Search This Blog

Friday, 30 December 2022

HEKAHEKA MSITUNI - 5

    


Simulizi : Hekaheka Msituni 


Sehemu Ya Tano (5)


“Sasa tunafanyaje hapa?” Inspekta Tom Green aliuliza.

“Tunahitaji boti” Latoya aliongea.

SASA ENDELEA

“Tutaipata wapi maana muda unazidi kusonga mbele na nina imani wale jamaa kule kambini watakuwa wameligundua hili na watakuwa tayari wameanza kutusaka?” Inspekta Tom Green aliongea akiuliza.

“Ngoja nichunguze mazingira” Latoya aliongea.
Latoya alianza kuzunguzunguka ukingoni mwa mto akitafuta kama anaweza kupata chombo ambacho kingewawezesha kusafari kwa maji.

“Heeeeey!”

Latoya alipiga kelele akimwita Inspekta Tom Green upande ule ambako alikuwako. Inspekta Tom Green alimbeba Martin na kuanza kwenda kule alikokuwa Latoya.

“Tuna mtumbwi hapa. Nadhani utatufaa” Latoya aliongea akimwonyesha Inspekta Tom Green mtumbwi uliokuwa ukingoni mwa mto.

“Safi sana!” Inspekta Tom Green aliongea huku uso wake ukionyesha tabasamu la furaha. Alimpakia Martin Samweli haraka haraka.

Baadaye Latoya naye alipakiwa na kisha mtumbwi ulianza kuongozwa majini. Safari iliendelea kwa muda mrefu huku Inspekta Tom Green na Latoya wakiwa makini kujikinga na hatari yoyote ambayo ingetokea.

“Mwanipeleka wapi? Ninyi ni akina nani?” Martin Samweli aliuliza. Kwa sasa alikuwa amerejewa na fahamu baada ya kuzimia kwa muda mrefu sana.

“Nadhani habari zetu ulikwishazipata tangu hapo awali. Sina haja ya kurudia tena kuongea kitu ambacho nilikwishakiongea!” Latoya aliongea.

Hapo ndipo kumbukumbu za Martin Samweli zilipomrejea. Alikumbuka kila kitu toka alipovamiwa kule kambini na huyu mwanamke.

“Mmejipalia makaa. Hamtafika kokote kabla Kanali Edson hajawanasa” Martin Samweli aliongea.

“Sisi ni watu tusiokamatika. Safari hii huyo kamanda wako ndiye ambaye atakamatwa” Inspekta Tom Green aliongea.

“Unajidanganya. Tena naamini kwa sasa kamanda atakuwa njiani kuja kuwanasa!” Martin aliongea huku akicheka.

“Wewe ndiye ambaye unajidanganya. Sisi tupo katika kazi hii kwa muda mrefu. Kamanda wako hafahamu hata kidogo kama sisi tuko katika misitu hii. Anachokifahamu ni kwamba wewe umetoroka kambini kwa sababu umeasi jeshi na unakwenda kuungana na serikali. Huo ndiyo ujumbe ambao niliuacha pale kambini. Kwa sababu wazifahamu siri nyingi za jeshi hili basi kwa sasa unasakwa kama dhahabu” Inspekta Tom Green aliongea akicheka.

“Shiiiit! Mmeniangamiza ninyi mbwa. Makoko akinikamata atanichinja kabisa!” Martin aliongea akiporomosha machozi.

“Yes, sasa uamuzi ni wako. Kuendelea na safari ili ukatoe msaada kaw mheshimiwa Rais na ufutiwe makosa yako kisha uishi kwa amani kama shujaa wa Taifa au urudi kwa Makoko kukifuata kifo chako cha kikatili. Na kumbuka kwamba Makoko pamoja na BMM yake mwisho wake ni sasa!” Inspekta Tom Green aliongea.

Martin Samweli hakujibu lolote zaidi ya kubaki akiporomosha machozi. Wababe hawa walikuwa wamemuweza hasa. Alikuwa amebaki njia panda.

Safari ilikuwa ikiendelea katika mto ule. Mtumbwi ulikuwa ukiteleza juu ya maji mithili ya nyoka juu ya majani. Inspekta Tom Green alikuwa akipiga makasia kuuongezea kasi mtumbwi ule. Latoya na Martin Samweli walikuwa wamekaa juu ya mtumbwi ule huku Martin Samweli akiwa bado amefungwa mikono yake kwa nyuma.

Ni wakati huohuo ndipo sauti ya chopa ilianza kusikika ikija upande wao kuufuata mto. Jeshi la Kanali Edson Makoko lilikuwa limeshawakaribia.

“Yes, mambo ni moto sasa. Muda wa kuucheza muziki wetu umekwishakaribia!” Inspekta Tom Green aliongea huku akiiseti vema bunduki yake aina ya AK 47.

“Yes, ngoja tuwaonyeshe namna wababe vile tunafanya!” Latoya alijibu naye akiiseti bunduki yake aina ya AK 47.

“Jamani mnifungue mikono. Nitauawa mimi!” Martin alilalamika akiomba kufunguliwa mikono yake.

“Bado hatujakuamini. Unaweza ukatugeuka. Waonesha una kichwa kigumu cha kuelewa mambo na kuchukua maamuzi sahihi. Hii ndiyo njia salama kwako!” Inspekta Tom Green aliongea.

“We mbwa wewe! Nasema nifun ……..!” Martin Samweli hakuweza kuimalizia kauli yake.

Chopa ya wale waasi ilikuwa imekwishawakaribia. Kombora lilikuwa limeachiwa na lilitua pembeni yao na kufumuka.

“Diiiiiiive!” Inspekta Tom Green alipiga kelele.
Wote walijirusha ndani ya maji pindi kombora jingine lilipotua juu ya ule mtumbwi na kuusambaratisha.

“Ha ha ha haaaaaa! Kwisha habari yao. Halafu kumbe yuko na wengine?” askari mmoja kwenye chopa aliongea.

“Basi leo wameingia choo cha kike!” askari mwingine naye aliongea.

Inspekta Tom Green aliogolea chini kwa chini ndani ya maji huku akiwa amemshika mkono bwana Martin Samweli. Baadaye wote waliibukia ng’ambo yam to mahali ambapo palikuwa na kichaka.

“Yaani wewe kenge ni mnyama kabisa. Utaniua wewe!” Martin alilalamika. Inspekta Tom Green hakujibu chochote.

“Nifungue tafadhali, nitashindwa kujitetea na hawa jamaa wataniua!” Martin aliongea huku sasa machozi yakimtoka.

“Hii ni nafasi yako ya mwisho ya kujisafisha. Ukifanya ujinga tu, basi kumbuka sisi ni zaidi ya shetani!” Inspekta Tom Green aliongea huku akizikata kamba za mikono zilizomfunga Samweli.

Wakati huo huo Latoya alimrushia Martin bunduki aina ya AK 47.

“Ahsante sana. Sasa tuingie uwanjani. Mimi naufahamu vema msitu huu. Nitawaongoza!” Martin Samweli aliongea akiikoki bunduki yake.

Inspekta Tom Green na wenzake walianza kuchanja mbuga ndani yam situ ule. Walikuwa wakikimbia huku wakiongozwa na Martin. Msitu ule kwa sasa ulikuwa umetapaa wanajeshi kila mahali.
*******


Inspekta Tom Green na wenzake walianza kuchanja mbuga ndani yam situ ule. Walikuwa wakikimbia huku wakiongozwa na Martin. Msitu ule kwa sasa ulikuwa umetapaa wanajeshi kila mahali.

SASA ENDELEA

Baada ya mwendo kidogo kuna kikundi cha askari kama saba wa jeshi la BMM kiliwaona akina Inspekta Tom Green. Hapo ndipo mapambano ya risasi yalipoanza. Ilikuwa ni hatari kubwa sana kwani eneo lile la msitu lilipambwa kwa mivumo ya risasi ambazo zilikuwa zikikohoa kutoka katika bunduki za kila upande. Ndani ya dakika kumi mahaini wale walikuwa wamekwishakandamizwa na kupoteza uhai wao. Akina Inspekta Tom Green waliendelea kusonga mbele.

Dakika kumi mbele walikutana na muziki wa kundi la wanajeshi kama kumi na mbili ambao walikuwa na silaha nzito. Inspekta Tom Green na wenzake ndiyo walikuwa wa kwanza kuwaona wanajeshi wale.

“Sasa hapa tunapaswa tutumie akili!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Yap!” Martin Samweli alijibu.

“Tunatakiwa tutawanyike. Latoya utajipeleka na kujikamatisha kwa wanajeshi wale. Mimi nitashambulia kutoka kushoto na wewe Martin utashambulia kutoka kulia. Latoya unajua nini cha kufanya ikitokea hali hiyo!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Rodger that boss!” Latoya alijibu.

“Haya tutawanyike!” Inspekta Tom Green aliamuru na wote walitawanyika.

Latoya alijipeleka kwa askari wale na kunyoosha mikono juu ishara ya kusalimu amri. Wanajeshi wale walifurahi sana kwani waliona kama wamekwishapunguza sehemu ya kazi yao. Wanajeshi wale walimsogelea Latoya huku bunduki zao zikiwa tayari mikononi.

“Wenzako wako wapi?” mwanajeshi mmoja aliuliza huku akimpiga Latoya ngumi moja ya tumbo.

“Wameuawa!” Latoya alijibu huku akiigiza huzuni.

“Ha ha ha haaaaa! Pumbvu sana. Kazi kwisha!” mwanajeshi mmoja aliongea.

Ghafla mashambulizi ya risasi yalianza kutokea kila upande wa wanajeshi wale. Hapo ndipo Latoya naye alipowaonyesha uwezo wake. Mithili ya umeme alimfuata mwanajeshi mmoja na kumkandika ngumi ya uso na kisha alichomoa bastola iliyokuwa imewekwa katika mfuko wake kiunoni. Alianza kuwacharaza risasi wanajeshi wale huku akijiviringisha huku na huko kuepa risasi za maadui.

Baadaye maadui wote walikuwa chini wakiwa wameuawa. Wazee wale wa kazi walikutana tena na kupena mikono ya pongezi.

“Safi sana Martin!” Inspekta Tom Green alimpongeza Martin.

“Ahsante sana. Sasa tunakikaribia kijiji. Pale kuna bwana mmoja ambaye ana chopa. Tunapaswa kwenda kuiiba chopa ile ili itutoe kutoka hapa msituni maana safari ni ndefu sana kutoka hapa na hakuna namna yoyote ya usafiri tunayoweza kuipata!” Martin alijibu.

“Sawa. Tufanye hivyo pasi kupoteza muda!” Inspekta Tom Green aliongea.

Wote walianza kukimbia kutoka eneo lile walilokuwepo kuelekea kijijini huku wakichukua tahadhari kubwa sana.
******
Kijiji kilikuwa hakina wanajeshi kabisa. Wanajeshi wote walikuwa wameelekea ndani yam situ kwenye uwanja wa vita. Wananchi wote waliambiwa wajifungie ndani kwani kulikuwa na mapigano ambayo yalikuwa yakiendelea. Hali hii ilifanya kijiji kiwe kitulivu kabisa.

Kwa upande wao akina Inspekta Tom Green ilikuwa ni safi kabisa kwani iliwawezesha kufika katika nyumba ya mwanajeshi yule ambaye alikuwa akimiliki helkopta bila ya tatizo.

Kwa bahati nzuri mwanajeshi yule naye alikuwa amekwenda kwenye uwanja wa vita kwa kutumia gari. Akina Inspekta Tom Green hawakupenda kuipoteza fursa ile. Waliifungua milango ya chopa.

Kwa kutumia utundu mkubwa Inspekta Tom Green aliweza kuiwasha chopa ile. Chopa iliposhika moto, Inspekta Tom Green aliipaisha na kuanza safari ya kuuacha msitu ule. Huku msituni wanajeshi waliendelea kuwasaka akina Inspekta Tom Green wakiamini kwamba walikuwa bado wamenasa mle msituni.
*******
Saa nne za usiku Inspekta Tom Green, Latoya pamoja na Martin Samweli waliingia jijini Kano. Moja kwa moja chopa ile ilielekezwa mpaka katika hospitali ya rufaa ya Taifa ya Kano. Maafisa wote wa usalama hawakuamini kile ambacho walikuwa wakikiona. Chopa ilipotua, Inspekta Tom Green, Latoya pamoja na Martin Samweli walishuka. Inspekta Tom Green alianza kumwongoza Martin kuingia hospitali.

“Dokta Morgan, huyu hapa ni Martin Samweli. Naomba kazi ya kuokoa maisha ya Rais iendelee!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Ahsante sana Tom. You guys you are the bests!” dokta Morgan aliongea huku akimpokea Martin Samweli na kumwomba amfuate ndani ya hospitali.

Maafisa wote walipiga makofi na kushangilia. Hawakuamini kama Inspekta Tom Green na Latoya walikuwa wameweza kuifanikisha kazi ile.

“Chifu naomba uongee na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi waweze kutuma jeshi kule Masolo. Wale jamaa wametawanyika ovyo kutokana na moto tuliowawashia. Mpaka sasa wanahaha kutusaka. Huu ndio muda muafaka wa kuwavamia na kuwatawanyisha. Mashambulizi ya anga ndiyo yanafaa zaidi kwa kambi ile!” Inspekta Tom Green aliongea.
“Sawa Tom” Chifu alijibu.

“Na pia wakumbuke kwamba kijiji cha kwanza wanaishi watu wa kawaida. Eneo linalofuata ndiyo kambi yenyewe ya BMM. Watumie ramani hii ambayo itawaongoza vizuri kabisa!” Inspekta Tom Green aliongezea.

“Umesomeka Tom” Chifu aliongea huku wakati huo akiwa ameanza kufanya mawasiliano na waziri wa ulinzi pamoja na mkuu wa jeshi.
******
Ghafla hali ya hewa pale hospitalini ilichafuka. Kanali Edson Makoko pamoja na baadhi ya wanajeshi wa jeshi lake walivamia hospitali ile. Kumbe Kanali Edson Makoko alikuja kutambua kwamba Martin Samweli alikuwa ameshirikiana na akina Inspekta Tom Green na walikuwa wametoroka kule msituni.

Na pia alikuja kutambua kwamba misheni ya kumwua Rais ambaye aliitekeleza hapo awali haikuwa na mafanikio. Rais alinusurika lakini alikuwa mahututi hospitalini. Pia alifahamu kwamba Rais alikuwa akihitaji damu na damu ambayo ilikuwa ikimfaa ilikuwa ni ya bwana Martin Samweli ambaye alikuwa ni askari wake. Na hii ndiyo sababu ya akina Inspekta Tom Green kumtorosha bwana Martin kule msituni Masolo.

Sasa Kanali Edson Makoko yeye mwenyewe aliamua kuja jijini Kano na kuendesha operesheni ya kumwua Rais pamoja na yule askari aliyemsaliti.
*******

Sasa Kanali Edson Makoko yeye mwenyewe aliamua kuja jijini Kano na kuendesha operesheni ya kumwua Rais pamoja na yule askari aliyemsaliti.

SASA ENDELEA

“Code 002 …. Code 003 …. Code 004 and Code 005. Are there?” Inspekta Tom Green aliongea kupitia kifaa chake cha mawasiliano.

“Tunakupata poa kabisa toka huku nje. Yaani huku nje hali ni tete kabisa!” Amina alijibu.

“Sasa mimi nitacheza huku ndani na ninyi mtacheza kutoka nje kuja ndani. Hakikisheni hakuna kiumbe chochote chenye asili ya hawa waasi kinachotoka salama hapa!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Rodger that boss!” Hashim alijibu.

“Haya wazee, mambo ni moto. Sasa naomba mwende kwenye chumba cha mheshimiwa Rais mkaimarishe ulinzi huku. Mimi nitacheza nao hawa kunguni na nitahakikisha hawafiki huko!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Sawa kijana!” Chifu aliongea na kuwaongoza wenzake huku bastola zao zikiwa mikononi.

Inspekta Tom Green aliwaamuru manesi na madaktari kufunga milango ya mawodi na ofisi. Pia aliwaambia wawatulize wagonjwa watulie pindi yeye anapopambana na wale wahaini. Manesi na madaktari walifanya kama vile ambavyo Inspekta Tom Green alikuwa amewaamuru kufanya.

Wakati huohuo Kanali Edson Makoko pamoja na jeshi lake walikuwa wamekwishaanza kuingia ndani ya hospitali. Huko ndani walipokelewa na Inspekta Tom Green wakati nyuma walisindikizwa na maafisa wale wengine wa BSA pamoja na maafisa wengine wa Idara mbalimbali za usalama.

Polisi na Jeshi la wananchi pia walikuwa wamewasili pale hospitali kuwasha moto. Hakika mambo yalikuwa ni bambam. Ulikuwa ni mpambano mzito sana ambapo askari waasi waliuawa sana. Hakuna hata mmoja ambaye aliachwa. Vile ambavyo walitegemea na kuaminishwa na kamanda wao ilikuwa tofauti kabisa.

Naye Inspekta Tom Green upande wa ndani alizidi kuwashusha na kuwaounguza wote ambao walijaribu kuingia ndani ya hospitali. Hakika moto wa Inspekta Tom Green ulikuwa ni balaa. Hata Kanali Edson Makoko mwenyewe ilifika kipindi alishangaa. Hakutaka kuamini kama Inspekta Tom Green alikuwa ni binadamu wa kawaida.

Mtu wa mwisho kusalia katika jeshi la Kanali Edson Makoko alikuwa ni Kanali Edson Makoko mwenyewe. Na sasa alikuwa amekutana ana kwa ana na Inspekta Tom Green. Na kwa bahati nzuri walikutana kila mmoja bunduki yake ikiwa imeisha silaha.

“Umeniharibia sana. Nitahakikisha nakuua kikatili sana!” Kanali Edson Makoko alifoka.

“Hapa umekutana na mwamba. Nadhani ingelikuwa vema kama ungelikuwa unasali kumwomba Mungu msamaha kwa dhambi ambazo umezitenda. Unayekwenda kufa ni wewe!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Haya na tuone sasa!” Kanali Edson Makoko aliongea huku akimjia wanguwangu Inspekta Tom Green.

Kanali Edson Makoko aliachia konde zito ambalo Inspekta Tom Green alilipangua kwa mkono wake wa kushoto. Kanali Edson Makoko aliliachia konde jingine ambapo Inspekta Tom Green alibonyea na kuliepa.

Baada ya hapo Inspekta Tom Green alimbandika Kanali Edson Makoko konde moja tu zito kwa mkono wake wa kulia ambapo Kanali Edson Makoko alishindwa kuyahimili maumivu ya konde lile. Alijishika taya lake kwa maumivu huku akipiga kelele.

Inspekta Tom Green hakutaka kumpa nafasi kabisa. Alirusha teke kali ambalo lilimpata Kanali Edson Makoko tumboni. Kanali Makoko alijikunja na kulishika tumbo lake akiugulia maumivu. Ni wakati huo ndipo ambapo Inspekta Tom Green alianza kumpa dozi ya ngumi na mateke ya mfululizo.

Kanali Edson Makoko alilainika na kuwa zaidi ya mlenda. Inspekta Tom Green alihitimisha mchezo kwa kuukamata mkono wa Kanali Edson Makoko na kuuvunja. Kanali Edson Makoko alilia sana kwani maumivu ambayo aliyapata yalikuwa ni makali sana. Wakati huohuo askari walifika na kumtia nguvuni.

“Wekeni ulinzi wa kutosha sana kwani mtu huyu ni hatari sana. Ana mengi sana ya kuijibu serikali” Inspekta Tom Green aliongea.

Kanali Edson Makoko aliondolewa pale na kupelekwa cjhumba cha matibabu huku akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa polisi pamoja na wanajeshi. Baadaye hali ilikuwa tulivu kabisa pale hospitali. Mheshimiwa Rais aliendelea kupewa matibabu. Aliongezewa damu mara baada ya kuitoa katika mwili wa Martin Samweli.
******
MSITUNI MASOLO

Katika msitu wa Masolo nako mambo yalikuwa ni moto sana. Wanajeshi wa Jeshi la wananchi waliuvamia msitu na kuanza kupambana na waasi. Waasi wa kikundi cha BMM walishambuliwa vilivyo na kuteketezwa kabisa. Hawakuwa na pa kukimbilia.

Wale waliosalia walikamatwa na kushikiliwa mateka. Kambi yao iliteketezwa na kusambaratishwa kabisa. Hakuna alama yoyote ya BMM ambayo iliachwa. Na huo ulikuwa ndiyo mwisho wa BMM.
******
Kanali Edson Makoko alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya uhaini. Alionekana na makosa na alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja na adhabu kali sana.
Matibabu ya mheshimiwa Rais Ditric Mazimba yalichukua kama miezi miwili ambapo alirejea kuwa ahueni kabisa.
Bwana Martin Samweli alisamehewa makosa yake na kupongezwa kama mzalendo wan chi ya Bantu kwa kukubali kuokoa maisha ya Rais wake.

Pia Inspekta Tom Green pamoja na maafisa wenzake wa BSA walipongezwa kwa namna ya pekee kwa kazi kubwa ambayo waliifanya. Rais aliwapa shukrani za pekee sana.
Chifu naye alipongezwa kwa kuwapika vijana imara kabisa kwa usalama wa Taifa.
**** MWISHO ***

HEKAHEKA MSITUNI - 4

    


Simulizi : Hekaheka Msituni 


Sehemu Ya Nne (4)

  
    

Simulizi : Hekaheka Msituni 

Sehemu Ya Nne (4)





“Kuingia katika kikosi cha waasi halafu na kumchukua mwanajeshi mmoja miongoni mwao. Duh! Jambo hili kweli mtihani mzito sana!” afisa mwingine naye aliongezea kumuunga mkono yule wa mwanzo.



“Kwa hiyo kwa kusema hivyo mnamaanisha nini? Mna maana kwamba tumwache mheshimiwa Rais apoteze maisha?” Chifu aliuliza.



“Hapana, tulikuwa tunajaribu kuweka wazi ugumu wa jambo lililopo mbele yetu” yule aliyetoa kauli mara ya kwanza aliongea.



“Kauli zenu ni za kukatisha tama. Kwa sasa tunatakiwa tufikirie namna ya kulitatua tatizo hili na si kukatishana tama!” Chifu aliongea huku akionyesha wazi kwamba alikuwa amekerwa na kauli za maafisa wale wa mwanzo.



“Tusamehe ndugu!” maafisa wale waliomba radhi.



“Mimi nitakwenda katika misitu ya Masolo. Nitaingia katika kikundi cha waasi cha BMM na nitamleta bwana Martin Samweli hapa!” Inspekta Tom Green aliongea.



Maafisa wote pale walishindwa kuamini kile ambacho walikuwa wakikisikia. Walihisi huenda Inspekta Tom Green alikuwa ameanza kuchanganyikiwa. Haikuwa rahisi kwa mwanadamu wa kawaida kufanya maamuzi yenye kuhatarisha maisha kwa kiasi kile.



Ukiachilia mbali kuhatarisha maisha lakini maamuzi yale yalikuwa hayawezekani. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kuingia katika kambi ile na akatoka salama kabisa. Kwanza ataingiaje pasi kupoteza maisha kabla hata hajaingia katika kambi ile maana ulinzi ambao ulikuwa katika kambi ile haukuwa wa kawaida. Kauli ya Inspekta Tom Green iliwafanya maafisa wale wapigwe na butwaa la mwaka.



Ni Chifu pekee ndiye ambaye hakushangazwa na kauli ya Inspekta Tom Green. Yeye alimfahamu kijana wake huyu kwamba alikuwa na uwezo wa pekee sana. Alikuwa na uwezo mkubwa sana katika tasnia nzima ya ujasusi pamoja na mapigano.



Alikuwa na uwezo wa kupambana na jeshi kubwa kwa wakati mmoja na akatoka na ushindi. Kwa upoande wake maamuzi ya Inspekta Tom Green aliyabariki kwa moyo mkunjufu kabisa. Hakuwa na wasi hata kidogo katika moyo wake.



“Heeee! Itawezekanaje?” afisa mmoja alishindwa kujizuia na kuamua kuuliza.



“Hili ni jambo la uzalendo linalohitaji moyo wa pekee. Ukiwa na moyo dhaifu huwezi kufanya jambo kama hili. Rais wetu anahitaji msaada kwa sasa katika kuyaokoa maisha yake. Nina imani na kijana wangu. Ataikamilisha misheni hii!” Chifu aliongea.



Maafisa wengine walikuwa bado wameduwaa. Hawakuwa wameyaamini maneno ya Chifu. Waliona jambo lile kama haliwezekani kabisa.



“Nimesema nitaifanya shughuli hii. Wakuu hebu ondoeni shaka zeni na tufokasi zaidi katika afya ya Rais” Inspekta Tom Green aliongea.



“Dokta Morgan naomba schedule to the deadline!” Inspekta Tom Green aliongea akimtazama dokta Morgan ambaye alikuwa ameshikilia nyaraka fulani mkononi.



“Kwa sasa tumefanikiwa kuizuia damu isiendelee kuvuja katika jeraha. Kwa kiwango cha damu kilichopo katika mwili wa Rais, hatakuwa na maisha marefu kama hataongezwa. Kwa makadirio ni masaa tisini na sita. Yaani tuna siku nne kabla ya mheshimiwa Rais hajapoteza maisha kama hatoongezwa damu!” dokta Morgan aliongea.



“Siku nne nyingi sana kwangu. Kabla ya masaa tisini na sita nitakuwa hapa na Martin Samweli. Dokta Morgan trust me. I will bring you Martin Samweli before the deadline!” Inspekta Tom Green aliongea.



“Nakuamini sana kamanda. Naamini kila kitu kitakwenda salama kabisa na Rais atarejea katika kiti chake salama” dokta Morgan aliongea.



“Wakuu, naomba nikaanze safari. Sina muda wa kuendelea kupoteza!” Inspekta Tom Green aliwaaga wale wakuu wa usalama.



“Nadhani ninahitaji kwenda na kijana wangu kwa maandalizi. Tutakutana baadaye kidogo wakuu!” Chifu naye aliongea akianza kuondoka akiambatana na Inspekta Tom Green.

******

KATIKA OFISI ZA BSA



“Wazee, kama ambavyo nilizungumza hapo awali, nina misheni kubwa sana katika misitu ya Masolo ambako ninatakiwa nimlete bwana Martin Samweli mwanajeshi kutoka kikosi cha waasi cha BMM kwa ajili ya blood donation kwa mheshimiwa Rais” Inspekta Tom Green aliongea.



“Kwa nini tusiende wote mkuu maana misheni hii ni ya hatari” Inspekta John Michael aliongea.



“Kama ulivyokwishasema kwamba misheni hii ni ya hatari sana. Hatutakiwi kukirisk kikosi chote. Acha niende mwenyewe. Ninawamudu wale jamaa katu hawawezi kunipa shida!” Inspekta Tom Green aliongea.



“Uko sahihi kabisa mkuu. Pekee wawaweza wale jamaa but you need mya company!” Latoya aliongea.



Inspekta Tom Green alibaki kimya akimtazama Latoya. Hakufahamu ajibu nini.



“You don’t have to say no. tutakwenda pamoja!” Latoya alisisitiza.



“Yes boss. Unahitaji kampani ya Latoya!” Hashim naye alisisitiza.



“Ok, hebu kajiandae tuanze safari kwani hatuna muda wa kupoteza. Muda ni finyu sana kwetu!” Inspekta Tom Green aliongea akimtazama Latoya.



“Rodger that boss!” Latoya alijibu na kusimama kwa ajili ya kwenda kujiandaa.

******





“Ok, hebu kajiandae tuanze safari kwani hatuna muda wa kupoteza. Muda ni finyu sana kwetu!” Inspekta Tom Green aliongea akimtazama Latoya.



“Rodger that boss!” Latoya alijibu na kusimama kwa ajili ya kwenda kujiandaa.



SASA ENDELEA



NDANI YA CHOPA



“Kwa jinsi uhitaji wa damu hii ulivyokuwa wa muhimu, tunahitaji kutumia siku moja tu kuhakikisha kwamba tumempata bwana Martin Samweli na kumfikisha Kano” Inspekta Tom Green aliongea.



“Ni kweli usemayo kamanda. Lakini naona mazingira ya kambi ile siyo rafiki kuitimiza misheni hii kwa haraka kiasi hicho” Latoya aliongea.



“Umeongea sahihi kabisa Latoya. Ni kweli katika kambi ile kwa mujibu wa ramani imegawanyika katika sehemu mbili. Kwanza kabisa kuna makazi ya wananchi wa kawaida na upande wa pili kuna kambi ya jeshi. Sasa katika misheni hii tunatakiwa tuvifanye vile visivyowezakana viwezekane. Sisi ni askari wenye mafunzo ya hali ya juu. Naamini hili litawezekana. Kumbuka maisha ya Rais kwa sasa yapo mikononi mwetu!” Inspekta Tom Green aliongea.



“Kuvamia kambi ni jambo dogo. Ugumu ninaouona hapa ni namna ya kumshawishi askari huyu kuondoka na sisi” Latoya aliongea.



“Hiyo itawezekana tu. Akikataa basi itatubidi kutumia njia ya pili yaani kuhakikisha kwamba anafika Kano ndani ya muda uliopangwa apende asipende!” Inspekta Tom Green aliongea.



Wakati huo chopa iliendelea kukata anga. Rubani alikuwa makini kabisa kuhakikisha kwamba anakiongoza chombo katika hali ya usalama. Kipindi hicho chote Inspekta Tom Green pamoja na Latoya waliendelea luzungumza hiki na kile katika kuiboresha mikakati yao ya uvamizi katika kambi ile ya waasi. Mioyo yao ilikuwa na ari kubwa sana ya kufanya misheni ile kwa mafanikio ili kuyaokoa maisha ya mheshimiwa Rais.



Mwendo wa masaa matano uliwafikisha katika eneo la misitu ya Masolo.



“Nadhani wewe utushushe hapa na ugeuke kurejea Kano. Eneo hili kwa sasa siyo salama kabisa. Haitakiwi waasi hawa wabaini uwepo wetu mapema kabla ya misheni kukamilika!” Inspekta Tom Green aliongea.



“Sawa mkuu!” rubani alijibu huku akiishusha chopa ile mahali fulani ndani yam situ.



Baada ya hapo Inspekta Tom Green na Latoya walishuka. Chopa ilipaa na kurudi ilikotoka.



“Haya mama. Let’s start the game!” Inspekta Tom Green huku akibeba begi lake ambalo lilikuwa na silaha.



“Rodger that darling!” Latoya alijibu huku naye akilibeba begi lake mgongoni.



Baada ya hapo walianza safari ya kusonga mbele huku silaha zao zikiwa mikononi mwao. Walikuwa makini sana kila walipotembea kwani walifahamu kwamba msitu ule ulikuwa ukimilikiwa na waasi hivyo hatari yoyote yaweza kutokea.



Mwendo wa saa moja uliwafikisha katika kijiji ambacho kilikuwa kikimilikiwa na waasi lakini walikuwa wakiishi raia wa kawaida. Hii ina maana kwamba utawala uliokuwepo katika kijiji kile ulikuwa ni utawala wa waasi chini ya Kanali Edson Makoko.



Inspekta Tom Green na Latoya hawakutaka kupita katika kijiji hiki. Hii ilikuwa ni kwa sababu za kiusalama. Walichokifanya ni kuambaa ambaa pembezoni mwa kijiji kile na kuendelea kusonga mbele wakiifuata ramani ya msitu ule ambayo walikuwa nayo.



Baada ya muda fulani wa kutembea, hatimaye walianza kuyaona majengo ya kambi ya jeshi. Majengo hayo vilikuwa ni vibanda ambavyo vilikuwa vimejengwa kwa miti na kuezekwa nyasi wakati vingine viliezekwa kwa bati.



“Haya sweetheart, tumekwishafika tayari. Ngoja tuwaonyeshe shoo moja matata sana!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Yes darling, let’s pop in!” Latoya alijibu.



Walianza kutembea kwa tahadhari kubwa sana mpaka walipokifikia kibanda cha kwanza ambacho kilikuwa kimejengwa miti na turubai.



Walipochunguza vizuri kuna kitu walikigundua. Vibanda vile vilikuwa na majina. Majina yale yalikuwa ni ya askari ambao wanaishi ndani ya vibanda hivyo.



Mungu alikuwa upande wao kwani kibanda ambacho walikuwa wamekifikia kwa mara ya kwanza kilikuwa kimeandikwa Martin Samweli hii ikimaanisha kwamba mtu wao ambaye walikuwa wamemfuata ambaye ni Martin Samweli alikuwa akiishi ndani ya kibanda kile.



Inspekta Tom Green alimwonyesha ishara Latoya kwa kutumia kichwa chake na Latoya alijibu kwa kuonesha idara ya dole gumba. Hii ilimaanisha kwamba alikuwa amemwelewa Inspekta Tom Green. Kwa tahadhari kubwa sana Latoya alizama ndani ya kibanda kile huku Inspekta Tom Green akiwa anaangalia usalama upande wa nje.



Kwa wakati huo yalikuwa ni majira ya saa nane za mchana. Martin Samweli alikuwa amejipumzisha juu ya kitanda chake ndani ya kibanda kile usingizi ukiwa umempitia. Latoya alimgusa Martin Samweli kumuamsha ambapo Martin alishtuka ghafla na kuishika bastola yake mkononi.



“Wewe ni nani na umefuata nini hapa!” Martin Samweli alifoka huku akimtazama Latoya.



“Naitwa Latoya. Ninatoka Kano. Nimekuja hapa kwako kwa sababu nina shida kubwa sana. Na sina muda mrefu wa kuendelea kuwepo hapa!” Latoya aliongea.



Martin Samweli alimtazama Latoya usoni na kuvutiwa na sura nzuri nay a kirembo ya Latoya. Sura ile ilimfanya Martin Samweli apunguze munkari wake kwani aliamini mwanamke huyu hawezi kuwa hatari kwake. Na hili ndilo kosa kubwa sana alilolifanya. Alikosea sana kumwamini Latoya. Hakufahamu kwamba Latoya alikuwa ni mwanamke hatari zaidi ya hatari yenyewe.



“Una shida gani?” Martin Samweli aliuliza.



“Hali ya mheshimiwa Rais ni mbaya sana kwani amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu. Kuna uhaba wa damu ya kumwongezea. Rekodi zimeonyesha kwamba damu yako ndiyo inafanana na ya mheshimiwa Rais” Latoya aliongea.



“Unasemaje wewe kenge. Yaani huyo mtu unayemsema ni adui yangu namba moja. Kwanza ilikuwa inafahamika kwamba amekufa, kumbe amenusurika. Halafu nashangaa umefikaje hapa pasi kuonekana!” Martin Samweli aliongea huku sasa akiwa amemwonyeshea Latoya bastola.



“Martin Samweli nadhani kuna mambo mengi sana ambayo mnapotoshwa na huyu kiongozi wenu Kanali Edson Makoko. Yeye anachokitaka ni kuwatumia ili aweze kutekeleza adhma yake ya kuwa Rais wa Bantu. Ninachokuomba kuwa mzalendo na itetee nchi yako!” Latoya aliongea.



“Hebu ondoa ngonjera zako hapa!” Martin Samweli alizidi kufoka.

****





“Martin Samweli nadhani kuna mambo mengi sana ambayo mnapotoshwa na huyu kiongozi wenu Kanali Edson Makoko. Yeye anachokitaka ni kuwatumia ili aweze kutekeleza adhma yake ya kuwa Rais wa Bantu. Ninachokuomba kuwa mzalendo na itetee nchi yako!” Latoya aliongea.



“Hebu ondoa ngonjera zako hapa!” Martin Samweli alizidi kufoka.



SASA ENDELEA



“Hebu fikiria athari zitakazopatikana na vita ambayo mnataka kuianzisha. Hebu fikiri ni maisha ya watu wangapi wasio na hatia ambayo yatapotea. Fikiria kama katika wahanga wa vifo hivyo wanakuwepo watu wa familia yako. Ni uchungu kiasi gani utaupata? Hebu kuwa mzalendo kwa kuokoa maisha ya Rais. Hakika utatangazwa shujaa wa Taifa na makosa yako yote yatafutwa!” Latoya aliongea.



“Nimekwambia nyamaza kunguni wewe. Kwanza inabidi nikuripoti ili uweze kukamatwa na kuuawa kidudumtu wewe!” Martin Samweli alifoka.



“Samahani sana brother. Hilo haliwezi kutokea!” Latoya aliongea.



Wakati huohuo aliipangua bastola ya Martin Samweli na kisha alimbandika ngumi ya uso. Martin Samweli alihisi nyotanyota. Kabla hajatahamaki mateke matatu mfululizo yalitua kichwani kwake na kumbwaga chini.



Baada ya hapo Latoya alimpa Martin Samweli pigo la nyuma ya kisogo ambalo lilimfanya apoteze fahamu. Latoya aliibonya batani Fulani katika saa yake ambapo muda huohuo saa ya Inspekta Tom Green kule nje ilipiga mlio. Inspekta Tom Green aliingia haraka sana ndani ya kibanda kile. Ndani ya kibanda aliweza kuushuhudia muziki ambao alikuwa ameucheza Latoya.



“Ha ha ha haaaaa! You are the beast!” Inspekta Tom Green aliongea huku akimbeba Martin Samweli begani mwake.



Baada ya hapo safari ya kutoka katika kambi ile ilianza. Mwendo ulikuwa ni wa haraka sana. Mbele kidogo waliweza kuliona gari ambalo lilikuwa limeegeshwa. Walimwingiza Martin Samweli ndani ya gari lile. Inspekta Tom Green aliliwasha na kasha waliondoka kutoka eneo lile.

*******

Mwendo wao ulikuwa ni wa kasi sana. Ndani ya muda mfupi walikuwa wamekwishakikaribia kile kijiji ambacho kinamilikiwa na waasi. Pale waliamua kutumia akili ya kikomando. Waliamini kwamba kama wangelipita na gari lile pale kijijini, basi waasi wangeliweza kushtuka na kuanza kuwaandama.



Inspekta Tom Green alichepusha gari kutoka barabarani na kuliingiza ndani ya msitu. Aliliingiza ndani kabisa na kasha alisimama. Kwa wakati huo bwana Martin Samweli alikuwa bado amezirai. Na alikuwa amefungwa mikono yake ili kama ataamka basi asiweze kuleta matata.



“Now we walk!” Inspekta Tom Green aliongea.

“Yes ofcourse!” Latoya alijibu.



Walishuka kutoka kwenye gari. Inspekta Tom Green alimbeba bwana Martin Samweli begani na kisha safari ya kusonga mbele ilianza.

*******

KAMBINI BMM



“Mkuu kuna tatizo limejitokeza!” mwanajeshi mmoja aliongea mbele ya Kanali Edson Makoko.



Hii ilikuwa ni ndani ya ofisi ya Kanali Edson Makoko ambaye alikuwa bize toka asubuhi akiuandaa mpango wa mapinduzi.



“Tatizo gani?” Kanali Edson Makoko aliuliza.



“Martin Samweli ametoroka kambini” mwanajeshi yule aliongea.



“Una maana gani?” Kanali Edson Makoko aliuliza tena.



“Ameasi mkuu. Ameacha ujumbe kwamba ameamua kurudi serikalini na kuomba msamaha” mwanajeshi yule aliongea.



“Shiiiit! Asakwe mara moja na kurudishwa hapa. Anaifahamu siri na mipango yetu mingi sana!” Kanali Edson Makoko alifoka.



Wakati wanaondoka baada ya kumteka Martin Samweli, Inspekta Tom Green aliacha ujumbe kwamba akijifanya ni Martin Samweli ndiye ambaye aliuacha. Kitendo hiki kilikuwa na maana kubwa sana kumbuka kamba maafisa hawa wa BSA kila jambo walitendalo, hulitenda kwa kutumia akili kubwa sana.



“Ita paredi mara moja. Mbwa huyu ni lazima arejeshwe hapa mara moja!” Kanali Edson Makoko alifoka.



“Sawa mkuu!” mwanajeshi yule alijibu huku akipiga saluti na kuondoka mle ofisini.



Baada ya dakika mbili king’ora kilisikika pale kambini. King’ora hiki kiliashiria kwamba kulikuwa na hali ya hatari ambayo ilikuwa imetokea. Wanajeshi kutoka kila kona ya kambi ile walianza kukusanyika katika uwanja mkubwa sana pale kambini ambao hutumika kwa ajili ya paredi.



Baada ya kujipanga katika mistari mingi iliyonyooka, Kanali Edson Makoko aliwasili eneo lile. Kila mwanajeshi alikuwa kimya akiwa na shauku ya kusikia ni nini kilikuwa kimetokea.



“Soldiers, kuna tatizo moja limetokea. Kuna mmoja miongoni mwetu ameasi jeshi na sasa yuko mbioni kwenda kujikabidhi kwa serikali. Mwenzetu huyu ni askari Martin Samweli!” Kanali Edson Makoko alitulia kidogo.



“Haaaaaa!” wanajeshi wote walishangaa.



“Sasa bwana huyu anazijua siri zetu nyingi pamoja na mipango yetu yote. Akifika mikononi mwa serikali tu, basi itakuwa ni rahisi sana kwa serikali kutuvamia na kutushinda. Hivyo basi ninaagiza kwamba ndani ya muda mfupi bwana huyu awe amerejeshwa hapa akiwa mzima kabisa. Nitamuua kwa mkono wangu!” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Haya tawanyikaaaaa!” Kanali Edson Makoko alifoka.



Wanajeshi walianza kutawanyika na kwenda katika ghala la kuhifadhia silaha. Walichukua silaha na kisha waliingia msituni tayari kumsaka bwana Martin Samweli. Kulikuwa na askari wa miguu ambao walikuwa na mbwa maalum, kulikuwa na askari wa anga pamoja na askari wa miguu. Kwa kifupi jeshi la Kanali Edson Makoko lilikuwa limekamilika hasa.

*******

Safari ya Inspekta Tom Green, Latoya pamoja na mateka wao ilikuwa bado inaendelea ndani ya msitu wa Masolo. Mateka wao alikuwa bado yupo katika hali ya kupoteza fahamu. Hii kwa kiasi kikubwa iliwapa urahisi wa kusonga mbele pasi upinzani kutoka kwa mateka wao. Kwa sasa walikuwa eneo ambalo lilikuwa na mto mkubwa sana. Hiki kilikuwa ni kizingiti kikubwa sana katika kuendelea na safari yao.



“Sasa tunafanyaje hapa?” Inspekta Tom Green aliuliza.

“Tunahitaji boti” Latoya aliongea.

*****





“Sasa tunafanyaje hapa?” Inspekta Tom Green aliuliza.

ITAENDELEA

ITAENDELEA

HEKAHEKA MSITUNI - 3

    


Simulizi : Hekaheka Msituni 


Sehemu Ya Tatu (3)


Simulizi : Hekaheka Msituni 

Sehemu Ya Tatu (3)





Kumbe haikuwa imejulikana. Mheshimiwa Rais Ditric Mazimba alikuwa katika hatari kubwa sana. Walinzi hawa wawili ambao walikuwa wakilinda hapa mlangini walikuwa ni wanajeshi kutoka katika kikundi cha uasi cha Bantu Military Movement. Walikuwa hapa kwa shughuli maalum ambayo walitakiwa kuitekeleza kwa haraka sana na kwa ufanisi mkubwa. Kwa mara nyingine tena Kanali Edson Makoko alikuwa amefanya mambo yake.



Mlinzi mwanajeshi mmoja aliitoa kadi yake mfukoni na kuipachika katika mashine maalum ambayo ilikuwa pale mlangoni. Baada ya hapo alibonyabonya namba kadhaa na mlango ulifunguka. Hatimaye mlinzi yule aliufungua mlango ule taratibu na kisha aliingia ndani.



Kwa wakati huo mheshimiwa Rais Ditric Mazimba alikuwa amekwishalala. Askari Yule mmoja aliyekuwemo mle ndani naye alikuwa amepitiwa na kausingizi kidogo hivyo alikuwa amejiegesha kitini.



Bila ya kupoteza wakati mwanajeshi yule alikirusha kisu chake ambacho kilitua katika shingo ya mlinzi yule na kuzama katika koromeo. Mlinzi yule alianguka chini na kuanza kutapatapa huku akikoroma kuupigania uhai wake.



Upande wa nje ya chumba alicholala mheshimiwa Rais Ditric Mazimba yule askari inchaji aliendelea kufanya doria ya kuyazungukia maeneo yote ambayo yalikuwa yamewekewa ulinzi. Ghafla kichwa cha askari yule afisa inchaji wa ulinzi kilichemka haraka haraka, alihisi palikuwa na tatizo katika chumba cha mheshimiwa Rais.



Katika mlango wa chumba kile alionekana amesimama askari mmoja wakati pale walikuwa wamepangwa askari wawili.



“Huyu mwingine ameenda wapi?” inchaji yule alijiuliza swali lile kwa sauti ya chini. Baadaye aliamua kwenda kuangalia palikuwa na tatizo gani pale.



“Mwenzako yuko wapi?” askari yule inchaji aliuliza.

Askari yule ichaji hakupata jibu kutoka kwa mlinzi yule. Alichokipata ni ngumi kali ambayo ilifuatiwa na teke ambalo lilimkalisha chini. Kisu kilirushwa kumfuata pale chini lakini alikiona na kukikwepa. Hapo ndipo askari yule inchaji alipotambua kwamba walikuwa wameingiliwa na maisha ya mheshimiwa Rais yalikuwa hatarini.



Kutoka pale chini alijibinua na kusimama dede tayari kwa mashambulizi. Alijipanga kwa mapigo ya karate ambapo jambazi yule mlinzi naye alifanya vivyohivyo. Jambazi yule alirusha pigo la mkono ambapo askari inchaji alibonyea na kuliepa. Teke kali lilimfuata lakini nalo alilikinga kwa mikono yake yote miwili.



Ndipo naye askari inchaji alipomfyatua teke jambazi yule na kumfya ale mweleka. Alipotaka kusimama alitulizwa kwa ngumi mbili mfululizo ambazo zilifuatia na pigo la karate katika koo lake. Pigo lile lilizikata kabisa pumzi za jambazi yule na hatimaye alikata roho. Kwa kujiridhisha askari inchaji yule alichomoa bastola na kumimina risasi katika kichwa cha jambazi yule.



“Section A ….. Section B …. Section C …. We have the situation! Over!” askari inchaji aliongea katika kifaa chake cha mawasiliano akiwataarifu walinzi wote katika ikulu ile kwamba walikuwa wamevamiwa.







“Section A ….. Section B …. Section C …. We have the situation! Over!” askari inchaji aliongea katika kifaa chake cha mawasiliano akiwataarifu walinzi wote katika ikulu ile kwamba walikuwa wamevamiwa.



SASA ENDELEA



Askari inchaji yule alichomoa kadi yake maalum na kuitumbukiza katika mashine maalum iliyokuwa katika mlango wa chumba ambamo alikuwa amelala mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba. Bastola ikiwa mkononi aliusukuma mlango ule mara baada ya kufunguka na kisha aliingia ndani kwa tahadhari kubwa sana.



Askari inchaji yule hakuamini kile ambacho alikiona mkle ndani. Mlinzi wa Rais alikuwa chini amelala akiwa maiti. Katika kitanda alionekana mheshimiwa Rais akiwa amelala huku mtu mmoja akiwa amekishika kisu kilichokuwa kikimeremeta kwa makali tayari kwa kushusha pigo moja kwa mheshimiwa Rais.



Askari inchaji yule alipiga hesabu za haraka haraka. Kufumba na kufumbua alizimimina risasi mfululizo kuelekea kwa jambazi yule.



Lakini askari inchaji yule alikuwa amechelewa. Kisu kilikuwa kimeshuka na kuzama katika tumbo la mheshimiwa Ditrick Mazimba. Jambazi yule naye alikuwa amepigwa risasi nyingi sana ambazo zilimwangusha chini akiwa maiti.



Tukio lile lilitisha sana. Ikulu ndogo ya Soweni ilikuwa imechafuka. Upekuzi mkubwa sana ulianza kufanyika ili kubaini kama kulikuwa na majambazi wengine ambao walikuwa wamesalia miongoni mwa walinzi wa ikulu ile.



Wakati huo huo hali ya mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba ilikuwa mbaya sana. Madaktari bingwa wa wilaya walikuwa wamewasili pale ikulu na walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya mheshimiwa Rais.



Wakati huohuo kuna helkopta ambayo ilikuwa njiani ambayo ilikuwa inatakiwa imsafirishe mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba kutoka pale Soweni mpaka katika mkoa wa Dolayo ambako mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba angesafirishwa kwa ndege mpaka jijini Kano ambako angepatiwa matibabu.



Taarifa za kuvamiwa mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba pale ikulu ndogo ya Soweni zilikuwa zimefanywa siri kubwa sana. Hii yote ilikuwa ni kwa ajili ya sababu za kiusalama.

*******

“BMM oyeeeee!”

“Oyeeeee!”



“Bantu mpya safiiiiiii!”



“Saaaafiiiiiiiii!”



Hii ilikuwa ni salamu kati ya Kanali Edson Makoko na wanajeshi wake wa BMM pindi alipokuwa amekutana nao kwa dharura. Hii ilikuwa ni pindi alipopata mrejesho wa uvamizi wa kumwua mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba ambao ulikuwa umefanywa na vijana wake.



Kanali Edson Makoko alikuwa na furaha sana. Furaha ambayo alikuwa nayo siku ile hakuwahi kuwa nayo hapo kabla katika maisha yake. Habari ambazo alikuwa amezipata zilikuwa ni habari njema sana kuwahi kutokea katika maisha yake. Habari zile zilikuwa ni muhimu zaidi ya chakula ambacho alikuwa akila.



Wafuasi wa Kanali Edson Makoko walikuwa walimeibaini furaha ambayo bosi wao alikuwa nayo. Hii iliwafanya nao wawe na furaha kubwa sana. Hii ilikuwa ni kwa sababu bosi wao Kanali Edson Makoko anapokuwa na furaha basi hufanya sherehe kubwa sana pale kambini. Watu hunywa na kulewa sana. Pia wanawake Malaya huletwa pale kambini ambapo wanajeshi huburudika kwa kulala nao kimapenzi. Hii ndiyo sababu kuu iliyowafanya wanajeshi wale kufurahi.



“Nina habari njema sana ambazo ninataka niwaletee leo hii!” Kanali Edson Makoko alianza kuongea.



“Kama ambavyo niliwahi kuwataarifu kipindi furani hapo nyuma kwamba Rais Ditrick Mazimba ndiye ambaye alimwua mzee wetu Shukuru Kizibo. Siku zote jambo hili lilikuwa likinitesa sana kwani nilikuwa nikiumia sana kwa unyama huu ambao Rais alikuwa ametutendea. Unyama ule ambao alikuwa ametutendea lilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu. Aliturudisha nyuma katika harakati zetu kwa hatua nyingi sana” Kanali Edson Makoko alitulia kidogo na kuwatazama wanajeshi wao namna ambavyo wanaipokea taarifa yake.



Wanajeshi wote kwa wakati huo walikuwa kimya kabisa. Mioyo yao ilionyesha kuguswa sana na kuchomwa na habari zile ambazo Kanali Edson Makoko alikuwa akiwapa. Hii hasa ilitokana na namna ambavyo walikuwa wamemzoea marehemu mzee Shukuru Kizibo.



“Binafsi sikupenda kuona mwanaharamu yule akiendelea kuvuta pumzi ya dunia hii. Nilitaka na niliazimia kumfanya aulipe uovu wake. Sikutaka kusubiri mpaka siku ya mapinduzi itakapofika. Kwa sababu yeye alikuwa ameyakoroga mambo, basi nasi ilibidi tuyakoroge vilevile” Kanali Edson Makoko aliendelea kumwaga cheche.



Wanajeshi waliendelea kuwa kimya wakiwa na shauku ya kutaka kujua ni jambo gani ambalo limetokea ambalo kiongozi wao Kanali Edson Makoko alikuwa akitaka kuwaambia. Mioyo yao ilikuwa na shauku kubwa sana.



“Basi hapo nilianza kuandaa mpango wa kuhakikisha Rais Ditrick Mazimba anatoweka duniani. Mpango huu nilikaa na kuupanga kwa muda mrefu sana kwani ulikuwa ni mpango ambao ulikuwa unahitaji umakini wa hali ya juu sana hasa ukichukulia hadhi ya mtu ambaye alikuwa akitakiwa kuondolewa duniani” Kanali Edson Makoko alitulia kidogo.



“Mpango wangu lipokamilika, basi niliuingiza katika utekelezaji. Niliwateua wanajeshi wawili miongoni mwenu kwa ajili ya kuutekeleza mpango huu. Kwanza kabisa ninaleta kwenu habari za huzuni kwani wale wenzetu wawili wameyapoteza maisha yao. Waliuawa wakiwa wanautekeleza mpango huu” Kanali Edson Makoko alitulia kidogo akiwatazama wanajeshi wake ambao waliviinamisha vichwa vyao kwa huzuni.



“Lakini hatupaswi kuhuzunika sana kwa sababu wenzetu wale walikuwa ni wazalendo ambao walikuwa wamejitolea maisha yao kwa ajili ya kuyatetea maslahi mapana ya jeshi la BMM na wananchi wa Bantu kwa ujumla” Kanali Edson Makoko al;itulia kidogo.



“Habari njema ni kwamba mpango wetu huu umefanikiwa kwani wenzetu wale walifanikiwa kumwua Rais Ditrick Mazimba. Hivyo ninatangaza rasmi kwamba Rais Ditrick Mazimba ameuawa na kisasi cha kifo cha kiongozi wetu kimelipwa. Jambo pekee ambalo tutakuwa nalo kwa sasa ni maandalizi ya mpango wa mapinduzi. Tunatakiwa tuifyekelee mbali serikali nzima ya Bantu. Viongozi hawa hawastahili kabisa kuendelea kuwepo madarakani” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Hureeeeeeeee!” wanajeshi wote walipiga kelele za shangwe huku wakizinyanyua juu bunduki zao.



Walionyesha kuwa na furaha kubwa sana kwa habari hizi ambazo walikuwa wameletewa na kiongozi wao. Habari hizi ziliwafanya warukeruke kwa furaha. Hawakuamini kama kilio cha kisasi kwa mtu ambaye alikuwa amemwuua kiongozi wao kilikuwa kimesikika.



Lakini wanajeshi hawa hawakufahamu siri kubwa sanaambayo ilikuwa nyuma ya mambo yale. Wao waliendelea kulishwa unga wa sumu ndani ya fikra zao.

*****





Lakini wanajeshi hawa hawakufahamu siri kubwa sanaambayo ilikuwa nyuma ya mambo yale. Wao waliendelea kulishwa unga wa sumu ndani ya fikra zao.



SASA ENDELEA



“Kwa sasa ninatangaza sherehe za ushindi. Kwa muda wa wiki nzima iktakuwa ni sherehe hapa kambini ambapo tutakunywa pombe na kuburudika. Yaani raha na starehe za aina zote zitakuwepo hapa kambini kwa muda wa wiki nzima!” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Hureeeee! Long live our Cornel!” wanajeshi walipiga kelele za furaha huku wakimimina risasi ovyo angani.

******

OFISI ZA BSA JIJINI KANO



Habari zakuvamiwa mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba zilikuwa zimeifikia ofisi ya Idara ya usalama wa Taifa ya BSA. Habari hizi hazikuwa njema hata kidogo. Maafisa waandamizi wakiongozwa na mkuu wao yaani Chifu walikuwa wamekusanyana na kujaribu kutafakari ni vipi tukio baya kama lile liliweza kutokea. Hali ya ulinzi na usalama wa Rais ilikuwaje mpaka mahaini hao wakaweza kujipenyeza na kufanya maafa yale?



Waliamini kwamba ni lazima kulikuwa na uzembe katika kikosi cha usalama wa Taifa na kikosi cha ulinzi na usalama wa Rais.



Wakati huu Dokta Morgan aliwasili katika ofisi za BSA kwa ajili ya kufanya mazungumzo muhim sana na Chifu.



“Karibu sana dokta” Chifu alimkaribisha dokta Morgan



“Ahsante sana Chifu” dokta Morgan alijibu.



“Karibu uketi hapo” Chifu alimwelekeza dokta Morgan mahali pa kuketi katika sofa.



“Starehe!” dokta Morgan alijibu.



“Nadhani umekwishasikia kile ambacho kimetokea kwa Rais wa Jamhuri ya Bantu” Chifu alianza kuongea.



“Ndiyo Chifu. Nimesikia” dokta Morgan alijibu.



“Basi hali ni mbaya dokta. Maisha ya mtukufu Rais Ditrick Mazimba yako hatarini sana” Chifu alitulia kidogo na kumtazama dokta Morgan.



“Nimepokea ujumbe kutoka Idara ya usalama wa Rais ikulu. Wananiomba msaada wa kuokoa maisha ya Rais. Hii ina maana kwamba taaluma yako pamoja na umahiri wako katika tiba vinatakiwa sasa katika kuyaokoa maisha ya Rais. Nadhani umenielewa dokta!” Chifu aliongea.



“Nimekuelewa Chifu. Naamini Mungu atasaidia na maisha ya mheshimiwa Rais yatakuwa salama kabisa” dokta Morgan aliongea.



“Ok, basi nifuate kwa zoezi hilo linaanza sasa!” Chifu aliongea.



Chifu alisimama na kuanza kutoka mle ofisini huku akifuatwa na dokta Morgan. Moja kwa moja walienda mpaka mahali ambapo maafisa waandamizi wa BSA walikuwepo wakifanya mazungumzo.



“Attention! Kama vile ambavyo kila mmoja ana taarifa, ni kwamba mheshimiwa Rais amevamiwa na kuchomwa kisu katika ikulu ndogo ya Soweni. Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba hali yake mpaka sasa ni mbaya. Kwa sasa yuko njiani analetwa hapa Kano. Atakuwepo katika hospitali ya Kano kwa ajili ya matibabu ya awali kwa ajili ya kuweka afya yake katika hali ya usalama!” Chifu alitulia kidogo na kuvuta funda la mate.



“Nadhani mpaka hapo mtakuwa mmefahamu kazi nzito ambayo iko mbele yetu kama Idara ya usalama wa Taifa. Kwanza kabisa itakuwa ni kuwatafuta watu waliofanya uhaini huo. Na pili ni kuhakikisha kwamba hakuna jambo linguine la hatari ambalo litampata mheshimiwa Rais” Chifu aliongea.



“Sawa mkuu!” maafisa walijibu kwa umoja.



“Kwa sasa Code 001 utakiongoza kikosi. Naomba umfikishe dokta Morgan mpaka katika hospitali ya rufaa ya Taifa ya Kano ambapo yeye atasimamia matibabu ya mheshimiwa Rais. Wengine wote pia myahakikisha kwamba mnafanya track katika eneo lote la hospitali ile ili kuhakikisha kwamba hakuna hatari nyingine ambayo itakuwa imepangwa. Hii ndiyo misheni ya awali. Misheni nyingine mtapata taarifa” Chifu aliongea kwa msisitizo.



“Sawa mkuu umeeleweka!” maafisa wote walijibu kwa pamoja huku wakionyesha munkari mkubwa.



“Haya nendeni sasa” Chifu aliongea na kasha aliondoka kutoka eneo lile.



Maafisa wale walijiandaa kwa haraka sana. Baada ya kujiandaa walimchukua dokta Morgan na kuanza msafara wa kuelekea katika hospitali ya rufaa ya Taifa ya Kano.

*******

HOSPITALI YA RUFAA YA TAIFA YA KANO



Mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba alikuwa amefikishwa katika hospitali ya rufaa ya Taifa ya Kano. Madaktari walikuwa wakihaha huku na huku katika kuhakikisha kwamba hali ya mheshimiwa Rais inakuwa ahueni.



Dokta Morgan daktari kutoka Idara ya usalama wa Taifa ya BSA ndiye alikuwa daktari ambaye alikuwa ameteuliwa kuhakikisha kwamba maisha ya mheshimiwa Rais yanakuwa salama. Sababu za kumpendekeza na kumteua daktari huyu ilikuwa ni kutokana na umahiri wake katika masuala ya tiba.



Hali ya ulinzi kuzunguka eneo lote la hospitali ile ilikuwa imeimarishwa sana. Askari mbalimbali kutoka katika idara mbalimbali za usalama wa Taifa walikuwa wametapakaa kila mahali katika kuhakikisha hakuna hatari yoyote ambayo inatokea kwa mheshimiwa Rais.



“Hali ni mbaya. Mheshimiwa Rais amepoteza damu nyingi sana. Hivyo anatakiwa kuongezewa damu haraka sana!” dokta Morgan aliongea mbele ya wakuu wa idara mbalimbali za usalama.



“Sasa si aongezewe haraka dokta?” mkuu wa idara ya usalama wa Rais ikulu aliongea.



“Uko sahihi mkuu. Nadhani kila mmoja anawaza kama ambavyo wewe wawaza. Lakini kuna tatizo kubwa sana” dokta Morgan aliongea.



“Tatizo gani dokta?” Chifu aliuliza.



“Damu ya mheshimiwa Rais ipo katika kundi maalum. Watu ambao wana damu ambayo ipo katika kundi hili ni wachache sana. Hivyo hii inaleta ugumu katika upatikanaji wa damu ya kumwongezea mheshimiwa Rais” dokta Morgan aliongea.



“Duh!” wakuu wale wa Idara za usalama wa Taifa walijibu kwa pamoja wakionyesha kuchoka kabisa kwa majibu yale kutoka kwa dokta Morgan.



“Sasa tunafanyaje dokta?” afisa mwingine aliuliza



“Kwa mujibu wa rekodi zilizopo ni kwamba hapa nchini kuna watu sita ambao wana damu ya kundi hili la mheshimiwa Rais. Hawa watano rekodi za upatikanaji wao hazijawekwa vizuri. Lakini yupo huyu mmoja ambaye rekodi zake zipo clear kabisa!” dokta Morgan aliongea.



“Basi huyo aletwe hapa mara moja pasi kupoteza muda” Chifu aliongea.



“Kwa mujibu wa rekodi zilizopo ni kwamba hapa nchini kuna watu sita ambao wana damu ya kundi hili la mheshimiwa Rais. Hawa watano rekodi za upatikanaji wao hazijawekwa vizuri. Lakini yupo huyu mmoja ambaye rekodi zake zipo clear kabisa!” dokta Morgan aliongea.



“Basi huyo aletwe hapa mara moja pasi kupoteza muda” Chifu aliongea.



SASA ENDELEA



“Huyu bwana anaitwa Martin Samweli. Ni askari jeshi katika jeshi la BMM. Hapo awali alikuwa ni mwanajeshi katika Jeshi la wananchi wa Bantu lakini baadaye aliasi na kujiunga na kikundi cha waasi cha BMM” dokta Morgan aliongea.



“Mungu wangu!” wakuu wale waliongea kwa pamoja vinywa vyao vikiwa wazi kabisa kuonyesha kukata tama kabisa.



“Hii ina maana kwamba inatakiwa kwenda katika kikundi hicho cha waasi na kumchukua huyu bwana ili aje awe msaada hapa kwa maisha ya mheshimiwa Rais” dokta Morgan aliongea.



“Aiseee! Hapa tuna changamoto kubwa sana. Litawezekanaje jambo hili?” afisa mmoja alihoji.

ITAENDELEA

   

ITAENDELEA

HEKAHEKA MSITUNI - 2

    


Simulizi : Hekaheka Msituni 


Sehemu Ya Pili (2)


Simulizi : Hekaheka Msituni 

Sehemu Ya Pili (2)









“Sasa katika wiki hili nitafanya mchakato wa kuacha kazi. Kuacha kazi kwangu hakutakuwa katika mfumo wa kawaida. Kutakuwa ni kwa kutoweka tu kazini. Naamini jeshi litanisaka lakini halitanipata. Na pia ndani ya wiki hili litafanya ziara ya kuangalia ni mahali gani katika nchi hii ambapo patatufaa kuweka kambi ya jeshi letu” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Basi sawa. Nadhani tutawasiliana kwa kila hatua” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



SASA ENDELEA



“Jambo la msingi unatakiwa uandae magari kama matano hivi ambayo tutaanza nayo katika matumizi hapo kambini” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Hilo ni jambo dogo sana kwangu. Idadi yoyote ya magari ambayo unayataka, utayapata” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



Baada ya hapo wawili hawa waliendelea na mazungumzo yao ambayo yalichukua muda mrefu sana. Mazungumzo yao yalikuwa ni katika kuimarisha na kuboresha mikakati kuelekea jambo lile la uundwaji wa jeshi mpaka mapinduzi ya kijeshi ambayo watayafanya hapo siku za mbeleni.



Bwana Shukuru Kizibo alionekana ni mtu mwenye furaha sana kukutana na Kanali Edson Makoko na kufanya naye mazungumzo. Aliona kama mipango yake inaelekea kutimia kwa urahisi kabisa tofauti na vile ambavyo alidhani hapo awali. Hii ilimpa chachu ya kuendelea kusonga mbele na michakato ya uundwaji wa jeshi.

********

BAADA YA MIAKA MIWILI

Kikundi cha waasi Cha Bantu Military Movement (BMM) kwa sasa kilikuwa kimekuwa. Kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa na jeshi kubwa sana kwa sasa. Kilikuwa kikiendesha jharakati zake za uasi kutoka katika misitu ya Masolo misitu mikubwa ambayo ilikuwa ikipatikana kusini mwa nchi ya Bantu.



Serikali ya Bantu chini ya Rais Ditrick Mazimba ilikuwa ikijaribu kupambana na kikosi hiki pasi mafanikio ya kukiangamiza. Kilikiwa ni kikundi ambacho kilikuwa na nguvu sana. Kilikuwa kimejiimarisha kila mahali kuanzia silaha, chakula mpaka huduma za afya. Kikundi hiki kilizidi kuwa tishio kadri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele.



Kanali Edson Makoko alizidi kupata umaarufu mkubwa sana kwani ilisemekana ndiye aliyekianzisha kikundi hiki mara baada ya kulisaliti jeshi la wananchi wa Bantu kuacha kazi na kuacha kazi na kutorokea katika misitu ya Masolo.



Lakini iliaminika kwamba mbali na Kanali Edson kuwa kiongozi wa kikundi hiki, lakini kulikuwa na mkono wa mtu mkubwa mwenye pesa ambaye alikuwa akikifadhili kikundi hiki. Lakini hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa akifahamu mfadhili wa kikundi hiki. Watu wengine walifika mbali kwa kuwaza.



Walihisi huenda kulikuwa na nchi fulani huko Ulaya ambayo ilikuwa ikikifadhili kikundi hiki kwa silaha na huduma mbalimbali. Hakuna hata mmoja aliyefahamu kwamba bwana Shukuru Kizibo ndiye ambaye alikuwa mfadhili mkuu wa kikundi hiki.



Bwana Shukuru Kizibo alikuwa na furaha muda wote kadri alivyokuwa akiyaona maendeleo na mafanikio ya kikundi hiki. Aliona kama ndoto zake za kuwa Rais wa Bantu zilikuwa jirani sana kutimia. Aliamini kwamba alikuwa jirani kabisa katika kuishangaza dunia na kuifanya isiamini kile ambacho itakuwa ikikishuhudia.



Kwa upande wake Kanali Edson Makoko alikuwa na furaha kubwa sana pengine kumpita hata bwana Kizibo. Hii hasa ni kwa sababu ndoto zake za kuwa na pesa pamoja na nguvu zilikuwa zimetimia. Mpaka sasa alikuwa amekwishamchota bwana Shukuru Kizibo pesa nyingi sana.



Bwana Shukuru Kizibo yeye kwa upande wake hakuwa akifahamu kwamba alikuwa akihujumiwa na Kanali Edson Makoko. Yeye alimwamini mwanajeshi huyu muasi kwa kiwango chote cha uaminifu. Alikwishausahau ule usemi wa wahenga usemao ‘Kikulacho ki nguoni mwako’



Yalikuwa ni majira ya usiku bwana Shukuru Kizibo alikuwa amejaa tele nyumbani kwake. Alikuwa ametulia yeye na familia yake wakiyafurahia maisha. Bwana Kizibo alikuwa na familia ya mke na watoto watatu.



Bwana Shukuru Kizibo aliipenda sana familia yake. Alitaka muda wote iishi maisha ya raha mustarehe. Hakutaka ipate shida hata kidogo. Jambo hili ndilo ambalo lilimfanya kila uchao azidi kupambana katika miradi yake ili aweze kuingiza pesa nyingi sana.



Bwana Shukuru Kizibo alipata ugeni ambao hakuutaraji. Ugeni huu ulikuwa ni wa Kanali Edson Makoko. Nasema ugeni huu hakuutaraji kwa sababu, kwa siku ile hakuwa na miadi kabisa ya kukutana na Kanali Edson Makoko. Alichofahamu ni kwamba Kanali Edson Makoko alikuwa msituni akiendelea na shughuli zake za kijeshi.



“Karibu sana bwana Makoko!” bwana Shukuru Kizibo alimkaribisha Kanali Edson Makoko katika chumba chake cha mazungumzo kwa kumpa mkono na kasha kumwonyesha mahali pa kuketi.



“Nashukuru sana bwana Kizibo. Vipi hali yako pamoja na familia?” Kanali Edson Makoko alijibu na kusabahi.

“Sisi tuko salama kabisa. Mungu anazidi kutupigania” bwana Shukuru Kizibo alijibu.



“Vipi, naona leo umenitembelea kwa ghafla pasi miadi. Vipi kwema kweli huko kambini?” bwana Shukuru Kizibo aliongea akiuliza.



“Huko kwema kabisa bwana Kizibo. Ondoa shaka kabisa kwani kila kitu kipo salama kabisa” Kanali Edson Makoko alijibu.



“Nafurahi kusikia hivyo. Haya nipe maneno rafiki yangu. Shughuli zinaendaje huko?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.



“Shughuli zinaenda vema kabisa. Jeshi linazidi kuwa imara na tishio kabisa kwa serikali. Yaani kwa sasa serikali inakosa kabisa usingizi kwa kutuhofia. Na hili ni jambo jema kabisa katika kuelekea mafanikio ya adhma yetu” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Sawasawa, hizo ni habari njema kabisa kuzisikia” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Sasa bwana Shukuru Kizibo, mimi na wewe tumetoka mbali sana. Tumeshirikiana mambo mengi sana katika michakato yetu. Umekuwa msaada mkubwa sana mpaka hapa tulipofikia. Ninapaswa kukushukuru sana kwa hilo” Kanali Makoko aliongea na kumtazama bwana Shukuru Kizibo usoni.



“Usijali bwana Makoko kwani jambo hili ni la kwetu sote” bwana Shukuru Kizibo alijibu.



“Sasa bwana Kizibo, mimi nimekuja kukuaga na kukutakia safari njema” Kanali Edson Makoko aliongea maneno ambayo yalikuwa ni magumu sana kwa bwana Shukuru Kizibo kuyaelewa.



“Una maana gani bwana Makoko? Umepata wapi taarifa kwamba mimi nasafiri? Mbona mimi sina ratiba ya kusafiri kwa sasa?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza kwa mshangao.



“Ni kweli bwana Kizibo lakini ratiba yaw ewe kusafiri nimeitengeneza mimi. Na nimekuja hapa kwako kwa ajili ya kukusafirisha!” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Unasemaje bwana Makoko?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.

Bwana Shukuru Kizibo hakulipata jibu la swali lake kwani alijikuta akitazamana na mtutu wa bastola ambao ulikuwa umeelekezwa katika paji lake la uso.







“Unasemaje bwana Makoko?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.

Bwana Shukuru Kizibo hakulipata jibu la swali lake kwani alijikuta akitazamana na mtutu wa bastola ambao ulikuwa umeelekezwa katika paji lake la uso.



SASA ENDELEA



“Hapana bwana Makoko, huwezi nifanyia hivi” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Pole sana bwana Shukuru Kizibo. Ninahitaji sana pesa, mali, umaarufu pamoja na cheo. Uwepo wako utakuwa ni kikwazo katika kufanikisha adhma yangu. Uliyoyafanya mpaka sasa kwa nafasi yako yanatosha. Sasa unapaswa kusafiri na uniache mimi hapa duniani nikiendelea kuyafaidi maisha” Kanali Edson Makoko aliongea kwa tambo.



“Hapana bwana Edson. Usifanye hivyo tafadhali. Kama wataka pesa mimi nitakupa kiasi chochote ukitakacho!” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Hapana bwana Shukuru. It’s too late to decide. Maamuzi na mipango hii nilikwishaipanga muda mrefu sana!” Kanali Edson Makoko alijibu.



Bwana Shukuru Kizibo alibaki ameyatumbua macho yake. Hakuamini kile ambacho kilikuwa kikitokea. Alijihisi kama yuko ndotoni. Alijilaumu sana kwa kumwamini mwanajeshi huyu ambaye alikuwa ni hatari kama nyoka.



Alichobaki kukifanya kwa muda ule ni kumwomba mwenyezi Mungu amwepushe na kikombe kile ambacho kilikuwa ni kigumu sana kukinywa. Hakufahamu kama alikuwa na uwezo zaidi wa kumshawishi Kanali Edson Makoko kuyabatilisha mawazo yake.



Risasi moja ambayo ilitoka katika bastola ile yenye kiwambo cha kuzuia sauti ya Kanali Edson Makoko ilipenya katika paji la uso la bwana Shukuru Kizibo. Risasi ile ilitokeza nyuma ya kichwa na kukifumua kabisa kisogo cha bwana Shukuru Kizibo. Mwili wa bwana Shukuru Kizibo ulidondokea juu ya meza.



Baada ya hapo Kanali Edson Makoko alikichomoa kisu chake kikali kutoka katika ala yake na kuikatakata shingo ya bwana Shukuru Kizibo.



Alipotoka hapo Kanali Edson Makoko alienda mpaka sebuleni ambako familia ya bwana Shukuru Kizibo ilikuwa imetulia ikitazama televisheni. Huko nako Kanali Edson Makoko alifanya mauaji ya kutisha nay a kinyama sana. Aliikatakata miili ya wanafamilia wale na kuitenganisha vichwa na viwiliwili vyake. Hakika hali ilikuwa inatisha sana katika jumba la tajiri Shukuru Kizibo.



Baada ya kuridhishwa na mauaji ambayo alikuwa ameyafanya, Kanali Edson Makoko alitoweka kutoka katika eneo lile huku akiwa ameyabeba mabegi kadhaa ambayo yalikuwa yamejaa fedha. Pesa hizi zilikuwa ndani ya jumba lile la marehebu Shukuru Kizibo.

******

Mauaji ya bwana Shukuru Kizibo na familia yake yaliishtua nmchi nzima ya Bantu. Watu wengi walishangaa kwa mauaji ya kikatili kama yale kufanywa na binadamu. Mauaji yale yalivihangaisha sana vyombo mbalimbali vya usalama mchini Bantu kujua sababu hasa ya mauaji yale.



Iliaminika huenda ulikuwa ni uhasimu wa kisiasa ndiyo ambao ulipelekea mauaji yale. Lakini wengine waliamini kwamba bwana Shukuru Kizibo kama mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa, alikuwa na maadui wengi katika biashara zake. Huenda alikuwa amedhulumiana na mfanyabiashara mwenzake ambaye aliamua kulipa kisasi kwa kutekeleza mauaji yale.



Lakini zote hizo zilikuwa ni hisi tu. Hakuna upande hata mmoja ambao ulikuwa na jibu sahihi. Siri ya vifo vile alibaki nayo marehemu Shukuru Kizibo pamoja na Kanali Edson Makoko.



Msiba ule ulilitingisha Taifa zima la Bantu kwa sababu bwana Shukuru Kizibo alikuwa ni mtu mkubwa sana katika medani za siasa. Pia alikuwa na umaarufu mkubwa sana katika sekta ya biashara. Hivyo umaarufu wake ulikuwa umetapakaa Bantu nzima na kuvuka mipaka yake.



Wafuasi wa chama chake cha siasa waliomboleza sana. Waliona kama wamepata pengo kubwa sana ambalo lilikuwa ni vigumu sana kuzibika. Bwana Shukuru Kizibo alibaki kuwa ni mtu wa kukumbukwa katika historia ya chama chake.



Serikali ya Bantu nayo iliumizwa na vifo vile kwa sababu bwana Shukuru Kizibo alikwua na umuhim mkubwa sana katika medani za siasa ya Bantu. Pia Taifa lilikuwa limepoteza nguvu kazi kwani bwana Shukuru Kizibo alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana ambapo biashara zake zilikuwa zikiingizia nchi kipato kikubwa sana. Hivyo msiba huu ulikuwa umegusa kila kona miongoni mwa wananchi na nchi nzima ya Bantu kwa ujumla.

*******

“BMM oyeeee!” Kanali Edson Makoko aliongea kwa nguvu.

“Oyeeeeee!” wanajeshi walijibu wakizinyanyua bunduki zao juu.



Hii ilikuwa ni katika paredi ambayo ilikuwa imeitishwa katika kambi ya BMM huko katika misitu ya Masolo.



“Kama ambavyo mmesikia ni kwamba, mzee wetu bwana Shukuru Kizibo pamoja na familia yake wameuawa kikatili sana. Hili ni pigo kubwa sana kwetu kwani mzee yule alikuwa ndiye mfadhili wetu mkubwa!” Kanali Edson Makoko alitulia na kuwatazama wanajeshi wake ambao walikuwa wamejawa na nyuso za huzuni.



“Ninaamini na ninafahamu kwamba mauaji haya yamepangwa na kutekelezwa na Rais Ditrick Mazimba kwa sababu ndiye alikuwa hasimu wake mkubwa. Nadhani leo ndiyo mmeuona unyama ambao Rais huyu anao!”



Kanali Edson alizidi kutema cheche akimchafua Rais Ditrick Mazimba ndani ya fikra za wanajeshi wale. Kwa kifupi wanajeshi wale walikuwa wakilishwa sumu mbaya nay a hatari sana ya kuichukia serikali yao. Kanali Edson Makoko alikuwa anajua sana kucheza na saikolojia ya wanajeshi wale.



“Sasa je, kuuawa kwa bwana Shukuru Kizibo ndiyo iwe mwisho wa harakati zetu za kuhakikisha tunaichukua dola?” Kanali Edson Makoko aliuliza kwa mzuka mkubwa.



“Hapanaaaa! Haiwezekani kabisaaaaaa!” wanajeshi wale walijibu kwa umoja kwa jazba kubwa sana.



“Nami nawaunga mkono kwa kusema haiwezekani. Nitawaongoza nma nitahakikisha tunampindua Rais mnyama na shetani Ditrick Mazimba. Kifo cha mlezi na mfadhili wetu ni lazima kilipwe!” Kanali Edson Makoko alifoka kwa jazba huku wanajeshi wakishangilia kwa kuzinyanyua silaha zao juu.



“Hatuna sababu ya kuendelea kumwacha shetani huyu akivuta hewa ya dunia hii kwa raha mustarehe wakati ndani yake amejaa ushetani kwa kutokomeza roho za watu wasio na hatia!” Kanali Edson aliongea.



“Lazima auawe! Tunataka Bantu mpyaaaa!” wanajeshi wale walipiga kelele wakimshangilia sana Kanali Edson Makoko.

Wanajeshi wale hawakuifahamu siri ambayo ilikuwa nyuma ya pazia. Hawakufahamu kwamba kiongozi wao huyu ambaye alikuwa mbele yao ndiye ambaye alikuwa anahusika na mauaji yale. Laiti wangelifahamu hilo, kamwe wasingebaki pale kumsikiliza mahubiri yake. Ni lazima wangeanzisha vurugu kubwa sana.



Lakini Kanali Edson Makoko alikuwa na akili kubwa sana. Alikuwa amesajili watoto katika jeshi lake ili iwe rahisi kwake kuuteka ufahamu wao. Alichofanya ni kuupandikiza ukatili ndani ya vichwa na mioyo yao. Aliwalisha sumu ya ukatili dhidi ya binadamu. Kadri walivyozidi kuwa wakubwa basi walizidi kuwa ni watu wa hatari sana ambao walikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yoyote ya kikatili pasi kusita.

******







Lakini Kanali Edson Makoko alikuwa na akili kubwa sana. Alikuwa amesajili watoto katika jeshi lake ili iwe rahisi kwake kuuteka ufahamu wao. Alichofanya ni kuupandikiza ukatili ndani ya vichwa na mioyo yao. Aliwalisha sumu ya ukatili dhidi ya binadamu. Kadri walivyozidi kuwa wakubwa basi walizidi kuwa ni watu wa hatari sana ambao walikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yoyote ya kikatili pasi kusita.



SASA ENDELEA



Rais Ditrick Mazimba alikuwa ni Rais kipenzi cha watu wengi sana nchini Bantu. Alikuwa ni Rais ambaye alifanikiwa kuwaunganisha wanabantu na kuwafanya kuwa kitu kimoja. Alikuwa ni Rais ambaye alikuwa ameleta upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi. Rais Ditric Mazimba alikuwa ni Rais ambaye alipinga sana ufisadi na aliapa kupambana nao mpaka tone lake la mwisho la jasho lake.



Pia Rais Ditrick Mazimba aliwawajibisha viongozi na watumishi wote wa serikali ambao walikiuka katiba ya nchi na kuamua kwenda kinyume nayo. Jambo hili lilisababisha Bantu kuanza kufikia mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi ambayo haikuwahi kufikia hapo awali.



Rais Ditrick Mazimba alikuwa ametenga miezi miwili ya kufanya ziara katika nchi nzima ya Bantu. Katika kipindi hicho cha miezi miwili aliamini kwamba atakuwa ametembelea kila eneo katika nchi ya Bantu. Na kwa sasa alikuwa amekwishaianza ziara yake.



Katika ziara hii alikuwa akiwatembelea wananchi wa Bantu na kusikiliza kero zao ambazo zilikuwa zikiwakabili. Hii ilikuwa ni kawaida kabisa kwa mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba kufanya hivi kila baada ya kipindi fulani. Jambo hili lilimuongezea thamani Rais huyu mbele ya wananchi. wananchi waliona kwamba alikuwa ni Rais ambaye alikuwa akiwajali sana.



“Eneo hili la Matutu halina mahali pazuri penye hadhi na usalama wa kulala Rais. Labda mpaka katika eneo la Soweni mji unaofuata kutoka mji huu” mkuu wa Wilaya ya Soweni alikuwa akiongea na maafisa usalama ambao walikuwa katika msafara ule wa Rais.



“Pana umbali gani kutoka hapa?” afisa usalama mmoja aliuliza.



“Ni takribani kama saa moja na nusu!” mkuu wa wilaya alijibu.



“Tutafika usiku” afisa mwingine alichangia. :Hakika, lakini hii si nzuri” afisa mwingine naye aliongea.



“Basi tunaomba ufanyike utaratibu wa kuhakikisha kwamba mahali salama panaandaliwa” afisa usalama mmoja aliongea.

“Usijali. Mahali pako salama na pia pako tayari muda wote!” mkuu wa wilaya aliongea.



Kwa wakati ule yalikuwa ni majira ya saa kumi na mbili za jioni. Magari ya msafara wa Rais yalikuwa yakizidi kutimua vumbi kwa mwendo wa kasi sana. Walitaka wahakikishe kwamba wamefika Soweni kabla masaa hayajaenda sana na giza halijawa zito sana. Madereva ambao walikuwa wakiyaendesha magari yale walikuwa ni mafundi hasa katika udereva. Walikuwa wakijua kuyamudu magari yao ambayo yalikuwa yakirindima vilivyo juu ya barabara.

*******

Msafara ule ulifika salama katika mji wa Soweni. Mji huu ulikuwa umechangamka na ndiyo yalikuwa makao makuu ya wilaya ya Soweni.moja kwa moja mkuu wa wilaya aliuongoza msafara ule mpaka katika ikulu ndogo mahali ambapo mheshimiwa Rais angelala.



Ulinzi ambao ulikuwa mahali hapa ulikuwa ni mzito sana. Maafisa usalama na walinzi mbalimbali walikuwa wametapakaa kila kona ya ikulu hii ndogo mjini Soweni. Hii yote ilikuwa ni katika kuhakikisha suala zima la usalama linaratibiwa na kutekelezwa vema kabisa.



Inchaji wa ulinzi na usalama katika alikuwa akitembelea kila kona ya ikulu ile kuhakikisha kwamba mambo yalikuwa yanakwenda sawa sawia. Askari huyu alikuwa makini sana katika utendaji wa kazi yake.



Nje ya chumba ambacho alikuwemo Rais palikuwa na walinzi wawili. Ndani ya chumba ambacho Rais alikuwemo kulikuwa na mlinzi mmoja ambaye alikuwa akihakikisha usalama kwa kiongozi huyu wan chi unakuwa sawa.



Yalikuwa ni majira ya kuelekea saa nne za usiku, askari walinzi pale nje ya chumba alimokuwemo mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba walitazamana na kukonyezana.

ITAENDELEA


ITAENDELEA

HEKAHEKA MSITUNI - 1

   


Simulizi : Hekaheka Msituni 


Sehemu Ya Kwanza (1)



IMEANDIKWA NA : KALMAS KONZO 

********************************************************************************

Simulizi : Hekaheka Msituni 

Sehemu Ya Kwanza (1)





Bantu Military Movemnt (BMM) killikuwa ni kikundi cha waasi ambacho kilikuwa kikiendesha harakati zake kusini mwa nchi ya Bantu. Kikundi hiki kilikuwa kina nguvu sana na kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele ndivyo ambavyo kilikuwa kikizidi kujiimarisha. Kikundi hiki kilikuwa kimeiimarisha kwa jeshi kubwa pamoja na silaha nyingi na za kisasa. Kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele kikundi hiki kilizidi kuwa tishio kwa serikali ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa ikiongozwa na Rais Ditrick Mazimba.



Kwa upande wake mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba alikuwa ni Rais kipenzi cha wengi. Wannanchi wengi wa Bantu walimpenda sana Rais huyu kwani alikuwa ni Rais ambaye alikuwa akiwajali sana. Alikuwa ni Rais ambaye alikuwa anajali utu na kutambua thamani ya binadamu. Alikuwa ni Rais ambaye alikuwa akiwajali wananchi wake na kuwasaidia kwa kadri ya uwezo wake na wa serikali yake.



Hata wananchi wenyewe waliwashangaa wale wanajeshi ambao walikuwa wakiendesha harakati za mapinduzi. Waliwaona kama walikuwa ni wendawazimu. Na kwa mtazamo dhahiri ni kweli wanajeshi wale hawakuwa na sababu nyingine ya uasi wao kwa serikali zaidi ya uroho wa madaraka. Ilikuwa ni uendawazimu kuendesha harakati za uasi kwa serikali sikivu na yenye kuwajali wananchi wake kama serikali ya Bantu.



Hata Umoja wa Mataifa ulikuwa ukilipigia kelele suala la waasi wale kila uchao. Umoja wa Mataifa ulikuwa ukiwarai waasi wale kuweka silaha zao chini na kukaa meza moja ya mazungumzo ya amani na serikali ya Bantu ili waweze kueleza shida yao hasa ilikuwa ni nini?



Wanajeshi wale hawakutaka kusikiliza rai za Umoja wa Mataifa pamoja na taasisi mbalimbali ambazo zilikuwa zikijihusisha na haki za binadamu duniani. Wenyewe waliendelea kudai tu kwamba Rais Ditrick Mazimba pamoja na serikali yake hawakustahili kuwepo madarakani.



Harakati hizi za uasi zilikuwa zikiendeshwa na Kanali Edson Makoko mwanajeshi muasi kutoka katika Jeshi la Wananchi wa Bantu. Mwanajeshi huyu alikuwa ameacha jeshi na kuingia msituni ambako aliwakusanya wanajeshi kadhaa ambao walimuunga mkono na kuanzisha kikundi cha uasi. Walitafuta silaha na kuzidi kujiimarisha.



Katika kujijengea uwezo kiuchumi kikundi hiki kilianza kufanya shughuli za ujambazi ambapo kilivamia na kupora mali na pesa kutoka kwa watu makampuni na taasisi mbalimbali. Hii ilikifanya kikundi hiki kizidi kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi.

Baadaye wanajeshi hawa walianza kuwateka watoto na vijana na kuanza kuwafunza matumizi ya silaha na baaddaye kuwaweka katika jeshi. Kikundi hiki sasa kilianza kuwa tishio kwa nchi zilizopakana na Bantu pamoja na Afrika nzima kwa ujumla.



Harakati hizi za uasi zilianza miaka saba iliyopita ambapo palikuwa na uchaguzi mkuu nchini Bantu. Uchaguzi huu ulikuwa ni wa Rais, wabunge pamoja na madiwani. Ulikuwa ni uchaguzi ambao ulikuwa na changamoto nyingi sana. Na huu ndiyo ulikuwa uchaguzi ambao ulimwingiza madarakani mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba katika kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi.

Uchaguzi ule ulikuwa na mchuano mkali sana kati ya mahasimu wawili wakubwa wa kisiasa nchini Bantu. Mahasimu hawa walikuwa ni mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini Bantu kwa kipindi kile bwana Shukuru Kizibo.



Wanasiasa hawa walichuana vikali sana kila mmoja akimwaga sera zake ambazo aliamini kwamba zitawavutia wananchi wa Bantu kumpa kura. Kila mmoja alijiona ni bora kuliko mwenzake.



Katika uchaguzi ule bwana Shukuru Kizibo alijipa asilimia kubwa sana ya ushindi kwa sababu yeye alikuwa akitokea katika chama kikuu cha upinzani nchini Bantu.



Chama hiki kilikuwa na nguvu sana na kilionyesha kuwa na wafuasi wengi sana. Wafuasi wa chama hiki walikuwa ni wafuasi ambao walikuwa na ashki kubwa sana ya kuchukua madaraka ya uongozi wa serikali ya Bantu.



Uchaguzi ule uliendeshwa kwa vurugu nyingi sana. Wananchi hawakutulia hata kidogo kwani kila mmoja kwa upande wa chama chake alijihesabu kwamba ni mshindi wa uchaguzi ule.

Uchaguzi ulifanyika kwa muda wa siku moja na baada ya hapo uhesabuji wa kura ulianza. Katika kipindi chote cha kuhesabu kura, wananchi walikuwa wakifanya vurugu nyingi sana. Wafuasi wa chama pinzani walikuwa wakitaka muda wote wawe jirani na vyumba ambamo shughuli ya kuhesabu kura ilikuwa ikiendelea.



Dhumuni lao kubwa hasa lilikuwa ni kuzilinda kura zisiibiwe. Walitamani hata kulala hapohapo. Jambo hili liliwafanya waingie mgogoro na vyombo vya usalama ambavyo vilikuwa vijiraibu kuwatawanya. Baada ya siku tano za kuhesabu kura, hatimaye majibu yaliwekwa hadharani hasa kwa kura ya urais kwani majibu ya ubunge na udiwani yalikuwa yametoka mapema. Mheshimiwa Ditrick aliibuka kidedea kwa uchaguzi ule na kutangazwa kuwa mshindi.



Jambo hili lilimkasirisha sana bwana Shukuru Kizibo pamoja na wafuasi wa chama chake ambao walianzisha vurugu kubwa sana. Vurugu zile ilikuwa kubwa sana ambapo wafuasi wa chama kile pinzani walikuwa wakipambana na vyombo vya usalama vya nchini Bantu.



Katika ghasia zile watu takribani elfu moja na mia moja waliuawa. Bwana Shukuru Kizibo alijikuta akishikiliwa na polisi na baada ya vuguvugu la uchaguzi kwisha na Rais mpya kutangazwa, alipelekwa mahakamani. Alionekana na hatia na mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka kumi na tano gerezani. Hukumu hiyo iliwahusu wafuasi wa bwana Shukuru Kizibo ambao walimsaidia katika kufanya vurugu zile.



Lakini baada ya mwaka mmoja wa kutumikia adhabu ile, mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba alitoa msamaha kwa bwana Shukuru Kizibo na wafuasi wake. Hii yote ilikuwa ni katika kutafuta amani na utulivu wa kisiasa nchini Bantu.



Kwa upeo wake uliojaa busara mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba alidhani kwamba kwa kufanya vile atakuwa ameutatua mgogoro wa kisiasa ambao ulikuwa ukifukuta nchini Bantu baina ya chama tawala na chama kikuu cha upinzani. Yaani ilikuwa ni afadhali ambapo bwana Shukuru Kizibo alikuwa akishikiliwa gerezani.



Kumpa msamaha mfanyabiashara na mwanasiasa huyu lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo mheshimiwa Rais Ditrick Mazimba alikuwa amelifanya. Kosa hili lilimgharimu sana na muda wote huwa anajilaumu kwa kuchukua maamuzi yale ambayo yapo kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Bantu.



Bwana Shukuru Kizibo aliporudi uraiani tu alianza kufanya vuguvugu la uasi wa chini kwa chini. Lengo lake kubwa lilikuwa ni hapo baadaye kuja kufanya mapinduzi makubwa sana ambayo yataistaajabisha dunia.



Bwana Shukuru Kizibo alikuwa ameyadhamiria hasa mapinduzi haya. Hakuwa na huruma hata kidogo kwa raia wenzake wa Bantu juu ya madhara ambayo yatatokea katika utekelezaji wa mapinduzi hayo. Kwa sasa alikuwa amechafukwa kabisa. Moyo wake kwa sasa haukuwa tofauti na moyo wa mnyama mkali na katili wa mwituni.

*******







Bwana Shukuru Kizibo alikuwa ameyadhamiria hasa mapinduzi haya. Hakuwa na huruma hata kidogo kwa raia wenzake wa Bantu juu ya madhara ambayo yatatokea katika utekelezaji wa mapinduzi hayo. Kwa sasa alikuwa amechafukwa kabisa. Moyo wake kwa sasa haukuwa tofauti na moyo wa mnyama mkali na katili wa mwituni.



SASA ENDELEA



Kwanza kabisa bwana Shukuru Kizibo alianza kwa kuumiza kichwa ni namna gani atapata jeshi ambalo litamuunga mkono katika mapinduzi yake aliyoyakusudia. Aliwaza sana lakini mwishoni alikuja kujipa moyo kwamba katika dunia hii kila kitu kinawezekana. Aliamini kwamba kwa kutumia pesa ambayo alikuwa nayo, basi angeweza kuunda jeshi imara ambalo litaweza kupambana na serikali kwa mafanikio makubwa.



Jambo la kwanza ambalo alipanga kuanza nalo katika kuutekeleza mchakato ule lilikuwa ni kumpata mwanajeshi mmoja ambaye ndiye angekuwa inchaji katika kuelekea kuliunda jeshi ambalo alikuwa akilitaka.



Mwanajeshi huyu ambaye alimhitaji kuwa inchaji alitaka awe ni mwanajeshi wa ngazi ya juu jeshini ambaye amehudumu jeshini kwa muda mrefu hivyo anafahamu mbinu mbalimbali za kijeshi.

*******

Kanali Edson Makoko alikuwa ni mwanajeshi mtumishi katika Jeshi la wananchi wa Bantu. Alikuwa ni mkuu wa kambi ya jeshi ijulikanayo kama KJ 05. Kanali Edson Makoko alikuwa amelitumikia jeshi kwa muda mrefu sana. Alikuwa ni mwanajeshi ambaye alikuwa ana sifa kubwa sana katika Jeshi la wananchi wa Bantu. Alikuwa ni mwanajeshi makini kabisa ambaye hakuwa akipenda utani pindi linapokuja suala la kazi.



Sambamba na hilo pia Kanali Edson Makoko alikuwa ni mwanajeshi mwenye sifa ya ukatili kupita kiasi. Yeyote ambaye alikuwa amekosea na kuingia katika anga zake, basi hakika alipata tabu sana.



Sifa hizi na zingine kedekede ndizo ambazo zilimfanya apande vyeo harakaharaka. Na sasa alikuwa ni mkuu wa kambi KJ 05 kambi ambayo ilikuwa ni muhimu sana kwa jeshi la wananchi. Kambi hii ilikuwa inatunza silaha mbalimbali za jeshi na pia ilikuwa na gereza la kijeshi ambapo wafungwa wa kijeshi walikuwa wakifungwa humo.



Kanali Edson Makoko alikuwa na kasoro moja tu katika maisha yake. Kanali Edson Makoko alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na tamaa sana. Hakuwa ni mtu wa kutosheka kwa chochote alichonacho au akifanyacho.



Tabia hii ilimfanya awe ni mtu wa matumizi makubwa sana kuliko kipato ambacho alikuwa akikipata. Hii ilimfanya muda mwingi asiwe imara kiuchumi.



Kanali Edson Makoko alianza kufikiria namna mbadala ya kuweza kuongeza kipato tofauti kabisa na mshahara ambao alikuwa akipokea. Aliamini kwamba kwa kufanya hivyo basi maisha yake yangeliweza kumnyookea.



Na ni katika wakati huu ndipo ambapo alizipata habari za siri za mfanyabiashara maarufu nchini Bantu bwana Shukuru Kizibo za kutaka kufanya mapinduzi kwa serikali. Kanali Edson Makoko aliona kwamba hii ilikuwa ni fursa pekee kwake ambapo angeweza kutengeneza pesa nyingi sana ambazo angezitumia vyovyote apendavyo mpaka anaingia kaburini. Hii ilikuwa ni kwa kushirikiana na bwana Shukuru Kizibo kaika kuyatekeleza mapinduzi yale.

*******

Bwana Shukuru Kizibo alikuwa ametulia ndani ya baa ijulikanayo kama Oceania Bar. Chupa moja ya pombe kali aina ya Silicov inayotengenezwa nchini Urusi ilikuwa tuou. Hii ilimaanisha kwamba bwana Shukuru Kizibo alikuwa amekwishaimaliza pombe ile. Chupa ya pili kwa sasa nayo ilikuwa imekatwa robo.



Bwana Shukuru Kizibo alikuwa ni fundi mkubwa sana katika kukata masanga. Alikuwa na uwezo wa kunywa pombe nyingi sana pasi kulewa chakari. Kichwa chake kilikuwa ni kizuri sana. Hata watu wake wa karibu walimshangaa sana.



Pia pombe ni kitu ambacho bwana Shukuru Kizibo alikuwa akikipenda sana katika maisha yake. Bwana Shukuru Kizibo anapokuwa na mawazo mengi sana kichwani mwake, basi hupenda kujituliza kwa kuzitandika chupa nyingi za pombe kali.



Na kama ambavyo nilikudokeza hapo awali ni kwamba bwana Shukuru Kizibo kwa sasa alikuwa na mawazo mengi sana muda wote. Mawazo yake yalikuwa ni katika kuelekea kuliunda jeshi lake ambalo litashiriki katika mapinduzi ya serikali ya Bantu.



Akiwa katika burudani yake ile ya pombe, ghafla mhudum mmoja wa baa ile ambaye alikuwa ni mlimbwende hasa alikuja katika meza ya bwana Shukuru Kizibo. Mkononi alikuwa ameshikilia gazeti. Mlimbwende yule aliliweka gazeti lile mbele ya bwana Shukuru Kizibo. Pasi kusema chochote mlimbwende yule aligeuka na kuanza kutembea kuelekea kule ambako alikuwa ametoka.



Bwana Shukuru Kizibo alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni nini ambacho kilikuwa kikiendelea. Hakuelewa ni kwa nini mlimbwende yule alikuwa ametenda kitendp kile. Kwa kweli hakuelewa maana yake.



Baadaye aliamua kulichukua gazeti lile ili aweze kupitisha macho yake ndani. Akiwa katika kulifunufunua, ghafla kipande cha karatasi kilidondoka kutoka kurasa za katikati za gazeti lile.



“NAOMBA KUKUTANA NAWE HAPA NJE KATIKA GARI LAKO. NI MUHIMU SANA HASA KWA MIPANGO YAKO!” huu ulikuwa ni ujumbe ambao ulikuwa umeandikwa juu ya karatasi ile.



Macho ya bwana Shukuru Kizibo yalibaki yakiwa yameduwa juu ya maandishi ambayo yalikuwa yameandikwa katika karatasi. Pia kichwa chake kilikuwa kikiwaka moto kujaribu kuutafakari na kuuelewa ujumbe ule ambao ulikuwa umeandikwa katika karatasi ile.



Baadaye bwana Shukuru Kizibo alikiinua kichwa chake na kujaribu kumtazama mrembo yule ambaye alimletea gazeti lile ambalo lilikuwa na kipande kile cha karatasi chenye ujumbe lakini hakuweza kumwona. Alijaribu kuangazaangaza macho yake katika ukumbi wa baa ile huenda macho yake yangeweza kumwona mtu ambaye alikuwa ndiye mhusika na ujumbe ule, lakini aliambulia patupu.



Hapo awali alitaka kuupuuza ujumbe ule lakini upande wa pili wa akili yake ulimkataza kufanya vile. Upande ule wa akili yake ulimsisitiza kuitikia wito kwani hakufahamu umuhimu wa wito ule.



Bwana Shukuru Kizibo aliinyanyua chupa ile ya pombe kali na kupiga mafunda mawili ya mfululizo. Baada ya hapo alisimama na kuanza kutembea. Alipopiga hatua ya pili bwana Shukuru Kizibo alitaka kupiga mweleka ambapo alijishikilia katika kiti ambacho kilikuwa pembeni yake. Alitulia kidogo na kuuweka mwili wake sawa. Baada ya hapo alianza kutembea kuelekea nje ya baa ile kuitikia wito ule.



Dakika tatu zilitosha kumfikisha mpaka mahali ambapo alikuwa ameliegesha gari lake. Aliangaza macho yake kama angeweza kumwona mtu ambaye alikuwa akimhitaji lakini hakufanikiwa. Baadaye aliamua kuingia ndani ya gari ili aweze kumsubiri mtu huyo akiwa ndani ya gari.



Aliuingiza ufunguo wa gari katika tundu la mlango na kasha aliuzungusha. Baada ya hapo alikikamata kitasa na kukinyanyua. Mlango ulisalimu amri na kufunguka.

********





Aliuingiza ufunguo wa gari katika tundu la mlango na kasha aliuzungusha. Baada ya hapo alikikamata kitasa na kukinyanyua. Mlango ulisalimu amri na kufunguka.



SASA ENDELEA



Bwana Shukuru Kizibo alipigwa na butwaa mara baada ya macho yake kumwona mtu mmoja akiwa amekaa pembeni ya siti ya dereva.



“Wewe ni nani na umeingiaje humu ndani wakati mlango wa gari nilikuwa nimeufunga?” bwana Shukuru Kizibo aliporomosha maswali mawili mfululizo huku akimtazama mtu yule ndani ya gari lake.



“Acha maswali ya kitoto. Ingia ndani ya gari acha kupoteza muda. Hilo ni jambo dogo sana” Kanali Edson Makoko aliongea. Bwana Shukuru Kizibo hakujibu kitu. Alichofanya mi kuingia ndani ya gari kama vile ambavyo aliamriwa.

“Habari yako bwana Shukuru?” Kanali Edson Makoko alimsabahi bwana Shukuru Kizibo.



“Salama tu. Wewe ni nani na umefuata nini hapa?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.



“Usijali bwana Shukuru. Nitajitambulisha na utanifahamu kwa kina” Luteni Edson Makoko alijibu.



“Kwanza kabisa naitwa Kanali Edson Makoko mwanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Bantu. Mimi ni mkuu wa kambi ya jeshi ya KJ 05” Kanali Edson Makoko alianza kujitambulisha.



Ghafla mwili wa bwana Shukuru Kizibo ulishikwa na ganzi. Pombe aliyokunywa yote ilimtoka na macho aliyatumbua mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango. Utambulisho ule ulimshtua sana.



Hakufahamu ni nini ambacho kilikuwa kinaendelea. Alihisi huenda harakati zake za mapinduzi zitakuwa zimevuja na sasa wanajeshi walikuwa wamekuja kumsomba na kumpeleka kizuini. Alichoka sana. Ubongo uligoma kufanya kazi kwa muda.



“Ok, wahitaji nini kutoka kwangu bwana Makoko?” bwana Shukuru Kizibo alijitutumua na kuuliza swali.



“Kuwa mpole bwana Shukuru Kizibo. Hautakiwi kuwa na jazba kama ambavyo ninakuona ulivyo. Mimi nimekuja hapa kwa kheri kabisa na wala si kwa shari. Hivyo kuwa huru kabisa bwana Shukuru Kizibo!” Kanali Edson Makoko aliongea akimtoa wasiwasi bwana Shukuru Kizibo.



“Nimekuwa nikikufuatilia kwa muda mrefu sasa harakati zako kisiasa. Hakika wewe ni mtu wa pekee sana ambaye unastahili kupongezwa na kuungwa mkono!” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Ahsante sana!” bwana Shukuru Kizibo alijibu.



“Sasa mimi nipo hapa kwa ajili ya kukuunga mkono. Nahitaji kukuunga mkono kwa huo mpango ambao unao. Mpango wako unahitaji watu kama sisi” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Mpango gani? Mbona sikuelewi” bwana Shukuru Kizibo alijibu huku akihisi kwamba Kanali Edson Makoko alikuwa akimtega.



“Usijifanye huelewi bwana Shukuru Kizibo. Nadhani nilikwishakwambia hapo awali kwamba hupaswi kuwa na woga kwani mimi nimekuja hapa kwa kheri na si kwa shari. Hebu tuache utoto na tuongee mambo ya maana” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Sasa nitaamini vipi kama haupo hapa kwa ajili ya kunikaanga?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.



“Wewe ulikuwa una shida ya kupata wanajeshi kwa ajili ya kuunda jeshi. Sasa ni kwa nini unashindwa kuniamini kama mimi nipo tayari kwa ajili ya kukuunga mkono?” Kanali Edson Makoko aliuliza.



“Jambo linalonitia hofu ni kwamba, wewe ni mtumishi wa jeshi. Sasa utawezaje kushiriana name pasi kuleta matatizo jeshini?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.



“Hilo ni jambo dogo sana bwana Shukuru Kizibo. Mimi niko tayari kuacha jeshi kwa ajili ya kuuratibu na kuutekeleza mpango huu. Mpango huu ni muhimu sana kwangu kuliko huduma yangu jeshini. Mimi mwenyewe nilikuwa na ndoto za kuufanya mpango huu kwa muda mrefu sasa lakini sikuwa nimepata mtu wa kuweza kushirikiana naye. Nadhani kwa sasa Mungu amejibu maombi yangu na amekuleta wewe kwangu. Usiwe na shaka bwana Shukuru Kizibo” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Unajua wanipa mtihani mzito sana. Lakini ngoja nikuamini. Nadhani mimi pamoja nawe kwa ushirika wetu tutaweza kulifanisha jambo hili kwa mafanikio makubwa sana. Jambo la muhimu ni kuaminiana. Jambo hili ni jambo ambalo lina matunda makubwa sana hapo mbeleni. Ni jambo ambalo litayabadilisha kabisa maisha yetu na tutaishi kama wafalme mpaka tunaingia kaburini” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Kuhusu uaminifu kwangu ondoa shaka. Nadhani mimi ni mtu sahihi ambaye ulipaswa kunishirikisha mpango huu kwani sote tuna mawazo yanayooana. Wewe hesabu mafanikio tu bwana Shukuru Kizibo” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Sasa tunaanzia wapi mchakato huu huu maana ni kwa muda mrefu nimekuwa ninashindwa namna ya kuanza?” bwana Shukuru Kizibo aliuliza.



“Hili ni jambo dogo sana. Kwanza kabisa tunatakiwa kuunda jeshi. Mchakato huu utatuhitaji kuwa na bajeti ya kutosha kwani tutahitajika kuwa na silaha za kutosha pamoja na chakula cha kutosha pia” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Kuhusu bejeti, hilo lisikupe hofu hata kidogo. Nimejipanga vilivyo katika kuhakikisha mchakato huu unafanikiwa. Hivyo masuala yanayohusu ffedha wala yasikuumize kichwa. Itakuwa ni utekelezaji tu” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Safi sana. Hizo ni habari nzuri. Basi kama hali iko hivyo basi mchakato huu utafanikiwa mapema sana. Kama nilivyosema hatua ya kwanza itakuwa ni kulikusanya jeshi. Katika jeshi letu kutakuwa na watu mchanganyiko. Kutakuwa na wanajeshi wenye taaluma ya jeshi na pia kutakuwa na watu wa kawaida ambao ni vijana na watoto”



“Tutahitajika kuweka kambi kubwa mahali Fulani msituni ambapo tutakuwa tumepachagua. Tutaendesha mafunzo ya kijeshi kwa watoto hao pamoja na vijana. Niamini, jeshi letu litakuwa ni jeshi lenye nguvu sana!” Kanali Edson Makoko aliongea maneno ambayo yalimfurahisha sana bwana Shukuru Kizibo.



“Umebnifurahisha sana bwana Makoko. Maneno yako yananifanya nizidi kukuamini na pia kuamini kwamba kuna mafanikio makubwa sana mbele yetu. Hakika leo nimempata mtu sahihi kabisa katika mipango yangu” bwana Shukuru Kizibo aliongea.



“Usijali bwana Shukuru. Kila kitu kitakwenda kama ambavyo kimepangwa” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Sasa katika wiki hili nitafanya mchakato wa kuacha kazi. Kuacha kazi kwangu hakutakuwa katika mfumo wa kawaida. Kutakuwa ni kwa kutoweka tu kazini. Naamini jeshi litanisaka lakini halitanipata. Na pia ndani ya wiki hili litafanya ziara ya kuangalia ni mahali gani katika nchi hii ambapo patatufaa kuweka kambi ya jeshi letu” Kanali Edson Makoko aliongea.



“Basi sawa. Nadhani tutawasiliana kwa kila hatua” bwana Shukuru Kizibo aliongea.

*******

ITAENDELEA

    
ITAENDELEA

Blog