi aliongea huku akipokea ile hela huku akifurahi, maana ilikuwa bahati kubwa sana kupewa pesa kubwa kama ile.



Sarah alitoka mpaka nje huku akibuluta begi lake la matairi, alipofika mbele ya guest kama bahati vile alikutana na dalali yule aliyemuagiza amtafutie chumba, dalali alikuwa ndani ya gari ndogo ambayo umbo la gari hiyo na bei nahisi vililingana,



"Dada ndio nimekufuata, tena nimekuwahi maana naona unaondoka" Dalali aliongea huku akitabasamu,



"Nilikuwa naondoka ila nilitaka nianzie kijiweni kwako kukuangalia ulipofikia. Vipi umefanikisha?" Sarah alimuuliza dalali,



"Ndio, nyumba imepatikana na hapa nilikuja kukuchukua ukapaangalie" Dalali aliongea,



"Haina shida, je naweza kuhamia leo endapo nitapapenda?" Sarah aliuliza,



"Leo?" Dalali aliuliza huku akishangaa,



"Ndio, nataka nihamie leo kama patanipendeza" Sarah alijibu,



"We twende tukapaangalie, kama mtafikiana makubaliano na mwenye nyumba, utahamia tu" Dalali alijibu,



"Niingie kwenye gari au?" Sarah alimuuliza dereva,



" ingia twende" Dalali alijibu.



"Naruhusiwa kukaa mbele?" Sarah aliuliza,



"Ni wewe tu uamuzi wako" Dalali alijibu,



"Nadhani nyuma ni pazuri" Sarah alijibu.



**************************



Ingawa Taita na vijana wake walikubaliana kuwa saa moja ndipo kuwe na kikao pale Vin hotel kwa ajili ya kumjadili binti msumbufu aliyewafanyia shambulio, lakini kuna mkali anaitwa Tekso, yeye aliamini kuwa tayari anapokaa Sarah kumejulikana, basi ni lazima vijana waende muda huo kuangalia uwezekano wa kumpata Sarah.



Tekso alitoa mpaka ramani kutokana tu na mawalisiliano ya hawali baina ya Tekso na kijana aliyetumwa akamchukue Sarah hawali, pia vile vinasa sauti alivyovitega Sarah kwenye nyumba ya Taita na baadae Tekso alipokuja kuvichakachukua ndipo alipoweza kugundua huyo mtu aliyevitega hivyo vinasa sauti anapatikana Wapi.



Tekso baada ya muswada wake kupitishwa na Taita, Tekso aliwachukua vijana takribani sita na kuingia nao ndani ya gari aina ya land cruiser, wakaondoka kwa kasi ili kujaribu kumuwahi Sarah.



Land cruiser waliyopanda vijana wa Taita iliwasili katika maeneo jirani na guest aliyokuwa akihishi Sarah, walichofanya vijana wa Taita ni kuzuia ile Barabara yote ambayo ilikuwa inaingiza na kutoa magari yaendayo kule mtaa wenye guest, uzuri ni kwamba barabara yenyewe ilikuwa moja tu, kama ni kamari basi walikuwa wametupa kete ya ushindi.



kisha Tekso alitelemka na kuanza kutembea kwa mguu kuelekea kwenye hiyo guest, aliamua kufanya hivyo mara baada ya simu yake kuonesha kuwa yupo jirani tu na hiyo guest. Tekso aliambatana na vijana wengine wawili.



Vijana wengine walibaki na gari, tena gari yenyewe walikuwa wameisimamisha katikati ya barabara kwa ajili ya kuweza kusimamisha gari zote ili wazikague kama huyo binti wanaemtafuta atakuwepo, ingawa hawakumjua ila walipewa wajihi wake kwa nje, waliambiwa ni mwembamba na ana kimo cha wastani, kwa hiyo walichokuwa wanafikiri wale vijana ni kukamata wasichana wote wembamba wenye kima cha wastani wataowahisi kwa namna moja au nyingine.



Baada ya dakika moja tu ya kukaa barabarani kwa vijana wa Taita na gari yao, walishuhudia gari ndogo ikitokea upande ule wa guest na kuelekea upande walipo wao, vijana hawakuwa na pupa, waliisubiri ile gari ilivyokuja mpaka ilipowakaribia, ile gari ndogo ikasimama kutokana na kutokuwa na nafasi ya kupita, vijana wa Taita wakashuka na kwenda kugonga kwenye kioo cha dereva wa ile gari ndogo kwa maana ile gari ilikuwa na vioo vya Giza.



Dereva wa gari ndogo akashusha kioo, alikuwa ni yule dalali wa Sarah, vijana wa Taita wakamsalimia,



"Unaweza kutufungulia milango kuna mtu tunamtafuta" Kijana wa Taita aliongea huku akimuangalia Dalali,



"Hakuna mtu zaidi yangu ndani ya gari" Dalali alijibu baada ya kufikiria kwa muda, vijana wa Taita wakamtilia shaka,



"Basi fungua milango" kijana mmoja akaongea kwa hasira,



"Hakuna mtu, si nimeshawaambia" Dalali aliongea,



"Mbona mnambeleleza sana" kijana mwingine aliongea huku akimuwekea bastola usawa wa kichwa yule dereva,



"Haya fungua milango" Kijana aliongea huku akiwa hana mzaha hata kidogo, dalali akalegeza kamba, aka unlock milango yote, kisha kwa pupa vijana wa Taita wakakimbilia kufungua milango ya nyuma ya ile gari ya dalali.........





Baada ya kufungua milango hawakukuta mtu ndani ya gari,



"Niliwaambia nipo peke yangu, mbona mnanichelewesha? kwanza nyie ni wakina nani, mbona hamjajitambulisha?" Dalali aliuliza kwa kulalamika lakini hakujibiwa kitu, vijana wa Taita walikuwa bize na upekuzi wa gari.



Walipekua na walipojiridhisha ndipo wakamruhusu dalali aondoke, Dalali aliondoka huku akinung'unika sana, alihisi hakutendewa haki kabisa.



Vijana wa Taita wakaendelea kusimama pale huku wakiendelea na kazi ya kukagua kila chombo cha usafiri kinachoingia na kutoka eneo lile.



**********_**



Tekso akiwa na vijana wawili walifanikiwa kufika mpaka guest ile aliyokuwa anaishi Sarah, waliweza kufika kaunta na kumkuta dada wa mapokezi akisugua kucha zake,



"Karibuni kaka zangu, vyumba vipo" Dada wa mapokezi aliongea kwa uchangamfu,



"Hapana hatuna shida na vyumba, kuna dada tunamtafuta anaishi hapa" Tekso aliongea huku akimtazama Dada wa mapokezi aliyekuwa na mwili mkubwa, uswahilini tunawaita vibonge,



"Yukoje?" Dada wa mapokezi akauliza,



"Mwembamba na ana kimo cha wastani, mweupe" Tekso alitoa jibu kulingana na maelezo ya Taita,



"Ameondoka muda sio Mrefu" Dada wa mapokezi alijibu,



"Atarudi muda gani?" Tekso aliuliza,



"Yaani ameondoka moja kwa moja, amesema anaenda kuishi kwa rafiki yake kwa kuwa kuishi hapa ni gharama. Ni ndugu yenu kwani?" Dada wa mapokezi aliuliza,



"Ameondoka muda gani?" Tekso aliuliza huku akiwa amekata tamaa,



"Sasa hivi tu, yaani hana hata dakika tano" Dada wa mapokezi alijibu na kufanya Tekso awaze kwa muda,



"Ameondoka na usafiri?" Tekso aliuliza,



"Ndio, amechukuliwa na gari ndogo nyeusi" Dada wa mapokezi alijibu na kufanya Tekso akumbuke kuwa alipishana na gari ndogo nyeusi iliyokuwa na vioo vya Giza (tinted),



"Ebu wapigie simu wenzako waulize kama wameiona hiyo gari pale njiani" Tekso aliongea huku akimgeukia kijana mmoja waliyeambatana nae, yule kijana akatoa siku mfukoni na kubonyeza vitufe kadhaa kisha akaiweka simu sikioni, baada ya sekunde akaanza kuongea na upande wa pili wa siku na kisha akakata,



"Hiyo gari wameiona ila wanadai ndani alikuwepo mtu mmoja tu, mwanaume" Kijana aliyeongea na simu alimpa taarifa Tekso,



"Dah, kwa hiyo inawezekana huyo dada bado yupo mtaa huu huu?" Tekso aliwauliza wenzake,



"Kama hawajamuona basi inawezekana yupo" Kijana mmoja alijibu,



"Dada unaweza kunipeleka chumba alichokuwa anahishi?" Tekso alimuuliza Dada wa mapokezi,



"Lakini kaka yangu hamjajitambulisha" Dada wa mapokezi aliongea,



"Utatujua baadae, nipeleke katika chumba alichokuwa anaishi" Tekso aliongea na kisha Dada wa mapokezi akatoka kaunta na kuelekea moja kwa moja katika chumba alichokuwa akikaa Saraha na kukifungua mlango kisha akaingia na nyuma yake alikuwa Tekso, baada ya kuingia ndani Tekso akaanza kukichunguza kile chumba kama ataambulia chochote, ila hakubagatika kupata kitu chochote, akatoka nje huku akifuatwa na dada wa mapokezi.



Walielekea mpaka kaunta,



"Unaweza kutusaidia jina lake?" Tekso alimuuliza yule dada, na kufanya yule dada achukue daftari lake la orodha ya wageni walichukua vyumba na kuanza kupekua kutafuta jina la Sarah ila hakuliona, akarudia tena pia hakuona,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Jina lake halionekani" Dada wa mapokezi aliongea,



"Kwani wewe hulijui jina lake?" Tekso alimuuliza,



"Silijui" Dada wa mapokezi alijibu na kufanya Tekso amuangalie tu bila kuongea kitu, kisha akawaamuru vijana wake waondoke eneo hilo.



Tekso na vijana wake wakaenda mpaka walipokuwa wenzao na gari lao, wakaongea maneno mawili matatu kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka zao.



******************



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog