Search This Blog

Friday 18 November 2022

SALA YA SARAH - 5

 





    Simulizi : Sala Ya Sarah

    Sehemu Ya Tano (5)









    Usiku ule Vin alirudi ndani ya chumba chake ndani ya Vin hotel huku mawazo juu ya kuponea kifo mikononi mwa Sarah yakiwa yamemkaa kichwani.



    Vin akafungua friji na kutoa soda, akaimiminia kwenye bilauri na kuinywa taratibu, kisha akasimama na kuvua koti la suti, akaliweka ndani ya kabati,



    "Alafu mwisho amemjeruhi mlinzi na kuniambia nikimbie kabla polisi hawajafika, huyu mwanamke ni nani? au anataka kuniteka akili ili baadae anitumie?" Vin aliwaza huku akijitupa kwenye kochi lililopo ndani ya chumba hicho.



    Vin alitamani kwenda hospitali muda huo ili amueleze kilichotokea, ila alihofu muda huo ingekuwa ngumu kupewa ruhusa ya kuingia hospitali kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana.



    "eti dada yangu, dada gani shetani?" Vin aliendelea kujiuliza na muda huo mlango wa chumba chake uligongwa. Akainuka na kwenda kufungua, alimkuta Trigger akiwa amesimama mlangoni,



    "pita ndani, vipi umefanikiwa kumpata Harry?" Vin alimuuliza Trigger,



    "hapana, nimezunguka sana nimemkosa" Trigger alijibu,.



    "atapatikana tu" Vin aliongea huku akikaa vizuri kwenye kochi,



    "hata nyumbani hajarudi, au hukukaa sana?" Trigger aliuliza,



    "alikuja Sarah aisee" Vin aliongea kwa upole,



    "umemmaliza? au nini kimetokea?" Trigger aliuliza kwa shahuku ya kutaka kujua,



    "Tumepambana sana, ila mwisho wa siku alinizidi uwezo na kuniwekea bastola kichwani, ila ghafla akawa mpole na kuniita mimi mdogo wake" Vin aliongea kwa sauti tulivu na kumfanya Trigger ashtuke,



    "Alafu?" Trigger akauliza,



    "ebu Trigger kuwa muwazi, Sarah ni nani?" Vin aliuliza kwa utulivu,



    "yule ni shetani, anatakiwa kufa" Trigger aliongea huku akiwa ana wasiwasi,



    "amesema mimi ni mdogo wake na kweli ameshindwa kuniua ingawa alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Je mimi ni mdogo wake kweli?" Vin aliuliza huku mkono ukiwa shavuni, ila Trigger alisita kujibu, alihisi Vin kuna kitu amekijua,



    "aisee tutaonana kesho" Trigger aliongea huku akiinuka kwenye kiti,



    "hujanijibu wewe, Sarah ni dada yangu?' Vin aliuliza huku akiwa amemshika mkono Trigger, Trigger akasimama na kumgeukia Vin, kisha Trigger akafikiri kwa muda,



    "ndio, Sarah ni dada yako" Trigger alijibu na kumfanya Vin ashtuke..................





    "Dada yangu? Kivipi?" Vin aliuliza kwa mshangao,



    "kwa sisi watanzania mwanamke yoyote anaweza kuwa dada yako, hiyo ndiyo maana yangu" Trigger alijibu,



    "kwa hiyo sina unasaba nae?" Vin aliuliza,



    "unasaba utoke wapi na wakati wewe umezaliwa marekani na unaishi uko, kama ungekuwa na ndugu yako si baba yako angekuambia? Muda mwingine utumie akili bwana" Trigger aliongea kumshawaishi Vin,



    "unaweza kwenda" Vin aliongea huku akiuachia mkono wa Trigger,



    "lakini umenielewa, si ndio?" Trigger aliuliza,



    "nenda Kaka, si umeshanijibu?" Vin aliongea kwa ukali na kumfanya Trigger aondoke huku akitabasamu, ila pia alikuwa na wasiwasi na kitendo cha Vin kuhoji unasaba wake na Sarah.



    ****************



    Sarah alifika nyumbani kwake huku akiwa na uchungu sana, kitu ambacho kilimpa uchungu ni kile kitendo cha kukuta familia ya Harry yote imekufa,



    "kwanini Vin ameua watu wasio na hatia?" Sarah aliongea kwa uchungu huku akilia,



    "Sarah mama, vipi mbona unalia?" Babu yake aliuliza huku akiingia sebuleni kutoka chumbani kwake,



    "babu nimemuona Sebastian mdogo wangu, ila naona amekuwa katili sana" Sarah alitoa habari ya kushangaza kwa babu yake,



    "umemuona wapi na umejuaje huyo ni ndugu yako?" Babu yake Sarah aliuliza,



    "si zile alama ulizonielekeza, nimeona anazo mbili sehemu kama ilipo ya kwangu" Sarah aliongea kwa uchungu,



    "ebu mchunguze tena, maana utotoni kwenu uliwahi kumuunguza na uji, kwa hiyo ana baka la moto mgongoni, ebu kamchunguze" Babu yake Sarah aliongea kwa udadisi,



    "nitafanya hivyo, ila yule ni yeye tu, nakumbuka sana siku ile Taita anachoma nyumba yetu, alituchukua mimi na Seba na kutupakia kwenye gari lake, ila baadae Harry akamshauri anishushe mimi na kunirudisha ndani, kisha wao wakabaki na Seba. Na ndio maana mwili wa Seba hakuonekana baada ya nyumba kuungua na hakuna aliyejua huo mwili ni wapi ulipo?" Sarah aliongea na kufanya babu yake atingishe kichwa kuonesha amekubaliana nae,



    "au nipeleke nikamuone" Babu yake Sarah aliongea,



    "sipajui anapokaa, alafu hata nikikupeleka bado hatokujua" Sarah aliongea,



    "sasa utafanyaje ili akujue? " Babu yake Sarah aliuliza,



    "dunia ya leo imeendelea, tutatumia hata sayansi" Sarah alijibu,



    "mama lakini angalia mapambano hayo, usije ukapoteza uhai" Babu yake Sarah alimuonya,



    "mzee, kusanya nguo zako zote muhimu, kesho tunahama hapa" Sarah aliongea huku akiinuka kwenye kochi na kuingia ndani na kumuacha babu yake akiwa anashangaa maamuzi ya ghafla ya mjukuu wake.



    ******************



    Asubuhi ya leo Sajenti Minja aliamkia ofisini kwake, alipofika alifungua makabrasha yanayohusu kesi ya Sarah, akayapitia na mwisho akaona atafute chanzo cha ugomvi wa Taita na Sarah.



    "sasa kama Sarah ana ugomvi na Taita, na kwanini aende akaiteketeza familia ya Harry jana? Huyo Harry ni nani?. Sarah ana hatia, na nikiendelea kumlegezea kamba anaweza kufanya mauaji ya kutisha sana" Sajenti Minja aliongea peke yake huku akiifunga kabrasha la kesi ya Sarah, kisha akainuka na kutoka mpaka eneo ilipo kaunta ya polisi,



    "chukua askari watano na gari, hakikisha wanabeba bunduki zenye risasi, alafu nifuateni" Sajenti Minja alitoa agizo kwa askari aliyemkuta hapo, kisha Sajenti Minja akaelekea kwenye gari yake na kuingia, akawa anasubiri agizo lake litimizwe.



    Baada ya dakika tano, gari ya polisi ilikuwa tayari imeshajaa askari waliokuwa na silaha, Sajenti Minja akawasha gari yake na kuiondoa, huku nyuma gari ya polisi ilikuwa ikimfuata.



    Walitembea kwa mwendo wa muda kidogo, kisha Sajenti Minja akaisimamisha gari yake mbele ya geti la nyumba ya Sarah, na ile gari ya polisi ikasimama ikasimama. Sajenti Minja akatelemka, na kupatwa mshangao, alikuta geti la nyumba ya Sarah likiwa na kufuri, akasogelea jirani na geti na kuchungulia,



    "askari wawili nifuateni" Sajenti Minja aliongea kisha akarudi nyuma hatua mbili na kukimbia kwa kasi kuelekea getini, alipofika aliruka na kukamata geti kwa juu kisha akajivuta na kuangukia ndani ya geti.



    Askari wakabaki nje wakiwa wanashangaa namna mkuu wao alivyoingia ndani, hawakuwahi kudhaii kama anajua kufanya vitu kama hivyo, walijua ni mzembe tu,



    "nyie mnafanya nini uko nje, ingieni" Sajenti Minja aliongea kwa ukali na kufanya wale askari wa nje wagutuke, na wao wakaingia ndani kwa mtindo huo huo alitumia Sajenti Minja.



    Sajenti Minja alikuta gari ya Sarah ikiwa imeegeshwa ndani, alipojaribu kufungua mlango akakuta imefungwa, akaanza kuelekea moja kwa moja kwenye mlango wa sebuleni, napo akakuta kumefungwa na kufuri kubwa, Sajenti Minja akaishika ile kufuri na kuutingisha, kisha akazunguka upande wa nyuma wa nyumba na kukuta kufuri nyingine.



    Sajenti Minja akatoa simu yake mfukoni na kujaribu kupiga namba ya Sarah, ikawa haipatikani, akatabasamu,



    "tuondokeni" Sajenti Minja akaongea kisha akaanza kuondoka na kufanya askari wengine wakamfuata, walipofika getini wakatoka kwa mtindo ule ule walioingia nao, walipofika nje Sajenti Minja akawaruhusu askari wengine waondoke, kisha yeye akaingia kwenye gari yake na kuliondoa kwa mwendo wa haraka.



    Safari ya Sajenti Minja iliishia katika hotel ambayo alikuwa anakaa Dokta Pendo, alifika na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Dokta Pendo. Alipofika mlangoni aligonga hodi, lakini hakujibiwa, akarudia tena lakini bado hakukuwa na jibu,



    "anaoga au?" Sajenti Minja alijiuliza huku akirudia tena kupiga hodi, lakini hakuna aliyejibu, akaamua asukume mlango ila ulionekana umefungwa. Sajenti Minja akatoa simu na kupiga namba ya Dokta Pendo, haikupatikana, Sajenti Minja akarudisha simu mfukoni kisha akaamua arudi mpaka mapokezi,



    "samahani dada, yule binti wa chumba namba kumi na tisa ametoka?" Sajenti Minja alimuuliza Muhudumu,



    "yule aliyevunjika miguu?" Muhudumu naye akauliza,



    "huyo huyo" Sajenti Minja akajibu,



    "ameondoka na yule dada ambaye anakujaga hapa, yule mwenye nywele ndefu" Muhudumu aliongea na kufanya Sajenti Minja aelewe huyo dada ni Sarah,



    "wameondoka muda gani?" Sajenti Minja aliuliza,



    "mapema sana, saa kumi na mbili asubuhi" Muhudumu alijibu,



    "sawa basi, ngoja nikuachie namba yangu, wakirudi utanipigia" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa simu yake mfukoni,



    "wakirudi? Yaani wameondoka moja kwa moja na funguo wamerudisha, na deni lote amelipia yule dada" Muhudumu alijibu na kumfanya Sajenti Minja ashtuke,



    "sawa" Sajenti Minja aliongea na kutoka zake nje huku akiwaza ni wapi Sarah alipoelekea na Dokta Pendo?



    Sajenti Minja aliingia ndani ya gari yake na kuondoka huku akiwa hajui ni wapi ataanzia kumtafuta Sarah.



    *******************



    Mtaa mmoja wa uswahilini sana, anaonekana Harry nyakati za usiku akiwa amevaa suti yake nyeupe, haikuwa safi kama anavyokuwa kila siku, suti ilikuwa chafu sana, tokea siku ya tukio la familia yake kuuawa, Harry hakuwahi kubadili nguo.



    Harry hakuwa na viatu, mguu mmoja ulikuwa na soksi moja nyeusi na mguu wa pili haukuwa na kitu, ulikuwa peku.



    Harry alitembea mwendo wake wa haraka haraka huku akiongea na kucheka peke yake, hakuwa na akili timilifu, akili zake ziliyumba kutokana na familia yake kuteketea yote kwa wakati mmoja.



    Safari ya Harry iliishia chini ya daraja ambalo chini yake hakukuwa na maji mengi yakipita, ila kulikuwa na uchafu kiasi, Harry alivyofika alivuta mabox kadhaa aliyokuwa ameyachomeka ukutani na kuyatandika chini, kisha akalalia huku akiongea peke yake.



    Wakati akiwa amelala hapo, alihisi mtu akimgusa mgongoni,



    "leo sijalala upande wako, usinisumbue" Harry aliongea kwa ukali kisha akacheka, ila bado alihisi mtu akimgusa tu, Harry akageuka kwa hasira na sura yake ikakutana na Sarah,



    "mwisho umekuwa hivi, elimu yako imeishia hapo" Sarah aliongea kwa sauti ndogo huku akimtazama Harry. Harry akanyanyuka na kukaa,



    "Sarah umekuja, umekuja kuniua?" Harry aliuliza na kisha akacheka kwa sauti kubwa,



    "ukitaka kufa utakufa, hukumbuki ahadi niliyokuambia hawali, kuwa sitokuua mpaka utakapotaka?" Sarah aliuliza na kutabasamu,



    "utanichoma moto?" Harry aliuliza huku akicheka,



    "hapana, moto utachomwa akhera" Sarah aliongea na kutabasamu,



    "nani alikuonesha nilipo? Je familia yangu imezikwa vizuri kwa heshima?" Harry aliuliza huku machozi yakimtoka,



    "hakuna aliyenionesha ulipo, kuhusu familia yako ni kwamba wamezikwa, wamezikwa vizuri tu, ni vizuri ukienda kuyaona makaburi yao" Sarah aliongea kwa huruma baada ya kuona machozi ya Harry,



    "Sarah, Taita amenigeuka, amemtuma Trigger auwe familia yangu, na vin nae ameshiriki" Harry aliongea kwa uchungu,



    "malipo ya kazi uliyomfanyia ni hayo" Sarah alijibu,



    "je unahitaji nikusaidie kwenye kesi yako?" Harry aliuliza,



    "bado nahitaji msaada wako" Sarah aliongea,



    "hakuna mahakama itayokubali kusikiliza ushahidi wa kichaa, mimi ni kichaa Sarah, najijua" Harry aliongea na kufuta machozi,



    "wewe malaya upo huku, ni vizuri nimewakuta wote" ilikuwa sauti ya Vin, alitokea ghafla na kumuelekezea Sarah bastola, Harry akaangusha kicheko,



    "muue, muue tu" Harry aliongea huku akicheka na Sarah nae hakuwa na la kufanya,



    "usaliti umekufanya umekuwa kichaa" Vin aliongea kwa hasira huku akimtazama Harry,



    "kichaa ni nani kati yangu na yako?" Harry aliuliza huku akicheka,



    "mpumbavu wewe, unajiona mzima?" Vin alimuuliza Harry huku bastola yake ikiwa bado amemuelekezea Sarah,



    "Sarah muangilie huyu, msamehe kwa kuwa hana akili timamu" Harry aliongea huku akimtazama Sarah,



    "wewe bwabwaja hapo ukimaliza nikufumue ubongo wewe pamoja na huyu malaya" Vin aliongea kwa dharau huku akitabasamu,



    "Dada yako unamuita malaya? Ndio maana nakuita kichaa" Harry aliongea na kucheka na kumfanya Vin ashangae,



    "Seba mimi ni dada yako, ukweli anajua huyu na Taita" Sarah aliongea kwa upole huku akimuangalia Vin,



    "Dada yangu kwa maana ya mtoto wa shangazi yangu, Baba alishaniambia ukweli, ila undugu haupo tena kwa kuwa umemuua mama yangu" Vin aliongea kwa hasira,



    "majinuni wewe, bila mimi hata wewe ungekufa, mimi ndiye niliyetoa wazo la wewe kuondolewa kwenye moto, vinginevyo wewe, mama yako na baba yako wote mngekuwa marehemu" Harry aliongea na kucheka kwa nguvu,



    "una maana gani?" Vin aliuliza,



    "Baba yako na mama yako wameshakufa, Taita ndiye aliyewaua kwa moto na kisha akakulea wewe kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kuzaa" Harry alijibu na kumfanya Sarah machozi yamtoke baada ya kauli ya Harry na kuamini sasa kuwa Sebastian mdogo wake ndiyo huyo Vin,



    "mnanichezea akili nyinyi wajinga" Vin aliongea kwa hasira,



    "wewe ni mdogo wangu, na kukuhakikishia tu kwa kutokukuua siku ile nyumbani kwa Harry, na pia kingine ni kwamba una baka mgongoni, baka la moto, nilikuunguza na uji wakati tukiwa watoto" Sarah aliongea na kumfanya Vin ashtuke, ni kweli ana baka mgongoni, hakuna mtu aliyewahi kuliona hilo baka, uwa analificha sana kwa maana mwanajeshi wa marekani hutakiwi kuwa na kovu lolote mwilini, kwa hiyo hujitahidi sana kulificha kovu lake.



    "Taita ni mbwa tu, anakutumia na mwisho wa siku atakuua kama alivyokutuma uniue" Harry aliongea huku akicheka,



    "kama huamini twende tukapime DNA, wewe ni msomi najua unajua DNA haiongopi" Sarah aliongea huku akimuangalia Vin aliyekuwa bado ameshika bastola,



    "hapana, msiniletee maigizo" Vin aliongea huku akili yake na maneno yake vikianza kupingana.



    Sarah akachomoa bomba la sindano kutoka kwenye mfuko wa nguo yake, kisha akajichoma kwenye mshipa mkubwa wa mkononi na kuvuta damu, baada ya hapo akachomoa bomba la sindano na kulifunga kwa juu, kisha akamtupia Vin,



    "utachunguza kwa muda wako" Sarah aliongea na kisha akageuka kwa lengo la kuondoka,



    "ukipiga hatua nakuua" Vin alimtahadharisha Sarah,



    "mjinga kweli, muue tu, muue dada yako ili Taita awe shujaa na wewe uwe umemalizia kizazi chako kwa upumbavu wako" Harry aliongea huku akimtazama Vin,



    "kama uliweza kuua watu wanne wa familia moja, sitoshangaa ukiniua mimi mtu mmoja" Sarah aliongea na kuanza kuondoka taratibu bila kujali bastola aliyoelekezewa na Vin,



    "Sarah, nadhani nimekusaidia kwa mara ya kwanza leo, nimeongea ukweli mbele ya mdogo wako, sijasema ukweli ili unisamehe, nimeongea ukweli kwa kuwa sitaki huyu Vin afuate njia niliyopita mimi kwa Taita. Vin kama umeua familia yangu ni sawa, umeniua mimi pia, nimekusamehe kwa kuwa umelipa kisasi cha mimi kushiriki mauaji ya wazazi wako wewe na Sarah" Harry aliongea huku machozi yakimtoka, ila hakuacha kucheka.



    "usiongee upuuzi wa kunivuruga akili, nitakuua wewe" Vin aliongea kwa hasira huku akimgeuzia bastola Harry,



    "siogopi kufa, sioni sababu ya kuishi sasa, maisha yangu yameshaisha, natamani sana kufa, sihitaji kuishi tena. Bora nife nikaiombe radhi familia yangu kwa maana wamekufa kwa upumbavu wangu" Harry aliongea kwa uchungu, hakuwa akicheka tena alikuwa akilia,



    "kwa hiyo unataka kufa?" Vin aliuliza huku huruma ikianza kumuingia,



    "Niue kama unaweza, sihitaji kuishi" Harry alijibu huku akilia, ila bila mtu yoyote kutegemea, Sarah kwa kasi ya ajabu alitoa bastola yake na kumfyatulia Harry risasi mbili za kichwa, Harry akafa pale pale, na huo ndio ukawa mwisho wake.



    Vin akapigwa na butwaa huku akiwa haelewi ni kwanini Sarah amefanya vile.



    Sarah akageuka na kuanza kuondoka taratibu huku Vin akiwa anamuangalia na bastola yake ikiwa mkononi.........









    Sarah aliendelea kutembea mwendo wa wastani mpaka akapotea machoni kwa Vin.



    Baada ya dakika mbili za Sarah kupotea, Trigger alitokea na kumkuta Vin akiwa ameganda na bastola yake ikiwa mkononi, na pembeni yake alikuwepo Harry akiwa amekufa,



    "umemaliza kazi tayari" Trigger aliongea huku akiumulika mwili wa Harry,



    "Alafu alishaanza kuwa teja, huoni bomba la sindano hilo" Trigger aliendelea kuongea baada ya kuona bomba la sindano ambalo Sarah alitumia kujitoa damu. Muda wote ambao Trigger alikuwa akiongea Vin alikuwa kimya tu.



    "huyu Harry ambaye alikuwa hapendi hata harufu ya sigara leo hii anajidunga Unga?" Trigger aliongea huku akinyanyua mguu wake kwa minajili ya kutaka kukanyaga lile bomba la sindano, ila kabla mguu wake haujafikia lile bomba, Vin alimsukuma Trigger na kumfanya apepesuke huku akirudi nyuma,



    "hilo bomba amelileta Sarah, lina damu yake" Vin aliongea huku akiinama kuliokota lile bomba la sindano,



    "ina maana Sarah alikuwepo hapa?" Trigger aliuliza kwa mshangao,



    "na yeye ndiye aliyemuua Harry" Vin alijibu,



    "sasa hiyo damu ya nini?" Trigger aliuliza,



    "Sarah anadai yeye ni ndugu yangu, ameniachia hiyo damu ili nikaipime nihakikishe kuwa yeye ni dada yangu" Vin aliongea na kumfanya Trigger apate wasiwasi,



    "usimsikilize, anakuchezea tu akili" Trigger aliongea kwa kujiamini,



    "inawezekana, ebu tuondoke eneo hili" Vin aliongea huku akianza kupiga hatua,



    "Mkuu si ulitupe tu hilo bomba la sindano, sasa unaenda nalo wapi?" Trigger alimwambia Vin,



    "hakuna sababu ya kulitupa, ni muhimu pia kusikiliza malalamiko ya adui yako, unaweza kuyatumia kumuangamiza" Vin alijibu huku akiliweka lile bomba la sindano kwenye mfuko wa koti lake la suti,



    "huyu Sarah anataka kuleta vita nyingine hapa" Trigger aliongea kwa sauti ndogo ambayo haikumfikia Vin,



    "Sasa Vin akijua Sarah ni ndugu yake, wabaya si tutakuwa mimi na Taita?" Trigger alijiuliza huku nae akipiga hatua kuelekea upande alipoelekea Vin.



    ***************



    Tukio la kufa kwa Harry wakati linatokea Aisha alikuwa jirani kabisa, alikuwa umbali wa mita mia mbili huku heaefone zikiwa masikioni mwake, alikuwa anasikia kila kitu kilichokuwa kinaongelewa kati ya Vin, Sarah na Harry.



    Aisha kutokana na kumfuatilia Harry kwa muda kidogo ndio akafanikiwa kujua eneo analolala Harry na akatega vinasa sauti hivyo ili ajue Harry anakaa na nani?



    Na siku hiyo Aisha ndio alipanga siku ya kwenda kummaliza Harry, ila wakati amefika na kutazama mazingira ndipo alipomuona Sarah akielekea eneo hilo, ikambidi asubiri aone Sarah anakwenda kwa lengo gani, ndipo pia baadae akamuona Vin pia akielekea usawa huo, hapo ndipo alipoamua atulie na kusikiliza ni kipi kitafuata.



    Alisikia yote mpaka tukio la Harry kupigwa risasi na Sarah. Na mwisho akamuona Sarah akitoka na kuelekea kwenye gari yake, Aisha akatoka mafichoni na kwenda kwenye kugonga kwenye kioo cha gari ya Sarah, Sarah akashtuka na kushusha kioo,



    "fungua mlango bibie, acha uoga" Aisha aliongea huku akitabasamu,



    "kwanini nikuogope?" Sarah aliuliza huku akimfungulia mlango wa gari Aisha, Aisha akaingia na kukaa,



    "ondoa gari" Aisha aliongea,



    "unaelekea wapi?" Sarah aliuliza huku akiwa bado hajaondoa gari,



    "twende popote tu, utaniacha mbele hapo" Aisha aliongea na kisha Sarah akawasha gari na kuliondoa,



    "ulikuwa unanifuatilia?" Sarah aliuliza,



    "hapana, nilikuwa namfuatilia Harry, ila nashukuru kwa kazi uliyoifanya to kumuua" Aisha aliongea na kutabasamu,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "kwanini ushukuru?" Sarah aliuliza,



    "kwa maana hata mimi nilikuwa na mipango huo wa kumuua leo, ila wewe umeifanya hiyo kazi" Aisha aliongea,



    "sawa, si unaweza kushukia hapa, maana ninapoenda sitopenda upajue" Sarah aliongea huku akiwa anaegesha gari ili Aisha ashuke,



    "nina ombi moja" Aisha aliongea,



    "sema" Sarah aliongea,



    "nilikuwa nasikiliza maongezi yenu kupitia vinasa sauti, nimegundua kuwa ulifanyiwa unyama mkubwa sana na Taita, pia nikafikiria kuwa kwa namna moja au nyingine wewe peke yako huwezi kupambana na huyo Taita" Aisha aliongea na kumeza mate,



    "kwa hiyo wamekutuma kunitisha?" Sarah aliuliza kwa jeuri,



    "hapana, ninachotaka ni kukusaidia kumaliza machungu yako" Aisha aliongea,



    "sihitaji msaada, nilianza mwenyewe na nitamaliza mwenyewe" Sarah alijibu,



    "kumaliza huwezi, kwenye utata ni kwa huyo mdogo wako aitwae Vin, yule ameshamezeshwa chuki dhidi yako na Taita anajua kabisa huwezi kumuua Vin, ila Vin ndiye atakayekuua wewe" Aisha aliongea na kufanya Sarah amtazame,



    "siwezi kumuua eee? Sawa ngoja muone, nimemuacha mara mbili, kama wamekutuma waambie waendelee kuhesabu" Sarah aliongea na kutabasamu,



    "hawajanituma na wala sina uhusiano nao, ni ubinadamu tu ndio umenisukuma kukusaidia" Aisha aliongea,



    "ubinadamu? Kwa hiyo ubinadamu unafanya unisaidie kuua binadamu wenzako?" Sarah aliuliza,



    "kwani wewe unaeua sio binadamu?" Aisha aliuliza,



    "Sarah sio mtu, Sarah ni mnyama au malaika, sihishi kwa malengo, naishi kwa maarifa ya kulipa kisasi, nikishaimaliza kulipa kisasi, naweza kufa kwa amani kwa maana sitokuwa na deni" Sarah alijibu,



    "sawa, endelea na mambo yako" Aisha aliongea na kufungua mlango,



    "sawa, na wewe endelea na ya kwako" Sarah alijibu na wakati huo Aisha alikuwa anatelemka kwenye gari, kisha akafunga mlango na Sarah akaiondoa gari yake.



    "watu wengine wendawazimu kweli, baada ya kugeukana ndio aje kutaka kunisaidia?" Sarah aliongea huku akikanyaga mafuta ya gari na kufanya gari iongeze mwendo.



    ***************



    Vin na Trigger walipotoka eneo ambalo alifia Harry, wakaelekea moja kwa moja kwenye gari, Trigger ndio alikuwa dereva, akawasha gari na kuiondoa. Kipindi chote hicho Vin alikuwa na mawazo,



    "nikurudushe hotelini au unaenda hospitali kumuona mzee?" Trigger aliuliza,



    "nipeleke hospitali" Vin aliongea,



    "vipi, unaumwa?" Trigger aliuliza,



    "fanya kama nilivyokuagiza" Vin aliongea na kumfanya Trigger akae kimya.



    Trigger aliendesha gari mpaka nje ya hospitali moja ya kisasa, kisha akasimamisha gari na vin akashuka, Trigger nae akaamua ashuke.



    Vin alielekea moja kwa moja mpaka eneo la mapokezi na akaomba aonane na Daktari, akaelekezwa mahala ofisi ya daktari ilipo, akaingia na kumuacha Trigger eneo la mapokezi akimsubiri.



    Harry akaingia katika chumba cha Dokta na kumkuta mwanaume wa makamo akiwa amevaa koti jeupe na mbele yake kulikuwa na kibao kilichomtambulisha kama daktari.



    Vin akakaa kwenye kiti na kumsalimia Dokta.



    "nahitaji kupima DNA" Vin aliongea,



    "kwa ajili ya kutaka kujua nini?" Dokta aliuliza kwa utulivu,



    "kuna mtu anadai mimi ni ndugu yake, kwa hiyo nataka kuthibitisha Kama ni kweli" Vin aliongea,



    "hapo itabidi tuwapime damu, huyo mtu yupo wapi?" Dokta aliuliza,



    "sijaja naye" Vin alijibu,



    "basi itakubidi kesho uje naye ili tuwatoe damu kwa pamoja" Dokta aliongea,



    "ila damu yake ninayo hapa, aliitoa mbele ya macho yangu" Vin aliongea huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake la suti na kutoa bomba la sindano lenye damu ya Sarah na kumpa daktari,



    "kama hivyo ni sawa, je wewe upo tayari kutolewa damu yako muda huu?" Daktari aliuliza,



    "Mimi nipo tayari" Vin alijibu, kisha daktari akavuta karatasi iliyokuwepo juu ya meza na kuandika maelezo kadhaa likiwemo jina la Vin.



    "chukua hii karatasi uende maabara" Daktari aliongea huku akimpa Vin karatasi,



    "maabara ipo kwa wapi?" Vin aliuliza,



    "ukifika mapokezi utauliza" Daktari aliongea na kisha Vin akachukua bomba la sindano lenye damu ya Sarah na kutoka nalo mpaka eneo la mapokezi,



    "maabara ipo upande upi?" Vin alimuuliza dada aliyekuwepo hapo,



    "nyoosha na hii korido mpaka mwisho mlango wa kushoto" Dada wa mapokezi alijibu na kisha Vin akaelekea maabara, alipofika uko aliwapa ile karatasi aliyopewa na Daktari na kisha wakamtoa damu.



    "urudi kesho saa kumi jioni" mtu wa maabara alimwambia Vin,



    "nikija nije huku moja kwa moja?" Vin aliuliza,



    "hapana, utaenda kwa daktari uliyempa maelezo" Mtu wa maabara aliongea na kisha Vin akatoka zake mpaka eneo la maabara na kumtaka Trigger waondoke.



    Wakatoka mpaka nje na kuingia kwenye gari,



    "nipeleke hotelini" Vin aliongea,



    "ila mzee anaweza kuruhusiwa leo, kwa nini tusiende wote hospitali?" Trigger aliuliza,



    "nipeleke hotelini" Vin aliongea kwa msisitizo na Trigger hakutaka kuongea tena, aliamua kufuata maelezo ya Vin.



    Njia nzima ukimya ulitawala, hakuna aliyemuongelesha mwenzake, wakati Vin aliwaza utata wa undugu baina yake na Sarah, na kipindi hicho hicho Trigger alihisi Vin ameanza kugundua kitu kuhusu undugu Sarah.



    Trigger alifika Vin hotel na kuegesha gari kwa nje na kisha Vin akafungua mlango na kutelemka,



    "mzee akikuulizia nimwambiaje?" Trigger alimuuliza Vin,



    "mwambie sijisikii vizuri, nimepumzika" Vin alijibu,



    "sawa" Trigger alijibu huku akijiandaa kuondoa gari, Vin akageuka haraka,



    "usimwambie kama tumekutana na Sarah" Vin akamwambia Trigger,



    "kwanini?" Trigger akauliza,



    "nitamwambia mwenyewe kesho" Vin alijibu,



    "na kuhusu kifo cha Harry?" Trigger aliuliza,



    "unaweza kumwambia, ila epuka kumtaja Sarah" Vin aliongea na kuondoka zake.



    ****************



    Sarah alivyomshusha Aisha aliendelea kuendesha gari lake kwa mwendo wa kasi, alikuwa akielekea kwenye makazi yake mapya ambayo hayakuwa mbali sana na mjini, aliamua kununua nyumba nyingine na kuhamia uko kwa ajili ya kuwakwepa watu wanaopafahamu kwake hasa polisi. Alikuwa hataki usumbufu wa aina yoyote. Na uko kwenye makazi mapya alikuwa akihishi na dokta Pendo na babu yake.



    Sarah alifika mpaka kwenye hiyo nyumba yake mpya na kufungua geti, akaingiza gari, kisha akashuka na kwenda kufunga geti.



    Akazunguka nyumba yake kwa lengo la kukagua, hakuona kitu chochote cha hatari, alipomaliza kukagua akaamua aingie ndani, akafungua mlango wa sebuleni na kuingia ndani, alipotupa macho kwenye makochi akashuhudia Dokta Pendo na babu yake wakiwa wamefungwa kamba mikononi na miguuni na mdomoni waliwekwa plasta ya kuzuia kupiga kelele. Sarah akiwa akajiuliza ni nani aliyefanya hivyo, akahisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake, kwa kuwa ni mtaalam akagundua hiyo ni bastola na pia akajiuliza huyo mtu ni nani?



    "hutakiwi kugeuka nyuma" Sauti nzito ya kiume iliongea na kufanya Sarah kutoitambua sauti hiyo, kwa maana hakuwahi kuisikia hata mara moja,



    "wewe nani?" Sarah aliuliza kwa ujeuri ili kumuadaa na ikiwezekana amuotee kwa pigo, ila mtu badala ya kujibu, alimpiga Sarah kofi zito la shingoni,



    "na ukiendelea kuuliza bila ruhusa, utaumia zaidi" Mtu yule aliongea na kumfanya Sarah agundue huyo mtu hakuwa akifanya utani..........







    "kakae pale kwenye kochi uungane na wenzako" Sauti ile iliongea kwa mamlaka na kumfanya Sarah akakae na hapo akaweza kuiona vizuri sura ya yule mtu aliyemteka, alikuwa ni Strategic,



    "kumbe Sarah mwenyewe ndio wewe, mbona hufanani na unyama unaoufanya?" Strategic aliuliza lakini Sarah hakujibu, strategic akatoa simu na kubonyeza namba anayoijua yeye, kisha akaiweka simu sikioni na kuisikiliza wakati ikiita,



    "hoya Vin, nimefanikiwa kumteka Sarah, vipi nimmalize?" Strategic aliuliza,



    "ooh, hapana, muache" Vin alitoa kauli iliyomshangaza Strategic,



    "kwanini nimuache mkuu?" Strategic aliuliza kwa mshangao?



    "nitakuja kukueleza, wewe muache tu, na usimdhuru" Vin aliongea,



    "sawa mkuu" Strategic alijibu na kukata simu, kisha akamtupia jicho Sarah na kumuangalia kwa dakika kadhaa,



    "bahati yako, tutakutana siku nyingine" Strategic aliongea na kisha akaelekea kwenye mlango na kuufungua kisha akaondoka.



    Baada ya Strategic kuondoka, Sarah alivuta bastola yake na kutoka mbio mpaka nje, hakukuta mtu,



    "mpuuzi huyu" Sarah aliongea kwa hasira huku akirudi ndani. Alipofika ndani aliwafungua kamba Dokta Pendo na babu yake,



    "muda gani aliingia hapa?" Sarah aliuliza wakati akimaliza kumfungua kamba Dokta Pendo,



    "kama nusu saa hivi iliyopita" Babu yake alijibu,



    "amepajuaje hapa?" Sarah aliuliza lakini hakuna aliyejibu kwa maana hakuna aliyejua.



    "hii ni hatari Sarah, yaani wamepajua mpaka hapa?" Babu yake Sarah aliuliza huku akisikitika,



    "itabidi tuhame na hapa, tuhamie hotelini sasa" Sarah aliongea huku akikaa kwenye kochi,



    "hakuna sababu ya kuhama, sasa tutahama hama mpaka lini?" Dokta Pendo aliuliza,



    "tunahitaji kuwa sehemu salama, kwa kuwa hawa manyang'au wameshajua tunapoishi, wanaweza kuja kutushambulia" Sarah aliongea,



    "kama angekua na lengo la kutuua angetumaliza mapema tu, ila mbona amekuachia?" Dokta Pendo aliuliza,



    "Vin itakuwa ameanza kuelewa kitu kati yangu na yeye, ila isiwe sababu ya kujiamini kiasi cha kuwa huru muda wote, itabidi tukiwa ndani mlango yote ya geti ifungwe" Sarah aliongea kwa utulivu,



    "mama nadhani ungeachana nao tu, watakumaliza hawa" Babu yake Sarah aliongea,



    "hilo haliwezekani, hata nikiachana nao bado wao hawatoachana na mimi, watataka tu kuniua au kuwaua watu wote mlio upande wangu" Sarah alijibu,



    "shoga pambana, maji umeshayavulia nguo" Dokta Pendo aliongea kwa ya upole,



    "usimshauri mwenzako ujinga, je akifa utajisikiaje?" Babu yake Sarah aliuliza kwa ukali,



    "je wakati wewe unamchongea kwa polisi ulikuwa unajisikiaje?" Dokta Pendo aliuliza huku akinyanyuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea chumbani na kumuacha Sarah akitabasamu,



    "usimsikilize maneno yake huyo mwenzako, hana nia nzuri na wewe" Babu yake Sarah alimwambia Sarah,



    "Mimi namsikiliza shoga yangu, nampenda kwa maana amenisaidia mambo mengi" Sarah aliongea kwa utani huku akielekea chumbani akicheka,



    "mabaradhuli nyie, ukifa shauri yako" Babu aliongea kwa hasira huku akimtazama Sarah anavyoondoka.



    **********************



    Sajenti Minja alihisi kuchanganyikiwa, na kilichomchanganya Sajenti Minja ni kupotea kwa ghafla kwa Sarah huku akiwa na Dokta Pendo. Sajenti Minja akili yake ikamtuma aende uwanja wa ndege kwenda kukagua watu waliokwenda nje ya nchi ndani ya wiki hii, aliamini huenda Sarah ametoroka nchini baada ya kufanya mauaji ya familia ya Harry.



    Sajenti Minja alichukua gari na kwenda moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege, alipofika haikuwa rahisi kukubaliwa kufanya kazi yake, ilimbidi ampigie simu waziri wa wizara husika na kumueleza lengo lake, kisha waziri akapiga simu uwanja wa ndege na kuwaamuru wamuache Sajenti Minja afanye kazi yake.



    "nenda kwenye chumba namba saba, uko ndipo kuna orodha yote" Mfanyakazi Mmoja alimuelekeza Sajenti Minja huku akimpatia kibali ambacho kilimtambulisha Sajenti Minja kama mtu maalum na aachwe afanye kazi yake.



    Sajenti Minja alielekea moja kwa moja mpaka chumba kilichokuwa na mlango uliochorwa namba saba na kisha akabonyeza kengele iliyokuwepo hapo mlangoni, na mlango ukafunguliwa na msichana, Sajenti Minja akamsalimu na kisha akamuonesha kile kibali, akaruhusiwa kuingia ndani na kukuta watu kama watano wakiwa bize na computer, kila mtu alikuwa na computer yake.



    Sajenti Minja akawasalimia, kuna waliotikia na wengine walikuwa bize kubonyeza computer zao.



    "samahani jamani, mimi ni askari, nimekuja kuangalia orodha ya watu waliotoka nje ya nchi ndani ya wiki hii" Sajenti Minja aliongea kwa sauti tulivu na kufanya watu wote wamuangalie,



    "ni wengi sana bro, au labda ueleze shida yako ni ipi hasa?" Kijana mmoja mtanashati alimuuliza Sajenti Minja,



    "kuna mtu anatafutwa na serikali, sasa nataka kujua kama yupo ndani ya nchi au ametoroka?" Sajenti Minja aliuliza,



    "una kibali cha kuruhusiwa kufanya ukaguzi ndani ya ofisi hii?" Yule kijana akamtupia swali jingine Sajenti Minja,



    "anacho, waoneshe" Dada aliyemfungulia mlango Sajenti Minja alijibu huku akimtazama Sajenti Minja na kufanya Sajenti Minja awaoneshe kile kibali alichopewa,



    "tupe jina lake tafadhali" Yule kijana aliongea,



    "Sarah Isack" Sajenti Minja aliongea huku akiandika jina la Sarah kwenye karatasi na kisha yule kijana akaliingiza lile jina kwenye computer yake na kubonyeza sehemu iliyoandikwa "search", baada ya muda jina la Sarah likatokea kwenye computer ya yule kijana,



    "bro, huyo mtu jina lake limeaonekana kwa mara ya mwisho mwaka mmoja uliopita, tena imeonesha alikuwa akiingia kama mtalii kutoka nchini uingereza" Yule kijana alimpa maelezo Sajenti Minja,



    "hakuna sehemu iliyoonesha akitoka?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ipo, ila imeonesha alitokaga miaka ishirini iliyopita na amerudi mwaka uliopita" Kijana alijibu,



    "na sehemu ya kutoka imeonesha ametoka kwenda wapi, na ametoka kwenda wapi na kufanya nini?" Sajenti Minja aliuliza,



    "imeonesha alitoka kwenda uingereza, na alienda kwa ajili ya masomo" Kijana alijibu,



    "dah, hii report yenu hapa ni ya abiria wa uwanja huu tu au ni report ya viwanja vyote?" Sajenti Minja aliuliza,



    .



    .

    "ni ya viwanja vyote vya Tanzania" Yule kijana alijibu,



    "sawa, asante kwa ushirikiano wako" Sajenti Minja aliongea huku akianza kuondoka,



    "au bro kwa kukushauri, ni bora ukaangalie na vituo vya mabasi, huenda ametumia njia ya mabasi kusafiri mpaka Kenya, alafu akifika Kenya ndio achukue ndege" Kijana aliongea huku akimtazama Sajenti Minja,



    "nashukuru, ngoja nikafanye hivyo" Sajenti Minja alijibu, ila kiukweli aliona hiyo njia ni ngumu sana kuitumia kwa kuwa stand ya mabasi haina utaratibu maalum wa kukata tickets na kuifadhi kumbukumbu.



    Sajenti Minja alirudi mpaka sehemu alipochukulia kibali, akakirudisha na kisha akashukuru. Akatoka zake mpaka nje ya eneo la uwanja wa ndege na kisha akaingia kwenye gari lake.



    Wakati akiwa anajiandaa kuwasha gari yake, simu yake iliita na kupokea,



    "Minja anaongea" Sajenti Minja aliongea,



    "tumeokota mwili ukiwa na majeraha ya risasi" Mtu wa upande wa pili aliongea,



    "mmemtambua?" Sajenti Minja aliuliza,



    "tumemtambua kupitia kitambulisho chake" Mtu wa upande wa pili alijibu,



    "sawa, mpelekeni hospitali na mruhusu uchunguzi ufanyike, mimi nakuja" Sajenti Minja aliongea na kukata simu, kisha akaondoa gari.



    ***************



    Trigger alifika hospitali na kumkuta Taita akiwa amekaa kitandani,



    "Vin yupo wapi?" Taita aliuliza,



    "anadai hajisikii vizuri, amerudi hotelini kupumzika" Trigger alijibu,



    "na mmefanikisha kumuona Harry?" Taita aliuliza,



    "tutaongea baadae, je kuna habari mpya?" Trigger aliuliza,



    "mpya sina, ila cha muhimu ni kwamba nimeruhusiwa" Taita aliongea,



    "kwa hiyo tunaondoka?" Trigger aliuliza,



    "ndio, ebu nisaidie kusimama" Taita aliongea huku akisimama na Trigger aksmsaidia kwa kumshika mkono na kisha wakaelekea mpaka nje, wakaingia kwenye gari na kisha Trigger akawasha gari na kuondoka.



    Walifika nyumbani kwa Taita na kisha Taita akafikia kukaa kwenye kochi,



    "mzee, Harry ameuawa" Trigger aliongea baada ya Taita kukaa,



    "ameuawa au mmemuua?" Taita aliuliza,



    "Sarah ndio amemuua" Trigger alijibu,



    "umejuaje kama Sarah amemuua?" Taita aliuliza,



    "wakati Sarah akimuua Harry, Vin alikuwepo na yeye ndiye aliyemuona" Trigger alijibu,



    "sasa kwanini Vin hakumuua Sarah?" Taita aliuliza,



    "kuna kitu cha ajabu sana kimetokea, Sarah anamuaminisha Vin kuwa yeye ni dada yake, na leo ametoa damu na kumpa Vin akaipime ili ahakikisha" Trigger aliongea na kumfanya Taita ashtuke,



    "na vin ameamini?" Taita aliuliza,



    "itakuwa, maana alipitia hospitali na kwenda kuacha damu ya Sarah" Trigger aliongea,



    "hii hatari, itabidi uende hiyo hospitali ukasimamishe huo mpango" Taita aliongea,



    "kwa njia gani?" Trigger aliuliza,



    "kaongee na Dokta akupe hayo majibu" Taita aliongea,



    "na akikataa?" Trigger aliuliza,



    "ua" Taita alijibu,



    "sawa mkuu, hiyo kazi itafanyika kesho" Trigger alijibu.



    ***************



    Siku iliyofuata Vin alipata wazo jipya, aliona ni bora amtume Strategic aende maeneo ya hospitali kuimalisha ulinzi mpaka mida ya saa kumi ambao ni muda Vin alitakiwa kufika kuchukua majibu.



    Vin alifanya hivyo kwa maana alihisi huenda Sarah anaweza kufika eneo la hospital na kumteka Dokta na kumshurutisha aandike majibu ya uongo ya DNA, bado Vin hakuwa na imani na Sarah.



    Strategic alifika eneo la hospital kuimarisha ulinzi, hakuwa akimjua Dokta muhusika, ila alichoenda kufanya ni kumuwinda Sarah endapo atakuja eneo hilo.



    Muda ulizidi kwenda tu, ilipofika saa kumi, strategic alimshuhudia Trigger akifika eneo lile, strategic akataka kushuka ila akaamua auchune tu ndani ya gari, akatoa simu na kumpigia Vin,



    "nimemuona Trigger eneo hili" Strategic aliongea,



    "amekuja kufanya nini?" Vin aliuliza,



    "sijui kwa kweli" Strategic alijibu,



    "amekuona?" Vin aliuliza,



    "hapana" Strategic alijibu,



    "endelea kukaa hapo na ufuatilie amefuata nini?" Vin aliongea baada ya kuhisi huenda Trigger ameenda kwa ajili ya kuchunguza ni kipi Vin alikifuata siku iliyopita,



    "sawa mkuu" Strategic alijibu.



    Huko ndani Trigger alipitiliza mpaka ndani kwa Dokta na kumkuta akiwa anajiandaa kuondoka, akamsalimu,



    "Dokta nimetumwa nifuate majibu ya damu" Trigger aliongea,



    "na nani?" Dokta aliuliza,



    "mdogo wangu alikuja jana hapa na bomba la sindano lililokuwa na damu" Trigger aliongea na kumfanya Dokta amkumbuke Vin,



    "sasa kijana, hapa haturuhusiwi kumpa mtu majibu ya mwingine, ni vyema angekuja mwenyewe" Dokta aliongea huku akipekua pekua karatasi juu ya meza yake,



    "kwa hiyo haiwezekani?" Trigger aliuliza,



    "hiyo haiwezekani" Dokta alijibu na kisha Trigger akaondoka kwa hasira.



    Baada ya Trigger kuondoka, Dokta alipekua zile karatasi mezani na kuchukua karatasi moja ambayo ilikuwa na majibu ya DNA ya Vin, akaitia kwenye bahasha ya njano.



    Trigger alitoka na kusimama mlangoni, akili yake ikamtuma arudi ndani ya ofisi ya daktari. Trigger akageuka na kusukuma mlango, akaingia,



    "nipe majibu niliyotumwa, vinginevyo amani itapotea" Trigger aliongea huku akiichomoa bastola yake na kumuelekezea Dokta, Dokta akapata mshtuko na kujikuta akiichomoa bahasha moja ya njano na kumpatia Trigger, Trigger akafungua na kusoma maelezo ya juu katika karatasi, alikuta kumeandikwa " DNA TEST" na chini ya hayo maneno kulikuwa na jina la Vin na Sarah.



    Trigger akaitudishia ile karatasi ndani ya bahasha na kisha akamtupia jicho Dokta,



    "Trigger akikuoneshea bastola uwa haishushi chini mpaka itoe risasi" Trigger aliongea huku akitabasamu na kumfanya Dokta macho yamtoke,



    "unamaanisha nini?" Dokta aliuliza kwa hofu, ila Trigger hakujibu, badala yake alimfyatulia Dokta risasi mbili na kisha Dokta akaanguka chini. Trigger akafungua mlango na kutoka zake kimya kimya na bahasha mkononi utasema hajatoka kufanya tukio la kinyama........







    Trigger alitoka mpaka nje ya hospitali na kuingia kwenye gari lake, akawasha na kuondoka.



    Strategic alikuwa akishuhudua hayo yote, akaichukua simu yake na kumpigia Vin,



    "Trigger ndio anatoka muda huu" Strategic aliongea,



    "yupo peke yake?" Vin aliuliza,



    "ndio yupo peke yake, ila mkononi ameshika bahasha" Strategic aliongea,



    "wakati akiingia ulimuona nayo hiyo bahasha?" Vin aliuliza,



    "hapana" Strategic alijibu,



    "poa, nipo njiani nakuja" Vin aliongea na kukata simu.



    Strategic akaendelea kukaa eneo lile huku akiwa makini sana kuangalia watu wanaotoka na kuingia.



    ********



    Dada wa mapokezi wa eneo la hospital ndio alikuwa mtu wa kwanza kupata mshangao kwa kuwa hakumuona Dokta akitoka wakati muda wake wa kutoka ulikuwa umefika, na kawaida ya huyu Dokta uwa hachelewi kutoka hata kwa dakika, muda ukifika uondoka hapo hapo.



    "Lydia, mbona leo Dokta amechelewa kutoka, au ana kazi?" Dada wa mapokezi alimuuliza mwenzake,



    "kumbe bado hajatoka? Ila atakuwa ameshatoka bwana, yule mzee hawezi kuwepo mpaka muda huu" Mwenzake alijibu huku akiwa hana uhakika,



    "bado bwana, si angepita kusaini hapa, mbona sioni sahihi yake? au leo amepitiwa?" Dada wa mapokezi alimbishia mwenzake huku akifungua kitabu cha maudhurio ya wafanyakazi,



    "tatizo lako Anita wewe mbishi, ngoja nikuhakikishie" Mwenzake aliongea huku akielekea kwenye mlango wa Dokta, alipofika aligonga hodi ila hakujibiwa,



    "yupo?" Dada wa mapokezi aliuliza,



    "nagonga hodi sijibiwi" Mwenzake alijibu huku akirudia tena kupiga hodi,



    "ebu sukuma mlango" Dada wa mapokezi alimshauri mwenzake ambaye nae alikubaliana na ushauri huo, akasukuma mlango na kutupa macho kwenye kiti cha Dokta ila hakumuona,



    "si nilisema? Ameondoka" Mwenzake alipaza sauti kumuelekea dada wa mapokezi,



    "basi leo kapitiwa, maana hata mlango uwa ahachagi wazi pindi akiondoka" Dada wa mapokezi aliongea, ila mwenzake hakumsikia, akili yake ilikuwa kwenye michilizi ya damu iliyokuwa ikionekana chini ya meza, akainama na kuchungulia, akauona mwili wa Dokta ukiwa umelala sakafuni na damu ikiwa imetapakaa, akapiga kelele na kumfanya mwenzake ashtuke, nae akaungana na mwenzie kwenda kushuhudia hicho kitu kilichomfanya mwenzake apige kelele, nae baada ya kuoneshwa akajikuta anapiga kelele na kufanya baadhi ya wagonjwa na wafanyakazi wa ile hospitali kujaa mlangoni ili nao waweze kuona ni kipi kimetokea kwenye chumba hicho cha Dokta.



    *****************



    Vin alifika eneo la hospital na kuegesha gari yake, kisha akatelemka na kuanza kuelekea ndani ya jengo la hospitali, alipofika usawa ilipo gari ya Strategic, Vin alimuoneshea ishara ya dole gumba na kumfanya Strategic atabasamu.



    Vin akaingia ndani ya jengo la hospitali, ila alikuta hali tofauti, alikuta yule daktari aliyemchukua vipimo siku iliyopita akiwa amewekwa kwenye kitanda cha matairi na kufunikwa shuka mwili mzima, kwa maana hiyo alikuwa amekufa. Baadhi ya watu na wafanyakazi wengine wa ile hospitali walikuwa wakilia kwa uchungu, Vin akaonekana kuchanganyikiwa kidogo, akaelekea ilipo ofisi ya mapokezi na kuwakuta wadada wawili wakiwa na macho mekundu kuashiria walikuwa wakilia muda mfupi uliopita,



    "poleni" Vin aliongea kwa upole,



    "asante" wale wadada walijibu kwa pamoja,



    "ni kitu gani kimetokea?" Vin aliuliza,



    "hakuna anayeyajua, yaani tumekuta Dokta amepigwa tu risasi" Dada wa mapokezi alijibu,



    "kwa hiyo huduma zimesitishwa?" Vin aliuliza,



    "ulikuwa na shida gani?" Dada wa mapokezi alimuuliza,



    "nimekuja kuchukua majibu yangu, nilipima jana" Vin aliongea,



    "nenda katika chumba cha Dokta uliyempa maelezo" Dada wa mapokezi aliongea,



    "chumba nadhani ndio hicho ambacho huyo Dokta aliyepata matatizo" Vin alijibu,



    "kwa hapo itabidi usubiri utaratibu mwingine, maana polisi wamezuia watu kuingia kwenye kile chumba mpaka uchunguzi ukamilike, na isitoshe kila majibu ya wagonjwa uwa ndani ya ofisi ya daktari husika" Dada wa mapokezi alijibu,



    "kwa hiyo hamjabahatika hata kumuona mtu aliyefanya tukio, hii hospitali si ina camera?" Vin aliuliza,



    "polisi ndio watafanya uchunguzi, kuna mtu wanamsubiri, ila kwa sisi tunamuhisi kijana mmoja ambaye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuingia ofisi hiyo ya Dokta" Dada wa mapokezi alijibu,



    "huyo mtu yukoje?" Vin aliuliza,



    "mweupe mrefu, ana michoro mwilini, mkononi amejichora bastola" Dada wa mapokezi aliongea, ila kwa maelezo hayo tu, Vin alimtambua mtu huyo anaezungumziwa ni Trigger,



    "atashikwa tu" Vin aliongea na kisha akawa anaelekea nje huku mawazo yakiongezeka na kujiuliza kwanini Trigger amemuua yule daktari?



    Vin alitembea mpaka kwenye gari la Strategic na kuingia,



    "mbona hatuambiani hapa hospitali kuna nini? Maana umemiagiza niangalie kama Sarah amefika, mara namuona Trigger, mara na wewe unakuja nakuona umepitiliza ndani. Au mzee mnataka aletwe hapa kwa matibabu zaidi?" Strategic aliuliza huku akitabasamu,



    "Trigger ameua muda ambao ulimuona eneo hili" Vin aliongea kwa unyonge,



    "ndio maana nimewaona polisi na baadhi ya watu wakipishana maeneo haya. Amemuua nani?" Strategic aliuliza,



    "jana kuna vipimo nilikuja kupima hapa, sasa nahisi huenda Trigger alikuja kuchukua majibu kwa nguvu, na tena Dokta aliyekufa ni yule yule niliyekuwa nae jana, na nimeshtuka sana mara baada ya kukumbuka kuwa uliniambia kuwa Trigger ametoka na bahasha ya njano, huenda ndio majibu yangu hayo" Vin aliongea kwa upole,



    "mbona sielewi, hivyo vipimo ni vya nini mpaka Trigger achukue majibu kwa kutumia bastola?" Strategic aliendelea kuhoji na kumfanya Vin akae kimya kwa muda na kujikuna kichwa,



    "jana nilivyokuagiza ukamuue Sarah, tulikutana na Sarah kabla hujakutana nae wewe, na akanitolea damu na kudai mimi ni ndugu yake, na hii ni mara ya pili. Sasa mara baada ya kunipa ile damu, nikapita hospitali nikiwa na Trigger na kuchukua vipimo vya DNA, majibu ndio nilitakiwa nifuate leo. Ndio maana nikazuia kwanza usimuue Sarah mpaka nijue ukweli, na pia nikakutuma uje umuwinde Sarah hapa kwa maana anaweza kuja na kumshurutisha Dokta aandike majibu ya uongo ili aonekane ni ndugu yangu" Vin aliongea kwa utulivu na kumfanya Strategic ashushe pumzi nzito,



    "wewe unahisi kwanini Trigger amewahi kuja kufuata majibu? Tena mpaka ametumia nguvu ya ziada?" Strategic aliuliza,



    "sasa hapo ndipo napata mashaka, huenda kuna kitu anakificha. Wewe umekaa muda mrefu na Trigger na baba yangu, na wewe peke yako ndio nimetokea kukuamini na ndio maana nakushirikisha kwenye mambo yangu. Tafadhali sana naomba uniambie ukweli wowote unaoujua kuhusu mimi, kwa maana mimi sijakulia hapa, historia inaonesha nilienda marekani tangu nikiwa mtoto" Vin aliongea,



    "dah, sijui nikuambiaje? Ila nilishawahi kuwasikia Harry na Trigger wakisema Taita sio baba yako, ni mjomba wako tu, ila hawakujua kama niliwasikia" Strategic alitoa habari nyingine mpya kwa Vin, hapo sasa kichwa cha Vin kikaparaganyika,



    "hawajasema baba yangu ni nani?" Vin aliuliza,



    "nilisikia wakisema kuwa wazazi wako walikufa kwenye tukio la nyumba kuungua na moto" Strategic aliongea na vin akakumbuka maneno ya Harry na Sarah kuhusu kifo cha wazazi wake,



    "kingine unachokijua kuhusu mimi?" Vin aliuliza,



    "hakuna zaidi mkuu" Strategic alijibu,



    "sawa, basi we nenda kaendelee na shughuli zako, nikikuhitaji nitakutafuta" Vin aliongea huku akishuka kwenye gari ya Strategic,



    "poa boss" Strategic alijibu,



    "ila ukiwa na Trigger na mzee usiwaeleze kama umeniona au umekutana na mimi siku za karibuni, hiyo ni kwa ajili ya usalama wako tu, maana Trigger akijua unanisaidia kupata ukweli wangu, anaweza kukuua" Vin alimtahadharisha Strategic,



    "sawa, haina shida" Strategic alijibu na kisha Vin akaelekea kwenye gari yake na kuondoka.



    Strategic nae akawasha gari yake na kuiondoa eneo hilo la hospitali.



    ***********************



    Sajenti Minja alipotoka uwanja wa ndege, alielekea moja kwa moja katika hospitali ambayo aliambiwa kuna mwili wa mtu ambaye ulikotwa chini ya daraja la taka umepelekea uko.



    Sajenti Minja alifika hospitali na kuwakuta baadhi ya askari wakiwepo eneo hilo, aliwasalimu,



    "uchunguzi wa mwili uliookotwa umeanza?" Sajenti Minja aliuliza,



    "bado, ila wamemaliza muda huu kumtoa risasi mbili zilikuwepo kichwani mwake" Askari alijibu,



    "zipo wapi?" Sajenti Minja aliuliza,



    "twende" Askari yule aliongea huku akiondoka na Sajenti Minja akimfuata kwa nyuma.



    Walielekea mpaka kwenye chumba kimoja kidogo na kuingia, yule askari akavaa mipira mkononi na kufungua kabati dogo ndani ya kile chumba na kutoa mfuko mdogo wa nylon, ulikuwa na risasi mbili.



    Sajenti Minja nae akavaa mipira mkononi na kuitoa risasi moja, akaitambua kwa haraka sana, ni zile risasi anazozitumiaga Sarah,



    "aliyeuawa mmemtambua?" Sajenti Minja aliuliza kwa pupa,



    "jina lipo kwenye kitambulisho chake, anaitwa Harry William, ni mfanyakazi WA TaV Company" Askari alijibu na kumfanya Sajenti Minja apate mwanga sasa, alikuwa anamjua Harry vizuri, na alikuwa akijua kuwa hiyo company aliyokuwa akifanyia kazi ni company ya Taita,



    "kwa hiyo baada ya familia yake kuuawa siku zilizopita, leo hii wamemuua yeye?" Sajenti Minja aliuliza na kufanya mwenzake asielewe anachokimaanisha.



    "una maana gani?" Mwenzake aliuliza,



    "kwa hilo jina ulilonitajia hapo, huyo marehemu ndiye yule mtu familia yake tuliyoikuta wote wamekufa kwa kupigwa risasi" Sajenti Minja aliongea,



    "kwa hiyo huu ni muendelezo? Inaweza kuwa ni mauaji ya madai au visasi" Mwenzake aliongea,



    "yote yanawezekana" Sajenti Minja aliongea na kuvua ile mipira mkononi na kuelekea nje ya kile chumba.



    *******************



    Vin alivyotoka hospitali, alielekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Taita, alivyofika hakugonga hodi, aliingia moja kwa moja sebuleni na kumkuta Taita na Trigger wakiwa wamekaa na juu ya meza kulikuwa na bahasha ya njano yenye jina lake, Vin bila hata ya kumsalimia mtu, akaenda moja kwa moja kuchukua ile bahasha, hapo Trigger na Taita wakapata wasiwasi,



    "mko salama?" Vin aliuliza huku akikaa kwenye kochi na mkononi akiwa na ile bahasha ambayo Trigger aliichukua hospitali,



    "safi tu" Trigger alijibu huku akiinuka kwenye kochi.



    Vin akaitoa karatasi iliyokuwa ndani ya bahasha, Vin akaanza kusoma, kila neno alilokuwa akilisoma ndipo uso wake ulizidi kubadilika, ilionesha wazi hasira zilivyokuwa zinaongezeka.



    "mzee, baadae kidogo" Trigger aliongea huku akianza kuondoka,



    "unaenda wapi? Rudi Kaa hapa, leo mtanieleza ukweli wa haya majibu" Vin aliongea kwa hasira huku akiichomoa bastola yake na kumuelekezea Trigger..................







    Trigger na Taita wakapatwa na mshtuko, ila Vin hakuonekana kujali,



    "kulikuwa na sababu gani ya kumuua Dokta na kuchukua majibu haya kwa nguvu?" Vin aliuliza huku akitoa macho kwenye ile karatasi na kumuangalia Trigger,



    "Mimi ndiye niliyemtuma" Taita alijibu,



    "kwanini umtume? Unadhani ni sahihi wewe kuingilia mambo yangu?" Vin aliuliza kwa hasira,



    "nilifanya hivyo baada ya kusikia Sarah anataka kwenda kufanya shambulio hospitali, ilinibidi nimtume Trigger ili upate majibu yako yakiwa salama" Taita alijibu,



    "ni upuuzi unaongea, ila endeleeni kufanya vitu kama hamna akili timamu" Vin aliongea kwa hasira,



    "leo umeamua kunikosea hadabu kwa ajili ya majibu ya hospitali?" Taita aliuliza kwa ukali,



    "nyie ndio mmenikosea adabu" Vin alijibu kwa hasira,



    "jamani msigombane kwa vitu visivyokuwa na maana" Trigger aliongea,



    "na wewe ni mnafki sana, kama mwanamke" Vin aliongea kwa hasira huku akimtazama Trigger,



    "kwanini boss?" Trigger aliuliza,



    "sijui" Vin alijibu huku akiinuka na ile karatasi yake ya majibu na kuondoka nayo na kuwaacha Taita na Trigger wakiangaliana.



    "hili ni tatizo" Trigger aliongea kwa sauti ndogo,



    "mpuuze, achana nae" Taita aliongea,



    "kwa hali ilivyo, hatokuwa sawa kumpuuza" Trigger aliongea,



    "kwa hiyo unataka kufanyaje?" Taita aliuliza huku akimtazama Trigger,



    "inabidi tumwambie Strategic amfuatilie Vin kwa kila hatua anayoifanya, isije baadae akaujua ukweli, naona muda huu anatafuta sana ukweli" Trigger aliongea,



    "hilo ni jambo jema, muagize Strategic afanye hivyo" Taita aliongea,



    "sawa, baadae basi" Trigger aliongea,



    "sawa" Taita alijibu kisha Trigger akaondoka zake.



    ***********************



    Vin aliondoka pale huku akiwa na maswali mengi sana kichwani mwake, kifupi Vin alichanganyikiwa kutokana na majibu aliyoyaona kwenye cheti, majibu yalikataa kuwa Vin na Sarah sio ndugu, sasa kilichomchanganya ni kitendo cha Trigger kwenda kuiba yale majibu, alihisi huenda kuna namna imefanyika, alihisi huenda Trigger alimshurutisha daktari aandike majibu ya uongo, au Taita na Trigger hawakuwa na uhakika na aina ya majibu yatakayotoka.



    Vin alifika Vin hotel na kuingia moja kwa moja kwenye chumba chake, alipofika ndani akatoa simu na kupiga namba anayoijua yeye,



    "upo wapi?" Vin aliuliza,



    "nipo maeneo ya Vin hotel" Strategic alijibu,



    "njoo chumbani kwangu" Vin aliongea kisha akakata simu, baada ya dakika tano Strategic alikuwa chumbani kwa Vin,



    "vipi?" Strategic aliuliza baada ya kuingia,



    "bado nahitaji msaada wako" Vin aliongea huku akivua shati,



    "ongea tu boss" Strategic aliongea,



    "majibu ya vipimo nimeyapata, ila hayaoneshi kama sarah ni ndugu yangu" Vin aliongea,



    "sasa tatizo lipo wapi?" Strategic aliuliza,



    "tatizo hayo majibu sijayapata moja kwa moja, ingekuwa nimeyapokea mimi kutoka mikononi kwa Dokta ni sawa, ila nimeyakuta tu juu ya meza pale nyumbani, sasa sijui kama yamebadilishwa au yapo sawa" Vin alijibu,



    "unahitaji msaada gani?" Strategic aliuliza,



    "nahitaji utafute ukweli kupitia kwa Trigger" Vin aliongea,



    "sawa, nitafanya hivyo, ila endapo tutapata mtaalam wa kuweka vitega sauti ili nikiwa naongea nae uwe unapata taarifa moja kwa moja" Strategic aliongea,



    "hiyo kazi ndogo, nitaifanya mimi hapa" Vin aliongea,



    "sawa, nadhani uifanye sasa hivi" Strategic aliongea kisha Vin akaenda kwenye begi lake na kulifungua, kisha akavitoa viwaya waya vingi na kuviweka juu ya meza,



    "sasa itabidi niziweke ndani ya shati mbele usawa wa kifungo cha juu" Vin aliongea,



    "waya zote hizo unaniwekea?" Strategic aliuliza,



    "we nakuwekea mic (maiki), hizi nyaya zinabaki hapa" Vin aliongea huku akicheka, na kipindi hicho simu ya Strategic ilikuwa ikiita,



    "Trigger" Strategic aliongea huku akimtazama Vin,



    "pokea, ila usimwambie kama tupo wote na wala usimwambie kama tumeonana leo" Vin alimtahadharisha Strategic na Strategic akaitikia kwa kichwa kuonesha amekubaliana na maneno ya Vin,



    "mkuu" Strategic aliongea baada ya kupokea simu,



    .



    "upo wapi bwana mipango?" Trigger aliuliza,



    "nipo town" Strategic alijibu,



    "na mimi nipo town, njoo tuonane" Trigger aliongea,



    "sawa mkuu, nipe dakika kumi" Strategic alijibu,



    "fresh" Trigger alijibu na kukata simu.



    "sijui ananiitia nini?" Strategic aliongea baada ya kukata simu,



    "nenda kumsikiliza, chukua na hii mic ipachike kwa ndani" Vin aliongea huku akimpatia mic na Strategic akapokea na kuipachika ndani ya shati lake.



    "usiniangushe mista, wewe ndio tegemeo langu kwa sasa" Vin aliongea huku akiziunga nyaya zake kwenye lap top.



    "tupo pamoja kaka" Strategic alijibu huku akiondoka kwa mwendo wa haraka.



    Strategic alienda mpaka kwenye gari yake na kuingia, kisha akaiondoa kwa mwendo wa kasi. Alipofika maeneo ya mjini alitoa simu yake na kumpigia Trigger na kumuuliza ni wapi alipo? Trigger akamuelekeza kisha Strategic akaelekea uko moja kwa moja.



    Strategic aliegesha gari nje ya hotel moja na kupitiliza moja kwa moja mpaka eneo la ndani ambalo lilikuwa na uwazi ambao ulitokana na bwawa la kuogelea lililokuwepo hapo ndani. Strategic akatupa macho kushoto na kulia, akaweza kumuona Trigger aliyekuwepo amekaa pembeni ya bwawa ambapo kulikuwa na kijitanda kidogo na meza ambayo Trigger alitumia kuweka pombe kali.



    Strategic alitembea mpaka sehemu alipo Trigger, akakaa,



    "kachukue glass tuendelee" Trigger alimwambia Strategic,



    "hapana, pombe situmii" Strategic aliongea huku akitabasamu,



    "kaagize utakacho basi" Trigger aliongea,



    "ngoja, Muhudumu akipita hapa nitamuagiza" Strategic aliongea,



    "sasa bwana kuna jambo nimekuitia, ni kuhusu vin" Trigger aliongea,



    "amefanya nini?" Strategic aliuliza,



    "aisee Vin anatakiwa afuatiliwe kwa ukaribu sana, kwa maana kwa sasa Sarah anamzuzua, anadai ni ndugu yake" Trigger aliongea,



    "hiyo habari nimeisikia muda mrefu sana, kwani ukweli ni upi kuhusu undugu wao?" Strategic alianza kumchimba Trigger huku akijua fika Vin anasikia kila kitu,



    "wale ni ndugu, ila juzi Vin alienda kupima damu hospitali, ila vipimo vimeonesha hawana undugu, hapo ndio tulishangaa" Trigger aliongea kwa mshangao,



    "kwa hiyo majibu ya vipimo Vin ameyapata?" Strategic aliuliza,



    "ametukuta nayo mimi na Taita, amekasirika sana na ndio maana nataka umfuatilie" Trigger aliongea,



    "kwani wazazi Vin wapo wapi?" Strategic aliuliza,



    "ni habari ndefu, ila kifupi ni kuwa wameuawa wote, tena waliteketea kwa moto" Trigger alijibu,



    "sasa ikawaje Vin akapona, au hakuwepo ndani?" Strategic aliuliza,



    "Vin nilimtoa mimi kabla nyumba haijaungua, niliwatoa yeye na Sarah baada ya Harry kumshauri Taita, ila baadae Harry huyo huyo akasema ni bora Vin abaki ila Sarah arudishwe ndani kwenye moto, nikamuingiza Sarah ndani, ila kosa ambalo nalijutia mpaka leo ni kutokumfunga Sarah, hiyo ilisababisha Sarah afanikiwe kutoka salama, ila sijajua alitumia mbinu zipi?" Trigger aliongea,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kwa hiyo baba yake Sarah ndiyo baba yake Vin?" Strategic aliendelea kuchunguza,



    "ndio, ila majibu ya hospitali yanaonesha hawana undugu" Trigger alijibu,



    "sasa kwanini Taita aliwaua wazazi wa Vin alafu akachukua Vin, si bora angemuua na Vin?" Strategic aliuliza,



    "bwana we, kwanza Taita na mama yao Vin na Sarah walikuwa ndugu, yaani mtoto wa mkubwa na mdogo, tena walizaliwa wao tu, baada ya baba zao kufa tatizo likaja kwenye mirathi, hapo ndipo ugomvi ulipoanzia" Trigger alijibu,



    "ila nadhani njia bora ilikuwa ni kuwaua wote, yaani Vin na Sarah, sasa mlivyowaacha hai ndio matokeo yake hayo kila siku vurugu na Sarah" Strategic aliongea,



    "huyu Vin tulimuacha hai na tukamfuta kumbukumbu zake zote, huyu alitakiwa awe mrithi wa Taita kwa maana Taita hana uwezo wa kuzalisha" Trigger aliongea na kumfanya Strategic ashangae,



    "kumbukumbu zinafutwa? Zinafutwaje?" Strategic aliuliza kwa mshangao,



    "zinafutwa hospitali, ila uwa zinarudi baada ya muda fulani, ila kwa Vin inakuwa ngumu kumbukumbu kumrudia kwa maana tulimfuta wakati akiwa mdogo sana, alikuwa na miaka minne" Trigger aliendelea kuongea bila kujua maongezi yao yote Vin anayasikia,



    "ni hospitali gani hiyo mliyoitumia, maana na mimi ni bora nifute za kwangu kwa maana stress zitaniua" Vin aliuliza kwa utani huku akicheka,



    "tulifanyia hospitali kuu ya mkoa, na dokta aliyetufanyia alikuwa ni baba mmoja alikuwa akiitwa Innocent Malle, sijui hata kama yupo hai, maana kipindi kile alikuwa na muonekano wa kuwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, si unajua siku hizi watu hatuishi sana?'" Trigger aliongea na kugida ile chupa yenye pombe nyeupe mfano wa maji,



    "kipindi hicho mkuu ulikuwa na umri gani?" Strategic aliuliza huku akicheka,



    "nilikuwa chalii sana, nilikuwa na miaka ishirini na mbili, sasa hivi ni miaka ishirini imepita tangu tukio lile lifanyike" Trigger aliongea na kumfanya Strategic ashangae,



    "ni muda sana, sasa acha mimi niondoke" Strategic aliongea,



    "fanya hiyo kazi niliyokuagiza, hakikisha Vin hajui chochote, maana wewe unaweza kumwambia haya yote tuliyoongea hapa" Trigger aliongea huku akimtazama Strategic,



    "nitamwambia muda gani wakati huyo Vin mi siendi naye sawa, ananata sana" Strategic aliongea huku akicheka,



    "mmarekani yule, lazima awanatie" Trigger aliongea huku akicheka na kipindi hicho Strategic alikuwa akitoka zake.



    *****************



    Vin alikuwa bize akifuatilia maongezi kati ya Trigger na Strategic, sasa alianza kupata mwanga kidogo, ila kilichomchanganya ni matokeo ya vipimo kuonesha hana undugu na Sarah, na kipindi hicho amemsikia Trigger akidai Sarah na Vin ni ndugu,



    "sihitaji kumuamini yoyote, kati ya Sarah wala Taita, bora nirudi marekani nikaendelee na maisha yangu" Vin aliongea peke yake huku akiwa na hasira, kisha akaizima lap top yake na kuingia bafuni.............





    Sajenti Minja bado alikuwa anachanganywa na matukio ya kutisha yanayotokea mfululizo, baada ya kutoka hospitali kufuatilia uchunguzi wa kifo cha Harry, Sajenti Minja alipokea simu nyingine iliyomtaka afike hospitali binafsi ambapo kulikuwa na tukio la daktari kupigwa risasi.



    Sajenti aliendesha gari lake mpaka eneo la tukio na kutelemka, akaelekea moja kwa moja mpaka ndani ya jengo la hospitali na kukaribishwa na wafanyakazi, akawasalimia,



    "nani alikuwepo kipindi tukio linatokea?" Sajenti Minja aliuliza,



    "hakuna mtu anayejua ni muda gani tukio limetokea, ila kuna wadada wapo hapa walimuona mtu wa mwisho kuingia kwenye chumba cha Dokta" Daktari mmoja alimjibu Sajenti Minja,



    "wapo wapi hao wadada?" Sajenti Minja akauliza,



    "ni hao hapo waliokaa mapokezi" Daktari alijibu na kumfanya Sajenti Minja awasogelee, kisha akawasalimia wale wadada wawili warembo, anita na lydia.



    "nasikia nyie ndio mmemuona mtu wa mwisho kuingia kwenye hicho chumba?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ndio, sisi tupo hapa muda wote, kwa hiyo mtu yoyote anayeingia kwenye chumba hicho cha daktari tunamuona" Lydia alijibu,



    "huyo mtu yupoje?" Sajenti Minja aliuliza,



    "sura yake hatujaikariri vizuri, ila ni mwanaume mweupe, amenyoa upara na ana michoro mwilini" Lydia alijibu huku Anita akitikisa kichwa kuashiria kuwa maneno ya mwenzake yapo sawa. Kwa maelezo hayo tu, kichwa cha Sajenti Minja kikafananisha huyo mtu aliyeelezewa hapo na akayakumbuka maneno ya mlinzi wa Harry kuhusu mtu kama huyo kuonekana nyumbani kwa Harry kabla ya kifo cha familia ya Harry.



    "Trigger" Sajenti Minja aliongea huku akiwa ameangalia chini na kufanya wale mabinti wasielewe kitu chochote.



    "mzee hii hospitali haina camera za kunakiri matukio?" Sajenti Minja alimuuliza daktari,



    "kwa bahati mbaya hatuna afande" Daktari alijibu,



    "Daktari aliyekutwa na hilo tukio amefanyiwa uchunguzi?" Sajenti Minja aliuliza,



    "yupo, ametolewa chumba cha upasuaji nusu saa tu iliyopita, hali yake sio mbaya sana, anaweza kuongea" Daktari alitoa jibu lililofanya Sajenti Minja ashtuke,



    "kumbe hajafa?" Sajenti Minja aliuliza kwa mshangao,



    "yupo hai, zile risasi zilimpiga mkononi na kifuani upande wa kulia" Daktari alijibu,



    "naweza kuongea nae?" Sajenti Minja aliuliza,



    "inawezekana tu, twende ukaongee nae" Daktari alijibu huku akianza kutembea na kisha Sajenti Minja akamfuata.



    Walielekea mpaka kwenye wodi moja na kuingia, akamkuta yule Dokta aliyepigwa risasi akiwa amelala, ila mwili tu, macho yalikuwa wazi,



    "askari huyu, amekuja kukujulia hali" Daktari aliyeongozana na Sajenti Minja aliongea kumfahamisha mwenzake,



    "karibu bwana" Dokta aliyepigwa risasi aliongea huku akilazimisha tabasamu, kisha wakasalimiana na Sajenti Minja,



    "unaweza kunieleza mlolongo ulivyokuwa mpaka ukawa kwenye hali hiyo?" Sajenti Minja alimuuliza yule Dokta aliyepigwa risasi,



    "kuna bwana alikuja, akawa anataka majibu ya vipimo ambavyo sio vyake, nikamkatalia, akatoka nje yule bwana, ila kwa utaalam wangu wa saikolojia, nikamsoma yule bwana na kugundua kuwa ni lazima arudi tena baadae, tena alionekana atarudi kwa shari kwa sababu hata muonekano wake ni wa kihuni, amejichora chora michoro mingi mwilini. Basi baada ya yule kijana kuondoka, nilichofanya ni kuchukua karatasi nyingine na kujaza vitu vya uongo, kisha juu nikaandika jina la mtu ambaye anadai amemtuma, uzuri ni kwamba huyo kijana ambaye alikuja kuchukua vipimo nilikuwa nimemkariri kwa kutokana na aina ya vipimo alivyochukua. Basi wakati nikiwa nimemaliza kuweka majibu ya uongo, nikachukua karatasi na kuiweka kwenye bahasha, kisha nikaandika jina la muhusika juu ya bahasha, ndipo mlango ulipofunguliwa na kisha huyo kijana akaingia, akanitolea bastola na kunitaka nimpe majibu, nikampa yale ya uongo ili niokoe uhai wangu" Dokta aliyepigwa risasi aliongea,



    "na kwanini umpe ya uongo?" Sajenti Minja aliuliza,



    "huwezi jua yale majibu alikuwa anayataka kwa sababu ipi, na pia majibu ya vipimo ni siri inayobaki kati ya muhusika na dokta, kwa hiyo sikuona sababu ya kumpatia majibu ya ukweli" Dokta alijibu,



    "tokea tukio limetokea, muhusika mwenye majibu hayo amekuja?" Sajenti Minja aliuliza,



    "nimesikia amekuja na kuuliza, alivyoambiwa hali iliyotokea, ameondoka amesema atakuja baadae au kesho" Daktari ambaye aliongozana na Sajenti Minja alijibu,



    "ni vipimo ambavyo vinahusu nini?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia yule Dokta aliyejeruhiwa,



    "DNA TEST, alileta damu na pia yeye akatoa damu kwa ajili ya kuangalia kama wana uhusiano wa kindugu" Dokta aliyejeruhiwa alijibu,



    "majina ya huyo mtu unayakumbuka?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ni Vin Dennis nafikiri, na alikuwa anataka kulinganisha damu yake na Sarah Isack" Dokta aliyejeruhiwa alijibu na kufanya moyo wa Sajenti Minja upate mshtuko,



    "sawa, basi endapo huyo mtu mwenye majibu atakuja tena, naombeni mchukue namba yake, nikija tena mtanipatia" Sajenti Minja aliongea huku akiinuka,



    "sawa, sijui tukutambue kwa jina gani afisa?" Daktari aliyeongozana na Sajenti Minja aliuliza,.



    "Joel Minja" Sajenti Minja alijibu huku akiondoka na yule Daktari mwingine alimsindikiza.



    **************



    Sarah siku ya leo hakuwa na ratiba maalum, alichoamua ni kuchukua simu yake kisha akaitafuta namba ya simu ya Vin kupitia mtandaoni, kisha akajaribu kupiga ile namba, ikawa inaita,



    "habari" Sarah aliongea baada ya upande wa pili kupokea simu,



    "nzuri" Vin alijibu kifupi,



    "upo wapi muda huu?" Sarah aliuliza,



    "naongea na nani?" Vin aliuliza,



    "Sarah naongea" Sarah alijibu,



    "nipo hotelini, Vin hotel" Vin alijibu,



    "ninaweza kukuona?" Sarah aliuliza,



    "njoo Vin hotel, ila hakikisha hakuna mtu atakayekujua" Vin aliongea kwa msisitizo,



    "sawa, ndani ya nusu saa nitakuwa nimefika" Sarah aliongea na kukata simu, kisha akaingia bafuni kuoga, baada ya hapo akachukua baibui refu na kuvaa, kichwa akakivika mtandio mkubwa na zaidi alijifunga huo mtandio kama mama mtu mzima,



    "vipi shoga, leo unaenda kuonana na sheikh nini? Maana sio kwa mtandio huo" Dokta Pendo alimuuliza Sarah,



    "naelekea Vin hotel, kuna mtu naenda kumuona mara moja" Sarah alijibu huku akitabasamu,



    "kwa wema au vurugu zako tu?" Dokta Pendo aliuliza,



    "kwa wema shoga, huoni hata mavazi nimevaa ya kistaharabu?" Sarah alijibu kwa mtindo wa kuuliza,



    "sawa shoga" Dokta Pendo aliongea,



    "huyu mzee yupo wapi?" Sarah alimuulizia babu yake,



    "alikuwa ametandika mkeka kule nyuma ya nyumba, nadhani alikuwa anataka Kulala" Dokta Pendo alijibu,



    "poa basi, akiniulizia mwambie nimeenda kununua mahitaji ya nyumbani, usimwambie kuwa nimeenda Vin hotel" Sarah Alimwambia Dokta Pendo,



    "usijali shoga, usisahau kuniletea castle za kopo" Dokta Pendo aliongea huku akitabasamu,



    "tokea umepona umekuwa mnywaji kweli, nitakuletea shoga, na huyo mlevi mwenzio nitamletea na za kwake pia" Sarah aliongea huku akicheka,



    "haya bwana" Dokta Pendo aliongea huku akifurahi na kipindi hicho Sarah alikuwa akielekea nje, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka na kumuacha Dokta Pendo akifunga geti kubwa la nyumba.



    Sarah aliendesha gari kwa mwendo wa haraka kidogo ili asitoke nje ya muda ambao amemuahidi Vin, na alikuwa anakwenda kwa Vin kwa lengo la kutaka kujua kuhusu kama Vin alifuatilia vipimo vya damu au alimpuuza?



    Sarah alifika Vin hotel na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Vin, akagonga mlango, baada ya sekunde chache mlango ulifunguliwa na Vin mwenyewe, akamkaribisha Sarah, Sarah akaingia na kukaa kwenye kochi,



    "mbona ulivyofika hukunipigia simu?" Vin alimuuliza Sarah,



    "sikuwa na sababu ya kufanya hivyo wakati chumba nakijua vizuri" Sarah alijibu huku akitabasamu,



    "umejuaje nakaa katika chumba hiki?" Vin aliuliza,



    "muda tu najua, na kama ningeamua kukudhuru, ningekudhuru mapema tu" Sarah aliongea kwa kujiamini,



    "isingekuwa rahisi kunidhuru" Vin nae alijibu kwa kujiamini,



    "angalia pale" Sarah alimuonesha Vin pembeni ya dirisha, kulikuwa na kitu kama cha kuwekea ua,



    "si ni urembo wa kuwekea ua?" Vin aliuliza,



    "kaangalie kwa karibu zaidi" Sarah aliongea na kumfanya Vin ainuke aende kuangalia, haukuwa ni urembo wa kuwekea maua, aligundua hilo bomu, akashtuka,



    "rudi ukae dogo, sina nia mbaya" Sarah aliongea na kufanya Vin ageuke na kumtazama,



    "sasa kama huna nia mbaya si ulitoe?" Vin aliuliza huku akijiuliza hilo bomu liliwekwa lini,



    "njoo tuongee, nitalitoa tu" Sarah aliongea huku akicheka na kumfanya Vin aende kukaa huku akiwa hajiamini kabisa,



    "nambie umefikia wapi? Ulienda kupima damu?" Sarah alimuuliza Vin,



    "yeah, nilienda kupima, ila majibu yameonesha hatuna undugu" Vin aliongea huku akipekua chini ya meza na kuitoa ile bahasha yenye majibu ya vipimo, Sarah akaichukua na kuifungua kisha akasoma kwa Muda,



    "umepima hospitali moja tu?" Sarah aliuliza huku sura yake ikiwa haina nuru aliyokuja nayo,



    "kama majibu yameonesha hivyo, hata uende hospitali kumi bado itakuwa hivyo hivyo" Vin aliongea huku akitabasamu,



    "umeyaamini?" Sarah aliuliza,



    "ningependa kuyachukua mimi ningeyaamini, ila alienda Trigger, na ubaya zaidi aliyachukua kwa nguvu, amemuua mpaka daktari" Vin aliongea,



    "sasa bado hujapata jibu ni kwanini afanye hivyo, huoni kuna kitu wanakuficha?" Sarah aliuliza,



    "ni kweli, na kuna maelezo haya nilitumia mtu anisaidie kuyapata" Vin aliongea huku akiwasha lap top yake na kumsikilizisha Sarah maongezi yaliyokuwa yanafanyika baina ya Trigger na Strategic.



    Sarah akasikiliza tangu mwanzo mpaka mwisho wa yale maongezi, muda wote machozi yalikuwa yakimtoka tu kutokana na maneno ya Trigger,



    "baada ya kusikiliza hayo maneno umeamua kufanya nini?" Sarah alimuuliza Vin huku akifuta machozi,



    "nimeamua niruds marekani tu, maana bado mnanivuruga" Vin aliongea huku akirudia kuiweka sauti ya Trigger,



    "kabla hujaondoka, unatakiwa uende ukamtafute daktari aliyetajwa na Trigger hapo, anaweza kukupa mwanga, uzuri na hospitali ambayo wanadai walitumia kukufutia kumbukumbu wameitaja" Sarah aliongea,



    "na kama amekufa?" Vin aliuliza na kumfanya Sarah atabasamu,



    "usipende kujikatisha tamaa, mtoto wa kiume inabidi upambane ili ujue ukweli wa maisha yako" Sarah aliongea huku akitabasamu na muda alisimama, alikuwa anataka kuondoka,



    "sawa, nitafanya hivyo" Vin alijibu kivivu,



    "kafanye leo, muda bado upo, mimi naondoka, nitakupiga simu usiku" Sarah aliongea huku akiwa bado amesimama, ila ghafla mlango ulifunguliwa na akaingia Trigger, mkononi akiwa na bastola, Vin akamuangalia Sarah na kisha akatabasamu.



    Sarah akabaki ameduwaa huku akiishangaa hiyo hali na wakati huo asijue atapambana vipi angali hana silaha yoyote hata kisu tu au kiwembe..................?





    "ooh samahani, kumbe upo na shemeji" Trigger aliongea huku akirudi nyuma na kutoka nje, uzuri ni kuwa hakuweza kumtambua Sarah kwa kuwa Sarah alimpa mgongo na pia mavazi aliyokuwa ameyavaa Sarah yalikuwa ni mapana na ya kiutu uzima, ikawa shida kwa Trigger kumtambua.



    "subiri, Kaa hapo usitoke, ni Trigger huyo" Vin aliongea huku nae akitoka nje kumfuata, Sarah akakaa ila kwa tahadhari, aliamini chochote kinaweza kutokea.



    Vin alitoka na kumkuta Trigger akiwa amesimama nje ya mlango,



    "vipi kuna chochote?" Vin alimuuliza Trigger,



    "mzee anakuita, ameniagiza nikufuate" Trigger aliongea,



    "sasa hivi nina mgeni, nitakuja huko muda wowote, kwanini hamkunipigia simu?" Vin aliuliza,



    "kwa kuwa niliamini nitakukuta tu" Trigger alijibu huku akitabasamu,



    "poa, mwambie nakuja" Vin aliongea na kisha Trigger akaondoka zake.



    Vin akarudi ndani,



    "kuna usalama?" Sarah alimuuliza Vin,



    "upo, mzee ananiita mara moja" Vin aliongea,



    "nenda kwanza kamtafute daktari niliyokuambia, mzee wako utaenda kumuona baadae" Sarah aliongea,



    "hilo suala nalifuatilia muda huu" Vin alijibu,



    "sawa, ni naenda" Sarah aliongea huku akisimama,



    "Kaa hapo kwanza, subiri" Vin aliongea huku akitoa simu yake, kisha akabonyeza namba ya Strategic,



    "upo hapo nje?" Vin aliuliza kwenye simu,



    "ndio mkuu" Strategic alijibu,



    "umemuona Trigger akiondoka?" Vin aliuliza,



    "ndio, ameondoka muda sio mrefu" Strategic alijibu,



    "poa" Vin alijibu na kukata simu, akamgeukia Sarah,



    "unaweza kuondoka sasa" Vin alimwambia Sarah,



    "ina maana umeweka ulinzi nje?" Sarah aliuliza huku Akitabasamu,



    "ulinzi muhimu" Vin alijibu na kumfanya Sarah aondoke huku akitabasamu.



    Vin akakaa kwenye kochi na mawazo juu ya Sarah yakamuanza tena, kuna upande ulikuwa unakubali Sarah ni ndugu yake, ila kuna upande ulipinga kabisa hilo suala.



    "ngoja nifuatilie ukweli kuhusu mimi kwanza, suala la undugu litafuata baadae" Vin aliongea na kunyanyuka, kisha akaelekea kwenye kabati na kuchagua suti, kisha akavaa na kutoka nje.



    Alitoka mpaka nje na kuingia kwenye gari lake, kisha akatoa simu na kumpigia Strategic,



    "umeniona?" Vin aliuliza baada ya simu kupokelewa,



    "vizuri sana" Strategic alijibu huku akicheka,



    "njoo kwenye gari yangu, kuna sehemu nataka twende" Vin aliongea kisha akakata simu.



    Baada ya muda mchache Strategic aligonga kioo cha na kumfanya Vin afungue mlango,



    "wewe ni mwenyeji mji huu?" Vin alimuuliza Strategic,



    "ndio, vipi kwani?" Strategic aliuliza,



    "nataka niyafuatilie maongezi ya Trigger mliokuwa mkiongea naye, kwa hiyo muda huu nipeleke hospitali kuu ya mkoa" Vin aliongea,



    "sawa, na Trigger alivyokuja alikuwa na habari gani?" Strategic aliuliza huku akiwasha gari,



    "alikuja kuleta taharifa kuwa mzee ananiita" Vin alijibu,



    "ooh, sawa" Strategic aliongea huku akiondoa gari.



    Safari yao iliishia katika hospitali kuu ya mkoa, Vin akatelemka na kumuacha Strategic ndani ya gari.



    Vin akaingia moja kwa moja mpaka eneo la mapokezi na kumkuta mwanamke mtu mzima akiwa amekaa, Vin akamsalimia,



    "namuulizia Dokta mmoja anaitwa innocent Malle" Vin aliongea huku akimtazama huyo mama,



    "mhmm...anafanya kazi hapa? Mbona simjui? Au ni hawa vijana wanaofanya field?". Mama yule aliuliza maswali mfululizo na kumfanya Vin atabasamu,



    "hapana, alishawahi kunitibu miaka ishirini iliyopita, alikuwa mfanyakazi wa hapa, nilikuwa nje ya nchi sasa nimrudie, na nataka nionane nae na sikuwa na sehemu nyingine ya kumuulizia zaidi ya hapa" Vin aliongea na kumfanya mama ashangae,



    "miaka ishirini ni mingi mwanangu, ebu nenda chumba kile unaweza kupata msaada" Mama yule aliongea huku akimuelekeza Vin kwa kutumia kidole chake cha shahada.



    Vin akaelekea moja kwa moja mpaka kwenye hicho chumba, akagonga hodi na kuruhusiwa kuingia, akamkuta kijana mmoja akiwa amekaa,



    "karibu" Kijana alimkaribisha Vin,



    "asante" Vin aliitikia huku akiwa hajui aanzie wapi kueleza shida yake,



    "nakusikilza boss" Kijana aliongea huku akimtazama Vin,



    "namuulizia Dokta Innocent Malle" Vin aliongea,



    "yupo, unashida gani?" kijana alijibu na kumshangaza Vin,



    "umemjuaje wakati wewe ni kijana na kwa makadirio huyo Dokta atakuwa amestaafu miaka mingi nyuma?" Vin aliuliza huku akitabasamu,



    "Mimi ndio mtu ambaye nashughulika na wafanyakazi wastaafu wa hii hospitali, ndio maana nimemtambua kwa urahisi huyo mzee" kijana alijibu huku akitabasamu,



    "nitampata wapi kwa sasa?" Vin aliuliza,



    "una shida naye ipi?" kijana aliuliza na kumfanya Vin acheke,



    "alikuwa ni daktari wa familia yetu kipindi nikiwa mdogo, nilisafiri kwa muda mrefu sana, sasa nimerudi na nimeona ni vyema nimtafute" Vin aliongea,



    "ok, yupo, ngoja nikupitie namba yake ya simu" Yule kijana aliongea huku akibonyeza vitufe vya kompyuta yake.



    "si atakuwa amezeeka sana?" Vin aliuliza huku akijifanya anamjua,



    "umri umeenda, ila bado ana nguvu" Kijana alijibu huku akimpatia Vin karatasi yenye namba za simu za Dokta Innocent Malle



    "asante sana" Vin alipokea kile kikaratasi na kushukuru, kisha akaanza kuondoka huku zile namba akiziingiza kwenye simu yake, alitoka mpaka nje kwenye gari na kupiga namba ya simu ya Dokta Innocent Malle, simu iliita kisha ikapokelewa na Dokta mwenyewe, Vin akaomba aonane nae, ingawa ilikuwa ngumu kukubaliwa kwa haraka, ila baada ya kuomba sana, Dokta Innocent Malle alikubali kuonana na Vin, akamuelekeza nyumbani kwake.



    Vin akamgeukia Strategic na kumwambia pa kumpeleka, strategic akawasha gari na kuiondoa kwa mwendo wa wastani.



    Iliwachukua nusu saa tu Strategic kufika nje ya nyumba ambayo walielekezwa, waliitambua kutokana na namba ya mtaa na namba ya nyumba pia. Strategic akaegesha gari na kisha wakatelemka, wakabonyeza kitufe cha getini ambacho kilikuwa ni kengele, baada ya dakika moja geti lilifunguliwa na Kijana mmoja ambaye alilingana umri na Vin,



    "karibuni" Kijana aliongea,



    "asante" Vin aliitikia huku akiingia ndani, walipoingia ndani walikutana na mandhari nzuri, nyumba ilikuwa na uwanja mkubwa ambao ulipandwa miti mingi ya matunda iliyosababisha kivuli kipatikane kwa asilimia kubwa. Vin na Strategic waliendelea kuitazama ile nyumba huku wakionekana kuvutiwa na mazingira ya pale.



    "karibuni" Kijana aliyewakaribisha aliongea huku akiwaelekeza kakibanda kadogo kalichoezekwa kwa nyasi, ambapo ndani ya kakibanda hako kulikuwa na meza kubwa iliyozungukwa na makochi ya sofa ambayo yalikuwa makuu kuu ila yalipendeza kukaa sehemu ile.



    "karibuni" Kijana aliongea tena baada ya Vin na Strategic kufika ndani ya kibanda kile,



    "shukran sana" Vin alijibu huku akikaa kwenye kochi,



    "nyie ndio mliopiga simu mnataka kuongea na mzee?" Kijana aliuliza huku akiwaangalia,



    "ndio, ni sisi" Vin alijibu,



    "msubirini kidogo" Kijana aliongea na kuelekea ndani, baada ya dakika mbili kijana alirejea huku mkononi akiwa na chupa mbili za chai na ndoo yenye vikombe vidogo vya udongo, akaweka mezani.



    "chupa hii ina kahawa na hii ina chai ya kawaida, mtajihudumia mtakacho" Kijana aliongea na kurudi zake ndani na kuwaacha Vin na Strategic wakitazamana.







    ********************



    Sarah alivyotoka Vin hotel kuongea na Vin, aliamua kupitia super market kwa ajili ya kununua vitu vya nyumbani. Aliingia super market na kuchukua mahitaji yake, alipomaliza alienda kwa mpokea pesa ambaye alivihakiki vitu vya Sarah na kisha akamtajia malipo, Sarah akalipa na kutoka na vitu vyake mpaka nje, akaviingiza ndani ya gari na kisha akaingia kwenye gari na kuanza kuondoka.



    Wakati Sarah akiwa anaondoka eneo hilo, ndio muda ambao Sajenti Minja alikuwa anaingia hapo, wakati wakapishana, Sajenti Minja alitupia jicho kwenye gari alilopo Sarah, akamtambua.



    Alichofanya Sajenti Minja ni kupishana na gari ya Sarah kisha akageuza gari yake na kuanza kumfuatilia Sarah, alitaka kujua ni wapi anapokaa. Sajenti Minja kwa kutumia akili zake zote za kipelelezi aliendelea kuifuatilia gari ya Sarah huku akiwa makini kutumia mbinu tofauti ili Sarah asimgundue kwa maana alijua Sarah ni mtu hatari kwa hiyo kwa vyovyote vile ni lazima na yeye atakuwa makini kila wakati.



    Gari ya Sarah ilizidi kwenda mpaka kwenye mtaa mmoja uliokuwa mgeni machoni kwa Sajenti Minja, kisha Sarah akasimamisha gari lake mbele ya nyumba moja ambayo ilikuwa ngeni pia kwa Sajenti Minja. Sajenti Minja nae akasimamisha gari lake mbele ya nyumba ambayo hakuijua, aliamua afanye hivyo ili hata Sarah akishuka kwenye gari yake asiweze kutilia mashaka



    Umbali wa eneo aliposimama Sarah na eneo ambalo Sajenti Minja aliegesha gari yake, ulikuwa ni umbali mrefu sana, kilichomsaidia Sajenti Minja ni barabara kuwa nyoofu, kwa hiyo aliweza kumuona Sarah vizuri sana kwa kila hatua aliyokuwa anaifanya.



    Sajenti Minja alimshuhudia Sarah akishuka kwenye gari yake na kisha akaenda kufungua geti, akamshuhudia tena Sarah akirudi ndani ya gari na kuiingiza gari ndani ya geti, baada ya sekunde chache aliweza kuona geti likirudishiwa.



    Sajenti Minja akatoa simu yake mfukoni, kisha akatoa kichwa ndani ya gari na kumsimamisha kijana mmoja aliyekuwa akipita, akamsalimu,



    "dogo huu mtaa unaitwaje?" Sajenti Minja aliuliza,



    .



    "tambeleya" Dogo alijibu na kisha Sajenti Minja akashukuru na dogo akaendelea na safari. Sajenti Minja akapiga simu, baada ya muda mtu wa upande wa pili akapokea simu,



    "upo ofisini?" Sajenti Minja aliuliza baada ya simu kupokelewa,



    "ndio mkuu" Mtu wa upande wa pili alijibu,



    "chukua gari mbili zikiwa na askari wenye silaha, alafu nitakuelekeza unifuate" Sajenti Minja aliongea na kukata simu, aliamua kuchukua askari wengi kwa maana alihufahamu utata wa Sarah kwenye mapambano.



    Baada ya dakika kumi simu ya Sajenti Minja iliita, ilikuwa namba ya yule askari aliyempigia muda mchache uliopita, Sajenti Minja akapokea na kisha akamuelekeza ni wapi alipo, akakata simu.



    Baada ya dakika ishirini gari mbili za polisi zikiwa na askari wakutosha na wote wenye silaha walisimamisha gari pembeni ya gari ya Sajenti Minja, Sajenti Minja akashuka na kuingia kwenye gari la mbele la polisi,



    "twende" Sajenti Minja alimwambia dereva ambaye alifuata maelekezo mpaka mbele ya nyumba aliyoingia Sarah, Sajenti Minja akashuka kwenye gari na kisha akawataka askari wote watelemke, waliposhuka wakamzunguka Sajenti Minja,



    "mnachotakiwa ni kuivamia hii nyumba, mtu yoyote mtayemkuta humu mkamateni, haya vamieni" Sajenti Minja aliongea kwa amri kisha askari wakavamia kwa fujo ile nyumba huku Sajenti Minja akija kwa nyuma yao.



    Askari walivamia nyumba na kuizunguka yote, ila mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ulikuwa umefungwa kwa ndani, na taa ya ndani ya nyumba ilikuwa imewashwa,



    "mliopo ndani jisalimisheni" Sajenti Minja aliongea kwa sauti kubwa, ila hakuna mtu aliyetoka, badala yake wakashuhudia taa za ndani zikizimwa zote,



    "lete bunduki" Sajenti Minja alimwambia askari aliyepo jirani yake, askari akampatia Sajenti Minja bunduki, Sajenti Minja akarudi nyuma kisha akafyatulia risasi kadhaa eneo la kitasa, baada ya hapo akaupiga mlango take, mlango ukafunguka,



    "twendeni ndani" Sajenti Minja aliamrisha na askari kama kumi aliongozana nao kuingia ndani na wengine walibaki nje wakiimarisha ulinzi..........





    Sajenti Minja na vijana wake wakavamia ndani ya ile nyumba huku wakitumia tochi zao, walikagua nyumba nzima hawakubahatika kukuta mtu katika hiyo nyumba, nyumba yenyewe haikuwa na fenicha yoyote ndani,



    "atakuwa ametuzidi akili" Sajenti Minja aliongea huku akitoka nje na baadhi ya askari wakabaki ndani wakiendelea kukagua.



    "Mkuu huku nyuma kuna ngazi inayoonesha kuna uwezekano wa huyo mtu kuwepo juu ya nyumba" Askari aliongea na kumfanya Sajenti Minja azunguke nyuma ya nyumba na kukuta ngazi ikiwa imeegeshwa ukutani, Sajenti Minja akapanda mpaka juu ya nyumba na kukuta kuna eneo zuri tu la kukaa watu, na zaidi alikuta kuna viti viwili na meza moja katikati ya vile viti.



    Sajenti Minja akasogea kwa karibu huku akiongeza umakini wa macho, akaona damu ikiwa chini ila imeganda, Sajenti Minja akainama na kuigusa ile damu ila hakuambulia kitu, damu ilionekana ya muda mrefu. Sajenti Minja akatupa jicho juu ya meza na kuona ganda la risasi likiwa lipo juu ya meza, Sajenti Minja akahisi eneo hilo kuna mtu alipigwa risasi ila ni siku nyingi sana. Sajenti Minja akatoa simu mfukoni na kupiga picha kadhaa eneo hilo, kisha akatelemka chini,



    "hamjabahatika kuona kitu chochote uko ndani?" Sajenti Minja aliuliza askari waliokuwa ndani,



    "hakuna kitu mkuu" Askari mmoja alijibu,



    "sawa, nyie ondokeni kaendeleeni na shughuli zenu" Sajenti Minja aliwaruhusu askari waondoke, askari wakaondoka na kumuacha peke yake huku akijiuliza ile nyumba ni ya Sarah au ya nani?



    ,



    "atakuwa amekimbia, ila mbona gari yake ameiacha ndani?" Sajenti Minja alijiuliza bila kupata jibu sahihi, akaamua atoke nje na kuanza kuelekea sehemu ilipo gari yake, kwa kuwa aliegesha umbali mrefu kidogo ilimbidi atembee taratibu huku akigeuka kila muda kuiangalia ile nyumba aliyoingia Sarah, ila kabla Sajenti Minja hajaifikia gari yake, alikutana na watu watatu waliomsimamisha, walikuwa ni vijana wawili na mzee mmoja, kati ya wale vijana wawili, Sajenti Minja alimkumbuka kijana mmoja ambaye alimsimamisha hapo hawali na kumuuliza jina la mtaa huo.



    Yule mzee na Sajenti Minja wakasalimiana,



    "Mimi ni balozi wa huu mtaa, huyu kijana amekuona ukiwa na polisi na umeingia nyumba ile" Mzee aliongea huku akioneshea kwa kidole nyumba aliyoingia Sarah,



    "umekuja wakati muafaka mzee, mimi ni afisa wa polisi, kuna mtu aliingia kwenye nyumba ile, huyo mtu anatafutwa na polisi" Sajenti Minja aliongea huku akimpatia balozi kitambulisho chake, balozi akakipokea na kukiangalia, kisha akampa kijana mmoja ambaye nae alikipokea na kukikagua kisha yule kijana akamtupia jicho balozi na kutingisha kichwa chake kwa kukipeleka juu, kuashiria amekubaliana na alichokiona katika kitambulisho,



    "mmemkamata?" Balozi aliuliza huku akimrudishia kitambulisho Sajenti Minja,



    "hapana, ila kwa namna alivyoingia na kuondoka, inaonesha wazi ni mtu ambaye anaifahamu vizuri ile nyumba" Sajenti Minja aliongea,



    "watakuwa vibaka tu, kwa maana mwenye hiyo nyumba tangu ameinunua alirudi mara moja tu kuweka geti la mbele, ila kutokea hapo sijawahi kumuona tena" Balozi alimjibu Sajenti Minja,



    "ila huyo mtu tunayemtafuta ameingiza na gari kabisa ndani ya geti, tena hilo geti alifungua na funguo kutoka mfukoni mwake" Sajenti Minja aliongea na kumfanya balozi atoe macho,



    "ameingia na gari? ebu twende" Balozi aliongea huku akianza kuondoka na wale vijana wakamfuata na nyuma alikuwepo Sajenti Minja.



    Walifika mpaka katika ile nyumba na kuingia, kweli waliikuta gari ndani ya geti, Balozi akazidi kushangaa, kisha Balozi akauendea mlango wa kuingilia sebuleni na kuukuta ukiwa umeharibiwa vibaya na risasi,



    "sasa kama mnasema aliingia ndani na nyie mkavunja mlango, kwanini hamkumkuta ndani?" Balozi aliuliza huku akishangaa,



    "ndio maana nikasema kuwa huyo mtu anaijua vizuri hii nyumba" Sajenti Minja alijibu,



    "ebu twende upande wa nyuma" Balozi aliongea huku akielekea nyuma ya nyumba na Sajenti Minja na wale vijana wakamfuata.



    "ebu vuta hilo dirisha" Balozi alimwambia kijana wake ambaye alilivuta dirisha na likanyanyuka zima zima Kama mlango wa mbele wa genge, Sajenti Minja akili zikamwambia huenda Sarah alifanya kitu hicho, sasa swali likabaki ni nani aliyezima taa?



    "kwani mzee huyo mmiliki wa hii nyumba ni nani?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ni kabinti kamoja hivi kadogo dogo, kanaitwa salama sijui" Balozi aliongea,



    "hapana mzee, anaitwa Sarah" Kijana mmoja alimrekebisha Balozi huku akimcheka, huo ukawa mwiba kwa Sajenti Minja,



    "basi ndiye huyo aliyeingia hapa, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuua na kuteka, anaitwa Sarah Isack" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa simu yake na kumuonesha Balozi picha ya Sarah,



    "ndiye huyu haswaaa mmiliki wa hii nyumba, sasa unaponiambia ni muuaji unanichosha kabisa" Balozi aliongea huku akitabasamu kwa mshangao,



    "vijana pandeni uko juu ya nyumba alafu mmuambie Balozi kuna nini?" Sajenti Minja alimwambia wale vijana kisha kijana mmoja akapanda na kusema alichokiona, Balozi akazidi kushangaa,



    "tulikuwa hatujui kama ni mtu hatari hivyo?" Balozi aliongea,



    "mkae mkijua hivyo, na muda wowote akirudi tena hapa, mnitaharifu" Sajenti Minja aliongea huku akiwapa karatasi ngumu yenye namba yake ya simu, kisha akaondoka zake na kumuacha Balozi na vijana wake wakilizungumzia hilo tukio la kushangaza lililotokea mtaani hapo.



    ********************



    Sarah wakati akitoka super market hakuweza kumuona Sajenti Minja, ila baadae wakati akiwa njiani kurudi kwake ndipo alipogundua kuna gari inamfuatilia, hakujua hiyo gari ni ya nani, ilimbidi atulize macho yake na kuiangalia hiyo gari kwa umakini mkubwa na kuitambua hiyo gari ni Sajenti Minja, alichofanya Sarah ni kumpoteza maboya Sajenti Minja.



    Sarah alibadili njia na kuelekea upande ilipo ile nyumba, sio kwamba haikua nyumba yake, ile ni nyumba yake ambayo alimnunulia babu yake kutokana na pesa aliyopewa na Taita wakati ule Taita alipokuwa mateka wa Sarah, kama unakumbuka Taita alimpa agizo Trigger la kumpatia pesa Sarah. Sasa Sarah baada ya kuipata ile pesa alinunua nyumba ambayo alifanya kama fidia kwa babu yake baada ya nyumba ya babu yake kuchomwa moto.



    OK, tuendelee tulipoishia.

    Baada ya Sarah kugundua anafuatiliwa, aliamua aende moja kwa moja kwenye hiyo nyumba, Sarah baada ya kuingiza gari ndani alifunga geti kisha akatoa bidhaa ndogo ndogo alizotokanazo super market na kuziweka kwenye pochi yake kubwa, kisha akadandia ukuta na kumchungulia Sajenti Minja na kumuona akiongea na simu, sarah akahisi huenda Sajenti Minja anaita polisi zaidi.



    Sarah akafungua mlango na kuingia ndani, alitaka kuzima taa ili atokee dirisha la nyuma ambalo ni bovu, ila aliona unit za luku ni chache na umeme utazima muda wowote, Sarah akatabasamu na kutokea dirishani, kisha akapanda ukuta na kutua upande wa pili, akapotea eneo hilo na kwenda mtaa wa pili na kuchukua bajaj iliyompeleka nyumbani kwake.



    ********************



    Vin na Strategic wakiwa wamekaa kwenye viti huku wakizitazama zile chupa za chai, waliweza kushuhudia mlango wa mbele ukifunguliwa na akatoka mzee mmoja mwenye mwili mkavu, ingawa umri ulionekana kumtupa kidogo ila bado alikuwa na nguvu za kutembea mwenyewe bila tatizo.



    Yule mzee alitembea mpaka alipowafikia Vin na Strategic, kisha Vin na Strategic wakasimama na kumsalimia, akaitikia kwa uchangamfu,



    "mbona hamjaweka vinywaji bwana, wekeni msiogope" Mzee aliongea huku akikaa kisha kijana wake yule aliyewapokea wakina Vin akammiminia kahawa kwenye kikombe kidogo,



    "Mimi ndio Dokta Innocent Malle, haya na nyie mjitambulishe sasa ili tujuane" Yule mzee aliongea huku akitabasamu,



    "Mimi naitwa Vin Denis, huyu ni rafiki yangu tu amenisindikiza, mimi hasa ndio mwenye shida" Vin aliongea huku akitabasamu pia,



    "kupitia jina bado sijakujua, huenda ninaweza kukujua baadae baada ya maongezi" Dokta Innocent Malle aliongea na kucheka,



    "kweli Dokta" Vin nae alikubaliana nae,



    "twende kisomi sasa, nenda moja kwa moja kwenye lengo la wewe kunitafuta mimi" Dokta Innocent Malle aliongea na kunywa kahawa kidogo,



    "kuna kitu kina utata kidogo kuhusu maisha yangu, kwanza kabisa mimi ni mtoto wa Taita, lakini bado kuna habari zinasema Taita sio baba yangu ila alinichukua kipindi nipo mdogo na kunifuta kumbukumbu zangu zote, na hiyo kazi ya kufuta kumbukumbu uliifanya wewe" Vin aliongea na kumuangalia Dokta Innocent Malle ambaye muda wote wa maelezo hayo alionekana yupo kawaida, wala hakushtuliwa na maelezo ya Vin,



    "ujue kijana mimi ni mtu mmoja mkweli sana, hasa kwenye jambo linalolenga maisha ya mtu moja kwa moja, unaona hii nyumba, hii nyumba nilijenga kwa pesa ya Taita, kipindi kile cha nyuma serikali ilikuwa haina uwezo wa kutoa mshahara na mtu ukanunua Kiwanja kikubwa kama hiki na kujenga nyumba kubwa hivi.



    Sasa hapa point yangu ni ipi? ndio, miaka ya nyuma Taita alikuja hospitali na kuniomba nimfanyie kazi ya kumfuta kumbukumbu mtoto mdogo wa umri wa miaka minne, kisheria ni kosa kupoteza kumbukumbu za mtu tena bila sababu ya msingi, ila kwa maelezo waliyonipa ilibidi nikubali kufanya jambo lile Kaa ajili ya kumsaidia mtoto, kwa maana yule mtoto ningemuacha akue huku akiwa na akili na kumbukumbu ya zamani, basi maisha yake yangekuwa mafupi sana, ni lazima tu angeuawa na Taita kwa maana yule mtoto angeutambua na kuukumbuka unyama waliofanyiwa wazazi wake, ni lazima yule mtoto angetaka kulipa kisasi akiwa bado hajakomaa vizuri kimwili na kiakili" Dokta Innocent Malle aliongea na kushushia na kahawa,



    "unyama upi waliofanyiwa wazazi wake?" Vin aliuliza huku akimeza mate,



    "Harry alikuwa rafiki yangu sana, Harry ndiye aliyeniunganisha na ile kazi ya Taita, kwa hiyo kwa maelezo ya Harry aliniambia kuwa wazazi wa yule mtoto walichomwa moto wakiwa ndani ya nyumba, ila hakuniambiaa ni nani aliyefanya hivyo, ila hapa juzi juzi kabla Harry hajafa alikuja kuniomba nihifadhi familia yake kwa kuwa kuna tatizo, alisema kuna watu wanataka kuiteketeza familia yake, akiwemo baba yako Taita na msichana mmoja aliyemtaja kwa jina la Sarah, na nilipomuuliza ni kwanini Taita ambaye ni rafiki yake wa karibu anataka kumuua? Alinijibu kuwa ni kisa cha miaka ishirini iliyopita, ambacho ndicho hicho cha wazazi wa yule mtoto niliyempoteza kumbukumbu, alidai Sarah ni mtoto aliyeokoka kwenye moto ule na alipotea kwa muda mrefu, ila amerudi na lengo lake inaonekana ni kulipa kisasi kwa Taita na watu walioshiriki kuwaua wazazi wake. Hiyo ndio ilikuwa sababu ya Harry kuwindwa na Sarah.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na nilipomuuliza kwanini Taita nae anataka amuue, alinijibu kuwa alimwambia Taita Kuwa yeye Harry anataka kuondoka na kukimbia mapambano dhidi ya Sarah, hilo ndilo lilikuwa kosa, na pia anadai kuna siku alimuoneshea Taita bastola wakiwa hospitali, lakini alishangaa kuona akipigwa risasi ingali yeye Harry hakufyatua hizo risasi, na hata bastola yake haikuwa na risasi, huo ndio ukawa uadui kati ya Harry na Trigger na mtoto wa Trigger ambaye nadhani ni wewe" Dokta Innocent Malle aliongea huku akimnyooshea kidole Vin,



    "sasa hapo mbona sijapata jibu bado ni nani haswa aliwachoma wazazi wa yule mtoto?" Strategic aliuliza,



    "kijana una umelewa mdogo sana, yaani habari yote niliyozungumza na bado hujapata jibu, kwanini hujiulizi ni kwanini Sarah anataka kulipa kisasi cha kifo cha wazazi wake na mlengwa mkubwa ni Taita? hujiulizi kwanini Harry alikubaliana na hoja za Sarah na ndio maana akataka akimbie? Hujiulizi ni kwanini Taita anaficha ukweli kwa yule mtoto aliempotezea kumbukumbu na kumdanganya kuwa yeye ndio baba yake?" Dokta Innocent Malle aliongea,



    "mzee, huyo mtoto mwenyewe ndio mimi" Vin aliongea akitegemea Dokta atashtuka,



    "mbona ulishajitambulisha mapema, vijana mnapenda sana kurudiarudia mambo na ndio maana mnadumaa kiakili, kisa cha mimi kukupa hii habari yote ni baada ya wewe kusema kuwa Inasemekana ulifutwa kumbukumbu zako ukiwa mdogo, yaani hapo tu ulikuwa umeshajitambulisha, na ndio maana na mimi nikaongea yote ninayofahamu kuhusu hilo tukio" Dokta Innocent Malle aliongea huku akitabasamu,



    "kwa hiyo hapo point kubwa ni kwamba mimi sio mtoto wa Taita?" Vin aliuliza,



    "hapana, hapo point kubwa ni kwamba ulifutwa kumbukumbu zako wakati ukiwa mtoto, Sasa hilo suala la wewe kuwa sio mtoto wa Taita, hicho ni kijipengele kilichopatikana kwenye maelezo ya point kubwa" Dokta Innocent Malle alijibu huku akitabasamu,



    "labda una chochote cha nyongeza?" Vin alimuuliza Dokta Innocent Malle,



    "Mimi ndio nilipaswa kukuuliza wewe hilo swali, kwa maana wewe ulikuja kuuliza na mimi kazi yangu ni kujibu" Dokta Innocent Malle aliongea na kumfanya Strategic atabasamu kwa namna mzee huyu alivyokuwa anajibu,



    "je ulisikia jina langu la hawali kabla sijafutwa kumbukumbu?" Vin aliuliza huku akiamini huyo mzee hawezi kujibu hilo swali,



    "Sebastian Isack, hilo ndilo jina lako nililiandika kwenye daftari la vipimo" Dokta Innocent Malle alijibu na kumfanya Vin atoe macho,



    "kwa hiyo mimi na Sarah Isack ni ndugu!? Mbona vipimo Vinapinga?" Vin aliuliza,



    "hilo suala sijui, cha muhimu nenda kamuulize Taita, anaweza kukusaidia zaidi, au yule kijana wake mweupe mwenye michoro mwilini" Dokta Innocent Malle alijibu,



    "au mzee nikamchukue Sarah uje utupime?" Vin aliuliza,



    "hapa ni nyumbani na sio hospitali, alafu mimi ni daktari mstaafu, sio daktari tena" Dokta Innocent Malle alijibu huku akitabasamu,



    "nisaidie tu" Vin aliongea,



    " wewe unaamini Sarah ni ndugu yako?" Dokta Innocent Malle aliuliza huku akiinuka kwenye kiti,



    "si mpaka vipimo vioneshe hivyo" Vin alijibu,



    "Sarah sio ndugu yako kijana, jamani muda wangu wa maongezi umeisha, ngoja niende kupumzika kidogo" Dokta Innocent Malle aliongea huku akiondoka na Kijana wake akimfuata kwa nyuma, wakati huo Vin akiwa ameduwaa tu baada ya kuambiwa kuwa Sarah sio ndugu yake,



    "utata unaendelea, mzee ameianzisha mwanzo taharifa ya habari" Strategic aliongea huku akipiga mihayo.......





    "kumbe mzee unalijua hilo suala, kwanini hukuniambia mapema sasa?" Vin aliuliza wakati mzee akiondoka,



    "Mimi sijui chochote, ila si umesema majibu ya vipimo yanasema Sarah sio ndugu yako? Basi labda huenda ni kweli Sarah sio ndugu yako" Dokta Innocent Malle aliongea na kuondoka zake na kumfanya Strategic atabasamu,



    "mzee kala chumvi za kutosha, ndio maana anatuvuruga" Strategic aliongea huku akiinuka kwenye kiti,



    "ndio tunaondoka au?" Vin aliuliza huku akimuangalia Strategic,



    "si ndio, au tunakaa tunasubiri nini wakati mzee ndio ameshamaliza hivyo" Strategic aliongea huku akielekea kwenye geti la kutokea nje na kumfanya Vin amfuate bila kuongeza neno.



    Waliondoka mpaka kwenye gari na kuingia, strategic akawasha gari na kuliondoa kwa mwendo wa wastani,



    "nadhani umeshajua kuwa Taita sio baba yako, unafanyaje sasa baada ya hapo?" Strategic aliuliza,



    "unadhani nitafanya sasa, mimi nafahamu Taita ni baba yangu, hata kama sio baba yangu wa damu, kwa namna alivyonilea tu, naamini yeye ni baba yangu" Vin aliongea huku akitazama chini,



    "ila katika maelezo ya yule mzee, amesema pia Taita ndio aliwaua wazazi wako, wewe hilo umelichukuliaje?" Strategic aliuliza,



    "sio jambo zuri, ila wazazi wangu siwajui na sijajua upendo wao ulikuwa vipi kwangu, ila kwa namna Taita anavyopenda, naamini inatosha kabisa kuamini hakuna mtu muhimu kwangu kama huyu" Vin aliongea kwa utulivu,



    "Sarah anataka kumuua Taita, utamzuiaje wakati umeshajua Sarah ni dada yako?" Strategic aliuliza,



    "Sarah sio dada yangu kwa maana hakuna vipimo vilivyothibisha hilo, na kama kweli lengo lake ni kumuua baba yangu, basi ni lazima yeye afe kwanza" Vin aliongea huku macho yake yakiwa mbele,



    "aisee upo kwenye mtihani mzito sana" Strategic aliongea kwa huruma,



    "mapito tu haya" Vin alijibu na kulalia kiti cha gari.



    *******************



    Siku ya leo, Sajenti Minja aliamua aende moja kwa moja kwa Taita, alitaka kumuuliza kuhusu kutekwa kwake kwa maana yeye Sajenti Minja ndiye aliyepewa jukumu la kuifuatilia ile kesi, na kitu cha pili alichokuwa anaenda kukiuliza ni kuhusu kifo cha Harry, kwa sababu Harry alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya Taita.



    Sajenti Minja alifika nyumbani kwa Taita na kushangaa kwa namna nyumba ilivyokuwa kubwa.



    Sajenti Minja akaenda getini na kumkuta mlinzi, akamsalimu na kujitambulisha huku akimuonesha mlinzi kitambulisho chake, mlinzi akaongozana na Sajenti Minja mpaka sebuleni kwa Taita na kumkuta akiwa amekaa anasoma gazeti. Sajenti Minja akamsalimu na kujitambulisha, akakaribishwa kwenye kochi.



    "naona hali yako imeimarika mzee, mara ya mwisho kukuona ulikuwa chumba cha watu mahututi" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,



    "namshukuru Mungu, amenipigania sana" Taita aliongea huku akielekea kwenye friji na kurudi na chupa ya juisi, akampatia Sajenti Minja,



    "nashukuru, je unakumbuka ni kipi kilikutokea kabla hujapoteza fahamu?" Sajenti Minja aliuliza,



    "nakumbuka machache tu, nakumbuka nilitekwa na watu ambao siwajui, ila hawakutaka kunifanya chochote, walinipiga tu nikapoteza fahamu, zaidi ya hapo sikumbuki kitu" Taita aliongea, ila ulikuwa uongo mtupu,



    "na baada ya kutoka hospitali hao watu hawajakusumbua tena?" Sajenti Minja aliuliza,



    "hapana, sijui kwa baadae" Taita alijibu,



    "Harry alikuwa mfanyakazi wako, je kifo chake familia yake sio muendelezo wa tukio lako? Jibu unavyohisi wewe" Sajenti Minja aliongea,



    "siwezi kujua kwa maana walioniteka mimi hawakuniambia chochote wanachohitaji, kwa hiyo inakuwa ngumu kuhisi kitu" Taita alijibu,



    "unamfahamu Sarah?" Sajenti Minja aliuliza na kipindi hicho Vin alikuwa anaingia,



    "simfahamu" Taita alijibu na kumfanya Vin ashangae kidogo,



    "ni nani? Kwa nini uniulize kuhusu yeye?" Taita alimuuliza Sajenti Minja,



    "ni mwanamke ambaye anafanya uharifu mwingi hapa mjini, nilitaka kujua kama unamfahamu" Sajenti Minja aliongea huku akishangaa kwanini Taita anadai hamjui Sarah wakati ni mtoto wa dada yake,



    "wewe ni polisi?" Vin alimuuliza Sajenti Minja,



    "ndio" Sajenti Minja alijibu,



    "sasa kwanini unataka kumuhusisha huyo Sarah na baba yangu?" Vin aliuliza,



    "sikutaka kumuhusisha, niliuliza tu kama anamfahamu" Sajenti Minja alijibu na kipindi hicho Trigger alikuwa anaingia, Sajenti Minja alipomuona Trigger alishtuka kidogo,



    "ni mwanaume mweupe mwenye michoro mwilini, ana kipara na mkononi ana mchoro wa bastola" Sauti hiyo ya mdada wa mapokezi wa hospitali ilimrudia Sajenti Minja kichwani, Sajenti Minja akamtupia jicho Trigger ambaye alikuwa anakaa kwenye kochi pembeni ya Taita,



    "kwema hapa?" Trigger alisalimia baada ya kukaa,



    "kwema" Sajenti Minja alijibu huku akiweka simu yake vizuri ili ampige picha Trigger bila mtu kujua, kitu kingine alikuwa anamuangalia mikononi ili aweze kuuona mchoro wa bastola, ila hakufanikiwa kwa maana Trigger alivaa shati la mikono mirefu.



    "mzee nadhani nimemaliza, nitarudi siku nyingine" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka na tayari alikuwa ameshafanikisha kumpiga picha Trigger,



    "sawa, unaitwa nani?" Taita aliuliza,



    "Joel Minja, ila ukinitafuta kwa jina la Sajenti Minja ndio utanipata kwa haraka" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,



    "karibu tena" Taita aliongea na kisha Sajenti Minja akaondoka zake huku akiwa na lengo la kwenda hospitali kumuonesha Daktari picha ya Trigger ili amthibitishie kuwa aliyempiga risasi ndio huyo au sio?



    "anataka nini huyu?'' Trigger aliuliza baada ya Sajenti Minja kuondoka,



    "unamfahamu?" Taita alimuuliza,



    "hapana" Trigger alijibu,



    "ni askari, anamfuatilia tukio langu la kuokotwa nikiwa sina fahamu" Taita alijibu,



    "anajua chochote?" Trigger aliuliza,



    "hamna anachojua" Taita alijibu na kumfanya Trigger atabasamu.



    *****************



    Sarah baada ya kumtoroka Sajenti Minja katika siku iliyopita, hii siku ya leo aliamka na wazo tofauti kabisa, alipanga aende hospitali ambayo Vin alifanyia vipimo vya DNA, alitaka kwenda kuchunguza ni vipi majibu ya vipimo yawe tofauti.



    Sarah hakuwa na gari kutokana na gari yake moja ile Range Rover nyeusi kuiacha kwenye nyumba yake ya zamani na hakutaka kutembea nayo tena kutokana na polisi kuikariri, na gari yake ya pili ndio ile aliyoiacha kwenye nyumba nyumba yake nyingine baada ya kumkimbia Sajenti Minja.



    Sarah alitoka nyumbani kwake taratibu mpaka barabarani na kuchukua bajaj iliyompeleka moja kwa moja katika hospitali ambayo Vin alifanyia vipimo vya DNA.



    Sarah akamlipa dereva bajaj na kisha akatelemka na kuelekea moja kwa moja ndani ya jengo la hospitali, aliingia ndani na kuwakuta wadada wawili wakiwa eneo la mapokezi,



    "karibu" Mdada mmoja muongeaji sana anayeitwa Anita alimkaribisha Sarah,



    "asante, nimekuja kufanyiwa vipimo" Sarah aliongea huku akijitahidi kutabasamu,



    "andika jina lako hapo, kisha nenda chumba kile kuonana na Daktari" Anita aliongea huku akimpatia Sarah daftari aandike jina lake, Sarah akachukua daftari na kuandika jina, kisha akaelekea katika chumba cha daktari.



    "huyu mdada yupo kama mzungu, zile sijui ni nywele zake au amevaa wigi!?" Anita Aliongea wakati Sarah akiingia chumba cha daktari,



    "na wewe nae umizidi ufukunyuku, kila mtu akipita lazima umtete kidogo" Lydia shoga yake ambaye uwa pamoja eneo hilo aliongea,



    "kwa hiyo nakukera?" Anita aliuliza huku akimtazama lydia,



    "ndio, wewe inaelekea hata mimi nikikupa mgongo tu unanisema" Lydia aliongea huku akijinyoosha,



    "eeh!! Yamekuwa hayo tena shoga? Basi nitafunga mdomo" Anita aliongea huku akicheka,



    "we endelea tu, kuna vingine vya kurithi, wenzio wanarithi mali wewe unarithi umbea" Lydia aliongea huku akiondoka na pia akicheka,



    "unaenda wapi sasa?" Anita alimuuliza mwenzake,



    "chooni" Lydia alijibu,



    "sawa" Anita alijibu kisha akatoa kioo kwenye pochi yake na kujitazama usoni.



    Sarah alielekea moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha daktari na kumkuta mtu mama mzima akiwa amekaa, Sarah akamsalimu,



    "haya dada sema una shida gani?" Daktari ambaye ndiye huyo mama mtu mzima, alimuuliza Sarah,



    "nimekuja kupima ujauzito na typhoid" Sarah aliongea na kumfanya daktari atabasamu,



    "unahisi dalili gani mpaka uje upime ujauzito?" Daktari aliuliza,



    "kichefu chafu tu, alafu nachagua sana chakula" Sarah aliongea huku akiangalia mazingira ya kule ndani,



    "jina lako?" Daktari aliuliza huku akiwa ameshikilia karatasi mkononi,



    "Sarah isack" Sarah alijibu na kisha daktari akawa anaandika andika katika karatasi,

    .



    "itabidi upime na maralia, kwa maana hizo dalili ulizosema pia ni dalili za maralia" Daktari aliongea huku akiendelea kuandika,



    "eti eeeh?" Sarah aliongea huku akimuangalia daktari,



    "Shika hii karatasi, pita nayo mpaka mlango wa mwisho kushoto, utaingia humo kuchukuliwa vipimo" Daktari aliongea huku akimpatia Sarah karatasi, Sarah akatoka nje huku akiendelea kuchunguza ni mtu yupi anaweza kumdadisi na akampa taharifa nzuri juu ofisi ya daktari aliyepigwa risasi, kwa maana Sarah alipanga kuivamia hiyo ofisi na kuifanyia upekuzi, hakujua kama huyo daktari bado yupo hai.



    Sarah akaingia katika chumba cha vipimo na kumkuta dada mmoja, wakasalimiana kisha Sarah amampatia yule dada ile karatasi aliyotoka nayo kwa Daktari, yule dada akaichukua na kuisoma, kisha akaanza kumchukua Sarah vipimo kulingana na maelekezo ya karatasi aliyoisoma, baada ya vipimo vyote kukamilika, yule dada alimruhusu Sarah aondoke,



    "samahani, baada ya muda gani nifuate majibu?" Sarah alimuuliza yule dada,



    "nusu saa tu" yule dada alijibu na kisha Sarah akatoka eneo lile, akaamua arudi kukaa eneo la mapokezi huku akiwa ameshafanya upelelezi wake wa kutosha juu ya ile hospitali na kugundua kuwa haina ulinzi wa kutosha na pia hata camera za kunakiri matukio yanayoendelea hospital hapo, hakuna.



    Sarah alijivuta na kukaa kwenye viti vilovyokuwa hapo eneo la mapokezi, kulikuwa na runinga iliyokuwa ikionesha mambo mbalimbali yanayotokea duniani.



    "Dada hizo ni nywele zako au umeshonea?" Anita aliuliza na kufanya Sarah ageuke na kutabasamu,



    "ni zangu" Sarah alijibu huku akitabasamu,



    "una nywele nzuri kweli, mpaka nimezitamani" Anita aliongea huku akitabasamu,



    "ni matunzo tu" Sarah alijibu na kukaa kimya.



    "nasikia eti mlivamiwa na majambazi siku za karibuni?" Sarah aliuliza huku akawageukia wale wadada wa mapokezi,



    "tulivamiwa na mtu tu, sio Jambazi, alivamia chumba cha daktari na kumpiga risasi" Anita alijibu,



    "khaa jamani, watu wana roho ngumu, kwa hiyo alivyompiga akamuua?" Sarah aliuliza huku akionesha kuogopeshwa na hilo tukio,



    "bahati nzuri daktari hajafa, yupo hai" Anita alijibu na kumfanya Sarah ashtuke, hakutegemea kukutana na hiyo habari,



    "aah bora, amepelekwa nje ya nchi kwa matibabu?" Sarah aliuliza,



    "yupo hapa hapa hospitali, amelazwa" Anita alijibu,



    "na wewe sio unajibu kila swali unaloulizwa, wengine wanaweza kuwa ndio wale wale majambazi wanataka kuja kummalizia" Lydia aliongea kwa sauti ndogo ambayo haikumfikia Sarah, ila aligundua kuna kitu huyo dada anamuonya mwenzake.



    "na wewe hujui hata kuhisi watu, huyu dada alivyo hivi anawezaje kuwa Jambazi, kwanza mzuri hadi raha" Anita alimjibu Lydia kisha akamgeukia Sarah na kutabasamu,



    "mnatakiwa muweke ulinzi wa kutosha, ipo siku wanaweza kuvamia tena na wakaleta madhara makubwa zaidi" Sarah aliongea kwa utulivu,



    "sijui bwana uongozi wenyewe, nadhani wanashughulikia hilo suala" Anita alijibu na kisha ukimya ukatawala. Kipindi chote hicho cha ukimya Sarah alikuwa anafuraha ya kusikia kuwa daktari hajafa na pia alikuwa anataka kujua ni wodi ipi daktari amelazwa ili baadae aje kuongea nae vizuri,



    "kuliko kuja baadae kuleta kashkash hapa, ni bora tu nimjulishe Vin kuwa daktari ni mzima" Sarah alijiwazia moyoni kwake na kipindi hicho alitakiwa aende kwa daktari kuchukua majibu yake,



    "muda unakimbia, yaani nusu saa imeshafika?" Sarah aliongea huku akitabasamu baada ya kuitwa jina na kutakiwa kuingia chumba cha daktari kufuata majibu.



    Baada ya dakika kumi Sarah alitoka kwenye chumba cha Daktari na kuelekezwa aende nje ya jengo ila ndani ya uzio wa geti, kuna duka la dawa, aonyeshe karatasi aliyopewa na Daktari, amuoneshe muuzaji wa duka la dawa na kisha atapatiwa dawa zake.



    Sarah alifika ndani ya duka na kumuonesha muuzaji karatasi na kupatiwa dawa husika, Sarah akalipia pesa na kisha akawa anaelekea nje kutafuta usafiri wa kumrudisha kwake huku kichwani akiwa na haraka ya kufika nyumbani na kumpigia simu Vin ili amjulishe kuwa yule daktari aliyepigwa risasi, hakufa.



    Wakati Sarah akiwa na haraka zake na kipindi hicho ndicho Sajenti Minja alikuwa ametoka nyumbani kwa Taita huku akija hospitali ili kumuonesha daktari picha ya Trigger ili athibitishe kuwa ndiye mtu aliyempiga risasi.



    Sarah akiwa amesimama nje ya geti akisubiri bajaj, alishangaa mtu akiwa amesimama mbele yake kabisa, tena jirani na bastola ikiwa mkononi mwake usawa wa kifua cha Sarah,



    "za mwizi arobaini" alikuwa ni Sajenti Minja, aliongea kwa sauti ya dharau na kumfanya Sarah apigwe na butwaa, hakutegemea kama anaweza kufanyiwa shambulio la ghafla namna ile,



    "nyoosha mikono mbele" Sajenti Minja aliongea kwa amri na Sarah akatii, hakuwa na ujanja tena. Sarah akanyoosha mikono yake mbele back kisha Sajenti Minja akamfunga pingu, akamkamata mkono mpaka kwenye gari la Sajenti Minja ambalo lilikuwa ng'ambo ya barabara, akamfungulia mlango na Sarah akaingia kwenye siti ya mbele ya gari, Sajenti Minja akatoa pingu nyingine na kumfunga Sarah miguuni, kisha akatoa kamba kwenye buti na kukifunga kiwiliwili cha Sarah kwenye siti, yaani alimbana haswa, kisha Sajenti Minja akaingia kwenye gari na kumtazama Sarah, Sajenti Minja akacheka,



    "bila kukufunga namna hiyo kama mbuzi kabebwa kwenye pikipiki, unaweza ukanishangaza, kwa maana wewe sio mtu wa kawaida" Sajenti Minja aliongea na kuwasha gari, Sarah alikuwa kabanwa vibaya, hata kujitingisha alikuwa hawezi........









    Sajenti Minja akawasha gari yake na safari ya kwenda kituoni ikaanza, njia nzima hakuna aliyemuongelesha mwenzake, Sarah alikuwa akisali msaada utokee, huku Sajenti Minja alikuwa akishangilia kwa kumkamata muharifu wake kwa urahisi namna ile,



    "hivi wewe uwaga unanitafutia nini?" Sarah alimuuliza Sajenti Minja, alionekana ana hasira,



    "swali gani la kipuuzi hilo unauliza wakati unajua mimi ni polisi na wewe ni muharifu" Sajenti Minja aliongea kwa dharau,



    "itafika kipindi nitaanza na wewe kwa maana umekua kama kikwazo kwangu, nitakuondoa wewe kikwazo ili nifanye kazi yangu kwa uhuru" Sarah aliongea kwa hasira,



    "sasa haya ni maajabu yametokea, kikwazo ndio kimekuzidi uwezo leo" Sajenti Minja aliongea na kucheka,



    "sawa, huu ni mchezo, bado haujaisha, yoyote anaweza kushinda" Sarah aliongea kwa sauti ndogo ila ilimfikia kwa uzuri tu Sajenti Minja,



    "mchezo eeh? Kuua watu ni mchezo?" Sajenti Minja aliongea huku akiegesha gari nje ya kituo,



    "wewe ndio unaona naua, ila wao ndio wanajua ninachokifanya dhidi yao" Sarah alijibu wakati Sajenti Minja akitelemka katika gari,



    "hiyo hainihusu, mimi nipo upande wa sheria tu" Sajenti Minja aliongea huku akifungua mlango wa upande wa Sarah, kisha akamfungua kamba na kisha akamfungua pingu zote, za mikononi na miguuni.



    "Sidhani kama utaleta usumbufu eneo hili, mimi sio mkofofi, ila nikichokozwa uwa sio mtu mzuri kabisa" Sajenti Minja alimuonya Sarah mara baada ya kumfungua pingu, kisha akamtelesha na kumshika mkono, wakawa wanaelekea ndani ya kituo.



    "twende ofisini kwangu, kuna maswali ya kujibu" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amemshika mkono Sarah.



    Wakaelekea moja kwa moja mpaka ofisini kwa Sajenti Minja na Sarah akawekwa kwenye kochi,



    "nina maswali machache tu, Taita ni nani yako?" Sajenti Minja aliuliza,



    "mjomba angu" Sarah alijibu,



    "mbona yeye anadai hakujui?" Sajenti Minja na Sarah akacheka,



    "inaweza kuwa sawa, kwani hajawahi kuona ndugu hawajuani?! " Sarah alihoji,



    " kwanini ulimuua Harry?" Sajenti Minja aliuliza,



    "Mimi? Ooh sawa ndio ni mimi niliyemuua, ila alitaka mwenyewe kufa" Sarah alijibu huku akitabasamu,



    "alitaka mwenyewe kufa? alitakaje kufa?" Sajenti Minja aliuliza,



    "aliyesema amechoka kuishi, hana furaha kwa maana familia yake imeuawa yote" Sarah alijibu,



    "na mahakamani ukisema huo ushenzi unaweza kupona?" Sajenti Minja aliuliza huku akimshangaa Sarah,



    "mahakamani? Sidhani kama naweza kufikishwa mahakamani kwa kitendo hicho" Sarah alijibu kwa kujiamini,



    "kwanini uliiua familia ya Harry?" Sajenti Minja aliuliza,



    "na wewe upo kama mpuuzi, nitaiuaje familia isiyo na hatia? Najua ni uchungu kiasi gani mtu anaupata anapopoteza familia, nisingeweza kuiua familia Harry" Sarah alijibu,



    "sasa kama unajua ni uchungu kupoteza watu muhimu maishani, kwanini ulimuua Harry?" Sajenti Minja aliuliza,



    "nilimuua baada ya familia yake kufa, hakuwa na furaha tena, alitaka akaungane na familia yake" Sarah alijibu,



    "umesema wewe hujaua familia ya Harry, ni nani ameiua familia ya Harry?" Sajenti Minja aliuliza,



    "Taita, Taita na vibaraka wake" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti afikirie kidogo, kisha akaitoa simu yake na kubonyeza bonyeza,



    "unamjua huyu?" Sajenti aliuliza huku akimuonesha picha ya Trigger,



    "Trigger, huyu ndio kiongozi wa mauaji yanayotokea chini ya Taita" Sarah alijibu,.



    "unajua kuwa huyu ndiye aliyefanya shambulio la kumuua daktari pale hospitali ulipotoka?" Sajenti Minja aliuliza,



    "sijui" Sarah alijibu baada ya kuhisi hilo swali ni la mtego,



    "Alafu na yule kijana mwingine anayependa kuvaa suti, ni nani kwa Taita?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kumkumbuka Vin na maneno aliyowahi kuambiwa na mlinzi wa Harry kuwa kabla familia ya Harry haijaangamia, mtu wa mwisho kuingia alikuwa ni Trigger na huyo kijana mmoja anapenda kuvaa suti,



    "yule anaitwa Vin, hata ile Vin hotel inatokana na jina lake" Sarah alijibu,



    "ndiye mtoto wa Taita?" Sajenti Minja aliuliza,



    "hapana, yule ni mdogo wangu" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja amtolee macho,



    "mdogo wako? Au mdogo wako kwa kuwa Taita ni mjomba wako?" Sajenti Minja aliuliza na kumfanya Sarah atabasamu,



    "mdogo wangu kwa maana ya kuchangia baba na mama" Sarah alijibu na sasa ikawa zamu ya Sajenti Minja kucheka,



    "kivipi?" Sajenti Minja akauliza,



    "kivipi, vipi? Hujaelewa nilichokueleza?" Sarah akauliza huku akimshangaa Sajenti Minja,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "iweje Vin awe ndugu yako alafu awe anakaa vyema na Taita, ingali wewe hauishi vyema na Taita?" Sajenti Minja aliuliza,



    "yupo gizani yule, na siku akipata mwanga, hakutakuwa na wa kumzuia" Sarah alijibu na kumfanya Sajenti Minja abaki ndani ya Fumbo,



    "nitakuuliza swali la mwisho, je ugomvi wako wewe na Taita ulitokana na kifo cha wazazi wako?" Sajenti Minja aliuliza,



    "liweke vizuri swali lako hili jibu liwe jepesi, kwa maana wakati wazazi wangu wakifa nilikuwa na miaka sita tu, nisingeweza kugombana na mtu mzima" Sarah alijibu,



    "Taita baada ya kuiangamiza familia yako ndipo ulipomchukia?" Sajenti Minja alimuuliza Sarah,



    "hilo sio swali, ni jibu" Sarah alijibu,



    "na mwisho wa yote ni nini?" Sajenti Minja alimuuliza,



    "mwisho ni chini, ama yeye ama mimi" Sarah aliongea huku hasira zikionekana wazi machoni mwake,



    "mwisho ni jela, tena kabla vifo havijatokea zaidi, ni lazima ufungwe sasa, ni lazima ushtakiwe Sarah" Sajenti Minja aliongea kwa sauti tulivu,



    "hilo halitotokea, mkae mkijua kwamba mimi sishikiki, mimi ni moto. Kama mlishindwa kumkamata Taita na mlijua ana tuhuma, basi msitegemee kunishka mimi, hakuna atayebaki salama" Sarah aliongea kwa hasira na kumfanya Sajenti Minja acheke,



    "we mpuuzi kweli, yaani upo mikononi mwa polisi alafu unaleta jeuri?" Sajenti Minja aliuliza huku akicheka,



    "labda mniweke ndani ya chupa, tena chupa ya chuma" Sarah aliongea huku bado akiwa na hasira, na kipindi hicho mlango wa ofisi ya Sajenti Minja ulikuwa unagongwa,



    "ingia" Sajenti Minja alijibu hodi na kutupia macho mlangoni, aliingia mwanamke aliyevaa kofia ya cap, alipoingia alifunga mlango kwa ndani, wakati Sajenti Minja akishangaa tukio hilo, yule dada aligeuka na mkononi alikuwa na bastola, kisha akaiondoa ile kofia kichwani na kubaki uso wazi, alikuwa ni Aisha,



    "afande tulia hivyo hivyo, ukijitingisha sikuachi, si unakumbuka nilichomfanya mwenzako mara ya mwisho ndani ya ofisi hii?" Aisha aliuliza huku akitabasamu na kumfanya Sajenti Minja atulie kama gogo, alikumbuka tukio la Aisha alilowahi kulifanya hapo,



    "na wewe unazubaa nini? Nyanyuka na umfunge huyo afande" Aisha aliongea huku akimtazama Sarah, Sarah hakuupenda ule msaada wa Aisha, aliamini unamuongezea matatizo tu, ila kwa muda huo hakuwa na la kufanya, alitaka kuwa huru.



    Sarah aliinuka na kwenda kumfunga pingu Sajenti Minja, kisha Aisha akatoa bomu na kuchomoa pin na kumuwekea lile bomu mdomoni mwa Sajenti Minja, kisha akamfunga na plasta ngumu,



    "sasa bomu la nini, usimuue bwana" Sarah aliongea kwa ukali huku akimtazama Aisha,



    " twende, hii kwa ajili ya usalama wetu" Aisha aliongea huku akifungua mlango kisha wakatoka taratibu huku Aisha akiwaaga polisi wengine kwa furaha zaidi na kumfanya Sarah ashangae huku akijiuliza hilo tukio Aisha alipanga kulifanya kwa kushirikiana na askari wengine au?



    Aisha aliongoza nje kwenye gari moja dogo jeusi na kuingia, kisha Sarah nae akaingia upande wa pili,



    "kwanini sasa umemuwekea bomu?" Sarah aliuliza huku akimuangalia Aisha,



    "ni bomu ndio, ila haliwezi kulipuka kwa kuwa nilishaliharibu, na bila kumfanyia hivyo huenda angepiga kelele baada ya sisi kutoka" Aisha aliongea na kumfanya Sarah ashushe pumzi,



    "ulijuaje nipo hapa?" Sarah alimuuliza Aisha,



    "nilishajitolea kukusaidia, popote uendapo nipo nyuma yako" Aisha aliongea,



    "lakini kumbuka kuwa huu msaada unaonipa unazidi kuniharibia tu, kwa maana hapo umeniongezea kosa polisi, nimeonekana nimemtoroka askari" Sarah aliongea,



    "nataka uwe huru ukamilishe kisasi chako" Aisha aliongea,



    "na mbona wakati tunatoka polisi ulikuwa ukiagana vizuri na askari?" Sarah alimuuliza Aisha,



    "wakati naingia nilijitambulisha ni mpenzi wa Sajenti Minja na niliongea nao kwa ucheshi kabla hawajanielekeza ilipo ofisi ya Minja" Aisha aliongea,



    "nishushe hapa" Sarah aliongea na kisha Aisha akasimamisha gari na Sarah akashuka,



    "nashukuru, ila nakupa onyo tena, sihitaji msaada kutoka kwako, vinginevyo na wewe utakuwa katika hatari" Sarah aliongea ila Aisha hakujibu kitu, aliondoa gari huku akiongeza sauti ya radio,



    "kama ungekuwa hutaki msaada si ungeendelea kubaki polisi, kwanini ulikubali kuondoka na mimi" Aisha aliongea peke yake huku akitabasamu.



    Sarah baada ya kuachia na Aisha, alichokifikiria kwa muda huo ni kumpigia simu Vin na kumpa taharifa juu ya daktari aliyepigwa risasi kuwa hajafa. Sarah akaitoa simu mfukoni na kuitafuta namba ya Vin na kupiga.



    *******************



    Sajenti Minja hakuwa katika hali nzuri, mikono yake ilifungwa pingu iliyoambatanishwa na kiti na mdomoni alikuwa na bomu lilipachikwa na juu ya Bomu kulikuwa na plasta ngumu iliyolizuia bomu lisitoke mdomoni kwa Sajenti Minja. Sajenti Minja hakuweza kutoa hata sauti, muda wote alikuwa kimya huku akimuomba Mungu amletee msaada na pia miale ya machozi ilikuwa ikimchomoza machoni.



    Baada ya kukaa muda mrefu bila kupata msaada, Sajenti Minja aliinuka na kiti na kwenda mpaka mlangoni, kwa kuwa mlango ukifunguliwa unafungukia kwa ndani, hiyo ikawa shida shida nyingine, hakuweza kuuvuta mlango, ikabidi augonge mlango kwa kutumia kiti. Baada ya kuugonga kwa muda kidogo, wenzake wa nje walisikia, mmoja wao akaenda na kuusukuma mlango, akamkuta Sajenti Minja akiwa amefungwa kila sehemu, yule askari akakimbilia moja kwa moja kubandua plasta ya mdomoni, Sajenti Minja akakwepesha mdomo na kumuonesha kwa ishara kuwa amfungue pingu, yule askari akafungua pingu Sajenti Minja, kisha Sajenti Minja akaibandua plasta taratibu na kisha akalitoa bomu mdomoni na kutoka nalo nje kwa lengo la kwenda kulitupa baharini, ofisi yao na bahari vilikuwa jirani, baada ya yule askari mwingi kugundua Sajenti Minja amemshika bomu, ikabidi nae aanze kukimbia kutoka nje na wakati huo Sajenti Minja nae alikuwa anaanza kukimbia, tatizo mlango ulikuwa mdogo, wote wakakutaniana mlangoni na kudondoka chini, bomu likamponyoka Sajenti Minja, wakilalamika chini huku wote wakipiga kelele wakijua mwisho wao umefika, lakini wakashangaa bomu halilipuki, mwenzake akanyanyuka bila kuangalia mbele, alitaka akimbie akajikuta akilikanyaga lile bomu, akaanguka tena chini ila bomu halikulipuka, liliseleleka mpaka jirani kwa Sajenti Minja, Sajenti akalitupia jicho na kuona lile bomu lina uwazi mkubwa kwa juu, akashangaa, maana hakuna bomu la namna ile duniani, Sajenti Minja akaliokota na kuliangalia kwa karibu, akagundua ndani ya lile bomu kuna karatasi, akazitoa zote na kuziweka pembeni, bomu halikuwa na kitu, lilikuwa "empty"



    Sajenti Minja akajicheka mwenyewe huku akimuangalia mwenzake ambaye alikuwa ameshapoteza fahamu muda mrefu tu mara baada ya kukanyaga bomu.



    "hawa wanawake wapumbavu sana" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu, kisha akakumbuka kitu,



    "Sarah alivyotoka hospitali alifuata nini?" Sajenti Minja alijiuliza kisha kwa haraka sana akawa anatoka nje, alipanga kwenda hospitali,



    "nendeni mkamtoe mwenzenu ofisini kwangu, mlazeni nje chini ya miti" Sajenti Minja aliwaambia askari wawili waliokuwa wamesimama wakipiga soga, kisha Sajenti Minja akaenda kwenye gari yake.......................

    .



    **, ***7****



    Vin, Taita na Trigger wakiwa sebuleni wanaongea, simu ya Vin iliita, ilikuwa karibu na Trigger, Trigger akaiokota na kumpa Vin, ila Trigger alibahatika kuona jina la mpigaji, alikuwa ni Sarah,



    "vipi?'" Vin aliongea baada ya kupokea simu,



    "yule daktari aliyekupima hajafa, nilienda hospitali kufanya uchunguzi" Sarah aliongea na kumfanya Vin ashtuke,



    "Daktari hajafa? Yupo wapi?" Vin aliuliza,



    "amelazwa pale pale" Sarah alijibu,



    'pale pale?, poa ngoja niende" Vin aliongea na kukata simu, kisha akatoka kwa haraka bila kuaga mtu na kufanya Taita amtupie jicho Trigger,



    "alikuwa anaongea na Sarah, nimeona jina kwenye kioo" Trigger aliongea,



    "Daktari gani ambaye wanamzungumzia?" Taita aliuliza,



    "hata mi sijui" Trigger alijibu



    "wewe, sio yule uliyempiga risasi juzi ukaondoka na majibu?

    " Taita aliuliza kwa mshangao na kumgutusha Trigger,



    "ila hata Vin akienda haitomsaidia, majibu si ameyaona na hayaoneshi undugu walionao" Trigger aliongea,



    Usiwe mjinga wewe, je huyo daktari akihojiwa na akikutaja wewe kwa Vin, ni picha gani Vin atapata?" Taita aliuliza kwa hasira,



    "kwa hiyo?" Trigger aliuliza,



    "nenda kammalize muda huu kabla hawajaongea chochote na Vin" Taita aliongea,



    "Ila kweli eeh?" Trigger aliuliza na kunyanyuka kwa haraka, nae akatoka ndani kwa kasi kuwahi gari ili aende hospitali na kufika kwa haraka kabla ya Vin.



    ***, **************



    Alitangulia Trigger kufika mapema hospitali, haikuingia ndani, akawa anazunguka nje ya jengo huku akitumia madirisha kumtafuta daktari anayemtaka na mkononi akiwa na bastola.



    Vin alifika hospitali na kwenda mapokezi, akajitambulisha na kisha akauliza kama ni kweli Dokta yupo hai, akajibiwa ndio, akaomba kuongea nae kidogo, wadada wa mapokezi wakaenda kumpa ombi la Vin yule daktari, Daktari akakubali kwa maana aliona huo ndio muda muafaka wa kumpatia Vin majibu ya kweli.



    Vin akaingia mpaka katika wodi aliyolazwa daktari na kumkuta akiwa amekaa, Daktari alipomuona Vin alifurahi sana, wakasalimiana,



    "bora umekuja, maana nilikuwa naweza nitakupataje?" Daktari aliongea,



    "nilikuja hata siku ile ulipopigwa risasi, nikakukuta haupo kwenye hali nzuri, pole sana" Vin aliongea kwa furaha,



    "sasa kijana kuna mtu alifuata majibu yako, nikampatia kwa sababu alikuja kishari, ila majibu ambayo yamethibitishwa kitabibu yapo" Daktari aliongea na kumfanya Vin atoe macho,



    "yapo wapi daktari?" Vin aliuliza huku akitabasamu, ila wakati daktari anataka kujibu alisita na macho akayatupia dirishani ambapo Vin aliupa mgongo upande huo wa dirisha, Vin ikambidi atake kugeuka ili aone daktari anachotaka kusema, ila kabla hajageuka alisikia mlio wa risasi na kushuhudia mwili wa Daktari ukiwa umejaa damu na ilionesha amekufa, Vin akatoa bastola yake na kugeuka upande wa dirishani kwa kasi, akamshuhudia Trigger akiipachika bastola yake kiunoni kisha akatabasamu na kutoka akikimbia. Vin akapigwa na butwaa huku bastola yake ikiwa mkononi, akaona bora atoke nje ajaribu kumfukuzia Trigger, ila Vin hata kabla hajainua mguu, mlango wa wodi ulifunguliwa na Sajenti Minja akiwa mkononi na bastola na nyuma yake walikuwa wafanyakazi wa ile hospitali,



    "weka bastola chini, nyanyua mikono juu" Sajenti Minja aliongea kwa amri huku bastola yake akiwa ameelekeza usawa wa kichwa cha Vin...... Vin akanyong'onyea akatupa bastola chini, hakuwa na ujanja kwa maana alikamatwa akiwa na ushahidi wa bastola mkononi.....





    "weka silaha chini" Sajenti Minja aliongea kwa ukali huku akimuangalia Vin, Vin akaweka silaha chini huku akitabasamu, maana alikamatwa na ushahidi kabisa.



    "ongoza mbele" Sajenti Minja aliongea kwa amri na kufanya Vin aanze kupiga hatua huku akiwa bado anatabasamu, tabasamu la mshangao kutokana na tukio lililotokea ghafla. Wakati Vin akitaka kuanza kupiga hatua, Daktari Aliyepigwa risasi alimshika mkono,



    "kumbe hajafa?" Vin aliuliza kwa mshangao huku akimuangalia,



    "majibu ya vipimo vyako yapo ndani ya ofisi yangu" Daktari aliongea kwa tabu huku akiwa anatoka damu puani na mdomoni,



    "Dokta mimi ndiye niliyekupiga risasi?" Vin alimuuliza huku akiwa amemuinamia, Daktari akatingisha kichwa kwa maana ya kukataa, Sajenti Minja akampiga kikumbo Vin na kusogea karibu na Daktari,



    "unamjua huyu?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuonesha picha ya Trigger, Daktari akaitikia kwa kichwa kumaanisha anamjua,



    "huyu ndiye aliyekupiga risasi mwanzo?" Sajenti Minja aliuliza na Daktari alitingisha kichwa na kujibu ndio,



    "ndio huyo huyo amempiga na sasa hivi" Vin aliongea kwa sauti,



    .



    "eti ni kweli?" Sajenti Minja aliuliza na Daktari akakubali kwa kutikisa kichwa na kumfanya Vin ashukuru Mungu kwa kumuepusha na balaa lile,



    "huyo mtu alikuwepo humu?" Sajenti Minja aliuliza tena ila daktari hakujibu tena, mwili ulikakamaa na kisha akatema damu nyingi kwa mkupuo na kukilaza kichwa chake pembeni, kwa maana hiyo daktari alikuwa amekufa,



    "sogeeni tutoe huduma" Dokta mwingine aliwapangua wakina Sajenti Minja na kisha akamsogelea yule daktari aliyekufa na kuanza kusikiliza mapigo yake ya moyo, hakutaka kuamini kirahisi kama mwenzake amekufa.



    "wewe twende" Sajenti Minja aliongea kibabe huku akimvuta Vin,



    "unanipeleka wapi sasa wakati daktari amesema mimi sijampiga risasi?" Vin aliuliza kijeuri,



    "wewe twende, una kesi nyingi za kujibu ukiitoa hii ya kumshambulia daktari kwa risasi" Sajenti Minja aliongea na kumsukuma mbele Vin,



    "sawa, basi ngoja nipewe majibu yangu, si umemsikia daktari amesema yapo ofisini kwake" Vin aliongea huku akimtazama Sajenti Minja,



    "we dada, ebu njoo" Sajenti Minja alimuita dada wa mapokezi,



    "abee" Dada wa mapokezi aliitikia baada ya kufika, alikuwa ni lydia,



    "ingia kwenye ofisi ya yule daktari aliyepigwa risasi, kuna cheti cha mtu nakihitaji, wewe jina nani?" Sajenti Minja aliongea kisha akamgeukia Vin,



    "Vin Denis, kama yatakuwa yapo ndani ya bahasha, basi juu ya bahasha kutakuwa kumeandikwa "DNA TEST, Vin Denis and Sarah isack" Vin aliongea,



    "wewe umejuaje yameandikwa hayo yote, kama sio lenu moja kati yako na yule aliyempiga risasi daktari?" Sajenti Minja aliuliza huku akimuangalia Vin,



    "mara nyingi hospitali nyingi duniani uwa zinatumia mfumo huo" Vin alijibu,



    "wewe kama utayapata majibu au utayakosa uje nje unipe taharifa" Sajenti Minja alimwambia lydia,



    "sawa" lydia alijibu huku akielekea ofisini kwa Dokta mkuu kwenda kumuomba ruhusa ya kuingia kwenye ofisi ya daktari aliyepigwa risasi.



    Sajenti Minja akatoka na Vin mpaka nje na kumpakia kwenye gari, kisha akawa anamsubiria dada wa mapokezi.



    Baada ya dakika kumi na tano dada wa mapokezi aliwafuata na kuwapatia bahasha ya kaki yenye majibu ya vipimo vya Vin, Vin akatabasamu,



    "nipe, ni majibu yangu hayo na wala sio yako" Vin aliongea baada ya kumuona Sajenti Minja akiyapokea na kuyaweka pembeni yake. Sajenti Minja hakutaka kujibu kitu, aliwasha gari na kuiondoa.



    Walifika mpaka kituo cha polisi, na kisha wakashuka wakawa wanaelekea ndani,



    "koplo Rama anaendeleaje?" Sajenti Minja alimuuliza askari aliyekuwepo kaunta, alimuulizia yule askari aliyekanyaga bomu na kupoteza fahamu.



    "imebidi apelekwe hospitali, inaonekana presha inamsumbua" Askari aliyeulizwa alijibu na kumfanya Sajenti Minja aelekee ofisini kwake huku akitabasamu.



    Sajenti Minja aliingia ofisini kwake na kupanga vitu vizuri kutokana na purukushani ya Bomu feki la Aisha, baada ya hapo akakaa kwenye kiti,



    "kuna maswali machache nataka unijibu kwa ufasaha zaidi ili urudi uraiani" Sajenti Minja aliongea huku akimtazama usoni Vin,



    "nitajibu ninavyojua, sasa wewe ndio utajua nimejibu kwa ufasaha au lah!" Vin aliongea huku nae pia akimuangalia usoni Sajenti Minja,



    "sawa, je unaweza kunionesha kibali cha umiliki wa silaha yako?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ninavyo vibali, vipo nyumbani" Vin alijibu,



    "swali la pili, huyu mtu aliyempiga risasi daktari, jana tu nimemkuta upo nae kwenu, wewe na Taita, kwa maana hiyo ni lazima kuna kitu mnakijua juu ya hilo tukio alilolifanya" Sajenti Minja aliongea,



    "nadhani naweza nikawa najua, ila kwa hisia tu" Vin alijibu,



    "nieleze unachokijua" Sajenti Minja aliongea,



    "ni hayo majibu ya hospitali, nadhani hakutaka niyapate hayo majibu ya hospitali kutokana na sababu nisizozijua" Vin aliongea,



    "siku ile kwenye kifo cha familia ya Harry, mlinzi alikuona na wewe ukiingia nyumbani kwa Harry kabla familia ya Harry haijauawa, mimi napenda nikuweke hatihani kutokana na vifo hivyo" Sajenti Minja alimueleza Vin,



    "ni kweli nilionekana, ila sikuua mtu" Vin aliongea,



    "Sarah ni nani yako?" Sajenti Minja huku akimuangalia,



    "Sarah sikuwa namjua wala sikuwahi kumjua, ila inasemekana ni ndugu yangu wa damu" Vin alijibu,



    "kwanini useme humjui, alafu useme inasemekana, kwani hamjawahi kukua pamoja?" Sajenti Minja aliuliza,



    "bado nasema inasemekana kwa maana inadaiwa wakati mdogo nilifutwa kumbukumbu zangu na nikaanza upya" Vin alijibu,



    "hiyo haiwezekani, mtu kufutwa kumbukumbu?" Sajenti Minja alibisha huku akicheka,



    "hata mimi iliniwia vigumu kuelewa hilo jambo, ila nilielewa baadae nilipokutana na Daktari aliyefanya hilo jambo" Vin alimueleza Sajenti Minja,



    "hilo jambo lilifanyika katika hospitali za hapa nchini?" Sajenti Minja aliuliza,



    "ndio, uzuri ni kuwa hata daktari wake bado yupo hai ingawa jambo hilo lilifanyika zamani sana" Vin alijibu



    "mwaka gani?" Sajenti Minja aliuliza,



    "miaka ishirini iliyopita, inasemekana baada ya nyumba yetu kuchomwa moto na wazazi kufariki" Vin alijibu, na kufanya Sajenti Minja aikumbuke ile report iliyofungwa mara baada ya askari aliyekuwa akiifuatilia ila kesi ya nyumba ya baba yake Sarah kuuawa, ile report iliandikwa miili iliyopatikana imeteketea kwa moto ni mitatu, yaani wa baba yake Sarah, mama yake Sarah na mfanyakazi wa ndani, huku mwili wa mtoto wa kike aitwae Sarah ulikutwa nje ya nyumba, na mwili mmoja wa mtoto wa kiume hakuonekana,



    "wewe ni Sebastian?" Sajenti Minja aliuliza,



    "Sarah uwa ananiita hivyo, ila mimi naitwa Vin" Vin alijibu na kumfanya Sajenti Minja achukue ile bahasha yenye majibu ya vipimo vya DNA na kuifungua, kisha akaanza kusoma taratibu, ilimchukua dakika tano kuisoma kisha akamtupia jicho Vin,



    "ulisema daktari aliyekufuta kumbukumbu yupo, anakaa wapi?" Sajenti Minja aliuliza ila safari kwa upole zaidi na kumfanya Vin ashangae, kisha Vin akamuelekeza Sajenti Minja,



    "hivi unajua ugomvi wa Sarah na Taita ni ugomvi wa kisasi baada ya wazazi wa Sarah kuuliwa na Taita?" Sajenti Minja alimuuliza Vin,



    "ndio" Vin alijibu,



    "utafanyaje ukigundua kuwa Taita sio baba yako ila aliwaua wazazi wako?" Sajenti Minja aliuliza,



    "siwezi kufanya kitu, kwa maana siwajui wazazi wangu, Taita ndio mzazi wangu" Vin alijibu,



    "sawa, nenda, ila uje kesho ukiwa na nyaraka za umiliki wa silaha uliyonayo" Sajenti Minja aliongea na kumfanya Vin ajisachi, kisha akatoa kitambulisho na kukitupa juu ya meza ya Sajenti Minja, Sajenti Minja akakiokota na kukiangalia, akashtuka,



    "nitakutafuta nitapokuhitaji"Sajenti Minja aliongea huku akimrudishia kitambulisho,



    "naomba na majibu yangu ya hospitali" Vin aliongea kwa upole kisha Sajenti Minja akaichukua ile bahasha na kumpatia,



    "kafungulie nje, nataka kutoka" Sajenti Minja aliongea baada ya kuona Vin anataka kutoa karatasi iliyopo ndani ya bahasha.



    Vin akatabasamu na kutoka nje huku Sajenti Minja nae akiwa kwa nyuma yake, Sajenti Minja alipanga kuelekea kwa Dokta Innocent Malle muda huo, alikuwa anataka kwenda kumuhoji kutokana na maelezo ya Vin.



    *****************



    Trigger alivyotoka hospitali alirudi nyumbani kwa Taita na kumkuta akiwa sebuleni,



    "umefanikisha?" Taita alimuuliza Trigger,



    "kazi imefanyika, ila Vin yupo hatarini" Trigger aliongea,



    "yupo hatarini kivipi?" Taita aliuliza huku akionekana kushtuka,



    "wakati nampiga daktari risasi, Vin alikuwa katika chumba cha daktari, na isitoshe polisi walikuwa eneo hilo" Trigger alijibu,



    "umekosea sana, je Vin amekuona?" Taita alimuuliza,



    "ameniona ndio" Trigger alijibu,



    "umekosea Trigger, sasa atakufikiriaje?" Taita aliuliza kwa kulalamika,



    "kama kutufikiria vibaya mbona tayari ameshatufikiria vibaya, muda wote wanaongea na Sarah, wanasaliana, unadhani wanaongea nini kama sio kutumaliza, huoni hata Sarah hatusumbuhi siku hizi? itakuwa kuna mipango wanaipanga na ikikamilika watatudhuru" Trigger aliongea,



    "Vin hawezi kunifanyia hivyo" Taita aliongea kwa kujiamini,



    "ulijua ipo siku hatokuamini wewe kama baba yake na akaamua kwenda kupima ili apate ukweli, usimuamini mtoto asiekuwa wako, maana anakugeuka muda wowote" Trigger aliongea na kumfanya Taita afikiri kidogo,



    "basi nitamwambia arudi marekani akaendelee na mambo yake" Taita aliongea,



    "mzee Vin ni wa kuuawa tu, maana ukweli ameshaanza kuujua ukweli kuhusu kifo cha wazazi wake" Trigger aliongea,



    "siwezi kumuua vin" Taita alijibu huku akitabasamu,



    "mzee utakurupuka kukiwa kumekucha, elewa pia jana Vin alikuwa kwa Dokta Malle" Trigger aliongea na kumfanya Taita ashtuke,



    "alienda kufanya nini?" Taita aliuliza kwa hofu,



    "sijui kilichoongelewa, ila wewe unadhani wataongelea nini kama sio habari zile zile za miaka ishirini iliyopita?" Trigger aliuliza,



    "wewe umejuaje Vin alienda kwa Dokta Malle siku iliyopita?" Taita aliuliza,



    "nilimfuatilia jana kwa kila hatua, maana hata Strategic nakosa imani nae" Trigger alijibu,



    "basi nenda kwa Dokta ukamuohoji Vin alifuata nini pale?" Taita alimuagiza Trigger,



    "sawa" Trigger alijibu na kuondoka huku akiwa na hasira.



    ******************



    Sajenti Minja hakupata tabu kuipata nyumba ya Dokta Innocent Malle kwa maana Sajenti Minja aliujua mji vizuri.



    Sajenti Minja alifika na kuiegesha gari yake nje ya nyumba ya Dokta Innocent Malle, kisha akabonyeza kengele, baada ya dakika moja yule kijana aliyewapokea wakina Vin siku iliyopita alienda na kufungua geti,



    "habari yako? Dokta nimemkuta?" Sajenti Minja aliuliza,



    "yupo, karibu" Kijana aliongea huku akiacha nafasi Sajenti Minja apite, Sajenti Minja akaingia ndani ya geti na kumkuta Dokta Innocent Malle akiwa amekaa kwenye viti vya nje akinywa kahawa, Sajenti Minja alimsalimu,



    "mzee mimi ni polisi, kuna maswali kidogo naomba unisaidie kujibu" Sajenti Minja aliongea huku akiweka kitambulisho juu ya meza kisha Dokta Innocent Malle akakichukua na kukikagua na mwisho akaridhika kuwa Sajenti Minja ni polisi kweli,



    "mimina Kahawa kwanza alafu ndio tuendelee kuulizana" Dokta Innocent Malle aliongea huku akitabasamu, kisha Sajenti Minja akamimina kahawa kwenye kikombe na kugida fundo moja,



    "mzee naomba unisaidie kueleza tukio la mtoto aliyeletwa kwako kufutwa kumbukumbu, hilo tukio lilitokea miaka ishirini iliyopita" Sajenti Minja aliuliza na kumuangalia Dokta Innocent Malle,



    "kweli mmeamua, jana tu huyo mtoto alikuja hapa kuniuliza, hama kweli ukweli haufichiki, hata uhufiche miaka Mia, ipo siku utajitokeza tu" Dokta Innocent Malle aliongea na kisha akaelezea mkasa mzima ulivyokuwa, hakuficha kitu,



    "huyo kijana mweupe mwenye michoro mwilini uliyemtaja kama kijana wa kazi wa Taita, amefanana na huyu?" Sajenti Minja alimuuliza Dokta Innocent Malle huku akimuonesha picha ya Trigger iliyokuwa kwenye simu ya yake,



    "ndio huyu haswa, ingawa hapa anaonekana mtu mzima kidogo" Dokta Innocent Malle aliongea huku akiiangalia ile picha,



    "hii picha nimeipiga leo, nilikuwa kwa Taita nafuatilia ile kesi yake ya kutekwa na kutupwa" Sajenti Minja aliongea,



    "sasa mbona juu ya hiyo picha umeandika muuaji?" Dokta Innocent Malle aliuliza,



    "choo kipo wapi, nikitoka chooni nitakujibu hilo swali, hapa haja ndogo imenishika kidogo kutokana na kahawa" Sajenti Minja aliuliza na yule kijana akamuelekeza Sajenti Minja akaelekea chooni.



    Kipindi Sajenti Minja akiwa chooni ndicho kipindi ambacho Trigger alikuwa anaingia kwa Dokta Innocent Malle. Trigger aliingia na kukaa kwenye kiti kile kile alichokalia Sajenti Minja, kisha akamsalimia Dokta Innocent Malle,



    "bado upo imara, ni muda sana tangu tuonane" Trigger aliongea huku akitabasamu,



    "siku mbili hizi mmenikumbuka, jana kaja Vin, leo wewe" Dokta Innocent Malle aliongea huku akitabasamu,



    "na kilichonileta ni suala hilo hilo la Vin" Trigger aliongea,



    "ebu hama kwenye hicho kiti, kuna kijana mmoja polisi ndio amekaa hapo, ameingia uwani, nae amekuja kwa masuala hayo hayo ya Vin," Dokta Innocent Malle aliongea na kumfanya Trigger ashtuke na kuitupia jicho simu ya Sajenti Minja iliyokuwepo mbele yake na kuiona picha yake ya ikiwa na maandishi " MUUAJI" Trigger akashtuka zaidi,



    "yuko wapi polisi mwenyewe?" Trigger aliuliza huku akiibeba simu ya Sajenti Minja,



    "ameelekea uko nyuma, chooni" Dokta Innocent Malle alijibu na wakati huo Sajenti Minja alikuwa akirejea, Sajenti Minja alipotokezea akamuona Trigger akiwa ameshika simu yake, Sajenti Minja akashtuka na kusimama, kitendo chake cha kusimama tu ghafla, Trigger akatoa bastola na kumnyooshea,



    "kumbe ulivyokuwa pale kwa Taita hukumfuata yeye ila ulinifuata mimi?" Trigger aliuliza huku bastola yake ikimuangalia Sajenti Minja,



    "kwanini unasema hivyo?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa anajua kabisa kuwa Trigger ameiona picha yake kwenye simu yake yeye Sajenti Minja, na kipindi hicho Dokta Innocent Malle na mwanaye walikuwa wamepigwa na butwaa huku wakiwa hawajui la kufanya,



    "hii picha umenipiga leo maana hata nguo nilizovaa ni hizi hizi, alafu unajifanya ulimfuata Taita" Trigger aliongea huku akionesha ana hasira,



    "telemsha bastola basi nikueleze vizuri" Sajenti Minja aliongea huku huku akiweka tabasamu la bandia na kumfanya Trigger pia atabasamu,



    "Trigger uwa hashushi silaha mpaka itoe risasi" Trigger aliongea huku akiendelea kutabasamu na kuikoki bastola yake, Sajenti Minja akashtuka,



    "una maana gani kusema hivyo?" Sajenti Minja aliuliza huku akitetemeka, ila Trigger hakujibu, akamfyatulia risasi Sajenti Minja, Sajenti Minja akatupwa chini na kunyooka kama mti mkavu, Dokta Innocent Malle na mwanae wakabaki wameshika midomo kwa mshangao,







    "hiyo ndio maana yangu" Trigger aliongea huku akimuangalia Dokta Innocent Malle na pia akitabasamu..........







    "kumbe hili jambo sio jepesi kama nilivyodhani?" Dokta Innocent Malle aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja aliyekuwa amelala sakafuni,



    "ili nisilete madhara makubwa zaidi, naombeni tuondoke wote kama mlivyo" Trigger aliongea huku akimtazama Dokta Innocent Malle,



    "tuondoke twende wapi?" Kijana wa Dokta Innocent Malle aliuliza kwa ukali,



    "usibishane na mtu ambaye ana silaha moto" Dokta Innocent Malle alimuonya kijana wake,



    "simameni na mfanye nitakacho mimi" Trigger aliongea kwa mamlaka kisha Dokta Innocent Malle na Kijana wake wakasimama,



    "ila ulikuja kwa lengo la kutaka kujua nilichoongea na Vin?" Dokta Innocent Malle aliuliza,



    "mzee sitaki maswali, tii nilichosema kabla sijatumia risasi nyingine" Trigger aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja aliyekuwa anainuka huku akiwa na damu nyingi begani, Trigger akamkimbilia na kuichomoa bastola ya Sajenti Minja iliyokuwepo kiunoni,



    "naona leo umeamua kuonesha uhodari wako wa kuua?" Sajenti Minja alimuuliza huku akitabasamu,



    "sijakuua bado, ila hilo linaweza kutokea saa zijazo" Trigger aliongea huku akimsukuma Sajenti Minja. Kisha Trigger akatoka nao mpaka nje alipoegesha gari yake,



    "we dogo Kaa upande wa dereva, mzee utakaa nyuma pamoja na mimi, wewe mwela utakaa mbele na dogo" Trigger aliongea na kisha watu wakafanya kama Trigger alivyoagiza,



    "utaendesha gari kulingana na maelezo yangu, usipofuata maelezo utakuwa umeniruhusu nikuue" Trigger aliongea huku akiwa ameikamata bastola yake vyema, ila hakumuelewa hakumuelekezea mtu.



    Yule kijana aliendesha gari huku kukiwa na ukimya wa kutosha baina ya mateka, sauti iliyosikika ni ya Trigger tu, ilikuwa ni sauti ya maelekezo iliyoambatanishwa na vitisho.



    Ile gari iliingia moja kwa moja kwenye nyumba moja ambayo ndiyo kambi ya Taita, ila kipindi hiki haikuwa na walinzi kama zamani, nyumba ilikuwa na mlinzi mmoja tu wa getini.



    Baada ya gari kuingia, wa kwanza kushuka alikuwa Trigger, kisha na wengine wakashuka, walielekea moja kwa moja mpaka nyuma ya ile nyumba ha kukuta kuna viti vitatu vikiwa vimeizunguka meza moja na pembeni ya vile viti kulikuwa na nguzo za chuma kama tano zilizochimbiwa chini na kulikuwa na kamba zimezungushiwa kwenye hizo nguoo,



    "wafunge kila mmoja na nguzo yake" Trigger alimwambia Sarah yule kijana waliyemkuta getini, yule kijana akaanza na Sajenti Minja kumfunga, kisha akamalizia na wengine,



    "wewe rudi getini, hakikisha mtu yoyote haingii humu, isipokuwa Taita tu" Trigger aliongea kwa kumsisitizo,



    "haina shida mkuu" Kijana alijibu huku akiondoka na kumuacha Trigger na mateka wake.



    "sasa tunaweza kuendelea, naanza na wewe askari, kwanini unanitafuta mimi?" Trigger aliuliza huku akivuta kiti na kukikalia mbele ya Sajenti Minja,



    "sikuwa nakutafuta, kama ningekuwa nakutafuta ningeshakukamata" Sajenti Minja alijibu,



    "unanituhumu kwa mauaji, nimemuua nani?" Trigger aliuliza swali la pili,



    "Dokta wa polisi, umefanya hayo mauaji leo hii" Sajenti Minja alijibu huku akimtazama Trigger,



    "kuna ushahidi gani labda?" Trigger aliuliza,



    "kabla hajafa aliongea mwenyewe" Sajenti Minja alijibu,



    "aliongea? amenijuaje?" Trigger aliuliza kwa kebehi huku akicheka,



    "nadhani kutokana na ile picha ya kwenye simu yangu, kwa maana siku ya kwanza unafanya jaribio la kumuua alikuona" Sajenti Minja alijibu,



    "Alafu siku hizi nimekuwa mzembe sana, nalenga ila siui, sijui kwa nini?" Trigger aliongea huku akitabasamu kwa dharau,



    Kisha akanyanyua kiti na kusogea usawa wa Dokta Innocent Malle, ambaye muda wote alikuwa akitabasamu,



    "mzee utanisamehe sana, ila sitokuua endapo utanijibu swali langu vizuri, je Vin umemuambia ukweli kuhusu familia yake?" Trigger aliuliza huku akimuangalia Dokta Innocent Malle,



    "ukweli kuhusu familia yake ipi? Mimi nimemwambia ukweli kuhusu tukio lake la kufutwa kumbukumbu, na sijui kuhusu kitu kingine'' Dokta Innocent Malle aliongea huku akitabasamu,



    "ooh vizuri sana, je kulikuwa na umuhimu gani wa kumwambia hayo yote?" Trigger aliuliza,



    "nadhani kila mwanadamu anatakiwa ajitambue" Dokta Innocent Malle alijibu na kumfanya Trigger atikise kichwa huku akitabasamu,



    "je kuna mtu ana swali?, kabla sijafanya kitu cha kutisha yoyote mwenye swali aulize" Trigger aliongea huku akiinuka kwenye kiti,



    "Mimi nina maswali matatu tu, naomba ushirikiano wako" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Trigger,



    "uliza kamanda'" Trigger aliongea huku akicheka, alikuwa akimdhiaki Sajenti Minja,



    "nataka kujua kuhusu familia ya Sarah, ni kweli Taita aliichoma moto?" Sajenti Minja aliuliza na kumfanya Trigger afikirie kidogo,



    "sasa hivi vitu vyote vipo wazi, kila mtu anaujua huo ukweli, jibu la hilo swali unalo, labda kama una swali jingine" Trigger alijibu na kumfanya Sajenti apate uhakika kuwa Taita ndio aliyeiangamiza familia ya Sarah,



    "leo nimeona majibu ya Vin, yanaonesha yeye na Sarah ni ndugu, je mlitumia njia gani kuwatenganisha?" Sajenti Minja aliuliza,



    "maswali yako ya kipuuzi, yanapoteza muda tu, hilo swali ulilouliza jibu lake analo huyo mzee Dokta" Trigger alijibu huku akivua shati,



    .



    "ni muda wa kuua huu, nitaanza kwako kwenda kulia" Trigger aliongea huku akitoa risasi tatu kwenye mfuko wa suruali na kuzipachika kwenye bastola yake, kisha akamtupia jicho Sajenti Minja na kumnyooshea bastola usawa wa kichwa,



    "Trigger akikunyooshea bastola uwa haishushi mpaka itoe risasi" Sajenti Minja aliyakumbuka maneno hayo ya Trigger kisha Sajenti Minja akafunga macho na kuuma meno kwa nguvu, alijua kinachofuata ni kifo, Trigger baada ya kumuona Sajenti Minja akiwa kwenye hali ile, Trigger akaachia cheko moja baya sana huku akiwa Bado ameielekeza bastola yake usawa wa kichwa cha Sajenti Minja.



    ******************



    Vin alipotoka polisi alirudi hospitali na kuchukua gari yake, kisha akaelekea moja kwa moja nyumbani kwa Taita na kumkuta Taita akiwa anatazama runinga,



    "Trigger yupo wapi?" Vin aliuliza huku akikaa,



    "sijui hata alipoelekea, vipi kwani?" Taita aliuliza,



    "mzee kwanini mnatumia silaha kufanya mauaji ili mfiche tu ukweli juu ya chimbuko langu?" Vin aliuliza kwa sauti tulivu na kumfanya Taita ashtuke,



    "kwanini unasema hivyo mwanangu?" Taita aliuliza kwa upole,



    "Sarah ni ndugu yangu, hata ungeniambia mapema tu wala nisingebadilika, wewe bado ni baba kwangu" Vin aliongea huku akiwa ameangalia chini,



    Huyo Sarah atakudanganya mpaka lini? majibu si uliyaona yalionesha hamna undugu wowote" Taita aliongea kwa ukali,



    "yale majibu aliyaleta Trigger, mimi nimekuja na majibu yangu niliyopewa na Daktari mliyemuua leo" Vin aliongea na kuitupa ile bahasha juu ya meza, kisha Taita akaikota na kuitoa karatasi ya ndani, akaanza kusoma na kisha akatabasamu,



    "wewe unaamini hii? Huu ni ujanja wa Sarah tu wa kukuharibu akili" Taita aliongea huku akitabasamu,



    "huu ni ujanja ee? Na hii je?" Vin aliongea na kuitoa simu yake kisha yakaanza kusikika maneno ya Dokta Innocent Malle wakati alimueleza Vin habari za miaka ishirini iliyopita, Taita alikaa kimya huku akifuatilia yale maneno,



    "sasa hata huyu Dokta huenda ametumwa na Sarah, mbona wewe Vin ni msomi tu ila unashindwa kujua upi ni ukweli na upi ni uongo?" Taita aliuliza huku akiyatupa yale majibu juu ya meza,



    "sasa aongee nani ndio nimuamini? Maana kila anayeniambia ukweli unadai anatumwa" Vin aliongea,



    "hakuna wa kumuamini, labda ningeongea mimi au Trigger, hapo ndipo ungeamini" Taita aliongea huku akimtazama Vin,



    "wewe au Trigger ee? Sawa, je na hii sauti ndio unaiamini?" Vin aliuliza huku akifungua lap top yake kisha akaweka yale maneno ya Trigger aliyotumiwa Strategic kama mtego, baada ya maneno kuisha, Taita alihisi nguvu kumuishia miguuni, maana Trigger ndio mtu pekee ambaye alikuwa akimuamini muda huu, alishangaa kusikia kuwa nae ametoa siri hiyo.



    "bado unapinga?" Vin aliuliza huku akimuangalia Taita aliyekuwa amekaa kimya,



    "Strategic ameamua kunigeuka, umemtumia ili uujue ukweli" Taita aliongea kwa sauti iliyokata tamaa,



    "Trigger ameongea maneno mengi, ila ninachotaka ukubali tu kuwa mimi sio mwanao na pia unihakikishie Sarah ni ndugu yangu" Vin aliongea huku akimtazama Taita aliyekuwa ameinamisha kichwa chini,



    "Sarah ni ndugu yako, mimi sio baba yako" Taita aliongea huku akimtazama Vin,



    "hicho ndicho nilichokuwa nakihitaji, sasa nipo huru, pamoja na yote hayo bado wewe ni baba yangu, sina baba mwingine mwenye kunipa upendo kama wewe" Vin aliongea huku machozi yakimtoka, ila Taita hakuonekana kusikiliza maneno ya Vin, Taita alikuwa kama amechanganyikiwa, yaani siri aliyoificha muda mrefu imekuja kugundulika kizembe namna hiyo, tena mtu wa karibu ndiye aliyeivujisha.



    "Baba, Trigger yupo wapi?!" Vin aliuliza huku akiwa bado analia,



    "ameenda kwa Dokta Malle" Taita alijibu bila kutarajia,



    "tafadhali mzuie asiue zaidi, ukweli umeshajulikana na haina haja ya kuua zaidi" Vin alimsisitiza Taita huku akilia,



    "hapana, siwezi kumzuia, wote waliosababisha ukweli ukajulikana ni lazima wafe" Taita aliongea huku akiwa hana mzaha,



    "unachosema kitatokea moyoni kwako?" Vin aliuliza huku akitokwa na machozi,



    "uwa sitanii, na sasa nataka nikuoneshe roho yangu ilivyo, nilificha sana tabia yangu nilipokuwa na wewe" Taita aliongea kwa ujasiri,



    "hapana aisee, ngoja nikamsaidie Dokta Malle" Vin aliongea huku akiinuka,



    "Vin subiri, nenda chumbani kwangu kaniletee dawa kwenye droo ya chini ya kabati" Taita aliongea kisha Vin akakimbia ndani haraka, Vin aliyoingia tu chumbani, Taita akainuka na kukimbilia mlango, kisha akamfungia Vin kwa nje, Vin akashtuka,



    "mzee ndio unafanya nini sasa?" Vin aliuliza kwa hamaki huku akiwa ndani,



    "Vin tulia uko kwanza, acha Trigger atimize majukumu yake" Taita aliongea na kurudi kukaa kwenye kiti, kisha akampigia simu Trigger na kumuamuru amuue Dokta Innocent Malle na wote wataokuwa kikwazo eneo hilo.



    Wakati huo ndani Vin alikaa kitandani huku akiwa hana la kufanya, wazo likamjia, akachukua simu na kumpigia Sarah,



    "vipi Seba" Sarah aliongea baada ya kupokea simu,



    "Dada wahi kwa Dokta Malle, anauawa muda wowote" Vin aliongea na kumfanya Sarah ashangae kuitwa dada na Vin,



    .



    ..



    "anauawa na nani?" Sarah aliuliza,



    "mzee amemtuma Trigger akamuue, tafadhali kamsaidie" Vin aliongea kwa haraka haraka,



    "huyo Dokta Innocent Malle ndio nani?" Sarah aliuliza,



    "ndio huyo aliyenifuta kumbukumbu, sasa mzee anataka amuue kwa sababu alinieleza ukweli" Vin alijibu,



    "anaishi wapi?" Sarah aliuliza na kisha Vin akamuelekeza na kukata simu, Vin akajilaza kitandani huku akiwaza na kuwazua.



    ****************



    Sarah baada ya kukata simu, aliondoka Moja kwa moja na kwenda kuchukua boda boda iliyomfikisha mpaka mtaa alioelekezwa, akashuka na kumlipa dereva boda boda, kisha akakaa sehemu pembezoni mwa ukuta huku akiwa na mshangao, kwa maana aliikuta gari ya Sajenti Minja ikiwa nje ya ile nyumba pia,



    "huyu nae amejuaje hili tukio? Au Vin alimwambia?" Sarah aliwaza huku akiiangalia gari ya Sajenti Minja, Sarah akataka atoe simu ili amfahamishe Vin juu ya uwepo wa Sajenti Minja pale, ila kabla hajapiga simu aliona geti la mlango wa nyumba ya Dokta Innocent Malle ukifunguliwa, kisha akawaona watu wakitoka ndani ya ile nyumba, wa kwanza na wa pili hakuwatambua, ila wa tatu alimtambua, alikuwa ni Sajenti Minja aliyeonekana ana damu nyingi begani, na mtu wa nne akamtambua, alikuwa ni Trigger, alikuwa amemshika bastola na alionekana akiwa anawaamrisha wenzake,



    "mshenzi huyu amewateka wenzake" Sarah aliongea huku akicheka na kuwashuhudia wakiingia kwenye gari na kuondoka.



    Sarah hakutaka Kupoteza muda, akaangaza kushoto na kulia hakuona usafiri wa kuchukua, akakunja uso kwa hasira, akaamua aanze kukimbia kuelekea upande ule wakina Trigger walipoelekea, ila kabla hajapiga hatua za kutosha, kuna gari ilikuja kusimama pembeni yake,



    "ingia" Alikuwa ni Aisha, aliongea huku akitabasamu, Sarah hakutaka kubisha, akafungua mlango na kuingia, kisha Aisha akaiondoa gari kwa kasi,



    "unajua ninapoenda?" Sarah alimuuliza Aisha,



    "si unamfuatilia Trigger na mateka wake?" Aisha aliuliza,



    "yap, umejuaje?" Sarah aliuliza,



    "popote uendapo nipo nyuma yako, ulipowaonea wewe, na mimi niliwaonea hapo hapo" Aisha alijibu kisha ukimya ukachukua nafasi yake.



    Waliifuatilia ile gari mpaka walipoona imeingia kwenye nyumba moja hivi, hiyo nyumba wote waliitambua, Aisha akasimamisha gari,



    "pale kuna walinzi wengi, tutaingiaje?" Aisha aliuliza,



    "wewe pitia getini, mimi nitazunguka nyuma ya nyumba" Sarah alitoa wazo,



    "Alafu? yaani sijaelewa maana yako" Aisha aliuliza,



    "wewe si wanakujua baadhi ya walinzi? Nenda kawapotezee muda kwa kuwalaghai na hadithi za uongo, utanisubiri mimi niingie kwa ndani, ukiniona tu anza kushambulia" Sarah aliongea,



    "poa" Aisha alijibu kisha akaelekea getini, Sarah yeye akaamua kuizunguka nyumba na kupitia kwa nyuma.



    Aisha akaenda mpaka getini na kumkuta kijana akiwa anaimarisha ulinzi,



    "niitie Trigger" Aisha aliongea bila salamu,



    "hayupo, kwanza wewe nani?" Kijana aliuliza huku akiwa amemkazia sura Aisha aliyekuwa anashangaa ndani kuona kweupe, hakuna walinzi kama alivyozoea, aisha akaona asipoteze muda, akakishika kisha cha yule kijana na kukibamiza getini, geti likapiga kelele,



    "aaaaagh, nimebugi" Aisha alijilaumu huku akimuachia yule kijana na kudondoka chini kama mzigo, kisha Aisha akawa anakimbia kuingia ndani, hakujua kama mateka wapo nyuma ya nyumba na Trigger.



    Huko nyuma kile kishindo cha geti kilimshtua Trigger na kumfanya haache zoezi la kumpiga risasi Sajenti Minja ambaye alikuwa amefunga macho akisubiri kumalizwa.



    Trigger akashusha bastola chini na kuanza kunyata taratibu kuelekea mbele ya nyumba ili aone kuna nini, alipotokeza ndipo akamuona mwanamke akikimbia kuelekea ndani,



    "stop, weka mikono juu" Trigger aliongea huku akimuangalia Aisha,



    "Trigger, mi Aisha" Aisha aliongea huku akitabasamu, Trigger akafyatua risasi kumtisha,



    "Mikono juu, habari zako ninazo" Trigger aliongea kwa hasira na kumfanya Aisha anaswe kwa urahisi, kisha Trigger akamkokota Aisha mpaka nyuma ya nyumba na kuanza kumfunga kwenye nguzo kama wenzake,



    "nilikuwa nakutafuta sana wewe, tulikukosa kukuua na bomu nikasikia eti na wewe umepanga kutuua? Trigger hauliwi na malaya" Trigger aliongea kwa dharau huku akiwa anamalizia kumfunga Aisha, kisha Trigger akageuka nyuma ili arudi kwenye kiti, ila alishtukia kishindo chepesi nyuma yake, akageuka kwa haraka akakutana na teke kali lililotua kwenye mkono na kufanya bastola yake iruke mbali,



    "Trigger, professional killer" Sarah aliongea huku akiwa amemuelekezea bastola Trigger, Trigger akapigwa na bumbuwazi, huku asijue namna sarah alivyoingia na wakati huo Sajenti Minja na Aisha wakipata ahueni wakiamini Sarah atawaokoa,



    "nenda mbele, twende tukakae pale kwenye viti" Sarah aliongea na kumfanya Trigger atembee mpaka kwenye kiti na kukaa, kisha Sarah nae akakaa upande wa pili na meza ikawa kati yao,



    "ule mchezo tulioucheza mara ya mwisho tulipokutana, nataka tucheze na leo ingawa siku ile ulinizidi kete" Sarah aliongea na kufanya Trigger atabasamu huku wale wengine waliofungwa wakiwa hawaelewi ni kitu gani kinaendelea,



    Sarah akatoa bastola kiunoni na kuitupa mbele ya Trigger, kisha nae akazitoa risasi zote kwenye bastola aliyoishika mkononi na bastola akaiweka mezani, alafu akachukua simu yake na kuitega sekunde thelathini na kuiweka mezani, hapo wote wawili wakawa wanaziona sekunde zinavyohesabu.



    Sajenti Minja akashtuka baada ya kugundua mchezo wa Sarah, na wakati huo Aisha akatabasamu akiamini Sarah yupo na wepesi sana, kwa hiyo atamshinda Trigger,



    "wewe Sarah acha upuuzi njoo utufungue, atakuua huyo" Sajenti Minja aliongea kwa sauti ila wala Sarah hakuonekana kumjali, akili na macho yake yalikuwa makini na bastola mezani.



    Zilipobaki sekunde kumi, Sarah akatoa risasi mbili, moja akaiweka mbele ya Trigger na nyingine akaweka mbele yake. Sekunde zikazidi kuhesabu kwa kushuka chini, ilipofika sekunde ya sifuri hapo Sarah kwa Kutumia wepesi wake aliiokota risasi na kuiweka kwenye bastola kwa kasi ya ajabu sana, ila wakati akiinuka kichwa kumuangalia Trigger, hapo Sarah alikutana na ajabu la mwaka, tayari Trigger alikuwa ameshamaliza kila hatua na bastola yake ilikuwa inaangaliana na uso wa Sarah. Sio Sarah tu aliyeshangaa hilo tukio, mpaka Sajenti Minja na Aisha walikuwa midomo wazi kwa namna Trigger alivyokuwa mwepesi kwenye masuala hayo ya michezo ya silaha za moto.



    Sarah akainuka ili akimbie, ila alijigonga kwenye kiti na kuanguka chini, kisha bastola ikamponyoka na kudondoka mbali, Sarah akaishiwa ujanja na wakati huo Trigger aliinuka na kumfuata Sarah aliyekuwa amelala chini, Trigger alivyomfikia Sarah aligusisha bastola yake na paji la uso wa Sarah, Trigger akatoa cheko kubwa sana, huku Sarah jasho likimtoka,



    "Trigger akikuoneshea bastola uwa haishuki chini mpaka itoe risasi" Sajenti Minja alijikuta anaongea peke yake bila kujua ila sauti yake ilisikika vyema kwa kila mtu,



    "yeah, hiyo ndio kanuni yangu" Trigger aliongea huku akicheka na kufyatua risasi kwenye kichwa cha Sarah, watu wote katika eneo hilo walifunga macho.....................









    Ila Sarah akaupiga mkono wa Trigger kwa chini na yeye akabonyea kidogo, ile risasi ya Trigger ilivyotoka iliondoka na baadhi ya nywele za Sarah, Sarah akashika kichwa huku Sajenti Minja na Aisha wakiwa hawaamini wanachokiona, kumbuka kwenye bastola ya Trigger kulikuwa na risasi moja tu, kwa hiyo baada ya kumkosa Sarah akataka aiwahi ile bastola iliyomponyoka Sarah, ila kwa wepesi wa Sarah aliinuka na kiti na kumpiga nacho Trigger kichwani, Trigger akadondoka chini, kisha Sarah akajibetua na kuokota bastola yake, kisha akamnyooshea Trigger aliyekuwa yupo chini,



    "una lolote la kuongea labda?" Sarah alimuuliza Trigger huku akitabasamu, ila Trigger hakuonekana kutaka kujibu kitu, alikuwa yupo chini,



    "inuka ukae kwenye kiti hapo juu" Sarah Alimwambia Trigger, ambaye alitii agizo,



    "nisaidie kujibu hili swali, kulikuwa na ulazima gani kuwachoma wazazi wangu moto?" Sarah aliuliza huku akijishika kichwani eneo risasi ilipomkosa,



    "maswali ya nini? Kama umeamua kuniua niue, sitojibu swali lolote kuhusu watu waliokufa" Trigger aliongea na kucheka, Sarah akaona huu muda sio wa kubembelezana, akamfyatulia risasi ya mguu na Trigger akatoa ukelele wa maumivu, kisha Sarah akatoa risasi nyingine na kuzijaza kwenye bastola yake, akampiga risasi nyingine Trigger, ila hii alimpiga kwenye mguu wa pili na kumfanya Trigger alie kama mtoto, kufikia hapo Trigger hakuwa na uwezo wa kutembea kwa maana miguu yote ilikuwa imepigwa risasi.



    Sarah akainuka na kwenda sehemu alipofungwa Aisha na kumfungua,



    "mfungue huyo mzee" Sarah alimwambia Aisha ambaye alifanya kama alivyoagizwa, baada ya Dokta Innocent Malle kufunguliwa akashukuru sana kwa Sarah,



    "mzee ondoka, nenda nyumbani" Sarah aliongea kwa ukali,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "mama siwezi kuondoka, nimekuja na Kijana wangu hapa" Dokta Innocent Malle aliongea huku akimuangalia yule kijana wake,



    "Aisha mfungue na huyo, ondokeni moja kwa moja nendeni nyumbani, msipite sehemu yoyote kutoa taharifa" Sarah aliongea kwa msisitizo,



    "nifungueni na mimi" Sajenti Minja aliongea huku akiwatizama,



    "huyo mfungue uondoke nae, mpeleke sehemu umfungie alafu utanitaharifu ulipo, nitakuja ngoja nimalizane na huyu mwamba" Sarah alimwambia Aisha kwa sauti ndogo ambayo Sajenti Minja hakuweza kusikia,



    "mbona mnanong'ona? Mnataka kunifanya nini?" Sajenti Minja aliuliza kwa utani huku akicheka,



    "ngoja tukuachie kamanda, ila ukiachiwa ondoka, sitaki ujihusishe na hii kazi hapa niliyonayo" Sarah aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja,



    "hakuna tabu" Sajenti Minja alijibu huku akiwa na wazo endapo ataachiwa atawageuzia kibao.



    Aisha akaenda kwenye nguzo aliyofungiwa Sajenti Minja na kuanza kumfungua taratibu mpaka akamaliza, alipomaliza tu Sajenti Minja akatoa bastola yake,



    "haya wewe jiunge na mwenzako hapo, mpo chini ya ulinzi" Sajenti Minja aliongea huku akimsukuma Aisha,



    "wewe mpumbavu kweli" Aisha aliongea kisha akajizungusha na teke kali lililoipiga bastola ya Sajenti Minja na kufanya ianguke,



    "tulia hivyo hivyo, Aisha mfunge kamba huyo" Sarah aliongea kwa hasira huku akimuangalia Sajenti Minja,



    "nilikuwa nawadanganya tu" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,



    "hatuna utani" Aisha aliongea na kumchota mtama Sajenti Minja, kisha akamkimbilia na kumkamata mikono kwa nyuma na kumfunga kamba,



    "haya tuondoke" Aisha aliongea huku akimuinua Sajenti Minja na kuanza kumkokota kuelekea nje.



    Wakaelekea kwenye gari aliyokuja nayo Aisha kisha Sajenti Minja akawekwa upande wa kushoto wa dereva na Aisha akaingia upande wa dereva,



    "unanipeleka wapi?" Sajenti Minja aliuliza,



    "uwa unapenda mziki?" Aisha aliuliza huku akimuangalia,



    "hujanijibu swali langu" Sajenti Minja aliongea tena,



    "tunaenda clab, ndio maana nikauliza hupendi mziki?" Aisha alijibu huku akitabasamu, Sajenti Minja akahisi akilegea anaweza kutekwa kizembe, akamsukuma na bega Aisha, Aisha akapiga breki ya ghafla na Kumfanya Sajenti Minja akose balance kutokana na kamba alizofungwa, Sajenti Minja akakigonga kioo cha mbele cha gari kisha Aisha akamvuta kwa nguvu na kumpiga ngumi ya shingo iliyopelekea Sajenti Minja apoteze fahamu, kisha Aisha akakilaza kiti alichokalia Sajenti Minja, akakanyaga mafuta na gari ikatembea mbele.



    "haka kajamaa kana mbinu za kizamani kweli, sema tu kamenikuta siku hizi nina ubinsdamu, vinginevyo asingekuwa hai huyu" Aisha aliongea kwa hasira kisha akaingiza gia.



    Aisha aliendesha gari kwa muda wa dakika ishirini, kisha akaiingiza kwenye nyumba moja ndogo iliyokuwa katika uzio mkubwa, kisha akamtoa Sajenti Minja, akajaribu kumbeba akashindwa, akaamua ambulute mpaka ndani, akamuingiza katika eneo moja la wazi na kumfunga katika dirisha lililokuwa na nondo, kisha Aisha akashusha pumzi ndefu kutokana mchoko alioupata baada ya kumvuta Sajenti Minja.



    "nipumzike kidogo kisha nimrudie Sarah nikamtazame kama ameshaondoka" Aisha aliongea huku akikaa sakafuni, kwa maana eneo hilo halikuwa na viti.



    *******************



    Taita aliendelea kukaa sebuleni huku mawazo yakionekana kumzidi, akasimama na kwenda kwenye friji akatoa maji ya baridi na kuyanywa kwa pupa, kisha akarudi kwenye kochi na kutafakari kwa muda, akatoa simu yake na kubofya namba anayoijua yeye, kisha simu akaweka sikioni na kuisikiliza kwa namna inavyoita ila simu haikupokelewa,



    "huyu Trigger mpuuzi sana, yaani ni mzito sana kupokea simu" Taita alilaumu huku akikaa kwenye kochi, kisha akainuka na kwenda kwenye friji tena, akatoa pombe kali na kurudi nayo kwenye kochi, akatoa kizibo na kuigida kwa hasira, chupa ilipofika nusu akaishusha huku akiwa amekunja uso kutokana na ukali wa pombe yenyewe, akaiangalia simu yake tena na kufikiri kwa muda, kisha akaitafuta namba anayoitaka na kubonyeza, simu ikaanza kuita, iliita kwa muda na haikupokelewa, akaitupa simu kwa hasira,



    "hawa watu vipi? au wameanza kunidharau?" Taita alijiuliza huku akiiangalia simu yake iliyoangukia juu ya kochi, ila akahisi mlango wa sebuleni unafunguliwa, akatupia macho mlangoni kwa haraka na kumuona Strategic akiingia,



    "wewe mbona nakupigia simu hupokei?" Taita alimuuliza kwa hasira,



    "sikuona sababu ya kuipokea wakati nilikuwa hapo nje, ndio maana nimekuja" Strategic alijibu huku akitabasamu,



    "unatakiwa upokee na usikilize ninachosema, au ulijua nataka niseme nini?" Taita aliuliza kwa hasira,



    "nisamehe mkuu" Strategic aliongea baada kuona Taita ana hasira kubwa sana,



    "unapajua kwa Dokta Innocent Malle?" Taita alimuuliza Strategic na kumfanya Strategic afikirie kidogo,



    "hapana, hata Dokta mwenyewe simjui" Strategic alijibu ingawa alikuwa anapajua,



    "aaaaagh, nikikupa ramani si utaamka?" Taita aliuliza,



    "ndio mkuu" Strategic alijibu kisha Taita akachukua karamu na karatasi na kuanza kuchora chora, aliporidhika akampatia ile karatasi Strategic,



    "si utaelewa hapo?" Taita aliuliza,



    "ndio mkuu" Strategic alijibu,



    "nenda kamuangalie Trigger, nimemtuma uko, nampigia simu hapokei" Taita aliongea,



    "endapo nitamkosa?" Strategic aliuliza,



    "nipigie sure nenda kule kambini" Taita aliongea,



    "sawa" Strategic alijibu,



    "ukimkuta nipigie simu ili niongee naye" Taita aliongea,



    "sawa" Strategic alijibu kisha akaondoka kwa haraka kuwahi kwenye gari, alipoingia kwenye gari simu yake iliita, alipoitazama aligundua ni Vin, akapokea simu haraka,



    "nipo ndani hapa kwa mzee, nimesikia ukiongea nae, mimi amenifungia chumbani, je unaweza kuja kunisaidia kunifungulia mlango" Vin aliongea haraka haraka,



    "upo chumba kipi?" Strategic aliuliza,



    "chumba cha mzee" Vin alijibu,



    "hapo siwezi kukusaidia, maana yeye yupo sebuleni na huwezi kwenda chumbani kwake bila kupitia sebule" Strategic alijibu,



    "basi naomba unisaidie kitu, nenda kwa Dokta Malle na umuwahi Trigger, ameenda kufanya mauaji, nilimpigia simu Sarah ila sijajua kama amefanikisha au vipi? Kwa maana hapokei simu zangu" Vin aliongea haraka haraka,



    "sawa nitawahi, sasa kwanini mzee amekufungia ndani?" Strategic aliuliza,



    "tutaongea baadae, wewe nenda kwanza, mimi najua mzee atafungua tu mlango baadae" Vin aliongea,



    "poa" Strategic aliongea na kukata simu, kisha akawasha gari na kuiondoa kwa kasi.



    ***********************



    Sarah baada ya kuachwa na Aisha, alimgeukia Trigger na kumuangalia kwa hasira, Trigger alikuwa amekaa chini huku akiugulia maumivu ya kupigwa risasi za miguuni, hata kutembea hakuweza.



    "unajisikiaje?" Sarah alimuuliza Trigger ila Trigger hakujibu kitu, Sarah akamfuata na kuanza kumvuta kuelekea ndani, tena alimshika mguu na kumfanya Trigger asikie maumivu maradufu.



    Sarah alimvuta Trigger mpaka eneo la ndani ya nyumba ambayo ilikuwa kama sebule kwa maana kulikuwa na makochi na meza na ukutani kulikuwa na runinga bapa ya kisasa, tena yenye ukubwa wa kiwango cha juu.



    Sarah akatafuta kiti cha mbao ambacho kilikuwa eneo pembeni na sebuleni, alikikuta kikiwa na viti vingine vingi vya mbao vilivyoizunguka meza moja kubwa, Sarah akatambua ile ni sehemu ya kupata chakula. Sarah akakivuta kile kiti na kurudi nacho sebuleni, kisha akamchukua Trigger na kumkalisha juu ya kile kiti, alafu akaenda kwenye chumba ambacho alishawahi kutekewa,. Akaingia katika kile chumba na kurudi na kamba, kisha akaanza kumfunga Trigger kwa kumuambatanisha na kile kiti cha mbao,



    "unataka kunifanyaje?" Trigger aliuliza huku akicheka kwa dharau, Sarah hakujibu kitu, alitabasamu tu.



    Baada ya Sarah kumaliza kumfunga Trigger, Sarah alitoka mpaka nje ya nyumba huku akiwa amebeba ndoo na mpira wa maji mfupi, Sarah alitoka na kwenda kwenye gari alilokuja nalo Trigger, kisha akafungua tank la mafuta na kuingiza ule mpira kwenye tank kisha upande wa pili akauingiza mdomoni kwake na kuvuta mafuta, kisha akauelekezea mpira katika ndoo aliyoenda nayo, mafuta yakawa yanatoka kwenye tank na kujaa kwenye ndoo.



    Sarah aliporidhika na kiwango cha mafuta, alifunga tank na kuondoka na ndoo mpaka sehemu alipomuacha Trigger,



    "Mimi nadhani tuitimishe, maana tumewindana sana na leo mwenye bahati kabahatika" Sarah aliongea huku akimuangalia Trigger,



    "unataka kunichoma moto?" Trigger aliuliza huku akicheka,



    "ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga, malipo ni hapa hapa duniani" Sarah aliongea huku akimmiminia mafuta Trigger na kisha mafuta mengine akayamwaga eneo lililomzunguka Trigger, eneo ambalo hakuweka mafuta ni mlangoni tu,



    "una lolote la kunishauri au kunisifia?" Sarah aliuliza huku akitabasamu, Trigger akainua kichwa na kumtazama, macho ya Trigger yalikuwa mekundu sana,



    "kama nimeshindwa kukuua mimi, Vin atakuua" Trigger aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtoka, Sarah akatabasamu na kuamini ni maneno ya mkosaji, Sarah akanyoosha bastola yake kwenye eneo lenye mafuta, alitaka kulipua sasa, simu yake ikaita, ilikuwa ni namba ya Aisha,



    "vipi?" Sarah aliongea baada ya kupokea simu,



    "upo wapi?" Aisha aliuliza,



    "kwani wewe upo wapi?" Sarah nae akauliza,



    "nipo njiani nakufuata hapo kambini kwa Taita" Aisha aliongea,



    "sipo, nimeshaondoka, nimeenda nyumbani kupumzika" Sarah alidanganya, hakutaka mtu yoyote aende eneo hilo,



    "sasa huyu afande nimfanyaje?" Aisha aliuliza,



    "usimuachie, nitakutafuta baadae" Sarah aliongea,



    "poa" Aisha alijibu kisha akageuza gari na kurudi alipomuacha Sajenti Minja.



    Sarah akakata simu, kisha akaelekeza bastola sehemu yenye mafuta na kufyatua risasi, mafuta yakashika moto na kuanza kutembea kumuelekea Trigger, Trigger akatabasamu,



    "siku zangu za mwisho zimekuwa za taabu sana, wewe mtoto umekuja kuharibu kila kitu" Trigger aliongea huku akicheka na moto ulikuwa umeshamfikia ukamvaa na Trigger akaanza kupiga kelele na pia nyumba yote ikashika moto.



    **************



    Strategic alienda mpaka kwa Dokta Malle, akamkosa Trigger, hata Dokta mwenyewe hakumkuta.



    Strategic akatoka mpaka kambini kwao, alipofika getini alishangaa kuona nyumba nzima ikiwa imeshika moto, strategic akataka atelemke, ila akili yake ikamwambia hata akishuka kwa moto ule hawezi kuokoa kitu chochote.



    Strategic akachukua simu yake ili ampigie Taita na kumpa taharifa juu ya moto huo, lakini bahati mbaya simu yake ilizimika kwa maana iliisha chaji. Strategic akaondoa gari ili kwenda kutoa taharifa kwa Taita juu ya moto huo.



    *************



    Ndani ya nyumba, Sarah alikuwa amesimama pembeni akimuangalia Trigger namna anavyoungua na jinsi anavyojitahidi kuupigania uhai wake. Moto ukazidi kushika kasi mpaka poa la nyumba likaanza kutoa sauti kama linaachia, Sarah akaona bora aondoke, aliamini Trigger hawezi kupona kwa ule moto.







    Sarah akageuka nyuma ili aondoke, ila kutokana na ule moto kumuunguza Trigger kwa kiasi kikubwa, kamba alizofungwa zilikuwa zimeungua na kuisha, sasa wakati Sarah amegeuka aondoke, Trigger akamshika Sarah mguu na kuuvuta kumzuia asiondoke ili wote waungue, Sarah akageuka ili ammalize Trigger na risasi, ila mbao moja kutoka juu ya paa ikaachia na kudondoka, ikamuangukia Sarah kichwani, Sarah akadondoka na kupoteza fahamu, na muda huo moto ulishazunguka nyumba nzima na paa zikiwa zinaanguka tu, yaani nyumba ilikuwa inajifunika.



    Sarah alivyopoteza fahamu, Trigger akaanza kujivuta kwa mikono, alitambaa mpaka akafikia bastola ya Sarah, kisha Trigger akajivuta mpaka mpaka kwenye ndoo ya maji na kuibeba kisha akajimwagia maji kwa maana moto ulikuwa bado unawaka, sasa Trigger alipata ahueni baada ya moto kuzimika, akaifungua bastola na kuona ina risasi za kutosha, akaifunga na kumuelekezea Sarah kichwani, Trigger akatabasamu,



    "bora tufe wote" Trigger aliongea huku akitabasamu, moto ulikuwa umemuunguza vibaya sana, mwili mzima........................





    Sarah alivyopoteza fahamu, Trigger akaanza kujivuta kwa mikono, alitambaa mpaka akafikia bastola ya Sarah, kisha Trigger akajivuta mpaka mpaka kwenye ndoo ya maji na kuibeba kisha akajimwagia maji kwa maana moto ulikuwa bado unawaka, sasa Trigger alipata ahueni baada ya moto kuzimika, akaifungua bastola na kuona ina risasi za kutosha, akaifunga na kumuelekezea Sarah kichwani, Trigger akatabasamu,



    "bora tufe wote" Trigger aliongea huku akitabasamu, moto ulikuwa umemuunguza vibaya sana, mwili mzima, Trigger akaacha ghafla kutabasamu, machozi yakaanza kumtoka, akalia kwa uchungu, akageukia ndoo ya maji na kuibeba, akammwagia maji Sarah, Sarah akakurupuka na kumkuta Trigger akiwa ameshika ndoo ya maji na bastola. Sarah baada ya kuzinduka na kumkuta Trigger katika hali ile, akajua kabisa Trigger amemmwagia maji ili amzindue.



    Trigger akawa anamuangalia Sarah huku machozi yakimtoka na pua bastola akiwa amemnyooshea Sarah, Trigger akaigeuza bastola na kumrushia Sarah,



    "toka nje, hii nyumba inaanguka sasa hivi" Trigger aliongea huku akilia na kumfanya Sarah ashangae huo wema wa Trigger,



    "Sarah toka nje, nenda nje ujiokoe uende ukatimize ndoto zako" Trigger aliongea huku akilia, hapo huruma ikamuingia Sarah, akasimama huku machozi yakimtoka, alimuonea huruma Trigger kwa namna moto ulivyomfanya, aliungua vibaya, hakuweza kutazamika mara mbili.



    "twende nje, nitakusaidia kutoka" Sarah aliongea kwa upole huku akilia,



    "hata nikitoka sitoweza kukaa muda mrefu, ni lazima nitakufa tu" Trigger aliongea kwa huruma,



    "hapana usiseme hivyo, nimekusamehe kwa kila baya ulilonifanyia, nakuomba tutoke nje" Sarah aliongea,



    "Sarah toka nje, hichi kifo ni haki yangu, wala sitokulaumu" Trigger aliongea kwa hasira huku akimuangalia Sarah,



    "usiseme hivyo, twende nje" Sarah aliongea,



    "hapana, Sarah nenda mama, leo nilikuwa na uwezo wa kukuua, ila sikutaka kufanya hivyo, nilitaka ukakamilishe matakwa yako, pia nilitaka nikuoneshe upande wangu wa pili, mimi ni mzazi na nina mtoto ambaye nampenda sana, hajui wala hawezi kukubali mimi ni mtu mbaya kutokana na jinsi ninavyoishi nae, sasa leo ule upendo nimehamishia kwako" Trigger aliongea kwa huzuni huku akilia na kumfanya Sarah azidi kulia zaidi.



    "bado una nafasi ya kuishi, usikate tamaa" Sarah aliongea kwa huzuni,



    "nafasi ambayo unaona ninayo, naomba niitupe, sitaki kuishi nikiwa katika hali hii" Trigger aliongea kisha akachukua ile ndoo ambayo Sarah alikuwa ameweka petrol, Trigger akajimwagia petrol kisha akaokota kipande cha mbao kilichokuwa na moto na kugusisha katika mwili wake na hapo moto ukamshika tena, Sarah akaanza kulia kwa sauti huku akimtazama Trigger aliyekuwa ametulia huku moto ukazidi kummaliza. Sarah akamnyooshea Trigger bastola na kumlenga kichwa, kisha akaruhusu risasi itoke, risasi ikatua kwenye kichwa cha Trigger na kummaliza pale pale, Sarah hakutaka Trigger ateseke zaidi, alimuonea huruma.



    Na hiyo ndiyo ikawa safari ya mwisho ya Trigger, Sarah alipata hofu sana kila akiuangalia mwili wa Trigger, akakiri kifo cha moto ni kifo kibaya sana, akavuta picha namna wazazi wake walivyokuwa wanaungua, akajikuta machozi yanazidi kumtoka.



    Nyumba ilizidi kuungua, Sarah akageuka nyuma na kugundua hata mlango anaotakiwa kupitia tayari wote umeshika moto, hakuna njia tena, na moto ulizidi kupamba katika kile chumba, Sarah akaiendea ndoo ya maji na kubeba, kisha akamwaga maji mlangoni na kufanya moto upungue kidogo, alafu maji mengine akajimwagia mwilini kisha kwa kasi ya ajabu alipita kwenye ule moto na kuelekea nje, alipotoka ndani ya nyumba fulana yake ilichanwa ilikuwa imeanza kushika moto, akaivua na kuitupa, sasa mtihani mwingine uliomkabili ni kutoka nje akiwa kifua wazi ilihali yeye ni binti.



    "potelea mbali" Sarah aliongea kisha akawa anaelekea upande wa mbele kwenye geti, alitembea mpaka getini na kumkuta yule kijana mlinzi wa getini akiwa amelala, hakuwa na fahamu kutoka muda ule alivyopigwa na Aisha.



    Sarah akamuinamia yule kijana na kumvua fulana, kisha akaivaa yeye. Sarah akataka kufungua geti ili atoke nje, ila alisikia sauti za watu zikiokea nje, na walionekana ni watu wengi, walikuwa ni majirani na wapita njia, walijaa nje ya nyumba ya kambi ya Taita wakishuhudia nyumba ikiteketea.



    Sarah akaamua ahairishe mpango wa kutokea getini, akaona bora atumie njia aliyotumia kuingilia. Sarah akaenda nyuma ya nyumba na na kuukwea ukuta, kisha akaangukia upande wa nyuma ambapo kuna nyumba nyingine, lakini ilionekana hakuna mtu anayeishi katika hiyo nyumba.



    Sarah akasogea karibu na bomba lililokuwepo katika nyumba hiyo na kujaribu kufungulia maji, yakatoka.



    Sarah akaanza kunawa uso wake na sehemu ambazo alihisi ni chafu kutokana na moto aliopambana nao ndani, kisha akaenda mpaka kwenye geti la hiyo nyumba na kujaribu kufungua, akagundua limefungwa, Sarah akarudi nyuma kisha akalifuata lile geti kwa kasi, alipokaribia umbali wa hatua mbili, Sarah aliruka na kulikamata lile geti kwa juu, kisha akajivuta na kuangukia nje, alipotua chini akatupia macho kwenye kambi ya Taita na kuona namna watu walivyojaa wakishuhudia jinsi nyumba inavyoteketea kwa moto.



    Sarah hakutaka kusogea, akaenda zake upande wa kushoto na ile nyumba ikawa ameipa mgongo. Sarah alitembea kwa mwendo wa dakika mbili akapishana na zimamoto, lilikuwa linaelekea upande ambao Sarah ametokea.



    Baada ya kutembea kwa muda Sarah akatoa simu na kuangalia namba anayoitaka, kisha akapiga na simu ikaanza kuita,



    "Aisha upo wapi?" Sarah aliuliza baada ya mtu wa upande wa pili kupokea simu,



    "nipo sehemu moja hivi huku uswazi" Aisha alijibu,



    "upo na huyo afande?" Sarah aliuliza,



    "nipo nae" Aisha alijibu,



    "muachie, angalia namna nzuri ya kumuachia ili asikugeuzie kibao" Sarah alimwambia Aisha,



    "kwanini nimuachie? Huna mpango nae?" Aisha aliuliza,



    "sina tatizo nae, nilitaka umshike ili nimalizane na Trigger kwanza" Sarah alijibu,



    "kwa hiyo Trigger umemalizana nae?" Aisha aliuliza,



    "tayari" Sarah alijibu,



    "poa" Aisha alikata simu na kumgeukia Sajenti Minja ambaye alikuwa akiyafuatilia maongezi yao,



    "vipi?" Sajenti Minja aliuliza kwa wasiwasi baada ya kuona Aisha akimuangalia sana,



    "nataka nikuachie" Aisha aliongea huku akimsogelea Sajenti Minja,



    "sawa, ni jambo jema" Sajenti Minja aliongea huku akifurahi,



    "ila siwezi kukuachia kienyeji, nakujua wewe ni polisi, endapo nitakuachia kienyeji unaweza kunigeuka" Aisha alimtahadharisha Sajenti Minja,



    "sasa unataka uniachiaje?" Sajenti Minja aliuliza kwa wasiwasi, ila Aisha hakujibu, badala yake alimpiga Sajenti Minja ngumi nyepesi iliyotua katika shingo na kumfanya Sajenti Minja apoteze fahamu, kisha Aisha akamfungua na na kuanza kumvuta kumpeleka nje, alimvuta na kumuweka kwenye gari, kisha akaondoka nae na kwenda kumtupa mahali anapopajua yeye.



    **********************



    Strategic alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Taita, akaegesha gari kwa nje kisha akashuka na kuingia ndani moja kwa moja,



    "mbona nakupigia siku hupatikani wewe?" Taita aliuliza kwa hasira,



    "simu ilizimika" Strategic alijibu kwa uoga,



    "Trigger umemkuta?" Taita aliuliza,



    "kwa Dokta Malle sijamkuta Trigger, ila pia nimeenda kambini pia sijajua kama yupo" Strategic alijibu,



    "sasa hujajua kama yupo kwani hukuingia ndani?" Taita aliuliza,



    "sijaingia, nimekuta ile nyumba inaungua, tena moto mbaya ulikuwa unawaka" Strategic alijibu na kumfanya Taita ashtuke,



    "sasa si ungeingia ili ujue ndani kuna nini?" Taita aliuliza kwa hamaki,



    "kwa jinsi nyumba ilivyokuwa imeisha, ndani hakuwezi kubaki kitu, kwa hiyo sikuwa na sababu ya kuingia" Strategic alijibu,



    "ebu twende" Taita aliongea huku akisimama na kuelekea nje na kumfanya Strategic amfuate kwa nyuma.



    Taita alitembea na kutoka nje ya geti na kumpita mlinzi wa getini aliyekuwa amesimama kwa wasiwasi, alimuogopa sana Taita,



    "usiruhusu mtu aingie humu, ila Trigger peke yake" Taita alimwambia mlinzi wa getini,



    "sawa bosi" Mlinzi alijibu kwa ukakamavu na kumfanya Strategic acheke chini chini, Taita akaenda nje na sasa Strategic alikuwa amemfikia mlinzi,



    "nenda kamfungulie Vin, yupo katika chumba cha mzee" Strategic aliongea kwa sauti ndogo na kumfanya mlinzi ashangae,



    "Mimi siruhusiwi kutoka getini" Mlinzi alijibu Kaa sauti ndogo pia, strategic akatoa noti ya elfu kumi na kumrushia mlinzi,



    "unataka miujiza kama iendelee?" Strategic alimuuliza mlinzi na mlinzi akaitikia kwa kichwa kukubsliana nae,



    "kafanye nilichokwambia, hakika utashuhudia muujiza huu wa pesa ukiendelea kukutembelea" Strategic aliongea huku akiondoa na kumuacha mlinzi akiokota ile elfu kumi aliyotupiwa.



    Strategic akaelekea mpaka nje na kumkuta Trigger ameshaingia kwenye gari, strategic akawasha na kuindoa kwa kasi.



    Haikuwachukua muda mrefu sana kufika eneo la tukio, walikuta watu wengi wakiwa wamejaa nje ya nyumba na zaidi zimamoto walikuwa wakiendelea na kazi yao ya kuzima moto.



    Trigger alitelemka kwenye gari na kutaka kuingia moja kwa moja getini, ila askari waliokuwepo walimzuia,



    "mnanizuia kuingia kwenye nyumba yangu?" Taita aliuliza kwa hasira na pia baadhi ya majirani walikuwa wakiwapigia kelele polisi wakimtambulisha Taita ndiye mwenye hiyo nyumba,



    "hatujakuzuia, ngoja zimamoto waruhusu, si unaona mzee bado wanaangaika kuzima?" Askari mmoja alimueleza Taita,



    "wakati najenga sikupangiwa, iweje mnipangie muda wa kuingia?" Taita alihoji kwa hasira,



    "muachieni apite" Sauti ya askari mmoja wa zimamoto iliongea na kufanya askari wa pale getini wamruhusu Taita aingie. Taita alipita ndani ya geti na kukuta moto umeshazimwa ila bado kuna baadhi ya sehemu kulikuwa na moshi mzito,



    "hakuna mtu ndani?" Taita aliuliza,



    "hatujui kwa maana bado hatujakagua, moto ukipoa tutaangalia" Askari wa zimamoto alijibu na kumfanya Taita aanze kuzunguka zunguka huku akiwa na wasiwasi.



    Baada ya nzima moto ulikuwa umepoa kabisa, askari wa zimamoto kwa kushirikiana na wananchi wakaanza kutoa poa lililoangukia ndani na kuangalia kama kuna watu waliongua.



    Baada ya muda mchache waliweza kuupata mwili wa Trigger, ila hakuna mtu aliyeutambua kutokana na kuharibika vibaya, hata Taita mwenyewe hakuweza kuujua.



    "sasa kama wewe mwenye nyumba umeshindwa kumtambua marehemu, au kulikuwa na watu wangapi wanaishi humu?" Askari mmoja aliuliza,



    "ni mlinzi tu pekee, tena mmeniambia mmemkuta getini akiwa hana fahamu. Sasa huyo mlinzi ndio anaujua ukweli" Taita aliongea kwa hasira,



    "sawa, nadhani sisi tumemaliza kazi yetu" Askari wa zimamoto aliongea na kuwahimiza wenzake waondoke na kumuacha Taita akiwa amesimama akiiangalia nyumba yake.



    ,



    "huu mwili unaweza kuwa wa Trigger kweli?, ila Trigger hawezi kufa kizembe" Taita alijiuliza huku akitoka nje, akaingia kwenye gari na kumuamuru Strategic aelekee hospitali ambayo mlinzi wa getini alipelekwa.





    Taita alienda mpaka hospitali na kwenda katika wodi aliyolazwa mlinzi wake wa getini, alimkuta tayari fahamu zimemrejea,



    "ni nani aliyekuwa ndani ya nyumba kabla nyumba haijawaka moto?" Taita aliuliza moja kwa moja bila hata kumjulia hali mlinzi,



    "nyumba haijawaka moto?, nyumba ipi?" Mlinzi aliuliza kwa maana wakati nyumba



    ikiungua yeye alikuwa amepoteza fahamu kwa hiyo hakuna anachojua,



    "wewe vipi?, hujui kuwa nyumba imeungua?" Taita aliuliza kwa hasira,



    "mzee mimi nilipigwa na mwanamke ambaye simjui, nikspoteza fahamu, kwa hiyo sijui kitu kingine kilichoendelea" Mlinzi wa getini alijibu na kumfanya Taita ajiulize huyo mwanamke ni nani?



    "huyo mwanamke yupoje?" Taita aliuliza,



    "ana mwili wa wastani, ana nywele ndefu na ni mweusi" Mlinzi alijibu na kumfanya Taita ajiulize huyo mtu ni nani? Kwa maana Sarah hayupo hivyo, Sarah ni mwenye kiasi na mwili wake ni mwembamba,



    "sasa huyo mwanamke alikuwa anataka nini? Au alikupiga tu bila sababu?" Taita aliuliza,



    "alikuwa anamuulizia Trigger, na Trigger alinizuia nisiruhusu mtu aingie ndani, kwa hiyo nikagoma kumruhusu huyo mwanamke kuingia, ndio akanipiga" Mlinzi alijibu,



    "Trigger alikuwa ndani?" Taita aliuliza kwa wasiwasi,



    "ndio, alikuwa na wanaume watatu ambao alikuwa amewateka" Mlinzi alijibu na kumfanya Taita achanfanyikiwe, maana alizidi kuvurugwa na asijue ni nani aliyeungua,



    "wapoje hao wanaume?" Taita aliuliza,



    "mzee mmoja na vijana wawili" Mlinzi alijibu na kumfanya Taita ageuke na kuondoka, maana aliona mlinzi anamvuruga tu.



    *************



    Sajenti Minja fahamu zilipomrudia, sehemu ya kwanza aliyofikiria kwenda ni katika kambi ya Taita, maana hali aliyoiacha haikuwa hali salama.



    Sajenti Minja alisimamisha boda boda iliyomchukua mpaka eneo lile la kambi ya Taita, aliukuta umati wa watu ukiwa unatawanyika baada ya moto kuwa umezimika, hata kikosi cha zimamoto hakukikuta, kilikuwa kimeshaondoka, kilichomshangaza Sajenti Minja ni Kukuta ile nyumba ikiwa imeteketea kabisa wakati yeye aliiacha ikiwa nzima kabisa, sasa swali alilojiuliza ni ule moto ni wa kuwashwa na mtu au umetokea bahati mbaya?



    "aisee ndani ya nyumba kulikuwa na mtu kweli?" Sajenti Minja alimuuliza dada mmoja aliyekuwa jirani nae,



    "wameukuta mwili wa mtu" Yule dada alijibu kwa huzuni,



    "mwanamke au mwanaume?" Sajenti Minja aliuliza,



    "wameukuta wa mwanaume" yule dada alijibu na kumfanya Sajenti Minja ahisi huenda Sarah ameamua kumchoma moto Trigger.



    Sajenti Minja akatoka pale na moja kwa moja akaenda kwa Dokta Innocent Malle, akamkuta akiwa na Kijana wake, Sajenti Minja akawajulisha wanatakiwa wahame pale kwa muda kwa ajili ya usalama wao. Kisha Sajenti Minja akachukua gari yake na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Taita, akaingia moja kwa moja mpaka ndani na kumkuta Vin akiwa amekaa sebuleni huku akiwa bize kubonyeza simu,



    "mzee yupo wapi?" Sajenti Minja aliuliza baada ya kuingia,



    "ametoka, vipi?" Vin aliuliza,



    "mzee nadhani yupo hatarini, muda wowote Sarah anaweza kumdhuru" Sajenti Minja aliongea,



    "kwanini unasema hivyo?" Vin aliuliza,



    "Sarah ametoka kumuua Trigger muda si mrefu, tena kile ni kifo kibaya" Sajenti Minja aliongea kwa masikitiko,..



    .

    .

    ..



    "mzee nampigia hapokei simu, ila sitokubali Sarah amuue, nitamlinda mzee kwa nguvu zote, yule ni baba yangu hata kama sio wa halali" Vin aliongea kwa ukali,



    "ila mimi hapa nimekuja kumkamata mzee wako, kwa maana baada ya kufuatilia kila kitu kuhusu vifo vya wazazi wako na Sarah nadhani nimeshakusanya ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mzee wako" Sajenti Minja aliongea,



    "hapana, hiyo kesi si inanihusu mimi kama mwenye wazazi waliouawa? Basi nasema nimemsamehe Taita, sitaki umkamate" Vin aliongea kwa ukali,



    "usichukulie hasira, hii kesi ilifunguliwa na familia ya baba yenu, kwa hiyo mwenye uwezo wa kuifunga hii kesi ni babu yenu tu, pia nadhani endapo nitamkamata Taita, itakuwa salama kwake kwa kuwa kukaa kwake urahiani ni kukaa karibu na kifo, kwa maana inakuwa rahisi kwa Sarah kumfikia" Sajenti Minja alijaribu kumueleza Vin,



    "hapana, usitumie kigezo hicho kumtia hatiani mzee wangu" Vin aliongea kwa kujiamini, na kipindi hicho Taita alikuwa amerudi na amekaa nyuma ya mlango akisikiliza maongezi kati ya Vin na Sajenti Minja.



    "usibishane na sheria wewe, na hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, Taita lazima nimkamate na akajibu mashtaka" Sajenti Minja aliongea kwa kujiamini pia,



    "kwa ushahidi Upi?" Vin alihoji,



    "ngoja nikujibu kwa kifupi tu, Sarah amenipa ushahidi wa maneno yote aliyoongea Harry kabla hajafa, pia kuna mtu anaitwa Strategic, amenipa maongezi yake na Trigger, aliyarekodi kupitia lap top yako, pia leo muda mfupi kabla Trigger hajafa, aliongea ukweli wote wakati akiwa ametuteka'" Sajenti Minja aliongea na kumfanya Vin achoke,



    "Strategic nae amekupa ushahidi? Mbwa wangu mwenyewe leo amening'ata?" Vin aliongea kwa upole na wakati huo sasa Taita aliamua ajitokeze sebuleni,



    "Trigger amekufa? Au nimesikia vibaya?" Taita aliuliza huku akimtazama Sajenti Minja,



    "ndio amekufa, na wewe upo hatarini pia" Sajenti Minja alijibu,



    "mzee ebu ondoka nchini, ikiwezekana chukua hata ndege ya kukodi muda huu" Vin alimwambia Taita,



    "hiyo haiwezekani, mzee upo chini ya ulinzi" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Taita,



    "kwa kosa gani?" Taita aliuliza kwa dharau,



    '"kwa mauaji yaliyotokea miaka ishirini iliyopita, uliua familia ya Isack kwa kuiteketeza na moto" Sajenti Minja aliongea,



    "mzee, huyu anatuvuruga tu, mzee ingia ndani uangalie vitu muhimu na uondoke haraka, hii nchi haifai tena" Vin aliongea kwa msisitizo na kufanya Taita aanze kwenda chumbani kuchukua vitu vyake muhimu,



    "simama mzee" Sajenti Minja aliongea huku akiichomoa bastola yake na kumuelekezea Taita, Vin akaona akifanya uzembe mzee wake atakamatwa, Vin akarusha teke nw kumpiga Sajenti Minja, Sajenti Minja akapepesuka, kisha Vin akaokota mto wa kochi na kuurusha kuelekea kwenye mkono wa Sajenti Minja, mto ukaipiga ile bastola na kudondoka chini, Vin akachomoa bastola yake na kumuelekezea Sajenti Minja,



    "mzee harakisha uondoke" Vin aliongea baada ya kumzidi ujanja Sajenti Minja.



    Taita akaingia chumbani na kisha alirudi sebuleni baada ya muda mchache huku mkononi akiwa na begi dogo,



    "Vin mwanangu tuondoke" Taita aliongea huku akimtazama Vin,



    "mzee wewe nenda, kwa hali ilivyo hapa, nikishusha bastola chini utakamatwa" Vin alimwambia Taita,



    "mpige risasi huyo ili tuondoke, sitaki nikuache mwanangu" Taita aliongea kwa upole.



    "hapana mzee, siwezi kumpiga risasi, cha muhimu wahi kuondoka na uende mbali, ukifika nitaharifu" Vin aliongea ila Taita aliweka msimamo waondoke wote, Vin alimbembeleza na mwisho Taita akakubali kuondoka, alimsogelea Vin na kumbusu katika paji la uso wake, kisha akageuka na kuanza kuondoka,



    "mzee, ondoka peke yako, usimuamini mtu yoyote, hata Strategic" Vin alimsisitizia Taita ambaye aliitikia kwa kichwa na kisha akageuka na kutoka nje, sebuleni akawaacha Sajenti Minja ambaye alikuwa mateka wa Vin.



    "elewa kuwa hili unalofanya ni kosa, unamsaidia muharifu kutoroka" Sajenti Minja alimwambia Vin ambaye alikuwa ametulia na bastola yake mkononi,



    "sawa, acha nifanye kosa kwa ajili ya kumsaidia mtu anayenipenda" Vin alijibu na kumfanya Sajenti Minja acheke.



    Baada ya nusu saa ya kumshikia bastola Sajenti Minja, Vin aliamini baba yake atakuwa ameshaondoka na kufika mbali, Vin akateremsha bastola na kuitupa chini, kisha akanyoosha mikono juu kujisalimisha kwa Sajenti Minja.



    Sajenti Minja akashangaa, ila kwa haraka akamkimbilia bastola na kuikota, kisha akamfuata Vin na kumfunga pingu, kisha akaanza kutoka nae nje.



    Alivyotoka nje, Sajenti Minja akatoa simu mfukoni na kumpigia Sarah, aliona huyo ndio mtu mzuri ambaye anaweza kumsadia kumkamata Taita kwa muda huo.



    Sajenti Minja akatoa akapiga simu,



    "sarah naomba unisikie kwa umakini mkubwa, nina ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Taita, sasa basi hapa nipo kwake, Taita amenitoroka na nahisi ameelekea uwanja wa ndege, fanya ukamuangalie na ukimpata nitaharifu, usimfanye chohote" Sajenti Minja aliongea kwa kusihi,



    "kama mmeamua kumfungulia kesi sawa, ngoja niende kumuangalia" Sarah aliongea kwa utulivu na kukata simu.



    Muda huo wa jioni ndio muda ambao Sarah alikuwa amefika nyumbani kwake kutoka katika kambi ya Taita. Baada ya Sarah kupokea taharifa hizo kutoka kwa Sajenti Minja, alichofanya ni kuingia ndani na kubadili nguo, alivaa suruali nyeusi na koti jeusi la kike, kisha ile mask yake akaitia ndani ya mfuko wa koti, kisha akamuaga Dokta Pendo na babu yake na kuondoka zake huku akifurahi kitendo cha Sajenti Minja kuamua kumfungulia kesi Taita, aliamini haki itatendeka.



    Ilimchukua muda mchache tu kwa Sarah kufika nje ya majengo ya Kiwanja cha ndege, aliamua kutumia usafiri wa boda boda kwa maana ndio ulikuwa wa haraka. Sarah alivyofika nje aliangaza kila upande aone kama anaweza kuiona gari yoyote ya Taita, kwa maana alikariri asilimia tisini ya magari ya Taita. Baada ya kuangalia kwa muda, hakuweza kuona gari katika eneo hilo.



    Sarah hakuwa na uhakika kama ni kweli Taita anaweza kuwa yupo au hayupo, mwisho akajiaminisha huenda Taita labda alikuja na gari nyingine ambayo Sarah haijui, Sarah akaamua aingie ndani ya jengo huku akiamini labda Taita yupo ndani, ila wakati akiinua mguu ili aanze kuelekea ndani, alishuhudia gari ya Taita ikiegeshwa, Sarah akasita na kuanza kuifuata kwa kujificha ficha, na kwa kuwa giza lilikuwa linaanza kushika kasi, haikuwa rahisi kwa Taita kumtambua Sarah kwa urahisi.



    Taita akafungua mlango, akashuka na begi lake, mara ghafla akawekewa bastola kichwani na Sarah,



    "rudi ndani ya gari mjomba" Sarah aliongea huku akimuangalia, Taita akataka kupiga kelele, Sarah akamuwahi kwa kumpiga ngumi kali ya kisogo, Taita akalegea na kuanguka, Sarah akamuingiza ndani ya gari kisha akamvua koti la suti na kulichana, kisha akatengeneza kamba na kumfunga mikono, kisha akamfunga kwa kumuambatanisha na kiti cha gari, Sarah akaingia kwenye gari na kuliondoa.



    Baada ya muda mchache Taita akazinduka na kujikuta na kamba mwilini,



    "unaenda kuniua?" Taita aliuliza,



    "hapana, nakupeleka polisi ili sheria ifuate mkondo wake" Sarah alijibu na kumfanya Taita acheke,



    "sheria za nchi gani? Sheria za hii nchi zinafuata mkondo wa pesa, wewe unadhani nikipelekwa mahakamani nitafungwa" Taita aliuliza huku akicheka,



    "utafungwa tu, ushahidi si upo" Sarah alijibu,



    "ningefungwa siku nyingi tu kwa maana hata madawa ya kulevya nimekamatwa nayo mara nyingi tu, ila naachiwa, we unadhani serikali inaweza kumfunga mtu anayoisaidia fedha za kufanya mambo yao?" Taita aliuliza kwa dharau na kumfanya Sarah sasa abadili muelekeo wa gari, aliona ni kweli Taita hawezi kufungwa.



    Sarah aliendesha gari mpaka nyumbani kwa Taita, kisha akashuka na kumkuta mlinzi yupo getini, Sarah akampiga mlinzi na kumfanya apoteze fahamu, Sarah akamshusha Taita na kumuingiza ndani, akamfunga kwenye kiti kama alivyomfanya Trigger, kisha yeye akakaa kwenye kochi,



    "kazi nzuri" Taita aliongea huku akitabasamu,



    "sipo hapa kwa ajili ya kuongea, nimekuja kuitimisha agano" Sarah aliongea huku akivaa kinyago chake,



    "agano? Agano uliwekeana na nani?" Taita aliuliza,



    "unaikumbuka ile sala niliyoomba nikiwa mdogo? Leo hii inatimia" Sarah aliongea huku akisimama,



    "unawaka kama moto? Ebu waka nikuone" Taita aliongea kwa dharau na kumfanya Sarah atanue mikono yake, kisha akaikutanisha na moto ukatokea kwenye viganja vya mikono yake, Taita akashangaa,



    "umeona sasa?" Sarah aliuliza huku akicheka na kumfanya Taita ashikwe na bumbuwazi, Sarah akamsogelea Taita na kuuweka ule moto kichwani, Taita akaanza kuungua, Sarah akawa anamtazama tu namna Taita anavyoangaika, kisha Sarah akauzima ule moto,



    "moto ukiwaka kichwani utakufa mapema" Sarah aliongea na kisha akaanza kuchana makochi ya sofa na kuanza kumfunga nayo Taita mwilini, aliporidhika akawasha moto, Taita akaanza kuungua na kipindi hicho Sarah akaanza kuwasha moto kwenye kila chumba, nyumba nzima ikawa na moto sasa, Sarah akarudi na kumuangalia Taita namna anavyoungua.



    Mkononi kwa Sarah alikuwa na pete ambayo ndio ilikuwa inatoa moto, alipewa na jeshi kama silaha pindi awapo kwenye hali ngumu.



    ****************



    Sajenti Minja alifika polisi huku akiwa na vin, akamuingiza kwenye ofisi yake kwa ajili ya kumuhoji, ila kabla hawajaanza mahojiano, alifika mlinzi wa getini kwa Taita na kuwapa taharifa kuwa Taita ametekwa na mtekaji amejifungia ndani ya nyumba, Sajenti Minja akataka aende ila mkuu wa polisi akamzuia,



    "kila siku unashindwa kumkamata huyo dada, leo hiyo kazi nitafanya mimi" Mkuu wa polisi aliongea kisha akatoka na askari katika gari tano, wote walikuwa na silaha.



    Wale askari walifika mpaka nyumba kwa Taita na kukuta nyumba nzima inawaka moto na katika dirisha la sebuleni alisimama Sarah akiwa anawaangalia, kisha alivyoona ni askari, Sarah akashusha pazia.



    Askari wakaamua watoe tangazo kuwa mtu yoyote aliyepo ndani ajisalimishe, lakini Sarah hakutaka atoke, badala yake alikuwa anatafuta njia ya kutoroka.



    Sarah akatokea mlango wa nyuma, ila alipofungua mlango tu akakoswa na risasi, akagundua ameshazungukwa kila upande, Sarah akarudi mpaka dirishani na kutoa bastola yake, alikuwa ameshapaniki kwa kitendo cha kukoswa na risasi, Sarah akafyatua risasi iliyompiga askari mmoja na kuanguka chini.



    mkuu wa polisi akaamuru vijana wake waishambulie, polisi wakaanza kufyatua risasi kuelekea dirishani, moja ikampata Sarah kifuani na kuanguka chini, huku risasi nyingine zilimpiga Taita aliyekuwa anafuka moshi baada ya moto kumteketeza, baada ya zile risasi kumpiga Taita, alikufa pale pale juu ya kiti.



    Nje mkuu wa polisi akawaamuru askari wawili wasogee dirishani wakaangalie kama wamemuua mtekaji, wale askari wawili wakasogea mpaka dirishani, ila Sarah akawapiga risasi na wakafa palepale.



    Mkuu wa polisi akaamuru tena washambulie, askari wakapiga tena risasi mfululizo na mbili zikampiga Sarah, moja ilimpiga Sarah mkononi na nyingine ikampiga kwenye mbavu, Sarah akaanguka chini na bastola ikamtoka, Sarah akawa anapumua kwa shida huku akiwa na mawazo ya kujisalimisha, kwa maana aliona ameshazidiwa, aliona akiendelea kupambana atafia ndani kwa kuwa alishazungukwa.



    Kwa upande wa nje, mkuu wa polisi aliomba msaada wa jeshi, aliamini inawezekana mtu wanaepambana nae sio wa kawaida, na muda huo Vin na Sajenti Minja walikuwa wanawasili.



    Vin alivyoona hali ilivyo, alianza kulia tu, aliamini Taita hawezi kuwa mzima kwa namna ule moto ulivyokuwa unawaka.



    Baada ya muda mchache, wanajeshi walifika, wakawaambia askari warudi nyuma, kisha wao wakakaa mstari wa mbele, na amri ikatolewa kuwa lazima huyo mtekaji auawe kwa maana ameshaua askari watatu, wanajeshi wakajipanga kushambulia, na walikuwa na mabomu ya sumu, ndio walipanga kuyarusha ndani.



    Sarah aliweza kuona kila kitu kupitia dirishani, alikata tamaa, aliona njia bora ni kujisalimisha,



    Wanajeshi wakarusha bomu, likaingia kupitia dirishani, kisha wakasubiri kwa muda, mara ghafla mlango wa mbele ukafunguliwa, akatoka Sarah mikono ikiwa juu, ila kutokana na amri waliyopewa wanajeshi, walianza kumpiga risasi nyingi mfululizo na asilimia tisini ya hizo risasi zilimpiga kuanzia kichwani mpaka shingoni.



    Sarah akapiga magoti, lakini bado waliendelea kumpiga risasi, mwisho Sarah akaanguka chini na kukata roho huku kile kinyago chake kikimuachia na kuanguka pembezoni mwake.



    Kiongozi wa jeshi akaonesha ishara na wanajeshi wakaacha kupiga risasi, kisha kiongozi wa jeshi na polisi wakaisogelea ile maiti na kuigeuza, risasi zilikuwa zimemuharibu vibaya uso wake, alikuwa hatizamiki mara mbili.



    Vin alikuwa analia huku akisikitika kuwapoteza watu wawili kwa wakati mmoja, yaani Taita, na Sarah ambaye ni dada yake.



    Sasa askari wote wakaruhusiwa kwenda kuuangalia ule mwili, hapo Sajenti Minja ndipo akapata nafasi ya kuuangalia ule mwili,



    "umekufa, ila hukustahili kufa, ungeachwa hai ili ulisaidie taifa, ni mtu muhimu sana wewe" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni, kisha akaondoka huku akicheka.



    Vin aliendelea kulia huku akiiangalia ile cheni ya Sarah shingoni, hakika ilimuuma, aliendelea kuuangalia ule mwili wa dada yake uliokuwa umelala chini,



    "tuondoke, una kesi ya kujibu" Sajenti Minja alirudi na kumchukua Vin ambaye alikuwa na uchungu mkuu.



    Huku nyuma mwili ule ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa, huo ndio ukawa mwisho wa Sarah na Taita.







    Siku iliyofuata asubuhi, Sajenti Minja aliamkia hospitali, kuna kitu alikuwa anakihisi, ndio maana baada ya kuuangalia mwili wa Sarah siku iliyopita, alicheka ingawa aliongea maneno mazito.



    Sajenti Minja alifika hospitali na kuonana na Daktari, bahati nzuri daktari wa zamu siku hiyo alikuwa ni Dokta Pendo, wakasalimiana,



    "mmeshafanyia uchunguzi huo mwili wa Sarah?" Sajenti Minja alimuuliza Dokta Pendo,



    "tayari, kila kitu kipo kwenye ripoti, ipo ofisi ya Dokta mkuu" Dokta Pendo alijibu, ila kilichomshangaza Sajenti Minja ni kuona Dokta hana hata uchungu wakati aliekufa ni rafiki yake.



    Sajenti Minja akaelekea ofisi ya Dokta mkuu na kuchukua ripoti ya ya mwili wa Sarah, kisha akaondoka huku akiwa hana imani na ule mwili unaosemekana ni wa Sarah,.



    Wakati Sajenti Minja akiwa anatoka, alisikia akiitwa kwa nyuma, alipogeuka alikutana na dokta Pendo,



    "samahani, una namba ya Vin?" Dokta Pendo alimuuliza Sajenti Minja,



    "ndio" Sajenti Minja alijibu,



    "naomba unipatie" Dokta Pendo aliongea na kisha Sajenti Minja akatoa simu na kumsomea Dokta Pendo zile namba za Vin, Dokta Pendo akanakiri kwenye simu yake na kisha Sajenti Minja akaondoka huku akiwa na wasiwasi sana juu ya mwili wa Sarah.



    Dokta Pendo baada ya kuridhika kuwa Sajenti Minja ameshaondoka eneo lile, aliipiga ile namba ambayo alipewa na Sajenti Minja, simu ikaanza kuita,



    "hallow, naongea na Vin?" Dokta Pendo aliuliza baada ya simu kupokelewa,



    "yeah, ndo mimi" Vin alijibu kwa sauti ya upole,



    "unaweza kuonana na mimi leo?" Dokta Pendo aliuliza,



    "wewe ni nani kwanza?" Vin aliuliza,



    ,



    "ooh, kumbe sijajitambulisha? Mimi ni Dokta wa hii hospitali hapa yenye mwili wa dada yako Sarah" Dokta Pendo aliongea,



    "kuna nini?" Vin aliuliza,



    "tuonane kwanza, utajua tu" Dokta Pendo aliongea,



    "nitakuja baadae hapo hospitali" Vin aliongea,



    "hapana, sitaki tukutane hospitali, njoo kanisa kuu la roman, mjini nitakuwepo hapo saa moja jioni, ukifika ingia moja kwa moja ndani ya kanisa" Dokta Pendo alitoa maelezo,



    "kwanini kanisani?" Vin aliuliza,



    "nahitaji tukae eneo lenye amani ili tuongee vizuri" Dokta Pendo aliongea,



    "sawa, nitakuja" Vin aliongea na kukata simu, kisha Dokta Pendo akashusha pumzi ndefu na kuirudisha simu mfukoni. Kisha akaenda kuendelea na kazi.



    **************



    Sajenti Minja aliibeba ile report mpaka ofisini kwa mkuu wake, mkuu wa polisi akaifungua ile report na kuanza kuisoma, aliisoma kwa muda wa dakika ishirini kisha akavua miwani na ile report akairudisha kwenye bahasha.



    "ujue huyu mwanamke hajaua polisi watatu pekee?" Mkuu wa polisi aliongea huku akimtazama Sajenti Minja,



    "kuna wengine tena?" Sajenti Minja aliuliza,



    "kule ambapo kuna mlango wa nyuma, tumekuta polisi wote wamekufa, na pia kulikuwa na michirizi ya damu iliyoenea mpaka juu ya ukuta" Mkuu wa polisi aliongea,



    "hapo una maana gani?" Sajenti Minja aliuliza,



    "inawezekana watekaji walikuwa wawili, ila mmoja ametoroka" Mkuu wa polisi aliongea na kumfanya Sajenti Minja aanze kuziamini hisia zake juu ya ule wa Sarah,



    "kwa hiyo unataka kusema tumtafute huyo mtekaji tena?" Sajenti Minja aliuliza,



    "tena hiyo kazi ifanyike usiri mkubwa, yaani ni mimi na wewe, hatakiwi mtu mwingine kujua hii habari" Mkuu wa polisi aliongea,



    "sawa mkuu" Sajenti Minja aliongea, kisha mkuu wa polisi akainuka na kutoka nje ya ofisi na kumuacha Sajenti Minja akicheka peke yake.



    Sajenti Minja alikaa kwenye ile ofisi kama dakika tano hivi, kisha akainuka na kuelekea nje, akaingia kwenye gari na kurudi hospitali, safari hii alirudi kama mpelelezi, sio kama mtu aliyefuata report.



    Sajenti Minja baada ya kufika eneo la hospital, aliingia ndani ya jengo na lengo lake kubwa lilikuwa ni kutaka kujua kama Dokta Pendo bado yupo hapo..



    Baada ya Sajenti Minja kukagua kama dakika kumi, aliweza kugundua kuwa Dokta Pendo bado yupo. Sajenti Minja akatoka nje na kuingia kwenye gari lake, kisha akachukua gazeti na kuanza kusoma, kila mtu aliyekuwa anatoka ndani ya jengo la hospitali, Sajenti Minja alikuwa akimuangalia.



    Baada ya masaa matato, Sajenti Minja alimshuhudia Dokta Pendo akitoka, kisha Dokta Pendo akaingia kwenye gari dogo na kuondoka, Sajenti Minja akaanza kuifuatilia ile gari.



    Dokta Pendo aliendesha gari bila kufahamu kama anafuatiliwa, gari ilienda mpaka kwenye nyumba ya Sarah, kisha Dokta Pendo akatelemka na kuingia ndani ya geti.



    Sajenti Minja kama kawaida yake akaegesha gari kwa mbali na kusubiri huku akijiwekea muda kuwa baada ya saa kadhaa atatelemka na kwenda kuchunguza kwa umakini zaidi.



    Saa la kwanza likaisha, saa la pili likakatika, la tatu pia. Saa la nne likiwa mwishoni bila kuona mtu akiingia wala kutoka, Sajenti Minja akafungua mlango ili atoke, ila kabla hajashusha hata mguu, alishuhudia geti la nyumba ya Sarah likifunguliwa, Sajenti Minja ikambidi afunge mlango wa gari na kutupa macho getini kuona nani anaetoka.



    Alimshuhudia Dokta Pendo akitoka huku akiwa ameongozana na babu yake Sarah, walionekana wakiongea na kucheka kwa furaha, ila Sajenti Minja hakuweza kujua wanachoongea kwa kuwa alikuwa mbali,



    "Sarah amekufa kweli? Mbona wanaongea na kufurahi?" Sajenti Minja alijiuliza huku akiiangalia gari waliyopanda Dokta Pendo na babu yake, ile gari iligeuzwa na kisha ikawa inaondoka kuelekea upande aliopo Sajenti Minja, Sajenti Minja kuona hivyo, akalala kwenye siti ili wasimuone, ile gari ikapita na kisha Sajenti Minja akawasha gari yake na kuigeuza, akaanza tena kuifuatilia ile gari.



    ****************



    Mishale ya saa moja usiku, Vin alitelemka Katika gari nje ya kanisa, kisha kwa hatua za haraka akawa anaelekea ndani ya kanisa, alifika na kuingia ndani, kisha akasimama nyuma ya kanisa na kuangaza macho, hakuweza kumuona mtu mwingine isipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa akibandua karatasi sehemu tofauti ndani ya kanisa, alikuwa akibandua kwa kufuata mstari kwa maana karatasi zilikuwa nyingi, Vin akatupa jicho kwenye karatasi moja iliyopo pembeni yake, ilionekana kufanana na zile karatasi zinazoondolewa na yule mwanamke.



    Vin akatupia jicho ile karatasi na kuisoma,



    "eee Mungu naomba nikiwa mkubwa niwe nawaka kama moto"



    "sala hii iliombwa na mtoto mdogo aitwae Sarah Isack mnamo tarehe //-//-//"



    Vin akajikuta anashangaa na kumtupia jicho yule mwanamke, kisha yule mwanamke nae akamtupia jicho Vin, Vin akazidi kushangaa kwa maana yule mwanamke alikuwa ni Aisha,



    "itoe hiyo karatasi na uje nayo huku" Aisha aliongea na kugeuka kisha akaelekea benchi la mbele na kukaa.



    Vin akaitoa ile karatasi na kwenda nayo moja kwa moja mpaka alipokaa Aisha na kisha akampatia ile karatasi,



    "Mimi ndiye niliyetaka uje hapa, Kaa hapo" Aisha aliongea na kumfanya Vin ashangae,



    "kuna nini?" Vin aliuliza huku akikaa,



    "pole kwa msiba wa baba yako, nadhani umeumia sana kwa hilo" Aisha aliongea kwa huzuni,



    "uchungu lazima uwepo, nimeumia kwa kweli, ila sina chuki dhidi ya dada yangu Sarah, ingawa amefanya hayo yote, ila nimeumia sana kwa namna alivyokufa, sikutaka afe, niliamini yeye ni mtu pekee mwenye upendo wa dhati kwangu" Vin aliongea kwa hisia,



    "ile siku ya hilo tukio hata mimi nilifanikiwa kuingia ndani ya ule moto kuja kumuokoa sarah" Aisha aliongea na kumfanya Vin ashangae,



    "kwanini hukumuokoa sasa?" Vin aliuliza kwa pupa,



    "ilikuwa hivi, siku ile nilifika pale nikiwa na mtoto wa Trigger, tutakuta askari wamejaa mpaka kule nyuma ya nyumba, sasa itabidi tupambane nao, mimi na mtoto wa Trigger tukafanimiwa kuingia ndani, tukakuta Sarah ameshapigwa risasi tatu, tukambeba ili tutoke nae, tukakuta kule nyuma askari wengine wameongezeka, ikabidi tumuweke Sarah chini kwa maana alikuwa yupo kwenye hali mbaya, kisha mimi na mtoto wa Trigger tukaanza kupambana, mwisho askari tukawapunguza, tukakubaliana mimi nimbebe Sarah kisha mtoto wa Trigger atanilinda kwa kuendelea kuwapiga risasi askari wachache waliobaki.



    Ila mtoto wa Trigger akasema njia rahisi zaidi ya kumsaidia Sarah baada ya kutoka, ni yeye mtoto wa Trigger kujisalimisha kwa maana polisi hawatoendelea kumtafuta Sarah kwa maana tulikuwa na wasiwasi huenda polisi wetakuwa wamewekwa njia zote za mtaa ule, basi tukakubaliana hivyo na kisha kile kinyago cha Sarah na mkufu nikampatia yule binti, kisha nikambeba Sarah na kutoka nae nje huku yule binti akipambana na askari kadhaa ambao wangeniletea madhara.



    Nikafanikiwa kutoka na Sarah na kisha nikampeleka kwenye gari huku nikiwa na imani yule binti wa Trigger atakuwa amejisalimisha na nikapanga nitaenda kumuokoa usiku mkubwa, ila nikashangaa kusikia wanajeshi wamemuua yule binti" Aisha alimaliza kuongea kwa huzuni,



    "kwa hiyo Sarah yupo hai?" Vin aliuliza,



    "Sarah yupo" Aisha aliongea na kumfanya Vin apate furaha upya,



    "yupo wapi?" Vin aliuliza,



    "kabla sijakujibu, Sarah ameniagiza kuwa huo mwili wa huyo binti wa Trigger, uchukue na uuzike kwa heshima, jina la huyo binti anaitwa Sarah, hilo ni jina alilopewa na Taita, ni jina la bibi yao Taita, bibi yao Taita ndio aliowazaa baba yake Taita na mama yenu aliyeitwa Margret" Aisha aliongea,



    "nitafanya hivyo, je Sarah yupo wapi?" Vin aliuliza,



    "twende nikupeleke" Aisha huku Akiinuka na zile karatasi, Aisha akaelekea moja kwa moja mpaka kwenye shimo la taka na kuzitupa zile karatasi na kisha akazichoma moto, baada ya hapo akaingia kwenye gari la Vin na wakaanza safari, walikuwa wanaenda Kiwanja cha ndege.



    Vin ilimbidi aendeshe gari kwa mwendo mkali ili kuiwahi ndege, walifika uwanjani na kisha wakatelemka na kuingia ndani ya jengo, kwa mbali Vin aliweza kumuona Sarah akiwa anaongea na dokta Pendo na mzee asiyemfahamu, Vin ikambidi akimbie kumuwahi Sarah, alipomfikia alimkumbatia kwa hisia,



    "nakupenda sana Sarah" Vin aliongea kwa hisia huku akitokwa na machozi,



    "nakupenda sana Sebastian isack" Sarah alijibu huku pia machozi yakimtoka, kisha wakaachiana na Sarah akamtambulisha Vin kwa babu yao, basi furaha ikaongezeka maradufu,



    "ila huyu mzee naenda nae uingereza, atarudi baada ya miezi miwili" Sarah alimwambia Vin,



    "na mimi nitakuja huko kwa ajili yako, nahitaji muda wa kukaa pamoja na nyinyi, baada ya wiki mbili nitakuja" Vin aliongea na wakati tangazo lilisikika likiwataka abiria wanaoenda uingereza kupitia Kenya waende wakafanyiwe ukaguzi ili waingie kwenye ndege, Sarah na babu yake wakaagana na watu pale, kisha Sarah akamsogelea Aisha,



    "kuna gari range Rover nyeusi, Dokta Pendo atakupatia utembelee, alafu Vin akija uingereza, uje naye" Sarah aliongea huku akiwa amemkumbatia Aisha,



    "usijali" Aisha alijibu huku akitabasamu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya lisaa limoja, ndege aliyopanda Sarah iliruka na kuiacha ardhi ya Tanzania.



    Vin, Aisha na Dokta Pendo wakatoka nje, kisha Vin akaagana nao na kuingia ndani ya gari na kuondoka, pia Aisha na Dokta Pendo wakaingia kwenye gari lao na wakaondoka.



    Pale kwenye uwanja wa ndege kulikuwa na mwanaume akiyafuatilia yale matukio kwa umakini mkubwa, alikuwa ni Sajenti Minja, baada ya kila mtu kuondoka eneo lile Sajenti Minja alitabasamu na kuwasha gari yake,



    "hakuna cha kufuatilia, Sarah kaondoka na mambo yamefika mwisho" Sajenti Minja aliongea na kuiondoa gari yake kuelekea upande tofauti kabisa na ule walioondokea wakina Aisha.



    ***********MWISHO************


0 comments:

Post a Comment

Blog